Sehemu Ya Tatu (3)
Nilikua ni muoga sana kwa wakati huo. maana nilitokewa na sura ambayo naifahamu kabisa. na sii mwingine bali alikua ni BABA YANGU MZAZI ndio alinijia. ila hakunifanya chochote zaidi ya kuniambia
"umekuja mjini? utapata shida sana mwanangu... kama kuna mtu alikuambia usije mjini ni bora ungelimsikiliza huyo mtu"
"kwani hakua ni wewe?"
"hapana sio mimi"
"na huyo mtu ni mwanamke au mwanaume?"
"mi pia sijui"
Alikua akiongea kabisa lakini nikimshika hashikiki kabisa. Ghafla alitoeka bila kujua kaondokaje hapo mbele yangu... lakini kidogo moyo ulikua na amani kwakua hakua mtu mbaya. Lakini pia nilikua nina wasi wasi kuusu ile stori alioniambia jamila japo hakuimalizia yote. Niliamka pale chini huku nikiwa na maumivu mengi sana katika mwili wangu. Nilipanda kitandani na kujipumzisha zangu maana nilikua naumwa na vile vidonda vya mguu
BAADA YA WIKI MOJA KUPITA
Na leo ni siku ya juma tatu asubuhi. Nilipiga zangu mswaki kisha nikawa namsubiri broo atoke ili niongee nae kuusu kazi.. maana namtegemea yeye kuhusiana na jambo hilo... Kweli punde si punde broo alitoka na kuwasha gari yake. nami nikamfuata kabla hajatoka getini hapo
"shkamoo broo?"
"marahaba vp?"
"poa tu"
"vp kuna tatizo?"
"Hapana hakuna tatio ila kuna kitu naitaji tu kukuambia"
"ni kitu gani hicho?"
"Aaaaa ni kuusu kazi broo.. kwan si unajua nimeacha familia hivyo naomba unifanye na mimi niwe na mchakariko wa hapa na pale"
"sasa familia yako inaniusu nini mimi?? kama umekuja mjini chakalika mwenyewe mzee hapa ni mjini"
"lakini broo si unajua mimi sina ninaemfahamu zaidi yako?"
"sasa skia, tena umeitibu kuanzia sasa hivi nakupa wiki moja tu ya kuwepo ndani ya nyumba yangu"
Aliongea hivyo kisha akaondoka zake kazini. nilibaki na maumivu tuu juu ya majibu yake Yani ni bora nisingemwambia,
Basi baada ya broo kutoka mara mkewe alitoka na kunikuta nimejiinamia pale pale nje. Alianza kuniongelesha mambo ya ajab ajabu tu
"we vp mbona umesimama hapa? Eheheeeeeeee halooo unajipendekeza kua ndugu wakati hamuna hata undugu loooo aibuuu"
"hapana shemeji ka"
"weeeeeeeeeee ukome na jina lako hilo.. toka lini nikaolewa na kaka ako?"
"huyu mtu huyu ni kaka angu kabisa na kama kakuambia kua hana ndugu basi huyo kakudanganya"
"mimi sinashida na kuzijua porojo zako hizo"
"lakini shemu mbona mi sina kisa na nyinyi lakini naona unanichukia tu bure"
"hebu nipishe mimi kinyago mkubwa wewe"
"mmhh sawa ila vp chai ipo?"
"chai? chai ipi hio? au ulipeleka mkundu pale kupika hio chai? au baba yako kaleta sukari huku ndani?"
"bac nisamee shemeji"
"nimesema hilo jina silitaki kwanini husikiii? ( paaaa...kibao )"
Alinipiga kibao cha mkononi tena mkono ule ule weye maumivu makali
"Aaaaaaiiiiiiiiii umeniumiza aisee"
"kufa kabisa mwana kidagala we.. mschiuuuuuu Usiojua ndugu na kuja kumng'ang'ania hatibu wangu...Eti hatibu ni ndugu yaaanguuuu nyooo"
Aliongea mengi sana kisha akaondoka na kuelekea saluni kutinda nywele...
Ghafla mfanya kazi alitokea na kuniinua pale chini niliposukumwa na shemeji...
"pole kaka"
"asante sana dada angu"
"ivi kweli ni ndugu yako huyu baba?"
"ndio ni ndugu yangu"
"mmhh pole sana kaka angu.. na vp umekunywa chai?"
"mnhh wala sijanywa dada angu"
"ok nenda kule ndani kwako nakuletea chai ila uinywe fasta fasta asije kuku kuta"
"naomba nisindikize basi maana nilivyosukumwa. niliutikisa huu mguu"
"usjali kaka angu"
Dada jamila alikua akinionea huruma sana. hivyo aliweza kunikokota hadi kule stoo kwangu ninapolala siky zote.
Baada ya kuniacha ghafla aliniletea chai na chapati.. nilianza kuzila haraka haraka na kuzifakamia kwa spidi ili nisije kukutwa na shemeji...
Nilichua dakika mbili tu kuimaliza chai ile. Basi hadija alichukua vyombo vyake na kufuta ushahidi wa kua nilikunywa chai...
BAADA YA SIKU MOJA KUPITA
na sasa ni mida ya jioni kama saa 10 hivi nilikua nimekaa sebuleni naangalia tv.. Mara jamila alikuja hadi hapo sebulenihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"eti we mkaka? kwanini usiongee na kaka yako kwa haya anayokufanyia shemeji yako?"
"mmhh dada angu.. kaka yangu mwenyewe yupo hivyo hivyo alivyo huyu shemeji... Kwasababu nakumbuka jana nilimuambia anifanyie mpango wa kazi Lakini sikuamini kwa majibu alionipa kwakweli"
"najua yatakua yamekuumiza sana hayo majibu"
"ni sana kuliko unavyofikiria"
Basi mfanya kazi aliondoka baada ya kuskia honi ya gari ikilia...
Nami nilikua na wasi wasi juu ya honi ile. maana kama ni shemeji basi nijijue kua nitakuja kugombezwa muda si mrefu. Nilikua nimetulia tu nacheki zangu filamu fulani hivi ya kibongo..
Ghafla shemeji alitokea pale sebuleni Na kuniangaliaaaa bila kupesha hata jicho...
"hee hee hee hee hee nani kakuruusu ukalie sofa zangu?"
"shkamoo?"
"kamuamkie baba ako kuzimu mbwa wewe shuka kwenye sofa zangu haraka"
Nilishuka fasta kwenye sofa za watu kisha nikakaa chini huku uwoga ukinijaa telee
"afu nani kakuambia uwashe tv?"
"nimewasha mwenyewe"
Nilidanganya ila aliewasha ni jamila hivyo nikakubali kosa.. mana siwezi kumsingizia mtu wa watu japo ni yeye ndio kafanya hilo kosa la kuniwashia tv...
"ushakua fundi na kichwa wa hii nyumba ee?"
"hapana shemeji"
"nyamaza mbwa wewe usiejua hata ndugu zako... mschiuuuuu ( msunyo )"
Mara jamila katokea na kumkuta shemeji akinisukuma na teke kwenye ule ule mguu unaouma
"dada usimfanye hivyo kaka wa watu"
"shiiiiii kimya na wewe... nitakugeuzia kibao wewe oohoo nadhani umenisahau wewe... kwanza nenda kwenye kazi zako"
Mara mlinzi nae alikuja huku akiwa kashikilia kirungu chake mkononi
"kuna nini hapa dada?"
"si huyu mwehu kaja kufungulia tv utafikiri ni kwake vile. mbwa huyu"
"lakini dada? huyu si ndugu yake na mzee?"
"ana undugu wapi huyu wala hawana hata undugu... usikute hata ni jirani yake tu"
"kwahio kumbe hana undugu?"
"hawana undugu hawaaa"
"eeeee makubwa"
Mtoto wa kiume nilikua nimetulia tu kimyaa sina nikianza kulengwa na machozi na kujuta kwanini nilikuja mjini.
Manyanyaso yalizidi kuwepo katika nyumba hii kila siku sikosi kuuziwa na shemeji. kwani nilikua kama nakomolewa katika nyumba hii. ila maisha ya ndugu ndivyo yalivyo hivyo sio cha kufanya kwani hata sasa hivi yenyewe nimepewa wiki moja tu. ya kuwepo hapa katika nyumba yake.
Sasa siku moja niliitwa sebuleni na nilihisi kutakua na kikao cha familia..Lakini cha ajabu nilimkuta shemeji analia kabisa na anaonekana kua na hasira na mimi. ila kwakua sikua na kosa lolote lile kwahio sikupaswa kuwa muoga juu ya hilo.....
"rashidi?"
Broo aliniita huku akiniangalia kwa hasira mno. na hapo ndipo woga uliponijaa teleee.
"ndio broo?"
"umekuja mjini kutafuta maishaa au umekuja kugombana?"
"kugombana? kugombana na nani?"
"unajifanya hujui?"
Nilikula kibao cha mbali mbali na kuanza kulia ghafla tu....... Na silii kwa maumivu ya kibao bali nalia kwa kusingiziwa jambo ambalo silifahamu kabisa...
"sijui kitu broo"
"umemfanyaje shemeji yako?"
"Eee mungu wangu... Eti shemeji nimekufanya nini mamii?"
Shemeji alianza kupayuka yote anayoyajua yeye kuusu nilichomfanyia... ila mi siui nimemfanyia nini kwakweli
"hatibu yaani huyu mtu wako ni wakuja kunitusi mimi? Yaani huyu kinyago wako ni mtu wa kunirushia mkono kweli? Siamini kama naweza kutukanwa na kugombezwa na kinyago kama huyu.. na usipoliangalia hili mimi narudi zangu kwetuuuu"
Alikua akiongea huku akilia kwa uchungu kuashiria ni kweli nilimtukana lakini sio kweli
"haaaaaaaaaa shemeji mbona mi sijakufanya chochote mamii?"
"nimesema hivi? usipolifanyia kazi mimi naondoka zangu kwetuu"
"hapana mke wangu.. hawezi kukufanya uondoke bali yeye ndio aondoke ila sio wewe...... rashidi? sasa nasema hivi kachukue kila kilicho chako na uondoke zako ulipotoka"
"broo broo sasa na usiku huu ndugu yangu nitalala wapi kaka?"
"mimi sitaki kujua hizo shida zako... kwanza ulikuja mikono mitupu.. kwahio naomba unyooke getini haraka"
"kaka naomba unisamee kaka sintorudia tena"
Niliomba msamaha kwa kosa ambalo hata silifahamu kabisaaa...
Daaahh mtoto wa kiume leo ndio nimeamini kweli ndugu sio wa kuishi nao na hawana msaada wowote... na sio kila mwenye ndugu mjini ana maisha mazuri bali wengine tunavumilia tu.. kwani hata hayo mateso sikuanza leo. lakini nimevumilia hadi nimefikia kufukuzwa katika nyumba za watu.. Nilitoka moja kwa moja huku nikiwa na mguu wangu wa tatu ( magongo ) Nilifunguliwa geti lakini mlinzi nae roho ya huruma pia ilimjia ghafla tu
"mmhh ndugu yangu kiukweli sina cha kukuseidia ila chukua hii elfu 10 na hili koti langu vikuseidie tu ndugu yangu... na naomba unisamee sana kwani mateso yako ni tuu mach kwakweli"
"usijali kaka tupo pamoja na nakushukuru kwa huruma yako"
Sasa kabla sijatoka nje mara jamila nae kaja huku akiwa muoga muoga
"chidi? nakuombea tu ufanikiwe huko uendako kwakweli ila mimi sina cha kukupa zaidi ya huu mshahara wangu wote nakupa wewe na chukua hiki kitenge kitakuseidia hata kujifunika chidi.. uende salama"
Jamila alinipa shilingi Elfu 30 ambao ni mshahara wake alioupokea juzi tu...
"nami nashukuru sana kwa ukarimu wenu nami naami mungu hatoniacha peke yangu"
Sasa nikiendelea kuwashukuru mara ghafla niliskia sauti ya broo
"kuma mayo bado hujaondoka tuu?"
Nilitoka mbio baada ya kuskia hivyo ila imeniuma roho kwa kutukaniwa mama yangu... ila sijali yote ni maisha tu... na naamini ipo siku na mimi nitatusua tu...... Daahh nilikua nipo hapo getini nikiendelea kufikiri pakwenda..
Niliangalia tu juu ya mbigu na kuongea neno moja tu
"ONE DAY YES"
Nilikua najifariji kwa maneno niliokua nikiongea mwenyewe kwani wakati huo nilikua nina hasira na maumivu ya mwili. Kwa kufukuzwa na kaka yangu wa damu kabisa Kisa ni mwanamke? daahh siamini kabisa kama leo nipo nje ya nyumba ya kaka yangu tena tajiri mkubwa hapa jijini arusha.....
Basi nilipotoka pale nilizunguka nyuma ya nyumba hio ya broo. wakati huo ilikua ni mida ya saa 4 usiku afu kuna baridi kali huku mvua ikianza kunyesha, Niliingia kwenye nyumba moja ya jirani na hapo. nyumba hio ilikua haijaisha kujengwa hivyo nilivaa lile koti la mlinzi na kutandika boksi ndani ya nyumba hio ambapo kulikua na vinyesi vya watu na pia ilikua ni kama nyumba ya mambwa.. kwani ilikua haina hata madirisha ya chuma ( magrili ) yaani ilikua ni behewa tuuu..
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kiukweli usingizi hauji kabisa kwani ndani ni ndani na nje ni nje.. Nimelala na vinyesi karibu nimelala na madogi pembeni.. Yaani nilikua kama mnyama vile. Lakini mungu sii asumani siku hio ilikwisha na sasa ni asubuhi....
Niliamka asubuhi sana kama saa 11 hivi alfajiri, Nilianza kujikokota na magongo yangu huku nikipita katika moja ya njia ambazo hata sizijui kwakweli.... Nilipita mahari na kukutana na vijana fulani hivi
"we vp saa hizi unatoka wapi?"
"mmhh?"
"mmhh nini? sema unatoka wapi?"
"asee natoka kulala jamani"
"ok ni furu areef sasa Ebu changia kidogo tupate ata dawa kidogo"
"dawa gani tena? kwani na nyie mnaumwa?"
Walinishangaa huku wakikonyezana kihuni
"oyaaa we wa wapi wewe? ata dawa ujui? ebu toa ata jala kimtindo areef"
Mmhhh sasa kwa vile walivyo vaa nikajua tu hawa ni wauni na nikikaa vibaya kale kapesa nilichopewa na jamila na mlinzi wataichukua hawa..
"ebana jodaa unae sanda areef?"
Eee sasa kuskia sanda nikajua heee apa kifo changu kimefika. lakini sana sio sanda kama sanda.. bali ni kikaratasi fulani cha kuekea bangi... ila mimi nilikua sijui kua ndio kinaitwa hivyo..
"jamani sasa sanda za nini tena ndugu zanguni?"
"afu we boya acha kutuzingua wewe tutoa iyo chambi tusepe Ama nini jodaa?"
"ni yechu yechu areef Au kama vp mbust kichere azinduke uyo"
Sasa niliposkia kubust nikajua hapa visu vya tumbo vitaniusu. maana mijitu ya arusha kwa fujo ndio wenyewe....
Niliona hawa wanaitaji pesa na kwakua nilikua na shilingi elfu 40 niliopewa na wafanyakazi wa broo... nilijisachi ili niwape ata elfu tano. maana wakisema wanisachi watachukua zote. Nilipata elfu tano kisha nikawapa...
"vp mbona umetoa kwa kuesabu? au una zingine nini? ebu tuone"
"Asee sasa si nishaawapa hio wazee?"
"Heeeeeee unamfokea nani we boya? nakuuliza kimbarata unamkoromea nani?"
"niachieni bhana"
"vunga we chalii tutavunja huu mguu mwingine we boya"
"lakini asee nimewakosea nini ndugu zangu?"
Walianza kunisachi huku mmoja kanishika. ila sikua na uwezo wa kuleta fujo kwani sikua na nguvu ya aina yeyote ile maana mguu mbovu mkono wenyewe pia mbovu tena ndio kwanza hata kupona havina hata dalili. Basi nilitulia tu kama dudumizi na kuchomolewa pesa zote nilizokua nazo...
"jamani nipeni ata iyo elfu 10 moja tu. maana jana sijala kabisa wazee"
"nani mzee wewe? peleka usambaa kwenu uko"
"oya jodaa mtemee iyo ng'ora yake ( simu yake ) kwanza haiuziki hii mpe tu"
"chukua uchafu wako endelea kutumia"
"wazee ata kaki basi niachieni"
Daa niliambulia kupewa simu yangu tu maana haiuziki kabisa...
Jamaa waliondoka na pesa yangu yote. na wakati huo mtoto wa kiume sina mbele wala nyuma na wala sijui kazi nitapata wapi na hata kama nikipata kazi je? nitaifanyaje? maana mguu na mkono wake havina kazi kabisa.... Basi niliendelea zangu kuchechemea na kuelekea mahali ambapo hata sipajui kabisa... kwani hata stend yenyewe tu siijui. Niliondoka hapo mpaka nimekutana na lami
Nikicheki saa ilikua ni mida ya saa 1 kasoro asubuhi... Kiukweli nilikua ni mtu mwenye njaa sana hivyo sikuona haya wala aibu ya kuelekea dampo na kutafuta hata chochote cha kutia tumboni.... maana jana nilifukuzwa kabla ya chakula. afu ukizingatia vyakula vyenyewe ndio hivyo...
Nilianza kutafuta ata maskonzi yaliotupwa kwenye dampo hilo. Nilikua sina kifurushi chochote nilichokibeba hivyo nilikua nipo mimi na gongo langu moja. Nilianza rasmi kula vyakula vya dampo. watu walikua wakinisikitia sana kwasababu shida zangu mimi zilipitiliza kikomo. kwani nilikua naumwa na afu bado sijapona afu bado hata usafi sina...
Sasa yapata wiki moja toka nifukuzwe na ndugu yangu.
Staili ya kula dampo na kulala dampo nilishaizoea maana sikua na pakula wala pakulala. na ulema wangu upo pale pale....
Siku ya leo dampo halikua na chakula hivyo nilianza kutembelea madampo yote makubwa makubwa na kukosa chakula kabisa.... Sasa nitafanyaje? maana hata kazi nashindwa kuomba maana sintoweza kufanya kazi kutokana na ukilema nilionao... Niliingia kwenye hotel ndogo ndogo na kuanza kuchangua madude ya kuekea vyakula vibovu... ambavyo kwangu naviona kama almasi vile. nilikutana na makapurwa wenzangu na kuungana nao na kuwa kitu kimoja.... Lakini mbaya zaidi wenzangu walikua ni waizi wa kupindukia. kwani wanajulikana hapo mjini kwa uizi.
WADUDU WA DAMPO ndio jina lao wanalotumia kujiita... Nilianza kujiunga nao rasmi kwakua wenzangu wanazijua sehemu zenye vyakula hivyo nami sikutaka kuwaacha wafanye yao. Walianza kunipa masharti yao na kuniambia kua
"sikia we mtu... Afu we ni msambaa Ee?"
"ndio"
"Aahahahahahaha duuu"
Walicheka kwa wote huku wakiangaliana.. . sasa nikajiuliza kua watu kama hawa wenye shida ya kupindikia nao wanafurahia kama mtu na pesa zake... Nami niliona haina haja ya kufikiria sana kuusu maisha....
"sikia we chaliii... ivi utaweza kazi wewe?"
"aaahh broo nitaweza"
"hahahahahahah uuu sasa taweza kukimbia wewe?"
"lakini nikipona nitaweza"
"sasa we pona kwanza afu ungana na sisi. maana sisi kazi zetu ni kukimbia muda wote. nadhani utakua umenielewa"
"sawa ila kwani hio kazi yenu haina seksheni zingine tofauti na hio?"
Mara mmoja akatoa wazo fulani
"ooiiii dadu?"
"sema totoo?"
"mimi nina wazo juu ya hilo"
"lete wazo"
"unaonaje huyu chalii akawa MR MAP?"
"yes safi sana totoo coz umetoa wazo zuri sana"
Niliuliza hio map ni nini
"wazee hio map ni kazi gani hio?"
Totoo ndio alinijibu kwa ufasaha tena bila kunificha kitu chochote
"sikiliza bhana naniii nani vile ulisema?"
"rashidi"
"ok sikiliza bhana rashidi... sisi kazi zetu ni uizi tu, tena uizi wetu hauchagui muda... yaani sisi tukiona pesa mahali hua hatuogpi kitu, hata kama askari wapo...hivyo ukiambiwa uwe mr map... basi ujue tumekuchagua uwe unatuangalizia muonekano wa pesa... mfano tukikutuma katika jongo fulani basi kazi yako wewe ni kuangalia njia za kutoke na njia za kuingilia.... yaani kwa kifupi utakua mchora ramani wetu maana wewe huwezi kukimbia.. kwahio hicho ndio kitengo chako kuanzia sasa hivi"
Kabla sijakubali nilianza kukumbuka familia yangu huku machozi yakinitoka kwa fujo. Na kukumbuka mateso yote ya nyuma mpaka sasa daahhh bora nikubali tu
"poa nimekubali jamani nifanye kazi na nyie"
Basi na mimi nilianza kua miongoni mwa watu wabaya tena makapurwa ( wachafu ) wa kutupwa
Siku moja tulikua katika hotel moja hivi ndogo ndogo tukitafuta chakula cha mchana katika zile ndoo za kuekea uchafu ( dastbin ) Tukiwa tunagombea makoko ya pilau.... Sasa mara kulitokea gari moja kali na kushuka mtu mmoja mwenye pesa zake. Na alifika hapo kwa kuja kumuona mtu.. maana alikua kama anaangaza angaza macho.. Alirudi kwenye gari na sikujua alichokifanya pale
"oyaaa chidi? nafasi yako ihusike pale"
"nafasi gani tena?"
"chora map tuanze kazi babaaa"
"daaahhh wezee kweupe ivi wazee?"
"sisi tulishakuambia kua hatuchaguagi muda"
"lakini wazee mbona mzee wa watu hana hata shida yule muislamu wa watu"
"hizo huruma za kisenge senge sisi ndio hatuzitaki sawa? tushaibia hadi mama zetu sembuse yeye??"
"oyaaa chaliii soma ramani chapu tuanze kazi"
"ok poa nipeni muongozo basi"
"nenda pale karibu yake msalimie afu muombe hela kama vile omba omba Akupe asikupe sisi tujulishe kama mkwanja upo tuvamie chapu"
"daah poa ngoja nijaribu"
"sio ujaribu..sisi hatuna hizo mambo za kujaribu"
"poa"
"na ukitusalitiii utajuata kuzawa duniani"
"acheni mkwara basiii"
"we nenda kafanye kazi bhana chalii"
Basi mtoto wa kiume kwa mara ya kwanza ndio naianza kazi ya uizi.... Sikusita kumsogerea yule mzee na kumsalimia.
"shkamoo mzee?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"marahaba ujambo? Khaaa vp kijana mbona una vidonda kila mahari karibia mwili mzima?"
"daahh mzee wangu we acha tu ni maisha mzee"
"ok haya ulikua unasemaje?"
"mzeee? haki ya mungu vile mzee mi sijala toka jana mzee wangu.. sasa naomba uniseidie angalao hata senti nikapate hata skonzi kavu tu"
Nilikua nalia machozi ya uongo na kweli huku nikimuangalia kwa umakini sana huyu mzee...
Sasa ghafla mzee alitoa kitita cha pesa na kuanza kuhesabu moja baada ya nyingine.... Na kunipa pesa isiopungua elfu 50 tena ni mpyaaaaaa..........
Nilishindwa kuamini macho yangu.. maana hua naambiwa matajiri hua hawaseidiagi watu...
"saa nyingine unapomuomba mtu pesa usijaribu kumtaja mungu kabisa. maana wengine hatumuamini mungu sisi.. sawa?? kwahio hizo haki ya mungu zako ni huko huko unapoishi ila sio kumtajia mtu haki ya mungu... umenielewa?"
"ndio mzee asante sana na mungu akuja oooo samahani mzee kwa kusema mungu"
"najua sio kosa lako kijana"
Sasa mtoto wa kiume nilisahau kazi ilionileta hapo... mpaka wenzangu wakanishtua kwa mbaliii
"oyaaa unauweka sana chalii"
Nilitikisa kidole cha mwisho kuashiria "ngojeni kwanza" Sasa mzee alianza kuniuliza maswali
"umefanya nini mpaka umevunjika miguu mikonoo hebu ona sasa mabendeji yenyewe yamechafukaa ni nini kilikukuta kijana?"
"mzee ni maisha tu.. kwani nilipata ajali mzee"
Sasa kuangalia ndani ya gari niliona brifkesi iliofunuliwa. afu imejaa wekundu wekundu tupuuu... Duuuu nilipepesa macho kinafki na kujifanya sikuziona zile pesa...
"pole sana kijana wangu... pole sana. ila nahitaji nikupeleke hospitalini kijana"
Mara wale jamaa wakaanza kuja bila kuwapa ruksa ya kuja.....
Sasa nikajiuliza kua nimuambie kua watu hao wanaokuja sio wazuri au nisimuambie?? maana mzee keshaonesha kuniseidia kunipeleka hospitalini.... Nilimuangalia yule mzee kisha nikawaangalia na hawa WADUDU WA DAMPO wanavyokuja huku wakiwa wameshika visu..... na walisema nikiwasaliti kitu watanifanya sitokaa kusahau hadi kufa
Niliona hapa hakuna jinsi zaidi ya kumseidia tu mzee... nilianza kuondoka taratibu huku nikasema kwa upole ili wale wadudu wasisikie kitu. na asikie mzee tu
"mzee mabandidu hao wanakuja"
"eee?"
Sasa mzee hakuskia vizuri Afu wadudu ndipo walipofika na kumpora ile brifkesi... Sasa kukimbia kwao walinisukuma mimi na kudondoka chini... ili mzee asijue kua nipo nao. Roho iliniuma sana kuona mzee wa watu akichanganyikiwa huku akija kuniamsha pale nilipoangukia....
"vp kijana upo salama kweli?"
"ndio mzee nipo salama.. ila si upige simu polisi mzee?"
"ahahaha hakuna shida kijana kwani huo ni ujana wao ndio unawasumbua tu"
"lakini wanaonekana kama wamechukua kitu mzee"
"ndio wamechukua kiasi kidogo cha milioni 10 tu."
"haaa mzee pesa zote izo unasema ni kiasi kidogo?"
"ndio kwa hata hapa kuna mtu nimekuja kumpa msaada sasa ndio nilikua namsubiri"
"daaahh mzee wangu nashukuru sana mzee wangu kwani unaonekana kunijali sana mzee"
"usijali kijana kwani napenda kujali bina damu kuliko pesa... ila vp si upo salama kijana?"
"ndio nipo salama mzee usijali"
"hawajakuumiza kweli maana wamekusukuma kweli aisee"
"usijali mzee wangu nipo salama kabisa"
"ok chukua hii biznesi kadi yangu utanitafuta ili tuendelee kuseidiana kijana sawa?"
"sawa mzee nshukuru sana mzee wangu"
Mzee aliwasha gari na kuniacha pale chini nikiwa najiuliza na kujilaumu kwa ujinga nilioufanya kwa mtu kama huyu.. Lakini haina shida nilitoka na kuelekea maskani tunapoishi na kuwakuta machizi wanaesabu pesa
"afu we msenge unzingua sana wewe... mbona ulianza kupiga story na yule mzee?"
"Eee asee uyu chalii anazingua kichizi kama vp tumtemeni wazee"
"ni kweli we jomba uezi kazi"
Walikua wakiongea kila mtu yake huku mimi nikiwaangalia tu, Sikuwajibu chochote
Mara totooo katoa wazo fulani
"oyaa dabu? mtoe chake asepe awezi kazi na sisi"
"oyaa wazee sio kua siwezi bhana si mnajua ndio dei ya kwanza hii?"
"waapi wewe ulikua unapiga stori pale"
"sawa lakini ilikua ni hali ya kumlegeza kimtindo tuu"
Wakaangaliana kisha wakanisamee kwa kosa nililolifanya leo
"sawa tunakutema ila uboya mwingine atutaki sawa?"
"poaa"
Sasa nikajiuliza kua kama hawa jamaa wanapiga pesa ndefu hivi? kwanini wasiache? maana mi naamini nikipiga hata milioni moja naacha uizi kabisaa..
Walinikatia chakwangu huku wakiniambia kua
"pesa tunazopiga hua tunafanya maendeleo hivyo na wewe fanya maendeleo"
"sasa kama mnafanya maendeleo mbona mpo hivyo makapurwa na bado mnakula vyakula vichafuu Afu mbaya zaidi uizi hamuachi"
Walicheka huku wakiangaliana tu.. na mmoja kusema kua
"usituone hivi.. sisi tuna mijengo kwa kazi hiii tulionayo... wengine wanamiliki mabiashara yao hapa mjini ila hatutaki kuisaliti kazi kwasababu ndio imetutoa kimaisha. hivyo wewe hulingani na sisi hata kidogo...kikubwa kaza buti na wewe uwe kama sisi"
"yaani unataka kuniambia wewe una nyumba?"
"Aaahhh sio nyumba tu.. bali mpaka magari na mabiashara tunayo ila hatutaki kujulikana kwa jamiii"
"mmhhh yaani mnanishangaza wazee"
"utashangaa sana ila we kaza buti tu"
Nilibaki kimya maana kuona watu wana mijumba na migari kwa ajili ya uizi.. na uizi wao haujali muda.. yaani kikubwa paonekane na pesa tu
Walinipa kiasi cha shilingi laki 5.... nilichokifanya ni kwenda hospitalini na kwenda kuchekiwa kwanza.... Nilibadirishwa mabendeji yote na kupakwa dawa.. Iligarimu shilingi laki moja kubadiri mabendeji yote... Sikutaka kukaa pale hospitalini kama walivyotaka nikae miezi 6 kwanza eti ili vipone... heeee angejua maisha yangu yalivyo asingesema kitu... Basi niligoma kukaa hospitali na kutoka zangu mtaani.....
Cha pili nilienda M-pesa na kuanza kutuma pesa nyumbani kwani angalau sasa hivi hata tisheti nabadili kuliko mwanzo nilikua nina nguo moja tu tena ni zile nguo za broo ambazo kiuno cha suruali utafikiri ilivaliwa na MADILUU
"habari broo?'
"poa vp?"
"poa.. asee naitaji kurusha pesa kwa watu tofauti tofauti"
"ok hakuna shida"
Nilianza kumrushia mama angu shilingi laki moja... kisha na mke wangu nikamrushia kiasi kama hicho hicho cha laki moja.... bila kumsahau kaka yangu juma nilimrushia shilingi elfu 50 tu.... Nimefanya hivyo kwasababu pesa yenyewe haikai hata kidogo na nikisema niiweke nitashangaa na mimi nimeibiwa... Nikijicheki mfukoni nimebakiwa na laki moja na nusu.. nilinunu vocha na kuanza kuongea nao na kuwaeleza kila kilichonitokea juu kufukuzwa kwa kaka.... kisha nikamalizia na mke wanguhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"jamani mume wangu nimekumis kweli yani"
"usijali mke wangu... kwani ndio naendelea kutafuta hivyo"
"ila inaonekana kaka yako kakutaftia kazi nzuri"
"nini? yaani mi na na na AAAAOO ookee Eee kazi nzuri ndio"
Sikutaka ajue maswaibu yalionikuta kwani namjua mke wangu ana roho ndogo sana hivyo naweza kumtafutia matatizo kama nitamuambia kua nilipata ajali afu kaka yangu amenifukuza kwake... kwahio sitaki mke wangu ajue.. japo mama na broo nimeshawaambia kila kitu ila yeye mke wangu sitaki ajue.
"sasa hivi utakua umenenepa ee?"
"nani mimi?"
"sasa naongea na nani kwani?"
"mmhh ungejua wewe wala usingesema"
"nisingesema kwa jinsi ulivyo bonge"
"acha utani bwana.. ebu nipe saidi niongee nae nimemisi kweli boy wangu"
"heee aongee?? ulimuachia mdomo nini?"
"aaahhh mfinye kidogo ata nimsikie bwana"
"bwana mi sitaki kwani si utakuja"
"aaahhh bwana nimemmis side wangu"
"haya basi unamsikia?"
"haaaaaaa we umemfinya sana wewe mbona hanyamazi?"
"si ulitaka umsikie wewe"
"aisee usikute umemuumiza aiseee wewe"
"Enhee kwaio utakuja lini?"
"mmhh sijui hata nitakuja lini"
"bwana baba saidi njoo mi nimemisi hio nanii?"
"usijali nitakuja"
"mmhhh haya mwaya kama ndio unatususa"
"afu sikia naomba sasa hivi mtoto anywe liuji la ulezi.. na sio dona tena sawa?"
"mmhhh unampenda mwanao wewe"
"sanaaaaa yani kuliko hata wewe"
"nini? basi namfinya tena"
"aaaaaaahh we basi nakupenda hata wewe eeee?"
Basi ilikua ni moja ya utani mimi na mke wangu... juu ya kakijana ketu
Basi nilirudi zangu maskani baada ya kuongea na familia yangu.
"oii chidi? vp naona umeenda kucheki mguu sio?"
"ndio asee si unajua bana nina muda sijabadirisha hata bendeji asee"
"ni furu fururu areef"
BAADA YA WIKI MOJA KUPITA
Tulikua zetu mtaanzi na nguo chafu chafu ili tuonekane makapurwa zaidi
"aseee chidi? yule broo vp tumlie rada nini?"
"ndio... ila mbona kama anaingia pale benki?"
"nenda basi kachore map Afu kama mkono una uzani utushtue kwa ng'ora au sio?"
"poa"
.
Basi kama kawa na magongo yangu nilisogea hadi karibu na benki nikijifanya kuomba omba pesa pale kumbe nia yangu ni kuchora ramani fulani... Kwa kumsubiri umtu alieingia ndani ya benk hio.
punde sii punde yule mtu alikua anatoka na brifkesi yenye uzani kidogo. Niliwatumia sms chapu na kuja kufanya yao.... Kama kawa hua hatukosei
Nilijikuta kazi ya uizi naizoe kadri kila siku zinavyozidi kwenda. Nilikua naijali sana familia yangu. mpaka wananiambia kua huenda nafanya kazi T.R.A nini.... maana sijawahi kuwarushia kiasi kidogo hata siku moja... Nilitikea kuipenda kazi ya uizi lakini kitu kinachoniuma zaidi ni kuibia watu wasio na hatia yaani hatuchagui wa kumuibia.... hata awe mwema kiasi gani. Hicho ndicho kinachoniuma kwakweli. maana labda ingefaa tuwaibie mafisadi.. wazee wa Richmond au Epa au Escrow.. kuliko kuibia hata mtu anaeganga pia haachwi duuu.... leo niliamua kuiacha kazi ya uizi kabisa..
"asee dabu, totoo, chuda, ngati? mi naacha kazi"
"aaaaaaa sasa ni swaga gani izo? au unaacha ili utuchomee nini jombaa?"
"sina maana hio kua naacha ili niwachomee ila naitaji nifungue biashara yangu binafsi"
"Eeee? ushapata pesa sasa unatulingia si ndio?"
"wazee mi naomba tuelewane kua siachi kwa ubaya jamani"
"kwaio hebu tuambie kilichokufanya uache kazi ni kipi haswa?"
"tatizo ni kwamba hamuangalii mtu wa kumuibia... afu mi napenda kuacha tu bila hata ya sababu.. kwahio naombeni mniache niache kazi hiii"
"okee poa kwaheli kaka na tunakuombea biashara njema eee?"
Nilitoka zangu maskani japo hawakupenda niondoke ila najua hapo nitakua nimejenga chuki juu yao. Lakini sikujali kitu kwani nimelelewa katika madhingira ambayo ni ya kihuruma huruma na kumjali mtu hivyo uizi kama huu ilikua ni shida tu ndio ilinifanya niwe mwizi......
Basi kutokana na nilikua na vipesa pesa kidogo. hivyo nilipangisha chumba cha biashara ambacho kipo bara barani. lakini nitakua nikilala humo humo ndani.... Sasa kwakua sijaanza biashara yangu ya mtumba na viatu.. nilifungua kashuu shaini kangu ili nijichukulie vimia mia vya kushona na kupaka rangi viatu vya watu...
Toka niachane na wale jamaa sasa yapata kama wiki moja hivi. Na maisha yalikua yanaenda vizuri tu tena ni bora sana kuliko kua muizi...
Sasa nikiwa zangu nje ya fremu yangu ya biashara ( chumba ) nilishangaa kuona askari wakija pale nilipo na kunisomba mzima mzima...
"ooyaa broo kwani nimefanyaje asee?"
"utajulia mbele ya kituo pumbavu sana nyie"
"ok ngoja basi nifunge chumba changu broo"
"tweeeendeeee"
"broo fremu yangu ipo wazi na ndipo ninapoishi broo"
Kiukweli askari ni watu wa ajabu sana. kwani huezi amini alinibeba hadi kwenye gari na kuondoka na mimi. nilibaki kuiangalia fremu yangu ikiwa wazi... na pesa zote zipo kule ndani katika begi langu... Nilihisi kuonewa kabisa. Sijakaa vizuri mara meseji imeingia..
Kuisoma hivi.. iliandikwa
"tumeanza kuchoma kabla hujatuchoma. sasa we nenda kapotelee huko"
Roho iliniuma sana kuona kua ni watu niliokua nao ndio walinichomea ili nipotelee
"wewe yaani unachezea simu mbele yetu? hebu ile hio simu"
Simu yangu ilichukuliwa na afande mmoja na kuitupa kwenye mtaro
"aaaaaYaaaa afande namba zangu aisee afande"
Alianza kunipiga vibaya mno kabla hatujafika hata kituoni aiseeee...
Tulipofika kituoni tulishushwa vijana kadhaa tuliokamatwa siku hio... kwanza tuliwekwa sero. ili tufunguliwe mashtaka...
"afande? huyu kijana kesi yake ni kubwa mno"
"kwani ana kesi gani?"
"afande huyo kijana ndio kiongozi wa WADUDU WA DAMPO"
"haaaa haaaaa haaaaaa haaa pumbavu sana kumbe ni kakijana kadogo tu? mi nilijua ni MIDUDU YA DAMPO kumbe ni VIDUDU VYA DAMPO? pumbavu sana wewe"
Nilianza kupigwa virungu katika magoti na viwiko vya mikono... Nilipoangalia kwa pembeni niliona mijamaa kama miwili hivi nayo ipo sero na sijui yana makosa gani.. ila walikua wananiangalua kweli. Mpaka niliogopa...
"sikia kijana. hapa sero una siku tatu tu.. za kuwepo hapa na asipotokea mtu wa kukuekea dhamana basi ni jela moja kwa moja sawa kijana?"
"nyie nipelekeni tu.. kwani sina hata mtu ninaemtegemea hapa mjini. na sina hata ndugu hapa mjini"
"wewe kaa tu kwa sheria za sero ila zikipita siku tatu ndio utakwenda jela"
Hii ndio mara yangu ya kwanza kuwekwa sero ( mahabusu ) nilikua naogopa sana kwakweli maana sijawahi kuingia jela wa sero... sasa leo ndio kwanzaa nakutana na mijibaunsa humu sero.....
Ilipofika mida ya saa 12 jioni tuliletewa ugali mkubwa na maharagwe. Daaahhh maharagwe yenyewe yalikua ni uozo tupu. yaani mpaka wadudu unawaona kabisa lakini huruusiwi kuchambua. yani ukikuta dudu we kula tu. sasa nilikua mimi ndio kwanza wala siwazi maana nishakula wadudu sana kule dampo. kwahio siwazi kula ugali na maharagwe mabovu.. Sasa cha ajabu niliona wala mabaunsa wawili wakiletewa wali. kana kwamba kama una pesa basi ugali na maharagwe havikuhusu tena..... Nilitamani ule wali na samaki ila sema pesa sina....
Mara yule baunsa alinisogezea sahani yake na kuniambia nile mimi hio sahani. haaa nami sikuvunga niliisogeza sahani ile na kuutandika ule wali.......
Baada ya kumaliza sasa nimeshiba tukaambiwa sasa ni muda wa kulala. Heee nilishangaa kuambiwa tulale saa hio hata saa moja usiku bado.. Ila utafanyaje. tulilala afu tukaambiwa hakuna kugeuka wala nini.. hadi saa 8 usiku ndio kugeuka upande wa pili.... daahhh usingizi ulikua hauji kwa kuziwazia pesa zangu kule kwenye ile fremu kule na sijui kwanini nilisahau kuzitupia M-pesa... duuu naombea kutokee msamaria mwema afunge tu ile fremu bila kuikagua kitu....
Ilipofika saa 8 usiku nyapara alipiga fimbo chini na kusema kua
"upande wa pili sasa"
Watu wakageuka na ambae hajageuka anakula fimbo... maana tumejipanga kama ndizi.
Sasa saa ngapi sijaskia yule baunsa akiniulizia na usiku huo.
"oyaaa we dogo mgeni uko wapi?"
Iiiiiiii nilianza kuogopa kwa kuskia hivyo.
"oya nyapara?"
"sema babu?"
"yule dogo kalalia wapi?"
"yupi uyo?"
"yule aliokula nguvu zangu"
"aaaa sijui kalalia wapi.... we dogo uliokula wali wa watu uko wapi?"
Niliskia ila nikavunga kama sisikii vile
"aisee njoo umtafute mwenyewe bhana"
Aiseeee tumbo lilinikata kwa uoga... huku nikijiuliza huyu jamaa ananiulizia wa nini sasa? Saa hizi usiku wote huu.... Yule jamaa alikuja hadi maeneo tuliokuepo... sasa kulikua kuna jamaa wa karibu yangu ananijua
"oyaaa we si ndio unatafutwa wewe"
"Aaaaa vunga chalii yanguu"
"nivunge nini bana we jitokeze tuu... au hadi aje aniamshe mimi nini?"
"vunga basi jombaa"
"mmh tatizo unapenda kula vya watu"
"oyaaa mbona unakula mdomo sana asee"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"we utajua mwenyewe bhana"
Sasa kumbuka sero au jela hua hakunaga taa wala nini. na ndio maana tulikula mapema.
"oya we dogo si nakuita kuma mae wewe"
Nilinyamaza kimyaaaaaa
"oyaa nenda bhana utafanya tuje tuamshwe sisi wengine"
"aisee vunga chali yangu tukitoka ntakutoa we vunga tu"
"aiseee mi nasema ujue... maana hata mimi jana niliponea chupu chupu"
"kwani ananitafutia nini uyu jamaa?"
"heeeeeee hujui?? nenda kalipe wali wa watu uko"
Mara nyapara kanijua kua ndio mimj
"aisee babu mtu wako uyu apa asee"
"yuku wapi kuma mae?"
Aisee nilikuja kubebwa juu juu huku napelekwa kule alipokua analala yeye.... Aisee nilianza kupiga kelele japo haikuseidia kitu aseee
"afandeeee afandeeeee uuuuuuuwiiiiii afandeeee aaaa afandeeeee?"
Nilipiga kelele lakini wapi.... tena huku tena namuona nyapara anakuja na katochi cha simu... huku akisema
"afande keshalala na mke wake huko.. we tulia nawe upate wako... ili upunguze ulafi wa kupenda vyakula vya watu... pumbavu wewe.... Aisee babu eee? shika katoshi hako mulikia"
Nilikua sina jinsi ya kujitetea juu ya hilo, maana kila mtu humo ndani alikua yupo kimyaaa wakiskilizia tu mambo fulani yaendeleee nikaona wacha nipige hata kelele kidogo nimuite afande aje atoe msaada kidogo maana nikichelewa tu apa napakatwa na uyu jamaaa.. tena ukizibgatia nina mguu mbovu na mkono wake.. hee yaani ndio kabisaaa
Basi mtoto wa kiume nilianza kupiga mayowe makubwa ya kumuita afande, lakini makelele yangu yote hayakufanya kitu chochote
"afande keshalala na mke wake huko.. we tulia nawe upate wako... ili upunguze ulafi wa kupenda vyakula vya watu... pumbavu wewe.... Aisee babu eee? shika katoshi hako mulikia"
Yaani niliposkia tu hivyo yaani nikajua leo sina changu yani ni lazima niliwe 0714 maana nimekula wali wa watu na samaki mkubwaaa
Sasa tukiwa katika msumbuano japo sina nguvu ila kukubali ndio mbinde....
Ghafla kuliwaka mwanga mkalii. yaani kulikua kama kuna umeme hivi. ila taa yenyewe haionekani ilipo Yaani hata mwanga wa umeme ukiuona utajua tu huu mwanga unatokea wapi lakini huu hauonekani chimbuko lake. na umewashwa kama umeme vile.... Sasa kwa hali ile kila mtu alianza kushangaa kwa kuona mwanga wasioutegemea maana chumba tulichopo hakuna umeme wala kibatali au mwanga wowote ambao utatoka hata kwa jirani.... Sasa hata waliolala waliamka na kushangaa mwanga huo wa kimaajabu na mwanga wenyewe una rangi ya balbu za tambi... yaani zile balbu ambazo zimejivingiisha kama tambi tambi vile... au rangi ya choblaiti. Kiukweli wote hakuna ambae hakua ila mimi nilitambua tu. kwani vitu kama hivi vilishanitokea sana tu.
Na hapo ndipo nilipo ponea chupu chupu ya kulipia chakula cha watu maana kila mtu alikua muoga. tulikaa macho huku mguu wangu ukiwa unauma sana maana lile lijamaa sijui lilikua linataka kunikunja staili gani daahh Kiukweli namshukuru sana huyu aliewasha mwanga wake wa maajabu. Watu wengine walikua wanaomba ardh ipasuke waingie chini... Maana ni ajabu kubwa mahabusu au sero au jela kuwepo na taa usiku... itashangaza sana
Basi tulikaa macho vile vile tukiushangaa mwanga. mpaka ilipofika mida ya saa 12 asubuhi na ule mwanga nao ukapotea.. ila saa hio hakuna mtu ananitamani tena. ilipofika mida ya saa nne niliitwa na kuulizwa ulizwa maswali ya hapa na pale
"rashidiiii?"
"ndio afande?"
"njoooo"
Nilikwenda tena kwa adabu zote na taazima kabisaaa
"ndio afande?"
"Eheeeee tunahitaji utuonyeshe wenzako wako wapi?"
"mmhh afande mi sijui walipo"
"utapotelea jela kijana oohoo we wateteee tu"
"mzee hapo walipokua wakiishi mwanzo wamehama. na sikujui huko walipohamia"
"utakua unajua wewe... rudi sero kesho mtoa azabu akija utasema yote"
Nilirudi sero huku nikiwa na wasi wasi juu ya maisha yangu na familia yangu kwa ujumla.... Sasa sijakaa vizuri mara kuna vijana wawili wengine wameletwa. ila siwafahamu kabisa
Kesho yake mida ya jioni tuliitwa mahabusu wote, na kuulizwa kua kuna wale waliomaliza siku tatu humu sero.. hivyo muda wao wa kuingia jela umefika... kwahio naita kwa majina Aliita kwa majina lakini mimi sikuitwa maana ndio nina siku ya pili toka nije hapo sero. Walitoka wale mabaunsa wote. mpaka lile lijamaa huku likiniangalia kwa hasira hio daahh nikawaza kua kama na mimi nikienda jela ni lazima nikutane nalo huko huko.. Nilianza kuogopa sana.
Waliitwa wengi sana na tukawa tumebakia mahabusu kama watano hivi.
Watatu ni sisi ambao tumebakiza siku moja tu tuende sero... na wawili ni wale walioletwa jana
Basi wote tuliulizwa kua kama tuna watu huko au namba za simu tuwapigie....
Sasa kila mtu alianza kutoa namba za watu wao ili kuwapigia waje kuwatoa. ila mimi ninayo namba ya yule mzee alionipaga biznesi kadi yake ambayo imepata mwezi sasa toka anipe... sasa naona hata aibu kumpigia maana ni muda sana umepita sikumsalimia wala nini, Nilipiga kimya tu na kutulia kua sina mtu wa kumpigia wala ninaemtegemea kuja kunitoa.
Sasa ilipofika mida ya saa 11 jioni mara kuna gari ilisimama hapo nje ya sero na kutoka mwana mama mmoja hivi ambae kapiga miwani na uchungi juu... lakini ile gari aliokuja nayo kama naifahamu vile... Alikuja na kusalimiana na ma afande kisha akamuulizia mtu wake
"samahani kuna kijana wangu huku anaitwa kelvin?"
"aaa kelvin huku wapo wawili sasa sijui we unamtaka kelvin nani? au ngoja tuwaite wote tu..... Oyaa sogeeni huku kidogo"
Tulitoka kwa wote na kumkuta yule mama ila sikumjua maana alitingishia tintedi...
"heee we kijana na wewe upo huku?"
Sasa ndio nimemjua baada ya kuvua ile miwani... alikua ni yule dokta ambae ndi alinipokea hospitali na ndio alinipa lifti ya kunipeleka hadi kwa broo siku zileeee kama unakumbuka.... sasa amekuja kumuekea zamana mwanae kelvin...
"mama angu si unajua tena maisha? nimesingiziwa tu. kwani kikundi nilichosingiziwa nilisha kiacha muda mrefu tu."
"mmhh pole sana kijana.. naa kaka yako vp hakuja kukuona?"
"mama yangu weee... kaka alishanifukuza siku nyingi sana mama angu"
"Ooh pole sana kijana wangu..... Sasa afande? mimi nawataka wote wawili"
"mmhh haina shida mama ila huyu kijana kakesi kake ni kakubwa kidogo mama"
"haijalishi hata kama kaua... ila naomba nimuekee mzamana"
"sawa hakuna shida mama.... Haya tokeni nyie wawili"
Tulitoka mimi na yule kelvin wake. Kisha mama akachojoka kiasi fulani cha pesa na kumpa afande mkuu ili aizime hii kesi isifike popote. Kisha tukaingia kwenye gari na kuondoka hapo kituoni.
"vp kijana una pakuishi?"
"mmhh mama angu nilikua ninapo lakini sidhani kama patakua salama kweli.. kwani nilipokamatwa nilikua sijafunga mlango"
"ok usijali nyumbani kwangu kuna sehemu kubwa tu hivyo wala usijali kabisa... ila twende huko kwenye sehemu yako ili tukaihakikishe kabisa"
"sawa"
Tulipofika kwanza tulikuta watu wamejaa kweli
Nilishuka kwenye gari na kusogea kwa spidi ili niangalie vitu vyangu vipo au havipo.
Daahh nilipofika tu nikaskia watu wakianza kuning'ang'ania
"si huyu hapa jamani?"
"nimefanyeje jamani?"
"viatu vyetu tunavitaka"
"jamani mimi nilipata shida jamani"
Mara baba mwenye nyumba kaja kwa spidi kali.
"we kijana kwanini uliacha nyumba yangu wazi? kama ulikua hupataki si ungesema kuliko kuacha wazi?"
"ivi nyie mnalalamika kiivyo na wakati mimi nimepoteza vitu vyangu vingi na vya thamani nyingi tu afu nyie mnaanza kuniambia mambo ya hovyo tu"
"yaani we mjinga umetuuzia viau vyetu afu unaongea pumba?"
Mara yule mama akaingilia kati na kusema kua
"samahanini jamani. huyu kijana ndio nimetoka kumtoa sero sasa hivi na alikamatwa na polisi hapa hapa kwenye fremu yake"
Sasa Watu ndio wakaanza kufungukwa na akili sasa.... Yule mama hakuendelea kuongea bali aliniambia tuondoke nami nikapanda zangu gari na kuondoka.. kwani hakuna nilichoambulia katika nyumba ile zaidi ya kukutana na matusi tu. huku nyumba ikionekana kupangishwa tena....
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulifika nyumbani kwa mama huyo na kuingia ndani pamoja na kijana wake
Nilika zaidi ya siku mbili hapo kwake
Siku moja yule mama aliniita tukiwa wawili tu.. na kuniambia kua kuna kazi anahitaji kunipa.. je? nitaiweza?
"kijana? kuna kazi imejitokeza vp utaiweza?"
"ni kazi gani hio mama angu? na nitafanya tu ila kikubwa ni malipo mazuri tu"
"mmmh kwa malipo hua wanalipa laki 2 kwa wiki"
"nini? Eti laki 2 kwa wiki?"
"ndio..ila inahitaji ujasiri wa hali ya juu sana"
"Eeee mungu wangu anipe nini mimi Eee? anipe tu kidonda nifukuze nzi tu"
"ila utaweza kazi yenyewe?"
"mmhh mama mbona wantisha tena?"
"ah ah nimekuuliza tu"
"mi nadhani hakuna kazi inayoshindikana hapa mjini"
"ok kwanza unatakiwa uwe jasiri, pili uwe na nguvu, tatu usiwe muoga, nne kua mvumilivu, na tano uwe mshapu na mwepesi na usiwe wa kulala usiku.... je utaiweza?"
"na mimi nasema hivi nitaiweza tu ila... je? ni kazi gani?"
Nilikua natamani kusikia hio kazi ni kazi gani, maana inalipa vizuri mno na najua sitokaa muda mwingi nami nitakua na chumba changu mwenyewe.
Nilikaa kwa umakini sana ili nisikie kazi ambayo nitapewa.. kwani nimetokea kuipenda ghafla tu japo siijui kazi yenyewe. sasa mama au dokta akaongea hio kazi yenyewe kua
"utaweza kukaa mochwali?"
"haaaaaaa kule wanapokaa maiti?"
"ndio"
"maaama yangu eee sijui kama nitaweza dokta"
"ah ah wewe si umesema hakuna kazi inayoshindikana hapa mjini?"
"ndio hakuna lakini sio hio mama... hio kazi ni ngumu sana"
"ugumu wake upo wapi?"
"mmhh lakini ile kazi si ya wazee ile?"
"wala tu sio wazee hata vijana wanaiweza sema hofu tu ndio imewajaa"
"mmhh labda nijaribu mama lakini sidhani kama nitaiweza kwakweli"
"sio ujaribu we fanya kazi bwana"
"mmhh sawa"
"ok kesho jiandae basi ili twende wote"
"sawa"
Yaani hamu na kazi tena iliniisha kabisaaa maana ni kazi inayotaka ujasiri na nguvu nyingi.. Basi sikua na jinsi ya kukataa juu ya hilo. kwani alienitaftia kazi ndio huyo huyo alienihifadhi nyumbani kwake. hivyo kama nitakataa nitaeleweka vibaya katika nyumba hio
BAADA YA SIKU HIO KUPITA
Na sasa ni mida ya saa 2 asubuhi tukiwa tunajiandaa andaa ili nikapewe kazi na mama huyu ambae ndio dokta mkuu wa kike.. ila kuna mkuu wa kiume hivyo wapo madokta wawili wakuu... Basi tulimaliza kujiandaa kisha tukapanda gari na kuondoka zetu huko hospitalini kwao. Njiani nilikua najiuliza sana kuusu hio kazi, maana ni kazi ambayo kiukweli sikuipenda hata kidogo japo ina malipo mazuri. lakini sijaipenda kabisaaaaa
Basi hatukuchukua muda tukafika hospitali hapo.... huku nikiwa na wasi wasi mwingi mno kutokana na hio kazi ninayoenda kupewa. Tuliingia ndani na kwenda mpaka ofisini kwao ambapo niliandikishwa kama mfanyakazi kabisa. waliniuliza maswali maswali ambayo niliyajibu sahihi lakini ni kwa heshma ya yule mama.... Baada ya kuandikishwa kikazi pale nilipelekwa kwenye eneo langu la kazi... Ambako nilikuta wazee wazee wamekaa kwenye ofisi zao huko huko mochwali. ila wazee wenyewe wapo kama machizi vile... afu kulikua kunanuka bangi na maviroba tu ( pombe ya pakti ) Nilifikishwa pale na kukutana na wenzangu. ila hakukua na kijana yeyote maeneo hayo, kana kwamba kijana nitakua mimi tu katika seksheni hii ya mochwali... Daahh kwanza niliogopa kuona hivyo visanda vilivyofunikwa chini.....
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment