Search This Blog

Thursday 27 October 2022

ONE DAY YES - 5

 http://pseudepigraphas.blogspot.com/2019/12/one-day-yes.html

    Chombezo : One Day Yes

    Sehemu Ya Tano (5)







    Lakini ile anashuka tu Aisse kuna kitu nilikiona ambacho nilisha wahi kukiona sehemu fulani ila sikumbuki sana

    Aisee sikuvumilia kitu nilimuita maana mooyo ulishanienda mbio...

    "we dada wewe?"

    Hakuitika ila aligeuka tu na kuniangalia....

    "vp hio miguu yako mbona ipo hivyo?"

    Hakunijibu kitu bali alipotea tu katika madhingira ya kutatanisha... Nami na uoga wangu nikapanda gari na kuendesha kwa spidi mno huku nikiwa nahema juu juu kwa kuona mtu akipotelea mbele ya macho yangu.....



    Nilifika nyumbani na kushuka ndani ya gari huku nikiwa nimebeba nguo za side wangu.... nilipitiliza mpaka ndani chumbani na kutulia kwanza huku nikiwa nimelala chali kitandani. nikiendelea kumkumbuka yule msichana wa kwenye gari...



    Mara ghafla nikaanza kusikia sauti huku ikijirudia rudia mithili ya mtu aliopo kwenye shimo fulani hivi....

    "umefanya kosa, fanya kosa, fanya kosa"

    Nilikua najiuliza kuusu hio sauti inayoongea humu ndani ya nyumba tena ipo juu ya siling bodi.

    "yule mwanamkee mwanamkee, mwanamkee.... ni adui yetu. adui yetu, adui yetu.... kwa kosa hilooo, hiloo, hiloooo,..... unapaswa utoe sadaka ya mbuzi wa kike aliozaa uzao mmoja tuuu, tuuu, tuuu, tuuu.... tena fanya hivyo usiku wa leoooo, leoooo, leooo, leooo"

    Heeeee sasa nikajiuliza kwani yule mwanamke ni nani? ila sikupata jibu kwa wakati huo



    Nilitoka tena kwa wakati huo na kwenda katka mabanda ya mbuzi kisha nikanunua mbuzi aliozaa uzao mmoja..... Kisha nikaja nae mpaka nyumbani

    Sasa nikawa nimekaa nae mahali nikisubiri maelekezo juu ya mvuzi huyu



    "mpeleke machinjioni kule katika kampuni yetuuuu, yetuuu, yetuuu"

    Nilifanya hivyo mara moja ili tu pesa zangu zisiishe. maana niliambiwa nisipofanya nitapoteza pesa zangu zote.. na kuikaribisha mikosi mingi katika maisha yangu



    Nilifika machinjioni na kukuta pako kimya sana, kwani ilikua ni mida ya saa 6 usiku, hivyo nilimlaza mbuzi yule na kwenda kuchukua kisu mahali ambapo kuna chungu kilichosimamishiwa kwa juuu....



    Lakini nilipoenda kuchukua hicho kisu nilisikia sauti za watu wengi wakilia kwa mateso wanayo yapata. Mmhhh ikabidi nizifatilie hizo sauti ambazo zinalia na kutaka msaada fulani..... Sasa kumbe hiiii sehemu ina korongo refu kweli. nilisogelea na kuchungulia kidogo huko chini ya korongo...

    "mungu wangu eeee"

    Nilijisemea hilo neno lakini ghafla kichwa kilianza kuniuma na karibia naelekea kule korongoni kunako watu wanaolia......



    Nilijikuta nimedondoka chini kwa kizungu zungu nilichokua nacho. Nilipodondoka pale chini, Nilikua naskia vishindo vingi mno ambavyo vilikua vikipiguza chini ya aridhi, Nilishindwa kuelewa kuusiana na jambo hilo.



    Lakini ghafla niliskia sauti ikiniambia

    "amka uchinje kinyamaa, nyamaa, nyamaa"

    Nilijikuta nimepata nguvu na kuamka na nguvu mpya... Nilimshika yule mbuzi na kumuelekezea kibla kwa kunitolea kafala juu ya makosa yangu. sikukawia kuchinja, Nilimchinja mbuzi yule tena bila hata wasiwasi juu ya hilo nililolifanya. Lakini baada ya kuchinja? ghafla nilisikia watu wakilia katka ile damu ambayo ndio imetoka sasa hivi katika shingo ya huyo mbuzi, Nilishindwa kuelewa kwanini nayasikia sana mauza uza toka niingie katika kampuni hii? Nilijiuliza sana kuhusiana na jambo hilo lakini sikupata jibu sahihi kuhusu milio hio.... Basi niliweka kisu pale chini na kuondoka zangu, Lakini nilipokaribia kutoka getini niliskia sauti ikicheka kwa sauti kisha ikaniambia..

    "safi sanaaaaa..... umefanya jambo jema sana, Ilaaa utakapo pata taarifa fulani huruhusiwi kutoa choziiiiii, choziii, choziii, choziiii"

    Mmhhh nilishindwa kumuelewa huyo mtu kua alimaanisha nini. Basi mlinzi alifungua geti kisha nikatoa gari langu. na kuelekea nyumbani kwangu. Huku nikiwa na furaha ya hapa na pale kwa kusamehewa kosa langu. Mida hio ilikua ni mida ya saa 7 usiku Lakini nilipofika pale kwenye kona karibia na pepsi katika barabara ya njiro..... nilishangaa kuona mtu akiwa kasimama katikati ya barabara huku akiwa anavuja damu shingoni, tena alikua kavaa gauni heupeee pyeee..... Nilianza kuogopa hapo barabarani na kushindwa kuendesha gari, hivyo nilibaki tu nimeduwaa kama dudu vile,

    Lakini punde sii punde niliona yule mtu katoweka ghafla bini vuu... Niliwasha gari na kutoka mbiooo. Hadi kufika nyumbani kwangu, Nilijitupia kitandani bila hata kuvua viatu na kuulazimisha usingizi ili nipotezee kwa kile kilichonitokea muda si mrefu....

    ***********************************

    Mara nilianza kusikia sauti ya mwanamke akilia huku akisema



    "mume wangu, mume wangu, mume wangu, Tafadhali sana mume wangu.. naomba utoke huko ulikoo, ulikoo, ulikoo, Kwani kampuni ulioajiriwa sio kampuni ya binaadamu, binaadamu, binaadamu, kwa sasa umeshaniua mkeo na utaendelea kutumaliza sisi... familia yako inalia kwa kufiwa na ndugu kila siku...... Mume wangu? naomba utoke kwenye hilo kundi. kwani tayari umeshatuua mimi na mwanao, mwanao, mwanao, mwanao"

    ************************************



    "Noo Noo sio kweli we side wangu side wangu hawezi kufaa"

    Nilikurupuka kitandani huku jasho likiwa linanitweta vibaya... Daahh kumbe nilikua naota eti nimeua mke wangu na mtoto.. Daahh haitokaa kutokea hata siku moja kumuua side wangu na mke wangu. siwezi kabisa. Niligundua nimelala na viatu hivyo nilivua viatu huku nikifikiria hii ndoto ambayo nimeiota muda sii mrefu, Afu ni mke wangu ndio kanijia katika ndoto huku... tena huku akilia kwa sauti ya huruma.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sijui ni kwanini nimekosa namba za nyumbani. maana hii ndoto imenishtua sana, Daahh niliendelea kulala huku nikiwa na hamu ya kwenda nyumbani kuiona familia yangu. kwani kwa sasa nimeshakua tajiri wa kutupwa, yaani nimekua bnge la tajuri.....



    BAADA YA MIEZI MIWILI KUPITA



    Siku zilizidi kwenda na pesa nazo zilizidi kunielemea kwa wingi mno, maana rumu yangu yote inanukia pesa tu. na hata kitambi kimeanza kuota..... Nilikua ni mtu ninaependa starehe sana Nilikua natembea na wanawake wawili wawili tena kwa kumwaga pesa kibao... naweza kulala na mwanamke mmoja kwa shilingi milioni 1 tena bila kupunguza kitu. Kiukweli nilikua ni malaya sana, yani hakuna demu ninayemkosa mbele ya macho yangu, hata awe nani



    Basi nilikua natoka zangu NOVO hotel nikiwa nimekumbatia mademu wawili wawili tena nikiwa nimelewa chakali, Lakini nilipofika karibu na gari yangu Nilimuona yule msichana ambae nilishawahi kumkuta ndani ya gari yangu.... ni kama miezi miwili mitatu hivi imepita toka nionane nae.

    "afu wewe dada wewe? miezi michache iliopita ulinisababishia kesi ya mimi na bosi wangu kisa wewe tu,, umesababisha mpaka nimeenda kukaua kambuzi kawatu kisa ni wewe tu... Kwahio naomba sana usinizoee tena"

    Sasa hawa wasichana niliokua nao waliniona labda mimi ni kichaa au ndio kichaa kinaanza.. maana walishangaa kuona naongea na gari tu. lakini ukweli ni kwamba wao hawamuoni huyo niliokua nikiongea nae Hivyo waliona labda ni uchizi wangu au ni pombe ndio zinanisumbua akili yangu, Kwahio waliamua kuniacha pale na kuondoka zao, ila ni kwasababu nilishawakatia chao na ndio maana wameondoka



    Niliendelea kumsemesha yule mschana wa kiislamu ambae hayupo kibinaadamu kama sisi ila sijui ni nani,

    "dada tafadhali sana naomba usinisogelee maana tukigusana tu kwangu itakua ni kesi kubwa kwa bosi wangu, hivyo kaa mbali na mimi kwani hua sipendi kuchinja vimbuzi vya watu hovyo hovyo tu"



    Ghafla yule dada aliongezeka mara 4 na wale wanne walikua wamevaa nguo nyeupe pyeeee, Nilianza kuogopa ghafla na kujikuta sina ulevi tena, Alafu wale watu walikua hawapo tena, Niliwasha gari na kukimbia mbio za kuelekea nyumbani kwangu.....



    sasa kufika tena nyumbani kwangu nilikutana na gari ya mzee joakimu... yule mzee alieniunganisha na hii kampuni yao,

    Nilimkuta pale nje akiwa kapaki gari akinisubiria



    "mbona unakimbiza gari hivyo kuna nini?"

    "aaaahh ni matisho tu ndio nayaona"

    "matisho gani sasa?"

    "kuna mdada ananifatilia sana na sijui ni nani... ila tuyaache hayo vp mbona hujaingia ndani mzee?"

    "Ahahaha usijali kijana kwani kuna ujumbe nimeagiziwa nikuletee"

    "Na nani? Bosi nini asee?"

    "ndio"

    "Ehe ujumbe gani huo?"

    "leo saa 8 usiku kuna kikao cha wafanyakazi wote.... kwani tumekaa muda sana bila kutoa sadaka"

    "oookee hakuna shida. kwahio leo tunakua wote ndani ya uwanha?"

    "ndio.. ila hakikisha unakuja na mbuzi dume"

    "Aaayaaaa Acha utani mzee kupanda vyeo? duuu ila sasa mbuzi saa 3 hii nitamtoa wapi mzee?"

    "mimi mwenyewe sina. na ndio natarajia kwenda katika mabanda sasa hivi"

    "basi twende wote mzee"

    "sawa ila mimi ndio naenda sasa hivi"

    "sawa haina shida we twende tu"

    "kwahio hata ndani huingii?"

    "apana siingii kabisa"

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Basi tulikwenda katika mabanda ya mbuzi yaliopo katka maeneo ya machinjioni ya nyama za kuuza kama kwenye mabucha hivi. Tulinunua kila mtu mbuzi wake na kumuweka ndani ya gari, Tulikus tuna furaha kwa kufanikisha mbuzi wetu.......

    Kila mtu alienda makwao kujiandaa na mkutano wa usiku wa leo ambao utajumuisha wafanya kazi wote wa kampuni hiii.



    Ilipofika mida ya saa 8 usiku tulikutana katika tempo moja ambalo kulikua na kama ukumbi fulani hivi maana kulikua na viti mithili ya kanisa. Afu kule mbele nikiangalia nilikua naona shimo tu katika eneo la steji... ambapo mkuu au bosi ndipo atakaposimamia.... nikiangalia watu wote humo ndani tulikua tumevaa majoho meusi yenye mistari miekundu, Huku kila mtu akiwa kashika mbuzi wake kwa ajili ya kafala la kujitolea mikosi,



    Mara ghafla mkuu ameingia katika steji na kuanza kuongea

    "nashukuru sana kwa kuwaona mpo wote tena kwa furaha sana.... ila nadhani kila mmoja amekuja na kinyama chake?"

    Tuliitikia kwa wote huku tukisema

    "ndiooooo mkuu"

    "sawa kabisa.... sasa nadhani kila mtu ana kisu chake maalum cha kujichinjia knyama huyo... sasa naanza kuita majina. na ukisikia jina lako. unatakakiwa hapo hapo ulipo weka chungu chako chini na umchinje mbuzi huyo na hakikisha damu yake iingie katika hicho chungu sawa?"

    1. "keneth Dominic?"

    "ndioo"

    "nipe jinsia ya mbuzi"

    "ni mbuzi wa kike"

    "ok chinja"

    Baada ya huyo ikafata

    2. "Ashishy Mpacha?"

    "ndio mkuu?"

    "jinsia?"

    "mbuzi wa kike"

    "chinjaaa"

    3. "Denic Jackson?"

    "ndioo"

    "jinsia?"

    "beberu"

    "chinjaaa"

    4... "masanza kemchoz?"

    "ndioo"

    "jinsia?"

    "kajike"

    "chinjaa"

    5... "khalfan yusuph?"

    "nipoo"

    "jinsia"

    "mbuzi wa kike"

    "chinjaa"

    6... "Ally Jfour?"

    "nipo mkubwa"

    "jinsia ya mbuzi"

    "kondoo"

    "nani kakuambia ulete kondoo?"

    "ooo sory mkuu kumbe ni kabeberu"

    "chinjaa"

    7..."Swaaleh Twalha?"

    "ndio?"

    "jinsia"

    "wa kike mkuu"

    "chinjaaa"

    8...."Oswald A halla?"

    "ndiooo"

    "jinsia"

    "mbuzi mchanga"

    "chinjaaa"

    9...."Issa juma?"

    "nipo"

    "jinsia?"

    "kajike mkuu"

    "chinjaa"

    10...Ommy mtupa?"

    "nipo mkuu"

    "jinsia"

    "beberu"

    "chinjaaa"

    Walikua watu tupo wengi sana tulikua tupo kama watu 500 hivi

    sasa mkuu aliiita na kuita mpaka ikafikia zamu yangu ya kuchinja kinyama changu

    "rashidi tandu kingazi?"

    "ndioo"

    "jinsia"

    "mbuzi dume mkuu"

    "chinjaaaa"

    Nilimchinja mbuzi wangu na damu ile ya mbuzi ikaingia ndani ya chungu.... sasa huku nikiendelea kuikamulia damu iingie vizuri katika chungu... ghafla kuna jina nililiskia likiitwa. na jina hilo nalifahamu kabisa... na si mwingine bali ni kaka yangu yule alienifukuza kule kwenye nyumba yake.... heee kumbe na yeye ni mmoja kati ya wafanyakazi wa hii kampuni?.... Lakini sawa haina shida ila je? yeye kaja na kinyama gani cha kujitolea sadaka?

    "hatibu tandu kingazi?"

    "nipooo"

    "jinsia?"







    Nilikua nasubiri ndugu yangu aitaje jinsia ya mbuzi wake,

    "hatibu tandu kingazi?"

    "nipooo"

    "jinsia?"

    "wa kike"

    "chinjaa"

    Duuu kumbe yeye alikuja na mbuzi wa kike.

    Ila nashangaa sana kumuona broo nae yupo katika hii kampuni ya kitajiri kiasi hiki, afu kumbe sisi ndugu zake tulikua tunakufa na njaa kiasi hiki, Duuuu kweli pesa ni mwana haramu .. Lakini namlaumu mwenzangu tu? mbona mimi mwenyewe toka niingie katika hii kampuni sijakanyaga hata siku moja kule kijijini, Basi waliisha wote kuchinja vinyama vyao kwa kujiwekea ridhiki za pesa nyingi..



    Baada ya kumaliza kuchinja vinyama hivyo. Mkuu alitoa agizo kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiii,

    "nadhani mnajua kua pesa yetu haitumiki katika njia mbili.... na ili kujua njia hizo basi muulize aliokuleta ili ujue kabisaaa..... Nadhani sina la ziada ila papo hapo ulipo beba chungu chako kisha tuelekee katika kampuni yetu"

    Tulitoa kwa mstari utafikiri ni wana kwaya fulani hivi,



    Lakini tulipofika njiani tukielekea kule kwenye kampuni... maana huku tulikua katika ukumbi mmoja ambao ni kama tempo lao la ibada, Sasa kwa jinsi tulivyokua tukitembea kwa mistali tena tukiwa tumevaa majoho utafikiri ni wanafunzi waliohitimu vyuo vikuu...

    Sasa nilikumbuka siku moja niliona kitendo kama hiki. Watu wakiwa wamebeba vitu fulani katika vifua vyao. huku wameinama chini, Kumbe wale watu ndio walikua ni hawa. ila siku ile niliona kidogo tu maana nilipatwa na usingizi wa ghafla siku ile, na nilipokuja kuzinduka ndio nikakutana na kwato za ng'ombe mbele yangu, Sasa nikaanza kujiuliza hiii ni kazi gani hii ya kubebana na madamu hivi??? Mnhhh Aiseee kesho lazima nimuulize mzee. ili anipe jibu sahihi kuhusu hii kazi ni kazi gani? ili isije kua tunatumikia mashetani bure....

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Basi tulifika katika kampuni na kupitiliza moja kwa moja hadi katika lile korongo, Kisha tukaimwaga ile damu kule chini kunakolia watu, na baada ya kumwaga damu wale watu walionekana kunyamaza, kiaskwamba wamezikubali kafala zetu.......



    BAADA YA SIKU MBILI KUPITA



    Na leo ni siku nyingine nikiwa nyumbani kwangu, Nilikua naangalia visuruali nilivyomnunulia side wangu pamoja na mama yake Bila kumsahau dada yangu na mama yangu pia. Lakini nikiwa naangalia nguo hizo ghafla kuna simu iliingia Niliitoa simu kisha nikaipokea.... Alikua ni mzee ndio ananiita katika ofisi yake binafsi...

    Sasa katika hali ya kuangalia namba zangu za simu, nilikutana na jina SABRINA sasa nilipoona hili jina ndio nikakumbuka kua tanga nilikua na demu aitwae sabrina, na namba zake za simu ndio niliziweka kichwani kwa urahisi, maana si demu wangu



    NADHANI HATA WEWE NAMBA YA MPENZI WAKO IPO KICHWANI



    kwani namba ya mke wangu nilishindwa kuiweka kichwani kwakua ilikua ni mpya hivyo sikuweza kuishika.... pia ya kaka yangu sikuishika kabisa kwani ilikua ni ngumu... ila namba ya sabrina nakumbuka ilikua ni maziro ziro mengi tu, Sasa kwakua ndio namba pekee ninayoijua hivyo niliiweka kwenye simu na kuipiga. Ilikua inaita duuuuuu naomba iwe ndio yenyewe

    "halooo?"

    "eee halo mambo?"

    "poa tu nani mwenzangu?"

    "aaa naitwa rashidi"

    "rashidi nani?"

    "si rashidi tandu"

    "mmhh mi sikujui"

    "ok kwani wewe unaitwa nani?"

    "mimi naitwa sabrina"

    "yesi hata huyo niliempigia pia anaitwa sabrina"

    "mmhh mi sikujui bhana.. Enhee shida yako?"

    "aaahh kuna namba ya ndugu yangu nilikua naitaka sasa sijui utamjua?"

    "mhh sasa kama wewe sikujui je? yeye nitamjuaje?"

    "kwani dada we si upo tanga maeneo ya kikokwe au?"

    "ndio kwani we ni nani?"

    "mimi naitwa rashidi ambae ni kijana tuliokua tunalima kwenu mimi na kaka yangu juma"

    "haaaaaaaaaaaaaa chidi? mungu wangu umepotelea wapi jamani? huku kwenu ni majanga kila siku ya mungu"

    "majanga gani tena? haloo haloo haloo jamani sabrina haloo?"

    Daaahh simu ilikata aiseee Nilijaribu kupiga tena huku mapigo ya moyo yakinienda mbio. Daahhhh

    "Samahani namba ya mteja unayopiga haipatikani tafadhali jaribu tena baadae.... Thank you for cho"

    "Aaaaaaaaaaaiiiiiiiii mambo gani tena haya daaa Asa tena hapatikaniki jamani aaaaaiiiii"

    Niliondoka hapo nyumbani kwa hasira huku nikielekea kwa yule mzee. maana kama unakumbuka aliniita niende ofisini kwake



    Niliwasha gari na kutoka mbio huku nikiwa na wasiwasi juu ya familia yangu. kua kuna majanga Sasa ni majanga gani hayo? Nilitoka kwa spidi sana na kufika kwa mzee huku nikihema juu juu kama mbwa mzee.

    "shkamoo mzee?"

    "marahaba vp?"

    "safi tu..Aaaa umeniita nafikiri?"

    "ndio nimekuita nije nikupe data nzima ya kampuni yetu jinsi inavyokwenda"

    "aaaa wala siihitaji hio data mzee labda usubiri mpaka nirudi kijijini. maana nina mpango wa kwenda kesho"

    "uende kijijini kufanya nini?"

    "naisi kuna matatizo mzee"

    "hupaswi kwenda popote pale"

    "Nini???? labda unifunge jela ila kwa swala la kwenda lipogo tuu"

    "sasa kijijini unakwenda kufanyaje?"

    "aseee mzee mbona una maswali mengi hivyo? si naenda kuisalimia familia yangu"

    "familia gani tena? na wakati familia yako ndio hizo pesa ulizonazo"

    "mzeee naomba tueshimiane mzee maana nitatamani kukuvuruga sasa hivi... maana nilikua nakuheshim sana ila heshima naona imeshuka tayari sasa"

    "sikia kijana... ulioyafanya ni mambo makubwa sana hivyo hupaswi kupaniki endapo utayasikia mambo hayo"

    "mambo gani?"

    Mara simu yangu iliita... nikaitoa mfukoni na kuangalia namba ilikua ni ya sabrina..

    "haloo sabrina ulisema kuna nini kwetu?"

    "huyo ndugu yako juma unaemsemea ndio huyo anaezikwa leo au?"

    "unasema ndugu yangu anazikwa leo?"

    "ndio... si yule kaka yako mliokua mkilima nae vibarua? afu kama mkorofi korofi hivi?"

    "vigezo vyote hivyo ni vyake lakini kwa huyo anaezikwa sio kaka yangu"

    "wewe ivi unajua kua nipo maeneo ya kwenu"

    "upo kwetu?"

    "ndio na tunasubiri kuzika tu. kwani hata baba yangu ninae hapa"

    "we we .... we ....we ..we unamjua mke wangu?"

    "aakaa simjui"

    "oooo shit ebu mpe baba yako niongee nae"

    Nilianza kuongea na yule mzee ili nijue huyo jamaa anaezikwa ni nani.. Sasa ile nataka niongee na baba yake sabrina..



    Ghafla huyu mzee akanipokonya simu yangu,

    "khaaa we mzee vp bhana ebu nipe simu yangu bhana"

    "hapana sikupi maana hii simu ndio inakupa kiburi cha kujua kila kitu"

    Nilimshangaa mzee akitoa betri katika simu yangu.... kisha akaikata kata laini na kuipasua ile simu yangu. Nilishindwa kumuelewa hivyo nikabaki kumuangalia tu kwa hasira

    "sikiliza kijana.. kama msiba umetokea huko kwenu. ni kweli kuna msiba.... na unaruhusiwa kwenda kumzika ndugu yako. ila kwa sharti moja tu"

    "Ebu endelea ongea nikuskie"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "hupaswi kulia wala kusikitika yaani tena unapaswa kucheka kabisaaa sawa?"

    "wewe ni mpumbavu nini wewe"



    Nilimtukana kisha nikatoka zangu na kuwasha gari kwa spidi huku nikitokwa na machozi.. Nilielekea Eapoti kuchukua ndege binafsi....



    Kama unavyojua usafiri wa ndege sio daladala. hivyo ilinichukua lisaa limoja hadi kufika nyumbani... niliondoka na helkopta binafsi.



    Kweli nilikuta watu wamejaa pale nyumbani kwetu. Lakini kitu kilichonishangaza nilikutana na wanafunzi wa vyuoni. Sasa nikajiuliza na hawa wanafunzi nao ni vipi.... Sikupata jibu sahihi kuhusiana na hao wanafunzi wa vyuoni.



    Cha kwanza kabisa nilikimbilia kuingia geto kwangu. Na kukuta hakuna hata mtu tena kulikua kumevurugika sana. basi nikajua mke wangu na mwanangu watakua wapo kwa mama kule...... Wakati huo watu wananishangaa mimi tu..



    Nilipofika nyumba kubwa yaani kwa mama.... daaahhh sikuamini macho yangu,



    "Yaani hapa nyumbani kulipita sunamiiiiiiii au kulikua na ugonjwa wa ghafla?"

    Nilijisemea mwenyewe huku nikilengwa na machozi kwa mbali Na nilipewa sharti moja tu la kutokulia wala kusikitika Sasa kwa hali hii kweli nitavumilia kweli? mungu wangu....



    Nilishindwa kuelewa kwa mambo nilioyakuta pale nyumbani, Yaani sikuamini macho yangu kiukweli nilikuta maiti mbili ya dada yangu pamoja na kaka yangu. Lakini sasa cha kushangaza ni kwamba sikua namuona mke wangu kwani nilijua nitamkuta akiwa huku kwa mama....



    Kwa usalama nilioukuta ni kwamba nilimkuta mama yangu pamoja na bibi yangu tu.... Nilimkimbilia mama yangu Lakini mama alionekana kukasirika sana juu ya mimi kupotelea mjini na kuwaacha ndugu zangu wakiisha mmoja baada ya mwingine. Nilikua nalengwa na machozi juu ya vifo hivi, kwani mimi mwenyewe nilijua ni kaka juma tu, kumbe hadi dada yangu aseeeee duuuu.. Nilikua natamani kulia ila nikifikiria yale masharti duu hata machozi yanakata yenyewe



    Nilijifanya kulia tu kwa uongo na kweli ili mama anionee huruma maana kakasirika kweli, Nilimkuta pia na bibi yangu mzaa mama wakiwa katika hali ya kulia kweli kweli, yaani hata muda wa kuomba msamaha nilikua sina, Niliingia ndani na kuwaona ndugu zangu waliokua wamelala moja kwa moja na siwezi waona tena, Nilitamani kulia kabisa Japo nilikua nimevaa suti ya maana lakini sikutaka kuvumilia kitu,



    Nilitoka zangu nje huku tukisubiri muda ufike waende wakazikwe.... Lakini cha kushangaza simuoni mke wangu kabisa, sasa sijui kaenda kwao au sijui kasafiri na yeye, Maana hata ile geto yetu haina hata mvuto tena kwani imeshakua banda la kuku.. . sasa mke wangu atakua yupo wapi?. Nilipotoka nje nilikutana na mzee yule ambae ni baba yake na sabrina,

    "shkamoo mzee?"

    "marhaba kijana hujambo?"

    "sijambo mzeee"

    "pole sana kijana..ila ndio hivyo kila marefu hayakosi kua na ncha, hivyo tumewapoteza ndugu zako, hivyo basi tu ni kazi ya mungu kijana"

    Mara ghafla sabrina katokea huku nae machozi yakimlenga kwa msiba huu, kwani dada yangu pia alikuaga ni best yake. kabla hajaenda chuo... hivyo anamkumbuka sana kiasi flani



    Ilifika mida ya kuzika ndugu zangu. hivyo nami nilishiriki katika mazishi yale, Na tuliwazika katika shamba letu la bondeni kule....



    Ila nilipofika hapo shamba niliona utofauti mkubwa sana, na sikua na mtu wa kumuuliza zaidi ya mama yangu.... Basi mazishi yalifanyika vizuri na mimi pia nilitupia mchanga huku watu wakiniangalia kwa jicho baya, Maana nimekuja na ndege binafsi. sasa wanashangaa kuona nimekuja na ndege afu huku kijijini wazazi wangu wanalala kwenye nyumba ya majani,



    Tulimaliza kuwazika wote na hatmae sasa narudi kule nyumbani, ili nikampooze mama angu. kwani katika watu walioumizwa na msiba huu ni yeye peke yake, Niliwakuta wote yeye na bibi pamoja na wamama wengine waliokua wakimpa pole, Huku wakimbembeleza sana. aisee nilitamani kulia asee yaani nilitamani kulia kabisaaa. Ila nikikumbuka kua mzee aliniambia kua pesa hii haiseidii ndugu wala kumseidi masikini...



    Yaani kama unakumbuka siku ile mkuu wetu alisema kua tumieni pesa mnavyotaka ila kasoro sehemu mbili tu... na nilipomuuliza mzee pale ofisini kwake aliniambia kua pesa ya kampuni hiii haiseidii ndugu wala maskini yeyote yule na katika majengo ya ibada pia hairuhusiwi......



    Niliona sasa hii ni kazi gani? kazi isioseidia hata familia? Hapana mi siwezi... Niliona kua siwezi kuondoka bila kumjengea mama yangu nyumba, Yaani mwanae nina pesa kiasi hiki mpaka naumwa, afu leo nimuache katika nyasi? haiwezekani... Pale pale nilianza kuagiza tofari na mawe ili nyumba ijengwe



    Lakini kila nikitoa pesa watu wanairudisha na kusema kua pesa hio haitumiki...... sijakaa vizuri mara niliskia sauti ambayo sikujua ilipotokea,

    "hahahahahah Aaaahahahaha tulikuambia usimseidie mtu hata awe nani, pesa hizo zinatumika vizuri sana. ila kwakua sio destuli zetu kuseidia watu. hivyo hao hao watu wataiona hio pesa haitumiki ila wewe tu ndio utaiona... sasa unahitajika urudi mjini sasa hiviiii, hivii, hiviii, hiviiii"



    Sauti hio ilikua ni sauti ya mkuu wetu wa ile kampuni,

    Niliingia ndani kwetu na kumkuta mama yangu akiwa na huzuni muda wote.

    "mamaa? baomba unisamee mama angu nilikua natafuta maisha mama angu"

    Nilianza kulia ili wanionee huruma.,...

    "mamaa? mimi bado ni mwanao tu lakini mbona kaka hatibu hajawahi kurudi. ila bado tu unampenda mama?"

    Bibi alinisamee na mama pia ilibidi tu anisameee maana mimi bado tu ni mtoto wake hata iweje

    "lakini mama? lile shamba la bondeni umeliuza nini?"

    "mwanangu kweli nina shida kubwa sana ila siwezi kuuza hazina za watoto wangu siwezi kabisa mwanangu"

    "sasa mbona lina makaburi mengi vile? maana mi najua kulikua na kaburi la baba tu.... Afu mama saidi kaenda kwao au kaenda wapi? maana toka nije hapa sijamuona kabisa"

    "mwanangu? yaani huna taarifa yeyote kuusu mkeo?"

    "mamaa mimi simu nilipotezaga hivyo hata namba zake sina za kwako sina za kaka juma yenyewe sina sasa ningejulia wapi mama angu?"

    "mwanangu? kwanza pole sana kwani hata mimi nilikua nampenda sana mjukuu wangu ila ndio hivyo"

    "mamaaaaa mbona sikuelewi?"

    "hayo makaburi yaliozidi kwenye shamba lenu ndio mkeo na mtoto wake"

    "u. u. u. u. u. uuuuu unase...unasemaje mama?"

    "alianza mtoto wako... na ni kama miezi 8 hivi toka mtoto wako afariki.. kisha haikupita hata miezi mitatu. mkeo nae akafariki dunia.. hivyo yale ndio makaburi yao...

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aiseeeee niliambiwa nisilie lakini hapa haki ya mungu sinyamazi... Nilitoka hapo nyumbani kama kicha na kuelekea shamba bondeni huku nikilia kwa uchungu mkubwa sana... yaanu kama ungeniona jinsi nilivyo basi hata wewe usingeacha kulia. nilifika kwenye kaburi la mtoto wangu na kugalagala kwa uchungu huku nikilia kama mtoto mdogo...

    "saidiiiii mwananguuu aiiiiiii kidume changu hicho kimekufa uuuuuuuuwiiiiii aaaaaaaaahhhhhoooooo uuuuuuuuu mke wangu eeeeeeeee mama saidi eeeeeeeeeee saidi wangu saidi wangu eeeeeee.... mwanangu amkaaa nimekununulia majinsi makali kinyama aseee uuuuuwiiiiiiii.... we mama saidi weeeee nimekununulia tentemente sita na madera kumi uuuuuuywiiiiiii mama saidiii weeeeeeeee mwanangu said? said? saidiiiiiiiiiiii Ahahaha uuuuuuuuwiiiiii uuuiiiiiiii eeeee mungu nimekukosea nini mimi? nimeenda mjini kwa kuitafutia familia yangu afu leo wamekufa wote uuuuuiiiiiiiiiu ooooooo mungu wangu wainue basi hata niwaone.... aaaaaaahhhh saidi baba amkaaa.. mke wanguuuuuuuuu aaahahaha uuuwiiuuu......"



    Kiukweli siku hio nilikua kama kichaa vile, na niliamua kulala hapo hapo na jioni yote. maana watu walikuja kunichukua lakini sikutaka kuondoka kabisa katika makaburi hayo,

    Na watu nao waliniacha pale pale huku nikiwa nimechafuka suti yangu kwa kuyagala galia makaburi hayo.. Nililala pale bila kumuogopa mtu wala mnyama yeyote yule. Nililala pale mpka asubuhi



    Asubuhi mida ya saa mbili watu wananikuta nimechakaa vumbi kama katuni... yaani nimelia mpaka macho yanauma. Watu walinichukua huku nikileta fujo kua sitaki kutoka hapo kabisa kwani. nina hamu na familia yangu....

    Nilibebwa juu juu tena kwa nguvu kweli. Walinipeleka hadi nyumbani na kuniacha hapo, Yaani nilikua ni mtu wa kulia tu muda wote. sina wa kujivunia tena kama mtoto....



    Nilikaa nyumbani kama siku mbili nzima Sili sinywi wala sikua na raha hata kidogo....... Basi na leo ni siku ya kuondoka ila siamini kama namuacha mama yangu bila hata kumuachia senti tano....... Sikuamini macho yangu kama kweli mama yangu nimuache katika maisha kama haya na wakati mwanae nina pesa mpaka nazichezea? Hapana hii kazi sio ya kufanya kabisa na siitaki tena...



    "mwanangu yani unaondoka na kuniacha hivi? mwanangu sina hata pesa ya kula"

    Yaani kumsikia tu mama yangu akilalamika hivyo nilianza kushikwa na hasira hizo......



    Lakini ghafla nilimuona mtu mmoja akiwa kasimama kwenye mti. na nilimjua mtu huyo... na nilimfuata mpaka pale alipo.

    "umeona madhara ulio yafanya?"

    Aliniambia huyu mdada mwenye miguu kama ng'ombe wa kienyeji..

    "kwani mi nimefanyaje tena?"

    "ooohh hujui? ok chukua hii pesa mpelekee mama yako afu tuondoke"

    Alinipa bahasha moja nzito na nilipoichungulia ilikua imejaa noti za kibongo tuuuu... Sikutaka kuuliza wala nini. nilimpelekea mama yangu na kumkabidhi bahasha ile.

    "mamaa nilitaka kukujengea nyumba ila muda wa kuwepo tena hapa kijijini sina hivyo chukua hizi pesa utaendelea kujenga jenga tu mwenyewe taratibu tu mama angu"

    "mwanangu nashukuru sana mwanangu, ila jua nimebaki na wewe tu na huyo bedui mwenzio lisiotaka kuja kwao.. nakuombea mwanangu"

    "asante mama na wacha mi niende maana nimekuja na ndege iko pale uwanjani"

    "nashukuru mwanangu na nakuombea safari njema na uendelee kufanikiwa mwanangu"

    "haya mama.. ila upatie na bibi ya ugolo maana kahasi kuniomba ya ugolo kweli yani"

    "sawa mwanangu nitampa bibi yako usijali"



    Niliondoka huku nikijiuliza maswali mengi kua,

    "je? kama ningetafuta pesa yenye kutumika na kila mtu... mbona ingelikua ni furaha ya hali ya juu... ila hii nionayo ni kazi gani hasa. ambayo pesa yake ni marufuku kuseidia ndugu au masikini wenye shida?"

    Nilijiuliza maswali hayo huku machozi madogo madogo yakinilenga lenga kimtindo. kwani tayari nimeshaitilia mashaka hii kazi nilio nayo sasa hivi.... ambayo kila miezi 3 tunatoa kafara.....



    Nilifika kwenye ule mti na kumkuta yule mschana mrembo kweli afu mweupeeeee.

    "kwaio?"

    Nilimuuliza hivyo. maana tayari nimeshamzoe na hali yake ya king'ombe ng'ombe.

    "twende"

    "mimi nimekuja na ndege lakini?"

    "najua ila kuna mahari nataka nikupeleke nikakuonyeshe kitu"

    "kitu gani?"

    "we twende tu"

    "ok ngoja nimjulishe rubani aondoke zake"



    Basi baada ya hapo nilijikuta ninefika eneo fulani hivi liliojaa gold na madhahabu kibao. yaani hata kitanda chenyewe ni gold tupu.

    "sikia chidi. katika kikosi ulichojiunga nacho sii kikosi cha kawaida"

    "kivipi labda"

    "wewe hapo ulipo tayari ni member wa freemason"

    "nani? mimi au?"

    "ndio ni wewe"

    "hapana siwezi kua freemason hata siku moja"

    "sasa ndio hivyo. na kama huamini ona pale"

    Alifungulia tv moja iliopo ukutani na kunionyesha jnsi nilivyoanza kumchinja mtoto wangu siku ile... afu nikaona na siku ambayo nilimchinja mke wangu... afu nikaona na

    "aiseeee basi zima tu zimaaa aaaaaaiiiiiii uuuuuuuuwww kumbe nimewaua kwa mikono yangu... uuuuwiiiiii aaaaahhhh mungu wanguu aaaaiiiiii"

    Nilijikuta nlia kwa mara nyingine.... huku nikiiangalia mikono yangu ilioua familia yote.

    "sikia sio wewe peke yako ndio ulioua.. bali hata kaka yako yule hatibu ni mmoja kati ya kundi hilo... na yeye ndie aliemuua dada yako wa kike na pia wewe mwenyewe upo kwenye prosesi ya kutolewa kafara na huyo ndugu yako. hivyo kua makini sana"

    "eeeeee mungu wangu ee kumbe hata kaka yangu ni freemason pia?"

    "ndio....tena yeye alianza na baba yenu"

    "haaaaaaaa yani ni kumbe broo ndio alimuua baba?"



    Niliamka kwa hasira na kuzunguka hapo kwenye hicho chumba

    "samaani dada naomba nitoke eneo hili"

    "hupaswi kutoka kwenda mahali"

    "dada naomba sana nitoke nipo chini ya miguu yako"

    "ok ila hupaswi kuendelea nao"

    "sawa nimekusikia."



    Baada ya dakika kadhaa tu nilijikuta nipo uraiani.... sikupoteza muda nilielekea moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya mzee

    "we mzee kuma mae zako... we mzee kwani ilikuambia uniunganishe na hili kundi lenu? kwanini umeniungasha mzee? si ungeniacha na umaskini wangu ee? kwanini usingeniambia kwanini? ona sasa mimi sina hata ndugu kisa ni huu ufreemason wenu"

    "Aaaaaaahahahahahaha kumbe ulikua hujui? na hakuna jinsi ya kutoka tena, afu isitoshe mkuu anakuita kule..... tena wamekuekea kikao wewe. nenda ukawasikilize"

    "kuma mae wewe"

    "haijalishi kitu hata utukane matusi yote"

    Ani nilikua natetemeka kweli kwa hasira za hali ya juu... Niliitisha gari yangu ikaletwa kisha nikaelekea huko kwenye ofisi zao...

    Ila nilipoingia tu yule mdada alinikataza nisiingie.. lakini sikumsikia maana nilikua nana hasira ya kugombana na huyo LUSIFA mwenyewe ambae haonekaniki, Nilipoingia kweli niliwakuta wapo kwenye kikao cha kunijadili mimi. Nilifika kwa hasira zangu nyingi na kutulizwa juu kwa juu.. kabla hata sijaongea nikaskia

    "umefanya makosa mengi sana kwenye kampuni hii... tulikuambia ukifika kwenye msiba usilie... lakini kwa jeuli yako umelia... tukakuambia kua hatutaki uwe na yule mschana husikiii... alafu bado umetoka kumgombeza mkuu wako ofisini kwake.... sasa kwa adhabu ya makosa hayo inakuja hivi"

    "weeee lusifa acha usenge wewe mimi nimeua ndugu zangu wote afu unasema usenge wako hapa we ni hanisi nini wewe?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "hilo ni kosa lingine.... na adhabu yake ni hiii.... .

    1... katuletee albino watatu uliowaua wewe mwenyewe

    2.... basi la mtei leo limejaza vizuri sana hivyo nataka lidondoke pale darajani

    3.... na mama yako tunamtaka

    Kama utavikosa hivi vitu basi tutakutoa kafara wewe mwenyewe..na vitu hivyo vifanyike leo leooo, leoo, leoo, leoo, leoo, leoo"



    Nilishtuka sana kuskia hivyo, kwani kuua albino watatu? au kuua umati wa watu. kusa ni mimi tu? hapana

    "kwanini lakini mnafanya hivi?"

    "hatutaki maswali, haya uliyataka mwenyewe hivyo maswali nengi ni marufuku kwetu"

    Sikua na jinsi ni lazima nivifanye hivyo vitu nilivyoagizwa kutoka kwa wakuu hawa.

    "basi mi naacha kazi yenu na pesa zenu na majumba yenu magari yenu kila kitu chenu chukueni na sivitaki tena"

    "ahahahahahahaha huezi kukitoa katika ulimwangu mpya na mpana.. au The New World Order... ama WWW ( WORLD WIDE WEBSITE ) huezi kutukimbia katika ulimwengu huu mpana na wenye kukamata kila mtu mwenye akili mbovu kama yako... sasa ili uendelee kuishi tufanyie hizo kazi haraka"

    "lakini kwanini mnakua makatili kiasi hiki? basi nipeni chaguo kati ya hivyo nipunguzieni basi"

    Niliomba wanipunguzie japo hata mbili tu, maana kuteketeza basi la mtei au albino watatu au mama yangu. sii kazi ndogo asee..

    "ok tunakupunguzia mbili na ubaki na hizi mbili"

    "ndio kabisa asante. ila ni zipi sasa?"

    "mama yako au wewe mwenyewe. na ukifanikiwa kumuua mama yaki basi na cheo tunakupandisha tena"

    Daaahh nilichoka kabisa kusikia hivyo. maana nilijua swala la mama yangu limetoka, lakini ndio kwanzaa lipo palepale.... Nililia sana kuona vile.......



    Basi sikua na jinsi ya kufanya bali nilitoka pale huku nikijifikiria mara mbili mbili kuusiana na swala hilo la kujipeleka mimi au nimtoe mama angu afu niendelee kula pesa zangu?

    Lakini kabla ya yote nimeona niende kwa yule dada akanipe ushauri juu ya hili



    Sasa kwakua sikua na mahari pakumpatia hivyo kuna kitu alinipa ambacho niki kigusa tu anakuja nilipo. Na ni kweli haikuchukua muda mrefu nilishangaa yupo nyuma yangu Wala sijui amekujaje, Alinishika tu mkono na kunipeleka mahali ambapo nilitoka muda sii nrefu, yaani pale kwenye chumba ambacho kina gold chumba choteee.

    Sasa yeye alikaa mahari huku akiniambia

    "chidi? najua kwa sasa una mawazo mengi sana kuusu hivyo ulivyoambiwa na mr lusifa. ola hutakiwi kutekeleza hata kimoja"

    "kwanini nisitekeleze? lazima nifanye hivyo maana bila hivyo nitakufa asee"

    "bora ufe kuliko kuendelea kuuwa watu"

    "kwaio nifanyaje dada angu?"

    "kifupi ni kwamba achana nao hawa watu..... na hata mwanzo nilikuambia siku ile nilipokukuta kwenye toroli umelala.. nikakuambia kabisa nikiachana na wewe kuna mwingine atakuja.... sasa ndio huyo keshakufanya muuaji tayari"

    "afu Eeheeeee nimekumbuka hebu niambie wewe ndio ulienipeleka hospitalini siku ile?"



    SASA HAPA WE MSOMAJI KUA MAKINI... MAANA HAPA KINAONGELEWA KILA KITU AMBACHO KILITOKEA HUKO NYUMA NA HUKUKIJUA.. SASA HAPA NDIO ATAELEZA YOTE SASA... ILA KAMA HUKUIANZA MWANZO HII STORI BASI UJUE HUTOELEWA KITU CHOCHOTE KILE



    "sikia nikuambie rashidi, mimi nilikua ni binaadamu kama wewe, ila wakuu wa majini wa nchikavu waliona kua mimi nafaa kuwa mmoja wao, hivyo nikawa mbali na binaadamu na kua jini wa nchikavu. ila ni majini wa wa nchikavu na wasio na hatari yeyote ile.... Toka nilipoingia katika sekta hio nilikaa muda mrefu bila kua na mahusiano ya kimapenzi na binaadamu, japo naweza kujiweka katika hali ya kibinaadamu na kuishi na binaadamu..... katika kundi letu sisi kulikua na vijana wawili na wasichana wanne, hivyo kulihitajika kijana mmoja ili tuwe saba... kwani sheria yetu hua tunakua waschana wanne na wavulana watatu na sio kila mtu inaweza kumuangukia, bali kuna vigezo vya kiroho lazima uwe navyo ndio ujiunge na majini. na nafasi hio ilikuangukua wewe kabla hujaingia katika ushetani. Hivyo wakuu wangu waliniambia nikufuatilie mwanzo mwisho ili nijue matendo yako, na kuweza kukupeleka kwa wakuu wangu... Na mara ya kwanza kukufatilia ilikua ni hapa



    ***********************************

    "Broo tuache masihara bwana mbna mnarusha mawe?"

    "nani karusha mawe wewe?"

    "ok poa twendeni"

    Tulianza safari huku tukipiga stori za hapa na pale



    Lakini ghafla niliguswa usogoni mithili ya mtu alienisodoa...

    "aiseee broo mbona mi sielewi?"

    "nini wewe?"

    "nani kanigusa kwa nyuma?"

    "sasa mimi nipo mbele nitakugusaje kwa nyuma?"

    "eeeehh??"

    "Eeenhh eee eee Eeee nini sasa?"

    "eeee?"

    **********************************



    Na mara ya pili nilikuja ndani kwako usiku na kukuonya kua usiende mjini maana nilishayaona maisha amvayo ungeishi,



    na mara ya tatu nilikufatilia siku ile ulipokua unakwenda kwenye mdumange... kile kitendo sikukipenda kwani ulikua una mke na mtoto... afu pia mimi mwenyewe nilishaanza kukupenda taratibu, hivyo sikupenda uende kwenye mdumange.. na ndipo nilipowatuma wenzangu waanze kukuzuia... na wa kwanza ni yule uliemuona kwenye mti siku ile.... kisha baada ya muda nikatokea na kukurudisha kwenu...



    Na siku nyingine ni pale kwenye ajali. ile ajali haikua kosa la dereva bala mule ndani ya gari kulikua kuna baadhi wengine sio watu. ila wewe na wengine mliwaona kama watu... ile gari ilipinduliwa na mfanyakazi mmoja wa kampuni hio ulionayo kwa sasa..... nae alipewa azabu kama hio uliopewa wewe.. na ilikua mfe wote mliopo katika magari yote mawili.. ila ulipona kwasababu mimi nilikua nyuma yako... na nakumbuka kuna muda nilikushika macho ili uone yanayofanyika tofauti na macho yako ya kawaida sasa pale ulipojifanya unaweza kutoka nje ndipo ulipopigwa kibao na kupoteza fahamu kabisa.



    walikuchukua wale watu kisha wakakutenga mahari ili wakuuwe kiukatili. ila walipoona kua wewe ni wa muhimu kwao hivyo wakakuacha pale pale chini ukiwa huna fahamu.... nami ndipo nilipokuchukua na kukukabizi kwa yule mama dokta....... Na hapo ndipo wakaanza kukufatilia kwa kumtuma yule mzee.... na hata hivyo yule mzee na wale WADUDU WA DAMPO ni kitu kimoja hivyo ulikua ukisomewa wewe tu uingie katika chama chao hicho cha mauaji



    Na sehemu nyingine nilipokufatilia ni pale mochwali ulipotaka kusex na maiti yule... hivyo nilitumwa tu nidhibitishe kama kweli ungefanya nae?



    Na sehemu nyingine ni pale nilipokukuta umelala katika mkokoteni, Na ndipo freemason walipotoka katika tempo lao walilokwenda kutolea kafara... na wangelikuona basi ingelikua ni shida na tatizo kwao... hivyo nami pale pale nikakupa usingizi wa ghafla... na ulipozinduka asubuhi ndipo ulipokutana na kwato za ng'ombe.. nilikuambia maneno machache tu kisha nikaondoka...



    Na sehemu nyingine ni pale ulipokua unachinja mbuzi mchanga... hua sisi hatunaga sheria ya kumzuia mtu kwa kile alichoamua yeye bali tunamuambia tu kwa mdomo... ila mimi nilijitahidi kukushika mikono lakini bado ulikua hutaki.... kwani yule ndio alikua ni mwanao saidi, ila wewe ulijua ni mbuzi mchanga.



    Na sehemu nyingine ni pale uliponikuta nipo ndani ya gari yako... na kunifanya univute kiisia mpaka nikakupa mate yangu japo wewe ulijua kua nimefuata pesa zako lakini hapana... Na pale pale kama unakumbuka nilishtuka. Sasa pale ni mkuu wangu alinionya nisirudie tena jambo kama lile... na ndio maana sikuendelea kukaa kabisa.. na ndipo ulipopewa adhabu ya kuchinja mbuzi aliozaa uzao mmoja tu... ila yule hakua mbuzi bali alikua ni mkeo...... Na pale kwenye korongo ambapo watu wanalia? huko chini kuna watu aina ya mashetani. ambao ndio husababisha wewe na mwingine kuwa na pesa. yaani vile wanavyolia ndivyo na pesa inavyoingia katika akaunti yako au chumbani kwako.. maana wameshaifurahia damu ya ndugu au mke au mtoto. au mama...



    Na sehemu nyingine ni pale NOVO hotel ambapo ulikua umeshika wadada wawili wawili. tayari kwa kusex nao.... kitendo kile sikukipenda kabisa kwakua hata mimi nilikua na chembe chembe za mapenzi na wewe....



    Na sehemu ya mwisho ni pale nilipokuja tanga kukuchukua Baada ya kuwazika ndugu zako.



    Haya hebu niambie mungu ataweza kukusamee kwa dhambi ulizozifanya? na sasa bado wataka ukaendelee kuuwa tu. ivi unaona raha tu kuuwa si ndio?"



    MMNHHH KIUKWELI DADA KAONGEA MENGI SANA



    "sasa mimi nitafanyeje? maana nitakufa"

    "nimeshakuambia ni bora ufe.. ila sio wakuue wao bali ujiue mwenyewe na kifo cha mateso ndipo utaweza kusamehewa dhambi zako.... na kuweza kuwarudisha watu wote uliowaua kwa mkono wako... kwani watu hao hawakufariki bado. na hata kuzika mumezika migomba tu. ila watu wapo hai kabisa jambo sio kwa dunia hiii.... hivyo wanatakiwa kukombolewa kwa kutumia damu yako tena ujiue kwa hiali yako wewe mwenyewe. ila sio wakuuwe wao"

    "haaaaaa kwahio nikijiua mimi na familia yangu itarudi kuwa hai?"

    "ndio"

    "oooo bora nifanye hivyo saidi wangu na mama yake na kaka yanguuu na pia dada yangu warudi aseer"

    "hapana dada yako hawezi kurudi kwani hukumuua wewe, bali dada yako aliwawa na kaka yako hatibu... hivyo haitowezekana kwa yeye kurudi labda atubu kwa kukiua kama wewe"

    "niue basi familia yangu irudi... kwani ni bora waendelee kuishi wao kuliko mimi"

    "sio uuliwe na mtu bali ujiuwe mwenyewe na kifo cha mateso sana.... kama vile kujitupia gholofani... au kujitupia katika moto au maji.. na hivyo vyote havipo katika ulimwengu huu, bali vipo mahali nitakupeleka... kwani huko kuna ukubwa wa mara 70 ya vitu vya duniani... yaani khama ni gholofa huni hata chini... na kama ni ukali wa moto basi ni mara 70 ya duniani.... na kama ni maji basi ni zaidi ya sunami yaani ni sunami mara 70 sasa chagua moja uende wapi?"



    "bora hio gholofa"

    "kwahio umeridhika?"

    "ndio mama nimeridhika... ila nipe basi hata denda la mwisho kwani si unajua sirudi tena?"

    "kurudi utarudi ila sio kwa sura hio wala kwa jina hilo bali utakua ni mtu mtakatifu... hivyo ukirudi tu utanikuta. ila nikikupa denda kwa sasa utaniletea shida kwa mkuu, kwani alishanikataza kuusu hili.... ila bado nakupenda chidi. hivyo hata mimi sio kua napenda ukajiue ila ni njia ya kukutengenezea njia mzuri"



    Sasa alipomaliza tu kuongea Tulijikuta tupo juu ya gholofa... yaani hilo gholofa hakuna kabisa na sio kua hakuna kwa hapa tanzania? bali ni kwamba hilo gholofa sijawahi ona na wala hakuna na halitowahi kuwepo duniani kote...



    "ngoja kwanza chidi... nakuomba fungua moyo wako juu ya hilo. kwani ukienda kwa roho mkunjufu ndio utafanikiwa. ila ukiwa hupendi hata hao ndugu zako hawatorudi kabisa. kwani hukupenda kuwarudisha"



    Kwa jinsi alivyokua anaongea nilihisi kama ndio ananichelewesha kufa vile... hivyo nilijitupa bila kufikiria kitu huku nikifumbs macho kwa upepo ambao ulikua ukinipuliza.

    Yaani gholofa ilikua ni ndefu kiasi kwamba hata ukimwaga tenki la maji halifiki ng'ooo. maana ni parefu mnooo..



    Nguo zangu zote zilikua zikichanika kwa upepo mkali ambao ulikua ukinipitia nikiwa nashuka chini..... Huezi amini nilihisi kama robo saa imeshapita lakini hata katikati sijafika..... Nilikua naomba tu nisijeku, Lakini ghafla nilikutana na moto mkali ulioanza kunichoma kwa mbali.... Sasa nilipokua naukaribia ule moto ambao ndio 7 mara 70....



    Nilishangaa naitwa huku nikisukumwa sukubwa na kuambiwa

    "we sheby? sheby mwanangu amka uende shule"

    "Eee? Nini nyie bwana mi nataka kuikomboa familia yangu nimeiua yote"

    "we mtoto una nini hebu amka bwana ona sasa umechelewa shule"

    "haaaaaa ni saa ngapi mamaa?"

    "si saa 4 hii mwanangu, kwani ulikua unafanya nini? hebu ona jasho lilivyokutoka"



    HAAAAAAAA KUMBE NILIKUA NAOTA AISSE DUUUU TENA WALA SIITWI RASHIDI.... JINA LANGU NI SHARBINY RASHIDY TENA BADO I MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU......



    "mamaa? kuna ndoto nimeiota"

    "ndoto gani hio mwanangu?"

    "mamaa? nilikua na mke na mtoto afu nimeota eti nimeua ndugu zangu afu kuna dada mmoja akaniambia ili niwarudishe watu hao nilio waua eti nijitupe kwenye gholofa nife, ndio wafufuke"

    "jamani mwanangu pole sana... na washindwe na walegee kabisa hao waliokuotesha jamani"



    Mama angu alikua ananipenda sana kupita kiasi......

    "kwaio utaenda shule?"

    "ndio mama ntaenda tu"

    "utachapwa mwanangu usiende"

    "ah ah wacha nikachapwe tu"



    SASA ONE DAY YES IMEISHIA HAPO JUUU..... ILA STORY YA ONE DAY YES INA MUENDELEZO WAKE AMBAO JINA NI TOFAUTI NA HILO



    YAANI MUENDELEZO WAKE UTAKUA NA JINA TOFAUTI LA STORY... ILA CHIMBUKO LA MUENDELEZO NI HIO ONE DAY YES..



    KWAHIO ONE DAY YES ILIKUA NI NDOTO TU.... SASA HUUU NDIO MUENDELEZO WAKE AMBAO UTAKUA NA JINA LIGINE......



    KWAHIO ~ONE DAY YES~ IMEKWISHA KWA STAILI HIO...



    ILA NAWAONJESHA KIONJO CHAKE AMBACHO SIKUAMBII JINA LA STORY HIII ILA BUNIA JE? INAITWAJE



    HEBU TUONJE KIONJO KWANZA



    story hiii mimi ni mtoto wa kitajiri ile mbaya... na wakiume nipo mimi mwenyewe na nina dada zangu wawili wenye asili ya kiarabu. kwani mama yangu yeye pia ana asili ya kiarabu.....



    Ninae dada yangu ambae ana umri wa miaka 25 huyo ni wa kwanza na keshamaliza shule muda tu... kisha ninae dada yangu mwingine ambae tumefuatana.. yeye ana umri wa miaka 22 na yeye bado yupo kidato cha 4... afu anafatiwa na mimi kidume sharbiny rashidy mwenye umri wa miaka 20 na yupo kidato cha 3.... familia yetu ilikua ni familia ya kitajiri sana yaani tulikua ni matajiri waliopindukia....



    Ila katika watoto wote wa mzee rashidy mimi peke yangu ndio nilikua nina rangi tofauti na dada zangu wote. Ila nyumba yetu imezungukwa na wafanyakazi wengi mno. kama kwa raisi vile kumbe ni kwa mtu tu wa kawaida...



    "mwanangu utaenda kesho tu"

    "mamaa mi sijawahi kukosa kwenda shule hivyo nisipoenda naisi kama nitaumwa yani"

    "mmhh haya ila njoo unywe chai basi"

    "nitakula huko huko mamaa"

    "mwajabu? we mwajabu?"

    "abee dada?"

    "umeona mtoto wangu anaenda shule na njaa?"

    ndani kwetu tulikua tuna mfanyakazi ambae ni mtu mzima kabisa na ndio alionilea mimi toka nikiwa mtoto.... hivyo roho inaniuma sana pindi ninapoona anafokewa kwa ajili yangu,

    "kakaa njoo unywe chai"

    Aliniita yule mdada wa makamo kabisa tena hata sio mdada ni mmama kabisa. kwani alitulea mimi na dada zangu wote, lakini dada zangu asa huyu mdogo hua hamueshimu huyu mama na sijui ni kwanini....

    "mamii nimeshiba usijali"

    Nilimuambia kwa kwa utaratibu na heshma zote alizonilea yeye mwenyewe.

    "sheby mwanangu, sema ukirudi unataka ule chakula gani?"

    Alioniuliza ni mama yangu mzazi

    "aaaa chochote tu mamaa"

    "yaani we mwajabu humuulizi mtoto atakula nini umeuchubua tu"

    "mamaa mbona ivyo lakini?"

    "amna mwanangu ni huyu mtu naona hakujali kabisa yani"

    "ok nitakula ugali na mrenda"

    "haaaaaaa sheby mwanga chakula gani hicho cha kishenzi hivyo?"

    "mamaa kwani hicho mbona pia ni chakula"

    Mara mami kazi akaingilia katihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "lakini dada kama kapenda mwenyewe kula labda tumuache tu"

    "hapana mwanangu hawezi kula matapu tapu hayo... afu wewe mwajabu umenilelea mtoto wangu vibaya sana wewe"

    "nisamee dada"



    Nilichukua BMX yagu ambayo hua naendaga nayo shule pindi ninapopitwa na school bus, Hua shule ninayosoma ni shule ya serikali iitwayo

    ASHRAF SEMINARY SEC SCHOOL ni shule ya kiislamu ambayo ina maadili mema kila idara....



    MWISHO

ONE DAY YES - 4

 http://pseudepigraphas.blogspot.com/2019/12/one-day-yes.html

    Chombezo : One Day Yes

    Sehemu Ya Nne (4)





    "sasa huyu si kilema huyu ataweza kazi kweli? maana mguu una bendeji na mkono pia. sasa itakuaje hapa?"

    Aliuliza mzee mmoja wa makamo kabisa

    Kisha akajibiwa na mama huyo kua

    "ataweza tu kwani kukija maiti yeye asihusike ila aangalie kwa wale maiti wageni kama kuna atakaetikisa mguu kua ni mzima atolewe"

    "ooo kwahio huyu ndio mwangalizi tu?"

    "ndio"

    "mmhh ni sawa ila hapa si tupo shift kwahio aje jioni kwa ajili ya usiku"

    Yaani niliposkia shift ya usiku ndio nilipagawa kabisaaaaa

    Maana mimi nilitegemea kua nitafanya kazi mchana ili iwe afadhali kidogo. lakini kumbe ni mambo ya shift tena duuu.... sikua na jinsi ya kukataa juu ya hilo maana ndio kazi hii



    Basi mama alinipa elfu 2 ya nauli ili nirudi nyumbani kwa muda huo, maana yeye ndio kafika kazini hivyo.. Basi nilirudi nyumbani nikiwa nimejawa na mawazo telee huku nikijihisi kama sina thamani na haya maisha. kwani kuletwa kwenye seksheni kama hiii ni jambo linaloniumiza kichwa sana,

    Nilitamani jioni isifike mapema maana nahisi kama sitoiweza hii kazi, licha ya kwamba kitengo nilichopewa ni kuangalia tu wale maiti wapya kama kuna ambae bado hajafa basi atolewe katika chumba hicho



    Daa Jioni nayo ndio hiooo imefika na ni muda wa kwenda kazini. hivyo sikutaka kuchelewa Nilipanda daladala na kuelekea maunt meru kunako job yangu... Yaani nikisema maunt meru, utafikiri nafanya kazi ya maaaana kumbe ni mochwali tu..

    Nilifika hospitali na kupitiliza moja kwa moja hadi kwenye kipande hicho cha kuangaliana na maiti. Niliingia mida ya saa moja kasoro jioni, nikawakuta wengine nao ndio walikua wanaingia kwa shift za usiku..

    Nilikaribishwa vizuri tu na kuanza kupewa namna ya kufanya... na kuambiwa kua sitoweza kupokea maiti pindi inapokuja hapo ndani.. kutokana na ukilema wangu wa mguu na mkono. hivyo sitoweza kubeba. kwahio nimepewa seksheni ya kuwakodolea macho tu....



    Waliokuepo shift za mchana waliondoka zao na kwenda kupumzika. kisha nasi tukalianzisha gurudumu la hapo mochwali



    Tulikaa sana maeneo hayo kwani kwa siku hii ya leo hakukua na maiti mpya ilioletwa nikiona. hivyo zilizopo chini ni zile za toka jana.



    Sasa muda si muda alikuja maiti mmoja wa kike..sasa wale wazee wa kuipokea na kuiosha kazi ni kwao. Waliipokea maiti na kuanza kuiosha na usiku huo mida ya saa 8 hivi ila hapo mochwali kuna taa nyingi sana kiasi kwamba utafikiri ni mchana.... Basi waliandaa maji na kumueka sehemu ya kuoshea maiti.. kwa kawaida huku mochwali hua hakuna wanawake hivyo maiti inayokuja yeyote ile iwe ya kike iwe ya kiume... basi itaoshwa na mwanaume. swaga za wakike aoshwe na wakike hakunaga hio ni kwenu Au labda mumuoshe kwanza huko kwenu ndio mumlete mochwali, na pia akioshwa ni pesa mbele hakuna mkopo. hawaoshwagi bure.. Sasa mtoto wa kiume nilikua zangu nimetulia huku nikiwa kama nasinzia sinzia hivi.. Nilishtuliwa na maji ambayo nilimwagiwa na jamaa mmoja hivi aliokua akiiosha ile maiti



    "unalala lala nini we boya?"

    "daa samaani mzee"

    Huku hua hakuna hata vijana wote ni wazee

    "we kijana unavuta bangi?"

    "hapana mzee"

    "pombe je?"

    "pia situmii mzee"

    "ugoro je?"

    "yaani situmii kilevi chochote kile"

    Waliangaliana huku wakicheka kwa kejeli.. lakini sikuwajali kitu. niliendelea kuwakazia macho wale maiti waliopo chini, ila usingizi nao ulikua ukinisumbua kiasi fulani hivi.. kwaio nilikua nasinzia sinzia kimtindo

    Sasa usingizi ukienda kukolea niliwasikia wale jamaa wakiambiana kua

    "aisee bado wamoto kabisa asee"

    Sasa nikajiuliza kua? kama huyo dada bado ni wa moto? kwaio atakua hajafa sio? Nilijiuliza sana huku nikianza kufumbua macho taratibu huku nikiwaona wanavyomsugua yule maiti huku wakimuinua inua mapaja yake.

    "oyaa anafaa huyu tena bado hajakaza"

    Sasa nikajiuliza anafaa kwa kazi gani? nikaona bora nuvunje ukimya bwana

    "jamani kwani vp? ni bado ni mzima huyo dada sio? ngoja nilete kibaskeli basi ili tumpeleke kwa wagonjwa wengine"

    Heeeeee niliangaliwa na wale jamaa huku wakinitafakari kunipa jibu fulani hivi baya baya... Lakini walisita kusema kitu hivyo wakaendelea kuosha mait ile huku kama naona kama wanaitamani maana dada mwenyewe alikua sii haba... yaani tako ni tako kweli sio mchezo. na hilo paja sasa..

    "we dogo njoo"

    Waliniita kiubabe ubabe huku kama wanampapasa papasa maiti yule. maana kuosha imekua kupapasa papasa matt na mapaka yake....

    "ndio mzee?"
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "vp dogo?"

    "poa tu"

    "sikia dogo humu ndani maiti ikiletwa na kuandikiwa kua keshakufa. basi hata kama kwa bahati mbaya hajafa afu ukamuona yupo hai? huruhusiwi kutoa taarifa popote pale"

    "haaaa kwanini sasa?"

    "unajua ni kwanini?"

    "sijui"

    "mtu tayari keshaandikiwa kufa na faili lake limewekwa X hivyo akizinduka hapa mochwari hua anamaliziwa. ili tusiwaharibie madokta wengine vibarua"

    "haaaaaaa kwanini lakini mfanye hivyo?"

    "we vp mbona huelewi? jakobo? hebu lieleweshe hili toto, maana halinielewi kabisa yani"

    "sikia dogo... hua dokta pale anapoandika kua mtu huyu tayari ni mfu na faili lake lipo katika orodha ya wafu. basi huyo hapaswi kupona kama atakua ni mzima.. maana tukimuacha awe hai huyu mfu.. basi yule dokta atafunguliwa mashtaka kwa kumfosi mtu kifo afu ataonekana pia wengine waliokufa basi ni yeye kawaua hivyo hatutaki kupoteza vibarua vya wenzetu kwa mtu ambae keshaonekana kua mfu.. nadhani umenielewa hapo?"

    "mmhh nimekuelewa ila sidhani kama ni sahihi kufanya hivyo"

    "ok tunajua huo ni ugeni tu. bali utazoea na tena utawamalizia wewe mwenyewe kwa bereshi"

    "haaaaaaaa mnawamaliziaga kwa kuwapiga na bereshi?"

    "sasa je?"

    "mungu wangu eeeee?"

    Daaahhh kiukwwli nilichoka kabisa kusikia maneno kama hayo ambayo walikua wakisema

    Nikaona ngoja niwaulize kuhusu huyu mait wa kike hapa

    "Eti mzee? vp mbona kama mnamtomasa tomasa huyo dada wa watu?"

    "kwani we unaonaje? huyu lazima aliwe.. na sio sisi tu hata wewe ni lazima umle?"

    "nimle?? nimle kivp sasa?"

    "jakobo hebu muonyeshe mfano huyu"

    Sasa nikawa nipo makini kuona huo ulaji wenyewe.. sasa hawa jamaa wapo watatu na mimu ni wanne.. niliona wawili wamempanua panuuu kama msamba vile afu yule mwingine aliiingia kati.. aiseee mungu wangu eee wanasex na maiti duuu... kumbe ndio maana niliskia neno

    "aisee bado wamoto bwana yaani hajakaza kabisa" kumbe nia yao ilikua ni kusex nae yule maiti...

    Sasa hawa ambao wameshika wakawa wananiongelesha kua

    "dogoo we tulia tu kwani hawa watu wakiwa njiani hua wanaringa sana sasa hii ndio dawa yao"

    "lakini mjue ni zambi hio wazee wangu nyie"

    "heeeee sikuhizi hata mtoto wa miaka mitano ana dhambi hivyo hatudanganyiki"



    Kiukweli haviangaliki kabisa kabisa kwani walikua wakifanya kwa zamu huku wamempanua miguuu... yaani kama kifo cha mende vile. maana si bado hajakauka hivyo bado alikua ni mlaini.... sasa mimi nilikua nimeinamia chini kwani nilihisi hata nikiangalia nitajiona na mimi namkula huyu mdada mrembo kweli sii haba... ila ukafiri kama huu kaamwe mi siwezi kufanya maisha yangu yote... ni bora umbake mtoto mdogo kuliko kusex na maiti...



    Sasa nilipokua nimejiinamia nilishtuliwa na sauti ilionipasua tumbo kwa uoga wa lile neno

    "we dogo?'

    "naam mzee mshaamaliza?"

    "ndio... Sasa ni zamu yako uje kula"





    Kiukweli sikua naipenda ile tabia tena ndio watanifanya niache kazi kwa tabia yao mbaya kama hii. Nilikua nimejiinamia zangu kichwa chini huku nikitafakari mbele ya maisha yangu itakuaje?......

    Sasa nilipokua nimejiinamia nilishtuliwa na sauti ilionipasua tumbo kwa uoga wa lile neno

    "we dogo?'

    "naam mzee mshaamaliza?"

    "ndio... Sasa ni zamu yako uje kula"



    Nilistuka kuskia hivyo kua imefika zamu yangu ya kwenda kusex na maiti.... Eee mungu wangu haya ni maisha gani tena. Nilianza kulia kama mtoto ili nisiambiwe niende nikalale na maiti.... Maana hio ni laana kubwa mno kulala na mait.

    "we dogo ni kwamba husikii au?"

    "mzee mi siwezi mzee"

    "huezi kwanini? Utaweza tu njoo"

    "apana mzee sitaki kufanya hio laana"

    "kwaio sisi tunachokifanya ni laana sio?"

    "sijui ila kwangu ni hivyo"

    "kwahio utamla au humli?"

    "hapana simli"

    "Aaahaaa sasa kuanzia leo tusikuone humu ndani... na pia tutakusingizia kua huyu mtu alikuja mzima afu wewe ukasex nae na kummalizia kabisa"

    "Aaaa sasa mzee ndio nini hivyo?"

    "tuambie utakula huli?"

    "ok basi nitakula lakini sio huyo labda aje mschana mwengine maana huyo si keshakauka"

    "safi sana kwa kukubali haya kaa utulie pale"

    Niliongea vile ili wasinilazimishe kwa muda huo. Basi walimuosha tena baada ya kumaliza kazi yao ya kusex nae.. Eti wanamtoa janaba



    Nilikaa pale lakini roho ilikua ikiniuma sana kwa kuona ukafiri unaoendelea humu ndani.



    BAADA YA SIKU 4 KUPITA



    Nikiwa bado naifanya kazi yangu vyema ndani ya hospitali. Nilikua kila siku naombaga asiletwe maiti wa kisicha. maana maiti MZEE, MTOTO, MWANAUME hua hawashuhuliki nao. ila wanata msichana kuanzia miaka 18 mwisho 40... kwaio kuanzia 40 hawakugusi kwasababu Eti hana joto. Kwaio kila siku nilikua namuomba mungu wawe wanakuja maiti watoto na wazee na wanaume tu... kwani wakija wasichana nitaambiwa nilale nao kimapenzi



    Sasa siku hio nilikua zangu nimetulia kwenye kiti huku nikiwa na wasiwasi wa hapa na pale.. maana nywele zilishaanza kunisisimka kua kuna kitu kitatokea. hivyo niliingiza simu yangu mfukoni.. maana nilikua naichezea ili kupoteza fikra za humo ndani... kwani watu wanaokaa mochwali ni lazima wawe walevi au wavuta bangi. tena kwa kila muda. na ndio maana hawa wazee wameshachizika kiakili........ Sasa mida hio ilikua ni mida ya saa 8 usiku.. nilikua peke yangu pale mochwali... kwani wazee walienda chooni kuvuta bangi na kunywa pombe...



    Sasa nikiwa nashangaa shanga humo ndani. Taa zilianza kuzima zima afu zinawaka. Nilishindwa kuelewa ni shida gani hio?

    Sasa nikiwa naendelea kuushangaa umeme ukikata na kurudi..

    Nilishangaa kuona majokofu yalioekea maiti yakianza kufunguka yenyewe... Yaani yalikua yanajivuta afu yanajirudisha ndani... Maana majokofu yenyewe yapo kama droo ya meza au hata kabati... ZILE DROO ZA KUVUTA sasa ndio kama haya majokofu... Sasa yalikua yanafunguka kwa kushindana Kwa kufunguka na kujifunga, Niliona au huenda ni wenge langu nini, Nilishindwa kuvumilia hivyo nikachukua gongo langu la kutembelea. Kisha nikaamka huku nikiangalia majokofu kwa umakini wa hali ya juu sana, Sasa sijakaa vizuri mara kwenye jokofu moja ukatokea mkono wa mtu.... Nilipasukwa na roho huku mapigo ya moyo yakienda mbio. Mara mwingine kainua kichwa juu.... Aaahh nilishindwa kuvumilia aisee nilianza kukimbia huku nikichechemea....... Sasa cha ajabu na cha kushangaza Niliona na wale maiti wa chini wakianza kutetemeka kama vile wanaskia baridi. Daaahh yaani hapo hata kukimbia nilishindwa na kubaki naburuzika tu chini.... sasa nikiwa najitaidi kukimbia kwa magoti,, ghafla nikashikwa mguu kwa nyuma na maiti mmoja. mpaka nikaona huenda akawa ni mzima huyu mtuu..

    nilianza kupiga kelele nyingi kweli

    "mzeeeeee uuuuuwiiiiii wazeee njoooniiii uuuuuuuwuiiiiiiii uuuuuuuu wazeee nakufaaa ooiooooiiiiiiii jamani njooniiii aaayaaaaa uuuuuyuuu"

    Mara yule mtu akaniachia mguu.... aisee niliruka sarakasi utafikiri sio kilema... niliruka hadi mlangoni na kukutana na hawa wazeee

    "nini wewe unaamsha wagochwa huko wodini?"

    "mzeee we acha tu mzee ni majanga"

    "kuna nini?"

    "daahh mzee yale madude yalikua yanafunguka yenyewe Afu pale chini kuna mtu ni mzima pale"

    "hahahahahahaha ivi una akili wewe? watu wameshakufa wale"

    "mzeee kuna mmoja hajafa pale. maana kanishika mguu"

    "Aaaahahahahaha Aaaahahahahaha dogo wacha kunichekesha wewe nani kakuambia maiti anashika mtu?"

    "mzee mzee mzee we subiri tu utaona mwenyewe"

    "acha uga mtoto...na ndio maana michwali hakutakiwi vijana wadogo kama nyie"

    "Eeheee mzee umeona katingisha mkono umeonaaa?"

    "aaa we unatukatia tu stimu zetu... oyaa twendeni tukaendelee kupombeka bwana.. mwacheni huyu dogo anazingua tu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Aaaise hamuniachi tena asee.. walai vile twendeni wote huko huko"

    "Acha ujinga we dogo kaa hapo si tukamalizie vinywaji"

    "sitaki bhana na kama ni kazi na ife tu"

    "kwaio utaki kazi tena?"

    "mi skai peke yangu kule"



    Nilienda nao huko wanapokaa wao maana huku ndani kumesha chafuka kabisaa hakufai, Nilienda kukaa nao huko nje wanakovuta bangi zao japo mimi sikua navuta..



    BAADA YA SIKU 2 KUPITA



    Na leo ni usiku mwingine na wa mwisho kwa wiki.. Ilikua ni mida ya saa 9 usiku ikiwa ni siku ya jumaapili yaani kukipambazuka tu nachukua pesa yangu ya wiki afu nifikirie kuendelea. Sasa ilipofika saa 9:30 kulikuja gari imebeba maiti wengi ambao walipata ajali usiku huu... Nikaanza kujisemea kua hii ndio gundu hii daa..

    Walikuja maiti wa kila lika na wengine ni majeruhi wakapelekwa huko kwenye wodi zao.. na maiti wote wakaletwa humu ndani.. afu walikua wametapakaa damu chungu nzima... yaani hawatamaniki wala hawaangaliki..

    "dogo leo kuosha kutakuusu maana maiti ni nyingi sana"

    Nikaona sio mbaya pia kwani ni kazi yangu

    Basi maiti wote wakawekwa mahali pakuoshea maiti kisha tukaanza kuwaosha... ila wenzangu walikua spidi sana maana wamezoea.... kwahio baada ya kama nusu saa hivi tukawa tumemaliza kuwaosha hivyo tukawatoa wale pale chini na kuwaweka kwenye jokofu afu hawa wapya ndio walale chini



    UNAJUA UKIMPELEKA MAITI WAKO AU HATA KAMA KAFIA PALE PALE HOSPITALI... BASI KAMA ATAPELEKWA MOCHWALI KULE, UJUE HATOWEKWA KWENYE JOKOFU MOJA KWA MOJA.. KWASABABU YA KUMUANGALIA KWANZA KAMA NI MZIMA... HIVYO HAWEKWI KWANZA HUKO KWENYE BARAFU.... ANAWEKWA CHINI KWA SIKU MIJA AU MASAA KADHAA KWA UHAKIKA WA KWAMBA NI MFU NDIO AWEKWE HUKO... ILI WASIJE WAKAINGIZA MTU AMBAE YUPO HAI NDANI YA JOKOFU... HIVYO ANAWEKWA CHINI KWANZA NDIPO APANDE JUUU....... SASA HAPO TULIWATOA WALE WA TOKA JANA NA WA MASAA KADHAA YALIOPITA AFU TUNAWAWEKA HAWA MAITI WA LEOO



    Basi tulifanya hivyo na kuwaweka ndani ya jikofu kisha wapya tukawalaza chini. Baada ya hapo nikawaona wazee wanagawana pesa. nikana wacha nisogee huenda na mimi nikapata hata buku moja...

    "we unaenda wapi?"

    "mnhh Ah Ah mi naangalia tu"

    Wakawa wanaendelea kugawana pesa za kuoshea maiti ambazo zimekuja hivi punde...

    "afu uyu dogo kaosha maiti wangapi?"

    "kaosha mmoja tu"

    "haaaaaa yaani maiti karibia 25 kaosha mmoja tu?"

    "ndio"

    "we dogo ivi unafanya kazi au unatutegea tu?"

    "lakini mzee si unaona mi nilivyo kilema mzee"

    "hakuna cha ukilema hapa"

    "basi wakija wengine nitajitaidi"

    "ndio ivoo haya chukua hii buku 5 utulie... afu yule dada uliemuosha umeshampa mambo fulani?"

    Nikastuka huku nikijiuliza kua wasije wakanilaza na maiti hawa

    "ndio aaa tena ni mtamu kweli?"

    Nilidanganya kua nimesex nae lakini siafanya hivyo

    "ivi we unatudanganya hadi sisi?"

    "kweli vile mzee nimemla"

    "njoo.... hebu niambie huyu kaliwa huyu?"

    "ndio"

    "joni ebu lete kondom arudie tuone.... asilete utani apa"

    "lakini mzee kwani ni lazima?"

    "ni lazima ndio...we utakaaje na sisi utuchore tu"

    Daaahhh ililetwa kondom aisee ili nisex na yule dada aliekufa...

    "haya sema unakula au hauli"

    Sasa kabla sijaanza kula niliona watu ukutani wamesimama afu wananiangalia mimi. na hawa watu wamevaa magauni meupeee afu mmoja kavaa gauni jeusi...

    "aisee mzee wale ni akina nani?"

    "ntakutia mkonzi huo we dogo.. unamtisha nani? ivi pale na akili yako kuna watu pale?"

    "mzee kweli watu wale pale"

    "sikia nikuambie hapa leo huruki lazima umridhishe huyu mtoto wa kike"

    "mi sifanyi hio tabia"

    "lakini dogo ukumbuke kua umeshamaliza wiki tayari.....hivyo usishangae ukatoka bila hata senti"

    "kwanini mzee nikose pesa?"

    "ili ulipwe ujira wako haya shika kondom hiii anza kazi"

    "mzeee"

    "niniiii kama hutaki useme ila asubuhi ukitoka unanyooka nyoooo njee bila hata malipo. na si hivyo tu ni hurudi tena"

    Sasa nikafikiria laki mbili kweli niziache? hapana aiseee yaani kisa ni kumla huyu demu....

    Afu nikiangalia wale watu naona bado wananiangalia tu kama video flani hivi... yaani wanataka washuhudie ninachokifany......

    Lakini nilikua nawaza pesa yangu itaishia chini kweli? kisa ni kutosex na huyu dada.....

    "oyaa okoa muda bwana unaona nje kunaanza kupambazuka ujue"



    Nikaona potelea mbali nikaichana ile pakti na kuitoa kondom nje..... yaani kile kitendo tu cha kuitoa ile kondom na kutaka kuivaaa

    Nilijikuta nikianza kutetemekwa na mkono mpaka miguuu.... kana kwamba ninachokitaka kukifanya ni ufirauni uliopitiliza..

    Nikiangalia wale watu waliopo ukutani walikua wameinamisha vichwa vyao chini mithili ya watu wenye aibu fulani hivi........

    "dogo vp mbona umeduaa?"

    Nilikua nawaza jinsi ya kuanza huo mchezo wa kusex na maiti wa kike. daa kiukweli sikuipe ile tabia ya kusex nao hivyo niliamua kugoma na kama n pesa bora nikose kabisaa kuliko kufanya ufirauni ambao hata shetani mwenyenyewe hakai eneo hilo.

    "ivi we una kichaa? yaani ufanye kazi wiki yote hio afu uje kuacha pesa yako leo?"

    "mzee nimesrma hivi nasubiri tu kupambazuke niondoke zangu. kuliko kufanya huu ushenzi usio na kichwa wala mguu"

    Baada ya kuongea vile niliwaona wale watu waliokua pale ukutani wakiwa wameondoka. kana kwamba walikua wanataka wanishuhudie kitu nilichokua nataka kukifanya kwa wakati huo. Kweli niliwakatalia hawa wazee kwa kuonesha msimamo wangu zaidi. Baada ya hapo nilienda zangu mahali nikakaa ili nisubiri kupambazuke ili niondoke kazini tena naacha kabisa...

    "oyaa dogo mbona umekaa kiuzuni hivyo?"

    "ivi mnaona mlichokua mnanilazimisha ni sahihi kweli?"

    "Aaahh sikia dogo... unajua sisi hatutali kukaa na mtu ambae yupo tofauti na sisi.. kwasababu mshahara tunapokea sawa na kazi pia tunafanya sawa sasa kwanini na vitendo tusiendeane sawa?"

    "naacha kazi yenu"

    "ila chunga mdomo wako huko mtaani"

    "wala ata simwambii mtu"

    "tunafurahi kwakua tutakua huru.. maana mambo mengi ulikua unatubana sana.. kwasababu kuna saa zingine tunakula 0714 ila mbele yako hatukulifanya hilo"

    "mzeee sihitaji stori zako hapa"

    "mmhh sawa kijana ila nakutakia safari njema"



    Baada ya masaa mawili kupita. Na sasa ni saa 1 kasoro asubuhi.. walikuja watu wa shift ya mchana na kuingia kazini nasi wa shift ya usiku tukatoka kwa kwenda kupumzika.....



    Wenzangu walipitia ofisini kuchukua malipo yao ya wiki lakini mimi sikupitia kwa maana waliniambia kama nitapitia pesa basi wataweza kunisemea kwa boss wao kua.. nilifanya kitendo fulani na mtu aliokua mahututi na kumsababishia kifo chake...

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini nilipokua natoka nilikutana na yule mama akiwa anaingia kazini. nilitamani nisimuone kabisa maana najijua kazi ndio naacha hivyo. maana sitoweza kulala na maiti kamwe..

    "Ee kijana nakuona ndio unatoka? vp umechukua pesa yako?"

    Nilikaa kimya na kuangalia tu chini kama kondoo... Mama labda alihisi kitu fulani kuusu mimi hivyo alinishika mkono na kuenda nae ofisini....



    Tulipofika ofisini kwake mama alianza kunihoji baadhi ya maswali fulani tu..

    "vp kijana wangu? mbona leo huna raha kabisa?"

    "mmhhh mama ni kweli sina raha kwani leo nimeamua kuacha kazi"

    "kwanini chidi? Na ukiacha kazi hii utafanya kazi gani tena?"

    "mama wacha nikafanya hata kazi za mtaani tu... ila hii siiwezi kabisa"

    "ooopppsss hata hivyo nilijua tu kua utaacha... kwani kazi hii inahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana"

    "ndio mama kwaio nilikya tu naomba ruksa yako juu ya kuiacha kazi hii maana wewe ndio umenileta hapa"

    "sina cha kukuzuia, ila pesa yako umechukua?"

    "mngh hapana sijachukua"

    "kwanini sasa? hebu twende kwa boss"



    Alinishika mkino na kuelekea huko kwa bosi ambako ndiko mshahara unapotoka kwa wafanyakazi wa mochwali. Tulipofika tuliwakuta wale wazee wakusaini saini pesa zao. Walishangaa kuingia nikiwa na dokta mkuu. na kunidhania kua huenda nikawa nimemwambia kwa ushenzi wanao, Tulipofika pale mama aliongea na yule boss kisha nikakatiwa mshiko wangu.... kumbe hawa jamaa hawakujua kua nililetwa na huyu mama. hivyo waliogopa mno kuona nipo karibu na dokta mkuu, japo sikumgusia jambo hilo.



    "chidi ila nakuomba usihame nyumbani, kama una shuhuli zako we fanta tu lakini sijakufukuza nyumbani sawa?"

    "sawa mama"

    "nenda nyumbani basi ukanywe chai"

    "ndio naenda mama usijali"



    Nilitoka pale na kuelekea kwa yule mama...

    mama huyu ana mtoto mmoja wa kiume na mmoja wa kike ambae bado ni mdogo kama miaka 8 hivi na wa kiume ndio yule kelvin ambae tulikuaga wote sero... ila kelvin yeye ana hurka ya uhuni sana. hua hatulii kwao wala halalagi kwao siku nyingine asile kwao... yaani duu janga hilo....



    Sasa nilipofika hapo nilimkuta house girl akiandaa andaa mambo ya chai huku akionja

    "Eee hata kuandaa nako kunaonjwa?"

    Katoto kalijichekesha kinafki huku kakirembua... lakini kwa muda huu mimi sikua na hamu ya mapenzi na mtu yeyote yule. Kichwa changu kilikua bize juu ya maisha yangu... Nilikua ni mtu wa kuwaza kila siku ya mungu..



    Lakini nikiwa hapo sebureni nilikua naangalia tv. hivyo nikasikia maswala ya kusafisha nyota. na wakaweka na namba zao kabisa.. tena alikua ni mtu wa kigoma huyo mganga... Nilizichukua namba zake huyo sultani msafisha nyota.....

    Nilikua nina shaukua ya kuijua nyota yangu na vp je kuhusu maisha yangu? Mbona kila kazi kwangu ni ngumu na za ajabu tuuu..



    Ilipofika asubuhi niliamkia safari, ila sikumuaga mtu kua naenda wspi zaidi ya kuwaambia kua naenda mihangaikoni. Nilienda kupanda mabasi yaendayo kigoma ili nikakutane na huyo mganga ambae anaangalia nyota za watu......



    Safari ilituchukua masaa 8 njiani.... nilipofika kigoma nilimuulizia huyo mganga ili nikakutabe nae. na mganga huyo pia naskia anatoa utajiri wa hali ya juu kama utatimiza vigezo vyake...

    Nilionyeshwa mganga huyo na kufika hadi kwake. nikiwa na maswali mawili tu.... KUANGALIA NYOTA NA UTAJIRI

    "Olile olile, olile olile olile ooo naskia harufu ya mgeniiiiiiiiii karibuu"

    Daahh ilikua ni mikwara ya mganga kujifanya kaniona na wakati bado sijafika mlangoni kwake...

    basi nilifika kama ilivyo ada ya waganga hua hawanaga nyumba za maana kwa kazi zao.. yaani wanaishi katika vibanda ya majani au kuzungushia nguo... kisha kazi yao iendeleee....



    Nilipofika kwanza kajifanya kajua shida yangu.

    "kijanaaaaaaa najua unataka utajiriiiii"

    "ndio ndio broo"

    "usiseme broooooooo... sema hewalaaaaa sawa?"

    "sawa babu"

    "kwanza unataka kujua nyota yako?"

    "hewilooo"

    "sio hewilooo pumbavu...sema hewalaaa"

    "sawa sawa babu"

    "unataka kung'arisha nyota yako?"

    "heeeewaaaalaaaaa"

    "basi weka mkono wako hapa kwenye maji kisha fumba macho"

    Nilifanya kama alivyotaka mganga huku akinishika kichwa changu na kukitikisa kwa nguvu

    "ooooooo kijanaaaaaaa una maswaibu mengi sana... na nyota yako imefunikwa na ndugu yako..."

    "ndugu yangu??? ndugu yangu nani huyo?"

    "sema kwanza hewalaaaa"

    "niambie kwanza ni ndugu ganii?"

    "sema hewalaaa"

    "hewala"

    "eeeeeee hapo sasa ruksa kuulizaaa"

    "nataka kumjua huyo ndugu yangu"

    "ni ndugu yako na ana pesa nyingi sana.... na bila nyita yako atafirisikaa... maana utajiri wake ulikua ni wakooooooooo"

    "haaaaaa kwanini babu? sasa utaniseidiaje?"

    "ndiooo inawezekanaaaa ilaa utaweza masharti yakeee?"

    "ndio nitaweza"

    "sema hewalaaaa"

    "Aiseee babu unanichosha na hio hewala yako bhana"

    "sema hewalaaa"

    "Aaaahhhh hewalaaaa"

    "Shart la kwanza nenda ukalete panya aliezaliwa akiwa hana mkia"

    "heeeeeeeeee sasa nitamtoa wapi huyo?"

    "sharti la pili, nenda kalete jogoo mwenye mguu mmoja"

    "Duuuuuuuu"

    "shart la tatu nenda kalete ngozi ya kichwa ya kaka yako tajiri"

    "ah ah kwa hili swala la nyota hebu tuliache kwanza. . maana siwezi kuleta hivyo vitu mimi"

    "sema hewalaaa"

    "aaaa aiseee ubasumbua daaa Hewalaaaaaa"

    "teileeeee sema kingine kilichokuleta"

    "nataka kuwa fogo"

    "pumbavu majini yangu hayajui hilo neno la fogo"

    "aaaaa babuu si nataka kua zimba"

    "unaleta utanu sio?"

    "hapana babu"

    "haya sema hewalaaa"

    "aayaaaaaa Haya hewalaaa"

    "haya ulikua unasemaje?"

    "utajiri"

    "teileeee mizimu imekusikia na inataka kukupa mashart utayawezaaa?"

    "ntajaribu tu"

    "sisi hatutaki ujaribuuuuu"

    "Eee haya"

    Nilikua natetemeka ile mbaya maana naskia watu wengi ni matajiru kupitia huyu mzee... hivyo nilikua naamini atanipa utajiri wa kudumu...

    "kwanza kabisa njia za utajiri zipo aina tatu. je wewe wataka ipi?"

    "mmmhhh mi sijui hata moja babu"

    "sawa sawa sema hewalaaa"

    "hewalaa"

    "kuna njia ya kupata utajiri kupitia kuku"

    "kuku?? heee ngoja nikawanunue. ni kuku wangapi unataka?"

    "tulia kijanaaaa sio kuku huyo unaemjua wewe"

    "sasa ni kuku yupi?"

    "kuku tunae sisi... na kuku huyo tunamrushia punje za muhindi zipataza 7 akila zote 7 basi utajiri pamoja na uhai wako utadumu kwa miaka hio saba"

    "heeeeeeee na kama akila punje moja je?"

    "utaishi kifalme kwa mwaka mmoja"

    "heeee kwahio itategemea na ulaji wake?"

    "teileeeee"

    "haaaa Aaa hio sitaki... na je nikija na kuku wangu?"

    "haifai"

    "mmmn haya nyingine"

    "nyingine ni kufa kwa siku 7 afu hio siku ya saba ndio ufufuke ukiwa nyumbani kwako... na hio unapaswa uwe na mke mjasiri. ili aweze kuokota wale wadudu wanaotoka katika mwili wako"

    "heeeeee kwaio nitaoza kabisa?"

    "ndio.... tena utakufa moja kwa moja kama mke wako atapiga kelele"

    "apana pia hio siitaki.... ehe na hio ya tatu?"

    "ya tatu ni kuzuiliwa kitu fulani kwa miaka fulani"

    "mmhhh sijakuelewa hapo babu"

    "yaani utakapokua tajiri unaweza kupewa shart moja kati ya haya..... KULALA CHINI YA SAKAFU MIAKA YAKO YOTE, KULALA CHOONI MIAKA YAKO YOTE, KUTOKUA NA MAHUSIANO MIAKA YAKO YOTE, KUTEMBEA PEKU MIAKA YAKO YOTE, KUVAA NGUO CHAFU MIAKA YAKO YOTE, KUTEMBEA NA VIATU AU KANDAMBILI TOFAUTI MIAKA YAKO YOTE, KUVAA NGUO TOFAUTI MIAKA YAKO YOTE..... na vyote hivyo utavifanya ukiwa ndani ya utajiri"

    "eee mungu wangu...sasa raha ya utajiri ukuapi hapo? bira nikagange tu mtaani ila hio siwezi... ila hio ya kutembea peku ngoja nikaifikirie hio sawa babu?"

    "hewalaaaaa hakikisha ukirudi njoo na jogoo wa ngama"

    "sawa babu... ni shing ngapi?"

    "weka chochote hapo kwenye ungo"

    Niliweka kama elfu 20 hivi kisha nikawa natoka nje

    "toka kinyume nyume na usigeuke nyumaaaaa"

    Daaahhh nilipotoka nilikimbia mbio huku nikijiuliza kuusu yale masharti ya kua mchafu au kulala chooni... Sikupata jibu nichague lipi kati ya yale mart..

    Nilipanda gari na kurudi zangu arusha japo ngefika usiku.. maana nimepanda gari saa 11 jioni ambalo ni kama private car ( gari binafsi ) Walinipa kama lift tu kwa haya magari makubwa....



    Nilifika arusha usiku karibia saa 6 hivi. najiuliza pakulala kwa muda huo. maana sio vizuri kwenda kugonga kwenye nyumba ya watu kule kwa dokta. Nilizunguka hapo mjini kwa kutafuta sehemu ya kulala ila sio gesti bali natafuta chobisi....

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa bahati nzuri nikakuta mikokoteni imepakiwa mahari nami sikujiuliza sana. niliingia ndani ya mkokoteni mmoja na kujifunika na kisalfeti cha mkaa.....



    Usingizi ulikuja vizuri tu. kwani maisha ya tabu ni kama changamoto kwangu na pia nime yazoea sana tu. Nililala huku nikiota tu yale mavitu ya mochwali.. hivyo na kunifanya usingizi ukate kabisa ... sasa nikiwa nashangaa shangaa kwa kuinua tu kakichwa niliona msalagambo wa watu wengi wasiopungu mia hivi.. wakiwa kama wamebeba vibakuli flani afu kama vina maji kwa ndani. Walikua wamevaa majoho kama vile maaskofu fulani.... na majoho hayo yana mstari miekundu kwa pembeni..

    Sasa nikiwa bado nashanga ghafla nilipatwa na usingizi nisio utarajia. tena sikua nasinzia wala kua na usingizi... lakini nilijikuta nimelala ghafla tu



    Nilipokuja kuzinduka ilikua ni mida kama saa 11 arfajili ambako niliskia tu muazana msikitini.. ndio nikajua ni saa 11.. sasa nikiwa najifikicha macho ili kuutoa uchovu wa usingizi. nilishangaa kuona Kwato za ng'ombe zikiwa zimesimama mbele yangu... ila cha ajabu ni kwamba simuoni huyo ng'ombe mwenyewe kwani nilikua naona kwato tu...



    Lakini cha ajabu na cha kushangaza ni kwamba mkono wangu na mguu wake vilikua haviumi kabisa. tena sijiskiii kua na ukilema tena kwani hata yale mabendeji ya mkono na mguu sikuyakuta tena... Nilishangaa sana kuona kua siba mguu mbovu wala mkono ... kiufupi ni kwamba nimepona kabisa. ila sijui nimeponaje, maana najua jana nimelala nikiwa na mabendeji ya kutosha lakini cha ajabu leo siyaoni tena.... sasa nikiwa bado najishangaa



    Mara ghafla zile kwato zikarudi nyuma... saa hio mimi mavi debe yaani kukimbia siwezi. wala kuongea siwezi

    Sasa leo kwa mara ya kwanza ndio namsikia sauti yake... ila sikua namjua kwa sura wala nini. kwani hapa naona kwato tu...

    Na sauti yake ilikua ikijirudia rudia hivi mithili ya mwangwi...

    "usiogope siogope siogope"

    Ilikua ni sauti ya kike tena nzuri kupitiliza

    "nimetumwa na mkuu, na mkuu na mkuu"

    Ukisoma hivyo mara mbili mbili ni kwamba ndivyo sauti yake inavyojirudia kama vile upo ndani ya shimo fulani hivi au korongoni au ndani ya karavati ama daraja....

    "umetumwa na nani? afu we kwani ni nani?"

    "damu yako, damu yako, damu yako"

    "heee damu yangu?"

    "damu yako ina thamani kubwa sana mbele yetu, mbele yetu"

    "tafadhali sana dada angu naomba unisamee kama nina kosa"

    "nasema tunakuitaji, kuitaji, kuitaji"

    "mh mh hapana siwezi kwenda kwa watu nisiowajua"

    "Nimesema tunakuitaji uwe upande wetuuuuu, wetuuu, wetuuuu, wetuuu...... Damu yako pia inaweza kupambana nao, nao, nao.....ila ukikataa pia unaweza kuungana nao nao, nao, nao, nao, ....sasa chagua moja... kwenda kulia ama kushotoooooo, shotoo, shotoo, shotoo, shotooo?"

    Alikua akiongea kwa sauti kubwa utafikiri anautangazia umati fulani hivi. Nami nikawa najiuliza huko kulia ni akina nani? na huko kushoto ni akina nani?...... Nilijikakamua kuuliza japo kwa upole kidogo

    "Sasa kwani wewe upo upande gani?"



    Niliuliza huku nikijawa na uoga mwingi mno, Maana nilikua naongea na mtu ambae simuoni sura wala mwili, bali nilikua naona miguu ya ng'ombe tu. Yaani nilikua natetemeka kwa kusikia sauti ya mtoto wa kike afu simuoni wala nini. Lakini toka nilipomuuliza yeye alikaa kimya. na haikuchukua muda niliona zile kwato za ng'ombe zikitoweka bila kutembea.. yaani zilipotea katika madhingira ya kutatanisha. ila sasa nimebaki na maswali juu ya huyu mwanamke... Je? huyu ndio yule anaenifatilia toka kijijini au huyu ndio huyo upande wa kushoto? Nilijiuliza maswali mengi mno lakini sikupata jibu hata moja litakalo nitoa wasiwasi juu ya mtu huyu..... Na pia nataka kujua yule alienipakata na kunipeleka hospitali siku ile ya ajali, Nikiangalia madhingira niliona tayari kumesha pambazuka. yaani ilishafika muda wa saa 12 asubuhi. Ambapo niliendelea kuwepo pale pale kwenye mikokoteni iliopakiwa kwa mapumziko, Ilipofika saa 1 asubuhi Walikuja wenye mikokoteni yao, na kuniuliza uliza maswali kadhaa ya kwanini wamenikuta hapo.. nami sikuficha shida yangu... Hivyo walinielewa na kunipa mpaka tena ya kwenda kubebana na mikaa kutoka mahali fulani mpaka mahali fulani.. Tulipomaliza kubeba magunia ya mikaa tulienda katika soko la kirombero. ambako tulipewa dili ya kubeba karoti na makabichi... Kiukweli siku hio ilikua kama siku ya neema kwangu... kwani kazi zilikua nyingi mpaka raha. Sasa ilipofika mida ya saa 10 hivi jioni Ambapo ni muda wa kugawana mshiko nzuri kwa kazi ambayo tumeifanya...

    "jamani leo tumepiga kazi kweli au kisa ni huyu mgeni nini?"

    Aliongea jamaa mmoja ambae ni mmoja wetu tuliokua nae mchana kutwa

    "usikute ni huyu mgeni kaja na ridhiki huyu"

    Walikua kama wananisifia hivi. Ila mi nilikua kimya tu nasubiri mshiko..

    "sasa we mgeni kama buku 2 na jero"

    "haaaaa broo? ani kazi yote ile unanipa buku 2500?"

    "weee weee dogo nitakubutua mangumi sasa hivi ujue?"

    "basi broo yaishe"

    "yaishe nini maamae wewe, au ubajifanya unajua pesa sana sio?"

    Nilikua natokwa tu na machozi maana nilikua najituma kwa nguvu zote nikitegemea leo sikosi kiasi cha elfu 20 safiiii..... lakini huezi amini Eti nimepewa elfu 2 tu... Nilinyoosha ni mikono juu na kumshukuru mungu. Na kulitaamka lile neno langu la ONE DAY YES kwani naamini sitokua masikini siku zote, kwani mimi ni mtu wa kupigana na maisha.. .



    Nilitoka hapo nikiwa nafuta machozi ya huruma. na kwenda katika kihotel kidogo kilichopo maeneo ya stendi kwa ajili ya kwenda kupata chochote cha kuweka tumboni. Nilifika hapo nikala msosi wa buku moja... na kuongea na broo mmoja hivi aliopo katka mgahawa huo,

    "shamoo broo?"

    "maraaba vp?"

    "poa tu broo.... aaa broo nilikua nina shida kidogo"

    "shida gani?"

    "vp apa sipati ata kakazi cha kuosha vyombo broo?"

    "duuuu hapa waoshaji wanatakiwa wanawake dogo"

    "vp ata kwenye chipsi pale siwezi kukaa pale?"

    "kweli kabisa.. kwani pale kwenye chpsi sina mtu.. ila una uzoefu wa kupika chipsi?"

    "Daaa kiukweli sina kaka angu lakini mimi ni mtu mzima na ukinielekeza tu baweza"

    "ok usijali kazi utapata ila si unajua kua biashara haitegemeki?"

    "kivp labda?"

    "Yaani mara leo tumeuza mara kesho tusiuze. ila siku tukiuza utatoka na buku 2 na siku tusipouza utatoka na buku 1 tu au sio?"

    "sawa broo haina shida"

    "ila hata vyombo utaosha osha kidogo sawa?"

    "sawa broo"

    Basi mtoto wa kiume nilianza kazi siku ile ile. Ila kazi zilikua ni nyingi mno... kwani kumenya kukata na kukaanga ilikua ni mimi tu... siku zote hizo bado naishi kwa yule mama dokta....



    Siku zilizidi kwenda na leo ilikua ni siku fulani ya usafi.... hivyo manispaa ya jiji la arusha walikuja katika kimgahawa chetu na kuanza kutuuliza maswali ya hapa na pale.. kisha wakataka rushwa ya shilingi laki moja.. Ambayo ilikua ni ngumu kuipata maana walisema hiki kibanda kinatakiwa kitolewe, kwakua kulikua kuna msafara wa raisi kwa kutembelea jiji la arusha.. ila kama atatoa rushwa hio wataachwa. kwani hilo ni jukumu lao kutoa vibanda vilivyopo karibu na barabara ya lami..... Yule jamaa hakua na hio pesa hivyo kibanda kilivunjwa kiubabe na manispaa ya jiji hilo.. kwaio kama kibanda kimevunjwa na manispaa ya jiji hili. hivyo kwa upande wangu nitakua sina kazi tena. Hivyo nikaanza tena kazi ya kutafuta kazi, Nilikaa karibia siku tatu bila kazi



    Siku fulani nikiwa natafuta kazi katika masoko. hata nipate ya kuuza mtumba pia haina shida. Nilipitia sokoni pale nikakuta watu wanabeba magunia ya viazi na makaroti kwa kuingiza katika gari au kutoa.



    Niliomba nafasi sehemu hio na kupata kazi ya ukuli ( kibega au mbeba mizigo ) Nilianza ile kazi lakini sikuiweza kwa maana ya afya yangu ilivyo ndago. kwani yalikua ni magunia ya haswa Kama kilo 100 hivi. Sasa kilo 100 na mimi mwenyewe nina kilo 45.. duuuu si itakua ni kifo hicho??? Nilijaribu gunia moja ila sikufika nalo mbali likanidondokea na kuniumiza kiasi fulani. ila sikuendelea tena maana ningekufa. ..... Kwani mungu hapendi kusikia unafanya kazi huku ukinung'unika hovyo...



    Sasa baada ya kuumia nilikua nimetulia zangu mahari huku nikiuguza maumivu ya gunia.... Niliskia honi ikipiga mahari. Jikaona aahhh labda ni honi honi zao hizi hivyo sikumfatilia huyo mpiga honi Kwani nilikua nimejichokea kwa kuanguka na gunia la karoti, Nilikua kama nasinzia hivi huku nikiwa sina hata pakuenda kula na mchana huo. kwani naona hata aibu ya kwenda kula kule kwa yule mama dokta... hua napenda nile jioni tu. na sio mchana



    Nilikua hapo chini ya mti fulani karibu na barabarani.

    Niliendelea kuisikia ile honi nikaona kama inanisumbua vile. Haikupita hata dakika tano mara nilishikwa bega kwa nyuma na mtu nisiemfahamu kua ni nani, Hivyo niligeuka na kumuangalia huyo alienigusa

    "Aaaaaaahhh shkamoo mzee"

    "marahaba kijana hujambo?"

    "aaa sijambo mzee wangu"

    Alikua ni yule mzee alienipaga biznesi kadi yake na kunipa shilingi elfu 50.. tena kwa bahati mbaya aliibiwa shilingi milioni 10 na WADUDU WA DAMPO kama unakumbuka hata mimi nilikua mmoja wao, na ndio nilikua nchora map wao....

    "vp si nilikupa namba zangu unitafute kijana?"

    "ndio mzee ila ile kadi ilipoteaga mzee wangu"

    "ooo pole sana kijana wangu na vp umekula?"

    "mmhhh mzee kula kwangu ni kwa mnyato sana mzee. yaani hapa unavyoniona sijala toka asubuhi"

    "kwanini kijana ufe njaa na wakati una mwili wa kufanya kazi? afu vp mbona huna yale magongo yako?"

    "mzee we acha tu, Kwani hata mimi sijui nimeponaje kwakweli"

    "mmhh pole sana kijana... basi twende tukale pale novo"

    "Novo??"

    "ndio au hupendi?"

    "mzee mzee ivi na hali yangu hii naweza kuingia novo kweli?"

    "aaaahahahaha usijali hapa upo na mtu mzitooo hebu twende bwana"

    "sawa mzee"



    Novo ni hotel moja ya kifahari sana hapa jijini arusha... kwa jina halisi inaitwa ~Mount Meru Hotel~ sasa ukisikia Neno NOVO basi ujue ni huko....

    "mbona kijana una nguvu za kufanya kazi tu?"

    "mzee mzee? ni kweli naweza kufanya kazi yeyote ile. ila sasa kama unavyojua serikali yetu ilivyobana kazi hivi?, ulizani nitapata ajira mzee?"

    "kijana wanguuu usiseme hivyo, mbona kazi zipo nyingi tuuu... we niambie kama kweli unataka kazi nikitafutie.. tena ni kazi ya maana kijana?"

    "mzee hata sasa hivi kama ipo nipeleke. ila isiwe ya watu waliosoma sana. maana mimi ni darasa la saba mzee"

    "usijali hilo kwani kazi zetu sisi hua hazina haja ya elimu"

    "lakini si zina malipo mazuri mzee?"

    "mmhhh mi sisemi ila utajionea mwenyewe huko huko"



    Tulifika Novo hotel kisha nikapiga diko la kitajiri ambalo ni binge ya msosi, Tulikula tena kwenye meza moja bila ubaguzi wowote, Baada ya kula tulitoka na kuelekea ofisini kwake.... kiukweli alikua ana ofisi kali utafikiri ni ofisi ya raisi Haaa palikua panapendeza sana kiukweli,



    "ila kijana utaiweza kazi?"

    "mzeeee hakuna kazi inayoshindikana hapa mjini mzee"

    "nakuuliza tena. utaiweza kazi kijana?"

    "mmhh mzee mbona tunatishana tena"

    "ok usijali... kazi utapata endapo utakuja na wenzako watano ukiwa wewe ni wa sita"

    "mmhhh mzee mimi hapa mjini sina ninaemfahamu hata mmoja kwakweli kwahio sina wa kukuletea mzee"

    "yaani hata watu wawili utakosa?"

    "ndio mzee wangu"



    "mmmhh unaonekana huna nia na kazi wewe"

    "mzeee na mateso haya kweli nisiwe na nia na kazi mzee?"

    "ok kazi ipo ila kuna kiingilio kinahitajika"

    "kiingilio?? kiingilio gani tena?"

    "unahitajika ulete mbuzi mchanga"

    "mbuzi mchanga? sasa mbuzi mchanga wa nini tena?"

    "huyo ni kwa ajili ya kukutolea mikosi na laana zote"

    "Aaaaaaa okeeeee sasa mi sijui pakumpata huyo mbuzi mtoto"

    "nitakuelekeza pakumpata mbuzi huyo.. na chukua hii laki 5 kwa ajili ya kwenda kumnunua mbuzi huyo"

    "heeeeee huyo mbuzi anauzwa laki 5?"

    "hapana bali hio nyingine utatumia tu"

    "asante mzee wangu nashukuru sana"

    "usijali kijana, kwani ni jukumu letu kuwaseidia vijana kama nyie"

    "kwahio sasa nitampeleka wapi huyo mbuzi?"

    "aaaaa kwanza kabisa twende nikupeleke katika kampuni yetu kuubwa kabisa"

    "sawa mzee"



    Tulitoka hapo na kupanda gari yake kali kuliko

    "kijana gari kama hizi kwako zitakua kama viatu tu"

    "aaaa wapi mzee.... usawa wenyewe ndio huu wa manati?"

    "mi sisemi bali utajionea mwenyewe tu"

    Tulikua tunapiga stori za hapa na pale huku tukielekea katika kampuni yao ambayo ina wafanyakazi wengi kuliko kampuni yeyote hapo jijini arusha.....



    Tulifika katika jumba moja kubwaaaaa lenye uwanja usiopungua heka kumi.. yaani utafikiri ni kiwanda fulani hivi kumbe ni kampuni yao huyu mzee....



    "hapa ndio kwenye kampuni yetu na hata huyo mnyama unapomleta utamleta hapa hapa ndani"

    "Eeeeeeee mzee hii yote ni kampuni yenu hii?"

    "ndio kabisa"

    Niliingia huko ndani kwao... duuu yaani kuanzia getini ni tailizi mwanzo mwisho hadi tumeshuka kwenye gari ilikua ni full tailizi duuu mpaka naogopa kuikanyaga aisee.. . Basi tuliingia pale ndani ambapo ndipo kwa sekretali. ila huyu mzee sikupita nae huko

    "kijana? utanikuta huko mbele sawa?"

    "wewe unakwenda wapi tena mzee?"

    "utapewa maelekezo yote hapo"

    Mmmhhh nilishindwa kuelewa hapa inakuaje hapa...

    Mmm basi nilipitia huko kwa sekretali wa kampuni hii na kuongea nae

    "karibu"

    "asante... aaa kuna mzee kaniambia utanipa maelekezo ili nikakutane nae huko mbele"

    "oohoooo basi pitia hapo mbele.. utakuta sinki la kunawia maji... utanawa kwa maelekezo utakayosikia hapo"

    "maelekezo???"

    "ndio we nenda tu"

    Nilishangaa kusikia mambo ya kuelekezana... afu mbaya zaidi wafanyakazi wenyewe wapo siriasi na hawakuangalii usoni...

    "ukifika pale bisha hodi"

    Basi nilianza kutembea taaratibu huku nikiwa na wasiwasi mwingi mno, maana nipo katika jengo kubwa ambalo sijawahi kuingia hata siku moja, Nilipofika hapo nilipoambiwa nibishe hodi? nilifanya kama nilivyo ambiwa na secretari kua nikifika hapo mlangoni basi napaswa kubisha hodi...

    "hodi, hodi, hodi,

    Nyumba ilikua inatoa sauti mara mbili mpaka nikawa naogopa. maana naisikia sauti yangu ikijirudia rudia

    "karibu, karibu, karibu,"

    Niliitikiwa na mtu ambae sikua namuona ila hakukua na giza wala nini..... kwani taa ndio zilichukua nafasi ya giza katika nyumba hio. hivyo kuona giza humo ndani ni ndoto...

    Kwakua sauti ya huyo mtu alionikaribisha ilikua ni nzito na ya kiume hivyo nilimsalimia huyo mtu

    "shakamoo, kamoo, kamoo, kamoo?"

    "marahaba hujambo kijana, kijana, kijana?"

    "sijambo, sijambo, sijambo, sijambo"

    "kwanza unaitwa nani?, nani, nani?"

    "naitwa rashidi, rashidi, rashidi"

    "una ndugu?, ndugu, ndugu?"

    "ndio, ndio, ndio"

    "kwahio una familia kubwa tu, kubwa tu, kubwa tu?"

    "ndio ninayo, ninayo, ninayo"

    Nilijibu hivyo ili kama ni mshahara nipewe mkubwa. maana najua familia yangu ni kubwa mno... na inanitegemea mimi

    "sawa kabisa Sasa sogelea hio sinki na unawe mikono yako na kusema kua ( naunawa umasikini na kuingia utajiri ) anza sasa, sasa, sasa, sasa"

    Niliisogelea ile sinki la kunawia kisha nikataamka hayo maneno alioniambia mwanzo

    "tayari nimemaliza, maliza, maliza"

    "sawa kabisa Sasa kwakua umekosa kutuletea wafanyakazi watano. hivyo itakugarimu kuleta mbuzi mchanga sawa? sawa, sawa?"

    "sawa nzee, sawa mzee, sawa mzee"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "sawa kabisa unaweza kwenda kwa kupanda hio ngazi, ngazi, ngazi"



    Baada ya hapo nilipanda ngazi fulani ambazo nimeelekezwa kisha nikashuka na kumkuta yule mzee kakaa sebuleni. Yaani hio sebule yenyewe ni kama uwanja yani duuuu... afu hio Tv saaa... ndio kituko kabisaaa... maana tv utafikiri ni ukuta mzima duuu...

    "vp kijana tayari?"

    Aliniuliza yule mzee huku kama haamini amini kama nimepita salama huko nilipotoka......



    BAADA YA SIKU HIO KUPITA



    na sasa ni siku nyingine tena nikiwa tayari nimeshampata yule mbuzi aliotakiwa kule ofisini..... Tulipanda gari na mzee kisha tukaondoka zetu kuelekea huko kwenye ile kampuni..



    Tulipofika tuliingia nyuma ya huo mjengo ambao upo kimya sana siku zote.

    Nilishangaa kukuta vijana wenzangu wakiwa wamejipanga mstari huku wakiwa wameweka mbuzi wao chini kila mmoja. tena walikua wameshika visu. Nilisikia tu

    "tulikua tunakusubiri wewe"

    Ni mkuu wa kampuni hio ndio aliniambia mimi..

    Basi nami nikaweka kambuzi changu chini kisha nikaletewa kisu kimoja kikali na cha ajabu kweli... Ila sikujali kitu.

    Lakini nikiangalia hawa watu wengine ambao wanashuhudia uchinjaji huu. walikua wamevaa majoho kama maaskofu vile.... na nikivuta kumbu kumbu ni kama vile kuna mahari niliwaona hawa watu... ila sikumbuki sana....



    Mara mkuu akatoa amri kua

    "haayaaa kila mwenye kinyama chake achinje mwenyewe kwa kujiondolea mikosi na balaa katika maisha... Kila mmoja aanze kushika kichwa cha mbuzi wake na kuweka kisu sawaaa"

    Tulifanya maelekezo tunayopewa na mkuu huyo ambae haonekani sura kwani nguo alioivaa imemfunika usoni kabisa.....



    Lakini cha ajabu na chakushangaza mkono wangu ulioshika kisu ulikua unavutwa na mtu nisiemuona... tena huyo mtu inaonekana labda hataki nichinje kinyama hicho. hivyo nilikua kama napambana nae vile..

    "mkuu mbona kuna mtu ananipokonya kisu?"

    "nimesema chinjaaaaaaa.... naesabu mpaka tatu nione visu vyenu vikichuruzika damu sawa?"

    Tukaitikia sisi ambao tumeshika visu

    "sawa mkuuu"

    Lakini bado nilikua napokonywa kile kisu ila sikua nataka kupokonywa kwa maana ataniharibia maisha yangu kwa kutojitolea mikosi na mabalaa kwa kutumia mbuzi huyu....

    "1…………2……………3......... Nani bado hajachinja kinyama chake??"



    Kiukweli nilikua ni mtu nisiwezaga kuchinja, kwani hata kijijini kwetu nilikua naogopaga kuchinja hata kuku. Hivyo hata hapa katika uchinjaji huu. Niweza lakini ni kwa mbinde sana.......

    "1…………2……………3........... Nani bado hajachinja kinyama chake??"

    Tuliitikia kwa wote tena kwa sauti

    "wote tumechinja mkuu?"

    "safi sana, pongezi kwenu?"

    Lakini kwa upande wangu roho ilikua ikiniuma sana. na sijui ni kwanini... Sikukaa muda machozi yalinitoka kwa wingi utafikiri nimepigwa nyundo ya kichwa. Kiukweli roho yangu ilikua ikiniuma sana huku machozi mengi yakinitiririka kwa wingi. Ila sikujali kikubwa ni kwamba nashukuru kwa kujitolea mikosi na mibalaa ya hapa na pale.....



    Tulipotoka pale machinjioni tuliingizwa katika chumba kimoja kama darasa vile. maana lilikua lina vitu na vimeza vyake. ni kama sehemu ya mkutano yani ila imekaa kama darasa.

    Tulipoondoka tuliviacha vile vinyama pale pale nje. ndio tukaingia katika hicho chumba fulani kwa ajili ya mahojiano zaidi, Tulikaa kimya sana maeneo hayo na mkuu wa hii kampuni alikuja na kutupa mpangilio mzima wa kazi, Tulikua kimya kwa kumsikiliza huyo mkuu

    "habari zenu vijana?"

    Tuliitikia kwa wote huku kila mtu akiwa katika wasiwasi wa mahojiano hayo, ( Interview )

    "salama tu mzee"

    "sawa kabisa... aaaa kampuni yetu sisi hua haipendi kuajiri mtu mwenye mikosi na mabalaa aliotoka nayo kwao... hivyo kila unaemuona hapa kwenye kampuni hii basi ujue kafanya kama hivyo ulivyochinja kinyama hicho"

    Tulikua makini sana kwa nasaha ambazo tulikua tukipewa kwa wakati huo

    "kwahio hapa leo tupo pamoja ila tutakua tukikutana kwa siku ya vinyama tu.. au iwe tusionane kabisa, hivyo kuhusu kazi ni kwamba mumeshaipata hivyo kabla hamujaanza kazi kuna masharti munayopaswa kuyajua"

    Aliposema hivyo watu wakaanza kuangaliana kwa kujiuliza uliza kua ni masharti gani hayo?

    Ila hatukua na jibu zaidi ya mkuu Hivyo tuliendelea kumsikiliza kwa umakini

    "kwanza kabisa kila miezi miwili ni lazima tuchinje vinyama.. kwa ajili ya kujilinda na watu wabaya.... pili pesa ya kampuni hii unapaswa uitumie unavyotaka ila kasoro sehemu mbili tu. ndio hupaswi kuitoa, na ya tatu hutakiwi kulalamika kua huna pesa na wakati kampuni yetu ni kisima cha pesa... nadhani masharti yetu ndio hayo tu. je? mutayaweza?"

    Tukaitikia kwa wote tena kwa furaha

    "ndiooooooooo"

    "sawa kabisa.. kwahio ukitoka hapa utamuona aliekuleta kisha atakuonyesha makazi yako mapya.. kwani sisi hua tunampa mtu kazi pamoja na nyumba na gari... hivyo vyote utamuona aliokuleta hapa.."



    Yaani kwa hizi nasaha zilizokua zinaongelewa na huyu mkuu wetu zilinifurahisha sana... kwani kutoa nyumba gari na kadhalika ni dhahiri kua maisha yangu tayari yameshakua ya kitajiri. Basi tuliendea kumsikiliza mkuu kwa masharti ya kampuni yake hio.

    "vp kuna mwenye swali lolote?"

    Aliinuka kijana mmoja hivi niliokua karibu nae

    "mkuu nina swali moja tu"

    "uliza"

    "ulisema tutumie pesa jinsi tunavyotaka..ila kasoro sehemu mbili tu. je? hizo sehemu ni zipi?"

    "swali zuri sana... Kwa hizo sehemu hautoambiwa leo. bali utaambiwa na mtu wako aliekuleta na sio leo lakini. hivyo umuulize baada ya kuchinja kinyama cha pili sawa?"

    "sawa mkuu"

    "sasa kuanzia leo mpaka maisha yako yote umeshajiunga na kampuni ya POWER TO PEOPLE ( NGUVU KWA WATU ) hivyo kujitoa yaweza garimu maisha ya mtu... kwahio kueni makini sana na kazi zenu...na nawatakia maisha marefu na yenye upendo juu yenu. ahsanteni sana"



    Mahojiano au interview ilikwisha na sasa kila mtu anapelekwa katika makazi yake mapya ya kitajiri...

    "vp kijana? umeona kampuni yetu ilivyo na ubinaadamu?"

    "daaahhh mzee siku zote ulikua wapi mzee? Eee hebu ona sasa na mimi naweza kusimama mbele za watu na kutoa ushauri fulani na ukasikilizika vizuri.... kiukweli mzee nakushukuru sana mzee wangu yaani nashukuru sana mzee wangu"

    "usijali kijana kwani sisi ni watu wa kumseidia mtu.. na mimi naamini mungu asingeweza kukuseidia maisha yako yote"

    "mmhh kwanini mzee useme hivyo?"

    "nasema hivyo kwasababu kama mungu anaseidia watu basi wewe leo ungeshakua tajiri. lakini ona umekua tajiri kupitia binaadamu mwenzako"

    "ni kweli kabisa hata mimi naamini mungu haseidii aisee"

    "umeona eee?"

    "kabisa"



    Tulikua tupo kwenye gari tukielekea huko njiro ambako pia kaka yangu anaishi huko huko maeneo ya njiro.. Tulifika katika nyumba hio na kufunguliwa geti na mlinzi... Tulishuka katka gari na kuanza kuikagua nyumba mpyaaa....

    "hii sasa ndio nyumba yako ya maisha yako yote"

    "haaaaaaa mzee acha utani mzee... heeeee na zile gari tatu pale ni za nani?"

    "nilikuambia kua gari kama hizi kwako zitakua kama viatu tu... sasa zile ni gari ulizonunuliwa na kampuni yako.. na huko ndani kuna droo za pesa ambazo utachukua kiasi cha kama milioni 10 hivi ukafanye shoping ya nguo"

    "haaaaaa mzee acha utani. yaani milioni 10 nifanye shoping ya nguo tu?"

    "ndio.. au huamini? njooo uone mabegi ya pesa kwa ajili yako"

    Niliongozana na mzee hadi ndani ya chumba changu cha kulalia. na kufungua mabegi fulani yaliojaa pesa za kitanzania aina shilingi elfu kumi kumi tuuuu... mabegi yalikua yapo mawili yaliojaa pesa tupu, Nilishangaa kwa kuona vile

    "mzee hizi pesa zote ni zangu?"

    "na bado huu ni mwanzo tu"

    "mh mh Hapana mzee naomba uniambie hii ni kazi gani inayotoa malipo ambayo hata raisi mwenyewe halipwi hivi"

    "ndio maana ukaambiwa kampuni yetu ni ya kipekee sana duniani kote... na ina matawi katika dunia nzima"

    "sasa hizi pesa nimelipwa kwa kazi gani nilioifanya?"

    "hizi pesa zimetoka katika supa maketi ambayo itakua ni kitengo chako cha kazi na wewe ndio msimamizi wa supa maketi hio... hivyo haya ni mauzo tu"

    "toobaaa yarabi roo yangu... kwahio mimi kazi yangu itakua ipo kwenye supa maketi?"

    "yaani wewe ndio boss wa hio supa maket"

    "aaaaiseee nashukuru sana mzee wangu. nashukuru sana mzee kwa kunifanya na mimi nionekane mtu mbele ya watu"

    "usijali kijana.. naaa vp gari unaweza kuendesha?"

    "hapana mzee siwezi kabisa"

    "ok nitakufundisha mimi mwenyewe na tutakwenda kukutafutia leseni yako sawa kijana?"

    "sawa mzee wangu"



    BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA



    Leo nilikua katika ofisi yangu ndani ya supa maketi. ambayo ndio naimiliki....

    Kiukweli natamani sana familia yangu ije mjini. kwani kijana wao nimekua na pesa mingi mno kuliko hata kaka yangu hatibu. Nilikua nina usongo wa kwenda kwake kumringishia utajiri lakini haina maana kuenda huko..... Basi leo Ilipofika mida ya jioni nilitembelea katika moja ya maduka makubwa makubwa kwa ajili ya kununu nguo za mtoto wangu.. Japo sijui kwa sasa ana umri gani. maana ni muda mrefu sana sijawasiliana nae muda mrefu, kwasababu namba zao hua sinaga kabisa. kwani toka siku ile simu yangu itupwe mferejini na wale askari. hivyo sikua na namba yeyote ya huko kijijini.



    Sasa nilipotoka katika duka la nguo nilimkuta mtu kakaa ndani ya gari yangu afu kama kainamia chini kichwa chake. tena yupo kwa mbele afu kavaa nguo nyeusiiii.... Ilikua ni mida ya jioni jioni kama saa 12 hivi. Basi kwakua ni gari yangu sikusita kuifungua na kuingia na mizigo yangu ya nguo za saidi...

    Kwanza nilitamani kumuona lakini sikuweza kumuona kwakua alikua kajiinamia. Nilimuuliza tu

    "samaani sijui ni nani mwenzangu?"

    Sikujibiwa ila alionekana kuamka tu na kuniangalia.. . ... Alikua ni msichana mmoja mzuri sijapata kuona dunuani kote. yaani alikua ni mweupe afu ni mzuri wa ajabu na anaonekana ni mtu wa heshma sana. afu pia alikua kavaa hijabu na uchungi wa kawaida tu.... Sasa nilipomuona hivyo nikajua huyu ni muislamu tu hivyo nilimsalimia kiislamu tu

    "asalam aleykhu?"

    Alikua pia yupo kimya na kuniangalia tu huku machozi kama yakimtoka vile.... nilishindwa kutambua hii mambo inaendaje sasa..

    "unaineka mstaarabu sana lakini roho yako imejawa na tamaa nyingi sana"

    Aliongea hivyo nami nilikua namsikiliza tu kwa utumbo wake anao uongea.

    "ulikua ni kijana mzuri sana ila tamaa imekupoza sana..... Sasa hebu niambie hizo nguo umemnunulia nani?"

    "kwanini uniulize hivyo? we kama wataka pesa semaaaaa... najua mshaanza kujigonga gonga kwangu na kujufanya una heshma na wakati ni kahaba tu wewe"

    "kijana wacha zarau zako utaishia pabaya"

    "pabaya?? hahahahahahaha Eti pabaya.. pabaya na wakati nilipotoka ndio pabaya.. weee manzi ni vipi wewe?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ok nashukuru kwa dharau zako ila hizo nguo utavaa mwenyewe"

    "Aaaaaahahahahaha Aaaaahahahahahaha uuuuwiiiii..... ungejua nina kidume cha mbegu wala usingesema kua nitavaa mwenyewe.. sasa kwa taarifa yako nina kidume hicho we acha tu... na nina mpango wa kwenda kuwachukuwa wotee na mama yangu waje kula maisha mjini umenielewaaaa Aaahahahahahahaha uyooo mbona upo kimya?"

    "umeongea sana ila mimi sina cha kuongea. lakini najua utalia sana... kwani tayari umeshanunua kilio ndani ya moyo wako"

    "waaaapi weweeee hayo ni maneno ya mkosaji tuuuu"

    "sawa nashukuru kwa kutokunisikiliza maneno yangu"

    "sawa sasa vp mdada una mchumba wewe?"

    Hakunijibu alibaki kuniangalia tuu kwa muda mrefu kisha akasema

    "kwani si una mke wewe? sasa mimi ni wanini tena"

    "aaaaa we ni mrembo sana njoo basi karibu mamiii... tena kama ni pesa hapa ndio kisima chaooo"

    Heeeee sasa mdada alikua anakuja kweli kunipa denda eti....na mimi nilijua ni utani... huezi amini nilikula denda bila wasiwasi huku nikiwa namshika shika mbavu zake.... nilimminya matiti yake madogo dogo na yaliosimama.... Lakini ghafla alishtuka kama mtu alioitwa vile. Kisha papo hapo aliniachia na kushuka ndani ya gari.....







    ITAENDELEA

Blog