Search This Blog

Thursday 27 October 2022

ONE DAY YES - 5

 http://pseudepigraphas.blogspot.com/2019/12/one-day-yes.html

    Chombezo : One Day Yes

    Sehemu Ya Tano (5)







    Lakini ile anashuka tu Aisse kuna kitu nilikiona ambacho nilisha wahi kukiona sehemu fulani ila sikumbuki sana

    Aisee sikuvumilia kitu nilimuita maana mooyo ulishanienda mbio...

    "we dada wewe?"

    Hakuitika ila aligeuka tu na kuniangalia....

    "vp hio miguu yako mbona ipo hivyo?"

    Hakunijibu kitu bali alipotea tu katika madhingira ya kutatanisha... Nami na uoga wangu nikapanda gari na kuendesha kwa spidi mno huku nikiwa nahema juu juu kwa kuona mtu akipotelea mbele ya macho yangu.....



    Nilifika nyumbani na kushuka ndani ya gari huku nikiwa nimebeba nguo za side wangu.... nilipitiliza mpaka ndani chumbani na kutulia kwanza huku nikiwa nimelala chali kitandani. nikiendelea kumkumbuka yule msichana wa kwenye gari...



    Mara ghafla nikaanza kusikia sauti huku ikijirudia rudia mithili ya mtu aliopo kwenye shimo fulani hivi....

    "umefanya kosa, fanya kosa, fanya kosa"

    Nilikua najiuliza kuusu hio sauti inayoongea humu ndani ya nyumba tena ipo juu ya siling bodi.

    "yule mwanamkee mwanamkee, mwanamkee.... ni adui yetu. adui yetu, adui yetu.... kwa kosa hilooo, hiloo, hiloooo,..... unapaswa utoe sadaka ya mbuzi wa kike aliozaa uzao mmoja tuuu, tuuu, tuuu, tuuu.... tena fanya hivyo usiku wa leoooo, leoooo, leooo, leooo"

    Heeeee sasa nikajiuliza kwani yule mwanamke ni nani? ila sikupata jibu kwa wakati huo



    Nilitoka tena kwa wakati huo na kwenda katka mabanda ya mbuzi kisha nikanunua mbuzi aliozaa uzao mmoja..... Kisha nikaja nae mpaka nyumbani

    Sasa nikawa nimekaa nae mahali nikisubiri maelekezo juu ya mvuzi huyu



    "mpeleke machinjioni kule katika kampuni yetuuuu, yetuuu, yetuuu"

    Nilifanya hivyo mara moja ili tu pesa zangu zisiishe. maana niliambiwa nisipofanya nitapoteza pesa zangu zote.. na kuikaribisha mikosi mingi katika maisha yangu



    Nilifika machinjioni na kukuta pako kimya sana, kwani ilikua ni mida ya saa 6 usiku, hivyo nilimlaza mbuzi yule na kwenda kuchukua kisu mahali ambapo kuna chungu kilichosimamishiwa kwa juuu....



    Lakini nilipoenda kuchukua hicho kisu nilisikia sauti za watu wengi wakilia kwa mateso wanayo yapata. Mmhhh ikabidi nizifatilie hizo sauti ambazo zinalia na kutaka msaada fulani..... Sasa kumbe hiiii sehemu ina korongo refu kweli. nilisogelea na kuchungulia kidogo huko chini ya korongo...

    "mungu wangu eeee"

    Nilijisemea hilo neno lakini ghafla kichwa kilianza kuniuma na karibia naelekea kule korongoni kunako watu wanaolia......



    Nilijikuta nimedondoka chini kwa kizungu zungu nilichokua nacho. Nilipodondoka pale chini, Nilikua naskia vishindo vingi mno ambavyo vilikua vikipiguza chini ya aridhi, Nilishindwa kuelewa kuusiana na jambo hilo.



    Lakini ghafla niliskia sauti ikiniambia

    "amka uchinje kinyamaa, nyamaa, nyamaa"

    Nilijikuta nimepata nguvu na kuamka na nguvu mpya... Nilimshika yule mbuzi na kumuelekezea kibla kwa kunitolea kafala juu ya makosa yangu. sikukawia kuchinja, Nilimchinja mbuzi yule tena bila hata wasiwasi juu ya hilo nililolifanya. Lakini baada ya kuchinja? ghafla nilisikia watu wakilia katka ile damu ambayo ndio imetoka sasa hivi katika shingo ya huyo mbuzi, Nilishindwa kuelewa kwanini nayasikia sana mauza uza toka niingie katika kampuni hii? Nilijiuliza sana kuhusiana na jambo hilo lakini sikupata jibu sahihi kuhusu milio hio.... Basi niliweka kisu pale chini na kuondoka zangu, Lakini nilipokaribia kutoka getini niliskia sauti ikicheka kwa sauti kisha ikaniambia..

    "safi sanaaaaa..... umefanya jambo jema sana, Ilaaa utakapo pata taarifa fulani huruhusiwi kutoa choziiiiii, choziii, choziii, choziiii"

    Mmhhh nilishindwa kumuelewa huyo mtu kua alimaanisha nini. Basi mlinzi alifungua geti kisha nikatoa gari langu. na kuelekea nyumbani kwangu. Huku nikiwa na furaha ya hapa na pale kwa kusamehewa kosa langu. Mida hio ilikua ni mida ya saa 7 usiku Lakini nilipofika pale kwenye kona karibia na pepsi katika barabara ya njiro..... nilishangaa kuona mtu akiwa kasimama katikati ya barabara huku akiwa anavuja damu shingoni, tena alikua kavaa gauni heupeee pyeee..... Nilianza kuogopa hapo barabarani na kushindwa kuendesha gari, hivyo nilibaki tu nimeduwaa kama dudu vile,

    Lakini punde sii punde niliona yule mtu katoweka ghafla bini vuu... Niliwasha gari na kutoka mbiooo. Hadi kufika nyumbani kwangu, Nilijitupia kitandani bila hata kuvua viatu na kuulazimisha usingizi ili nipotezee kwa kile kilichonitokea muda si mrefu....

    ***********************************

    Mara nilianza kusikia sauti ya mwanamke akilia huku akisema



    "mume wangu, mume wangu, mume wangu, Tafadhali sana mume wangu.. naomba utoke huko ulikoo, ulikoo, ulikoo, Kwani kampuni ulioajiriwa sio kampuni ya binaadamu, binaadamu, binaadamu, kwa sasa umeshaniua mkeo na utaendelea kutumaliza sisi... familia yako inalia kwa kufiwa na ndugu kila siku...... Mume wangu? naomba utoke kwenye hilo kundi. kwani tayari umeshatuua mimi na mwanao, mwanao, mwanao, mwanao"

    ************************************



    "Noo Noo sio kweli we side wangu side wangu hawezi kufaa"

    Nilikurupuka kitandani huku jasho likiwa linanitweta vibaya... Daahh kumbe nilikua naota eti nimeua mke wangu na mtoto.. Daahh haitokaa kutokea hata siku moja kumuua side wangu na mke wangu. siwezi kabisa. Niligundua nimelala na viatu hivyo nilivua viatu huku nikifikiria hii ndoto ambayo nimeiota muda sii mrefu, Afu ni mke wangu ndio kanijia katika ndoto huku... tena huku akilia kwa sauti ya huruma.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sijui ni kwanini nimekosa namba za nyumbani. maana hii ndoto imenishtua sana, Daahh niliendelea kulala huku nikiwa na hamu ya kwenda nyumbani kuiona familia yangu. kwani kwa sasa nimeshakua tajiri wa kutupwa, yaani nimekua bnge la tajuri.....



    BAADA YA MIEZI MIWILI KUPITA



    Siku zilizidi kwenda na pesa nazo zilizidi kunielemea kwa wingi mno, maana rumu yangu yote inanukia pesa tu. na hata kitambi kimeanza kuota..... Nilikua ni mtu ninaependa starehe sana Nilikua natembea na wanawake wawili wawili tena kwa kumwaga pesa kibao... naweza kulala na mwanamke mmoja kwa shilingi milioni 1 tena bila kupunguza kitu. Kiukweli nilikua ni malaya sana, yani hakuna demu ninayemkosa mbele ya macho yangu, hata awe nani



    Basi nilikua natoka zangu NOVO hotel nikiwa nimekumbatia mademu wawili wawili tena nikiwa nimelewa chakali, Lakini nilipofika karibu na gari yangu Nilimuona yule msichana ambae nilishawahi kumkuta ndani ya gari yangu.... ni kama miezi miwili mitatu hivi imepita toka nionane nae.

    "afu wewe dada wewe? miezi michache iliopita ulinisababishia kesi ya mimi na bosi wangu kisa wewe tu,, umesababisha mpaka nimeenda kukaua kambuzi kawatu kisa ni wewe tu... Kwahio naomba sana usinizoee tena"

    Sasa hawa wasichana niliokua nao waliniona labda mimi ni kichaa au ndio kichaa kinaanza.. maana walishangaa kuona naongea na gari tu. lakini ukweli ni kwamba wao hawamuoni huyo niliokua nikiongea nae Hivyo waliona labda ni uchizi wangu au ni pombe ndio zinanisumbua akili yangu, Kwahio waliamua kuniacha pale na kuondoka zao, ila ni kwasababu nilishawakatia chao na ndio maana wameondoka



    Niliendelea kumsemesha yule mschana wa kiislamu ambae hayupo kibinaadamu kama sisi ila sijui ni nani,

    "dada tafadhali sana naomba usinisogelee maana tukigusana tu kwangu itakua ni kesi kubwa kwa bosi wangu, hivyo kaa mbali na mimi kwani hua sipendi kuchinja vimbuzi vya watu hovyo hovyo tu"



    Ghafla yule dada aliongezeka mara 4 na wale wanne walikua wamevaa nguo nyeupe pyeeee, Nilianza kuogopa ghafla na kujikuta sina ulevi tena, Alafu wale watu walikua hawapo tena, Niliwasha gari na kukimbia mbio za kuelekea nyumbani kwangu.....



    sasa kufika tena nyumbani kwangu nilikutana na gari ya mzee joakimu... yule mzee alieniunganisha na hii kampuni yao,

    Nilimkuta pale nje akiwa kapaki gari akinisubiria



    "mbona unakimbiza gari hivyo kuna nini?"

    "aaaahh ni matisho tu ndio nayaona"

    "matisho gani sasa?"

    "kuna mdada ananifatilia sana na sijui ni nani... ila tuyaache hayo vp mbona hujaingia ndani mzee?"

    "Ahahaha usijali kijana kwani kuna ujumbe nimeagiziwa nikuletee"

    "Na nani? Bosi nini asee?"

    "ndio"

    "Ehe ujumbe gani huo?"

    "leo saa 8 usiku kuna kikao cha wafanyakazi wote.... kwani tumekaa muda sana bila kutoa sadaka"

    "oookee hakuna shida. kwahio leo tunakua wote ndani ya uwanha?"

    "ndio.. ila hakikisha unakuja na mbuzi dume"

    "Aaayaaaa Acha utani mzee kupanda vyeo? duuu ila sasa mbuzi saa 3 hii nitamtoa wapi mzee?"

    "mimi mwenyewe sina. na ndio natarajia kwenda katika mabanda sasa hivi"

    "basi twende wote mzee"

    "sawa ila mimi ndio naenda sasa hivi"

    "sawa haina shida we twende tu"

    "kwahio hata ndani huingii?"

    "apana siingii kabisa"

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Basi tulikwenda katika mabanda ya mbuzi yaliopo katka maeneo ya machinjioni ya nyama za kuuza kama kwenye mabucha hivi. Tulinunua kila mtu mbuzi wake na kumuweka ndani ya gari, Tulikus tuna furaha kwa kufanikisha mbuzi wetu.......

    Kila mtu alienda makwao kujiandaa na mkutano wa usiku wa leo ambao utajumuisha wafanya kazi wote wa kampuni hiii.



    Ilipofika mida ya saa 8 usiku tulikutana katika tempo moja ambalo kulikua na kama ukumbi fulani hivi maana kulikua na viti mithili ya kanisa. Afu kule mbele nikiangalia nilikua naona shimo tu katika eneo la steji... ambapo mkuu au bosi ndipo atakaposimamia.... nikiangalia watu wote humo ndani tulikua tumevaa majoho meusi yenye mistari miekundu, Huku kila mtu akiwa kashika mbuzi wake kwa ajili ya kafala la kujitolea mikosi,



    Mara ghafla mkuu ameingia katika steji na kuanza kuongea

    "nashukuru sana kwa kuwaona mpo wote tena kwa furaha sana.... ila nadhani kila mmoja amekuja na kinyama chake?"

    Tuliitikia kwa wote huku tukisema

    "ndiooooo mkuu"

    "sawa kabisa.... sasa nadhani kila mtu ana kisu chake maalum cha kujichinjia knyama huyo... sasa naanza kuita majina. na ukisikia jina lako. unatakakiwa hapo hapo ulipo weka chungu chako chini na umchinje mbuzi huyo na hakikisha damu yake iingie katika hicho chungu sawa?"

    1. "keneth Dominic?"

    "ndioo"

    "nipe jinsia ya mbuzi"

    "ni mbuzi wa kike"

    "ok chinja"

    Baada ya huyo ikafata

    2. "Ashishy Mpacha?"

    "ndio mkuu?"

    "jinsia?"

    "mbuzi wa kike"

    "chinjaaa"

    3. "Denic Jackson?"

    "ndioo"

    "jinsia?"

    "beberu"

    "chinjaaa"

    4... "masanza kemchoz?"

    "ndioo"

    "jinsia?"

    "kajike"

    "chinjaa"

    5... "khalfan yusuph?"

    "nipoo"

    "jinsia"

    "mbuzi wa kike"

    "chinjaa"

    6... "Ally Jfour?"

    "nipo mkubwa"

    "jinsia ya mbuzi"

    "kondoo"

    "nani kakuambia ulete kondoo?"

    "ooo sory mkuu kumbe ni kabeberu"

    "chinjaa"

    7..."Swaaleh Twalha?"

    "ndio?"

    "jinsia"

    "wa kike mkuu"

    "chinjaaa"

    8...."Oswald A halla?"

    "ndiooo"

    "jinsia"

    "mbuzi mchanga"

    "chinjaaa"

    9...."Issa juma?"

    "nipo"

    "jinsia?"

    "kajike mkuu"

    "chinjaa"

    10...Ommy mtupa?"

    "nipo mkuu"

    "jinsia"

    "beberu"

    "chinjaaa"

    Walikua watu tupo wengi sana tulikua tupo kama watu 500 hivi

    sasa mkuu aliiita na kuita mpaka ikafikia zamu yangu ya kuchinja kinyama changu

    "rashidi tandu kingazi?"

    "ndioo"

    "jinsia"

    "mbuzi dume mkuu"

    "chinjaaaa"

    Nilimchinja mbuzi wangu na damu ile ya mbuzi ikaingia ndani ya chungu.... sasa huku nikiendelea kuikamulia damu iingie vizuri katika chungu... ghafla kuna jina nililiskia likiitwa. na jina hilo nalifahamu kabisa... na si mwingine bali ni kaka yangu yule alienifukuza kule kwenye nyumba yake.... heee kumbe na yeye ni mmoja kati ya wafanyakazi wa hii kampuni?.... Lakini sawa haina shida ila je? yeye kaja na kinyama gani cha kujitolea sadaka?

    "hatibu tandu kingazi?"

    "nipooo"

    "jinsia?"







    Nilikua nasubiri ndugu yangu aitaje jinsia ya mbuzi wake,

    "hatibu tandu kingazi?"

    "nipooo"

    "jinsia?"

    "wa kike"

    "chinjaa"

    Duuu kumbe yeye alikuja na mbuzi wa kike.

    Ila nashangaa sana kumuona broo nae yupo katika hii kampuni ya kitajiri kiasi hiki, afu kumbe sisi ndugu zake tulikua tunakufa na njaa kiasi hiki, Duuuu kweli pesa ni mwana haramu .. Lakini namlaumu mwenzangu tu? mbona mimi mwenyewe toka niingie katika hii kampuni sijakanyaga hata siku moja kule kijijini, Basi waliisha wote kuchinja vinyama vyao kwa kujiwekea ridhiki za pesa nyingi..



    Baada ya kumaliza kuchinja vinyama hivyo. Mkuu alitoa agizo kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiii,

    "nadhani mnajua kua pesa yetu haitumiki katika njia mbili.... na ili kujua njia hizo basi muulize aliokuleta ili ujue kabisaaa..... Nadhani sina la ziada ila papo hapo ulipo beba chungu chako kisha tuelekee katika kampuni yetu"

    Tulitoa kwa mstari utafikiri ni wana kwaya fulani hivi,



    Lakini tulipofika njiani tukielekea kule kwenye kampuni... maana huku tulikua katika ukumbi mmoja ambao ni kama tempo lao la ibada, Sasa kwa jinsi tulivyokua tukitembea kwa mistali tena tukiwa tumevaa majoho utafikiri ni wanafunzi waliohitimu vyuo vikuu...

    Sasa nilikumbuka siku moja niliona kitendo kama hiki. Watu wakiwa wamebeba vitu fulani katika vifua vyao. huku wameinama chini, Kumbe wale watu ndio walikua ni hawa. ila siku ile niliona kidogo tu maana nilipatwa na usingizi wa ghafla siku ile, na nilipokuja kuzinduka ndio nikakutana na kwato za ng'ombe mbele yangu, Sasa nikaanza kujiuliza hiii ni kazi gani hii ya kubebana na madamu hivi??? Mnhhh Aiseee kesho lazima nimuulize mzee. ili anipe jibu sahihi kuhusu hii kazi ni kazi gani? ili isije kua tunatumikia mashetani bure....

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Basi tulifika katika kampuni na kupitiliza moja kwa moja hadi katika lile korongo, Kisha tukaimwaga ile damu kule chini kunakolia watu, na baada ya kumwaga damu wale watu walionekana kunyamaza, kiaskwamba wamezikubali kafala zetu.......



    BAADA YA SIKU MBILI KUPITA



    Na leo ni siku nyingine nikiwa nyumbani kwangu, Nilikua naangalia visuruali nilivyomnunulia side wangu pamoja na mama yake Bila kumsahau dada yangu na mama yangu pia. Lakini nikiwa naangalia nguo hizo ghafla kuna simu iliingia Niliitoa simu kisha nikaipokea.... Alikua ni mzee ndio ananiita katika ofisi yake binafsi...

    Sasa katika hali ya kuangalia namba zangu za simu, nilikutana na jina SABRINA sasa nilipoona hili jina ndio nikakumbuka kua tanga nilikua na demu aitwae sabrina, na namba zake za simu ndio niliziweka kichwani kwa urahisi, maana si demu wangu



    NADHANI HATA WEWE NAMBA YA MPENZI WAKO IPO KICHWANI



    kwani namba ya mke wangu nilishindwa kuiweka kichwani kwakua ilikua ni mpya hivyo sikuweza kuishika.... pia ya kaka yangu sikuishika kabisa kwani ilikua ni ngumu... ila namba ya sabrina nakumbuka ilikua ni maziro ziro mengi tu, Sasa kwakua ndio namba pekee ninayoijua hivyo niliiweka kwenye simu na kuipiga. Ilikua inaita duuuuuu naomba iwe ndio yenyewe

    "halooo?"

    "eee halo mambo?"

    "poa tu nani mwenzangu?"

    "aaa naitwa rashidi"

    "rashidi nani?"

    "si rashidi tandu"

    "mmhh mi sikujui"

    "ok kwani wewe unaitwa nani?"

    "mimi naitwa sabrina"

    "yesi hata huyo niliempigia pia anaitwa sabrina"

    "mmhh mi sikujui bhana.. Enhee shida yako?"

    "aaahh kuna namba ya ndugu yangu nilikua naitaka sasa sijui utamjua?"

    "mhh sasa kama wewe sikujui je? yeye nitamjuaje?"

    "kwani dada we si upo tanga maeneo ya kikokwe au?"

    "ndio kwani we ni nani?"

    "mimi naitwa rashidi ambae ni kijana tuliokua tunalima kwenu mimi na kaka yangu juma"

    "haaaaaaaaaaaaaa chidi? mungu wangu umepotelea wapi jamani? huku kwenu ni majanga kila siku ya mungu"

    "majanga gani tena? haloo haloo haloo jamani sabrina haloo?"

    Daaahh simu ilikata aiseee Nilijaribu kupiga tena huku mapigo ya moyo yakinienda mbio. Daahhhh

    "Samahani namba ya mteja unayopiga haipatikani tafadhali jaribu tena baadae.... Thank you for cho"

    "Aaaaaaaaaaaiiiiiiiii mambo gani tena haya daaa Asa tena hapatikaniki jamani aaaaaiiiii"

    Niliondoka hapo nyumbani kwa hasira huku nikielekea kwa yule mzee. maana kama unakumbuka aliniita niende ofisini kwake



    Niliwasha gari na kutoka mbio huku nikiwa na wasiwasi juu ya familia yangu. kua kuna majanga Sasa ni majanga gani hayo? Nilitoka kwa spidi sana na kufika kwa mzee huku nikihema juu juu kama mbwa mzee.

    "shkamoo mzee?"

    "marahaba vp?"

    "safi tu..Aaaa umeniita nafikiri?"

    "ndio nimekuita nije nikupe data nzima ya kampuni yetu jinsi inavyokwenda"

    "aaaa wala siihitaji hio data mzee labda usubiri mpaka nirudi kijijini. maana nina mpango wa kwenda kesho"

    "uende kijijini kufanya nini?"

    "naisi kuna matatizo mzee"

    "hupaswi kwenda popote pale"

    "Nini???? labda unifunge jela ila kwa swala la kwenda lipogo tuu"

    "sasa kijijini unakwenda kufanyaje?"

    "aseee mzee mbona una maswali mengi hivyo? si naenda kuisalimia familia yangu"

    "familia gani tena? na wakati familia yako ndio hizo pesa ulizonazo"

    "mzeee naomba tueshimiane mzee maana nitatamani kukuvuruga sasa hivi... maana nilikua nakuheshim sana ila heshima naona imeshuka tayari sasa"

    "sikia kijana... ulioyafanya ni mambo makubwa sana hivyo hupaswi kupaniki endapo utayasikia mambo hayo"

    "mambo gani?"

    Mara simu yangu iliita... nikaitoa mfukoni na kuangalia namba ilikua ni ya sabrina..

    "haloo sabrina ulisema kuna nini kwetu?"

    "huyo ndugu yako juma unaemsemea ndio huyo anaezikwa leo au?"

    "unasema ndugu yangu anazikwa leo?"

    "ndio... si yule kaka yako mliokua mkilima nae vibarua? afu kama mkorofi korofi hivi?"

    "vigezo vyote hivyo ni vyake lakini kwa huyo anaezikwa sio kaka yangu"

    "wewe ivi unajua kua nipo maeneo ya kwenu"

    "upo kwetu?"

    "ndio na tunasubiri kuzika tu. kwani hata baba yangu ninae hapa"

    "we we .... we ....we ..we unamjua mke wangu?"

    "aakaa simjui"

    "oooo shit ebu mpe baba yako niongee nae"

    Nilianza kuongea na yule mzee ili nijue huyo jamaa anaezikwa ni nani.. Sasa ile nataka niongee na baba yake sabrina..



    Ghafla huyu mzee akanipokonya simu yangu,

    "khaaa we mzee vp bhana ebu nipe simu yangu bhana"

    "hapana sikupi maana hii simu ndio inakupa kiburi cha kujua kila kitu"

    Nilimshangaa mzee akitoa betri katika simu yangu.... kisha akaikata kata laini na kuipasua ile simu yangu. Nilishindwa kumuelewa hivyo nikabaki kumuangalia tu kwa hasira

    "sikiliza kijana.. kama msiba umetokea huko kwenu. ni kweli kuna msiba.... na unaruhusiwa kwenda kumzika ndugu yako. ila kwa sharti moja tu"

    "Ebu endelea ongea nikuskie"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "hupaswi kulia wala kusikitika yaani tena unapaswa kucheka kabisaaa sawa?"

    "wewe ni mpumbavu nini wewe"



    Nilimtukana kisha nikatoka zangu na kuwasha gari kwa spidi huku nikitokwa na machozi.. Nilielekea Eapoti kuchukua ndege binafsi....



    Kama unavyojua usafiri wa ndege sio daladala. hivyo ilinichukua lisaa limoja hadi kufika nyumbani... niliondoka na helkopta binafsi.



    Kweli nilikuta watu wamejaa pale nyumbani kwetu. Lakini kitu kilichonishangaza nilikutana na wanafunzi wa vyuoni. Sasa nikajiuliza na hawa wanafunzi nao ni vipi.... Sikupata jibu sahihi kuhusiana na hao wanafunzi wa vyuoni.



    Cha kwanza kabisa nilikimbilia kuingia geto kwangu. Na kukuta hakuna hata mtu tena kulikua kumevurugika sana. basi nikajua mke wangu na mwanangu watakua wapo kwa mama kule...... Wakati huo watu wananishangaa mimi tu..



    Nilipofika nyumba kubwa yaani kwa mama.... daaahhh sikuamini macho yangu,



    "Yaani hapa nyumbani kulipita sunamiiiiiiii au kulikua na ugonjwa wa ghafla?"

    Nilijisemea mwenyewe huku nikilengwa na machozi kwa mbali Na nilipewa sharti moja tu la kutokulia wala kusikitika Sasa kwa hali hii kweli nitavumilia kweli? mungu wangu....



    Nilishindwa kuelewa kwa mambo nilioyakuta pale nyumbani, Yaani sikuamini macho yangu kiukweli nilikuta maiti mbili ya dada yangu pamoja na kaka yangu. Lakini sasa cha kushangaza ni kwamba sikua namuona mke wangu kwani nilijua nitamkuta akiwa huku kwa mama....



    Kwa usalama nilioukuta ni kwamba nilimkuta mama yangu pamoja na bibi yangu tu.... Nilimkimbilia mama yangu Lakini mama alionekana kukasirika sana juu ya mimi kupotelea mjini na kuwaacha ndugu zangu wakiisha mmoja baada ya mwingine. Nilikua nalengwa na machozi juu ya vifo hivi, kwani mimi mwenyewe nilijua ni kaka juma tu, kumbe hadi dada yangu aseeeee duuuu.. Nilikua natamani kulia ila nikifikiria yale masharti duu hata machozi yanakata yenyewe



    Nilijifanya kulia tu kwa uongo na kweli ili mama anionee huruma maana kakasirika kweli, Nilimkuta pia na bibi yangu mzaa mama wakiwa katika hali ya kulia kweli kweli, yaani hata muda wa kuomba msamaha nilikua sina, Niliingia ndani na kuwaona ndugu zangu waliokua wamelala moja kwa moja na siwezi waona tena, Nilitamani kulia kabisa Japo nilikua nimevaa suti ya maana lakini sikutaka kuvumilia kitu,



    Nilitoka zangu nje huku tukisubiri muda ufike waende wakazikwe.... Lakini cha kushangaza simuoni mke wangu kabisa, sasa sijui kaenda kwao au sijui kasafiri na yeye, Maana hata ile geto yetu haina hata mvuto tena kwani imeshakua banda la kuku.. . sasa mke wangu atakua yupo wapi?. Nilipotoka nje nilikutana na mzee yule ambae ni baba yake na sabrina,

    "shkamoo mzee?"

    "marhaba kijana hujambo?"

    "sijambo mzeee"

    "pole sana kijana..ila ndio hivyo kila marefu hayakosi kua na ncha, hivyo tumewapoteza ndugu zako, hivyo basi tu ni kazi ya mungu kijana"

    Mara ghafla sabrina katokea huku nae machozi yakimlenga kwa msiba huu, kwani dada yangu pia alikuaga ni best yake. kabla hajaenda chuo... hivyo anamkumbuka sana kiasi flani



    Ilifika mida ya kuzika ndugu zangu. hivyo nami nilishiriki katika mazishi yale, Na tuliwazika katika shamba letu la bondeni kule....



    Ila nilipofika hapo shamba niliona utofauti mkubwa sana, na sikua na mtu wa kumuuliza zaidi ya mama yangu.... Basi mazishi yalifanyika vizuri na mimi pia nilitupia mchanga huku watu wakiniangalia kwa jicho baya, Maana nimekuja na ndege binafsi. sasa wanashangaa kuona nimekuja na ndege afu huku kijijini wazazi wangu wanalala kwenye nyumba ya majani,



    Tulimaliza kuwazika wote na hatmae sasa narudi kule nyumbani, ili nikampooze mama angu. kwani katika watu walioumizwa na msiba huu ni yeye peke yake, Niliwakuta wote yeye na bibi pamoja na wamama wengine waliokua wakimpa pole, Huku wakimbembeleza sana. aisee nilitamani kulia asee yaani nilitamani kulia kabisaaa. Ila nikikumbuka kua mzee aliniambia kua pesa hii haiseidii ndugu wala kumseidi masikini...



    Yaani kama unakumbuka siku ile mkuu wetu alisema kua tumieni pesa mnavyotaka ila kasoro sehemu mbili tu... na nilipomuuliza mzee pale ofisini kwake aliniambia kua pesa ya kampuni hiii haiseidii ndugu wala maskini yeyote yule na katika majengo ya ibada pia hairuhusiwi......



    Niliona sasa hii ni kazi gani? kazi isioseidia hata familia? Hapana mi siwezi... Niliona kua siwezi kuondoka bila kumjengea mama yangu nyumba, Yaani mwanae nina pesa kiasi hiki mpaka naumwa, afu leo nimuache katika nyasi? haiwezekani... Pale pale nilianza kuagiza tofari na mawe ili nyumba ijengwe



    Lakini kila nikitoa pesa watu wanairudisha na kusema kua pesa hio haitumiki...... sijakaa vizuri mara niliskia sauti ambayo sikujua ilipotokea,

    "hahahahahah Aaaahahahaha tulikuambia usimseidie mtu hata awe nani, pesa hizo zinatumika vizuri sana. ila kwakua sio destuli zetu kuseidia watu. hivyo hao hao watu wataiona hio pesa haitumiki ila wewe tu ndio utaiona... sasa unahitajika urudi mjini sasa hiviiii, hivii, hiviii, hiviiii"



    Sauti hio ilikua ni sauti ya mkuu wetu wa ile kampuni,

    Niliingia ndani kwetu na kumkuta mama yangu akiwa na huzuni muda wote.

    "mamaa? baomba unisamee mama angu nilikua natafuta maisha mama angu"

    Nilianza kulia ili wanionee huruma.,...

    "mamaa? mimi bado ni mwanao tu lakini mbona kaka hatibu hajawahi kurudi. ila bado tu unampenda mama?"

    Bibi alinisamee na mama pia ilibidi tu anisameee maana mimi bado tu ni mtoto wake hata iweje

    "lakini mama? lile shamba la bondeni umeliuza nini?"

    "mwanangu kweli nina shida kubwa sana ila siwezi kuuza hazina za watoto wangu siwezi kabisa mwanangu"

    "sasa mbona lina makaburi mengi vile? maana mi najua kulikua na kaburi la baba tu.... Afu mama saidi kaenda kwao au kaenda wapi? maana toka nije hapa sijamuona kabisa"

    "mwanangu? yaani huna taarifa yeyote kuusu mkeo?"

    "mamaa mimi simu nilipotezaga hivyo hata namba zake sina za kwako sina za kaka juma yenyewe sina sasa ningejulia wapi mama angu?"

    "mwanangu? kwanza pole sana kwani hata mimi nilikua nampenda sana mjukuu wangu ila ndio hivyo"

    "mamaaaaa mbona sikuelewi?"

    "hayo makaburi yaliozidi kwenye shamba lenu ndio mkeo na mtoto wake"

    "u. u. u. u. u. uuuuu unase...unasemaje mama?"

    "alianza mtoto wako... na ni kama miezi 8 hivi toka mtoto wako afariki.. kisha haikupita hata miezi mitatu. mkeo nae akafariki dunia.. hivyo yale ndio makaburi yao...

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aiseeeee niliambiwa nisilie lakini hapa haki ya mungu sinyamazi... Nilitoka hapo nyumbani kama kicha na kuelekea shamba bondeni huku nikilia kwa uchungu mkubwa sana... yaanu kama ungeniona jinsi nilivyo basi hata wewe usingeacha kulia. nilifika kwenye kaburi la mtoto wangu na kugalagala kwa uchungu huku nikilia kama mtoto mdogo...

    "saidiiiii mwananguuu aiiiiiii kidume changu hicho kimekufa uuuuuuuuwiiiiii aaaaaaaaahhhhhoooooo uuuuuuuuu mke wangu eeeeeeeee mama saidi eeeeeeeeeee saidi wangu saidi wangu eeeeeee.... mwanangu amkaaa nimekununulia majinsi makali kinyama aseee uuuuuwiiiiiiii.... we mama saidi weeeee nimekununulia tentemente sita na madera kumi uuuuuuywiiiiiii mama saidiii weeeeeeeee mwanangu said? said? saidiiiiiiiiiiii Ahahaha uuuuuuuuwiiiiii uuuiiiiiiii eeeee mungu nimekukosea nini mimi? nimeenda mjini kwa kuitafutia familia yangu afu leo wamekufa wote uuuuuiiiiiiiiiu ooooooo mungu wangu wainue basi hata niwaone.... aaaaaaahhhh saidi baba amkaaa.. mke wanguuuuuuuuu aaahahaha uuuwiiuuu......"



    Kiukweli siku hio nilikua kama kichaa vile, na niliamua kulala hapo hapo na jioni yote. maana watu walikuja kunichukua lakini sikutaka kuondoka kabisa katika makaburi hayo,

    Na watu nao waliniacha pale pale huku nikiwa nimechafuka suti yangu kwa kuyagala galia makaburi hayo.. Nililala pale bila kumuogopa mtu wala mnyama yeyote yule. Nililala pale mpka asubuhi



    Asubuhi mida ya saa mbili watu wananikuta nimechakaa vumbi kama katuni... yaani nimelia mpaka macho yanauma. Watu walinichukua huku nikileta fujo kua sitaki kutoka hapo kabisa kwani. nina hamu na familia yangu....

    Nilibebwa juu juu tena kwa nguvu kweli. Walinipeleka hadi nyumbani na kuniacha hapo, Yaani nilikua ni mtu wa kulia tu muda wote. sina wa kujivunia tena kama mtoto....



    Nilikaa nyumbani kama siku mbili nzima Sili sinywi wala sikua na raha hata kidogo....... Basi na leo ni siku ya kuondoka ila siamini kama namuacha mama yangu bila hata kumuachia senti tano....... Sikuamini macho yangu kama kweli mama yangu nimuache katika maisha kama haya na wakati mwanae nina pesa mpaka nazichezea? Hapana hii kazi sio ya kufanya kabisa na siitaki tena...



    "mwanangu yani unaondoka na kuniacha hivi? mwanangu sina hata pesa ya kula"

    Yaani kumsikia tu mama yangu akilalamika hivyo nilianza kushikwa na hasira hizo......



    Lakini ghafla nilimuona mtu mmoja akiwa kasimama kwenye mti. na nilimjua mtu huyo... na nilimfuata mpaka pale alipo.

    "umeona madhara ulio yafanya?"

    Aliniambia huyu mdada mwenye miguu kama ng'ombe wa kienyeji..

    "kwani mi nimefanyaje tena?"

    "ooohh hujui? ok chukua hii pesa mpelekee mama yako afu tuondoke"

    Alinipa bahasha moja nzito na nilipoichungulia ilikua imejaa noti za kibongo tuuuu... Sikutaka kuuliza wala nini. nilimpelekea mama yangu na kumkabidhi bahasha ile.

    "mamaa nilitaka kukujengea nyumba ila muda wa kuwepo tena hapa kijijini sina hivyo chukua hizi pesa utaendelea kujenga jenga tu mwenyewe taratibu tu mama angu"

    "mwanangu nashukuru sana mwanangu, ila jua nimebaki na wewe tu na huyo bedui mwenzio lisiotaka kuja kwao.. nakuombea mwanangu"

    "asante mama na wacha mi niende maana nimekuja na ndege iko pale uwanjani"

    "nashukuru mwanangu na nakuombea safari njema na uendelee kufanikiwa mwanangu"

    "haya mama.. ila upatie na bibi ya ugolo maana kahasi kuniomba ya ugolo kweli yani"

    "sawa mwanangu nitampa bibi yako usijali"



    Niliondoka huku nikijiuliza maswali mengi kua,

    "je? kama ningetafuta pesa yenye kutumika na kila mtu... mbona ingelikua ni furaha ya hali ya juu... ila hii nionayo ni kazi gani hasa. ambayo pesa yake ni marufuku kuseidia ndugu au masikini wenye shida?"

    Nilijiuliza maswali hayo huku machozi madogo madogo yakinilenga lenga kimtindo. kwani tayari nimeshaitilia mashaka hii kazi nilio nayo sasa hivi.... ambayo kila miezi 3 tunatoa kafara.....



    Nilifika kwenye ule mti na kumkuta yule mschana mrembo kweli afu mweupeeeee.

    "kwaio?"

    Nilimuuliza hivyo. maana tayari nimeshamzoe na hali yake ya king'ombe ng'ombe.

    "twende"

    "mimi nimekuja na ndege lakini?"

    "najua ila kuna mahari nataka nikupeleke nikakuonyeshe kitu"

    "kitu gani?"

    "we twende tu"

    "ok ngoja nimjulishe rubani aondoke zake"



    Basi baada ya hapo nilijikuta ninefika eneo fulani hivi liliojaa gold na madhahabu kibao. yaani hata kitanda chenyewe ni gold tupu.

    "sikia chidi. katika kikosi ulichojiunga nacho sii kikosi cha kawaida"

    "kivipi labda"

    "wewe hapo ulipo tayari ni member wa freemason"

    "nani? mimi au?"

    "ndio ni wewe"

    "hapana siwezi kua freemason hata siku moja"

    "sasa ndio hivyo. na kama huamini ona pale"

    Alifungulia tv moja iliopo ukutani na kunionyesha jnsi nilivyoanza kumchinja mtoto wangu siku ile... afu nikaona na siku ambayo nilimchinja mke wangu... afu nikaona na

    "aiseeee basi zima tu zimaaa aaaaaaiiiiiii uuuuuuuuwww kumbe nimewaua kwa mikono yangu... uuuuwiiiiii aaaaahhhh mungu wanguu aaaaiiiiii"

    Nilijikuta nlia kwa mara nyingine.... huku nikiiangalia mikono yangu ilioua familia yote.

    "sikia sio wewe peke yako ndio ulioua.. bali hata kaka yako yule hatibu ni mmoja kati ya kundi hilo... na yeye ndie aliemuua dada yako wa kike na pia wewe mwenyewe upo kwenye prosesi ya kutolewa kafara na huyo ndugu yako. hivyo kua makini sana"

    "eeeeee mungu wangu ee kumbe hata kaka yangu ni freemason pia?"

    "ndio....tena yeye alianza na baba yenu"

    "haaaaaaaa yani ni kumbe broo ndio alimuua baba?"



    Niliamka kwa hasira na kuzunguka hapo kwenye hicho chumba

    "samaani dada naomba nitoke eneo hili"

    "hupaswi kutoka kwenda mahali"

    "dada naomba sana nitoke nipo chini ya miguu yako"

    "ok ila hupaswi kuendelea nao"

    "sawa nimekusikia."



    Baada ya dakika kadhaa tu nilijikuta nipo uraiani.... sikupoteza muda nilielekea moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya mzee

    "we mzee kuma mae zako... we mzee kwani ilikuambia uniunganishe na hili kundi lenu? kwanini umeniungasha mzee? si ungeniacha na umaskini wangu ee? kwanini usingeniambia kwanini? ona sasa mimi sina hata ndugu kisa ni huu ufreemason wenu"

    "Aaaaaaahahahahahaha kumbe ulikua hujui? na hakuna jinsi ya kutoka tena, afu isitoshe mkuu anakuita kule..... tena wamekuekea kikao wewe. nenda ukawasikilize"

    "kuma mae wewe"

    "haijalishi kitu hata utukane matusi yote"

    Ani nilikua natetemeka kweli kwa hasira za hali ya juu... Niliitisha gari yangu ikaletwa kisha nikaelekea huko kwenye ofisi zao...

    Ila nilipoingia tu yule mdada alinikataza nisiingie.. lakini sikumsikia maana nilikua nana hasira ya kugombana na huyo LUSIFA mwenyewe ambae haonekaniki, Nilipoingia kweli niliwakuta wapo kwenye kikao cha kunijadili mimi. Nilifika kwa hasira zangu nyingi na kutulizwa juu kwa juu.. kabla hata sijaongea nikaskia

    "umefanya makosa mengi sana kwenye kampuni hii... tulikuambia ukifika kwenye msiba usilie... lakini kwa jeuli yako umelia... tukakuambia kua hatutaki uwe na yule mschana husikiii... alafu bado umetoka kumgombeza mkuu wako ofisini kwake.... sasa kwa adhabu ya makosa hayo inakuja hivi"

    "weeee lusifa acha usenge wewe mimi nimeua ndugu zangu wote afu unasema usenge wako hapa we ni hanisi nini wewe?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "hilo ni kosa lingine.... na adhabu yake ni hiii.... .

    1... katuletee albino watatu uliowaua wewe mwenyewe

    2.... basi la mtei leo limejaza vizuri sana hivyo nataka lidondoke pale darajani

    3.... na mama yako tunamtaka

    Kama utavikosa hivi vitu basi tutakutoa kafara wewe mwenyewe..na vitu hivyo vifanyike leo leooo, leoo, leoo, leoo, leoo, leoo"



    Nilishtuka sana kuskia hivyo, kwani kuua albino watatu? au kuua umati wa watu. kusa ni mimi tu? hapana

    "kwanini lakini mnafanya hivi?"

    "hatutaki maswali, haya uliyataka mwenyewe hivyo maswali nengi ni marufuku kwetu"

    Sikua na jinsi ni lazima nivifanye hivyo vitu nilivyoagizwa kutoka kwa wakuu hawa.

    "basi mi naacha kazi yenu na pesa zenu na majumba yenu magari yenu kila kitu chenu chukueni na sivitaki tena"

    "ahahahahahahaha huezi kukitoa katika ulimwangu mpya na mpana.. au The New World Order... ama WWW ( WORLD WIDE WEBSITE ) huezi kutukimbia katika ulimwengu huu mpana na wenye kukamata kila mtu mwenye akili mbovu kama yako... sasa ili uendelee kuishi tufanyie hizo kazi haraka"

    "lakini kwanini mnakua makatili kiasi hiki? basi nipeni chaguo kati ya hivyo nipunguzieni basi"

    Niliomba wanipunguzie japo hata mbili tu, maana kuteketeza basi la mtei au albino watatu au mama yangu. sii kazi ndogo asee..

    "ok tunakupunguzia mbili na ubaki na hizi mbili"

    "ndio kabisa asante. ila ni zipi sasa?"

    "mama yako au wewe mwenyewe. na ukifanikiwa kumuua mama yaki basi na cheo tunakupandisha tena"

    Daaahh nilichoka kabisa kusikia hivyo. maana nilijua swala la mama yangu limetoka, lakini ndio kwanzaa lipo palepale.... Nililia sana kuona vile.......



    Basi sikua na jinsi ya kufanya bali nilitoka pale huku nikijifikiria mara mbili mbili kuusiana na swala hilo la kujipeleka mimi au nimtoe mama angu afu niendelee kula pesa zangu?

    Lakini kabla ya yote nimeona niende kwa yule dada akanipe ushauri juu ya hili



    Sasa kwakua sikua na mahari pakumpatia hivyo kuna kitu alinipa ambacho niki kigusa tu anakuja nilipo. Na ni kweli haikuchukua muda mrefu nilishangaa yupo nyuma yangu Wala sijui amekujaje, Alinishika tu mkono na kunipeleka mahali ambapo nilitoka muda sii nrefu, yaani pale kwenye chumba ambacho kina gold chumba choteee.

    Sasa yeye alikaa mahari huku akiniambia

    "chidi? najua kwa sasa una mawazo mengi sana kuusu hivyo ulivyoambiwa na mr lusifa. ola hutakiwi kutekeleza hata kimoja"

    "kwanini nisitekeleze? lazima nifanye hivyo maana bila hivyo nitakufa asee"

    "bora ufe kuliko kuendelea kuuwa watu"

    "kwaio nifanyaje dada angu?"

    "kifupi ni kwamba achana nao hawa watu..... na hata mwanzo nilikuambia siku ile nilipokukuta kwenye toroli umelala.. nikakuambia kabisa nikiachana na wewe kuna mwingine atakuja.... sasa ndio huyo keshakufanya muuaji tayari"

    "afu Eeheeeee nimekumbuka hebu niambie wewe ndio ulienipeleka hospitalini siku ile?"



    SASA HAPA WE MSOMAJI KUA MAKINI... MAANA HAPA KINAONGELEWA KILA KITU AMBACHO KILITOKEA HUKO NYUMA NA HUKUKIJUA.. SASA HAPA NDIO ATAELEZA YOTE SASA... ILA KAMA HUKUIANZA MWANZO HII STORI BASI UJUE HUTOELEWA KITU CHOCHOTE KILE



    "sikia nikuambie rashidi, mimi nilikua ni binaadamu kama wewe, ila wakuu wa majini wa nchikavu waliona kua mimi nafaa kuwa mmoja wao, hivyo nikawa mbali na binaadamu na kua jini wa nchikavu. ila ni majini wa wa nchikavu na wasio na hatari yeyote ile.... Toka nilipoingia katika sekta hio nilikaa muda mrefu bila kua na mahusiano ya kimapenzi na binaadamu, japo naweza kujiweka katika hali ya kibinaadamu na kuishi na binaadamu..... katika kundi letu sisi kulikua na vijana wawili na wasichana wanne, hivyo kulihitajika kijana mmoja ili tuwe saba... kwani sheria yetu hua tunakua waschana wanne na wavulana watatu na sio kila mtu inaweza kumuangukia, bali kuna vigezo vya kiroho lazima uwe navyo ndio ujiunge na majini. na nafasi hio ilikuangukua wewe kabla hujaingia katika ushetani. Hivyo wakuu wangu waliniambia nikufuatilie mwanzo mwisho ili nijue matendo yako, na kuweza kukupeleka kwa wakuu wangu... Na mara ya kwanza kukufatilia ilikua ni hapa



    ***********************************

    "Broo tuache masihara bwana mbna mnarusha mawe?"

    "nani karusha mawe wewe?"

    "ok poa twendeni"

    Tulianza safari huku tukipiga stori za hapa na pale



    Lakini ghafla niliguswa usogoni mithili ya mtu alienisodoa...

    "aiseee broo mbona mi sielewi?"

    "nini wewe?"

    "nani kanigusa kwa nyuma?"

    "sasa mimi nipo mbele nitakugusaje kwa nyuma?"

    "eeeehh??"

    "Eeenhh eee eee Eeee nini sasa?"

    "eeee?"

    **********************************



    Na mara ya pili nilikuja ndani kwako usiku na kukuonya kua usiende mjini maana nilishayaona maisha amvayo ungeishi,



    na mara ya tatu nilikufatilia siku ile ulipokua unakwenda kwenye mdumange... kile kitendo sikukipenda kwani ulikua una mke na mtoto... afu pia mimi mwenyewe nilishaanza kukupenda taratibu, hivyo sikupenda uende kwenye mdumange.. na ndipo nilipowatuma wenzangu waanze kukuzuia... na wa kwanza ni yule uliemuona kwenye mti siku ile.... kisha baada ya muda nikatokea na kukurudisha kwenu...



    Na siku nyingine ni pale kwenye ajali. ile ajali haikua kosa la dereva bala mule ndani ya gari kulikua kuna baadhi wengine sio watu. ila wewe na wengine mliwaona kama watu... ile gari ilipinduliwa na mfanyakazi mmoja wa kampuni hio ulionayo kwa sasa..... nae alipewa azabu kama hio uliopewa wewe.. na ilikua mfe wote mliopo katika magari yote mawili.. ila ulipona kwasababu mimi nilikua nyuma yako... na nakumbuka kuna muda nilikushika macho ili uone yanayofanyika tofauti na macho yako ya kawaida sasa pale ulipojifanya unaweza kutoka nje ndipo ulipopigwa kibao na kupoteza fahamu kabisa.



    walikuchukua wale watu kisha wakakutenga mahari ili wakuuwe kiukatili. ila walipoona kua wewe ni wa muhimu kwao hivyo wakakuacha pale pale chini ukiwa huna fahamu.... nami ndipo nilipokuchukua na kukukabizi kwa yule mama dokta....... Na hapo ndipo wakaanza kukufatilia kwa kumtuma yule mzee.... na hata hivyo yule mzee na wale WADUDU WA DAMPO ni kitu kimoja hivyo ulikua ukisomewa wewe tu uingie katika chama chao hicho cha mauaji



    Na sehemu nyingine nilipokufatilia ni pale mochwali ulipotaka kusex na maiti yule... hivyo nilitumwa tu nidhibitishe kama kweli ungefanya nae?



    Na sehemu nyingine ni pale nilipokukuta umelala katika mkokoteni, Na ndipo freemason walipotoka katika tempo lao walilokwenda kutolea kafara... na wangelikuona basi ingelikua ni shida na tatizo kwao... hivyo nami pale pale nikakupa usingizi wa ghafla... na ulipozinduka asubuhi ndipo ulipokutana na kwato za ng'ombe.. nilikuambia maneno machache tu kisha nikaondoka...



    Na sehemu nyingine ni pale ulipokua unachinja mbuzi mchanga... hua sisi hatunaga sheria ya kumzuia mtu kwa kile alichoamua yeye bali tunamuambia tu kwa mdomo... ila mimi nilijitahidi kukushika mikono lakini bado ulikua hutaki.... kwani yule ndio alikua ni mwanao saidi, ila wewe ulijua ni mbuzi mchanga.



    Na sehemu nyingine ni pale uliponikuta nipo ndani ya gari yako... na kunifanya univute kiisia mpaka nikakupa mate yangu japo wewe ulijua kua nimefuata pesa zako lakini hapana... Na pale pale kama unakumbuka nilishtuka. Sasa pale ni mkuu wangu alinionya nisirudie tena jambo kama lile... na ndio maana sikuendelea kukaa kabisa.. na ndipo ulipopewa adhabu ya kuchinja mbuzi aliozaa uzao mmoja tu... ila yule hakua mbuzi bali alikua ni mkeo...... Na pale kwenye korongo ambapo watu wanalia? huko chini kuna watu aina ya mashetani. ambao ndio husababisha wewe na mwingine kuwa na pesa. yaani vile wanavyolia ndivyo na pesa inavyoingia katika akaunti yako au chumbani kwako.. maana wameshaifurahia damu ya ndugu au mke au mtoto. au mama...



    Na sehemu nyingine ni pale NOVO hotel ambapo ulikua umeshika wadada wawili wawili. tayari kwa kusex nao.... kitendo kile sikukipenda kabisa kwakua hata mimi nilikua na chembe chembe za mapenzi na wewe....



    Na sehemu ya mwisho ni pale nilipokuja tanga kukuchukua Baada ya kuwazika ndugu zako.



    Haya hebu niambie mungu ataweza kukusamee kwa dhambi ulizozifanya? na sasa bado wataka ukaendelee kuuwa tu. ivi unaona raha tu kuuwa si ndio?"



    MMNHHH KIUKWELI DADA KAONGEA MENGI SANA



    "sasa mimi nitafanyeje? maana nitakufa"

    "nimeshakuambia ni bora ufe.. ila sio wakuue wao bali ujiue mwenyewe na kifo cha mateso ndipo utaweza kusamehewa dhambi zako.... na kuweza kuwarudisha watu wote uliowaua kwa mkono wako... kwani watu hao hawakufariki bado. na hata kuzika mumezika migomba tu. ila watu wapo hai kabisa jambo sio kwa dunia hiii.... hivyo wanatakiwa kukombolewa kwa kutumia damu yako tena ujiue kwa hiali yako wewe mwenyewe. ila sio wakuuwe wao"

    "haaaaaa kwahio nikijiua mimi na familia yangu itarudi kuwa hai?"

    "ndio"

    "oooo bora nifanye hivyo saidi wangu na mama yake na kaka yanguuu na pia dada yangu warudi aseer"

    "hapana dada yako hawezi kurudi kwani hukumuua wewe, bali dada yako aliwawa na kaka yako hatibu... hivyo haitowezekana kwa yeye kurudi labda atubu kwa kukiua kama wewe"

    "niue basi familia yangu irudi... kwani ni bora waendelee kuishi wao kuliko mimi"

    "sio uuliwe na mtu bali ujiuwe mwenyewe na kifo cha mateso sana.... kama vile kujitupia gholofani... au kujitupia katika moto au maji.. na hivyo vyote havipo katika ulimwengu huu, bali vipo mahali nitakupeleka... kwani huko kuna ukubwa wa mara 70 ya vitu vya duniani... yaani khama ni gholofa huni hata chini... na kama ni ukali wa moto basi ni mara 70 ya duniani.... na kama ni maji basi ni zaidi ya sunami yaani ni sunami mara 70 sasa chagua moja uende wapi?"



    "bora hio gholofa"

    "kwahio umeridhika?"

    "ndio mama nimeridhika... ila nipe basi hata denda la mwisho kwani si unajua sirudi tena?"

    "kurudi utarudi ila sio kwa sura hio wala kwa jina hilo bali utakua ni mtu mtakatifu... hivyo ukirudi tu utanikuta. ila nikikupa denda kwa sasa utaniletea shida kwa mkuu, kwani alishanikataza kuusu hili.... ila bado nakupenda chidi. hivyo hata mimi sio kua napenda ukajiue ila ni njia ya kukutengenezea njia mzuri"



    Sasa alipomaliza tu kuongea Tulijikuta tupo juu ya gholofa... yaani hilo gholofa hakuna kabisa na sio kua hakuna kwa hapa tanzania? bali ni kwamba hilo gholofa sijawahi ona na wala hakuna na halitowahi kuwepo duniani kote...



    "ngoja kwanza chidi... nakuomba fungua moyo wako juu ya hilo. kwani ukienda kwa roho mkunjufu ndio utafanikiwa. ila ukiwa hupendi hata hao ndugu zako hawatorudi kabisa. kwani hukupenda kuwarudisha"



    Kwa jinsi alivyokua anaongea nilihisi kama ndio ananichelewesha kufa vile... hivyo nilijitupa bila kufikiria kitu huku nikifumbs macho kwa upepo ambao ulikua ukinipuliza.

    Yaani gholofa ilikua ni ndefu kiasi kwamba hata ukimwaga tenki la maji halifiki ng'ooo. maana ni parefu mnooo..



    Nguo zangu zote zilikua zikichanika kwa upepo mkali ambao ulikua ukinipitia nikiwa nashuka chini..... Huezi amini nilihisi kama robo saa imeshapita lakini hata katikati sijafika..... Nilikua naomba tu nisijeku, Lakini ghafla nilikutana na moto mkali ulioanza kunichoma kwa mbali.... Sasa nilipokua naukaribia ule moto ambao ndio 7 mara 70....



    Nilishangaa naitwa huku nikisukumwa sukubwa na kuambiwa

    "we sheby? sheby mwanangu amka uende shule"

    "Eee? Nini nyie bwana mi nataka kuikomboa familia yangu nimeiua yote"

    "we mtoto una nini hebu amka bwana ona sasa umechelewa shule"

    "haaaaaa ni saa ngapi mamaa?"

    "si saa 4 hii mwanangu, kwani ulikua unafanya nini? hebu ona jasho lilivyokutoka"



    HAAAAAAAA KUMBE NILIKUA NAOTA AISSE DUUUU TENA WALA SIITWI RASHIDI.... JINA LANGU NI SHARBINY RASHIDY TENA BADO I MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU......



    "mamaa? kuna ndoto nimeiota"

    "ndoto gani hio mwanangu?"

    "mamaa? nilikua na mke na mtoto afu nimeota eti nimeua ndugu zangu afu kuna dada mmoja akaniambia ili niwarudishe watu hao nilio waua eti nijitupe kwenye gholofa nife, ndio wafufuke"

    "jamani mwanangu pole sana... na washindwe na walegee kabisa hao waliokuotesha jamani"



    Mama angu alikua ananipenda sana kupita kiasi......

    "kwaio utaenda shule?"

    "ndio mama ntaenda tu"

    "utachapwa mwanangu usiende"

    "ah ah wacha nikachapwe tu"



    SASA ONE DAY YES IMEISHIA HAPO JUUU..... ILA STORY YA ONE DAY YES INA MUENDELEZO WAKE AMBAO JINA NI TOFAUTI NA HILO



    YAANI MUENDELEZO WAKE UTAKUA NA JINA TOFAUTI LA STORY... ILA CHIMBUKO LA MUENDELEZO NI HIO ONE DAY YES..



    KWAHIO ONE DAY YES ILIKUA NI NDOTO TU.... SASA HUUU NDIO MUENDELEZO WAKE AMBAO UTAKUA NA JINA LIGINE......



    KWAHIO ~ONE DAY YES~ IMEKWISHA KWA STAILI HIO...



    ILA NAWAONJESHA KIONJO CHAKE AMBACHO SIKUAMBII JINA LA STORY HIII ILA BUNIA JE? INAITWAJE



    HEBU TUONJE KIONJO KWANZA



    story hiii mimi ni mtoto wa kitajiri ile mbaya... na wakiume nipo mimi mwenyewe na nina dada zangu wawili wenye asili ya kiarabu. kwani mama yangu yeye pia ana asili ya kiarabu.....



    Ninae dada yangu ambae ana umri wa miaka 25 huyo ni wa kwanza na keshamaliza shule muda tu... kisha ninae dada yangu mwingine ambae tumefuatana.. yeye ana umri wa miaka 22 na yeye bado yupo kidato cha 4... afu anafatiwa na mimi kidume sharbiny rashidy mwenye umri wa miaka 20 na yupo kidato cha 3.... familia yetu ilikua ni familia ya kitajiri sana yaani tulikua ni matajiri waliopindukia....



    Ila katika watoto wote wa mzee rashidy mimi peke yangu ndio nilikua nina rangi tofauti na dada zangu wote. Ila nyumba yetu imezungukwa na wafanyakazi wengi mno. kama kwa raisi vile kumbe ni kwa mtu tu wa kawaida...



    "mwanangu utaenda kesho tu"

    "mamaa mi sijawahi kukosa kwenda shule hivyo nisipoenda naisi kama nitaumwa yani"

    "mmhh haya ila njoo unywe chai basi"

    "nitakula huko huko mamaa"

    "mwajabu? we mwajabu?"

    "abee dada?"

    "umeona mtoto wangu anaenda shule na njaa?"

    ndani kwetu tulikua tuna mfanyakazi ambae ni mtu mzima kabisa na ndio alionilea mimi toka nikiwa mtoto.... hivyo roho inaniuma sana pindi ninapoona anafokewa kwa ajili yangu,

    "kakaa njoo unywe chai"

    Aliniita yule mdada wa makamo kabisa tena hata sio mdada ni mmama kabisa. kwani alitulea mimi na dada zangu wote, lakini dada zangu asa huyu mdogo hua hamueshimu huyu mama na sijui ni kwanini....

    "mamii nimeshiba usijali"

    Nilimuambia kwa kwa utaratibu na heshma zote alizonilea yeye mwenyewe.

    "sheby mwanangu, sema ukirudi unataka ule chakula gani?"

    Alioniuliza ni mama yangu mzazi

    "aaaa chochote tu mamaa"

    "yaani we mwajabu humuulizi mtoto atakula nini umeuchubua tu"

    "mamaa mbona ivyo lakini?"

    "amna mwanangu ni huyu mtu naona hakujali kabisa yani"

    "ok nitakula ugali na mrenda"

    "haaaaaaa sheby mwanga chakula gani hicho cha kishenzi hivyo?"

    "mamaa kwani hicho mbona pia ni chakula"

    Mara mami kazi akaingilia katihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "lakini dada kama kapenda mwenyewe kula labda tumuache tu"

    "hapana mwanangu hawezi kula matapu tapu hayo... afu wewe mwajabu umenilelea mtoto wangu vibaya sana wewe"

    "nisamee dada"



    Nilichukua BMX yagu ambayo hua naendaga nayo shule pindi ninapopitwa na school bus, Hua shule ninayosoma ni shule ya serikali iitwayo

    ASHRAF SEMINARY SEC SCHOOL ni shule ya kiislamu ambayo ina maadili mema kila idara....



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog