Search This Blog

Monday 19 December 2022

FUPI LAKINI TAMU - 1

 

IMEANDIKWA NA : EDGAR MBOGO


*********************************************************************************


Chombezo : Fupi Lakini Tamu 


Sehemu Ya Kwanza (1)




Siku iliyo zaa mambo na kizaa zaa, siku ambayo sito kaa ni isahau, ilikuwa ijumaa, siwezi kuisahau japo nilikuwa mdogo sana, ilikuwa ijumaa ya yapasaka, mwanzoni mwa mwezi wa nne, sikumbuki tarehe, ila nakumbuka sikukuu yapasaka, sababu uwa napenda sana siku kuu, asa kipindi hicho cha utoto, anasimulia shuhuda wetu, bwana Prosper, wacha umsikie mwenye akisimulia mkasa huu.******


Ilikuwa mwaka tisini nambili, mwezi wan ne, ijumaa ya pasaka, wakatolic wanaiita ijumaa kuu, mwanzoni kabisa mwa mwenzi wanne, yani week ya kwanza ya mwezi huo wa nne, wakati huo nilikuwa na miaka kumi na moja tu! nilikuwa nasoma darasa la tatu, wakati huo tunaishi Mbezi kwa Yusuph, mita kama mia tano toka barabara kuu ya morogoro, kipindi hicho apakuwa na nyumba nyingi kama ilivyo sasa, nyumba zilikuwa moja moja, zikipakana na vichaka na mapori madogo madogo, ilikuwa mida ya mchana, nilikuwa mimi na kaka yangu mkubwa Denis, tunatoka nyumbani, tunaelekea kanisani, siunajuwa mambo ya ijumaa kuu.


Nakumbuka ilikuwa imepita week moja tu! toka kaka amekuja likizo fupi ya pasaka, akitokea songea alikokuwa anasomea udoctor, kwenye chuo cha Pelamiho, kinacho milikiwa na wazungu wakatolic, (kipindi hicho, sijuwi kwa sasa) ukweli nikwamba kaka alikuwa kama mgeni hapa mtaani, sababu muda mwingi akuwa anakaa hapa nyumbani, mimi na kaka tumepishana miaka kumi na mbili, wakati mimi na miaka kumi na moja yeye alikuwa anamiaka ishilini na tatu, hapa katikati kulikuwa na dada zangu wawili na kaka moja, jumla yetu tulikuwa watano, hao wengine kipindi hicho walikuwa mashuleni, sababu walikuwa wanasoma bweni, ata Sophia nilie mfwatia, nae alikuwa anasoma ST Joseph huko hanga monaster songea, kipindi hicho alikuwa darasa la sita.


Nakumbuka asubuhi yake kulinyesha mvua kubwa sana na kutengeneza vidimbwi, na vibwawa vidogo vidogo, baba na mama wao walisha tangulia kanisani na gari lao, walikuwa wanamiliki aina ya volxwagon, watoto wenzangu walikuwa wanaliita mgongo wa chura,


Sasa basi, wakati tunavuka kwenye nyumba moja, ambayo ndio tungeweza kusema jirani zetu, sababu akukuwa na nyumba nyingine kati kati yetu, nika shangaa kumwona kaka Denis akitazama nyumba ya jirani kwa mshangao, nikajuwa anatazama gari la kina Eve, ambalo lilikuwa linatoka pale kwao, lakini aikuwa hivyo nilivyo tazama vizuri, nikagundua kuwa kaka Denis alikuwa anawatazana wakina Eveline na mama yake mdogo, waliokuwa wanakuja kwa miguu, upande huu tuliokuwa sisi, wakiwamevalia vizuri sana, (nikawaida ya mama mdogo kuvaa vizuri) wote walikuwa wanalitazama gari lao, aina ya suzuk pajero, (gari la kifahari kwa kipindi hicho) ambalo lilikuwa linaondoka, pale kwao, taratibu likikwepa vidimbwi vya maji, huku Eveline na mama yake mdogo, wakilipungia mkono, huku kaka akimkodolea macho ya kustaajabu, mama mdogo wake Eveline, nikakumbuka kuwa kaka akuwa anamfahamu mama mdogo, (ndivyo na mimi nilivyo kuwa na mwita mama mdogoeake Eveline) kutokana kuwa mama mdogo, siyo mkaaji sana, wa hapa mbezi, yani kwa kina Eveline, japo nilikuwa ni mdogo kwa umri, lakini na kubari kuwa, mama huyu alikuwa ni mzuri sana, na anavutia kwa kula mwanaume, ata mimi na nautoto wangu alinivutia.


Gari lilipo fika usawa wetu, nika gundua kuwa ndani yake alikuwepo mama na baba Eveline na dada yao wa kazi, awa ndio majirani wetu, wa karibu sana, na awakutupita moja kwa moja, baba Eveline, ambae alikuwandie dereva aka lisimamisha lile gari, karibu yetu, “ujambo bwana Denis” alisalimia baba Eveline, akimlenga kaka yangu, ambae alikuwa amenishika mkono, “sijambo shikamoo mzee” kaka uwa anapenda kuamkia japo baba Eveline, alikuwa nikijana, lakini ata hivyo alikuwa mkubwa kwa kaka, kama ilivyo kuwa kwa mke wake, kwa mkadilio, ningesema wana miaka 34, “marahaba” waliitikia wote kwa pamoja, huku mama Eveline, akiongeza, “naona doctor umekuja kula pasaka” alisema mama Eveline, nae ni mzuri kiasi flani, lakini siyo kama yule mdogo wake, yani mama mdogo, walio zidiana miaka sita, yani yule alie kuwa anakuja na na Eveline, wakionekana kuulamba kwa mtoko, yeye alikuwa na miaka ishilini na nane, na hapo kati kati yao kulikuwa na kaka yao, alie kuwa na miaka 31, ila kwakipindi hicho alikuwa South Africa, ana endelea na biashara zake, ambazo zilimsaidia sana, pamoja na kuwawezesha ndugu zake wawili, yani mama Eveline na mdogo wao ambae tulikuwa tuna mwita mama dogo, ambae ndie huyu alie kuwa na Eveline, “ndiyo nimekuja toka jumamosi” alijibu kaka Denis, ambae upole ni tabia yake, wakati huo mama mdogo na Eveline, walikuwa wanazidi kutusogelea pale tuliposimama.


Mimi nika mtazama Eveline au Eva, ambae tulikuwa tunalingana umri, na tulikuwa tunasoma wote, nakucheza pamoja, tuka tabasamuliana, kwa furaha, ukihisi kuwa safari yetu itakuwa moja.


Baada ya salam na maswali na majibu, mwisho baba Eveline akasema, “Denis sisi tunaelekea morogoro, kwenye easter conference tunarudi jumatatu, naomba uwe unapita pita hapa nyumbani, kutazama usalama kwa awandugu zako” kaka akuwa na shida, aka kubari na kuahidi kufanya hivyo, kisha wakina baba Eveline wakaondoka zao, huku wakiwa wamejaza mabegi kwenye gari lao, ambalo lilijaa kiasi kwamba wawili awa, wange kosa lift ya kwenda huko waliko kuwa wanaenda.


Naam mala baada ya wakina baba Eveline kuondoka, iliwaona kaka na mama mdogo wana tazamana, kama vile kuna jambo wanataka kuambizana, lakini kila mmoja akasita, na kushindwa kuongea, wakaishia kutabasamuliana, hapo mimi na Eveline tukawa tuna sikilizia, kuona wataanzaje kusemeshana, au wata chuniana, unajuwa kwanini, ebu sikia kwa umakini sababu ambayo ilitufanya tuwe na hamu ya kuwasikia awa wawili wakiongea.******


Sababu ni kwamba, toka huyu mama mdogo alipo kuja hapa kwakina Eveline, zilikuwa zimepita week mbili, na hii ingekuwa ya tatu, hivyo kaka akuwa anamfahamu, maana safari hii mama mdogo, ndiyo alikuwa amesaana tofauti na zamani ambapo alikuwa anakuja na kuondoka, alikuwa akiongozana na mbaba mmoja hivi, ambae wakina Eveline walikuwa wanamwita baba mdogo, wakitokea kigamboni, walikuwa wana kuja na gari lao, nakumbuka kwa muundo wake na jina la kwanza, tulikuwa tuna liita Toyota Double cabin, sababu lilikuwa na sehemu mbili ya kukaa watu, na nyuma lilikuwa wazi, kwaajili ya kuwekea mizigo, na pengine kubebea abilia, katika hali ya shida.


Nili mfahamu vizuri mama mdogo, ambae jina lake ni Irene, kutokana na kwamba muda mwingi nilikuwa na shinda na Eveline, kama siyo nyumbani kwao, basi nyumbani kwetu, tukicheza michezo mingi tu! ikiwemo ile ya kuitana baba na mama, tukiweka makopo yetu na kuigiza tuna pika na kula kama mume na mke, ilifiki kipindi ata wazazi wetu, ambao ni marafiki sana, wakawa wanatuita wakwe, wakitania kuwa mimi ni mchumba wa Eveline.


Safari hii tokea mama mdogo afike pale mbezi kwa Yusufu, yani nyumbani kwa kina Eve, akiwa peke yake, bila yule mwanaume wake, yani baba mdogo, sikumwona akienda kazini, wakati alikuwa anafanyazia kazi mamlaka ya mapato, na kwafedha alizo kuwa nazo kipindi hicho mama mdogo, siyo wa kukaa kwa dada yake muda wote huu, lakini kwa hali ya utoto, sikuweza kujiuliza sana, ila nilicho kifahamu, nikwamba, kwa uzuri na umalidadi wa ma’mdogo Irene, vidume avikuwa mbali, vilifukuzia kwa udi na uvumba penzi la mwana mke yule, ambae ni mzuri kweli kweli, kila mala vikiwa avipungui nyumbani kwa kina Eveline, basi vingekuja na kuomba kuonana na madogo, na kusimama pale nje wakiongea kwa muda mrefu, na mwisho wasiku wakaondoaka wakiwa awaja ambulia kitu, yani walikuja watu wa aina mbali mbali, wakiambatana na vijizawadi flani flani ambavyo, ni kama vile vinguo vizuri vizuri, mikate na choklet bila kusahau pipi, ambazo mimi na Eve, tulikuwa tuna pewa na kuvi kamua kisawa sawa, ila walitukela mabishoo, wao walimletea mauwa rose na card, lakini hao wote waliishia kupewa karenda za kupewa majibu yao, kipindi hicho kutongoza ilikuwa ni kazi ngumu kidogo.


Tena uwa tulikuwa tuna penda sana kumsindikiza mamdogo, kila sehemu anapoenda, asa mbezi anapoenda kutembea au kununua vitu, maana tulikuwa tuna ambulia offer za pipi nazani wengi amzifahamu, zile za sukari ambazo zilikuwa na rangi rangi, biscuit na vitu vingine vingi, ambavyo mama mdogo Irene alipewa na wanaume au kununua kwa fedha alizo kuwa anapewa na wanaume hao,


Nakumbuka siku tatu zilizo pita, kabla ya leo, (siku ya ijumaa kuu) ma’mdogo alituchukuwa mimi na Eveline, tukaenda mbezi, lakini wakati tuna karibia barabarani, ambapo nyumba na makazi ya watu, zilikuwa nyingi, sambamba na maduka, kuna jamaa mmoja ambae kwa umri anaweza kuwa kama baba yake Eveline, alitufwata na kuanza kuongea na ma’mdogo, tuna mfahamu sababu ni muuza duka, na mala nyingi sana uwa ana mwongelesha ma’mdogo, na kumpatia ela, napengine sisi kuambulia pipi, kutoka kwenye duka lake, “Irine, mbona jibu langu unanizungusha, yani week ya pili sasa, kama unashindwa kuniambia moja kwa moja, we! niandikie ata kwenye kikaratasi alafu watume awa watoto waniletee” alisema kwa sauti yenye rafudhi ya kipemba na yakubembeleza yule jamaa, ambae na mfahamu vizuri, uwa anauza moja ya duka kubwa, kati ya maduka yaliyopo pale mtaani, kwa Mpemba, “unajuwa sipendi nikupe jibu ambalo litakufanya ujisikie vibaya” alijibu mama mdogo, ambae kwa watoto watukutu kama John bonge, angesha mtamani na kusimamisha dudu, maana alikuwa mnono, kuanzia hips na makalio, tumbo dogo, mguu wabia, zile chupa za zamani, kifua cha wastani tumbo dogo, vilivyo fanya shape yake kuwa ya coca cola, zamani kuna mwanamziki wa Jamaica aliimba coca cola shape, (search you tube unaweza kuupata) “ok! Irine, sasa chukuwa hii japo kidogo, lakini utatumia siku kuu, mimi nita kuja ijumaa usiku, maana shemeji yako aliniambia anasafiri kwenda morogoro, na kama utaitaji chochote niambaie” alisema yule jamaa, ambae duka lake lilikuwa limeandikwa kwa Mpemba Shop, hivyo watu wengi uwa wanamwita Juma Mpemba, huku akimpa Irine, yani mama mdogo kitita cha fedha noti za shilingi mia mia, sikujuwa ni kiasi gani lakini baadae nika juwa kuwa zilikuwa ni shiringi elfu moja, zilikuwa na thamani kubwa, kipindi hicho, maana anakumbuka, nguo yangu ya sikuku mwaka ule, ilinunuliwa kwa shilingi mia mbili, nilimwona ma’mdogo anashangaa kwa kiasi kukibwa cha fedha alicho patiwa na na Juma Mpemba…






Hapo Juma mpemba, ambae alikuwa anakaa mitaa ule ule, na wake zake wa wiwli ambao kilammoja alisha pata nae watoto, bi mkubwa akiwa na watoto wanne, bi mdogo alikuwa na watoto wawili wa kike, ambao katiyao wawili tulikuwa tuna soma nao, akatuacha tuondokezetu, sisi na mama mdogo tukaondoka zetu kuelekea Mbezi mwisho, ambako tulipita bara bara ya zamani, huku mala mala kwa mala, tukipishana na vidume vilivyo msemesha mama mdogo, maneno ambayo ayakuni flaisha, “we! mwanake ebu simama tuzoze kidogo” kuzoza ni kuongea, au kujadiriana jambo flani, wengine walipiga miluzi, na mambo mengine ya kuhudhi, Kitu ambacho mimi na Eveline tuligundua, ni kwamba ma mdogo apendi kuongozana wala kuwa karibu na wanaume, japo akuwa na ujasiri wa kuwapa majibu ya mojakwamoja kuwa akuwa tayari kuwa nao kimapenzi, na kwa uzuri wake, ilikuwa vigumu kuepuka usumbufu wa wanaume hao.


Nakumbuka wakati tupo mbezi sokoni, kuna jamaa mmoja muuza samaki, ambae pia anakaa kule mtaani kwetu, namkumbuka kwa baiskeri yake, ambae kwenye main guide (medigadi) nyuma ya tairi, aliandika Wakwetu, alimweleza mamdogo maneno kama yale aliyo elezwa na na Mpemba, yani yule muuza duka, mwisho jamaa huyu muuza samaki wakavu, aka funga kambale wawili na kumpa ma’mdogo Irine, “nenda kale nyumbani, nazani nitakuja ijumaa, shemeji yako uwa anapenda sana kusafiri kipindi kama hiki” mpaka hapo tulikuwa tumesha sikia ahadi mbili, ambazo binafsi siku msikia mamdogo akitoa majibu, ya kukubari ahadi zile, au kuzi kataa, na licha ya hivyo tulisha ona kikataa kuongea na wanaume wengi sana.*****


Leo mimi na Eveline tulitaka kuona kama ma’mdogo atakubri kuongozana na kaka Denis, na ukichukuia hii ndio njia ya kwa mpemba, na leo ndio siku ambayo mpemba aliahidi, kuja kwa kina Eva, na kweli wazazi wa Eva walishaondoka, kuelekea mrogoro, “Pross unaenda kanisani bila kumpitia mchumba wako?” alisema ma mdogo, huku akinichezea kichwani, sikujuwa ni jibu nini, nikajichekesha huku na mtazama kaka Denis, “na juwa Popa uwezi kumkimbia mchumba wako, na hivi alivyo pendeza, si watu watakuibia huko kanisani” alijibu kaka, japo mwanzo siku lielewa jibu lile, na kulichukulia kiwepesi, lakini nikaelewa, baada ya kumsikia mama mdogo ambae alianza kukutabasamu kidogo, akijibu, “Eva mwambie Poross, ni wasi wasi wake tu!, aibiwi mtu” kwa maneno, nikama ilitoa kibari cha kuongozana, tukaanza kutembea kuelekea Mbezi kanisani, safari ilianza kimya kimya, na baada ya kutembea kama mita mia mbili hivi, kaka akaanza uchokizi, “Eve, leo umependeza utazani ndio siku ya siku kuu, mpaka Popa anaona wivu” hapo Eveline aka mtazama ma’mdogo, nikama alikuwa ana msubiri amjibie, mana tulisha ufahamu ule mtindo wao wakuongea, “Eva mwambie Pross, ndio kawaida yetu kupendeza” hapo kaka Denis akacheka kidogo, nikifwatia mimi kumsaidia kucheka, ata Eva nae kacheka, ma’mdogo yeye aliishia kutabasamu, huku safari ikiendelea, tukikaribia madukani.


Nika mwona ma’mdogo anaongeza mwendo, kila tulipo karibia maduka, huku akiwa amemshika mkono Eva na kumfanya apate shida kuruka vidimbwi vyamajini, “Pross mwambie Eva atembee taratibu, atacha uaviatu vyake vizuri” kiukweli kutokana na sura ya kaka Denis, na umri wake mdogo zaidi ya ma’mdogo, usinge weza kuwa fikilia vibaya, ilionyesha wazi kuwa ma’mdogo nimkubwa kwa ma’mdogo Irene, “Eva mwambie mchumbma wako, hapa kuna wa doezi, ndio maana tuna arakisha” alijibu mamdogo, hapo akuna ambae akujuwa kuwa anaambiwa kaka Denis, hivyo atukuwa na budiku ongeza mwendo, ili kuufwata mwendo wa ma’mdogo.


Lakini aikusaidia, maana ile tuna livuka duka la mpemba tu, Juma mpemba akachomoka toka dukani kwake akiwaacha wateja watatu waliokuwa wana subiri huduma, “Irene leo wapiti mbio mbio, kama wafukuzwa” alisema Mpemba huku akitukimbilia, “tumechelewa kanisani” alijibu mamdogo, huku anasimama, “Pross mshike mkono mchumba wako, mtangulie taratibu” alisema Ma’mdogo, huku anamwachia mkono Eva, ambae alienda kuudaka mkono wa kaka wa kushoto, “ujambo kijana?” alisalimia Juma Mpemba, na kaka akaitikia, kisha aka mwamkia, mpemba akaitikia, na sisi tukiwa tuna ndelea kutembea taratibu, huku wote watatu tuna tupa macho ya wizi kumtazama ma’mdogo, ambae akutumia muda mrefu, tukaona aona anaambiwa mamneno flani na kupewa kitu flani ambacho tulijuwa itakuwa ni fedha, kisha akatukimbilia, huku Juma Mpemba akisisitiza kuwa mamdogo asi sahau kupitia wakati wa kurudi.


“Pross, utani kumbusha kupitia wakati wa kurud” sikuelewa kwanini mamdogo alikuwa mwepesi wa kupokea fedha na vitu vya watu, wakati walikuwa wana mlalamikia kuwa akuwapa jibu walilo kuwa wanaliitaji, ambalo ata kwa udogo wangu nilijuwa, ni kuwa kubaria wamle kitumbua, “tuta kukumbusha” hapo nilijibu mimi, maana kaka Denis alikuwa kimya, nikama alikuwa anatafakari jambo, ukimya ambao ulimwambukiza ata ma’mdogo, na hapo safari ikawa kimya kimya, mpaka tulipofika kanisani, na tuka tawanyika, wakati sisi tukielekea sehemu walipo kaa wanaume, Eve na ma’mdogo, wakaelekea upande wa wanawake.


Saa kumi jioni tayari tulisha toka kanisani, nakumbuka nikama kulikuwa na dalili yamvua nyingine kushuka jioni ile, maana wingu lilitanda kwelikweli, juu ya anga, niliingiwa na unyonge, maana sikuona dalili ya kaka kuwatafuta wakina ma’mdogo, ukweli safari ya kuwa na kaka Denis, sikuipenda ata kidogo, kwanza akuwa na ela ya kununua pipi, maana zaidi ya shilingi sita ambazo tulizogawana yeye akichukuwa shiringi tano na mimi shilingi moja, ambazo tulizitoa sadaka, akuwa na ela nyingine, na alicho nikela zaidi, ni kitendo cha kunilazimisha nitoe sadaka, maana nilitaka kuibana, ili nikanunue pipi wakati wa kurudi.


Nilitoka kanisani nikiwa nimenuna kwa hasira, na mbaya zaidi ndio tulikuwa tunaondoka, bila kuwasubiri wa kina Eva na ma’mdogo, ambao najuwa kabisa wata faidi pipi wakati wakurudi, lakini nahati ikawa upande wangu, maana ile tuna ikamata barabara huku kaka amenisika mkono, katikati ya kundi la watu waliokuwa wanatoka kanisani, mala nika stuka, mtu ame nigusa begani kutoka nyuma yangu, kutazama nyuma alikuwa ni Eva, aliekuwa ameshikwa mkono na ma’mdogo Irene, nakumbuka nilijisikia amani kubwa moyoni mwangu, maana nilitabasam mpaka wana Eva walijuwa kuwa nilikuwa nawaitaji, kutokana na kugeuka kwangu, kaka Denis akageuka kutazama nyuma, macho yake yaka kutana na macho ya mamdogo, ambae alitabasamu kidogo, japo kaka nikama alilipotea zilie tabasamu la mama mdogo, “Pross, una mwacha mchumba wako, umsindikizi sokoni” aliuliza Mamdogo, hapo sikuangaika kujibu. nilijuwa lile swali ni la kaka, wakati huo watu wengi waliokuwa wana elekea majumbani mwao, walikuwa wanamshangaa ma’mdogo , kwa uzuri wake, wengiwao wakiwa ni wanaume, ambao awakujali kuwa wapo na wakezao, au familia zao, maana licha ya kupendelewa uzuri wa sula na umbo. pia ma’mdogo, alikuwa anajipenda sana, kwa urembo na mavazi, “Porss, uogopi kufumaniwa na wenyewe” aliniuliza kaka, hakika nilishindwa kumwelewa kaka Denis, na ukichukulia nilikuwa na juwa kuwa safari za mamdogo ni zakufaidi, nika jibu mwenyewe, “siogopi” huku nikijitoa mkono wangu, kwa kaka ambae nilisha ona kuwa hakuwa na mpango wa kuongozana na mama mdogo, pengine kwa wivu au roho ilimuuma, kwa kile kilicho ketoa pale kwa mpemba, “eti Pross utafumaniwa nanani wakati wewe ndie mwenye mchumba” alisema ma mdogo, ambae nilimtafthiri juu juu, sikujuwa alikuwa ana maanisha nini, “mh! Pross Eva ana kupa moyo, wakati wewe siyo hadhi yake” alisema kaka, wakatu huo walikuwa wanaongea kwa sauti ya chini, “wala asikutishe Pross we jiamini, kwa ni wenye ela ndio wananini, kama ela si tunazo zakwetu”, alisema mama mdogo huku anamtazama kaka kwa macho ya tabasamu, na kuzodoa, “poa twenzetu, lakini sisi yetu macho” alisema kaka na wakati huo alikuwa ananidaka mkono, kisha tukaelekea mbezi sokoni.********


Safari ilianza kimya kimya, huku na watathimini kaka na mamdogo Irene, kaka licha ya kuwa mrefu kiidogo kuliko mamdogo, na mwili mkubwa, kiasi, lakini bado alionekana kuwa ni mdogo kwa umri, wakati ma’mdogo alionekana wazi kuwa ni mkubwa, lakini alikuwa anavutia sana, japo nilikuwa mdogo sana, lakini niliona jinsi mama mdogo alivyo kuwa anavutia, maana ukiachia umbo lake ambalo wakubwa walikuwa wanaliita namba nane pia alikuwa na sura nzuri, na alipenda kujilemba kila wakati, na kwenya mavazi ndio usiseme, ila alikuwa mpole sana, tofauti na zamani, alipokuwa anakuja kuwatembelea wakina Eve.


Wakati tuna endelea na safari, mimi na Eve tuligundua tabia mpya ya wakina kaka na mamdogo, maana mala kwa mala walikuwa wanatazamana usoni na kuishia kutabasamuliana, huku mala nyingi kaka aki tazama kwenye makalio ya mamdogo, ambae alikuwa mbele yatu, ame mshika mkono Eve,


Baada ya kutoka pale kanisani kituo cha kwanza kilikuwa kwenye maduka ya karibu na stend kakaribu kabisa na sokoni, hapo mamdogo akanunu biscut box moja, na kutu gawanyishia mimi na Eva, alafu safari ikaendelea kimya kimya, kuingia sokoni, “Eve mwulize mchumba wako kamaana penda kachumbali tununue nyanya” nilimsikia mamdogo, akimwambia Eva, na kwa kuwa tulisha zowea kuwa kila swali anajibu kaka, wote tuka mtazama kaka, “kwani we Pross unakulaga kwa kina Eva?” aliuliza kaka Denis, na hapo ma mdogo akaongea wazi wazi wazi, “kwani vibaya akila kwa mchumba wake?”


Hivyo ndivyo ilivyo kuwa kila kilicho takiwa kuulizwa kaka ilipitia mimi na alicho takiwa kuulizwa mamdogo aliulizwa Eva, ilimladi nikama walikuwa wanakwepa maongezi ya moja kwamoja, kwetu ilikuwa kama burudani, lakini tulipenda kuona ndugu zetu au watu wetu wakaribu, wakiwa wakiwa pamoja, maana usingeweza kumkuta mamdogo akiongozana na mwanaume kama hivi, kingine kilicho changia pengine ni umri mdogo wa kaka Denis,


Nakumbuka tukiwa sokoni, wakati tuna pita sehemu ya wauza samaki, tuka kutana na yule jamaa anae mpaga mamdogo hela na samaki, mama mdogo nikama akutaka kupitia, wala kuonekana mbele ya yule jamaa ambae baiskeri yake imeandikwa wakwetu, ukweli nazani siyo peke yangu ata Eva alitamani tupitie, ili tupewe ela ya pipi, lakini mama mdogo akuonyesha dalili ya kupitia, ndio kwanza alikuwa anaongeza mwendo.


Nakumbuka bahati ikuwa upande wetu, maana wakati nataka nimkumbushe mama mdogo kupitia kwa wakwetu, na Wakwetu alikuwa wakwanza kutuona, alipotuona tu! akatuita, “Irene vipi wangu mbona unanipita kama jiwe la kilomita?” aliuliza Wakwetu, akiwa mbali kidogo na sisi, hapo ma’mdogo akujibu, ila aka mtazama kaka Denis…






Ambae nikama alijifanya kupotezea hivi, alafu mama mdogo akamtazama Eva, “Eva nisubirini hapo, niongee na mjomba” alisema mamdogo Irene na kumfwata Wakwetu, nikawaona wanaongea mambo flani flani, nikama mamdogo alikuwa anakataa kitu alicho kuwa anaambiwa na Wakwetu, lakini baada ya maongezi ya dakika kadhaa, tuka mwona kama wanakubariana, tuka mwona Yule jamaa akichagua samaki wawili wakubwa aina ya kambale, na kuwa weka kwenye mfuko, kisha akatutazama pale tulipo, “we dogo, unazubaa nini njoo uchukue mboga” alisema Wakwetu, nikamwona kama mamdogo, nikama alikuwa anamkataza, asimwite kaka, lakini alisha chelewa kaka Denis aliwafwata wakina mamdogo, na sisi tukimfwata nyuma yake, “beba mboga hii ya kula jioni, mbona unazuba sana dogo” alisema Wakwetu na kaka akatabasamu huku anapokea ule mfuko wa kambale, “shikamoo” alisalimia kaka Denis, “malahaba dogo” aliitikia wakwetu, kisha akamtazama madogo, ambae alikuwa ametazama chini kwa aibu, “sikunyingine utakiwi kuja sokoni we mtume tu huyu dogo, si atanikumbuka?” alisema Wakwetu kwa majisifu, mamdogo aliishia kutabasamu, kaka ndie alie jibu, “nitapakumbuka” niliona mamdogo akimkata jicho kaka Denis.


Baada ya hapo mamdogo akaaga na kisha tuka ondoka zetu, huku wakwetu akisisitiza, kuwa baadae atakuja nyumbani kwa kina Eva, “sawa utanikuta” kwa haraka haraka, nilisha wasikia watu wawili waki toa ahadi za kuja kwakina Eva ndani ya usiku mmoja.


Kagiza kalisha tanda, likiongezewa na wingu kubwa la mvua, ambayo inge shuka muda wowote, tulitembea kimya kimya, kila mmoja alisha choka, na mizunguko, sasa mimi na Eva tulikuwa tume shikwa mikono na mamdogo, kaka alikuwa amebeba mazaga yote aliyo nunua mamdogo sokoni, tulipofika pale dukani kwa kwa juma mpemba, nikamwona mamdogo akipita kwa kujificha ficha akisaidiwa na giza lililo kuwepo, lakini wakati tuna pita, tuka gundua kuwa mpemba akuwepo dukani kwake, na baada yake alikuwepo mke wake, yani mmoja kati ya wakezake, hapo safari ikaendelea kimya kimya, ikonyesha mamdogo na kaka Denis awajazoweana bado, kiasi cha kupiga story, wakati mwingine nilizania kuwa, ni kutokana na kuzidiana umri, au ni ile tabia ya mamdogo kuto kupenda mazungumzo mengi na wanaume, japo cha ajabu akuwa anawakataa waziwazi, na vitu vyao alikuwa anachukuwa.


“Pross, leo si utakula nyumbani kwetu” aliuliza mamdogo, hapo nika mtazama kaka kama atatoa jibu gani, lakini akawa kimya, “pross ujuwe mchumba wako leo yupo peke yake, anaogopa, si utakuja kuchaza nae kidogo?” safari hii mamdogo aliongea kwa sauti ya kubembeleza, “labda kaka akinileta” kwamala ya kwanza nilijibu mwenyewe, kweli nilikuwa na hamu ya wali na kambale, mana kipindi hichi wali ni moja ya vyakula nilivyo kuwa navipenda kupita kiasi, hapo hapo nika msikia Eva akinisaidia, “eti kaka Denny, si utamleta pross?” aliuliza Eva, “ngoja kwanza tuka age nyumbani, alafu nita mleta” hapo moyo wangu ulitabasamu kwa furaha, wali kambale siyo mchezo, maana katika kumbukumbku zangu tulimwacha dada anabandika maarage kwaajili ya jioni, siyo kwamba wazazi wetu walikuwa awana uwezo kifedha, ila ndio utaratibu walio jiwekea, kama mchana tuta kula ugari samaki au nyama, basi usiku wali maarage, na leo ndio ijumaa kuu, basin i maharage kwakwenda mbele.




ITAENDELEA




0 comments:

Post a Comment

Blog