Search This Blog

Monday 19 December 2022

KITU MNATO - 3

  



Chombezo : Kitu Mnato 


Sehemu Ya Tatu (3)




Akajitahidi kumsahau ikashindikana kivipi amsahau mwanaume wake wa kwanza?!




Akajipa moyo avumilie danis atabadilika,alijidanganya kwa kweli!,akawa katika maumivu makali ya mapenzi




***




Ili ajifariji!,pengine ni uchunguzi au ni ushamba wa mapenzi SHAMIM akataka kufahamu ni kipi kilichomgeuza Dani's?!


Akaamua kutembelea sehemu ambazo Danis aliwahi mpeleka




Kwa minajili ya kujifariji sambamba na wivu!




Ha haaa haaaaa haaaa eti pengine angemfumania Denis na mwanamke mwingine aliye mbadilisha na kumuona yeye hafai!




Mapenzi ni uchizi , shamim yalimgeuza kichaa!,katika mahoteli, walokuwa wanapenda kutembelea akawa anaweka mtego bila mafanikio




Wengine wanauliza eti si angeenda kwake?!




Kumbuka Denis ni mtoto wa kigogo je ni mlinzi yupi angemruhusu aingie?!




Aliwazalo mjinga ndilo linalotokea,na siku ya siku mtego wake ukatega!




Ni katika ile supamarket kubwa mjini pale,supamarket iliyomilikiwa na bwana HAKEEM!




NI SIKU AMBAYO ATOISAHAU KATIKA MAISHA YAKE




Kivipi?! Nini kilitokea katika siku hiyo?!




*******




SEHEMU YA 06




Ni wakati akiendelea kuchagua vitu katika "super market" ile ghafla kuna kitu kikamwambia atazame upande zilipo nguo na viatu vya kiume!, kutazama tu!....




Ni wazi alihisi macho yake yanamdanganya!,




Au pengine alimfananisha kutokana na kumuweka sana moyoni!


Ila akili yake na macho yake vikazidi kumsisitizia kwamba hakukosea yule ni Danis wake




Wakati akiendelea kumshangaa ghafla Danis naye akageuza shingo kuangalia upande ule alipo Shamim


Akaonesha wazi kushtuka!,


Hakutegemea kumuona binti yule mahali pale!




Na hivi alikuwa na binti mwenye asili ya chotara au shombeshombe,aliyejaliwa uzuri wa sura na hata muonekano wake aliendana na Danis


Kiukweli waliendana,...




mapenzi yana nguvu zaid ya greda au break down hilo lilidhibitika pale ambapo Shamim alipoanza kuchepuka kuelekea ule upande aliopo Dani's...




"Tuondoke mpz!"




Ghafla Danis akamwambia mpz wake,ambaye alipigwa na butwaa, kwa kuwa ilikuwa ni ghafla,akabaki kushangaa,alipo ona binti hamueleewi akamshika mkono na kuanza kumvutia nje!




Shamim hakukubali akatoka!, kabla hawajaingia ndani ya gari akaita tena kwa sauti kubwa "Daniiiiiiiis!"




Wote wakageuka,ila DANIS akawa akimvuta mkono shombeshombe yule waingie ndani ya gari!


Ghafla naye akasita,akasimama na kumnyooshea mkono Shamim aliyekuwa akichepuka kuwafata




"Yule ni nani?!" Binti yule akauliza,Danis akakosa la kujibu!




"Si ninakuuliza wewe yule ni nani?!" Shombeshombe akazidi kuhoji safari hii sura yake ikibadilika kutokana na jinsi alivyoikunja


Tayari Shamim Alisha wafikia,kama mjuavyo wa uswahilin ni wa uswahilini tu!




Kutokana na kuzidiwa na wivu aliokuwa nao Shamim akaanza kumchamba (kutukana)binti yule akishusha lawama Kali kwa DANIS, watu wakawazingira!




"Sikutegemea kama ungenifanyia hivi Danis kipi ulitaka nikakunyima wewe,kumbuka wewe ndo nilikuzawadia usichana wangu ukanipa ahadi kem kem kwamba hutoniacha yako wapi?! Yako wapi Danis, umeutia moyo wangu simanzi, sononeko la milele yote kwa sababu ya huyu kikaragosi....




" inatosha mamaaa, Mimi si kikaragosi nitakufanya kitu mbaya usinisahau katika maisha yako!,"




yule Dada shombeshombe akajibu mashambulizi,hasira zilimkaa kooni Shamim akashindwa kuzituliza akamvamia Yule Dada pasina kumjua vizuri kwa lengo la kumtandika!




Waandishi wa habari "shilawadu!" walianza kuwasili wakiwapiga camera,




"wakosaje kwa mfano?!"




tayari Danis alishawatumia meseji polisi baada ya dakika chache difenda ikawasili ni kama supamarket imevamiwa 'ffu' wakashuka na kumuweka Shamim chini ya ulinzi mkali




Akituhumiwa kumletea fujo mtoto wa waziri Danis pamoja na mtoto wa baloz wa Oman nchini Tanzania bi Salha mrisho




Kivipi iwe kesi ndogo!,kivipi waandishi wasiiripoti au kuiweka picha ya Shamim mbele ya magazeti yao kusudi iuze?!


Mtoto wa waziri na wa baloz iwe kesi ndogo?!...


'Unaleta masikhara nini?!'




Shamim aliangukia pabaya,ni wazi aliangukia pua,ni nani angemuokoa katika janga hilo!,kwa kipigo kikali akapandishwa juu ya gari kupelekwa polisi!




****




Mzee Side mtukutu alifura kwa hasira!,mkononi alikuwa kashika mkanda! Akihema, sambamba na kufoka!




Mke wake alilia mpaka sauti ikakatika,ni baada ya kushukiwa na dhahma ya kipigo kikali kutoka kwa mume wake yule




"Unafuga maradhi lazima nikuadhibu,upo kimya mwanao Malaya wa kutupwa unanyamaza tu sasa uso wangu mi ntauweka wapi?!"




Mzee yule aliongea akijinyanyua na mkanda wake,bila huruma akaushusha katika mwili wa mke wake, mkewe alipiga magoti akiomba msamaha! Ila hilo alikusaidia




"Mtoto wa waziri anamtaka kwa nguvu!!!




Hii ni too much asiyefunzwa na wazaziye atafunzwa na ulimwengu ngoja sasa akaozee jela ndo ataijenga tabia,sitofika polisi kamwe nawe mwana hizaya unyanyue milonjo yako hapa uende kule utautambua uongozi haya kaniandalie maji nikakoge Mimi!"




Akamalizia mzee yule akitiririka jasho kwa kazi ya kuadhibu aliyoitoa, kwa haraka mkewe akanyanyuka na kwenda kuandaa hayo maji!


Uchungu wa mwana aujuaye mama,bado mama yule alizidi kumlilia mwanaye kipenzi pasina kujua ataokokaje katika mikono ya wenye nazo nao wakiwa mafukara wa kutupwa na mwenzake ndio ivyo kasha Susa!






***




Gari ya kifahari toleo jipya Mali ya japan,hii ilimilikiwa na matajiri wachache mjini pale


Ilipiga "break" kituo kikuu cha polisi,




Mlango wa upande wa dereva ukafunguliwa mguu ulobeba kiatu kilichopigwa kiwi tena cha thamani kikakanyaga ardhi!,mguu wa suruali ya kitambaa kilichong'aa na kunyooka kwa kupigwa pasi "ikapasika" kikafatia




sambamba na mkono ulotokeza ulobeba mkono wa shati la thamani ulokuwa mfupi na kuwezesha kuonekana kwa saa ya mkononi yenye madini ya dhahabu katika kopo la saa yenyewe na almasi katika Mikanda yake,Mwisho mwili wote ukachomoza toka katika gari ile,




Alikuwa ni kijana " smart" na "mtamu" machoni mwa wadada wa kileo,


Mkononi alishika simu ndogo tu yenye gharama kubwa,hakashuka!




"But" hakuwa peke yake "no" bali upande wa pili wa mlango pia alishuka mtu akiwa na bahasha kubwa mkononi


Huyu alikuwa ni wakili wa jamaa huyo!




Je huyo jamaa ni nani?!,bila shaka wengi wenu mnatamani kumfahamu, usoni alipambwa na tabasamu jepesi akaongoza wakili wake akimfata kwa nyuma wakaelekea uelekeo wa kituo kile!




Ni wakati alipofika kwenye mlango wa kuingilia kuna watu walikuwa wanatoka, mwanaume kwa mwanamke ikabidi wasubiri pembeni watoke kwanza ndo waingie!




Mwanaume Yule alokuwa akitoka alipofika usawa wa jamaa yule kama alimtambua,akasimama wakaangaliana kwa sek kadhaa pasina yoyote kuongea lolote , yule mwanamke shombeshombe alokuja na yule jamaa akabaki amepigwa na butwaa




"Hakeem!?" Jamaa Yule akaita,lakini Hakeem akuonesha kujali wala kumnyenyekea,jambo hilo likamshangaza jamaa yule,tabasamu aliloliachia likayeyuka na mwenyewe bila iyana akapisha njia




"Lakini ni nini kinachoendelea hapa Danny?!" Salha binti shombeshombe akaoji akimshangaa mpz wake yule!,




"wala usijali mpz tuondoke!"




Danis alisema kumwambia mpz wake yule wakapiga hatua kutoka nje ya kituo kile




Naye Hakeem na wakili wake wakazama ndani




"Naitaji kumtolea dhamana mshtakiwa"




Hakeem akaongea kwa kujiamini,na kuwaacha maaskari wote katika bumbuwazi!,kivipi na wakati yeye ndo angekuwa kipaumbele kumdididimiza kwa kumchafulia "super market" yake jina?!




Hawakujua kilichopo ndani ya moyo wa kijana yule,mapenzi ya ghafla yalomvamia pindi alipomuona binti yule,




Ni wakati ule akiwa ofisini kwake ghafla anasikia sauti za makelele nje ya ofisi yake ile,akajinyanyua na kutoka,mapenzi ni hisia uja pale unapo ona, moyo wake ulipasuka alipomuona kwa Mara ya kwanza binti yule




Maneno ya uchungu aloyatoa kumwendea Danis yalimwingia kisawasawa,akabaki ameganda pasina kuchukua hatua yoyote walinzi walipotaka kwenda akanyoosha mkono juu kuwazuia,japo tendo lile alikuonwa na mtu nje ya walinzi wale!




Hisia Kali za mapenzi zilimsukuma kwenda kuingilia,naaam akanyanyua mguu wake kuelekea pale kwenye varangati ila kabla ajafika akasita baada ya polisi wale kuja na kumchukua mzobemzobe binti yule




Hakeem akarudi ofisini kwake,ila akili haikuwa sawa,mchomo mkali wa mapenzi ulimchoma na kumpa maumivu makali,alikuwa katikati ya msitu mzito wa mapenzi na wakumwokoa alikuwa hatarini ili kupona kwake ilikuwa lazima amwokoe kwanza mwokozi wa mapenzi yake




Uwezo wa kumwokoa alikuwa nao ila je jamii ingemchukuliaje?!,kumsaidia muhalifu!, hapana! Ila ile ndo nusra ya moyo wake,iwavyo na iwe!...




Akachukua simu na kupiga namba za wakili wake,na kumuitaji pale ofisini,baada ya dakika kadhaa wakili wake yule akawasili akamweleza juu ya dhumuni lake la kumsaidia Dada yule!




Kwa pamoja wakatoka na kuingia ndani ya gari,kwa safari ya kuelekea kituoni na ndivyo ilivyokuwa!




"Una uhakika na unachosema?!"




Insp wa jeshi la polis akauliza aliyepewa jukumu la kusimamia kesi ile




"Bila shaka afande!" akajibu Hakeem uso wake ukichanua tabasamu!




"Ok right! Fata tu maelekezo!" Insp Nurdin akamalizia akimpa fomu ajaze naye akampa wakili wake wakajaza kila kitu baada ya kukamilisha wakaondoka zao! Huku nyuma afande Jane akaitwa akamtoe mshtakiwa




***




Bado alikuwa na maumivu mazito katika kichwa chake!


Kidonda cha mapenzi huwa ni kigumu kupona, hasa yule ulomtegemea akikuweka pabaya




Shamim alijiinamia selo,akipambana na maumivu makali ya kichwa,maumivu yalotokana na kulia pamoja na mawazo mazito katika kichwa chake!




Ghafla mlango ukafunguliwa na askari Yule wa kike akamuita!


Kwa haraka Shamim akajiinua na kuelekea kwa mkuu wa kituo alipoitajika




"Umepata dhamana ila unapaswa kila siku urejee hapa kusighn,fata sheria zote za dhamana!"




Shamim akaduwaa!, kapata dhamana?!, kivipi?! Na ni nani huyo alomthamini?!,katu akutaraji jambo hili, hamu ya kumjua mtu huyo ikamvaa,bila kusita akauliza




"Je ni nani alomthamini?!"




Yule mkuu wa kituo kwa tabasamu jepesi akamwambia "ni bwana Hakeem?!"




'Hakeem?! Ni nani hasa mtu huyo,' ni wazi jina ilo lilikuwa geni kabisa katika masikio yake na ni vipi ampe dhamana?! Lazima kuna kitu akutaka kujidanganya




"Hakeem mkurugenz wa HAKEEM SUPERMARKET"




mkuu yule wa kituo baada ya kumuona binti kapigwa na butwaa akamtajia kabisa muhusika!




Naaam ni kama Shamim aliona wingu likifunguka na kuona yaliyomo ndani yake kwa mshangao ulompata!, akauacha mdomo wazi akipigwa na butwaa! Mpaka yule askari akamshangaa ila binti alikuwa na haki ya kushangaa!....




Kwanza Hakeem mwenyewe hakuwa na mazoea naye,hawakujuana kivipi aje amtolee dhamana?!,zaid ya kuwa mteja katika super market yake ile hakukuwa na la zaidi baina yao!,hata kama ni wewe ndugu msomaji lazima ungeshangaa!




Kisa tu unaenda kununua bidhaa "nakumat supamarket" Leo umepatwa na matatizo yalopelekea hata kuchafua jina super market ile ila mmiliki wake anakuja kukutolea dhamana!?




Ila akahisi pengine ni MUNGU tu, akapewa vitu vyake alivyokuja navyo, akapanda daladala kuelekea nyumbani akaoge abadilishe ndipo aelekee katika super market ile kupeleka shukrani zake za dhati!




Mapokezi alokutana nayo akuyatarajia pengine alitegemea wazazi wake wangefurah kumuona mwanao ambaye wiki nzima alikuwa ndani,ikawa tofauti baba yake alikuwa kama mbogo alojeruhiwa , pasina kuuliza ametokaje! Wala kumsikiliza akamshushia kipigo akimtuhumu kwa umalaya!




Akuishia hapo mwisho akamfukuza pale nyumbani!,akimwambia aende kwa wanaume wake!




Shamim angeenda wapi?!, alilia akapiga magoti ila mzee yule alikuwa na roho mbaya,hata mama yake alipotaka kuingilia walichanganywa wote!




Ili kumnusuru mama yake,ikabidi Shamim ajiondokee!,japo akujua ni wapi anapoelekea!




'Naamin hii ni dunia yangu!,dunia yangu peke yangu'




Alilalamika akiwa anaendelea kutembea,pasina kujua anaelekea wapi! Yote hayo kisa mapenzi?!


Ghafla akamkumbuka Hakeem! Na Nia yake ya kumtembelea kutoa shukran!,akaanza kuchepuka kuelekea palipo na usafiri akapanda na kuelekea kwa mwanaume yule,ambaye akujua atampokeaje na lipi lengo lake la kumsaidia!.....




****




Bado mapigo ya moyo wake yalimwenda mbio,alifanikiwa kufika katika supar market ile na kuelekea katika ofisi ya mmiliki bwana Hakeem!




Wafanyakazi wengi alopishana nao walimwangalia kwa jicho baya kama wamekutana na shetani,kwani wengi walimuona ni mkosaji!,akuwajali!,akafata njia mpaka mapokezi




"Naitaji kuonana na mmiliki wa super market hii"




ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog