Search This Blog

Monday 19 December 2022

MWALIMU ALITAKA - 5

  

  

Chombezo : Mwalimu Alitaka 


Sehemu Ya Tano (5)




Nikweli leo hii Juned alitimiza ahadi, kwa kuleta gari kubwa la mizigo, ambalo lilipakiza mizigo yote, mpaka nguo zao, huku wakibakiza zile nguo chakavu ambazo, zisinge faa kuvaliwa, wakaondoka vizuri tu, pale nyumbani ambako walipanga kwa miaka mitatu, wakaelekea mjini, ili kuanza safari ya kuelekea Namabengo, huku bwana Peter Mbilinyi, akiwa amekaa nyuma kabisa ya gari kule walikoweka mizigo, amevalia nguo alizokuwa anafanyia kazi ya kupakiza mizigo kwenye gari, yani hii suruali ya chakavu ya kitambaa na shati la rangi ya damu ya mzee, chini akivalia viatu vya wazi, yani sendo, Monica na kaka yake Juned wakiwa wamekaa mbele pamoja na dereva.


Naam lakini walipofika mjini ndipo mazingaombwe yalianza kutokea, maana walisimama maeneo ya soko kuu, kisha Juneid akashuka toka kwenye gari, na kuzunguka upande wa nyuma wa gari yani kule kwenye mizigo, “shemeji hee! shuka basi tuka nunue vyakula kwaajili ya njiani siunajuwa tunasafari ndefu” alisema Juned akimwambia Mbilinyi, ambae kiukweli mfukoni kwake akuwa na ata shilingi moja, akaona kweli hiyo ni nafasi yake ya kusaidiwa na shameji yake huyu, ambae kiukweli yeye mwenyewe alisha msaidia sana, kwa kupitia Monica, “kweli bwana shemeji, maana saa nne hii nimesha anza kusikia njaa”alisema Mbilinyi, huku anashuka toka kwenye bodi la gari lile la mizigo, na kuungana na shemeji yake huyo kisha waka ingia ndani ya soko, ambapo walikatiza na kutokea upande wapili wakielekea kwenye hotel moja wa waarabu, lakini ile wanataka kuingia ndani, mala Juned akasimama ghafla, “dah! wakati mwingine utazani umetumwa, yani mkojo unabana eneo kama ili” alilalamika Juned huku anatazama kushoto na kulia, kabla ya kutazama upande wa sokoni, kule walikotoka, “shemeji naomba unisubiri kidogo, nika jisaidie kwenye choo cha kulipa cha soko” alisema Juned na bila kusubiri, jibu la uitikio la Mbilinyi, akaondoka zake mbio mbio, kuelekea upande ule wa sokoni, akimwacha Mbilinyi ana msindikiza kwa macho mpaka alipopotelea ndani ya soko.


Naam hapo Mbilinyi alisimama kwa muda wa nusu saa, bila kumwona hsmeji yake akirudi toka chooni alikosema anaenda, akaongeza tena dakika kumi, akaona bado kimya, “mh! huyu alibanwa na mkojo au ana harisha?” alijiuliza Mbilinyi, huku anatazama ndani ya hotel, na hapo akakumbuka kitu, “hapana inamaana hii hotel aina choo” alijiuliza Mbilinyi, kabla ajaanza kutimua mbio kurudi alikotokea, yani upande ule wa sokoni, akiamini kuwa monica na kaka yake wamesha mwingiza mjini, maana ata mwenendo wa Monica kwa siku za usoni akuwa anauelewa vizuri.


Nakweli Mbilinyi alipofika pale alipo liacha lile gari la mizigo akulikuta lile gari, akatazama huku ana huku, pengine lime sogezwa mbele kidogo, lakini akuona dalili yoyote ya uwepo wa gari lile, akawauliza watu waliokuwepo pale jirani, kama waliona wakati lile gari linaondoka, nao waka mwambia kuwa lile gari liliondoka pale muda mrefu uliopita, nimala tu baada ya mwenzao, kuingia ndani ya gari lile, na kwa mujibu wa wajihi wa mwenzao huyo, Mbilinyi aligunduwa kuwa ni Juneid.


Mbilinyi alizunguka mji mzima wa songea kulitafuta lile gari, pengine angeliona sehemu lina shusha mizigo, lakini akufanikiwa kuliona gari ilo, na ndipo alipochukuwa uamuzi wakwenda kwa Rafiki mmoja wa Monica wazamani, ambae alikuwa anaishi mfaranyaki, mschana ambae alimfahamu miaka mingi iliyopita wakati anamtongoza Monica, “samahani shemeji hivi Monica atakuwa ameenda wapi?” aliuliza Mbilinyi kama alie changanyikiwa, ni mala baada ya kumsimulia kila kitu Rafiki huyu wa Monica, “shemeji tatizo ulimuamini sana Monica, na kufanya kosa la kumfanya kuwa mke, yani nakushauri wala usijusumbue kumtafuta, kwa jinsi ni navyo mfahamu yeye na mpenzi wake Juned watakuwa wamesha uza vile vitu, na sasa wana kula raha tu!” alisema yule mwanamke, ungesema labda anamwonea huruma Mbilinyi, ila yeye mwenye aliona kama anasimangwa, sababu wakati anaanza mapenzi na Monica walikuwa ni marafiki wakubwa walioshibana, na huyu mwanamke alishiriki kutumia fedha zake, na hapo ndipo Mbilinyi alipogunduwa rathmi kuwa amesha kuwa amesha ibiwa, nakuwa kama amezaliwa upya…




umbani kwa yule mwanamke, huku roho inamuuma sana, asa akikumbuka kuwa siku zote alikuwa anamchukulia Juned kama shemeji yake kumbe alikuwa ni mume mwenzie, na fedha alizokuwa anapeleka kwa wazazi kumbe zilikuwa zinaenda kwa Juned ambae ni hawara wa monica hakika roho ilimuuma sana Mbilinyi ambae alitembea taratibu pembezoni mwa barabara ya rami, kuelekea Luhuwiko, kwenye ile nyumba aliyo kuwa anaishi, ambako alikuta mwenye nyumba ameshafika pamoja na mnunuzi, wanafanya makabidhiano, huku wakianza kuchoma vitu vilivyo bakia, yeye alicho kifanya ni kuchambua baadhi ya nguo ambazo aliziona zita mfaa katika kubadiri, nizile alizo ziacha kwamba singefaa kwa matumizi, kisha akaondoka akiwa hana ata shilingi moja, akilazimika kutembea tena kwamiguu kueleka mjini, mpaka mtaa wa majengo ambako anaishi mwanae mkubwa yani Richard, ikiwa ni miaka na miaka, toka mtelekeze na kuishi na mama Jackline na mwanae Jackline, akamweleza kilicho mkuta, na kwamba amekuja pale kuomba ifadhi wakati anatafuta kazi yoyote itakayo msaidia, “hivi kwa hakiri zako unazani nitaweza kukusaidia we mzee, yani umesahau yote uliyo tufanyia, kwa kututelekeza sisi na mama?” alisema Richard ambae aliongeza kuwa, “kwasasa sina uwezo wakukusaidia kwa lolote, sababu sina kazi, KAHURU ime fungwa, na fanyakazi wote tume ondolewa” alisema Richard ambae akumpatia baba yake ata maji ya bomba japo apooze kiu iliyokuwa inamkabiri.


Kuona hivyo mzee Mbilinyi akaenda kwa Gogfrey, ambae ni mdogo wa Richard, akiwa ni mtoto wake wa pili, kwa mke wake wakwanza, nae ilikuwa kama ilivyo kuwa kwa Richard, “si uende kwa mama Jack, ambako walikufanya utukimbie sisi na mama” alisema Godfrey wakati anamfukuza baba yake, mida hiyo ilikuwa ni saa kumi na mbili za jioni.


Naam hapo ndipo mzee Mbilinyi alipo kumbuka kuwa mama Jackline pia alikuwa na nyumba ya kuishi, japo aliikumbuka ile ya zamani aliyokuwa amepanga, lakini aliona inaweza kuwa msaada kwake, hivyo akaanza safari kuelekea bomba mbili, huku akiamini kuwa huruma ya wanawake inge msaidia kupata ifadhi, na ndipo alipoenda kukuta tofauti na livyo tegemea, ukiachilia kukuta jumba moja kubwa la kifahari, eneo lile, pia alishangaa kuwaona mke wake wazamani na binti yake Jackline wakiwa katika mwonekano wa kipekee, yani walipendeza vibaya mno, ni wazi walikuwa katika Maisha mazuri sana.*****


“Ndio maana nipo hapa, naomba unisaidie mke wangu, hakika nimejifunza siwezi tena kuwa telekeza” alisema mzee Mbilinyi ambae muda wote wa simulizi yake alikuwa akiongea kwa msikitiko, huku Jackline na mama yake wakimsikiliza kwa macho makavu ambayo ayakuwa na huruma, tofauti na Michael, “pole sana mzee ni mitihani katika Maisha” alisema Michael ambae aliguswa sana na simulizi ya mzee Mbilinyi, yani baba mkwe wake, asa kipengele cha kutimuliwa na watoto wake, ambao pia walisha ondolewa kwenye kampunzi iliyo filisika ya KAHURU, “asante kijana wangu, hakika lime kuwa somo kwangu naomba mnisamehe, kwa yote yaliyotokea” aliongeza tena bwana mbilinyi, “baba Jacjk sisi tulisha kusamehe, asa baada kuona umesha amua kutukataa kabisa, na kuacha yule mwanamke akitoa maneno ya kashfa kwa binti yako, na ilo nilicha lichukuwa kama soma kwangu, na binti yangu, kuwa cha mtu ni chamtu, ukiazima akita kustili kwa muda mrefu, kwamaana mume wa mtu ni sumu, hivyo naomba uende kwa mkeo mama God, na uniombee msamaha, kuwa sitorudia kukufwata tena” alisema maam Jackline, na hapo ndipo Mbilinyi alipoamua kuangua kilio kabisa, akiomba asamehewe, na kupewa na fasi nyingine, “mke wangu mimi nakupenda wewe, naomba unisamehe” alisema Mbilinyi, huku anapiga magoti, macho yakimtoka, akiamini kuwa huruma ya mke wake itapita kwake, “we piga magoti, lia utakavyolia, lakini sirudii kosa tena” alisema mama Jackline, kwa sauti kavu kabisa, hapo mbilinyi akaona kuwa, msamaha wake unaweza kupatikana kwa kupitia Jackline binti yake, “Jackline mama, naomba unisaidie kumbuka mimi ni baba yako….” lakini kabla ata ajamaliza akadakwa juu kwa juu, “weeeee! tena ishia hapo hapo, naomba utoke nje, mala ya mwisho wewe na mkeo milinifukuzia mlangoni, na wewe ondoka haraka, si umfwate huyo mwanamke wako” alisema Jackline kwa sauti yenye Jazba.


Sasa ilikuwa vurugu, mzee Mbilinyi akimbeleza Msamaha, huku Jackline na mama yake wakimtaka aondokea pale nyumbani kwao, maana walichukizwa na mambo aliyo wafanyia, ilifikia hatuwa wakaanza kumshika na kutaka kumtoa nje kwa nguvu, ndipo Michael uzalendo ukamshinda na kuamua kuingilia kati, “samahani mama, samahani mama Eric, naomba mwacheni kwanza” alisema Michael huku akiwasogelea na kumshika mzee Mbilinyi, ambae aliona kuwa ukombozi ume mfikia, maana ukweli ni kwamba, akuwa nasehemu ya kwenda, na njaa ilikuwa inamchamanda vibaya sana, “baba Eric usije ukaanza kurefusha mambo, eti unataka kumshauri mama amsamehe, kumbuka kuwa huyu ni mume wa mtu, na amesababisha mpaka sasa, wakina kaka God wananichukia vibaya sana” alisisitiza Jackline, ambae akuonyesha dalili ya utani, “sawa mama Eric, lakini huyu mzee usiku huu ataenda wapi, lazima ukumbuke kuwa anaitaji msaada watu, pengine ajatia chochote tumboni, na kama ulivyo msikia kuwa, nyumba aliyokuwa anaishi imesha nunuliwa, na mbaya zaidi ameibiwa vitu vyake vyote” aliongea Michael kwa msisitizo, “sawa baba, sasa unataka kusemaje? lakini siyo kulala hapa kwangu” alisema mama Jackline, kwa sauti ya kukaza, “sinamaana yakuwa alale hapa kwako, ila tusi mfukuze namna hii maana tuna weza kumsabishia matatizo ya kihakiri na kiafya, labda tufanye jambo moja, tumwulize kama kuna msaada anaweza kuuitaji, ili kuanza Maisha mapya” alisauri Michael ambae ata mzee Mbilinyi alipo omba asaidiwe kufika kijijini kwao Mawengi, huko Ludewa, yeye akatoa fedha kiasi cha Tanzania shilingi laki mbili, pengine unge linganisha na milioni mbili kwa sasa, wakamkatia tiketi usiku ule pamoja na kumnunulia baadhi ya vifaa na nguo, ambazo angeenda kuanzia Maisha huko kijijini Mawengi, kisha waka mpeleka kwenye guest moja kubwa na nzuri yenye hadhi, ya #Nyumbani_peace_lodge, ambapo alipumzika na siku ya pili akawai basi la kwanza liendalo Njombe, ambako angepata usafiri wa kwenda Ludewa akishukia Mawengi kilomita kadhaa kabla ya kufika Ludewa, hakika Mbilinyi aliumia sana roho yake, huku akimlahani Monica kwamba akutwe na mabaraha makubwa.*******


Naam Richard na Godfrey, wakiwa hawana kazi yoyote, ni baada ya kampuni waliyokuwa wanafanyia kazi yani KAHURU, kufungwa, walikaa kwa miezi kadhaa, huku wakiishi kwa kutegemea kazi za muda mfupi, yani vibarua, ambazo zilikuwa na malipo madogo, tofauti na Malipo yao ya zamani, wakiwa katika kampuni ya KAHURU, hakika azikusadia chochote, katika Maisha yao ya kila siku, nakuanza kusababisha migogoro na usaliti katika ndoa zao, wake zao wakitoka na kuanza kugawa vitumbua vyao kwa wanaume wengine ilikujipatia maitaji madogo madogo kama walivyozoweshwa na waume zao, hakuna kati ya God na Richard alie lizika na Maisha yale, na Maisha yao yalizidi kuwa magumu zaidi wakati flani ambao walizikosa ata zile kazi za muda.


Hapo wakaanza kusaka kazi huku na huku, ili kupunguza ugumu wamaisha, uliokuwa unawakabiri, bila mafanikio yoyote, adi mwezi mmoja baadae waliposikia kuwa, kuna Kampuni mpya binafsi, ya usafirishaji, inaitwa Eric Transpoter, ambayo kwa sasa ina ajiri wafanyakazi, ambao ni madereva na mafundi wa magari, huku wakisikia kuwa mishahara ya kampuni hiyo mpya yenye magari mapya, ilikuwa ni mikubwa na minono, pamoja na posho nyingi zilizo nenepa kwa wafanyakazi watakao ajiriwa kampunini hapo “si kampuni ya mtoto wa yule mzee Eric, mwenye kampuni ya Bief” alisema Gody wakati anamsimulia kaka yake, hivyo wakakubariana wabebe vyeti vyao, na kuelekea huko kunako ofisi za kampuni hiyo mpya, pasipo kujuwa kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo ni mdogo wao Jackline.


Naam God na kaka yake Richard, walifika kwenye ofisi za Eric Transpoter, na kujiunga na wenzao kadhaa, waliokuwa wamefika pale ofisini, kwaajili ya kuomba kazi, kwenye kampuni mpya, ata muda ulipofika nao walikusanya vyeti yao, na kusuburi kuitwa majina yao ili kuingia ndani, katika mahojiano, huku wakiyatazama magari mapya kabisa ya mizigo aina ya Nissan Diesel.


Dakika chache baadae majina yakaanza kuitwa, watu waliingia wawili wawli mpaka watatu watatu, na kila alie itwa aliingia ndani na kufanyia mahojiano, kisha kutoka na dalili ya majibu moyoni mwake, wapo waliofurahi na wapo walio toka na uzuni, baada ya kuona dalili za kushindwa kukidhi vigezo, na wote wakaondoka wakiambiwa waje Kesho kuchukuwa majibu lasmi, “Godfrey Mbilinyi, Richard Mbilinyi na Tuzo Ngonyani” yalisikika majina yakiitwa wakainuka watu watatu, ambao ni Richard na mdogowake Godfrey, pamoja na mtu mwingine ambae ni Tunzo Ngonyani, waliinuka na kuigia ndani, ambako walikuta watu wanne waliokaa mbele ya meza ndefu, watatu wakiwa ni wanaume na mmoja ni mwanamke.


Naam walipoingia mle ndani watatu wale macho yao yalikuwa kwa wale wanaume watatu ambao waliamini kuwa ndio wenye uwezo, wa kuhoji kuhusu, udereva na ufundi, na siyo yule mwanamke ambae muda huo alikuwa ameinamisha kichwa mezani, yupo busy anaandika kitu flani, nazani kuhusu mahojiano yale….……






“ok! bwana Richard Mbilinyi, cheti chako kina onyesha kuwa wewe ni dereva, je unadaraja gani la lessen?” aliuliza mmoja kati ya wanaume wale watatu, huku mwingine akitupa swali kwa Tuzo Ngonyani, na mwingine kwa Godfrey, na ata walipojibu, yakafwatitia maswali mengine, huku alie uliza mwanzo akimuuliza mwingine, kwamaana waliuliza kwa kuchanganya, na hawamu ya mwisho kabisa wakashtuka sauti ya kike ikiuliza, “mnaahidi kuifanyia nini kampuni endapo mtaajaliwa” wote wakamtazama yule mschana kwamaana mbili tofauti, upande watuzo, alimtazama mwanamke alie muuliza swali ili ampatie jibu, ila kwa God na Richard waligeuka kumtazama mwanamke yule kwakumshangaa nibaada ya kuitambua sauti yake kuwa, ni mdogo wao Jackline, “tuanze na Tuzo Ngonyani” alisema Jackline akimtaka Tuzo kujibu swali lile, huku God na kaka yake wakitazamana kwa machi ya kujiuliza, kama vile “umeona kaka” ndio mfano wa swali walilo ulizana wawili awa, “nitafanya kazi kwa juhudi kuiletea faida kampuni, maana naamini kuwa mafanikio ya kampuni ndiyo mafanikio yangu” lilikuwa jibu la Tuzo, akamwona yule mwanamke ambae ni Jackline anaandika, na alipo ,a;oza akamatzama Richard, “hapo kaka yangu, unaweza kueleza utaisaidiaje kampuni endapo utaajiliwa?” aliuliza tena Jackline, kwa na mna ambayo ungesema amjuwi mtu huyu, yani ndio mala yake ya kwanza anamwona, ukweli Richard alikuwa bado katika mshangao, kwanza kabisa nikama alikuwa anajuliza Jackline anafanya nini maali pale, je amepata kazi, kama ndiyo basi ameajiliwa lini, aya basi aJackline ni mmoja wa watu wanao simamia uajiri, je kutokana na mambo walyo mfanyia ata waajiri yeye na mdogo wake, “nita fanya kazi kwa uaminifu na juhudi kubwa” alijibu Richard, na hapo Jackline aka andika kitu kwenye karatasi yake mezani, na alipomaliza akamtazama Goodfrey, ambae kama kaka yake, bado alikuwa anajiuliza kuhusu atima yake mbele ya mdogo wao Jackline, lakini alijipa moyo kuwa mle ndani kuna watu wa nne, yakwamba Jackline, siyo peke yake mwenye kutoa maamuzi, “na wewe bwana Godfrey Ngonyani, eleza jinsi uatakavyo isaidia kamupuni hii changa” alisema Jackline kama ilivyokuwa kwa Richard yani kamavile akuwa anamfahamu, “nitafanya kazi kwa juhudi, kutokana na uwezo wangu katika fundi wa magari, ilikuakikisha kampuni inaendelea” alijibu Godfrey, na Jackline akaandika mambo mawili matatu, kisha akawatazama wote watatu kwa zamu, “ok! majibu yenu Kesho” alisema Jackline ambae uongeaji wake, usingeweza kuutambua kama alikuwa amekasirika au yupo katika hali ya kawaida, “ila awa wawili wakina Mbilinyi, sijuwi ndugu, wanauzoefu mkubwa, maana waliwai kufanya kazi katika kampuni ya KAHURU, hivyo wanaweza kuwa wazuri katika kazi zao” alisema mmoja kati ya wale wanaume watatu, kitu ambacho kiliwashangaza wakina Richard, baada ya kusikia Jackline akutoa jibu kama lile, baada ya kuulizwa swali lile, “sidhani kama ili ni muhimu kumbuka tuna vigezo vyetu” alisema Jackline ambae aliagiza waitwe watu wengine.


Naam wakina God na Richard walitoka mle ndani, wakiwa wanasugua vichwa kwa maswali ambayo hakika yasingeweza kupata majibu yake, “hivi kaka imekuwaje Jack ame badirika vile, yani anaonekana anaela nyingi sana, amekuwa zaidi ya zamani, alafu amepataje ile kazi anaonekana kama nayeye ni boss pale?” aliuliza Godfrey wakiwa na Tuzo, wanaelekea mjini kati, “ata mimi sijuwi, lakini uwezi kujuwa mambo ya wanawake, na vile alivyo jaliwauzuri kama mama yake, mimi naofia asije aka tunyima kazi tu” alisema Richard, ambae alionekana wazi kuofia jambo ilo, “lakini hayupo peke yake, lazima wale jamaa wata tusaidia we siulisikia yule mmoja alivyosema?” alisema Godfrey, akijipa moyo, “kwani nyie mna mzungumzia nani, yule dada wa pale Eric Transpoter?” aliwauliza Tuzo, baada ya kukaa muda mrefu bila kuongea chochote akiwasikiliza ndugu wale, ambao leo amekutana nao kwa mala ya kwanza, “ndiyo ni yeye tuna mzungumzia, vipi unamfahamu” aliuliza Richard, “kwani nyie amumjuwi yule dada, yule ndie boss pale, yani ni mke wa mtoto wa mzee Eric, siuna mjuwa yule dogo anaitwa Michael, wanamtoto mmoja anaitwa Eric ndie mwenye jina la kampuni, wanafedha kama taka taka” alisema Tuzo, akimwaga sifa kwa Jackline, na kuwafanya Richard na mdogo wake watazamane, kwa mshangao, “mh! au amefananisha huyu, Jack ameolewa na Michael toka lini?” aliuliza Godfrey kwa sauti ya mshangao, huku anamtzama Tuzo, ili kumtathmini, kama alikuwa anamwonekanano wa kuongea ukweli au alikuwa anatania, mana siyo siri, achana na unapomzungumzia mzee Eric mwenye, ambae ni Tajiri mmoja mkubwa sana mjini songea, sasa ni pale unapomzungumzia Kijana mdogo Michael, ambae ni mmoja wa matajiri wenye umri mdogo pale mkoani, na sifa yake kubwa ni kuto kupenda makuu, wala majivuno, na habari zilizo zagaa mitaani ambazo zilikuwa na ukweli kwa hasilimia nyingi, ni kwamba waschana wengi walikuwa wanatamani kuwa na kijana huyu, iwe wale wasio olewa, waliokuwa wanatani kuwa mke wa kijana huyo, pia ata wake za watu, wapo waliotamani kuwa na kijana huyo, achana na wanafunzi au mabinti wadogo, ambao penzi la kijana huyu, alikuwa ni moja kati ya ndoto zao, “mh! kwani nyie mpowapi, mbona hiyo hipo wazi kabisa, tena jamaa ame mjengea mama mkwe zinga la jumba, kule bomba mbili kanisani, karibu na kiwanda chake M Mills” alisema Tuzo, na kuzidi kuwachanganya wakina Richard, ambao nikama waliona wanaumbuka, “kwahiyo hii Eric Transporter ni yakwake?” aliuliza Richard kwa sauti ya mshangao wakuto kuamini, “ndiyo maana yake, ni ya kwake na mume wake, kwani vipi mna mfahamu yule mwanamke?” aliuliza tuzo.


Hapo kikapita kimya kifupi, kama vile wanategeana kujibu, na mwisho wakajikua wana jibu kwa pamoja, “ni dada yetu” hapo walijibu kwapamoja, lakini Godfery akaongeza, “tumechangia baba” hapo Tuzo akasimama kabisa na kuwafanya wakina Richard pia wasimame pia, na Tuzo akawatazama kwa zamu kwa macho ya mshangao, akitumia sekunde kama sekunde tano,kisha akaachia kicheko cha mwaka, “mh! acheni utanani nyie” alisema Tuzo huku akiendelea kuchekea huku anaanza kutembea tena, na wakina Dod nao wakaanza kumfwata, maana wote walikuwa wanaelekea upande ule, wa kati kati ya mji, “kama ni dada yenu sasa kwanini amjuwi kama ni mke wa Michael Eric, au amuelewani maana siwezi kushangaa kuona ndugu wanapopata uwezo kidogo, uwa wana watenga na kuwa nyanyasa ndugu zao, wasio na uwezo kifedha” alisema Tuzo, ambae ni kama aliongea ukweli, juu ya kile walichokifanya wakina Godfrey, ambao walimtenga kabisa Jackline, ambae aliwasaidia sana kipindi walipokuwa, hawana uwezo kifedha, hivyo wakatazamana kwa macho ya kujisuta, “sasa jamaa, sisi tunaeleka majengo” alisema Godfrey na bila kusubiri jibu la Tuzo, yeye na kaka yake wakachepukiau[pande wa kulia na kukamata chochoro ya maduka ya Velis, wakimwacha Tuzo amesimama na kuwatazama kwa mshangao, maana ilikuwa ni ghafla sana, kwa wao kuaga na kuondoka.


Naam wawili awa walitembea kimya kimya, kwa mwendo mrefu kidogo, kila mmoja akiwaza tukio lile, siyo tu kumkuta Jackline pale ofisini na kuambiwa kuwa ni boss, ila pia kumwona amenawili na kupendeza wakiambiwa kuwa ni mke wa kijana Tajiri Michael Eric, “lakini kaka unazani ataweza kutuajiri kweli?” aliuliza God wakiwa wamekaribia sehemu ambayo walitakkiwa kuachana kila mmoja aelekee nyumbani kwake, “labda kutokana na chuki zake, lakini sizani kama tumewai kumfanyia jambo baya” alisema Richard, na hapo God akamtazama kaka yake kwa macho ya mshangao, “kaka umesahau, tulivyokuwa tuna kata kumsaidia kipindi kile anashida?” aliuliza Godfrey, kwa sauti ya kukumbusha, “lakini kutoa msaada si inategemea uwezo wa mtu, kwani nilazima, na sisi tume omba kazi siyo msaada” alisema Richard kwa kujiamini, “sawa kaka, achana na msaada tulio mnyima, sasa vipi kuhusu maneno tuliyo kuwa tuna mtolea,, ikiwa ni pamoja na kumshutumu kuwa mama yake alisababisha baba akamwacha mama” alisema God na hapo wakakaa kimya, kila mmoja akijaribu kuvuta kumbukumbu ya kile walicho mfanyia Jackline, ikiwa pamoja na naneno yakashfa, waliyo yatoa wao na wake zao, kama siku ile alipokuja kuwaomba msaada kuhusu mtoto wake, alie kuwa anaumwa, “kaka atuna ujanja, inabidi twende kwa Jack, tukamwombe atusaidie” alisema Godfrey, kwa sauti ya kinyonge, “lakini God unazani ata tusikiza kweli, maana kuna maneno mengine atukustahili kumweleza wakati ule, atakama atukutaka kumsaidia” alisema Richard ambae nikama alikuwa amekata tamaa, “ila kaka, mimi naamini kuwa ana weza kutusaidia, Jack anamoyo wa huruma sana, si unakumbuka kipindi kile baba ametunyima fedha za matibabu ya mama, yeye ndie aie tupatia fedha za matibabu” alisema God akijipa moyo, “hiyo aijarishi God, kumbuka wewe ulimfanyia nini baada ya yeye kukusaidia” alisema Richard kwa sauti ya uzuni….……






Na hapo God akuwa na la kusema, na Richard akaendelea, “hapa ndio naona kuwa sina tofauti na baba, ni wabinafs sana, tuna jijari wenyewe, tume kuwa wadhaifu kwa wanawake ambao awakutushauri vizuri kuishi na ndugu zetu” alisema Richard, ambae kama unge msikiliza ungegundua kuwa alikuwa katika majuto makubwa sana,


Basi wawili awa awakuwa na cha kufanya, zaidi ya kukubariana kuwa Kesho waende kusikiliza majibu ya maombi yao, wakaagana na kuelekea majumbni mwao huku nafsi zao zikiwasuta vibaya sana, awakujuwa kile ambacho kinaenda kutokea majumbani kwao, ambacho pengine kingewapa machungu makubwa zaidi.


picha linaanza kwa upande wa Richard, ambae alipofika nyumbani akuweza kumkuta mke wake, zaidi ya watoto wao wawili, ambao walionekana wazi kuwa walikuwa na njaa, “Alex mama yupo wapi?” aliuliza bwana Richard kaka mkubwa wa Jackline, huku anamtazama moto wake mwenye miaka sita, “sija mkuta, mi nime mkuta Joy (Joyce) yupo peke yake analia” alisema Alex ambae alikuwa ame mshika mtoto wa kike mwenye umeri wa miaka miwili, ambae uso wake ulionekana wazi kuwa na alama ya machozi yaliyokauka.


Richard alitazama muda kwenye simu yake, na kuona kuwa ilikuwa ni saa saba, za mchana, ni masaa matatu toka Alex arudi toka shuleni, kwa hiyo toka muda muda huo mke wake alikuwa ameondoka hapo nyumbani akimwacha binti yao mdogo, pale nyumbani peke yake, maana dada wakazi walisha mwondoa muda mrefu uliopita baada ya kuona awawezi tena kumlipa, kutona na kuwa hakuwa na kazi, “vipi mmesha kula?” aliuliza Richard huku ana mchukuwa Joyce toka kwa Alex, “aujala baba, ata Joyce njaa inamuuma” alisema Alex, hapo bwana Richard hakiri yake ika mpeleka moja kwa moja kuwa mke wake atakuwa ameenda kuliwa kitumbua, maana ndiyo tabia yake mpya, aliyo ianza tokay eye akose kazi, yani amefikia hatua hii, anatelekeza mtoto sababu ya wanaume wake” aliwaza Richard, huku akiwa anatembea kuelekea chumbani ambako alikuta chumba kichafu, Joyce alisha kojoa, kitandani hapo, akuna alie badiri shuka, “ebu kwanza” alisema Richard huku ana toa simu yake na kupiga namba za mke wake, ambazo ziliita ila kupokelewa, aka piga tena akiwa amepandisha hasira mpaka kiwango cha mwisho, na safari hii iliita kidogo tu! kisha ikapokelewa, kwanza alikutana na sauti kubwa ya mziki, ambayo iliambatana na kelele za watu waliokuwa sehemu kama vile bar au sehemu ya ulevi, “hallow hivi unamana gani kuwatelekeza watoto kama hivi?” alisema Richard kwa sauti iliyojaa hasira, “hoyaaa! mbona unapiga simu za watu alafu unaanza kubwabwaja hovyo?” ilikuwa ni sauti nzito ya kiume ya kilevi, ambayo ilimshtua sana Richard, ambae alitoa simu sikioni na kuitazama namba aliyopiga, pengine alikosea, lakini aliona kuwa ni namba ya mke wake, akairudisha sikioni, “we nani, na mwenye simu yupo wapi?” aliuliza Richard kwa sauti ya ukari pia, lakini akujibiwa kitu zaidi akasikia sauti ya mtu alie pokea simu akisema, “hoya ebu, msikilize huyu fala wako siulisema mmesha achana?” hapo ata Richard alijikuta akisisimkwa na mwili wake, ni msisimko wa wivu na uchungu, “achana nae huyo mjinga nimesha mwachia watoto wake sina mpango nae tena” Richard aliweza kumsikia vyema mke wake akiongea, kwa sauti ya kilevi, kisha simu ikakatwa, “huyu Malaya akirudi leo, nita mfanyia kitu mbacho ato sahau katika Maisha yake” alijiwazia Richard akiwa amejawa na machungu makubwa sana, kisha akaanza kuandaa chakura kwaajili ya watoto na yeye mwenyewe, na ndio wakati ambao, aligundua, kuwa ata chakula kilichikuwepo mle ndani, kilikuwa ndio cha mwisho, na kwamba Kesho asipopata fedha yoyote, basi anaweza kuuwa watoto kwa njaa.


Naam baada ya kumaliza kupika na watoto wakiwa wamesha kulan a yeye kuosha vyombo, akaingia chumbani kuweka sawa katika swala la usafi, na wakati anaendelea na usafi wa mle chumbani, aligundua kuwa, nguo nyingi na vitu vya mke wake, avikuwepo mle ndani, lakini nikama akujari sana, ila wakati ana tandika kitanda ndipo alipokuta kipande cha karatasi, alipotazama kwa haraka haraka, akagundua kinamaandishi, ya kalamu ya wino, ambayo yameandikwa na mkewe, ambae anaufahamu vyema mwandiko wake, “nazani nimeondoka na vitu vyangu tu! nime kuachia kila kitu chako, kuanzia watoto mpaka bakuri ndogo ya mwisho, naomba usinitafute kuanzia leo, nimeenda kuanza Maisha mapya na mwanaume nimpendae” ukweli kuachwa ni uzuni kubwa kuachwa ni machungu, yani japo mke wake alikuwa ni mgawa kitumbua hovyo, lakini uwezi amini, kama Richard aliumia rohoni vibaya sana.


Naam hapo Richard alitulia kidogo, akijaribu kutafakari Maisha yakuwaje baada yaleo, maana ukiachilia ukosefu wa fedha za kuwalisha wanae pia, nani ana mlea binti yake mdogo, wakati wakati yeye akiwa kwenye miangaiko yake, lakini badaa ya kuwaza kidogo akapata wazo la kupeleka watoto kwa maam yake, “lakini mama Maisha yake yenyewe yanatutegemea sisi, atawezaje kukaa na watoto awea” aliwaza Richard ambae mwisho aliona kuwa kwa mama yake ndio sehemu pekee iliyobakia, kuwapeleka watoto wake ambao walikimbiwa na mama yao, hivyo akawachukuwa watoto na kuanzisha safari ya kuelekea kwa mama yake kuwapeleka, ili wakakaae huko mpaka atakapo pata kazi, ata kuja kuwachukuwa.


Lakini basi ile anafika kwa mama yake aka shangaa kumwona Godfery akiwa na mtoto wake, moja wapekee wakiume, mwenye unao karibiana na wa Alexmtoto wa kaka yake, nae alikuwa anamleta kwa mama yake, “God imekuwaje tena na wewe unamleta Johnson huku, wakati mke yupo?” aliuliza Richard kwa mshangao, “kaka afadhari yaliyo kukuta wewe” alisemaGod kwa sauti iliyo jaa machungu ya wazi wazi kabisa, “he! kitokea nini God, aliuliza Richard ambae yeye tayari alishasimulia mkasa wake.


Hapo God akatulia kidogo, kabla ya akuanza kusimulia kilichotokea, nimaksaulio anzia mala tu walipo achana, na kila mmoja kuelekea kwake, na yeye Richard alipokaribia nyumbani kwake, akamwona Johnson kijana wake, alie kuwaanacheza na wenzake akitoka mbio na kufwata uelekeo wa yumbani kwao, kitendo kilichomshangaza ata bwana Godfrey, ambae alipaza sauti, “John!!!!!!!we John ebu subiri” lakini bado, Johson aiendelea kukimbia upande wa nyumbani, hapo Godfrey machale yaka mcheza, hivyo akaamua kuongeza mwendo, kuwai nyumbani ambako palibakiza kama mita mia mbili.


Naam japo Godfery alijitaidi kutembea kwa haraka, ilikumuwai mwanae Johnson, lakini akuweza ata kuvuka kona mbili tayari alisha mpoteza Johnson, na alipokaribia nyumba aliyo panga aliyokuwa anaishi na mke wake na mtoto wao, akamamwona mwanaue mmoja, anatoka kwenye mlango wa nyumba yake, haraka haraka, akionekana mwenye mashaka makubwa, na kilicho mvutia zaidi kwamtu hyo ambae ata kwaumri alimzidi kama miaka kumi na nane au ishilini, Godfrey, wakati huo God alikuwa na miaka therathini na mbili, akuwa amevaa shati, na viatu alikuwa ameshika mkononi, huku Johnson, akitangulia mbele yake na kumwonyesha njia, “we mzee unaenda ebu simama hapo hapo” alisema God huku anatoka mbilo kumfwata yule mzee, alie kuwa anakaribia miaka hamsini, ambae kuona hivyo, akaanza kukimbia kufwata chochoro, za mtaa ule wa majengo, huku Johnson akirudi ndani kwa haraka, “mwiziiiiiiiii!” alipiga kelele Godfrey.


Hapo sasa, ile kelele moja tu! iliwatoa watu toka ndani ya majumba yao na kuanza kumwandama yule jamaa ambae akufika mbali, akajikuta amesha zungukwa na wananchi wenye hasirakali, ambao walimvuruga na kumgombania kama kitenesi mdomoni mwa mbwa, ambapo ndani ya dakika chache baadae nazani ata mama yake mzazi asinge weza kumtambua, kwajinsi alivyo chakaa, “jamani mimi siyo mwizi” alisema yule mzee kwa sauti ya shida, ambayo ilimezwa na damu nyigi zilijaa mdomoni mwake, zilizosababishwa na kung’oka kwa meno kadhaa mdomoni mwake, “kama siyo mwizi wewe ni nani? na ulikuwa unataka nini nyumbani kwa Mbilinyi” aliuliza mmoja kati ya watu waliokuwepo mahali pale, “ni yule mwanamke ……. niyule mwanamke alisema ajaolewa” alisea yule jamaa, ambaeakuna kiungo ambacho akikuguswa katika mwili wake, kwa kipigo, na hapo ndipo God alipogunduwa kuwa huyu jamaa alikuwa ametoka kula kitumbua cha mke wake.


Na God aliporudi nyumbani kwake haraka ilikwenda kuhoji kuhusu mke wake, akauta amesha ondoka, akimwacha Johnson ambae alieleza jinsi alivyotumwa na mama yake, kwenda kukaa barabarani, iliaangalie kama akimwona ana tokea amjulishe mala moja, “ndiyo maana nime amua nimlete hapa” ndivyo Godfrey alivyoitimisha mkasa wake, hapo mama yao aliwapa pole watoto wake wawili, ambao ndio tegemeo lake, “nikweli mlimtendea vibaya, atukumsaidia pale alipoitaji msaada wetu, japo yeye aliwai kutu saidia, na alilifanya ilo kama sehemu ya wajibu wake, nitaenda nyumbani kwa mama yake, ” alisema mama yao, ambae ndie alieongoza chuki zidi ya Jackline na mama yake, kutokana na kuchukuliwa mume wake, “mh! mama ata kuelewa kweli?” aliuliza Richard kwa sauti ya kukata tamaa, “nazani atanielewa tu! nazani kwa sasa ugovi umekwisha, hakuna kitu tunacho gombea, baba yenu kwa sasa yupo Kijiji na anaendelea na Maisha yake” alisema mama Godfrey, ambae alizamilia kwenda kumwona mama Jackline kwa aajili ya watoto wake wawili, ambao walikuwa wanaitaji kupata kazi, asa kwakipindi hiki ambacho wanapitia wakati mgumu, “sawa mama lakini akikataa we achana nae” alisema God, kabla awajaondoka zao, kila mmoja kuelekea nyumbani kwake, akiwa anaishi kama mwanaume kapela, yani asie na mke. wakimwacha mama yao anajiandaa kuelekea bomba mbili kwa mama Jackline. *****


Naam ni miezi michache ilikuwa imepita, toka mzee Mbilinyi aende Kijiji kwao huko makete, hakuna mtoto wala mmoja kati ya wake zake aliemjari, na kati yao mwenye uwezo alikuwa ni mmoja tu, yani mama Jackline pekee, siyo mama God wala Monica, ambae kwa sasa atukujuwa kilicho kuwa kinaendelea juu yake, baada ya kutoroka na vitu vya bwana Mbilinyi.


Nisiku ile ambayo wakina God waligundua kuwa dada yao, au mdogo wao, Jackline, ambae walimtenga na kumyima msaada huku waki saidiana na wake zao kumtolea maneno ya kashfa, wakisahau kuwa, undugu wa damu auna talaka, na leo hii ndiyo siku ambao, walitendewa maovu makubwa na wake zao hao, kiasi cha kutengana nao kabisa, tena kwa njia za aibu.


Leo Jackline aliona wazi mwanzo wa kaka zake kuanza kuitaji msaada wake, lakini alipokumbuka maneno ya kashfa, waliyo mtamkia wao na wake zao, “siwezi kuwapa kazi, na wao wavune walicho panda”aliwaza Jackline akiwa ofisini kwake, anakagua majina ya watu waliopita katika usajiri, ambapo baada ya kukagua kwa muda flani, akayaona majina ya kaka zake, “lakini ni kaka zangu, wanaitaji msaada wangu, na wana watoto” aliwaza Jackline huku moyo wake ukiingiwa na huruma, “lakini hapana siwezi kuwa saidia ngoja kwanza nikamwelezeMichael na mama nisikie wata semaje” alijisema Jackline au mama Eric au mwalimu Jack, kisha akaweka harama kwenye majina yale mawili, na kuendelea kukagua majina mengine, huku anavuta kumbu kumbu maneno ya kashfa, aliyotolewa na kaka zake wakishirikiana na wifi zake. 






*****Saa kumi za jioni mama God alishuka toka kwenye dala dala, la soko kuu mshangano, katika kituo cha sanga one, pale bombambili, na kuanza kuifwata barabara ya vumbi (enzi hizo) iendayo matalawe, kupitia kanisani, na lipofika mtaa wa kanisani, akachepuka upande wa kulia, kuingia kwenye mtaa ambao kwamacho tu! unge utambua kuwa ni mtaa wa watu wenye kipato cha chini au wasio na kipato kabisa, kutokana na mwonekano wa nyumba za mtaa huo, ata mama Richard ya mke wa bwana Mbilinyi wa kwanza, alitembea huku akiwaza kuwa ata ile nyumba aliyo kuwa anaishi mke mwenzie, yani ile ya zamani, kama itakuwa ime rekebishwa basi ni kidogo sana.


Lakini hisia zake iligonga mwamba dakika kumi baadae, baada ya kufika mwisho wa barabara ile, na kujikuta amufikia ukuta wa M Mills Company, bila kuiona nyumba ambayo hipo hakirini mwake, akasimama na kutazama aliko toka, akaziona nyuma nyingi zikiwa zime jipanga pembezoni wa barabara, yani kushoto na kulia, akaanza kuzitazama nyumba zile moja baada ya nyingine, huku akiiacha nyumba ya kwanza kabisa toka pale alipo, ya mkono wake wakushoto, ambayo ni nyumba nzuri sana, siyo tu kwa mtaa ule ila, ni kwa sehemu nyingi sana, mkoani hapa, nyumba ambayo ata mume wake akuwai kupanga wakati wa utumishi wake, nyumba ambayo kama una hakiri, zilizo ungwa na plasta, ungewezakusema hipo pale kimakosa.


Lakini baada ya kuangalia kwa muda mrefu, huku akizidi kuvuta kumbu kumbu zake, sehemu ilipo nyumba ya mama Jack, ambazo mwisho zilimleta tena pale kwenye nyumba ile mpya ya kisasa, yenye harufu ya utajiri, nje ikipambwa na bustani nzuri ya mauwa, mbali mbali, yaliyomea vye majuu ya zuria lanyasi za koka, “mh! inawezekanaje, ngoja kwanza nika ulize pale pale” alijisemea mama God, huku akianza kutembea, kuelekea kwenye nyumba ya ile kubwa ya kisasa, huku mamacho yake yakijaribu kuendelea kukagua nyumba za jirani, kama angeona nyumba ambayo imefanyiwa ukarabati, lakini mpaka anafika kwenye yumba ile ya kisasa akuweza kuiona nyumba ambayo ina mwelekeo wa nyumba kama ile, ambayo hipo kichwani mwake.


Mama God aliusogelea mlango wa nyumba ile ya kifahari, ambayo licha ya kuvua kandambili zake, lakini bado aliona kama akustahili kukanyaga, sakafu ya nyumba ile, kwa miguu yake, iliyo chafuka kwa vumbi jekundu, la songea, huku aki akikaribishwa na sauti ya music wa chini, wa taharabu, ningependa kuutaja jina lawimbo, ulikuwa unaitwa doctor nipasue, wa mwana music flani mkongwe wa kike wa music huo.


Mama Godfrey akagonga mlango kwa tahadhari, akiofia na kujilinganisha yeye alivyo na mazingira ya nyumba ile ya kisasa na ya kitajiri, “karibu subiri nakuja” ilisikika sauti ya mschana toka ndani, sambamba na vishindo vyepesi, vya miguu peku peku, kabla ajasikia mlango ukifunguliwa, na kuibuka kwa mschana mmoja wa kawaida alie valia kanga kwa mtindo wa Lubega, juu ya gauni flani la mauwa mauwa, “shikamoo!” alisalimia yule mschana, huku akimtazama mama God, ambae alikuwa anamtazama pia yule mschana, huku moyoni akijisemea kuwa hapa siyo kwa mama Jackline, maana akuwa na mototo mwingine wakike, zaidi ya Jackline, “Malahaba mwanangu, samahani nilikuwa naulizia kwa mama mmoja hivi alikuwa anakaa hapa kwenye nyumba moja ya zamani, kabla aijajengwa hii nyumba” alisema mama God kwa sauti iliyojaa mashaka kidogo, yule mschana akaonekana kushangaa kidogo, “mh! yumba nyingine?” aliuliza yule mschana kwa sauti iliyoja mshangao, “ndiyo mwanangu, kuna mama alikuwa anakaa hapa na binti yake, na mjukuu wake mdogo, yupo kama msomalia hivi, ananyuwele ndefu nyeusi” alielekeza mama Godfrey, “mh! au anaitwa mama Jack?” aliuliza yule mschana, “aswaaaaa! anaitwa mama Jack, kumbe unamfahamu” alisema mama God huku usowake ukichanuwa kwa tabasamu, ata yule mschana pia alitabasamu, “sasa anakaa wapi?” aliuliza mama God akiwa na tumaini la kumpata mama Jackline, “anakaa hapa, lakini sasa hivi hayupo, bado ajarudi, yupo mjini dukani kwake” alisema yule mschana, aliekuwa amesimama mlangoni, akimtazama mama God alie simama nje akiutazama mlango wa nyuma ya mama Jackline, kiitazama kwamacho ambayo ya mshangao mkubwa sana, akishindwa kuamini, kile alicho kisikia kuwa ile nyumba mbele yake ndiyo anayoishi mama Jackline, mshangao ambao ata yule mschana aliuona wazi wazi, “unasema kweli we binti?” aliuliza mama God kwa sauti ya mshangao, huku akimtazama huyu mschana, ambae bado akujuwa ni nani hapa kwenye nyumba hii, “kweli ayupo, anarudi saa kumi na mbili au saa moja?” nazani awakuelewana vizuri, hapo mama God akajishtukia kuwa alikuwa ameshangaa, kiasi cha kuonekana wazi wazi, hivyo akazunga, “hooo! kumbe nime wai sana, hen! uwa anarudi saa ngapi?” aliuliza mama God huku akitafakari mafaniko ya huyu mwanamke, ambae akutaka kuamini kama ndie yeye, “lakini unaweza kumsubiri kama unashida nae” alisema yule mschana, na hapo mama God akaona ni bora amsubiri, kuliko kuondoka pasipo kufanikisha alicho kifwata.


Naam mama God aliingia ndani na kuchagua sehemu ya kukaa akutaka kwenda kukaa kwenye viti ya meza ya chakula, akiona kuwa pale kwenye makochi ata chafua, “njoo ukae huku, nikuwashie video” alisema yule mschana, na hapo kwa wasi wasi, na uchaguzi, mama God akaenda kukaa kwenye moja ya kochi lililo itazama TV, kumbuka miaka hiyo ya tisini bidhaa hiyo ilikuwa ni adimu kidogo, unge weza kufahamu ilo dakika kumi baadae baada ya kuwasha video, zikaanza kusikika hodi, watu wanakuja kutazama video, watu walika mbali mbali, wengi wao wakiwa ni wakike, na iliwalazimu kukaa chini, wakichelewa kuchafua makochi ya mama Jack, na kitu ambacho msomaji inakupasa kutambua, ni kwamba kwa kipindi hicho mtaa huo wa kanisani, television ilikuwa nyumbani kwa mama Jack, na kule kanisani tu!, na television ambayo, wana jamii wa mtaa ule, wangeweza kuitazama, ni ile ya nyumbani kwa mama Jackline pekee.


Mama God licha ya kukaribishwa ndani, bado akuamini kuwa pale ndiyo kwa mama Jackline, yani nyumbani kwa mwanamke, aliemchukulia mume, na kisha kutelekezwa kama ambayo yeye mama God alitelekezwa, na mume huyo yani mzee Peter Mbilinyi, “amepata wapi hizi fedha za kujengea nyumba kubwa kama hii, na huyu binti ni nani, mbo na akuwaga na mtoto mwingine” aliwaza mama God ambae uzaolendo ilimsinda na kuamua kuuliza, “samahani binti, wewe unamwita nani huyo mama Jack” aliuliza mama God, akimtazama yule mschana alie kuwa amekaa nzae karibu, “mimi ni mfanyakazi wake, kwani na wewe ni nani wake mama Jack?” hapo ilikuwa ni swali jibu kwa swali, “mimi ni dada yake, sija mwona muda mrefu sana” alijibu mama God akishindwa kujitambulisha vizuri akichelea kubadirikiwa na kuondolewa mle ndani endapo ata eleza ukweli akihisi kuwa mama Jackline amesha simulia juu yake kwa kila mtu, na ameweka wazi jinsi anavyo mchukia, kutokana na ugovi yeye mama God, na wanae wakina Godfrey na Richard kuufanya wakudumu, licha ya kutendewa wema mala kadhaa, “hoooo! kumbe mama anadada yake” alisema yule mschana wakazi, huku wakiendelea kutazama video, na watu wakiongezeka kila dakika zilivyo pita, “inamaana baba Eric, anafedha nyingi kiasi cha kumjengea mama Jack, nyumba kama hii?” alijiuliza mama God huku, akipepesa macho, kutazama kushoto na kulia ndani ya nyumba ile, yenyekila sifa ya kuitwa ya kifahari, na kukaliwa na mtu mwenye fedha.*****


Naam baada ya kutoka ofisini, mida ya saa moja na robo, Jackline akichukuliwa namumewe Michael, wakaelekea nyumbani, huku tayari Jackline akiwa amesha wapotezeakaka zake, kwamaana ya kuwa chinjia baharini, kwamba akuwana mpango wa kuwaajiri, yeye na mume wake walimpitia mtoto wao Eric, na kuelekea nyumbani kwa mama yake kule bombambili, kwenda kumsalimia kama ilivyo kawaida yao, huku njiani Jackline akimsimulia mume wake, jinsi usajiri wa wafanyakazi ulivyokuwa na jinsi alivyowaona kaka zake, ambao walikuja kuomba kazi, “walishangaa kweli kweli, nazani awakutegemea kama watanikutapale” alisema Jackline ambae sasa alikuwa mzuri mala dufu, “nazani uliwahoji vizuri, na uta wahukumu kutokana na sifa zao na uwezo wao, siyo matukio ya zamani waliyo kufanyia” alisema Michael alie kuwa anaendesha gari, “mh! Michael sidhani kama ilo nilahisi hivyo, nivigimu kwa sifa zao kuweza kufuta kile walicho nifanyia” alisema Jackline, na hapo Michael akatabasamu kidogo, akimalizia na kicheko kidogo, “Jack, wewe ni mama sasa, utakiwi kutunza kinyongo moyoni, kumbuka kuwa ndugu zako wanafamilia zao, zinazo wategemea, isitoshe hao ndio wajomba wa Eric” alisema Michael, kwa sauti ambayo nikama ilikuwa ina msihi, na kumshauri mke wake, “lakini walikataa kumsadia fedha kidogo ya matibabu, na walisema kama nimeshindwa kumlea, ni mwache afe” alisema Jackline, kwa sauti ambayo nikama ilikuwa inaanza kushikwa na hasira mpya, “sidhani kama kwa sasa wataweza kufanya waliyo yafanya mwanzo” alisema Michael kwa sauti iliyojaa busara, “Michael sidhani kama wamejirekebisha, labda waonyeshe kufahamu ubaya walio ufanya, ndipo na mimi nita amini kuwa wamejirekebisha” alisema Jackline huku safari inaendelea.


Naam wawili awa wakiwa waesha maliza kupandisha mlima wabomba mbili na kufika stendi ya bombambili inayofahamika kwa jina la kwa Sanga one, Michael alipungaza mwendo na kuingia upande wakushoto, kufwata barabara ya Kanisani, na ile wanakata kona waka shtuka kumwona mtu mmoja mzee wa makamo, alie kuwa anatembea kwa shida, kwa msaada wa fimbo moja kubwa yani gongo, Michael akasimamisha gari, ili kumpisha mzee huyu, alie valia nguo chakavu, zilizo ambatana na koti kubwa jeusi, nalo chakavu kama kofia yake ya duara, ambayo ilipoteza rangi yake ya hasiri, na kuwa nyekundu siyo nyekundu, udhurungi siyo udhurungi, ambae alikuwa anavuta taratibu ile barabara, kwa mwendo wa kujivuta akisaidiwa na fimbo kubwa, siyo mkongojo, ni ni gongo kubwa kabisa, ambalo lilionekana wazi kuwa lilipokatwa kwenye mti alikuangaikiwa kuwekwa katika mwonekano mzuri, kwa mtu kutembelea.


Kitu cha kushangaza, yule mtu ambae anaoekana ni mzee wa makamo, alipofika kati kati ya barabara, alilitazama lile gari ambalo lilikuwa lina mmulika wka taa zake angavu, kisha akabadiri uelekeo na kuanza kulifwata, gari la wakina Michael, ambao walimkodolea macho huku kila mmoja akitabiri akinacho fuata, awakuweza kuondoa gari, sababu alikuwa anatembea, usawa wagari mpaka alipo lifikia, ndipo alipo anza kuambaa mbaa ubavuni mwa gari ilo, la ifahari, aina ya range rover, upande wa kushoto, yani alikokuwa amekaa Jackilne, huku Eric akiwa amekaa, seat ya nyuma yya gari lile, na yeye akimtazama mzee yule, ambae alionekana wazi kabisa kuwa anajambo la kuongea na mtu aliepo ndani ya gari ili, maana alikuwa amelikazia macho, japo wao awakuweza kuuona uso wake, ni kutokana na kofia chakavu ya duara aliyo ivaa, kuona hivyo na kwa uoga wakike, mama Eric yani Jackline, akaanza kupandisha koo haraka, kablam zee yule alie karibia dirisha la mlango wake, ajamfikia, “samahani…. samahani naomba unisikilize……” alisema yule mzee, kwa sauti ambayo ilionekana wazi kuwa katika maumivu, au kuelemewa na mzigo wa shida….. 






Ambae alishindwa kuongeza mwendo, lakini jackline akumsikiliza akaendelea kupandisha kioo, kama ujuwavyo miaka hiyo kioo kilipandishwa kwa kuzungusha kile kishikio chake.


Naam Jackline kabla ajafikia nusu, aka Michael akamzuwia, “subiri kwanza” alisema Michael huku wote wakimtazama yule mzee, “habari za leo jamani” ilikuwa ni sauti ambayo japo ilikuwa ni ya kizee, lakini ilionekana wazi kuitaji msaada, toka kwa walipo ndani ya gari, “salama shikamoo mzee wangu” alisalimia Michael lakini kwa upande wa Jackline alionekana anamtazama yule mzee kwa macho ya mshangao na kuto kuamini, unge sema kuna jambo ameligundua kwa yule mzee, “marahaba kijana wangu, samahani naomba unisaidie chochote kijana wangu nipo katika matatizo makubwa” alisema yule mzee kwa sauti iliyotia huruma, “ok! msaada gani mzee wangu?” aliuliza Michael kwa sauti ambayo ilijaa heshima na busara, huku bado Jackline akiwa ana mtazama yule mzee, ambae sasa alikuwa busy na Michael, kwa mshangao, “chochote mwanangu, maana toka asubuhi sijara chochote, na kama unavyoniona nina ulemavu wa mguu, sina uwezo wakufanya kazi yoyote” alisema yule mzee kwa sauti ambayo kama unge isikia kwa wakati huo, hakika unge shikwa na huruma kuu, “ok! kwa hiyo una itaji fedha siyo?” aliuliza Michael huku akianza kujipapasa mfukoni, “hivi kimetokea nini mpaka umekuwa hivi, ujalipwa mafao yako?” Michael alimsikia Jackline akiuliza kwa mshagao, na yeye akiwa amesa ibuka na wallet yake akamtazama mke wake, kwani mama Eric unamfahamu huyu mzee, na alikuwa mfanyakazi?” aliuliza Michael kwa mshangao, na wakati huo yule mzee nae akainua uso kumtazama mama Eric, yani Jackline, ambae alikuwa anamtazama Michael, na zani akuiona sura yake, “mh! kwani umemsahau huyu mzee, si mwalimu Haule, yule mwalimu wa nidhamu, walikuwa wanamwitaga Njwanga?” alisema Jackline, kwa sauti ya kukumbusha, iliyo onyesha bado ilikuwa katika mshangao, hapo wote wawili wakamtazama yule mzee, ambae Jackline alimtambua kama mwalimu Njwanga, ambae alikuwa bado amemkodolea macho Jackline akingoja ageuke, na safari hii alipogeuka alimtambua vyema, “He! Miss Jack” alisema yulemzee kwa sauti ya mshangao, kabla ajamtazama tena Michael ambae safari hii alimtambua, “hoooo! ticha ni wewe” Michael alipiga kelele zamshangao, akiwa ameshikilia wallet mkononi.


Kiukweli mzee huyu, ambae kama ukusoma mkasa huu toka mwanzo, uwezi kumtambua kama Jackline alivyo mtambua, alipo watambua wawili awa, alionekana kushtuka vibaya sana, na kushikwa na fadhaa, maana uso wake ulimshuka na hapo akageuka na kuanza kuondoka, tena kwa haraka, huku akionekana wazi ameingiwa na uoga, “tafadhari mwalimu, usiondoke kwanza”alisema Michael huku ana endesha gari na kulihegesha kwenye hotel moja iliyopo pembeni mwa barabara ile upande wakulia kwao, jina wacha niliifadhi, “michael unamtaka wa nini huyu, mwache aende zake” alisema Jackline huku akigeuza chingo yake na kumtazama mwalimu Njwanga kupitia kioo cha pembeni yake, kilicho kuwa kimeshushwa nusu, akamwona anatembea kwa haraka kuelekea upande ule wa kushoto wa barabara, “subiri kwanza, mama Eric, uwezi kuona kuwa tunaitaji kujuwajambo kutoka kwake” alisema Michael ambae alionekana kuhisi kitu flani kutokana na hali ya mwalimu Njwanga,ambae akuwa amemwona toka siku aliyo mtengua baadhi ya viungovyake vya mwili.


Michaela lisimamaisha gari akashuka haraka, “tafuteni mezanzuri kisha kaeni mnisubiri” alisema Michael huku ana tembea kwa haraka kuelekea upande wapili wa barabara, hku macho yake ameyakaza kwa mwalimu Njwanga, ambae alikuwa anajitaidi kujikongoja na lile fimbo lake mkononi. ******


Mida hii mama Jackline, ndiyo alikuwa anaingia nyumbani kwake, alisimamisha gari lake aina ya Toyota Crester, toleo zee kwa sasa tunavyoweza kuliita, lakini kwa wakati huo, lilikuwa nit oleo jipya kabisa la Toyota, mama Jackline akashuka toka kwenye gari lake baada ya kulizama engine yake, na kulifunga vizuri milango ya gari ilo, akiwa amesha chukuwa mkoba wake, na kuelekea ndani.


Alipofika mlangoni akakutana na viatu vingi kweli kweli, akastaajabu kidogo, maana watu wale alijuwa fika kuwa wamekuja kutazama video, lakini utaratibu wake ni kwamba, video uwa ina washwa mida ambayo yeye anakuwa amerudi nyumbani, lakini leo imewashwa mapema, na tukio kama ili utokea pale panapo kuwa na ugeni, hivyo mama Jack, akaingia ndani mwake, akiwa na mambo mawili kichwani mwake, kama kuna mgeni ni nani, na kama akuna mgeni kwanini dada yake waka kazi amewasha video mapema kabla yeye ajarudi.


Ile anaigia ndani akakutana na umati wawatu, waliokuwa wamekaa chini, kasoro watu wawili tu, yani dada wakazi na mama mtu mzima mmoja, ambae alikuwa amempa mgongo, akajuwa kuwa huyo ndie mgeni alie washiwa video, hivyo akasogea karibu na kochi lile, “karibu sana pole kwa kusubiri” alisema mama Jackiline ambae badoakuwa ameiona sura ya mgeni wake, hapo mama God akageuka kumtazama mama Jack, “asante lakini, aichoshi nime liwazwa na videomuda wote, mpaka nikaombea uchelewe zaidi” alisema mama God, kwa sauti ambayo, ilikuwa na vichembe chembe vya utani, huku akimtazama mama Jackline ambae alikuwa amekodoa macho kwa mshangao, kumwona mama God mahali pale, “karibu… karibu.. sana, habari za siku” alisema mama Jack, ambae kichwani mwake alihisi kuwa akukuwa na usalama kwa ujio wa mama God pale nyumbani kwake, “asante……asante sana, habari nzuri kidogo, lakini kwakweli kwa upande mwingine siyo zuri, ndio maana nime kuja kukuona” alisema mama Godfrey kwa sauti ya upole, ambayo kidogo ilimpa moyo mama Jack, na kuona kuwa usalama ulikuwepo, “basi hakuna tatizo, wacha nikabadiri nguo mala moja alafu tuongee, alisema mama Jackline, na kueleka chumbani kwake, huku akiwaza mama God atakuwa na shida gani, maana siku za nyuma ilikuwa wakikutana kama hivi ni ugomvi mkubwa.*******


Jackline akiwa amekaa na mwanae pale bar, na mwanae Eric, huku akiwaza na kutafakari mambo aliyofanyiwa na mwalimu Njwanga, kiukweli akuelewa mume wake anataka kufanya nini kwa yule mzee, kama ni msaada au kumwongezea kipigo, lakini kwa mwonekano wa Michael, alikuwa na nia ya kumsaidia yule mzee, ambae yeye Jackline au mama Eric, alikuwa anaamini kuwa ule mguu anao uvuta kwa msaada wa lile gingo, nikipigo kile kile cha miaka iliyipita, alicho pewa na Michael, “samahani mtakunywa nini” Jack alishtuliwa na sauti ya kike, ambayo aikuwa ngeni masikioni mwake, japo alipuuzia ufahamu ule, sababu akuwa na mazowea nasehemu kama zile, za ma bar na mahotel, kihasi cha kufahamiana na wahudumu, “lete soda mbili za orange” alisema Jackline huku anafungua mkoba wake na kutoa noti ya shilingi elfu mbili za kitanzania, wakati huo soda moja ilikuwa inauzwa shilingi mia moja hamsini, akamkabidhi yule dada, ambae mwanzo akuwa amemtazama usoni, na ile wakati ana mkabidhi, ndio akainua uso wake na kumtazama, mhudumu yule alie kuwa anapokea ile elfu mbili.


Naam hapo Jackline akajikuta amatoa macho kwa mshangao, pasipo kuamini anacho kiona, siyo tu kwakuwa anamfahamu yule Mhudumu, siyo kwamba alimshangaa kwakuwa anafanya kazi pale bar, sababu kazi ni kazi, ilimradi unalipwa kutokana na kazi hiyo, ambayo inafahamika ata serikalini, maana mpaka sasa kuna vyuo binafsi na vya serikali, vya kufundisha jinsi ya kutoa huduma za vinywaji na vya kula, katika maeneo ya wazi, nay a kijamii, yani public services, ukweli kilicho mshangaza ni jinsi, mtu huyu anae mfahamu kumwona akiwa amedhoofika mwili, uso una makovu, kama gari la mkaa, au nguo ya mvuta sigara, au vidole vya mkaanga samaki (ni utani tu), “ni wewe mama mdogo?” aliuliza Jackline kwa sauti iliyo jaa mshangao, huku macho ameyatoa, kumtazama huyo mama Mdogo, kama vile akuamini alicho kiona, “he! Jack” alisema yule mwanamke kwa kushuka, ikionekana wazi kuwa hapo mwanzo, alikuwa ajawatambua wateja wake, na alishtuka vibaya sana, “Jack, wewe ndie umeshuka kwenye lile gari?” aliuliza tena mama mdogo, mwenye uso wenye vilaka, “ndiyo mama mdogo, nipo na baba Eric, ametoka mala moja, kunamtu anaongea nae hapo ng’ambo” alisema Jackline, huku bado akionyesha mshangao wawazi kabisa.


Naam huyu ni Monica yani mke wa mwisho wa mzee Mbilinyi, nazani wengi walitamani kujuwa kilicho mtokea mwana dada Monica……..






*******Michael tembea kwa haraka mpaka alipo mfikia mwalimu Njwanga ambae alionyesha wazi kumkimbia yeye, “samahani mwalimu naomba usimame tuongee” alisema Michael, huku ana mshika mkono mwalimu Njwanga, akimzuwia asiendelee kutembea, “samahani kijana naomba unisamehe, najuwa nilikukosea sana lakini adhabu uliyonipatia inatosha, ebu ona, mpaka sasa nimeshindwa kutibu mguu, mfumo wameno mpaka sasa aijakaa sawa” alilalamika mwalimu Njwanga, kwa sauti ya kuomboleza, iliyotia huruma, kiasi cha Michael kuingiwa na uzuni kubwa, maana niwazi kuwa, ukilema aliokuwa nao mwalimu Haule ulitokana na kipigo alicho mpatia usiku hule, “pole mwalimu, inamaana shule ilishindwa kukutibu?” aliuliza Michael, kwa sauti ya fadhaha, “kwakweli nilifukuzwa kazi mwezi mmoja baadae, baada ya mwalimu Jack, kufukuzwa kazi, sababu ni matokeao ya uchunguzi uliowekwa na bodi ya wazazi, juu yangu, kuhusishwa na kutembea na wanafunzi, na ilipo bainika nika fukuzwa shule mke wangu akanikimbia, yeye na watoto, na mimi nika poteza haki zangu, nikikosa ata shilingi moja ya kujikimu, ndio maana unaniona nipo hivi, yani hapa nilipo sijara toka asubuhi, na sina dalili za kula tena leo” alisimulia mzee Njwanga, “pole sana mzee, ebu twende pale bar,ukapate chakula, huku tunaangalia cha kufanya,ili uweze kupatiwa maibabu” alisema Michael,na hapo akiwa amini kinacho mtokea, mwalimu Haule au Njwanga kama wengi walivyopenda ukumwita, alimfwata Michael alie kuwa anaongoza kuelekea kule bar, alikomwacha mke wake na kijana wao mdogo Eric.*******


Naam baada ya kumaliza kuoga na kubadiri nguo, alizo kuwa amerudi nazo toka dukani kwake, alikoshinda toka asubuhi, mama Jackline ambae muda wote, alikuwa anajiuliza sababu ya mama God kuja pale nyumbani kwake, pasipo kupata jibu la kweli, zaidi yay ale ya kukisia, alitoka chumbani kwake na kuelekea sebuleni, ambako kiukweli watu bado walikuwa wanazidi kujaa sebuleni, kwaajili ya kutazama filamu, iliyokuwa imewekwa kwenye deck ya mkanda mkubwa (ndivyo zilivyoitwa) “sasa dada mimi nipo tayari, nazani tuka kae jikoni ilitungee vizuri, hapa atutoweza kusikilizana na hizi kelele za video” alisema mama Jack, mala baada ya kumfikia mama God, ambae aliinuka na kuongozana na mama Jackline kuelekea jikoni, ambako walimkuta dada wakazi ananzisha mapishi, kitu ambacho alikumbuka baada tu! ya kumwona mama mwenye nyumba, “umejiziuka na video mpaka una sahau kumpikia mgeni” alisema mama Jack, wakati wanaingia jikoni, na dada wakazi akakosa jibu.


Kwakifupi mama God alishangazwa na mapokezi ya upendo na upole ya mama Jackline, ambae kiukweli yeye na vijana wake, walimtengenezea ugomvi mkubwa sana, “dada mimi nimekuja, japo nikikumbuka mambo ya zamani, ukweli naona aibu, asa baada ya kujuwa kuwa, niligombana na kukuchukia bule, wakati sisi wote ni ndege tulio nasa kwenye tundu moja, lililotegwa na mwindaji mwenye uchu, ambae alipomaliza njaa zake, aliondoka na kwenda kuwinda sehemu nyingine” alisema mama God ikiwa ndio wanzo wa maongezu yake na mama Jackline alie kuwa anasikiliza kwa umakini, huku akiitikia kwa kichwa kukubariana na mama God, kwakweli hatukuwa na aja ya kugombana sisi wenyewe, maanaisinge badiri tabia ya Peterwala matokeo ya mambo aliyo tufanyia, kwakweli nakili kabisa mimi na watoto wangu, ndio tulio endekeza ugomvi, muda wote, japo wewe na mwanao Jack, mlijitaidi kusogea karibu yetu, na kutufanya ndugu” alisema mama God na hapo mama Jack akasema, “lakini dada ulikuwa na haki ya kufaya vile, hakuna kitu kibaya kama kuona mumeo anakutelekeza kwaajili ya mwanamke mwingine, na anakuachia watoto, ambao kwa kiasi kikubwa bado wanaitaji, huduma za baba yao” alisema mama Jackline ambae moyoni mwake alisifu kitendo cha mama huyu, alie wai kumnyakulia mume wake, kuwa ni cha busara sana, kuamua kumaliza tofauti zao, japo alikuwa amajiuliza ime kuwaje mpaka akaamua kufanya vile, kwamba kuna mtu kamshawishi, au ameona nini mbeleni, “lakini ilikuwa mbaya sana, mama Jackline, yani mpaka leo hii umeniona nime kuja hapa, nimeona tulikofikia ni hatari, mfano leo wakina God walikutana na dada yao, yani wametazamana kama watu wasio juwana” alisema mama God, na hapo ndipo mama Jackline akapata picha iliyojificha, kuwa kuna jambo wakina God wanaitaji toka kwa Jack, ndio maana mama yao amekuja nakujifanya waya malize.


Nikweli dakikachache baadae mama God akanza kueleza shida za wanae, kuanzia kufungwa kwa kampuni waliyokuwa wanafanyia kazi mwanzo, mpaka tabia za ajabu, za wakwe zake, yani wake wa wakina God, na ata tukio la leo, la kufumanianana na kuachana, mwisho akaeleza jinsi wanae wanavyo angaika kwa kusa ajira, “wakaniambia mama nenda kwa mama mdogo, anaweza kutusaidia kuongea na dada Jack, na sisi tupate pa kujishikiza” hapo mama Jack akapata picha kamili, ni kwamba wakina God wanaitaji msaada toka kwa Jackline sasa kwa yale waliyo mfanyia wanashindwa kuongea nae, na msaada wenyewe ni kuwapatia kazi, sasa ugumu ukaja ni kwamba yeye atamjibu nini, wakati mwenye mamlaka ni Jack mwenyewe, na kabla mama Jack aja jibu kitu, mama God akaongezea, “kwakweli hali ni mbaya, mpaka sasa sijuwi wale watoto kule nyumbani watakula nini, kama wataa siku chache mbele bila kazi, basi tunaweza kufa kwa njaa, naomba tusahau yaliyopita tuwasaidie watoto, wana wajukuu wetu, tume shaunganisha undugu” alisema mama Godfrey, kwa sauti ya kubebembeleza na kusisitiza.


Hapo mama Jack akashusha pumzi ndefu, huku sura ameinamisha chini, alifanya hivyokwa sekunde kadhaa, kabla aja inua na kumazama mama God, “sawa ntajaribu, lakini kiukweli inabidi tubadirike, isiwe kama mwanzo, aliwasaidia walipoitaji msaada, na walipo fanikiwa wakaanza kumtusi na kumtenga, kama vile awajuwi” alisemamama Jack, kwa sauti ya msisitizo, hapo mama God lilimwingia kweli kweli, maana ata yeye akuweza kuwashauri watoto wake, juu ya swala ilo. ******


Ilikuwa hivi, Monica akiwa na mpenzi wake Juneid, walifanikiwa kumtoroka bwana Mbilinyi, walienda moja kwa moja mpaka Mehenge B, ambako walipanga kukutana na mtu ambae wange muuzia, vile vitu vya mzee Mbilinyi, ambae walimkuta nyummbani kwake, anawasubiri, naealiwapatia fedha zao kiasi cha laki mbili na nusu, fedha ambayo kwa kipindi hicho tungeithaminisha na million zaidi ya kumi shilingi za kitanzania, na wao wakaondoka zao kurudi mjini, ambako walienda kwenye hotel moja nzuri, yenye hadhi ya hali ya juu, nakuchukuwa chumba ambacho wange kaa kwa siku kadhaa, wakati wanatafuta nyumba zuri ya kukaa, kipindi hicho ungeweza kupanga yumba nzima kwa elfu hamasini,maana chumba kilikuwa kinalipiwa kwa shilingi elfu moja tu, kwa mwezi mzima.


Maisha pale Hotelini yalianza vizuri sana, mchana wa siku ile, wawili awa waliingia upande wa bar, na kuanza kunywa pombe kwa fujo, huku Monica ambae alikuwa ana lewa kwa kasi, akujuwa kuwa mwenzie Juneid alikuwa ana tegea katika unywaji wa pombe, yani wakati Monica anakunywa chupa ya tatu, au ya nne, Juneid alikuwa anakunywa chupa ya kwanza, na mpaka mida ya kulala, ilipowadia, yani mida ya saa sita za usiku, waliingia kulala, na ata Monica akukumbuka muda ambao alipitiwa na usingizi, alishtuliwa na mlango uliokuwa una gongwa kwa fujo, Monica alitazama pembeni yake na kujikuta, alikuwa peke yake, pale kitandani, akahisi kuwa Juneid alikuwa bafuni akaenda kuchungulia, lakini akumwona, akahisi kuwa ametoka na kwenda kuagiza vitafunwa au supu, hivyo akajifunga shuka na kwenda kufungua mlango, akakutana na mhudumu, wa hotel ile, “dada ni saa tano kasoro sasa, unatakiwa kuabdhi chumba” alisema Mhudumu ambae alikuwa na vifaa vya kufanyia usafi, “lakini tulisema tutakaa hapa kwa siku nyingi, sasa kwanini unasema nikabidhi chumba” alisema Monica huku anamtazama mhudumu kwa mshangao, “ata manager alisema hivyo, lakini yule mwenzio amelipa ela ya leo, tu! wakati anaondoka, na amesema na wewe ukioamka utaondoka pia” alisema mhudumu, ambae alirududi nyuma kidogo na kufunga mlango ili ampishe Monica avae nguo zake, na aweze kuondoka.


Baada ya mlango kufungwa Monica ambae akuelewa ilicho tokea, akatazama mle chumbani, ili kuona kama kuna dalili za uwepo wa Juneid au kama atarudi tena maali pale, lakini akuona kitu chochote cha Juneid, zaidi ya begi lake kubwa lililojaa nguo zake, na hapo akakummbuka kuwa Juneid akuwa amekuja na mzigo wowote, maana ata nguo za Mbilinyi waliziacha kwa mteja wao, “Juneid ameondoka, mama yangu weeee, nitampata wapi” alisema Monica huku anajishika kichwa, macho ameyatoa kama ame mwaga uji wa ugari washughuri…




.


Nikweli huo ndio ilikuwa mwanzo wa Maisha magumu kwa Monica, ambae siyo tu kuibiwa fedha na kukimbiwa na Juneid, ila pia, akuwa na sehemu ya kwenda kuishi wa sasa, ata Rafiki yake ambae, alikuwa anaishi nae kipindi kile ajakutana na Mbilinyi, alishagombana nae, hapo akaanza kuzunguka kwenye ma bar, na kudandia wanaume waliokuwa wanakunywa pombe, huku akikodoamacho akitarajia kuwa ange mwona Juneid sikumoja.


Nikweli miezi miwili baadae, Monica alifanikiwa kupajuwa anapoishi Juneid, ni baada ya mjumbe mmoja kumtonya, nae akusubiri aambiwe mala mbili, akaelekea Msamala kwa mahuki, ambako alielekezwa kuwa Juneid ana patikana, na ukweli ni kwamba akudanganywa, alifika nyumba aliyo elekezwa, “tena Mbela yake kuna maduka mawili, moja la kawaida na jingine la vyakula” alikumbuka maelekezo hayo mwana dada Monica, ambae hakiri yake ilikuwa ni kurudiana na Juineid na pengine kupata kiasi cha fedha, toka kwa mpenzi wake huyo alie mtoroka, kama ata kuwa nayo, sababu alihisi kuwa una uwezekano mkubwa wa wa kuwa amesha ishiwafedha hizo, kiasi cha kuamua kuja kupanga huku Msamala.


Monica ambe alihisi kuwa maduka yale ayakuwa mausiano na watu wanao kaa kwenye nyumba ile kubwa ya nyuma ya maduka yale, ambayo alielekezwa kuwa Juneid anakaa pale, na alikuwa na uhakika kuwa Juneid alikuwa amepanga, ndani ya nyumba ile, sababu alikuwa na fedha nyingi alizo ziiba toka wake, akaona ni vyema akapeleleze kwa mmoja kati ya wauza duka, wa maduka yale makubwa yaliyo sheheni bidhaa, ambayo kwa muda ule ayakuwa na wateja, lakini alipoyasogelea, akakuta ni duka moja tu, lilikuwa na muuzaji, yani lile la kawaida lenye bidhaa mchanganyiko, “karibu” alikaribisha muusaji ambae ni mwana dada walika lake, mzuri wa sura, atukuona mwili asa maeneo ya chini, sababu alikuwa amekaa kwenye kiti, na kuzuiwa na meza ambayo pia ilijaliwa na bidhaa, kama makopo ya aina mbali mbali za pipi, Big G, biscuit na vitu kama hivyo, ambae pia alikuwa amempakata mtoto mdogo wa umri wa kama mwaka mmoja na miezi mitatu au minne, “sijaja kununua kitu, kuna jambo nataka kuulizia” alisema Monica kwa sauti kavu, ambayo nikama ilikuwa ina jijaza hasira, pasipo kuitikia ile karibu wala kusalimia, “aina shida unaweza kuniuliza” alisema yule mwana mke muuza duka, mwenye mtoto, ambae alikuwa na dalili zote zakuwa ni mstaarabu, “kuna kaka mmoja anaitwa Juneid, sijuwi unamfahamu, maana nasikia amepanga kwenye hii nyumba, hapo nyuma” aliuliza Monica, kwa sauti ile ile kavu, japo alijitaidi kujiweka katika hali ya kawaida, lakini kiukweli, akuweza kuficha la moyoni mwake.


Monica akamwona yule mwanamke akitabasamu kidogo, “vipi una shida nae gani” aliuliza yule mwanamke, huku uso wake ukiwa umetawaliwa na tabasamu, “sizani kama kuna ulazima wa wewekujuwa nina shida nae gani, nacho taka kujuwa ni kwamba amepanga hapa au nyumba ya jirani” alisema tena Monica, ambae ata afya yake ilishaanza kupauka, kwa kukosa matunzo mazuri, “ok! lakini sizani kama kuna ubaya kwa mimi kujuwa shida yako kwa mume wangu” alisema yule mwanamke muuza duka, kwa sauti yake ya upole, akiwa bado amekaa na mwanae mdogo.


Naam kusikia vile Monica aka achama mdomo kwa mshangao, “usiniambie, toka lini Juneid anamke, au ume mfananisha?” aliuliza Monica, kwa mshangao, “mh! mbona mimi na baba Tina tuna miaka miwili sasa, toka tuna kaa mfaranyaki, tulikuwa tumepanga, na sasa tume nunua hii nyumba na kufungua maduka haya, alisema yule mwaname, huku ana tabasamu, akujuwa kama ana chokonyoa moyo wa mwenzie kwa kijiti kikavu, “inamaana siku zote nilizo kuwa na Juneid aliuwa ana nithariti?” aliuliza kwa sauti iliyojaa hasira monica huku ana mtazama yule mwanamke, kwa macho yaliyo jawa na ghazab, za wazi kabisa, “mh! sasa samahani, unaongelea nini, inamaana uliwai kutembea na mmume wangu” safari hii yle dada muuza duka aliuliza kwa sauti ya mshangao, ambayo iliashilia kuwa akupendezwa na taarifa ile, “unashangaa nini wakati wewe na mwala ya mwenzio mmenitaperi, na le outa ni tambua mala ya mkubwa” alisema Monica huku ana jivuta kidogo pale mezani na kunyoosha mkono kwa ghafla kumzabua kofi la usoni, yule mwanamke mstaarabu, ambae alipiga kelele la yowe, ambalo alikusaidia kitu, zaidi alimwona Monica ndio kwanza ana tafuta sehemu ya kupita ilimwingilia kule ndani, “baba Tinaaaaa!” alipiga kelele yule mwanamke ambae ndie mama Tina, akijaribu kuomba msaada kwa mume wake, kitu ambacho Monica akujari, zaidi aliendelea kutafuta njia palembele, kwa kujaribu kusukuma ile meza, “leo utanitambua we mshenzi, siunapenda kuchukuwa wanaume wawatu” alisema Monica kwa hasira, huku ana ulaza mkono wake juu yameza na kusikuma kama vile anapangusa ile meza, nakuangusha chuni makopo yote ya pipi liyokuwa mezani.


Sasa ile ana anza kupanda juu ya meza iliaingie ndani ya duka, aka shtuka akidakwa mguu na kuvutwa kwanguvu kurudi nyuma, kilikuwa kitendo cha ghafla, na cha kushtukiza, ambacho Monica akukitegemea, hivyo aliteleza na kujigonga vibaya mezani, akibamiza kidevu chake kwenye kingo ya meza, “mama na kufaaaaaa!” alipiga kelele Monica, ambae siyo tu! kujibamiza mezani, nakuanza kuvuja damu, pia alipitiliza chini na kujibamiza sakafuni, akifikia uso, na kuubamiza kwa nguvu, kiasi cha kutoa kishindo kikubwa, safari hii Monica alishindwa kutoa ata sauti, akajaribu kujiinua, huku damu zikimchuluzika, toka mdomoni kwa Monica, “mshenzi sana wewe ume fwata nini hapa?” ilikuwa ni sauti ya kiume toka kwa mwanaume aliesimama nyuma yake, nasasa alikuwa anainua mguu na kumkanyaga mgongoni, kwamaana ya kumkandamiza, (wangoni wanasema kutimba) kitendo kilicho sababisha Monica arudi tena chini na kujibamiza uso wake, “utaniuwa Juneid” alipiga kelele Monica ambae kila alipo kuwa anaongea, damu zili toka kwa wingi mdomoni mwake, lakini aikusaidia, maana kipigo kiliendelea kumshukia Monica, “utajuta kuja hapa we mbwa” alisema yule mwanaume ambae ndie yule yule Juneid.


Naam dakika kumi baadae tayari watu walisha jaa eneo lile la duka, nan a sasa Monicaalikuwaamesha poteza fahamu, huku uso wake ukiwa ume pasuka pusaka kwa vidonda, damu zikimvuja usoni kwa wingi sana, ukweli ni kwa msaada wa raia wema, ambao walimtoa Monica mikononi mwa Juneid, na kumkimbiza kituo cha polisi kabla awaja mpeleka Hospital, huku polisi wakienda kumkamata Juneid, kwa kosa la kumshambulia Monica.


Monica alipatiwa matibabu, kwa kushondwa nyunzi nyingi sana usoni kwake, kuficha vidonda ambavyo, vilikuwa vimetawara usoni mwake, mishono ambayo iliubadirisha uso wa Monica kwakiasi kikubwa sana, na kumfanya aonekane kituko, miezi minne baadae, Juneid ali hukumiwa miaka miwili jela, huku Monica akiingia mtaani kuendelea kusaka wanaume wakumsaidia kupata fedha ndogo ndogo, biashara ambayo aikumsaidia tena, sababu ya mwonekano m baya wa sura yake, na mwisho akabahatika kupata kazi kwenye hii hotel, kama mhudumu wa upande wa vinywaji, huku siku zote akimkumbuka sana Mbilinyi, ambae alimpa Maisha mazuri na yeye kujifanya mjanja, kwa kujiongeza na Juneid, ambaae pia alisha jiongeza ka mke wake, ambae kabla ata awaja kutana, alikuwa wamesha peana ujauzito.


Ukweli leo hii Monica ambae mala ya mwisho alimwona Jackline akiwa amekuja kuomba fedha zamatatibabu ya Eric, alishangaa sana kumwona Jackline akiwa na mwonekano wa kitajiri kabisa, ukiachilia kuja na gari la kifahari pia ata mwonekano wa mavazi yake na mwanae Eric, “mamdog…” kabla Jackline ajamaliza kuongea alicho taka, Monica aligeuka na kuondoka…






. endelea….


Pasipo kuwasikiliza wala kupokea fedha yao ya vinywaji, na kuwaacha wakina Jackline na mwanae wakimshangaa, awakujuwa jinsi moyo wake ulivyo mchoma.


Na wakati wana tafakari juu ya mama mdogo Monica, mala akaingia Michael akiwa ameongozana na mwalimu Njwanga, ambae sasaalikuwa anatembea huku ameinamisha kichwa chini, kwa aibu, maana alishindwa kuwa tazama usoni, kwa yale aliyo ya sababisha siku za nyuma, kwa wapenda nao awa.


Kwa kifupi mwalimu Njwanga ambae aliona wazi kuwa msaada hupo mbele yake, aliomba msamaha kwa mwalimu Jackline, na kusema kuwa, licha ya kugundua kuwa mwalimu huyu alitaka mwenyewe, kupewa dudu siku ile, lakini alifanya aliyo yafanya, kwa kumsingizia Micahel kubaka, kutokana na wivu aliokuwa nao, sababu na yeye alitamani kupewa kitumbua na mwalimu Jackline.


Michael na Jackline walimsamehe mwalimu Njwanga, na kumpatia kiasi cha fedha ambacho kinge msaidia matibabu, na kuanzia Maisha, japo chamoto alisha kiona, nao wakaagana na wakina Jackline Michael na Eric, wakaondoka zao, kuelekea nyumbani kwa mama Jackline, huku njiani mama Eric yani Jackline alimsimulia mume wake jinsi alivyo kutana na mama yake mdogo, yani Monica, na jinsi mwonekano wa uso wake ulivyo, “meondoka ghafla bila kutumbia chochote, utazania sisi ndio tulio mwaribu sura yake” alisema Jackline, kama vile anamtazania mama yake mdogo.*******


Yap, wakati huo huo, mama God ambae alikuwa amesha maliza kueleza kilicho mleta pale kwa mama Jack, yani mke mwenzie, akaakaaga na kujiandaa kuondoka, “unge subiri chakula kidogo” alishauri mama Jack, jambo ambalo mama God alipinga kwa kudai kuwa licha ya kwamba akuwa na fedha ya kununulia chakula, pia aliwaacha watoto kule nyumbani, ambao walikuwa awanaitaji msaadae wake, kiukweli moyo waimani ulimwingia mama Jack, ambae ni mmoja kati ya watu walio sababisha, kushuka kwa Maisha ya mama huyu, hivyo akaona akuwa na budi kumsaidia kwa fedha kidogo, “basi sawa wacha nikachukuwe funguo za gari, nikupeleke mpaka bale stendi, pia uta…..” kabla ajamaliza kuongea mama Jacklne wakashtuka wageni wakiingia mle jikoni, “bibi.. bibi…. bibi…” ni tabia ya Eric kumshangilia bibi yake.


Huyu alikuwa ni Jackline, ambae likuwa amemwacha mume wake kule sebiuleni, na yeye kumfwata mama yake jikoni, akiuongozana na Eric, na klule alimkuta mama God. ******


Kwakifupi, baada ya kusikiliza kwa umakini maelezo ya mama yake mkubwa, Jackline alisamehe kila kitu, na kuamua kuwapa kazi kaka zake, yani God na Richard, ambao waliomba msamaha binafsi wakieleza kuwa awata rudia tena kile walicho kifanya miaka ya nyuma, wakaa ahidi kushirikiana nae kama ndugu.


Jackline, na Michael walimsaidia mama mkubwa sehemu ya kukaa, yani walimjengea nyumba ndogo nzuri, ambayo alikaa na wajukuu zake watatu, ambao baba zao yani Richard na Godfrey walijitaidi kuhakikisha kuwa fedha na maitajio yote ayakosekani pale nyumbani.


Kuna wakati na mama God aliitaji mschana wakazi, kwaajili ya kumsaidia majukumu madogo madogo ya pale nyumbani, asa kumtazama yule mtoto mdogo wakike wa Richard, na alitoa kazi kwa mama mmoja ambae alikuwa anafahamiana nae, nae akamweleza kuwa kuna dada mmoja mkubwa kidogo, alikuwa anaitaji kazi yoyote na alikuwa tayari kwa mshahara wowote, kutokana na ugumu wa Maisha.


Hapo ndipo ilipotokea sito fahamu, ni mala baada ya kuletewa huyo dada wakazi, ambae aliwaacha midomo wazi, siyo kwasabu ya umri wake mkubwa kiasi, hapana ni sababu alikuwa ni yule mke wa zamani, waRichard, ambae aliwaacha watoto na kujongomea na mwanaume, akisema kuwa ajachukuwa chochote kwa Richard na wala ajasahau chochote, hivyo akukuwa na sababu ya yeye kurudi pale wala kutafutwa.


Ukweli mke wa Richard akuamini alicho kiona, maana alikuta Maisha yame badirika katika familia ile, yamekuwa ni mazuri sana, maisha ya kutamanisha, sizani kama wewe msomaji unge mwakiri mama huyu, ambae alianza kujiliza na kuiomba msahama, kwamba alilubuniwa tu, na tena shetani akampitia, na kwenda kumwacha pale bar, “sikujuwa kama yule mwanaume alikuwa na lengo la kuniaribia Maisha yangu, niligundua kuwa alikuwa anafamilia yake, na kwamba alitaka kunirubuni tu!” alijitetea mke wa Richard ya wifi yake Jackline, ambae akuna alie msikiliza na kuona bola akimbilie kwa wifi yake, ili akaombe msaada wa kuombewa msamaha, huko nako kiukweli ata Michael akuweza kumshawishi, mke wake kutoa msamaha kwa wifi yake huyo, ambae alipoona kuwa amegonga mwamba, akaondoka zake na kutokomea tisiko kujuwa.


Na week moja baadae Jackline akiwa ofisini kwake, akajiwa na polisi, ambao walieleza kuwa kuna mtu ameokotwa, amkiwa katika hali mbaya, ya kiafya, majeruhi mwili mzima, ikionekana wazi kuwa amefanyiwa michezo ya ajabu na watu wanao hisiwa kuwa, ni wakukodishwa mala baada ya kumfumania, na mume wamtu, na alipopata fahamu na uwezo wa kuongea, polisi waliitaji kujuwa ndugu zake, “akasema kuwa wewe ndie mtu pekee unaweza kutoa msaada, kwasasa yupo hospital ya mkoa, tunaitaji kwenda kukukabidhi, mgonjwa wako” alisema askari polisi alie onekana kuwa ndie mkubwa wao, kusikia hivyo Jackline aliinuka haraka, na kuingia kwenye gari la kazini, yani la kampuni yake, na kuongozana na polisi mpaka pale hospital, ambako alionyeshwa mgonjwa, mwanzo akumtambua kutokana na bandage alizo pandikwa usoni, kuficha majeraha, “mh! mbona hii sura ningeni, eti dada unanifahamu?” aliuliza Jackline, huku akijaribu kumtazama vizuri mgonjwa pale kitandani, “wifi ume nisahau, mimi mama John” alisema yule mwanamke, alie kuwa amelala kitandani, “mh! mama John, umanaanisha mke wa God?” aliuliza Jackline, kwa sauti ya mshangao, “ndiyo mimi, wifi nime vamiwa na watu wananisingizia kuwa ninatembea na mume wamtu” alisema mama John, mke wa Godfrey yani kaka yake Jackline, “sasa kwanini unasema kuwa mimi ndie mtu wa pekee, ninae weza kukusaidia baada ya kumtaja mume wako?” aliuliza Jackline ambae sasa nikama alianza kupandwa na hasira, “wifi naomba unisaidie niligombana na baba John, hivyo naitiaji kuongea nae kishapona”alisema mama John kwa sauti inayo tia huruma, “kwa hiyo unaitaji msaada kwangu, unakumbuka kauri uliyo niambia mala ya mwisho nilipoutana na wewe?” aliuliza mama Eric, ambae kiukweli akuwa na utani ata chembe usoni kwake, “jamani wifi, yale yalisha pita, nisaidie mwenzio nipo kwenye matatizo” alisema mama John kwa sauti iliyotia huruma, hapo Jackline akamgeukia, kuu wapolisi alie ingia nae mle ndani, wakiwa pamoja na mkurugenzi wa ile hospital, “jamani huyu dada mimi siyo mtu wake wakaribu, naomba muulize vizuri pengine anaweza kuwa tajia mtu wake wakaribu” alisema Jackline ambae aliaga na kuondoka zake, “we manamke kama una mume siutuambie anapatikana wapi tuka mwite aje kukusaidia” alisema mkuu wapolisi, kwa sauti iliyoanza kuonyesha hasira, “baba yangu, kama huyu mwenye huruma kuliko wote kwenye familia yao ame nikataa sizani kama kuna mwingine anaweza kunionea huruma, naomba mnisaidie nipate nafuu, kisha niondoke” alisema mama John, ambae siyo tu kushangazwa na jinsi Jackline alivyo pendeza na kuonekana wazi kuwa katika Maisha mazuri, pia alishangazwa na jinsi polisi walivyo mzungumzia kuwa ni mmoja kati ya waschana walio olewa na matajiri, “we dada ulimfanya nini huyu mwanamke, anauwezo mkubwa wakifedha si angekusaidia katika aya matatizo, au liachana na mumeo ukafwata mwanaume mwingine?” aliuliza yule polisi, ambae alipoona mama Johna ameshindwa kujibu, akamwachia maamuzi yule mkurugenzi, ambae alisema kuwa watamsaidia apate nafuu kisha wange mwacha aondoke.


Naam ata taarifa ilipomfikia God mwenyewe mambo yalikuwa ni hay ohayo, akuweza tena kurudiana na mwanamke huyu, hivyo ndio ukawa mwisho wa kutanga tanga kwa mama John, ambae alishindwa kumshahuri mume wake namna ya kuishi na ndugu, na ata mambo yalivyo wa haribikia, yeye akaona jibu ni kusaka wanaume.


Kwa kifupi kila mmoja alivuna alicho kipanda, japo kuna msahama, lakini kumsamehe asie juta wala kulijuwa kosa ni, sawa na kazi bule, asante sana kwa kufwatilia makasa huu, ambao nusu yake ni hadithi ya kweli, simulizi hii iwe kumbuku mbuku, kwa kaka Michael Haule, (siyo Michael Eric) pumzika kwa amani, na wegine wote walio tajwa humu, kama wazima, basi waishi Maisha marefu, na waliotangulia, basi wapumzike kwa amani, jiandae kwa mkasa mwingine wenye kiwango kidogo cha ukweli ndani yake, na majina ya ubunifu






MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog