IMEANDIKWA NA: RAMAH JUNIOR
**************************************
Chombezo : Mke Changudoa
Sehemu Ya : Kwanza (1)
''
"kaka vipi?"....... "poaw mzima wewe?"....... "mimi mzima za siku?"........ "njema kabisa"..... "karibu sana muda mrefu sana hatujaonana kaka"...... "aiseii we acha tu"....... "ngoja tuite tax twende nyumbani"...... "sawa kaka"...... "tax tax njoo" aliita tax wakapakia wakaondoka, wakiwa njiani maongezi yaliendela, "hassan kwahiyo umeoa kaka" huku wakicheka, "ndio nimeoa"...... "kwa yale yaliyokukuta nilijua huwezi kuoa tena?"..... "ni kweli nilipanga hivyo nisio kabisa lakini nilipata mtu sahihi wakati sahihi nimeoa"...... "natamani kumuona shemeji sijui anafanania vipi?"...... "hahahaa acha zako bwana juma"...... "kweli hassani"..... "umeacha ukorifi lakini"....... "sasa mimi nikiacha ukorofi wewe utatetewa na nani?"....... "daaah kweli aisey, ulikuwa unanitetea sana enzi zile"...... "ulizidi upore rafiki yangu." wakacheka, walikuwa ni marafiki wawili jumana hasan, hasan akasema "dereva, ingia hapo kushoto tumeshafika" walifika nyumbani kwa hassan, walimlipa dereva wa tax kisha wakaingia ndani.
Walibisha hodi, wakajakufunguliwa na binti wa makamo, "asalam alyekum, karibuni" binti yule ambaye alikuwa anaonekana kujistiri vizur alisalimia na kuwapokea mizigo na kuingiza ndani. "karibu sana rafiki yangu hapa ndio nyumbani"...... "ahsante sana hasani" wakiwa wanaongea akaja mtoto mwenye miaka kama mitatu hivi, "asalam alyekum" alisamilia, japo aliitamka kwa shida hiyo salamu ila ikielewek vizur, kisha akasogea mpaka kwa hasan, "njoo hapa binti yangua" hasan akasema, "juma huyu ni binti yangu, anaitwa, sarha" juma akasema "duuuh bro kweli siku nyingi mpaka mtoto amefika hapa. Hongera sana lakini" hasan akamwambia binti yake "nenda kamuite mama, mwambia baba amekuja na mgeni" sarha akaenda kumuta mama yake.
"maji au juice?" hasan alimuuliza juma, juma akasema "naomba maji" hasani akamtolea maji kwenye friji na akachukua grass kisha akampatia juma, "karibu kaka"...... "ahsante sana, kaka umejitahidi sana, nyumbq yako nzuri halafu umepata sehemu nzuri huku hakuna umbea kabisa"....... "yes huku hakuna umbea, japo mimi sikuwa nakupenda ila mke wangu ndio alichagua huku" wakiwa wanaongea, sarha akaja "baba mama aswali" hasan akangalia saa akaona ni saa kumi na robo, "aaah kweli muda wa swala huu?" juma akasema "kaka hongera umepata mke anaswali swala tano?"...... "twende basi tukaswli na sisi?"...... "sawa" waliamka na kwenda kuswali. Baada ya nusu saa walirudi kutoka msikitini na kuingia ndani, walipoingia walimkuta mke wa hasani amekaa siting room anawasubiri, "asalam alyekum" alisalimia, hasana na juma waliitikia, hasan akambusu mke wake, juma akasema, "huyu ndio mkeo?".... "ndio?"....... "unamfahamu?"
"hapana ila nimeshangaa kuona umapata mke mzuri, pia anaoneka mpole na mwenye tabia njema"...... "ooooh sawa vizur. Mke wangu huyu ndio juma, ni rafiki yangu toka utotoni ila yeye alikimbia nchi na kwenda kwenye nchi za watu"...... "nafurahi kukufahamu shemeji karibu sana"....... "ahsante sana"..... "karibuni mezani nimewaandalia chakula" juma na hasan walisogea mezani wakaanza kula. Mkenwa hasan akaondoka na kuelekea zake chumbani, wakabaki juma na hasan "bro umepata bonge la toto yaani pale kavaa dela, sijui akivaa jeanz au kimini"...... "jumaa bhana yaani bado unawaza ushetani ushetani tu"...... "hapana ila najaribu kuvuta picha tu"....... "acha ujinga"...... "ila tuache utani rafiki yangu, kupata mwanamke mzuri kama huyu wako, halafu akakubali kukaa ndani, tena sio ndani tu akawa anafanya ibada na hataki anasa, ni agharabu sana sana tena"...... "ni kweli rafiki yangu ila kika kitu kinawezekana endapo nia ya dhati ikiwepo"..... "jinsi akivyomzuri hivi, yaani ikifika weekend utasikia baby twende club, au twende band"..... "nashukuru toka nimemuoa mke wangu hajawahi kuniambia hizi habari, japo kuna siku huwa naamua kumtoa, nampeleka sehemu tunakula tunakunywa tunaenjoy maisha, tukirudi amefurahi"
"sarha tulia nikusuke mama" mke wa hasan alikuwa yupo na mwanae akimsuka, pembeni kulikuwa na binti mwengine, "dada kwani ili uolewe inabidi uweje?"...... "ana kwanini unasema hivyo mdogo wangu?"...... "nafurahia sana maisha mnayoishi na shemeji natamani na mimi kuolewa, na mume anipende kama nyinyi mlivyo"...... "mdogo wangu ndoa zinamapito mengi sana, hivyo usione tu picha ya nje, ukiingia ndani utachoka, ila mimi nashukuru sina magumu kwenye ndoa yangu. Ila omba sana mungu jitahidi kufanya ibada, maana mungu ndio hupanga na kuaamua, hivyo muombe akupe mume bora"..... "sawa dada nashukuru kwa ushauri, maana mimi nilikuwa najia ndoa ni vita ila kwenu ndio nimejua ndoa ni furaha"...... "kwanini"..... "mmmmh dada wewe acha tu"...... "kuna nini kwani ana hebu nambie"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment