Search This Blog

Wednesday, 15 March 2023

MKE CHANGUDOA - 5

  


Chombezo : Mke Changudoa

Sehemu Ya : Tano (5)



Jennifer akanyamaza kidogo kisha akaendelea kusema, "baada ya kufungua mlango kwa nguvu na kuingia ndani, akaniangalia kisha akasema, kwahiyo wewe utanifanya nini? Nimeshamnunulia amua sasa cha kufanya, na naweza kufanya ninachotaka kama hutaki ondokeni hapa kwani mimi nina shida na nyinyi? Mama alinyamaza kimya, hakuongea neno, baba akaniangalia mimi kisha akasema na wewe, unajifanya unamdomo mdomo sana nitakuonyesha uwanaume wangu, kisha akaondoka zake. Nikamuuliza mama yangu, kwana baba yangu yu wapi ni bora niende kwa baba yangu, alichonijibu mama kikinifanya kuzidisha chuki na wanaume nilizidi kuona kuwa hakuna faida ya kuolewa, kutokana na aliyopitia mama yangu?"......"mama yako alikwambia nini?"


"sitaki kulikumbuka jibu la mama kwani mpaka leo naona kama ni mateso makubwa ndani ya moyo wangu, japo siwezi kulisahau, siwezi kulifuta kamwe! Mama yangu alisema, yeye alikuwa ni binti mrembo sana kijijini kwao, na hakuna mtu ambaye aliacha kumsifia, hivyo kutokana na uzuri wake wengi walivutiwa naye na kutaka hata kumuoa, lakini alikuja mjomba wake ambaye yeye anaishi huku dar sijui kama ni mzima mpaka sasa au laah, hivyo mama alichukuliwa na mjomba wake akaja dar, maisha ya dar yalizidi kumbadilisha mama na kuonekana mrembo zaidi, jambo pekee ambalo mama alinisisitizia kipindi chote hicho alikuwa ni mwari hajawahi kukutana na mwanaume yoyote yule, aliendelea kujitunza sana, mjomba ake mama akamtafutia mama kazi ya kibanda cha simu akawa anapigisha simu, enzi hizo simu za mkononi hqzikuenea watu walikuwa wanatumia simu ya mezani. Mama alifanya kazi pale kwa muda, mjomba wake mama akaanza tamaa za kumtaka mama, alianza kumshawishi kila mala alale naye lakini mama alikata. Hali hiyo ikampelekea mama kuogopa kurudi nyimbani mapema maana alikuwa anajua akiwahi kurudi atasumbuliwa na mjomba wake, hivyo alikuwa akichelewa kufunga ama akiwahi kufunga basi harudi nyumbani anatafuta sehemu anakaa kisha ndio anarudi nyumbani. Alichosahau mama ni kuwa alikuwa akimkimbia adui mmoja na kiwakaribisha kundi la maadui, laiti angelijua ni bora angekuwa tu anarudi nyumbani mapema, ila hakuweza kujua, kutokana akili yake ilikuwa ikiwaza kusumbuliwa na mjomba wake tu"


Jennifer akaomba maji, anifar akaamka na kumchukulia maji kwenye friji, kisha akamuwekea kwenye glass na kumpa anywe, jennifer alikunywa funda moja la maji kisha akaweka glass chini na kuendelea kusema, huku akilazimisha tabasamu, "mama yangu alipenda kunywa maji kama hivi hakika naendelea kumkumbuka sana, mungu ailaze roho yake mahala pema peponi." waliitikia "amiin" kisha juma akauliza "nini kiliendelea wakati mama yupo kwa mjomba?" jennifer akajibu, "mama aliendelea kurudi usiku, hapo ndio siku moja wahuni wakamlia rada, wakamgoja kwenye kichochoro wakambaka, walikuwa wanne wote walimuingilia, ukumbuke alikuwa ni bikra, hivyo maumivu yake hayaelezeki yalikuwa makubwa sana tena zaidi ya neno lenyewe. Mama aliahindwa kusimama, nguvu zilimuisha hatimaye akapoteza fahamu kabisa, alikuja kustuka yupo hospital, amewekea drip. Nesi alipokuja akamuuliza nani amempeleka pale akaambiwa ni raia wema tu, hivyo mama ilimlazimu aombe simu ampigie mjomba wake.


Mjomba wake alifika alipofika akamuuliza nini kimetokea, mjomba hakuonekana kukasilika, alilipa bill zote pale hospita na baada ya masaa kadh aliruhusiwa kurudi nyumban, lakini alipofika nyumban hali ikawa tofaut, mjomba wake akanza kumtukana mama na kumzihaki kwamba alikula pesa ya mwanaume halafu akaamka ndio maana wamembaka kumbe wala haikuwa hivyo. Mama aliendelea kujiuguza mpka alopokuwa sawa, aliporudi alipokuwa anafanyia kazi, pamewekwa mtu mwengine. Hivyo akawa amekosa kazi, akawa yupo nyumbani tu. Hiyo ilikuwa fursa kwa mjomba wake kuona ndio wakati wa kuzidisha usumbufu kwa mama, lakini mama alikataa, mama aliendelea kukataa huku akisema anaumwa, aliendelea kusema hivyo kwa muda. Mpaka pale mjomba ake alipoamua kumpeleka hospital na kupimwa, majibu yalibadilisha kabisa direction ya maisha ya mama, kwani alikutwa ni mjamzito, hapo ndipo mjomba wake akaamua kumtimua mama na kurudi kijijini, kijijini nako wazazi wake wakamtimu kwa kumuita malaya. Maisha yakaanza kuwa magumu, hakuwa anajua anaenda wapi?"


"baada ya hapo nini kilifwatia?" jumaa aliuliza, jennifer akasema, "akawa mtu wa kutanga tanga, akawa hana sehemu maalum, miezi tisa ikawa kama miaka, lakini hatimaye mungu akamsaidia akajifungua salama, ndipo nikazaliwa mimi. Mtoto ambaye baba yake hajilikani?" Jennifer akaanza kulia, kwa uchungu sana, huku akisema, "wanaume watu wabaya sana yaani mnahalibu maisha ya mabinti wengi sana, mnaua ndoto zao, mnaivunja mioyo yao, na hamna huruma mimi sijawaji penda na sijui kama naweza kupenda tena, moyo wangu unachiki dhidi yenu yaani nawachukia sana, ndio maana nikipata nafasi ya kuwaumiza nafanya hivyo sina huruma kabisa." annifer akasema,"nyamaza kipenzi usilie, ni kweli kwamba samaki mmoja akioza ni wote ila, kumbuka wanasema ni wote kutokana na ile harufu inayotoka kwenye tenga la samaki, lakini ukimchukua huyo mmoja aliyeoza, ukamtupa wale wengine watabaki wazuri kwa ajili ya matumizi, ni kweli uchafu wa baadhi ya wanaume unachafua hadhi ya wale wanaume wanaojitambua. Jennifer kipenz hiyo chuki naomba ipunguze sawa mama?" Jennifer akamwangalia annifer kisha akasema,"annifer wewe hujui tu, hujui nini kimenikuta unajua kama nimempoteza mama yangu hivi unajua?"........ "nini kimetokea kwani, hebu tueleze" machozi yaliifuta makeup yote ya Jennifer, yaliufunika uzuri wake na kuijaza huzuni sura yake, annifer alijitahidi kjmbembeleza Jennifer ili aweze kunyamaza, "punguza kulia basi kipenzi, nyamaza"


"mpenzi wangu, naomba nyamaza nipo hapa kwa ajili yako, pleas usijari nitahakikisha unakuwa na furaha, acha kulia" juma aliongea hayo, Jennifer akasema, "nakosa imani na wanaume sina kabisa sina, kama mtu aliyenilia alivunja moyo wangu vipi wewe juma utaweza?" Jennifer akaendelea kwa kusema, "unajua mnaona ni rahisi lakini sio rahisi hivyo?"...... "hebu tuambie ni nini kimetokea kwani" jennifer akafuta machozi kisha akasema, "mama baada ya kunizaa mimi alitafuta kibarua akawa anafanya kazi maisha yakawa yanaenda, ndipo akakutana na baba ambaye ndio mlezi wangu, wakakubaliana na kuanza kuishi wote mama anadai mwanzoni alikuwa ni mtu mwema lakini baadaye akabadilika akawa kama shetani akawa anampiga mama, anamwingilia kinyume na maumbile basi yaani ilikuwa vurugu vurugu. Mama alivyomaliza kunisimulia akasema, hakikisha maisha yako yana kuwa siotegemezi kwa wanaume maana sio wakuwaamini, hiyo ndio ilikuwa siku ya mwisho mimi kuongea na mama, ndio siku ambayo niliiyona sura yake na tabasamu lake. "........." kwani nini kilitokea baada ya hapo?"


"siku iliyofwata asubuhi na mapema mama akiamka na kuelekea sokoni, hakuniamsha maana alishaambiwa na baba asiende na mimi sokoni, hivyo mimi nikawa nipo nyumbani, nilikuwa chumban kwangu nimelala, mala nikastuka baada ya kuhisi kuna mtu ameingia chumbani kwangu, nilipofungua macho nilimuona baba akiwa ananiangalia, alipoona nimiamka akasema, usiogope, hapo akanisogelea na kunishika nikasogea pembeni, akanambia usiogope, kisha akanisogelea tena, na kuniambia nataka nikufundishe mchezo mzuri na mtamu, nikamwambia sitaki kufundishwa mchezo wowote, alipoona sitaki akanifwata na kunishika, akanifunua night dress yangu akaichana chupi yangu, akaniminya na na na?" Jennifer alishindwa kumalizia akawa analia, hassan akasema," alikubaka????"



"ndio alifanya hivyo, ila alipoingiza tu, mama alikuwa amefika, na sijui alijuwa amesahau nini? Moja kwa moja aliingia chumbani kwangu akamkuta baba ndio yupo kwenye halakati hizo, mama alichukua kiti akampiga nacho baba, baba akageuka naye bila huruma akachukua kiti kile kile akampiga nacho mama, mama akaanguka chini, siuweza kuvumilia, pembeni yangu kulikuwa na kipande cha nondo nilimpiga baba cha kichwa, alianguka akafa, nikaita majirani, wakaja tukamuwahisha mama hospital lakini hakufika hata hospital akawa amefariki. Tulizika watu wawili, pale tulipokuwa tunaishi walikuwa hawajui mama kwao ni wapi hivyo alizikwa pale, baba naye alizikwa pale kwako ndip kwao. Nilibaki pekee yangu, sikuwa na mtu wa kunisaidia, sikuwa na ujuzi wala sikuwa najua ni wapi napata pesa. Shida kwangu ziliongezeka maisha yakwa magumu sana kwangu, hakuwahi kutokea jirani wala ndugu wa kunipa msaada na hii yote ni kutokana na marehemu baba alivyokuwa akiishi na majira zake, hakuwa anataka ukaribu wala kujihusha na watu, tena mama akienda hata kwenye shughuli ya jirani akirudi basi anapigwa, majiran walikuwa wanaogopa hata kuniongelesha kwa kumuogopa baba, hivyo hiyo hali ilinijengea wakati mgumu, ukizingatia nilikuwa mdogo sikuwa naweza kujitgemea. Siku moja nilikuwa na njaa sana sikula siku iliyopita na nililala na njaa, na siku hiyo kama ingeisha ingekuwa ni siku ya pili, nikiwa sijui nifanye nini akaja msichana mrembo sana akaniuliza habari yako? Nikamjibu mbaya, akaniuliza tena kwanini? Nikamwambia njaa inaniuma leo siku ya pili sijala. Alinichukua na kunipeleka nikale, baada ya hapo nilimsimulia kuhusu mimi, hapo ndio akanichukua na kuja naye mjini alinambia kuwa nisiwaamini wanaume. Na maneno yake yalikuja kutimia, siku ambayo alikufa mkononi mwangu?" Jennifer machozi yalimzuia kuongea maana yaliziba uzuri wake, huzuni ilitawala iliwagusa mpaka waliokuwa wanamsikiliza.


Ukimya ulitawala, kibaridi cha huzini kilitanda mahala pale, Jennifer hakuwa nasehemu kavu kwenye uso wake, mashamvu yake yalikuwa yamejawa na michilizi ya machozi, macho yake yalikuwa ni kama chemchem isiyokauka, juma alitoa kitambaa chake na kumfuta machozi Jennifer, huku mkono wake ukiwa unampapasa kwenye mgongo. "nini kilimkuta mpaka akafa mkononi kwako?" hassan akahoji, Jennifer akasema, "niliyopitia yawezakuwa ni kitabu cha kuwafunza wengine ujasiri, dada yule akawa dada yangu toka siku aliyonikuta na njaa akanichukua nikaja naye mjini alikuwa amepangisha, chumba na sebure, nilishini naye vizur sana takriban miezi sita, nikapa mpenzi ila hatudumu akaniacha nikabaki nalia hovyo, hapo ndio akaniambia usipende wanaume, watakuumiza kila siku penda pesa zao. Nikamwambia nifanyenini? Akasema kuwa kama mimi, ili upate mwili wangu lazima utoe pesa tena sio ndogo. Hapo ndio akaanza kuniingiza kwenye kazi ya uchangudoa. Niliona ni ngumu ila taratibu nikaanza kuzoea."


"Nikaona ni kazi nzuri kwani, siumi moyo wala siteseki, sina muda wa kusema nisipojibu meseji baby atanunua, mimi ilikuwa tunakutana leo tunaishia leo leo, mambo ua kugandana hayakuwepo, kijiwe kikaanza kuchanganya nikapata kwangu nikahama, yule dada yangu aliyenisaidia akanambia amefanya kazi hii kwa muda sasa na amefika hatua anatamani kuolewa. Nilimwambia sawa, lakini unasema wanaume ni waongo je utaolewa na nani? Akanambia labda anaweza kubahatisha, siku zikaenda, siku moja akanambia njoo nikuonyeshe shemeji yako, nikaenda kumuona, alikuwa ni mkaka anapesa, mzuri na alionekana mwenye heshima zake, nilimtakia kila la kheri. Walikuwa wenye furaha, lakini kumbe uwongo na hulka la kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja ni wameumwa navyo wanaume, siku moja nikiwa na dada yangu, alikuja mama wa makamo akatusalimia kisha akasema, kati yenu nani sasha? Dada akasema mimi, yule maka akaniuliza na wewe unaitwa nani? Nikajibu naitwa Jennifer, akasema hili liwefundisho kwako Jennifer achana na wanaume za watu usijaribu kuwa na mume wa mtu, tafuta wako, mtengeneze na mtunze, baada ya hapo yule mama alitoa bastora na kumpiganayo sasha ya kichwa, dada yangu aliyenileta mjini naye akaanguka chini, nikamshika akakata roho akiwa kwenye mikono yangu, inauma sana, ni ngumu kuwaamini wanaume siwezi ni bora uniache jumaa?"


Jennifer aliamka na kutaka kuondoka, annifer akamzuia akamwambia,"hapa huondoki, hakuna kwenda sehemu nyengine, kama hutaki kuolewa ni vyema ukabaki hapa, umepitia magumu mengi, umepitia uchafu mwingi basi inatosha, kaa na mimi hapa, utavaa nguo zangu, utakula chakula changu, utalala ndani kwangu, mimi nina ofisi ndogo, tutaenda wote kutafuta ridhiki, achana na hiyo kazi, huna mama huna baba, huna ndugu, wengi ni marafiki tena sio marafiki wema. Siwezi kuruhusu tena urudi huko, nataka uwe mwema nataka kikao hiki kiwe ni moja ya kutubu kwako, machozi na maneno yako yakawe tiba kwenye moyo wako. Wewe ni rafiki yangu historia zetu zimefanana, wewe ni ndugu yangu, wewe ni mdogo wangu, wewe ni damu yangu baki tuanze safari mpya ya maisha." annifer akaendelea kwa kusema,"tunapaswa kufuta yote ya zamani, tunapaswa kuandika ukurasa mpya, tunatakiwa kurudi kwa mungu, tuanze kufanya ibada, huo moyo mgumu uweze kuondoka, Mungu anaweza kufanya yote amini hilo, mimi haikuwa rahisi ila nimeweza"


Maneno ya annifer yaliingia taratibu kwenye masikio ya Jennifer, yakaanza kupenya kwenye ubongo wake, annifer akaendelea kwa kusema, "Huwezi kuwa mke kama huwezi kuondoa hiyo roho iliyokuvaa, chuki itaendelea kukuumiza miaka yote, na haitakupa faida, hivi jiulize kazi unayoifanya ya kuuza mwili wako huoni kama ni hatari kwa afya yako? Huoni kama wewe huna ndugu, jiulize ukizeheka ni nani atakusaidia na huna mtoto? Mimi nina mtoto wangu huyu wa kike nashukuru ndio rafiki yangu, ndio ndugu yangu naamini kabisa hata kama hatanisaidia sana lakini hata niacha nizalilike. Unapaswa kutafakari, hilo maana umri haurudi nyuma, unazidi kukua unazidi kuupunguza umri wa kuwepo duniani." annifer aliendelea kwa kusema,"njoo huku twende" annifer alimshika mkono Jennifer na kumpeleka kwenye moja ya chumba ambacho hakikuwa na mtu, "jennifar hiki chumba hakina mtu, nyumba yangu ina vyumba vinne, wewe utalala hapa, hiki ndio chumba chako, hapa ndio utaishi." annifer alimaliza kwa kusema, "nakupenda kwa ajili ya Allah"


Maneno hayo yalimfanya Jennifer atokwe na machozi na kisha kumkumbatia annifer, kisha akasema "annifer umekuwa rafiki mwema, umeongea maneno ambayo sikutarajia kuyasikia, nashukuru sana, nipo tayari kuishi hapa, lakini mimi sijui chochote kuhusu dini, sijawahi batizwa wala sijapewa kipaimara, sijaenda madrasa wala sijaenda msikitini, sijui chochote." annifer akasema,"utachagua kama uwe mwislamu kama mimi au mkristo, kama utakuwa muislamu basi nitakuelekeza kila kitu na utajua maana hata mimi nilikuwa kama wewe, sikuwa na dini, sikuwa na elewa uwislamu wa ukristo, nikachagua uwislamu mwanzo nilichagua kwasababu ya mume wangu ni mwislamu lakini baadae nikavutiwa na mafundisho yake nikaamua kubaki kwenye dini hii. Sijui wewe utachagua wapi?"......"Na mimi nataka kuwa wewe, niite annifer yaani mimi annifer na wewe annifer maana annifer na Jennifer yanafanana hivyo sitakuwa mbali na jina hilo."...... "sawa karibu sana mimi nitakufundisha kila kitu utakaa na mimi hapa?" mke wa hassan akamsilimisha Jennifer kisha akampleka Jennifer bafuni, akaoga akamtolea nguo akabadilisha kisha wakirudi siting room, hapo mke wa hassan akasema, "jennifar ataishi hapa, na kuanzia sasa ataitwa annifer, ili mututofautshe mimi niiteni mama sarah, annifer sasa ni muislam nitajitahidi ajue kila kitu, swala na vingine" juma na hasan walifurahi sana lakini juma akawa na swali kichani je vipi swala la ndoa amelikubali?


"kwasasa naomba mumuache annifer, mpaka pale akili yake itakapotulia, ili afanye maamuzi sahihi" mama sarah alionge maneno hayo na kuongeza kuwa, "annifer amepitia mengi magumu, ni kama mimi lakini binadamu tunatofautiana kwenye swala zima la kuyabeba matatizo, tunatofautiana kwenye kufanya maamuzi, hivyo hatupaswi kumlazimisha sana tukazidisha kumuathiri akili yake hivyo ni vyema tukamuacha akafikili taratibu" mama sarah alipomaliza kusema hayo, juma akasema, "shemeji nakushukuru sana lakini pia niombe radhi kwa niliyokufanyia huko nyuma, sikuwa najua kuwa wewe ni mwema hivi? Sikuwa najua kuwa unajielewa kiasi hiki? Mwanzo nilikuwa najua changudoa hawezi kuwa mke, niliposikia kuwa ulikuwa ni changuduoa nikataka kukujaribu kumbe nilikuwa na kosea, kumbe huwa wengi hufanya bila kupenda, ni kutokana na maisha jinsi yalivyo, huwa wamekutana na mengi. Naombeni sana radhi. Sasa nimejua kuwa hisia zinaweza mpenda yoyote kwani nilipojua kuwa wewe ulikuwa changudoa nikajiuliza bro wangu hassan amefwata nini kwako? Nikawa sijui kuwa mapenzi ni kitu cha siri, lakini pia hisia huweza kwenda pahala popote na bila kizuizi. Naombeni sana radhi sasa nimejua kuwa kila mtu anathamani yake, hivyo tunapaswa kuheshimiana kwani hujui mtu huyo atakuwa msaada wapi?"


Juma aliendela kusema,"Nimeamini sasa ukimuona mtu amempenda mtu mwengine usihoji maana kuna siri ndani ya moyo wake, kuna mengi yamefichika. Nisameheni wote nimejifunza" hassa aksaema, "uliwahi mtongoza mke wangu?"...... "niseme wazi nilijaribu kumshawishi japo sikumwambia nampenda ila nilijaribu kumshawishi, nilifanya hivyo, nisamehe sana kaka" mama sarah akasema, "mume wangu kuna siku niliwahi kukwambia angalia kuhusu marafiki zako sijui unakumbuka?" hassana akajibu "ndio nakumbuka mke wangu"...... "basi nilikuwa namaanisha hivyo nilikuwa sitaki kuwa wazi maana kama ningesema mngegombana na sitaki kuamini kama ungempa nafasi ajielezee, ila leo amejielezea mwenyewe, tena amejielezea kwa kirefu sana na sio kama ipo haja ya kumuwekea kifundo moyoni, inapaswa kumsamehe na marafiki na maisha yaendelee"...... "nimekuelewa mke wangu, maana hata Mtume wa Allah ametufundisha kuhusu kusamehe amesema tusamehe palo tunapoombwa msamaha lakini pia tunapswa kuwasamehe hata wale ambao hawajaomba msamaha. Ili nasi tunapoomba msamaha kwa Allha tusamehewe."........ "shemeji mimi nimekusamehe sina kinyongo na wewe." juma akasema "ahsante shemeji nashukuru sana" hassan naye akasema, "juma tumepitia vingi mimi na wewe, tumekoseana mala nyingi sana kuna makosa ambayo labda saa hizi tusingekuwa wote hapa lakini tuliyamaliza."


Hassan akaendelea kusema, "mimi niseme tu wewe ni bindamu na binadamu ni wazaifu tumeumbiwa kukosea, hivyo sina budi kukusamehe. Wewe ni ndugu yangu hivyo sina kinyongo na wewe nimekusame ondoa shaka juu ya hilo." juma akasema, "nawashukuru sana kwa kunisamehe, hakika wewe ni ndugu yangu, nawashukuru sana, niseme ahsante kwa yote umekuwa ndugu mwema kwangu ukiniongoza kwenye mengi ukinisaidia vingi. Naomba Mungu atujaaliye tuwendelee kuwa hivi, atupe afya njema na baraka tele." wakiwa wanaongea simu ya annifer ikaita, wote wakawa wanamuangalia annifer, annifer hakupokea simu, simu ilipokata akaizima akatoa laini na kuivunja vipande vipande, hassan akauliza,"mbona unavunja laini?"


Walisubili jibu kutoka kwa annifer, lakini hakulitoa. Mama sarah akasema "huwezi kubadilika kama bado unamarafiki wa zamani ambao wanatabia zile zile, hata nami nilibadilisha laini na sikutaka watu wajue naishi wapi, hivyo annifer yupo sawa" baada ya maongezi ya muda mrefu juma na hassan waliaga na kuondoka zao kwenda mjini. Annifer na mama sarah walianza kufundishana mambo kadha ambayo ni muhimu muhimu, "ulijifunza wapi hivi vyote?" annifer alihoji, mama sarah akasema, "vingi amenifundisha mume wangu japo pia kwa sasa nahudhulia darasa la kina mama pale msikitini hivyo naendelea kujifunza vingi"....... "na mimi naweza kwenda kwenye darasa au siruhusiwi"...... "kwanini usiruhusiwe? Unaruhusiwa kwenda nitaenda na wewe kesho jioni maana leo hamna darasa"...... "sawa nitafurahi nikijua kama wewe?"...... "utajua tu annifer"...... "mbona nasikia wale vijana wanao uza laini huko nje?"....... "subiri" mama sarah akamuita binti yake wa kazi, alipokuja akamwambia, "nenda kaangalia kama kuna wale vijana wanauza laini, waite watusubiri hapo nje" Nintendo alitoka nje, baada ya dakika tagu alirudi na kusema, "wanawasubiri hapo nje" mama sarah na annifer walitoka nje wakawakuta wale vijana wakasajiliwa laini mpya, annifer akaiweka kwenye simu, na kuanza kutumia laini nyengine.


Upande wa rafiki zake annifer(Jennifer) waka wanapiga simu ya annifer haipatikani, "huyu Jennifer amepatwa na nini? Simu iliita mala moja sasa hivi haipatikani"...... "au amepata danga atakuwa kazini"...... "hapana sio kawaida yake angesha sema huwa anatoa taarifa"..... "kwani alipoondoka alisema anaenda wapi?"...... "alisema anaenda kwa yule mwanaume ambaye anataka kumuoa"....... "mmmmmh nina wasi wasi sana"....... "ngoja tuone kama asipopatikana mpaka kesho utabidi twende polisi na tuanze kumtafuta maana nijuavyo mimi hana ndugu yule"....... "Ni kweli halafu yule mwenyewe ndio boss wetu hapa, maana sisi wote tunaweza kosa soka ila sio yule"...... "watu wanazaliwa na bahati zao bibi wewe" walicheka kwa sauti na kisha wakasema "weeeeweeeeee" muda ulizidi kusogea hatimaye giza likaingia. Jamani tujiandaeni twendeni kazini. Marafiki wa annifer wakajianda na kwenda kutega mingo. Walienda kufanya biashara ya kuza miili. Upande wa annifer na mama sarah walikuwa wakianda chakula, mala walikuja juma na hassan, wakasalimiana na kisha waliketi na kuanza kula chakula kwa pamoja, "annifer anakichwa chepesi sana anashika halaka ukimwelekeza mashaAllah"...... "mashaAllah, ni jambo jema Mungu azidi kumsimamia inshaAllah" wakaitikia wote InshaAllah. Wakiwa wanakula na kimya kimetawala, sarah akasema, "Mama na wewe utava suruali kama ile ya mamdogo mchana?" waliangaliana kisha mama sarah akasema, "ile suruali sio ya mamdogo, ile suruali ni baba ile, mama yako mdogo ameibiwa nguo zote ndio maana akava kwanza ile, ndio maana umeona sasa hivi amevaa nguo hizo" sarah aksema, "masikini, pole mamdogo basi nikupe na mimi baibui langu uvae, waizi watu wabaya, tuishi wote hapa usiende tena huko hapa hawatakuibia sawa mamdogo" annifer alitamani kulia macho yake yalianza kabisa kujaa machozi na huzuni, annifer akasema, "nitaishi na wewe hapa sawa sarah, siondoki"..... "safi sana, nitakuwa rafiki yako, kama vile mimi na mama, huwa tunasoma hadithi mimi na mama, na wewe utasoma na sisi haditi tukimaliza kula sawa" sarah alikuwa ni binti mdogo sana lakini maneno yake yalimfariji annifer, na kuona kuwa yupo kwenye mikono salama.


Alfajiri mama sarah akamuamsha annifer ili waswali, akamuelekez kwa vitendo baadhi ya vitu kish wakaswali, walipomaliza wakaweka darasa wakaanza kuelekezana vitu mbali mbli vya dini. Kulipambazuka na jua likaanza kuchomoza wakaanza kufanya shughuli za nyumbani kisha annifer akasema, "nahitaji kwenda kule nilipokuwa nataka kwenda kuwaaga, pia nichukue baadhi ya vitu vyangu, lakini pia nataka wasije nitafuta, maana najua watakuwa na wasi wasi wasije enda polisi bure"...... "ok sawa usijari tutamwambia baba sarah twende" walijianda na kiisha hasana, juma, annifer na mama sarah wakaondoka kuelekea kule alikokua anakaa annifer. Safari ya masa mawili wakawa wamefika, walipofika annifer alibisha hodi, na kuingia ndani, "khaaaaa wewe ndio wakuvaa baibui?"


Wote wanne walishanga kumuona annifer vile, "haya Jennifer umekutwa na mangapi shoga angu?" annifer hakuwajibi akaingia chumbani akavuta begi lake akachukua vitu vyake vya muhimu vyote kisha akatoka, "mbona na mabege tena vipi mbona hivyo?" annifer akawaza majibu ya haraka haraka akaona akisema ukweli itakuwa shida maswali yatakuwa mengi, akaona bora adanganye, "acheni niwahi nina msara hivyo sitaki muingie kwenye huu msara, akija mtu yoyote kuniulizia mwambie hamnijui wala hamjui nilipo, sawa?" annifer akatoka mbio mbio akaondoka zake, aliwaacha wenzie na maswali kibao.


"itakuwa amefanyaje?"...... "sasa unamuuliza nani wote tupo humu ndani tutajuaje?"....... "au kaiba?"..... "yule muwoga sana hawezi kufanya hivyo?"....... "mmmmh sasa sijui kafanya nini?" ukimya ukatawala, mmoja akasema, "nahisi inawezekana yule jamaa anayesema anataka kumuoa labda wamekubaliana sasa anatafuta njianya kutukimbia"....... "hiyo sio kweli, hivi unamjua Jennifer wewe?"........ "kwahiyo unahisi sio hivyo?"...... "ndio itakuwa kitu chengine, Jennifer anawachukia wanaume sana ndio maana nakwambia inawezekana kaiba au kamzingia mwanaume sasa kuna kesi ila kupenda hapana nakata"..... "mmmmh ok sawa acha tumpotezee, ngoja tuangalie kwanza asije kubebe na vitu vyetu"....... "hilo neno halafu tumejisahau kabisa" waliingia chumbani wakakagua sehemu zote, "huyu atarudi umeona nguo zake nyingi anazozipenda kaziacha kabeba chache sana"...... "kabeba tu perfume, mafuta cheni, heleni, na nguo kidogo"...... "basi huyu atarudi anasikilizia upepo tu"...... "tuachane naye tuendelee na mishe zetu" waliendelea na mambo yao bila kuwa wanaujua ukweli kuhusu Jennifer ambaye sasa anaitwa annifer. Upande wa Annifer aliingia kwenye gari na kuwaambia hasan na jumaa, "twendeni sina ambacho nimbacho kina niweka eneo hili tena, naenda kuanza maisha mapya" hasan na juma waliangalia, juma akawasha gari wakaondoka zao. Wakiwa njiani hassan akasema "tupitie mjini tumnunulie annifer nguo maana anaswali hivyo anahitaji nguo za kuswali maana naamini nguo zake za zamani nyingi sio nzuri" walikubaliana na kuelekea mjini kumnunulia nguo annifer.


Walifanya shopping na kisha kurejea nyumbani. "Ahsanteni sana nashukuru kwa upendo na wema mnaoendelea kunionyesha mungu awabariki sana" hassn akasema, "usijari kuwa huru, hapa ni kwako". Maisha yaliendelea, mama sarah aliendelea kumfundisha annifer mafundisho ya dini na mengine mengi, pia alianza kwenda naye kwenye madarasa ya jioni ya kina mama msikitini, mama sarah hakuishia hapo akaanza kumfundisha kazi mbali mbali, alikuwa akienda naye kwenye saloon yake, alikuwa akienda naye kwenye duka lake la miamala ya kifedha kwa njia ya simu, walianza kuwa marafiki wazuri walishibana kwenye mambo mema, "mama sarah, muda wa swala huu nenda kaweke udhu tuswali acha kuchezea simu" annifer ilikuwa anamkumbusha mama sarah muda wa ibada. Hapa ndio lile neno la kusema, shetani pia anaweza kuwa malaika, ndio linatimia. Kwani kila mmoja ananafasi ya kuwa mtu mwema. Siku moja annifer akiwa anatoka nyumbani anaenda ofisi kwa mama sarah, akiwa njia ilisimama gari nzuri sana na ya gharama, "habari yako mrembo" annifer akageuka kuangalia ni nani anamsalimia, alipomuona alitaka kuondoka lakini akakumbuka, kuwa muungwana hakatai salamu, aliitikia salamu, kisha akataka kuondoka, yule mzeee wa makamo ambaye alikuwa ndani ya gari akasema, "samahani mrembo naomba dakika moja tu niongee na wewe?"...... "nina halaka sana sijui kama utaweza kuongea upesi niwahi"........ "sawa usijari, mimi sina maongezi marefu sana, kwa kifupi mimi leo sio mala ya kwanza nakuona, ila ni mala ya kwanza kuongea na wewe, kwa kifupi nimevutiwa na wewe, naomba uwe mke wangu, niruhusu nikuoe nimekupenda"....... "hivi umechanganyikiwa au?"....... "hapana nina akili zangu timamu, nakupenda?"


"nimekuelewa, uwe na siku njema" annifer aliondoka akawa amemuacha mzee yule pale akiwa hajui kuwa amekubaliwa au amekataliwa. Annifer alienda kwenye shughuli zake, akafanya kazi mpaka Jioni alipofunga ofisi. Alipofiia nyumbani alimkuta mama sarah, wakasalimia na kisha akaenda bafuni akaoga, alipotoka akamfwata mama sarah, wakaanza kupiga story, "annifer rafiki yangu, nimekaa na wewe huu ni mwezi watatu, nafurahia kuwa na wewe umebadilika na kuwa mtu mwema, nafurahi kukuona ukiwa mtu mpya Mungu akubariki sana kipenzi" mama sarah aliongea hayo, annifer naye akasema, "amiin rafiki, shukrani nyingi zikuendee wewe rafiki yangu, umekuwa na mimi bega kwa bega, nawe Mungu akubariki sana kipenz chagu"..... "amiin"...... "nina kitu nataka kukwambia"...... "niambie tu annifer"..... "Sasa nipo tayari kuishi na mwanaume, nahitaji kuwa na kwangu sasa, nafurahi kuona maisha yenu wewe na shemeji hapa mnavyoishi, ni maisha mazuri yanavutia, naamini ni muda sahihi na mimi kuolewa"...... "waoooow yaani nimefurahi kusikia hivyo, maana jana tu shemeji juma ametoka kunambia jambo hilo hilo?"..... "mbona mimi haniambie au hanitaki tena?"...... "ingekuwa hakupendi angekuwa anakuhudumia kweli? Anakupenda sana ila tulimsihi akuache utulize akili yangu, mpaka pale utakapo amua kwa hiyari yako"..... "sasa nipo tayari"..... "kwahiyo nimwambie?"...... "ndio mwambie, mwambie nipo tayari kuwa mke wake"..... "sawa mpenzi nitamwambia, usiku nitamwambia mume wangu, yeye ataenda kumwambia rafiki yake."..... "sawa nashukuru" maongezi yaliendelea mpaka muda wa chakula ulipofika wakenda kula, kabala hawajamaliza kula hassan aliingia, akasalimia na kisha kuketi na yeye akajiunga na kuaanza kula. Walipomaliza kula. Hassan akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake.


Muda wa kulala ulipofika, mama sarah alimwambia mume wake kwa utulivu na mahaba makubwa, "mume wangu, nina jambo la kheri nataka kukwambia"..... "jambo gani mke wangu?"..... "ni kuhusi aniffer, annifer amesema yupo tayari kuolewa na juma"..... "MashaAllah, Mungu ni mwema, hatimaye sasa ufahamu wake umerudi sasa ni wakati wa kuishi na mume wake kesho panapo majaariwa nitaongea na juma, kisha nitasimamia maandalizi yote ndoa iweze kufungwa halaka iwezekanavyo."..... "sawa mume wangu fanya hivyo" baada ya maongezi hayo wapendao walila. Asubuhi na mapema hassan alimpigia simu juma aweze kuja nyumbani.


Juma alipokuja akakutana na hassan wakazungumza, "annifer yupo tayari sasa kuolewa, ametamka kwa hiyari yake, naomba kukuuliza kaka hutamuumiza binti wa watu? Usije mfanya akarudi kwenye maisha yake ya mwanzo, hakika ukifanya hivyo moto wa jahannam yatakuwa makazi yako"...... "bro nakuahidi nitakuwa mume mwema, nitampenda na kumheshimu."...... "sawa haina shida, inatulazimu tufanye maandalizi ya ndoa"...... "ni kwanini tusifanye kesho kutwa ijumaa?"...... "sawa ngoja tuwaite hawa wanawake" juma alimuita mke wake pamoja na annifer. "annifer nilikuwa naongea na juma hapa na amefurahi sana kuona umekuwa Tayar maana amekusubiri kwa muda mrefu, sasa tumependekeza ndoa iwe kesho kutwa ijumaa hapo msikitini" annifer akasema, "sawa shemeji mimi nipo tayari hata ikiwa sasa". Wote walikuwa na furaha kusikia hivyo.


Maandalizi yalifanyika, ijumaa ilipofika ndoa ilifungwa, Ndoa ilifungwa saa saba mchana, baada ya ndoa, juma na annifer walielekea airport na kwenda zao hanemoon zanzibar. Walifurahia wiki mbili za mwanzo za ndoa yao. Walipomaliza hanemoon walirudi nyumbani na kuendelea na maisha ya kawaida. Annifer na juma wakiishi kwa amani na wana mtoto mmoja. Annifer hajawahi kuacha kufanya ibada hata siku moja, naye juma kwa sasa naye anaswali swala tano kama mke wake.

***********MWISHO*************




0 comments:

Post a Comment

Blog