Chombezo : Mke Changudoa
Sehemu Ya : Nne (4)
Juma yeye ndio alikuwa anatoka lodge amekaa siku tatu na niffer, "niffer kama nilivyokwambia nataka uwe wangu pekee yangu nenda fikilia hilo, naomba kakae chini ulifikilie kwa kirefu sana"..... "mimi ni ndege ila ndege mimi sio kuku wala njiwa mimi ni kunguru, ni ngumu kunifuga sijui ufanye nini, mazoea yameshanijengea tabia tayari hii biashara imekuwa kama tabia yangu, ni ngumu kuacha ni ngumu sana"..... "nenda nyumbani nitakufwata baadaye sawa"...... "ok kwaheri" waliagana na kila mmoja akaenda njia yake, juma alipofika nyumbani alimkuta hasan yupo getini kwake, "kaka vipi umekuja muda mrefu" juma akimuukiza hasan, hasan akajibu, "ndio nipo muda sana hapa, nagonga mlango, napiga simu ila hupatikani"..... "kaka nimekamatika pabaya, vipi lakini".... "poa kaka, umekamatika kivipi?"...... "ngoja nifungue mlango tuingie ndani?" juma alifungua mlango wakaingia ndani na kuketi siting room, akachuku simu yake akaweka chaji. "leo siku ya tatu sijakanyaga humu ndani"....... "ulikuwa wapi juma?"..... "sikuwa mbali sana ila nilikuwa nipo nimejificha na mtoto mmoja hivi mzuri"..... "yaani mimi naumiza kichwa ndugu yangu yupo wapi kumbe wewe unakula raha tu"..... "ndugu yangu nisamehe lakini nimekutana na msichana, utazani under 18 kumbe anaenda kwenye 30, yaani kitu 'mang'anyu' yaani ngoma inanata hivi, nilichanganyikiwa nikatapagawa, nimeshindwa kujizuia nayaka kuoa kabisa"..... "huyo mwanamke unamjua vizur lakin?"...... "mimi simjui nimekutana naye tu baa ila nataka nimuoe"...... "hukuwa na plan za kuoa umepewa nini ndugu yangu?"..... "kaka wewe acha tu yaani sijui nisemeje"..... "kwahiyo unaplan gan?"..... "nataka kuoa hakuna chengine?"...... "hebu nambie huyo msichana umemkuta mazingira gani? Pia umeshamwambia kwamba unataka kumuoa?"...... "ukweli ni kuwa yule ni changudoa, na pia nimemwambia ila amenijibu yeye ni kunguru siwezi mfuga"...... "duuuu pole kaka"...... "pole ya nini"...... "si anakuchomolea huyo demu, halafu wewe ndio ushapenda?"...... "ndio nimependa, ila najishangaa iweje nipende kwa haraka hivi, kwanini nisipate mwanamke anayejiheshimu na kujitunza, ningepata mke kama wako, bro umepata mke yaani nakuambia ukweli?"...... "Ahsante".... "najishangaa sana kumpata mke wa hivi yaani najikuta naweweseka kabisa, nimekuaje lakini?"..... "juma, mapenzi huwa hayabishi hodi wala hayatoi taarifa, lakini pia ubaya kuhusu hisia za mapenzi hazina macho zenyewe ni kipofu, hivyo kuna wakati hukuingiza sehemu ambayo hukuitegemea, hivyo basi kwakuwa ndio hisia zimekupeleka huko, ombi langu kwako, usiache akili, zitumie akili zangu vizuri, fanya kila kitu kwa umakini laa sivyo utakuja juta"....... "sasa nifanyaje na nimeshampenda?"...... "tutatafuta namna ya kufanya ondoa shaka?"....... "utaenda kuongea naye?"...... "nitajaribu kufanya hivyo?"
Upande wa niffer alikuwa yupo na mashosti zake wakipiga story, "basi bwana bwana yule asitangaze ndoa"..... "eeeh ilikuwaje? Umempa nini mtoto wa watu"....... "labda kampa tope"....... "nyie mnajua kama mimi pamoja na uhuni wote ila tope sitoi"....... "sasa ndio utuambie umemfanya nini?"..... "inaonekana hajawahi kutana na wanawake ambao wanajishughulisha kitandani, mimi niliimiliki show, nilimburudisha haswa, nilikotro kila kitu, kuna muda mpaka alitamani kupiga kelele kwa raha" '"hahaha hahaha" walicheka kwa pamoja "yaani nilimpa show".... "na sindio alitaka show" simu ya niffer ikaita "nyamazeni juma anapiga" akapokea "yes haloo"...... "mambo vipi niffer"..... "niko poaw za wewe?"....... "mimi mzima sijui kwako?"...... "fresh nambie"...... "niffer naomba tuonane baadaye nina mazungumzo na wewe pleas usikatae"...... "unajua ulikaa na mimi siku tatu, bado unataka na leo"...... "ila si nimekulipa vizur au?"...... "kwahiyo na hayo maongezi pia utanilipa"..... "nitakulipa ndio wewe njoo"...... "saa ngapi?"...... "jioni saa kumi"..... "sawa nitakujibu"
Juma alikata simu kisha, hasan akamuuliza juma, "eeeh amekubali au amekataa?"..... "hapana hajakataa ila pia hajakunari"...... "amesemaje sasa"...... "amesema atanijibu baadaye, kwahiyo nitamtafuta baadaye"........ "ok sawa haina shida ni jambo zuri"...... "sasa tutamwambia nini ili akubali maana yule ameshazoea kujiuza atakubali kweli?"....... "atakubali usijari bwana"...... "watu hawataniseme kweli?"........ "mbona unawasi wasi sana, inshi maisha yako usifwate watu wanasema nini?"...."sawa bro nipe moyo"....... "sasa acha niende home kwanza maana nilikuwa na wasi wasi sana na wewe, tuonane jioni sawa"....... "sawa haina shida" hassan aliondoka na kurudi nyumbano kwake.
Niffer naye akiwa na rafiki zake waka wanaongea, "shoga limekuganda hilo"......"mwenzangu yaano huyu nwana amenong'ang'ania utazani ruba",,,,,,, "tatizo mnatoa ufundi wote, jnatakiwa unampa maufundi kidogo tu, sasa wewe unampa vyote vya uvunguni huoni kama ni balaa hilo"....... "daaah sasa sijui anamaongezi gani na mimi?"....... "wewe nenda ukifika utajua anakuitia nini?"....... "sawa nitaenda nikamsikilize" mazungumzo baina ya niffer na wenzie yaliendelea. Upande wa hassan alikuwa yupo na mke wake wamekaa chumbani wanaongea na kijadili, "mke wangu jumaa anataka kuoa?"...... "mbona ghafla hivyo?"..... "hata mimi nimeshangaa sijui kimemkuta nini sijui yamemkuta mangapi?"....... "masikini yaani hata siamini kama ndio yeye"....... "mambo yanabadilika mke wangu, ila ni jambo la kher naye akiwa na mke"....... "yeah ni sabin mume wangu"...... "ok tuachane na hayo, vipi naona niwakati sahihi wa kupata mtoto wa pili au unasemaje mke wangu"...... "sawa mume wangu"........ "basi itabidi tuanze kumtafuta tuombe mungu sasa aje dume"....... "hahahaha, likija jike?"...... "basi nitashukuru kwani ni mipango ya mungu siwezi kuipinga"....... "ni kweli mume wangu hata mimi natamani aje wa kiume ila mungu ndio mpangaji"...... "sawa nakupenda mke wangu nakupenda sana kipenzi changu"....... "nakupenda pia mume wangu, wewe ndio mficha aibu zangu, wewe ndio unanipa furaha, ni wewe uliyenitoa kwenye ushetani, nakupenda mpaka kufa laazizi"....... "ahsante mke wangu"....... "kuna wakati najiuliza ni kwanini nisingejuana na wewe mapema, nikaishi maisha haya ya furaha?"........ "kila jambo huwa na wakati wake mke wangu hivyo usiseme sana, mungu pekee ndio hujua, wakati gani ni sahihi"...... "ahsante sana kwa kuniamini, ahsante sana kwa kunipa heshima nashukuru sana sana kipenzi"....... "sawa love ngoja nikaoge kidogo ili nijiandae kutoka kwenda mjini nataka kumpeleka huyu jumaa"......... "sawa mume wangu acha nikakuandalie maji bafuni" mke wa hassan akaenda kumwandalia mume wake maji kisha akatoka na kimwambia mume wake, "tayari nenda kaoge mume wangu" hassan alichukua taulo na kwenda kuoga, alipomaliza alikuta mke wake ameshamwandalia nguo za kuvaa, akavaa na kuondoka.
Hassan na juma walikutana wakawa wanamsubiri niffer, "vipi kwani uliongea naye tena"......"ndio niliongea naye mala mbili akasema atakuja"...... "basi acha tumsubiri subiri"..... "sawa tumsubiri japo nina wasi wasi sana natamani nighairi"...... "kwanini?"..... "unajua yole hana mapenzi ya dhati na mimi, hivyo hata akikubali kuolewa je vipi swala la dini atakubali kweli?"...... "hapo kwenye dini sasa ndio shughuli hapo"...... "kama vipi tuache tu hili swala"..... "hapana usikate tamaa tutafanikiwa wala usijari"...... "yule anakuja sasa utamwambia nini ili akubali?"
"punguza pressure juma" walikaa kimya mpaka niffer alipofika, niffer aliwasalimia kisha akaketi, juma akasema, "karibu sana niffer"..... "ahsante sana"...... "niffer huyu mbele yako anaitwa hassan, yeye ni rafiki ila kwa sasa ni kama ndugu yangu maana tumekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka kumi sasa"...... "nafurahi kukufahamu hassan"..... "nafurahi pia"..... "hassan huyu ndio mrembo anayefanya nakosa raha, huyu ndio niffer aliyeniteka"..... "niffer umempa nini ndugu yangu maana hakuwa na nia ya kuoa kabisa sasa nashangaa ghafla tu anataka kuoa" niffer akajibu kwa kusema, "wala sijampa cha ajabu, ni yeye tu mwenyewe?"..... "sawa sasa niffer, naomba uwe muwazi, maana ndugu yangu amesema anataka kukuoa sasa sijui wewe unasemaje juu ya swala hili? Kwanza umempenda?" niffer alimwangalia juma kisha akasema, "changudoa huwa hapendi, huwa anafanya mapenzi kama biashara nikwambie tu ukweli miki naishi kwa kuuza mwili wangu, unanilipa nakupa utamu"...... "ila unapaswa kuolewa sasa na kuacha hayo mambo, unapaswa kuwa na nyumba yako"...... "nafahamu hasan lakini mimi sijui kama nitaweza kutulia ndani, mimi sina wikiend, siku zote naenda club na bar, ukinikosa forty forty, utanikuta triple seven, au viwanja vingine unadhani nitaweza kweli?"...... "mimi naamini unaweza ukiamua amua sasa"...... "sijui kama naweza"
"niffer wewe ni mwanamke, naamini ndoto za wanawake ni kuwa na familia kuwa na mtoto hivyo ndio mimi najua"...... "hassan sijuwa kama nitaweza sijuwa kiukweli, natamani lakini siwezi yaani naogopa kuja kufanya vitu vya hovyo sitaki kukutia doa"...... "niffer naomba ukae ufikilie hili kwa makini usikae kuangalia watu, hakikisha unaangalia kesho yako"..... "nitafikilia ila sidhani kama naweza, nani aliwahi kujaribu kuacha hii kazi akaweza? Hamna hayupo?"...... "yupo na kuhakikishia yupo, na ameweza kufanya hivyo, kwanini wewe uwogope"...... "siamini labda aje hapa aniambie yeye amewezaje?"....... "naweza kuongea naye kama atakubali kuja kuonana na wewe basi nitakwambia. Leo nipo na nafasi na hii ndio nafasi yenu pia kuhakikisha mnajitahidi kunishawishi juu ya hili"
Juma akasema "bro kama anaweza kuja mwambie aje, anisaidie kwenye hili"...... "kuongea naye sio shida ila inshu ni kuwa hapendi watu waijue historia yake, anachotaka nikuitengeneza kesho yake hivyo ni kama tutakuwa tunamkumbusha machungu na maumivu ambayo yeye anajaribu kuyasahau" niffer akasema, "anaishi wapi twende?"..... "anaishi nyumbani kwangu"....... "basi twende naamini atakubaki kuongea na sisi"....... "naogopa sana niffer ila kwakuwa lengo letu sio baya basi twendeni" walianza safari mpaka nyumbani kwa hassan. Mwendo wa takriban dakika ishirini mpaka kufika nyumbani kwa hassan. Walifika wakashuka kwenye gari na kuingia ndani. Waliingia ndani na hasan kuwakaribisha, walikaa na kisha hasan alimuita mke wake. Alipofika tu siting room, niffer akasema, "khaaa anifah?"...... "kwani unamjua?"
Hassan na juma wote walishanga kuona jennifer na Anifah wanajuana, anifaha alisalimia kisha aliketi, niffer akasema, "ndio maana moyo wangu ulikuwa unanisukuma kuja huku, habari yako za miaka mingi?" anifah akajibu "nzuri tu habari yako"...... "siamini kweli ni wewe?"...... "kwanini huwamini?"....... "naomba nijue umewezaje kuwa mke wa mtu, tena unavaa hivyo, juma anataka kunioa lakini sijui kama nitaweza kukaa ndani sijui"...... "unaweza kila kitu ni kuweka nia na kufanya maamuzi sahihi, acha nikwambie kitu huwezi ishi maisha ya kuruka ruka kama ndege hali yakuwa wewe ni binadamu. Kumbuka huwishi hapa duniani milele, pia unapaswa kuelewa kuwa unachofanya sio sahihi. Mimi naamini kabisa kunasababu imekufanya uwe hivyo ulivyo uwongo kweli?" niffer alifikilia, akiwa anafikilia anifar akasema,"mimi nilikuwa kama wewe, nilifanya kila aina ya starehe ni stly gani siijui, ni burudani gani siijui, ni party gani sijafanya ila maisha ya uhuni na kuruka ruka nimeona haya maana wala faidi yoyote. Mimi kwakifupi niliingia kwenye kazi hiyo kwa sababu, ya maisha magumu lakini pia ninkutokana na chuki ambayo nilikuwa nayo, wakati nikiwa mdogo nilikuwa nikimuona mama yangu anapigwa na baba, anatukanwa na kunyanyaswa sana. Baba hakuwahi kwenda shamba wala hajawahi kufanya jambo zuri zidi ya mama."
"Nakumbukw siku moja mama alinambia, 'nateseka ila ili wanangu mkuwe unaona maisha yangu hayana furaha kabisa, nimekuwa mtu wa huzuni sana'. Nilikuwa nikawa nayaona hayo, lakini hiyo hali haikuwa kwetu tu, bali hata kwenye baadhi ya nyumba pale kijijini kwetu, niliamini labda inawezekana kuna sababu lakini sikuwahi kuijua. Nilianza kukuwa na kuvunja ugo, nikawa msichana sasa. Katika makuzi nikaanza kuwa na mahusiano nikiwa darasa la sita, lakini kijana niliyekuwa naye akawa na mwanamke mwengine. Nikajiuliza hii inasababishwa na nini? Nikaendelea kukua hivyo hivyo nikapa mahusiano mengine, nikapenda mwaname ambaye nilimpenda naye akaja kunitenda nikasema acha nisome kwanza, nikamaliza form four, nilipomaliza mama akasema itabidi uwolewe mwanangu umekuwa sasa, lakini kabla sijaolewa nilipata mwanaume ambaye alionyesha kunipenda sana.
"nisiwe muwongo hapa nilipendwa na kupenda sana, nakumbuka jioni alikuwa anakuja nichukua tunaenda mazoezini wote, wiki ende tunaenda wote kutembea, alinifanya nijisikie vizur muda wote, alinifanya nimpende sana. Alikuwa ni kijana mpole mcheshi na mzuri pia, nilimpa mwili wangu, akafanya anachotaka, nami zikumzuia, alinilazimisha kuniingilia kinyume na maumbile nilikataa sana lakini mwisho alinambia kama nisipokubali basi anatafuta mtu mwengine kwakuwa nampenda ikanilazimu nikubali, aliniahidi atafanya siku moja tu halafu hatutafanya tena, lakini waswahili husema ukishakula nyama ya mtu hutaacha utaendelea nisawa na mtu aliyeonja buyu la asali. Aliendelea kuniingilia nyuma kila tukikutana, nilijua sio jambo zuri lakini kwakuwa mpenzi wangu anafurahi basi acha nimpe atakacho, nilikubali hayo kutokana na hali ya nyumbani kwetu, nyumbani hakukuwa na amani, pia pesa haikuwepo hivyo yeye ndio alikuwa msaada wangu, alikuwa akinipa pesa na kuniliwaza. Pale nilipokuwa na mawazo basi alijitahidi niweze kufurahi. Lakini naukumbuka msemo wa mama alisema wanaume wameumbwa na tamaa hawaridhiki kamwe ndipo maana mungu aliwaruhusu waoe wake wawili mpaka wanne, japo leo hii naamini kwamba kila mtu na hurka yake, wapo wanaume wametulia na kuridhika. Kijana yule alichonifanyia kikaniingiza kwenye unywaji wa pombe, uvutaji sigara na nikawa sipendi tena?"....... "alikufanyia nini?"
Annifer alikuwa analia, machozi yalitoka alishindwa kabisa kujizuia, hassan alisogea karibu ya mke wake na kuanza kumbembeleza, na kumtia moyo ajikaze. Hassan alimfuta machozi mke wake na kumuomba aendelee, "mke wangu acha kulia, hayo yameshapita, jikaze" annifer akasema, "inauma sana, ndio maana huwa sipendi kuyakumbuka yaliyopita, kwani historia yangu ni mbaya ni yenye kuumiaza, lakini pia ni isiyofaa kwenye jamii"...... "hatuwezi kukijaji kwa jana yako, ila kwa leo yako, kwani hata shetani anaweza kuwa malaika kama atatubu zambi zake. Hata nawe sasa umekuwa mwema kwani umeacha yote hivyo acha kulia mpenz wangu, punguza munkari love" anniffer alivuta pumzi kisha akaanza kwa kusema, "mpenzi wangu yule alinitenda, alinisaliti, lakini ni bora tu angenisaliti kimya kimya, alifanya wazi nikaona, mbaya zaidi alinisaliti na ndugu yangu, alilala na mtoto wa baba yangu mdogo, inamaana alikosa wanawake wengine? Niliumia sana kutuchanganya, kuna wakati usiri unamadhara yake, nikajilaumu maana mdogo wangu alinambia dada kwanini hujanambia kama unatoka n huyu kijana? Na kweli sikumwambia. Hivyo hakuwa anajua na sio kosa lake, lakini yule kijana alifanya makusudi. Toka hapo nikawa naamini kuwa wanaume sio wakuwapenda nikaanza kujiingiza kwenye ukahaba, ulevi na uvutaji sigara, nilifukuzwa kijijini. Sikujari nikaondoka nikaja dar, nikaendelea na maisha yangu ya uzinzi na kujiuza. Nilipata kile ambacho nataka, nilipata pesa lakini pia nilipata penzi, leo nikiwa na huyu kesho nipo na mwengine, hayo ndio maisha yangu"
Jennifer akamuuliza annifer, "sasa ilikuwaje ukaamua kuacha ile kazi na kuolewa? Maan mimi najua ukifanya ile kazi wewe ni kunguru na tunajua kuwa hakuna anaweza kufuga kunguru" annifer akasema, "Jennifer sikuacha kwa siku moja, hapana ila ilichukua muda japo sio mrefu, kwanza kabisa mimi mwenyewe nilichoka lakini pia, siku moja nililala na mume wa mtu, yule mwanaume nililala naye mpaka asubuhi, asubuhi yule mwanaume alipigiwa simu, na mke wake, mke wake alikuwa analia na kulalamika, maneno yake yakanichoma sana, alikuwa akisema, "unaacha familia yako, unaenda kulala na malaya, makahaba, ambao hawajari familia yako, mimi mke wako ninaye kufuria, kupikia na kukufanya upendeze hunijari, ila elewa hao ni wapita njia hapa utarudi tu. Na nikwambie haya unayowafanyia wanao, watakuja kukufanyia wewe uzeeni usilalamike. Na mwambie hiyo mwanamke uliyenaye kuwa, atafute mume wake, ampendezeshe, sio asubiri wenzie wampendezeshe mume wao wamchukue, mwambie atengeneze wakwake wanaume wamejaa tele. Maneno hayo yaliniingia akilini lakini niliumia baada ya kusikia akisema, wanao jana wamelalia uji, hapa ndio nilipatwa na simanzi sana, maana usiku huo tulitumia pesa nyengi sana na yule mwanaume kwahiyo nikashangaa ni vipi anawaacha watoto wake na njaa. Nikajiona mkosefu sana nikajiona sina faida, nipo kwa ajili ya kuwaumiza wanawake wenzang hapo ndio nikaanza kuona ile kazi haina faida ila nikawana najiuliza nitafanya nini nikiach?" annifer alikaa kimya kidogo akijifuta machozi.
"Jennifer unaweza ukiamua, mimi niliamua nikamuomba mungu anipe mtu mwema nitulie, hapo ndio nikakutana na hassan nashukuru hassan akaonyesha nia ya kunioa nami siku kataa nilikubali, japo nilimpa mikakati yangu, naye akakubali na kunitimizia, baada ya kapo nikarudi nyumbani kijijini nikaenda kuomba radhi wazazi, nashukuru wakanisamehe, na hapo ndio tukaanza mikakati ya ndoa." Jennifer akasema,"duuuuuh pole sana na hongera sana kwa kuthubutu, ila mimi sijui kama nitaweza."...... "unaweza wewe na mimi kuna tofauti gani? Unanini hasa mpaka ushindwe? Kuna lipi baya ambalo linafanya wewe ushindwe kabadilika?"....
. "juma hata nioa nikisema, na mimi najiona kabisa sifai kuolewa bora nibaki hivi ni livyo, mimi ni zaidi ya shetani." annifer akamwangalia sana Jennifer kisha aksema, "najua unaweza kuwa unahistori mbaya zaidi lakini haijariahi ila ni ukweli kuwa unaweza, ukiamua yote yanawezekana, ukisha amua basi anza kuswali kama tulivyoelekezwa, hapo ndio utaanza kubadilika" juma akasema, "Jennifer sijui umekumbwa na nini? Ila nikwambie tu ukweli, mimi siwezi kukuacha lakini pia nitakuwa pamoja nawe siku zote, nakupenda sana, naomba usiwe na was wasi kipenzi changu" Jennifer akasema, "wewe hujui tu niliyopitia, hujui roho yangu jinsi ilivyongumu, ungejua wala usinge sema hivyo?"....... "kwani umekutwa na nini?
"sijui nianzie wapi? Na sijui nitumie maneno gani?"....... "anzia popote, ongea chochote tutaelewa"....... "mama yangu alikuwa anaishi na mwanaume asiyempenda ili tu mimi nipate mahitaji, mwanaume huyo alikuwa mshezi, alikuwa akifanya chochote kwa mama yangu. Nilikuwa nikikua nikiona hayo, baba yuoe wa kambo hakuishia hapo, baada ya miaka kumi na tano mimi nikiwa binti wa miaka kumi na saba, siku moja nilizisikia vurugu chumban kwa mama, baba alikuwa akidai mtoto, akisema mama yangu ni gumbu hazai, mama akawa anamjibu kama ni gumba jennifer amamtoa wapi? Hivyo ugomvi ukazidi, baba akaona kama mama anamkesea adabu ni kama vile anamuona yeye ndio tasa. Alimpiga sana na kumuumiza. Kisha baba akaondoka zake. Nilimkuta mama yangu anavuja damu. Nikisikitika sana nilimwambia mama, twende hospital akakataa, nikachukua dawa na kumsafisha sehemu alizoumia. Nikimwambia mama tuondoke pale maana manyanyaso ni makubwa sana. Lakini mama alikataa sikujua ni kwanini alikataa nikimsihi sana lakini wapi? Haikuishia hapo baba aliporudi, alimuingilia mama kwa nguvu mbele yangu nikiona, ulikuwa uzalilishaji, sijui alikuwa ananifundisha nini?" Jennifer alianza kulia na kushindwa kuongea, anifer akamsogelea Jennifer na kumkumbatia, na kumsihi,"nyamaza mpaka mpenzi, pole sana hayo ndio maisha, yana mwisho na mwisho wa kuyasahau ndio huu, huu ndio wakati wa kufungua ukurasa mpya. Nyamaza kipenzi changu, nyama Rafik" annifer alimfuta machozi Jennifer.
Jennifer aliendelea kuongea kwa kusema, "baada ya tukio lile nilikuwa naona aibu kumwangalia mama yangu sikupenda alichofanyiwa, baada ya siku kadha baba alikuja chumbani kwangu akanambia, wewe unakula na kula bure, nimekusomesha mpaka sasa unamaliza form four sasa itabidi ukipie vyote, sikumuelewa alimaanisha nini na alikuwa ana lengo gani? Maisha yaliendelea, japo hayakubadilika, nilifanya mtihan wa kidato cha nne, na tulipohitimu tu, nikawa nashinda nyumban, maana siendi shule. Nilikuwa naenda na mama sokoni kuuza matunda lakini baba alikata akasema sipaswi kwenda sokoni natakiwa nibaki na nyumba niwe nailinda. Kumbe alikuwa na malengo yake. Mama alinambia bakia nyumban, huyu baba yako asije leta matatizo, nikamuuliza kwani huyu ndio baba yangu mzazi? Mama akanambia ukweki hapana sio yeye, nikamuuliza baba yangu yupo wapi? Mama akasema ni story ndefu mwanangu ila ipo siku utajua. Wakati tunaongea hayo kumbe baba anatusikiliza akaingia ndani, na kuanza kumfokea mama, alimpiga makofi na ngumi, kisha akambeba na kumpeleka chumbani, alimchania nguo na kumuingilia kingono kwa nguvu, mama hajawahi kuenjoy ndoa wala tendo lenyewe. Tabu hizikuishia hapo, baba akahamia kwangu, nikiwa nabaki nyumbani, akawa ananiletea zawadi mala nguo, mala hichi na kile, nashanga siku moja akanilietea shanga. Nilistaajabu sana"....... "kheeh alikununulia shanga?"....... "ndio alininunulia, tena sio moja zilikuwa nyingi, akisema wewe ni binti mzuri na mdogo unapaswa uvae hizi shanga, utapendeza sana binti, nilipokea na kusema ahsante, lakini baba alikuwa akiniangalia kwa jicho ambalo hakupaswa kuniangalia vile. Haikuishia hapo mama aliporudi nilimwambia kuwa baba alininunulia shanga, mama akakasilika kwani alijua sio jambo jema. Wakati tuanongea baba kumbe alikuwa nje anatusikiliza, akaingia ndani kwa hasira"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment