Search This Blog

Wednesday 15 March 2023

BEKI TATU MCHARUKO - 1

 

IMEANDIKWA NA: UNKNOWN

**************************************

Chombezo : Beki Tatu Mcharuko

Sehemu Ya : Kwanza (1)


“Shogaa yule mfanyakazi nimeshampata ni wewe tu uje kumchukua maana kadada kenyewe kamekaa kazungukazungu kasije kuniibia mume haka”.


“Mhhh!! Uzungu huo vipi, kwahiyo ndo umenitafutia huyo aje kuwa mke mwenzangu au? Kwani amna wadada wengine tofauti na hao?”.


“Natania bana ni kwamba huyu dada alikuwa anafanya kazi za ndani kwa wazungu so huenda ame adapt tabia zao, ila sio nasema eti tabia zake mbaya, wala mwenzio kenyewe kametulia tu lakini kazuri ni wewe tu ukiwekee mipaka.”


Yalikuwa mazungumzo kati ya Mama Johnson na shoga yake mama Wazir.Mama Johnson alikuwa amempa mama wazir kazi ya kumtafutia dada wa ndani wa kumsaidia shughuli mbalimbali za nyumbani kwani ndio kwanza alikuwa ameajiriwa baada ya kuhangaika kutafuta kazi tangu miaka sita iliyopita alipomaliza chuo.


Mumewe alikuwa daktari katika hospitali moja ya binafsi jijini darn a walikuwa na watoto watatu ambao tayari walikuwa mashuleni.Watoto hao wa kiume wa mwisho alikuwa na umri wa miaka kumi na sita akiwa kidato cha pili aliitwa John, wa pili kutoka mwisho aliitwa Lameck na wakwanza ama mkubwa wao aliitwa Jonson, huyu alikuwa akichukua shahada yake katika chuo kikuu cha dar, mlimani.


Kazi nyingi za ndani kama kupika kufua na kufanya usafi pale nyumbani zilimlazimu mama Johnson kutafuta mdada wa kazi kwani kwa sasa angekuwa anachelwa kurudi nyumbani mara nyingi majira ya saa kumi na mbili kama sio saa moja.


Basi baada ya kuafikiana mama wazir na mama Johnson walikubaliana kuwa binti huyo wa kazi afike siku iliyofuata ili mama Johnson amfundishe kazi maana siku mbili baadaye alitakiwa kuripoti kazini.

0754232253. Watsp for more story


Ijumaa majira ya saa nne asubuhi gari ya mama wazir ilipaki nje ya geti la nyumani kwa mama Johnson.Kutoka siti ya mbele akashuka msichana wa umri wa miaka ishirini na tatu.Msichana huyu alivaa kipensi chekundu kilichoyabana makalio yake makubwa na sijui kama ndani alivaa kitu kwani nymama laini ya tako ilionekana ikicheza huku na kule bila kuwepo kwa dalili ya chupi.


Juu alivaa tisheti laini tu iliyokuwa na kikatuni cha mdada aliyetoa ulimi nje, miguuni alivaa zake visendo vya manyoya na vikuku vya dhahabu.Alikuwa na ngozi laini inayongaa balaa kiasi kwamba baada ya mama Johnson kumuona tu akatamani amrudishe alipotoka kwani moja kwa moja alijua lazima mume aibwe.


“Mhh! Nashukuru umemfikisha salama, ila duh sijui kama kazi ataweza maana anaonekana slay qeen sana”Mama Jonson alisema baada ya kumfikia mama wazir.


“Dada wala usijali miye kazi naweza mavazi sio kigezo cha kumjaji mtu uwezo wake wa kazi we leta kazi nipe nifanye”Alijibu mfanyakazi huyo baada ya kusalimia na kujitambulisha kwa jina la Fetty.


“Shogaa miye nimekufikishia fetty wako ondoa shaka ni mchapakazi maana jana kukaa kwangu tu kafagia hadi kwa kuku”Alisema mama Wazir akaaga na kuondoka, akamuacha mama Johnson akiendelea kumshangaa fetty na vituko vyake.


“Haya karibu twende ndani”Alisema mama Johnson na kuburuza begi la Fetty wakaenda hadi ndani.Fetty akakaribishwa chakula akakaa na kula.Baada ya kula akaenda kubadili nguo ambapo alivaa kitisheti chake akajifunga uapnde wa khanga na kuingia bustanini kumwagilia na kupalizi maua yaliyokuwa yamezongwa na majani.


“mhh kweli kanapambana haka, ila kwa tabia nyingine sijajua”Älisema mama Johnson muda huo akimchungulia Fetty kupitia dirishani aliyekuwa akiendelea na kazi bustani ingawa ilishafika usiku wa saa moja.


Wakati Fetty akiendelea na kazi pale nje mara honi ya gari ilisikika.Mlinzi akafungua geti na ndipo ilipoingia gari ya baba Jonson aliyekuwa ndio kwanza katoka kazini.Wakati akielekea kupaki taa za gari yake zikapiga moja kwa moja mpaka sehemu alipokuwa Fetty.Paja jeupe lililojaa la fetty pamoja na mbongoko wake vikamfanya mze asimamishe gari na kushusha kioo.

ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog