Search This Blog

Wednesday 15 March 2023

HAPPY BIRTHDAY SELINA - 1

 

IMEANDIKWA NA: UNKNOWN

**************************************

Chombezo : Happy Birthday Selina

Sehemu Ya : Kwanza (1)


Nikiwa zangu maeneo ya Kinondoni manyanya kijiweni mida ya usiku saa moja, nilisikia simu yangu ikiita mfukoni halafu nikaitoa na kutazama, ilikuwa simu kutoka kwa Selina mtoto rafiki wa mdogo wangu wa kike.

"Shikamoo kaka" Alisema selina baada ya mimi kupokea simu

"Marahaba vipi mdogo wangu?" nilimuuliza

"Pouwah....Mary yupo wapi?" Aliniuliza

"Ameenda kwa shangazi huko Kibiti atarudi wikiendi"

"Doooh nikajua yupo hata aje anipe kampani nyumbani

Hayupo"

"Sawa, mimi nipo home, wazazi wangu wameenda Tanga kwenye shughuli ya dada"

"ok" Nilisema kwa mkato

"Sina hata raha, Mbaya zaidi wameenda wakati mbaya maana kesho ni kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa"

"Pole sana kwa kweli" Niliongea

"Asante....sina hata mtu wa kunimwagia maji mwaka huu ntajimwagia mwenyewe haha" Alisema huku akicheka cheka kwa furaha

"Hahaha....sawa bana mi nipo kijiweni hapa nikitoka saa tatu hivi nitakucheki" Niliongea

"Powa"

Selina alikata simu na mimi nikaagiza kahawa na kashata nikawa najibirudisha.

Baadaye nilirudi nyumbani.

*

Kwa kawaida yangu mimi huwa nalala saa saba nane usiku nikiwa nacheza zangu online.

Siku hiyo sijui hata ilikuwaje, yaani ile imefika saa sita kamili nilipost kwenye status "Happy birthday Selina Mungu akujaalie miaka 500 ya uhai" Nilipomaliza nilizima data nikawa nacheza gemu la mpira kwenye simu taratibu

Baada ya saa saba nililala usingizi wa pono ambao nilikuja kushtuka saa mbili asubuhi na kupokea simu kutoka kwa Selina huyo huyo niliyemtakia miaka 500

Niliipokea huku nikilalama ananitoa kwenye usingizi wangu mtamu vile.

"Selina" Niliongea baada ya kuipokea

"Shikamoo kaka" Alisema

"Marahaba...vipi?" Niliuliza

"Poa.....nakushukuru sana kaka" Aliniambia

"Kwa kipi?"

"Umeniwish birthday umekuwa mtu wa kwanza kuniwishi yaani saa sita kamili ukapost hata mimi bado sijajipost jamani" Alisema nikacheka

"Hahahaa....na nilifanya makusudi ningekuwa huko Msasani ningekuja kukumwagia maji"

"Hahaha....njoo unimwagie" Alisema mtoto wa kike huku akicheka

"Hahha ntakuja" Nilimtania tu wala sikuwa na mpango wa kwenda kwake

"Poa saa ngapi unakuja?" alisema huku akiwa serious kabisa

"Weee nakutania mimi siji kwako"

"Mmmj njoo bhaasi, niko mwenyewe hata hamna raha huku nyumbani" Aliniambia

"Mmh.....haya poa ntakuja"

"Saa ngapi?" Aliniuliza

"Saa nane mchana"

"Poa thanks"

"Ok" Nilisema

Selina alikata simu na mimi nikajilaza kujilazimisha usingizi lakini kiukweli usingizi haukuwepo kabisaa.

Moyoni nilikuwa nina mpango niende ufukweni nikale upepo fulani hivi mwanana ndipo nilipoamka na kuingia mtandaoni kidogo.

*

Ikiwa ni mida ya saa 7 mchana, nilikuwa zangu beach nikiwa najipatia raha muda wote peke yangu kwani mpenzi wangu alikuwa mbali sana huko Karibia na Bagamoyo.

Simu iliita ni Selina "Aaah kanasumbua haka kanadhani naenda kweli?" Nilijisemea huku nikijishauri nipokee au nisipokee.

Iliendelea kuita mpaka ikakata mi sikupokea. Mara message

"Umefika wapi, nimeshaandaa Pilao, kuku na vinywaji" Alisema nikasoma mate kidogo yanidondoke maana hivyo vyakula nilivimiss sana. Lakini sikutaka kujibu.

Baada ya dakika mbili aliongeza "Ukifika utaniambia" Alituma halafu akapiga mi nikapokea

"Vipi?" Nilisema

"Hauko serious, mbona hausemi umefika wapi nishaandaa kila kitu" Alisema kwa hasira

'Hivi wewe upo serious kwamba unadhani nakuja?" Niliuliza

"Mmmh kaka Jof acha basi hizo mi nimetumia pesa nyingi nilizoachiwa nikijua unakuja sasa unanitia hasara khaa" Alisema

"Basi sawa ngoja nije basi" Nilisema

"Eeh bana njoo"

"Poa"

Nilibaki na mawazo kibao kwamba kumbe alikuwa anamaanisha niende kweli, anyway nilijitia moyo nikasema acha niende nikasherekee naye ili asikasirike.

Niliondoka pale kwa kuwa nilikuwa nimeoga kabla ya kutoka nyumbani, mi sikujali nilienda kupanda gari na kuondoka moja kwa moja kuelekea nyumbani kwao Msasani.

Nilipofika kwao nilikuwa sipajui maana sikuwahi kufika kabla hivyo nilimuandikia ujumbe

"Niko msasani stand nielekee wapi?"

"Kuna duka limeandikwa Offline Shop. Nyuma yake kuna barabara, angalia mbele kabisa utaona Nyumba tatu zinafanana nenda hapo mi utanikuta" Alinitumia ujumbe mtaalam

Nilipoinua uso kutazama kweli niliona hilo duka hivyo nikafuata maelekezo nikaona nyumba zilee nikasogea mpaka kwenye nyumba ndipo nilipomuona barazani kwao akiwa anachezea simu.

"Seliiiiiii" nilisema kwa furaha nikaona ameinuka alikuwa amejisokotea kitenge kuanzia kifuani mpaka chini ya magoti na alikuwa mwembamba sana

"Shikamoo" Alisema

"Marahaba....kumbe kwenu hapa" Nilisema

"Yeah karibu ndani" Aliniamboa halafu tukaingia ndani mpaka sebuleni yaani ndani kulikuwa kunanukia vyakula sio kawaida.

Mtoto selina alichokifanya alisimama mbele yangu "Hujaniletea zawadi ya birthday" Aliniambia

"Hahah...nimesahau"

"Ok twende tukale" Alisema huku akinivuta mkononi wote tukaenda mezani na kuketi.

Alinipakulia chakula na viepe halafu paja la kuku akaweka juu ya viepe

"Utamaliza kweli?" Alinitania

"Sijui ila vinavutia"

"Hahaaa....ngoja nipakue changu" Alisema na kuanza kujipakulia msosi mi nikawa namuangalia tu

"Unajua kupika sana sasa kwanini usimfundishe mdogo wangu?" niliuliza



"Hahha....mlete"

Binti alimaliza kupakua akaninawisha mikono Lakini ya kwake yeye hakunawa. Akaketi

"Mbona hujanawa?" Nilimuuliza

"Kaka....mi nimezaliwa leo siwezi kula peke yangu mimi mtoto natakiwa nilishwe" Alisema huku akinitazama sana usoni

"Hahaha" nilicheka na kuchukua paja la kuku nikampelekea mdomoni akapokea na kumega kidogo halafu akaanza kutafuna..


****

ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog