Search This Blog

Wednesday 15 March 2023

MKE CHANGUDOA - 3

  


Chombezo : Mke Changudoa

Sehemu Ya : Tatu (3)


Juma alikasirika kuondoka pekee yake nalishaona wasichana warembo pale baa, lakini akashindwa kufanya chochote. Walifika nyumbani, na kila mtu akaingia kulala. Asubuhi na mapema juma na hasan walitoka na wakenda mbezi beach kuonana na dalali wa nyumba, wakapelekwa kwenda kuona nyumba, juma akaipenda wakafanya utaratibu wa malipo, siku hiyo hiyo juma akaatafuta watu wafanye usafi ili ahamie, akaenda mjini kutafuta vitu vya ndani. Walihangaika siku nzima kufanya manunuzi, mpaka giza linaingia siku iliyofwata wakamalizia, kisha wakaanza kupanga vitu kwenye nyumba. Palipendeza sana nyumba ilikuwa yakisasa na vitu vyote vyakisasa, makochi, tv, meza na vyengine vingi. Baada ya kukamikisha juma akasema "sasa twende nikakamikishe ahadi yangu" waliondoka kuelekea sehemu wanauza magari, juma akanunua gari mbili moja toyota harrie nyengine rav 4 new model, juma akamwambia hasan "wewe chukua hii rav 4 au unataka gari gani?" hassan akamuuliza muuzaji "samahani ni gari gani inaringana thamani na hii rava 4?" akatajiwa aina ya magari akasema "nipatie toyata athletics" wakaandikiwa wakapatiwa card za magari na vitu vyote kisha kila mmoja akawasha gari yake nakuondoka.


Juma alienda kwake, na hasan akaenda kwake. Hasan alipofika nyumbani alimuita mke wake aone gari lao. "mume wangu umepata wapi pesa?"....... "mke wangu sikuwa na pesa ya kununu gari ila juma alinambia akija ataninulia gari kama ahsante"........ "ahsante kwa lipi? Umemefanyia nini?"....... "siwezi kuhesabu niliyomfanyia, ila kubwa mimi ndipo nilimpatia mchongo wa kwenda south kufanya kazi?"....... "kwanini hukwenda wewe?"....... "mimi nilikuwa nakazi tayari, halafu yeye alikuwa hana kazi hivyo sikuwa na tamaa niliamua kumconect yeye, aende akafanye maana ni kama ndeugu yangu"...... "kwahiyo ndio amekununulia gari"...... "ndio"...... "sawa ikawe kheri in shaa Allah" hasan na mke wake wakaingia ndani, Upande wa juma yeye alikuwa anawaza aende kiwanja gani? "hapa sijui niende wapi lakini inatakiwa nong'oe mtoto mkari sana" alijisemesha mwenyewe, akapata jibu aende the great. Akaingia bafuni akajiandaa akaondoka zake. Alipofika alikaa meza ile ile waliyokaa siku tatu zilizopita, akaletewa kinywa akawa anakunywa mala akawaona wale wasichana tena akawaita, wakaja akawaagiziia pombe, kisha stor zikaanza, mmoja ya wale wasichana akauliza, "juzi ulikuja hapa mlikuwa watatu?" juma akajibu "ndio, yule ni rafiki angu na mke wake" wale wasichana wakaangaliana kisha wakacheka, "kheeeeeh kunguru toka lini akafungwa?"...... "ndio nashangaa" jumaa akawa haelewi akauliza "mbona siwaekewi vipi kwani" mmoja akamjibu juma kwa kusema, "kwahiyo yule msichana ni shemeji yako?"...... "ndio ni shemeji yangu"...... "yule changundoa ndio shemeji yako?"...... "unasemaje?"

**********ITAENDELEA**************



"kama huamini wewe mpe pesa kama hakupi utamu"....... "Inamaana mnamjua vizur"....... "hatuwezi msingizia bhana"....... "nuinyi mlimuona lini akijiuza"....... "siku hizi machangudoa wamebadilisha fashion ya kujiuza, unazani utawakuta barabarani kama zamani? Kila kitu kila kitu kinabadilika"...... "mmmmmh sitaki kuamini hilo ila acha iwe hivyo" waliendelea kunywa na story mbili tatu, muda ulivyoenda juma akaona bora aondoke zake, wale wasichana wakamuuliza, "kwa hiyo nunaenda kulala pekee yako? Hutaki campan?" juma akasema, "mimi mgeni hapa hivyo nakaa kwa rafiki yangu na unabidi nirudishe hit gari yake mwenyewe anaenda kazini kesho"... "sasa si unaipeleka halafu tunaenda logde kupumzika mimi na wewe au unasemaje?"....... "tuonane kesho nitakuwa free kwaherini" juma aliondoka.


Wale wasichana walibaki pale wakiendelea kupata vinywaji, "yaani angekubali tu kuondoka na mimi angelia kilio cha mbwa mwizi asubuhi"...... "kwaninavyokujua wewe ungemkomesha"....... "anaonekana kabisa mgeni yule"....... "ningempa vitu adimu akachanganyikiwa kisha akilala tu anapigwa pesa asubuhi akiamka kweupe, halafu nambembeleza"..... "mnalia wote mmeibiwa".... "khaa yani namuigizia kama vile sijui kitu"....... "nakubalia jeshi langu"....... "mjiji hapa lazima akili iwe kubwa."


Asubuh na mapema juma alienda nyumbani kwa hasan, alipofika alikuta hasan ndio anataka kutoka kwenda kwenye mizunguuko yake ya kazi ya kutafuta ridhiki, "asalam alyekum kaka" walisalimiana, kisha hasan akasema "sikutegemea kupokea mgeni saa hizi ndio maana natoka"....... "aaaah nimewakumbuka nikaona nije niwaone kabla sijaenda kwenye mishe zangu"....... "ok sawa karibu sana ndugu yangu"....... "ahsante sana, shem ameamka?"..... "yule akisha swali halali tena?"....... "aaaah sawa, anapunguza dhambi sio"........ "unamaana gani?"....... "achana nalo hilo swala, kwahiyo unaenda wapi?"....... "mimi naenda town maana naweza kupakia niende tunduma kupeleka mafuta"....... "aaaah sawa basi sawa mimi nitabaki nashemeji nikimlinda au unasemaje?"....... "mke wangu hana shida ya kulindwa analindwa na mungu pekee yake"...... "unamuamini sana shem inaonekana si ndio?"..... "ndio kwanini nisimuamini".... "sasa unaenda na gari au?"...... "hapana naliacha, kwasababu kama nikipakia naondoka zangu"..... "basi ngoja nikupeleke na gari yangu, nikirudi ndio nitamuona shemeji"...... "poaw twende" juma na hasan wakaondoka kuelekea kigamboni.


Walifika na juma akamuacha hasan yeye akaondoka zake, akanijibu wa njiani simu yake ikaita, "oya vipi kaka nikufwate au?"..... "hapana nimepata zari hapa, naenda kupaki than nasepa"...... "oooh poa kwahiyo home huji kuchukua nguo?"...... "nguo zangu zipo kwenye gari mimi standby"..... "oooh poaw basi ukiondoka utanambia mwamba"...... "poaw" juma alitabasamu kisha akajisemea moyoni, 'ngoja nione utamu wa shem asijilie pekee yake, hapa acha nipite supermarket ninue mazaga kisha nimpelekee shem' juma alipitia kweli supermarket na kununua vitu kisha alipomaliza alianza safari ya kuondoka kwenda nyumban kwa hasan, alipofika alibisha hodi akakaribishwa na binti wa kazi wa hasana, akaingia ndani na kuketi, baada ya kusalimiana juma akauliza "dada yako yupo wapi?"....... "yupo ndani"...... "muite" binti akaondoka na kwenda kumuita mke wa hasani. Juma alikuwa anawaza anaanzaje kumuingia shemeji yake, akakumbuka maneno ya wale mabinti wa baa kwamba mpe pesa uwone, akatabasamu akijua atampata, na kusibitisha kuwa ni changuduo kweli. Akiwa anafikilia simu yake ikaingia sms, "mwamba mimi naamsha" ile sms ikamfanya juma afurahi, "hili bwege linaondoka safi sana, acha nimsaidie majukumu" mala alifika mke wa hasan, "ooooh shem salam alyekum"..... "walyekum salam shem kwema"..... "kwema"...... "nimekuletea zawadi shemeji"...... "oooh asante sana shemeji mungu akubariki"...... "usijari sana" mke wa hasan akainama kuchuku ile mizigo apeleke ndani, juma akasema "nenda halafu uje nina jambo nataka kukwambia, mke wa hasan alipeleka vitu ndani kisha akachukua simu akampigia mume wake," amekuja juma hapa"...... "ameniambia atakuja hapo"...... "vipi unaondoka au safari hamna nikuhesabu chakula cha mchana?"...... "sijajua ila usinihesabu naweza kurudi ama nisirudi?"...."sawa mume wangu, shemeji anasema anamazungumzo na mimi"..... "nenda kamsikilize anasemaje?"....... "sawa mume wangu" mke wa hasan akaenda siting room akakaa kisha akamuuliza juma, "shemeji eeh unamazungumzo gani?"..... "mbona unaogopa wakati mkubwa wewe?"...... "ukubwa unahusiana nini na kuogopa"...... "ok basi haina shida, nahitaji hii iwe siri"..... "siri tena?"...... "nahitaji tuwe wote usiku wa leo, maana hasan si anasafiri"...... "unasemaje shemeji?"


"Nataka nikupeleke viwanja vya bata ambavyo hasan hawezi kukupeleka, kila siku mabaibui na madera ngoja nikupeleke sehemu ukaone mambo ya dunia yanavyokwenda twende tukatumie pesa twende ukaenjoy" mke wa hasan alikuwa akimsikiliza tu juma akimwaga sera, "mtoto mzuri kama wewe hutakiwi kuwa hivi? Unatakiwa kuwa na gari yako, na maisha yako"...... "kwahiyo unanichukuliaje mimi?"......"kawaida na lengo ni wewe uwe na furaha"...... "ok subiri" mke wahasan akaamka kisha akaenda chumbani kwake akachukua zawadi alizoletewa na juma akatoka nazo akampa juma mzigo wake kisha akafungua mlango na kusema, "naomba uwondoke, beba mizigo yako ondoka, mimi sio kuku kama utanidanganya kwa punje za mtama naomba uwondoke, usije hapa kama hasan hayupo, pleas ukitaka huu ujinga wako nisimwambie hasan basi kaa mbali na mimi, ukija hapa njoo na hasan au subiri hasan akiwepo ndio uje, laah sivyo nitakuzalilisha" juma akasema "kwani shem tatizo liko wapi, kwani ukitoka na mimi nani atajua, pia hatuendi jufanya chochote kibaya, tunaenda kutembea tu than tunarudi"...... "mimi sio mjinga kama unavyonifikilia, nasema toka nyumbani kwangu" juma akaondoka zake, "mbonw unaacha mizogo yako beba katagute wakumpa"..... "hiyo nilikununulia wewe chukua"....... "nimesema sitaki chukua mizigo yako" mke wa hasan akamtimua juma, juma akaondoka zake na kuelekea kwake.


Jioni juma alichukua tax hadi the great ambako alipanga kuonana na wale wasichana alikaa na kuagiza kinywaji kisha akaanza kunywa na kuanza kuwasubiri, akiwa amekaa mala akaja msichana mmoja kati ya wale aliyokuwa nao siku moja iliyopita, "karibu"..... "ahsante"..... "wenzio wako wapi naona upo pekee yako"......."wale kila mtu kapata ubavu wake kasoro mimi"...... "kwahiyo sahizi wapo kwenye sarakasi"....... "hahahahaha, acha kunichekesha mimi"..... "basi usijari wewe leo utakuwa na mimi au uanasemaje?"..... "sina neno juu ya hilo, kikubwa pesa tu"...... "kwanini unasema kikubwa pesa"...... "sasa unadhani nitaishije mjini bila pesa?"...... "basi usijari utaishi kiboss kama mimi sawa?"...... "usiwaze kuhus mimi"....... "nataka uwe wangu yaani kila siku tuwe wote utaweza kweli?"....... "sijui"..... "ok sawa maliza kinywaji tuondoke"...... "sawa ila vipi kuhusu yule manzi umejua kama ni changu?"...... "mmmmh sijui ila sijasibitisha hilo"...... "sawa haina shida" walikunywa kisha wakaamua kuondoka na kwenda kupumzika. Walipofika logde, juma aliingia bafuni akaoga, kisha na yule mrembo naye akaingia bafuni alipotoka akaenda kukaa kwenye mapaja ya juma, juma akauliza, "ulisema unaitwa nani?"..... "naitwa niffer"...... "mrembo kama jina lako"...... "ahsante love" wakaanza kutomasana na kisha kupeana penzi.


Hasan alirudi nyumban kwake majira ya saa nne usiku akamkuta mke wake anamsubiri, alipoingia mke wake alianza kulia, hasan akasema "unalia nini mke wangu" mke wa hasan akasema, "kuna yoyote anajua storia yangu?"...... "hapana sijamwambia yoyote?"....... "sipendi kujaribiwa, nitakuja kumtukana mtu waambie rafikinzako mimi sio malaya, waambie kabisa wajue"..... "kuna nini kwani?".... "mume wangu acha niishie hapo, ila unamarafiki wa ajabu sana sana"...... "bado zikuelewi, yaani sielewi kabisa"........ "usiwaze mpenzi wangu, usiwaze mume wangu mimi nakupenda, umeniheshimisha kuniweka ndani na kunifanya kuwa nathamani, imani yako uliyoweka kwangu sitaki kuivunja, sitaki kukuangusha acha niendelee kuweka uwaminifu wangu kwako yaani sitovunja uwaminifu wako, nakupenda mume wangu nakupenda sana kipenz changu."......"nakupenda sana love, mama wa mwanangu, ila sijui nini kimekusibu laazizi"...... "sitaki musisalimiane, sitaki pia mgombane, ila ninachotaka kusema unapokaa na rafiki zako waambie, mimi sio rahisi hivyo, halafu kama wanataka kunijua kiundani waje niwaambie kuhusu mimi. Wengine washamba tu, mimi sio mshamba kama wao"....... "bado unaniacha njia panda"...... "twende ukapumzike mume wangu najua umechoka, ila sitakuja kukusaliti niamini, ipo siku utakuta nimemoiga rafiki yako makofi si unanijua vizur?"...... "khaaa usije nipa kesi nakujua wewe yaani ukimkamata mtu kama juma yule unaua mwenyewe mbovu mbovu yule"..... "sasa mwambie asinipime kina changu kirefu"...... "asikupime?"


"ndio asinipime"....... "kwani anakupima?"....... "hapana ila natoa tahadhari tu?"........ "ok sawa haina shida, twende ndani" waliingia ndani hasan akaenda kuoga kisha wakapanda kitandani na kulala. Upande wa juma yeye alikuwa na dada poa wake wakiendelea kupeana mapenzi moto moto, "Umezaliwa wapi mbona fundi hivi?" juma alijikuta anamuuliza niffer, niffer akasema "mimi kwetu bara mbona"..... "unajua sana yaani raha mpaka utosini"...... "ahsante sana" waliendelea kusifiana na kupeana raha mpaka asubuhi. Juma akachanganyikiwa na penzi la niffer akamzuia niffer kuondoka, "naomba usiondoke baki hapa, baadaye nataka twende ukapaone kwangu, wewe ni mzuri, unajua mapenzi tulia na mimi kipenzi"...... "utaniweza mimi wewe?"....... "ndio nitaweza"...... "sawa haina shida" wali baki pale logde kwa siku mbili wakipeana uroda. Hassan alishikwa na wasi wasi na kuanza kumtafuta juma akipiga simu ikawa haipatikani, akatuma sms lakini hazikujibiwa alikuwa na wasi wasi sana. Mke wa hasan akamuuliza hasan "mbona unaonekana haupo sawa mume wangu?"..... "ni kweli sipo sawa, namtafuta juma toka jana hapatikani leo ni siku ya tatu hatujaongea sio kawaida sijui amepatwa na nini?" mke wa hassan aliwaza sana alitamani kusema ukweli lakini akaona atawagombanisha marafiki ambao sasa ni kama ndugu, "mume wangu atakuwa yupo sawa, kama kuna tatizo angeshakupa taarifa itakuwa yupo salama"....... "mke wangu unajua mimi na juma hata kipindi yupo south ilikuwa lazima tuwasiliane kila siku, sasa sijui kakumbwa na nini?" mke wa hasan alimbembeleza mume wake, na kujaribu kumsihi na kumliwaza, hassan akauliza "mke wangu ile siku ya mwisho alivyokuja hapa hakuna tatizo lolote lilitokea?" mke wa hasan akastuka hasan akasema "mbona unastuka kuna nini?"...... "swali lako limenistua maana sikutegemea, ila hakujatokea kitu chochote baina yetu"....... "sawa acha mimi nijiandae nitoke niende nikamwangalie kwake" hasan alienda kujianda na kisha kuondoka kwenda kwa juma.

ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog