Search This Blog

Wednesday 15 March 2023

SHINDIKANA - 3

  


Chombezo : Shindikana

Sehemu Ya : Tatu (3)







Pia kwa mbali nilianza kuzihisi dalili za upendo wa dhati kwa huyu kahaba. Niliona kabisa








kwamba nilikuwa nimezimika na nimekufa juu yake. Nilikuwa natamani muda wote niwe naye.








Nikavaa ngio zangu na kasha nikaondoka kutoka katika chumba kile cha gesti. Kwa upande wa wakati ilikuwa ni majira ya saa mbili usiku. Niliona leo niwahi kurudi nyumbani kwani nikichelewa yaweza tokea vita kuu ya tatu ya dunia ambayo itakosa msuluhishi.




**********












“Hello! Niambie mdogo wangu”. Ilikuwa ni sauti ya mama Careen akiongea na simu mchana huu wa leo.








“Safi tu sista”. Upande wa pili wa simu ulijibu.








“Vipi, mbona kimya sana? Yaani uko kimya utadhani hauko katika jiji hili!?”. Mama Careen aliongea.








“Nipo dada yangu. Nitakuja siku moja kukutembelea”. Upande wa pili wa simu uliongea.








“Sawa tu bwana. Yaani tunaishi utafikiri si ndugu?”. Mama Careen alilalama katika simu.






“Kwa nini wasema hivyo dada?”. Uliuliza upande wa pili wa simu.








“Sasa ni mwaka wa ngapi hatuonani? Humjui shemeji yako wala mwanangu. Kila nikikuuliza, waniambia uko katika jiji hilihili la Kano. Hivi hii ni haki kweli mdogo wangu?”. Mama Careen aliongea.








“Punguza moto dada yangu. Natambua nimekosa. Safari hii wala sitakuangusha. Nitahakikisha kwamba ninakuja kukutembelea wewe pamoja na familia”. Upande wa pili wa simu uliongea.








“Lakini hayo si ndiyo maneno yako kila wakati? Mara oooh! Nakuja kesho halafu ooooh! Nimepata udhuru nitakuja wiki ijayo. Hebu jifunze adabu wewe mtoto. Yaani unavyonikera natamani mpaka kukutapika!”. Mama Careen aliendelea kuongoa huku sasa akionesha dhahiri kwamba alikuwa amepandwa na jazba.








“Dada yangu nisamehe. Amini safari hii sitakuangusha nitakuja kukutembelea”. Upande wa simu uliongea.








“Haya wewe ndiye mwamuzi. Ukipenda njoo na usipopenda usije. Mimi sitakuwa na neno nawe kuanzia sasa. Wewe si mtoto mdogo wa kushinda tunakumbushana mambo madogo kama haya wakati waelewa wazi ni jambo la msingi”. Mama Careen aliendelea kufoka.








“Vipi mama Careen, mbona wazozana na simu?”. Nilimwuliza mama Careen mara baada ya kuwa ameacha kuongea na simu. Na kwa wakati huo mimi nilikuwa nimetoka chumbani ambako nilikuwa nikijiswafi mwili wangu.








“Nilikuwa naongea na mdogo wangu”. Mama Careen alijibu kwa kifupi huku jazba ikiwa bado haijapungua.








“Anhaaaa! Yule ambaye ulishawahi niambia kwamba yupo hapahapa Kano?”. Nilimwuliza mama Careen huku nikimtazama usoni.








“Ndiye huyohuyo. Yaani mimi ananikera sana huyu mtu. Yaani mambo yake ni ya kitoto utafikiri ni mtoto mdogo”. Mama Careen aliongea.








“Mh! Yakupasa umsamehe kwani ndiye nduguyo wa pekee”. Nilijaribu kumtuliza.








“Ushaanza na wewe mambo yako. Yaani wewe ndiye unayefuga ugonjwa!”. Mama Careen alinigeuzia kibao.






“Mh! Basi mama yaishe. Mimi natoka kidogo. Nitarejea baadaye”. Niliaga ili kuepusha shari kwani namfahamu fika huyu mwanamke.








“Sasa ole wako uchelewe kurudi leo. Utanieleza kwa nini jogoo hatagi”. Ilinipata hiyo nikiwa navuka kizingiti cha mlango.








Yaani mwanamke alikuwa na shari huyu balaa! Hakuna siku ambayo tungekaa kwa amani na kufurahi kwa pamoja kama mume na mke.








Muda wote ilikuwa ni kuzozana na kutoleana maneno ya kashfa ambayo muda mwingine yaliambatana na vipigo vya hapa na pale. Vipigo vya aina zote vidogo na vikubwa ambavyo mara nyingi vilikuwa vikihatarisha uhai wa ndoa yetu.








Ama kweli mke nilikuwa naye. Na sikuwa na ujanja juu ya mke wangu kwani alikuwa ni mwanamke ambaye nilimchagua mwenyewe na kumwoa wala sikuchaguliwa na mtu yeyote.








Sikulazimishwa na mtu yeyote kumwoa mwanamke huyu bali ni kwa mapenzi yangu mwenyewe. Niliamua kuingia mkataba wa maisha kwa kula naye kiapo cha ndoa takataifu tena ya kanisani ambayo ilishuhudiwa na mashuhuda wengi sana.








Kwa wakati huo mawazo yangu yalikuwa juu ya kahaba wangu mrembo. Niliamua siku ya leo niipitishe nikiwa naye kwani sikuwa na shughuli nyingine ya kufanya. Niliamua niende nikampe mapenzi motomoto nami nipate burudani tamu ambayo huwa naikosa kutoka kwa mke wangu kutokana na kisirani chake.








“Hello! Mambo”. Niliongea katika simu mara baada ya kuingia katika sehemu nilipohifadhi namba za watu wangu mbalimbali na kulichagua jina la kahaba mrembo ambalo nilikuwa nimelisevu likisomeka PATRICK.








Niliamua kuisevu namba ya kahaba kwa jina la Patrick ili kuepusha maswali kutoka kwa mama Careen endapo angeamua kuipekua na kuifukunyua simu yangu.








Niliamua kuichukua tahadhari hiyo kwani nilimfahamu fika mama Careen kwamba alikuwa ni mwanamke ambaye alikuwa akipenda sana udambwidambwi.








“Poa vipi mzima wewe?”. Upande wa pili wa simu uliongea kwa sauti ya kumtoa nyoka pangoni.






“Mimi niko fresh kabisa”. Nilijibu.








“Eeeeeenheee! Lete maneno”. Upande wa pili wa simu uliongea.








“Maneno yatoke wapi zaidi ya kukumiss tu”. Nilijibu huku nikiendelea kutembea.








“Ha ha ha ha haaaaaaa! Yaani wewe unimiss mimi badala ya kummiss mkeo!”.








“Aaaah! Najua huwezi kuamini lakini ukweli wenyewe ndiyo huo”. Nilijibu.








“Haya unanimiss kwa lipi sasa?”. Alihoji Yule mrembo katika simu.








“Nakumiss kwa yale mambo matamu sana ambayo huwa unanipa. Mambo haya huwa siyapati kwingine kote zaidi ya kwako”. Niliongea.








“Acha kunichekesha bwana. Ina maana kwa mkeo huwa hupati?”.








“Amini hebu nielekeze nyumbani kwako nije sasa hivi maana ugwadu nilionao ni balaa!”. Nilimsisitiza Yule mrembo.








“Heeeeee! Uje kwa nani?”.








“Jamani si nakuja kwako? Kwani kuna ubaya gani? Mi wala siyo simba kusema huenda nikakung’ata ukafa!”. Nilimchombeza Yule mrembo kwa maneno matamu na laini.








“Ila una vituko wewe mwanaume sipata ona. Huwa unanipa raha sana kwa maneno yako. Haya basi njoo mtaa wa Jalawa ukifika hapo nipigie nami nitakuja kukuchukua”. Hatimaye yule mrembo alikubali kuniruhusu niende kwake.










“Nd’o hivyo kisura. Hebu kubaliana na ushauri na maoni yangu”. Nilimwambia yule mrembo pindi tulipokuwa chumbani kwake kabla hata hatujayaanza yale mambo yetu.






“Lakini we mwanaume ni wa ajabu sana. Yaani hivi umekomaa kabisa mimi niachane na shughuli hii ambayo ninaifanya”. Yule mrembo aliuliza.








“Ninakimaanisha kile ambacho ninakiongea”. Nilimwambia.








“Ok, lakini hivi unafahamu kwamba hii biashara ndiyo ambayo inaniweka katika jiji hili la Kano?”. Mrembo aliuliza.








“Ndiyo nafahamu fika na kwa uwazi kabisa”.








“Sasa kama wafahamu, je, ni kwa nini wataka mimi niiache hii shughuli? Hivi huoni maisha yangu yatakuwa magumu sana na jiji hili litanishinda?”. Mrembo aliongea huku akinitazama usoni kwa macho yake malegevu.








“Mimi nimejitolea kukusaidia kwa kila kitu katika maisha yako”. Niliongea kumtoa hofu yule mrembo malkia.








“Basi naomba nikuulize swali”. Mrembo aliongea.








“Uliza tu wala usijali”. Nilimruhusu.








“Hivi ni kwa nini umeamua kuyafanya haya yote ambayo umekusudia?”. Swali hilo lilitua katika ngoma za masikio yangu.








“Nimeamua kuyafanya haya yote kwa sababu ya upendo wa dhati ambao ninao juu yako”. Nilimjibu.








“Acha propaganda zako bwana. Wewe utampendaje kahaba?”.








“Upendo hauchagui. Popote pale mtu aweza kupenda bila kujalisha tabia, dini, sura, rangi au kabila la mtu”. Niliongea huku nikimtazama usoni.






“Mh! Hii kali sasa. Je, kwa nini usimpende hivyo mkeo?”. Yule mrembo aliniuliza swali moja la msingi sana na ambalo lilinichoma sana moyo.








“Mke wangu hatupatani hata kidogo. Yaani mpaka inafika kipindi huwa najilaumu ni kwa nini nilimwoa mwanamke yule. Mwanamke ana gubu, mwanamke ana inda, mwanamke amejaa kisirani toka unyayoni mpaka utosini”. Niliongea hayo kwa uchungu sana mpaka yule kahaba akanionea huruma.








“Mh! Usimseme hivyo mkeo”. Yule mrembo aliongea huku akinikuna kifuani.








“Ni kweli haya nikuambiayo. Laiti ungemshuhudia huyu mwanamke kwa vitimbi anavyonifanyia, ungenionea huruma”. Niliongea.


ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog