Search This Blog

Thursday 9 March 2023

UNO LA MASIKINI - 1

  

IMEANDIKWA NA : UNKNOWN

***************************************

Chombezo : Uno La Masikini

Sehemu Ya Kwanza (1)

e" alisema mmoja wa marafiki zake


"sina hela shoga angu, ipo kwenye Tigo pesa halafu hamna wakala hapa" alisema Christina ambaye kwa kifupi walizoea kumuita Tina


"sasa sikiliza Tina" shoga mwingine alidakia "mimi mama ameniagiza nimsaidie kupeleka hela yake kwa mama Shanta ningewalipia, hivyo cha muhimu kama unataka kutulipia basi nakupa hizi za mama halafu ulipe ili baadaye tukitoka ukaweze kutoa iliyoko kwenye simu unigee nipeleke nilipoagizwa"


"mmmh sawa" alisema Tina


Basi walifanya kulipia walichokitaka halafu wakaelekea mpaka sehemu ambazo kulikuwa na wavuvi wengi waliokuwa wakivua na walikuwa ni wanaume kama ilivyozoeleka hii kazi wanawake ni mara chache sana


"broo nisevu nipate hii kazi man nina shida sana" alisema kijana mmoja mchafu mchafu sana aliyekuwa akibembeleza kupewa kazi ya uvuvi maana hakuwa na vifaa vya kuvulia. 


"bwana mi sina kazi mzee vipi mbona huelewi?" yule mwenzake alimjibu kwa hasira na kupanda ngalawa wakaanza kuzama katikati ya bahari na kuanza kufanya mambo


Ghafla lilitokea bonge laa nyoka lilikuwa likikatiza mitaa ile, sasa Tina alipoliona aliogopa sana akaanza kukimbia bila kujali anakimbilia wapi. 


Mwisho wa siku alizama hadi kwenye maji baharini


"Nyokaaaa" alisema mmoja wa mashoga zake, ndipo yule kijana alipogeuka na kukutana na bonge la nyoka


Ilibidi yule kijana atafute lirungu halafu akaanza kulikandamiza kichwani joka lile mpaka likafa


"daaah asante kaka yangu" alisema msichana mmoja pale


"usijali" yule kijana alisema huku akiifuta mikono yake na kuanza kutembea. 


"Tina yuko wapi?" alisema msichana mmoja ambaye alikuja na kina Tina 


Wote walishtuka wakaanza kupiga kelele baada ya kumuona Tina akitapatapa kwenye maji, walianza kupiga kelele


"jamani Tina anakufa auwii, Wee kaka njoo msaidie mwenzetu" walisema wakipiga kelele


Yule kijana aliekuwa akitembea aligeuka na kumuona binti huyo Tina akiwa anajaribu kujiokoa kwenye maji lakini anashindwa, ilibidi jamaa avue suruali yake akabaki na bukta la Chelsea halafu akavua tisheti yake na kuingia ndani ya maji kwa ajili ya kwenda kumuokoa binti


Aliogelea mpaka pale binti alipokuwa akitapatapa akaanza kumsaidia kwa kumvutia kifuani mwake. 


Binti yule ambaye alikuwa ameshalegea kwa kunywa maji alijikuta akimuangukia kifuani kijana yule kwa bahati mbaya akajikuta amepitisha mkono kwenye bukta la kijana huyo akakutana na kipande cha ndizi kilichokuwepo ndani. 


Aliutoa mkono wake haraka halafu akajiegesha vizuri ili kijana yule ambebe mpaka kule ufukweni mwa bahari. 


Kweli kijana alimtoa akampeleka nje ya maji na kuanza kumkandamiza tumboni ili atapike maji. 

*

Jioni kila mtu alikuwa amesharudi katika makazi yake ya kudumu Tina bado alikuwa na rafiki yake ambaye alikuwa anaishi kwake kwa muda maana walisoma naye. 


"Shoga yangu ungekufa ujue" alisema binti yule aliyefahamika kwa jina la Jane


"jamani acha tu Jane nimepagawa eti yani sijui hata nilishindwaje kuogelea pale karibu hivyo"


"mi mwenyewe nilishangaa" 


"hivi yule kijana aliyenisaidia ni wa wapi?" Aliuliza


"sijui, itakuwa ndiyo kakuibia simu yako alipokuwa anakuokoa"


"sio kweli haiwezekani" Tina alikata katakata


"kweli vijana wale wahuni sana si unaona hata alivyo mchafu"


"ila kweli Jane, ila haina shida labda ndiyo mshahara wake wa kunikomboa kesho nitanunua nyingine kipindi nikienda kurenew laini yangu?"


"sawa shogaa" Jane alisema


Baadaye walipolala, usiku usingizi ulikuwa wa taabu sana, kila mara Tina alikumbuka jinsi ambavyo kijana yule alivyomuokoa akajikuta anamshukuru kimoyo moyo

'Mungu ampe nguvu apate kazi anayoitaka jamani kaka watu' alitafakari binti kimoyo moyo


Alikumbuka jinsi kijana yule alivyomvuta kwa bahati mbaya akajikuta ameshika pingili ya mua ya kijana yule

'mh mwembamba lakini ana ndizi mshare kabisa jamani' Binti alipata tabu sana kutoka na jinsi jamaa alivyomsaidia 'mmh kesho ntaenda kumuona kama atakuwepo'

Alijikuta amemuwazia mtu ambaye ndiyo mara ya kwanza kumuona yaani mpaka akaaishia usingizini akiwaza imekuwaje kijana yule akajitokeza kama mkombozi.... Je ITAKUWAJE (usikose sehemu ya pili) 




#Tulipoishia

Alijikuta amemuwazia mtu ambaye ndiyo mara ya kwanza kumuona yaani mpaka akaaishia usingizini akiwaza imekuwaje kijana yule akamsaidia....


#Endelea sasa

Asubuhi na mapema Tina aliamka huku akiwa ameimiss Instagram yake, alitakiwa pia aende maeneo ya Makumbusho kuna video alikuwa akacheze huko yeye na msanii Harmonize


Ilibidi afanye kujiandaa haraka haraka yeye pamoja na Rafiki yake Jane wakachukua bajaj na kuelekea maeneo ya Makumbusho, walifika moja kwa moja hadi katika ofisi kuu za Tigo kwa ajili ya kurenew line ya Tina iliyopotea jana kwenye simu


"Naomba namba ya NIDA tafadhali" alisema mhudumu


"19960218312540000322" Tina aliitaja na yule muhudumu alimsaidia kufanya process za kurudisha laini ile


"Njoo weka kidole cha pili hapa"


Tina alisogea taratibu na kufanya kama alivyoagizwa


Baada ya kumaliza kila kitu yule kijana alianza kumchokoza


"Christina"


"Abee"


"Na mimi nichukue hii namba nini?" aliuliza kijana yule baada ya kumuona binti anavyong'aa


"Haina shida" alijibu binti


"Poa basi nitakucheki"


Binti na rafiki yake waliondoka moja kwa moja na kuchukua tena Bajaj hadi maeneo ya Kariakoo ili kuweza kununua simu mpya na kali


"Sijui tutawahi kurudi"


"Kwanini tusiwahi? ni chapu tu bana" Jane alisema


Walienda hadi Kariakoo na kuvuta simu nzuri ya laki nne halafu Tina akatia laini yake na kuunga bando ili kui-update


"Samahani Tina hatutafanya video leo tutafanya kesho" alituma sms Jose wa Mipango ambaye ni Rafiki wa karibu sana wa Harmonize


"Jamaaniii hawafanyi ile video leo" alisema Tina 


"Whaaat" Jane aliuliza


"SMS hii hapa" alisema Tina huku akimuonyeshea ujumbe Jane


Basi ilibidi waondoke na kurudi mitaa ya kwao huko Kimara lakini wakiwa njiani Tina alianza mbwembwe


"Jane, twende zetu kule kwa wavuvi tukasafishe macho"


"Mmmh shoga angu, kule tena umepapendea nini?" aliuliza


"We twende tu nataka nikamshukuru yule kijana aliyenisaidia jana"


"Makubwa shoga angu, wewe ni wa kummiss kijana yule mchafu?"


"Wewe twende bana au wewe tangulia nyumbani ukapike mi nakuja" alisema Tina


"Aya mi naenda nyumbani bwana nimechoka zangu"


"Powa basi"


Baadaye kidogo kila mtu alifuata mambo yake, Jane nyumbani na Tina Baharini kuwaona wavuvi


Leo Tina alipofika mule alimkuta yule kijana akiwa amejiinamia analia sana, leo alikuwa amevalia pensi ya rangi ya Maziwa, na fulana nyeusi


"wewe kaka mambo" binti aliongea kwa mshtuko baada ya kumuona mtaalam akilia


"Safi da.. Da kwema" alisema huku akijifuta uso na kufuta machozi ili binti asishtuke


"Kwema, mbona unalia" alisema


"Hapana silii dada angu"


"Haulii vipi wakati unaonekana macho mekundu na sauti ni ya huzuni hiyo, niambie ukweli kaka"


"Daaah dada yangu ni wiki sasa ninahudhuria hapa sipati kazi, nina njaa sana sijala tangu jana asubuhi najihisi kufa eti" kijana yule alisema


"Oooh jamani, pole sasa usilie, twende hivi" alisema binti na kumshika mkono akaanza kumvuta, jamaa lililegea kwa njaa


"Kwanza unaitwa nani kaka?" binti aliuliza


"Naitwa Tino" alisema "Kwa kirefu Agustino" alimaliza


"Ahaaaa mimi mwenyewe naitwa Tina, haha kwa kirefu Christina" alisema na kutabasamu huku akimuangalia yule kijana ambaye naye alitoa tabasamu kwa mbali sana "Kwa hiyo Tino na Tina" binti alisema


"haya sawa, sasa unanipeleka wapi?" mtaalam aliuliza


"Ukale"


"No hizi hoteli ni za ghali sana dada angu"


"usijali mimi ndiyo nalipia"


Basi walienda hadi hotelini wakala wote, binti akalipa hela za kutosha, halafu akamchukua Tino wakatoka hadi nje ya hoteli


"Wewe umeshiba sasa Tino?" binti aliuliza huku akimkagua mtaalam kwa macho legevu yaliyoonesha kumjali sana mshikaji


"ndiyo nimeshiba sana dada yangu asante" alisema jamaa na kuinama kidogo kwa nidhamu ya hali ya juu


"Haya basi powa, unakaa wapi?" aliuliza binti huku akiwa anafungua pochi yake na kutoa noti moja ya 5000


"Boko" alijibu Tino


"Haya hii itatosha nauli na kula Maana nahisi hauna mke wewe" binti aliongea akiwa anatabasamu huku akimkabidhi ile noti


"Asante jamani, mimi sina mke pia"


"Haya, samahani unaweza chukua namba yangu halafu ukaniandikia message hata na simu ya rafiki yako maana kesho kutwa nataka nije nikusalimie nione unapoishi wewe" alisema binti kisha akachukua kitambaa na kujifuta kidogo usoni


"nitajie tafadhali"


"Una pakuandika?" aliulizia


"wewe taja tu"


"Hee unaweza kushika kichwani kweli?" binti aliuliza


"We taja usiwaze" Tino alisema akiwa anatabasamu


"Haya, 0654433281" alitaja binti haraka haraka


"Poa" Tino aliongea binti akashtuka


"Tino, haupo serious kama hutaki namba yangu wewe sema wala sikulazimishi ah" binti alisema kwa hasira huku akiifunga pochi yake na kuondoka kwa hasira


"Vipi kwani Tina?" Jamaa aliita kwa mshangao


Tina alipoondoka alikuwa akifoka sana kwa hasira

"Mwanaume mwenyewe huna chochote halafu unaringa, unahisi mimi nakutaka au, yani mshenzi kweli mfyuuuu" aliondoka binti kwa hasira na kupanda bajaji huyo akasepa zake nyumbani. 


"Ehee niambie shogaangu" alisema Jane baada ya kumuona mwenzake "Haiwezekani Tina haiwezekani, yaani wewe umempenda masikini kama yule"


"nani kakuambia nimempenda na we mi silipendi lipumbavu lile, mwanaume gani hana hata nguo za kung'aa naweza kupiga naye hata picha kweli?" binti alisema huku akiwa anavua hereni zake akiwa bado ana hasira na Tino alivyomtambia kuandika namba yake


"umemuona lakini?" Jane aliuliza


"Usinitajie yule mpumbavu bwana taja watu wenye hela zao" Binti alisema kwa hasira


"Oooh ningesahau shoga, Mheshimiwa kanipigia anadai hupatikani eti kwenye voda" alisema Jane


"Aaaah Voda si imepotelea kwenye simu jamaani, ile mi nilisajili kwa kitambulisho cha mtu ndo maana nashindwa kurenew" alisema binti


"ahaa, nilimueleza kwamba umepoteza simu sasa kasema eti mkutane JingoMoja Hotel usiku wa leo" alisema Jane


"mmmmmh nitampiga kizinga atakoma" alisema Tina


"sasa unafikiri hatotaka mfanye"


"Hata akitaka ni kimoja tu si najua lizee lile haliwezi kunichosha mimi bado mbichi, embu hujapika shoga?" Tina aliuliza


"Nimepika mwaya check kwenye Hotpot, kitu kitamu we"


"Hahahaaaaa, nakukubal Baby Jane huuuu kelele ya kwanza kwa Shoga ake" waliongea maneno mengi huku wakiwa wananyoosha vidole vitatu juu si unajua waswahili tena


"wee" Jane alijibu wote wakacheka


**

Usiku saa nne kamili Tina alipanda gari na kwenda mpaka, JingoMoja Hoteli ikiwa ni bonge la hoteli mjini hapo. 


Binti alikuwa amependeza balaa, na leo alitakiwa kwenda kuonana na lizee liheshimiwa ambapo katika serikali hii alikwa ni Waziri wa sanaa na michezo, Mh Regnald Mwasoka Kalumbile


"Hey, 072" binti alikutana na wapambe wa muheshimiwa wakamuelekeza chumba cha kwenda kumkuta mheshimiwa kwa signal. 


Binti alienda moja kwa moja akaingia chumbani huko alikuwa ameandaliwa vizuri na alikuwa anahitajika amburudishe muheshimiwa kwa siku hiyo usiku kucha kwa bei ghali. 


Hizi ndo zilikuwa kazi za mabinti hawa wawili na ndizo ziliwaweka mjini, walifanya pia kazi ya kucheza video za mastaa mbali mbali hata kwenye wimbo wa Darassa uitwao Muziki walionekana.....ITAENDELEA




Kisa chenye ukweli ndani yake


??©?

Mida ya asubuhi Tino aliwahi kuamka, akachukua simu ya mwenzake na kutoa lock maana yeye hakuwa na Simu


Kama utani aliandika namba ya Tina ambayo alikuwa ameikariri alipotajiwa na Tina ilikuwa 0654433281


"Mambo" aliitumia sms namba ile wakati huo Tina alikuwa akivaa nguo kwa ajili ya kwenda kwenye video shooting huko Makumbusho.


Binti aliisoma sms na kujibu "Poa nani?" alijibu kwa mbwembwe


"Tino" 


Kwanza cha kwanza binti alipoisoma ile message aliushika moyo wake kwa sababu uligonga kwa kasi ya ajabu. Hakuamini kama kijana angeshika namba yake kiurahisi wakati alimtajia mara moja tu namba


"Haupo serious Tino" alimtext huku akiketi vizuri


"Kwanini?" Tino aliuliza


"Kwa sababu haiwezekani wewe uishike namba yangu kirahisi rahisi vile"


"hahaa mbona kawaida na wee" alisema Mtaalam


"Hahaa Genius" binti aliandika kwa furaha


"Whose number is this?" aliuliza kwamba namba anayotumia tino ni ya nani maana alimwambia kwamba hana simu


"Unasemaje mbona sijaelewa kiingereza" Tino alisema


"Daaah, Samahani sikujua jamani nimekuuliza hii namba unayotumia ya nani?" alisema binti halafu akamgeukia Jane "Hahaa Shoga angu nachati na Tino hajui kiingereza hata kidogo" binti alisema kwa dharau kidogo


"Tino ndo yupi?" aliuliza Jane


"Yule kijana mvuvi na we" binti alisema


"Hahahaaa"alicheka tena


Mara tino alijibu message "sawa, simu ni ya mshikaji wangu aitwaye Dickson"


"Powa, nitakucheki mida naenda kishuti video ya Harmonize"


"Harmonize???" mshkaji alishtuka sana


"Ndiyo mbona kama umeshtuka"


"Msanii mkubwa sana huyo mbona" alisema mtaalam


"Kawaida" alijibu binti "Byee mwaya baadaye nitakutafuta"


Ilibidi Tino amrudishie simu Dickson, bila hata kufuta namba ya Tina. 


Dickson akaweka simu mfukoni na kuelekea zake kwenye Jobu lakini Tino akaketi zake chini huku akitafakari namna ya kupata kazi


Hata hivyo Tina na Jane wakiwa kwenye bajaj walikuwa wakipiga story za kudanga


"ina maana jana Mheshimiwa alionyesha shoo au ndo hamna uno kabisa" Jane aliuliza


"Kimoja tu chali nikasepa mimi"


"Bila hela?" Jane alipenda hela sana


"Weee alinipa hela yangu, ila Unajua Tino ni mstaarabu sana?" Binti alisema alijikuta akimchanganya Tino kwenye story zisizomuhusu


"Toba, Tino katoka wapi tena huku? We Tina nimeshtuka ushampenda yule kijana mchafu bila kujua" Jane aliongea


"Hapana siwezi nikampenda yule, mimi sipendagi mwanaume wewe"


"Haya tutaona" Jane alisema


Safari yao ilishia katika maeneo ya Derm Plaza, hapo ndipo walitakiwa washuti kideo cha wimbo mpya wa Harmonize ambao pia jina halikujulikana kwa watu wengi maana ulikuwa haujatoka.


Kulikuwa na shamra shamra Hanscana huyu hapa, Jose wa Mipango, Konde Boy huyo hapo, Ibraa Tz n.k


"Mtotooo" Hanscana alianza mbwembwe


"Hahahaha, wewee Hanscana ushaanza" binti alisema 


"Nikumbatie basi jamaniiiiii" Hanscana alimtania


"Sitakiiiiii" Alisema binti


"sawa, na ntamwambia kaka Kondeboy asikulipe shauri yako" 


"Hahaha bwana, embu kwanza nitumieni wimbo huo niusikilize kidogo"


"Weee ukausambaze wakati hautoki siku za karibuni, utasikilizia hapa na kuuacha hapa hapa" Alisema Konde


"Haya bwana"

"Tushuti vipande vya kwanza sasa, wee nendeni mkabadilishe mavazi" Hanscana alisema


Basi ilikuwa ni shamra shamra za kuchukua video tu mpaka usiku ndiyo waliweza kurudi nyumbani


"Mambo" Tina alituma sms kwenye namba ya Dickson ajue kama ataweza kuchat na Tino


"Safi, samahani Sipo home nikifika nitampa Tino achat na wewe" alisema Dickson mara Binti akampiga


"Hallooo mambo kakaa angu, usisahau please and please unisaidie niongee naye" alisema binti


"Usijali maa" mtaalam alijibu


"pouwaaaah" Alisema Tina na kukata simu


"Daaaaah kudadadeki huyu demu gani ana sauti kama hii, halafu ndo anamsumbua Tino kudadadeki" Alisema Dick kwa mshangao


Ilibidi aingie whatsapp aangalie DP ya huyo binti ili ajue ana kasoro gani hadi amtafute Tino 


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog