Search This Blog

Thursday, 19 May 2022

HEHEEE. KANTANGAZEEE!!! - 5

 











    Chombezo; Heheee. Kantangazeee!!!
    Sehemu Ya Tano (5) 




    Ninafumbua macho yangu, ninashangaa nipo kitandani nimelala. Ninajaribu kuvuta hisia mahala nilipo, ninashindwa kung’amua mara moja kuwa nipo wapi na



    kwa nini.

    Ninainua mkono wangu ninauona mzito. Ninautazama kwa nini mzito, ninauona mpira mwembamba ukiwa katika mkono wangu wa shoto! Ninautazama vizuri



    ninaiona sindano imeuchoma mkono. Ninaufatilia huu mpira ninauona umeelekea juu. Ninainua macho yangu kuutazama ulipoendea, ninauona ulipoishia kuna



    Dripu ikiingia mwilini mwangu! Ninapata wasiwasi Dripu tena, ninaangaza huku na kule, ninaviona vitanda vingine vikiwa na watu wamelala. Ninawatizama



    kwa makini ninayaona maandishi meusi katika shuka nyeupe yanasomeka AMANA HOSPITAL. Ninajiuliza ina maana mie nipo hospitali?! Ninavuta hisia



    imekuwaje hadi niwe hapa, ninakihisi kichwa changu kinauma na kinakuwa kizito!

    Ninatulia sijui nifanye nini uzito kwa kichwa changu unazidi kunielemea. Nikiwa nimelala ninamuona mtu anasogelea katika kitanda changu. Ninamtazama kwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    makini ninamuona ananikenulia meno yake anatabasamu.

    Ninamtazama bila kumsemesha ingawa sura yake siyo ngeni usoni mwangu. Ila kumbukumbu zangu ni chenga tupu.

    “Pole Dobe, nimekupigia simu yako imepokelewa na mtu mwengine amenambia umeanguka unapelekwa Amana Hospitali ndiyo nikangoja muda wa kuwaona



    wagonjwa saa kumi hii jioni, nimekuja kukutazama pole sana.”

    Ninamtazama kwa makini na sauti yake ninaiingiza katika mizani yangu ya akili ninaiona kama nimeshaongea nayo kabla ya leo.

    “Wewe ni nani kwani na nani alikupa namba yangu ya simu?!”

    Ninamuuliza nikimtazama usoni kwake. Ninamuona anatabasamu kijinga.

    “Ama kweli Dobe umeumia, hivi ni kweli mie umenisahau?! Inaonesha wewe umeangukia kichwa kwani usingeweza kunisahau hivihivi tu. Namba ya simu



    umenipa wewe mwenyewe!”

    Majibu yake hayo ninavuta tafakari lakini sikumbuki kama nimempa namba yangu.

    “Wapi nilipokupa namba yangu wewe?”

    Ninamuuliza kwa hamaki lakini ananituliza kwa mkono wake na kisha ananambia kwa utuo.

    “Pole sana Dobe utapona tu usijali, mie ninakwenda kulipia matibabu yako kisha niwaulize madakitari kama wanaweza kukuruhusu, ikiwa utaruhusiwa basi



    tutakwenda sote nyumbani kwangu, sawa Dobe?”

    Ninabung’aa tu ninatoa macho sijui nimjibu nini kwani, simkumbuki, kichwa changu kinazidi kuwa kizito sasa ninasikia kama muungurumo ndani ya kichwa.

    Ninamtafakari mtu huyu anaponambia akanilipie huduma za matibabu, anazidi kuniumiza kichwa. Ninamuona anaondoka nami ninamtizama kwa nyuma, hadi



    anaingia katika chumba.

    Ninatazama kule ndani ya chumba nikiwa hapa nilipo, ninamuona yule mgeni akizungumza na watu waliovaa nguo nyeupe, wakioneshea kidole kwangu. Mara



    ninamuona mwanaume mmoja kutoka katika chumba kile akinijia hadi kitandani.

    Muungurumo kichwani kwangu na upepo mwingi ninauhisi ukitembea kutoka upande mmoja kwenda mwengine!

    “Unaendeleaje sasa hivi?”

    Ananiuliza huyu mtu alietoka kwa wenzake.

    “Niendelee nini wakati mie ninataka kuwahi kazini kwangu mnanichelewesha tu hapa, hebu kaniwashie mashine yangu nimpe huduma Baby Girl Mwanamtama,



    yupo hapo ananisubiri!!!”

    Ninaposema maneno hayo ninamuona huyu mtu alievaa nguo nyeupe ananikazia macho.

    “Mbona unanitisha wewe, mie pia dereva ujue kama wewe vile, unabisha nikuwekee gia sasa hivi?! Mwambie Baby Girl Mwanamtama apande mbele wewe ukae



    nyuma niwapeleke beach mkapunge upepo!!!”

    Kila nikizungumza, ninamuona huyu bwana ananishangaa. Atatingisha kichwa chake kwa masikitiko!

    Na mie ninamuigiza kwa kutikisa kichwa changu kama yeye! Ninapofanya hivyo ninamuona huyooo anageuza alipotoka huku akisikitika.

    Mara baada ya muda kidogo ninamuona ananijia akiwa ameongozana na wenzake waliovaa nguo nyeupe.

    “Dobe hujambo mpenzi wangu?”

    Mwanamke mmoja ambae amevalia nguo nyeupe na kikofia kidogo cheupe juu ya kichwa chake ananiuliza.

    Kabla sijamjibu ninatabasamu kwa sauti kubwa.

    “Karibu tule chakula, kisha umpe na Baby Mwanamtama nae ale.”

    Mara ninawaona wakitazamana kisha wakiinua vichwa vyao juu chini kwa pamoja. Nami ninawaigiza pia huku ninacheka sana!

    Mara ninawaona wananikamata, kisha huyu mwanaume ananichoma na kitu chenye ncha kali.

    “Huyu bado amechanganyikiwa kwa dawa na maumivu ya kichwa. Kwa hiyo bado anachanganya habari, sindano hii itakwenda hadi kwenye ubongo. Atakaa sawa



    taratibu, fahamu zake zitamrejea.”

    Ninayahisi maumivu makali sana, mwili unanilegea, nguvu zinanishia kwa haraka. Kiza kinatanda machoni.

    SAA TATU BAADAE.



    Ninainuka kitandani ninakaa kitako kitandani huku mwili wangu ukiniuma sana. Ananijia mtu mbele yangu nisiemfahamu.

    “Vipi Dobe hujambo?”

    “Sijambo nasikia njaa sana, na kichwa nakisikia kizito sana, kwani kimetokea nini?!”

    Ninamuona huyu mtu anatikisa kichwa kisha anatabasamu.

    “Pole sana Dobe, kwani hakika ulikuwa ni mwehu saa tatu zilizopita. Hapa upo Hospitali Amana, mie ni Daktari Mwaky Shola. Uliletwa hapa ukiwa



    umeangukia kichwa sehemu ya kichogo, hivyo MEDULA OBLANGATA ilicheza kidogo. Ulianguka mara baada ya kupewa habari za msiba, hii ni kwa mujibu



    wa watu waliokuleta hapa walivyoeleza.”

    Ninamtazama kwa makini huyu bwana, hakika ninamuona amevaa mavazi ya utabibu meupe mwilini mwake. Vifaa vya kupimia mapigo ya moyo, vikining’inia



    kifuani mwake.

    “Dokta umesema msiba, msiba, msibaaa, aaaagh Baby Girl hapana usife mpenzi, bado ninakuhitaji mpenzi. Siamini kama umeniacha hivi”

    Kumbukumbu zangu zinanijia kwa kasi. Ninakumbuka msiba wa Mwanamtama, ndiyo uliyonifanya nianguke ila sikutambua kutokea nilipoanguka



    kilichoendelea nyuma yangu, hadi sasa hivi kumbukumbu zinaponirejea tena.

    “Dobe nyamaza kulia, wewe ni mwanaume. Ulimpenda Baby wako, lakini Mungu amempenda zaidi yako. Tumeumbwa kwa udongo, tutarudi kwa udongo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mbele yake nyuma yetu. Jikaze kwani hili limeshatokea. Ukiendelea kuwaza jambo hili unaweza kudata bure, kwani saa chache zilizopita kama siyo juhudi zetu,



    hakika ulishakuwa chizi kabisa. Unaulizwa Kunde wewe ulikuwa ukijibu Choroko!”

    Ninainua uso wangu ninamtazama daktari kwa uchungu, kisha ninashika kichwa changu, machozi yananitoka mtoto wa kiume. Moyo unaniuma. Kweli kifo



    kimeumbwa, lakini pia msiba huwa mchungu kwa mtu wako wa karibu.

    “Jikaze ndiyo ukubwa huo, kisha hapa hospitali siyo mahala pazuri, kama ukiwa hivyo ulivyo itabidi tukulaze, sasa unaweza kupata maradhi ya kuambukiza hapa



    bure, matokeo yake ukawa ulikuja na kadha ukaondoka hapa na kadha wa kadha. Jikaze ili ukaugulie nyumbani, kwani hii dripu ikesha tu na hali yako ikiwa hivi



    unavyo jifahamu, basi tutakupa ruhusa, kwani gharama za matibabu umeshalipiwa tayari hudaiwi.”

    Ninamtazama huyu Dakitari anaponambia kuwa gharama za matibabu, nimeshalipiwa ninashindwa kumuelewa.

    “Dokta ni nani alienilipia mie gharama za matibabu?”

    Dokta ananitazama kisha ananambia.

    “Alipokuja kukutazama ulikuwa bado upo kwenye maruwe ruwe ya dawa na maumivu. Hivyo ukashindwa kumfahamu. Ila ametaka jina lake tulihifadhi



    tusikutajie kwa vile na wewe hukuweza kumtambua alipokuja awali, ila amesema kabla ya kukupa ruhusa tumpigie simu, ili akufate akuchukue kwani amejinadi



    kuwa wewe ni mtu wake wa karibu sana!”

    Maneno ya Dakitari yananifanya nisahau uchungu wa kufiwa na nimpendae, nishughulike na huyo mtu alienilipia ambae kumbe alinijia hapa mie nikiwa



    nimechanganyikiwa hata nikashindwa kumtambua.

    “Samahani Dokta ninaomba unitajie japo jina lake tu, au umbile lake namna alivyo, au jinsia yake tu kwani nipo njia panda hapa.”

    Lakini Dakitari anakataa kata kata kunambia kwa madai eti analinda usiri aliowekeana na mteja wao.

    Ninakuwa mpole ninasubiri Dripu lishe, mara ninakumbuka simu yangu. Ninajipapasa kuitafuta mifukoni mwangu.

    “Unatafuta kitu gani?”

    Dokta ananiuliza, bila shaka kunipima kama nipo sawa bado au laa.

    “Natafuta simu yangu.”

    Ninamjibu kuwa ninatafuta simu, anaingiza mkono mfukoni mwake ananionesha simu yangu anayo yeye!

    “Simu yako nimekabidhiwa mie, na waliyokuleta hapa, hivyo mie ndiyo nimeizima ili kukataa usumbufu wa kelele ya simu hapa wodini, lakini pia wewe



    mwenyewe hukuwa na uwezo wa kumjua mtu aliekutembelea tu, sembuse simu? Hivyo nitakukabidhi ukiruhusiwa mie nipo na wewe hadi saa nne usiku.”

    Ninakubali maneno ya dokta kwa shingo upande, kisha ninakaa kimya nikitafakari mustakabali wa maisha yangu. Nilipotoka, nilipo sasa na ninapokwenda.

    Ninapata kugutuka kitu, dokta anaitazama Dripu ikiwa inaishia.

    “Dokta samahani sana.”

    Dokta ananitazama kisha anasogea karibu name kinisikiliza.

    “Dokta nimeshafika hapa tafadhali ninaomba unipime Virusi vya Ukimwi kabisa ili nijijuwe.”

    Dokta ananitazama kwa makini.

    “Kwa nini unataka kupima Virusi Dobe?”

    “Ili nijue afya yangu.”

    Namjibu kwa mkato. Dokta anatikisa kichwa juu chini.

    “Baadhi ya watanzania wanataka kupima Virusi, kwa sababu ya mambo makuu matatu. Kwanza kama mpenzi wake akiwa amemwambia amepima amekutwa na



    maambukizi. Pili kama amesikia mwanamke/mwanaume aliewahi kufanya nae Ngono zembe amekufa kwa Ukimwi. Na tatu mtu akiwa anakonda na heshi



    kupatwa na maradhi nyemelezi, ndiyo anataka apime afya yake. Lakini wakutaka kupima ili watambue afya zao ni wachache sana.”

    Dokta anaposema maneno hayo ananichoma moja kwa moja moyoni mwangu, kwani mie sababu yangu ya kupima hasa ni baada yakusikia baby Mwanamtama ni



    muathirika, na ameshakufa tayari.

    Dokta anakwenda kuchukua vipimo vyake, kisha anakuja navyo nilipo. Anaitazama Dripu yangu inamalizia matone ya mwisho kadhaa. Anaifungua mkononi



    mwangu, sindano inatoka na damu.

    “Basi imekuwa kheri Dobe damu hii hii inatosha kupimia sitokutoboa tena.”

    Anaposema maneno hayo damu yangu anaidondoshea katika kifaa maalumu cha kupimia kama umeambukizwa virusi au laa. Mkono wangu ananiwekea Pamba



    yenye spirit ananambia niishikilie kwa muda ili damu isitoke, nami ninafanya hivyo.

    Anakitazama kipimo changu ananitazama usoni.

    “Dobe umeshawahi kupima VVU siku za nyuma?”

    “Hapana Dokta sijawahi kupima VVU.”

    Ninamjibu hivyo ili asianze kunipa majibu kwa matokeo ya kulinganisha na vipimo vya nyuma bure.

    “Ok umeoa wewe?”

    “Hapana sina mke.”

    “Una mchumba au bibi unaeishi nae?”

    “Dokta nambie tu bwana kama nishaukwaa. Unanizungusha bure tu. Mara mke mara mchumba au Bibi, mie mwanaume rijali nitakosa wapi mambo hayo?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nichane tu kama nishaungua nijijuwe.”

    Dokta anakitazama kipimo changu, kisha ananitazama.

    “Dobe nikikwambia kuwa umzima hujaathirika utafanyaje? Na nikikwambia umeathirika vile vile utafanyaje?”

    Yaani hapa napigwa maswali ya mitego tu aaah.

    “Dokta haya maswali yenu ya namna hii ndiyo mnawafanya watu wafe kwa presha nyie. Sasa nikiambiwa mzima nifanyeje kama sikufurahia kuwa



    nimesalimika?! Na ukinambia nimeukwaa ni lazima nitahuzunika, hakuna mtu anaepima virusi vya Ukimwi, kisha aambiwe ameambukizwa akafurahi au



    akaweka Rusha Roho (KIGODORO) nyumbani kwake, nambie tu nijue moja. Maana unanichosha kabla hata ya majibu”

    Ninamwambia huyu Dokta huku mapigo ya moyo yananienda mbio kinoma wahaka umenizonga, mashaka yamenijaa! Jasho linanitoka kama maji. Kifupi sina



    amani kabisa. Kupima siyo kazi mjamani, bali unapopokea vipimo ndiyo utaijua Junjunlai!







    “Haya nimekusikia Dobe, sasa kipimo kinaonesha wewe……!”

    Dokta anakatishwa kumalizia kunambia majibu yamgu na mtu anaefika hapa huku akinikenulia meno yake.

    Moyo wangu unastuka ninapomuona, damu inatembea kwa kasi katika mishipa yangu. Inanizidisha jasho kunimwaika.

    “Dokta anaendeleaje Dobe kwa sasa, keshakuwa vizuri?”

    Dokta ananigeukia mie huku akiacha kunimalizia kipimo changu, anamjibu yeye.

    “Mungu ni mwema kwa kweli. Ametupa ushindi na Dobe anaendelea vizuri sana”

    Anasema maneno hayo kisha ananambia.

    “Dobe huyu ndiyo aliekulipia gharama za matibabu yako“

    Ninabaki kinywa wazi kabisa. Huyu ndiyo aliyonilipia?!!!





    Ninamuona mlipaji na mfadhili wangu anatabasamu.

    “Asante sana Jesca kwa mchango wako wa hali na mali.”

    Ninamwambia mfadhili wangu nae anainama kupokea shukurani hiyo.

    “Pole sana Dobe, ninakusubiri ili tuondoke sote nyumbani ukapumzike.”

    Jesca ananambia maneno hayo huku anatabasamu.

    “Asante ila ninaomba falagha kidogo ninamaongezi na Dokta.”

    Dokta nae anamthibitishia hilo la falagha. Jesca au SHEMALE anatoka nje ya wodi, huku akiwa na wingi wa kujiamini.

    “Dokta sasa naomba unambie hayo majibu tafadhali usinizungushe tena, wakaja watu wengine.”

    Ninamwambia Dokta huku nimemkazia macho kwelikweli.

    “Dobe punguza wahaka kwani nilikuwa nakueleza ila yule mfadhili wako akaingilia kati hivyo nikashindwa kutoa majibu mbele yake. Natambua majibu ya VVU



    ni siri ya mpimaji na anaempima.”

    Dokta anasema maneno hayo kisha anainamisha macho yake kukitazama kipimo, alichokuwa nacho mkononi mwake, kisha ananigeuzia macho yake nami



    ninamtazama kwa makini.

    “Dobe kipimo chako kinavyosoma hapa, inaonekana hujaathirika bado. Ila kitu cha kuzingatia hapa ni kwamba. Ikiwa umepata maambukizi katika siku mbili, au



    tatu nyuma, huwezi kuonekana katika kipimo kuwa umeathirika. Ila ninakushauri ukae kutoka tarehe ya leo uliopima hadi upate miezi mitatu upime tena. Ikiwa



    hapo hutoonekana umeathirika basi tunasema utakuwa upo salama. Ingawa unashauriwa pia katika kipindi hiki cha mpito upime mara tatu kwa uhakika zaidi,



    lakini ujichunge na ngono zembe.”

    Dokta anaponipa majibu, mwili wangu unarowana zaidi na jasho, kama nimekoga na nguo!

    Kweli mie mzima?! Kuanzia leo na siku zijazo, sitaki tena kukaza iwe mbele au nyuma. Ninaacha kabisa.

    Ninajisemea kimoyomoyo huku nikiuona mwili wangu unapata nguvu kubwa sana. Ninayatafakari maneno ya Dokta kisha ninamgeukia.

    “Dokta samahani sana, ninaomba nichome sindano uniuwe mkuyati wangu usiwe na nguvu tena!”

    Ninamwambia kwa dhati, kwani inaweza kuniangaaza, kisha ikanipa mashaka bure.

    “Sikia Dobe. Usifanye jambo hilo hata mara moja katika maisha yako. Uanaume wa mtu ni uume imara wenye nguvu. Unapotaka kujichoma sindano kisha



    utafanyaje ikiwa Mungu atakupa maisha marefu, si utadhalilika bure? Lakini ninakushauri kabla hujafikiria mara mbili jambo hilo, basi ungoje miezi mitatu



    ipite ili upime tena. Majibu ya baada kipimo hicho ndiyo yatakupa muelekeo.”

    Furaha imenijia katika nafsi yangu sana kwani moyo wangu ulikuwa tayari ushanyong’onyea.

    “Dokta naomba simu yangu na ruhusa, nishapona mie.”

    Dokta anatabasamu kisha ananambia. Subiri nikuandikie ruhusa na simu yako nitakukabidhi utakapokuwa unaondoka.”

    Dokta ananambia maneno hayo kisha anapiga hatua anakwenda ofisini kwake. Hakika amefanya hekima sana kubakia na simu yangu, lau angelikuwa



    ameshanikabidhi nisingengoja hiyo ruhusa yenyewe ningesepa tu.

    Ninamuona SHEMALE jesca anaingia huku macho yake ameyatizamisha mahala nilipo. Anatembea kwa kujiamini hadi ananifikia nilipo.

    “Dobe pole sana, nilikupigia simu leo akaipokea kijana mmoja akanambia mwenye simu umepata matatizo umeanguka, hivyo umeletwa hapa ndiyo nikaja lakini



    namna niliyokuona nayo mwanzo, nikatambua hakika ulikuwa unaumwa sana. Kwani nilishangaa kuwa ulikuwa ukinikataa kuwa hunitambui. Ila madakitari



    nilipokwenda kuwaeleza hali yako wakakupa huduma bora baada yakuwaambia gharama zote za matibabu nitatoa mie, wakanitaka nitoe kabisa nami sikusita

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kufanya hivyo.”

    “Jesca asante sana kwa mara nyingine kwa msaada wako. Haya uliponipigia simu bila shaka ulikuwa na jambo ulilonitafuta nalo, je umeshanipata sasa niambie.”

    Ninamuona Jesca akitabasamu kama kawaida yake.

    “Dobe ulinambia unajifikiria hivyo nikakupigia simu ili nijue ulipofikia kwani nafasi ya kazi ninayotaka kukupa, ina watu wengi wanayoitaka. Hivyo



    nisingependa unijibie hapa laa, ningependa unijibu tukitoka hapa tukifika nyumbani.”

    SHEMALE amekaza nami ninajua anachotaka ila amechelewa sana. Sasa hivi sitaki tena kuwa kama awali, nishakoma kabisa. Hata kama nipewe nini sitaki tena.

    “Sawa nimekusikia. Ila nitaomba tukaongelee nyumbani kwangu kwani sijui hata kupoje tangu nilipoondoka. Mama mwenye nyumba wangu amefariki nawao



    ndiyo walionisababishia haya hadi nikawa hapa.”

    SHEMALE ninapomwambia maneno hayo, ninamuona anabadilika sura na kuwa mtu aliechukia, japo hakupenda kunionesha machoni.

    “Sawa Dobe nimekuelewa hakuna neno nitafanya utakavyo ili uwe na amani.”

    Ninafarijika kwa kukubaliana na mawazo yangu.

    Dokta anawasili ananipa cheti changu na dawa za kwenda kutumia ili afya yangu izidi kutengemaa. Ananipa simu yangu kisha ananipa mkono na kuagana nami.



    Ninageuka ninashika njia kuelekea nje ya wadi ya wagonjwa. SHEMALE Jesca hachezi mbali namimi, ninamuona anaunga tela kwa karibu kabisa.

    Ninatoka hadi nje ya jengo, Jesca ananielekeza gari yake alipoiegesha ninamfata na tunapoifikia gari yake, anatoa lock za milango tunafungua milango na kuingia



    ndani. Jesca anawasha gari tunaanza safari kuelekea Tabata Segerea.

    Mwendo wa kimya kimya ndani ya gari hakuna mwenye kumsemesha mwenzake.

    “Jesca washa radio basi kwani naona ni kimya tu kama tunawenda kuzika.”

    Ninaanzisha mazungumzo na yeye hanijibu bali anafanya vitendo anawasha radio kwa sauti ya wastani, kisha macho yake mbele anaendesha kwa umakini kabisa.



    Tunakwenda katika mwendo huo hadi tunafika Tabata Segerea nyumbani kwangu. Lakini ninapoukaribia mlango wa nyumba, ninapigwa na butwaa. Mlango



    umefungwa umetiwa kufuli kubwa kuonesha hakuna kuingia mtu tena humu ndani!

    “Haya Dobe fungua mlango tuingie ndani tuzungumze.”

    Jesca ananambia maneno hayo kama haoni kuwa mlango umefungwa na kufuli na mie sina funguo yake. Ninajiuliza ninaishishe sasa. Sijui msiba ulipo, lakini



    hata kama imeamriwa nyumba ifungwe sawa sina ubishi juu ya hilo lakini kuna vitu vyangu. pamoja na nguo ninazipataje?”

    Ninawaza sipati jibu la maswali haya.

    “Dobe vipi tena mbona tunaganda nje tu, kulikoni au umesahau ufunguo wako?”

    Ninamtazama kisha ninautazama mlango kwa kukata tama

    “Mie wakati nimeondoshwa hapa sikuwa na fahamu. Hivyo sitambui funguo ya kufuli hii ilipo, lakini pia mlango huu huwa haufungwi na kufuli!”

    Ninamjibu Jesca aliekuwa anataka kunitia ujinga kwa kumuweka nje.

    “Ok kwa hiyo unakubaliana na mimi sasa kuwa tukazungumzie nyumbani au bado unataka kuzungumzia kwako?”

    Ninatafakari kwa kina kisha ninajiuliza ikiwa nitaendelea kukataa kwenda kwa Jesca na hapa ndiyo mlango ushatiwa kufuli nitakuwa mgeni wa nani? Lakini pia



    maisha bila kazi nitaishije. Ninapofikiria hivyo ninajikuta ninakubaliana na Jesca kwenda nae nyumbani kwake kwa shingo upande.

    “Usiwe na wasi Dobe, kwangu pia ukitaka kulala nina vyumba vya kutosha, ikiwa hapa hutofunguliwa tena mlango sawa?

    “Sawa.”

    Jesca anafurahi hadi jino la mwisho, huku akitangulia kwenda kwenye gari. Nami ninamfata kwa karibu. Mie sipendi kabisa kwenda kwake lakini ninafanyaje,



    kwani sasa nimekuwa wakuogopwa kama ukoma!

    Jesca anaingia garini kisha ananifungulia mlango niingie nami ninajiachia kwenye gari yake habari sipati. Jesca anaendesha gari tunatokomea hadi katika wilaya



    ya Kinondoni, Nyumbani kwake anapiga honi geti linafunguliwa anaingiza gari hadi ndani. Tunapofika ninapitishwa moja kwa moja hadi chumbani kwake,



    ninafikishiwa kitandani!

    “Dobe punguza nguo zako kusudi zisijikunje, upumzike kwanza nifanye maarifa ya chakula tule kabisa kisha tutaanza mazungumzo yetu.

    Ninamjibu sawa kisha Jesca ananiletea Khanga nivae ili kunusuru nguo zangu zisikunjike. Kwa adha ya Khanga ilivyonisibu, inabaki kidogo tu nikatae kuivaa!

    Ninazivua nguo zangu, ninavaa Khanga, kisha ninajibwaga kitandani . Jesca anachukua nguo zangu anatoka nazo nje.

    “Muda unakwenda, sasa hivi itaingia magharibi.”

    Ninamwambia Jesca ili ahimize hicho chakula.

    “Usiwe na wasi bwana Dobe utakula sasa hivi.”

    Ninakuwa mpole ninasubiri chakula kwani utumbo sasa ninausikia kuwa unadai amana yake.

    Ninaiwasha simu yangu kutazama ujumbe wowote kama umetumwa, lakini naona simu haina jipya.

    Jesca anabeba nguo zangu anaondoka nazo nami simfatilii ninajilaza tu kitandani bila kujua ameelekea wapi katika hiki chumba chake chenye choo ndani.

    Baada ya dakika kama ishirini na tano hivi Jesca anaingia na chakula anaweka chumbani kwenye meza ndogo.

    “Haya ulilalamika njaa chakula hichi hapa ushindwe mwenyewe.”

    Nitamtazama Jesca kisha ninatabasamu kichovu.

    “Asante sana kwani wadudu wa njaa wananitakua siyo mchezo.”

    Ananinawisha maji kisha ananipa chakula katika sahani, ninaanza kula kwa haraka kwani hali mbaya sana tumboni. Ladha ya chakula ninachokula hakiingii katika

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    chakula cha Baby girl hata robo! Ninakula nifanyeje nisije kufa kwa njaa.

    Jasho linanitoka kwa wingi, ninamaliza kula ninaingia msalani ninashindwa kuyaamini macho yangu kwa kitu ninachokiona!

    Nguo zangu jesca amezitia kwenye beseni la maji, ameweka na sabuni ya unga juu zimerowana ndembendembe!

    Ninazihakiki kama ndizo nguo zangu hasa, ninazitambua ndizo. Ninashindwa kwenda haja ninatoka ninamkuta akiondosha vyombo.

    “Jesca sasa ndiyo umefanya nini? Mbona nguo zangu umeziroweka tena wakati mwenzako sina nguo za kuvaa zaidi ya zile?”

    Anatabasamu kijinga!

    “Nisamehe mpenzi kwa kuziweka nguo zako katika hali ya kuziandaa kuzifua. Nguo zilikuwa na vumbi kama nini, huwezi kuwa na mie kisha uwe mchafu



    Dobe.”

    Nikiwa ninatafakari kuhusu nguo zangu, mara mlango wa chumbani unabishwa hodi. Jesca anainuka kwenda kumsikiliza anaegonga mlango nami ninaingia



    chooni kujihifadhi lakini pia kufanya haja zangu.

    “Ohooo karibu shoga yangu, karibu sana. Mbona umepotea hivi jamani kwema?”

    “ Kwema Shoga. Kabla sijakuzungumza kilichonileta acha kwanza niende chooni kujisaidia kwani kojo limenibana saa nyingi kweli!”

    Sauti hiyo ninaisikia kwa fasaha, mwili wangu unapata ganzi. Ninakuwa na hasira sana ninawaza akiniharibia hapa na nguo zangu zisharowekwa kwenye maji,



    nikitimuliwa nitatoka vipi?! Kichwa kinauma kwa mawazo. Huyu amefata nini huku? Ninajiuliza.





    “Msalani kuna mtu shost fanya subira kidogo.”

    Ninamsikia Jesca akimwambia Njasi maneno hayo, nami ninasikiliza maneno yao, haja imeniruka imekwenda mbali nami kwani huyu keshakuwa siyo mtu mzuri



    kwangu.

    “Hee?! Makubwa haya shost! Choo chako umuingize mgeni kwani choo cha wote hukumuonesha? Au mchuchu huyo Jesca?!”

    “Haloooow, Kanchomekee!!! Chezea mie wewe utalala hoi!”

    Jesca ninamsikia akicheka cheko la kedi, nami ninazidi kuvutika na mazungumzo yao. Umbea umenishika Siendi haja kubwa, wala ndogo. Nimebaki chooni



    kama mende!

    “Sasa kama ndiyo mchuchu yupo chooni, basi mie nakwenda zangu shost, nikuache upige show yako kwa utuo.”

    Njasi anamwambia Jesca nami ninaombea aruhusiwe tu ende zake kwani akikaa huyu chango mzaa maradhi ataniharibia tu. Anaweza kusababisha nikaondoshwa



    na Khanga tena huyu!

    “Hapana shost, huwezi kuondoka hivyo juu juu, kama nywele za kichwani, nipe huo ubuyu kwanza kisha umsalimie shemeji yako, ndiyo wende zako. Mtu



    umeniacha kwenye Taharuki, kisha utaondokaje uniache ninaning’inia bure. Mwenzako ukimtia nyege ni budi ummalizie kabisa!”

    Ninamlaani Jesca kama nini! Sasa anisalimie mie ili iweje?! Huyo Njasi siku hizi ni nuksi tu, amegeuka Mung’unye aharibikia ukubwani! mwache apige bunda



    bwana aaah atazingua tu huyo! Ninajisemea kimoyomoyo chooni, haja sina kabisa imekimbia.

    “Shost mbona nimeyakanyaga mwenzako?! Nimejitia utaalazi wa kupiga show na mtu muathirika, nika shere nae mkuyati, kumbe shost ninajiingiza katika



    Mkenge! Huyo bwana mwenzangu ni fundi wa Matentelee lakini mmmmh sina amani hapa nilipo nina mashaka utasema nadaiwa na Kijumbe!”

    Njasi keshaanza yake sasa! Nikimuacha hadi amalizie story yake hapa ninatolewa Dima na Khanga kama siyo uchi kabisa! Maana hii siyo Kantangazee tena naona



    itakuwa ni Kanchomekee!

    “Hehee Shost usinambie, nani huyo kwani?!”

    Jesca anapofika hapo uzalendo wa kukaa chooni tu kusikilizia ubuyu, unanishinda ninaamua kujichanganya, ili japo Njasi aone haya kwa vile uso umeumbwa na



    haya, asimalizie kusema mineno yake ya falaka!

    Ninatoka chooni huku ninajifanya kujikohoza kwa nguvu, ili niwateke wanyamaze kuzungumza habari zangu na za Baby wangu. Alietangulia mbele ya haki



    ambae sitomsahau maishani mwangu.

    Ninamuona Njasi akigeuza sura yake haraka kwangu nilipo ili aonane na huyo mchuchu wa Jesca, uso wake na wangu unakutana macho yake ninayaona



    yanatahayari!

    “Haya nenda kwanza chooni, shem wako keshatoka kisha unimalizie ubuyu wangu.”

    Jesca anamwambia, lakini Njasi bado alikuwa amepigwa na butwaa kwani Khanga anayoniona nayo hapa, siyo aliyonishuhudia nikiondoka nayo kutoka kule kwa



    Qeenlyn. Hivyo akili yake bila shaka inamwambia nishacheza show sana hapa!

    “Shost huyu ndiyo mchuchu mwenyewe?!”

    Njasi anamuuliza Jesca kwa mshangao, huku akiyaangaza macho yake huku na kule.

    “Naam shost humkumbuki huyu wewe, anaitwa Dobe alikuwa pale katika Massage Sinza, kijana amenikaa rohoni huyu, kila siku nakumbuka mambo yake.”

    “Mmmmh”

    Ninamsikia Njasi akiguna kisha anashusha pumzi nzito.

    “Shost ninaomba nisindikize tu mara moja, kwani huo mkojo wenyewe ushaniruka kabisa. Hapa nipo sawa ila ukiuma nitapiga hodi nyumba yoyote ili nijistiri.”

    Ninaumiza kichwa mara moja, ninaona Njasi anataka kwenda kunimaliza akiwa peke yake na Jesca, wakati akisindikizwa.

    “Heeeh! Njasi ulinambia mkojo umekubana saa nyingi na ulipofika hapa tu ukataka wende chooni, sasa kimekusibu nini hata iwe huna tena haja?!”

    Jesca anaposema maneno hayo, kabla ya Njasi hajajibu lolote ninadakia.

    “Jesca my love, tunamsindikiza wote mgeni haachwi mtu hapa!!!”

    Ninamuona Njasi ananitazama kwa kuninyali, yaani ananiona kama vile ninasambaza VVU, angejua mwenzake nipo safi mbona na yeye angeyataka Matentelee?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kumbe Binaadamu anakuthamini ukiwa mzima na kumtimizia haja zake, ila unapopatwa na matatizo tu wanakutenga! Ama kweli kila mchuma janga hula na



    wakwao.

    “Dobe ninakutangaza sasa hivi, tena ukome tabia yako hiyo nakwambia!”

    Ninamtazama kwa dharau, ninatambua anataka kunitangaza kuwa nishaungua, ama kweli jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.

    “Heee?! Umtangazee tena, amefanya nini? Hebu nambie shoga yangu, kwani ninaona kama una kitu ambacho unakificha vile. Nikiunganisha matukio tangu



    ulipokuja hapa ukiwa na furaha, na sasa ulivyobadilika hasa baada ya kumuona Dobe, tafadhali niambie nini kinachoendelea?! Ni sababu gani hasa iliyokuleta



    kwangu?!”

    Jesca anamgeuka Njasi, nami ninataka kumkomesha pia maana amenidhalilisha vyakutosha. Japo sina ubishi Njasi ni mzuri wa umbo na mambo, lakini kila



    kizuri hakikosi kasoro, na kasoro yake ndiyo hii, ana dharau sana yaani.

    “Jesca shoga yangu, naomba unisikilize kwa makini.”

    Njasi anaposema maneno hayo ninaanza kumkemea kimya kimya ashindwe. Maana naona sasa anamwaga mboga, itabidi na mie nimwage ugali ili twende sawa.

    “Nakusikiliza shoga yangu nambie, usinifiche chochote.”

    Jesca ameshajaa upepo, anawahaka wa kujua hayo mambo.

    “Labda nikuulize tu shost wangu, na naomba unambie ukweli. Dobe umeshatembea nae hata mara moja?”

    “Bado shoga yangu.”

    “Kama bado nakushauri achana nae, Dobe siyo mzima ni muathirika.”

    Anaposema hivyo mie ninaangua kicheko kikubwa sana, huku sina wasiwasi kabisa. Jesca anashangaa sana.

    “Ameathirika?!”

    Jesca anamuuliza shoga yake. Mie ninaendelea kucheka kwa nguvu.

    “Sasa wewe nae unacheka nini? Jambo la hatari wewe unachekelea?!”

    Jesca ananiuliza kwa mshangao.

    “Ndiyo ujue kuwa huyo si mzima, virusi aliyvokuwa navyo, bila shaka vishampanda kichwani ameshadata!”

    Njasi anasema maneno hayo, lakini hajui mwenzake ninamfanya yeye aonekane kama anaetia fitina vile.

    “Hebu nambie maana ushanichanganya shost huyu anaumwa nini?! Yaani ameathirika na VVU? Wewe umemjuaje?”

    Jesca anamuuliza Njasi, nami sasa ninakaa kimya nisije kufikirika nimedata kama kule hospitali bure.

    “Nilipokuja hapa, nilikwambia kuwa nimeshere mkuyati na muathirika? Basi mkuyati wenyewe ni wa huyu bwana. Mwanamtama ameathirika na VVU anakula



    dawa na mumewe ameshakufa kwa Ukimwi, na hivi ninavyoongea na wewe huyo Mwanamtama nimepata habari nyepesinyepesi kuwa ameshafariki dunia. Hivyo



    Dobe kwa kuwa ndiyo alikuwa mpenzi wake, ninahisi sote mie na Dobe tumeathirika. Nakupenda shoga yangu, ndiyo maana ninakutakia mema. Kama utaona



    ninakuzibia rizki yako, haya endelea ila utakuja kunikumbuka.”

    Njasi anamalizia nukta yake ya mwisho ya kuharibu, nami ninatabasamu kwa kujiamini kabisa.

    “Mmmmh makubwa haya sasa, Dobe kuna ukweli wa maneno haya?!”

    Jesca ananiuliza huku amenikazia macho.

    “Jesca hayo ni maneno ya mkosaji anayoyasema shoga yako. Mie ni mzima kama chuma sina virusi nipo tayari twende hospitali yoyote unayoijua wewe, na



    kuiamini kwa vipimo vyao ili tukapime sote humu ndani. Huyo amekuuliza wewe kama umeshatembea na mie, Je?! wewe una Uke wakutembea nami?! Huyu ni



    fitina anaumia kwa nini mie nifanye show na wewe! Kwani ndiyo chaguo langu, wanawake nimeshafanya nao show wengi tu. Ila mtu wa namna yako, ni shida



    sana kukutana nae, huyo amejaa wivu tu.”

    Ninaamua na mie kumgeuka kwani ninachelea kutolewa dima na Khanga, na kule kwa Baby kuna kufuli unadhani nitakuwa mgeni wa nani kama siyo kwenda



    kulala vituo vya basi. Na huu upande wa Khanga nao niliokuwa nao na baridi hili, itakuwaje? Na hao Mazabania utawaachia wapi, kama hawajataka kula



    Ashaakum nikilala?! Hapa hatoki mtu yaani ninapambana hadi hatua za mwisho.

    “Njasi wewe umejuaje kama Dobe ameathirika?! Kwa sababu ametembea na muathirika au umepima nae?”

    Njasi anakosa jibu la maana lenye msingi.

    “Ok mie kwa bahati nzuri ninavipimo ndani kwangu. Nilipokuwa safari Marekani nilipata kuhudhuria semina moja ya SHEMALES nikapewa vipimo vingi tu,



    vingine nimegawa lakini vingine ninavyo hapa hapa ndani, mnaonaje sote tukapima tukaujua ukweli wa haya?!”

    “Safi sana tufanye hivyo, kwani Njasi amenidhalilisha sana, ameshasababisha nitembee uchi huyu, keshanitangaza sana kuwa mie ninao, kama ulivyomsikia hapa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Naona leo utakuwa umekata mzizi wa fitina kabisa.”

    Ninadakia kumwambia Jesca, ninamuona Njasi anarudi matawi ya chini kwa namna nilivyokuwa nimejiamini kupita kiasi. Jesca anafungua kabati lake anatoa



    bahasha kubwa katika droo la kabati, kisha anatoa vifaa vya kupimia VVU ambavyo havina tofauti kubwa sana na vile nilivyopimia leo hospitali.

    “Ninaomba nianze mie kwanza kupimwa.”

    Ninasema kwa kujiamini sana. Jesca anachukua spiriti anachukua pamba, anaichovya kwenye spiriti kisha ananisugua kidogo na hiyo pamba katika kidole cha



    kati, ananitoboa na sindano maalumu damu inatoka. Kisha damu yangu anaikinga katika hicho kifaa cha kupimia, matone kadhaa yanadondokea hapo. Jesca



    anatoa ufafanuzi wa namna ya kuelewa matokeo ili sote tuone kwa macho yetu.

    “Hichi kifaa baada ya dadika mbili tu, kitakuwa kimeshaisoma damu hii, na ikiwa imeiona haina maambukizi itachora mstari mmoja mwekundu hapo mbele, na



    kama ikiwa na maambukizi itachora mistari miwili hapo hapo.”

    Jesca aliposema maneno hayo, anakiweka hichi kifaa katika meza ya kioo iliyokuwa hapa chumbani, kifaa kinakaa sawa na mie ananipa pamba niweke katika



    kidole changu ili kukata damu isitoke zaidi. Macho sita yanakitazama hichi kifaa huku tukiwa kimya kabisa, mara mstari mmoja mwekundu unachora katika



    kifaa hiki! Ninainua uso wangu ninamtazama Njasi, ninamuona anatahayari anakuwa hana amani kama mtu aliefumaniwa.

    “Haya kantangazee sasa kama sina VVU, siyo unitangazee kuwa ninavyo tu, ukatangaze na hili la kupima mbele yako pia!”

    Ninamwambia Njasi ambae anakuwa hana neno, maneno yote yamemkauka kabisa kinywani mwake. Jesca ananibusu busu zito mbele ya Njasi.

    Mmmmmwaaaaaaaaaaaaaah Mie ninamtazama Njasi kwa jicho la husuda.

    “Haya zamu yako Njasi upime na wewe mbele yetu, kwani usiwe hodari kutangaza ya watu tu, na wewe pia tukutambue tukatangazane vizuri.”

    Ninamwambia Njasi, huku nikiwa na furaha na najiamini sana, kuwa japo hapa kwa vipimo hivi siwezi kuondoka na Khanga, hivyo kwa hilo tu ninajiamini.

    “Haya shost unahukumu kwa macho kisa tu kuna mtu ameambukizwa basi na wewe unaona mwengine aliekuwa nae atakuwa nao, VVU havipo hivyo. Wapo



    watu mke na mume wanaishi mmoja ana virusi vya VVU na mwengine hana kabisa, na wanafanya mambo yote ya ndani ya kuta 4. Ila ni muhimu tu



    mkishajitambua kuwa mmoja ni muathirika, mvae kinga ili msiambukizane”

    Njasi anasogea apime lakini ninamuona anabadilika uso wake, mapigo ya moyo yanamuenda mbio kama mshale unaosababisha sekunde! Jesca anamtoboa na



    kukinga damu yake katika kile kifaa, kisha kama ilivyokuwa kwangu sote tunatazama kipimo hiki kwa makini. Mara baada yakusomwa kwa kipimo macho yetu



    yanashuhudia kipimo kile kikileta majibu, Ninamtazama Njasi usoni, ninamuona machozi yanamtoka!!!





    Analia siyo kwa furaha hata kidogo bali majibu yake, yametoa alama au mistari miwili kuonesha damu yake inamaambukizi ya VVU.

    Jesca anamtazama usoni shoga yake kwa masikitiko.

    “Njasi Katangazee sasa kuwa umeathirika, wewe si hodari wakutangaza wenzako?”

    Ninamwambia maneno hayo kwa kedi bila kumhurumia kwa chochote kwani Mungu amemungaaza na mie ninamueleleza!

    “Dobe usiseme hivyo yaliyompata Kibeku na ungo yatamfika, kama umefanya Sexy na Njasi, basi amini muda huu ni wa mpito tu, usimcheke muathirika kwani



    huwezi kujua baada ya miezi mitatu na wewe utakuwa katika hali gani!”

    Jesca ananambia maneno ya kuonya ila hajui namna mwanamke huyu alivyonidhalilisha akasababisha nikatembea na upande wa Khanga ya kiuno.

    “Hata kama nitaonekana hivyo potelea mbali, lakini sasa sina! Huyo shoga yako amefikia kusema kuwa niogopwe kama Ukoma! VVU hakuumbiwa mwanamke



    wala mwanamme, hakuumbiwa mtoto wala mtu mzima, mbona alikuwa ananitangaza hata alipokuwa hana majibu ya kipimo cha damu yangu, lakini alikuwa



    akinituhumu kuwa nimeathirika, sasa imekuwa kinyume chake. Adhaniwae ndiye, kumbe siye, hii itakuwa fundisho kwa jamii nzima.”

    Ninasema maneno hayo huku sasa haja ikiwa imekata kabisa, yaani nina furaha hapa kupindukia.

    “Jesca pima na wewe tujue afya yako sie umeshatujua tayari, pima na wewe tukatangazane.”

    Ninamwambia maneno hayo huku nikiwa sitanii kabisa. Jesca ananitazama kisha ananambia.

    “Mie sina tatizo na kupima ninautaratibu wa kupima kila mwezi, nitapima mbele yenu nanyi mshuhudie.”

    Baada yakusema hayo anachukua kifaa maalum cha kutobolea anakifungua kutoka katika plastic lake anajitoboa, kisha anachukua kifaa cha kupimia anakinga



    damu yake matone kadhaa, anasubiri majibu ya kipimo. tunakitazama kipimo. Njasi anakitazama kipimo akiwa macho yake yamemjaa machozi. Kipimo kinatoa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    majibu mstari mmoja tu mwekundu unatokezea juu ya kipimo kile kuonesha kwamba damu iliyopimwa haijapatwa na maambukizi.

    “Mie nina bahati mbaya, jamani yaani Dobe awe mzima kisha mie nimeathirika?”

    Njasi anasema maneno hayo huku akilia na mie tu.

    “Kwa hiyo ulikuwa ukinambia mie nimeathirika kwa vile wewe umetembea na mie na ulijitambua kuwa ushaumia?”

    Ninamtolea maneno ya kejeli, kwani amenikera kupita kiasi.

    “Njasi kama lililokuleta kwangu ni kunambia Dobe ameathirika, imekuwa kinyume chake shost, je una lolote lingine au?!”

    Jesca anamgeukia Njasi anamfahamisha maneno hayo huku, akimtazama usoni.

    “Hapana shoga yangu, nimekuja na mengine ila kwa sasa yote yamenishia nakwenda zangu.”

    “Nenda tu Njasi, huna jipya na fitina zako.”

    Ninamjibu kisha anageuza sura yake ananitazama.

    “Kantangazee!!!”

    Ninamwambia huku nimemkazia macho.

    “Dobe sipendi unavyofanya mambo ya visasi namna hivyo hebu badilika.”

    Jesca ananambia, lakini hanibadilishi mawazo yangu. Njasi anaaga na kutoka nje ya nyumba ya shoga yake. Jesca anamsindikiza kisha anarudi na kunikabili.

    “Dobe sijapenda ulivyokuwa ukimuangaaza shoga yangu hata kidogo!”

    “Ahaa ila yeye alivyonieleleza wewe umefurahi si ndiyo?!”

    Ninamjibu huku nikiwa nimechukia sana. Mie nimetembezwa na upande wa Khanga yeye aliona vizuri?

    “Ok nimekuelewa naomba niende home mara moja kuna jambo la muhimu sana nikafate.”

    Ninamwambia Jesca ili nisepe zangu mbele kwani mambo ya kunyonyeshana Nembe Dume mtoto wa kiume siyo mazuri.

    Mahaba ya SHEMALE pamoja na ya shoga wa kiume, ukikwambia umnonye kinembe chake, tambua unakula Mkuyati yabisi! Ukiweza kula hiyo kitu yaani



    ndiyo unamnyonya hapo. Mie mmmh swaga hizo siziwezi pamoja na ubalamaki wangu wote.

    “Sasa utakwendaje na nguo zako nimeziroweka?”

    “Nitafutie hata bukta nitavaa na fulana zako hamna neno.”

    Ninamjibu na yeye ananambia.

    “Bahati mbaya bukta, suruali na fulana zangu zote zipo kwa dobi. Vinginevyo wende na Khanga tu.”

    Majibu hayo yananinyima amani kabisa. Ninaamua kutoka na Khanga kwani sina amani na mahali hapa kabisa. Jesca anadhani ninatania, kwamba sitoweza



    kuondoka na khanga lakini ninatoka kweli chumbani na nyumbani kwake, ninatembea nikiiacha nyumba yake. Ninakata mitaa hadi kwa madereva wa Bodaboda.



    Wanaponitazama wote wananishangaa sana, lakini mie ninauchuna kama nimevaa suti vile kumbe nina upande wa Khanga tu.

    “Ndugu yangu naomba unistiri, nguo zangu zimetiwa kwenye maji na mpenzi wangu na mie ninatakiwa kufika nyumbani kwangu, hivyo nimeamua kutoka hivi



    nilivyo. Naomba unipeleke nyumbani kwangu Segerea nitakupa pesa yako tukifika nyumbani.”

    Dereva wa bodaboda ananithaminisha kutoka juu hadi chini, kisha anajishauri sana hatimae, anapanda chombo chake kuonesha amekubaliana nami.

    Ninapanda nyuma ya piki piki yake, safari ya Segerea inaanza. Ninaumiza kichwa matukio yanayonitokea yameharibu kabisa maisha yangu. Dereva wa bodaboda



    anakatisha mitaa anacheza pembeni mwa barabara mara katikati ya barabara, hatimae tunafika nyumbani kwangu. Katika ajabu ninayoiona nyumba mlango



    ninaukuta upo wazi. Lakini hakuna dalili ya mtu ndani ya nyumba! Ninamwambia dereva wa Bodaboda anisubiri ili niingie ndani nimpe pesa yake, ananisubiri



    usawa wa mlango huku akinitumbulia macho.

    Ninaingia ndani kimya kimya hadi katika mlango wa chumbani kwangu, nao ninaukuta pia upo wazi! Moyo unanienda mbio, ninatia shaka huenda tushaibiwa



    tayari!

    Ninaingia taratibu hadi chumbani kwangu, hamadi nakiona kitu siyo cha kawaida! Ninaliona kawa limefunikwa katika sinia ikiwa juu ya stuli! Ninashangaa sana.



    Ninashindwa kustahamili ninaamua naiendea Stuli na nalishika kawa kwa kitetemeshi cha mikono, ninalifunua taratibu hamadi macho yangu yanapatwa na ganzi



    na makengeza makuu! Ninalifunika haraka sana, huku ninashika mkono wangu katika moyo wangu, kwani mapigo ya moyo yamenilipuka sana. Mara



    ninagutuliwa na milio ya honi ya Bodaboda. Ninafunika tena Kawa vizuri mahala pake, ninakwenda nilipoiweka pesa yangu aliyonitunza hayati Mwanamtama,



    ninaichukua pesa ninatoka nje ninampa dereva wa bodaboda, ninamshukuru nae anashukuru kwa uaminifu wangu kisha anaondoka zake.

    Ninarudi ndani lakini ninapitiliza hadi uani kuona kama nitamuona mtu alieufungua mlango na kuweka mambo yale katika sinia kisha akafunika na kawa tena



    chumbani kwangu. Ninafika uani ninaangalia uwa wote lakini sioni mtu, ninakwenda chooni kutazama kama kuna mtu napo pia nakuta hola! Ninarudi na



    kugonga chumba cha hayati Baby Girl Mwanamtama, labda ameingia katika chumba hicho, ninagonga sana lakini sipati majibu, wala hakuna mtu anaeniitikia

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    gonga yangu. Mlango umefungwa kwa funguo hakuna dalili za kuwa ameingia mtu chumbani humo.

    Jasho linanitoka sana, moyo unanienda mbio kama saa mbovu. Nani sasa alieufungua mlango mkubwa pamoja na wa chumbani kwangu, kisha aniwekee mambo



    yale chumbani kwangu? Lakini kama haitoshi awezaje ende zake auache mlango wazi?! Akili yangu inakataa kufanya kazi sawasawa juu ya kadhia hiyo, ninahisi



    labda huyo mtu aliefanya haya atakuwa amekwenda dukani, ninakaa sebuleni kwa muda mrefu kumsubiri lakini hakuna mtu yeyote anaekuja ndani humu.



    Ninapata shaka labda mapepo ndiyo yananifanyia mchezo huu, lakini sitaki kuamini sana mambo hayo. Ninarudi chumbani ili nikaone kama sinia nitalikuta tena



    pamoja na mambo niliyoyaona katika sinia. Ninaingia chumbani ninalikuta kawa lipo ninalitazama. Ninapiga hatua hadi katika stuli iliyobeba sinia iliyofunikwa



    na kawa, ninalifunua tena kwa mara nyingine kawa, kuhakikisha nilichokiona awali nitakikuta tena au nitaona mauzauza mengine? Ninapotazama katika sinia



    ninaona kile nilichokiona awali ndicho kilichomo ndani yake! Macho yananitoka pima ninatazama kwa makini, naanza kuingiwa na wasiwasi. Wasiwasi



    unaonipata ni kwa haya niyaonayo, ninaona kama vile yana mkono wa Hayati Baby Girl Mwanamtama! Naam nawaza hivyo kwani sijapatapo kuona kitu kama



    hicho kwa mwanamke yeyote tangu nimeanza matentelee zaidi yake.

    Ndani ya sinia kuna chakula kimewekwa. Ni ndizi zilizopikwa kwa nazi shatashata, na nyama ya kusaga ikiwa imetupiwa juu yake! Hii nyama ya kusaga



    imetupiwa kwa mpango maalum, kiasi imechoreshwa neno DOBE kwa herufi kubwa, kisha chini kumepambwa na maneno yaliyoandikwa kwa herufi ndogo,



    welcome. Ninatafakari nani ananifanyia haya ananitia uchungu mie, kwani kwa baby mbali yakupata mapenzi mazito, lakini pia nilikuwa nasoma maada, vihendo



    na mizungu mingi sana. Ninahisi labda ninaota au labda jinamizi la mapenzi linanitokea kwa kumpenda kwangu kulikopindukia Baby girl. Ninatizama huku na



    huko lakini sipati kitu chengine cha maana. Ninafikiri mara mbili ninaamua kwenda kunawa mikono, bila hata kubadili nguo, tena bila woga, ninakusudia kula



    kwani chakula kimewekwa chumbani kwangu, basi mie ndiye mlengwa! Ninaamini labda nimetangazwa kwa ndugu na jamaa wa Mwanamtama, hivyo ameamua



    kunirithi labda. Ninapiga msosi mtamu hadi ninapopata kula pahala penye lost palipoandikwa jina langu ndipo ninapokutana na kitu, kinachonirusha roho yangu



    Sarakasi ya shufani kwa fadhaa!!! Haaaaaah!

    Mapigo ya moyo yameongeza kasi yake mara dufu. Nini hiki jamani mbona hivi?! Karatasi ipo ndani ya Nyloni nyeusi, imewekwa kwa kukusudiwa, kwani



    imetiwa humo ili isirowane na chakula.

    Natafakari kwa muda, hatimae naichukua ninaitazama kwa makini, moyo wangu unanituma niifungue nione hiyo karatasi inayoonekana kwa shida humo ndani,



    ili nitambue ina nini.

    Ninaifungua taratibu ninaiachanisha na mfuko na ninaiona kwa uwazi. Laahaula moyo wangu ninauhisi kusimamisha mapigo yake! Siamini macho yangu kwa



    mara nyingine. Ninahisi nipo ndotoni na si kweli hiki nilichokuwa nacho mkononi mwangu.

    Ninayafikicha macho yangu kwa mkono wangu wa kushoto, ninatizama tena na tena lakini siipati tofauti.

    “Mungu wangu, mungu wangu nini hii tena?”

    Najikuta nayatamka maneno hayo, nikiwa nimechanganyikiwa sana.

    Ninaigeuza nyuma, nakutana na kitu kingine kinachoyavuta macho yangu, nakunifanya niyakodoe pima kama fundi saa, aliepoteza nati. Ninajikaza kiume ili



    nisipoteze fahamu kwani akili imezidiwa na mawazo ya vitu ninavyokutana navyo. Sijawahi katika maisha yangu yote,kuona ndani ya chakula nawekewa picha!



    Ndiyo picha tena ya mtu alieniingiza katika ulimwengu wa mahaba, ambao hakika ni mpya kwangu pamoja na Matentelee yangu yote. Baby Girl atabakia kuwa ni



    fundi kwangu asie na mpinzani, katika kuogelea bahari ya mahaba. Mwanamtama ni Profesa wa mapenzi..

    Picha niionayo ni ya kwake, najiuliza nani ameiweka katika chakula hiki?! Nikiwa bado ninastaajabu kuwekewa picha, nyuma ya picha hiyo kumeandikwa



    maneno, yanayonitatiza zaidi ya sana.





    Dobe Boy, uwa la roho yangu nilipo ninakuwaza. Miss you sana, nimeyamiss Matentelee yako, njoo nilipo nikusabilie vyote!

    Maneno hayo yameandikwa nyuma ya picha kipande ya Baby Girl Mwanamtama, au naweza mwitwa Nyakanga wa Manyakanga.

    Akili inaniduru kwa kuwa mwisho wa maneno hayo, kumeandikwa tarehe ya siku ya leo! Yaani maana yake ujumbe huu umeandikwa leo hii hii! Japokuwa siujui

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mwandiko wa Mwanamtama, lakini sipati uelewa kama haya niyasomayo yameandikwa naye. Nafsi yangu inakataa kwa vile Baby Girl ameshakufa! Angewezaje



    kuandika ujumbe nae ni maiti? Angewezaje kupika chakula hiki ilihali mwili wake alipo, hawezi hata kumpangusa sisimizi anaemtambaa?!

    Haya, anaponambia niende alipo akanisabilie vyote, nende kaburini au alikuwa na maana nife tukakutane huko Ahera?!!! Mmmmh sidhani! Hapo ndipo mawazo,



    akili, na fikra zinaposhindwa kufanya kazi zao sawasawa.

    Najaribu kuhisi labda kuna mtu upande wa marehemu, ameamua kunichezea picha hiyo nichanganyikiwe. Ninajiuliza kwa nini afanye hivyo! Kisha iweje?



    Chakula kinanitumbukia nyongo, ladha yake inanipotea, nakiona kama mauzauza tu hivi.

    Nimebung’aa tu kama mwehu, akili imesimama kwa muda. Mara mlio wa simu unanirudisha tena katika ufahamu wangu. Ninashangaa kwani mie sina simu



    nilipo, hii inayolia ni ya nani? Nageuka upande simu inapolilia ninavuta hatua hadi kitandani kwangu, ninaufata mlio unapotokea. Ninauinua mto, hatimae



    ninaiona simu ya kisasa aina ya Verssed Platnum Android ikiendelea kuita, nami ninabaki kuikodolea macho.

    Najiuliza na kujipa majibu labda huyo alieleta chakula atakuwa ameisahau simu yake!

    Mara simu inakatika kwa kutokupokelewa. Moyo wangu unakataa mawazo kuwa alieleta chakula, ameisahau simu yake kwa sababu imewekwa sehemu kwa



    kukusudiwa bila shaka. Ingelikuwa kusahauliwa ingekuwa sehemu yakuonekana kirahisi, lakini siyo chini ya mto, tena mto wa pili badala ya uliokuwa mbele,



    lazima kuna kitu hapa.

    Ninapeleka mkono wangu ilipo simu, ninaiinua ninaishika. Nikiwa najiandaa kuibonyeza niione namba iliyokuwa inapiga, simu ikaanza kuita tena. Ninaitazama



    namba naiona ni ngeni machoni mwangu. Ninajiuliza mara mbili niipokee au nisiipokee?

    Nikiwa katika kujiuliza, moyo nao unaongeza mapigo lakini unanisukuma niipokee. Ila inanitahadharisha niwe kimya nisiseme hata “Halow.”

    Kwa mkono wenye kitetemeshi ninaipokea na kuiweka sikioni mwangu bila kusema neno. Upande wa pili nao unakaa kimya,nadhani unasubiri sauti yangu!



    Ninakaa hivyo kwa dakika mbili hakuna neno kwangu wala kwa mpigaji, ninaamua kuikata. Mara ninasikia mlio wa gari likisimama nje ya nyumba. Nikahisi



    mwenye simu sasa amefata simu yake. Haraka nikairejesha ilipokuwa kisha nikaubwaga chini upande wa khanga niliojistiri nao, nikavuta suruali yangu ya jinzi



    nikaivaa na kuwa tayari kwa lolote litalojiri nipambane nalo.

    Sekunde zilikatika, dakika zikaenda lakini sikusikia mlango wa gari ukifunguliwa kisha kufungwa. Nikapata shauku nitoke nje kuitazama.

    Ninapiga hatua moja tu simu inaita tena upyaa.

    Nikawa kati sijui nende nje kutazama gari, au nibakie ndani nipokee simu. Nikaona nende nje haraka ikiwa anaeipiga yupo nje ninaweza kumuona nikamtambua.

    Haraka ninavuta fulana iliyokuwa katika msumari wa mlango, ninaitupia kwa haraka mwilini huku ninatembea.

    Nikiwa nje ninaishuhudia gari ndogo aina ya IST yenye vioo vya kiza, ikiwa mlango wa abiria upo wazi.

    Ninashangaa kwani sehemu mlango ulipokuwa wazi, hakukuwa na mtu. Najiuliza kwa nini asiufunge alipotoka? Ninaisogelea gari kwa karibu kwa kupitia



    mlango uliokuwa wazi ninaweza kuona ndani ya gari hiyo kukiwa patupu hamna mtu ndani.

    Eboo nini maana yake?

    Ninajisemea kimoyomoyo, hatimae ninaamua kurudi ndani, ninajipa moyo labda dereva kaamua kutokea kwa abiria pengine mlango wake umegoma kufunguka,



    na kwamba atakuwa ameenda dukani. Mara wazo linanijia ghafla kuwa maduka hapa yapo mawili na yote ninaweza kuyaona nikiwa barazani. Ninageuka kwa



    haraka na kuyatazama maduka hayo ninaona katika duka moja, watoto wadogo wawili bila shaka wananunua pipi. Katika duka la pili kulikuwa hakuna mtu.



    Watu walikuwa wakipita na hamsini zao hakuna aliekuwa anashughulika na mie.

    Nikakata shauri niingie ndani. Ninaona lazima nifanye kitu, tena nifanye haraka.

    Ninaingia ndani na kuelekea moja kwa moja kwenye nguo zangu, ninaanza kufungasha niondoke mahala hapa nitokomee mbele kwa mbele. Ninafungasha vitu



    vyangu, lakini kabla sijesha kufunga simu inaita tena. Ninaamua niipokee kisha nimtukane mitusi nende zangu.

    “Halow.”

    Ninasema kwa hasira, huku nikijiandaa kuteremsha kamusi ya matusi, lakini masikio yangu, yanapoisikia sauti ya upande wa pili, yanatahayari. Mdomo wangu



    unapata kigugumizi, maneno yananikauka kinywani, nabaki kuwa msikilizaji.

    Sauti hii, sitaki kukubali, hapana siyo!

    Ninajisemea moyoni peke yangu. Nguvu zinanisha, ninashindwa kuendelea kusimama nakaa kitako kitandani. Machozi yananitoka sina habari, na sijui kwa nini



    yananitoka.

    Nikiwa katika mawazo, bado simuni mawimbi ya sauti ya upande wa pili, yanarindima masikioni mwangu. Upande wa pili unaendelea kuzungumza kwa utuo na



    ufasaha wa hali ya juu. Mzungumzaji anajua anachokifanya. Hatimae ninatanabahi ninajibu swali ninaloulizwa simuni.

    “Ndiye mwenyewe Dobe Boy, hujakosea hata kidogo”

    “Amini nikwambiayo na fata maelekezo niliyokupa, haraka usishangae!”

    Busu mwanana ninapigwa na simu inakatwa.

    Ninaendelea kuishikilia simu sikioni kwangu, japo haiongei, nazama kwenye lindi la fikira hatimae, ninaisikia katika mawazo sauti ikinambia taratibu.

    Amini nikwambiayo na fata maelekezo niliyokupa, haraka usishangae.

    “My God!”

    Ninatamka maneno hayo kisha ninaiweka simu mfukoni mwangu, ninakurupuka mbio.

    Ninafika barazani ninaingia ndani ya gari IST, ninaufunga mlango wa abiria, kisha ninatazama kupitia vioo vya pembeni na cha ndani ya gari, kama kuna mtu



    anaenifatilia, sioni mtu kila kitu kipo sawa.

    Ninainama chini ya kiti cha dereva, kama maelekezo niliyopewa katika simu, ninauona ufunguo ya gari. Ninauchukua na kuiwasha gari, ninatia gia naingia

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    barabarani, naitafuta Ubungo.

    ********

    Naegesha gari katika maegesho ya Hoteli Sharom nyuma ya kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani.

    Ninashuka nakwenda mapokezi, ninamkuta muhudumu wa mapokezi, akizungumza na simu.

    “Nikusaidie kaka yangu tafadhali.”

    Ananambia huku ananitazama usoni, kisha anaikata simu aliyokuwa akizungumza nayo.

    “Naitwa Dobe boy.”

    “Ahaa sawa, ninazo taarifa za ujio wako, chukua lifti panda gorofa ya tatu, ukishuka kwenye lifti tu chumba unachokitazama ndicho kinakuhusu.”

    Majibu hayo ya muhudumu ninataka kuhoji vitu, lakini ninaona siyo sehemu yake, kwa vile wahaka umenijaa, ninaamua kuingia kwenye korido ninaufungua



    mlango wa kioo, ili nende kwenye lift, kabla sijamaliza kuufunga mlango, ninalisikia jina langu likitajwa nyuma yangu.

    “Dobe Boy, ndani ya nyumba.”

    Ninageuka nyuma ninamuona muhudumu akiongea na simu ya mezani.

    Ninahisi labda anamfahamisha mwenyeji ujio wangu. Sijali wala sirudi nyuma. Nasonga mbele ninaufungua mlango, kisha ninauachia mlango ujifunge nyuma



    yangu. ninaziendea lifti, ninaibonyeza ili ifunguke, Lifti ipo chini nilipo haifanyi khiyana inafunguka milango yake ninajichoma ndani.

    Ninaibonyeza namba tatu, kuiruhusu lifti ili ikifika ghorofa hiyo isimame, chombo kinainuka juu, hadi ghorofa ya tatu, kinasimama milango inafunguka



    ninatoka nje ninatizamana ana kwa ana na mlango wa chumba ninachotakiwa kuingia.

    Mapigo ya moyo, yanaongezeka kasi yake. Ninashusha pumzi ndefu. Ninaukabili mlango wa chumba, ninagonga kwa adabu.

    Simu mfukoni mwangu, inaanza kuita. Ninaitoa na kuitazama namba inayopiga, ninaiona ni hii, hii inayofanya niwe pahala hapa muda huu.

    “Halow, nimeshafika.”

    “Najua, nimekuona tangu unaegesha gari. Hapo chini ya maegesho”

    “Sawa nifungulie, mlango kwani hii milango inafunguliwa na Kadi, nami sinayo.”

    “Natambua Dobe, ndani ya dakika sifuri utafunguliwa huo mlango.”

    Simu inakatwa ninabaki namaswali yasiyojibika. Nitafunguliwa mlango, ina maana siyo yeye anifungulie?

    Nikiwa bado natafakari, mara lifti inafunguliwa na dada mmoja amevaa sare mithili ya yule alienipokea mapokezi. Anatoka ndani yake, akiwa na Kadi mkononi.



    Ananisalimu kisha anaionesha ile Kadi katika mlango upande wa kulia, mlio mdogo ninausikia kuonesha kuwa Kadi imesomwa.

    Anaushika mlango anaufungua, lakini haingii ndani. Ila ananikabidhi Kadi, ananiashiria nipite ndani.

    Ninaingia chumbani, ninapokelewa na harufu nzuri ya uturi.

    Ninaufunga mlango, nakielekea kitanda lakini ninapofika kitandani, ninasita kidogo. Ninasita kwa sababu kuna kitu kimenifanya nisite. Hakuna katika hoteli zote



    Duniani zinazoweza, kufanyika kitu hiki. Au niseme katika kutembea kwangu, sijawahi kukutana navyo.

    Ninatupa macho huku na kule. chumba ninakiona kitupu hamna mtu.

    Macho yangu ninayarejesha, kwenye kitanda, ninatizama nakujikuta ninasoma kimoyomoyo.

    WELCOME AGAIN DOBE BOY

    Maandishi hayo yameandikwa kwa herufi kubwa,

    kwa Mashada ya asumini juu ya kitanda.

    Chumba kipo tulivu, shuka na mazingira yapo safi. Nikiwa katika kushangaa, ninasikia mlio wa mlango wa kioo ndani ya chumba unafunguliwa.

    Ni mlango wa sehemu ya kupungia hewa, ambayo ipo nje ikiwa imeachanishwa kwa aluminium na kioo kikubwa ndani ya chumba hicho. lakini kwa uzito wa



    mapazia, siyo rahisi kutambua kama kuna mlango. Ninakuwa makini zaidi kuona nani anaeingia, mara ninauona mguu wake ukiingia ndani, mara nusu ya mwili



    wake unaonekana, hatimae wote ninamuona ameingia.

    Ninapotazamana nae, nashindwa kuamini macho yangu. Moyo wangu ninauhisi kushindwa kufanya kazi sawasawa. Miguu inanisha nguvu, kitete kinanipata,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    fahamu nazo ninazihisi kwa mbali zikinitupa mkono. Kizunguzungu kimenivamba, macho yanitanda kiza, siwezi kutazama sawasawa, ninajihisi kuupiga



    mweleka wa chali. Kwa mbali sana ninahisi mikono laini ikinidaka, lakini siwezi kusikia anachokiongea, ninapoteza fahamu.



    MWISHO


0 comments:

Post a Comment

Blog