Search This Blog

Thursday 19 May 2022

SORRY MADAM - 5

 





    Chombezo : Sorry Madam

    Sehemu Ya Tano (5)



    ILIPOISHIA

    "Una masaa ishirini na nne, kuleta kiasi cha pesa milioni mia moja, kumuokoa mke wako na mwanao Junio, la sivyo WATAKUFA"

    "Wewe ni na.....?"

    Simu ikakatwa, nikabaki nikiwa nimeitazama simu yangu, mapigo ya moyo yakinienda mbio.

    ENDELEA

    Nikageuza gari langu, nikalirudisha sehemu nilipo lichuku.Nikashuka haraka na kuelekea chumbani kwangu. Kitu cha kwanza kukifanya, nikachukua kadi zangu mbili za benki, nakuziweka kwenye mfuko wa jinzi niliyo ivaa. Nikachukua sweta langu lenye kofia, japo Dar es Salaam kuna joto kali, ila ikanilazimu kulivaa, hivyi hivyo. Nikasimama nje ya chumba changu kilichopo ghorofani, kila mtu nikamuona anashuhulika na mambo yake.

    Kitu kinacho zidi kuniumiza kichwa ni jinsi ukuta wa jumba hili ulivyo mrefu, huku juu ukiwa umezungushiwa nyanya zilizo na umeme wenye volt nyingi sana.

    "Chaji"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijisemea mwenyewe, nikachukua chaji ya simu yangu. Nikatoa walet yangu mfukoni, nikaikuta ina noti mbili za dola mia pamoja na na shilingi elfu sabini. Chakushukuru Mungu, nikaliona gari lakukusanya mataka taka likiingia getini, nikashuka kwa haraka pasipo kusemeshana na mtu, nikafika sehemu lilipo simamishwa, ambapo wafanyakazi wake wapo bize kwa kukusanya matakataka yaliyopo kwenye mindoo mikubwa.

    Kwa haraka nikabingiria kwa haraka na kuingia chini, ya gari hili kubwa la taka taka. Nikashikilia kwenye, bomba zilizopo chini ya gari hili. Baada ya dakika kumi, wakawa wamemaliza, tukafanikiwa kutoka getini pasipo askari kugundua kitu cha aina yoyote. Kutokana gari hili linapita kwa kila nyumba zilizopo kwenye maeneo ya nyumba za eneo hili, likasimama kwenye nyumba ya tatu kutoka lilipo jumba la mama.

    Nikatoka chini ya gari pasipo mtu kuniona. Nikakodi pikipikia kuelekea benki ya posta. Niliwa njiani simu yangu ikaita, ikawa ni namba ngeni, ila ni yatanzania.

    "Mmm"

    "Shem mimi Blanka upo wapi?"

    "Naelekea benki ya posta, upo wapi?"

    "Nimetoka huku saloon nimeazima simu ili nikupigie, sijui tunaweza kuonana sasa hivi, kwa maama leo hatuto rudi nyumbani na kesho ndio harusi yako"

    "Upo wapi?"

    Manka akanielekeza sehemu alipo, ikanilazimu kughairi safari ya benki na kwenda alipo yeye. Ilituchukua kama dakika kumi na tano kufika alipo Blanka kwenye mgahawa mmoja ulio jificha sana, kutona na uwenyeji wa dereva huyu wa bodaboda, aliweza kupafahamu. Nikamlipa dereva pesa anayo nidai, nikaingia ndanibya mgahawa kama Blanka alivyo nielekeza, nikamuaona amekaa kwenye kona moja ya huu mgahawa ambao si rahisi mtu yoyote kumuona, kutokana na kigiza kilichopo ndani ya huu mgahawa.

    "Mbona shemu umevaa hivyo?"

    "Mama alikua haitaji mimi kutoka nje'

    "Ahaaa sasa hapa napata picha"

    "Picha gani?"

    "Nilimsikia akizungumza asubuhi na dada Sheila, kwamba huto toka, sasa sikuwaelewa wanamaanisha nini"

    "Ehee kabla hujaniambia ulicho hitaji kuzungumza jana, mbona umetumia namba ambayo si yako?"

    "Nimehofia kutumia namba yangu kuwasiliana na wewe kutokana toka juzi namba za watu wote mule ndani zimeunganishwa na namba ya mama, zikiingia na kutoka lazima kwake zipitie"

    "Mmmmm hata yangu?"

    "Yako sijajua, ila nahisi pia itakua kwenye mlolongo huo huo"

    "Poa tuachane na hilo, wewe na Sheila muma undugu wa kivipi?"

    "Ahaaa ni story ndefu kaka yangu, ila kiufupi Sheila si ndugu yangu wa kuzaliwa wala wa ukoo"

    "Sheila nilimsaidia kipindi fulani alitekwa, sasa nilimuokota porini akakaa sana kijijini kwetu Tulimuuguza hadi akapata nafuu ndipi alipo rudi huku, akaamua kulipa fadhila zake kwa kuniendeleza na masomo"

    "Ahaaaa kwa maana nilikua ninajua Sheila hana ndugu"

    "Kweli hana, mimi ni ndugu yake wa hiyari"

    "Kitu nilicho hitaji kukuambi wewe kama kama yangu, Sheila anatabia zilizo nipelekea leo kuzungumza hichi nimacho taka kukizungumza"

    Blanka akashusha pumzi na kunitazama usoni, kisha akapiga fumba la juisi yake aliyo agizia.

    "Kabla hawajaja kuja huku marekani, dada sheila alikua akinilazimisha kumtoa mimba aliyo kua nayo"

    "Ng....ngooja kwanza, kimba gani?"

    "Hii aliyo kua nayo, kwani kipindi anakuja huko ulipo kua, alijigundua ana mimba ya ya wiki kam moja na nusu"

    "Ñgoja mimba ya wiki inaweza kuonekana?"

    "Ndio inategemea na maumbile ya mwanamke wengine hadi mwezi ndio wanaiona"

    "Basi nilikataa kumtoa, akaniambia atajua nini cha kufanya. Alipo kuja huko sijui kama mulikutana kimwili au laa?"

    Kwa upande mmoja kichwa kikaanza kunikoroga kwa hasira, huku upande wa pili ikiwa ni nafuu kwangu kuepukana na jukumu la ndoa.

    "Nilikutana naye"

    "Na umaamini mimba ni yako?"

    "Mi sijui?"

    "Kwani siku ulipo onanana naye alikuaje?"

    "Mimi wala sielewi hapa nahisi kuchanganyikiwa"

    "Tulia shem wangu, ila kuna kidhibitusho kingine ñgoja nikuonyeshe"

    Blanka akatoa simu yake, akaminya minya na kunipa niangalie baadhi ya meseji alizo zipiga picha zikiwa kwenye simu ya Sheila zikionyesha akijibizaba na mwanaume aliye mtia mimba.

    Sheila alikakua àkimlazimisha mwanaume huyo, akubali yeye kutoa mimba kwani mumewe amesha rudi.

    "Huyo jamaa yake unamjua?"

    "Ndio, tena ngoja nikuonyeshe"

    Blanka akachukua simu yake akaminya minya baadhi ya sehemu anazo zijua mwenyewe, akanikabidhi tena simu yake.

    Moyo wangu ukazidi kukosa amani, baada ya kumuona John akiwa amekbatiana na Sheila, tena wakinyonyana midomo yao

    "Huyo jamaa, anadai anafanya kazi kwenye shirika la ndege la Ufilipino, na huja mara chache sana hapa Tanzania"

    Mwili mzima ukazidi kunitetemeka kwa hasira kali, huku nikimtazama John ambaye hadi sasa hivi, amechukua kila kitu kutoka kwenye mikono yangu. Kuanzia mali za baba yangu hadi Sheila mwanamke niliye tokea kumuamini sana.

    "Alafu hafi sasa hivi, kuna mpango ambao Sheila ameupanga na huyo jamaa yake, sasa sijajua ni mpango gani. Mara nyingi Sheila ananiambia mambo yanakaribia kuiva, tutakua matajiri sana"

    ”Ila shem ninakuomba usinitaje, kwani Sheila anaweza kuniua mimi"

    "Hawezi kukuua, nakuomba ufwatilie huo mpango ulio jificha"

    "Sawa nakuahidi nitalifanya hilo, na vipi huto jamaa unamjua?"

    "Hapana?"

    "Mbona anajuana sana mama, na huwa anakuja nyumbani, anadai ni rafiki yako?"

    Kabla sijamjibu Blanka simu yangu ikaingia meseji kwa namba iliyo nipigia mara ya kwanza kutoka Somalia

    (Jinsi unavyo kaa kimya, ndivyo jinsi unavyo karibisha vifo vya familia yako)

    "Shitiii"

    Nikajikuta nikiibamiza simu mezani, kabla haija anguka chini, Blanka akaiwahi kuidaka, akausoma ujumbe ulio ingia kwenye simu yangu

    "Ni familia gani?"

    "Nitakuambia, fanya urudi Saloon, ila usimuambie mtu yoyote chochote kuhusiana na kuonana kwetu"

    "Sawa nimekuelewa shem"

    "Ukiinipigia simu piga kwa namba nyingine kama vipi tafuna namba mpya"

    "Sawa niyafanya hivyo shem"

    Nikawa wa kwanza kutoka ndani ya mgahawa, nikakodi pikipiki hadi benki ya posta, nilipo hifadhi kiasi changu kikubwa cha pesa.

    "Samahani, nahitaji kutoa pesa"

    "Nilizungumza na jamaa, mmoja ambaye ni muhudumu"

    "Chukua fomu ya kutolea hapo juu"

    "Sihitaji fomo hiyo kwani nataka kutoa kiasi kikubwa cha pesa"

    Muhudumu akanitazama kwa macho ya mshangao

    "Unataka kutoa kiasi gani?"

    "Milioni mia na hamsini"

    "Mmmmm, ngoja nikukutanishe na meneja, nisubirie hapo"

    Jamaa alaondoka na baada ya kuda akarudi na kuniomba niongozane naye, nikaingia ofisini kwa meneja, nikamueleza shida yangu niliyo nayo, akaniomba namba ya accounti yangu, nikampa akaminyaminya batani za computer yake, kisha akanitazama huku alivua miwani yake.

    "Samahani, bwana Eddy hii akaunti yako imefungiwa"

    "Imegungiwa?"

    "Ndio na agizo hilo, hili limetoka ofisi ya waziri mkuu, masaa kama mawili yaliyo pita"

    "Sababu?"

    "Ahaaa tumeambiwa tuifunge kwa àgizo la waziri mkuu"

    "Asante"

    Nikachukua kadi yangu, na kutondoka sikutaka kuuliza nini chanzo cha akaunti yangu kufunguliwa kwani natambua mama ndio chanzo. Nikaenda benki ya bacrays ambapo, nikakutana naajibu ya kufungiwa, kwa akaunti yangu mbaya zaidi sina akaunti nyingine zaidi ya hizi mbili.

    Nikaipiga namba ya simu ya Phidaya, ikaita kwa muda na kupokelewà na jamaa aliye nipigia simu muda asubuhi

    "Nimazo pesa zenu, niambieni ni wapi mupo nizilete"

    "Ohoo Mr Eddy, fwatà maelekezo tutakayo kupa"

    "Kwanza kabla sijaonana na nyinyi, nahitaji kuzungumza na mke wangu"

    "Subiri"

    Baada ya dakika moja, simu akakabidhiwa Phidaya

    "Eddy usitoe chochote"

    Sauti ya Phidaya ilisikika, ikiambatana na mlio wa risasi kisha simu ikakatwa, nikajaribu kupiga tena huku mwili mzima ukinitetemeka ila haikupatikana tena, na saa yangu ya mkononi ikinionyesha yamesalia masaa kumi na tano tu.



    Nikabaki nikiwa nimeizhik simu yangu nisijue nini cha kufanya. Nikapata wazo la kumpigia mmoja wa waongozaji wa tangazo la magari ya Ford, ambaye alitokea kuwa rafiki yangu sana

    "Smith, mimi Eddy"

    "Vipi kaka, mbona unahema sana?"

    "Nahitaji msaada wako"

    "Upo wapi?"

    "Nipo Dar es Salaam, umesha rudi Marekani?"

    "Hapana, bado nipo Dar, labda kesho kutwa naweza kuondoka kuna vipande vya lile tangazo, vinamapungufu, tumeamua kuvitengeneza upya"

    "Ahaa mupo wapi?"

    Smith akanielekeza walipo, nikakodi tena pikipiki hadi walipo kwenye moja ya godauni, ambapo wamepafanya kama studio, wakitumia 'blue screen' wakitengeneza mazingira kama ya Arusha.

    "Vipi Eddy mbona kama una wasiwasi?"

    "Kaka nina matatizo makubwa sana"

    Nikanza kumuadisia Smith, tukio moja baada ya jengine, sikumficha kitu cha aina yoyote.

    "Eddy nakuahidi hakuna kitakacho haribika, nitakusaidia kaka yangu"

    "Pesa yote hiyo utaitoa wapi Smith, wakati bado upo Tanzania?"

    "Njoo uone"

    Tukaingia ña Smith kwenye moja ya chumba, ambapo tukakuta Mtu anaye fanana na mimi kila kitu.

    "Huyu nane ni nani?"

    "Tumemtafuta mtu wa kufanana na wewe, ili aweze kurekebisha baadhi ya vipande, tulijaribu kukupigia simu ila hatukukupata"

    Hapa ndipo nilipo amini duniani watu ni wawili wawili, Jamaa hadi kuzungumza anafanana na mimi.

    "Umaitwa nani?"

    "Fred"

    "Duuu jamaa anafanana na mimi"

    Nilizungumza huku nikiwa ninacheka kwani sikuamini kukutana na mtu anaye fanana na mimi, kwa asilimia zaidi ya tisini.

    "Eddy huyu umnaonaje kakakusaidia katika swala zima la wewe kuoa"

    "Apo Smith umenena jambo la maana"

    "Alafu una bahati kwa maana ndio amemaliza kushooti vipande tulivyo vikosea"

    Nikaanza kumuelezea fredy historia yangu yote kuanzia mwanzo hadi mwisho, nikamuelezea mazingira yate ya nyumbani, pamoja na mtafaruku uliopo kati yangu na mama

    "Nimekuelewa Eddy, ila huoni kwamba itakua hatati siku wakigundua kwamba mimi sio wewe?"

    "Hawawezi kugundua, kikubwa ni weww kuwa karibu sana na mimi, kila jambo ambalo utaona linakutatiza nijulishe kwa njia ya meseji"

    "Ila kuna kitu kingine ambacho ni kigumu"

    "Kitu gani?"

    "Na mimi nina mke, ila bado sijamuoa"

    "Ahaaaa Fredy, hii ni ishu kati yangu mimi na wewe, pia nitakupa kiasi chochote cha pesa"

    "Utachukua muda gani kurudi, kutoka kuko Somalia?"

    "Haitazidi mwezi mmoja"

    "Ahaa kaka, huoni nitampoteza mke wangu"

    "Mkeo anaishi wapi?"

    "Mbagala rangi tatu"

    "Ndipo ulipo kua ukiishi wewe?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ndio ninapo ishi"

    "Fanya hivi, mimi ninakupeleka nyumbani kwetu, mimi nielekeze kwako, nitazungumza na mkeo"

    Fredy akajifikiria kwa dakika kadhaa, akakakubali kuufanya mchezo wa hatari, uliopo mbele yetu. Ikanilazimu kumnunulia Fredy kama nilizo vaa, pamoja na simu inayo fanana na mimi. Nikatafuta laini mpya ya kuwasiliana na Fredy tu, kwani ya kwangu imeunganishwa na namba ya mama.

    "Bado nini hapa"

    "Sweta ulilo vaa wewe"

    "Twende nitakupa mbele ya safari"

    Tukaingia kwenye gari ya Smith, tukaelekea nyumbani kwetu, ambapo nikakuta basi kubwa, lililo toka kuwachukua ndugu kutoka stendi ya ubungo, walio toka mikoa tofauti kuja kushuhudia harusi yangu, wakishuka na kuingia ndani, huku wengine wakicheza kwa furaha.

    Nikampa Fredy sweta langu na kujifunika kichwa chake, akajichanganya na wanandugu hao, walio landuka kwa kucheza kwa furaha, wengine wakionekana kulewa chakari. Fredy akafanikiwa kuingia ndani pasipo kustukiwa. Nikampigia simu

    "Sasa chumba chako ni kipi?"

    "Si umeona kuna nyumba tatu?"

    "Ndio"

    "Sasa wewe, pandisha kwenye hilo gorofa lenye rangi ya pinki, achana na hayo majengo mawili yenye ghorofa mbili mbili"

    "Mbona zote zina rangi sawa"

    "Hilo jengo la katikati, ndio upande, si umeliona?"

    "Ndio naelekea"

    Smith akawasha gari, tukaondoka, huku simu yangu ikiwa hewani

    "Nipo ndani"

    "Pandisha ngazi hizo utakuta kirdo ndefu, nyoosha hadi mwisho chumba cha mwisho kushoto ndio changu"

    Japo ni jambo la hatari tunalo lifanya mimi na Fredy ila hapakuwa na njia nyingine zaidi ya kufanya hivyo.

    "Nimesha ingia chumbani kaka, nipazuri sana"

    "Sasa kazi kwako, ila hakikisha huwi muongeaji sana, usije ukachapia baadhi ya vitu"

    "Nimekupata, demu anaitwa Sheila?"

    "Ndio"

    "Poa, kaka kukiwa na shida nitakueleza"

    "Sawa"

    Moja kwa moja tukaelekea Mbagala, hadi nyumbani kwa Fredy, kutokana Smith anapafahamu haikuwa shida kwangu kupajua. Tayari yaamekatika masaa manne yamesalia masaa kumi na moja kabla sijapeleka pesa ya kumkomboa Phidaya na mwanangu Junio.

    Kitendo cha kushuka kwenye gari, nakastukia nikiguswa kwa nyuma, kugeuka nikakutana na Manaka akiwa amejitanda kanga mbili mwilini mwake

    "Karibu sana mume wangu"

    Nikasita kidogo kuitikia salamu yake, ila Smith akanikonyeza kuaahiria kwamba huyo ndio mke wa Fredy

    "Safi"

    Nilijibu kwa kifupi, kwani ukweli ni kwamba Manka ni dada yangu, niliye potezana naye muda mrefu sana. Mara ya mwisho kukutana naye ni ile siku, nilipo kua nimetekwa na Mzee Godwin, na kupelekwa kwenye ngome yake, iliyokuwa milimani.

    "Mbona hivyo mume wangu, umechoka nini?"

    "Yaa nimechoka sana"

    "Ahaaa pole sana"

    Manka akauleta mdomo wake, kwangu. Ikanilazimu kuupokea japo kiroho ngumu, japo kuwa tulisha wahi kupeana penzi, hadi akapata ujauzito ulio toka kwa kupata ajali.

    "Twendd ndani, Smith karibu ndani"

    Manka akatagulia huku, tukifwata nyuma. Tukaingia kwenye chumba kimoja tu wanacho ishi yeye na Fredy, ambapo kimekosa nafasi kutokana na ukubwa wa kitanda pamoja na ndoo za maji, vistuli viwili.

    "Mume wangu, umekuja hata kunipigia simu, au ulidhani utanifumamia?"

    "Ndio, nilitaka kukufumania"

    "Mmmm jiamini mume wangu, acha wivu"

    "Wivu lazima, kila mtu na chake"

    "Sikuwezi"

    "Shem, tumekuja kukuchukua kukupeleka kwenye makazi mapya, ambayo tumekubaliana na bwana mkubwa hapa"

    "Wee"

    "Ndio"

    "Jamani, kweli Mungu ni mwema, nahisi vicheko vya wapangaji dhidi yetu vitakwisha"

    "Usijali, wewe chukua nguo tu, tuondoke usiku huu huu"

    "Hata kula"

    "Kula tutakula mbele ya safari"

    Manka akachukua nguo zake chache na kuziweka kwenye mkoba wake, hadi hapa sikujua Smith anatupeleka wapi, tukatangulia kutoka nje na kumuacha Manka akiagana na wapangaji wezake

    "Smith hivi jamaa alikua akifanya kazi gani?"

    "Alikua akiuza maji baranarani, ndipo nilipo muona. Mara ya kwanza nilijua ni wewe ila baada ya kumuhoji ndipo nilipo gundua kwamba sio wewe. Ndio tukaamua kufanya naye kazi"

    Sikutaka kumueleza Smith kuhusiana na Manka, tukaingia kwenye gari na kwenda maeneo ya Mbezi kwa Msuguri, ambapo kampuni ilimnunulia Fredy nyumba kubwa, na yakupendeza. Manka akaonekana kama kuchanganyikiwa kuiona nyumba hii, ambayo ni mpya kabisa.

    "Ohhh Fredy nakupenda sana"

    Manka alizungumza huku, akinibusu mdomoni mwangu, tukaingia ndani, tukakuta kila kitu kinacho paswa kuwepo ndani ya nyumba nzuri kipo. Manka akawa kama mtu aliye changanyikiwa, kila chumba akaanza kuingia.

    "Kaka hapa nitaondokaje?"

    "Usijali tutaondoka tuu, niachie mimi kila kitu"

    Simu yangu, ikaita na kukuta ni Fredy anaye piga, ikanilazimu kutoka nje kwenda kuipokea

    "Vipi?"

    "Kaka nimeulizwa, pete za ndoa zipo wapi?"

    "Nani kakuuliza?"

    "Mama"

    "Kwenye droo ya kitanda hapo, fungua utaziona"

    "Poa, ila mama hajastuka"

    "Hawawezi kustuka, hembu kata simu kuna simu kwangu inaingia"

    "Poa"

    Fredy akakata simu, nikapokea simu inayo ingia kupitia laini nyingine ya simu iliyopo ndani ya simu, yangu inayo ingia laini mbili

    "Utatuletea utani si ndio?"

    Sautii ya mwanaume anaye zungumza lafudhi ya kisomali, niliisikia kupitia simu yangu

    "Ninawatania kivipi?"

    "Tunataka hizo pesa, sasa nakuongezea masaa mengine ishirini na nne, ole walo usilete pesa nakata kichwa cha mkeo"

    "Nitawapatia tu hizo pesa"

    Simu ikakatwa, nakujikuta nikishusha pumzi

    "Unaongea na nani?"

    Sauti ya Manka ikaniatua, nikageuka nyuma, nikamkuta akiwa amesimama akinitazama

    "Kuna jamaa zangu, niliwakopa pesa yao ndio wanayo ihitaji"

    "Ahaa tena ufanye ukamlipe baba mwenye nyumba pesa yake kwa maana ananisumbua"

    "Sawa nitakupa asubuhi, ukamlipe"

    "Na kesho unakwenda Marekani, mbona hujaniambia?"

    "Kwani mke wangu, tumekaa tukaongea"

    "Sasa Fredy, umeacha hadi Smith ndio aniambie"

    "Kwani shem, nikizungumza mimi ni sawa amezungumza yeye, kama nilivyo kuambia kuna mikataba anakwenda kusaini, akirudi utamsahau kwamba alikua ni muuza maji wako"

    Hapa ndipo nikaamini, Smith anaakili kubwa ya kutengeneza matukio makubwa pasipo mtu mwengine kustuka kwa haraka.

    "Kaka Fredy, mimi ngoja niwaache nitakuja kukuchukua saa kumi na moja alfajiri, ili kuwahi ndege"

    "Sawa kaka"

    Smith akanishika mkono, tukatoka nje ya geti, ambapo tulimuacha Manka akirudi ndani.

    "Eddy kwa leo hapa tumefanikiwa, sasa ni hapo kukipambazuka tuifikirie familia yako"

    "Nakushukuru sana kaka, yaani nilikua nimechanganyikiwa kabisa"

    "Tupo pamoja, kesho nitakuja na pesa ya kumuachia huyu mkeo mpya, ili imsaidie kwa kipindi chote utakapo kua nje ya nchi"

    "Asante sana kaka"

    Smith akapanda gari, na kuondoka, nikarudi ndani, nikamkuta Manka akimalizia kupanga sahani mezani, kwa ajili ya chakula alicho kikuta kimesha pikwa na dada wa kazi ambaye, kipindi tukiingia ndani, yeye alikua amelala.

    Tukala msosi, na kuelekea katika chumba ambacho tayari Manka alisha ingiaza nguo zake. Manka kwa haraka akavua nguo zake na kuingia bafuni

    "Mmmmm leo kazi ninayo"

    Nilijisemea huku nikisikilizia maji yanayo mwagika bafuni. Manka akatoka bafuni, pasipo kua na kitu chochote mwilini mwake. Akajirusha kitandani jilipo lala. Akaanza kufanya uchokozi kama wafanyao wanawake walio shikika na hamu nzito ya kukutana kimwili na mwanaume.

    Manka akaanza kunivua nguo moja baada ya nyngine, nilipo baki na boksa akaonekana kustuka kodogo

    "Vipi?"

    "Fredy umekula nini?"

    "Kwa nini?"

    "Mbona, nanilou yako imekua kubwa, tofauti na siku zote?"



    "Ahhh kuna... kuna videngo Smith alinipa, ndio vimeifanya iongezeke kua hivi"

    "Mmmmm, vidonge gani hivyo?"

    "Ahaaa mimi sijui."

    "Hujui, na ilikuaje akakupa?"

    "Manka, mambo mengine ni yakiume"

    "Fredy umeniitaje?"

    "Si Manka"

    Manka akaonekana kunitazama vizuri, usoni mwangu kwa macho yaliyo jaa umakini mkubwa. Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, macho yake yakatua kwenye kifua changu, akanitazama vizuri kwa umakini.

    Akaipeleka mkono wake kwenye kifua changu, nakuanza kukipitisha kiganja chake kutoka eneo moja la kifua changu kwenda eneo jingine la kifua changu.

    "Hizi alama umezitoa wapi?"

    Nikajitazama na kujikuta na makovu, ya risasi nilizo wahi kupigwa siku za nyuma kwenye kifua changu, kovu moja likiwa limetokana na yeye kunipiga risasi kipindi cha nyuma.

    Sikuweza kumjibu kitu chochote, Manka kwani nikijikanyaga zaidi, naweza kuharibu kila kitu.

    "Mbona hunijibu?"

    "Sijui hata nikujibu nini, kwani hujawahi kuliona hili kovu?"

    "Fredy leo hii, unataka kunuliona mimi ji mgeni wa mwili wako?"

    "Labda siku zote, hukuwa makini na kunitazama"

    "Ftedy, ni mara ngapi ninakunyonya kifua chako?"

    "Nahisi leo huna hamu na mimi"

    Nikanyanyuka kitandani, huku nikijifanya nimekasirika, kumbe ni njia ya kukimbia kikaangio cha maswali ambayo jimeanza kufeli kwa asilimia sifuri.

    "Na huku mgongoni umefanyaje?"

    Manka akanitandika swali jengine, nikiwa naingia mlango wa bafuni. Nikaingia haraka haraka kuepuka kujibu, hata hamu ya kuoga ikaanza kuniishia.

    'Nikimueleza ukweli, nitaharibu kila kitu'

    'Sasa leo nitamuepuka vipi huyu Manka?'

    'Kwenye jina, nahisi nimevuruga, au sio Manka?'

    'Ndio yeye bwana, isije nao wakawa wawili kama mimi na Fredy?'

    Niliendelea kujiuliza maswali, mengi pasipo kujipatia jibu. Huku maji ya bomba la mvua yakiendelea kushuka mwilini mwangu, yakiitotesha boksa yangu ninayo ogopa kuivua.

    "Yameanza lini kuoga na boksa?"

    Sauti ya Manka, ikazidi kumistua, kwani hata alivyo ingia humu bafuni sikuweza kumsikia, kutokana na msongo mkubwa wa mawazo.

    "Eheee"

    "Fredy, mbona leo sikuewi. Nimekuuliza maswali yangu, hukanijibu nakuja huku nakukuta umeegemea ukuta, nini tatizo?"

    "Ahaa naifikiria safari ya kesho"

    "Mmmm haya mwaya, ila mmmmm"

    Manka akatoka, bafuni nakujikuta nikishusha pumzi nyingi.

    "Asiniumize kichwa mimi, ninamambo mengi ya kufanya"

    Nilizumgumza kwa hasira huku, nikijipaka sabuni, na kuivu bosa yangu. Nikamaliza kuoga na kurudi ndani, nilamkuta Manka amesha jifunika kwa shuka, macho yake akiwa amenikodolea mimi.

    Kiunyonge kikapanda kitandani, nikajilaza taratibu.

    "Fredy, natambua kila siku ulikua unahitaji kujua historia yangu ya nyuma, ila nikawa ninakuficha."

    "Leo nimeona uwe ni muda muafaka, wa kuzungumza na wewe, ili kama utaniacha uniache kwa amani."

    Manka alizungumza kwa sauti ya untinfe iliyoa anza kumpeleka kwenye hisia ya kulia.

    "Natambua umenifwatilia sana, hadi kulifahamu jina la Manka"

    "Fredy, mimi siitwi Maria kama, unavyo nijua. Jina langu halisi ni Manka Godwin"

    Manka alizungumza, huku machozi yakianza kumwagika.

    "Fredy, niliweza kukupenda, japo hukua na uwezo kunifanya chochote kama wafanyavyo wanaume wengine kwa wapenzi wao."

    Hapa ndipo nilipo anza kupata picha halisi kwamba Fredy hana nguvu za kiume.

    "Yote ni kwasababu ya kumpenda mwanaume, aliye fanana na wewe, samahani kwa kile nitakacho zidi kukizumgumza, ila natambua utakwenda Matekani, labda Mungu anaweza kukufungulia milango yako zaidi na kuwa suprestar"

    'Laiti angejua, nakwenda Somalia, wala asinge kuzungumza haya'

    Manka taratibu, akajivuta na kukaa kitako kitandani.

    "Huyo mwanaume, niliweza kumjeruhi, kwa risasi."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Lakini baby hayo yote yametokea wapi, njoo tulale"

    Manka akanigeukia, akanitazama kwa macho makali, hafla akanikalia kiunoni mwangu na kuanza kuninyonya midomo yangu. Akawa kama mithili ya mbogo, aliye jeruhiwa kwa rusasi, hakutaka kunipa nafasi ya kumuandaa, alainike ili iwe rahisi kufurahia mchezo huu, unao pendwa na watu wengi sana duniani.

    Manka akawa kama mtu aliye kaa, kwa kipindi kirefu pasipo kukutana kimwili na mwanaume. Kwani kelele zake zilitawala chumba kizima. Hadi tunamaliza akabaki akiwa amenikalia kiunoni, huku jasho likimwagika.

    "Your not a Fredy"(Wewe sio Fredy)

    Manka alizungumza, huku akinitazama machoni, jasho likimdondoka.

    "Wewe ni Eddy, kwani penzi hili ulinipa miaka mingi ya nyuma"

    "Eddy! nani mimi?"

    Nilibabaika, kwani tayari Manka ameutambua ukweli wa mambo.

    "Eddy, nilijua umekufa"

    "Mimi sio Eddy"

    "Wewe ni Eddy, risasi niliyo kupiga ilitua hapa"

    Manka akaniminya sehemu aliyo wahi kunipiga risasi kwa bahati mbaya.

    "Mwili wako, ninaujua Eddy. Harufu yako haiwezi kuniondoka puani mwamgu, nilikutafuta miaka mingi, nikakukosa, nilimuona Fredy nikawa naye kama faraja ya kunikumbusha uwepo wako"

    Manka alizungumza huku, akinitazama kila mahala.

    Sikua na lakuzungumza zaidi ya kukaa kimya, kwani kitu anacho kizungumza Manka ni ukweli, kabisa na hajakosea sehemu yoyote ya mazungumzo yake.

    "Manka nahitaji kujua ukweli?"

    Sikuona sababu yà kuendelea kuminyana na Manka, kubisha kwamba mimi si Eddy, bali ni Fredy, ambaye hadi sasa hivi nimeguñdua kwamba ana idhaifu mkubwa, kitandani.

    "Kwahiyo mama, hataki kumuona huyo Juñio na mama yake?"

    "Ndio hapa, ninakazi ya kuwaokoa wao"

    "Nitakusaidia kama, kaka yangu. Tusahau mambo ya kitandani, kwani yameshapita"

    Uamuzi wa Manka, ukanishangàza kiasi cha kunifanya niaze kufarijika moyoni mwangu, kwani ukombozi wa familia yangu, unaweza kua wa asilimia mià. Kitu kilicho nitatoza ni kujua wapo Somalia sehemu gani.

    Kama Smith alivyo ahidi, alfajiri na mapema, honi ya dari lake tukaisikia, ikipiga nje ya geti. Kutokana tulisha jiandaa, tukatoka na kuelekea nje ya geti

    "Shem naye anakwenda Màrekani?"

    Smith mimi, nakwenda Somalia hakuna cha Marekani hapa"

    Smith akabaki akishangaa, kwani hakutarajia kusikia anacho kisikia. Nilamueleza Smith, historia kati yangu na Manka.

    "Haya bwana nyinyi wajanja, sasa nitawapitisha Arusha, mutaingia Kenye, kisha Somalia"

    "Sawa"

    "Kenya kuna rafiki yangu, anafamya kazi kwenye shirika la mdege, mitawakabizi kwale naye atawafanyia mchàkato wa kuingia Somalia"

    "Sawa"

    Tukatumia takribani masaa, sota kufika Arusha, kitu cha kwanza baada ya kufika Arusha, tukaitafuta namba ya Phidaya kupitia 'Caller Tracker' ambayo, iliweza kutusaidia kuijua sehemu, alipo Phidàya

    Tukajatibu namba ya mtekaji, aliye nipigia kwa mara ya kwanza, nayo tukakuta inapatikana katika eneo hilo hilo, alipo Phidaya.

    Tulafanikiwa kuingia nchini Kenya, kwa kuwahonga askari wa mpakàni. Tukafika jijini Nairobi, ambapo Smith akatukabidhi kwa rafiki yake, akatuachia pesa ya kutosha, kiasi kipatacho milioni ishirini, za kitanzania.

    Tukanunua baadhi ya nguo, zakitusaidia katika kazi iliyopo mbele yetu.

    Hatukuweza kutumia usafiri wa gari, kuhofia kuchelewa, tukakodi boti ndogo ya kwenda kwa mwendo kasi, kila sehemu zilizo na vizuizi vya askari, tuliweza kuwapa chochote kitu, na kufanikiwa kupita pasipo tatizo. Tumaingia nchini Somalia, majira ya saa nane usiku

    Manka akanipeleka kwà rafiki yake ambaye siku za nyuma, alikua akifañya kazi ya kigaidi, katika kundi la mzee Godwin, lililo sambaratishwa, baada ya kiongozi wao Mzee Godwin, kutiwa nguvuni, na jesi la Tanzania, na kufungwa kwenye gereza, lisilo julikana.

    Manka akasalimiana na dada huyu mrefu kwenda juu, mwili wake umejengeka, na anaonyesha ni mtu wa mazoezi.

    "Umemtoa wapi huyu?"

    Dada huyu alizungumza huku akiwa ameninyooshea bastola yake, ambayo sikujua hata ameichomolea wapi, kwenye mwili wake

    "Amina tulia bwana, huyu nahisi unamjua?"

    "Ndio maana nikakuuliza, umemtolea wapi?"

    Manka akamuelezea rafiki yake huyo kila kitu, kuhusiana na kutekwa kwa familia yangu, Amina akahitaji kiasi cha shilingi milioni mbili katika kuifañya kazi yetu.

    Nikampa milioni moja na nusu, kwa makubaliano ya kazi ikikamilila ninampa laki tano, iliyo salia.

    "Ahaaa, hiyo sehemu, ninaijua. Kwanza walio mteka pia nahisi ninawajua"

    Amina alizungumza baada ya kumuelezea sehemu, sehemu walipo Phidaya na Junio.

    "Ngoja kupambazuke, tutakwenda kupachunguza, usiku tukapige ambushi ya kufa mtu. Kama zile tulizo kua tukizifanya tukiwa na mzee G"

    "Amina hapo umenena"

    Manka alizungumza huku, akinyanyuka akielekea sehemu ilipo tv kubwa. Akaiwasha ila haikuwaka

    "Hii tv yako vipi?"

    "Ipige kwa juu hàpo itawaka"

    Manka akafanya kama alivyo elekezwa, na kweli ikawaka

    "Mmmm, hii tv yako kiboko, hadi makofi ndio inawaka"

    "Hiyo tv ya kibabe, hapo mwizi akiiba ataumbuka"

    "Haaaaa, king'amuzi chako ni kipi"

    "DSTv"

    "Ngoja nitafute movie za ngumi, nikikumbushie"

    Manka akaanza kubadilisha chaneli moja kwenda nyiñgine.

    "Manka hembu weka chanel yoyote ya Tanzania"

    Manka akaanza kutafuta chanel za Tanzania, na kufanikiwa kupata chaneli ya shirika la utangazaji Tanzania TBC1. Tukakuta kipindi cha kumekucha, ambapo kuna baadhi ya magazeti yanasomwa.

    "Katika gazeti la burudani, ukurasa wake wa mbele linakicha cha habari kinachosema, NDOA YA MTOTO WA WAZIRI MKUU YA....."

    Tukajikuta tukikitazama kioo cheusi cha Tv hii, kwani ilizima gafla

    "Wanesha kata umeme wao,"

    Amina alizungumza huku akinyanyuka kwenye sofa. Kwa hataka nikawasha simu yangu, niliyo kua nimeizima, nikajaribu kuingia kwenye mitandao ya kijamii, ila kukawa na tatizo la internet. Tukastushwa na sauti ya Tv, kwani umeme umerudi gafla na hatukuwa tumeizima.

    "Watatuunguzia, vitu ahaaaa"

    Amina alizungumza huku macho urmetu yakielekea kwenye Tv, tukitazama kipindi cha magazeti kilionyesha, picha moja iliyopo kweñye gazeti, likiwa limetobolewa sana kwa risasi.

    "Hiyo ni picha ya ukurasa wa mbele katika gazeti hili la Jambo leo, ikibebwa na kichwa chà habari kisemacho, MTOTO WA WAZIRI MKUU NA MKEWE WATEKWA NA WATU WASIO JULIKANA, NA RISASI ZARINDIMA ENEO ZIMA LA KANISA"

    Mtangazaji alizungumzà, huku akifunua kurasa ya ndani, akidai kwenda kuisoma taarifa hiyo kwa urefu zaidi.



    Manka akazima tv, na kuiweka rimoti mezani, akionekana kupatwa na mawazo ya gafla.

    "Mbona umezima"

    Nilimuuliza kwa sauti ya upole sana

    "Eddy, hichi ni nini ulicho kifanya kwa Fredy wangu?"

    "Nisikili......"

    "Eddy hapa hakuna cha kusikiliza, umemsababishia mwenzako matatizo makubwa sana"

    "Ndio nalitambua hilo, ila natambua kwamba hajauliwa, lazima atakua hai"

    "Una uhakika gani, hata kama Fredy hajiwezi kitandani, lakini nimempenda hivyo hivyo."

    Manka alizungumza huku akiwa amekasirika sana, machozi yakaanza kulowanisha uso wake.

    "Oya mboma mimi siwaelewi?"

    Amina alituuliza baada ya tukio lililo tokea, kushindwa kulielewa. Nilamuelezea kwa ufupi, akanielewa vizuri

    "Sasa wewe, Manka huo ni unafki sasa. Tangu lini ukamlilia mwanaume?"

    "Amina hujui tu maumivu, niliyo kua nayo nampenda Fredy tena sana"

    "Hembu sikia, ishu hapa ipo hivi. Tunakwenda kwa hao mafala walio teka mke wa bro, tukimaliza tunakwenda kwa hao mafala wengine walio teka Fredy"

    Amina alizungumza huku akiwasha sigara yake kwa kiberiti cha kutumia gesi.

    "Yaani hapa nguvu zote zimeniishia"

    "Zimekuishia kisa mwanaume. Mbona umekua fala sana mtu wangu?"

    "Manka niliye kua namjua mimi ni yule wakazi, sasa Manka wewe wa kulia lia kisa mwanaume sijui umetokea dunia gani. Hembu nyanyuka tukafanye kazi"

    "Siendi popote"

    ”Nini wewe, sasa maana ya kuja hapa ni nini?"

    "Siendi"

    Mgomo wa Manka ukaañza kunipa wasiwasi mkubwa, dalili mbaya ya mpango nilio upanga mbele yangu nikaanza kuuona ukianza kuharibika.

    "Manka nini unafanya, nini uliniahidi kulifanya juu ya familia yangu?"

    "Sawa Eddy ila elewa siendi popote"

    "Sikia Eddy asikuchanganye, mziki wako nauelewa vizuri. Twende tukapige job"

    Manka akanyanyuka na kuingia ndani, kwa Amina. Amina akamfwata kwa nyuma kwenda kuzungumza naye. Nikawasha Tv, ila nikaikuta tarifa hiyo ikiwa imekwisha, nikajaribu kuitafuta kwenye chanel tofauti, pia sikuipata.

    "Oya mtu wako amekataa bwana, tujiandae twende tukapachunguze, kisha usiku twende"

    "Poa"

    Tukajiandaa, nikavaa miwanani pamoja na kofia, tukaingia kwenye gari la Amina na kuondoka.

    "Hilo begi lina nini?"

    Nilimuuliza Amina, àliye beba begi la mgongoni, alilo liweka siti ya nyuma.

    "Lifungue"

    Nikalichukua, nikalifungua. Nikakuta kamera moja aina ya Canoon, bastola tatu, magazine kumi na mbili, na mabomu manne yakurusha kwa mkono.

    "Mmmmmm"

    "Mbona umeguna?"

    "Kazi leo ipo"

    "Ahaaa ulizani nimchezo, hii ni Somalia bwana, kuingia nirahisi ila kutoka ni ngumu"

    Amima alizumgumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari lake. Chakumshukuru Mungu, htukukutana na polisi barabarani. Mwendo wa dakika arobaini na tano, tukafika kwenye majengo ya magorofa machakavu, yaliyopo nje kidogo ya mji wa Mogadishu. Amina ajasimamisha gari pembeni na kuitoa simu yake, akaniomba namba ya simu ya jamaa aliye nipigia, akaipiga, baada ya muda ikapokelewa, akaanza kuzungumza na jamaa kisomali, ambacho sikielewi kabisa.

    "Amesemaje?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimuuliza Aminà baada ya kumaliza kuzungumza na jamaa huyo.



    "Anasema yupo hapa"

    "Ulimuambia kwamba wewe ni nani?"

    "Hapana nimemuambia nahitaji kufanya nao biashara ya mafuta"

    "Kwahiyo watakuja hapa tulipo?"

    "Hapana nilitaka kufahamu kwamba wapo hapa"

    Tukakaa ndani ya gari zaidi ya nusu saa, sikuwa ninaelewa nini maana ya Amina.

    "Tunasubiri nni hapa?"

    "Usiwe na hataka utaona"

    Tukaendelea kusubiri zaidi ya masaa mawili, magari makubwa aina ya Scania yakatoka yakiwa na matela nyuma. Yakaingia barabara ya lami, na kuondoka kwa mwendo wa taratibu. Amina akawasha gari, taratibu tukaanxa kuyafwata.

    "Tunaelekea wapi?"

    "Tunayafwatilia hayo magari moja wapo ndipo alipo mke wako?"

    "Umejuaje?"

    "Hawa jamaa huwa wanafanya biashara ya kuuza wañawake wanao wateka katika nchi za ulaya, ambapo huku wanakwenda kuuzwa kwenye makasino na mabaa makubwa kwa ajili ya ngono"

    "Sasa hapa wanawapeleka wapi?"

    "Hii moja kwa moja wanakwenda baharinia àmbàpo wanawasafirisha kutumia meli"

    "Mmmmmmmm"

    "Usigune hii ndio dunia bwana"

    Amina alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari"

    Nikaanza kuzitoa bastola moja moja, na kuanza kuzikagua kama zina ubora kwa maana nimatambua chochote kitatolea muda wowote tuliwa kwenye hio safari ambayo hadi sada hivi sitambui kama kuma udhibitisho wowote wa Phidaya kuwa ñdani ya magari haya yenye makontena makubwa.

    Kadri tulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi mahari hayo yalivyo zidi kuyoyoma, Amina hakukata tamaa, kila magari yalipo kunja naye akakunja pasipo kuhofia kama wahusika wameugundua, uwepo wetu wa kuwafwatilia kwa nyuma.

    "Usiyafwate kwa ukaribu zaidi watatustulia"

    "Usiogope"

    "Kivipi"

    "Hakuna kitakacho jitokeza"

    "Mmmm"

    Kitu ninaçho kiamini maishani mwangu, ni kuto kumuamini mtu yoyote, mbaya zaidi wale nilio waamini wote walinifamyia unyama wa hali ya juu, nikajikuta nilihangaika na kuteseka vibaya mno. Akili yangu ikaanza kumfikiria Amina, sikuhitaji kumpa uaminifu wa aina yoyote. Magari tuliyo yafwata, tukayashuhudia yakikunja kushoto mwa barabara na kuiacha barabata ya la lami na kuingia barabara ya vumbi. Amina akasimamisha gari

    "Mbona umesimamisha gari?"

    "Huku walipo ingia ni hatari sana"

    "Kwahiyo itakuaje?"

    "Itatulazimu kwenda kwa miguu, kutokana sio mbali saña na hapa"

    Tukashuka kwenye gari, tukachukua silaha zetu, kila mmoja akachukua silaha yake, tukaanza kuchanja mbuga kwa kutumia miguu. Kigiza kwa mbali kilisha anza kujitokeza, huku saa yangu ya mkononi ikinionyesha ni saa kumi na mbilo na robo. Tukatembea zaidi ya dakika kumi. Tukafika kwenye moja ya fensi , iliyo zunguka majengo machakavu, ambayo yapo pembezoni mwa bahari. Tukapenya kwenye fensi hii, iloyo na uwazi mkubwa kidogo.

    Kwa mwendo wa haràka, wenye umakini, tukafanikiwa kufika kwenye moja ya nyumba. Tukashuhudia jinsi watoto wengi wa kike wakishushwa kwenye magari hayo. Amina akachukua kamera yake, na kuanza kurekodi matukio yote yanayo endelea, huku akizivuta karibu sura za wasichana hao, weñgine walipaswa kuwa mashuleni, ila ndio hivyo wametekwa.

    Nikamuona Phidaya akisukumwa, kitoka kwenye gari alilo kuwepo, kuanguka kwake chini, kukanifanya nitake kujitoa muhanga, ila Amiña akaniwahi

    "Umataka kufanya nini?"

    "Mke wangu yule"

    "Kwahiyo? Hembu tumia akili, wewe huoni walivyo wengi. Unadhani utapona?"

    Amina alizumgumza huku akiwa amenikandamiza ukutani kwa nguvu zake zote.

    Nikamshuhudia askari mmoja akimpiga Phidaya mgongoni kwa kutumia kitako cha bunduki mgongoni, baada ya Phidaya kukataa kunyanyuka, chini.

    "Amina tunasubiria nini?"

    "Ngoja kua mvumilivu"

    Amima akiwa anaendela kurekodi, nikalichunguza eneo zima, nilawaonà askari wote katika maeneo walio kaa. Nikachukua kiwambo cha kuzuia sauti na kukifumga kwenye bastola yangu. Nilipo hakilisha kila kitu kipo sawa, sikuhitaji kusubiri, nikaanza kufyatua risasi kwa askari mmoja baada ya mwengine, nilianza kuwamaliza pasipo wao kujijua wanakwisha, kutoka na bastola yangu kuto kutoa mlio wa aina yoyote. Ñikaanza kusonga mbele pasipo kuhofia kitu cha anai yoyote, huku nikowa nahasira kali dhidi ya askari walio mtesa mke wangu

    Askari hao wakastuka, baada ya Amina kumlenga mmoja, kwa bahati mbaya akamkosa na risasi ikapiga katika tairi la gari moja na kulifanya litoe mlio. Yakaanza majibizani ya rusasi kati yetu na watekaji hawa, haikuwa kazi rahisi kwani, wengine waliongezeka wakitokea kwenye meli waliyo kua wakiisubiria kuja kuwabena Phidaya na wezake.

    "Nimezaliwa siku moja, nitakufa siku moja"

    Nilizungumza baada ya kuona mashambulizi yakianza kutuelemea upande wetu, isitoshe risasi zilitupungukia. Ikatulazimu kuokota baadhi ya bunduki za askari walio fariki, Kusema kweli, Amina anajua kujituma, jinsi anavyo piga risasi unaweza kuhisi ni mwanaume, kumbe ni mwanamke. Kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi tulivyo zidi kuanza kuwamiliki maadui zetu, wengi tuliweza kuwaua, hadi tukafanikiaa kufika katika eneo wipo lala chini Phidaya na wenzake. Maadui zetu wakaanza kukimbia ovyo, baada ya mashambulizi kuwa makali sana. Ikawa ninafasi kwetu kuhakikisha wanaondoka kabisa, wengine wakaingia kwenye meli yao.

    "Unakwenda wapi?"

    Amina aliniuliza baada ya kuniona nikikimbili kwenye meli hiyo, ambayo hadi kuwashwa kwake na kuondoka ni shuhuli kubwa sana.

    "Walinde hawa"

    Nikadi kukimbia, huku mkononi mwangu nikiwa nimebeba bumduki aina ya AK 47, walizo kua wakitumia hawa maadui. Nikafanikiwa kuingia ndani ya meli, Kazi yangu ikawa ni moja tu, kuhakikisha haondoki adui hata mmoja katika eneo hili. Nikafanikiwa kuwateketeza karibia wote.Taratibu nikaanza kunyata kuelekeà chumba cha manahoza, kitendo cha kufungu mlango, nikastukia nikirudishwa nyuma kwa kupigwa teke la uso. Kwa bahati mbaya nikajikuta nikiiachia bunduki na ikaangukia mbali nami.

    Nikanyanyuka na kukutana na jitu refu kwenda juu. Nikamtazama vizuri jinsi alivyo jazia misuli yake, kwa haraka haraka nikamfananisha na mwana mereka mmoja nchini Mareni, anayevitwa 'BIG SHOW'. Likanza kurusha makonde ambayo nilianza kuyakwepa, kutokana na urefu wake, ninamfikia kiunoni, kwa kimo changu. Katika kukwepa kwangu, akanibahatisha kunitandika teke moja, la miguu. Nikajikuta nikianguka kifudi fudi. Akaninyanyua na kuñirusha kwenye mapipa yaliyopo karibu nasi, nakunisababishia maumivu karibi mwili mzima.

    Likanifwata na kujaribu kuniinua, ila nikalikwepa. Kwa haraka nikanyanyuka, nikaanza kumpiga mateke ya miguu. Likanza kuyumba. Nikazidisha juhudi ya kulipiga miguuni hadi likaànnguka chini. Ñikaiokota bunduki yangu, nikataka kufyatua risasi ila hapakuwa na risasi iliyo toka.

    Likaanza kucheka kwa dharau. Huku taratibu likinyanyukà. Nikaitoa magazine na kuikuta haina risasi hata moja. Nikaanza kurudi nyuma kwenda kilipo chumba cha manahoza. Nikaingia ndani, nalo likazidi kumifwata. Ndani ya chumba hichi nikakuta, masanduku mawili yaliyo wazi, huki yana pesa nyingi dola za kimarekani. Ninaamini mtu huyu ndio alikua mnunuzi wa wasichana hawa. Likaanza kunirushia mskonde mazito. Sikutaka kurudi nyuma zaidi ya kukabiliana nalo, kufa na kupona. Baadhi ya ngumi zake zikawa zinanipata kisawa sawa mwilini mwangu. Sikulaza damu, na mimi nikazidi kujituma kupigana, huku ngumi zangu nikijitahidi kupiga kwenye sehemu za viungio vya mwili wake. Taratibu likaanza kulainika, hata ngumu kurusa likaanza kushindwa kwani, nilimpiga sana kwenye viungio vya mabega, tena kwa kujaribu kupanda kwenye baadhi ya meza, ili kumfikia kwenye mabega yake.

    Nikafanikiwa kuona sime mbili zikiwa zimechomekwa kwenye moja ya kabati la vioo. Nikazichukua zote mbili na kusimama, nikilisubiria jitu hili kunyanyuka, baada ya kuanguka chini.

    Likafungua moja ya droo, likkatoa bomu la kutega kwa sekunde

    "We are going to die, kid”(Tunakwenda kufa mtoto)

    Lilizungumza huku likiminya minya batani za bomu hilo, kwa haraka nikakimbia, mguh mmoja nikakanyaga kwenye meza, nikajinyanyua juu, sime moja nikàishusha kwenye mkono wake ulio shika bomu na kukatika, bomu likaangukia pembeni, jamaa akaanza kulia kwa maumivu makali huku damu ikiwa inàmtoka kwa wingi, mkononi mwake.

    Nikaliokota bomu, nikakuta zimebaki dakika mbili, kabla halijalipuka. Nikamkata mkobo wake wa pili, na kumzidishia maumivu. Nikatupa sime pembeni, nikachua masanduku ya pesa na kuyafunga, bomu likawa limebakisha dakila moja na sekunde kumi.

    "Your going to die grand paaa"(Unakwenda kufa babuu)

    Nilizungumza huku nikilichukua bomu na kulidumbukiza kwenye mshati wake. Nikayabeba masanduku haya yenye kilo kilo moja zsidi ya ishirini. Yakanifanya nishindwe kutembea kwa kasi. Nikazidi kujotahidi kukimbia huku nikiwa nimeyabeba. Mlipuko mzito ukaanza kusikika nyuma yangu, ukitokea kwenye chumba cha manahoza. Pembeni nikaona dirisha la kioo, nikalivunja kwa kutumia masanduku haya ya chuma, nikajirusha kwenda chini, kwenye maji huku nikiiacha meli ikizidi kulipuka kwa moto mkali.



    "Your going to die grand paaa"(Unakwenda kufa babuu)

    Nilizungumza huku nikilichukua bomu na kulidumbukiza kwenye mshati wake. Nikayabeba masanduku haya yenye kilo kilo moja zsidi ya ishirini. Yakanifanya nishindwe kutembea kwa kasi. Nikazidi kujotahidi kukimbia huku nikiwa nimeyabeba. Mlipuko mzito ukaanza kusikika nyuma yangu, ukitokea kwenye chumba cha manahoza. Pembeni nikaona dirisha la kioo, nikalivunja kwa kutumia masanduku haya ya chuma, nikajirusha kwenda chini, kwenye maji huku nikiiacha meli ikizidi kulipuka kwa moto mkali.

    ENDELEA

    Kitendo cha mimi kuzama, ndani yà maji ikawa ndio pona pona yangu, kwani moto mkubwa ulizidi, kurindima juu ya maji, Masanduku yenye pesa yakaanza kunishiñda nguvu, ikanilazimu kuyaachini, yakazidi kwenda chinni. Taratibu nikaanza kujilegeza mwili wangu na kuanza kw, hadi nikatolea usawa wa bahari.

    Nikailuta meli ikiendelea kuteketea kwa moto mkali, nikatazama sehemu nilipo waacha Amina na wezake ila sikuzioa gari mbili zilizo kua zimewabeba.

    Wasiwasi wangu, ukawa juu ya Phidaya, ikanilazimu kuogelea kuelekea ukingoni mwa bahari. Kitendo cha kufika ukingoni mwa bahari, kundi la watu si chini ya saba, wamesimama mbele yangu huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. Nikajikuta nikiishiwa ujanja nisijue nini nifanye

    "Toka nje ya maji"

    Jamaa aliye valia kilemba kichwani mwake aliniamrisha niweze kufamya alicho agiza. Nikawatazama vizuri, nikagundua hawa ni miongoni mwa wale wali mteka mke wangu Phidaya. Nikatoka huku mwili wangu wote ukiwa umelowa kwa maji.

    "Piga magoti kabla hatujakumwaga ubongo"

    Nikapiga magoti taratibu, sikuwa na ubishi kwani tayari nipo chini ya ulinzi wao. Wakaanza kunong'onezana, walizungumza kisomali. Macho yangu yakatazama kila pande ila sikuona magari yote mawili.

    "Umeharibu biashara yetu mshenzi wee"

    Jamaa alizungumza, huku akinipiga teke la kifua lililo niangusha chini. Sauti ya simu ya upepo ya mmoja wao ikasikika ikizungumza

    "Mkuu wasichana wametukimbia tayari wamefika kwenye mikono ya wanejeshi wa UN. Over"

    Nikuona mkuu wao akianza kuzunguka zunguka mithili ya mwenda wazimu aliye changanyikiwa. Akaanza kujipiga piga kichwani kwa mkono hadi kilemba kikaanguka chini, akanigeukia, huku akiwa amenikodolea mimacho mikali iliyo jaa hasira kama chui.

    Akaanza kunisogelea sehemu, niliyo piga magoti chini, huku mkono wake mmoja ukichomoa bastola aliyo ichomeka kwenye mkanda wa suruali yake. Nikamtazama kila hatua anayo ipiga kumifwata nilipo, hatua moja kabla hajanifikia. Nikauvuta mguu wake kwa nguvu, akaanguka chini, kwa kasi ya akabu nikamuwahi, kumpiga kabali, iliyo wafanya watu wake kuzikoki bunduki zao wakiwa tayari kwa kufyatua risasi

    "Waambie watu wako waweke silaha chini, lasivyo nakuvunja koromeo lako"

    Nilizungumza huku, nikizidi kuliminya koo la jamaa huyu, mwenye mwili mwembamba kiasi ila ulio komaa. Watu wake wakashusha silaha zao chini, hapakuwa na sehemu nyimgine ya kukimbilia zaidi ya kurudi nyuma, kuelekea kwenye maji.

    "Musitufwate"

    Nilizungumza kwa sauti ya ukali, iliyo wafaya watu wake kusimama wakinikodolea mimacho. Nikafika ukingoni kabisa wa bahari. Nikawatazama jinsi walivyo duwaa, pasipo kusubiri kitu chochote, nikaizungusha shingo ya mkubwa wao, na kuivunja kabisa, nami nikajirusha kwenye maji. Nikawacha wakimkimbilia bosi wao, niliye muacha akiwa eanguka katika sehemu tuliyo simama.

    Mwanga wa moto, wa meli inayo endelea kuteketea, ukanisaidia kuona vitu vilivyomo ndani ya maji. Nikayaona masanduku ya pesa. Nikaanza kuyafwata sehemu yalipo angukia. Kabla sijayafikia, mikawaona jamaa wakijirusha ndani ya maji mmoja baada ya mwengine, lengo lao kubwa ni kunifwata mimi sehemu nilipo. Ikanilazimu kubadili muelekeo na kuachana na masanduku ya pesa.

    Kasi yao ya kunifwata ikazidi kuongezeka. Nikapanda juu kwa kasi ili kupata pumzi itakayo nisaidia kupambana na jama hawa

    Nilastukia mmoja wao akinivuta ndani ya maji huku akiwa amenishika miguu. Nikaanza kupambana nao, huku wezangu wakiwa na visu vikali. Japo katika maisha yangu nimekutana na mambo mengi sana kuhusiana na kupambana na maadui, ila hawa wasomali ni mziki mwingine. Sikutaka kukubaliana na kushindwa japo, visu vyao mara kadhaa vimejikata kata maeneo ya mikononi, kila nilipo kua nikijaribu kuvizuia visinifikie mwilini mwangu.

    Nikafanikiwa kupata kisu cha jaa, mmoja niliye mtoboa macho, kwa vidole vyangu, ikamlazimu kukiachia kisu hicho. Nikazidi kupambana nao pasipo kukata tamaa, Nikazidi kuwapunguza hadi nikawamaliza kabisa. Nikaogelea taratibu hadi eneo nilipo zama mara ya kwanza na masanduku ya pesa. Nikavuta pumzi yakutosha kisha nikazama tena ndani ya maji. Nikayachukua yote, hivyo hivyo nikajikaza kupanda tena juu, na nikafanikiwa kutokeza juu kabisa. Nikatoka nayo hadi nchi kavu, nikatazama usalama wa kila eneo, nilajiridhisha hakuna mtu atakaye nidhuru. Taratibu nikaanza kujikongoja, huku mwanga wa mbala mwezi ukinisaidia kuona niendapo. Japo mwendo wangu ni wakuchoka sana, ila nikajika kutembea hivyo hivyo.

    "Baba mwema ni yule anaye ipigania familiavyake"

    Nilijifariji hulku nikisonga mbele, nikafanikiwa kufika sehemu tulipo liacha gari la Amina. Kwa bahata nzuri nikalikuta. Nikayaingiza masanduku yote ndani ya gari. Sikuikuta funguo ya gari, ikanilazimu kukata nyaya mbili za hasi na chanya, zilizopo pembeni ya mskani. Nikazikutanisha kwa pamoja gari ikawaka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hahaaahaaaaa"

    Nilianza kucheka mimi mwemyewe baada ya gari kuwaka, nikaligeuza kwa haraka na kurudi katika sehemu tulipo toka na Amina

    Gari ikaanza kutoa mlio wa kuishiwa na mafuta, kwa kumbulumbu zangu, kuna sehemu niliona sheli, na sehemu niliyopo hadi sheli ilipo si mbali sana. Nikafanikiwa kufika ilipo sheli, saa ya kwenye gari inaonyesha ni saa kumi na mbilo asubuhi. Nikafungua sanduku moja nilachomoa noti kadhaa za dola mia, japo zimetota kwa maji, ila hazijaharibika.

    Nikazungumza na muhudumu, akanijazia tanki la gari. Nikampa noti tatu za dola mia, kisha nikaondoka na kumuacha akishangaa kwani nikiasi kikubwa sana cha pesa ukilinganisha na mafuta aliyo niwekea kwenye gari.

    Safari ya kurudi, kwa Amina ikaanza, njia nzima nikawa makini kwa kila gari lililo karibu yangu.

    Nikafanikiwa kufika nyumbani kwa Amina, nikalisimamisha gari sehemu anapo lisimamisha, nikashuka ndani ya gari, nilitizama kila kona ya yumba, nikaridhika na usalama. Nikashusha masanduku ya pesa ndani ya gari. Nikaingia nayo ndani.

    Niajikuta nikiyaweka chini, kwa haraka, hii nibaada ya kukuta damu nyingi zikiwa zimetapakaa kwenye sakafu, pamoja na sehemu ya ukutani. Mapiga ya moyo yakaanza kuniendaa mbio. Nikaanza kufwata michuruziko ya damu iliyo elekea chumbani mwa amina kabla sijufikia mlango wa chumbani kwake, kitu kizito kikangia kupitia dirishani. Kikaanza kutoa moshi mkali ulioa anza kunipalia, nikagundua ni bomu la machozi, lililo ambanata nailio ya risasi iliyoanza kusikika ikitokea nje.



    Ikanilazimu kulala chini haraka haraka, risasi zikazidi kumiminika zikipigwa kupitia maditishani, ambayo ni yaviol na tayari yamesha vunjika vibaya mno. Kitu kilicho nichanganya sikujua risasi hizo zinatokea upande gai, na mbaya sijajua watu hawa nj waaina gani, na wanamalengo ganjni kwangu. Nikatamba haraka na kuyachukua masanduku ya pesa nikaufungua mlango wa chumba cha Amina, nukayasukumia ndani, na mi nikaingia nikiwa ninatambaa, japo moshi huu, mkali uliendelea kunipalia na kuyafanya macho yangu kumwagikwa na machozi mengi. Nikamkuta polisi akiwa ameuawa ndani ya chumba cha Amina, huku risasi kadhaa, zikiwa zimekichangua kichwa chake vibaya. Nikafunga mlango kwa ndani, nikaatafuta maji ya kunawa usoni, ila sikuyapata. Nikavua shati langu nililo livaa, nikalikojolea na kulitotesha vizuri kwa maji mengi. Nikajifunika usoni, kidogi hali ya kumwagikwa kwa machozi ikapungua. Risasi zikaendelea kurindima, nikawa ninajiuliza watu hawa huwenda wakawa ni wendawazimu, kutokana risasi zao wanazimalizia katika kuzifyatua pasipo malengo, isitoshe ukuta waa nyumba hi, kidogo ni imara sana, na risasi kupenya si rahisi sana.

    Nikatafuta kila koa ya chumba kama kuna kitu cha kuweza kunisaidia kuepukana katika adha hii ya kuingia mikononi mwa watu amwa watu ambao hadi sasa hivi sijajua kama ni poliai au laa. Katika kuyembea tembea ndani ya chumba cha Amina, nikahisi mlio fulani kutokea chuni ya kapeti lililo tandazwa chumba kizima. Nilalifunua kwa haraka na kukuta, mfuniko wa chuma, ulio fungwa kwa kufuli. Nikaanza kutafuta jinsi ya kuufungua mfuniko huu, kwakutumia ncha ya sanduku moja wapo, ñikafanikiwa kulivuñja kufuli. Nikalifungua, nikakuta ngazi ya kushuka chini, kwa haraka nikashuka japo kuna giza totoro, ila nikajiamini. Kufika chini ya ngazi, nikahisi kuna kitu, kinanigusa kichwani, nikaupeleka mkoni wanguna kushika, nikakuta kijikamba, katika kukivuta chini, taa karibia nne, zilizopo ndani ya chumba hichi zikawaka. Bunduki nyingi za kila aina nikaziona zikiwa zimepangiliwa vizuri kwenye kuta za handaki hili, nikapnda juu haraka, nikayasukumia ndani masanduku ya pesa, nikajibanza kwenye moja ya kuta, yenye dirisha, nikachungulia nje. Nikaona watu wakikatiza katiza kwenye miti mingi ya hii, nyumba. Mikononi mwao wakiwa na silaha. Kitendo cha wao kukimbia kimbia kwenye miti hii, ni kubadilishana nafasi za kufyatua risasi. Kitu kilicho nifanya nigundue hawa si polisi, hii nikutokana na vilemba vyao walivyo jifunga, pamoja na mavazi yasiyo na sare maalumu.

    "Jamaa wamekuja hadi huku"

    Nilijisemea, mwenyewe huku nikiendelea kuwatazama jinsi wanavyo fyatua risasi zinazo piga kwenye kuta ya nyumba hii.

    'Wameanza mimi, nitamaliza'

    Nilizungumza, huku nikishuka kwenye ngazi za kuingia kwenye handaki. Nikanza kufungua makabati manne yaliyopo humu ndani, nikayakuta yakiwa na bunduki pamoja na silaha kadhaa, nikakuta kisanduku cha kuhifadhia, vitu vya huduma ya kwanza. Nikafungua na kuchukua clip bandeji, nikajifunga sejemu nilizo pata majeraha ya kukatwa na visu. Nilipo hakilisha nipo salama, nikachukua bunduki, aina ya SMG, nikachukua na magazine kumi, zilizo jaa risasi.Nikachukua shati langu, nililo lilowanisha kwa mikojo, nikajifunga kichwani. Nikapanda juu, nikakuta hali ikiwa imetulia. Nikaanza kusikia minong'ono ikitokea sebleni, iloashiria jamaa, wamesha ingia ndani. Nikajibanza pembeni ya ukuta wenye mlango, taratibu nikakifungua kitasa, Na kuuvuta mlango taratibu, nikauachia, nikañza kusikia hatua za mtu akija chumbabi.

    Nikashañgàà, kunuona mtoto mdogi wa kike mwenye umri chini ya miaka kumi na tato, akiwa ameshika bunduki huku akimshangaa, polisi aliye lala chini.

    "Amefia huku"

    Alizungumza pasipo kuniona nyuma ya mlango, nilipo simama. Akaiweka bunduki yake chini na kuanza umpapasa askari huyu, nikasogea pembeni kidogo, ili asinione, kwa bahati mbaya nikagusa kikopo chenye poda kilichokua juu ya 'dreasing table'

    na kikaanguka chini na kumfanya binti huyo kugeuka haraka, tukakutana macho kwa macho.

    Kumbukumbu za wanakijiji walio vamiwa na John, na kuuliwa watoto wao kikatili, wasio na hatia yoyote. Ikapita kichwani mwangu kwa haraka, nikajikuta nikomuonea huruma binti huyu ambaye hastahili kifo kwa wakati huu. uzuri wa binti huyu, kidogo unaendana na Phdaya wangu, Macho yake, pua yake, midomo yake ni kama Phidaya. Nikawa katika dimbwi zito la kumtathimi binti huyu, nikastukia kuona mtu aliye valia sutlruali ya jeshi, akiingia ndanj ya chumba hichi, huku akimfokea binti huyu, akimuuliza mbona anachelewa kutoka.

    Nikafyatua risasi kadhaa kwa jamaa, huyu na akaanguka chini. Binti akajribu kuchukua bunduki yake, ila nikawahi kujirusha na kuisukumia pembeni. Jamaa waliopo sebleni, wakaanza kufyatua risasi nyingi katika chumba tulichopo. Nikamnyanyua binti huyu aliye chamganyikiwa na kumsukumiza kwenye ukuta usio pitisha risasi. Nikaanza na mimi kujibu mashambulizi ya watu hawa.

    "Babaa, Babaa usiniache mwenyewe"

    Binti huyu alianza kulia, huku akimtazama mzee, huyu niloye mpiga risasi na kufa mbele ya macho yake.

    Nikaendelea, kujibu mashambulizi ya jamaa hawa, walio sebleni wakakimbjlia nje. Nikatoka sebleni, huku nikiendeleà kujibu mashambulizi yao. Nikasikia sauti zikiwaashiria waondoke, haraka eneo hili kwani mkubwa wao amekufa. Ndani ya dakika tano, ukimya ukatawala nje ya nyumba. Nikarudi ndani ya chumba na kumkuta binti huyu akiwa amemuegemea baba yake, aliye jitahadi kumnyanyua hadi akamkalisha kitako.

    Binti huyu akanyanyuka, haraka na kunifwata mlangoni nilipo simama. Akaanza kunipiga piga kifuani huku akilia.

    "Umemuua baba yangu"

    "Kwa nini umuue baba yangu?"

    Aliendelea kunipiga kifuani, mwangu sikumjibu kitu chochote, akaendelea kunipiga kifuani mwangu, nikajikuta nikimtandika kofi moja la shavuni lililo muangusha chini, nakumfanya atulie kimya.

    Nikakaa kitanda huku, nikiwa nimejichokea sana. Nikajihi maumivu kwenye paja langu la mguu wa kushoto, nikajichunguza vizuri na kugundua nina jeraha risasi, iliyo nikwaruza, ila haikuingia ndani ya mguu wangu.

    "Mungu, hivi kwanini maisha yangu si yaraha?"

    Nilijikuta nikizungumza mwenyewe huku nikitazama maiti mbili zililo lala chini, sikujua hata hii maiti ya askati imetokea wapi. Ubaya wa hii sehemu, nyumba ipo msituni, na imezingirwa na miti mingi, kiasi kwamba si rahisi kwa watu wa kawaida kupafikia.

    Nikazitoa maiti zote mbili, nukuziweka sebleni, Nikaigia chini kwenye handaki, nikajitibu jeraha la risasi iliyo nipunyua. Nikachuku silaha na risasj zakutosha nikazipeleka kwenye gari, nililo likuta lipo salama salmin. Nikarudi na kuchukua masandukuvya pesa kabla sijatoka binti akapiga chafya. Nilayaweka chini nà kumsogelea karibu, nikamnyanyua na kumuweka kumkalisha.

    "Unaitwa nani?"

    "Eheeee"

    "Jina lako ni nani?"

    Akabaki akiwa amenitazama tu, pasipo kunijibu kitu cha aina yoyoye.

    "Nipo wapi?"

    "Upo duniani"

    Nilimjibu hivyo kutokana ninatambua kwamba alipoteza fahami kwa kofi zito nililo mtandika. Akanyanyuka na kutazama mazingira ya chumba, nikamuona jinsi anavyo zitazama damu zilizo tapakaa chini.

    "Kumetokea nini?"

    "Hakuna, twende zetu"

    Tukatoka chumbani, akafika sebeni, akaitazama maiti ya bana yake. Nikashangaa kumuona akianza kuupiga mwili wa baba yake mateke huku akianza kulia.

    "Kufa kufa kufa"

    Alizungumza huku akizidi kuutandika mateke mwili wa baba yake, nikabaki nikiwa nimeduwaaa nisijue nini kinacho endelea



    Ikanilazimu, kumshika huyu binti, nakumuweka pembeni ili asiendelee kupoteza muda wa sisi kuondoka katika eneo hili kwani hatutambui ni kitu gani kinaweza kutokea ndani ya dakika moja inayofwata mbeleni. Tukatoka nje huku binti akiendelea kumwagikwa na machozi mfululizo. Tukaingia ndani ya gari, nikaliwasha kama nilivyo liwasha mara ya kwañza kwa kuviunganisha vijiwaya hasi na chanya.

    "Usiondoke"

    Msichana alizungumza mara baada ya gari kuwaka. Akashuka ndani ya gari na kuzunguka nyuma, ikanilazimu na mimi kushuka. Akainama na kuchungulia uvunguni mwa gari, akaingiza mkono wake, alipo utoa nje, akawa amesheka bomu la kutega

    "Limebakia dakika tatu lilipuke, tuondoke haraka kwani yapo mengi eneo hili"

    Binti huyu alizungumza huku akiliweka taratibu chini bomu alilo lishika.

    "Kwahiyo mengine yapo humu ndani?"

    ”Yapo kwenye nyumba"

    Tukaingia ndañya gari, kitendo cha kuingiza gia, ili kuliruhusu gari hili kuondoka. Likazima gafla, nikajaribu kuviunganisha vijiwaya, ila gari halikuwaka.

    "Endesha nisukumu”

    Nilizungumza huku nikishuka kwenye gari, na kumpisha binti kwenye mskani. Nikazunguka nyuma, nikalitazama bomu lililopo karibu, linaonyesha imesalia dakika moja na sekunde kadhaa, kabla halijalipuka, wasiwasi wangu mwengine ni kwenye mabomu, yaliyo wekwa kwenye nyumba, sijajua yametegwa kwa muda gani. Kwa jinsi nilivyo jeruhiwa mwilini mwangu na kuchoka ikanilazimu kujikaza liume kusukuma gari, hili ambalo sikujua limepatwa na nini hadi haliwaki. Taratibu likaanza kusogea, nikazidi kujikakàmua kuendelea kulisukuma lizidi kwenda mbe, huku mara kwa mara binti huyu akijaribu kuliwasha. Kwa bahati nzuri, kwenye njia ya kuingilia nyumbani kwa Àmina kuna kiporomoko, kidogo, kilicho lifanya gari kuongezeka mwendo.

    Gafla gari likawaka, huku likitoa moshi mwingi.

    "Ingia twende"

    Nikalikimbilia gari, lilipo, kwani lilikua limeniacha kwa umbali fulani baada ya kuwaka. Kabla sijashika kitasa cha kufungulia mlango wa gari, nyuma tulipo iacha nyumba ya Amina, tukaanza kusikia milipuko mikubwa ya mabomu

    "Twete twende"

    Binti huyo alizungumza huku, akinitazama, nikajitosa ndani ya gari na binti hiyu akaliondoa kwa kasi kwenye eneo tulilopo, na mabomu yakaendelea kulipuka nyuma yetu.

    ***

    Tukafika kwenye moja ya kijiji, chenye nyumba chache sana, zilizo achana achana na kujengwa na udongo wa mfinyanzi. Akasimamisha gari kwenye moja ya kijumba, akashuka kabla hajafikka mlangoni mwa kijumba hicho akarudi nilipo ndani ya gari.

    "Hapa ni kijijiji kwetu, ndipo nilipokua nikiishi”

    Alizungumza huku akiwa anachungulia kwenye dirisha la gari hili upande wa siti ya dereva alipo kua amekaa yeye.

    ”Kuna usalama?"

    "Katia nchi hii, hakuña eneo lenye usalama”

    "Unaweza kushuka ñdani ya gari"

    "Ahaaa wewe nenda, nitakungojea hapa hapa"

    "Sawa ñisubirie"

    Akaingia ndani, mimi nikashuka kwenye gari na lufungua kwenye buti ya gari, nikatoa bunduki, yenye risasi za kutosha kisha nikarudi kukaa kwenye siti niliyo kaa, muda wote màcho yangu, yakawa yanatazama kila kona ya barabara, kuhakikisha ninapata usalama wangu, kwani niliyo yafanya dhidi ya watu nilio pambana nao nina imani wananitafuta kona zote za nchi hii ya Somalia.

    "Mbona anachelewa kutoka huyu?"

    Nilijiuliza baada ya zaidi ya lisaa zima kupita pasipo binti kutoka ndani ya kajumba haka kilicho kidogo sana.

    Nikataka kushuka, ila mlango ukafunguliwa wa kijumba hichi. Binti akaja nilipo

    "Samahani kaka yangu, kwa kuchelewa nilikua nikifanyà fanya usafi, kidogo nyumba ilijaa vumbi"

    "Ahaaa, ulinipa wasiwasi, nikajua umepatwa na tatizo"

    "Hapana karibu ndani"

    Nikashuka kwenye gari, nikazunguka nyuma gari, nikatoa masanduku ya pesa, binti akabeba silaha tulizo nazo. Tukaingia ndani, nikaona vyumba viwili tu ndani ya kijumba hichi, nikabaki niliwa najiuliza ni usafi gani alikua akiufanya binti huyu, ulio chukua zaidivya lisaa zima.

    'Au kuna njama kapanga?'

    Nilijiuliza kimoyo moyo, huku nikiendelea kuchunguza eneo zima la humu ndani.

    "Kaka twende huku"

    Tukaingia kwenye moja ya chumba kati ya viwili vilivyomo humu ndani, kwenye chumba hichi kuna ngazi, zakushuka kwenda chini. Sikuamini macho yangu baada ya kukuta seble kubwa, iliyo pangiliwa vizuri na inamasoma makubwa. Kuna milango kadhaa kwenye kuta za seble hii ikiashiria kwamba, nimilango ya kuiñgilia ndani ya vyumba vilivyopo chini ya handaki hili.

    "Karibu kaka"

    "Asante"

    "Jisikie upo nyumbani."

    Nikayaweka masanduku yangu chini, huku nikiendelea kuchunguza sehemu nzima, iliyo tengenezwa kwa utadi wa hali ya juu. Huku kukiwa na taa nyingi, zaukutani zinazo waka kwa mitindo tofauti tofauti

    "Kwa nini munapenda kujenga nyumba zenye mahandaki?"

    "Nikutokana na usalama wetu"

    "Duuu"

    "Pasipo kufanya hivi, tunaangamia. Watoto wengi wanatwekwa na kwenda kufanyishwa kazi mbali mbali, ikiwemo ya kigaidi"

    "Yule uliye kua ukimpiga ni nani?"

    "Baba yangu"

    "Baba yako!?"

    "Ndio, ila si mzazi. Ni baba mlezi, yeye kwenye kundi la kigaidi, watoto hua tunamuita baba"

    "Ahaaa"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Alafu sijalijua jina lako, mimi jinairwa Shamsa Al Seif"

    "Eddy, Eddy Godwin"

    "Umetokea wapi?"

    Shamsa alizungumza huku, akifungua friji lililopo hapa sebleni, akatoa soda mbili za kopo na kunirushia moja.

    "Nimetokea Tanzania"

    "Kweli?"

    "Ndio kwani vipi?"

    "Hiyo nchi ninaisikia tu, kwamba ina amani. Basi najua watu wake hawajui kutumia silaha kama ilivyo sisi."

    "Ni kweli, watu wengi hawajui kutumia silaha, kutokana na amani iliyopo. Ila ukiwa na matatizo utaweza kujua tu"

    "Ahaaaa, wewe ni askari?"

    "Hapana"

    "Mmmm mbona, unajua mbinu nyingi za kijeshi?"

    "Kawaida tuu. Ila wewe imekuaje ukawa katika kundi la magaidi?"

    "Kule, niliingia pasipo kupenda. Siku tulipo kua njiani kurudi nyumbani, kwenye ule msitu ule tulio upita, walituvamia na kumuua baba, na mama wakaniteka mimi, nikiwa na miaka tisa"

    "Ndipo walipo niunga kwenye kundi lao, wakawa wakinitumia kwenye matukio kadhaa ya ualifu"

    "Mmmm pole sana, ilikuwaje mukavamia pale?"

    "Pale tulipewa mchongo na jamaa mmoja, kwamba wewe unapesa nyingi sana, baada ya kumpa yeye pesa nyingi"

    "Ndipo jamaa, fulani wakawa wanakifwatilia pasipo wewe kujua. Ndipo ukafika kwenye ile nyumba. Kutokana hatukuwa mbali na ile nyumba. Ndio maama tulikuvamia mara baada ya wewe kuingia ndani"

    "Duu!"

    "Ndio hivyo, mara baada kupiga risasi nyingi, tukajua utakua umekufa ndipo tulipo amua kuingia ndani. Tulivyo zikuta zile damu sebleni, zikielekea chumbani

    Tukajua utakua umejeruhiwa ndipo tulipo ingia ndani na kukuta ule mwili wa askari. Ila nilibaki nimeduwaa baada ya kukuona ukiwa unanitazama kwa macho ya guruma, pasipo kuniua"

    "Baba alikua akinifokea nitoke nje kwani tayari walisha tega mabomu"

    "Sasa kwa nini, wasizifwate pesa nilizo kua nazo?"

    "Huwa wananitoa mimi kama chambo, laiti baba angeingia mule ndani, asinge kutana na tukio kama hilo basi tungesaka chumba kizima kujua ni wapi zilipo pesa, ila kutokana ulimuwahi basi ikawa kama hivyo ilivyo tokea"

    Shamsa, alizungumza huku akikizungusha zungusha kikopo cha soda yake. Machozi yakaanza kumwagika taratibu.

    "Sikupenda kuua, sikupenda niwe katili katika umri huu. Nilihitaji nisome nitimize malengo yangu ya kuwa Daktari"

    "Ila sijajua kama yatatimia tena"

    "Kwani una umri gani?"

    "Miaka kumi na saba"

    "Unataka kusoma?"

    "Ndio"

    "Basi tumuombe Mungu"

    Siku nzima tukashindia kunywa soda, hapakuwa na chakula chakupika. Shamsa akanisaidia kunisafisha majeraha yote mwilini mwangu. Akanipaka dawa nyingine aliyo ichukua kwenye kabati moja humu ndani

    "Hii inakausha vidonda, haraka. Nakumbuka baba alikua akinipaka hii kipindi nikipata majeraha"

    "Baba yako alikua anafanya kazi gani?"

    "Yeye alikua daktari na mama pia alikua dajtari, walikua wakifanya kazi kwenye shirika la msalaba mwekundu, hadi wanakutwa na mauti walikywa wanatoka kazini"

    "Pole sana"

    "Asante. Asili yangu mimi ni bara la Asia, ila mama alikua msomali. Walikutana na baba kwenye kazi yao ya udaktari ndipo walipo oana."

    Shamsa alizungumza mambo mengi juu ya familia yake, hapa ndipo nikatambua hakupaswa kuwa katika hali kama hii. Usiku kucha sikulala, ila Shamsa yeye alipitiwa na usingizi. Nikamlaza vuzuri kwenye sofa. Nikaanza kukagua picha moja baada ya nyingine. Zilizo bandikwa kwenye kuta za seble hii. Nyingi ni za Shamsa alizo piga na wazazi wake. Nikaingia kwenye vyumba vinee vilivyopo humu ndani, vyote nikakuta vina usalama wa kutosha na hapakuwa na mtu aliye jificha kama, hisia zangu zilivyo kua zikinituma.



    Asubuhi kulivyo pambazuka, nikamuamsha Shamsa, akaingia bafuni kuoga na kuvaa nguo nyingine. Alizo dai ni za mama yake, kwani zakwake zilikua ndogo kwake. Tukachukua kila kilicho chetu, tukaondoka na kwenda mjini talipo makao makuu ya umoja wa mataida kwenda kuitazama familia yangu. Ikatuchukua takribani masaa manne kufika Mogadishu, tukaingia kwenye moja ya hoteli. Tukala chakula, kuyaweka matumbo yetu sawa kisha tukaendelea na safari yetu

    "Eddy kwenye hayo masañduku kuna nini?"

    "Pesa"

    "Pesa!!?"

    "Ndio"

    Ilimlazimu, Shamsa kushangaa, kwani sikumueleza chochote kuhusiana na pesa hizo. Akasimamisha gari pembeni, kutokana yeye ndio dereva tangu mwanzo wa safari, kutokana na yeye kuwa mwenyeji katika nchi hii.

    "Pesa za nchi gani?"

    "Marekani"

    "Mmmm itabidi, tutafute sehemu tuzihifadhi"

    "Kwanini?"

    "Endapo tutakamatwa nazo, zitachukuliwa na serikali, na sisi tutaingia mikononi mwa jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano"

    "Sasa itakuaje?"

    "Hata mimi sijui kwani, tunapo kwenda nilazima tukaguliwe, ili kuruhusiwa kuingia kwenye hiyo kambi ya wakimbizi, inayo lindwa na wanajeshi wa umoja wa mataifa"

    Ushauri wa Shamsa ukaniingia kisawa sawa akilini mwangu. Nikabaki nikiwa nawaza ni wapi kwa kuziweka hizi pesa kutokana ni nyingi sana, japo sijazihesabu. Nikafikiria nimtafute Smith, anisaidie katika hili, ila pesa haina urafiki na anaweza kunibadilikia, ikawa ni tatizo jengine.

    "Kuna benki ya bacrayse hapa?"

    "Ndio, imefunguliwa wiki mbili za nyuma"

    "Nipeleke"

    Tukaghairi safari, Shamsa akageuza gari na kunipeleka kwenye banki ya Bacrayse. Nikaingia na masanduku yangu, huku nikiwa ninajiamini. Tukafika mapokezi kabla sijazungumza kitu nikastukiwa nikiguswa bega kwa nyuma. Nikageuka na kukutana na sura ya Madam Mery, akiwa amevalia suti yeusi huku akiniwekea tabasamu pana usoni mwake.

    "Za masiku mengi Eddy"

    Alianza kunisalimia, nikabaki nikiwa nimemkodolea macho nisgindwe kumjibu chochote. Nikameza fumba zito la mate huku Shamsa akibaki akinitazama.

    "Eddy"

    "Mmmmm za kwako"

    Nilimjibu huku nikijenga tabasamu la kinafki usoni mwangu.

    "Bosi kile kikao kimebakisha dakika kumi na tano kabla hakijaanza"

    Muhudumu mmoja wa kike aliye valia sare, pamoja na kitambulisho cha benki hii, alimuambia Madam Mery.

    "Sawa, kisogeze muda nina mgeni muhimu hapa wakuzungumza naye"

    "Sawa madam, nisogeze muda kiasi gani?"

    "Fanya lisaa"

    Mfanyakazi huyo aliondoka, madam Mery akaniomba twende ofisini mwake. Nikamtazama Shamsa, akakubali tuongozane naye, pasipo kujua ni uadui gani uliopo kati yangu na Madam Mery ambaye kidogo umri umesha anza kumsogea. Tukaingia ofisini kwake, na kukaa kwenye viti vilivyopo kwenye ofisi yake, yenye kibao kidogo kilichopo kwenye meza yake ya kisasa kilicho andikwa, 'Chief Exacutive Mery J.Shirima'

    Inamaana yeye ni meneja mkuu, wa benki hii. Madam Mery akanitazama kwa muda, huku akikoaa cha kuzungumza, taratibu nikaanza kukichomoa kisu changu kilichopo kwenye soksi ya mguu wa kushoto, kwa ajili ya kuikata shingo ya madam Mery aliye, nifanyia ukatili mkubwa, akishirikiana na washenzi wezake John na Victoria.



    Shamsa akanishika mkono, ulio kua ukichomoa kisu kutoka katika soksi. Akanikonyeza huku akinionyesha camera ya ulinzi, iliyopo kwenye moja ya kona ya ukuta wa ofisi hii. Nikakirudisha kisu nilipo kitoa. Nikabaki nikimtazama madam Mery kwa macho makali, yaliyo jaa hasira.

    "Eddy ninatambua kwamba una hasira na mimi"

    Madam Mery alizumgumza na kukaa kimya huku, akiyakwepesha macho yake kutazamana na macho yangu.

    "Sikupenda kufanya kile walicho kufanyia John na nwenzake. Roho yangu iliniuma sana pale nilipo sikia kwamba umekufa."

    Madam Mery alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Shamsa akasimama na kupiga hatau hadi mlangoni.

    "Eddy nipo nje ninakusubiri"

    Nikamuitikia Shamsa kwa kutingisha kichwa kumuashiria kwamba nimekubali yeye kutoka nje ya ofisi. Madam Mery akatoa kitamba kwenye pochi yake na kujifuta machozi yaliyo tapakaa usoni mwake.

    'Huyu mnafki kweli"

    Nilijiseme kimoyo moyo huku nikimtazama madam Mery usoni mwake.

    "Eddy moyo wangu ulikosa amani, nilijaribu kutafuta japo kaburi lako, nije nipige magoti nikuombe msamaha"

    "Ila sikuweza kufanikiwa katika hilo, ila nilikuka kupta amani pale nilipo kuon kwenye tangazo la magari, ndipo nilipo tambua kwamba upo hai"

    Madam Mery alizumgumza huku alinyanyuka kwenye kiti chake na kuja nilipo. Akapiga magoti chini, na kuushikilia mguu wangu wa kulia, huku aliendelea kulia kwa uchungu.

    "Eddy ninakupenda sana, ndio maana nilikupa nafasi ya kuishi tena duniani"

    "Nakuomba unisamehe, ninakuomba unipe nafasi ya msamaha wako, ili niweze kuishi kwa amaani"

    Suti ya uchungu, na yamajozi ya Madam Mery ikaanza kuilainisha hasira yangu, iliyo ganda kama barafu. Nikamnyanyua na tukasimama, akanikumbatia kwa nguvu huku akiendelea kutoa kilio cha kujutia makosa aliyo yafanya. Japo hasira bado inanisukuma niweze kumfanyia madam Mery jambo la ukatili, ila nikazidi kujitahidi kuweza kuepukana na kufanya tukio lolote baya.

    "Eddy nisamehee'

    Madam Mery aliendelea kuzungumza huku akilia kwa uchungu.

    "Ni...mekusamehe"

    Nilijitahidi kukifungua kinywa changu, kujibu nilicho mjibu Madam Mery, japo muda sote kinatetemeka kwa hasira kali. Taratibu Madam Mery akaniachia, na kunitazama machoni mwangu. Tukabaki tukiwa tumetazamana kama dakika tatu, hisia kali ya mapenzi iliyo pelekea kuyakumbuka matukio kadhaa ya nyumà dhidi ya penzi letu, na madam Mery. Zikanifanya mwili mzima kusisimka, taratibu ñikaupelekà mdomo wangu, ulipo mdomo wa Madam Mery ila akaukwepesha usikutane na mdomo wangu.

    "Eddy sio sasa"

    Madam Mery akanichia na kurudi, kilipo kiti chake, nikabaki nikiwa nimemtazama kwa mAcho yaliyo jaa matamanio mengi.

    "Umetuletea pesa nini?"

    "Eheee!"

    Nilibaki nikiwa nimemshangaa Madam Mery, huku hisia za mapezi, zikiupelekea mwili wangu kuishiwa kabisa na nguvu. Taratibu nikakaa kwenye kiti changu.

    "Eddy sio kwa sasa, hiyo kamera hapo juu ukutani inarekodi kila kitu kinacho endelea humu ndani."b

    Madam Mery alizungumza huku, akinionyeshea kamera iliyopo ukutani.

    "Ni pesa ulizo beba?"

    "Eheeee"

    "Una akaunti ya benki hii?"

    "Ndio"

    "Hembu nitajie"

    Nikamtaji madam Mery namba ya akaunti yangu, akaiingiza kwenye computer iliyopo hàpa mezani mwake. Baada ya muda akanigeuzia kioo cha çumputer hii, aina ya 'DELL'. Nikaona taarifa za benki yangu, ikiwemo picha na jina langu kamili.

    "Ila inaonyesha kwa Tawi la Tanzania umefungiwa, kwa nini?"

    "Ahaaa ni mama, ndio alinifungia"

    "Sawa, ngoja nimpigie simu muasibu"

    Akampigia simu muasibu wake kwa kupitia simu ya mezani. Tukiwa tunamsubiri muàsibu madam Mery akanipatia kokadi chenye namba ya simu yake.

    "Mimi nitakwenda kwenye kikao, kama utaondoka pasipo kuonana na mimi basi utanipigia kuniambia ni wapi ulipo"

    "Sawa"

    Akaingia jamaa mrefu, mweusi kiasi aliye valia suti, nikatoka naye ofisini na kwenda kwenye chumba chenye mashine za kuhifadhia pesa.

    Zoezi la kuzihesabu pesa likaanza, halikuchukua muda sana tukawa tumepata kiwango cha pesa ambacho ni dola za kimarekani milioni saba. Sawa na bilioni kadhaa kwa pesa ya tanzani. Nikatoa dola laki moja na nyingine zilio salia zikaingizwa kwenye akaunti yangu.

    "Eddy hatuwezi kwenda kwenye kambi ya wakimbizi muda umesha pita"

    Shamsa alizungumza huku tukitoka kwenye mlango wa benki.

    "Kwani ni saa ngapi sasa hivi?"

    "Saa tisa mchana na muda wa kuingia pale, ni kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nanechana"

    "Sasa itakuaje?"

    "Ni hadi kesho"

    "Nasi tutafute sehemu ya kulala"

    "Sawa, ila kama ukihitaji iwe rahisi sisi kuingia ndani mwa kambi tunaweza kununua vitu kama mifuko ya mchele, sabuni, mafuta ya kupikia. Tukifika pale tunawaambia sisi tunatoa msaada"

    "Wee dogo una akili sana"

    Kila wazo alilo litoa Shamsa, sikulipinga. Tukaanza kazi ya kutafuta alivyo sema. Ikatulazimu kununua na nguo ambazo zitatufanya tuonekane kweli ni watoaji msaada. Ikatulazimu pia kununua gari, jengine aina ya pickup lililo tuwezesha kubeba mizigo hiyo. Tukakodi vyumba viwili kwenye hoteli moja kubwa yakitalii, iliyopo katikati ya mji wa Mogadishu, ambapo usalama wake kidogo ni wauhakika

    Mida ya saa mbili, usiku nikampigia simu madam Mery simu, nikamuelekeza sehemu nilipo. Akaniambia nimpe dakila kadhaa atafika sehemu tulipo.

    "Una uhakika utalala naye?"

    Shamsa aliniuliza swali mara baada ya kuksta simu.

    "Kwa niki umeuliza hivyo?"

    "Kwa maana yule mama nina mjua vizuri sana"

    "Ana nini?"

    "Ni mke wa waziri wa fedha hapa nçhini. Na mumewe ni mmoja wa watu hatari hapa Somalia"

    "Nisinge penda kukuona unajiingiza kwenye matàtizi ambayo hayakuhusu. Wewe kwa sasa jaribu kuiangalia familia yako"

    Shamsa alizungumza maneno, yaliyo nifanya nibaki kimya nisijue nini cha kujibu.

    "Usiku mwema nakwenda kulala, ila nilicho kueleza kiweke akilini. Tutaonana asubuhi"

    Shamsa akanyanyuka, kitandani mwangu, akapiga hatua hadi mlangoni akafungua na kutoka. Nikabaki nikiwa nà msongo wa mawazo, nikiiwazia familia yangu. Kijiusingizi kikaanza kunipitia taratibu, kila nilipo jaribu kuitazama saa ya ukutani, masaa yalizidi kuyoyoma pasipo Madàm Mery kutokea.Mida ya saa sifa usiku, nikasikia mlango ukigongwa taratibu. Nikanyanyuka, nikiwa nimeishika bastola yangu, iliyopo chini ya mto. Nikasimama pembeni ya mlango.

    "Nani?"

    Niliuliza kwa sauti ya chini, ambayo mtu aliyopo nje ya chumba ataisikia vizuri.

    "Mery"

    Ilikua nisauti ya Madam Mery nikashika funguo, iliyopo kwenye kitasa nikaizungusha tatatibu, huku nikiwa makini kwa lolote litakalo jitokeza. Nikaufungua mlango, nikakuta Madam Mery akiwa amevalia baibui jeusi, bila ya salamu kaingia ndani. Nikachungulia nje kwenye kordo, hapakuwa na mtu. Nikafunga mlango.

    Madam Mery akanikumbatia kwa furaha, huku akihema mihemo yenye pumzi moto, iliyo katiza mara kadhaa kwenye shingo yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mbona umeche......."

    Madam Mery akaniwahi kuninyonya mdomo sangu, na kuikatisha sentensi yangu. Fukuto zito la mzhaba likatukamata miiili yetu. Nikalivua baibui la Madam Mery na kulitupa kando. Tukaendelea kunyonyàña midomo yetu, nikamnyanyua na kumuweka kitandani, tukasndelea kupeana burudani za mwili.

    Saa kumi alfajiri Madam Mery akastuka, kutoka usingizini, baada ya kupitiwa na uchovu wa penzi zito tulilo peana usiku mzima.

    "Unakwenda wapi?"

    "Nyumbani"

    "Usiku wote huu?"

    "Kuna kazi nakwenda kuifanya"

    Madam Mery alizungumza kwa wasiwasi, huku akiingia bafuni, akaoga na kurudi chumbani, Akavaa haraka sana, akanifwata kitandani, akanipiga busu mdomoni.

    "Kesho Eddy"

    Madam Mery akatoka haraka, hadi nikabaki nikishangaa.Saa kumi na mbili Sahamsa akaingia chumbani.

    "Eddy za kazi"

    "Kazi?"

    "Ndio kazi uliyo ifanya jana usiku na mtu wako?"

    Nikastuka, Shamsa akatoa simu, niliyo mnunulia jana, akanirushia kitandani. Nikaona video ya jinsi madam Mery alivyo kuja, chumbani kwangu Nikichungulia na kuufunga mlango.

    "Huyo ni mimi niliye rekodi hiyo video, pasipo nyinyi kujijua. Piga picha siku wakiwa ni watu wa huyo waziri, itakuaje?"

    "Jibu unalo, siñà haja ya kukusimulia kitakacho tokea. Amka twende tulipo panga"

    Nikajikuta nikianza kumuogopa Shamsa, sikukua kama atanifwatilia kwa ukaribu kiasi hichi. Nikajiandaa, tukalata kifungua kinywa na kuelekea ilipo kambi ya wakimbizi, huku Shamsa akiwa ndio dereva.

    Gafla Shamsa akafunga breki kali, huku akijitahidi kumkwepa mtu aliye lazwa barabarani akionekana hajitabui. Gari, likafanikiwa kusimama.

    "Eddy usishuke, hili eneo sio salama"

    "Ngoka kwanza"

    Nikavua koti langu la suti, pamoja na tai. Nikaichomoa bastola yangu na kuanza kutembea kwa tahadhari, kwenda alipo lala mtu huyo, huku macho yangu yakiwa makini kila sehemu. Nikafika sehemu alipo mtu huyo. Kwakutumia mguu nikamgeuza. ili niione sura yake, kutokana amelala kifudi fudi. Moyo ukanipasuka baada ya kukuta ni Amina rafiki wa Mnka, akiwa ameuawa kikatili, huku macho yake mawili yakiwa yameng'ofolewa



    Huku yakitoka funza wadogo wadogo, harufu kali ya mwili wa Amina, haikunizuia kuchuchumaa kumtazama vizuri. Mwili wake tayari umeanza kuharibika kutokana na kujeruhiwa vibaya kwa mapanga, sikuweza kuusogeza pembeni ya barabara, kutokana na baadhi ya nyama za mwili wake, kushikamana na barabara hii ya lami. Nikajikuta machozi yakianza kunilenga lenga, nikatazama pande zote ya eneo tulilopo hapakuwa na dalili yoyote ya mtu kutokea zaidi ya Shamsa aliye simama, nje ya gari letu akinitazama kwa kitu ninacho kifanya.

    Nikazidi kujihisi uchungu baada ya kukisogeza kichwa cha Amina kwa kutumia bastola yangu, na kukuta ubongo wote ukiwa nje. Huku sehemu ya pembeni, upande wa kushoto ikiwa imepasuliwa vibaya mno.

    "Ahaaa"

    Nikajikuta nikitoa sauti ya uchungu, huku nikisimama. Wasiwasi ukaanza kunijaa moyoni mwangu, wa kwanza kumfikiria ni mke wangu Phidaya, ambaye kwa mara ya mwisho alikua na Amina, ambaye ni huyu amelala hapa barabarani, akiwa tayari ni mfu. Nikaanza kupiga hatua za taratibu kurudi kwenye gari. Nikafungua mlango wa gari pasipo kumsemesha chochote Shamsa, ambaye naye aliingia ndani ya gari na kuliwasha. Akanitazama kwa muda jinsi machozi hanavyo nitiririka kwenye mashavu yangu pasipo kutoa mlio wowote wakulia. Akawasha gari na kuondoka eneo hili taratibu.



    Mwendo wa takribani lisaa lizima, sikufungua kinywa changu kuzungumza na Shamsa, ambaye mara kwa mara aliniita pasipo kumjibu chochote. Akasimamisha gari kwenye moja ya sheli ya mafuta. Akashuka na kuzungumza na muuzaji wa mafuta kisha yeye akaingia kwenye duka lililopo hapa kwenye sheli. Picha kadhaaa, za Amina alivyo nisaidia kwenye tukio la kuiokoa familia yangu, zikaanza kunijia kichwani. Hadi picha ya mwisho ya mwili wake, ulio haribika ndio ikagota kwenye ubongo wangu, unao shuhulka na kumbukumbu. Nikaichomoa bastola yangu haraka na kuinyoshea kwa mtu aliye chungulia kwenye kioo cha upande wa Shamsa.

    "Ohhhhhhhh"

    Sauti ya dada, muhudumu wa sheli hii, niliisikia. Macho yake akawa meyatoa kwenye bastola niliyo mnyooshea. Nikamuona jinsi anavyo tetemeka kwa woga. Jasho jingi likaanza kunimwagika. Huku nikiyang'ata meno yangu kwa hasira kali, iliyo changanyika na uchungu wa kutamani kulipiza kisasi kwa yeye aliye muua Amina.

    "Eddy unafanya nini?"

    Shamsa alizungumza huku akiufungua mlango wa gari, akausogeza mkono wangu pembeni ulio shika bastola. Akaweka bidhaa alizo zinunua siti ya nyuma.

    "Samahani dada, pesa yako hii hapa."

    Shamsa alizungumza huku akimpa dada huyo, pesa anayo dai kwa mafuta aliyo tuwekea kwenye gari. Shamsa akafunga kioo, akawasha gari na tukaondoka.

    "Eddy unatatizo gani, nji nzima unakazi ya kumwagikwa na machozi, nakuuliza hutaki kunijibu?"

    Shamsa liniuliza kwa sauti ya ukali, huku akinikodolea macho. Nikairudisha bastola yangu nilipo ichomoa kwenye kiuno, ilipo kua imebanwa vizuri kwa mkanda wangu wa suruali.

    "Geuza gari turudi, kwenye ule mwili"

    "Nini, hivi Eddy umechanganyikiwa?"

    Shamsa alizungumza huku, akifunga breki za gari na kulisimamisha kando ya barabara.

    "Nimekuambia geuza gari turudi, kwenye ile maiti."

    "Eddy tumia akili, mtu humjui, ya nini kujifanya msamaria mwema, kwa matatizo yasiyo yako. Tumebakisha kilomita moja tufike, wewe unataka turudi tena kilomita ishirini nyuma? Ahaaa siwezi kufanya ujinga kama huo."

    Shamsa alizumgumza kwa kujiamini sana. Nikamtazama kwa macho makali yaliyo jaa hasira na uchungu. Nahisi atambui ni nini anazungumza.

    "Tunarudi au haurudi?"

    Ilinibidi na mimi kuzungumza kwa sauti ya hasira, iliyo mstua Shamsa, ambaye kwa kipindi kifupi nilicho kaa naye, amenizoea sana.

    "Eddy, fikiria juu ya familia yako, fikiria juu ya mwanao na mkeo. Kwa nini unataka kufanya vitu vitakavyo kuhatarisha usalama wako, na kukutenga na familia yako?"

    "Fikiria hilo, hii nchi haina usalama kama umavyo fikiria wewe, jiulize yule ni kwanini amuauwa na kutupwa pale barabarani, piga picha ni mimi au wewe ndio tumetupwa pale barabarani, utajihisi vipi?"

    Shamasa alizungmza kwa sauti ya upole huku machozi yakimwagika, nikabaki niliwa ninafikiria ni nini cha kufanya. Sikuwa na uwezo wa kuhairisha safari ya kwenda kwenye kambi ya wakimbizi ilipo familia yangu, na kurudi kuuchukua mwili wa Amina ambao tayari umesha haribika vibaya mno, na hata niiuchukua nisingeweza kuuzika leo, pia endapo polisi watanikamata na mwili huu, wataniweka kuzuizini hadi watakapo fanya uchunguzi ambao sijajua utachukua muda gani kukamilika.

    "Eddy, natambua wewe ni mtu mwema. Ila si kwa kila kitu unatakiwa kufanya wema, mengine inapo kupasa kufanya ukatili fanya hata kama mtu unamtambua. Ila kama atakuwa adui yako wewe fanya kwani ukimuacha atakudhuru wewe"

    Shamsa alizungumza maneno yaliyo nifanya nianze kukata tamaa, juu ya mwili wa Amina, uliopo barabarani.

    "Washa gari tuendelee na safari"

    Shamsa akafanya kama nilivyo muagiza. Safari ikaendelea.

    "Kwani unamtambua marehemu?"

    "Ndio"

    "Eheeee ni nani yako!?"

    "Anaitwa Amina, ndio aliye nisaidia katika kuiokoa familia yangu, hadi ikachukuliwa na jeahi la umoja wa mataifa. Na wakapelekwa kwenye hiyo kambi ya wakimbizi kwa usalama wao zaidi"

    "Mmmm, kuna kitu kinacho endelea hapa. Kuwa makini Eddy. Yaani hii nchi anaye kuua huwezi kumdhania kabisa. Laiti ningeamua kukuua mimi si ningekuua siku tulivyo kutana. Ila uliniacha kwasababu ni mtoto."

    "Ndio"

    "Ndio unatakiwa kuwa makini, na hata watoto wadogo, kwani huku watoto pia wamepandikizwa roho za chuki na ugaidi"

    "Ile nyumba iliyo lipuka ni ya yule dada, aliye uwawa"

    "Weee, acha utani!?"

    "Utani wa nini sasa?"

    "Ndio ukweli huo."

    "Mungu ailaze mahali pema, roho ya marehemu"

    "Amin"



    Taratibu nikaanza kupata picha ya siku nilivyo rudi, nyumbani mwa Amina na kukuta mwili wa askari aliye kufa. Wasiwasi ukazidi kuongezeka baada ya kumkumbuka Manka, ambaye tulimuacha kwenye nyumba ya Amina na sikumkuta na hadi sasa hivi sifahamu ni wapi alipo.

    "Ngoja niipate familia yangu kwanza"

    Nilizungumza, huku Shamsa akisimamisha gari, kwenye megesho ya nje ya geti, la kuingilia katika kambi ya wakimbizi.

    Tukaacha bastola zetu ndani ya gari, tukashuka na kwenda kwenye kijumba kidogo, kilicho jengwa kwa ajili ya ofisi ya wanajeshi wanao simama getini, kuangali ni nani anaye ingia na kutoka ndani ya kambi hii. Wakatukagua kabla ya kuingia kwenye ofisi hiyo. Kisha wakaturuhusu kuingia ndani ya ofisi, baada ya kuridhishwa na kutukagua kwetu.

    "Mumesema nyinyi, niwatoaji misaada si ndio?"

    Mwanajeshi mmoja, alituulizaa kwa lugha ya kifaransa, huku akitutizama machoni kwa umakini.

    "Ndio"

    Nilimjibu kwa kujiamini, huku nikizichunguza nguo alizo vaa, zikionyesha bendera ya nchi ya Ufaransa kwenye bega la mkono wake wa kushoto, huku mkono wa kulia kukiwa na kitambaa cheupe, kilicho andikwa kwa maandishi makubwa yenye rangi nyekundu 'MP'.

    "Mumetokea wapi?"

    "Ohhh Eddy karibu"

    Kabla sijamjibu, aliingia mwanajeshi, mwenye nyota tatu begani, wanajeshi walio kuwemo ndani ya hii ofisi wakampigia saluti. Ikanibidi kuipokea salamu yake kwa tabasamu huku nikimpa mkono. Japo sifahamiani naye, na wala sina kumbukumbu ni wapi nilionana naye.

    "Jamani huyu ndio yule jamaa aliye okoa familia ya balozi wa Marekani nchini Afrika kusini."

    Wanajeshi wengine wakaanza kutabasamu na kunipa mikono ya pongezi hata wale walio nisemesha kwa kifaransa, wakazungumza kingereza japo, kifaransa ninakijua kidogo. Nikatoka na mkubwa wao aliye jitambulishwa kwa jina la Jonson, tukafika lilipo gari letu. Tukapanda wote watatu. Tukaingia getini, bila ya kukaguliwa kutokana tupo na mkubwa wao huyo mwenye nyota tatu begani mwake.

    Tukafika sehemu ya kitengo cha wanao pokea misaada, inayo letwa ndani ya kambi hiyo. Tukatambulishwa, na kuwakabidhi misaada yetu. Nikawaomba waniangalizia jina la Junio na Phidaya, katika orodha ya wakimbizi walio pokelewa kipindi cha hivi karibuni. Mama anaye husika na kutunza kumbukumbu za majina ya wakimbizi, akawasha computer iliyopo ndani ya ofisi hii. Akaandika jina la Junio

    "Junio nani?"

    "Junio Eddy"

    "Yeah wametokea saba hapa"

    Aliniita na kunionyesha majina hayo ya kina Junio Eddy yakiwa saba yamejipanga vizuri.

    "Hembu andika jina la Phidaya"

    Akaandika haraka, ila computer, ikaonyesha hakuna jina kama hilo. Nikajaribu kuandika mwenyewe ila pia jibu likawa ni moja, kwamba Phidaya hayupo, kwenye orodha hiyo.



    Tukaondoka kuelekea kwenye mahema ambayo, wanaishi wakimbizj na pis tunaweza kuwapata Junio, hema la kwanza, tukakuta Junio huyo ni mtu mzima, mwenye umri zaidi yangu. Kila Junio tunaye onyeshwa si mwanangu, kwani wote wamezidi umri wa Junio wangu. Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, baada ya Junio sita nilio onyeshwa na sio mwanangu. Tukafika kwenye hema ambalo walidai tutampata Junio huyo mwengine waliye nieleza ni mtoto mdogo.

    Tukakuta watu wengi kiasi wakiwa wamekusanyika nje ya hema hilo, huku wakiwa na huzuni machoni mwao. Muhudumu mmoja kati ya wanne tulio ongozana nao, akamfwata muhudumu, anaye onekana ni daktari aliye kuwepo nje ya hema hilo akizungumza na watu. Waka non'gonezana, na daktari huyo akatutizama, kisha akawaomba watu wanao msikiliza, wamsubiri kidogo azungumze nasi.

    "Huyu ni dokta Martin, ndio mganga mkuu wa hii kambi"

    Jamaa, alitutambulisha kwa dokta huyo, mwenye asili ya Uingereza na anaumri mkubwa kiasi.

    "Walikua wakimuulizia Junio Eddy"

    Dokta akakaa kimya kidogo, huku akinitazama machoni, Shamsa akanishika mkono wa kulia vizuri, kutonana na yeye kuchoka kwa kuzunguka kwenye kambii hii kubwa, huku jua kali likituchoma, ipasavyo.

    "Ohhh Junio Eddy, tunetoka kumzika masaa mawili ya nyuma"

    "Nini doktar?"

    Mstuko wangu, uliwafanya hata watu walio kua wakimsikiliza doktar huyo kunigeukia mimi.

    "Ndio, tulimkuta na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, na yeye ndio mtu wa kwanza kuugua ugonjwa huo ndani ya kambi hii. Na hapo nilikua nikitoa mafunzo kwa watu wengine endapo wataona mtu mwenye dalili hizo watufahamishe haraka iwezekanavyo."

    Sikuweza kuyazuia machozi yangu kunimwagika, Shamsa akawa wa kwanza kunikumbatia kwa nguvu huku akinibembeleza.

    "Mwanangu amekufa kabla sijamuona"

    "Hapana Eddy ni kazi ya Mungu, jikaze usilie mbele za watu"

    Shamsa alizungumza huku, akinibembeza, Shamsa akanishika mkono, tukaondoka huku nikimuacha Jonson akizungumza na daktari huyo pamoja na wahudumu, tulio kuja nao, wakionekana kustushwa na ugonjwa huo ambao ni hatari sana duniani.

    "Eddy jikaze, wewe ni mwanaume. Usilie kila mmoja akajua unamatatizo"

    Shamsa aliendelea kunifariji, huku tukizidi kutembea kurudi getini. Kundi kubwa la watoto, wenye umri kama miaka kumi hivi, tukalikuta limekusanyika kwenye moja ya mti, huki wakishangili watoto wawili wanao rushiana makonde. Nikajifuta machozi na kwenda walipo watoto hao, nikapita katikati yao, na kumkuta mtoto mmoja akiwa amelazwa chini, na mwenzake amwe nguvu kumpita yeye.

    Nikawatennganisha, nikamnyanyua mtoto aliye chini, ambaye sura yake kidogo imevimba, kutokana na kichapo hicho.

    "Musipigane sawa, watoto wazuri"

    Nilijikaza tu, kuzungumza hivyo. Sikutaka kuwataza machoni watoto hawa, ili wasigundue kwamba ninalia. Nikapita kati kati yao, nikabaki nikimshangaa Shamsa, akiwa ameduwaa, akiwatazama watoto hao.

    "Shamsa twende"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Eddy ngoja"

    Shamsa alizungumza, huku akipiga hatua akipita katikati ya watoto hao. Akamfikia yule aliye pigwa, anaye onekana kuvimba sura yake. Akamtazama vizuri, kisha akanitazama na mimi.

    "Eddy"

    "Mmmm"

    "Huyu ni mwanao"

    Shamsa alizungumza, huku akimtazama mtoto huyo, niliye anza kumtazama kwa umakini.

    "Mtoto unaitwa nani?"

    Shamsa alimuuliza mtoto huyo, ambaye na mimi nikaanza kupata mashaka naye, japo sura yake imevimbishwa kwa ngumi za mwenzake na kuifanya iumuke kiasi, ila anafanana kidogo na mimi.

    "Jack"

    Kulitaja jina la Jack, maumivu ya kufiwa na Junio wangu yakarudi upya, kwani hakuwa Junio wangu.

    "Jack nani?"

    "Mama hajaniambia baba yangu anaitwa nani"

    "Mama yako, yupo wapi?"

    "Yupo kule, ninapo kaa"

    "Twende ukatuonyeshe"

    Shamsa akamshika Jack mkono na kuongozana naye.

    "Eddy twende, umashangaa nini?"

    Shamsa aliniambia kwa sauti ya chini, nikawafwata kwa nyuma, huku nikimchunguza vizuri mtoto huyu kwa nyuma. Sikutaka kuwema asilimia mia kwamba ni mwanangu, kwani tayari amesha nichanganya, kwa jina lake la Jack. Tukaona moshi mwingi, ukienda juu. Ukitokea kwenye mahema ya mbele yetu, Jack akajichomoa mikononi mwa Shamsa na kuanza kukimbia kuelekea moto ule unapo tokea. Ikamlazimu, Shamsa naye kumkimbiza kwa nyuma, mimi sikuwa na hata nguvu za kukimbizana nao, zaidi yakuwafwata kwa nyuma. Wakawahi kufika kwenye mahema yanayo ungua kwa moto. Nikafika na kumkuta Jack akilia huku akimuita mama yake, ambaye anahisi yupo ndani ya hema hilo. Huku watu wengine wakiendelea kuzima moto kwa kutumia mchanga, kwani hapakuwa na moto wa kufanyia hivyo.

    "Jack, Jack"

    Sauti ya msichana, ilisikika nyuma yangu, kabla sijageuka, kumtazama dada huyo nikajikuta nikipigwa kikumbo kwa nyuma, dada huyo akanipita na kukumbatia na Jack, huku dada huyo akinipa mgongo, na sikuiona sura yake. Tukabaki tukitazamana na Shamsa, huku mimi nikiwa sina la kuzungumza.

    "Ulikuwa wapi mwanangu"

    Sauti ya dada huyu, ikazidi kunipa ushawishi wa kutaka kumgeuza, ili kuiona sutmra yake kwani inaendana na sauti ya Phidaya, japo imejaa mikwaruzo mingi, kama mtu ansye ugua kifua kikali.

    "Nilikua na hao hapo.'

    Jack akanyoosha kidole kwangu, na kumfanya mama yake anigeukie. Phidaya, akanitazama kwa mshangao mkubwa, huku machozi yakianza kumlenga lenga. Kukondeana kwa Phidaya, kumembadili sana, muonekano wake. Mashavu yake yameingia ndani, akionekana kukosa lishe bora kwa muda mrefu. Mavazi aliyo yavaa, yanechakaa, sana na yanazidi kumuonyesha anamatatizo mengi, nywele zake za ndefu, zimejaa masponji mengi, ya godoro alilo lalia. Kiufupi Phidaya amechakaa sana kwa shida alizo pitia.

    Taratibu Phidaya akasimama, akanisogelea huku machozi yakimwagika. Nikataka kumkumbatia, ila akanizuia, nisifanye hivyo.

    "Phida.."

    Kofi zito kutoka kwa Phidaya likatua shavuni mwangu, lililo mfanya Shamsa kustuka. Phidaya akaachia msunyo mkali na kumshika mkono Jack.

    "Junio tuondoke"

    Phidaya alizumgumza kwa hasira, na kuanza kuondoka na mwanaye, wakijichanganya katikati ya watu walio kusanyika hapa.



    Sikuhofia kukatiza katikati ya watu, kuwafwata Phidaya na mwanagu Junio. Furaha moyoni nwangu ikawa imezaliwa upya kuiona familia yangu. Iliyo nigharimu maisha yangu katika kuitafuta hadi leo kuitia machoni kwa mara ya pili, ukiachilia siku ya kwanza Junio alivyo zaliwa mbele ya macho ya watu wengi akiwemo Shatani John na Victoria.

    "Phidaya, Phidaya"

    Nilimuita Phidaya niliye mkaribia, kumfiki. Akasimama na kunitazama kwa macho makali sana, yaliyo jaa hasira huku machozi yakimwagika taratibu.

    "Unakwenda wapi mke wangu, kumbuka nimehangaika kwa ajili yako, nimejitolea maisha yangu kwa ajili yako na mwanangu. Kwa nini unanikasiriki, kosa langu ni nini haswa?"

    Nilizungu huku machozi yakianza kunitiririka.

    "Nimekua muuaji kwa ajili yako, nimefanya kila niwezalo kufanya kwa ajili yako, ila umaona yote hayana dhamani si ndio?"

    "Eddy nyamaza. Nilikuomba usioe, ila kwa nini ulioa. Umeniacha nahangaika, naishi maisha ya kitumwa na mwanangu. Tumekua watu wa kubadilisha majina kwa ajili yako. T...."

    "Phidaya mimi sijaoa mwanamke yoyote, nilijitoa kufa na kupona kuwakomboa nyinyi mukiwa kwenye maroli kwenda kuuzwa nchi za nje. Nimefanya kosa?"

    "Eddy acha uongo, haukuwa wewe, uliye tuokoa, Umemuoa mwanamke aliye nidhalilisha na kuniita mimi malaya, mimi?"

    "Phidaya, achana na hayo maneno. Njoo tukamlee Junio. Twende tukaishi kwa amani na upendo. Unatambua ni mazingira gani ulimzaa Junio, huku na mimi nikiwa kwenye tabu gani."

    "Junio sio mwanao, ni mwanangu peke yangu. Junio twende zetu"

    Phidaya alizungumza huku akimshika mkono Junio, na kumvuta waondoke ila Junio akagoma kwenda popote.

    "Mama uliniambia mtu, akiniuliza baba yangu ni nani, nimuambie simjui. Ila Eddy ni baba yangu, mara ngapi ulikua ukimpigis simu. Anamapenzi ya dhati na sisi. Mama nimechoka kuishi maisha haya ya ukimbizi. Mpe baba nafadi yake, aonyeshe ni jinsi gani anavyo tupenda."

    Japo Junio kiumri ni mdogo, ila maneno aliyo yazungumza huku akilia yakanifanya mwili wangu kusisimka. Phidaya akamtizama Junio kwa macho ya mshangao, kisha akanitazama na mimi.

    Nikafungua vifungo vya shati langu, nikakivua na kumpa Shamsa anishikie.

    "Majeraha yote haya, nikwaajili ya kuiokoa familia yangu. Mwili wangu haukua na dhamani juu ya kuziokoa nafsi zenu. Msikilize anacho sema mwanao. Anahitaji malezi yetu sote. Tafadhali mke wangu, rudi mikononi mwangu au unataka mwanangu aendelee kuishi maisha haya ya shida. Tazama jinsi sura yake ilivyo umuka kwa kupigemwa na wezake. Je unataka awe hivi kila siku?"

    Nilizungumza kwa uchungu, huku nikipiga magoti chini, sikujali ni idadi ngapi ya wagu walio tuzunguka wakitushangaa. Junio akamshika mkono mama yake.

    "Mama, unanifundisha niwe mpatanishaji kwa walio gombana. Mshike baba mkono anakupenda"

    Phidaya aliendelea kulia kwa uchungu, sura yake yote ikabadilika na kuwa na uwekundu fulani, kutokana na kulia kwa uchungu sana.

    "Nakuomba mama, patana na baba anakuhitaji bado"

    Maneno ya Junio yakamlainisha Phidaya. Taratibu Phidaya akarudi sehemu niliyo piga magoti, na yeye akapiga magoti chini, huku akilia. Kwa nguvu akanikumbatia. Nikamvuta Junio wangu, naye nikamkumbatia huku sote machozi ya furaha yakitumwagika. Watu walio tuzunguka wakaanza kupiga makofi, yafuraha. Shamsa akabaki akinikonyeza huku akitabasamu.

    "Nakupenda mume wangu"

    "Nawapenda wote"

    Tukaendelea kukumbatiana kwa furaha.

    "Eddy muda"

    Shamsa alininong'oneza baada ya kuona tunakumbatiana sana. Tukanyanyuka, nikambeba Junio wangu ambaye kwa sasa anatarajia kufikisha umri wa miaka mitano.

    "Nitakufanyia sherehe kubwa siku ya kuzaliwa kwako"

    Nilimuambua Junio, huku tukielekea kwenye ofisi kukamilisha taratibu zote za kuwachukua Phidaya na mwanangu, na kuwa mikononi mwangu.

    "Kweli baba"

    "Ndio unataka ifanyikie wapi?"

    "Mama kule kwa kina yule mchezaji uliye ninunulia mpira wenye jina lake ni wapi?"

    "Brazil"

    "Ndio, dady nataka huko huko na mimi nikawe mchezaji mpira"

    "Usijali mwanangu, unaweza kucheza mpira?"

    "Ndio baba nataka niwe kama Ronaldo"

    "Sawa mwanangu utakuwa, tena kabla sijasahau, huyu ni Shamsa, mdogo wangu. Kwa sasa atakuwa dada yake Junio"

    "Kweli dady?"

    "Yeah"

    Nikambusu Junio kwenye paji la uso, jambo lililo zidisha furaha kati yetu sote wanne.

    ***

    Kitendo cha ndege kutua kwenye uwanja wa ndege nchini Brazil, likawa ni jambo la kumshukuru Mungu, sote tukafungua mikanda ya siti zetu tulizo kalia, ikiashiria kwamba safari yetu immefika mwisho. Tukatoa mabegi yetu ya nguo, katika sehemu tulipo yaweka. Tukatoka ndani ya ndege kama abiria wengine. Tukafika eneo la kukaguliwa, tukafanikiwa kupita pasipo kusumbuliwa, juu ya hati zetu za kusafiria. Tulizo zikata nchini Kenya tukisaidiwa na rafiki wa Smith, aliye tukutanisha naye kipindi tunatoka Tanzania mimi na Manka, ambaye hadi sasa sijui yupo wapi.

    Kwa msaada wa ramani tuliyo pewa na rafiki wa Smith, juu ya miji yote mikuu nchini Brazili, ikatusaidia kutufikisha kwenye hoteli tuliyo kusudua kufikia tangu tukiwa nchini Kenya. Hoteli hii inapatikana pembezoni mwa fukwe za bahari zijulikanazo kwa jina la 'Copar Carban'.x

    Sehemu tuliyo chukua kwa ajili ya makazi ya wiki mbili, ina vyumba vitatu, seble, kubwa pamoja na xjiko kubwa. Kila chumba kimejimudu kwa huduma zote muhimu kama choo na bafu.

    "Eddy hapa umelipia bei gani?"

    Phidaya alizungumza huku akikagua kagua chumba chetu cha kulala, chenye hadhi ya nyota tano.

    "Kwa siku ni dola elfu sabini"

    "Mmmmm kwa chumba hiki au?"

    "Kwa sehemu yote, hii"

    "Kweli una pesa ya kuchezea, hii ni birthday ya mwanao mambo ni haya, Je siku ya ndoa yetu itakuaje"

    "Ndio ujiulize sasa, nataka kuihakikishia dunia nzima kwamba ninakupenda mke wangu"

    Phidaya akanikimbilia, nilipo simama. Akanirukia na kuning'inia kifuani kwangu. Huku miguu yake akiipitisha kiunoni mwangu na kuikutanisha nyuma.

    "Wewe ni mwanaume jasiri, i wish wanaume wote wangekua kama wewe. Ninaamini furaha ingepatikana katika ndoa nyingi."

    "Ni wachache wenye moyo kama wangu. Ila kikubwa nimekupata wewe na mwanangu, ninaamini furaha itarudi upya"

    Phidaya hakusita kuusogeza mdomo wake, karibu na mdomo wangu. Akanitazama kwa muda, kisha kwa haraka akaanza kuunyonya mdomo wangu. Kutokana na nguvu nilizo nazo, sikuweza kutetereka, kwani fujo anazo zifanya Phidaya mdomoni mwangu, huku nikiwa nimembeba, mtu unaweza kuanguka chini.

    Nikamlaza kitandani, huku akiendelea kuninyonya lipsi zangu, mikono yangu nikaishusha kifuani mwake, na kuanza kuzichezea chuchu zake. Kwa raha anazo zipata Phidaya, akajikuta akifumba macho yake. Nikazidi kuutadhimini uzuri wa Phidaya. Hapa ndipo nilipo jilaumu, kwa nini nilikua na magubegube, Sheila na Madam Mery. Kwa kupitia kioo kikubwa, kilichopo kwenye kitanda chetu. Nikamuona Junio akiwa amesimama mlangoni huku akiwa ameshika mpira alio nunuliwa na mama yake. Mdomo wake akiwa ameulegeza akishangaa tunacho kifanya. Nikamuona naye Shamsa, akisimama nyuma ya Junio, wote walikua na safari ya kuingia chumbani kwetu. Shamsa akamfumba macho Junio, aliyeganda akishangaa kama mshumaa wa pasaka. Shamsa akamyanyua Junio taratibu huku akiwa amemfumba macho. Akanikonyeza, na mimi nikamuonyesha ishara ya dole gumba kwa kutumia mkono wa kulia huku mkono wa kushoto akiendelea kuchezea chuchu za Phidaya. Shamsa akatabasamu, taratibu akaurudishia mlango wetu, huku mkono alio mziba macho Junio akiutumia kuufungia mlango, na kumpa fursa Junio kushangaa vya mwisho mwisho.

    "Eddy ni nini hicho?"

    Phidaya aliniuliza huku akiyafumbua macho, yake kutazama kila kona ya chumba.

    "Kitu gani?"

    "Kilicho gusa mlango"

    "Hakuna kitu bby"

    Phidaya akapotezea, na kuendelea na zoezi la kuunyonya mdomo wangu. Huku kila ma}ra akihakikisha ananigusa kila kona ya mwili wangu. Tukavuana nguo tulizo zuvaa, na kubaki kama tulivyo zaliwa.

    ***

    Sote tukajikuta tukiwa tumechoka, kutokana na mechi tuliyo ipiga, saa ya ukutani inatuonyesha ni saa tisa alasiri. Huku mechi tukiwa tumeianza saa sita mchana, uzuri ni kwamba tulifika nchini Brazil, saa kumi na moja alfajiri na hadi tunafika hotelini, ilikua saa sita kasoro.

    Phidaya akashuka kitandani huku, akiyumba yumba

    "Eheee leo Eddy umenikomoa, hadi miguu imepoteza nertwork. Kweli wewe ni baba Junio. Sikukosea kuzaa na wewe"

    "Hata wewe ulinikamia, hapa nina kiu"

    "Kiu ya nini tena? Kama ni yakitandani ahaaa usije ukaniua bure"

    "Kiu ya maji"

    "Ahaa ndio umalizie matamshi yako"

    Phidaya akafungua friji, akatoa chupa ya maji, akanirushia kisha yeye akaingia bafuni. Sikuamini kwamba ipo siku nitakuja kumpata mke wangu. Hapa ndipo nilipo tambua, ukijibidiisha kwa kila jambo zuri, mwisho wake nifuraha.

    "Eddy Eddy"

    Phidaya aliniita kwa sauti ya juu, iliyo nistua. Nikanyanyuka haraka na kukimbilia bafuni. Nikamkuta akiwa amesimama kwenye bomba linalo mwaga maji kwa mfumo wa kama mvua.

    "Una nini mke wangu"

    "Hahahaaaa, kumbe unanipenda. Nimekuita tuje kuoga."

    Phidaya akanivuta karibu yake, na kunikumbatia.

    "Kelele nyingine tutakuja kuuana kwa....."

    Phidaya akauwahi mdomo wangu kwa kukiwekea kidole chake, ili nisimalize kuzungumza nililo hitaji kuzungumza"

    "Shiiii kila mtu na chake. Nisipo kutania wewe nimtanie nani?"

    "Ahaa..."

    Fhidaya akaniziba mdomo wangu kwa mdomo wake. Busu alilo nipa likanifanya nikae kimya.

    "Hii ni siku yetu, sitaki kelele zako"

    "Sawa bosi Phidaya"

    "Am not your boss"

    "But."

    "Am your wife, mother of your child"

    "Mama Junio"

    "Ndio maana yake"

    Tukamaliza kuoga, kisha tukarudi chumbani, Phidaya akanichagulia nguo za kuvaa, zinazo endana na mazingira ya kupungia upepo kwenye fukwe. Tukatoka sebleni. Hatukuwakuta Shamsa na Junio, tukatazama kwenye vyumba vyao ila hatukuwaona.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Watakuwa kwenye fukwe"

    "Sasa watakwendaje pasipo kutuaga"

    Phidaya alizungumza huku akiwa amekasirika, akafungua mlango na kutoka, nikabaki nikicheka, kutokana hakulishuhudia tukio la Junio na dada yake. Tukafika kwenye fukwe iliyo jaa watu wengi. Tukawakuta wakicheza mpira na watoto wengine, huku, Shamsa akiwa refa wao.

    Junio alivyo tuona akakatisha mchezo na kuja tulipo huku akifwatana na Shamsa.

    "Mbona mumeondoka bila kutuaga?"

    "Mama tuliwaku..."

    Shamsa akawahi kumziba mdomo Junio huku akitabasamu. Mimi nikawa nimeielewa maana ya Shamsa kumziba mdomo Junio.

    "Wangetuaga saa ngapi mke wangu wakati mlango tulifunga?"

    Phidaya akashusha pumzi, akibaki anatushangaa sote.

    "Mumeshinda ninyi leo"

    Sote tukabaki tukimcheka Phidaya aliye nuna, kisa tu hajaagwa na wanae.

    Usiku ukapita salama salmini, kulipo pambazuka tukaanza mizunguko ya kununua vitu kwa ajili ya siku ya kuzaliwa ya Junio, iliyo bakisha siku mbili hadi ifike. Tukazunguka maduka kadhaa, hadi inafika mchana ikatulazimu kuingia kwenye mgahawa mmoja kupata chakula cha mchana.

    "Jamani mumesha wahi kula hivyo vyakula mivyo agiza au ndio ushamba. Musije matumbo yakawauma, bado tuna mizunguko mingi"

    Nilizungumza kwa kuwatani. Kila mmoja akajibu anauhakika na chakula alicho kiagizia hakita mletea madhara yoyote. Kila mtu akaletewa chakula chake, Phidaya akawa ndio mtaja majina ya vyakula vilivyo wekwa mezani kutokana na kuvifahamu vizuri.

    Tukamaliza kula, nikalipa pesa wanayo tudai. Tukatoka na kuvuka barabara upande wa pili, kwenda kwenye duka moja la viatu.

    "Dady nimeusahau mpira wangu"

    "Wapi?"

    "Pale chini ya meza, tuliyo kaa"

    "Chagueni viatu, ngoja nikachukue huo mpira.

    Nikawaacha mimi nikarudi kwenye mgahawa tulio toka. Nikafika kwenye meza, tuliyo toka kukaa muda si mrefu. Nikaukuta mpira wa Junio anao upenda kuliko kitu chochote. Kitendo cha kunyanyuka, nikamshuhudi Sheila na John wakiingia ndani ya mgahawa huu, wakitafuta sehemu ya kukaa, pasipo wao kuniona.



    Nikabaki nikiwa ninawashangaa, hadi wakapata sehemu ya kukaa pasipo wao kuniona. Nafsi moja ikawa inanishawishi kwenda walipo kaa, ila nafsi moja ikawa inanikatiza kufanya ujinga kama huo kwani sehemu nilipo iacha familia yangu si salama kabisa. Na linaweza kuwa kosa kubwa sana la kupotelewa tena na familia yangu. Nikaendelea kuwatazama jinsi wanavyo onekana ni wenye furaha sana. Sheila hakuonyesha dalili yoyote kuwa na ujauzito kutokana na nguo alizo zivaa zimembana sana mwili wake.

    Nikapiga hatua hadi mlangoni, nikasimama huku nikifikiria ni nini nimfanyie John kwa yale yote aliyo nitendea kipindi nikiwa mikononi mwake. Jasho lililo changanyika na hisia kali ya asira taratibu likaanza kunimwagika. Huku likiambatana na mapigo ya moyo yalio nifanya nijihisi vibaya. Kwa haraka hali hii ninakumbuka ilinitokea kipindi nikiwa ofisini mwa balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, pale alipo ingia John na Victoria, wakiwa miongoni mwa wageni walio alikwa na balozi huyo.

    Nikajikaza na kutoka nje ya mgahawa. Nikatafuta sehemu nikashika nguzo moja kati ya nguzo kadhaa zilizopo pembezoni mwa barabara. Kizunguzungu kilicho nishika gafla taratibu kikaanza kupungua taratibu, huku jasho likiendelea kunimwagika usoni. Kitu kilicho nichanganya ni matone kazaa ya damu, yaliyo anza kutoka puani.

    "Ohhh Mungu wangu, nini hichi?"

    Nilijisemea huku nikiyatazama matone ya damu yanayo dondoka chini.

    "Sir you need help?"(Muheshimiwa unahitaji msaada)

    Askari mmoja anayelinda kwenye mgahawa huu, aliniuliza baada ya kunitazama tangu nikiwa ninatoka nje, mpaka ninashikilia nguzo hii ya taa za barabarani.

    "I need water"(Nahitaji maji)

    Akaingia ndani ya mgahawa, akatoka akiwa ameshika chupa ya maji. Akaifungua, na kunikabidhi. Nikajimwagia kichwani kidogo, kisha nikanawa usoni kutoa damu zilizo churuzika kutoka puani mwangu.

    Nikasubiri kama dakika tano, mwili kidogo ukapata nguvu za kutembe. Nikamshukuru mlinzi, nikavuka barabara na kwenda kwenye duka nilipo waagiza Phidaya awachagulie wanae viatu. Nikawakuta wakiendelea kuchagua chagua viatu wanavyo vipenda.

    "Mbona umelowa kichwani?"

    Phidaya aliniuliza huku akinigusa gusa kichwani mwangu.

    "Kichwa kidogo kilikua kinaniuma, ndio nikanawa kichwani"

    Ilinibidi kumdanganya Phidaya kwa maana vita yangu na John, nitaka niimalize mimi nwenyewe japo Phidaya naye alihusika katika mateso yote tuliyo sababishiwa na John.

    "Hiii damu nayo imetoka wapi?"

    Aliniuliza huku akinishika kwenye kifua changu akinionyesha matone kadhaa ya damu.

    "Dady hapo je, nimependeza?"

    Junio alisimama mbele yetu, huku akiwa amevalia viatu aina ya Supra, huku akiwa ameshika miwani iliyo endana na viatu alivyo vivaa, ikanilazimu kumjibu Junio kwanza na kulikwepa swali la Phidaya.

    "Yeah umetokelezea mwanangu."

    "Je nikivaa hii miwani?"

    "Umekua kama Michael Jackson"

    Junio akanifwata nilipo simama, tukagonganisha mikono, akaondoka akiwa amefurahi sana.

    "Huo ubishoo mwanao ameridhi kwa nani?"

    "Nikuulize wewe baba mtu, mtoto anapenda kuvaa vitu vizuri kama anajua kuvinunua"

    "Muache bwana ndio muda wake huu wa kupendeza"

    "Sawa tuachane na hayo, nijibu hizo damu umetoa wapi?"

    "Tutazungumza nyumbani"

    "Eddy umetoka kupigana?"

    "Hapana mke wangu"

    "Ila ni nini?"

    "Sijapigana mke wangu. Hembu nenda ukawaambie hao wanao wafanye haraka turudi hotelini. Sijisikii vizuri"

    Phidaya akanitazama machoni kwa umakini, kisha akawafwata Shamsa na Junio, sehemu walipo.

    Nikasimama kwenye ukuta wa vioo wa hili duka ulio elekea sehemu ulipo mgahawa, nilipo waacha John na Sheila. Dakika kama tatu, nikamuona John na Sheila wakitoka kwenye duka hilo. Wakaingia kwenye gari moja yakifahari iliyo simama baada ya wao kusimama nje.

    Nikastukia nikiguswa kwa nyuma, nikageuka na kumkuta Phidaya akiwa amesimama nyuma yangu, huku macho yake yakielekea lilipo gari walilo panda Jonh na Sheila.

    "Unashangaa nini?"

    Phidaya aliniuliza.

    "Nashangaa magari"

    "Alafu ile gari nimeipenda"

    "Iipi?"

    "Ile lililo ondoka nje ya mgahawa"

    Nikagundua Phidaya hajamuona John, laiti angemuona asinge zungumza maneno kama haya.

    "Nitakununulia"

    "Mmmm ila inaonyesha ni gari la gharama sana"

    "Hakuna shida, tutatafuta tununue na sisi, lakwetu"

    "Haya njoo uwalipie hawa wanao viatu vyao walivyo vichagua"

    Nikafika sehemu ya kulipia nikakuta viatu vya Junio na Shamsa vikiwa vimepangwa kwenye meza moja kubwa na kila mmoja amechagua pea ya viatu zaidi ya kumi.

    "Eheee vyote hivi munakwenda kuvaa au kuweka mapambo?"

    "Kuvaa"

    Shamsa alinijibu huku akitabasamu.

    "Mmm haya bwana"

    "Ila kaka ndio watoto hao, usilalamike"

    Jamaa muhudumu alizungumza kiswahili nakutufanya sote tushangae.

    "Unajua kiswahili?"

    "Ndio kaka, nilikulia Nairobi Kenya. Ila kaka familia yako ipo vizuri sana"

    "Asante"

    "Huyo mwanao wa kike amefanana sana na mama yake na huyo wa kiume ni chata yako kabisa."

    "Etieer ehee"

    "Ndio, hongera sana, umejua kuchagua."

    Jamaa, alikua mzungumzaji sana, ila kusema ukweli Shansa anafanana sana na Phidaya, kuanzia rangi za mwili hadi sura zao. Japo mara kadhaa, Phidaya alikua akikataa hajafanana na Shamsa.

    "Ni kiasi gani nadaiwa?"

    Janaa akaminya batani ya mashine iliyo mbele yetu. Ikatoa bei ya pamoja ya viatu vyote.

    "Hembu weka hiyo miwani kwenye meza"

    Junio akaweka miwani kwenye meza, vilipo viatu. Mashine ikaongeza bei.

    "Ni dola elfu moja na miatano"

    Nikatoa pochi yangu, nikatoa dola mia mia kumi na tano na kumkabidhi muhudumu. Wafanyakazi wengine wakachukua viatu na kuviweka kwenye mifuko.

    "Jamani kuuliza si ushamba. Hivi hiyo meza ndio inahesabu bei za vitu vinavyo wekwa juu yake?"

    Nilimuuliza muhudumu baada ya kuona tukio hilo, lililo nishangaza sana.

    "Ndio, inarahisisha kazi na kutoa shida ya wateja kulalamika kwamba tunawazidishia bei wateja. Ukiweka hapo kitu chochote kinacho uzwa humu ndani ya duka letu, basi bei inatoka kama hapa mulivyo ona, kwahiyo hakuna mabishano."

    "Haki ya Mungu, hii mashine ikiwekwa kwenye maduka ya wachaga watafilisika"

    "Wachaga wa Tanzania?"

    "Ndio"

    "Ahaaa kwa nini?"

    "Unajua kitu kama cha dola tano, watakuanzia kukuuzia dola kumi, ukiwa mjinga wana kula ila ukiwa mjanja utashuka nao hadi bei halisi"

    "Haaaaa, kwani wewe kaka kabila gani?"

    "Ahaa kabila hapo...."

    "Hapo nini si ujibu, kigugumizi cha nini?"

    Phidaya alidakia kwenye mada niliyo kua nikizungumza na muhudumu.

    "Mimi mwenyewe ni mchaga ila nimechanganyia na mpare"

    "Mungu wangu, hayo makabila nasikia ni wabaili sana kwa nchi ya Tanzania?"

    "Waongo hao, hukuna kitu kama hicho, tena ndio makabila yanayo ongoza kwa kutumia pesa bila kuijutia."

    "Mmmmm"

    "Usigune si unaniona mimi haoa ninavyo wapapendesha wanangu. Ngoja tuondoke kaka tumezunguka sana"

    "Sawa kaka ninaitwa Salim"

    "Mimi ni Eddy, huyu mke wangu na hawa ni wanangu"

    "Karibuni sana"

    "Asante"

    Kwa uchangamfu wa jamaa huyu, ukanifanya mwili wangu kurudi katika hali ya kawaida hata, hasira niliyo kua nayo dhidi ya John ilanipotea. Tukatoka nje ya duka. Tukakodisha taksi hadi Hotelini, moja kwa moja nikaingia chumbani kwetu, nikawaacha Phidaya na wanae wakiendelea na kujipima pima nguo na viatu walivyo nunua. Nikachukua simu iliyopo mezani, nikaipakata mapajani, nikaingiza namba za simu ya Blanka mdogo wa Sheila. Kwa bahati nzuri simu ikaanza kuita. Ikaita kwa muda hadi ikakata. Nikajaribu kuipiga tena ikaita kwa muda mrefu, kabla haijakata ikapokelewa.

    "Haloo"

    Nilizungumza, ila Blanka hakuitikia.

    "Blanka"

    "Wewe nani?"

    Blanka alizungumza kwa sauti yaupole, iliyo jaa wasiwasi mkubwa.

    "Upo sehemu gani?"

    "Wewe nani kwanza?"

    "Eddy"

    "Eddy gani?"

    Nikaanza kupata wasiwasi dhidi ya Blanka nikahisi nimekosea namba, kwani hata namba yenyewe sikuwa naikumbuka kivile.

    "Kwani wewe upo nchi gani?"

    "Tanzania, kwani wewe ni Eddy gani au ndio hii mimamba ya Fremasoon? Hata kama munanichukua hamuwezi kunichukja damu ya Yesu imenifunika, washenzi nyinyi"

    Simu ikakatwa nikabaki nikiwa ninashangaa, sikujua maneno yote hayo yametokea wapi.

    "Labda nimekosea, ila sauti mbona niyake?"

    Nilizungumza huku nikiirudisha simu mezani nilipo itoa, nikaingia bafuni, nikaoga na kurudi chumbani. Nikakuta simu ikimalizia kuita na kukatika. Nikafungua kabati lenye nguo zetu, nikiwa ninaendelea kuchagua chagua nguo ya kuvaa, simu ikaita tena. Nikaipokea na kuiweka sikioni. Huku nikisubidia kuisiki sauti ya Blanka

    "Eddy toka uje kuwaona wanao walivyo pendeza"

    Haikuwa sauti ya Blanka bali ni Phidaya ndio alizungumza.

    "Sawa nakuja"

    Nikakata simu, nikamaliza kuva na kutoka sebleni. Nikawakuta Shamsa na Junio wakiwa wanapigwa pigwa picha na mama yao, kusema ukweli wamependeza sana.

    "Kaa na wewe hapo niwapige picha"

    Phidaya alizungumza, akiniomba nikae kwenye sofa walilo kaa Junio na Shamsa. Huku akiwa ameshika camera aina ya Cannon D7 tuliyo inunua kwa ajili ya kuchukua matukio baadhi katika siku ya kuzaliwa kwa Junio.

    "Nitapigaje picha na nguo hizi?"

    "Kwani zina nini, hembu kaa bwana"

    "Haya mwaya mamyto"

    Nikakaa katikati ya Shamsa na Junio. Phidaya akawa na kazi ya kutupiga picha huku, tukiwa tunabadilisha mikao tofauti tofauti.

    "Hizi picha tunazitupia facebook"

    Phidaya alizungumza huku akitufwata kwenye sofa tulilo kaa akituonyesha picha tulizo piga.

    "Zimependeza"

    Shamsa alizungumza huku akiwa na furaha sana, kwani nimeamua kuifanya familia hii kuishi kwa amani, chochote watakacho hitaji kutoka kwangu, wakipate kwa muda muafaka.

    "Haya na wewe mamyto kaa niwapige picha"

    Phidaya akakaa katikati yao, na mimi nikaanza kuwapiga picha huku nao wakibadilisha miako tofauti tofauti.

    "Nizamu ya baba na mama"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shamsa alizungumza huku, akinifwata nilipo simama.

    "Ile laptop mumeifungua kwenye boksi lake"

    "Bado"

    "Itoe"

    "Ngoja nikaichukue ipo chumbani kwa Junio"

    Shamsa akaingia chumba cha Junio, akarudi akiwa na boksi lenye laptop tuliyo nunua. Akaitoa na kuiweka mezani. Nikampa kamera, tukapiga piçha kadhaa nikiwa na Phidaya kisha tukapiga tukiwa na mtoto wetu Junio.

    "Yaani facebook leo watakoma"

    "Kwànza muna account ya hiyo facebook au unasema tu watawakoma"

    "Nitafungua, mimi Eddy, nifungulie kwa jina gani?"

    "Mr and Mrs Eddy"

    "Jina gani hilo? Mwaya Shamsa fungua kwa jina la Eddy family"

    Phidaya alipendekeza jina lake, lililo nilazimu mimi kulikubali tu kishingo upande. Tukamaliza kupiga piga picha, nikaingia ndani kujipumzisha huku nikiwaacha wao wakifanya shughuli zao.

    ***

    Jioni Phidaya akaniamsha kwa ajili ya kupata chakula cha jioni. Nikatoka na kukuta Shamsa akichezea chezea laptop huku Junio akicheza game ya mpira kwa kutumia deki ya 'Play station 4' niliyo mnunulia kama moja ya njia ya kukuza kipaji chake cha kucheza mpira.

    "Eddy njoo uone"

    Shamsa aliniita kuangalia anacho kifanya kwenye laptop.

    "Cheki hadi sasa hivi nina marafiki mia tano"

    "Ahaaa mimi nilijua una kitu cha cha maana kumbe ni hao marafiki"

    "Ndio wanaendelea kuniomba urafiki na kukoment kwenye picha zetu."

    "Acheni munacho fanya ni muda wa msosi"

    Nilizungumza huku nikiwatazama Junio na Shamsa.

    "Huyo Junio wako hataki kubanduka kwenye hiyo tv na migemu yake"

    "Junio, Junio"

    Wala Junio hakunisikia ninavyo muita, nikatazama jinsi anavyo wachezesha wachezaji wa timu aliyo ichagua kwenye game hiyo. Nikamtazama mchezaji wake anayekwenda kufunga goli, kabla hajafika golini nikachukua rimoti ya tv na kuizima

    "Dadyyyyyyyy"

    "Ni muda wa kula"

    "Nifainali dady"

    "Eheee ni muda wa kula, utaendelea baadaye"

    Ilibidi nimfokee kidogo Junio, taratibu akanyanyuka na kukaa kwenye meza ya chakula huku akiwa na sura ya kukasirika.

    "Junio ukinuna unatisha"

    Shamsa alimtania Junio na kumnya azidi kununa huku machozi yakimlenga lenga.

    "Eddy umeniharibia mtoto"

    "Kwa nini?"

    "Amechukua hasira zako zote, japo ni mdogo ila kanajifanyaga kababe. Kalikua nakazi ya kupigana na wezake kule kambini"

    "Kwangu atanyooka. Tena Junio ukiendea kununa, sikufanyii sherehe na vitu vyote navirudisha madukani tulipo vinunua"

    "Am sorry dady"(Samahani baba)

    "Nime kusamehee"

    Furaha ya Junio ikarudi kama kawaida, Tukamaliza kula chakula.

    "Asante dady"

    "Asante Eddy na Mama"

    Shamsa na Junio wakamaliza kula na kutushukuru, kila mmoja akarudi katika shuhuli yake. Tukasaidia na Phidaya kutoa vyombo tulivyo kula na kuvipekeka jikoni. Uzuri wa hotel hii, unaweza kujipikia chakula chako ukiwa unahitaji kufanya hivyo. Tukasaidiana kuviosha vyombo.

    "Ehee niambie zile damu ulizitoa wapi?"

    "Tutazumgumza kitandani"

    "Sawa"

    Tukamaliza kuonysha vyombo na kuvipanga vizuri, tukawaaga watoto wetu na kuingia chumbani wao wakaendelea na mambo wanayo yafanya. Phidaya akapitiliza bafuni kuoga, baada ya muda akarudi na kujirusha kitandani.

    "Nasubiria hayo mazungumzo"

    Nikashusha pumzu huku nikimtazama Phidaya anaye hitaji nimuambie ni nini kilicho nikuta.

    "Nina tatizo mke wangu"

    "Tatizo! Tatizo gani?"

    "Kipindi fulani nilipo kua Afrika Kusini nilifanyiwa uchunguzi na kubainika nina ugonjwa wa hasira ambao, nikikasirika sana damu puani hua zinanitoka, pamoja na mwili kushikwa na kizungu zungu"

    Nilimfinya Phidaya juu ya ugonjwa wa saratani(Canser), ambao niligundulika unaninyemelea.

    "Mmmm leo ni nini kilicho kukasirisha?"

    Nikamtazama Phidaya kwa macho ya kumdadisi kama anaweza kuhimili kile nitakacho kwenda kumuambia.

    "Nilikumbuka, kitu licho nifanyia John. Nikajikuta nikiwa nimemasirika sana"

    Ilinibidi nimdanganye tena kwani hakuwa jasira kwa lile nililo panga kumueleza kuhusiana na John

    "Ni hilo tu au kuna jengine?"

    "Hakuna jengine zaidi ya hilo"

    "Ila baba Junio, kama ni huyo John, achana naye. Kikubwa umesha ipata furaha yako"

    "Una uhakika na unalo lizungumza?"

    "Kama mimi nimesha msamehe japo sihitaki kuonana naye. Kwa maana nikimuona nitatamani nimuue?"

    Nikamchunguza Phidaya nikagundua ana usingizi unao mnyemelea, hata anacho kizungumza hakzingatii.

    "Kwanza Junio alivyo zaliwa, aliwapeleka wapi. Hadi mukawa munazungumza na mimi?"

    "Ni stori ndefu, kesho tutazungumza tukiwa tumetulia. Ila msamehe tuu"

    "Siwezi kumsamehe, hadi nichukue kila kitu alicho nichukulia mikoni mwangu"

    "Utavichukua vitu vipi?"

    "Vingi tu"

    "Mtu mwenyewe yupo huko Afrika kusini utampataje?"

    "Nitampata tu"

    Katikati ya mazungumzo Phidaya akapitiwa na usingizi, mzito ulio tokàna na uchovu wa kutwa nzima. Saa ya ukutani inaonyesha ni saa saba usiku.

    Sikuwa na hata lepe la usinguzi, nikaibeba simu ya mezana na kwenda nayo sebleni, ambapo nikamkuta Shamsa akiwa amepitiwa na usingizi. Huku Junio akiwa amejilaza kwenye sofa.

    "Shamsa amka ukalale"

    Shamsa akanyanyuka kiuvivu, akaifunga laptop.

    "Niachie laptop hiyo"

    "Usiku mwema"

    Shamsa alizungumza huku akipiga miyayo ya uchovu. Nikamnyua Junio na kumuingiza chumbani kwake, huku akiwa usingizini. Nikamlaza kitandani na kumfunika vizuri na shuka.

    Nikarudi sebleni na kukaa kwenye kiti chenye meza iliyo na laptop. Nikaifungua na kukuta ikiwa bado ipo hewani kwenye mtandao wa Facebook. Nikatazana tamzama alicho weka Shamsa, Picha moja niliyo piga mimi, Junio na Phidaya inaonekana ikiwa na maoni mengi ya watu. Ikanivutia niyafungue. Kitu kilicho nistua ni baadhi ya maoni ya watu yakionyesha masikitiko yao juu ya kifo changu. Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi huku wasiwasi ukinijaa. Nikataona maoni ya Blanka aliyo yaandika kwa herufi kubwa.

    'MBONA SIELEWI NI NINI HICHI?"

    Nikachukua simu na kumpigia Blanka tena, safari hii akapokea haraka.

    "Blanka mimi ni Eddy"

    "Ndio sauti yako nimeikumbuka, jana ulivyo piga nilikua usiku nimelala"

    "Vipi kuna lipi jipya?"

    "Jipya bwana, ni mhabari juu ya kifo chako"

    "Kifo changu, kivipi?"

    "Ndio, kitu kilicho nifanya nijue hujakufa ni picha nilizo ziona hii asubuhi facebook, ukiwa na familia yako. Hapo ndipo nikakumbuma uliniambia unakwenda kutafuta familia yako"

    "Sasa kifo changu kipi?"

    "Tumemzika majuzi juzi Eddy aliye uawa pamoja na dada Sheila"

    "Fredy aneuawa?"

    "Ndio, walitekwa kwenye arusi yeye na Sheila, ila hadi sasa mwili wa Sheila haujapatikana"

    "Sasa nakuomba usimuambie mama kuhusiana na hii ishu."

    "Eddy mama ana hali mbaya sana, amepararaizi baada ya kifo chako, hali, hanywi yupo yupo tu"

    "Nini?"

    "Ndio hivyo, dokta wake amesema tunaweza kumpoteza mama muda wowote kuanzia leo. Hapa nilipo nimechanganyikiwa"

    Nikakata simu, mwili mzima nikawa kama umezizima, picha ya Jonh na Sheila zikanijia kichwani jinsi walivyo kua na furaha, nilipo waona kwenye mgahawa.

    "John nilazima ulipe kwa hili. Nikatuua kwa mkono wangu mwenyewe, ole mama yangu afe, nitakufanya kama Derick"





    Kila nilicho kifikiria juu ya adhabu nitakayo mpa John, sikupata jibu la uhakika. Nikazima kila kitu na kurudi chumbani kwetu. Nikajilaza kitandani taratibu huku mawazo yakiendelea kuniandama. Kikubwa nikawa ninamfikiria sana mama yangu. Sikulala hadi kunapambazuka.

    "Umeamkaje baby?"

    Phidaya alinisalimia mara baada ya yeye kuamka.

    "Safi vipi?"

    "Ahaaa poa, alafu nimeota ndoto mbaya kama nini?"

    "Ndoto gani?"

    "Nimeota John amekuja hapa tulipo, akiwa na wale watu wake, akatufunga kamba, sote wanne, kisha wakatuweka hapo sebleni. Wakamwaga mafuta ya petroli kila sehemu, na kuwasha moto wao wakaondoka. Ndio nikastuka"

    "Mmmm hakuna kitu kama hicho"

    Niliamua kumfariji Phidaya, kwani sikupenda apoteze amani asubuhi hii, ambayo tunaendelea kujiandaa na maandalizi ya sherehe ya kuzaliwa kwa Junio wetu.

    "Hapa nilipo mapigo ya moyo yananienda mbio."

    Nikamvuta karibu yangu na kumlaza kifuani mwangu, taratibu nikaanza kuzichezea nywele zake ndefu na laini.

    "Tulia mke wangu"

    "Eddy naogopa"

    "Umaogopa nini mke wangu"

    "Nahisi familia yangu, itapata shida tena. Tena hii itakua kubwa kuliko ya kwanza"

    "No baby usiyape nguvu, mawazo hayo mimi nipo. Nitahakikisha hakuna kitakacho haribika wala mtu kunyanyua mkono wake juu ya familia yangu nipo tayari kwa lolote hata kufa ili mradi familia yangu iishi kwa amani"

    "Kweli baby?"

    "Ndio kama aliweza ile mara ya kwanza basi hii ya pili, hato weza kamwe"

    Nilizungumza huku nikiwa na jazba ya hasira, kwani hadi hapa ninavyo zidi kumfariji mke wangu, tayari John amesha yaweka maisha ya mama yangu mashakani. Taratibu Phidaya akaanza uchokozi wa kitandani, sikuwa na hiyana zaidi ya kumpa haki yake anayo stahili kama mke wangu. Hadi tunamaliza kila mmoja akawa kwenye furaha isiyo simulika, kwani wote tulifika kwa wakati mmoja mwisho wa mechi yetu.



    "Ngoja nikaandae kifungua kinywa"

    "Sawa"

    Phidaya akanyanyuka na kuingia bafuni, akaoga na kutoka. Akavaa nguo alizo amua kuvaa kwa siku hii yaleo na kwenda nje. Nikachukua simu ya mezani, nikaziingiza namba za Blanka na kumpigia. Simu ikaita baada ya muda ikapokelewa.

    "Vipi hali ya mama?"

    "Kuna mabadiliko kidogo?"

    "Mazuri au mabaya?"

    "Mazuri, nilimuonyesha mama picha yako ukiwa na mkeo na mwanao. Kidogo mama alianza kufungua kinywa huku akitabasamu"

    "Hakusema chochote?"

    "Hapana, alitabasamu tu na kutingisha kichwa kama mtu aliye furahi kwa kuiona hiyo picha"

    "Poa nitakuja"

    "Kwani upo wapi?"

    "Nitakuambia siku nyingine. Kwaheri"

    Nikakata simu, baada ya kumuona Junio akiingia chumbani huku akilia jambo lililo nistua sana.

    "Mona unalia?"

    "Mamy kanipiga"

    Kidogo mapigo ya moyo yakanitulia.

    "Kisa nini?"

    "Eti hataki nimsaidie kupika chai"

    "Ni hilo au kuna jengine"

    "Nihilo dady"

    "Mwanao ni muongo"

    Phidaya aliingia huku akionekanana kukasirika.

    "Amefanyaje?"

    "Nimemuambia asicheze mpira ndani, likawa halinielewi. Mpaka akaipiha Tv ya ukutani ikaanguka"

    "Imevunjika?"

    "Hapana, haijavunjika. Tena huku nje usitoke ubaki humu humu na huyo baba yako. Sitaki kukuona huku nje sawa?"

    Phidaya alizunguilmza na kutoka nje, nikamnyanyua Junio na kumtupia kitandani nilipo na kumfanya aanze kucheka na kufurahi.

    "Huo uronaldo wako, uwe unaufanyia nje sawa mwangu?"

    "Sawa dady, twende tukacheze nje"

    Junio alizungumza huku akinivuta mkono, nikatizama saa ya ukutani inaonyesha ni saa tatu asubuhi.

    "Nenda ukaningoje sebleni nioge mara moja"

    "Ok dady"

    Junio akatoka nikaingia bafuni na kuoga, kisha, nikavaa nguo za mazoezi na kutoka nje.

    "Munaenda wapi?"

    Phidaya alutuuliza baada ya kutuona tukitoka mlangoni bila ya kuaga.

    "Ufukweni"

    "Kifungua kinywa tayari"

    "Anzeni tu sisi tunakuja"

    "Eddy mbona unapenda kumuendekeza huyo mwanao, kila anacho taka unamfanyia"

    Nikamfwata Phidaya na kumbusu mdomoni.

    "Tunakuja baby, Shamsa yupo wapi?"

    "Yupo jikoni anamalizia kupika"

    "Ok tunakuja"

    Tukatoka na Junio, tukaingia kwenye lifti na kushuka hadi chini, tukitokea gorofa ya saba, yalipo makazi yetu. Tukaelekea kwenye fukwe zilizopo pembezoni mwa hotel hii. Kitu kilicho nishangaza ni jinsi Junio alivyo maarufu kwa watoto wezake ambao tuliwakuta hapa ufweki. Wakaunda timu mbili huku nami nikiwa timu pinzani na Junio. Wakanichagua kua goli kipa na sikuwa na jinsi. Magoli ya viayu tuliyo yaweka hayakuzuia mechi kuanza, huku golikipa wa timu ya Junio, akiwa mzee mwenye mjukuu wake kwenye timu yangu.



    Hapa ndipo nilipo pata fursa ya kumtazama Junio vizuri, nakugundua anakipaji kikubwa cha kucheza mpira. Mara kadhaa akawa anapiga mashuti mazito golini mwangu, ambayo niliweza kuyanyaka vizuri. Huku wachezaji wa timu yangu wakinisifia kwamba ninaweza kazi ya kulinda goli. Kitendo cha kuinyaka mipira, ndivyo jinsi Junio alivyo ongeza juhudi ya kucheza na kupiga mashuti mazito golini.

    "Kumbe na wewe ni kipa mzuri?"

    Mzee wa timu ya Junio ambayo hadi sasa hivi hakuna goli alilo fungwa, aliniuliza tulipokua tukibadilishana magoli, baada ya dakika kumi na tano alizo tuwekea refa wetu kuisha.

    "Najaribu tuu"

    "Hapana, kuna kitu nimekiona ndani yako na huyo mwanao"

    "Kitu gani?"

    "Muna vipaji vikubwa sana, hakikisha unamuendeleza mwanao katika fani hii, atafanikiwa sana na atakuwa mchezaji mkubwa sana duniani"

    Sauti ya filimbi ikatustua mimi na huyu mzee, huki refa akituomba kila mmoja akakae kwenye goli lake, tukafanya kama alivyo tuelekeza.

    Mpira ukaanza, japo kuna tifutifu jingi kwenye hii fukwe, ila Junio, anakimbia kuliko watoto wezake ambao mara kadhaa, walikua wakianguka anguka.

    Shuti kali alilo lipiga Junio, akiwa karibu yangu, likanipita katikati ya miguu yangu na kwenda mbali kidogo na sehemu tunayo chezea mpira. Nakuwafanya Junio na timu yake kushangilia ushindi wa goli hilo walilo kua wakilitafuta kwa juhudi mara baada ya kipindi cha pili kuanza.

    "Hahaaaa haaaaaa"

    Nilimuona Phidaya akicheka, huku akiwa na kamera yetu. Nikatambua moja kwa moja anacheka goli, nililo fungwa na Junio.

    "Junio kachukue mpira sijui umeenda wapi"

    Nilimuambia Junio aufwate mpira wake ambao yeye ndio aliuona sehemu ulipo elekea. Junio akaongozana na wezake wawili kwenda kuutafuta.

    "Unacheka nini?"

    "Nakucheka wewe, ulivyo fungwa na huyo mwanao, njoo uone hili goli lilivyo ingia"

    Nikamfwata Phidaya alipo, akanionyesha video aliyo rekodi, goli lililo pita katikati ya miguu yangu

    "Mwanao amekupiga tobo"

    "Huyu mtoto, ananguvu za miguu kama hadi ananiogopesha, skija golini"

    "Ndio hivyo tumepata mchezaji, mzuri tusubirie atakaye kuja sijui atakuwaje"

    "Huyo naomba awe wa kike"

    "Kweli ehee"

    "Au wewe unataka aweje?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Vyovyote Mungu atakavyo tubariki, nenda uwanjani wamesha rudi na mpira"



    Mechi ikaendelea huku mipira mingi ikielekezewa golini kwetu, baada ya wachezaji wangu kuchoka sana. Ikanikazimu mara kadhaa nikaiokote mipira inayotoka nje ya goli letu. Mpira mmoja ukapigwa na mchezaji wa timu ya Junio, ukaenda mbali kidogo. Nikaanza kuukimbiza kwa bahati mbaya ukagonga glasi mbili za juisi zilizo wekwa kwenye kijimkeja, huku pembeni yake akiwa amelala, kifudifudi msichana mmoja, aliye valia chupi na sidiri, akiota jua na juisi zikamwagikia ubavunini.

    "Ahaaaaa jamani"

    Akanyanyuka, kitendo cha kunitazama usoni akastuka, kwani ni Sheila. Macho yake akabaki akiwa amenitumbulia. Sikuonyesha dalili yoyote ya kustuka kwani tayari ninatambua kitu kinacho endelea na anatambua kwamba mimi ni marehemu niliye zikwa wiki kadhaa za nyuma.

    "Am sorry Madam"(Samahani bibie)

    Nilibadilisha sauti yangu na kuifanya ya besi. Nikauokota mpira na kuondoka pasipo kutazama nyuma. Nikafika uwanjani, muda wa kucheza ukawa umeisha. Nikamuona Sheila, kwa mbali akiondoka akielekea kwenye hoteli ya pembeni yetu, huku akiwa amejifunga kipande cha mtandio kiunoni mwake. Akaingia kwenye hoteli hiyo yakifahari kama ya yakwetu.

    'Sipo nao mbali'

    Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiondoka na familia yangu. Tukafika ndani na kumkuta Shamsa akiwa anatusubiria sisi, ili tupate kifungua kinywa.

    "Jamani mbona mumejaa michanga hivyo?"

    Shamsa alituuliza baada ya kutuona mimi na Junio tukiwa tumechafuka sana.

    "Si hiyo mijimipira yao. Nendeni mukaoge la sivyo hamuli leo"

    "Jamani ndio munatutelekeza na mwanangu"

    "Ndio nendeni mukaoge"

    Nikataka kuokota soseji moja ila Phidaya akaniwahi kunidaka mkono

    "Hembu tuachie uchafu wako, nenda ukaoge tunasikia njaa wezenu"

    "Tangu lini njaa ikasikika"

    "Banaa ehee hivyo hivyo"

    "Sema nahisi njaa, sio nasikia njaa"

    "Eddy mbona mchokozi lakini, unakuka kuniudhi mapema yote hii"

    "Naombaaaa"

    "Nini?"

    "Kasoseji kiduchuuuuuu"

    "Jamani huyu mwanaume mmero ahaaaa"

    Phidaya akanikatia kipande kidogo cha soseji na kunilisha.

    "Mambo si ndio hayo, kamuogesheni Junio nasikia maji yanamwagika tu huko bafuni kwake."

    Nikaingia bafuni kwetu na kuanza kuoga, huku nikiwa na furaha ya mpango wanguy wa kumteketeza John, unaanza kukamilika, kutokana Sheila hajanistukia kwamba ni Eddy mimi na sio Fredy waliye muua.

    Nikarudi sebleni nikiwa nimevalia nguo nyengine. Tukapata kifungua kinywa. Tukapamba eneo zima la sebleni kwa ajili ya kesho, siku ya kuzaliwa kwa Junio. Phidaya na Shamsa wakasaidiana kutengeneza keki kubwa. Nikavaa sweta lenye kofia pamoja na miwani nyeusi. Nikawaaga kwamba nakwenda kununua vitu baadhi kwa ajili ya kesho. Nikafika kwenye hoteli ya jirani yetu, inayo onekana mmiliki akiwa ni mmoja kutokanana kufanana majengo yake kufanana sana.

    Nikaikuta gari ya John kwenye maegesho ya hoteli hii, nikatafuta sehemu ya watu kukaa, nikajipatia kinywaji taratibu nikaanza kushusha tumboni mwangu, huku nikitazama anayetoka na kuingia kwenye hoteli hii yenye watu wengi tofauti na yakwetu, iliyo tulia sana.

    Hadi kagiza kanaingia sikumuona John wala Sheila wakiwa kwenye eneo hili, nikahisi kukata tamaa ya kuwaona. Nikapiga fumba la mwisho la juisi yangu ninayo kunywa. Nikasimama na kujiweka sawa, kabla sijatoka nikawaona John na Sheila wakiitoka ndani ya lifti, iliyo toka gorofa za juu, wakielekea hadi sehemu ilipo kaunta ya vinywaji. Wakaagizia vinywaji, baada ya muda kidogo John akambusu Sheila na kwenda maeneo ya vyooni.

    Nikaelekea sehemu alipo Sheila, nikasimana upande wake wa kushoto. Taratibu nikavua miwani na kuiweka juu ya meza kubwa iliyopo hapa kaunta.

    Nikamuonyesha muhudumu mzinga wa whayne ninao uhitaji, jambo lililo mfanya Sheila kunitazama huku akiwa amenitumbulia mimacho. Mwili mzima ukaanza kumtetemeka kwa woga, hata simu yake kubwa aliyo ishika ikaanguka chini.

    Nikalipa pesa ya mzinga huo, nikamuona John, akiwa anatoka kwenye mlango wa chooni. Nikavaa miwani yangu, taratibu na kuanza kuelekea mlango wa kutokea nje. Huku John akipita nyuma yangu bila ya kunijua. Kwakupitia kioo cha mbele yangu, nikamuona Sheila akininyooshea kidole, mimi huku, akizungumza na John, aliyekua akimbembeleza kutokana, analia kwa woga. Nikatoka nje ya mlango wa hotel. hii.

    "Am sorry brother, please wait for me"(Kaka samahani naomba unisubirie tafafadhali)

    Niliisikia sauti ya John, ikiniita kwa nyuma na kunifanya nisimame huku chupa yenye whyne, nikiishika vizuri, kwa lolote litakalo tokea kati yetu, huku nikimsubiria kwa hamu anifikie nilipo.



    Nikawaona polisi wawili wakija mbele yangu, jambo lililo nifanya nishindwe kufanya kile nilicho hitaji kukifanya mbele ya John. Nikapiga hatua kwenda mbele, huku nikiipuuzia sauti ya John inayo niomba nisimame. Sikuelekea kwenye hoteli yetu kuepukana na kugundulika sehemu ninayo ishi. Nikafika kwenye kundi la watu wanao elekea barabarani, nikajichanganya nao. Nikageuka nyuma na kumuona John akiendelea kunifwata kwa nyuma

    'Ngoja nimpeleke peleke huyu mwehu'

    Nikazidi kutembea kwa mwendo wa kawaida, hadi nilipo fika kwenye moja ya eneo lililo tulia. Nikasimana na kugeuka nyuma na kumkuta John akiwa ananikaribia kunifwata.

    "Brother....."(Kaka.....)

    John hakumalizia sentensi yake na kubaki akinitumbulia mimacho.

    "Can i help you?"(Ninaweza kukusaidia?)

    Nilimuuliza John anaye nishangaa, huku sauti yangu nikiifanya nzito, tofauti na sauti ninayo itumia siku zote na iliyo zoeleka na watu wengi.

    "You... you kno......"(Una.....una jua)

    John alibabaika kiasi kwamva hata hata alicho kipanga kuzungumza kilimtoka kichwani.

    ”Samahani nilikufananisha"

    John alizungumza huku akiondoka kwa aibu, na kutazama tazama chini. Kitu kilicho nifanya nishindwe kumdhuru John ni kamera za ulinzi zilizo fungwa barabarani. Ambazo zipo kwa ajili yàkuchukua matukio yote yatakayo tendeka barabarani hususani ya madereva wanao kwenda kwa kasi. Na endapo ningefanya lolote baya ingekuwa ni viguu kwangu kutoka nje ya nchi hii ya Brazili.

    Nikamuona John, akirudi Hotelini, ambapo si mbali sana na sehemu tulipo. Ikapita taksi, nikaisimamisha na kuingia ndani, mikamuomba dereva anifikishe kwenye hoteli niliyo fikia jambo lililo mshangaza dereva taksi kwani umbali huo, mtu anaweza kutembea kwa miguu.

    "I will pay you"(Nitakulipa)

    Dereva taksi akafanya kama nilivyo muagiza. Njiani tukampita John, akirudi hotelini, wala hakuweza kuniona mimi ndani ya gari. Nikafika hotelini. Nikampa dereva kiasi anacho kihitaji. Kabla sijashuka nikamuona John akiingia kwenye hoteli waliyo fikia huku, akitembea kwa mwendo wa haraka akionekana kumuwahi mpeñzi wake Sheila.

    ***

    Nikaingia ndani na kuwakuta Phiday na wanae wakitazama movie kwenye tv, kubwa iliyopo sebleni.

    "Mbona umechelewa kurudi?"

    Phidaya aliniuliza huku akinyanyuka kwenye sofa, akanipokea chupa ya whyne niliyo ibeba. Akanibusu mdomoni.

    "Nilikya nashangaa shangaa mji tu"

    "Mmmm masaa yote hayo?"

    "Ndio, pia kuna kazi nilikua nikiifanya, nitakuambia nikiwa nimetulia"

    "Sawa, muda wa chakula, tulikua tunakungoja wewe"

    "Dady umesha wahi kuiona movie ya Death Race?"

    "Hapana"

    "Njoo uicheki"

    Nikakaa sehemu alipokua amekaa Phidaya, katikati ya Shamsa na Junio

    "Jimovie lenyewe ndio wanauana hivyo?"

    Nilimuuliza Junio baada ya kushuhudia tukio la filamu hiyo, ikionyesha mtu akiuliwa vibaya na gari moja kubwa, lenye watu wanao piga risasi.

    "Yeaaah wamelipuka, dady cheki kule cheki"

    Junio alizidi kupendezewa kwa tukio la gari hilo kubwa kugonga kwenye vyuma vyenye ncha kali na kulipuka vibaya.

    "Sasa Junio mwanangu, hapo ni kipi kinacho kufurahisha?"

    "Dady lile jigari likubwa lilikua likiwashambalia Frank Sting na Joe"

    "Eddy narudia tena kukuambia, kwamba umeniharibia mtoto. Hapo hajaanza shule, anawajua masteringi wa movie hizo kama ndio wazazi wake"

    "Usimlaumu hata mimi nilivyo kua mtoto nilipenda kutazama sana movie. Junio stering anaitwa nani?"

    "Jansan Stathan au Frank Sting"

    "Mmmm haya baba, nyanyuka ukale movie yako naiwekaa pause, ukimaliza utaendelea"

    Tukanyanyuka sote, na kukaa meza yachakula.

    "Shamsa mbona kama haupo sawa?"

    "Najisikia sikia kichwa kinauma"

    "Umekunywa dawa?"

    "Hapana, ila kitapona. Nahisi ni jinsi tulivyo tazama tv muda mrefu, imechangia kichwa kuuma"

    "Mmmm pole fanya ule, kisha ukameze dawa. Sawa mwanangu?"

    "Sawa baba"

    Kwa mara ya kwanza Shamsa kuniita baba, jambo lililo nishanga

    za sana kwani siku zote alizoea kuniita Eddy. Furaha ikazidi kuongezeka moyoni mwangu. Kwa kuona Shamsa akiniheshimu kama baba yake mzazi.

    "Shamsa utaniambia nikupe dawa gani, kwa maana mimi ni dokta"

    "Kweli mama?"

    "Ndio nilikua dokta, muulizeni huyo baba yanu, tumetokea wapi?"

    "Natamani nisome kwa juhudi, ili niwe dokta kama baba na mama yangu"

    Shamsa alizingumza kwa sauti yaunyonge iliyo jaa huzuni.

    "Usijali utakuwa, tutahakikisha tunakupa chochote utakacho kutoka kwetu"

    Phidaya alizungumza huku akimshika shingo Shamsa kumfariji, kutokana Phidaya anatambua historia nzima ya Shamsa baada ya mimi kumuadisia, tukiwa ndani ya ndege tukija Brazili.

    Tukamaliza kula, kabla kila mtu hajaendelea na shughuli yake nikawaomba wanisikilize kwa dakika chache.

    "Nilipotoka, nilikwenda kupiga simu. Kuwasiliana na nyumbani nchini Tanzania."

    Niliwaongopea kutokana simu nilipila siku mbili za nyuma.

    "Nilitaka kujua hali ya mama, ila nikaambiwa kwamba ni mgonjwa sana, amepalalaizi na hawezi kufanya kitu chochote"

    Nikamuona Phidaya akistuka kwa taarifa hiyo.

    "Sasa imekuaje!?"

    "Matatizo nahisi ni mambo yao yakisiasa, wamechezeana."

    Ilibidi kuficha kwamba John ndio chanzo wa tatizo la mama, baada ya kumuua Fredy ninaye fanana naye sana.

    "Dady wamemchezea bibi mziki?"

    Swali la Junio likatuashiria kwamba haelewi kitu tunacho kizungumza kwa wakati huu.

    "Eheee"

    "Kina nani hao?"

    "Watu tu utakwenda kuwaona mukienda Tanzania"

    "Ngoja Eddy, umesema tukienda Tanzania, ina maana wewe hauendi?"

    "Kuna kazi itanilazimu kuifanya hivi karibuni, itawalazimu nyinyi kwenda kabla yangu."

    "Kazi gani?"

    "Nilikuambia nitakuambia, nikitulia mke wangu"



    Tukamaliza mazungumzo, nikaondoka na kuingia chumbani kwetu, nikafanya maandalizi ya kulala, baada ya muda Phidaya akaingia na kukaa kitandani

    "Baby ni kazi gani inayo kufanya ubaki huku peke yako"

    Phidaya aliniuliza kwa sauti ya upole, huku akinichezea chezea kifua changu.

    "Yakumuua John"

    "Kumuua John!!?"

    "Ndio, nimemuona leo, na ninatambua anapo ishi."

    "Sa..sa sasa itakuwaje akituona, si atatuua?"

    "Kwa sasa hawezi kuniua"

    Nikaanza kumuadisia Phidaya kuanzia mipango ya harusi ilivyo pangwa, hadi kuuawa kwa Ftedy.

    "Kwahiyo wanaamini wewe umekufa?"

    "Ndio maana yake, nahitaji mutangulie nyumbani mimi niimalizie kazi hiyo ya kumuua yeye kwa mkono wangu."

    "Eddy kuwa makini, sihitaji kukupoteza katika hili"

    "Usijali mke wangu, nipo makini tena sana"

    Tukakumbatiana na Phidaya. Akaingia bafuni akaoga, kisha akarudi kitandani na kujilaza.

    "Unajua mama anaweza akapona?"

    "Ataponaje?"

    "Sisi madaktari, tunambinu za kuwafanya watu walio paralaizi, kuweza kutembea tena"

    Maneno ya Phidaya yakanipa matumaini mapya juu ya uwezekano wa mama yangu kupona.

    "Mjkienda Tanzania, kuna mtu atawapokea"

    "Atatujua?"

    "Ndio picha zenu anazo"

    "Sawa ila nakuomba Eddy, urudi"

    "Nitarudi mke wangu. Tena ngoja nimpigie uzungumze naye"

    Nikachukua simu ya mezani na kumpigia Blanka.

    "Ndio kaka"

    "Hali ya mama inaendeleaje?"

    "Kidogo anaonyesha matumaini, japo si sana"

    "Msalimie wifi yako"

    "Anajua kiswahili au ndio kuch kuch hotae?"

    "Anajua mbona, tena zaidi yako"

    Nikampa simu Phidaya akazungumza na Blanka, kisha Phidaya akanirudishi simu.

    "Ehee kesho kutwa watakuja Tanzania. Watafutie nyumba maeneo ya Masaki au Mbezi beach mimi nitarudi wiki moja baadaye"

    "Kaka pesa sina kwa sasa"

    "Watakuja na pesa zao wenyewe"

    "Poa kaka Eddy sasa nikawapokee Ubungo au wapi?"

    "Kwa akili zako hujajua hii namba inatokea nchi gani. Kama ni yatanzania kawapokee Ubungo, kama ni ya nchi za watu wakukute uwaja wa ndege"

    "Haaaaaa haya mwaya kaka"

    Nikakata simu nikimuacha Blanka akicheka kwa jibu nililo mpa.

    Usiku mzima ukawa ni usiku wakuwaza jinsi gani nimuue John pasipo mimi kutiwa hatiani, na kujisababishia matatizo mapya. Nikamuacha Phidaya peke yake kitandani akiwa amepitiwa na usingizi, mimi nikaelekea sebleni. Kitendo cha mimi kukaa kwenye kochi, Shamsa akatoka chumbani kwake.

    "Mbona hujalala, hadi sasa hivi?

    "Nimekosa tu usingizi, baba"

    "Kichwa bado kinauma?"

    "Hapana, kichwa hakiniumi, ila kuna jambo linaniumiza sana akili yangu"

    "Jambo gani?"

    "Nikuhusiana na hiyo kazi unayo hitaji kuifanya. Naomba na mimi niwepo"

    "Noo Shamsa, hii vita ni yangu na yule John niliye kuadisia"

    "Sawa Eddy, ila nahitaji kuwa karibu nawe kutokana wale wezangu wananitafuta kila kona ya dunia hii"

    "Kwa nini wanakutafuta?"

    "Huwa kwenye kundi lile mtu akitekwa basi nilazima atafutwe popote alipo, kuhofia kutoa siri zao"

    "Mmmmm"

    "Na mbaya zaidi, wanashirikiana na Al-Kaida ambao nilisha wahi kufanya kazi kwenye kundi hilo zaidi ya mara nane"

    Nikabaki nikimshangaa Shamsa kwani hii habari anayo niambia ni ngeni kwenye masikio yangu na niyahatari kupita zote nilizo wahi kuzisikia kwenye maisha yangu. Kwani kundi la Al-Kaida, linatafutwa na nchi kubwa hususani Marekani. Je vita ya mimi peke yangu nitaiwezaje.

    "Nikiwa na familia yako, ninahofia kuitia matatizoni kwa ajili yangu, na wale wanavyo jua ni kwamba umeniteka"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Picha za zenu mulizo ziweka Facebook nahisi ndio chanzo?"

    "Hizo ndio zilizo niharibia mimi kila kitu, najuta kuziweka. Wanenitumia ujumbe facebook"

    "Upo wapi?"

    Shansa akanyanyuka na kuingia chumbani kwake, akarudi akiwa ameshika laptop. Akaiweka mezani na kuufungua ujumbe alio tumiwa ambao umeandikwa kwa maandishi ya kiarabu.

    "Yana somekaje?"

    "Wanasena hivii. MIKONO YAO INAVUJA DAMU, ILIYO SABABISHWA NA WEWE. TUTAKUTAFUTA DUNIA NZIMA. DAMU YAKO ITAKUWA KINYWAJI CHETU."

    Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, huku wasiwasi mwingi ukiwa umenijaa moyoni mwangu. Nikamtazama Shamsa jinsi alivyo poteza raha.

    "Tutafanyaje Eddy na huu ujumbe ni wakwako?"

    Sikujua hata nimjibu nini Shamsa zaidi ya kumtazama tu machoni.

    "Eddy hapa nilipo raha yote imetoweka moyoni mwangu, sijui hata tunawakimbiaje?"

    "Fanya hivi, ifute hiyo account"

    "Alafu?"

    "Nitajua ni jinsi gani ya wewe kwenda Tanzania. Natambua kuwa kule mutakuwa mupo salama zaidi"

    "Una uhakika?"

    "Ndio ninao uhakika huo. Ila nakuomba uandamane na familia yangu"

    Shamsa akakaa kimya kama dakika tano, huku akiwa amesongwa na msongamano wa mawazo kichwani mwake.

    "Nitakwenda nao kuhakikisha wanafika salama"

    "Asante Shamsa"

    "Wewe je, usalama wako utakuaje?"

    "Hilo musilihofie sana, nilipo toka nimbali sana"

    Nikamfwata na kumkumbatia Shamsa. Nikamruhusu arudi kulala. Mimi nikaendelea kukaa sebleni nikiwa sina amani moyoni mwangu kabisa, huku mawàzo mapya ya Al-Kaidah yakinitawala kichwani

    ***

    Muda wa sherehe ya Junio ikawadia, tuliamua kuialika familia ya jirani yetu. Ambaye alikubali kujumuika nasi, akiwa na mke wao na mtoto mmoja. Ili kuinogesha sherehe, tukaimba wimbo wa siku ya kuzaliwa unao tumika kuibwa katika siku za kuzaliwa.

    ¶Happy birthday to you×2¶¶

    ¶Happy birthday ni ya Junio, Happy birthday to you¶¶

    Junio akaizima mishumaa iliyopo juu ya keki kwa kuipuliza kwa nguvu. Mama yake akaanza kukata vipande vidogo vidogo vya keki. Baada ya kumaliza Junio akaanza kutulisha mmoja baada ya mwengine.

    "Jamani kuna kitu nahitaji nikifanye, mbele yenu"

    Nilizungumza huku nikitabasamu, nikawafanya watu wote kukaa kimya wakisubiria kitu hicho ninacho taraji kukifanya. Taratibu nikamfwata Phidaya alipo, nikapiga magoti huku nikitoa kisanduku kidogo mfukoni mwa suruali yangu, kilicho hifadhi pete ya dhahabu, niliyo inunua siku tulipokua tukifanya manunuzi ya vitu vya Junio, pasipo mtu yoyote kujua hilo.

    "Phidaya, upo tayari kuwa mke wangu?"

    Nilizungumza kwa sauti ya unyonge na kumfanya Phidaya kuanza kumwagikwa na machozi yafuraha.

    "Ndio Eddy"

    Nikauchukua mkono wa kushoto wa Phidaya, na kuivisha pete kwenye kidole kinacho paswa kuvishwa pete ya uchumba. Watu wote wakapiga makofi ya furaha, huku jamaa tuliye mualika akichukua picha za video kwa kamera yetu. Phidaya akaninyanyu na kunikumbatia kwa nguvu huku akilia kwa furaha sana.

    "Nakupenda Eddy mume wangu"

    "Nakupenda pia mke wangu"

    Hatukujali uwepo wa watu waliopo ndani ya seble yetu, tukajikuta mimi na Phidaya, tukinyonyana midomo yetu, kwa hisia kali za kimapenzi, zilizo changanyika kwa furaha nzito.

    "Mmmm sasa tusherekee"

    Shamsa alizungumza huku akiwasha redio kubwa iliyopo sebleni hapa. Kusema kweli japo ni sherehe ya watu wachache, ila ilitupa furaha kubwa sana mioyoni mwetu, huku kila mmoja akionekana kuridhika kwa matukio yote yanayo endelea katika sherehe hii.

    Hadi inafika jioni kila mmoja akawa amechoka kwa kucheza mziki. Nikatoka na jamaa, niliye mualika kwenda nje kupunga upepo huku Phidaya akibaki na mke wa jamaa, aliye jitambulisja kwa jina la Jordan, pamoja na watoto wetu

    "Nimefurahi sana kaka Eddy kunialika kwenye sherehe hii ya leo, kusema kweli ipo boma sana"

    "Hata mimi nafurahi kwa kuja kwako, hivi wewe ni mwenyeji wa wapi?"

    "Florida Marekani. Wewe je?"

    "Tanzania"

    "Safi sana, alafu kama nilisha wahi kukuona kwenye matangazo ya magari ya Ford yaliyo zinduliwa mwaka huu?"

    "Ndio mimi"

    "Du kumbe nipo na mtu mkubwa"

    "Kawaida hivi unajishuhulisha na nini?"

    "Mimi ni mzalishaji wa movie Hoolywood"

    Tuliendelea kuzungumza mambo mengi na jamaa hadi majira ya saa tatu usiku tukarudi juu gorofani. Tukajumuika na familia zetu kupata chakula cha usiku, kisha wao wakaondoka na kurudi vyumbani mwao.

    ***

    Mipango ya kukata tiketi za ndege katika shirika la KLM kwa kupitia mtandao likakamilika usiku. Muda wa ndege kuondoka ni saa tano asubuhi, ikatulazimu kufika uwanja wa ndege saa nne asubuhi, ambapo, nikakabidhiwa tiketi tatu nilizo zikata usiku wa jana. Nikawakabidhi kila mtu tiketi yake pamoja na namba za Blanka niliye mpa taarifa juu ya kuupokea ugeni wa familia yangu.

    Nikamkabidhi Junio na Shamsa kila mmoja kiasi cha dola elfu ishirini, wazitunze na zitawasaidia kukiwa na tatizo lolote. Nikamkapa Phidaya dola laki moja na nusu za kumsaidia.

    "Nakuomba hizo pesa uzitumie vizuri, japo kwa Tanzania ni pesa nyingi sana, ila kuwa nazo makini"

    "Sawa baba Junio"

    "Walinde wanangu"

    "Nitawalinda, nakuomba na wewe ujilinde mume wangu ninakuhitaji zaidi ya chochote kwenye maisha yangu"

    "Sawa mke wangu"

    Nikamkumbatia Phidaya, kisha nikamfwata Junio.

    "Mlinde mama sawa?"

    "Sawa dady"

    "Nakuaminia wewe ni mwanaume"

    Nikamkumbatia Junio na kumpa tano. Nikamfwata Shamsa aliye onekana muda wote macho yake yakiwa juu juu.

    "Vipi?"

    "Hakuna, kitu baba"

    "Ok kuwa makini na familia nzima. Ninakuamini huto niangusha. Mlinde mdogo wako na mama yako"

    "Sawa dady"

    "You call me dady again?"(Umeniita baba tena?)

    "Ndio, unanipa mapenzi bora kama niliyo kua nikiyapata kwa baba yangu.Mungu akubariki"

    "Asante kwa kulitambua hilo"

    "Nakutakia kazi njema dady"

    "Nanyi pia nawatakia safari njema"

    Nikawakumbatia wote watatu, nikawaacha waelekee kwenye foleni ya mizigo yao kukaguliwa. Mimi nikaondoka, nikachukua taksi iliyo nifikisha kwenye maduka ya urembo. Nikanunua ndevu bandia.

    "Jamani nimepungukiwa na dola kumi nisaidieni tu kuipata hii pochi"

    "Hatushushi bidhaa zetu, bei ni hiyo tu, chukua pesa yako uondoke dada"

    "Lakini jamani kuweni na utu, katika hili. Dola kumi pia munashindwa kunipa hii pochi"

    Niliyafwatilia mazungumzo ya muhudumu na dada mmoja aliye shika pochi, aliyo onyesha kuipenda sana. Nikatoa dola mia na kumpa muhudumu huyo anaye bishana na dada huyo anaye onekana ni muongeaji sana.

    "Chenchi itakayo baki utampa huyo dada"

    Nilimuambia muhudumu huyo, huku nikiwatazama machoni. Nikachukua mfuko wangu nilio nunua vitu ndani ya duka hili ikiwemo sura ya bandia. Nikatoka nje ya duka na kutazama tazama uwezekano wa kupata usafiri wa taksi.

    "Naitwa Prety wewe je?"

    Dada niliye mlipia pochi dukani, alizungumza huku akiwa amesimama pembeni yangu. Huku akiwa amebeba jifuko kubwa lenye vitu vingi ndani yake.

    "Eddy. Taksi"

    Niliita taksi inayo katiza pembeni yetu.

    "Hapana wewe nenda"

    Prety alimruhusu dereva wa taksi hiyo kuondoka jambo lililo anza kunikera.

    "Mimi nina gari yangu, ile pale nyekundu"

    Alinionyesha kagari kadogo, kanako fanana na gari la mchekeshaji maarufu duniani Mr bean.

    "Lile ndio gari lako?"

    "Ndio twende tukapande"

    Prety akanishika mkono hadi kwenye kagari hako. Akanifungulia mlango nikaingia, kisha yeye naye akaingia.

    'Mungu wangu hiki kikipata ajali hatutoki humu'

    Nilijisemea kimoyo moyo.

    "Unakwenda wapi?"

    Nikamtajia hoteli ninayo kwenda, akaonekana kufurahi.

    "Mimi ninakaa hoteli ile ya pili yake. Nina mwaka sasa ninaishi pale"

    "Una kazi gani inayo kufanya ukae pale kwa kipindi chote hicho?"

    "Ohoo mimi ni mtaalamu wa mambo ya mtandao, chochote unacho hitaji kwenye mtandao ninaweza kukutafutia"

    Prety ni muongeaji sana, kiasi kwamba nikajikuta nikiwa ninamshangaa.

    "Kabla hatujafika kwako, twende ukapaone kwangu kisha ndio uende kwako"

    "Kwa nini?"

    "We twende tu"

    Nikaanza kumtilia mashaka huyu Prety, isije akawa ametumwa na John. Nikajipa moyo hawezi kunifanyia chochote. Tukafika hotelini, tukaelekea kwenye chumba chake kilicho gorofa ya tano

    Chumba chake kimejaa computer si chini ya kumi na zote zimewashwa. Akaanza kuminya moja baada ya nyingine akitazama ujumbe ulio ingia.

    "Hapa ndio kwangu, jisikie huru"



    Nikashangaa kumuona Prety akivua sura yake, aliyo nayo. Ndipo nilipo gundua ni sura ya bandia. Akabaki na sura yake halisi ambayo ni nzuri sana.

    "Mbona unashangaa?"

    "Nashangaa kukuon unavua sura ya bandia"

    "Yaa unajua mimi ni Mrashia, dili zangu nyingi ni wizi katika mabenki makubwa na watu matajiri duniani. Huwa siwezi kuifanya kazi yangu kwa sura yangu halisi"

    "Kwa nini unakua mwizi?"

    "Ndio kipaji changu, njoo uone"

    Akanipeleka kwenye chumba kimoja, kilicho jaa mitambo mingi kiasi, pamoja na picha nyingi za wasichana kwenye ukuta

    "Hii mitambo huwa ninaitumia kutengeneza sura za wasichana ninao hitaji kufamana nao.

    "Mmmm"

    Akanionyesha jinsi ya anavyo tengeneza sura hizo za bandia. Sikujua ni kwanini emeniamini kwa muda mfupi.

    "Kwa nini umeniami na kunileta chumbani kwako. Kama mimi ni askari je?"

    "Hakuna mtu mwenye kuwajua askari wa nchi yoyote duniani kama mimi. Ungekua askari wala pesa yako nisinge ipoke"

    Tukarudi sebleni ambapo akanipa kiti nikae nitazame tazame jinsi anavyo weza kuiba vitu kwa mtandao hususani pesa ndani ya mabenki.

    Katika kufungua fungua baadhi ya picha nikamuona John na Sheila.

    "Hembu rudisha nyuma hiyo picha niione vizuri"

    Akafanya kama nilivyo muagiza, nikaitazama vizuri picha hiyo.

    "Hawa ni najirani wangu, nimegundua nao ni matajiri sana. Nipo kwenye mpango wa kuwaibia pesa zao benki. Tena nimesha jenga urafiki na huyu dada."

    "Anaitwa nani?"

    "Coletha Agray"

    Nikashangaa jinsi Sheila alivyo badilisha jina.

    "Ahaaa naomba unionyeshe chooni"

    Prety akaniobyesha chooni, nikaingia huku nikijitahidi kuficha wasiwasi wangu wa kuwajua John na Sheila. Baada ya muda nikasikia Prety akimkaribisha Coletha ambaye ndio Sheila, Nikatoka chooni na kujibanza sehemu ninapo weza kuiona seble vizuri. Nikamuona Sheila akikaa kwenye sofa, huku akiwa na tanasamu na furaha.

    'Sheila kifo chako kitakua cha taratibu taratibu, sina haraka na wewe'

    Nilijisemea komoyo moyo huku nikimtazama Sheila au Coletha Agrey. Anavyo shusha mafumba ya juisi aliyo andaliwa na Prety

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Prety kila nikija nakuta Tv yako ukiwa umeizima huwa uitazami"

    "Coletha muda huo nadhani ninao"

    Sheila akanyanyuka na kuichukua rimoti iliyopo mezani, akaiwasha Tv, kabla hajarudi kukaa kwenye kochi simu yake ikaita.

    "Umesharudi?"

    "Nakuja basi nipo hapa kwa P"

    Moja kwa moja nikahisi Sheila atakuwa anazungumza na John.

    "Huyo mwanaume ameaharudi"

    "Kwani alikuwa ametoka?"

    "Ndio alitoka kuna watu wake alikwenda kuzungumza nao. Kuna kazi amewapa"

    "Kazi gani hiyo?"

    "Ni story ndefu ngoja nikamsikikilize nikimaliza nitakuja kukuadisia"

    Sheila akatoka, nikarudi sebleni na kumkuta Prety akiendelea na mambo yake.

    "Mbona umechelewa kutoka chooni?"

    "Hakuna"

    "Yule dada niliye kuonyesha kwenye picha akiwa na mumuwe ametoka hapa ndani muda si mrefu"

    "Ahaaa, mimi ngoja niondoke"

    "Sasa Eddy, niachie namba yako ya simu"

    "Sina simu ila natumia ya chumbani kwangu ambayo ni yamezani!"

    "Ok basi chukua yakwangu. Usiku kuna sherehe nahitaji twende wote"

    "Kabla sijasahau. Nahitaji unitengenezee sura nyingine"

    "Kwa nini?"

    "Nahitaji tu, sura nyingine"

    "Poa mida ya saa moja usiku nipigie, itakuwa tayari."

    "Asante Pretty"

    Nikachukua mizigo yangu, nikatazama kila sehemu ya kordo, nikaiona imetukia hakuna fujo za watu. Nikatbea hadi kwenye lifti, nikaminya batani na kuingia. Nikafanikiwa kufika kwangu pasipo kuona dalili yoyote ya mtu kunifwatilia. Huku akilini mwangu nikkiwazia kazi ya John aliyo wapa hao watu wake.

    Nikavitoa vitu vyote ndani ya mfuko nilio uchukua. Nikasimama mbele ya kioo, nikaanza kujibandika ndevu za bandia nilizo zinunua, muonekano wangu wa sura umebadilika kwa kiasi kikubwa, hadi mimi mwenyewe nikaanza kujishangaa. Kwani nimekuwa kama mtu mwenye umri wa miaka kama thelathini na tano kwenda juu.

    "Muda sasa umewadia wakulipa kwa kila aliye nikosea"

    Nilizungumza huku nikizipaka nywele zangu, dawa inayo itwa 'brich' iliyo zifanya nywele zangu kuwa na rangi ya dhahabu.



    Nikachukua suti yangu nyeupe, nikaiweka kitandani, nikachukua viatu vyeupe na kuviweka kitandani kisha. Nilipo hakikisha kila kitu nilicho kua nimefikiria kukifanya. Nikarudi sebleni na kuiwasha tv yangu. Huku nikisubiria mida ya saa moja usiku itimie ndio nitoke kuelekea kwa Pretty.

    Nikakumbuka Pretty amenipatia namba yake ya simu.Ilanilazimu kurudi tena ndani, kuichukua simu yamezani. Nikaziingiza namba za simu yake, ikaita baada ya muda ikapokelewa.

    "Hii ndio namba yako?"

    "Ndio"

    "Kazi yako imekamilika njoo, mida ya saa kumi na mbili. Kama nikuvalia unaweza kuja kuvalia huku huku"

    "Sawa nipe dakika chache nitafika hapo"

    Nikakata simu, nikachukua nguo zangu na kuziweka kwenye begi la mgongoni. Nikalipo hakikisha usalama upo nikatoka na kufunga ndani kwangu. Nikaelekea gorofa la pili alipo Pretty. Nikamkuta akiwa ananisubiria.

    "Eheee mbona hiyo?"

    "Ni moja ya hatua za kubajibadilisha"

    "No Eddy umetiaha bwana"

    "Mmmmm"

    "Kweli njoo nikupambee"

    Tukaingia kwenye chumba, anacho tengenezea sura za bandia. Nikakaa kwenye moja, akanitoa ndevu zabandiia, kisha akanivisha sura yabandia iliyo nifanya nionekane kijana mzuri na mwenye umri sawa na huu wangu.

    "Hii kwenye kuivua si itauma sana?"

    "Ndio nilazima iume sana, kutokana hapo imeshikana na ngozi, tena gundi yake ni imara sana."

    "Alafu kama nilijua vile, kuziweka hizi nywele brich. Vimeendana sana"

    "Umeona ehee"

    Sikutamani kuondoka mbele ya kioo kujitazama sura hii niliyo wekewa kwani si rahisi kwa mtu yoyote kugundua huu mchezo nilio ufanya.

    "Nimekutengenezea kitambulisho chataifa, sasa kwenye jina nimepaacha wazi, sijajua niweke jina gani?"

    "Henry Derulo"

    "Haya bosi"

    Tukarudi kwenye mitambo ya Pretty akamalizia kutengeneza kitambulisho changu, chenye uraia wa brazili, akanipiga picha kwa sura hii ya sasa hivi na kuiscan na kukimalizia kukitengeneza kitambulisho.

    "Kwanza hiyo sherehe inahusiana na mambo gani?"

    "Maswala ya kibiashara, ila kuwa watu ninakwenda kuwawinda. Yaani nikifanikiwa nitapiga pesa ndefu sana"

    "Mmmmm sawa"

    "Muda ndio unakwenda sasa"

    "Ingia kwenye hicho chumba changu, badilisha tu nguo humo ndani"

    Nikaingia chumba cha Pretty kilicho pabwa vizuri. Nikaingia bafuni na kuoga. Nikavaa suti yangu, iliyo nikaa vizuri mwilini.

    "Waoooooo your looking so handsome"(Waooooo unaonekana mzuri sana)

    "Kweli?"

    "Ndio yaani sikutarajia utapendeza hivyo"

    "Asante"

    "Sasa ngoja tumechishe"

    "Poa mimi nimesha maliza ngoja nitoke nje"

    "Subiri kuna kitu ambacho nahitaji kikae mwilini mwako"

    Pretty akafungua droo ya kabati lake akatoa saa nne za dhahabu, pamoja na cheni na dhahabu.

    "Chagua utakayo penda uvae"

    Nikachagua nilizo zipenda, nikazivaa nakutoka nje ya chumba na kukaa sebleni. Baada ya dakika kama kumi hivi Pretty akatoka akiwa amevalia gauni refu jeupe.



    "Umependeza sana Pretty"

    "Asante Eddy, alafu unajua kwamba wewe ni mzembe sana?"

    "Kwa nini?"

    "Hujaniuliza nimekijuaje kiswahili?"

    "Ahaaa hiyo ni lugha kubwa, sio ajabu mtu mweupe kuzungumza kiswahili"

    "Ahaa ninajua lugha karibia kumi na moja zilizopo duniani"

    "Hongera kwa hilo, ila niite jina moja la Henry na si Eddy"

    "Poa kitambuliaho chako hichi hapa"



    Tukafika maeneo ya maegesho ya magari akalisogelea gari moja aina ya 'Jaguar'. Akaingia, nami nikwmafwatia. Sikushangaa binti kama huyu kumiliki gari kama hii yakifahari. Mwendo wa nusu saa tukafika kwenye moja ya gorofa refu, nje kukiwa na watu wengi hususani wapiga pucha wanao chukua tukio moja baada ya jengine. Pretty akauingiza mkono wake katikati ya mkono wangu wa kushoto nilio kuwa nimeukunja kidogo. Taratibu tukaelekea ndani tulipo kuta watu wengi sana. Prety akanipa simu moja.

    "Tuwasiliane kwenye hiyo simu kuna namba moja tu humu ambayo niyangu"

    Pretty alizungumza huku akiniachia mkono na kwenda upande mwengine, ambapo alianza kusalimiana na watu nahisi anafahamiana nao.



    Nikatafuta sehemu iliyo tulia, nikakaa, huki nikiendelea kitazama mazingira ya ukumbi huu wagorofa. Kama zilivyo kumbi za madisco makubwa. Macho yangu yakatua kwa John na Sheila wanao ingia ndani ya ukumbi huu wakionekana kuwa na furaha sana.

    Wakasalimiana na baadhi ya watu aaliopo ndani ya ukumbi huu. Nikawa makini sana kwa kila hatua anayo ipiga John na Sheila ndani ya ukumbi huu. Sikutaka niwapoteze hata kidogo kwani muda muafaka wa mimi kufanya malipo kwa kila walicho kifanya umewadia

    Muongoza sherehe akatuomba tuoande kwenywe ukumbi wa gorofani. Ndipo kwenye makutano makubwa yatukio zima lililo tuleta hapa. Nikamshuhudia Pretty akiwa na jibabu moja lakizungu, wakionekana niwapenzi kwa maana Pretty anajiachia sana, mara kadhaa alimpiga mabusu ya mdomoni mzee huyo. Tukiwa kwenye gazi zakupanda kwenda gorofani, Pretty akanishika mkono kisiri pasipo zee hilo kuona chochote, akaniachia funguo za gari huku akinikonyeza.



    Tuakuta viti vingi, kila mmoja akaka kwenye kiti anacho kihitaji yeye. Sikukaa mbali na walipo John na Sheila. Kila muda macho yangu yakawa kwao. Taa zote zikazimwa. Tv kubwa yenye uwezo wa kila mtu kuona kiancho onyeshwa kwenye tv hiyo, likawashwa. Sauti ya kipaza sauti ikatujulisha kwamba kila mtu aliye kaa kwenye kiti chake pembeni kuna kitufe kidogo chenye uwezo wa kufanya kazi kama maiki.

    "Karibuni mabibi na mabwana kwenye mnada wetu wa uzinduzi wa gari ambalo nilakipekee"

    Sauti ya dada huyo ilizungumza huku picha ya gari hilo kikionyeshwa kwenye Tv kubwa, iliyopo mbelw yetu.

    "Hili gari, sifa ya kwanza haliingii risasi, hwala likipigwa bomu halilipuki"

    Si mimi tu niliye guna, bali hata wapembeni yangu aliguna.

    "Gari hii niyakisasa, kwani unaweza kuigeuza na kuwa katika muundo wa ndege, na likapaa angani kwa umbali wa mile nne kwenda juu."

    "Mmmmm"

    Na spidi yake likiwa angani linakwenda kwa mwendo kasi kama wa ndege za jeshi Jet"

    Mwanadada huyo aliendelea kutupa sifa za gari hilo lililo zidi kutushangaza sote tuliopo ndani ya ukumbi huu. Kila alicho tueleza ndicho kilicho kuwa kikionyeshwa kwenye tv hiyo kubwa, jinsi gari hilo linavyo fanya kazi. Kusema ukweli lilinivutia, mbaya zaidi gari hilo limetengenezwa moja tu.



    Taa zote zikawashwa baada ya dada huyo kumaliza kulielezea sifa zakumwaga gari hilo, lililo tengenezwa kwa vyuma vigumu, pamoja na madini ya dhahabu. Muda wa gari hilo, lililetwa mbele yetu, kila mmoja akapata fursa ya kuliona, kwa macho yake.

    Watu wakaanza kutaja bei za kulinyakua gari hilo, akiwemo John.

    "Paund laki nne"

    John alizungumza nakuwafanya watu kumtazama. Kwani ni pesa nyingi.

    "Paundi laki nne na nusu"

    "Paundi laki tano"

    "Paundi laki sita"

    John aliendelea kuminyana na vigogo matajiri wenye peaa zao waliomo ndani ya ukumbi huu.

    "Paundi laki nane"

    John alizungumza nakuufanya ukumbi mzima kuzizima, huku sauti ya dada anaye pigisha mnada akihesabu taratibu.

    "Pauni milioni moja na nusu"

    Nilizungumza kwa kujiamini sana, watu wote wakageuka na kunitazama. John na Sheila wakanitazama kwa macho yamshangao.

    "Kwa mara ya kwanza kwa bwana nani?"

    "Henry Derulo"

    "Kwa mara ya kwanza kwa bwana Henry"

    "Kwa mara ya pili kwa bwana Henry"

    "Milioni mbili paundi"

    John alizungumza huku akinitazama.

    Nikamuona Sheila akitabasamu sana.

    "Pauni milioni nane"

    Nilizungumza kwa kujiamini nikamuona John akifumba macho yakukaya tamaa, kwani pesa niyo itaja nikubwa sana katika ulimwengu wetu huu. Nilitaja pesa hiyo huku nikiwa sina pesa hiyo.

    Nikamuona John akinong'onezana na Sheila.

    "Paumi milioni kumi"

    John alizungumza, na kunifanya nimpigie makofi kwa ishara ya kumpongeza.

    John akafanikiwa kuwa mshindi wa gari hilo. Baada ya zoezi hilo kila mtu akaendelea na kujipa burudani ya kutembea popote ndani ya ukumbi huo na ujipatia burudani tofauti tofauti.

    "Eddy wewe ni nani?"

    Pretty aliniambia baada ya kunifikia.

    "Mimi ni Henry, kwani vipi?"

    "Pesa yote umeitoa wapi uliyo kuwa umeitaja?"

    "Usijali ni pesa ndogo"

    "Ndogo mmm.."

    "Nakuona upo na tajiri"

    John alizungumza baada ya kutufikia tulipo akiwa na Sheila

    "Hapana wewe ndio tajiri,"

    Nilimjibu John huku nikitabasamu.

    "Naitwa John huyu ni mke wangu Coletha"

    Nikatabasamu kwanu ushindi wa kuwateketeza John na Sheila.

    "Naitwa Henry"

    "Tunaweza kuwa marafiki na kushirikiana katika biashara kama hivi?"

    "Ndio tunaweza kuwa"

    John akanipa mkono huku akinikumbatia pasipo kujua mbaya wake nimerudi.





    Pretty akamtazama John kwa umakini huku akionekana kuwa na mshangao mkubwa.

    "Unafurahia nini?"

    "Kuna mpango niliupanga na vijana wangu, kuhusiana hiyo ndege"

    "Unataka kusema wewe umehusika kwenye mpango wa hiyo ndege kulipuka?"

    Pretty alimuuliza John huku akimkodolea macho ya wasiwasi. Mimi hata nguvu ya kunyanyuka kwenye kochi sikuwa nayo hii yote ni kwakuiwazia familia yangu.

    "Ndio"

    "Kwanini?"

    Kuna mjinga nilimuua, sasa ulikua muda wakuiteketeza famia yake"

    Nikastukia kumuona Pretty akinyanyuka kwa hasira na kumrukia John, hadi sofa alilo likalia wakaaanguka nalo. Sheila akasimama kwa haraka na kumchomoa Pretty aliyekuwa akimshambulia mumewe kwa kumpiga kwa makofi mfululizo.

    "Wewe ni gaidi"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pretty alizungumza kwa hasira, huku mimi nikiwa nimepigwa na bumbuazi lililo nifanya nishindwe kufanya kitu cha aina yoyote.

    "No no nakudanganya Pretty"

    John alizungumza huku akicheka.

    "Muongo wewe"

    "Kweli Pretty siwezi kufanya kitu kama hicho. Kwanza nitaanzia wapi. Eti Henry kweli ninaweza kufanya jambo hili?"

    Nilitabasamu tu, hata kinywa changu kikashindwa kufunguka. Tangu nizaliwe sijawahi kukumbana na hali ya mshangao kama hii, iliyo nimaliza nguvu zote.

    Pretty akafungua mlango na kutoka huku akiubamiza kwanguvu. Jambo lililo nistua na kurudi kwenye hali yangu yakawaida. Nikanyanyuka kwa haraka na kumfwata Pretty ndani kwake

    "Nilazima nimpeleke polisi nikamstaki"

    Pretty alizungumza kwa hasira huku akiingia chumbani kwake. Nikamfwata na kumkuta akiwa amekaa kwenye kitanda huku akilia.

    "Pretty nisikilize, kitu kimoja"

    "Nahitaji zile video mbili kama una flash zihifadhi sawa"

    Pretty alibaki akiwa amenikodolea macho. Nikatoa simu mfukoni na kuingiza namba za Blanka. Ikaita kwa muda mrefu, kisha ilapokelewa.

    "Blanka wamefika?"

    "Hawajafika"

    Jibu la Blanka likanifanya nizidi kuchanganyiliwa, hadi mwili ukawa unanitetemeka kwa woga kwani swala la akufiwa nafamilia tena kwa wakati mmoja, sikuliwazia kichwani mwangu.

    "Hawajakupigia?"

    "Hapana hawajanipigia"



    Nikakata simu nakushusha pumzi kubwa, nikabaki nimesimma pasipo kuzungumza kitu chochote na Pretty. Nikamshika mkono Pretty na kumnyanyua juu.

    "Twende kwangu"

    "Kufanya nini?"

    "Twende tu"

    Tukatoka sebleni, Petty akaziingiza video zote mbili kwenye flash, kisha akachukua begi lake lenye laptop.

    Tukaondo hadi nyumbani mwangu. Kitu cha kwanza nikaifwata simu ya chumbani kwangu. Nikamiinya kitufe cha kusikiliza ujumbe wa sauti, ili kutambua kama kuna ujumbe wowote wa suti ulio ingia nikiwa sipo.

    "Eddy mume wangu, mbona hupokei simu?"

    Ilikuwa nisauti ya Phidaya, kwenye ujumbe wa kwanza wasauti

    "Tumeamua kubadilisha safari, tupo Marekani kwa sasa. Shamsa ndio alitoa pendekezo la sisi kubadilisha safari. Ukipata ujumbe huu usiwe na wasiwasi, tupo salama na kesho tunakwenda Tanzania. Nakuupenda mume wangu"



    Ujumbe wasauti, ukawa umekwisha. Nikashusha pumzi nyingi, huku tabasamu pana likiwa usoni mwangu. Nikatoka sebleni na kumkuta Pretty akiwa anaminya minya batani za laptop yake.

    "Unafanya nini?"

    "Nachapisha habari za kumchafua John kwenye mtandao na kuituma hii video ya mauaji"

    "Hapana usifanye hivyo"

    "Kwanini?"

    "Nataka kumuua John taratibu"

    "Kumuua taratibu!?"

    "Ndio"

    Nikaanza kumuadisia historia nzima ya maisha yangu. Kuanzia nilivyokua shule na John hadi leo ni adui yangu.

    "Sasa kwanini hutaki tumuue sasa hivi?"

    "Pretty mpango wangu ni mrahisi sana. Nataka kumuua kwa kifo chakumzalilisha na kumtesa sana."

    "Ila familia yangu ipo salama"

    "Kweli?"

    "Ndio"

    Pretty akanikumbatia kwa furaha, huku machozi yakimwagika kwani historia yangu ilimuuzunisha sana.



    Siku ya pili, tukakutana na John na Sheila wakiwa kwenye maandalizi. Ikamlazimu Pretty kuwaomba msamaha kwa kile kilicho jitokeza jana mchana. Hii ikiwa ni moja ya mpango wetu wa kumteketeza John na Sheila, pasipo wao kujua chochote.

    "Nilijua tu nihasira, mimi nimemsamehe"

    John alizungumza huku akimpa mkono Pretty.

    Ikawa ni furaha kubwa sana kwa John, na Sheila wake. Wakiamini urafiki wetu utaendelea kama kawaida na laiti wangejua wasinge ruhusu kujipendekeza kwetu.

    ***

    Siku ya harusi ya John ikawadia, mimi na Pretty tukawa nimiongoni mwa waalikwa kwenye sherehe hii ndani ya kanisa hili kubwa la Roman katolic.

    "Kila kitu umekipanga sawa?"

    Nilimuuliza Pretty mara baada ya kufika kanisani, tukishuka kwenye gari yetu aina ya BMW, tulilo linunua jana kwa kazi moja tu iliyopo mbele yetu.

    "Kila kitu kipo powa mpenzi"

    Kabla sijazunguza chochote simu yangu ikaita kwa namba ya Blanka, ndio inayo nipigia.

    "Nipigie bwana"

    Blanka alizungumza kwa furaha, ikanibidi nikate simu na kumpigia.

    "Ndio kaka Eddy. Kweli wewe nikiboko"

    "Kwanin?"

    "Yaaani toto lako nikopi na wewe yaani umefanya kazi kubwa kulitafuta"

    "Kwani wamefika?"

    "Ahaaa ndio nipo hapa uwanja wa ndege nimewapokea yaani weee acha tuu. Ninafuraha yakufa mtu"

    "Hembu mpe Junio simu nizungumze naye"

    "Dady tumefika Tanzania"

    "Umemuona antie?"

    "Ndio, ila kuna joto kali"

    "Poleni mwanangu, mpe mama simu"

    Nikasikia sauti ya Junio ikimuita Phidaya, furaha ikazidi kuongezeka moyoni mwangu, nakujiamini zaidi kwamba kazi yangu inazidi kuwa nyepesi zaidi.

    "Mume"

    "Niambie mke wangu"

    "Safi, tumesha fika Tz yaani hapa nijoto"

    "Sasa hivi nisangapi?"

    "Saa.....saa tano inakwenda saa sita usiku"

    "Poleni kwa uchovu"

    "Yàani wee acha tu, yaani tumetoka Marekani jana alfajiri, tunashukuru Mungu ndege tuliyo panda haikupita kwenye nchi nyingi"

    "Ilikuwaje mukaenda Marekani?"

    "Hilo swali muulize mwanao Shamsa"

    "Mpe simu"

    "Vipi wewe"

    "Ahaaa safi baba"

    "Hembu sogea pembeni uniambie nini kilitokea?"

    "Wee acha baba, kipindi tupo uwanja wa ndege kuna jamaa nilikua ninamtilia mashaka, sasa tulipo maliza kukaguliwa. Kipindi sasa tunaelekea kupanda basi lile linalo wapeleka watu kwenye ndege"

    "Ndio"

    "Basi roho yangu ilisita, nikamuambia mama hatuwezi kuondoka. Nashukuru mama alinielewa ikatulazimu kuuza tiketi kwa kisingizio tumepata msiba wa gafla Marekani"

    "Tukaweka booking kwa ndege iliyokua inaondoka saa moja usiku, basi tukaondoka"

    "Duuu umefanya la maana sana mwanangu. Una habari?"

    "Ya nini?"

    "Ile ndege, mulio kuwa mukitaka kupanda. Imelipuka"

    "Weeee"

    "Na mtu uliye kua unamtilia mashaka ndio huyo John"

    "Yupoje?"

    "Mrefu kiasi, mweusi si sana na ana macho makubwa hivi"

    "Ahaaa nilimuona pale ulivyo ndoka basi akawa anatutizama sana"

    "Mimi aliniona?"

    "Hakukuona kutokana alikuja dakika kama tatu hivi baada ya wewe kutuacha"

    "Hei ibada inataka kuanza"

    "Pretty alizungumza kwa sauti ya chini huku akinionyesha ishara nikate simu.

    "Ok nitawapigia baadaye"



    Nikakata simu, shamsa akanishikaa mkono, tukaingia kanisani. Tukakaa viti vya mbele huku, tukiwa na hamu yakuwashuhudia maharusi wetu. Mlio wa kinanda, wakuwaruhusu maharusi kuingia kanisani, taratibu ukaanza kulia. Vitoto vidogo vipatavyo kumi, vitano vikiwa vya kiume na vitano vikiwa vya kike wakawa wametangulia mbele, huku John na Sheila wakifwata kwa nyuma.

    "Mpango mbona kama utaaribika?"

    Nilimuuliza Pretty kwa kumnong'oneza kwa sauti ya chini, pasipo mtu mwengine kusikia nilicho kizungumza.

    "Usijali, naiaminia timu yangu"

    Pretty alinipa matumaini makubwa ya kuifanya kazi yangu. John na Sheila wakafika mbele yakanisa. Ukubwa wa hili kanisa ukanifanya niwe makini sana kutazama walinzi wa John ni wapi.

    Ibada ikaanza huku nasi tukipiga ishara za msalaba, kama wafanyavyo waumini wengine.



    Maubiri ya hapa na pale yakafanywa na mchungaji, anaye fungisha ndoa hii. Huku akituahusia tusilipize baya kwa ubaya.

    'Kakosa chakuhubiri huyu'

    Nilijisemea kimoyo moyo, baada ya kusikiliza maubiri yake kwa umakini, na yote nikahisi yananihusu mimi.



    Muda wakuvishana pete ukawadia, Prettyakatoa simu yake kwenye pochi yake.

    "Unataka kufanya nini?"

    "Subiri uone"

    "Coletha Agray upo tayari kumpokea John, kuwa mume wako wa maisha, kwenyeshida na raha, afya na magonjwa hadi pale kifo kitakapo watenganisha?"

    "Ohooooo aiiiiii mmmmmmmmm"

    Sauti za mahaba zilisikika kutokea kwenye vipaza sauti vilivyomo humu kanisani. Kila mmoja akawa amekodoa mimacho kila upande. Gafla tv zote zilizo kuwemo ndani ya kanisa hili, zikabadilisha picha kutoka katika matukio yanayo endelea humu kanisani hadi kwenye video ya ngono, aliyo cheza Sheila miaka kadhaa ya nyuma.



    Kila mtu akajikuta mdomo wazi, ila tukio hilo ninatambua Pretty ndio amelifanya litokee. Nikamuona Sheila akitazama chini, huku mchungaji akiweka miwani yake vizuri, akitazama tv iliyopo pembeni yao. John akaanza kuhaha, huku akizungumza na msimamizi wake hata kama kuna jinsi ya kuzisimamisha video hiyo ifanyike.

    Sheila akashindwa kustahimili kusimama, akadondoka chini na kutulia akazidi kumchanganya John, aliye livua koti lake kwa kuchanganyikiwa. John amampokonya kipaza sauti mchungaaji

    "Wewe mshenzi uloye ziweka hizi video zitoe kabla sinakuua"

    John alizungumza huku mishipa ya shingo ikiwa imemsimama, huku jasho jingi likimwagima kama maji.

    Video zikabadilika na kuionyesha sura yangu, halisi, huku chini kukiwa na maandishi makubwa R.I.P EDDY, ikaja picha ya Victori, akiwa na John. Huku maandishi yakiandikwa R.I.P VICTORIA.

    John akabaki akiwa ameitumbulia macho tv hiyo. Akaifwata Tv na kuinyanyua, akaibamiza chini. Gafla taa zote za kanisani zikazima, huku kagiza kwa mbali kakitanda ndani ya kanisa. Watu wakaanza kuchanganyikiwà mara baada ya moshi mkali, wa mabomo ya machozi kuanza kutapakaa ndani ya kanisa. Nakuzidi kumchanganya John aliye fura kwa hasira kali.



    Mirindimo ya risasi, ikaanza kurindima ndani ya kanisa, jambo lililo pelekea watu kulala chini, huku wakipiga mayowe.

    "Pretty mbona sielewi?"

    Milimuuliza Pretty baada ya kuona hali inazidi kuwa ngumu, Watu walio valia nguo nyeusi wapatao kumi, wakaingia ndani ya kanisa, huku sura zao zikiwa zimezibwa na vinyago, mikononi mwao wakiwa waneshika silaha nzito

    "Hata mimi sielewi"

    Pretty alinijibu huku akionekana kuto kuelewa ni nini kunacho endelea, kwani si tukio tulilo lipanga kutokea.



    Kundi la watu hao, nikawashuhudia wakimnyanyua juu, John aliye legea sikujua wamemfanya kitu gani. Wakambena na Sheila juu na kutoka nao nje yakanisa.

    "Twende"

    Nilimuambia Pretty huku tukinyanyuka na kutoka nje ya kanisa huku tunakimbia. Tukalikuta gari jeusi, kubwa likiondoka kwa kasi nje yakanisa. Nikakimbia hadi lilipo gari letu, huku Pretty naye akinifwata kwa nyuma. Nikaingia na kuwasha gari. Ikawa ni kazi yangu kulifuluzia gari hilo lililo wabeba Sheila na John ambao wapo kwenye mpango wangu wa kuwaangamiza na sikujua hawa walio vamia na kumteka ni kina nani.

    Pretty akabaki kunishanga, kwa jinsi undeshaji wangu ulivyo kama kichaa. Kwani niliyapita magari yaliyo mbele yangu, pasipo kupunguza mwendo kasi wa gari.

    "Ohhh Eddy tunafwatwa kwa nyuma"

    Kwakupitia kioo cha pembeni, nikaona gari nne za polisi zikitufwata kwa kasi huku zikipiga ving'ora.

    "Tulia usiwe na wasiwasi"



    Kwa uzoefu wangu, katika kuendesha magari haya ya kampuni ya BMW, ulinisaidia sana kuweza kumudu mwendo kasi wa gari, la maadui lililo wabeba John na Sheila. Polisi hawakukata tamaa kuendelea kutukimbiza kwa nyuma. Nikastukia kuona gari la watu majambazi, wakifungua mlango wa nyuma, wakasimama jamaa wawili wakiwa kwenye mavazi yao yale yale walioyo ingia nayo kanisani, kila mmoja wao akiwa na bunduki zao zinazo toa risasi pamoja na mabomu pale wanapo hitaji kufyatua mabomo hayo.

    Mara nyingi bunduki za aina hii wanatumia wanajeshi wakimarekani, hususani wale wanao kwenda kupambana na vikundi vya kigaidi katika nchi za Iraq na nyinginezo zenye vikundi vya kigaidi.

    "Eddy......Eddy.......Eddy"

    Pretty alizungumza hivyo baada ya kuona watu hao. Umakini wangu wote ukahamia kwao. Wakaanza kupiga risasi zisizo na idadi, kuelekea tulipo sisi. Nilicho kifanya ni kubadilisha njia na kupitia kwenye barabara ya pembeni, ambayo magari yake yanarudi kutoka upande ninao tokea mimi.

    Katika siku nilizo jitahidi kuendesha gari, zaidi ya uwezo wangu ni siku ya leo. Mbaya zaidi magari mengi ya upande niliopo yananifwata, kila ninavyo yakwepa ndivyo ajali ya magari mengine yanavyo zidi kubamizana, kutokana na kunikwepa mimi.

    "Eddy rudi upande ule"

    "Watatuua"

    "Kwani ni kina nani?"

    "Sijui mimi"

    Ptetty akakaa kimya na kuniacha nifanye lile ninalo liweza katika kuyaokoa maisha yetu, kwa maana yapo hatarini kutoweka endapo nitafanya kosa la kugongana na gari lolote. Nikazishubudia gari za polisi jinsi zinavyoshambuliwa na magaidi hao hadi zikapoteza muelekeo.

    Nikafanikiwa kulirudisha gari upande ninao paswa kupita, Nilicho kifanya kwa wakati huu, nikuhakikisha ninalipita gari hilo kwa kasi kubwa. Kabla sijachukua uamuzi huo, wakakatiza kulia na kuingia kwenye barabara iliyo nyooka sana. Sikukata tamaa na mimi nikakafanikiwa kukunja huko huko japo gari lilinizidi nguvu, likayumba kidogo, kutokana na kukunja gafla. Nikafanikiwa kuliweka sawa na kuendelea kulifukuzia.



    "Wanaelekea kwenye msitu wa Amazon"

    Pretty aluzungumza huku akitaza simu yake inayo inyesha ramani ya eneo tulipo.

    "Sasa Eddy si tuhairishe kuwafwata"

    Pretty alizungumza akionekana kukata tamaa. Sikumjibu chochote zaidi ya kufanya kile kilicho niweka ndani ya gari hili. Nikafanikiwa kulipita gari hili na kuwa mbele yao. Nimejiamini kuwa mbele kutokana na barabara kunyooka tu.

    "Unaweza kuendesha kwa mwendi huhuu?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ndio"

    "Njoo ukae hapa"

    Nikampisha Pretty kwenye siti niliyo kalia kwa utaalamu mkubwa pasipo kupunguza mwendo kasi wa gari, nikarukia siti ya nyuma. Nikalichunguza gari hili vizuri, jinsi linavyo kuja kwa kasi nyuma yetu. Nikafungua mlango wa nyuma

    "Eddy unataka kufanya nini!?"

    "Nahitaji kwenda juu ya hari hili"

    "Umechanganyikiwa wewe?"

    "Punguza mwendo"

    "Alafu si tutakufa?"

    "Nahitaji uwe sawa na hili gari"

    "Nini?"

    "Fanya hivyo"

    Pretty akageuka nakunitazama kwa macho yamshangao.

    "Funga mlango"

    Nikafanya alivyo hitaji, akafunga breki za gari, kisha akakanyaga breki za gafla huju akilkgeuza kwa mtindo wa kuchora duara, jambo lililo mchanganya dereva wa gari la majambazi hao, Akajitahidi kulikwepa gari letu, linalo endelea kuzunguka huku lilichora duara.



    Tukalishuhudia gari hilo likitoks barabarani, na kulivas jiwe kubwa lililopo pembezoni mwa barabara, na kulipelekea gari hilo kubinuka nakuanza kubingiria. Pretty akaluweka sawa gari na kuelekea lilipo gari la majambazi hao. Nikashuka kwenye gari haraka, nikamkuta dereva wao akijitahidi kutoka ndani ya gari hilo. Huku akiwa ameumia vibaya usoni mwake.

    Nikaiwahi bunduki yake, nikamtwanga risasi mbili za kichwa. Kwa mwendo wa tahadhari nikazunguka nyuma, kulipo na mlango wa kuingilia ndani. Nikaufungua taratibu, watu wote waliomo ndani nikakyta wakiwa katika hali maututi, Nikamvuta John nje, nikamvuta na sheila nje. Nikarudi ndani ya gari hili lililo lala ubavu, naada ya kubingirika zaidi ya mara kumi mfululizo.

    Kila aliye kua na hali mbaya nikamsindikaza kwa ridasi kadhaa. Akabaki mmoja akiwa anatetemeka huku akiniomba nisimuue.

    "Nani aliye watuma?"

    Nilimuuliza huku, mdomo bunduki nikiuelekezea kichwani mwake.

    "Ni...Mad......ame Mery"

    Alizungumza huku damu zikimtoka mdomin mwake.

    "Yupo wapi?"

    "Yu..po......"

    Hakuimalizia sentensi yake, akakakata roho. Kuhakikisha amekufa nikamtandika risasi yakichwa. Nikatoka nje ya gari na kumkuta Pretty akiwa amesimama pembeni ya miili John na Sheila.

    "Wamekufa au?"

    'Wapo hai"

    "Sasa si uwaue?"

    "Bado ninakazi nao"

    Nilizungumza huku nikikagua moja ya bastola niliyo ichomoa kwa majambazi walio waua ndani ya gari.

    "Kazi gani?"

    "Utaiona"

    Tukawabeba na kuwaingiza ndani ya gari, Pretty akaniambia kuna nyumba yake, ipo maemdeo ya karibu ya msitu wa Amazoni. Tukatembea kama kilomita sita hivi, tukafika kwenye ntumba yake iliyopo juu ya mlima. Manzari yake nimazuri sans, na ninyumba iliyo jengwa kwa ustadi vizurii na inagorofa moja kwenda juu.

    "Hapa ni kwako kweli?"

    "Ndio"



    Tumawaingiza ndani, John na Sheila ambao hadi sasa hivi hawajitambui na sura zao zimejaa damu. Nikawajalisha kila mmoja kwenye kiti chake, huku nikiwa nimuwavua nguo na kubakiwa na nguo za ndani. Kila mmoja nikamfunga kwa kamba gumu ya manila.

    "Unakwenda kuwafanyaje?"

    Pretty aliniuliza baada ya kulimaliza zoezi langu, nililo kuwa nimelifanya.

    "Utaona, hadi asubuhi watakuwa wamesha zinduka. Tukatoka ndani ya chumba tulicho waingiza John na Sheila.

    "Unahitaji kinywaji?"

    "Ndio"

    Pretty akafungua, friji na kutoa mzinga wa pombe kali akaja nao kwenye sofa nililo kalia, huku nikitazama taarifa ya habari, kukua nini kunacho endelea katika nchi hii, hususani mwa tukio la leo.

    "Hawajatujua"

    Pretty alizungumza baada ya kutazama taarifa hiyo kwa muda kidogo.

    "Nahisi"

    "Hivi umejifunza wapi kuendesha gari?"

    "Sijajifunza popote, kikubwa ni kujituma"

    Pretty akanitazama usoni mwangu, akapiga fumba moja la pombe kali, kisha akanivutia kwake na kuanza kuninyonya mdomo

    "Pretty stop, nina mke"

    Nilizungumza huku nikimzuia kuendelea kufanya anacho kifanya

    "Mmmm samahani Eddy"

    Pretty alizungumza kwa aibu, huku akiyakwepesha macho yake na yangu yasikutane kwa pamoja.

    "Usijali"



    Hatukulala hadi, kuna pambazuka. Nikawa wa kwanza kuingia kwenye chumba walichopo John na Sheila. Nikawakuta wakiwa wamezinduka, huku wakiwa hawaelewi wamefikaje hapa.

    "Henry rafiki yangu asante sana kwa kuja"

    John alizungumza baada ya kuniona nikiwa nimesimama mbele yao.

    "Pole, jana nikaona harusi imevurugika?"

    "Ndio kaka yaani sijui ni mshenzi gani aliye fanya hivi? Tufungue basi kaka"

    "Nitawafungua, ila nimemuoji mmoja akadai ni Madam Mery, ndio amewatuma sijui unamjua huyo?"

    John akakaa kimya akionekana kumfikiria mtu niliye mtajia

    "Ahaaas ndio ninamjus huyu mama ni mshenzi sana, ila nifungue kaka tuondoke nitakuadisia mbele ya safari"

    "Usalama hapa upo mzuri tu. Wala usijali ndugu"

    "Shem tufungue jamani"

    Sheila alizungumza huku akimwagika na machozi.

    "Usijali shem, Pretty anaanda vifaa vya kusafisha majeraja yenu"

    "Huyo madam, anataka nini kutoka kwako?"

    "Anataka mali zake"

    Nilimuoji John katika hali ya upole, pasipo kumfanya astuke kwamva mimi ni nani.

    "Mali gani?"

    John akamtazama, Sheila kisha akanitazama na mimi.

    "Kuna jamaa, tulipanga sote wawili tumuangamize tuchukue mali za bana yake sasa, sijamrudishia ndio maana ameamua kuanza vita na mimi. Haki ya Mungu nitamuua huyu mwanamke wee ngoja niwe sawa.Na yeye ndio aliye tuzalilisha kanisani"

    "Ahaaaaa, pole sana kaka. Huyo jamaa anaitwa nani?"

    "Huyo niliye mchukulia mali?"

    "Ndio"

    "Eddy Godwin"

    "Ndio kama huyu"

    Nilizungumza huku nikiibabadua sura yangu ya bandia, hadi ikatoka yote na kubaki na sura halisi. John na Sheila wakabaki wakiwa wame nitumbulia mimacho. Mwili mzima wa John ukaanza kutetemeka, hadi mkojo ukaanza kulowanisha boxer yake na kutapakaa chini.

    "Eddy kuna....."

    Pretty alinyamaza baada ya kuingia ndani ya chumba hichi, na kunikuta nikiwa na sura yangu halisi. Pretty akapiga hatua hadi nilipo huku akiwa amebeba sinia kubwa lenye vitu vyenye makali mengi, kama kisu na vifaa vya oparesheni vitumikavyo hospitalini. Huku mkono wake mwengine akiwa ameshika bomu lakutega.

    "Pretty...!!!"

    Sheila aliita huku akimshangaa, Ptetty aliye simama mbele yao.

    "Haya wewe kidume kizima kujikojolea humu ndani ni nini?"

    Pretty aliuliza, huku akiwa na anamcheka John.

    "Hawezi kukujibu, sasa hivi"

    "Hahaa, haki ya Mungu kumbe ubane wa bure"

    "John rafiki yangu, Sheila mke wangu wa zamani niwaulize kitu"

    Sheila akajibu kwa kutingisha kichwa akiashiria niulize tu.

    "Munapenda niwakate kate, kate vipande vigogo vidogo kama nyana. Au mufe kwa bomu hili, litakalo wachangua vipande vidogo vidogo"

    Sheila badala ya kujibu, akaangua kilio likubwa kilichonifanya nimtandike ngumi nzito ya shavu, hadi taya ikapinda, huku meno baadhi yakianguka chini.



    "Ahaaaaa fu**"

    John alijikuta akitukana kwa kitendo nilicho mfanyia mke wake. Sheila akaendelea kuangua kilio cha majuto sana.

    "Nipe kisu"

    Pretty akanipatia kisu chenye makali, John akabaki akiwa amenitumbulia mimacho, huku hakiema kwa woga. Nikamkita John kisu cha kwenye paja, la mguu wake wa kulia.

    "Mamaaaa.."

    John alilia kwa uchungu, ulio changanyika na maumivu makali.

    "Ahaa kuna kitu nahitaji ukifanye kabla haujakufa"

    Nilizungumza huku, nikikizungusha kusu kilicho zama kwenye paja lake, John akazidi kutoa mlio wa machozi.

    "Kuna mali zangu, ulizo zichukua wewe na ulivyo mjinga ukaamua kumdhulumu Madam Merry. Sasa nazihitaji zote zirudi kwangu"

    "Na....ru..disha"

    "Sawa kama utazirudisha"

    "E...ddy tusa...mehe"

    Sheila alizungumza kwa sauti iliyo legea, kutokana na ukosefu wa meno yake mdomoni na kuvunjika kwa taya yake.

    "Tena wewe usizungunze. Ni mwanamke gani usiye na huruma katika maisha yangu. Ulipanga kuniua mimi ili muchukue mali za mama yangu. Kwa bahati mbaya ukamuua Fredy. Mtu niliye fanana naye. Leo hii unasema kwamba niwasamehe"

    Nilizungumza kwa hasira huku nikimtazama Sheila jinsi anavyo vuja damu.

    "Nimezaliwa na roho ya kiatili, na sijawahi kumsamehe mtu abaye kwenda kinyume na mimi."

    Nikachukua mkasi mkubwa kiasi. Nikashika kidole kimoja cha John na kukichomeka katikati ya mkasi.

    "Ngoja ngoja usinikate nikuambie ukweli"

    John alizungumza huku akiendelea kulia hadi makamasi yakaanza kumwagika puani mwake.

    "Mali zote nilizo zichukua, kuma mtu ndio mmiliki kabisa na mimi ndio nilikua ninamsimamia"

    "Nani?"

    "Mzee Godwin na.....na yupo Oman, ndipo yalipo makazi yake"

    Ikawa ni taarifa nyingine mpya kwani mzee Godwini ninavyo fahamu mimi amefungwa. Ila gereza alilo fungu ndio sikulifahamu.

    "Mmmm kwahiyo, hajafumgwa yeye?"

    "Haa....hajafumgwa na mtu aliye kua akishirikiana naye ni madam Mery"



    Nikakaa kimya huku nikimtazama John usoni mwake. Sikuhitaji kumuonea huruma John hata kidogo. Nikakikata kidole chake kwa kutumia mkasi na lukitenganisha na vidole vinne vilivyo bakia kwenye mkono wake.

    "Nahitaji namba za akaunti zako zote za benki"

    "Ehee tena ngoja nichukue laptop"

    Pretty alizungumza huku akitoka kwenye chumba tulichopo. Ptetty akarudi akiwa na laptop yake.

    "Tunaweza kuzihamisha hizo popote pale kwenye akaunti ya benki"

    Pretty alizungumza huku akiminya minya batani za laptop yake.

    "Kwanza una akaunti ngapi?"

    "Eheeee?"

    "Hujanisikia eheee"

    Nikachukua koleo, nikalichomeka kwenye sikio la John, la upande wa kushoto na kuanza kulibana taratibu.

    "Nakuambia hiviiii, una akaunti ngapi za benki"

    Nilizungumza kwa sauti ya kumnong'oneza John

    "Tano tano"

    John alijibu kwa sauti ya juu.

    "Kumbe unanisikia vuzuri. Ila una ihakika ni tano?"

    Nilizungumza huku nikiminya zaidi sikio lake

    "Zipo saba, nyimgine ni....ni ni...."

    "Ni..ni ni sizihitaji kuzisikia, una akaunti ngapi?"

    "Kumi"

    Nikajikuta nikicheka kwa maana kili ninavyo zidi kulibana sikio lake ndivyo kila alivyo zidisha kutaja idadi ya akaunti zake za benki.

    "Tutajie namba ya akaunti na beki"

    John akataja namba ya kwanza, huku akimwagikwa na machozi.

    "Ni ya benki gani?"

    Pretty alimuuliza, huku akiendea kuminya batani za laptop yake.

    "Co-operative"

    "Ya London?"

    "Ndio"

    "Yes Eddy, imesoma, tunaomba namba ya siri"

    John akataja, Pretty akaiingiza na kusubiria kwa muda kidogo.

    "Ohoo My God, Eddy njoo uone"

    Nikaliachi sikio la John na kwenda alipo Pretty. Akanionyesha kiasi cha pesa kilichopo kwenye akaunti hiyo. Ambacho dola za limarekani bilioni kumi.

    "Eheeee, John mwanangu, kumbe wewe nintajiri hivi. Ukiambiwa utakufa na kuziacha hizi"

    Nilizumgumza huku nikimcheka John, ambaye uhai wake upo mikononi mwangu. Nikamtajia Ptetty namba za akaunti yangu ambayo nahitaji wazihamishe pesa hiyo.

    "Ohoo wanataja alama ya dole gumba la John ili waweze kudhibitisha kuzihamisha kwenda kwenye akaunti yako"

    "Wanataka la upande gani, hilo dolr gumba?"

    "Kulia"

    Nikachukua mkasi wangu na kumfwata John alipo.

    "Nina kazi na kidole chako"

    "Eddy kikatie chini chini kidogo ili kifiti hapa"

    Pretty aliniambia, John akanitumbulia mimacho akihisi kwamba sinto fanya hilo swala. Nikalikamata dole gumba la kulia na kulikata kwa nguvu. Sheila akatoa ukelele, kama yeye ndio aliye katwa.

    "Kinacho kuliza na wewe? Nahisi hili tukio si geni kwako, kwani Derick yule malaya wako naye alikufa kama huyu"

    Nikakichukua kidole cha John na kwenda sehemu alipo kaa, Pretty.

    "Kisuuze kwanza bwana, si unaona kimejaa damu"

    Nikakisuuza vizuri kidole cha John kwa kutumia maji, nikampa Pretty akakiweka kwenye kifaa kingine, alicho chomeka waya wake kwenye laptop. Mwanga mwekundu ukapita kwenye kidole cha John,

    "Hapo kinafanyaje?"

    "Nina kiscan. Yes kimesoma"

    Pretty akanionyesha, kidole kimefanana na alama ya dole gumba iliyopo kwenye benki hiyo.

    "Sasa pesa hapa tunaweza kuihamisha"



    Pretty akaanza kufanya, kazi ya kuhamisha pesa hiyo kwenye akaunti yangu.

    "Asilimia zinakwenda taratibu?"

    "Kwa nini?"

    "Pesa nyingii hii"

    Kama robo saa, pesa, yote ikawa imekamilika luhamishiwa kwenye akaunti yangu. John akaendelea kututajia akaunti zote anazo zimiliki na zote zina pesa nyinhi tu. Pesa nyingine nilimpa ruhusa, Pretty akazihamishia kwenye akauti yake.



    Hadi inafika majira ya saa kumi jioni, tukawa tumelikamilisha zoezi zima la kumfilisi John kwenye maakaunti yake ya benki.

    "Vifo vyenu nahitaji viwe vya taratibu mno"

    Nilizungumza huku nikinywa juisi, aliyo nipa Pretty, hii ni baada ya kukaa kwa muda mrefu pasipo kula chocho.

    "Eddy nisamehe kaka, kwani haya yote niliyafanya kwa tamaa"

    "Ahaaa tamaaa?"

    "Pretty ile video ya mauaji ya Victoria iweke mtandaoni, kila mtu ajionee ukatili wa huyu mjinga"

    "Sawa bosi"

    Pretty akamuonyesha John, ile vodeo jinsi alivyo muua Voctoria, John akabaki akitokwa na machozi mengi. Sheila naye akabaki akikodoa mimacho, hata kuzungumza alishindwa kutokana na taya kuvunjika.

    "Una jengine la kuzungumza?"

    John akatingisja kichwa kwamba hana la kuzungumza. Nikachomoa bastola, kiunoni mwangu. Nikaifunga kiwambo cha kuzuia sauti.

    "Yupi awe wa kwanza kufa?"

    Hakuna aliye nijibu zaidi ya woye kukaa kimya. Nikampiga John risasi za miguu, kwenye magoti, kisha nikachukua kishoka kidogo cha kukatia nyama. Nikakata viganja vyake vya mikono yote miwili.



    Yote niliyo yafanya Pretty na Sheila waliyashuhudia kwa macho yao mawili. John alilia kwa uchungu mkubwa huku akiniomba nisimuue ila sikumpatia msamaha wa aina yoyote. Nikamgeukia Sheila na kumtazama kwa macho yaloyo jaa chuki na hasira kali.

    "Ed.."

    Sheila aliniita, kabla hajamaliza kuliita jina langu, nikampiga risasi tano za kifuani mwake, nikachukua bomu, lakutega. Nikaliweka mbele ya John huku nikiwa nimelitega dakika tano lilipuke.

    "Kifo hichi ndicho unacho stahili John"

    Nikamaliza kumpiga John risasi za miguu yake yote, hadi nilipo hakilisja hatoweza kusimama wala kulishika bomu hilo, kwani hana tena viganja vya mikono.

    Tukatoka na Pretty hadi nje, Pretty akachukua gari lake jengine na tukaliacha gari tulilo kuja nalo, kuepuka kukamatwa na polisi. Tukaondoka eneo la nyumbani, hatukufika mbali sana nyumba nzima ikalipuka huku John na mwili wa Sheila vikiwa ndani.

    "Eddy inabidi ukatubu kwa Mungu wako"

    Pretty alizungumza huku akiendelea kuendesha gari kwa kasi. Tukaingia kwenye barabara ile tuliyo pita jana, iliyo nyooka. Tukaingia mjini majira ya saa mbili usiku, ambapo tukaelekea moja kwa moja hotelini.

    Nikafika chumbani kwangu na kuchukua kila kilicho changu, nikarudisha funguo kwa wahusika

    Nikatoka nje na kumkuta Ptetty akinisubiri ili anisindikize uwanja wa ndege. Nikaingia ndani ya gari na tukaondoka eneo la hotelini.

    "Eddy kuna kitu nitahitaji nikuambie kabla hukaondoka"

    "Kitu gani?"

    "Mimi ni mpeleleIi wa kikosi cha CIA, nilipewa zamana ya kukulinda na serikali yangu ya Marekani."

    Nikastuka kusikia aliyo niambia Pretty.

    "Usistuke kwa maana bado matatizo kwako hayaja kwisha"

    "Una maanisha nini?"

    "Baba yako, anakutafuta ili akuue"

    "Wewe unejuaje?"

    "Mim ni mpelezi ni lazima nilihisi hilo. Ninacho kusihi sasa nenda Tanzania na uipeleke mbali familia yako la sivyo watauawa"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pretty alizungumza kwa msisitizo mkubwa, ulio ifanya akili yangu kuanza kumfikiria mzee Godwin. Tukafika uwanja wa ndege, kabla ya kushuka, kutoka ndani ya gari akanisogelea na kunibusu mdomoni

    "Nakitakia safari njema Eddy"

    Ptetty alizungumza kwa sauti ya unyonge huku machozi yakimlenga lenga. Nikaupitisha mkono wangu kwa nyuma, nikakiasogeza kichwa chake karibu yangu, tukanyonyana midomo yetu kama dakika tatu na kumuachia, huku akihema kwa pumzi nzito iliyo jaa mahaba.

    Nikafungua mlango na kushuka, nikachukua begi langu lililopo kwenye buti. Nikamtazama Pretty aliye kataa kushuka kwenye gari, machozi yakawa yanamtiririka.

    "Pretty bye"

    Pretty hakunijibu kitu zaidi ya kuendelea kulia kwa uchungu mwingi. Nikaelekea sehemu ya kukatia tiketi kwa bahati nzuri nikapata tiketi moja ya ndege, iliyokua ikiondoka nusu saa badaye. Nikasimama kwenye foleni ya watu wanao kaguliwa na mizigo yao, ili kuelekea kwenye ndege.

    "Eddy Eddy"

    Nikageuka nyuma na kumuona Pretty akija kasi, huku akilia. Ikanibidi nitoke nje ya foleni, Pretty akanirukia na kunikumbatia kwa nguvu. Machozi yakazidi kumtomka

    "Eddy usiende popote, ninakupenda sana"

    Ptetty alizungumza huku akiendelea kulia, akaniachia na kusimama huku akinitazama.

    "JAMANI NINAMPENDA EDDY GODWIN, NAHITAJI ANIOE"

    Nilimshangaa Pretty akizungumza kwa sauti kubwa, iliyo wafanya watu wote kututazama. Bila ya aibu Ptetty akanikumbatia na kuanza kuzinyonya lipsi zangu, jambo lililo wafanya watu wote kupiga makofi ya kushangilia





    Ikanilazimu kumtoa Pretty kwenye mwili wangu, taratibu.

    "Ptetty"

    Nilimuuita kwa sauti ya upole, huku nikimtazama machoni mwake.

    "Mmmmm, nakupenda sana, ila ninakuomba kitu kimoja tu unisaidie kwa wakati huu"

    "Kitu gani?"

    "Ninakuomba, uniruhusu nikaiweke familia yangu katika sehemu salama."

    "Eddy nimekuzoea sana. Ninakuomba twende wote"

    "No no, nitarejea mama, kwa ajili yako, ninakuomba uniruhusu katika hilo."

    Pretty akakaa kimya huku akinitazama machoni mwangu, machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake.

    "Promise me"(Niahidi)

    "Nitarejea mpenzi, kwa ajili yako"

    "Kweli?"

    "Ndio"

    Ilinilazimu kutumia akili nyingi na busara kubwa kumdanganya Pretty la sivyo nisinge ondoka na hata ndege niliyo ibahatisha kwa ajili ya usafiri nisinge ipata.

    Pretty akanikumbatia tena, akunibusu mdomoni, huku akilia, nikamfuta machozi kwa kutumia viganja vyangu.

    "Nitarudi baby"

    "Ok, safari njema"

    Pretty alizungumza kwa kujikaza, kwa maana uchungu alio kuwa nao ni mkubwa sana

    "Kuwa makini, Eddy"

    "Na wewe pia"

    Pretty akaniruhusu kuondoka, nikapiga hatua za haraka hadi kwenye foleni ya ukaguzi. Nikavua vitu vinavyo hitaji kuvuliwa ikiwemo, mkanda wa suruali, saa ya mkononi, viatu na simu yangu nikawakabidhi. Nikafanikiwa kupita salana kwenye kitengo hicho, nikachukua kila kilocho changu na kwenda kujumuika na wasafiri wengine.

    Tukaingia ndani ya ndege, huku nikiwa ninafuraha sana, kwani ni muda wa kwenda kumuonyesha mama yangu, familia yangu aliyokua akiikataa kisa wao ni waarabu ambao mara nyingi alidai mke wangu ni gaidi, kumbe Sheila ni gaidi mkubwa aliye kuwa amejificha kwenye familia yake.

    Nikakaa kwenye siti yangu, ambapo pembeni nikamkuta mtu akisoma gazeti kubwa, lilolo ificha sura yale huku kichwani mwake akiwa na kofia kubwa.

    "Hi...!!"

    Nilijipendekeza kusalimia, kwani si uungwana kukaa siti moja na mtu pasipo kusalimiana naye. Akalishusha gazeti lake chini kidogo, ndipo nilipo pata nafasi ya kuiona sura yake vizuri.

    Ni mzee wamakamo aliye enda umri kidogo, anaasili ya kiarabu, huku ndevu zake zikiwa za rangi nyeupe.

    "Hakunijibu kitu zaidi ya kunitazana kwa sekunde kadhaa, kisha akalirudisha gazeti lake usawa ulio kuwepo awali na kuufunika uso wake kabisa.

    "Mmmmm"

    Niliguna, huku na mimi nikifunga mkanda wa siti niliyo kalia, nikatoa simu yangu na kumpigia Blanka

    "Vipo dogo"

    "Safi kaka, huku lini?"

    "Kama wiki hivi, ndio nitarudi, wapo wapi hao"

    "Mlimani city, kuna vitu tumekuja chukua"

    "Ahaaa, nyumba mulipata?"

    "Ndio, tulipata ya kukodi"

    "Poa mida"

    "Hutaki kuwasalimia leo?"

    "Baadaye nitawasalimia"

    Nikakata simu na kuiweka kwenye mfumo wa 'Airplane mode' kisha nikairudisha mfukoni, nikaminya minya batanani za kitv kilichopo mbele yangu, nikaweka filamu ninayo ipenda na kuanza kuitazama, huku nikiwa nimevaa earphone, zinazo tumika kusikilizia sauti ya filamu hiyo, hii nikuepuka kumbuguzi mwenzako uliye kaa naye, huku tukisubiria ndege kuwashwa na kuondoka.

    Taratibu mashine, za ndege zikawashwa, tukaashiriwa na muhudumu, wa kike aliyopo ndani ya ndege hii, kupitia vipaza sauti vilivyomo ndani ya ndege kwamba kila mmoja ajifunge mkanda na kutulia kwenye siti yake, kwani ndege muda wowote itaweza kuondoka. Muda mchache baadae ndege ikacha ardi ya nchi ya Brazili, jambo lililo nipa furaha kubwa kwani tukio nililo mfanyia John na mkewe wake, laiti kama ninge kamatwa ningeozea jela, maisha yangu yote

    'Asante mungu'

    Nilijisemea kimoyo moyo huku nikijiweka sawa kwenye siti yangu

    **

    Mzee aliye kaa pembeni yangu, akalikunja gazeti lake kwa haraka. akachunguli nje kwa kupitia kioo kilichopo pembeni yake, kutokana na giza hakuweza kuona chochote, akalifunga dirisha na kukiziba kioo hicho.

    Akanitazama huku akionekana kuwa na wasiwasi mwingi sana. Akavua kofia lake ambalo mara nyingi hupendwa kuvaliwa na watu wanao jiita 'Cow boys'(Ng'ombe wa kiume). Akaliweka pembeni huku jasho likianza kumwagika, jambo lililo anza kunipa wasiwasi na mashaka makubwa dhidi yake.

    Akaanza kuzungumza maneno yakiarabu yaliyo nipa wasiwasi, kwani maneno yake ni kama ya yule mtu aliye jilipua nikiiwa hotelini, nchini Iraque, akapelekea mimi kupelekwa kwenye hospitali, ambayo nilikutana na Phidaya kwa mara yaa kwanza, akiwa kama daktari aliye nitetea kufa na kupona, pale madaktari wezake walipokua wakihitaji kunikata mguu.



    Mzee huyo akavua koti la suti yake akabakiwa na shati lililo tuna mbele, kwa haraka nikamshika na kuchana shati lake hadi vifungo vikakatika.

    "Bomuuuuuu"

    Nilijikuta nikizungumza kwa sauti ya juu, baada ya kukuta bomu linalo kwenda kwa kasi sekunde zake, zinazo onekana kwa rangi nyekundu, alilo lifunga tumboni mwake. Watu wote waliopo siti za mbele wakanyanyuka na kuanza kupiga kelele, huku wengine wakimuita Mungu wao. Nikataka kuondoka mzee akaniwahi kunidaka mkono, kila nilipo jaribu kuondoka, akanishinda nguvu. Nikalishuhudia bomu lilifika kwenye namba za sifuri, likiashiria lipo tayari kwa kulipuka.

    "Buuuuuuuuupuuuuuuuuu"

    Bomu likalipuka, na kutuchangua sote tuliomo ndani ya ndege

    **

    Nikastuka kutoka usingizini, huku nikihema sana, macho yangu yakatua kwenye kiji tv kadogo kalichopo mbele yangu, kikionyesha tukio la filamu hiyo, ikiwa na mlipuko wa bomu, kwenye moja ya kipande chake, niliyo kuwa nikiitazama kabla sijapitiwa na usingizi. Nikavua earphone huku ikinilazimu kumgeukia mzee aliyopo pembeni kwa haraka, nikalivuta gazeti lake alilo kua akiendelea kulisoma na kumfanya astuke huku akinitumbulia mimamcho yamshangao.

    "What....!!?"(Nini....!!?)

    Mzee aliniuliza, huku akiendelea kunitumbulia mimacho, nikampiga kisukusuku cha uso, kilicho mfanya akae kimya, huku damu za puani zikianza kumchuruzika. Nikamfungua vifungo vya shati lake, nikakuta hana kitu chochote alicho kifunga tumboni mwake zaidi ya msalaba mkubwa alio uvaa shingoni na kuning'inia tumboni mwakr, nikakichomoa kitambulisho alicho kichomeka kwenye mfuko wa shati lake.

    'Rev: Frank Dismas'

    Kitambulisho chake kilionyesha ni mchungaji, wa shirika la misaada duniani

    "Am sorry"(Nisamehe)

    Nilizungumza huku nikimuachia mchungaji huyu, niliye muona kama ni gaidi, aliye jifunga bomu. Hakunijibu chochote zaidi ya kukaa kimya, huku akizifuta damu zake puani kwa kutambaa. Tukio nililo lifanya juu ya huyu mchungaji, halikuonwa na watu wengi, kutokana na wao kalala, kwa uchovu wa safari hii.

    Hamu ya kuendelea kukaa kwenye siti hii, ikanipotea kabisa, kwa maana mchungaji huyu hakuzumgumza chochote na mimi, wala sikujua kama amenisamehe au laa. Akanyanyuka na kuniomba nimpishe, nikafanya hivyo. Akaelekea maeneo ya chooni, huku mara kadhaa akigeuka nyuma na kunitazama mimi, kama mtu mwenye wasiwasi mkubwa na mimi.

    "Huyu mzee vipi"

    Nilizumgumza huku, nikiedelea kumtilia mashaka, moyo wangu nikaulazimisha kumuamini mzee huyu, ila ikakataa kumuamini kabisa. Nikanyanyuka na kuelekea kilipo choo. Kitendo cha kufika mlagoni tu, nikamkuta naye anafungua mlango, akanitazama kwa muda.

    "Buuuuupuuuuuuuuu"

    Alinisemesha maneno, nisiyo yaelewa huku akitabasamu kidharau. Nikabaki nikimshangaa, kwa jinsi alivyo nifanyia huyu mzee, kwa mara ya kwanza nilimuota ila hii ya pili ni kitu kinacho fanyika kiukweli. Nikamtazama, akielelea kwenye siti, huku nikiendelea kumyafakari mzee huyu maana ya kunifanyia hivyo ni nini, na nikwanni amenifanyia mimi peke yangu.

    "Chizi nini huyu? au ni kile kisukusuku, nilicho mpiga?"

    Nilijisemea mwenyewe huku nikiingia chooni.

    Nikafungua zipu ya suruali yangu, kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo. Kabla sijaanza nikahisi kuna kijimlio kikitokea chini ya sinki la kunawia mikono. Ikanilazimu kusitisha zoezi zima, nililo kua nikihitaji kulifanya, taratibu nikainama na kuchungulia. Nikakuta bomo, lililo tegwa, kama lile nililo mtegeshea John, huku likiwa limebakisha dakika mbili na sekunde kadhaa kabla halijalipuka.

    "Mungu wangu"

    Nikatoka chooni haraka, kila niliye mtazama ndani ya ndege, amesinzia, huku baadhi wakiwa wanatazama filamu kwenye tv zao. Sikumuona mzee niliyekuwa nimekaa naye kwenye siti moja, kwani siti zetu mbili zote zilikuwa tupu.

    "Amekwenda wapi huyu mchungaji?"

    Nilizungumza huku nikiendelea kupepesa macho huku na kule.

    Kusema kweli, sikuwa na ujuzi wa kutegua mabomu, nilicho kuwa nikikijua katika mabomu ni kutega tu. Nikamuona muhudumu mmoja mwanadada, akimfunika shuka, mtoto mmoja, aliye lala muda mrefu.

    Nikamfwata na kumuomba, anisikilize shida yangu.

    "Do you speak English or Swahili?"(Je unazungumza Kingereza au Kiswahili?)

    Nilimuuliza dada huyu, huku jasho likinimwagika usoni, Kwani mimi ndio ninafahamu ukweli unao endelea ndani ya ndege hii, iliyo beba watu wengi si chini ya mia mbili na hamsini, huku watoto na wamama wakiwa ni wengi ndani ya ndege, mbaya zaaidi kwa dakika chache kila kitu kitakuwa kimesambaratika hata miili yetu pia.

    "Kswahili pia nazungumza"

    Aliniambia huku akinitazama machoni kwa umakini. Nikamshika mkono hadi nje ya mlango wa kuingilia chooni.

    "Ninakuomba unisikilize kwa umakini, kuna bomu humu chooni, na limebakisha dakika kulipuka...."

    "Bomuu....Mungu wangu!"

    Dada huyu alishangaa huku akinitumbulia mimacho usoni, ilinibidi kumziba mdomo asizungumze kwa sauti kuashiria watu wengine kuanza shida, zitakazo pelekea sote kupotea kwa uzembe wetu.

    "Hakuna haja ya kushangaa"

    Nikamvuta na kumuingiza chooni, mikamuonyesha bomu lilipo, Sote tukajikuta tunashangaa kutokana bomu hilo limebakisha sekunde hamsini na tisa, kabla halijalipuka na sote hapa hatujui jinsi ya kulitegua, na muhudumu akaanza kulia, akijaribu kunikumbatia kwani mwisho wetu umefika



    "Una chochote cha kukatia"

    Nilizungumza huku nikimtoa muhudumu huyu, mwilini mwangu, kwani kukumbatiana kwetu sio suhulisho la bomu hili kuacha kuacha kulipuka. Hakunijibu zaidi ya kubabaika, kwa mawenge yaliyo mchanganya kupita maelezo. Akaanza kujipapasa huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga, akatoa, kikatia kucha(Nail cutter), akaitupa chini huku akiendelea kuikagua mifuko ya nguo zake alizo zivaa. Kwa haraka nikaokota kikatia kucha, nikapiga magoti chini, huku nikiwa ninajiamini kwa lile ninalo kwenda kulifanya.

    Sekunde za bomu hili, zikazidi kurudi nyuma, huku zikiwa zimebakia sekunde thelathini na mbili kabla halijalipuka. Nikaanza kuzichambua nyaya nyingi ndogondogo zipatazo ushirini, zikiwa na rangi tofauti tofauti.

    "Ishirini na tano"

    Muhudumu aliniambia, huku macho yake akiwa ameyatumbulia kwenye bomu, linalo zionyesha sekunde hizo, zinavyo rudi nyuma.

    "Mungu wangu"

    Nilizungumza huku nikizidi kuchanganyikiwa, kwani sikujua ni waya upi unanipasa kuukata, ili kulizuia bomu hili kuto kulipuka.

    "Kumi na tano"

    Nikashika nyaya moja nyekundu na kuikata, chakushangaza, bomu likaendelea kurudisha sekunde zake nyuma.

    "Nane"

    Nikazidi kuchanganyikiwa, na kukata wanya mweusi, hali ikawa ni ile ile.

    "Tano"

    Mikono yote, ikazidi kutetemeka hadi nikaangusha kikatia kucha, nikakiokota kwa haraka, hata kukaa mkononi vizuri, nkawa ninashindwa kukishika.

    "Tatu"

    Nikamuona muhudumu, akipiga ishara ya msalaba akiashiria mwisho wetu ndio unakaribia, nikashika waya wa rangi ya kijani, sekunde ikawa imebaki moja, nami nikawa nimeukata. Sekunde hiyo ikasimama hapo hapo na bomu kuzima. Nikashusha pumzi nyingi, huku mwili wangu wote ukiwa umesha vuja jasho lakutosha hadi shati nililo livaa, likawa limelowana kabisa. Kumtazama muhudumu nikamkuta akiwa ameyafumba macho yake huku jasho likimwagika shingoni nwake.

    "Tumefanikiwa"

    Nilizungumza kwa sauti ya unyonge huku nikimtazama usoni muhudumu, akayafumbua macho yake taratibu, huku akihema. Akalitazama bomu nililo lichomoa na kulishika, akabaki akiwa ameduwaa. Akanishika mkono taratibu na kuninyanyua, akanikumbatia huku akilia kwa furaha.

    "Asante Mungu, kweli wewe ni mwema. Hakuna kama wewe"

    Alizungumza huku akiendelea kulia, nakunifanya na mimi machozi kunimwagika kwani sikutarajia kama nitaweza kufanikiwa kulitegua bomu hili, taratibu akaniachia, huku akijifuta machozi usoni

    "Unaitwa nani?"

    "Eddy, Eddy Godwin"

    "Am Tasiana, from Arusha Tanzania"(Mimi ni Tasiana natokea Arusha Tanzania)

    "Mimi pia natokea Tanzania, ila A leve nilisoma Arusha"

    "Waooo, nashukuru kukufahamu"

    Tasiana akanikumbatia kwa mara ya pili, akawasiliana na marubani wa ndege hii, kupitia kijisimu kidogo wanacho kitumia kuwasiliana, wakamuomba tuelekee kwenye chumba walipo, tukiwa na bomu hilo, ila tuhakikishe hakuna abiria atakaye liona, ili kuto hatarisha amani ya walio wengi.

    Tasiana akachukua mfuko mtupu, mweusi. Akaliweka bomu, nikaongozana naye hadi chumba cha marubani. Tukawaelezea hali halisi juu ya tukio zima na jinsi mchungaji Frank, alivyo nipa vitisho nikiwa ninapishana naye kwenye mlango wa chooni.

    "Hakuna aliye toka ndani ya ndege, ngoja tukifika Afrika kusini, tutafanya upelelezi kabla watu hawaja ruhusiwa kushuka kwenye ndege"

    Rubani mmoja alizungumza huku akilitazama tazama bomu hilo nililo mpatia.

    "Ukimuona si utamkumbuka?"

    "Ndio, nilikuwa nimekaa naye ila simuoni kwenye siti yetu"

    "Ulikaa siti gani?"

    Nikamtajia rubani, huyo herufi ya siti niliyo kuwa nimekaa, akatazama mkanda mzima, kwenye kiji tv chao kidogo unao rekodiwa na kamera zilizo tegwa kila kona ya ndege. Tukamuona mzee huyo akiingia kwenye moja ya chumba walicho dai ni stoo, chenye gazi za kushukia chini, kunapo hifadhiwa mizigo mikubwa mikubwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ngoja nimfwate"

    Nilizungunza kwa kujiamini, huku nikiwatazama marubani hawa wapatao wanne, huku wawili wakiwa niwasaidizi.

    "Itaweza kumkamata?"

    "Nitahakiksha nalifanikisha hilo"

    Wakanitazama machoni, mkuu wao akanipa ruhusa.

    "Tuongozane"

    Tasiana aliomba tuongozane pamoja.

    "Wewe baki, ngoja nikajaribu kulifanya na hili kama nitafanikiwa"

    "Tafadhali twende pamoja"

    Tasiana aling'ang'ania kwenda, ikanibidi nimkubalie tu. Tukaongozana hadi kwenye chumba hicho, pasipo wasafiri wezangu kuelewa kitu gani kinacho endelea, hakikuwa chumba kikubwa sana, kwani kina ngazi zakushuka chini kulipo na mizigo mikubwa. Tukafanikiwa kushuka chini, kwa wingi wa mizigo iliyo fungwa kwenye mifurushi mikubwa, ilitufanya tubaki tukiwa tumesimana na kuduwaa.

    "Atakuwa wapi?"

    Tasiana aliniuliza kwa sauti ya chini, huku tukiendea kupepesa pepesa macho yetu kila kona ya eneo hili lilolo kubwa.

    "Nifwate nyuma na kuwa mkimya"

    Tukaanza kupita kwenye vinjia, vilivyo tenganishwa kwa maburungutu makubwa ya mizigo. Nikaanza kupata wasiwasi, baada ya kukuta shati alilo kua amelivaa mzee yule, likiwa chini. Tasiana akataka kuliokota ila nikamzuia asifanye hivyo.

    "Kwa nini nisiliokote?"

    Nikatingisha kichwa nikimuashiria Tasiana asifanye chochote dhidi ya shati hilo.Tukalipita, hatua kumi mbele, tukakuta suruali aliyo kuwa ameivaa.

    Kwa kutumia mguu nikaisogeza kuitazama kama kuna kitu kimefunikwa, ila hatukuona kitu.



    Arufu ya moshi wa sigara, ukaanza kuingia kwenye pua zetu, ulitokea upande wa pili wa sehemu ilipo mizigo hiyo. Tukapiga hatua za tahadhari hadi sehemu inapo tokea harufu ya moshi huo wa sigara, tukakuta kipande cha sigara kikiwa chini, kikiendelea kuteketea taratibu.

    "Yumo humu humu"

    Tasiana aliniambia huku akitazama tazama kila kona ya hili eneo. Nkakikanyaga kipande cha sigara hadi kikazimika. Nikapiga hatua mbili mbele, nikastukia kitu lizito kikinipiga kifuani mwangu na kuniangusha chini, nikaamka kwa haraka kutazama ni nini kilicho nipiga.

    Mtu aliye valia nguo nyeusi tupu akawa amesimama mbele yangu, huku amevalia kinyago kilicho ificha sura yake, mkono wake wa kulia, ameshika chuma kifupi alicho toka kunipiga nacho muda mchache ulio pita.

    "Buuuuuuuupuuuuuuuuuu"

    Alizungumza maneno kama aliyo niambia mzee yule nilipo kuwa nikipishana naye mlangoni mwa chooni.

    "Rudi nyuma"

    Nilimuambia Tasiana, naye akafamya hivyo. Taratibu nikavikunja vidole vya mikono yangu, na kugeuka kuwa ngumi.

    "Hahaaaaaa"

    Mtu huyo alicheka, kwa dharau kubwa huku akiendelea kunitazama machoni mwangu. Nikarusha ngumi kadhaa, ila akazikwepa zote na kunitandika chuma cha mgongo kilocho nifanya nitoe ukelele mkali wa maumivu.

    Nikajipanga tena kufanya mashambulizi kwa mtu huyu, kila nilivyo zidi kupambana naye, ndivyo jinsi alivyo nizidi kwa mbinu za kupigana.

    Akakitupa chini chuma chake alicho kishika na kukunja ngumi, akiashiria tunapigana kwa mkono, sikukata tamaa ya kupamba naye, baadhi ya ngumi na mateke niloyo mpiga, kidogo yakanipa matumaini ya kuamini nitamudu. Ila naye hakuwa nyuma katika kurusha makonde mazito tena yaliyo shiba kwa ujazo mzuri tu wa ngumi, kwani akinipiga konde moja nilazima nilisikilizie kwa sekunde kadhaa.

    "Eddy utakufaa"

    Tasiana aliniambia huku akinitazama jinsi ninavyo vuja damu, zikitokea chini kidogo ya jicho la kushoto baada ya kupigwa ngumi nzito, niliyo jitahidi kuizuia kwa mikono yangu, ila ilipita hovyo hiyo na kunipasua sehemu hiyo.

    "Kama humuwezi tuondoke"

    Nikamtazama Tasiana jinsi anavyo zungumza kwa wasiwasi, nikatingisha kichwa kuashiria kwamba bado sijashindwa. Nikaitazama miguu ya mtu huyo jinsi inavyo irusha rusha kwa haraka akinifwata, nikatambua anatumia upiganaji wa kichina unao itwa 'kung fu' na mimi sikuwa na mfumo maalumu wa kupigana ndio maana nikajikuta nikipigwa kizembe, kiasi hichi.

    'Mtu anaye pigana kung fu, wewe tazama miguu yake na mikomo yake kabla hujafanya shambulizi lolote kwake'

    Niliyakumbuka maneno ya mzee Godwin, kipindi akinifundisha utotoni, hadi mtu huyu ananikaribia nikawa nimemtazama kwa umakini, anavyo kuja kwa kasi. Akarusha mateke kazaa, nikaweza kuyakwepa na kumpiga ngumi ya tumbo iliyo mrudisha nyuma na kumfanya ajipinde kiasi.

    Tukaanza kuyumbishwa, hii ni baada ya ndege kuanza kutua, kwa bahati mbaya Tasiana akateleza na kuangukia sehemu aliyopo mtu huyo. Akamkamata Tasiana na kukichomoa kisu chake na kumuwekea Tasiana shingoni.

    Katika kurupushanani za ndege kutua kwenye ardhi, Tasiana akafanikiwa kumtoa mtu huyo kinyago cha usoni mwake, sikuamini kumuona Mzee Godwin, kwani muda wote nilivyo kua nikipambana naye nilihisi kuwa ni yeye, hii nikutokana na mapigo aliyo kuwa akiyatumia kushambuliana na mimi, ila sikuwa na uhakika kama ni yeye. Nikiwa nimeduwaa kumtazama Mzee Godwin, aliye endelea kujitazama kwa macho makali, nikastukia kumuona Tasiana akianguka chini, huku amechomwa kisu cha tumboni.

    Mzee Godwin, akanifanyia ishara ya kunichinja kwenye shingo kisha akaondoka, na kumuacha Tasiana akiendele kuugulia kwa maumivu makli. Nikataka kumfwata mzee Godwin, ila Tasiana akaniita kwa kuhitaji msaada wangu, ili kuyaokoa maisha yake yaliyopo hatarini kupotea.

    "Eddy nisaidie ninakufaa, mimi"



    Nikakimbia hadi sehyemu alipo angukia Tasiana, kwa haraka nikamuweka vizuri huku kichwa chake akiwa amekilaza katika mkono wangu wa kulia, huku mkono wangu mwengine ukiwa na kazi ya kuzizuia damu zilizo kuwa zikimwagika kuto kuendelea kutoka katika jeraha lake alilo chomwa na kisu.



    “Eddy ninakufa mimi”

    “No huwezi kufa Tasiana”

    Niliendelea kumfariji Tasiasa, huku nikiwa ninaendelea kusubiria ndege kuweza kutua kwenye ardhi, kwani sehemu tuliyopo ilinilazimu kuweza kuegamia moja ya mzigo ili tusianguke. Kwa kutumia kijiisimu kidogo alicho kuwa anakitumia Tasiana, nikaweza kuomba msaada kutoka kwa wahudumu wengine. Hadi ndege inasimama kabisa ardhini, hali ya Tasiana kusema kweli haikuwa nzuri kiasi cha kumfany ayafuyafumbe macho yake, huku mapigo ya moyo yakimuenda taratibu sana.



    Tukasaidiana na wezake kumpa huduma ya kwanza. Nikiwa ninaendelea kutafakari ni nini cha kufanya huku nikizunguka zunguka sehemu tuliyopo. Nikauona mwili wa mtu, ukiwa umelala chini na umesukumizwa chini ya moja ya mzigo mkubwa huku miguu yake ikiwa imetokezea kwa nje.



    Nikamuita mmoja wa polisi kati ya polisi wanne walio ingia sehemu tulipo, kwa kusaidiana naye tukamvuta na kumtoa nje, sikuamini kumuona yule mchungaji akiwa ameuawa kikatili huku macho yake yakiwa yamepasuliwa na inavyo onekana ameminywa kwa vidole vigumu hadi yakapofuka.



    “Unamjua huyu?”

    Aliniuliza kwa lugha ya kingereza, nikamtazama machoni askari kisha nikatingisha kichwa kwa kumuashiria kwamba ninamfahamu mtu huyo. Akawaita wezake kuja kulishuhudia tukio hili la kinyama.

    “Inabidi twende kituoni kwa mahojiano zaidi”

    Askari mmoja alizungumza huku akinitazama machoni.

    “Sawa, ila kwa sharti moja tu”

    “Lipi?”

    “Nahitaji kubadilisha hizi nguo zimejazana damu kama ninyi munavyo niona”

    “Kwa hilo hakuna tatizo”



    Kilicho niokoa dhidi ya hawa askari kuto kunichukualia mimi kama muhalifu, ni kwa jinsi marubani walivyo waeleza juu ya tukio zima la kutegua bomu lililo kuwa limetegwa ndani ya ndege hii. Nikatafutiwa nguo nyingine, nikazibadilisha  na kutoka sehemu ya juu ambapo nikakuta baadhi ya abiria wakiwa wameketi kwenye siti wakisubiri safari iiendele, huku wengine wakiwa katika mlolongo wakishuka na kukaguliwa.



    Nikamuona Tasiana akiingiazwa kwenye gari la wagonjwa na kuondoka katika eneo la uwanja wa ndege, sikufahamu wanakwenda katika eneo gani. Nikashuka kwenye gazi za ndege huku nyuma yangu nikiwa nimeongozana na askari wawili. Baadhi ya waandishi wa habari walikatazwa kunipiga picha yoyote, huku mmoja wa askari akisikika akiyazungumza maneno haya mara kwa mara pale alipokuwa akisogezewa maiki za waandishi wa habari.



    “HUYU JINA LAKE NI EDDY NA WALA SI GAIDI”

    Maneno yake yakazidi kunipa matumaini ya kuamini kwamba kile kilichopo mbele ya maisha yangu hakita kuwa kigumu sana kwani sina hatia yoyote katika hilo. Tukaingia kwenye moja ya gari la polisi lenye rangi nyeusi, huku tukiwa na askari wawili wenye pikipiki kubwa nyeupe zenye kupiga king’ora, mmoja akiwa mbele na mwengine akiwa nyuma.

    “Mbona munanipeleka kwenye mahojiano huku kukiwa na askari wengie?”

    “Hii ni kwaajili ya usalama wako kwanza, ndani ya nchi hii, ugaidi umekidhiri sana, hususani kwa mtu ambaye anahitajika kutoa msaada wa kukamatisha mtu au kundi kubwa la watu wakiwemo matajiri na viongozi serikalini, bila ya kumfanyia ulinzi wa kutosha basi anaweza kuuawa”



    Askari alizungumza huku nikiendelea kutazama pikipiki ya askari inayo kuja nyuma yetu. Tukafanikiwa kufika kituo cha polisi salama salmin, nikapelekwa kwenye moja ya ofisi kwa ajili ya kukutana na mkuu wa kitengo hicho cha mahojiano

    “Hembu nielezee tukio zima jinsi lilivyo tokea kwenye ndege”

    Mzee wa makamo alimiuliza swali hilo, huku tukiwa tunatazama machoni. Nikamuelezea kila kitu kilivyo kuwa ndani ya ndege hadi maafa ya Tasiana kuchomwa kisu nikiwa pamoja naye.



    “Muuaji ulifanikiwa kuiona sura yake?”

    Nikafikiria kwa sekunde kadhaa, ikanilazimu kuktaaa kwamba sikumuona sura yake. Kutokana na kinyago alicho kuwa amekivaa usoni. Ila ukweli ni kwamba ninatambua kila kitu kuhusiana na Mzee Godwin na endapo nitawaeleza ninamtambua, nitalazimika kujibu maswali mengi ambayo yangenipotezea muda wangu mwingi. Baada ya kuridhika na mahojiano yangu, wakanipeleka, hospitali kupatiwa matibabu ya majeraha yangu kisha wakanipeleka hotelini kwa ajili ya kulala, hadi kesho nitakapo endelea na safari yangu ya kuelekea nchini Tanzania.



    Usiku kucha nikiwa ndani ya Hoteli sikuweza kupata usingizi hata kidogo, swali lililo niumiza akili yangu ni kwanini hadi leo mzee Godwin anachuki juu yangu.  Sababu ya mimi kuwa ni mtoto wa pacha mwenzake haikuwa kubwa sana yakunifanya niwe adui yake aliye tumia muda wake mwingi katika kunisaka kila kona ya dunia ila kuiangamiza nafsi yangu.



    “Kuna kitu kinacho endelea hapa, ambacho mimi sikifahamu, itabidi nifwatilie kwenye kumbukumbu za mama.”

    Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kulala kwenye kitanda, huku macho yangu yakitazama feni linalo zunguka taratibu juu ya chumba hichi.

    Asaubuhi na mapema nikawahi kuamka ili kuiwahi ndege niliyo kuwa nikisafiria kwenda nayo Tanzania, kwani ililazimika ndege hiyo kuzuiwa kwa muda ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika kabla haijaendelea na safari yake kuelekea mashariki mwa Afrika. Nikafika uwanja wa ndege nikiwa nimevalia kofia kuepuka watu wengi kunitazma tazama mimi, nikaingia kwenye kitengo cha usafirishaji ambapo nikakabidhiwa hati yangu ya kusafiria pamoja na mizigo yangu iliyo kuwa imehifadhiwa hapo.



    “Ndege itaondoka muda gani?”

    Nilimuuliza muhudumu wa ndege yetu, baada ya kukabidhiwa kila kilicho changu na mamlaka husika walio kuwa wamevishikilia vitu vyangu.

    “Saa tisa jioni, tunasubiria kupata ruhusa ya kuondoka hapa uwanja wa ndege, kutoka katika ofisi za Interpol”

    “Ahaa basi ngoja nikazunguke zunguke mjini mida ya saa saba nirudi”

    “Sawa”

    “Hivi yule mwenzenu, amepelekwa hospitali gani?”

    “St Hellen Hospital”

    “Sawa, nitamuomba dereva taksi anipeleke hapo”

    “Sawa”



    Nikaiacha mizigo yangu kwa muhudumu huyu wa ndege ambaye nilikuwa nikizungumza naye, nikatoka nje na kumuomba dereva  taksi kunifikisha katika hospitali hiyo niliyo mtajia jina. Nikafika hospitalini nikaelekea moja kwa moja sehemu ya mapokezi ambapo nikamuomba muhudumu kunipeleka kwenye chumba alicho lazwa Tasiana. Wakanipeleka na kunionyesha chumba chake, nikaingia na kumkuta akiwa amelala.



    Huku akiwa amezungukwa na mashine nyingi zinazo msaidia kupumua. Nikamtazama dada wa watu jinsi alivyo mzuri, nikajikuta mchozi yakinimwagika kwani pasipo mzee Godwin sidhani kama angelala kwenye kitanda hichi kwa wakati kama huu, tana akiwa hajitambui kabisa. Nikaivua saa ya dhahabu, niliyo pewa na Pretty na kuiweka pembeni mwa kichwa chake, kama zawaidia itakayo msaidia baada ya kupata nafuu kwani saa hii ni ya gharama sana.



    “Ninakuomba hii saa, akiamka muambie umepewa na Eddy”

    Nilimuambia nesi huyu ambaye amevalia mavazi ya watakatifu wa kike(masista), akaniahidi kuitunza hadi Tasiana atakapo pona na ataufikisha ujumbe wangu kama nilivyo muambia. Nikaondoka na kurudi uwanja wa ndege, nikaichukua mizigo yangu na kukaguliwa vizuri, kisha nikaruhusiwa kwenda ndani ya ndege. Baada ya masaa kadhaa, safari ikaanza kuelekea Kenya kisha inamalizikia Tanzania. Muda wote ndani ya ndege nikawa ninamuomba Mungu katika kunisiaidia ili kuweza kufika nchini Tanzania salama salimi.



    Hadi tunafika Kenya, hapakuwa na Tatizo lolote ndani ya ndege, tukakaa Kenya kwa masaa kadhaa, kisha safari ya Tanzania ikaanza, ambayo ikatuchukua masaa machache kuingia katika anga la Tanzania. Ndege ikatua kwenye uwanja wa Mwalimu J.K Nyerere, nikasali sala ya kumshukuru Mungu kwa kuweza kunifikish salama Tanzania. Hadi ninatoka nje ya uwanja moyo wangu ukawa umetawaliwa na furaha kubwa sana kwani ni muda wa mimi kuiona familia yangu japo Pretty aliniambia niipeleke mbali na Tanzania, familia yangu ila siwezi kuufanya ujinga kama huo.



    “Hapa ndipo ninapo nilipo zaliwa, siwezi kwenda sehemu yoyote”

    Nilizungumza huku nikitazama mandhari tofauti tofauti yaliyopo nje ya uwanja huu, nikamuita muhudumu kati ya wahudumu wanao zunguka zunguka ndani ya uwanja huu

    “Samahani ni wapi wanapo uza lini za simu?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ”Nyoosha kulia, utaona maduka ya simu ukifika hapo utajua ni mtandao gani unahitaji kuutumia”

    “Asante”

    Nikaenda nilipo elekezwa, nikawakuta wadada kadhaa wakiwa wanawahudumia watu wengine, na mimi nikajichochochomeka kati ya wateja, nikaelezea shida yangu, nikatenmgenezewa lini mpya ya simu kwa bahati nzuri wakaniambia nikiweka tu salio laini hiyo itaanza kufanya kazi.

    “Niwekee”

    Nikatoa noti ya dola mia na kumpa dada huyo, aliye nisajilia laini yangu.

    “Hapo utajua unaniwekea vocha ya kiasi gani”

    Akabaki amenitumbulia mimacho akinitazama machoni kwa mshangao, akaanza kuminya minya simu yake huku akinitazama usoni mwangu kana kwamba ananifananisha na mtu fulani ila anashindwa kuniambia ni mtu gani. Akaniingizia salio la laki moja, kabla sijaondoka akaniita



    “Samahani kaka”

    “Bila samahani”

    “Sijui nimekufananisha au laa”

    “Umenifananisha na nani?”

    “Mtoto wa waziri mkuu aliye zikwa miezi iliyo pita”

    “Sasa dada yangu kama mtu amezikwa atatembeaje?”

    “Hapana unaweza kuwa ni pacha wake”

    “Hapana, kwani huyo mtoto aliye zikwa, walisema ana pacha wake?”

    “Hapana”

    “Basi si mimi”

    “Ila naye anaitwa Eddy”

    “Majina tu yamefanana”

    Nikamuaga dada huyu na kuondoka zangu, nikatafuta sehemu iliyo tulia na kumpigia simu blanka

    “Dogo upo wapi?”

    “Home nani?”

    “Acha ujinga hujui sauti yangu”

    “Ohoooo kaka Eddy”

    Nilimsiki Blanka akizungumza kwa furaha kubwa.

    “Nisikikilize, njoo unichukue uwanja wa ndege ila usimuambia mtu kama nipo hapa”

    “Nakuja sasa hivi nipe dakika kumi nitakuwa hapo”

    “Powa”



    Nikakata simu, kutokana nimefika mida hii ya saa sita mchana, nina amini barabarani hakuna foleni nyingi zinazo weza kumfanya akachelewa sana. Nikatafuta sehemu na kukaa. Ndani ya robo saa nikamuona Blanka akishuka kwenye gari aina ya Haria, akaanza kutazama pande zote za sehemu wanapo tokea wageni, nikamfwata hadi sehemu nilipo. Akanikimbilia na kunikumbatia kwa furaha sana.

    “Eheee mbona usoni una plasta?”

    “Ahaaa nilipata kajitatizo kadogo”

    “Mmmmm pole”

    Blanka akizungumza huku akilichukua begi langu na kulibebe, tukaingia kwenye gari na kuianza safari.

    “Tunaelekea kwa mama au kwa kina Junio?”

    “Kwa kina Junio kwanza. Ila mama anaendeleaje?”

    “Mama kidogo ana kiunafuu”

    “Mungu ni mwema atapona”

    “Ni kweli”



    Tukafika katika jumba ambalo ndipo ilipo familia yangu, mlinzi akatufungulia geti, nikamuona Shamsa akicheza na Junio kwenye moja ya bustani yanye majani yaliyo katwa vizuri. Walipo liona gari la Blanka, Junio akakatisha mchezo na kuja kasi kwenye gari kumpokea shangazi yake. Junio alipo niona akageuza kumfwata Blanka na kuzunguka upande wa pili wa gari ambapo, akanirukia kwa furaha. Nikamkumbatia huku machozi yakinilenga lenga kwa furaha. Shamsa naye hakuhitaji kubaki nyuma, akanikumbatia kwa furaha kubwa.

    “Hamujambo?”

    “Hatujambo dady”

    “Mama yupo wapi?”

    “Anapika jikoni”

    Nikambebea Junio na kumshika mkono Shamsa, sote tukaingia ndani, Junio akaanza kumuita mama yake.

    “Nini bwana, umesha anza makelele yako Junio”

    Niliisikia sauti ya Phidaya ikitokea jikoni akionekana kumkemea Junio aliye kuwa akimuita muda wote.



    “Shiiiiiii”

    Niliwanyamazisha, nikaelekea jikoni ambapo nikamkuta Phidaya akiwa bize akikata kata nyama. Nikamnyatia kwa nyuma taratibu na kumziba macho yake. Akatulia kwa sekunde kadhaa huku akishika shika mikono yangu.

    “Eddy”

    Phidaya aliita kwa sauti ya upole, iliyo jaa furaha kwa mbali. Nikavitoa viganja vyangu machoni mwake, akanigeukia na kunitazama. Kwa furaha kubwa Phidaya akanikumbatia huku akiruka ruka kama mtoto. Bila hata salamu, akaniwahi mdomo wangu na kuanza kuninyonya mdomo wangu, alipo ridhika akaniachia, huku machozi ya furaha yakimwagika.



    “Baby”

    “Ndio mke wangu”

    “Nimekumicjeee”

    “Hata mimi mke wangu”

    Furaha ikarudi upya kwenye maisha yangu, nikamshukuru MUNGU kwa kuweza kunikutanisha tena na familia yangu, wakiwa katika hali nzuri ya furaha na afya nzuri. Tukapata chakula cha mchana, baada ya kumaliza sikuhitaji kupoteza muda, sote tukaelekea nyumbani kwa mama. Wahudumu wa mama wakaanza kunishangaa sana, ila sikuwalaumu kutokana wanatambua kwamba mimi nimefariki. Blanka akanitambulisha kwa daktari anaye muhudumia mama.



    “Hali ya mama inaendeleaje?”

    “Tumuombe Mungu atamponya, huku nami nikiendelea kuhakikisha ninayaokoa maisha yake kadri ya uwezo wangu”

    Dokta Angelina alizungumza huku akinitazama. Nikamuomba dokta Angelina kuingia chumbani kwa mama, akaniruhusu bili kipingamizi. Taratibu nikaufungua mlango wa chumba cha mama na kuingia ndani, nikamkuta mama akiwa amelala kitandani huku amekondeana sana. Sikuamini kama nitamkuta kwenye halii hii mbaya. Nikapiga hatua hadi kwenye kitanda chake, taratibu nikapiga magoti chini huku machozi yakinilenga lenga. Nikamshika mkono wake wa kulia, ulio chomekwa sindano ya dripu la maji, sura ya mama imebadilika sana huku imekunjamana kwa kukonda, mashavu yake yameingia ndani huku nywele zake zikiwa na rangi ya kahawia.



    “Mama”

    Niliita huku machozi yakianza kunimwagika taratibu, nikarudia tena kumuita ila hakuniitikia kabisa.

    “Mama, mwanao Eddy nipo hapa. Nakuomba ufumbue macho yako japo unione mama yangu. Sikufa mama nipo hai, nimerudi tena nyumbani……”

    Kidogo mwili wa mama ukatingishika, nikajikuta nikiwa nimemkazia macho nikimtazama machoni mwake, taratibu akayafumbua, akakigeuza kichwa chake upande wangu, akanitazama kwa muda huku akiwa amenishangaa



    “Mama ni mimi Eddy, mwanao wa pekee”

    Mama akaendelea kunitazama, baada ya muda akatabasamu akishiria kufurahi uwepo wangu. Nikamuunga mkono na mimi nikatabasamu huku nikitokwa na machozi ya furaha kidogo. Gafla mama akayafumba macho yake, mwili wake ukaanza kutetemeka, hali ikazidi kuwa mbaya baada ya kuanza kuirusha rusha miguu yake kwa nguvu hadi kitanda kikaanza kutingishika tingishika. Nikazidi kuchanganyikiwa zaidi  baadaya ya mapovu kuanza kumtoka mdomoni, na mwili wake ukizidi kukakamaa.

    “Doktaaaaa Doktaaaaa……………..!!!!”

    Niliita kwa sauti ya juu, ya kuchanganganyikiwa kwani hali ya mama, ilizidi kuwa mbaya kiasi kwamba nikaanza kuhisi kumpoteza duniani mama yangu kipenzi.



    Daktari akaingia haraka, ndani ya chumba tulichopo. Kwa haraka akaanza kumuhudumia mama huku akiniomba niweze kutoka nje nimuache aifanye kazi yake kiufasaha. Nikatoka nje huku machozi yakinimwagika. Phidaya akanifwata kwa haraka baada ya kuniona ninatokwa na machozi mfululizo

    “Baby kuna nini?”

    “Mama anakufa”

    Phidaya kwa haraka akaingia ndani ya chumba cha mama na kuufunga mlango, Shamsa akamchukua Junio na kumpeleka nje, kwani hakustahili kuendelea kushuhudia matukio yanayo endelelea kwa muda huu, ukitegemea kwamba umri wake bado ni mdogo sana. Blanka naye akaanza kutokwa na machozi, akanifwata na kunikumbatia

    “Ohhh Mungu saidia mama yetu apone, kwa nini inakuwa ni hivi jamani?”

    Blanka alizungumza huku akiwa ameendelea kunikumbatia, machozi yakimwagika. Tukaendelea kusubiri nje kwa muda mrefu pasipo Phidaya wala doka Angelina kutoka nje. Wasiwasi juu ya kifo cha mama ukazidi kunipanda, mara kadhaa nilihitaji kwenda kuufungua mlango ili kutazama hali ya mama ila Blanka alinizuia akiniomba niweze kuwapa muda walipo ndani kufanya wanacho kifanya kwa muda huu.

    Baada ya masaa kama manne Phidaya akawa wa kwanza kutoka ndani ya chumba huku jasho likimwagika usoni mwake.

    “Baby vipi?”

    Nilianza kumuuliza Phidaya mara tu alipo simama mbele yetu, akatutizama kwa sekunde kadhaa, mimi na Blanka kisha akashusha pumzi nyingi, iliyo nizidisha kuchanganyikiwa.

    “Tumejitahidi kadri ya uwezo wetu katika……katika kumuokoa mama, na…..naa….na….”

    Kigugumizi cha Phidaya kikaanza kunipa wasiwasi ulio nifanya na mimi, kijasho chembaba kuanza kunimwagika usoni mwangu.

    “Nini mbona huzungumzi?”

    “Hali ya mama, si nzuri sana ila bado anapumua kwa kutumia mashine”

    “Anasumbuliwa na nini?”

    “Mmmmm alipata mstuko ulio pelekea mapigo yake ya moyo kwenda kwa spidi kubwa iliyo mfanya awe katika hali kama ile ila kwa sasa amerudi katika hali yake ya kawaida”

    Niliona Phidaya akinichanganyia mada, mara aniambie hali yake ni mbaya mara aniambie hali yake imerudi kama kawaida. Nikataka kuingia chumbani ila Phidaya akanishika mkono.

    “Kwa sasa mama anabadilishwa nguo na Angelina”

    Nikamtazama Phidaya machoni, kwa kuhitaji kujua anacho kizungumza kina ukweli wowote ndani yake.

    “Blanka nenda kamuangalie mama”

    Nilimuagiza Blanka, taratibu akapiga hatua za kuelekea chumbani kwa mama, nikabaki na Phidaya tukiwa tumetazamana usoni. Baada ya muda Blanka akatoka akiwa ameongozana na dokta Angelina.

    “Vipi?”

    “Mama anaendelea vizuri kidogo”

    Blanka alizungumza, jambo lililo anza kunipa faraja kidogo moyoni mwangu. Ila Angelina akaniambia siwezi kumuona mama kwa wakati huu kutokana amepumzika.

    ***

    Hali ya mama ikaanza kurudi taratibu kadri ya siku zilivyo zidi kukatika, afya ya mwili wake ikaanza kujijenga taratibu baada ya matunzo mazuri anayo pewa na dokta Angelina pamoja na Phidaya. Kumbukumbu taratibu zikaanza kumrejea na kuwatambua watu baadhi jambo lililo zidi kutufurahisha katika familia yetu. Alipo kaa sawa nikamuelezea mama mpango wote alio kuwa ameupanga Sheila dhidi yake.

    “Kumbe yule mtoto alikuwa mshenzi kiasi kile eheeee?”

    “Ndio mama, hata yule Fredy wamemuua wao”

    “Aiseee, ila kama umesha waua hakuja haja tena ya kuwaadisia kwa maana, hicho ndicho walicho vuna kwa yale mauovu waliyo yafanya”

    “Ni kweli mama”

    “Pia nisamehe Eddy wangu, kwa kuto kukusikiliza na kumuona mke wako hana maana kwangu, nikidhani waarabu wote ni magaidi”

    “Hakuna haja mama ya kuniomba msamaha kwa maana mimi pia nimekukosea mengi”

    Nikamkumbatia mama, akiwa kitandani amelala, ikawa ni moja ya ukurasa mwengine tulio uanza kimaisha kama mama na mwanaye. Phidaya akamuanzishia mama mazoezi ya kujifunza kutembea asubuhi na mapema pamoja na jioni, kwani kutokana na kuparalaizi, aliweza kupoteza uwezo wa kutembea na kuzungumza vizuri.

    Ndni ya miezi nane mfululizo ya mazoezi pamoja na kupewa dawa za kuipa nguvu mifupa yake pamoja na mwili kwa ujumla, mama akaanza kujimudu kutembea mwenyewe kwa kutimia fimbo maalumu inayo msaidia pale anapokuwa amechoka sana. Furaha ikazidi kuongezeka katika familia yetu, huku mama akizidi kuipenda familia yangu, hadi ikafikia hatua akaanza kutulazimisha mimi na Phidaya tuweze kufunga ndoa mapema, itakavyo wezekana.

    “Mama tutafunga tu ndoa”

    Phidaya alizungumza huku akiwa amemshika mkono mama, akimfanyisha mazoezi ya jioni ya kutembea tembea kuzunguka nyumba.

    “Sawa, unajua mukikaa sana, pasipo kufunga ndoa mutapata uvizu wa kufunga ndoa”

    “Ila mama tulikuwa tunakusubiria wewe upone ili nimuoe mke wangu, mtarajiwa”

    “Ndio nimesha pona sasa, unaona ninaweza hata kutembea mwenyewe, ninakula mwenyewe”

    “Hahaaaaaa”

    Mimi na Phidaya tukacheka kwa jinsi mama alivyo kuwa akiruka ruka, akiashiria kwamba amepona kabisa

    “Mama angalia usije ukaanguka”

    “Siwezi kuanguka, hembu niachie uone leo situmii fimbo kutembea, nitatembea peke yangu”

    Phidaya akamuachia mama, na mimi nikaishika fimbo yake anayo itumia kuitembelea. Taratibu mama akaanza kupiga hatua za kutembea. Jambo lililo tushangaza sote, kwani kutoka kitandani hadi leo anaweza kutembea mwenyewe ni kwa msaada wa mwenyezi Mungu ndio umemfikisha hapa.

    “Munaona munaona naweza kutembea mwenyewe”

    Kadri tulivyo zidi kwenda mbele ndivyo jinsi mama alivyo zidi kuongeza mwendo wa kutembea kwa haraka, japo ule mwendo wake nilio kuwa nimeuzoea haujarudi bado.

    “Bibi……!!!.”

    Junio alimshangaa bibi yake, baada ya kukutana naye akitembea mwenye, kwani amesha zoea kumuona akitembea kwa msaada wa mtu pemben au fimbo yake ya kisasa, inayo tumia umeme wa kuchaji.

    “Twende twende”

    Mama alimuambia mjukuu wake, wakaendelea kuongozana, wakaanza kushindana kutembea kwa haraka. Mimi na Phidaya tukabaki tukiwa tunawatazama.

    “Asante Mungu wewe ni muweza wa kila jambo”

    Phidaya alizungumza huku akimtazama mama anavyo cheza na mjukuu wake. Hapa ndipo nilipo amini kwamba usimdharau mtu usiye mjua kwa maana hujui atakuja kukusaidia katika lipi, na endapo kama mama alivyo kuwa amemkataa Phidaya sidhani kama leo hali yake inge tengemaa na kutembea mwenye. Kwa ni watu wachache sana wanao paralaizi, na kurudi katika hali zao za kawaida.

    “Nikuoe lili mke wangu?”

    “Hata leo hii”

    “Kweli?”

    “Ndio”

    Nikamkumbatia Phidaya wangu, mwanamke aliye weza kunisaidia katika kipindi changu chote cha maisha yangu, hadi nimefikia hatua ya kubahatika kupata mtoto aliye zidi kuongeza furaha kwenye mioyo yetu. Tukaanza kupanga mipango ya harusi, ambayo hatukuhitaji watu wengi wahudhurie, kwani tunaifungia katika viwanja vya hapa nyumbani kwa mama na si kanisani kama wapendavyo watu wengi sana katika nchi hii ya Tanzania.

    “Kabla hamujaingia kwenye ndoa, mimi ninaombi moja tu”

    Mama alizungumza mara baada ya kumaliza kikao cha mwisho cha harusi, yetu kilicho hudhuriwa na marafiki wa chache wa mama wengi wao wakiwa ni wafanya kazi wa serikalini.

    “Ombi gani mama?”

    “Nahitaji, Junio aishi kwangu”

    “Sawa mama hilo halina tatizo na wenyewe mumesha zoeana”

    Phidaya alizungumza kwa furaha huku akimtazama maama usoni,

    “Baba mtu mbona hazungumzi?”

    “Mama mimi kwenye hillo sina tabu, tutamtafuta mdogo wake Junio”

    “Huyo ndio atakuwa wa kwenu, ila huyu ni wakwangu nataka amrithi baba yako”

    Sote tuajikuta tukicheka kwani mama, tangu apone amekuwa muongeaji sana, Junio mwenye tulipo mfikishia habari za kuhamia nyumbani kwa bibi yake moja kwa moja alifurahi sana, kwani ni mara kadhaa alikuwa akikaa kwa bibi yake hata wiki mbili bila hata ya kurudi kwetu.

    “Kwahiyo dady mimi nitakua siji huku?”

    “Utakuwa unakuja kusalimia, pia sisi tutakuwa tunakuja huko”

    “Ila ukienda kwa bibi yako, uli mtindo wako wa kuchungulia chungulia madirishani ukiwa gorofani siku utaanguka hilo bichwa lako livunjike”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “P usimuombee mtoto hivyo”

    “Huju mtoto wako asikii, mkorofi kama nini, na ukichukulia bibi yake atakavyo kuwa anamdekeza basi atazidi kuwa mkorofi”

    Phidaya alizungumza huku akimtazama Junio aliye jikausha baada ya kuambiwa hivyo na mama yake katika hali ya ukali, sikutaka nimtetee sana Junio kwani mama naye anapaswa kuchukua nafasi yake kama mama, ikanilazimu kubadilisha mada.

    “Shamsa mwanangu wewe je unahitaji nini?”

    “Mimi nahitaji kusomea udaktari kama mama hapa”

    “Ahaaa sasa inabidi tutafue vyuo vya udaktari, ambavyo vinatoa elimu bora”

    “Unataka nje ya nchi au humu ndani ya nchi?” Phidaya alimuuliza

    “Nje ndio kwenye elimu bora”

    “Sawa tafuta tafuta chuo ambacho, wale watu wako hawata weza kukudhuru, wala kukufikia kiurahisi”

    “Sawa baba”

    Shamsa akaaga na kwenda chumbani kwake, naye Junio akaaga na kwenda chumbani kwake, tukabaki mimi na mke wangu mtaraijiwa Phidaya. Nikamnyanyuka kwenye kiti nilicho kikalia na kumbeba mke wangu na kwenda naye chumbani.

    “Leo mbona umenibeba muwe wangu?”

    “Ninachukua mazoezi ya siku ya harusi yetu, kwa maana kwa sasa umenenepa”

    “Mmmmm ndio unibebe jamani?”

    “Ndio mke wangu”

    Phidaya akanivuta kitandani na kuanza kunipa haki ya tendo la ndoa, linalo stahili sisi kuweza kulipata kama mmoja ya furaha katika mahusiano yetu.

    ***

    Siku ya harusi ikawadia, watu si chini ya thelathini wakawa wamehudhuria kwenye harusi yetu tuliyo ifanya nyumbani kwa mama yetu, hatukuhitaji kwenda kanisani kuepuka maswala ya kigaidi kama yaliyo tokea kwenye harusi ya kwanza ya Fredy na Sheila. Hatua zote za ndoa, zikaendeshwa na mchungaji kama vile anavyo ziongoza akiwa kanisani

    ”NDIO NIMEKUBALI NA MUNGU ANISAIDIE”

    Phidaya alijibu swali la mchungaji alilo ulizwa kama yupo tayari kuishi na mimi milele hadi pale kifo kitakapo tutenganisha. Taratibu nikamvisha pete mbele ya mashahidi walio kuja kushuhudia tukio hili, akiwemo raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Muheshimiwa Praygod Makuya.

    “EDDY GODWIN Je upo tayari kuishi na PHIDAYA EDDY, kuwa mke wako kwenye shida na raha tabu na shinda, hadi pale kifo kitakapo watenganisha?”

    Ilibidi Phidaya achukue jina langu la Eddy kwani, jina la baba yake lilikuwa la kiarabu, na siku zote hakulipenda jina la baba yake kutokana na matatizo yao ya kifamilia.

    “NDIO NIMEKUBALI NA MUNGU ANISAIDIE”

    Phidaya akanivisha pete, huku machozi ya furaha yakimwagika. Nikataka kumbusu ila mchungaji akatuzuia kwa kutumia ishara ya mkono

    “BASI NINAWATANGAZA YA KWAMBA EDDY NA PHIDAYA, MUMEKUWA MWILI MMOJA. SASA BWANA EDDY UNARUHUSIWA KUMBUSU MKE WAKO”

    Baadhi ya waalikwa wakacheka kwa tukio hilo, kwani nilimvuta kwa haraka Phidaya na kumbeba na kuanza kumnyonya mdomo huku sote tukiwa tumefumba macho yetu na kuwaacha mapaparazi kupiga picha kwa tukio hilo.

    Nikamuachia Phidaya, akawapa mgongo waalikwa na kulishika vizuri uwa lake, alilo kuwa amelishika tangu anafika kwenye hii bustani ya maua tunapo fanyia shuhuli hii. Akalirusha na Blanka akafanikiwa kulidaka, ikiashiria kwamba katika familia hii, Blanka atafwatia kuolewa.

    Sherehe ikaendelea kufanyika huku kila mtu akitupa pongezi ya kufunga ndoa, muheshimiwa raisi akatufwata sehemu tulipo mimi na Phidaya.

    “Hongera sana vijana”

    “Asante muheshimiwa”

    “Kuna kitu nahitaji nikupe kama zawadi”

    “Kitu gani muheshimiwa?”

    “Nahitaji kukupa nafasi ya uwaziri wa ulinzi je utaimudu hiyo kazi?”

    Tukatazamana na Phidaya, ambaye akanikonyeza kwamba niweze kukubaliana na ombi hilo la muheshimiwa Raisi.

    “Ndio muheshimiwa”

    “Basi ukimaliza mapumziko ya harusi uje ofisini kwangu nikupe majukumu hayo rasmi, kabla sijatengua baraza la mawaziri kutokana mama yako ameomba kustafu katika kuitumikia serikalini na yeye alikuwa ni waziri mkuu”

    “Sawa muheshimiwa raisi, nimekuelewa asante sana”

    Raisi akatupa mikono kisha akatuacha tukiendelea na kusheherekea,

    “DADY, MOM NINAWAPENDA SANA”

    Junio alizungumza huku akiwa amesimama mbele yetu, taratibu Phidaya akachuchumaa na kumkumbatia mtoto wetu, nami nikachuchumaa na kuwakumbatia wote kwa pamoja.

    “Tunakupenda pia mtoto wetu”

    “Ila dady, mimi nataka kuanza shule”

    “Ohhhh basi mwaka ujao utaanza kusoma sawa mwanagu”

    “Ndio baba”

    Phidaya akampiga busu Junio upande wa kushoto, kisha nami nikampiga Junio shavu upande wa kulia, mpiga picha akatuomba tunate hivyo hivyo kwenye pozi letu, tukapiga picha ya tukio hilo.

    “Yeaaaahh”

    Tukapiga picha nyingi tukliwa na mtoto wetu kama kumbukumbu ya maisha ya baadaya. Usiku wa siku hiyo hatukutaka makuu sana, ya kwenda kusheherekea nje ya nchi, tukepelekwa katika hoteli ya Serena, ambapo ilitupasa kukaa hapo wiki mbili, kwa ajili ya kuanza ukurasa mpya wa maisha kama mume na mke.

    “EDDY UNATAKA NINI NIKUFANYIE MUME WANGU”

    Phidaya alimiuliza swali, tukiwa kitandani, mara baada ya kumaliza kuoga na kujitupia kitandani.

    “Nahitaji unipatie mtoto mwingine”

    “Kweli”

    “Ndio mke wangu”

    “Basi njoo tumtengeneze, mwengine kwani leo nipo katika siku hatari”

    “Kweli?”

    “Ndio baba Junio”

    Phidaya akajigeuza na kunikalia mapajani mwangu na kunitazama kwa macho malegevu, mkono wake mmoja akaupeleka kwenye swichi, iliyopo pembeni ya kitanda na kuzima taa, giza likatawala ndani ya chumba chetu na shuhuli ya kumtafuta mtoto mwengine ikaanza taratibu, huku kila mmoja akifurahia utengenezaji wa mtoto wetu huyu mpya, ambaye jina lake hatukulijua ataitwa nani.

    MWISHOOOOO…

0 comments:

Post a Comment

Blog