Search This Blog

Thursday, 19 May 2022

MY MOMY’S FRIEND - 5

 





    Chombezo : My Momy's Friend

    Sehemu Ya Tano (5)



    Nikamaliza na taratibu pua zangu zikaanza kukutana na manukato mazuri na sikujua ni kitu gani kilichopo ndani ya boksi.Nikalifungua na kukuta kipande cha boksi kilicho tengenezwa kama mfuniko na nikakisika kwenye kishikizo kilicho licho tengenezwa kwenye kipande hichi na kujikuta nikipata mstuko mkali huku mwili mzima ukitetemeka kwa woga na kuhisi ninacho kiona ni kama filamu ya kuigiza hii ni baada ya kuviona vichwa viwili vilivyo jaa damu huku kimoja kikiwa ni cha mke wangu Juliana na kingine kikiwa ni cha Pretty shemeji yangu na pembeni nikakuta kikaratasi chenye ujumbe unasomeka

    {HUU NI MWAZO TU WA VITA YETU NA WEWE}

    Nikahisi nguvu za mwili zikianza kuniishia nikajaribu kutazama tena kwenye boksi ili kuhakikisha ninacho kiona ni kweli au ninaota,ila hakuna kilicho badilika zaidi ya kuviona vichwa viwili cha mke na shemeji yangu.Gafla taa za jumba langu zikazima na nikastukia kuona vioo vya dirsha la sebleni likivunjika na gafla moshi mwingi ukaanza kutawala ndani kwangu na nikagundua ni bomu la machozi na kwa haraka nikapandisha gorofani nikaanza kusikia milio ya bunduki ikiteketeza mali zangu za dhamani zilizopo sebleni kwangu.Nikaingia chumbani kwangu huku nikiwa na wasiwasi mwingu kwani sikujua maadui zangu ni kina nani na wana lengo gani kwangu.Nikaacha kujiuliza maswali ambayo fika sikujua kama ninaweza kupata majibu yake kwa haraka nikaingia bafuni na kuchukua taulo nililo likuta bafuni na kulichovya kwenye maji kisha nikaliweka vizuri na kujivunga maeneo ya kuanzia puani hadi mdomoni

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikafungua droo yangu ya kitanda na kutoa bastola yangu kisha taratibu nikaanza kupiga hatua za kwenda nje huku nikiwa makini sana.Nikawashuhudia madui wawili wakifungua chumba alichokuwa akilala Ptetty huku sura zao wakiwa wamezifunika kwa vitambaa vyeusi huku mikononi mwao wakiwa na bunduki zenye uwezo mkubwa,Nikafyatua risasi kadhaa kwenye miili yao na kuwafanya waanguke chini na kupoteza maisha.Nikatembea kwa tahadhari hadi kwenye miili yao nakuziokota bunduki zao na nikazivaa mgongoni kupitia mkanda wa ishikizo za bunduki hizo.

    Nikajibanza kwenye ukuta na kutazama chini na kuwaaona wengine wawili wakiendelea kutafuta kana wataniona kwenye vyumba vya chini,nikanyuta taratibu huku bastola yangu nikiwa nimeishika vizuri,Shambulizi lagu likwa ni la haraka kiasi kwamba maadui zangu wakaanza kuchanganyikiwa kwani hakua aliye tegemea kuwa ninaweza kufanya tukio kama hilo.Ndani ya dakika tano miili ya maadui zangu ikawa imelele chain huku jasho jingi likinimwagika.Nikaanza kuchunguza kila sehemu ya ndani ya nyumba yangu sikuona mtu yoyote,Kabla sijatoka nje kwenye boksi lenye vichwa vya familia yangu nikasikia mlio ukipigw kwa nguvu na kwa ujuzi wangu nikatambu kuwa ni bomo la kutega ndio lipo ndani ya biksi na mlio wake huu linaashiria limebakisha sekunde kadhaa kabla halijalipuka.Nikaanza kuchanganya miguu kwa haraka kuelekea nje na kabla hata sijafika mbali nikajikuta nikirushwa hewani na kuangukia kwenye moja ya bustani iliyupo kwenye eneo la jumba langu huku mgongoni shati langu likiwaka moto.

    Nikajigaragaza chini hadi moto ukazima na macho yangu yakaishuhudia nyumba yangu ikiteketea kwa moto mwingi,Machozi yakaanza kunimwagika kwa uchungu na hasira kubwa.Gari za polisi zikaanza kuja huku zikiwa zimeongozana na gari za zima moto,watu wa huduma ya kwanza wakanichukua na kuniingiza kwenye gari lao la wagonjwa na kuanza kunifanyi matibabu ya haraka kwa sehemu zote nilizo ungua kwa moto.Sikutaka kuzungumza na mtu yoyote na moyoni mwangu nikabeba kisasi kikubwa cha mtu aliye sababisha mauji ya mke wangu na hadi hapa nilipo sikuweza kumjua ni nani yupo nyuma ya tukio zima

    Jeshi la zima moto wakajitahidi kuzima moto kwenye jumba langu ambalo linateketea kwa moto mkali na wakafanikiwa ila sehemu kubwa ya jumba langu ikawa imeungua.Polisi wakanichukua hadi kituoni kwa kunifanyia mahojiano na nikawaelezea kila kitu kilicho tokea kwenye jumba langu ndipo wakanichukua kwenda katika hospitali ya Taifa kwenda kutazama miili ya wanawake wawili ambayo iliokotwa pembezoni mwa bahari ikiwa haina kichwa.Nikafika hospitalini na kuikuta kweli ni miili ya yake wangu na Prety huku ikiwa imejeruhiwa sana kwa kupigwa

    Uchungu na simanzi ikazidi kunitawala katika maisha yangu,nikawasiliana na Priscar na akanifwata kwenye hotel ambayo nipo kwa ajili ya kunifariji

    “Eddy wewe unavyo hisi ni nani yupo nyuma ya pazia katika hili tukio zima”

    “P hata mimi mwenyewe sitambui yaani hapa ninajionea mauza uza kabisa”

    “Pole sana Eddy.....”

    “Ila nilazima nijue ni nani ambaye amefanya hili tukio na nilazima nilipe kisasi katika hili”

    Nilizungumza kwa uchungu huku nikimtazama Priscar

    “Nitakusaidia Eddy kwa lolote litakalo tokea mbele yako”

    “Kweli?”

    “Ndio Eddy “

    ***

    Baada ya mazishi ya mke wangu na shemeji yangu niliyo yafanya pasipo familia yao kujua.Lengo nikiwa ni kuhakikisha ninampata muuaji wa mke wangu na kumuua kama alivyo mfanya mke wangu na shemeji yangu ndio nitakuwa huru kuwajulisha wazazi wa Juliana juu ya tukio hilo.Nikauza kila kitu ambacho ninamiliki kwa hapa Italia na gari yangu ya dhamani nikamkabizi Priscar. Moja kwa moja nikapanda ndege ya shirila la Qatar Airways inayoelekea nchini Pakistani.Mawazo mengi yakazidi kukiandama kichwa changu nikikosa jibu ni nani muhusika wa kifo cha mke wangu

    “Samahani,kaka”

    Dada mmoja alizungumza pembeni yangu,nikajikuta nikustuka kwani kuanzia macho,sura,pua,rangi ya mwili wake vinafanana na mke wangu Juliana ila kitu ambacho wanatofautia na vimo kwani huyu dada ni mrefu kidogo kuliko mke wangu ambaye alikuwa ni mfupi kidogo



    Nikaendelea kumtazama kuanzia chini hadi juu,kitu kilicho nishangaza zaidi ni kumuona akiwa amevaa gauni la harusi,nikachomoa ‘earphone’ nilizo kuwa nimezichomeka masikioni zikiniburusha na mziki laini nilio kuwa nimeufungulia kwa sauti ya chini sana kiasi kwamba hata mtu akinisemesha ninaweza kumsikia

    “Samahani,tunakuomba uweze kujumuika nasi kwenye harusi yetu”

    “Wapi?”

    Niliuliza swali,huku nikitazama siti za abiria wengine ila nikakuta wezangu wote hawapo kwenye siti zao na wala sikujua ni wapi walipi elekea.

    “Shemu ya pili,nyanyuka twende”

    Sikuwa na haja ya kubisha zaidi ya kujintanyua kwenye siti yangu,Tukaingia upande wa pili wa ndege na kukuta watu wengi wakiwa na glasi mikononi mwao zenye mvinyo.Kwa aibu nikasimama nyuma kwani watu wote ndani ya gari ndege walikuwa wakinitazama.Dada akapitiliza hadi sehemu alipo simama mume wake ambaye anaonekana ni rubani wa ndege hii.

    “Ulikuwa wapi mjukuu wangu?”

    Bibi mmoja wa kizungu aliniuliza na kunifanya nitabasamu

    “Nilikuwa ni melala bibi?”

    “Basi watu walikuja kukuita ila hukuamka tuakadhani hujisikii kuja,ila kutokana bibi harusi alihitaji watu wote kujumuika kwenye hii harusi yake,ndio maana akaamua kuja kukuita”

    Bibi alizungumza kwa sauti ya chini ya kuninong’oneza

    “Asante kwa taarifa”

    Mchungaji akanza kuendesha misa ya ndoa,kila hatua ambayo anaifanya inanikumbusha siku ya ndoa yangu nikiwa na Juliana kanisani.Taratibu uchungu na hasira vikaanza kuutawala moyo na mwili wangu

    “Unamuona huyu binti?”

    Bibi alizungumza na kunitoa kwenye dimbwi la maumivu huku akimyooshea bibi harusi kidole hadi akatutizama

    “Ndio”

    “Baba yake ndio mmiliki wa hili shirika”

    “Ahaaa”

    “Ndio,maana akaamua kuifunga ndoa yeka kwenye ndege yeye mwenyewe huyu binti nirubani”

    “Ahaa”

    “Ndio”

    Sikuwa na hata hamu ya kuzungumza na huyu bibi,kitendo cha kuvalishana pete maharusi kikawadia,nikajikuta nikimwagikwa na chozi la tarativu.Nikaiinamisha sura yangu chini watu wasinione,nikashindwa kabisa kuendelea kutazama tukio hilo.Nikinyanyua sura yangu na macho yangu yakakutana na bibi harusi.Nikatoka sehemu tulipo na kuelekea kwenye chooni.Nikajifungia mlango kwa ndani.Machozi yakazidi kuntawala,picha mbali mbali zikaanza kunijia kichwani kwangu,nikaanza kuona picha za mke wangu kwenye fikra zangu.Kicheko,tabasamua lake,jinsi anavyo lia

    Nikiwa ninaendelea kuitazama kwenye kioo,gafla ndege ikayumba kidogo na kunifanya nijibamize kwenye ukuta ika sekunde kadhaa ikakaa sawa,nikajipa matumaini itakuwa ni tatizo la marubani kwani karibia wengi wapo kwenye sherehe ya marubani wezao.Nikashushe pumzi,hata kabla sijamalizia kushusha pumzi nikaanza kusisikia milili ya bunduki.Kutokana na ujuzi nikajua milio ya bunduki hizi ni ‘Short gun’ bastola aina ya Browinging NSF na AK47

    Kengele ya hatari ikaanza kugonga kichwani kwangu.Nikazisikia kelele za vilio kutoka kwa abiria wezangu.Nikashika kitasa cha kuingilia chuooni na kuufungua mlango taratibu,nikachungulia nje na kuona watu walio valia nguo za jeshi na kujifunga vitambaa kichwani huku sura zao wakiwa wameziziba kwa vitambaa hivyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikaufunga mlango na kuanza kufikiria ni nini nifanye kwa maana kila sehemu wameizingira na watu wote wapo chini ya ulinzi wa askari hao ambao sikujua wameingiaje kwenye ndege.Nikatizama juu ya choo na kuna sehemu ta kufunguka.Kutokana choo sio kikubwa sana niliwaza kuiweka mikono yangu na miguu katika kuta za miguu na kuanza kupanda juu taratibu,nikafanikiwa kuufungua sehemu ya juu kwenye choo,Nikachungulia na kukua kuna uwazi mkubwa ambao ninaweza kuingia mimi kama mimi.Nikajivuta juu na kuingia na kuparudishia kama palivyo kuwa.Nikakaa kwa muda ila milio miwili ya risasi niliyo isikia ikanifanya nianze kutambaa taratibu sehemu ilipo tokea.

    Kwa bahati nzuri nikapata uwazi wa kuchungulia sehemu ambayo ndipo kulikuwa kunafanyikia sherehe.Nikamuona bwana harausi akiwa anafuja damu kifuani huku mke wake akiwa amemlalia kifuani akilia kwa uchungu.Jamaa mmoja alizungumza kwa lugha ya kiarabu ambayo ninaielewa vizuri

    “Wamarekani wote wanyooshe vidole juu”

    Walio ielewa lugha ya kiarabu nikawashuhudia wakinyoosha vidole juu,wakaamrishwa kusimama.Wakasimama watu kama sita na wote wakapigwa risasi pasipo na huruma na wote wakaangu chini.Nikazidi kuchanganyikiwa kwani watu hawa hawana huruma hata kidogo,Nikaanza kumuona mmoja wa watekaji wa ndege akianza kutazama juu sehemu niliyo jificha mimi.Wasiwasi ukazidi kunijaa baada ya kumuona akiichomoa bastola yake kiunoni na kuielekezea sehemu nilipo mimi.Kabla hajafyatua risasi mwenzake mmoja akamnong’oneza,wakazungumza kwa sekunde kadhaa kisha jamaa wakaondoka.Nikashusha pumzi nyingi kwani jamaa angeamua kufyatua risasi nisingekuwa hai tena duniani

    Nikatulia kwa muda nikifikiria kitu cha kufanya,nikarudi kinyuma nyuma hadi sehemu kilipo choo.Nikajigeuza taratibu pasipo kugonga sehemu yoyote ya pembeni kuepuka kusikika kama kuna mtu juu ya dari la ndege.Nikakisogeza kijimfuniko nilichokuwa nimekifungua wakati ninapanda juu.Kabla sijamaliza kukifungua nikastukia kumuona mmoja wa watekaji akiingia kwa kasi sana chooni,kwa haraka akaishusha suruali yake na kuanza kutoa haja kubwa kwa kasi sana,inavyo onekana tumbo lake linamuuma sana.Bunduki yake aina ya AK47 akaiweka pembeni huku kifungua kitambaa chake ili kukipa kichwa hewa na kuendelea kujikamua kutoa uchafu ulio tumboni mwake.Nikamalizia kukifungua kisha nikaanza kushuka tararibu nikiwa nimetanguliza kichwa na na mikono huku miguu yangu nikiwa nimeipanua na kuibananisha kwenye kona za tundu hili lilolotengenezwa kwa mfumo wa pembe nne.

    Nikamkaribia mtekaji pasipo yeye kujua,nikamgusa kwa kidole sikio la kushoto akajifuta akidhani kuwa ni mdudu ndiye aliye mtambali

    “Hi”

    Nilimstua na akaangalia juu na kunipa fursa ya mimi kukishika kichwa vizuri na bila ya huruma nikaivunja shingo yake kwa haraka,nikashu sehemu nilipo.Nikaufunga mlango kwa ndani.Nikaanza kazi ya kumvua jamaa ngoa alizo zivaa,nikavua nguo zangu na kuvaa za kwake.Nikajifunga kitambaa kama walivyo jifunga wao.Nikavaa gloves nilizo zikuta kwenye mfuko wa suruali yeka na uzuri ni kwamba zitanisaidia kuificha ngozi yangu ya mwili.Nikamvalisha nguo zangu kwa haraka na kumuweka nyuma ya mlango,nikafungulia maji ya choo na kukisafisha choo kisha nikafungua mlango na kutoka nje.Nikakutana na jamaa mwengine na akaniongelesha kiarabu uzuri nikwamba ninakifahamu vizuri

    “Choo chao kizuri?”

    Aliniuliza akidhani kwamba mimi ni mwenzake

    “Ndio”

    Nilimjibu kwa ufupi huku sauti yangu nikuwa nimeiweka katika lafudhi ya kiarabu

    “Mimi naogopa sana kutumia vyoo ndani ya ndege”

    “Kwa nini?”

    “Sipendi tuu,nimezoea kwetu Pakistan kila kitu kinakuwa safi”

    Nikaanza kupata wasiwasi kuwa hawa jamaa ni Al-kaida ambao nilikuwa nao kundi moja kipindi nikiwa nchini Pakistani.

    “Mwanangu tukimaliza kupiga hii dili mimi ninaoa”

    Alizidi kubwabwanya maneno,sikutaka kumdhuru mapema kwani ninahitaji habari nzima ya kwanini wao wapo humu ndani ya ndege na pia wameingiaje ingiaje

    “Kweli”

    “Walah naapa,nitaoa mwanamke mzuri kambi zima kule hakuan mwenye kumpata”

    “Mmmmm”

    “Hivi Abdul unalichukuliaje hili swala ya mkuu Bin Isack kututumia sisi kama mbwa wake,alafu mafanikio anayapata yeye?”

    Swali lake likanihakikishia kuwa hawa ni miongoni mwa wezangu wa Al-kaida na hii safari ni yakwenda kujiunga upya tena kwa ajili ya mafunzo zaidi ya kigaidi.

    “Kawaida”

    “Abdul wewe unasema kawaida kwasababu upo karibu sana na Bin Isack,sisi kinakajamba nani, tunakazi ya kutumwa.Kama tukifanikiwa kuitulisha tege hii salama basi yeye anachukua maasilimia yote sisi tutapata nini?” “Achana na hizo habari”

    Sauti yangu nikazidi kuiwea katika mfumo wa kiarabu na kumfanya mtekaji kuamini kua mimi ndio Abdul.Akili yangu ikiwa inatamani niendelee kukausha kutazama kitu ambacho kitatokea.Ila roho yangu bado inatamani kuwasaidia watu wanao uawa kwa kupigwa risasi pasipo kuwa na sababu yoyote.Nikawachunguza kwa umakini nafasi zao zote walizo jitega nikaona wapo katika mapozi ya kawaida si yakujiweka tayari kwa chochote kwa maana, tayari ndege wameiweka chini ya ulinzi mkali.Nikasimama huku bunduki yangu ikiwa mkononi

    “Abdul unakwenda wapi?”

    Jamaa aliniuliza pasipo kujua

    “Chumba cha marubani”

    “Huko mkuu hataki twenda, anataka tubaki huku huku”

    Kitu kingine ninacho jiuliza juu ya huyu jamaa, ina maana hajaniona kimo changu au Abdul anaye msema yeye anaendana kimo na mimi.Sikuwa na jinsi zaidi ya kubadilisha muelekeo wangu na kwenda sehemu walipo wekwa abiria chini ya ulinzi mkali.Nikawakuta watekaji wengine sita wakiwa makini sana na watu walio lala chini huku mikono yao wakiwa wameiweka kichwani

    “Nani ni mtoto wa tajiri wa hii ndege”

    Sauti kali ilisikia nyuma yangu na kunifanya nigeuke na macho yangu yakakutana na jamaa ambaye nilipigana naye siku tukiwa kambini Pakistani na yeye ndio kiongozi wa hili kundi,sura yake hakuifunika na kitambaa na kunifanya nimkumbuke vizuri kabisa.Macho yake yakawa na kazi ya kuwatazama watu walio lala chini, kuna jamaa mmoja akawa anamzuia mwanamke anaye fanana na mke wangu Juliana, asinyanyuke.Jamaa akamuona na kwa hasira jamaa akampiga risasi ya kichwa jamaa aliye kuwa akimzuia bibiharusi

    “Nyanyuka”

    Jamaa alimuamrisha bibi arusi kunyanyuka, huku kingereza chake kikiwa ni kibovu kilicho changanyikana na kiarabu.Akamchukua bibi harusi na kuondoka naye.Sikuwa na haja ya kubaki ndani ya hichi chumba.Nikaanza kumfwatilia kwa nyuma pasipo yeye kujua kama ninamfwatilia.Akaingia naye kwenye chumba cha marubani na kumpa simu

    “Zungumza na baba yako”

    Alizungumza huku bastola yake akiwa ameiweka kichwani mwa bibi harausi anayemwagikwa na machozi wakati wote, Hii ni baada ya kumpoteza mumewe aliye toka kufunga naye ndoa dakika chache zilizo pita

    “Baba, tumetekwaa” Alizungumza huku akilia

    “Usijali mwangu, nitatuma pesa utaokolewa mwanangu”

    Jamaa akampokonya simu bibi harusi na kuiweka sikioni mwake

    “Tunataka kiasi cha dola bilioni mbili za kimarekani, tumuachie mwanao”

    “Nitatuma”

    Mazungumzo ya simu yaliweza kusikika vizuri kutokana na simu hiyo kuiungani na vipaza sauti vilivyopo ndani ya ndege hii,Nikashusha pumzi na kuondoka katika eneo hili.Kabla sijafika mbali nikasikia nikiitwa nyuma yangu.Nikageuka na kukutana na jamaa aliye mchukua bibi harusi akinitazama kwa macho makali huku mkononi mwake akiwa ameishika bastola yake

    “Vua kitambaa chako”

    Moyo ukastuka na kujikuta nikiwa ninamtazama kwa umakini,Macho yangu yakatua kwenye mkono wake wa kulia ulio shika bastola yake na kukuta kidole chake kipo kwenye traiga na muda wowote anaweza akafyatua risasi katika mwili wangu.Mkono mmoja nikaupeleka kwenye kitamba nilicho jifunga kichwani mwangu na kuziba sura yangu na kuyaacha macho yangu tuu.Nikaanza kukivua kuanzia nyuma huku macho yangu yakiwa makini kuitazama bastola yake, kwa haraka nikakimalizia kukivua kitambaa na jamaa akabaki akiwa ameduwaa

    “Ni wewe nguruwe.......!!?”

    Jamaa hakuonekana kutegemea kama ipo siku atakuja kukutana tena na mimi, Kabla hajafanya kutu cha aina yoyote nikamrushia kitambaa cha usoni, hata kabla hajachukua maamuzi ya aina yoyote,akili yangu ikwa tayari imesha amuu kufanya shambulizi la kufyatua risasi kazaa,zilizotua kifuani mwa jamaa na kumuangusha chini. Nikajibanza kwenye siti ya ndege na kuanza kuchambuliana na watekaji wengi walipo maeneo mbali mbali ya ndege.Kazi yangu ikawa ni moja tuu.Kufyatua risasi kwa mlengwa ninaye kusudia kumpiga risasii.Shambulizi langu likaanza kuzaa matunda kila muda unavyo zidi kwenda,Nikatoka kwenye siti na kuaanza kunyata kuelekea sehemu walipo tekwa kwatu.Nitendo cha kufungua pazia nikakuta watu wote wakiwa wamesimamishwa huku miko ikiwa juu na sikuwaona ni wapi walipo majambazi



    Nikastukia risasi moja iliyo tua kwenye kifua changu,nikajiangusha chini kitu kilicho nisaidia ni jaketi la kuzuia risasi nililo livaa.Jamaa watatu wakajichomoza katikati ya watu na kuanza kupiga hatua za kunifwata sehemu nilipo anguka huku bunduki zao wakiwa wamezitanguliza mbele.Hatia chache kabla hawajanifikia nikaichomoa bastola kwa haraka na kuwafyatulia risasi zilizo waangusha chini,Wengine watutu walio salia wakajichomoza katikati ya watu,huku wakifyatua risasi hii ni baada ya kuona wezao wamekufa,Nikatambaa kwa haraka na kuingia kwenye moja ya uwazi mkubwa wa shiti ulio karibu yangu.Jamaa wakajitokeza huku wakinyata wasijue ni wapi nilipo.Nikajinyanua kwa haraka na kuwafyatulia risasi za vichwa kila mmoja na wote wakaanguka chini

    Nikahakikisha kila sehemu ipo salama kabla sijawaruhusu watu kukaa kwenye siti zao nikastukia kumuoa bibi harusi akitolewa chumba cha urubani na jamaa ambaye naye amevaa nguo za kirubani akiwa amempiga kabali bibi harusi na kumuwekea bastola kichwani

    “Weka silaha yako chini kabla sijakufumua kichwa chako”

    Taratibu nikaiweka bastola yangu chini huku nikimtazama jamaa kuanzia kichwani hadi miguuni,

    “Rudi nyuma”

    Jamaa alinimrisha na nikatii, hapa ndipo nikagundua kuwa kuna njama iliyo tendeka kati ya rubabi huyu pamoja na magaidi waliokuwa wameiteka ndege.Nikasimama pembeni ya maiti moja ya gaidi iliyo lala chini, kwa kutumia jicho la pembeni nikaichunguza maiti vizuri kuanzia juu hadi na kuiona bastola ikiwa imechomokwa maeneo ya kiuno cha maiti,

    “Wewe ni nani hadi, uzuie mipango yetu”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jamaa alizungumza huku akifoka, nikamtazama bibi harusi kwa umakini.Macho yangu yakaanza kumpa ishara bibi harusi ila hakuelewa ni kitu gani ambacho ninamuambia afanye, kwani nilimuashiria aweze kumpiga kisukusuku jamaa aliye mkaba ili niweze kufanya tukio ambali litaweza kuyapoteza maisha ya jamaa.Ikanibidi kutumia akili ya kuzaliwa tofauti na jinsi nilivyokuwa nikihitaji kwa bibi harusi kuweza kufanya kile ambacho ninahitaji mimi akifanye.Nikatabasamu huku nikimtazama jamaa na kumfanya ashangae shangae

    “Angalia nyuma yako”

    Nilizungumza kwa sauti kali na kumfanya jamaa kutazama nyuma, kwa haraka nikaichomoa bastola iliyopo kwenye mwili wa maiti ya gaidi na kufyatua risasi moja iliyotua kichwani mwa gaidi na akaanguka chini na kumfanya bibi harusi kuyafumba macho yake huku akitoa ukelele wa woga.Nikapiga hatua hadi alipo bibi harusi

    “Upo salama dada”

    Nilizungumza na kumfanya ayafumbue macho yake, nikampita huku bastola nikiwa nimeishika vizuri mkononi mwangu.Nikaingia chumba cha marubani na kukuta marubani wawili wakiwa wemepigwa risasi na ndege ikiwa inakwenda nyenyewe huku inatoa mlio wa hatari na kutokana sina utaalamu wa ndege nikabaki nikiwa nimeshangaa

    Akaingia bibi harusi kwenye chumba cha marubani,bila hata ya kunisemesha akaanza kumvuta rubani aliye kaa kwenye kiti cha kulia.Kutokana hana nguvu ikanilazimu kumsaidia kumchomoa rubani huyo na kumuweka pembeni kisha yeye akakaa kwenye kiti.

    “Mtoe huyo na wewe ukae”

    Alizungumza kwa sauti ya juu, nikafanya hivyo pasipo kuuliza kitu chochote,Nikakaa kwenye kiti cha pembeni, nikavaa earphone kama alivyo fanya bibi harusi.Akanza kuminya minya baadhi ya batani ambazo mimi wala sielewi matumizi yake yapo vipi

    “Funga mkanda”

    Sote tukafunga mikanda iliyopo kwenye situ huku ndege ikiendelea kutoa ukelele ambao unaashiria kuwa hali si shwari,

    “Jamani, ndugu abiria mulia baki kwenye hii ndege ninawaomba mukae kwenye siti zenu na kufunga mikanda ya siti”

    Bibi harusi alizungumza kwa kutumia kifaa kidogo cha kunasa sauti kilichopo pembeni yake.Taratibu ndege ikaanza kulala upande wangu wa kulia

    “Shika hicho kifaa hapo”

    Alinionyesha kitu chenye vishikizo viwili ambavyo jina lake vinaitwa ‘Control Wheel’ ambazo zipo pande zote mbili.Nikaanza kuirudisha upande wa kulia kwa kutumia nguvu niyingi sana hadi ndege ikakaa sawa.Ila ndege bado ikaendelea kuyumba sana na bado ikazidi kutoa kelele

    “Ohhh MUNGU wangu tusaidie”

    Ni maneno ambayo yalitoka mdomoni mwa bibi harusi na sikujua amefikiria nini hadi kuzungumza hivyo.

    “Unaitwa nani?”

    Bibi harudi aliniuliza jina langu

    “Eddy”

    “Mimi naitwa Jolin”

    Alizungumza huku akiendelea kuminya minya baadhi ya batani, gafla tukaanza kusikia mtikisiko mkubwa ulio toke kwenye ndege na kuifanya ndege ianze kwenda mrama,kelele kutoka nyuma walipo abiria walio salia ndani ya ndege zikasikika na hali ya wasiwasi ikazidi kuongezeka kati yetu.Joline akaanza kupiga ishara ya msalaba na kuyafumba macho yake.Kwa nguvu zangu tena nikaishika control wheel na kuanza kuminayana nayo nikijitahidi ndege kuweza kuirudisha katika hali yake ya kawaida

    Misuli yote ya mwili ikazidi kujitokeza huku nikijikaza kwa nguvu zangu zote kuweza kuiweka ndege sawa, jasho jingi likaendelea kunimwagika, juhudi zangu taratibu zikaanza kuzaa matunda kwani ndege ikaanza kurudi katika kukaa sawa

    “Nisaidie”

    Nilizungumza na kumfanya Jolin ambaye nahisi anahisi maisha yake yanakwenda naye akaishika control wheel yake na kuanza kutumia nguvu zake na kuendelea kujaribu kuiweka ndege sawa.Cha kumshukuru Mungu ndege ikakaa sawa.Hatukuweza kusikia mawasiliano yoyote kwenye earphone zetu tulizo zivaa masikioni mwetu,

    “Eddy tumepoteza mawasiliano”

    “Inakuwaje sasa?”

    “Hata mimi sijui”

    Kifaa kinacho itwa ‘Direction finder’ kikatuonyesha kuwa tunapo elekea ni kusini mashariki

    “Kwani tulikuwa tunaelekea wapi?”

    “Tulikuwa tunaelekea kaskazini”

    Kifaa kingine kinacho itwa Altitude Indicator, mashale wake ukaanza kurudi nyuma kwa kasi, gafla injini zote za ndege zikazima, kwani tuliweza kuligundua hilo kupitia kifaa kinachoitwa ‘Systems Information Display’

    “Mungu wangu”

    Jolin alizungumza huku macho yakiwa yamemtoka, jasho jingi likaanza kunimwagika na mapigo ya moyo kwa sasa yakawa hayana budi kwenda mbio.Kwa kasi ya ajabu ndege ikaanza kwenda chini, huku imetandulia mbele.Macho yetu yakaiona bahari iliyopo chini yetu

    “Mungu, baba ninatambua kuwa mimi ni mtenda makosa.Nikakuomba unisamehe dhambi zangu zote nilizo zifanya na kuzitenda.Amen”

    Niliomba kimoyo moyo, machozi yakaanza kunimwagika kwani ninatambua hali ambayo tunaiendea sasahivi ni kifo wala si kitu kingine.Jolin akawa na kazi ya kupiga kelele, zilizo ungana na abiria wengine wa nyuma, tukio la kuangua kwa ndege kipindi nikiwa nimekwenda kumuokoa mke wa raisi likaanza kunijia kichwani mwangu

    “Safari ile nilipona, hii je?”

    Nilijiuliza swali ambalo sikupata jibu lake.Sote tukaishuhudia jinsi ndege inavyoingia kwenye bahari na kwenda kina kirefu, hata vijitaa vidogo vilivyokuwa vikiwaka ndani ya ndege vikazima na kusababisha giza kubwa, mbaya zaidi ajali tumepata wakati wa usiku.Nikaufungua mkanda wa siti yangu, huku maji yakianza kuingia taratibu kwenye ndege.Nikamfungua Jolin mkanda wake

    “Unajua kuogelea?”

    Nilimuuliza kwa sauti kubwa kwani, kelele nyingi, za watu wanao omba msaada zilinifanya niweze kuuliza kwa sauti hii

    “Ndio”

    Kutokana ndege, katika uangukaji wake imetangulia mbele, ikatulazimu kuanza kutambaa kuelekea juu huku tukisaidiwa kwa kushika siti, tukafanikiwa kutoka katika chumba cha marubani.Upande wa abiria tukakuta ni taa mbili tuu ndizo zinawaka na mwanga wake wenyewe ni wakucheza cheza.Maji yakazidi kujaa, ndani ya ndege, hii nikutokana, kuna dirisha moja limepasuka na kusababisha maji kuingia kwa wingi.Kila mtu akawa na kazi ya kuliita jina la Mungu wake, ili aweze kufanya muujiza wowote ambao utusaidia kutuokoa kwenye ajali hii

    “Nisikilizeni jamani”

    Nilipaza sauti yangu kwa nguvu huku nikizungumza kwa lugha ya kingereza, baadhi ya watu wakanyamaza na kunisikiliza

    “Jamani, hii ni ajali.Hatuna budi kujiokoa kwa njia yoyote, basi hatuwezi kuendelea kukaa humu ndani na kufa na haya maji yanayo ingia humu ndani.Ni bora hata tukatoka na kwenda kufia nje ila si humu ndani”

    “Ninacho kipendekeza mimi, tusaidiane kuugungua mlango wa ndege, tujitahidi kutoka humu ndani”

    Watu wakaanza kulalamika, kila mtu akaanza kuzungumza lake, wengine wakaendelea na kuangua vilio kwa sauti ya juu huku wakiliita jina la MUNGU.Japo ninatambua jambo ninalo lifanya nilahatari sana ila sikuwa na jinsi

    “Vua gauni lako la harusi”

    Nilimuambia Jolin na akatii kwa haraka, nikausogelea mlango wa ndege, jamaa mmoja wa kizungu akanifwata sehemu nilipo na sote tukashika kitasa cha ndege kilicho kaa muundo wa duara na kuanza kukizungusha kwa kutumia nguvu zetu nyingi.Taratibu tukafanikiwa kukizungusha kitasa hadi kikafunguka.Maji mengi yakaanza kuingia kwa kasi ndani ya ndege, tukasubiria hadi yakaanza kujaa kwa kiasi fulani na kasi yake ikapungua,Huku tukiwa tumezibana pumzi zetu tukaanza kutoka kwenye ndege mmoja baada ya mwengine.

    Kila mmoja akawa na kazi ya kujiokoa kivyake akijaribu kupanda juu, ili kutokea usawa wa bahari.Nikazidi kujitahidi kuelekea juu yapo mwanga wa mbala mwezi ninauona kwa mbali ila nikazidi kujikaza kwa juhudi zangu zote.Taratibu nguvu na pumzi zikaanza kuniishia, walio shindwa walianza kunywa maji mengi na ikawa ndio safari ya mwisho ya maisha yao.Picha ya mke wangu ikaanza kunijia kichwani kwangu, picha ya kichwa chake kilivyokuwa ndani ya boksi ikazidi kunijia kichwani mwangu

    “Hapana, siwezi kufa bado ninakazi ya kufanya”

    Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kujikaza kupanda juu, kadri jinsi nilivyo zidi kupanda juu, kuutafuta usawa wa bahari nikazidi kupata mafanikio ya kuijioko, ndani ya dakika ishirini nilizo kaa ndani ya maji, nikafanikiwa kutokeza usawa wa bahari huku nikiwa ninahema sana, miili ya watu ambao walishindwa na safari nikaikuta ikiwa ipo juu ya maji ikiwa inaelea elea.Kwa kuchunguza kwangu sikuweza kuuona mwili wa Jolin, watu wachache wakaanza kuibuka ndani ya maji, nikajilegeza na kuufanya mwili wangu kuelea elea juu ya maji, nakaendelea kuvuta pumzi hadi nikaridhika na kuanza kazi ya kumtafuta ni wapi alipo Jolin.Wasiwasi ukaanza kunijaa kwani sikuweza kumuona Jolin

    “Jolin, Jolin”

    Nilianza kuitwa kwa sauti ya juu, sikupata matokeo yoyote ya kuisikia sauti ya Jolin, nikavuta pumzi nyingi na kuzama tena ndani ya maji,nikajaribu kuyaangaza macho yangu ndani ya maji ila sikufanikiwa kumuona yoyote akija kutoka chini.Nikajitokeza tena kwenye kina cha bahari

    “Eddy”

    Niliisikia sauti nyuma yangu, nikageuka na kumkuta Jolin akiwa amechoka sana, nikamsogela na kumkumbatia.

    “Upo salama?”

    “Ndio, Eddy”

    Hatukujua hata tupo kwenye bahari gani, kila mmoja akawa na kazi ya kuomba, watokee japo wasamaria wema waweze kutusaidia katika kujiokoa.Cha kumshukuru Mungu, hakuna baridi sana wala mawimbi ambayo yangeweza kutudhuru.Hadi kunapambazuka ndipo tukaanza kuziona boti nyingi zikija katika eneo tulilopo.Nikazivua nguo za magaidi na kubakiwa na nguo ya ndani.Nimefanya hivi ili kuepukana na usumbufu wa kuhusishwa kama gaidi waliotaka kuiteka ndege.Boti za waokoaji zikatuzinguka na kuanza kutupa msaada wa huduma ya kwanza

    ***

    Tukafikishwa kwenye moja ya hospitali kubwa ya jeshi, sikuweza kuijua jina lake kutokana na jina lake kuandikwa kwa lugha ambayo siitambui.Ikawa ni siku ya huzuni kwa wale ambao walipata habari juu ya ajali ya ndege, ambayo walikuwemo ndugu zao

    “Here is where?”( Hapa ni wapi?)

    Nilimuuliza daktari mmoja aliye valia suruali ya kijeshi

    “Here is Egyp”( Hapa ni Misri)

    “Thank you”( Asante)

    Kutokana, hali yangu haikuwa mbaya sana, nikaanza kutembela wezangu katika wodi nyingine ambapo wamelazwa, huku nikiwa nimevali manguo ya wagonjwa wanao lazwa kwenye hospitali hii.Kwa bahati nzuri nikakutana na Jolin akiwa wodi moja huku pembeni kukiwa na wanaume wanne walio valia suti nyeusi, mwanaume wa tano akiwa ni mzee kidogo wa makamo, akiwa amevalia suti nyeupe.Jolin alipo niona akaachia tabasamu pana usoni mwake hadi mzee aliyopo pembini yake akanitazama. Nikasimama, Jolin akainiita kwa ishara, nikapiga hatua hadi kitandani kwake

    “Father, this is the boy whom I tell you, that has helped me in fighting enemies, who wasted your flight”(Baba huyu, ndio kijana niliye kuambia kuwa amenisaidia katika kupambana na maadui walio iteka ndege)

    Mzee akanitazama, kuanzi juu hadi chini, akanipa mkono wa shukrani.Akaendelea kuuingisha mkono wangu, kisha akanikumbatia huku akinipiga piga mgongoni

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Congratulations teen”(Hongera sana kijana)

    “Thank you, dad”(Asante, sana baba)

    Nilijibu kwa unyenyekevu, na kusimama pembeni ya kitanda alicho lazwa Jolin.Jolin akamuomba baba yake atoke ili azungumze na mimi, Baba yake hakuwa na lakubisha zaidi ya kutoka akiongozana na walinzi wake

    “Your father is very rich eheee?”(Baba yako ni tajiri sana, eheee?)

    Nilimuuliza Jolin, huku nikikaa kwenye kitanda

    “Yes, he is one of the owners the airline, which we found it accidentally”(Ndio, yeye ni miongoni mwa wamiliki wa lile shirika la ndege, tuliyo pata nayo ajali)

    “Congratulation ahaaa”(Ahaaa, hongereni)

    Jolin akanitazama kwa muda machoni, huku akiminya minya vidole vyake vya mikoni

    “Eddy”

    Aliniita

    “Eheee”

    “Thank you for your support which is me, for I did not expect mint bytes will be saved me in the accident”(Asante sana kwa masaada wako ulio nipa, kwa maana sikutarajia kama nitaweza kuokoka kwenye ajali ile)

    Jolin alizungumza kwa sauti ya unyonge, huku kwa mbali machozi yakianza kumlenga lenga

    “Has lost very important person, I my life, my joy swept spot, canker has entered the life which I think will be able to recover as”(Nimempoteza mtu muhimu sana, kwenye maisha yangu, Furaha yangu imeingia doa, imeingia donda la maisha ambalo sizani kama linaweza kupona)

    Jolin alishindwa kuyazuia machozi yake kumwagika

    “Eddy I lost my husband, I just stayed with the ring, I enyoy married life, I enjoy living life to the man i love, Why me, eheeee”(Eddy, nimempoteza mume wangu, nimebaki na pete tuu, Sijafurahia maisha ya ndoa, sijafurahia maisha ya kuishi na mwanaume ninaye mpenda, Kwa nini mimi, eheee?)

    Ikanibidi, nimkumbatie Jolin na kuanza kumbembeleza, taratibu

    “Shiiii.......call courage, God will help you find someone who would granted for everything”(Shiiii...piga moyo konde, Mungu atakusaidia utapata mtu atakaye kujali kwa kila kitu)

    “Eddy, I think if it would be possible to find a man as, Samson”(Eddy, sizani kama inaweza kutokea kupata mwanaume kama, Samson)

    Ikawa ni kazi yangu ya ziada kuendelea kumbembeleza, Jolin hadi akanyamaza.Nikatumia muda wangu mwingi kumpigisha stori za kumchekesha ili arudi katika hali ya uchangamfu

    “Eddy is married?”(Eddy unamchumba?)

    Jolin aliniuliza swali lililonifanya nikae kimya, na kujikuta nikiwa mnyonge gafla, kila ninapo mtazama Jolin, ninaikumbuka twasira ya mke wangu Juliana

    “I told you the other day”(Nitakuambia siku nyingine)

    “Why not today?”(Kwa nini isiwe leo?)

    “ Aahaa’ll tell you just”(Aahaa nitakuambia tuu)

    “Why, Eddy you where you are?”(Kwani, Eddy wewe kwenu ni wapi?)

    “Tanzania”

    “True”(Kweli?)

    “Yes, you do?”(Ndio, wewe je?)

    “I us is England, where I live with dad”(Mimi kwetu ni Uingereza, kule ninaishi na baba)

    “Mothers do?”(Mama je?)

    “Mother is Brazilian, and dad were divorced since I was a five year old daughter”(Mama yupo Brazil, waliachana na baba tangu nikiwa binti wa miaka mitano)

    “Ahaaaa”

    Siku ya pili tukaruhusiwa kutoka hospitalini, kutokana na tukio ambalo nimelifanya ikamlazimu Jolin kuniomba kwenda naye Uingereza japo nikapaone anapoishi yeye na baba yake Mzee Marcus Thomas, Tukapanda ndege aina ya Jet ambayo inamilikiwa na mzee Marcus Thomas, ila muda wote nikiwa ndani ya ndege sala yangu kubwa ni kuto kupata ajali ya aina yoyote

    “Eddy, mbon upo kimya?” Jolin aliniuliza

    “Hapana”

    “Ila, kwa maana safari nzima upo kimya?”

    “Kuna vitu ninaviwaza”

    “Vitu gani?”

    “Nitakuambia, siku nikipata muda wa kutulia”

    “Kwa sasa?”

    “Tupo safarini, tumuombe MUNGU atusaidie katika safari yetu nzima”

    Kila ninavyo mtazama Jolin ndivyo kumbukumbu juu ya maisha yangu na mke wangu Julina inavyozidi kunitawala kichwani mwangu, nikajikuta machozi yakinilenga lenga, jambo ambalo nikajaribu kujizuia ili Jolin asigundue kitu cha aina yoyote

    “Eddy mbona machozi yanakumwagika?”

    “Ahaaa, nikiikumbuka ile ajali basi furaha inaniishia”

    “Ohh usizungumze hivyo, utanfanya niuzunike na mimi”

    "Sawa”

    Safari ikaendelea, na chakumshukuru MUNGU, tukafika Uingereza pasipo kupata tatizo lolote katika safari yetu.Ila kitu kikubwa ambacho kinaendelea kuutafuna ubongo wangu kwa kiasi kikubwa ni juu ya kumjua muuaji wa mke wangu Juliana, tena akiwa na ujauzito wa watoto wangu mapacha na shemeji yangu Prety.Tukafika katika jumba la Mzee Marcus Thomas, siku hii kwangu katika maisha yangu ni tofauti sana kutokana mapokezi niliyo yapata nitofauti sana na jinsi nilivyokuwa nikijifikiria kichwani mwangu.Asalimia ya watu wote waliomo kwenye hili jumba la Mzee Marcus Thomas wakatokea kunisalimia huku sura zao zikijawa na furaha iliyo kubwa sana.

    Kitu cha kwanza kufika katika jumba la Mzee Marcus Thomas, akanikabithi kwa wafanyakazi wake wanao shuhulika kwa maswala ya mitindo, wakaniweka sawa kuanzia nywele zangu ambazo zinasiku kathaa hazijapata kitana wala kupakwa mafuta, isitoshe uso wangu umetawaliwa na ndevu nyingi, kwani tangu afariki mke wangu sikuwa na muda hata wakujitazama usafi wa kichwa changu.

    Mzee Marcus Thomas akaandaa sherehe ndogo ya kumkaribisha mwanaye Jolin ambaye muda wote usoni mwake ametawaliwa na tabasamu lililozidi kuufanaya uzuri wake kuongezeka mara dufu.Muda wa sherehe ukawadia na tukaingia kwenye ukumbi mkubwa uliopo kwenye jumba la mzee Marcus Thomas, kitu amacho kimeanza kunishangaza ni kwamba sherehe inafanyika huku watu wakiwa wamesimama wima, na ukipendelea unaweza kupatiwa kinywaji kwenye glasi ambayo wahudumu wapo kwa kazi hiyo.

    “Eddy jisikie huru kama upo nyumbani, kwa maana wewe kwa sasa hivi ninakuhesabia kama mtu muhimu sana katika familia yangu, umefanya jambo la kihistoria ambalo kama usinge kuwepo ninaamini sasa hivi ningekuwa ninakovu kubwa sana katika maisha yangu, kwani Jolin ni mwanangu wa pekee na ninampenda sana kupita kitu chochote”

    Mzee Marcus Thomas alizungumza huku machozi yakimlenga lenga huku mkononi mwake akiwa ameshika glasi ya mvinyo, watu wakaanza kupiga makofi huku taa kubwa yenye mwanga mweupe ikinimulika mimi, mzee Marcus akaniomba niweze kupita mbele kwenye jukwaa dogo alilo simama, nikatii, mzee Marcus akaupitisha mkono wake mmoja begani, na kuanza kunipiga piga

    “Sikupata mtoto wa kiume katika maisha yangu, ila ninaimani sasa nimepata”

    Mzee Marcus alizungumza huku akinitazama usoni

    “Eddy kama huyo jali, unaweza kuwa mwanangu, kuanzi leo”

    Sikujua ni kwanini, huyu mzee ametokea kuniamini kiasi cha kuniomba kuwa mwanaye, laiti kama angetamua kuwa nimefanya matukio mengi ya kikatili wala asinge thubutu hata nikanyage nyumbani kwake, nikamtazama kwa muda kisha nikatingisha kichwa kuashiria kwamba nimemkubalia

    “Kweli”

    “Ndio nimekubali baba”

    Mzee Marcusa akanikumbatia kwa nguvu nyingi, kisha akamuita Jolin ambaya taratibu machozi ya furaha yalianza kumwagika, akatukumbatia sote kwa pamoja, kisha akawageukia watu waliopo ukumbini

    “Jamani, hawa ndio watoto wangu, warithi wa utajiri wangu, kwa sasa ninamiaka 75, siku yoyote ninaweza kuondoka duniani, nawapenda sana wanangu”

    Nikajikuta ninashindwa kuyazuia machozi yangu, na taratibu nikajikuta nikidondosha chozi,

    “Eddy, ninakuomba umlinde mdoo wako, natambua kwamba unamoyo wa kipekee sana”

    “Sawa, baba”

    Kila kinacho nitokea nikawa ninaona kama ni ndoto katika maisha yangu, muda wa sherehe ukaisha, kutokana na uchovu kila mmoja akaingia kwenye chumba chake.

    ***

    Maisha yakazidi kusonga mbele, huku uhusiano wa kifamilia kati yangu na Mzee Marcus pamoja na mwanae Jolin unazidi kuongezeka, ikafikia hadi hatua Mzee Marcus akaanza kunieleza siri zake za ndani ambazo anadai katika maisha yake hajawahi kumuadisia mtu wa aina yoyote zaidi yangu mimi

    “Ila Eddy kitu ninacho kwenda kukumbia ninakuoma usimuambie mtu wa aina yoyote, hata Jolin mwenyewe”

    Mzee Marcus alizungumza huku akikaa vizuri kwenye kiti kilichopo kwenye moja ya bustani zake kubwa

    “Sawa baba”

    “Katika kipindi cha nyuma, nilibahatika kupata mwanamke ambaye nilimpenda sana, kiasi kwamba nilitokea kumuamini kwa kila kitu.”

    “Yule mwanamke, niliamua kufunga naye ndoa ambayo kwa hapa Uingereza kwa kipindi kile ninaweza kusema ni miongoni mwa ndoa zilizokuwa zakitajiri, kwa maana nilitumia takribani Dola milioni ishirini”

    “Mmmm”

    Ilinibidi kuguna kwa maana kiwango anacho kitamka Mzee Marcus kwa Tanzania ni kiwango kikubwa sana cha pesa ambacho kusema ukweli ukikimiliki unakuwa miongoni mwa matajiri watakao leta fujo mjini

    “Yaaaa, sikuona hasara sana nikukwasababu nilimpenda sana yule binti, basi katika maisha yetu ya ndoa yaianza kuingia migogoro pela tu tulipo mpata huyu, Jolin”

    “Kwa nini?”

    “Ndio ninapokuja huko”

    Mzee Marcus akatazama pande zote za bustani alipo hakikisha hakuna mtu aliyopo karibu, akachukua glasi yenye juisi na akapiga fumba moja kisha akanitazama na kuendelea kuzungumza

    “Kadri jisni Jolin alivyokuwa akikua, nilianza kupata wasiwasi kwani sikuona dalili zozote za Jolin kufanana na mimi, basi kipindi Jolin anatimiza miaka minne nikaamua kwenda kumpima DNA pasipo mama yeke kujua”

    “Majibu yalivyo toka, nilitamani ardhi ipasuke na inimeze kwa maaana nilikuwa vipimo vikiwa ni tofauti sana kwani, ilionyesha Jolin kwamba sio mwanangu wa damu”

    Mzee Marcus alizungumza huku akinitazama machozi yakimlenga lenga

    “Basi nilipo muhoji mama Jolin juu ya ukweli kuhusiana na Jolina, akaniambia kwamba alimuiba Jolin hospitalini, na yeye kwa kipindi chote alikuwa na mimba bandia”

    “Kwa hiyo baba, kipindi hicho cha mama alivyo kuwa mjamzito wewe hukujua au ulikuwa hulali nae?”

    “Kitu ambacho nilikuwa ninakijutia sana kwenye maisha yangu ni kipindi mke wangu alipo kuwa mjamzito aliniambia kwamba anakwenda kujifungulia kwao na kwasheria za kimiza zao nilikuwa siruhusiwi kumuona mke wangu kipindi chote cha miezi tisa ya ujauzito, na kutokana nilikuwa ninamuamini sikuwa na tabu juu ya hilo, kikubwa nilikuwa ninafanya maandalizi ya kumpokea motto”

    “Mmmm, pole sana baba”

    “Nimesha poa mwanangu, hilo ndilo lililo pelekea kumuacha mke wangu, na kuanzi hapo sikuwamuona tena kwenye maisha yangu, na nilikuja kusikia kwamba amefariki kwa kasna kwani kitendo cha mimi kumuacha kilimuthiri sana kisaikolojia, akawa mlevi wa sigara na pombe kali.”

    “Jolin aliniambia kwamba mama yake yupo?”

    “Ndivyo anavyo jua ila ukweli ni kwamba mama yake ambaye ni mke wangu hadi sasa hivi yeye ni mfu”

    “Jolin hasumbui kumuona mama yake?”

    “Anasumbua, sana ila ninatumia mbinu zangu za kumliwaza hadi inafikia kipindi anamsahamu mama yake, na hadi sasa hivi unamuona amekuwa mtu mzima ila ndio hivyo hamtambui mama yeka wa mzazi”

    “Ulisha wahi kufwatilia juu ya mama yake, mzazi?”

    “Hapana na sikupata muda huo kabisa”

    “Kwa nini?”

    “Ninampenda sana Jolin japo sio damu yangu, ila kusema ukweli ninampenda sana.Ila lengo la mimi kukuambia haya yote ninahitaji kukupa kazi ya kumtafuta mama mzazi wa Jolin popote duniani na nipo tayari kugaramika kwa kila kitu ili mradi siku nimuone Jolin wangu akiwa na furaha, na jinsi unavyo muona kwa kipindi hichi yupo kwenye majonzi makubwa ya kumpoteza boyfriend wake”

    Sawa baba, nipo tayari kwa kazi hiyo ila kikubwa ninaomba kufahamu hospitali ambayo mke wako alijufungulia

    “Mmmmmm, hiyo hospitali ipo bara la America kusini, sasa nchi ndio hapo sikufahamu kwani mke wangu alinidanganya kwa kipindi chote cha ujauzito kwani kwao yeye ni bara hili la uingereza sasa yeye akaenda bara la America na hiyo nilikuja kujua baada ya sisi kugombana”

    Nikaanza kupata msukumo wa hisia, juu ya wazazi wa Juliana na kuhisi kwamba kutakuwa na ukweli unao endelea katika familia hiyo japo hadi sasa kuna muda wa takribani miezi miwili sijawasiliana nao, kwani sijaamua kuliweka bayana swala la mauaji ya Juliana na Pretty.



    Baada ya mazungumzo kuisha kati yangu na mzee Marcus kitu cha kwanza kukifanya baada ya kuingia chumbani kwangu, nichukua simu yangu ya mkononi na kutazama kama ina salio la kutosha na kukuta kiasi kikubwa cha kutosha kupiga simu kwenda nchi yoyote

    Nikaingiza namba za simu za nyumbani kwa nilipo iacha familia ya Juliana, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya simu kuanza kuita, kitu kikubwa ambacho ninajiuliza, endapo simu ikapokelewa nitazungumza kitu cha aina gani, ikaita hadi ikakata, nikarufdia tena kupiga simu ikaita na kukata.Nikarudia mara mbili mfululizo ila jibu likawa kama lilivyo

    “Watakuwa wametoka”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijipa moyo kwa maana simu ninayo ipiga ni simu ya mezani.Nikatoka chumbani kwangu na kumkuta Jolin akiwa amejilaza kwenye sofa huku amekumbatia picha mbili zilizowekwa kwenye frame, huku machozi yakitiririka kwenye uso wake.Nikakaa pembeni yake na kunyanyua na kichwa cheke nikakilaza kwenye mapaja yangu

    “Mbona unalia?”

    Jolin hakunujibu kitu chochote zaidi ya kunigeuzia picha alizo zikumbatia, hapo ndipo nilipo kutana na sura ya mama yake ambaye mzee Marcus aliniambia kwamba ni mke wake na picha ya pili ni picha ya mpenzi wake ambaye alipigwa risasi kwenye ndege siku ya harusi yao

    “Eddy nilimpenda sana mpendi wangu, lakini ndio hiyo tena, furaha yangu imebaki kwa mama yangu tuu”

    “Eddy, mama yangu aliniacha nikiwa mdogo sana, ila sijui ni kwanini baba anakataa nisionane na mama”

    Jolin alizungumza huku akimwagikwa na machozi

    “Jolin” Niliita kwa sauti ya chini

    “Mmmm”

    “Mama ni muhimu sana kwenye maisha, pia baba ni muhimu sana kwenye maisha.Wote wana uhiano sawa, ila kwangu mimi sikuweza kupata nafasi hiyo ya kuwa na baba na mama yangu alifariki na kuzikwa pasipo mimi kujua chochote”

    Jolin akanyanyuka taratibu na kukaa kitako na kunitazama kwa macho yaliyo jaa huruma

    “Nimepitia shida nyingi sana, taabu nyingi, ila yote hayo nikukosa upendo wa mama na muongozo wake, aliniacha kipindi nikiwa mdogo sana”

    Nilizungumza huku machozi yakianza kunitiririka

    “Eddy, tafadhali ninakuomba usilie”

    Jolin alizungumza huku akinitazama machoni mwangu, huku taratibu akinichezea shingo yangu, Jolin akaendelea kunitazama machoni mwangu na taratibu akayafumba macho yake kisha akaanza kuusogeza uso wake kwangu na kuzikutanisha lipsi zake na zangu.Tukashindwa kuzizuia hisia za mapenzi zilizopo kati yetu, Jolin akanyanyuka na kunishika mkono wangu na taratibu tukaanza kupandisha ngazi kuelekea juu ghorofani kilipo chumba chake.Kitu cha kwanza kuingia kwenye chumba chake ikawa ni kazi ya kunyonyana lipsi zetu huku kila mmoja akijitahidi kumsararua mwenzake nguo alizo zivaa,

    “Kumbuka kwamba wewe ni dada yangu?”

    “Ila si wa damu moja”

    Jolin alizungumza huku akizidi kunikumbatia, kimoyo moyo nikawa na faraha kubwa kwani tangu afariki mke wangu sikuwa na hamu hata ya kujiingiza kwenye mahusiano na mwanamke wa aina yoyote hadi nimalize kazi ya kuwatafuta wale wote walio sababisha mauaji ya mke wangu Juliana.Nikaanza kumburudisha Jolin hadi akaanza kuapia kuto kuniacha daima kwenye maisha na kuniomba niwe mume wake

    “Usijali nitakuwa mume wako”

    “Kweli Eddy?”

    “Ndio mpenzi wangu”

    Kila mtu alipo ridhika kwa burudani ya kitandani, tukaingia bafuni na kuanza kuoga

    “Kesho ninasafari ya kwenda Marekani” Nilimuambia Jolin huku nikiwa imemkumbatia maji ya bomba la mvua yakimwagika katikati yetu

    “Kufanya nini?”

    “Kuna swala ninalifwatilia”

    “Twende wote”

    “Hapana, ninakwenda mara moja kuna vitu ninavifwatilia kisha baada ya siku mbili nitakuwa nimerejea”

    “Kweli mume wangu”

    “Ndio”

    Jolin alianza kunibatiza jina la mume hata kabla ya harusi kupitishwa, Tukamaliza kuoga na kurudi chumbani

    ***

    Nikakamilisha mipango yote ya safari kueleka nchini Marekani, nipanda ndege majira ya saa sita usiku, na kutokana Marekani nimekuwa ni mzoefu sana, haikuwa ni ngumu kwa safari ninayo iendea.Safari nzima nikawa ninakazi moja tu ya kumuomba Mungu aweze kunifikisha salama, Safari ikatuchukua masaa takribani nane kufika katika bara la Amerika ya kaskazini, Cha kumshukuru Mungu ndege imetua salama, nikakodisha taksi hadi kwenye moja ya hoteli.

    Sikutaka kufikizia ilipo familia ya Juliana kuepuka kuulizwa maswali ya kwanini nimekaa kwa kipindi kirefu pasipo kuwasiliana nao.Kutokana nimefika mida ya asubuhi, nikajipumzisha hadi mida ya saa nane mchana na kuamka, nikaelekea kwenye maduka ya nguo, nikatafuta sweta kubwa lenye kofia, nikanunua na kulivaa.Nikaelekea kwenye stendi za treni za kwenda kwa kasi zinazo pita chini ya ardhi nikaingia na moja kwa moja ni kaelekea mji wa las Vegas, haikuchukua muda mwingi kufika kwenye mji huo, nikakodi taksi hadi kwenye nyumba yangu nilipo iacha familia ya Juliana

    Mapigo ya moyo yakaaza kunienda mbio baada ya kukuta gari nyingi za zima moto, pamoja na gari za polisi zikiwa zimesimama nje ya nyumba wanayo ishi familia ya Juliana, huku kikosi cha zima moto wakijitahidi kuuzima moto unao iteketeza nyumba yangu, kwa haraka nikashuka kwenye gari baada ya dereva kuisimamisha gari

    “Kaka pesa yangu”

    Dereva alizungumza kwa kingereza cha kihuni huku naye akishuka kwenye gari

    “Bei gani unanidai”

    “Dola mia”

    Nikatoa noti ya dola mia, japo natambua kiasi alicho niambia amenidhulumu ila sikutaka kufwatilia hilo, nikaanza kujipenyeza katikati ya watu nikitaka kwenda kushuhudia ni kitu gani kilicho tokea

    “Hei huruhusiwi kuingia huko”

    Asakari mmoja alinizuia baada ya kuniona nikielekea kuvuka kwenye utepe wao walio ufunga kuzuia watu wesikaribie kwenye tukio la ajali ya moto

    “Familia yangu”

    Nilizungumza huku nikiwa sijielewi, waokoaji, nikawaona wakitoka wakiwa wamebeba mwili wa mama mmoja, nikapiga hatua za haraka kwenda kumtazama, sikuamini kumkuta ni mama Juliana akiwa ameungua mwili wake vibaya sana kwa moto, machozi yakaanza kunimwagika, huku askari zaidi ya watatu wakiwa wananizuia nisimkaribie mgonjwa

    “Jamani yule ni mama yangu, tafadhali ninawoamba niongee naye japo kidogo”

    Hakuna askari ambaya aliendela kunisikiliza zaidi ya kujitahidi kuniondoa katika eneo la tukioa, watu wambao wananijua walijitahidi kunishika kunituliza kwani machozi mengi yanazidi kunitiririka, nikaishuhudia miili mingine ya wadogo zake Juliana, John na Jackson wakiwa wameteketa miili yao kwa moto, nikawashuhudia wakiingizwa kwenye mifuko mikubwa myeusi, ikiashiria kwamba tayari wameshakufa.N

    “Pole sana, Eddy”

    Mama mmoja alizungumza, nikamkumbuka mara moja kutokana alikuwa ni jirani yangu, akanishika mkono na kunipeleka ndani kwake, akili na mawazo yote yamevurugika kichwani kwangu

    “Eddy mwanangu, najua kwa sasa umechanganyikiwa.Nikakuomba upate kikombe cha kahawa kwanza”

    Mama Mac Mahon alizungumza huku akinikabidhi kikombe cha kahawa.Nikakipokea taratibu

    “Ni kitu gani kilicho tokea?”

    Nilimuuliza kwa sauti nzito iliyojaa mikwaruzo

    “Mimi nilisikia mlipuko mkubwa, kwa utaalamu wangu wa kijeshi ni bomu la kutega ndilo limsababisha haya yote”

    Mama Mac Mahon alizungumza huku akinitazama kwa macho yaliyo jaa huruma, nikasimama kutoka kwenye kiti nilicho kaa, nikaelekea kwenye kioo cha dirisha na kuona gari la wagonjwa likiondoka kwa kasi huku likiwa linaliza ving’ora vyake.

    “Mama…….!!”

    Nilizungumza na kutoka nje kwa haraka, huku nikiwa ninawasi wasi mwingi, Mama Mac Mahon akanifwata kwa nyuma na kuniomba niingie kwenye gari lake na kuanza kuifukuzia gari ya wagonjwa kwa nyuma

    “Eddy, jikaze mwanangu upate japo nguvu, tambua kwamba wewe ni mwanaume”

    “Ila mama inaniuma”

    “Ndio, ila acha kulia”

    Mama Mac Mahon alizungumza huku akinipatia kitambaa chake kwa ajili ya kujifuta machozi yanayo nimwagika.Tukafika hospitali na kumkuta mama Juliana akipokelewa na manesi kumuwahisha katika chumba maalumu cha wagonjwa wahututi.Nikambia kwa haraka hadi kilipo kitanda alicho pakizwa juu yake, kwa bahati nzuri akayafumbua macho yake na kuniona, akanipa mkono na kuwaomba manesi wasimamishe kitanda

    “Ed…dy mwa….naaaangu, aliye fanya haaya ni ra….is…..”

    Mama Juliana hakuweza kuendelea kuzungumza, akakaa kimya na kuwafanya manesi kumkimbiza katika chumba walicho kikusudia, na sisi tukabaki tukiwa tumesimama nje ya mlango wa kuingilia kwenye chumba alicho ingizwa.

    Kwa kupitia kwenye kioo cha mlango, nikawashuhudia madaktari wakijitahidi kuyaokoa maisha ya mama Juliana ila tayari walisha chelewa kwani mashine inayo hesabu mapigo ya moyo inaonyesha mstari mmoja mrefu wa kijani, ikiashiria mama Juliana ameshafariki.Nikajikuta nikitafumba macho yangu na kusimama pembeni ya mlango huku machozi yakianza kunimwagika upya, taratibu mama Mac Mahon akanifwata na kunikumbatia kwa huzuni kubwa, huku na yeye machozi yakimwagika

    ***

    Mipango ya mazishi, ya mama, John na Jackson ikaanza kupangwa na jeshi la polisi nchini Marekani, huku likiwa ni pigo jengine katika maisha yangu kwani nimepoteza watu wa karibu sana katika maisha yangu.Hadi wakati huu sikufahamu sehemu alipo baba Juliana,

    “Mama Mac Mahon mbona simuoni mzee?”

    Nilimuuliza mama Mac Mahon, tukiwa tumekaa kwenye vit vilivyo pangwa makaburini, tukiendelea kuyasikiliza mazungumzo ya padre

    “Aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa, wiki mbili za nyuma”

    Nikauzuia mstoko wangu, na moja kwa moja nikaanza kuhisi hali ya hatari inatawala kwenye maisha yangu.Nikaanza kujiuliza ni nini chanzo haswa hadi familia ya Juliana kuuawa kikatili kiasi hichi, eneo zima la makaburi limetawaliwa na ulinzi mkali wa askari wa vitengo tofauti, huku swala zima la mazishi likiwa limetawala vyombo vingi vya habari kwa mauaji ya kitatili

    Nikasimama kwenda kutoa heshima ya mwisho, nikiwa kama mwana familia wa pekee, wakafwatia watu wangu wa karibu ambao muda wote walikuwa wakiendelea kunifariji.Nikaishuhudia miili ya wapendwa wangu ikishushwa kwenye makaburi yao matatu, huku ikiwa ndani ya majeneza yaliyo tengenenezwa vizuri

    “Kulia haina haja, kikubwa ni kuutafuta ukweli basi”

    Nilizungumza taratibu huku nikiingalia miili jinsi inavyo anza kufukiwa, mazisha yakamalizika.Nikaondoka na mama Mac Mahon ambaye kwa muda wa siku sita nimekaa kwake tukisubiria kufanyikwa kwa mzishi ya wapendwa wangu

    “Mama kuna kitu ambacho kinaendelea kwenye hii familia”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndio hata mimi pia ninahisi hivyo, ila ngoja tusuburie ripoti ya CIA watasemeje”

    “Watachukua muda gani kuchunguza, mauji haya yote?”

    “Sijafahamu ila ninaimani watachukua muda mrefu kidogo, ili kujua nani ni wahisika wa haya mauaji”

    Tukamaliza mazungumzo na mama Mac Mahon, nikatoka nje na kwenda hadi ilipo nyumba yangu.Nikasimama kwa muda kuitazama jinsi ilivyo poteza uzuri wake, nikatoa simu mfukoni na kupiga baadhi ya picha na kurudi ndani

    “Mama Mac Mahon, leo ninaomba niende sehemu mara moja nikatulize akili”

    “Sawa Eddy, ila utahitaji usafiri?”

    “Yaa kama itawezekana”

    “Kuna gari yangu nilinunua juzi juzi ni mpya, nitakupa unde nayo huku uendapo”

    “Asante mama Mac Mahon”

    Mama Mac Mahon akaingia ndani kweke akatoka na funguo mkononi, akaniomba aknionyeshe hilo gari lake jipya, tukaingia kwenye ukumbi wake wa kuhifadhia magari, akafungua turubai moja alilo lifunikia gari kale

    “Hii ni gari yangu mpya Lamborhgin Hurcan LP 610-4, kuwa nayo muangalifu”

    “Sawa mama”

    Akanikabithi funguo, katika magari yane thamani kubwa duniani hili nimiongoni mwa magari haya.Nikaingia ndani ya gari na kuona hakuna kitu kigeni sana kwangu, nikaliwasha na kulitoa nje hadi barabarani kwa mwendo wa taratibu, nikashusha kioo na kumpungia mkono mama Mac Mahon na kuondoka kwa mwendo wa taratibu wa kumridhisha Mama Mac Mahon.Nikaelekea kwenye cassino moja ambalo huingia matajiri peke yao, nikaingia ndani ya Cassino na kutafuta sehemu yenye kigiza na kukaa.Nikaagiza mzinga wa pombe kali, huku nikitazama wasichana wanao cheza pasipo nguo wakiendelea kitoa burudani kwenye bomba ndefu zilizomo ndani yah ii Cassino



    Nikaanza kushusha mafumba ya pombe kali, ambayo kooni inapita kwa shida sana, ilinilazimu kufumba macho pale kila nilipo imeza.

    Pembeni yangu, nikamuona msichana akiwa amejilaza kwenye meza, huku pembeni alipo kilaza kichwa chake kukiwa na unga unga mwingi, ambao ni mamawa ya kulevya.Sikutaka kumfwatilia sana zaidi ya kuendelea kupiga mafumba ya mzinga ambao nimeuagiza.Kichwa kikaanza kukulea kwa pombe, msichana aliye jilazwa kwenue meza yake akasimama kwa unyonge, huku anayumba sana.Kwa bahati mbaya akaniangukia ikanilazimu kumdaka kabla hajafika chini

    “Samahani”

    Alizungumza kwa sauti ya ulevi, nikamsaidia kunyanyuka, akanitazama kwa muda machoni mwangu na kunikumbatia kwa furaha, ikanilazimu kumzuia kuendelea kunikumbatia

    “Niache wewe”

    “Ohhhh Eddy wangu”

    Nikastuka baada ya kumsikia akilitaja jina langu na akarudia tena kunikumbatia, kwa furaha

    “Eddy mimi ni Lilian”

    Alizungumza huku akinikumbatia kwa mara ya tatu, nikabaki nikiwa ninamshangaa kwa maana Lilian ninaye mjua mimi, amehukumiwa kifungo cha maisha kama gaidi aliye tafutwa kwa kipindi kirefu sana, pia hataa sura yake haionyeshi kwamba ni Lilian niliye mzoea

    “Mbona sura yako ipo hivyo”

    “Njoo”

    Akanishika mkono na kuniingizwa kwenye moja ya chumba, kilicho tulia, na kina sofa moja pamoja, kitanda na kioo kikubwa, kilichopo ukutani

    “Eddy, ni muda mrefu mimi na wewe hatukuonana”

    Alizungumza huku akijitazama kwenye kioo

    “Ndio ila sina uhakika kama wewe ni Lilian ambaye ninakutambua”

    “Ndio mimi, unakumbuka kwamba tulipata wote ajali ya ndege, tukiwa na mke wa raisi wa Pakistani?”

    Nikaanza kuamini kwamba huyu ndio Lilian kwa maana, tukio alilo nitajia ni miongoni mwa matukio ambayo sinto weza kuyasahau katika maisha yangu.

    “Ndio ninakumbuka?”

    “Kwanza ninakuomba unisamehe kwa yale yote ambayo nimekufanyia, pasipo ya mimi wala ndege ile siku isinge pata ajali, kwa kipindi chote nilikuwa ninatambua ya kwamba umefariki dunia”

    “Nimekusamehe”

    Lilian akaanza kuzichomoa kope za bandia alizo zibandika machoni mwake, hapo ndipo sura halisi ya Lilian ikaanza kunijia kichwani mwangu

    “Eddy mwenzako nilikamatwa, na kuhukumiwa kifungo cha maisha”

    “Sasa imekuwaje upo tena uraiani?”

    “Pesa ndio kila kitu, mama aliweza kunisimamia hadi nikatoka na kuwa huru, japo ilimgharimu kiasi kikubwa cha pesa”

    “Vipi, wale jamaa zako bado upo pamoja nao?”

    “Wale Al-khaida?”

    “Ndio?”

    “Hapana, tangu nifungwe nikaja kugundua kwamba wale ndio walisababisha mauji ya dada yangu kipenzi kipindi alivyokuwa anakuokoa wewe ulipokuwa mikononi mwa jeshi la marekani.Kuanzia kipindi hicho nikawachukia kupita maelezo”

    Lilian alizungumza kwa sauti ya unyonge mmo, huku taratibu akiwa akikaa kwenye kitanda

    “Kwa sasa unafanya kazi gani?”

    “Ninamiliki hili Cassino, mama yangu ameamua kunifungulia mtaji ili niweze kuachana na maswala ya kigaidi”

    “Vipi wewe unashuhulika na maswala gani?”

    “Sina. Ila kuna kazi iliyopo mbele yangu, japo ni ngumu ila nitafanikiwa ninaimani katika hilo”

    Nikaanza kumuadisia Lilian maisha yangu yote kuanzia siku nikiwa, nimeokolewa na baba Juliana, hadi siku ambayo nimeshuhudia familia ya Juliana ikiteketea kwa moto

    “Leo ndio nimetoka kuwazika wapendwa wangu”

    Lilian akabaki akiwa ananitazama kwa macho yanye alama ya kujiuliza na anaonekana kama anahisi anawaza kitu akilini mwake

    “Eddy hao watu walio fanya hivyo ninatambua, karibia wote”

    “Unauhakika na unayo yasema?”

    “Siwezi kukudanganya kwenye kitu kama hichi”

    Lilian alizungumza huku akinitazama kwa macho makali, akasimama na kunifwata kwenye sofa nililo kalia, akanikalia mapajani mwangu

    “Nipe leo na kesho, nitakuletea picha za wale wote walio husika kwenye mauaji ya familia yako”

    Lilian akanibusu mdomoni kisha akanyanyuka na kurudi kitandani na kukaa, ukimya ukatawala katikatui kama dakika tano huku, nikiwa na hasira ya kutaka kuwatambua wale wote walio husika katika mauji ya familia yangu.Nikasimama na kutoka bila hata ya kumuaga Lilian, nikatoka nje na kuingia ndani ya gari langu na kuondoka eneo la Cassino kwa kasi ya ajabu

    (xiii)

    ***********************************************

    Baada ya siku mbili, nikarudi kwenye Cassino anali miliki Lilin, kwa bahati nzuri kitendo cha mimi kuingia tu, akaniona na kunifwata akanishika mkono na kuingia kwenye chumba ambacho tuliingia siku ya kwanza ninfika kwenye Cassino lake.Akapiga hatua hadi kwenye kitanda chake, akafunua godoro na kutoa baasha kubwa ya rangi ya kaki na kunifwata sehemu nilipo kaa mimi

    “Humu ndani kuna picha za wale wote walio husika kwenye mauji ya familia yako”

    “Wewe umewajuaje?”

    “Nimewajua kutokana wengi wao, wanakuja kwenye hii Cassino langu, na baada ya kunywa sana wanakuwa wapo wazi wazi katika kuzitoa siri zao, isitoshe hawa wasichana wote waiomo humu ndani nimewafanya kama wapelelezi wangu, kila habari inayo endelea duniani, na hata mipango ya kinyama ikiwa inapangwa, kwa kutumia uzuri walio nao, wanaweza kupata taarifa kiurahisi”

    Lilian alizungumza kwa sauti ya chini iliyo jaa msisitizo, nikato picha moja na kukutana na sura ya jamaa ambaye sikuwahi kumuona katika maisha yangu na anaasili ya kichina

    “Huyo anaitwa Jong Lee, ni miongoni mwa wauaji wanao tumiwa na mama mmoja kutoka Afrika, ila huyo mama sijapata kumjua, inavyo semekana ni tajiri mkubwa sana katika bara la Afrika”

    Kila picha ambayo ninaitoa, sijawahi kukutana na sura za hawa watu, nikatoa picha kumi na nne zenye sura tofauti tofauti za wanaume ambao Lilian anakiri ndio walio husika kwenye kifo cha familia ya Juliana

    “Umetoa picha ngapi?”

    “Zipo kumi na nne”

    “Kuna moja umeisahau, ni kadogo hivi”

    Ikanibidi kuurudisha mkono wangu kwenye bahasha na nikatoa picha ndogo, yenye muundo wa ‘passport size’ nikaigeuza sehemu yenye picha, nikastuka baada ya kukuta sura ya Caro ikiwa katika picha hii ndogo

    “Huyo ndio, mtoa oda mkuu wa mauaji ya familia yako”

    Nikajikuta nikisimama huku taratibu, hasira ikiinza kunipanda kifuani mwangu, nikamgeukia Lilian, akatingisha kichwa akionekana kutilia msisitizo wa kwamba Caro anahusika katika mauaji ya familia yangu

    “Na wiki iliyo pita huyo dada alikuwepo hapa kwenye Cassino alikuja na muwe wake, naye yumo kwenye hizo picha”

    Lilian akazichukua picha nilizo ziweka kwenye sofa na kuanza kuzichambua moja baada ya nyingine

    “Eheee, huyu hapa”

    Lilian akanikabidhi picha ya jaamaa mmoja mwenye asili ya kiafrikast, nikazishika kwa pamoja huku nikiwa ninahasira kubwa sana kwenye moyo wangu

    “Unamkumbuka Don, Yule kaka yangu aliye tusaidia kule Oman?”

    “Ndio”

    “Kwa sasa ni marehemu, aliuawa na huyo jamaa, ambaye ni mume wa huyo dada, jina lake anaitwa Xaviela, kama sijakosea”

    “Ndio jina analo jiita kwa sasa?”

    “Kwani anajina jingine?”

    “Ndio, jina lake anaitwa Caro”

    “Kumbe unawajua…..!?”

    “Ndio, ninamjua, na sasa nitahakikisha ninaangamiza mmoja baada ya mwengine kwa kutumia mkono wangu huu, mumewe anaitwa nani”

    “David, baba yake ni mmiliki wa hizi sheli za Gapco, zilizo sambaa kote duniani, na nikijana mwenye pesa sana”

    “Wana kipindi gani cha mahusiano?”

    “Wanamuda sana, ila sijajua ni miaka mingapi na huyo ndio aliye suka mfumo mzima wa kuwaua watu wako wa karibu na anakujua vizuri sana”

    “Nilazima niwaue yeye na huyu malaya wake”

    Nilizungumza huku nikiutazama mkono wangu unao tetemeka kwa hasira kali

    “Ila Eddy kuwa makini sana, kwa maana hao watu ni matajiri sana na wanamkono mrefu sana angalia wasije wakakuangamiza”

    “Usihofu juu ya hilo, je upo tayari kunisaidia?”

    Lilian akabaki akiwa ananitazama machoni, akionekana kushikwa na kigugumizi kikali cha kunijibu kitu ambacho anahitaji kunijibu

    “Nakuomba, unisaidie katika hili”

    “Eddy”

    “Naam”

    “Sipo tayari kuyaweka tena rehani maisha yangu, nimekusaidia katika hilo msaada wangu kwa hapo unatosha sana”

    Lilian alizungumza kwa sauti ya upole yenye kunibembeleza, nikamtazama kwa umakini na kuzichukua picha alizo zishika kisha, nikaziingiza ndani ya bahasha na kupiga hatua za kuelekea kwenye mlango

    “Eddy”

    Lilian aliniita kwa sauti ya upole, nikageuka na kumtazama

    “Samahani kama nitakuwa nimekuudhi, kazi njema”

    “Asante”

    Nilimjibu Lilian na nikafungua mlango na kutoka, nikafika nje na kuingia kwenye gari langu na kuondoka, nikielekea nyumbani kwa mama Mac Mahon.Nikiwa umbali kidogo na ilipo nyumba ya mama Mac Mahon nikaliona gari moja lilitoka kwenye geti la mama Mac Mahon, gafla nikajikuta damu ikaanza kunisisimka, nikaanza kuhisi jambo la hatari, nikaisimamisha gari yangu nyumba mbili kutoka ilipo nyumba ya mama Mac Mahon.Ukimya wa barabara ya kuendea sehemu ilipo nyumba ya mama Mac Mahon, haukuniogopesha sana, Macho yangu yakawa na kazi ya kutazama kila sehemu ya barabara kama kuna usalama wowote.Nikafika ilipo nyumba na kukuta geti likiwa wazi, jambo ambalo si lakawaida kwa Mama Mac Mahon kuliacha geti lake wazi na isitoshe kuna gari imetoka kweke muda si mrefu

    “Au aliniona, ndio maana ameamua kuacha geti wazi?”

    Nilijiuliza swali ambalo lilikosa jibu kichwani mwangu na kujikuta nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kuingia ndani.Nikaanza kuingia ndani huku nikiwa, makini sana.Nikaufungua mlango wa kuingilia ndani kwenye nyumba, nikakuta vitu vikiwa vimechanguliwa, japo kuna giza ila niliweza kuiona hali ya vitu kuwa katika kuchanguliwa, nikatambua kwamba kuna jambo ambalo limetokea, sikuwa na silaha yoyote, zaidi ya mikono yangu, nikajiweka tayari kwa chochote.Nikendelea kupiga hatua nikastukia nikiteleza na kuanguka chini, jambo lililo niogopesha sana

    “ Shitiii”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikanyanyuka haraka, ndipo nilipo gundua kuna michirizi mingi ya damu kwenye sakafu ya kisasa iliyopo ndani ya hili jumba la mama Mac Mahon.Nikazidi kuongeza umakini huku nikiendelea kwenda mbele nikiifwata michirizi sehemu ilipo elekea.Nikapandisha ghorofani, sikuamini macho yangu baada ya kuuona mwili wa mama Mac Mahon ukiwa umening’inizwa kwenye feni la sebleni kwake, akiwa tayari amefariki dunia.Nikatazama kila sehemu ya sebleni, nilipo hakikisha hakuna mtu ikanilazimu kuwasha taa, nikakuta kikaratasi chenye maandishi kikiwa kimebandikwa kwenye ya mama Mac Mahon

    (KILA HATUA UNAYO PIGA TUPO NYUMA YAKO, NA KILA ANAYE KUSAIDIA NI ADUI KWETU, NA SASA TUNAELEKEA UINGEREZA KWA BABA YAKO FEKI MZEE MARCUS, NAKUPENDA SANA EDDY WANGU)





    Nikajikuta nikishusha pumzi nyingi, huku nikimtazama mama Mac Mahon jinsi anavyo vuja damu kwenye shingo yake akionyesha amechijwa kwa kitu kikali sana.Sikujua hata nifanye nini, nikafikiria kupiga simu polisi ila nikaona kwamba haita saidia kwani kesi inaweza kurudi kwangu

    “Nikitoroka si ninaweza kujulikana kwamba mimi ndio muuaji?”

    Nilizungumza mimi mwenyewe, nikafikia maamuzi ya kupiga simu polisi, na kuwaomba kufika katika nyumba ya Mama Mac Mahon.Baada ya muda nikaanza kusikia ving’ora vya gari za polisi vikisimama nje ya jumba ya Mama Mac Mahon, nikatoka nje na kwenda kuwachukua polisi na kuingia nao ndani, kila aliye uona mwili wa mama Mac Mahon akabaki akishika mdomo wake akionekana, kushangazwa na mauaji mengine ya kikatili

    Polisi wakaanza kufanya kazi ya kuushusha maiti ya mama Mac Mahon na kuuiingiza kwenye mfuko mwesi wa kuhifadhia maiti, wakanichukua na kwenda nao katika kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi

    “Mimi, nilikuwa ninatoka matembezi usiku, wakati ninarudi nikaiona gari ikitoka kwa haraka kwenye geti la nyumbani, ikanilazimu kusimamisha gari yangu mbali kidogo na nyumbani, nikatembea kwa miguu hadi nyumbani ndio nikakutana na hali kama hiyo”

    Ni maelezo ambayo niliwapa polisi walio hitaji maelezo kutoka kwangu, wakanihaidi kuanza kulifanyia uchunguzi swala la mauaji ya mama, Mac Mahon, ikanilazimu kuwauliza juu ya uchunguzi juu ya familia yangu

    “Uchunguzi bado unaendelea na wahalifu wakikamatwa ndio utaelezwa”

    Ni majibu aliyo nipa mkuu wa upeleleze anaye fwatilia mauji ya familia yangu,, jambo ambalo nikaanza kulitilia mashaka kwani hapana muhamko wowote wa wao kufwatila ni kina nani walio husika na mauji ya familia yangu.Asabuhi na mapema nikarudishwa nyumbani kwa gari ya polisi, cha kwanza kukifanya ni kupiga simu Uingereza kwa mzee Marcus kwa bahati nzuri akapokea

    “Eddy tulijaribu kukupigia simu kwa kipindi lakini hukupokea, umepatwa na nini?”

    “Baba nitakuambia ila kikubwa nakuomba mchukue Jolin na wewe muende nchi yoyote mukaweka makazi ya siri kuna watu wanakuja kuwafanyia kitu kibaya”

    “Ni kina nani?”

    “Baba siwajui, ila kikubwa ninakuomba muweze kuondoka haraka hata kama inawezekana sasa hivi mupande ndege na musimuambie mtuo yoyote ni wapi munapo elekea”

    “Sawa nitafanya hivyo”

    Nikakata simu, nikaingia ndani kwangu na kuchukua koti langu la kujikinga na baridi, nikalivaa na kurudi ndani ya gari, safari ikaanza kuelekea kwenye Cassino la Lilian, nikafika na kukuta wahudumu wakiwa wanafanya usafi

    “Samahani nimemkuta mkurugenzi wenu?”

    Nilimuuliza mmoja wa wahudumu

    “Amesafiri, nahisi ataondoka na ndege ya saa tano asubuhi”

    “Anaelekea wapi?”

    “Ungereza mama yake anaumwa alipigiwa simu hii asubuhi”

    “Una namba yake?”

    “Ndio, ila kiukweli hapendi namba yake itolewe kwa watu wasio julikana”

    “Samahani, mimi ananijua sana, nakuomba unipatie nitampigia hapa hapa mbele yako ili ujue kwamba ninafahamiana naye”

    Muhudumu akanitazama kwa macho ya kunichunguza, kisha akatoa simu yake mfukoni na kunitajia namba za Lilian, nikaziingiza kwenye simu yangu na kuzipiga.Simu ikaaita hadi ikakata, nikapiga kwa mara ya pili simu ikaata na kupolekewa

    “Eddy ninazungumza”

    “Vipi, umeipata wapi namba yangu?”

    “Nimepewa hapa ofisini kwako, upo wapi?”

    “Nipo nyumbani kwangu, ninajiandaa kwenda uwanja wa ndege nasafiri”

    “Nielekeze nije nikufwate kwako”

    Lilian akanielekeza kwake, hapakuwa ni mbali sana na ofisini kwake, nikamuga muhudumu na nikaingia ndani ya gari na kuanza safari kwa mwendo wa kasi kidogo, kwani inakwenda saa nne kasoro asubuhi, nikafika kwenye jumba la kifahari la Lilian, nikafunguliwa geti na mlinzi nikaingia ndani, na Lilian akatoka kunipokea

    “Lilian ninaomba msaada wako mwengine”

    “Upi?”

    “Hali ya jamaa kuendelea kuangamiza watu wote walio karibu yangu imeanza ninakuomba uwe makini katika hil kwa maana ninaona wananifwatilia kwa ukaribu sana”

    Nilizungumza huku nikimkabidhi, Lilian kikaratasi kilicho achwa kwenye maiti ya Mama Mac Mahon

    “Umekitoa wapi hiki kikaratasi?”

    “Kuna mama nilikuwa ninaishi naye, alinifadhili, jana usiku wamemuua na kuniachia hicho kikaratasi”

    “Mmmm?”

    “Usishangae na kama unaelekea Uingereza twende wote kwa maana kuna hali nyingine huku inakwenda kutokea”

    Lilian akanitazama kwa umakini, akamalizia kuweka nguo zake kwenye begi, kisha tukaingia kwenye gari langu na safari ikaanza, ukimya ukatawala ndani ya gari huku sote tukiwa na mawazo mengi, japo ninaendesha gari ila ukweli mawazo yananipekekesha puta kiasi kwamba kichwa ninakihisi kinapata moto

    “Eddy hiyo gari unayo tufwata nyuma umeiona?”

    Lilian alizungumza huku akitazama kwenye kioo cha pembeni, nikayatupia macho yangu kwenye kioo cha pembeni na kuliona gari jeusi likitufwata nyuma yetu kwa mwendo wa taratibu, nikaongeza mwendo nao jamaa wakaanza kuongeza mwendo, nikipunguza na wao wanapunguza.

    “Hawanijui hawa?’

    Nilizungumza huku nikiaanza kuongeza mwendo kasi wa gari langu, kadri jinsi ninavyozidi kuongeza mwendo ndivyo jinsi na wao wanavyo ongeza mwendo

    “Saa ngapi?” Nilimuuliza muda

    “Saa nne na dakika thelathini na tato”

    “Ndege inaondoka saa ngapi?”

    “Saa tano na dakika kumi?”

    “Tuna dakika ishirini na tano, piga simu uwanja wa ndege waniwekee tiketi na mimi”

    Lilian akafanya kama nilivyo muagiza, nikawa na kazi ya kukatiza mitaa, kwa mwendo wa kasi, kwa uwezo mkubwa wa mwendo kasi wa gari langu, niliweza kuwapoteza jamaa walio kuwa wakitufwatilia, chakushukuru Mungu hakuna askari ambao walitufukuzia kutokana na mwendo kasi wa gari, tukafika uwanja wa ndege na kushuka, kutokana nina hati yangu ya kusafiria haikuwa ngumu, nikakabidhwa tiketi ambayo Lilian alisha ilipia.

    Hadi tunaingia ndani ya gari hapakuwa na mtu yoyote ambaye, tulimuhisi anatufwatilia, tukaanza safari ya kuelekea Uingereza huku wakati wote nikiwa makini kumchunguza kila mtu ambaye yupo karibu yangu, au anapita karibu ya siti ambayo nimekaa.Tukafanikiwa kufika uingereza salama salimini cha kwanza kukifanya baada ya kutoka nje ya uwanja wa ndege nikampigia simu mzee Marcus

    “Baba mupo wapi?”

    “Kwa sasa tupo ndani ya ndege binafsi, tunaelekea Canada”

    “Upo na Jolin?”

    “Ndio”

    “Mpe simu”

    “Eddy mambo vipi?”

    “Safi, ni hivi hakikisha munakuwa makini kwa kila kitu huko Canada, na ninakuomba usipende kwenda sehemu hatarishi sawa”

    “Sawa, ila Eddy kuna nini, kwa maana sielewi ninaona munanipeleka peleka?”

    “Nitawaambia sawa”

    “Sawa”

    Nikakata simu na kuirudisha mfukoni

    “Ulikuwa unazungumza na nani?”

    Lilian aliniuliza swali, mara baada tu ya kuingia ndani ya taksi ya kukodi

    “Yue baba yangu wa hiyari niliye kuambia?”

    “Ndio walio muandika kwenye kikaratasi?”

    “Ndio”

    “Mmmm kazi ipo, sas isije wakawa wamesha fika hapa Uingereza, na hapa tunakwenda nyumbani kwa mama isije wakawa wanaendelea kukufwatilia?”

    “Kikubwa ni kuwa makini”

    Tukafika katika jumba la mama yake Lilian, na sote tukaingia ndani na kupata mapokezi mazuri kutoka kwa ndugu wa Lilian

    “Eddy jisikie upo nyumbani”

    “Nashukuru”

    Baada ya mapumziko ya muda mfupi Lilian akaniomba niingie kwenye chumba ambacho mama yake amelazwa na you chini ya uangalizi mkali wa madaktari alio waajiri, sikuamini macho yangu baada ya kuingia na kukutana na bibi Vanessa akiwa amewekewa mipira ya kuhemea na hali yake ikuwa mbaya kupita maelezo, machozi yakaanza kumwagika Lilian taratibu, huku akipiga hatua akikifwata kitanda alicho lala mama yake, ambaye mimi mara yangu ya mwisho ni kuonana, na bi. Vanessa ni nchini Kenya baada ya jengo kubwa la bishara tulilo kuwepo kuivamiwa na kundi la waasi la Al-Shabab.

    Bi.Vanessa akayafumbua macho yake na kumtazama Lilian, anakunyanyua mkono mmoja na kumshika Lilian nywele zake, hakuweza kuzungumza kutokana na hali yake kuwa mbaya sana, akaigeuza sura yake na kunitazama mimi, akaachia tabasamu pana na kuninyooshea mkono mmoja wa kuniomba nimfwate sehemu alipo lala, nikamsogelea, huku kwa mbali machozi yakiwa yananilenga lenga kwa mbali, akaunyanyua mdomo wake taratibu huku akiniita jina langu kwa sauti ya chini isiyo toka vizuri masikioni mwangu

    “Eddy mwanangu”

    “Ndio mama”

    Lilian akabaki akiwa anashangaa kwa maana, hakuamini kama ninajua na mama yake, akatutushika mikono pamoja na Lilian, huku akitutizama machoni

    “Pendaneni, na mushirikiane kwa pamoja, eddy ulijitoa maisha yako kwa ajili yangu, basi na wewe uwe Lilian ujitolee kwa mwenzako”

    Bi Vanessa alizungumza kwa sauti ya chini sana huku kwa mbali akiwa anatetemeka mwili mzima, kila kitu ambacho Lilian anakisikia kwake bado haamini, anaona kama ni ndoto kwenye macho yake.Bi Vanessa akatutingisha mikono yetu taratibu, huku akiwa anatabasamu, gafla hali yake ikaanza badalilika, hata mashine ambayo inahesabu mapigo yake ya moyo ikaanza kuchira mstari mmoja huku asilimia zake zikianza kurudi chini hadi zikifika kwenye sifuri.Lilian akaanza kumtingisha mama yake kwa nguvu huku akilia, madaktari wakatuomba tutoke nje wamshuhulikie mgonjwa.

    “Niacheni, mama yangu amekufaaa”

    Lilian alizungumza kwa sauti ya juu huku akijitahidi kujitoa mikononi mwa madaktari wanao muomba kutoka nje, ukweli ni kwamba Bi Vanessa tayari amefariki dunia na madaktari, wanamfariji tuu Lilian kuweza kutoka nje ya chumba.Nikafumba bi Vanessa macho yake ambayo yalikuwa wazi, huku na mimi nikijizuia kuyamwaga machozi yangu.Nikamshika Lilian na kumnyanyua juu na kumtoa nje ya chumba.Ni pigo jengine kwenye maisha yangu ya kushuhudia kifo cha watu ambao nilishuhulika nao kwenye maisha yangu kipindi cha nyuma.Nikawa na kazi moja ya kumbembeleza Lilian kunyamaza kulia, japo imenichukua kipindi kirefu kwa Lilian kunielewa ila akanielewa na kunyamaza kulia.

    Ndani ya kipindi cha wiki moja na nusu, tukawa tunaandaa maandalizi ya kuuzika mwili wa Bi Vanessa, japo kwa muda wote Lilian alipotewa na furaha kwenye maisha yake.Baada ya tukio zima la mazishi kufanyikwa, ikatulazimu kuondoka London na kwenda jijini Liverpool kwenye fukwe za bahari kupuumzika kwa ajili ya kuanza kazi rsmi ya kuwatafuta maandui zangu wote walio wateketeza wapendwa wangu

    ***

    “Eddy bado upo fiti kwenye matumizi ya bunduki?”

    “Sana tuu, unadhani mafunzo yote niliyo yaata nchini, Pakistani nimeyasahau”

    “Wachaa wee, alafu ninasikia kwamba, Yule mama anashirikiana na kikundi cha Al-Khaida”

    “Nani, mama Caro?”

    “Ndio, na tunatakiwa kuendelea kuwa makini sana katika kazi yetu hii, mimi nimefanya kutokana na wewe uliamua kujitolea maisha yako kwa ajili ya mama yangu kipindi mupo huko maangoni”

    “Asante ila ninakuomba ufanye kwa moyo mmoja”

    Tulizungumza na Lilian, huku tukiwa tumejilaza kwenye fukwe za bahari, na upepo mzuri kutokea baharini ukiwa unaendelea kutupepea taratibu.

    “Kazi tunaianza lini”

    “Siku yoyote kuanzi leo, kutokana mimi ninazijua njia zao hazita tuwia ugumu kulifanya hilo kwa pamoja”

    Kutoka, tulisha wahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi mimi na Lilian, haikuwa ngumu kati yetu kuyarudisha upya mapenzi yetu.Tukaanza kutafuta watu wanao weza kutuuzia silaha kwa njia haramu(kununua silaha pasipo kufwata shria za kijeshi).Tukakutana na kikundi kimija wanachi jiita kwa jina ‘Black Devil’(Shetani mweusi), kinacho shuhulika na maswala ya uhalifu nchini Uingereza.Tukakutana na mkuu wao ambaye kwa kiasi cha pesa tulicho nacho tuliweza kumshawishi kununua baadhi ya silaha ambazo, tunaamini zitaweza kutusaidia katika swala zima la kuteketeza kila ambaye nimemuona kwenye picha alizo nipa Lilian.

    Tukarudi nyumbani, tukiwa na shehena ya bunduki, pamoja na magazine zilizo jaa risasi za kutosha, zote zikiwa kwenye begi kubwa, tulilo libeba kwa kutumia gari letu dogo aina ya Ferrari.Tukaingiza begi ndani pasio mfanya kazi yoyote kugundua kitu tulicho kibebe ndani ya begi.Cha kwanza kukifanya baada ya kuingia ndani, tukaziweza silaha zote juu ya kitanda chetu cha kulalia na kuanza kukagua bunduki moja baada ya nyingie ambazo zipo ishirini aina tofauti tofauti.

    “Nakwenda kuchukua vinywaji sebleni”

    “Powa”

    Lilian alizungumza, na kutoka nje na kuniacha mimi nikiendelea kukagua silaha moja baada ya nyingine hadi nikamaliza, Lilian akaingia ndani akiwa amebeba mzinga wa pombe kali pamoja na glasi mbili

    “Eddy hembu washa Tv, haraka na uweke BBC nikuonyeshe huyo mama ambaye ni katili”

    Nikachukua rimoti na kuwasha Tv kwa haraka, kama alivyo niambia Lilian na kuweka chaneli ya shirika la utangazaji nchini Uingereza BBC, sikuamini macho yangu baada ya kukuta taarifa ya kuapishwa kwa raisi wa kwanza ukanda wa Afrika Mashariki, ambaye pia ni raisi wa kwanza mwanamke nchini Tanzania, ambaye ni mama Caro.

    Nikashusha pumzi nyingi, nikijiuliza imekuwaje kuwaje hadi mama Caro amepata kuwa raisi, ni swali ambalo hata Lilian mwenyewe alibaki akiwa ananitazama kwa maana hata yeye mwenyewe hakulijua hilo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kazi imesha kuwa ngumu”

    Nilizungumza huku nikiwa ninamtazma Lilian kwa macho makali?”

    “Kwa nini unasema hivyo?”

    “Huyo mwanamke amesha kuwa na mkono mrefu, isitoshe kwa sasa amekuwa ni raisi hatuwezi kufanya kazi kiurahisi kama nilivyo kuwambia”

    “Mmmmm, sasa tutafanyaje tuache?”

    “Hatuwezi kuacha”

    “Nisikilize mpenzi wangu, katika kazi hizi, kamwe usidhubutu kuweka moyo wa kusita sita, kwa maana kazi yako itakuwa ni ngumu sana kuifanya, pili utajikuta unakufa pasio kuweza kuikamilisha kazi yako.Kikubwa ni kupambana kiume, hilo ndilo jambo la msingi sawa”

    Lilian alizungumza kwa umakini huku akinitazama machoni, akionekana kumaanisha kwa kile ambacho anakizungumza

    “Sawa”

    Tukaanza kazi ya kuwatafuta kwa kutumia mtandao wa satelaiti wale wote ambao wameusika katika mauaji ya mke wangu na familia yeka kwa ujumla.Kwa uzoefu mkubwa wa matumiza ya ‘laptop’ haikuma shida sana Liliana kuweza kujua ni wapi walipo wale alionionyesha, uzuri wake aliweza kuziingiza saura moja baada ya nyingine kwenye mtandao, na kufanikiwa kuanza kuzipata moja baada ya nyingine

    “Kuna huyu, Lucas, anaonekana yupo hapa nchini kwenye jiji la Manchester”

    Lilian alizungumza huku akinionyesha kialama chekundu kinacho waka na kuzima kwa mtu aliye iingiza sura yake, kwenye laptop ndogo tunayo itumia kwa kazi hiyo.

    “Inatulazimu twende sasa, hivi tusije tukamkosa”

    “Powa”

    “Na tukimpata huyu tutajua mengi sana kuhusiana na jinsi ya kuwapata wengine”

    Kila mtu akachukua bastola mbili zenye magazine zilizo jaa risasi za kutosha pamoja na viwambo vya kuzuia kelele, za sauti ya risasi inpokuwa inatoka.Tukaingia kwenye gari na sote tukiwa tumejiandaa kwa tukio lililopo mbele yetu, kutoka na mimi kuto kuwa na kibali cha kuendesha gari kwa masafa marefu, ikamlazimu Lilian kufanya kazi ya uendeshaji wa gari

    Tukafanikiwa kufika kwenye mgahawa alipo Lukas, kwa kufwata ramani tunayo ipata kuoitia Laptop yetu, tukasimamisha gari pembezoni mwa barabara

    “Atakuwa yupo ndani”

    Lilian alizungumza huku akitazama kiilama chekundu kinacho waka na kuzima, nikaichukua picha ya Lukas, na kushuka kwenye gari na kiingia ndani ya mgahawa huku simu yangu nikiwa nimeiweka sikioni nikipata maelekezo ya moja kwa moja

    “Upande wako wa kulia Eddy unamuona nani?”

    Lilian alizungumza kupitia simu yake,

    “Kuna meza za watu kama sita hivi zina watu walio kaa wakila”

    “Piga hatua kama sita mbele huo upande wa kulia”

    Nikapiga hatua alizo niagiza Lilian za kwenda mbele zaidi

    “Simama hapo hapo ndipo alipo Lucas”

    Nikamuona jaa mmoja aliye valia miwani nyeusi na koti jeusi aina ya lezar akiwa amekaa na msichana mdogo apataye miaka saba wakiata chakula.Nikamtazama jaa jinsi anavyo endelea kula nikasikia mwanaye akimuita jamaa baba, jambo lililo anza kunipa kikwazo cha kufanya tukio langu papo kwa papo

    “Eddy fanya tuondoke ninakusubiria”

    “Ngoja kwanza Lily”

    “Kwani kuna nini?”

    “Ngoja kwanza”

    Nikakaa kwenye meza ya pembeni na kumuagizia muhudumu Juisi ya embe, nikiendelea kuvuta subira ya kupata nafasi ya kutekelea adhima yangu ya kumuua jamaa

    “Baba kesho ni siku yangu ya kuzaliwa, utanipa zawadi gani?”

    Binti alizungumza huku akimtazama baba yake

    “Ohhh mwanagu kesho nitakununulia cheni nzuri ya kupendeza, iliyo tengenezwa kwa madini ya dhahabu”

    Mazungumza ya Lucas na mwanaye yakazidi kunizuia, kwani hali ya kuwa na huruma kama baba ikaanza kunijaa moyoni mwangu, huruma yangu yote ikaangukia juu ya motto wa Lucas ambaye kesho ni siku yake ya kuzaliwa, nikahofia kumpotezea furaha yake

    “Nakupenda sana baba yangu, nakuombea kwa Mungu usife haraka, ili niendelea kufaidi upendo wako, ningetamani kama mama naye angekuwepo sema ndio hivyo ametangulia mbele za haki”

    Japo ni mototo mdogo ila anazungumza mambo ambayo kusema kweli moja kwa moja yakaugusa moyo wangu.

    “Eddy ni nini unafanya?”

    Lilian alizungumza kwa sauti ya ukali, kwani aliona kwa kipindi chote ninacho kaa ndani ningekuwa nimesha maliza kazi iliyo nipeka ndani.Lucas akamkumbatia mwanaye,

    “Naomba kwenda chooni mara moja”

    Lucas akamuaga mwanaye na kusimama, na kuelekea chooni, nikamtazma binti wa Lucas na kumuona akiendelea kunywa juisi iliyopo kwenye kopo lake kwa kutumia mrija.Nikasimama na kwenda moja kwa moja chooni, kitendo cha mimi kufungua mlango nikakaribishwa na bastola niliyo wekewa kichwani mwangu na Lucas

    “Ohhh Bwana Eddy, unadhani kwamba sikufahamu wewe, tena ninashukuru kwa maana umejileta mwenyewe na kunirahisishia kazi ya mimi kuata zawadi nono kutoka kwa mama”

    Lucas alizungumza huku akinipapasa na kuichomoa bastola yangu kiunoni nilipo kuwa nimeichomeka kwenye mkanda wa suruali yangu, kwa kutumi kona ya jicho langu la kushoto, nikawa na kazi ya kumtazama Lucas kwa umakini mkubwa, akaichomeka bastola yangu kwenye kiuno chake

    “Funga mlango kwa ndani?”

    Aliniamuru na mimi nikatii, akaniamuru kuonyoosha mikono juu na nikafanya kama anavyo hitaji, Lucas akaitoa simu yangu mfukoni na kuanza kuichunguza na kuikuta ikiwa ipo hewani, akaiweka sikioni mwake

    “Ohhh wewe ndio up…….”

    Sikumpa nafasi ya kumalizia sentesi yake, nikampiga teke la shingo lililo myumbisha na kujibamiza kwenye ukuta na bastola yake aliyo ishika ikaangukia pembeni, nikamshika koti lake na kulizungusha kwa utaalamu mkubwa, na kukifunika kichwa chake kwa haraka, nikaichoa bastola yangu kwenye kiuno chake.Kisha nikampiga vigoti viwili vya kifuani na kumfanya atoe ukelele wa maumivu makali, nikamsukuma na akaanguka chini

    “Nani aliye kutuma?”

    Nilimuuuliza kwa sauti ya ukali huku nikiwa nimemnyooshea bastola kichwani mwake

    “Nenda kamlale mama yako mzazi”

    Lucas alinitukana tusi, lililo nipandisha hasira, mguu wangu wakulia ukatua kwenye sehemu zake za siri na kuzidi kumzidisha maumivu Lukas

    “Sema ni nani aliye kutuma”

    Lucas akaendelea kunitukana matusi ya nguoni jambo ambalo, likanifanya kuanza kumshushia kipigo ambacho sikuwahi kukitoa kwa mtu yoyote aliye nikosea, japo katika maisha yangu ya nyuma nimeua watu wengi.Gafla mlango ukagongwa na kuisikia sauti ya simu inayo ita ya mtu aliyepo nje ya mlango

    “Baba simu yako inaita?”

    Nilisikia sauti ya mtoto wa Lucas ikizungumza, Lucas akataka kuiga kelele ila nikamuwahi kumziba mdomo.

    “Baba simu yako?”

    Mtoto wa Lucas aliendelea kuzungumza huku akigonga mlango,

    “Sema ni nani aliye kutuma lasivyo ninakuua wewe na mwanao”

    Nilizungumza huku nikiwa nimepiga kabali ya shingo Lucas na mkono wangu mwengine ukawa na kazi ya kukiziba kinywa chake

    “Ni mama Getrude”

    “Ndio nani?”

    “Mama Caro”

    Lucas alizungumza kwa sauti ya maumivu kwani kabali niliyo mpiga ninahakikisha anazungumza ukweli wote anao utambua

    “Kwa nini, muliua familia yangu?”

    “Alisema, hao ndio wanao kuficha wewe, anataka akurudishe mikononi mwake”

    “Ili iweje?”

    “Mimi siju…”

    “Baba upo salama kweli?”

    Mtoto wa Lucas alizungumza huku akiendelea kugonga mlango, nikamuamrisha Lucas kujibu swali alilo ulizwa na mwanaye

    “Ndio mwanangu”

    “Bibi, anasema twende tukamchukue uwanja wa ndege”

    “Na..kuja nenda kakae”

    “Sawa baba”

    Nikaendelea kumkaba kabali Lucas na kuzidi kumuhoji maswali, juu ya mtandao wa Mama Caro, akaanza kunitajia sehemu moja baada ya nyingine ambayo ninaweza kuwapata watu walio husika kwenye mauji ya familia yangu

    “Ninakuachia huru kwa ajili, kesho ni siku ya mwano ya kuzaliwa la sivyo ningekuua”

    Nilimuambia Lucas huku nikimsukumiza chini, akionekana kuchoka sana kwa kiigo kikali nilicho mpatia, nikaichukua bastola yale na kuiweka mfukoni mwangu, nikaiokota simu yangu na kuiweka mfukoni, kisha nikatoka chooni na kurudi kwenye gari nilipo muacha Lilian

    “Vipi mbona umechelewa, umefanikiwa?”

    “Ndio, amenisaidia kupata kujua ni wapi walipo watu wengine”

    “Kama kina nani?”

    “Wote ambao umenitajia kwenye picha na ameniambia kwamba kwa sasa wapo barani Afrika”

    “Nchi gani?”

    “Somalia, ndio walipo jificha kukwepa mkono wa majasusi wa Kimarekani”

    Tulizungumza na Lilian huku akiendelea kuendesha gari, sikutaka kumuambia ukweli kuhusiana Lucas kwamba nimemuacha hai.Tukafika nyumbani salama salimi, kitu cha kwanza, kukifanya baada ya kufika nyumbani nikawasha Tv na kutafuta chaneli ambayo inaonyesha juu ya kuapishwa kwa Raisi mpya wa Tanzania Bi.Getrude au kwa jina ninalo lijua mimi ni Mama Caro

    Nikfanikiwa kupata, chaneli moja ikionyesha marudio ya kuapishwa kwa raisi mpywa wa kike nchi Tanzania.Hapakuwa na mabadiliko sana kwa Mama Caro kwani sura yake ndio ile ile, umbo lake ndio lile lile, labda kikubwa ambacho kimebadilika umri wake kusogea mbele ila bado anamvuto sana.



    “Nilizama nimuue huyu mwanamke”

    Nilizungumza kwa sauti nzinto na kumfanya Lilian kunitazama kwa macho makali

    “Inatubidi twende Somalia”

    Lilian alizungumza, huku akiendelea kunitazama

    “Kuna mtu nitahitaji kupta msaada wake?”

    “Nani?”

    “Priscar”

    “Ndio nani?”

    “Utamjua”

    Kutokana namba ya simu ya Priscar niliikremisha kichwani, nikahukua simu yangu na kuipiga kwa bahari nzuri ikaaita, baada ya muda ikapokelewa na Priscar mwenyewe

    “Eddy hapa”

    “Ohh Eddy, mambo vipi?”

    “Si safi, nahitaji msaada wako”

    “Upo wapi kwani?”

    “Uingereza wewe je?”

    “Nipo bado, Italy”

    “Ninakuja”

    Sikutaka kuzungumza mazungumzo marefu kwenye sifu kuhofia mawasiliano yangu kukamatwa na jeshi la polisi wanashuhulika na maswala ya simu zinazotoka nje ya nchi na kuingia ndani ya nchi ya uingereza

    ***

    Siku ya pili tukatua kwenye kiwanja cha ndege nchi Italia kwa ndege tuliyo kodi kwa safari hiyo.Kutokana sote si wageni nchini Italia, haikutusumbua sana kukodi chumba kwenye Hoteli moja ya kitali, nikampigia simu Priscar na akaniahidi kuja siku ya pili yake.Mimi na Lilian hatukutoka nje na tukawa na kazi ya kupanga mbinu za kuvamia kikosi cha mama Caro kilichopo nchini Somalia,

    Tukafanikiwa kupanga mbinu saba za kuteketeza kikosi cha mama Caro.Asubuhi na mapema simu yangu ikaita na Priscar akaniarifu kwamba ameshafika kwenye Hoteli niliyopi, nikamuelekeza kwenye chumba nilichopo, baada ya dakika kadhaa akaingia kwenye chumba ambacho topo mimi na Lilian

    “Karibu sana Prisca”

    “Asante”

    Nikafanya utambulisho kati ya Lilian na Priscar na kila mmoja akaonekana kumfurahia mwenzake kwa historia yake fupi ya maisha yao ya nyuma.

    “Priscar nakukumbuka, ile siku tupo kwenye boti si ndio ulidumbukia kwenye maji ukiwa na jamaa mmoja hivi”

    “Swadataa ndio mimi, japo siku ile kila mmoja alikuwa na kazi ya kujiokoa yeye mwenyewe.”

    Nikamueleza Priscar kila mpango tulio upanga ila kikubwa hatukujua sehemu husika walipo kikundi cha mama Caro, japo Lucas amenitajia ni nchini Somali

    “Duu, Somalia mimi ninaijua yote, na kikundi kikubwa ambacho kinanguvu nchini humo ni Al-Shabab”

    Priscar alizungumza, huku akitutizama

    “Kwa hili utanisaidiaje ndugu yangu?”

    “Eddy mimi na wewe tumetoka mbali, na bado na mimi ninahitaji msaada wako”

    “Msaada wangu wa nini tena?”

    “Wa kulipiza kisasi cha yale yote ambayo mama Caro aliwafanyia wazazi wangu”

    “Peke yangu siwezi, kwa ushirikiano wetu wote watatu tutaweza”

    Nilizungumza huku nikiwatazama Lilian na Priscar

    “Ndio tunaweza”

    Kwa mamoja tukaikutanisha mikono yetu ya kulia huku ikiwa imekunja ngumi kuashiria kukubaliana kwa pamoja na kuungana kwa pamoja

    “P mwanao anaendeleaje?”

    “Yupo Marekani kwa babu yake mzaa baba”

    “Eddy kuna babu yangu, yupo nchini Cuba, yeye ni jasusi twendeni huko atatusaidia”

    Lilian alizungumza na sote tukamuunga mkono, Siku ya pili kwa kutumia ndege tuliyo ikodisha aina ya Jet, inayo beba abiria wachache ikatupeleka kisiwa cha Cuba.Tukafika kwenye moja ya mji unaitwa Trinida, ambapo ndipo anapo ishi babu yake Lilian.Tukafika kwenye nyumba yake iliyopo pembezoni mwa bahari na imejitenga sana na makazi ya watu, huku ikiwa imezungukwa na miti mingi iliyo ifanya nyumba hiyo kuonekana kama ipo msituni

    “Babu”

    Lilian alimkimbilia babu yake na kumkumbatia baada ya kufika tu kwake.Wakakumbatiana kwa muda, huku wote wakiwa na furaha, mimi na Priscar tukabaki tukiwa tumesiama na mabegi yetu ta nguo, tukisubiri wamalize kusalimiana

    “Baba hawa ni rafiki zangu, huyu mwanaume anaitwa Eddy na huyu msichana anaitwa Prisca”

    Tukampa mikono babu yake Lilian, huku akionekana kufurahishwa na uwepo wetu katika eneo lake

    “Jamani huyu ni babu yangu mzaa baba, yangu naamini Eddy baba unamjua”

    “Ndio, wanafanana kiasi”

    “Yule ni mwanangu seme ndio hivyo amefariki, katika umri ambao bado hakufikika kwenye malengo yake aliyo kuwa akiyahitaji kufika”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akatukaribisha ndani, kitu ambacho kinanishangaza ni maisha ya ukimya katika eneo hili, kwani mzee anaishi peke yake pasipo kuwa na msaidizi wa aina yoyote japo umri wake unaonekana ni mkubwa sana.Baada ya Lilian na Priscar kuandaa chakula, tukala kwa pamoja, huku babu yake aliye jitamulisha kwa jina la Calyto, akituadisia mambo mengi enzi zake za ujana

    “Hadi leo, bado serikali ya Marekani, wananitumia katika ushauri wa mambo ya kijasusi”

    “Duuu babu na umri huo?” Lilian aliuliza

    “Ndio umri sio tatizo, kikubwa ni akili yangu inafanya kazi kwa kiasi kikubwa, wiki iliyo pita mkuu wao wa kikosi cha kijasusi alikuja hapa kunieleza juu ya mauaji ya familia moja huko Marekani, nikawaambia jinsi ya kufanya ila bado hawajanipa jibu ni wapi walipo fikia”

    “Walikueleza ni familia gani?”

    “Ahaaa jina la lile familia limenitoka, ila wanadai kwamba baba alipigwa risasi, mke na vijana wawili wakiume walilipuliwa na bomu nyumbani kwao”

    Macho yangu yakatazama na Lilian, kisha tukamgeukia babu tena

    “Babu, hiyo ndio familia yangu”

    Mzee Calyto akaonekana kustuka kidogo, na kunitazama kwa macho ya umakini.Ikanilazimu kuanza kumuadisia mkasa mzima wa familia yangu, kutoka alipo uliwa mke wangu akiwa mjamzito pamoja na mdogo wake ambaye ni Pretty.Hadi ninamaliza kuadisia machozi yakawa yananitiririka machoni mwangu.Mzee Calyto akanichukua na kuniingiza kwenye moja ya chumba chenye viti viwili pamoja na meza.

    Akaanza kunihoji maswali juu ya mkasa mzima wa maisha yangu, nikamuadisia tangu nikiwa kijana mdoho hadi hapa nilipo fikia,

    “Pole sana Eddy”

    Mzee Calyto alizungumza huku akishusha pumzi kwani, historia ya maisha yangu inaoenekana kumgusa sana moyoni mwake

    “Kuanzia kesho, nitawafundisha mbinu zote za kijasusi ambazo hata watu wengine hawajajifunza, ili ukalipize yale yote waliyo kufanyia wabaya wako”

    “Sawa babu”

    Saa kumi na moja alfajiri mlango wa chumba nilicho lala ukagongwa kwa nguvu, nikasimama na kwenda kuufungua, huku nikiwa na malepe ya usingizi, nikastikia ngumi ikitua kwa nguvu kwenye pua yangu, kabla sijajiweka sawa nikastukia teke lililo niangusha chini kama mzigo

    “Vaa, muda wa mazoezi”

    Mzee Calyto alizungumza huku akinirushia, mavazi ya jeshi amoja na viatu, huku yeye akiwa tayari amevaa mavazi hayo, akatoa ndani kwangu na kuufunga mlango kwa nguvu.Nikanyunyuka huku nikiwa na maumivu, nikavaa nguo na viatu alivyo nipa.Nikatoka nje na kukuta Lilian na Priscar nao wakiwa wamevalia mavazi kama niliyo yavaa mimi, mzee Calyto akaingia kwenye gari yake aina ya jeshi, isiyo funikwa juu, na kutuamrisha kuanza kuikimbiza gari hiyo kwa miguu.

    Tukaanza kufanya kama alivyo tuagiza, kila jinsi gari inavyozidi kwenda ndivyo nasi tulivyo ongeza mwendo wa kukimbia, umbali kutoka nyumbani hadi huku tulipo unapata kama kilomita si chini ya kumi na tano, huku kila mmoja akiwa, amechoka kwani hakuna ambaye alitarajia kukimbia umbali mrefu namna hii.Wakati wa kurudi Mzee Calto akatupakiza kwenye gari lake, huku Lilian na Priscar wakiwa hoi kupita maelezo.

    Baada ya kufika nyumba majira ya saa moja asubuhi, Mzee Calyto akatuamuru kwenda pembezoni mwa bahari kufanya mazoezi mengine ambayo kwetu sote ni mapya, kila mmoja akawa na kazi ya kulalamika kuchoka kupita malelo, huku Lilian akishindwa kustahimili hadi ikafikia hatua akaanza kumwagikwa na machozi, ila Mzee Calyto hakumuonea huruma hata kidogo.

    Mazoezi ya viungo yakaendela kwa siku saba mvululizo hadi tukawa tumeyazoea, hata umbali wa kukimbia ukawa umezoeleka, tukaanza kufanya mazoezi mengine ya kuvamia kwa kutumia silaha nzito za kivita, kutokana sote ni wazoefu katika matumizi ya bunduki, hayakutuwia ugumu sana kuyaelewa, japo silaha nyingine za kivita ndio mara yatu ya kwanza kuzitumia katika maisha yatu, zoezi zima likatuchukua kadri ya siku tano tukawa tumesha maliza, na kuhamia kwenye mazoezi mengine yanayo husiana na jinsi ya kuambana bila silaha

    Japo mzee Calyto ana umri mkubwa ila kusema kweli you fiti sana kwenye kuigana, mbinu zake zikazidi kutukomaza hata yale mavunzo ambayo niliyapaya nchini Iraq hayana maana sana, tukahamia kwenye mafunzo ambayo kila mmoja kwa mara ya kwanza tulivyo ambiwa na mzee Calyto tukaona hana nia nzuri kwenye maisha yetu

    “Ni lazima mufanye, sio ombi ni amri”

    Mzee Calyto alizungumza huku akitutizama, muda mchache kabla ya kumaliza kula chakula cha usiku.Kama kawaida asubuhi na mapema, tukaamka, na kuingia kwenye helcoptar ya Mzee Calypto.Akaipaisha juu sana na kuelekea kwenye kina kirefu cha bahari,

    “Kila mmoja awe tayari, kuruka kwako vibaya ndio kutakua wewe maumivu au kufa, mutakuwa munaifwatisha hii chopa yangu, ukizubaa utapotea baharini, Tumeelewana”

    Mzee Calyto alizungumza kwa sauti kubwa, na kila mmoja aaliyasikia maelekezo yake vizuri na hapakuwa na aliyekuwa na swali

    “Nahesabu mpaka tatu muwe mumesha ruka, Sawa”

    “Ndio”

    Nilijibu peke yangu, ila Lilian na Priscar haku ambaye alijibu chochote zaidi ya sote kutazama machoni.Mzee Calyto akaanza kuhesaba kwa sauti ya juu, hadi inafika tatu, Priscar akawa wa kanza kujitosa kwenye maji, akafwatia Lilian kisha nikamalizia mimi kuruka, kusema kweli upepo mkali ukanifanya, nishindwe kupumua vizuri, kufumba na kufumbua nikajikuta nikiwa nimedumbukia kwenye maji ya bahari na kwenda chini kwa umbali kiasi, nikuulegeza mwili wangu, kumbukumbu za siku tuliyo pata ajali ya ndege ya abiria ikaanza kunijia kichwani mwangu kwa kasi sana.

    “Nikiwa mjinga nitakufa”

    Nilizungumza kimoyo moyo, kwa haraka nikaanza kuogelea kwenda juu, hadi nikatokeza kwenye kina cha bahari, nikawaona Lilian na Priscar wakiwa wanaifwata helcoptar ya Mzee Calyto inapo elekea.Nikaanza kuogelea kwa haraka na mimi, kutokana na mazoezi ya kukimbia, sana, yamenisaidia kutengeneza pumzi ambayo, inanisaidia sana kwenye kuogelea.Ikatuchukua zaidi ya dakika arobaini na tano kufika ukingoni mwa bahari, sote tukiwa hoi sana

    “Ahaa kudadadeki, huyu mzee atatuua”

    Nilizungumza huku nikiwa nimejilaza kwenye, mchanga nikitazama jua linalo nipiga usoni, huku nikihema sana.

    “Hongereni, mumebakisha zoezi moja, ambalo mukifanikiwa katika hilo basi hata nyinyi mutafanikiwa kwenye kazi yetu”

    Mzee Calyto alizungumza dakika chache baada ya kumaliza kula chakula cha usiku.

    “Linaanza lini?”

    “Kesho ni jumamosi, ninawapa mapumziko, muende mjini mukatembee ila jumatatu kama kawaida”

    “Ndio mzee”

    Kila mtu akaingia kwenye chumba chake, asubuhi tukafanya mazoezi ya kawaida kuvieka vingo vyetu sawa, mchana tukapata chakula na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kufanya matembezi katika sehemu ambayo tutaiona sisi inatufaa.Kila mtu akavalia nguo ambayo inampendaza kila akijitazama, nikachukua bastola zangu mbili moja nikaichomeka kiunoni na nyingine nikaichomeka kwenye kiatu changu aina ya ‘Travota nilicho kivalia na jinsi nyeusi, pamoja na setwa jeusi lenye kofia juu.

    “Eddy endesha gari basi”

    Lilian alizungumza huku akinirushia funguo ya gari aina ya Ford, ambayo ni mali ya mzee Calyto.Sote watatu tukaingia ndani ya gari na safari ikaanza, huku nikifwata maelekezo ya Lilian ni wapi nielekee,kutokana mwenzetu ni mwenyeji sana katika mji huu.Tukaingia kwenye moja ya Clabu, na kutafuta sehemu iliyo na kigiza na kukaa.

    “Liliy mbona macho yapo juu juu, unatafuta nini?”

    Nilimuuliza Lilian baada ya kumuona kutazama tazama kila pande, ya ukumbi sikujua anatafuta kitu gani



    “Ahaa kuna kitu natafuta”

    “Kitu gani?”

    “Niakuambia”

    Priscar akawa na kazi ya kusikiliza miziki kwenye kiredia kidogo aina ya ‘MP3 Player’ kwa kutumia ‘earphone’.Lilian akamuita muhudumu na kumnong’oneza, pasipo sisi kusikia, muhudumu akanyoosha mkono kwenye mlango mmoja na Lilian akatingisha kichwa na kutoa noti ya dola mia na kumkabidhi muhudumu, na akaondoka

    “Umema ya nini?”

    “Ahaaa, hakuna kitu”

    Nikaanza kupata mashaka na Lilian kwa maana, tangu tuingie kwenye ukumbii huu wa starehe hajatulia kabisa

    “Nakuja”

    Lilia akatuaga na kuondoka na kuingia kwenye mlango ambao, muhudumu alimuelekeza.Nikamchomoa Prisar earphone moja ya sikio la kushoto

    “Hivi unamuelewa Lilian kweli?”

    “Kwa nini?”

    “Wewe hujamuana, jinsi alivyo kuwa humu tangu tuingie?”

    “Mbona hiyo ni kawaida tuu, labda mziki umemchanganya?”

    “Unasilaha?”

    “Ndio”

    Tukaendelea kunywa vinywaji taratibu huku nikiwa na kizi ya kuutazama mlango ambao Lilian ameingia, nikatazama saa yangu ya mkoni na kugundua zimepita dakika thelathini tangu Lilian kuingia kwenye mlango alio elekezwa na muhudumu.

    “P, nilinde”

    Nilizungumza huku nikinyanyuka

    “Eheee, unasema?”

    Priscar alizungumza huku akivua earphone moja kwenye sikio lake akionekana kuto kusikia nilicho kizungumza

    “Nimekuambia nilinde, ninakwenda kwenye ule mlango pale sawa?”

    “Powaa”

    Priscar alijibu kwa sauti ya juu, nikapiga hatua hadi kwenye mlango, nikatazama pande zote za ukumbi hapakuwa na mtu ambaye ananifwatilia kila mmoja alikuwa bize kwa mabo yake, wengine wakicheza mziki.Nikavungua mlango taratibu na kuingia, nikakutana na ngazi zakupanda kwenda juu, nikaichomoa bastola yangu ya kiunoni na kuanza kupanda kwenda juu taratibu kwa umakiki wa hali ya juu.Nikakuta kordo ndefu yenye vyumba vingi, nikajikuta nikishusha pumzi nyingi kwani sikujua Lilian ameingia kwenye gani.Nikaanza kupiga hatua kwenda mbele, uzuri wa vyumba hivi vinamapazia tu na hakuna milango, kila chumba kina watu wakifanya mapenzi, nikawa na shughuli ya kuchungulia chumba kimoja baada ya kingine, hadi ninafika chumba cha kumi na moja nikamkuta Lilian akiwa amejilaza kwenye sofa, huku meza iliyopo pembeni ya sofa hilo kukiwa na pakti ya madawa ya kulevya

    “Shitii”

    Nilizungumza huku nikiachia mshunyo mkali, nikaingia na kumstua Liliana kutokana amepitiwa na usingizi mzito, nikamtingisha hadi akazinduka kutoka usingizini, japo amelewa sana kupita maelezo.Nikaichomeka bastola yangu kiunoni na kumnyanua Lilian na kumuweka begeni

    “Eddy”

    “Nini”

    “Umekasirika”

    “Hembu funga domo lako”

    “Niambie basi mpenzi wangu, unanipenda kweli?”

    Lilian aliendelea kuropoka, maneno yaliyo nikera sana.Gafla nikastukia Lilian akiichomoa bastola yangu ya kiunoni, nikasikia milio miwili ya risasi mgonini mwangu, ikanibidi kugeuka kwa haraka, Lilian akaruka kutoka mgongoni mwangu, nikawashuhudia jamaa wawili walio kuwa na bundiki wakiwa wameanguka chini, baada ya kupigwa risasi na Lilian.Kelele za wasichana waliokuwa kwenye vyumnba wakiwashuhulikia wateja wao, zikaanza kusikika, wakatoka jamaa wengine pembeni ya mlango ambao nimesimama wakiwa na bunduki huku wakiwa hawana nguo hata moja kwenye miili yao, nikafanya chumba

    shambulizi moja la haraka kwa kuwapiga mateka kwenye mikono yao na kuziangusha bunduki zao, Wakiwa wanaendelea kushangaa, Lilian akawazawadia kila mmoja risasi ya kichwa na wakaanguka chini.

    Tukaanza kukimbia kueleka chini, kwenye ngazi tukakutana na Priscar akiandishwa kwa haraka, alivyo tuona tu, tukastukia akichomoa bastola yake na kutuekezea na kufyatua risasi, iliyo pita kati yetu mimi na Lilian, na kusikia kishindo nyuma yetu mtu akianguka.Tukageuka na kukuta jamaa, kikiwa linavuja damu mwilini mwake

    “Unashabaha nzuri”

    Lilian alimsifu Priscar na sote tukaanza kushuka kwa haraka, ukumbini tukakuta watu wakichanguna na kuminyana kuwahi kutoka nje ya ukumbi baada ya kusikia milio ya risasi.Tukaminyana kutoka mlangoni na kufanikiwa, kutoka salama salimi, tukafika kwenye maegesho ya gari letu na kuondoka kwa kasi

    “Mupo sawa?”

    “Ndio”

    Tukafika nyumbani, kila mmoja akaingia kwenye chumba chake na kulala.Jumatatu asubuhi, kama kawaida yetu tukafanya mazoezi ya kunyoosha viungo.Mzee Calyto akatupa kila mmoja kisu chake, na kutuomba tuache bunduki zetu, tukaingia kwenye gari lake na kuanza safari ya kwenda tusipo pajua.Akasimamisha gari lake kwenye kibao kimoja cha msitu mkubwa, kilicho andikwa ‘NYAMANA FOREST, DANGEROUS ANIMAL’(MSITU WA NYAMANA, WANYAMA WAKALI)

    Mzee Calyto akatoa karatasi moja gumu na kulifungua, na sote ndio tukatambua kwamba ni ramani, akaliweka juu ya boneti ya gari lake na kuanza kutuelekeza, kitu kimoja baada ya kingine, na sote tukawa tumeelewa alicho tuelekeza

    “Kumbukeni, huu msitu una simba, chatu, chui, na wanyama wengine wakali, umakini wenu na uhodari wenu, utawaokoa kutoka ndani ya huu msitu, kwa kawaida munakaa siku mbili zaidi ya hao ninaimani mutakuwa wote MUMEKUFA.”

    Mzee Calyto alizungumza huku akitutizama machoni

    “Babu chakula je?”

    “Kuna matinda, mito, kumbukeni nilicho waelekeza kwenye ramani muweze kutoka salama, nawatakia safari njema, nendeni sasa”

    Sote tukawa tumebaki tumesimama kama masanamu, yanayo subiri kuamrishwa, japo tumeamrishwa ila wasiwasi ulianza kuonekana machoni kwa kila mmoja wetu.Tukakumbatiana kwa pamoja kisha tukaanza kutembea kuingia kwenye msitu, huku sote tukiwa makini, na visu vyetu vikiwa mikononi.Kadri tunavyo songa mbele ndivyo giza lilivyo anza kutawala anga, kila sehemu ambayo tulikuta matunda hatukusita kuchuma kuyapoza matumbo yetu yaliyo tawaliwa na njaa.Giza likatanda agani, cha kumshukuru Mungu, mwanga wa mbalamwezi, utatusaidia kwa kiasi kikubwa kusonga mbele,

    “Jamani tupumziken, tumetembea sana”

    Priscar alizungumza huku akionekana kuchoka sana

    “Powaa”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Lily saa yako inaonyesha ni saa ngapi?”

    Lilian akaminya saa yake inayo toa mwanga, nikamuona akinyong’onyea na sura yake kuzidi kupoteza matumaini

    “Ndio kwanza saa nne na robo”

    Kabla sijazungumza kitu chochote, tukaanza kusikia mngurumo wa mnyama ambaye sikuwahi kuisikia sauti yake kwenye maisha yangu

    “Shiiii, huyo ni anaconda, tena hapo yupo na mwanaye”

    Lilian alizungumza kwa sauti ya chini sana, nikajikuta hofu ikianza kunitawala kwani, nyoka aina ya anaconda nimezoea kuwaon kwenye filamu tuu, sasa leo ninakutana naye.Tukaegemeana migongo, na kutengeneza engo ya pembe tatu, huku kila mmoja akiwa na kazi ya kutazama upende wake, tuakaendelea kuisilizia sauti ya joka hilo alilo tueleza Lilian ila halikutokea, na baada ya muda sauti hiyo ikapotea masikioni mwetu.Hatukuwa na sababu ya kupumzika tena kwenye eneo hili, ikatulazimu kwenda mbele, kuepuka hatari ya wanyama wakali.Hadi inafika saa kumi na moja alfajiri tunamshukuru Mungu hatujakutana na kitu cha aina yoyote kibaya, kidogo tukapata nafasi ya kupumzika

    “Jamani kuna bwawa pale ngoja nikanywe maji, ninakiu sana”

    Priscar alizungumza huku akinyanyuka na kwenda kunywa maji, kwa mwendo mrefu Lilian amechoka kupita maelezo, Gafla tukasikia kelele za Priscar zikitokea kwenye bwawa, nilipo yahamishia macho yangu sehemu alipo, sikumuona, na kelele zake zinaishia kwenye maji.Tukasimama kwa haraka na kwenda alipo zama Priscar.Kitu kilicho tustusha zaidi ni baada ya kuona damu zikianza kuelea juu ya maji na hatukujua ni kitu gani kilicho mchukua Priscar, nikataka kujirusha ndani ya maji ila Lilian akanizuia

    “Na wewe unataka kwenda kufa ndani ya hayo maji?”

    “Mwenzetu si umemuona amezama?”

    “Hata kama ila unatakiwa kuwa makini, kama yeye kazama na wewe unataka kwenda, unajua anechukuliwa na kitu gani hadi na wewe uende”

    Lilian alizungumza hukua akiendelea kunishikilia mkono wangu, maji ya eneo zima yakawa yamebadilika rangi na kuwa mekundu, jambo lililo anza kunitia simanzi na kuamini kwamba tayari tumesha mpoteza Priscar

    ”Eddy hatuna haya ya kuendelea kukaa hapa, tuondoke zetu”

    “Ngoja kwanza”

    Nikaendela kuyatazama maji, ila nafsi moja ikawa inasita kuondoka katika eneo hili, nikachomoa kishu changu, na kuanza kupiga hatua za kuingia kwenye maji, kabla sijafika haya maji na kifuani nikastukia kuhisi kittu kikisimama nyuma yangu, nikageuka haraka sana na kumkuta Priscar akiwa analivuta joka kubwa alilo lipasua maeneo ya tumboni mwake

    “Eddy njoo unasaidie kuvuta hili jidude”

    Tuakasaidiana kulivuta jijoka hadi nje ya maji, mimi na Lilian tukabaki tukimshangaa Priscar kwa tukio alilo lifanya

    “Ahaaa lile zoezi la kuogelea limenisaidia sana”

    Priscar alizungumza huku akilikanyaga jijoka hili linalo tisha sana kwa muonekano wake

    “Umeliuaje uaje?” Lilian alimuuliza swala Priscar

    “Pale nilipokuwa ninapiga kelele ndipo lilipokuwa limemichapa na mkia wake, na kunizamisha ndani ya maji, kila lilipokuwa linakaribu kuniviringisha, nikawa ninalichoma kwa kishu na kufanikiwa kulipasua tumo lake”

    Priscar alizungumza kwa kujiamini, nikatafuta kamti na kukachonga vizuri, nikakikata kichwa cha joka hilo na kukichoma na mti, na kuendelea na safri yetu huku tukifwata malekezo ya Mzee Calyto.Mchana kutwa tukaendelea na safari yetu hadi tukafanikiwa kutoka upande wa pili wa msitu ambapo, tukakuta kijiji kidogo kiasi.Kila walipo tuona, wakabaki wakitushangaa haswa mimi niliye beba kichwa cha joka hili.Tukaiona gari ya mzee Calyto ikiwa imesimama nje ya kijai Motel kimoja.Kelele za watu kutushangilia pasipo kuelewa wanacho kishangilia haswa ni nini, zikawafanya watu waliopo ndani ya kijimotel hicho kuytoka nakuanza kushangaa.

    Hata mzee Calyto mwenyewe akabaki akiwa anatushangaa, akatufwata na kutukumbatia kwa pamoja

    “Hongereni sana”

    “Asante babu”

    Lilian akawa wa kwanza kujibu, wakatukaribisha ndani ya kijimotel

    “Sijaamini kama mutarudi siku hii, mawazo yangu nilijua mutarudi kesho mchana tena mukiwa pungufu”

    “Pungufu kwa nini babu?”

    “Hilo joka mulilo liua limeleta shida sana kwa vinana ambao wanachukua mafunzo kama yeni”

    Mzee Calyto alizungumza huku wanakijiji wakiwa wanatutizama, wakituzingira sehemu tuliyo kaa huku kila mmoja akizungumza lake kwa kunong’oneza na mwenzake.Wanakijiji hawakusita kuonyesha furaha yao waliyo kuwa nayo juu yetu.Wakaamua kutufanyia sherehe ndogo, usiku kucha, asubuji na mapema tukarudi nyumbani kwa Mzee Caltyto.Tukaanza kazi moja ya kukusanya data za sehemu zote walipo watu walio husika katika mauaji ya mke wangu na familia yake. Kwa msaada wa rafiki wa mzee Calyto waliopo nchini Somalia wakaweza kutupatia, na kutuambia kwamba kundi hilo lipo katika mji uitwao Kismayo pembezoni mwa bahari ya India.Tukajiandaa kwa kila kitu, tukakusanya silaha za kutosha na kuziweka ndani ya boti ya kwenda kwa masafa mrefu, inayo milikiwa na Mzee Caltyto, ambayo alizawadiwa na shirika la kijasusi CIA baaya ya kumaliza kipindi cha utumisha kazini.

    “Nawatakia safari njema, na tuwe tunawasilianakwa kila hatua ambayo mutakuwa munapiga”

    Mzee Calyto alizungumza huku akitukumbatia mmoja baada ya mwengine akionekana kujawa na huzuri ambayo hata sisi wenyewe ilianza kututawala



    “Sawa mzee”

    Tukampigia saluti kwa ishara ya kumuaga, na sote tukaingia kwenye boti, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu tulicho ishi na mzee Calyto ilitokea kumzoe kama babu yetu, na hakusit kutueleza siri nyingi za nchi mbalimbali katika maswala ya kijasusi ikiwemo Tanzania, ambapo alidai alisha wahi kufanya kazi katika ubalozi wa Marekani baada ya mashambulizi ya balozi za Marekani zilizopo mashariki mwa Afrika, kutoka katika kikundi cha Al-Khaida.Kutokana Lilian anajuzi wa kuendesha boti, akawa ndio nahodha wetu katika safari nzima kutoka bahari ya Atlantic, kaskazini mwa bara la Amerika hadi bahari ya Hindi.Nisafari iliyo tuchukua takribani wiki moja, kutokana na umbali, na kuvizia kupita kwenye badhi ya nchi, kwenye ukanda wa bahari zao usiku wa manene.Tukafanikiwa kufika nchini Somalia, na hadi tunafika kwenye mji wa Kismayo yapata saa saba usiku, kwa usalama zaidi tukaisimamisha boti yetu mbali kidogo kutoka ulipo mji, tukavaa mavazi maaluu ya kuingilia ndani ya maji, yenye mitungi ya gesi itakayo tusaidia kuhema ndani ya maji.Tukabeba silaha zetu zote na kuzama ndani ya maji na kuogelea hadu ufukweni.Tukapokelewa na mmoja wa marafiki zake mzaa Calyto tuliye kuwa tunazungumza naye kwa kupitia simu, na alituambia ni miongoni mwa wanafunzi wake katika maswala ya kikomandoo na yeye anafanya kazi katika jeshi la Somalia,

    “Karibuni kwa jina ninaitwa bwana, Ally Sadick”

    Alijitmbulisha na sisi tukajitambulisha kwake na akatupeleka nyumbani kwake, kwa siri sana pasipo watu kutuoa, ambapo anaishi na mkewe pamoja na mwanaye wa kike mwenye umri wa miaka saba.Hatukulala na akaanza kutuonyesha ramani ya sehemu walipo watu wa mama Caro.Pamoja na picha za majengo ya sehemu ya sehemu walipo

    “Aisee hiyo kambi mbona ipo kama sinagogi?”

    Niliuliza huku nikiwa nimeishika picha inayo onyesha kambi hiyo kwa juu kwani, kambi hiyo imejengwa majumba yapatayo kumi ya kifahari

    “Ahaa yule mama anapesa chafu, amemwaga pesa katika kuijenga hiyo kambi, watu wake wakifanya matukio huku wanakuja kukimbilia hapo?” “Kwa haraka haraka ina watu kama wangapi?”

    “Kama hamsini hivi, kutoka mataifa mbali mbali”

    “Kwa nini, serikali haiwakamati watu kama hawa?”

    Nilimuuliza swali baada ya kumaliza kuelekezwa

    “Ahaaa ukiwakamata leo kesho wanaachiwa, ukichunguza sana utaona kuna ukiritimba ndani yake”

    “Ahaa”

    “Ndio hivyo, yaani sisi tunafanya kazi kwa shinikiza sana, kwamaana unaweza kujua mtu fulani amehusika na mauaji ya watu au mtu fulani, ila ukitaka kwenda kumkamata utakuta viongozi wanao mlinda yule mtu wanakujia juu, na usipo kuwa makini wanaweza hata kukuua na wewe mwenyewe”

    “Mmmm kwahiyo nyinyi munaishije, katika utendaji wenu wa kazi?”

    Lilian aliMuliza swali Ally

    “Hivyo hivyo tu ndio maana vikundi vya kigaidi kila siku vinazidi kuongezeka”

    “Poleni sana” “Asante na kama tunakwenda kuvamia kikundi hicho cha magaidi, basi inatupasa kufanya shambulizi zito litakalo wafanya waweze, kuteketea kirahisi”

    Tukaanza kupanga mipango ya jinsi ya kuivamia kambi hiyo, ya mama Caro ambaye kwa sasa ni raisi.Tukamaliza kupanga tulicho kiamua kupanga, hada asubuhi, ndipo tukajipumzisha, huku tukilindana zamu kwa zamu, ili kuutoa uchovu wa usingizi.Mida ya saa moja kamili usiku tukapata chakula cha kuyaweka matumbo sawa, na kama tulivyo panga, Lilian na Priscar wakavaa nguo za kiraia, kama wanazo vaa wasichana wanao jiuza kisha na sisi tukabeba mabegi yetu yenye silaha za kutosha ikiwemo na mabomu ya kutega pamoja na mabomo ya kurusha kwa mkono.

    Lilian na Priscar wakatangulia kwenye clubu moja ambayo ipo karibu sana na kambi hiyo ya watu wa mama Caro, huku wakiwa wamevaa vifaa maalumu vya wasasiliano, ambavyo nivyakupachika kwenye sikio, na ningumu sana kwa mtu kuviona, hii ni kutokana na nywele zao kuwa ni ndefu sana.

    “Tumesha fika”

    Lilian alatutaarifu kupitia vifaa hivyo vya kunasa sauti, ambavyo hata sisi tunavyo tumevivaa kwenye masikio yetu.

    “Powa sisi tupo njiani tunakaribia kufika kwenye kambi” “Priscar amapata askari mmoja nahisi ni mkuu wao, naona anashikwa shikwa” “Haaa kuweni makini”

    “Powa”

    Mimi na Ally tukafika kwenye kuta ya kambi hii iliyo jengwa kwa umahiri mkubwa mithili ya gereza la wafungu.Tukawa na kazi ya uparamia ukuta kwa kutumia vivaa tulivyo vaa mikonino na miguuni, vyenye ncha kali za kuweza kunasa kwenye ukuta pasipo kuanguka.Tukatumia dakika, mbili kupanda ukuta na kushukia ndani pasipo mtu yoyote kutuona

    “Tupo ndani?”

    Niliwajulisha Lilian na Priscar na kuwasikia wakizungumza na wanaume hao wanao zungumza lugha ya kingereza, tukaanza kazi ya kutega mabomu jengo moja bada ya jingine, hadi tukamaliza majumba yote kumi.

    “Tupo ndani”

    Niliisikia sauti ya Lilian ikitupa taarifa sote

    “Tuna dakika kumi na tano kutoka kabla majengo hayajalipuka”

    “Tumekupata”

    Lilian na Priscar kila mmoja alijibu kwa muda wake.Tukawa makini sana katika kucheza na saa zetu za mikononi kuangalia muda jinsi unavyo kwenda kwani tukichelewa tunaweza kuwa miongoni mwa watakao lipuka katika mabomu tuliyo yatege

    “Nimemuua mmoja wao”

    Priscar alizungumza, baada ya kukamilisha kazi ya kumuua mmoja wa watu alio kua nao.

    “Nice”

    Mimi na Ally tukaanza kazi ya kuwanyonga mlizi mmoja baada ya mwengine, pasipo wao kujistukia

    “Dakika kumi zimesalia”

    Nilitoa taarifa kwa Lilian na Priscar

    “Nimemaliza, ila limenisumbua hilo”

    Lilian alizungumza na kunifanya nitabasamu.Tukawaelekeza sehemu tulipo na kuwakabithi nguo za kuvaa ambazo ni zakijeshi hadi tukavaa kwa pamoja.Zimesalia dakika dato kabla ya mabumu kulipuka, wezangu wakaanza kupanda ukuta kama jinsi tulivyo ingia.Kabla sijapanda ukuta nikasikia sauti ya mtoto mchanga akilia kwenye moja ya dirisha, nikapiga hatua za haraka kwenda kuchungulia na kukuta mmto wa miezi kama sita au saba akiwa kwenye moja ya kitanda huku mama yake akifanya mapenzi na jamaa, nikataka kuondoka ila nafsi ikasita

    “Eddy tuondoke, unafanya nini huko ndani?”

    Lilian alizungumza

    “Ngoja kunaishu ninafanya, tangulieni ninakuja”

    Nikatazama saa yangu ya mkononi na kuona zimesalia dakika tatu kwa mabumu kulipuka, kutokana dirisha halina nondo, limetengenezwa kwa viooo tu ikanilazimu kutoa bastola yangu na kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti, kitu cha kwanza kukifanya ni kufyatua risasi zilizotua kwenye mwili wa jamaa, nikakikumba kioo na kuingia ndani na kumfanya msichana huyo kuanza kupiga kelele.Sikua na haja ya mama yake, nikamnyanyua mtoto na kumkumbatia mama mtu akachomoa bastola chini ya mto, kabla hajafanya chochote nikampiga risasi mbili za kifuani, na kusababisha kufyatua risasi moja pembeni, iliyo toa mlio mkubwa.Nikatokea na dirishani, kutokana mtoto nimembeba na khang yake aliyokuwa amefunikiwa, nikamfunga mbele ya kifua changu

    Zimesalia sekunde hamsini kabla mabomu hayajaanza kulipukua, nikaanza kusikia milio ya risasi ikitokea kwenye chumba ambacho nimemchukua mtoto, mchanga anaye endelea kunililia kifuani kwangu.Nikaanza kupambana na jamaa, ambao mlio wa bastola ndio uliwastua.Nikaiona pikipiki aina ya Honda ikiwa imeegeshwa pembeni ya mlango wa kuingilia kwenye jumba nililo muiba mtoto.Nikaikimbilia kwa haraka cha kushukuru Mungu, nimeikuta na funguo, nikaiwasha na kuanza kulilenga geti la kuingilia kweye jumba hili la kifahari, huku nikiendelea kupambana na askari hawa wanao stuka sasa hivi.

    Milipuko ya mabomu ikaanza kulipuka kwenye majumba moja baada ya jingine, nikazidi kuvuta mafuta ya pikipiki hadi kulifikia geti na kwabahati nzuri nikakuta lipo wazi, upenyo unaoweza kupitisha pikipiki, nilicho kifanya ni kukanyaga breki ya tairi ya nyuma, na tairi ikaanza kuserereka na kuniwia urahisi kupenya kwenye upenyo huo wa geti ulio kaa upande.Hadi ninafanikiwa kutoka kwenye geti, ninamshukuru Mungu hapakuwa na risasi hata moja iliyo nipiga mimi na mtoto niliye mbeba

    “Mupo wapi?”

    Niliwasiliana na kina Lilian wakaniambia sehemu nilipo, kambi ya watu wa mama Caro ikazidi kuteketea kwa moto mkali, huku kuta zake zikishuka na kudondoka chini.Nikawakuta Ally wakinisubiri

    “Eddy na huyo mtoto vipi?”

    Lilian akawa wa kwanza kuniuliza swali

    “Nimemuokoa”

    “Kazuri hako”

    Nikamkabithi mtoto Priscar na wao wakatangulia na gari na mimi nikawa na kazi ya kuwafwata kwa nyuma.Mapigo ya moyo yakaanza kuniaenda mbio baada ya kukuta myumba ya Ally ikiteketea kwa moto, ikionekana kuna shambulizi lililo fanywa dakika chache zilizo pita

    “Shiti”

    Nikaaiachia pikipiki na kuruka pembeni, nikachomoa bastola yangu na kujiweka tayari kwa shambulizi.Ally akachomoka haraka ndani ya gari baada ya kuisimamisha na kutaka kukimbilia ndani ya nyumba yake ila nikamuwahi kumzuia

    “Kuna mke wangu humu ndani na mwanangu niache”

    “Ally tulia, huwezi kufanya chochote sawa”

    “Eddy nimekuambia niache”

    Ally akanipiga kisukusuku cha tumbo na kunifanya nimuachie, kabla hajafika mbali na mimi nikamrukia na kumdaka mguu na kumzuia asiende sehemu yoyote.

    “Tulia wewe, utakwenda kufa huko ndani, si unaona nyumba imesha teketea”

    Ally hakutaka kunisikia, akaanza kunipiga mateke kwa mguu ambao sijamdaka, ikanilazimu na mimi kujibu mashambulizi yake, na nikafanikiwa kumuwahi kupiga kabali, iliyo anza kumtuliza taratibu hadi akatulia

    “Eddy utamuua mwenzio hembu muchie” Lilian alinivuta, mikono yangu baada ya kumuona Ally ametulia kimya baada ya kumkaba sana.Nikamuachia Ally, huku nikihema na jasho jingi likinimwagika.Nikamvuta hadi kwenye gari, na kumlaza nyuma ya siti ya gari akiwa amepoteza fahamu.Sote hatukujua ni nani, aliye husika na maangamizi ya familia ya Ally

    “Ingieni kwenye gari?”

    Nilizungumza huku nikifungua mlango wa gari, upande wa dereva

    “Eddy hembu subiri mara moja”

    Priscar alizungumza huku akitazama kwenye kichaka kimoja, akamuweka mtoto kwenye siti ya gari na kuichomoa bastola yake, sote tukawa makini kutazama, kwenye kichaka hicho, ambapo kuna watu wawili walio jificha.Priscar akawaamrisha watu hao kutoka kwenye kichaka kwa kutumia lugha ya kisomali.Wakasimama na ndipo tukagundua kwamba ni mke na mtoto wa Ally.Tukawaingiza ndani ya gari yetu aina ya Randrover na kuondoka katika eneo la yumba ya Ally

    ***

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tukakodi vyumba viwili kwenye Hotel moja ya kitalii yenye, kwa kutumia mngongo wa Ally, kwa kitambulisho chake cha ujasusi.

    “Ally hivi unahisi ni nani atakuwa ni muhusika kwenye, jaribio la kuiteketeza familia yako”

    “Watakuwa ni Al-Shabab, hii nikitokana na mahojiano niliyo yafanya na mke wangu.”

    “Kisa kitakuwa ni nini, hadi wakufanyie hivi?”

    “Ni maswala ya kazi kwa maana ni siku nyingi wananitafuta kuniangamiza”

    Tukajikuta tukinyamaza na macho yatu tukiyahamishia kwenye Tv iliyopo chumbani kwetu.Ikizungumzia kuteketea kwa jengo la watalii tulilo liteketeza jana usiku

    “Unaona ujinga wa hii nchi, wanasema kwamba ni jengo la kitalii wakati ni kambi ya magaidi”

    Ally alizungumza kwa hasira kubwa huku akiitazama Tv.Kitu kingine kilicho niacha hoi ni baada ya kusikia kwamba raisi wa Tanzania ambaye ni mama Caro ametuma salamu za rambirambi kwa nchi ya Somalia

    “Itanibidi kwenda Tanzania”

    “Kufanyaje?” “Kuna kazi nitakwenda kuifanya mara moja kisha ndio nirudi huku Somalia”

    “Sawa, tungeende wote ila hali ya usalama wangu na familia yangu ni mdogo sana”

    “Usijali kwa hilo”

    Nikawajulisha Lilian na Priscar juu ya safari yangu ya kwenda nchini Tanzania, na kila mmoja akawa tayari ya kuungana na mimi kwenda nchini Tanzania





    “Priscar itabidi ubaki na mtoto”

    “Eddy namjua mama Caro A to Z kwahiyo, nitabidi twende sote”

    Sikuwa na jinsi yakuwakubalia wote wawilikatika kuendelea na kazi yetu ya kuwaangamiza wale wote walio nifanyia mabaya juu yangu, Tukamuachia Ally mtoto wa kike ambaye nilimuuokoa kwenye kambi tuliyo ivamia

    “Sasa huyo mtoto ni muite jina gani?”

    Ally aliniuliza baada ya kumkabithi mtoto ambaye kwa sasa ni mali yangu

    “Muite Xaviela”

    “Sawa muheshimiwa” Tukaondoka na kumuacha Ally na familia yake hotelini na sisi tukaondoka muda wa usiku hadi sehemu tulipo acha boti yetu huku tukiwa na kiasi cha kutosha cha pesa tulizo toka nazo Uingereza, ikatulazimu kuogelea pasipo kutimia nguo maalimu za kuogelea kutokana zimeungua kwenye nyumba ya Ally, katika vyumba tulipo kuwa tumezihifadhi.Tukaikuta boti yetu kama tulivyo iacha na safari ya kwenda Tanzania ikaanza usiku kucha na tukafika pwani ya Tanga salama majira ya saa kumi na moja asubuhi pasipo kukamatwa, tukaiacha boti yetu umbali mrefu kidogo ulipo usawa wa bahari na kuingia nchi kavu

    “Nashukuru Mungu kwa kufika nyumbani kwa mara nyingine tena”

    Nilizungumza kimoyo moyo, tukaanza safari kwa kutembea kwa miguu hadi kwenye kituo cha daladala za mwambani.Tukapanda dalala hadi stendi kuu ya mkoa wa Tanga na kupanda basi hada jijini Dar es Salaam na kufika majira ya jioni, tukachukua chumba kwenye moja ya Hotel ya bei ya kawaida, kuepuka kujiweka karibu sana na polisi, japo tumevaa nguo za kirai, ila muda wote tulikuwa makini kwani mabegi yetu yana silaha na vifaa vya maangamizi.

    “Kazi iliyopo mbele yetu ni ngumu sana, na tutambua ya kwamba hili tunalo kwenda kulifanya ni jambo ambalo litatuwia ugumu kwenye maisha yetu, pale tu ambapo tutakamatwaa”

    Nilizungumza huku nikiwatazama Priscar na Lilian walio kaa kwenye kitanda mara baada ya kupata chakula cha jioni

    “Najua tumeshirikiana pamoja, ila katika hili ninaomba ushirikiano wa kumchunguza mama Caro, jinsi ratia yake inavyo kwenda ila katika hayo mengine niachieni mimi mwenye, sitaki muingie kwenye mkono wa serikali”

    “Eddy ni kwanini unazungumza hivyo?” Lilian aliniuliza

    “Ni kazi hatari sana, kazi ya kumuua raisi ni ngumu sana, ila nilazima afe tuu.Ila nitakapo hitaji msaada wenu nitawaambia”

    “Sawaa”

    Siku ya pili ikawa ni siku ya Lilian na Priscar kutoka nje ya hoteli na kwenda kufanya upelelezi wa maisha mazima ya raisi ila mimi, sikutaka hata sura yangu ionekane nje kuofia usalama wangu, kwani ninatambua mama Caro mkono wake ni mrefu sana.Muda wa jioni Priscar na Lilian wakarudi wakiwa na tabasamu katika sura zao

    “Eddy kazi nahisi itakuwa ni rahisi kwako”

    Lilian alianza kuzungumza baada ya kukaa

    “Kwa nini?”

    “Wiki ijayo ni harusi ya mtoto wa raisi”

    Lilian akanirushia gazeti lenye taarifa hiyo, nikaisoma kwa umakini na kutambua ni wapi harusi hiyo inapo fungwa na siku yake ya sherehe.

    “Eddy katika siku hiyo, sisi tutakusaidia kutika ulinzi wako tu”

    Priscar alizungumza kwa kujiamini jambo lililo nifanya nifarijike sana moyoni mwangu.Tukawa na kazi ya kuhama hoteli moja kwenda hoteli nyingine kwa ajili ya usalama wetu binafsi na pia tusitiliwe mashaka na watu wanao tuona.Siku ya harusi ikawadia, ambayo ni jumamosi, jiji zima la Dar es Salaam limezizima kwa amani, huku story kubwa ikiwa ni harusi ya mtoto wa kike wa raisi.Ulinzi ulizidi kuhimarishwa kila kona ya jiji, huku viongozi mbali mbali wa nchi za jirani hadi na mbali wakija kushuhudia sherehe ya kiistoria nchini Tanzania.

    Suti aliyo nunulia Lilian siki mbili zilizo pita, maalumu ya siku hii, nikaivaa vizuri na kunikaa mwilini mwangu, na kuonekana mtu wa tofauti sana.Nikachukua bastola yangu na kuichomeka kwenye soksi, kisha Priscar akachukua ndevu za bandia na kubandika, sehemu ya chini ya pua yangu(mustachi).Zilizo nibadilisha sana muonekako wangu wa sura

    “Eddy umebadilika sana”

    Priscar alizungumza huku akinichana nywele zangu ndefu kidogo.

    “Utasema yeye ni bwana harusi?”

    Lilian akaongezea neno lililo tufanya tucheke sote, japo Lilian anaasili ya kizungu ila maisha mikikimiki amayezoea sana.Lilian akanisogelea na kunipiga busu la mdomoni

    “Safari njema Eddy”

    “Asante”

    Priscar akanifwata na kunikumbatia huku akiachi tabasamu pana

    “Eddy pigania haki yako kwenye maisha yako, na hii pia iwe kwa ajili ya maisha yako na yamama yako aliye uawa na huyu mshenzi”

    “Sawa”

    Nikavaa miwani ndogo iliyo nifanya nionekane kama daktari, nikawakumbatia wote kwa pamoja, kisha nikawaachia nikafungua mlango na kuwaacha ndani, saa ya mkononi inanionyesha zimesalia dakika thelathini kabla ya harusi kuanza kwa maana gazeti na vyombo vyote vya habari nchini Tanzania viliutaarifu uma kwaba arusi inatarajia kuanza saa tisa na nusu kwenye moja ya kanisa kubwa lililopo maeneo ya kivukoni.Nikakodi bodaoda ya pikipiki, ili kuwahi kanisani, pia kuepuka foleni za magari.Nikafika kanisani zikiwa zimesalia dakika kumi, kila mtu ambaye anaingia getini anakaguliwa kwa kutumia mashine za maalumu zinazo weza kutambua kama mtu anaye ingia humo ana silaha au la

    Nikaona kundi la wapambe wa bwana, wakiwa wamesimama nje ya geti la kanisa wakisuburi kuwasili kwa bana harusi, cha kumshukuru Mungu, suti za rangi ya kijivu walizo zivaa, zinaendana na mimi, na hadi mashati pamoja na kiua kidogo kilichopo pembeni, ya koti la suti vimeendana.

    “Lilian alijua nini?”

    Nilijisemea kimoyo moyo, nikapiga hatua hadi sehemu walipo na kuwasalimia, na wote wakaitikia kwa furaha kwani kila mmoja, anafuraha kwenye moyo wake.Ndani ya dakika mbili gari la kifahari lililo pambwa vizuri, likasimama mbele yatu na wezangu wakanza kushangilia na mimi ikanilazimu kujichetua kama wao na kuanza kucheza, walinzi wakatufungulia geti na kutuacha wapambe wa bwana kupita hata bila kutukagua, na sura ya David ambaye ni bwana harusi nimesha iona kweny picha ni kati ya wale watu wangu ambao ninawatafuta kwa udi na uvumba.Nilipo fanikiwa kuingia ndani ya kanisa nikajidai nikitoa simu yangu mfukoni na kuachana nao waendelea kuruka ruka na bwana harusi wao.

    Meseji ikaingia kwenye simu yangu kutoka kwa Lilian

    (Hiyo suti nilikuchwagulia na sare za wapambe wa bwana harusi)

    Ikanibidi nicheke na kutafuta sehemu ya kukaa na nikapata kwenye benchi la katikati na kukaa mwanzoni mwa benchi hilo.Macho yangu yakatua kwa mama Caro aliye kaa mbele kabisa, pamoja na wanandugu wengine wakicheka na kufurahi

    Matarumbeta kutoka nyuma ya kanisa yakatufanya watu wote tugeuze shingo zetu na kutazama nyuma, nikashuhudia kundi kubwa la vijana wadogo wa kike wakiwa wamevalia magauni meupe, wakiwa na vijikapu vidogo na kazi yao ikiwa ni kurusha maua juu angani.Nyuma yao wamesimama wadada wakubwa wanne nao wakiwa wamevalia nguo nyeupe tupu, na nyuma yao nikamshuhudia Caro akiwa ameshikwa mkono na mzee mmoja wa makamo, na wakaanza kupiga hatua za taratibu kwenda mbele ya kanisa.Wapiga tarumbeta waliopo nyuma ya bibi harusi wakaendelea kupiga matarumbeta yao kwa nguvu kadri ya wanavyo weza ili mradi kuchangamsha kanisa

    Wakafika hadi mbele ya kanisa, ambapo mzee aliye mpeleka Caro akamkabidhi Caro kwa mume wake kisha mzee huyo akaenda kukaa karibu na mama Caro.Mchungaji akaanzisha ibada, na kutuomba tukae, Ibada ikazidi kwenda mbele, huku muda wangu wote nikiwa na kazi ya kuwatazama askari walio sambaa ndani ya kanisa huku wengine wakiwa wamevalia nguo za kiraia

    “Wapo wengi”

    Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kutazama kila upande kwa umakini, Caro na mume wake wakavishana pete, huku kila mmoja akionekana kumrithia mwenzake katika shida na raha, wakasaini vyeti vyao vya ndoa, na kutuonyesha wageni waalikwa na kusababisha shangwe na nderemo kuzidi kutawala kwenye kanisa.

    Baada ya muda maharusi wakaanza kutoka nje ya kanisa huku wakitanguliwa na wapambe wao kama walivyo ingia awali.Waalikwa wote tukanyanyuka na kuendelea kushangilia, macho yangu yote yakawa yapo kwa Mama Caro, nikapiga hatua za kumsogelea mama Caro, ambaye ametawaliwa na furaha nyingi sana usoni mwake, kiasi cha kujisahau kwamba yeye ni raisi, na anajichanganya na wapambe wake.Nikafanikiwa kumsogelea kwa karibu sana, hadi tunafika nje ya kanisa, nikapata nafasi ya kusimama nyuma yake, kwa haraka sana nikamuwahi kumpiga kabali, huku nikiichomoa bastola yangu na kumuwekea kichwani,

    Watu wakaanza kutawanyika, na kutukimbia huku wakipiga kelele, nikafyatua risasi moja juu na kuzidi kuwachanganya wageni waalikwa, askari karibia hamsini walio kuwepo kwenye eneo hili, bunduki zao wakawa wamenielekezea mimi

    “Wekeni silaha zenu chini, kabla sijamuua raisi wenu”

    Nilizungumza huku nikiendelea kumkaba kwa nguvu Mama Caro, ambaye anaendelea kutapa tapa mikononi mwangu.

    “Eddy…..!!” Caro akaniita huku akinishangaa, kwani hakutarajia ujio wangu kwa wakati huu

    “Ni mimi?”

    Nikazibandua ndevu za bandia na kuivua miwani niliyo ivaa na kusababisha Caro azidi kunishangaa

    “Eddy, tafadhali, nakuomba umuache mama yangu”

    “Ahaaa nimuache mama yako, kwanza mama yako ni shetani, na wewe mwenyewe ni mtumwa wa shetani.”

    Nilizungumza kwa sauti kubwa huku nikiendelea kumkaba mama Caro na bastola yangu nikiwa nimeielekezea kichwani mwake

    “Bila ya huruma, muliiangamiza familia yangu, mulimchinja mke wangu kama kuku na kunizawadia kichwa chake, hamkujali kama mke wangu ni mjamzito, laa hasha mukaona haitoshi, mukaiangamiza familia yake, baba na mama yake, wadogo zake.”

    Nilizungumza huku machozi yakinimwagika, waandishi wa habari hawakuwa nyuma kwa kuchukua matukio yote yanayo endelea kanisani

    “Leo hii, mutasema kwamba nimuache raisi, wenu ambaye ni shetani aliye vaa ngozi ya kondoo, my mommy’s friend, umeyaharibu maisha yangu, nimekuwa ni mtu wa kuishi kwa maumivu, nimekuwa ni mtu wa kuruka ruka mithili kunguru asiye na makazi maalumu, kwanini”

    Baadhi ya watu, wakaanza kutokwa na machozi, kwani ninazungumza kwa maumivu makali sana yalio uvunja moyo wangu

    “Eddy…Eddy” Mama Caro aliniita kwa sauti ya kukwaruza, ikanibidi nilegeze kidogo mkono wangu kumsikiliza anacho taka kuzungumza ni nini

    “Eddy ninakuomba unisamehe, niliyafanya hayo yote kwa ajili ya upendo wangu kwako, ninakupenda kuliko jinsi unavyo fiki….” “Wewe ni muongo, tazama, sina mke, sina mtoto, roho yangu imejaa ukatili kwa ajili yako wewe mwanamke.Nilitamani nije kuwa mtu mwema kenye maisha yangu, ila nimekuwa ni mtu wa kuua kila niapojisikia kufanya hivyo, naona hakuna haya ya mimi na wewe kuishi, nilazima TUFE”

    “EDDY USIFANYE HIVYO”

    Sauti kali kutoka katikati ya kundi la watu ilizungumza, ikanilazimu kugeuka upande wa getini inapo tokea sauti hiyo, macho yangu yakakutana na macho ya Christina mpenzi wangu wa zamani huku uso wake ukiwa unavuja jasho jingi, huku pembeni yake akiwa amesimama na bibi yake ambaye umri wake umekwenda

    “Eddy kunamambo mengi huyatambui kwenye maisha yako, ila Getrude ninakuomba unisamehe, tena sana.Pia Eddy ninakuomba unisamehe mjukuu wangu”

    Bibi yake Christina alizungumza huku akipiga hatua za kuja sehemu ambayo tumesimama mimi na Mama Caro

    “Eddy, kama ukitaka kuniua, niue mimi wa kwanza”

    Bibi alizidi kuzungumza, huku mikono yake akiinyoosha juu, akiwa tayari kwa kufa.Nikabaki nikiwa nimemtazama kwa macho makali yaliyo jaa uchungu na hasira, ila ndani yake yakiwa na alama ya kujiuliza ni kitu gani kinacho mfanya huyu bibi kujiamini kiasi hichi

    “Simama hapo hapo la sivyo nitakuua”

    Nilizungumza huku bastola yangu nikiwa nimeielekezea kwa bibi Cristina, ila akazidi kupiga hatua mbele, nikafyatua risasi mbili chini, mbele ya miguu yake na kumfanya astuke na kupepesuka, Christina akamuwahi kumzuia bibi yake asianguke chini





    “Simama hapo hapo wewe mzee, nitakuua, sina huruma na mtu yoyote aliye kuwapo eneo hili”

    “Eddy, umekuwaje mpenzi wangu, ina maana humuanini bibi yangu?”

    “Shiiiiiiii nyamaza, malaya mkubwa wewe.Nikukuacha ukiwa ni mwenda wazimu usiyeye jielewa.Ukanifanya niingie kwenye matatizo kwa ajili yako” “Eddy, maisha yanabadilika, ndio nakubali kwamba nilikuwa ni mwenda wazimu, ilawasamaria wema ndio walio niokoa mimi.Usiku ule niliokolewa na wavuvi walili, baada ya kunikuta nikiwa ninashambuliwa na kung’atwa na mambwa wakali, waliniokoa japo damu nyingi zilikuwa zimenimwagika.” “Kwa kipata chao kidogo cha uvuvi, waliweza kunitibu hadi nikapona.Ndio nilikuumiza sana baada ya mimi kuolewa, ila tulisha yazungumza, na chazo cha mimi kuolewa na yule mwanaume ni Madam Getrude.”

    Christina alizungumza huku machozi yakimwagika akiendelea kumshikilia bibi yake

    “Na nilisha kuambia kwamba yule mwanaume sikufanya naye chochote, japo tumefunga ndoa ya kanisani.Sindano ya sumu aliyo nichoma madam Gedrude ndio iliyo pelekea mimi kuwa chizi, baada ya kugundua kwamba ninamahusiano ya kimapenzi na wewe.Nilikuwa kichaa, ila jina lako halikufutika kichwani mwangu, na kumbuka niliapa kuwa sintakuwa na mahusiano na mtu yoyote, ambaye ni tofauti na wewe.”

    Christina aliendelea kuzungumza huku machozi yakiendelea kumwagika kwa uchungu

    “Ila hayo yote, nilimsamehe madam Getrude na kuamua kuishi maisha ya kumkimbia kimbia, hadi leo nilipokuona ukitoka kwenye hoteli ambayo ninafanyia kazi, nilijaribu kukuita ila hukunisikia kwani tayari ulisha panda bodaboda.”

    “Christina nyamaza, munaona, huyu ndio munasema kwamba ni raisi, wa kuingoza nchi kama hii, iliyo jaa amani, upendo eheee”

    Nilizungumza huku nikiwatazama wananchi wanaoa endelea kutuangalia, macho yangu wakati wote yakawa makini na askari wote walio ninyooshea bunduki.

    “Eddy kumbuka kwamba, mimi ni mpenzi wako, nilikutengeneza na kuwa kijana mzuri, ila wivu wangu nd…”

    “Mama, ina maana ulikuwa na mahusiano na Eddy?”

    Caro alimuuliza mama yake swali huku machozi yakimwagika usoni mwake

    “Ndio mwanangu, Eddy nilimpenda sana na nilimlinda kwa kila msichana ambaye alimtamani, basi sikusita kushuhulika naye”

    “Mama kwanini hukuniambia mapema ahaaaa”

    Christina alizungumza huku akirusha rusha mikono akionekana kuchanganyikiwa sana, mume wake akajaribu kumshika mkono ila akamsukuma

    “Niache na wewe, mama kwanini lakini eheee, Carry unadhani atakuita wewe nani?”

    “Bibi, kwani si mtomto wako na David?”

    Mama Caro aliuliza huku mikono yake ikiendelea kuushika mkono wangu nilio mkaba kabali

    “Carry ni mtoto wa Eddy na si mtoto wa David”

    Watu wakaanza kushangaa, hata David mwenyewe akabaki akiwa anamtazama Caro kwa mshangao, sikujua huyo mtoto wanaye mzungumzia ni yupi kati ya watoto wengi walio valia suti nyeupe

    “Carolina, i..na maa…na Carry si mwanag….u?”

    David aliuliza kwa kigugumizi, huku akimtazama Caro na jasho jingi likimwagika usoni

    “Samahani David, huo ndio ukweli Carry sio mwanao, na baba alisi wa Carry ni Eddy”

    Gafla David akamvuta askari mmoja na kumpokonya bastola aliyo ishika na kabla hata ajamfyatulia risasi Caro, nikafyatua risasi mbili zilizo tua kifuani mwake na kumuangusha chini, kila mtu akabaki akishangaa.Askari wanashindwa kunifanya kitu chochote kutokana Raisi nimemuweka chini ya ulinzi wangu

    “Eddy usiendelee kuua” Bibi Christina alizungumza kwa upole na unyenyekevu, huku akinitazama machoni mwangu.Akameza fumba la mate na kuanza kuzungumza kwa sauti iliyo jaa upole

    “Eddy mimi nilikuwa ni nesi, ninaamini unalitambua hilo.Mama yako na Getrude walikuwa ni marafika sana, hadi urafiki wao ukafikia kipindi wakapata ujauzito pamoja, kutoka kwa mwanaume ambaye aliweza kuwachanganya mama yako na Getrude kimapenzi.”

    “Mwanaume yule, ndio baba yake Caro, ila kutokana na uzuri wa kimaumbile wa mama yako alitokea kumsaliti mke wake ambaye ni huyo Getrude uliye mshika, ndipo ilipo tokea mama yako kupata ujauzito.”

    “Kwa upendo wa marafiki kati ya mama yako na Getrude, ukazidi kuongezeka siku hadi siku.Hadi siku ambayo mama yako anapata uchungu wa kujifungua, wakaja pamoja kwenye hospitali niliyo kuwa ninafanyia kazi, Gatrude akiwa amemsindikiza mwenzako, huku yeye akiwa pia ni mjamzito” Nikajikuta nikianza kumuachia mama Caro taratibu nikiendelea kumsikiza Bibi Christina kwa umakini mkubwa

    “Niliificha siri hii kwa kipindi kirefu sana, cha maisha yangu.Kuhofia usalama wangu, ila leo sina budi kuiweka hadharani.”

    “Getrude alipata naye uchungu, mara baada ya kumfikisha mama yako hospitalini, ikatulazimu kuwaingiza chumba kimoja kwa ajili ya wao kujifungua”

    Ukimya ulitawala katika eneo zima la kanisa na mtu wa pekee ambaye alisikika sauti yake ni bibi Christina.

    “Katika kujifungua kwao, wote walibahatika kupata watoto wa kiume, ila mama yako na Getrude walipoteza fahamu, baada ya watoto wao kuwa na kilo nyingi tofauti na watoto wa kawaida.”

    “Ila kitu kilicho nisikitisha ni baada ya mtoto aliye mzaa mama yako, kufariki duania, na mtoto ambaye ni wewe, uliendelea kupumbua, Samanani sana Getrude”

    Bibi Christina alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake,nataratibu akapiga magoti mbele yetu mimi na mama Caro

    “Kutokana wewe, tayari ulisha kuwa na binti ambaye ni Caro, ili kuifanya furaha ya rafiki yako kuendelea kudumu, ikanilazimu……”

    Bibi Christina aligoma kuzungumza, na kunifanya nimuachie kabisa Mama Caro na kuendelea kubaki na bumbuwazi

    “Ilinilazimu, kumchukua Eddy, na kumpa rafiki yako, na wewe tukakakupa mtoto aliye fariki, kwa hiyo EDDY NI MWANAO WA KUMZAA”

    Mwili mzima nikahisi, ukiishiwa nguvu, kila mtu ambaye alikuwa katika eneo hili akabaki mdomo wazi, mama Caro akanitazama mara moja, na nikastukia akiniangukia, na akapoteza fahamu, kwa haraka pasipo kuuliza nikafyatua risasi mbili zilizo tua kichwani mwa bibi Christina na kukichangua kichwa chake,

    “Husahili kuishi tena duniani, wewe ndio chanzo cha matatizo”

    Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiitupa bastola yangu nikaitupa pembeni na kunyosha mikono yangu juu, kujisalimisha mikononi mwa polisi.

    Christina akabaki akiwa anashangaa, akimtazama bibi yake anaye vuja damu nyingi kichwani, simu yangu ikaita na kuichoma mfukoni na kuipokea

    “Eddy, tunakuona turuhusu tuue askari wote walio kusogelea?”

    Ilikuwa ni sauti ya Lilian akizungumza

    “Hapana, musifanye hilo”

    Nikaiachia simu chini na ikachanguka, askari tayari walisha nisogelea, wengine wakimuwahi kumpa huduma ya kwanza muheshimiwa Raisi, huku wengine wakinivisha pingu za mikononi.Kabla hawajaninyanyua mtoto mmoja wa kiume mwenye umri si chini ya miaka saba akanisogelae kwa haraka na kunikumbatia huku machozi yakimwagika

    “Nakupenda, baba yangu”

    Alizungumza huku akinikumbatia kwa nguvu, askari wakaanza kutoa mikononi mwangu na kumkabidhi kwa Caro, ambaye bado anaendelea kumwagikwa na machozi.Askari wakaninyanyua na kunisimamisha, gafla Christina akasimama mbele yangu, huku akiwa na bastola akininyooshea mimi

    “Eddy umemua bibi yangu, kipenzi cha maisha yangu na wewe huna buni nikuu……”

    Kabla hata Christina hajamaliza kuzungumza, risasi moja ikatua shingoni mwake na kukitengenisha kichwa na kiwili wili chake.Na kwaharaka nikatambua kwa ni bunduki aina ya Snaiper ndio ina uwezi wa kufanya kazi hito, kwa jicho langu la pembeni, nikaangalia kwenye moja ya gorofa lililo mbali kidogo na kanisa, juu kabisa nikawaona Lilian na Priscar wakiwa wameshika bunduki zenye uwezo wa kupiga risasi masafa marefu.Wakanitazama kwa sekunde kadhaa na kuondoka zao, pasipo askari kuniona na mimi nikaingizwa kwenye gari ya polisi nikiwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi.

    ***

    Nikakaa rumande mwezi mzima na kesi yangu ikaanza kusikilizwa kwenye mahakama kuu ya Tanzania.Shtaka la kwanza ni kujaribu kumua meheshimiwa raisi na staka la pili ni kumuua bibi Christina na David.Kwa makosa hayo yote matatu nikahukumiwa kifungo cha maisha jela.

    Watu wengi wamejipanga nje ya mahakama wakisuniri nitolewe nje baada ya kuhukumiwa kifungo hicho.Ulinzi mkali ukazidi kuhimarishwa kila kona na kila pembe ya mahakama.Nikatolewa nje huku nikiwa nimefungwa pingu mikononi pamoja na myororo miguuni.Nikatazama pande zote walizo jaa watu, nikawaona Lilian na Priscar wakiwa wamesimama wakinitazama kwa macho yaliyo jaa ishara ya kutaka kufanya chohote cha hatari.Ila nikawakataza wasifanye lolote juu yangu

    Nikastukia kumuona Carry akija na kunikumbatia tena huku akilia kwa uchungu, askari wakataka kumtoa ila nikawaomba nizungumze naye, taratibu nikapiga magoti chini na kuipitisha mikono yangu, katikati yangu na kumkumbatia kwa uchungu huku machozi yakinimwagika

    “Carry”

    “Mmmm”

    “Mimi nani yako?”

    “Baba yangu”

    “Unanipenda?”

    “Ndio ninakupenda baba”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Safi, mama na bibi wapo wapi?”

    “Mama nimemuacha kwenye gari, ila bibi amesema atahakikisha anakuua”

    Carry alizungumza kwa sauti ya chini, ya kuninong’oneza.Jambo alilo niambi likanistua kidogo kwani mama yangu mzazi bado anakisasi na mimi

    “Kasema lini?”

    “Juzi alipokuwa akizungumza na Mama, ila baba yangu nitahakikisha haufi”

    Carry alizungumza kwa kujiamini hadi nikabaki nikiwa ninashangaa kwani mtoto mdogo kama yeye kuzungumza kitu kama hichi nilazima inastaajabisha

    “Nakupenda sana baba yangu”

    Carry akanibusu kwenye paji la uso na kujitoa mikononi mwangu, na kuwapisha askari kufanya kazi yao ya kunipeleka ndani ya gari, nikageuza shingo kuangalia sehemu walipo, ila sikuwaona.Nikaingizwa ndani ya gari la wafungwa ambalo ni maalumu, na sijawahi kuliona kwani limetengenezwa na chuma pande zote kasoro matairi yake.Waandishi wa habari na wananchi wakanipiga picha za mwisho nikiwa ndani ya gari na safari ya kulekea katika gereza nisilo lijua kwenda kutumikia kifungo cha maisha ikaanza.



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog