Chombezo : My Momy's Friend
Sehemu Ya Tatu (3)
ILIPOISHIA
Mama Caro akainama na kunipiga busu la mdomoni kisha nikamfuta machozi usoni.Mama Caro akasimama huku akionekana akikitafuta kijiko alicho kitupa chini.Akainama taratibu kisha akasimama huku akiwa ameshika pakti moja ya kondom huku akionekana kushangaa na kunitazama kwa macho makali huku sura akiwa ameikunja.Moyo ukanipasuka kwa woga ila nikajikaza kuuzuia wasi wasi wangu
ENDELEA
“Eddy hii kondom ya nani?”
Kabla sijajibu akaingia daktari na kumtazama Mama Caro kwa jinsi alivyo ishika kondom huku akinitazama
“Aisee samahani mama hawa wafanya usafi watakuwa wamezidondosha hizi kondom kwa maana zikakaa huku kwenye kaati”
Dokta alizungumza huku akiichukua kondom kutoka mikononi mwa Mama Caro na kufungua kabati na kuiweka katika oksi la kondom alilo litoa nesi Matha kisha akaufunga mlango wa kabati.Kidogo mapigo ya moyo yakanituli.
“Dokta sasa inakuwaje mpaka boksi za Kondom kukaa katika wodo za wagojwa?”
“Tunafanya hivi kutokana pale mgonjwa anapo ruhusiwa tunampa kwa ajili ya kwenda kujikinda na maradhi”
“Ahaa hapo kidogo nimekuelewa”
Mama Caro akakaa pemeni yangu huku akiwa anakiosha kijiko alicho kuwa amekitupa chini na akaanza kunilishaa taratibu.Dokata akanichoma sindano ya kutuliza maumivu kisha mama Caro akaendelea kunilisha.Baada ya kumaliza kunilisha akaondoka.Mida ya saa nne asubuhi Caro akaingia katika chumba nilicho lazwa nikashangaa kumuona hatembelei gongo.Akanifwata kitandani na kunikumbatia kwa furaha
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Eddy nilidhani umetukimbia?’
“Hapana mpenzi umekuja na nani?”
“Na dereva nimemuacha hapo nje anaongea na simu”
“Ahaa ila vipi nyumbani?”
“Nyumbani si kwema kutokan wewe haupo”
“Tumuombe MUNGU nitarudi siku si nyingi”
“Ila pole Eddy wangu kwa kuumwa”
“Asante si unajua matatizo tumeumbiwa wana damu”
“Ndio na mimi kipindi nilipo pata ajali niliwaomba waalimu wasimjulishe mama hadi hali yangu ilipoanza kukaa sawa ndio wakampigia mama na hata mwenyewe alivyokuja kunichukua alishangaa kwani alinikuta kidonda kinaenda kupona”
“Ahhaa mimi hapa sijui nitapona lini kwa maana mguu ndio kwanaza umepasuliwa upya”
Akaingia dereva tukasalimiana kisha akasimama pembeni ya kitanda
“Kaka Eddy unaonaje maendeleo?”
“Kidogo nina nafuu”
‘Kweli hata mimi naona kwa maana ile siku tumekuja katika ile hospitali tuliyo kukuta hata kumbukumbu zako hazikuwa sawa”
“Kweli kaka ila hapa nashukuru kumbukumbu zimerejea kidogo ninaweza kukumbuka kila kitu”
“Daaa kaka pole sana.Sasa sister Caro Maza amenipigia simu kuna mzigo wake nikauchuke post kisha nimplekee ofisini je utabaki hapa hadi muda gani?”
“Nitakupigia simu”
“Powa kaka Eddy ngoja mimi niwakimbie kidogo”
“Haina tabu kaka tutaonana baadaye”
Dereva akatoka na kutuacha mimi na Caro.Caro akabaki amenitazama kwa macho ya huruma mpaka chozi likamdondoka
“Eddy siamini kama nimekuona tena?”
“Kwa nini?”
“Unajua kunisiku moyo wangu ulikosa raha kabisa na mida ya jioni hivi nikajikuta nguvu zote zikiniishia na jinsi mama alaivyo niadisia nikajua ndio siku wewe uliyo pata ajali”
“Alafu kipindi ninapata ajali ndio ilikuwa muda ninarudi nyumbani nikiwa kwenye boda boda”
“Ulikuwa umekunywa?”
“Hapana sikuwa nimekunywa”
Nikajikuta nafsi ikinisuta kwani muda wa mchana wa siku niliyopata ajali nilikunywa whyne nyumbani kwa Clara.Tukaendelea kupiga story na Clara hadi muda wa mchana dereva alipo rudi akiwa ameongozana na mama Caro
***
Baada ya miezi miwili nikapona na kurudi katika hali yangu ya kawaida.Ni siku ya jumamosi ambayo mama Caro amepanga kunifanyia shere ya kupona na kurudi nyumbani.Tukaelekea katika hoteli moja maarufu iliyopo katika fukwe za bahari ambapo mama Caro amekodi ukumbi na kuwaalika marafiki zake matajiri pamoja na wafanyakazi baadhi.Tukafiaka ukumbini mida ya saa moja na nusu usiku huku mimi nikiwa dereva wa gari tulilo panda na mama Caro na mwanaye.Nikiwa nadani ya suti nyeusi iliyonibana mwili pamoja na shati jeupe na tai nyeusi vikanifanya kupendeza mpaka mimi mwenyewe nikajikubali
Caro kwa usiku huu amevalia gauni refu jekundu lenye mpasuo hadi kwenye paja na kuufanya mguu wake wa bia kuonekana huku makalio yake makubwa yakiwa yamejichora vizuri katika gauni lake hilo.Kila tulipo pita tukiwa tumeongozana watu hawakusita kuficha hisia zao za kutupongeza na kutuambia tumependeza.Mama Caro kwa upande wake amevalia vitenge vyake ambavyo ni vya gharama sana na alitengenezewa mtindo wa pekee wa mavazi na mwana mitindo wa kampuni yake ya simu ambaye huwatengenezea mavazi wacheza matangazo ya video ya kampuni
Tukakaa katika vitu maalumu vya mbele na tukawa tunawatazama waalikwa huku Mama Caro akiwa amekaa katikati yetu.Sherehe ikaanza huku kila wakati MC alitusifia na kumwagia sifa nyingi Mama Caro kwa kuwa na watoto wazuri.Ila akilini mwangu nikawa ninajiuliaza ni ina maana watu hawajui kuwa Mama Caro si mama yangu wa kunizaa.Ila sikutaka kuyapa mawazo hayo ruhusa ya kuitawala akili yangu kwani muda tulio nao ni muda wa furaha
Muda ukawadia wa Mama Caro kuzungumza nasaha juu ya sisi watoto wake wawili
“Ninaamini kwamba nyinyi ndi ndugu ambao munapendana sana.Machache ambayo ninataka kuwaambia ni kwamba ninawaomba sana watoto wangu muwe na moyo wa upendo kwa watu wengine kwani Mimi mama yenu nilizaliwa katika familia masikini na kwajuhudi zangu na pamoja na Mungu kunisaidia leo hii ndio munaniona jinsi hii nilivyo.Pia ninawaheshimu kila mmoja wenu pasipo heshima leo hii naamini asinge kuwepo mtu wa kumuajiri kwahiyo nina wahusia Caro na Eddy muwe na heshima na upendo kwa kila mmoja asanteni”
Watu wakapiga makofi na mama Caro akakaa kati kati yetu kisha muongoza sherehe akaniomba na mimi nisimame ili nizungumze mawili matatu.Kusema kweli sikuwa na kitu cha kuzungumza ila ikanilazimu kusimama na kuzungumza machache
“Kwanza ninamshukuru mama yangu kwa kunifanya leo nionekane hivi pamoja na dada yangu Caro hapa kwani pasipo wao sasa hivi ningekuwa kilema au hata kufa kwani ajali yangu niliyo ipata ilikuwa ni mbaya……….”
Nikakaa kimya huku machozi yakianza kunitiririka huku nikimtafuta Christina ukumbini lakini sikumuona nikajua moja kwa moja atakuwa hajaja
“Ila cha kumshukuru Mungu leo nimepona na ninaendelea na shuguli zangu za kawaida.Pia hata wale mulio kuwa munakuja kunitembelea hospitali nawasukuru sana.Pia hata nyinyi mulio niombea nawashukuru pia.Asanteni”
Ukumbini watu wakapiga makofi na kumpa nafasi Caro kuzungumza machache.Baada ya muda Caro akamaliza kuzungumza na sote pamoja na wageni waalikwa tukapata chakula cha pamoja.Kisha mziki ukawekwa na tukaanza kucheza.Simu yangu ikaita kutokana na kelele za mziki ikanilazimu kutoka nje kwenda kuipokea,hadi ninafika nje ikawa tayari imekata na sikujua ni nani anaye nipigia kutokana namba ilikuwa ngeni katika simu yangu.
Nikawakuta walinzi wakimbeba juu juu mwanamke ambaye anaonekana ni kichaa na kwenda kumuweka katika fukwe za bahari mbali kodogo na ukumbi kwani anang’ana’ania kuingia ndani ya ukumbi na kumfanya mdoli wake aliye mbeba kuanguka.Nikapiga hatua na kuufwata mdoli wake ulipo angukia na kuanza kwenda kwenye fukwe za bahari.Nikautana na walinzi wa waliokuwa wamembeba chizi yule ikabidi niwasimamishe
“Mume mpeleka wapi yule dada muliyekuwa mume mbeba?”
“Tumempeleka kule ufukweni analia lia lia huku akimtaka Eddy ambaye sisi hatumjui”
Moyo ukanipasuka na kuanza kujiuliza tangu lini kichaa akanijua,ila nikajipa mmoyo na kujua atakuwa amesikia jina langu likitajwa ukumbini.Hali ya hewa haikuwa nziri sana kwani mitone tone vya mvua vilianza kunyesha.Nikapiga hatua za haraka kwenda ufukweni nikamuona kichaa anaye niulizia.
Nikamuona ikachezea chezea maji huku nywele zake zilizo kaa changu changu sikuweza kuiona sura yake vizuri kwa umbali niliokuwepo.Nikazidi kupiaga hatua za haraka na nikamfikia kutokana amenigusa mgongo nikalazimaka kumshika bega.Akageuka haraka na sote wawili tukajikuta tua shangaana huku mimi mapigo yangu ya moyo yakianza kunienda mbio na woga mwingi ukiuvaa mwili wangu
“Eddy Eddy……Eddy huyooooo katoka kazinii hiiiii na mdoliii mkubwaaaaa”
Nikajikuta nashindwa kuyazuia machozi yangu huku hadi wakati huu siamini kitu ninachokiona mnele yangu na na kuanza kujiuliaza ni kitu gani kilicho mpata Christina ambaye alikuwa ni mpenzi wangu na yeye ndiye alie nipeleka hospitalini.Nikazidi kupatwa na huzuni na kujua Christina amekuwa kichaa ni kutokana na jinsi anavyo imba nyimbo zake huku akiruka ruka na kunizunguka
“Tina Tina”
“Hahaaaaa haaaaa haaaaaaa”
“Ni kitu gani kimekupata!!?”
“Hahaha unikamati ngo’ooo”
Christina alizungumza huku akinikimbia kimbia kila nilipokuwa ninajaribu kumkamata.Christina akaanza kukimbia kwenda mbele kwenye ufukwe ambapo kuna giza jingi.Ikanilazimu nianze kumkimbiza.Hakunipa shida hadi kumpata na kumlaza chini
“Tina ni nini kimekupata mke wangu”
Nilizungumza huku nikiwa ninatokwa na machozi na kumfanya Christina kuendelea kucheka chaka,Mvua ikazidi kuongezeka na kuwa kubwa ikanibidi nimnyanyue na kuvua koti langu na kumvalisha na kwenda kumuweka chini ya mti wa mkoko ili mvua isitupige sana.
“Njaaaaaa njaaaaa uma mimi”
“Tina unasikia njaa?”
“Njaa uma mimi”
Christina alizungumza huku akiwa analia.Nikavua mkanda wa suruali yangu na kumfunga miguuni kisha nikavua na tai yanga na kumfunga kwenye mikono ili asinikimbie pindi nitakapo kwenda kumchukulia chakua
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tina ninakuja mpenzi wangu nakwenda kukuchukulia chakula sawa”
“Njaaaaaa”
Nikasimama na kuanza kukimbia sikutaka mtu yoyote atambue kuwa Christina yupo sehemu hii kwani ninahisi kuna kitu kitakuwa kimetokea hai yeye kuwa katika hali ya ukichaa.Nikafika kwenye mlango wa kuingila ukumbini huku nikiwa nimelowa mwili mzima na kuanza kujifikiria jinsi ya kuingia ukumbini.Nikastukia nikiguswa bega kwa nyuma.Nikageuka na kukuta ni Mama Caro wakiwa na Caro
“Eddy ulikuwa wapi mbona umelowana na mvua hivyo?”
“Nilikuwa kule kwneye maegesho ya magari”
“Sasa jamani mwangu mbona umeondoka bila kutuaga umeyufanya tupate wasiwasi kama nini?”
“Eddy koti liko wapi?”
“Koti nimeliacha kwenye gari”
“Twende zetu nyumbani kwani hapa sherehe imesha isha?”
“Kwani sasa hivi ni saa ngapi?”
“Saa sita na nusu”
“Wale wapishi wamesha ondoka?”
“Siku nyingi wameshaondoka hapa tulikuwa tunakutafuta tuondoke”
Akili yangu ikaanza kufanya kazi kama kompyuta huku nikiwa natafuta jinsi ya kuwadanganya uongo utakao kuwa unafanania na ukweli.Mama Caro akanishika mkono na tukaanza kuelekea kwenye maegesho ya magari huku tikiwa tunakimbia kujikinga na mvua isitunyeshee sana huku Caro akifwata kwa nyuma yetu nyuma yetu.
Nikastukia mkono wa Mama Caro ukiniponyoka kweye kiganja changu na kustukia akiwa chini huku akiwa amekaa kitako.Nikajua moja kwa moja ameteleza
“Mama umeumia?”
“Hapana wanangu nipo powa japo mguu nahisi kama umestuka”
Tukasaidiana na Caro kumyanyua na ikatulazimu tutembee taratibu hadi kwenye gari huku mimi nafsi yangu ikiwa na wasiwasi juu ya Christina niliye muacha ufukweni.
“Eddy hembu tuwahi nyumbani kwani hapa mguu nauhisi kuvuta”
“Mama isije ukawa uevunjika ?”
“Hapana sijavunjika ni mstuko tu”
Sikuwa na jinsi zaidi ya kuwasha gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi huku maombi yangu kwa Mungu ni alinde Christina asipatwe na chochote.Nikasfunga breki kali za gari mbele ya suppermakert inayofanaya kazi masaa 24
“Caro nipe elfu ishirini hapo kuna kitu ninunue”
Caro akanipa elfu theladini nikashuka kwenye gari nikaingia ndani ya supermakert na kununua vifuko viwili vya soseji pamoja na nyama za kopo.Kisha na kurudi ndani ya gari na kuendelea na safari huku nikitembea na spidi mita 120 hadi Mama Caro akanishangaa kwani hakuwahi kuniona nikiendesha gari kwa mwendo mkubwa kiasi hicho.Tukafika nyumbani na kushuka kwenye gari huku Mama Caro akiwa anachechemea,Nikapitiliza hadi jikoni na kunza kuzikaanga soseji pamoja na nyama za kopo ambazo zimesagwa.
“Eddy unanjaa?”
Caro aliniuliza huku akiwa amesimama kwenye mlango wa kuingila jikoni
“Best mimi wala sikushiba.Vipi mama yupo wapi?”
“Nimetoka kumchua mguu wake na ameshapanda kitandani hapa mimi mwenyewe nahisi usingizi kama nini”
“Powa baby ngoja mimi nile kwanza ndio nilale”
Caro akanisogelea na kuninyonyalipsi zangu kisha akanimalizia na busu la shavuni kisha akaondoka
“Wee Caro usisahau kuzima taa za sebleni”
“Nimeshazima kaka yangu”
Nikamaliza kupika na kukiweka chakula kwenye hotpot ambalo lina kishikizo na kukiweka chakula juu ya friji,Nikaingia ndani kwangu kwa ajili ya kubadilisha nguo ili nimuwahi Christina katika fukwe za ya bahari nilipo muacha.Nikavaa haraka na kurudi jikoni nikastuka kumkuta Mama Caro akiwa anakula chakula nilichokuwa ninakipika na mbaya zaidi mvua inaogezeka huku ikiwa inaandamana na radi nyingi
“Eddy mimi mwenyewe nilikuwa na njaa kama nini sema huu mguu ulinichanganya”
Nikabaki kimya huku nikitafakari nini cha kumwambia mama Caro kwa maana anazidi kunichanganya
“Eddy nbona umesimama huli chakula?”
“Nitakula tuu baby”
“Alafu Eddy nina hamu na wewe miezi miwili hatujakutana hapa kila nikikuangalia mwili wangu unanisisimka”
“Mbona unaniangalia mpenzi wangu hunijibu kitu au nimekuudhi kwa kula chakula chako?”
“Hapana baby…….Nashangaa kama umeweza kula chakula changu kutokana nahisi kama hakija iva si unajua mapishi kwangu ni zero”
“Mmmmm Eddy hapa…unajua kupika hapa nilipo najisikia raha burudani”
Mama Caro akanisogele huku akiwa na kipande cha soseji mdomini na kunipa kwa kutumia mdomo,sikuwa na haja ya kukataa zaidi ya kukipokea na kukila.Akanishika kiuno na kusisogeza nyuma hadi nikaegemea kwenye friji.Mama Caro akaanza kuninyonya lipsi zangu huku akianza kutoa mihemo mzito na pumzi iliyo jaa joto kali
“Baby Caro anaweza akatusikia tutafanya kesho”
“Hawezi kutusikia yeye yupo gorofani atatusikia vipi?”
“Huwezi jua nakuomba basi mmm”
Mama Caro hakunielewa akazidi kunikumbatia huku mkono wake mmoja akiushusha kwenye koki yangu na kuanza kuichezea.Nikautoa mkono wake kwenye koki yangu na kuushikisha kwenye kiuno changu
“Baby nakuomba unielewe sipwendi Caro atambue kuwa wewe na mimi tuna mahusiano najua una hamu na mimi ila tulinde amani yetu humu ndani”
“Eddy sawa kama vipi nakuomba twende ndani kwangu”
“Baby wewe mwenyewe unajijua jinsi unavyotoa vilio kwa sauti ya juu huoni kama itamfanya asikie”
“Leo nipo radhi nisitoe sauti yoyote ya kumfanya asikie”
“Hapana nakuomba please baby”
Mama Caro akakaa kimya huku akinitazama kwa macho malegevu,akaninyonya tena lipsi zangu kisha akaniachia kiuno
“Edy tambua kuwa nimeshikika mwenzio naenda kulala ila bado sijatosheka”
“Usijali kesho nitakuridhisha hadi wewe mwenyewe utafurahi”
Mama Caro akarudia kuninyonya tena lipsi zangu kisha akafungua mlango wa jikoni na kutoka.Kidogo nikashusha pumzi.Nikakirudisha chakula kilichopo kwenye sahani na kukiweka kwenye hotpot na klifunga vizuri.Nikaanza kufungua makabati nikitafuta mfuko wa kuliweka hotpot,nikastuka mlango ukifungulia na akaingia Caro akiwa na na kagauni kakulalia huku macho yake yakiwa yanaonekana kuwa na usingizi mwingi
“Eddy bado hujalala tu?”
“Bado hapa natafuta sahani?”
Caro akacheka huku akipiga miayo huku akiwa anashika kiuno
“Eddy mpenzi wangu nahisi umeshaanza kuwa mzee”
“Kwa nini?”
“Sahani si hii hapa tena inaonekana ulikuwa uweiwekea chakula”
“Hapana nimeiona ila natafuta sahani safi”
“Sahani safi si zinakaa hapo juu ya kabati kwenye droo ya kwanza”
Kwa kuzuga ikanibidi nifungue kwenye droo na kutoa sahani na kuiweka juu ya friji ambalo ni fupi kisasi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ngoja nikalie chakula ndaani kwangu”
“Sawa mimi nimekuja kuchukua maji nikanywe dawa nahisi kichwa kinaniuma”
“Pwa usiku mwema”
“Eddy mbona unaniaga hivyo”
Nikamuelewa Caro anamaanisha nini,nakamsogelea na kumbusu mdomoni kisha nikatoka haraka huku nikiwa nimelishika hotpot na sahani mkononi.Nikapiga hatua za haraka za kwenda nje nikafanikiwa kufungua mlango wa nje pasipo Caro kunisikia.Mvua imezidi kuongezeka tofauti na mwanzoni na ya sasa hivi inaandamana na radi kubwa,Nikafungua mlango wa gari ili niondoke nalo nikahisi mama Caro atanisikia na mbaya zaidi dirisha la chumba chake kilichopo gorofani lipo upande wa mbele wa geti la kutokea katika jumba hilo.Sikuona haja ya kutumia garii nikaufunga mlango wa gari na kuelekea getini.
“Oyaa ninatoka kuna sehemu nina kwenda ila usimwambie mtu yoyote sawa”
“Powa kaka ila..”
“Hakuna cha ila wewe jua kuwa nina toka sawa”
“Powa mkuu”
Nikafungua geti na kuachana na mlinzi nikaangalia pande zote za barabara nikaona zimetulia hakuna uwepo wamtu yoyote,Saa yangu ya mkononi inanionyesha ni saa nane kasoro usiku.Nikaanza mwendo wa haraka kuelekea katika barabara ya kaskazini kotoka lilipo jumba la Mama Caro kadri ninavyozidi kutembea ndivyo miguu yangu ikaanza kuongeaza mwendo na nikajikuta nikianza kukimbia huku mvua ikizidi kupiga.Mara kwa mara nikajikuta nikisimama huku nikiwa ninahema kutokana na kuchoka na pia kukosa mazoezi ya kukimbia kwa kipindi kirefu na kunilazimu kupumzika kwa dakika kadhaa kisha nikaendelea na kukimbia
Nikafika maeneo ya ufukwe wa Hoteli tuliyo fanya sherehe muda mchache uliopita na kuongeza mwendo wa kutembea huku nikiisogelea sehemu nilipo mfunga Christina.Wasi wasi ukaanza kuniingia baada ya kukuta sehemu niliyo muacha Christina imejaa damu huku yeye mwenyewe akiwa hajupo.Kwa mwaga wa radi nikaona damu zikiwa zimechuruzika zikielekea wa mashariki kutoka sehemu nilipo,nikaanza kuifwatisha michuruziko ya damu na nikajikuta nikizidi kutembea kwa urefu mkubwa pasipo kujua nitaifika mwisho wa michuruziko hiyo ya damu.
Sikukata tama zaidi ya kuongeza mwendo huku wakati mwengine ikifikia hatua nikisimama huku nikisubiria mwanga wa radi upige ndio nione sehemu damu hizo zinapo elekea,Woga wote uliniondoka na kujawa na ujasiri huku akili yangu ikiwa inawaza ni jinsi gani nitampata Christina na nikajikuta nikisahau ya nyuma aliyo nifanyia ya kuolewa na mwanaume wengine tofauti na makubaliano yetu.Nikajikuta nikistuska gafla na kusimama huku shingo yangu nikiigeuza taratibu nyuma kuangalia kitu gani kinacho nguruma.
Macho yangu yakakutana na mbwa mkubwa mwenye macho makali huko meno yake meupe nyenye ncha kali akiwa anayaonyesha onyesha kila akinguruma.Akili yangu ikaanza kufikiria kitu cha kufanya kwani nikikimbia kitakuwa ndio chanzo cha mbwa huyu kunidhuru kwa kuning’ata.Mwanga wa radi ukapiga tena nikaliona eneo zima nililopo lina mabomba makubwa yanayoingia baharini huku yanapo toka kuna mitungi mikubwa ya mafuta huku kukiwa kumezungushiwa fensi ya waya mgumu uliosukwa na kuweka matundu matundu makubwa kiasi hku kukiwa na kibao kikubwa kilicho andikwa ‘DANGER’ na kuchorwa kichwa cha fuvu la mtu huku likiwa na mifua miwili iliyochomoza pembeni huku ikiwa imejenga muundo wa X .Huku kibao kingine kikiandikwa ‘ULINZI MKALI HAURUHUSIWI KUPITA ENEO HILI’
Nikaunyanyua mkono wangu taratibu ulio shika hotpot la chakula na kila nilivyozidi kulinyanyua ndivyo mbwa aliyo zidisha mngurumo.
“Ohoo Mungu wangu nisaidie”
Nikajikuta nikiomba sala ila nikaona pasipo kufanya juhudi za kujiokoa katika jimbwa hilo hakika nitaangamia.Nikalifungua Hotpot lenye chakula na kulirusha upandea wa kulia kwangu wenye bahari na kuanza kukimbia kwa kasi ya ajabu huku nikijihisi uzito kutokana na mchanga wa ufukweni kulowana na maji na kunifanya kasi ya kukimbia kuwa ndogo.Cha kushangaza mbwa hakukifwata chakula changu zaidi akanza kunifukuza.Sikujua hata nguvu za kukimbilia zimetokea wapi kwani mahatua ninayo yapiga yakanifanya kumuacha mbwa kwa umbali kidogo.Nikawa na kazi ya kupenya chini ya mabomba makubwa huku mara kadhaa nikiwa ninajigonga.Mbwa hakukata tama na mimi na akazidi kunikimbiza,nikaanza kuona matumaini yakinitoweka baaya ya mbele yangu kuona tochi tato zikija kwa kasi na moja kwa moja nikatambua watakuwa ni wlinzi wa eneo hilo.Nikakunja kona kali kuelekea upande wa baharini na kumfanya mbwa kupitiliza kidogo ila akageuka na kunifwata.Nikaingia baharini na kuanza kuogelea kuelekea nisipo pajua.Milio ya risasi nikaisikia nyuma yangu ila sikujua kama inanifwata mimi.Nikastuka kuona boti mbili ndogo zikija upande wangu kwa kasi ya ajabu huku zikiwa na na taa kubwa
Nikavuta pumzi nyingi kisha nikazama ndani ya maji na kuanza kuogelea kuzifwata boti zinapo tokea huku nikiwa nipo umbali kidogo kutoka juu.Boti zikasimama gafla huku matochi yake yakiwa yanaelekezwa kwenye maji wakiwa wananitafuta mimi gafla vitu vyenye ncha kali vikaanza kuingia ndani yamaji na nikatambua zitakuwa ni risasi.Nikaanza kuhisi pumzi zikianza kuniishia na kila nilipo jaribu kuogelea kwenda mbele ndivyo nilivyozidi kuishiwa na nguvu na kuanza kuhisi kifo kipo mbele yangu
Nikaendelea kuogelea kwa nguvu zangu zangu zote kuelekea katika giza mbali kidogo na boti za watu wanao nitafuta zilipo simama,Nguvu za mwili wangu zikazidi kuniishia sikuwa na jinsi zaidi ya kuamua kujilegeza mwili mzima na kuanza kuelea huku nikijitahidi kuvuta pumzi itakayo nisaidia kuzama tena ndani ya maji.Gafla mwanga mkali wa zile boti zikanimulika huku sauti ya mwanaume inayotoka kwenye kipaza sauti ikiniamuru kujisalimisha lasivyo wataniua kwa kunishambulia na risasi.Sikuwa na ujanja zaidi ya kuendelea kuelea juu ya maji katika eneo nililopo na wakaja na boti zao na kunizunguka huku mitutu ya bunduki zao zikinielekea mimi.Kwa esabu ya haraka haraka jamaa wanapata kumi na mbili kwenye boti zote huku wakiwa wamevalia nguo nyeusi tupu na wengine wakiwa wamevalia makofia yaliyo wabakiza macho na kuficha sura zao.Wakaniamuru nipande mwenyewe kwenye boti moja wapo.Nikapanda huku nikiwa na mashaka nikiwa ninawatizama tizama kwa kuweweseka huku baridi kali ya baharini iliyo andamana na upepo mkali ikiwa inauumiza mwili wangu ulio lowana na maji.Gafla nikastukia kitu kizito kikinipiga kichwani na kkuzimia hapo hapo
***
Nikastushwa na maji mengi yaliyo nipiga usoni kwa nguvu na kunifanya nizinduke kwenye hali ya kuto jielewa.Ila sikuelewa jinsi dunia ilivyo kaa kwani vitu vyote vilivyopo mbele yangu ninaviona vimekaa kichwa chini miguu juu, nikajichunguza vizuri nikagundua nimefungwa kichwa chini miguu juu huku mikono yangu ikiwa imefugwa kwa nyuma na kujikuta nikiyumba yumba kama nyama ya buchani.Sikuweza kutambua mara moja mtu aliye simama mbele yangu ni mwanaume au mwamke kutokana na kuvaa kofia iliyo mziba uso mzima kasoro macho yake kama wale watu walio niamuru nipande kwenye boti huku mkono mmoja akiwa ameshika kindoo kidogo cha lita tano huku mkono wake mwengine akiwa ameshika bunduki aina ya SMG.Nikaanza kuhisi maumivu makali katika kichwa nikakumbuka ni kile kitu kizito nilichopigwa kwa kustukizwa wakati wakinikamata.
“Hei sema wewe ni nani kabla bosi wangu hajafika?”
Hapo ndipo nikagundua mtu aliye simama mbele yangu ni mwanamke kutokana na sauti yake kuwa nyembamba huku akiniuliza kwa sauti ya chini chini ya kuninong’oneza.
“Mimi ni Eddy?”
“Eddy gani?....Ongea kitu cha kueleweka wewe si…….”
Kabla hajamaliza mlango ukafunguliwa nawakaingia wanaume watano huku wanne wakiwa na bunduki mikononi huku wakiwa wamevalia nguo nyeusi huku mmoja wao akiwa amevalia nguo za kawaida huku akiwa anaonekana kuto kuwa na silaha yoyote na anaasili ya kiarabu.Akawaamuru wezake kunifungua na wakafanya hivyo na kunaliza chini kwenye vumbi lililo changanyikana na maji niliyo mwagiwa muda mchache ulio pita.
“What’s yorur name ?”(Jina lako ni nani?)
Nikakaa kimya kwani sikuelewa ameniuliza kitu gani.Ikamlazimu yule dada kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili
“Anakuuliza unaitwa nani?”
“Ninaitwa Eddy”
“Ohh Mr Eddy are you a spy?”
“Anakuuliza wewe ni mpelelezi?’
“Hapana”
“He say no”(Anasema hapana)
Jamaa akawaamuru jamaa alio ingia nao wenye miili mikubwa na iliyo jazia misuli kuniinua chini na kunikalisha kwenye kiti huku mikono yangu ikiwa imefungwa kwa nyuma.Jamaa akanisogelea hadi nikaanza kutetemeka ila yeye akawa anatabasamu na kunifanya niyaone meno yake yaliyotengezezwa kwa madini ya dhahabu yaking’aa vizuri kwenye kinywa chake.Gafla jamaa akanibana kwenye sehemu zangu za siri kwa kutumia kiganja chake cha kushoto na kunifanya nianze kupiga kelele huku machozi yakinimwagika
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“I say are you are Tanzanian SPY?”
“Anasema wewe ni mpelelezi wa Kitanzania”
“Haaa….haaaapanaa”
Nilizungumza kwa tabu huku machozi yakinimwagika kama maji na jamaa akazidi kuziminya sehemu zangu za siri.Jamaa akaniachia na kunyoosha mkono kwa mmoja wa watu wake alio ingia nao kama anamuomba kitu.Jamaa aliye nyooshewa mkono akatoa kolea na kumkabidhi jamaa
“You don’nt want to saya who are you?”
“Anasema hukati kusema wewe ni nani?’
“Jamani mimi ni Eddy na wala si mpelelezi”
Nilizungumza huku nikilia kama mtoto mdogo na kumfya jamaa azidi kuniminya sehemu za siri huku akitafsiriwa na dada aliye iziba sura yake kasoro macho yake na akaniachia kwa muda huku akinitazama kwa hasira.Jamaa akanisogelea na kunishika sikio langu kisha na kilibana kwa koleo lake na kuanza kulivuta.Kusema kweli maumivu ninayo yapata hayasimuliki kwani mwili mzimaa umepoteza ile furaha ya kuuitwa ni mwili wa binadamu.Nikazidi kutoa kelele za vilio vilivyo ambatana na maumivu makali nikastukia ngumi nzito ya jamaa ikitua kwenye shavu langu na kuhisi mtikisiko mkali kwenye taya zangu za meno.Jamaa kwa hasira akaanza kuzungumza lugha ambayo sikuielewa hata kidogo ila dada akanitafsiria
“Analalamika anadai wewe lazima utakuwa ni mpelelezi na umemtia hasara ya mamilioni ya pesa za kimarekani”
“Jamani jamani dada yangu mwambiea mimi si mpelelezi ni mtu mwema tu…..Nilikuwa nikimtafuta mpenzi wangu baharini”
Dada akazunumza kwa lugha ya jamaa anayo zungumza,nikastukia teke zito kutoka kwa jamaa likatuua kifuani kwangu na kuniangusha mimi pamoja na kiti changu chini kisha jamaa akatoa ishara ninyanyuliwe haraka.Machozi yakazidi kunidondoka huku damu za pua zikianza kunimwagika.Jamaa akanishika masikio yangu mawaili kwa kutumia miganja vyake na kuninyanyua kwenye kiti na kunisogeza karibu yake akanitazama kwa macho yaliyo jaa hasira.Kichwa kikali kutoka kwa jamaa kikatua kwenye paji la uso wangu na jikuta nikianguka chini huku jamaa akinisindikiza na teke la tumbo lililozidi kunipa maumivu makali
“Dada yangu nakuomba umuambie jamaa mimi sihusiki na chochote”
Dada akazungumza kwa lugha ya jamaa anayo zungumza na kumfanya jamaa kuwa kama Mbogo aliye jeruhiwa kwa risasi.Jamaa akaniweka chali na kunikalia tumboni na kuanza kunishushia mokonde mazito yaliyotua usoni mwangu hadi mmooja wa alio kuja nao akamshika mkono akimzuia asiendelee kunitandika mangumi ambayo ninahisi yameuharibu uso wangu kwa kiasi Fulani japo sijajiona
“Sir you will kill this men remember we need him go give us full information”(Muheshimiwa utamuua huyu mwanaume.Kumbuka tunahitaji habari nzima kutoka kwake)
“Fuc*k you…..shate up your fuc**ng mouse am gona kick your as*”(Mse** wewe funga huo mdomo nitakuto** huo mk***u wako)
Jamaa alizungumza huku akiichomoa bastola yake kwenye soksi na kumuelekezea mwenzake na kumfanya arudi nyuma kwa woga.Jamaa akanitazama huku bastola yake akinikandamizia kwenye paji la uso wangu.Nikaanza kusali sala ninayo ijua mimi mwenyewe kwani tayari kifo kimesimama mbele yangu na sikuwa na matumaini ya kuishi tena,Mapaigo ya moyo yakaenenda na kwasi ya ajabu huku kwa mbali yakisikika jinsi yanavyo dunda.Jamaa akanyanyuka na kuondoka huku akizungumza lugha isiyo eleweka akilini mwangu huku watu alio ingia nao wakimfwata kwa nyuma
“Anasema ujifikirie cha kumjibu kipindi atakaporudi”
“Da…da yangu mi….mi sijui nini nimefanya…..”
Nlizungumza kwa tabu sana kwani mdomoni ninamaumivu makali yanayopelekea kuhisi kama dunia kwangu inaweza kuwa ndio mwisho wake.Kabla hajazungumza chochote mlango ukafunguliwa wakaingia mijitu mingine miwili yenye miili mikubwa kama micheza myereka kwa haraka haraka nina wafananisha na ‘Under Taker’ au ‘Big Sow’.Mmoja akaninyanyua na kuniweka begani mwake na akaanza kutoka ndani ya chuma nilichokuwa,Kusema kweli sikujua ni wapi wanapo nipeleka ni nikajikuta muda wote nikikwa ninalia kama mtoto mmdogo huku damu zikiendelea kunichuruzika puani na usoni.
Kwa kipigo nilicho kipata kikanifanya sehemu ya chini ya jicho langu moja kuvimba na kuacha uwazi mdoogo sana wa kuona huku jicho langu la pili likiwa limejaa machozi na kusababisha hata nisione vizuri ni wapi ninapo elekea.Harufu kali ikaanza kutawala katika pua zangu na nikajitahidi kutazama katika chumba nilicho ingizwa nikaona damu nyingi za binadamu zikiwa zimetapakaa kwenye ukuta na sakafu za chumba hicho huku kukiwa na fimbo za mkia wa samaki mmoja anaye itwa taa.Kitu kingine kinacho changia chumba nilicho ingizwa kuwa na harufu kali na mbaya ni kutokana na miguu ya binadamu iliyo katwa na ipo pembeni ikiwa imeoza huku ikishambuliwa na funza walio jazia kwa unene
Jitu lililo nibeba likanibwaga kwa nguvu chini na kujikuta nikiuangukia mkono ule nilio vunjika kwenye ajali na nikausababisha ukastuka kidogo.Wakaanza kuzungumza lugha ambayo sikuielewa ila nikakumbuka kuna movie moja ya wamarekani wamecheza na wasomalia ambao walikuwa wameiteka meli ya Mafuta ya wamarekani pamoja na manahodha wake,nikakukumbuka kipande kimoja cha jambazi wa kisomali alipokuwa akimfokea nahodha wa meli kwa kuto kuwaonyesha walipo wafanya kazi wengine.Lugha na lafudhi wanazo zungumza hawa jamaa moja kwa moja nikajua nimekamatwa na wasomali.Jamaa wakaanza kujibizana wao kwa wao huku kila mmoja akihitaji kufanya anachohitaji kukifanya kwangu mimi japo sielewi wanacho kizungumza ila kwa vitendo nikaona jinsi wakinihusisha katika mabishano yao.Jamaa lililo nibeba likaninyanyua na kuzivuta nguo zangu zote nilizo zivaa na kuzichana chana na kubakiwa na boxer,Mwili mzima ukaanza kunitetemeka na maumivu yote nikayaweka kando na kuhisi jamaa anaweza kuniingilia kinyume na maumbile nikajiweka tayari kwa lolote hata nife lakini si kwa kuingiliwa kinyume maumbile nikiwa ninajiona.
Jamaa akaanza kufungua mkanda wake huku akicheka cheka ila mwezake akamzuia na kumwambia kitu ambacho sikuelewa ni kitu gani na kumfanya jaa kuacha kuufungua mkanda wa suruali wake na kuchukua moja ya fimbo ya mkia wa taa kisha akasimama mbali kidogo na mimi,Akarusha fimbo moja ikajikunja mwilini mwangu kisha akaivuta hapo ndipo nikahisi ninakufa kwani kila anapo ivuta fimbo hiyo ndivyo nyama ya mwili wangu inavyo chomoka katika sehemu zote fimbo hiyo itanapo pita kwani inavijimiba vigumu.Nikashuhudia idadi kubwa ya fimbo zikitua juuu ya mwili wangu na kuzidi kunichanganya kiasi kwamba mwili wangu wote ukajaa damu.
“Mungu wangu kama kunakitu kibaya nimekifanya duniani nakuomba unisamehe”
Nikajikuta nikizungumza maneno hayo huku machozi yakinimwagika ila jamaa hakujali kulia kwangu zaidi ya kuendelea kunicharaza mikii ya taa.Jamaa mwengine akatoka ndani ya chumba huku sura yake kwa mbali machozi yakiwa yanamlenga lenga.Baada ya muda akarudi akiwa anaburuza mpira mnene na akazungumza kwa sauti kubwa na mtu wa nje kisha baada ya muda maji yakafunguliwa na yakatoka kwa kasi katika mpira alio ushika jamaa na kuuelekezea kwangu.Maji mengi yaliyochanganywa na chumvi yakanirusha hadi kwenye ukuta na kuniangusha chini ila jamaa hakuacha kunimwagia.Taraibu nikaanza kuona sura za watu ninao wapenda zikipita taratibu katika ubongo wangu ikiwemo mama yangu mzazi.Nikaiona sura ya Mama Caro jinsi usiku alivyokuwa akila chakula changu nilichokuwa nimekipika kwa ajili ya Christina ambaye hadi sasa hivi sijui yupo hai au amekufa.Nikaiona sura ya Caro akiwa anatabasamu huku akicheza mziki ukumbini kwenye sherehe yangu ya kukaribishwa nyumbani.
Mawazo yangu yangu yakakatika gafla baada ya mlango kufunguliwa na akaingia yule dada ambaye hadi sasa sura yake sijaiona.Akazungumza kwa lugha ya kisomali na kumfanya jamaa anaye nimwagia maji kusitisha zoezi na kunifwata nilipo jikunyata kama kifaranga kilicho nyeshewa na mvua kali.Akanivuta na kunisimamisha na kuniachia gafla nikajikuta nimeanguka chini kama mzigo kwani miguu yangu yote imepoteza nguvu.Jamaa wakaanza kunicheka na kumfanya dada aliye ingia kuzungumza kwa sauti ya ukali na kuwafanya jamaa kunyamaza kimya na yule aliye nimwagia maji kuninyanyua tena na kunishika bega na tukaanza kuondoka huku mimi na mijamaa tukiwa tumetangulia mbele huku msichana akawa anatufwatia kwa nyuma huku tukiwa tunapita kwenye kordo yenye giza kidogo na sikujua ni wapi wananipeleka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikastukia kusikia kishindo kizito pembeni yangu huku nikiwa nina pepesuka nikajikuta nikitazama ni nini kilicho tokea, nikashangaa kumuona lile jitu lililokuwa likinichapa limeanguka chini kama mzigo na kulifanya jamaa lililo nishika mkono kugeuka na kumkuta mwenzake akiwa chini,Nikashangaa kumuona msichana tuliye kuwa naye akimfyatulia rasasi na bastola yake aliyo ifunga kiwambo cha kuzuia sauti na risasi kama nnne zikatua kwenye kifua cha jamaa aliye nishika na kumfanya naye aanguke kama mzigo na mimi kwa kiwewe nikajikuta nimelala chini,kitendo cha majamaa kuuliwa kilitendeka ndani ya dakika mbili .Msichana akanishika kwapa na kuninyanyua na mkono wangu mmoja akiupitisha kwenye shingo yake na kwa mwendo wa haraka haraka tukaanza kuondoka eneo hilo.
Tukashuka kwenye ngazi zinazoelekea chini ya arthi na tukatembea mbele kufwata njia iliyo na giza huku msichana akiwa amewasha simu yake ikiwa na tochi.Tukatembea kwa mwendo wa kama lisa zima huku mara kwa mara akiniambia nikaze mwendo hata kama wezake alio wasaliti watakuwa wanatufwatili wasitukute.Tukakuta mlango wa chuma mbele yetu huku ukiwa umefungwa na kufuli lenye nyororo ndefu yenye kufuli kubwa lililo jaaa kutu,akaniegemeza ukutani na kukaa mbali kidogo na mlango na kuanza kulilenga kufuli kwa kutumia bastola yake na risasi kadhaa zikalifanya kufuli kufunguka na akauvuta mlango kwa nguvu kisha akanirudia kunishika kama alaivyo nishika kwa mara ya kwanza na kutoka nje.Tuakatokea kwenye msitu wenye miti iliyo kaushwa na jua kali tukalikuta gari likiwa limefichwa kwenye kichaka aina ya Land Rover new Model.Akatoa funguo ya gari hilo na kuliwasha kwa kutumia rimoti ya gari hilo lenye namba za usajili zisizo za Tanazania hapo ndipo nikapata uhakika kuwa sipo Tanzania
Akaniingiza ndani ya gari na kunilaza katika siti ya nyuma na kunifunika na shuka aina ya blangeti na kunibakiza kichwa.Akaondoa gari kwa kasi ya ajabu huku nikirushwa rushwa kutokana na gari kuingia katika mashimo shimo na inavyo onekana barabara ni mbovu.Nikashiindwa kujua nijilaze kivipi kwani kila sehemu ya mwili wangu imejaa vidonda vinavyo uma kupita maelezo
“As….ante kw…a kunio…koa”
Usijalii umetokea Tanzania?”
“N…dio”
“Mkoa gani…?”
“Dar….”
“Karibu Somalia”
“Nmefikaje fikaje…..?”
Kabla hajanijibu swali langu nikastushwa na breki kali za gari alizo zifunga na kunifanya nijigonge kwenye siti za mbele.Nikajinyanyua taratibu huku maumivu ya vidonda vyangu vikiongezeka na kwakupitia uwazi wa siti mbili za mbele na kiio cha mbele ya gari hilo nikaona kizuizi cha polisi huku wakiwa na bunduki zao mikononi na mbwa wakubwa mithili ya mbwa alaiye nikimbiza katika ufukwe wa bahari
“Tulia hivyo hivyo na jifinike hilo blangeti.Polisi wanakagua magari”
Dada alaizungumza na sikuwa na haja ya kumuuliza swali kwani hali alisi nina iona mwenyewe la hali hiyo ikaufanya mwili wangu kuanza kutetemeka huku yeye akivua kofia alilo livaa na kuziweka vizuri nywele zake ndefu na nyingi na kunifanya nishindwe kumuona sura yake vizuri,Nikajifunika mwili mzima nikaanza kusikia kucha za mbwa zikikwaruza kwaruza kwenye mlango wa gari katika siti ya nyuma huku wakibweka kwa sauti ya juu
Mwili mzima ukaendelea kunitetemeka sikujua itakuaje kwani nilisikia askari wakianza kuzungumza kwa sauti ya ukakali huku wakimfokea dada alaiye niokoa kutoka mikononi mwa magaidi wezake,nikastukia mlango ukigongwa kwa nyuma na kitu kizoto sikutaka kujua ni nini zaidi ya kuendelea kuling’ang’ania blangeti langu lililo nifunika kuanzia miguuni hadi kwenye kichwa changu.Gafla nikastukia gari likiwashwa na kurudishwa nyuma kwa kasi ya ajabu kisha likakunja kona ya gafla huku nikizisikia breki zinavyo fanya kazi yake ya kulisimamisha gari hili kitendo kilicho nipelekea kujigonga kwenye mlango.Nikasikia gia namba moja ikiingizwa kwa kasi huku mbili ikirukwa na kukimbilia kwenye gia namba tatu na kulifanya gari lizidi kukumbia
Nikaanza kusikia milio ya risasi ikija upande wetu nikajikaza taratibu nikanyanyua kichwa changu huku nikichungulia kwa kupitia kioo cha nyuma ili nijue ni wakina nani wano turushia.Nikaona gari mbili aina ya Ford zikiwa na vingora zikija kwa kasi huku askari wake wakiwa wamejitokeza kwenye vioo vya gari hizo wakifyatulia risasi gari letu
“Rudisha kichwa chako chini”
Dada aliye niokoa alizungumza kwa sauti kali na kunifanya nikirudishe kichwa changu chini na kujifunika na blangti langu.Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo sauti za vingora ilipungua na baada ya muda kidogo sikuzisikia tena ikanilazimu kukinyanyua tena kichwa changu kama mara ya kwanza kuchungulia ni nini kimewapata askari waoa tufukuzia.Sikuziona gari zozote zinazo tufwata na sehemu tuliyopo ni barabara ya msituni sikuona dalili ya kuwa na uhai wa mtu au nyumba katika msitu huo ambao umejaa miti mingi
“Tupo wapi?”
“Msituni”
“Wale polisi waliokuwa wakitufwata?”
“Nimewapoteza na huku sina hakika kama wanaweza kutufikia”
Sikuwa na swali la kuuliza zaidi ya kukaa kimya,Ila kitu kingine kilicho niogopesha ni kumuona dada akiwa amelivaa tena kofia lake lililo mbakisha macho tu.Safari ikaaendelea kama umbali wa kilomita 10 gafla akalisimamisha gari lake kisha akashuka huku mkononi kwake akiwa na bastola aina ya M1911 mbayo inaingia risasi 45 katika magazine yake.Akauchunguza msitu kwa umakini kisha akarudi ndani ya gari
“Eddy unaendeleaje?”
Aliniuliza huku akiliwasa gari lake na safari ikaendelea wala sikujua ni wap tunapo elekea
“Bado mwili unaniuma sana?”
“Usiwe na shaka tumebakiza kama kilomita moja na nusu tufike kwenye kijiji kimoja ambapo kuna mtu ninaye mfahamu”
Safari ikaendelea huku gari akizidii kuiongeza mwendo ambao endepo tutakanyaga kitu chochote kilicho kaa vibaya lazima tutaanguka.Tukafika katika kijiji kimoja ambacho ni kidogo chenye nyumba chache za watu huku watu wengi wakiwa wamevalia nguo nyeupe kwa upande wa wanaume na kwa upande wa wanawake wangiwao wamevalia mabaibui meusi.Kila mmoja akaanza kutushangaa ila na mimi ikanibidi nianze kushangaa baada ya kuwaona watoto wadogo wakiwa wamevalia mikanda ya risasi huku wakiwa na bunduki zenye uwezo mkubwa ambazo mara nyingi kwa Tanzania nina waona nazo polisi
“Eddy nisubiri ninakuja”
Akashuka ndani ya gari na kuingia ndani ya nyumba iliyojegwa kwa udongo aada ya muda akarudi akiwa ameongozana na vijana wawili wakiwa wamebeba machela kisha wakanishusha kwenye gari na kuniweka juu ya machela na wakaniingiza ndani ya nyumba hiyo ambayo muonekano wake wa nje ni mmbaya.Cha kustaajabisha nikaona jamaa wakishuka kwenye gazi kwenda chini na wakaingia katika mlango ambao ndani ya chumba hicho kuna taa nyingi huku kukiwa na wodi vitanda vingi vya wagojwa pamoja na madaktari
“Eddy usiogope hii ni hospitali ipo chini ya ardhi huku utapatiwa matibabu na utapona”
Dada niliye kuja naye alizungumza huku akinishika kiganja changu cha mkononi huku jamaa walio nibeba wakizidi kupiga hatua kuelekea mbele kwani ukubwa wa chumba hicho kina uwezo wa kukusanya watu wengi huku sehemu nyini zikiwa na milango sikujua ni milango ya kuingilia wapi.Tukaingia katika chumba kimoja chenye taa nyingi na nikakuta madaktari watatu wakiwa wamevalia nuo za kijani huku wakijifunga vitambaa vya kijani vilivyo ziba pua zao na midomo yao.Wakaniweka juu ya kitanda kicha mmoja wao akachukua sindano na kunichoma na nikaanza kusikia mwili wangu ukizizima na kufa ganzi kabisa.
Madaktari wengine wakawa na kazi ya kunifuta damu iliyo toka hadi ikanikauka,baada ya zoezi hilo wakaanza kazi ya ya kunishona katika mwili wangu sehemu zote nilizo chanika huku sehemu nyingine wakiniweka bandeji ikiwemo kwenye jicho langu lililokuwa limevimba.Baada ya huduma waliyo nifanyia nikaipelekwa kwatika chumba cha kwangu peke yangu cheche kitanda kimoja na kikti komoja tuu
“Eddy utapona”
“Nashukuru dada yangu yaani nitazidi kukushukuru pale utakapo nisaidia nikirudi nyumbani nchini Tanzania”
“Kurudi Tanzania hilo sio gumu kwangu ila na mimi nitakuomba kitu kimoja ambacho nitafurahi ukikitekeleza kwa ajili yangu”
“Kitu gani hicho”?
“Nataka ukanilipizie kisasi katika familia moja iliyopo nchini Tanzania”
“Familia gani hiyo?”
“Familia ya Mama Caro”
Moyo ukanipasuka na kujikuta nikimtazama dada katika macho yake ila kutokana na jikofia lake sikumjua kuwa yeye ni nani,ila nikajifariji kwamba anaweza akawa mama Caro mwengine tofauti na niye mjua mimi
“Mama Caro yupi?’
“Nitakuambia ni yupi”
Akatoka nje ya chumba bila hata kuniaga na kunifanya nizidi kujiuliza maswali mengi ambayo yanakosa majibu baada ya muda akarudi akiwa amebeba mfuko wenye chakula na kukaa katika kiti na kuanza kunilisha chipsi taratibu
“Eddy katika maisha si kila mwanadamu anakuwa ni mbaya….Ila kuna watu wanamsababisha yeye akawa ni mbaya na roho ya kikatili”
“Kwa nini unazungumza hivyo?”
“Kwa sababu…..Mimi nina historia ndefu sana katika maisha yangu.Baba yangu alikuwa ni msomali alikwenda Tanzania miaka mingi ya nyuma na kwabahati nzuri akapata mwanamke wa Kitanzania ambaye ni mama yangu.Kwa bahati nzuri mama yangu alikuwa ni mafanya biashara mzuri na mwenye pesa zake kiasi kwamba akawa anafahamiana na watu wengi kiasi kwamba akajijengea maarufu mzuri.Ila umaarufu wake ulikuja kupotea gafla baada ya kupakaziwa kuwa anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kitu mbacho kilikuwa si kweli……Ila katika kesi ile mama yangu alitumia kiwango kikubwa sana cha pesa na ikanilazimu mimi kuiba pesa ili kumuokoa mama yangu……Ia juhudi zangu zilifanikiwa ila nikaanza kutafutwa nchi nzima…..Ila kitu kingine kilicho sababisha furaha yangu ipotee katika maisha yangu ni siku nilipoona kupitia taarifa ya habari nikiwa nipo nchini Kenya mafichoni juu ya mauaji ya wazazi wangu wote wawili ndipo hapo nilipo amua kuwa katili kiasi kwamba sina huruma na mtu yoyote anayeingia katika 18 zangu”
Nilikaa kimya huku nikimsikiliza kwa umakini dada aliye niokoa kutoka katika mikoto ya magaidi wezake.
“Samahani dada yangu unaweza kuivua kofia yako uliyo ivaa?”
“Kwa ajili yako nitalivua”
Akasimama na kugeuka akanipa mgongo kisha taratibu akaivua kofia yake na kuziweka nywele zake vizuri kisha akageuka na kunitazama.Moyo wangu ukastuka na kujikuta macho yangu nikiwa ninayatoa huku nikiwa siamini mtu aliye simama mbele yangu ni PRISCAR msichana aliyekuwa akifanya kazi katika kampuni ya mama Caro na pia aliiba pesa nyingi za kampuni na kumfanya mama Caro anifukuze ofisini kwake
“Priscar…..!!?”
“Abeee”
“Ni wewe?”
“Ndio Eddy”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mbona sauti yako imebadilika?”
“Eddy ilinilazimu kuweza kubadili mfumo wangu wa kuzungumza kwani niliamini ukiisikia sauti yangu utaikumbuka”
Priscar alizungumza huku mahozi yakimwagika akapiga hatua na kuja kukaa pembeni yangu kutokana nina dripu la damu katika mkono wangu wa kushoto hku mmkono wa kulia ukiwa na dripu la maji sikuweza kmshika Priscar
“Priscar kwanini hukunifahamisha siku zote sehemu uliyopo”
“Eddy nisinge weza kufanya hivyo kutokana wewe upo karibu sana na mama Caro na kitu kingine ambacho Eddy nilikigundua kati yako wewe na mama Caro ni kwamba yule sio mama yako mzazi”
“Nani alikuambia juu ya hilo swala?”
“Unajua nini Eddy tuachane na hiyo mada kwani sihitaji chuki yangu iwe juu yako tena kwani wewe ulikuwa pia upo miongoni mwa watu nilio panga kuwwangamiza ili toho yangu iridhike”
Ikanilazikmu kukaa kimya kwani nikileta ujinga wowote ninaweza kujikua ninakufa pasipo kutegemea.Priscar akanitazama kwa macho makali kisha akaachia msunyo mkali na kusimama
“Eddy namchukia sana Mama Caro tena sana kwani yeye ndio chanzo cha familia yangu kusambaratika na yeye pia ndio chanzo cha mama yako kupotea katika mazingira ya kutatanisha”
Nikastuka na kujikuta nikijiweka vizuri huku mapigo yangu ya mbiao yakianza kunienda mbio kiasi kwamba nikahisi kupagawa na kigugumizi cha gafla kikanipata
“Mb…ona mama yangu a….mes….hakufa”
“Eddy acha kuwa mjinga wewe umeona wapi mtoto mwenye mama yake hayashuhudii mazishi ya mama yake kama ilivyo kuwa kwako wewe,kwani walishindwa kukusubiria wewe hadi uzinduke ndio wakazike?”
“Priscar mbona sikuelewi unanichanganya?”
“Na utachanganyikiwa sana ila ukweli ni kwamba mama yako hajafariki na isitoshe yupo mikononi mwa Mama Caro”
“Wewe umejuaje…..?’
“Eddy ninayo yajua mimi ni mengi sana luliko ulivyo kuwa ukinichukulia na mama yako hakuwa na ugojwa wa aina yoyote kama daktari alivyo kuambia kuwa anaumwa kisukari na ugojwa wa moyo ila alikula sumu iliyowekwa kwenye chakula na sumu hiyo huwa hutumia masaa zaidi ya kumi na mbili hadi mtu afariki huwa inamuua taratibu unakumbuka ile siku uliyo mpeleka mama yako hospitali kabla ya hapo aliletwa na nani nyumbani kwenu”
Nikafumba macho na kuanza kufikiria siku ambayo mama alirudi nyumbani kwa mara ya kwanza kumbukumbu ziligoma kujua ali;etwa na nani kwani siku hiyo ninavyo hisi sikuwepo nyumbani.Ila nilicho kikumbuka nilikuta alama za matairi ya gari nje kwetu na inavyo onekana kulikuwa na mtu alikuja na gari.Ila kitu kingingine ninacho kikumbuka nilimkuta mama akiwa anakula nyama.Sikutaka kula kutokana nilitoka kufakamia mipilau atika maulidi ya watu mtaa wa pili kutoka ninapo ishi
“Sikujua aliletwa na nani?”
“Aliletwa na mama Caro na yeye ndio aliye mpatia mama yako sumu zilizo kuwa kwenye chakula alicho kuwa akikila”
“Priscar hayo yote wewe umeyajuaje?”
“Eddy ni……..”
Priscar akakaa kimya baada ya kuingia daktari na wakaaanza kuzungumza lugha yao nisiyo ijua kisha daktari akatoa sindano na kunichoma kwenye bega kisha akatoka
“Amekuchoma sindano ya kukaausha vidonda haraka”
“Inauma”
“Tuachane na hilo swala la sindano ila nataka ujue kitu kilichokupata wewe katika maisha yako na yangu”
“Priscar umejuaje kuwa mama yangu hajakufa na yupo mikononi mwa Mama Caro”
“Eddy nilitumiwa sana na mama Caro…….Alinifanya kuwa kijakazi wa matukio yake ya ajabu ajabu sana…..na kila kitu alichokuwa akikifanya nilikuwa ninampa ushauri mimi……Kwangu nilitambua kuwa ni mtu mzuri sana kutokana tanu nikiwa mtoto alikwa rafiki wa mama yangu na pia aliweza kuchukua mbinu nyingi za mafanikio kutoka kwa mama yangu hadi akafika pale alipo sasa hivi na yeye ndiye aliye nishawishi mimi kusomea maswala ya mawasiliano na kuniajiri katika kampuni yake”
Nikashusha pumzi nyingi huku nikiaanza kufikiria ni kitu gani cha kufanya kwani kila kitu alicho nieleza Priscar kiliendana na ukweli ila nikashindwa kuelewa ni kwanini mama Caro aliamua kufanya kitu kama hicho.Gafla tetemeko la ardhi likatokea na kuanza kutetemesha vitu pamoja na sisi na kama dakika tatu mbeleni likaacha na hali ikawa shwari
“Tumevamiwa hilo ni bomu lililo pigwa na ndege za kijeshi”
Mapigo ya moyo yakaanza kuniaenda mbio huku kwa mbali tukaanza kusikia milio ya risasi ikirindima nje.Priscar akatoa bastola yake na kuikoki vizuri na kuanza kupiga hatua kuelekea njee huku akiniacha kitandani na madripu yangu
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio huku kijasho chembamba kikianza kunimwagika,Mlio ya risasi na mabomu ikazidi kusikika nje ila kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo ilivyozidi kupungua hadi ikafikia uwakati kukawa kimya kabisa,Gafla taa zote zikazima na giza kali kupita maelezo likatawala eneo zima la chumba nilichopo.Nikajikausha kimya kitandani huku nikisikilizia ni kitu gani kinacho endelea na mbaya zadi kama alivyo niambia Priscar kwamba sehemu hii nilipo ni chini ya ardhi
Nikaanza kusikia miguu ya watu ikija eneo nililopo nikajitahidi na kuzitoa sindano za dripu zilizopo kaika mikono yandu kisha kwa haraka nikahuka kitandani kutokann na giza sikuweza kukimbia kwenda sehemu yoyote ila kitu kilicho nisaidia ni usawa wa kitanda kilichopo karibu yangu na nikaingia chini ya kitanda nilichokuwa nimelalia japo kuwa chini kina auwazi mkubwa ila nikajificha hivyo hivyo ni bora watu wanao kuja ndani wanikute chini ya kitanda kuliko juu ya kitanda
Mlango ukafunguliwa kwa kupigwa kwa teke na kujibamiza ukutani kwa nguvu,nikazidi ktetemeka kiasi kwamba nikajikuta ninazidi kuchanganyikiwa.Miguu ya mtu mmoja ikaanza kuzunguka zunguka ndani ya chumba nilichopo na gafla ikasimama karibu yangu.Jamaa akapiga risasi mbili ukutani kisha kazidi kutembea tembea akizunguka.Gagla milio mingi ya risasi ikaanza kusikika mlanoni huku vilio vya watu wakiugulia maumivu na kudondoka chini kama mizigo ya magunia
Risasi nyingi zikazidi kurindima ndani ya chumba na kuzidi kunipagawisha kwani tangu kuzaliwa kwangu sina kumbukumbu kama nilisha wahi kusikia milio ya risasi kama ninayo isikia katika chumba hichi nilichopo.Baada ya kama dakika tano ukimya mwingi ukatawala ndani ya chumba.
“Eddy Eddy”
Nikasikia sauti ya Priscar ikiniita na kunifanya kukaa kimya huku nikiisikilizia tena,akarudia tena kuniita ikanibidi niitike.Nikatoka chini ya kitanda nikaona mwanga wa simu aliyo ishika Priscar nikaaza kupiga hatua za kumfwata hadi sehemu aliyo simama.
“Wamekudhuru?”
“Hapana”
“Nishike koti tutoke humu ndani”
Nikashika koti Priscar kwa nyuma na tukaanza kwenda njee.Tulitembea kwa msaada wa mwanga hafifu wa tochi hadi tukafika nje na kukuta hali ya kijiji ipo tofauti kama nilivyo ingia kwani nyumba nyingi zinawaka moto na maiti za wana kijiji zikiwa zimesambaa eneo zima ila kunaa baadhi ya watu wakiwa wamesalimika huku wengine wakiwa ni wamejeruhiiwa vibaya na baadhi yao kupoteza viungo vya mwilini mwao.Gari tulilo kuja nalo nikaliona likiteketea kwa moto.
“Eddy jikaze mpenzi wangu tutembe hali ya hapa sio nzuri kabisa”
“Sawa ni nini kimetokea?”
“Ni wale wezangu walikuja kutuvamia wakitutafuta mimi na wewe”
“Wamejuaje kwamba mimi na wewe tupo hapa”
“Kuna kifaa fulanikipo sehemu za mgongo wangu kilichomekwa kipindi ninajiunga nao.Huwa kina tumika kama kifaa cha alama na kila sehemu ninayo kwenda kwenye mitambo yao lazima wataniona”
“Wakana kuonaje onaje?”
“Kwa alama nyekundu ila nitahitaji unitoe na tukiendelea kukaa hapa ndivyo jamaa watazidi kuja kwani hawa tulio waua ni badhi na ninajua lazima watakuja wengine”
Tukaanza kutokomea msituni japo mwili wangu umejawa na maumivu makali ila nikajikaza na kuzidi kusonga mbele japo tunapo kwenda hatupajua
“P nimechoka mwenzako naomba tupumzike”
“Eddy jikaze baba yangu la sivyo tutakufa”
“Hakuna mtu anaye tufwata”
“Eddy mpenzi wangu hembu jikaze wewe ni mtoto wa kiume je upo tayari kufa kirahisi kiasi hicho unacho taka?”
Maneno ya Priscar yakanipa nguvu kiasi na kuanza kupiga hatua za kwenda mbele.Mawingu yakaanza kujikusanya taratibu na kwa kadri tunavyo zidi kwenda mbele ndivyo yalivyo jikusanya na na matone ya mvua yakaanza kudondoka taratibu
“Eddy tuongeze mwendo”
Kusema kweli mwili mzima umechoka kiasi kwamba nikatamani ardhi ipasuke ili niingie,Mvua ikazidi kuongezeka huku ikiandamana na upepo mkali tukaingia chini ya jiwe kubwa lenye uwazi ukubwa lengo ni kuweza kujikinga na mvua.Priscar akavua koti lake na kunivalisha kisha akabakiwa na nguoyake nyeusi aliyo ivaa.Akatoa kisu kikubwa na kunikabithi mkononi kisha akavua shati alilo livaa na kunigeuzia mgongo
“Eddy umeiona hiyo sehemu yenye alama ya mshono?”
“Ndio”
“Ichane kwa kisu kisha utoe kitu utakacho kiona”
“Haaaa P siwezi”
“Eddy wewe ni mwanume acha kuwa na roho nyepesi kiasi hicho”
“Ila…”
“Eddy hakuna cha ilaa fanya nilicho kuambia”
“Mmmm siwezi”
Nilizungumza huku nikimrudishia Priscar kisu chake nikastukia akigeuka huku akinielekezea bastola yake
“Eddy utafanya au haufanyi nilicho kuambia?”
“Sa..aawa”
Sura ya Priscar ilbadilika kiasi kwamba nikahisi atanipasuaubongo kwani Priscar wa sasa hivi sio kama Priscar wa zamani.Akageka na kunielekezea mgongo na nikaanza kumchana sehemu aliyo nielekeza huku mikono ikiwa inanitetemeka kiasi kwamba nikaanza kukosea kosea
“Eddy fanya haraka”
Nikajikaza na kupapasua na kukuta kidude kidogo kilicho kama kifuniko cha kalamu kisha nikakitoa na kumfanya Priscar kutoa miguno ya maumivu ila akajikaza na kulivaa shati lake huku damu zikiwa zinamtoka.Kwa mbali tukaanza kusikia milio ya mbwa wengi wakibweka huku sauti hizo zikija eneo letu
“Wanakuja”
“Wakina nani?”
“Wezangu tukimbie”
Tukaanza kukimbia huku Priscar akiwa yupo mbele yangu hapo ndipo nikapata fursa ya kumchunguza Priscar vizuri na kugundua kuwa kuna amepungua mwili kwa kiasi kikubwa na kuwa mwembamaba hata makalio yake yaliyo kuwa makubwa yamepungua.Kelele za mbwa zikazidi kutusogelea kiasi kwamba nikaongeza kasi ya kukimbia na kumpita Priscar adi mimi wemnyewe nikajishangaa nguvu nimezitolea wapi kwani kwa wakati huu hata maumivu ya mateso sikuyasikia kivile japo jicho langu moja lina plasta kubwa
Mlio mwengine ukaongezeka na moja kwa moja sikuwa na haja ya kumuuliza Priscar ni kitu gani kwani ni Helcoptar ndio inayotoa mlio huo.Ila kadri nilivyo zidi kukimbia nikaanza kuhisi kitu nyuma yangu ikanilazimu kugeuka na kujikuta nikistuka kwani sikumuona Priscar na kujikuta nipo peke yangu katika kinjia nilicho pita.Roho moja ikawa inanishauri nikimbie ila nyingine inanishauri nirudi nyuma kumtafura Priscar.Milio ya mbwa ikazidi kukaribia eneo nililo kuwepo mimi na kunifanya nianze kukimbia kwenda mbele huku moyoni mwamngu nikimuomba Mungu anisamehe kwa kushindwa kumuokoa Priscar
Kasi yangu nikaanza kuhisi si chochote nyuma ya mbwa anayenikaribia kunifikai nikiwa nina geuka geuka nyuma nikajikuta miguu ikigongana gongana na kunifanya nianguke chini kama mzigo ila gafla nikamuona mbwa akitoa kijimlio cha maumivu na kulala chini huku damu nyingi zikimwagika.Nikatizama mbele yangu na kumkuta Priscar akiwa amesimama kwa mabali huku bastola yake akiwa amaeilekezea kwangu
“Nyanyuka na ukimbie”
Nikanyanyuka na kuanza kukimbia huku nikiwa ninajiuliza ni kivipi Priscar alikimbina na kupita njia nyingine kiasi kwamba ninamkuta amesimama mbele yangu.Niamfikaa na tukaanza kukimbai huku mvua ikisabaisha matope mengi kiasi kwamba mara kadhaa nilijikuta nikianguka chini na kujikuta nikichafuka mwili mzima kwa matope.Priscar akaingia kwenye pango moja lenye giza na mimi nikamfwata na tukaanza kutembea kwenda mbela kwa kutumia mwanga wa simu yake.Popo wengi walimo ndani ya pango hilo wakazidi kuniogopesha ila sikuwa najinsi.Tukafika sehemu yenye uwazi mkubwa na kuka kwa ajili ya kujipuumzisha kwani mimi nahisi nimechoka sana kumpita Priscar
“Priscar”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Bee”
“Hivi kweli tutakuwa hai?”
“Eddy cha msingi umuamini Mungu”
“Kusema kweli nimeka tama ya kuishi sina hata hamu ya kunyanyuka hapa niendelee mbela kwani tunapokwenda hatupajui”
“Eddy wewe ni mwanaume unasema maneno ya kukatisha tama kiasi hicho je mimi mtoto wa kike unataka nisemeje?”
“Sawa P ila tambua hapa mimi hapo nilipo mwili wangu hauwezi kuhimilii hii mikiki mikiki kwani nahisi nitapoteza maisha yangu muda si mrefu”
“Eddi tambua ya kuwa Mugu alikuwa na wewe kuanzia mawazo wa safari yako ya kuja huku hadi hapo ulipo fikia kwani ulidahani utakutana na mimi?”
“Hapana Priscar yaani kama ni kujilazimisha nimejilazimisha sana katika kukimbia ni vyema tukajisalimishe?”
“Eddy Eddy kile kipogo ulicho kipata pale kilikuwa ni nisu hembu piga picha yule mkubwa wetu angerudi pale unadhani itakuwaje?”
“Priscar hivi huku ninmefikaje fikaje
“Ile siku ambayo ulitekwa wewe sisi tukikuwa tupo katika fukwe za Tanzania lego letu lilikuwa ni kwenda kuvamia kiwanda cha mafuta.Ila tukiwa katika harakati za kuanza kukivamia ndio tukakuona wewe ukiingia kwenye maji ndio ikatulazimu tukuteke na kitu kingine zile risasi wezangu walizo kuwa wakikupiga wewe milio yake ikawastua wanajeshi askari wa majini na kusababisha zoezi letukukwama.Tulikuwa tumeicha meli yetu mbali kutoka katika fukwe za Tnazani”
“Kwa hiyo mulitumia meli kuja nchini Somalia?”
“Ndio kitendo ulicho kifanya kilimchukiza sana bosi wetu na laity kama ningechelewa kurudi angekukata kiungo kimoja kimoja hadi ungekufa na kile chumba ulichoingizwa na wale mabaunsa ndio chmba cha watu wanao enenda kinyume na taratibu zetu kukatwa katwa viungo vyao”
“Priscar sijakuelewa katika kitu kimoja ulicho niambia wakati ule”
“Kitu gani?”
“Mama yangu amakuaje akawa hai na kama yupo hai mbona harudi nyumbani?”
“Eddy hujamjua vizuri mama Caro……Yule mwanamke ni Mafia kiasi kwamba mtu yoyote atakaye enenda kinyume na yeye lazima amuue,Alisha wahi kunimbia kuwa yeye alimuua mumwe wake kwa mkono wake mwenyewe”
“Weee”
“Usishangae yule mama ana mkono mrefu”
“Mkono mrefu kivipi?”
“Yaani anawatu wengi ambao humsaidia katika kazi zake za kigaidi wengi wao ni viongozi seriklini wa ngazi za juu”
“Eddy usinyanyuke kaa hivyo hivyo kuna kiktu nyuma yako”
Priscar alinistua sikujua ni kitu gani kinachomfanya aniambie nikae jinsi nilivyo kaa huku macho yake yakitazama nyuma yangu huku taratibu akiichomoa bastola yake gafla mwanaga wa simu tunao utumia ukaizima huku ukitoa mlio ukiashira kuwa simu imekwisha chaji
Nikasikia milio miwili ya risasi kutoka eneo tulilopo na kujikuta mwili mzima uki nitetemeka kiasi kwamba nikahisi haja ndogo ikitaka kunitoka.Ukimaya wa sekunde kadhaa ulio andamana na giza totoro ndani ya pango likanafanya nizidi kuogopa kwani hata Priscar hakuzungumza kitu chochote na wala sikusikia uwepo wake katika eneo tulilopo
“P…P”
Niliita kwa sauti ya chini ili niweze kujua ni kitu gani kilicho msibu ila mwenzangu hakuitika na kunifanya nizidi kutetemeka galfal nikashtukia nikizibwa mdomo na mtu aliyopo nyuma yangu
“SHIIII……”
Nikatambua ni sauti ya Priscar ila sikujua ni kwanini ameniziba mdomo,taratibu akaanza kunivuta nyuma na tukasimama huku akiwa nyuma yangu na akaanza kuninong’oneza
“Eddy hii sehemu sio nzuri”
“Kuna nini?”
“Kuna wanyama wa wabaya na wakuogopesha”
“Wametokea wapi?”
“Sifahamu hata mimi”
Tukatulia kama daki tano tukisikilizia kuna kitu gani kitakacho endelea ila ukimya ulitawala hatukusikia kitu cha aina yoyote kikijisogeza ndani ya pango tulilopo.
“Eddy nishikilie kiuno”
Nikamshika shati na tukaanza kutembea kwa hatua za taratibu huku sote tukiwa hatujui ni wapi tunapoelekea kutokana na giza kuwa kubwa na hatukuwa na kitu chochote kinacho weza kutusaidia kuona mbele wala pembeni,tukapiga hatua kama hamsini mbeleni tukaanza kuhisi mgurumo wa kitu kizito kikitokea mbele yetu,Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio gafla nikastukia Priscar akipontoka kwenye viganja vyangu na kuanza kupiga kelele zinazo elekea upande wa kushoto kwangu huku akionekana kupelekwa ndani zaidi katika pango hilo,nikiajipa moyo na ujasiri ukautawala mwili wangu kisha nikaanza kupiga hatua kufwata zilipo elekea sauti ya Priscar huku miguu yangu ikibahatisha eneo la kukanyaga.
Nikazidi kwenda mbele huku nikizisikia kelele za Priscar kwa mbali akiomba msaada huku akilitaja jina langu na kunifanya nizidishe hatua,nikapata wazo la kuutafuta ukuta wa eneo hilo kisha nikaanza kuufwata taratibu ila kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo sauti za Priscar zikaanza kufifia masikioni mwangu hadi ikafikia kipindi nikawa simsikii kabisa.Nikajipa moyo na kuzidi kupiga hatua kwenda mbele ila kutokana na hali yangu ya kuumwa kuwa si nzuri nikajikuta nguvu za mwili zikianza kuniishia huku hali ya kuchoka ikiutawala mwili wangu na kujikuta machozi yakinimwagika kwa uchungu kwani sikujua ni kitu gani kilicho mnyakua Priscar.Nikajiegemeza kwenye ukuta wa pango hilo huku nikitafuta pumzi ya kuweza kuendelea na safari ya kumfwatilia Priscar,gafla nikahisi kuna vitu vikinipandia katika miguu yangu kwa ufahamu wangu wa haraka haraka nikatambua nii wadudu Fulani wadogo wanao itwa SIAFU hii nikutokana na harufu yao kutawala puani mwangu na mmoja mmoja akaanza kuning’ata na mbaya zaidi wakawa wananing’ata sehemu zenye vidonda.
Nikaanza kuruka ruka huku nikiwatoa mwilini mwangu kwani maumivu ninayo yapata ni zaidi ya mauvivu kiasi kwammba inafikia hatua ninajikuta nipo katika hali ngumu huku nikianza kukihisi kifo kikianza kunitawala.Nikajitahidi kwenda mbele zadi hata ule utaratibu wangu wa kutembee kuufwata ukuta nikajikuta ninausahau na kutembea tembea kama mtu aliye changanyikiwa na ugumu wa maisha,Nikajikuta nikijigonga kwenye mawe makubwa na kuanguka chini mara kadhaa ila sikukata amaa zaidi ya kunyanyuka na kusonga mbele kiasi kwamba kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo nilivyo poteza matumaini ya kuishi duniani
Hatua mbili mbeleni nikajikuta nikianza kuelea hewani huku nikienda chini kwa kasi ya ajabu nikatambua nitakuwa nimeingia kwenye shimo kubwa,Ila kadri jinsi ninavyo zidi kwenda chini ndivyo nilivyozidi kuuona mwanga wa taa ambao ni wa rangi ya njano.Nikayafumba macho yangu huku nikimuomba MUNGU wangu kuweza kuniongoza katika kudondoka kwangu kwani mawazo na fikra zangu nikajua nilazima nitakwenda kutua chini kwenye jiwe kubwa au sehemu yoyote ngumu na ndio utakuwa mwisho wa uhai wangu,nikiwa bado nipo kwenye mawazo ya kufikiria chini ninapo elekea gafla nikajikuta nikitua kwenye kwenye kitu chenye asili ya nyavu ila ina uasili wa mpira kwani ilinirudisha tena juu kwa kiasi Fulani na kutua tena katika eneo hilo la nyavu na kutulia
Jicho langu moja likafumbuka na kuanza kulichunguza eneo hilo taratibu na kuona mafuvu megi ya vichwa vya binadamu pamoja na mifupa mingingi ikiwa imezagaaa sehemu mbali mbali katika eneo hilo lenye taa za nyingi za CHEMLI zilizo ning’inizwa kwenye kuta za dehemu hiyo yenye ukubwa kiasi huku nyavu niliyo lalia ikiwa hewani na kushikiliwa na baadhi ya kamba kubwa zilizo fungwa katika kuya nne za eneo hilo.Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kuliona shati la Priscar likiwa limening’inizwa kwenye moja ya kamba huku likiwa limelowana damu nyingi.Ukimya wa eneo hilo ukazidi kuniogopesha na kujiuliza ni viumbe vya aina ani ninavyo ishi katika eneo hili ambalo sidhani kama binadamu anaweza kuishi ila kitu kinacho nichanganya zaidi ni jinsi ya mpangilio wa vitu vilivyomo ndani ya eneo hilo kwani kuna CHUNGU kikubwa na cheusi kilicho wekwa kwenye mafiga makubwa matatu huku chini yake kukiwa na moto mwingi ukichemsha vitu ambavyo sikujua ni vitu gani
Gafla nikaanza kusikia sauti ya msichana akipiga vigelegele na makofi na sikujua ni wapi mtu huyo alipo,vigelegele vikazidi kuongezeka kwa kasi huku vikisikika katika kila upande wa eneo hili.Wasi wasi ukazidi kunitawala moyoni mwangu na gafla nyavu niliyo ilalia ikaanza kushushwa chini na vijitu vifupi na vyeusi sana na vina mabichwa makubwa tofauti na miili yao kiasi kwamba wanaogopesha hata kuwatazama mara mbili mbili.Vijitu hivyo vikaanza kujitokeza na kuzidi kuwa vingi kabla hata sijafika chini vikajipanga na kunibeba juu juu na nyavu yangu na wala sikujua vinanipeleka wapi huku vikizidi kupiga vigele gele kwa sauti ya juu na kuzidi kuyaumiza masikio yangu na kunipa wasiwasi mwingi
Nikastukia vikinirusha kwenye moja ya chumba kilicho jegwa na miti aina ya MIANZI ambayo ni migumu sana na si rahisi kuvunjika kisha vikaondoka huku vikikimbia.Mlio wa ngoma inayo onyesha ni kubwa kiasi ikaanza kusikika kutoka katika lile eneo nilio kuwepo matra ya kwanza na kujikuta nikianza kupata wasi wasi.Nikarudi hatua mbili nyuma na kustuka kuwa kuna kitu nitakuwa nimekikanyaga kwenye nikageuka taratibu na kukuta ni Priscar akiwa amelala kifudifudi hajitambui.Nikachuchumaa haraka na kumgeuza na kumkuta sura yake ikiwa amechafuka kwa tope jingi.Nikamstua kwa kumtingisha mara kadhaa ila hakuamka.Nikaanza kumsugua kwa kutumia kiganja changu eneo la katikati ya maziwa yake kwa kasi ya ajabu hadi ikafika hatua akastuka na kunyanyuka kwa kasi huku akionekana kuwa na wenge(amechanganyikiwa).Nikamdaka na kumziba mdomo kwani alianza kupiga kelele
“SHIIII P NYAMAZA”
“Eheee eheee”
“Tulia usipige kelele”
Nilimanyamazisha Priscar na akanitazama kwa muda kisha akanikumbatia kwa furaha kwani hakuamini kuniona mimi katika eneo hilo,baada ya muda Priscar akaniachia na kujifuta machozi yaliyokuwa yakimtoka
“Priscar ilikuwaje hadi ukafika huku?”
“Eddy sijua hata lile lililokuwa limenibebda lilikuwa ni jinyama la aina gani?”
“Limekudhuru?”
“Hapana”
“Inavyo onekna hawa si binadamu wa kawaida cha msingi hapa tutafuta jinsi ya kutoroka”
“Eddy tutatokea wapi?”
“Priscar hilo la kutokea wapi si lamsingi ila cha msingi ni kujua ni jinsi gani tunaweza kutoka humu ndani”
Tukiwa tunaendelea kujadiliana na Priscar jinsi gani tutoke tukazisikia sauti za vigelegele vikija katika eneo tulilopo tena za wakati huu ziliongezeka na sote tukajua wataukuwa wanatufwata sisi.Ila tukastukia watu wawili wamakamo mmoja akiwa mwanaumemzee na mwengine akiwa bibi kizee wenye asili ya kizungu wakirushwa ndani ya chumba kingine kilicho tengenezwa na mianzi kama chumba chetu kama nilivyo rushwa mimi kisha wakaondoka kwa huku wanakimbia
“P hivi hawa ni binadamu au?”
“Ni binadamu ndio ila watu hawa hula nyama za watu wanaitwa Canibal”
“Weee kwa hiyo mimi na wewe tutaliwa nyama?”
“Inawezekana”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sikutaka niendelee kumuuliza Pridcar maswali zaidi ya kuwaza ni jinsi gani ninaweza kutoka ndani ya kijikibanda hicho kilicho tengenezwa kwa miti migumu huku kikiwa kimufungwa na kufuli kubwa kiasi kwamba sio rahisi kulifungua.Bibi wa kizungu akawa na kazi ya kulia huku akionekana kumlaumu mume wake
“My husband met us see now what I tell you this your observations about these people does not have any benefit in our lives he find whatever you see now?” (Mume wangu unaona sasa yaliyo tukuta,nilikuambia huu uchunguzi wako juu ya hawa watu hauna manufaa yoyote katika maisha yetu unaona sasa kinacho tukuta? )
“My wife pray God will help us in this” (Mke wangu tumuombe Mungu atatusaidia katika hili)
“What do you think is God who will hear the prayers of people who are desperate to life as we?” (Unadhani ni MUNGU gani atakaye sikia maombi ya watu wenye tamaa ya maisha kama sisi?)
“My wife calmed emotions will come into this cave Believe me, and when we come here we have a massive wealth through this video we took”( Mke wangu tuliza jazba tutatoka katika hili pango niamnini mimi,na tukitoka hapa tutakuwa na utajiri mkubwa kupitia hii video tuayo ichukua)
“One whole silly that your camera does not have any benefits at this time”( Kwanza zima hiyo kamera yako ya kipumbavu haina manufaa yoyote kwa wakati huu)
“The young among you there is someone who can speak English?” (Vijana kati yenu kuna mtu anaye weza kuzungumza kingereza? )
“Yes, Im able to talk”( Ndio mimi nina weza kuzungumza)
Priscar aliitikia huku akimtazama yule mzee na mimi nikawa kimya kwani sikuwa ninakifahamu kingereza kutokana na elimu yangu kuwa ni ya msingi niliyo ipata miaka mingi iliyo pita
“Do you have nothing to sav?”(Muna kitu chochote cha kujiokoa?)
“No we do not”(Hapana hatuna)
“Ohhhhh my God you see now the youth and also have nothing to save?”( Ohhhhh Mungu wangu unaona sasa hao vijana nao pia hawana chochote cha kujiokoa?)
“My wife is not blame how do you think I will now”( Mke wangu unavyo nilaumu unadhani mimi nitafanyaje sasa )
“But you are the cause of all this I told you we should not Afrika.Do you see now we leave our children orphans?”(Ila wewe ndio chanzo ya haya yote nilikuambia tusije Afrika.Unaona sasa watoto wetu tunawaacha yatima?)
“I HAVE SPOKEN TO FOOL YOUR MOUTH SHUT AND KEEP SILENT”( NIMESEMA FUNGA MDOMO WAKO WA KIPUMBAVU NA KAA KIMYA)
Mzee alizungumza kwa sauti ya juu ya kumfokea mke wake huku akimshika nywele za kichwani mwake na kumtingisha tingisha kiasi kwamba bibi wa watu akakaa kimya huku akitetemeka.Gafla vijitu viwili vikaja na a kwenda katika banda la wazee wa kizungu kisha vikapiaga miluzi wakaja vijitu vingine nane huku vikiwa vimeshika mishale na kufungua mlango wa kibanda cha wale wazee na kumtoa babu wa kizungu nje ya kibanda na kuanza kumshambulia kwa kumpiga na mishale kisha wakambeba juu juu na kuondoka naye na kumuacha bibi wa watu akilia kwa woga huku mimi nikiwa kama siamini kama haya yote yanatokea mbele ya macho yangu tena katika sehemu nisiyo itegemea kuifika katika maisha yangu huku akilini nikijiuliza zamu itakayo fwata itakuwa ni ya nani
Cha kumshukuru Mungu mlango wa bibi wa kizungu uliachwa wazi alicho kifanya Priscar ni kumuomba bibi anyamaze kulia na atazame lengo zima la kuweza kujioko ndani ya pango hili lenye vijitu vya ajabu.Bibi akafuta machozi yake kisha akatoka ndani ya kibanda alichokuwepo kisha akaja kusimama mbele ya kibanda chetu
“Prisca muambie basi atafute kitu avunje hilo kufuli”
“Sasa nifanyanye?”
Mimi na Priscar tukabaki tunamshangaa bibi wa kizungu kwani hatukujua kama anaweza kuzungumza Kiswahili tena Kiswahili kizuri cha kueleweka
“Bibi unaweza kuzungumza Kiswahili?”
“Ndio ninaweza.Hapa mimi nitafanyaje?”
“Tazama tazama kwenye hayo mawe kama kuna jiwe lolote linaweza kuvunja hilo kufuli”
Priscara alizungumza na kumfanya bibi aanze kutazama tazama chini huku akitafuta jiwe linaloweza kumsaidia katika kulivunja kufuli.Bibi akatulia kwa sekunde kadhaa na kuanza kujipapasa kwenye suruali yake aliyo ivaa kisha akatoa kiberiti cha gesi na kipande cha waya kigumu kisha akalisogelea kufuli na kukiwasha kiberiti cha gesi na kuanza kulichoma kufuli kwa chini katika sehemu ya kuingizia funguo
“Ndio unafanyaje?”
Ilinibidi nimuulize bibi kwani sikuelewa lengo lake ni lipi
“Kijana subiri utaaona”
Bibi akaendelee kulichoma kufuli kwa chini kwa dakika zisizo pungua tano kisha akavua tisheti yake na kulishika kufuli kwa kutumia tisheti yake kutokana kufuli limepata moto na kisha akaanza kulichokonoa kwa kutumia kipande cha waya alicho nacho.Bibi akiwa anaendelea tukaanza kusikia vigelegele vikija upande wetu na kumfanya bibi aanze kuwewesekea kiasi kwamba akakiangusha kipande cha waya alichokishika.Gafla kelele za vigelegele zikanyamaza na hatukuajua kama vijitu hivyo vipo sehemu tuliyopo sisi au vimekenda sehemu nyingine
Bibi akaokota kipande cha waya na kuendele kulifungua kufuli,Priscar akamuomba bibi amsaidie katika kulifungua kufuli hilo na bibi hakuwa mbishi zaidi ya kumpisha Priscar ambaye akaitoa mikono yake na ajaribu bahati yake.Kama dakika mbili hivi Priscar akafanikiwa kulifungua kufuli na tukatoka ndani ya kibanda hicho.Bibi akaokota Video Camera ya mume wake na akatuomba tumfwate kwani anaitambua njia ya kutoka ndani ya pango hilo.Tukaanza kupandisha katika ngazi zilizo chongwa katika ukuta wa pango hilo na tukaanza kupita juu pembezoni ukuta wa pango wenye kijinjia chembamba ambacho usipo kuwa makini nilazima utadondoka kwenda chini ambapo kuna ukumbi mkubwa ulio jaa vijitu vikionekana kuwa na kikao huku yule mzee wa kizungu akiwa amefugwa kamba kwenye miguu na mikono na kutanuliwa mithili ya mbuzi anaye chunwa ngozi huku kijitu kimoja kikimtoa utumbo wake pamoja na moyo
Priscar akamziba bibi mdomo kwani alianza kulia baada ya kumuona mume wake akiwa tayari amepoteza maisha na kuchanguli mwili wake na kutolewa vitu vingi vya ndani kiasi kwamba katika mazingira ya kawaida inatisha na kuogopesha.Ikanibidi mimi nitangulie mbele japo siijui njia na kumlazimu Priscar kuwa na kazi ya ziada ya kumbembeleza bibi wa kizungu atuongoze njia.Gafla vikatokea vijitu viwili mbele yangu huku vikinikodolea macho huku midomo yao wakiwa wameifumbua na kunionyesha meno yao mabaya yaliyo na mpangilio mbaya huku mikononi mwao wakiwa wameshika virungu
Sikutaka vinizoe nikarusha kofi kwa kutumia mkono wa kulia na likatua kwenye kichwa cha kijitu kilichokuwa mbele yangu na kukifanya kiyumbe na kuanguka kwenda chini kulipo na mkutano wa wezake huku kikipiga kelele na kuwafanya wezake walipo chini kukipisha na kikaangukia kwenye jiwe na bichwa lake likapasuka.Kijitu kingine kikawa bado kinamtazama mwenzake aliye anguka nilicho kifanya ni kumsukuma naye akamfwata mwenzake naye akapata kama kilicho kipata mwenzake wa kwanza na kufanya mkutano kuvunjika na wakaanza kuchanguka kwa kasi huku ikionekana wanakuja katika sehemu tuliyopo
Bibi wa kizungu akaacha kulia na kuja mbele yangu na kuanza kuongoza njia huku akiwa na anakimbia na sote tukamfatwa kwa nyuma.Kila tulivyozidi kwenda mbele ndivyo vijitu vilivyo zidi kutufwata kwa kasi ya ajabu hadi wakatukaribia,nikaokota mawe mawili yenye ncha kali kisha na kuwaomba Priscar na bibi wa kizungu watangulie mbele na waniache mimi
“Eddy siwezi kukuacha kama ni kufa tufe sote lakini sio useme nikuache”
“Priscar nimekumbia wewe ndenda na sihitaji mubaki katika sehemu hii sawa”
“Edd…”
“Priscar nimesema nenda”
Priscar hakuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kukimbia na bibi wa kizungu kisha nikasimama na kuwasubiria vijitu vinavyo kuja kwa kasi kwani katika sehemu niliyo simama kuna kona ambayo sio rahisi kwa wao kuona mbele tulipo sisi.Nikajiweka tayari kwa kila kitu na kwajinsi mwili wangu ulivyo jeruhiwa nikaamini sina umuhimu wa kuishi tena duniani na nikajitolea kufa kwa ajili ya Priscar na bibi wa kizungu.Kijitu cha kwanza kikajitokeza huku kikiwa kasi kuifwata njia tuliyopo sisi,Nikakapiga teke na kikaanguka huku kikitoa kilio cha maumivu makali kiasi kisha nikakikita na ncha ya jiwe kwenye kichwa chake na kikaanza kutingishika kurusha rusha viguu vyake huku kikionekana kupoteza maisha.Nikajibanza tena kwenye kona niliyokuwa nimejibanza na sekunde kadhaa vikaja vijitu vingine kama vinne na kusimama wakimshangaa mwenzao jinsi anavyo pepesuka.Nikavivamia na kuanza kuvikita kita ncha za mawe navyo vikaanza kunishambulia kwa fimbo na virungu vyao walivyo vishika
Nikajitahidi kwa nguvu zangu zote kupambana navyo kiasi kwamba kila nikizidi kuviua ndivyo jinsi vilivyo zidi kuongezeka kwa kasi huku wakinidandia kwenye mwili mwangu na kuanza kuning’ata.Sikutaka kukubali kufa kizembe na roho ya kikatili ikazidi kunitawala na kuzidi kuvinyonga bila huruma huku vingine nikivibamiza kwenye ukuta wa pango.Vikaanza kunizidi nguvu na kujikuta nikiianza kwenda chini taratibu huku vikiendelea kining’ata na kunipiga virungu,nilicho kilinda ni macho yangu wasiweze kuyadhuru.Galfa mlio wa bunduki aina ya gobore ukasikika na kuvifanya vijitu vyote kuniachia na kuanza kukimbia kuelekea katika sehemu waliyo tokea,nikabaki nikiwa nimejilaza chali huku mwili wangu ukivuja damu na maumivu makali yakitawala kila sehemu ya mwili wangu
Nikamuona Priscar akiwa amesimama pembeni yangu akiwa ameshika bunduki aina ya gobore katika mkono wake huku akinitazama huku akionekana kunishangaa,Akanipa mkono na mimi nikampa wakwangu kisha akanivuta kutoka chini nilipo ilalia miili mingi ya vijitu nilivyo viua.Nikanyanyuka kisha mkono wangu mmoja nikaupitisha upande wa nyuma wa shingo Priscar kisha tukaanza kutembea kuelekea nisipo pajua.Mwendo wa dakika kumi tukawa tumefika nje ya pango na kumkuta bibi akiwa kwenye gari aina ya Landrover.Akatufungulia mlango na wakasaidiana na bibi wa kizungu kuniingiza ndani ya gari na safari ikaanza,kutokana na maumivu makali nikajikuta nikipoteza fahamu na sikujua ni kitu gani kinacho endelea
***
Nikayafumbua macho yangu na kujikuta nimezungukwa na madaktari wawili wa kizungu wenye ndevu nyingi huku kando yao akiwepo Priscar na bibi wa kizungu,Priscar akaachia tabasamu pana lenye furaha kisha akaanisemesha
“Eddy unajisikiaje?”
“Vizuri”
Nilizungumza huku nikimtazama Priscar na bibi wa kizungu kisha macho yangu nikayapeleka kwenye mwili wangu na kujikuta nikiwa nimefungwa na bandeji nyingi kwenye kila kona ya mwili wangu ila cha kumshukuru Mungu sikusikia maumivu ya aina yoyote
“P tupo wapi?”
“Tupo Kenya”
“Mmmm tumefikaje fikaje?”
“Pale tulipo tokea ilikuwa ni Mpakani mwa Kenya na Somalia”
“Ahaaa”
“Priscar madaktari wanasema wanaomba tumuache mgonjwa apumzike”
Priscar akatoka ndani ya chumba pamoja na bibi wa kizungu na kuniacha na madaktari ambao mmoja wao akatoa kichupa kidogo kwenye koti lake chenye maji ya rangi ya kijani huku kikiwa na kijikaratasi kidogo kilicho andikwa Poison(Sumu) na kuchorwa picha ya fuvu la binadamu kisha akatoa sindano na kufyonza dawa iliyopo ndani ya kichupa hicho huku daktari mwengine alilifungua koti lake na kunionyesha bastola aliyo ichomeka kwenye kiuno chake akiniashiriaa nikae kimya na nisilete fujo ya aina yoyote la sivyo ataniua
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi kwamba nikajikuta jasho likianza kunitoka kila nilipo jifikiria kupiga kelele nikaona haita saidia kwa mimi kuweza kupona au kutoka katika mikono ya wauaji hao ambao sikujua kwanini wanataka kuniua.Kabla hawajafanya chochote mlango ukafungulia na Priscar akaingia na kuwafanya madaktari hao kujikausha kimya na kujifanya wanaandika andika kwenye vijadaftari vyoa vidogo
“Eddy bi.Vanessa amekwenda Air port kututafutia passport za kusafiria”
Priscar alizungumza huku akikaa karibu yangu na kunifanya nimfinye kisiri siri kwenye paja lake hadi akastuka
“Eddy mbona unanifinya….?”
Daktari mmoja akanikonyeza na kwa ishara akanionya nisiseme kitu chochote la sivyo atanimaliza.Priscar akatulia kidogo kisha akatabasamu na kuinama akitaka kunibusu,Gafla daktari aliyeshika sindano akaiishusha kwa kasi ili imchome Priscar mgongoni ila kwa kasi ya ajabu Priscar akarusha teke la aina yake lililotua kwenye mkono wa daktari aliye ishika sindano na kuifanya sindano kuangukia pembeni,daktari mwengine akataka kutoa bastola yake ila akajikuta akirushwa ukutani kwa teke kali kutoka kwa Priscar ambaye sikuamini kama anaweza kufanya vitu vikubwa kiasi hicho.Priscar akarusha ngumi nne zilizotua kifuani mwa daktari aliyekuwa ameshika sindano na kumfanya ataoe ukulele mkali kiasi kwamba akajikuta anaanguka chini.Kabla daktari aliyekuwa na bastola hajanyanyuka akajikuta kidevu chake kikipigwa kwa kigoti na Priscar kilicho mfanya atokwe na damu nyingi mdomoni kisha Priscar akaiokota bastola kabla hajawafyatulia risasi mmoja akaanza kuji tetea huku akiinyoosha mikono yeka juu
“Usituue kwanza ngoja tuzungumze ukweli”
Nikazidi kushangaa kuona daktari wa kizungu akizungumza Kiswahili huku machozi yakimwagika yakiandamana na damu za pua zinazo mchuruzika kama maji
“Nani aliye watu”
“Kuna…..kuna…..kuna nanilio mmoja”
“Nanilio nani zungumza kitu cha kueleweka kabla sijakifumua kichwa chako?”
“Kuna Msomali mmoja ametulipa pesa ili tumuue huyu kijana kisha tukumalizie na wewe”
“Waooo anaitwa nani?’
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Daktari akamuliza mwenzake aliyepigwa kigoti na kuumfanya mmdomo ushindwe kufunguka vizuri na hata anacho kizungumza hakieleweki
“Jina lake sikumbuki vizuri”
“Ahaa humkumbuki eheee?”
Priscar akarusha teke likampiga daktari anaye zungumza naye kwenye shingo na kumfanya kichwa chake kijigonge ukutani na akaanza kulia kama mtoto mdogo
“Nimekumbuka nimekumbuka…….Anaitwa Muntarih jina lake jengine silijua”
“Amewalipa kiasi gani cha pesa?”
“Kla mmoja dola elfu hamsini za kimarekani”
Priscar akatabasamu kisha akanitazama huku akinikonyeza akiwa anaendelea kunitzama dokta aliye pigwa kigotia akaupeleka mkono wake taratibu hadi kwenye sindano iliyo anguka chini na kuiokota taratibu kwa ishara ya macho nikamjulisha Priscar na akamdeukia daktari na kumkuta akijiaandaa kumchoma sindano hiyo na Priscar hakufanya makosa risasi mbili zikiandamana na milio mikubwa zikatua kichwani mwa daktari huyo na akafarika hapo hapo.Ukimya mkali ukaanza kutawala ndani ya chumba huku daktari aliyekuwa akizungumza na Priscar kwa kubabaika akiwa haamini kitu kilicho tokea kwa mwenzake.Priscar akapiga hatua hadi dirishani na kuchungulia nje
“Eddy tutoke kuna askari wanankuja hapa tupo ghorofa ya tano hadi wakifika huku wasitukute”
Priscar alizungumza huku akichomoa sindano ya dripu nililokuwa nimechomekwa kwenye mkono wangu wa kushoto.Japo mwili wangu una maumivu sikuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kujitahidi kutembea.Tukatoka nje na kukuta watu wengine wakiwemo madaktari na wagonjwa wana jiweza wakikimbia wakiokoa maisha yao.Nikajua moja kwa moja milio ya risasi iliyo sikika ndio inawafanya wakimbie kimbie na sisi tukajiunga kwenye msafara wa watu wanao kimbia huku tukielekea zilipo lifti na kukuta zimejaa watu wanao jiokoa maisha yao
Priscar akanishika mkono na tukaanza kushuka kwenda chini kwa kutumia ngazi za ghorofa hilo huku watu wengine wakiungana na sisi.Tukapishana na askari njiani wenye bunduki zao wakipandisha kuelekea ghorofani kujua ni nini kilicho tokea.Tukafika chini na kuunganana na watu wengine wanao elekea getini na kufanikiwa kutoka katika geti la hospitalini hapo na kwabahati nzuri tukakutana na Biibi Vanessa akiwa amesimama nje ya gari lake huku akionekana kuchanganyikiwa kwa hali aliyo ikuta hapa hospitalini.
“Ohoo asante Mungu kwa kuwakuta mumetoka salama”
Bibi Vanessa alizungumza huku akitukumbatia kwa furaha kisha tukaingia ndani ya gari lake na kuondoka
“Sijafanikiwa kupata Visa itatubidi twende Tanzania kwa kupitia njia ya Arusha na kama kuna uwezekano tukapande ndege katika uwanja wa KIA”
“Mungu wangu mimi Tanzania ninatafutwa itakuaje?”
“Kwani P kuna safari ya kwenda wapi?”
“Mimi na bibi tulipanga ukipata nafuu sote twende kwake Marekani tukakae huko kwa muda tukisubiria hali itulie kisha ndio turudi Tanzania.Ninaamini wewe mwenyewe unajionea hali halisi ya mambo?”
“Hivi huyo Muntarih ndio nani?”
“Ni yule jamaa aliye kupatia mateso kule Somalia na ndio alikuwa kiongozi wangu”
“Sasa kwa nini anataka kuniua?”
“Yule jamaa ni hatari sana na hakuna mtu aliye ingia kwenye ngome yake na kutoroka na endapo atatoroka atamtafuta popote atakapo kwenda na anamtandao mkubwa sana”
“Wanangu kwani kuna kitu gani kilicho tokea?”
“Bibi kama nilivyo kuelezea pale awali kuwa tulitokea Somalia ila pale ulivyo ondoka wale madaktari ulio waacha walikuwa ni maadui na wakataka kumuua Eddy pamoja na mimi na katika kupambana nao ndio nikafanikiwa kumuua mmoja kwa kumpiga risasi ndio maana ukakuta watu wanatoka wakiokoa roho zao”
“Mungu wangu….!! Ina maana Priscar mwanangu umeua?”
‘Bibi bila kufanya hivyo sisi ndio tungeuliwa sasa hapo kipi bora sisi kufa au hao kufa?”
“Basi itabidi tutafute duka la nguo mubadilishe ni lazima kamera za ulinzi zitalinasa tukio mulilo lifanya?”
“Kwani kwenye kile chumba hizo camera zipo?”
“Ndio ile hospitali kila sehemu ina camera kasoro vyooni na mbaya zaidi Camera zake zimechimbiwa ukutani na si rahisi kwa mtu kuziona labda kwa wakati wa usiku huwa zinzwasha taa nyekundu”
“Mmmmm Priscar huo msala”
“Tena mkubwa”
Bibi akasimamisha gari pembezoni mwa barabara na tukashuka kisha tukavuka upande wa pili wa barabara na kuingia kwenye jengo kubwa lenye maandishi makubwa na inavyoonekana ni duka kubwa sana
“Eddy hili ndio duka kubwa hapa Kenya”
“Ngoja kwanza bastola yako iko wapi?”
“Niliitupa kwenye maua kule kule hospitali”
Tukaingia ndani ya duka hilo huku tukikaguliwa mlangoni na maaskari kwa kutumia vifaa maalumu japo askari baadhi wakaanza kunishangaa kwa jinsi nilivyo jaa bandeji kwenye mwili wangu
“Kijana ngoja kwanza”
Kuna askari mmoja mzee akanizuia na kuwafanya Priscar na Bibi Vanessa kusimama kusikilizia ni kitu gani anachotaka kuniambia huku kwa mbali nikianza kumuona Bibi Vanessa anavyoanza kupata wasiwasi
“Mbona mwili wako umetawaliwa na bandeji nini kimekupata?”
“Nimeruhusiwa hospitali nilipata ajali”
“Ajali ya nini?”
“Ajali ya pikipiki”
“Ahaaa pole sana kijana”
“Asante”
“Ila unaendeleaje?’
“Vizuri”
“Ok nakutakia manunuzi mema”
“Na wewe pia nakutakia kazi njema”
Nikaachana na askari na kuingia ndani ya duka hilo lililo jaa watu wengi wa mchanganyiko wa kila ain huku likiwa na gorofa kwenda juu.Tukaanza kupita katika sehemu zinazo uzwa nguo na kuanza kuchagua nguo moja baada ya nyingine kisha nikaingia kwenye chumba maalumu cha kubadilishia nguo na baada ya muda nikatoka na kumkuta Priscar na yeye amebadilisha nguo zake na kuvaa nyingine na kumfanya azidi kuonekana mzuri kama alivyokuwa Tanzania
“Eddy mwanangu kuna hivi vidonge nimekununulia vya kupunguza maumivu”
“Ninakunywa vingapi?”
“Unatafuna viwili kila baada ya masaa kumi na mbili……Kama mutahitaji kula chukueni hii pesa mimi ngoja niende kwenye huduma za Internet Cafee ili niwasiliane na mafanyakazi wangu anitumie ndege ije kutuchukua”
“Sawa bibi Vanessa”
“Na kama mutaona ninachelewa basi nendeni mukanisubiri kwenye gari nitakuja kuwakuta huko huko”
“Sawa bibi usujali kwa hilo”
Priscar akazichukua pesa sikujua ni kiasi gani alicho achiwa kisha bibi Vanessa akaondoka na kutuacha tukiwa tumesimama tukitafuta sehemu ya kwenda kununua chakula
“Mmmm P huyu bibi anaonekana anapesa nyingi ehee?”
“Tena anapesa nyingi si mchezo yeye na mume wake wanamiliki ndege za mizigo,wana shule ambayo huyu bibi ndio msimamizi na wanafundisha lugha ishirini kubwa duniani ikiwemo Kiswahili”
“Ahaa kumbe ndio maana huyu bibi anazungumza Kiswahili vizuri?”
“Ndio…nimeongea naye vizuri pia amaniambia kuwa wanamiliki hospitali kubwa tuu ya upasuji wa mifupa ila mume wake ndio alikuwa daktari”
“Masikini ninamuonea huruma kwa jinsi mume wake alivyokufa kifo kibaya”
“Wee acha tuu pale alipo anajikaza mwenyewe ila amekusifia na kusema wewe ni bidamu wa pekee”
“Kivipi mimi ni biadamu wa pekee”
“Amesema hajawahi kuona mtu anayekubali kufa kwa ajili ya wezake kama ulivyo fanya kwa vile vijitu na yeye amepenga kutusaidia hadi pale sisi tutakapo ridhika na maisha yetu”
Tulikapata sehemu inayo uzwa chakula ndani ya jengo hilo,tukanunua nyama ya kuchoma na soda za kupo na kutafuta sehemu na kukaa na kuanza kula taratibu huku tukishangaa shangaa baadhi ya vitu vya ajabu ajabu vinavyo uzwa ndani ya jengo hilo huku likiwa na idadi kubwa ya watoto na wamama wanao nunua vitu
“P hembu niambei ni kwanini ulijiunga na kikundi ulichokuwa umejiunga?”
“Eddy ndio yalinifanya kujiunga huko nilipokuwa nimejiunga lengo langu kuu nikulipiza kisasa kwa mama Caro kwa vitendo alavyo vifanya juu ya maisha yangu”
“Sawa P ila inabidi uwe na moyo wa kusamehe”
“Eddy hicho kitu kwangu hakiwezekani na siwezi kufanya kitu kama hicho na nilazima nilipize kisasi kwa mama Caro.Yeye ndio ameyafanya maisha yangu kuwa ya kutanga tanga na dunia na nimekuwa mtu katili kiasi kwamba sistahili kuwa uraiani……Eddy mimi nimeua watu wengi tena sana”
Priscar alizungumza kwa sauti ya unyonge huku akitokwa na machozi mengi hadi baadhi ya watu wanaopita karibu na sehemu tuliyo kaa wakawa wanatushangaa
“Priscar usilie”
“Eddy niache nilie nimekuona wewe kidogo nina imani kuwa ninaweza kubadilika kitabia…..Eddy mimi ilikuwa ikipia wiki bila kuua kwangu ilikuwa ni dhambi na watu wengi nilio kuwa nikiwaua ni wanaume ambao ninawachukia kupita maelezo”
Priscar alizungumza huku machozi yakimwagika kwa uchungu,nikanyanyuka kwenye kiti na kumsogelea Priscar kisha nikamkumbatia taratibu na kuendelea kumbembeleza.
“Eddy ninakupenda sana ila najua sinto weza kuwa na wewe katika maisha yako…sistahili kuitwa mama.Naogopa kuzaa watoto wenye roho za kikatili ambao mwisho wa siku watakuja kuisumba familia”
“Hapana P unaweza kuzaa ila watoto jinsi tutakavyo walea ndivyo watakavyo kuwa….kwa hilo unalo lisema litashindikana”
“Eddy najua fika kuwa kuzaa kwangu sio tatizo ila ukweli kuhusu wewe na Christina ninaujua kiasi kwamba nahofia kumuibia rafiki yangu kipenzi”
“Wewe na Christina mulikuwa ni marafiki sana?”
“Ndio tena sana….na Christina alinieleza jinsi mulipo toka hadi mulipo fikia ndio maana nilipo toroka sikuhitaji niwasiliane na wewe……na kuna siri kubwa sana katika ndoa ya Christina?”
“Siri gani?”
Kabla Priscar hajanijibu huku nikiwa nimemkumbatia nikamuona mwanamke wa kiarabu akiwa amevalia baibui nyeusi akitoa bastola yake kwenye kibegi chake kisha na kufyatua risasi kadhaa upande wetu.Nikamsukuma Priscar na sote tukaanguka chini na kelele za watu zikaanza kutawala ndani ya jengo tulilopo.Upande wa kulia kwangu nikawaona wanaume wawili weusi wakiwa na bunduki aina ya AK47 wakizipiga risasi hewani huku wakiwaamrisha watu kulala chini
“Eddy tumekwisha jamaa wamekuja hadi huku”
Watu hawakulielewa tamko la watu hao wenye bunduki na wakazidi kukimbia kimbia,nikawashuhudia watu wakiangushwa chini kwa kupigwa risasi na wengine kulia kwa maumivu makali.Mimi na Priscar tukaanza kutambaa kama wanajeshi vitani na kuingia kwenye moja ya duka la vyakula na kuanza kuchungulia na kuona watu wenye bunduki wakiongezeka na kufikia saba huku wakiwa wamevalia nguo nyeusi huku wamejifunga vichwa vyoa na vaitambaa aina ya vikoi.Watu wengi wakazidi kupoteza maisha kwa kupigwa risasi huku wengine wakilala chini na kuvifunika vichwa vyao
“Priscar ina maana jamaa wamuetufwata sisi?”
“Itakuwa hapa sijui tutafanya nini?”
“Shitii Bibi Vanessa sijui yuko wapi?”
Nilizungumza huku nikichungulia kweye mlango wa kioo wa duka tulilo ingia na kumuona jamaa mmoja akipiga piga risasi ovyo kwenye kila duka lililo jengwa kwa ukuta wa vioo na kadri anavyo piga risasi ndivyo jinsi anavyo geukia kwenye duka tulilopo sisi.Kwa haraa tukajisogeza na kujificha nyuma ya friji kubwa na baada ya dakika moja tukasikia risasi zikivunja vioo vya duka tulilopo.
Tukakaa kimya kwa muda kidogo tukisikilizia hali itakayo endelea nje ya eneo hilo tulilopo huku sote tukiwa tunatokwa na jasho jingi.Tukaanza kusikia hatua za watu wawili zikiingia kwenye duka tulilopo huku wakizungumza ile lugha niliyo isikia Somalia.Priscar akainiomba nimpishe kwenye sehemu niliyo kaa mimi kisha akajibanza kwa umakini huku akiwa amechuchumaa tayari kwa kitu cha aina yoyote.Gafla sauti za watu hao zikanyamaza nikajinyanyua taratibu nikichungulia na nikawaona jamaa wakiwa wanakula soseji huku wakionekana kunogewa
Mmoja akatoka na kumuacha mwenzake akiendelea kufakamia soseji na mikate huku akijishushia na soda ya cocacola.Akajifuta mdomo kwa kutumia jitambaa lake alilo kifunga kichani kisha akapiga hatua mbili za kutoka nje gafla kikopo cha Milo kikadondoka kutoka kwenye sehemu vilipo upande wa kulia na sehemu tuliyo jificha sisi na kumfanya jamaa kugeuka haraka huku buduki yake akiishika vizuri na kuanza kunyata taratibu kuelekea kikopo kilipo anguka.Priscar akanyanyuka na kwa mwendo wa tahadhari akapiga hatua za kumfwata jamaa ambaye hakumuona Priscar.
Priscar akamkaba jamaa shingo kwa nyuma na bila hata ya huruma akamvunja shingo kisha akaichukua bunduki ya jamaa na mkanda wa risasi kisha akampapasa jamaa na kumkuta na kisu kikubwa pamoja na bastola kisha akarudi sehemu niliyopo
“Unaweza kutumia bastola”
“Hapana”
“Unaiona hii ukiirudisha nyuma mata moja hapa unakuwa muziweka risasi tayari kutoka na ukiminya huki kwa kukirudisha nyuma risasi hutoka…..Ila usije hapa ukaparudisha mara mbili utakuwa umezifunga risasi zisitoke”
“Ahaa kwa hiyo hapa ninaikoki mara moja kusha huku ninakirudisha mara moja”
“Eheee”
Haikuwa ngumu kuelewa anacho nielekeza Priscar kabla hata hajaikoki bunduki yake vizuri akaingia yule gaidi aliye muacha mwenzake na sikufanya makosa nikafanya kama alivyo nielekeza Priscar na kujikuta risasi zikichomoka kwenye bastola na kutua kwenye mwili wa jamaa na kumuangusha chini.Priscar akanyanyuka huku akiwa ameuvaa mkanda wa bunduki kama walivyo vaa magaidi na kuanza kupiga risasi kuelekea nje ya duka tulipo na kuwapata baadh ya magaidi.Sikuamini kama Priscar ananguvu za kuhimili vvishindo vya bunduki aina ya Ak47 kwani ni bunduki ambayo uliwa lege lege ni lazima itakupa shida katika kuitumia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Eddy usishangae fanya nilivyo kuambia”
“Sawa”
Tulizungumza kwa sauti ya juu ili tusikilizane hii ni kutokana na milio ya bunduki inayo rindima ndani jengo hilo.Nikaanza kufyatua risasi kuelekea magaidi walipo ila nikajikuta nikiwakosa kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kutumia vitu hibyo.Gafla Priscar akapiga ukulele mkali na kuniangukia na sote tukajikuta tukianguka chini
Kwa haraka nikamsogeza Priscar pembeni na kujificha kwenye moja ya chumba kilicho na bidhaa za watoto za kuchezea huku akiwa anachuruzika danu kwenye paja la mguu wa kushoto na kumfanya alie kwa uchungu.Nikalichana shati langu nililo livaa na kumfunga Pricar sehemu ya juu ya jereha lake ili damu isiweze kumwagika sana.Risai za magaidi zikazidi kupigwa kwenye chumba tulichopo uzuri wa chumba tulichopo ukuta wake umejegwa kwa saruji(cement) kiasi kwamba ni ngumu kwa risasi kuingia
“Eddy”
“Naam”
“Nakupenda sana”
“Na mimi pia ninakupenda”
“Nakuomba utafute njia ya kutoka humu ndani”
“Na wewe?”
“Mimi hata nikifa nihaki yangu”
“Hapana nakuomba usieme hivyo Priscar”
“Eddy kweli nakuomba utafuta jinsi ya kutoka humu ndani”
Priscar alizungumaza huku akiishika bunduki yake vizuri na kuanza kujivuta taratibu akitaka kuchungulia kwenye mlango tulio ingilia katika chumba hicho.Nikamvuta Priscar na kumkumbatia
“Pricar ninakupenda tena sana nakuomba tupambane hadi dakika ya mwisho…..Sipo tayari kukuona unapoteza maisha”
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga na kumfanya Pricar kuanza kulia kwa uchungu
“Eddy nakupenda pia ila sina jinsi nilazima nife kwa ajili yako nakuomba utafute pa kutoke tafadali fanya hivyo”
Ikanilazimu kuichukua bunduki ya Priscar na kuiweka pembeni kisha nikachukua kipande cha shati kilicho bakia na kukifunga mbele ya bunduki ya Pricar kisha nikaanza kuitanguliza taratibu kwenye mlango kuashiria tunajisalimisha
“Eddy nini unafanya…..?”
“Tujisalimishe mpenzi wangu hatuna jinsi”
“Eddy una akili kweli….? Hivi unawafahamu hao watu vizuri eeehee”
“Priscar ninajua nini ninacho kifanya……Tazama wati walio kufa pasipo sababu ya msingi .Kama hida yao ni sisi ni bora tujialimieshe kuliko kuwaacha watoto na wanawake kufa”
“Edd hata kama ila hupaswi kukubali kirahisi rahisi…”
“Sawa niache na mimi nife ila sio wewe”
Priscar akajitahidi kunyanyuka kwa hasira ili anizuie ila nikajikuta nikimukuma na akaangukia pembeni na kuendelea kukifanya nilicho nikikifanya.Milio ya risasi ikanyamaza kwa muda nikachungulia na kuwaona jamaa wawili ambao ni magaidi wakija katika chumba tulichopo kwa mwendo wa kunyata huku bunduki zao zikiwa zimeelekea upande nilio kuwepo mimi.Nikajitokeza huku bunduki nikiwa nimeinyoosha juu kwa kutumia mikono yangu .Jamaa wakaanza kuzungumza lugha ya kiomali ambayo sikuwa ninaielewa ila mmoja wao akaniomba nipigea magoti na bunduki kuiweka mbali na sehemu niliyo kuwepo
Priscar naye akajitokeza akiwa ameisnyanyua mikono yake juu huku akiwa anatokwa na machozi kisha akapiga magoti kama nilivyo piga mimi na jamaa wakaja na kutuomba tulale chini kifudu fudi huku mikono tukiwa nimeiweka kichwani.Jamaa wakachukua kamba na kutufunga kwenye mikono na kutunyanyua kwa nguvu kishana kutusogeza kwa wezao wengine ambao wapo ndani ya jengo hilo.
Jamaa wakatuweka chini ya ulinzi wao mkali kisha baadhi wakaingia ndani ya maduka na kuvaa nguo nyingine tofauti na nguo walizo nazo na wakafanya hivyo hivyo kwa zamu hadi wakamaliza kuvaa na kuwaamrisha watu wote waliomo ndani ya jengo hilo kusimama juu
Idadi kubwa ya watu wamekufa ikiwemo watoto wadogo nikajikuta roho yangu ikiniuma kiasi kwamba nikajikuta machozi yakianza kunimwagika taratibu.Jamaa wakawaamriha watu wasimame kwenye mlango mkuu kisha wakatushika sisi na Priscra na kutumarisha kuingia katika chumba kimoja chenye ngazi kwenda ardhini.Tukaingia ndani ya chumba kikubwa chenye maboksi makubwa mengi na kwa haraka haraka nikatambua ni chumba cha kuhifadhi bidhaa katika duka hilo.
Jamaa wakatuamrisha kwenda mbele zaidi na kukuta kuna tobo kubwa katika ukuta wa chumba ukionekana umetoka kuvunjwa muda sio mrefu ila kutokana tumetekwa sikuwa na mtu wa kuweza kumuuliza kuwa ni nani aliye uvunja ukuta huo.Tukaingia katika shimo hilo na kukuta njia ya mfereji wa maji machafu na uliojegwa vizuri kwa saruji(Cement) na kwaukubwa amabao humuwezesha mtu kupita pasipo kuinama
Jamaa tulio nao wakawasha tochi zao huku wawili wakitangulia mbele kuongoza njia huku jamaa wanne wali na bunduki wakiwa nyuma yetu na bunduki zao.Nikazidi kuumia moyo wangu baada ya kumuaona jaa mmoja akimshika shika Priscar kwenye makalio yake kila alipo jaribu kuhitaji kupumzika kwani umbali tuliopo ni mrefu kutoka tulipo toka katika duka walilo kuwa wametuteka na mbaya zaidi Priscar anajeraha la risasi kwenye paja lake na kitu kinachozidi kuniumiza kichwa juu ya risasi iliyopo kwenye paja la Priscar huku damu zikiwa zinamwagika njia nzima.Nikaanza kujilaumu kwa uamuzi nilio kuwa nimeuchukua wa kujisalimisha na mipango yangu ni kumuokoa Priscar ila hadi sasa hivi matumaini ya kumuokoa yakaanza kunipotea taratibu na kujikuta nikipata ujasiri wa kuwaza nini nifanye
Kwa mbali tukaanza kuuona mwanga ukituokea kwa juu huku ukiwa umejichora kwa alama ya duara,Tukafika katika sehemu yenye mwanga na kuna ngazi ya kupandia kwenda juu na inavyo onekana ni shimo maalumu ila sikujua ni himo gani,Akaanza kupanda jamaa mmoja na kutoka nje na kusikia jamaa akizungumza na watu wengine.Kisa yule jamaa akachungulia na kuzungumza na wezake ambao wakatuamrisha tuanze kupanda ngazi japo mikono yetu wammeifunga kamba.Jamaa akaanza kuniukuma nianze kuapanda kwenda juu na sikuwa na jinsi nikapanda juu na kutoka nje ya shimo hilo na kukuta nipo mbele ya watu wapatao kumi na tano wakiwa wamevaa nguo nyeusi huku wakiwa na bunduki zao mikononi mwao wakiwa wamenielekezea mini huku mmoja kati ya watu hao akiwa amenipa mogongo na sikujua ni nani.
Priscar akatoka akiwa anatetemeka mwili mzima na huku akitembea kwa kuchechemea na upepo mkali wa bahari uliopo katika eneo hiliukazidi kuufanya mwili wa Priscar kuzidi kutetemeka.Jamaa laiye tupa mgongo akageuka taratibu na kujikuta nikistuka baada ya kumuona ni yule jamaa aliye nitesa kipindi nipo nchini Somali na kwajina Priscar aliniambia jamaa anaitwa Muntarah.
“Eddu umeona sasa ulicho kifanya?”
Priscar alaizungunza kwa sauti ya kuninong’oneza huku akinisogelea karibu na sehemu niliyo simama.Sikuweza kumjibu Priscar kwani jamaa taratibu alipiga hatua za taratibu huku akionekana kuwa na furaha usoni mwake ambapo ameshika bastola huku akiichezesha chezesha.
sAkaanza kutuzunguka taratibu huku akicheka kwa suati ya kejeli kisha akasimama mbele ya Priscar na gafla akampiga kichwa kikali Pricar na kumyumbisa kwa kasi na akaanguka chini huku mikono yake ikiwa bado imefungwa.Jamaa akarusha teke na kutua juu ya tuombo la Priscar na kufanya atoe ukulele mkali ulio zidi kuniogopesha na kujikuta mwili mzima ukinitetemeka kwa woga.Jamaa akashusha ngumi nzito ikatua kweny tumbo la Priscar na kumfanya ajikunje kiasi kwamba nikataka kwenda kumaidia ila jamaa wakazikoki bunduki zao na kunifanya niitishe uamuzi wangu.
Jamaa akanitazama kwa jicho kali kisha akasimama na kunifwata nilipo na kusimama mbele yangu na akanza kunitazama kwa hasira.Ngumi zipatazo sita zikatua kifuani na kuniangusha chini na kwa kasi ya ajabu jamaa akaja kunikalia tumboni na kuchoma kiu kilali kwenye kiuno cheka na kukinyanyua juu na kuanza kukishusha kwa kasi sana kikielekea maeneo ya jicho langu upande wa kushoto
“WAIT PLEASE……….!”(TAFADHALI SUBIRI)
Priscar alizungumza huku machozi yakimtoka na kumfanya jamaa kusitisha zoezi analo lifanya huku ncha ya kisu chake ikiacha umbali wa sentimita chache kutua juu ya jicho langu
“Don’t kill him please”(Tafahdali ninakuomba usimuue)
Jamaa akasimama na kumtazama Priscar kwa hasira kisha akawaamuru watu wake kutunyanyua chini tulipo anaguka na wakatubeba na kutuingiza ndani ta magari yao kisha safari ikaanza huku magari hayo yakitembea pembezoni mwa ufukwe wa bahari.Tukafika kwenye miti mimgi ya mikoko na wakatushusha kisha wakaanza kutulazimisha tutembee,Nikamuomba jamaa anifungue kamba ili niweze kumbeba Priscara ambaye hawezi kutembea kabisa.Nikambeba Priscra mgongoni cha kushukuru Mungu nimekunywa dawa za kuondoa maumivu na sikuweza kusikia muumivu yotote kwenye majeraha yaliyopo kwenye mwili wangu
Tukaingia kwenye moja ya boti iliyo na ukubwa na unaweza kusema ni Meli na kukuta watu wengine ambao ni askari wa kigaidi.Nika staaajabu kuona watu wengine wenye asili ya uingereza wakiwa wamefungwa vitambaa machoni huku wakiwa chini ya ulinzi mkali.Askari mmoja akatuelekeza kwa ishara na kutuonyesha chumba kimoja na tukaingia kwenye chumba hicho chenye uzuri wa hali ya juu kisha akasimama pembeni yetu.Nikamkalisha Priscar taratibu juu ya kochi lililopo ndani ya chumba tulicho ambiwa tuingie ndani ya boti hiyo inayo onekana ni boti ya kitali.Hali ya Priscar ikazidi kuwa mbaya kiasi kwamba nikajikuta ninazidi kupata wasiwasi kwani imefikia hatua mwili wake kuanza kutetemeka sana huku damu zikimwagika kwenye jeraha lake
“Kaka ninaomba unisaidie dawa nimtibu Priscar”
Nilizungumza na askari mmoja,akanitazama kwa muda kisha akapiga hatua na kuingia kwenye moja ya chumba kilichopo kwenye boti hii kisha akarudi na kisanduku kilicho chorwa msalaba mwekundu kisha akanirushia na nikakinyaka.Nikakifungua na kuchukua pamba nikaipaka dawa aina ya Methylated spirit na kuchana nguo ya Priscar sehemu iliyo na jeraha la risasi kisha nikaanza kuisafisha kwa kutumia pamba hiyo na kumfanya Priscar kutoa kelele za maumivu makali.Ikanilazimu niweze kumpa Priscar kipande cha nguo iil aweze kujifunga mdomoni ili iwe rahisi kuzuia kelele anazo zipiga kwani katika chumba tulichopo kuna askari mmoja tu mwenye bunduki na ndiye aliye nisaidia vifaa hivyo vya matibabu.
“Anarisasi ndani?”
Nikashangaa kumuona askari akiniuliza swali kwa kutumia lugha ya kiswahilia
“Ndio”
Askaria akatoka ndani ya chumba nilichopo kisha akarudi tena ndani akiwa na chupa ya pombe kali aina ya Wisky kisha akanikabidhi
“Unaweza kutoa risasi?”
“Nitajaribu”
“Fanya fasta fasta kabla mkuu hajaja”
“Asante sana kaka”
Nikazidi kuona ni maajabu ambayo Mungu ameamua kunitendea kwa siku ya leo kwani jamaa ameweza kunionyesha wema ambao sikuutegemea kama unaweza kuja kunitokea kwa watu hao wanao sifika ulimwenguni kuwa na roho za kikatili kiasi kwamba wakikukamata sio rahisi kwa wao kuweza kukuacha hai
Nikaimimina pombe aliyo nipa jamaa kwenye kidonda cha Priscar kisha na kusababisha sehemu hiyo kuaza kutoa mapovu madoo madogo ikionekana sehemu hiyo inaunguzwa na pombe hiyo ambayo ni kali
“Anza kuiminya hiyo sehemu kwa pembeni kuweza kuipandisha risasi kiurahisi”
Askari akanipa maelekezo na nikaanza kufanya kama jamaa alivyo nielekeza,Priscar akaanza kuto kelele na kwa kadri ninavyo mminya ndivyo rishasi ikapanda juu hadi ikatoka,Nikachukua bandeji na kuanza kumfunga Priscar kwenye jeraha lake na kuvirudiha vitu nilivyo vitumia kwenye kisanduku chake kisha nikampa askari na kukirudisha alipo kitoa na kurudi ndani ya chumba huku akijifanya kama hajui kinacho endelea
“Nashukuru kaka kwa msaada wako”
“Powa naitwa Salim”
“Mimi naitwa Eddy”
“Priscar huyo alikuwa ni kama dada yangu kipindi tupo Somalia kwahiyo sina budi na mimi kulipa fadhila zangu alizo nitendea”
“Kumbe munajuana?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndio mimi pia ni Mtazania mwenzake nimetokea Zanzibar”
“Salim”
Priscar aliita kwa sauti ya chini iliyo jaa mikwaruzo na uchungu wa kulia kwa muda mrefu huku akionekana kuchoka sana
“Ndio dada”
“Bado unanikumbuka?”
“Ndio ninakukumbuka dada yangu”
“Vizuri…..Nakuomba uniue mimi kwa kunipiga risasi”
“Kwanini dada yangu unataka nikuue?”
“Sitaki Muntarah anikamate na kunirudihs kwenye himaya yake na kunitumikisha mbwa”
“Dada siwezi kabisa”
“Nakuomba Salim”
“Dada siwezi kufanya hivyo kwani Mkuu bado anakupenda sana”
“Salim mdogo wangu fanya hicho nilicho kuambia”
“Priscar unataka ufe uniache?”
“Eddy sio hivyo wewe hujui ni jinsi gani huyu mwanaume alivyo nitesa,Alinitumikisha kama mbwa asiye na mapumziko”
“Priscar najua hawezi kukugusa kama mimi nipo hapa.Nipo tayari kufa kwa ajili yako”
“Eddy jifo ni kitu kingine na kila mtu amezaliwa kwa siku yake na atakufa kwa siku yake…..Kwahiyo niache mimi nitangulie”
“Priscar unanipenda?”
Kabla Priscar hajanijibu akaingia mkubwa wao akiwa ameongozana na askri wengine wawili wakiwa na sura za kutisha kiasi kwamba sidhani kama wanauruma,Jamaa akawasha Tv iliyomo ndani ya boti hiyo na kuanza kutafuta chaneli ya kutazama ndipo akapata chaneli moja inayoitwa CITIZEN inayoonyesha taarifa ya habari.Nikaaona jinsi watu wanavyotoka kwenye duka kubwa tulilo kuwepo wakiwa wanakimbia kimbia kila mmoja akiiokoa maisha yake
“Magaidi hao wenye silaha kali zakivita waliweza kugeukana na kuanza kurushiana risasi wao kwa wao na zifwatazo ni picha za video za magaidi hao zilizo naswa na kamera za ulinzi zilizopo ndani ya jengo hilo”
Muandishi wa habari alizungumza na kunifanya niwe makini katika kuzitazama picha hizo moja baada ya nyingine,Nikastuka baada ya picha yangu kuwa ya tatu kutoka kwa watu wanao sadikika kuwa nii magaidi.Picha ya nne ikawa ni picha ya Priscar huku muandishi wa habari akiongezea maneno baada ya picha ya Priscar kuwa juu ya kioo cha tv tunayo itazama
“GAIDI HUYU WA KIKE NI MWAKA WA PILI SASA ANATAFUTWA NA ASKARI WA TANZANIA NA KENYA NA NIGAIDI HATARI SANA NA YOYOTE ATAKAYE FANIKISHA KUKAMATWA KWAKE DONGE NONO LITATOLEWA NA SERIKALI YA TANZANIA”
Nikamtazama Priscar kwa jicho la kuiba na kumkuta na yeye akifwatilia taarifa hiyo kwa umakini wa hali ya juu na akaachia msunyo mkali ulio wafaya askari wa kigaidi kumtazama kisha wakaendelea kuitazama taarifa ya habari huku picha nyingine za magaidi zikiendelea kuonyeshwa
“Priscar?”
Mkuu wa magaidi akamuita Priscar na kumfanya aitikie kwa sauti ya chini inayo kwaruza kwaruza
“Why you try to run away?”(Kwa nini ulijariu kukimbia?)
“Muntarah ulinitumikisha sana kwa kazi zisizo na maana na sasa ninahitaji amani”
“Amani kumbuka bado mkataba wako na mimi haujaisha”
“Hata kama haujaisha ila nimechoka kuua watu wasio na hatia,Tazama ninavyo tafutwa karibia Afrika mashariki nzima wewe unadhani itakuwaje siku nikikamatwa?”
“Ukiwa na mimi huwezi kukamatwa…….Priscar kumbuka ahadi yangu kwako ni ipi….Nimepanga kukuoa leo hii lasivyo ninamuua huyu kinyago wako mbele ya macho yako”
Nikabaki kimya huku nikimtazama Priscar anaye lia kwa uchungu huku akionekana kukata tama ya maisha
“Abdulah nimesha kueleza mapema kuwa mimi sikupendi…Mwanaume gani ambaye huna huruma na mwanamke wako unakazi ya kunitumikisha kwa kazi za mauaji”
“So unataka nifanye kile nilicho dhamiria kukifanya? SI NDIO?”
Abdulah alizungumza kwa sauti ya juu na kunifanya nistuke pale bastola yake alipo iweka kichwani kwangu tayari kwa kufyatua risasi.Nikafunga macho na kuomba sala fupi ya kutubu dhambi zangu ambayo hata kama nikifa ninaweza kuingia mbinguni japo sijajua kama itakuwa imekubaliwa mbinguni au laa.
“Abdulah nakuomba umuache huyo kijana kama wa kumuua niue mimi yeye hana makosa yoyote”
“Wewe siwezi kukuua kutokana wewe ndio malikia wangu nimepoteza muda wangu kukutafuta wewe na kama ninge waagiza vijana wangu waniletee kwangu ukiwa upo mfu isinge chukua muda.Ila niliwataka waniletee wewe ukiwa hai.Ni nani aliye mpiga Priscar risasi?”
Swali la mkuu wao likawafanya askari watatu waliomo ndani ya chumba kuanza kutazamana kisha mmoja akazungumza kisomalia kisha akatoka nje na baada ya muda wakarudi wakiwa wamengozana na askri sita na kusimama mbele ya bosi wao ambaye aliwauliza kwa luhga ya kisomalia na mmoja wao akanyoosha mkono juu huku mwili ukimtetemeka nikajua watakuwa wameulizwa swali walio ulizwa wezao watatu.Gafla askari aliye nyoosha mkono akanguka chini huku kichwa chake kikivuja damu nyingi hii ni baada ya kupigwa risasi na bosi wake
Wezake wakamtoa ndani ya chumba huku wakiwa wamembeba kama mzoga wa mnyama aliye kufa na kufanya damu kuchuruzika eneo wanalo pita
“Priscar umeona….? Nimeua kwa ajili yako kwani wewe ndio malikia wangu.Kama hutaki basi hizi risasi zilizo baki humu ndani ya bastola yangu zitamalizikia mwilini mwako huyu mshenzi mwenzako ambaye sijui amekushawishi nini hadi ukamtorosha”
“Huyu si mwenzangu bali ni ndugu yangu?’
“Ndugu yako huyu, Mbona hujawahi kuniambia kuwa una ndugu?”
“Nilikuongopea huyu ndia ndugu yangu na anaitwa Eddy na si mpelelezi kama ulivyo dhania”
“Ohoo Eddy unabahati sana ingekuwa sio ile taarifa ya habari kuonyesha na wewe ni miongoni mwa magaidi wanao tafutwa basi wewe leo ungekuwa ni chakula cha samaki.”
Jamaa kwa mara ya kwanza kuliita jina langu kidogo mapigo ya moyo yakaanza kutulia taratibu kiasi kwamba nikarudi katika hali ya kawaida
“Eddy wewe ni dokta?’
Jamaa aliniuliza swali na kumfanya Prscar kulijibu kabla ya mimi sijatoa jibu
“Wala sio dokta”
“Sijakuuliza wewe?”
“Mimi sio dokta nilikuwa ni mfanya biashara”
“Basi usijali bwana mdogo nitakufanya kuwa zaidi ya mfanya biashara…..ila kwa sharti moja kazi zote anazo paswa kuzifanya Priscar utazifanya wewe”
“Kazi zipi?”
“Kuua,kusafirisha madawa ya kulevya…..na kazi nyingine ni wewe unizalie mtoto mzuri kama alivyo huyu ndugu yako”
“Wewe mpumbavu nini nani akuzalie kama ni kuniua niue ila sio kufanya kazi yako hiyo ya kijinga”
“Waooo unahitaji kifo?”
“Ndio nipo tayari kufa ila si kufanya kazi hizo za kikijinga”
“Eddy usizungimze hivyo nakuomba uwe mpole”
“Priscra nipo tayari kufa kwa ajili yako ila kama si kuonana hapa tena tutaonana mbinguni”
Nilizungumza huku machozu yakinimwagika kwa uchungu na kumfanya Priscar azidi kumwagikwa na machozi.Jamaa akanielekezea bunduki yake na kuiweka kwenye paji lau so wale na nilabaki nikimtazama kwa hasira ya hali ya juu.Jamaa akampiga risasi Salim ya kichwa na kumfanya apoteze uhai wake hapo hapo
“Huyo ndio msali wangu wa kwanza…….Eheee bwana Eddy rudia sentesi yako tena?”
“Nimesema siwezi kufanya kazi zako za kijinga na nipo tayar kufa kwa ajili ya Prisca na tambua ya kwamba hukupendi na mimi ndio mwnaume wake wa kwanza kumtoa bikra”
Muntarah akawa kama mtu aliye changanyikiwa akanitazama kwa hasia huku bastola yake kisha akaminya kishikizo cha bastola yake kinacho ruhusu risasi kutoka na hakuna kilicho toka ikiashiria risasi za bastola yake zimekwisha.Muntarah akawamrisha watu wake kunikamata na kunivisha kitambaa chenye rangi nyeusi huku mikononi mwamgu wakinifunga kamba aina ya manila huku wakiwa wameielekezea nyuma kisha wakanitoa ndani ya chumba hicho na kubaki nikizisikia kelele za Priscar akiomba wasiende kunifanyia kitu kibaya.Sikujua ninapelekwa wapi kwani upepo mkali ulianza kuunyanyasa mwili wangu na kwa haraka aharaka nikajua nipo nje ya boti hiyo.Jamaa wakaniamarisha kuweza kupiga magoti chini na nikafanya hivyo
Gafla mapigo ya moyo yakanipasuka baada ya kusikia milio ya risasi ikitokea pembeni yangu huku kukiwa na kitu kilicho dumbukia ndani ya maji.Nikazisikia sauti za watu wakilia kwa uchungu huku wakizungumza kwa lugha ya kingereza ambayo kidogo inanipiga piga chenga.Mlio wa risasi ukasikika tena na kusikia mtu huyo akidumbukia kwenye maji ya bahari.Milio mingi ya risasi ikasikika kwa wingi kama ndani ya dakika moja kisha ikakata.Nikastukia nikivuliwa kitambaa nilicho valishwa na kukutana na sura ya msichana wa kizungu akiwa amashika bastola mkononi mwake,Akanifungua kamba za mikononi kisha akanijumisha na wetu wengine watatu alio waokoa na kutuomba tutafuta sehemu tujifiche huku yeye akiendelea na shuguli ya kuwatafuta magidi ndani ya boti hiyo kwani sehemu tuliyo kuwepo ni juu ya boti kiasi kwamba wale walio pigwa risasi wote walidumbukia kwenye maji ya bahari
Akili yangu ikamfikiria Priscara haraka nikaokota moja ya bunduki iliyopo chini kisha nikaichunguza kama alivyo ichunguaza Priscar tulipo kuwa kwenye duka kubwa kisha nikaikuta ina risasi za kutosha kwenye Magazine yake.Kwa mwendo wa tahadhari nikaanza kushuka chini vilipo vyumba vya boti hiyo huku nikiwa makini na sikujua yule dada wa kizungu ameelekea wapi
Nikakutana na gaidi mmoja nikafyatua risasi zilizo mpata kifuani na akaanguka chini na kufa,nikazidi kupiga hatua kuelekea mbele huku nikiwa makini na safari hii sikuwa na huruma ya aina yoyote na bunduki niliyo nayo haikunisumbua katika utumiaji wake.Nikachungulia kwenye chumba cha manahoza nikakuta wamejazana askari wa kigaidi wakiwa wamewashikilia manahodha wa kizungu ambao wanaonekana ndio watumishi halali wa boti hiyo.Nikafyatua risasi nyingi kwa umakini wa hali ya juu huku kitendo hicho nikikifanya kwa haraka sana na risasi kadhaa zikatua juu ya askari wa kigaidi na baadhi yao wakapoteza maisha hapa hapo ila wengine wakawa wamejilaza chini wakilia kwa maumivu makali
Nikamsogelea kila askari mmoja wa kigaidi na kumchunguza kama yupo hai au amekufa na niliye mkuta yupo hai nikampiga risasi ya kichwa na ikawa ndio safari yake ya mwisho kuwepo katika maisha haya.Nikawafungua manahodha wa meli hiyo wapatao sita na wakaanza kunishukuru kwa kitendo cha kuwaokoa.Nikatoka na kutafuta sehemu kilichopo chumba nilicho muacha Priscar,Kutokana sikuwa mzoefu wa sehemu hiyo na mbaya zaidi vyumba hivyo vimefanana fanana sana kiasi kwamba sio rahisi kuweza kujua mara moja ni chumba kipi walichopo wao.Nikaona michuruziko ya damu ikiwa imetoka kwenye moja ya chumba nikakumbuka kuna yule askari aliyempia risasi Priscar alitolewa na wezake katika chumba tulichokuwepo huku damu zake zikiwa zinachuruzika kila eneo alilokuwa akipitishwa
Nikashika kitasa cha mlango huo na kuanza kukisukuma taratibu kuelekea ndani huku nikiwa nimeishika bunduki yangu kwa umakini zaidi nikiwa nipo tayari kwa lolote litakalo jitokeza mbele yangu.Hadi mlango unafika mwisho nikaukuta mwili wa Salim ukiwa pale pele ulipo kuwepo na sikukuta mtu yoyote na kilicho nijulisha zaidi kuwa chumba nilichopo ndicho kile tulicho ingizwa nikipande cha nguo nilicho mpa Priscar aking’ate kipindi ninamtibu jeraha lake.Nikatoka kwa haraka na kuanza kuelekea njia ambayo sikuipita huku nikiwa makini kwa lolote litakalojitokeza.Gafla taa ndani ya Boti zikazima na na kusababisha giza kali kwani tayari usiku ulisha tawala anga,kutokana njia niliyo kuwepo ilikuwa imenyooka nikazidi kupiga hatua kuelekea mbele huku akilini mwangu nikimuwaza Priscar tuu na sikuwa tayari kuona anaolewa na Muntarah.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikastukia bunduki yangu ikiniponyoka mkononi kwa teke kali lililo piga kwenye mikono yangu na kunifanya nirudi nyuma kidogo nikitazama ni nani aliye nipiga japo kuna giza kiasi katika sehemu hiyo ambayo mwanga hafifu wa mwezi uliingia kupitia madirisha madogo yaliyomo ndani pembezoni mwa sehemu hiyo
Akasimama msichana wa kizungu mbela yangu huku akiwa na kisu mkononi mwake na akajiweka kwa mkao wa kupigana.Nikakunja ngumi kwenye mikono yangu huku nikiamini akijaribu kusogea mbele yangu nitakacho mfanya atajua yeye na mola wake.Mwanamke akarusha teka lilikaribia kunipata kifuani mwangu ila nikarudi nyuma na kulifanya teke hilo kutua chini pasipo kunipata.Akaja kwa kasi huka kisu chake akiwa amekishika vizuri katika mkono wake wa kushoto.Nilicho kifanya mimi ni kurusha teke kali sikujua hata uwezo huo ulitokea wapi ila akalipangua kwa mkono wake wa kulia na kunifanya niyumbe hadi ninakaa sawa ngumi kali ya msichana huyo ikatua kwenye pua yangu na kunifanya nianze kujisikia nyota nyota huku damu zikianza kunichuruzika kama maji.Mwanamke akakaa kama awali huku miguu yake ikiwa ameipinda kidogo na kubonyea chini kidogo huku mikono yake akiwa ameikunja ngumi
Nikajipangusa damu zinazo nimwagika kisha na mimi nikamuiga mkao alio ukaa huku namimi nikikunja ngumi na kwa mbwembwe nikaanza kunesa nesa kama anavyofanya Bruce Lee kwenye filamu zake na kutoa kijimlio kama cha paka huku kidole changu kimoja kikimuita kwa ishara anifwate.Macho ya msichana wa kizungu yakanitazama chini hadi juu kisha akanitisha kama anakuja nikajikuta nina simama na kurusha ngumi zilizo ishia hewani ila mwenzangu akawa sehemu ile ile aliyo simama.Ikanibidi nirudie mkao wangu kwa haraka huku nikiongeza mbwembwe na mimi nikajaribu kumtisha msichana wa kizungu.Nikastukia ngumi kadhaa zikitua kifuani kwangu wala sikujua zimefikaje na zikanifanya nirudi nyuma,Nikamchunguza msichana wa kizungu jinsi alivyo kaa ila nikajua hana bunduki ya aina yoyote na hata kisu alichokuwa amekishika hakikuwepo mkonono mwake sasa sikujua ni wapi alipo kiweka
Nikageuka nyuma yangu na kuona kuna mlango ambao nilikuwa ninaukaribia kuufikia kipindi nilipo kuwa nimatoka ndipo nikakutana na msichana huyo ambaye ndiye aliye tuokoa kipindi tulipokuwa tunapigwa risasi na askari wa kigaidi.Nikaesabu kimoyo moyo moja mpaka tatu na kugeuka kwa kasi ya ajabu na kuanza kukimbia kuelekea ulipo mlango hadi ninaufikia nilikuwa nimemuacha msichana wa kizungu kwa umbali kidogo ila yeye mwenyewe anakuja kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba akinikamata nahisi ndio mwisho wa maisha yangu.Nikashika kitasa cha mlango na moyo ukanipasuka baada ya kuukuta umefungwa na mbaya zaidi ni ile milango inayo tumia funguo kadi inayoweza kufungulia milango ya aina hiyo na isitodhe umeme umekatika ndani ya boti hiyo na sikujua sababu ni nini na kujikuta nikikata tamaa
Nikageuka na kutazama msichana wa kizungu na kukuta anakaribia karibu yangu huku akiwa kasi nikajipa moyo kuwa ataweza kunisamehe ila nikiwa katika imani yangu hiyo nikastukia ngumi nyingine ikitua kwneye kifua changu na kuniegemeza kwenye mlango huo.Nikarusha ngumi na mimi kujiokoa kwani nikiendelea kuwa mjinga msichana huyo anaweza kuniua ila ngumi hito ikapita hewani na haikupata msichana huyo.Nikarusha kofi kali likatua kwenye shavu la msichana huyo na kumfanya apepesuke kama nilivyo pepesuka mimi kwa mara ya kwanza alivyo niandika ngumi ya pua.Nikamrukia huku bega langu likiwa limemlenga msichana huyo kwenye tumbo kama wanavyo fanya watu wa Mereka na wenyewe wanaiita ‘SPEAR’ na nikampata vizuri na kutufanya wote tuanguke chini kama mizigo huku msichana wa watu akitoa ukulele wa maumivu makali.Nikajua huu ndio wakati wangu wa mimi kutawala nikamkalia kwenye tumbo lake na kuanza kumpiga vibao kadhaa kwenye mashavu yake na kustukia nikiangukia mbele ya msichana huyo baada ya teke lake kunipiga kwa mgongoni.Nikanyanyuka kwa haraka na mimi nikajikuta nikitua chini baada ya mshichana huyo kunipiga kwa bega lake sehemu ya tumboni kama nilivyo mfanya mimi na maumivu niliyo yapata hayaelezeki
Akakaa tumboni mwangu kwenye maumivu makali na kuanza kunishambuli kwa ngumi ambazo niliweza kuzizuia kwa kutumia mikono yangu niliyo ibananisha kwa nguvu na hazikuwa rahisi kwa ngumi hizo kutua juu ya uso wangu.Nikaishika kwa haraka mikono ya msichana huyo huku nikihema kwa kuchoka
“Bwana eheee nimechoka kupigana na mimi sio gaidi”
Nilizungumza huku nikiendelea kuhema kwa nguvu na kumfanya binti huyo kutulia huku akinitazama kwa mshangao huku na yeye damu zikimchuruzika puani.Akasimama na kunipa mkono kisha akaninyanyua kwa kunivuta.
“Naitwa Lilian”
“Mimi naitwa Eddy”
“Unajina kama la kaka yangu”
“Hee umekijua vipi Kiswahili?”
“Nimesoma na kukijua kwani nilunga niliyokuwa nikiipenda tangu utotoni”
“Umeokea wapi….?”
“Calfonia Marekani wewe je?”
“Dar Tanzania”
“Waoo huo mji nilisha wahi kuutembelea”
“Kweli?”
“Ndio”
Nikawaona kwa kutumia vidirisha vilipo karibu yetu Muntarah na Priscar wakipita kwa nje huku Muntarah ikimshika Priscar shingoni huku akiwa amemuelekezea bastola kwenye kichwa chake wakirudi nyuma nyuma wakielekea kwenye ukingo wa boti hiyo.Nikaanza kukimbia kuelekea kwenye ule mlango ulio fungwa huku Lilian akinifwata kwa nyuma na kwakutumia nguvu zangu zote nilizo nazo nikaurukia kwa kuupiga kikumbo hadi ukaanza kulegea.Tukarudi nyuma na Liliana na sote tukaurukia hadi ukavunjika na kujikuta tukiwa tumengukia karibu na walipo simama Muntarah na Priscar.
“Eddy”
Priscar aliniita huku Muntarah akizidi kumkaba kooni na bastola yake ikiwa ameielekezea upande wetu.
“Ukisogea hatua hata moja ninamuua Priscar”
Muntarah alizungumza huku akizidi kurudi nyuma huku akiwa anamburuza Priscar ambaye anakataa kwenda anapo hitaji Muntarah.Gafla Muntarah na Priscar wakajirusha kwenye maji ya bahari mimi na Lilian tukabaki tumeshangaa.Kabla sijapiga hatua tukasikia sauti za kiume zikitumarisha tusimame kama tulivyo nikageuka kutazama ni nani anaye tumuamrisa na kukutana na askari wapatao wanne walio valia nguo nyeusi na mikononi mwao wakiwa na bunduki huku nguo zako zikiwa zimeandikwa kwa maandishi makubwa yenye rangi nyeupe FBI
Askari wakatusogelea mimi na Lilian na kutuamrisha tupige magoti kisha wakatufunga pingu za mikononi na wakaanza kuwasiliana na wezao ambao sikujua wapo wapi.Ndani ya dakika kumi zikaja Helcopatar zipatazo tano zikaanza kuizunguka boti tuliyopo huku askari wengine wakishuka kwenye Helcoptar hizo kupitia kamba ndefu
“Eddy”
“Mmmm”
Kabla Lilian hajaniambia kitu cha aina yoyote askari wawili wakatunyanyua na kutuvalisha majaketi yasiyo ingiza risasi{bullet proof) kisha wakatufunga kamba kwenye viuno na mabegani na kamba hizo zikaanza kutupeleka juu kuelekea kwenye moja ya Helcoptar ya askari hao ambao siku zote wanasifika kwenye maswala ya kuzuia magaidi.Tukapokelewa na askari wengine walio valia makofia yaliyo wabakisha macho tuu katika muonekano wao na kwaharaka haraka unaweza kuwafananisha na Maninja katika filamu za kichina ua kijapani,Nikashangaa kumuona askari mmoja akimpa mkono Liliana wa kumkaribisha katika helcoptar hiyo ila mimi nikastukia nikichomwa sindano ya shingoni na usingizi mzito ukanipitia
***
Kwa mbali nikasikia mlango wa chuma ukifunguliwa nikajitahidi kuyafumbua macho yangu ili kuona vizuri nipo wapi nikajikuta nikishindwa kutokana na macho yangu kutawaliwa na ukungu mwingi.Wakasimama watu wawili mbele yangu huku mmoja akiwa ni ni mwanamke,Wakanitazama kwa muda kisha mmoja wao akatoka na kumuacha mwanamke akiwa amesimama mbele yangu.Akanishika kwenye shingo na kwa kitu cha baridi na kunifanya mwili kusisimka na macho kuanza kuangaza vizuri.Msichana mweusi kiasi akaendelea kunitazama huku akiendelea kunipaka mafuta yenye ubaridi mwilini mwangu hapo ndipo nikagundua nipo uchi huku mikono yangu ikiwa imenyooshwa juu huku kila mkono mmoja ukiwa umefungwa kwenye kona ya chumba hicho kwa kutumia mnyororo mrefu
Miguu yangu nayo imefungwa na minyororo na ikatanuliwa kwa upana kiasi na kunifanya nianze kuhisi maumivu kwenye misuli ya mapaja yangu.Akaendelea kunipaka mafuta hayo ambayo sikujua yanakazi gani mwilini mwangu.Akamaliza akatoka ndani ya chumba na nikabaki peke yangu.Nikakitazama chumba kwa umakini na kukuta hakina kitu cha aina yoyote zaidi ya kioo kikubwa kilichopo mbele yangu ambacho ni cheusi na sikuweza kuona nje ya kioo hicho kuna nini.Taa kali mfano ya taa zinazo fungwa kwenye viwanja vya mpira zikawaka mbele yangu na kunipiga machoni na kusababisha maumivu makali kwenye macho yangu na nikajitahidi nikuyafumba ili nisiendelee kuumia zaidi na joto kali likatawala mwilini mwangu na kusababisha mafuta niliyo pakwa mwilini kuanza kuchuruzika kama maji huku yakiwa yanauchoma mwili wangu kiasi kwamba nikaanza kupiga kelele za kuomba msaada
Ila hakuna aliye weza kusikia kilio changu kwani mwanga wa taa zikazidi kuuchoma mwilini mwangu na gafla zikazimwa na taratibu maumivu yakaanza kunipungua mwilini mwangu.Akaingia askari mwenye umbo kubwa lililo kaza kwa misuli huku akiwa na urefu kwenda juu kiasi kwamba japo nina urefu wa wastani ila ninamfikia kifuani.Nguo zake nyeusi kwenye bega lake zimechorwa ramani ya marekana huku kukiwa na maandashi madogo yanayo someka U.S.A ARM.Askari akanisogelea karibu na uso wangu na kunitazama kwa umakini kisha akanipiga ngumi moja ya tumbo na kunifanya nitoe ukulele mkali huku damu zikinivuja mdomoni mwangu
“Wewe ni gaidi?”
“Hahaaa haa pana”
Jamaa akacheka na kunipa mgongo na gafla akageuka na kunitandika teke kali la tombo na kunifanya nirushwe juu kiasi na kusababisha mikono yangu kuanza kuchanwa na vifungio vya nyororo hizo.Machozi yakazidi kunitoka huku mwili wangu ukitawaliwa na maumivu makali ya tumbo.
“Wewe ni miongoni mwa wasomali tunao watafuta….Je tunahitaji kuijua gome yenu ipo wapi?”
“Mimi sijui chochote…”
“Una uhakika?”
“Ndioooo”
“Sawa”
Jamaa akafungua begi alilo ingia nalo ndani ya chumba hicho na kutoa vifaa viwili vyenye vishikizo na ncha kali huku vikiwa vina nyaya ndefu na akazichomeka kwenye soketi ya umeme na kuvikutanisa na kutoa miale ya umeme ambayo hufanana na miale ya radi kisha akanisogelea na kunitazama
“Una uhakika wewe hujui ni wapi walipo wezako?”
“Sijui na mimi sio Msomalia ni mtanzania”
“Ohhhh Tanzania hakuna watu magaidi kama wewe”
“Kaka mimi sio gaidi”
Jamaa akavibandika vivaa alivyo vishika kwenye mwili wangu na kujikuta nikianza kutetemeka mwili mzima huku maumivu makali yakiutawala mwili wangu hadi kichwani mwangu kisha akavitoa na kurudia swali lake kuwa mimi ni gaidi ila nikaendelea kubisha na kumfanya jamaa kunibandika vifaa vyake vya umeme na kuufanya mwili wangu kutingishwa na maumivu makali yakazidi kuutawala mwili wangu na kujikuta nikianza kuishiwa nguvu hadi ikafikia kipindi siwezi kuzungumza kitu cha aina yoyote.Jamaa akaniachia na wakaingia askari wengine wawili wenye asili ya kimarekani na kunifungua kwenye nyuroro nilizo fungwa na kunivalisha nguo za rangi ya chungwa(Njano kama ya soda za mirinda) ambazo zipo kama maovaroli ya mafundi gereji.Wakanivisha mnyororo mrefu kwenye miguu yangu na kuiwezesha kutembea vizuri bila shida ya aina yotote na pia mikononni wakanifunga pingu za kawaida
Kusema kweli sikuwa na guvu za kuweza kutembea hata hatua tano ila jamaa wakazidi kunihimiza kuweza kutembea huku mara kwa mara nikaanguka chini na kuninyanyua na kuendelea na safari.Sikujua ni wapi jamaa wananipeleka kwani tunapita kwenye moja ya kordo ndefu kuelekea mbele na ikiwa na taa hafufu zisizo na mwanga mkali.Wakanikabidhi kwa askari wengine ambao wamejazia miili yao na wana bunduki ambazo tangu nizaliwe sijawahi kuziona.Tukaingia kwenye moja ya ukumbi mkuwa wenye wanajeshi wengi ambao kila mmoja anaendelea na shunguli yake wengine wakiwa wanatengeneza ndege ndogo za kijeshi aina ya jeti
Wakanipeleka kwenye moja ya chumba kinacho onekana ni ofisi kisha wakanipa chakula ambacho sikuwahi kukila hata siku moja katika maisha yangu na mdomoni mwangu hakikuwa na ladha ya aina yoyote kiasi kwamba nikajikuta nikijilazimisha katika kukila kutokana na njaa kali niliyo nayo.Akaingia mtu aliye valia koti jeupe na kufungua begi lake lililo jaa vifaa vyaa vya hospitalini kisha akanichoma sindano kwenye mkono wangu wa kushoto na kunipa vidonge nimeze baada ya muda nikaanza kuuhisi mwili wangu ukipata nguvu na maumivu yakinipungua mwilini.Akanichana kwenye mkono wangu kulia na kuniingiza kifaa kidogo kisha akaanza kunishona kwa nyuzi kiasi kwamba sikuelewa lengo lake ni nini haswa
Wakaingia jamaa wawili mmoja wao akiwa mweusi na mzeekiasi na mwengine akiwa na asili ya Kimarekana huku wote wakiwa wamevalia suti nyeusi na jamaa mweusi kwenye suti yake kukiwa na kialama kilicho chorwa bendera ya Tanzania na hapo ndipo nikaanza kupata matumaini ya kuachiwa huru
“Huyu ni mtanzania ambaye amehusika kwenye tukio la mauaji nchini Kenya na kuiteka boti ya kifahari ya Kimarekani”
Jamaa mwenye asili ya Kimarekani alizungumza huku akinitazama na nikabaki nikitazamana na mzee huyo ambaye ninahisi ni Mtanzania
“Mimi ni balozi wa Tanzania hapa nchini Pakistani nimekuja kudhibitisha kwamba wewe ni Mtanzania kweli au sio Mtanzania”
“Mzee wangu mimi ni Mtanzania halisi kabisa na wala sijahusika katika mauaji hayo kama wanavyo sema hawa jamaa”
“Mbona sura yako sio ya kitanzania?”
“Ahaaa Mzee mimi ni mtanzani kabisa…..Napajua Dar,Mwanza,Tabora…..”
“Kuijua mikoa ya Tanzania sio sababu ya kukufanya wewe uonekane ni Mtanzania”
“Sasa mzee hata hici Kiswahili ninacho kizungumza ni cha Tanzania kabisa”
“Siamini kama huyu ni Mtanzani na katika historia ya nchi yangu hatujawahi kuwa na mtanzania gaidi”
“Kwahiyo muheshimiwa huyu sio Mtanzania?”
“Ndio sio mtanzania kabisa nyinyi mfanyeni jinsi munavyo taka”
Mzee aliye jitambulisha ni balozi wa Tanzania nchini Pakistani akatoka ndani ya ofisi hiyo akiongozana na mtu aliye ingia naye na kunifanya machozi kuanza kunimwagika kiasi kwamba nikahisi huo ndio mwisho wa maisha yangu.Na sifa moja waliyo nayo hawa jamaa wakikukamata na nchi yako ikakukana basi tambua kinacho fwata hapo ni kifo ambacho dunia nzima hawatajua umeuawa kwa jinsi gani.Daktari anaye nihudumia akaniazama kwa huruma kisha akanipa kitambaa chake na kujifuta machozi
“Wanakupeleka kwenye gereza la magaidi omba Mungu isiwe hivyo”
Daktari alizungumza huku akinifunga bandeji kwenye sehemu aliyo nishona kwa nyuzi na kunifanya nimtazame
“Wewe ni sawa na mdogo wangu hii ni siri ninakuambia…….Hichi kifaa nilicho kiingiza humu ndani kitawaonyesha hawa jamaa sehemu yoyote ambayo wewe utakwenda…..unacho paswa ni kuwa mtulivu katika safari yako”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dokta alizungumz kwa sauti ya chini ya kunong’oneza kiasi kwamba nikajikuta nikizidi kuogopa kwani katika maisha yangu swala la kufungwa sikuwahi kulitarajia.Wakaingia askari wawili walio na bunduki wakanishika mikono na kuhakikisha pingu walizo nifunga zipo vizuri.Baada ya kuridhishwa wakanivalisha koti lisilo pitisha risasi(Bullet proof) na kutoka nao ndani ya chumba hicho
Wakanisimamisha mbele ya wanajeshi kumi walio jipanga mstari huku wakiwa wamevalia miwani nyeusi na wakiwa na bunduki zao mikononi huku wakiwa na majaketi yasiyo pitisha risasi kama yangu huku sare zao zikiwa na rangi ya kaki hadi viatu walivyo vivaa.Jamaa mmoja akatoa amri na wote kwa kasi wakaingia kwenye magari yao ya kijeshi yaitwayo Hammer yapatayo sita yenye rangi ya kaki.Kisha wakaniingiza kwenye moja ya gari la aina hiyo na zote zina fanana kwa ukubwa wa maumbo.Geti kubwa katika ukumbi huo likafunguka na gari zikaanza kutoka moja baada ya nyingine huku gari nililopo mimi likiwa kati kati kata ya magari sita yaliyo ongozana kwa pamoja.
Askari nilio kaa nao siti ya nyuma huku wakiwa mameniweka kati kati hakuna hata mmoja aliye nisemesha na wote ni wazungu na nimmoja wao aliye kaa siti ya pembeni mwa dereva akawa anazungumza kwa sauti ya juu na kumfanay dereva wao ambaye ni mwanamke kucheka kwa furaha na sikuelewa wanazungumza kitu gani kwani kingereza chao cha kimarekani ni kigumu tofauti na waingereza wenyewe.Safari ikazidi kusonga mbele huku ikakatiza kwenye jagwa lenye vilima lima vingi vya mchanga huku gari zikienda kwa kasi ya ajabu na mwanga wa jua ukianza kupotea taratibu ukilikaribisha giza kulitawala anga.Sikuweza kupata usingizi kwani nilihitaji kujua ni wapi ninapo pelekwa japo daktari aliniambia ninapelekwa gerezani ila hakunitajia ni gereza gani.Kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo giza lilivyo zidi kutanda angani,Gafla gari zote zikasima na kuwafanya askari waliomo ndani ya gari letu kuziweka bunduki zao tayari kwa chochote kitakacho tokea huku wakivaa vifaa Fulani kwenye macho yao vinavyo fanana na darubini
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kuanza kusikia milio mingi ya risasi ikitokea kwenye magari ya yaliyopo mbele yetu.Askari walio kaa na mimi kwenye gari letu wakafungua milango na kujirusa njena wakapiga magoti na kuanza kupiga risasi kuelekea mbele walipo wezao na kumuacha derava wao akijaribu kulirudisha gari kwa nyuma huku akiyagonga magari ya nyuma ili kuweza kupata nafasi ya kupita.Akaligeuza gari kwa haraka na kuelekea tulipo kuwa tunatokea sisi kisha akalisimamisha na kushuka na bunduki yake na kunitoa ndani ya gari na kunilaza chini kisha akajibanza kwenye gari akiwa karibu yangu na kuanza kupiga risasi kuelekea walipo wezake.Milio ya mabomo ikaanza kusikika huku magari ya wanajeshi hao yaliyopo mbele yetu yakianza kulipuka moja baada ya jengine na kuifanya sehemu hiyo kutawaliwa na mwanga wa moto wa magari yanayo ungua
Katiaka maisha yangu sikuwahi kutegemea kama itatokea siku nitashuhidia majibizano ya bunduki kama hayo.Nikawaona jamaa wawili wakijitokeza kwenye kilima cha mchanga kilichopo karibu yetu huku wakiwa wamevalia vitambaa kichwani na moja kwa moja nikajua watakuwa ni waarabu huku mikononi mwao wakiwa wameshika bunduki zao.Kwa haraka nikajinyanyua na kuichomoa bastola iliyopo kiunoni mwa askari huyo wa kike kisha nikafyatua risasi sita kwa haraka na kuwafanya jamaa hao kuanguka chini na kuwafanya askari huyo kunitazama kwa mshangao kisha akaendelea kufanya mashambulizi kwa waarabu hao wenye hasira kali.Sikujua hata niliichomoa chomoa vipi bastola hiyo kwani kitendo nilikifanya katika muda mfupi hadi kifo cha waarabu hao walio taka kutuua kukamilika.Wanajeshi wengi wa kimarekani wakazidi kufa kwa shambulizi la gafla la waarabu hao.Askari wa kike akanifungua pingu za mikononi na mnyororo walio nigunga miguuni na mimi nikaendelea kufanya kazi ya kuwashambulia waarabu hao na mbaya zaidi tupo jagwani na hakuna hata sehemu ya kujificha zaidi ya gari tulilo nalo.Askari wa kike akaingia kwenye gari lake na mimi nikaingia na kwakasi tukaanza kuelekea sehemu tusiyo ijua na kuwaacha askari wengine wakiendelea kupambana na waarabu hao.Gafla kwa nyuma nikaona gari mbili zikija kwa kasi huku risasi zikipiga gari letu kwa nyuma
Askari niliye naye akaniomba niendeshe gari hilo lililopo kwenye mwendo wa kasi kiasi,tukabadilishana kwa utaalamua wa hali ya juu na askari akakaa siti ya nyuma na kuanza kujibu mashambulizi ya watu wanao tufukuzia na mimi nikawa na kazi ya kuendelea na kazi ya kuendesha gari hilo japo sina uzoefu wa kuendesha gari jangwani ila nikajitahidi kuliendesha kwa mfumo wa kukunja kunja kona mithili ya nyoka anaye tambaa kwa kasi ili kuyazuia matairi hayo kuingia kwenye mchanga.Kwa mbali nikaanza kuiona miti mingi na kunifanya nipate matumaini ya kuyakanyaga mafuta kwa kwenda mbele zaidi ili kuikaribia miti hiyo.Mwendo wa dakika kumi na tano nikawa nimeifikia miti hiyo na kukuta barabara ndogo inayo wezesha gari hilo kupita bil shida ikiingia ndani yam situ huo wenye giza kali ila kilicho nisaidia ni taa za gari hilo
Nikazidi kulipeleka gari kwa kasi na kwakutumia kioo cha pembeni nikashuhudia gari mbili zinazo tufukuza zikizidi kuja kwa mwendo wa kasi na nikazidi kupata wasiwasi baada ya ukimya kutawala kwenye siti ya nyuma alipo askari wakike wa kimarekani ambaye anajibu mashambulizi ya waarabu hao.Nikageuka na kumkuta akiwa amejilaza huku damu zikimwagika kwenye shingo yake,Nikaachia mkono mmoja kwenye mskani wa gari kuanza kuivuta bunduki yake kabla sijaifikia akanishika mkono huku akitetemeka na kunikabdhi picha ndogo na kwa shida akazungumza akiniomba niwatafute watu walipo kwenye picha hiyo ambayo nikaiweka mfukoni mwa nguo nililo livaa.Galfa nikaanza kuhisi matairi ya gari yakiwa hayatembei kwenye ardhi na nikageuka kutazama mbele na kuliona gari nililomo likisuka kwa kasi kwenda chini kwenye korongo kubwa huku likielea hewani
Nikaanza kuminyana na mlango wa gari katika kuufungua na kwabahati nzuri nikafanikiwa na kujirusha na mimi nikajumuika na gari hilo kwenda chini kwa kasi na gafla nikajikuta nikitua kwenye miti ya eneo hilo na kuanza kupigiza kwenye matawi ya mti huo ambao kadri ninavyozidi kwenda chini ndivyo ninavyozidi kujigonga na kasi ikaanza kupungua na kujikuta kikoti cha kuzuia risasi nilicho kivaa kikinasa kwenye moja ya tawi la mti huo na kubaki nikining’ia hewani huku taratibu nikihisi maumivu makali yakiutawaka mwili wangu na damu zikizidi kunimwagika na sehemu niliyopo kutoka juu ya mti huo hadi chini kuna umbali mkubwa na kuna mawe marefu yaliyo chongoka na nikaanza kuhisi tawi lilolo ninasa likianza kukatika kwa kushindwa kuhimili uzito nilio nao
Gafla nikaanza kuhisi sauti ya mnyama ikikoromoa nyuma yangu kwa haraka haraka nikajua sauti ya mnyama huyo ni chui.Nikageuka taratibu na kutazama nikakutana ni mnyama ambaye sijawahi kumuona katika maisha yangu na wala hakuwa chui kama mawazo yangu yalivyokuwa yakinipelekea,Akazidi kunguruma guku macho yake yakiwa ni makali kupita maelezo huku meno yake yenye ncha kali akinionyesheshea kwa ishara ya kutaka kuning’ata.Akaanza kupiga hatua za taratibu kunifwata kwenye tawi lililo nizuia na kutokana na uzito wetu tawi kikashindwa kustahimili uzito na likakatika na tukaanza kwenda chini kwa mwendo wa kasi huku nikijitahidi kwa juhudi zangu zote kuweza kushika japo tawi la mti mmoja na kujikuta nikishindwa kufanya hivyo.Kabla sijafika chini ili mwili wangu upige kwenye jiwe lenye ncha lali nikafanikiwa kushika kwenye tawi jembaba la mti huu kiasi kwamba umbali kutoka sehemu nilipo hadi kwenye jiwe sio mbali sana.Mnyama aliye kuwa akinitishia nilishuhudia akipasuka kichwa baada ya kutua kwenye jiwe kubwa na kusababisha nizidi kuogopa
Maumivu makali ya mkono wangu ulio shikilia kijitawi kidogo ukaanza kunipa wasiwasi na mara kadhaa nikajitahidi kubadilisha mikono katika kukishikilia kitawi hichi ili nisiendelee kuumia.Gafla kwa mbali ndani ya msitu nikaanza kuona taa za gari zikija kwa kasi katika eneo nililopo na nikaanza kuogopa.Ubaya wa sehemu niliyopo siwezi kwenda juu wala kusogea pembeni na nikisema niende chini ndio utakuwa mwisho wa maisha yangu.Akilini mwangu nikaanza jua watakuwa ni wanajeshi wa kimarekani ambao waliniweka kifaa maalumu kwa ajili ya kuniona mimi kila sehemu ninayo kwenda.Kadri dakika zinavyo zidi kukatika ndivyo gari hizo zipatazo mbili zilivyo zidi kuja kwa kasi katika eneo nililopo na ndani ya dakika nne hivi zikawa zimesimama chini ya mti niliopo.Wakashuka jamaa wenye asili ya kiarabu na kuufanya moyo wangu kuanza kudunda na kujua jamaa hawa ndio wale walio kuwa wakitukimbiza huku mmoja wao akionekana na ndevu nyingi na urefu mkubwa na kujikuta nikiwa nikizidi kuogopa na kukiona kifo kipo mbele yangu na huu ndio utakuwa mwisho wa maisha yangu,Nikataka kujiachia kwenye katawi ka mti ili nife kuliko kuingia mikononi mwao ila jamaa akanizuia kwa ishara nisifanye ninachotaka kukifanya.Wakajipanda watu wapatao sita wenye miili mikubwa huku wakiwa wameshikana mikono na wakaniomba niweze kujirusha kwenye mikono yao.Jamaa akazidi kuniomba kwa ishara niweze kufanya hivyo na kwa ushawishi wake nikagundua ni mtu mzuri kwangu japo wamebeba bunduki zenye uwezo mkubwa wa kivita.Nikajirusha na jamaa wakanidaka kwa kutumia mikono yao na kunisimamisha wima na nikabaki ninatazamana na kamaa
“Una kifaa chochote kwenye mwili wako?”
Jamaa mwenye ndevu nyingi aliniuliza kwa lugha ya Kiswahili kidogo wasiwasi ukaanza kupotea
“Kivaa gani?”
“Kifaa chochote ulicho ingizwa kweye mwili wako?”
“Kipo?”
“Wapi?”
Nikamuonyesha sehemu niliyo fungwa bandeji na mmoja wao akaanza kuifungua na kukutana na nyizi nilizo shonwa masaa mengi yaliyopita.Akachukua visu vya kufanyia oparesheni na kunichana bila hata kutumia ganzi na kukitoa kifaa nilicho ingizwa na daktari kwenye kambi ya wanajeshi wa marekani.Wakanipakiza kwenye gari na tukaondoka eneo hilo kwa kasi.Tukatokeza kwenye barabara ya lami na kuona kibao kimeandikwa na maandishi makubwa ya kiarabu huku chini yake kukiwa na maandishi mengine ya kizungu KA LABGH ROAD.Tukaingia kwenye mji mdogo na tukaupita na kwenda umbali wa kilomita tatu na kufika kwenye mji uliopo pembezoni wenye ukimya mkubwa huku kukiwa na kambi moja tu iliyo zungukwa na ukuta mrefu kama wa gereza na mti mingi na mirefu kwenda juu huku kukiwa na ulinzi mkali kiasi kwamba si rahisi mtu wa nje kuona ndani na mtu wa ndani kuona nje zaidi ya askari na ulinzi walio simama juu ya kuta hizo wakiwa na bunduki zao
Geti kubwa likafunguliwa na magari yetu yakaingia na kukuta mahema mengi yaliyo makubwa kiasi na kukiwa na viwanja vikubwa vyenye ndege za kijeshi aina tofauti tofauti pamoja na vifaru vya kupigania vita.Tukashuka ndani ya gari na jamaa akanifata sehemu nilipo
“Karibu bwana Eddy kwenye kambi ya Al-khaida jina langu ni Mohamed Bin Isack watu wengi wamezoea kuniita BIN ISACK”
Akanipa mkono na mimi nikampa wa kwangu japo unamaumivu makali ila nikajitahidi kupotezea ila kadri jamaa anavyo nitingisha nikajikuta nikikunja sura yangu kwa mauvivu
“Unamaumivi......?”
“Ndio”
Jamaa akazungumza na wezake kwa kutumia lungha ya kiarabu na mmoja akatoa blangeti kwneye gari na kunifanika kwani katika eneo tulilopo kuna baridi kali kiasi kwamba iliwaladhimu kunipataia huduma hiyo.Tukaongozana na tukaingia kwenye moja ya nyumba na nikagundua ni hospitali.Akanikabidhi kwa madaktari na akaniambia atarudi asubuhi.Madaktari wakanipiga picha ya X-rays na kungundua nina mpasuko kwenye mfupa wa moja ya mguu ambao kipindi nipo Tanzania nilipata ajali ya pikipiki.Wakananichoma visindano vingi kwenye eneo la mguu nilipo na jeraha hilo na ndani ya dakika mbili sehemu ya jeraha ikaanza kuvimba na sikuweza kuhisi maumivu ya aina yoyote na wakachukua vivaa vyao na kunichana kisha wakaanza kuniingiza vitu ambavyo sikujua ni vitu gani na mbaya zaidi hawakunichoma hata sindano ya usingizi na kila walicho nifanya niliweza kukiona.
Wakamaliza na kunishona kisha wakanipaka dawa yenye uasili wa mafuta na kuvitoa vijimiba walivyo nichoma na kunifunga bandejii.Kila eneo la mwili nililo pata michubuko na vidonda wakalifanyia matibabu na ndani ya masaa mawili wakawa wamemaliza.Wakanioandosha kwenye kitanda walicho nifanyia Oparesheni na kunilaza kwenye kitanda cha matairi kisha wakakisukuma kitandani hicho kutoka katika chumba nilichopo na kuniingiza kwenye chumba kingine.Wakanitundikia dripu la maji na wao wakatoka ndani ya chumba hicho.Maswali mengi yakazidi kuniumiza kichwa kwani sikuju sababu ya waarabu hao kunisaidia mimi na kitu kingine walijuaje kama mimi ninapelekwa sehemu nyingine na wanajeshi wa Kimarekani hadi wakakatisha msafara huo
Sikupata usinhizi hadi asubuhi na akaingia BIN ISACK kwenye chumba nilichopo kama alivyo niahidi jana usiku na akasimama kando yangu
“Habari yako bwana Eddy?”
“Salama”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hali yako ipo vipi?”
“Kidogo maumivu sina yamekwisha”
“Usijali Mungu atakupa uheri wa afya na utapona haraka”
“Amen”
“Pole kwa maswaibu yote yaliyo kukuta”
“Asante......Ninaweza nikakuuliza swali?”
“Unaweza?”
“Imekuwaje kuwaje hadi mukanisaidi mimi na wakati mimi siwatambui nyinyi?”
“Swali nzuri bwana Eddy....Na nitakueleza kwa ufupi tu kwani ninataka nikampolee Lilian......Kipindi unataka kupelekwa Marekani kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano ikashindikana ikawalazimu wanajeshi walio kukamata kuweza kukuleta katika base kubwa ya jeshi la Marekani iliyopo hapa Pakistani na kila kilicho kuwa kikiendelea sisi tuliweza kupata taarifa kutoka kwa Lilian ambaye ni mshirika wetu wa upelelezi nchiniMarekani....Na Lilian aliweza kupata taarifa kutoka kwa dada yake aliopo kwenye kambi hiiyo ya Wamarekani”
Jina la Lilian halikuwa geni sana kwangu nikahisi atakuwa ni Lilian niliye kutana naye kwenye boti ya kifahari ya watalii ambayo ilitekwa na kundi kutoka Somalia
“Kwa maelezo zaidi atakuja kukueleza yeye mwenyewe Lilian kwa maana anakuja hapa kambini kukutana na wewe”
“Yeye kwa sas hivi yupo wapi?”
“Yupo kwenye ndege akitokea Marekani ndani ya nusu saa ninatakiwa niwe Air port nikimsubiria”
“Sawa”
Jamaa akatoka ndani ya chumba na kunifanya matumaini ya kuishi yaanze upya kutawala moyoni mwangu.Wakaja madaktari wawili wakanihudumia na kwa kunibadilisha nguo na kunivalisha nguo maalumu ambazo hutumiwa mara nyingi na wagonjwa.Wakaniletea mikate ya slesi na mayai mawili pamoja na chai ya maziwa nikala nikilipa tumbo langu ufufuo kwani kutokana na njaa niliyo kuwa nayo furaha yangu haikuwa nzuri ila baada ya kula furaha ikaongezeka mara dufu.Ndani ya lisaa moja wakaingia Bin Isack na Lilian kwenye chumba nilichopo na kwa jinsi Lilian alivyo vaa kwa haraka haraka sikuweza kumtambua ila alivyo tabasabu nikakumbuka siku tuliyo kuwa kwenye boti
“Eddy unaendeleaje?”
Lilian alaizungumza huku akinipa mkono wa salamu
”Vizuri tuu sijui wewe?”
“Mimi kama unavyo niona nipo powa na ninafuraha kujua kuwa upo hai”
“Hata mimi ninamshukuru Mungu?”
“Bin Isack mtu mwenyewe niliye kuwa nainakuambia kupitia simu ndio huyu ndio huyu hapa kwa wakati mchache nilio kaa naye niligundua ana uwezo mkubwa amboa atatusaidia kwenye kazi zetu”
“Nimemuona hata mimi nina imani hiyo”
“Eddy karibu sana....na hapa ni Pakistani na ujisikie nyumbani?”
“Sawa ndugu zangu nawashukuru kwa upendo na ukarimu wenu”
Hali yangu ya mwili ikazidi kuimarika kadri siku zinavyo zidi kwenda na nikiajikuta nikipendwa na watu wengi kutokana na uchangamfu wangu na kujitahidi katika kujifunza lunga ya kiarabu na kingereza,Ndani ya wiki mbili nikawa nimepona kabisa majeraha ya mwili wangu na nikaanza kujumuika rasmi katika mafunzo ya kijeshi yanayo tolewa ndani ya kambi hiyo.Na juhudi yangu ikanifanya niwashawishi waalimu wanao tufundisha mafunzo ya kijeshi kunitengea muda wangu wa ziada wa kufanya mazoezi na wakazidi kunifundisha hadi mbinu zao za ndani kiasi kwamba kuna kundi la wezangu ambao nipo nao wakaanza kunichukia.Kama kawaida yetu ya kuoga pamoja wanaume tuliopo kwenye kambi hii na leo nilimechafuka sana kutokana na kufanya mazoezi kwenye matope kiasi kwamba mwili wangu haukutamanika.Nikaingia bafuni na kukuta wezangu wakiendelea na kuoga.Nikavua nguo zangu nikiwa ninashika boxer ili niivue nikastukia jamaa mmoja akinisukuma kwa nyuma huku akizungumza maneno ya kiarabu ambayo ninayaelewa
“Wewe muamfrika mjinga huwezi kuchukua utemi katika kambi hii”
“Sijakuelewa?”
“Wewe umetoka huko kwenye nchi zako za kis*** na kuja huku ili iweje”
Jamaa alizungumza kwa kutumia kiarabu na mimi nikawa ninamjibu kwa lugha hiyo hiyo,Jamaa akazidi kunisukuma na kurudi nyuma na kiwafanya watu wanao oga kusitisha kazi zao na kuanza kushangilia huku wakiliimba jina la mwenzao aweze kunipiga.Jamaa akarusha teke ambalo likanipiga kwenye bega na kuniyumbisha kiasi
“Sihitaji fujo na wewe”
“Wewe fala wa kaifrika ndio maana huwezi kupigana na ngozi nyeupe kama sisi”
“Nashukuru kwa hilo ila sihitaji ugomvi”
“Nenda zako huko kamalale mama yako mwenye akili za kimalaya kama zako”
Maneno ya jamaa yakapenya kwenye moyo wangu na kujikuta nikipandwa na hasira na kwajinsi wezake wanavyo mshangilia ndivyo jamaa akazidi kujiftua huku akitunisha tunisha misuli yake na tangu siku ya kwanza ninaanza mazoezi jamaa alikuwa anaonekana ni mbabe sana kwa wezake na hata kwenye holi tunalo lala yeye huwa mtu wa kuwaamrisha wezake katika kufanya kazi mbali mbali hata kazi ya kuvalishwa viatu alimpa jamaa mmoja ambaye ni mnyonge nyonge na anaumbo dogo ambalo hawezi kufanya chochote mbele ya jama
Wezake wakaanza kunijambisha huku wakinizomea kutokana sikujibu kitu cha aina yoyote.Jamaa akanisogelena na kuninyooshea kidole cha kati cha mkono wa kushoto ikiwa ni maana ya tusi.Nikakunja ngumi kwa haraka na kabla jamaa hajashusha kidole chake chini nikakipiga ngumi nzinto na kumfanya jamaa kukishika huku akiinama kwa kuugulia maumivu makali.Nikampiga kigoti cha kidevuni na kumfanya jamaa kunyanyuka huku akiwa ameushika mdomo wake na akatema mate yaliyo changanyika na damu.Watu wakaanza kutuwekea daura kubwa kwa ajili ya kupigana,jamaa akakunja ngumi huku akiruka ruka.Nikaitazama miguu yake jinsi anavyo ifanya kisha akapiga hatua na kurusha teke jingine na nikainama chini na likapita kwa juu na kwa haraka nikiwa nimeinama ngumi yangu ikatua sehemu za siri za jamaa na kumfanya ajishike huku akipiga kelele za maumivu makali na akaanguka chini huku akiwa analia na kulifanya bafu zima kukaa kimya wakinitazama
Nikapiga hatua na kusimama kwenye moja ya bomba la mvua na kufunga maji na kuanza kuoga na jamaa akanyanyuliwa na wezake na wakatoka bafuni,Kila mmoja akaanza kunipa pongezi kwa kitendo nilicho kifanya na sikujua ni kwanini wananipa pongezi
“Yule jamaa alikuwa anajifanya ni mbabe sana”
Alizungumza jamaa mmoja huku akinipa mkono wa pongezi na nikajikuta nikitabasamu pasipo kuzungumza chochote.Nikamaliza na kwenda kwenye holi tunalo kaa na kumkuta jamaa akiendelea kulia kwa maumivu huku akiwa amejilaza kwenye kitanda chake cha juu na wezake walipo niona wakaanza kurudi nyuma wakiniogopa
“Jamaa anaendeleaje?”
Niliwauliza kwa kutumia lugha ya kiarabu na kuwafanya jamaa kuanza kutazamana na hakuna aliye weza kunipa jibu la uhakika na jamaa mmoja akamnyooshea kidole mwenzao niliye mpiga na akatingisha kichwa akimaanisha bado hali ya jamaa sio nzuri,Nikapanda juu ya kitanda changu na kufungua begi langu la nguo na kuvaa suruali za jeshi na shati lake nikamalizia kuvaa viatu ambavyo navyo ni vya jeshi kabla sijafunga begi langu nikaiona picha niliyopewa na askari wa kike wa Kimarekani kipindi tupo ndani ya gari.Sikuzote sikuweza kuitazama ni picha ya watu gani ila kadri jinsi ninavyo zidi kuziangalia sura za watu wawili hao zikanijia kichwani na kujikuta nikianza kujiuliza maswali mengi sana japo binti mdogo anaye onekana kwenye picha hiyo ameweka mtindo wa nywele zake kiupande na kuziba jicho moja ila nikajua ni Liliana na mama anaye onekena ni pembeni ya mtoto huyo ni Bibi Vanesa ambaye tulimuacha nchini Kenya.Nikaiingiza mfukoni picha hiyo na kutoka ndani ya holi letu na kawaida ya kambini hapo ni lazima watu kuvalia sare za jeshi hili masaa yote utakayo kuwa upo nje ya holi lako la kulalia.
“Eddy unaitwa”
“Na nani?”
“Na Bin Isack kwenye ofisi za R one”
Nikaongozana na jamaa hadi kwenye ofisi hizo na kumkuta akiwa na Lilian ambaye siku kadhaa aliniaga anakwenda Iran kuna uchunguzi anakwenda kuufanya
“Eddy pole kwa mazoezi”
“Kawaida kamanda Bin Isack”
“Ninapata sifa zako kwa waalimu wenu wanadai upo vizuri”
“Ninajitahidi kufanya yale wanayo nielekeza ili niwe mpiganaji mzuri”
“Eddy mambo vipi?”
“Salama”
“Nina habari nzuri kwako”
“Habari gani Lilian?”
“Kpindi ninaondoka hapa nilikwenda moja kwa moja hadi Italy ambapo niliweza kumuona Priscar akiwa na yule jamaa aliye toroka naye na ushahidi wa picha huu hapa”
Lilian akania picha mbili kubwa zinazo waonyesha Priscar na Muntarah wakiwa wanatembea kwenye moja ya mtaa wa Italy
“Hapo niliweza kuwafwatilia na kugundua wanaishi kwenye mtaa mmoja ambao nitakuambia jina leke nitakapo likumbuka”
“Asante Lilian ila kuna kitu nahitaji kukuuliza?”
“Kitu gani?”
“Unamfahamu Bibi Vanessa?”
“Ndio ninamfahamu ni mama yangu mzazi.Wewe umemjuaje?”
Nikajikuta nikistuka na taratibu nikiwa mnyonge sikujua ni jinsi gani nimuelezee Lilian juu ya mazingira ambayo tulimuacha mama yake kwani sikujua kama yupo hai au amekufa
“Eddy mbona umekuwa mnyonge gafla....Unamjua mama yangu?”
“Ndio nina mfahamu sasa sijui kama......Yupo likini?”
“Ndio yupo ila nimemuacha Marekani akiwa na huzuni kubwa akiwalilia rafiki zake anao dai wamefariki kwenye tukio la kutekwa nchini Kenya”
“Amekuambia hao rafiki zake?”
“Hakunitajia hao rafiki zake ila kitu kingine kinacho mpa upweke ni kifo cha baba kilichotokea kwenye mapango walikwenda kufanya uchunguzi wao”
Nika kaa kimya na wala sikutaka kujitaja ni mimi ndio miongoni mwa rafiki zake ila kitu kingine kinacho nichanganya nii picha.Nikataka kuitoa mfukoni ili nimuonyeshe Lilian nikajikuta nikisita
“Bin Isack unajua hadi leo sijapata simu kutoka kwa dada yangu sijui watakuwa bize kwenye shuhuli zao”
“Labda inaweza ikawa hivyo kwani hata simu yake ya mkononi haipatikani?”
“Haipatikani na nilijaribu kumpigia rafiki yake wa karibu katika kambi yao naye pia hakupatikana”
“Samahani lakini Lilian kwa kuwaingilia maongezi yenu?”
“Bila samahani”
“Dada yako anajishuhlisha na nini?”
“Yeye ni Luteni katika kambi ya jeshi la Marekani lililopo hapa Pakistani na yeye ndio alikuwa msaada mkubwa sana katika kutupa habari juu ya msafara wako wa kupelekwa katika gereza la Guatenama”
“Mmmmm sasa yeye alikuwepo kwenye huo msafara?”
“Hapana aliniambia hato husika na chochote ila alinimbia kuwa watakwenda Ukrein kuzuia machafuko yanayo endelea katika nchi hiyo”
Nikashusha pumzi ila hisia zangu zikawa na nguvu ya kuhisi dereva wa kike niliyekuwa naye kwenye gari alikuwa na dada yake Lilian ila sikutaka kuzungumza kitu cha aina yoyote.
“Bin Isack pia nilikwenda Somalia na kufanya uchunguzi wa wapi inapatika kambi ya wale jamaa walio iteka boti ya mama nikafanikiwa kuipata”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lilian akaweka picha za majengo zipazo kumi mezani na kumfanya Bin Isack kuanza kutazama picha moja baada ya nyingine huku akitingisha kichwa akionekana kufurahishwa na juhudi za Lilian ambaye kwa mtazamo wa haraka haraka unaweza ukasema ni mwanamke mastaarabu wa kuoa na kumuweka ndani
“Kazi nzuri na hii kazi utabidi ukaifanye na Eddy ili aweze kupata uzoefu”
“Mim!!?”
Ndio kwani kazi yako ndio imeanza hivi na wewe tunahitaji ufanikiwe kwenye mipango yako kwani nina imani una mipango yako binafsi akilini mwako”
“Itakuwa lini?”
“Baada ya wiki mbili zijazo na ukirudi unaingia msituni”
Sheria moja ambayo tunafundishwa katika kambi hiyo ni kuto kukataa maagizo yanayo tolewa na mkuu wako na inakulazimu kuweza kukubali kila utakacho ambiwa pasipo kuuliza maswali zaidi ya matatu.Giza likatanda juu ya anga na Lilian akaniomba nikapate naye chakula kwenye moja ya mgahawa uliopo nje ya kambi hiyo.Ikanilazimu kuvaa tisheti ya jeshi pamoja na kofia na nikamalizia na koti nililokuwa nimelivaa,Nikaichomeka bastola yangu kiunoni na nyingine nikaichomeka kwenye soksi huku zote zikiwa na risasi za kutosha.Tukaingia kwenye gari ndogo na tukatoka kweye kambi na kushika barabara ya kuelekea mjini ila sikujua panaitwaje ikanibidi nimuulize Lilian kwa sababu hiyo ndio siku yangu ya kwanza kutoka nje ya kambi hiyo tangu nilipo ingia
“Tunaelekea wapi?”
“Tunaelekea katika jiji linaitwa KARACHI”
“Ahaaa karachi ninapasikia sikia”
“Ila tunapo kwenda sisi ni kwenye mji ulipo nje kidogo ya jiji la Karachi na mji wenyewe unaitwa GADAP TOWN”
“Ahaaa”
Ndani ya masaa moja na nusu tukaifikka kwenye mji alio niambia Lilian na tukaingia kwenye moja ya hoteli ambayo ni kubwa na ina watu wengi.Tukatafuta sehemu iliyo jificha na yenye kigiza giza na kukaa.Lilian akaangizia chakula na baada ya muda muhudumu akaleta chakula na taratibu tukaanza kula huku tukipiga stori za hapa na pale na nikamuelezea maisha yangu ya nyuma katika hali ngumu niliyo pitia ila sikumuadisia kama nilikutana na mama yake
“Pole sana Eddy ila tambua katika maisha changamoto kama hizo zipo”
“Kweli ila na wewe ni kwanini ulijiunga kwenye kundi hili la magaidi?”
“Nilipenda tu kwani tangu nikiwa mtoto mimi na dada yangu tulikuwa tunapenda sana katika maisha yetu ya ukubwani tuwe wanajeshi ila kadri tuivyokuwa tukikua mwenzangu akazidi kulipenda jeshi la nchi yetu ila mimi nikatokea kuichukia nchi yangu ndio nikaamua kujiunga na hawa jamaa”
“Kuna malipo wanayo kupa?”
“Ndio pale ni sasa sawa na kazini na wewe ukimaliza mafunzo utaanza kulipwa mshahara”
Tukaendelea kula na kadri muda unavyo zidi kwenda tukajikuta tumezoeana na Lilian kiasi kwamba akaanza kunishika shika kifua changu huku akikisifia ni kizuri na nikikubwa.Kimoyo moyo nikajisemea laiti angenijua huwa sibipiwi waka asingwe fanya anacho kifanya.Akauweka mkono wake juu ya paja langu na taratibu akaanza kuusogeza na ukatua juu ya koki yangu na akaendelea kuupapasa na kuifanya koki yangu kujibu mapigo na kusimama na hadi nikahisi mishipa yake inaweza kupasuka kwa hasira.Nikaushika mkono wa Lilian na kuuweka kando ili asiendelee kufanya anacho kifanya
“No Eddy leo sikurudishi kambini”
“Kwanini?”
“Nataka nipate joto lako”
“Huoni kuwa itakuwa ni tatizo kwangu nikilala nje ya Kambi?”
“Bin Isack hawezi kusema kitu chochote juu yangu na pia hakuna mtu atakaye kuuliza kususiana na hili na endepo atatokea basi muambie akamuulize mkuu wake”
Sikuwa na unjanja wala swali lolote na kitu kingine kilicho nifanya nikubaliane na Lilian ni kutokana katika maisha yangu sikuwahi kupata mwanamke wa kizungu.Tukalipia chumba kwenye hoteli tuliyopo na tukapanda kwa kutumi lifti hadi gorofa ya kumi ambapo ndipo kilipo chumba chetu.Tukaingia na alichoa anza kukifanya Lilian ni kuvua nguo moja baada ya nyingine na akabakiwa na bikini kisha akajirusha kitandani na kuanza kuniita kwa mapozi,Nikavua koti nililo livaa na nikapanda kitandi na kuanza kumnyonya Lilian lipsi zake huku taratibu nikianza kuyaminya minya maziwa yeke malaini.Lilian akanifungua mkanda wa suruali yangu na kuanza kunivua suruai yangu na ikanilazimu nijilaze kitandani ili aweze kunivua viatu na kuimalizia suruali yangu niliyo ivaa
Nikamuona Lilian akitulia na taratibu na akaanza kuupandisha mkono wake na kuona ameishika picha ambayo nilipewa na dada yake na nikajua itakuwa imeanguka. Akanitazama kwa umakini kisha jicho lake akalirudisa kwenye picha na akashuka kitandani haraka na kuiwahi bastola iliyopo juu ya meza na kunielekezea mimi
“Eddy hii picha umeipata wapi?”
“Alinipa dada mmoja wa kimarekani kwenye gari lililopata ajali”
“Unataka kusema dada yangu amekufa?”
Lilian alizungumza kwa sauti ya kufoka huku machozi yakimwagika na kulowanisha mashavu yake,Nikabaki nimemtizama na gafla nikaona vivuli vya watu wawili vikipita karibu na dirisha letu huku watu hao wakionekana wakiwa na bunduki na wananing’inia kwa kamba huku wakijiandaa kuingia kwenye dirisha letu ambalo ni dirisha la kioo.Nikaichomoa bastola yangu niliyo ichomeka kwenye soksi na kufyatua risasi mbili kuelekea kwenye kioo na kumfanya Lilian kuinama chini
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment