Search This Blog

Thursday 19 May 2022

TOTO LA KIMANGA - 2

 





    Chombezo : Toto La Kimanga

    Sehemu Ya Pili (2)



    Chirs aliendelea kusubili ujio wa shemsa ila akazidi kuona kimya tu na kibaya zaidi hakuwa na hata na namba ya simu ya shemsa,

    *sasa mbona huyu naye haji au amegairi? Kweli kuna watu dunia hii hawana shida ya pesa mtu unamuitia pesa zote zile alafu analinga kuja kuzichukua?

    Chirs alisubili dakika zikaenda zikawa masaa hatimae jua likaanza kuzama mawinguni na kiza kikaanza kuchomoza,

    *hapa ni bora mimi niondoke naona huyu binti hana shida ya pesa*

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***** ***** *****

    Upande wa chaz baada ya kuchukua pesa aliamuwa kuondoka na kwenda sehemu kusiko julikana,

    *hapa nikupanga hotel ya kifahari nikae kwanza hakiri yangu ifikilie itafanya nini? Chirs utanisamehe kwa maana sijafanya hivi kwa ajiri ya kukukomoa ila nimefanya hivi kwa ajiri ya ujinga wako wa kutaka kurudisha hizi pesa ili hali unajua kabisa hali yetu,



    **** v"v ******

    Shemsa na dada yake nyuso ziliwashuka kwani mama yao alikuwa na karatasi inayoonyesha zile pesa zilipokuwa zimetoka na pia alikuwa na ushahidi wa makubaliano ya shemsa na huyo aliyempa hizo pesa,



    "sikia niwambie kama nilivyokuwa numewaeleza kuanzia leo sitaki kuwaona hapa niacheni kama ni kufa basi nitafia hapa,



    "mama tusamehe kweli tumekosea sisi wanao tuko chini ya miguu yako mama yetu mama tusamehe wanao,



    Shemsa na dada yake walipiga magoti na kumbembeleza sana mama yao ila mama aligoma kutoa msamaha matokeo yake alizidi kuwafukuza,



    Hatimae doctor aliingia kwenye chumba alichokuwemo mama shemsa na kukuta hali ya sitofahamu ndani ya chumba hicho,



    "Jamani kuna nini mbona kelele namna hiyo?



    Mama shemsa hakuchelewa alimwambia doctor awafukuze,

    "dokta nifukuzie hawa watu humu na kuanzia leo wasikanyage humu ndani,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "haya sawa mama haina shida,

    Haya Jamani naombeni mtoke humu ndani maana kadiri mnavyozidi kumsemesha mama yenu mnaomuongezea tatizo mnajua kabisa anaumwa uti wa mgongo,



    Shemsa na dada yake hawakuwa na jinsi walitoka nje huku wakiwa hawaamani kilichotokea ndani walipofika nje walianza kulaumiana,



    "Shemsa haya yote umeyasababisha wewe,



    "dada huu mda siyo wa kulaumiana ni wakati wa kufikilia tutatue vipi hili tatizo,



    "haya niambie pale ulipo pokea simu uliruka kuwa pesa zimepatikana je ni zile pesa zilizopotea ama kuna zingine..?



    "Ndio zile zile pesa,



    "ehee kwa hiyo aliyekupigia simu alikuambiaje?



    "aliniambia tukutane kaliakoo nikazichukue ila naona mda umekwenda sana,



    "shemsa fanya haraka twende tukazichukue kama ningejua ni zenyewe toka saa zile ningekuambia ukazifuate,



    Shemsa na dada yake mbio waliondoka kuelekea kaliakoo kunifuata pesa kwa chirs,



    Shemsa na dada yake waliondoka mbio kwenda kaliakoo kufuata pesa kwa chirs,

    "sijui tutamuwahi mda wote ule alionipigia mpaka sasa sijamfikia,

    "tikikuta hayupo unampigia simu atuambie alipo tumfuate,

    "tatizo lililopo sina namba yake,

    "shemsa hebu acha ujinga huna namba yake kivipi?

    "namba aliyotumia ni namba ya meneja wa bank kama nilivyo kueleza huyo kaka alienda bank kutafta mawasiliano yangu ndio meneja wa bank akanipigia kupitia namba za bank akanipa niongee naye,

    "lakini mdogo wangu bado nakulaumu ulivyo ongea naye ungemwambia akutajie namba zake,

    "hapo ndipo nakubali nilikosea sikuwa na mawazo hayo kabisa si nilijuwa nitawahi kwenda,

    "ongeza sipidi basi maana nahisi kama vile gari haitembei?

    ***** "v" ******

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Chirs baada ya kukaa kwa mda mrefu bila kumuona shemsa aliona bora aondoke,

    *kama angelikuwa na shida ya hizo pesa angekuwa ameisha fika ila inaonekana hana shida ya pesa acha mimi niondoke zangu*

    Chirs aliondoka maeneo hayo na kuamuwa kurudi geto kwao,

    ***** "v" *****

    Mda ule alipotoka chirs hata dakika 5 hazikupita shemsa na dada yake walifika Katika eneo la makutano,

    Shemsa alitoka kwenye gari akaanza kuangaza macho huku na kule kuona kama atapata kumuona chirs,

    "shemsa inamaana humuoni huyo kaka?

    "simuoni yaani simuoni kabisa naona atakuwa ameondoka,

    "jaribu basi hata kuulizia hao wakina kaka kama wamemuona?.

    Shemsa alijisogeza kwa wale machinga ili awaulize kama wamemuona chirs pale,

    "Habari yako kaka?

    " nzuri karibu dada mrembo hapa kuna urembo kama vile hereni na bangiri n.k,

    "kaka sihitaji vipuri ila nina shida naomba kuuliza kama umemuona kijana mmoja maji ya kunde mrefu hivi,

    "Mhh hapa dada wanapita watu wengi sana,

    Shemsa alihama akaenda kuulizia kwa machinga mwingine,

    "huyo kijana kama vile nimemuona hapa alafu kaondoka mda sio mrefu hapa hata dakika tano hazijapita hebu ngoja nimuulize huyu jamaa,

    "oya kebo yule jamaa aliyekuwa hapa mda mrefu kaenda wapi?

    "Karudi ma getoni kwake,

    "kuna tunda lake hapa lilikuwa linamtafta,

    "dada shuka geto mchizi kakuweiti sana bila mafanikio,

    "sipafahamu kaka yangu ningelikuwa nimeisha ondoka,

    "shemeji sikia njoo usubili kuna mchizi anapajua akija atakupeleka huyo jamaa yako si anaitwa chirs?

    "Ndio yeye huyo,

    Jamaa mmoja alidakia,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " haa kumbe ni chirs yule wa mtaa wa kati kitaa flani kwa kina kiba,

    Jamaa mwingine,

    "Ndio kitaa hicho wapeleke basi,

    Dada yake shemsa alionesha tabasamu kwani hakuamini kama wamepata mtu anayepajua kwa chirs,

    "shemeji twendeni niwapeleke,



    Chirs aliondoka kuelekea nyumbani baada ya kumsubili shemsa pasipo na mafanikio yoyote yale,



    Chirs alipofika alingia ndani ila akashangaa kukuta mlango uko wazi alafu chaz hayumo ndani,



    *mmhhh huyu chaz ameachaje mlango wazi wakati anajua kabisa humu ndani kuna pesa*



    Chirs mapigo ya moyo yalimuenda mbio kwani tayari alianza kupata wasi wasi huenda pesa zitakuwa hazipo,

    Chirs alianza kuangaza huku na kule huku akitamani macho yake yake yakutane na mfuko wa pesa,

    Chirs kadili alivyozidi kupapasa macho huku na kule ndivyo kadili alizidi kuchanganyikiwa kwani mfuko wa pesa alikuwa hauoni wala dalili za kuwepo kwa chaz hazikuona kabisa,



    Chirs alikaa chini kutokana na kuishiwa nguvu,

    Alipotupa jicho mezani ulipokuwa mfuko wa pesa aliona karatasi akaichukua akaifungua ili kujuwa maneno yaliyomo,



    # rafiki yangu chirs sijachukua pesa kwa kwa ajiri ya kukukomoa naomba unisamehe sana Niliona upeo wako utatufanya kuwa masikini daima najua nimekukwaza kwani hizi pesa najua ulitaka kuzirudisha kwa yule binti mrembo ila mimi mawazo yangu yalikuwa tofauti na yako,

    Najua kwa jinsi unavyompenda yule binti utaumia sana kukosa hizi pesa,

    Naomba unisamehe kwani najua kabisa nitakuwa chanzo kukukwamisha kupata penzi la binti yule mwenye hizi pesa,

    Nisamehe sana ndugu yangu chirs#🌝



    Chirs Akiwa hapo chini alianza kuliya huku akikumbuka alipotoka yeye na chaz,

    *chaz rafiki yangu umesahau shida ngapi tumepitia mimi na wewe umesahau yote tuliyosaodiana mpaka leo hii unavunja urafiki na undugu kwa sababu ya pesa kweli chaz.?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Chirs akiwa Katika mawazo alisikia hodi mlangoni akaitika hodi



    "karibu mlango uko wazi,



    Chirs alishangaa kumuona shemsa akiwa na dada yake wakiingia ndani,



    "karibuni Jamani karibuni,

    "asante habari yako kaka chirs....?

    "nzuri karibuni tupo,

    "asante sana,



    Dada yake na shemsa alikuwa kimya huku ameshika pua yake akiashiria kuwa anasikia harufu mbaya ndani ya chumba kile,



    Shemsa alizidi kupiga story na chirs za hapa na pale kuhusu pale wamefikaje nani kawaleta,

    Ila dada yake shemsa alionekana kuchukua hali ile kabisa akatoa neno,



    "shemsa hebu mwambie akupe huo mzigo twende hali ya Hewa imenishinda kuvumilia,



    "dada hebu kuwa msitaarabu basi mbona hivyo.......?



    Shemsa alimkanya dada yake kuacha kauli zile za kebehi,



    "shemsa usiniambie maneno yako ya shombo hapa tumefuata pesa tu hatukufuata maongezi,



    Walianza kujibizana utazani hawakuja pamoja,

    Nilipoona hivyo niliingilia kati,,



    "Jamani msigombane someni hii karatasi kwanza,



    Niliwapa karatasi ya ujumbe ujumbe Wa chaz wakausoma,



    "wewe kaka usituekitie hapa tunachohitaji ni pesa tu wala si kingine,



    "la sivyo pita hapa twende polisi,



    Dada yake shemsa alianza kunipiga makofi huku akinivuta shati akitaka kunipeleka polisi,



    "Dada acha achaaa nini unafanya nini niniiiiiii.?..........



    "dada acha achaaa nini unafanya nini niiiiiii?.



    "wewe shemsa funga bakuli yako funga kabisa yaani pesa ziibiwe hivi hivi? Hapa ni lazima nimfikishe polisi,



    "hivi dada kama kweli chirs angekuwa mwizi angehangaika kunitafta anirudishie pesa zangu kweli?



    "haya kuhangaika kukutafta sasa pesa ziko wapi alizokutaftia?



    "dada uelezwe vipi barua ya ndugu yake aliyekimbia na pesa ametuonesha sasa ulitaka atuoneshe nini kingine ili uamini?



    "huyu ni jambazi tu hakuna kingine nakushangaa shemsa unapomtetea mwizi kama huyu,



    "chirs siyo mwizi wala siwezi kumtuhumu kwa kitu ambacho kinaonekana hakukifanya angekuwa mwizi asingehangaika kuitafta kiasi hiki,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati yote yakiendelea mimi nilikuwa na mawazo mengi sana kichwani na pia nilikuwa najiona mjinga mbele ya shemsa na dada yake na kitu kingine kilichokuwa kinanitesa ndani ya moyo wangu ni chaz kumchukua zile pesa za shemsa na kuniingiza Katika mgogoro na familia ya kina shemsa,



    Shemsa aliongeza bidii ya kunitetea mpaka nikahisi faraja ndani ya moyo wangu ila kadiri majibishano yalivyo zidi kuendelea kati ya shemsa na dada yake yalionekana kuelekea kubaya mpaka dada yake akapiga simu kwa ndugu yake akamuelekeza tulipo akaja alipofika aliambiwa aulize kwa chirs ataoneshwa,



    Huyo ndugu yao ambaye walimuita baba mdogo alifika akiwa na rafiki yake walipoingia baba yao mdogo alitoka kwanza nje akidai anaenda kuegesha gari vizuri,



    Rafiki yake aliyekuwa amebaki ndani alianza kusimuliwa jinsi mambo yalivyo na yeye bila kuvuta subira alianza kuniadhibu moja kwa moja kwa kunipiga mateke na ngumi za kutosha,



    "wewe mbwa sema pesa ziko wapi sema wewe mpumbavu pesa zilipo?



    Jamaa alinipiga kwa sifa kwa kuwa alikuwa anaona sura za warembo wale na kilichomsisimuwa zaidi ni kuona anasapotiwa na dada yake shemsa,



    Shemsa alionekana kuumia moyoni mpaka uso wake ulibadilika na kuonesha mistari kwenye paji la uso hiyo ilitosha kuyajuza macho yangu kuwa anaumia,

    Alivumilia ila akaona haina jinsi akaamuwa kuongea,



    "wewe weweeeee hebu muache unampiga kama unapiga ngoma kwanza hayakuhusu haya,



    Yule jamaa alimuangalia dada yake shemsa kisha akahoji swali kwa dada yake shemsa,



    "hey vipi huyu ndugu yako mbona anamtetea jambazi?



    "mimi mwenyewe nashangaa ila Endelea kupiga mpaka aseme pesa zilipo,



    Jamaa aliporudi kutaka kunipiga shemsa alisimama mbele yangu kwa bahati mbaya yule jamaa akawa amempiga teke la paja shemsa na kuanguka chini,



    Hapo ilikuwa kama kanichaji niliinuka kama upepo kutoka chini jamaa nilimpiga ngumi zisizo na hesabu nikamsindikiza na teke lililompelekea kuchomoka mlangoni na kuangukia nje,



    Shemsa na dada yake walishangaa hawakuamini kama nilikuwa na uwezo ule wa kupigana walibaki wametoa macho wasiamini kilichokuwa kimetokea mbele yao,

    Yule jamaa akiwa na baba yao mdogo na akina shemsa waliingia wameshika mnyororo na kisu mkononi dada yake na shemsa alishangilia huku akisema,



    "uweni kabisa huyu ni jambazi tena jambazi sugu,



    shemsa alisimama kwa taabu kisha akasema,



    "hauliwi mtu hapa ila tutauwana kwani roho zenu mbaya nazijuwa sasa mkimuuwa chirs labda mhakikishe na mimi mmeniuwa,





    Shemsa alikuwa mkali kama mbogo kwa jinsi alivyokuwa sikutegemea kama anaweza kukunja sura kiasi kile na kubadili sura kuwa kama mtu aliye chomwa sindano ya shingo,



    Dada yake alianza kutoa maneno ya shombo kama kawaida yake,



    "shemsa nasema hivi lazima chirs atoe hizo pesa awe nazo asiwe nazo atajua yeye,



    "sasa sikia nikwambie kitu kimoja Najima hizo pesa hukumkabizi kwa hiyo huna uharali wa kudai hizo pesa na kama unamshutumu kuwa ni mwizi sema alichokuibia nini?



    Najima ambaye ni dada yake na shemsa aliishiwa pozi akabaki kutoa macho asijue cha kufanya,

    Baba yake mdogo na rafiki yake waliingilia kati baada ya kuona Najima ameshindwa kufurukuta kwa maneno aliyopewa shemsa,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "huyu kijana lazima afike polisi iwe isiwe kwasababu ni mwizi na sijui ni kwanini unamtetea?



    "umpeleke polisi amekuibia nini? Kama kuna alichokuibia mpeleke hiyo polisi,



    "hivi shemsa unapopayuka hivyo unakuwa unapayukia nani? Sasa nimesema hivi wewe kijana pita hapa twende polisi,



    Aliongea huku akinivuta mkono na mimi nikakaza mkono, nilipokaza mkono alinipiga kofi la shavuni bila ya kuchelewa na mimi nilimpiga kofi la shavuni,

    Alipoona hivyo alirusha ngumi na mimi nikarusha mapambano yalianzia yule mwenziye aliyekuwa pembeni alipoona hivyo aliingia kati na kuanza kumsaidia mwenziye kwa kunipiga,

    Shemsa alipoona hivyo aliona isiwe tabu na yeye akaingilia kati alichofanya alinyanyua ubao uliokuwa ndani akampiga nao baba yake mdogo na pale pale akaanguka chini na kuanza kutoa damu puani na mdomoni,



    ****** **** ******

    Mama shemsa akiwa hospital alikuwa akiwaza mengi sana kuhusu familia yake haswa suala lililokuwa linampa presha ni suala la watoto wake kutafta pesa za kumtibisha kwa njia isiyo salama,



    *siamini kama mwanangu shemsa alitumia hakiri yake kukubali zile pesa za mashariti ya kipuzi maana namjua mwanangu vizuri hanaga masuala ya kishenzi,

    Najua Najima ndie atakuwa amemshauri hakuna mwingine Najima ni mwanangu ila huwa simuamini kabisa,



    Mama huyo akiwa Katika mawazo mengi sana mgonjwa mwenziye waliyekuwa wamelazwa chumba kimoja alimuuliza,



    "vipi ndugu yangu mbona una mawazo mengi sana?



    "wanangu wananichanganya sana kuumwa kwangu imekuwa taabu sana wanatafta pesa za kunipeleka India kutibiwa ila huo utaftaji wa hizo pesa ndio sijaupenda kabisa,



    "hajaupenda kivipi wakati wanahangaikia uzima wako?



    "shemsa ni mwanangu ninaye mpenda kuliko kitu chochote kile najua anahangaika kwa sababu yangu ila pesa alizotumiwa kutoka ulaya zilikuwa zina mashariti magumu kwa mwanangu kwani mtoa pesa alitoa pesa kwa shariti kumuowa shemsa,



    "sasa kuna ubaya gani kama aliahidi kumuowa? Mbona kwa binti kuolewa ni jambo la furaha sana?



    "ndoa ni maridhiano na nafsi kukunjuka juu ya hiyo ndoa kwa hiyo mwanangu mwanangu nafsi yake haikuridhia bali alikuwa amekubali kwa sababu ya pesa ya kunitibu,



    "Kweli unampenda mwanao hakika wewe ni mzazi bora angekuwa mzazi mwingine angekubali ili apone,





    Baada ya baba yao mdogo kuanguka chini Najima akiwa na yule jamaa aliyekuja na baba yao mdogo walianza kumpepea huku wakimfuta damu zilizokuwa zikimtoka,

    Shemsa alipoona hivyo alimshika mkono chirs akamsogeza pembeni alionesha kuna jambo alitaka kumweleza,



    "Chirs nakuomba utoke hapa kila kitu nitakikabili mimi hapa sawa? Nenda basi acha kushangaa,



    "shemsa kabla sijaenda naomba nikueleze kitu kimoja Nilicho nacho moyoni mwangu,



    "kitu gani tena chirs wakati tuko kwenye matatizo?.



    "sikia shemsa ni kwamba mimi nakupenda sana tena sana kwa hiyo nakuomba unielewe kwa hilo japo mimi ni masikini lakini ni tajiri wa moyo wa kukupenda wewe hapo,



    "sawa chirs nenda tutayaongea siku nyingine tukionana wewe nenda kwanza sawa chirs,



    Shemsa alimwambia chirs huku akimsukuma atoke pale alipo,



    "shemsa kwaheri ila nakupenda sana nielewe nifikilie sana shemsa usiangalie umasikini wangu, Mimi ni masikini ila tajiri wa pendo lako ukiwa na mimi utafaidi utajiri wa kupendwa,



    "sawa chirs nimekuelewa basi nenda, Nenda basi chirs kama unanipenda nielewe uondoke hapa,



    Chirs aliona isiwe tabu akaondoka huku akiwa hajapenda kabisa kumuacha pale shemsa ila ndivyo hivyo tena ilibidi atii amri ya shemsa ili kumuonesha kuwa anampenda na anamuheshimu,



    Huku upande wa pili ndani shemsa akiwa anawaza maneno ya chirs aliyomwambia mda mchache uliopita TOTO LA KIMANGA likajikuta linatoa chozi machoni mwake kwa kukumbuka maneno yale, *Shemsa nakupenda japo kuwa mimi ni masikini ila ni tajiri wa kukupenda wewe*

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    # kwanini chirs aseme kuwa yeye ni masikini ina maana aliona nitamkataa kwa umasikini wake? Hapana mimi shemsa siangalii pesa ila Nahitaji mwanaume mwenye penzi la ukweli na atakae nidhamini na kunijari mimi kwangu pesa sizipi uzito sana kwani unaweza kupata pesa ila ukakosa penzi la kukufariji na kujikuta unaingia kwenye penzi la majuto maisha yako yote ukakosa amani ukawa binaadamu wa kuliya tu,



    Shemsa akiwa Katika mawazo alishitushwa na kofi la shingo alipogeuka akakutana na kofi la shavuni,

    Aliyekuwa anampiga hakuwa mwingine alikuwa ni baba yake mdogo aliyezinduka kutoka nusu kifo kwani alikuwa amezimia,



    "yaani shemsa unanipiga mimi wewe ni kunipiga na ubao mpaka kuzimia kwa hiyo ulikusudia kuniuwa si ndio?



    Shemsa alizidi kuwa kimya huku akisikilizia maumivu ya makofi aliyopigwa moja la shingo na jingine shavuni,



    "sasa leo shemsa nitakupiga mpaka nihakikishe unashindwa kutembea,



    Shemsa akiwa hana hili wala lile alishituka yuko chini kwa kutokana na teke alilopigwa na baba yake mdogo akiwa bado chini alipigwa teke la mbavu lililopelekea shemsa apige kelele ya maumivu aliyoyasikia,



    ***** ***** *****

    Upande wa tatu kwa Mr john bosi wake na shemsa aliendelea kupanga namuona atavyompata mtoto wa kike shemsa aweze kuwa Katika himaya yake,



    "eehhee Mr john niambie mpango gani utakao ufanya ili umpate shemsa ili hali umesema mtoto wa kike hashitushwi na pesa wala vitu vya dhamani?



    "Nina mipango miwili na yote ni ya kimafia,

    Mpango wa kwanza ni wa kumteka na kumhifadhi kwenye nyumba nzuri alafu nikawa nambaka mpaka nihakikishe namtia mimba hapo hapo ujanja wake utakuwa umekwisha au unasemaje wewe kuhusu huo mpango?



    "duuhh hapo john nimekukubali huo mchongo upo juu kama ni reseni basi ni daraja C,



    John alikamilisha mpango wake na moja kwa moja akaanza kujipanga kuukamilisha mpango wake dhidi ya shemsa,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog