Search This Blog

Thursday, 19 May 2022

MY MOMY’S FRIEND - 4

 





    Chombezo : My Momy's Friend

    Sehemu Ya Nne (4)



    ILIPOISHIA

    Lilian alizungumza kwa sauti ya kufoka huku machozi yakimwagika na kulowanisha mashavu yake,Nikabaki nimemtizama na gafla nikaona vivuli vya watu wawili vikipita karibu na dirisha letu huku watu hao wakionekana wakiwa na bunduki na wananing’inia kwa kamba huku wakijiandaa kuingia kwenye dirisha letu ambalo ni dirisha la kioo.Nikaichomoa bastola yangu niliyo ichomeka kwenye soksi na kufyatua risasi mbili kuelekea kwenye kioo na kumfanya Lilian kuinama chini

    ENDELEA

    Ni kajirusha kutoka kitandani kwa utaalamu mkubwa huku bastola yangu ikiwa mkononi na kujibanza kwenye ukuta na nikaipandisha suruali yangu kwa haraka na kujiweka tayari kwa mashambulizi.Lilian akajificha kwenye ukuta mwengine na tukabaki tumetazamana huku tukiwasubiri watu wano taka kuingia kupitia dirasha waiingie

    “Eddy lala chini”

    Nikafanya kitendo nilicho ambiwa na risasi nyingi kutokea mlangoni zikapiga katika eneo nililo simama,Nikatambaa kwa haraka na kujibanza katika mlango wa kuingilia bafuni na kumuacha Lilian akiwa na kazi ya kufyatua risasi kuelekea katika mlango wa kutokea nje,Lilian akaja sehemu niliyo simama huku akiwa anahema na sote tukawa tunasubiria kupambana na watu wanao tushambuli na hatukujua ni wakina nani.Gafla moshi mkali ukaanza kutawala ndani ya chumba chetu na kwaharaka tukatambua ni bomu la machozi na sote tukaingia kwenye bafu na kukuta choo cha kukaa tukatazama kila upande hakuna sehemu ya kutokea

    “Eddy hakuna pa kutokea”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikumjibu Lilian zaidi ya kufungua mfuniko wa choo na kwa haraka nikaanza kukisogeza kikalio cha choo kwa kutumia nguvu hadi kikavunjika na kuacha shimo linaloweza kuturuhusu kupenya kwa wembamba tulio nao.

    “Inatubidi tupenye kwenye hili shimo”

    “Eddy......”

    “Hakuna jinsi”

    Japo kuna harufu kali ila sikuwa na jinsi ya kufanya nikatanguliaza miguu na kuanza kuporomoka kwenye bomba kubwa linalo pitisha kinyesi cha binadamu huku Lilian akifwatia kwa nyuma.Kutokana tupo gorofani kasi ya kushuka chini ni kubwa kiasi kwamba nikaanza kupata wasiwasi wa huku chini tunapo elekea na kutokana na giza sikuweza kuona ni wapi tutakapo angukia.Nikajikita migua yangu na kimono katika kuta za bomba ili kuweza kupunguza kasi ya kushuka chini.Nikazidi kujikaza katika kukita miguu yangu na mikono hadi ikafikia hatua nikasimama na Lilian akaja kusimama kwa miguu yake kuikanyaga mabega yangu

    “Eddy mbona umesimama?”

    “Chini sina uhakika kama ni salama”

    “Sasa tufanye nini?”

    “Kaa kama nilivyo kaa”

    Lilian akaipanua miguu yake na na mikono yake na sote tukabaki tukia katika mkao huo na chakumshukuru Mungu mazoezi yaliweza kutusaidia kwa kiasi kikubwa katika kukaa kwa muda mrefu japo miguu na mikono ilizidi kupata maumivu makali

    “Eddy”

    “Naam”

    “Nimechoka”

    “Jikaze Lilian”

    “Twende tuu chini”

    “Lili hatuwezi kujua kama chini tutaingia kwenye shimo la kinyesi au tutatokelezea sehemu gani”

    “Sasa itakuwaje?”

    “Tupande juu”

    “JUU....!!?

    “Ndio”

    “Eddy akili yako inafanya kazi kisawa sawa”

    “Ndio ila ninaona ni bora turudi juu kuliko kwenda chini inaweza ikawa ni hatari sana kwetu”

    “Na unataka tukatokelezee katika kile chumba?”

    “Ndio ninahisi jamaa watakuwa wameondoka”

    “Eddy siwezi kufanya hivyo kwani kurudi juu itahatarisha maisha yetu zaidi”

    “Niamini mimi”

    “Eddy”

    “Niamini”

    Tukaanza kurudi juu huku tukitumia nguvu nyingi kiasi kwamba ilitubidi mara kwa mara tuweze kupumzika japo harufu kali ya kinyesi ilizitesa pua zetu.Tukatumia muda wa zaidi ya lisaa kufika katika shimo la choo cha chumba tulichopo kisha Lilian akachungulia

    “Hakuna mtu”

    Lilian akatoka kwa tahadhari kubwa kisha na mimi nikatoka kwa uangalifu kisha nikachungulia kilipo chumbani na kukuta hakuna mtu wa aina yoyote zaidi ya vitu vilivyomo ndani ya chumba kuaribiwa kwa risasi nyingi.Miili yetu haikutamanika katika muonekano wetu kwani tulijaa vinyesi kuazia juu utosini hadi chini.Hakuna aliye weza kumsemesha mwezake zaidi ya sote kujisimamisha kwenye bomba la mvua na kuyaruhusu maji kushuka kwenye miili yetu.Nikazivua nguo zote na na kubaki kama nilivyo zaliwa nikajifunga shuka kama wafanyavyo kabila la kimasai kisha na Lilian akavaa nguo zake alizokuwa amezivua kipindi tunaingia ndani humu na kushukuru Mungu bastola yangu niliyokuwa nimeichomeka kiunoni inafanya kazi ila bastola zetu mbili zilipotelea kwenye shimo

    Harufu kali ya kinyesi haikusita kutuandama sote wawili,Nikachungulia katika mlango wa kutokea katika chumba chetu na kukuta kordo ya eneo hili ikiwa kimya na hapakuwa na dalili ya mtu kukatiza.Nikatoka huku nikiwa nimetangulia mbele na gafla mlango wa chumba kimoja ukafunguliwa akatoka bibi kizee na akabaki ananishangaa jinsi nilivyo vaa.Naikamnyooshea bastola na akaanza kutetemeka kwa ishara nikamuomba arudi ndani kwake na sote tukaingia ndani kwake na kumkuta mume wake akiwa amejilaza kitandani

    “Mukipiga kelele sinto sita kuwaua”

    Niliwaambia kwa lugha ya kiarabu ambayo ninaizungumza vizuri bila wasiwasi

    “Jamani munataka nini?”

    “Nahitaji nguo”

    “Hizo hapo mlangoni”

    Mzee alinionyesha nguo zake nikazishusha kabla sijazivaa Lilian akanifwata na kuanza kunipulizia pafyumu yenye haruu kali

    “Umeito wapi?”

    “Nmeikuta kweye kapochi cha huyo bibi pamoja ni hii funguo”

    Nikazivaa nguo za mzee wa watu ambazo ni suruali ya kitambaa na koti la suti huku likiwa na kofia yake nyeusi watu wengi tumezoea kuwaona watu wanao jiita COW BOYS wakizivaa.

    “Gari yenu ipo wapi?”

    Lilian aliwauliza kwa kutumia lugha ya kiarabu na wakatuelekeza sehemu lilipo kisha tukawaomba masamaha kwa usumbufu na kabla hatujatoka Lilian akajifunga mtandio wa bibi alio kuwa amejifunga kisha tukatoka ndani ya chumba huku tukiwa makini kila tunapoelekea.Tukawa na kazi ya kushuka kutumia ngazi na tulihofia kutimia lifti kwani hatukujua watu walio kuwa wakitushambulia wapo katika eneo la Hoteli au wamesha ondoka.Tukafika kwenye mlango wa kutokea tukachunguza kila kona ya eneo hilo na kuwakuta watu wakiendelea na shunguli zao kama hakuna tukio lolote lililo tokea.Tukapiga hatua za haraka hadi kweye eneo tulilo elekwezwa ilipo gari ya wazee wa watu na Lilian akaminya batani iliyopo kwenye kishikizo za funguo na tukaona gari moja likiwaka taa ikiashiria ndio gari linalo endana na funguo hizo

    Tukalisogelea na kukuta ni gari aina ya LAMBORGHIN LP 610-4 magari yanayotumiwa na askari wa nchini Italia na yameingizwa sokoni siku si nyingi na inavyo onyesha wazee hawa ni matajiri sana kwani kwa mtu wa kawaida ni vigumu kumilika gari la kifahari kama hili.Tukapanda ndani ya gari huku Lilian akiwa ni dereva akaliwasha na tukaanza kulifwata geti kuu la Hoteli na kabla hatujatoka Lilian akafunga breki za gari na tukabaki tukitazama gari za polisi ndogo zinazo ingia kwa kasi katika hoteli hii.Lilian akaanza kulirudisha gari nyuma kwa kasi kisha akafunga breki likageuka nakutazama sehemu tuliyo tokea.Akatia gia namba mbili na kukanyaga mafuta na gari lilaanza kwenda kwa kasi katika sehemu ya bustani ya maua na gari nne za polisi nazo zikawa nyuma yetu zikitufwata kwa kasi ya hali ya juu.

    Lilian akaanza kulipitisha gari katika sehemu iliyopangwa viti vya wateja na kuwafanya watu walipo kukimbia kuzipisha gari zetu kupita.Tukapata nafasi ya kutokea kwenye barabara kwa kutumia geti dogo lisilo tumiwa na watu katika kupitia na kwa uimari wa gari tulilo nalo tuliweza kuligonga geti hilo na likabomoka na ikawa rahisi kwetu kupita.Lilian akawa na kazi ya kuziongeza gia za gari hili na mwendo wa gari ukafika hadi kwenye spidi mita 280.Hichi ni kiwango cha juu kilichopo kwenye gari hili kiasi cha kuzipoteza gari za polisi.Gafla tukaanza kuuona mwanga mkali ukitumulika kutokea juu,Nikachungulia na kukuta ni Helcoptar ya polisi.

    “Waoooooo”

    Lilian alishangilia na kunifanya nimemshangae

    “Mbona unahangaa?”

    “Nakuona unashangilia wakati tupo kwenye hatari”

    “Usihofu nataka niwadhihirishie kuwa mimi ni dereva”

    “Huku tunapo elekea ni wapi?”

    “Kunaitwa KALABAGH BOAT YARD”

    Lilian akanijibu huku akikunja kona kali na kuifanya gari kuserereka na kuyumba kidogo kisha likakaa sawa na kuaanza kuifwata barabara inayoelekea kwenye sehemu inayo onyesha ni baharini kwani kwa mbali kuna boti nyingi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wee si ni baharini?”

    “Ndio wewe tulia Eddy tatizo lako ni nini?”

    Nikajifunga mkanda wa gari na kuikoki bastola yangu na nikavuta pumzi nyingi kisha nikazitoa kwa pamoja nikitumia pua kisha nikasubiria kitu anacho taka kukifanya Lilian.Risasi nyingi zikaanza kupiga barabarani kutoka kwa askari walipo kwenye Helkoptar na kumfanya Lilian kuanza kuliyumbisha yumbisha gari ili kuzikwepa risasi.Mbele yetu tukaona geti la nyaya ngumu na Lilian akalivaa na kuwafanya askari waliopo kwenye kibanda cha pembeni mwa geti hilo kuanza kutufyatua risasi.

    “Eddy fungua mkanda wa gari”

    “Kwa nini”

    “Gari naipekeka baharini wewe fungua mkanda”

    Nikafanya kama alivyo niambia na Lilian akaanza kunyosha nji inayo elekea baharini na ndani ya dakika kadhaa gari letu nikaingia ndani ya maji na kuanza kuzama taratibu kwenda chini.Nikafungu mlango na kutoka huku pumzi zangu nikiwa nimeziziba na nikaanza kuogelee kwenda juu na nikatokeza juu.Nikastuka baada ya kutokumuona Lilian akitokeza sehemu niliyopo,Nikavuta pumzi nyingi na kuzama tena ndani ya maji na kwamsaada wa taa za gari zinazo waka huku likielekee chini nikamuona Lilian akiomba msaada.Nikaanza kushuka kwa kasi hadi nikalifikia gari na kumkuta Lilian akiwa anajitahidi katika kuitoa nguo yake iliyonaswa kwenye mlango wa kutokea kwenye gari.Nikamsogelea na kumshika mdomoni na kumpulizia pumzi niliyo nayo kwani nilianza kumuona akilegea kwa kukosa pumzi kisha kwa kutumia nguvu nikaivuta nguo yake hadi ikachanika kisha sote tukaanza kurudi juu huku.Tukielekea eneo jengine tukiwa tumezama ndani ya maji ili hata kama polisi watapiga risasi katika eneo lilipo zama gari letu wasitupate

    Tukatokea kwenye moja ya boti iliyopo kwenye eneo hili huku tukihema sana kwani kwa kitendo cha kukaa ndani ya maji zaidi ya dakika kumi na tano sio kidogo.Helkoptar ya polisi ikawa na kazi ya kuzunguka katika eneo ambalo gari letu lilidumbukia.

    “Eddy asante”

    “Usijali”

    Nikapanda kwenye boti ambayo si kubwa kwa uangalifu na kuchunguza eneo la ndani na kuwakuta vijana wawili wakiwa wamezama kwenye dibwi kubwa la mapenzi.Sikutaka kuwastua nikatoka na kumstua Lilian kwa ishara na yeye akapanda kwenye boti kisha tukaingia ndani ya chumba walichopo vijana hao na kuwafanya wastuke

    “Ohhhhh musituue”

    Jamaa wa kiume alizungumza kwa kiarabu huku akitetemeka

    “Sisi sio wauaji ila tunahitaji funguo ya hii boti”

    “Ni...ni nayoo?”

    Jamaa akanirushi funguo na nikapita hadi sehemu ya kuendeshea na kabla sijaiwasha kwakupitia kioo cha mbele cha boti nikaona boti za polisi zikikagua boti moja baada ya nyingine huku wakiwatoa watu waliomo ndani ya boti hizo.Nikasikia ukulele mkali nyuma yangu na nikageuka haraka na kumkuta Lilian akiinama chini akiokota bastola huku msichana tuliye mkuta ndani ya boti akiwa ameanguka chini akilia kwa maumivu makali

    “Vipi Lily?”

    “Ni huyu chiki ananitishia bastola”

    “Ina risasi?”

    “Ndio”

    “Eneo zima tumezingirwa”

    “Weee”

    “Ndio njoo uone”

    Tulizungumza Kiswahili ili kuwafanya vijana hawa kuto kuelewa tunacho kizungumza,Lilian akasogea hadi katika eneo nililopo na kuzishuhudia boti za polisi zikiendelea na kazi ya kututafuta.Gafla kijana wa kiume akaanza kukimbia kutoka nje ya boti huku akipiga kelele za kuomba msada.Nikampokonya bastola Lilian na kumpa funguo kisha nikapiga hatua za haraka na kumuwahi kijana huyo na nikamkuta amesimama nje ya chumba cha boti akipunga mikono juu akiomba msaada na kuwafanya askari wenye boti kuanza kuja eneo tulilopo kwa kasi huku mwanga mkali wa Helcoptra ukitumulika sehemu tuliyo simama



    Nikampiga kabala kwa nyuma huku bastola nikimuwekea kwenye kichwa chake na sikuwa na masihara hata kidogo,Nikamuamrisha kunyoosha mikono yake juu jambo lililowafanya askari kushindwa kufanya kitu cha aina yoyote.Askari kwa kutumia kipaza sauti wakaniomba nijisalimeishe na niweke silaha yangu chini na mimi nikapaza suati huku nikizungumza lugha ya kiarabu

    “MUKIJARIBU KUFANYA KITU CHOCHOTE CHA KIJINGA TUTAWAUA HAWA VIJANA”

    Kauli yangu ikawafanya askari kukaa makini huku bunduki zao wakiwa wametuelekezea sisi,Helcoptar ya polisi ikazidi kutumulika kwa mwanga wake mkali,Nikstukia boti ikiwaka na kuondoka kwa kasi na kutufanya tunyumbe kidogo na kuanguka chini kitendo kilichosababisha polisi kuanza kufyatua risasi zilizopiga pembezoni mwa boti na nikamvuta kijana hadi ndani na kumkuta Lilian akijitahidi kuzikwepa boti za polisi zilizo tuzunguka.Nikamsukuma kijan kwa hasira na akakaa kwenye sofa huku akilia kwa uchugu

    “UNATULETEA UJINGA SISI SI NDIO”

    Nilizungumza huku bastola yangu nikiwanyooshea hao vijana wawili na sikuweza kusikia milio ya risasi kwa nje

    “Kaka nisamehee”

    “Funga bakuli lako ku** wewe unadhani ninamchezo”

    Nikaikoki bastola yangu na kabla sijafyatua risasi kijana akanipigia magoti huku mikono yake ikiwa imeshika mguu wangu mmoja

    “Kaka seme chochote ila usiniue baba yangu atakupa kiasi chochote cha pesa utakacho kihitaji”

    “Sina haja ya pesa za baba yako ila kwa kitendo ulicho kifanya nilazima nikuue”

    “Hapana Hapana Hapana kaka nakuomba usiniue......Mimi baba yangu ni Raisi sema chochote atakupatia”

    Nikamtazama Lilian na yeye akanigeukia na akatingisa kichwa akiashiria nimuache kijana na nisimfanye chochote kitakacho mdhuru,Simu iliyojengewa ukutani ikaita kwa mlio mkali,nikaitazama kwa muda kisha nikaichomo akwenye sehemu ilipo chomekwa kisha nikaipokea

    “Wewe ni mshenzi gani uliye mteka mwanangu?”

    Sauti ya kizee ilizungumza kwa ukali huku mzungumzaji akionekana kuwa na wasiwasi mwingi

    “Wewe ni nani?”

    “Mimi unaniuliza ni nani......Pumbavu wewe mimi ni raisi wana nchi yako”

    “Ahaaa Raisi.....Nikusaidie nini Mr President?”

    “Pumbavu wewe mrudishe mwanangu”

    “Waooo mwanao hatoweza kurudi sasa hivi labda uwazuie hao askari wako wasiendelee kutufwata”

    Nilizungumza kwa dharau kiasi kwamba nikazidi kumpandisha hasira Raisi wa nchi na kwangu sikuwahi kutegemea kama itatokea siku nitakuja kuzungumza na Raisi wa nchi ya Pakistani

    “Nataka kuzungumza na mwangu......”

    Nikamuwekea jamaa simu masikiioni na akaanza kuzungumza huku akilia kwa uchungu

    “Baba baba fanya lolote uniokoe baba”

    “Kuwa mpole mawangu nitakuokoa”

    Nikaitoa simu sikioni mwa kijana na kuirudisha sikioni kwangu taratibu na nikajikoholesha kidogo kisha nikazungumza kwa sauti ya upole

    “Muhesimiwa Raisi nakuomba ufanye kitu kimoja....Mimi nitamuua mwanao endapo tuu utakiuka haya nitakayo yahitaji kwa sasa.Kwanza zuia askari wako wasitufwatilie tunapo kwenda.....Mbili maongezi yako na yangu yasiunganishwe kwenye mtandao wa taifa.....Tatu nikihitaji chochote kwa muda wowote unipatie la sivyo ninakwenda kumuua mwanao na damu yake itakuwa mikononi mwako na familia yako”

    “Shiiit”

    Simu ikakatwa na nikairudisha katika kishikizo cheka na kuchungulia kwenye kioo cha nyuma na sikuona boti yoyote ikitufwata wala Helcoptar ya polisi

    “Lily umechoka?”

    Nilizungumza Kiswahili na kuwafanya vijana wabaki wakitutizama wasijue tunacho zungumza ni nini

    “Hapana nipo powa”

    “Saa ngapi saa hizi?”

    “Kumi kasoro usiku”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Boti inamafuta yakutosha?”

    “Mmmmm yanatosha kwa mwendo tunao kwenda nao......Eddy njoo uendeshe kuna kitu nahitaji kukifanya”

    Nikasimama sehemu ya kuendeshea na Liliana akafungua kwenye moja ya kikabati kidogo kilichopo ndani ya boti na kuanza kuchangua changua vitu kisha akatoa kisu na akafungua sehemu ya juu ya boti na nikaona nyaya nyingi zilizopo kwenye shemu hiyo kisha akaanza kuzichambua moja baada ya nyingine huku baadhi akiaanza kuzikata kisha akapafunika kama palivyo kuwa

    “Ulikuwa unafanya nini?”

    “Nilikata mawasiliano ya rada kwani wakikaa kwenye mitambo yao wanatuona tunapo elekea ila kwa sasa hawata weza kutuona”

    “Vizuri”

    Lilian akapiga hatua hadi alipo kijana wa kiume na kuchuchumaa taratibu na akamshika kidevu na kuzungumza naye na lugha ya kiarabu

    “Kijana unaitwa nani?”

    “SEIF KHAN AL-BASHIR”

    “Eddy hawa jamaa wana majina marefu mmmm...Kama mzizi wa bangi”

    Nikabaki nikicheka na kuendelea kuendesha boti hii ambayo inakwenda kwa mwendo wa kasi sana

    “Seif ni wapi ilipo contor system ya hii boti?’

    Lilian alizungumza kwa sauti ya upole huku akiendelea kukishika shika kidevu cha mtoto wa Raisi

    “Sijui mimi”

    “Ohhh hujui?’

    “Ndio dada”

    Nikastukia kusikia kibao kikitua kwenye mwili wa mtu nikageuka na kumkuta binti akiwa amejikunja huku akilia na Lilian akawa na kazi ya kukichezesha kiganja chake akikipoza kutokana na kibao kizito alichompiga msichana wa watu

    “Iko wapi?”

    “Sijui dada yangu”

    Lilian akazishika nywele msichana kwa nguvu na kabla hajampiga kichwa jamaa akamzuia huku akimuomba asifanye hivyo

    “Usimpige iko pale kwanye ukuta fungua kwenye hiyo picha hapo utaona utaiona”

    Lilian akanyanyuka na kuitoa picha kubwa iliyobandikwa ukutani kisha akakuta mlango wa chuma na pembeni yake kuna batani zenye namba

    “Dogo namba ya siri hapa ni ngapi ngapi?”

    “18...23....999”

    Lilian akaminya namba alizoambiwa na sehemu hiyo ikafunguka na taratibu kukatoka kifaa ambacho hadi Lilian alipo kifungua ndipo nikagundua ni Laptop.Akaiwasha na akaanza kuminya minya baadhi yabatani sikujua anaminya nini kisha akamgeukia Seif na kumita.Akakichukua kidole gumba cha mkono wa kshoto wa Seif na kukikandamiza kwenye sehemu iliyopo pembeni ya Laptop hiyo kisha akamruhusu kurudi kwenye sofa

    “Lily unafanya nini hapo?”

    “Kuna mawasiliano ambayo ninayatafuta?”

    “Mawasiliano ya wapi?”

    “Yes i got it”(Ndi nimeyapata)

    Lilian alizungumza huku akifaurahi na akaendelea kuminya baadhi ya batani na nikaanza kusikia sauti za watu wakizungumza kutokea kwenye spika za laptop hiyo

    “Eddy njoo uone”

    “Nitakujaje wakati hapa ninaendesha hii boti”

    “Izime”

    Nikapunguza mwendo wa boti kisha nikaizima na kwenda alipo simama Lilian na kuona video inayowaonyesha viongozi wa serikali wakiwa kwenye moja ya ukumbi wakijadiliana

    “Ni viongozi wa wapi hao?”

    “Wa Pakistani....Huyu hapa ndio Raisi uliyetoka kuzungumza naye muda mfupi ulio pita”

    Tukaa kimya huku tukisikiliza mipango wanayo ipanga juu ya kumuokoa mtoto wake

    “Tumewapoteza kwenye rada na mara ya mwisho walikuwa wakielekea Magharibi Kaskazini ambapo ukitoka Karachi Magharibi Kaskazini yeetu ni Iran”

    Mzee mmoja aliye valia nguo za jeshi zenye vyeo vingi aliwaelekeza wezake kupitia kioo kikubwa kinachofunika ukuta wote wa eneo walilopo

    “Lily umeyanasa vipi haya mazungumzo?”

    “Eddy hivi vitu havinisumbui sana na hapo unapo waona wanatutafuta na nilikata nyaya za rada na Satelait haziwezi kutukamata na hakuna Rada ya nchi yoyote itakayoweza kutunasa”

    “Mmmm kweli wewe ni mtaalamu...”

    “Sir Unaturuhusu kwenda kupeleka vijana katika bahari ili kuwasaka kwa udi na uvumba hawa watekaji?”

    Kiongozi mwengine ambaye sikujua ni askaria au laa hii ni kutokana na uvaaji wake wa suti nyeusi ambayo ni vigumu kujua shughuli anayo ifanya alimuuliza raisi na kumfanya akae kimya kwa muda.Lilian akaminya moja ya batani na kusababisha sura yake kuonekana kwenye kioo kilichopo kwenye ukumbi walipo viongozi

    “NISIKILIZENI KWA UMAKINI”

    Suati ya Lilian ikawastua viongozi wote na kuwafanya wakigeukie kioo hicho na wakakaa kimya wakimsikiliza Lilian

    “SISI SIO WATEKAJI WALA MAHARAMIA....ILA MUSIHITAJI VIJANA WENU KUINGIA KWENYE MATATIZO MUSIYO YATARAJIA......ENDAPO MUTASUBUTU KAFANYA MUNACHO KIPANGA MUTAWAPOTEZA VIJANA WENU”

    “Binti munahitaji nini ili mumuachie mwanangu?”

    “Muheshimiwa Raisi tunacho kihitaji sisi ni kuwa Salama katika safari yetu”

    “Mwanangu je?”

    “Mwanao......Nitakujulisha ni wapi uje kumchukua ila kwa masharti mawili tu”

    “Tunakusikiliza”

    “Tutawapigia simu na kuwaambia ni wapi mtoto wako na msichana wake walipo....Mbili tunahitaji kiasi cha milioni 200 za kimarekani la sivyo futa mawazo kama ulikuwa na mtoto wa kiume katika maisha yako”

    Nikawashuhudia viongozi kadhaa wakishika vichwa wakionekana kuchanganyikiwa kiasi kwamba wengingine machozi yakianza kuwalenga lenga

    “Milioni 200 za kimarekani ni nyingi sana hizo na inakariia bajeti ya serikali”

    Raisi alizungumza huku machozi yakimwagika na msaidizi wake akawa na kazi ya kumfuta

    “Ooooh ni nyingi basi tufanye hivi nahitaji kisima kimoja cha nyuklia na muwakabishi AL-Kaiida ndani ya masaa 12 kuanzia sasa”

    Viongozi wote wakashika vichwa na wakazidi kupagawa kwani katika swala zima kisima cha nyuklia ambazo ni silaha tishio duniani zitazidi kulipa ndugu kundi la AL-KAIDA katika ufanyaji wake wa kazi

    “Ohhh tutakupa hiyo milioni 200 ya kimarekanni munayo ihitaji ila kwa kisima tunakuomba utusamehe”

    “Sawa ila nimebadilisha mawazo sio milioni 200 tena nahitaji 500 milioni za kimarekani,Sihitaji swali”

    Viongozi wakakaa kimya na sura ya Lilian ikapotea kwenye kioo chao na tukabaki tukiwatazama kiasi kwamba ukimya ulitawala ndani ya ukumbi wao wa mikutano

    “Eddy kwa hii dili tuakwenda kuwa matajiri”

    “Tumuombe Mungu itiki”

    “Hapo sio kumuomba Mungu kwani Mungu sidhani anaweza kusaidia watu tulio poteza roho za huruma kama sisi”

    “Ok nini tunafanya sasa?”

    “Hawa mawazo yao wanajua sisi tunaelekea Iran ila nimepata wazo?”

    “Wazo gani?”

    “Tupige mwendo hadi Muscat kwani kutoka hapa tulipo Muscat ipo Kasini Magharibi”

    “Sio mbali lakini?”

    “Nimbali kidogo”

    “Mafuta yatatosha kwenli”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tutajua mbele ya safari”

    Lilian akarudi kwenye kiendesheo cha boti hii ambayo kwa muonekano wake ni boti ya kifahari sana kwani muundo wake na vifaa vyake vipo tofauti sana na boti nyingine nilizo zoea kuziona.Safari ikaaendelea huku mwanga ukizidi kutawala kwenye anga ikiashiria kunapambazuka.Kwa mbali tukaanza kuona mji mzuri na wakuvutia

    “Liliy pale ni wapi?”

    “Ndio Muscat hii nchi tunayo iendea inaitwa United Emirates(Umoja wa nchi za kiarabu)”

    “Ahhh ndio Oman huku?’

    “Hujakosea”

    “Nilikuwa ninapasikia pasikia”

    Ukimya ukatawala ndani ya boti na gafla Lilian akasimamisha boti na ikanilazimu nichunguli kwenye kioo nikaziona boti mbili zikija kwa kasi huku zikiwasha ving’ora na nikajua ni polisi wa majini

    “Tunafanyaje?”

    “Wewe tulia nitamalizana nao?”

    Lilian alizungumza huku akianza kuvua nguo moja baada ya nyingine na akabakiwa na chupi na sidiria,Akamtazama Seif kwa sekunde kadhaa kisha akamyooshea mkono

    “Nipe pesa yote uliyo nayo”

    “Seif akatoa kiasi chote chapa pesa na sikujua ni kiasi gani kwani sikuweza kukihesabu,Lilian akaziweka vizuri nywele zake kisha akaniomba nisitoka ndani ya boti na nikawafunika Seif na mchumba wake blangeti kubwa na kuwapa onyo endapo watajaribu kuleta fujo nitawaua.Liliana akatoka na kusimama kwenye ukingo wa boti na kuanza kuzungumaza na askari ambao wameizunguka boti yetu kwa kutumia lugha ya kingereza

    “Wewe ni nani?”

    “Mimi ni mtalii ninatokea Iran nimekuja Muscat kupumzika”

    “Tunaomba hati yako ya kusafiria”

    “Ohh jamani niliisahau kwa kuwa niliona ninatumia usafiri wangu binafsi”

    “Ila si unatambu kila nchi inautaratibu wake?”

    “Ndio ninatambua ila jamani ninawaomba munisamehe”

    “Kwa hilo hatuwezi kukusamehe kabisa na pandeni mukaikague boti”

    Askari amabeye ni mkuu nilisikia akiwaamrisha wezana na kunifanya bastola yangu kuikoki vizuri huku nikiwa tayari kwa lolote litakalo jitokeza huku nikiwa nimejibanza kwenye kochi

    “Subirini jamani kwani munashindwa kuniamini mimi?”

    “Hamuaminiki nyinyi hembu pandeni mukaka...”

    “Ohh jamani hembu nitazameni vizuri kuanzi chini hadi juu kweli ninaweza kufanya chochote kibaya....Kwanza mimi bado mdogo..Ngozi yangu bado laini....mmm leo mkuu nataka nikupe kitu roho inataka”

    Askari wengine wakajisahau kama wapo kazini baada ya kuyasikia maneno ya Lilian wakaanza kushangilia huku wakimshabikia mkuu wao aweze kukubali ofa aliyopewa na Lilian

    “Sawa sawa nimekuelewa....Utafikizia Hoteli gani?”

    “Nichagulie wewe mpenzi”

    “Ohhh basi chukua hii ni kadi yangu ina namba za simu na ukifika kweye hoteli yoyote chukua chumba kwa jina langu pesa itakatwa kwenye akaunti yangu”

    “Asante je unapenda leo nikukalie mikao gani ukiwa unanishuhulikia kitandani.....?”

    Maneno ya Lilian yakazidi kuwachanganya maaskari hususani kiongozi wao na nikawasikia wakijichekesha chekesha kiasi kwamba nikabaki nikijisemeo kimoyo moyo laiti wangejua wasinge furahi kijinga kiasi hichi

    “Yoyote mtoto mzuri”

    “Panda hapa juu”

    Askari mkuu akapanda alipo Lilian na akavutwa na kuanza kunyonywa mate na Lilian na kuwafanya askari wazidishe kelele za kushangilia.Askari mkuu akataka aingie ndani na Lilian ila Lilian akamzuia

    “Utafaidi usiku mzima wala usiwe na wasiwasi”

    “Kidogo tuu”

    “Ohhh badae utafaidi usijali mpenzi leo mimi ni chakula chako cha usiku mzima”

    Mkuu wa askari anaonekana kuchanganyikiwa na kitendo alicho fanyiwa na Lilian,Nikamsuhudia akishuka kwenye boti yetu huku suruali yake akiiweka weka vizuri sehemu ya mbela na akapanda kwenye boti aliyo jia nayo katika eneo hili

    “Mrembo mbona boti yako kwa hapo ulipo simama imetoboka inavyoonekana ni matobo ya risasi”

    “Ndio kuna siku maharamia walitaka kuiteka baoti yangu ila namshukuru Mungu niliwakimbia”

    “Pole sana mrembo”

    “Asante....”

    “Ngoja basi niondoke nikaendelee na mishuhuliko mingine ila usisahau kunipigia”

    “Sawa nakupenda Mwaaaaaa”

    “Nakupenda pia”

    Askari wakaondoka na boti zao na Lilian akarudi ndani huku akijifuta futa mdomo wake akavaa nguo zake na kuiwasha boti na tukaendelea na safari tukielekea ufukweni,Tukaisimamisha boti yetu kwenye sehemu maalumu kisha Lilian akamshika mtoto wa Raisi kiuno na kwajinsi walivyo endana mtu unaweza ukasema ni wapenzi.Mimi nikamshika mkono msichana japo alianza kugoma goma ila nilipo muonyesha bastola akatulia.Tukaanza kutembea kwenye fukwe ya bahari tukielekea baharini huku mtoto wa raisi akiwa ameibeba Laptop iliyokuwepo kwenye boti na baada ya muda tukafika kweye barabara na kukodi Taksi

    Mimi,Seif na msichana wake tukakaa siti ya nyuma huku Lilian akikaa siti ya mbele,Akamuomba dereva atupeleke hadi kwenye mtaa mmoja amabao jina lake sikuweza kulikariri haraka haraka.Tukashuka na kuingia kwenye gorofa moja na kukuta watu wengi wakiwa na Silaha mikononi na baada ya kumuona Lilian wakazihusha silaha zao chini

    “Ohhh Lilian mdogo wangu hujambo?”

    Alitokea jamaa mwenye ndevu nyingi na akamakumbatia Lilian huku akionekana kuwa na furaha sana

    “Sijambo kaka aisee umebadilika na hizo ndevu?”

    “Mdogo wangu majukumu mengi haya niambie za wapi kwa maana nikikuona wewe basi nijue kuna tatizo?”

    “Wala hujakosea kaka yangu nahitaji msaada wako tena wa hali na mali?”

    “Ehee twende ofisini kwangu?”

    “Kabla hatujaenda ngoja nikutambulieshe kwanza?”

    “Sawa”

    “Huyu hapa anaitwa Eddy na mshiriki wangu mpya katika harakati za kutafuta maisha.....Na hawa wawili ni vitega uchumi vitakavyo tupatia maisha mazuri”

    “Hahaaaa Lilian mdogo wangu hujaacha tuu masihara yako?”

    “Kaka mimi sikutanii ila huyu ni mtoto wa Raisi wa Pakistani”

    “Duuu Bingo hiyo”

    Nikampa mkono jamaa na akanitingisha kwa kunipima nguvu na ukakamavu wangu ila nikamshinda kwa nguvu kwani mazoezi yalinisaidia sana katika kuimarisha misuli yangu na jamaa akanivuta na tukatazamana usoni huku kila mmoja akimtolea mwenzake jicho na baada ya muda jamaa akatabasamu na kuniachia mkono wangu

    “Eddy huyu kaka yangu anaitwa Patrick ni mtoto wa baba yangu mdogo”

    “Nashukuru kukufahamu”

    Tukaingia kwenye lifti huku Sief na mchumba wake wakiwekwa chini ya ulinzi mkali wa jamaa tulio wakuta na wakaingizwa kwenye chumaba kimoja ambacho madirisha yake yote yananondo na nivigumu sana kwa wao kujaribu kutoroka na isitoshe chumba kipo gorofani.Tukaingi kwenye moja ya ofisi na jamaa akatukaribisha vinywaji na na tukaanza kunywa taratibu huku yeye na Lilian wakipiga stori wakikumbushana maisha yao ya nyuma.Lilian akaifungua Laptop na kuanza kuminya batani anazo zijua yeye mwenyewe kisha akapata mawasiliano ya moja kwa moja kutoka ikulu na safati hii akawa anazungumza na Raisi akiwa ofisini kwake

    “Mwano yupo katika hali salama muheshimiwa raisi ila makubaliano yetu nahitaji yaweze kukamilika ndani ya masaa 24 kuanzia sasa”

    “Sasa hizo pesa tutawaleteaje?”

    “Kuna namba ya benki nitawatumia na nitahitaji muzitume asilimia 80 ya hizo pesa na asilimia 20 ya pesa naziitaji kwa makabadhiano ya mkono kwa mkono”

    “Mupo wapi sasa?”

    “Sinto kuambia ila nitakuambia ni wapi muniletee hizo pesa.Bye”

    Lilian akakata mawasilano na kukimalizia kinywaji chake kilichopo ndani ya glasi kisha akashusha pumzi kidogo na kumgeukia kaka yeke

    “Kaka mbona kama una mawazo hivi?”

    “Kuna shangingi moja limenitapeli pesa yangu na hapanafikiria jinsi ya kulisaka”

    “Kiasi gani cha pesa”

    “Nilimpa dola milioni 10 kwa kuiendeleza kampuni yake ila hadi sasa hivi ninaona kimya hajanilipa”

    “Ila kaka na wewe hujaacha tabia ya kuwa na wasichana...Hembu tafuta mwanmke wa kuona na sisi siku tuje kuitwa mashangazi”

    “Bado bado kwanza”

    “Huyo shangingi mwenyewe yupo wapi?”

    “Sijajua hata yupo wapi ila nilikutana naye Malyesi akiwa na mwanaye na tukakubaliana mwanaye akipona mguu basi aniozeshe mtoto wake”

    “Kaka umekuwa mzembe kiasi gani hadi ukadanganyika kiasi hicho?”

    “Lily sio uzembe ila kusema la ukweli mtoto wake ni mzuri na nimuafrika....Yaani katika maisha yangu sikutarajia kama ipo siku nitakutana na binti mzuri kama yeye”

    Lilian akaanza kucheka hadi machozi yakaanza kumwagika

    “Unacheka nini sasa?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nakucheka na hiyo mindevu yako unavyo zungumza Eti msichan mzuri sana sijuii nini?.Kaka nakuonea huruma,Sasa wewe unajua ni nchi gani ya Afrika walipo tokea”

    “Ndio waliniambia wanatokea Kenya”

    “Na hiyo kampuni iliyo endelezwa kwa pesa zako inaitwaje?”

    “Kwenye kampuni hapo kidogo nilipotea wala sikuaka kumuhoji sana mawazo yangu yalikuwa ni kumpata yule msichana”

    “Duuu hii kali kaka yaani kumbe na ujanja wote huo umekamatika kwa Mkenya mmoja”

    “Mtoto kaumbika ile mbaya ninavyo kuambia kaumbika sio masihara...Ngoja nikuonyeshe picha zake”

    Jama akaminya minya batani za kumoyuta yake kisha akaigeuzia tulipo na moyo wangu ukanipasuka kiasi kwamba kajasho kakaanza kunitoka.Sura ya Caro na Mama yeke ndizo zilizopo kwnye kioo cha kumpyuta hiyo na kumbukumbu zangu zikanikumbusha siku Mama Caro alipo pigiwa simu kwenda Malyesia kumchukua Caro alipo pata ajali ndio wakakutana na Patrick niliyopo naye

    “ILA SIKU NIKIJA KUMTIA MIKONONI HUYU MAMA ATANITAMBUA NA NITAFIDIA KWA KUWACHUKUA MTU NA MAMA YAKE NA WOTE WATAKUWA WAKE ZANGU”



    Nikabaki nikiwatazama pasipo kuonyesha hali yoyote kama ya kuweza kuwafahamu Caro na Mama yake ambao kwangu ni miongoni mwa watu walio nisaidia maishani mwangu isitoshe nimeshaanza kujenga chuki dhidi yao hii ni baada ya Priscar kunieleza ukweli wote kuhusu wao.

    “Eddy unaweza kuwafahamu hawa watu?”

    “Lilian katika maisha yangu sijawahi kuwaona watu kama hao ndio kwanza ninawasikia hapa”

    “Kaka mimi kwenye hili nitakusaidia na wewe pia nitahitaji unisaidie katika kuzipata pesa kutoka serikali ya Pakistani”

    “Wewe kwenye hili utanisaidiaje saidiaje?”

    “Mimi Kenya ninaijua vilivyo kwahiyo swala la kuwapata hao watu kwangu litakuwa ni dogo sana”

    “Ndio maana Lliy ninakupenda kwani wewe upo makini sana na unapenda kujitolea sana katika kunisaidia katika ishu zangu”

    Wakaendelea kupanga jinsi ya kuwapata mama Caro na Caro huku kichwani mwangu na mimi nikianza kupanga mipango ya jinsi gani ninaweza kuwasaidia japo moyo wangu unapinga na akili yangu katika maamuzi ya kuwasaidia.Tukabadilisha nguo na kutoka na Lilian huku tukitumia gari la kaka yake na kufika kwenye moja ya Hoteli kubwa ya kitali na kuchukua chumba kimoja chenye hadhi huku akitumia kadi ya polisi ambaye alimpatia masaa machache yaliyo pita katika kulipia chumba.

    Tukaagizia chakula na kikaletwa na muhudumu ndani ya chumba tulicho fikizia na tukuanza kula taratibu huku tukiwa kimya na kichwa changu kikawa na mawazo ya jinsi gani ninaweza nikarudi Tanzania pasipo serikali ya Tanzania kunikamata kwa makosa ya uvanmizi wa duka kubwa la kibiashara nchini Kenya kwani hadi sasa hivi ninahesabiwa kama gaidi.

    “Eddy unanishauri nimpigie yule askari kwanza aje au tufanye kwanza?”

    “Tufanye nini?”

    Lilian akanyanyuka kwenye kiti chake alicho kikalia na kunilalia kwenye mapaja yangu na tukaanza kunyonyana midomo yetu huku Lilian akionekana kuwa na hamu kubwa ya kufanya mapenzi na mimi.Nikaishusha suruali yake aina ya jeans aliyo ivaa na mkono wangu mmoja ukaingia kwenye ikulu yake na kuanza kuichezea taratibu na kumfanya azidi kupagawa na kuzidisha kasi ya kuninyonya lipsi zangu ambazo ni kivutio kwa wanawake wengi na ninakumbuka kipindi nipo shule ya msingi watu walikuwa wakinitania kwa jina la Malipsi

    Lilian akaanza kufungua vifungo vya shati langu na kuanza kuzichezea nywele nyingi zilizomo kwenye kifua changu ambacho kimejengeka vizuri kwa mazoezi mazito niliyokuwa nikiyafanya nchini Pakistani.Lilian akazidisha uchokozi wa kuendelea kunyonya viziwa vyangu vya kifuani na mimi nikamvua tisheti yake na akabakiwa na sidiria kisha nakayabananisha maziwa yake kwa pamoja na kuanza kuyatomasa taratibu taratibu,Nikamvua mikanda ya sidiria na kuitupa pembeni kisha taratibu nikaanza kuzinyonya chuchu zake zilizo laini na nikamnyanyua na kumuweka kitandani huku kila mmoja akijitahidi kushika viungo vya mwenzake ili kufurahishana zaidi katika kipindi hichi ambacho tunamatatizo.Lilian akanivua suruali yangu na mimi nikaimalizia ya kwake na taratibu akaanza kuichua koki yangu huku akiipaka paka mate na akaizamaisha mdomoni mwake na kuanza kuinyonya taratibu

    Nikaipanua miguu yake na mimi nikaanza kuinyonya ikulu yake ambayo inamuonekano mzuri wa kuvutia.Ikawa ni kazi ya kunyonyana kiasi kwamba kila mmoja akazidi kuonyesha utaalamu wake katika kazi hiyo.Nikamgeuza na kupanua miguu yake na kazi ikaanza huku kila mmoja akiianza kwa kasi ya ajabu.Lilian akazidi kutoa kelele za raha huku mara kwa mara akibadili lugha za kuzungumza hadi baadhi ya maneno nikawa siyaelewi ameyatolea wapi.Mechi ikazidi kuwa kali kiasi kwamba nikazidi kutumia ujuzi wangu wote katika kumpagawisha Lilian ambeya kwa uzuri amejaaliwa japo ni mwembamba na hama maungo makubwa kama walivyo wanawake wa Kiafrika

    Mechi ikaisha hulu Lilian akionekana kuridhika hata nilipo muomba kuendelea akakataa.Tukaingia bafuni na kuoga na kuzivaa nguo zetu kisha akaichuka simu iliyupo ndani ya chumba hichi na kupiga namba za simu zilizopo nyuma ya kadi aliyo pewa na Mkuu wa askari.Akamuelekeza askari aliye kutana naye na akaahadi atafika sehemu tulitopo baada ya dakika ishirini.Kila mtu akaiweka bastola yeke vizuri huku zote tukiwa tumezifunga viwambo vya kuzuia sauti na hivi husaidia pale unapofyatua risasi kuto kuweza kusikika na watu hata walio karibu.Baada ya dakika ishirini mlango ukagongwa na mimi nikaenda kusimama nyuma ya mlango na Liliana alasimama mlangoni na kufungua huku bastola yake akiwa ameichomeka kwenye suruali na kuifunika na tisheti

    “Ohh mpenzi wangu karibu ndani”

    “Asante binti mzuri....Umependeza sana”

    “Asante”

    Jamaa akaingia ndani na mimi nikamuwekea bastola kwenye kisogo cha kichwa chake na kumuomba aweze kutulia kama alivyo la sivyo nitaweza kikifumumua kwichwa chake.Lilian akanza kumkagua askari huyo aliye anza kutetemeka na kuchukua bastola zake mbili na kisu chake kisha nikamuamuru kukaa kwenye kiti kilichopo ndani ya chumba hichi

    “Binti ni nini unafanya?”

    “Tulia na fanya kila nitakacho kihitaji wewe ukifanye”

    “Ha...haya sio makubaliano yetu lakini?”

    “Ndio hivyo inakulazimu kukubaliana na mimi kwa kila nitakacho kumrisha la sivyo nitakuua?”

    Macho ya askari yakanitazama kwa umakini na mimi nikaanza kumchunguza kwa umakini kuanzia kichwani hadi miguuni na nikagundua anakitu alicho kificha kwenye bega leke la kushoto.Nikaichomeka bastola yangu kwenye kiuno na kuchukua kisu cha jamaa na kulichana shati lake na kukuta amejifunga kifaa maalumu cha kunasia sauti ambacho ninavyohisi kinapeleka moja kwa moja mawasiliano katika makao makuu yake polisi aliyo toka.Nikakichomoa na kukivunja kisha nikaanza kumkagua sehemu moja hadi nyingine na nikamvua viatu vyake na kukuta vimevungwa kamera ndogo ambayo inaweza kuchukua video kwa eneo kubwa

    “Ametusaliti”

    Nilizungumza kwa Kiswahili na kumfanya Lilian kunielewa vizuri na tukaanza kusikia ving’ora vya magari ya pili vikisimama kwenye hoteli hii.Nikachungulia chini nikaona askari wengi wakishuka kwenye magari yao

    “Kaka ninahitaki msaada wako sasa hivi”

    Lilian alizungumza kupita simu ya mezani kisha nikampiga kabali kwa nyuma mkuu wa polisi na kumnyanyua kwenye kiti kisha nikamuwekea bastola yangu mgongoni na tukatoka kwenye chumba.Tukaanza kupiga hatua za keelekea nje huku tukiwa makini kupita maelezo

    “Waamrishe askari wako wasifanye chochote cha kijinga la sivyo tunakuua”

    “Saa....awaa”

    Tukafika nje na askari wengi wakiwa wamejificha kwenye magari yao huku bunduki zao wakiwa wametuelekezea sisi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “MUSIFAFYATUE RISASI WAACHENI WAPITE”

    Mkuu wa polisi alizungumza huku nikiaendelea kumshika kwa nyuma na bastola yangu nikiihamishia kichani kwake.Gafla tukastukia askari wakidondoka mmoja baada ya mwengine,hii ni baada ya gari zipatazo sita zilizo na jamaa wenye bunduki zenye uwezo wa juu kuanza kuwashambulia Askari.Tukafanikiwa kuingia kwenya moja ya gari la polisi huku nikiwa nimemuweka mkuu wao chini ya ulinzi na tukaondoka kwenye eneo hili kwa mwendo wa kasi huku gari za jamaa walio tusaiidia zikitufwata kwa nyuma na kutuwekaea ulizi dhidi ya askari walinao zifukuzia gari zetu kwa nyuma.Tukafika kweye maoja ya jago kubwa na nitofauti na jengo la mwanzoni na gari zetu zikaingia.Kuna jamaa akaminya moja ya batani na ardhi ikafunguka na gari zote zikashuka chini na kukuta kuna gereji kubwa iliyojaa watu wengi wakifanya kazi na Lilian akalisimamisha gari tulilo jia katia sehemu yenye magari mengi na tukashuka

    “Eddy usioope huku pia ni kwetu”

    “Nimekupata”

    Nikamshusha mkuu wa polisi na kumkabidhi kwa mijamaa miwili iliyo jazia na kabla hawajampeleka sehemu yoyote wakaanza kumtwanga mangumi mazito yaliyo uchakaza uso wa mkuu huyo wa polisi na sura yake ikatawaliwa na damu nyingi.Wakambeba na wakamdning’iniza kwenye moja ya mnyororo mkubwa na kumpisha Lilian azungumze naye

    “Kwanini ulikuja kutuchunguza?”

    “Naomba munisemehe”

    “Sio jibu la swali nililo kuuliza”

    “Mi....mimi nilitumwa na serikali ya Pakistani kuja kuwachunguza”

    “Eheee wakakuambi kitu gani kuhusu sisi?”

    “Hawajaniamba kitu chochote”

    Mkuu wa askari alizungumza huku akilia kama mtoto mdogo.Lilian akachukua mashine ya kukatia mabati magumu na kuiwasha nikajikuta nikistuka baada ya kumuona akiukata mguu wa askari huyo pasipo kuwa na huruma hadi akauachanisha na mwili na kumfanya mkuu wa askari kulia kiasi kwamba kelele zake zikazizidi kelele za vyuma vinavyo gongwa gongwa ndni ya gareji hii.

    “Sema walikuambiaje?”

    “Walisema niwakamate na watanipatia donge nono?”

    “Ahaa kwahiyo ukapingana na makubakiano yetu si ndio”

    Lilian alizungumza kwa sauti ya ukali huku sura yake ikiwa imekunjana kiasi kwamba akaanza kuwa mwekundu kwa hasira

    “Haaa...ahapana”

    Lilian akaiwasha mashine yake na kuisogeza kwenye mguu mwengine wa mkuu wa askari na kabala hajaukata akanitazama na kuizima mashine na akanikabidhi mashine na kuniomba nimkate jamaa mguu

    “Lilin siwezi kufanya hicho kitendo”

    “Kwanini?”

    “Hiyo adhabu uliyo mpa inatosha”

    “Eddy fanya la sivyo utanijua mimi vizuri”

    Lilian alizungumza huku akionekana hana masihara kabisa na anacho kizungumza.Nikaiwasha mashine na kumtazama kwenye sura mkuu wa polisi na kujikuta nikimuonea huruma.Nikaizima mashine na kumkabadhi Lilian na akaiachia na kuanguka chini.Akanitazama kwa macho makali kisha akatoa bastola yake na na kufyatua rasi mbili zilizotua kichwani mwa Mkuu wa polisi na mwisho wa maisha yake ukafikia hapo.Nikashusha pumzi nyingi huku nikijishika kiuno nikastukia mdomo wa bastola ya Lilian ukitua kichwani kwangu huku macho yake yakiwa yamebadilika kiasi kwamba akazidi kutisha sura yake na uzuri ambao nimezoea kumuona nao umepotea kiasi kwamba nikajikuta nikimeza fumba kubwa la mate kwa woga kwani sikuwahi kumuona Lilian katika hali kama hiyo

    Lilian akanitazama kwa muda kisha akapiga rasasi nyingi hewani kwa hasira hadi bastola ikaisha risasi na akaondoka kwa kasi huku akisunya sunya na akaingia kwenye moja ya chumba na nikataka kumfwata majamaa mawili yalio jazia miili yao yakanizuia huku wakiwa wamenikunjia ngumi.Nikawatazama kwa umakini watu waliomo ndani ya gereji hii na kugundua kila mmoja anabunduki yake na mbaya zaidi sikujua ni sehemu gani ninaweza kutoka ndani ya jengo hili hata kama nikihitaji kutoka.Lilian akatoka ndani ya chumba alicho ingia na huku akiwa ameshika bastola mbili mikononi mwake zisizo fungwa kwa kiwambo chocho cha kuzuia sauti.

    Akaoa ishara kwa majamaa walio nizuia na wakanishika na kutaka kunining’niza kwenye sehemu walio mning’iniza mkuu wa polisi.Akili yangu ikafanya kazi haraka haraka na nikaichezesha mikono yangu kwa nguvu na kujichomoa mikononi mwa mijamaa na kwa haraka nikaichomoa bastola yangu kiunoni huku nikiruka sarakasi hewani na mtu wa kwanza kumfyatulia risasi ni Lilian ila akazikwepa na kujificha kwenye moja gari linalo tengenezwa.Nikakimbia na kuingia kwenye moja ya mferiji ambao hutumiwa na mafundi gereji katika kuzifungua gari kwenye sehemu za chini.Watu wote walipo ndani ya gereji wakastushwa na tukio hili na wakaanza kupiga rasasi zao kelekea katika sehemu niliyopo.Nikaegemea kwenye ukuta wa mfereji huku bastola yangu nikiikoki na kugundua ndani ya sehemu hii kuna kijimlango.Nikakifungua na kuingia na nikatokea kwenye sehemu ya kuhifandhia vifaa vya magari.Nikaanza kuichunguza sehemu nzima na kugundaa hakuna mtu wa aina yoyote.Nikashuka kwenye ngazi zinazoelekea chini na kukuta mlango mmoja ulio fungwa na kufuli kubwa.Nikalipaga risasi tatu hadi likavunjika na kuufungua mlango na kukutana na bunduki nyingi zikiwa zimehifadhiwa ndani ya chumba hichi.Kwa haraka nikaanza kutafuta bunduki yenye uwezo mkubwa wa kunisaidia kwenye mapambano kati yangu na watu wa Lilian ambaye ameshakuwa adui yangu.Nikafanikiwa kuipata bunduki aina ya AK-47 ambayo ni bunduki iliyogunduliwa na Mrusi bwana Mikhali Khalashnikov mwaka 1942 na nimiongoni mwa bunduki zinazotomiwa na majeshi mengi duniani ikiwepo Urusi yenyewe

    Nikaikuta na risasi za kutosha kwenye magazine yake na nikachukua jaketi lakuzuia risasi(Bullet proof) na kuvaa vizuri na nikachuka na baadhi ya bastola zenye uwezo mzuri wa kupiga risasi kwa masafa marefu pasipo risasi kupungua uwezo wake wa kasi.Nikakusanya magazine za kutosha na kuziweka kwenye mfuko yangu.Nikabeba mabomo ya machozi na maboyo ya moto ambayo yanarushwa kwa mkono kisha nikachukua kofia la kuzuia moshi wa mabomo ya machozi.Nikashusha pumzi ya kutosha na kutoka ndani chumba na kabla sijafika katika sehemu ya ngazi nilizo shuka nikaona miguu ya watu wawili ilishuka.Nikajibanza kwenye ukuta na kuuvaa mkanda wa bunduki ya AK-47 na kuiweka mgongoni na kuitoa moja ya bastola yangu na kuishika vizuri,Jamaa wakaanza kunyata huku wakitazama tazama kila eneo la sehemu ya chumba.Nikawafyatulia risasi nyingi za kustukia na wakaanguka chini na kufa kisha nakaanza kupanda kwenye ngazi huku nikitambua kabisa jamaa watakuwa wakinisubiria nje kwa hamu

    Nikalivaa kofia la kuzuia moshi wa mabomo ya machozi kisha nikafika kwenye kijalango nilicho ingilia na kutoa mabumo mawili ya moto ya kurusha kwa mkono(Grenade) kisha nikafungua mlango na kuyatoa vipini vyake na kuyarusha juu ya mtaro na nikaufunga mlango na kuisikia milipuko ya mabomo hayo.Nikashukua mabomo mawili ya mwachozi na kuyarusha kwa nje na kusubiria kwa muda kisha nikatoka ndani ya chumba na kuwakuta jama wakikohoa sana nikaongezea kurusha mabomu ya machozi mawili na kusababisha sehemu nzima kutawaliwa na moshi mwingi.Nikaanza kufanyatua risasi kwa kila niliye muona ndani ya gereji na sikuwa na muda wa kumuhurumia mtu kwani tayari Lilian aliingiwa na roho ya kikatili dhidi yangu.Nikazidi kuwafaytulia jamaa risasi na mabomo ya moto na kuifanya sehemu nzima ya eneo kutawaliwa na moshi wa magari yanayo ungua huku nikitafuta sehemu ya kutokea ndani ya gereji.

    Nikafika kwenye sehemu iliyo na batani nyingi na kuanza kuminya moja baada ya nyingine hadi nikafanikiwa kufungua lango kubwa linalo nyanyuka kwa juu na nikaingia kwenye moja ya gari aina ya GMC ambayo kwa mara nyingi yanapatikana nchini Marekani na hutumiwa sana na majasusi wa Kimareni na sikujua hawa jamaa wamelipatia wapi.Nikaliwasha na kutoka katika sehemu ya chini ilipo gereji.Nikakutana na gari zipatazo saba zikiwa zimetanda katika lango kuu la geti na watu waliomo ndani ya magari hayo wakaanza kukanyaga mafuta kama madereva wanajindaa kwa mashindano ya magari.Nikafungua mlango wa gari langu na kushuka nikatoa mabomo ya mkono na kuyarusha sehemu walipo jamaa na kusababisha mlipuko mkubwa wa magari baadhi.Jamaa wakaanza kunifyatulia risasi nyingi na mimi nikaichukua bunduki yangu AK-47 na kuanza kujibu mashambulizi ya jamaa na kutokana na uzoefu wa matumizi ya bunduki ni kuwa na shabaha nikafanikiwa kuwaua baadhi.Nikaingia ndani ya gari na kukanyaga mafuta kwa nguvu na kuifanya gari kuongeza mwezo huku nikizifwata gari zilizo tanda mbele yangu na kuwafanya baadi ya madereva wa magari hayo kuyasogeza njiani magari yao na kunipa nafasi ya kupita na kutokea kwenye barabara tuliyoigilia

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gari tatu za watu wa Lilian zikaanza kunifukuzia kwa nyuma na kunifanya niongeze mwendo huku nikiingia kwenye mitaa ambayo tangu nizaliwe sikuwahi kuingia.Nikafika kwenye moja ya makutano ya watu wengi na kivua jaketi la kuzuia rasasi na kuiweka bunduki yangu AK-47 pembeni ambayo inauzito kiasi na kushuka ndani ya gari na kuzichomeka bastola zangu kwenye sehemu ambazo sio rahisi mtu kuziona na kushuka ndani ya gari na nikajichanganya kwenye watu wengi ambao kila mmoja anaenendelea na mishuhuliko yake.Nikaingia kwenye moja ya duka na kuchukua kanzu na kitamba cha kujifunga kichwani.Nikavivaa kwa haraka huku muuzaji wa duka akinisaidia kunifunga vizuri huku akinisifia nimependeza vizuri kisha nikaanza kutoka na kumfanya muuzaji kunizuia

    “Pesa yangu”

    Nikatoa bastola na kumuelekezea mzee huyu kwenye kifua na kumfanya anze kutetemeka na kwa bahati nzuri ndani ya duka hakuna mtu wa aina yoyote zaidi ya sisi tu

    “Nahitaji pesa zako”

    Muuza duka akanionyesha droo ya kuhifadhia pesa na nikaifungua na kutoa kiasi cha kutosha cha pesa na kuiziweka kwenye mfuko wa kanzu na kumuonya muuza duka ambaye ni mzee wa makamo asipige kelele ya aina yoyote la sivyo nitamuua.Nikajichanganya na watu wanaoendelea na safari zao.Sikuwaona jamaa wakinifwata kutokana na wingi wa watu,nikafika kwenye gorofa moja lililoandikwa kwa maandishi ya kiarubu ambayo ninayaelewa vizuri na kugundua ni Hoteli ya watu wenye maisha ya kawaida.Nikafika hadi mapokezi na kulipia chumba kimoja na kujifungia ndani.

    Nikaa kwenye kitanda kwa muda huku nikiwa nimechoka kupita maelezo nikazitoa bastola zangu nne pamoja na magazin zipatazo nane na kuziweka juu ya kitanda,nikazitoa pes zote zilizopo kwenye kanzu na kunza kuzihesaba taratibu na kukuta ni dola elfu tatu za kimarekani ni sawa na milioni nne na laki nane za kitanzani.Katika mbinu moja ambayo waalimu wangu wakipakistani waliyo nifundisha ni kuwa mmbunifu wa kutenegeza hati feki za kusafiria.Nikazirusisha pesa mfukoni na kuzichomeka bastola zangu kwenye kila sehemu ambayo nilizichomoa na magazin zake nikazeweka kwenye mifuko ya surali yangu.Nikatoka ndani ya chumba na kwenda kumuuliza muhudumu sehemu ambayo ninaweza kupata maduka ya vitabu(Stationary) na akanielekeza ni mtaa wa pili kutoka katika sehemu niliyopo.Nikatoka na tarayi kagiza kwa mbali kalishaanza kutawala anga.Nikatembea kwa uangalifu wa hali ya juu na kufika kwenye moja ya duka ambalo linauza vitu ambavyo ninavihitaji na kukuta wasichana wawili wakiuza na wakaanza kunichangamkia baada ya kuniona

    Nikaagizia vitu ninavyo hitaji na mmoja wao akanza kuvitafuta na kunikabidhi na kabla sijalipa na simu ya mmoja wasichana hao ikaita na akaipokea huku akionekana kuwa na wasiwasi mwingi.Nikashangaa kusikia akiongea Kiswahili kizuri ambacho nivigumu kwa waarabu wengi kuzungumza Kiswahili kama anacho kuzungumza

    “Baba amefariki.......!!?”

    “Sawa sawa ngoja niombe ruhusa kwa bosi wangu ninawaomba musimzike hadi nije”

    Akakata simu huku akionekana kuchanganyikiwa kwa taarifa aliyo ipata huku machozi mengi yakimwagika,Mwenzake akamtuliza na kumuuliza ni kitu gani kilicho tokea na nikagungundua kwamba mwenzake hafahamu Kiswahili zaidi ya kiarabu

    “Baba ameariki ncini Tanzania”

    “Weee pole sana tatizo lilikuwa ni nini?”

    “Mdogo wangu ameniambia kuwa aliumwa gafla”

    “Mungu wangu sasa itakuwaje?”

    ‘Inabidi niende Tanzania leo hii”

    “Bosi kweli atakuruhusu?”

    “Ata kama hata niruhusu itanibidi niende tuu”

    “Pole sana rafiki yangu”

    “Asante”

    “Ila Mariam ukiende nakuomba unikimbuke nimesha kuzoea rafiki yangu”

    “Sawa rafiki yangu”

    Mariam akachuku baibui lake na kulivaa na kujifunga kitambaa kilicho yabakisha macho yake tu na akachukua pochi yake na kumuomba rafiki yake afunge mapema.Akatoka nje ikanibidi nilipe pesa ya nilivyo vichukua na kutoka ndani na kumuona akiingia kwenye moja ya Taksi na ikaondoka ikielekea upande wa mashariki.Nikaita taksi nyingine na mimi nikaingia na kukaa siti ya nyuma na kumuomba dereva aifwatilie gari aliyopanda Mariam.Taksi aliyopanda Mariam ikasimama kwenye moja jemgo mabalo kwa haraka nikalifanhamu,Ni jengo ambalo tuliingia na Lilian kipindi tunafika hapa Oman tukitokea Pakistani na ndipo walipo mtoto wa Raisi wa Pakistani.Dereva wa taksi niliyo panda akasimama taksi gafla kwa mbali na lilipo jengo alilo ingia Mariam huku akionekana kuogopa kufika kwenye eneo aliloshuka Mariam

    “Mbona unasimama?”

    “Ameingia kwenye makao makuu ya Don”

    “Don ndio na nani?”

    “Don ni mtu hatari sana na anauwezo wa kufanya chochote kinachoweza kumdhuru mtu pasipo serilali kumfanya lolote”

    “Huyo Don ni nani?”

    “Jamaa mmoja anaitwa Patrick na hapa Oman yeye ndio anaye ogopewa na kila mtu na jamaa ni mtu wa kujichanganya na watu wengine ila anaroho mbaya sana”

    “Sasa kwa nini wewe umelisimamisha gari hapa?”

    “Kila mtu anayekwenda kusimama pale kwenye lile jengo nilazima afwatiliwe na watu wa Don Patrick na wakikukamata wanakutesa kiasi kwamba useme kitu gani kilikusimamisha nje ya jengo lake”

    “Mbona mwenzako kasimamisha gari lake pale?”

    “Yule jamaa ni mgeni nahisi hamfahamu Don vizuri”

    “Sawa unanidai kiasi gani cha pesa”

    “Dola 15”

    Nikatoa kiasi anacho kihitaji na kushuka ndani ya gari na kuanza kutembea kwa umakini na kabla sijalifikia jengo la Don Patrick nikajibanza kwenye moja ya gari lililo simamishwa barabarani na kuwaona Patrick na Mariam wakitoka wakiwa ndani ya gari na kuondoka wakielekea upande mwingine.Nikavunja kioo cha gari lililosimamishwa kwa kutumia kitako cha bastola na kuuingiza mkono wangu na kufungua mlango wa upande wa dereva na kukata nyaya za kuwashia gari na uzuri ni kwamba nilishawahi kufanya kazi gereji kwa Mama Caro na haikuwa ngumu kwangu kuliwasha gari kwa njia hii ambayo mara nyingi hutumiwa na wezi wa magari

    Nianza kufwata njia aliyo elekea Don Patrick ambaye ni kaka yeke Lilian na kulifikia gari lao kwa ukaribu.Wakasimama kwenye moja ya duka kubwa na wakashuka na Mariam na kuingia kwenye duka hilo linaloonekana ni duka lan guo,na mimi nikashuka ndani ya gari na kuingia ndani ya duka na kumuona akimchagulia chaguli nguo Mariam.Nikaanza kujifnya na mimi nikikagua kagua nguo kama mnunuzi hadi nikawafikia kwa nyuma na kuitoa bastola yangu na kumuwekea Don Patrick kwa nyuma pasipo Mariam kuona tukio hili

    “Ninamazungumzo na wewe”

    Don Patrick akastuka baada ya kuniona na akamuomba Mariam aendelee na kuchagua nguo anazo zihitaji,Mimi na Don Patrick tukatoka kwenye duka hili huku nikiziona kamera za ulizi zikiwa zimesambaa katika eneo zima tulilopo.Nikamuingiza kwenye gari langu na kukaa naye siti ya nyuma huku akionekana kunidharau japo anawoga na mimi

    “Bwana mdogo huwezi kunifanya chochote huu ni mji wangu”

    “Sikiliza wewe mpuuzi sikuja hapa kujua kama huu ni mji wako au wa baba yako ninacho kihitaji mimi ni mtoto wa raisi na mpenzi wake tu”

    “Hahaaaa unachekesha sana wewe unadhani ni kirahisi kiasi hich.....”

    Nikampiga kichwa cha pua na kumfanya atoe mguno mkubwa huku damu zikianza kumchuruzika zikitokea puani na bastola yangu nikizidi kumgandamiza kwenye mbavu zake

    “Utanipa hao vijana au hunipi?”

    “Nakupatia”

    “Fanya maswasiliano na watu wako na ukileta ujinga nitakuua sawa”

    Don Patrick akatoa simu yake na kuminya baadhi ya namba na kuzungumza na mmoja ya watu wake na kumuomba awachukue watoto wawili na awalete katika sehemu tuliyopo

    “Na mwambie asiandamane na watu wengine la sivyo nakutoa uhai wako”

    “Karimu hakikisha unakuja peke yako na hao watoto na ufanye haraka”

    Don Patrick akakata simu na kuanza kujichekesha huku akipiga mluzi unao endana na wimbo wa kuchi kuchi hotahe wa Shar Khan

    Tukasubiri ndani ya dakika kumi gari nyeusi ikasimama nyum yetu na Don Patrick akanitaarifu kuwa gari iliyo simama ndio yenye watoto wa raisi wa Pakistan.Tukashuka ndani ya gari na mtu aliye mtuma akashuka na akaufungua mlango wa nyuma wa gari hiyo na kumuona Seif na mwenzake wakiwa wamefungwa vitambaa vyeusi kwenye macho na mikono yao ikiwa imefungwa kamba

    “Mwambie awafungue”

    “Wafungue bwana hao vijana”

    Karim akawafungua Seif na mwenzake kisha nikampokonya Karim funguo ya gari na kuingia ndani ya gari alilo kuja nalo Karim na kuondoka nikiwaacha wakiwa wanashangaa.

    “Musiogope nimewaokoa sawa Seif”

    “Sawa kaka”

    "Fungeni mikanda ya gari"

    Kwa kupitia kioo cha pembeni nakaona gari la Don Patrick likija kwa kasi nyuma yetu na gafla nikajikuta nikifunga breki za gari huku nikijitahidi kuizungusha gari na kugeuka na ikitokea tulipo toka hii ni baada ya kuona gari zipatazo tatu zikija kwa kasi mbele yetu huku zikiwa zimetanda barabara mzima huku watu waliomo ndani ya gari hizo wakitufyatulia risasi



    Nikakanyaga mafuta kwa kasi na kuachia Mbeki za gari langu na kulifanya magurudumu yake kwenda kwa kasi na kuelekea kwenye sehemu ambayo tulikuwa tumetokea na kuanza kulilenga gari la Don Patrick huku nikiwa nimejiandaa kwa chochote kile kitakacho toke.Gari ya Don Patrick ikatukwepa na kwenda kugonga kwenye mlango wa duka moja na kuanza kuwaka moto.Nikazidi kuogeza mwendo wa gari langu na watu wa Don Patrick wakaendelea kutufukuzia kwa nyuma huku wakizidi kutumiminia risasi nyingi

    “Seif unaweza kuendesha gari?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimuuliza Seif kwa lugha ya kiarabu ambaye ameinama chini kwenye siti yeye na mpenzi wake ili risasi zinazopigwa nyuma zisiwapate kwani tayari kioo cha nyuma kilisha pasuliwa kwa risasi

    “Ndio”

    “Hamia siti ya mbele”

    Seif akahamia siti ya mbela na nikampisha kwenye siti niliyo ikalia na tukio la siku nilipokuwa nimekamatwa na wanajeshi wa Kimarekani likaanza kunijia kichwani na kukumbuka jinsi dada yake Lilian alivyonikabidhi gari kwa ajili ya kuliendesha na kwabahati mbaya akafariki kwa kupigwa risasi alipokuwa akipambana na waarabu waliokuwa wakipambana na wanajeshi hao.Seif akakaa kwenye siti ya gari na kundelea kuendesha gari letu lililopo kwenye mwendo wa kasi huku na mimi nikihamia kwenye siti ya nyuma alipo mchumba wa Seif na nikazitoa bastola zangu na kuhakikisga zipo tayari kwa mashambulizi na kuanza kufyatua risasi kuelekea walipo watu wa Don Patrick

    Nikawa ninahakikisha kila risasi moja inampiga mtu mmoja yapo wao risasi zao wakawa wanazifyatua pasipo kuwa na mpangilio maalumu.Nikampia dereva wa gari lililokuwa linatusogelea kwa karibu na kusababisha gari lao kuanza kupoteza muelekeo na kuanza kupinduka na kubingiria na kufanya gari moja la nyuma dereva wake akashindwa kulikwepa gari lililokuwa likibingiria na kulivaa na kusababisha ajali mbaya na kukawa kumebakia gari moja linalo tufwata kwa nyuma kwa mwendo wa kasi

    Kwa uendeshaji wa Seif nikajikuta nikimkubali kwani kila jinsi tunavyokwenda ndivyo jinsi tulivyozidi kuwaacha watu wa Don Patrick ambao gari lao lilipasuka matairi yao na kusababisha kushindwa kuendelea kwa mashindano tunayo yafanya.Seif akalisimamisha gari kwenye kichochoro kimoja na sote tukajikuta tukishusha pumzi na nikawa wa kwanza kushuka kwenye gari huku kilemba changu nikikivua na kukitupa ndani ya gari na kulichunguza eneo zima na kugundua ipo salama na kuwaruhusu Seif na mpenzi wake kushuka ndani ya gari nakuliegemea

    “Kaka tunafanya nini?”

    “Seif inatubidi tufanye mpango kurudi Pakistani”

    “Seif mimi ninasikia njaa”

    Mpenzi wa Seif alizungumza na kutufanya tumtazame kisha Seif akamsogelea na kuanza kumbembeleza taratibu huku akimuambia asijali kwani kila kitu kitakuwa sawa

    “Seif mpenzi wako anaitwa nani?”

    “Kajol”

    “Anajina zuri”

    “Asante kaka”

    Nikaingia ndani ya gari na kuchukua kitambaa changu cha kichwani kisha nikatoka na kujifunga kichwani vizuri na kuanza kutembea hadi sehemu yenye bararaba na kutazama usalama na kukuta kila kitu kipo sawa kwa ishara nikawaita Seif na mpenzi wake na wakanifwata na tukaanza kutembea kwa miguu tukitafuta sehemu yanye mgahawa tuweze kula japo tayari imeshatimu saa sita usiku.Kwa bahati nzuri tukakuta Motel moja na kuingia na kukuta watu wachache na tukatafuta sehemu na kukaa na kuagizia chakula kitakacho tutosha na kuanza kula taratibu baada ya kuletwa na muhudumu tuliye muagizia

    “Seif hivi unashuhulika na maswala gani?”

    “Mimi nimesoma chuo cha udereva wa magari na maswala ya techonilogia ya computer”

    “Ahaa ndio maana upo vizuri kwenye kuendesha gari?”

    “Ndio kidogo ninajitahidi kwani nimeshawahi kushirika mashindano ya magari mwaka jana”

    “Ahaaa Kajoli mbona upo kimya”

    Kajoli akanitazama kwa muda kisha akaachia msunyo uliotufanya tubaki tunashangaa na akaanza kuzungumza lugha ya Balochi ambayo sikuwa ninaielewa

    “Anasemaje mpezni wako?”

    “Anadi kuwa wewe na mwenzoko ndio vyanzo vya sisi kupata shida huku ugenini”

    “Ahaaa”

    Tukaendelea kula huku nikiwa tanatazma Tv kubwa inayoonyesha matangazo ya kombe la dunia ambalo limebakisha siku mbili katika kuanza kwake nchini Brazil.Seif akaniomba noti moja ya dola mia nikampatia na akaenda mapokezi na akazungumza na muhudumu kisha akapewa simu ya mezani nikataka kumfwata ila nikatulia kungalia ni nini anataka kufanya.Akaweka mkonga wa simu sikioni kwake na baada ya sekunde kadhaa akaanza kuzungumza taratibu

    “Baba mdogo mimi nipo salama tuu”

    “Ok basi tunakuja muda si mrefu ila usimuambie baba”

    Akaurudisha mkonga wa simu kwenye sehemu yake kisha akamlipa muhudumu pesa anayo ihitaji na kurudi sehemu tuliyo kuwepo na akakaa

    “Nimezungumza na baba mdogo na amesema twende kwake kama huto jali?”

    “Baba yako mdogo anashuhulika na nini hapa”

    “Yeye ni miongoni mwa wenye hisa kwenye shirika la ndege la Fly Emirates na nitajiri mkubwa sana hapa Oman”

    “Huoni utanihatarishia maisha yangu kwani ninatafutwa na serikali ya baba yako”

    “Mimi ndio nitazungumza naye kwa maana ananielewa vizuri sana na pia nilimuambia asimuambie baba”

    Nikaanza kufikiria kitu cha kufanya kwa maana bado sikuwa ninamuamini Seif moja kwa moja kwani hata Lilian mwenyewe ambeye nilikuwa ninamuamini alinieuka pasipo kuwa na sababu ya muhimu na Seif nikahisi anaweza kunibadilika muda wowote.Nikamkubalia ila nikawa nimejiandaa tayari kwa chochote na tukakodi taksi ikatupeleka kwenye mji wa Abu Dhabi na kuingia kwenye Hoteli yenye maandishi makubwa kwenye sehemu ya juu kwenye gorofa yanayosomeka NOVOTEL HOTEL.

    Seif akaingia akazungumza na muhudumu na akamuulizia baba yake mdogo na muhudumu akapia simu na akazungumza na mtu anayempigia na baada ya muda akakata simu na kutuomba tuingie ndani na tupande kwenye orofa ya 22 ndio tutakutana na huyo tunaye muulizia.Tukaingia kweye lifti na baada ya muda tukafika kwenye gorofa ya 22 kisha tukatoka na kwenye lifti na kukuta walinzi walio valia suti nyeusi na wakaanza kutukagua mtu mmoja baada ya mwengine.Mlinzi akaonekana kustuka baada ya kuniona mimi nikahisi wameambia kuhusiana na habari zangu ila nikawa mpole na kusuiria watakacho niambia.Wakaniamrisha ninyooshe mikono juu na nikatii wakanikagua na kuzitoa bastola zangu zote na magazine nilizo kuwa nazo.Akaja mzee aliye valia kanzu nyenye rangi ya dhahabu na kusalimiana na Seif na Kajoli ila kwangu akagoma na kunitazama kwa muda kisha akamgeukia Seif na kumuuliza swali

    “Huyu ni nani?”

    “Huyu ni mtu aliye tuokoa mimi na mpenzi wangu”

    “Mbona baba yako amenitumia picha za watu wawili na huyu akiwa ni mmoja wapo kati ya wale walio wateka”

    “Ndio ila huyu ametukumboa kutoka mikononi mwa wale walio kuwa wametushikilia na nimtu mzuri tu na usimtilie mashaka kwani pasipo yeye tusingeweza kuwa hapa”

    Mzee akanitazama kuanzia juu hadi chini kisha akarudia tena kwa mara mbili kisha akanipa mkono na mimi nikautazama kwa muda na kumpa wa kwangu na kusalimiana naye

    Akatukaribisha kwenye seble yenye vitu vingi vya dhamani na tukakaa huku mimi nikitazama kila kona ya seble hiyo kwani hata wakitaka kunifanyia kitu chochote nijue jinsi ya kujiokoa.Akawaagiza wahudumu wake kutuletea vinywaji na baada ya muda vikaletwa kabla sijakinywa machale yakanicheza na nikamuomba Seif nibadilishane naye kinywaji na yeye akachukua changu na kabla hajakinywa simu ya baba yake mdogo ikaita na akipokea na kutufanya tusitishe zoezi la kunywa vinywaji tulivyo pewa

    “Ametekwa......!!”

    “Na nani tena?”

    “Sawa subiri nitakupigia ila mwanao yupo kweye hali salama na ninaye sasa hivi hapa”

    “Sawa”

    Baba mdogo wa Seif akakata simu na kutufanya sote tubaki tukimtazama na yeye akatutizama kwa muda na kuanza kuzungumza

    “Seif mama yako ametekwa”

    “Nini?”

    “Ndio mama yako ametekwa”

    Seif akanyanyuka kwenye sofa akionekana kuchanganyikiwa kwa tukio alilo ambiwa na machozi yakaanza kumwagika taratibu.Kajoli akasimama na kuanza kumtazama Seif na kujikuta na mimi moyo ukianza kuingiwa na huruma.Akaja mlimzi mmoja akiwa na Laptop mkononi huku akiwa ameifunua na kuiweka mbele ya bosi wake

    “Shiiiti ndio huyu msichana tena”

    “Ndio mkuu”

    Nikaanza kujiuliza ni msichana gani aliye fanya tukio hilo na sikupata jibu la haraka haraka

    “Tutafanyaje mkuu?”

    “Ngoja nimuulize kaka”

    Baba mdogo wa Seif akatoa simu yake na kupiga baadhi ya namba na kuiweka sikioni na kuanza kuzungumza na mtu aliyepo upande wa pili na sauti nikawa ninaisikia

    “Anahitaji bilioni mbili za kiamarekani?”

    “Kaka hiyo ni pesa kubwa cha msingi tutafute njia nyingine na si kufanya hivyo anavyo taka yeye”

    “Amesema atamuua mke wangu ndani ya siku mbili kama nitakuwa sijatimiza hizo pesa”

    “Ila kaka ninawzo hapa”

    “Wazo gani?”

    “Nina yule kijana ambaye aliwateka Seif na mpenzi wake ila yeye amewageuka wezake na inavyo onekana anaweza akatusaidia kwenye hilo”

    “Huyo mpumbavu munaye hapo.......Mkamateni mara moja kwani anaweza akakuja kuwachunguza”

    “Kaka tuliza jazba huyu kijana anaonekana ni mtu mwema”

    “Nimesema....”

    Baba mdogo wa Seif akakata simu na kunitazama kisha akaishika laptop na kusimama na kuja kukaa kwenye sehemu niliyo kaa mimi na kunionyesha picha ya Lilian akiwa amepiga na mama mmoja wa kiarabu huku akiwa amemuwekea bastola kichwani

    “Nina imani unamjua huyu msichana vizuri”

    “Ndio”

    “Kwa sasa yupo mchini Brazil ambapo amemteka huyu mke wa kaka yangu ambaye ni mama yeka Seif.Sijui katika hilo utanisaidiaje?”

    “Umesema yupo Brazil?”

    “Ndio shemeji yangu alikwenda kama miongoni mwa wawakilishi wa ufunguzi wa kombe la Dunia sasa ndio amekamatwa na huyu binti ambaye ulishirikiana naye”

    “Wapo Brazil eneo gani?”

    “Sijajua hadi sasa hivi ila huyu binti anahitaji dola za kimarekani bilioni mbili ambazo ni nyingi sna kwetu kuweza kuzitoa”

    Nikaanza kufikiria jinsi ya kukabiliana na kazi iliyopo mbele yangu,nikamtazama Seif aliye jikunyata kama kuku huku akilia na roho ya imani ikanijia taratibu nikatingisha kichwa nikikubaliana na kazi hiyo

    “Nimekubali”

    “Asante sana kijana na tupo tayari kukulipa kiasi chochote cha pesa utakacho kihitaji”

    “Sawa ila kwa sharti moja tuu”

    “Sharti gani?”

    “Ninahitaji serikali ya kaka yako kunitoa kwenye idadi ya watu inayo watafuta kama magaidi”

    “Hilo halini shida”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tukaubaliana na baba mdogo wa Seif ambaye alijitambulisha kwa jina la MAHAMOUD na mipango ikapangwa haraka ya kusafiri kuelekea Brazil pasipo Raisi wa Pakistani kutambua hilo kwani inaonekana hayupo tayari kaniona niikiwa ninalishuhulika tatizo la kutekwa kwa mke wake.Wakanipatia pesa ya matumizi ya kutosha na sura yangu ikatengenezwa vizuri na kupandikizwa ndevu za bandia zilizo nibadilisha sura yangu na kunipa muonekano wa tofauti sana na nivigumu sana kwa mtu gunigundua kama mimi ni Eddy.Wakatengenezea kitambulisho cha FBI ambacho si rahisi kwa mtu kugundua kama ni bandia kwa maana kimetengenezwa na wataalamu walio somea mambo ya utengenezaji wa vitu hivyo.Jina langu kwenye hati yangu ya kusafiria ikabadilishwa jina na nikaitwa Jack Lee na safari ikaanza majira ya saa kumi na moja asubuhi kwa kutumia ndege za shirika la Fly Emirates iliyo na uwezo wa kubeba abiria 250 kwa safari moja

    Ndege ikapita usawa wa bahari ya Altetic kaskazini na moja kwamoja kukaelekea Brazil pasipo kutua kwenye nchi yoyote

    “Kaka unahitaji kinywaji gani?”

    Msichana mrembo mwenye asili ya kizungu ambaye ni muhudumu kwenye ndege hii akasimama mbela yangu huku akiwa amevalia sketi fupi huku shati lake akiwa amelichomekea kweye sketi yale hiyo na huku katai kadogo kakiwa kameiipendezesha shingo yake na kichwani kwake kukiwa na kofia nyekundu ndogo iliyokaa upande kidoo na kuziacha nywele zake ndefu zikininginia na kuufanya uzuri wake kuwa maradumu

    “Kaka nikuletee kinywaji gani?”

    “Ohhh naomba juisi ya maembe”

    “Je utahitaji na kitu kingine?”

    “Labda soseji na yai moja”

    “Sawa subiri baada ya muda”

    Akaondoka na kubaki nikimtazama kwa nyuma jinsi sketi yake inavyo cheza kwa nyuma sehemu yake ya makalio na kunifanya niaanze kuvutiwa naye.Baada ya muda akaniletea nilivyo muagizia na akaniwekea kwenye sehemu ya kuwekea iliyopo kwenye siti niliyo kaa na kabla ajaondoka ikanibidi nimuulize

    “Samahani dada unaitwa nani?”

    “Angelin Danson”

    “Mimi ninaitwa Jack Lee”

    “Ohh unajina zuri sana”

    “Asante na la kwako pia ni zuri sana”

    “Nashukuru kusikia hivyo”

    “Sijui ninaweza kupata mawasiliano yako?”

    “Kwa sasa siruhusiwi kufanya hivyo nipo kazini labda ndege mwisho wa safati nitakupatia”

    “Sawa”

    Akaondoka na nikaanza kupata kazi ya kusali ili safari iende haraka kwani ninahamu sana ya kufika nchini Brazi ambapo imebaki siku moja kuanzishwa kwa kombe la dunia nchini humo.Badaa ya masaa manne na nusu sauti ya kiume ikitokea kwenye vipaza sauti vya ndani ya ndege ikatuomba tujifunge vizuri mikanda yetu kwani ndege inajiandaa kutua kwenye ardi ya nchini Brazil na baada ya muda matairi ya ndege yakaanza kugusa ardhi nakusimama.Angelin akanifwata na kunipa kikaratasi kidogo na kunikonyeza kisha akaendelea na kazi zake na mimi nikalitoa begi langu lenye nguo na pesa kadhaa kwenye sehemu ya kuwekea mizigo kisha nikaanza kushuka kwenye ndege.Tukaingia kwenye basi kubwa lililo tupeleka kwenye mlango wa kuigilia sehemu ya kotukea hii nikwasababu ya ndege yetu kusimama mbeli kutokana na wingi wa ndege zilizopo eneo hili la uwanja na sote tukashuka na kuingia ndani na kupanga foleni sehemu ya kotokea na kuanza kukaguliwa mmoja baada ya mwengine

    Ulinzi wa uwanja wa ndege umeimarishwa kwa kiasi kikubwa na askari wengi wamesambaa kila kona ya eneo la uwanjwa wa ndege huku wakiwa na silaha na baadhi yao wakiwa na mbwa wakubwa.Dada anayepiga mihuri kwenye hati za kusafiria akanitazama kwa muda kwa macho makali huku akiwa ameishika hati yangu ya kusafiria na kuanza kupata wasiwasi labda amenistukia ndevu zangu za bandia nilizo wekwa kisha akatabasamu na kuzungumza kwa lugha ya kingereza

    “Karibu sana bwana Jack Lee katika sheree za kombe la dunia Brazil”

    “Asanate”

    Nikachukua hati yangu ya kusafiria na kutoa nje na kuita taksi na kumuomba dereva anipeleke kwenye hoteli nzuri

    “Kaka hoteli nyingi zimejaa wageni”

    Alizungumza kingereza kibovu ila nilimuelewa vizuri

    “Sasa ni wapi kwenye hoteli ambayo ninawezaa kupata?”

    “Ngoja tuzunguke zunguke ila sidhani kama tunaweza kupata hoteli ya wewe kufikzia si unatambua mashindano yamebakisha masaa kuanza kuna watu waliweka oda za hoteli mwezi mmoja kabla”

    “Sawa ninaomba msaada wako”

    Kutokana na foleni ya magari mengi japo barabara inauwezo wa kupitisha gari manne kwa wakati mmoja ila zote zimejaa magari ikatulazimu kutembea kwa mwendo wa taratibu huku mara kwa mara tukisima kuifwata foleni iliyopo mbele yetu.Taksi yetu ikasimama sawa na gari nyeusi ya kifahari ambayo watu wengi tumezoea kuziita Six Doar(Milango sita) na ambayo madirisha yake hayakufungwa nikajikuta nikitazama msichana aliye kaa siti ya nyuma kwenye siti hiyo na kugundua ni Caro kwani kwa pembeni yake nikamuona mama yeke akiwa anazungumza na simu na kujikuta nikitaka kumuita ila mdomo ukashindwa kwa kigumizi



    Magari yakaanza kuondoka taratibu huku nikilishuhudia gari alilo panda Caro na mam yake lilikunja kona ya kushtoto huku gari letu likinyoosha barabara ya moja kwa moja nikashindwa hata kumuambia dereva akunje kona na kulifwatilia kutoka na wingi wa magari yaliopo katika barabara hii.Safari ikaendelea mbele ikanilazimu kumuuliza dereva ni wapi tunapo kwenda kwa maana sikuelewa dereva anaipeleka wapi na mbaya anaminya minya simu yake kama mtu anaye andika meseji

    “Huu ni mji gani?”

    “Huu ni mji wa Rio de Janeiro huu ndio mji mkuu wa utalii”

    “Ahaa kweli tunaweza kupata vyumba vya kulala?”

    “Tutabahatisha na pia nimecheki rafiki yangu mmoja ameniambia kuna vyumba kwenye moja ya hoteli kwenye fukwe za Copacabana”

    Sikuwa na cha kuuliza zaidi ya kuitoa simu yangu mfukoni na kuanza kupiga picha za sehemu zinazo nivutia na haikuchukua muda sana dereva akasimamisha gari lake kawenye moja ya jengo la gorofa lililo andikwa maandishi makubwa Windsor Copa Hotel na akaniomba tushuke kwa pamoja.Akanitolea begi langu kwenye buti ya gari kisha akamkabidhi muhudumu aliye toka kutupokea.Nikamkamlipa dereva wa taksi kiasi cha pesa anacho nidai kisha akaniachai namba yake ya simu endapo nitamuhitaji iwe rahisi kwa mimi kumtafuta.Tukaingia hotelini na moja kwa moja muhudumu aliye libeba begi langu akaniongoza hadi sehemu ya mapokezi na kwabahati nzuri nikafanikiwa kupata chumba cha kulala japo ni cha bei ya gharama sana hii ni kutokana na wateja wengi waliopo katika nchi ya Brazil kulishuhudia kombe la dunia ila sikuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kulipa kiasi cha dola za kimarekani laki moja na ishirini ni sawa na pesa ya kitanzania shilingi milioni miambili na laki nne kwa mwezi mzima nitakao kaa brazil nikiwa ninaendelea na uchunguzi wa kumtafuta Lilian aliye mteka mke wa raisi wa Pakistan

    Nikaifungua laptop yangu iliyo unganisheshwa moja kwa moja na ofisi ya Mahamoud mdogo wa raisi wa Pakistan na kwabahati nzuri nikamkuta yupo hewani na kwakutumia mtandao wa viber ikawa ni rahisi kwa sisi kuzungumza tukiwa tumeonana,nikavaa eyephone masikioni na kuanza kuzungumza na Mahamoud

    “Tumshukuru Mungu kama unmefika salama”

    “Ndio mkuu ila hamujapata sehemu ambayo Lilian amemshikilia shemeji yako”

    “Tumefanikiwa kuipata kwani simu ya mwisho yake ya mwisho kutupigia tumegundua yupo katika fukwe za Copacabana katika sehemu inayoitwa Atlantico Praia”

    “Ngoja kwanza niitafute subiri kwa dakika moja”

    Nikaifungua simu yangu sehemu ya internet na kuingiaza jina la hotel aliyo nitajia na ndani ya sekunde kadhaa ikafunguka na kutoka sehemu niliyopo mimi katika hoteli ya Windsor sio mbali sana na alipo Lilian

    “Nimeipata mkuu”

    “Sawa hapo ndipo alipo sasa niambie ni wapi ulipo ili wale vijana wenye silaha waje kukuletea”

    “Mimi nipo katika hotel ya Windsor ukiwaambia tu hivyo watealewa”

    “Sawa ngoja niwape namba yako ya simu waje kukutana na wewe”

    “Sawa”

    Nikakata mawasiliano na Mahamoud kisha nikaifungua sehemu aliyopo Lilian kwa kutumia Laptop yangu na kuiona kwa ukubwa hotel aliyopo na matumaini ya kuifanikisha kazi yangu kwa urahisi ikaanza kuzaa matunda.Ndani ya dakika kumi simu yangu ikaingia ujumbe mfupi wa meseji ukiniomba nichungulie dirishani na nikafanya hivyo na kuliona gari jeusi likiwa limesimama nje ya hotel hii na kumuona msichana mwembamba aliye valia nguo nyeusi akiniitya kwa ishara .Nikatoka chumbani kwangu na kupafunga vizuri na kutoka nje na nikavuka barabara na kwenda sehemu ya pili ya barabara alipo msichana na akaniomba niingie kwenye gari alilo kuja nalo ambalo ni Range rover Sport

    Nikaingia na yeye akanifwatia kwa nyuma na kutokana na vioo vyake ni vyeusi hapakuwa na mtu yoyoyte wa nje kuweza kuona ndani zai ya sisi watu wa ndani kuona nje.

    “Ninafikiri wewe ni bwana Jack Lee?”

    “Ndio ni mimi”

    “Ninafurahi kukutana na wewe jina langu ninaitwa Matlda De Santos Jr”

    “Nashukuru kwa kusikia hivyo”

    “Niliagizwa na bosi wangu kukuletea huu mzigo”

    Msichana alizungumza huku akitoa brofcase nyeusi na kunikabithi nikataka kushuka ila akaniomba niifungue kuhakikisha mzigo nilio pewa ni sahihi.Nikaifungua na kukuta bastola moja yenye magazine yake pembeni inayo ingia risasi zipatazo arobaini na tano

    “Vipo kamili”

    “Sawa na endapo utahitaji msaada wowote piga hii namba”

    Matilda De Santos Jr akanikabidhi kikaratasi kidogo na kabla sijashuka ndani ya gari sote tukaiona gari ndogo ya polisi ikisimama mbele yetu na askari wawili wakashuka ndani ya gari lao na kuanza kupiga hatua za kuja lilipo gari letu na kugonga kwenye kioo cha upande wa dereva na Matlda De Santos Jr akafungua kiio na wakaaza kuzungumza kibrazil ambacho zikuwa ninakielewa

    Polisi mmoja alizungumza kwa kufoka huku akishika kitasa cha mlango akikivuta nje ili Matilda kushuka kwenye gari ila kutokana na mlango kufungwa kwa ndani ikawa ni ngumu kwake kufungua

    “Wanahitaji nini?”

    “Wamesema nimesimamisha gari sehemu ambayo sio husika na pia muda wagari hii kutembea barabarani umekishwa”

    Nikatoa kitambulisho changu cha FBI na kuwaonyesha maaskari hawa na wakabaki kimya wakinitazama kwa umakini kisha wakaniomba msamaha kwa kingereza kibovu na wakaondoka zao.Matlda De Santos Jr akaniaga na mimi nikashuka ndani ya gari na kurudi chumbani kwangu na kuifungua broofcase iliyo na bastola yangu kuikoki vizuri na nikaifunga kiwambo cha kuzuia sauti.Nikajilaza kitandani ili kuusubira muda ukatike ndio niweze kufanya kazi yangu kwa usahihi.Sikuuruhusu usingizi kuyateka macho yangu na hdi inatimu saa mbili usiku sikuwa nimelala na nilicho kifanya ni kuvua nguo zangu nilizo jia kisha nikavaa nguo nyingine zenye rangi nyeusi na juu yake nikavaa koti jeusi pamoja ni viatu vyeusi na bastola yangu nikaichomeka kwenye soksi na nilipo hakikisha ipo salama nikatoka ndani ya chumba changu na kwenda sehemu ya kupatia chakula

    Nikaagizia chakula ambacho nilisha wahi kukila ambacho ni mchanganyiko wa viazi na mboga za majani.Nikala kwa haraka na kuondoka zangu na safari ya kuelekea ilipo hotel aliyopo Lilian ikaanza huku nikisaidiwa na simu yangu niliyo iseti kitu kinacho itwa ‘Map Direction’(muongozo wa ramani) na nikafanikiwa kufika kwenye hotel aliyopo Lilian japo nimetumia muda mrefu hadi kufika sehemu hii kutokana na umbali kutoka sehemu nilipokuwa na nilitumia miguu.Nikaingia kwenye hotel na kukuta watu wa aina mbali mbali wakiwemo mashabiki wa mpira wa timu ya Spain,Nikatafuta sehemu yenye kigiza na kukaa na kuagizia juisi na kuanza kunywa huku nikiyasoma vizuri maeneo ya ndani ya hotel.Nikamshuhudia Lilian akitoka kwenye lifti ya sehemu hii akiwa amevaa kofia kubwa huku na yeye akiwa amevalia jezi ya mpira ya nchi ya Spain huku nywele zake akiwa ameziweka kwa mtindo wa kuufunika upande mmoja na si rahisi kwa mtu yoyote kuweza kumgundua kirahisi ila kwangu si ngumu kutokana na nimemzoea sana.Nikamuona akitafuta sehemu ya kukaa kisha akaadizia kinywaji na akaanza kuchezea simu yake huku akipiga pia picha kwa watu wanao cheza ngoma za kispain katika ukumbi wa hotel.Lilian akaendelea kuga picha huku akionekana kuwa na furaha na kinywaji anacho kunywa nikagundua ni pombe kwa kulidhibitisha hili nikaitoa simu yangu mfukoni na kuweka sehemu ya video camera na kuizoom chupa iliyopo kwenye meza ya Lilian na kutokana na uwezo mkubwa wa simu yangu nikafanikiwa kuyasoma maneno yaliyo andikwa Alcohol 55% na kugundua ni kiwango kikubwa cha kilevi kilichopo kwenye kilevi hicho.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikaaanza kuyahisi maumivu makali ya tumboni huku kizunguzungu kikianza kunitawala.Nikajikaza na kumuomba muhudumu kunionyesha chooni na nikaanza kuelekea kwa kujikaza na nikafanikiwa kufika pasipo kuanguka na moja kwa moja nikakimbia sehemu yenye ya bomba la maji na kuanza kuyafungua na kuanza kuyanywa kwa fujo kwani nikagundua kwenye juisi niliyo kunywa niliwekewa sumu.Nikaanza kujitapisha kwa nguvu guku nikivichomeka vidole vyangu mdomoni hadi nikaanza kutapika kila nilicho kila.Nguvu za mwili wangu nikahisi zikiwa zimeniishia kwa kiasi kikubwa na kujikuta nikiwa nimeinama chini kwenye sinki la maji huku mara kwa mara nikitema mate yaliyo bakia mdomoni yenye mchanganyiko wa sumu

    Kwa kupitia kioo kilichopo pembeni nikashuhudia watu wanne wakiingia ndani ya bafu wakiwa na nondo mikononi huku miili yao wakiwa wameichora chora kwa rangi nyeusi huku wakiwa wamevalia hereni wenye masikio yao na pua zao japo ni wanaume ila sikuelewa kilicho wafanya kuvaa hivyo ni nini.Japo nimeishiwa nguvu kwa kiasi fulani ila nikahisi wana mpango mbaya na mimi kwani walinong’onezana kwa muda kisha wakaanza kupiga hataua za taratibu za kunifwata sehemu niliyo simama na kabla wawajanifikia nikaeuka kwa teke kali lililotua kicwani kwa mwenzao mmoja aliyekuwa ametangulia mbele na kumpeleka chini na kumfanaya aanguke chini na kuwafanya wezake kunifwata kwa kasi huku wakiyarusha magongo yao na kunifanya niwe na kazi ya ziada ya kuyakwepa kila walipo yarusha

    Nikajikaza katika kurusha ngumi ambazo ziliwapata kila aliye jaribu kuisogeza sura yeke mbele yangu.Japo nao wanafanikiwa kunipia kwa magongo kwenye mgono wangu ila na mimi nikajikaza kufanya juhudi ya kuwapia mapigo mazito yaliyo wachanganya kiasi kwamba watatu wakawa wameanguka chini na akabaki mmoja akiwa ameishika kisu huku akiwa anantetemeka,Nikakipiga teke mkono wake ulio shika kisu na kumfanya akiachie kisu na kikaangukia pembeni na akabaki akiwa amesimama,Nikaunyanyua mguu wangu wenye bastola kisha nikaichomoa na kumelekekezea na kumfanya azidi kupagawa kwa woga

    “Nani aliye watuma?”

    Nilimuuliza kwa sauti ya ukali huku nikitumia lugha ya kingereza

    “Ha...jatu..tutuma mtu”

    “Una uhakika”

    “Ndio”

    Nikaikoki bastola yangu na kumeelekezea na kumfanya atetemeke zaidi na akapiga magoti huku akilia

    “Ni bosi huwa kila mteja mgeni anaye ingia humu ndani tusiye muelewa tunamuwekea sumu ya kisha tunamchuulia pesa zake”

    “Bosi wako anaitwa nani?”

    “Lilian”

    “Yeye ndio mmiliki wa hii hotel?”

    “Ndio”

    “Kwa hiyo na mimi muliniwekea sumu?”

    “Nd...io”

    Nikamtazama kwa muda kisha nikaichomeka bastola yangu kiunoni na nikapiga teke la kifuna akawaangukia wezake na akabaki akiwa amelala huku damu zikimtoka puani.Nikanawa mikono yangu kisha nikajimwagia maji kichwani ili kupunguza joto kali lililo tokana na sumu na kupumzika kwa dakika tati kisha nika kufungua mlango wa chooni na kwenda nje ila kabla sijaufika mbali na vyoo vya wanaume nikamshuhudia Lilian akimalizikia mgongo akiingia kwenye vyoo vya wasichana.Nikaichomoa bastola yangu na kupiga hatua hadi kwenye mlango wa vyoo vya wanawake na kusimama nikimsubiri Lilian atoke.Kila muda ulivyozidi kukatia ndivyo Lilian alivyo kawia kutoka ndani ya chuo na wasichana waliingia na kutoka ile yeye hakutoka.Uvumilivu ukanishinda nikakitoa kitambulisho changu FBI na kukining’iniza shingoni kisha nikaingia ndani na kuwakuta wasichna wakimsaidia mmsichana mmoja aliye vuliwa nguo na kuwa kama alivyo zaliwa na kunifanya nistuke baada ya kuziona nguo za Lilian zikiwa pembeni kwenye ndoo ya kuwekea uchafa.Nikatoka kwa haraka chooni na kusimama nje huku nikimtazama kila msichana aliyopo kwenye eneo la karibu na choo na nikatambua nilazima Lilian alitoka nikiwa nimesimama pele pale nje ya choo pasipo mimi kujua

    Nikapata wazo la kwenda kwenye ukumbi na kwa baati nzuri nikamuona mke wa raisi wa Pakistan akiwa amesimama kwenye pembe ya ukuta wa ukumbi na kunifanya nizidi kupiga hataua za haraka.Hatua chache kabla sijamfikia kikastukia teke kali likitua kifuani kwangu na kuniangusha chini n kuwakumba baadhi ya watu wanao cheza ngoma za kispain na macho yangu yakalishuhudia jitu kubwa lenye misuli likisimama mbele yangu na kuninyanyua na kunipiga kuchwa na kuwafanya watu wanao cheza ngoma kuacha kucheza na kutuwekea duara huku wakishangilia.Nikamuona Lilian akiwa amevalia sweta lenye kofia akisimama pembeni ya mke raisi wa Pakistan huku akiwa amemuwekea bastola ya mbavu ilitomfanya mama wa watu kutulia kimya.

    Nikasimama huku damu za pua zikinichuruzika na kukaa mkao wa kupigana huku viganja vyangu vikiwa vimekunja ngumi na wala sikujua bastola yangu imeangukia wapi jitu likanifwata kwa fujo na kujikuta nikijitahidi kulipiga ngumi za tumboni ila nikashindwa kuelewa kama huyu ni mtu wa kawaida au laa kwani hakutikisika na kikastukia chupa ikitua kichwani kwangu na kunifanya nianguke chini na kujikuta nikianza kuliona giza kwenye macho yangu na nikapoteza fahamu



    ***

    Nikayafumbua macho yangu taratibu na kujikuta nikiwa nimezungukwa na watu sita wenye miili iliyo jazia msuli huku mikono yangu ikiwa imedugwa pigu na miguu yangu ikiwa imefungwa mnyororo mgumu huku mwilini mwangu nikiwa sina nguo hata moja na baada ya muda kidogo nikamuona Lilian akija huku amemshika mke wa raisi wa Pakistan nywele zake na kumvuta na kumfanya mama wa watu kupiga kelele za kuomba msaada,Akamsukumia mke wa raisi na akany kwa na baunsa mmoja kisha Liliana akaichukua video camera ndogo aina ya HDV na kuiwasha na kukabidho baunsa mmjo.

    “Eddy unajihisi wewe ni mjanja sana zaidi yangu?”

    Lilian alizungumza huku akiniinamia na mikono yake ikaanza kunishika shika kifuani kwangu

    “Eddy mimi sina moyo wa kumpenda mwanaume wa aina yoyote na usione jinsi ulivyo nivua nguo ndio utafanikiwa kunitawala mimi hicho kitu kwangu ni kigumu sana......Umemfanya kaka yangu kupata ajali mbaya na sasa yupo hospitalini basi na wewe leo nahitaji ucheze mchezo mmoja utakao mfurahisha raisi wako aliye kutuma”

    Lilian akasimama na kwaishara akamuamrisha baunsa mmoja kumvua nguo mke wa raisi wa Pakistan na akabaki kama alivyo zaliwa na bansa aliye na video camera akaendelea kuyachukua matukio yanayo endelea.Lilian akawaomba mabaunsa wanne walio bakia kuvua nguo zao na wao wakabaki kama walivyo zaliwa na wakaanza kuishika shika koki zao hadi zikasimama

    “Eddy kuna kamchezo kadogo unacho takiwa kukafanya hapa ni chagua moja kati ya haya mawili ninayo kwenda kukuambia.......Moja ni kufanya mapenzi na mke wa rahisi kinyume na maumbile na video yako nimtumie raisi wako aliye kutuma au mbili hawa jamaa wanne wakuingilie wewe kinyume na maumbie kwa zamu hadi haja zao za mwili ziwaishie”



    Lilian alizungumza kwa sauti iliyo jaa dharau na taratibu akaniinamia huku kidole chake akikipitisha kwenye shavu langu na kwaharaka nikainyanyua mikono yangu na kuipitisha kwenye shingo yake na kumkaba kwa kutimia pingu kitendo kilicho mfanya kuanza kupiga kelele na kwajinsi anavyozidi kupiga kelele na mimi nilivyozidi kumkaba

    “Waamrishe watu wako kusimama mbali na mimi”

    Lilian akafanya kama nilivyo muagiza na watu wake wakasimama mbali na mimi huku wakionekana kuisubiria nafasi yoyote ya kuweza kunivamia mimi

    “Mama nakuomba uvae nguo”

    Nilizungumza kwa kutumia lugha ya kingereza na kumfanya mke wa raisi kuvaa tisheti kubwa la baunsa mmoja lililo mfanyakuonekana kama amevaa gauni.Nikaendelea kumkaba Lilian kiasi kwamba rangi ya mwili wake ikaanza kuwa nyekundu kwa maumivu.Tukasimama huku nikiendelea kumkaba Lilian kiasi kwamba akaanza kuishiwa na nguvu.Mke wa raisi akamsogela baunsa mwenye video kamera na kuichukua kisha akatoa akatoa kijimkanda kidogo kinacho hifadhia vitu vina vyo rekodiwa(divu) na kukishika nikamuomba atafute funguo kwenye suruali za mabaunsa zilizopo chini na kwaharaka akaanza kuikangua suruali moja baada ya nyingine na akafanikiwa kuipata fungua ya gari na akaendelea kukagua kwenye susuruali nyingine na akafanikiiwa kuipata funguo ya pingu niliyo fungwa

    “Wote laleni chini?”

    Nilizungumza kwa lugha ya kingereza na kuwafanya mabausa kunishangaa shangaa na inavyo onekana hawaitambui lugha ya kingereza.Lilian akazungumza kwa lugha yenye maumivu na ya yakukoroma na kuwaamrisha mabaunsa wake kulala chini na wakatii.

    “Maari yenu yapo wapi?”

    “Hu.....k...u”

    Lilian aliznungumza kwa sauti ya kukata kata kama mtu anaye taka kukata roho na moja kwa moja tukaelekea kwenye sehemu aliyo tuonyesha.Mkwe wa raisi akafungua mlango wa gari alilo tuonyesha Lilian na sote tukaingia ndani ya gari

    “Mama unaweza kuendesha?”

    “Ndio”

    Mke wa raisi wa Pakistan akawasha gari na tukaondoka wa kasi katika eneo tulilopo na kwakutumia pembezoni mwa kiganja cha mkono naikampiga Lilian kwenye mshipa wake wa fahamu na kumfanya apoteze fahamu.Mke wa raisi sikujua ni wapi anapo elekea ikanilazimu kumuuliza

    “Tunaelekea wapi?”

    “Kwenye ubalozi wa Pakistan kuomba msaada zaidi?”

    “Hapana nakuomba usiende huko?”

    “Kwa nini?”

    “Sihitaji uende huko?”

    “Mimi nahitaji twende huko”

    “NIMESEMA SIHITAJI UENDE KWENYE UBALOZI HUO”

    Mke wa raisi hakutaka kunielewa zadi ya kuongeza mwendo wa gari na kwa haraka nikapita siti ya mbele na sikuona aibu kama nipo kama nilivyo zaliwa cha msingi ni kuweza kumzuia mke wa raisi kufanya anacho kihitaji kukifanya kwa wakati huu.Mguu wangu mmoja nikauingiza katikati ya miguu ya mke wa raisi na kuusukuma mkuu wake mmoja na kukanyaga breki za gari kwa nguvu na kulifanya ari kuaanza kuserereka na kwa harakaka nikapiga mshipa wake wa fahamu uliopo shingoni mwake na kumfanya apoteze fahamu kama Lilian ambaye hadi sasa hivi hajitambui.Na kwakutumia nguvu nikajitahidi kulisimamamisha gari pasipo kuanguka na nikafanikiwa na kwaharaka nikamnyanyua mke wa raisi na kumuweka siti nyuma alipo Lilian

    Kitemdo cha gari langu kusimama kwa kupitia kioo cha pembeni cha gari nikaziona gari mbili za polisi zikija kwa kasi katika eneo nililo simama na kwaharaka nikamsogeza mke wa raisi pembeni na kuliwasha gari ila kwa bahati mbaya halikuwaka na tayari gari za polisi zimesha simama mbela yangu na polisi wapatao wanne wakashuka huku wakiwa na bunduki mikononi na wakiniamuru niweze kushuka

    Nikawatazama kwa muda nataratibu mkono wangu nikapeleka sehemu yenye funguo ya gari kisha kwa haraka nikaliwasha gari na kulirudisha kwa nyuma huku nikiwa nimeinama chini na kuwafanya askari kuanza kunifyatulia risasi zao kiasi kwamba nikioo cha mbele kikapasuka ila sikujali zasi ya kuligeuza gari langu na kugeuka tulipo tokea na kwa kasi nikaanza kuliendesha huku nikiwa ninakatiza kwenye mitaa yenye nyumba zilizo babana na kwa bongo tumezoea kuziita nyumba hizo ni uswahilini na kufanikiwa kuiingiza gari kwenye kijiuchochoro kidogo na kuwafanya askari wana nifukuza na magari yao kupita pasipo kuniona,cha kumshukuru Mungu katika sehemu niliyo simama kuna kamba nyingi za nguo na nikatokati ya gorofa mbili ambazo huishi watu wangi wenye maisha duni

    Nikautoa mkono wangu mmoja na kuvuta suruali iliyo anikwa kwenye kama hizo na kuivaa kisha nikashuka kwenye gari na kuwafanya watu waliopo kwenye eneo hili kuanza kunishangaa huku wakiwa wananong’onezana nong’onezana.Nikawachungulia Lilian na mke wa raisi na kuwakuta wapo salama kila mmoja anapumua japo wamepoteza fahamu ila hapakuwa na aliye jeruhiwa.Akanisogelea kijana mmoja mwenye nywele nyingi na anaonekana ni machachari sana

    “Kaka uanahitaji msaada?”

    “Ndio....Ninaweza kupata uwanja wa ndege ulio karibu na hapa?”

    “Ndio kuna uwanja unaitwa AUGOSTO SEVERO INTERNATIONAL AIR PORT”

    “Kwani hapa ni wapi?”

    “Hapa ni Sao Paulo do Potengi ila kuna urefu kidogo hadi sehemu ulipo uwanja wa ndege”

    “Unaweza kunipeleka?”

    “Ndio ila utaidi unilipe na kwa usalama zaidi inabidi kuutumia usafiri wangu na sio wakwako”

    “Sawa nitakupa kiasi utakacho kihitaji”

    “Nisubiri”

    Jamaa akaondoka na mimi nikarudi ndani ya gari na kumsubiria baada ya dakika kama tano jamaa akarudi akiwa na gari jeusi na kulisimamisha mbele ya gari langu kisha akashuka na kuniomba niingie kwenye gari lake.Nikafangua mlango nakumshusha mke wa raisi huku nikiwa nimembeba begani na kumingiza ndani a gari kisha ninirudi na kumbe Lilian na kumuingiza ndani ya gari

    “Broo inabidi pesa iongezeke”

    “Sawa”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimjibu jamaa huku nikiwa ninajijua sina hata shilingi kumi mfukoni kwangu na safari ikaanza huku jamaa akipita njia anazo zijua yeye mwenyewe

    “Hao ni kina nani?”

    “Ni ndugu zangu”

    “Ndugu zako mbona hata hufanani nao?”

    “Yaaa ila tambua kuwa ni ndugu zangu”

    “Mimi ninaitwa Joo wewe je?”

    “Lee”

    “Ahaaa sasa sasa una hati za kusafiria?”

    “Sinai la ninaweza kupata ndege ya kukodi?”

    “Za kukodi zipo...kwani wewe unaelekea wapi?”

    “Pakistan”

    “Ohoo kama ni Pakistan basi utapata japo ni za gharama sana”

    “Je tunaweza kupata ndege hata ya kuia hivi?”

    Nikastukia jamaa akisimamisha gari huku akishusha pumzi nyingi akionekana kustushwa na swali langu

    “KUIBA.....Mmmm mbonaitakuwa ni ngumu sana?”

    “Kwa hiyo siwezi kupata?”

    “Ngoja kuna jamaa zangu ni watengenezaji wa ndege ninaweza kuzungumza nao sasa una pesa ya kuwalipa?”

    “Ndio”

    “Basi ngoja tugeuze safari kwani wao wanaishi Pernambuco”

    “Sawa”

    Safari ya kuelekea walipo jamaa zake ikaanza na kutokana si mwenyeji sana wa nchini Brazil na baada ya muda tukafika kwenye jengo kubwa na Joo akapiga honi ya gari lake na eti likafunguliwa na akaaingiza gari lake

    “Musishuke hadi nitakapo kuambia sawa?”

    “Sawa”

    Joo akashuka na kusalimiana na wezeke ambao wanajishuhulisha kwenye kuchomelea chomelea vyuma na huku sehemu nyingine kukiwa na ndege ndogo ndoo zinazo tengenezwa.Joo akaingia kwenye moja ya ofisi na kukaa kwa dakika zaidi ya tano kisha akatoka na kuja kwenye gari na kuniomba nishuke na nikafanya hivyo huku nikiwa kifua wazi na tukaingia kwenye chumba na kumkuta jamaa mwenye mwili mkubwa ulio chorwa chorwa michoro mingi akiwa amekaa kweye kiti kikubwa chenye uwezo wa kuhimili uzito wake huku pembeni yake kukiwa na wasichana wawili wali valia chupi na sidiria wakimshika shika kwenye sehemu za mwili wake

    “Huyo ndio anahitaji ndege”

    Jamaa alizungumza kwa lugha ya kingereza huku sauti yake ikiwa ni nzito kiasi kwamba inaogopesha unapo isikia

    “Ndio bosi”

    “Mbona anaonekana hana chochote?”

    Joo akanitazama akishindwa kulijibu swali la bosi wake ikanilazimu mimi kumjibu

    “Pesa mimi ninayo labda museme munahitaji kiasi gani?”

    “Milioni 65 za kimarekani kwa ndege aina ya jeti inayo ingia watu 15”

    “Je ninaweza kukodi?”

    “Ndio ukikodi itakuwa ni milioni 12 za kimarekani”

    “Bora kukodi ila munaweza kunisaidia”

    Jamaa akanipa simu yake na nikaziingiza namba ya simu za Mahamoud na ikaaita baada ya muda akaipokea

    “Nani?”

    “Mimi Jack Lee”

    “Ohh nilikuwa ninakutafuta kwa muda sijakupata vipi umefanikiwa?”

    “Ndio na ninao wote wawili?”

    “Nani na nani?”

    “Shemeji yako na binti aliye mteka shemeji yako”

    “Ohh basi fanya urudi”

    “Nahitaji ndege ya kukodi itakayo weza kunirudisha hadi huko”

    “Unahitaji kiasi gani tukiingize kwenye hilo shirila unalo taka kukodi ndege”

    “Wanahitaji kiasi cha milioni 15 za kimarekani”

    “Sawa tutumie namba yao ya akaunti na ndani ya dakika kumi na tano tutakuwa tumezituma”

    Nikaibana sehemu ya kunasia sauti kwenye simu na kumuomba bosi wa Joo kunipatia namba yao ya akaunti na akaniandikia kwenye kikaratasi na kuniwekea mbela yangu na kuanza kumtajia Mahamoud tarakimu za akaunti na akaniomba nisubiri ndani ya dakika alizo niambia pesa itakuwa tayari kisha nikakata simu na kumkabidhi bosi wa Joo simu yake

    “Kuna ongezeko la milioni tatu na utanipatatia mimi sawa?”

    “Sawa”

    Ndani ya dakika ishirini na tano simu bosi wa Joo ikaaita na akaniambia ni namba yangu ndio inapiga.

    “Tayari tumeziingiza”

    “Sawa”

    Nikamuomba bosi wa Joo kuziangalia kwenye akaunti yake kupitaia kumpyuta yake iliyopo mezani kwake na kukuta meseji inayo ashiria kuwa pesa walizo zihitaji zimeingia kweye akaunti yake.

    “Una akaunti na wewe nikuingizie hizi pesa zako”

    “Sina ila sininaweza kufungua akaunti kupitia mtandao”

    “Ndio ila kwa urahisi kuna benki moja ipo uinereza inaitwa Co-opetarive Bank hiyo karika maswala ya kufungua akaunti kwa kupitia mtandano ni rahisi sana”

    “Sawa ninaomba msaada katika hilo”

    Joo akapewa jukumu la kufanya kazi ya kunifungulia akaunti kwa njia ya mtandao na ndani ya dakika kumi na tano wakawa amefanikiwa kunifungulia akaunti yangu ya benki na namba za siri nikaziiniza pasipo wao kuziona kisha bosi wa Joo akazituma pesa zilizo zidi kwenye akaunti yangu na nikahakikisha zimeingia na mimi nikamtumia Joo laki moja za kimarekani kwenye akaunti yake kama malipo kisha tukatoka kweye ofisi na kurudi sehemu lilipo gari na kuwakuta Lilian na mke wa raisi wakiwa hawaja zinduka.Nikambeba begani kisa mke wa raisi akabebwa na Joo begani na tukaongozana na bosi wake hadi kwenye kiwanja kikubwa chenye ndege nyingi na tukaingia kwenye ndege moja nzuri ya kisasa kisha tukawakalisha Lilia na mke wa raisi kwenye siti na kuwafunga mikanda kisha Joo na bosi wake wakashuka na nikabaki na rubani wawili wenye asili ya kizungu

    “Karibu bwana Jack Lee”

    “Asante”

    “Tunaelekea nchi gani?”

    “Oman”

    “Sawa”

    “Bwana Jack Lee tunakuomba ufunge mkanda ndege inaanza safari yake”

    Rubani mmoja aliniambia na nikakaa siti ya karibu na Lilian na kufunga mkanda na taratibu ndenge ikaanza kutembea ardhini na baada ya muda ikaanza kuiacha ardhi ya nchini Brazil na ndani ya dakika kadhaa tukawa angani na Lilian akazinduka na akabaki akinitazama akikosa la kuzungumza

    “Unajisikiaje?”

    “Kwani nipo wapi”

    “Kwenye ndege”

    “Tunaelekea wapi?”

    “Hupaswi kujua”

    Lilian akataka kunyanyuka ila nikamzuia kwa mkono huku mkono wangu ukiwa umeyashika maziwa yake

    “Lilian huwezi kucheza na mimi”

    Lilian akatulia kimya huku akichungulia nje kwa kupitia dirisha la kioo lililopo pembei yake na asielewe ni wapi tunapo elekea.Mke wa raisi wa Pakistan akazinduka huku akionekana kuchoka.Nikachukua koti kubwa lililopo kwenye siti yangu na kumpa ajifunike ila macho yake yalipo muona Lilian akaanza kukunja sura kisha akafungua mkanda wa siti na akanyanyuka kwa hasira na kutaka kumvamia Lilian ila nikamzuia

    “Wewe msichana ni mshenzi sana nitahakikisha unafungwa”

    “Huwezi kunifunga wewe mwanamke”

    Lilian alizungumza huku akisimama kwenye na kutaka kumvamia mke wa raisi na ikanilazimu kumuachia mke wa raisi na kumshika Lilian ambaye mziki wake ninaufaamu vizuri na nikamkalisha kwa nguvu kwenye siti.Nikastukia kitu kizito kikipita kwenye sikio langu na kumfanya Lilian kuinama chini na kuishuhudia mtungi wa gesi(fire extinguisher) ukikipasua kioo cha dirisha la ndege na kusababisha upepo mkali kuingia ndani ya ndehe na kutufanya turushe na mlio wa kelele ukaanza kusikika kwenye vipaza sauti vya ndege na taa zake zikazima na zikawaka taa nyekundu na ndege ikaanza kutumba huku ikaanza kubinuka binuka na kusababisha vioo vingine kupasuka na upepo ukaizidi kuingia ndani ya ndege na kuifanya kunza kwenda chini kwa kasi ya ajabu



    Kila mmoja akaanza kuliita jina la Mungu wake kwa jinsi anavyo weza yeye mwenyewe ili hata kama kuna uwezekano wa muujiza wowote wa kuokoka kweye ndege hii inayo kwenda chini kwa kasi kuweza kutokea ili roro zetu ziweze kusalimika.Hali yakujigonga kwenye sehemu mbalimbali za ndege zilizo sababishwa na mzunguko wake ikaendelea kiasi kwamba kelele za mkwe wa raisi ambazo nilikuwa kizisikia masikioni mwangu akiliita jina la MUNGU wake sikuweza kuzisikia tena kiasi kwamba nikaanza kupata wasiwasi kuwa kuna kitu kibaya kilicho mpata tofauti na sisi.Hata Lilian naye aliniita mara mbili tu na kusikia akizungumza neno NAKUFA na sikuisikia tena sauti yake

    Katika kufumba na kufumbua nikastukia nikiusikia mlio mkubwa wa ndaege yetu kugonga kwenye maji mengi na taratibu nikaanza kuona maji mengi yakiingia ndani ya ndege yetu na kusababisha giza kali ambalo sikuweza kumuona mtu wa aina yoyote zaidi ya kuanza kutafuta upenyo wa aina yoyote katika kuyaokoa maisha yangu huku ndege yano ikaanza kuzama taratibu kwenda chini.Sikujali majereha mengi niliyo nayo mwilini mwangu ila cha msingi ni kuweza kuiokoa roho yangu.Nikapata nafasi ya dirisha la ndege lilopasuka kioo chake japo ni dogo nikatumia nduvu zangu za kila ina kujipennyeza hadi nikafanikiwa kutoka ndani ya ndege kitendo ambacho kilinichosha zaidi na kujikuta nikipoteza pumzi nyingi na maji kadhaa yakaanza kuingia mdomoni mwangu na taratibu nikajikuta nikiyafumba macho yangu na nguvu zikiniishia kabisa na nikaanza kuelee juu ya maji na giza jingi likanitawala machoni mwangu na sikujua ni kitu gani kinacho endelea kwenye eneo nililopo



    ***

    Kelele kwa mbali zikaanza kusikika masikioni mwangu ila kila nilopo jaribu kuyafumbu macho yangu sikuona kitu cha aina yoyote zaidi ya giza zito lilolo nitawala machoni mwangu na kujikuta nikistuka na wasiwasi ukianza kunitawala.Nikajaribu kuinyanyua mikono yangu ili nijishike machoni ila haikuweza kunyanyuka kutokana na uzito na maumivu makali niliyo yahisi kwenye mikono yangu.Nikaanza kupiga kelele za kuomba msaada kwa watu na baada ya dakika kidogo nikasikia sauti ya msichana ambaye kwa kukadiria umri wake utakuwa ni chini ya miaka 18 akizungumza lugha ambayo sikuweza kuielewa na baada ya muda kidogo nikasikia sauti za watu wazima wakizungumza pembeni ya kitanda changu ila kitu kinacho tufanya tusielewane ni lugha kutofautiana.Nikasikia ukimya ukitawala ndani ya chumba huku sauti ya mwanaume akizungumza na msichana mwengine ambaye sauti yake sikuweza kuisikia awali kisha msichana huyo akaanza kuzungumza kwa lugha ya kingereza niliyo ielewa vizuri

    “Unajua kuzungumza kingereza?”

    “Ndio”

    Akawatafsiria watu alio kuwa nao kwa lugha ambao kwa upande wangu sikuweza kuwaona zaidi ya giza jingi lililo tanda kwenye macho yangu na sikujua kama nimekuwa kipofu au laa.

    “Unaitwa nani?”

    “Eddy”

    “Unatokea wapi?”

    “Brazil”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mimi naitwa Juliana na hapa upo nchini Suriname”

    “Suriname ndio wapi?”

    “Ipo kwenye bara la Amerika ya kusini kaskazini kidogo mwa nchi ya Brazil ambayo ndipo unapo tokea wewe”

    “Nimefikaje fikaje”

    “Ni history ndefu kidogo ila kwa ufupi tu ni kwamba uliokotwa na baba yangu siku tatu zilizo pita katia bahari ya Atlntic kusini wakati wa usiku alipokuwa akivua na wezake...Ndipo wakaamua kuchukua jukumu la kukusaidi na kukuleta hapa na siku zote mbili za nyuma haukuweza kuonyesha matumaini yoyote ya kuishi kutokana na mwili wako kuharibika vibaya kwanye sehemu za mikononi na usoni”

    Ikawa ni habari nyingine mpya katika maisha yangu na sikujua ninaonekana vipi nikatamani nipate japo nafasi ya sekunde kadhaa kuuona mwili wangu jinsi ulivyo kwa maana ninahisi kuwa nipo kwenye muonekano mbaya kama nilivyo ambiwa

    “Kwa hiyo mimi nimekuwa kipofu?”

    “Hapana haujawa kipofu”

    “Ila....mbona sioni sasa?”

    Nilizungumza huku nikiwa ninalia kwa ndani na wala sikuhisi machozi yakimwagika kwenye mashavu yangu zaidi ya kusikia maumivu makali kwenye mishipa ya kichwa changu

    “Ila kuna dawa ya asili umepakwa kwenye macho yako ili yaweze kurudisha uwezo wa kuona tena”

    “Itachukua muda gani?”

    “Ndani ya wiki zaidi ya mbili hadi tatu na mikono yako imevunjika kwahiyo imefungwa magongo maalumu ili kuiwezesha kunyooka na kuirudisha katika hali yake ya kawaida”

    Nikabaki kimya huku nikijitadhimi mwili wangu kwa jinsi unavyo onekana ila sikupata picha halisi kichwani kwangu zaidi ya kuendelea kulia na kujikuta nikianza kumuomba Mungu kuweza kushusha baraka zake katika kuniponya

    Siku zikazidi kukatika na kwenda mbele huku kila siku nikianza kuhisi mabadiliko mapya kwenye mwili wangu hii ni kutokana na dawa ambazo ninapakwa kila asubuhi kwa mtindo wa kuchuliwa kwenye mikono yangu japo sichomwi sindano yoyote ya ganzi ili kuepusha kuhisi maumivu ila nikawa na kazi ya kuvumilia maumivu makali ninayapata kwa muda wa kuchuliwa na mzee ambaye ameniokota ila sikuweza kuzungumza naye kutokana na yeye kuto kuwa na uwezo wa kuzungumza kingereza.Taratibu mikono yangu ikaanza kupata nguvu ya kunyanyua japo kikombe cha chai na mazoezi maalumu ya kunyanyua kindoo kidogo chenye maji nusu yakaanza kila siku asubuhi na jioni hii ni kuirudishia mikono yangu nguvu na endapo nitazembea basi ninaweza kuparalaizi(uwezo wakupoteza nguvu katika sehemu za mwili) kitu ambacho sikuhitaji kinitokee kwenye maisha yangu

    Siku zote nilizoea kutembelea na fimbo ya kuniongoza njia kwani macho yangu bado hayakuweza kuona kabisa,Na rafiki yangu wa karibu akawa ni Juliana ambeye ndio anajua kuzungumza kingereza lugha pekee inayoweza kutuunganisha mimi na yeye na kuelewana naye vizuri tofauti na wezake.Ni siku ya jumapili ambayo ndio siku yangu ya kwanza kutoka kwenda kanisani tangu nilipo ukotwa baharini na nifuraha kubwa kwa Juliana ambaye ameninunulia nguo mpya

    “Eddy umependeza?”

    “Asante July kwani ni watu wachache sana wenye roho za kibinadamu kama wewe na familia yako japo siwaoni kwa macho yangu haya mawili ila ninaamini Mungu atanipa uwezo wangu wa kuona”

    “Usijali Eddy Mungu tunaye muabudu na kumlilia kila siku ninaamini atayasikia maombi yetu na utapona na kurudi katika maisha yako ya kawaida”

    “Kweli hata mimi ninaliamini hilo ndio maana kila siku ninaomba na kusali ili niweze kurudi katika hali yangu ya kawaida”

    Tukaendelea kuzungumza mengi huku tukiwa tanatembea kuelekea kanisani kwenye ibada ya asubuhi huku akiwa amenishika mkono kwa ajili ya kuniongoza

    “July hivi hapa kunaitwaje?”

    “Kuna itwa Pokigron ni mji ulio jaa wavuvi wengi”

    “Ahaa kunaonekana ni kuzuri ehee?”

    “Kidogo ila sio sana ila kwa sisi tumesha zoea kuishi hapa”

    “Aaaa natamani hata siku niweze kupaona”

    “Usijali kwa hilo Eddy utaweza kupaona

    Tukafika kanisani na Juliana akaniongoza hadi kwenye benchi za kukaa na kwakutumia fimbo yangu ya kutembelea nikahakikisha ni kweli sehemu ninayo kaa ni kwenye bechi na taratibu Juliana akanishika mkono na kunikalisha.Mahubiri yakaanza huku wakizungumza kwa lugha yao na kidogo mchungaji anaye ongoza ibada hiyo akawa anachanganya na kingereza kidogo na mimi nikaawa nina elewa anacho kizungumza na kitu kikubwa anacho kisisitizia leo Mungu atatenda miujiza kwa wale wenye matatizo mbali mbali.Ukaanza kuibwa wimbo ambao kwa jinsi unavyo imbwa kwa utaratiu wa hali ya juu nikagundua ni wimbo wa kuabudu.

    Juliana akanishika mkono na akaninong’oneza na kuniambia kuwa mchungaji amewaomba wenye matatizo kupita mbele.Moyoni mwangu nikasikia nguvu kubwa ikinisukumu nipite mbele na sikuidarau zaidi ya kuitii na taratibu nikapita mbele huku Juliana akiwa amenishika mkono wangu na tukasimama kwa pamoja.Watu wakanyamaza kuimba wimbo na mchungajia akaanza kuomba hapo ndipo nikagundua tupo wengi tulio pita mbele ya kanisa kwani kwa jinsi mchungaji anavyo omba ndivyo jinsi watu wenye mapepo ndivyo wanavyo anguka na kupiga kelele.Nikahisi kitu kingine kikipita kwenye mwili wangu na kuhisi moto mkali ukiipiga mikono yangu na kunifanya nistuke kiasi na kuiachia fimbo niliyo ishika na ndani ya dakika nikaihisi imepata nguvu na maumivu yakanitoweka

    Misuli ya mikono yangu ikaanza kukunja kama kawaida na nikaanza kuinyanyua juu kitendo ambacho sikuweza kukifanya na kabla sijasimama mbele ya kanisa nilikuwa nikijikaza tu katika kuishika fimbo yangu na sikutaka mtu yoyote ajue juu ya maumivu yangu hii nikuhofia kuwakatisa tama Juliana na familia yao ambao wananihudumia kwa juhudi zao zote.Tukaombwa turudi kwenye sehemu zetu za kukaa,ila kwa upande wa macho yangu sikuona lolote lililo tokea ila nikajikuta nikimshukuru Mungu kwa uponyaji wake wa mikono yangu.

    Tukarudi nyumbani huku njiani nikiwa nina furaha sana kiasi kwamba hata mwendo wangu wa kutembea ukaongezeka na kumfanya Juliana mara kwa mara kunipunguza mwendo wangu kwani kuna kipindi nilinusurika kuingia kwenye mtaro ulipo kando kando ya barabara.Tukafika nyumbani na kukuta chakula cha mchana tayari

    “Eddy tule haraka kuna sehemu ninataka twende tukapunge upepo”

    “Wapi?”

    “Baharini kidogo na wewe leo ukapate pate kajiupepo”

    “Sio mbali na hapa?”

    “Hapana ila kwa hapa nyumbani hadi baharini sio mbali ila hiyo sehemu ninayo itaka mimi ni kwenye fukwe zilizo tulia mbali kidogo na nyumbani hapa”

    “Sawa ila umemuaga baba?”

    “Baba hana neno na isitoshe na mimi ni mtu mzima”

    “Sawa”

    Tukamaliza kula na tukaaga nyumbani kwao na safari ya kuelekea anapo sema yeye ikaanza na njiani watu wengi wakaanza kupiga miluzi ambayo sikujua ina maana gani

    “Mbona watu wanashangilia?”

    “Ahaa vijana wa huku uwazoee kwa maana wanapenda sana kutongoza wasichana na leo kusema kweli hata mimi nimependeza”

    “Ahaa daaa natamani ningekuona”

    “Usijali ipo siku utaniona Mungu ni mwama wa kila jambo”

    “Kweli.....Vipi tunakaribia kufika?”

    “Kama dakika tatu hivi zimebakia tutakuwa tumesha fika”

    Kweli ndani ya muda alio usema Juliana tukawa tumefika kenye fukwe za bahari ambazi Juliana alinieleza hapo awali na ilikuwa ni rahisi kwangu kuelewa kwamba sehemu tuliyopo ni salama na haina watu hii ni kutokana na mbinu za kijesi nilizo fundishwa nchini Pakistani kwani masikio yangu kwa wakati wote yakawa na kazi ya kusikilizia endapo hata akitokea mtu tofauti na Juliana katika eneo tulilopo nitafahamu

    “Eddy hapa ni kwenye fukwe ambayo ninaipenda sana na mara nyingi ninapokuwa ninamawazo huwa ninakuja huku kupoteza mawazo ya hapa na pale”

    “Hivi kuna watu?”

    “Hapana watu hii ni kutokana na jinsi ya kulivyo mafichoni”

    “Ahaaa July hivi wewe unafanya kazi gani?”

    “Mimi ni mwalimu wa shule za msingi na pale nyumbani kwetu mimi ndio wakwanza na nina wadogo zangu sita wananifwata wa kike wawili na wakiume wanne jumla tupo saba......Wewe jee mumezaliwa wangapi kwenu””

    “Nimezaliwa peke yangu”

    “Ohhoo hongera sana.....kwa maana sisi maisha yetu ni magumu sana kiasi kwamba mimi na baba pale nyumbani tumekuwa tegemezi”

    “Sasa wewe kama wewe una mpango gani kwenye maisha yako?”

    “Mimi nilifaulu masomo ya juu ya chuo katika maswala ya utalii ila kutokana na hali duni ya maisha tuliyo nayo skuweza kwenda na hapa nimeamua kujishikiza kwenye moja ya shule ili kidogo nikipata pesa ninakwenda kusoma”

    “Kwani unakwenda kusoma wapi?”

    “Italia ndipo nilipo panga kusoma na itakuwa ni rahisi sana kwangu kupata kazi itakayo niwezesha katika kuisaidia familia yangu na kuikomboa kwenye janga kubwa la umasikini”

    Nikamsimulia Juliana historia yangu ya maisha kwa ufupi ila kuna baadhi ya mambo sikuweza kumuambia ikiwemo swala langu ugaidi.Hadi ninamamaliziz kumsimulia shida na tabu nilizo zipitia nikahisi Juliana akitokwa na machozi

    “July...?”

    “Bee”

    “Kwa nini unalia?”

    “Eddy kumbe umepitia matatizo makubwa kiasi hicho?”

    “Ndio na bado ninaendelea kuyapitia....Mimi sina baba wala mama na hapa sijui ni kitu gani kitakacho weza kutoke tena kwenye maisha yangu”

    “Eddy usiseme hivyo Mungu anakupenda”

    “Amen”

    Kwa kumfurahisha Juliana nikamshika pua yake na kuiminya kidogo na kugundua ana pua ndogo kiasi na kumfanya Juliana kuruka na kuaanza kucheka kisha nikamuachia mkono wake na kwa kutumia fimbo yangu niliyo itanguliza mbele nikaanza kukimbia taratibu na kumfanya Juliana kuanza kunipigia kelele za kuniomba kuacha kufanya hivyo.Kabla sijasimama naistukia migu yangu ikillivaa gogo dogo kiasi na kujikuta nikianguka kifudi fudi na uso wangu ukapiga kwenye mchanga mwingi ulipo kwenye fukwe za bahari

    “Mungu wangu Eddy umesalimika”

    Juliana alizungumza huka akunishika mngongoni na kunigauza taratibu na kabla sijamjibu nikahisi mstuko kwenye mishipa ya macho na maumivu makali yakapiata kwa wakati mmoja kwenye kichwa changu hadi nikaisi kichwa kinaweza kupasuka

    “Eddy unanisikia....?”

    “Ndio”

    “Vipi umeumia?”

    “Ngoja kwanza”

    Nikatulia kama dakika tano nikakianza kukihisi maumivu yakipungua taratibu hadi yakakatika kabisa

    “Twende ukanawe uso?”

    “Fimbo yangu iko wapi?”

    “Hii hapa”

    Juliana akaninyanyua kwa kunivuta mkono na taratibu tukaanza kupiga hatua za kuelekea kwenye maji ya bahari yalipo,Kabla hatujayafika Julinana akaniomba nivue viatu kisha akanikunja suruali yangu kwenda juu ili isiwe rahisi maji kuniingia kwenye sururali yangu.Tukaingia kwenye maji na taratibu Yuliana akaanza kuninawisha uso kwa maji ya bahari,kadri jinsi anavyoninawisha ndivyo nikaanza kuuona mwanga kwa mbali huku nyama za macho yangu zilizo ziba zikaanza kuachia taratibu.Nikaanza kuyachukua maji kwenye kiganja changu na mimi nikaanza kujiosha kwa fujo usoni mwangu na kujikuta nikianza kuyaona macho yakifumuka kiasi kwamba nikaanza kuhisi chumvi chmvi ya maji haya ya bahari kuingia kwenye macho yangu

    “Eddy taratibu unajitotesha”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Juliana alizungumza ila sikumuelewa na nikaendelea na zoezi langu la kuyaosha macho yangu huku nikiyafikicha pamoja na majo ya bahari yenye chumvi hadi yakaanza kumwaga machozi na nikaaza kuuona mwanga vizuri.Nikamgeukia Juliana na kumkuta akiwa ameinama akichota maji mengine ili aninawishe usoni na akanyanyuka taratibu huku mkono wake wakulia ukiwa na maji kwenye kiganja chake na akabaki akinishangaa kabla hajakileta kiganja chake usoni mwangu nikamshika mkono wake na kuuzuia na kumfanya azidi kunishangaa

    Mshangao wa Juliana ukanipa wakati mzuri kuanza kumtathimi uzuri wake alio pewa na Mungu,Macho yake makubwa kiasi yenye mduara umeiweka sura yake katika uzuri ulio kamilishwa na pua yake ndogo kiasi na lipsi zake zilizo ndogo kiasi ila zimekusanya nyama zilizo tengenezwa vizuri na kuzifanya kuwa na unene kiasi ulio nipa hata kigugumizi cha kuzungumza

    “Eddy unaona?”

    “NDIO”

    “Kweli......!!?”

    “Ndio July”

    “Hivi idole vingapi?”

    “Viwili”

    “Hivi?”

    “Vitano”

    “Nimevaa nguo za rangi gani?”

    “Sketi nyeusi na shati jeupe lenye madoa doa meusi”

    Juliana akanirukia kwa furha na mikono yangu ikamshika kwa nyuma kumzuia asianguke na hapa ndipo nikagundua kitu kingine kwa Juliana kwani amepewa umbo dogo kiasi ila lenye kiuno kizuri kilicho kusanya makalio makubwa kiasia mbayo yameendana na miguu ya bia.Nywele ndefu zinazo mfika mgongoni na zilizo laini na kulala vizuri kwa mchano alio uchana wa kuzipeleka nywele zake nyuma zikazidi kuipendezesha rangi yake ya mwili ambayo ni chokleti inayo ng’aa

    Nikaanza kumzungusha Juliana kwa furaha na kujikuta sote tukianguka chini huku akiwa amenilalia kifuani kwangu na sote tukabaki tukiwa tumetazamana kwa dakika kadhaa na taratibu Juliana akayafumba macho yake na kuanza kuzishusha lipsi zake hadi zikakutana na zangu na kwa upole wa hali ya juu na nikazipokea lipsi zake na kunza kunyonyana taratibu huku maji yakiwa yametufunika sehemu za miguu yatu na sehemu zetu za juu zikiwa zimelala sehemu yenye mchanga ulio lowa maji

    Juliana akazidi kuninyonya lipsi zangu na safari hii akaongeza kasi ya kuninyonya kiasi kwamba akaanza kutoa pumzi nyingi zilizo ziamsha hisia zangu za mapenzi,Mikono yangu ikaanza kazi yakuyaminya minya makalio yeke na kumfanya Juliana kuaza kuguna.Mkono wangu mmoja ukaifungua zipu ya sketi ya Juliana na kuuingiza mkono wangu na kabla sijaifikia ikulu yake nikastukia akinyanyuka kwa haraka huku akikimbia akielekea sehemu yenye majani yaliyo tulia na ikanilazimu na mimi kumfwata kwa nyuma huku nikwa nimevibeba viatu vyetu

    Nikamkuta Juliana akiwa anatokwa na machozi ambayo kwa wakati huu sikujua kama ni machozi ya furaha ama huzuni

    “July una lia nini?”

    “Siamini Eddy kama umepata uwezo wa kuona tena”

    “Mungu ameweza kuyasikia maombi yetu na leo kweli ametenda muujiza katika maisha yangu”

    “Kweli Eddy ina bidi tukatoe shukrani kanisani”

    “Kweli July”

    Nikaupitisha mkono mmoja kwenye shingo ya Juliana na kumvutia kwangu nakutaka kumbusu mdomoni ila akakwepesa lipsi zake na kujikuta nikimbusu shavuni mwake

    “Eddy wakati wake bado wa kufanya hayo unayo itaji tuyafanye”

    “Kwanini?”

    “Mimi bado ni bikra na niliapa kwa MUNGU mume wangu atakaye nipa ndio atakaye itoa hii itakuwa ni kama zawadi yangu kwake”

    “Ohoo samani kwa hilo?”

    “Hakuna tatizo”

    Kutokana imesha timu saa moja usiku ikatulazimu kurudi nyumbani taratibu na kabla hatujafika mbali kidogo na ufukwe wa bahari nikakumbuka nimeisahau fimbo yangu ya kutembela ikatulazimu kurudi na kwa msaada wa mwanga wa mwezi tukaanza kuitafuta kila sehemu tulizo kuwa tumepitia na ikatuchukua kama dakika ishirini katika kuitafuta na kwabahati nzuri Juliana akaiona ikiwa imeezama kidogo kwenye mchanga ulio lowa maji.

    “Hii itakuwa ni ukumbusho wangu kwenye maisha yangu kwamba ilitokea siku nilikuwa kipofu”

    “Kweli unatakiwa kuitunza vizuri ili hata siku uweze kuwaonyesha watoto wako”

    “Kweli”

    Tukaendelea kuzungumza huku tukitembea kwa mwendo wa kawaida huku moyoni mwangu nikiwa nimetawaliwa na furaha isiyo elezeka.Tukiwa kwenye njia isiyo na nyumba nyingi za watu tukamuona mtu mmoja akitokea kwenye jumba buvu akisimama mbele yatu huku akiwa na panga linalo ng’aa vizuri kutokana na mwanga wa mwezi pamoja na upya wake,na kwaharaka Juliana akarudi nyuma na kusimama mgongoni mwangu

    “Eddy hawa wakaka walinitongoza siku nikawakataa”

    “Ni kina nani?”

    “Ni wavuta bangi na wanakula sana unga wa kulevya pia niwakabaji na niwaizi sana wameshindikana na askari wa eneo hili”

    Juliana alizungumza kwa haraka haraka huku sauti yake ikiwa ni yakunong’oneza na kwa woga alio nao anatetemeka kiasia kwamba haidi amening’ang’ania shati langu kwa nyuma.Vijana wakaanza kuongezeka na kusimama mbele yangu na idadi yao ikafikia kumi huku wengine wakiwa na magongo na mapanga.

    “Eddy kuna wengine nyuma”

    Nikageuka na kuwakuta wengine wakiwa wesimama huku wakiwa hawajavalia mashati kiasi kwamba wakawa wameitunisha misuli yao wakinionyesha vifua vyao vya mazoezi na kwa haraka wanafika watano huku mikononi mwao wakiwa wameshika visu huku wakivuta bangi zenye kutoa moshi mwingi



    “Juliana usiondoke nyuma yangu sawa?”

    “Sawa”

    Tukaanza kupiga hatua za kuwafwata wavuta bangi walio simama mbele yetu huku nikiwa nimejiandaa kwa jambo lolote litakalo tokea.Nikaanza kushangaa baada ya jamaa kutupisha na tukapita kati kati yao kisha wakarudi kusimama kama walivyo kuwa wamesimama hapo awali.Wavuta bangi hao wakaanza kujibishana na wale jamaa wengine walio kuwa nyuma yetu kisha wakaanza kufwatana kwa kasi na ugomvi mkubwa ukazuka kati yoa huku wakipigana mapanga na marungu walio kuwa nayo na sikujua chanzo kikuu cha ugomvu huu ni nini.

    “Eddy tuondoke kwa maana polisi watafika hapa muda si mrefu”

    Sikutaka kumbishia Juliana zaidi ya kuondoka katika eneo ambalo wavuta bangi hawa wanaendelea kupigana.Kabla hatujafika nyumbani nikaishika fimbo yangu na kuyafumba macho yangu na Juliana akanishika mkono na taratibu tukaanza kuelekea nyumbani na kuwakuta wazazi na wadogo zake Julina wakiwa wapo nje wanatusubiri.Juliana akawasalimia wazazi wake na wakatujulia hali ya sehemu tulipo toka na hatukuhitaji wafahamu kuwa mimi ninaona hadi wakati tulipo maliza kula Juliana akawaita wazazi wake pamoja na ndugu zake kisha akawaeleza juu ya hali yangu kisha akaniruhusu niyafumue mamcho yangu jambo lililo wafanya wazazi na ndugu zake kufurahi kwa kile wanacho kiona mbele yao na kila mmoja akanikumbatia kwa furaha ila kitu lilicho nishinda ni lugha wanato izungumza

    Juliana akawa na kazi ya kunifundisha lugha yao wanayo izungumza na kutoakana akili yangu ni nyepesi katika kuyaelewa mambo haikuwa ngumu kuweza kusahau kwa kile nilicho fundishwa na ndani ya wiki tatu nikafanikiwa kukijua kidutch kukizungumza na kukiandika ambayo ni lugha kuu inayotumika katika nchi hii ya Suriname.Makovu ya sura yangu yakaendelea kupona kadri ya siku zilivyozidi kwenda hadi sura yangu ikarudi kwenye muonekano wa kawaida japo nikabaki na alama ndogo ndogo za mikononi na usoni.Kila siku jioni baada ya Juliana kurudi kazini tunakwenda kanisani katika mazoezi ya kwaya ya vijana ambayo Juliana ni miongoni mwa waimbaji wakuu na kujikuta kila siku zinavyo zidi kwenda ndivyo jinsi nilivyo pendezwa na uimbaji wao na kujikuta na mimi nijijiunga katika kuimba katika kwaya yao.

    Maisha yangu yakamgeukia Mungu na kuachana na mawazo ya kikatili niliyo nayo juu ya maisha ya kulipiza kisasa kwa wale wote walio nikosea.Uimbaji wangu ukazidi kuongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda na nikawa kivutio kikubwa sana kwa watu wengi jambo lililo wafanya watu wengi kunipenda akiwemo mchungaji mkuu wa kanisa Bwana Leopard Vandisel ambaye akaanza kunifundisha mambo mengi juu ya kumuamini Mungu na siku zote akawa ananiomba nikubaliane naye katika kulitumikia kanisa

    Nikakubaliana na mchungaji Leonard Vandisel Nikaanza kulitumikia kanisa kwa juhudi zangu zote na maarifa hadi ikafikia kipindi nikaanza kupata uwezo wa kuhubiri katika siku jumamosi katika misa za vijana na maisha yangu ya nyuma yakawa ni ushuhuda tosha kwa wale wasio nijua japo kuna baadhi ya vitu kama mauaji na umalaya sikuyaweka hadharani

    “Mtumishi Eddy”

    Kijana mmoja aliniita nikiwa ninatoka nje ya kanisa huku nikiwa nimeshika biblia yangu na kunifanya nisimame nikimsubiria kunifwata sehemu niliyo simama

    “Naam”

    “Kusema kweli leo nimependa mahuiri yako”

    “Asante ila haya yote unatakiwa kumrudishia sifa Mungu kwa maana yeye ndio aliye nipa hii karama ya kuhubiri”

    “Kweli mtumishi....Unajau tangu ulipo anza kuhubiri wewe hizi siku za jumamosi kuna vijana wengi sana wanakuja kusikiliza yale unayo yahubiri kusema kweli Mungu akubariki na kukuongezea katika kipawa chako cha kuhubiri”

    “Hata wewe Mungu akubariki”

    Kijana akatoa boksi dogo kiasi kwenye begi lake na kunikabidhi na nikamuuliza ni la nini ila akaniomba nifungue nitajua kuna nini.Nikafungua na kukuta simu nzuri aina ya NOKIA Lumia925

    “Mtumishi ninafahamu ya kuwa hapa unajitolea ila nimeamua kukupa zawadi ya hii simu itakuwa inakusaidia katika matumizi yako ya kuwasiliana na sisi na watu wengine humo ndani kuna namba yangu nimeisave kwa jina la Fred”

    “Asante sana na Mungu akubariki bwana Fred”

    “Amen”

    Nikaondoka huku nikiwa nimejawa na furaha moyoni mwangu kwani tangu nianze kukaa katika nchi hii sikua na pesa ya aina yoyote zaidi ya kumtegemea Juliana kwa kila kitu ambacho nitakuwa ninakihitaji.Nikafika nyumbani na kukutana na mdogo wa kike wa Juliana anayeitwa Pretty na baada ya kuniona akanifwata kwa haraka huku akionekana kuwa na wasiwasi

    “Kaka Eddy mama ameanguka chooni na kuumwa gafla na hali yake sio nzuri”

    “Yupo wapi?”

    “Ndani kwake”

    Tukaongozana na Pretty hadi ndani kwa mama yeka na kumkuta mama akiwa amelala kitandani huku akiwa anahema kwa shida sana.Nikaisikia sauti ndani yangu ikiniomba niweze kumewekea mkono mama Juliana ambanye na mimi nilizoe kumuita mama na nikaanza kuomba kimoyo moyo kiasi kwamba nikaanza kuhisi nguvu nyingi zikitoka kwenye mwili wangu na kupitia mkono wangu nilio uweka juu ya kifua chake zikaingia mwilini mwake na akaanza kutingisha miguu yake kama mtu anayekata roho na nikaanza kupata wasiwasi na kutaka kuutoa mkono wangu ila sauti iliyo niambia niuweke mkono wangu kifuani kwa mama ikanirudia na kuniomba nisiutoe mkono wangu na nizidi kuomba kwa juhudi nyingi

    Nikazidi kuomba na kukemea vitu vyote ambavyo vilikuwa vimetumwa mwilini mwa mama na baada ya muda mama akaanza kutapika vitu vya ajabu vikiwa na rangi nyeusi

    “Pretty lete maji na chumvi”

    Nikauweka mkono mgongoni mwa mama na kuzidi kuomba na mama akazidi kutapika hadi ikafikia hatua akaanza kutapika irizi na nywele nyingi za mtu pamoja na kucha na kumfanya Pretty abaki akishangaa kwa kitu kinachotoka kwa mama.Nikamnywesha mama maji niliyo yachanganya na chumvi kiasi kisha akaendelea kutapika hadi ikafikia hatua yale yote aliyo tupiwa kwenye mwili wake yakawa yameisha na akarudi katika hali yake ya kawaida japo nguvu nyingi za mwili zilimuishia.Nikamtoa mama nje na kumuacha Pretty akifanya usafi ndani kwa mama

    “Eddy ninakushukuru sana mwanangu”

    “Usijali mama yangu sifa zote zinatupasa tuzirudishe kwa Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi anayesema hakuna litakalo shindikana mbele zake”

    “Amen mwanangu ni kweli hayo husemayo”

    “Ila mama usirudi nyuma katika maisha ya kumtegemea Mungu japo tunajua kuwa maisha ni mihangaiko ya hapa na pele ila Mungu pia ananafasi yake katika kumshukuru kwa yote yale tunayo yafanya”

    “Kweli mwanangu”

    Tukaendelea kuzungumza mengi na mama ambeye siku zote yeye na baba muda wa wao kwenda kanisani ni adimu sana kiasi kwamba kwa mwezi wanaweza kwenda mara moja au wasiende kabisa.Pretty akaleta chakula na nikaanza kumlisha mama kwa utaratibu na kwa jinsi ninavyo mpenda mama huyu mtu unaweza ukasema ni mama yangu mzazi

    “Eddy mwanagu ni lini utaoa?”

    Swali la mama likanipa wakati mgumu sana wa kulijibu kwani hadi sasa hivi sikuwa na mtu wa kumuoa japo moyoni mwangu nimetokea kumpenda Juliana mtoto wao wa kwanza ila kutokana na kazi yangu ya utumishi ninajikuta ninashindwa kumueleza ukweli Juliana juu ya upendo wangu kwake

    “Ahaa mama kuoa nitaoa”

    “Lini?”

    “Mungu pale atakapo nipa mke yule ambaye nitaamini ni mke mwema kwangu si unajua kuwa kila kitu kina wakati wake mama yangu”

    “Eddy mwanangu natambua ya kwamba wewe si mtu wa nchi hii na July alitusimulia kuhusiana na maisha yako wewe na familia yako.....Ila jana usiku mimi na baba yenu tuliona tuwaite wewe na July na tuwaeleze juu ya swala zima la ndoa kama mutaridhiana muweze kufunga ndoa”

    Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama mama ambaye sikutegemea kuwa ipo siku atakuja kunimbia kitu anacho kizungumza

    “Kweli mama hilo unalo lisema ila sijajua juu ya upende wa July kwamba atalichukuliaje hili swala la ndoa kwa maana hatujawahi kuzungumzia kitu kinacho itwa mapenzi siku hata moja”

    “Ngoja kwanza....Wewe unampenda Juliana?”

    “Ndio mama”

    “Basi nitaongea naye na.......”

    “SIPO TAYARI KUOLEWA WAKATI HUUU MAMA”

    Sote tukastuka na kugeuka nyuma na kumkuta Juliana akiwa amesimama nyuma yetu na anaonekana mazungumzo yetu ameyasikiliza kwa muda mrefu.Sikuwa na kitu cha kuzungumza zaidi ya kukaa kimya huku nikiwa ninatizama chini kwa aibu.Mama akanyanyuka kumshika mkono Juliana na kwenda naye ndani.Baada ya muda nikapata wazo na kujikuta nikinyanyuka na mimi kwa haraka na kwenda kusimama nje ya mlango wa chumba walichopo Juliana na mama wakizungumza na kumsikia Juliana akilia

    “Ni kijana mtulivu,mstaarabu sana mwenye upole na usahimilivu...Hivi mwangu Juliana unadhani ni nani asiye mtamani Eddy kwanza muangalie jinsi alivyo barikiwa uzuri wa pekee kijana wa watu ana kila sifa za kuitwa mwanaume”

    “Ila mama Eddy amekosa sifa moja”

    “Sifa gani mwangu?”

    “Hana kazi....hana pesa unadhani haya maisha tutayamudu vipi...Hao watoto tutakao zaa tutawamudu vipi..Mimi mwenyewe sina kazi ya kueleweka mimi ninapambana kutafuta pesa ya kuiongoza familia yetu Jack,John,Pretty wote wananitegemea mimi niwalipie ada na nikipata mzigo mwengine wa Eddy hivi unadhani itakuwaje mama?”

    “Sawa mwanangu ila Eddy Mungu atamsaidia na yeye atapata kazi”

    “Ila mama na wewe umesahau kitu kimoja?”

    “Kitu gani?”

    “Umesahau kuwa mimi ninamchumba wangu na sasa hivi yupo masomoni na nyinyi nyote munamjua na tayari nilisha mleta kwenu na nyinyi mukampokea kwa mikono miwili”

    “Sasa mtu amekwenda kusoma huko ulaya mwanangu unadhani sasa hivi atakuwa amekosa msichana wa kumuoa na isitoshe yule kijana kwao ana pesa unadhani atakuwa bado anakukumbuka....Sema mwenyewe huu ni mwaka wa ngapi tangu huyo Lameck wako akuambie yupo masomoni?”

    “Hata kama mama”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sio hata kama seme mwenyewe huu ni mwaka wa ngapi?”

    “Mwaka wa sita”

    “Sasa mwaka huu ni wasita unakwenda wa saba unadhani bado atakuwa anakukumbuka tuu”

    “Mama ninampenda sana Lameck na sio Eddy samahani sana na hilo”

    Nikajikuta chozi likinimwagika na maumivu ya sasa hivi ninayafananisha kama maumivu niliyo pewa na Christina msichana ambaye niliye kuwa ninampenda kiasia kwamba nikaamua kumsomesha kwa mshahara wangu wa kufanya kazi gereji ili tuje kuwa na maisha mazuri ila mwisho wa siku nikajikuta nikishuhudia ndoa ya Christna na mwanaume mwengine.Nikageuka na macho yangu yakakutana na Pretty akiwa ananitazima,nikaanza kupiga hataua za kutoka nje

    “Kaka Eddy mbona unalia?”

    Sikumjibu Pretty na kumuacha akiwa anasikiliza mazungumzo kati ya mama yake na Julina

    Moja kwa moja nikaenda kwenye fukwe ambazo mara kwa mara tulikwenda na Juliana kupunga upepo na kupunguza mawazo.Maumivu makali yakazidi kuutesa moyo wangu huku nikikumbuka maneno ya Juliana yakiwa yanajirudia rudia akilini mwangu

    {HANA KAZI....HANA PESA UNADHANI HAYA MAISHA TUTAYAMUDU VIPI...HAO WATOTO TUTAKAO ZAA TUTAWAMUDU VIPI..MIMI MWENYEWE SINA KAZI YA KUELEWEKA MIMI NINAPAMBANA KUTAFUTA PESA YA KUIONGOZA FAMILIA YETU JACK,JOHN,PRETTY WOTE WANANITEGEMEA MIMI NIWALIPIE ADA NA NIKIPATA MZIGO MWENGINE WA EDDY HIVI UNADHANI ITAKUWAJE MAMA?}

    Nikaitoa simu niliyo pewa na Fredy na kuanza kuichunguza vizuri katika vitu vilivyomo ndani ya simu kisha nikafungua sehemu ya kuingilia internet na kuingia kwenye email(barua pepe) yangu na kukuta meseji nyingi kutoka kwa watu mbali mbali.Nikafungua barua pepe moja niliyo tumiwa na benki ya Co-perative iliyopo London wakinijulisha kuwa salio langu la pesa lipo kiasi cha dola za kimarekani milioni 3 na hii ni kawaida ya benki hii kutuma meseji kwa wateja wake kila mwezi wanao hifadhi pesa kwenye benki yao.

    “Asante MUNGU kumbe pesa yangu bado ipo?”

    Nilijisemea kimoyo moyo kisha nikafungua mtandoa wa GOOGLE na kutazama kinacho endelea kwenye serikali ya Pakistani na kukuta habari ikielezea juu ya kupatikana kwa mke wa raisi na kukiwa na picha zinazo muonyesha mke wa raisi akiwa amelazwa hospitalini baada ya kuokolewa kwenye ajali ya ndeke huku ikisadikika watu walio okolewa ni wanawake wawili tu ikiwemo Lilian ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha kwenye mahakama kuu ya kimataifa inayohusika na maswala ya kigaidi inayoitwa The Hague.

    Kitu ambacho wanakiamini duniani ni kwamba mimi nimefariki duniani pamoha na miili mingine miwili ya marubani inayosemekana hadi sasa haijapatikana.Nikaingia kwenye barua pepe na kufungua barua pepe niliyokuwa nikiisoma kutoka benki na kuichukua namba ya simu ya benki na kuipiga.Cha kumshukuru Mungu imeita kwa muda kisha ikapokelewa na sauti ya kike huku akizungumza kingereza

    “Hapana ni makao makuu ya benki ya Co-operative kutoka jijini London Uingereza na unazungumza na Bi.Colnelia Mack Antony tukusaidie nini?”

    “Kwa jina ninaitwa Jack Lee nina akaunti yangu namba 1212986-4567Co ninahitaji msaada wa kuweza kujua ni jinsi gani ninaweza kutoa pesa nikiwa nchi nyingine”

    “Wewe sasa hivi upo nchi gani?”

    “Nipo nchi ya Suriname”

    “Subiri kidogoa”

    Sikukata simu na kuiacha hewani nikisubiria jambo atakalo nieleza Bi.Colnelia Mack Antony na baada ya muda akazungumza

    “Nimeipata akaunti yako bwana Jack Lee na tutaweza kututumia pesa zako pele utakapokuwa na akaunti ya Benki katika nchi uliopo na hapo unaweza kutumia benki inayoitwa De Surinaamsche”

    “Sawa asante je sininaweza kutoa kiasi chochote nitakacho kihitaji?”

    “Ndio unaweza na pia makato yake yatakuwa ni madogo”

    “Asante kwa msaada wako”

    “Na wewe pia na endelea kutumia benki yetu kwa huduma nzuri zaidi”

    Nikakata simu huku moyoni mwangu nikianza kupata matumaini ya kuacha kumtegemea Juliana ambeye amekiri kwa mama yake kuwa mimi ni mizigo.Nikarudi nyumani na kumkuta Pretty akiwa amekaa njee akiwa anajisomea vitabu vyake vya masomo akujiandaa na mitihani yake ya sekondari

    “Pretty unaijua benk ya De surinaamsche?”

    “Ndio napafahamu”

    “Unaweza kunipeleka”

    “Kwa muda huu watakuwa wamefunga tena na leo ni jumamosi labda kwa jumatatu ndio tunaweza kwenda”

    “Sawa...Hivi ni mbali na hapa?”

    “Sio mbali sana kwa maana tutapanda daladala”

    “Sawa Mungu akibariki jumatatu asubuhi utanipeleka”

    “Sawa”

    Siku nzima Juliana hakunisemesha kitu cha aina yoyote hadi tukaenda kula na mimi nikaingia kwenye chumba ambacho ninalala na wadogo wawili wa kiume wa Juliana ambao wapo shule ya sekondari

    “Kaka Eddy leo umenunu simu mpya?”

    “Ndio mdogo wangu”

    “Ahee bei gani?”

    “Ni pesa nyingi tuu”

    “Aaaa inaingia Facebook?”

    “Ndio”

    “Naomba niingie kwenye akaunti yangu nicheki meseji zangu kwa maana hii ya kwangu mtandao unasumbua”

    “Sawa”

    Nikampa simu Jackson mdogo wa Julina anaye mfwatia na akaaza kufanya anayo yajua yeye na mimi sikuwa na haja sana ya kumfwatilia zaidi ya kuipanga mipango yangu ya kujikidhi kimaisha kwa pesa nitakayo itao benki kwani nimeamua kuanza maisha yangu na mimi na kuachana na utegemezi.

    “John njoo uone”

    “Kuna nini?”

    “Njoo bwana”

    John akanyanyuka kitandani na kumfwata Jackson sehemu alipo na wakaanza kuitazama kitu kinacho onekana kweneye simu yangu

    “Wee huyu si ni Lameck”

    “Ndio ametupia picha za harusi yake tena masaa matano yaliyo pita ndio amefunga ndoa kanisani”

    “Hapo ni nchi gani?”

    “Yupo Ital”

    “Je na dada Juliana naye ndio kusema....?”

    “Mmmm....twendeni tukamuonyeshe”

    “Ngoja kwanza Jack?”

    “Nisubiri nini tumuonyesheni picha kwamba yeye amepigwa kibuti na huyo mchumba wake”

    “Jack hembu hiyo simu”

    Jackson akanyanyuka na kunifwata hadi nilipo kaa na kunionyesha picha na kulikumbuka jina la Lameck ambaye ni mchumba wa Julina ambaye anamsubiria siku zote kuja kuolewa

    “Yaani kaka Eddy huwezi kuamini huyu jamaa alikuwa ni mchumba wa dada July na leo hii tunaona picha zake hizi za ndoa”

    “Mmmm Huyu ndio Lameck?”

    “Ndio”

    “Basi nisikilizeni wadogo zangu mimi ninacho waomba musimueleze kitu chochote July nitajua mimi jinsi ya kuongea naye”

    “Sawa ila jamaa anatabia mbaya sana”

    “Ndio....Ila Mungu atampigania dada yenu sawa?”

    “Sawa kaka Eddy”

    Nikamuachia Jackson simu akaendelea na shughuli yake na mimi nikapanda kitandani na kulala.Asubuhi nikaamka na kutokana ni siku ya jumapili tukajiandaa kwa kwenda kanisani na leo hii idadi ya waendaji kanisani ikaongezeka wakiwemo baba na mama na ikatulazimu tutafute usafiri wa kukodi

    “Wee Jackson simu yako ina hela ya kupiga kwa maana simu yangu sasa hivi haina vocha?”

    “Ndio dada ila unataka kumpigia nani?”

    “Nampigaia dereva taksi aje kutuchukua”

    “Sawa ila dada July usiitumie vocha yangu yote kuna jamaa nahitaji kuwapigia”

    “Sawa siitumii yote ninamuita tuu hapa alafu niwekee sehemu ya namba kabisa kwa maana hiyo simu yako siwezi kuitumia”

    “Powa tayari wewe ingiza namba yake”

    Juliana akachukua simu ya Jacksom na akaandika namba za dereva taksi akizitoa kwenye simu yake na kuziingiza kwenye simu ya yake kisha akampigia na akamuomba aje nyumbani kisha akakata simu.Ila nikaanza kuiona sura ya Juliana ikanza kubadilika huku macho yake akiwa amayafumbua sana akiitazama simu ya Jackson na nikaanza kuyashuhudia machozi yakimwagika Julina na gafla akadondoka chini na kupoteza fahamu.Nikanyanyuka kwa haraka kutoka kwenye kiti na niakakimbia hadi sehemu alipo angukia na kabla sijamgusa Julina nikaiokota simu ya Jackson na kubaki nikiwa nimeshangaa picha inayo onekana kama wallpaper katika simu hii ikimuonyesha Lameck mchumba wa Julina akiwa anamvisha pete mke wake mpya wa ndoa kanisani na sikikujua ni kwanini Jackson aliamua kuiweka hii picha kwenye simu ya yake wakati nilimkataza kuhusiana na dada yake kujua kitu kinacho endelea kwa mchumba wake anaye mpenda



    Wadogo wa kiume wa Juliana wakaja sehemu alipo anguka dada yao na nikamkabidhi Jackson simu yake cha kumshukuru Mungu dereva wa taksi ndio amesimamisha gari yake nje.Nikambeba Juliana na kumuingiza ndani ya gari ikamlazima baba na mama nao kuingia ndani ya gari na safari ya kwenda hospitali ikaanza.Nikaanza kusali kimoyo moyo huku nikimuomba Mungu amuwezeshe Juliana kuweza kupata nafuu ili aweze kuzungumza na mimi,Tukafika hospitalini na madaktari wakatupokea kwa haraka na Juliana akapelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na sisi tukabaki nje tukiwa tunasubiria majibu ya madaktari ni nini watakacho tuambia.Nikaanza kupata wasiwasi baada ya kuwaona madaktari wakiingia na kutoka katika chumba alicho ingizwa Juliana na kila ambaye tulijaribu kumuuliza juu ya hali ya mgonjwa alituomba kuweza kusubiri kwani kwa madai wanasema wao sio waongeaji kwa hali ya mgonjwa

    Nikajikuta nikipiga magoti na kuegemea kwenye kiti nilicho kuwa nimekikalia na kuanza kuomba kimoyo moyo huku machozi yakinimwagika kiasi kwamba nikatawaliwa sana na uchungu moyoni mwangu ila sikukata tama zaidi ya kuendelea kuliita jina la Mungu wangu kwani yeye ndio kimbilio la maisha yangu kwa sasa.Daktari mmoja mzee wa makamo akasimama mbele ya baba na mama na kunifanya nisimamishe maombi yangu na kumsikiliza kwa kitu anacho kihitaji kukizungumza

    “Nyinyi ndio wa husika wa mgonjwa aliyopo ndani?”

    Daktari aliuliza kwa lugha ya kidutch amabayo ninaielewa vizuri

    “Ndio”

    “Ninawaomba munifwate”

    Mimi na baba tukanyanyuka na kumfwata daktari na kumuacha mama akiwa amekaa na sisi moja kwa moja tukaingia ndani ya ofisi ya daktari na mimi nikasiama na baba Akaka kwenye kiti kilichopo pembeni ya meza ya daktari

    “Daktari hali ya mwangu inaendeleaje?”

    “Sio nzuri hata kidogo”

    Moyo ukanipasuka kiasi kwamba nikahisi ninaweza nikaanguka kwa mstuko na nilicho kifanya ni kuegemea ukutani na kumsikiliza daktari ni kitu gani anachoweza kukizungumza kwa wakati huu

    “Mwanao amepata tatizo la mishipa inayo peleka damu kwenye ubongo kuweza kupasuka kiasi kwamba seli hai za ubongo imekufa kutokana na kuzibwa na damu iliyokuwa ikivuja kwa wingi kwenye kwenye ubongo na hii inatulazimu kuweza kumfanyia upasuaji wa kichwa haraka iwezekanavyo kwanza tuweze kutoa damu inayoweza kuganda kwenye ubongo wake na jinsi tutakavyo chelewa ndivyo jinsi mwanaoa atakavyoweza kupata uwezekano mkubwa wa mwili wake kuparalaizi”

    Moja kwa moja nikajua daktari anazungumzia ugonjwa wa kiharusi na kujikuta nikiwa sina cha kufanya.

    “Gharama za upasuaji ni kiasi gani?”

    “Ni dola za kimarekani elfu ishirini na tano”

    Kwa mahesabu yangu ya haraka kichwani mwangu kiasi hichi kinaweza kukaribia kama shilingi milioni arobaini na moja na laki mbili na nusu za kitanzania kiasi mbacho kilimfanya baba kunigeukia na akanitazama kwa macho yanayo ashiria kuwa hicho kiasi hakipo.

    “Dokta hizo pesa munazihitaji kwa lini?”

    “Leo ua munaweza mukaingia mkataba na hospitali na mukaandikisha vitu vinavyoweza kuwa na dhamani kama hiyo ili opareshini kuweza kufanyika”

    Baba akanyanyuka na kumuomba daktari atusubiri kwa muda kisha na sisi tukatoka nje na kusimama pembeni kidogo ya ofisi

    “Mwangu Eddy hapa tunafanya nini?”

    “Baba kwani wewe una kiasi gani cha pesa?”

    “Mimi mwanangu kiasi nilicho kuwa nacho cha akiba ni dola ishirini tuu ambayo nilitaka nimpe Pretty pesa ya kwendea kwenye mtihani wake wa kumaliza nusu muhula na biashara ya samaki imekaa vibaya sasa ni mwezi samaki hawaonekani kabisa baharini”

    “Baba ngoja kwanza”

    Nikatoa simu yangu mfukoni na kuipiga namba ya benki kisha nikapiga hatua kama tano kutoka alipo baba Juliana na simu yangu ikapokelewa

    “Hapana ni makao makuu ya benki ya Co-operative kutoka jijini London Uingereza na unazungumza na Bi.Colnelia Mack Antony tukusaidie nini?”

    “Mimi ni bwana Jack Lee”

    “Karibu tena bwana Jack Lee”

    “Nina ombi moja je ninaweza kupata hizi pesa zangu kwa lini labda?”

    “Utakapo weza kufungua akaunti kwenye benki ambayo nimekuelekeza nasi tunahitaji namba ya akaunti yako na sis i tunaweza kutumi hiyo pesa na ukamilishaji wake unaweza kuwa ndani ya nusu saa”

    “Sawa asante”

    Nikakata simu na kurudi sehemu ambayo amesimama baba anayeonekana kutawaliwa na mawazo mengi

    “Baba unaweza ukakopa hoyo pesa sehemu na ndani ya siku mbili tatu mimi nitakuwa nimeirudisha?”

    “Mmmmm sidhani kama ninaweza kupata.....?”

    “Fikiria fikiria kwa mtu yoyote wa karibu ambaye tunaweza kupata hiyo pesa kwa haraka ili tuweze kuyaokoa maisha ya Juliana”

    “Ngoja kuna mfanya baiashara mmoja ambaye hapo mwazoni nilikuwa ninampelekea samaki ngoja nikazungumze naye kisha nitakujulisha kama tumefikia wapi?”

    “Sawa baba yangu”

    Baba akaingia ofisini mwa daktari ni kumuomba atusubiri kwa muda kidogo na sis tutarejea na kiasi cha pesa wanacho kihitaji na akamuomba waanze kumfanyia upasuaji Juliana kama kuna uwezekano huo.Tukarudi na kumkuta mama akiwa macho yake yamemvimba kwa kulia na baba akamuomba akae atusubiri na sisi tunakwenda nyumbani kuchukua nguo za Juliana.Ilimlazimu baba kumdanganya mama kuhofia kumsababishia wakati mgumu

    “Baba nimepata wazo wewe nenda kwa huyo mfanya biashara ila mimi ngoja niende kanisani kuzungumza na mchungaji Leopard kama anaweza kutuchangia kiasi kidogo cha pesa”

    “Sawa mwanangu utaweza kufika kanisani mwenye?”

    “Ndio njia ninazikumbuka na sinto weza kupote baba yangu”

    Tukaachana na baba na mimi niikanza kazi ya kutembea kwa haraka nikielekea kanisani huku nikibahatisha bahatisha njia za kupita na ilipo nilazimu kuomba msaada wa kuelekezwa nikafanya hivyo hadi nikafika kanisani na kukuta watu ndio wanatoa sadaka.Nikatoa kitambaa changu na kujifuta jasho kisha nikapiga hatua za haraka hadi kiti cha mbele karibu na lilipo kapu la kutole sadaka na macho yangu yakaanza kuhesabu vitita vya pesa vinavyowekwa na matajiri ambao wamekuja kuchangia harambee ya upanuzi wa kanisa.Maombi yangu yakahamia kwenye ibada iishe mapema ili niweze kuzungumza na na mchungaji.Baada ya lisaa ibada ikasha na watu walipo anza kutawanyika nikamfwata mchungaji Leonard na tukasalimiana na nikaanza kumuelezea tatizo lililo mpata Julina ambaye amatamvu vizuri sana kutokana na umahhiri wa uimbaji katika kwaya ya vijana

    “Doooo pole sana mwanangu”

    “Asante mchungaji yaani hapa nimechanganyikiwa na sina hata senti tano yaani ninakuomba kama kuna uwezo wowotw mchungaji ninakuomba unisaidi japo hichi kiasi cha pesa alafu mimi nitakusrudishia”

    “Mwanangu kusema kweli kwa hilo mimi siwezi kukusaidia kwasababu hata mimi ninamatatizo yanayo weza kufanana na yako japo yangu nimesha anza kuyatatua......Nina mwanangu wa kiume alipata ajali wiki mbili za nyuma na yeye nimempeleka nje ya nchi yupo Marekana kwahiyo kunapesa nyingi sana inahitajika”

    “Mmmmm sasa mchungaji nitafanyaje......?”

    “Hata mimi sijui labda umuombe Mungu atakusaidia katika hilo?”

    “Mchungaji nipo chini ya miguu yako ninakuomba basi hata unipatie kiasi kidogo hata robo ya hiyo pesa nikalipe hospitlini tafadhali”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Eddy mwanangu ninakuomba usinipigie magoti kwa maana sihitaji kusujudia anaye stahili kupigiwa magoti ni MUNGU tuu muumba mbingu na ardhi”

    Nikaendelea kumbembeleza mchungaji ila akakataa kata kata na mbaya zaidi nikaona wazee wakanisa wakiyaingiza makapu ya liyo jaa noti yapatao matatu na kuanza kushirikiana na mchungaji kuzihesabu moja baada ya nyingine.Nikaanza kuisikia sauti rohoni mwangu ikiniambia kuwa ninaweza kuwamudu wote kwa kuwapiga na kuzichukua pesa ila roho nyingine iliniomba nisifanya ninaho shawishiwa na roho hii moja ambayo nimegundua ni roho ya shetani

    “Eddy tunakuomba utoke kwani haya mahesabu hayakuhusu”

    “Sawa mchungaji”

    Nikanyanyuka taratibu huku moyoni mwangu nikiwa nimejawa na uchungu kiasi kwamba kwa mbali machozi yakaanza kunilenga lenga.Moja kwa moja nikarudi nyumbani na kumkuta baba akiwa anawatembeza watu wawili wenye vitambi na walio valia nguo za gharama sehemu za nyumba na sikusita kumfwata na kumuuliza

    “Baba unafanya nini?”

    “Nataka niiweke rehani nyumba mwanangu kwa maana sina pa kutoa pesa”

    “Ohhhoo baba nyumba ndio kila kitu sasa unapo iweka rehani unadhini wakina Pretty watakwenda kukaa wapi?”

    “Hapana ni bora niiweke reheni hii nyumba na ndani ya wili moja nitakuwa nimepata pesa hiyo na nitawarudishia na yule mwenye cheni nyingi za dhahabu ndio niliye mfanya biashara niliye kuambia”

    “Baba hiyo ndani ya wiki moja hiyo pesa utaitoa wapi?”

    “Usijali mwanangu najua wewe pia unapigana katika kuzipata hizi pesa....Japo sijui ni wapi nitazitoa ila tutajua mbele ya safari”

    Baba alizungumza kwa uchungu kiasi kwamba nikabaki nikimuhurumia na nikamshuhudia akienndelea kuwatembeza wafanya biashara hawa katika sehemu mbali mbali za nyumba kisha wakamaliza na akaingia nao ndani ya gari na akainiomba na mimi pia nijumuike kwenda nao kwenye ofisi yao.

    Tukafika kwenye ofisi za huyu mfanya biashara na akatukaribisha ndani na akatutolea mikataba na tukaanza kuisoma taratibu na kitu kilicho nipa wasiwasi ni kipengele kinachosema

    “MKOPWESHAJI ANAPOSHINDWA KUREJESHA DENI NITAKALO MKOPESHA NDANI YA WIKI MOJA NITAMFILISI MALI ZAKE NA KUMFUNGA KIFUNGO CHA MIEZI SITA JELA KWA USUMBUFU ATAKAO NIPATIA”

    Ikanibidi nimnong’oneze baba ili aweze kujioneka kitu kilicho andikwa na yeye akaaniambia yopo tayari kwa lolote.Baba akachukua kalamu na kisha akasaiini kwenye sehemu anayo paswa kusaini kisha na jamaa naye akasaini na sahidi wake naye akasaini na wakaniomba na mimi pia kusaini kama shahidi wa baba Juliana.Nikawatazama machoni na kwaharaka haraka nikahisi kuna mchezo ambao unaweza kuchezewa kwani tunasaini pasipo kuziona pesa zilipo

    “Pesa zipo wapi?”

    “Zipo wewe saini tuu”

    “Ninaziomba nizione na kwenye mkataba unaonyesha anaye kopa anachukua dola elfu stini ninaziomba mutuonyeshe kwanza”

    Jamaa akamnong’oneza msaidizi waka na akatoka ofisini na baada ya muda akarudi akiwa na mfuku wa lailoni ulio na vibunda vya pesa na kwaaraka nikawaomba niweze kuvihesabu na wakaniruhusu na nikavihesabu na kukuta nikiasi cha dola elfu stini ambacho baba amekihitaji.Nikachukua kalama na kusaini mkataba kama shahidi wa baba na tukachukua mfuko wa pesa na kuubeba na kabla mimi sijatoka nikasikia jamaa akimnong’oneza msaidizi wake na kutokana na umakini wa mafunzo niliyo nayo nikaweza kuwaelewa ni nini wanacho kimaanisha kwa maana jamaa amemuomba mtu wake kutufwatilia

    “Hapa na hospitali sio mbali kwahiyo tunaweza kutembea kwa miguu haina haja ya kukodi taksi”

    “Sawa baba”

    Tukaanza kutembea huku nikiwa ninamfwata baba kwa nyuma na macho yangu yote yakawa makini kwa wakati wote na ndipo nikagundua kuna watu wanne wanatufwatilia kwa nyuma pasipo baba kujua.Ikanilazimu kuongeza mwendo hadi baba akashangaa na jamaa nao wakaeongeze mwendo.Tukafika karibu na hospitali nikasimama na kumkabidhi mfuko wa pesa baba kisha nikamuomba akimbie kuelekea mlango wa hospitali ila akaanza kusita sita asielewe ni nini ninamaanisha.Nikaguka na kuwakuta jamaa wakiwa karibu kabisa na mimi na mmoja wao akatoa kisu na kuanza kunifwata kw akasi huku kisu akiwa amekitanguliza mbele.

    Nikarusha teke la kumstukiza jamaa na likampiga tumboni na kumfanya aanguke chini na wezake watatu wakanifwata na kunizunguka hapo ndipo nikamshuhusia baba akikimbia kama hana hakili vizuri na nikamshuhudia akiingia kwenye mlango wa hospitali hapo ndipo nikapata amani.Janamaa wakanza kunivamia kwa pamoja kiasi kwamba nikajituama kwa sana kataika kuiachia mikono yangu kwenye kutupa ngumi zilizo wapata jamaa na sikusita kuizuia miguu yangu kurusha mateke pale nilipo jisikia kauanya hivi kiasi kiasi kwamba jamaa wakaanza kuchanganyikiwa kwani kila mmoja niliweza kumpiga kwenye sehemu ambayo atayasikia maumivu kwa kiasi kikubwa.Na jamaa ambaye ni msaidizi wa mfanya biashara tuliye mkopa alipoona mambo ni mzito akainama na kuichomoa bastola yeke kwenye soksi na hata kabla hajanyannyuka nikampiga teke kwenye mkono alio shika bastola na ikaangukia pembeni na nikaiokota na kuwaamuru wote kupiga magoti huku wakiwa wanavunja na damu sehemu mbali mbali hususani kwenye sehemu za juu ya macho yao nilizo zipasua kwa ngumi

    Gafla nikasikia breki kali za gari zikisimama pembeni kidogo na nilipo mimi na nikageuka na kukuta ni gari za polisi zikiwa zimesimama na wakashuka askari walio na bastola mikononi mwao na kuniamrisha niweke silaha yangu chini.Nikatii na kuiweka silaha yangu chini na kuinyoosha mikono yangu juu na askari wapatao sita wakatufwata na kutufunga pingu kwa nyuma na kabla sijaingia kwenye gari nikamuona baba akitoka hospitali na akaonkana kushangaa zaidi kwa kitendo anacho kiona mbele yake.Nikaingia kwenye gari la polisi ambalo ni muundo wa taksi na moja kwa moja tukapelekwa kwenye kituo cha polisi na kuwekwa mahabusu pamoja na jamaa nilio toka kupambana nao

    Jamaa nilio pigana nao hakuna hata mmoja aliye nisemesha na walijitenga nami na ndani ya masaa mawili bosi wao akaja na akawatolea dhamana na hakuamini kuniona na mimi nikiwa nipo ndani na akawauliza watu wake ni nini kilicho nipeleka mimi ndani ya mahabusu hiyo

    “Bosi jamaa huyu ndio aliye tufanya sisi tuingie humu ndani”

    “Yaani nyinyi mumemshindwa huyu kibaraka mmoja?”

    “Bosi huyu jamaa anamapigo ya kijeshi na si mtu wa kawaida kama ulivyo dhania?”

    “Na pesa jee?”

    “Pesa mzee kaondoka nazo”

    “Shiitiii”

    Nikabaki nikishangaa kwa maana mazungumzo yao waliyafanya mbele ya polisi huku waiwa wemejiamini kupita maelezo.Bosi wao akanionyeshea ishara ya kunichinja kwa kutumia kidole gumba cha mkomo wake wa kulia kisha akaondoka na watu wake wakamfwatia kwa nyuma.Nikatafuta sehemu ya kukaa huku nikimuomba Mungu aniepushie majariu yakiopo mbele yangu kwa maana tayari shetani ameanza kujiinua kwenye maisha yangu haya.Siku ya kwanza ikakatika pasipo kumuona baba Juliana wala ndugu yoyote wa Juliana kuja maabusu nilipo shikiliwa na polisi na mbaya zaidi sikuweza kuletewa chakula.Siku ya pili na yatatu ikakatika pasipo kupata msaada wowote kutoka kwa familia ya Juliana na ndipo nikaanza kupata wasiwasi kwa kitu kitakacho kuwa kinaendelea uraiani.

    “Wewe ni siku ya tatu hatuoni ndugu wala jamaa kuja kukutembelea unaishije?”

    Askari mmoja wa kike aliniuliza huku akinichungulia nikiwa nyuma ya mlango wa ndondo uliotengenezwa kama mlango wa kufungia mahabsu.

    “Watakuja tuu”

    “Au wewe sio raia wa nchi hii nini?”

    Swali la askari likanistua kwani siku zote japo ninaishi kwenye hii nchi ya Suriname sikuwa na uraia wala hai ya kusafiria ambayo ianweza kunionyesha kuwa ninastahili kukaa siku kadhaa ndani ya hii nchi jambo ambalo ni kinyume na sheria kwenye nchi nyingi dunia.

    “Mimi ni raia?”

    “Una uhakika?”

    “Ndio”

    “Sasa mbona ndugu zako wala rafiki zako hawaji kukuwekea dhamana kwa maana ukikaa humu ndani zaidi ya wiki unapelekwa gerezani”

    Ikawa ni habari mpya kwamgu kiasi kwamba nikajikuta nikaanza kupata wasiwasi na kitu kingine kilicho nitesa zaidi ni njaa kali iliyo nikamata

    “Naomba msaada wako dada yangu”

    “Mimi nitakusaidiaje wakati wewe ni mwalifu”

    “Huwezi jua kama ipo siku na mimi ninaweza kukusaidia kwani milima haikutani ila binadamu tunakutana”

    “Mimi cha kukusaidia hapo labda ni chakula na si kingine zaidi ya hapo”

    “Nitashukuru kwa hilo je ninaweza kupata simu yangu japo niwasiliane na ndugu na jamaa”

    “Ngoja askari wengine wapungue kwa maana muda wa kwenda kula chakula cha machana umekaribia”

    “Sawa dada yangu nitashukuru sana kwa masaada wako na Mungu akusaidie”

    “Usijali”

    Askari wa kike akandoka na baada ya muda akarudi akiwa na kifuko cheuisi chenye soseji nyingi na soda ya kopo kisha akanipa kisiri na hakutaka wezake waweze kuona.Askari wakaanza kupungua kwenye kituo na kama madai ya askari wa kike aliye tokea kunisadia alivyo dai kuwa huo ndio ndio muda wao wa kwenda kula,Akaja kwa haraka sehemu nilipo na kunipa simu na nikaiwasha simu na kumpigia Fredi kwani ndio namba pekee iliyopo kwenye simu yangu na nikamuelekeza kituo nilichopo na akaniaidi atakuja muda si mrefu na kujikuta nikianza kupata furaha ya kurudi uraiani.Baada ya lisaa Fred akaja na kufwata hatua zote za kunitoa mahabusu na nikaachiwa huru

    “Mimi ninaitwa Afende Sofia”

    “Na mimi ninaitwa mtumishi Eddy”

    “Ooohoo wewe ni mtumishi wa Mungu?”

    “Ndio”

    “Ahaa pole sana”

    “Asante”

    Tukaondoka kwenye kituo cha polisi huku nikimshukuru sana Fred na nikamuelezea chanzo cha nipelekea mimi kuwa katika mikono ya polisi

    “Hivi Fredy wewe unafanya kazi gani?”

    “Nina mihangaiko tuu ya kimaisha hapa mjini”

    “Ahaaa nakushukuru sana ndugu yangu”

    “Usijali mtumishi ila mimi nimekuja hapa mara moja ngoja nirudi kwenye mishuhuliko yangu kuna ishu ninakwenda kuifanya mida ya saa kumi na hapa niliwakimbia wezangu mara maoja”

    “Ni ishu gani ndugu yangu unaifanya?”

    “Ni kazi ya kawaida ila Mungu akibariki kesho nitakutafuta ili tuweze kuzungumza vizuri juu ya maisha yangu”

    “Sawa asante sana kwa upendo na ukarimu wako na Mungu akubariki sana katika kazi yako unayo kwenda kuifanya”

    “Amen mtumishi”

    Tukaachana na Fredy na akanilipia pesa ya taksi ambayo ikanipeleka hadi hospitalini na nikaelekea katika chumba ambacho niliacha Juliana akiwa amelazwa na nikajikuta nikipata wakati mwengine mgumu baada ya kukuta Juliana akiwa hayupo.Nikiwa ninaendelea kushangaa shangaa nikamuona Prety akipandisha ngazi za kuelekea gorofa ya juu,nikamkimbili huku nikimuita jin lake kwa sauti ya juu

    “Wewe kijana acha kelele tambua hapa ni hospitalini”

    Daktari mmoja alinikemea na kunifanya ninyamaze na kwabahati nzuri Pretty alisha nisikia,Pretty akanisalimia huku akinikumbatia na machozi yakanza kumwagika

    “Pretty mbona unalia?”

    “Ni baba?”

    “Amefanyaje.....”

    “Amepigwa risasi na watu tusio wajua”

    Mappigo ya moyo yakaanza kunieda mbio huku moja kwa moja akili yangu ikiwa inamuhisi ni mfanya biashara ambaye tulimkopa pesa na kitu nilicho kigundua kwa huyu mfanya biasha ni kwamba anakukopesha pesa na hata kabla hujazitumia anakutumia watu wanakupokonya kisha anaendelea kukudai

    “Yupo wapi?”

    “Amelazwa kwenye wodi ya juu....Na sisi sote tunajua kuwa wewe pia umeuawa kwani tangu siku ulipokuwa na baba hatukukuona tena”

    “Mdogo wangu nitakuadisia ila twende tukamuone baba”

    Tukapandisha ngazi na kwenda katika wodi ya wanaume na kumkuta baba akiwa amefugwa bandeji kwenye kifua huku amefungwa mashine ya gesi inayo msaiidia katika kuhemea,Nikakaa pembeni yake huku nikimtazama kwa masho ya masikitiko

    “Mama yupo wapi?”

    “Mama yupo kwenye wodi ya wanawake anamuangalia dada July”

    “Upasuaji wake umekwendaje?”

    “Wanasema unakwenda vizuri ila hadi sasa hivi hajazungumza wala kujitindisha na hali yake sio nzuri kabisa”

    “Je na watu walio mpiga baba risasi wamekamatwa?”

    “Wakamatwe na nani....Hii nchi kaka Eddy yaani ina matabaka kiasi kwamba mnyonge hana haki mbele ya sheria hata kama muhalifu atajulikana basi hawezi kuchukuliwa sheria”

    “Mmmm wewe unawajua?”

    “Wakina nani?”

    “Walio mpiga baba risasi?”

    “Hapana ila nahisi ni lile jifanya biashara ambalo baba alikuja nalo nyumbani kwa maana limesha anaza kuleta vitisho eti tuhame mule ndani kwani nyumba yetu baba ameiweka rehani”

    Nikaanza kupata picha kwani kwani kwa ishara ambayo mfanya biashara alinifanyia kipindi nikiwa mahabusu ilianza kunipa mashaka kwa kiasi kikubwa na kutambua kwamba hii nchi mwenye pesa ndio mwenye haki kwa maana alifanyia mbele ya polisi na hawakunya kitu cha aina yoyote.

    “Twende ukanionyeshe kwenye chumba alichopo mama na Julina”

    Tukatoka kwenye wodi za wanaaume na tukapanda ngazi kuelekea gorofa inayo fwata na nikamkuta mama akiwa na amejiinamia huku akiwa ameshika tama.Mama baada ya kuniona akanyanyuka na kunikimbila na kunikumbatia kwa furaha

    “Mwnangu Eddy upo hai?”

    “Nipo hai mama yangu....Juliana anaendeleaje?”

    “Hali yake ndio kama hivyo unavyo muona na tangu alivyo toka kufanyiwa upasuaji haja tingishika wala kufumbua jicho lake na hapo alipo analishwa kwa mipira”

    “Mmmmm ila MUNGU tunaye muomba atamsaidia atapona na atarudi kwenye hali yake ya kawaida”

    “Ulipatwa na nini mwanangu?”

    “Mama nilishililiwa na polisi basi wakaniweka ndani na leo ndio wameniachia”

    “Tatizo lilikuwa ni nini?”

    “Ile siku t

    lipo toka kuchukua pesa za matibabu kuna watu walituvamia mimi na baba ila nikapambana nao na polisi wakatukuata tukiwa tunapamba na ndipo hapo walipo tukamata”

    “Ohoo pole sana mwanangu kwa maana tulijua na wewe pia umepigwa risasi kama baba na tulipo watuma Jack na mwenzake kukufwatilia habari zako ila hawakupata jibu la msingi”

    “Ahaaa cha msingi ni kumshukuru Mungu kwani nipo salama”

    “Ila baba yule mfanya biashara ambaye mumechukua pesa zake anakazi ya kutupa vitisho kama nini na amesema kuwa wiki ni hii anahitaji pesa yake na lasivyo atamchukulia mzee sheria ya kumfunga na jinsi unavyo muona baba hali yake kitandani ilivyo ni kama Juliana”

    “Nimekuelewa mama yangu ngoja nichakarike na ndani ya siku mbili hizi nitazipa”

    Nikamuomba Pretty tutoke nje ya chumba na kumuomba anielekeze sehemu ilipo benki ya De surinaamsche”

    “Kwa kukuelekeza huwezi kupajua labda twende wote”

    Tukamuaga mama na hatukumuambia ni wapi tunapoelekea na tukapanda mabasi yanayokwenda kwa kasi hadi kwenye benki iliyipo kwenye jiji la Paramaribo na nimbali kidogo na ilipo hospitali na tukaingia na moja kwa moja tukafika kwa muhudumu anaye wahudumia wateja

    “Nikusadie nini kaka?”

    “Ninaomba kujua taratibu za kufungua akaunti kwenye hii benki”

    Akanipa karatasi inayoonyesha vigezo vya mtu ambaye anaweza kufungua akaunti katika banki hii na kujikuta nikiguna baada ya kusima kisoma kifungu cha sita

    (MTEJA ANATAKIWA KUWA NA KITAMBULISHO CHA URAI,KAZI,MAKAZI AU HATI YA KUSAFIRIA)

    “Kaka Eddy mbona unaguna?”

    “Kuna ishu hapa inanipa wasiwasi”

    “Ishu gani?”

    “Kweny kitamulisho hapa si unaju kuwa mimi sio raia wa hapa”

    Nikastukia nikiguswa bega na kugeuka na kukutana na Afande Sofia huku akiachia tabasamu na kunifanya na mimi nitabasamu pasipo kuwa na sababu ya msingi

    “Kumbe wewe sio raia wa nchi hii?”

    “Hapana nilikuwa ninamsimulia mdogo wangu story moja....Mbona huku?”

    “Tumeletwa lindo huku kwani ndio mida ya benki kufunga mahesabu....Huyo ndio mdogo wako?”

    “Ndio.....Pretty huyu ni askari ambaye alinifanyia mpango wa mimi kuachiwa leo huru anaitwa afande Sofia”

    “Shikamoo”

    “Marahaba”

    “Mdogo wako mzuri”

    “AHaaaa kawaida”

    “Munatatizo gani?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimekuja kuf...........”

    Kabla sijaimalizia sentesi yangu tukasikia milio mingi ya risasi zinazo pigwa hewani na jamaa wapatao sita wakaingia ndani ya benki huku wakiwa wamevalia nguo nyeusi sura zao wakiwa wamezifunika na vitambaa vyeusi na wakabakisha macho yao tuu.Milio ya risasi ikawafanya watu kuchanganyikwa na kuanza kukimbia kimbia na na wakaanza kuwashambulia watu wanao kimbia na kuwaua baadhi ya askari waliokuwa wakijaribu kujibu mashambulizi ya majambazi hao kwa haraka nikaichomoa bastola aliyopo kiunoni mwa Afande Sofia na kuanza kufyatua risasi za haraka huku nikurukia kwenye sehemu yenye meza ya chuma isiyoingiza risasi na kuwaacha Pretty akiwa amelazwa chini na Afande Sofia.Kutokana na ushapu wangu wa matumizi ya bunduki nikafanikiwa kuwapiga risasi za vichwa majambazi watatu na wengine baada ya kuona wezao wakiwa chini huku wakivunywa na damu ikawalazimu kukimbia na nje kwenyewe wakakutana na askari ambao wakawashambulia kwa risasi nyingi na kuwafanya kupoteza maisha yao,

    Nikanyanyuka kutoka kwenye sehemu niliyokuwa nimejificha huku bastola nikiwa nimeishika kwa vizuri na kusisogela miili ya majambazi ili kuhakikisha kama wamekufa au laa.Nikaanza kuwafunua vitambaa vyao mmoja baada ya mwengine na mtu wa tatu nikajikuta nikistuka baada ya kumkuta Fredy kijana aliye nisadia kunitoa mahabusu na ndiye aliye nipa simu ninayo itumia





    Afande Sofia akanisogelea na kuniomba bastola yake na nikamkabidhi huku moyoni mwangu nikiwa ninajihisi vibaya kwa kitendo cha kumuua Fredy

    “Wewe ni mpigaji mzuri wa bunduki”

    Afande Sofia alizingumza huku akinishika bega na kulipiga piga kwa kunipa pongezi

    “Kawaida”

    “Unaonekana umesha wahi kuwa amwanajeshi?”

    “Kwa nini unazungumza hivyo”

    “Inaoenekana tuu kwa jinsi ulivyo kwa maana kwa mtu wa kawaida hawezi kupiga mapigo kama unayo yapiga wewe”

    “Kweli sijawahi kuwa mwanajeshi....ila ninapendelea sana kuangalia mapigano ya kwenye filamu za kama kina John Rambo na wengineo”

    Tukasitisha mazungumzo yetu baada ya polisi wengine kuingia na kuanza kufanya mpango wa kuiondoa miili ya majambali walio fariki,Shuhuli ya ufungaaji wa akaunti ukasitishwa na benki ikasimamisha shuhuli zake na kututangazia itafunguliwa ndani ya wiki moja mbeleni jambo ambalo kwangu ni mtihani mkubwa kwani jaama tuliye mkopa anaendelea kutusumbua na zimebaki siku chache hadi wiki moja aliyo tupa kukamilika

    “Kwani kaka Eddy huku benki wewe unapesa uliyo iweka?”

    “Hapana Pretty ila kuna pesa zangu ninahitaji zisairishwe kutoka Uingereza na zije huku”

    “Kiasi gani?”

    “Nyingi nyingi tu ambayo inaweza kutusaidia katika kuwauguza baba na Julian pamoja na kulipa deni la yule mfanya biashara tuliye mdai”

    “Ahaaa ila daaa yaani hata mimi mwenyewe nimechanganyikiwa sijui haya yot yametokea wapi”

    “Kikubwa ni kumuomba Mungu atuongoze”

    Tukaendelea kuzungumza huku kila mmoja akiwa amejichokea hususuni mimi kwani hapa mfukoni sikuwa na hata senti tano ila cha kumshukuru Mungu ni kwamba Pretty ana kiasi kidogo kinachoweza kutusaidia kwenye nauli ya kurudia nyumbani,Tukapanda basi za kwenda kwa kasi na safari hii tukafikizia nyumbani na kuwakuta Jackson na John wakiwa wamejilaza nje na milango ya nyumba ikiwa imefungwa na kwa makufuli

    “Haya mbona mume lala nje?”

    “Shikamoo kaka Eddy?”

    “Marahaba?”

    “Mbona mumelala nje”

    “Jamaa wamekuja kufunga kwenye nyumba yao?”

    “Wakina nani?”

    “Si yule jamaa ambaye baba alimkopa pesa anadai tusipo lipa ndani ya masa haya machache anakuja kuivunja apandishe gorofa”

    “Jamani huyu jamaa mbona ana roho mbaya...Eti kaka Eddy kwani mulikubaliana naye vipi?”

    “Prety mdogo wangu hilo niachieni mimi nitajua jinsi ya kulitatua”

    “Utalitatua vipi wakati hata benki kwenye ndio hivyo haito fanya kazi ndani ya wiki nzima”

    “Musijali je na haya makufuli nayo vipi?”

    “Ndio hivyo bro jamaa wamekuja na makufuli mapya hayo sijui ya namna gani kwani sijawahi kuyaona kabisa ukilishika tuu linapiga makelele”

    Nikatafuta sehemu na kujiegesha huku nikiwa ninamawazo ya nini nifanye ili kuweza kuzipata pesa ambazo ninazihitaji kwa wakati huu ili kuepukana na nyumba ya Baba Julian kuvunjwa.

    “Huu niwakati wangu wa mimi kulipa fadhila kwa yake yote ambayo familia hii imenitendea”

    Nilijisemea kimoyo moyo huku nikizitazama nyota na anga zinavyo ng’ara kiasi kwamba nikajikuta nikianza kuziesabu nyota ila nikashindwa,Nikaishusha sura yangu taratiu na kujikuta nikipata uchungu baada ya kumuona Pretty binti mdogo wa miaka 15 akijikunyata pembeni ya kaka zake huku machozi yakimwagika na isitoshi kipindi cha hali ya hewa tulicho navho kwa wakati huu ni cha baridi kali

    “Nani ana kibereti cha gesi?”

    Wote wakanitazama na mmoja mmoja akatingisha kichwa akiashiria hana hicho kiberiti,Nikasimama na kuyasogelea makufuli yapatayo manne na kuyachunguza moja baada ya jingine pasipo kuyashika na nikagundua yana kijibetrii kidogo kinacho lifanya kufuli hilo kutoa kelele

    “Nani ana funguo yoyote hapo”

    John akanipa funguo ya makufuli ya kawaida na nikalisogelea kufuli moja na kuiingiza funguo na ikakubali japo lilianza kupiga kelele na nikaanza kulitekenya taratibu kwa utaalamu mkubwa hadi likaanza kufunguka taratibu hadi ikafika hatua likafunguka kabisa kisha nikauungua mlango ambao unaingia katika chumba tunacholala na kuwafanya Jackson na wadogo zake kunifwata chumbani.Nikatafuta suruali yangu nyeusi na kuivaa kisha nikachuku tisheti nyeusi na sweta jeusi lenye kijikofia kwa nyuma na kukivaa

    “Kaka Eddy unakwenda wapi?”

    “Ninataka kwenda hospitli”

    “Ahaaa”

    “John ninaomba begi lako la shule”

    John akatoa madaftari yaliyopo kwenye begi lake na kunipatia

    “Kuna bisibisi yoyte humu ndani?”

    “Ya nini kaka Eddy?”

    “Si munajua huu ni usiku kwahiyo ninaweza nikavamiwa na vibaka”

    “Ahaa ngoja nizitafute”

    John akaanza kutafuta vifaa nilivyo muagiza na akafanikiwa kuiona pamoja na nyundo moja na wakanikabdidhi kwa lengo ya kuweza kunisaidia endapo nitakutana na watu wabaya njiani

    “Hakikisheni munafunga mlango kwa ndani na asitoke njee”

    “Sawa”

    Nikamkabidhi Jackson simu yangu kisha nikatoka nje na kujiweka vizuri nguo zangu huku nikijifunga vijimikanda vya kikofia cha sweta nililo livaa kisha nikaanza kupiga hataua za haraka huku nikielekea kanisani.Ndani ya dakika kama saba nikafika kwenye uzioa wa michongoma iliyo ota na kujipanga vizuri na nikaanza kutafuta sehemu yenye upenyo na nikafanikiwa kuiona japo miba miba mingi imenichoma ila nikavumilia.Sikuweza kupitia kwenye eneo la mbele kwenye geti kuepuka kukutana na walinzi wanaolinda kwenye kanisa hili.Nikatoa kitambaa cheusi mfukoni na kujifunga kwenye uso kuanzia sehemu ya puani kushuka chini na kuacha macho yangu

    Nikazunguka sehemu ya nyuma kwenye ofisi ya mchungaji na kukuta kukiwa kumefungwa,nikatoa bisibisi niliyopewa kisha nikaitupukiza kwenye sehemu yenye kitasa cha mlango na kwakutumi nyundo nikaanza kuvunja vishikizo vilivyomo ndani ya kitasa hivyo na kwa kadri nilivyo zidi kupiga piga ndivyo kitasa kilivyozidi kulainika hadi kikaachi na mlango ukafunguka.

    Nikaingia ndani na moja kwa moja nikaliendea kabati ambalo siku zote ndili linahifadhia pesa za sadaka,cha kumshukuru Mungu ni kwamba ninafahamu sehemu ambayo mchungaji anaificha funguo ya kufungulia kabati hili.Nikatumia funguo kwa kufungulia kabati na nikafanikiwa kukuta vibunda vya pesa vikiwa vimepangwa vizuri,Kwa haraka nikafungua zipu ya begi langu na kuanza kuingiza vibunda vya pesa kwa haraka na sikuacha hata hata senti tano,Nilipo hakikisha kila kitu kipo sawa nikafungua mlango huku begi langu likiwa limejaa pesa,Nikasimaa nje ya mlango na kuangalia pande zote za kanisa na sikumuona mtu yoyote akiwa katika eneo hili.Nikaanza kupiga hatua za kuelekea kwenye sehemu nilipo pitia na nikapenya kwenye sehemu uwazi kwenye michongomo na kitendo cha kusimama nikakutanana na askari watatu waliopo doria

    Wakaanza kunifwata huku wakia wamezishika virungu na wakaanza kuniita na wakiniamrisha kusimama ila kwangu sikuweza kutii na kuaanza kukimbia na kuwafanya waanze kunikimbiza huku wakipiga vilimbi ambayo kwa haraka nikajua wanaawaashiria watu walio lala kuweza kutoka.Nikasimama gafla na kuwageukia askaria ambao haikuwa rahisi kwa wao kusimama kwa haraka na wakajikuta wakinipita na wakasimama kwa mbele yangu na kungigeukia na kuaanza kunisogele

    Nikaruka teke moja lililotua kifuani kwa mmoja wa askari na kumungusha chini na kwawafanya askari mmoja kuchomoa bastola kwenye kiuno chake na kabla hajainyanyua vizuri nikaupiga mkono wake na akaiangusha pembeni na nikaanza kupambana na polisi kiasi kwamba nikawazidi uwezo na hadi mwisho wa siku wakawa wamelala chini huku kila mmoja akiugulia kwa maumivu makali,Nikaiokota bastola ya askari kisha nikaondoka zangu na nikatamua kuwa hawajaweza kuiona sura yangu kutokana na jinsi nilivyo ificha kwa kitambaa.

    Nikafika moja kwa moja nyumbani na kugonga mlango na John akauliza ni nani na nilivyo muambi ni mimi akanifungulia mlango na nikaingia ndani na kuwakuta Jackson na Pretty wakiwa wamelala.

    “Kaka mbona unavujwa na jaso hivyo?”

    “Nilikuwa ninakimbia”

    John akarudi kitandani na begi nikaliweka chini ya uvungu na nikabadilisha nguo zangu na kuvaa nguo zangu nyingine na nikakaa kwenye kiti kwani sikuweza kupanda kitandani kutokana na kitanda nafasi yake kujaa kwa ugeni wa Pretty aliye lala na kaka zake.Asubui na mapema na nikaamka na kuchukua begi lenye pesa na kufungu na kutoa vibunda viwili vya pesa nilizo ziiba kanisani na kulirudisha begi uvunguni na kutoka nje na kuzihesabu pesa na hazikufikia idadi ya pesa tunazo daiwa na ikanilazimu kurudi tena ndani kutoa vibunda viwili ndani ya begi langu na kulificha uvunguni na nikatoka nje na kuvihesabu na nikapata idadi kamili ya pesa tunato daiwa na nikavichomeka kwenye mifuko ya suruali niliyo ivaa

    Nikaanza safari ya kwenda ofisini kwa mfanya biashara yuliye mkopa na kwa bahari nzuri nikamkuta anashuka kwenye gari akitaka kuingia ofisini kwake na baada ya kuniona akaonekana kustushwa baada ya kuniona

    “Usiniogope nimekuja kulipa kiasi chote cha pesa ambacho munanidai”

    Jamaa akabaki akinitazama huku walinzi wake ambao wawili ninakumbuka nilipambana nao siku walipo kuwa wananifwatilia mimi baba.

    “Twende ofisini kwangu”

    Tukaingia ofisini kwake na nikamuwekea vibunda vya pesa mezani kwake na nikamuomba anipe karatasi za mikataba na kafavyo na akanikabidhi na nikazichana mbele yake na akavihesabu vibunda vya pesa na kukuta ni pesa kamili ambayo tulimkopo

    “Ninaomba funguo za nyumbani kwetu”

    Jamaa akanikabidhi fungua na nikanyanyuka kwenye kiti na kabla sijaufikia mlango wake akaniita na nikamgeukia

    “Kama huto jali ninaomba tuzungumze”

    “Ongea ninakusikiliza”

    “Ninaomba uketi kwenye kiti”

    “Hata nikiwa nimesimama ninaweza kuzungumza”

    “Unafanya kazi gani?”

    “Kwani tatizo lako wewe ni nini?”

    “Ninahitaji kuja kwani wewe unaonekana ni mtu hatari kwahiyo nilihitaji kuweza kukuajiri kama mfanyakazi wangu”

    Nikasima kwa muda huku nikiyatafakari maneno ya jamaa aliyo nimbia na nikapiga picha ya maisha niliyo nayo kwa sasa na nikapiga hatua za kurudi kwenye kiti ambacho nilikuwa nimekaa

    “Ni kazi gani ambayo unahitaji kuniajiri?”

    “Kwanza ninapenda kujitambulisha ninaitwa Paul Heamen wewe je?”

    “Eddy

    “Kazi ambayo ninahitaji kukuajiri kusimamia kazi zangu zinazo endelea kwenye migahawa na nitakuwa ninakulipa kwa wiki”

    “Kiasi gani utakachokuwa unanilipa?”

    “Kwa wiki nitakulipa dola elfu kumo na tano za kamarekani”

    “Na kazi yenyewe inaanza lini?”

    “Siku yoyote ambayo utakuwa tayari”

    “Sawa nitakupa jibu”

    Nikanyanyuka na kuondoka zangu na kurudi nyumbani na kufungua milango ambayo imefungwa,

    “Kaka Eddy funguo umezipata wapi?”

    “Nilikwenda kuzichukua na hivi shule unadaiwa kiasi gani?”

    “Pesa ya mitiani ni dola elfu moja”

    “Basi ingia ndani ukajiandae je Jack na John wapo wapi?”

    “Wamesha kwenda shule”

    “Powa jiandae nitakupa pesa”

    Pretty akaingia ndani kwake na mimi nikaingia chumbani kwetu na kulitoa begi la pesa na kutoa kiasi cha matumizi na nikamkabidhi Pretty dola elfu mbili na akaondoka na nikabaki peke yangu nyumbani na nikaanza kazi ya kuzihesabu pesa nilizo nazo na kukuta ni kiasi cha dola za kimarekani laki sita na sabini ambacho ni sawa na bilioni karibia mbili za kitanzani.Ila roho yangu ikajikuta ikipata shida sana katika kuziiba sadaka za kanisani.Nikazirudisha ndni ya begi na nikalificha na kuelekea hopsitali na nikakuta hali ya baba kidoo inaridhisha

    Siku zikazidi kwenda huku kanisani wakitoa tangazo na urejeshwaji wa pase ambayo imeibiwa japo nusu yake kiasi kilicho ibiwa ndani ya kipindi cha wiki mbili na endepo itakuwa haijarudishwa wachungaji na watu wote watafunga na kuomba kumlaani mtu aliye zichukua pesa hizo.Nikazidi kukosa amani huku roho moja ikinishawishi kuto kurudisha huku nyingine ikiniomba nirudishe

    “Eddy mwangu mbona swiki hii unaonekana kama mtu aliye poteza amani moyoni mwake?”

    “Hapana mama kawaida si unajua kuumwa kwa baba na Juliana kwangu inaiuma sana”

    “Ni sawa mwangu ila inakupasa usiwe hivyo kwa maana itakupa shida sana ila Mungu tunaye muabudu atakwenda kuwapa uzima na watapona”

    “Kweli mama”

    Nilizungumza na mama kwa unyonge na laiti angetambua kitu kilicho nifanya ili kuikomboa nyumba yao kwa pesa za wizi sikujua angesemaje.Zikawa zimesalia siku mbili kabla ya waumi kuingia kwenye mfungo na maombi ya kumuombea mtu au watu waliofanya wizi huo,na kila nilipo lisikia tangazo hili likitangazwa na mchungaji kwenye ibada nilijikuta mwili ukisisimka na kukosa nguvu kabisa

    “Mtumishi Eddy umejiandaaje na mfungo hao majambazi walio iba pesa za rambi rambi ya ujenzi wa kanisa?”

    Mchungaji aliniuliza baada ya iada ya jumapili kwisha

    “Nimejiandaa vizuri mchungaji na ninaimani kwamba Mungu anakwenda kufanya kitu juu ya watu hao”

    Nilizungumza kwa kujikaza tu ila kusema ukweli moyoni mwangu nilijihisi shida sana.Tukaendelea kuzungumza na mchungaji mambo mengi kuhusiana na mfungo hua ambavyo watu wamejwa na uchungu kwani pesa hizo walizichangisha miezi kwa miezi kufikia malengo yao

    “Sasa kwanini musiziweke benki?”

    “Tulipanga kuziweka benki ila nilihisi kitu kweli na siulisikia wale majambazi walio vamia benki?”

    “Ndio”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Na kama tungeziweka ingekuwa ni shida sana ila kusema kweli huyu mtu aliye ziiba hizi pesa Mungu amuangalie kwa jicho jengine na itatulazimu ulinzi wa kanisani hapa uongezwe maradufu....”

    “Hadi sasa hivi polisi wanasemaje juu ya mtu huyo?”

    “Waseme nini wakati polisi wenye ni wazembe kama nini wanasema wanafwatilia”

    “Ahaa tuendelee kupata wepesi wa kumuombea huyo mtu aliye iba kupewa wepesi wa kuzirejesha”

    “Kweli Mungu ampe wepesi huo”

    Nikarudi zangu nyumbani na muda wa usiku kila nilipo jaribu kulala nikajikuta ninashindwa kwa kuwazia hizi pesa nilizo nazo.Nikanyanyuka kitandani na kulichukua begi lililo na pesa na nikaziweka kwenye mfuko mkubwa na nikauingiza ndani ya begi kisha safari ya kwenda kanisani na simu yangu ya mkononi inaonyesha ni saa saba usiku.Nikafika kwenye uzio wa kanisa na kuutoa mfuko wenye pesa na kuurusha kwa ndani bila mtu yoyote kuniona kisha nikarudi nyumbani na moyoni nikajihisi amani ikitawala,Asubuhi na mapema simu yangu ikaita na kukuta ni namba ya mchungaji na kujikuta mapigo yakinienda mbio na kuanza kujiuliza maswali mengi hata kabla ya kuipokea simu yake

    “Shikamoo mchungaji”

    “Marahaba umeamkaje?”

    “Salama sijui wewe?”

    “Nimeamka salama pole bwana kwa kukuamsha mapema”

    “Hakuna tatizo”

    “Nimetoka kuzungumza na walinzi wa pale kanisani na wamedai kuwa wamezipata pesa zilizo ibiwa”

    “Kweli mchungaji?”

    “Kweli japo zimepungua kidogo”

    “Sawa mchungaji inatubidi sifa zote tumrudishie Mungu”

    “Amen asubihi njema”

    “Na wewe pia”

    Nikamaliza kuzungumza na mchungaji na kama kawaid yangu ya kwenda asubuhi hospitali kuwajalia hali wagonjwa.Nikaongozana na Jackson pamoja na John hadi hospitali na kumkuta mama akiwa anatokwa na machozi huku akiwa amejiinamiana chini huku akiwa amekaa nje ya chumba alicho lazwa Juliana na sote tukajikuta tukipata wasiwasi

    “Mama kuna tatizo gani?”

    “July mwanangu...mana weee”

    Mama alizungumza hukua akiunyoosha mkono wake mmoja wenye chumba alicho lazwa Juliana na kujikuta nikisimama na kwenda kuufungua mlango na kujikuta nikizidi kuchanganyikiwa kwani Juliana hakuwepo ndani ya chumba.

    “Mama July amekwenda wapi?”

    “Kule”

    Mama alinionyesha sehemu yanye kordo ndefu na nikaanza kutembea kwa hatua za haraka huku jasho likinimwagika japo kuna baridi kali,Jackson ndiye aliweza kunifwata kwa nyuma ila John nahisi alishindwa kwa mstuko.Sikujua hata ni wapi tunapoelekea na kwabahati nzuri nikakutana na daktari aliye tuhudimia siku ya kwanza

    “Samahani dokta niaamnini unanikumbuka?”

    “Ndio ninakukumbuka”

    “Mgojwa wangu yupo wapi?”

    Daktari akanitazama kwa macho ya kujiuliza kisha kwa ishara akaniomba nimfwate nyuma na tukafanya hivyo hadi ofisini kwake na nikakaa kwenye kiti komoja ila Jackson akabaki akiwa amesimama huku sura yake ikiwa imelowana kwa machozi

    “Dokta acha kujishika shika basi niambie Juliana yupo wapi?”

    “Hali ya mgonjwa wenu hadi hapa ninavyo zungumza ni mbaya sana na muda wowote kuanzia sasa tunaweza kumpoteza”

    “Kwa nini dokta?”

    “Hali yake imebadilika gafla na sisi kama sisi madaktari tunapendekeza mupige hatua moja mbeleni”

    “Dokta hembu nyoosha maelezo”

    “Mgonjwa wenu munaatakiwa kumpeleka nchini Marekani kwa matibau zaidi kwani hapa bara la Amerka ya kusini hakuna hospitali itakayoweza kumuhudumia kwani anatokwa na majimaji kwenye masikio nayaharufu mbaya sana”

    “Mungu wagu ni kiasi gani cha pesa kitafanikisha hilo?”

    “Kwenye laki nne au tano kwa pesa za Kimarekani”

    Nikajikuta nikiishiwa pozi kwani hadi jana usiku nilikuwa na kiasi hicho cha pesa nilicho kiiba kanisani na hapa nilipo sina hata senti tano na kujikuta nikijutia ni kwanini nilizirudisha pesa nilizo ziiba





    Nikabaki nikiwa sina cha kuzungumza na hata Jackson mwenyewe anaonekana kuwa katika hali ngumu sana,nikabaki nikiwa nimejiinamia chini huku nikiyasikilizia mapigo yangu ya moyo jinsi yanavyo kwenda kwa kasi ya ajabu na sauti ya daktari ndiyo ikanistua kidogo

    “Hembu nawaombeni mulitazame na hilo tena kwa maana tusipo muwahisha nilazima ndugu yanu ataiaga dunia?”

    Nikamtazama dokta kwa macho ya sito fahamu kisha nikanyanyuka haraka na kuufungua mlamo na kutoka nje na kuaanza kutembea kwa mwendo wa kasi nikielekea na nikastukia nikishikwa shati kwa nyuma na ikanilazimu kugeuka na kukuta ni mama ndio anaye niita

    Mwangu unakwenda wapi jamani?”

    “Mama ninakwenda kutafuta pesa ya kumuokoa mke wangu Juliana japo natambua mimi sipo moyomi mwake ila kwa hili inanipasa kusimama kama mwanaume mwenye uwezo wa kuitwa mwanaume.Mama nina mikono inafanya kazi...ninamiguu inatembea na inanguvu,sina mapungufu yoyote mwilini mwangu kwahiyo mama ninakuomba uniache nifanye kile ninacho stahili kukifanya”

    Nilizungumza kwa uchungu kiasi kwamba Mama Juliana anakanishika mashavu yangu huku akimwagikwa na machozi kisha akanishika akanibusu kwenye paji la uso

    “Mungu akutangulie mwanangu”

    “Amen mama”

    Nikaondoka na kumuacha mama akiwa amesimama akiniangalia kwa uchungu,nikasimamisha taksi ya kukodi na ikanipeleka hadi ofisini kwa Paul Heamen na kujikuta nikishuka ndani ya gari pasipo kulipa

    “Kaka inakuwaje kuhusu pesa yangu”

    “Nikakulipa nisubiri dakika tatu ninatoka

    Nikamuacha dereva taksi akinisubiri na nikaingia kwenye jengo kubwa la gorofa ambalo linatawaliwa na Paul Heamen ambaye ni tajiri sana.Nikampita sekretari wake pasipo kumsemesha kitu cha aina yoyote

    “Kaka samahani kunakikao....Bosi anakikao muhimu sana”

    Sikumsikiliaza sekretari anaye nifwata kwa nyuma huku akinikimbilia na nikakutana na walinzi wake wawili wakiwa wamesimama mlangoni na wakanizuia

    “Ninashida na bosi wenu”

    “Ngoja ana kikao”

    “Nahitaji kuonana naye wakati huu”

    “Tumekuambia ana kikao muhimu nenda kamsubirie kule”

    “Muna niruhusu au hamuniruhusu?”

    Jamaa aliye simama upande wa kushoto kwangu akamkonyeza mwenzaka na sikujia wanapeana ishara gani ila nikastukia jamaa wa upande wa kulia akinishika bega kwa nguvu na kunivuta shati langu na kujikuta nikimtandika kisukusuku cha pua na kumuangusha chini.Nikamuwahi mwenzake na kumtapiga kabali na kumpiga kigoti cha uso na kumfanya atoe mguno wa maumivu na nikashika kitasa cha kuingila ofisini mwa Paul Heamen na nikaufungua kwa nguvu na kujikuta nikitazamana na mitutu ya bunduki ipatayo kumi ikinitazama mimi huku watu hao walio zishika bunduki zao wakiwa wamezikunja sura zao,Paul Heamen akanitazama kwa macho makali kisha akawaamuru watu hao kushusha silaha zao chini

    “Eddy ni nini unafanya?”

    “Nikekubaliana na kazi yoyote utakayo niambia”

    Nikamuachia jamaa na akatoka nje kisha Paul Heamen akanionyesha sehemu ya kukaa na nikajumuika na watu waliopo kwenye kikao hicho huku wakionekana ni matajiri sana

    “Kwanza niwatambulishe kwetu nyote kwamba huyo aliye ingia hapa kwa fujo ndio Eddy ambaye nilitoka kuwaambia muda mchache ulio pita japo sijawahi kufanya naye kazi ila kwa upeo wangu wa hizi kazi zangu ninaweza kumuamini”

    Watu wote wakanigeukia na kunitazama kisha wakamgeukia bwana Paul Heamen ambaye ndio anaye onekana ndio mkuu wa kikao hichi

    “Utawezaje kumuamni mtu usiye mjua bwana Heamen?”

    “Ninaimani naye”

    “Sasa hii kazi ilivyo kuwa ngumu unadhani ataiweza?”

    “Bwana mbona kijanamwenyew ninamuona mzembe mzembe”

    Matajiri hawa wakaanza kubishana wenyewe kwa wenye wapo waliopo upande wangu na wa wengine wakabisha nisipewe kazi ambayo hadi sasa hivi sikuelewa ni kazi ya aina gani wanayo ihiitaji mimi kuifanya

    “Ngojeni ni kazi gani munayo ihitaji mimi niifanye?”

    “Wewe nyamaza huwezi kujua chochote tunacho paswa kukufanya na kama Heamen umetuhitia ujinga kama huu na uwape watu wako kazi ya ajabu kama hii mimi naachana na nyinyi na ninajitoa na sihitaji hata kuwemo kwenye hiyo serikali yenu”

    Mzee mmoja alizungumza huku akijaribu kunyanyuka na mimi nikasimama na kupiga hatua za haraka hadi sehemu ambayo mzee huyu amesiama na kumsogelea karibu na uso wake na kumtazama kwa sura ya hasira na kuifanya ofisi nzima kukaa kimya wakisubiria kuona ni kitu gani kitakacho tokea

    “USIMDHARAU MTU USIYE MJUA UTAUMIA”

    Mzee akarudi taratibu na kukaa kwenye kiti chake kisha na mimi nikarudi kwenye kiti chagu na watu wote wakakaa kimya na wakisubiri ni nani atakaye anzisha mazungumzo mapya

    “Mmmm...tuendelee,bwana Eddy kuna kazi ambayo tunataka tuweze kukukabidhi japo ni kazi ngumu ila tumeona kwamba tukupe kama utaiweza tuweze kufanya makubaliano”

    “Ni kazi gani?”

    “Tunahitaji uweze kumuua Raisi wa nchi hii na tutakupa kitita kikubwa cha pesa utakayo ihitaji wewe”

    Nikakaa kimya huku nikiawaangaki watu waliomo ndani na moja kwa moja wazo la Juliana kuumwa likanija kichwani kwa haraka na kujikuta nikiiweka dini pembeni na kukubali kuichukua kazi hii.Wato wote wakatabasamu hata yule mzee aliye onekana kuto kunikubali akajikuata akiwa wa kwanza kupiga makofi na wezake wakafwatia

    “Ila ninaombi moja?”

    “Ombi gani?”

    “Hii kazi ninaifanya peke yangu sihitaji msaada wa mtu wa aina yoyote sawa”

    “Sawa”

    “Je malipo yangu ni kiasi gani?”

    “Tutakulipa dola za kimarekani milioni 10”

    “Kama ni milioni kumi siwezi kuifanya hiyo kazi”

    “Kwani wewe unataka kiasi gani cha pesa?”

    “Mlioni 50 kama hamuwezi basi kazi fanyeni wenyewe”

    Ukimya ukatawala ndani ya chuma huku wazee hawa waliopo ndani yah ii ofisi wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini huku wakiwa hawana la kuzungumza.Baada ya muda Paul Heamen akakohoa kidogo kisha akazungumza

    “Ni kweli hicho kiasi cha pesa tukijichanga tunaweza kukupiata mimi nitatoa milioni 25 kama raisi mtarajiwa”

    “Mimi nitatoa milioni mbili”

    Wakajichanga change hadi ikafikia idadi ya milioni 50 za kimarekani ambazo ni kiwango kikubwa sana cha pesa ambacho kwa mwanachi wa kawaida kama mimi nikikipata nikiwa kwa Tanzania ninakuwa ni miongoni mwa mabilionea.Wakaanza kunielekeza jinsi ya kumuua Raisi wao huku wakidai siku mbili zijazo Raisi wao atakuwa katika masafara wa gari la wazi katika sikukuu ya uhuru wa nchi yao na ndio kipindi ambacho nitapaswa mimi kukamilisha adhama ya kumuua Raisi huyo

    Nikatoka nje na kumkuta dereva taksi akinisubini na kumuomba sekretari niliye mkuta kumlipa dereva huyo na akafanya kama nilivyo miagiza.Nikaondoka na mmoja wa wafanyakazi wa Paul Heamen ambaye ni muhasibu mkuu wa kampuni yake hadi benki ambapo nikafungua akaunti mpya kwa kutumia kitambulisho kilicho tafutwa ndani msaa machache na kinaonyesha kuwa mimi ni miongoni mwa wananchi wa nchi hii.Akaniingizia kiasi cha milioni 25 kama kitangulizi cha kazi ya kuumua Raisi na kitu nilicho kidundua ni jinsi gani wanavyo nifwatilia kwa kila hatua ninayo pitia hii ni kuepuka kuwakimbia kabla sijaifanya kazi yao.

    Nikafika hopsitalini na kukuta mama akiwa hana la kufanya kwani kitu likicho subiriwa ni jinsi gani Juliana atakavyo weza kusafirishwa kupelekwa nchini Marekani kwa matibabu zaidi.Nikamtafuta daktari ambaye alida kuwa ni lazima Juliana asafirishe nje ya nje ya nchi ili maisha yake yaweze kuekolewa

    “Vipi umepata hicho kiasi cha pesa?”

    “Ndio ila je ninaweza kulipia safari nzima kwa kutumia cheki?”

    “Ndio”

    “Basi ninaomba nifanye hivyo na ninahitaji kuisafirisha familia yangu nzima hadi baba yangu aliye lazwa kwenye hii hospitali?”

    “Sawa inawezekana kufwanya hivyo ila gharama zitaonezeka na wanaweza kwenda wakiwa chini ya uangalizi wa hospitali”

    “Gharama zake zitakuwa ni kiasi gani?”

    “Itaenda hadi kwenye dola laki tisa na nusu za kimarekani”

    “Sawa basi ninaomba nizilipe zote kwa mkupuo”

    Daktari akabaki akinitazama akionekana kunishangaa kwani hakuamini kamaninaweza kuwa na kiasi chote hicho cha pesa.Akanionyesha sehemu ya kifanya utaratibu mzima wa kuwasafirisha Juliana na baba kama wagonjwa huku Mama,Jackson,Pretty na John wakiwa wanakwenda kama waangalizi wa wangojwa.Tukakamilisha malipo kwa njia ya mtandao kwa kukihamishia kiasi cha pesa wanacho kihitaji kutoka kwenye akaunti yangu ya benki hadi kwenye akauti ya hospitali.Nikawapa taarifa mama na ndugu wa Juliana na wakaonekana kufarhi sana

    “Kaka Eddy wewe huendi na sisi?”

    “Pretty nitakuja mdogo wangu”

    “Na safari itaanza mida ya saa tano usiku na mutaondoka na ndege ya hapa hospitalini na kila kitu kipo tayari na nimesha weka maandalizi ya hospitali mutakayo fikia hoteli na vitu vingine mutajua pindi mutakavyo fika hopspitali”

    Mama akanikumbatia huku machozi yakimwagika kwa furaha,akanishika mkono na kunivuta pembezoni na sehemu walipo wadogo wa Juliana

    “Mwanangu Eddy hizi pesa zote umezitoa wapi?”

    “Mama nimepewa na mchungaji ila ameniambia kuwa nisimuembie mtu wa aina yoyote kutokana ni pesa za ramirambi za ujenzi wa kanisa”

    “Ohhh Mungu ashukuriwe mwanangu……Sasa kwanini wewe hauendi?”

    “Mimi nitakuja ila kuna mambo ninayaweka sawa”

    “Na yatachukua muda gani kuisha?”

    “Kama siku mbili au tatu hivi”

    “Sawa mwanangu Mungu unaye muabudu akulinde na akuongezee ufanisi kwenye kazi yako ya kuwafundisha watu wa MUNGU”

    “Amen mama”

    Laiti kama mama angetambua kuwa ninamsalaba mzito mbele yangu wale asinge niombea kwa mtindo alio niombea kwani kila nilipowaza jinsi ya kumuua Raisi asiye na hataia kisa ni roho ya madaraka ya kina Paul Heamen an rafiki zake nikajikuta roho ikiniuma kiasi kwamba nikatamani nitoroke ila nikaona itakuwa ni tatizo kubwa sana katika maisha yangu

    Nikiwa ninaendelea kuzungumza na mama nikamuona Afande Sofia akiingia katika moja ya ofisi yah ii hospitali,nikatizama kila kona na sikumuoana mtu ambaye ninaweza kumtilia mashaka na nikamumbia mama ninakuja mara maja kisha nikaingia kwenye ofisi aliyopo Afande Sofia

    “Eddy vipi mbona juu juu?”

    “Nikakuomba tuzungumze”

    “Nini tena rafiki yangu?’

    Nikamtazama daktari aliyopo ndani yah ii ofisi na kuona hastaihili kuijua hii siri ninayo hitaji kumuambia Afande Sofia.

    “Dokta unaweza ukatupisha kwa muda?”

    “Bila shaka”

    Afande akatoka nje na nikaufunga mlango wa ofisi kisha nikamvuta Afande Sofia kwenye moja ya chumba na kumugandamiza ukutani

    “Kuna ishu inataka kutokean na ninahitaji tuweze kucheza dili mimi na wewe?”

    Nilizungumza kwa sauti ya chini ya kunong’oneza

    “Ishu gani?”

    Nikaanza kumuelezea kiufupi Afande sofi na hadi ninamaliza mumelezea akabaki akiwa amenitumbulia mimacho huku akitetemeka

    “Nikakuomba ufanye kama nilivyo kuagiza sawa”

    “Sawa Eddy”

    “Na sihitaji mtu wa aina yoyote kuweza kujua nilicho kueleza”

    “Sawa Eddy niamini katika hilo”

    Nikamuchia Afande Sofia na nikatokana ndani ya ofisi na kurudi walipo mama na wanae.Nikawaagiza Jackson na John waelekee nyumbani ili kuweza kuandaa maandalizi ya safari

    “John hakikisheni hakuna anaye jua kuwa munasafiri”

    “Sawa kaka Eddy”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikutaka kuiacha Familia ya Juliana peke yake kwani ninajua kuna hali ya hatari inaweza kutokea kwa wakati wowote na kama ningewaacha ingekuwa ni shughuli nyingine mpya.Johna na Jackson wakarudi wakiwa wamebeba mabegi yao ya shule na nikaamini hakuna aliye gundua kuwa wanasafiri,Kutokana na hopsitali kuwa na kiwanja chake cha ndege na ikawa ni rahisi kwa safari ya Juliana na ndugu zake.Mida ya saa tano usiku wakaingi a kwenye ndege ya hospitali yenye uwezo wa kwenda masafa marefu kiasi kwamba safari ya kwenda marekani sio numu sana japo watatua kwenye nchi moja kabla hawajaendelea na safari

    Wakapakia wote huku Juliana hali yake ikiwa ni mbaya sana na kwa masaada wakaenda na mmoja wa madkatari ambaye kazi yake ni kama kuna hatari yoyote inaweza kujitokeza kati wagonjwa ataweza kuishuhulikia kiurahisi,ndege ikaancha ardhi na kupaa angani na moyoni mwangu nikapata amani na kujua sasa kazi iliyo baki ni kujilinda peke yangu.

    Nikarudi nyumbani na kuchukua baadhi ya nguo zangu chache kisha nikaelekea hotelini na kuchukua moja ya chumba cha bei ya kawaida na makazi yangu yakahamia hapa kwa muda

    ***

    Siku ya sherehe za uhuru zikawadia na gari moja ya kifahari ikasimama nje na simu yangu ikaingia meseji kutoka kwa Paul Heamen akioniomba niingie ndani ya hiyo gari na nikafanya hivyo na kukuyana na jamaa mmoja akiwa amevalia suti nyeusi.Tukafika sehemu ofisini kwa Paul Heamen na nikapitliza ofini kwake na hatukakaa ofisini kwake na akanipeleka kwenye moja ya chumba kilichopo ndani ya jengo lake hili na kukuta chumba kikiwa na makabati mengi ya chuma.Akafika kwenye moja ya kabati na kufungua kabati hilo kwa kuuingiza namba za siri na likafunguka na kukuta silaha nyinyi za kila aina na akaniomba niweze kuchagu silaha ambayo ninaweza kuitumia na nikachague yenye uwezo wa kupiga masafa ya mbali na nilipo hakikisha inafanya kazi vizuri nikaifungua na kuigawanyisha vipande vipande na kuiweka kwenye begi lake maalamu

    “Kuna suti hapa”

    Akadungua begi jengine na kukuta limejaa aina nyingi za suti na nikachagua suti nyeusi kisha kabla ya kuvaa shati nikavaa kizuizi cha risasi(bullet proof) kisha nikava shati na suti na kujiweka sawa,Saa yangu ikaonyesha yamesalia masaa mawili kabla ya maandamano ya raisi kutembea kwenye gari la wazi,Nikaingia ndani ya gari nililo jia na likanipeleka hadi kwenye mnara mmoja wa kanisa kubwa wenye kengele kubwa ulio karibu na barabara na nikapanda juu kabisa kwenye mnara na kutoa bunduki yangu na kunaza kuiunga vizuri hadi ikakamilika na nikaifunga kiwambo cha kuzuia risasi kisha nikairekebisha lensi ya bunduki hii na kuweza kuiona vizuri barabara amayo raisi atapita

    Ikawa ni kazi ya kuhesabu dakika kwani saa sita na dakika tano raisi atapita kwenye barabara ambayo ipo mbali kidogo na mnara wa kanisa na wananchi tayari walisha jipanga barabaani wakiwa na vipeperushi vya miaka sabini ya uhuru wa hii nchi.Zikiwa zimesalia dakika mbili nikaanza kuona gari za askari walinda usalama zikianza kuoita kwa kasi huku zikiwasha ving’ora vyao vikiashiria raisi hayupo mbali na eneo hili

    Nikajilaza chini vizuri huku miguu miwili ya bunduki ikiwa imejikita chini vizuri na nikawa ninaendelea na kazi yangu ya kuivu lensi yangu na ikawa inanionyesha magari yawanausalama kwa ukaribu.Pikipiki za pilisi zipatazo sita zikaanza kupita katika mwendo wa taratibu na baada ya muda kidogo nikaliona gari la raisi lililo wazi kwa juu likipita taratibu huku akiwa amesimama na pembeni akiwemo mke wake na wote wakiwa wanapunga mikono.

    “Ehee MUNGU wangu nisamehe”

    Nilazungumza na kupiga ishara ya msalaba na kwakutumia lensi yangu nikamvuta raisi kwa ukaribu zaidi huku mshale mwekundu ukiwa emesimama juu ya paji lake la uso,Nikamuona anavyo tabasamu kwa mara ya mwisho na roho ya kikatili ikanivaa moyoni mwangu na nikakivuta kitufe cha kuiruhusu risasi kufyatuka na ndani ya sekunde kadhaa nikamshuhudia raisi akianguka chini na wanachi wakaanza kushangaa shangaa.Nikamaliza kufunga bunduki yangu kisha nikaiweka ndani ya begi na lake na kabla sijashuka kwenye ngazi za mnara simu yangu ikaita na kukuta ni Paul Heamen ndio anaye piga

    “Hongera bwana Eddy na pesa yako ninaiingiza sasa hivi benki”

    “Asante”

    Nikaka simu na kuizima kabisa na laini nikaitoa na kuing’ata ng’ata kisha nikashuka kwenye mnara na moja kwa moja nilaelekea kwenye vyoo vya kanisa na kuzunguka sehemu yalipo mashimo yake ya kuhifadhia uchafu na nikalifunga moja na kuliingiza begi lenye bunduki na nikahakikisha hakuna aliye lishuhudia tukio langu na moja nikaingia kwenye choo kimoja wapo na nikajisaidia haja ndogo

    “Tumsifu Yesu kristo”

    Nilistushwa na sauti ya padri na kunifanya hata haja ndogo yangu kuikatisha

    “Milele Amen”

    Padri akaingia kwenye moja ya kijikichumba kidogo na nikaona akivua joho lake na kuliweka kwenye mlango wa choo ambao ni mfupi kidogo na nikajua kabisa anajisaidia haja kubwa.Nikwalichukua joho kake na kumfungia kwa njea kisha nikalivaa vizuri joho lake na kidogo nikawa nina muonekano kama wachungaji wengiene japo sikuwa na rozari wala kola inayo onyesha kuwa mimi ni mchungaji.Moja kwa moja niapita katika geti linalo tokezea upande wa baharini na kumkuta Afande Sofia akiwa kwenye boti ndogo inayokwenda kwa kasi na kwaishara akaniita na nikafika kwenye boti na tukaondoka kwa kasi katika eneo hili

    “Vipi kazi haikuwa ngumu?”

    “Hapana ilikuwa raisi”

    “Hivi Eddy narudia tena kukuuliza ulisha wahi kuwa askari?”

    “Ndio ila sio askari kama wewe”

    Tukatembea kwa umbali mrefu hadi tukafika kwenye manohari iliyo simama na Afande Sofia akasimamisha boti na tukashushiwa ngazi na watu walio valia nguo za kiaskari kisa tukaingia ndani ya manohari kila mmoja akaanza kunipongeza kwa kazi niliyo ifanya.Mimi na Afande Sofia tukaingia kwenye moja ofisi na kumkuta Raisi akiwa amekaa kwenye sofa na mke wake na alipo niona akanyanyuka na kunipa mkono

    “Kijana kazi nzuri uliyo ifanya”

    “Asante mkuu”

    “Jamani mpatieni kinywaji bwana Eddy”



    ***

    (Siku mbili kabla)



    Mazungumzo yangu kati ya Afande Sofia ilikuwa ni jinsi gani ninaweza kumuokoa raisi amabaye hadi sasa hivi nimepewa jukumu la kumuua katika siku ya sikukuu ya uhuru

    “Ishu ambayo ninahitaji tuzungumze mimi na wewe ni kwamba niahitaji ukamape raisi abari hii kwamba Paul Heamen na kundi la wafanya biashara wezake wanataka kumuua ili wachukua madaraka kilazima”

    “Mmmm itakuwaje?”

    “Hapo hakuna cha itakuwaje….Ila ili kuwapoteza waambie wamtengeneneze mtu ambaye atafanana kabisa na raisi na mke wake na siku ya sikukuu wapiti kama kawaida na mtu huyo ajifanye kama raisi na mimi nitampiga risasi”

    “Utampiga risasi akifa?”

    “Hato kufa kuna risasi za aina mbili kuna risasi moto na baridi na mimi nitatumia risasi baridi ila ahakikishe kwamba anavaa bullet proof itakayo mpa ulinzi zaidi hata kama nitakosea kumpiga sehemu nyingine”

    “Je na huyo mke wake?”

    “Pia watafute mwanamke wa kutengeneza ambaye atajifanya kama mke wa raisi wahakikishe kuwa wanafanana naye vizuri sawa”

    “Sawa kwani kuna mtaalamu mmoja tunaye pale kituoni ambaye ni mtegenezaji wa sura bandia pamoja na miili bandia ninaamini kazi hiyo itamfaa”

    “Ndio na huyo raisi wa bandia hakikisheni kuwa awi machepere machepere na ahakikishe amkarii vitendo raisi wenu kuanzia kutabasamu hadi kila aina ya pozi lililopo usoni mwake”

    “Sawa Eddy”

    “Na kipindi tukio hilo linafanyika hakikisheni raisi anakuwa yupo mbali kabisa na eneo la mji sasa utajua ni wapi mutakwenda kumuweka”

    “Je wewe hilo tukio utalifanyia wapi?”

    “Nitalifanyia kwenye ule mnara mrefu wa kanisa na nikiwa pale ninaweze kuuona mji kwa chini vizuri”

    “Basi mimi nitakusubiri geti la nyuma la kanisa kwani kuna gati linalo tokea upande wa baharini na usiokee kwa njia ya mbele”

    “Sawa usijali kwa hilo”

    ***

    Mipango tuliyo ipanga mimi na Afande Sofia ikaenda sawa kama tulivyo panga na tukawa na kazi ya kuwaangalia wananchi kupitia Tv ya taifa wakiwa wamejawana uchungua na huzuni na baada ya daktari aliuye mpokea raisi feki kusema kuwa raisi huyo hali yake sio nzuri kabisa na mida wowote anaweza lupoteza maisha.Sherehe nzima iliingia doa kwani wa raisi wao kipenzi ndio hivyo tena amepata tatizo la kupigwa risaisi na mtu wasiye mjua hadi wakati huu

    “Una mpango gani kijana?”

    Raisi aliniuliza huku akiwa na furaha usoni mwake

    “Nina mpango wa kuifwata familia yangu Marekani”

    “Ndio nyumbani?”

    “Hapana wamekwenda hospitali”

    “Basi tunaweza kukupeleka kwa ndege ya serikali kwa maana mchango na ujasiri ulio uonyesha ni mkubwa sana”

    “Sawa muheshimiwa”

    “Je ni lini unahitaji kwenda huko”

    “Hata leo”

    “Sawa ngoja niwasiliane na makao makuu wafanye kshuhuli ya wewe kusafiri pia kama huto jail nitakuzawadia mojawapo ya nyumba yangu ya kifahari iliyopo Italia hiyo itakuwa ni kama malipo yangu kwako na ninahitaji ukaishi mbali na hapa mabara haya ya Amerika”

    “Asante muheshimiwa”

    Mawasiliano yakafanyika na ikanilazimu kuweza kubadilisha mavazi kisha nikapanda kwenye helcoptar ya jeshi hadi uwanja wa ndege na nikaagana na Afande Sofia na akanipigia saluti kama heshima kisha nikapanda ndege ya serikali na ndani ya masaa machache tukawa tunalitafuta anga la bara la Amerka ya kaskazini.Tukafika nchi marekani na moja kwa moja nikaelekea katika hospitali walipo Juliana na wazazi weke haikuwa raisi kwangu kupotea kutokana jina la hospitali nililifahamu na kwabahai nzuri nikawakuta ndugu wote wa Juliana wakiwa wapo kwenye sura za kuchangamka na walipo niona furaha yao ikaongezeka mara dufu

    Hali ya baba ikaendelea kuwa nzuri siku hadi siku pi hali yaJuliana nayo ikaendelea kuwa nzuri na kutupa matumaini na ndani ya wiki kadhaa baba akawa amepona kabisa na kwa uapenda wa Juliana akawa kidogo anaweza kuzungumza ziruri japo kumbukumbu zake zikawa zimepotea.Katika kufwatilai kwenye mitandao ya kijamii nikagundua kuwa Paul Heamen na wezake wamekamatwa na bado hawajahukumiwa.Nikiwa katika tabasamu pana simu yangu ikaingia meseji

    {EDDY NILAZIMA UFEEE SIKU YOYOTE KUANZIA SASA}



    Nikaisoma meseji mara mbili mbili na nilipo ichunguza namba nikatambua ni namba kutoka nchini SURINAME kitu kingine kilicho anza kuniumiza kichwa kwamba ni nani aliye ijua namba yangu hii wakati ni mpya kabisa.Nikajaribu kuipiga nama iliyo nitumia meseji ila nikakuta haipatikana

    “Kaka Eddy”

    “Naam”

    Kuna jamaa mmoja alisema ni mtumishi wa Mungu kotaka Suriname aliniomba namba yako nikamtumia…amesha kupigia”

    “Ahaaa hapana bado hajanipigia”

    Ilinibidi nimdanganye kwa maana ningemuambia amenitumia meseji angesema amesemaje

    “Huyo aliye kuomba alikuwa ni mwanamke au mwanaume?”

    “Alikuwa ni mwanamke”

    “Jack siku nyingine mtu akikuomba namba yangu ninakuomba usitoe pasipo mimi kujua”

    “Sawa kaka Eddy”

    Hali ya Juliana ikaendelea kuhimarika siku hadi siku hadi ikafikia kipindi akaawa anakumbuka kila jambo la nyuma.Kutokana nina pesa ya kutosha nikaamua kununua nyuma katika mji wa Las Vegas japo ilinighaimu kiasi kikubwa cha pesa ila kwangu ikawa ni moja ya hatua kubwa kimaisha na nikafungua mradi mkubwa wa mgahawa ambao mama na Pretty wakawa ni wasimamizi wakubwa huku tukiendelea kumuombe Juliana aweze kupona kabisa

    Baada ya mwezi mmoja Juliana akaruhusiwa kurudi nyumbani huku hali yake ikiwa ipo vizuri kabisa na kwakipindi chote akiwa hospitali sikuweza kumgusia kuhusiana na maswala ya upendo,Nikiwa kwenye sehemu ya juu ya nyumba yangu ambayo ni ya gorofa nikiwa ninatadhimini juu ya nini nifanye kuhusiana na maisha ya mbeleni Juliana akanifwata hukua akiwa katika sura ya tabasamu

    “Eddy mbona unamawazo?”

    “Ahaa kuna maswala fulani ambayo kidogo ninayafikiria”

    “Maswala gani?”

    “Ninampango wa kumfungulia baba japo kampuni ila hadi sasa hivi sijajua ni kampuni gani nimfungulie”

    “Mmmm ni vizuri…Ila leo ninaomba nizungumze na wewe”

    “Kuwa huru”

    “Eddy ninakushukuru sana kwa msaada wako ambao umeweza kunifanyia…ni msaada ambao kamwe sinto weza kuusahau katika maisha yangu.Umekuwa ni mtu muhimu sana kwenye maisha yangu umenifanya familia yangu kutoka katika hali moja mbaya ya kiuchumi na sasa hivi tunaweza kusema na sisi ni miongoni mwa watu wenye kipato kizuri cha maisha nashukuru sana”

    Juliana alizungumza kwa sauti ya upole nay a unyenyekeva na akataka kunipigia magoti ila nikamzuia

    “Hapana usinipigie magoti kikubwa ni kumshukuru Mungu katika kulifanya hilo na ninampango ukaendelee na masomo yako ichini Italia ili ndoto zako ziweze kukamilika na mimi nitarudi nyumbani Tanzania….”

    “Eddy unataka kutuacha sisi na nani?”

    “Juliana hata nikikaa hapa furaha yangu haito weza kukamilika kama vile nitakavyo kuwa nipo nyumbani Tanzania….Pia ninahitaji kwenda kusali kwenye kaburi la mama yangu…Huu ni mwaka wa tatu nipo mbali na nchi yangu ni vyema mimi nikarudi”

    “Eddy….siwezi kuishi mbali na wewe nimekuzoea,ninakuhitaji uwe nuru ya maisha yangu.Mimi ni mwanamke niliye weza kujitunza hadi leo hii bado ninausichana wangu…..Eddy nahitaji kukupa zawadi ya usichana wangu kwani kwa sasa hakuna mwanaume yoyote ambaye anaweza kuwa katika moyo wangu zaidi yako…japo mwanzoni nilikuwa nimemuhifadhi mtu mwengine ila kwa alicho nifanya siwezi tena kuwa naye”

    Juliana alizungumza kwa sauti ya upole huku machozi yakimtoka,nikamuangalia kwa muda kisha taratibu nikanyanyuka kwenye kiti nilicho kaa na kumfwata taratibu hadi sehemu alipo kaa na nikapiga magoti chini na mikono yangu nikaiweka kwenye mishavu yake kisha nikamvuta taratibu karibu ya mdomo wangu na tukaanza kunyonyana midomo yetu kwa hisia kali huku moyoni mwangu nikiwa ninafuraha kwani kusema kweli Juliana aliweza kuziteka hisia zangu kwa kiasi kikubwa japo nilisha wahi kutembea na wanawake wengi kwa kipindi cha nyuma

    “Mghhhmmm”

    Tulisikia mguno nyuma yetu na kujikuta tukiachiana na macho yangu yakakutana na baba akiwa amesimama pembeni yetu huku sura yake ikiwa na tabasamu kubwa na sote tukajikuta tukipatwa na aibu na akachukua kitai nilicho kikalia na akakaa pembeni ya Juliana huku akitutizama na nikashindwa hata kusimama kwa aibu

    “Eddy na Juliana”

    “Mmmm”

    “Natambua kuwa sasa nyinyi ni watu wazima na ambao munastahili sasa kuwa na familia yenu ambayo itakuwa ni ya furaha….”

    “Eddy mwanangu ninakuomba uweze kumuoa mwanangu na kumtunza vizuri na yeye aje siku aweze kuitwa mama na sisi tuweze kuitwa babu na mama yenu aitwe bibi”

    Tukabaki tukitabasamu pasipo kumjiu baba kitu chochote na baba akasimama na kuniomba nikae kwenye kiti cha alicho kuwa amekaa na akatushika mikono yetu ya kulia na akatubariki kama mzazi na akaniruhusu rasmi niweze kumuoa mwanae

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tukaanza kufanya maandalizi ya ndoa na nikawaalika baadhi ya marafiki zangu ambao nimezoeana nao,Upendo kati yangu na uliana ukazidi kuongezeaka siku hadi siku na kila muda tukatamani siku ya ndoa yetu iweze kufika haraka ili tuweze kufunga pingu za maisha.

    Siku ambayo tuliisubiri kwa hamu kubwa sana ikawadia na kila mmoja ambaye tulimualika akatamani kutuona tukiwa kwenye mavazi ya wana ndoa,Nikafika kanisani nikiwa na mpame wangu huku sote tukiwa tumevalia suti zilizo endana na miili yetu na kutufanya tuweze kupendeza,Ndugu na jamaa ambao niliweza kuwaalika wamefika kanisani na kila nilipo pita nikielekea mbele ya kanisa waliweza kushangilia kwa furaha na katika masha yangu ya shida niliyo pitia sikuamini kama ipo siku nitaweza kuwa ndani ya suti na mimi nikafunga ndoa

    Tukakaa kwenye viti vilivyo andaliwa na tukaanza kumsubiri bibi arusi ambaye analetwa na baba mkwe.Shangwe na vigelegele vikatawala kanisani bada ya Juliana kuanza kuingia kwenye mlango wa kanisa.Kusema kweli Juliana uzuri wake uliweza kuongezeka mara dufu kwa jinsi tabasamu lake lilivyo tawala usoni mwake likazidii kuufanya uzuri wake kuongezeka

    Mchungaji kwa ishara akaniomba nikampokee Juliana ambaye amevalia gauni refu jeupe lenye kuburuzika nyuma huku sura yake ikiwa imefunikwa na kitambaa chepesi.Baba akamuachia mkono Juliana na mimi nikakaa kwenye upande wa kulia alipo toka baba na tukapiga hatua hadi sehemu ambayo mchungaji alituonyesha tuweze kukaa.Ibada ya ndoa ikaanza huku muda wote jicho langu moja likawa na kazi ya kumtadhimini Juliana baada ya muda mchungaji akatuomba tusogee mbele na akatoa pete ambazo mpambe wangu alimkabidhi kabla ya sisi kuingia kanisani,akaziombea na kunikabidhi na kuniuliza swali la kwamba nipo tayari kumuoa Juliana na kuwa mke wangu katika shida na raha magonjwa na taabu

    “NDIO NIMEKUBALI NA MUNGU UNISAIDIE”

    Makofi na vigelegele vikashamiri na mchungaji akanikabidhi pete na nikaunyanyua mkono wa Juliana juu na kuzungumza maneno ya kiapo cha ndoa kisha taratibu nikaishusha pete kwenye kidole cha mkono wa kushoto wa Juliana na kuzifanya kelele za shangwe zizidi kuongezeka

    Juliana naye akaulizwa na yeye maswali niliyo ulizwa mimi na akajibu kuifasaha kisha akakabidhiwa pete na akanivisha kidoleni na watu walio fika kanisani kuanza kushangilia kwa furaha

    “Uaweza ukamfunua shela”

    Mchungaji akaniruhusu kumfunua Juliana kitambaa kilicho funika sura yake kisha nikamvuta karibu yangu na kumpiga busu zito mdomoni na picha nyingi za watu tulio wakodisha kwa kazi hiyo zikatawala.Tukamaliza kazi ya kuweka saini kwenye vyeti vya ndoa na tukatangazwa kuwa tumekuwa mume na mke

    Tukatoka na kuingia kwenye gari la kifahari ambalo nililinunua kwa ajili ya harusi yetu tuu na tukaelekea kwenye moja ya busatani ambayo ipo kwenye hotel ambayo ndio tunafanyia sherehe na tukapigwa picha nyingi za ukumbusho.Baada ya muda tukaingia ukumbini ambapo sherehe yetu imehudhuriwa na watu wengi kiasi na baada ya sherehe kuisha tuapelekwa kwenye chumba cha gharama kubwa am acho tunakaa hapa kwa wiki moja kama mapumziko

    Furaha ikazidi kutawala kwenye maisa yatu huku nikijisifu kimoyo moyo kuwa nimepata zawadi kutoka kwa Mungu kwani ni mara chache sana kwa wasichana wa dunia ya sasa hivi ukawakuta wana bikra zao.Tukajifungia siku mbili ndani bila kutoka nje huku tukipeana kila linalo stahili kupeana kama wana ndo na siku zote vyakula tulikuwa tunaletewa ndani ya chumba chetu na wahudumu wa hii hoteli

    “Mke wangu hembe rudisha hiyo chaneli uliyo itoa”

    “Chaneli ipi?”

    “Hiyo ya habari hembu weka mara moja”

    Juliana akaweka chaneli ya aliyokuwa ameipitsha kisha akarudi kitandani nikaanza kuisikiliza habari ya ziara ya raisi wa Suriname bwana Jacob Daniel ambaye yupo nchini hapa Marekani kwa dhiara ya kikazi ya siku tatu

    “Raisi kuna kitu aliniahidi?”

    “Kitugani?”

    “Nitakumbia ngoja nifanye mpango wa kuonana naye”

    “Utamuonea wapi?”

    “Nitauliza tuu”

    Nikachukua simu yangu na kuwasiliana na mpambe wangu wa harusi na nikamuomba afwatilie juu ya wapi alipo raisi wa nchi yangu na akaniomba nimpe muda atanijulisha.Baada ya nusu saa akanipigia

    “Kaka Eddy”

    “Mmm vipi umejua ni wapi alipo?”

    “Ndio tena cha kumshukuru Mungu yupo kwenye hiyo Hotel mulipo nyinyi”

    “Kweli?”

    “Kweli inabidi mukaulizie”

    “Asante ndugu yangu”

    “Vipi shemeji hajambo?”

    “Huyu hapa zungumza naye”

    Nikampa simu Juliana na mimi nikashuka kitandani na kufungua begi letu lililo jaa nguo mpya na kanza kutoa nguo moja baada ya ngingine

    “Mume wangu vaa hiyo suruali ya jinzi na hiyo tisheti nyeusi”

    “Na viatu gani nivae?”

    “Hizo travota nyeusi utatokelezea sana”

    “Na wewe vaa tutakwenda pamoja”

    “Wapi?”

    “Si kwenda kumuona Raisi”

    “Nimechoka mume wangu”

    “Twende bwnaa mke wangu”

    Nikamfwata Juliana kitandani na kuanza kumtekenya tekenya na nikambeba na sote tukaingia bafuni na kuoga kisha tukarudi na kuvaa nguo ambazo tulichaguliana na tukatoka nje ya chumba chetu.Nikamuuliza mmoja wa wahudumu wa hoteli na akanielekeza ni wapi alipo raisi wa nchi tuliyo toka.Tukaelekea kwenye sehemu tuliyo elekezwa na kwa bahati nzuri nikakutana na Afande sofia akiwa miongoni mwa walinzi wa raisi

    “Kaka Eddy za masiku”

    “Salama”

    Nikamtambulisha Afande Sofia kwa Juliana na kutokana Raisi alikuwa na kikao ikatulazimu kumsubiria nje.Ndani ya dakika ishirini tukaruhusiwa kuingia kwenye ukumbi wa mkotano ambapo raisi baada ya kuniona akanikumaka vizuri na tukasalimiana na nikamtambulisha Juliana na raisi akanipongeza kwa uamuzi nilio uchukua wa kuoa

    “Aisee itabidi nikielekea hivi Italia twende sote nikakukabidhi nyuma niliyo kuahidi”

    “Sawa muheshimiwa ninashukuru sana”

    Tukaendelea kuzungumzia kuhusu maswala ya Paul Heamen na watu wake na kunihakikishia kuwa usalama juu yangu upo vizuri na hakuna mtua ambaye ataweza kunigusa.Tukawataarifu baba na mama juu ya safari yetu ya kwenda Italia kuhamia kwenye makazi mapya na wakatubariki na kututakia kila laheri kwenye mipano yetu.Tukawa ni miongoni mwa abiria wa ndege ya raisi wa nchi ya Suriname na ndani ya masaa kadhaa tukafika nchini Italia na akapokelewa na waziri mkuu wa nchi hii.Mimi na mke wangu Juliana tukafikizia kwenye hoteli ambayo raisi na watu wake walifikizia

    Siku ya pili yake mida ya saa mbili usiku baada ya Raisi kumaliza mikutano yake akatupeleka kwenye jumba la kifaharia ambalo akanikabidhi na kuniandikisha kama mmiliki wa jumba hilo na ikawa ni zaidi ya furaha katika maisha yangu pamoja na mke wangu wa pekee

    Ndani ya wiki moja tukaanza kuwa wenyeji kwenye mji wa Roma ambapo ndipo jumba letu lilipo na kwakipindi hichi kifupi tulicho kaa tukaweza kufahamiana na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu nchini hapa na ikaturahisishia sisi kuishi pasipo kusumbuliwa katika maswala ya uhamiaji

    “Mume wangu kuna kitu nahitaji kukuambia?”

    “Kitu gani?”

    “Leo nilizungumza na mama akaniambia kuwa Pretty na yeye anahitaji kuja kuishi nasi huku”

    “Ni vizuri tufanye mpango aje asomee mambo ya Hoteli ili apate ujuzi zaidi katika kazi anayo ifanya na mama”

    “Alafu hapo umezungumza mume wangu je na mimi nitasomaje?”

    “Utasomaje kivipi mbona sikuelewi mke wangu?”

    “Nina habari nzuri”

    “Habari gani mke wangu?”

    “Ninajihisi mabadiliko kwenye mwili wangu na ninaona ni ujauzito”

    “Kweli?”

    “Kweli mume wangu”

    Nikajikuta nikimkumbatia Juliana kwa fauraha na sikutaka kupoteza muda tukaingia ndani ya gari letu na kumpeleka kwenye hospitali inayo husiana na wanawake tuu na daktari wakachukua vipimo na kweli akanidhibitishia kuwa Juliana ni mjamzito

    “Na kitu kingine ambacho ninakupongeza bwana Eddy ni kwamba mke wako anaujauzito wa mapacha ya watoto wa kike”

    Nikawa kama mtu aliye changanyikiwa kwa furaha na kujikuta nikizunguka zunguka kwenye ofisi ya daktari huku nikishangilia,nikamfwata Juliana kitandani na kumnyanyua na kuanza kumbusu mdomoni wala sikujalia kama daktari yupo

    “Bwana Eddy inabidi mke wako awe katika uangalizi mzuri ambao hauta weza kumletea madhara ya watoto kuudhurika tumboni na isitoshe ni kwamba watoto wanaonekana wana afya kubwa na nzuri”

    “Asante dokta usijali kwa hilo”

    Tukatoka hospitali na kitu cha kwanza nikampigia simu mama mkwe na kumpa taarifa hiyo ambayo ikawa ni moja ya taarifa nzuri ambayo ikazidisha faraha katika familia zetu.Ndani ya siku mbili nikakamilisha swala la safari ya Pretty kuja kuishi nasi huku Italia na kitu kizuri ni kwamba ataweza kukaa na dada yake ambaye kwa sasa ninamlea kama yai ambalo sinta penda kusikia kwamba mimba yake itaharibika na ili mwanaume ukamilike hata uwe na pesa vipi ila mtoto ni kitu cha muhimu sana.

    Siku ya kwenda kumpokea Pretty ikawadia na nikamuacha Juliana nyumbani na mimi nikafika kwenye uwanja wa ndege na kumsubiria Pretty ambaye ndege yao itawasili baada ya nusu saa lijalo.Nikaelekea kwenye mmoja wa gahawa ulipo jirani sana na uwanja wa ndege japo kupata juisi huku nikivuta vuta muda kwa ajili ya kumpokea mdogo wa mke wangu

    Nikatafuta sehemu nikakaa na kuagizia juisi ambayo ninahitaji na muhudumu wa kike akaniletea juisi niliyo muagiza kwa baati mbaya akajikwaa na juisi ikanimwagikia kwenye shati nililo livaa na kumfanya aanze kuniomba msamaha

    “Wewe mbona unakuwa ni mshenzi sana unaona unawamwagia wateja juisi”

    Nilisikia sauti ya kike ikija nyuma yangu na mwanamke anaye foka akafika kwenye sehemu niliyo kaa na ikanibidi nimtazame na macho yangu yakakutana na Priscar ambaye mara ya mwisho kuonana naye ni kipindi tulipo tekwa na kundi la kigaidi na yeye alitoroka pamoja na mkuu wa kundi hilo

    “EDDY”

    “Ndio Prisca”

    Nikasimama na kukumbatiana naye kwa furaha kisha tukaachiana na kutazamana kwa muda huku sura zetu zikijawa na furaha kubwa

    “Eddy umekuwa mbaba”

    “Hata wewe umekuwa mmama”

    “Eheee kweli binadamu tunakutana…wewe nenda zako tutaonana baadaye”

    Muhudumu akaondoka na Prisca akakaa kwenye kiti cha pembeni na tukaanza kuzungumza mambo mengi ya nyumba

    “Vipi Prisca hujasumbuliwa kwenye maswala ya kigaidi?”

    “Ahaa walinisumbua kipindi fulani ila mambo yakaisha kabisa na nimeamua kuwa mtu mwema sasa na mungu amenibariki nina mtoto mdogo mmoja wa kiume ana miaka miwili na nusu”

    “Dooo hongera sana mimi mwenyewe ninataraji kuitwa baba”

    “Weee ahaa ndio maana nakuona una pete ya ndoa kidoleni”

    “Ndio vipi umeolewa na nani?”

    “Na mzungu mmoja ambaye ndio amenifungulia huu mgahawa”

    “Hongera sana vipi Tanzania ulisha wahi kwenda?”

    “Ndio na mama Caro anakutafuta hadi kwesho”

    “Wee anacho taka kutoka kwangu haswa ni nini?”

    “Sijajua ila kunaswala la mama yako itabidi hilo Eddy ulifanyia mpango wa kumtoa alipo ninaimani atakuwepo hai hadi leo”

    Kabla sijazungumza simu yangu ikaingia namba ya mezani na nikaipokea na kuisikia sauti ya Pretty

    “Shemeji nimesha fika naomba uje kunichukua”

    “Sawa nipo hapa karibu ninakuja”

    Nikakata simu na kumtazama machoni Christina

    “Vipi tena?”

    “Kuna shemeji yangu ninakwenda kumpokea hapo uwanja wa ndege hilo swala nitakutafuta tuzungumze vizuri”

    “Sawa naomba simu yako nikuandikie namba yangu”

    Priscar akaandika namba yake ya simu na nikaipiga kwenye simu yake ikaita,tukaagana na nikaondoka na kuelekea uwanja wa ndege na nikamkuta Pretty kwenye sehemu za wageni.Akanikumbatia kwa furaha na safari ya kwenda nyumbani kwangu ikaanza huku Pretty akinisimulia mamo aliyo yaacha nchini Marekani.Furaha ya Juliana ikazidi kuongezeka baada ya kumuona mdogo wake

    Maisha yakazidi kuendelea huku ujauzito wa Juliana ukikua taratibu na kuzidi kuhimarisha upendo kati yetu.Asubuhi ya siku ya leo ninakikao na jamaa ambao wanashuhulika na maswala ya urembo na lengo lao kubwa ni endapo watoto wangu watakapo zaliwa waweze kuingia mkataba na mimi na wawe wanazitumi picha za wanangu kuwemo kwenye matangazo ya urembo wa watoto hii yote ni kutokana na wao kumuona mke wangu na wanaamini kuwa watoto watakao zaliwa watakuwa ni wazuri kama mama yao au zaidi ya mama yao

    “Mumu wangu alafu leo nitakwenda mjini na Prety kutazama kile chuo ambacho atahitajika kwenda kuanza masomo”

    Juliana aliniambia huku akinifunga tai vizuri

    “Sawa mke wangu ila kama ni gari usiendeshe wewe muambieni dereva awapeleke”

    “Sawa mume wangu”

    Juliana akanibusu mdomoni na akanibebea begi langu lenye laptop hadi kwenye maegesho ya magari yaliyopo kwenye hili jumba letu la fahari na akaliingiza kwenye gari na kunifwata upande wa dereva na kukiingiza kichwa chake ndani ya gari na kunibusu tena huku macho yake yakiwa na huzuni

    “Mbona una huzuni mke wangu?”

    “Hapana mume wangu ila ninakuomba uweze kuwa makini huku huendapo ninahisi kuna jambo ambalo sio zuri litakutokea”

    “Jambo gani mke wangu?”

    “Usije ukanisaliti tuu mke wangu”

    “Siwezi kufanya hivyo niamini mimi”

    “Sawa ninakupenda sana mume wangu”

    “Ninakupenda pia kuwa makini”

    “Usijali”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikambusu tena mke wangu na nikavuta kidogo na kulibusu tumbo lake kisha nikawasha gari na kuondoka.Njia nzima nikawa ninayafikiria maneno ya mke wangu kuwa anahisi kuna jambo baya litanipata na njia nzima nikawa nipo makini sana katika uendeshaji wa gari langu aina ya Ferrari.Nikafika kwenye makao makuu ya ofisi ya kampuni ninayo taka kuingia nayo mkataba na nikatoa simu yangu na kumjulisha mke wangu kuwa nimefika salama

    “Na sisi ndio tunajiandaa kwenda chuoni na Pretty anahitaji kukusalimia”

    “Mpe simu”

    “Shemeji vipi?”

    “Salama”

    “Mbona umeondoka bila hata kuniaga?”

    “Ulikuwa umelala shem wangu”

    “Na huyu mke wako amekuwa mvivu kama nini?”

    “Kwa nini?”

    “Humfanyishi mazoezi”

    “Basi nikirudi leo nitamfanyisha mazoezi”

    “Sawa shem itakuwa vizuri”

    “Mpe simu mama kijacho”

    “Ehee mume wangu”

    “Nitazima simu nikiwa kwenye kikao sawa”

    “Sawa mume wangu nina kupenda sana”

    “Hata mimi pia ninakupenda mke wangu”

    Nikakata simu na kupokelewa na wahusika na baada ya muda tukaanza kikao na ikanilazimu simu yangu kuzima.Kikao hakikuwa kifupi kama nilivyo dhania kwani muda tulio uchukua kujadiliana ni jinsi watakavyo weza kuwatumia watoto wangu tukatumia zaidi ya masaa tisa kwani ilinilazimu kuweza kutafuta wanasheria wangu wapatao wanne watakao weza kulisimamia hili swala hata kama ikitokea nimefariki.Baada ya kikao wakaniomba nijumuike nao kwenye sherehe fupi ya kumuaga bosi wao ambaye anastaafu na alikuwa ni mtu wa makamo kidogo.Nikakumbuka uiwasha simu yangu mida ya saa moja usiku ili kumpa taarifa mke wangu.Nikajaribu kupiga simu na kukuta haipatikani na sikuwa na wasiwasi sana,mida ya saa mbili usiku nikawaaga na kuondoka zangu

    Nikajitahidi kuiendesha gari yangu kwa kasi na nikafika nyumbani kwangu na kukuta mazingira ya giza na nitaa za kwenye kuta ndizo zinazo waka ila si za ndani.Nikaanza kupata wasiwasi kwani si kawaida kwa nyumba yangu inapo fika wakati wa usiku kuzimwa taa.Nikashuka kwenye gari na kuanza kutembea kwa umakini hadi kwenye mlango wa kuingilia ndani na kukuta boksi kubwa likionyesha ni maboksi yanayoletwa na shirika moja la usafirishaji la DHL.Nikalipiga piga kwa mguu na kuliona ni zito kiasi na nikafungua mlango na kuwasha taa za sebleni na kutoka nje na kuliingiza boksi hili

    Nikapanda gorofani huku nikiliita jina la mke wangu na sikusikia jibu la aina yoyote na nikajaribu kupiga simu yake nikakuta haipatikani na wasiwasi ukazidi kunijaa zaidi.Kwa bahati mbaya zaidi sikuwa na namba ya simu ya Pretty

    “Ni nini kimempata mke wangu….? Au ni chaji ya simu imemuishia….? Mmmm hata kama ingekuwa imemuishia angenijulisha?....angenijulisha vipi wakati simu na mimi nilizima akhaaaa”

    Nikajikuta nikizungumza peke yangu huku nikijikuna kichwa changu na nikashuka hadi sebleni na nikapitiliza moja kwa moja haid jikoni na kuchukua kisu na kurudi nacho sebleni na kuanza kukata gundi iliyo tumika kufungia boksi hili huku nikipiga mluzi.Nikamaliza na taratibu pua zangu zikaanza kukutana na manukato mazuri na sikujua ni kitu gani kilichopo ndani ya boksi.Nikalifungua na kukuta kipande cha boksi kilicho tengenezwa kama mfuniko na nikakisika kwenye kishikizo kilicho licho tengenezwa kwenye kipande hichi na kujikuta nikipata mstuko mkali huku mwili mzima ukitetemeka kwa woga na kuhisi ninacho kiona ni kama filamu ya kuigiza hii ni baada ya kuviona vichwa viwili vilivyo jaa damu huku kimoja kikiwa ni cha mke wangu Juliana na kingine kikiwa ni cha Pretty shemeji yangu na pembeni nikakuta kikaratasi chenye ujumbe unasomeka

    {HUU NI MWAZO TU WA VITA YETU NA WEWE}



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog