Search This Blog

Thursday 19 May 2022

SORRY MADAM - 4

 





    Chombezo : Sorry Madam

    Sehemu Ya Nne (4)



    ILIOISHIA

    “Bye….”

    Nikaanguka chini, huku nikilalia tumbo na giza nene taratibu likaanza kuyafunika macho yangu, na kwambali nikaanza kuisikia sauti ya Dorecy ikiliita jina langu kwa uchungu

    ENDELEA

    Sikuweza kusikia kitu chochote kinacho endelea kwenye masikio yangu

    ***

    Kwa mbali nikaanza kuhisi sauti za watu wakizungumza taratibu, nikajaribu kuyafumbua macho yangu kutazama ili nione ni kina nani, ila ukungu mwingi uliojaa machoni mwangu sikuweza kuwaona vizuri.

    “Eddy”

    Nilisikia sauti ikiniita masikioni mwangu, ambayo inaendana na sauti ya mke wangu Phidaya, nikageuza shingo yangu kutazama sehemu inapo tokea sauti hiyo, nikawaona watu wawili wakiwa wamesimama huku mmoja akiwa amevalia mavazi meupe huku wapili nguo zake zikiwa na rangi mchangayiko.

    “Eddy mume wangu upo salama?”

    Sauti ya Phidaya ikaendelea kupenya masikioni mwangu, nikajaribu kuzungumza ila kinywa changu nikakikuta kikiwa ni kizito sana, Nikabaki nikimtazama Phidaya mke wangu, aliye valia gauni lenye rangi machanganyiko, mkono wa Pihidaya ukapita kwenye sura yangu, kisha mwanaume aliye valia nguo nyeupe akamshika na kumuondoa ndani ya chumba

    Hali yangu ya afya ikazidi kuhimarika siku hadi siku, nikiendelea kupatiwa huduma na madaktari ambao sikuwafahamu, zikapita siku kadhaa nikiwa kitandani nikiendelea kuuguza majeraha yangu ya mwili mzima huku Phidaya akija kunitembelea kila siku, ila kitu kikubwa ambacho ananificha ni jinsi ya mimi kufika katika hospitali hii

    “Baby ngoja mimi nirudi hotelin”

    Phidaya alinyanyuka kiuvivu huku tumbo lake likiwa kubwa kiasi, kutokana na ujauzito wake alio kuwa nao

    “Ngoja kwanza”

    Nilimuambia Phidaya huku nikimshika mkono wake wa kushoto, uliokuwa karibu yangu

    “Kwa nini huniambii ukweli, juu ya kufika kwangu hapa”

    “Eddy nilisha kueleza kwamba, nitakujibu mume wangu siku ukiwa umepona vizuri, hili swala halina haja ya wewe kulijua kwa wakati huu

    “Hata kama, kwani kukuuliza jinsi ya mimi kufika hapa imekuwa ni shida, si ndio?”

    “Hapana mume wangu, ila kikubwa ni wewe afya yako kuwa katika hali ya uzima”

    “Powa kama hutaki kuniambia chochote ninakuomba uende zako”

    Nilizungumza kwa hasir huku nikimtazama Phidaya aliye simama pembeni ya kitanda changu,

    “Baby umekasirika?”

    “Hapana, wewe nenda”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Phidaya akaanza kupiga hatua za kuondoka kuelekea ulipo mlango wa kutokea katika chumba cha hospitalini, kabla hajaufikia nikamstua

    “Na usipo nikuta, usijilaumu”

    Ikamlazimu Phidaya kugeuka na kunitazama kwa macho ya mshangao mwingi, taratibu akarudi na kukaaa kwenye kiti, huku sura yake ikiwa na huzuni kidogo

    “Mume wangu ni kwanini unazungumza maneno kama hayo, unajua ni jinsi gani unavyo utesa moyo wangu”

    “Tatizo sio kuutesa moyo wako ila tatizo ni kwanini hutaki kuniambia ukweli juu kufika kwangu hapa, kwa mtazamo wangu hapa si Iraq, siwezi kuendelea kukaa sehemu ambayo siijui ni wapi nikifa j…?”

    “Eddy inatosha…”

    Phidaya alinikatisha na kuzungumza kwa sauti kubwa ya ukali huku machozi yakimwagika usoni mwake, akanitazama na macho yake makubwa kiasi ambayo tayari yalisha anza kubadilika rangi na kuwa mekundu kiasi

    “Eddy unajua ni jinsi gani, tabu niliyo ipata hadi kukuleta hapa eheeeee? Ulikuwa ni mfu wewe usiye jitambua, umeyafanya maisha yangu kuwa ni yakuwindwa kama kitu cha thamani kwa ajili yako”

    Phidaya alizungumza kwa sauti ya ukali iliyo jaa hasira

    “Utaka kujua kwamba hapa ni wapi si ndio?”

    Swali la Phidaya likaniacha mdomo wazi huku nikishindwa kujua ni jinsi gani nimjibu

    “Si unataka kujua, mbona uzungumzi?”

    “Ndio”

    Nilijibu kwa unyonge baada ya kumuona Phidaya akinijia juu

    “Hapa Manila, Philipines”

    “Ndio wapi?”

    “Ndio hapa”

    Phidaya alinijibu kwa ufupi huku akinitazama machoni, akanyanyuka na kupiga hatua za haraka hadi shemeu ulipo mlango akafungua na kutoka, nikajikuta nikishusha pumzi nyingi, huku nikuutazama mlango aliotoka Phidaya.Kitu kikubwa ambacho kunaniumiza kichwa ni juu ya kwanini Phidaya hataki kunieleza ukweli jinsi ya yeye alivyo fika hapa

    Siku mbili zikapita pasipo kumuona Phidaya, jambo lililoanza kuzua wingi wa maswali kichwani mwangu, huku nikijiuliza ni nikwanini sijkumbili hizi hajatokea.

    “Au hao watu wanao muwinda ndio wamemteka?”

    Niswali jingine lililotokea kuniumiza kichwa change, kutokana nimeshaanza kuruhusiwa kutoka nje ya maeneo ya hii hospitali iliyojaa watu wenye asili ya bara la ulaya na asia.Sikuwa na rafiki zaidi ya kuzunguka kila eneo la hospitali huku nikiwa nimevalia nguo nyeupe zinazo fanana na wangonjwa wengine wanao zunguka zunguka katika eneo hili la hospitlini

    Baada ya kuhisi kuchoka nikaamua kurudi kwenye chumba change, kabla sijakifikia nikawaona jamaa wawili walio walia nguo nyeusi pamoja na miwani wakiingia ndani ya chumba change, ikanilazimu kujibanza kwenye moja ya kona ya ukuta kutazama kujua ni kitu gani amacho kitaendelea, baada ya dakika kama tatu hivi jamaa wakatoka na kuondoka, jambo lililo anza kunipa mashaka mengi

    “Niende au nisiende?”

    Nilijiuliza huku mwili mzima ukinitetemeka, nikatazama mlango wa chumba changu kisha nikajipa matumaini mimi mwenye kwamba hakuna kitu kibaya kitakacho tokea juu yangu, nikaanza kupiga hatau za kwenda kilipo chumba change, nikafika kwenye mlango na kukishika kitasa, nikashusha pumzi na kufungua mlango taratibu.Nikamkuta Phidaya akiwa amekaa kwenye kiti pamoja na mwanamke aliye valia baibui jeusi, huku usoni mwake akiwa amejiziba na kubakisha macho yake, nikawatazama kwa muda huku nao wakinitazama, msichana aliye vaa baibui akajifungua uso wake na kujua kwamba ni Dorecy

    “Mbona unashangaa?”

    Dorecy aliniuliza huku akinyanyuka kwenye kiti nilicho kikalia

    “Hapana”

    “Karibu ndani ukae”

    Nikapitiliza moja kwa moja na kukaa kitandani mwangu, na kuwatazama Phidaya, aliye nunu na Dorecy ambaye sura yake ipo kawaida tu

    “Ninafuraha kukuona tena ukiwa hai Eddy”

    “Asante”

    “Niliwaagiza watu wangu wakakutafute huko nje, kutoka tulilkuja muda mrefu hatukuona, ila tulivyo wauliza manesi wakadai kwamba upo kwenye maeneo ya viwanja vya michezo”

    Dorecy aliendelea kuzungumza huku akiwa amesimama akinitazama kitandani sehemu nilipo kaa

    “Ila vipi bado unamaumivu ya vidonda vya risasi?”

    “Hapana vimesha kauka”

    Ukimya ukatawala ndani ya chumba huku kila mmoja akiwa yupo kimya akimtazama mwenzake aanze kuzngumza.Phidaya akasimama na kutaka kutoka ndani ya chumba ila Dorecy akamkamata mkono

    “Shoga yangu ninakuomba utulize hsira usiondoke”

    “Sioni sababu ya mimi kuendelea kukaa hapa”

    “Ndio ninatambua ya kwamba unahasira sana, ila ninakuomba utulie kwani kuendelea kuwa na hasira haitasaidia kupatana kwenu”

    Dorecy aliendelea kuzungumza huku akiwa ameushika mkono wa Phidaya aliye vimba kwa hasira, sikujua ni kitu gani ambacho kimemkasirisha Phidaya hadi ikafikia hatua ya yeye kunichukia kupita maelezo.Phidaya akarudi na kukaa kwenye kiti chake alichokuwa ameka

    “Eddy natambua ya kwamba hujui ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa wakati huu, ila utaelewa tuu”

    “Kwani mke wangu unatatizo gani?”

    “Nani mke wako?”

    “Haaaa”

    Ilinibidi kushangaa tu kwani sikulitarajia jibu kama hili la Phidaya kunijibu mimi, kwaishara Dorecy akaniomba ninyamaze kimya kwamaana ananijua mimi vizuri sana pale ninapokuwa nimekasirika

    “Eddy ile siku ambayo ulipigwa risasi kule porini, mume wangu alinichukua mimi pamoja na mtoto, akiamini kwamba wewe umeshafariki.Walinipeleka hadi nyumbani, ila kwa siri sana nilizungumza na hawa walinzi wangu wawili nilio kuja nao huku”

    “Walienda kukuchukua kule porini nakunipele kwenye moja ya hospitali pasipo Khalid kugundua kitu cha aina yoyote.Kwa kipindi chote ulipokuwa kwenye hospitali ya siri, ukifanyiwa matibabu ya kuyaokoa maisha yako, niliendelea kulifanyia kazi ombi lako la wewe kumtafuta mke wako, hadi nikafanikiwa kimpata”

    Tulinyamaza kimya mimi na Phidaya tukimuacha Dorecy akizungumza,

    “Baada ya kukutana na bibie hapa, nilimueleza kila kitu juu yako, na maisha yetu ya nyuma, kitu ambacho sikukijua ni kwamba kunabadhi ya mambo ambayo wewe hukumuadisia mkeo na mimi nikajikuta nikumuadisi”

    “Phidaya alikasirika sana, na kukiri kwamba hakufahamu wewe, ila nileiendele kumbembeleza ili asifikie hatua ya kukutenga wewe, nashukuru Mungu kwamba alinielewa, kumbe kunakipindi kunatukio ambalo mulilifana wewe na yeye, ambalo kule Iraq hadi leo munatafutwa na serikali ya kule”

    “Ngoja kwanza, tukio la mimi kutoroshwa hospitali ndilo lilolofanya sisi kutafutwa?”

    Nilimuuliza Dorecy na kumfanya Phidaya kunitazama kwa jicho kali lililo jaa hasira

    “Ndio, ila kuna ishu Khalid alitaka kukufanyia wewe na Phidaya akaiingilia kati na kuwa adui namba mwengine wa Khalid”

    “Jambo gani hilo?”

    Hata kabla Dorecy hajanijibu tukasikia milio mingi ya risasi kwenye kordo yetu huku kelele za watu wagonjwa na manesi wakike zikisikia jambo lililo tustua sote ndani ya chumba



    Milio ya risasi ikaendelea kurindima nje ya chumba tulichopo na kuzidi kutupagawisha sote tuliopo ndani ya chumb hichi, wasiwasi mwingi ukawa kwa Dorecy ambaye fika anaoenekana kuchanganyikiwa

    “Eddy hao ni watu wa mume wangu”

    Dorecy alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka, nikapiga hatua za haraka hadi dirishani na kuchungulia chini ambapo kuna umbali wa ghorofa mbili kwenda chini.

    “Hatuwezi kutoka humu ndani”

    Nilizungumza huku nikiwatazama Dorery na Phidaya

    “Itakuwaje sasa?”

    Phidaya alizungumza huku machozi yakimwagika kwa wingi.Nikapiga hatua hadi mlangoni, nikachungulia kwenye sehemu ya kuingizia funguo, nikamshuhudia jamaa mmoja akitandika risasi ya kichwa mzee mmoja aliye ambiwa alale chini ila akaleta kiherehe cha kujinyanyua, ndipo akakutana na maafa hayo ambayo ni yakinyama sana.

    Gafla simu ya Phidaya ikaita na kutufanya sote kumgeukia na kumtazama kwa macho ya mshangao, kwa kiwewe alicho nacho akashindwa hata kuikata na kujikuta akiiachia na kuanguka chini, nikachungulia tena kwenye tobo la kuingizia funguo na kumuona jamaa aliye muua mzee, akiutazama mlango wetu kwa umakini.

    “Ingieni bafuni”

    Nilizungumza kwa sauti ya chinichini, Dorecy akamshika mkono Phidaya na kukimbilia kwenye bafu liilopo humu ndani ya chumba changu.Jamaa akapiga hatua hadi ulipo mlango uku bunduki yake aina ya ‘short gun’ ikiwa mkononi mwake.Nikajibanza nyuma ya mlango, huku mapigo ya moyo yakinienda mbio kiasi kwani bado sijaiamini afya yangu kwa kiasi kikubwa kutokana na majeraha ya risasi yaliyopo mwilini mwangu.Mlango taratibu ukafunguliwa, nikaanza kuona kiatu cheusi kikitangulia mbele, jamaa akasimama kwa muda, gafla simu ya Phidaya iliyo anguka chini ikaanza kuita tena na kumfanya jamaa kupiga hatua za taratibu hadi sehemu ilipo anguka simu na kuiokota.Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, kwani endapo jamaa atageuka nyuma nilazima ataniona.Akaitazama simu ya Phidaya kwa muda na kuitupa chini na kuchanguka, akatazama mlango wa kuingilia bafuni ambapo ndani yake yupo Phidaya na Dorecy

    Simu ya jamaa ikaita, akaitoa kwenye koti lake, akaipokea nakuiweka sikioni mwake, akazungumza kwa lugha ya kiarabu, nikastukia kumuona jamaa akichomoka kwa kasi, ndani ya chumba pasipo kuniona nyuma ya mlango, ving’ora vya gari za polisi, nikaanza kuvisikia na kunifanya nishushe pumzi nyingi, na kujikalia chini, huku jasho jingi likimwagika.Ndani ya dakika kadaa askari kadhaa wakawa wameingia katika sehemu tulipo, Dorecy na Phidaya wakatoka bafuni, askari na madaktari walio salimika katika vamizi la majambazi hawa

    ***

    Wagonjwa tulio salimika tukahamishwa kwenye hospitali moja, inayo milikiwa na jeshi la nchi ya Philipines, matiibabu yangu hayakuchukua muda mrefu sana, nikaruhusiwa kutoka hospitalini na kuhamia kwenye hoteli ambayo Phidaya anaishi kwa siri sana, na amelipiwa gharama zote na Dorecy ambaye tayari amerudi kwa mume wake.

    “Phidaya,itatubidi turudi Tanzania”

    Nilizungumza huku macho yangu yakimtazama Phidaya aliye jilalia kiuvivu kwenye kitanda, huku akiwa tumbo wazi akilichezea chezea kwa kiganja chake tumbo lake lenye kiumbe ndani

    “Si usubiri niweze kujifungua kwanza”

    “Hatuwezi kuishi hapa, pasipo sisi kuwa na kazi, unadhani tutayamudu vipi haya maisha?”

    “Sawa mume wangu, je tukirudi huko Tanzania, tutafikia wapi wakati umesha sema kwamba mama yako alitekwa na baba yako mkubwa”

    Nikamtazama Phidaya kwa muda, kwani kitu alicho kizungumza kinamaana kubwa sana kwangu, isitoshe sijajua ni hali gani inayo endela kati ya mzee Godwin na mama yangu.Nikanyanyuka taratibu na kuisogelea computer iliyopo kwenye meza humu chumbani kwetu, ambayo imeunganishwa na huduma ya Internet.Nikaiwasha taratibu, baada ya muda nikafungua mtandao wa Google

    “Unataka kufanya nini?” Phidaya alizungumza huku akipiga hatua na kuja kukaa kwenye kiti nilicho kikalia mimi

    “Kuna mtu nataka kumtafuta”

    “Nani?”

    “Baba yangu mzazi, anaishi Afrika kusini”

    “Mmmm sawa”

    Nikaliingiza jina la baba yangu mzazi kwenye sehemu ya kutafutia, kwenye mtandao huu ambao unasadikika ndio mtandao mkubwa duniani kote, ulio kusanya mambo mengi sana, ndani ya sekunde kadhaa nikawa nimefanikiwa kulipata jina la baba yangu mzazi pamoja na historia yake, cha kumshukuru Mungu nikakutana na taarifa nyingine iliyo nipendezesha moyoni mwangu, kwani ameingia kwenye orodha ya matajiri kumi nchini Afrika kusini huku yeye akiwa nafasi ya nne kutoka juu.

    “Inabidi twende nyumba ni kwa baba”

    “Sawa mume wangu”

    Phidaya hakuwa na pingamizi na maamuzi yangu niliyo yachukua, nikaanza kufwatilia hati za kusafiria kuelekea Afrika kusini, kutuokana na pesa ambazo Dorecy anatusaidia, sikupata tabu sana katika kukamilisha maswala usafiri wa ndege.Siku ya pili tukakusanya kila kitu kilicho chetu kwenye hoteli ambayo tunaishi, tukakodi Tanksi hadi uwanja wa ndege, muda wa kupanda ndege ulipo wadia, tukaungana na wasafiri wengine na kuingia ndani ya ndege, na taratibu safari ikaanza, huku moyoni mwangu nikimuomba Mungu atufikieshe salama, kwani kumbukumbu za ajali iliyo tokea nchini Kenya kipindi nikitokea Afrika Kusini, inaendelea kuzunguka ndani ya kichwa changu kama mkanda wa filamu.Phidaya kwa kudeka muda wote kichwa cheka amekilaza kifuani mwangu, huku akiimba nyimbo za kunibembeleza kwa sauti ya chini

    “Baby” Nilimuita kwa sauti ya upole

    “Mmmmm”

    “Naomba niende msalani”

    “Sawa, ila usichelewe mume wangu”

    Phidaya alinijibu taratibu huku akijinyanyua, kifuani kwangu taratibu, nikasimama, na kuanza kupiga hatua za kuelekea chooni, nikaingia ndani ya choo na kumaliza haja zangu zote, nikanawa uso wangu ili kuutoa uchovu na usingizi unao ninyemelea usoni mwangu.Nikafungua mlango, gafla nikastulia kitu chenye ncha kali kikinikita mgongoni mwangu, na sauti ikasikika kutoka nyuma yangu

    “Tulia kama ulivyo upo chini ya ulinzi, Mr Eddy”



    Mwili ukanisisimka na kujikuta nikitulia kimya, huku kwa mbali mapigo ya moyo yakianza kunienda mbio, ila sauti niliyo isikia nyuma yangu haikuwa ngeni masikioni mwangu, nikatamani kugeuka na kutazama nyuma ila sikuwa na uwezo kutokana nipo chini ya ulinzi wa mtu huyu.

    “Oya wewe bwege kweli, kijiko pia kinakutisha”

    Mtu aliye nyuma yangu alizungumza huku akizunguka na kuja mbele yangu, macho yangu yakakutana na John, rafiki yangu wamuda mrefu tangu tukiwa shule ya sekondari, akiwa amevalia mavazi maalumu kama watumishi waliopo kwenye hii ndege, nikashusha pumzi nyingi na kubaki tukitazamana.Tabasamu likatawala usoni mwa John na mimi pia nikajikuta nikitabasamu na kukumbatiana naye huku tukipigana pigna migongoni kwani, nimiaka kadhaa imepita pasipo sisi kuonana

    “Eddy mwanangu, aahaa nikitambo sanaa”

    Johna alizungumza kwafuraha huku tukiachiana

    “Kweli mwanangu, haya mbona huku tena kwenye ndege?”

    “Ndugu wee acha tuu, maisha mwanangu yanabadilika”

    “Ndipo unapofanyia kazi?”

    “Nipo training(mafunzo), napata pata ujuzi”

    “PCB wewe umekuwaje, umekuja kwenye ndege huku, au ndio hiyo elimu ya Tanzania, HKL anakuwa mkaguzi wa fedha, wakati Mathematics amenyoosha mswaki?”

    Nilizungumza kwa utani huku nikiwa nafuraha usoni mwangu

    “Ahaaa kaka, ndio maana yake, huku tumeingia hivyohivyo tuu, tena kwa masaada wa mama yako ndipo aliniunganisha huku”

    Taarifa ya John ikanistua kidogo nakujikuta nikaanza kumfkiria mama yangu

    “Mama yangu yupi?”

    “Haaa kwani Eddy wewe una mama gani mwengine?”

    “Hapana nimekuuliza hivyo kutokana nina maana yangu?”

    “Mama yako ambaye kwa sasa ni waziri wa usafirishaji, ametoka kwenye kitengo cha Afya”

    “Unataka kuniambia kwamba mama yangu yupo hai?”

    “Ndio yupo hai, tena yeye anakutafuta wewe”

    “John umeniacha njia panda hemb……..”

    Sikuimalizia sentesi yangu, msichana mmoja aliye valia mavazi kama John, alimuita John kwakutumia lugha ya kingereza

    “Am coming”(Ninakuja)

    John alimjibu msichana aliye muita huku akimtazama usoni mwake

    “Sasa Eddy, ngoja mimi nikaendelee na majukumu ndugu yangu”

    “Sawa ila kaka nahitaji tuzugumze zaidi”

    “Usijali kwani wewe unaelekea wapi?”

    “Afrika kusini, kwa mzee”

    “Mzee gani tena, kwa maana baba yako amefungwa?”

    “Eheee”

    “Kwani Eddy ulikuwa wapi siku zote”

    “John”

    Sauti ya msichana aliye muita John mara ya kwanza ilisikika tena, ikimuita kwa msisitizo

    “Kaka baadaye”

    John aliondoka kwa kupiga hatua za haraka kwenda katika sehemu alipo itwa, nikashusha pumzi kwa mara nyingine, huku kichwa changu kikiingia mawazo mapya katika maisha, kwani kwakipindi hichi, nilichokaa mbali na nchi yangu sikujua ni mambo yapi yaliyo endelea kwenye nchi yangu, na pia sikujua ni kitu gani lilichotokea kati ya mama yangu na mzee Godwin, baba yangu mkubwa ambaye kwa mara ya kwanzi nilidhani kwamba ni baba yangu mzazi.Nikarudi kwenye siti yangu, huku nikiwa nafuraha usoni mwangu

    “Mbona umechelewa kurudi ulikuwa na nani?”

    Phidaya aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu, nikajikuta nikitabasamu kwa furaha na kumtazaka usoni mwake

    “Mke wangu, ninafuraha wee acha tuu”

    “Furaha gani tene hiyo?”

    “Kwanza nimekutana na rafiki yangu wa kipindi kirefu sana”

    “Nani?”

    “Nitakuambia tukitulia”

    “Ahaaa eheee, sawa bwana”

    Phidaya alizungumza kwasauti yakudeka huku akigeukia uapande wapili wa siti yake, nikaupitisha mkono wangu mmoja kwenye kiuno chake na kumvuta karibu yangu na kichwa chake akakilaza kifuani kwangu taratibu

    “Umekasirika?”

    “Ndio”

    “Nisamehe mke wangu”

    “Sikusamehe, hadi uniambie umekutana na nani?”

    Nikamuadisia Phdiaya, historia fupi kati yangu na John, nikamuelezea kuhusiana na maisha ya mama yangu japo hakunieleza kwa undani, sana kuhusiana na maisha yaliyo jitokeza kwenye familia yangu ila moyoni mwangu kidogo nikipata matumaini yakumuona mama yangu, hadi namaliza kumuadisia Phidaya, mwenzangu tayari usingizi umepitia nakulala fofofo.Baada yamasaa kadhaa, sauti ya msichana ilisikika kwenye vipaza sauti vilivyomo ndani ya ndege, akituomba tufunge mikanda kwani ndege ipo karibuni kutua katika uwanja wa ndege wa ‘Johannesburg’.Ndani ya dakika kadhaa ndege ikatua kwenye uwanja na abiria wakaanza kushuka mmoja baada ya mwengine, John akafika hadi kwenye siti yetu, ambapo ametukuta tunatoa toa mabegi yetu katika sehemu ambayo tumeyaweka

    “Huyu ndio, John ambaye nilikuwa nikikuambia”

    Nilimtambulisha John kwa Phidaya

    “John huyu ni mke wangu, anaitwa Phidaya”

    “Ahaaaa, habari yako shemeji”

    Phidaya na John wakasalimiana kwa muda huku wote wakiwa wanafuraha, John akatuomba tumsubiri nje ya uwanja, yeye nawezake wakimalizia hatua za makabidhiano ya ndege, nawahudumu wengine ambaoa watarudi kwenye safari ya mzunguko wa ndege hiyo.Tukakaguliwa mimi pamoja na mke wangu Phidaya, tukatoka nje ya uwanja wa ndege na kutafuta sehemu yakukaa, Ndani ya dakika kumi na tano John akaja katika sehemu tuliyo kaa, kutokana ipo wazi sana kwa watu kutuona

    “Jamani, sijui nyinyi wezangu munaelekea wapi?” Jonh alituuliza

    “Sisi tunasafari yakuelekea kwenye Cap town”

    “Munaonaje tukafikizia Hotelin leo, kisha kesho muweze kwenda kwakutumia usafiri watreni za umeme”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    John alitushauri, sikuwa nakipingamizi kutokana hatukumaliza mazungumzo na John juu yakitu ambacho kimetokea kwenye maisha ya miaka michache iliyo pita, tukakidisha taksi iliyotupeleka kwenye hoteli moja iitwayo ‘Mondior Concorder’ iliyopo pembezoni mwa barabara ya Albetina Sisulu, tukafanikiwa kupata vyumba viwili vyenye hadhi nzuri kwawageni kulala

    “Baby mimi najisikia kuchoka, nitapumzika zangu ndani”

    Phidaya alizungumza mara baada ya kuingia katika chumba tulicho chukua

    “Kwanini?”

    “ Kuna chakwanini wakati nimekuambia kwamba nimechoka, hivi unadhani hili jitoto lako humu ndani halinichoshi?”

    “Mmmm mke wangu na wewe kwakudeka, haujambo”

    “Nini”

    “Yaishe mama kijacho”

    “Wewe niudhi tuu”

    Phidaya alizungumza huku akijilaza kitandani taratibu, kwa jinsi mwili wa Phidaya ulivyo umbika, umekuwa nikivutio kizuri kwangu ambacho sichoki kikitazama kila muda na dakika zake zinavyo zidi kukatika

    “Kweli hapa nimepata mke”

    Nilijisememea kwasauti yachini chini, nakumfanya Phidaya kunitazama kwamacho makali, akaachia msunyo mkali na kujiweka vizuri kitandani, kutoka tayari kumeshaanza kupambazuka, sikuona haja ya mimi kuendelea kulala kitandani, kusimama kwenye dirisha la chumbani chetu lenye kioo kikubwa, na kuaanza kuuangalia mji huu jinsi ulivyo jengeka kwa majengo yaliopo kwenye mpangilio mzuri

    “Huji kulala hapo umesimama kama mshumaa wapasaka, maana yake ni nini?”

    Phidaya alizungumza huku akitumbulia macho yake, makubwa kiasi

    “Mke wangu saa hizi, saa kumi na mbili na nusu, nitalala nini?”

    Phidaya akajifunika kwashuka gubigubi, kwa jinsi ujauzito wa mke wangu ulipo fikia, unampelekesha kama mtoto mdogo kwani kila analo lifanya nikituko kwangu.Asubuhi namapema nikakutana na John kwenye mgahawa uliopo chini ya hoteli hii, akaanza kuniadisia kila kitu amcho kilitokea kwapindi kizima nilipokuwa sipo nchini Tanzania

    “Mama, yupo salama kabisa na nijuzi kati tu, hapa nilikuwa naye kwenye ndege yetu inayo elekea Tanzania, alikuja huku kwa mambo yake binafsi”

    “Ehee ilikuwaje?”

    “Siku ambayo ilikuwa ni graduation(mahafali) yakumaliza kidato cha sita ndipo, siku ambayo nilikutana na mama wakati wausiku.Ile siku nakumbuka ilikuwa nijumamosi, wakati wausiku nilikuwa na demu mmoja sidhani kama utakuwa unamfahamu”

    “Alikuwa ni mwanafunzi?”

    “Ndio, anaitwa Catherina?”

    “Simkumbuki”

    “Nahisi alihamia kipindi wewe, umeshaondoka, kama unavyojua mwanangu maisha ya shule, tuliamua usiku kwenda sehemu yakujificha kule msituni, ambapo tulianza, kufanya yetu kwenye kichaka”

    “Mmmm, hukuwa na pesa ya chumba nini?”

    “Ahaaa hoteli zote zilijaa wageni, waliokuja kwenye sherehe, kipindi tunafanya yetu, kwa mbali tulianza kusikia vishindo vya watu wakitembea kwenye eneo tulilopo, ikatulazimu kukatisha mautamu yetu, nakujikuta tukijificha kwenye kichaka chetu”

    “Tuliwashuhudia watu hao wakiitupa miili ya watu wawili, huku wote wakibishana nakudai kwamba watu hao tayari wameshafariki, walipo watupa, wakaondoka zao na kutuacha sisi, tukiwa tunatetemeka”

    “Sasa mulikuwa munatetemeka nini?”

    “Weee, Eddy wewe unazungumza tuu, kukutana na watu kama wale si kitu kidogo, mbona Catherina alijikojolea kwa woga”

    “Dooooo” Nilijikuta nikicheka

    “Sijui hata ujasiri niliupatia wapi, nikajikuta nikipiga hatua za kwenda kutazama sehemu walipo tupwa watu wale, japo Catherina alikuwa na wasiwasi, kufika ile sehemu, nikastukia kuona mmoja wao akistuka na kutoa ukelee, kumcheki vizuri wapili naye nikagundua kwamba yupo hai, ambaye ni mama yako, Ila miili yao ilikuwa imedhohofika sana, tena sana, ilinilazimu kwenda kumuomba, Lucas gari lao”

    “Lucas nani?”

    “Lucas Martin, tuye jamaa wa HKL aliyekuwa anajisikia sana”

    “Ahaaa nimemkumbuka”

    “Alikuwa anatembeala na gari ya baba yake, aliyokuja nayo kwenye mahafali, basi tuliwapeleka kwa bibi yangu aliyepo pale pela Arusha yeye ni nesi, ila nilifanya nisiri sana watu wasijue kutokana mazingira tuliyo wapata, yalikuwa nihatarishi sana.Bibi yangu alianza kuwafanyia matibabu hadi afya zao zikawa salama”

    “Huyo mtu wapili alikuwa ni nani?”

    “Ni Sheila, ambaye kwa sasa, anaishi kwa mama”

    “Ahaa sasa ilikuwaje kwa mzee Godwin”

    “Sasa hapo ndipo nilipopata kujua kwamba, mchongo wote wakutekwa kwa mama yako, aliyesababisha kutekwa kwake ni Mzee Godwin ambaye kwa sasa, ananyea debe gerezani”

    Habari aliyo nipa John, ikajenga furaha iliyojawa nashauku yakutaka kutaka kumuona mama yangu,

    “Kwenye ndege umesha ajiriwa au bado?”

    “Ndio ninamalizia mafunzo,”

    “Kwa nini umekuwa muuhudumu wa ndege wakati, mipango yetu ilikuwa ni kuwa madaktari bingwa?”

    “Kaka, PCB mbaya mwanangu, nilizungusha”

    “Ulizungusha…..!!?”

    “Ndio ndugu yangu, nilipata zero, ila sijutii sana kwani muda mwingi niliutumia sana na Catherina”

    “Na huyo Catherina alipata ngapi?”

    “Ahaaa naye pia alizungusha, japo alikuwa HKL, ila alizungusha”

    “Poleni sana”

    “Asate, eheee na wewe umemtolea wapi huyu bibie muarabu si muarabu, mzungu si mzungu?”

    Nikaanza, kumuadisia John mkasa mzima wa maisha niliyo pitia kuanzia siku nilipokuwa nikitafutwa Tanzania na kukimbilia nchini Kenya ambapo ndipo, safari yangu yakwenda nchini Iraq ilipo anza, nikamuelezea jinsi nilivyokutana na Phidaya, na alivyokuwa msaada mkubwa sana kwenye masha yangu

    “Ninampenda sana Phidaya”

    “Unauhakika?”

    “Ndio, asilimia mia”

    “Mmmmm ni yule Eddy ninaye mjua mimi, au kwa maana wewe ulikuwa mzee wa Gologolo”

    “Hahaaaa, nimkekuwa mtu wangu, hapa nipo kwenye majukumu yakuitwa baba”

    “Safi ndugu yangu, ila nakutobolea siri moja?”

    “Siri gani?”

    “Sheila anakupenda sana, na hapa yupo anakusubiria wewe”

    “Mmmmm,”

    Nilijikuta nikiguna, huku mapigo yamoyo yakianza kunienda mbio, mwili mzima ukaanza kusisimka, na nywele kichwani zikaanza, kunisisimka, jambo ambalo kwenye maisha yangu halikuwahi kutokea siku hata moja.Nikasimama haraka huku akilini mwangu nikmfikiria Phidaya

    “Eddy unakwenda wapi?”

    “Chumbani”

    Nilizungumza huku nikizidi kupiga hatua za haraka, nikaingia kwenye lifti pamoja na John, ambaye alikuwa akinifwata kwa nyuma, ikasimama kwenye ghorofa ya tatu, kama jinsi nilivyo minya batani ya ghorofa hii ambayo niyatatu, nikaanza kukimbia kuelekea chumbani kwangu, nilipo muacha mke wangu akiwa amelala, wasiwasi mwingi ukiwa umenitawala, nikafika kwenye mlango wachumba changu, nikaufungua kwa nguvu, kitu cha kwanza kutazama nikitandani, nikastuka kukuta mke wangu hayupo huku shuka jeupe lililo tandikwa juu yakitanda likiwa limejaa damu nyingi, jambo lilizozidi kustua mimi na John



    Nikakimbilia kwenye mlango wa kuingilia bafuni, ila sikufanikiwa kumuona Phidaya, joto kali la mwili likaanza kuambatana na woga ambao tangu kuzaliwa kwangu sikuwahi kuupata siku hata moja, nikatizama kila shemu ya chumba hadi chini ya uvungu ila sikumuona mke wangu, machozi kwa mbali yakaanza kunilenga lenga, huku nikijaribu kutafakari ni nini nifanye

    “Kwani alikuwa humu ndani?”

    Nilijikuta nikiachia msunyo mkali, baada ya John kuniuliza swali ambalo jibu analo kichwani mwake, kwani muda nilipokuwa ninatoka nilikuwa nipo mwenyewe, na sote tumekuta damu juu yakitanda iweje aniulize kwamba alikuwepo humu ndani, nikatoka kwa hatua za haraka, huku shati nililo livaa likiwa linavuja jasho jingi, sana

    “Sasa Eddy unakwenda wapi?”

    John aliniuliza huku akinifwatwa kwanyuma tukielekea zilipo lifti za ghorofa hili, sikumjibu John chochote kwa maana ninahisi, hatambui nini umuhimu wa mke, isitoshe mke mwenye kiumbe change tumboni, kupotea katika mazingira yakutatanisha, tukaingia kwenye lifti ambayo kuta zake nne zina vioo, nikawa na kazi yakujitazama jinsi macho yangu yanavyo tiririsha machozi yanayotoka pasipo kuwa na kilio, huku wekundu ukiwa umetawala kwenye macho yangu, John akanipa kitambaa chake ili nikisaidie kufuta machozi

    “Nimepata wazo, hembu twende kwenye chumba cha ulinzi kwa maana humu ndani kuna kamera za ulinzi kila kona”

    John alizungumza huku akinitazama usoni, wazo lake kidogo likarudisha ufahamu kwani kitu ninacho kifikiria ni Phidaya na kiumbe change, kitarajiwa

    “Samahani dada”

    John alizungumza na muhudumu mmoja kwa kingereza, mara baada ya sisi kutoka kwenye lifti iliyo tufikisha chini kabisa katika eneo tulilokuwepo

    “Bila samahni?”

    “Ninaomba kuuliza ni wapi kwenye chumba cha CCTV camera”

    “Kwani kuna tatizo?”

    “Ndio lipo, kuna dada mmoja, ni mjamzito amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha, mume wake alimuacha chumbani akiwa amelala ila tulipo kwenye hatujamkuta”

    “Mmmm kuseme ukweli, mimi sijaona dada mjamzito akitoka, labda chakuwasaidia nyinyi, nikuwapeleka kwa meneja na yeye ndio atatoa idhini ya nyinyi kupelekwa kwenye hicho chumba”

    “Asante dada”

    Sikuchangia neon lolote zaidi yakuwasikiliza John na muhudumu jinsi wanavyo zungumza, huku macho yangu yakitazama kila upande wa sehemu tulipo simama, nikastukia nikuvutwa mkono na John ambao tayari walishaanza kuondoka na kuniacha mimi nikiwa nimesimama kama sanamu, lakuongozwa na betrii

    “Kaka, usijali shemeji atapatikana, ninaimani hawezi kuondoka humu ndani ya Hoteli kwa hali ile”

    John aliendelea kuzungumza huku tukipiga hatua tukimwafwata dada, huyu kwanyuma, tukaingia kwenye moja ya chumba ambapo macho yangu hayakuwa ngeni kwa mtu aliye kaa kwenye kiti hichi huku akionekana kwamba ndio meneja wa hii hoteli

    “Meneja kuna, hawa wageni wa…..”

    Meneja wake akainua mkono, kwa ishara ya kumkatisha mfanyakazi wake, na meneja wake akapiga hatua za haraka hadi sehemu nilipo simama mimi, huku akiwa ametabasamu usoni mwake, akanikumbatia kwa furaha, hapa ndipo nikapata uhakika kwamba ni mlinzi wa baba, ambaye kuna kipindi alinipeleka kwenye benki, nikatoe pesa kwa ajili ya kununulia siku ila ndipo nilipokutana na Sheila baada ya jamaa kumkuta akiminyana na Sheila aliyekuwa amechanganyikiwa

    “Eddy umekuwa mkubwa mdogo wangu”

    Jamaa alizungumza huku akitabasamu, na mimi nikajikaza niweke tabasamu lakinafki ili mradi tu nisalimieane naye

    “Eddy mbona kama umepoteza furaha usoni mwako, unatatizo gani?”

    Nikamuelezea jamaa jambo linalonisumbua,bila kupoteza muda akaniomba tuelekea chumba maalumu chenye video nyingi zinazoonyesha maeneo mbalimbali ya hotel, tukaanza kuonyeshwa matukio yaliyo pita muda mchache kwenye eneo la chumba chetu kilipo, tukashuhudia kumuaona mwanake aliye valia baibui lililo mficha sura yake akiingia ndani ya chumba change, muda mchache baada ya mimi kutoka, ndani ya dakika kadhaa akatoka akiwa amembeba mke wangu, kwenye mikono yake huku akiwa amemfunika kwa shuka jeupe, kama mtu aliye uwawa.

    “Peleka mbele kidogo”

    Jamaa alizungumza na kumfanya muongozaji wa video hizi kupeleka picha za video mbele kidogo, ambapo tukamshuhudia mwanamke huyo ambaya hadi sasa, hivi sura yake hatukuiona, akimuingiza mke wangu kwenye gari yawagonjwa na kuondoka naye, pasipo watu kumshuhudia

    “Ujinga huu, ulipo kuwa unafanyika mulikuwa wapi?”

    Jamaa alizungumza huku akimfokea mfanyakazi wake anaye ongoza mitambo ya kamera za ulinzia, mwili mzima ukaanza kunitetemeka na kujikuta nikizidi kuchanganyikiwa pasipo kujua ni kitu gani ambacho, nilimemkosea huyu mwanamke aliye mteka mke wangu, kila mmoja akabaki kimya akimtazama mwenzake asijue nini chakufanya

    “Sasa hapa itakuwaje?”

    John alizungumza na kumfanya jamaa, ambaye hadi sasa hivi jina lake silifahamu kutokana sikuwa na mazoea naye sana kipindi yupo nyumbani kwa baba, akatoa simu yake na kuminya baadhi ya namba na kuiweka simu yake sikioni, akaanza kuzungumza lugha ya kizulu, ambayo kwangu si ngeni sana japo siifahamu.Akamaliza kuzungumza na simu na kututazama

    “Nimewasiliana na makao makuu ya polisi hapa ‘Johannesburg’ na wameniambia wanaanza kulifanyia kazi muda huu”

    “Sa..sa umesema wanafanyia kazi?”

    Nilizungumza kwa kiwewe kikubwa huku nikimtazama jamaa

    “Ndio wameshaanza kulifanyia kazi, kwani nimewatajia hadi namba za gari kuhakikisha wanalinasa gari husika”

    Jasho halikuacha kunitiririka japo kuwa ndani ya chumba hichi kuna baridi nzuri yajutosha, jamaa akamuomba mtu wake azitume picha za gari na mwanamke hukyo makao makuu ya polisi kupitia mtandao(internet), ili kuzidi kuwarahisishia kazi askari polisi

    “Eddy usiwe na wasiwasi, kama tukio limefanyika kwenye hoteli hii basi, muhalifu aliye mteka mke wako atapatika tu”

    “Ila mke wangu atakuwa amesha fariki”

    Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga, twasira za sura ya mke wangu masaa machache ya nyuma yaliyo pita zikaanza kunisumbua kichwani mwangu, nikajikuta nikianza kujilaamu nikwanini nilitoka chumbani kwangu na kumuacha Phidaya wangu akiwa amelala peke yake, jamaa akasogea pembeni na kuzungumza na simu, sikujua anazungumza na nani, baada ya muda akarudi tulipo

    “Eddy nilikuwa nikizungumza na baba yako, na yupo njiani anakuja”

    “Baba yake!?”

    John aliuliza huku akiwa ameshangaa, sikutaka kumjibu kitu chochote zaidi ya kujikalia zangu kwenye kiti huku mapigo ya moyo yakianza kunienda mbio, ndani ya dakika ishirini, mlango ukafunguliwa na akaingia baba akiwa na walinzi wake wanne walio valia suti nyeusi pamoja na miwani, nikanyanyuka kwenye kiti na kukumbatiana na baba huku akionekana kuwa nafuraha usoni mwake, kwani hakuamini uwepo wangu, jamaa akaanza kumuelezea baba kila kitu kilicho tokea na kumuonyesha baadhi ya video hizo za mwanamke aliye mteka mke wangu

    “Pole sana Eddy”

    Baba alinipa pole na mimi nikaiitikia kwa sauti ya chini, tukatoka ndani ya chumba nikiwa nimeongozana na baba pamoja na walinzi wake, huku jamaa na John wakifwata kwa nyuma, tukakuta polisi wakiwa wanafanya vipimo kwenye chumba change

    “Mumefikia wapi?”

    Baba alimuuliza mmoja wa polisi

    “Hii damu, inaonekana si damu ya mauaji”

    “Kivipi?” Baba aliuliza tena

    “Inaonekana mtekaji alimwaga damu kwenye shuka kutoka kwenye pakti za kuhifadhia damu”

    Askari alituambia huku akituonyesha pakti mbili za kuhifadhia damu, walizo zitoa ndani ya chumba changu baada ya kukifanyia uchunguzi sana

    “Ila mtekaji atapatikana kwa maana inaonekana hajatoka mbali sana na hapa”

    Polisi alizungumza, ila moyo wangu haukuwa na furaha hata kidogo japo wanadai kwamba ni damu ndizo zilizo mwagwa kwenye shuka la chumbani kwetu, tukatoka na baba hadi sehemu ya kupumzikia, ukimya ukatawala kati yetu, hapakuwa na aliye zungumza kitu chochote zaidi ya mimi kutazama tazama mandhari yaliyomo humu ndani

    “Eddy, ulikuwa wapi mwanangu?”

    “Baba, ngoja hayo mazungumzo tutayazungumza baada ya kufikia muafaka kutambua ni wapi alipo mke wangu”

    Nilizungumza kwasauti nzito iliyo jaa hasira ndani yake, baba alinielewa na kukaa kimya hakutaka aendelea kunigusia kuhusiana na kitu cha aina yoyote.Simu ya baba ikaita na akaanza kuzungumza na mtu aliye mpigia

    “Eddy twende sehemu, lile gari lawagonjwa limepatikana”

    Baba aliniambia mara baada ya simu kukata, nikawa wakwanza kunyanyuka kwenye kiti na kuanza kuongozana, tukaingia kwenye gari huku John akiingia kwenye gari ya jamaa ambaye ni meneja wa hoteli.Tukatembea umbali wa kilomita kumi, tukafika pembezoni mwa mlima na kuwakuta polisi wengi wakiwa wamelizingira gari lawagonjwa, kwa umbali kidogo ambalo pembeni limezungushiwa mabomo yakutega yapatayo sita, bomo moja nikaliona likiwa limebakisha sekunde hamsini huku zikiendelea kurudi nyuma taratibu

    “Phidaya”

    Nilianza kukimbia kuelekea lilipo gari lawagonjwa polisi wakanidaka, na kunizuia nisiendelee kwenda mbele, gafla mlipuko mkubwa ukalipuka kwenye gari na kusababisha polisi walio nikamata kuniangusha chini na kunifunika na miili yao waliyo valia nguo maalumu zinazo zuia kuadhirika na vipande pande vya vyuma vitokanavyo na mabomu endapo vitawaangukia

    “Phidayaaaaaaaaaaaaaaaaaa”

    Nilizungumza kwa sauti ya juu huku machozi ya uchungu yakinimwagika usoni mwangu, huku nikilishuhudia gari alilopo mke wangu likiteketea kwa moto mkali



    Askari wa kikosi cha zima moto wakaanza kulishambulia gari la wagonjwa kwa kutumia mipira mirefu inayotoa maji kwa kasi kiasi kwamba, moto ukaanza kupunguza makali yake ya kuteketea, amchozi yalizidi kunitoka huku askari wakiendelea kunizuia nisikaribie eneo ambalo lipo gari, wakanikabidhi kwa walinzi wa baba, ambao waliendelea kunishika.Si mimi tu ambaye nipo kwenye huzuni, ila hata rafiki yangu John, machozi yalianza kumtoka, na kuzidi kunizidishia hisia ya kumwagikwa na machozi mengi

    “Eddy, jikaze mwanangu”

    Baba alizungumza huku akinikumbatia, akiendelea kunipigapiga mgongoni ikiwa ni ishara ya kunituliza hasira na uchungu ambao nimeupata, askari wengine wakaanza kazi ya kuchambua kama kuna kitu kilicho salia kwenye gari, ikiwemo kupata udhibitisho wa kama kuna mwili wa mtu ambaye alikuwepo ndani ya gari, mwili mzima ukazidi kunitetemeka kwa woga, kila ninapojaribu kutazama gari lililo teketea kwa moto, dua yangu kubwa ni kumuomba Mungu aweze kutenda miujiza Phidaya asiwepo ndani ya gari hilo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Askari mmoja akatufwata sehemu nilipo simama mimi pamoja na askari wa baba, huku mkononi mwake akiwa ameshika kibegi kidogo, na viganjani mwake akiwa amevaa gloves nyeusi.Akamsalimia baba, kasha akatusalimia na sisi, akamuomba baba wazungumze pembeni, baba akatii ombi la askari huyo, sikusikia kitu ambacho wanakizungumza

    Mlio wa simu ya John, ukanistua kutoka katika dimbwi kubwa la mawazo na kujikuta nikimgeumkia na kumtazama kwa macho yaliyo jaa huzuni nyingi, John akaitazama simu yake kwa muda huku akiwa amekunja ndita, akaipokea na kukaa kimya

    “Nani mwenzangu?”

    John alizungumza baada ya sekunde kadhaa ya simu yake kuwa sikioni

    “Hapana, mimi ninawapa watu wengi namba yangu, kwahiyo usipo taja jina lako mimi siwezi kutambua kwamba wewe ni nani?

    John alizungumza kwa sauti ya ukali huku macho yake akiya pepesa pepesa

    “Wee mwendawazimu nini, usinichangenye”

    John alizungumza huku akiachia msunyo mkali na kukata simu yake, nikaanza kupiga hatua kulifwata gari lililo teketea ambapo kuna askari, pamoja na madaktari wakiendelea kufanya uchunguzi na vifaa vyao maalumu.Nikafanikiwa kufika pasipo mtu yoyote kunishika mkono, nikakuta wakiyapiga picha, mafuvu mawili ya watu, yaliyo tekete kwa moto, ikiashiria kwamba miili yao, imesha teketea, nikajikuta nikianguka chini kama mzigo, kutokana na kuishiwa na guvu za mwili wangu.

    Madaktari wakaniwahi kunipa huduma ya kwanza, ikiwemo kuniwekea mashine ya kunisaidia kuhema, japo fahamu hazijanipotea, ila sikuwa na uwezo wakuuamuru mwili wangu kufanya kitu, ambacho ninakihitaji, machozi yakaanza kunichuruzika, kumbukumbu za gari kulipuka dakika chache zilizo pita zikaanza kunijia kichwani mwangu, nikaanza kuisikia sauti ya Phidaya kwa mbali ikiniita masikioni mwangu, nikataka kunyanyuka, ila madaktari wakanizuia nisinyanyuke

    “Mwanangu atapona?”

    “Ndio mzee atapona, ni mstuko tu, ndio umempata ulio pelekea yeye kuishiwa na nguvu, kidogo na uwezo wa moyo wake ulishindwa kudunda kama inavyo paswa ufanye”

    Daktari mmoja nilimsikia akimjibu baba, huku wezake wakiniinyanyua kwenye machela, waliyo kuwa wameniweka wakinipatia huduma ya kwanza na kuniiingiza ndani ya gari.John akawahi kuingia ndani ya gari la wagonjwa, lililokuja muda mchache baada ya mimi kuanguka chini.

    “Eddy”

    John aliniita, na kumtazama taratibu, pasipo kumjibu kitu chochote, kwani hata kuzungumza kumenishinda kabisa

    “Mungu, atasaidia kila kitu kitakuwa sawa”

    John alizungumza kwa kunifariji tu, kwani ukweli halisi nimeshaujua, kwamba Phidaya sipo naye tena duniani, kwani mafuvu mawili ni yawatu ambao nimeyakuta kwenye gari, yanaashiria kwamba ni mke wangu ni marehemu.

    Wakanishusha kwenye gari, wakaniweka kwenye kitanda cha kusukuma, manesi wawili wakaanza kukisukuma kitanda nilicho lalia hadi kwenye moja ya chumba na kuniingiza humu, nikakuta madaktari wawili wakiwa ndani ya chumba wakiwa tayari kwa kunihudumia.Wakanichoma sindano kwenye mkono wangu wa kushoto sehemu ya mshipa wa damu, kasha waniwekea baadhi ya vifaa kifuani kwangu, ambavyo sikuelewa kazi yake ni nini.Wakamaliza kufanya kazi yao, ya kunihudumia na kutoka ndani ya chumba, msongamano wa mawazo ukazidi kunipelekesh, huku sura ya mke wangu Phidaya ikiwa haichezi mbali na fikra zangu

    “Eddy I love you”(Eddy ninakupenda)

    Sauti ya Phidaya ikaendelea, kusikika kwenye masikio yangu, nikajitahidi kuyazungusha macho yangu kila pande ya chumba kutazama kama nitaweza kumuona mke wangu ila sikufanikiwa, kuiona sura yake.Baada ya masaa manne mlango ukafunguliwa na akaingia baba pamoja na John, kila mmoja anaonekaa kuwa na huzuni, baba akasimama pembeni ya kitanda change, huku John akikaa sehemu ndogo ya kitanda nilicho lalia

    “Unajisikiaje mwangu”

    “Safi”

    Nilimjibu baba kwa sauti ya chini, iliyo jaa mkwaruzo

    “Baba, yale mafuvu yapo wapi?”

    Baba hakunijibu zaidi ya kumtazama John, kisha wakanitazama hakuna aliye jibu swali langu, ila macho yao nikatambua kwamba yanakitu wanacho kijua ila wananificha

    “Ahaa…., inabidi kwamba…… Ahaaa kesho urudi nyumbani, ukapumzike kwa muda kidogo ili uwe sawa”

    Baba alizungumza kwa kubabaika, nikamtazama John, akatizama chini baada ya macho yangu kukumbana na macho yangu.Simu ya baba ikaita ikambidi atoke nje kwenda kuipokea

    “John niambie ukweli mke wangu amekufa?”

    “Eddy………………”

    John aliniita, nikabaki nikimtazama pasipo kumuitikia.Ukimya ukatawala, kama dakika mbili John hakunijibu swali langu nililo muuliza.Kijimlio kifupi kikasikika kwenye simu ya John iliyopo mfukoni, ikamlazimu kuitoa simu yake, mfukoni.Akasoma meseji aliyo ingia, akanitazama kwa jicho la kuiba na kuitazama tena meseji anayo isoma

    “Kaka hembu soma hicho kilicho indikwa”

    John akanipa simu, kabla sijaisoma meseji iliyopo kwenye simu, baba akaingia ndani akiwa ameongozana na madaktari walio, nitibu muda mchache ulio pita, wakafika kwenye kitandani nilicho lala.Daktari mmoja akanitoa vifaa walivyo niwekea kifuani,

    “How do you feel?”(Unajisikiaje?)

    Daktari mmoja aliniuliza

    “Najisikia powa”

    Daktari wa pili akaniwekea kifaa kigo cha kusikilizia mapigo ya moyo, akamtazama baba

    “Kwa sasa yupo salama, tunaweza kumruhusu kurudi nyumbani”

    “Shukrani daktari”

    Baba alizungumza, huku akimpa mkono dokta, wakanipa vidonge vya kuupa mwili wangu nguvu, nikaruhusiwa kutoka hospitalini, tayari giza lilisha anza kutawala anga, kwa mbali, ikiwa ni majira ya jioni, tukaingia kwenye gari moja mimi pamoja na John, huku baba akiwa katika gari lake jengine

    “Uliisoma ile meseji?”

    “Ngoja noisome”

    Nikaitoa simu mfukoni na kumpa John anitolee namba za siri alizo ziweka kwenye simu yake upende wa meseji kisha akanirudishia

    {KAA MBALI NA HII VITA KATI YANGU MIMI NA EDDY, UTAUMIA}

    Nikairudia kuisoma tena meseji kwa msisitizo, kisha nikamtazama John, huku mapigo ya moyo yakianza kunienda mbio

    “Nani aliye ituma hii meseji?”

    “Mimi wala sijui, kutoka hata namba yenyewe haionekani”

    “Mmmmmm, ulimuonyesha mtu mwengine tofauti yang?”

    “Pale ilipokuwa inaingia, ndio nikakukabidhi hiyo simu”

    Nikashusha pumzi kubwa huku nikiendelea kumtizama John machoni, nikajaribu kuipiga namba iliyo tuma hii meseji ila haikenda zaidi ya kukatika.Tukafika nyumbani kwa baba, mazingira nikayakuta yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana, kuanzia nje hadi ndani, sikumkuta yule mama wa kambo aliyekuwa akinisumbua akili yangu kipindi nilipokuja kwa mara ya kwanza

    “Una mpango gani, juu ya hili Eddy?”

    Baba aliniuliza mara baada ya mimi, kukaa kwenye moja ya sofa lililopo hapa sebleni, nikakaa kimya kwa muda kabla sijamjibu baba, kwani akili yangu ikaanza kutafakari juu ya meseji aliyo tumiwa John, inavyo onekana mtu huyo ananijua mimi vizuri ndio maana ameamua kunifanyia unyama wa kumuangamiza mke wangu

    “Sijajua baba”

    Jibu langu, likamfanya John kunitazama kwa mashangao

    “Ngoja tupate ripoti ya polisi juu ya muhusika, wa tukio zima kisha tutajua nini cha kufanya”

    “Sawa baba”

    Baba alizungumza na kuanza kupandisha ngazi kuelekea ghorofani, nikasikia sauti ya kike ikizungumza na baba, ikanilazimu kusimama kutazama ni nani anaye zungumza naye, macho yangu yakakutana na macho ya mototo wa mama wa kambo, ambaye kipindi ninakuja kwa mara ya kwanza nyumbani kwa baba, yeye alikuwa chuo akisoma

    “Waoooo kaka Eddy”

    Alinikimbilia na kunikumbatia kwa furaha, sikuamini macho yangu kwani mimi na yeye kidogo kuta tofauti zilizo tokea kipindi cha nyuma, hususani swala la mimi kumpiga mama yake

    “Za huku utokapo?”

    “Si salama”

    Nikamuona John akimshangaa huyu dada yangu, akataka kumpa mkono ila akasita, ikanilazimu nimtambulishe mimi

    “Dada huyu ni rafiki yangu anaitwa John, na John huyu ni motto mwengine wa baba yangu”

    “Nashukuru kukufahamu”

    John alizungumza huku akimpa mkono dada yangu

    “Eddy unatabia mbaya”

    “Kwa nini dada?”

    “Hadi leo hulitambui jina langu”

    “Ahaaa”

    Nilibaki nikitabasamu tu, kwani ni kweli jina lake sikuwa ninalikumbuka vuzuri

    “Mimi ni Victori”

    “Ahaaa, kama lilikuwa likinijia kwenye akili yangu vile?”

    “Kwenda kulee, ulikuwa hulijui”

    Alizungumza kwa utani, huku akiichezea chezea mikono yangu, tukatizamana kwenye macho kwa sekunde kadhaa, sote tukajikuta tukiwa kimya

    “Mama yupo wapi?”

    Nilimuuliza na kumfanya apooze gafla, akaniachia mikono yangu na kwenda kukaa kwenye moja ya sofa, huku machozi yakimlenga lenga, akainyanyua sura yake kidogo na kunitazama

    “Mama, amesha fariki”

    Alizungumza kwa sauti ya upole huku machozi yakianza kumtoka, nikapiga hatua hadi alipo kaaa, nikamkumbatia, huku na mimi hisia za mke wangu kufa, zikaanza kunijia kichwani

    “Eddy kwa nini unalia?”

    “Mke wangu amekufa”

    “Weeee”

    Victoria alistuka baada ya kusikia maneno haya

    “Amefariki lini?”

    “Leo”

    “Leoooo?”

    “Ndio”

    “Kwa nini?”

    “Amefariki kwa mlipuko wa bomu baada ya kutekwa, na mtu asiye julikana”

    John akabaki akitutizama jinsi tunavyo zungumza mimi na dada yangu, Victoria akanikumbatia kwa nguvu na kuanza kunibembeleza kwa hisia kali, tukaachana na stori za kufa kwa mke wangu, tukaendelea kuzungumza kuhusiana na mambo mengine, muda wa chakula ukawadia na sote tukakaa kwenye meza maalumu ya chakula, nikagundua kitu kutoka kwa John, wakati wote alikuwa na kazi ya kumtazama Victoria kwa macho ya kumtamani.Tukamaliza kula mimi na John, tukaelekea kwenye chumba change

    “John mbona ulikuwa unamtazama sana Victoria?”

    “Hapana”

    “Mmmmm john wewe hakuna cha hapana, au umempenda nikuunganishine”

    “Ahaaa Eddy, ila ngija kuna kitu ninakichunguza, kikikamilika nitakuambia”

    “Kitu gani?”

    John akautazama mlango wa kuingilia humu ndani ya chumba change, akapiga hatua za taratibu huku akiniomba ninyamaze kuzungumza, akaliweka sikio moja kwenye mlango, huku mkono wake mwingine ukishika kitasa cha kufungulia mlango, akaanza kuufungua taratibu, mimi nikawa na kazi ya kumtazama jinsi anavyo fanya.Akauvuta kwa nguvu, macho yetu yote yakakutana na Victoria akiwa amevalia nguo ya kulalia, inayo onyesha nguo yake ya ndani

    “Vicktoria vipi?”

    Nilimuuliza Victoria baada ya yeye kushindwa kuzungumza kitu kinacho mfanya asimame nje ya mlango wetu, akaanza kuvunja vinja vidole vyake kwa aibu, akamtazama John, ambaye hakuwa amezungumza kitu cha aina yoyote, akamshika John shati lake, kisha akamvuta karibu yake na kumpiga busu la mdomo na kunifanya nibaki nikiwa ninamshangao

    “I need you John”(John, ninakuhitaji)

    Victoria alizungumza huku akimsukumia John ndani ya chumba, changu, kama simba mwenye njaa Victoria akamsukumiza John kitandani na kuanza kumvua shati, lake, kwa aibu ikanilazimu mimi kutoka ndani ya chumba nikawaacha waendelee na mambo yao



    Nikaelekea moja kwa moja jikoni, nikachukua maji ya kunywa kwenye friji lililopo humu jikoni, kisha nikakaa kwenye kiti kirefu ambacho nacho kipo humu ndani ya chumba.Mawazo yakaanza kurudi upa juu ya mtu aliye mteka mke wangu na kumuua kinyama kwa kumlipua kwa bomu

    “Nilazima nilipize kisasi kwa yoyote aliye husika katika hili”

    Nilijiapiza kimya kimya huku nikiyatazama maji yaliyopo kwenye glasi niliyo ishika mkononi mwangu, nikaitazama saa ya ukutani na kukuta ikionyesha ni saa sita kasoro dakika ishirini, usiku

    “Hawamalizi na sasa hivi”

    Nilizungumza huku nikinyanyuka kwenye kiti na kutoka nje, na kuwakuta walinzi wakizunguka zunguka kaimarisha ulinzi wa jumba hili la baba yangu, sikutaka kuzungumza na mtu wa aina yoyote zaidi ya kubatazama mandhari mazuri yalipomo kwenye eneo hili

    “Hei”

    Nilimuita mlinzi mmoja aliye kuwa anakatiza karibu yangu

    “Ndio bosi”

    Kwa bahati nzuri mlinzi huyu alinijibu kwa Kiswahili

    “Ninaweza pata usafiri muda huu”

    “Kivipi?”

    “Nina maanisha ninaweza kupata gari, lolote lenye funguo”

    “Unataka kwenda wapi usiku huu?”

    “Kuna sehemu ninahitaji kwenda”

    “Kwa hapo, ndugu siwezi kukusaidia kwani bosi hajatoa ruhusa ya mtu yoyote kutoka na usafiri, tena muda huu wa usiku”

    “Ahaa powa asante”

    Nikaachana na mlinzi na kurudi ndani, nikafika hadi mlango wa kuingilia chumbani kwangu, nikaweka sikio la upande wa kulia, nikasikia miguno ya mahaba ikiwa inaendelea ndani ya chumba change.

    “Mmmm kazi kweli kweli”

    Nikapata wazo la kwenda chumbani kwa Victoria japo kuegesha kichwa change kidogo, hii ni kutokana na uchovu mwingi.Nikaingia na kuwasha taa, kitu cha kwanza nikakutana na mwanga wa simu ya Victoria, ikionyesha ni muda mfupi kuna meseji au simu ilipigwa.Nikapiga hatua hadi kitandani ilipo, nikaichukua na kutazama, na kukuta missed call na namba ambayo haikuwa na jina lolote.Nikafungua kipochi chake kilicho kuwa pembezoni mwa simu, nikakuta noti kumi za dola mia mia

    “Yess, kazi yangu imeanza kukamilika”

    Nikazichomoa noti hizo, na kuzidumbukiza kwenye mfuko wa jinzi langu, ambapo kuna simu ya John, aliyo nikabidhi muda wa mchana.Nikatazama salio kwenye simu ya Victoria nikakuta lipo lakutosha, nikaiweka mfukoni, nikafungua kabatini kwake na kukuta makoti mengi makubwa ya baridi.Nikachukua koti jeusi na kulivaa, nikachukua kofia ya kuzuia baridi na kuivaa, nikatoka nje ya chumba cha Victoria.Kutokana ni mzoefu sana wa jumba hili la baba haikuwa, ngumu sana kwangu kutoroka pasipo walinzi kunioa, nikatoka nje ya ukuta wa jumba hili, kwa kuuruka, nikaanza kutembea kuelekea barabara kuu, kwa bahati nzuri nikapata taksi

    “Nipeleke kwenye uwanja wa ndege, wa ‘Johannesburg’, itakuwa ni bei gani?”

    “Dola mia”

    “Sawa”

    Kutokana nina kiasi cha kutosha cha pesa, sikuwa na haja ya kumbembeleza dereva huyu, japo ninatambua amenipiga kizinga, kutokana na ugeni wangu, tukatumia dakika ishirini kufika uwanja wa ndege.

    “Unaweza kunisubiri?”

    “Bili shaka”

    Nikampa dereva taksi pesa yake, nikaelekea sehemu ya huduma kwa wateja, na kuwakuta dada kadhaa wakiwa wamejipanga wakizungumza na baadhi ya abiria waliopo kwenye eneo hili

    “Samahani dada”

    “Bila samahani, nikusaidie nini?”

    “Juzi usiku, kuamkia jana nilifika hapa na ndege ya shirika la nchini Philipines, kuna kitu ninahitaji kukipata kwenye kwenye safari ile”

    “Kitu gani?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dada huyo alinijibu kwa umakini, huku akinitazama usoni

    “Nahitaji video zilizo rekodiwa kwenye safari nzima, kutoka Philipines hadi hapa South Africa”

    “Eheeeee, kaka yangu, mbona hiyo ni kazi kubwa sana, na kwakitengo changu, mimi siwezi kukusaidia”

    “Unaweza, nitakupa pesa yoyo……”

    Mngurumo(vibration) wa simu ya Vivtoria, ukaanza kutetemesha mfuko wangu, ikanilazimu kuitoa simu yake na kukuta meseji ikiwa imeingia, nikaifungua ila nikakutana na batani nyingi zikiniomba niiingize neno la siri ili niweze kuifungua meseji hiyo

    “Akhaaaa”

    Nilijisemea mwenye baada ya kushindwa kuifungua meseji hiyo, nikamgeukia dada niliyo kuwa nikizungumza naye, nikakuta akimalizia kumnong’oneza rafiki yake, aliye kaa kiti cha pembeni yake

    “Niambie sasa dada, inawez……”

    Akanikatisha mazungumzo yangu, kwa kunikonyeza kwa jicho lake kubwa kiasi, akanionyeshea ishara kwa macho nitazame juu yangu, nikakuta kameta ya ulinzi ikinirekodi

    “Nifwate”

    Alizungumza kwa sauti ya chini, akajinyanyua kwenye kiti alicho kalia, akatoka kwenye chumba walichopo nikaanza kuongozana naye kuelekea anapo kwenda yeye, tukapandisha kwenye ngazi, sikujua ni wapi ananipeleka.Tukafika kwenye moja ya ukumbi wenye viti vingi, vya kupumzikia.Akatafuta sehemu iliyo tulia na kuniomba nikae

    “Eheee kaka ulikuwa unasemaje?”

    Nikamuelezea nini ninacho kihitaji, akaniomba nimsubiri kama dakika kadhaa atarudi na kitu ambacho ninahitaji, ila akaniomba nimpatie malipo ya awali, na tulikubaliana nimpatie dola mia tano kwa kazi atakayo nifanyia.Nikaito simu ya John na kufungua upande wa picha, nikajikuta nikistuka baada ya kuzikuta picha za John na Victoria wakiwa pamoja, kwenye fukwe za bahari, ila sikujua ni nchi gani.Nikazidi kwenda mbele na kukuta picha nyingi wakiwa pamoja, hapa ndipo nikagundua kuna mahusiano ya kimapenzi kati ya John na Victori

    “Ahaaa, ndio maana nilivyo kuwa ninawatambulisha John alistuka, kumuona Victori….”

    Nilijisemea mimi mwenye, kimoyo moyo, huku nikiendelea kuzitazama picha walizo piga pamoja, nikaingia upande wa namba za simu na kuanza kuandika jina la Victoria na kukuta likiwa limeandikwa ‘MY WIFE V’, Nikajaribu kuipiga namba, ikaingia kwenye simu ya Victoria na kutokea jina la ‘BABY JOHN’

    “Wamejuana juana vipi?”

    Ni moja ya swali lililo anza kuniumiza kichwa change, kabla sijajipatia jibu kichwani mwangu, muhudumu akarudi akiwa ameshika laptop ndogo mkononi mwake.

    “Chukua hii, nenda chooni, katazame kuna video nimeiiba ndani kwenye chumba cha mawasiliano”

    “Powa”

    “Fanya haraka mimi ninakusubiria hapa, nenda moja kwa moja kwenye ile kordo kunja kulia, utakuta vyoo”

    Nikanyanyuka katika sehemu nilipo kaa, moja kwa moja nikaelekea katika sehemu alipo nielekeza muhudumu huyu, nikaingia kwenye choo cha wanaume, nikaifungua laptop aliyo nipa na kukuta faili moja lili andikwa video, nikalifungua

    Nikaanza kuona mkanda wa video, katika ndege ya shirika la Philipines, video hii imerekodiwa kwa kamera za ulinzi lilizipo kwenye ndege tulio kuja nayo, nikaanza kuona abiria wakiingia, ikiwemo mimi na Phidaya.Ikanilazimu kuisimamisha video mara moja baada ya kumuona Victoria akiingia ndani ya ndege hii, ila alikaa siti ya nyuma kabisa, pamoja na abiria mwengine.Katikati ya safari nikamuona John akiwa anazungumza mara kwa mara na Victoria, pia nikaona jinsi John alivyokuwa akizungumza na mimi.Hadi ndege inafika, na sisi tunatoka kwenye ndege nikaumuona John akizungumza na Victoria, wakakumbatiana kwa pamoja na kila mmoja akaondoka zake

    Kwa kamera zilizopo nje ya uwanja wa ndege, nikamuona Victoria akiingia kwenye moja ya gari jeusi na kuondoka huku, mimi na Phidaya tukiwa tumekaa katika sehemu tuliyo kuwa tumekaa na kuondoka pamoja na John.Nikashusha pumzi nyingi, nikapata kumbukumbu za haraka kuhusiana na gari ambalo aliingia Victoria kwani nililiona likiwa kwenye maegesho ya hoteli tuliyo kuwa tumefikizia.

    Nikaifunga laptop, na katikti yake nikaweka noti tatu za dola mia mia, ili kukamilisha malipo ya dola mia tano, kutokana tayari nilisha mlipa dola mia mbili kama utangulizi wa kazi, nikarudi na kumkuta akiwa ananisubiri.Nikakaa kwenye kiti nilicho kuwa nimekalia, wakaingia askari wawili ndani ya ukumbi tuliopo, wakatutizama kwa umakini mimi na muhudumu na kuanza kupiga hatua za kuja sehemu tulipo kaa

    Nikastukia kumuona muhudumu akinishika mashavu yangu, akaanzak kuinyonya midomo yangu, huku macho yake yakiwatazama askari wanao karibia kufika kwenye meza yetu

    “Mmgghhh”

    Askari mmoja aliguna na kumfanya muhudumu huyo kuniachia taratibu, akatabasamu na kuwafanya askari hao watabasamu, akazungumza nao kizulu

    “Sizibuna ukuthi kungani muna?”(Mbona munatabasamu?)

    “Sibona lapho nabasekweni”(Tunaona upon na shemeji)

    “Yebo, nabasemzini zakho lokhu”(Ndio shemeji yenu huyu)

    “Siyakubongela thina kudlule”(Hongera sisi tunapita)

    “Esizayo efanayo”(Sawa baadaye)

    Askari wakaondoka na ku kutuacha sisi tukiwatazama

    “Haita jirudia tena”

    Muhudumu alizungumza huhu akijifuta mdomo wake, kwa kitambaa

    “Pesa yako nimeibananisha katikati ya laptop, asante”

    “Sawa”

    Nikanyanyuka na kuondoka, nikatoka nje ya uwanja wa ndege na kuingia katika taksi niliyo kuja nayo, nikamuomba dereva anipeleke ilipo hoteli tuliyo fikizia, njia nzima moyo wangu ukawa na maswali mengi kati ya John na Victoria wamejuana vipi

    “Ahaaa, ila inaweza kuwa ni mambo ya kidunia”

    Nilijisemea mwenyewe na kumfanya dereva taksi kunitazama, tukafika kwenye hoteli, tukasimama kwenye maegesho yamagari, nikashuka kwa bahati nzuri nikaliona gari alilo ondoka nalo Victoria, nikapiga hatua hadi lilipo na kuchungulia kwenye dirisha, lake, sikukuta mtu ndani.Mlio wa mbwa na tochi za walinzi zikanistua, wakaniamuru nisimame kama nilivyo huku mikono yangu nikiinyoosha juu

    Wakafika katika sehemu nilipo simama na kunza kunikagua, ila askari mmoja akastuka baada ya kuniona, akawanong’oneza wezake, ambao walikuwa wameninyooshea bunduki zao, wakazishusha chini

    “Samahani bwana bosi”

    Askari huyo alizungumza huku akijaribu kutengeneza tabasamu la kinafki usoni mwake, huku akionekana kutahayari kwa kitendo walicho nifanyia

    “Hii gari ni yanani?”

    “Ahaa, hili gari ni la mkurugenzi Victoria”

    “Yeye yupo wapi?”

    “Alikuja nalo juzi usiku, ila kutokana sikuingia mchana zamu sijajua aliondoka vipi”

    Nikajaribu kuuvuta mlango wa gari upende wa dereva na likafunguka.Nikaufunga mlango nikaondoka na kuwaacha walinzi wakiulizana maswali kadhaa, nikafika kwenye chumba cha kurekodia video zote zinazo chukuliwa na kamera za ulinzi.Sikuamini macho yangu baada ya kuwakuta wafanya kazi wawili wa chumba hichi, wakiwa uchi wa mnyama, wakifanya mapenzi na msichana, anaye onekana ni kahaba



    Walipo niona wakastuka, na kila mmoja akasimama sehemu yake, huku msichana wanaye fanya naye mapenzi akiziwahi nguo zake zilizo kuwa juu ya meza, na kujifunika katika sehemu zake za siri.Nikawatizama jinsi wanavyo babaika, sikutaka kuwasemesha kitu cha aina yoyoye zaidi ya kwenda zilipo computer nyingi

    “Kuna video ninazihitaji”

    “Sawa sawa bosi”

    Akawasha computer moja, nikamuelezea, video ninayo ihitaji ni ile ya siku nilipokuwa ninafika hapa hotelini, nikaanza kuyaona matukio yote tangu nikiwa ninaingia na Phidaya sebleni, katika usiku ule nilimshuhudia John akizungumza na Victoria katika sehemu ya vinywaji, baada ya mimi na mke wangu kuingia ndani ya chumba chetu cha kupumzikia.Nikawaona wakiingia kwenye moja ya chumba ambacho si kile John alicho kichukua

    “Mnamjua huyu?”

    Nilimuonyesha John kwa kutumia kidole changu’’

    “Huyu ndio tunamjua, mara kwa mara huwa anakuja na mkurugenzi Victoria”

    Nikaona mwanamke mwengine akiingia ndani ya chumba alichokuwa John na Victoria, huku akiwa amevaa baibui lililo mficha sura yake na kumbakisha macho tu

    “Huyo aliye ingia ni nani?”

    Jamaa akairudisha nyuma video, hadi sehemu anayo ingia mwanamke huyo ambaye, ndiye aliye mteka na kumuua mke wangu.

    “Mlimuona kipindi akiingia ndani ya hicho chumba?”

    “Hapana bosi”

    “Iendeleze”

    Jamaa akaiendeleza video, inayo onyesha watu wakiingia na kutoka kwenye vyumba vyao, kutokana na camera hizo zimetengwa kwenye kordo ya hoteli hii.Baada ya muda nikamuona John akitoka ndani ya chumba hicho, akaondoka zake, baada ya dakika chache akatoka Victoria na kuondoka, ila msichana huyo hakutoka hadi inatimu muda wa asubuhi ndipo naye akatoka, hapa ndipo nilipo ipata picha kamili kwamba kuna mchezo ambao ninachezewa na John pamoja na Victoria.Nikajikuta nikiwa ninahasira dhidi ya John na Victoria ambao wanaonekana wana siri kubwa sana waliyo ificha

    “Huyo msichana alikwenda wapi?”

    Wakanionyesha video ambayo tuliiangalia muda baada ya mke wangu kutekwa na msichana huyo ambaye hadi sasa hivi sura yake sikuweza kuijua

    “Hembu nitolee hizo picha zake”

    Jamaa akanitolea picha za msichana huyo aliye vaa baibui, kwa kutumia mashine ya ‘Printing’ nikaikunja karatasi yenye picha ya msichana huyo na kuiweka mfukoni mwangu, nikatoka nje ya chumba na kurudi nilipo muacha dereva taksi, huku moyoni mwangu nikiwa ninahasira ya kwenda kutembeza kipigo kati ya John na Victoria hadi waseme ukweli ni wapi alipo mke wangu.

    “Nirudishe kule tulipo anzia safari yetu”

    Nilimuambia dereva taksi naye akatii, safari ikaanza kwa mwendo wa kawaida huku saa iliyopo kwenye simu ya John ikionyesha ni saa kumi na moja na dakika kumi, alfajiri.

    “Ongeza mwendo dereva tuwahi kufika”

    Nilimuamrisha dereva taksi, akazidisha mwendo kasi wa gari kutoka spidi ya themanini hadi mia moja na thelathini, gafla nikastukia kumuona derava taksi akipiga kichwa kwenye mskani wa gari, huku akitoa mlio wa maumivu, makali, gari ikayumba na kutoka kwenye barabara, huku vitu vigumu vikipiga kwenye kioo cha mbele cha gari, na upande wa pembeni wa gari.

    Kwa akili ya haraka nikagundua kwamba ni risasi zinazo piga kwenye gari letu, lilili poteza muelekezo na kusababisha lizunguke kutokana na miguu ya dereva kufunga breki za gafla na kuyazuia matairi yote kutembea.Nikabaki nikiinama chini, huku nikijitahidi kuushika mskani wa gari kuhakikisha gari haizidi kupoteza muelekeo.Risasi zisizo ni milio ya bunduki zikazidi kumiminika kwenye vioo vya gari tulilopo, sikujua hata zinatokea wapi.Chakumshukuru Mungu, gari ikapiga kwenye mti mkubwa ulio pembezoni mwa barabara na kulisabaisha lisimame na kutulia.Mianga mikali ya taa za pikipiki nikaziona zikija kwa kasi kwenye sehemu gari lililopo

    “Nimepona…….?”

    Nilizungumza huku nikijipapasa mwili mzima, sikujihisi maumivu yoyote kwenye mwili wangu, zaidi ya vioo vingi, vidogo vidogo vilivyo vunjwa kwa risasi, kuniangukia kwenye koti nililo livaa pamoja na suruali yangu, kwa haraka nikajirusha kwenye siti ya nyuma ya gari, jamaa wenye pikipiki wakazidi kulisogelea gari nililomo.Sikutaka kujua kwamba dereva taksi ni mzima au amekufa, nilicho kifanya ni kuufungua mlango wa nyuma upande ambao gari imepiga kwenye mti.Nikatambaa haraka hadi nyuma ya mti na kujibanza, huku nikihema sana.Nikachungulia nikawashuhudia majamaa kama sita wenye pikipiki kubwa, wakiwa wamevalia makoti, makubwa meusi, huku wakiwa na bunduki mikononi mwao zilizo fungwa viwambo vya kuzuia sauti

    Wakasimama mita chache kutoka lilipo gari, na kuanza kulishambulia tena kwa risasi, na kuzidi kunipa woga mwingi.Dakika kama tano hivi zikakata kwa majamaa kulishambulia gari letu kwa risasi, nyingi, nikachungulia kidogo, nikamuo jamaa mmoja akipiga hatua za taratibu hadi ilipo gari na kuichungulia ndani, na kuonekana akistuka sana

    “Hayupo muhusika”

    Alizungumza kwa sauti ya juu, huku akiwatazama wenzake, anaye onekena ni mkubwa wao akatoa simu, na kuminya minya na kuiweka sikioni, gafla simu ya Victoria ikaanza kutetemeka mfukoni mwangu, kutokana kuweka mlio ulio katika mfumo wa mtetemeko(vibration).Nikaitoa kwa haraka mfukoni mwangu na kwabahati nzuri ikawa imesha jipokea kotokana na kuibabatiza kwenye mfuko wangu wakati ninaitoa kwa haraka mfukoni mwangu, kutokana ni ‘screan touch’ nikasikia sauti ikitoka kwenye simu iliyo pigwa ikizungumza kwa sauti ya juu kidogo

    “Bosi muhusika hatujampata”

    Maneno hayo yanafanana na jamaa anaye piga simu hiyo, nikachungulia na kumuona jamaa akiishusha simu yake kutoka sikiooni mwake

    “Vipi”

    “Bosi azungumzi chochote”

    “Inakuwaje sasa?”

    “Hivi mnauhakika hii ndio taksi, tuliyokuwa tukiifwatilia aliyo ipanda huyo Eddy?”

    Mkubwa wao aliuliza

    “Ndio hii, hembu mpigie bosi, kwenye ile namba yake nyingine”

    Jamaa mmoja alimshauri mwenzake na kuinyanyua tena simu yake na kuiweka sikioni, nikajikuta nikiitumbulia mimacho simu ya Victoria nikisikilizia kuingia kwa simu hiyo.Ila haikuingia nikamsikia akizungumza

    “Bosi tumemkosa Eddy”

    “Tumefwatilia, tumefanya shambulio la gafla ila hatujamuona”

    “Sawa, bosi”

    Jamaa akakata simu na kuwatazama wezake

    “Oya Jumbe, bosi anasemaje?”

    “Anasema tuhakikishe tunarudi na kichwa cha Eddy, la sivyo atavikata vichwa vyetu”

    “Mmmm”

    Jamaa mmoja akaguna, huku akishusha pumzi nyingi, mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, hapa ndipo nikapata uhakika wa Victoria ndio adui yangu namba moja na ndio yupo nyuma ya mpango mzima wa kumuua mke wangu akishirikiana na John, rafiki yangu wa karibu

    “Kama atakuwepo atakuwepo eneo, haya tumt……..”

    Kabla ya mkuu wao, anaye itwa Jumbe hajamalizia sentesi yake, sote tukastushwa na sauti ya simu ya John, iliyopo mfukoni mwangu.Nikasimama kwa haraka huku nikiwatazama jamaa, ambao nao wakanitazama huku akionekana kutokuamini macho yao, nisawasawa na mtu aliye okota embe dodo chini ya mti wa mpapai

    “Kamaataaaaaaa mshenzi yule”

    Jumbe alizungumza huku akininyoosheaa kidole, kwa haraka nikaanza kukimbia nikieleka kwenye msitu huu, ambao ulikuwa na barabara tuliyo kuwa tunapita.Taa za pikipiki wanazo ziendesha jamaa, zikazidi kunifwata kwa nyuma kwa mwendo wa kasi, nikazidi kukimbia kuelekea nisipo pajua huku nikikatisha katisha kwenye miti, nikikwepa risasi nyingi zinazo kuja nyuma yangu

    “Eheee Mungu wangu, nisadie mie”

    Nilizungumza huku nikiendelea kukimbia, nikafanikiwa kupandisha kwenye kilima chenye mawe mengi makubwa ambayo si rahisi kwa pikipiki kupita, nikazidi kuongeza mwendo wa kukimbia, huku nikihema sana, Nikazidi kupandisha mlima huku nikijitahidi kwa kadri yangu, kutafuta sehemu ambayo ninaweza kujibanza na kuwakwepa jamaa wana nitafuta

    Nikafanikiwa kuingia kwenye moja ya mwamba wenye tobo kubwa, sikujali kama kunaweza kuwa na kutu cha hatari ndani ya mwamba huu, zaidi nilicho kijua mimi ni kujibanza huku, jasho jingi likinimwagika, kutokana na mwanga mzuri wa mbalamwezi nikawaona watu hao wakiendelea kutazama huku na huku na kuzidi kwenda mbele wakiamini kwamba nimekimbilia juu kabisa kwenye milima.Walipo potea kwenye macho yangu, nikaanza kurudi nyuma tulipo toka, safari hii nikijitahidi kufunga breki za miguu yangu, kuhakikisha sianguki kwani kasi niliyo nayo ya kushuka mlimani si ndogo, ikitokea bahati mbaya nikakosea kushuka nilazima kichwa kipige chini, hapo kuna mawili, kuvunjika vunjika mifupa au kufa kabisa

    Simu ya John ikaanza kuita mfukoni mwangu, nikaitoa na kukuta jina la ‘My Victoria’ huku pembeni kukiandikwa namba 2.Ikimaanisha ni namba ya pili kuwekwa kwenye simu hii, nikajibanza sehemu, yenye jiwe kubwa na kuitazama kwa muda, huku nikijaribu kuyalazimisha mate kupita kwenye koo langu lililo kauka kwa kiasi kikubwa, na taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni

    “Hahahaaaa, Eddy, rafiki yangu, si kila unaye muona kwako ni mwemaaaaa, wengine ni maadui.Kumbuka Tanzania wewe ulijifanya ni mjanja kunionea na kunidhalilisha kwa kunipiga, sasa ni muda wako wakudhalilikaaa, Ahahaaaaaaha”

    Sauti ya John ilisikika huku, akizungumza kwa dharau na kucheka sana.Asira ikazidi kunipanda huku mwili mzima ukinitetemeka kwa hasira iliyo kali

    “Ohhhh kaka Eddy, kumbuka mimi sio ndugu yako.Baba yako kwa nyege zake alimchukua mama yangu kutoka mikononi mwa baba yangu, kwa kutumia pesa zake, kisha wewe ukamtesa mama yangu na kumfanya afe, you’re a loser…………”(….., wewe ni mpotezaji)

    Sauti ya Victoria ilisikika huku wote wawili wakionekana kufurahia ushindi walio upata dhidi yangu

    “Wait bro Eddy, ukirudi nyumbani utamkuta baba yako ni maiti, love you baby boy Eddy, mwaaaaaaa”(Subiri kaka Eddy……., nakupenda Eddy mtoto wa kiume,……)

    Nikajihisi, mwili ukipasuka kwa hasira nikataka kupiga hatua moja mbele, ila kuna kitu kigumu kikanigusa kwenye kichwa changu upande wa kulia

    “Ohhhh lete simu yako”

    Ni sauti nzito ya mmoja wa majambazi walio tumwa na Victoria, kuja kuniangamiza.Taratibu akapita mbele yangu, huku bunduki yake akiwa ameielekeza kichwani kwangu

    “Utanaka simu eheeee”

    Nilizungumza kwa kujiamini, huku nikimtazma kwa macho yaliyo anza kudondosha machozi ya asira pamoja na uchungu mwingi.Kwa haraka nikairusha simu juu, na kumfanya jambazi kuiangalia jinsi inavyo kwenda juu kwa kasi, nikaushika mkono wake wenye bastola, na kuvivunja vidole vyake vya mkono ulio shika bastola, akainama huku akitoa maumivu makali ya kuumia huku akilalamika.Nikampiga kigoti cha mso na kumfanya asimame, huku akiyumba yumba.Ngumi niliyo ikunja vizuri, ikatua kwenye shingo yake, ikampeleka chini, simu yake ya upepo aliyo kuwa ameishika na mkono mwengine ikaanguka chini huku sauti ya mkuu wake ikisisika

    “G umepatwa na nini, eheeee”

    Akanyanyuka na kutema mate pembeni yaliyo changanyikana na damu, ikiashiria kuna sehemu kwenye kinywa chake imepata itilafu.Akarusha teke, nikainama chini, na kujizungusha kwa haraka, nikaichota miguu yake na kumbwaga chini kama mzigo wa kuni.Macho yangu yakatua kwenye bastola iliyo anguka karibu yangu, nikaiokota kwa haraka, jamaa akanishika mguu wa kulia na kuuvuta, ikapelekea mimi kuangukia mgongo na kuichia bastola ikasogea pembeni kidogo.Jamaa akaniwahi kunikalia tumboni, akaanza kunikaba koo kwanguvu nyingi kwa kutumia mkono wake ambao sijauvunja vidole, nikajitahidi kuminyana naye, huku mkono wangu mmoja nikiupeleka ilipo bastola, Jamaa akazidi kuniminya koo langu, hadi nikajihisi kuanza kufanya mawasiliano na malaika mtoa roho

    ‘UKIWA MWANAUME HUTAKIWI KUKATA TAMAA KIRAHISI, PAMBANA HADI DAKIKA YA MWISHO, HATA KUUA IKIBIDI FANYA HIVYO, ILI TU UWE MSHINDI’

    Nimaneno ya baba yangu mkubwa mzee Godwin, kipindi alipokuwa akinifundisha mazoezi ya kupigana, nilipokuwa kijana wa umri mdogo sana, na maneno yake haya alikuwa akiniambia pale anaponizidi ikiwemo kunipoga kabala.Nikazidi kuupelekea mkono wangu sehemu yanye bastola, kidole change kimoja cha katikati, mkono wa kulia, kikaanza kuivuta taratibu bastola, hadi ikafika kwenye vidole vyangu vyote vitano vya mkono wa kulia.Sikuuliza zaidi ya kuvuta traiga, ya bastola mara sita na kuziruhusu risasi sita kutoka kwenye bastola, na kupenya kwenye mbavu za jambazi huyu, akaanguka pembeni yangu huku akivuta pumzi yake ya mwisho

    Nikasimama na kumtizama jambazi huyu jinsi anavyo hangaika hangaika, nikafyatua risasi mbili, zikaingia kichwani mwake, akatulia tuli, nikaiokota simu ya John pamoja na simu ya upepo ya jambazi iliyo anguka

    “Upo wapi G wewe, tukufwate?”

    Suti ya mkuu wao ambaye anaitwa Jumbe, ilisikika vizuri kwenye spika za simu hii

    “Zamu yenu inafwata”

    Nilizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo mingi, nikaipiga simu ya upepo kwenye jiwe kubwa, ikapelekea kuchanguka changuka vipande vingi.Nikakaanza kushuak kwenda chini, kwa bahati nzuri nikakuta sehemu walipo zisimamisha pikipiki zao, nikapanda kwenye moja ya pikipiki, nikaiendesha kwa kasi hadi umbali kidogo na zilipo nyingine, nikashuka na kurudi zilipo nyingine, nikaziangusha chini zote, nikazifungua mifuniko ya matanki ya mafuta, kisha nikarudi nilipo iacha pikipiki niliyo ichukua.Nikafyatua risasi mbili, zilipo pikipiki na kusabisha zilipuke zote

    Nikaondoka kwa kasi, huku nikiotea otea njia ya kurudi barabarani, nikafanikiwa kutokeza kwenye barabara niliyo ifahamu, kwani ndio barabara kuu ya kurudi nyumbani kwa baba.Nikazidi konyeza mwendo kasi wa pikipiki, kimoyo moyo nikiapa kuwaua John na Victoria kwa mkono wangu mimi mwenye.Hadi ninafika nyumbani kwa baba imesha timu saa kumi na mbili asubuhi

    “Nifungulieni geti nyinyi”

    Niliwafokea walinzi wa getini, waliokuwa wakinihoji maswali, ikanilazimu kulivua kufia la pikipiki, ndipo wakanitambua ni mimi, wakafungau geti na kuingia ndani kwa kasi, walimzi wakabaki wakinishangaa, nikafika mlangoni na kuisimamisha pikipiki, kwa haraka nikashuka huku bastola yangu ikiwa mkononi, nikapandisha ngazi kwa haraka nikielekea kwenye chumba change, nikaupiga teke mlango, ukafunguka, chumbani sikukuta mtu zaidi ya kitanda kilicho changuliwa mashuka.Nikaelekea chumba cha Victoria, ila sikuwakuta.Nikaelekea chumba cha baba yangu, nikawakuta walinzi wake wawili wakiwa wamesimama mlangoni, ila mmoja akanizuia nisiingie

    “Mzee amepumzika, hadi muda wake wa kuamka ukifika ndio, unaruhusiwa kuingia”

    “Nini wewe”

    “Hiyo ni sheria na si ombi”

    “Unajua mimi ni nani?”

    “Hata kama, ila muda wa mzee kuamka ni sambili kamili kwa sasa jaturuhusu mtu kuingia ndani ya chumba hichi”

    Nikamshika tai mlinzi anaye nisemesha upuuzi wake, nikamvuta na kumuangusha chini, mwenzake akataka kunishika ila kwa haraka nikaielekeza bastola yangu, kwenye pua yake, akabaki kimya akinitumbulia mimacho yake.Nikausukuma mlango wa chumba cha baba, nikamkuta akiwa anazunguka zunguka kwenye feni lililo juu, huku akiwa amefungwa kwa kamba ngumu, mdomoni mwake akiwa amefungwa kwa plasta kubwa, huku miguu na mikono yake ikiwa imefungwa kwa kamba.Nikabaki nikiwa nimeduwa, nikastukia walinzi nilio gombana nao mlangoni wakinipita kwa kasi na kukimbilia anapo ning’inia baba na kuanza kumshusha huku wakiwasiliana na wezao kuomba msaada.Machozi ya uchungu yakaanza kunimwagika, walinzi wakazidi kujazana chumbani kwa baba yangu, huku daktari wake akijitahidi kumpatia baba huduma ya kwanza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikamuona daktari akitingisha kichwa baada ya kuweka sikio lake kwenye, kifua cha baba, na kukuta mapigo yake ya moyo yakiwa yamesimama, ikiashiria kwamba ni marehemu tayari.Sikutaka hata kukisogelea kitanda cha baba, nikatoka ndani ya chumba, huku nikiwa nimefura kwa hasira kali.Sikujua hata walipo John na Victori, na wao ndio wamesababisha mauji ya baba yangu.Simu ya John ikaita, na kukuta ni namba ngeni ndio inayo ita, nikaipokea haraka

    “EDDDYYYYYYYYYY UPO WAPI KAKA”

    Sauti ya John ilisikika kwenye simu

    “Mshenzi, mpumbavu, nikikukamata nitakunyonga kama mulivyo fanya kwa baba yangu”

    “Hhaahahaaaaa kumbe umefika nyumbani….Ohhhhh boy, huwezi fanya chochote kwani hujui nilipo”

    “Kaka Eddy, mwaya samahani kwa kumuua baba yako”

    Sauti ya Victoria ilisikika, alizungumza kwa dhara kubwa sana.Sikutaka kumjibu chochote, nikaikata simu, na kuingia kwenye mtandano wa goole, nika ‘download’, apps inayoitwa google map pamoja na ‘mobile location tracker’, inayo saidia kujua ni wapi namba ya simu iliyo pigwa inapatikana.Nikaiingiza namba ya simu iliyo nipigia, kitendo cha dakika moja nikafanikiwa kuletewa alama inayo onyesha ni wapi namba hiyo ya simu ipo na kuna umbali gani kutoka hadi sehemu nilipo.Nikatoka nje ya kupanda pikipiki yangu, na kuondoka kwa kasi, huku nikifwata jinsi simu inavyo nielekeza sehemu ninapoweza kuwapata John na Victoria

    Ndani ya nusu saa nikawa nimefika kwenye moja ya mtaa, wenye watu wengi wanao onekana ni wavuta bangi, na sehemu niliyo simama pembeni kuna kundi la vijana walio choka choka na maisha, huku mmoja akiwa aimeishika simu ambayo alitumia John kunipigia, nikashuka kwenye pikipiki kwa kujiamini sana hadi sehemu walipo simama.Nikawasalimia ila hapakuwa na aliye ijibu salamu yangu, nikagusa bega aliye ishika simu akageuka, huku sura yake akiwa aimeikunja, akavuta fumba kubwa la msokoto wake wa bangi, kisha taratibu akaupulizia usoni mwangu, kitendo chake kikanipandisha hasira dhidi yake, nikampiga kidoti na sehemu za siri na kumfanya atoe ukelele, wezake wakataka kuingialia huku wakichomoa visu vyao, nikatoa bastola, nikawaelekezea moja baada ya mwengine akaanza kuondoka kwa kukimbia, akijaribu kuyaokoa maisha yake, nikabaki na mwenye simu

    “Nani kakupatia hii simu?”

    “Ehhheee?”

    Nikamzaba kofi la shavu, hadi nikahisi na mimi maumivu makali kwenye kiganja change, kutokana nakutumia nguvu nyingi, jamba lililo sababisha vidole vyangu kujitokeza kwenye shavu la jamaa huyu

    “Ni dada mmoja hiviii”

    Jamaa alizungumza huku akilia, kama mtoto mdogo

    “Huyo dada yupo wapi?”

    “Sijui mimi”

    Nikaikoki bastola yangu, na kuisokomeza mdomomi mwake, macho yangu yaliyo jaa asira yakazidi kumtazama jamaa huyu, ambaye mwanzoni alijihisi ni mbabe sana

    “Na..ongea….”

    Nikaichomoa bastola yangu mdomoni, ili kumpa nafasi ya kuzungumza

    “Alimpa mtoto mmoja hivi, nikampokonya na kuichukua mimi”

    Jamaa aliendelea kuzungumza huku akimwagikwa na machozi mengi

    “Unanidanganya….?”

    “Kweli, ila nawafahamu wale”

    “Wanapatikana wapi?”

    “Kuna godauni moja lipo hapo mbele, ndipo zilipo biashara zao”

    “Twende unipeleke”

    Nikaiacha pikipiki, tukaanza kutembea kwa miguu kuelekea lilipo godauni analo lizungumzia jamaa, hapakuwa mbali sana, tukafika kwenye moja ya jengo kubwa lenye geti kubwa

    “Simama na ugonge”

    Jamaa akasimama na kuaza kugonga, mimi nikasimam pembeni kodogo, huku nikiwa nimejificha.Geti likaanza kufunguliwa kwenda juu, akachungulia mlinzi mmoja mwenye bunduki mkononi mwake, sikutaka kuuliza zaidi ya kufyatua risasi iliyo tua kichwani mwa mlizi huyo, jamaa niliye kuja naye akaanguka chini kwa presha, nikaingia ndani ya godauni hili, lenye maboksi mengi, walinzi waliopo humu ndani wakanza kunishambulia kwa risasi, zilizo nikosa kutokana na kujificha kwenye nguzo moja,

    “Stop fireee”

    Niliisikia sauti ya Victoria ikiwaamrisha watu wake kuacha kupiga risasi, nikashusha pumzi nyingi huku nikilishuhudia geti likishushwa chini na kufungwa

    “Eddy natambua kwamba ni wewe, hapo ulipo ninahesabu hadi tatu ninaomba ujitokeze”

    Victoria alizungumza kwa sauti ya juu, niliyo isikia vizuri masikioni mwangu

    “Mojaaaaaaa,”

    Nikashusha pumzi nyingi, huku nikichungulia kuona sehemu alipo, sikuamini macho yangu baada ya kumuona John akiwa amemshika Phidaya, anaye lia, huku akiwa amemuwekea bastola ya kichwa

    “Mbiliiiiiiiiiii”

    Nikamtazama mke wangu aliye pauka sana uso wake, nikamtazama tumboni mwake na kukuta tumbo lake lipo vilevile, ikiashiria bado ni mjamzito

    “Ta……….”

    Nikajitokeza kwenye nguzo niliyo jificha, walinzi kama hamsini, bunduki zao zote zikawa zimeelekea kwangu, nikaanza kutembea kuelekea katika sehemu walipo simama John, Phidaya na Victori, huku bastola yangu ikiwa mkononi mwangu

    “Eddy mume wangu”

    Phidaya akataka kunifwata, ila John akamshika nywele zake na kumvuta kwa nyuma, hadi akatoa ukelele akijaribu kuzishika nywele zake, John akaachia tabasamu pana usoni mwake, taratibu akianza kulishika tumbo la mke wangu.

    “Eddy, umepata mke nzuri sana”

    Victoria alizungumza kwa sauti ya dharau, John akamkumbatia Phidaya kwa nyuma, kitendo kilicho anza kunikasirisha, mikono ya John ikashuka taratibu hadi kwenye sehemu za siri za Phidaya, akaanza kumlazimisha kulifunua dera(gauni) lake, ili aizishike sehemu za siri za Phidaya, sikuvumilia kitendo cha John kumfanyia mke wangu unyama kama huo, nikaminya traiga ya bastola yangu, kwa bahati mbaya nikakuta bastola imeisha risasi, nikastukia nikipiga goti moja chini, huku damu zikianza kuvuja kwenye paja la mguu wangu wa kulia ulio pigwa risasi na John, aliye onekana kukasirishwa na kitendo change cha kujaribu kumuua

    “Baby usimuue sasa hivi, bado hukumu yake”

    Victoria alizungumza huku akimtazama John aliye fura kwa hasira nyingi, akitaka animalizie kunipiga risasi nyingine.Geti likafunguliwa, yakaingia magari manne aina ya BMW, zinazo fanana rangi, ambayo ni nyeusi yakasimama nyuma yangu, wakashuka wanaume nane walio valia suti nyeusi pamoja na miwani, maumivu ya mguu yakazidi kuniandama, huku kilio cha mke wangu, kikizidi kuniumiza.Akashuka mwanamke mmoja aliye valia suti yeusi, pamoja na kofia kubwa nyeusi, huku macho yake akiwa ameyafunika na miwani yeusi, nywele zake ndefu, zikiwa zimeufunika uso wake, akanipita na kusimama sehemu alipo simama Victoria, wakakumbatiana kwa furaha, kisha akaelekea sehemu alipo simama John, akamkumbatia huku wakizungumza chini chini.

    Akageuka nyuma na kunitazama mimi, taratibu akavua miwani yake, akafwatia kofia lake kubwa, taratibu nywele zake akazisogeza pembeni, nikabaki nikistuka baada ya macho yangu kutazamana na macho ya Madam Mery.Mwalimu aliyekuwa mpenzi wangu kipindi ninasoma

    ”Mambo Eddy”

    Alinisalimia huku akitabasamu, akpiga hatua za taratibu na kusimama mbele yangu, taratibu akachuchumaa, kidole chake kimoja akakiweka chini ya kidevu changu, kisha akazilete lipsi zangu karibu, akihitaji kunibusu, nikausogeza mdomo wangu pembeni, ila akanishika kwa nguvu na kuninyonya midomo yangu kwa kutumia nguvu, jambo lilizidi kumliza Phidaya mke wangu, madam Mery akaniachia na kusimama

    “Mmmmmm ladha yako ya mate, imezidi kuwa tamu, baby wangu.Au huyu mwanamke wako wa kiarabu ameiongezea?”

    Alizungumza kwa dharau, akamfwata Phidaya, nikastukia kumuona Phidaya akimzaba kofi la shavu Madam Mery, huku akisindikiza kofi hilo kwa mate yaliyo tua usoni mwa madama Mery, aliye anza kuchecheka kwa dharau.Madam Mery akampiga ngwala Phidaya, na kumfanya aangukie mgongo, na kutoa ukelele mkali wa maumivu, mguu mmoja wa madam Mery ukatua kifuani kwa Phidaya, madam Mery akanyoosha mkono, wake wa kulia akiomba kitu.Mlinzi wake mmoja akampa bastola, iliyo tengenezwa kwa dhahabu tupu.Akaikoki tayari kwa kumfyatulia mke wangu risasi

    “MERY Tafadhali ninakuomba usimuue mke wangu”

    Nilizungumza huku machozi yakinimwagika kwa uchungu mwingi, Phidaya akawa na kazi ya kulia huku akimuomba Mungu wake, amlaze mahali pema peponi

    “Please SORRY MADAM, don’t kill my wife…..Kama mtu wa kumuua ni mimi na si yeye”(Tafadali bibie, ninakuomba usimuue mke wangu………)

    Niliendelea kuzungumza huku machozi yakinimwagika kwa wingi usoni mwangu, Madam Mery akanitazama kwa macho makili kisha akmachia Phidaya, na kurudi nilipo simama mimi.

    “Eddy, mimi ni mwanamke katili sana, ulikuwa hujui ni jinsi gani ninavyo mpenda Derick, ulimuua kinyama sana.Ulimkatakata kama kuku, na kumbanika.Wewe ni binadamu wa aina gani eheee? Unajua ni uchungu gani nilio upata juu ya kifo cha mume wangu wa ndoa Derick”

    Madam Mery alizungumza kwa uchungu mwingi, huku aknitazama kwa macho makali sana, akanipiga teke la kifua, lililo niangusha chini, kwakutumia kitu chake chenye ncha kali ya kisigino, akanikanyaga kwenye jeraha langu na kuzidi kunipa maumivu pamoja na uchungu.Madam Mery akamngong’oneza Victoria, ambaye naye alimuuta mtu wake mmoja aliye ondoka katika eneo hili.

    “Eddy nilikupenda ila siwezi kukuacha mzima hata kidogo”

    Madam Mery aliendelea kuzungumza huku mara kadha akiniminya kwenye jeraha langu la risasi, meza kubwa ikaletwa na watu wa Vitoria, wakaninyanyua na kuniweka juu ya meza hiyo, wakanifunga kamba kwene kila mkono na ziichanua, huku watu wawili wakiwa wanazivuta kamba hizo, kila mmoja upande wake.Wengine wawili wakaifunga miguu yangu na kila mmoja akaivuta upande wake.

    Jamaa mmojaa akamkabidhi madama Mery upanga wenye kumeremeta kwa rangi yake, madama Mery akapiga hatua hadi kwenye meza niliyo lazwa mimi, akanitazama kwa macho ya dharau

    “Nafanya hii, kwa ajili yakulipiza kisasi cha mume wangu”

    “Ngoja kwanza, nipo tayari kufa, ila ninakuomba usimuue mke wangu”

    Nilizungumza kwa ujasiri, nikiwa nipo tayari kwa kufa, Madam Mery akalinyanyua panga lake juu, akalishusha kwa kasi kwenye mkono wangu wa kulia



    Nikatoa ukulele mkali, ulio mfanya madam Mery kusitisha zoezi lake kuukata mkono wangu, panga lake likiwa limesimama sentimita chache kutoka ulipo mkono wangu

    “Madam, ninakuomba unisamee”

    Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagika usoni mwangu, madam Mery akanitazama kwa macho ya hasira yaliyo jaa ukatili mkubwa, akawatazama Victoria na John ambao macho yao yote yalikuwa kwetu

    “Natambua kwamba mimi nimkosaji sana kwako, ninastahili kufa mbele yako, ila si mbele ya macho ya mke wangu.Mtazame jinsi alivyo katika hali yake.Mule ndani amebeba kiumbe kama ulicho kuwa umekibeba wewe, miezi tisa, na Derick akakiangamiza mbele yetu.Yule ni mwanamke mwenzako ambaye anauchungu kama wewe”

    Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagilka usoni mwangu, madam Mery kwa mbali machozi yakaanza kumlenga lenga, macho yake yamebadilika rangi na kuwa mekundu kiasi huku sura yake ikiwa imejaa mikunjo kwenye paji lake la uso akinitazama kwa uchungu sana

    “Mery mimi pia ni binadamu, kumbuka ni mambo mangapi tuliyafanya tukiwa pamoja, vuta kumbukumbu ni vitu vingapi tulishiriki tukiwa pamoja, Eheeee, leo hii unataka kuimwaga damu yangu, leo hii unataka kunisulubu kikatili, le……..”

    “Eddy STOP TALKING”(Eddy nyamaza kuzungumza)

    Madam Merry alizungumza kwa sauti ya juu, yenye uchungu ndani yake.Akalitupa chini panga lake alilokuwa amelishika.Machozi mengi yakaanza kumbubujika usoni mwake, John na Vivtoria wakabaki wakimtazama madam Mery, ambaye taratibu alianza kupiga hatua za kuelekea kwenye gari lake alilo kuja nalo

    “Madam Vipi?”

    John alizungumza huku akimwafwata madam Mery kwa nyuma

    “John ninakuomba uniache”

    Madam Mery aluzungumza huku akiunyanyua mkono wake mmoja akimzuia John asimfwae anapo elekea

    “Ila madam haya sio makubaliano yetu”

    “John sipo sawa nimekuambia usinifwate”

    Madam Mery alizungumza kwa sauti ya ukali, huku machozi yakiendelea kumchuruzika usoni mwake.

    “Sasa Madam tumfanye nini Eddy?”

    Madam Mery akageuka kwa hasira, hadi John akastuka kidogo, akanitazama jinsi machozi yanavyo nimwagika, akayafumba macho yake kwa sekunde kadhaa, akionekana akifikiria kitu cha kufanya juu yangu.

    “Kesho nimkute akiwa hai”

    Madam Mery alizungumza kwa sauti ya upole, kisha akaelekea lilipo gari lake, akafunguliwa mlango na mlinzi wake, akaingia ndani ya gari na wakaondoka zao.John akalisindikiza magari ya Madam Merry yanayotoka kwenye geti kubwa la Godauni, lilipo fungwa taratibu John akanigeukia, akanitazama kwa macho ya dharau huku Victoria akiwa amejichokea, kwani ninaamini mipango yao waliyo kuwa wameipanga dhidi yangu imeharibika.John akamfwata Victoria sehemu alipo simama, wakanong’onezana kwa muda kisha wakamtama Phidaya ambaye muda wote, amejilaza chini huku machozi yakimwagika kwa uchungu

    “Mchukueni huyo Malaya mumrudishe mulipo mtoa”

    John aliwaamrisha watu wake, wakamnyanyua Phidaya na kumbeba juu juu, japo anajitahidi kujitoa mikononi mwa watu walio mbeba, huku aikiliita jina langu kwa sauyti ya juu, ila hakuifanikiwa kujitoa mikononi mwao

    John akapiga hatua hadi katika sehemu nilipo fungwa, akanitazama kwa muda, huku macho yake yakiwa yamejaa dharau kubwa, akanitemea mate ya usoni, akiyasindikiza kwa kofi zito lililo tua kwenye shavu langu la kushoto

    “Mmmmmm Eddy, unajisikiaje?”

    John alizungumza huku akivifikisha viganja vyake, na kuvipuliza taratibu taratibu.Akanishika sikio langu la upande wakulia, akaanza kulivuta kwa nguvu zake zote, nikaendelea kuugulia maumivu ndani kwa ndani, sikutoa sauti yoyote kwenye kinjwa changu

    “Waooo, unajifanya komandoo usikii maumivu eheeee?”

    John alizungumza, huku akiliachia sikio langu.Akaanza kunitandika vibao mfululizo kwenye mashavu yangu, hasira ikazidi kumiliki nafisi yangu.

    “John, tumpeleke kisimani, hapo unajisumbua bure”

    Victori alitoa wazo ambalo John alilikubali, wafanyakazi wao wakanishusha kwenye meza, majamaa wawili wakanibeba kwenye mabega yao. kama wawindaji walio beba swala waliye muua kwenye mawindo yao.Tukaingia kwenye moja ya ukumbi mkubwa wenye mwanga hafifu, unao pita kwa kutumia madirisha machache yaliyopo juu yake.Wakanibwaga chini, na kunifanya nitoe mguno wa maumivu kutokana na kujiumiza sehemu ya paja langu, nililo pigwa risasi

    Taa kubwa zenye rangi nyeupe zikawaka na kulifanya eneo zima la ikumbu kuponekana vizuri, kuna mashimo makubwa mawili, kwa haraka nikatabua ndio hivyo visima wanavyo vizungumzia, mabaunsa walio kuwa wamenibeba, wakaufunga mwili wangu kwa kamba ngumu aina ya manila.

    “Eddy utakufa kifo kibaya sana”

    John alizungumza huku akiwa ameniinamia

    “Usiombe nikatoka, kwenye mikono yeno, utajuta”

    Nilizungumza kwa kujiamini sana, John akaanza kucheka kwa dharau, huku akinipiga piga mashavuni mwangu

    “Eddy huwezi kutoka mikononi mwangu, nakujua wewe vizuri sana.Huwezi fanya chochote dhidi yangu.Muda wako umekwisha kaka”

    “Angalia wakwako ndio utakuwa umekwisha”

    John akaanza kunipiga mateke mfululizo kwenye mbavu zangu, nikaendelea kutoa sauti ya maumivu ila John hakunionea huruma zaidi ya kuendelea kunipiga kwa nguvu zake zote

    “Mchukueni na mukamdumbukize kwenye kisima”

    John aliwaamrisha watu wake, wakanibeba, kabla hawajaondoka na mimi, Victoria akawazuia.Akapiga hatua hadi sehemu tulipo simama

    “Eddy nakupenda kaka yangu, kwaheri”

    Victoria alizungumza huku akinibusu shavuni mwangu, akawarusuhu watu kuonipeleka kwenye kisima kilichopo kwenye huu ukumbi, kwa jinsi walivyo nifunga kamba mwili wangu sikuweza kufanya kitu cha aina yoyote zaidia ya mwili wangu kunyooka moja kwa moja, mithili ya mtu aliye fariki dunia.Wakanifunga kwenye kamba nene, tartibu wakaanza kunishusha kwenda chini, taratibu.Giza jingi lililo tawala ndani ya shimo hili, likazidi kuniogopesha na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa.Nikastuykia nikigusa chini, kwenye shimo hili lenye futi zaida kumi na mbili.

    Gafla nikaanza kuhisi vitu vidogo vidogo vikinitambalia mwilini mwangu, nikastukia mwili wangu ukianza kupata maumivu maklali yaliyo tokana kung’atwa na wadudu wadogo ambao sikujua ni waduudu wa aina gani, jambo lililo nifanya nitoe ukelele mkali sana



    Wadudu wenye meno makali, wakazidi kuushambulia mwili wangu jambo lililo nifanya nizidi kuchanganyikiwa na kuanza kukiona kifo kikisimama mbele yangu, nilicho kuwa nikikisubiria ni pumzi yangu kukatika name niesabike kama mfu kati ya mamilioni ya watu walio tangulia mbele za haki, masaa kadri yalivyo zidi kukatika ndivyo jinsi nilivyo zidi kupata maumivu makali yasiyo mna kikomo, ikafikia kipindi kelele na maumivu yangu hayakupata msaada wa aina yoyote kutokwa kwa mtu yoyote

    “Eheee Mungu ninakuomba unisaidie”

    Niliamua kumkumbuka Mungu wangu, kama kuna uwezo wowote ambao anaweza kunipatia, kwa wakatui huu, sikua na ubishi wa aiana yoyote kwani ndio tayari nipo kwenye shimo la kifo.Giza likaanza kutoweka taratibu na mwanga mkali wa jua ukitokea juu ya paa lililo funguliwa muda mchache uliopita ikiashiria kwamba asubuhi nma mapema kumepambazuka, hapa ndipo nikagundua aina ya wadudu wanao nishambulia kwamba ni ng’ee wadogo wadogo wenye meno kali sana.Nguvu za mwili wangu zikaanza kuniishia kadri ya muda unavyo katika, mwili mzima wote umevimba kwa maumivu makali niliyo yapata.

    Nikaanza kuzisikia kelele za watu wakizungumza ndani ya ukumbi huu, huku kutikana na umbali niliopo kwenda chini kwenye kwenye shimo sikuelewa ni mazungumzo ya aina gani ambayo wanayanzungumza, taratibu nikaaza kuvutwa kwenda juu, na nikatolewa ndani ya shimo na watu walio niiingiza ndani jana

    “Duu huyu jamaa ana roho yap aka, bado yupo hai”

    Jamaa mmoja alizungumza huku akinitazama na kunigeuza geuza kwa mguu wake alio valia kiatu kigumu sana, na kila alipokua akinmigusa katika mwili wangu, kwangu ilikuwa ni maumumi makali yasiyo elezeka

    “Si bora tumuue tuu”

    “Tukimuua unadhani bosi atatuelewa?”

    “Sasa mtu ameumuka kiasi hichi unadhani kwamba atapona huyu?”

    “Sina uhakika ila tusubiri hao mabosi wetu wakija watoe uamuzi juu ya hili”

    Jamaa waliendelea kushauriana huku wakiwa wamenizunguka, katika sehemu waliyo nilaza huku kamba waliyo izungusha mwilini mwangu ikiendelea kubaki kama walivyo nifunga, jamaa mmoja ajachukua ndoo ya maoja na kutoka nje, wakabaki jamaa watatu wakiwa wamenizunguka. Huku wakiwa wanavuta sigara zao.Jamaa aliye toka na ndoo akarudi na kuisimamisha pembeni yangu

    “Umeweka nini humo?”

    “Kuna maji ya yabaridi nahitaji kumuogesha huyu mwehu”

    Jamaa pasipo kufikiria mara mbili ni maumivu ya aiana gani nitayapata, akaanza kunimwagia kuanzia juu hadi chini huku akiungana na wezake katika kunimwagia maji hayo, yaliyo zidi kuviumiza vidonda vyangu.

    “Cheki jinsi anavyo babaika”

    Mmoja alizungumza huku akininyooshea kidole, wakinicheka jinsi ninavyo garagara chini na kulia kwa maumivu makali ninayo yapata mwilini mwangu

    “Bosi anasema mumtoe, mumpeleke kule kwenye godauni”

    Jamaa mmoja aliye ingia muda si mrefu aliwapa wezake ujumbe walio anza kuutekeleza ndani ya dakika moja mbeleni, nilidhani watanibeba kama walivyo fanya jana walipokua wakiniingiza ndani ya ukumbi huu. Wakaanza kuniburuta huku wakiwa wanaivuta kamba waliyo nifunga nayo.Tukafika kwenye godauni la jana, nikamkuta John akiwa na Victoria wamesimama wakitungojea tutokee katika sehemu tuliyo simama

    “Habari za asubuhi Mr Eddy”

    John alizungumza huku akinizunguka zunguka katika sehemu niliyo lazwa, hata kinywa changu hakikuwa na nguvu ya kufunguka kutokana na maumimu makali niliyo yapata kutoka kwa wadudu walio nishambulia usiku mzima

    “Ninaimani leo inakuwa ni siku ngumu sana kwako”

    John aliendelea kuzungumza huku akiwa amesimama pembeni yangu akinitazama chini, sukuamini Yule John niliye kua nikimsaidia mambo mengi kipindi tunasoma leo hii ndio mtu anaye nifaniyia ukatili wa aina hii

    “Mtoeni Yule Malaya”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walinzi wao wakatii agizo walilo ambiwa na mkuu wao ambaye ni John, ndani ya dakika kadhaa wakarudi wakia wameongozana na mke wangu Phidaya, ambaye amechakaa kwa kiasi kikubwa huku nywele zake zikiwa zimechanguka kama mwenda wazimu, uzuri wake wote umepotea kwenye sura yake, sura yake imejaa alama nyingi za vidole ikishiria kwamba kuna mtu au watu walimpiga muda mchache ulio pita

    “Eddy ninakumbuka kipindi tunasoma kombi ya PCB, ulikua unapenda sana kuwapasua vyura kuona ni kitu gani kipo ndani ya matumbo yao, sasa leo na mimi ninahitaji kumpasua mke wako nione ni kitu gani ambacho amekibeba ndani ya tumbo lake hadi likawa kubwa kiasi hichi”

    John alizungumza huku akianza kuvaa gloves nyeupe, macho yangu yakakutana na macho ya Phidaya ambaye muda wote anabubujikwa na machozi mengi usoni mwake, akaanza kutingisha kichwa pasipo kutambua ni nini maana ya yeye kukitingisha kichwa chake

    “Ohhh naona wifi anahuzuni sana, ila John nimepata wazo”

    Victoria alizunguimza huku akimtazama John anaye chagua chagua kisu kikali kwenye moja ya meza fupi iliyomo ndani ya godauni hili

    “Wazo gani mke wangu”

    “Mimi ninaona tumpe uchaguzi wifi yangu kipenzi”

    “Ehee endelea mama”

    “Mimi ninaona achague kati ya haya mambo mawili, kumfanyia upasuaji na ukitoe hicho kiumbe cheke au amuue mume wake kwa mikono yake yeye mwenyewe”

    Nikamuona jinsi Phidaya alivyo stuka na kuzidi kumwagikwa na machozi mengi usoni mwake, nikamtazama Phidaya ambaye amechanganyikiwa kwa mambo aliyo ambiwa na Vicvtoria

    “Yeee hilo ni wazo zuri mpenzi, yaap Shemeji, uamuzi upo mikononi mwako, una dakika mbili za kujifikiria, wewe kuondoka duniani, au wewe kumuondoa mume wako duni ani”

    John akaivua saa yake ya mkononi na kumkabidhi Phidaya, akimuomba afanye kama alivyo agizwa.Phidaya akanitazama mimi kwa macho yaliyo jaa uchungu kisha akamtazama John anaye piga mluzi, ulio jaa dharau.

    “Dakika zinakwisha shemeji”

    Phidaya akajiinamia chini, kisha akanyanyanyua kichwa achake na kunitazama tena kwa mara nyingine pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote.Akamrudishia John saa yake kisha, akanyoosha mkono wake kwa John akiashiria kwamba kuna kitu anakiomba

    “Nini?”

    John alimuuliza Phidaya aliye baki amemnyooshea mkono mmoja pasipo kusema kitu cha aina yoyote

    “Kisu”

    John akatabasamu na kuchagua kisu kikubwa kiasi chenye ncha kali na kinacho ng’aa, akamkabidhi Phidaya, aliye kishika vizuri na kuanza kupigha hatua hadi sehemu niliyo lala, macho yangu yakanitoka kwani sikuelewa Phidaya anataka kufanya kitu cha aina gani

    “Eddy ninakuomba unisamehe, nafanya hivi kwa ajili ya mwanangu aliye tumboni mwangu, ninaimani nizawadi tosha uliyo nipatia mimi”

    Phidaya alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake na kunitazama kwa macho makali.Machozi yakaanza kunimwagika taratibu

    “Phi…d….”

    “Shemeji usimsikilize huyo muue”

    John alizungumza kwa sauti kali, iliyo zidi kumtetemesha Phidaya aliye changanganyikiwa

    “Usipo muua ninakufumua tumbo lako hilo, kubwa hilo sasa upo tayari kupoteza maisha yako na mwanao?”

    John aliendelea kuzungumza kwa sauti ya ukali na yajuu kiasi

    “Hembu jitazame wewe mwenyewe, jinsi ulivyo mzuri, mwanamke mwenye kupendeza, hadi sasa hivi sijatambua ni kwanini unapata tabu kwa ajili ya mpumbavu mmoja, ambaye sijuu mumekutana wapi”

    John aliendelea kumshawoshi Phidaya kufanya anacho hisi kwao kitakuwa ni furaha

    “Wifi, mbona wanaume wapo wengi tuu, utapata wanaume wazuri zaidi ya huyo mume wako, huu ni wakati wako sasa, uhai wako upo juu ya mikono yako”

    Victoria naye aliamua kusema kitu juu ya Phidaya aliye anza kuchanganyikiwa na kujikuta akiwa amekishika kisu kwa mkono mmoja, taratibu Phidaya akaikutanisha mikono yake kwa pamoja katika kishikizo cha kisu, taratibu akaanza kuinyanyua juu akijiandaa kikishusha kwenye mwili wangu na wala sikujua ni wapi kitwakwenda kutua

    “I say kill him”

    John aliendelea kuzungumza kwa kufoka huku akimtazama Phidaya anaye mwagikwa na jasho mwili mzima, sikuwa na uwezo wa kufanya kitu cha aina yoyote kutokana mwili wangu wote imefungwa kwa kamba

    “Eddy am sorry”

    Phidaya akakishusha kisu kwa nguvu, kabla hakijatua kwenye kifua changu akakisimamisha na kukitupa pembeni na kuniangukia kifuani mwangu na kunikumbatia huku akilia kwa sauti ya uchungu

    “Nakupenda mume wangu, wewe ni baba wa wanangu, siwezi kukuua kwani sijui nitamjibu nini mwanangu pale atakapo uliza yupo wapi baba”

    Phidaya alizungumza huku akiendelea kunikumbatia kifuani mwangu, machozi yakeendelea kunimwagika huku nikimtazama Phidaya, Phidaya akasimama kwa hasira na kumtazama John

    “Kama unataka kuniua niue tu, ila siwezi kumuua mwanaume wa maisha yangu, niliye jiapiza kwamba sinto weza kumuacha katika maisha yangu yote hadi ninaingia kaburini”

    Phidaya alizidi kuzungumza kwa hasira huku akiwa amelishika tumbo lake kwa mkono wa kulia, akichechemea na kumfwata John aliye pigwa na butwaa

    “Ni mangapi aliyo kusaidia rafiki yako Eddy, ni vitu vingapi alivyo kutendea Eddy, leo hii unataka kumuangamiza mbele yako, unataka kupelekeshwa na huyo mzungu wako.Kumbuka huyo sio muafrika mwenzio, kumbuka huyo ndio aliye kunyanyasia wazazi wako.Leo hii bado unaende………”

    Victori akapimtandika Phidaya kibao kilicho muangusha chini, ila Phidaya akanyanyuka na kusimama, huku akiyumba yumba mithili ya mlevi.Gafla nikaanza kuona maji maji mengi yakichuruzika kwenye miguu ya Phidaya, ambaye alianza kulishika tumbo lake, huku akilia kwa uchungu mkali sana.Nikaanza kujibiringisha taratibu nikilisogelea eneo alilo lala Phidaya huku akiendelea kulia kwa uchungu

    “Eddy……”

    Phidaya aliita huku akilia kwa uchungu, miguu yake akiwa aimeipanua, jasho jingi likianza kumwagika

    “Ba……by p..usssh”

    Nilizungumza kwa kujikaza huku nikiwa sina msaada wowote kwa mke wangu, John na watu wake wakabaki wakiwa wametukodolea mimacho huku wengine wakicheka kwa dharau, Victoria akataka kuja sehemu tuliyopo mimi na Phidaya ila John akamzuia, huku akimshika mkono

    “Acha tuone watafanyaje”

    John alizumngumza kwa dharau

    “Push baby”

    Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagika usini mwangu Phidaya akazidi kujikakamua, huku akiendelea kulia, kutokana Phidaya ni nesi kidogo kuna mbinu za uzalishaji aliana kuzitumia kwani hapakuwa na msaada wowote kwake zaidi ya mimi kumchochea kwa maneno aweze kumsukuma mtoto atoke nje

    “Anakuja baby anakuja”

    Phidaya alizungumza kwa uchungu huku akiendelea kuzidi kujikakamua kumzaa mtoto wetu, wazo likanijia haraka, japo ninamaumivu makali mwili mwangu ila nikajigeuza haraka na kuiweka miguyu yangu karibu na miguu, ya Phidaya aliye zidi kujikaza katika kumleta kiumbe change duniani

    Nikamshuhudia mwanangu akitoka taratibu na kufikizia kwenye miguu yangu, Phidaya akajitahidi hadi mtoto wangu wa kiume akalala kwenye miguu yangu, iliyo fungwa kamba kwa pamoja

    “Duuuu hongereni sana”

    John alizungumza huku akiichomoa bastola yake kiunoni

    “John unataka kufanya nini?”

    Victori alizungumza, huku akimtazama John aliye anza kuifunga bastola yake kiwambo cha kuzuia sauti

    “Sifanyi chochote mke wangu”

    John akanisogelea hadi sehemu tuliyo jilaza, akanitazama kwa muda, mimi pamoja na mwanangu aliye anza kulia

    “Mwanao ni mzuri sana”

    John alizungumza huku akimtazama mwanangu pamoja na mama yake aliye jilaza, akiwa ameishiwa nguvu za mwilini mwake

    “Goodbye my friend”(Kwaheri rafiki yangu)

    John alizungumza kwa sauti ya upole nikastukia risasi kadha zikitua kifuani mwangu na kuninyamazisha kimya katika sehemu niliyo lala

    Sauti ya milio ya ndege nikaanza kuisikia kwa mbali kwenye masikio yangu, taratibu nikajaribu kuyafumbua macho yangu kuweza kuona n kitu gani kinacho endelea ila, ukungu mwingi umawa umetawala kwenye mboni yamacho yangu, jamvo lililo nifanya nisione kitu cha aina yoyote, nikajaribu kupapasa katika sehemu niliyo lala, nikagundua kwamba nimelalia kitanda cha kamba, ila sikuweza kutambua ni sehemu gani niliyopo.Muda jinsi ulivyo yoyoma ndivyo nilivyo weza kugundua kwamba eneo nililopo, kuna watu wanao zungumza lugha nisiyo ijua

    "Nipo wapi?"

    Nilijarivu kuzungumza huku nikijitahidi kunyanyuka kutoka katika kitanda nilicho lala ila milono ya watu si chini ya wanne wakanirudusha kulala tena kwebye kitanda.Sauti za wanaume pamoja na wanawake zikaendelea kupenya kwenye masikio yangu, nilipo anza kusikia milio ya watoto wadogo wakicheza na wengine kulia ndipo nilipo amini kwamba eneo hili ni salama kwa maisha yangu

    Nikawasikia wakiendelea kunong'oneza, mara sauti ya kike ikasikika, ambayo sikuweza kuisikia tangu wàlipo anza kuzungumza watu hawa, ambao hadi sasa hivi siwezi kuwaona vizuri zaidi ya vivuli vyenye giza, vilivyo simana pembeni ya kitanda nilicho kilalia.Nkasikia wakiyazungumza maneno niliyo yasema dakila kadhaa za nyuma nikiwauliza kwamba hapa nilipo ni wapi

    "Hei"

    Sauti ya msichana hiyo ilinisemesha, ila sikujua anataka kusema kitu gani

    "Nipo wapi, dada?"

    Nliyarudia maneno yangu niliyo yazungumza hapo awali

    "Unazungumza kiswahili wewe?"

    Msichslana huyo aliniuliza, kwa lugha ya kiswahili jamvo lililo nifanya nizidi kufarijika moyoni mwangu na kuamini kwamva nimepata mwokozi katika wakahi huu mgunu nilio nao katika yangu maisha

    "Ndio, ndio dada"

    Niliitikia kwa haraka ila hata ninaye zungumza naye asibadili mawazo ya kunisaidia mimi

    "Unaitwa nani?"

    "Eddy, Eddy dada yangu"

    Nikamsikia msichana huyo akizungumza na wezake huubakilitaja jina langu, kwa wezake ambao ninaamini hawaijui lugha ya kiswahili tunayo zungumza

    "Umetokea wapi?"

    "Tanzania dada yangu"

    "Ulikuja huku kufanyaje?"

    "Wapi, kwani hapa ni wapi?"

    Kabla sijajibiwa nilicho kiuliza nikasikia sauti za watu waliomo ndani ya chumba wakisalimia kwa pamoja kwa kutumia lugha wanayo izungumza, sauti nzito ya mwanaume ikaitikia na kuwafanya watu wote kukaa kimya ndani ya chumba tulichopo

    "Mumesema, ameamka?"

    Mwanaume huyo alizungumza kiswahili cha kuvuta maneo, akionekana kwamba hakifahamu vizuri

    "Ndio baba, na anazungumza kiswahili"

    "Amesema ametokea wapi?"

    "Tanzania, ila hajanitaji ni sehemu gani"

    Mwanaume huyo akaendelea kuzungumza kilugha chao, baada ya muda akatoka ndani ya chumba tulichopo

    "Eddy baba amrsema tukuache upumzike"

    "Ndoja kwanza, unaitwa nani?"

    Msichana huyo akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akajikoholesha kidogo kuliweka koo lake vizuri kisha akanijibu kwa upole

    "Nitakujibu, ukiwa vizuri"

    Nikamsikia akitoka ndani ya chumba nilichopo, nikajipapasa kifuani mwangu, na kukuta kitambaa kigumu kikiwa kimefungwa kuzunguka usawa wa kifua changu chote

    "Ehee Mungu warehema, nisaidie mimi mja wako"

    Nilizumgumza kwa sauti ya chini, huku nkihisi machozi yakinitiririka pembezoni mwa macho yangu.Kumbukumbu za maisha yangu ya nyuma nilipo kua bado mdogo zikaanza kunijia kichwani mwangu, picha ya sura ya mana yangu ikaanza kunijia kichwani na iukumbuka baadhinya matukio ya furaha aliyo kua akinifanyia

    'Eddy mwanangu jaribu kuishinda hasira yako'

    Nimaneno ya mama, niliyo anza kuyakumbuka vizuei na hili tukio lilitokea kipindi nilipo mpiga mwenzangu nilipo kua chekechea hadi akapoteza maisha akiwa anakimbizwa kupelekwa hospitalini

    'Usiwe mjinga na wewe utakubali vipi kupigwa na mwanaumwe mwenzio'

    Nimanenoya mzee Godwin, alipo kua akinifundisha mbinu za kupigana baada ya kupugwa sana na wezangu nilipo kua darasa la kwanza

    'Mwanaume halisi, hupambana hadi dakika ya mwisho ya uhai wake'

    'Hata ikiwezekana kutoa roho ya mtu wewe toa tu, ili mradi uwe msindi'

    Nimaneno menfine ya mzee Godwin alipokua akinifundisha kadei siku zilivyokua zikienda jambo ambalo alinifanya na mimi ka katili na roho ya kinyama tangu nilipo kua mdogo.

    'Uwe unasamehe saba mara sabini, kwani Mungu anawasamehe wale wote walio mkosea'

    Nimaneno mengine ya mama, alipokua akinifundisha kusoma biblia kabla ya kulala, kwani alipenda kunikuza katika mazingira ya kidini na kumujua Mungu

    'Mimi baba yako, nihodari sana wa kuua pale ninapo kua kwenye uwanya wa vita, risasi yangy moja inapo toka kwenye mdomo wa hii bastola yangu, hua nilazima imuangamize mtu'

    Maneno ya Mzee Godwin yakaendelea kujirudia kwenye akili yangu, siku hii alikua akinifundisha kulenga shabaha kwa kutumia bastola take tukiwa shambani, tulipo kwenda kuwinda nguruwe pori waliokuwa wakila mihogo yetu

    'Jitahidi kumuomba Mungu mwanangu kwani yeye ndio muweza wa kila jambo, usimruhusu shetani akaitawala roho yako'

    Mana alijitahidi kadri ya uwezo wake kunishawushi kuwa kijana mwema. Maumivu makali yaliyo changanyika na uchungu moyoni mwangu, yakaanza kunitawala, hapa ndipo nilipo gundua, maisha yangu yameharibika kwa kufwata maneno ya baba, na kuyaacha maneno ya mama, ambae siku zote alinihasa niwe kijana mwema, mbaya zaidi baba niliyekua nikimuamini kwa kila alicho niambia, mwisho wa siku amekuja kya adui yangu namba moja, hii ni baada ya kugundua kwamba mimi sio mtoto wake, bali ni wapacha mwenzake

       Siku zikasonga mbele nami ndivyo nilivyo zidi kupata unafuu wa machi yangu, pamoja na kifua changu ambacho kilipigwa baadhi ya risasi na rafiki yangu John, ikafika kipindi macho yangu yakapona kabisa kutokana na kutibiwa kwa dawa za kienyeji zilizo nipa uponyaji huu, hapa ndipo nikaruhusiwa kutoka njie ya nyumba ya nyasi niliyo kuwa nimekaa kwa kipindi kirefu kidogo, mazingura ya wanakijiji yakanishangaza kwani mavazi waliyo yavaa, yametengenezwa na ngozi za wanyama, hususani wanaume, vinguo vyao vya chini, ni ngozi ili juu ya vjfua wapo vifua wazi.Nikiwa ninaendelea kuwashangaa wanakijiji hawa, ambao nao pia wanaonekana kunishangaa kwa jinsi nilivyo, jamaa mmoja mwenye misuli mikubwa na mweusi akanifwata na kwaishara akaniomba nimfwate nyuma, sikuwa mbishi nikaanza kumfwata huku tukikatiza kwenye mitaa tofauti ya kijiji hichi chenye nyumba nyingi, zilizo tengenezwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi juu ya mapaa yao.Tukafika kwenye moja ya jumba kubwa lililo zingirwa na wanaume wenye vifuavyenye miraba miine, wengine hasi miraba sita, mikononi mwao wakiwa wameshika mikuki lamoja na ngao, na muda wote wakiwa makini na kila iangiae katika jumba hili, lililo jengwa kwa aina yake

    Tukaingia kwenye moja ya ukumbi mkubwa ambao nikakutana na wasichana wengi walio vifua wazi, hiku sehemu zao za siri zikiwa zimefunikwa kwa vijingozi vidogo, mikononi mwao wameshika mikia ya simba, na farasi ambayo wanaitumia kumpepea kila anaye ingia sehemu hiyo.Jamaa akanionyesha sehemu ya kusimama, akaniacha hapa na kuondoka zake, niliwa ninaendelea kusimama sauti nzito ya mwanaume nikaisikia ikitokea kwenye nyumaa ya pazia lililopo kwenye ukumbi huu ikiniita jina langu, akatoka mwanaume wa makamo, aliye valia ngozi ya chui, mwilini mwake huku kwenye bega la kushoko kukiwa na kichwa cha chui huyo,

    "Unaonekana sasa unaendelea vizuri sio?"

    "Ndio kwa sasa ninaendelea vizuri kiongozi"

    "Safi ila mimi siitwi kiongozi bali ninaitwa chifu Kambute"

    "Chifu KAMBUTE?"

    "Ndio, karibu uje kuketi hapa karibu yangu"

    Nikapiga hatua hadi kwenye kiti chaje kilicho tengenezwa kwa miti migumu sana, nikakaa pembezoni mwa kiti cheke kama alicyo niamuru kufanya.

    "Kwanza pole kwa yaliyo kukuta bwana Eddy"

    "Asante sana chifu Kambute"

    "Vijana wangu walikuokota kwenye moja ya mto, ambao naji yake, yanakwenda kwa mfumo wa maporomoko, ulikutwa ukiwa na hali mbaya walikuchukua na kukuleta hapa nikawaamuru wakujenge kibanda chako, ili waganga wangu waweze kukufanyia huduna hadi leo ukapona"

    "Asante sana chifu Kambute"

    Nilizungumza huku nikipiga magoti chini, kama ishara ya kumshukuru kwa alicho nifanyia. Akaniruhusu ninyanyuke na kukaa kama nilivyo kaa mwanzoni

    "Nilifurahi sana kusiki kwamba unajua kuzungumza kiswahili fasaha, na pia nilifurahi kusikia umetokea Tanzania"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwa nini Chifu Kambete?"

    "Mwaka 1975, baba yangu alinipeleka nchini Tanzania, kwenda kusoma,ambapo alibikabidhi kwa rafiki yake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kipindi hicho alikua ni raisi wa nchi ya Tanzania"

    Ilinibidi nimshangae chifu huyu, kwani ninaimani anaitambua vizuri Tanzania, japo hadi sasa hivi sijijui nipo wapi

    "Kipindi hicho cha makaburu hapa nchini Afrika kusini, hakiwaruhusu watu wengi kupata elimu, na ukibagatika kupata elimu basi ni yamasharti makubwa inayo fundisha utamaduni wao. Baba yangu alinipeleka kule kisuri, kutokana alikua ni chifu katika kijiji hichi cha Kambute, Nilikaa Tanzania kwa Miaka zaidi ya kumi na tano, ambapo, nilibahatika kuzaa na mwanamke mmoja, alikua akiitwa Maria"

    Sauti ya chifu kidogo, ikapungua uzito wake, huku machozi yakianza kunlenga lenga usoni mwake,

    "Maeia alikufa, kipindi mwanangu akiwa na umri wa miaka mitatu, ilinilazimu kurudi naye huku, ambapo nilimkuta baba akiwa katika hali mbaya sana, naye hakukaa sana alidariki dunia kutokana na magonjwa yawakumbayo wazee wengi."

    Kijistori cha chifu kilinisisimua mwili wangu sikujua ni kwanini ameamua kuzungumza maneno mengi kwangu.

    "Pole sana chifu"

    "Nimesha poa"

    Chifu Kambute, hakuendelea kuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kuondoka na kuagiza nibadilishiwe mavazi nivae kama walivyo vaa wao. Japo kwangu ni ngumu sana kuvaa nguzo za wanyama kama nguo ili ilinibidi kufanya hivyo.Taratibu nikaanza kuyazoea mazingira ta watu wa hichi kijiji, chifu akaniomva niingie kwenye jeshi la kijiji hichi, ambapo nikaanza kufundishwa taratibu jinsi ya kutumia silaha za asili katika kupambana, ikiwemo kutumia majambia makali. Nilistushwa na makofi ya mtu yakitokea nyuma yangu, baada ya kufanya vizuri katika mapambano yangu na jamaa mmoja miongoni mwa askari katika eneo la kufundishiwa kupigana

    "Hongera sana"

    Sauti ya msichana huyu haikuwa ngeni sana kwangu, kwani niliisikia kipindi nilipo kua bado ni mgonjwa wa macho. Msichana huyu ni mrefu kiasi, huku umbo lake likia limekaa kimazoezi sana, japo ni mrembo kisura ila mazingira aliyo kiweka ni tofauti sana na mazingira wanayo jiweka wasichana wanao jijua wai niwarembo, msichana huyu akachomoa upanga wake, akashuka kwenye farasi aliye mpanda na kuja katika eneo nililo simama, askari wote wakatuzunguka.

    Gafla msichana huyu akaanza kunishambulia kwa haraka kwa kutumia upanga wake nkali ni mrefu kiasi, ikanilazimu na mimi kujitetea kwa upanga wangu. Kila nilivyojaribu kujikinga na upanga wangu ila msichana huyu anaonekana hodari sana katika kutumia upanga, nikastukua akinipiga mtama na kuanguka chini, huku ncha ya upanga wake ikielekea kwenye koo langu

    "Vipi unahitaji kuendelea kupambana?"

    Aliniuliza huku akihema sana na jasho lilimwagika kwani mapigano tuliyo yafanya nimajali kupita maelezo. Kutokana na kuchoka sana sikuwa na haja ya kuendelea kupambana naye, akanipa mkono na kuninyanyua juu

    "Ninaitwa Lutfia"

    Alijitambulisha jina lake, nikataka kuzungumza jina langu akanizui

    "Unaitwa Eddy, ulisha niambia jina lako"

    "Wewe ndio yule uliye, zungumza nami siku ya kwanza?"

    "Ndio mimi, ila unahitaji kufanya sana mazoezi, ili kuwa askari mzuri"

    Lutfia alizungumza huku akimpanda farasi wake

    "Jioni tutaonana nina mazungumzo na wewe"

    "Wa....."

    Tatari Lutfia alisha ondoka na farasi wake na kuniacha nikiwa nimeshangaa.Nikarudi katika kibanda changu ninacho ishi, nikakaa kwenye kitanda changu cha kamba, huku jasho likinimwagika, nikajichunguza msili wangu nikagundua kuna mabadiliko makubwa sana kwani kifua changu kimekua kikubwa na kugawanyika kama askari wengine, hii nikutokana na mazoezi magunu niliyo patiwa kwa kipindi kirefu tangu afya yangu ilivyo tengemaa

    "Kuna haja ya kuondoka, siwezi kuendelea kuishi kwenye mazingira haya"

    Nilizungumza mwenyewe, nikaletewa chakula kama kawaida ya mama huyu anàye niletea chakula.Nikamaliza kula na kuelekea kwenye mto ambao tunautumia kuoga askari wa kijiji hichi kila ifikapo jioni. Nkawakuta baadhivya askari wakioga, nikavua kinguo cha kingozi changu, amoja na upanga wangu ambao muda wote ninatembea nao, nikaingia kwenye mto na mimi nikaanza kuoga.

    Kwa mbali nikamuona Kutfia akiwa amesimama kwenye moja ya kilima kilichopo karibu na mto huu, nikawatizama askari wote wanao oga nikawaona wapo bize na stori zao, Lutfia akaniita kwa ishara, nikatoka ndani ya mto na kuvaa kingozi changu, nikazuga zuga na kuondoka pasipo askari wezangu kustukia kitu chochote. Nikapandisha hadi eneo alipo Lutfia, akaniomba nilande kwenye farasi wake, sikusita sana, nikapanda na kukaa nyuma yake na kuondoka katika ene hili, akanipeleka kwenye moja ya msitu akamsimamisha farasi wake, sote tukashuka.

    "Nifwate?"

    Tukaingia ndani zaidi ya msitu, ulio tulia sana ukiwa hauna kelele za viumbe wengine zaidi ya kusikia hatua zetu tunazo tembea.

    "Huku ni wapi?"

    Lutfia hakunijibu zaidi ya kugeuka na kunitaza, akapiga hatua hadi sehemu niliyo simama, akanitazama usoni mwangu kwa muda, akaipitisha mikono yake shingoni mwangu, akauleta mdomo wake karibu na mdomo wangu ila nikaukwepesha, mdomo wangu, na taratibu nikaichomoa mikono yake, shingoni mwangu. Nikatoa upanga wangu na kuanza kupiga hatua za taratibu, kuelekea mbele tulipo kua tunakwenda kwani kuna kitu nilihisi.

    Gafla nikastukia kusikia kelele za Lutfia, nikageuka nyuma haraka nikakuta akiwa ameshikwa na mijitu minne yenye nguvu huku sura zao zikiwa zimechorwa, kadri nilivyo zidi kuishangaa ndivyo ilivyo zidi kuongezeka na kufika ya mijtu kumi na saba huku akiwa na marungu makubwa mikononi mwao



    Nikaushika upanga wangu vizuri, nikijiandaa tayari kwa mashambulizi dhidi ya hii mijitu, iliyo tisha. Tararibu ikaanza kunizunguka, huku ikiwa imeshika marungu yao kwa umakini.

    "Mungu nusaidie"

    Nilizungumza kimya kimya huku nikiendelea, kuushikilia upanga wangu ambao una urefu kiasi. Gafla majitu hayo yakaanza kunishambulia, kutokana na uzoefu nilio upata dhidi ya kutumia upanga, haikuniwi ugumu wowote katika kujibu mas uh ambulizi ya kijitu hii, inayo onekana haiña mbinu kabisà za kupambana, kwani ninajikuta nikiimaliza kijinga kwa kuikata vichwa vyao

      Kwa bahati nzuri, Lutfia akapata nafasi ya kujitoa kwenye mikono ya mijitu iliyo mkamata, likawa ni zoezi moja tu, lakuhakikisha tunaishambulia mijitu hii hadi tunaiua yote, kutokana na uhodari wetu wakupambana, tukafanikiwa kuiua yote, jambo lililo tupa uhakika wa sisi kuishi

    "Eddy umechoka?" Lutfia aliniuliza

    "Hapana sijachoka"

    "Tuondoke hili eneo si salama"

    Tukapanda kwenye farasi, na kuindoka katika eneo tulilo kuwa. Tukàfika karibu na kijiji, nikashuka kwenye farasi na kumuacha Lutfia atangulie kududi, ili kuepusha hisia mbaya zitakazo jengwa miongoni mwa wanakijiji, dhidi yetu.

      Nikafika kwenye kijumba changu, sikuingia ndani nikatafuta mti uliopo karibu na kijumba changu nikapanda, kutokana ni usiku sikuhitaji nilale ndani, kwani bado nimapema

    "Nimepakbuka nyumbani" Nilijisemea kimya kimya

    "Nitarudije lakini?”

    "Hakuna jinsi nilazima nitoroke hapa ki....."

    Nikastushwa na mlio mkali wa king'ora kilichopo hapa kijijini, moti mkali kutoka kilipo kijiji, ukaniogopesha na kunifanya nikae kwa umakini, kuchunguza ni nini kinacho endelea, kelele za wamama na watoto zikazidi kurindina kijiji kizima, huku moto ukiendelea kuteketea. Kwa haraka nikashuka juu ya mti, nikaanza kukimbia kuelekea kilipo kijiji, kabla sijafika, nikashuhudia jinsi wanakijiji wanavyo uliwa na watu wenye bunduki, pamoja na mabomo yakurusha kwa mkono

    "Ohhh Mungu wangu!"

    Nilihamaki huku nikiwa, sihui chakufanya. Baadhi ya askari wakijiji, wameanguka chini baada ya kushambuliwa kwa risasi, kitu kiluchozidi kunichanganya ni baada ya kumuona Lutfia akiwa amezingirwa na watu hao wenye bunduki nzito na mara nyingi bunduki hizi hutumika kwenye vita vya mataifa makubwa kama Marekani.

    "Upanga hauto saidia chochote"

    Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kujibanza kwenye mti mkubwa, nikishuhudia jinsi wanakijiji wanavyo patishwa matesona watu hao.

    Mlio mkali wa helcoptar, ukasikika ukitokea mashariki mwa kijiji, nikaichungulia Helcoptar hiyo, nikaishuhudia ikitua taratibu sehemu yenye uwazi, ambapo ndipo walipo kusanywa wanakijiji, pamoja na chifu wao. Askari mmoja kati ya wengi walio kishambulia kijiji, akakimbilia hadi sehemu ilipo Helcoptar, akafungua mlango, wa helcoptar.Akashuka mwanadada mmoja aliye valio nguo nyeusi, kuanzia juu hadi chini, huku kichwa chake akikivisha kofia nyeusi, huku baadhi ya nywele zake akizishusha eneo la uso wake na kufucha jicho moja kama anavyo fanya mwanadada, mwanamuziki Rihana.

    Akashuka jamaa mwengine, ambaye naye amevalia nguo nyeusi, kofia pamoja na miwani nyeusi. Wakapiga hatua hadi, walipo wanakijiji walio wekwa chini ya ulinzi. Wakaanza kuwakagua wanaume wote, walio amrishwa kupiga magoti, huku mikono yao wakiwa wamevishika vichwa vyao. Jamaa huyo akaanza kurusha rusha mikono kama mtu aliye changanyikiwa, baada ya kukagua wanaume wote, akaivua kofia yake na kuitupa chini.

    Nikastuska, baada ya kuiona sura ya mtu huyu, ambaye usoni mwañgu si mgeni sana japo jiña lake, bado halinijii kichwani kisawasawa, akamfwata chifu, aliye pigishwa magoti kwa amri ya wa ajeshi hao. Akaichomoa bastola yake kiunoni na kuielekezea kichwani mwa chifu

    Kutokana na umbali waliopo sikuweza kusikia nimaswali gani anayo muuliza çhifu, anaye kuwa mbishi kujibu, gafla nikamuona Lutfia akimsukuma jamaa huyo aliyekuwa akihitaji kumfyatulia baba yake risasi, kwa jinsi vitendo anavyo vifanya Lutfia, vinaashiria kumuimba jamaa huyo, amuadhibu yeye na si baba yake.

    Jamaa akamtandika Lutfia kichwani, kwa kutumia kitako cha bastola yake, nakumfanya chifu anyanyuke kwa hasira, kabla hajamkabili jamaa huyo, msichana aliye shuka naye kwenye Helcoptar, akafyatua risasi kadhaa zilizo muangusha chifu chini kama gogo kubwa.

    "God...!"

    Niligamaki, huku nikimshuhudia Chifu, anavyo tapatapa chini, akikata roho, askari mmoja wa kijiji akajaribu kunyanyuka, ila akarudishwa chini kwa risasi, alizo pigwa kwenye miguu yake. Jamaa akachukua kipaza sauti na kuanza kuzungumza

    "Natambua upo hapa kijijini, nipo hapa kwa ajili yako, rafiki yangu kipenzi Eddy"

    Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio hukunikijiiza swali, ni kwanini hawa watu wapo kijijini kwa ajili yangu.

    "Hutaki uje tupige stori? Njoo basi rafiki yangu Eddy. John nipo hapa ninakusubiri"

    Hasira ikazidi kuyaongeza kasi mapigo yangu ya moyo, picha kadha kichwani mwangu zikaanza kujirudia kwa kasi, kama mkanda wa video, unao rudishwa nyuma. Picha za kumbukumvu zikasimama, katika tukio la John, kunipiga risasi za kifua baada ya mke wangu Phidaya kujifungua, miguuni mwangu

    "Ohhhh Eddy, hutaki? Basi ngoja niondoke zangu.Ila kabla sija ondoka nina ujumbe kutoka kwa mke wako na mwanao Jimy"

    Maneno ya John yakazidi kunichanganya, sikua na lakufanya kwabi askari wake wapo zaidi ya hamsini na wote wana bunduki mikononi mwao.

    "Mke wako, na mwanao wanakuhitaji rafiki yangu. Ndio maana nikaamua kuja kukutafuta, baada ya kusikia upo hài. Kaka mimi na wewe ni marafiki wa damu. Tafadhalu njoo twende nyumbani, ukamuone Jimy wako"

    Maneno ya John yaliyo jaa ushawishi, wakibinadamu sikuyapa nafasi katika kichwa changu, kwani asinge fanya alicho kifanya kwa wanakijiji wezangu

    "Ohhh ngoja nimpigie simu, umsikie mkeo"

    John akatoa simu yake mfukoni, akaiweka sikioni mwake kwa sekunde kadhaa, kisha ajaisogeza karibu na kipaza sauti chake

    "Mume wangu Eddy, ninakupenda sana.Nimeishi mbali nawe kwa miaka mitatu sasa, ninakuomba urudi nyumbani, mwanao ananisumbua kila siku kusema baba, baba."

    "Nakuomba Eddy wangu, urudi. Ngoja nimsikilizishe mwanao simu. Jimy talk to dady"(....Jimy zungumza na baba)

    "Halloo Dady, where are you? I mis you. Came back home"(Halloo baba, upo wapi? Nimekukumbuka, rudi nyumbani)

    Sauti ya mtoto mdogo ilisikia vizuri masikioni mwangu, jambo lililozidi kunitatiza nakunipa wakati mgumu sana, japo sauti ni yamke wangu Phidaya ila sikufanya maamuzi yoyote kwenye kichwa changu

    "Muambiw baba, umekua wa kwanza darasani"

    Sauti ya Phidaya ilimuamrisha mtoto huyo anaye semekana niwakwangu

    "Dady nimekua first in class"

    Mtoto, alichanganya kiswahili na kingereza, jambo lililo nipa wasisi wa kuhisi kuna kamchezo kanacho endelea katikati yao. John akakata simu na kujikoholesha kidogo

    "Eddy umesikia hiyo. Mke wako, mwanao, wote wanakuhitaji wewe. Njoo twende zetu rafiki yangu"

    John alizungumza huku akitazama kila pande ya eneo walilopo, akitarajia kuniona, tarativu nikajikuta nikikaa chini, huku machozi yakinimwagika. Nikautazama upanga wangu kwa umakini, kisha nikachungulia walipo, nikamuona John akikikamata kitoto kimoja chenye umri wa miaka kama mitatu

    "Eddy mwanao anafanania na huyu"

    John ilizungumza huku akimbembeleza bembeleza mtoto huyo, anaye lia kwa sauti ya juu, hii ni baada ya kutolewa kwenye mikono ya mama yake aliye lazwa chini

    "Eddy muda unakwenda, njoo tuondoke. Sasa hivi ni saa saba usiku. Unasubiri ninj rafiki yangu. Au unataka ukae na hawa watu wako, walio vaa nusu uchi eheees?"

    John aliendelea kuzungumza huku, akizunguka zunguka katika eneo walilopo, mkononi akiwa na mtoto aliye endelea kupaza sauti ya mayowe.

    Gafla John akamgeuza mtoto, kichwa chini, miguu juu, huku akiwa amemshika kwa mkono mmoja, mguu wakulia.

    Kitendo cha John kumshika, mtoto huyo hivyo, kikanikumbusha jinsi Derick alivyo mshika mtoto wangu, niliye zaa na Madam Mery.

    "Eddy hujui ni jinsi gani, ninavyo chukia kupotezewa muda. Huku mijitoto inayo lia kama hii, inavyo zidi kunicchanganya akili yangu"

    John akakitupa kipaza sauti chini, pasipo kua na huruma, akachomoa bastola yake na kuzimimina risasi kadhaa tumboni mwa mtoto huyo, na kumtupa chini kama mzoga

    "Fuc......"

    Nilizidi kupandwa na hasira iliyo ufanya mwili wangu wote kutetemeka. Vilio vya wamama vikazidi kuutesa moyo wangu, nikamuona John akikiokota kipaza sauti, huku akicheka kwa dharau

    "Ohhhhh Eddy, naondoka, ila hili ulilo liona linakwenda kumkuta mwanao Jimy"

    John akamrushia kipaza sauti, msichana aliye kuja naye, naye akamkabidhi askari mwengine kipaza sauti. Wakaondoka, wakaingia kwenye Helcoptar yao na kuondoka.

    Askari wao wakaondoka kwa umakini, na kutokomea pasipo julikana.

    Nikasubiri kwa muda, wa nusu saa, ndipo taratibu nilipo anza kutembea walipo wanakijiji wanao omboleza kwa machungu, vifo vya wapendwa wao. Kila mwanakijiji anaye niona, ananitazama kwa macho makali yaliyo jaa jazba.

    Macho yangu yakakutana na macho ya Lutfia, aliye pembeni ya mwili wa baba yake, aliye fariki dunia. Nikatembea kwa haraka hadi ulipo mwili wa chifu, kabla sijaugusa, nikastukia, Lutfia akinisukuma kwa nguvu na, nikaanguka chini

    "Eddy, hupaswi kuugusa mwili wa baba yangu. Haya yote wewe ndio chanzo. Umekisababishia kijiji changu matatizo...."

    "Lutfia ila si mimi niliye waua hawa wote"

    "Wewe, ni chanzo Eddy, nakuanzi sasa hivi ninakuomba uondoke kijijini kwangu, la sivyo utakwenda kuungana na kifo cha hawa wote walio tangulia mbele za haki"

    Lutfia alizungumza kwa msisitizo, huku machozi yakimwagika, ñà kifua chake kikipanda na kushuka kwa kasi akionekana kujawa na jazba kubwa dhidi yangu.



    "Lu....."

    "Eddy nimesema ondoka"

    Lutfia alizungumza kwa kupaza sauti, hadi wanakijiji wote wakatutizama sisi, natambua hawajui lugha tunayo izungumza ila, matendo yanaashiria kwamba Lutfia hataki kuniona mbele ya macho yake. Nikamtazama Chifu, huku machozi yakinilenga lenga. Midomo ya Lutfia, inatetemeka kwa kufura kwa hasira, uzuri wake alio kua nao umetoweka kabisa. Taratibu nikauweka chini upanga wangu, kisha nikasimama na kutazamana na Lutfia aliye nitumbulia mimacho kiasi cha kunifanya nimuogope. Kila mwana kijiji ninaye mtazama sura yake imetawaliwa na majonzi mengi, wamama wengine wakiwa wanalia kwa uchungu huku wakigara gara kwenye vumbi, wakionyesha ni jinsi gàni, walivyo umizwa na tukio zima lililo tokea muda mchache ulio pita.

    Sikumuangali mtu yoyote usoni zaidi ya kugeuka na kuanza kutembea kwa mwendo wa haraka, ulio changanyika na hasira kali. Nikafika kwenye kijumba changu, nikachukua kibuyu changu, ninacho hifadhia maji ya kunywa, nikachukua na kisu changu cha akiba, na kutoka nje ya kibanda changu. Nikautizama mji jinsi unavyo teketea kwa moto, hasira dhidi ya John ikazi kunipanda. Nikaanzà kutokomea msituni, nikijaribu kutafuta njia ya kutokea kwenye kijiji hiki, kutokana na hasira pamoja na uchungu ulio nitawala moyoni mwangu, nikajikuta nikitembea hadi kuna pambazuka, pasipo kuchoka.

      Nikafika kwenye moja ya mlima mrefu, ulio zingirwa na miti mingi, kwa mbali nikaanza kusikia mngurumo wa gari, likipita eneo la karibu na mlima huu, kwa haraka nikashuka, nikiufwatisha mgurumo huo ni wapi unapo tokea. Kwabahati nzuri nikaiona barabara ya lami, iliyo chongwa kwenye mlima huu. Matunaini ya kufika ninapo pahitaji yakaanza kunijia moyoni mwangu.

    Nikasimama, katikati ya barabara. Sikuona aibu kwa jinsi nilivyo vaa nusu uchi, huku sehemu zangu za siri, zikiwa nimezifunika na ngozi ya chui. Mlio wa gari sikuusikia tena, kwani ninahisi lilisha pita, kabla ya mimi kuifikia barabara. Nikaendemea kuzunguka zunguka maeneo ya barabara, nikijaribu kusubiria kama ninaweza kupata usafiri.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gafla gari moja ndogo, likapita kwa kasi pasipo kufanikiwa kulipungia mkono, ila halikufika mbali sana, likasimama. Dereva wa gari hilo akaanza kulirudisha nyuma kwa kasi, hadi sehemu nilipo simama. Kioo cha upande wa dereva kikashuka, nikamuona mvulana mmija wa kizungu, àkiwa na mchumba wake, wakabaki wakinishangaa kwa jinsi nilivyo vaa.

    Binti wa kizungu akatoa kamera yake, aina ya digital, na kuanza kunipiga picha, huku akiwa amesimama upande wa lili wa gari, nikaanza kuwafwata taratibu

    "Casey get in the car"(Casey ingia ndani ya gari)

    Mvulana huyu, alizungumza kwa haraka baada ya mimi kilikaribia gari lao, kabla hajafanya chochote, nikawahi kuingiza mkono kupitia upenyo wa kioo alicho kifungua. Nikachomoa funguo ya gari lao, nakulifanya lizime. Jamaa akashuka, huku akiwa amekasirika, akajaribu kunirukia, ila nikamuwahi kumtuliza kwa ngumi ya shingo iliyo muangusha chini na kuzimia hapo hapo.

    Msichana akajaribu, kukimbia ila nikamuwahi na kumdaka, nikambeba begani na kumrudisha ndani ya gari. Nikachomoa kisu changu na kumuwekea kooni mwake huku kidole changu kimoja kikimpa ishara ya kukaa kimya la sivyo nitamkata kichwa. Nikaufunga mlango wake, ña kuzunguka upande wa pili, sehemu alipo anguka mpenzi wake. Kwa haraka nikamvua nguo mpenzi wake, na kuzivaa mimi japo hazinitoshi sana ila nikazilazimisha kukaa mwilini mwangu.

    Nikachukua soksi za jamaa, na kumkandamiza nazo mdomoni, kisha nikamnyanua na kufungua, uoande wa pili wa gari. Kwa bahati nzuri nikakuta kamba, kwa haraka nikamfunga miguuni na mikononi. Kisha nikamuwena vizuri nyuma ya gari, hii yenye viandishi vidogo vilivyo andikwa Verosa, kisha nikafunga, nikarudi alipo mpenzi wake.

    Nikamkuta akihangaika na simu yake, akijaribu kupiga namba anazo zijua yeye, kwa bahati mbaya, maeneo tuliyopo hakuna mawasiliano.

    Nikampokonya simu yake na kuiweka mfukoni mwangu

    "Ukijaribu kufanya ujinga wowote, nitakuu"

    Nilizungumza kwa sauti ya ukali nikitumia lugha ya kingereza, jambo lililo mfanya binti huyo kushangaa, kwani nahisi alijua kwamba mimi ni mtu misiye jua lugha yoyote zaidi ya lugha ya jamii niliyo tokea

    Nikawasha gari na kuondoka, huku mara kwa mara niki muamrisha binti huyu kunielekeza barabara ya kufika kwenye mji wowote. Mwendo wa karibia masaa tisa, tukafika kwenye moja ya mji wenye nyumba, nyingi sana zilizo tengenezwa kwa mbao

    "Hapa ni wapi?"

    "Soweto"

    Casey alinijibu kwa kifupi huku, akiwa amenuna, kwani hajafurahishwa na uwepo wangu mimi, ndani ya gari hili. Nikasimamisha gari nje ya baa moja, iliyo tulia sana,

    "Mbona umesimamisha gari?"

    "Nahisi njaa, nahitaji kula, nipatie pesa"

    Casey akanitazama kwa woga, taratibu akaingiza mkono wake kwenye, mfuko wa suruali aliyo ivaa, akatoa noti moja ya dola mia na kunikabidhi, nikafungua mlango, kabla sijashuka, nikamgeukia Casey.

    "Shuka ndani ya gari, tuongozane"

    Casey hakuwa na kipingamizi zaidi yakushuka kwenye gari, tukaingia ndani ya baa hii kwa bahati nzuri tukakuta, sehemu wanauza chakula

    "Wewe unaitwa nani?"

    Casey aliniuliza kwa sauti ya chini, huku tukiendelea kukisubiria chakula tulicho kiagiza

    "Eddy"

    "Una jina kama la mchumba wangu"

    "Yupi, huyo niliye mfungia kwenye buti ya gari?"

    "Hapana, huyo ni kaka yangu, mpenzi wangu yupo hospitali"

    "Anaumwa na nini?"

    "Alishambuliwa na majambazi, wiki moja iliyo pita"

    "Ohoo pole saña, ila hali yake inaendeleaje?"

    "Sio nzuri, kwani yupo chini ya uangalizi wa madaktari, kwani alipigwa risasi nne za kifua, alipokua anapeleka pesa benki"

    Casey alizungumza kwa sauti yaunyonge huku kwambali nachozi yakimlenga lenga, tukachukua chakula tulicho kiagiza na vinywaji, tukarudi kwenye gari

    "Eddy nakuomba kitu kimoja"

    "Kitu gani?"

    "Ninakuomba umfuñgulie kaka yangu, nahisi atakuwa anajihisi njaa"

    Casey aliniomba kwa utaratibu, nikamtazama kwa umakini, machoni mwake

    Nikamkabidhi mfuko wa chakula nilicho kishika, nikazunguka nyuma ya gari, nikajifikiria kwa muda kisha nikakishika vizuri kitasa cha kufungulia buti ya gari.

    Kabla sijafungua, gari ya polisi, ikasimama nyuma yangu, jambo lililo nifanya nisitishe zoezi, nikaanza kuondoka, nyuma ya gari

    "Hei kijana"

    Sauti ya askari mmoja ikaniita, nikageuka kwa kujiamini, na kuwatazama askari wawili walio simama mbele ya gari lao, dogo linalo endana na gari ninalo liendesha.

    "Njoo"

    Nikapiga hatua kurudi walipo, askari hawa walio zichomeka bastola zao viunoni mwao

    "Fungua, buti ya gari. Tunahitaji kukagua gari yako"

    Alizungumza askari mmoja huku akinifwata sehemu bilipo simama, nikaanza kuchanganyikiwa baada ya Casey kushuka ndani ya gari na kuja tulipo

    "Ofisaa"

    Casey alimuita askari mmoja, aliye simama akitutiza, Casey akanitazama kwa macho makali, jambo lililo wafanya askari hao kuipeleka mikono yao kwenye bastola zao walizo zichomeka viunoni.



    Nikataka kurudi nyuma, ila nikajikuta miguu ikipata uzito wakutekeleza azma yangu ya kurudi nyuma. Askari wakazichomoa bastola zao, kwa haraka wakatusukuma mimi na Casey, tukaanguka chini.

    "Laleni chini"

    Askari mmoja alizungumza kwa sauti ya juu huku akianza kutambaa, wakielekea ilipo baa, tuliyo toka muda mchache. Milio ya risasi ikaanza kurindima, ndani ya baa, nikatazama vizuri, nikashuhudia kundi la majambazi walio valia makofia meusi vichwani mwao, yaliyo bakisha sehemu za macho yao, wakiwamrishà watu waliomo ndani ya baa hiyo kutoa walivyo navyo.

    Ikawa kama mkanda wa kuigiza, kwani majambazi hao walianza kuwashambulia askari hao walio kua wakitambaa, mmoja wao, akapigwa risasi ya kichwa na mmoja wa majambazi, na ukawa ndio mwisho wa askari huyo, aliyetoka kuzungumza na Casey muda mchache ulio pita.

    Nikamtazama Casey, na kumuona akijaribu kunyanyua kichwa chake kuchungulia upande walipo majambazi hao, na akaanza kupiga mayowe yaliyo wafanya majambazi kutazama eneo lilipo gari, letu.

    "Weka kichwa chako chini, Casey"

    Nilizungumza kwa sauti ya ukali, huku nikibingiria kwa haraka, na kumuwahi Casey aliyekuwa ameshikwa na butwaa, akimshuhudia askari aliye zungumza naye, jinsi ubongo wake ulio changanyikana na damu, ulivyo sambaa chini.

    "Heiii, nisikilize wewe"

    Nilizungumza huku nikimpiga piga Casey mashamvuni, ili arudi katika hali yake ya kawaida.

    "Eheeee!"

    Alizungumza huku akiwa amenitumbulia mimacho, asijue nini azungumze. Gari yetu ikaanza kushambuliwa kwa risasi na majambazi hao, huku sisi tukiwa upande wa pili wa gari hili. Nikatazama upande lilipo gari la polisi, nikachungulia kupitia durisha la gari, tulilopo nikao majambazi wawili wakilisogelea gari letu huku wakiendea kuzimimina risasi kwenye upande wa pili wa gari letu.

    "Hei Casey, unaweza kutambaa?"

    "Heee"

    "Unaweza kutambaa?"

    Casey akanijibu kwa kutingisha kichwa kwamba anaweza.

    "Nakuomba, utambae uende lilipo gari lapolisi"

    "Eddy una akili kweli wewe, unataka na mimi nife kama hao polisi?"

    Casey alizungumza kwa sauti ya kuto kujiamini huku akinitazama usoni, huku jasho likimtiririka.

    "Fanya kama nilivyo zungumza"

    Nilizungumza, huku nikiwachunguli majambazi hao, wanao zidi kulisogelea gari letu lilipo.

    Casey hakuwa na uchaguzi mwengine zaidi yakufanya nilivyo muambia kufanya. Kwa haraka akatambaa hadi lilipo gari la polisi na kujibanza huku akihema sana, macho yake yote yakawa kwangu. Ukimya ukatawala gafla, kwani majambazi waliacha kupiga risasi, nikachungulia nikawakuta wakinong'onezana, mmoja akaanza kunyata taratibu, akilisogelea gari nililopo, huku bunduki yake akiwa ameiishika vizuri mkononi mwake.

    Nikakichomoa kisu changu, na kukishika kwa mkono wangu wa kulia. Taratibu nikanza kuhesabu moja mpaka tatu, kitendo cha jambazi huyo kuufungua mlango wa gari, upande wa dereva, ikawa ninafasi yangu kufanya shambulizi la kukirusha kisu changu kwa nguvu zangu zote, kisu changu

    kikatua shingoni mwa jambazi aliye simama, hatua chache toka gàri lilipo, akatoa ukelele ulio mduwaza mwezake, aliye karibu yangu. Kwa haraka nikapanda juu ya gari, nikajizungusha kwa kasi, kwakuitumia miguu yangu, na kumpiga kichwani jambazi, akaanguka chini. Nikawahi kuochomoa bastola iliyo kiunoni mwake, na kumpiga risasi kadhaa za tumbo.

      Nikakimbia kwa haraka, hadi kwenye moja ya gari, lililopo kwenye maegesho ya hapa baa, nikajibanza kutazama ni kitu gani kinacho endelea ndani ya baa. Jambazi mmoja akajitokeza mlangoni kuwachungulia wezake, alipo waona wamelala chini, akarudi ndani kwa haraka, sekunde kadhaa wakatoka majambazi wanne, wakaanza kufyatua risasi zao ovyo, pasipo kujua muhusika mkuu wa mauaji ya wezao wawili yupo wapi.

    Sikuhitaji kufanya makosa, ambayo yangenigharimu maisha yangu. Kwa haraka nikanza kufyatua risasi zilizo wapeleka chini, majambazi wote wanne, Nikatoa magazini ya bastola, nikskuta imebakiwa na risasi nne tu.

    "Shitii"

    Nilizungumza huku nikiirudisha kwa harana Magazine hiyo ndani ya bastola, nikanyanyuka kwa umakini, nikaanza kukimbilia katika mlango wa kuingilia baa.

    Nikachungulia na kuwakuta watu wote wakiwa wapo chini ya ulinzi mlali wa majambazi sita waliomo ndani ya baa hii, iliyo kusanya wateja wengi.

    Jambazi mmoja, akajisumu kutoka nje, nikamrukia kwa nyuma na kumkaba kabali, huku nikimvuta pembeni kabisa ya mlango. Taratibu jambazi huyu akaanza kuiaga dunia, kwa nguvu zangu zote nikaivunja shingo yake.

    "Nisalimie huko uendapo"

    Nikamlaza chini, taratibu nikachukua bunduki yake àina ya 'Short Gun', Nikamvua jaketi lakuzuia risasi alilo livaa, nikaanza kushangaa baada ya kuguñdua jambazi huyu ni mwanamke.

      Nikalivua kofia lililopo kichwani mwake, sikuamini macho yangu, kwani ni binti mdogo sasa, jinsi anavyo onekàña usoni mwake.

    "Umekosa nini, binti mzuri kama wewe?"

    Nilizungumza huku nikilivaa jaketi la kuzuia risasi. Kazi ikawa ni moja tu, kuhakikisha ninawamaliza mambazi wote. Haikuwa ngumu kwangu, kwani ndani ya dakika kadhaa nikafanikiwa kuwaua majambazi wote ndani ya baa hii. Mtu mmoja akaanza kupiga makofi, mwenzake wa pembeni naye akafanya hivyo, watu wote waliomo ndani ya baa wakaaendelea kunipigia makofi kwa kazi nzuri niliyo ifanya.

    "Asanteni"

    Nilizungumza, kwa kizulu jambo lililo zidi kuwafurahisha, walio na simu zao wakawa na kazi ya kunipiga picha, huku wengine wakichukua video. Casey akanifwata na kunikumbatia, huku akitokwa na machozi

    "Vipi?"

    Nilimuuluza kwa wasiwasi, huku kitu cha kwanza kukifikiria kichwani mwake ni kaka take, niliye muacha ndani ya buti ya gari lililo shambuliwa vibaya kwa risasi.

    "Umeyaokoa maisha yangu"

    Casey alizungumza huku akiendelea kulia

    "Casey tuondoke"

    Sauti ya kaka yake ilisikika, na kutufanya sote tutizame mlangoni na kumkuta àkiwa amesima, huku akiwa na nguo ya ndani tu. Akajistukia mwenyewe baada ya watu wote, kumshangaa.

    "Naweza kupiga simu?"

    Casey alimuuliza mmoja wa wahudumu aliye valia sare kama wahudumu wengine

    "Ndio"

    Casey akaonyeshwa simu iliyo kwenye moja ya ukuta ndani ya hii baa, akaniachia na kwenda kupiga simu, baada ya kumaliza akarudi nilipo simama

    "Nimempigia simu baba, atafika muda si mrefu"

    Ving'ora vya gari za polisi vikafika katika eneo la tukio

    "Kumbe hawa nao hawana tofauti na wabongo"

    Nilijisemea kimoyo moyo, huku nikiwatazama askari hawa wakiingia kwa mbwembwe ndabi ya baa hii huku, wakiwa na bunduki mikoni mwao

    "Weka silaha yako chini"

    Askari mmoja aliniamrisha huku, wakinielekezea bunduki zao.

    Nikashangaa wazee wawili wakisimama mbele yangu huku, mikononi mwao wakiwa wameshika chupa za bia.

    "Nyinyi muda wote mulikua wapi? Huyu kijana yeye ndio aliye waua majambazi wotw hawa, bila aibu munakuja sasa hivi"

    "Kwanza hamshangai, jinsu tulivyo mzingira huyu kijana, munadhani ni jambazi?"

    Wazee hawa walipokezana kuwatandika maswali askari hawa, walio baki wakibabaika wasijue nini chakuwajibu wananchi hawa waliopo ndani ya hii baa. Askari wakaachana na mimi, wakaanza kushuhulika na miili ya majambazi hao. Kundi kubwa la waandishi wa habari walio kuja baada ya askari kufika, wakaanza kunihoji naswali ambayo sikuyajibu hata moja.

    "Eddy baba yangu amekuja"

    Casey alizungumza huku, akinishika mkono na kutoka ndani ya baa. Nijakuta gari nne , nyeusi zinazo fanana, aina ya GVC, zika zimejipanga pembeni, huku zikiwa na vijibendera vidogo vya marekani. Walimzi wapatao kumi, walio valia suti nyeusi, pamoja na miwani nyeusi, wakashuka kwenye magari hayo. Kaka yake Casey akaongoza zilipo gari hizo, huku mkononi mwake akiwa ameshika kamera ya Casey, akashuka mzee mmoja mwenye mvi kichwani mwake.

    "Eddy yule ni baba yangu"

    Casey alizungumza huku akiendelea kunishika mkono nielekee zilipo gari hizo.

    "Ngoja kwanza, siwezi kwenda kwa baba yako nikiwa kwenye halii hii"

    "Wewe twende baba yangu hana tatizo"

    Casey alizungumza huku akiendelea kunivuta, tukafika zilipo gari zao, akakumbatiana na baba take.

    "Baba, huyu ni shujaa aliye yaokoa maisha yangu. Anaitwa Eddy"

    "Eddy huyu ni baba yangu, ni balozi wa Marekani, hapa Afrika kusini"

    Nikampa mkono, baba Casey naye akaupokea wa kwangu huku akiachia tabasamu pana.

    "Asantw kijana kwa kazi nzuri uliyo ifanya"

    "Asante mzee"

    Casey akamuomba baba yake niweze kujumuika nao kwenda wanapo ishi, ikawalazimu walunzi kunikagua, mwili wangu kamakuna kitu kinaweza kuwadhuru. Wakachukua bastola yangu, wakaniruhusu kuingia ndani ya gari.

      Sikupanda gari moja na Casey na baba yàke, gari nililo panda likari wawili walio kaa siti ya mbele mmoja akiwa ni dereva. Kwangu ikawa kama bahati kukutana na balozi huyu wa Marekani. Japo mama yangu ni waziri wa nchini Tanzania, ila sikuweza kubahatika kukutana ni viongozi wa nchi kubwa kama Marekani. Katika siti niliyo kaa, nyuma ya siti ya dereva kuna Tv ndogo inayo onyesha, vipindi mbalimbali. Matangazo ya kituo cha television kinacgo itwa ENEWS, kikaanza kuonyesha tukio la majambazi walio kufa, huku ikisadikika kundi hilo la majambazi lilikuwa likitafutwa na jeshi la polisi la Afrika kusini, zaidi ya miaka mitano sasa, pasipo mafanikio.

    'NI MTU MMOJA TU, AMEWEZA KULISAMBARATISHA KUNDI HILO HARAMU'

    Nimaneno ya mtangazaji wa taarifa hiyo, huku picha za video zikinionyesha, walivyo kua wakinihoji.

    "Wewe ni askari?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mlinzi mmoja aliniuliza, pasipo kugeuka nyuma kunitazama

    "Hapana"

    "Umewezaje kutumia silaha?"

    "Nilifundishwa na baba yangu, yeye alikua ni mwanajeshi"

    "Yupo wapi?"

    "Amesha kufa"

    Nilidanganya, huku nikiangalia saa ndogo iliyopo pembezoni mwa dereva, ikionyesha ni saa sita usiku. Nikageza shingo yangu kutazama pembezoni mwa barabara, ambapo kuna bonde kubwa na endapo dereva akikosea basi tukianguka, huko bondeni tutakua tutasagika sagika bibaya,na isitoshe gari zote zipo kwenye mwendo kasi sawa kwa uzoefu wangu, spidi wanayo tembelea ni zaidi ya spidi mita mia moja. Matone matone ya mvua yakaanza kutotesha vioo vya gari letu tulilo panda, ambalo ni lapili kutokà mbele, kati ya msafata wa magari manne yaliyo ongozana. Kitu ninacho wasifu madereva hawa, ni utaalamu wao kukunja kona, bila kupunguza mwendo wa magari yao, zilizopo kwenye hii bararaba iliyo chogwa kitaalamu, pembezoni mwa mlima ninao weza kuufanan uliopo mkoani Iriñga ni Tanzania.

    Nikiendelea kuitadhimini barabara hii, gafla nikastukia kuliona gari la mbele yetu, nikinyanyuliwa hewani na kitu kama bomu kutegwa, likazunguka hewani mara kadhaa na kutua chini, kitendo kilicho mfanya dereva wetu kufunga breki za gafla, zilizo lifanya gari kuserereka na kuligonga gari lililo anguka na kulisukumia bondeni, kwenye korongo refu, huku matairi ya mbele ya gari letu yakianza kutangulia kwenye korongo, huku ya nyuma yakijitahidi kubaki barabarani.



    Macho yangu yote, yakahamia kwenye gari inayo kuka nyuma yetu kwa kasi kubwa, huku dereva wake akijitahidi kufunga breki zake, akitumia juhudi zake zote

    Nikajiluta nikiyafunga macho yangu, kwani kitu kinacho fwata sekunde chache, ni dereva huyo, kutusindikiza kwenye korongo kama alivyo fanya dereva wetu, kwenye gari lilil kua mbele yetu.

    Dakika kama mbili, hivi niliendelea kusikilizia ni nini kitatokea, kwetubila haikuwa hivyo. Mwanga mkali wa taa za gari lililo kua nyuma yetu, ukaendelea kunipiga machoni, ni sentimita chache sana, toka lilipo simama gari lililopo nyuma yetu, huku gari letu, likianza kunesa taratibu.

    "Tutulie hivi hivi"

    Dereva alizungumza huku akihema sana, askari walio kwenye magari ya nyuma wakashuka kwa haraka, kwenye magari yao, wakaja nyuma ya gari letu na kuanza kujitahidi kulivuta kwa nyuma. Kutokana na uzito wa gari ikawa ni kazi ngumu sana kwao kulivuta. Ikawalazimu kulishikilia na kutuomba tushuke haraka.

    Sikutaka nipoteze muda, nikaufungua mlango wa nyuma katika siti niliyo kaa na kutoka nje haraka iwezekanavyo, huku walinzi nilio kua nao ndani ya gari wakitokea kupitia mlango nilio pitia mimi.

    Walinzi wakaliachia gari, likaporomoka kwenye korongo. Nikiwa ninatazama huku na kule, nikawaona watu wakiwa juu kidogo ya mlima wakijipanga kwa ajili ya kufanya shambulizi

    "Shitiii"

    Bila hata ya kuomba, nikachomoa bastola moja ya mlizi aliyo ichomeka kiunoni mwake. Nikafyatua risasi mbili kwa jamaa aliye shika bunduki aina ya 'Snaiper' ambayo ni hatari sana, kutokana na uwezo wake mkubwa.

      Mashambulizi yakaanza rasmi, na watu hawa ambao ndio walio tegesha bomu barabarani. Ikawa ni ambushi moja ambayo hakuna aliye itarajia kama inaweza kutokea kwa wakati huu, askari wawili wakapigwa risasi na kufa hapo hapo.

    "Gari la balozi ni lipi?"

    Nilimuuliza mlinzi mmoja, niliye simama naye karibu, tukiendelea kujibu mashambulizi ya wavamizi hawa, ambao wanapig a risasi kama wendawazimu

    "Lile la mwisho"

    "Nilinde"

    Jamaa akaendelea kuwafyatulia majambazi risasi, huku mimi nikikimbia pembezoni mwa kuta ya mlima huu, jambo lililo gumu kwa majambazi kuweza kuniona. Nikafika lilipo gari la balozi, nikamkuta akiwa ameinama kwenye siti yeye pamoja na wanae, wakimuomba Mungu wao

    "Muheshimiwa unaniamini?"

    Nilimuuliza balozi mara baada ya kuingia ndani ya gari na kukaa, katika siti ya dereva.

    "Ndio nakuamini."

    Kutokana gari halikuzimwa, likanirahisishia wepesi wa kufanya jaribio la kumuokoa balozi pamoja na familia yake. Nikaangalia upenyo ulio achwa na gari, lililo simaba barabarani, nikaamini unanitosha kupita.

    Mlinzi akanipa ishara nipite, yeye anaendelea kupambana na wavamizi hawa. Nikafanya kama alivyo agiza, kalilazimisha gari kupita kwenye uwazi wa gari lililopo barabani, chakushukuru Mungu likapita, ikawa kazi ni kwangu kuhakikisha ninasonga mbele.

    Japo kuna risasi kadhaa zilipigwa kwenye gari letu, ila hapakuwa na iliyo adhiri matairi zaidi ya kuvunja vioo vya pembeni. Kwa mwendo kasi wa gari hili, ulinifanya niwe makini kwa kila kona ninayo kunja barabarani.

    "Ohhh Mungu wangu! tunafwatwa nyuma"

    Kaka yake Casey alizumgumza huku, akichungulia kwenye kioo cha nyuma kilicho jaa matundu ya risasi. Sikutaka hata kutazama nyuma kuzihofia kona za papo kwa papo, huku nyengine zikiwa ni kali sana.

    "Wapo wangapi?"

    ”Pikipiki mbili na gari ndogo tatu"

    "Muheshimiwa unaweza kutumia, silaha?"

    "Eheee?"

    Balozi alibabaika kwenye kunijibu swali nililo muuliza. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuongeza mwendo kasi wa gari, ninalo liendesha. Tukafanikiwa kuingia kwenye barabara iliyo nyooka, hapa ndipo nikapata wakati mzuri wa kuwatazama wanao tufwata kupitia kioo changu cha pembeni.

    "Hawa vijana ni kina nani?"

    "Siwajui muheshimiwa"

    Waendesha pikipiki, nikawaona wakilikaribia gari letu, kutokana na mwendo wao mkali. Nikapunguza mwendo taratibu

    "Mbona unapunguza mwendo?"

    Balozi aliniuliza huku akitetemeka, hata sauti yake haikutoka vizuri

    "Najua nini, nafanya"

    Nilimjibu kwa kujiamini, huku macho yangu yote yakiwa kwenye kioo cha pembeni nikiwatazama jinsi majambazi hao wakija kwa kasi, Nikakanyaga breki kwa nguvu zangu zote, huku nikilizungusha gari kwa mtindo wa duara, jambo lililo wafanya waendesha pikipiki hawa kulivaa gari letu, na kila mmoja akarushwa vibaya na kuangukia upande wake wa barabara.

    Kutokana na uhodari wa gari hili, halikuweza kuyumba wala kuzima. Ila kilicho, niogopesha ni jinsi gari ilivyo geuka na kutazama tulipo tokea ambapo kuna gari mbili ndogo zinatufwata, na mbaya zaidi zipo karibu kutufikia.

    Ikanilazimu kulirudisha gari kinyuma nyuma ili nipate, japo nafàsi la kuligeuza, nitakavyo jua mimi.

    Nikiwa ninaendelea kurudi nyuma kwa mwendo wa kasi japo si sana nikaliona, gari tulili liacha sehemu tuliyo vamiwa likaja kwa kasi nyuma ya gari hizi mbili ndogo, zinazo tukimbiza.

    "Ohhh wamelichukua hata hili"

    Nilizungumza huku nikijitahidi kupata nafasi ya kuligeuza gari hili, ila kwa bahati mbaya upande nilio kuawepo mimi kuna gari kubwa la mizigo, likija kaa kasi huku dereva wake akijitahidi kunipigia honi, nimpishe upande wake, lasivyo anatugonga.

      Nikalirudisha kwa haraka upande wa kushoto ambapo ndipo ninapo stahili kupita, dereva wa gari ambaye alikuwa upande mmoja na mimi, nikastukia akigongana uso kwa uso na gari hilo la mizigo, tukio lililo mstusha mwenzake ambaye nipo naye upande mmoja. Akajikuta akifunga breki, bila hata ya kutegemea gari lililo kuwa nyuma yake, likamvaa na yote kwa pamoja yakatoka nje ya baranara huku yakizunguka, na kutimua vumbi jingi, huku vyuma vya magari yao vikisagika ikiashiria kwamba yana gongonga kwenye mawe makubwa yaliyopo pembezoni mwa barabara.

    Nikakanyaga breki, kusimamisha gari. Nikashusha pumzi nyingi, huku nikilitazama vumbi likielea angani.

    "Kila mmoja yupo salama?"

    "Ndio"

    "Ndio"

    "Ndio"

    Kila mmoja alijibu kwa wakati wake, nikatazama upande wa mbele tulipo tokea, sikuona gari lolote likija, saa iliyopo pembeni yangu inaonyesha ni saa kumi na moja alfajiri. Taratibu nikaliemdesha gari hadi, hadi zilipo gari hizi mbili.

    "Bakini ndani ya gari"

    Nilizungumza kwa kujiamini, nikaichukua bastola yangu niliyo kuwa nimeiweka pembeni mwa siti, niliyo kalia. Nikafungua mlango wa gari na kushuka, huku nikiwa makini sana na tayari kwaa lolote litakalo jitokeza mbele yangu.

    Nikafika ilipo gari ndogo, na kumkuta dereva akiwa amelalia mskani wake, ulio mbana maeneo ya kifuani. Nikamchunguza na kugundua bado anahema kwa shida, huku damu zikimtoka puani na mdomoni.

    "Ni...ss..aid..ie"

    Aliniomba msaada huku akinitaza kwa macho yaliyo mtoka. Mithili ya mtu aliye kwabwa na kitu kizito kooni.

    "Nani aliye kutuma?"

    "Nisa....i..die...ni.tamtaj....a"

    Nikaikoki bastola yangu kuziandaa risasi kutoka, kidole changu kimoja kikianza kuivuta traiga, taratibu, huku nikiwa nimemuelekezea bastola kichwani kwake.

    "Nakuuliza kwa mara ya mwisho. Ninani aliye watuma?"

    Jamaa alipo litazama shimo dogo, la kutolea risaai la bastola, akayarudisha macho yake usoni mwangu.

    "J....oh..n"

    Jamaa, alinijibu kwa shida kubwa sana, na kichwa chake kikalegea, akiashiria ameiaga dunia. Kwa hasira nikamsindikiza huko aendapo kwa risasi moja iliyo tua kichwani mwake.

    Nikasikia sauti ya mtu akikohoa kwenye gari, tulilo liacha sehemu ya tukio.

       Nikaanza kutembea kwa umakini, huku bastola yangu nikiishikilia vizuri, nikamkuta yule amlinzi tuliye muacha eneo la tukio, akiwa amekaa chini huku ameliegemea gari, mkono wake mmja akiwa amejishika tumboni mwake, kunapo vuja damu nyingi, sura yake ikiwa imechanika chanika kwa kuchwana na vipande vya vioo vya gari.

    Alipo niona akatabasamu kidogo, huku akikohoa na kumwaga madonge ya damu mdomoni mwake.

    "Muheshimiwa yu..po salama?"

    "Ndio yupo salama"

    Nilimjibu, huku nami nilipiga goti chini, nikijaribu kumtazama ni nini kilicho mpata sehemu ya tumbo.

    "Asante kwa msaada wako, wewe ni mwanaume shujaa."

    Alizungumza huku, akitabasamu na kukohoa juu.

    "Damu nyingi, imenitoka. Suwezi pona"

    Alizumgumza maneno haya baada ya kujaribu, kumpa huduma ya kwanza. Akanishika mkono wangu wa kulia

    "Toa pochi yangu, kwenye......mfuko wa nyuma"

    Nikaitoa pochi, akaniomba niifungue na kitu cha kwanza kukiona na kitambulisho chake chenye jina la George Jr.

    "Fungua, upande wa pili"

    Nikafungua na kukuta, picha mbili moja akiwa mdogo na nyingine akiwa amesimama na msichana aliye nifanya niitumbulie mimacho picha hiyo.

    "Chukua hii chane, naomba umtafute dada yangu anaitwa Victoria, umkabidhi hii cheni."

    George Jr. Alinikabishi cheni aliyokua ameivaa shingoni mwake. Huku taratibu, akianza kuyapepesa macho yake. Akanyayua mkono wake taratibu, huku alitetemeka, akanipigia saluti na kukata roho.

      Taratibu machozi yakaanza kunimwagika, nikayafunika macho yake kwa kupitia kiganja cha mkono wangu wa kulia. Nikageuka nyuma, nikamkuta baloIi akiwa amesimama na watoto wake, huku Casey machozi yakimwagika. Nikanyanyuka taratibu, na kwenda lilipo gari na kuingia. Nikaitazama picha ya George aliyopiga na Victoria. Nikajikuta donge la hasira likinibana kifuani mwangu.

    Nikasikia milio ya helcoptar, nikawasha gari kaa haraka, ila Casey akanikimbilia

    "Eddy tupo, salama hao ni wanajeshi wa Marekani, wanakuja"

    Casey alizumgumza huku, akichungulia dirishani. Helcoptar mbili zikashuka hewani na kusimama, katikati ya barabara. Wakashuka wanajeshi wengi, wenye bunduki mikononi. Balozi akaanza kuzumgumza nao, huku kaka yame Casey, akipewa nguo ajisitiri mwili wake.

    Wakatuchukua, sote wanme na kuondoka huku, Helcoptar nyingine ikibaki, na wanajeshi kadhaa wakiupima pima mwili wa George Jr.

    Tukafika makao, makuu ya jeshi la Marekani lililopo hapa, nchini Afrika kusini. Tukapewa huduma za kwaza ikkwemo vifungua kinywa, kwani hatukupa chakula kwakipindi kirefu. Matumbo yalipo kaa sawa, nikatambulishwa mm wa baadhi ya wakuu wa jeshi. Wengi wao wakanisifu kwa kazi nzuri na pevu, niliyo ifanya.

    Tukapelekwa kwenye moja ya hoteli kubwa, tukiwa chini ya uangalizi mkali wa jeshi. Balozi Brayan Daniel, hakusita kunitambulisha kwa kila rafiki yake ambaye, huku akinimwagia sifa kedekede. Tukakaa hotelini, kwa siku nne, ambapo Balozi Brayan Daniel akaendelea na majukumu yake ya kazi, huku akiniomba niwaliende watoto wake kwa kipkndi kifupi kabla hatujaenda Marekani, kuhudhuria mazishi ya askari walio kumbwa na tukio la uvamizi.

      Mida ya saa sita mchana, ikafika gari katika hoteli tuliyopo, huku akija muwakilishi wa balozi, akituomba twende ofisini kwake, tukakutane na baadhi ya viongozi wa hapa nchini Afrika kusini. Tukajiandaa, kila mmoja akavalia mavazi tuliyo numuliwa siku kadhaa, tumaingia ndani ya gari, huku mimi nikiwa makini kuhakilisha Casey na kaka yake wapo salama salmini.

    Tukafika kwenye ofisi za ubalozi wa Marekani, tukapokelewa vizuri na kupelekwa kwenye ofisi za balozi, ambapo tulimkuta yupo na watu baadhi, wanao onyesha kua ni viongozi. Tukakaa kwenye viti vilivyo andaliwa kwa ajili yetu.

    "Jamani mutatiwia radhi kidogo kwa kuchelewa kufika kwenye halfa hii"

    Sauti ya John, ilisikika kutokea mlangoni, akiingia akiwa ameongozana na Victoria, mpenzi wake.Pasipo kutazama waliopo ndani ya ofisi John na Victoria, wakakaa kwenye viti vyao na kukamilisha idadi ya watu ishirini na tano, tuliomo humu ndani, Nikaivua miwani yangu nyeusi niliyo ivaa, nikamuona John, akilegeza mdomo wake kwa kunishangaa, huku naye Victoria akiinamisha kichwa chini kwa aibu, wasiju nini cha kufanya. Huku nikiwakazia macho yaliyo jaa hasira kali kama Simba.

    Ukimya wa sekunde kadhaa, ukakatiza huku macho yangu nikiyahamisha kutoka kwa John, kwenda kwa Victoria. Swali la kwanza kujiuliza ni kuhusiana na John anahusika kivipo kwenye huu mkutano, hiyo moja mbili anamahusiano gani na balozi wa Marekani bwana Brayan Daniel.

    "Nashukuru kwa kufika kwenu, kwa maana nyinyi ni wachache kati ya wengi nilio tamani wafike hapa."

    Balozi B.Daniel alizungumza huku akiwa amesimama.

    "Lengo langu la kuwaita hapa, ndugu zangu, ni kumtambulisha shujaa wangu, aliye jitolea kuyaokoa maisha yangu na familia yangu.”

    "Huyu ninaye mzungumzia hapa si mwengine bali ni Eddy Godwin."

    Balozi alininyoonyea mkono, watu wote wakapigaiwemo Jonh na Victoria.

    "Japo nimepatwa na pigo, lakuwapoteza vijana wangu, kumi katika shambulio lile, Ila kusema ukweli ni jbo la kumsukuru sana Mungu, kwa kijana Eddy kujitokeza na kuweza kuitetea nafsi yangu. Pasipo kujali yeye ni nani, ila ni kitu kikubwa sana kufanywa na mtu wa kawaida."

    Kila muda ulivyo zidi kwenda, ndivyo nilivyo jikuta nikizidi kupandwa na hasira kali, hata yañayo zungumzwa ndanivya hichi chumba sikuweza kuyasikia hata kdogo.

    Matukio baadhi aliyo yafanya John, yakanza kunisumbua akilini mwangu, taratibu nikajikuta nikitokwa na machozi ya uchungu sana. Casey akaniangalia kwa muda, kwa haraka akanifwata nilipo kaa

    "Eddy una tatizo gani?"

    Watu wote wakabaki wakitutizama mimi na Casey. Mapigo ya moyo hayakusita kunienda mbio hadi nikaanza kujihisi kizungu zungu. Nikaanza kujishangaa, baada ya kuona jinsi matone ya damu yakianza kunitoka puani

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Muiteni dokta"

    Nikajaribu kunyanyuka, ila kizunguzungu kikali, kikaniyumbisha kabla sijaenda chini, Casey aksniwahi, akisaidiana na kaka yake.

    Macho yakaanza kujaa ukungu mwingi ulio nifanya niwaine watu wawili wawili. Nikamuona John, akitabasamu. Huku akinyanyuka kwenye kiti alicho kikalia.

    "Tupeni nafasi, tumuhudumie."

    Sauti za madkari, nilizisikia kama sauti ya kengele zinazo gongwa.

    "Nakufa"

    Nilizungumza kwa sauti ya chini, sana, huku nikizidi kujihisi vibaya.

                   ***

       Nikastuka gafla, kabla sijanyanyuka, nikastukia nikirudishwa chini, kitandani na dada mmoja aliye valia mavazi meupe.

    "Tulia kaka yangu."

    "Nipo wapi?"

    "Hospitali"

    "Kwañi ninaumwa?"

    "Ndio"

    Nikatizama pembeni, nikaona dripu la maji likishusha kiwango cha maji kwenye, mishipa ya mkono wangu wa kushoto, kupitia mrija wake mwembamba ulio unganishwa na sindano yake na kuchomwa kwenye sehemu ya kukunjia mkono.

    "Unajisikiaje?"

    "Vizuri"

    "Basi tulia, dripu hili likiisha, unaweza kuruhusiwa"

    "Litachukua muda gani?"

    "Mmmmm masaa kama mawili hivi, kwani ndio nimekuwekea muda huu"

    Nikajichnguza mwili wangu, na kujikuta nikiwa na mavazi niliyo yavaa, mchana. Saa ya ukutani inaonyesha ni saa moja jioni. Nesi akatoka ndani ya chumba, dakika jadhaa akaingia Casey na kaka yake.

    "Unaendeleaje Eddy?" Çasey alizungunza.

    "Nipo poa"

    "Pole kaka Eddy"

    "Asante Bruño"

    "Baba yupo, na daktari, wanazungumza kuhusiana na tatizo lako"

    "Daktari amesema nina tatizo gani?"

    "Amesema kwamba, una...."

    Bruno akamziba Casey mdomo asizungumze, anacho taka kukisema kwa muda huu.

    "Hapana kaka Eddy, huna tatizo mwaya."

    Nikatabasamu huku nikimtazama, Bruno na Casey, nikatambua kwamba kuna tatizo tu, ila nahisi wameambiwa wasizungumze.

    "Mbona umemziba mwenzako mdomo?"

    "Hapana, anapenda kuongea ongea sana huyu."

    "Si uniaçhe, nizungumze.."

    Bruno akamziba tena mdomo, Casey na kujikuta wakianza kugombaba, kama jawaida yao.

    "Heii jamani acheni kugombana”

    Casey akatoka chumbani kwa hasira na kuubamiza mlango. Bruno akaachia msunyo mkali na kukaa katika sofa lililomo ndani ya hichi chumba.

    "Bruno hivi, mbona unapenda kugombana na Casey?"

    "Ahaa domo lake, lipo wazi sana"

    "Sawa, hivi yule jamaa aliye ingia, baada ya sisi kufika una mfahamu?"

    "Yule ndio nina mfahamu, ni rafiki mkubwa sana wa baba"

    "Tangu lini?"

    "Kivipi yani?"

    "Namaanisha wamejuana lini?"

    "Tangu mwaka jana, tunakuja hapa Afrika kusini, tukitokea Marekani."

    "Ahaaa"

    "Tena yule John, ana roho nzuri sana. Haswa yule mke wake."

    "Chanzo cha baba, kua rafiki na yule John. Walitoa Hotel yao sisi kuishi tangu tunakuja hadi tulipo pewa nyumba, tuliyo andaliwa. Kwani balozi aliye pita kabla ya baba, alifariki kwa ajali ya ndege."

    "Kwa hiyo vitu vyake havikuamishwa, kwenye ñyumba tunayo ishi, sasa hivi. Ikatulazimu kuishi Hotelini, John akajitolea hoteli yake tuishi bure kwa kipindi chote"

    "Ahaaa"

    "Hata ile Hotel tunayo kaa sasa hivi ni ya John na mke wake"

    "Kweli?"

    "Ndio"

    "Kumbe nimatajiri dana ehee?"

    "Ndio nimatajiri sana, ila nasikia kwamba utajiri wao ni wakuridhi, kutoka kwa baba yake Victoria, ambaye kwa sasa ni marehemu"

    Nikastuka, huku nikimtazama Bruno, akili yangu ikaenda moja kwa moja katika tukio walilo lifanya John na Victoria kutaka kumuua baba yangu.

    "Huyo baba yake, Victoria anaitwa nani?"

    "Kwakeli simfahamu, ila nilisikia kwamba baba yake alijinyonga, chumbani kwake. Inasadikika alikuwa na ugonjwa wa kichaa"

    Nikahisi mwili wangu, ukisisimka, kwani John amechukua, kila kitu kwenye maisha yangu. Kuanzia mali za baba yangu. Hadi familia yañgu.

      Muda wa kuruhusiwa, ukawadia. Daktari akaniomba azungumze na mimi. Tukaingia ofisini kwake na kukaa kwenye viti vilivyomo humu ndani.

    "Tumekufanyia uchunguzi wa kina, tukakukuta na matatizo mawili kwenye mwili wako. Endapo hayata fanyiwa uharaja wa matibabu, unaweza kupelekea kifo chako. Bwana Eddy."

    Daktari alizungumza huku akinitazama machoni mwangu. Wasiwasi haukuacha kunitawala usoni nwangu.

    "Ninaumwa na nini Daktari?"

    "Tatizo la kwanza, ni hasira iliyo pitiliza kiwango. Ambayo ikikupanda sana, inapelekea mfumo wako wa mapigo ya moyo kukuenda kasi sana. Moyo unapeleka kasi damu kwenye mishipa mbali mbali mwilini mwako. Na ndipo kuna baadhi ya damu, zinatoka puani mwako."

    "Ukishindwa kujizuia hasira yako, itapelekea mishipa ya damu kupasuka, hapo utakua ni mwisho wako wa kuishi duniani"

    "Tatizo la pili, tumegundua kwamba, unayemelewa na ungonjwa wa Saratani, ya damu."

    Nikahisi mwili mzima ukifa ganzi, kwani sikifikiria kama nitaumwa nà ugonjwa wa Canser, tena ya damu

    "Ila usiwe na wasi, nimezungumza na muheshimiwa, utakwenda kufanyiwa matibabu Marekani. Na saratani itakwenda kupona, kwani ndio ipo kwenye hatua za mwanzoni mwanzoni."

    Daktari akanikabidhi dawa, za kunywa pale nitakapo jihisi vibaya.

    "Siwezi kufa hadi nirudishe, kila kitu alicho kichukua John kutoka mikononi mwangu.”

    Nilizungumza kimoyo moyo huku, nikitoka chumba cha daktari, nikajumuika na balozi, pamoja na wanae kurudi hotelini.

                                                                                                              ***

      Siku mbili, zikapita na hali yangu ikazidi kuimarika. Kila asubuhi nikawa na jukumu la kufanya mazoezi, ili kuuimarisha mwili wangu. Nikiwa nimevalia nguo za mazoezi, raba pamoja na earphone, nikibrudika kwa mziki, kupitia Ipad aliyo nipa Casey, jana usiku. Nikaendelea kukimbia barabanani, huku saa yangu ya mkononi, ikinionyesha ni saa kumi na moja alfajiri.

    Katika barabara ninayo kumbia, hakuna wa watu wengi, zaidi ya mtu mmoja mmoja, ninao kutana nao wakifanya mazoezi kama mimi ya kukimbia.

    Nikamkuta dada mmoja aliye vali, suti ya kijivu, Akionekana kuchanganyikiwa, kwani gari lake analo liendesha, limepata pacha tairi la mbele.

    "Samahani kaka"

    Aliniita baada ya kumpita kidogo, nikavua earphone zangu, na kugeuka kumsikiliza ahahitaji kuzungumza na mimi kitu gani.

    "Ndio"

    "Nakuomba, unisaidie kubadilisha tairi la hili gari."

    Nikamtazama juu hadi chini, pasipo kumjibu chochote. Nilipo ridhika na udadisi wangu, nikamsogelea.

    "Kwani ilikuaje?"

    "Nimekuta tu tairi, likiisha upepo"

    "Toa hilo jengine"

    Akazunguka nyuma ya gari lake kwa haraka, akatoa tairi pamoja navifaa vingine vya kusaidia kubadilishia tairi la gari. Nikaanza kazi ya kulifungua tairi lenye pancha, huku yeye akiwa na kazi ya kunibadilisha kila spana nitakayo muomba anipatie.

    Haikuchukua muda sana, nikamaliza kumfungia tairi lake jipya.

    "Asante sana"

    "Usijali"

    Akafungua mlango wa upande wa dereva, na kutafuta kitu. Kutokana sikuhitaji kulipwa, nikaanza kuondoka babla sijapiga hatua hata sita nikasikia akiniita.

    "Kaka subiri uchukue zawadi yako"

    Nikageuka, sikuamini macho yangu kwani, nikakutana na bastola aliyo ishika huyu dada, akinielekezea mimi

    "Tulia hivyo hivyo, ukijaribu kupiga hatua nitakufumua ubongo wako."

    Alizungumza huku akiwa ameishika, bastola yake kwa mkono mmoja, huku mkono mwingine akiwa na simu.

    "Ninaye hapa"

    Alizungumza kupitia, simu yake. Wala sikujua ànazungumza na nani. Mbaya zaidi siwezi fanya chochote kutokana hii barabara imenyooka sana, na haina sehemu ya kujificha. Gari nne nyeusi, zenye muundo wa gari kama zinazo bebea pesa za mabenki, zikafunga breki katika eneo tulilopo. Wakashuka watu walio valia ñguo nyeusi, makofia meusi yaliyo waficha sura zao, na kubakishs macho yao tu. Kila mmoja mkononi mwake ameshika bundiki, na wote wakanizungu huku wakinitazama kwa umakini.



    Mmmoja wao akatoa amri ya mimi kuiamsha mikono yangu juu, nikatii pasipo kubishana. Akatoa amri nyingine ya mimi kulala chini, hapo ndipo nilipo anza kuleta ubishi, kwani siwezi kukamatika kirahisi.

    Kitendo cha mimi kusogeza mguu nyuma, nikastukia kitu chenye ncha kali kikinichoma mgongoni, kwa haraka nikaupeleka mkono wangu nyuma, kwa ajili ya kukichomoa. Nikakuta ni sindano

    yenye dawa, iliyo anza kuvinyong'onyeza viungo vyangu vya mwili. Taratibunikajikuta nikianza kuishiwa na nguvu. Nikaanguka chini, kila nilipo jaribu kunyanyua hata mkono sikuweza, nikajikuta nikiwatazama watu hao walio nikaribia na kuninyanyua. Nikastukia kitu kizito kikinipiga, kichwani, giza kali likanitawala machoni mwangu.

                ********

    "Eddy.... Eddy"

    Nisauti nyororo, iliyo anza kuisikia taratibu, ikipenya masikioni mwangu. Taratibu nikayafungua macho yangi, nikakutana na sura ya kike, huku kichwa chache kikiwa kimejaa nywele nyingi nyeusi na zilizo ndefu sana.

    Macho yake makubwa kiasi, na yadura kiasi, yaliendelea kunitazama huku akiwa ameniimamia, kutoka katika kitanda nilicho kilala.

    "Karibu tena duniani" Alizungumza huku akiwa ametabasamu.

    "Duniani?"

    "Ndio duniani"

    "Kwani nilikua, sipo duniani?"

    Hakuzungumza chochote zaidi ya kusimama, pembeni ya kitanda nilicho lala.

    "Kwa jina ninaitwa dokta, Agines, nimtaalamu katika maswala ya saikolojia"

    "Ngoja, hapa ni wapi?"

    "Upo Washinton DC, Marekani"

    "Ahaaaa?"

    "Usishangae, ninaimani kwamna unatambua, nitukio gani ulilo lifanya kwa ajili ya hii nchi, nasi tumeamua kukuweka karibu nasi na kukusaidia kwa kila jambo"

    Akafungua pazia, kubwa lililopo kwenye moja ya ukuta, hapa ndipo nilipo anza kuona majengo makubwa yaliyopo katika mji huu, ambapo ndipo yalipo makao makuu ya serikali ya nchi ya Marekani.

    "Tutahakikisha tunakufanyia kila unacho kihitaji"

    Akaniandalia chakula, akaniomba nile.

    "Ukimaliza kula, kuna watu nitahitaji uonane nao"

    "Wakina nani?"

    "Utawaona tuu"

    Nikamaliza kula, akanionyesha bafuni, nikaoga na kurudi kitandani, huku nikiwa nimejifunga taulo.

    "Unaweza kuvaa"

    "Mbele yako?"

    "Kwani kuna tatizo lolote, tambua kwamba mimi nitakuwa pamoja nawe kwakipindi cha siku tisini"

    "Za nini?"

    "Eddy vaa bwana, watu hao wanakusubiri."

    Nikamtazama kwa muda, nikavua taulo, nikachukua nguo moja baada ya nyingine alizo zipanga kwenye kitanda.

    "Umependeza sana"

    "Asante"

    "Upo tayari"

    "Ndio"

    Tukatoka ndani ya chumba, hichi kilicho tengenezwa kwa mfumo wa wakisasa, tukaingia ndani ya lifti na kushuka chini, hapa ndipo nilipo gundua ghorofa tuliyokuwa ni ya hamsini kutoka chini.

    Tukafika chini, kabisa tukaongozana hadi nje ya ghorofa hili, tukakuta gari karibia sita zenye muundo mmoja wa milango sita zikitusubiri sisi.

    Tukaingia kwenye moja ya gari, na gari zote zikaondoka.

    "Tunapo kwenda ni wapi?"

    "Ahaaa utapaona usiwe na wasiwasi"

    Akanipa glasi iliyo jaa whyne

    "Ninaamini unatunia hiki kinywaji?"

    "Ndio"

    Nikaendelea kutazama jinsi mji huu ulivyo jengeka, kwa majengo marefu. Tukafika kwenye mojo ya geti kubwa, gari zote zikaingia kwa pamoja.

    Tukashuka mimi na Agie, tukapokelewa na mdada mmoja aliye valia suti nyeusi. Akatupeleka kwenye moja ya meli, iliyo simama pembezoni mwa bahari

    "Ni nani huyo tunakwenda kuonana naye?"

    "Eddy mbona una haraka, utamuona tu"

    Tukaingia ndani kabisa ya meli hii ya kifahari, kila niliye mtazama alionekana kutabasamu. Wengine wakadiriki kunisalimia, kwafuraha.

    "Tuingue humu chumbani"

    Tukaingia kwenye moja ya chumba kilicho humu ndani ya meli hii. Tukakuta baadi ya watu wanao onekana ni wanamitindo.

    Wakanichukua vipimo vya mwili wangu, wakaanza kunishonea nguo ya mtindo nilio uchangua kati ya mitindo mingi, waliyo nionyesha.

    "Agie mbona, mimi sielewi?"

    "Huelewi nini Eddy?"

    "Mambo yote haya, munanifanyia kwa maana ipi?"

    "Eddy kama nilivyo kuambia, inatupasa kulufanyia kitu kama kukulipa fadhila ya uliyo fanya kwa raia wa Marekani"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hata kama, ila bado haijaniingia akilini!"

    "Kwa nini?"

    "Ni watu wangapi, walikufa kwa ajili ya wamarekani muliwafanyia hivi?"

    "Ndio ila kila mmoja ana bahati na nafasi yake kwenye maisha. Kwahiyo nafasi yako no hii"

    Ndani ya lisaa, nguo niliyo hitaji kushonewa ikawa imekamilika, wakanipa niijaribu, kutokana na uzoefu wao, hawakukosea kitu hata kimoja.

    "Ni muda wakutoka kwenda kukutana na watu nilio, kuahidi utaonana nao"

    Nikashusha pumzi huku nikimtazama Agie, ambaye naye, alibadilisha nguo alizo kuja nazo na kuvalia gauni, refu jekundu.

      Tukatoka tukiwa tumeshikana mikono, sauti yakiume, kupitia kipaza sauti nikaisikia ililitaja jina langu, ukumbi wote ukafura kelele za makofi. Watu walizidi kushangilia huku wakianza kuimba wimbo wa Happy birtday, wakiashiria ni siku yàngu ya kuzaliwa.

    Agie akanipeleka hadi mbele ya ukumvi kwenye sehemu iliyo nyanyuka kidogo. Kwa matatizo yalivyo nizonga, hata siku yangu ya kuzaliwa sikuikumbuka.

    Ukimya ukatawala ndani ya ukumbi, huku watu wakinisubiri nizungumze kitu chochote.

    "Kipindi, nilipo kuzaa, nilitambua kwamba ipo siku utakuja kua mtu muhimu kati ya watu wengi ulimwenguni humu"

    Sauti ya mama, ilinistua, kupitia vipaza sauti vilivyomo humu ndani, nikatazama pande zote za ukumvi ila sikumuona mama.

    "Usipate shida ya kunitafuta, nipo hapa mwanangu"

    Nikamuona mama, akisimama katikati ya watu huku mkononi mwake akiwa ameshika kipaza sauti.

    "Leo maombi yàngu, Mungu ameyasikia. Nilikutafuta kwa miaka mingi mwanangu. Hadi leo nimekuona"

    Mama alizungumza huku akipiga hatua akija mbele nilipo, mashafu ya mama yakaanza kujaa machozi, yanayo mtiririka kutoka machoni mwake.

    "Umekua mwanangu, hadi leo unatimiza miaka ishirini na tato, kweli umekua mwanangu"

    Nikashikwa na kigugumizi hata sikuweza kuzungumza, mama akanikaribia na kunitazama usoni mwangu, nami nikashindwa kuyazuia machozi yangu. Tukajikuta tukikumbatiana kwa pamoja na kuwafanya watu, waliopo ukumbini kupiga makofi

    "Nakupenda sana mwanangu, Eddy"

    Sikutarajia kama ninaweza kukutana na mama yangu, baye nimepotezana naye kwa kipindi kirefu sana

    "NA...KU..PENDA PIA MAMA"

    Nilizungumza huku, machozi yakinimwagika, yakiendana na sauti iliyo jaa kigugumizi. Kati ya watu walio simama ukumbibi, nikamuona Sheila, akipiga makofi huku akimwagikwa na machozi ya furaha



    Taratibu mama akaniachia na kunibusu kwenye paji la uso wangu. Akasimama pembeni yangu nakuniomba nizungumze chochote, kwa watu walio nifanya sasa hivi kuwa na furaha.

    "Siamini, kitu ninacho kiona mbele ya macho yangu."

    Nilizungumza huku nikijifuta machozi yafuraha yanayo nimwagika usoni mwangu.

    "Sina kitu kingine chakuzungumza zaidi ya kusema asanteni, nyinyi nyote. Mulio nikutanisha na familia yangu. Asanteni sana."

    Nikamapa kipaza sauti, muendeshaji wa shughuli hii, mama akaninishika mkono na kunipeleka kwenye moja ya meza, iliyo na kitu kikubwa kilicho funikwa na kitambaa cheupe.

    "Eddy tunakuomba ufunue hicho kitambaa"

    Muongozaji wa shughuli alizungumza nami nikafanya kama alivyo zungumza. Sikuamini kuona keki kubwa, iliyo tengenezwa kwa muonekano wangu.

    Nguo zilizo tengenezwa kwenye, keki hii, ni zile nilizo kua nimezivaa siku nilivyo kua katika mapambano, ya kumuokoa balozi wa marekani na familia yake, huku mkononi nikiwa nimeshika bastola. Wadada wawili walio valia sare nzuri za suti zenye rangi ya 'cream' wakasimama karibu yangu na kuanza kuikata kekii hii, yenye maandishi yaliyo andikwa kwenye kibao cheusi ambacho nacho pia ni keki, yanayo someka

    (Wewe nishujaa wa maisha yangu na familia yangu, hongera kwa siku yako ya kuzaliwa)

    Wakamaliza kukata vioande vya keki, kisha muongoza sherehe akaniomba nianze kumlisha mtu nimpendaye. Nikamuanza mama, kisha nikamuita balozi Brayan, pamoja na familia yake. Nafasi yangu ya mwisho nikamuita Sheila, ambaye katika, ziku alizo pendeza ni leo. Ukumbi wote ukakaa kimya, kusikilizia ni kitu gani ninaweza kukifanya, baada ya Sheila kusimama mbe yangu, akisubiria mimi nimlishe keki. Nikachukua moja ya kipande, nikakiweka mdomoni mwangu, kisha taratibu, nikakipeleka mdomoni mwa Sheila, watu wote waliopo ukumbini, wakatusindikiza kwa kupiga makofi.

    "Nakupenda mume wangu"

    Sheila lizungumza, huku machozi yakiendelea kumbubujika usoni mwake.

    "Ninakupenda pia, mke wangu"

    Tumaendelea, kunyonyana midomo yetu mbele ya mama, pamoja na watu wote walio hudhuria sherehe yangu ya kuzaliwa.

    Mziki wa taratibu ukafunguliwa, kila mtu aliye na mpenzi wake, hakusita kumshika alipo jisikia, nakucheza taratibu. Nikaanza kucheza na Sheila baada ya muda, nikabadilishana na mzee mmoja aliyekuwa akicheza na mama, akahamia kwangu

    "Eheee Eddy mwanangu umekua, mbaba, hadi nakushangaa"

    "Kwa nini mama?"

    "Mara ya mwisho kukuacha ulikuwa kijana mdogo"

    "Ndio hivyo mama"

    "Ehee ulikua wapi kipindi chote, nilikutafuta hadi nikakata tamaa na kujua kwamba umefariki?"

    "Usijali mama, nitakuadisia, ila vipi baba?"

    "Yule shetani!"

    Kwa jinsi mama, alivyo zungumza alinifanya, nitabasamu, kwani alionekana kukerwa sana na mzes Godwin

    "Ndio, huyo huyo Shetani"

    "likamatwa, nakufungwa"

    "Amefungwa wapi?"

    "Ahaa Embu achanana na hizo habari mwanangu, tuendelee kusherekea"

    "Sawa, je kazini umerudi?"

    "Ndio nimerudi kitambo sana, sasa hivi mimi ni waziri mkuu"

    "Kweli mama?"

    "Ndio mwanangu, ila kunakitu kimoja nahitaji ukitekeleze hivi karibuni"

    "Kitu gani mama?"

    "Nahitaji uniletee mkwe, na sihitaji mwanamke mwengine isipo kua Sheila"

    "Sawa mama"

    "Usiseme sawa, nahitaji pia na mjukuu wa kucheza naye, nina miaka hamsini sasa, hata kuitwa bibi, sijaitwa bado"

    "Ila mama, mi.."

    Nikajikuta nikinyamaza gafla, sikutaka kumuambia mama, kama nina mtoto, nimezaa na Phidaya, ila kitu kunacho nifanya nisizungumze, ni kuto kumuoba mwanangu.

    "Ila nini?"

    "Mtoto ni najaliwa ya Mungu"

    Nilibadilisha mada haraka, ili mama asielewe nini kinacho endelea moyoni moyoni mwangu.

    "Ndio hapo muombe, kwa Mungu awajalie, mumpate"

    "Unataka wa kike au wakiume?"

    "Mimi yoyote, ili mradi awe mjukuu wangu"

    Mama akarudi kwa mzee mwenzake, nami nikarudi kwa Sheila, tukaendelea kuburudika ma miziki inayo badilika badilka kila wakati.

    Tukaongozana na Sheila hadi eneo la juu la Meli hii, hapa ndipo nikagundua kwamba meli, inatembea, kwani sehemu tuliyopo sasa, ni katikati ya bahari na magorofa yote sikuyaona, zaidi ya jua linalo zama kwa mbali, nakutengeneza rangi nzuri kama nyekundu kwenye, mawingu.

    Tulibaki kutazamana na Sheila, pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote, kila mmoja, anatafakari kitu cha kuzumgumza kwa wakati huu.

    "Eddy"

    Sheila aliniita kwa sauti ya chini na yaupole.

    "Mmm"

    "Ninakupenda"

    "Ninakupenda pia"

    "Kweli?"

    "Ndio"

    Kwa haraka, Sheila akaniparamia, mwilini mwake, huku mikono yake akiipitisha, shingoni mwangu na kuikutanish nyuma yangu, tukaanza kunyonyana midomo yetu, huku kila mmoja akitoa nihemo ya mahaba. Kila mmoja ana hamu na mwenzake, jambo liito tukuta tukianza kupapasana kila kona ya mwili, huku mikono yangu nikiipeleka kwenye makalio ya Sheila, yaliyo makubwa kiasi na malaini.

    "Eddy stop, stop"

    "Nini?"

    "Hii sehemu si sahihi, twende huku"

    Sheila akanishika mkono na kushuka ngazi, tukaelekea sehemu yenye vyumba, akafungua moja ya chumba, tukaingia ndani. Macho yangu yakanza kukishangaa hichi chumba kwani kwenye madirisha yake mawili, unaona samaki walio chini ya maji.

    "Unashanga nini?"

    "Hichi chumba kipo chini ehee?"

    "Ndio, kipo kwa ajili yetu,"

    Sheila alizunfumza huku akifungua mikanda ya viatu vyake virefu, Sheila akanifwata na kunikumbatia, huku akiendelea kuninyonya mdomo wangu.

    Kwa jinsi mahaba, yalivyo tuchanganya, sote tukaangukia kitandani, na kuendea kutomasana, kila kona ya mwili, huku tukisaidiana, kuvuana nguo, tukabaki kama tulivyo zaliwa, na tukazama kwenye dimbwi zito la mahaba.

    ******

    Safari ya kufika kwenye bandari ya Mombasa, nchini Kenya, ilitugharimu siku kumi na sita, usiku na mchana, kupiti meli hii ya kifahari, yenye huduma za kila aina. Katika kipindi chote cha safari, niliweza kukutana na watu maarufu, wengine nikaingia nao mikataba ya matangazo kwenye makampuni yao mbalimbali, ikiwemo kampuni ta magari aina ya Ford.

    Kwa mikataba niliyo ipata, imeaniingizia kiasi cha pesa zaidi ya milioni thelathini za dola ya kimarekani. Pia ndani ya meli, niliweza kutengeneza matangazo mawili, moja likiwa la mafuta ya nywele kwa ajili ya wanaume, na jengine lilikua ni kwaajili ya kuchangia wahanga wa ugonjwa wa Ebola.

    Tukapanda ndege ya kukodi, hadi uwanja wa CIA uliopo mkoani Arusha. Mama akatangulia Dar es Salam, akatuacha mimi na Sheila, nikimalizia kufanya baadhi ya matangazo niliyo ingia mikataba. Na mengine yalisha anzs kurushwa kwenye baadhi ya vituo vikubwa duniani, kama BBC, SKYSPORT, BEINGSPORT na vinginvyo.

    "Mume wangu kuna simu yako inaita"

    Sheila alizungumza huku, akiwa ameishika simu yangu. Tukiwa kwenye moja ya eneo tulilo panga kumalizia, kipande cha mwisho cha utengenezaji wa video, ya tangazo kwa ajili ya magari ya kampuni ya Ford

    "Nani?"

    "Namba mpya, sijui ya nchi gani?"

    Nikachukua simu yangu na kuipokea na kuiweka sikioni kusikiliza ni nani anaye piga

    "Eddy mimi ni Casey, nimeona tangazo lako yaani, kaka umejitahidi"

    "Asante mdogo wangu, mbona tena namba mpa upo wapi?"

    "Nimerudi Canada kusoma, namalizia muhula wa mwisho"

    "Ahaa sawa, asante"

    "Nilimaliza tuu kaka, kabla sijakwenda Afrika kusini, nitakuja Tanzania nikae kae na wifi"

    "Usijali mdogo wangu, baadaye kidogo kuna kazi naifanya watu wananisubiria mimi tu"

    "Ahaa sawa kaka yangu, ngoja nikuache baadaye"

    "Sawa"

    Nikakata simu na kumrudishia Sheila, mimi nikaingia kwenye gari ninalo fanyia tangazo.

    "Baby simu yako inaita tena"

    "Nani?"

    "Namba ngeni?"

    "Pokea muambie, ninakazi nafanya"

    Nikaendelea kufwata maelekezo, ninayo pewa na muongozaji wa tangazo, nikimuacha Sheila akiendelea na kuzungumza na simu.

    Nikafanikiwa kumaliza, tangazo hili, lililo kua gumu, kidogo kwangu kulifanya. Tukatlrudishwa kwenye hoteli tuliyo fikizia, na dereva wa kampuni hii ya Ford. Tukaingia kwenye chumba chetu, huku nikiwa nimechoka kiasi

    "Eddy mama ameniambia tarehe ya harusi, waliyo panga kwenye kikao?"

    "Tarehe ngapi?"

    "Kumi"

    "Ahaa si wiki mbili zimesalia"

    "Ndio"

    "Wameiharakisha, sana"

    "Kwani tatizo lipo wapi, kwanza hapa nina habari njema kwetu"

    "Habari gani?"

    "Sijaziona siku zangu, nahisi nimenasa tayari"

    "Ina maana una mimba yangu!"

    "Ndio mume wangu, mimba ni yako, kwani hakuna mwengine zaidi yako aliye nigusa mimi"

    Nikamfwata Sheila na kumkumbatia kwa furaha, huku nikimzungusha zungusha hewani na kumsimamisha chini, huku nikimbusu busu mdomoni mwake

    "Ngoja kwanza, baby nahitaji unijibu swali langu?"

    "Uliza tu mke wangu nitakujibu haraka haraka"

    Nilizungumza kwa furaha, kwa huku nikilisubiria kwa hamu swali ka mke wangu mtarajiwa Sheila

    "PHIDAYA NI NANI YAKO?"

    "Eheeee!"

    "Hujanisikia nirudie au?"

    Sheila alizumgumza, huku akinitazama kwa sura iliyo anza kujikunja kwa hasira kali.



    "Ohhh baby, huu sio muda muafaka wa kulizungumzia hilo, tuzungumze juu ya harusi yetu."

    "Eddy nahitaji kulijua hilo, nililo kuuliza"

    "Sheila unanipenda?"

    "Ndio, ninakupenda ndio maana nilikaa, bila ya kuwa na mwanaume nikikusubiria wewe"

    "Ok ninakuomba tuachane na hiyo mada, kinacho paswa ni....."

    "Nikujua Phidaya ni nani kwako"

    Sheila alizungumza huku akiwa ame itumbulia mimacho, kwa mbali machozi yakianza kumlenga lenga. Kitu kilicho anza kunichanfanya ni namna gani amemjua Phidaya.

    "Sipo katika wakati mzuri wa kulizungumzia hilo swala sasa hivi, ninakuomba tuliache"

    "Eddy, Eddy, Eddy"

    Sheila alizungumza, huku aking'ata meno yake, kwahasira huku machozi yakimtiririka mashavuni mwake.

    Akaitoa simu yangu kwenye kipochi chake, akafungua fungua baadhi ya mafaili, na kunigeuzia kwangu.

    "Hii ni nini?"

    Nikaiona picha ya Phidaya, akiwa na mtoto anaye fanana na mimi, ambaye John, alinibia anaitwa Junio

    "Eddy kwa nini, hukua mkweli kwangu, kwa nini uliamua kuzaa na mwanamke mwengine wakati unatambua mimi nipo?"

    Sheila alizungumza huku akiwa ameishika simu yangu, na kunisogezea karibu na uso wangu ili nimuone mtoto huyo, ambaye kila kitu amefanana na mimi. Hata mama akimuona hata kua na haja ya kuuliza huyu ni mtoto wa nani.

    Nikaikwapua simu yangu, kutoka mkononi mwa Sheila, na kukaa kitandani huku nikiendelea kumtazama mwanangu huyu mwenye mvuto wa kila aina.

    "Eddy, ni kosa gani nilikufanyia lakini, hadi ukaamua kunisaliti ehee?"

    "Au kwasababu mimi ni muafrika, ukaona ukazad na huyo muarabu?"

    "Au sikua mwanamke sahahi kwenye maisha yako si ndio?"

    Sheila alizungumza huku akiendelea kulia kwa uchungu, huku akinitazama usoni mwangu. Kwa upande mmoja, nifaraja kumuona mwanangu japo kwa picha ila kwa upanfe mwengine imeanza kuniletea uchungu kwani sikuhitaji mtu yoyote atambue nina mtoto, hadi nitakapo amua mimi kufanya hivyo.

    "Eddy si ninazungumza na wewe, lakini?"

    "Ninakuomba unyamaze"

    "Eddy siwezi kunyamaza, dhamani yangu mimi ipo wapi?"

    "Sheila funga bakuli lako, unataka dhamani gani zaidi ya mimi kukuoa wewe, au unataka nimuue huyu mtoto si ndio?"

    Nilizumgumza kwa kufoka huku nikimtazama Sheila, aliye anza kurudi nyuma baada mimi kunyanyuka kitandani kwa kasi. Sheila alianza kutetemeka, baada ya kugundua nimekasirika, sana.

    "Hii ishu ibaki kuwa mimi na wewe, sihitaji mama atambue sawa?"

    "Kwa nini, hutaki ajue?"

    "Hilo sio ombi, bali ni amri"

    Nilizungumza na kutoka nje, kwenda sehemu ya kupumzikia, ambapo kuna baa kubwa tuu

    "Nikusaidi nini?"

    Dada muhudumu, alizungumza huku akinitazama machoni

    "Una pombe kali?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Aina gani?"

    "Nipe yoyote, ili mradi iwe pombe kali"

    "Nusu glasi, au glasi nzima?"

    "Lete mzinga mzima"

    Dada huyu akanitazama mara mbili mbili, usoni na kuondoka.

    "Hii picha ameitoa wapi huyu mwanamke?"

    Nilijiuliza huku nikiendelea kuitazama picha iliyopo kwenye simu yangu. Nikapata wazo la kuingia kwenye mtandao wa Whatsappp, ila sikuona picha yoyote iliyo ingia kupitia mtandao huo. Nikaingia Viber ila sikuona chochote.

    Muhudumu akaweka mzinga wa pombe kali mezani

    "Usiniwekee glasi wewe nenda nayo"

    Muhudumu akaondoka

    "Wewe dada, ni bei gani?"

    "Huo ni elfu semanini"

    Nikatoa walet mfukoni na kutoa noti kumi za shilingi elfu kumi, nikamakabidhi muhudumu, akanipa asante na kuondoka. Nikaanza kufakamia mafumba ya pombe, iliyo ngumu kumeza kooni mwangu, ila muda mwengine, ikanilazimu kufumba macho ninapo imeza.

    Nikiwa kwenye dimbwi la mawazo, mlio wa simu, yangu ukanistua. Sikujua ni namba gani inayo piga kwa haraka nikaipokea na kuiweka sikioni

    "Eddy umeoa?"

    Nisauti ya Phidaya, ilisikika upande wa pili wa simu, nikajikuta nikipatwa na kigugumizi cha kulijibu swali hilo, baada ya Sheila kukaa kwenye kiti cha karibu yangu.

    "Ngoja nitakupigia"

    Nikakata simu, na kumtazama Sheila aliye kaa mbele yangu.

    "Eddy umeanza lini kunywa?"

    "Kwani vipi?"

    "Nimekuuliza tuu"

    "Ninakuja"

    Nikanyanyuka na kumuacha Sheila peke yake mezani, nikaingia chooni na kuipiga namba aliyo ipiga Phidaya, ikaita kwa muda ikapokelewa

    "Wewe nani?"

    Nilisikia sauti ya mtoto ikizungumza, nikakaa kimya kusikilizia

    "Mama kuna mtu amepiga simu yako, hazungumzi"

    Mtoto huyo niliye amini kwamba ni Junio nilimsikia akizungumza

    "Haloo"

    Nikaisikia sauti ya Phidaya akizungunza

    "Yaa ni mimi Eddy"

    "Najua hilo"

    "Sawa, namba yangu umeitoa wapi?"

    "Hilo sio jukumu lako, ila kitubalicho kifanya huyo mwanamke wako sihakipenda"

    "Amefanya kitu gani?"

    "Ameniita mimi malaya, changudoa ninajipendekeza kwako, ila kitu ambacho nitakifanya hato kuja kusahau"

    Nikajikuta nikishusha pumzi huku nikifikiria nikipi nizungumze.

    "Ila Eddy sina haja ya kukuambia ni wapi tulipo toka, kama kukuua mimi ningekua nimesha kuua nikiwa na kuimbe chako tumboni mwangu"

    "Niliweza kuvumililia kwa kila jambo, ili mradi nisikupotezee wewe. Mimi na mwanangu tunaishi kama watumwa, tunaishi maisha ya shida ya kutanga tanga. Hatuna pakuishi, hatuna pa kula kwa ajili yako."

    "Nimetoroka kwa shida mikononi mwa John, hadi sasa hivi nimekua mwanamke wa kuishi kitumwa kwa ajili yako, hembu fikiria yote niliyo yafanya kwako kuanzia siku ulipo kua hospitalini, hadi siku najifungua mwanao mbele ya macho yako, tena kwa kudhalilika mbele ya watu wengi, ila sikujali hilo nilifanya kwasababu ya kukupenda."

    Maneno ya Phidaya yakaanza kunitoa machozi taratibu huku maumivu makali yakinitawala moyoni mwangu.

    "Leo hii mimi ninaitwa malaya, na huyo mwanamke wake"

    "Phidaya, nakuomba unisamehe, hilo. Upo wapi?"

    "Nipo Somalia, Mogadishu"

    "Upo kwa nani?"

    "Eddy nimekuambia sina sehemu ya kuishi, najishikiza kwa kufanya vibarua vya ndani. Kikubwa kinacho niumiza ni mwanangu, kuishi maisha ya shida tangu nilipo mzaa, hivi unahisi ni lini mwanao ataishi kwa furaha?"

    Phidaya alizungumza pasipo kunipa nafasi yakuzungumza.

    "Eddy ninakuomba usioe, tambua kua ninakupenda sana na mimi nina mwanao. Siku njema"

    Phidaya akakata simu, nikajaribu kupiga simu tena haikupatikana tena.

    Nikajikuta pombe iliyo anza kunichukua, ikaaanza kunititoka kichwani kauli kazaa za Phidaya zikaanza kujirudia rudia kichwani mwangu

    'Eddy usioee.......Kitu nitakacho kifanya hato kuja kusahau'

    Nikatoka chooni na kurudi alipo Sheila, nikakuta akiwa amejiinamia chini

    "Bora umerudi, mama anataka turudi Dar kesho"

    "Poa, twende tukalale"

    ******

    Safari nzima yakurudi Dar es salaam, sikuwa na raha, kila nuda nikajikuta nikimkumbuka Phidaya na mwanangu. Hadi tunafika uwanja wa ndege wa J.K NYERERE, sikuwa na raha kabisa moyoni mwangu japo kila muda nilitabasamu usoni mwangu kumfanya Sheila asielewe ni kitu gani kinacho niumiza moyoni mwangu.

    Tukapokelewa na mama, pamoja na wapambe wake, safari ya mwenda kwenye makazi mapya ya mama ikaanza. Kutokana tunatembea kwa mfumo wa msafara ulio ongozea na gari ya polisi, haikutuchukua muda mwingi barabarani. Tukafika nyumbani na kukuta wana ndugu ambao kipindi cha nyuma sikuwahi kuwaona. Nikatambulishwa kwao, ila sikuhitaji kuwajua sana kwani, kipindi tunamatatizo wao hawakuonekana

    Siku zikazidi kusonga mbele, huku maombi yangu yakimuomba Mungu siku ya ndoa yangu isifike kwani ninahisi itakua ngumu sana. Roho moja, ikawa inahitaji nimuoe Sheila, huku rohi nyingine, ikikataa kabisa kumuoa Sheila, ikinishawishi niende Somalia, kuitafuta famili yangu

    'Baba mwerevu ni hule anayekufa akipigania, familia yake'

    Nimaneno yaliyo jirudia rudia kichwani mwangu.

    **

    Macho yangu yaliyo jaa mwangavu, wakutizama kila pande ya kanisa, yaliendelea kufanya kazi hiyo. Nikazidi kujotahidi kumuangalia kila aliye fika kanidani hapa kuishuhudia ndoa yangu. Sheila aliye pambaa vizuri, anatabasamu kila muda nilimtazama usoni mwake.

    Mchungaji, akaniba nizitoe pete kwa ajilo ya kuziombea, nilafanya hivyo na kumkabidhi

    Akaziombea na kunikabidhi pete moja kwa ajili yakumvisha Sheila, nikamtazama mama yangu aliye valia nguo za dhamani.Akanikonyeza akiniashiria niweze kumvisha Sheila. Ukimya kanisani pote ukatawala, kila mmoja akinisubiria kufanya hilo. Vishindo vya viatu aina ya kokoko, vikaanza kusikika kutokea nyuma, ulipo mlango wa kanisa.

    Ikatulazimu watu wote kugeuka kutazama, ninani anaye ingia kanisani. Nikajikuta nikitamani ardhi ipasuke, ili inimeze. Hakua mwengine, bali ni Phidaya aliye valia viatu vya juu, huku mkono wake wakulia ukiwa umemshika Junio, wakitembea kwa haraka kuja mbele tulipo.

    Miaani nyeusi aliyo ivaa Phidaya, ikawafanya walinzi wa mama kumfwata, ili wamzuie, ila kila aliye mtazama Junio, alijikuta akisita kumgusa Phidaya, kwani we alitambua ni kitu gani kinacho endelea

    "Phi....."

    "Shiiiiii"

    Phidaya alinizuia nisiseme chochote, akasimama hatua chache toka tulipo simama.

    "Junio, yule ndio baba yako, ndio Eddy"

    Sheila mwili mzima, unamtetemeka, Junio akaliga hatua kabla ya kufika nilipo

    "Junio"

    Phidaya aliita na kumfanya mwanae ageuke kumtazama, nikamuona mama akinyanyuka huku akimtazama Junio kwa macho makali yaliyo jaa mshangao.

    "Umemuona baba?"

    "Ndio"

    "Nakupenda mwanangu"

    Phidaya alizungumza huku, alifungua zipu ya koti lake. Akalichanua, macho yangu yakatua kwenye bomu, alilo lifunga kwenye koti hilo, lililo bakisha sekunde tano kabla halijalipuka, Junioa akapiga hatua za haraka kwenda alipo simama mama yake, hata kabla hajamfikia, tukastuki mlipuko mkali, ulio turusha watu wote, ndani ya kanisa hili.



    "Eddy....Eddy"

    Nikastuka, baada ya mama, kunitingisha mara kadhaa.

    "Tumesha fika, tushuke."

    Msafara wa gari za ulisha fika kwenye maegesho ya magari, nje ya duka kubwa la kuuza suti kutoka nchi mbalimbali duniani, hususani Italia na Markani.

    Usingizi mfupi ulio nipitia kwa muda mchache, niliwa ndani ya gari, umenifanya niote ndoto iliyo anza kuniogopesha sana.

    Nikamtazama mama kwa umakini, nikajiweka vizuri shati nililo vaa, nikashuka ndani ya gari.

    "Vipi umaumwa?"

    Mama aliniuliza huku tukiingia ndani ya hili duka, lililopo maeneo ya posta.

    "Hapana"

    "Sasa mbona hujachangamka, nini tatizo?"

    "Nahisi ni uchovu wa usingizi"

    Tukaanza kupitia suti moja baada ya nyingine, sikuwa na amani kabisa moyoni mwangu. Isitoshe zimesalia siku mbili kabla ya mimi kufunga ndoa na Sheila.

    "Hii umeipenda?"

    Mama alinionyesha suti moja yeñye rangi nyeupe yenye maua, mazuri.

    "Yap"

    Mama akanitazama usoni kwa umakini, huku akijaribu kunichunguza, akanigusa kwenye shingo na kiganja chake, ili kuona kama nina tatizo lolote, ila akakuta joto la mwili wangu lipo kawaida tu.

    "Nenda ukaijaribishe basi"

    Nikaingia moja ya chumba kilichopo hapa ndani ya duka. Nikajaribu suti aliyo nichagulia mama. Ikawa imenikaa vizuri mwilini mwangu.

    "Mkuu hapa upo bomba"

    Jamaa mmoja muuzaji alinisifia baada ya mimi jutika ndani ya chumba hichi, nikiwa nimevalia suti hiyo. Kila nilipo mtazama mama, nikawa ninakumbuka mlipuko nilio uota kanisani.

    "Hapo mkeo atafurahi sana"

    "Hongera kaka, umependeza sana"

    Baadhi ya watu ndani ya duka, hawakusita kuniambia ukweli, wa kupendeza kwa jinsi nilivyo vaa. Mama alipo ridhia, akalipia suti hiyo, nikaivua na kurudi ndani ya gari.

    'Junio umemuona babà?'

    Sauti ya Phidaya, ilianza kujirudia rudia kichwani mwangu. Jambo lililo nikosesha amani kabisa moyoni mwangu.

    "Mama, tunaweza tafuta sehemu tukazungumza?"

    Nilimuuliza mama mara baada ya yeye kuingia ndani ya gari

    "Tutazungumza nyumbani"

    "Hayo nataka tuzungumze nje ya nyumbani"

    "Dula, hembu tupitisheni hapo Serena"

    Mama alumuambia fereva wake, akawasiliana na wezake waliopo kwenye gari moja ya mbele na nyingine gari moja lililopo nyuma yetu. Msafara ukabadilika kama alivyo sema mama, tukafika serena Hotel, nakupokelewa na wahudumu. Tukatafuta sehemu iliyo tulia na kaa mimi na mama, hata mlizi wake, wa kike aliamua kukaa mbali kidogo na ilipo meza yetu, asisikie tunacho kizungumza.

    "Heee una lipi la kuzungumza?"

    "Mama, ninaamini kwamba nilisha wahi kukukosea mimi kama mwanao wa pekee."

    "Ila uliweza kunisamehee, kwani mtoto kwa mama, hua akui. Kama tunavyo sema sisi waswahili"

    "Ndio mwanangu, nalitambua hilo"

    "Màma, kunakitu ninahitaji nikuombe?"

    "Omba tu mwanangu, usipo niomba wewe ni nani atakaye niomba mwengine"

    Nikashusha pumzi tataribu, huku nikitazama chini, kwani hata ujasiri wa kumtazama mama, machoni ulinipotea gafla.

    "Mama...."

    "Mmmm"

    Nikajikuta nikishusha pumzii kwa nguvu. Kila nilicho taka kukizungumza kikanipotea gafla kichwani mwanfu, nikajikuta nikibaki.

    "Zungumza mbona umekaa kimya?"

    "Nilitaka kukuambia kua...."

    "Kua nina kupenda sana mama yangu. Upendo wangu sijawahi kuweka bayana kwako. Mama yangu wewe ni mfano mzurikwenye maisha yangu

    Hakuna mama kama wewe"

    Maneno yangu, yakapelekea hadi mama kulengwa lengwa na machozi.

    "Nakupenda pia mwanangu, nipo tayari kuupoteza utajiri wañgu, ila si wewe mwanangu"

    "Japo wamama wengi, hawapendi kuwaomba misamaha watoto wao, ila kwangu nitofauti."

    "Eddy mwanangi, ninakuomba unisamehe"

    "Nikusamehe kwa kipi mama?"

    Mama akajifuta machozi kwa kitambaa, chake. Akavichukua viganja vyangu, na kuvikutanisha kwa pamoja.

    "Najua matatizo yote, yaliyo kupata chanzo ni mimi. Niliamua kuzaa na mdogo wa Gidwin kwa ajili ya....."

    "No mama, hlo nilisha kusamehe, siku nyingi. Haikuwa kisa lako kufanya vile, pia nashukuru kwakuzaa na baba yangu, ila si godwin"

    Mama akakaa kimya, hakutarajia kama nitazungumza kitu kama hicho. Kabla hatujazumgumza, simu yangu ikaita, nikaitoa mfukoni na kukuta Sheila ndio anaye piga.

    "Mume"

    "Mmm"

    "Mumefikia wapi?"

    "Tupi Serena"

    "Na nani upo?"

    "Kwani nyumbani, nilitoka na nani?"

    ”Mama"

    "Sasa inakuaje, unauliza kwamba nipo na nani?"

    "Samahani mume wangu, kama nimefanya kosa"

    "Poa"

    "Piga picha unitumie whatsapp, nimekumis mume wangu"

    "Poa"

    "Jamani Eddy, mbona unanijibu kihasira, kuna kitu nimekuudhi?"

    "Hujaniudhi, ngoja nitakupigia"

    "Nitumie basi picha sasa hivi, ukiwa na ma.."

    Nikakata simu, kabla hata Sheila hajamalizia, sentensi yake

    "Mbona unamjibu mwenzako kihasira?"

    "Hapana mama, yeye anataka picha ya eneo nililopo, naona ananisumbua"

    "Ndio lazima akusumbue, kutoana na mimba aliyo ibeba. Na mwamke akiwa katika kipindi hicho usidhubutu kumuudhi, anaweza kuchukua maamuzi ua ajabu, baadaye ukaja kujutia"

    "Nimekuelewa mama"

    "Lete, simu yako nikupige picha umtumie"

    Nikampa mama simu, akanza kunipiga picha, kadhaa

    "Tayari?"

    Nilimuuliza mama

    "Ndio ngoja nizitazame kama, umetokelezea"

    Nikajikuta nikicheka kwani, sikujua kama mama naye anayatambua maneno ya vijana, kama kutokelezea. Nikaiona sura ya mama, ikibadilika taratibu, huku mikonjo kadhaa ikiwa kwenye uso wake.

    "Huyu nani?"

    Mama akanionyesha picha ya Phidaya, akiwa na Junio.

    "Ahaaa... huyo ni, ni, ni n......."

    "Nani?"

    Rafiki yangu"

    Nilijibu kwa kubabaika sana, mama akanitazama kwa macho makali sana, usoni mwangu.

    "Huyu mtoto?"

    "Eheee"

    "Hujanisikia vizuri au?"

    Mama aliniuliza kwa sauti ya ukali, nikajikuta nikikosa cha kujibu.

    "Mam..."

    "Huyu ni nani kwako?"

    "Mama huyo ni Junio"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Eddy ni ujinga gani umefanya, unazaa na hawa magaidi, Unataka ulipuliwe na mabomu ehee?"

    Mama alipo zungumzia swala la julipuka kwa mabomu, moyo wangu ukanza kunienda mbio, kiasi cha kumbukumbu kadhaa za ndoto niliyo iota ndani gari ikanijia kichwani mwangu, kama mkanda wa filamu.

    "Eddy, laiti ungejua, binadamu ninao wachukia ni huo waarabu"

    "Hivi unawaju vizuri kweli wewe?"

    "Ila mama..."

    "Edddy hakuna cha ila hapa, kwa nini hujasema, kwba una mwanamke umezaa naye?"

    "Mama ninakuomba, utulize jazba, nataka nikuelezee kila kitu juu ya huyo msichana"

    "Kwanza ni mtu wa nchi gani?"

    "Iraque"

    "Mungu wangu, Eddy mwanangu umeingia pabaya"

    "Maa sio pabaya ninampenda sana huyo mwanake ni mama wa mwana....."

    Kibao kikali kikatua shavuni mwangu, kitendo kilicho mganya hadi mlinzi wa mama akastuka.

    "Funga bakuli lako, mbwa wewee. Habari ni hii, simtambui huyo malaya wako wa kiarabu, na wala sikitambui hicho kingurue chako.Ninaye mtambua ni Sheila tuu na mjukuu wangu ajaye."

    Mama alizungumza kwa hasira, huku machozi yakimtiririka mashavuni mwake

    "Mama, mwanamgu ni ngurue?"

    "Kama ulivyo sikia"

    Mama akanyanyuka, na kuanza kuondoka huku akitazama chini, ili watuwasiguñdue kwamba analia.

    "Mama sinto muoa Sheilaa"

    Nilizunguza kwa sauti ya juu, iliyo mfanya mana kugeuka kwa hasira na kurudi nilipo simama

    "KAMA MIMI SIJAKUWEKA, TUMBONI MWAÑGU MIEZI TISA, HUTO MUOA SHEILA, ILA KAMA NILIKUZA KWA UCHUNGU, BASI UTAMUOÀ SHEILA."

    "HICHO KIBESI CHAKO WAPANDISHIE HAO WASICHANA WAKO, ILA SI MIMI MAMA YAKO. USIPO ANGALIA NITAMPOTEZA HUYO MBWA WAKO NA KITOTO CHAKE"

    Mama alizungumza na kupiga hatua tatu mbele akanigeukia na kwaishara ya kidole chake, akaniamrisha nitangulie kwenye gari, huku yeye na mlinzi wake wakifwatia nyuma.



    Katika siku ambayo nimejisikia vibaya ndani ya moyo wangu ni siku ya leo, sikutegemea kama mama yangu anaweza kumkataa mwanangu mbele yangu japo sijamuona, ila muonekano wa kwenye picha una dhihirisha kwamba Junio ni mwanangu wa damu. Kila nilipo mtazama aliye keti, pembeni ya siti yangu. Moyo ukazidi kuniuma, kiasi cha kutamani nishuke ndani ya gari, nitembee hata kwa miguu kurudi nyumbani.

    Tukaafika nyumbani nikawa wa kwanza kushuka ndani ya gari. Sikuelea chumbani kwangu kuepusha kelele za Sheila, ambaye muda wote, mama anamchukulia Sheila kama mtoto mdogo. Chochote anacho kihitaji anakipata.

    "Shem, mbona umekaa huku bustanini, peke yako”

    Sauti ya ndugu wa Sheila anaye itwa Blanka, niliisikia ikinisemesha, nyuma yangu

    "Hapana nina punga punga upepo"

    "Ahaaa, basi nilijua kwamba hjarudi na mama"

    "Nimerudi"

    Blanka akakaa pembeni yangu, huku akivua viatu vyake na kuvisogeza pembeni

    "Shem mbona kama, haupo sawa, unaumwa?"

    Nikatingisha kichwa kumjibu Blanka

    "Sasa n nini tatizo shem wangu? Sasa hivi ulitakiwa uwe ndani unafuraha"

    "Hapana, nina furaha"

    "Shem huna furaha, au dada amekudhi?"

    "Hapana, kuna maswala yangu yakibiashara kidogo ndio ninayafikiria"

    "Ahaaaa, ila shem kuna kitu nahitaji kukuuliza"

    "Kitu gani?"

    "Unampenda kweli dada Sheila?"

    Ikabidi nimtazame Blank vizuri machoni mwake.

    "Mbona umeniuliza hivyo?"

    "Yaa nàhitaji kujua, kwa maana kuna vitu hapa nyuma vilikua vinaendelea"

    "Sijakuelewa, vitu gani vilikua vinaendelea?"

    "Kuna mambo alikua anayafanya dada Sheila, kwa upande wangu sijayapenda isitoshe anakwenda kufunga ndoa na wewe, sizani kama anastahili kua mkeo"

    Moyo ukaanza kunienda mbio, nikamgeukia vizuri Blanka, kabla sijamuuliza kitu, nikamuona mama akija sehemu tulipo.

    "Ina bidi uongeze juhudi kwenye masomo, isitoshe unasoma masomo ya udaktari, ujitahidi sana"

    Ilinibidi kubadilisha mada, ili mama asielewe ni kitu gani tunazungumza. Chakumshukuru Mungu Blanka alinielewa maana yangu ya kubadili mada tuliyo kua tukiizungumza.

    "B wezako wanakutafuta kule ndani"

    "Ahaa sawa mama"

    Blanka akanyanyuka na kuondoka, mama akakaa sehemu nilipo. Ukimya wa sekunde kadhaa ukakatiza, sikua na kitu cha kuzungumza.

    "Hivi Eddy, ni nani aliye kuroga?"

    "Hakuna"

    "Nimempigia mchungaji simu, aje kukuombea"

    "Ili iweje"

    "Eddy wewe si bure, utakua umerogwa"

    "Mama na elimu yako hiyo yote yaani una amini kwamba mimi nimerogwa?"

    "Tena sana, na aliye kuroga amesha fariki"

    Laiti kama añgekua si mama yangu, aliye nibeba tumboni mwake miezi tisa, ningemtandika ngumi, ambayo asinge isahau maisha yake yote.

    "Na kama nilivyo kuambia, mtoto uliye naye mimi simtambui, na huyo mama yake naye simtambui. Sasa ole wako unidhalilishe kwa wageni nilio waalika. Haki ya Mungu naapa nitakuachia laana."

    Mamà akanyanyuka, nakujifunga tenge lake vizuri.

    "Na sitaki siku hata moja huyo mwanangu Sheila ajue, kwamba unamtoto. Akijua na kuchukua maamuzi mabaya utajuta"

    Mama àkaondoka na kuniacha nikibaki nikimsindikiza kwa macho, yaliyo jaa hasira.

    Kitu kilicho anza kuniumiza kichwa, nikuhitaji kujua ni mambo gani aliyo kua akiyafanya Sheila, kipindi ambacho mimi sikuwwepo. Nikaanza kuamini kwamba Blanka atakua ni msaada mkubwa sana kwangu.

    Usiku sikuamini kumuona mchungaji akiwa ameketi kwenye sofa za sebleni, akizungumza na mama. Wakaniita, nikajumuika nao kwenye mazungumzo, mimi na mchungaji tukaingia kwenye chumba cha maombi, kilichopo ndani ya hili jumba jipya la mama.

    Bila hata mchungaji kuniuliza swali, lolote akaanza kuniombea huku akiuweka mkono wake juu ya kichwa changu

    "Pepo mchafu uliyopo ndani ya kichwa cha huyu kijana toka kwà jina la Yesu kristo"

    Mchungaji aliendelea kuniombea huku akinisukuma sukuma kichwa changu. Zaidi ya nusu saa mchungaji aliendelea kunisalia

    ”Mchungaji, nimechoka kupiga magoti kama mapepo sina si tuachane na hii biashara bwana"

    "Ohhhh shagara bagharaa, pepo wewe mchafu huwezi jibizana na mimi mtu wa Mungu, hapo ulipo toka kwa jina la Yesu"

    "Mchungaji tuheshimiane bwana, sina pepo wala nini. Hembu fanya jengine la maana"

    "Pepo pepo mchafu tokaaaaaa"

    Nikaona mchungaji hanielewi, nikasimama, akabaki kunitazama machoni mwangu, huku akizungumza maneno, nisiyo yaelewa.

    ”Nisikilize mchungaji, nahisi huyo Mungu iyepo ndani yako sidhani kama ni Mungu huyu tunaye muabudu. Hembu rudi ulipo toka kasime vizuri hiyo biblia yako uje tena kuniombea. Matatizo yaliyopo hapa ni kati yangu mimi na mama yangu sawa?"

    Nilizungumza kwa sauti ya ukali na yachini, jambo lililo mfanya mchungaji kunitumbulia mimacho. Nikafungua mlango na kwenda chumbani kwangu, na kulala.

    Asubuhi na mapema, nikaamka. Nikafanya mazoezi kama kawaida yangu, nikaenda kwenye nyumba wanayo ishi watoto wa kike, na ndipo anapo kaa Sheila, nilitenganishwa nàye ili nisimuone hadi siku ya harusi yetu. Nikamtafuta Blanka ila sikumuona

    "B amekweñda wapi?"

    "Wametoka na bibi harusi, leo wamekwenda saloon kuanza kupambwa"

    "Saloon gani?"

    "Labda mpigie wifi mwenyewe umuulize"

    Nikaachana na mdogo wangu, ambaye nilitambulishwa sikujua hata ametokea wapi, ila wote ni ndugu. Nikampigia simu Sheila ila haikupatikana, nikajaribu kupiga simu ya Blanka ñayo haikupatikana. Nikajaribu kupiga ya ndugu mwengine niliye hisi atakua mpambe kwenye msafara huo, simu yake ikaita baada ya muda akaipokea

    "Dada upo na hao maarusi?"

    "Ndio, tupo Saloon moja inaitwa Rich Power Women au R.P

    W"

    "Ipo wapi?"

    "Màeneo ya huku posta"

    Akanielekeza walipo, akanieleza simu za Sheila na Blanka, zimezima chaji.

    Nikaingia kweñye moja ya gari, kwa lengo la kwenda kuzungumza na Blanka, nikafika getini nikashangaa kuona halifunguliwi na askari wanao linda.

    "Vipi fungueni basi geti"

    "Muheshimiwa ametuambia kwamba wewe hàuruhusiwi kutoka"

    "Nini?"

    "Ndio, tunafwata agizo lake, samahani kwa usumbufu muheshimiwa"

    Askari mmoja, aliniambia huku akiwa ameshika bunduki yake aina ya SMG pamoja na mbwa mkubwa, na anaye onekana mkali sana.

    Nikatoa simu yangu na kumpigia mama, aliye kwenda kazini, alfajiri na mapema.

    "Mama ni mambo gani unayo nifanyia lakini?"

    "Mambi gani?"

    "Ndio umewapa amri hawa askari wako mimi nisitoke nje?"

    "Ndio, utatoka kesho siku ya harusi yako tu. Hiyo sio ombi bali ni amri"

    Mama akakata simu, nikabaki nikiwa nimeitazama simu yangu, huku nikihema kwa hasira. Ikaingia namba ngeni kwenye simu yangu, iliyo nistua sana moyo wangu. Taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.

    "Haloo bwana Eddy"

    Nilisikia sauti ya kiume

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nani wewe?"

    "Hauna haja ya kujua mimi ni nani, Ila nina habari njemaa sana kwako"

    "Una masaa ishirini na nne, kuleta kiasi cha pesa milioni mia moja, kumuokoa mke wako na mwanao Junio, la sivyo WATAKUFA"

    "Wewe ni na.....?"

    Simu ikakatwa, nikabaki nikiwa nimeitazama simu yangu, mapigo ya moyo yakinienda mbio.



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog