Chombezo : Sorry Madam
Sehemu Ya Tatu (3)
ILIPOISHIA
Nikapata matumaini ya uwepo wake na moja kwa moja nikaufungua mlango wake na sikuamini macho yangu baada ya kumkuta akiwa ananyonyana denda na mwanaume mwengine ambaye kwa haraka nikamtambua ni Derick mume wa madam Mery
ENDELEA
Sheila akastuka sana kuniona nikiwa nimesimama mbele yao,hata Derick ambaye mimi na yeye ni maadui kama paka na paya akakastuka sana na wakaachiana.Macho yangu kwa hataka nikayazungusha katika enoe la chini kutafuta kitu kizuri ambacho ninaweza kupambana nacho ila sikuona.Nikatazama nje nikaona kupande cha mbao kilicho chongonga vizuri na kina unene mkubwa kiasi.Nikakifwata kwa haraka na kurudi ndani na kumkumba Derick ambaye alikuwa anakimbilia kuufunga mlango kwa ndani,akaanguka vibaya na kunipa nafasi ya kuanza kumshambulia kwa haraka.Kwa nguvu zangu zote nikakitulisha kipande cha mbao kwenye magoti yake na kumfanya anguke chini akitoa ukulele wa maumivu makali.
Sheila akaanza kubabaika kwani siku zote ananijua nikiwa na hasira ninakuwa ziadi ya mnyama mkali,kwa kutumia kigoti ya mguu wa kulia nikakitulisha kwenye kidevu cha Derick na kumfanya arushwe juu kidogo huku meno kadhaa yakidondoka sakafuni
“EDDY UTAMUUA.....”
“Wewe Malaya funga bakuli lako”
Derick akajaribu kurusha teke,nikalidaka huku nikimtazama kwa hasira.Nikamsukuma na akajigonga kwenye kabati lenye Tv na redio kubwa.Derick akaanza kutokwa na machozi akijaribu kuniomba msamaha ila sikumuelewa kabisa kwa kitu anacho niambia.Kwa kutumia gongo nikaanza kumshambulia kwenye miguu yake,nikitumia nguvu zangu zote kuiamiza kwa kipande cha mbao na kuzidi kumpa maumivu Derick.Sheila akanidandia mgongoni akijaribu kunizuia,Nikageuka na kumshika Sheila kichwa chake na kumtazama kwa macho makali.Nikampiga kichwa kichwa cha uso na kumfamya ayumbe kama tiara,nikampiga buti nililo muangushia kwenye sofa na kuanza kulia kwa maumivu kalali.
Nilipo hakikisha miguu ya Derick haifanyi kazi yoyote,nikaingia jikoni na kuchukua kishoka cha kukatia nyama chenye makali,kabla sijatoka nikaona kamba ikiwa kwenye mfuko.Nikavichukua kwa pamoja na kutoka sebleni na kumuona Derick akijiburuza akijaribu kwenda nje huku akilia.Nikaishika miguu yake na kumburuza hadi alipo Sheila,
“Eddy mpezi wangu,nakuomba unisamehe....nisikilize nakuomba”
Sikuwa na haja ya kumsikiliza Sheila,nikamshika Sheila kichwa chake na nikachukua vipande vya vitambaa vya masofa na kumkandamiza navyo mdomoni na kumfanya ahangaike agaike,Nikamfunga kwenye mikono na miguu.Derick wakati wote anakoroma kwa kulia na maumivu.Nikatoka nje na kulifunga geti na kurudi ndani na kuufunga mlango wa kuingilia
“Sheila naamini mimi kwako si wakusimuliwa,ninaroho ya binadamu na Shetani.....leo nahitaji unijue mimi ni nani?”
Nilizungumza kwa hasira na sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo mingi.Nikamshika Derick mkono wake wa kulia,kumbukumbu ya mwanangu alivyompiga chini ikapita kwa haraka kichwani kwangu,nikanyang’ata meno yangu kwa hasira.Nikachukua kishoka na vidole vya Derick nikavilaza sakafuni huku nikivikandamiza kwa kutumia mkono wangu wa kushoto
“No...Usinifa.......”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nishoka kikatua kwenye vidole vyake na kuvitawanyisha kwenye sakafu,Dericka akatoa ukulele mkali ila nikamzaba ngumi ya shavu na akabaki akigugumia.Sheila akabaki akiwa ameyatoa macho kama amepigwa mshale wa mgongo.Nikavikunyanya vidole vyake vyote na nikaviweka kwenye meza ya kioo.
“Derick leo utakufa kifo cha taratibu kama mwanangu ulivyo mfanya.”
Nikavua tisheti niliyo ivaa,nikaingia jikoni na kuchukua sahani na kurudi nayo ndani sebleni.Nikamfunga Derick akamba za miguu,Nikamsokomeza vitambaa na yeye kwenye mdomo.Nikauchukua mkono wake wa kushoto ulio na vidole vyake kamili.Nikamtazama machoni kwa macho ya dharau,kisha nikaupitisha katikati ya miguu yangu na akabaki akinitazama,Nikaizungusha miguu yangu na kuusababisha mkono kutoa mlio wa kuvunjika mifupa iliyopo kwenye mkono wake.Dericka akaendelea kulia huku akigaragara chini.Nikaibaeba sahani yenye vidole hadi jikoni,nikaweka kikaangio kwenye jiko la gesi na kuliwasha,nikamimina mafuta mengi ya kula kisha nikavidumbukiza vidole vyote kwenye kikaangio na kuongeza moto ili viive haraka na kurusi sebleni.
Sheila akanitazama huku machozi yakimwagika,Mlio wa simu kutoka kweney mfuko wa suruali ya Derick ukaanza kusikika.Nikaitoa simu yake ikiita na kukuta ni madam Mery ndio anapiga simu kwani imeandikwa ‘wife’ na pembeni kuna picha yake.Nikamtazama Sheila na kumfwata,nikamshika nywele za kichwa chake
“Sikia wewe Malaya,zungumza na huyu mjinga mwenzako.Jitambulishe kuwa wewe ni mke mwenzake sawa?”
Sheila akatingisha kichwa,simu ikakata na baada ya muda ikaanza kuita tena,Nikamtoa Sheila vitambaa mdomoni.
“Zungumza naye”
Nikaminya kitufe cha kupokea na kuiweka simu iwe kwa sauti kubwa(Laudspeker) na kuisikia sauti ya madam Mery ikaanza kuzungumza
“Haloo mume wangu”
“Wewe mshenzi nimekuambia achana na mpenzi wangu.”
“Kwani wewe ni nani na namba ya mume wangu umeipataje?”
“ Hadi hapo ujaelewa tuu,mimi ni mke mwezio”
“Jamani kwa nini uanifanyia hivyo wewe dada kumbe wewe ndio umeficha mume wangu wiki nzima harudi nyumbana”
“Mjini hapa”
Nikaikata simu na kuizima huku nikijiuliza maswali ni kwanini Madam Mery aliamua kurudia na mume wake baada ya tukio la kuuawa kwa mwanangu
“NA YEYE LAZIMA AFE”
Nilizungumza kwa sauti ya hasira huku nikimtazama Sheila,nikamdumbukiza tena Sheila vitambaa vya mdomoni.Nikakimbilia jikoni na kukuta vidole vya Derick vikiungulia kwenye mafuta,Nikazima jiko na kuvitoa kwenye vikaangio na kuviweka kwenye sahani,Nikaona nyanya mbili juu ya friji,nikazikataka kata vizuri na kurudi sebleni nikiwa nimeishika sahani,Nikaviweka juu ya meza na kumgeuza Derick aliye lala kifudi fudi akiugulia maumivu.
“Derick nimekukangia miskaki iliyonona,karibu ule”
Derick akanitazama kwa macho ya hasira,nikamuitamia na kuvitoa vitambaa mdomoni mwake kisha nikachukua kidole kimoja na kukikandamiza mdomoni mwake,Gafla akanitemea kidole usoni na kuzidi kunipandisha hasira na nikaanza kumshindilia ngumi za pua hadi ikatepereka na kumwaga damu nyingi.
Nikajibwaga kwenye sofa huku nikimtazama Derick nikifikiria nini cha kumfanya ili apate uchungu kama nilio upata mimi kipindi alipo muua mwanangu.Nikapata wazo ambalo likanifanya nisimame na kumburuza Derick hadi nje kisha nikarudi ndani na kumchukua Sheila na kumbeba begani,Nikafungua mlango wa gari na kumuingiza upande wa dereva huku mikono na miguu yake nikiwa bado nimeifunga kwa kamba.Nikaaingia ndani na kuchukua kishoka changu na kurudi nje nikamchukua Derick na kumlaza chini ya gari,nikaingia ndani ya gari na kuifungua mikono ya Sheila
“Washa gari lako”
Nilizungumza huku kishoka nikiwa nimekiweka kwenye shingo yake.Sheila akaanza kutetemeka na akafanya kama nilivyo muagiza
“Endesha gari lako umkanyage huyo mwehu wako”
Sheila akatingisha kichwa,akiashiria kukataa.Nikamtoa vitambaa ambavyo nilimsokomeza mdomoni
“Endesha gari”
“Huoni tutamuua”
Nikamzaba Sheila kofi la shavu,na kumfanya kuweweseka na akakanyaga mafuta na gari ikasogea mbele na kupanda kwenye mwili wa Derick kama imepata kwenye matuta yaliyo tengenezwa barabarani.Nikashuka kwenye gari na kumkuta Derick akiwa yupo katika hali mbaya,kwa kutumia kishoka changu nikamkata Derick kichwa chake na kukirusha ndani ya gari alipo Sheila na kumfaya akarupuke kwa woga
“Sheila Sali sala yako ya mwisho,unamfwata mwehu wako kuzimu”
Nilizungumza kwa sauti nzito isiyo na huruma hata kidogo
“Eddy ni nini kimekupata unakuwa naroho mbaya kiasi hicho”
Sheila alizungumza kwa woga huku akitetemeka,Nikapiga hatua za taratibu hadi sehemu aliyo simama pembezoni mwa gari,
“Wewe ni mtu wa kunisaliti mimi?”
Swali langu likamfanya Sheila kutingisha kichwani,Nikamshika mkono na kuanza kumburuza hadi tukaingia ndani na kumsukumia kwenye sofa
“Eddy,kumbuka mimi na wewe tumetoka mbali........nilikuwa nipo radhi kufa kwa ajili yako.Leo hii huioni dhamani yangu kwanini lakini Eddy”
Sheila alizungumza huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi,Hasiri ikazidi kunipanda kila nilipo kumbuka tukio la wao kukumbatia na Derick
“Eddy mimi nilijua kuwa wewe umeniacha,Tazama nilikuokoa kwenye ndege nikawa nipo tayari mimi kufa ili wewe upone,Ila hata siku moja sijakuona hospitalini.Niliiungua kwa ajili yako wewe.Ila dhamani yangu ipo wapi au kwa sababu mimi ni mwanamke ndio unaamua kuninyanyasa?”
Sheila alizidi kuzungumza kwa uchungu na kunifanya niwe kimya nikimtazama huku asira ikinishuka
“Eddy nipo tayari kufa,Nichinje kama ulivyo mchinja Derick,NICHINJE”
Sheila alinamisha kichwa chake mbele ya miguu yangu na kujikuta nikikinyanyua kishoka changu juu kwa hasira machozi yakinimwagika taratibu
“Eddy ,najua nitakwenda kuzimu kwa maana nimekukosea sana.Ila sistahili kuendelea kuishi mip tayari uniue.”
Nikakitupa kishoka kwa nguvu kwenye meza ya kioo hadi meza ikavunjika.Taratibu nikakaa chini huku nikimwagikwa na machozi,Sheila akainyanyua sura yake iliyo lowana machozi na kuniangalia kwa uchungu
“Eddy kwa nini umeua,ulishwa kutuambia kiustarabu”
Kiganja cha mkono wangu wa kulia kwa haraka kikatua shingoni mwa Sheila na kuanza kuibana kwa nguvu,mikono ya Sheila ikawa na kazi ya kuuzuia mkono wangu usiendelee kuibana shingo yake
“UNAMAJUA DERICK VIZURI WEWE?”
“Mm..mmmmmmmm.....?”
Nikaiachia Shingo ya Sheila na kumfanya asogee mbali kidogo na nilipo mimi.Ukimya ukatawala kati yetu huku ikisikika mihemo yangu ya hasira jinsi inavyo panda na kushuka.
“Eddy ninakupenda sana,tena sana.Maishani mwangu nilikuambia kuwa sijawahi kupenda mwanaume yoyote kama wewe.Umenifundisha mengi Eddy,Upendo,Ujasiri,Huruma......Ila mimi sio kosa langu kuwa na Derick”
“Ila?”
“Derick mimi alinisaidia sana kipindi nipo Kenya,Sikuwa na mtu wa kunilipia hata pesa ya hospitali ambayo nilikuwa ninatibiwa.Aliweza kunihudumia kwa kila jambo,alininunulia dawa za gharama kuwa zilizo nisaidia ngozi yangu kurudi katika hali ya kawaida kama awali.Nilikuwa nimebabuka mwili mzima mimi,nilikuwa sitamaniki na......”
“Ukaamua kumpa mwili wako?”
“Sio kama niliamua kumpa mwili wangu,Aliweza kunishawishi na wewe sikujua ni wapi ulipo.Nilijariu kukuulizia shule ambayo ulikuwa unasoma ila sikupata jibu”
Nikaachia tabasamu la dharau lililo jaa hasira nzito inayo ifanya royo yangu kutamani niyanyofoe masikio ya Sheila,nikawa ninajikaza nisifanye kitu ninacho kiwaza
“Tangu tupoteane,imepita kipindi gani?”
“Miezi mitatu”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ulishindwa kuzizuia hisia zako hadi utakapo niona?”
Sheila akaa kimya huku macho yake akiyakwepesha kukutana na macho yangu yalio jaa ukali kama chui aliye jeruhiwa mwili wake kwa risasi.
“Dawa yako ipo jikoni”
Nilizungumza huku nikinyanyuka na kwenda njee,Nikauvuta mwili wa Derick na kuutoa chini ya gari,Nikaurudi ndani na kumkuta Sheila akiwa amejinamia chini akilia
“Funguo ya handaki lako iko wapi?”
“Ndani?”
“Wapi?”
“Kwenye dreasing table yangu”
Nikamtazama Sheila kwa muda,nikafunga mlango wa kutokea nje kwa funguo zilizokuwa zikining’inia ndani ila kumfanya Sheila asikimbie kwenda sehemu yoyote.Nikaingia chumbani kwake na kuiona rimoti ndogoi iliyopo juu ya kakabati kake kadogo kalicho jaa vipodozi.Nikaichukua kabla sijaondoka kwa bahati mbaya nikaangusha kichupa cha mafuta,nikakiokota na kukirudisha juu sehemu kilipo kuwa ambapo chini yake kuna karatasi iliyo geuzwa upande wa pili ambao hauna maandishi yoyote,Nikaichukua karatasi na kuigeuza upande wa pili
Nikaanza kusoma maandishi yaliyo andikwa kwa muandiko wa kulala na juu yake kuna jina la hospitali ambayo dokta huyo ndio ameandika vipimo vilivyo anza kuufanya mwili wangu kurudi katika hali ya hasira kali.Vipimo alivyo viandika daktari vinaonyesha Sheila ni mjamzito wa mimba ya wiki mbili na kwa pembeni yake baba wa mtoto ni Derick Malki
“ANAMIMBA YA DERICK....?”
Nilijiuliza swali ambalo jibu lake ninalo kichwani,Nikiwa ninaendelea kuitazama karatasi yangu ni kama Mungu aliye niambia nitazame kwenye kioo,Nikauona mkono wa Sheila akiwa ameunyanyua juu huku akiwa ameshika kishoka nilicho kuwa nacho mimi.Nikakikwepa na kuruka pembeni,Sheila akakirusha kishoka,nikainama na kikanikosa na kutua kitandani.Kama gari iliyo poteza breki zake,nikajirusha na kwakutumia bega langu la mkono wa kulia,likatua tumboni mwa Sheila na sote tukaanguka chini,Sheila akaanza kutoa kilio cha maumivu.Nikainyanyua ngumi yangu na kushusha kwa kasi na kabla haijafika usoni mwake nikaisimamisha na kumtazama jinsi alivyo fumba macho akiogopa mzigo utakao shuka kwenye uso wake
“UNATAKA KUNIUA WEWE MALAYA SI NDIO?”
Sheila hakunijibu chochote zaidi ya kuwa kimya.Nikampiga vibao vinne vya mashavu ili kuiweka akili yake sawa.
“Upendo wangu kwako usije ukageuka ukawa kifo chako,Sheila....nimezaliwa siku moja nia nitakufa siku moja,Hakuna kama mimi Eddy na hatotokea kama mimi.PUMBAVU”
Nikamalizia na kibao cha tano kilicho mfanya azidi kuwagikwa na machozi.Nikamnyanyua na kumuweka begani nikakichukua kishoka changu na tukatoka nje.Nikambwaga kwenye sofa kama zigo wa kuni na kabla sijatoka nje Sheila akaniita
“Nini?”
“Naomba unisamehe,haikuwa akili zangu”
“Zilikuwa akili za nani?”
“Ni shetani amenipitia,nikatamani kukuua”
Sheila alizungumza huku akiwa amejishika tumbo lake.
“Sheila mimi sina roho mbaya,ila inapobidi niwe na roho mbaya itakuwa.Mimi siwezi kumuua mtoto wa Derick uliye naye tumboni kama yeye alivyo fanya kwa mwanangu”
Sheila akakosa la kuzungumza na mimi,nikaufungua mlango na nikatoka nje,Kwa kutumia kirimoti nikaufungua mlango wa handaki na kisha nikabeba mwili wa Derick hadi ndani.Nikarudi juu na kuchukua kicha chake na kuingia nacho ndani.Nikalichunguza handaki na kugundua lina majiko mengi ya umeme ambayo yana sehemu ya kuwokea mikate.Nikaisogeza meza kubwa iliyipo pembeni yangu na nikauweka mwili wa Derick juu
“Eddy”
Sauti ya Sheila ikanifanya nimgeukie,Akainisogelea karibu na kunishika mkono wenye kishoka
“Hii roho ya kikatili umeitoa wapi?”
“Kwenye kazi zangu huwa sihitaji kuingiliwa,Ondoka kabla sijafanya maamuzi mabaya kwako”
“Eddy,mimi ndio nilikuwa ninakupunguza hasira zako.Hakuna mwanamke ambaye aliweza kufanya hivyo kama si mimi au mama yako”
“Mama anakutaka uende nyumbani,amekutafuta kwa kipindi pasipo mafanikio yoyote.Nakuomba twende sote kwa mama leo”
Nikayatazama macho ya Sheila na kuyaona yanamaanisha kitu anacho kizungumza.
“Rudi ndani?”
“Unataka kuufanya nini huo mwili?”
“Rudi ndani usiniulize chochote”
Sheila taratibu akasogea pembeni yangu.Pasipo kuwa na haruma nikaanza kuucharanga kwa kishoka mwili wa Derick,Nikaufanya mwili wa Derick kuwa katika vipande vipande.Nikaliwasha jiko kubwa lenye visahani vinne vya kupikia.Nikaviingiza vipande vya mwili wa Derick.
“MUNGU ninaomba unisamehe katika hili”
Niliomba sala ya msamaha kwa Mungu wangu,Nikaifanya kazi yangu ya kuvikausha vipande vya mwili wa Derick hadi nikamalizia na kichwa chake kwa kukipasua.Nikaviweka kwenye turubai kubwa la kufunikia gari la Sheila kisha nikatoka nje,Nikamkuta Sheila kusafisha sehemu zote zenye damu.Macho ya Sheila yamevimba kidogo kwa kulia huku mashavu yake yakiwa na alama za vidole vyangu
“EDDY,hii ni siri kati yangu mimi na wewe.”
“Ukiitoa nikufanye nini?”
“Nifanye chochote upendacho”
“Sawa”
Tukasaidia kufamya usafi,Nilipo hakikisha hakuna uchafu wa ina yoyote tukarudi ndani na Sheila akawa wa kanza kuoga kisha nikafwatia na mimi,nikavaa suruali ya Sheila ambayo inanitosha na tisheti yake hii ni kutokana na kutokuwa na nguo.Mida ya saa mbili usiku tukafunga safari hadi nyumbani kwa mama,Sheila akapiga honi na geti la nyumba likafungulia na akaingiza gari hadi sehemu ambayo kuna magari yetu mengine.Nikashuka ndani ya gari ila Sheila akaniomba atangulie.Akaufungua mlango na kuanza kumuita mama ambaye niliisikia sauti yake akiitika.
“Ohoo karibu mwanangu”
Nikawachungulia ndani na kumuona Sheila akikumbatiana na mama.Nikaingia na kumfanya mama kunishangaa kwa muda huku akionekana kama kuto amini kwa kile anacho kiona mbele yake.Kwa Furaha mama akanikumbatia na sote machozi yakaanza kunimwagika.Mama akanikaribisha ndani huku akiwa na furaha kubwa
“Mwanangu Eddy ndio umevaa nini?”
Mama alinitazama kuanzia juu hadi chini na kumfanya Sheila kucheka
“Nimempisha pamba zangu zimemtoa chikopa kama nini?”
“Mwanangu ungekuwa mwanamke ungevutia kama nini”
“Mama.....!!”
“Ndio....ila ndio hivyo umezaliwa dume la mbegu”
Mama akatukaribisha mezani na kutakapa chakula cha usiku.Kutokana na mawazo mengi sikuweza kuzungumza sana na mama.Nikapanda gorofani kulala,nikajitupa kitandani ila usingizi haukunichukua kabisa.Tukio la uuwaji wangu wa kikatilii ulianza kunisumbua sana akilini mwangu.Taswira ya madam Mery ikaanza kukisumbua kichwa changu,Nikanyanyuka na kwenda cumbani kwa mama.Niifungua droo yake ambayo anahifadhia astola yeke.Kwa bahati nzuri nikaikuta.
Nikaitazama na kuikuta na risasi za kutosha,Nikafungua droo nyingine na kukuta pesa za kutosha,Nikachukua kibunda kimoja na sikujua idadi ya pesa iliyopo.Nikashusha pumzi vya kutosha,nikatoka chumbani kwa mama nikiwa ninakatiza kwenye kordo nikirudi chumbani kwangu nikayasikia mzungumzo ya mama na Sheila
“Wee unataka kuniambia kuwa mwangu amekuwa na roho mbaya kiasi hicho?”
“Ndio mama,Mbele ya macho yangu amemuua mwanaume mmoja ambaye anadai kuwa alimuulia mtoto wake”
“Mtoto?”
“Ndio mtoto ila sijajua huyo mtoto amezaa na mwanamke gani?”
“Ina maana Eddy alikuwa na manamke mwengine zaidi yako?”
“Ndio mama,Imeniuma sana mama yangu”
“Ila mama chonde chonde ninakuomba usimuambie Eddy chochote kwa maana,amekuwa kama mtu aliye changanyikiwa”
“NANI KACHANGANYIKIWA”
Nilishindwa kuvumilia ikanibudi nizungumze,taratibu nikiwa ninashuka kwenye ngazi na mkononi nikiwa nimeshika bastola na kuwafanya mama na Sheila kustuka
Sheila kwa haraka akarudi nyuma ya mama na kujificha,Mama akanitazama kwa macho yaliyo jaa mshangao
“Eddy mwanangu unataka kufanya nini?”
“Nataka kujua huyu mwanamke kwa nini amesema kuwa mimi nimechanganyikiwa”
“Hujachanganyikiwa mwanangu,tulikuwa tunazungumza kuhusiana na baba yako mzee Godwin kwamba amechanganyikiwa”
“Mama na wewe unashiriki zambi ya uongo?”
“Kweli mwanangu,aliniambia kuwa amemuona sehemu fulani katikati ya jiji akiwa anaruka ruka”
Nikamtazama mama kisha nikakaa kwenye sofa na kuiweka bastola pembeni yangu.Sheila akabaki akinitazama huku akiwa hana la kuzungumza.Wote wakaka na kunitazama,ukimya ukatawala ndani ya dakika kadhaa mama akaamua kuuvunja ukimya.
“Eddy na hiyo bastola yangu unakwenda nayo wapi?”
“Kuna kazi ninataka kwenda kuifanya”
“Eddy mwanangu,hembu niambie ni nini tatizo linalo pelekea kuwa na roho kama hiyo kwa maana umerudi hujazungumza na mimi vitu vingi zaidi ya kwenda kulala?”
“Mama bado mimi nipo,tutazaungumza kila kitu”
“Sawa,ila kwanini ume......”
Nikauona mguu wa Rahma ukiukanyaga mguu wa mama na kumfanya asiimalizie sentesi yake.
“Kwa nini umekaa huko mbali pasipo kuwa kunijulisha?”
“Huyo hajakuambia?”
“Yeye atajuaje mtoto wa watu?”
“Ahaa mama hiyo mada tutazungumza kesho.Oya ninaomba funguo”
“Za nini?”
Sheila alizungumza kwa sauti ya upole na yenye unyeyekevu mkubwa
“Funguo za gari na nyumba yako.”
Sheila akafungua pochi yake na kunipa.
“Mbona umevaa nguo hizo hizo ulizo kuja nazo?”
Nikajitazama kuanzia chini hadi juu,nikarudi chumbani kwangu na kuvaa nguo zangu vizuri,nikaichomeka bastola kiunoni mwangu na kuifunika na tisheti nyeusi niliyo ivaa,nikurudi sebleni.
“Wewe twende basi home”
Sheila akatazama na mama kisha akanitazama na mimi
“Mmmm nitalala na mama”
“Hutaki au?”
“Eddy muache mwenzako alale hapa,kwani huku kwake unakwenda kufanya nini?”
“Kulala”
Nikataka kutoka na mama akaniita
“Bastola yangu ipo wapi?”
“Nimeirudisha”
“Wapi?”
“Kwani mama ilikuwa wapi?”
“Basi baba nenda salama”
Nikatoka na kuufunga mlango vizuri.Nikasimama pembeni ya dirisha na kusikilizia ni nini mama na Sheila watakizungumza,kwa kupitia uwazi ulioachwa na dirisha nikawaona wakikaa kwenye sofa
“Mbona mwanangu amebadilika namna hii?”
“Mama wee acha tuu,Eddy mimi ninampenda ila kwa hapa alipo fikia ninamuogopa mama”
“Mmmm usimuogope”
“Mama Eddy kuna kipindi alipokuwa na hasira mimi nilikuwa nikimtuliza na kumsogelea,ila sasa hivi mmmmmm ni bora nimtoroke toroke hadi atakapo kaa sawa”
“Itabidi nitafute madaktari watakao muhudumia”
“Ni kweli mama,yaani mtu anazungumza kwa sauti nzito kama simba dume”
“Ila mwanangu huyu anaugonjwa wa asira,mimi wala simshangai sana kwani kuna kipindi akiwa mdogo alisha wahi kumuua mwenzake shule kwa kumpiga na chupa ya soda kichwani”
“Weeeee?”
“Ooohhh ilikuwa ni kesi kubwa kilicho muokoa ni udogo wake kwa alikuwa na miaka mitano”
“Mama ina maana Eddy kuua hakuanza leo?”
“Eddy mwangu akiwa na hasira si mtu wa kumsogelea,nilisha mpeleka hadi kwa wachungaji wamuombee ila wapii.Nilijaribu kutafuta wana saikology labda wakae nao ila imeshindikana.Kila dawa ambayo niliambiwa inafaa kwa kipindi hicho kuwa kama kitulizo cha ugonjwa wake ila wapi?”
“Mmmm”
“Yaani na haya matatizo yaliyo tokea hichi kipindi cha hivi karibuni naona pia yanachangia sana”
Nikataka kuondoka niwahi ninapotaka kwenda ila swali la Sheila likanifanya nipige hatua kadhaa kurudi dirishani
“Kweli mama,Hivi mzee Godwin yupo wapi?”
“Hadi leo sijamuona,Mimi mwenyewe ninafanya uchunguzi nije kumuona ila hadi sasa hivi sijapata jibu”
“Mama tutasaidiana katika hilo,yule mzee ni muuaji sana”
Sikuona haja ya kuendelea kusikiliza mazungumzo yao zaidi ya mimi kuondoka,Nikaingia ndani ya gari na mlinzi akanifungulia geti na kuondoka,Nikafika kwenye kituo cha kuongeza mafuta.Nikajaza tanki la gari na kulipa kiasi ambacho kimegharimu kiasi hicho cha mafuta.Njia nzima nikawa ninafikiria ni wapi alipo Mzee Godwin.Nikafika nyumbani kwa Sheila na kushuka kwenye gari na kufungua geti,nikaliingiza gari ndani na kufunga geti.Nikafungua ndani na kuchukua kirimoti cha kufungulia sehemu ya kuifadhia gari,Nikaingia na kuchukua turubai lenye mwili wa Derick ambao niliubanika vizuri
Nikauingiza ndani ya buti la gari na kulifunga vizuri,nikafunga kila sehemu kama nilivyo iacha,kabla sijatoka nikakumbuka simu ya Derick niliiacha sofa nikiwa nimeizima,Nikaingia ndani na kuichukua ila sikuiwasha,Nikafungua geti na kutoa gari.Nikarudi kulifunga na safari ya kuelekea Arusha ikaanza,Kutokana ni usiku sana hapana magari mengi zaidi ya maroli ya mizig ambayo yanakwenda kwa kasi na usipo kuwa makini utajikuta ukigongwa.Nikazidi kuongeza mwendo na kimoyo moyo nikawa na kazi ya kumuomba Mungu nisipate ajali kwani mwendo ninao tembea nao endapo nitakubwa hata na baiskeli basi kitakaocho endelea kwenye kuanguka nahisi kitakuwa ni kifo tu.Kwa hofu nikapunguza mwendo kutoka spidi 250 hadi mia moja japo gari bado ipo kwenye mwendo mkali sana.
Mwanga mkali wa gari linalokuja nyuma yangu ukaanza kuniumiza macho,Nikapunguza mwendo na kumuwashia taa nikimuashiria apite kwani sikuweza kuendesha kwa jinsi taa zake zinavyo niumiza macho kupitia vioo vya pembeni.Nikashuhudia gari aina ya ‘HAMMER’ yenye rangi nyeusi na vioo vyake vyote vikiwa ni vyeusi na limefungwa likinipita,Haikuwa ni moja zikapita nyingine mbili zikiwa katika kwendo kama ilivyo gari ya kwanza
“Mmmmmm ni kina nani hawa?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijiuliza maswali,Na mimi nikaanza kuongeza mwendo wa gari langu.Jinsigari hizi zinavyozidi kwenda ndivyo nami nilivyodidi kuongeza mwendo,Nikaanza kuzikaribia kwa karibu.Nikawasha taa zote za gari langu ili na mimi nimtese dereva wa gari la nyuma.Nikashanga kuona gari mbili za nyuma zikitanda barabarani na kunizuia kupita.Nikaanza kupatwa na mashaka baada ya madereva hao kuanza mtindo wa kupunguza punguza mwendo gafla gafla na usipo kuwa makini unazigonga kwa nyuma.
Kwa mbele likawa linakuja lori ikatulazimu sote kubana upande mmoja kuliacha lipite na mchezo ukarudi na kuwa wa kuzuiana kupita.Hadi tunafika daraja la wami ndio gari hizo zikapunguza mwendo kulikwepa fuso lililo haribika pembezoni mwa barabara
Tukalimaliza daraja,nikaona jamaa wananichelewesha nikamuomba dereva wa nyuma kuweza kupita akaniruhusu,Nikiwa ninamaliza kuliacha gari la nyuma gari la pili kutoka mbele likatanda barabarani na kuongeza mwendo.Dereva wa gari la nyuma akaongeza kasi zaid na kutanda kwa nyuma wakawa wameniweka katikati.Kwenye kioo kidogo kilichopo pembeni ya mskani kwenye gari langu nikaanza kuwaka taa nyekundu na kutoa maandishi yaliyo andikwa kwa herufi kubwa.
{HABARI YAKO BWANA EDDY,GARI YAKO IPO KWENYE WAKATI MGUMU WA USALAMA.KAMA UNATAKA ULINZI MINYA HAPA AU UNAWEZA KUKATA}
Nikaminya sehemu yenye alama ya tiki(pato).Sikushangaa sana kwa maana hili gari aina ya BMW 007 limetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu na ninakumbuka Sheila aliniambia kwamba amepewa na Wamarekani weusi alio cheza nao filamu ya ngono.Gari ikaanza kurudi chini kidogo kisha vioo vyote kasoro cha mbele vikapitiwa na ukungu mweusi ambao sikujua ni wa nini.
Kwenye kioo kidogo nikaona gari la mbele na la nyuma,nikaonyeshwa jinsi zivyo ndani na idadi ya watu waliomo ndani wakiwa katika hali ya mifupa(mafuvu).Nikiwa ninashangaa shangaa nikastukia nikigongwa na gari ya nyuma na kunifanya nishindwe kulizuia gari na likamgonga gari la mbele.
Nikastukia kuona jamaa wawili kwenye gari la mbele wakichomoza kwenye vioo vya pembeni na kuanza kunishambulia kwa kutumia bunduki zao,Kitu kilicho nistaajabisha ni jinsi risasi hizo kushindwa kuingia ndani ya gari langu.Nikaanza kujiamini kuwa gari yangu imepata kweli ulizi,Nikakanyaga breki za gafla na kusababisha gari la nyuma kunigonga na kuanza kuzunguka barabarani kwa kasi na kuacha njia na kuvaamiti iliyopo pembezoni mwa barabara na kupinduka.Nikaachia breki na kulifukuzia gari la mbele ambalo kidogo liliniacha kutokana na mwendo wao wa kasi,Nikalisogelea kwa ukaribu,kila ninapo jaribu kulipita wananizuia.Nikaongeza mwendo,kutokana na gari yangu kuwa chini kidogo likaweza kupiga tairi za nyuma na kulifanya linyanyuke kidogo na dereva wake kushindwa kulimudu na kuanguka vibaya na kuanza kubingirika likiingia msituni.
Gari la mbele likapunguza mwendo na kutokana lipo mbali kidogo na mimi, likafunga breki za nguvu na kwa utaalamu mkubwa dereva wa gari hilo aliweza kuligeuza na likawa limegeuka nilipo mimi.Nikapunguza mwendo hadi nikasimama mita chache kutoka lilipo gari langu.Derevaa wa gari lililopo mbele yangu akaanza kuvuta mafuta huku akiganyaga breki na kuzifanya tairi za gari lake kuzunguka kwenye lami pasipo kwenda mbele na kuzifanya zitoe mlio fulani.Nikazima taa za gari langu na dereva akazima za kwake.Nikawasha za kwangu ila nikajikuta nikinshangaa dereva wa gari hilo kwani anafanana sana na Manka japo simuoni vizuri ndani ya gari hilo.Gafla nikalishuhudia roli linalo malizia kona iliyopo karibu na lilipo simama ‘Hammer’,Sikujua kama dereva wa Hammer ninaye mfananisha na Manka kama ameliona lori hilo au la kwani anaendelea kuzifunga breki za gari lake katikati.Nikazisika honi za lori zikimuashiria dereva wa Hammer kuondoka barabarani,ndani ya sekunde kadhaa nikastukia kuona lori likiligonga kwa nyuma Hammer na kulisogeza pembeni ya barabara na lori likapita pasipo kusimama.
Ukimya ukatawala kesemu nzima,nikataka kuondoka ila nikataka kujua niliye muona ni Manka kweli au sio yeye.Nikalisimamisha gari pembeni,nikaichomoa bastola yangu,nikafungua mlango na kushuka ndani ya gari.Nikatazama pande zote za barabara hapakuwa na gari lolote linalo kuja.Nikaanza kutembea kwa mwendo wa tahadhari hadi sehemu lilipo anguka gari la watu ambao ninahisi sio watu wazuri.Nikalisogelea taratibu.Nikachunguza ndani na kumuona mtu moja aliye kaa pembezoni mwa dereva akiwa amekitwa na kisiki cha mti kwenye kichwa na amefariki hapo hapo,Siti za nyuma zilijaa maboksi makubwa na hapakuwa na mtu wa aina yoyote.Dereva wa gari ambaye ni mwanamke aliendelea kujitahidi kutoka ndani ya gari pasipo kugungua kama mimi nipo eneo hilo.Akasimama huku nywele zake nyingi zikiwa zimemfunika usoni mwake,akakutana na mdomo wabastola yangu.Akajiweka nywele vizuri na nikahakikisha ni Manka kwani akawa ni wakwanza kuliita jina langu
“Eddy”
“Naam”
Tukakosa cha kuzungumza,Uvaaji wa Manka unaashiria kuwa ni jambazi kwani kuanzia juu hadi chini amevaa nguo nyeusi tupu zinazo endana na nguo za jeshi.Mikono yake amevaa gloves nyeusi.Kifuani amejifunga jaketi la kuzuia risasi(bullet proof).Kiunoni mwake anabastola mbili zilizo chomekwa kwa kwenye kiuno
“Umeumia?”
“Hapana”
“Tuondoke”
“Hapana ngoja kuna kitu tusaidiane”
“Nini?”
“Kutatoa haya maboksi”
Sikutaka kuuliza yana nini zaidi ya kusaidiana kwa pamoja kuyatao maboksi mawili makubwa kiasi.Kwa uzuri yakaingia kwenye gari langu siti ya nyuma.Manka akachomoa bastola yake na akaifunga kiwambo cha kuzuia sauti na kuftatua risasi kazaa kwenye tanki la mafuta ya gari lao na likalipuka.Akaingia ndani ya gari langu na safari ikaendelea.Dakika kumi nzima ndani ya gari hakuna aliye msemesha mwenzake.
“Eddy usiku huu unakwenda wapi?”
“Arusha”
“Kuna nini?”
“Kuna ishu ninakwenda kufanya na wewe je?”
“Nitakuambia tukitulia”
“Boksi zina nini?”
“Pesa”
“Pesa.....!!?”
“Ndio”
“Za nani?”
“Ndio maana ninakuambia nitakuambia tukitulia”
Nikazidi kuongeza mwendo na ndani ya masaa mawili tukawa tumefika Arusha.Tukafika hadi kwenye mtaa wa wachaga na tukaingia kwenye moja ya nyumba iliyo tulia sana.Manka akashuka kwenye gari na kufungua geti na mimi nikaliingiza gari ndani akafunga huku akitazama pande zote kisha akalifunga geti.Akafungua mlango wa nyumba hiyo na tukayaingiza maboksi yote ndani.Tayari mwanga wa jua ulisha anza kuchomoza kwa mbali ikiashiria ni asubuhi
“Oya mimi ngoja nikapige mishe ninayo itaka kisha nitakustua”
Nilimuambia Manka ambaye alianza kukata biksi moja kwa kutumia kisu.Nikashuhudia vibunda vya elfu kumi kumi vikiwa vimejaa ndani ya boksi
“Nimeshatoka kimaisha mpenzi”
“Mmmm....”
Manka akanirushi kibunda kimoja cha pesa kuku vingine akivitoa na kuvirusha rusha juu kwa furaha.Manka akanifwata na kunikumbatia kwa furaha huku akinipiga mabusu mdomoni
“Eddy furaha yangu imekamilika sasa”
“Kwa nini?”
“Nina pesa na nimekupata wewe,nilikutafuta kwa siku nyingi mpenzi wangu”
Wazo la Manka kuwa ni dada yangu likanijia akilini mwangu.Nilipo kumbuka kuwa baba yake ni baba mkubwa nikakaa kimya pasipo kujibu chochote.
“Nikupeleke sehemu ambayo unataka kwenda?”
“Hapana”
“Twendwe wote bwana”
“Ila ubadilishe nguo zako”
“Unadhani sina akili,nilazima nibadilishe”
Manka akaniachia na kuingia kwenye moja ya chumba.Baada ya muda akatoka akiwa amejiremba na mtu unaweza kumsahau kama yeye ndie aliyekuwa akiliendesha gari la majambazi.Nikalitoa gari nje,akafunga geti lake,akaingia ndani ya gari nasafari ikaanza.Nikalisimamisha gari nje ya geti la madam Mery
“Hapa kama napajua?”
“Ni kwa mwalimu wangu mmoja”
“Namjua si yule Mery?”
“Ndio,ila nisaidie kitu”
“Kitu gani?”
“Ninaomba ukagonge”
“Alafu”
Nataka kuingiza gari humo ndani”
Manka akashuka kwenye gari na kuaza kugonga geti,dakika kama mbili gati likafunguliwa na Madam Mery.Wakasimuliana kwa furaha na madam Mery.Kutokana na kufunga vioo vya gari langu madam Mery hakuweza kuniona.Madam Mery akazungumza kidogo na Manka kisha akafungua geti na Manka akarudi ndani ya gari.Nikawasha gari na kuliingiza ndani.Manka akawa wa kwanza kushuka,nilipo hakikisha madam Mery amefunga geti na kuanza kwenda ndani kwake ndipo na mimi nikashuka.Madam Mery akastuka kuniona.Akataka kuingia ndani ila akakutana na John rafiki yangu akiwa amevaa kibukta akiwa tumbo wazi ikiashiria John na Madam Mery wanamahusiano ya kimapenzi.John akapigwa na bumbuazi kana kwamba anasubiria kupigwa picha ya mnato hii ni baada ya kuniona
Sikuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kuzunguka nyuma ya gari,nikafungua buti ya gari na kutaka kulitoa turubai lenye mwili wa Derick,nikafikiri kwa muda kidogo kisha nikalifunga buti pasipo kulitoa turubai
“John niaje?”
“Ahaa....ahaa powa”
John alinijibu kwa kubabaika nikabaki nikitabasamua na kumfwata Manka sehemu alipo simama
“Jamani,hamutukaribishi ndani?”
Niliuliza na kumfanya madam mery kushtuka,akatabasabu kiwoga huku midomo yake ikitetemeka akishindwa hata kuzungumza anacho taka kukizungumza
“Nd...aaaniii kar..ibu....ni”
Manka akabaki akiwa anashangaa kwani hali ya kuzungumza kati ya Madam Mery na John zilibadilika kwa kiasi kikubwa.Madam Mery akaongoza msafara wa sisi kuingia ndani kwake,mtu wa mwisho kuingia ndani nikiwa ni mimi.Nikaufunga mlango na kwabahati nzuri nikakuta funguo ya mlango ikiwa inaning’inia mlangoni.Nilipo hakikisha nimeufunga mlango nikaidumbukiza fungoa mfukoni mwangu na kukaa kwenye moja ya sofa.
“Madma kwako kumebadilika”
Nilizungumza kinafki kwani hapakuwa na mabadiliko yoyote tangu nilivyo paacha siku ya mwisho ninapambana na muwe ndivyo nilipo pakuta.Kikubwa kilicho badililika ni vitambaa vya makochi ni meza mpya ya kioo
“John,masomo yanaendeleaje?”
“Masomo kidogo yapo vizuri”
John alizungumza kwa sauti ya unyonge nayaupole sana,huku sura yake ikiwa inatisama chini kwa aibu anashindwa hata kunitazama usoni
“Sasa,ndio munaingia kidato cha sita?”
“Ndio”
“Hongereni”
Wakati ninazungumza na John.Madam Mery na Manka walikaa kimya wakitusikiliza.Macho yangu nikayahamishia usoni mwa madam Mery ambaye naye hakutaka kabisa kunitazama usoni
“Wenyeji mbona mumepooza gafla?”
Manka alizungumza na kuwafanya John na madam Mery kunyanyua nyuso zao na wakazipamba kwa tabasamu ambalo kwangu ninajua ni tabasamu lililo jaa aibu na ninavyo hisi kila mmoja anaomba ardhi ipasuke na immeze
“Haaa sisi,tunazungumza”
Madam Mery alizungumza manene ambayo kama mtu mzima mwenye akili zake hawezi kuzungumza pumba kama hizi kwa maana kwa muda wote yupo kimya kama amejaza fumba la uji wa bada(uji wa unga wa miogo)
“Ngoja nikawaandalie hata chai wageni wangu”
Madam Mery alizungumza huku akinyanyuka.Nikamtazama na kutingisha kichwa nikiashiri nimekubali akafanye kazi hiyo.
“Manka yule ni rafiki yangu anaitwa John,John huyu ni Manka ni zaidi ya ndugu yangu”
“Nashukuru kwa kumfahamu”
Manka akanyanyuka na kumpa John mkono kama wa kusalimiana kwa mara nyingine tena
“Mimi ngoja niende msalani”
“Sawa”
Nikanyanyuka na kuondoka sebleni na kuwaacha Manka na John.Nikapitiliza moja kwa moja hadi jikoni na kumkuta Madam Mery akiwa ameuegemea ukuta,akionekana kuwa katika mawazo makali na mazito yanayo mfanya ashindwe hata kutazama maji yanayo mwagika kwenye jiko la gesi,baada ya kuchemka sana.Hadi ninazima jiko ndio madam Mery anastuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo
“Unawaza nini?”
“Aahaa hakuna”
“Siku hizi unaniongopea hata mimi?”
“Eheee,”
“Ehee,unaisoma au unaiandika?”
“Tuachane kwanza na hayo,mume wako yupo?”
“Nimeachana naye?”
“Umeachana naye,kisa ni nini kilicho wafanya muachane?”
“Wee acha tuu.Ila kila kitu wewe unakijua?”
“Mimi,mbona kama sikumbuki?”
“Eddy usinikumbushe ya nyuma”
“Kweli? Ok labda nikutokana na kupoteza kwangu kumbukumbu”
Nilizungumza kwa sauti ya upole kwa kumtega Madam Mery.Ukimya wa dakika kama tatu ukapita huku kila mmoja akiwa atamtazama mwenzake
“Mery”
“Una nipenda?”
“Ehee?”
“Unanipenda?”
“Mimi?”
“Wewe,ndio?”
“Ndio”
“Kwa nini umeamua kutembea na rafiki yangu?”
“Ehee.....ahaaa uun....ajua”
“Najua nini?”
“Wewe.....wewe ulikuwa umepotelea wapi sijui?”
“Hujanijibu swali langu”
“Ahaa Eddy tuachane na hilo bwana”
“Sawa.Nataka kuliona kaburi la mwanangu”
“Eheee”
“Hivi hizo Eheee zako ni za nini,Mimi sizipendi bwana”
“Eddy,Sikumzika mwanao”
Nikakaa kimya nikimtazama ni nini anataka kuniambia
“Ila ile siku nilikuwa nimechanganyikiwaa,na nilipomuwahisha mfanyakazi hospitalini.Nilipo rudi nilikuta mbwa wanamalizia kumla mwanao,huku wewe ukiwa umelaa pembeni”
Nikamtazama Mery kwa macho makali yaliyo anza kuchuruzikwa na machozi ya uchungu
“Wewe ni mama wa aina gani,Hujui dhamani ya utu wa kiumbe ulicho kiweka tumboni miezi tisa.Unaacha kinaliwa na mbwaa?”
“Eddy nilichanganyikiwa,Niliucha mlango wa ndani wazi.Na mbwa ile siku msichana wa kazi aliwafungulia na siku zote mchana wanashinda kwenye banda lao”
“Merry nidanganye kwa kingine ila sio kwa hili”
“Eddy ni kweli.Hata mimi ninauchungu moyoni mwangu kuona kiumbe changu kina.....”
Niliunyanyua mkono wangu kwa kasi na kutaka kumpiga madam Mery kofi la shavuni ila nikajizuia kabla halijatua shavuni mwake na kumfanya afumbe macho.Nikaushusha mkono wangu taratibu na kumtazama Madam Mery kwa macho makali nikaachia msunyo mkali,kabla sijazungumza kitu chochote Manka akaingia na akabaki akiwa anatutizama.Nikajifuta machozi na kutoka jikoni na kuwaacha wao wawili
“Naona umeamua kuniridhi kabla sijafa?”
Sauti yangu ilimstua John ambaye nimemkuta akiwa anapiga hatua za kunyata akielekea kwenye mlango wa kutokea huku nguo zake akiwa ameziweka begani
“Mbona unaondoka bila kuaga?”
John hakunijibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kubaki akiwa amesimama kama mlingoti wa bendera.Kwa ishara nikamnyooshea mkono arudi sehemu alipo kuwa amekaa.Akabaki akiwa amesiama asijue nini afanye,Nikaichomoa bastola kiunoni hapo ndipo nilipo mafanya John,kuanguka chini kama mzigo.Akajizoa zoa na kunipigia magoti
“Eddy....ni shetani amenipitia tu,ila sikukusudia mimi kulala na madam Mery”
John alizungumza huku akimwagikwa na machozi
“John,mimi sina ugomvi na wewe.Tutabaki kuwa marafika hadi mwisho wa maisha yetu.Hawa ni wanawake hawawezi kutugombanisha”
Maneno yangu yakamfanya John kuunyanyua uso wake na kunitazama machoni,akayashusha macho yake hadi shehemu ilipo bastola kisha akayarudisha macho yake usoni mwangu.Nikatambua kuwa anaihofia bastola niliyo ishika,Nikaichomeka bastola yangu kiunoni mwangu.Wasiwasi wa John kidogo ukapugua.Nikaunyuosha mkono wangu na kumpa John,akanipa na yeye mkono wake kisha nikamnyanyua na kumvuta juu na kukumbatiana naye.
“Eddy sijaamini ndugu yangu kama nitakuona tena”
“Hata mimi”
“Asante ka.....”
Sikumpa John nafasi ya kuzungumza chochote,kigoti cha mguu wangu wa kulia kikatua tumboni mwake na kumfanya ajikunje na kutoa ukulele mkoali.Nikamsukuma pembeni kwa nguvu,kwa haraka nikamfwata na kuanza kumpiga mateke ya mbavu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“HIVI UNAJUA UCHUNGU WA MWANAMKE ALIYE BEBA KIUMBE CHANGU?”
“JOHN UNANIJUA MIMI VIZURI,UNAJUA NI KITU GANI AMBACHO NINAKIFANYA KWA WALE WANAO JARIBU KUNIIBIA KITU CHOCHOTE KUTOKA KWANGU”
Nilizungumza kwa sauti ya juu huku nikiendelea kumpiga John mateke ya mbavu.Kelele za John zikawatoa kwa kasi jikoni Madam Mery na Manka
“Eddy mu......”
Manka alizungumza kabla hajaimalizia sentesi yake,niliichomoa bastola yangu na kumnyooshe na kusimama sehemu alipo.Madma Mery kwa haraka akarudi nyuma ya Manka na kujificha mgongoni mwake.
“Eddy kuwa mpole mpenzi wangu.Kwa nini unafanya hivyo?”
“Manka mimi sio mpenzi wako”
Manka akakaa kimya akinitazama kwa umaki akishindwa cha kuzungumza.Nikamtazma John ambaye amejikunja chini huku akilia.Nikairudisha bastola yangu kiunoni nikampiga John teke jengine la mbavu
“USIRUDIE”
Nikampa John mkono,akabaki akinitazama kwa woga.Nikainama na kuushika mkono wake kwa nguvu na kumyanyua na kumkumbatia
“Wanaume huwa ahtulii”
Nikamuachia John na kumkalisha kwenye sofa.Nikawageukia Manka na Madam Mery,tukatizamana kwa muda
“Mbwa wako wapo wapi?”
“Huko nyuma”
Nikatoa funguo na kufungua mlango na kutoka nje.Nikazunguka nyuma ya gari na kufungua biti ya gari na kutoa turubai lenye mwili wa Derick.Manka akatoka na kusimama mlangoni na akabaki akiwa amenitazama
“Umebeba nini?”
“Unataka kuona?”
“Ndio.”
“Muite huyo mwenzako”
“Nani?’
“Huyo Mery”
Manka akamuita Madam Mery,Madam Mery akatoka akiwa katika hali ya kiunyonge
“Shosti umeniambia umbwa wako wapo wapi?”
“Huku nyuma”
“Nimewaletea chakula,twende basi ukanionyeshe”
Madam Mery akashuka kwenye kibaraza na kuongoza kwenda nyuma ya nyumba yake kwenye mabanda ya mbwa.Kwa uzuri wa yumba ya madam Mery imezungushiwa ukuta ulio mrefu na si rahisi kwa mtu wa nje kuweza kuona chochote kinacho endelea ndani.Nikakuta mabanda manne nyenye mbwa wengi wakubwa kwa haraka ninaweza kuwafananisha na mbwa wa jeshi la polisi kitengo cha kutuliza ghasia(F.F.U)
“Mbwa walio mla mwanagu ni wapi?”
“Hao kwenye hilo banda kubwa”
“Mbona una mbwa wengi hivi”
“Huwa ninawauzia wachina,mbwa mmoja naweza akafka hata dola elfu tatu”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya unyonge.Nikaliweka turubai chini kabla sijalifungua,Manka akaniita
“Eddy naomba funguo za gari,kuna kitu nataka nikachukue ndani ya gari”
Nikaanza kujipapasa mfukoni,wakati ninatoa funguo simu ya mume wa madam Mery ikaanguka.Manka akataka kuiokota ila nikamzuia,Nikamkabishi Manka funguo
“Hakikisha John aondoki”
“Sawa”
Manka akaondoka na kumfanya Madma Mery kubaki kimya akiitazama simu ya mume wake kwa umakini hadi sura yake ikatengeneza mikunjo.Nikaiokota simu na kumpa Madam Mery
“Naomba unishikie hii simu”
“Eddy,hii simu kama ya mume wangu?”
“Ahaaa...wewe si umesema umeachana naye?
“Ahaaaa eheeee”
Madam Mery akabaki akinitazama,Nikalifungua turubai,nikamtazama machoni madam Mery na akastuka kuona viungo vya mwili wa mtu kwenye turubai nililo lifungua.
“Mbwa yupi likuwa mmero kwa kumtafuna mwanangu?”
Madam Mery akabaki akiwa anashangaa shangaa,nikaokota kipande cha mkono na kukirushia ndani ya banda la mbwa wakakivamia na kukigombania kwa haraka na kuanza kukila
“Kwa msosi huu lazima mbwa mmoja utamuuza hata kwa dola elfu kumi”
Madam Mery akabaki akiwa ameuziba modomo wake kwa kiganja cha mkono wake wa kulia.Nikachukua vipande viwili na kuvidumbukiza kwenye banda
“Ed.....si ni mume wangu?”
“Shiiiii,mume wako yupi? Wewe si umeachana naye?”
“Eddy mtu wako nimemfunga kamba,nilimkuta anataka kukimbia”
Manka alizungumza huku akisimama na kujishika kiuno na macho yake yakiwa kwenye turubai
“Eddy si mwili wa mtu huo.....!!?”
Manka alizungumza kwa mshangao
“Kwani vipi?”
“Umeutoa wapi?”
“Wee acha tuu”
“Ni mume wangu”
Madam Mery alizungumza huku akikaa chini,Gafla akaanza kutapika baada ya kuona ninatoa kipande cha utumbo ulio kauka na kuingiza kwenye banda la mbwa.Nikavirusha vipande vyote vya mwili wa Derick kwenye mamanda yote ya mbwa.
“Hichi kichwa Madma utachemsha kama supu ya mbwa wako”
Manka akanitazama kuanzia chini hadi juu,Madam Mery akazidi kutapika.
“Eddy you’re a Mouster”
Manka alizungumza huku akinitazama kwa macho makali.Akamnyanyua Madam Mery.Wakanza kuelekea ndani,Kichwa cha Derick nikakirudisha ndani ya turubai na kulibebe turubai langu na kulirudisha ndani ya buti la gari.Nikaingia sebleni na kumkuta madam Mery akiwa amelazwa kwenye sofa kubwa huku mwili mzima ukimtetemeka
“John yupo wapi?”
Nilimuuliza Manka,ila akakaa kimy akabaki akinitazama kwa hasira.
“Manka si ninaungumza na wewe?”
“Kamtazame huhko jikoni”
Nikaichukua simu ya Derick ambayo Madam Mery ameiweka pembeni ya sehemu aliyo lala
“Sory madam,nilifanya hivi kwa ajili ya damu yangu”
Nikaingia jikoni na kumkuta John akiwa amefungwa kama za mkono na miguuni huku amelazwa chini kifudifudi.Nikakaa pembeni yake
“John shule kunasemaje?”
Nilizungumza kwa dharua,huku taratibu nikimshika shika kichwa chake
“Eddy mbona umekuwa katili kiasi hichi,Unamtuma huyu mwanamke wako kunifunga hivi kama mwizi”
“Wewe unajionaje,Si ni mwizi.Laiti kama ungekuwa hujaniibia madam Mery haya yote yasinge tokea”
“Sawa Eddy,najua kama nimekuumiza ila si kunifanyia hivi.Laiti kama ungejua wema nilio kufanyia wala usinge nifanyia hivi”
“Wema gani?”
“Eddy mimi nimekufanyia mitiahani yako ya kuingia kidato cha sita na umefaulu vizuri”
“Kivipi,wakat wewe una mitihani yako?”
“Eddy mimi nilimuhonga mwalimu wa academy.Aliniruhusu nikufanyie mitihani.Sasa jana wakati ninakuja kumuuliza Madam Mery kuwa anataarifa yoyote kuhusiana na wewe ndipo alipo nishawishi hadi nikalala naye.Halikuwa kusudio langu mimi kufanya hivyo.Kwa bahati mbaya leo wewe ukaja na kutukuta katika mazingira kama hayo”
John alizungumza kwa upolenhadi roho ya huruma ikaanza kunijaa moyoni mwangu
“Eddy,wewe ni zaidi ya ndugu yangu.Kumbuka wapi tulipo toka.Kuanzia kidato cha kwanza tupo pamoja.Hadi sasa hivi,kwa nini lakini ndugu yangu”
“Ila John...wewe tangu kidato cha kwanza.Unajua jinsi nilivyo,mtu yoyote anaye jaribu kuniibia mimi kitu changu chochote nilazima akilipe kwa njia yoyote”
“Ndio ninalijua hili,Na madam aliniambia kitendo cha yeye kufanya hivi ni juzi,alimpigia mumuwe na akapokea mwanamke na akatukanwa sana ndio maana akaamu kunishawishi mimi”
“John.....”
“Naam”
“Nakuomba unisamehe kaka”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika
“Usijali kwa hilo kaka,ninatambua umefanya hivi kwa ajili ya hasira tuu”
“Ni kweli”
Nikaanza kumfungua John kama moja baada ya nyingine.Nikasimama na kumsaidia kumyanyua.
“Mbavu zinaniuma sana”
“Pole,nikupeleke hospitalini”
“Ahaa wee acha tuu nipo vizuri”
Jinsi John anavyo zungumza nilijihisi vibaya moyoni mwangu,nikaanza kujilaumu ni kwa nini nimempiga John pasipo kumuuliza chanzo cha yeye kunisaliti.Tukarudi sebleni na kumkuta madam Mery akiwa amelala na Manka akiwa pembeni yake.Manka akanyanyuka na kunishika mkono na tukatoka nje
“Eddy,japo mimi ni katili ila wewe umezidi”
“Manka naomba hiyo mada uiache”
“Eddy hata kama.Mwili wa binadamu mwenzako unaukausha kama nyama nya ng’ombe”
Nikaanza kumuadisia Manka kuanzia mwanzo wa ugomvi kati yangu mimi na Derick.Hadi ninamaliza kumuadisia Manka akabaki kimya.Tukakaa nyumbani wa Madam Mery hadi mida ya saa moja waote wanne tukapata chakula cha usiku kilicho pikwa na Manka japo Madam Mery anapata tabu sana ya kula.Mimi na John tukaondoka na kwenda shule nikiliacha gari la kwa Madam Mery.
“Leo kuna welcome form five”
Kawaida kwenye shule yetu kila wanafunzi wa kidato cha tano wanapo jiunga na shule yetu huwa hufanyiwa sherehe wiki tatu baada ya kujiunga na shule.Wezangu ambao nilipotezana nao kwa kipindi kidogo wakaonekana kunifurahia.Mida ya saa mbili tukaingia ukumbini huku nikiwa nimevaa swete lenye kofia.Tuliongozana wanafunzi wa kidato cha sita wapatao nane ila mwalimu ambaye machoni mwangu ni mpya akanisimamisha na kuwaacha wezangu kupita
“Vua kofia ya sweta”
Alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo.Nikiwa ninavua kofia,mkuu wa shule ambaye tunawindana kama paka na panya naye akawa anaingia ndani ya ukumbi huku akiwa ameongozana na mkuu wa shule.Akabaki akinitazama kwa hasira na kuanza kupiga hatua za haraka kunifwa huku mikononi mwake akiwa amekunja ngumi
Nikaanza kurudi nyuma huku nikimtazama mkuu wa shule,akazidi kuja kwa kasi ikanilazimu kusimama nikimtazama kwa umakini.Wanafunzi wote wakawa na hamu ya kuangalia ni nini ambacho atakifanya mkuu wa shule.Hatua chache kabla hajanifikia nikaifunua tisheti yangu sehemu ya kiunoni na kumuonyesha bastola niliyo ichomeka kiunoni.Kidogo akapunguza kasi hadi ananifikia munkari wote ulimuishia.
“Toka katika shule yangu”
Alizungumza huku meno yake ameyang’ata kwa hasira.Nikamtizama na macho makali na ukumbi mzima wa shule upo kimya hata kijiko kikianguka mlio wake utasikika vizuri.
“Sitoki”
Wanafunzi wote wakashangilia,mkuu wa shule akawatizama wanafunzi na wakakaa kimya
“Walinzi mupo wapi?”
Mkuu wa shule alizungumza kwa sauti kubwa,hapakuwa na mlinzi hata mmoja aliye nifwata kila mlinzi aliye niona kuwa ni mimi aliishia mlangoni na kusimama.Mmiliki wa shule akatufwata sehemu tulipo simama na mkuu wa shule
“Jamani,kuweni wapole.Mkuu unaniambisha bwana”
Mkuu wa shule akajifanya kama hamsikii muajiri wake,Kitu kinacho niumiza kichwa ni kwanini mkuu wa shule hadi leo yupo wakati amafanya mambo ya ajabu hadi muda huu hajachukuliwa hatua zozote.Akanisogea katibu yangu,nikastukia kibao kikali kikitua kwenye shavu langu.Nikataka kulipiza nikaisikia sauti ya John ikiniita jina langu na nilipo mtizama nikamkuta John akitingisha kichwa akiniashiria nisifanye chochote
Mkuu wa shule akanitandika kibao cha pili,Ila John akawa na kazi moja ya kuniomba hadi machozi yakawa yanamwagika,nisilipize chochote kwa mkuu wa shule.Machozi ya hasira yakaanza kunimwagika,huku kifua changu kikianza kutanuka kwa hasira kali,Akataka kunitandika kofi la tatu nikamdaka mkono wake.
“NITAKUUA”
Nilizungumza kwa sauti ya ukakamavu,huku macho yangu yakimtazama mkuu wa shule.Akajaribu kuuchomoa mkono wake kutoka kwenye mkono wangu ila akashindwa.John kwa haraka akaja na kuingia katikati yetu na kuniachanisha mkono wangu na mkuu wa shule na kunishika mkono na kuanza kunitoa nje
“Eddy achana naye huyo mzee”
Machozi yakazidi kunimwagika,pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote
“John niachie,tafadhali”
“Eddy siwezi kukuachia,nakujua.Tuliza kwanza hasira”
“John,yule mzee ananitafuta nini mimi?”
“Mpotezee bwana,hajui atendalo”
“John,mama yangu hata siku moja hajawahi kunizalilisha mbele ya watu kwa kunipiga.Sembuse yeye kikaragosi”
“Ndio,naelewa hilo Eddy ila punguza jazba”
Tukaingia kwenye moja ya darasa lililopo chini ya ukumbi kwani ukumbi upo gorofani.John akanikalisha kwenye moja ya kiti na yeye akakaa mbele yangu juu ya meza.Moyo na mwili wangu vyote vikawa vinajisikia vibaya sana kwa kitendo cha kuzalilishwa.Kwani katika maisha yangu tangu nikiwa mtoto sikupenda mtu kunizalilisha wala kunionea.Hata awe ni mkubwa vipi nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kupambana naye hata akinipiga basi ipo siku nitamvizia hata kwa mawe nimpige,ndio maana hadi hapa nimekua bondia mzuri tuu.Nikaichomoa bastola yangu kwa haraka John akanibeta na kunipokonya
“Eddy,unataka kufanya nini?”
“Lete hiyo bastola”
“Ahaa Eddy sikupi”
John alikimbia nyuma ya darasa,huku bastola akiwa ameishika mkononi.Nikamtazama kwa macho makali sana yasiyo pepeseka hata kidogo.Kwa haraka nikatoka mlangoni na kumfungia John kwa nje.Nikakimbia na kuanza kupandisha ngazi za kuelekea kwenye ukumbi.Kitendo cha mguu wangu wa kwanza kukanyaga sakafu ya ukumbini nikatazama wapi alipo mkuu wa shule.Nikamuona akiwa amekaa kwenye meza ya wageni waalikwa akiwa katikati ya waalimu wengine na mmiliki wa shule.Kwa kasi ya ajabu nikakimbia hadi alipo kaa na kujirusha na sote wawili tukaanguka na kiti,mbaya zaidi yeye akangukia mgongo na kunipa mimi nafasi nzuri ya kumkalia kwenye kifua chake na kuanza kumshambulia kwa ngumi zisizi na idadi kwenye uso wake
Kelele za wanafunzi kushangilia zikazidi kuongezaka,Waalimu walio karibu yetu wakaanza kunivuta,kuniachanisha na mkuu wa shule.Wakanisimamisha na kunipeleka pembeni.Mkuu wa shule akasimaa huku akitaka kunifwata ila waalimu wezake wakanizuia.Ukumbi mzima wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita wakawa na kazi ya kunishangilia huku wakilitaja jina langu na kupiga makofi
“EDDY......EDDY........EDDY........EDDY”
Mkuu wa shule akawazidi nguvu,waalimu walio mshika na kuja kutuvaa na waalimu ambao wamenishika mimi.Sote tukaanguka chini,kabla mkuu wa shule hajafanya chochote nikamuwahi kumdaka shingo na kumpiga kabali.Akaanza kunishindilia ngumi za mbavu,nikamuachia shingo yake na kumsukuma pembeni na kunyanyuka juu kidogo.Akanyanyuka kwa kasi na kunifwata,kabla hajanifikia nikaruka juu kwa kutumia mguu wangu wa kulia,nikautulisha kwenye kifua chake na kumuangusha chini.Waalimu wakaendelea kutushika,kelele za wanafunzi wezangu zikazidi kuongezeka.Hata ambao wawanijui vuzuri,nao pia wakawa katika mkombo wa kushangilia
“Nitakuua wewe kijana”
Mkuu wa shule alizungumza huku akiwa ameshikwa na wezake kwa nguvu.Nikabaki nikitabasamu kwa dharau zaidi nikamnyooshea kidole cha kati kama tusi.Ndio nikawa nimemfungulia hasira zake zote.Akajibabadua mikononi mwa waalimu wengine na kunifwata.Nikasikia mwalimu mmoja aliye nishika akiwaambia wezeke
“Hembu muachieni tuone atakacho kifanya,Mzee mgomvi kama nini”
Wote walio nishika wakaniachia,ila wakawa wamechelewa kwani mkuu wa shule alishafika mbele yangu na kuachia ngumi nyingi zilizo nijia kwa kasi mwilini mwangu.Kikubwa cha kwanza nilicho jilinda nacho ni sura yangu,Mikono yangu ikawa na kazi ya kuzizuia ngumi hizo zisiingie sana kwenye mwili wangu.Jinsi ninavyoziuia ngumi zake ndivyo jinsi ninavyo mpata wakati mzuri way eye kuzirusha ngumi zake.Nikaona ni ujinga
“Bora ngumi kumi kuliko mia”
Ni usemi ambao Mzee Godwin kipindi alipo kuwa akinifundisha kupigana utotoni alipenda sana kuniambia,akimaanisha nibora kupigwa ngumi kumi kuliko ukazuia ngumi miamoja.Nikaanza kuiruhusu mikono yangu kufanya kazi ya kumshambulia mkuu wa shule.Kila ngumi ambayo niliirusha sikukosea sehemu ya kupiga,kila ambapo ninahitaji kupapiga ndipo nilipo papiga.Nikaanza kumuona mkuu wa shule akishinda kustahimili,Nikazidi kuongeza kasi ya mashambulizi,Ngumi kama nne zikatu sehemu za njuu kwenye jicho lake la kulia na kuifanya sehemu hiyo kuchanika na kutoa damu nyingi.Mkuu wa shule akaanza kuyumba yumba akionekana kuchanganyikiwa
Nikampiga mtama ulio muangusha chini,akajaribu kunyanyuka ila akshindwa.Nikataka kumkanyaka kifuani,kwa haraka akanyanyua mikono yake juu
“EDDY NISAMEHE,NIMEKUKUBALI”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kauli yake ikasikiwa karibi na wanafunzi wote,ukumbi mmzima ukanyanyuka kwa furaha,Wanafunzi walio na simu ambazo haziruhusiwa shuleni ila kwa furaha wakazitoa na kuanza kupiga picha,huku wengine wakirekodi tukio zima.Walinzi wakamsimamisha mkuu wa shule na kumtoa nje ya ukumbi.Baadhi ya waalimu ambao wakikuwa wamenishika wakaanza kupiga makofi,ila mmiliki wa shule alipo watazama wakaacha mara moja na kujifanya wakiwanyamazisha kelele wanafunzi ambao hawakuacha kuficha furaha zao.Japo nimeumia baadhi ya sehemu katika mwili wangu ili nikabaki nikiwa nimesimama mbele ya wanafunzi wezangu huku nikiwa ninahema sana.Nikawanyamazisha wanafuni wezangu na wakakaa kimya wakisubiri nizungumze
“Rafiki zangu,ndugu zangu,nawashukuru sana kwa upendo wenu.Ninaimani kwa kitendo hichi nilicho kifanya,sizani kama sheria za shule zinaniruhusu mimi kuwa mwanafunzi halali wa hii shule”
“Nawatakia masomo mema na mungu awalinde”
Ukumbi mzima ukawa kimya,macho yangu yakawa na kazi ya kuwatizama wanafunzi wezangu.Kuna baadhi ya wasichana wa kidato changu wakashindwa kuyazuia machozi yao na kujikuta wakiwa wanamwagikwa na machozi.Mwalimu wa nizamu akanitazama kwa macho ya masikitiko kisha akawatazama wanafunzi wengine
“Wewe,wewe leteni simu zenu”
Mlwalimu wa nidhamu aliwanyooshea wanafunzi wawili walio zishika simu zao,wengine kwa haraka wakazificha.Wanafunzi walio itwa wakabaki wakimtazama mwalimu wa nizamu.
“Hamunisikii?”
“BOOOOOOOO”
Wanafunzi wote wakaanza kumzomea mwaliwa na nizamu,
“Tunataka haki zetuu...tunatakaaa hakizetu”
Wanafunzi mmoja alianza kuimba na wengine wakaitikia,sauti zikaendelea kurindima kwenye ukumbi,Sikujua ni haki gani ambayo wezangu wanaitaka.
“Waambie wezako wanyamaze bwana”
Mwalimu wa nizamu alizungumza kwa sauti ya kuninong’oneza huku akiwa na wasiwasi mwingi sana.Kwa jinsi ninavyo wajua wanafunzi wezangu,muda wowote anaweza kuanzisha fujo.Nikajaribu kuwanyamazisha na kweli wakanyamaza na kila mmoja nikamuomba kukaa kwenye kiti chake na wakatii
“Jamani,munataka nini?”
Niliwauliza na karibia kila mmoja akanyoosha kidole juu akiomba nafasi ya kuzungumza.Nikamchagua mwanafunzi mmoja akasimama na wengine wakakaa kimya
“Kaka Eddy kwanza hatumtaki mkuu wa shule”
“NDIOOOOOO”
Wakaitikia wote kwa furaha
“Pili tangu hii shule tumefungua,chakula tunacho kula ni kibovu,sio kama pale awali.Sasa hizo milioni mbili za ada kazi yake ni nini?”
“Semaaa babaaaa”
Msichana mmoja aliropoka kwa sauti ya juu
“Yangu ni hayo kaka”
Nikamchagua mwengine na akasimama
“Kaka Eddy kwa niaba ya wezangu,kwanza tunakuomba urudi shule.Pili tunakuteua kuwa kaka mkuu wa shule kuanzi sasa hivi”
Ukumbi mzima ukanyanyuka kwa furaha,Sikuamini na ukorofi wangu wote kama ipo siku nitakuja kukubalika shule nzima.Mwalimu wa nizamu akabaki kimya asijue nini cha kuzungumza
“Jamani asanyti kwa uchaguzi wenu.Ila swali langu ni Je nitaruhusiwa kurudi shule?”
“Ndiiooooo”
Lengo la swali langu,alijibu mwalimu wa nazamu ila nikashangaa wakijibu wanafunzi wezangu.Nikamgeukia mwalimu wa nazamu akabaki akiduwaa
“Ndio....ndio....ndio.....ndio”
Wanafunzi wezangu walipiga kelele za ‘NDIO’.Mwalimu wa nizamu akakubali kwa kunijibu Ndio
“Ila siku utakayo rudi uje na mzazi wako”
“Sawa”
Ratiba nzima ikavunjika,kama kaka mkuu mpya wa shule nikamuomba DJ kufungulia mziki na wanafunzi wakaanza kuserebuka.Furaha ikarudi moyoni mwangu,baadhi ya rafiki zangu wakanifwata na kunipongeza,Nikakumbuka kuwa John nimemfungia darasani.Nikaanza kushuka kwenye ngazi za kuelekea madarasani.
“Eddy...Eddy”
Nikasikia sauti ya kike ikiniita,nikageuka nyuma na kumkuta msichana mmoja ambaye sikuwahi kumuona siku hata mmoja ila sketi aliyo ivaa nikatambua watakuwa ni miongoni mwa wanafunzi wapya walio jiunga na kidata cha tano
“Samahani mwaya kaka Eddy”
“Bila samahani”
“Ninaitwa Hellen,najua utakuwa hunijui?”
“Ahaa umesha niambia jina lako,ndio nimesha kujua”
“Kweli kaka,nimeona nikikaa kimya pasipo kukupongeza nahisi leo nisinge lala vizuri”
“Kwa nini?”
“Ahaa sijawahi kuona mwanafunzi anaye jiamini kama wewe”
“Asante”
“Naweza kukupa zawadi?”
“Ndio”
Hellen akanifwata taratibu na kunibusu shavuni
“I LIKE YOU”
Alizungumza kwa sauti nyororo na taratibu akaondoka huku akinipiga busu la upepo(busu la mbali) huku akikichezesha kiganja chake cha mkono wa kulia akiashiria kuniaga.Nikaachana na Hellen na kufika katika mlango wa darasa nililo mfungia John.Nikaingia ndani na sikumkuta John,kabla sijatoka nikastukia meza iliyopo nyuma ya darasa ikianguka na John akasimama huku bastola akiwa ameielekezea kwangu
“EDDY NAKUUA,NALIPIZA KWA KILE ULICHO NIFANYIA LEO ASUBUHI”
John alizungumza huku akiwa anamaanisha kile anacho kizunguma kwani macho yake yamekuwa mekundu na machozi membaba yanachuruzika kwenye machavu yake na sura yake ikiwa imetawaliwa na mikonjo na tangu niwe na urafiki na John sikuwahi kumuona katika hali kama hii
Nikabaki nikimtazama John kwa macho yaliyo jaa mshangao mwingi.Nikajaribu kupiga hatua moja nyuma
“Ukisogea nakuchangua ubongo wako”
John alizungumza huku jasho likiwa linamwagika huku akitetemeka mwili mzima,nikameza fumba la mate ili kusawazisha koo langu kabla sijazungumza chochote
“John wewe leo hii ni wakunishikia mimi bastola?”
“I don’t care”(Sijali)
“Even if,remember am your friend......Real friend”(Hata kama,kumbuka mimi ni rafiki yako.....tena rafiki yako wa kweli)
Nilizungumza kwa hisia kali,kwa sauti ya chini sana ya unyenyekevu,kwa mbali machozi yakinilenga lenga
“Eddy usiniigize mkanda wa kuigiza,wewe nikatili sana wewe ni muuaji,wewe ni hustahili kuishi kwenye hii dunia.Kumbuka ulimuacha yule dereva wa watu wa shule aliye pata ajali,alikufa mikononi mwangu,kisa ulikuwa unamuendekeza yule Malaya wako Salome”
John alizungumza kwa uchungu,huku sauti yake ikiwa imebadilika sana.Ucheshi wote ulimpotea
“John,kumbuka tumefanya mambo mengi.Kumbuka ‘O’ level wewe uligongwa na nyoka tukiwa shamba la shule,Ni nani aliyekuwa wa kwanza kuyaokoa miasha yako”
Nilizidi kuzungumza kwa sauti ya upole sana kwani nikifanya ujinga wowote John anaweza akanifumua kichwa
“Hiyo sio kigezo Eddy,wewe sio rafiki wa kweli.Wewe ni muuaji Eddy”
Nikakosa cha kuzungumza,ikanilazimu nianze kutafuta njia nyingine ya kuepukana na tatizo lililopo mbele yangu.Nikaikazia macho bastola aliyo ishika John,nikavitazama vidole vyake nikagundua hakuna kidole hata kimoja kilicho ingia sehemu yenye traiga ya kufyatulia risasi,nikashusha pumzi nyingi na kutabasamu.Nikaanza kupiga hataa moja baada ya nyingine mbele huku nikiwa nimejiamini kupita maelezo
“Eddy ukinifwata nitakuua,ninakuapia haki ya Mungu”
John alizungumza kwa kubabaika,nikazidi kupiga hatua mbele zaidi huku macho yangu yakiwa kwenye vidole vya vilivyo ishika bastola.Hatua mbili kabla sijamfikia akakiingiza kidole kimoja kwenye sehemu yenye traiga ikanilazimu kusimama kama namba moja
“Eddy rudi nyuma,Moja........Eddy rudi nyuma,Mbili......”
Sikumpa nafasi John aendele na mchezo wake wa kunihesabia namba zake kama mtoto mdogo.Urefu wangu ukanisaidia kurusha teke lilikoupiga mkono wa John wenye bastola na ikaangukia pembeni kwenye meza na viti.John akataka kuikimbia bastola sehemu ilipo simama ila nikamuwahi kumshika shati lake na kumvuta nyuma hadi akaanguka chini.Nikaiwahi bastola na kitu cha kwanza nikaichomoa magazine na kuiweka mfukoni
John akanyanyuka na kunifwata kwa hasira hadi sehemu nilipo simama,akataka kunipiga ngumi,nikaikwepa na kurudi nyuma hatua haraka nne na kuacha umbali kidogo
“John usimtafute Mungu maneno”
Nilizungumza huku nikimtaza John machoni,hakunisemesha chochote zaidi ya kuendelea kuhema kwa hasira,Ili kuepusha mafarakano nikaanza kupiga hatua kuelekea mbele ya darasa kwenye mlango,Hellen akaingia akachungulia kwenye mlango
“Eddy nilikuwa ninak.......Eddy nyuma yakoo”
Nikageuka kwa haraka na kukutana na kiti alicho kirusha John,kwa juhudi zangu zote nikajitaidi kukikwepa kiti,ila nikawa nimechelewa na sehemu ya kuegemea kwenye kiti alicho kirusha John ikanipiga puani na kuniangusha chini.Kizunguzungu kikali kikanikamata huku damu zikaanza kunitoka puani.Nikajaribu kunyanyuka ila nikashtukia teke la kifua lililo nilaza chini
“Wee kaka,muachie mwenzako”
Hellen alizungumza huku akiwa amemshika mkono John,kofi zito likatua shavuni mwa Hellen na kumuangusha chini huku akito ukele mmoja tuu akatulia.John akanigeukia na kutaka kunivamia ila nikajitahidi hivyo hivyo kumpiga teke kwenye miguu yake na akaanguka chini.Nikajikaza kumtazama ila machoni mwangu ninaona vitu vya ajabu ajabu(mawenge mawenge) na kwambali ninaona vitu vilivyopo humu ndani ya darasa.John akaniwahi kunikalia kifuani na kanza kunitandika ngumi za uso nilizo zizuia kwa mikono yangu.
Nikauingiza mkono wangu mmoja ndani ya mfuko wenye magazine ya bastola na kuichomo,nikaishika vizuri na kumpiga nayo John ya kichwa na akaangukia pembeni.Sote tukabaki tukiwa tumelala huku mimi nikiwa ninatafuta chanel ya kichwa changu irudi vizuri kwani hadi sasa hivi inasoma no signal(hakuna mwasiliano).Nikaanza kujihisi vizuri kwa msaada wa ukuta nikaasimama huku ninayumba kama mlevi aliye pitisha kiwango cha ulevi.Nikatafuta kiti na meza,nikakaa huku kichwa changu nikiwa nimekilaza kwenye meza na damu za pua taratibu zikawa zinamalizikia kutoka.Nikashusha pumzi mara kadhaa na kusimama juu.
Nikamtazama John na kumuona akiwa anayafumbua fumbua macho yake,Hellen bado emejikunyata chini.Nikaiokota magazine na kuanza kuitafuta ilipo bastola.Nikaiona bastola na kuikota.Nikaichomeka magazine na kurudi kwenye kiti nilichokuwa nimekikaa na kusubiria John aamke.John akakaa kitako na kunitazama huku kwenye kichwa chake akivuja damu sehemu ya upande wa kichwa nilipo mpiga na magazine ya bastola
“John,ni nani aliye kuroga?”
John hakunijibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuendelea kunitazama.Tukatazamana na John kama dakika mbili kisha nikacheka kichoko cha kejeli na kusimama na kumpita.Nikachuchumaa na kumtazama Hellen
“Hellen”
“Mmmm”
“Amka”
Hellen akainuka huku akiwa na mawenge mawenge
“Unajisikiaje?”
“Ehee”
“Unajisikiaje?”
“Mmmmm”
Nikajua bado Hellen anakiwewe,nikamnyanyua na kumkalisha kwenye kiti na kumtazama John ambaye alianza kulia pasipo kuwa na sababu ya msingi
“Hujaingia kwenye idadi ya watu ninao wachukia na usitake uingie kwenye idadi hiyo”
Nikafungua mlango wa darasa na kuondoka huku bastola nikiichomeka kiuoni na kuifunika na sweta nililo livaa,nikashusha ngazi za gorofa la shule na kueleka zangu nyumbani kwa madam Merry.Kabla sijafika nikakuta gari ya polisi ikiwa nje ya nyumba ya geti la madam Mery.Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio,nikarudi nyuma na kutafuta sehemu yenye nyumba nikajibanza na kuangalia kitu kinacho endelea.Nikamuona Manka na Madam Merry wakiwa wanatoka kwenye geti wakiwa wanazungumza na askari mmoja.Wakasimama kwa muda nje huku wakizungumza na mimi
Askari akawaaga na akaingia kwenye gari na kuiwasha na kuondoka,nikawasubiri waingie ndani ya geti.Nikakimbia kwa kasi hadi kwenye geti na kulipiga kikumbo kabla Manka hajalifunga vizuri.Mstuko wa geti kufunguka ukamstua sana Manka na madam Mery.
“Yule ni nani?”
Wote wakaa kimya wakinishangaa kwani sweta zama limejaa damu
“Si ninawauliza nyinyi kenge,yule ni nani?”
“Mumekwenda kunistaki sio?”
Wakatazama,pasipo kunijibu swali langu.Nikichomoa bastola na kuwaishika mkono wa kushoto,kwani ni mkono wangu wenye nguvu kuliko mkono wa kilia.
“Eddy,sisi yule askari ni rafiki yetu tuu na naa......”
Manka alinijibu huku akipata kigugumizi cha hapa na pale
“Yaani wewe Manka leo hii ndio unaamua kwenda kunistaki polisi si ndio?”
“Hapana....yule ni naniliuuuu”
“Naniliuu nani?”
“Eddy mpenzi wangu ni.....”
“Wewe Mery koma mimi sio mpenzi wangu.Manka tambua mimi ni ndugu yako,Baba yangu ni baba yako sasa wewe endelea ku........”
Nikasikia milio ya magari polisi kwa mbali kidogo ikionekana kuja ilipo nyumba ya madam Mery.Nikaacha mazungumzo na kwaharaka nikaingia ndani ya gari na kuliwa,Madam Mery na Manka wakakimbilia ndani.Nikakanyaga mafuta kwa nguvu huku nimekanyaga breki na kuyafanya matairi ya gari kusereleka chini,nikalitazama geti lililo jifungua kidogo,nikajifunga mkanda wa siti yangu ya dereva na kushusha pumzi nyingi zilizo changanyikana na vichembe chembe vya damu vilivyo toka puani mwangu.Nikaachia breki za gari na kulifanya liende kwa kasi na kugonga geti na kufumba na kufumbua nikajikuta nikiwa nje huku geti ni kiwa nimelivunja.Nikakanyaga breki galfa na kuifanya gari kuzunguka mzunguko mmoja katikati ya barabara,ulio ifanya gari ya polisi iliyo tangulia kupita kwa kasi.Gari ya pili ya polisi ikanikwepa na kwenye kuuvaa ukuta wa madam Mery.
Uzuri wa gari hili,unaweza kutumia mfumo wa ‘MANUEL’ au ‘AUTOMATIC’ katika uendeshaji wake.Nikabadilisha mfumo kutoka Automatic hadi Manuel ambayo inaniruhusu kuingiza gia mimi mwenyewe tofauti na automatic gia zinajiingiza zenyewe.Kwa kioo cha pembeni nikalishuhudi gari la polisi likikunja kona kwa bahati mbaya likazima na dereva akawa na kazi la kuliwasha
“Muombeni mkuu wenu awanununulie magari mapya”
Nilizungumza huku nikiiachia breki na kuondoka kwa kasi.Namba za mbele na nyuma ya gari langu nikazigeuza kwa kuminya kitufe kinachofanya kazi hii ya kuzibadilisha namba hizi za gari.Sikupanga kurudi Dar es Salaam leo ila ikanibidi kufanya hivyo kwani tayari Arusha nimesha haribu hali ya hewa.Nikafika Moshi na kuendelea na safari yangu,gafla nikaona gari mbili nyeusi zikinifwata kwa nyuma kwa mwendo wa kasi
“Nani hawa?”
Zikazidi kunifwata kwa kasi kubwa,kila ninapojaribu kuongeza mwendo ndivyo nazo zinavyozidi kuongeza mwendo,Hadi nanafika Usangi bado zikawa katika kunifukuzia kwa nyuma.Nikaanza kuchangayikiwa pale gari moja lilipo nikaribia kwa ukaribu sana na kuanza kunigonga kwa nyuma.Nikajitahidi kwa uwezo wangu wote katika uendesha gari na hadi hapa nilipo fikia kwenye mwendi kasi wa miambili na arobaini,pembeni kilipo kioo kidogo kikaanza kunionyeshea vipicha vya watu walio bebe jenaza na kunindikia maandishi ya kuniomba kupunguza mwendo.Katika kona zote nikawa na kazi ya kukanyaga breki kidogo na kukunja mskani wa gari langu kama ni kushoto au kulia
Jasho jingi la woga likazidi kunimwagika japo nimewasha AC(air condition) ambayo inanisaidia kunipepea ila haikufua jasho.Kwa mwendo ninao kwenda nao nimewaacha jamaa kwa umbali kidogo,ila nao bado wanakuja kwa kasi.Hadi ninafika Mombo bado jamaa wananifwata,Akili moja nikawa ninawaza niingie katika kituo cha polisi Mombo kujisalimisha.Ila akili nyingine ikanikataza kabisa kufanya maamuzi ya kijinga kama haya
“Nitakuwa mpumavu”
Nikaendelea kwenda kasi,hadi ninafika Korogwe jamaa bado wananifwata.Machozi yakaanza kunilenga lenga.Sikujua ni kwanini machozi yananilenga lenga.Mtu ukiziona gari zetu unaweza kusema ni mbio za mashindano ya magari
“Hizi sio gari za polisi.”
Nilijisema kimoyo moyo huku nikiendelea kuzitazama kwenye kioo cha pembeni.Muda umeshatimu saa nane usiku,Nikafika segera na kunyoosha barabara ya kwenda Tanga bila kwasha taa ya pembeni inayo niashiria ninaingia wapi,nikakunja kwenye stendi mpya iliyopo hapa Segera na kuzifanya gari hizo zote kupita na ndipo nikagundua ni gari aina ya Range rover ndio maana mwendo wake ni mkubwa sana.Nikatokea upande wa pili wa stendi na kunyoosha barabara ya kweda Dar es Salaam.Nikazidi kukanyaga mafuta,nikaziona gari zilizo kuwa zikinifukuzia kwa nyuma zikija kwa kasi nyuma yangu
“Hawa ni kina nani?”
Nilizungumza kwa sauti ya juu.Nikazidi kuongeza mwendo ndivyo nazo zilivyo zidi kunifwata.Maeneo ya kabuki nikaliona gari kubwa aina ya Scania lilika mbele yangu kwa kasi huku limetanda barabarani.Nikabana upande wa kushoto niliopo ila dereva wa scania naye akabana nilipo,nikarudi kulia naye akanifatwa huko nilipo elekea huku akiniwashia taa zake zote.
Nikaachia msunyo mkali na kuirudiisha gari yangu upande wa kushoto nilipo toka na jamaa akanifwata nilipo,Sikuwa na budi zaidi ya kutoka nje ya barabara kuepika kugongana uso kwa uso na gari hilo.Gari ikaanza kunishinda nguvu badala ya kufunga breki kwa kuchangunyikiwa nikawa na kazi ya kuongeza kasi.Nikastukia gari ikaanza kupiaga kubingiria kwa kasi ya ajaba.Jinsi inavyobingiria ndivyo jinsi ninavyo jigonga ndani ya gari hadi giza jingi likayavaa macho yangu na kutulia kimya
Kwa mbali nikaanza kusikia milio ya ndege,nikajaribu kuyafumbua macho yangu ila kichwa changu nikakuta kinaniuma sana.Nikakajikaza sana na kuyafumbua macho yangu yakakutana na mwanga mkali wa juu unao ingi kwenye kioo cha mbele cha gari langu.Nikajaribu kujichunguza kwa umakini na kugundua mikono yangu imefungwa pamoja na mskani wa gari langu.Kila nanapovuta taswira ya sehemu nilipo,sijawahi kuiona siku hata moja.Miti mirefu iliyopo kwenye eneo zima lililo gari langu likazidia kunichanganya.
Baada ya muda kiogo nikastukia mlango ukifunguliwa na akasimama jamaa mwenye bunduki mbele yangu,huku akiwa amevalia mavazi meusi kuanzia juu hasi chini.Akanitazama kwa umakini kisha akaifungua mikono yangu na kunitoa ndani ya gari na kunitupa chini.Akaninyanyua na kuniweka begani,tukaanza kuondoka pasipo kuwezakujua ni wapi tunapo elekea,Hatua kadhaa mbele nikaona jumba kubwa lililo zungukwa na miti mingi ambayo kwa mbali huwezi kugundua kama kuna jumba kubwa kama hili
Tukaingia ndani na jamaa akanibwa mbele ya watu wapatao ishirini walio shika bunduki zao.Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi baada ya macho yangu kutazamana na Mzee Godwin ambaya jicho lake moja ameliziba na kitambaa cheusi.Mzee Godwin akatabasamua na kumuamuru mtu aliye nilete katika sehemu hii kunifungua mikono yangu.
“Eddy.....Eddy......Eddy my X-Son”
Mzee Godwin alizungumza kwa dharau kubwa huku akinizunguaka taratibu katika sehmu ambayo nimesimama.Kila niliye jaribu kumtazama sura yake haikuonyesha huruma hata kidogo japo kuna wasichana watatu ila nao sura zao zinaonekana zimejaa ukatili mkubwa.Kitu mabacho kinaniumiza
“Usishangae sana kwa maana vita yangu mimi na wewe bado inaendelea”
Kwa haraka ninakumbuka kwamba huyu mzee niliambiwa kuwa amechanganyikiwa sasa sijajua imekuwaje hadi leo anamiliki kundi kubwa la watu kiasi hichi,Gafla mzee Godwin akanipiga mtama ulio niangusha chini vibaya sana na kunifanya niaanze kutoa miguno ya maumivu
“Wewe ndio,chanzo cha kuipoteza mali yangu.Wewe ndio mtu uliye mteka mwangua.Wewe sio mwanangu niambie yupo wapi mwanangu?”
Maswali ya Mzee Godwin yanakizidi kunichanganya kwani sikujua mwanaye anaye mzungumzia ambaye anadai nimemteka ni nani
“Mi...mi mbona sikuelewi?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ahaa hunielewi?”
Mzee Godwin akanipiga teke la kifua na kunifanya nijikunje huku maumivu yakizidi kunitawala kwenye kifua changu.Machozi mengi yakaendelea kunitoka
“Ninakwenda kumuua mama yako?”
“Hapana baba.kumbuka kuwa mama ni mke wako wa ndoa.Mtu wa kuniua ni mimi hapa na wala si mama yangu.Nipo chini ya miguu yako”
Nilizungumaza huku nikiwa nimeishika miguu ya mzee Godwin,akarudi nyuma na kunipiga teke lililo ifanya mikono yangu kuuiachia miguu yake
“Yupo wapi,Manka mwanangu?”
“Manka,yupo Arusha”
“Arusha,Arusha.Ndipo ulip kwenda kumficha si ndio?”
“Hapana baba,mbona Manka yeye ndio aliye watoroka nyinyi?”
“Mimi sio baba yako na Manka mwangu hawezi kunikimbia mimi”
Mzee Godwin alizungumza kwa hasira huku akinitazama,Akamuomba mwenzake mmoja waya wa umeme ambao unene wake ni 1.5,Akaukunja mara mbili na kuanza kunichapa nao kwa fujo huku akinitukana mimi na mama yangu.Nikazidi kulia kwa uchungu mkubwa,maumivu mengi yakazidi kuusonga mwili wangu.Kila ninapojaribu kuizuia sehemu moja ya mwili wangu isichape basi sehemu nyingine ni lazima ichapwe kwa waya huu.Mzee Godwin bila ya huruma akachukua pakti mbili zenye unga mwekundu na kuanza kunimwagia mwilini mwangu,hapa ndipo nikagunda ni unga wa pilipili ndio anao nimwagia.
Mauimivu ninayo yapata hayana mfano,kikubwa ambacho ninakilinda ni macho yangu yasiingie pilipili hii.Mzee Godwin akawaamrisha watu wake wakamtafute Manka na kumleta hapa mara moja.Mimi wakaniburura na kuniingiaza kwenye chumba kimoja ambacho kina giza nene.Baada ya dakika kama mbili nikastukia taa tatu kubwa zikiwaka zenye mwanga mkali ambao ukaanza kuniungaza mwili wangu,jasho ambalo linanimwagika kutokana na mwanga mkali,likazidi kunichoma kwenye vidonda vyangu.Sehemu zote za majeraha ya mwili wangu,zikazidi kuniuma kiasi kwamba maumivu makali yakazidi kunitwala.Taa zikaendelea kuwa zaidi ya dakika kama kumi kisha zikazimwa.Nikabaki nikiwa nimekaa chini nimejikinyata mwili mzima huku nikiwa ninatetemeka kma nimepigwa na shoti
Nikaendelea kukaa ndani ya chumba kwa muda mrefu,sikujua jinsi masaa yanavyo kwenda,mlango ukafunguliwa na ikawasha taa ya kawaida,mbele yangu akasimama mwanamke mrefu mwenye mwili mmnene kiasi.Mikononi akiwa ameshika sahani yenye chakua kingi,akachuchumaa na kuniwekea
“Kama unaweza kula sawa,kama hutoweza kula acha”
Alizungumza na kutoka ndani ya chumba na kukifunga,nikaivuta sahani yenye chakula taratibu.Nikaanza kula wali uliopikwa vibaya kwani wala haukuiva vizuri,Sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kuula huku nikiwa nimejikaza.Mwili mzima unanitetemeka kwa maumivu makali,chakula kingi kinamwagika chini kutokana na mikono yangu kutetemeka sana kiasi kwamba hata kukishika chakula ninashindwa.Sikumaliza kukila chakula kutokana na kutetemeka sana mwili wangu,
Masaa yakazidi kwenda pasipo kujua nini muafaka wangu wa kukaa ndani ya hili jumba.Nikaanza kukichunguza chumba sehemu yote na kugundua kimefungwa taa nyingi zenye ukubwa mbali mbali,nyengine zinaukubwa kama taa zinazo fungwa kwenye viwanja vya mpira ndio maana zina mwanga mkali sana.Nikauchunguza mwili wangu na sehemu kubwa imeujeruhiwa.Nikiwa nimesimama nikastukia mlango ukifunguliwa,nikakaa kwa muda ila sikuona mtu akiingia ndani ya chumba.Taratibu nikaanza kupiga hatua za kwenda nje,nikachungulia wala sikumuona mtu wa aina yoyote.Nikapiga hatu na kwenda nje kabisa na sikuona mtu wa aina yoyote katika eneo hili
Nikazidi kwenda mbele na yumba nzima inavyumba vingi sana,nikaendelea kuchunguza hadi nikafika sebleni.Nikachungulia dirishani na kumuona mzee Godwin akiwa amesimama na watu wake wakilitazama gari linalo simama,baada ya gari kusimama wakashuka watu wawili walio valia mavazi meusi kish mmoja akafungua mlango wa nyuma akashuka Manka akiwa na Madam Mery.Mzee Godwin akamkumatia Manka kwa furaha ila Manka hakuonekana kuwa na furaha ya aina yoyote
“Mama yangu mbona huna furaha?”
“Baba kwa nini siku zote ulinificha?”
“Nilikuficha na nini mwanangu?”
“Baba kumbe Eddy ni ndugu yangu.Umecha hadi nimefanya naye vitendo vya ajabu nikidhani ni mtu wa kaiwada kama wengine”
Maneno ya Manka yakaibadilisha kabisa sura ya Mzee Godwin,akikunja kana kwamba amepigwa na mshale wa mgongo
“Ina maana Eddy amekubaka?”
“Sio amenibaka,Eddy alikuwa ni mpenzi wangu na hadi amenipatia ujauzito ila kwa bahati mbaya mimba ikatoka”
Mzee Godwin akajishika kichwa na kuzunguka mara mbili huku akisunya misunyo mkali
“Nitamuua Eddy leo mbele yako”
Mzee Godwin alizunguza na kuanza kupiga hatua za kuingilia kwenye mlango wa sebleni.Kabla sijafanya kitu chochote nikastukia nikishikwa kwa nyuma na kuzibwa mdomo
“Shiii”
Ilikuwa ni sauti ya kike,mwanamke aliye nishika kwa nyuma akaanza kunivuta kwa nyuma huku tukielekea gizani.Tukatokea upande wa pili wa nyumba kwenye miti mingi,ndipo nikagundua mtu aliye nishika ni yule dada aliyekuwa ameniletea chakula
“Kimbia kabla kifo hakija kukuta hapa”
Msichana alizungumza,huku akiwa amenitazama kwa macho makali,
“Asante”
“Amina ninaitwa”
“Eddy”
“Ninakujua,haya nenda”
Nikaanza kujikaza na kutokomea porini,Japo mara kwa mara ninaanguka ila nikazidi kujikaza na kwenda mbele,Giza likatawala anga na sikujua ni wapi nielekeaa,nikajiegemeza kwenye mti mmoja huku nikiwa ninahema sana kwani umbali nilio ukimbia ni mrefu sana.Nikiwa nimeegemea mti nikasikia milio ya mbwa kwa mbali.Nikatazama nilipo toka na kuona mianga mingi ambayo kwa muonekano ni mianga ya tochi na si watu wengine wanao nifwata ila ni Mzee Godwin na watu wake.Nguvu za mwili zimeniishia,nikaendelea kukimbia ila ikafikia sehemu nikashindwa kwenda mbela zaidi n kujikuta nikiangua chini na watu wa mzee Godwin wakazidi kunikaribia nilipo anguka,Nikasimama ila kabla sijapiga hatua hata moja nikastukia mbwa mmoja akinidaka mguu na kuniangusha tena chini
Kwa haraka nikaokota kigongo cha mti kilichopo karibu yangu, nikambamiza nacho mbwa cha kichwa na kumfanya atoe ukelele huku akiniachia mguu wangu.Nikarudia tena kumbamiza na kigongo kwa nguvu zangu zote hadi akalala chini na kutoa milio ya kuaga dunia, watu wa Mze Godwin hawakuwa mbali sana kutoka sehemu ambayo nipo, nikajikaza na kunyanyuka na kuendelea kukimbia kwa mwendo wa kuguchia kwani mwili mzima umejaa maumivu mengi yanayo nifanya nisikimbie sana.
“Mungu nisaidie”
Nimaneno ambayo hayakuacha kutoka kinywani mwangu, kila ninapozidi kwenda mbele ndivyo jinsi ninavyo choka.Milio ya risasi inayo tokea nyuma yangu ikazidi kunichanganya na kunifanya niaanze kwenda mbele.Mwanga wa mbala mwezi kiogo ukawa unanisaidia kuona mbele ninapo elekea, nikazidi kupanda mlima ambao unamajabali makubwa sana na yakutisha.Kwa haraka haraka kwa elimu yangu ya Jografia ambayo nimeisoma nikatambua sehemu hii nilipo itakuwa ni maeneo ya milima ya usambara, sema sehemu ndio siifaamu bado
Nikaingai kwenye moja ya jabali ambalo linashimo kubwa na kijibanza kwa ndani huku nikihema sana kwa huku woga mwingi ukiwa umenitawala.Mianga ya tochi ikazidi kunisogelea katika sehemu niliyo jificha, nikaendela kujibanza huku nimelala chini ndani ya chimo ili isiwe rahisi kwa wao kuweza kuniona.Nikawaona jamaa watatu wenye bunduki mkononi pamoja na tocho kubwa wakikipita nje ya jabali kubwa nililo jificha mimi.Wakapita na kuelekea mbele, nikawashuhudia watu wengi wanne wakiendela kutafuta kila sehemu
“Huyu jamaa, atauwa amekimbilia sehemu hii hii”
Jamaa mmoja alizungumza huku akiendelea kumulika mulika kwenye mawe mengine.Mmoja wao akasimama pembezoni mwa jabali nililopo mimi na kuanza kumulika mulika ndani na kunifanya nijibanze kwenye sehemu ambayo mwanga wake wa tochi hauta weza kunimulika.Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi baada ya jamaa kuanza kupiga hatua za kuingia ndani ya jabali,Nikastuka baada ya kuona joka kubwa lililo jiviringisha na kukificha kichwa chake likiwa ndani ya jabali, hii ni baada ya jamaa kumulika mulika kwa tochi yake.Mwanga wa tochi ukaanza kulifanya joka hili kuanza kujichezesha chezesha huku likaanza kujiachia, nikashusha pumzi huku macho yangu yakilitazama joka na jamaa ambaye anatembea kwa mwendo wa kunyata akiingia ndani ya pango huku akiwa ameshika bastola na tochi kwenye mikono yake.
Nikaanza kuhesabu moja hadi tatu kimoyo moyo na kuchomoka kwa kasi na kumpiga kikumbo jamaa na kumfanya kutoa ukelele ambao ukasababisha joka lililomo ndani ya jabali kujifyatua mwili wake, nikawa ninazisikia kelele za jamaa akito maumivu makali kwa nyuma na mimi nikazidi kutokomea nisipo pajua.Milio mingi ya risasi nikaisiki sehemu nilipo tokea na kunifanya nizidi kukimbia, sikujua hata nguvu za kukimbia zimetokea wapi.Niasimama kwenye moja ya mti na kuinama huku mikono yangu ikiwa imeshika magoti yangu na kuhema sana
“Simama, na mikono juu, lasivyo nitakifumua kichwa chako”
Sauti kali ya mwanaume niliisikia nyuma yangu ikiniamrisha, sikuwa na jinsi zadi ya kusimama huku mikono nikiwa nimeinyanyua juu.Nikataka kugeuka
“Usigeke, pumbavu”
Nikabaki nikiwa nimesimama, nikisikilizia mtu huyo ataniamrisha nifanye kitu gani kingine.Nikastukia akinishika mikono yangu kwa nyuma na kuishusha chini,nikageuza shingo yangu kwa haraka na kukutana na watu wawili wa mzee Godwin, huku aliye nishika akinigunga pingu mikoni.
“Nimekwisha”
Nilijisemea kimoyo moyo,jamaa wakanichukua safari ya kurudi katika ngome ya siri ya mzee Godwin,baba aliye nilea kuanzia utotoni hadi hapa nilipo fikia na siku zote niliamini ni baba yangu kumbe sivyo kama nilivyo dhania.
“Jamani, semeni kiasi chochote cha pesa mimi nitawapa ili tu muniachie”
“Pumbavu wewe, hatuna haja na pesa yako.Sisi kazi yetu ni moja tu.Kukurudisha mikononi mwa mkuu wetuu”
“Sikilizeni, nyinyi ninwanaume wezangu,Jaribuni basi kuniurumia.Mimi ni sawasawa na mdogo wenu.Hembu pigeni picha nikienda kuuawa, nyinyi mutafaidika na nini?”
Nilizidi kuashawishi jamaa waweze kuniachia ila hakuna ambaye ananisikiliza.Hadi tunafika kwenye jumba la mzee Godwin hakuna hata mmoja aliye nikubaloa ombi langu.Tukaingia sebleni na kumkuta Mzee Godwin amekaa na Manka pamoja na watu wake wengine, Kitendo cha mimi kufikishwa sebleni kikamfanya mzee Godwin kusimama kwa haraka na kuichoma kiunoni bastola yake na kukoki kabla hajanipiga risasi Manka akamzuia
“Baba, unataka ufanye nini?”
“Acha nimuue mshenzi mkubwa huyu”
“Baba ninakuomba,usimuue Edd......”
Mzee Godwin akamtandika Manka kibao kilicho muangusha chini Manka,akaninyooshea bastola huku akiwa amenilenga kichwani
“Najua unataka kunai,Ila ninakuomba nizungumze kitu kimoja”
Nizungumza kwa sauti ya upole sana
“Nampenda sana mama yangu, yeye ndio kila kitu kwangu.Ninakuomba nitakapo kufa usimsumbue, najua kulea mtoto ambaye si wako ni kazi kubwa na mbaya zaidi ulikuwa unajua kama ni wako”
“Nipo tayari kufa, ila ninakufa kwa ajili ya mama yangu.Please dady don’t hurt my mother”(..........tafadhali baba ninakuomba usimuumize mama yangu)
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika, sikuwa na ujanja wowote kwani sikujua ni jinsi gani ninaweza kujiokoa kutoka mikononi mwa Mzee Godwin
“Ila kumbuka baba, kumbuka baba yangu ni ndugu yako wa damu.Damu yake ni damu yako,iweje leo mimi niwe adui yako,iweje leo niwe kitu cha chuki,iweje leo mama yangu awe adui yako.Kumbuka alikuuinua kiuchumi.Kumbuka alikugharamia na kukutibu tatizo lako, ila vyote umeona hakuna kitu”
Nilizidi kuzungumza huku machozi yakiendelea kunimwangika, taratibu nikapiga magoti chini kisha nikainyoosha mikono yangu juu
“Unaweza kuniua ukihitaji”
Nilizungumza huku nikimtazama Mzee Godwin usoni, hakuonekana hata kuwa na lepe la huruma kwenye macho yake.Macho yangu nikayahamishia kwenye bastola yake na kukiangalia kidole chake kilicho ingia kwenye traiga kikianza kurudi nyuma taratibu,Gafla milipuko mkubwa nje ukasikika na kuwafanya watu wote tuliopo sebleni kulala chini.Risasi nyingi kutoka njee zikaanza kushambulia mlango wa kuingilia na kunifanya nitambae kutafuta sehemu ya kujificha nyuma ya soma ambalo halikubana ukutani.Watu wa mzee Godwin wakaanza kujipanga ndani na kuanza kujibu mashambulizi ya watu wanao fyatu risasi nje.
“Eddy”
Nilisikia sauti ya chini ikiniita pembeni yangu,nikatazama na kukutana na msichana aliye nifungualia mlango na kutoroka jana.
“Nifwate”
Nikatambaa kuelekea sehemu ambayo yupo pasipo watu wengine wote kuona kwani macho yao yote wameyaelekezea nje sehemu ambapo risasi zinatokea.Tukanyanyuka sote na kuanza kukimbia huku nikimfwata kwa nyuma.Tukazunguka hadi mbele ambapo risasi zinapigwa.Nikashangaa kukuta bunduki kubwa yenye kutumia risasi zilizo kwenye mkanda ikizipiga mlangoni huku sehemu yenye traiga ikiwa imefungwa na mpira,jambo linalo wazubaisha Mzee Godwin na watu wake wakidhania wanashambuliwa na maadui
“Usishangae mimi ndio nimefanya hivyo”
Alizungumza huku akinistua,akanirushia funguo za gari langu ambalo kidogo limebonyea sehemu za pembeni.Nikaingia ndani ya gari na kuichomeka funguo sehemu yake na kuliwasha, nikashusha pumzi na kumshukuru Mungu baada ya gari kuwaka bila ya matatizo.Ili nisitumie nguvu sana nikaibadilisha mfumo wa kuendesha na kuweka ‘automatic’ na kuliondosha kwa kasi katika eneo la jumba hili
“Asante dada”
“Na wewe pia asante”
Sikujua asante yangu inatokana na nini, akawa na kazi ya kunielekeza njia za kupita na kusema kweli si rahisi sana kwa watu kugundua sehemu lilipo jumba la mzee Godwin kwa maana lipo kwenye mlima mkubwa ulio jaa miti mingi na hapana nyumba ya mwananchi wa aina yoyote ambaye yupo kwenye huu mlima.Nikaendele kuliendesha gari kwa umakini huku mara kwa mara nikitazama kupitia kioo cha pembeni kama kuna gari zinanifwata ila sikuona gari lolote
“Nilijaribu kuliwasha hili gari lako ila nikashindwa”
“Hili gari si rahisi kwa mtu kuliiba kwani namba za siri ninazijua mimi mwenyewe”
“Mimi ninaitwa Dorecy”
“Ninashukuru kukufahamu”
“Kusha kusoto kwani mbele kuna geti na kuna watu ninaamini watakuwa wanatusubiria”
Nikakanyaga breki kidogo na kukunja kushoto nilipo elekezwa na kuiacha njia ambayo niyakunyoosha,
“Huku twende taratibu taratibu kwa maana kuna kona nyingi sana”
“Sawa”
Nika ninakwenda kwa mwendo wa kawaida ambao hata nikikutana na kona ya gafla niweze kukunja isitoshe sehemu ya upane wa pili wa barabara kuna korongo kubwa kwenda chini na laiti kama mtu unaanguka ni lazima ukafie chini huko kwani kuna mimawe mingi iliyo chongoka.
“Eddy simamisha gari”
Nikafanaya kama Dorecy alivyo niambia, akachomoa bastoa mbili kwenye mifuko ya suruali yake nyeusi aliyo ivaa na kunikabidhi moja.
“Unaweza kutumia?”
“Ndio”
Macho yate yakawa na kazi ya kutazama sehemu za juu kwenye milima ambayo kwa chini tunapita na gari.
“Endesha taratibu”
Nikafanya kama Dorecy anavyo niagiza,gafla tukaiona gari moja mbele yetu, aina ya pick up ikiwa na watu wenye bunduki zao huku mmoja wao akiwa ameshika bomo aina ya rocket ambalo upigaji wake analiweka begani na kulifyatulia.Sote tukafunga breki za magari yetu na majamaa wakaanza kushuka huku mwenye bomo akiwa ametuelekezea kwetu akijiandaa kutufyatulia
Mach yangu yangu yakawatazama jamaa walio shika bunduki mikononi mwao, wote wanaonekana wapo makini katika kutushambuli sisi.Kwa kupitia kioo pembeni, nikaangalia nyuma na kuona kuna kona ambayo ipo karibu na sehemu tulipo simama, Nikakanyaga mafuta na gari kuanza kuirudisha nyuma kwa kasi kubwa, jamaa wakaana kutushambulia kwa risasi ambazo kwa bahati nzuri hazikuingia kwenye gari, Kitendo cha kukunja tu, bomo alilo lifyatua jamaa likapita mita chache kutoka sehemu gari letu lilipo na kwenda kugongwa kwenye miamba na kusababisha mlipuko mkubwa na mawe yakaziba barabara kwa nyuma na kushindwa kurudi nyuma.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikafunga breki na kulisimisha gari, sote tuakashuka kwenye gari huku bastola zetu zikiwa mikononi,Tukaifungua milango ya gari na kujificha nyuma ya milango kwani uzuri wake haipitishi risasi.Bastola zetu zikawa zimeelekea kwenye kona ambapo tunatarajia majambazi kutokea.Ukimya wa kama dakika tatu ukatawala, hatukuona watu ambao wanajitokeza kwenye kona, nikataka kunyanyuka
“Eddy kaa chini”
Dorecy alizungumza kwa sauti ya ukali, nikatii kwa haraka na risasi ikapiga kwenye kioo cha gari katika mlango ambao nipo mimi.Dorecy akaanza kufyatua risasi zilizo elekea walipo majambazi, kila risasi ambayo ninaipiga mimi haikumpata mtu yoyote zaidi ya kupiga pembeni, hata kama mtu nimemlenga vizuri ila haikumpata
“Nakosea wapi?”
Nilizungumza kwa sauti ya juu
“Kaza mkono”
Dorecy alizungumza, huku akiendelea kufyatua risasi kwa majambazi ambao wanatoa vilio vya maumivu kila aliye pigwa na risasi.Nikaingia ndani ya mlango na kuufunga mlango wa upande ambao nipo
“Unafanya nini?”
“Ngoja nikuonyeshe”
Nikaiwasha gari na screen(kioo), kilichopo pembeni yangu kikawaka na kuniandikia maneno yaiyo nichosha
‘SYSTEM WEAPON EMPTY’ ikimaanisha hakuna silaha yoyote inayoweza kufanya kazi kwani zimeisha.
“Shitiii”
Nilizungumza huku nikiupiga mskani kwa kitako cha bastola
“Vipi?”
“Kuna, ishu nilikuwa ninaicheki kwenye hii gari.Imeisha”
“Ni nini?”
“Silaha, naomba hilo jaketi lako la kuzuia risasi”
Dorecy alinitazama kwa muda kisha akavua bullet proof yake na kunirushia upande niliopo, nilalivaa vizuri na mara nyingi nilikuwa nikimuona mzee Godwin akilivaa jinsi nilivyo livaa nikiwa mtoto mdogo.Kwani kuna siku nyumbani tulivamiwa na majambazia nyumbani, akatuvalisha sote kisha yeye alielekea kupambana nao na siri moja aliyo niambia ni kwamba jaketi hili linamionzi ambayo hata ukiwa umelengwa kupigwa risasi ya kichwa basi inaivuta na kukimbilia kifuani.
“Vipi huku, mbele mimi ngoja nipande hapo juu”
Nilimuambia Dorecy, nikapanda kwenye gemo ambalo lipo pembeni yetu, nikapanda hadi pasipo majambazi kuniona, nikatafuta sehemu nzuri ya kusimama ambayo nikawa ninawaona kwa chini, nikawahesabu kwa haraka na kuwaona wakiwa wamebaki wanne wamejibanza kwenye gari lao wakimsubiria Dorecy kujitokeza, Dorecy naye akawa amejibanza kwenye gari akiwasubiri wajitokeze
Nikaishika bastola vizuri, nikafumba jicho langu moja huku nikiitazama sehemu yenye mfuniko wa tanki la mafuta kwenye gari, nikameza mate mengi kisha nikafyatua risasi tatu mfululizo huku nikiwa nimeikaza mikono yangu, risasi mbili zikapiga pembeni, jambo lililo wachanganya jamaa.Risasi ya tatu ikapiga kwenye Tanki la mafuta na kulifanya gari kulipuka, huku likinyanyuliwa juu na jamaa wote wakarushwa pembeni.Hadi gari linatua chini milango na matairi yake yalichanguka vibaya.
Nikashuka kwenye gemo kupitia njia niliyo pandia na kumkuta Dorecy akiwa bado ameshika bastola yake akiielekezea walipo majambazi, nikatembea kwa mwendo wa tahadhari hadi ilipo gari ya majambazi, nikaanza kuhakikisha jambazi mmoja baada ya mwengine kama amekufa, ambaye ninamkuta kwenye hatua za mwisho za maisha yake nilampiga risasi ya kumsindikiza kuzimu
Nikageuka nyuma na kumkuta Dorecy akiwa ananitazama kwa macho ya mshangao, kwani haamini kama nitaweza kuwapiga risasi wezake ambao amewasaliti, nikarudi lilipo gari na kuingia, nikaliwasha hadi sehemu alipo, akafungua mlango na kuingia.Nilalipitisha pembeni gari langu taratibu kulikwepa gari linalo teketea na kuandelea na safari.Dorecy akaendelea kunielekeza njia hadi tukatokea barabara inayotokea Tanga kuelekea Moshi
“Eddy, ulisha wahi kuua?” Dorecy aliniuliza
“Swali gani sasa hilo?”
“Hapana, kwa mtu ambaye hazifanyi hizi kazi hawezi kuwa kufanya kama ulivyo fanya wewe”
“Nimefanyaje?”
“Ulivyo wapiga wale, risasi waliokuwa wakikaribia kufa”
“Kawaida”
Nilimjibu huku nikendelea kuendesha gari kwa umakini, macho yangu yote yakawa ni barabarani kuangali kama polisi wa usalama barabarani wapo au hakuna.Tukaingia kwenye Motel iitwayo Mombo Motel iliyopo kwenye barabara ya Mombo
“Una pesa?”
Nilimuuliza Dorecy
“Ndio”
“Kachukue chakula basi”
“Utakula nini?”
“Bufee,nyama chukua na soda za take way”
Dorecy akalivua shati lake na kubaki na vest ya kiume, akaziweka vizuri nywele zake ndefu, akaichomeka bastola yake kwenye buti la jeshi, mguu wa kulia na kushuka ndani ya gari.Kwa kupitia kioo cha pembeni nikawaona askari wa usalala barabarani, wakiingia kwenye geti la Motel wakiwa na pikipiki.Wakaisimamisha pikipiki nyuma ya gari langu na kunifanya nianze kupata wasiwasi, kwani sihitaji kumwaga damu tena katika eneo hili.Mmoja akaanza kulitazama gari langu vizuri, akaanza kulizunguka taratibu huku akilitazama kadi zake za usajili zilizo bandikwa kwenye kii cha mbele
“Anataka nini huyu?”
Nilijizungumzia kimya kimya, akanionyesha ishara ya kufungua kioo cha gari langu, akanitazama kwa sekunde kadhaa
“Habari yako afande?” Nilianza kumsalimia
“Salama, gari yako ilipata nini?”
“Kivipi?”
“Imebonyea pembeni huku?”
“Ilipata ajali, afande”
Nilizungumza huku mkono wangu wa kulia ukiwa umeishika bastola, huku nikiwa nimeficha pembeni ya siti yangu
“Unatakiwa ukaiyooshe, kwa maana gari ya kifahari inakuwa haileti picha nzuri”
“Sawa Afande”
“Insuarence yako nayo ipo katika siku za ukingoni”
“Yote nitayafanya, nikifika ikulu”
Niliingiza swala la ikulu kwa maana askari, anahisi kama mimi ni miongoni mwa askari, hii nikutoka na bullet proof niliyo ivaa
“Ahaaa, upo ikulu wewe?”
“Yaaa”
“Wezetu nyinyi wa ikulu muna kula kula pesa”
“Tunakua pesa wapi kaka, kazi nyingi kama hizi unazo ziona”
“Ila si kwa kila kazi unapata mkwanja mrefu?”
“Inategemea, na kazi”
“Ahaa sisi wa barabarani huku ni shida”
“Shida gani?”
“Ahaaa, madereva wenyewe wabishi kama nini”
“Wabaneni”
Nilizungumza huku nikijiamini sana, kwani tayari nimesha muingiza choo cha kike huyu askari.Dorecy baada ya kuwaona askari akastuka, ila akajikaza na kwajinsi alivyo vaa askari ninaye zungumza naye akazidi kuamini kuwa sisi ni askari kutoka ikulu.
“Habari yako, Afande?”
Dorecy alimsalimia askari
“Salama tuu, jamani ngoja niwaache muende”
“Asante afande kwa muda wako”
“Ila kaka kama kukiwa na nafasi basi, huko ikulu tukumukane”
“Usijali kaka yangu”
“Naomba namba yako ya simu”
“Nitajie yako kwa maana ninabadilisha badilisha namba za simu, si unajua kazi zetu hizi”
Askari akanitajia namba yake ya simu, tukaagana naye na kuondoka bila ya wao kutustukia juu ya kitu chochote
“Eddy, nimesikia ikulu?”
“Ahaaa mzembe yule, Alivyo niona nimevaa hivi akazani mimi ni askari”
Dorecy akaanza kucheka sana,
“Eddy your geniuse boy”
“Kwa nini?”
“Umemtekaje tekaje hadi kakuamini?”
“Njaa zake tuu yule, nahisi”
Safari ikaendela kwa mwendo wa kawaida, hadi tunafika Korogwe akawa ememalia kula, nikasimamisha gari pembeni na kumpisha Dorecy upande wangu wa dereva kisha mimi nikakaa upende alio kuwepo na kuanza kula.
“Eddy, tunaelekea Dar au wapi?”
“Dar”
“Unajua mimi sio mwenyeji wa Dar”
“Wewe ni mtu wapi?”
“Kagera na nimwanajeshi, ambaye nilikuwa upande wa baba yako.Alitushawishi hadi tukawa tunafanya kazi zake isitoshe yeye ni mkubwa hatukuwa na kauli juu ya hili, ndio maana ikafikia kipindi nikaamua kuwasaliti, niachane na kazi zake”
“Kwani, mulikuwa munafanya kazi gani?”
“Kazi nyingi tu za kigaidi, hadi kazi ile ya kukuteka wewe, mimi ndio nilikuwa muendeshaji wa gari la mbele”
“Wewe ndio ulikuwa kihere here sana kwenye kunimulika mataa”
“Ahaa tutafanyaje sasa, wakati bosi ndio kashasema”
“Na ile siku niliwapeleka”
“Ahaa wee acha tuu, nilikuwa ninaendesha gari hadi mikono inaniuma”
“Sasa, mulijuaje kuwa ninarudi?”
“Unajua ilikuje, mzee alimpigiwa simu na askari ambao, sijui walikuwa wanakukimbiza Arusha.Sasa, wale askari walikuwa wanataka kukufukuzia, ila mzee akasema wamuachie kazi yeye.Ndio maana ulistukiza gari zikiwa zinakufwata tuu”
“Mmmmm.....”
“Yaani hapa umeichokoza vita, na mzee wako anamkono mrefu sana”
“Mungu bariki nitayashinda”
“Yaa, kikubwa ni kupambana hadi dakika ya mwisho.Fungua hapo kuna bastola yako”
Nikafungua kwenye sehemu ya kuhifadhia vitu iliyopo mbele kwenye siti niliyo kaa, nikaikuta bastola ya mama
“Niliiweka, mimi hapo”
“Asante”
Hadi tunaingia Dar es Salaam, hatukupata tatizo la kusimamishwa na askari yoyote njiani, moja kwa moja tukaelekea nyumbani.Hadi tunafika nyumbani ilishatimu saa kumi na moja jioni, Dorecy akasimamisha gari sehemu ya magesho ya magari baada ya geti kufunguliwa.
“Karibu ndani”
“Asante”
Tukaingia ndani na Dorecy, sikumkuta mtu yoyote ndani, nikatoka na kwenda gaetini na kumuuliza mlinzi
“Mama yupo wapi?”
“Ni siku ya pili tangu aondoke jana na yule sister hajarudi”
“Sister gani?”
“Yule uliye kuja naye,majuzi”
“Sheila?”
“Ndio”
“Powa”
Nikarudi ndani na kuchukua simu ya mezani na kumpigia mama simu, ikaita kwa muda kisha ikapokea
“Mama upo wapi?”
“Eddy.....Eddy.Umecheza pata potea”
Niliisikia sauti ya Mzee Godwin ikizungumza kwa dharau huku akicheka,Wasiwasi ukaanza kunivaa
“Yupo wapi mama yangu?”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali
“Mama yako ame reast in peace”(.......amepumzika kwa amani)
Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, huku jasho jingi likimwagika midhili ya maji, Dorecy akasimama kwenye sofa na kunifwata sehemu nilipo, akanipokonya simu na kuishika mkononi
“Haloo.....Eddy........ulisema ufe wewe, kwa ajili ya mama yako.Ila kwa bahati mbaya mama yako ndio hivyo amesha tangulia mbele za haki”
Sauti ya Mzee Godwin iliendelea kusikika kwenye simu akizungumza kwa sauti iliyo jaa dharau
“Do you know, who will be the next to die?”(Je una unajua, ni nani atafwata kufa?)
“Hhahaahaaaa is your Sheila, na leo nimepata tunda lake kwa mara nyingine tena, Yupo so mwaaaaaaaaaa”(Hhahaahaaaa ni Sheila wako, ........)
“Enjoy your day, mr Eddy”(Furahia siku yako, bwana Eddy)
Simu ikakatwa, nikashindwa kuyazuia machozi yangu, kwa mara nyingine Mzee Godwin anawateka watu wangu wa karibu.Dorecy akanishika mkono na kunikalisha kwenye sofa, hasira taratibu ikaanza kupanda na kujikuta mwili wangu wote, ukianza kunitete, Dorecy akanitazama kwenye macho yangu.Mlango wa kuingilia ndani ukafunguliwa na kujikuta nikichomoa bastola yangu na kumuelekezea mlinzi aliye fungua mlango
“Ohooo, ni mimi kaka”
Alizungumza huku akiinyanyua mikono yake juu, huku mkononi akiwa ameshika gazeti
“Unataka nini?”
Nilimuuliza kwa sauti ya ukali
“Ka..ka kuna hili gazeti hapa.....”
“La nini?”
“Kukuuu.....”
“Nitolee kigugumizi chako, kabla sijakuua”
Mlinzi akaanza kutoka ndani
“Wee kaka samahni, hembu hilo gazeti”
Dorecy akanyanyuka na kwenda kulichukua gazeti, akalifungua na kuanza kulisoma huku akipiga hatua za taratibu akirudi sehemu ambayo alikuwa amekaa.Akakaa sehemu yake, sikuwa na haja ya kulitazama gazeti lake.
“Eddy”
Dorecy aliniita na kunifanya nimtazame, nikaikuta sura yake ikiwa imejaa mikunjano akionekana kuna habari iliyopelekea sura yake kuwa katika sura kama hii,Akanyanyuka na kukaa kwenye sofa nililopo mimi.
“Soma, hii habari”
Macho yangu yakatua kwenye maandishi meusi yaliyo andikwa kwa herufi kubwa zinazo onekana vizuri pasipo na shida yoyote
‘MTOTO WA WAZIRI WA AFYA (EDDY GODWIN), ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI KWA MAUAJI YA KIKATILI YA MFANYA BIASHARA WA MADINI JIJINI ARUSHA BWANA DERICK LAMBART NA MWILI WA DERICK KUWA CHAKULA CHA MBWA WAKE’
Chini ya maandishi haya makubwa kuna picha yangu, ya mama na Derick Lambart zikiwa zimeambataishwa kwenye mstari mmoja
“Eddy ni kweli?”
Dorecy alizungumza huku akinitazama machoni, sikumjibu zaidi ya kunyanyuka kwenye sofa, kabla sijamjibu Dorecy nikasikia mlio wa gari ukisimama nje ya geti.Cha kwanza nikazima taa za sebleni na kufungua pazia kidogo la dirisha linalo tazama kwenye geti,Nikawaona askari wawili wakizungumza na mlinzi huku wakionekana kulazimisha kuingia ndani kwa nguvu.
Dorecy akanyanyuka katika kochi alilo kaa na kunifwata nilipo simama,
“Shiit, wamejuaje kama upo humu?”
“Hata mimi sifahamu”
“So, inakuwaje?”
“Tuwauoe?”
“Eddy, usiongeze dhambi nyingine juu ya kuua.Uliyo yafanya yanatosha kwa sasa”
“Sasa wewe unanishaurije?”
“Ngoja nikuonyeshe”
Dorecy, akaanza kuvua nguo moja baada ya nyingine hadi akabakiwa na nguo za ndani(sidiria na chupi), na nguo zake akazificha nyuma ya masofa.Mlinzi alishindwa kuwazuia askari hao kuingia, Dorecy akaniomba nijifiche nyuma ya mlango wa kuingilia.Nikafanya kama alivo niagiza Dorecy, maaskari wakaanza kugonga mlango taratibiu.Dorecy akaisogelaa swichi ya kuwasha taa za sebleni, akaiwasha na kwenda kusimama ulipo mlango
“Fungua”
Nilizungumza kwa sauti ya chini sana, huku nikiwa nimeishika bastola yangu vizuri mikononi mwangu.Dorecy akafungua mlango akiwa katika hali ya nguo zake za ndani, zilizo ufanya mwili wake kuonekana vizuri na kuwa kivutio kizuri mbele ya wanaume marijali.
“Habai zenu maafande?”
Dorecy aliwasalimia, ila salamu yake haikujibiwa kwa sekunde kdhaa, kwa kupitia uwazi wa mlango nikwashuhudia askari wakiwa wamemtumbulia mimacho Dorecy
“Aha....aahaa Salama tu”
“Mmmm, labda niwasaidie nini?”
“Ahaaa”
Askari walibabaika, hawakujua hata wajibu kitu gani
“Karibuni ndani”
“Haya....haya”
Mmoja alizungumza huku akijilamba lamba mdomo wake, wakaingia ndani na Dorecy akaurudishia mlango, na kunnifanya niweze kuonekana vizuri na askari walio ingia ndani.Hawakuweza kufanya kitu chochote kwa sababu, nimeshika bastola, huku nikiwa sina masihara kabisa na kitu ambacho ninakifanya
“Nyoosheni mikono yenu juu”
Niliwaamrisha, wakatii huku wakitetemeka, Dorecy akaanza kuwapapasa na kuwachomoa bastola zao walizo zificha kwenye miguu yeo,Dorecy akawavua mikanda yao ya suruali
“Unawafanyaje?”
“Subiri uone”
Dorecy akaichukua mikanda yao ya suruali, nikawaamrisha waende kukaa kwenye masofa
“Nyinyi, mumekuja kufanya nini?”
Niliwauliza kwa sauti ya ukali
“Tu..lik..uku..ja, kukutaf...uta wewe”
Mmoja alizungumza huku akibabaika sana,
“Nani amewatuma?”
Dorecy alizungumza
“Eheee?”
“Nani amewatuma, au swali langu ni gumu kulijibu?”
Dorecy alizungumza, huku akiizungusha bastola ya mmoja wa polisi
“Ni..ni....nimzee Dodwin”
“Nilijua, tuu”
Dorecy alizungumza, huku akinitazama usoni.
“Simameni kwanza”
Niliwaamrisha na wakasimama, nikawaamrisha tena kuvua nguo zao, wakatii bila ya ubishi.Wakabakiwa na kaptula zao za ndani, nikaamrisha kulala chini, nikachukua pingu zao na kuwafunga mikononi, walio irudisha nyuma, Dorecy akachukua mikanda yao na kuwafunga miguuni kisha akaikutanisha miguu na mikono kwa mamoja na kuwafunga,
“Sasa ninahitai munijibu swali moja baada ya jengine?”
“Munaweza kuniambia ni wapi alipo mama yangu?”
Wakaa kimya, hakuna aliye nijibu hata mmoja.
“Ninarudia tena na tena kuwauliza hili swali.Ni wapi alipo mama yangu?”
“Si hatujuii”
“Hamujui eheee?”
“Ndio”
“Waangalie hawa”
Nikaondoka na kuingia jikoni, nikachukua ndoo ndogo na kuijaza maji mengi, kisha nikachukua fimbo moja ya fagio la kusimama na kurudi navyo sebleni, nikaanza kuwanyunyizia maji ya makalio
“Sasa, hapo utawachapaje?”
Dorecy aliniuliza
“Wafungue huo mkanda nilio wafunga na mikono”
Dorecy alizungumza huku akiendelea kuwanyooshea bastola aliyo ishika, nikamfungua mmoja mkanda ulio fungwa na pingu yake, nilipo hakikisha nimeiachanisha miguu na mikono, nikamvuta pembeni na kumwagia maji ya makalio.Nikaivunja fimbo, ya fagio kugawanyika katika vipende viwili nilivyo viona vinatosha
“Ninakuuliza ni wapi alipo mama yangu?”
“Sijuii mimi?”
Nikamchapa fimbo nne za nguvu kwenye makali, yenye bukta iliyo lowa maji mengi.Jamaa akawa amejikaza makalio yeka, nikamtandika fimbo nyingine nne kwenye mapaja yake, kidogo akaanza kutoa miguno ya maumivu
“Sijuii mimi?”
“Utajua tuu”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikaanza kumchapa fimbo zisizo na idadi maalumu ambazo ninajua ni lazima zitampa maumivu ya kusema ni wapi alipo mama yangu, japo mzee Godwin ameniambia kuwa mama amesha fariki, ila sikutaka kuamini kama ni kweli, hadi niuone mwili wa mama yangu ndio nitaamini kwambe amefariki dunia.Fimbo zisizo na idadi nikazidi kuzishusha kwenye makalio ya ya polisi huyu, na akazidi kumwaga machozi ya maumivu
“Huwa mimi ninawashangaa sana nyinyi, kazi yenu ni kulinda mali za raia.Huku kwenye matatizo mengine kama haya munafwata nini?”
“Sijuii,”
“Mimi leo nina wahakikishia kuwa mutajua”
Nikaendelea kumatindika fimbo zisizo na idadi hadi, sehemu ambazo nilizichapa zikaanza kuvimba na kuweka maalama ya fimbo
“Eddy, huyo kakataa kusema bwana, hamishia zoezi kwa huyu”
Dorecy alizungumza, nikamuacha ninaye mchapa na kumfwata mwenzake, nikamuandaa kama nilivyo muandaa mwenzake kabla sijamchapa Dorecy akanizuia
“Lete hiyo fimbo”
Nikamabidhi Dorecy fimbo moja, akamuweka askari vizuri, kwa nguvu zake zote akaishisha vimbo kwenye makalio ya askari na kumfanya atoe ukelele huku akiliita jina la mama yake.Dorecy akashusha fimbo nyingine mbili za nguvu na kumzidisha askari kutoa kelele
“Nasemaa, nasemaa”
“Sema sasa”
Dorecy alizungumza, huku akimwagikwa na jasho jingi,
“Yupo, kwenye mikono ya Mzee Godwin”
“Hilo tunalijua, tunacho kitaka sisi ni kujus ni sehemu gani ambayo yeye yupo?”
“Kule kwenye ule msitu”
Dorecy akanitazama usoni
“Napajua”
Dorecy alizungumza, akamtandika fimbo nyingine ya makalio na kuzidi kumliza askari huyu anaye onyesha bado ni kijana sana.
“Hawa dawa yao ni kuwafungia stoo”
Nilizungumza, huku nikikiondoa kindoo cha maji na kukipeleka jikoni, nikarudi sebleni na kumkuta Dorecy akimalizia kuvaa nguo zake.Nikatoka nje ya nyumba na kumfwata mlinzi getini
“Hawa wehu wamekuja na nini?”
“Kina nani?”
“Hawa askari?”
“Na gari yao ndogo, ipo hapo nje”
“Sasa ilikuwaje ukaacha waingie ndani?”
“Walinionyesha vitambulisho vyao”
Nikatoka nje ya geti na kukuta gari aina ya Corola ikiwa imesimama nje ya geti, nikarudi ndani na kuwaamrisha wanipe funguo za gari lao,
“Ipo kwenye hiyo suruali yangu”
Nikaiokota funguo ya askari aliyechapwa na Dorecy, nikatoka nje na kumuomba mlizi aniungulie geti, nikaingia ndani ya gari lao walilo jia na kuliingiza ndani ya geti na kwenda kulisimamisha nyuma ya yumba yetu pembezoni mwa ‘swimming pool’.Nikamuita mlinzi na kumuomba asaidiane na mimi kuwabeba askari hawa
“Tunawapeleka wapi bosi?”
“Nyuma ya nyumba huko”
“Ila kablwa hatujawapeleka, wavue viatu vyao”
Mlinzi akaanza kuwavua viatu kisha, tukamuanza yule niliye mchapa, kumbeba.Nikaingia kwenye nyumba ya nyuma, kwenye chumba ambacho chini kina handaki.Hata mlinzi mwenyewe akashangaa kwani hakuamini kama chumba hichi kina handaki, lenye ukumbi mkubwa.Tukamuingiza askari wa kwanza na kumfwata askari wa pili na kumuingiza, huku wote wakiwa wamefungwa miguu na mikono yao
“Hakikisha, hawatoki.Pia hakikisha unawapatia chakula mchana na jioni”
“Sawa bosi nimekuelewa”
“Pia hakikisha haingii, mtu yoyote akidai kuwa yeye ni askari au mpelelezi”
“Sawa”
Nikaachana na mlinzi yeye akarudi zake getini na mimi nikaingia ndani, nikamkuta Dorecy akimwalizia kuyafuta maji yaliyo tapakaa chini kwa tambaa.
“Eddy, uhisi njaa”
“Kwa mbali ninajihisi njaa”
“Kwenye friji, jikoni niliona nyama na soseji ngoja nipiki chakula”
“Powa, upendavyo wewe, mimi ninaingia chumbani huku juu”
“Sawa”
Nikaingia ndani kwangu, mazingira ya chumba changu kwa jinsi nilivyo yaacha, hapakuwa na tofauti sana.Nikaingia nikainama chini ya mvungu wa kitanda changu na kulikuta begi lenye madini, niliyo yatoa kwenye handaki.Nikakifungua na kukuta madini yapo kama yalivyo.Nikakirudisha kibegi chini ya mvungu, nikaingia bafuni na kuvua nguo zangu zote, nikasimama mbele ya kioo kikubwa kiichomo humu ndani ya bafu langu
Mwili wangu mzima umejaa, majeraha mengi, yaliyo tokana na mateso niliyo pitia siku chache za nyuma, nikajikuta machozi yakinimwagika kwani hata ule uzuri ambao Mungu aliniumba nao umetoweka kwa kiasi fulani.
“Kwa nini mimi?”
Nilijiuliza swali huki nikitokwa na machozi,
“Nimekuwa, hivi na roho ya kinyama”
“Gereza au kifo ndio mwisho wangu”
Nilizungumza huku nikiendea kumwagikwa na machozi mengi, malengo yangu yote niliyo jiwekea kuja kuwa daktari bingwa nchini Tanzania yametoweka kabisa, hapa ndipo nikaanza kuamini kwamba pesa haitimizi malengo ya mtu, kwani tangu nimezaliwa sikuwahi kuishi maisha ya shida kwani baba anapesa na mama ndio tajiri kupindukia, ila kwa sasa ndio wamekuwa maadui sana.Sikujua baba yangu wa damu anaendeleaje, kwani sikupata hata muda wa kukaa na mama na kumuuliza kuhusiana na baba yangu aliyepo Afrika kusini
Macho yangu, nikaendela kuyakaza kwenye kioo, nikiitazama sura yangu, iliyo jaa dhambi na ukatili ulio mkubwa.Sikupenda kuwa hivi, ila matatizo yakanibidi mimi kuwa hivi
“Mungu, nisamehe, mimi ni mwenye dhambi tena dhambi nyingi.Ila ninaomba nimuue Mzee Godwin tuu.Ili nikifa nife kwa amani”
Nilijikuta nikizungumza maneno haya ambayo sikujua ni kwanini nimeyazungumza, tena kwa sauti ya juu.Nikafungua bomba la maji ya mvua na kuasimama kwa muda chini ya maji haya yanayoendelea kutiririka mwilini mwangu.Mwili wangu umejawa na nongo nyingi sana kwani hata maji ambayo yanaingia kwenye kishimo kidogo cha hapa bafuni yanaonyesha jinsi mwili wangu ulivyo jaa uchafu.Nikaoga na kurudia kupiga mapovu manne ndipo, hali ya uchafu ikaondoka mwilini mwangu.Hata rangi halisi ya mwili wangu ikarejea.Nikamaliza na kurudi chumbani kwangu, nikiwa ninatafuta ni wapi lilipo taulo langu lipo, mlango wa chumbani kwangu ukafunguliwa na Dorecy
“Ahaaa sory Eddy...!!”
“Ahaaa bila samahani”
Nilizungumza huku mikono yangu nikiwa nimeiziba kweye sehemu zangu za siri
“Chakula tayari kule”
“Sawa, ninakuja”
Dorecy akatoka, nikavaa pensi, nikaelekea sebleni na kumkuta akiwa ananisubiria kwenye meza ya chakula
“Mbona, hukula chakula?”
“Nilikuwa ninakusubiria”
“Ohoo, ungeanza tuu”
“Hapana, itakuwa sio tabia nzuri sana kwa yule umpendaye”
“Kweli”
“Ehee, sisi kwetu hatujafundishwa hivyo”
“Sawa”
Nikakaa kwenye kiti, Dorecy akanitengea chakula changu na taratibu tukaanza kula,
“Kipindi nikiwa, Sunday school tulikuwa tunafundishwaga kusali kabla ya kula”
Nilizungumza
“Mulikuwa munafundishwaje?”
“Tulikuwa tunaomba, Ohh loard our father, bleas this food for this day, Welcome Dorecy”(.....baba yetu wa mbinguni, bariki hiki chakula cha leo, karibu Dorecy)
“Hahaaa, Eddy.Sasa mbona leo hujasali?”
“Ahaa weee acha tuu”
Tukaendelea kula huku nikitazamana mara kwa mara na Dorecy, nikanyanyuka na kuzunguka meza hadi alipo kaa Dorecy, nikasimama nyuma yake, mikono yangu nikaiweka mabegani mwake.Nikainama taratibu na kumbusu shavuni
“Dorecy”
“Mmmm”
“Ninakupenda”
Dorecy hakunijibu chochote, taratibu nikaanya kuinyonya shingo yake na kumfanya aanze kujichezesha chezesha kwa hisia.Nikamnyanyua kwenye kiti na kuanza kuinyonya midomo yake, huku nikaanza kumvua nguo moja baada ya nyingine.Tukajikuta tunazama kwenye dimbwi kubwa la mapenzi huku kila mmoja akijitahidi kumpa mwenzake raha ambayo anastahili kuipata kwenye dimbwi la mapenzi.Tukatumia kama dakika thelathini na nano kuburudishana hadi tunamaliza, tukavikuta vyombo vyote vipo chini huku sisi tukiwa juu ya meza tukitoa pumzi nyingi
Nikambeba Dorecy hadi chumbani kwangu, sote tukaingia bafuni, tukaoga na kurudi chumbani na kujitupa kitandani
“Eddy, unampango gani juu ya mama”
“Nataka nikamkomboe, siamini kama amekufa?”
“Japo sipendi kujua kilicho tokea kwenye familia yako hadi kukafikia huku, ila nakuhaidi tutashirikiana kudfa na kupona”
“Nitashukuru kwa hilo”
“Kingine, itabidi unyoe nywele zako....”
“Ili”
“Uvae zile nguo za askari, la sivyo utakamatwa kirahisi”
“Etii ehee?”
“Hapo hakuna cha Etii, inabidi iwe hivyo”
“Sawa, tutafanya asubuhi”
Kutokana na kuchoka kila mmoja akajilaza na usingizi mwingi ukanipitia,Nikawa wa kwanza kuamka nikaingia bafuni na kuoga, nikamuamsha Dorecy naye akaingia bafuni na kuoga.Nikachukua mashine ya umeme ya kunyolea na kumkabidhi Dorecy, akaanza kuninyoa nywele zangu zote na kunifanya nibadilike sana.
“Dory, nataka twende bank mara moja”
“Tukafanyaje?’
“Kuna ishu nakwenda kuiuzia benki”
“Benki gani?”
“CNB”
“Sawa, ila tumia hizo nguo za polisi”
“Powa”
Nikavaa, nguo za polisi,aliye chapwa na Dorecy, zikanitosha vizuri, nikazunguka lilipo gari la polisi nilipo liacha na kuchukua kofia moja ambayo ipo ndani ya gari, nikarudi sebleni na kuvaa viatu vya kiaskari
“Kama polisi kweli vile”
“Umeona eheee”
“Eddy una picha ndogo”
“Ya nini?”
“Kuna kitambulisho nataka nifoji hapa”
Nikaingia chumbani kwangu na kutoa picha ndogo ya na kukabidhi Dorecy, akaanza kazi ya kufoji kitambulisho kimoja cha polisi.Nikachukua bastola moja na kuichomeka kwenye viatu na kuifunika na sruali, nikachukua bastola nyingine na kuichomeka kiunoni.Nikavaa jaketi la kuzuia risasi, Dorecy naye akawa amemaliza kuvaa nguo zake, Nikaingia ndani kwangu na kuchukua begi lenye madini, nikaingia chumbani kwa mama na kuchukua funguo ya gari lake aina ya VX V8 na kutoka navyo nje
“Una endesha, niendeshe”
Nilimuuliza Dorecy
“Wewe endesha, huu mji wenu mimi siuelewi kabisa”
Tukaingia ndani ya gari na kuondoka nimasisitizia mlinzi asiruhusu mtu kuingia ndani ya nyumba yetu.
“Nimemaliza kukitengeneza kitambulisho chako”
Dorecy akanikabidhi kitambulisho changu, chenye jina la Edward Kilonzo, ni jina la askari aliye tandikwa bakora na Dorecy.Tukafika benk, kabla sijashuka Dorecy akanibusu shavuni.
“Ninakupenda Eddy wangu”
“Na mimi pia”
“Kwani humo ndani ya begi kuna nini?”
“Nitakuambia nikirudi”
Nikatazama mazingira yote ya benki na kuona yapo salama, nikashuka kwenye gari huku nikiwa na kibegi na kuanza kupiga hatua za kuelekea ulipo mlango wa benki, huku amcho yangu yakiwa makini sana.Nikafika hadi kwa muhudumu pasipo askari wa mlangoni kunigundua
“Dada habari yako?”
“Salama”
“Meneja nitamuona wapi?”
“Una mawasiliano naye?’
“Hapana ila, ninaujumbe kutoka kwa bosi wangu.Kuna huu mzigo nimeagizwa nimkabidhi yeye”
“Unalijua jina la meneja?”
“Ndio, anaitwa bwana Turma”
“Basi twende, nikupeleke ofisini kwake”
“Asante”
Tukaingia kwenye lifti na kupandisha gorofa ya kwanza, nikaingia ofisini mwa Bwana Turma ambaye ni rafiki mkubwa wa mama, na mimi ananifahamu vizuri sana.Kwa bahati nzuri nikamkuta hana mtu anaye zungumza naye
“Meneja unamgeni”
“Muambie aingie”
Muhudumu akaniruhusu kuingia ndani ya ofisi, kisha yeye akaondoka, nikaivua kofia yangu na kumfanya bwana Turma kutabasamu baada ya kuniona
“Eddy, umekuwa askari?”
Aliniuliza huku akicheka
“Hapana mjomba”
“Ila?”
“Ahaa vijimambo tu,”
“Ila ninasikia unatafutwa na polisi”
“Ndio, ila mjomba ninaomba msaada wako”
“Msaada gani?”
“Kuna haya madini, yanadhamani kubwa sana.Ninaomba niwauzie nyinyi kama benki na pesa yangu muiweke humu ndani, ipo siku MUNGU akibariki, mimi au mwangu anaweza akasaidiwa na hiyo pesa”
Bwana Turma akaniangalia kwa macho ya umakini, akaniomba nimuonyeshe hayo madini.Nikamfungulia begi na kumuwekea, kibegi juu ya meza.Akabaki akishangaa
“Umeyatoa wapi?”
“Hii ni mali ya mama, ninakuomba sana uniwekee”
“Wewe ulikuwa unayauza kwa kiasi gani?”
“Bilioni moja na nusu shilingi”
“Mbona nyingi sana”
“Hata haya madini, yanadhamani kubwa sana.Nikisema niuze kwa masonara si chini ya bilioni tano”
“Sawa mjomba nimekuelewa, ngoja nikawaite wahasibu na wanasheria wa benki tuwez kufanya biashara”
“Sawa mjomba”
Bwana Turma akatoka nje ya ofisi yake na kuniacha nikiwa ndani, nikakaa zaidi ya dakika kumi na tano, sikumuona bwana Turma kutokea, nikaanza kupata wasiwasi, labda amekwenda kuwaita askari.Nikanyanyuka na kukifunga kibegi changu, nikatizama kwenye kioo cha computer yake, iliyopo juu ya meza yake, kilicho gawanyika katika vipande sita vya picha za video za kamera za ulinzi na kuona gari aina ya Rangerover ikisimama kwa kasi nje ya Benki na wakashuka wasichana watano walio valia mavazi meusi huku wakiwa na bunduki mikonini mwao.Wakanza kuwashambulia askari huku walili wakiingia ndani ya benki na kuanza kuwashambulia askari na kuwaamrisha watu wote kulala chini.Nikamuona wakimuamrisha bwana Turma kuingia kwenye chumba ambacho ndicho wanahifadhia pesa
Japo ninaroho kidogo ya kikatili, ila kwa jinsi risasi zinavyo ngurumishwa nje na majambazi hawa, sikuthubutu hata kujaribu kutoka ndani ya chumba.Bastola yangu nikaishika vizuri kwa umakini huku macho yangu yakitazama kwenye kioo cha computer iliyopo juu ya meza.Nikawashuhudia wasichana wawili wakimuamrisha bwana Turma kuingia ndani ya chumba ambacho ni chakuhifadhia pesa.Wakaendela kuingiza pesa kwenye mifuko yao, nikamuona msichana mwengine akiingia akiwa na bunduki.Sikusikia kitu anacho kizungumza.Nikaanza kusangaa baada yakuwaona watu wakivuliwa nguo na kupangwa mstari katika mlango wa kutokea nje
“Wanataka kufanya nini hawa?”
Nilijiuliza swali ambalo jibu lake nikalipata baada ya kuona watu wakitolewa nje wakiwa uchi pasipo kuwa na nguo hata moja kwenye miili yao.Wasichana wakajichanganya kwenye kundi kubwa la watu wanaotoka wakiwa, wanakimbia.Nikaitumia nafasi hiyo na mimi kutoka ndani ya chumba huku kibeki changu nikiwa nimekifunga vizuri na kukishika kwenye mkono wangu wa kushoto huku mkono wangu wa kulia nikiwa nimeishika bastola yangu.Nikajichanganya kwenye watu na kukimbilia lilipo gari letu,Nikamkuta Dorecy akiwa amejiinamia kwenye gari, nikafungua mlango wa gari na kuingia ndani
“Eddy vipi huko?”
“Tuondoke, sikwema huku”
Nikawasha gari na kuliingiza barabarani kwa kasi ya hali ya juu,
“Eddy tunaelekea wapi?”
Dorecy aliniuliza huku akinitazama kwa macho makali, sikulijibu swali lake zaidi ya kuongeza mwendo kasi wa gari langu.Nikafika maeneo ya mataa na kukuta msongamano wa magari mengi yakiwa katika foleni
“Shiitii”
Nilizungumza huku nikiitizama gari ndogo ya polisi inayokuja nyuma yangu kwa kasi, wakionekana kunifwatilia mimi.Kutokana nyuma yangu hakuna gari, nikairudisha nyuma gari yangu, na kuingia barabara ya pili inayopitwa na watembea kwa miguu, Kazi yangu ikawa ni kupiga honi, huku nikiwa makini katika uendeshaji wangu.Watu wengi wakawa na kazi ya kulikwepa gari langu huku wengine wakijirusha kwenye mitaro kuepuka kifo
“Eddy angalia mbelee”
Dorecy alizungumza kwa sauti kubwa, kwani kuku gari la abiria linakuja mbele yetu kwa mwendo wa kasi, Kwa haraka sana nikakunja kushoto na kuzibaniza pikipiki za waendesha bodaboda zililozo pangwa barabarani wakisubiria wateja, kwa kupitia kioo cha pembeni, nikalishuhudia gari la abiria lilipoteza muelekeo na kuyakuma magari mengine na kusababisha ajali mbaya.Kwa ukubwa wa gari yangu haikuwa shida sana kuzikanyaga pikipiki mbili zilizopo mbele yangu.Nikapata kiupenyo cha kuingia barabarani na cakumshukuru MUNGU, hakuna magari ya foleni ambayo yanaweza kunizuia kuendelea na safari yangu, huku nikiwaacha waendesha pikipiki wakitoa matusi mengi juu yangu
Kwa mbali nikaliona gari, walilokuja nalo majambazi likichanja mbuga barabara ya kuelekea mkoani
“Wale ndio majambazi walio piga tukio benki”
Nilizungumza huku nililiinyooshea kidole gari la majambazi aina ya Rangerover.
“Mmmmm”
Dorecy aliguna, huku akinitazama machoni.Nikazidi kukanyaga mafuta na kuzidi kulisogelea majambazi, ambalo nalo linakwenda kwa mwendo wa kasi sana
“Eddy kuwa makini, wasije wakatushambulia”
“Powa”
Sikuona gari yoyote ya polisi inayokuja nyuma yetu, Nikazidi kulifukuzia gari la majambazi na gafla likakunja na kuingia porini
“Eddy nyoosha tuu, tusiwafate”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Powa”
Nikaachana na gari la majambazi na kuelekea zangu barabara inayokwenda mikoa ya Tanga na Arusha.Kwa mbali nikawaona askari usalama barabarani wakiwa wamesimama
“Eddy punguza mwendo”
“Huoni kama tutakamatwa?”
“Nitazungumza nao mimi”
“Dorecy”
“Fanya hivyo, la sivyo itakuwa ni tatizo kubwa”
“Powa”
Nikapunguza mwendo wa gari, na askari mmoja akatusimamisha, nikalisimamisha gari langu pembeni na askari huyo akaanza kuja kwa mwendo wa umakini, huku akilitazama gari langu.Nikaishika bastola yangu kwa umakini, ila Dorecy akaushika mkono wangu wa kushoto ulio shika bastola
“Tulia”
Dorecy alinizuia kufanya ambacho ninahaji kukifanya, kwa ishara askari akaniomba nifungua kioo cha gari upande nilio kaa mimi, nikatii kama alivyo hitaji mimi kufanya
“Habari yako afande”
Jamaa alianza kunisalimia, nikaachia tabasamu pana ambalo muda wowote ninaweza kulibadilisha
“Salama tuu, kaka”
“Mbona gari yako, mbele kidogo imebonyea?”
“Ahaaa kuna, mjinga alinibamiza kwenye mataa kule”
“Ahaaa, munaelekea wapi?”
“Nakwenda, Tanga mara moja kuna kazi hapo tumeagizwa na RPC”
“Kuna, gari tunaiwinda ya majambazi wamepiga tulio benki, ndio tupo tupo hapa, tunaisubiria”
“Ipoje hiyo gari?”
Polisi akaniwasha simu yake na kunionyesha picha cha gari hilo
“Nimetumiwa Whatsap hii picha”
Dorecy akaitazama picha ya gari ambalo, tulikuwa tumeongozana nalo
“Hii gari tumeongozana nayo”
Dorecy aliropoka na kunifanya nimgeukie na kumtazama kwa macho makali yaliyo jaa mshangao ndani yake
“Imengia wapi?”
Dorecy akaanza kumuelekeza askari gari sehemu ilipo ingia, askari akawajulisha wezake na sisi tukaondoka
“Dorecy umefanya nini?”
“Kwani tatizo lipo wapi?”
“Sio tatizo lipo wapi, wewe inakuwaje unawachomesha watu wa watu katika ishu zao”
“Sio ishu zao, kumbuka hata mimi ni askari”
“Hata kama”
“Sio hata kama, wewe hukuona ni watu wangapi walio uliwa nje ya benki”
“Ila sijapenda hiyo tabia sawa”
“Eddy, kumbuka hata wewe ni muhalifu”
“So”(Sasa)
Nilimjibu Dorecy kwa kifupi, huku nikiwa nimekasirika sana
“Sihitaji hicho kibesi chako”
“Unasemaje wewe?”
“Sihitaji hicho kibesi chako cha kijinga, nitakubadilikia sasa hivi, umenielewa?”
Dorecy alizungumza kwa sauti ya ukali, huku akinitazama kwa hasira.Kwa kona ya jicho la kushoto nikamtazama Dorecy na kugundua hajafunga mkanda, nikaongeza mwendo wa gari, gafla nikafunga breki za kustukisha na kumfanya Dorecy kupiga kichwa kwenye dasbord ya gari.Kwa haraka nikamuwahi kumshika shingo yake na kuiminya kwa nguvu
“Huwa sipendi, ujinga kwenye yangu maisha sawa?”
Niliminya Dorecy shingo yake kwa nguvu, huku nikimtakandamiza kwenye kwenye siti yake.Nikazichomoa bastola zake katika sehemu alipo ziweka, na kuziweka upande wangu.
“Wewe ni nani?”
Nilizumuuliza Dorecy huku nikiendela kuminya kwa nguvu kwenye siti yake aliyo kalia.Dorecy akawa na kazi ya kuushika mkono wangu ulio ishika shingo yake
“Ed...eddy ni...aachi...ee”
“Nitakuua, mwehu wewe”
Nikamuachia Dorecy, akaanza kukohoa huku akihema kwa kasi kwani kwa jinsi nilivyo mkaba ni nusu ya kuyaona mauti
“Upo na mimi, au?”
Nilimuuliza Dorecy na kumfanya aendelee kukohoa, nikabaki nikiwa nimemtazama kwa macho makali kama ya simba dume aliye uliwa mke wake, Dorecy akanitazama kidogo kisha macho yake akayakwepesha tena na macho yangu na kutazama chini huku akiendelea kukohoa.Nikaichukua bastola yangu na kumuelekezea Dorecy ya kichwa huku nikiwa nimeikandamiza kwenye nywele zake, nikamshuhudia Dorecy akitingishika mwili mzima
“Nimekuuliza, upo na mimi au?”
“Nipo na wewe”
Nikaachia msunyo mkali na kuishusha chini bastola yangu na kuwasha gari langu na kuendelea na safari.Hadi ninafika Segera ikanilazimu kusimamisha gari kwani sikujua ni wapi nielekee, kwani Arusha siwezi kwenda kutokana ninatafutwa,
“Mbona umesimamisha gari?”
“Nafikiria kwa kwenda”
Sote tukabaki kimya, kwa wakati huu sikuwa na uwe wa kwenda alipo mama, kwani sijajipanga vizuri na ukatili wa Mzee Godwin ninatambua vizuri sana, na nikienda kichwa kichwa ninaweza kufa nikiwa ninajiona
Twende Tanga”
Dorecy alizungumza
“Unapajua?”
“Ndio, kuna rafiki yangu kule atanisaidia pia kwa hili swala lako”
“Unamuamini?”
“Ndio Eddy”
“Pita basi huku, uendeshe hari kwani mimi sipajui Tanga”
“Sawa”
Dorecy akashuka kwenye gari na mimi nikahamia kwenye siti yake.Akaingia kwenye gari na safari ikaendelea, ila kwa muda wote nipo makini sana na Dorecy kwani anaweza kubasilika wakati wowote ikawa ni tatizo jengine kwangu
“Ulishawahi kufika Tanga?”
Dorecy alizungumza
“Hapana, ndio leo ninakwenda”
“Sawa”
“Kwa nini, umeniuliza hivyo?”
“Hapana, nilihitaji kujua tuu kama ulisha wahi kufika”
Nikamtazama Dorecy kwa umakini, kisha nikashusha pumzi nyingi.Safari ikaendelea huku nikimuomba Mungu, Dorecy asije kuniyumbisha hata kidogo kwenye mpango wangu wa kumuokoa mama yangu, ambaye siamini kabisa kama Mzee Godwin amemuua hadi sasa hivi.Japo ninausingizi mzoto, ulio tokana na uchovu wa hekaheka za jana hadi sasa hivi, sikuweza kabisa kuyaruhusu macho yangu kufumba kwani, litakuwa ni kosa kubwa sana kwangu na sukujua ni kitu gani ambacho Dorecy anakifikiria kichwani kwake kuhusiana na mimi.
Kila ninavyo jizuia kuyafumbua macho yangu, ikafikia kipindi nikajikuta nikishindwa kuvumilia, nikaiminya kidogo siti yangu kwa nyuma na kuiegemea vizuri na kulala, gafla nikamuona Mzee Godwin akiwa amemshika mama yangu na kumuweka juu ya meza kubwa, akaipanua miguu ya mama juu ya meza huku akisaidiana na watu wake, akaanza kumkita misumari, mirefu ya miguuni kisha, akampigilia misumari mingine kwenye viganja vya mikono yake, pembeni yupo Madam Mery na Manka wakishangilia jinsi mama anavyo fanywa
“Muue, kwani hata yeye mwanaye ameniulia mume wangu kikatili sana”
Madam Mery alizungumza huku akishangilia na kupiga makofi akifuahia sana kitendo kinacho endelea.Mama akazidi kulia kwa uchungu, huku damu nyingi zikiwa zinamiminika katika miguu ya viganja vya miguu yake
“Nimekuambia chinja kabisa huyo”
Madam Mery aliendelea kushangilia, Madam Mery akachukua mashine ya kupasulia miti mikubwa na kumkabidhi Mzee Godwin
“Weka dishi la maji chini”
Mzee Godwin alizungumza, Manka akalisogeza dishi la maji chini ya meza na kuliweka vizuri, na damu za mama zinazo toka kwenye mikono yake zikaanza kuingia ndani ya dishi.Mzee Godwin akaanza kuiwasha mashine ya kukatia miti hadi ikawaka, kwa kutumia mashine ya kukatia miti akaanza kuukata mguu wa kulia wa mama, na kuzidi kukizidisha kilio cha mama.Akaendelea kuikata miguu ya mama miguu ya mama.
Hakuishia hapo, kwa kutumia mkasi mdogo akaichana tisheti ya mama na kumuacha kifua wazi, akalishika zima moja la mama, akalinyonya kidogo kisha akachukua kisu kikali alicho kabithiwa na msaadizi wake na kukilikata zima la mama upande wa kulia jambo lilizidi kumuongezea mama uchungu, akaendelea kulia kwa maumivu anayo yapata
“G Niue tu, kuliko kunitesa hivi”
Mama alizungumza kwa sauti iliyo jaa vilio, mzee Godwin na watu wake wakaanza kucheka kwa dharau akiwemo, Manka na Madam Mery.
“Unataka kufa?”
“Bora nife, kuliko kunifanya hivi”
Mzee Godwin akalitupa ziwa la mama alilo likata ndani ya beseni, kisha kwa nguvu akakichoma kisu chake, tumboni mwa mama na kuuanza kumchana hadi utumbo wake ukatoka nje, kwa kutumia mashine ya kukatia miti akakikata kichwa cha mama na kukitenganisha na mwili wake
“Nooo”
Nilizungumza kwa nguvu, huku nikistuka na kujikuta nikiwa ndani ya gari hapa ndip nikagundua ni ndoto kwa kila kitu nilicho kuwa nimekiona juu ya mama yangu, jasho jingi likazidi kunimwagika na kulisababisha shati langu la pilisi kulowa kama nimemwagiwa maji mengi.Nikaendelea kutasikilizia mapigo ya moyo jinsi yanavyo kwenda, huku nikiwa nimetizama chini, nikageuza shingo yangu upande alio kaa Dorecy na sikumku.Nikanyua kichwa kwa haraka huku nikiwa na wasi wasi na kukuta gari ikiwa imesimama nje ya kituo cha polisi kilicho andikwa kwa maandishi makubwa
{KITUO CHA POLISI CHUMBAGENI TANGA}
Nikamuona Dorecy akitoka nje ya kituo, akiwa ameongozana na askari watatu wenye bunduki mikononi mwao, huku akinyoosha kidole sehemu ilipo gari, nikajaribu kufungua mlango ila nikashindwa na polisi nao kwa mwendo wa umakini wakazi kuisogelea gari yangu
Nikazidi kuchanganyikiwa, kwa jinsi askari wanavyo isogelea gari langu kwa umakini.Nikajipapasa mifukoni mwangu sikukiona bastola zangu jambo lililoufanya mwili wangu kupoteza nguvu zote na kubaki nikiwa ninawatizama hadi wanafika kwenye gari.Dorecy akawa wa kwanza kufungua gari na kuingia huku akishusha pumzi
“Jamani, huyu ni shemeji yenu, anaitwa Eddy, Eddy hawa ni rafiki zangu nilikuwa depo so ndio nimepitia hapa kuwaona”
Nguvu zote za mwili zikazidi kudidimia kwani nilidhani kuwa jamaa wamekuja kunikamata kwa makosa niliyo yafanya
“Kaka habari yako?”
Askari mmoja alinisalimia, hata nguvu za kumuitikia sikuwa nazo zaidi ya kukitingisha kiwachwa changu nikimaanisha kwamba nimemuitikia salamu yake
“Unaonekana umechoka mume wangu?”
Dorecy alizungumza huku akinishika kidevu changu
“Yeaah”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijibu kwa upole mwingi
“Kaka, mtunze bwana dada yetu, wewe si unaona jinsi alivyo mchuma wa huakika”
Askari mmoja alizungumza huku akiachia tabasamu usoni mwake
“Musijali kwa hilo”
Niliwajibu, kidogo hali yangu ikaanza kunirejea, hata mapigo ya moyo kidogo yakabadili muelekeo wake na kurudi katika mapigo yake 72 kwa dakika
“Huyu dada yetu kipindi tupo depo, Moshi alihamishwa na kupelekwa JWTZ”
“Kaka, hivi huchezei makofi mawili matatu, kwa maana shosti alikuwa mkorofi huyo”
Sote tukajikuta tulicheka, kwa maana sikutarajia kuwa hawa jamaa muda huu nitakuwa ninacheka nao kwa furaha kiasi hiki
“Hapana jamani, ubabe nimeacha siwezi kumpiga mume wangu, mwenyeni ninampenda kama nini?”
“Ahaaa Dorecy leo unapenda, kwa maana ninakumbuka afande Nyendeza alikutongozaga kipindi tupo porini, acha umporomoshee mangumi”
“Hahaaaa, yule alikuwa mwehu, Eti ananitongoza huku ananilazimisha kuninyonya denda hapo hapo, kwa nini nisimpige mangumi”
“Ahahaa, jamaa tulikuwa naye hapa Chumbageni, ila alihamishwa mwaka jana kapelekwa Handeni huko”
“Dooo, muache akakutane na watoto wa kizigua wamroge hadi akome”
“Haaaha, na ule weusi lazima wamtengenezee carolaiti ya tura”
Sote tukajikuta tukicheka kwa furaha kwani, mazungumzo ya hawa jamaa yamenifanya nijihisi mchangamfu gafla
“Unajua yule ndio chanzo cha mimi kupelekwa JWTZ?”
“Weee”
“Mama vile, si alikuwa anajiona mbabe.Sasa nilivyo mpiga ile siku ticha akaniita ofisini kwake na kunihoji hoji maswali, akaniambia tangu aanze kufundisha haijawahi kutokea afande wa kike kumpiga afande wa kiume”
“Ila alikupa kabahati”
“Kiupande mmoja ninamshukuru, kwa maana alinisaidia sana”
“Sisi bwana, bado tunakula ngwamba na wananchi, nakuona wewe upo kitengo kikubwa, hadi munatembelea na V8?”
“Dulla hembu acha utani?”
“Kweli Dore unadhani ni utani? Sisi tumesha telekezwa, tunakazi ya kutembelea vidifender hivi vilivyo choka, kila siku vinakazi ya kushinda gereji”
“Ahaaaa Dulla wewe ropoka usikiwe, utahamishiwa kitivo huko ukale makabichi”
Sote tukabaki tukiwa tunachekea kwa sauti ya juu hadi baadhi ya askari walio karibu nasi wakawa na kazi yakutushangaa
“Kwenye ukweli, inatubidi tuzungumze”
“Ni kweli, ila mmmmmm”
“Jamani, naona tukikaa sana hapa, hamuta enda lindo sisi ngoja tusepe”
“Kwani, munakwenda wapi muda huu?”
“Tunataka twende pande, jeshini”
“Mbona usiku, chukueni hoteli mulale, asubuhi na mapema mudimke”
“Etii?”
“Hakuna cha etiii, njia hiyo usiku sasa hivi sio nzuri”
“Kuna majambazi?”
“Mara mia kungekuwa na majambazi”
“Ila?”
“Kuna vituko vya ajabu, unaweza kukuta watu wanakatiza barabarani wakiwa na kanzu huku wanakwenda kuzika, ukisema uwapige risasi, kesho unakufa”
“Mmmmm”
Ilinibidi nigune
“Kaka Eddy wala usigune, hii ndio Tanga bwana, ukicheza vibaya wala humalizi siku”
“Sasa hapa ni wapi kwenye Hotel nzuri?”
Dorecy aliuliza
“Zipo nyingi, ni pesa yako tuu”
“Maeneo gani zipo?”
“Chuda si unapapata?”
“Ndio?”
“Sasa, ule mtaa ukikosa sehemu ya kulala ujue unabahati mbaya”
“Sawa jamani, ngoja tuondoke, nikisema tuendelee hapa tutakesha”
“Umeona eheee”
“Nishidaaa”
“Jamani, tutaendelea kuwasiliana”
“Tunawasiliana vipi wakati hatuna hata namba za simu ulizo tuachia”
“Simu sina”
“Haaaa, unaishije bila simu?”
“Nitachukua kesho”
“Sikia chukua simu yangu, mukifika sehemu mutakapo pata chumba utatujulisha, si unajua wewe sasa hivi ni mtu mkubwa kwetu, shemeji samahani bwana kwa kuipendekaza kumkabithi simu bibie, usije ukanihisi vibaya”
“Hamna shida, ndugu zangu pia mutakuwa mumetusaidia sana”
“Ndio maana nimekukubali shem wangu, ingekuwa jinga lengine hapa lingevuta mdomo kama yule bibi tuliye mkamata jana ameanguka na ungo wao wakichawi”
“Eheee, hayo mengine tena, mumeanza kukamata hadi wachawi?”
Dorecy aliuliza
“Ohoo, shosti huu mji bwana ahaaa, Juzi kati maeneo ya mwakizaro huko, tulipewa taarifa kuna bibi ameanguka na ungo, acha wananchi wamabamize mawe.Sasa sisi tukaitwa kumchukua, mwanagu kabibi kaze japo kamepigwa ila hakajafa, sasa huo mdomo alivyo uvuta mbele kama anapiga busu la karne”
Jamaa alizungumza na kuzidi kutufanya tucheke kwani alitoa mfano wa jinsi bibi huyo alivyo uvuta mdomo wake mbele
“John unafanana naye”
“Dullah hembu acha ujinga bwana”
“Hahaaa, jamani ngoja tuondoke”
“Sasa utaondokaje pasipo mimi kukuambia namba gani unipigie”
“Haya mwaya, niambie”
John akachukua simu aliyo mpa Dorecy, na kuandika namba na kumuonyesha Dorecy
“Haaaaa....!!”
Dorecy alihamaki
“Nini?”
“Mbona mba mbaya hivi, kama amba za majeneza”
“Ahaaa Dore sasa hizo dharau”
“Ahaaa kwa hiyo John na wewe unanunaga?”
“Hapanaaa”
“Unazani atanuna, anaogopa ukamfanaya kama shosti yake Nyandeza”
“Jamani, hembu achani utoto, hapa mume wangu ana njaa ngoja twende sehemu tukale kwanza kisha nitawapigia simu sehemu muje tunywe kidogo”
“Mambo si ndio hayo”
“Nyooo, John ndio maana pesa yako ya marupurupu unaimalizia kwenye pombe”
“Ahaaa nina shida gani, sina mke wala mtoto, acha niuponde ujana”
“John hadi sasa hivi huna mtoto!?”
“Wewe unaye?”
Dorecy akizungumza
“Ahaaa haya bwana, kwa herini”
“Sawa, bro Eddy mkumbushe bwana huyo kuja kunywa kidogo, si unajua tena katikati ya mwenzi huu, hali mbayaa”
“Powa kaka zangu, tupo pamoja”
Niliwajibu, Dorecy akafunga mlango wa gari na kuanza kuondoka taratibu,
“Tunaelekea wapi?”
“Kuna, hiteli hapo mbele inaitwa Nyinda Anex ngoja nikacheki kama tutapata chumba”
“Powa, hivi wale rafiki zako wanafanya kazi kweli?”
“Ahaaa, wale ni pumba, ningesema nikae nao pale.Tungekesha”
Tukafika kwenye hoteli aliyo niambia, Dorecy akashuka kwenye gari na kuniomba nimsubiri.Nikageuka siti ya nyuma na kukikuta kibegi changu cha madini, nikakifungua ndani na kukuta kikiwa kama kilivyo, hakuna kitu hata kimoja kilicho pungua.Dorecy akarudi na kuingia ndani ya gari
“Vipi umepata?”
“Vyumba vimejaa”
“Ahaa, mkosi huo”
“Ngoja twende, hapo mbele kuna Hotel ya ghorofa tuliipita”
“Powa, alafu bastola zangu zipo wapi?”
“Fungua hapo, pembeni utaziona”
Dorecy akanielekeza, nikafungua sehemu ya pembeni yangu kwenye siti na kuzikuta zote mbili, nikazichukua na kuzichomeka kwenye viatu, Tukafika kwenye Hotel moja inayo itwa Mtendele.Kama kawaida Dorecy akashuka na kuniacha kwenye gari, akaingia na baada ya dadika tano akarudi akiwa ameshika funguo ya chumba mkononi
“Nimepata”
Nikashuka ndani ya gari huko nikiwa nimeshika kibegi changu chenye madini, na sote tukaingia kwenye hoteli, hiyo iliyo tengenezwa vizuri kwa kwenda juu.Tukapandisha ghorofa ya tatu kilipo chumba chetu,
“Eddy, hivi hicho kibegi kina nini?”
“Nitakuambia, ila kikubwa kwanza, tuzungumze vitu vya maana”
“Hata kuoga hatuogi?”
“Tutaoga, kikubwa tuzugumze ni jinsi gani tutampata mzee Godwin?”
“Eddy, mzee Godwin anamtandao mkubwa sana, tena sana.Sio mtu wa kumuendea kichwa kichwa, wewe mwenyewe unaona jinsi alivyo kutia nguvuni, laiti ingekuwa sio mimi, sijui ungekuwa wapi hadi sasa hivi.”
“Sawa, ila kuna vitu ambavyo nahitaki kuvifahamu kupitia wewe”
“Uliza”
“Hivi ni watu gani ambao, mzee Godwin anashuhulika nao?”
“Ahaaa, ni wazito serikalini, ukumbuke kwamba yule ni mtu mkubwa sana kwenye hii nchi, pili utambue ni mkuu wa jeshi, yaani akitoka raisi katika mamlaka ya jeshi anafwata yeye, so huyo sio mtu wa kusema unamuendea kichwa kichwa.Nilazima tuwe na mipango ambayo itatufanya tuweze kumpata mama kwanza, kisha hao wengine watafwata”
Nikashusha pumzi zangu huku ninamtizama Dorecy kwa umakini machoni
“Eddy, lengo la mimi kukuleta huku ni wewe kwanza ukapate kwanza mazoezi ya kijeshi, japo wewe mwenyewe unajiona umekamilika ila bado, tena sana”
Dorecy alizungumza huku akinitazama machoni
“Kwani kupambana na mtu kuna ulazimu wa mazozi ya kijeshi?”
“Ingekuwa sio hivyo basi hata wauza mitumba wangeenda kupigana vitani”
Jibu la Dorecy likabaki likinipa msongamano wa mawazo
“Ila huoni kama baba atajua?”
“Baba gani?”
“Mzee Godwin”
“Ahaaa, huko ninapo kupeleka mimi, atakaye jua ni mimi na huyo ndugu yangu ninaye mfwata huko”
Dorecy alizungumza kwa kujiamini sana
“Sawa nimeku.....”
Nikastukia Dorecy akinivuta kwa nguvu na kuninyanyua kwenye sofa nililo kaa, nikastukia akinitandika kichwa cha uso kilicho niyumbisha huku nikiona giza kwenye macho yangu, zikiambatana na nanenane
“Ahaaa”
Niliropoka, ila nikastukia akinitandika ngumi mbili za kifua zilizo niangusha chini, nikachomoa bastola ya kwanza kwenye kiatu hata kabla sijaishika vizuri nikashtukia teke likitua kweny mkono wangu na kuiangushia mbali bastola, nikachomoa ya pili, hali ikawa kama hiyo hiyo ya kupigwa teke la mkono
“Unanipigia nini, sasa”
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga, nikajaribu kunyanyuka, ila nikaikuta miguu yangu ikipigwa na mguu mmoja wa Dorecy, nikajikuta nikirudi chini tena.Kwa jicho langu moja nilamchunguza Dorecy jinsi alivyo simama huku mikono yake akiwa ameikunja ngumi
Nikasimama kwa haraka, Dorecy akarusha ngumi, niliyo bahatika kuiona na kuikwepa.Kitendo cha mimi kuikwepa ngumi, nikastukia kigoti cha Dorecy kikitua kifuani mwangu na kujikuta nikinyanyuka kwenda juu mithili ya mtu aliyepigwa shoti ya umeme, nikastukia ngumi moja kali ikitua kwenye komo langu na kunisabanisha kunirudisha kwenye kochi huku macho yangu nikiwa nimeyafumba baada ya kuiona ngumi nyingine ikinijia kwenye uso, nikaisikilizia ila haikufika kwa wakati muafaka ikanibidi kufumbua macho na kujikuta nimetazamana jicho moja la bastola aliyo ishika Dorecy, huku ikiwa imesimama sentimita chache kutoka yalipo macho yangu
“Sali sala yako ya mwisho?”
Dorecy alizungumza huku sura yake ikiwa imejaa jasho jingi, na mikonjo iliyonifanya niamini huu ni mwisho wa maisha yangu mimi Eddy Godwin
“Dorecy umechanganyikiwa?”
Nilimuuliza Dorecy anayeonekana kumaanisha kile kitu anacho kizungumza, hakunijibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuendelea kunielekezea bastola yake kwenye sura yangu
“Eddy usimuamini kila unaye muona utaumia sawa?”
Dorecy alizungumza na gafla nikastukia akinipiga na kitako cha bastola kwenye kichwa changu, giza lililo andamana na maruwe ruwe kitanitawala taratibu katika macho changu na kwa mbali nikausikia mlango ukifunguliwa, baada ya muda kidogo sikujua ni kitu gani kinacho endelea
***
Nikahisi nikiguswa mgongoni, taratibu nikayafumbua macho yangu na kukutana na viatu vya mwanaume vikiwa vimesimama kando yangu, nikakinyanyua kichwa changu taratibu huku nikiwa ninamaumivu makali, nikakutana na sura ya mwanaume ambaye amevalia sare za wahudumu wa hoteli hii
“Kaka, habari yako”
Jamaa alinisalimia, huku akinitazama usoni mwangu.Sikumjibu cha kwanza kutazama ni kuangalia sehemu nilipo weka begi langu lenye madini ndani, sikuliona na kujikuta nikikurupuka na kusimama, nikaingia bafuni na kukuta kweupe hakuna mtu
“Kaka vipi?”
“Ku..kunaa dada hiv...i mrefu ume...muona wapi?”
“Yule uliye ingia naye jana usiku?”
“Jana, usiku? Eheee huyo huyo”
Niliungumza huku nikipiga hatua kuelekea kwenye dirisha, nikatamani kuanguka chini na kupoteza fahamu, kwani mwanga mkali wa jua nilio ukuta nje ya dirisha umenichanganya kiasi kwamba nimekosa la kuzungumza
“Yule mbona aliondoka usiku ule ule?”
“Shitii”
“Kwani, hamujuani?”
“Ehee”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hamujuani?”
Hata sikujua nimjibu vipi, muhudumu huyu aliye simama mbele yangu, nikajichunguza na kugundua kuna damu zilizo mwagika kwenye shati langu la kiaskari nililo livaa.
“Unamichirizi ya damu puani kaka”
Muhudumu alinionyesha, nikasimama kwenye kioo kilichopo kwenye hichi chumba na kujikuta ni kweli nilitokwa na damu za puani, ambayo kwa sasa imekauka.Muhudumu akanipatia taulo na nikaanza kujifuta
“Alafu, kuna askari walinionyesha picha yako mida ya asubuhi, na kuniuliza kama wewe upo kwenye hii hoteli nikwaambia kwamba uliondoka jana usiku”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, huku wasiwasi mwingi ukianza kunitawala
“Waliondoka?’
“Ndio waliondoka, ila sijajua kama watarudi tena au la”
“Asante ndugu yangu”
Nikatizama chini, na sikuona bastola zangu nikatambua ni lazima Dorecy atakuwa ameondoka nazo zote,
“Kaka kwani wewe ni askari kweli?”
Jamaa aliniuliza, nikamtazama kuanzia juu hadi chini, kwani maneno ya Dorecy aliyo niambia nisimuamini mtu yakaanza kunirejea kichwani mwangu
“Kwani vipi?”
“Nimeuliza hivyo kwa nia nzuri tu?”
“Nia gani?”
“Kwa maana picha ya sura yako, sio mara yangu ya kwanza kuiona kwenye mach yangu”
“Ulisha wahi kuiona wapi?”
“Wewe si ndio, Eddy?”
Sikustushwa sana kwa maana ninatambua kwamba ninatafutwa karibia nchi nzima ya Tanzania kwa tukio la kumuu Derick
“Mimi sio Eddy?”
“Sawa”
Nikatoka nje ya chumba, nikatizama kwenye kordo zote na kuona hakuna dalili ya kuwa na mtu, nikaanza kutembea kwa hatua za haraka kuelekea kwenye ngazi za kushuka chini, nikaanza kushuka kwenye ngazi ya kwanza, nikaisikia miguu ya watu wakikimbia na kunilazimu kuchungulia chini, nikaona kundi la askari wapatao sita wakipandisha ngazi kwa haraka huku wanne wakiwa na bastola na nyuma yao wakiwa wameongozana na mzee mwenye kitambi kwa haraka nikatambua ni meneja wa hii hoteli.Nikarudi juu haraka na kukutana na muhudumu niliyekuwa chumbani
“Tupandishe huku juu”
Aliniambia huku akitangulia kupandisha ngazi za kuelekea ghorofa ya juu, tukapandisha ghorofa ya juu na kutokea kwenye moja ya mlango wenye ngazi za chuma zilizo elekea chini.Tukaanza kushuka kwa haraka
“Huku ni nyuma ya holet”
Aliniambia, tukashuka hadi chini, tukakuta kijimlango kidogo, kilichopo kwenye ukuta na tuapita na kutokea kwenye hoteli nyingine niliyokuta kibao kikubwa kilicho andikwa ‘Macarios Hotel’
“Tupite huku”
Tukakatiza kwenye reli, na kushika barabara ya kuelekea magharibi kwetu na kutukea kwenye barabara moja inayopitisha magari mengi
“Hapa kunaitwa kwaminchi”
“Sawa”
Tukaendelea kukatiza mitaa, na kufika kwenye mtaa mmoja ulio na nyumba nyingi zilizo banana sana
“Hapa ni mwamboni”
“Kupo kama mbagala”
“Kwa nini?”
“Nyumba zake jinsi zilivyo”
“Karibu ndani”
Tukaingia kwenye nyumba iliyo chakaa kiasi fulani, akanikaribisha ndani kwake, ambapo kuna kitanda na kistuli kimoja, pamoja na nguo baadhi
“Karibu kaka”
“Asante”
Nikakaa kwenye kiti na yeye akaketi kwenye kitanda chake
“Kwa jina mimi ninaitwa Mbasa, ni mwenyeji wa bara, mkoa wa Shinyanga huko”
“Ahaaaa, kwanza ninashukuru kukufahamu, pili ninashukuru kwa kunisaidia”
“Kusaidiana ni jamba la kawaida, hususani kwa vijana kama sisi ambao tunatakiwa kuwa bega kwa bega katika kuhakikisha tunafikia kwenye malengo yetu”
“Nikuulize kitu Mbasa?”
“Uliza tuu”
Unawezaje kumsaidia mtu usiye mjua?”
“Kaka Eddy, mimi ninakujua na nimekuwa nikifwatilia habari zako kwenye magazeti jinsi unavyo tafutwa na jeshi la polisi kwa mauaji ya bwana Derick”
Nikamtazama jamaa vizuri, nikajitazama na mimi vizuri nikajisemea kimoyo moyo hata akitaka kuanzisha ugomvi, ninamudu tena sana
“Isitoshe, nilivutiwa sana na wewe”
“Kwa nini?”
“Umri wako na matukio yako uliyo yafanya ni tofauti”
“Sawa, ila ninakuomba usimuambie mtu juu ya uwepo wangu hapa kwako”
“Si wezi kwa maana ninahitaji tusaidiane”
“Tusaidiane?”
“Ndio, shida uliyo kuwa nayo wewe kidogo inaendana na yakwangu?”
“Shida gani”
***
“Nilizaliwa kwenye familia ya maisha bora, baba alikuwa anamiliki migodi ya madini, alikuwa ni tajiri sana.Ila niliaziliwa peke yangu kwa bahati mbaya mama yangu alifariki kwa ajali ya gari, nilikuwa darasa la sita”
“Baba alilazimika kumuona mwanamke mwengine, ambaye alikuwa ni binti mdogo kiasi na alijaliwa uzuri halisi kutoka kwa Mungu, kutokana na kazi nyingi za baba tangu, alitumia muda mwingi sana kuwa mbali na mama mdogo, ikafikia kipindi nikawa na mahusiano na mama mdogo”
“Badi mama mdogo alipata ujauzito wangu na mbaya zaidi niliwahi kubalehe haraka sana, ule ujauzito tuliulea katika mzingira ya kificho na ninacho mshukuru MUNGU, baba alisafiri kikazi kwenye Ujerumani na alikaa mwaka na nusu so ile ishu hakuijua”
“Mwanangu alizidi kukua pasipo baba kujua hilo, hadi anatimiza miaka mitatu, kama unavyo jua dunia haina siri baba yangu akaja kuligundua lile swala la mimi kuzaa na mama mdogo”
“Huwezi kuamini, kuna siku baba alituomba twende naye shambani, hatukuwa na kipingamizi kutokana tulikuwa hatujui kinacho endelea”
“Ngoja kwanza hapo mtoto wenu mulikuwa mumemuweka wapi?”
“Mtoto, tulimpeleka kwa dada yake yule mama mdogo, pesa za matumizi mimi ndio nilikuwa ninazipeleka pasipo baba kuelewa mchezo”
“Sasa tuifika shambani, tukiwa na mama mdogo, pamoja na baba.Tulikuta watu wake ambao mara chache huwa ninawaona ona, huwezi amini nilimkuta mwangu akiwa ametundikwa juu ya mti huku ngozi yake ikiwa imechunwa kama mbuzi aliye chunwa ngozi”
“Baba, yangu alitugeukia hapo hapo na kuanza kumshambulia mama mdogo kwa ngumi na mateke, huwezi ukaamini nilimshuhudia mama mdogo akichemshwa katika pipa lenye mafuta ya kula, huku akiwa hai, cha kumshukuru MUNGU, niliweza kufanikiwa kukimbia ila niligwa risasi za ya paja na kuanzia hapo sikuweza kumuona baba tena kwenye maisha yangu”
“Ila nilikuja kugundua kwamba baba pia alihusika na ajali ya mama”
“Kisa kilikuwa ni nini?”
“Hadi leo sijajua kisa kilikuwa ni nini hadi baba akaamua kumuua mama”
Nilimsikiliza Mbasa vizuri sana, kidogo yeye ana nafuu sana katika simu lizi ya maisha yake ya nyuma
“Baba yako anaitwa nani?”
“Godwin?”
Nikastuka, na kumtazama vizuri
“Mbona unastuka kaka Eddy?”
“Anaitwa Godwin, yupoje poje?”
“Mrefu kiasi, ni maji ya kunde kidogo, anamwili ulio jazia kidogo na pia anakovu kwenye mkono wake wa kulia, mama aliniambia baba alipataga ajali akiwa kijana”
Sifa ambazo Mbasa alinielezea zifanana na sifa za Mzee Godwin ambaye hapo mwanzo niliamini ni baba yangu ila ukweli ni kwamba ni baba yangu mkuwa, ila kitu kinacho nichanganya ni Mzee Godwin ninaye mjua mimi ni Mwanajeshi
“Ana kazi nyingine anayo ifanya ukiachilia na madini?”
“Ndio, nilikuja kushangaa siku nilipo sikia kwamba amepewa cheo cha kuwa mkuu wa jeshi wakati sijui hata jeshi yeye amekwenda lini?”
Nikajikuta nikishusha pumzi nyingi, nikamtazama Mbasa kuanzia juu hadi chini na kujikuta nikitingisha kichwa kwa kumuonea huruma
“Vita iliyupo mbele yetu ni kubwa sana”
“Kivipi?”
“Mbasa kwanza una umri gani?”
“Miaka ishirini”
Nikatabasamu, tabasamu lililo jaa uchungu kwa kumuonea huruma
“Adui yako ndio adui yangu”
Nilimuambia Mbasa na kumfanya abaki amenitumbulia mimacho,
“Kaka Eddy sijakuelewa bado?”
“Kwa sasa sio rahisi sana wewe kunielewa, ila utakuja kunielewa muda ukiwadia”
Sikutaka kumfafanulia kila kitu Mbasa, zaidi ya kuwa makini sana kwa kila jambo ninalo lizungumza, hii ni kutokana na moyo wangu kupoteza uaminifu juu ya kila anaye nisaidia.
***
Nikakaa nyumbani kwa Mbasa siku mbili mfululizo pasipo kutoka nje, na kila siku Mbasa akawa na kazi ya kunihadisia hali halisi inavyo endelea nje kuhuasiana na polisi wanao nitafuta, siku ya tatu nikaamua kutoka nje mida ya saa tatu usiku, nikiwa nimevalia nguo za mbasa ambazo kidogo kwangu ni ndogo, ila kutokana sikuwa na lakufanya nikaamua kufanya hivyo.Nikavalia kofia iliyo yaficha macho yangu na moja kwa moja nikaelekea kwenye moja ya baa inayo itwa kilimani, lengo langu ni kupata bia japo mbili ili kuiweka akili yangu sawa
Kama kawaida muhudumu mmoja akanisogelea huku akinitazama machoni mwangu, akisubiria nini niagize,
“Niletee, kilimanjaro ya moto”
“Sawa, naomba pesa”
Nikatoa noti ya elfu tano aliyo nipatia Mbasa mida ya jioni alipokuwa akielekea kazini kwake, kuingia katika zamu ya usiku.Muhudumua akaondoka na haikuchukua dakika nyingi akarejea akiwa na chupa bia niliyo muagiza
“Utatumia glasi?”
“Hapana, asante”
Taratibu nikaanza kuporomosha mafumba kadhaa ya bia, huku sehemu niliyo kaa inakigiza kidogo na nisehemu ambayo ninaweza kuwaona wanao ingia na kutoka kwenye hii baa.Baada ya muda kidogo nikawaona wasicha wawili wa kiarabu wakiingia kwenye baa hii, huku mmoja akiwa amevalia baibui na mwengine akiwa amevalia suruali ya jinzi pamoja tisheti iliyo mbana, wakasimama na kuanza kutazama tazama ni sehemu gani ambayo waneweza kupata viti na kwabahati nzuri meza niliyo kaa mimi ina viti viwili, na sehemu nyingine zimajaa watu.Wakapiga hatua za taratibu hadi sehemu niliyo kaa mimi
“Sahamani, tunaweza kuketi hapa?”
“Ndio munaweza”
Wakaa na mimi nikaendelea kunywa bia yangu ambayo, ninaishuhudia ikielekea ukingoni na muda wangu wa kukaa kwenye hii baa utakuwa umekwisha, ukimya ukatawala kati yetu na hakuna ambaye alimsemesha mwenzake, baada ya wao kugizia vinywaji wakawa na kazi ya kuchezea masimu yao makubwa ya kugusa na kidole
“Muhudumu”
Msichana mmoja alimuita muhudumu aliyekuwa anakatiza karibu yetu
“Mletee huyu kaka,kinywaji atakacho kihitaji yeye”
“Ahaa jamani mimi, hii moja inanitosha”
“Hapana, dada mwaya lete kinywaji kama anacho kitaka huyu kaka”
Sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana nao,
“Mimi naitwa Rajiti na mwenzangu anaitwa Sashah”
“Nashukuru kuwafahamu”
“Jamani hatupaswi kukujua jina lako?”
Nikatabasamu kidogo, huku nikiwa ninawatazama kwa macho ya uamakini kila mmoja kwenye sura yake
“Ninaitwa Thoma”
Niliwaongopea kuhofia jina langu la Eddy kuwa ni miongoni mwa majina yanayo tajwa kila siku katika vyomba vya habari
“Kuna kaka umefanana naye”
Sashah alizungumza, huku akiliiknja vizuri mikono ya baibui lake
“Nani?”
“Anaitwa Eddy”
Moyo ukaanza kunienda mbio huku mapigo ya kawaida yakibadilika na kuwa ya kasi sana kiasi kwamba nikaanza kujihisi vibaya
“Ahh….haaa sio mimi?”
Wakanitazama kwa umakini
“Samanani ninaomba niende msalani”
Nikawaaga na kunyanyuka, nikatamani kutoka nje ya baa ila macho yao yote tapo kwangu, nikamuuliza muhudumu ni wapi kilipo choo, akanielekeza na bahati mbaya kipo ndani ya baa hii na kama kingekuwa ni nje ingekuwa ni nafasi nzuri ya mimi kuwakimbia.Nikaingia chooni na kusimama kwenye moja ya kioo kilichomo humu ndani, nikaivua kofia yangu na kujitazama vuzuri
“Sijabadilika chochote usoni mwangu”
Nilizungumza kwa sauti ya chini, nikajiweka sawa na kuivaa kofia yangu na taratibu nikaanza kuelekea ulipo mlango, nikakishika kitasa cha mlango huku nikiwa ninahema sana, nikashusha pumzi nyingi na kuufungua mlango, nikapiga hatua mbili, gafla nikastukia nikizibwa pua na kitambaa chenye harufu ambayo tangu nizaliwe sikuwahi kuinusa, mtu aliye nikaba kwa nyma sikujua ni nani, na nilipo jaribu kuminyana naye, ndvyo naye alivyozidi kukikandamiza kitambaa puani mwangu na taratibu nikajikuta nguvu zikiniishia na nikapoteza fahamu.
***
Kwa mbali nikaanza kuona kitu nikiwa kinazunguka juu yangu, nikajaribu kuyakaza macho yangu, ila bado nikashindwa kuyafumbua, nikutokana na uchomvu mwingi ulio ambatana na usingizi mzito, nikajaribu kuinyanyua mikono yangu ila nikaihisi kuwa ni mizito sana, nikakigeuza kichwa changu upande wa kushoto na kukuta jamaa lenye miraba miine likiwa limekaa kwenye kiti, huku sura yake ikiwa na mindevu mingi sana.Hapa ndipo nilipo anza kugundua kwamba nimelala chali juu ya kindanda, sikuona kitu chochote kilicho ufunga mkono wangu, na sikuelewa ni kwanini nimekuwa mchovu kwenye mikono kiasi hichi
Nikaendelea kuvuta kumbukumbu ya nimefika vipi katika eneo hili, ila ubongo haukusoma kitu chochote zaidi ya kukumbuka kwamba nilikuwa nipo baa.Baada ya masaa kadhaa nguvu za mwili wangu zikaanza kurejea taratibu, nikapata nguvu hata ya kuyafumbua macho yangu hapo ndipo nikagundua kitu kinacho zunguka juu yangu ni feni
“Nipo wapi?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimuuliza jamaa, hakunijibu chochote zaidi ya kunitazamaa kwa macho makali, hukua akiendelea kuzichezea ndevu zake nyingi nyingi
“Nipo wapi?”
“Wee koma”
Jamaa alizungumza huku akininyooshea kidole, akionekana kukasirishwa na swali langu nililo tumia sauti ya ukali kumuuliza.Akasimama na kuitoa simu yake ya mfukoni
“Mtu wenu ameamka”
Sikujua anazungumza na nani, mapigo ya moyo yakaanza upya kudunda huku yakiandamana na wasiwasi mwingi, wazo la kwanza kunijia kichwani nikajua tarari nimeingia kwenye mikono ya Mzee Godwin, nikajaribu kusimama ila jamaa kwa haraka akaniwahi kunisukuma kitandani
“Ukilete ujinga jombaa nitakupoteza duniani?”
Nikazidi kuchanganyikiwa, baada ya muda wakaingia Rajiti na Sashah, wote wawili wamevalia suruali nyeusi na tisheti nyeusi, huku miguni wakiwa wamevaa, buti nyeusi
“Habari yako, Eddy?”
Rajiti alinisalimia, hapo ndipo nikadata kabisa na kutambua kwamba hawa si watu wazuri kwangu, kutokana niliwatambulisha kwa jina la Thomas, inakuwaje wananiita mimi Eddy
“Kamletee chakula”
Jamaa likatoka na kutuacha ndani ya chumba
“Eddy ninaimani utajiuliza imekuwaje hadi upo hapa” Sashah alizungumza
“Ndio”
Rajit akatoa picha mfukoni na kunirushia mimi kitandani nilipo lala, picha aliyo nirushia ina sura yangu na mama yangu zikiwa zimeambatanishwa kwa pamoja na kuitoa picha moja
“Usishangae sana, na kujiuliza ni wapi tumeitoa picha yako, kwa ufupi sisi tulikufwatilia kwa siku nyingi hadi jana tulipo fanikiwa kukupata” Rajit alizungumza
“Munataka nini kutoka kwangu?”
“Kikubwa tunacho kihitaji sisi ni wewe kukusaidia”
“Kunisaidia kivipi?”
“Utaelewa”
“Sisi ni wanajeshi wa kikundi cha Al-khaida, na kazi yetu kubwa ni kutafuta vijana wenye matukio makubwa kama yako, pia isitoshe tunahitaji kukupa msaada wa kumpata mama yako”
Baunsa akaingia huku akiwa amebeba sahani kubwa yenye vitu mbali mbali vya kufungua kinywa, akaviweka kwenye meza na kutoka nje
“Tunahitaji tukupeleke Iraq, yalipo makazi yetu kisha ukirudi Tanzania tukusaidia kwenye kazi moja tu”
Rajit alizungumza
“Kazi gani, unajua hadi sasa hivi sijawaelewa?”
“Eddy fungua akili yako, Tanzania nzima unatafutwa wewe, Je ukikamatwa ni wapi utapelekwa?”
“Gerezani” Nilimjibu Rajit
“Je upo tayari kuishi, gerezani?”
Swali la Rajiti likanifanya nikae kimya pasipo kumjibu chochote
“Hapa kwani nilipo ni wapi?”
“Hapa ni Mombasa, nchini Kenya.Jana tulisafiri usiku kucha hadi hapa”
“Kwa nini muniteke?”
“Ilitulazimu”
Rajiti na Sashah wakendelea kunishawishi hadi nikakubali kwenda nao Iraq kwani nikiangalia kwa jinsi maisha yangu yalivyo ya kuruka ruka kama ndege nikaona ipo siku nitanaswa kwenye jumba bovu.Akaja daktari mwenye asili ya kiarabu, waliye niambia anahusika na kazi ya kuchonhesha sura bandia, dakatari akanifanyia vipimo vya haraka na kazi ya kuchongesha sura nyingine itakayo kaa sawa kwenye uso wangu ikaanza mara moja.Ndani ya masaa sita tarari daktari akawa ameikamilisha kazi aliyo agizwa na Sashah.Kazi ya kupandikizwa sura bandia ikaanza mara moja, huku daktari akiifanya kwa umakini wa hali ya juu, haikuchukua muda mwingi sana kuvishwa sura bandia, nikaa lisaa moja kwenye kifaa ambacho daktari aliniambia kinaghusika na swala zima la kuikausha sura yangu mpya
Baada ya zoezi zima la kubadilishwa sura kuisha, Rajiti akanipa kioo niitazame sura yangu niliyo pandikizwa juu ya sura yangu halisi, sikuyaamini macho yangu kwani nimebadilika kupita maelezo hata mimi mwenyewe nikajisau
“Ebwaane eheee ni mimi kweli au naota?”
“Ni wewe, mbona hapo umetokelezea”
“Etii eheee?”
“Ndio”
“Hahaaaa”
“Sashah yupo wapi?”
“Amekwenda Mjini mara moja”
Sashah akarejea akiwa na furaha sana usoni mwake,
“Vipi kitu kimetiki nini?” Rajiti aluliza
“Ndio, chezea mimi wewe”
Rajiti akamkbidhi Sashah hati tatu za kusafiria, na akaanza kuzisoma taratibu
“Kweli wewe kiboko, kitu feki kama orijino”
“Ahaa, kila kitu kinawezekana duniani”
“Ila kipo kisicho wezekana” nilichangia mada
“Kama?”
“Kutengeneza pumzi ya mtu”
“Kweli”
“Mpe Eddy aone passport yake jinsi nilivyo itengeneza”
Sashah akanikabidhi hati yangu ya kusafiria iliyo na sura yangu mpya, huku jina langu likiwa ni Suleima Bin Yahaya
“Mbona jina ni hili?”
“Nisingeweza kuweka jina lako kutokana na wewe kuwa muhalifu, hapa mwenyewe nimetoka Jomo Kenyeata Airport na kuzikuta picha za sura yako zikiwa zemebandikwa kwamba unatafutwa”
“Mmmm”
“Unaguna? Tutakwenda na utaziona”
“Sawa bwana”
“Eheee umekata tiketi ya ndege ya saa ngapi?” Rajit aliuliza
“Saa sita uskuku”
“Ipo powa”
Tukaendelea kupiga stori za hapa na pele na nikawasimulia mkasa mzima wa nyuma uliopita kwenye maisha yangu, hadi ninamaliza wote machozi yakawa yanawamwagika
“Eddy pole sana”
“Asante”
Sashah na Rajiti wakabadilisha mavazi na kuvalia sketi ndefu nzuri na kuwafanya wapendeze sana, huku na mimi nikivalia suti kali waliyo nipa cha kushukuru Mungu imenikaa vizuri mwilini mwangu na kunifanya nionekane kama muheshimiwa wa kitengo fulani cha serikali.Tukaanza safari kwa kutumia usafiri wa gari yao ndogo, inayokwenda kwa kasi sana, kutokana ni usiku hapakuwa na magari mengi sana barabarani,Tukafika katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata, sote tukashuku na zimesalia dakika ishirini kabla ya ndege tunayo ondoka nayo kupaa angani.Moja kwa moja tuakelekea sehemui ya ukaguzi wa hati za kusafiria, Rajiti akawa wa kwanza kukaguliwa hati yake pamoja na mwili wake kwa kutumia kifaa cha ulinzi, akapita na kupewa hati yake iliyo tiwa muhuri na muhudumu wa kike anaye ifanya kazi hiyo huku akionekana kuwa makini sana, akafatia Sashah akakaguliwa kama alivyo fanyiwa Rajit na akafanikiwa kupia
Nikamkabidhi msichana hati yangu ya kusafiria cha kwanza akanitazama machoni, kisha hati yangu ya kusafiria akaiweka kwenye mashine inayotoa ripoti kwenye kioo kikubwa cha ‘computer’.Askari anaye kagua akaanza kazi yake ya kukipitisha kifaa chake kuanzia miguuni, msichana akanitazama kwa macho makali kisha akatazama tena kwenye kioo cha kumputer yake, nikatazama pembeni na kuwaona askari wawili walio shika mbwa wakubwa weusi wakianza kunisogelea, huku wakiwa na bubduki zao mikononi, kifaa cha ukaguzi kikaanza kutoa mlio wa kelele huku kikiwaka taa nyekundu kilipo fika maeneo ya shingoni
“Vua cheni yako”
Askari anaye nikagua aliniambia na kunifanya niivue cheni, niliyo ivaa shingoni mwangu.Akaendelea kukipitisha kifaa chake kwenye mgongo hadi chini kwenye miguu,
“Safari njema”
Dada aliyekuwa anaikagua hati yangu ya kusafiria alizungumza huku akinikabidhi hati yangu ya kusafiria, huku usoni mwake akiwa ameachia tabasamu pana lililo pendezeshwa na mwanya wake mwembamba.
“Asante na wewe pia kazi njema”
Nikapita kwenye kizuizi na kuwafanya Sashah na Rajiti kushusha pumzi nyingi kwani walihisi kwamba tayari nimeingia kwenye mikono ya askari, tukaingia ndani ya ndege, cha kushukuru Mungu, siti zetu tatu zipo sehemu mmoja, hatukukaa hata dakika nyingi, rubani akatuomba tufunge mikanda yetu kwani ndege itajiandaa kuruka muda sio mrefu.Ndani ya dakika kadhaa tukaanza kuiacha ardhi ya nchini Kenya
“Eddy” Rajiti aliniita
“Naam”
“Unajua kwamba unaonekana tofauti sana”
Alizungumza kwa sauti ndogo
“Kweli?”
“Ndio, umekuwa bonge la handsome”
“Mmmmm”
“Kweli vile”
“Jamani acheni kelele watu wamelala” Sashah alizungumza
“Ahaaa shauri yao, bwana”
Masaa yakazidi kusongo mbele, na ndege yetu ikatua baadhi ya nchi ambapo, baadhi ya abiria walishuka na kupanda abaria wengine na safari ikaendelea.Tukafika nchini Iraq, majira ya saa moja saa tisa alasiri huku sote tukiwa tumechoka kwa uchovu wa kukaa kwenye ndege takribani masaa kumi na tano, kutokana hatukuwa na mizigo tukawahi kupanga mstari wa kutokea sehemu ya kukaguliwa, huku moyoni mwangu nikiwa ni naomba sana nisiweze kushtukiwa kwa lolote, na nikafanikiwa kutoka njee ya uwanja wa ndege pasipo mtu yoyote kunistukia kwamba nimevalia sura bandia,
Sikuwa na sehemu yoyoote ninayo itambua na wenyeji wangu wakubwa ni Sashah na Rajit.Tukapanda kwenye taksi mojawapo iliyopo kwenye maegesho ya uwanja wa ndege na Sashah akazungumza kwa lugha ya kiarabu na dereva tuliye mkuta ndani ya teksi hii, Tukafika kwenye moja ya Hotel kubwa iliyo andikwa kwa maandishi ya kiarabu na kila kitu ambacho wanakizungumza Shasha na watu wengine, sikuweza kukifahamu kutokana siitamui lugha ya kiarabu
Sashah akamaliza kuzungumza, na wahudumu na akakabidhiwa funguo moja, akatufwata sehemu tulipo simama na Rajit, tukaingia kwenye lifti iliyo tupeleka hadi ghorofa ya sita, na tukaingia kwenye chumba ambacho Sashah alikodisha
“Eddy utakaa hapa siku mbili, ili uyazoee mazingira kisha tutaelekea makao makuu”
Sashah alizungumza
“Na nyinyi munakwenda wapi?”
“Sisi, tunakwenda kufwatilia mambo muhimu, kwa ajili ya kazi zetu, kikubwa ni wewe kuwa makini katika hili eneo.Tumekulipia chakula kila mahitaji utakayo yahitaji tumegharamia”
“Sasa jam….”
“Eddy hapo hakuna cha sasa kikubwa ni wewe kuwa makini, usipende kujitokeza tokeza kwa watu kwani watu wa huku hawana huruma, wana roho za kinyama.Yaani ukitembea sana wewe mwisho wako ni kule chini kwenye sehemu ya chakula”
“Sawa nimewaelewa, je nikihitaji hudumu ya kuwapigia wahudumu wa hii hoteli?”
“Kuna kitabu pale juu ya meza kwenye ile simu basi utaweza kuitumia hiyo sawa, na kabla sijasahau chukua hizi cuppon ukienda kuchukua chakula unaonyesha, zipo za ana mbili, moja ya chakula na nyingine ya kinywaji.Ukizipoteza baba utashinda njaa hizi siku mbili”
“Powa”
Sashah na Rajit wakaondoka na kuniacha nikiwa nimesimama, nikawasindikiza kwa macho hadi walipo funga mlango ndipo na mimi nikapiga hatua hadi kweye mlango na kuufunga kabisha kwa funguo na kurudi kujilaza kwenye kitanda kikubwa kilichomo ndani ya hii hotel.Nikanyanyuka na kusimama mbele ya kioo kikubwa na kujitazama sura yangu, kusema kweli nimebadilika kwa kiasi kikubwa
Nikavua suti niliyo ivaa na kuingia bafuni, nikaoga huku kichwani kwangu nikiwa nimejawa na mawazo yaliyo ambatana na maswali mengi juu ya wapi alipo mama yangu,
“Hii ni nafasi yangu ya mwisho kupambana na Mzee Godwin, nilazima nimuue kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
Nilizungumza huku nikiwa nimekiinamisha kichwa chwangu kwenye ukuta, huku nikiyatazama maji yanayo tiririka na kuingia kwenye kijishimo kidogo
“Ilipo fikia inatosha”
Nilizungumza huku nikishusha pumzi nyingi, nikamaliza kuoga na kurudi chumbani, saa ya ukutani inanionyesha inakwenda majira ya saa kumi na moja kasoro jioni.Nikapanda kitandani, kutokana na uchovu mwingi nikajikuta taratibu nikiwanza kusinzia hadi usingizi ukapitia kabisa
Nikastuka kutoka usingizini, na macho yangu yakakumbana na giza, nikashuka kitandani na kupiga hatua za ungalifu hadi sehemu ilipo swichi, nikawasha taa cha kwanza kukitazama ndani ya chumba ni saa iliyopo ukutani na kukuta ikionyesha ni saa nne na dakika kumi na nane usiku, nikavaa nguo zangu na kutoka nje ya chumba, nikashuka chini sehemu ya watu kujipatia chakula
Nikaa kweny moja ya meza, muhudumu akanifwata na kuniuliza kwa lugha kingereza ninatumia chakula gani, kati ya vyakula vilivyo orodheshwa kwenye Menyu yao.Kila chakula ambacho ninakisoma kwangu ni kigeni, nikaamua kuweka tiki kwenye chakula ambacho niliona jina lake linanipendeza, kinywaji nilicho kielewa kikubwa ni maji tuu ndio niliyo amua kuyawekea tiki
Muhudumu akaondoka na baada ya muda akarudi akiwa na chakula nilicho muagiza, nikajikuta nikishusha pumzi nyingi kwani chakula nilicho kiagiza, ni konokono wakiwa wamechemshwa vizuri huku wakiwa wamepambwa na nyanya zilizo katwa vizuri na kuwekwa pembezoni mwa shahani hiyo
“Mmmm, bora nirudi bongo, kwa staili hii”
Nikawatazama watu wengine kwenye meza zao, kila mmoja yupo bize na mambo yake, jamaa mmoja aliye kaa pembeni yangu nikamuona akiwekewa chakula kama changu na muhudumu aliye muagiza, bila hata ya kusita akaanza kutafuna nyama za konokono hao huku akishushia na soda.Kwa jinsi jamaa anavyo wala nikajikuta nikianza kujihisi kichefuchefu kwa mbali, kila ninapo watazama konokono wangu ndovyo jinsi kichefuchefu kinavyo ongezeka na kujikuta nikisimama na kumsimamisha muhudumu mmoja
“Where is Toilet”(Choo kipo wapi)
Nilizungumza huku kiganja cha mkono wangu wa kulia kikiwa mdomoni mwangu kuzuia kutapika, muudumu akanionyesha kwa kidole mlango wa kuelekea chooni, nikaanza kupiga hatua za kwenda kuufwata mlango huku ninatizama chini kwa bahati mbaya nikamgoga msichana mmoja mmrefu aliye nipa mgongo, na pochi yake ikaanguka
“So….”
Sikuweza hata kuimalizia samahani yangu, tayari kechefuchefu kilikolea, nikazidi kutembea kuelekea chooni, ila kwa msonyo alio uachia huyu dada ikanilazimu kugeuza kichwa kumtazama huku nikiwa ninatembea, macho yangu yakamshuhudia Dorecy akimalizia kunyanyuka huku akiwa ameshika kipochi chake kilicho anguka, kutokana na hali mbaya niliyo nayo sikuwa na budi kuingia chooni.Nikasimama kwenye moja ya sinki la kunawia mikono na kuanza kutapika, dakika tato mfululizo nikajikuta ninatapika hadi chakula nilicho kula ndani ya ndege.
Tumbo likaanza kunisokota, sikujua hata ni kitu gani kilicho nikumba kwa dakika chache hizi, ikanilazimu kujisaidia haja kubwa, kidogo nikapata nafuu ya tumbo kuniuma.Nikajiwek sawa na kunawa mikono yangu, nilipo hakikisha ninaonekana vizuri nikafungua mlango na kumkuta yule jamaa aliyekuwa anakula konokono akiwa amesimama juu ya meza huku mkoni mwake akiwa na bomu la kurusha kwa mkono, watu wote wakanza hulala chini huku wakipiga kelele, jamaa akafungua kikoti chake alicho kivaa na nikamshuhudia akiwa amejifunga mabomu mengine makubwa kama maane na akaanza kuzungumza kwa sauti ya juu kwa lugha ya kiarabu na neno nililo lielewa ni moja tu
“Walha wakhbar”
Kisha akalirusha juu bomu la mkoni, alilokuwa amelishika, huku mabomu mengine aliyo yavaa mwilini mwake yakisoma Zero nyingi zinazo onekana kwa rangi nyekundu
Fumba na kufumbua, nikajikuta nikiwa nimerushwa na kurudishwa nyuma ndani ya choo nilipo tokea, huku sauti kubwa ya mlipuko wa bomu ikisikika, sikujua hata nini kufanya kwani akili yangu ikakakosa maamuzi ya hataka ya kuamua, hadi ninaanza kupata chakufanya, tayari nimesha chelewa kwa maana kuta za choo zilisha anza kuporomoka na kusababisha upenyo mdogo sana.Nikazidi kuchanganyikiwa kiasi kwamba sikujua ni nini niweze, gafla nikashuhuda kifusi kikubwa cha mchanga kikilifunikia sehemu zima la chooni na taratibu nikaanza kupoteza pumzi na kulegea, na giza jingi likanitawala machoni mwangu
***
Nikaanza kuhisi kitu kikinistua kwenye kifua change, sikuweza kuelewa mapema ni vitu gani.Kelele za watu za watu mchanganyiko zikazidi kunipa hamasa ya kutamani kuona ni kitu gani kinacho endelea kwenye maisha yangu kwa wakati huu.Haikuwa rahisi sana kama ninavyo hitaji mimi kuwa, kwani kila kitu kinacho endelea kwenye ulimwengu huu niliopo ni chatofuti sana, na sijawahi kukiona hata siku moja mbele ya maisha yangu.Mwanga mkali ukasimama mbele yangu, na kundi kubwa sana la watu walio valia mavazi meupe yanayo ng’aa sana, wakiwa wapo kwenye marika tofauti kuanzi watoto wadogo hadi wakubwa, wote wakiwa wapo kwenye jinsia tofauti nikimaanisha jinsia ya kiume naya kike.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila niliye mtazama akaanza kutingisha kichwa, akionyesha kukaataa kitu na sikujua ni kitu gani ambacho anakikata, wakaanza kuninyooshea mikono ya kuniomba nirudi ninapotoka, sikujua ni wapi nilipo taoka kutokana sehemu nzima niliyo simama imetawaliwa na mwanga mweupe mtupu ambao sikuweza kuona ni wapi popote zaidi ya hawa watu walio simama mbele yangu
“Eddy, wakati wako bado.Rudi”
Sauti nzito ya kutetemesha ilisikika masikioni mwangu, na gafla nikisikia mstuko mkali kwenye kifua change ulio nifanya nistuke na kukaa kitako huku ninahema sana, na jasho jingi likiwa linanimwagika mwilini mwangu.Watu waliopo pembeni yangu walio valia mavazi ya kijana huku sura zao wamezifunika kwa vitambaa vinavyo fanana na mavazi yao, wajanirdusha haraka kulala kwenye kitanda.Nikaanza kuminyanana nao huku nikiomba waniachie
“Niachieni nyinyi, mimi mzima sijafaaaa”
Nilizungumza kwa sauti ya juu huku nikijitahidi kunyanyuka, ila wakazidi kunishikilia na kunikandamiza nisirudi kukaa, nikamuona dada mmoja akichukua sindano na kuichoma kwenye kwenye kichupa kidogo na kuvuta dawa nyingi kwa haraka
“Haaaaa, haaa unataka kuniua eheeee, kudadadeki nitakuua kwanza wewe”
Nilizungumza huku macho yangu nikiwa nimemtumbulia dada mwenye sindano, ila wezake wakajitahidi kunishika kwa nguvu zao zote, na nikamshuhudia dada akiichoma sindano kwenye mkono wangu wa kushoto, na kadri jinsi anavyoisukuma dawa ndivyo jinsi na mimi nilivyoanza kupoteza nguvu na usingizi mzito ukaanza kunitawala kila nilivyo jaribu kufumbua macho yangu nikashindwa kabisa
***
Nikastuka na kukuta, mashine ndogo ikiwa pembeni yangu ikionyesha mishale mishale ambayo imepinda panda, kujichunguza vizuri nikajikuta nikiwa nimevalishwa kitu kilicho funika pua yangu na mdomo wangu, sikuwa na nguvu za kufanya kitu chochote zaidi ya kuendelea kujilaza kwenye kitanda nilicho lazwa.Taa mbili nyeupe za chumba hichi hazikunipa uwezo wa kugudua kama huu ni usiku au mchana.Nikajaribu kujiinua ila nikashindwa na kuendelea kulala kitandani
Baada ya muda kidogo ukaingia nesi akiwa amebeba kisinia chenye sindano, pamoja na vichupa viwili vyenye rangi tofauti tofauti
“Unajisikiaje?” Aliniuliza kwa sauti ya chini iliyo jaa upole mwingi
“Vizuri”
“Vizuri, usiwe na wasi wasi upo sehemu salama na utapona sawa kaka”
Alizungumza huku akivaa gloves nyeupe kwenye mikono yake
“Kwani hapa nilipo nipo wapi?”
“Upo hospitali, ila kwa sasa tunajitahidi kukushuhulikie ili uweze kupona haraka”
“Kwani hapa ni Tanzania?”
“Hapana hapa ni Iraq”
“Mbona unazungumza Kiswahili kizuri”
Nilimuuliza huyu nesi mwenye asili ya kiarabu, akatabasamu na kuvuta dawa kidogo kwenye kichupa, kwa kutumia sindano kisha akachukua pamba na kuipaka dawa kidogo na kunipaka kwenye mkono wa kulia sehemu ya kikunjio, akanichoma sindano yanye dawa
“Pole eheee”
Alizungumza kwa sauti yepesi sana iliyo jaa upendo na upole
“Asante”
“Ikifika asubuhi nitakuja kukuchoma sindano ya kutuliza maumivu”
“Sawa”
Akakusanya kila kilicho chake na kutoka ndani ya chumba.Masaa yakazidi kwenye na kuzidi kukatika taratibu huku nikiwa nimesongwa na msongamano wa mawazo nikijaribu kuvuta kumbukumbu za hapa kufika hospitali ila sikukumbuka kitu cha aina yoyote, jina ambalo ninalo kichwani mwangu ni Tanzania, pamoja na lugha yangu ya Kiswahili ambayo kwangu ndio lugha ya Taifa
Wakaingi madaktari wawili wote wakiwa waarabu, wakanisogelea hadi kwenye kitanda nilicho lala na kuanza kuzungumza huku mmoja akianza kunishika mashavuni na kuniminya minya.Wakaendelea kuzungumza huku mmoja akiandika kwenye kijikitabu kidogo alicho kuja nacho.Mmoja akanifunua shuka na kumuonyesha mwenye kijikitabu mkononi sehemu ya mguu wangu, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kuuona mguu wangu wa kulia ukiwa umefungwa kitu kikubwa cheupe.Akaingia nesi wa jana usiku na kusimama pembeni ya madaktari hawa, huku akiwa ameshika kisinia chake cha jana usiku.Nikaanza kumuona nesi akitingisha kichwa akionekana kukataa mazungumzo ya madaktari hao
Wakaanza kubishana, na sikujua ni kitu gani wanacho bishana.Hadi ikafikia daktari mmoja wa aliyekuwa anazungumza na mwenzake anaandika akataka kumzaba kibaa nesi huyo, ila mwenzake akakataa na kumtoa nje, kuepusha ugomvi kutokea ndani ya chumba hichi.Nesi akaanza kuzunguka ndani ya chumba huku akimwagikwa na machozi na kuzidi kunichanganya kwani sikujua ni kitu gani kinacho mwaga machozi kwa kiasi hichi.
“Kuna nini?”
Nilimuuliza na kumfanya asimame na kunitazama, akautazama mlango na kwenda kuufunga kwa ndani, kisha akarudi na kukaa pembeni yangu huku akinifunika na shuka
“Eti nesi, kuna nini?”
Nilimuuliza kwa sauti ya upole iliyo jaa huzuni, akanitazama na machozi yakazidi kumwagika kiasi cha kuzidi kunichanganya mimi
“Watu wa huku, wana roho mbaya sana pale wanapo waona watu wenye ngozi yeupe”
Alizungumza huku akijifuta machozi yanayo mwagika kwa kutumia kiganja chake
“Kwa nini?”
Akanitazama kwa umakini na kwamacho yaliyo jaa huzuni kiasi cha kunifanya nihisi kuna jambo baya ila sikujua ni nini
“Kiufupi hawawapendi watu weusi, ndio maana wanafanya mpango wa kukukata huu mguu wako ulio vunjika”
Nilijihisi moyoni mwangu kama nimepigwa shoti ya umeme, kila nilivyo mtazama nesi sikujua nizungumze nini.Machozi yakaanza kunimwagika kama maji,
“Usilie, nitahakikisha unapona na hakuna mtu anaye weza kukufaniyia ukatili kama huo”
“Kwani umekatika?” Nilimuuliza kwa sauti ya upole sana huku nikiendelea kulia
“Hapana haujakatika, umefunjika mara mbili, ila nashangaa ni kwanini hapa wanapanga kuukata”
“Ila usilie, nipo radhi nipoteze kila kitu kwangu, ila si kukubali kuuona ubaguzi wa rangi kama huu.Kwa maana wakiukata kinacho fwatia hapa ni wewe kupelekwa katika kambi ya walemavu iliyopo Bangdad na kila siku hiyo kambi, walemavu wanakufa kwa njaa kali na mateso makali, na mbaya zaidi wengi wanao pelekwa kule ni wale ambao si raia wa nchi hii”
Maneno ya nesi yakazidi kuniogopesha na kuendelea kunipa wasiwasi mkubwa ulio zidi kunimwaga machozi yangu.
“Jikaze usilie, ngoja nikuchome sindano ya kutuliza maumivu na kukausha kidonda.Wakikuletea chakula tafadhali usile hadi nikuletee mimi”
“Sawa”
“Wanaweza kukupa sumu, ufe bure mtoto wa watu bila ya sababu maalumu”
Nesi alizungumza na kuendelea kunichoma sindano alizo niambia,
“Sasa hivi ninatoka, kazidi ninakwenda nyumbani kukuandalia chakula, hadi saa sita nitakuwa nimesha rudi kukuletea chakula na nikija nitakuja tuzungumze mengi.Ila vumilia njaa yako, usile chakula wala kunywa maji yoyote utakayo letewa na mtu wa aina yoyote sawa”
“Sawa, nashukuru kwa msaada wako nesi”
“Hata wewe nashukuru kwa uelewa wako, niite neshi Phidaya”
“Naitwa Eddy”
“Mungu mkubwa utapona na vua hiyo mashine”
Nikakivua kifaa nilicho kuwa nimevalishwa kwenye uso kisaha, nesi Phidaya akaondoka na kila kitu chake, baada ya muda kidogo akaingia nesi akiwa amebeba sahani nyenye chakula pamoja na maji kwenye glasi, akaviweka pembeni ya meza yangu na kunitazama usoni.Akawa anatamani kuzungumza na mimi ila anashindwa na nikahisi lugha zetu zipo tofauti sana.Akanza kunionyesha kivitendo kwamba chakula kipo mezani ninaweza kula, na mimi nikamjibu kivitendo kwamba nitakula, akatoka na kuniachia chakula mezani. Harufu ya chakula ikazidi kunitamanisha kuweza kukila kwani inavutia sana, ila kila nilipo jaribu kukumbuka maneno ya nesi Phidaya nilijikuta nikuwa ninakidharau
Baada ya muda mrefu kidogo nesi Phidaya akarudi akiwa emeshika mfuko mweupe wenye vyombo,
“Nani kakuletea chakula?”
“Nesi mmoja mfupi, mwarabu”
Nesi Phidaya akaachia msunyo mkali baada ya kumuambia nesi aliye niletea chakula hicho
“Ndio wale wale”
Akakisogeza chakula nilicho letewa akaniwekea chakula chake mezezani, akaanza kuninywesha taratibu uji alio uweka kwenye kikombe
“Watu wa huku hawana ubinadamu, ndio maana kila siku wanakazi ya kujitoa muhanga na mabomu yao”
“Hivi ni kwa nini?”
“Uchizi tu ndio unao wasumbua, kuna wanao amini kwamba ukijitoa muhanga, mbele za watu mbinguni utaingia moja kwa moja wakati ni uongo mtupu”
“Hivi unakumbuka kitu chochote cha nyuma?”
“Hapana”
“Ona sasa, wamekuchoma sindano ya kukupotezea kumbu kumbu, ndio maana nakuambia watu wa huku hawana maana”
“Wamenichoma sindano?”
“Ndio, na kuna kitu kinacho endelea, na ile siku ya oparesheni kama nisinge kuwepo ninaimani wangekumalizia, nikutokana katika watu walio okolewa wakiwa hai kwenye lile jingo wewe ni mmoja wao na idadi kubwa ya waarabu walikufa pale”
“Kwenye jengo, jengo gani?”
“Usiwe na haraka, hapa itabidi nifanye mpango wa kukutorosha la sivyo watakupoteza”
Maneno ya nesi Phidaya yakazidi kunipotezea imani moyoni mwangu na kunijaza moyo wa woga kwani imani ya kuwaamini madaktari wengine ikaanza kunipotea moyoni mwangu.Nesi Phidaya akamaliza kunilisha chakula alicho niletea na kunihaidi atarudi usiku kisha akaondoka zake
***
Masaa yakazidi kusonga, huku moyoni mwangu nikiomba sana nesi Phidaya atokee aje kunisaidia kwa maana kila daktari kwangu sikuweza kumuamini, kila nilipojaribu kuvuta subira sikuweza kumuona nesi Phidaya akiingia kwenye chumba change, mlango ukafunguliwa na kujikuta nikianza kutabasamu, macho yangu yakiwa na shauku ya kuweza kumuona nesi Phidaya.Nikashangaa kuwaona wale madaktari wa asubuhi wakiingia na kusimama pembeni yangu
Mmoja akafungua kitabu chake kilicho andikwa na maandishi ambayo akanionyesha na sikumuelewa ni maandishi ya lugha gani, akaniandikia tarehe kwenye kijikitabu chake na kuniambia kwamba hii ni tarehe ya leo, kish akaniandikia tarehe nyingine ambayo ni siku inayo fwata.Kisha akachora kijimguu na kukiwekea alama ya ‘X’ akiashiria kwamba kesho ndio siku ya mimi kukatwa mguu wangu.Alipo maliza kunionyesha kwa ishara wakatoka huku wakiwa wanacheka sana.
Hadi kunapambazuka sikuweza kumuona nesi Phidaya, hali ya hatari ikaanza kunijia kichwani mwangu na kuhisi nesi Phidaya anaweza kuwa amekutwa na matatizo, mlango ukafunguliwa na wakaingia manesi wawili pamoja na madaktari wale wawili.Wakaanza kufungua kitandana na kukishusha chini kidogo hadi kikafikia usawa mzuri wa kuweza kusukumwa.Pasipo hata ya kunisemesha wakaanza kunisukuma na kunipeleka nisipo pajua huku nyuso zao zikiwa na tabasamu ambalo sikuliewewa nini maana yeke
WAKAZIDI KUKISUKUMA KITANDA NILICHO LALIA HADI HADI TUKAFIKA KWENYE MAJA YA MLANGO AMBAO JUU KUNA MAANDISHI YA KIHARABU AMBAYO SIKUWEZA KUYAELEWA, NESI MMOJA AKAUSUKUMA MLANGO NA KUFUNGUKA, NA WAKANIINGIZA NDANI NIKIWA JUU YA KITANDA CHANGU, MWANGA MWEKUNDU WA TAA ULIOO NDANI YA CHUMBA UKAZIDI KUNIOGOESHA.CHUMBA KIZIME KIMEZUNGUKWA NA MASHINE MBALIMBALI AMBAZO SIKUJUA ZINAKAZI GANI.DAKTARI MMOJA AKACHUKUA MASHINE YENYE KIMVIRINGO MBELE, KISHA AKAKIWASHA NA KUANZA KUZUNGUKA, AKACHUKUA MOJA YA MIWANI KUBWA AMBAYO NI NYEUPE AKAIVAA NA KUANZA KUCHEKA KITU KILICHOO ZIDI KUNIOGOPESHA ZAIDI.
GAFLA TAA YA MWANGA MWEUE IKAWASHWA NA KUWAFANYA MADAKTARI NA MANESI, KUSTUKA, MACHO YETU WOTE TUKAYAELEKEZEA MLANGONI NA KUMUONA NESI PHIDAYA AKIWA AMESHIKA, BASTOLA HUKU JASHO JINGI LIKIWA LINAMWAGIKA USONI, AKAANZA KUZUNGUMZA KWA KIARABU NA TARATIBU MADAKTARI WAKANYOOSHA MIKONO JUU WAKITETEMEKA, AKAZUNGUMZA NENO LILILO WAFANYA MADAKTARI KUANZA KURUDI NYUMA KUTOKA KILIO KITANDA CHANGU.
“EDDY, WAMEKUFANYA CHOCHOTE KIBAYA?”
“HAPANA”
“POWA”
NESI PHIDAYA AKAZUNGUMZA NENO JENGINE LILILOWAFANYA MADAKTARI NA MANESI KULALA CHINI, SAKAFUNI HUKU MIKONO YAO WAKIWA WAMEIWEKA JUU YA VICHWA VYAO.NESI PHIDAYA AKANIFWATA HADI KITANDANI NA KUUITISHA MKONO WAKE MMOJA KWENYE, MGONGO WANGU NA KUNIOMBA NIWE KUSHUKA CHINI, JAPO NINAJIHISI MAUMIVU ILA NIKAJIKAZA KIUME KWANI KUENDELEA KUKAA HAOA KUTAHATARISHA MAISHA YANGU.
“JIKAZE BABA YANGU”
NESI PHIDAYA ALIZUNGUMZA HUKU AKIENDELEA KUNISHUSHA KWENYE KITANDA, AKANISAIDIA KUSIMAMA VIZURI, HUKU MUHIMILI WANGU WOTE WA KUSIMAMA NIKIUTEGEMEA KUTOKA KWAKE, NESI PHIDAYA AKAWATAZAMA WATU MADAKTARI WALIO LALA CHINI, AKAZUNGUMZA NENO LA UKALI LILILO WAFANYA MADAKTARI NA MANESI KUZIDI KUZIFUNIKA SURA ZAO CHINI PASIPO KUZINYANYUA JUU.TUKAFANIKIWA KOTOKA NJE YA CHUMBA WALICHO NIINGIZA, NESI PHIDAYA AKAFUNGA MLANGO KWA NJE NA SOTE TUKAANZA KUONDOKA TARATIBU HUKU NESI PHIDAYA AKIIFICHA BASTOLA YAKE NA BAADHI YA WAHUDUMU WAKABAKI WAKIWA WANATUSHANGAA.TUKATOKA NJE NA KUKUTA GARI AINA YA TAKSI IKIWA INATUSUBIRIA
“AHAAAA”
NILITOA MGUNO WA MAUMIVU BAADA YA MGUU WANGU NILIO VUNJIKA KUGONGWA KWENYE MLANGO NILIPOKUWA NINAJIAANDAA KUINGIA NDANI YA GARI, SITI YA NYUMA
“POLE EDDY”
“ASANTE”
NESI PHIDAYA AKANISAIDIA KUINGIA NDANI YA GARI NA KUFUNGA, KISHA YEYE AKAINGIA KWENYE SITI YA MBELE KWA DEREVA NA KUMUONGELESHA DEREVA KIARABU NA AKALIONDOA GARI LAKE KWA KASI.
“ASANTE SANA, NESI PHIDAYA”
“USIJALI NIPO KWA AJILI YAKO, ILA NINGEPENDA UNIITE PHIDAYA TU NA SI NESI PHIDAYA”
“SAWA”
NIKAENDELEA KUJILAZA KWENYE SITI YA NYUMA YA TAKSI TUIYO IPANDA, ILA KUNA MWANGA MKALI WA TAA UKAWA UNAINGIA KWENYE GARI LETU, IKANILAZIMA KUNYANYUA KICHWA CHANGU KUTAZAMA NYUMA, NIKAONA GARI NDOGO IKIJA KWA KASI SANA,
“PHIDAYA KUNA WATU WANATUFWATA NYU……”
KABLA SIJAMALIZIA SENTESI YANGU NIKASTUKA RISASI IKIPIGA KWENYE KIOO CHA NYUMA NA KUNIFANYA NIRUDI CHINI, NA KULALA KWENYE SITI YANGU.DEREVA AKAANZA KULALAMIKA, NA PHIDAYA AKAANZA KUMUHIMIZA DEREVA KUONGEZA MWENDO KASI WA GARI,RISASI ZIPATAZO NNE ZIKAINGIA KWENYE KIOO CHA NYUMA CHA GARI NA KUSHANGAA RAGI IKIAANZA KUYUMBA HUKU DEREVA AKIWA AMEULALIA MSKANI WAKE,
“SHIT DEREVA AMEPIGWA RISASI YA KICHWA”
PHIDAYA ALIZUNGUMZA KWA KUCHANGANYIKIWA KIASI KWAMBA NA MIMI NIKAANZA KUCHANGANYIKIWA, RISASI ZIKAENDELEA KUMIMINIKA NDANI YA GARI NA KUZIDI KUNICHANGANYA
“MTOE HUYO DEREVA”
NILIZUNGUMZA KWA SAUTI YA JUU, PHDIAYA AKAFANYA KAMA NILIVYO MUAGIZA, AKAUFUNGUA MLANGO WA DEREVA NA KUMSUKUMIA KWA NJE, KISHA AKAFUNGA MLANGO NA KUKAA KWENYE SITI YA DEREVA
“NIPE BASTOLA YAKO”
PHIDAYA AKANIRUSHIA KWA NYUMA BASTOLA YAKE, NIKAUCHUKUA MKANDA WA SITI WA SITI YA NYUMA NA KUANZA KUUVUTA NIKIJARIBU KUUKATA ILA NIKASHINDWA.NIKAMTAZAMA
“EDDY UNATAKA KUFANYAJE?”
“NATAKA KUKATA HUU MKANDA NIUFUNGE MGUU WANGU UNAVUTA SANA”
PHIDAYA AKAFUNGUA KWENYE KISANDUKU KILICHOPO PEMBENI YA SITI YA DEREVA, NA KUANZA KUTOA VITUVITU, VILIVYOMO NDANI YA KISANDUKU, AKABAHATIKA KUPATA MKASI NA KUNIKABITHI.NIKAUCHUKUA MKASI NA KUUKATA MKANDA WA SITI NA KUUFUNGA MGUU WANGU ULIO VUNJIKA, MAENEO YA MAPAJANI, HADI NILIPO HAKIKISHA KWAMBA NIMEUNGUZA MISULI KUVUTA, NIKAJILAZA VIZURI KWENYE SITI NA KUTOA MAGAZINE YA BASTOLA NA KUKUTA IKIWA NA RISASI ZA KUTOSHA.NIKAITAZAMA GARI INAYO TUFWATILIA, NIKASHUHUDIA JINSI INAVYO KUJA KWA KASI, AKACHOMOKA JAA MAA MMOJA KWENYE KIOO CHA GARI LAO HUKU AKIWA NA BUNDUKI AKIJIANDAA KUFYATU RISASI NYINGINE KWENYE GARI LATEU.NIKAANZA KUHESABU MOJA HADI TATU KIMOYO MOYO HUKU BASTOLA NIKIWA NIMEISHIKA KWA UMAKINI MKONONI MWANGU, NIKABANA UMZI KWA NGUVU, KISHA NIKAFYATUA RISASI TATU MFULULIZO KUELEKEA ALIPO JAAMA, KWA BAHATI NZURI RISASI ZOTE LILIATA KIFUANI NA KUSABABISHA KUNING’INIA TU
NIKAFYARUA RISASI NYINGINE MBILI KWENYE KIOO CHA DEREVA NA KULISABABISHA GARI LAO KUYUMBA, JAMBO LILILO PELEKEA GARI KUANZA KUSHUKA CHINI KWENYE KORONGO LILILO EMBEZONI MWA BARABRA, NA KUANZA KUBINGIRIA KWENDA CHINI.PHDAYA AKAZIDI KUONGEZA MWENDO WA GARI TUKIKATIZA KWENYE MILIMA, SIKUJUA NI WAPI TUNAPO ELEKEA ILA IKANILAZIMU KUWA MTULIVU
“UPO FRESHI EDDY?”
“NDIO NIPO POWA, TUNAELEKEA WAPI?”
“HUKU TUNAPO ELEKEA NI KWENYE SHAMBA LANGU, LA PAMBA”
“AHAA SAWA”
NDANI YA DAKIKA AROBAINI NA TANO TUKAWA TUMEFANIKIWA KUFIKA KWENYE SHAMBA LAKE, LENYE MITI MINGI YA PAMBA, TUKAINGIA NDANI YA SHAMBA HADI TUKAKUTA NYUMBA MOJA NZURI IKIWA KATIKATI YA SHAMBA NA IMEZUNGUKWA NA PAMBA NYINGI
“KARIBU”
PHIDAYA ALIZUNGUMZA HUKU AKISIMAMISHA GARI LAKE, AKAFUNGUA MLANGO NA KUSHUKA, AKAFUNGUA MLANGO WA SITI YA NYUMA AMBAPO NIPO, KISHA AKANISAIDIA KUSHUKA NDANI YA GARI, AKAENDELEA KUNISAIDIA KUTEMBEA HADI NDANI YA NYUMBA YAKE, NDOGO ILA IMETENGENEZWA KWA USTADI WA HALI YA JUU, AKAWASHA TAA NA TARATIBU AKANIKALISHA KWENYE MOJA YA SOFA KUBWA LILILOPO NDANI YA NYUMBA YAKE
“POLE SANA EDDY”
“NASHUKURU, HAPA UNAISHI NA NANI?”
“HUWA NINAISHI PEKE YANGU, MUDA WA MAPUMZIKO, KAMA LIKIZO na huwa ninanunua vyakula vinavyoweza kudumu hata kwa miezi sita pasipo kuharibika na kama unavyo ona, umbali kutoka huku hadi mjini”
“Ahaaa sawa”
Phidaya akaingia kwenye moja ya chumba kisha akarudi akiwa amebadilisha nguzo alizo kuwa amezivaa na kukaa kwenye moja ya sofa ambalo lipo karibu na sofa nililo jilaza
“Eddy kuna kitu nahitaji kukuuliza”
“Uliza kama huto jali”
“Wewe haswa ni nani?”
“Kivipi?”
“Nahitaji kujua ukweli kuhusu wewe, juu ya maisha yako na kazi zako”
Phidaya alizungumza huku akinitazama machoni, kwa umakini.Nikaanza kumuelezea Phidaya juu ya maisha yangu ya nyuma, kuhusiana na machafuko yanayo endelea kwenye familia yangu, japo kuna baadhi ya vitu sikuviweka wazi kwake, kama swala la kumuua Derick kikatili sana.
“Pole sana Eddy”
“Asante”
Sikuona haja ya kuendelea kukaa na sura bandia, ikanilazimu kuvua sura bandia nilivyo pandikizwa juu ya sura yangu japo inasababisha maumivu mengi, ila nilijikaza, na ikawa ndio mara ya kwanza kwa Phidaya kuiona sura yangu halisi
***
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hali ya mguu wangu kuendelea kuimarika huku vidonge vya kurudisha kumbukumbu anavyo nipa Phidaya vikaanza kufanya kazi, na taratibu kumbukumbu zangu zikaanza kurudi moja hadi nyingi, hali iliyoa anza kuleta matumaini kati yangu na Phidaya ambaye anaendelea kunipatia matibabu kila kukicha, kwa dawa na mazoezi ambayo Phidaya, ananipatia nikajikuta mguu ukianza kupona, hadi nikaanza kuacha kutembele gongo lililo kuwa likinisaidia kutembelea.Baada ya miezi minne nikawa nimepona kabisa hata maumivu ambayo nilikuwa nikiyapata yakawa yamekwisha kabisa
Katika kipindi ambacho tumeishi kwenye hili shamba la pamba, haikutokea hata siku moja mimi na Phidaya tukazungumzia swala zima la mahusiano ya kimapenzi, kwani heshima niliyo jijengea kwa Phidaya ni kama, dada na kaka
“Eddy hivi, una mchumba?”
“Hapana”
“Unamipango gani kwa sasa”
“Nahitaji kurudi, Tanzania kujua kama mama yangu yupo hai au lah”
“Nitakusaidia katika hilo pia”
Phidaya alizungumza huku akinitazama kwa macho malegevu, yaliyo jaa hisia kali za kimapenzi, akanisogelea sehemu nilipo simama na kunikumbatia kwa nguvu.Ikachukua kama dakika tano, Phidaya akiwa amenikumbatia mwilini mwangu.Phidaya akaanza uchokozi wa kama mwanamke akiwa anahitaji kitu muhimu kutoka kwa mwanaume.Kutokana na uzoefu wangu wa kuwajua wanawake, haikunia shida sana ikanilazimu na mimi kuanza kuonyesha makeke yangu ya mikono yangu kupita sehemu mbali mbali za mwili wa Phidaya, na taratibu tukajikuta tukizama kwenye dimbwi kuwa la mapenzi, na kadri ya jinsi tulivyozidi kupeana raha, ndivyo jinsi, hisia kali za upendo zilivyo zidi kukua kati yetu
Siku ya pili tukakubaliana kwenda mjini kufanya baadhi ya manunuzi ya vitu vya kuweka ndani, ikiwemo chakula kwani kinakaribia kuisha.Alfajiri na mapema tukaingia kwenye taksi ambayo tulikuja nayo kipindi tunatoroka kutoka mjini.Phidaya akawa ni dereva wa kuendesha hadi tukafika mjini, tukapitia benki ambapo Phidaya alichukua kiasi kikubwa cha kutosha kwa manunuzi tulio yapanga kisha, tukaingia kwenye maduka ya nguo, na akaninunulia nguo mpya
“Kuna duka flani la kike ninahitaji nikanunue nguo”
Phidaya alizungumza huku akiendelea kunichagulia nguo ambazo alihisi kwamba zitaupendezesha mwili wangu
“Lipo wapi?”
“Upande wa pili wa barabara, ili kufidia muda wewe chagua nguo utakazo ona zinatosha, nikuachie pesa, na utanikuta kwenye hilo duku”
“Nitalijuaje?”
“Ukivuka tu barabara upande wa kulia kwako, utakuta duka lina masanamu mengi yamevalishwa nguo za kike”
“Ahaaa powa”
Phidaya akaniachia kiasi cha kutosha na kuvuka upande wa pili wa barabara, mimi nikachagua nguo zangu kisha nikaelekea kwenye duka alipo Phidaya, nikamkuta akiwa anachagua nguo,
“Eddy hii inanifaa?”
“Ndio inakufaa”
Tukiwa tunaendelea kuchagua nguo akaingia mwanayume mmoja akiwa amebeba mkoba wa kike, akasimama akitizama tizama baadhi ya nguo, akatoa simu yake ambayo inaita nakuzugumza na simu, kisha akaikata na akasimama akitazama nje.Baada ya muda akaingia mdada aliye jitanda baibui lililo funika hadi macho yake huku tumbo lake kidogo likiwa ni kubwa akionekana ni mjamzito, dada huyo akavua baibui lake ndipo macho yangu yakamshuhudia Dorecy akiwa amesimama kiuvivu, huku mimba aliyo nayo ikionekana kumpelekesha sana, na kwabahati mbaya hakuniona mimi nilipo
Nikamtazama kwa makini jinsi anavyo zungumza na mume wake, hadi Phidaya akanigusa bega
“Mbona unamtazama sana yule dada wa watu?”
“Ninamfahamu”
“Unamfahamu?”
“Ndio”
“Ni nani?”
“Anaitwa Dorecy”
Tulizungumza kwa sauti ya chini huku, tukimtazama Dorecy akichagua chagua nguo na mume wake
“Huyu ndio yule msichana, aliye nipiga na kuondoka na kiasi kikubwa cha madini yangu”
“Ahaaa”
“Ngoja kwanza, nisubiri hapa”
Nilizungumza huku nikizunguka upande wa pili alipo Dorecy na mumuwe, nikajibanza kwenye moja ya kabati lenye nguo, simu ya mume wa Dorecy ikaita na kumlazimu kutoka nje kuzungumza na simu hiyo.Nikapiga hatu za umakini, hadi sehemu alipo simama Dorecy na kumgusa kwa nyuma.Akageuka, na kujikuta akinitazama kwa macho yaliyo jaa mshangao mkubwa kwani hakutarajia kuniona nikiwa katika eneo hili.Nikamvuta hadi kwenye sehemu ambayo si rahisi kwa watu kutuona, hii ni kutokana na wingi wa nguo zilizo pangwa
“Eddy..nisamehe”
“Sikia sina haja ya kuombwa msamaha, ninacho kihitaji ni madini yangu, la sivyo nitalitumbua tumbua hili jitumbo lako kama sikujui”
Nilizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa hasira pamoja na msisitizo mkali, mwili mzima wa Dorecy ukawa na kazi ya kutetemeka mithili ya mtu aliyepo kwenye baridi kali sana
“Yaaa, yaapo kulee”
Nikatazama juu kuchunguza kama kuna kamera yoyote ya ulinzi, ila sikuona, nikamtndika Dorecy kofi moja la kumuweka sawa
“Nimekuambia nahitaji madini yangu sawa?”
“Ndio, yapo kwa kule kule kwangu”
“Nitayapataje?”
“Eeheee?”
Nikaona Dorecy anababaika sana na kunipotezea muda, nikamtandika kibao cha pili ambacho nikizoto kuliko hata cha mara ya kwanza, hadi kuna dada mmoja akachungulia, nikajifanya nikimkumbatia Dorecy kama mpenzi wangu, dada aliye chungulia akaachia tabasamu na mimi, nikatabasamu kinafki ili airudishe sura yake alipo itoa.Alipo irudisha nikamuachia Dorecy na kumkuta sura yake imejaa machozi mengi
“Usijidai unalia kinafki, sasa leo nitakuzalilisha mbele ya mume wako”
“Hapana Eddy usifanye hivyo, mume wangu ni mtu mwenye pesa sana, atakudhuru wewe”
“Haaa na anidhuru kwahiyo pesa zake ndio unadhani kwamba ninaziogopa, si ndio”
Nilizungumza kwa hasira huku nikiwa nimeshika kiganja cha mkono wa kuliwa wa Dorecy na kukiminya kwa nguvu zangu zote.Dorecy akaanza kutoa kilio cha maumivu, simu yake aliyo ishika mkono wakushoto ikaita na kuona jina mume wake
“Pokea sasa”
Nilimuamrisha huku nikimuachia mkono, kabla ya kupokea nikamuona mume wake akija nyuma ya Dorecy
“Mumeo huyo hapo, ole wako uropoke”
Dorecy akajifuta machozi haraka, hadi mume wake anafika sehemu tuliyopo, sura yake imejaa uchangamfu wa gafla, wakazungumza kiarabu ambacho sikukielewa, nikashangaa mume wake akinipa mkono huku akiwa na tabasamu
“Eddy huyu ni mume wangu, anaitwa Khalid, nimemuambi kwamba tumesoma wote”
Nikatingisha kichwa, nikilipokea tabasamu la mume wake, tukaachiana mikono, kitu ambacho mume wake alikifanya na kuzidi kuniboa ni kumkumbatia Dorecy kwa nyuma na kuanza kumchezea chezea tumbo lake huku akizungumza maneno nisiyo yaelewa, Dorecy akanitazama machoni, na kugundua nilivyo kasirika
“Anasema, kwamba mtoto nitakaye mzaa atamleta Tanzania”
Dorecy alitafsiri maneno aliyo yazungumza mume wake
“Muambie hatutaki watoto kama wake, na utazaa Zombi kama sijakusoa”
Mume wa Dorecy akatabasamu baada ya Dorecy kumtafsiria nilicho kizungumza, na nina uhakika kwamba Dorecy alicho kizungumza sicho nilicho muambia
“Nataka, madini yangu, la sivyo nitakufanyia oparesheni bila ganzi ya hilo jitumbo lako”
Nilizungumza na kuachia tabasamu pana, kumfanya mume wa Dorecy kuto kuelewa kitu ninacho kimaanisha, nikawapa mikono na kuondoka zangu kurudi sehemuu nilipo muacha Phidaya
“Eddy umemaliza?”
“Ndio, ila kuna kazi nahitaji kuifanya peke yangu”
“Kazi gani?”
“Tutazungumza”
Phidaya akawa amesha maliza kununia alichokuwa anahitaji kukinunua, tukatoka nje na kuingia ndani ya gari
“Usiondoke kwanza, nataka tuwafwatilie Dorecy na mumewe sehenu wanapo ishi”
“Eddy mbona unanipa shuhuli nyingine”
“Zipi?”
“Hizo za kufwatilia hao watu, ujue kwamba tumekuja kutafuta nini huku”
“Powa nipatie pesa nikodo taksi”
“Utapakumbuka ninapo ishi”
“Wewe nipatie pesa”
Phidaya akanipatia kiasi cha kutosha cha pesa, nikashuka kwenye gari na yeye akaondoka, sikucheza mbali na mlango wa duka walipo Dorecy na mume wake, baada ya dakika kumi na tano nikawaona wakitoka kwenye duka, huku mumewe akiwa amebeba mzigo mkubwa wa nguo.Gari ya kifahari yenye milango sita ikasimama pembeni yao, akashuka jamaa aliye valia suti yenus na miwani nyeusi, akawafungulia mlango na wote wakaingia ndani ya gari na wakaondoka
Nikapiga mluzi kwa dereva taksi mmoja aliye kuwa ameisimisha gari yake upande wa pili wa barabara, akaja nilipo simama haraka, na nikaingia ndani ya gari
“Nilugha gani unayo tumia kuzungumza?”
Nilimuulizwa kwa kingereza, dereva taksi ambaye ni mzee wa makomo kidogo na kichwani mwake amejifunga kilemba
“Zote duniani, kiarabu, kingengereza, kiswahili, kichina na kadhalika”
Alinijibu kwa kingereza, nikamuomba alifwate gari la kifahari lilolo ondoka muda mchache sehemu hii, akatii, akafungulia mziki wa kihindi na kuanza kuimba huku akitingisha tingisha kichwa chake
“Mzee hembu kuwa makini na kazi yako. Utaipoteza hiyo gari”
Kijana mimi ile gari naijua hadi sehemu inapo elekea, ni gari la tajiri Khalid Bin Suley, baba yake alikuwa ni gavana wa hili jimbo”
“Kwa hiyo unamjua?”
“Vizuri sana, tangu akiwa mdogo, na nimwezi ulio pita amefunga ndoa na binti mmoja kutoka Afrika”
“Tuachane na hizo habari za ndoa, yeye anafanya kazi gani?”
“Ahaaa yule kijana, ni mshenzi kweli.Tangu baba yaka afariki basi yeye amekuwa ni muuzaji mkubwa sana wa madawa ya kulevya, kutokana ananguvu kubwa, wala hakuna mbweha polisi hata mmoja anaye msogelea”
“Ahaaa”
“Ahaaa, jamaa anamkono mrefu sana, akimtaka mtu kumchomoa duniani basi ni kitendo cha muda mfupi sana”
Maneno ya dereva taksi yakaanza kuniogopesha na kubaki nikiwa ninamtazama kwa umakini, ila nikajipa moyo kwamba shida yangu si yeye bali nimadini yangu tu.Tukaendelea kuifwatilia gari yake kwa ukakini, gafla dereva akaisimamisha gari yake
“Mbona umesimamisha?”
“Kijana hapa ndio mwisho wa mimi kufika, nikivuka tu hicho kibao hapo ujue haturudi”
“Haturudi kivipi?”
“Namaanisha tutakwenda kuuawa huho, ila jumba lake lile pale mbele”
Tukaishuhudia gari ya Khalid ikiingia kwenye gat kubwa ya jumba lake kifahari, hadi inazama ndani, nikajikuta nikishusha pumzi.Sehemu nzima tuliopo imependezeshwa na miti mirefu, pamoja na majani marefu kiasi yaliyo kolea kijani kikali, kiasi kwamba, ukipatazama lazima macho yafarahie mandhari ya eneo zima
“Ndio hivyo tena, gari imesha zama ndani kijana sasa sijui tunarudi pamoja, au unataka kwenda kudumbukizwa kwenye bwawa la mamba?”
“Turudi?”
Dereva taksi akasigeuza gari lake taratibu, kabla hajaliweka sawa barabarani, gari mbili nyeusi zikasimama barabarani na kuifunga barabara
“Ohoo nilikuambia kijana”
Dereva taksi alizungumza huku akianza kutetemeka mwili mzima.Wakashuka watu sita walio valia suti nyeusi huku mikononi mwao wakiwa na bunduki aina ya short gun.Mzee wa watu akaanza kuomba sala yake ya mwisho huku kajasho kembaba kakimwagika.Jamaa mmoja akaanza kupiga hatua za kuja lilipo gari letu, na kutuomba tushuke ndani ya gari, huku mikono yetu ikiwa juu.Nikajikuta nikiwa ninajiamini kupita maelezo, nikafungua mlango na kutoka nje huku mikono yangu ikiwa nimeinyoosha juu, akafwatia dereva taksi naye akafanya kama nilivyo fanya mimi
“Nyinyi ni kina nani?”
Jamaa alituuliza kwa lugha ya kingereza
“Sisi ttumepotea njia tu”
Nilimjibu jamaa kwa kujiamini, kiasi kwamba nikawa nimejiandaa kwa chochote ambacho kitakwenda kutokea.Jamaa akanisogelea na kuanza kunipapasa kuanzia chini hadi juu, akatoa kiasi cha pesa nilicho kuwa nacho mfukoni na kukitupa pembeni
“Inama kwenye gari”
Aliniamuru na nikafanya hivyo bila ya wasiwasi wa aina yoyote, nikamtazama mzee wa watu jinsi anavyo tetemeka hadi haja ndogo ikaanza kulowanisha surali yake aina ya panjabi aliyo ivaa.Jamaa akaanza kumpapasa mzee wa watu, hawakumuona na kitu chochote
“Ingieni kwenye gari lenu na muondoke haraka sana”
Asante sana baba yangu”
Mzee alijibu kwa haraka na kuingia kwenye gari, nikataka kuokota pesa zangu ila jamaa akanizuia na kuniamuru niingie kwenye gari huku akiwa ameninyooshea bunduki yake, wakazitoa gari zao barabarani na sisi tukaondoka, kwa mwendo wa kasi, njia nzima tukawa kimya, macho yangu nikayashusha sehemu ya mbele ya mzee wa watu na kujikuta nikianza kuchake kimoyomoyo
“Kufa kubaya?”
Nilijisemea huku nikicheka, hata mziki ambao mzee alikuwa anausikiliza akaona unampigia kelele, akaizima redio yake.Nikashangaa kuona mzee akisimamisha gari yake kwenye duka ambalo nilikuwepo
“Shuka kijana kwenye gari yangu, sitaki tena oda yako ya safari”
Mzee alizungumza huku akibabaika, nikashuka kwenye gari, hata pesa hakunidai, akaondoka kwa kasi na kutokomea mbele ya macho yangu.Nikabaki nikiwa nimesimama sikujua ni wapi nielekee, nikastukia nikiguswa bega kwa nyuma kugeuka nikakutana na Phidaya
“Wewe si umeondoka, mbona upo hapa?”
Phidaya alizungumza huku mkononi akiwa ameshika mfuko wa nguo zangu
“Nimerudi bwana”
“Una bahati kweli, nilisahau huu mfuko wako wa nguo, sijui ungerudije nyumbani na ubishi wako”
Phidaya akaita taksi na sote tukaingia ndani ya gari
“Gari umeiacha wapi?”
“Nimeiacha gereji, ina badilishwa rangi na kuwekwa kioo cha nyuma kipya”
“Umeshanunua hivyo vitu?’
“Ndio, vyote vipo kwenye gari”
Tuakfika hadi gereji na kukuta gari ikimaliziwa kufungwa kioo cha nyuma, huku rangi ikiwa imesha malizwa kupakwa
“Hii gereji ninaipenda kutokana huduma zao ni zaharaka, pia wanamitambo mingi”
“Ahaaa, ila ni kubwa”
“Ndio, vipi ulifanikiwa kufika lilipokuwa linakwenda lile gari?”
“Ndio, ila hatukufika kwenye jumba lenyewe, tulisimama kwa mbali”
Sikumuambia Phidaya kitu kilicho tupata kwa maana ningempa wasiwasi mwingi.Tukasubiri kwa masaa mawili, rangi iliyo pakwa kukauka, tukakabidhiwa gari yetu ikiwa katika muonekano mzuri na wakupendeza, tukaingia ndani ya gari safari ya kurudi nyumbani ikaanza
***
Nikaanza kuchukua mazoezi yangu binafsi, ya kuuweka mwili sawa, sikutaka kumuambia Phidaya lengo la mimi kufanya mzoezi hayo, kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo jisni mwili wangu ulivyo zidi kuwa mwepesi na kuhimarika kwa mazozi, nikaingia kwenye mazoezi ya matumizi ya bunduki, katika kulenga shabaha, hadi nikajiamini kwa matumizi ya silaha
“Eddy mbona kipindi hichi unajiweka bize kwa mazoezi hadi naogopa”
Phidaya alizungumza huku akinipa taulo, nijifute jasho linalo nimwagika baada ya kufanya mazozi makali ya kupiga push up na kukimbia kwenye milima muda huu wa asubuhi
“Mwanaume siku zote ni mlinzi wa mwanamke, na ninatakiwa kukulinda mke wangu”
“Mmmm kweli?”
“Ni kweli, ndio”
Phidaya akanivuta karibu yake na kunikumbatia kwa furaha huku akitoa mihemo mizito
“Ninafurahi kuwa na mume kama wewe”
“Hata mimi ninafurahi kuwa na mke kama wewe”
“Ila Eddy kuna kitu nahitaji kukuambia”
“Kitu gani?”
“Nimeanza kuziona dalili za ujauzito”
“Kweli….!!?”
“Ndio”
Ni habari nyingine mpya ya kunifurahisha kwenye maisha yangu, kwani kitu ambacho kitanipa furaha kwenye maisha yangu ya baadaye ni mtoto
“Itabidi uende kwa Tanzania, ukailee hiyo mimba”
“Eddy….niende Tanzania nikafanya nini?”
“Uende ukailee hiyo mimba, sitaki mwanagu azaliwe hapa”
“Na wewe?”
“Mimi nitakuja, pia ninataka ukaagalie hali halisi ya usalama Tanzania kwamba ninatafutwa au laa”
“Eddy siwezi kwenda sehemu yoyote bila ya kuwa na wewe, kumbuka nimeacha kazi kwa ajili yako, na hii hali nahitaji kuwa nawe karibu kila mara na kila dakika”
Hatukufikia muafaka na Phidaya, na akakataa kabisa kurudi Tanzania.Usiku wa saa nne baada ya Phidaya kulala, nikaamka taratibu kitandani, nikachukua bastola yangu na kuhakikisha ina risasi za kutosha, nikavaa nguo nyeusi ambazo si rahisi kwa usiku kuonekana vizuri pamoja na saa yangu ya mkononi, kisha nikachikua na koleo(playz).Kitu kilicho anza kunichelewesha ni funguo ya gari, ambayo sikujua ni wapi ilipo
“Huu mwanamke ameiweka wapi hii funguo?”
Nilijiuliza huku nikiendelea kuitafuta kwenye droo ambazo nilihisi inaweza kuwepo, nikatoka nje bila ya Phidaya kugundua kitu chochote, nikafungua kweye gari kwa bahati nzuri nikaikuta funguo ikiwa kwenye gari.Kuhofia Phidaya kusikia mlio wa gari, nikaanza kuisukuma taratibu hadi nikafika umbali kidogo wa shamba lilipo.Nikaingia kwenye gari na kuiwasha na kuondoka, safari ya kuelekea kwenye jumba analo ishi Dorecy na mumewe ikaanza huku njia nzima nikiwa ninahasira kali iliyo zidi kunisukuma kuliendesha gari kwa kasi kuwahi kufika katika jumba hilo
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikaisimamisha gari yangu kwenye kichaka kimoja, mbali kidogo na lilipo jumba hilo, nikashuka na kuanza kutembea msituni kwa kujiamini huku nikiwa makini sana, mwanga wa mbalamwezi ndio ulio nisaidia kuona mbele na shemu ninayo kanyaga.Nikafanikiwa kufika kwenye fensi ya nyaya, nikatoa kuleo na kuanza kukata moja baada ya nyingine hadi nikapata upenyo wa mimi kupita.Nikaendele kutembea hadi kwenye ikuta mrefu kiasi, nikatazama pande zote na sikuona dalili ya kumuona mtu.
Nikarudi nyuma, nikavuta kasi ya kupanda kwenye ukuta, kutokana na wepesi wa mwili wangu, halikuwa zoezi gumu la mimi kupanda juu ya ukuta huu, nikajivuta hadi nikafikia juu kasisa ya ukuta na kujilaza ili nisionekane, hapo ndipo nilipoanza kuona eneo zima la jumba la Khalid likiwa limetawaliwa na taa nyingi pamoja na ulinzi mkali wa askari walio na mbwa pamoja na bunduki nyingi.Nikamshuhudia mtu mmoja akiwa anapigwa na walinzi wapatao watano huku pembeni akiwa amesimama Khalid na Dorecy.Mtu huyo aliendelea kuomba msamaha ila walinzi hao hawakumsikiliza zaidi ya kuendelea kumshushia kipigo kitakatifu
Khalid akachomoa bastola yake na kumnyooshea mtu huyo, ila kabla hajafyatua akamkabidhi Dorecy bastola na kumuomba amuue mtu huyo, Dorecy bila ya huruma akafyatua risasi zilizo tua juu ya kichwa cha mtu huyo na kumsababishia kifo, nikashusha pumzi nyingi, kwani Dorecy amekuwa katili kiasi cha kuua mtu pasipo kuwa na huruma ya aina yoyote, nikiwa nifikiria cha kufanya nikastukia kitu kigumu kikinigusa kichwani mwangu, na kusikia sauti ya mwanaume ikiniamrisha nilale kama nilivyo na nisifanye kitu chochote la sivyo atauchangua ubongo wangu, taa kubwa lenye mwanga mkali likageukia sehemu ya sisi tulipo, juu ya ukuta na kuwafanya Khalid, Dorecy na watu wake kutuona.Na Khalid akaagiza mtu huyo kunishusha kwenye ukuta.
Nikashusha pumzi taratibu, jamaa akanigusa tena na ndunduki yake kwenye kichwa changu na kuniamrisha kushuka kwenye ukuta, kwa haraka sana nikajigeuza na kuichota miguu yote ya mtu huyo na kumfanya aangukie ndani kama mzigo wa kuni, nikajirusha na kuangukia nje ya sehemu ambayo nimetokea, cha kumsukuru Mungu sijaumia sehemu yoyote ya mwili wangu ambayo itanizuia mimi kukimbia.Nikanyanyuka haraka na kuhakikisha bastola yangu ipo sehemu nilipo iweka nikaikuta ipo.Kelele za ving’ora vya hatari vikanifanya nianze kukimbia kwa kasi zangu zote na kutokomea msituni, kelele za mbwa wengi, nikaanza kuzisikia nyuma yangu, na kadri ninavyo kimbia ndivyo jinsi zilivyo zidi kuja nyuma yangu kwa kasi kubwa.Milio ya bunduki ikazidi kunipa changamoto ya kukimbia kwani watu wa Khalid wapo nyuma yangu, nikajibanza kwenye moja ya mti baada ya kuona risasi zinazidi kuwa nyingi nyuma yangu.Kundi kubwa la walinzi wa Khalid wakazidi kunifwatwa kwa nyuma.
“Mungu bariki”
Nimaneo niliyo yasema kimya kimya moyoni mwangu, kisha nikaanza kujibu mapigo ya risasi niazo rushiwa kwa fujo, nikaendelea kuwafatulia watu wa Khalid na kuwaangamiza kila ambaye nilimfyatulia risasi.
Nikastukia kuona mwanga mkali wa ukinimulika kutoka juu, nikatazama na kukuta ni Helcoptar, nikaanza kusikia sauti kutoka kwenye kipata sauti ikiniomba nijisalimishe la sivyo nitauawa kwani sehemu nzima ya msitu imezingirwa, nikaitoa magazine ya bastola yangu na kukuta imebakiwa na risasi moja tu, na nyuma yangu kundi la watu wasio pungua ishirini, wananifwata kwa kuyata, huku wengine wakiwa awanatokea mbele yangu.Mwanga wa Helcoptar ukaendelea kunimulika kiasi cha kuninyongonyeza kabisa katika kupata matumaini ya kujiokoa.Sikuwa na jinsi zaidi ya kupiga magoti chini, huku miono yangu nikiwa nimeiinyoosha juu.Jamaa wakanizingira na wawili wakanisogelea nakuanza kunipapasa na kunitoa kila kitu nilicho kuwa nacho mfukoni mwangu kisha wakaninyanyua na kunifunga waya mgumu kwenye mikono yangu na safari ya kuelekea ilipo ngome ya Khalid ikaanza.
Ilituchukua mwendo wa dakika zisizo pungua kumi hadi kufika ilipo ngome ya Khalid, nikamuona Dorecy na mume wake wakiwa wamesimama kwenye moja ya ngorofa kubwa lililopo ndani ya ngome, macho yao yote yakiwa kwangu
“Ohooo karibu bwana Eddy”
Muyo ulinistuka sana baada ya kumsikia Khalid akizungumza kiswahili kizuri tu, kwa haraka nikayafikira maneno ya kejeli niliyokuwa ninazungumza na mke wake, nikiamini kwamba Khalid aelewi kitu ambacho ninakizungumza na mke wake.
“Naona umekuja kunitembelea, za masiku bwana Eddy?”
Sikumjibu Khalid zaidi ya kumtazama kwa macho makali katika sehemu ambayo amesimama, pamoja na mke wake
“Mpandisheni huku juu”
Aliwaamuru watu wake na wakaniingiza kwenye moja ya lango kubwa, tukaanza kupandisha ngazi kuelekea ghrorofani, wasiwasi wangu mkubwa ni juu ya mke wangu Phidaya, sijui akiamka asubuhi na kunikuta sipo ndani chumbani, ataamua kufanya maamuzi gani.
“Karibu Eddy, ninafurahi sana kukuona hapa, kwa kipindi hichi kingine.Vipi ulikuwa umekosea njia ya kuja hapa?”
Macho yangu yakagongana na Dorecy aliye valia dera refu, kutokana na ujauzito wake kuwa ni mkubwa.Khalid akazitazama ishara za macho kati yangu na Dorecy kisha akatabasamu.
“Naamini, mke wangu atakuwa na furaha sana kukuona hapa mwanadarasa wake, na munavyo onekana mulikuwa munasoma sana eheee”
“Hee baby, hembu acha maneno yako, mimi huyo Eddy hatukuwa na ushirikiano kwenye masomo”
Dorecy alizungumza kwa sauti nyororo iliyo mbembeleza mumewe, na taratibu akamsogelea mumewe na kuanza kuzichezea nywele za kifua cha mume wake
“Ohh mke wangu, sawa ila vipi, sijaielewa maana ya rafiki yako kuwa hapa?”
“Hata mimi sijui”
“Eddy, ni kwanini upo hapa?”
“Dorecy nipe mali yangu niondoke”
Nlizungumza kwa sauti nzito, na kumfanya Khalid kumgeukia mke wake
“Anakudai?’
“Ahaaa hapana ila sijui kachanganyikiwa huyo”
“Eddy, unamdai nini mke wangu?”
Kwa haraka Dorecy akanikonyeza, pasipo mume wake kumuona, nakuniomba nisizungumze kitu chochote mbele ya mume wake.Nikatabasamua na kumtazama Khalid
“Hapana, ile siku nilipo kutana na nyinyi kule dukani, Dorecy aliniambia kwamba siku moja nije kuwatembelea atanipa mali ya kutosha”
“Ohhh, mke wangu ni mali gani unataka kumpa Eddy?”
“Ni mtaji wa kufungua biashara, siku ile baby si nilikuwambia kwamba kuna bishara ya hoteli nataka kwenda kuifungua Tanzania, so nikaona mtu wa kumuweka awe Eddy kama msimamizi”
“Ahahaaaa hapo nimewaelewa, kwani mulianza kunitisha.Mfungueni”
Khalid aliwaamrisha watu wake wanifungue mikono yangu na wakatii kama bosi wao alivyo agiza, wakanifungua mikono yangu na akawaomba waondoke, Khalid akanikaribisha sebleni kwake, na tukaanza kuzungumza mambo mbalimbali ya maisha, jambo ambalo lilianza kunishangaza kwani Khalid niliye adisiwa na muendesha taksi sio huyu ninaye zungumza naye mbele yangu.
“Bwana Eddy, kunabinti atakuja hapa kukuonyesha chumba cha kulala, mimi ngoja nikapumzike na mke wangu, si unamuona jinsi hali yake ilivyo?”
“Hakuna shida shemeji”
Khalid akanyanyuka na Dorecy na kupandisha ngazi kwenda juu kabisa, macho yangu yakawa na kazi ya kuwachunguza walinzi walio simama kwenye kila kona ya jumba huili kuanzia ndani hadi nje.Akaja dada mmoja aliye valia chupi aina ya bikini na sidiria
“Nifwate”
Alizungumza kwa kingereza, pasipo kuuliza ni wapi ninapo elekea nikanyunyuka na kuanza kumfwata kuelekea sehemu anapo kwenda, tukapita kwenye moja ya kordo ndefu, nyenye wingi wa vyumba kila kona, akafungungua mlango mmojana na sote tukaingia.
“Unapenda nini, whyne, shampen, wicky au juis”
Aliniorodheshea idadi ya vinywaji ambavyo sivitumii kwa wakati huu ambao nipo kwenye ngome ambayo hadi sasa hivi sijajua usalama wangu upo kaika upande gani,kati ya kutoka salama au kutokamu ndani ya ngome hii.
“Sihitaji chochote, asante sana”
“Una hitaji huduma ya mwili wangu”
“Hapana ninashukuru”
Baada ya msichana kumjibu hivyo akajizoa zoa na kutoka ndani ya chumba changu na kuniacha nikiwa ninamawazo sana, nikazima taa za chumba kizima na kuwa giza totoro, nikaanza kuchunguza kuta moja baada ya nyingine, kutazama kama kuta kuwa na kamera zilizo fichwa kwenye kuta za chumba hichi, ambazo mara nyingi baadhi huwa zinachimbiwa ukutani, na zinatoa mwanga mwekundu kila unapo ziona kukiwa na giza.Nikamaliza kukizunguka chumba kizima na sikuona kitu cha aina yoyote, nikaipanga mito mitatu kitandani kama mtu aliye lala na kuifunika kwa shuka.Nikalisogelea dirisha taratibu na kulifungua, ukimya mwingi umetawala nje, kitu kikubwa ninacho kiona ni walinzi wakikatiza katiza kila kona ya ngome hii.
Kitu ambacho kinanifanya nishindwe kushuka kwenye chumba hichi ni kutokana, chumba kipo ghorofani na chini ni mbali sana, mwanga wa jitaa kubwa ukakatiza kwenye dirisha nililo simama na kwa haraka nikajibanza kwenye ukuta ili upite vizuri na walinzi wasione.Ukarudi tena ulipo tokea, kabla sijanyanyuka mlango wa chumbani kwangu ukafunguliwa taratibu na nikamuona Dorecy akiingia huku akiwa amevalia kagauni kakulalia
“Eddy”
Aliniita kwa sauti ya kunong’oneza, huku akielekea kitandani ambapp nimepanga mito vizuri kama mtu aliye lala.Akasimama pembeni ya kitanda changu, niaamini hakuniona kwenye sehemu niliyo simama, akakitazama vizuri mwili wa mito nilio ulaza kisha akakipandisha kigauni chake juu, na kuchomoa kisu kikali alicho kuwa amekificha kwa kukifunga kwenye paja lake kwa mpira kisha kwa haraka akakishusha na kutua kwenye mito jambo lililo nistua sana kuona Dorecy akizidi kuwa katili juu yangu
Dorecy akastuka baada ya kuona kisu kikinyanyuka na mto, ikamlazimu kufunua shuka kwa haraka kwa ajili ya kutazama kama kitandani kwangu kuna mtu, akajikuta akistuka zaidi baada ya kukuta ni mito ndio imejipanga, kwa haraka nikamrukia na kumsukimiza kitandani na kisu chake kikaangukia pembeni, nikakiwahi kukiokota kisu chake, kisha nikamuwahi kulikamata koo lake na kuliminya kwa nguvu zangu zote huku kisu nikiwa nimekinyanyua juu kwa mkono wangu wa kulia
“Unataka kuniua ehee”
Nilizungumza kwa hasira huku nikiendelea kuliminya koo lake na kumfanya atoa mlio wa kukoroma akishiria kukata roho
“E…ddy naa….”
“Hakuna cha kuomba, malaya mkubwa wewe, leo ndio utaijua jina langu la utotoni nilikuwa ninaitwa nani”
Niliendelea kukaba Dorecy koo lake, hadi akaanza kulegea, nikamuachia na kwaharaka nikashuka kitandani na kuivuta miguu yake na akaangukia mgongo kwenye sakafu, nikamnyanyua juu na kumpiga kabali kwa nyuma huku kisu changu nikikiweka kwenye tumbo lake.
“Eddy mpenzi wangu naomba unisamehe nilikuwa ninakutania tuu”
Dorecy alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.Sikutaka kuzisikiliza porojo zake kwa maana hakuna utani wa kuuana
“Ongoza njia”
“Eheee”
“Ongoza kwenda nje”
Nilizungumza huku nikikikandamiza kidogo kisu kwenye tumbo lake lenye mtoto ndani na kumfanya aanze kutambea huku mwili mzima ukimtetemeka, akafungua mlango, na kukutana na walinzi wawili wenye bunduki wakiwa wamesimama kwenye mlango wa chumba changu, hapo ndipo nikagundua kwamba nilikuwa ninalindwa nje nisitoke.Wakanielekezea bunduki zao, ila mimi nikazidi kumkaba kabali Dorecy huku kisu nikikikandamiza kwenye tumbo lake.
“Waambie washushe bunduki zao la sivyo nakufanyia oparesheni bila ganzi”
Dorecy akawaamuru watu wake waweze kufanya kama nilivyoa mauambia, wakatii kwa haraka, tukaanzaa kutembea kwenye kordo ndefu ya vyumba, huku walinzi wake wakitufwata kwa nyuma, sikuwa na woga wa aina yoyote kutokana bosi wao yupo chini ya mamlaka yangu.Tukafika sebleni na kukutana na walinzi wapata kumi wakiwa na bunduki zao wakitusubiria sisi kutokea kwenye seble hii.
“Eddy, sasa nimeijua rang yako”
Sauti ya Khalid ikanistua, nikamuona akitokea kwenye moja ya chumba huku akiwa amevalia nguo za kulalia na mkononi mwaka akiwa ameshika bastola
“Waamrishe watu wako kutupisha la sivyo ninamuua mke wako”
Nilizungumza kwa sauti kubwa, huku nikiendela kukikandamiza kisu kwenye tumbo la Dorecy ambaye muda wote machozi yanamwagika, kwa ishara Khalid akawaamrisha watu wake kutupisha, tukapita katikati yao huku muda wote nikiwa makini sana, nikiwatazama watu wa Khalid
“Ila Eddy unacheza makida makida kwenye nyaza za umeme”
Khalid alizungumza kwa kujiamini sana, sikujali maneno ya Khalid zaidi ya kumuamrisha Dorecy kutembea kuelekea nje.Tukafunguliwa mlango na walinzi wake baada ya Dorecy kuwaamrisha waweze kufanyan hivyo.
“Magari yenu yapo wapi?”
Nilimuuliza Dorecy kwa sauti ya ukali, taa kubwa lililopo katika jumba hili likawa na kazi ya kutumulika kila sehemu ambayo tunakwenda, macho yangu yote yakawa na kazi ya kutazama kila sehemu ya jengo hili kuangalia walinzi walio jipanga huku wote bunduki zao zikiwa kwetu, Dorecy akanionyesha moja yan jengo ambalo aliniambia kwamba ndipo yalipo magari, kwa hatua za umakini tukatembea hadi lilipo jengo hilo na kuingia ndani, ambapo nikakuta magari mengi ya kifahari takiwa yamepangwa kwa mpangilio mzuri.Macho yangu yakatua kwenye gari aina ya BMW inayo endana na gari ya Sheila aliyo pewa na wamarekani alio cheza nao filamu ya ngono.Nikaisogela huku nikiwa ninaendelea kumshika Dorecy shingo yake, nikajaribu kufungua mlango wa gari na ukafunguka, kwa bahati nzuri nikakuta funguo ikiwa kwenye siti ya dereva.
“Eddy si umesha fika sehemu uliyokuwa unahitaji, niachie sasa”
“Bado unakazi na mimi”
“Kazi gani jamani Eddy?”
“Utaijua mbele ya safari”
Nikamshukumiza Dorecy kwenye siti ya pembeni na mimi nikaingia, nikaiwasha gari na ikawaka pasipo tabu yoyote, cha kushukuru MUNGU mafuta ya gari yamejaa vizuri kwenye tanki lake, nikashusha pumzi nyingi huku nikijifunga mkanda wa gari
“Eddy Khalid atakuua”
Dorecy alizungumza kwa sauti ya chini huku, machozi yakiendelea kumwagika, sikutaka kumsikiliza sana Dorecy, nikairuduisha nyuma gari na kuiweka sawa kuelekea kwenye mlango wa kutokea kwenye jumba hili ambao ni wambao.
“Funga mkanda”
Nilimuamrisha Dorecy na akatii, nikaknyaga mafuta pamoja na breki na kuifanya matairi ya nyuma ya gari kuserereka kwa nguvu, nikaachia breki na kuifanya gari kuanza kwenda kwa mwendo wa kasi, nikaubamiza mlango na gari ikapita kwenye mlango bila ya shida.Taa kali zikapiga kwenye kioo cha gari langu na kunifanya nisione mbele vizuri, nikajikuta nikikanyaga breki kwa haraka, huku macho yangu yakikitazama ‘Kifaru’ kikubwa kilichopo mbele yatu.Nikatazama pembeni na kuona kuna bustani ya maua ambayo gari linaweza kupita pasipo shida yoyote.Nikatazam kifaru hichi ambacho mara nyingi hutumika jeshini katika vita.Mwanga wa Helcoptar ukaendelea kumulia kwenye gari letu,
“Shiti”
Nikakanyaga mafuta kwa haraka, kugeuza gari kwa kasi na kuuelekezea kwenye bustani ya maua, risasi nyingi za walinzi wa Khalid zikaanza kupiga kwenye gari yetu cha kushukuru Mungu hakuna risasi hata moja ambayo inaingia kwenye gari, nikaendelea kuipitisha gari kwenye bustania ya maua hadi nikafika kwenye barabara kubwa iliyopo ndani ya hili jengo la Khalid
“Njia hapa ya kutokea ni ipi?”
“Wewe nyoosha tuu mbele”
Dorecy akanipa ushirikiano mzuri paiso kupinga, nikazidi kunyoosha kwenye barabara aliyo seme Dorecy, huku mfululizo wa risasi ukizidi kuniandama kwa nyuma, mwanga wa Helcoptar ukazidi kutumulika
“Kunja kushoto”
Dorecy alizungumza na mimi nikafanya kama alivyo seme, kazi yangu kubwa ikawa ni kubadilisha gia kwenye gari na kuongeza mwendo kasi wa gari
“Kulia”
Nikakunja kulia kwenye kibarabara kidogo ambacho kwa mbele yake kuna geti dogo lililo wazi, nikazidi kuongeza mwendo kasi wa gari na kutoka kwenye ngome ya Khalid.Tukatokea kwenye barabara iliyopo kwenye kilima, huku pembeni ya barabra kukiwa kuna maporomoka marefu mithili ya barabara ya mlima Kitonga uliopo Mkoni Iringa nchini Tanzania.
“Unaijua hii barabara?”
“Ndio wewe twende”
Umakini wote nikazidi kuuweka kwenye barabara, kwani ina kona nyingi, na endapo nitafanya ujinga wa aina yoyote gari itabingiria kwenye maporomoko na ndio utakuwa mwisho wa maisha yangu na Dorecy.Helcoptar ya watu wa Khalid ikazidi kutufwata kila sehemu ambayo tunaelekea, kutokana na uzoefu wangu wa kuendesha gari kwenye barabara zenye makona mengi, haikuwa nguma kwangu kuhimili kona za hapo kwa hapo ambazo ni nyingi sana.
“Ukimaliza kona mbili hapo mbele kuna mporomoko mrefu kuwa makini”
Dorecy alizungumza, ushirikiano wake sikuuamini sana kutokana na yote aliyo nifanyia, nikazidi kuongeza mwendo kasi wa gari huku miguu yangu, ikiwa na kazi ya kucheza na breki.Tukafika kwenye kiporomoko ambacho Dorecy anazungumza kwa mbali kidogo nikaona taa za gari kwa haraka haraka zinapata kumi zikiwa zimeziba njia, kwa jicho langu la kushoto nikamuona Dorecy akitabasamu hapo ndipo nikagundua amaniuza, kwa kutumia kisukusuku changu cha mkono wa kushoto, nikambamiza nacho Dorecy pembeni ya shingo yake na kumfanya atulie kimya na kupoteza fahamu.Nikafunga breki za gari langu, umbali kidogo kutoka zilipo gari za watu wa Khalid, nikatazama kushoto kwangu ambapo kuna maporomoko marefu, hapakuwa na nyia ya aina yoyote.Kulia kwangu kuna ukuta mkubwa wa mlima, Helcoptar ikasimama na kuzidi kutumulika,
“Nitafanyaje?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijikuta nikijiuliza swali mwenye pasipo kupata jibu, kwa kutumia kioo cha pembeni nikaona gari nyingi zikija kwa kasi nyuma yangu, huku zikaanza kushuka kiporomoko ambacho ndipo nilipo.
“Bwana Eddy jisalimishe, wewe mwenyewe”
Niliisikia sauti ya Khalid ikitokea kwenye kipaza sauti juu ya Helcoptar yake,
“Siwezi kufa kijinga”
Nilizungumza mwenyewe huku nikiitazama Helcoptar ambayo inaendelea kumulika mwanga kwenye gari yetu
“Moja jisalimishe”
Khalid alianza kuhesabu, nikatimaza pembeni upande wa kushoto nikaona tobo kubwa kwenye gemo kubwa la mlima, gari za mbele yangu zikaanza kupandisha kilima huku za nyuma zikishuka kwa kasi, nikakanyaga mafuta, pamoja na breki zote kwa pamoja na kuyafanya matairi ya nyuma yakiserereka kwa nguvu gari za nyuma zilazidi kunisogelea katika sehemu ambayo nimesimama, kwa kasi nikakunja kulia na kuifanya gari yangu kuelekea kwenye tobo lilipo kwenye gemo la mlima, sikuamini kama gari yangu inaweza kuingia ndani ya tobo hili, sikumini macho yangu baada ya kukuta barabara iliyo chongwa ndani ya shimo hili, ambayo ipo ndani ya mlima
“Waoooo”
Nilijikuta nikipiga kelele a furaha baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya shimo hili, japo kuna giza jingi ila taa gari langu zikanisaidia kuona mbele vizuri sana.Gari za watu wa Khalid zikaendelea kunifukuzia kwa nyuma jambo lililo anza kunipa wasiwasi mwingi
“Wakinikamata watanila nyama”
Nilijisemea kimoyo moyo, nikamtazama Dorecy na kumkuta akiwa bado amepoteza fahamu, upana wabarabara hii iliyo chongwa ndani ya mlima ikazipa upenyo gari za watu wa Khalid kutanda njia nzima, huku baadhi ya gari zikijari kunipita ila niliwazui kwa kuwazibia njia kwa mbele.Wakaanza kunipiga risasi kwenye kii cha nyuma cha gari langu, nikazidi kuongeza mwendo wa gari langu, mbaya zaidi barabara hii haina hata kona zaidi ya kunyooka.
Risasi zao nyingi zikafanikiwa kutoboa kioo cha nyuma cha gari na kuzidi kunichanganya akili yangu, nikazidi kukanyaga mafuta hadi mshale wa spidi mita ukagota kwenye spidi ya mwisho ambayo ni mia mbili na hamsini.Nikazidi kwenda mbele, gafla nikakutana na kona ambayo kwa mwendo ambao ninao nikashindwa kukunja na kuisababisha gari kupiga kweney ukuta na kuvunja ukuta huu wa udongo, kufumba na kufumbua nikajikuta gari ikielea hewani, na kuanza kwenda chini kwenye miamba mikubwa ya mawe jambo ambalo lilinifanya niaanze kusali sala yangu ya mwisho kwani, ikitua chini mimi na Dorecy wote tutakuwa maiti
Gari ikazidi kwenda chini kwa kasi, gafla nikastukia gari ikiwa imekwama huku, tawi kubwa la mti likiwa limeingia dirishani la nyuma la gari na kuifnya iendelee kuninginia kwenye mti, nikashusha pumzi taratibu huku nikitazama chini, cha kumshukuru MUNGU, kutoka sehemu tulipo ning’inia hadi chini si mbali sana, nikaufungua mkanda wa gari nilio jifunga, nikamtazama Dorecy na kumuoana akiwa anainyanyua nyanyua shingo yake, akizinduka kutoka usingizini.Akanitazama kwa macho yakuchoka
“Eddy”
“Nini?’
“Yupo wapi Khalid?”
“Wee mwehu nini, jiulize mwenyewe”
Nilizungumza kwa hasira huku nikiufungua mlango wa gari, kuna tawi lipo karibu na mlango wangu, nikapiga makadirio ya macho na kuona ninaweza kuruka na kulikanyaga pasipo na wasiwasi wa aina yoyote
“Eddy unataka kwenda wapi, kwani hapa wapi?”
Dorecy alizungumza huku akitazama chini
“Hapa tupo mbinguni mama yangu”
“Mbinguni……!!?”
“Unauliza tena, hapa ukifungua mlango tuu umeshafika kwa sir God”
Nilizungumza kwa dharau, nikaruka kwenye tawi la mti, kwa bahati nzuri nikatua vizuri na kujiweka sawa mwili wangu, nikashuka kwenye mti taratibu na kufika chini pasipo shida ya aina yoyote, gafla nikasikia kelele za Dorecy akiniita jina langu, ikanilazimu nimtazame nikamuona akiwa ananing’inia, huku ameushikilia mlango wa gari uliopo upande wa siti yake
“Eddy niokoe mwenziooo, ninakufa mimi”
“Ukijiachia tuu unafika mbnguni, hapo tulikuwa kwenye geti la kuingilia mbinguni”
Nilizungumza huku nikimtazama Dorecy jinsi anavyo ning’inia huku akiirusha rusha miguu yake hewani
“Eddy nakufa mimi”
Dorecy aliendelea kuzungumza kwa sauti ya kilio, huku akiendelea kuning’inia hewani, nikatafuta sehemu yenye jiwe lililo kaa vizuri, nikakaa na kuendelea kumtazama Dorecy anaye endelea kuninginia hewani
“Eddy niokooe”
“Nikuulize kitu Dorecy?”
“Ehee” Alijibu huku akiwa amening’inia
“Hivi huku ulifikaje?”
“Nikuulize wewe, tumefikaje huku?”
“Ahaa unaniuliza mimi tena kwamba tumefikaje huku, unadhani kwamba mimi nilikuwa ni ndege iliyo kufikisha kwenye hii nchi?”
“Eddy tuachane na hayo, ninakuomba unisaidiea”
Dorecy alizungumza kwa sauti ya unyong, akiashiria kwamba amechoka sana
“Madini yangu yapo wapi?”
“Edd siwezi kukujibu hadi nishuke”
“Basi wewe si mjeda wa mzee Godwin, jishushe mwenyewe”
Nilizungumza huku nikinyanyuka kwenye jiwe, nikiendelea kulichunguza aneo zima la hii sehemu, nilipo hakikisha lipo salama na hakuna uwezekana na watu wa Khalid kufika katika sehemu tulipo nikarudi sehemu alipo Dorecy akiendelea kuning’inia huku akitoa kilio kwa mbali akilalamika kwamba anakufa
“Jiachie”
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama chini yake nikimtazama
“Ehee?”
“Hujasikia, jiachie nitakudaka na hilo jitumbo lako”
“Kweli Eddy?”
“Kama hutaki basi bwana”
“Basi najiachia”
Nikaitega mikono yangu usawa wa sehemu anayo ning’inia Dorecy, nikahesabu moja hadi tatu, Dorecy akajiachia na kutua kwenye mikono yangu, cha kushukuru MUNGU ametua vizuri kwenye mikono yangu, nikamsimamisha chini na kumuacha akiendelea kuhema kwa nguvu, kama bata mzinga.Nikaanza kupiga hatua za kuondoka katika eneo hili pasipo kusubiria asante ya Dorecy huku moyoni mwangu nikijikuta nikianza kusamehe kuhusiana na madini yangu, kwani hakuna uwezekano wowote wa mimi kuyapata kutokana na Khalid kujizatiti vizuri katika swala la ulinzi
“Edd….y”
Nilisikia sauti ya Dorecy ikiniita kwa unyonge nyuma yangu, nikasimama pasipo kutazama nyuma, nikashusha pumzi nyingi na kugeuka taratibu, nikamuona Dorecy akianza kukaa chini taratibu huku akiwa amelishika tumbo lake
“Eddy nakufa mimi, tumbo langu”
Dorecy alilalamika huku akiwa amelishika rumbo lake, nikaanza kupata mstuko baada ya kagauni kake ka kulalia alicho kivaa kukiona kikiwa kimelowa kwa damu sehemu zake za siri.Machozi ya uchungu yakaendelea kumtoka Dorecy, vilio vya Dorecy vikazidi kuongezeka, ikanilazimu kurudi kwa haraka katika sehemu alipo
“Eddy mtoto anatoka”
Dorecy alizungumza huku akipanua mapaja yake, wazo la kwanza kunijia kichwani mwangu, ni kukata nguo ya ndani aliyo ivaa Dorecy, macho yangu yakaendelea kumtazama Dorecy jinsi anavyo toa mayowe ya uchungu
“Eddy mwanangu uwiiiiiii”
“Yupo wapi?”
Nikastukia kofi zito ikitua kwenye shavu langu, kutoka kwa Dorecy ambaye anaonekana kukasirika, macho yake ameyatoa huku jasho jingi likimwagika kutoka na maumivu makali anayo yapata.
“Jikaze uzae”
Nilizungumza huku nikiishikilia miguu ya Dorecy ambayo ameichanua kwa kiasi fulani, nikaendelea kumuhimiza ajitahidi kumsukuma mtoto, kwani nilisha anza kuona dalili ya majimaji yanayotangulia kabla ya mtoto kuzaliwa.Taratibu nikaanza kuona kichwa cha mtoto kikianza kuchomoza
“Push kwa nguvu”(Sukuma……)
Nikaendelea kumuhimiza Dorecy kwa sauti ya juu, akaendelea kujitahidi kumsukuma mtoto wake atoke nje, nikaiweka mikono yangu karibu na kichwa cha mtoto na kuanza kukipokea kichwa chake taratibu
“Endelea mama, mabega yameshaanza kuchomoza”
Hadi mimi mwenyewe jasho likaanza kunitoka kwani si kazi ndogo ya kumzalisha mwanamke
“Eddyyyyyyyyyyyyyyyy”
Dorecy alizungumza kwa nguvu, huku akijikamua kwa nguvu zake zote na kumfanya mtoto wake kutoka na kuangukia mikononi mwangu, sikuisikia tena sauti ya Dorecy, katoto kake ka kiume, kenye mwili mdogo kakaanza kutoa kimlio kwa mbali, nikajikuta nikifurahi mimi mwenyewe, huku jasho likiendelea kunimwangika uso mzima, nikabaki nikimtazama mtoto huku kitomvu chake kikiwa bado kimeshikana na mama yake, ambaye amepotezafahamu kutokana na maumivu makali ya kujifungua
“Huyu mtoto amezaliwa kabla ya siku zake”
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama mtoto kwani ni mdogo kupindukia, kwa elimu yangu ya sayansi watoto wa aina hii huwa tunawaita njiti kutokana hajatimiza umri halisi wa yeye kuzaliwa kama watoto wengine wanaotimiza miezi tisa
Nikamtazama Dorecy kwa macho yaliyo jaa uchovu mwingi, kifua chake kwa mbali kinanyanyuka taratibu na kurudi chini, nikamsogelea na kumtingisha kidogo, ila hakuzinduka
“Hichi kitovu kinakatajwe?”
Nilijiuliza swali huku nikikitazama kitovu kilicho ungana kati ya mama na mtoto, nikamuweka vizuri Dorecy na kumlaza chali, nikamuweka mtoto wake juu ya tumbo lake kisha nikanyanyuka na kuanza kutafuta ni wapi ninapoweza kupata kitu chenye ncha kali cha kukikata kitomvu cha mtoto, kutokana kumesha pambazuka vuzuri ninaweza kuona kila kitu ambacho kinaweza kuwa chini, nikazunguka aneo la karibu na alipo Dorecy ila sikuona kitu kinachoweza kunisaidia kwa muda huu.Ikanilazimu kurudi sehemu nilipo muacha Dorecy, macho yangu yakangonana na macho ya chui, ambaye yupo hatua chache kutoka sehemu alipo lala Dorecy, ambaye muda wote hajitambui kutokana nakupoteza fahamu
“Mungu wangu”
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama chui ambaye anatoa mingurumo ya chini chini huku akilamba lamba mdomo wake wenye meno makli yenye ncha kali sana, nikachuchumaa chini taratibu pasipo kuyapepesha macho yangu, nikimtazama chui huyu, nikaokota kipande cha jiwe ambacho nimekikanyanga kwa mguu wangu wa kushoto, kisha nikasimama huku nikiendelea kumtazama chui huyu
“Shiiiii”
Nilitoa mlio huo, nikimfukuza chuki huyu ambaye taratibua alichaanza kupiga hatua za kumfwata Dorecy na mwanaye katka sehemu ambayo wamelala chini, chui akasita kidogo na kunitazama kwa macho yake makali
“Toka opo”
Niliendelea kuzungumza huku nikimtishia kwa jiwe ambalo nimelishika mkononi mwangu, mwili mzima ukaanza kunitetemeka baada ya chui kubadilisha muelekeo wake na kuanza kunifwata mimi kwa mwendo wa madaha katika sehemu ambayo nimesimama, kikataka kupiga hatua moja nyuma, gafla nikajikuta nikianguka chini kama mzigo, kitendo cha kujaribu kunyanyuka tayari Chui amenirukia kifuani kwangu, kichu cha kwanza kukiwahi katika kukishika ni shingo yake, nikakizuia kichwa chenye mdomo wake ulio jaa meno makali, usinidhuru kwenye mwili sura yangu,
Chui huyu akaendelea kunikwaruza na kucha zake, sehemu mbali mbali za mwili wangu, huku akijitahidi kuushusha mdomo wake kuing’ofoa pua yangu, nikaendelea kujikaza kwa juhudi zangu zote, uzito wa chui huyu ni mara mbili ya uzito alio nao mke wangu Phidaya, mikono yangu ikaanza kutetemeka kwa kuchoka, huku taratibi nikiendelea kujikaza kizuia shingo ya Chui huyu.
“Mungu wangu nisaidie mimi”
Niliendelea kuzungumza, huku mikono ikianza kuchuka taratibu chini, ikizidiwa uzito na kichwa cha chui huyu anaye onekana ananjaa kali, sikujali jinsi anavyo nikwaruza sehemu za mwili wangu kwa kutumia miguu yake ya nyuma na yambele yenye kucha kali sana, kikubwa ni kujitolea maisha yangu kwa ajili ya Dorecy na mwanaye niliye mzalisha
“Siwezi kufa kijinga”
Nikaanza kujitutumua kiume, huku nikiipandisha mikono yangu juu nikijitahidi kumtoa Chui huyu mwilini wangu, juhudi na nguvu zangu taratibu zikaanza kuzaa matunda, kwani nikafanikiwa kumgeuza chui na kumuegemesha kando.Mwili wangu mzima unavuja damu kataika sehemua alizo nikwaruza chui huyu, mikono yangu sikuiruhusu kutoka mikononi mwa chui huyu.Nikaanza kukidundiza kichwa chake chini, kwenye jiwe kubwa.Chui akazidi kupandisha hasira na kutoa pumzi kali iliyo anza kuyafanya macho yangu kumwagika machozi mithili ya mtu aliye pigwa bomu la machozi na askari wa kutulizaghasia
“Eddyyy”
Niliisikia sauti ya Dorecy ikiita kutoka katika sehemu alipo lala, nikageuza shingo yangu kumtazama sehemu alipo, nikamuona amekaa chini huku amemshika mwanaye, kitendo cha mimi kumtazama Dorecy kikawa ni kosa kubwa kwangu kwani chui, akanibinua kwa nguvu zake zote akaanza kunikwaruza huku meno yake akijaribu kuyakita kwenye paja langu la mguu wa kulia.Maumivu yasiyo na kifani yakaanza kuutesa mguu wangu, machozi ya uchungu yakanimwagika.Nikaokot kipande cha jiwe lilicho chongoka na kuanza kumkita nacho Chui cha kichwani mwake
Chui akazidi kuyakita meno yake kwenye paja langu, nia yake kuu ikiwa ni kunikata mguu wangu, nikazidisha kumbabiza kwa jiwe langu nililo lishika, kelele za maumivu zikaniendana na kasi yangu ya kukikita kicha cha chui kwa ncha ya kipande cha jiwe, kichwa cha Chui kikaanza kufumuka damu huku fuvu lake la kichwa likipasuka na ubongo wake kutoka nje, ikawa ni mwisho wa maisha yake
“Ahaaaa”
Nilizungumza huku nikilia kwa uchungu mkali, nikaushika mdomo wa Chui na kikauachanisha mdomo wake wenye meno yaliyo kita kwenye paja langu, japo maumivu ni makali sana ila nikajitahidi hivyo hivyo hadi paja langu nikalitoa kwenye kinywa cha Chui na kujilaza pembeni,Nikamtazama Dorecy sehemu aliyo kaa nikamuona akijitahidi kusota kuja sehemu niliyo jilaza mimi, huku sura yake ikiwa imejaa machozi mengi
“Usije”
Nilizungumza kwa sauti iliyo kwaruza sana huku nikimnyooshea mkono asifike katika sehemu nilipo mimi, nikajinyanyua taratibu huku damu zikendelea kuvuja kwenye paja langu.Chakumshukuru Mungu, Chui huyu meno yake, hayakufanikiwa kukutana na kutoa kipande cha nyama kwenye paja langu, au kuukata kabisa mguu wangu, nikaanza kutembea huku nikiuburuza mguu wangu ulio jeruhiwa hadi nikafika sehemu alipo kaa Dorecy
“Mtoto yupo hai?”
Nilimuuliza Dorecy huku nikimtazama mtoto wake aliye yafumba macho yake
“Ndio”
“Ohhh asante Mungu”
Nilizungumza kwa sauti ya kukwaruza sana huku damu zikiendelea kunimwagika mwilini mwangu, machozi yafuraha yaliyo changanyikana na uchungu yakaendelea kunitiririka usoni mwangu
“Eddy ninakupenda sana, samahani kwa yale yote niliyo kufanyia, ninaamini kwamba mimi ni binadamu ninaye weza kuhadaika kwa vitu vidogo sana.Sikustahili unisaidie, ilikuwa ni haki yangu kutafunwa na huyo chui mimi na mwanangu, ila wewe uliweza kujitolea maisha yako kwa ajliya yangu na mwanangu”
Dorecy alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, nikamtazama kwa muda jinsi anavyo endelea kulia kwa uchungu sana
“Usilie, nimekusamehe muda mwingi sana, hali yangu inazidi kuwa mbaya na hapa niporini, ninjua sinto weza kutoka nikiwa hai, kifo kitakuwa juu yangu, ninakuomba umtafute msichana mmoja anaitwa Phidaya, anamimba yangu nakuomba unisaidie kwa hilo pale nitakapo kuwa nimeshakufa”
“Hapana Eddy, huwezi kufa nakuomba usizungumze hivyo”
“Dorecy, damu nyingi inanitoka nilazima….”
“Edddyyuuu tazama nyuma yako”
Sauti kali ya Dorecy ikaniomba kugeuka nyuma na mimi nikafanya kama alivyo niambia, ila tayari nimeshachelewa risasi mbili kutoka kwa watu wa Khalid waliofika kwenye eneo hili, zikatua kifuani mwangu, na taratibu nikaanza kwenda chini, nikapiga magoti na kumtazama Dorecy, aliye yatoa macho yake huku akishangaa, kuto kuamini kitu anacho kiona
“Bye….”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikaanguka chini, huku nikilalia tumbo na giza nene taratibu likaanza kuyafunika macho yangu, na kwambali nikaanza kuisikia sauti ya Dorecy ikiliita jina langu kwa uchungu
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment