Search This Blog

Thursday 19 May 2022

TOTO LA KIMANGA - 1

 





    IMEANDIKWA NA : SEIF JABU





    *********************************************************************************



    Chombezo : Toto La Kimanga

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tanga raha, raha Tanga,

    Mh!!!!... Kaka Tanga raha, raha Tangaaaaa.....

    "chaz una maanisha nini?.

    "sikiliza chirs tanga raha, raha tanga, nina maana ya kwamba tanga ni sehemu yalipozaliwa mahaba,

    "chaz acha hizo ina maana unyamwezini unapaacha wapi?

    "chirs usiwe masikini wa kuona mbali tanga na tabora ni vitu tofauti kabisa,

    "chaz nakubaliana na wewe mahaba yamezaliwa tanga ila kaka sikia mahaba yamezaliwa tanga yakalelewa tabora yakakulia zanzibar,

    "una maana gani chirs?

    "kwani wewe huoni zile tabia za kuhendo waume siku hizi zinapwaya,

    "zinapwaya lakini hazijaisha chirs,

    "chaz nakwambia ukweli mapenzi yamebaki pemba tu huku kwingine ni masalia ya zamani,

    "chirs tuyaache hayo hebu tujadili leo tutaishi vipi maana hatuna hata unga humu ndani,

    "chaz tutaishi tu leo uhakika mbona,

    "uhakika kivipi?

    "mwarabu kasema taka zimekuwa nyingi kwa hiyo bila kupoteza mda twende kwanza tukapige kazi,

    "poa,

    Chirs na chaz walikuwa ni marafiki walioaminiana sana na kila mmoja alikuwa na ndoto zake ambazo alipanga kuzikamilisha,

    Upande wa chirs alikuwa na ndoto za kupata biashara ya kufanya na biashara aliyoona itamfaa ilikuwa ni biashara ya kuuza nguo za kike na viatu vya kike kifupi alijua umachinga utamtoa kimaisha,

    Upande wa chaz, yeye alikuwa na ndoto za kuwa machinga wa urembo yaani muuza urembo, chaz alikuwa na matumaini kuwa kazi ya urembo ingemtoa kimaisha na kuachana na maisha ya kazi ya kusomba taka,

    Na pia alikuwa na matumaini ya kuwa kazi ya kuuza urembo itampatia fursa ya kuchagua mwanamke mzuri anayempenda,

    Chirs na chaz walifika kwenye hotel ya mwarabu pale maeneo ya kaliakoo,

    "oya mwarabu ndio tumekuja hivyo,

    Poa fanyeni kweli basi,

    "poa,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Chirs na chaz walienda nyuma ya hotel ili kufanya kazi iliyowapeleka pale,

    Chaz na Chirs japo kuwa walikuwa wanafanya kazi za kuchafuka lakini walikuwa ni vijana smat sana kwani walipokuwa wanamaliza kazi walikuwa wanaoga vizuri na kisha wanabadili nguo na siku zote walikuwa wanatembea na ovaroli za kazi,

    "chaz sikia leo tukitoka hapa tupite soko kuu,

    "kufanya nini?

    "kuhemea,

    "alafu unajua kuwa kesho zamu yetu kununua umeme?

    "najua lakini maswala ya kesho ni ya kesho bwana,

    "poa,

    Chirs na chaz walifanya kazi yao wakaimaliza wakalipwa pesa yao wakazunguuka nyuma ya hotel wakaoga wanabadili nguo kisha zile za kazi wakaziweka kwenye kabegi wakachomoka walipopita hotelin mwarabu aliwaangalia kisha akawapa neno,

    "duh!!!!! Mmeuramba kama maofisa wa TRA,

    "mwarabu kupendeza kawaida yetu,

    "haya bwana,

    Chirs na chaz walitoka wakaingia mitaa ya kongo wakiwa Katika misele ya kuelekea soko la kaliakoo walikuwa wakitania njiani,

    "chaz unapenda wanawake wenye matako wewe?

    "Ndio njaa yangu hiyo kwani chirs wewe unazimika na aina gani ya wanawake?

    "mimi sema ukweli napenda mabinti waliobinuko kiaina wenye sura nzuri za mvuto na wenye madoido mengi mengi maringo kwa sana,

    "chirs wewe hakiri huna sasa binti mwenye maringo wewe mwenyewe si atakulingia?

    "haijalishi nitasota naye mpaka nimpate,

    "ngoja kwanza weee pimbi angalia ule mzingo ulivyofunga,

    "haaaaa haaaaa hapo siachii kitu lazima nitangaze njaa,

    "oyaa weee chirs unaenda wapi sasa?



    Chaz alijaribu kuniita ila sikumsikia kwani masikio yalikuwa utazani nimetia pamba hakili yangu yote iliwaza yule binti aliyekuwa mbele yangu,

    Nilimfuata kwa nyuma ila hakuwa anaenda mbali sana kwani nilimfuata hatua chache akawa ameingia ndani ya bank ya DTB tawi la kaliakoo,

    alipozama ndani mimi nilisimama nje kumsubili sekunde tano chaz alinifikia,

    "chirs mbona una mambo ya kijinga wewe?

    "mambo gani?

    "sasa wewe unamfuata yule dada kwa nyuma ili iweje?

    "ili nimjue hata sura yake tu,

    "ukiisha ijua sura utafanyaje?

    "nitajua cha kufanya,

    "sawa acha niangalie picha itakuwaje,

    Wakati wanabisha yule dada alinitoka ndani ya bank na wa kwanza kumuona alikuwa ni chirs mwenyewe,

    Chirs alishangaa sana baada ya kubahatika kumuona yule dada kwa ukaribu zaidi,

    "oooohhh mtoto wa kike anavutia sana....

    Chaz alishituka baada ya kusikia sauti ya Chirs na yeye akatupia jicho moja kwa moja mlango wa DTB akamuona yule binti na yeye akabaki ameduwaa kama mtu aliyepigwa shoti ya umeme mtoto wa kike alikuwa ameubwa akaumbika,

    Japo alikuwa ndani ya gauni lefu lakini uzuri wake ulionekana vizuri sana alikuwa ni binti mrefu wa wastani mwenye sura ndefu iliyo pambwa na macho makubwa kidogo yaliyolegea akikuangalia utazani anakulembua, alikuwa na pua ya kitusi rangi ya chungwa ndio ilikuwa ngozi yake alikuwa na umbo zuri lililokuwa limejikata utazani pingili za muwa kiuno kilikuwa kinaonekana kama kiuno na mgongo ulikuwa umejikata unaonekana ni mgongo,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ukiangallia upande mbele kifuani kama wewe ni mwanaume lijari ni lazima usisimke kwani mtoto wa kike alikuwa ana chuchu zilizosimama utazani miba ya porini ulikuwa ukiamuangalia ni lazima ugeuke mtoto wa kike alikuwa ana tumbo dogo dogo lililojitenga na kifua alikuwa ana shingo ndefu iliyopambwa na mistari mistari ukiangalia vibaya utasema amevaa cheni,

    Ukitupia macho midomo hapo ndio usiseme mtoto wa kike alikuwa ana midomo mizuri yenye umbo la kopa kwa luga raini utasema ana midomo ya love kwa fikira utafikilia kwamba hata kipande cha mhogo hawezi kumungunya kutokana na midomo yake jinsi ilivyokuwa ina pozi matata,

    Vijana walitoa macho ila hawakuwa peke yao kwenye kumshangaa mtoto wa kike kwani kila kidume alikuwa anakodoa macho na hata baadhi ya mabinti walimkodolea macho mtoto wa kike na wao walitamani kufikia hata nusu ya uzuri wa huyo binti,

    Chirs aliona Hapana lazima nimsemeshe mtoto wa kike,

    "dada dada dadaaaa..... daaa....

    Chirs alimuita huku akimfuata kwa nyuma binti huyo japo na kuita kote ila mtoto wa kike hakuitika aliendelea na safari zake mpaka chaz akamvuta chirs,

    "chirs mbona unakuwa pimbi wewe unaona una hazi ya kumsimamisha huyo dada kweli?

    "chaz achana na mimi bwana,

    Chirs alimwambia chaz kwa hasira,

    "poa ila unajitia aibu ndugu yangu ona watu wanavyokushangaa,

    "wanashangaa nini wakati wananionea gele hao,

    "sawa endeleaaaaa...

    Chirs aliendelea kuita kuona hata kama atabahatika kuongea naye japo hakuwa hata na point aliyopanga kuzumza,

    Akiwa bado anafuatilia nyuma Chirs Gafla yule dada aliingia duka la vifaa vya maofisini akanunua vitu mbali mbali kisha akatoka humo ndani ya duka akaendelea na safari zake,

    Alipotoka ndani tu yule binti Chirs alimuita kwa sauti,

    "dadaaaa.... daaada....

    Binti mrembo bila hiyana akageuka kumuangalia anayemuita,

    Alipokuwa akageuka yule binti Chirs alihisi kizunguzungu miguu akahisi imekufa ganzi akawewesuka,

    Akiwa Katika hali ile alisikia binti akiitikia sauti,

    "abeeeee......

    Chaz hakuwa mbali hali ile aliishuhudia na kusikia sauti ya mtoto wa kike na yeye alipoisikia alihisi kama anapigiwa kinanda masikioni akabaki ameduwaaaa,

    "kaka unasemaje?.....



    Chirs alitoka usingizini japo alikuwa hakulala,

    "dada mimi naitwa chirs nimekuona ukitoka dukani nikasema haitakuwa mbaya kama nikikusaidia kubeba mzigo wako angalau na mimi nikapata pesa ya kula kwa siku ya leo,

    Binti yule aliniangalia vizuri kuanzia chini mpaka juu kisha akaniambia,

    "chirs mbona mzigo wangu siyo mkubwa kivile naweza kuumudu tu bila hata msaada wa mtu,

    "dahh!!!... Basi sawa dada yangu naona siyo riziki yangu hii,

    "alafu kitu kingine kaka yangu mimi gari nimeipaki pale big born kwa sina mwendo mrefu sana kaka yangu,

    "sawa dada yangu nikutakie safari njema,

    "haya na wewe pia,

    Baada ya kuachana naye yule binti mimi niligeuka kuendelea na safari yangu Chaz aliniuliza,

    "vipi chirs kulikoni mbona mnyonge sana kiasi hicho?

    "Aaaahhhhh acha tu ndugu yangu nimeshindwa kutangaza neno langu la moyoni kwa yule matokeo yake nimeongea pumba tu,

    "chirs hebu niambie umeongea nini ili nijue kama umeongea vizuri au umeboronga,

    Chirs kabla hajaongea chochote kumwambia chaz alisikia sauti nyororo ikimuita,

    "chirs..... chirs....... Chirs..,

    Chirs aligeuza shingo upande wa pili wa balabala kuangalia ni nani anayemuita,

    Alipoangalia vizuri hakuamini machoni kwake baada ya kuona yule binti mrembo aliyeachana mda mchache uliopita ndie anayemuita chirs aliitikia kwa sauti kubwa,

    "naaaam dada aaa.....

    "njoo mala moja,

    Chirs alivuka balabala kama kichaa vile kwenda kuitika wito wa yule dada mrembo anaye muita,

    "naaaam dada nimesikia unaniita,

    "Ndio nimekuita, Nilicho kuitia hapa nilitaka nikupe haka kamzigo katakusaidia hata kwa siku ya leo,

    "sawa nitashukuru sana dada yangu,

    Kabla dada yule hajatoa mzigo aliotaka kumpa chirs kuna nyuma ilianza kupiga honi kuashiria ile gari ya yule dada ipishe njia,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "naona nimeziba balabala acha niende chukua mzigo wako huu na hii elf kumi,

    Kutokana na chirs kumzubalia zaidi yule dada mrembo hakusikia alichokuwa ana ambiwa na yule dada mpaka pale yule dada alipopaza sauti kwa kumuita,

    "kaka mbona umezubaa sana?

    " ooohh nisamehe mawazo yalikuwa mbali sana kwa dada yangu,

    "sawa, Chukua kamzigo haka kadogo alafu Chukua na hii elf kumi,

    "asante sana dada yangu mungu akulipe na akuongezee,

    "sawa na wewe pia, kwaheri,

    Dada yule mrembo aliondoa gari kwa sipidi kali sana kuelekea anakojua yeye,

    Baada ya kupewa mfuko ule na pesa sh. 10000 niliruka balabala na kwenda alipokuwa chaz,

    "vipi chirs umepewa nini?

    "nimepewa sh. 10000 na mfuko huu hapa unaouwona,

    "hebu ndani ya mfuko kuna nini?.

    Nilifungua mfuko kuangalia ndani yake kuna nini ila nilipo ufungua Nilibaki nimeduwaa na chaz alipo angalia ndani ya mfuko naye alipigwa na butwaa,

    "chaz ni macho yangu tu ndiyo yanayo ona hiki ninachoona au na wewe ndicho unachoona?

    "hata mimi mwenyewe siamini kile macho yangu inachokiona,



    Chaz na mwenzako waliondoka haraka Eneo lile na kwenda geto kwao kuhakiki kama kile wanacho kiona kwenye mfuko ni kweli ama ni si kweli,

    Baada ya kufika geto cha kwanza alichofanya chirs alifungua mfuko kisha akamwaga vilivyo kuwemo kwenye mfuko juu ya kitanda,

    "Haaa chirs hivi ni kweli ama naota hiki ninacho kiona?

    "mimi mwenyewe siamini hebu funga mlango vizuri mtu asije kuingia hapa gafla,

    Katika mfuko ule kulikuwa na pesa nyingi kama mil. 50 za kitanzania,

    Chirs na chaz walihesabu wameisha toka Ki maisha,

    "chirs sema ukweli tumetokamo Katika shimo la umasikini,

    Chaz alikuwa na furaha iliyopitiliza kifani ila kwa upande wa chirs aliye pewa ule mfuko wa pesa hakuwa na furaha yoyote ile ila alikuwa akiumiza kichwa ni kwanini dada yule amempatia kiasi kikubwa cha pesa?

    Hivi kweli ametoa kwa moyo wa kunipa au atakuwa amechanganya mifuko?

    Chirs alifikilia tukio zima lilivyokuwa akaona yule dada lazima alichanganya mifuko baada ya kuchanganywa na zile honi za gari iliyokuwa nyuma yake,

    "chirs unawaza nini mbona si kuelewi?

    "chaz ndugu yangu nawaza mengi sana kuhusu hizi pesa hakiri yangu inanituma kuwa yule dada hakudhamilia kunipa hizi pesa ila atakuwa amechanganya mifuko tu,

    "kwa hiyo sasa unasemaje hata kama atakuwa amechanganya mifuko?

    "mimi nafikilia kuangalia namna ya kurudisha pesa zake tu,

    "chirs wewe ni mwendawazimu eti? Yaani na umasikini wote huu tulio nao unaongea pumba za namna hiyo?

    "sasa nitakuwa na furaha gani ya kuwa tajiri kwa pesa za dhuruma?

    "dhuruma kwani umemdhurum nani? Hebu kuwa na hakiri chirs hii ni bahati sasa kama unataka kuipoteza fanya upuuzi wako uone tutakufa masikini,

    *** *** ***

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande wa pili ndani ya nyumba moja iliyopo maeneo ya masaki ndani kulikuwa kumetawala vilio,

    "Shemsa kwani hizo pesa umeibiwa kwa stairi kwani?

    "sijaibiwa na hata kama nitakuwa nimeibiwa basi nitakuwa nimeibiwa kimazingara,

    "sasa Shemsa tuliendelea kuliya hivi haitatusaidia chochote hapa kinacho hitajika ni pesa tu ili mradi tupate namna ya kumpeleka mama India kutibiwa,

    "sasa dada unaona tutapata wapi tena pesa mimi hapa nilipo account inasoma sh. Million mbili na laki nane tu,

    'sasa tutafanyaje kupata hizo pesa maana mimi nahisi kuchanganyikiwa,

    *** *** ***

    Katika hospital ya muhimbili mama Shemsa akiwa amelazwa akionekana ni mama mwenye kusikia maumivu makubwa kutokana na maradhi ya uti wa mgongo yanayo msibu licha ya kuteseka kwa maumivu mama huyo ila alikuwa akiteseka tena kwa maneno ya manesi waliokuwa wakimhudumia,

    "hivi wewe mama si una watoto wa kike wewe, iweje wasifanye hata ukahaba ili wakusafilishe ukatibiwe,

    Nesi mwingine akadakia kwa kumsapoti mwenzake,

    "mimi nashangaa watoto wenye wazuri wana figa za pesa sura za mauzo sauti za biashara alafu wanakalia uchumi wao bila hata kuutumia,

    Maneno yale yalimuumiza mama yule kuliko hata maumivu ya maradhi yake ila hakuwa na jinsi kwani hata nguvu ya kujipeleka chooni hakuwa nayo,

    *** *** ***

    Upande wa Mr John aliyekuwa mmiliki wa kampuni ya usafilishaji mizigo kila siku moyo wake ulimtekenya kupata penzi la binti shombe shombe aliyeitwa Shemsa,

    "Siyo siri rafiki yangu moyo wangu kwa yule mtoto mwenye asili ya kiarabu umefeli tena umefeli nikiwa juu ya mlima hata kuuzuwiya nimeshindwa,

    "John pale kwa yule mtoto lazima kila kidume aliyekamilika afunge breki pale, Yule mtoto ni kisu tena kisu chenyewe kina makari pande zote,



    "sasa nitampata vipi maana anamjua kabisa mke wangu,

    "wanawake wa siku hizi hawaangalii cha mume wa mtu wanaangalia pochi tu,

    "wewe sikia nikwambie shemsa ni binti tofauti kabisa na mabinti wengine unaowafahamu shemsa ni binti ambae hana tamaa na vitu vya dunia hadanganyiki kwa pesa wala magari ya kifahari,

    "sasa kama yuko hivyo unazani utamshawishi na nini huyo binti?

    Maana shetani wa mabinti ni pesa na vitu vya dhamani,

    "Kuna mpango ninao ufikilia nazani huo mpango utafaa kama nikiutumia vizuri,

    "ni mpango gani huo?.

    **** **** *****

    Chirs / chaz

    Chaz hakupendezwa kabisa na msimamo wa chirs wa kutaka kuzirudisha zile pesa kwa mwenye nazo,

    "sikiliza chirs sipingani na wewe kuhusu kuzirudisha hizo pesa ila nikuulize kitu kimoja huyo binti utampata vipi? Una namba zake za simu?

    "sina namba zake ula ninawazo la kwenda kumtafta kwa njia ya kupitia pale bank iwe isiwe lazima pale bank kutakuwa na data zake,

    "sawa basi fanya hima kimbiapo kabla hawajafunga,

    "sawa basi acha niende kabla hawajafunga,

    Chirs alichofanya alibadilisha shati na kuvaa shati jingine kisha akachukua mfuko wa pesa ila kabla hajapiga hatua chaz akamuita,

    "chirs sikia hebu acha ushamba unakuwa kama vile mtoto wa kijijini sasa ukienda na hizo pesa unazani ipo siku Utapata fursa ya kumleta tena hapa huyo binti?

    "ila kweli niende mikono mitupu nimwambie pesa ziko nyumbani alafu nije naye hapa,

    "Ndio ukifanya hivyo lazima akifika hapa umueleze hisia zako na pia akiona mazingira yako huenda atakusaidia chochote,

    ***** ***** *****

    Shemsa na dada yake walitoka nyumbani huku vichwa vyao vikiwa vimechanganyikiwa kuhusu zile pesa zilizokuwa zimepotea zaidi mil. 500

    Mtoko wa shemsa na dada yake ulikuwa ni wa kwenda kumuona

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Chirs alikaa kaliakoo kumsubili shemsa afike ila kuna kitu kilicho msumbua sana chirs Katika nafsi yake na kitu hicho hakikuwa kingine bali alifikilia ni namna gani ataanza kumweleza shemsa kuwa anapenda mpaka afikie sehemu shemsa amuelewe?

    *au nimwambie kuwa kama anataka pesa zake basi akubaliane kuwa na mimi kimapenzi?. Mhh ila itakuwa mtihani je kama akikataa alafu kaisha juwa kama mimi ndie mwenye pesa zake si itakuwa taabu kweli?

    Au bora nimpe pesa zake alafu ndipo nimwambie shida yangu yakuwa nampenda, Ila hapana nikimwambia baada ya kumpa pesa atachukulia kwa kuwa nimemsaidia ndio maana namweleza kuwa nampenda,

    Mawazo ya chirs yalikuwa ni mengi sana kuhusu nini afanye ili aweze kufikisha hisia zake kwa mtoto wa kike shemsa,

    Mda wote aliokuwa amesimama hakuna kitu kingine alichofanya zaidi ya kuwa anamuwaza shemsa na kufikilia nini ambacho atamwambia ili mradi ahakikishe shemsa anakuwa Katika himaya yake,

    ***** ***** *****

    Shemsa baada ya kupokea taarifa ya chirs kuwa wakutane ampe pesa zake shemsa aliruka ruka mbele ya mama yake na mpaka mama yake akashangaa,

    "wewe umekuwaje mbona sikuelewi?

    "mama wewe acha tu hapa nina furaha iliyopitiliza siamini kama pesa zangu zimepatikana,

    "pesa gani unazungumzia mbona sikuelewi wewe hebu niweke wazi,

    Shemsa alishituka akabaini kuwa Katika mpango wake na dada yake walipanga mama yao asibaini chochote kuhusu hizo pesa jinsi walivyozipata,

    Mama aliendelea kuuliza kuhusu hizo pesa na gafla uso wa shemsa ukawa mdogo kwani alishindwa ajitetee vipi kwa mama ili asiweze kubaini pesa zile alizitoa wapi?

    "shemsa niambie ukweli pesa gani unazungumzia?

    "mama ni pesa zangu nilizokuwa nazidai kwa mtu sasa ndiye aliyenipigia simu na kuniambia niende nichukue pesa zangu,

    "sikia shemsa mimi siyo mtoto mdogo wa kudanganywa sasa ninachosema ni kwamba sihitaji pesa zenu Katika matibabu yangu niachieni nife niacheni na ninawambia kuwa kuanzia leo sitaki kuwaona hapa kuja hata kunisalimia na nina wambia kuwa kama mkirudi hapa basi nitajiuwa mimi mwenyewe kwa mikono yangu,

    "mama mbona unaongea maneno makari kiasi hicho? Juwa kuwa sisi wawili ndio wanao pekee,

    "Sitaki watoto waliobadilika na kuwa malaya sitaki nimesema sitaki,

    "mama mamaaa nini unasema ni nini hicho sisi wanao unatuita malaya?

    Mama shemsa alijiinua kitandani kwa taabu akampiga kofi shavuni shemsa,

    Dada yake aliingilia kati na kumkanya mama yake,

    "mama nini unafanya unatutukana kwa ajiri ya kukusaidia? Na kutupiga?

    "bora kufa kuliko kuponywa na pesa za haramu nyie wanangu nimewasomesha dini nimewalea Katika maadili ya kidini sasa iweje leo mfanye upuuzi ili kunisaidia mimi?

    "mama wewe muislam safi na unajua kabisa kuwa kuhukumu kitu usichokijua ni dhambi,

    Mama shemsa aliinua mto akatoa karatasi moja nyeupe na nyeusi kisha akawatupia wanaye,

    "Haya ushahidi wa hizo pesa huo hapo na hapo semeni ni nani mnafiki?

    ***** **** ******

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog