Chombezo : Dada Emmy (Muuza Ubuyu)
Sehemu Ya Tatu (3)
Kitendo cha elly kuniuliza kwa hasira kilinishangaza na huku mwanzo tulianza kwa kuongea vizuri tu.
"Mbona unaniuliza kwa hasira hivyo?
" emmy wewe ni mchumba wangu na mke wangu ni lazima nikuulize" alijibu
"Jifunze kumsomà mtu yupo kwenye mood/hali gani ndipo uonyeshe hisia zako sipendi kufokewa elly na unajua hivyo"
Ukimya ulitawala simu ikiwa bado hewani nami sikutaka kujipendekeza nikakaa kimya tu. Wakati huo chakula kilikuwa karibu na kuiva ikabidi niiache simu pembeni na kuweka loudspeker kama hataongea nimjibu. Elly nae ni jeuri mno na nililijua hilo kipndi kile nilipomkosea akakaa muda mrefu bila kunitafuta nami nilipoomba sana msamaha bila kusamehewa niliamua kukaa kimya na shughuli zangu. Wanaume wengi upenda kunyenyekewa na wanawake na kujiona wao ni superior(bora) nasisi kutuchukulia km inferior(dhaifu) mimi sijawahi kuwa muumini wa dini hiyo mara zote napenda mwanaume hajue msimamo wangu kama tutawexana sawa km hatoweza ni sawa pia.
********************
Nilikaa mezani nikawa nasoma zangu geography maana nilichukua mchepuo wa HGL kwani tokea mwanzo niliyapenda sana masomo haya matatu na kuyafanya vizuri mno. Topic ya map(pratical geography) ni topic pekee ambayo mimi uipitia sana na ile ya physical geography. Nilishangaa kuona mlango unagongwa nilishtuka mno maana ilishafika saa nne na kule kwetu kijichi mida hiyo kunakuwa kimya mno ikabidi nifikirie mara mbili. Nikafungua mlango nikatoka mpaka getini nikauliza 'nani mwenzangu?
"Funguaa' ilisikika sauti ya elibariki.
" mmmh haya"
Niliguna kilichomfanya aje usiku ule nikahisi uenda alidhani sipo nyumbani au niko na mwanaume maana hana wivu yani anawexa kukunusa hata jasho haone umekumbatiwa huko utokapo au kwa namna yeyote ile. Akunisalimia akapita ndani mimi nikafunga geti kabla sijamalizia akaniita "weee usifunge geti fungua natoka muda si mrefu"
"Elly unaenda wapu usiku huu?
" we niambie gari yako ina mafuta?
"Elly jmn ndio unaenda wapi unajua sikuelewi"
"Emmy unaniumiza sana"
Aliongea hivyo akiwa anaingia ndani ya gari nilimshangaa nje kaasha gari yake anaondoka na yangu niliweza kumuona jinsi gani kavulugwa maana sikioni alikuwa anatoa maji kweny vile vitundu nilitetemeka kwani nilihisi mengi hasa hili la sam nikajua uwenda amelifahamu au kalisikia mahali.
"Bae niingize gari ndani?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
'Nakuja" alijibu na kuondoka.
Niliingia ndani ya gari yake ili niipaki ndani. Nilifanya hivyo kisha nikarudishia geti, nilirudi tena ndani ya gari nikawasha taa na kuanza kuchukuza kwenye dashbody nikafanikiwa kuona kijitabu kidogo km kinote book nikakichukua na kukifungua kurasa zake niliona majina ya watu wengi na namba zao za simu hadi salma niliiona namba yake na kikubwa nilifanikiwa kuipata line ya tigi ambayo ni private number nikaichukua wakati huo naendelea kuperuzi kweny kinote book nikaona jina limeandikwa sammy nilishtuka nikainote down ile namba, mbele kidgo nikaona jina limeandikwa mpango mzima nikalinote pia down.
***************"
Nilimuonea huruma elly na kumsihi aache kunywa vile pombekali ila hakunielewa aliendelea kunywa mpk akazima. Nilipata shida kumnyanyua kutokana na kuwa heavy weight(uzito mkubwa) ila nilifanikiwa kumfikisha kitandani kisha nikarudi sebureni kwenye simu yake nikaitazama nione mtu wake wa mwisho kuwasiliana nae alikuwa ni nani? Nilikuta ujumbe kutoka kwa sammy "bro tumejitahidi kumtafuta lakini hatujanikiwa" hapo tu nilianza kupata akili inawezekana huyu sammy ni mhusika katika kumteka nyara sam.
Haikuishia hapo nikaangalia ujumbe wa pili alikuwa ni salma japo alisaviwa sally ila namb yake naijua kichwani "please samahani elly kama umekasirika but nielewe nakupenda nimeshindwa kujizuia" niliumia moyoni hamna mfano kumbe salma anamtongoza elly roho iliniuma na hapo nikakumbuka tulivyokuwa marafiki wa karibu ananifanyia hivi niliona jumbe zake tatu ambazo elly hakuzijibu japo aliziona. Nikafungua sehemu nyingine nikaona jumbe moja ambayo alituma yeye elly kwa mtu ambaye namba zake azikuwa zimekuwa saved "sitaki kusikia huo ujinga anawezaje kutoroka na hapo upo wewe, sammy na julio kweli sitawaelewa" ujumbe huo ulitumwa saa 22:44 usiku ina maana ni muda mfupi tu alipokuwa ametoka kuelekea road kutafuta pombe zake ilibidi ninote ile namba pia kwa jina la unknown guy.
**********************"
Ilitimu saa kumi na moja kasoro bado nilikuwa macho nafikiria mengi sana juu ya sam na ukweli ambao elly anaujua na huyu kahaba ambye ananizunguka na kuact kuwa ni rafiki kumbe mshenzi anayetamani emy aanguke hata leo anipokonye mume. Niliamua kuwa endapo elibariki ataamka asubuhi nimwambie ukweli juu ya sam ila roho inasita maana atajua nimejua siri zake kupitia simu yake na hata ile line ya private number asipoiona atashuku bado nitakuwa sijasave tatizo. Sijui nililala saa ngapi ila nilijikuta nipo kwenye ndoto za hatarimno.
Siku hiyo elly alinichukua na kunipeleka tour moja ndefu ambapo ilikuwa ni ya kutembelea moja kati ya mbuga za wanyama nchini it was just fun journey(ilikuwa ni safari yenye furaha sana) nilipenda sana na haya yote elly alifanya ili tu kuufanya ubongo wangu na akili yangu usimfikirie mwanaume mwingine ila niyeye tu, tulifika mpaka kwenye hotel moja ya kifahari ambayo ufikia watalii ambao asilimia 70% ni outsiders(watalii kutoka nje). Tulispend pale siku ya kwanza ilikatika, sikuya pili yake tulitoka na kwenda umbali mrefu kutoka pale ilipo hotel au mbuga, ilikuwa karibu na waterfall(mteremko wa maji) mbele yetu kulikuwa na mwanaume aliyetupa mgongo akitazama upande ambao maji yanamwagika.
Tulimsogelea mpaka pale elly alipomuita "saaaam" nilishtuka lilipotajwa hilo jina kugeuka alikuwa sam niliyekuwa namuwaza mimi na kumfikiria kwa kipnd kirefu mno "the game is over" sam alijibu hapohapo nilisukumwa kwenye lile bonde kubwa la maji.
"Nooooooooooooo" nilipiga kelele palepale nilianguka kutoka kwenye sofa mpaka kwenye carpert. Nilikaa kwanza nikafikisha macho nikatazama picha yangu ukutani nikiwa nipo na elly nakumbuka siku nilipopiga nae ilikuwa beach moja kigamboni ina sunrise, si ngeni machoni kwangu ila tu ilibadili mwelekeo wa fikra zangu.
"Mmh hii ndoto ina maana gani mungu wangu" nilijiuliza maswali kimoyomoyo "mmh inaonyesha nisipokuwa makini ninaweza kuwapoteza wote wawili kwanini nisiseme ukweli tu" niliendelea kujiuliza maswali moyoni..
Nilikumbuka elly amelala ndani na muda si mrefu ataamka kwenda kwa job hivyo ilibidi niamke kumchemshea maji ya chai na kumkaangia angalau mayai pindi atakapoamka apate kifungua kinywa kabla ajaondoka kwa muda ule nilikuwa nimewahi sana(saa 12) ila nalikuwa nahitaji angalau nikasome maana siku mbili hizi sikufanikiwa kufika kabisa darasani.
Nilifanya kila kitu mpk mambo yalipokaa sawa niliingia chumbani nimuamshe elly akaoge tuondoke mapema.
Nilishangaa ambapo sikumkuta mtu nikajiuliza " huyu ameenda wapi na jana alilewa" nilipata wasiwasi nikatoka nje ya nyumba gari yake haikuwepo ikiashiria ameondoka nilirahumu mno kuwa mbali naye ila uzuri nina zile namba, sasa tatizo nitapata wapi mtaalamu wa kuongea kiswahili kama cha kichagga kama elibariki ili nitumie kuongea na wale watu ambao tayari niliikuwa na namba zao. "Nitapata akili nikishafika shule" nilijiandaa nikanywa chai na selesi moja tu nikavaa vizuri nakumbuka siku hiyo nilivaa skin jeans, simple nyeupe, blauzi nyeupe kiujumla nilipendeza kama nilivyojiona kwenye kioo kwani siku zote hakidanganyi.
Sikutumia muda mrefu kudrive maana kutoka kijichi mpaka kurasini nilitumia dakika 20 tofauti nikiwa peke yangu. Nilimtafuta mtu wa kuongea lafudhi ya kichagga ila nimalize utata kwangu na nijue kilichotokea uko nyuma.
*************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda mrefu ulikatika sikumuona elly kibaya aliondoka bila hata kuaga ila nakumbuka moja kati wale watu watatu aliniambia ukweli juu ya sam story ilikuwa hivi:
Kuna dada anaitwa salima alinipiga simu siku hiyo nilikuwa nipo na elibariki, tulikutana kama bahati nilikuwa naingia kwenye ukumbi wa ddc keko ndipo nilikutana na elobariki. Tuliongea mawili matatu ndipo alipopata simu kutoka kwa mdada salma alitoa maelezo mengi ila alionysha ni mtu mwenye kutaka kitu kwani alipomaliza ya moyoni akasema "please usijisahau" niliacha nafasi ya yeye elly anisumulia kama angehisi kufanya hivyo.
Wakati huo ndipo tulimkamata kijana huyo sam ambaye alichukiwa sana na elibariki kitendo kile kilisaidiwa na yule dada salma ambye alikuwa ni mtu pekee tuliyekuja naye.
"Mmh mlipitaje mlangoni" ilibidi niulize swali(emmy)
"Kuna mtu anaitwa Romney ni mtaalam wa it ndiye alitusaidia tukaja pale hotelini tukiwa na dawa za kupoteza fahamu ili tumchukue sam"
"Ina maana gani kufanya hayo yote na faida yake?
Emmy akauliza tena.
" ni mambi ya bosi wetu na wivu juu yako emmy"
"Sam yupo wapi sasa?"
Baada ya muda mrefu kupita nakumbuka kipindi flani nilipanga njama ya kumtorosha sam kuelekea handeni tanga kisha halale pale siku moja aende mombasa kenya kwa mama mkubwa wangu ili kujikinga mauaji maana elibariki alipanga kumuua na kumzika porini kuua ushahidi yani hapa nilipo cna maelewano na elly na wale wengine pia wanahesabika kama walimtorosha sam.
*************"
Niliumia roho ila sikukata tamaa baada ya kuongea na yule mkaka na kuniahakikishia sam yupo na namba zake pia anazo naweza kuwasilian naye. Huo ndio kama ulikuwa mwisho wa kuongea na yule kaka nilikuwa nilikuwa nipo temeke nakumbuka baada ya kurudi kuja kumuona mamdogo aliyekuwa mgonjwa muda huo nilitumia muda mwingi kuchat nilipita kichochoro kimoja nilikuwa naelekea dukani ghafla nilisikia naitwa pale pale niligeuza shingo nilikutana kitu kama flapeni usoni.....
Nilisikia maumivu makali usoni baada ya ile flampeni kutua usoni kwangu niliita sauti ya juu kisha nikapoteza fahamu palepale.
*****************
TURUDI KWA EMMY NA CINDY.
(Mpenzi msomaji napenda kukumbusha kuwa simulizi yote unayosoma huko nyuma ni hadithi ya emmy kwa rafiki yake cindy)..
"Mungu wangu!" Cindy alionyesha kushtuka kutokana na kusikia hivyo.
"Basi nikajikuta nipo hospitali ila nikiwa na maumivu makali sehemu za paji la uso"
"Enhee emmy story yako inavutia sana natamani kujua ilikuwaje?
Kabla hawajaendelea na simulizi emmy alinyanyuka akaenda kwenye friji akachukua juice na glass mbili ambazo aliweka juice na kurudi tena sebureni.
" enheee endelea na story" cindy alionysha kuwa na shahuku kubwa na ile simulizi.
"Shoga unapenda ubuyu wewe" aliongea emmy.
"Hahaaa sio hivyo nataka nijifunze mengi kutoka kwako" aliongea cindy.
"Aya mwaya kunywa na juice basi tuendelea leo si wikiend tutaongea mpk uchoke wewe"
************
Nilirejea nyumbani baada ya kupata nafuu, cha kushangaza sikuwahi kumjua aliyenifanyia lile tukio, angekuwa kibaka simu yangu na pesa zangu angechukua lakini haikuwa hivyo, nakumbuka siku hiyo ni salma ndiye aliyenifata hospitali na kunisaidia.
"Mamie tunapanda daladala au" aliuliza salma.
"Nooo tukodi bajaj mamie" niliketi pembeni yeye akatoka mbali kidogo kuulizia dereva bajaj kama tungeweza kupata usafiri, kusema ule ukweli sikuwa na imani hata punje ya kumuamini huyo salma sema nilijikaza tu kuongea nae ila ni mtu niliyemtoa moyoni kabisa hasa nikikumbuka yale matukio ya nyuma kitendo cha kuwa na mawasiliano na bwana wangu elibariki na kuunda njama ya sam kukamatwa hiyo tu iliniogopesha na niliamini ipo siku ataniua kabisa " na nina wasiwasi atakuwa ni yeye kanipiga na flampeni usoni, kweli mfadhili mbuzi" nilikatishwa mawazo yangu baada ya bajaj kuja mpk pale nilipokuwa.
*************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku zilikatika tukiendelea na ukaribu na salma kiasi kwamba wasiwasi juu yake ulianza kupotea, kuna wakati nilimuona kama mtu aiyetumwa kwa mpango flani na inawezekana ni kuniua hivyo sikutaka kabisa nimpe nafasi mno lakini yeye alikuwa akimbiliki kama kalio na chupi yani.
Taratibu nilianza kujenga imani nae kwani alinieleza mambo yake na matarajio yake kimaisha, nilikumbuka tulipotoka toka miaka3 tumekuwa wote mpaka leo hii 19/20 tumedum ya kupewa taarifa kuwa atakuwa huko kwa auty yake yule aliyenisimulia ile simulizi ,,,††††
Siku zilizidi kusonga nikiwa ni mtu mpole sana na nakumbuka kuna siku nikikawakumbuka wale watu wa kule hotel ambayo waliniahidi kuwa nami kwa kila hatua ni mimi ndye niliwasahau kwa kipindi hiki ila nilipanga ratiba ya kuonana nao kesho yake.
Ilipotimu asubuhu nikijiandaa na kumjulisha jimmy na william kuwa nitapita pale, ila nilipanga kukutana na mtu mwingine pia ila kibiashara zaidi maana biashara yangi ilinipa umaarufu wa haraka na kunifungulia wigo mpana ktk ufanisi wa kazi pia.
*****
"Emmy wewe una pass ya kusafiria? Aliuliza jimmy baada ya kuanza kikao
" hapana sina" nilijibu kwa kutingisha kichwa kabla ya kutoa sauti.
"Unajua elibariki anafanya biashara gani?aliuliza willy
," ndio anauza maduka na pia ana saluni zake" nilijibu kwa kujiamini.
"Sawa kuna mambo bado tunapeleleza tutakupa ripoti ya siku hizi mbili, sawa dada" alihoji willy
"Sawa nashukuru".
Nilitoka nikiwa mnyonge kwani nilitegmea mengi kutoka kwa wale jamaa ila ckukata tamaa ile safari yangu ya kwenda kenya bado nilikuwa naiandaa kwani kilichokuwa kinakwama ni anuania za sehemu niendako na yule jamaa anayedai/aliyesema sam yupo pia hakupatikana hewani. Nilijitupa kitandani nikiwaxa mengi ila nilishangaa willy akinipigia nikapokea haraka sana kwani nilijua kutakuwa na mpya.
" ndio emmy" ilisikika sauti
"Nakusikiliza kaka nipe ripoti"
.
"Sam unajua yupo wapi? Aliuliza swali kama la kuamsha hisia..
" willy kama unajua ukweli niambie sio unazunguka" nilikuwa mkali kidogo
"Sam yupi mombasa ni mwalimu shule ya awali huko" aliongea na kunishtua mno sikutegemea.
"Ila kama upo na elibariki sio mtu mzuri achana naye" aliongea zaid willy
"elibariki achana nae sio mtu mzuri" aliongea william
"Kwanini unasema hivyo?
" elibariki ni jambazi na kibaya zaidi anauza madawa ya kulevya anaweza kukuingiza matatizoni"
Nilibaki nimeduwaa nikashindwa kuzungumza chochote nilijisikia ganzi ya ghafla. Sauti ya william iliendelea kusikika ikiita kwenye simu baada ya kuona ukimya ukiendelea "eemmy emmy mbona kimya emmy" aliita karibu na kukata simu nikazungumza nae.
"Wewe umejuaje willy?
" ulinipa kazi ya kufatilia hiyo ndio ripoti ninayokupa"
"Sasa unanishauri nifanyaje?
" aaha hayo mapenzi siwezi kukushauri direct fanya hivi ila wewe utajua ufanyaje. Alijibu willy ila kichwani nilitengeneza taswira nyingi uwenda huyu ananiambia hivi atakuwa ananitaka kimahusiano kwahiyo kuja direct anashindwa au ni kweli ili jambo lipo na ndio maana mara nyingi elibariki akisafiri huwa hatoi taarifa na ndio miezi iliyopita alienda uko south kisha akanitumia tshs milioni kumi na gari ya spacio new modern hiyo tu inazidi kunipa maswali.
************************
Kadri siku zilivyozidi kwenda nilikuwa na ukaribu mkubwa na willy na salma. Mara nyingi willy alikuwa ananisaidia kimawazo na kunipa campaign mara zote nikitoka out kwasababu nilikuwa mpweke kwani sam hakuwepo na elibariki ameondoka sasa ni miezi miwili sina taarifa naye japo kuwa sio mara ya kwanza kufanya hivi amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara.
"Emmy nimekuletea zawadi nzuriii sijui kama utaipenda? Aliongea kwa tabasamu willy.
" wow! Nitaependa tu" nilikuwa na shahuku ya kujua ni nini hicho.
"Fumba macho kwa dakika mbili tu mpaka nitakapo kwambia fungua macho" aliongea willy huku akinyanyuka.
"Haya usichelewe ukizidisha dakika mbili nafungua" niliongea kwa utani uku nikifumba macho kama alivyosema.
Nilisikia movements/hatua za miguu japo sikupata fursa ya kuona ni nini kinachoendelea. Ilikuwa ndani ya dakika mbili kuekekea ya tatu ndipo akaniambia.
"Aya fungua macho supriseeeeee"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wow! Willy jamani what does it mean(kinamaanisha nini?)
" mimi kama mtu wako wa karibu nina haki ya kukufanyia hivi happy birthday to you" aliongea kwa bashasha kisha akanihug
"Willy am so excited(willy nimepatwa na msisimko) umejuaje my bday?
" mimi ni mtu wa karibu sana na wewe kujua tarehe ya kuzaliwa its a little thing sana(jambo dgo) niambie umeipenda?
"Saaana willy umenifanyia kitu kikubwa sana nashukuri mnoo"
Mbele yangu kulikuwa na keki kubwa ya ngazi mbili, gauni la pink lenye silver pembeni na saa ya silver, cheni ya silver na viatu pia rangi ya silver, aliniambia ameagiza kutoka france na kweli ukiangalia ni expensive alifanya kitu cha kipekee ambacho akuna aliyewahi kunifanyia.
"So what next/nini kinafata? Aliuliza jimmy.
" let us celebrate/tusherekehe"
"No no no invitee your family members, friends, classmates with you are neighbours am ready to prepare a bday party for you at any place(halika ndugu zako, marafiki, wanafunzi wenzako na majirani nipo tayari kukuandalia pati sehemu yeyote ile)
Aliongea willy kwa bashasha kubwa na kuonyesha kuwa ana pesa.
" willy we are too late ni mchana sasa hii tungeambia mapema" nilijitetea.
"Nooo waambie watakaokuja sawa nami nina friends nitawainvite pia" alijibu willy.
"Sawa jimmy asikose" nilisisitiza uwepo wa jimmy.
"Jimmy is around tuifanyie sinza hall na chakula na vinywaji nimeshaandaa sehemu tu ndo nilisubiri uamue ww" alizidi kunishangaza willy huyu.
"Jamani ulivyopanga ni hivyohivyo me sina cha kupinga"
***************
Kutimia saa mbili usiku nilipata fursa ya kutumiwa picha na rafiki yangu clere nasoma nae pia advance, ukumbi ulipendeza kwa harakaharaka ule ukumbi tu sio chini ya laki tatu, ujaweka wapambaji sio chini ya laki moja na nusu, bado vyakula inacost pia laki nnee au tatu na vinywaji kama laki mbili hivi. Ni jinsi gani willy alikuwa na pesa ya mchezo tu na ameweka historia maishani mwangu kwani sikuwahi kufanya sherehe ya kuzaliwa ukumbini zaidi ya vikeki kuliwa home tu basi.
Saa mbili na nusu niliingia ukumbini nikivaa yale mavazu aliyoninunulia aiseee nilikuwa kama queen kila mtu alishangaa maana pale tu nilivaa U$ 10000 full ni kiasi kikubwa sana kwa mavazi tu ila willy alifanya nathubutu kusema huyu jamaa anajua kucare.
Sikuamini kuona idadi ya watu vile nilikisia inaweza kuwa chini ya 20 au ikizidi 30 mwisho ila walikuwa watu karibia 80 au kuzidi sawa nilituma jumbe na kupiga simu ila salma nahisi alisaidia mno, maana wanasema sherehe ni watu.
Ulipofika muda wa zawadi nilitamani nipae tu maana nilipata zawadi hivyo vitenge, batiki, cheni, nguo za ndani na vinguo vya nje nilipata kwa wingi mwisho alikuja jimmy akiwa kabeba boksi kubwa kisha akalifungua na kuanza kunimwagia mtandio, saa, cheni mwisho akatoa simu ya iphone7 nilitamani kulia maana sikuwahi kufikiria kumiliki simu kama ile nilimkumbatia kwa muda mrefu kitu ambacho kilimfanya willy apate kawivu maana alinitazama alipotoka jimmy akaja yeye.
Nikawa nawaza atakuja na zawadi gani kushinda ya jimmy alipofika alicheza muziki kabla ya mziki kuzima.
"Mimi sina mengiiiii nasema hivi zawadi yangu hakuna atakayeifikia kama yupo aje hapa mbele tushindane" aliongea kwa jeuri ila kichwani tayari alikunywa pombe.
Nilimuona jimmy akija pale naye alikuwa kalewa hivyohivyo kikawa ni kituko marafiki hawa wawili walipokuwa wanabishana pale.
"Lipa kwanza zawadi zangu" alijidai jimmy.
"Hahaaaa jimy jimmy zawadi yenyewe iphone 7 mimi nampa gari zawadi yangu leo gari mama una gari aina gani?
Aliniuliza mimi willy
" natumia spacio new modern" nilijibu.
"Mimi nakupa harrier yangu ile kwanzia leo yako, kaka wewe unatoa nini kingine? Aliendelea na kiburi chake.
" aaaha kaka mimi nitapa chemba"
******************
BAADA YA SIKU MBILI.
Niliamkia shule ila asubuhi asubuhi willy alinipigia simu ya kunijulia hali maana muda huo ndio alikuwa anaingia kaxini
"Hiyo gari nitamtuma dereva akuletee vibali vyote tutaenda kubadilisha tra sawa?
* sawa kaxi njema"
"Nawe masomo mema usome sana etii" aliongeza willy
Nilinyanyuka kitandani nikiwaza huko shule itakuwaje maana hiyo jumamosi ilikuwa kufuru, ila sikujari sana wakati nipo kweny gari najaribu kuangalia maji ili nitoke nilisikia simu yangu inaita, niliacha ile kazi ili kusikiliza simu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/"Hey hallo nani? Niliuliza baada ya kuona namba ngeni
" mimi jimmy ni namba yangu ya airtel hii upo wapi emmy?
Aliuliza jimmy baada ya kujitambulisha
"Nipo home naelekea shule"
"Ukitoka shule uje kuna duka la nguo hapa nataka uje uangalie litakufaa nikupe liwe lako" aliongea kama utani
"Duka la nguo la nani?
" ni langu ila nataka nikupe wewe lipo sinza vartikani"
"Jamaniiiiiii kwanini unafanya hivi?
Niliuliza huku machozi yananilenga
" emmy mimi sipendi uongo nakupenda na nataka nikuoe naomba usikatae, mama mdogo yupo wapi?
Aliuliza
"Yupo anaishi temeke mikoroshini"
"Jamani mama akiyekulea anaishi huko mikoroshini na wewe unatembelea magari ya kifahari nyumba nzuri sio vizuri, mimi nataka nikupe nyumba uishi na mama"
Nilanguka palepale nikapoteza fahamu.
Salma alikuwa mtu wa kwanza kunikuta nikiwa chini nje ya gari yangu, alininyanyua akanifuta vumbi na kunitazama macho(kunyanyua kope) mithili ya daktari anampima mgonjwa mwenye malaria.
"Upo sawa? Aliniuliza salma
" yeah nipo sawa saa ngapi? Nilijibu swali kwa swali.
" nimejaribu kukupigia simu ipo hewani lakini uongei zaidi ya sauti ya redio(ndani ya gari)"
"Dah we acha tu simu yangu ni auto inajipokea muda mwingine ila tuyaache hayo unaelekea wapi now?
"Ninaenda karikoo kupeleka mzigo nilikuwa nataka nikuulize kwa mama suma supermarket nipeleke mzigo pia ndo naona uongei nikajua kuna tatizo"
"Ndio hivyo wangu nimepatwa na kizunguzungu cha ghafla nikaanguka nahisi ni uchovu maana nina siku ya tatu sijalala vizuri kama jana unaona tulikuwa na birthday party"
**********************
Mimi pale kituoni nilikuwa ni mwanafunzi wa kipekee sana hali iliyonifanya sio kuheshimika tu hata kupendwa na wengi licha ya kipato changu nilikuwa ni mtu wa kawaida sana, na hii yote imetokana na maisha niliyopitia huko nyuma, si walimu hadi wanafunzi wenzangu walikuwa wananipenda. Siku hiyo tulikuwa na presentation/kuwasilisha juu ya topic ya history2 "the emergence of USA as new capitalist super power" sisi tulichukua vipengele za mwanzo yani introduction/utangulizi wa mada, factors for rise of eropean capitalism and factors for demise/sababu za kukua kwa ubepari ulaya na kushindwa kwa ubepari kisha tukamalizia na factors for rise of USA as capitalist superpower.
Kundi langu lilikuwa ni kundi A ndio watu wa mwanzi kabisa, nilikuwa mimi, james, junior, sophia na ziada. Mimi nilijichagua kufanya introduction na kumaliza pia.
"Good aftrnoon class(za mchana darasa)" nilianza kwa kusalimia
"Afternoooooon emmy" waliitikia kwa nguvu kweli.
" infront of you am a leader of group A, we're going to discuss briefly about our main topic, are you ready?/mbele yenu ni kiongozi wa kundi A, tutaenda kuelezea kwa kifupi juu ya mada yetu kuu, mpo tayari? Niliuliza hivyo kwasababu kabla ujaelezea jambo lolote ni lazima ujui je watu unaongea nao wana usikivu juu ya unachotaka kuzungumza na kama jibu ni hapana kwa kufanya hivi unaweka tention yao ili kukusikiliza na ndio maana kwenye hadithi utasikia wanatumia maneno kama hadithi! Hadithi!, hapo lazima unategemea respond/majibu
"Yessssssss" walijibu wote.
"Initially USA was a British colony which got her independence in 4 july 1776 after 7 years battle/war with the British troops(kifupi USA lilikuwa ni koloni la mwingereza waliojipatia uhuru mwaka 4julai 1776 baada ya vita vya miaka saba7 dhidi ya jeshi la mwingereza) the USA regarded of 13states that got independence from great British and political joined to form US of america in 1787 who agricultural with industrial development in the north south after the american civil wars of 1861/65 usa entered the era of industrial development that enable them to compite with british in 20th Century (Us ilikuwa na Nchi 13 ambazo zilipata uhuru kutoka kwa mwingereza na baadae ziliungana na kuunda USA mnamo mwaka 1787 ambao walikuwa ni wakulima na wenye viwanda hii baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya wakulima na wamiliki wa viwanda mwaka 1861/65 baada ya kuisha kwa vita hivyo USA iliweza kuingia katika maendeleo ya viwanda na kuiwezesha kushindana na mwingereza kwanzia karne ya 20" nilipomaliza utangulizi niliona wanafunzi wakinipigia makofi
"Hongera emmy kweli unasoma, haya wengine" alinipongeza mwalimu na hii yote hakufundisha ila mimi tu nilipenda kutumia vitabu mblimbali kuandaa notes.
Baada ya mwalimu kutoka darasani wanafunzi wengi walinifata kuomba notes zangu wakaandike hivyo mmoja aliona vyema atumie ubaoni kuandika notes baada ya mwalimu kuzipitisha.
*************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikuwa mkimya mno nikisoma simulizi za mejah the plan boy ambaye mara nyingi uandika ktk page yake ya dimbwi la simulizi, kila mara zote anazotoa mwendelezo nimekuwa nikifatilia maana napenda sana fasihi maana ndicho kitu ninachosoma na uwependa kukosoa baadhi ya waandishi ambao hawafati kanuni za kiuandishi na wasiopenda kubadilika. Wakati namalizia kusoma simulizi ya " utamu wa mchezo" nilisikia simu yangu nyingine inaita ya line ya halotel. Nilikimbia fasta kuipokea sikufanikiwa kuigundua ni namba ya nani maana ilikuja bila jina.
"Emmy upo wapi? Ilisikika sauti nzito
" nipo nyumbani wewe nani?
Niliuliza kwa uoga kidogo
"Mimi ni rafiki yako, napenda uniite rafiki" aliongea yule mtu
"Sikujui wewe rafiki umenifahamu wapi?
" hahaaa emmy muuza ubuyu nakufahamu napenda kukwambia kitu emmy" iliongea ile sauti na kuendelea kunitisha
" kitu gani?
" emmy una mkono wa pesa, nyota yako inang'aa na usidhani wanaume wanakutaka bure kuna kitu wanapata kutoka kwako"
Alizidi kunitisha
"Wewe mbona sikuelewi"
" unaweza usinielewe leo ila kesho utanielewa ila kuwa makini kwani huyo elly amefanikiwa mambo mengi kupitia wewe hivyo nyota yako kali sana emmy"
Nilibaki mdomo wazi na kuanza kujiuliza kuna ukweli gani juu ya anayoongea yule kaka rafiki. Nilipoita sikuweza kupata mwitikio kwani simu ilikuwa imekatwa tayari.
Nilijiuliza maswali mengi sana baada ya simu kukatika yule kaka rafiki ni nani? Ila sikupata majibu niliendelea kuwa mpole nikarudi mezani taratibu nikashika simu yangu kubwa ikabidi nizime data maana hapo awali nilikuwa nasoma simulizi za mejah the plan maker.
"Mungu wangu leo tarehe 20 siku zinazidi kwenda karibia nifanye mtihani wangu wa kumaliza kidato cha sita eeh mungu wewe ndiye unajua maisha yangu natamani siku moja nifike chuo kikuu udsm"
Nilikuwa na determinations/matarajio makubwa hasa mbele yangu ni ili la kufika chuo akili na mawazo yangu yalikuwa uko tu. Nilitazama ratiba yangu nilikuwa natakiwa nisome geography, akilini mwangu nilitaka nisome geography2 maswali ila nilitazama mzigo niliokuwa nao geography 01 nikazuta begi langu nikatoa kitabu kilichoandikwa na zisti kamili cha physical geography nikaanza kusoma theories za structure of the earth nilianza na isostancy theory, kisha plate tectonic theory nikajihisi usingizi mzito nikaegemea kwenye kiti nikapitiwa na usingizi, ilikuwa michale ya saa7 usiku.
***************
05:43
Nilishtuka kutoka usingizi ndipo nilipogundua kumbe nilala palepale nikanyanyuka huku nikihisi mgongo unaniuma sana, ingekuwa siku za kawaida ningeenda kulala lakini mitihani inakaribia sikuweza kulala kabisa niliingia bafuni nikawasha maji ya uvuguvugu nikaoga ili mwili upate nguvu kisha nikarejea tena mezani kwaajiri ya kuendelea na ratiba yangu.
Ile asubuhi nilipitia topics za pratical geography hasa map na statistics nilihisi sehemu hiyo ndiyo nilikuwa na mapungufu mno, sikupenda kupoteza muda wangu kuwaza mengine ilibidi nizime simu kisha nisome intensive/kiundani maana kama nikiacha simu on atakurupuka jimmy atapiga au willy na sasa huyu aliyenipigia jana anayenipa stress kumfikiria ni nani/kaka rafiki nae ameongezeka hivyo nikikaa kuwafatisha sitafika mbali au malengo yangu ya kufika university of dar-es-salaam hayatatimia.
Nilisoma sana na niliona raha bado ya kusoma maana kuna raha ukisoma kitu alafu ukakielewa, ilifika saa moja kasorobo nikatoka mezani kisha nikaosha vyombo vyangu na kuanza kufanya usafi nyumba nzima kabla sitoa mapazia na vitambaa kwa ajiri ya kufua. Haikuwa kazi rahisi niliitaji yamkini kupata dada wa kazi lakin naye atafanya nini pale ndani na uku kazi nilihisi naweza kuzimudu mimi mwenyewe. Wakati nafanya usafi nilikumbuka kitu kilichonifanya nikae na kutafakari "hivi mimi nina maadui wengi sana? Ni nani anayeniandama hivi kila siku yanaibuka mapya nina nini mimi? Uenda anachosema kaka rafiki kweli inawezekana nina nyota kali maana sio rahisi wanaume waning'ang'anie mimi tu haya jimmy, willy na elibariki kuna kitu hapa" nilimaliza kuwaza kisha nikasimama na kuendelea na mengine.
**********************
Nilifika eneo ambalo jimmy aliniomba nifike japo nilitoa udhuru nyingi ila alinisihi hata kwa dakika kumi tu kisha nitaendelea na ratiba yangu nilikuwa suprised/shangazwa baada ya kuona duka zuri la nguo za watoto/baby shop za kila aina ambapo pia waliuza sabuni, maziwa ya lactose, pampers na kila kinachoitajika kwa watoto kwanzia mwezi mmoja mpaka miaka 7, kila aliyeniona alishangaa sikuweza kujua kwa haraka haraka wanashangaa nini ila inaonekana ujio wangu ulikuwa tayari umeshajulikana.
Baada ya kuzunguka duka zima jimmy alianza kunieleza baadhi ya mambi kuhusu kazini kwake.
"Unajua emmy wewe ni mwanamke wa ndoto za wanaume wengi, ufanani na mazingira uliyokulia kusema ukweli toka ile siku ya kwanza nilipokuona tukishughulikia suala lako lile(kesi ya sam) nilitokea kuvutiwa na wewe nikamwambia willy naye pia alionyesha kukubaliana nalo ila kumbe naye moyoni anakupenda sikujua, akaamua kuniwahi ila kwangu sikukata tamaa nimeamua kukuonyesha ni jinsi gani nakupenda nakupa duka hili liwe lako bby"
"Wow! Nashukuru kwa kuwa muwazi hata willy pamoja
na kufanya yote aliyofanya hakuwahi nitamkia kuwa ananipenda nakushangaa wewe kwa ujasiri wako" niliongea kwa ujasiri huku namtazama usoni nilimuona akitabasamu.
"Naomba nikubalie emmy"
"Usijari ila kusema ukweli mimi nina mtu ninayempenda yule sam niliyewahi kuwaambia hivyo nisingetamani anione msaliti na hapo badonatoka na elibariki kimakosa sitamtendea haki sam na elibariki eti kisa hawapo na pia utu wangu nitaonekana kama najiuza tu"
Niliongea huku machozi yananilenga.
"Hapana emmy hii itakuwa ni siri kati yetu hakuna atakayejua"
Alibisisitiza sana huku aking'ang'ania mkono wangu
"Hapana jimmy wakina emmy wapo wengu unawexa mpata mtu mwenye sifa kama zangu cha msingi usiwe na haraka ili kumpata"
Niliongea kabla sijaingia ndani ya gari yangu tayari kuondoka
"Pleaseee emmy nakusihi"
Sikutaka kumpa tena second chance nikaondoka
Akili na moyo vikawa vinashindana moyo unasema "chukua duka na alikuahidi nyumba ya kuishi na mama yako mdogo kubali" na akili inaniambia "no kumbuka wema wa elibariki usimsahau sam mtu unayempenda kwa dhati hayo ni yakupita hata kwa nguvu zako utapata siku moja" niliendasha gari nikiwa na migogoro nafsia ni lipi nifanye lipi niache. Mara nikasikia simu yangu inaita ilikuwa kwenye handbeg, moja kwa moja nilijua ni jimmy sikupokea ikaita mara ya pili nikiwa kwenye jam nikapokea ilikuwa namba ngeni.
"Nani mwenzangu"
"Rafiki yako, naitwa kaka rafiki"
"Eeh jamani wewe unanitakia nini lakini"
Niliongea huku nalia
"Usilie emmy napenda kukumbusha hao wanaume sio wazuri kwako jitenge nao" aliongea kaka rafiki
"Kwanini unafatilia maisha yangu wewe mkaka"
"Kwasababu wewe ni rafiki yangu'
" mimi sio rafiki yako nakuomba futa namba yangu"
Nilikuwa mkali kwake
"Sawa ila willy naye ataandaa mtego kwa ajiri yako kuwa makini, jioni njema"
"Kaka rafiki, kaka rafikiiiiii" niliita bila mafanikio
Niliwaza mtego gani ambao willy anataka aandae kwa ajiri yangu sikupata jibu hapo nilikuwa fire nilisikia simu inaita tena. Niliona jina pale willy "inawezekanaje hii" niliwaza kabla sijapokea sasa cha ajabu nilitazama kushoto nikamuona willy kwenye gari la pembeni yangu nilishtuka mno...
Nilitazama pembeni yangu nikamuona willy akaniangalia na kutabasamu huku simu yake ikiita bado , nilikumbuka maneno ya kaka rafiki nikaanza kuhisi jambo juu yake. Mara taa iliruhusu tupite nikapita nikielekea kariakoo niilitaza site mirror sikuweza kuona gari la willy nikajua tumeachana palepale fire, nilipita msimbazi hapo katikati nikaona carpets nzuri za uturuki nilitafuta parking nzuri ili niingie dukani na pia nilikuwa nahitaji nipite bookshop ninunue reviews za masomo yote kwanzia geography1&2, histry1&2, language1&2 na general studies.
"Habari za leo" nilisalimia
"Salama dada karibu" aliitikia muuzaji ambaye alikuwa ni mdada km mwarabu aliyechanganyika na uswahili
"Naomba hiyo carpet ya pink yenye mistari ya reds na purple"
Alisogea kunitolea carpet mimi nilichukua simu yangu na kujaribu kuangalia maana kuna jumbe zilikuwa zinaingia wakati nipo nadrive sikupata bahati ya kuzisoma. Zilikuwa ni nyingi mno kuna wateja wangu wa ubuyu, willy, jimmy na salma zikuzifungua kutokana na muda kuwa mdogo.
"Dada iangalie" aliniita yule mdada kunifanya niachane na simu nitazame yeye.
"Hiyo ni shilingi ngapi dada? Ilisikika sauti nyingine ya pembeni ila bado ckuitilia maanani
" ni laki nne na arobaini ila bei inapungua" alijibu yule dada
"Dada nimeipenda hii nipunguzie" nilijaribu kumuomba hapunguze bei.
"Hii hapa dada nimeshamlipia" aliongea yule kaka nikashangaa mno niligeuka kumtazama vizuri alikuwa ni willy.
Nilibaki mdomo wazi nikashindwa nisemaje kwa muda ule nilimtazama nikamtazama yule mdada muuzaji aliyekuwa anamwambia mkaka mmoja anibebee lile zuria mpka nitakapomwambia aliweke.
"Dada una usafiri? Aliuliza yule mdada sikumjibu bado nilikuwa nashangaa na willy alionyesha tabasamu pana mno ila mimi nikakumbuka maneno ya kaka rafiki " willy atakuandalia mtego kuwa makini" nilipokumbuka hivyo nilimgeukia yule dada muuzaji.
"Dada nashukuru naomba mpeni aliyelipia, willy asante ila sihitaji kwa sasa" nilimjibu willy na kuondoka kuelekea garini.
"Kuna wanawake wasumbufu namna hii" aliongea willy na kuondoka pia kuja upande wangu lile zuria likabaki mgongoni kwa yule kijana.
"Please naomba usinisumbue willy nilihitaji msahada wenu wakati nina kesi yangu, mmeshindwa kunisaidia mnaleta mapenzi mwambie na mwenzako mimi sina njaa kihivyo kama mna moyo wa kusaidia mkasaidie watoto yatima msinisumbue tena" nilimaliza nikafunta gari na kulock milango yote.
Nilihisi kichwa kinauma nikamuitaji sana kaka rafiki angalau anipigie simu anielekeze cha kufanya maana nilihitaji mfariji kwa wakati huu ila ckuwa nae hivyo kaka rafiki nilihisi ni mtu anayenitakia mema mno.
Ujumbe ukaingia niliwahi fasta kuufungua namba ngeni "emmy usirudi kijichi nenda kwa mama temeke" nilijibu
"Kuna nini kwani? Sikuweza kupata tena jibu zaidi ya nusu saa ilipita nikaamua kupiga simu
" namba ya mteja unayompigia haipatikani kwa sasa tafadhari jaribu tena baada, the number..." Nilikata simu kwa hasira
*************
Wakati nafika nyumbani(kwa mama mdogo) nilishangaa watu wakiingia kwenye gari aina ya noah wamembeba mdada aliyeonekana ni mgonjwa sana alikuwa amevaa dela nakumbuka, sikutilia maanani japo watu niliowaona nawafahamu niliendelea kutembea ghafla moyo ukawa mzito nikamsimamisha dada fulani anaitwa mwajuma "samahani kwani yule dada kapatwa na nini?
" haaaaa mwanaharamu mkubwa weee emmy sijawahi kuona mshenzi duniani kama wewe mpaka mama yako anazidiwa anataka kufa wewe ujui unatanua tu na vigari vya kuongwa, chefuuuuuu" aliishia kunishamba niliumia sana kwa yale maneno nikakimbia haraka kuwahi lile noah ambalo mlango wa abiria ulikuwa unafungwa.
Toba yarabi nafsi nilipohitaji kuingia nilipewa maneno ya kashfa ina maana pale mtaani hakuna aliyenipenda hata mmoja "toka tena ukome we mtoto kama umeshindwa kumlea mama yako tuache sisi tutamtunza ndo nyienyie freemason mnatoa ndugu zenu kafara ilo mfanikiwe kimaisha wee emmy wa kuvaa nguo za gharama namna hiyo mama yako hana hata hela ya kula toka sitaki kukuona" nilisimama nikaanza kulia huku nikimkumbuka mama yangu "emmy mwanangu ishi vizuri na wakubwa zako na hata wadogo waheshimu uwezi kujua atakayekusaidia nani, mheshimu mtu bila kujali anamuonekano upi utafanikiwa mwanangu" ni maneno ya mama kabla ajafa nimekuwa nikiyakumbuka ili ili ninalo bambikiwa leo sio.
"Mwajuma ni kweli emmy kamroga mama yake mdogo" nilisikia mnong'ono nikiwa nimesimama pale
"Wee uoni mtaa huu ni nani asiyejua kuwa emmy alikuwa maskini wa kutupwa nakumbuka alikuwa na nguo mbili tu tena gauni na dela muda wote unamkuta emmy na kanga haya ya leo haya kumiriki hadi nyumba, gari na kuvaa minguo ya gharama unafikiri ni nini kama sio ndumba" aliongea mwajuma bila wasiwasi hakujua ni jinsi gani ananiumiza.
"Iki kiama wengu watachomwa moto emmyhuyu alikuwa anakuja kwangu ananiazimisha nguo leo anaringa kisa kigari hicho simpendi huyu mdada hadi kinyaa" aliongea mwanaidi rafiki yangu wa kitambo
Niliendelea kulia hadi kimasi lilianza kunitoka na kichwa nacho kilianza kuniuma.
Niliondoka pale nikasogea hadi nyumbani mlango ulifungwa na funguo hazikuwepo pale nilipokuwa nimepazoea nikija nazikuta, nilimuona mpangaji jirani yetu mama bakari.
"Emmy kulikoni dada?
" shikamoo dada"
"Marahaba poleni ila hali ya mama yako haikuwa nzuri ulikuwa wapi kipindi chote?
Aliuliza mama bakari
" dada mama bakari mimi sijui lolote lile na kusema ukweli natuhumiwa kwa mambo nisiyoyafanya"
" emmy mdogo wangu mtaa mzima umekuwa gumzo wewe unaonekana umemroga mama yako ili upate mali nilivyosikia hivyo niliumia wanadai hata kumsaidia umsaidii chakula tu tuliwekeana zamu hapa kumuhudumia kweli emmy umeamua kufanya hivyo?
*mungu wangu mamdogo unanichumia dhambi bure, angalia mihamala hii nimekuwa nikituma laki kila wiki kweli simjari mama mdogo" nilifungua message na uzuri sikuzifuta sio kwamba nini nilikosa muda na mara ya mwisho aliniomba laki mbili hii niktumia.
"Kheeee kweli jamani mimi juzi hiyo ya.laki mbili aliniomba nimuandikie ujumbe hali yake ilikuwa mbaya"
"Sijui nifanyaje roho inaniuma kusingiziwa, ona message hii hapa namlazimisha aje kukaa pale kwangu unaona alichonijibu.
" mimi nimeshazoea maisha yangu ya temeke, ukitaka wewe mchukue rafiki yako salma uishi naye" ilisomeka hivyo
"Sasa napata picha emmy kuna kitu kinaendelea kati ya mama yako na baba mwenye nyumba na mama yako, na hii nakwambia siri mwisho niliwahi kumuona yule mkaka bonge akiwa nae(elibariki)'
Nilijikuta natokwa na machozi mama bakari alinitazama nikamuona nae machozi yakimtoka akanikumbatia kwa nguvu na kuniambia kwa sauti ya chini sana "emmy mdogo wangu usilie ndio ukubwa huo dada nakuomba wasamehe bure"
"Dada inauma kumbe kila nikipita hapa mtaani naonekana kituko hivi kweli mamdogo anaweza kunifanyia unyama huu"
"Emmy ebu kaa chini nikwambie jambo"
Niliamua kumsikiliza mama bakari nikachukua kigoda na kuketi huku nikimtazama usoni, nae alikaa kwenye mlango wake na kuanza kuongea huku mimi nikiwa bado namtazama ni nini anataka kuniambia.
"Emmy kama kusingiziwa wewe sio wa kwanza, kupitia shida emmy wewe sio wa kwanza na hata kusalitiwa wewe sio wa kwanza, emmy katika maisha yangu nimejifunza kusamehe mpaka hapa unionapo nimetendewa mengi nimesamehe nawe msamehe mama yako" aliongea mama bakari ila bado sikumuelewa kwangu yalikuwa ni maneno ya kawaida.
"Hivi kweli mama mdogo katembea na elibariki kabisa? Niliuliza kwa jazba
" tulia basi emmy mbona hivyo tunaongea wawili tu mbona hivyo"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mama bakari nakuheshimu wewe tu ila kile nitakachomfanyia hatasahau ngoja" niilizidi kutoa kilicho moyoni huku kifuani nilihisi kitu kama kiungulia.
"Hivi emmy wanaume unawajua kuliko mimi? Emmy usinione hapa nimepitia mengi kwenye mapenzi nimetendwa na hawa viumbe wanaitwa wanaume nilijuta kupenda niliwachukia wanaume nilimchukia hadi baba mzazi"
"Kheeeeeee" nilishangaa aliposema alimchukia hadi baba mzazi
"Usishangae emmy ndivyo ilivyokuwa"
"Ilikuwaje dada"
****************
FEEDBACK YA MAMA BAKARI KWA EMMY.
(KUMBUKA KUWA HII BADO NI SIMULIZI YA YALIYOMKUTA EMMY AKIMSIMULIA RAFIKI YAKE HIVYO TUWE MAKINI).
Nikiwa msichana mdogo(darasa 6) baba yangu alifukuzwa kazi aliyokuwa anaifanya katika shirika la reli tazara katika mkoa wa tabora. Kipindi hicho tulikuwa tunakaa kota za railway officers. Maisha yalibadili pindi tu tulipoama pale railway kota.
Kipindi kifupi kile mama alianza kufanya biashara ndogo ndogo za kuuza nguo kwenye gurio na mnadani, mimi fatuma(mama bakari) kila niliporudi shule nilikuwa naenda kumsaidia mama katika kuuza biashara yake, mambo yalizidi kubadilika hasa baba alipoanza kunywa pombe kitendo kilichopelekea fedha zote alizolipwa na shirika la reli kumalizika kwa pombe na wanawake..
Nilipomaliza darasa la saba sikubahatika kufaulu kuendelea na elimu ya sekondari hivyo rasmi nilijiingiza kwenye shughuli ndogo ndogo za kuuza vitafunwa na jioni kumsaidia mama mnadani siku zikazidi kwenda, ikafikia kipindi nikavunja ungo na kujiona sasa nimekuwa maana nilichelewa kuvunja ungo tofauti na rafiki zangu. Mara zote mama alikuwa akinihusia usafi(mwili na mazingira) maana tayari nilikuwa mwanamke na kikubwa zaidi juu ya kujiheshimu na kikubwa alinihusia juu ya kuwaogopa viumbe wanaoitwa wanaume.
Nilikuwa nikiyakumbuka mahusia ya mama kwani pamoja na kutongozwa sana na wanaume bado nilikuwa na msimamo, siwezi sema nilikuwa sipendi la hasha nilipenda ila niliogopa mama akijua yale nitakuwa matatizoni hivyo nilizidi kujitunza mpaka nilipofikia miaka 17 ambapo ndio nilipokutana na changamoto nyingi kutoka kwa mzazi wangu wa kiume/baba. Kuna kipndi tulikuwa na mama tunachelewa kurudi nyumbani kutokana na biashara kule sokoni baba alikuwa anamtukana sana mama mbele yangu matusi ya nguoni nilikuwa naumia mno ila sikuwa na jinsi maana nilikuwa mtoto tu kwao.
"Una akili kweli we mwanamke yani mwanao unampeleka kujiuza? Yani kujiuza wewe haitoshi mpaka unamuuza hadi mwanao shenzi sana wanawake ndio maana mimi nasema wanawake wote wasen*** tu" alikuwa akitoa kauli hizo kila siku japo muda tuliokuwa tunarudi ni saa moja jioni tu.
Kutokana na ile hali mama alianza kupata presha na miguu ilianza kujaa maji kiasi kwamba ukibonyeza unaasha alama, kwa mazingira hayo isingekuwa rahisi kufanya biashara hivyo mimi nilisimamia kila kitu nilijikuta nachoka mno maana asubuhi sana namke nikande ngani nipike chapati, maandazi kisha nichemshe chai kwa ajiri ya kwenda kuuza sokoni. Biashara nikimaliza hiyo saa tano asubuhi narudi kuandaa chakula nyumbani na kurudi tena sokoni kuuza nguo mnadani. Kuna wakati nilikuwa nadhurumiwa na wateja wakorofi mda mwingine wanaondoka na hela zangu ila bado sikuchoka maana bila hizo kazi familia yangu haitaishi.
Siku hiyo nikiwa narudi kutoka mnadani nimechoka hoi kuna kijana anaitwa jose alinisimamisha njiani namfahamu ni jirani yetu kwa mama haule nyumba ya tatu kutoka nyumbani. Alikuwa ananipenda muda mrefu huyo jose kipindi hicho yeye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha sita mimi ndo kama hivyo nilikuwa mdada tu wa nyumbani. Nilikuwa nampenda jose ila nilimuomba anitunzie heshima yangu tusifanye mapnzi hadi tutakapo kuja kuoana(nilikuwa bikra) alinishika mkono akanipusu na kunikumbatia hapo ghafla baba akatokea nilimuona jose akikimbia kuelekea porini mimi niligombezwa na kupigwa fimbo kama mtoto njia nzima huku nikipewa vitisho "nakwambia utanikoma malaya mkubwa kama mama yako"
Tulifika nyumbani akamwambia mama maneno ya uongo eti amenikuta nafanya mapenzi porini mimi nilishindwa kujitetea mama nae alizidi kunisema nikakosa amani moyoni na tangu siku hiyo baba alianza mambi ambayo sikuyaelewa mara aje chumbani kwangu au aje bafuni nikioga(bafu la makuti) akijifanya kajisahau nilikuwa nikikaa peke yangu nalia mno.
Nilifanikiwa kupata laki moja ambayo ilimuwezesha mama kupata matibabu na kuhudhuria mazoezi kila asubuhi. Jumapili asubuhi ni siku ambayo mama alianza kwenda hospitali yeye mwenyew mimi nilikuwa nje nafanya usafi wa vyombo na kufagia mazingira nikasikia naitwa ndani.
"Fatuma njooo" ilikuwa ni sauti ya baba
Nilirudi ndani kwenda kumsikiliza akaniruhusu niingie chumbani kwake na hapo ndipo aliponikamata na kunichania nguo na kunibaka nilipiga kelele ila sikupata msaada mithili ya kilio cha samaki. Alitumia zaidi ya masaa manne mpka kufanikiwa kunifanyia kile kitendo maana mna wote tulipigana ila baadae alinikaba na kunixidi nguvu, niling'ang'ania chumbani sikutaka kutoka ila mama akirudi anikute palepale.
"Fatuma twende uku" aliongea kama mtu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Samahani we mwanaume niache unachohitaji kingine kutoka kwangu ni nini? Wanawake siku zote ni dhaifu umetumia nafasi hiyo kunifanyia hivyo ulivyofanya nakuahidi sikuwahi na sitawahi kuwa na baba kama wewe ustahili kuwa baba na raana hii itakusumbua maisha yako yote mpaka unakufa" niliongea maneno kwa uchungu nikatoka chumbani.
Baada ya muda mama nae akaingia nikiwa chumbani najiangalia kweli sina bikra tena, kweli jose ataniamini mimi? "Fatumaaaaa nileteee maji mwanangu"/sauti ya mama ilinishtua nilivaa nguo yangu ya ndani haraka nikatoka ila nilisikia maumivu mno kiunoni na sehemu za siri.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment