Search This Blog

Thursday 19 May 2022

PENZI LA SHEMEJI - 4

 





    Chombezo : Penzi La Shemeji

    Sehemu Ya Nne (4)





    Bi mkubwa aliondoka kule kwa mganga na kwenda moja kwa moja nyumbani kwake ili ajiandae kwa safari ya kwenda Tanga

    Kabla ya kuondoka aliwapigia simu ndugu zake na mmewe na kuwataarifu kuwa ndugu yao amekamatwa kutokana na makosa ya kujeruhi na kubaka

    Baada ya kuwataarifu ndugu wale alipanda gari na kuanza safari ya kwenda Tanga kushughulikia tatizo

    Wakati akiiacha Segera akianza kupanda na njia ya kuelekea Tanga kilometa chache kutoka pale alishangaa kimuona mganga akiwa kasimama katikati ya barabara

    Alishtuka na kushika breki kwa ghafla na kwa bahati nZuri Mungu akawa upande wake akafanikiwa kusimama bila kumfikia yule mganga

    Mganga alicheka kwa sauti kubwa sana kisha akapotea

    Bi mkubwa akahaha na kushuka kutoka kwenye gari na kuzunguka kila upande kuona kama atafanikiwa kumuona mganga ila hakumuona

    Alirudi kwenye gari na kuendesha gari ila wakati huu kwa tahadhari na hakwenda kwa mwendo mkali tena

    Baada ya muda alijisahau na kuendelea na kasi kama mwanzo hasa mara baada ya ndugu wa mmewe kumpigia simu mara kwa mara wakitaka kujua maendeleo

    Alienda kwa speed kuba sana ila ghafla mbele yake akasimama bibi yake ambaye alifarii miaka saba iliyopita

    Bi mkubwa alipatwa na mshtuko mkubwa sana kumuona yule bibi yake ambaye aliamin alishafariki

    Kwa sababu ya ule mshtuko alichelewa kucheza na breki za gari yake na kukalibia kumgonga

    Alipofika kalibu hakuwa na namna akaona amkwepe ila ghafla yule bibi akageuka na kuwa mganga

    Bi mkubwa alikwepesha gari bila kuangalia eneo alilokuwa akiipeleka gari

    Alikuja kushtuka mti mkubwa ukiwa mbele yake

    Gari ile iligonga ule mti na kubilingika zaidi ya mara tatu

    Mama alitibiwa vizuri na wakafanikiwa kumtoa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ila hakuweza kurudisha fahamu zake

    Mimi nilishapewa ruhusa ila sikwenda popote bali nilibaki pale pembeni ya mama nikimwangalia muda wote machozi yakinitoka

    Nesi mmoja aliyekuwa na roho nzuri alikuwa ananinunulia chakula nakula wakati mama alilishwa kwa kutumia mirija

    "Mama yako amepooza sehemu moja ya upande wa mwili wake hivyo hataweza kufanya shughuli ya aina yeyote na pia anaweza kulala kitandani maisha yake yote"akasema Daktari

    Ilikuwa taarifa mbaya zaidi kuwahi kutokea kwa upande wangu kwa sababu nilikumbuka mara baada ya mama kuolewa na huyu mzee alikosana na nduguzake wote kwa sababu hawakupenda aolewe na huyu mzee

    Nililia sana siku hiyo mpaka nikataman kufa ili nisiendelee kuishi katika Dunia hii

    Baada ya siku tatu niliitwa na askari kwenda mahakamani ili kutoa ushahidi juu ya yule mzee

    "Ukitoa ushahidi wa kumuumiza ndugu yetu utafute pa kuishi na msirudi pale tena"ujumbe wa siri ulinifikia kutoka kwa ndugu za yule mzee

    Nilifikiria sana juu ya kumsaidia yule mzee kwa kusema uongo au nisimsaliti mama yangu ambaye alikuwa hoi kitandani

    "Mama akifa hawa watanilea kama mtoto wao wakati sina damu yao? Na je mama akifa atakuwa radhi na mimi huko aendako kwa usaliti wa aina hii?"nilikuwa najiuliza maswali mwenyewe

    Niliamua kusema ukweli wote na kweli nilipofika mahakamani niliongea ukweli halisi wa tukio lile

    Nilishaamua kutorudi pale tena bali nitajua cha kufanya kama mama atafariki

    Nilipotoka mahakama baada ya hakimu kutaja tarehe ya hukumu nilirudi hospital kwa mama yangu kipenzi

    "Mama nimeongea ukweli najua utakuwa na aman! Ningesema uongo najua usingekuwa radhi na mimi! Nitajua tutaishije ila lazima yule mzee apate haki yake kutokana na matendo yake"nilimwambia mama taratibu nikiamin ananisikia

    Wakati nikiwa pale Hospitalini mida ya usiku nikiwa nimelala pembeni yake mama kuna watu walionekana wamevaa nguo nyeusi wakirandaranda kwenye kile chumba kwa nje

    Nikanyenyuka taratibu na kwenda kalibu na mlango kisha nikatega sikio

    "Atakuwa hiki chumba! Ndiyo walisema wodi no 5! Lazima afe! Hawezi kumfunga ndugu yetu hivi hivi"niliwasikia wakinong'ona



     Bi mkubwa alipogonga ule mti kwa sababu alikuwa hajafunga mkanda alirushwa kupitia kioo cha mbele ya gari na akkumbana na ule mti

    Akapiga kichwa chake kwenye ule mti kikapasuka fuvu lake pale pale

    Haikuchukua sekunde nyingi kwa damu kuvujia kwenye ubongo na Bi mkubwa historia yake ikafungiwa pale

    Kama kawaida ya Watanzania tukio la ajali kama lile linapotokea cha kwanza wanachofikilia ni kuiba na si kuokoa maisha ya wahusika

    Moja kwa moja vijana waliowahi kufika pale walianza kunyofoa vifaa kwenye gari na vile vitu vingine alivyokuwa kabeba Bi mkubwa

    Raia walizidi kujaa eneo lile na wizi ukapungua ndipo simu zilipopigwa Polisi nao wakawaasiliana na wale askari wa usalama barabarani wakafika pale muda si mrefu

    Katika pekua pekua pale wakabahatika kupata kitabu cha kumbukumbu cha Bi mkubwa na humo wakapa namba za simu kadhaa

    Walichukua namba iliyoandikwa Mjomba na kufanya mawasiliano naye na kumweleza tukio lililotokea

    Kisha mwili wa marehemu ukapelekwa kuhifadhiwa Tanga mjini hospitalini

    Ndugu wa marehemu waliwasliana na ndugu wa mumwe ambaye alikuwa kizuizini kwa wakati huo

    Ndugu waakapanga safari ya kuelekea Tanga kushughulikia tatizo la ndugu wao na huyu mama ambaye alishakuwa marehemu

    Walipofika walianza taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kurudi Dar es salaam kwa ajili ya mazishi huku wengine wakibaki kuhangaikia dhamana ya yule mzee

    Siku ya kesi ndugu wale walijalibu kupenyeza ule ujumbe kwa Shamim ili wamtishe na asitoe ushahidi juu ya ndugu yao lakini wakashindwa

    Ndipo walipopanga kumuua Shamim ili shahid muhimu apotee na kwa sababu kesi ilihamishiwa Dar kwenye mahakama kuu basi itakapoanza kusikilizwa upya

    Walipofika walianza kutafuta chumba kile ambacho walipewa maelekezo ya kuwa ndipo Shamim na mama yake walipokuwa

    Shamim aliposikia akiongelewa kuuawa alishtuka sana

    "Mama yangu ndio wanataka kuniua? Nifanyeje hapa?"akawa anajiuliza

    Kutokana na utoto wake hakuwa na akili au uwezo wa kupambana nao na alipoelekea kwenye vioo alikuta vimefungwa na pia vina nondo hivyo asingeweza kupenya

    Akiwa anatetemeka sana pale aliskia wale watu wakifungua mlango wa chumba cha jilani na cha kwao

    Akashusha pumzi akiamini hawakuwa na nia naye labda ni huyo mtu wa chumba cha jilani

    Ghafla kashangaa wale watu wakifungua tena ule mlango na kutoka kisha wakaanza kubishana

    "Niliwaambia sio kule ni hiki hapa"mmoja aliwaambia wenzie

    Shamim hali akijua hatari iliyomkabili alijikuta bila kutarajia akipiga kelele kubwa sana

    "Majambazi wanataka kuniuaaaaaa!!! Nisaidieni majambazi wanataka kuniua"alipiga kelele kwa nguvu sana

    Wale jamaa pale nje waalishtushwa na shambulizi lile ambalo hawakulitarajia kabisa

    Mmoja akafungua mlango akitaka kmfata Shamim pale alipokuwa kajikunyata

    "Kaka hali imeshaharibika hapa hapafai! Achana naye twende"walimshika mwenzao na kujalibu kumshawishi asiingie

    Ila yule jamaa aliendelea kupambana ili aingie pale ndani

    "Wanataka kuniuaaaaaaaa!!! Nisaidieni jaman! Wananiua majambaziiiii!"aliendelea kupiga kelele

    Wale majambazi waliokuwa wakimzuia mwenzao walipoona anaendelea kulazimisha wakamuachia

    "tumekuzuia hujasikia! Sasa ukikamatwa ukatutaja kifo chako kitakuwa kinakuita"walimwambia

    Wakaondoka na kumwacha mwenzao

    Kelele zikaanza kuwa nyingi sana pale hasa kutoka wodi za jilani na ile ya kwao na Shamim

    Jamaa na yeye akashtuka ambo yameshaharibika tayali hivyo hakuwa na muda wa kutekeleza kile alichokipanga

    Kwa bahati nzuri wakati tukio lile linatokea mlinzi wa Hospitali ile alikuwa na askari wa doria waliopita eneo lile

    Hivyo wakati zile vurugu zinatokea walizisikia na wote wakaingia pale ndani kwa speed



      Askari wakishilikiana na walinzi walifanikiwa kuwadhibiti wale vijana waliokuwa wanataka kutekeleza lile tukio kwa Shamim



    Walipokamatwa walichukuliwa mpaka kituoni kwa mahojiano zaidi na sheria kuchukua mkondo wake



    Shamim aliendelea kukesha na mama yake pale Hospitalin huku baadhi ya wagonjwa wakimpa msaada pamoja na manesi wa chakula



    Siku mbili baadae mida ya usiku mama yake Shamim alianza kurisha miguu na kutapatapa



    Shamim akiwa usingizini alishtuka na kumkuta mama yake akiwa anatapatapa na kurisha miguu yake



    "Nesiii !!! Nesiiii!! Mama yangu! Mama yangu"alikimbia kuelekea chumba walichokuwepo manesi huku akipiga kelele na kuwaita



    Manesi walishtuka kutoka usingizini kwa sababu mara nyingi wakati wa usiku huwa hawana kazi nyingi hivyo kuuchapa usingizi



    Waliposhtuka kila mmoja alikurupuka na kudhani wakaguzi ndiyo waliokuja na hapo wanashtuliwa na mmoja wao



    Waliparamiana wakati wanagombania kupita kwenye kale kamlango huku wengine wakiumia



    Nje walikutana na katoto kadogo kakiwapigia kelele



    Kila mmoja alisimama akihema kwa mshangao!! Mpaka wakajiona wajinga kuumizana kwa sababu ya kale katoto



    Kila mmoja aliongea na kwake



    Wakutukana walimtukana Shamim matusi ya nguvu



    Wengine walitoa lugha wanazozifahamu ilimradi kujiridhisha nafsi zao kuwa kile kilichowapata



    Mmoja aliyefahamu kwa kina tatizo la Shamim alimuonea huruma na kumfata nyuma nyuma mpaka kwenye wodi aliyokuwa kalazwa mama yake



    Walimkuta akiwa kimya! Hatikisiki wala kuhema



    Nesi akajalibu kusikiliza mapigo ya mama yule ila hakusikia chochote



    Hakumwambia Shamim bali aliondoka mpaka kwenye chumba cha Daktari na kumpa taarifa ya kile kilichotokea



    Daktari alimfata Nesi mpaka kule kwenye wodi ile



    "Mtoe huyu mtoto hapa"akasema Daktari



    Nesi akamchukua Shamim na kumtoa pale wodin na kisha akarudi na kumsaidia Daktari



    Dokta alitumia dakika chache kufahamu kuwa yule mama hakuwa na uhai tena



    "Andaa utaratibu na mtu wa mochwari mmpeleke na huyu mtoto utafute namna ya kumwambia"akasema Dokta na kuondoka



    Nesi alienda na kumfata mtu wa chumba cha maiti na wakauchukua mwili wa mama yake Shamim na kuupeleka chumba cha maiti na muda huo Shamim alikuwa kaondolewa eneo analoweza kuona kinachoendelea



    Baada ya kumaliza hilo alimchukua Shamim na kwenda naye kwenye chumba cha Daktari



    "Shamim mama..."Dokta hakumaliza kuongea Shamim akamkatisha



    "Niambieni tu wala msiogope na kunificha au kutafuta namna ya kuniambia! Mama yangu amekufa?" akasema



    Waliangaliana na kushangaa ujasiri wa yule mtoto mdogo wa miaka kumi na mbili



    "Hatujasema hivyo Shamim"nesi akadakia



    "Najua ndiyo maana nauliza nilichungulia na kuona mkiutoa mwili wake kule chumbani kwa hivyo msizunguke zunguke jaman niambien kama kafa"akaongea tena ikakamavu



    "Ukweli ndo huo Shamim ila usife m..."Nesi alisema ila akakatishwa



    "Hilo ndiyo nilitaka kujua! Sasa mimi nina ombi moja pekee"akaendelea kuongea kijasiri sana



    "Ombi gan?"akauliza Dokta



    "Kwa sasa sina ndugu wala jamaa wakunisaidia kwa sababu sina uhusiano mzuri na kwa upande wa mama na pia baba naomba kama wazazi mnisaidie nimzike mama yangu kisha nitajua cha kufanya"akasema



    Ujasiri wa Shamim uliwashangaza saana Daktari na yule Nesi



    "Hilo halina tatizo binti tutashilikiana na Manispaa na kumzika mama yako kwa heshima zote kama binadamu wengine"akajibu Daktari



    "Nitashukuru sana kama mtanisaidia kwa hilo na Mungu awabariki"akasema Shamim



    "Usijal Shamim na pia mimi niko tayali kuishi na wewe kama mama hivyo usiwe na wasiwasi kabisa na maisha yako"akasema Nesi



    "Nahitaji msaada wa mazishi peke yake na sihitaji zaidi ya hapo! Najielewa na nitaweza kustahimili kuishi navyojua! Nashukuru kwa moyo wako wa wema lakini niseme tu kuwa msaada wako sitaupokea"akasema



    Kila mmoja alishangaa!!!





      Walijalibu kumshawishi Shamim akubali kwenda kuishi nao ila yeye alishikilia msimamo wake



    "Kwani dada wewe una mme?"akauliza Shamim



    "Ndiyo ninaye ila yeye ni msitaarabu hana matatizo"akajibu Nesi



    "Hakuna mwanaume msitaarabu na sitaki kabisa kuwaona wanaume kwenye maisha yangu,nawachukia sana tena sana wanaume"akasema Shamim



    " Lakin Shamim sio kila ukifanyiwa kitu kibaya na mtu mmoja basi unawahukumu wote tungekuwa hivyo basi tungewachukia binadamu wote mwanangu"akasema Nesi



    "Sidhani kama nahitaj kushauriwa juu ya hili! Najua wewe ni nesi na mwelewa hivyo unaweza nishawishi sana ila hunijui tu! Labda nikwambie sihitaj kuendelea na haya majadiliano naomba kama mnanisaidia kumzika mama mnisaidie tafadhali"akajibu Shamim



    Hawakuwa na uwezo wa kuendelea kubishana naye hasa kutokana na msimamo aliokuwa akiuonesha pale



    Hospital iliwasiliana na Manispaa ya Tanga na wakakubaliana kusaidiana kuuzika mwili wa mama yule siku inayofata mchana



    Shamim alipewa pesa kidogo na Nesi imsaidie mpaka kesho yake wakati wa mazishi aweze kuwepo ili kumuaga mama yake



    Alipotoka pale aliingia mtaani na kuanza kuzunguka zunguka mjini akiwa hana pa kwenda



    Kuna kipindi alienda mpaka kwenye ile nyumba waliyokuwa wakiishi na mama yake na yule mzee akakuta pamefungwa na hawezi kuingia



    Jioni ya siku hiyo alitafuta genge na kupata chakula kisha akajongea mpaka kwenye vibalaza vya maduka ya wahindi na kujilaza pale



    Usiku saa nane alishangaa anaota ndoto akimuona mama yake akihangaika kitandani akipigania roho yake kwa muda mrefi kusha akatulia



    Shamim alishtuka kutoka kwenye hiyo ndoto



    Alipoangalia pembeni yake alimuona mtoto mdogo wa miaka mitano hivi akiwa anatetemeka sana kama mgonjwa



    "Wewe"alijalibu kumuita akimtikisa



    "Eeee"kakaitika kale katoto



    "Unaumwa?"akauliza



    "Ndiyo nisaidie dada"kakasema kale katoto



    "Kwenu wap? Wazazi wako wako wap?"akauliza



    "Sina wazazi na sina kwetu"akajibu



    Shamim alipojalibu kumuhoji yule mtoto hakupata tena majibu ndipo akajua kuwa asipomsaidia anaweza kupoteza maisha mbele yake



    Alijitahidi akambeba yule moto mgongoni na kuanza safari kuelekea kwenye ile Hospital alipokuwa na mama yake



    Pamoja na yule mtoto kuwa mzito kulingana na umri wake ila alijikaza na kuendelea na safari mpaka alipofika Hospitalin



    Alielekea moja kwa moja kwenye ofisi ya Daktari na kwa bahati nzuri akakutana na yule Nesi mlangoni akiondoka mara baada ya kumaliza zamu yake kazini



    "Shamim vip tena? Na huyu ni nani?"akauliza



    "Tafadhali Nesi nisaidie huyu mtoto atibiwe kisha hayo mengine tutayajadili tafadhali"



    Nesi hakuwa mbishi alimbeba yule mtoto na kuongozana na Shamim mpaka kwenye wodi



    Alipofika alimhudumia yule mtoto kwa kumuwekea drip ya maji na pia ya dawa alipohakikisha kamuweka kwenye sehemu salama tena akimkabidhi Nesi mwenzake ndipo alipomuaga Shamim na kuondoka



    Siku iliyofata ilimkuta Shamim akiwa pale pale Hospialin akimsubiri yule mtoto aamke



    Muda wa kwenda kuzika ulipofika Nesi yule na baadhi ya watumishi waliokuwa wakiyajua matatizo yaliyomkuta Shamim waliongozana naye mpaka makaburin



    Manispaa ilimzika yule mama kwa heshima zote kama binadamu wengine



    Cha kushangaza wakati Shamim anatupa udongo kwenye kaburi la mama yake alikuwa mkavu kabisa bila kutoa chozi



    Alikuwa akiongea mwenyewe taratibu kitu ambacho hakuna aliyekuwa akikisikia



    Alipomaliza kutupa udongo kwenye kabuli la mama yake alirudi nyuma na kuacha warudishe udongo kwenye shimo lile



    Walipomaliza kulifukia lile shimo yule Nesi alimpatia Shamim ua na kwenda kuweka kwenye kaburi la mama yake



    "Nenda kwa aman mama yangu! Nitakukumbuka daima na nitakuenzi kwa kuwachukia wanaume"aliongea taratibu



    Wakati kila kitu kinatokea kuna mtu ambaye lengo lake halikujulikana ni lipi alikuwa akimfatilia Shamim kwa kila kitu alichokuwa akikifanya!!





      Siku moja nyuma kabla ya mazishi ya mma yake Shamim



    Alipokuwa akiongea na Dokta wakiwa na yule Nesi na kila mmoja kubaki na mshangao juu ya msimamo na ujasiri wa Shamim



    Kwa bahati mbaya au nzuri Dokta alipotoka pale Hospitalin hakuacha lile swala liishie pale bali aliporudi nyumbani alimsimulia mke wake kipenzi



    Bahati nyingine mbaya au nzuri pale nyumbani alikuwepo kijana mmoja waliyezoeana na Dokta na kujenga urafiki aliyekuwa akifanya biashara zake kutoka Somalia na kuleta Tanga



    Maelezo ya Daktari yule juu ya ujasiri na maisha ya Shamim ukamvutia sana



    "Nimepata vijana wawili boss"aliongea kwenye simu yule kijana



    "Wanatosha fanya uje moja kwa moja"akajibiwa



    "Hapana boss kuna kitu nimekisikia kutoka kwa huyu Daktari ninayefikiaga kwake ambacho kimenivutia sana"akasema yule kijana tena



    "Kitu gan?"akaulizwa



    Ikabidi yule kijana aelezee kisa alichokisikia kutoka kwa Dokta juu ya Shamim



    "Lakin unajua kuwa hatufanyi kazi na wanawake sio?"akaulizwa



    "Najua ila i think she is different and anawachukia sana wanaume so lets try her na pia nipe muda nimfatilia nijue kama anafaa isijekuwa ni sifa tu"akasema tena yule kijana



    "Ok do it lakini hakikisha unakuwa more than care nafikiri unajua kuwa i dont accept any mistacke"akajibiwa



    "I know boss! Let me do it pz"akajibu



    " Nakutakia mafanikio"akajibiwa na simu ikakatwa



    Ikabidi afatilie tukio la mazishi ya mama yake Shamim akiamin ndipo atakapopata nafasi ya kumuona Shamim



    Kweli kwenye maziko yale yaliyofanywa na Manispaa mwonekano wa Shamim ukamvutia kwa kiwango kikubwa yule kijana



    Alijitahidi kujipenyeza mpaka kuwa kalibu na Shamim ndipo akasikia akisema anawachukia saana wanaume



    Baada ya maziko yale msafara wa magari uliondoka pale makaburini kurudi Hospital na wale wa Halimashaur wakarudi maeneo yao



    Shamim alielekea hospitalin na kubaki akimuuguza yule mtoto aliyemuokota



    Jioni yule mtoto alipata fahamu



    " niko wap hapa?"aliuliza akiangaza macho yake eneo lile



    "hapa ni hospitalin mdogo wangu"akajibiwa



    "we ni nan?"akauliza tena



    "Mimi ni Shamim nilikusaidia tukiwa tumelala wote kibalazani usiku,we unaitwa nani?"akauliza



    "Naitwa Joan"akajibu



    Kabla hawajaendelea na majadiliano Nesi mmoja akaingia pale ndani akiwa na lugha chafu sana kwao



    "We mtoto umezoea kutibiwa hapa na kutolipa,tumekushtukia na huyo Nesi wako! Nakuahidi hapa lazima utalipa huondoki"akasema



    "Sio mimi niliyekwambia ubakwe au ufiwe! Kila mwenye matatizo akija kutibiwa bure patatosha hapa? Tulikusaidia wewe sasa unabeba mpaka chokoraa"akasema



    Maneno yale yalimuudhi sana Shami akajikuta akipandwa na hasira kali sana



    Akanyenyuka na kumfata yule Nesi

    Alipomfikia akachukua mkasi uliokuwa kwenye chombo chake cha kubebea vifaa akamchoma nacho mara mbili mkononi na kiunoni



    Yule Nesi akaanguka chini kwa maumivu makali akaanza kupiga kelele akihitaji msaada



    Shamim hakusubiri kukamatwa alienda na kung'oa drip za maji kwenye mkono wa Joan kisha akamshika mkono na wakaanza kukimbia kutoka kwenye jengo lile



    Walipokuwa wakikimbia yule kijana aliyekuwa akimfatilia Shamim akaona ni nafasi ya kutumia kuwaokoa kisha kumchukua Shamim



    Aliwahi getini na kuanza kuwachanganyia maelezo walinzi wakati kelele zikiendelea kusikika mpaka alipowaona Shamim na mwenzake wamefanikiwa kuvuka geti salama



    Walinzi walikuja kushtuka kuna tukio limetokea ndani wakati akina Shamim wakiwa wameshafika mbali



    Joan alikuwa kachoka ukiongeza na kule kuugua alikuwa anashindwa kukimbia kwa kasi sana



    Hivyo Shamim alimshika mkono kwenye uchochoro mmoja na kujificha kwenye kakibanda kadogo ka fundi viatu



    Yule kijana alikuwa speed sana akiwawahi akina Shamim ili ampate na kumpeleka kwa boss wake



    Aliwapita akina Shamim eneo lile bila kujua kuwa wamejificha pale



    Walipoona amepita waliyeamin ndye anayewafukuza awakamate kutokana na kitendo walichofanya waliondoka eneo lile



    Wakati wanavuka uchochoro ule kuingia wa pili walishangaa wamezungukwa na kundi la vijana





      Shamim akiwa na Joan walipotoka pale walipokuwa wamejificha walishangaa baada ya kukatisha mitaa michache wakawa wamezungukwa na kundi la vijana



    "Mtulie hivyo hivyo"wakasema



    Waliwasogelea huku Joan akiwa anatetemeka sana huku Shamim akiwa hana hofu yeyote ile



    "Oyaa huyo dogo sana huyu mkubwa anatufaa sana"akasema kijana mmoja



    "Mimi naona tufanye fasta"akasema mwingine



    Waliwavamia na kumsukuma pembeni Joan kisha wakamvamia Shamim



    Hakupiga kelele bali alijitahidi kupambana nao kwa nguvu zake zote ila kwa sababu ya wingi wao hakuweza chochote



    Hatimaye wa kwanza na wa pili wakafanikiwa kumuingilia kwa nguvu kimwili



    Alipata maumivu makali sana hasa kutokana na kuwa alikuwa hajapona vizuri majeraha ya kubakwa na baba yake yule wa kambo



    Wa tatu alipoingiza uume wake ili na yeye ambake Shamim alijikuta akipata nguvu za ghafla na kuwasukuma wale wengine kisha akamshika yule aliyekuwa kwenye zoezi



    Alimvutia kwake na kupeleka mkono wake chini kwenye maumbile ya yule kijana na kufanikiwa kuizikamata korodani za yule kijana



    Alizivuta kwa nguvu na yule kijana aliposikia maumivu akajalibu kumpiga ngumi Shamim ili amuachie



    Shamim alipoona wale wenzake na huyu kijana wakisogea eneo lile aliinama na kupeleka mdomo wake kwenye kiuno cha yule kijana kisha zile korodani akazihamishia mdomoni kwake na kuzing'ata kwa nguvu zake zote



    "Mamaaaaaaaaaaaa!!!!!! Nakufaaaaaaaaaaaa!!!"alipiga kelele yule kijana kwa nguvu



    Shamim alipojua katimiza lengo lake alimwachia yule kijana kisha akasimama kuwakabili wale wengine



    Wale vijana wengine nao walipoona yule kijana ambaye ndiye wanayemuaminia kuwa na nguvu kwenye kikundi chao akiwa pale chini akigaagaa waligeuza na kukimbia kila mmoja akipita njia yake



    Zile kelele zilimfikia yule Kijana wa Kisomali aliyekuwa mtaa wa jilani na huo akiwa tafuta akina Shamim



    Akageuza njia na kufata eneo ambalo alisikia kelele zikitokea



    Alipofika aliwaona Shamim na mwenzake wakiishilizia vichochoroni na yule kijana akiwa pale pale chini akigaa gaa



    Alimkagua yule kijana na kuona athari alizokumbana nazo kutoka kwa Shamim na kuamini kweli Shamim alikuwa gaidi wa uhakika



    "Atatufaa sana huyu"aliwaza



    Aliondoka pale na kuanza kuwafatilia akina Shamim huku akitoa simu yake na kumpigia boss wake kisha akamwelekeza tukio kamili la kilichofanywa na Shamim



    Shamim alipomchukua Joan kutoka pale chini walianza kukimbia na kukatisha baadhi ya mitaa ya mji ule mpaka wakatokea kalibu na bandari



    "Twende kulala kwenye zile meli kule" shamim alimwambia Joan



    "Huogopi dada kuwa tunaweza kukutana na vijana wengine wakorofi wakakufanya kama wale?"akauliza Joan



    "Unafikiri tutalala wapi mdogo wangu? Sisi hatuna wazazi wala ndugu hivyo twende tu tulale wakija wengine tutapambana"akasema Shamim



    "Sawa dada nakutegemea sana wewe sina ndugu zaidi yako "akajibu Joan



    "Usijal Joan"akajibu Shamim



    Waliondoka na kupenya sehemu za hatari sana mpaka wakafanikiwa kuingia kwenye vyumba vya meli zile



    Pale ndani waliwaona baadhi ya vijana wakiwa wamelala usingizi na hivyo wakajitahidi kupenya bila kuwashtua mpaka walipopata nafasi ya wazi wakalala



    Usingizi ulipowapitia ndipo adui wwalipofanya kazi yao



    Kwenye ndoto Shamim aliendelea kutokewa na lile tukio la kubakwa na yule mzee na pia picha nzima ya mama yake akiwa na jeraha lake shingoni akitapatapa na kukata roho



    "Mwanangu wanaume ni watu wabaya sana! Wamekuumiza sana mwanangu na kisha wakaniua! Wachukie na ukipata nafasi waumize sana"alisikia sauti ya mama yake akiwa ndotoni



    Alishtuka kutoka kwenye usingizi na kukuta kumeana kupambazuka na mwanga kutokeza huku watu wakianza kuendesha shughuli zaoe eneo lile



    Alipogeuka ili kumwamsha Joan akashangaa hayupo



    Akaanza kumtafuta pale ila hakumuona



    Alianza kuzunguka zunguka pale bandarini akimtafuta Joan ila hakumuona!!





      Shamim aliendelea kumtafuta Joan bila mafanikio kila upande na mwishowe akachoka



    "Atakuwa amechukuliwa? Au amenitoloka kwa kuniogopa?"alijiuliza



    Hakutoka kwa siku hiyo nzima eneo lile la bandari kabisa akitegemea kuna wakati atamuona Joan



    Ilipofika jioni ya saa kumi akiwa hajala aliamua kuzunguka kuelekea maeneo yenye magenge mengi ili apate japo kitu cha kuweka tumboni kutokana na njaa kali kumsumbua



    Alizunguka kwenye magenge mengi sana mwishowe akatafuta sehemu na kukaa kwenye gogo



    "Wee mtoto"sauti ya mama mmoja mwenye genge ilimshtua



    "Mimi?"aliuliza akigeuka



    "Ndiyo wewe njoo"akasema yule mama



    Shamim alinyenyuka na kuelekea kwenye lile genge la yule mama aliyekuwa anamwita pale



    "Kaa hapo"yule mama alimwelekeza sehemu ya kukaa



    Shamim alikaa na kusubiri maelekezo ambayo hakuyajua



    Yule mama alipakua wali sahani mpaka ikajaa na kuweka nyama na mchuzi wa kutosha kisha akampelekea Shamim



    "Kula mwanangu usiogope"akasema yule mama



    Shamim hakujiuliza tena bali alikula kile chakula kwa fujo kutokana na kuwa na njaa kali sana baada ya muda mfupi alikuwa kamaliza



    Mama yule aliichukua sahani yake na kisha akamuwekea chakula kingine na kumpatia nacho Shamim alikula kwa kasi na kilipokalibia kuisha akawa kashida



    "Ahsante sana mama"akasema



    "Usijal mwanangu"alisema yule mama



    Mama yule alittoka na baada ya muda mfupi alirudi akiwa na soda akampatia Shamim



    Shamim alikunywa ile soda mpaka akaimaliza



    "Ahsante sana mama,samahani mama naomba nikuoshee vyombo vyako"akasema Shamim



    "Hapana mwanangu,nitaosha wala usijal,wee endelea na mihangaiko yako ila usisahau kesho asubuh uje ule,na mchana,na jioni pia"akasema yule mama



    "Ahsante sana mama"akajibu



    Shamim aliaga na kuondoka eneo lile taratibu ila lile swla la kusaidiwa na yule mama huku akiwa hamjui likamuumiza akili sana



    "Sio rahisi mtu hanijui na wala simjui anisaidie hivi! Kutakuwa na jambo hapa"aliwaza



    Alipofika mtaa wa pili aliamua kufanya uchunguzi



    Alirudi kwa kutumia njia nyingine mpaka alipofanikiwa kufika kalibu na genge la yule mama akajificha na kuanza kufatilia nyendo za yule mama



    Muda mfupi aliona kijana mmoja akija mpaka eneo lile kisha akaongea kwa muda na yule mama kisha akatoa pesa na kumpatia



    Hakufahamu kama yule kijana ana uhusiano na ule msaada wake ila alitia shaka sana



    Aliondoka na kurudi bandarini kisha akategea tegea eneo lile huku akizunguka zunguka kuona kama anaweza kumuona Joan ila hakuona mtu



    Usiku kama kawaida aliingia sehemu yake na kulala usingizi mpaka asubuhi na kwa bahati nzuri siku hiyo hakuota zile ndoto zake



    Asubuhi alipoamka ili aondoke alishangaa kukuta kikaratasi kidogo pembeni yake

    Akakichukua na kukisoma



    "NAJUA UNATAMAN KUJUA ALIPO MWENZAKO JOAN! YUKO SEHEMU SAALAMA ILA UHAI WAKE UTATEGEMEA NA WEWE KUKUBALIANA NA MATAKWA YETU,NENDA KWA YULE MAMA ULIYEKULA JANA KWAKE NA UTAPATA MAELEKEZO YOTE" kiliabdikwa



    alishtuka sana



    Pale pale akakumbuka yule kijana aliyejadiliana na yule mama akahisi atakuwa anahusika na upotevu wa Joan



    Akaondoka na kukimbia kwa kasi mpaka kwenye lile genge la yule mama



    Kwa bahati mbaya akakuta hapajafunguliwa hivyo akakaa na kusubiri



    Baada ya muda mfupi yule mama alifika eneo lile na kumkuta Shamim amekaa akiwa kafura kwa hasira akimsubiria



    "Mwanangu hujambo? Mbona mapema hivyo?"akauliza yule mama



    Shamim hakumjibu kitu bado aliendelea kumwangalia kwa hasira kali sana



    "Joan yuko wap?"hatimaye akauliza



    "Joan yupo sehemu salama akipata huduma zote nzuri ila usalama wake utategemeana na makubaliano yako na hawa watu"akasema yule mama



    "Namhitaji Joan kabla sijafanya kitu kibaya hapa"akasema Shamim



    Yule mama alipigwa na butwaa katoto kadogo kama kale kumchimba mkwara





      Yule mama alimwangalia Shamim kutoka juu mpaka chini akashika kiuno kwa mshangao



    "Narudia tena! Unaniambia Joan alipo au hauniambiaa?"akafoka



    Yule mama hakumjibu bado aliendelea kumshangaa yule mtoto



    "Wewe mama mzima tena mzazi huna akili unanunuliwa na kumuuza mtoto mdogo kama yule na mimi angekuwa mwanao ungekubali kufanya hivyo? Ngoja nikuoneshe"akasema



    Shamim aliinama chini na kuokota jiwe kisha akamponda nalo ule mama kifuani



    Yule mama alipatwa na mshtuko na kujikuta akiangusha vyombo alivyokuwa amebeba kwa ajili ya kazi yake ile ya umama lishe



    Vile vyombo vilipoanguka Shamim aliinama na kuchukua kisu kutoka kwenye vile vyombo kisha akaanza kumfukuza yule mama huku akitoa matusi mengi ya nguoni



    Wakati lile timbwili linatokea yule kijana alikuwa kwenye gari aina ya Noah pembeni ya eneo lile akiwa na vijana wengine wakiangalia mchezo mzima ulivyokuwa ukiendelea



    Shami alipomfukuza yule mama mpaka kufika barabarani alishtushwa na gari ile kutaka kumgonga na kupaki pembeni yake na ghafla ndani yake wakatoka vijana watatu na kumkamata kwa nguvu kisha wakamwingiza ndani ya gari



    Baada ya kuingizwa kwenye gari alishikiliwa kwa nguvu huku akijalibu kupambana nao kwa kuwang'ata ila kwa sababu walikuwa vijana wenye nguvu walimzidi na kumbana mpaka akashindwa kufurukuta



    Gari ilitembea kwa dakika kumi na tano kisha ikaingia kwenye jengo kubwa lenye geti yenye fensi ya umeme



    Gari iliposimama walimshusha Shamim na kumuingiza ndani



    Shamim alikuta kwenye sebule ya ile nyumba kukiwa na watu wazima wawili wanaume na upande mwingine akiwa amekaa Joan



    Joan hakuwa yule aliyekuwa naye mtaani bali huyu alikuwa tofauti



    Joan alikuwa kapendeza sana,alivaa nguo nzuri na za kuvutia ingawa alionesha hali ya simanzi



    Joan alimkimbilia Shamim na kumkumbatia kisha wakalia kwa muda kabla ya kuachanishwa na wale vijana waliojazia miili yao



    "Shamim muulize mwenzako kama kuna kitu kibaya tumemfanya?"walimwambia



    "Hawajanifanya chochote dada ni watu wazuri"akajibu Joan kwa akili ya kitoto



    "Watu wazuri wangekuteka wakati nimelala? Niambieni mnataka nini?"akasema Shmim



    "Kazi ndogo tu,tunahitaji kukupa mafunzo ya uaskari ukafanye kazi yetu na sisi tutamsomesha Joan na kukufanya uishi maisha ya kitajiri,sisi hatuna shida ya kukubaka ka wale wahuni bali tunahitaji kuyabadilisha maisha yako na uishi kwa aman"wakamjibu



    "Na nikikataa kufanya kazi yenu?"akauliza



    "Tutamuua Jon hapa mbele yako na pia tutayafanya maisha yako machungu mara kumi zaidi ya sasa mpaka ukikubali kwa hiyo bora ukubali pasipokulazimishwa"wakamjibu



    "Dada kubali tu wasije wakaniua! Mbona sio watu wabaya?"akasema Joan



    Shamim alifikiria mara mbili mbili

    Hakutaka Joan afe na pia aliangalia umri wake endapo wale watu wakihitaji kutumia nguvu hataweza kushindana nao akaona akubali tu



    "Kama kweli wanayosema ni kweli acha niende tu nikishajifunza nikajua nitawageuka na kuishi mwenyewe na pia kulipa kisasi kwa wanaume"akawaza



    "Nimekubali"akajibu



    Lilikuwa jibu lililowafurahisha sana wote pale ndani



    Shami alipelekwa kwenye chumba maalum na huko akakuta mdada mrembo aliyempeleka na kumuogesha mpaka akatakata kisha akamvalisha mavazi mazuri na kumrudisha



    "Tutamsomesha mdogo wako kwa kiwango unachotaka na pia ukifanya kazi yetu vizuri utafurahi"walisema



    Chakula kililetwa akala na kunywa mpaka akashiba



    Baada ya muda wakaletwa vijana wawili wenye umri sawa na Shamim na kukalishwa pamoja naye



    "Shamim kutana na Abdul na Majid hawa ni vijana wenzako mtakaoondoka nao kwenda Mombasa kesho kwa ajili ya kuanza zoezi letu"alitambulishwa



    Wale vijana wakasimama na kwenda kusalimiana na Shamim



    Yule aliyetambulishwa kama Abdul alionekana kumchangamkia Shamim ila yule Majid hakumchangamkia na alionesha chuki ya wazi



    Baada ya hapo Shamim alipewa nafasi ya kushinda chumbani na Joan kwa mara ya mwisho kabla ya saafari



    " Unaonaje tukitoloka mdogo wangu,na wasiwasi hawa watu si wema huko tuendako?"akasema Shamim







      Joan alishtuka kusikia Shamim akimwambia watoloke



    "Dada tutoloke? Tutatoloka vip hapa na unaona nyumba imezungushiwa umeme?"akauliza Joan



    "Kwa hiyo we unanishaurije?"akauliza Shamim



    "Dada mimi nakushauri tufanye wanavyotaka kwa sababu sio watu wabaya! Wamesema watanisomesha na wewe watakufanya tajiri kubali tu"akasema Joan



    Shamim alitafakari maneno ya mdogo wake kwa kina ikabidi akubaliane naye kwa sababu hakuona namna ya kumuwezesha kutoloka na pia hakuona kama wale watu ni wabaya kwake



    Walipiga story na Joan mpaka usiku sana ndipo wakalala mpaka kesho yake asubuh



    Waliamshwa saa moja asubuh na baada ya kunawa uso wakapelekwa sehemu ya kulia chakula wakanywa chai nzito



    " Ni wakati wako kumuaga Joan kwa sababu mtatengana kwa muda ila tunakuhakikishia atasoma na pia tutajitahidi muwe mnaonana"akasema kiongozi wao



    "Atasomea wap?"akauliza Shamim



    "Atasomea hapa hapa Tanga na ndipo utakapokuwa ukiletwa kumsalimia,tuna mtu wetu hapa atakayetusaidia kwa hilo"akajibu yule kiongozi



    Joan na Shamim walikumbatiana hukumachozi yakiwatoka kwa sababu ya kuachana



    Baada ya muda walifika vijana wale wengine akina Majid na Abdul nao wakaungana na Shamim kisha safari ya kuelekea Mombasa kutoka Tanga ikaanza



    Ilikuwa safari ndefu na ya kuchosha kwa mtoto Shamim ambaye hakuwahi mzoefu wa safari ndefu ndefu kama hizo



    Walifika wakiwa wamechoka sana na moja kwa moja wakapelekwa mtaa ulioonekana kukaliwa na matajiri sana kutokana na majengo yaliyokuwa hapo kuonekana ya kisasa zaidi



    Walipoingizwa ndani walimkuta mzee mwenye asili ya kisomali akiwa anasubiri na wakapokelewa kwa heshima zote



    MIEZI SITA BAADAE



    "boss vijana wameiva kwenye mazoezi ya kutumia viungo vya mwili nafikiri tuwahamishie kwenye kitengo cha pili"alisema kijana mmoja mwenye asili ya kisomali akimweleza yule boss wao Mahmoud



    "Nahitaji uthibitisho"akasema



    Kijana mmoja aliyeaminiwa kwa mapambano akaletwa mbele yao na kuamrishwa wapambane nao



    Majid aliyeonekana kuwa na kiherehere alienda kichwa kichwa na kurusha ngumi za haraka zilizopanguliwa vizuri na yule kijana



    Wakati Majid akipambana wenzake walibaki kumwangalia yule kijana kwa mshangao kutokana na uwezo wake



    Majid aliruka hewani kwa Fly kick ili kuvunja shingo ya yule kijana ila yule kijana akawa amemsoma na kumkwepa kisha akamsindikiza na teke kali la mbavu mpaka kuvunja mbavu za Majid akashindwa kunyenyuka



    Abdul alienda naye kichwa kichwa akakutana na ngumi moja ya pua ka kudondoka chini kisha akazirai pale pale



    Ikaja zamu ya Shamim kupambana



    Hakukurupuka kama wenzake

    Alimfata yule kijana na wakaanza kupambana kwa kusomana kwa dakika nne kisha alijikuta akifanya kosa la kutaaka kumpiga yule kijana kwa kupaa hewani na kuchana msamba ila akakutana na ngumi kali sehemu zake za siri akatulia



    "Hawajaiva wapeleke kwenye zoezi la pili ila kila jioni warudishe kwenye mapigano ya kutumia viungo! Nawahitaji hawa vijana watatu kwa ajili ya hii kazi hivyo lazima waive"akasema



    WIKI TATU MBELE



    " tayali nyie mmeshakuwa miongoni mwetu hivyo mnaweza jikuta kwenye wakati mgumu mbele ya askari au watu wengine

    Tuna ishara tunazotumia kwa ajii ya kupashana habari"akasema kuongozi wao



    "Mfano unaweza kuwa umekamtwa na tunahitaji kwasiliana na wewe

    Huwa tunatumia alfabeti kwenye mawasiliano



    Ukijikuta kwenye wakati mgumu basi chochote kitakachokuja kwako kwa maandishi hata kama ni gazeti tafuta code zetu



    Mf

    123456

    234575

    452564

    123484



    Hapo utachagua code kuingana na zinavyofatana kama kwenye msitari wa kwanza unachukua ya kwanza,wa pili ya pili,wa tatu ya tatu mpaka mwisho mfano hapo juu ungetoa 1324



    na hili

    STQHKI

    EHMSYO

    AGINSO

    ANHMAJK

    ANHDONJ

    NAHSJNHD

    BAHSTJI



    ukikusanya herufi kwenye hizo hapo juu kulingana na malezo yangu kwa kupitia herufi za kuruka misari utapata neno SHIMONI na moja kwa moja utaelewa tunachomaanisha



    Na pia mfano unaweza kushikwa na maadui zetu hapo itabidi utumie....."alikuwa akieleza



      "Lakin mimi naona hizo code ni rahisi sana polisi kushtukia"akauliza Shamim

    "Wee naye unajifanya unajua kila kitu watajuaje sasa?"akauliza Majid

    Majid alishaonesha upinzani kati yake na Shamim tangu wanaanza mafunzo yale na kuanza kuiva

    "Hayo niliyotoa ni mawazo yangu na wala hayakuhusu"akajibu Shamim

    "Siyapendi haya malumbano yenu kabisa,haya Shami toa mawazo yako"akasema kiongozi

    " Mimi naona hata mjinga akiona code lazima atashtukia kuszisoma kwa staili hiyo hivyo bora zingegeuzwa juu chini ili iwe ngumu kuzisoma"akasema Shamim

    "Nashukuru kwa akili yako kufanya kazi haraka hivyo ila nilikuwa sijamaliza kuelezea hizi code huwa tunazitumia kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe kwenye mishe zetu ila unapojikuta umeshikwa tuna mbinu mbadala"akaeleza

    " ukikamatwa na unahitaji kuwasiliana na sisi kutupatia ujumbe basi tunatumia ishara za alama mf = hiyo ina onesha kuwa mambo yameharibika tuwe makini, na => ukiweka hivyo unamaanisha kuwa kuna mmoja wetu keshatuchoma....."

    Aliendelea kutoa mafunzo mengi sana kwa siku hiyo na kulingana na sheria zao walipaswa kuyakalili siku hiyo hiyo

    Baada ya mafunzo yale walirudishwa na kupewa huduma zote za muhimu

    Jion walikuwa wamepumzika kila mmoja chumba chake



    Majid aliona dalili za Shamim kumzidi kete kwa cheo kati ya vijana wote waliokuwa wakikuzwa na wale Wasomali hivyo akaona dawa pekee ni kumuondoa dunian ili abaki huru

    Aliamka na kuelekea chumbani kwa Shamim kwa tahadhari asiweze kushtukiwa na mtu yeyote yule mpaka akafanikiwa kuufikia

    Katika moja ya mafunzo ya awali kabisa waliyopewa wakati wanajiunga ni mafunzo ya kuishi kwa hisia

    Hata pale unapokuwa umelala unapaswa masikio yako na hisia zako kuwa macho ili kujikinga na chochote kinachoweza kutokea

    Akiwa kwenye usingizi wa kawaida sana tena wa kujiegesha alihisi kama mlango wa chumba chake unafunguliwa tena kwa taratibu kiasi cha mtu wa kawaida asingeweza kushtukia

    Hakutaka kuonesha mshtuko hivyo alitulia vile vile kama amelala usingizi na kweli akahisi nyayo za miguu zikisogelea eneo lile

    Ghafla alihisi kivuli kikiinuliwa juu kisha kikashushwa chini ghafla kikiwa kimelenga shingoni kwake

    Shamim alijivuta kwa chini kwa nguvu na lile jambia la Majid likakata kitanda

    Shamim akabinuka na kusimama nyuma ya Majid na Majid akajua ameshafanya kosa kubwa kwa sababu alilenga kummaliza Shamim wakati akiwa usingizini kisha apotee

    Aligeuka na lile jambia kwa speed ili amfyeke Shamim tumbo ila akakutana na teke kali sana kwenye mkono wake na lile jambia likaangukia pembeni

    Majid akafanya kosa la pili akainama ili alichukue tena lile jambia kosa ambalo Shamim alikuwa analisubiria

    Alipoinama tu Shamim alitua kwenye shavu lake la upande wa kulia na bongea la teke



    "aaaaaaaagh!!!"Majid alitoa ukelele wakati akipepesuka na kuangukia meza ndogo ya kioo iliyokuwa pale ndani na ikapasuka vipande



    Upande wa pili boss wa hawa vijana waliokuwa wanapambana alikuwa na kikao na vijana wake watatu

    " Nahitaji vijana waingie kazini na huko tutaona ujanja wao na tujue nani anaweza kutufaa na ni yupi ni mzigo"alisema

    " sawa boss ila yule binti ni hatari sana,itabidi hata sisi tuwe makini sana kwani anavyoelekea atakuja kuwa hatari zaidi"akajibu mmoja wao

    " Hilo hata mimi naliona ila mimi nashauri tumboreshee mambo yake na atatufanyia kazi nzuri sana,pia tunaweza mtumia kuwanasa baadhi ya adui zetu"akasema

    "Panga mizigo ya kusafirishwa kesho kwenda Dubai na yule kijana wa Tanzania pia apewe mzigo mkubwa sasa kwa sababu uaminifu umeanza kuonekana"akasema boss

    "Sawa boss ngoja nikaandae ule mzigo kisha niwashtue wawe tayali kwa hili"akasema

    "Hapana mimi nashauri nenda uwalete hapa niongee nao na kuwaweka sawa kisaikolojia "akasema

    "Sawa boss"akajibu

    Kijana yule akaondoka na kwenda kuwafata ili waje kuonana na boss wao

    Alipofika kwenye chumba cha Majid hakukuta mtu

    Akaelekea kwenye chumba cha Shamim!!!



      Majdi alipepesuka na kuanguka kalibu na kitanda

    Akayasikilizia maumivu kwa sekunde kadhaa na kunyenyuka kwa hasira kali sana ili alipe kisasi

    Kitendo hicho ndicho alichokisubiria Shamim kwani alijua yule akinyenyuka atakuja na hasira kichwa kichwa bila tahadhari

    Majid alitupa ngumi yenye uzito wa kutosha kwa Shamim aliyeiona na kuipangua vizuri kabla ya kuachia konde kali sana kwenye mbavu za Majid akakgugumia kwa maumivu na kuanguka chini

    Shamim akajiandaa kummaliza kabisa Majid kwa kuruka juu na kurudi na viwiko vya magoti ili atue tumboni kwa Majid

    Ghafla kitendo bila kuchelewa alijikuta akitandikwa teke mbili za tumbo akadondokea pembeni



    Yule kiongozi aliyetumwa kuwafata alipomkosa Majid aliamua kumfata Shamim

    Alipokalibia chumbani kwake ndipo akasikia vurugu za mapambano

    Alipochungulia ndipo alipomkuta Shamim akiandaa pigo ambalo aliwafundisha mwenyewe kwa ajili ya kummaliza adui akajua Shamim alidhamiria kummaliza Majid

    Akaamua kumwepusha Majid na kifo kwa kumsukumizia Shamim teke mbili za tumbo akiwa pale pale angani



    Shamim alipogeuka kuona aliyepambana naye akashangaa kumuona mkuu wao wa mafunzo ya mapambano ya ana kwa ana

    Akainuka haraka na kupiga magoti chini kisha akainamisha kichwa chake na kuonesha heshima

    Upande wa Majid alijalibu kunyenyuka ili kutoa heshima kwa mkuu wao akashindwa kutokana na maumivu aliyoyapata kwenye mbavu zake



    "Mambo gani haya mnafanya? Shamim? Majid umefata nini huku?"alifoka

    "Mkuu mimi nilikuwa najitetea kwa sababu mwenzangu alidhamiria kuniua"akasema Shamim

    "Nyamaza!!! Pumbavu sana nyie"akafoka



    Alimnyenyua Majid na kumtoa pale chumbani na kwenda naye nje

    "Na wewe nikukute chumba cha maongezi boss anakusubiri"akamwambia Shamim



    Shamim aliongoza mpaka chumba cha maongezi na kumkuta tajili akiwa kakaa anawasubiri



    "Vip mwanangu maisha yanaendaje?"akauliza

    "Yanaenda vizuri boss"akajibu Shamim



    Muda kidogo akaingia yule kiongozi wa mazoezi na mwanaume mwingine wameongozana

    "Boss itabdi Shamim aongozane na huyu Ally kwenda hukko"akasema

    "Kwanini? Na Majid yeye atafanya nini?"akauliza Boss

    "Majid nimemkuta chumbani kwa huyo Shamim na walikuwa wakipambana Shamim amemjeruhi vibaya ndiyo sababu ya kumuondoa kwenye safari"akaeleza

    "Ameumia kiasi kikubwa?"akauliza

    "Ndiyo ingawa sio sana,amevunjika mbavu mbili"akasema

    "Mwanangu nakuomba upunguze hasira kuna siku utakuja kuua mtu"akasema tajiri Mahmoud akimweleza Shamim

    "Mimi sina hasira boss ila alilenga kuniua ndiyo sababu nikajitetea"akajibu



    Maongezi yaliendelea huku Shamim akipewa maelekezo ya kazi ya uuzaji wa madawa ya kulevya na ubadilishanaji wa silaha waliokuwa wakienda kuufanya huko Dubai ili waje kuziuza kwenye vikosi vya Al shabab Somalia



    "Narudi tena! Uwe makini usionekane sura na pia kumbuka katika biashara nia yetu ni kutoka na mizigo yote miwili namaanisha tumepanga kumdhurumu"akasema boss

    "Nimekuelewa boss"akajibu Shamim



    Safari ikaandaliwa na mzigo mkubwa sana wa madawa ya kulevya ukapakiwa kwa ajili ya kusafirishwa kutoka Mombasa kwenda Dubai kupitia uwanja wa ndege ambao Mahmoud alishasambaza watu wake hivyo vijana wake walikuwa wanapita kirahisi huku mzigo ukivushwa na wale wale askari wanaohusika na ukaguzi bila kushtukiwa



    Siku ya safari Majid akiwa kachukia sana kutokana na kukosa safari aliyotegemea kumthibitishia boss wake kuwa anamzidi Shamim uwezo wa kazi akaikosa kwa kupigwa



    SIKU MBILI BAADAE



    Shamim alifunguliwa geti na kuingiza gari lake kisha akapaki eneo husika na kushuka kuelekea ndani

    Alimkuta boss akiwa kafura sebule nzima haikaliki kabisa

    Alikuwa akizunguka kutoka upande mmoja na kwenda mwingine huku akitoa matusi yote anayoyajua



    "mzigo ule ni mkubwa mno! Siwezi kuruhusu nitapeliwe kirahisi namna ile hata siku moja! Lazima mlipe kwa hilo Shamim!!! Shamim!!! Nilikuamin kumbe bora ningemwamin Majid i cant believe this u must pay"akafoka



      Alex ambaye ni kaka yako Junior akiwa kijana wa kitanzania aliyekulia huko kwenu Moshi na kuamua kuja Dar es salaam kutafuta maisha aliangukia katika mikono ya wauzaji wa madawa ya kulevya



    Alianza taratibu sana kupokea mizigo ya mabosi wake na kuisambaza mikoani huku akipata malipo mazuri na kujijenga kimaisha ila mwishowe akaunganishwa na wafanyabiashara wa nje

    Alex hakuwa na uwezo wa kuchukua madawa kwa pesa yake kutoka nje na uyaeta nchini Tanzania bali alikuwa akitumiwa kuyasafirisha kutoka huko kuja Tanzania

    Katika harakati zake hizo alijijengea jina kubwa kwa wale wauzaji wakubwa na kusababisha apate mbinu nyingi za uuzaji wa madawa

    Wale mabosi wake ambao walikuwa ni Waarabu waliokuwa wakiishi huko Urabuni walipopokea oda ya kupokea madawa ya kulevya na kuwauzia silaha wale Wasomali waliokuwa na Shamim aliwapangia mpango wale Mabosi wake jinsi ya kufanya ili wawatapeli akina Shamim ule mzigo

    Mipango ilienda kama walivyopana ila wao waliweka tahadhari ya kujua yawezekana na akina Shamim wakawa wanampango wa kuwazurumu kwenye mabadilishano

    Kosa walilofanya akina Shamim ni kutokuhisi kuwa wanaweza kugeukwa ila Alex na kikosi alichokuwa akikiongoza walichukua tahadhari mapema

    Shamim alipopewa maelekezo ya jinsi ya kuwahadaa wale Waarabu na kuondoka na mzigo aliamin kazi itaenda kuwa nyepesi

    "Ukishashuka uwanja wa ndege hakikisha mnafika eneo la makubaliano na wanafanikiwa kuuona mzigo halisi kwa sababu tutakupa mizigo ya aina mbili,halisi na usio halisi,wakishaujalibu na kugundua ni kweli nyie fanya kukataa kubadilishana siku hiyo"akasema boss

    "Sawa boss na je wakilazimisha tubadilishane? "akauliza Shamim

    "Wewe utabeba begi lenye madawa halisi wakati mnaenda na Abdul atabeba feki kisha utapanda gari yao na kuwaonesha mzigo kisha utaondoka nao,utapanga nao kubadilishana sehemu za bandarini ili wakukabidhi kontena zenye silaha zetu na uzikague zote kisha andikisha kila kitu na wapatie ule mzigo feki na wewe ondoka na kontena"akasema boss

    "Je wakiukagua tena pale pale na kugundua tumewahadaa?"akauliza

    "Kwenye mzigo Feki tumeweka bomu na Abdul ataliseti kabla ya kukupa na atabaki na remote ili ukishawakabidhi utafute namna ya kuwaacha umbali flani kisha Abdul atalipua na mchezo utaishia hapo"akajibu Boss

    "Sawa lakini wanaweza kutokufa wote na watakaobaki je?"akauliza Shamim

    "Ndiyo sababu ya kukupa mafunzo wewe na Abdul na yule mshenzi mwenzenu,mtakuwa na silaha za kutosha mtakazopewa na watu wetu tuliowapandikiza huko"akajibu boss

    "Uwanja wa ndege vip? Hatuwezi kupata shida?"akauliza Abdul

    " Kila sehemu tunayopeleka mizigo viwanja vilishasafishwa kabisa"akajibu

    Basi baada ya majadiliano na kuoneshwa mzigo na vifaa ya safari na kazi ile walipumzika na kusubiri safari yake kesho

    Asbuhi ya siku iliyofata Shamim alikuwa uwanja wa ndege mjini Mombasa kwa ajili ya Safari kwa kutumia shilika maarufu la usafiri wa anga Afrika mashariki la Kenya Airways kutoka Mombasa kwenda Nairobi kisha kupitia Cairo misri na kwenda Dubai

    " tufanye kazi bora ili tumfurahishe boss na kumfanya Majid aonekane si lolote,kkkiukweli simpenzi sana"alisema Abdul

    "Hata mimi simpendi kabisa sijui kwa nini tuko naye?"akajibu Shamim

    "Ila kuna siku yake! Nakuahid asipobadilika kuna siku atakuja kufa kwa mikono yangu mwenyewe"akasema Abdul

    Safari iliendelea huku wakipiga story kwa furaha sana na kutaniana kwa upendo kutokana na jinsi walivyoheshimiana

    Walifika Dubai baada ya mwendo mrefu sana na kushuka uwanja wa ndege walipokuwa wakitarajia kupokelewa na wenyeji wao

    Waliposhuka waliweka mabegi yao sehemu ya ukaguzi na yakafanikiwa kupita salama

    Timbwili lilianza mara baada ya kutoka nje ya uwanja ule wa ndege na kufanikiwa kuwaona wenyeji wao wakiwapungia mkono kwa ishara ya kuwapokea

    Walitembea kwa kujiamin kwa sababu walishafanikiwa kupenya kutoka uwanjani

    "Sor can we check your bag please but sor for it"waliskia sauti ikizungumza nyuma yao akimaanisha anataka kukagua mizigo yao

    Shamim alipogeuka alikutana na sura nne za kiarabu zikiwa zimevaa sare ambazo zilionesha ni za askari wa eneo lile

    Walitoa vitambulisho vyao kuthibitisha kuwa wao ni askari na si udanganyifu

    "Lakini tumeshakaguliwa ndani ya uwanja wa ndege"akajibu Shamim

    "Hilo sio tatizo dada,kumbuka ile ni mashine na inaweza kukosea hivyo tumewatilia mashaka tunaomba mizigo yenu yote tuikague"akasema mmoja wao



    "Tumekwishaaa!!!!"Shamim alijisemea taratibu



    Upande wa pili wa barabara kuna masterplan alikuwa anachekelea!!!!



     Shamim alijua wameshapatikana na hawana namna ya kujinasua kwenye lile tatizo lilowakabili ghafla bila kutarajia

    "Basi kama kuna tatizo naomba uingie kwenye gari tuongee mheshimiwa"alijalibu karata yake ya mwisho kwa kufanya ki2u ambacho kwa Tanzania ni maarufu sana kama kipoza roho na kimekuwa kikifanyika ili kujiepusha na matatizo na kwa sababu Askari wetu wengi masirahi yao ni kiduchu huku viongozi wakijilimbikizia mali nyingi

    "Hapana mama serikali yetu inatujali sana na wala hatuna njaa kiivyo,,we shuka ulete mizigo tuipekue ikiwa salama mtaenda"akajibu yule askari

    Shamim hakuwa na ujanja bali alishuka na Abdul wakatoa mizigo yao ikaguliwe

    Wale askari walifungua mizigo ile na kufanikiwa kukuta shehena kubwa sana ya madawa ya kulevya

    "Nini hiki dada? Mmeingiza madawa ya kulevya huku? Sisi tunahangaika kupambana na matumizi ya haya madawa ya kulevya kumbe nyinyi ndiyo mnaohusika?"alisema kwa hasira yule askari

    Shamim alimwangalia Abdul na kumwonesha ishara flani ya mawasiliano na kisha wakanyamaza bila kujibu chochote

    "Tunaomba mkapande gari ile pale twende kituoni"akasema yule askari

    Wakawa wapole na kwenda kwenye gari iliyoonekana kuwa ni ya polisi kabisa na ikaondolewa kuelekea pembezoni mwa mji

    Baada ya mwendo mrefu kidogo gari ile iliingia kwenye jengo dogo lililoonekana kuwa ni kituo cha polisi

    Walishushwa na kuingizwa ndani ya kituo na pale sehemu ya mapokezi walimkuta askari aliyewaandikisha na wakaacha ule mzigo pale ndani na kuingizwa kwenye chumba kidogo walichowakuta vijana wengine

    Walitulia mule ndani bila kujua hatma yao pale itakuwa nini hasa wakikumbuka kuwa bosi wao aliwaahidi kuwa pale uwanja wa ndege ana vijana wake na hawatasumbuliwa

    Baada ya kukaa pale ndani kwa zaidi ya nusu saa walifatwa na kufungwa vitambaa vyeusi machoni na kutolewa pale ndani

    Walipotolewa nje walipandishwa kwenye gari kisha likaondoka

    Mpaka mufa huo hawakuwa wameambiwa chochote kile cha kuwasaidia kutafuta namna ya kujinasua

    Gari lilitembea umbali wa kama saa moja na nusu kisha likasimama

    Wakatolewa kwenye lile gari na kukalishwa chini

    Wakati wamekaa pale chini wakashangaa wale waliowakalisha wanaondoka na kupanda gari walisikia tu gari likiondoka kwa kasi eneo lile

    Hawakujua kama wale watu wameondoka wote ama la!! Kwa sababu ya kufungwa macho na vitambaa

    "Abdul! Mbona kimya? Au wameondoka?"akauliza Shamim mara baada ya dakika tano kuisha hawasikii chochote

    "Hata mimi nashangaa kimya! Hebu nisogelee tufunguane"akasema Abdul

    Wakaanza kusogeleana mpaka wakafikiana na kukugasana ndipo wakageukiana na kushikana mikono na kuanza kufunguana kamba zile

    Shami alikuwa wa kwanza kufunguliwa ndipo akatoa kitambaa machoni na kumfungua na Abdul

    "Hapa tuko wap Shamim?"akauliza Abdul

    "Mmmmmmh!!! Tumetapeliwa Abdul! Wale sio askari"akajibu Shamim

    "Sio askari? Kwa nini? Na umejuaje?"akauliza Abdul

    "Huoni tumetelekezwa hapa!? Hawa shida yao ilikuwa yale madawa na wameyapata wameondoka na inavyoonesha watakuwa ni watu waliojua kila kitu kuhusu mzigo huu na nina wasiwasi ni wale wale tuliotaka kufanya nao biashara!"akasema Shamim

    "Mama yangu! Sasa tunafanyaje? Na boss tutamwambia nini? Si ndo Majid atapata cha kuongea kwetu?"akajibu Abdul

    "Yaan nimechanganyikiwa"akajibu Shamim

    "Huu mzigo ulikuwa mkubwa sana Shamim boss hatatuelewa cha msingi hapa tutoloke na tuishie mbali sana la sivyo atatua yule"akashauri Abdul

    "Hatuwezi kumtoloka Mafia! Ni ngumu! Utaenda wap ambapo hatakupata? Na labda nikuibie siri moja sisi tumeshapandikizwa cheap zenye GPS kwenye miili yetu tangu utoto na hatujui zilipopandikizwa kwamba tunaweza kuzitoa hivyo popote tutakapokuwa tutaonekana! "akajibu Shamim

    "Sasa tunafanyaje?"akauliza Abdul kwa wasiwasi

    "Hakuna zaidi ya kurudi Mombasa kwa boss"akajibu Shamim

    "Si atatua jaman?"akasema Abdul

    "Twende tu tutajua cha kufanya,akituua sawa ila asipotuua tutalipa kisasi"akajibu

    Ilibidi Abdul akubaliane naye ingawa alikuwa na wasiwasi sana

    Wakatembea kwa miguu mpaka walipopata barabara na kuomba lifti wakarudishwa mjini

    Uzuri wa safari za kwenda nchi za wenzetu tiketi zinakatwa kwenda na kurudi hivyo walirejea Mombasa salama

    Boss alikuwa kafura kwa hasira akiwasubiri!!!



      Ndege ya shilika la ndege la nchini Kenya ya Kenya Airways ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Moi Internation Airport katika jiji la Mombasa

    Milango ilifunguliwa taratibu na watu wakaanza kushuka mmoja baada ya mwingine

    Sura mbili moja ya kiume na moja ya kike zilionekana zikitokeza kwenye mlango wa ndege hiyo ila nyuso zao hazikuonesha hali yeyote ya furaha

    Walijua yawezekana hiyo ikawa siku hiyo inaweza kuwa ya mwisho hapa Dunian au kwa msamaha wa kiongozi wao wanaweza kupona hivyo walishuka na kuelekea kwenye milango ya kutokea eneo lile la uwanja wa ndege na kukaguliwa kama taratibu zinavyopaswa kisha wakatoka nje ya uwanja

    Pale nje waliwakuta vijana watatu akiwepo Majid wakiwa wamevaa suti nyeusi na wakiwasubiria

    Milango ilifunguliwa na wakazama ndani na magari yakaondolewa kwa kasi eneo lile

    Magari yale yaliishia kwenye mtaa wa watu wazito wa Miritini Estate na kuingia kwenye geti kubwa sana jeusi

    Gari ziliposimama walishuka na kuelekea ndani ya jengo hilo

    Walimkuta Mahmoud ambaye ni bosi wao aliyewaagiza katika safari hiyo

    "Nipe sababu tatu za uhakika zinazoniweza nisikuondoe Dunian?"akauliza kwa taratibu sana huku akionekana kuwa na hasira kubwa sana

    "Samahani bos naomba nafasi moja pekee"akasema Shamim

    "Unataka nafasi wakati umenifilisi Shamim? Si bora ningemuamin Majid? Shammm!!!"akafoka na kwa hasira akasimama

    "Take them to the place"akasema

    Walinyenyuliwa msobe msobe na kutolewa nje kisha wakaingizwa kwenye gari na safari ikaanza kutoka hapo kuelekea kwenye msitu wa Gedo forest ulioko nje kidogo ya mji ule wa Mombasa

    Safari ilichukua saa nzima na nusu kutokana na speed ya gari lile ikatumia njia ya mkato kuingia ndani ya poli lile

    Shamim alilifahamu lile eneo vizuri sana kutokana na kuwahi kufanya kazi kadhaa za mauaji eneo hilo kwa wale watu walioenda kinyume na zile taratibu zao hivyo alifahamu kuwa hakuna mtu anayepelekwa kwenye eneo lile na akatoka salama

    "Mungu nisamehe dhambi zangu zote na unipokee peponi"

    Alijikuta akisari peke yake kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya kigaidi hakuwahi kumkumbuka muumba bali mpaka hapo alijua kuwa hakuna namna ya kutoka

    Walipofika katikati ya msitu wa Gede walishushwa katika eneo mahsusi walilojenga kajengo kadogo sana ambako walikatumia kwa kazi hizo za mauaji

    Walishushwa na wakapigishwa magoti chini wakasubiri gari la mkuu wao mzee Mahmoud afike ili watimize lengo lao

    Kwa majid lile tukio alilifurahia sana kutokana na kujua kuwa Shamim akifa yeye atakuwa na nafasi kubwa sana katika utendaji wa kikosi kile

    Shamim alimuangalia Majid kwa hasira kuu huku Majid akimwangalia na kumjibu kwa kicheko cha kinafiki

    "Hhahahahahahahahah!!!! Ulijiona mjanja sasa umepatikana na kwa sasa huna ujanja lazima ufe"alisema



    Upande wa pili kilichotokea ulikuwa ni mchezo mdogo sana uliopangwa kitaalamu na Alex mwenyewe

    Aliwapa program nzima wale mabosi wake jinsi atakavyocheza ule mchezo nao wakambariki kwa kumpatia pesa aliyohitaji

    Alikipata kile kituo cha polisi na mkuu wake na askari wa zamu wakapokea fungu lao na kazi ikapangwa vizuri sana

    Wakati Shamim na Abdul wanakamatwa pale uwanja wa ndege Alex alikuwa sehemu katulia kwenye gari akiangalia ule mchezo unavyokuwa

    Alifatilia ule msafara mpaka pale kituo cha polisi na walipoingizwa ndani ya selo ile yeye akafika pale mapokezi na kupewa ule mzigo kisha akawakabidhi vijana watatu wa kufanya ile kazi

    Baada ya muda akina Shamim walitolewa ndani na kukabidhiwa kwa wale vijana kisha wakawapeleka nje kabisa ya mji na kuwatelekeza kisha wakarudi

    Wakati akina Shamim wakipelekwa kwenye msitu wa Gede nje ya mji wa Mombasa Alex akiwa na matajili wake walikuwa nje kidogo ya mji wa Dubai wakishelekea ushindi mkubwa walioupata wa kuwaua ndege wawili kwa jiwe moja tena kirahisi sana

    Walikunywa na kula huku wakimsifu Alex kwa kitendo kile



      Alipofika eneo lile Mohmoud aliwaangalia akina Shamim pale chini walipokuwa wamefungwa kwa muda kisha akatema mate kwa hasira

    "Unapaswa kufa Shamim! Huwa sina nafasi ya pili kwa anayefanya kosa kwangu"akasema

    "Najua hilo bosi ila naomba nafasi moja kukuthibitishia uwezo wangu na pia kukurudishia mzigo wako na baada ya hapo unaweza kuniua"akasema Shamim

    "Unaniahid nini?"akauliza Mahmoud

    "Kila kitu chako kitarudi at the right time boss naahidi"akajibu

    "Ok, kuna taarifa nimepokea kutoka kwa vijana wetu walioko kule kuwa kuna kijana yule niliyekuonya mwanzoni kuwa anashilikiana nao,yule Mtanzania kuwa ndiye aliyecheza mkanda mzima hivyo ili kupata chochote juu ya ule mzigo lazima tumtumie yule kijana"akasema Mahmoud

    "Huyo kijana yupo Tanzania? Au kule?"akauliza

    "Yupo kule bado ila makazi yake yako Dar es salaam ila wasiwasi wangu ni kuwa yawezekana ameikariri sura yako"akasema

    "Hapana sidhani inaweza kutokea kirahidi hivyo kwa sababu nilivaa miwani ila niamin boss siku chache nitakupa jibu nipe nafasi"akasema

    "Sawa wafungueni kamba nakupa nafasi moja ya mwisho fanya kazi kadri ya uwezo wako"akajibu

    "Usiwe na wasiwasi na mimi boss"akajibu

    Walifunguliwa na kurudishwa eneo lililokuwa na kambi yao kisha taratibu za safari ya Shamim ikapangwa

    Shamim alipelekwa saloon ya kisasa zaidi na kutengenezwa vizuri ule ukakamavu wake ukaondolewa na kutengenezwa vizuri kwa wiki nzima

    Baada ya matengenezo ya wiki nzima Shamim alibadilika sana umbile lake likaonekana sawia

    Uzuri wake ambao haukuwahi kupakwa poda wala make up yeyote kwa muda sasa ukang'aa sana na akaonekana mwanamke mzuri sana tena wa shoka ambaye akipita mbele ya mwanaume yeyote yule rijali lazima ageuke kumtazama



    Siku nne baadae ndani ya Supermaket moja Dubai ya Hareeous David alikuwa akitoka ndani ya jengo hilo baada ya kununua mahitaji yake muhimu ndipo akiwa anachezea simu yake aligongana na mtu

    "Ooooh! Sor m...."hakumalizia kutamka baada ya kunyenyua sura yake ili aone yule aliyemgonga ni nan?

    Mashalaaaah!!! Alikutana na binti wa kiafrika zaidi anayejielewa kuwa ni mzuri hasa kutokana na sura na umbo zuri sana alilojaliwa

    Aliganda akimwangalia yule mdada kwa makini kuanzia juu mpaka chini akajikuta mate ya uchu yakimtoka

    "Majitu mengine bana,sijui hayajielew! Hata halioni linapoenda"aliongea maksud kiswahili yule binti ingawa alifahamu kabisa kuwa wapo nchi ya watu na sio kila mtu mweusi aliyepo eneo lile ni mswahili ila alikuwa kazini na alitaka kucheza na akili ya David

    Yule binti alipotamka hivyo alisonya kwa nguvu kisha akageuka na kuondoka

    "Aaa! Wewe ni..."David hakumalizia kutamka kwa sababu aliyekuwa akiongea naye alikuwa keshapotelea ndani

    Akaganda akitazama kiuno cha yule mdada kilivyoumbika

    Kila alipokuwa akisogeza hatua yake moja kilikatika na kuligawa umbile lake vizuri sana

    "Hapa tutapona kweli mungu wangu? Mtoto kaumbika balaa na kumbe mswahili! Wallah simuachi"alijisemea

    Alitoka nje alipanda kwenye gari lake na kusubiri yule binti atoke ili amfatilie nyendo zake na kumfahamu ili aone kama anaweza fanikiwa

    Kama mpango ulivyoenda ndivyo ulivyofanyika

    "Mpuuzi anafanya tunavyotaka toka tuondoke"alisikiliza simu yake yule mdada akipata maelekezo

    Haraka akageuza na kwenda kupanda kwenye gari iliyokuwa ikimsubiria pale nje

    David alimwangalia yule binti akiingia kwenye ile gari

    Akasubiri ile gari ilipoondolewa na yeye akaanzza kuifatilia taratibu

    "He is working arcoding to our plan boss"aliongea yule binti kwenye simu

    "Nenda mpaka Swiz airways"akasema yule binti akimpa maelekezo yule dereva wake

    Gari ilielekea sehemu yenye ofisi ofisi

    David aliifatilia ile gari mpaka ikafika sehemu na kupaki yule binti akashuka na kuzama kwenye ile ofisi ya ndege na baada ya muda akatoka

    David alishuka na kuingia kwenye ile ofisi

    "Samahani kuna kitu nataka kupata taarifa zake nje ya utaratibu"alimwambia mdada wa mapokezi huku akitoa noti zenye thamani ya dola hamsin na kumkabidhi

    "Nahitaj kufaham huyu binti aliyetoka hapa alikuja kufanya nini?"aliuliza

    "Alikuja kukata tiketi"akajibiwa

    "Kwenda wap?"akauliza

    "Kwenda Tanzania"akajibiwa

    "Naomba kwa gharama yeyote nipate tiketi ya pembeni ya huyu binti na pia ya siku moja ya kusafiri naye tafadhali"akasema



     Mara baada ya kutoka kwenye zile ofisi za kukatia tiketi Shamim alipanda gari na kumpa maelekezo Abdul kuwa aendeshe kidogo kisha ashuke na kufatilia atakachokifanya Alex

    Alipoendesha na kufika sehemu akapaki na kushuka chini akimwacha Shamim akiendelea na safari

    Alex alirudi na kujibanza sehemu akiangali zile ofisi akamuona Alex akitoka ndani na kupanda gari kisha akatokomea

    Na yeye akaelekea kwenye zile ofisi na kumshawishi yule mhudumu kwa rushwa akapata taarifa za Alex

    Alex alirudi kwenye chumba alichopangiwa na wale mabosi wake na kupumzika akisubiri malipo yake na kisha arudi Tanzania

    Alipotulia alikosa usingizi kabisa kwani sura na ule urembo wa yule mdada uliendelea kumsumbua kila wakati

    Alitaman kuwa naye pale kitandani ili apate nafasi ya kuufaidi ule uzuri wake

    "Nikimpata yule demu natangaza ndoa! Silazi damu kabisa"aliwaza akiwa peke yake

    Siku mbili baadae Alex alikuwa kwenye uwanja wa ndege na wale mabosi wake kwa ajili ya safari ya kurudi Tanzania

    Aliagana nao mara baada ya kumkabidhi kilichochake na maagizo machache ya biashara yao kisha akaelekea sehemu ya kusubiria ili waondoke

    Akiwa amekaa pale alijalibu kuzungusha macho yake huku na kule ila hakumuona yule mdada

    Baada ya dakika chache alishangaa kuona watu wote waliokuwa wamekaa eneo lile wakigeuza macho yao kuangalia mlango wa kuingilia eneo lile

    Na yeye alipogeuza macho yake kutazama kule alistaajabu ya musa mara baaada ya kumuona yule yule mdada aliyekuwa akimsubiri

    Akiwa kavaa miwani ya jua iliyoonekana kuwa ya gharama huku shingoni akiwa na cheni ya dhahabu na akiwa kavaa blauzi iliyoacha tumbo na mgongo wazi na kisketi kifupi kilichoacha mapaja yake wazi

    Shamim alikuwa kapendeza sana kiwango cha watu wote waliokuwa pale wazungu kwa waafrika kumwangalia kwa macho ya matamanio

    "We mtoto ukikosea ukaingia kwenye kumi na nane zangu hatatoka! Lazima nimuoe"aliwaza

    Shamim alimpita kama hamuoni na kwenda kukaa kwenye benchi lililokuwa upande wa pili kutoka pale Alex alipokuwa

    Alipotoa miwani yake alimwangalia Alex kisha akageuza sura yake bila kumwongelesha kama hawajawahi kuonana

    Muda wa kuondoka ulipofka walielekezwa sehemu ya kupitia wakaelekea huko na baadae wakapanda kwenye ndege

    "Samahani dada umekaa kwenye siti yangu"Alex alimwambia Shamim

    "Hee!! Wewe tena? Haya pita"alijifanya kama ameshtushwa na Alex kukutana naye kwenye ndege

    Alimpisha Alex akapita na kukaa kwenye siti ya upande wa dirisha na yeye akakaa upande wa pili

    "Habari yako?"Alex alijitutumua na kusalimia

    "Nipoa vip na wewe kumbe ni Mtanzania?"aliuliza kama hajui vile

    "Tena haswa! Za tangu siku ile?"akauliza Alex

    "Sitaki kuongea na wewe kwa sababu siku ile uliniudhi sana kwa kunigonga maksudi"akajibu Shamim

    "Nisamehe dadangu,haikuwa maksudi bali bahati mbaya,nilijisahau na kuchezea simu"akajitetea Alex

    "Nimezidi kuchukia kwa sababu kumbe ni Mtanzania mwenzangu ndo ulinifanyia ubaya huku ugenini badala ya kuwa na urafiki?"akasema

    "Nisamehe tafadhali,ilikuwa bahati mbaya,by the way naitwa Alex mwenyeji wa Moshi ila mfanyabiashara wa Dar"alisema Alex akimpa mkono

    "Naitwa Lily ni mwenyeji wa Tanga ila mkaaji wa Dar na mjasiriamali"alijibu huku akiupokea mkono wa Alex

    Kwa Alex hiyo ilikuwa hatua kubwa sana kuelekea kumchukua Shamim aliyejiita Lily kwa sababu za kikazi

    "Vip Dar unaishi eneo gan Lily mrembo?"akauliza huku akichombeza

    "Mmmmmmh! Mrembo ntakuwa mimi? Hujawaona akina Wema?"akajibu

    "Hapana Lily wewe ni mrembo kiwango kikubwa sana hata hao unaowasema hawafiki kwako"akatoa sifa yeye akiamin anamlewesha Shamim

    "Ahsante ila me naishi Masaki"akajibu

    "Naomba unitembelee basi kwangi Kinondoni tafadhali kama hautajali"akatupa ndoano tena Alex

    Shamim aligeuka na kurembua jicho lake kama alivyoelekezwa na kocha wake kuwa jicho lake ni silaha ya kumuua mwanaume yeyote yule

    " aaaaah....



      Mahmoud alipopewa mpango wote wa namna ya kufanya aweze kurudisha mali zake na Shamim aliupenda

    "Niko tayali kutumia gharama zote kwako ilimradi unirudishie hizo mali zangu Shamim"alisema Mahmoud

    "Usijal boss i promice"akasema Shamim

    Maandalizi yalianza na akatafutiwa wamama waswahili haswa na wakamfunza mambo mbalimbali juu ya mapenzi na namna ya kumshika mwanaume yeyote yule hata kama ni Osama asiweze kufurukuta mbele yake

    Pia akapata nafasi ya kurembwa na kubadilishwa ule mwonekano wake wa kibabe na kuwa mlaini ndipo akapewa pesa na kila alichokihitaji na kuondoka kuelekea Dubai kukamilisha mpango wake kwa Alex

    Shamim na bosi wake waliamin kupitia Alex watajua namna ya kuwapata wale mabosi na kuzirudisha zile mali



    Lily au Shamim kwa jina asili walishuka kwenye uwanja wa ndege wa JK Nyerere wakiwa marafiki wakubwa na wenye ahadi ya kutembeleana

    Kila mmoja alipanda usafiri uliomfata eneo lile na kisha wakaondoka

    Upande wa Shamim alifikia kwenye nyumba aliyopangiwa kuitumia ikiwa na kila kitu katika kazi yao

    Alipofika aliingia kwenye chumba maalumu cha kazi na kukuta vijana watatu waliobobea kwenye teknolojia ya mawasiliano na computa wakicheza na kila kilichokuwa kikiendelea

    "Nimeweka tracking device GPS kwenye koti lake nafikiri mmeipata?"akauliza

    Wale vijana waliwasha screen moja kati ya zile na ikaonesha upande wa Alex akishuka kutoka kwenye gari na kisha kuingia ndani

    Mara baada ya kuingia alitoa simu yake na kupiga

    "Nimefika salama boss"alisema

    " Hey!...hey!....pz try to track all conversation from the caller pz"alitoa maagizo Shamim

    "Wor out boss but huwezi kuyasikia kwa sasa ila akimaliza everything will be revealed"akajibiwa na yule kijana

    Pale pale yule kijana akacheza na laptop yake alama nyekundu ikaonekana kwenye ile screen

    "okey...... Yes bos.....where?.......Deraj street?....ok.... Sunday evening... I will be there bos..thenx"akakata simu

    Mara baada ya kukata ile simu alielekea chumbani na kutundika koti lake kisha akaelekea kuoga

    Shamim na vijana wake waliirudia ile recordin ya mawasiliano ya Alex na wale mabosi wake na kupata picha nzima

    "Bos jumamosi napaswa kuwa Dubai nahitaji vijana wanne akiwe Abdul ila sitamhitaj Majid kwa ajili ya kazi.hawa jamaa watakutana na wanunuzi siku ya jumapli na huyu mshenzi atakuwepo"akamwambia

    "Shamim"akaita boss

    "Una ile dawa ya akili?"akaulizwa

    "Ndiyo boss"akajibiwa

    "Nenda kafanye mapenzi na huyo kijana we need more detail nakufahamisha tu sio kila kitu ni rahisi kama unavyofikiria it may be a trap"akasema Mahmoud

    "Boss do u think after sex he will reveal everthing to me?"akauliza Shamim

    " Plus drug tutapata kila tunachohitaj"akasema boss

    "Sawa mkuu"akajibu Shamim

    Baada ya kuongea na kiongozi wake Shamim aliwaambia vijana wake wajiandae na safari ya kwenda nyumbani kwa Alex usiku wa siku hiyo ili kumpatia ulinzi wa uhakika wakati akifanya kazi yake

    Aliendelea na shughuli zake na kisha akaingia kupumzika kwa sababu alijua usiku kuna shughuli nzito ya kufanya

    Jioni ya siku hiyo alimpigia simu Alex

    "Jaman nimekumiss"aliongea simu ilipopokelewa

    "Waooooh! Njoo nyumbani jaman"akajibu Alex

    " Poa nielekeze nakuja saa mbili"akasema

    "Mwambie dereva wako akulete Sinza bamaga kisha mnipigie niwaelekeze"akasema

    Shamim akajiandaa kwa safari ya kwenda kwa Alex kwa madhumuni mawili kufanya mapenzi na David ili amchanganye na kupata siri nzito ya wale Waarabu wa Dubai na pia kupata mzigo wa bos wake

    "Second room after the kitchen kwenye dari kuna ubao umerudishiwa, its a chember itumieni kuingia juu na kila kitu kitakuwa hapo"aliwapa maagizo vijana wake

    " catch you boss and we are ready"wakajibu

    Safari ikaanza Shamim akiwa na dereva wake huku nyuma kwa umbali wa mita mia mbli wakifata wale vijana wake

    Walipokelewa na Alex na kuelekea nyumbani kwake Mikocheni

    Walipofika dereva wa Shamim aliondoka na Alex akabaki na Shamim

    Shamim alikuwa kapendeza sana lakini maksudi kwa ajili ya kuikamata akili ya Alex yale mafunzo ya kimapenzi aliyopewa na style zote za kalichumbage.kitotatota na kindundunye alikuwa anaenda kuzifanyia practical tena akiwa anategemewa kutoka na habari nzito itakayosaidia mali za bosi wake zipatikane.



     Lily alipokaa sebuleni hakuzubaa alizungusha macho yake kijanja pale bila kushtukiwa na Alex mpaka akafanikiwa kuziona kamera zikiwa zimetanda pale ndani na akajua moja kwa moja kuwa ile nyumba itakuwa imezungushiwa kamera pia kila upande

    "Nisubiri kidogo mrembo"akasema Alex

    Alipoondika tu Lily au Shamim akatoa kifaa kidogo mfano wa kalamu na kufanya mawasiliano

    "Pz asiingia mtu kwanza humu mpaka niwape majibu kuna camera kila upande"akasema taratibu

    "Boss tubep na simu yake tunaweza kutegua kamera hizo"akajibiwa

    "Ok"akajibu

    Alitulia mpaka Alex aliporudi na kumkuta akimsubiri

    "sor kwa kukuacha peke yako ila kalibu kinywaji"akasema akimkabidhi

    "Usijal ila naomba simu yako dakika moja nimtumie sms msaidizi wangu kumpa maagizo"akasema Lily

    "Haina haja ya kutuma sms mpigie tu"akaongea akimpatia simu

    Shamim au Lily alichukua ile simu na kupiga namba yao ya kazi ikaita kisha akajifanya kuongea

    "Jitahidi kuwa makini na vitu vyangu"aliposema hivyo alikata

    Vijana wale mara baada ya kuipata simu ile wali activate vifaa vyao kwenye mashine waliyokuwa wakitembea nayo kwenye gari na kucheza na satelite na kuona kamera zote zilizokuwa zimetegwa ndani ya nyumba ile na wakafanikiwa kuzizima

    "Tumemaliza boss sasa unaweza kumtoa tufanye yetu"wakatuma sms kwa Shamim

    Shamim alipoipata ile sms alitafuta namna ya kumuondoa Alex pale ndani

    "Nimetoka kwangu sijala unaonaje tukienda Makumbusho na kula kidogo kwa sababu najua wewe ni bacherol"akasema

    "hapo umenena"akajibu

    Wakanyenyuka na kutoka kwa gari la Alex

    kwa sababu nyumba ilikuwa imefungwa waya za umeme na kuwa na kamera haikuwa na mlinzi

    Walipotoka pale nje wale vijana wa Shamim waliwaona na walipowap+ta tu wakaruka ukuta ule na kuzama ndani

    Shamim alienda na Alex mpaka Makumbusho kisha wakaagiza nyama choma kwa ndizi za kutosha wakala na kunywa mpaka wakashiba

    "Alex nikwambie kitu"akasema

    "Niambie mrembo"akajibu

    "Naomba usinifikirie vibaya jaman"akasema

    "siwezi mama nambie"akasema

    "Ni ngumu kwa mwanamke kusema ila ukweli nimetokea kukupenda sana,nahisi kukutana kwetu kuna maksudi flani"akaongea mkavu wa macho akimwangalia Alex

    "Nashukuru kusikia hivyo ila hata mimi nakupenda sana tena sana na nilishapanga kukwambia leo! Na nitafurahi ukiwa mke wangu"akajibu

    "Ahsante kama na wewe unanipenda baby twende kucheza mziki basi"akajibu kwa maksudi kwa sababu mpaka muda huo alikuwa hajapata majibu kutoka kwa vijana wake kama wamemaliza kazi ili warudi nyumbani

    Walicheza mziki kama dakika tano hivi na ujumbe ukaingia kwenye simu ya Shamim

    "Tumepata vitu vingi ila hatujapata cha kutusaidia juu ya mzigo hivyo tunakutegemea"meseji ilisema

    "Niachie vifaa hapo ndani niingia kazini"akajibu

    Pale pale akamwomba Alex waondoke kwa sababu alikuwa na hamu naye sana

    Waliondoka na kuelekea nyumbani

    Walipoingia ndani Alex alielekea kwnye korido na kubonyeza namba flani akagundua hali ni shwari kwenye nyumba yake bila kujua adui wake ndiye aliyekuwa naye pale

    Walielekea chumbani na kwa papara alizokuwa nazo Alex alimparamia Shamim ili waanze shughuli

    "Mbona papra baba? Tulia basi twende taratibu"akasema

    Alex akatulia na kumwacha Shamim afanye anavyotaka

    Alimvua nguo zake zote na kisha na yeye akavua nguo zake zote na kisha akambeba mgongoni na kumpeleka bafuni

    Alipomfikisha alimlaza kwenye sinki la kuogea kisha akatoa kiwembe cha topazi ambacho ni miongoni mwa vifaa vya kazi alivyowaambia vijana wake wamuachie

    Wakato Alex akishangaa alitanuliwa miguu kisha msitu wake wa solondo ukaanza kuondolewa taratibu wakati akitekenywa

    Alex alihisi anapaa angani kutokana na utam wa kuondolewa ule msitu

    Mara baa ya msitu kuisha Shamim alivua kyupi kyake na kuanza kumsugua Alex sehemu mbali mbali za mwili wake

    Alex aliendelea kufurahia zile raha alizokuwa akizipata

    "Nataka nikupe kitotatota unaijua?"akauliza Shamim

    "siijui mama nipe mambo jaman mwenzio"akajibu Alex



      Shamim alimbemba Alex na kumtoa kwenye sink lile na kumsimamisha kisha akajaza maji kwenye sink na kuachia sabuni na kumrudisha ndani yake akimlaza chali kisha akaukamata mhogo wa jang'ombe na kuubugia mdomoni kisha akaanza kuumung'unya taratibu ila kwa kubadilisha mikao huku vidole vyake vikizama masikioni na kuyachezea

    Alex alijihisi anapaa angani kwa raha alizokuwa akizipata akabaki kugugumia kwa raha

    "Utaniua mama!"alibaki kusema taratibu

    "Sitakuua baba ila hutanisahau"akajibiwa

    Aliendelea kunyonya ule mhogo kwa muda huku mikono ikiendelea kusambaa sehemu mbalimbali

    Kisha akaamua kupeleka pigo la mwisho kwa kuchukua maandazi mawili yaliyokuwa chini ya mhogo na kuanza kuyang'ata kijanja na taratibu bila kumuumiza kwa muda

    Kile kitendo kilipokuwa kikitokea Alex alihisi akielekea kufika mshindo na Shamim alipogundua akaamua kuumeza tena na kuongeza kasi ya kucheza nao mpaka Alex akamaliza

    Shamim akamtoa kwenye sink na kuingia yeye kisha akabinuka na kutengeneza style ya kitotatota

    Alex alibaki amepigwa na butwaa kwa sababu ile style ndiyo mara ya kwanza kuiona tangu amezaliwa pamoja na kujiamin kuwa ni nguli wa mapenzi

    Alibaki kumwangalia akijiuliza hivi akifanya akiwa vile si atamuua mtoto wa watu ila Shamim akaanza kulalamika Alex aanze

    Alex akasogea na kuzamisha kisha akaanza kushughulika kwa kasi

    Kama alijua atamuumiza Shamim alikosea

    Pamoja na mkao ule kuwa hatari Shamim alijua nini anafanya hivyo alimgeuza geuza na kiuno pale pale Alex mpaka akabaki kushangaa

    Alipata utam ambao hajawahi kuupata maisha yake yote

    Shamim alilenga kabisa kummaliza Alex kwa kubadilisha mikao pale ya ile style ya kitotatota mpaka Alex anamaliza hakuwa na nguvu japo za kusimama

    Alianguka chini na Shamim akambeba na kumrudisha kitandani na kumlaza

    "Pole sana baba kwa shughuli nzito mwaaaaah!"alisema Shamim huku akiinama na kumbusu maskioni Alex

    Alex aliruka juu kama kapigwa na shoti kisha akarudi kulala akiwa hana usemi

    "Babaaa"akaita Shamim taratibu

    "Mama sina hali mama niko hoi"akajibu

    "Usijal subiri uone"akasema Shamim

    Alinyenyuka na kuchukua jagi na kuchemsha maji kisha akayaweka kwenye kidishi kidogo na kuchukua kitambaa na kukilowanisha maji ya uvuguvugu

    "Geuka ulalie tumbo baba nikutoe uchovu"akasema Shamim

    Alex akigeuka na kisha Shamim akamkalia kiunoni na kuanza kumchua taratibu na kile kitambaa sehemu mbali mbali za mwili

    Alex aliona kama anayotendewa ni zaidi ya kawaida

    "Baba naomba kuuliza"akasema Shamim

    "Naomba kwanza unijibu mama huna mwanaume?"akauliza

    "Mimi ni mwanamke mfanyabiashara na sio kahaba! Na wala usinifikirie hivyo ila nimekupenda na nahitaji kuwa na wewe ndo maana nikakupa utam wote baba! Sasa je utanioa?"akauliza

    "Hata kesho ukitaka mama nakuoa sijawahi kupata raha kama hizi"akasema

    "Nitashukuru sana baba na nakuahidi kukupa mapenzi matam sana unajua nilishaumizwa sana hivyo sihitaji kuumizwa tena"akadanganya Shamim

    "Usijal mama"akajibu Alex

    "Baba kwani unafanya shughuli gan? Na ulikuwa umefata nini Dubai?"akasema Shamim

    "Mama nilikuwa kwenye biashara zangu na nafanya biashara za vinyago"akadanganya

    Shamim alikuwa ameshafaham sehemu yenye matata kwa Alex hivyo alichofanya ni kuipeleka ile taulo laini kwenye shingo ya Alex na kuanza kuisugua taratibu huku akipitisha na vidole vyake kwenye ile shingo na kuitekenya kidogo

    Alex alianza kulegea na kuishiwa nguvu akabaki kuhema na Shamim alipoona hivyo akaongeza majonjo

    "Niambie ukweli baba kumbuka naenda kuwa mkeo"akaongea kwa kubana pua Shamim

    "Niahidi utafanya siri mama"akasema Alex

    "Naahidi mme wangu kipenzi"Shamim aliongelea kwenye sikio la Alex huku akimpumulia taratibu sikion mpaka Alex akachanganyikiwa

    "Mama kuna biashara nawasaidia waarabu flani kule Dubai na hata juzi juzi kuna mzigo wa maana tumeupiga kutoka kwa Wakenya flani wenye asili ya Kisomali umenilipa vibaya sana"Alex akaanza kubwabaja



    Hicho ndicho alichokitaka Shamim akazidisha mbwembwe!!!



      "Kwani mnawatapeli vip hao mazoba na ni mzigo gan?"akauliza kimtego huku akimtekenya tekenya kijanja Alex

    "Wale waarabu wanauza silaha kwa Wasomali na wale Wasomali wanawapa madawa ila mimi sihusiki na wananitumia kama masterplan wao na hata mchongo wa sasa nimeupanga mwenyewe mpaka kuwaingiza mkenge wale mazoba"akajibu

    "Kwa hiyo huo mzigo mnao nyie? Na umekuingizia sana pesa?"akauliza tena

    "Kiasi flani umeniingizia pesa ndefu mpaka nafikiria kuachana nao wale waarabu na huo mzigo ni mkubwa sana nasikia wale waarabu wanakalibia kuupiga bei kwa wamexico flan"akajibu bila kujua

    Shamim au Lily akainama na kumbusu sikioni kisha akapeleka ulimi wake mdomoni mwa Alex

    Alex akapewa bonge la denda na kujikuta akisisimkwa mwili mzima

    "Watawauzia Wamexico? Na biashara itafanyikia wapi?"akauliza kimtego mara baada ya kumlainisha

    "Biashara itafanyikia kwenye kisiwa kidogo kiko nje ya mji kinaitwa Lisla ila mimi sitaenda kwenye biashara kwa sababu hiyo hakuna utapeli ni biashara halali na mimi huwa wananitumia kwenye utapeli"akasema

    Maneno aliyokuwa akiyataka Shamim ndo hayo

    Alipoona amejua kile alichokuwa kikitaka kwa wakati ule alimgeuza Alex na kumbinya shingoni kitaalam mpaka Alex akapoteza fahamu

    Alitoka kitandani kisha akavaa nguo zake na kisha akaufata mkoba wake

    Kwenye mkoba alitoa simu yake na kisha kucheza na teknolojia na zile camera zilizokuwa kwenye kile chumba zikazima

    Alipoona zile camera zimezima na haziwezi kumrekodi akampigia simu bos wake

    " Lisla island no location and the deal will be done there boss"akasema

    "Where are you now?"akajibiwa

    "Still with that bogus"akajibu

    "How is he? Is he the one who told u?"akajibiwa

    "he colapsed after ringer hint now i have to leave"akasema Shamim

    "No we still need him! Sleep there and tommorow we will begin the game"akaambiwa na simu ikakatwa

    Ikambidi Shamim arudi kitandani na kulala kwa sababu ya maelezo ya bosi wake aliyoona yana mantiki akiondoka anaweza kumshtua Alex na kuwapa taarifa wenzake wakabadili kila kitu na mchezo ukawa umehalibika

    Walilala mpaka asubuhi na Alex alipoamka hakukumbuka chochote kilichotokea kabla ya kulala

    Waliagana asubuhi hiyo Shamim akidanganya kurudi tena



    Siku mbili baadae Shamim alikuwa kwenye ndege akielekea Dubai na wale vijana wake

    Walipofika walipokelewa na vijana wengine na kupelekwa sehemu bosi wao alipofikia

    "Hakuna anayejua kuwa tuko hapa na vijana wetu wameshatupa uhakika wa jambo hili kwa sababu kuna boti saba zinazunguka kile kisiwa kwa ulinzi na wale wa Mexico wanatarajiwa kuingia mchana"akasema boss

    "Tunapaswa kuingia kazini muda huu huu bosi ili wale watukute"akajibu Shamim

    Majid alikuwa pembeni akiwaangalia akina Shamim huku akitamani apewe nafasi ya kuwepo kwenye tukio

    "Shami nenda surgey room we still need you na utaifanya kazi na timu yako"akasema bosi

    Shamim alielekea kwenye chumba cha upasuaji na kuwekewa sura ya bandia juu ya sura yake ambayo haikuathili chochote na alipotoka alikuwa tofauti

    Wakajiandaa na kisha wakapanda boti yao wakiwa wawili na Abdul na kuelekea kisiwani

    Walifika sehemu na kuona kwa mbali boti za ulinzi za maadui zao zkiwa zinazagaa kila sehemu

    "Its the time"akasema

    Wakavaa vifaa vya kuwasaidia kuogelea na mitungi ya hewa ya oksijeni kisha wakazama majini

    Shamim alikuwa kajiandaa na silaha zaidi ya kumi nyepesi za kutumia kwenye sehemu mbali mbali za mwili wake

    Waliogelea na kufanikiwa kufikiwa boti moja ya adui na kijishikiza pale

    Shmim alitokeza kwenye maji na kuwaona adui wamezubaa akatoa visu viwili na kutupa kwa pamoja vikatua kwenye shingo za wale watu

    Haraka haraka akawazamisha majini na huko wakagawana na Abdul kila mmoja akawavua nguo na kuzivaa

    Walipotokeza na kuingia kwenye boti walifanana na wale adui zao waliowaua

    Wakawasha ile boti na kuelekea kisiwani na njiani walipishana na boti za wenzao bila kugundulika



      Shamim na Abdul waliambaa ambaa na ile boti mpaka wakafika ufukweni na kushuka kisha wakaanza kuambaa ambaa na miti michache iliyokuwa kwenye kisiwa kile

    "Take the left side ili likitokea tatizo uweze kunisaidia"akasema Shamim

    Abdul alitkisa kichwa kama ishara ya kukubaliana naye kisha akaelekea upande ule wa pili na kumwacha Shamim akielekea upande mwingine

    Upande wa Shamim alifika sehemu ambayo alianza kuyaona majengo yaliyokuwa kwenye kisiwa kile na alipoyaona akaanza kutambalia tumbo taratibu akielekea upande ule

    Alifika sehemu akatulia na kutoa kiona mbali au darubini na kuanza kuangalia sehemu mbalimbali za jengo lile

    Alishangaa kuona askari wengi wakiwa wamevaa magwanda ya kijeshi wakiwa wanalizunguka eneo lile na kulilinda

    "Ina maana hawa watu wamejizatiti kiwango hiki?"alijiuliza kimya kimya

    Aliemdelea kuambaa na tumbo ila ghafla akashangaa akikutana na askari watatu wakiwa wamelizunguka eneo lile alilokuwa anaelekea

    Kwa bahati mbaya mmoja wao akamuona Shamim na akataka kutoa taarifa kwa wengine

    Kitendo kile Shamim alikiona kabla jamaa hajachukua maamuzi kisu kikali chenye sumu kwenye ncha yake kilitua shingoni pake

    Alianguka kwa kishindo na kusababisha wenzake wasikie na kugeukia pale

    Shamim alikuwa ameshajiandaa kukabiliana nao hivyo waliponyenyuka ili wachukue silaha zao Shamim alipiga hatua mbili za kasi na kuruka hewani kisha akatua kwenye shingo ya mmoja wa wale askari na kuivunja kisha akageuka haraka kukabiliana na yule mwingine

    Shamim alikuwa ameshachelewa tayali kwani yule askari kwa sababu alikuwa na mafunzo ya kutosha alishaona kila hatua aliyopiga Shamim hivyo akajua kosa la mwenzake ni kutaka kuokota ile silaha yeye akacheza na bastora iliyokuwa kiunoni

    Shamim alipogeuka alikutana na risasi tatu zikipenya kwenye upande wa juu wa bega lake la kushoto akadondoka chini

    Jamaa hakutaka kupoteza muda akapiga mluzi na kuwashtua wenzake

    Shamim alipokutana na zile risasi begani alianguka chini kama mzigo ila akajua yuko kwenye hatari kubwa hivyo akanyofoa kisu kisha kukitupa moja kwa moja shingoni kwa yule askari

    Kisu kilifika mahala husika ila kwa bahati mbaya kikafika wakati tayali yule askari alishapiga mluzi wa kuwataarifu wenzake

    Alipochomwa kisu chenye ncha kali yenye sumu na akatulia

    Shamim alianza kutambaa kutoka eneo lile huku damu ikiendelea kuvuja kwa kasi kutoka eneo lile ili asije akakutwa na wenzake na yule askari

    Hakufika mbali wale askari wakawa wamemfikia na kumzingira pale alipolala

    Alipewa kipigo kitakatifu pale pale chini kisha akabebwa na kupelekwa kwenye yale majengo

    Alipofikisha aliingizwa kwenye chumba kidogo sana ambacho aliweza kugeuka peke yake ila hakuweza kujisogeza kwingine

    Akiwa kwenye kile chumba alishangaa hewa kama ya kiyoyozi ikianza kuingia ndani ya kile chumba taratibu

    Polepole Shamim alianza kujua aina ya kifo alichoandaliwa

    Alipaswa kuzidiwa na baridi mpaka kuganda kisha mapigo yake yashindwe kupiga na hatimaye kusimama na maisha yake yawe yameishia pale

    Shamim akaanza kuona uwezekano wa yeye kupona ni mdogo



    Wamexico waliingia kwa helikopita binafsi wenye kile kisiwa na kupokelewa na wenyeji wao yaani wale waarabu kwenye uwanja mdogo wa ndege uliokuwa katika kisiwa kile

    Mara baada ya kupokelewa waliongozwa kuelekea kwenye lile jengo na wenyeji wao

    Walipitishwa korido mbalimbali mpaka kufikiwa ukumbi mdogo ila wakipekee wakaingia humo na kisha ule ukumbi ukaanza kuzama kuelekea chini ya ardhi

    Ulienda mpaka kwenye maji ya bahari ndipo wale Wamexico walipogundua kuwa kupitia kifaa maalumu walikuwa wanaenda kufanyia biashara kwenye maji

    Wakati wakianza kikao cha biashara kuna kijana mmoja aliingia na kumfata yule kiongozi wa kile kikundi cha Waarabu na kumnong'oneza

    "Kama ulivyotabiri boss amekuja na amenasa"alimwambia

    "Jinsia?"akauliza

    "Ya kike boss"akajibu

    "Mmalizeni sasa hivi na mniletee kichwa chake hapa"akasema

    "Sawa boss"akajibu



     Akiwa kajipumzisha nyumbani kwake Jabir Aboubakar Azizi akiwa anajiandaa kupokea wageni kutoka Mexico kwa ajili ya kufanya nao biashara ile kubwa aliyoamini kuwa itamnufaisha kuliko biashara zote ambazo alishawahi kuzifanya katika maisha yake yote

    Unga aliokuwa kaupokea kutoka kwa wale Wasomali ulikuwa wa gharama kubwa kwa sababu wale Wasomali walitegemea kwa kuuza ule unga walioupata kwa shida kutoka nchi moja ya Kusini mwa bara la Amerika walitegemea kupata silaha nyingi sana ambazo walishafanya majadiliano na kikundi chenye ushawishi mkubwa sana kwenye jimbo la Somaliland ili waweze kuipindua serikali ya jimbo hilo ambalo lilishajitenga kutoka Somalia na kujitangazia uhuru ingawa bado jamii za umoja wa mataifa hauutambui

    Mahmoud alikuwa mzawa halisi wa Somaliland na pia baba yake ni miongoni mwa wana mapinduzi waliopambana na hatimaye kufanikisha kuisaidia Somaliland kujiondoa kwenye utawala dharimu wa Somalia

    Lakini mara baada ya kufanikiwa kujitenga marafiki wakubwa wa baba yake walimgeuka na kumuua kikatili na kukalia madaraka

    Mahmoud alifanikiwa kutoloshwa na wafuasi wa baba yake mpaka Mombasa Somalia na huko ndipo alipojitengenezea kikundi chake kwa kusajili vijana aliowafundisha kama akina Shamim na Majid huku akiwajaza imani kali na mbaya sana juu ya utawala wa Somaliland

    Jabir alikuwa amejitahid kwa kadri ya uwezo wake wote kuimarisha ulinzi wa kisiwa cha Lisla ili ile biashara ifanyike kwa amani na hatimaye ahesabike miongoni mwa Mabirionea wakubwa wa Kiarabu

    Kijana wake mkubwa ambaye ndiye aliyekuwa mshilika mkubwa wa Alex akijulikana kama ABUU kwa kifupi cha Aboubakar jina la baba yake Jabir ndiye aliyehakikisha taratibu zote za kiusalama zinakuwepo

    Wakati wakijiandaa kuelekea kisiwani Abuu alipenyezewa taarifa kuwa yule mwanamke Gaidi kabisa na hatari wa kile kikundi cha Wasomali waliowadhurumu ule mzigo ameshaingia Dubai kwa ajili ya kufatilia mzigo wao

    "Hakikisheni kila sehemu kuna ulinzi wa kutosha pale kisiwani na chochote kitakachoonesha utofauti mtoe taarifa"alitoa maagizo

    "Sawa boss"akajibiwa

    Dakika hamsini baadae yeye na baba yake walikuwa kwenye Helikopita ndogo ambayo walikuwa wakiitumia kibiashara kwa ajili ya kwenda safari fupi fupi

    Ndani ya ile Helikopita kulikuwa na watu wengine wawili zaidi

    Wa kwanza alikuwa rubani na wa pili alikuwa Pyong kijana wa kijapani aliyekuwa kaiva vilivyo kwenye mafunzo ya karate kwa ajili ya ulinzi wao binafsi

    Walipofika kisiwani waliwapokea wageni wao na kuongoza moja kwa moja kuelekea kwenye chumba chenye lifti iliyowasafirisha kuelekea chini ya maji au bahari ili wafanyie biashara hiyo

    "Kalibuni sana katika eneo hili ambalo ni salama sana kwa ajili ya biashara"alisema Jabir

    "Sawa sawa mheshimiwa"wakajibu Wamexico

    Katika vitu alivyokuwa makini Jabir ni hawa Wamexico kwa sababu alijua maisha ya wafanya biashara wa kimexico kuwa ya kihuni na utapeli mwingi hivyo alimwacha yule kijana wa kijapanai kwa mbali kidogo ili likitokea tatizo aweze kutoa msaada

    Wakati anapewa taarifa na kijana wake kuwa kuna yule mwanamke waliyetegemea kuwa anaweza kuleta madhara kuwa amekamatwa

    "Boss tumemweka kwenye cold house i think two minutes from now she will be in hell"akajibiwa

    "Ok but you have to be sure that she is deady,everybody know how she is dangerous"akajibu

    "Wor out boss"akajibu yule kijana

    Wakati yule kijana aliyekuwa amemuinamia Jabir akimaliza kuongea naye na kunyenyuka ili aondoke alishangaa akikutana na pigo moja takatifu

    Aligeuka haraka ili kupambana na adui yake

    Na yule adui wake alimwachia nafasi ili amuone na kumfahamu kwa sababu alitegemea yule jamaa aoneshe mshangao

    Shamim alikuwa mbele yake na kweli alipigwa na mshangao

    Kama Shamim alivyotarajia jamaa alipopata mshangao alifanya kosa la kugeuka kumwangalia bosi wake hapo hapo akakutana na ngumi nzito kama ndoo ya maji shingoni

    Akayumbayumba na kuanguka chini

    Wakati kila mmoja akishangaa na kujiuliza kinachoendelea Shamim alipaa hewani kwa haraka na kisha akarudi chini kwa kutanguliza magoti ili atue usoni mwa Jabir ila Pyong akawa ameshausoma mchezo na kupaa kisha wakakutana hewani kwa pamoja!!!



      Unyevu unyevu ulizidi kupenya kwenye kile chumba alichofungiwa Shamim hali iliyomfanya ahisi kama anakalibia kuganda kabisa

    Simu yake maalumu ilikuwa imeshachukuliwa hivyo hakuwa na namna ya kujinasua kutoka pale ndani

    Ila hakukata tamaa alielekea kwenye kona ya kile chumba na kujikunyata huku baridi ikiendelea kumtesa

    Alifikia hatua akawa anahisi utumbo ukiganda tumboni kwa ile baridi

    "Niisipotafuta namna ya kujiokoa nitafia humu ndani na Abdul mwenyewe sijui yuko wap? Na kama yuko salama

    Akanyenyuka na kujalibu kutafuta upenyo wa kujalibu kujiokoa ila kwa bahati mbaya kile chumba hakikuwa na mlango bali kilikuwa na ukuta pekee ukiwa umeunganishwa na umeme pande zote

    Wakati akiendelea kuhangaika kutafuta upenyo alinyenyua macho yake na kuangalia juu na akafanikiwa kuona sehemu iliyofanyiwa ukarabati

    Akakunja ngumi yake na kwa nguvu zake zote akapiga ngumi eneo lile mpaka likapasuka

    Eneo lile lilipopasuka akafanikiwa kuona nyaya kadhaa zikipishana kutoka kushoto kuelekea kulia zikiwa nyeusi na nyekundu

    Akili kichwani na mpambanaji siku zote anapaswa kuwa mbunifu katika kila kitu anachokifanya

    Shamim alizivuta zile waya mpaka zikakatika na kumrusha kwa shoti

    Aliponyenyuka kutoka pale aliporushwa alizishika zile nyaya na kuziunganisha hasahasa kwenye ncha na pale pale zikatoa cheche kabla ya kulipuka kwa nguvu mpaka akaanguka chini

    Akiwa pale chini alishangaa cheche zikiongezeka na ghafla upande mmoja wa ukuta ukaanza kujitenga taratibu na kuachia nafasi

    Shamim akaelewa kuwa shoti imesaidia kufungua mlango hivyo akajiandaa kwa mapambano

    Kitendo bila kuchelewa askari wawili waliokuwa nje ya kile chumba wakimlinda wakaingia kichwa kichwa

    Wa kwanza alikutana na ngumi moja ya uhakika iliyombabatiza ukutani na akatulia pale kimya

    Wakati wa pili akitumia nafasi hiyo kushangaa alikutana na kabali moja matata iliyoibadilisha shingo yake kutoka kuangalia mbele na kuangalia nyuma na habari zake zikaishia hapo

    Shamim akatoka na kukuta chumba kidogo kwa nje lipoingia ndani akakuta kuna vifaa vyake vya kazi vikiwa vimehifadhiwa kule

    Akachukua kikoti chake kidogo kilichojaa zana za vita akakikagua na kukuta kila kitu kiko sawa akakivaa

    Akabeba na simu na vifaa vingine kisha akatoka taratibu akinyata

    Akatokeza kwenye veranda ndefu sana kiasi cha kumwogopesha

    Akawa anaambaa ambaaa pale na alipokalibia kuimaliza mbele yake wakaibuka wanajeshi wawili wakiwa na silaha

    Askari wale hawakuwa wamejiandaa kukutana na adui kwa wakati ule hivyo Shamim akatumia nafasi ile kuachia visu vyake kwa pamoja na speed vikatua shingoni

    Ilisikika miili peke yake ikidondoka chini huku watu wakiwa kimya

    Akaendelea na safari na kukuta chumba kimoja kikiwa na mlinzi akamzunguka kwa nyuma na kumtia kabari

    "Wameelekea wapi? Au uwafate wenzio kuzimu"alitamka huku akikaza mkono wake na kumuumiza yule askari

    "Hiyo hapo lifti itakupeleka chini ya maji ndipo walipoelekea"akajibu

    Hakupata nafasi ya kuomba kuishi kabla shingo yake haijageuzwa nyuma mbele na yeye akatulia chini

    Shamim akaaaingia kwenye lifti na kuzama mpaka kule chini

    Alijua ile lifti inaweza leta matatizo hivyo akafungua upande wa juu na kupanda na kutulia huko

    Lifti ilipofika chini wakaifungua na hawakukuta mtu yeye akapitia huko huko kuwaona kila walichokuwa wakikipanga

    Wakati yule jamaa anatoa taarifa yeye alikuwepo akimuona ndipo alipotokea na kumpa pigo takatifu



    Pyeong alikutana na Shamim hewani na kumpa pigo moja la mbavu lililompeleka chini moja kwa moja

    Wakati Shamim akigugumia kwa maumivu wale mabosi wa kiarabu na kimexico walijikusanya na kujalibu kutoloka

    Shamim akaliona hilo na kujizozoa pale chini akawahi na kuziba njia waliyotaka kupia

    Pyong akakurupuka akijua Shamim kwa pigo lile hana nguvu tena hivyo akamvaa akipanga kumpa pigo la mwisho ili ammalize

    Shamim akawa amesoma ule mchezo mzima

    Wakati Pyong akija na pigo la mwisho akitanguliza mguu wa kushoto kisha ageuke na kulia shamim alishamuona akakwepa wa kwanza

    Pyong alipogeuza mguu wa pili akawa katanua miguu Shamim alichana msamba na kumpa ngumi takatifu kwenye kijiji chake mpaka Pyong akapiga kelele kwa kichina



     Pyeong alikutana na maumivu makali sana sehemu zake za siri alipopigwa ngumi kali na Shamim akajikuta akienda chini bila kupenda

    Mabosi wale walipotaka kujalibu kupambana na Shamim alimpa mmoja pigo moja shingoni akalegea na kuanguka chini akapoteza fahamu wale wengine wakashtuka kuona kilichomkuta mwenzao hivyo wakatulia kuona hatima

    Pyeong hakutaka kuonekana mzembe alijinyenyua kutoka pale chini na kumfata Shamim

    Alijalibu kupambana kwa kutupa ngumi za mfululizo na mateke akitegemea kumchanganya Shamim ila zote Shamim aliziona na kupangua kirahii sana

    Pyeong akabadili mbinu na kutumia fly kick ili aweze kuivunja shingo ya Shamim

    Shamim alishamsoma alichotaka kukifanya na akamuwahi kabla hajapaa akampa teke kali sana la mguu na kisha akaachia ngumi nzito kama jiwe kwenye shavu za kushoto la Pyeong aliyekuwa hajajiandaa kwa lile pigo

    Ngumi ile ilimpata Pyeong kisawasawa akajikuta akitema damu ikiwa na mchanganyiko wa meno yake mawili akaanguka chini na kuamua kutulia na kusalimu amri

    Shamim akamfata pale chini na kumshindilia mateke ya haraka haraka kwenye mbavu na kumwacha akiugulia maumivu makali sana

    Aliwafata wale matajili ili awadhibiti na kuupata mzigo kisha aondoke eneo hilo kwani atakuwa amepata alichoagizwa kuchukua

    "Kuna mawili hapa! Mnipe mzigo niwaache hai? Au niwamalize na kuondoka"akasema

    "Mzigo gani unaoutaka?"wakamuuliza

    "Nahitaji mizigo yote miwili! Ule wa madawa mliotuzurumu na ule wa kwenu"akasema

    "Ile mizigo haipo hapa"akajibiwa

    "Iko wap?"akauliza

    "Iko godauni nje ya mji"akajibiwa

    Shamim alimwangalia kwa makini sana Jabir kisha akatoa ile bastora yake na kumchapa risasi ya mguu

    Kisha akafungua bega lake na kumwonesha kidonda

    "Hawa mbwa wako wamenijeruhi na risasi wakati nakuja hapa! Kwa akili yao walijua sitaweza kupambana nao! Na wewe ukatoa ruhusa niuawe ukidhani unapambana na paka? Sasa ni wakati wangu wa kuwaua mmoja mmoja! Mimi ni zaidi ya mnavyofikiria nyie! Amua unanipa mzigo? Nikumalize?"akafoka kwa hasira

    Jabir alilia kama mtoto huku akitetemeka kwani aliona uwezekano wa yeye kuishi umebaki mdogo ikabidi awe mpole

    "Nitakupeleka mpaka mzigo ulipo lakini niache hai tafadhali"akasema Jabir

    "Mimi sina tatizo na wewe kama utanipa mzigo! Amka na kuwa mpole"akasema

    Jabir alinyenyuka kwa shida na kufanikiwa kusimama akaanza kujikongoja kutoka eneo lile na kuingia kwenye lifti huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa Shamim

    Walipanda na lifti na kuwaacha kule chini wale wamexico na baadhi ya walinzi kule chini

    Walipotokeza kule juu walikuta baadhi ya wanajeshi wakiwasubiri huku wakitaka kumuweka chini ya ulinzi Shamim

    Shamim alimkwida vizuri Jabir kiasi cha kuwaomba wale wanajeshi wawe wapole ili maisha yake yawe salama

    Helikopita iliyowaleta kisiwani pale ikawashwa na Shamim na Jabir wakaingia ndani kisha ikaondolewa pale moja kwa moja kuelekea eneo ule mzigo ulipotunzwa

    "Tuko kwenye helikopita naelekea Ram road kama kilometa ishilini kutoka mjini kuna sehemu maalum mzigo ulipotunzwa naomba vijana waje kuchukua chetu"Shamim alituma mesage kwa Bosi wake bila Jabir kujua kinachoendela

    Helikopita ile iliendelea kuchanja mbuga mpaka kufika eneo la tukio kisha taratibu ikaanza kushuka na kufika ardhini

    Shamim alifungua mlango na kumtoa Jabir ndani kisha wakaanza kuongoza kuelekea mahali mizigo ilipokuwa

    Eneo hilo lilikuwa limezingirwa na wanajeshi wengi kama wale waliowaacha kule kisiwani

    "Unafikiri unaweza kuondoka na huu mzigo hapa salama?"Jabir akamuuliza Shamim

    "Tulia wewe mimi sio kama unavyonifikiria"akajibu Shamim

    "Kwanini usiwasaliti wenzako na kujiunga na mimi kisha nitakulipa mara kumi zaidi ya bosi wako anavyokulipa"akasema Jabir

    "Nitakuchakaza risasi sasa hivi ukiendelea kunipigia kelele"akasema Shamim

    Walipofika sehemu iliyojengeka kidogo waliingia ndani ya geti na huko akafanikiwa kuona makontena mengi sana

    "Unaonaje ukimuachia bosi wetu na sisi tumuachie mtu wako?"sauti ilitokea juu ghorofani

    Shamim alishtushwa na sauti hiyo akahamisha macho yake kuelekea kule juu

    "Abdul......"Shamim alimuona Abdul akiwa kachoka sana huku kalowa damu mpaka anatia huruma akiwa kaelekezewa bastora

    Akabaki njia panda!!!



     Baada ya kuachana na Shamim ili kila mmoja aelekee eneo lake Abdul alijongea taratibu mpaka upande wa pili wa zile nyumba za kisiwa kile

    Alipogeuka nyuma akafanikiwa kumuona Shamim akipambana na wale askari wawili

    Akageuza ili aende kumsaidia ila kabla hajamfikia akashangaa kuona kikundi kikubwa sana cha askari wakielekea Shamim alipokuwa

    Akasita na kushindwa kuendelea kwa sababu aliona asingeweza kupambana na askari wengi vile

    "Nifanyeje sasa hapa? Mbona majanga"akawaza

    Akageuka na kutafuta mnazi mmoja akajificha na kuanza kuangalia mchezo mzima wa kumkamata Shamim

    Askari wale walipoondoka na Shamim aliwafatilia kwa nyuma mpaka walipoingia kwenye yale majengo

    Akashindwa kuingia eneo lile

    Alirudi akajificha eneo moja akatoa simu ya kazi yenye uwezo mkubwa sana wa kusoma vitu hata visivyowezekana na kuwasiliana na bosi wao

    "Namba one kakamatwa"akasema

    "Sitaki maelekezo yeyote yale zaidi ya wewe kupambana mpaka umuokoe"akasema

    Abdul hakuwa na cha kujibu na simu ikakatwa

    Akageuka na kujalibu kuona kama kuna eneo anaweza kupenya kuingia

    Alizunguka mpaka eneo la nyuma na kuona walinzi wachache wakiwa eneo lile

    Akachagua sehemu iliyokuwa na dirisha na kukuta walinzi wawili peke yao akawanyemelea mpaka akawafikia

    Akatoa kisu na kurusha kikamchoma mmoja na yule mwingine alipogeuka kupambana akakutana na fly kick moja akatulia

    Akafungua lile dirisha na kuingia ndani akakutana na nyaraka nyingi sana mezani

    Alipojalibu kukagua hakuona cha kumsaidia

    Akatoka kwenye ile ofisi na kukuta korido yenye ofisi tatu zimefatana

    Akafata eneo zile korido zilipokuwa zikielekea na akatokea kwenye chumba kimoja na kukuta miili miwili ya askari alipochunguza akagundua wamefariki

    "Ina maana Shamim ameshafanya yake? Mmmmh!! Hii noma"akabaki kushangaa

    Akaachana nao na kuendelea kwenda mbele na akakutana na korido ndefu sana

    Alipotokeza tu akakutana na askari watano wakibeba miili ya wenzao

    Kwa bahati mbaya wakawa wamemuona

    Mmoja akageuka na kutoa silaha na Abdul akawa ameiona akatupa kisu kikatua shingoni kwake

    Akatoka speed kuwafata wale wengine ili kupambana nao ghafla akashangaa kuona mlango ukifunguliwa na askari wengi wakiingia eneo lile

    Akawa hana ujanja akatulia na kuwekwa chini ya ulinzi

    Alipewa kipigo cha uhakika kabla ya kupandishwa kwenye Helicopita na kupelekwa asikokujua mpaka kujikuta mbele ya Shamim akiwa kawekwa chini ya ulinzi

    "Shamim usikubali kujisalimisha! We chukua mzigo na uondoke! Hata nikifa hakuna shida"akasema

    "Kimbia tuone? Naanza kuhesabu moja mpaka tatu uwe umeweka silaha chini na kumwachia bosi wetu ama sivyo ubongo wa huyu nguchiro mwenzio utamwagika na kisha kufatia wako"akafoka yule askari aliyekuwa kamweka chini ya ulinzi Abdul

    "Moja.....mbii...."akaanza kuhesabu

    "Shamim usikubali,acha aniue kama anataka kuniua wewe timiza kazi ya bosi hatakuelewa"akafoka Abdul

    "Ta......"kabla hajamalizia

    "Acha!! Usimuue tafadhali"akasema Shamim

    Alishusha silaha yake na kumwachia yule bosi wao

    Vijana walipiga risasi hewani kwa ishara ya kumpokea bosi wao akiwa huru

    Jabir bosi wa kikosi kile alimfata yule askari aliyemuokoa na kumkumbatia kisha akachukua bastora yake na kuiangalia kwa makini kisha akamfata Shamim

    "Maisha yangu muda mfupi uliopita yalikuwa mikononi mwako ila kwa sasa maisha yako yako mikononi mwangu "akaendelea kutamba

    "Nahitaji jibu moja pekee na jepesi ili na wewe uendelee kuifurahia pumzi ya Dunia hii"akasema

    "Bosi wako yupo wapi kwa muda huu?"akauliza

    Shamim alimuangalia kuanzia juu mpaka chini kisha akamtemea mate usoni

    Jabir alimwangalia Shamim kwa hasira kisha akaikoki silaha yake na kumpiga risasi mguuni Shamim



     Shamim alianguka chini kama mzigo na kusikilizia maumivu makali kutokana na risasi ya pili aliyopigwa mguuni mara baada ya ile ya kwanza aliyokuwa kapigwa kwenye bega

    Miongoni mwa mazoezi waliyoyapata wakati wakiwa wadogo mpaka wanakuwa na kufikia hatua hiyo yalikuwa ni kuvumilia aina yeyote ile ya mateso ambayo wangekutana nayo

    Shamim mwenyewe alishawahi kupigwa risasi tatu mguuni na begani na kulazimishwa kupambana akiwa katika hali kama hiyo zaidi ya mara tatu wakati wakiwa kwenye mafunzo kwenye msitu wa Gobe huko Mombasa na kile kikundi cha Mahmoud

    Hivyo risasi ya pili aliyopigwa ilimsababisha asikie maumivu makali sana ila kwa nafasi nyingine alijilazimisha kuigiza kama aliyeumia sana na ambaye hawezi tena kusimama na kupambana na wale watu

    Igizo la Shamim likawashika wale Waarabu na kushawishika kuwa tayali walishammaliza na kuanza kujiandaa kudeal na Abdul

    "We malaya nimekupa option ya kujiunga na kikosi changu umekataa!! Basi subiri kifo ila kwanza ngoja nianze na huyu boya mwenzako kisha nitakumalizia wewe! Mnadhani mimi ni mwepesi kama mnavyodhani?"akasema kwa tambo Jabir

    Kosa lako moja ni ushindi kwa mwenzako na ndicho alichokuwa akisubiri Shami pale chini alipokuwa

    Jabir alichomeka ile silaha aliyokuwa nayo kiunoni na kugeuka kumwendea Abdul

    Wakati kila mmoja akijua Shamim amekwisha

    Shamim aliruka kutoka pale chini akiwa kachomoa visu vitatu kutoka kwenye soli yake ya viatu na kuviachia kwa kasi moja kwa moja vikafikia vifuani kwa wale walinzi waliokuwa wamemshikilia Abdul

    Wakati wakishtuka kwa kilichotokea Shamim alisharuka haraka na kutua kalibu ya Jabir

    Jabir alipoona walinzi wale wakianguka chini aligeuka kuonana na Shamim huku akipeleka mkono kiunoni ila cha kushangaza alikutana na sura ya Shamim pembeni yake

    Kiroho kikamshika ghafla,akabaki ameganda bila kujua achukue ile silaha ama aache

    Shamim aliiwahi ile silaha na kuichomoa kisha akampiga pigo moja Jabir akiwa kakaza mikono yake na kuvunja bega lake la kushoto kisha akamgeuza na kumfanya kama ngao yake

    "One mistake you loose Abdul"alimwambia mwenzake

    Abdul alijiangusha chini na kujivilingisha mpaka kwenye mwili mmoja miongoni mwa wale adui waliochomwa visu na Shamim akapeleka mikono yake na kuchomoa kisu kimoja na kukata kamba alizofungwa kisha akanyenyuka na silaha kali Ak-47

    Matendo hayo yote yalitokea ndani ya sekunde kadhaa ambazo wale adui wengine walikuwa hawajajitayalisha

    Abdul na Shamim walipeana ishara kwa macho kisha kila mmoja akaanza kushambulia wale adui kwa risasi za mfululizo

    Adui walichanganyikiwa kwa sababu kiongozi wao alikuwa amekamatwa na Shamim na kuwekwa kama ngao hivyo wakashindwa kuachia risasi kuelekea eneo lile wakihofia kumdhuru bosi wao na hilo likawa faida kwa Shamim akampa ishara Abdul aelekee alipoa

    Wakiwa upande mmoja wakaendelea kuachia risasi kama mvua kuelekea walipo adui bila kuwapa nafasi

    Adui wengi wakaanza kukimbia ovyo ovyo wakiogopa kufa kwa risasi na pia wakiogopa kumdhuru kiongozi wao

    Ghafla risasi zikawaishia akina Abdul

    "Abdul kaa na huyu boya wakati napambana na hawa! Hakikisha humpotezi"akasema Shamim

    Akamwachia Jabir kwa pigo moja takatifu lililomsukuma mpaka aliposimama Abdul na yeye akampokea kama mpira

    Shamim alijiviringisha akikwepa risasi mpaka kwenye kontena moja na kujificha

    Akawahesabu adui waliobaki wakawa hawazidi ishilini

    "Nitawaamaliza mwenyewe hawa maboya"akawaza

    Wakati wale adui wakijua Shamim hana silaha na kuanza kulisogelea lile kontena walizingire yeye alikuwa na mpango tofauti kichwani

    Walisogea taratibu wakipeana nafasi ya kulizingira kontena mpaka walipofika kalibu

    Walipozunguka kwa nyuma walishangaa kukuta patupu bila mtu

    Wakabaki kushangaa na kuanza kupeana ishara za kuulizana kaelekea wapi

    Kutoka juu ya kontena lile Shamim alitokeza na visu vyamfullulizo vyenye ncha kama zana za kininja ila vidogo na vyepesi na kuviachia kuelekea shingoni kwa wale jamaa



     Vijana zaidi ya kumi walikuwa chini kutokana na shambulizi lile na wale vijana wachache waliobaki wakachanganyikiwa kutokana na lile shambulizi la ghafla.

    Abdul akawa amewaona wale vijana wakijalibu kujiokoa kwa kukimbia na yeye akamwachia Jabir kidogo na kuwamaliza wale vijana kwa risasi.

    Kosa la Abdul kumwachia Jabir lilipelekea Jabir kutoka mbio eneo lile akimwacha Abdul akiwamalizia wale vijana.

    Abdul alipogeuka kumchukua Jabir akamuona kwa mbali akikimbia na kupotelea kwenye makontena yaliyojazana eneo lile.

    Kwa hamaki akaachia risasi kadhaa kuelekea alipokuwa Jabir.

    "AchaaaaaaaaAbdul....."Shamim alijalibu kumzuia Abdul ila akawa amechelewa tayali.

    Walikimbia kwa pamoja na kuelekea kule Jabir alipokuwa na kumkuta akiwa katika hatua zake za mwisho za uhai.

    "Bado tunahitaji kuupata mzigo Abdul na bila huyu hatuwezi kupata kitu! Anapaswa kupona"akasema Shamim.

    Abdul akashtuka kusikia maneno ya Shamim na yeye akajua kosa lake.

    Wakajalibu kuzuia damu iliyokuwa ikivuja kwenye majeraha kadhaa yaliyokuwa kwenye mwili wa Jabir ili japo aweze kuwajibu maswali yake ila hakuweza kuongea chochote na akatupa miguu kwa muda kisha akatulia.

    Kila mmoja alishika kichwa kwa hasira kutokana na kumpoteza mtu muhimu sana katika mpango wa kufanikiwa kupata mzigo waliotapeliwa.

    "Tunafanyaje sasa?"akauliza Abdul.

    "Hebu tujalibu kutafuta kwenye haya makontena tuone kama tunaweza kuupata ila nimechanganyikiwa"akasema Shamim.

    Walielekea sehemu yalipokuwa makontena yaliyoonekana mapya mapya na kuanza kuvunja makufuri na kukagua kama wanaweza kuambulia mizigo ile ila hawakupata kitu.

    Mara baada ya kukagua kwa muda walisikia vishindo vya watu wakielekea maeneo hayo na magari kadhaa.

    Walipochungulia wakagundua ni askari wengine wa kikosi hicho

    "Hatuna cha kufanya Abdul inabidi tuondoke! Ndo tumeshaukosa tena"akaongea Shamim kwa sauti ya kukata tamaa.

    Haikuhitaji mjadalaa kwa hilo wakaondoka eneo lile mpaka barabarani na kufanya mawasiliano na viongozi wao wakawaletea usafiri mpaka eneo lile kisha wakaondoka kurudi Hotelini.

    Walipofika ilikuwa lazima wakaripoti kwa Mahmoud ambaye alikuwa bosi wao.

    Walielezea kila kitu kilichotokea tangu mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari na kusubiri majibu ya bosi wao ambaye alikuwa kawapa nafasi moja ya upendeleo na wakishindwa walikuwa wanapaswa kupata adhabu kali sana.

    "Shamim kajiandae kuvaa uhusika wa Lily na uelekee Dar es salaam! Siko tayali kuuukosa huu mzigo! Nafikiri sihitaji kukwambia kuwa unapaswa kuishi na yule Mbongo mpaka nitakapoupata mzigo wangu! Kwa sababu yeye ndiye anayeweza kujua ule mzigo ulipotunzwa! Kwa kupitia mawasiliano au hata sasa anaweza kuwa anajua"akamaliza kuongea bosi.

    Maneno ya bosi yule hayakuhitaji mjadala na kwa Shamim alijua ni msamahamkubwa sana kwani alipaswa kuuawa kwa kosa la kushindwa kurudisha mzigo.

    Shamim aliondoka eneo lile na kurudi chumbani kwake kisha akachukua kompyuta mpakato na kisha akarudi kwenye mitandao ya kijamii na kumtafuta Alex

    "Kesho nakuja Tanzania baby!"akatuma mesage

    Alex aliipokea ile mesage kwa furaha sana bila kujua kuwa Shamim aliyeenda kuvaa sura ya Lily alikuwa kazini.

    Alipotoka chumbani kwake alipelekwa chumba kidogo cha upasuaji na kutolea ile sura ya bandia aliyovalishwa kisha akafanyia usafi kila sehemu ya mwili wake na kulembwa upya na yule mtaalamu wake wa mara ya kwanza na ile sura ya kazi ikamtoka na kubaki binti mrembo sana kama alivyokutana na Alex kwa mara ya kwanza super market.

    "Tiketi zako ziko tayali Lily! Unarudi Tanzania kwenye nyumba yako ya Masaki na pia ukiendelea na biashara zako za kutoa vifaa vya umeme huku na kupeleka kule"alipewa maelekezo.

    "Kila utakachokuwa unafanya kinapaswa kutufikia bila tatizo! Wale vijana wako wa kazi sita wapo tayali Tanzania wakikusubiri! Nakutakia safari njema na mafanikio! Kumbuka hupaswi kumpenda na unapaswa kupata taarifa za mzigo wetu kisha utamuondoa Duniani! Zingatia masharti! Na kwa heri!!"akamaliza kutoa maelekezo Mahmoud!!





    Maandalizi ya Shamim kurudi Tanzania kwa ajili ya kukutana na Alex ili kuhakikisha anapata uwezekano wa kujua ulipo mzigo wa bosi wake.

    Siku mbili baadae safari iliwadia na Shamim akakwea ndege na kuelekea Tanzania akiwaacha Abdul na Majid wakiwa na Bosi wao wakielekea Mombasa kwa ajili ya kusubiria majibu ya kazi aliyotumwa.

    Alifika Tanzania na cha kushangaza Alex hakuja kumpokea uwanja wa ndege bali vijana wale sita waliopangwa na bosi wake kufanya naye kazi kwa Tanzania ndiyo waliokuwa pale uwanjani kumpokea.

    "Nipe ripoti ya Alex"akauliza.

    "Amendoka saa mbili asubuhi na Emirates Airways kuelekea Dubai na anatarajiwa kurudi baada ya siku mbili kulingana na tiketi zake"akajibiwa.

    "Nipe ripoti ya Joan mdogo wangu"akauliza tena.

    "Amehamishiwa Kisumu na anamalizia kidato cha tatu ila afya yake ilileta mgogoro siku chache zilizopita na akapata matibabu kwa sasa yuko sawa kabisa"akajibiwa.

    "Location?"akauliza

    "Masaki bosi ila bishara ilisimama kwa muda tukitegemea kuifunga tukiamini utafaikiwa katika misheni yako"akajibiwa.

    "Fanya mawasiliano iendelee na pia hakikisha napewa kila kitakachokuwa kikiendelea upande wa Majid kule Mombasa najua anajipanga ila nahitaji kumshinda"akasema.

    "Ila bosi unapaswa usikutane kimwili na Alex kwa muda ili upate nafasi ya kupona majeraha yako ya mwili kwa sababu tumepewa ripoti ya wewe kupigwa risasi"akaambiwa

    Shamim akafungua bega lake na kuwaonesha wale vijana likiwa halina hata kovu moja.

    "sifanyi mambo kwa kukurupuka! Kuna siku nitawaeleza kilichotokea! Ila nilikuwa na bulletproof na ile risasi ya bega haikupenya ila niliigiza ili nipate nafasi ya kuingia kwao ila ile ya mguu iliniparaza na alama hii hapa"akasema akiwaonesha.

    "Lakini bosi anafahamu kuwa una majeraha!!Akauliza kwa mshangao mmoja.

    "Sio kila kazi unafanya na bosi zingine unafanya personal"akajibu.

    Muda wote wanajadiliana gari zilikuwa zikiendelea na safari ya kuelekea makazi aliyotengewa kutulia wakati wakiendelea na harakati zao za kupata siri ya sehemu silaha zilipopelekwa na ule mzigo wao.

    Walipokalibia kufika katika makazi yao simu ya ndani ya gari ile iliyotengenezwa kikazi zaid kuliko gari za kawaida ikaita.

    "haloo........simu yako bosi"alisema yule kijana aliyepokea simu.

    Shamim akapokea ile simu na kuweka sikioni.

    "Alex amefika huku leo ila inaonekana kuna uwezekano wakati akiwa huko alipigiwa simu na kuelekezwa kuhusu mambo ya mzigo! Hatuwezi kutrace call zake kwa sababu ya teknolojia wanayotumia hivyo usiku hakikisha unaingia na vijana pale na kucheza na camera za ile nyumba mpaka mpate conversation nzima yawezekana ikatupa mwanga"akasema bosi kwenye simu.

    "Sawa mkuu"alisema na kisha akakata simu.

    Gari iliendelea na safari mpaka Masaki kwenye makazi yao.

    Waliiingia na kupumzika huku wakipanga namna watakayocheza na camera zile ambazo zilishaonesha kuwa na mfumo mgumu kutumia wa teknolojia.

    Usiku walianza safari ya kuelekea huko kwenye nyumba ya Alex iliyokuwa Mikocheni.

    Walikuwa wamejiandaa kikamilifu kukabiliana na hali yeyote inayoweza kujitokeza eneo lile.

    Waliamini chochote kinaweza tokea kwa sababu Alex pia alikuwa mfanyakazi wa wale Waarabu wa Dubai.

    Walipofika walipaki gari yao kwa mbali kisha wataalamu wa teknolojia wakaanza kucheza na teknolojia ya kusoma zile camera.

    "pagumu bosi mpaka tuingie na kucheza na source ya hizi camera ndo tutaweza"akasema kijana mmoja.

    Vijana wakasogeza lile gari lao mpaka kalibu na ile nyumna kisha Shamim akavaa gloves na vifaa vyake vya kazi yakiwepo mavazi rasmi ya ile kazi kisha akatoka kwenye gari

    "Bosi unahitajika kuwa zaidi ya makini"akaambiwa.

    "Najua hilo usijal"akajibu.

    Shamim akarukia ukuta na kushika zile waya za umeme zilizolinda nyumba na zile gloves zake na kurukia kwa ndani.

    Alipotua ndani akaanza kunyata na kuelekea kwenye mlango wa kuingilia.

    Alipofika akatoa fungua zake feki na kuingiza kwenye tundu la kitasa.

    Kabla hajafungua akasikia kitu cha baridi kikigusa shingo yake.

    "Tulia hivyo hivyo! Ukijalibu kufanya ujanja wowote ule itakuwa mwisho wako"sauti nzito ikaamrisha.



     "Tulia hivyo hivyo! Ukijalibu kufanya chochote kila kifo ni haki yako"alisikia sauti ikimwambia.

    Shamim hakuwa na cha kufanya! Alitulia kama alivyoagizwa ila akijalibu kucheza na hisia zake kujua uwezo wa adui wake na pia lengo lake ni lipi!.

    "We ni nani na unatafuta nini hapa?"swali likarushwa kwake.

    Swali lile lilimfanya Shamim afahamu anayepambana naye si mtu anayejua chochote kile kuhusiana na kinachoendelea kwa Alex na wale waarabu na yeye!.

    Akaweka mawazo yake kuwa atakuwa mlinzi wa kawaida tu wa nyumba ile.

    "Nimekuuliza swali hujibu eee? Nitakusambaratisha sasa hivi nyang'au wewe! Jibu"akafoka yule mtekaji.

    Shamim akaendelea kunyamaza maksudi akimhesabia hatua yule jamaa afanye kosa la kujisogeza kalibu yake ili amalize mchezo ule.

    Kosa moja alilotaaka jamaa afanye ndilo alilolifanya.

    Akasogeza mguu wake kumfata Shamim ili amkabiri na kujalibu kutupa ngumi ili amdhibiti Shamim.

    Alichotaka Shamim kikatokea,alikwepa ile ngumi na kuachia pigo moja na kufanikiwa kuuvunja ule mkono wa yule mtekaji.

    "Aaaaaaaaaaagh!!"jamaa alitoa mguno wa maumivu makali sana.

    Shamim aligeuka na teke kali la mbavu akiwa kakomaza mguu wake kama anapiga jiwe au ukuta na mbavu za jamaa zikalia kama kijiti kilichovunjika kuonesha zimevunjika.

    "Aaaaagh!! Mamaaa!! Nakufa!"akapiga kelele.

    Shamim alimuwahi na kumpa pigo moja pekee la shingo na kumtuliza jamaa na kisha akatoa funguo zake na kuzama ndani hapo akiwa kajifunika nguo nyeusi mwili mzima kama ninja ili zile kamera zisiweze kumrekodi na akatambulika.

    Alielekea mpaka chumba maalumu cha kuongozea zile camera na kwenye Laptop iliyokuwa pale chumbani akaingiza USB na kisha akacheza na code za kompyuta ile akaiunganisha na wale vijana wake waliokuwa nje ya nyumba ile.

    Alitulia na vijana wakafanya kazi yao kisha wakampa ishara kuwa wamemaliza atoke.

    "Kuna mwili hapa naomba niutupe huko nje muupokee"alisema Shamim.

    Akaubeba ule mwili wa yule mtu aliyekuwa akipambana naye na kuutupa nje ya jengo lile na wenzake wakaupokea kisha akaruka ukuta na kutua nje na kuingia kwenye gari ikaondolewa.

    "Kuuacha huu mwili ingesababisha akirudi ajue kuna uvamizi ulifanyika kwake hivyo bora tuondoke naye ahisi labda hakuna kilichotokea"akasema Sshamim.

    "Sawasawa bosi"wakajibu vijana.

    "Vip kuna chochote mlichoambulia kwenye camera?"akauliza.

    "Tunaweza kuangalia wote hapa mkuu"akajibu.

    Kijana mmoja akawasha screen kubwa iliyokuwa kwenye lile gari na kisha akachomeka USB yake akaiunganisha na simu yake ya kiteknolojia kisha picha zikaanza kuonekana kwenye screen ile.



    Wakati wao wakiangalia zile picha upande wa pili Alex alikuwa na wale waarabu wakiusoma ule mchezo mzima.

    Walikuwa kwenye screen pana wakiangalia tukio zima lilivyokuwa likitokea kwenye nyumba ya Alex.

    Tangu siku ya kwanza camera zilivyoingiliwa walijua kuna kitu kimeenda tofauti na Alex akaamua kutafuta watalaam wa teknolojia kutoka nje ya nchi na kumsaidia kufunga sysytem ambayo hata uihack bado itaendelea kurekodi bila wewe kujua.

    Mpambano mzima wa Shamim na yule kijana na jinsi alivyoiba document kutoka kwenye camera na lapto zake alikuwa akiuangalia kwa makini akiwa kwenye chumba maalumu.

    "Lazima yule atakuwa yule mwanamke aliyemuua bosi wetu hapa! Cha msingi akamatwe akiwa mzima"alisema mmoja wa waliokuwa wakiitazama ile camera.

    "Tutafanyaje ili kuwakamata sasa?"akauliza mtoto wa Jabir

    "Nina watu wangu polisi! We subir uone"akajibu Alex.

    Akanyenyua simu na kupiga Tanzania kisha akaongea maneno machache pekee na kukata simu



    Shamim walishika barabara ya Shekilango na kuelekea Ubungo ili wapinde na kuelekea Kimara kisha wageuze gari ili kumpoteza yeyote anayeweza kuwa anawafatilia.

    Walipofika Romb Greeb View Hotel hapo kabla hawajafika Ubungo wakashangaa polisi sita wakiwapita na gari kasi kisha ikakata kona na kuwazibia njia.

    Wale polisi walishuka haraka kutoka kwenye gari na kutoa bunduki zao na kuwaweka Shamim chini ya ulinzi.

    Dereva aliyekuwa akiendesha gari ya akina Shamim alishtushwa na kile kitendo cha ghafla.

    Alishika breki ghafla sana ili ageuze ila akawa amechelewa kwa sababu gari yao ikawa imewafikia wale polisi kalibu sana.

    Shamim aka.......

     Shamim alishtushwa na lile tukio la kuwaona polisi mbele yake wakiziba njia na kuwanyoshea silaha.

    "Bosi tunafanyaje? Tuwamalize?"akauliza mmoja wa wale vijana.

    "Subiri kidogo! Usifanye papara isije kutugharimu"akajibu Shamim.

    Shamim alitoa simu yake na kupiga namba ya bosi wao.

    "Tumezingirwa na askari hapa tulipo na ni eneo lenye makazi ya watu na mbali na tunapoishi! Vip tuwamalize au?"akauliza.

    "Naona umeanza kufanya mambo kwa busara! Wamewaonesha silaha?"akaulizwa.

    "Ndiyo inaonekana wametonywa na mtu kuhusu sisi"akajibu.

    "Basi acha kupambana nao ila jisalimishe"akajibiwa.

    "Boss....."akakatishwa.

    "Nimesema jisalimishe! Wewe si umeshindwa kuwa makini? Jisalimishe"akafoka bosi wake.

    Shamim hakuwana ujanja wowote na alishapewa sifa za askari wa kitanzania kuwa wako fiti sana na wote huwa wanakuwa na silaha kali aina ya AK 47 tofauti na wale wa kule kwao Kenya ambao wapo wapo tu akaona akilianzisha inaweza kumletea shida na hata kujikuta akipoteza maisha.

    Alikata ile simu na kuwageukia wenzake.

    "bosi kaagiza tijisalimishe"akawaambia.

    "Haiwezekani bosi! Tujisalimishe na kesho sura zetu zizagae kwenye kile chombo cha habari? Me siko tayali"akajibu mmoja wao.

    "AbduMalick badilisha gari ndani kwa ndani hii mitambo yetu isilete shida na hizo silaha zenu tunzeni kwenye hii mashine hapa"akatoa maagizo.

    Maneno ya Shamim kwa wale vijana yalikuwa sheria kwa sababu walikuwa wakifanya kazi chini yake kwa muda mrefu sana.

    Gari ile iliyotengenezwa kwa muundo wa viti kubadilishwa kuwa vifaa vya kisasa vya kiteknolojia ilikuwa na uwezo wa kubadilishwa na kurudi katika hali ya kawaida bila binadamu yeyote kushtukia.

    Ni gari ambayo ilitolewa oda maaulumu na muundo wake wa kutengenezwa ukiwa uetolewa na Mahmoud mwenyewe kwa ajili ya kazi zao maalumu huko Japani.

    Na Wajapani hawakulemba walitengeneza gari ya kiwango cha juu kisha akakabidhiwa Shamim kwa ajili ya kazi za kikundi kile.

    Baada ya gari kubadilishwa na kutengeneza mwonekano mzuri wa kawaida Shamim alinyoosha mikono juu nje ya gari na kushuka taratibu.

    Askari wale walipatwa na mshangao kutokana na ile style ya Shamim.

    Wao kwa jinsi walivyoelekezwa walijua wanaenda kupambana na bonge la gaidi ambalo halikubali kushindwa.

    Mara baada ya Shamim kutoka wale vijana wake nao walitoka na kunyoosha mikono juu.

    Askari wale waliwakimbilia na kuwapigisha magoti chini kisha wakaanza kuwakagua kama kuna silaha yeyote waliyonayo.

    Cha ajabu tena hawakuwakuta na silaha yeyote ile.

    Wengine waliingia kwenye gari lile na kukagua kila sehemu ila bado hawakufanikiwa kuambulia chochote kile.

    Mmoja alitoa simu aina ya redio call ya kipolisi na kuanza kuongea.

    "Kikosi namba nne saba .....krooo....unanipata mkuu.......doria namba mbili.......nakupata afande.....tumewakamata afande........wapeleke kituoni over.........hawana kitu over........wapeleke hivyo hivyo nitakuja hapo muda si mrefu over......nimekupata over...."akamaliza.



    Alex akiwa na wale matajili wake walikuwa wakisubiria simu kutoka Tanzania kwa Askari waliyempa maagizo.

    Baada ya nusu saa tangu wampigie simu Alex alinyenyua simu yake na kupiga.

    "Ndiyo afande"akasema.

    "Wameshakamatwa ila naona kama sio wao kwa sababu hawajaonesha upinzani wowote ule na pia hawajakutwa na kitu chochote hatarishi"akajibiwa.

    "Walikuwa kwenye gari aina gan?"akauliza

    "Ni Range nyeusi kaka"akajibiwa

    "Ni wenyewe kaka si kuna mwanamke kati yao?"akauliza

    "Ndiyo yupo mwanamke mmoja!"akajibiwa.

    "Ndiyo wenyewe kamanda"akajibu.

    "Sidhani kaka! Hawa hawana japo dalili za ugaidi kaka"akaambiwa.

    "Kesho nitakuja hapo wewe watunze hao mpaka nifike kwa sababu tunamhitaji huyo mwanamke zaidi ya dhahabu kaka! Tafadhali taja kiasi gani chochote kile utapewa ila mwanamke huyo apatikane"akasema

    "Basi tutaongea ukija bosi"akajibiwa na simu ikakatwa.



    Wakati wote yule askari anaongea na Alex na Shamim alikuwa pale akimsikiliza

    "Nimekwisha!! Bora ningepambana nao"aliwaza



     Alex aliwaeleza wenzake hatua aliyofikia kuhusiana na kumkatamata Shamim.

    "Unahidi atakuwa yeye?"akaulizwa

    "Asilimia mia moja nyie mtaona wenyewe"akasema.

    "Tutakupa vijana wakusaidia ukipata shida na pesa ya kutosha! Na tunakutakia mafanikio katika hili"akaaambiwa.



    Upande wa Shamim mara baada ya wale askari kuwasiliana na kiongozi wao aliyewapa kazi ya kuwakamata waliwachukua ili wawapeleke Kituoni.

    "Mnatupeleka kituoni kwa kosa gan? Mmetukamata ila hamjapata chochote kile kibaya sasa kituoni mnatupeleka kwa minajili ipi?"akauliza Shamim.

    "Hatuhitaji maswari sawa? Sisi ni askari wa jeshi ra polisi hayo maswari utayauriza kituoni! Afande rikamate hiri rianamke risagane ndo rinareta ujinga"akaongea askari mmoja kwa lafudhi ya Kikurya.

    Shamim aliwaangalia wale askari na pia akawaangalia wale vijana wake.

    Akajiuliza afanyeje pale? Aende kituoni au ajiondoe vip pale??

    "hapa nikienda kituoni ntajiweka kwenye wakati mgumu! Hawa watakuwa wamepewa maelekezo! Kwa sababu hawawezi kukurupuka na kutuhisi! Na kama wamepewa maelekezo kunitoa ndani inaweza leta shida! Napaswa kutumia akili"alijisemea.

    Giza lilikuwa limetanda sana eneo lile kwa sababu ya kukatika kwa umeme na hiyo ikawa faida kwa Shamim.

    Ila eneo lile lilikuwa na makazi ambayo angeleta tafrani lingejaza watu wengi.

    Lakini pia akawaza kuwa angepambana na wale askari na kuwaachia majeraha ingeleta shida na polisi wangewasaka kwa nguvu sana.

    Pale pale akapata wazo lake na kuamua kulitumia.

    Askari wale wakati wakijalibu kuwanyenyua kutoka pale chini walipokuwa wamepiga magoti na hiyo ndiyo nafasi aliyokuwa akiisubiri.

    Askari aliyeenda kumnyenyua alimfata kichwa kichwa na kumshika mikono akiwa na dharau kuwa yule ni mtoto wa kike.

    Alipomshika Shamim alimpindua na kumbinua mkono kwa nyuma mpaka yule askari akahisi maumivu na kuachia ile silaha yake ining'inie kwa chini na Shamim akaiwahi na kuishika kisha akamkata yule askari na kumtumia kama ngao.

    "Wekeni silaha zenu chini au nimmalize huyu mwenzenu"akasema Shamim.

    Wale askari walipigwa na butwaa pale wakitafuta namna ya kumnasua mwenzao.

    Shamim hakuwapa nafasi ya kufikiria tena akafoka.

    "Sihitaji masihara hapa na naanza kuhesabu,moja.....mbili...."hakumalizia.

    "Basi....basi jaman"akasema mmoja wao na kuweka silaha yake chini.

    Wale wenzake walipoona yeye kaweka hawakuwa na namna na wao wakaziweka chini zile silaha.

    "Rudini nyuma hatua tano"akafoka Shamim

    Wakaanza kurudi nyuma taratibu mpaka walipofikisha hatua alizoomba.

    "Bebeni zile silaha zao J"akasema Shamim.

    Wale vijana wake wakaenda na kuokota silaha zile na kuwa nazo.

    "Na wewe kaungane na wenzako! Na hiyo redio call naiomba hapa haraka"akafoka.

    Yule askari aliyekuwa naye akaenda kujiunga na wenzao.

    Kisha wakatoa redio call na kumpa mmoja wa vijana wa Shamim

    "J nenda katoboe tairi za ile gari yao"akasema Shamim

    "Lala chini wote na msiinuke kabla hatujaondoka"akafoka Shamim.

    Wale askari hawakuwa na ujanja ikabidi walale chini na Shamim na wenzie wakaingia kwenye gari yao na kuigeuza kisha wakarudi mpaka Sinza Mori na kushuka kuelekea kwa Kakobe mpaka walipoishika barabara ya Sam Nujoma kuelekea Sheli ya Mlimani city wakatupa silaha nje ya gari na ile redio call kisha wakashika njia ya kuelekea Mliman chuo.



    Alex aliondoka kwa wale mabosi wake na kuelekea Hotelini kulala akiwa na amani kubwa sana kwani kuweza kumkamata Shamim jambazi wa kike aliyewasumbua kwa muda mrefu ingempa sifa kubwa kwa mabosi wake wale.

    Alilala usingizi mwololo mpala asubuhi!

    Kesho yake alianza safari kuja Tanzania akiwa na lengo la kumchukua Shamim ambaye yeye hakumjua kwa sura yake halisi kuwa ni yule mpenzi wake Lily bali kwa sura bandia kisha amkabidhi kwa vijana wa bosi wake wammpeleke Dubai kwa mabosi na yeye apewe donge nono!

    Wakati huo huo Shamim alikuwa uwanja wa ndege kukabiliana naye!!!



    Shamim alipofika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitulia sehemu ya kuwapokea abiria na kusubiri huku akiwa kawaacha vijana wake distance ndogo sana kutoka pale alipokuwa kakaa yeye.

    Wakati Alex anatokeza kwenye mapokezi ile akiwa na uso wa furaha akiwa hajui chochote kile kuhusiana na Shamim kuwaacha polisi solemba.

    Alipotokeza eneo la mapokezi akiwa na vijana wake wale aliokabidhiwa kutoka nje ya nchi ili akishampata Shamim awakabidhi kisha waondoke naye kwenda huko.

    Alipatwa na bumbuwazi pale alipomuona Lily akiwa amekaa eneo lile.

    "Lily.....au nimekosea?"alijikuta akiongea bila kutarajia.

    Lily au Shamim kama wengi wanavyomfahamu alinyenyuka bila kujibu neno na kumkumbatia Alex na kumbusu mbele za watu bila kuona aibu mashavuni kisha akahamia mdomoni.

    "Nilikumis sana baba"akasema Lily

    "Hata mimi pia mama nilikumis sana! Vip hapa? Au umekuja kunipokea?"akauliza Alex.

    "Hapana babaa! Ningejuaje unakuja? Kuna mtu ana vitu vyangu ndo nimekuja kumpokea"akasema.

    "Oooh!! Vip ameshafika tuondoke?"akauliza Alex.

    Wakati wanaongea wale vijana wa Alex walipita kama hawajuani na Alex.

    "Bado babaa! We nenda tutawasiliana nikishampokea huyu"akajibu Lily.

    "Poa mama! Mwaaaaa!!"akajibu Alex kwa kumbusu!.

    Waliagana na kisha Alex akaondoka na wale vijana wake.

    "Wameshaondoka bosi"akatumiwa ujumbe Shamim.

    Shamim au Lily aliondoka eneo lile na kupanda gari la vijana wake kisha wakaanza kumfatilia Alex na wale vijana wake kwenye lile gari lao.

    Alex alielekea moja kwa moja mpaka kituo cha polisi alichokuwa na mawasiliano na bosi wao kuhusiana na sakata la Shamim.

    Mpaka anafika pale kituno Shamim alikuwa akifatilia mchezo mzima.

    "Mkuu wenu nimemkuta?"akauliza Alex.

    "Yupo kwani wewe nan? Na una shida gan?"akauliza askari aliyekuwa kaunta.

    "Mwambie kijana wake kutoka Dubai"akajibu Alex.

    Yule askari alipiga simu ndani na kutoa maelekezo kidogo kisha akasikiliza na kukata.

    "Ingia mlango wa pili upande huu wa kulia"akasema yule askari.

    Alex aliongozana na vijana wake mpaka kwenye ile ofisi na kugonga na alipojibiwa akaingia.

    "Oooh!! Kijana wangu! Za ng'ambo?"akasema yule askari.

    "Salama za hapa bosi wangu?"akasema Alex.

    "Za hapa si nzuri sana"akajibu yule askari.

    "Kwanini zisiwe nzuri bosi wangu?"akauliza huku wasiwasi tayali ukiwa umeanza kutanda usoni pake.

    "Kwanza niambie watu wale wa jana ni watu wa aina gani? Kwa sababu mpaka sasa tumechanganyikiwa kabisa!"akajibu askari.

    "Mbona unanichanganya bosi wangu? Aina gani kivip? Kuna kitu kimetokea?"akauliza Alex huku akiwa tayali amehamaki.

    "Bana yule mwanamke sio mtu wa kawaida kabisa! Alichowafanyia askari wangu!!! Yaani we acha tu! Hapa nilipo vijana wangu sita wako makao makuu chini ya ulinzi na mimi nina kesi ya kujibu huko!"aliongea huku akiwa kajiinamia.

    "Hebu kuwa wazi tafadhali nini kimetokea? Na imekuwaje wawe chini ya ulinzi?"akauliza tena Alex.

    "Katoloka !?"akauliza Alex akiwa kahamaki.

    "Vijana walifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi yeye na wale vijana wake ila style aliyotumia kutoloka imetuweka matatizoni sana! Kwa sababu hakuna alama aliyoacha nyuma! Wakubwa wanauliza tulikuwa tunapambana na gaidi gan? Kwa sababu alifanikiwa kuwadhibiti vijana wangu na kuondoka na bunduki zao bila hata kuwapiga kofi hivyo serikali inaulizia bunduki zake na haiamini kuwa gaidi anaweza wekwa chini ya ulinzi usiwepo mlio wa bunduki au yeyote kati ya wale askari aliyejeruhiwa! Unaona kesi ilivyo ngumu?"akasema yule askari.

    "Unajua sijakwelewa kawatoloka kivip? "akauliza kwa mshangao Alex.

    "Nakwambia hata mimi vijana wangu siwaamini ila kwa sababu mimi ndiye niliyewatuma ndo maana naamini na amini usiamini hakuna aliyepigwa japo kofi ila wote hawana silaha zao na kawaida ya jeshi wana kesi ya kujibu"akajibu.

    "Aisee sikuele........"hakumalizia kuongea simu yake ikaanza kuita.

    "Nipigie baad........"alitaka kukata simu ila alichokisikia alibaki amepigwa na butwaa!!!



    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog