Search This Blog

Thursday, 19 May 2022

MUUZA MAZIWA - 4

 





    Chombezo : Muuza Maziwa

    Sehemu Ya Nne (4)





    “aaaaahh!! Jamani wifi wao!!”

    Aliongea kwa furaha baada ya kumuona mgeni aliyekuwa akigonga ni penina.

    “asante wifi , shikamoo!”

    Penina aliongea na kisha kumkumbatia wifi yake kwa furaha.

    “ marhaba wifi ,vipi masomo?”

    Aliongea huku akiipokea mizigo aliyo ibeba

    “naendelea vizuri tu wifi”

    “haya mungu akusaidie”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliongea lisa na kuelakea sebuleni , aliiiweka mizigo pembeni ya kochi na kasha kuelekea sehemuk ilipo friji. Penina, penina akaamua kuichukua mizigo ili aipeleke chumbani.

    “hapana wifi, hapana , hiyo iache hapo hapo nitaiingiza mwenyewe,, wewe kwanza kunywa juisi upumzike.“

    Aliongea lisa huku akiwa ameshikilia jagi lenye juisi pamoja na glasi, alifanya hivyo kwa sababu chumba anachotakiwa kulala penina ndicho chumba ambacho amemficha muuza maziwa.

    “usipate tabu wifi wangu kunywa juisi upumzike, nipo kwa ajili yako “

    Aliongea lisa huku akiibeba mizigo na kuelekea chumbani na kumuacha penina akinywa juisi taratibu.

    Alipoingia chumbani alimshutua muuza maziwa na kumweleza hali halisi.





    “kwahiyo nitatoka saa ngapi humu?”

    “ itabidi uvumilie mpaka usiku wifi akilala , mlango wa nje nitauacha wazi leo”

    Aliongea lisa

    “Sawa lakini vipi kuhusu chakula manaake niana njaa”

    “ usijali nitakuletea utakula humu humu , jitahidi usitoke nitajaribu kufanya mpango hata kamakabla ya usiku ikiwezekana”

    “poa”

    Muuza maziwa aliitikia

    “alafu nitaa……”

    Lisa alikatiza kauli yakebaada ya kusikia mlio wa kitasa kikifunguliwa. Haraka haraka muuuza maziwa aliingia kabatini na kisha lisa aliufunga mlango wa kabati hiyo kabla hata hajauachia mlango huo alisikia sauti nyuma yake.

    “wifi mbona unagombana na hilo kabati!?”

    Swali hilotoka kwa penina lilimfanya lisa ashikwe na kigugumizi cha ghafla huku akitoa maelezo ya kujikanyagakanyaga.

    “ah, mh, a-, u-n-a-j-u-a hi-li ka-ba-ti ni bo-vu”

    “limeharibika , ooh, mungu wangu!”

    Penina aliongea huku akilisogelea kabati hiloili kuiangalia sehemu ilipoaribika.

    “ah, hapana wifi usiiguse hapa nimeitegesha , iache hivyo hivyo mpaka atakapokuja fundi kulirekebisha”

    Aliongea Lisa haraka haraka.

    “okey”[sawa]

    Aliongea Penina huku akitikisa kichwa kuonyesha kwamba ameelewa.

    “nataka kuoga wifi”

    “na kweli manaake umechoka kweli kweli wifi yangu”

    Aliitikia Lisa haraka haraka kwani alijua huo ndio upenyo wa kumtoa muuza maziwa.

    Na kweli penina alipoingia bafuni lisa aliufungua mlango wa kabati haraka na kumtoa muuza maziwa , akala chakula haraka na kuanza safari ya kutoka nje ya nyumba hiyo , walipofika kwenye mlango wa kutokea muuza maziwa alimbusu lisa kwa mara ya mwisho , alipomaliza kufanya hivyo alitoka ndani ya chumba hicho na kutokeza koridoni ili atoke nje kabisa ya nyumba hiyo lakini kabla ya kufanya hivyo alisikia muungurumo wa gari, halikuwa gari lingine bali gari la Jerry mume wa Lisa.

    Hofu iliwaingia kwa ghafla na haraka haraaka walirudi tena chumbani kwa penina , ambapo kama kawaida alimfungia muuza maziwa kabatini, hawakuwa na njia nyingine tena bali hile waliyoipanga awali, muuza maziwa asubiri mpaka usiku wa manane Penina atakapo lala ndipo atoke kwani Lisa atauacha mlango wa kutokea wazi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lisa alipomaliza kumfungia muuza maziwa katika kabati alitoka nje ya chumba hicho,akiwa koridoni aligongana ana kwa ana macho na mumewe. Wote wawili waliinamisha vichwa vyao chini. Kwani kila mmoja aliona aibu kwa kumsaliti mwenzake.

    Lisa kwa muuza maziwa na Jerry kwa sekritari wake.

    “Ah, mmh, wifi amekuja , kakaribu!”

    Aliongea Lisa kwa kujiumauma huku akiwa na wasi wasi.

    “ asante amekuja saa ngapi?”

    “sio muda mrefu”

    “aah yuko wapi sasa nimsalimie?”

    “yuko bafuni anaoga”

    “Okey” [sawa]

    Aliitikia na kisha kuelekea chumbani kwake.

    Lisa nae alimfuata mumewe nyuma hukubado akiwa na hofu juu ya kugundulika kwa uwepo wa muuza maziwa ndani ya nyumba hiyo.

    “Pole na kazi dear”

    Aliongea Lisa huku akijibaraguza kwa kumvua tai mume wake, macho yake bado yalikuwa na aibu sababu bado alikuwa na wasi wasi kwamba labda mumewe amegundua chochote.

    “ah, asante mpenzi”

    Aliitikia Jerry huku akitabasamu, lakina nae pia tabasamu lake liliishia mdomoni tu moyoni nafsi ilimsuta .

    Maovu aliyoyafanya na sikritari wake ofisini kwake yalikuwa bado yakionekana katika kichwa chake.

    Akavua nguo na kuingia bafuni kuoga lisa nae alimfuata na kujumuika nae kuoga . Alifanya hivyo ili Jerry hasihisi chochote.

    Walioga huku kila mmoja akiwa hana habari na mwenzake. Kwani wote wawili walikuwa wamechoka, walipomaliza kuoga wakavaa na kasha kwenda sebuleni. Huko wakamkuta Penina akianga lia tv.

    “mdogo wangu huyo!”

    Jerry aliongea kwa furaha huku wakicheka.

    “kaka!”

    Penina aliitikia na kisha kumkimbilia kaka yake.



    “waoo!!!”

    Waliongea kwa pamoja na kisha kukumbatiana kwa furaha.



    “habari za masomo!?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “nzuri tu kaka, shikamoo!”

    Aliitikia Penina na kasha kumwamkia kaka yake

    “marhaba mdogo wangu>“

    Aliitikia salamu.

    “Penine kanenepa kweli safari hii, shule imempenda kweli.”

    Aliongea Lisa.

    “hapana wifi!?”

    Penina aliongea na kasha kucheka, ukweli ni kwamba kweli alikuwa amenenepa na kujengeka shepu kwa mahipsi na makalio yaliyo fungashika kiinye plus gwedegwede.

    Waliongea mengi wakiwa na furaha ya kuwa pamoja tena. Upande wa Lisa moyoni hakuwa na furaha hata kidogo, muda wote alifikiria jinsi ya kumtoa muuza maziwa ndani ya nyumba hiyo.

    Alifahamu fika jinsi swala hilo lilivyokuwa gumu kwani chumba alichomficha ndicho chumba atakacholala penina , hakuelewa angeweza vipi kumtoa muuza maziwa katika chumba hicho bila ya Penina kugundua.

    “sijui nitafanya nini mungu wangu?”

    Aliwaza bila kupata jawabu, hakuona aibu kumshikilikisha Mungu katika uovu wake.



    “atalala tu lakini , na hivi alivyochoka, na huo ndio utakuwa muda muafaka”

    Alizidi kuwaza,

    Hiyo ndio ilikuwa njia pekee aliyoitegemea alitumaini Penina atakapolala ndio uwe muda muafaka.

    “wifi vipi mbona utafikiri uko mbali sana!?”

    Penina aliuliza baada ya kugundua kwamba Lisa hayupo pamoja nao katika maongezi.

    “hapana nipo , mbona tupo pamoja!.“

    Aliitikia Lisa haraka haraka baada ya kuzinduka toka kwenye mawazo mazito aliyokuwa nayo.

    “kweli Lisa upo tofauti sana leo”

    Jerry nae alikazi

    “hapana jamani mbona nipo sawa!”

    Lisa alizidi kujitetea kwa nguvu zake zote kwani hakutaka mtu yoyote ahisi chochote kuhusiana na swala hilo la muuza maziwa, alichokifanya baada ya hapo ni kujaribu kujichekesha na kuonyesha kuwa ana furaha ili kupoteza kabisa hisia za mumewe pamoja na wifi yake.

    Waliongea kutwa nzima mpaka usiku ukaingia , baada ya chakula cha usiku kila mmoja alielekea chumbani kulala Jerry na mkewe chumbani kwao na Penina pia alielekea chumbani kwake.

    Wakiwa kitandani kwao si Jerry wala mkewe aliyeonekana kumjali mwenzake, kila mmoja aligeukia upande wake , kila mmoja alirizika na usaliti alioufanya mchana wa siku hiyo. Jerry alipotembea na Sekritari wake wakati Lisa alipotembea na muuza maziwa.

    Hakuna aliyejua maovu ya mwenzie kila mmoja alimuona mwenzake karanga bao na kumlalia mzungu wa nne.

    xxxxx- - - - xxxxxx—- - — xxxxxxxx



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa sita na nusu usiku Penina alishtuka toka usingizini , hii ni baada ya kusikia mlio wa kabati likifunguliwa , haraka alisogeza mkono wake kwenye swich ya taa na kuiwasha. Mwanga ulitanda chumba kizima . Penina hakuamini alipomuona mtu akiwa amesimama karibu kabisa na kabati huku kabati likiwa wazi.

    “kaka! , kaka!, mwizi! Mwizi!1”

    Penina alipiga yowe kwa hofu huku akimwangalia muuza maziwa vizuri.

    Muuza maziwa alikuwa akitetemeka mwili mzima, sauti ilikwisha fika chumbani mwa akina Jerry, Jerry alikurupuka na kumwamsha mkewe . Lisa alichanganyikiwa kusikia taarifa hizo alijua kwa vyovyote vile huyo atakuwa ni muuza maziwa.

    “mungu wangu, sijui nifanyeje mie!!”

    Aliongea Lisa kwa mshituko

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“utafanyeje nini?, twende au umesahau kwamba tuna Bastora!?”

    Jerry aliongea akiwa ameishikilia bastora yake kwa kujiamini. Hakujua kwamba mkewe hakuwa anaogopa mwizi bali alimhurumia muuza maziwa.

    Muuza maziwa alizidi kutetemeka hakujua afanye nini miguu yote iliishiwa nguvu alishindwa kusimama wima akaegamia kabati.

    “da– da—mi-mi si-o mwi-zi!-zi-zi”

    Aliongea muuza maziwa huku akitetemeka kupita kiasi.



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog