Chombezo : A Twin Sisters
Sehemu Ya Tatu (3)
"carl jua wewe ndo umenileta kwenye ulimwengu wa mapenzi lakini tazama una mwanamke mwingine na sijui kabla ya huyo ulikuwa nao wengne wangapi?"
"sio hivyo sophy huyu nimekutana nae baada ya kupotezana lakini usijari nakuja hapo nje unikumbushe yale mambo ya kipindi kilee" nililia sana baada ya kumaliza kusoma.
SONGA MBELE..
Nilitafakari mambo mengi na kukuta mazingira yaliyomkuta sophy yanaweza kunipata na mimi pia, carl ni mwanaume wangu wa kwanza na pia nimetokea kumpenda kuliko kitu ingine na yeye pia alionyesha kunijari sana kumbe ananing'ong'a laiti ningetambua mapema ningeachana nae ona sasa amerudia na sophy na huko kazini kwake sijuí anao wengne wangapi ila sophy ni mwanamke mwenzangu nitamuita na kumwambia ukweli najua atanielewa ila kwa carl ni lazima nimuonyeshe msimamo wangu. Ebu ngoja nikapate uhakika.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilinyanyuka nikawa kama naenda toilet huku nafanya uchunguzi wa kugundua ni wapi walipo nipate ushahidi. Mpaka naingia chooni sikuweza kumuona mtu nikawa nimesimama karibu na mlango wa sophy nikawa namsikia carl akimshukuru sophy kwa penzi motomoto alilompa na kumuahidi ni lazima afunge nae ndoa yani ahadi zote alizokuwa ananiambia mimi ndo zile zile alizokuwa anampa sophy nilirejea chumbani kwangu nikazima taa na kujifunika na blanketi.
Nilimuona carl anakuja huku ananyata nilimtazama tu ile anataka kulala nikawasha taa, akaumbuka alikuwa na boxer tu mwanaume mzima hata aya hana, akaanza kujibaraguza.
"eeh mpenzi upo nilienda chooni mara moja hapo vipi lakini?"
"poa tu, ebu angalia simu yako naona inaita sijui"
Nilimtazama alivyokuwa anatafuta maelezo ya kunipa baada ya kugundua ile simu aliificha ndani ya mto then anakuja kuiona nampa mimi mkononi, ataniambia lipi nimuelewe ngoja nimsikie atajiteteaje maana kichwani kwangu tayari nilishapata jibu la kumpa.
"mpenzi wangu naomba nisamehe huyu msichana ananitaka kwa nguvu tokea tupo shule lakini nakuomba unisamehe kwa yote"
"haya ebu tumuite huyo sophy atamwambie ukweli juu ya hilo"
"haina aja ya kumuita mpenzi wangu tuyamalize sisi wawili"
"haya sawa hamna tabu"
Nilimwambia lakini moyoni mwangu ajui ninachofikiria akaanza kunishika shika nikatoa mkono wake huko na kumwambia "kwani wewe haujalizika bado au niache na mimi nilale basi" nilitalala zangu mpaka ilipotimu saa moja asubuhi nikaenda kumuita sophy kipindi hicho carl alikuwa bado amelala. Baada ya sophy kuingia ndani nilimuamsha carl alipomuona sophy hakuamini macho yake akawa anatetemeka mwanaume mzima hata kuongea alishindwa aibu ilimjaa sijawai kuona.
"haya sophy karibu shoga yangu wala usiogope nakuomba uongee ukweli wako wote usifiche neno hata moja"
"kiukweli carl nimemjua tukiwa chuo na yeye ndo alikuwa mwanaume wa kwanza katika maisha yangu ilifikia kipindi alinipa ujauzito na hii yote kutokana na kuniforce tufanye ngono wakati nilikuwa kwenye tarehe mbaya baada ya kunipa ujauzito akawa ananikwepa sasa nikimpigia simu hapokei au anazima tokea hapo nikaashana nae mpaka leo hii namuona kwako"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"carl mimi na wewe tumekutana wapi? Si tumekutana casino tena wanapojiuza wanawake, uliambiaje kipindi tunakutana? Sasa ngoja nikwambie kitu umenisaidia mengi sana ila mimi sipendi kunyanyaswa hata kidogo nadhani unaweza kwenda ebu amka hapo kitandani uende kwako na kama mimba nitarea mwenyewe hata sihitaji msahada wako tena"
"flavian unanifukuza kweli?"
"carl usifukuzwe wewe umekuwa nani. Mama yangu au? Ebu toka bwana utaenda kuoga huko kwako" nilitoa viatu vyake na kumtupia nje huku natoa shuka ili atoke zake mimi siwezi kubembeleza mwanaume hata kama nilimpenda sana.
"flavian unanifukuza kweli"
"iiiih carl usifukuzwe umekuwa nani! Mama yangu au? Ebu toka nenda kwako bwana utaoga huko huko kwako" Nilitoa viatu vyake na kuvitupa kwa nje nikarudi ndani na kulitoa shuka ili aamke.
TIRIRIKA SASA.
"flavian haufanyi sawa wangu sio njia nzuri bwana hiyo"
"toka bwana wee na wewe si malaya tu utaniambia nini"
"baba nakuomba amka uwahi kwako hapa sikutaki"
Nilikuwa na hasira hatari na mimi katika maisha yangu sipendi kunyanyasika so sioni shida kumtimua mtu anayenifanyia ujinga. Carl aliamka akavaa suruali yake na kutoka nje kuchukua viatu vyake akavaa na kurudi tena ndani muda huo mimi nilikuwa nimesimama huku sophy akiwa amekaa kitandani, carl alinitazama na kuniambia.
"flavi kosa moja haliashi mke nakutakia maisha mema kama ukipata shida usisahau kunipigia simu hela hiyo hapo ya matumizi"
Niliendelea kumtazama ile hela akaiweka kitandani na kuondoka zake mimi nilianza kujifikiria kwa kile nilichokifanya kama ni sahihi au laa. Nilimuona sophy kama anataka kuniambia kitu lakini anasita nikamwambia "unasemaje sophy"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"nimetokea kukupenda sana flavian yani nimewahi kuwa na marafiki ila sijawahi kuona mwenye msimamo kama wewe naomba tuwe marafiki maana umenifundisha kitu kikubwa sana katika maisha yangu"
"usijari sophy nitakupenda kama ndugu yangu kwani hapa unaponiona sina ndugu zaidi ya pacha mwenzangu nae kama amenisusa wala haji hata kuniona nakuwa mpweke muda wote"
"usijari wangu mimi nakupenda sana naomba usijisikie upweke"
Alinikumbatia na huku kichwani nikiwa namfikiria flaviana mdogo wangu aliyenisusa hata akutaka kuniona kabisa, nilimtazama sophy nikawa namchukulia kama flaviana tu kwani yeye alikuwa mdogo kwangu au inawezekana tukalingana.
***
Mimi na sophy tulikuwa marafiki wakubwa sana kiasi kwamba akanitafutia kazi pale hotelini kwao traveta hotel iliyopo mpakani mwa tz na kenya na ilikuwa ni hotel kubwa ya kitalii. Niliweza kuweka pesa zangu kwenye account ili nije kuanzisha biashara yangu.
Siku ya wikiendi mimi na sophy tuliamua kwenda kwa yule mama ambaye alikuwa anatutunza mimi na flaviana, tulikuwa tunatembea mitaa hiyo ya njiro kwa miguu huku tunapiga stori zetu mara gari kubwa aina ya nissan terrano likaja kupiga breki mbele yetu na kioo kikafunguliwa kutazama alikuwa ni bamdogo peter aliyeenda ulaya kusoma toka nikiwa na miaka 10 leo nakuja kumuona akiwa na miaka 22 ni zaidi ya miaka kumi na mbili imepita.
"eeh flavian upo wewe?"
"nipo shikamoo"
"heee yani nimewaulizia sana kwa shangazi zako kila mtu anaonyesha hana muda na nyie ebu pandeni kwenye gari twende sehemu tukaongee"
"haa bamdogo tumekuja kumuangalia flaviana hapa maana sijaönana nae muda mrefu"
"wewe kwani wewe unakaa wapi hapa nyumbani vipi umeondoka?"
"ni stori ndefu bamdogo nitahadithia ngoja nimuangalie flaviana"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipiga hodi akafungua mlinzi aliyekuwa ananikumbuka nikamuuliza "vipi mama yupo?" akasema "ndio yupo" nikamuuliza tena "flaviana nimemkuta" hapo nilikuwa kama nimemkumbusha kitu.
"sesesese! Dada yani ukimuona uwezi kuamini sio flaviana unayemjua wewe"
"kwanini jamani mbona unanitisha"
"sasa hivi anajiuza hapa nina kama mwezi sijamuona"
"yani dada ukimuona sasa hivi uwezi amini amebadilika sana"
"mbona unanitisha amekuwaje?"
"sasa hivi anajiuza uwezi kuamini kama ni flaviana yule"
TIRIRIKA NAYO.
"bamdogo peter umesikia hayo?"
"eeh jamani imekuaje amefikia kote huko?"
"nitakwambia uncle"
"haya pandeni kwenye gari twendeni kwangu tukapafahamu"
Tulifika mpaka kwenye nyumba yake aliyoinunua ilikuwa ni nyumba kubwa sana na yenye uzio mkubwa mno humo ndani kulikuwa na bembea za watoto, swimming pool, garden house iliyozungukwa na maua mazuri ya rangi mbali mbali. Kwa pale bamdogo alikuwa peke yake na wafanyakazi mke wake yeye yupo dar, yeye baba anafanya kazi shirika la ndege la kenya "kenya airway" kwahiyo kipindi cha likizo ukitumia kuja kuspend na wanafamilia Tanzania. Tulikaribishwa kwenye garden nzuri penye upepo mwanana na maongezi yakaanzia pale.
"kwanza pole kwa kufiwa na wazazi, ila napenda kujua ilikuaje baada ya matatizo yale kuisha?"
"bamdogo ni story ndefu lakini kipindi msiba ulipokwisha tulikabidhiwa kwa bamkubwa ambaye familia ilimteua kama msimamizi mkuu wa mirathi lakini cha ajabu akutusomesha na kibaya zaidi akauza ile nyumba tuliyokuwa tunaishi tukaamia mtaani na kulala kwenye vibaraza vya watu tukikoswa koswa kubakwa nilijitahidi kutafuta kazi ya kufanza ila kazi zilikuwa ngumu kupatikana hata zikipatikana mpaka utoe rushwa ya ngono tumepata shida nakumbuka katika zungukazunguka zetu ndo tulipita hapa kama bahati yule mama aliyenunua hapa aliamua kutuchukua ndo mpaka leo yupo na flaviana mimi nilikataa kujiuza ndo nikaamua kuondoka ila ndugu hata mmoja akuwai kutujari kwa lolote matokeo yake flavi ameamua kujiuza"
Uncle aliumia sana akaanza kutoa machozi, nilimuonea hadi huruma tukanuia kumtafuta flaviana kwa udi na uvumba.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa ni ijumaa usiku tulimkuta club de casino akinywa mvinyo huku amevaa nguo fupi hamna mfano na mkononi alishka sigara nilimsogelea na kumvuta mkono mpaka nje alipokuwepo bamdogo peter nae aweze kujionea kwa mara ya kwanza "flaviana umepungukiwa na lipi mpaka upo huku?"
"maisha tu bamdogo usijari yote haya yatakwisha nikipata maisha safi hapa natafuta sembe"
***
Flaviana alipelekwa shule kenya akaanza sekondari mimi nikaenda kusoma mambo ya biashara chuo cha CBE hapo dsm tena mji wenye mrundikano wa watu na kila aina ya starehe. Sikutaka kuweka utani kwenye masomo kabisa kwani ndo kila kitu kwangu, nilimaliza certifate nikaunganisha na diploma nakumbuka matokeo yangu ya mwisho yalikuwa mazuri niliweza kucompite/kushindana na wavulana na kuwashinda hapo ndo nilianza kujulikana na chuo na wakufunzi pia.
Mark ni kijana aliye mwaka wa pili diploma nilimfahamu kupitia rafiki yangu scolastica wakati tunarejea hostel ndo tulianza kupiga stori mbili tatu akanipa namba yake ya whatsap akawa ananitumia picha, videos na music audios kiukweli he is charming/ni mchangamfu, nilianza kuchat nae kwa kutumia simu na ilikuwa ikifika saa nne usiku ni lazima tuongee. Hapohapo akaingizia mambo yake kama ujuavyo wanaume sio wavumilivu katika maswala haya, nilikuwa nawachukia wanaume na kwa wakati huo sikuhitaji mwanaume nilihitaji kufanya malengo yangu kama nikiwa nae basi ni rafiki.
"flavian me najua ni kiasi gani upendi wanaume lakini jua kama ilivyokuwa uwepo wa wabaya duniani basi hata wazuri wapo believe on me aliyekukosea ni mmoja usichukie dunia nzima"
"it can't be true kwani wewe umetoka sayari nyingine, nyie wanaume mnakuaga na maneno matamu kama utamu wa big g lakini ule utamu ukiisha unaona big g haifai tena, uwezi kunishawishi nikakubali maana nyie wanaume suruali mvaayo wote ni moja na fundi wenu ni mmoja"
Nilimpa maneno mark mpaka hakuwa hana pa kujitetea akabaki kijetetea kwa yaleyale lakini hakuwa na jipya nilimwambia nataka kulala nikamuaga na kukata simu.
Mark akuchoka aliendelea kunisumbua mara aniletée zawadi lakini wapi sikutaka kuzipokea zawadi zake nakumbuka hapo mwanzo alikuwa ni rafiki yangu mkubwa lakini nilianza kumchukia tokea aliponiambia upuuzi wake. Infront of majority nilimuumbua, ilikuwa hivi.
"flavian nimeandaa lunch kwa ajiri yako please naomba tuelekee basi"
"hivi mark unataka nini zaidi kwangu mbona nimeshakwambia tokea mwanzo kuwa sihitaji chochote kutoka kwako mbona unakuwa mgumu kuelewa lakini? Wewe ni msomi wa namna gani sio muelewa?
"naomba nisamehe sana flavi nafanya yote haya because of love please naomba nielewe tafadhari mimi sioni aibu kutetea penzi langu"
"bwana eeh kwani mwanamke ni mimi peke yangu khaa sitaki bwana"
Niliondoka zangu nikamuasha pale kasimama yupo na rafiki zangu sijui walikuwa wanamshauri nini mimi nilienda mpaka nyuma ya chuo nikaketi nikaweka earphone zangu nikawa nasikiliza music.
Kwa kipindi kile nilitokea kuwachukia wanaume tokea nilipoashana na carl nikatoa na mimba yake iliyokuwa na mwezi mmoja. Nakumbuka ilikuwa jumamosi jasmine aliniambia twende coco beach tukapunge upepo nilimkubalia tukajipanga hao mpaka coco sasa nilimshangaa mwenzangu yupo besy sana anachat nikitaka kuangalia anakwepesha simu nikasema ngoja nimuashe.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tuliagiza chakula na vinywaji tukawa tunakula huku tukitazama meli na watu wanaogelea mara ghafla mark alikuja pale nikajua ule ulikuwa ni mpango wao na jasmine na alipokaa tu jasmine alinyanyuka.
"jamani mimi ngoja ninyoshe nyoshe miguu nakuja muda si mrefu"
Niliitikia japo kwa shingo upande huku nikitamani nimfate, mark alianza kuangea maneno yake hata tention yangu haikuwa kumsikiliza maana ndo maneno yao ya siku zote, lakini kadili alivyokuwa anaongea nilianza kumuelewa kama kuna kitu cha maana anataka kusema akameza funda la mate na kusimama mbele yangu akanichum kwa nguvu bila ya mimi kutaka then akatoa pete ya uchumba na kunivalisha.
Nilibaki kushangaa inakuaje kwa mtu niliyemdharau akanivalisha pete ya uchumba ambayo hata carl akuwahi kufikiria kunifanyia hivyo zaidi aliishia kunitumia akanitia mimba na kuniasha nililia sana na kumkumbatia mark kwa machozi mengi yaliyoambatana na makamasi mepesi nisiamini kinachotokea.
Tulianza kupitia kwenye courtship/uchumba huku nikiendelea kumchunguza mark tabia zake lakini huyu mkaka alikuwa ni mwenye heshima, mpole, anajari wengne na pale chuo alipewa tuzo ya mwanafunzi bora mwenye nidhamu na ushirikiano mzuri na jamii iliyomzunguka, nilienjoy sana sana kuwa nae.
Nakumbuka kuna siku mimi na rafiki zangu pamoja na wanafunzi wengine tulipita kwenye notesbody kuangalia japo matangazo na matokeo ya mtihani wa semister ile ya kwanza. Wote tulistaajabu tulipoona mark ameongoza kwenye kozi yake na kumpita mbali sana anayemfatia. Kuna mdada alianza kuongea.
"unajua hapo mwanzo huyu mkaka nilijua wanampendelea ila baada ya kumuona niliamini kuwa kuna watu wamepewa mafunzo na wazazi wao sio bure"
"we acha ukimuona mkaka mwenyewe mpole ana muda na mtu huyu ndo anafaa kuwa rais wa wanafunzi sio yule mwakatobe"
Niliwaangalia wale wadada wakimsifia mark huku wanaondoka zao na kutuasha sisi tukiwashangaa, mara wakaja wavulana wengne inaonekana anasoma anasoma nao.
"ebwanaa kwa mara nyingine tena huyu jamaa anatukimbiza check point alizokuasha john?"
"hapa kuna upendeleo haiwezekani huyu jamaa anipite namna hii"
"bwana john wee kubali umeshindwa we point zote hizo bado unasema umeonewa"
Tuliondoka na kuwaasha wanabisha pale, na yule wanamuita john ndo alikuwa wa pili sasa amepitwa points nyingi lakini ataki kukubali kuwa amepitwa anaona kama kuna upendeleo.
****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliweza kufunga ndoa na Mark tena kanisani tukihudhuriwa na na watu wengi mno na bamdogo aliweza kughalamia kila kitu pale, na uzuri pia mark alipata kazi NMB tawi la mbagala zakhem kama wakala, nilifurahi sana kuolewa maana ndo lilikuwa hitaji kubwa la moyo wangu.
Nilianza maisha mapya ya ndoa nikiwa naenda shule na kurudi nyumbani kwangu kumuandalia mark mume wangu chakula na maji ya kuoga pindi arejeapo kutoka kazini. Hayo ndo yalikuwa majukumu yangu kama mama mwenye familia kilikosekana pale ni mtoto nae tulipanga baada ya mwaka tuzae.
Kila mtu alituonea gere baada ya kuona maisha yetu kawa watoto vile, ile asubuhi ilikuwa ni lazima tuoge pamoja ananipa dozi moja me naenda shule yeye anaenda kazini. Ni lazima anibebe mpaka nje na wakati wa kwenda kulala pia alinizoesha hivyo. Na kuna kipindi tukiwa tunaangalia tv pamoja najifanya nimelala ili nibebwe yani nilikuwa malkia kwenye dunia yangu.
Maisha yalisonga nilikuja nikapata ujauzito ila baada ya miezi miwili ile mimb ilitoka ikawa kila nikipata mimba inatoka mpaka mimba ya pili tena jumla mimba tatu na ile aliyonipa carl niliumia sana ila mpenzi wangu alinivumilia na kunifuta machozi kila niliapo alikuwa ni zaidi ya mume kwangu kuna muda nilimuita dadie maana kazi anayoifanya kama dadie at the sametime ni mume.
Mke wa bamdogo alikuwa anakuja sana pale nyumbani na kunishauri na alikuwa ni mama mzuri kwangu ila wakati tunaongea mara aliingia mume wangu mark akiwa kama ameshanganyikiwa akamsalimia mama juu juu akapitiliza chumbani niliamua kumfata ndani.
"mume wangu nini tatizo?"
"kazini kumetokea wizi mkubwa kwahiyo nimesimamishwa kazi"
Mke wa bamdogo alikuwa ananitembelea mara kwa mara pale nyumbani na alikuwa ananishauri kwa mambo mengi kusema ukweli alikuwa ni mama bora kwangu. Wakati tunaendelea na maongezi aliingia mume wangu mark akiwa kama amevurugwa alitusalimia juu juu akapitiliza chumbani kiukweli nilishtuka ikabidi nimfate nijue kilichomsibu.
"vipi mume wangu nini tatizo mbona hivyo?"
"mke wangu kuna wizi umetokea kazini nami nimehusishwa ndo nimesimamishwa kazi"
TIRIRIKA NAYO.
"jamani mume wangu upaswi kuwa hivyo matatizo kaumbiwa binadamu usiofu mume wangu haya yote yatakwisha"
"jamani mke wangu tutaishije hapa mjini huu ndio mwanzo wa kuumbuka na kwenda kuomba misaada kwa watu, na nina wasiwasi kesi isije kwenda mahakamani maana wizi umetokea kwenye kitengo ninachofanyia kazi mimi, masikini mimi nilianza kukubalika pale ofisini ndo haya yanatokea?"
"usijali mume wangu mungu atakusaidia utapata kazi sehemu nyingine"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimfariji mume wangu aliyekuwa amechanganyikiwa kabisa lakini baada ya kumpa kumpa kumbatio langu alitulia kama ndege kwenye kiota, tena nikamuandalia chakula akala na maji ya kuoga palepale alipata usingizi akalala.
Nilimweleza mamdogo yaliyomkuta mark alitamani hata kulia akatoa laki na nusu akanipa za matumizi kwani mara zote amekuwa akitumia pesa na bamdogo kupitia bank ya bacleys kwani yeye anafanya kazi kenya airport na huko ndo mdogo wangu/pacha mwenzangu flaviana.
Ile pesa tuliitumia kwa matumizi ya pale nyumbani na nauli yangu ya kwenda chuo na kibaya zaidi nilitakiwa kwenda field arusha pesa nayo haikuwepo nilikuwa kwenye wakati mgumu sana. Nakumbuka ilikuwa jumamosi asubuhi alikuja mtu na kugonga mlango nikafungua akanipatia bahasha na kuondoka hata akuingia ndani nikampelekea mume wangu ambaye alikuwa amepanga kutoka.
Ile barua ilikuwa inamtaarifu kuwa anahitajika mahakamani jumatatu saa4 asubuhi kichwa kilianza kumuuma ghafla akapoteza fahamu nilipata kibarua kumpepea mpaka alipozinduka nikaanza kumbembeleza hadi alipotulia. Yani mark hakuwa kwenda polisi hata mara moja hali hiyo ilimsumbua sana.
***.
Nilibaki kulia tu na kitanda nilikiona kikubwa mark akuwepo nami alikuwa mahabusu juu ya kesi, nilikuwa kwenye hali ya upweke sana hata mambo yangu hayakwenda vizuri.
Nilikuwa nawaöa rafiki zangu wakitoka na mabwana wenye hela zao na nilipata ushawishi mkubwa kutoka kwao lakini nilimuheshimu sana mume wangu na nafsi yangu iliona kama vile yupo karibu nami hivyo nilishindwa kufanya lolote baya juu yake.
Nilienda kwa mamdogo kumuomba pesa kidogo kwa ajiri ya matumizi lakini sikutegemea kauli aliyoniambia.
"mama kila siku utaomba hela mpaka lini najua mume wako hayupo lakini changamka mtoto wa kike wewe alaa"
"sasa mama unataka mimi nifanyaje?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"jitume mwanangu kwani unataka kusema wanaume huko barabarani na chuoni kwenu hawakufatifati?"
"wananifata mama lakini namuheshimu mume wangu"
"khaaa utakufa na njaa shoga me mwenyewe nitachoka mwenzangu kukuhudumia jitu zima na minanilii yako"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment