Search This Blog

Thursday 19 May 2022

SORRY MADAM - 2





    Chombezo : Sorry Madam

    Sehemu Ya Pili (2)



    ILIPOISHIA

    Nikauachanisha mkono wa Madam Mery kwenye mkono wangu kisha nikaanza kupiga hatua za haraka kuelekea getini

    “EDDY TAMBUA NIMEBEBA MWANAO NA MUME WANGU NIMEACHANA NAYE BAADA YA KUJUA MIMI NINAUJAUZITO AMBAO SI WAKE”

    Niksimama na kugeuka taratibu huku nikiwa ninamtazama Madam Mery anaye lia huku akiwa amekaa chini akionekana kuwa na uchungu na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa



    ENDELEA

    Nikapiga hatua za taratibu na kumnyanyua Madam Mery na kuanza kufuta machozi taratibu kwa kutumia kitambaa changu kisha tukaingia ndani na moja kwa moja tukapitiliza hadi chumbani kwake.Ukimya ukatawala kati yetu huku madam Mery akiendelea kulia chini chini na kichwani kwangu sikuwa na hata wazo la kulizungumza likaeleweka

    “Eddy”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naam”

    “Amini ya kwamba nina kupenda sana japo kuwa kiumri tume tofautana ila moyo wangu umeshindwa kumpenda mwanaume mwengine zaidi yako”

    “Acha kuniongopea......nilikuona ni mtu wa maana sana kipindi mapenzi yetu yalipo anza lakini leo hii unaniambia umeolewa tena na mapicha ya harusi yako unayambandika huku ukutani”

    Nilizungumza kwa sauti ya ukali kiasi kwamba Madam Mery akawa mpole pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote

    “Tena umeona gia yako ni kuniongopea kuwa wewe ni mjamzito,Unadhani mimi nitakubali kirahisi kulea mimba ambayo sielewi mwanzo wake ni upi wala mwisho wake”

    “Eddy najua unauchungu moyoni mwako kwa mimi kuolewa.....Ila Eddy mimi sikuwa na jinsi ya kufanya”

    “Ahaaaa hukuwa na jinsi ya kufanya kwani wewe ni mtoto mdogo ambaye ulibebwa juu juu na kupelekwa kanisani na kufungishwa ndoa eheee?”

    Madam Mery akazidi kulia kwa uchungu huku na mimi hasira ikianza kujaa kifuani kwangu hadi nikajikuta nikianza kutetemeka mikono

    “Eddy am sory?(Eddy samahani)

    “Samahani yako haiwezi kuchukua nafasi yoyote ndani ya moyo wangu kwasababu hujui ni jinsi gani nilivyo kuwa ninakupenda.....Leo hii unasema umeolewa na mimba ni yangu.Hainiingii akilini hata kidogo”

    “Eddy naomba nikuambie ukweli”

    “Ukweli kuhusu nini?”

    “Eddy kipindi nilipo anza mahusiano na wewe nilikuwa na mpezi wangu ambaye alikuwa Uingereza kimasomo....Alirudi mwezi ulio pita na akanifanyia suprize ya kunivalisha pete ya uchumba na tukafunga ndoa ila...”

    “Ila nini sasa kumbe siku zote una kazi ya kuniongopea na kumbe una bvwana wako nje ya nchi.Mbona nyinyi wanawake hampendeki mufwanye nini ili mujue munapendwa.....Wenyewe mukafanya vya kutosha ehee alafu mukajazana mimba leo hii unaniambia Eddy hii mimba ni yako.Si ndio munavyo danganyana”

    Nilizidi kuzungumza kwa sauti ya kufoka kiasi kwamba Madam Mery akanyanyuka kwa hasira na kunipiga kibao cha shavu na kuzidi kunipandisha hasira.Nikamshika koo Madam Mery na kumuegemeza ukutani huku nikimuangalia kwa macho yaliyo jaa hasira hadi machozi yakaanza kunimwagika

    “MERY NITAKUUA”

    “E...ddy we..ee niue nipo...radhi kwa hilo.Mimi siku zote nilijua UMEKUFA NDIO MAANA NIKACHUKUA MAAMUZI YA KUOLEWA”

    “Fuc* you”

    Nikamuachia madam Mery na kuanza kuvunja picha zilizo tengenezewa frame na kwahasira nikaanza kupiga ngumi ukutani hadi mikono ikaanza kuvuja damu.Madam Mery akapiga hatua moja ya kunifwata nikageuka kwa jinsi ya muonekano wangu tu ilitosha kumfanya asimame kama namba moja asipige hatue nyingine ya pili

    “Usinifwate nitakuua”

    “Eddy unajiumiza”

    “Nimekuambia niache...Sasa hivi huyu unaye zungumza naye ni mfu wa Eddy ila Eddy mwenyewe amekufa mwanzo leo mwisho leo sitaki kusikia unanitafuta”

    “Eddy jamani kwanini unanifanyia hivyo au kwasababu ninakupenda,kwa nini unanikatili kiasi hicho unataka huyu kiumbe huku tumboni akose baba?”

    “Baba yake si huyo anaye toka uingereza.....Ni mara mia ungenidanganya basi kuwa hiyo pete uliyo ivaa nip ambo lakini kabisa unalipanua domo lako EDDY NIMEOLEWA”

    Madam Mery akazidi kulia kwa uchungu na nikazidi kumuona ni muigizaji kwa maana kipindi cha mwisho kufanya naye mapenzi alilazwa hospitali kwa madai ya kuumwa ugonjwa wa malaria

    “Eddy siku tuliyofanya mapenzi ndipo nilipata mimba ya huyu kiumbe chako tumboni na wala sio mimba ya mume aliye niona”

    “Ahaaa kwahiyo unataka mtoto akizaliwa awe na rangi za Uingereza uingereza si ndio”

    “Eddy Eddy”

    ‘Eddy nini...kama mimba ni ya kwangu basi mumeo kaja kamalizia ukarabati wa rangi ya mtoto”

    “Eddy nyamaza sasa kumbuka mimi pia ni mwalimu wako”

    “Usinge nivulia nguo kama wewe ni mwalimu wangu......Sasa ni hivi sihitaji tena uhusiano na wewe sawa?”

    Nilizungumza kwa hasira huku nikipiga hatua za kuufwata mlango wa kutokea ndani ya chumba.Kabla sijaufikia Madam Mery akalishika shati langu kwa nyuma huku akilivuta hadi baadhi ya vifungo vikakatika nikageuka kwa hasira na kurusha ngumi iliyotua tumboni Madam Mery na kumfanya atoe ukulele mkali huku akijikunja na mikono yake ikiwa imelishika tumbo lake

    “Eddy Unaniua?”

    Madam Mery alizungumza na kuanguka chini na damu zikaanza kumtoka mdomoni,Hasira yote nikajikuta ikiniisha na nikipiga goti moja chini na kumtazama na Madam Mery na kumkuta akihema kwa shida kama mtu mwenye ugonjwa wa pumu,Gafla mlango wa chumbani ukafunguliwa na akaingia Madam Rukia na baada ya kumuona mwenzake yupo chini akaanza kupiga makelele huku akiwa anakimbilia sebleni.Nikanyanyuka kwa haraka na kutoka nje na kumkuta Madam Rukia akiminyana kuufungua mlango wa kutoka nje.Nikamshika kiuno na kumnyanyua juu juu na kumtupa juu ya sofa

    “Unataka kufanya nini?”

    Nilizungumza kwa sauti ya juu kiasi kwamba hadi mimi mwenyewe nikajishangaa kwani katika maisha yangu sikuwahi kuzunguamza kwa sauti ya namna hiyo

    “Eddy umemuua Mery”

    “Acha ufala una uhakika amekufa”

    “Ohooo Mama weee Eddy umeuaa ohooo majirani.......”

    Nikamuwai kumziba mdomo Madam Rukia anaye waita majirani wamsaidie na nikachukua vitambaa viwili vya makochi na kumsokomeza navyo mdomoni kisha nikavua mkanda na kuifunga mikono yake kwa nyuma.Kisha nikamnyanyua na kumuweka begani na kabla sijatoka njee nikasikia sauti ya Madam Mery akiomba msaada.Nikatoka hadi nje na kufungua buti ya gari na kumuingiza Madam Rukia na kwa uzuri nikakuta kamba ya manila ambayo nikaitumia kwa kumfunga miguuni

    “Ukileta upumbavu nitakwenda kukutupa sehemu usiyo ijua na sitaki using** sawa wewe Malaya”

    Madam Rukia akaitika kwa kutingisha kichwa akiashiria amenielewa ninacho kizungumza,Nikaifunga buti ya gari na kurudi ndani na kumkuta Madam Mery akiburuzika chini huku akiwa amelishika tumbo lake na damu zikiendelea kumtoka mdomoni.Nikanyanyua na kumuingiza ndani ya gari nikafungua geti na kulitoa gari nje kisha nikalifunga na kurudi ndani ya gari na kumpeleka Madam Mery katika hospitali ya mkoa.Manesi wakampoke Madam Mery na kuanza kumuhudumia nikabaki nikiwa ninajilaumu kwa kitendo nilicho kifanya.

    “Wewe ndio uliye mleta huyu mgonjwa?”

    “Ndio”

    “Nifwate ofisini”

    Nikaongozana na Mzee mmoja aliye valia koti jeupe na tukaingia ofisini kwake na nikakaa kwenye kiti nilicho kikuta na yeye akakaa kwenye kiti chake

    “Hali ya mgonjwa wako sio nzuri kwani kwa uchunguzi wa Utrasound tumegundua mfuko ake wa uzazi umepata mstuko na kupelekea mzunguko wa kiumbe kilichopo tumboni kwake kuhama kwenye njia”

    “Dokta nenda kwenye point maswala hayo mengine hembu yaache.Je mgonjwa wangu atapona au haponi”

    “Atapona ila itatulazimu tumfanyie upasuaji mdogo”

    “Utagharimu kiasi gani cha pesa?”

    “Laki saba”

    “Haaa kwenye hiyo lakisaba mtoto atakuwa hai au amekufa AU kuna chenchi ambayo itarudi?”

    “Hapa tunahitaji tumfanyie huo upasuaji leo hii la sivyo tunaweza kumpoteza mama na mtoto”

    “Hakuna punguzo la hiyo pesa”

    “Kijana hiyo ni kwa opareseni ndogo”

    “Hujuanielewe wewe ninaamana kwamba hamuwezi kunipunuzia hicho kiasi cha pesa”

    “Haiwezekani”

    Nikaitoa simu mfukoni nikiwa ninafikiria jinsi ya kumpaga Sheila hadi anipatie kiasi hico cha pesa.Moyo ukanipasuka baada ya kukuta missed call kumi za namba ambayo huitumia Sheila,Nikaipiga namba ikakatwa nikapiga kwa mara ya pili ikakatwa nikapiga kwa mara ya tatu ikapokelewa

    “Sheila ,mbona unanikatia simu wewe?”

    “Samahani kaka mgonjwa wako amekunywa vidonge vingi kwa lengo la kujiua ila tunajitahidi kuyaokoa maisha yake”

    “Wee......wee......nees....i imekuwaje haaad....i anywe sum...uu?”

    Nilipata kugugumizi cha gafla na kuzidi kuchanganyikiwa kiasi kwamba nikatamani ardhi ipasuke na inimeze kwani likiisha tatizo hili linaanza jengine kubwa kupita la kwanza

    “Hatukujua tatizo ni lipi lililo mfanya anywe vidonge vingi.Ila jitahidi uwahi kufika hapa hospitalini”

    “Haaa...yaaa nesi”

    Nikakata simu kwa haraka haraka nikaiweka mfukoni nikakumbuka nguo niliyo ivaa ambayo ni jeans inanibana ndio maana simu ikajiweka silence kutokana ni screan touch kujiminya minya kutokana na mishemishe nilizotoka kuzifanya muda mchache ulio pita.Nikatoa wallet yangu na kuchuomoa kiasi chote cha pesa kilichopo ndani ya wallet na kumuwekea daktari mezani

    “Hakikisha mgonjwa wangu anapona.Kama pesa imepungua nitakuja kuilipa”

    Nikafungua mlango na kutoka huku nikikimbia na nikapishana na manesi wakiwabeba baadhi ya wanafunzi wa shule yetu walio jeruhiwa katika vurugu zinazo endelea shuluni kwetu.Nikaliwasha gari na kuondoka eneo hospitali kwa kasi huku kichwa changu nikihisi kitapasuka kwa mawazo makali yaliyo nizonga.Nikajikuta nikikanyaga breki gafla kwa nguvu hadi gari ikaanza kuserereka barabarani huku nikijitahidi kumkwepa muendesha baiskeli aliye jiingiza barabarani na kukuta nikimvaa dada anaye tembea pembezoni mwa barabara na kumtupa kwenye mtaro uliopo mbembezoni mwa bararabara

    Nikatulia kama dakika tatu nikiyasikilizia mapigo ya moyo jinsi yanavyo nidunda yakienda sambamba na mwili wangu kutetemeka.Watu wenye hasira kali wakaanza kulisonga songa gari kangu huku wakiniomba nishuke kwenye gari.Nikapiga honi na kukunyaga mafuta na kuwafanya watu watawanyike na kulikwepa gari langu huku wengi nao wakijirusha kwenye mtaro.Kwa kupitia kioo cha pembeni nikaona pikipika zikinifukuzia.Nikaongeza mwendo na nikafanikiwa kuwapoteza kwenye macho yao na kuingia katika barabara ianyo elekea porini.Baada ya umbali wa kilomita 7 taratibu gari ikaanza kupunguza mwendo huku sauti ya kike ikiniambia niongeze mafuta haraka iwezekanavyo la sivyo gari itazimika

    Nikaliingiza gari kwenye kichaka na kulizima nikashuka na katika eneo zima nililopo hakuna nyumba ya aina yoyote na sijui kama kuna uwezekano wa binadamu kuishi katika eneo hili.Nikainama huku kichwa changu nikiwa nimekiweka kwenye sehemu ya juu ya gari huku machozi yakinitirikika na kwaharaka haraka nikaanza kuyakumbuka maneno ya mama alivyokuwa akiniambie nikasome.Nikaona kulilia sio suluhisho la mimi kuweza kupata msaada wa kujitoa ndani ya msitu huo kwani kuna umbali mkubwa sehemu niliyopo hadi barabarani.Nikakumbuka nimemuweka Madam Rukia kwenye buti la gari,nikazunguka kwa hatua za taratibu zilizo jaa uvivu na nikalifungua buti la gari na kumtoa vitambaa Madam Rukia bya mdomoni

    “Eddy wewe ndio umenifanyia hivyo”

    “Zungumza taratibu la sivyo nitakusokomeza hii mitambara”

    “Eddy una akili vizuri wewe?”

    “Usinivuruge na wewe”

    Nikalifunga buti la gari kwa nguvu na kuufungua mlango wa nyuma na kukaa na kumuacha madam Rukia akiniomba nimfungulie.Nikanyanyuka kwa hasira na kuulifunga buti na kumtazama madam Rukia kwa macho makali

    “Eddy naomba unifungue sinto piga kelele tena”

    “Ukipiga”

    “Nifanye chochote unacho taka”

    “Ole wako sasa unizingue nitakuacha huku huku porini”

    “PORINI....!!?”

    “Ndio porini kinacho kushangaza wewe ni kipi?”

    “Eddy jamani mbona unaroho mbaya hivyo umeamua kweli unilete huku porini”

    “Bwanaa wee sitaki maswali yako ya ajabu na kama unataka kukaa humu ndani ya hili buti wewe endelea kunikera”

    Nikamfungua kamba ya miguu madam Rukia kisha nikamtoa kwenye buti na akasimama kwa miguu yake.Nikamfungua mikono yeke na mkanda nikuaweka ndani ya gari na Madam Rukia akaanza kushangaa shangaa

    “Eddy huku ni wapi?”

    “Hata mimi sijui ni wapi?”

    “Umefikaje fikaje?”

    “Sitaki maswali hembu niache kwanza hapa kichwa kimevurugika”

    Madam Rukia akawa mpole na kukaa kwenye moja ya gogo la mti lililopo kwenye kichaka hichi huku sura yake ikianza kujawa na hofu na machozi yakaanza kumwagika taratibu

    “Eddy ina maana Mery ndio amefariki?”

    “Hajafa”

    “Hajafa wakati nimemuona kabisa ahemi?”

    “Nimekuambia hajafa”

    Nikaito simu yangu inayoita mfukoni na kukuta ni namba anayo itumia Sheila mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi kwamba nikasita kuipokea ikaita hadi ikakata,Ikapigwa tena na kuipokea pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote

    “Eddy mume wangu upo wapi?”

    Sauti ya Sheila ilizungumza huku akionekana kuchangamka kiasi kwamba nikabaki nikiwa na mshangao

    “Eddy mbona huzungumzi kitu chochote mume wangu?”

    “Wewe nesi si ameniembai kuwa umekunywa sumu?”

    “Tulikudanganya mume wangu........”

    “Kwanini sasa ulinidanganya?”

    “Nilipoona ninapiga simu hupokei nikajua utakuwa umekwenda shuleni kwenu kwenye vurugu ndio maana nikaamua kula mchongo na nesi”

    “Huo sasa ulio ufanya wewe ni ujinga.....Unaona sasa nimejikuta nipo porini?”

    Sheila akaanza kucheka huku nikisikia sauti nyingine ya nesi akicheka

    “Mume wangu huku porini umekwenda kufanyaje au umekuwa ndege”

    “Sheila kuna wakati wa utani na mwingine kuna wakati wa serious na ninavyo zungumza hivi sasa nipo kwenye msitu ambao sijui unaitwaje na gari imekata mafuta”

    “Wee.......kweli mume wangu acha kunitania!!?”

    “Nimesha wahi kukutania mimi?”

    “Hapana mume wangu sasa ilikuwaje?”

    “Bwana nilimgonga mtu barabarani ndio nikakimbikia huku porini baada ya watu kunifukuzia na laity ningekuja huko hospitalini ingekuwa ni majanga”

    “Mungu wangu sasa itwakuwaje mume wangu?”

    “Sijui hata itajkuwaje?”

    “Na mimi simu yangu imepotea jana kwenye ugomvi kuna majina ya watu ambao ningekuwa nayo ingekuwa rahisi kuwasiliana nao”

    “Sasas itakuwaje.......”

    “Nimekumbuka tazama kwe.......”

    Ukimya ukatawala kwenye sikio langu nikaitazama simu yangu na kukuta ikiwa imezima chaji

    “Madam una simu hapo?”

    “Sina simu zangu zote nimeziacha nyumbani kwa Mery”

    Nikajaribu kuiwasha simu yangu ila ikawa ina zima kiasi kwamba ikafika hatua hata nikiwasha haionyeshi mwanga wa aina yoyote.Nikangia ndani ya gari na kukunjua siti na kujilaza nikaanza kuyafikiria maneno ya mweisho ya Sheila yana maana gani

    “Tazama kwenye nini sasa?”

    Nikajikuta nikijiuliza swali nanikaanza kufungua kwenye kimlango kidogo kilichopo mbele ya siti ya abiria na nikakuta waya wa USB cha kushukuru Mungu unaingiliana na simu yangu.Nikaichomeka kwenye sehemu ya USB iliyopo kwenye gari na chaji ikaanza kuingia taratibu.Gafla nikasikia vishindo vya mtu akikimbia nikanyanyuka kwa haraka na kumuona Madam Rukia akipotelea kwenye miti nikalifunga gari na funguo nikaziingiza mfukoni na nikaanza kumkimbiza

    Kadri ninavyozidi kuongeza mwendo ndivyo jinsi Madam Rukia anavyo ongeza kasi ya kukimbia.Nikaongeza kasi ya kukimbia zaidi yake na nikafanikiwa kumnyaka na nikamlaza chini huku akijitahidi kujichomoa mikononi mwamngu huku akinipiga makofi mfululizo

    “Mbona unaabari za ajabu wakati wewe ni mtu mzima ulikuwa unakwenda wapi?”

    Mamda Mery akaendelea kunipiga makofi akiniomba nimuachie gafla nikaanza kusikia mazungumzo ya watu wakiulizana sauti ya kike inatokea wapi.Nikamziba mdomo Madam Rukia kwa kutumia kiganja changu kisha tukajificha kwenye miti iliyo banana.Watu hao wakendelea kutafuta huku na huku ila hawakutuona na baada ya muda wakaondoka zao.Madama Mery akanikumbatia huku akilia sikujua kilicho mliza

    “Unalia nini?”

    “Eddy nasukuru kwa kuniokoa”

    “Nimekuokoa wapi?’

    “Kwa maana kama ningekutana na hao jamaa wangenibaka”

    “Una uhakika gani kama wange kubaka?”

    “Nina uhakika kwani ndio kazi yao.Wanaitwa BLACK FOREST PEOLPLE”(Watu weusi wa msituni)

    Nikaanza kupata wasiwasi juu ya gari nililo liacha kwenye kichaka,nikamuachia Madma Rukia na akaanza kunifwata kwa nyuma hadi tukafika kwenye gari.Nikalikuta lipo katika hali yake ya kawaida kama nilivyo liacha.Simu yangu kidogo ikawa imeingia chaji nikaiwasha na kuipiga namba aliyo itumia Sheile ila mtandaao ukaanza kusumbua

    “Shiiti”

    “Nini Eddy?”

    “Network imekata kabisa”

    “Labda ujaribishe kusimama pele juu ya kile kisiki”

    Nikasimama juu ya jisiki cha mti ambao inaonekana ulikatwa kwa matumizi ya mbao nikaunyoosha mkono wangu juu ila mtandao haukukaa sawa na muda tayari ulisha songa sana huku baridi kali ikitawala ndani yam situ tuliopo.Hadi inafika saa moja usiku hatukuweza kupata mawasiliano kwenye simu niliyo nayo.Tukaingia ndani ya gari na kujifungia kwa ndani huku kila mmoja akiwa amejilaza kwenye siti yake akatafakari yanayo msibu

    Madam Rukia akaanza mchezo wa kunishika shika mapaja nikajikausha huku nikimsikilizia ni nini atakacho fwatia.Akanifinya na kunifanya nigune kwa maumivu makali kisha akauchukua mkono wangua ambao kwa sasa nikaanza kuhisi maumivu makali kwenye viganja vya mikono na akinishikisha kifuani kwake na nikaanza kuyaminya maziwa yake taratibu kiasi kwamba Madam Rukia akaanza kutoa mihemo ya nguvu

    “Tushuke kwenye gari humus into kufaidi”

    Madam Rukia akaniambia na sikuwa mbishi tukashuka kisha nikatafuta sehemu iliyo tulia ambayo sio mbali na lilipo gari.Madam Rukia akawa kama amelishwa pilipili kichaa kwa maana akaanza kazi ya kuinyonya koki yangu kwa fujo kisha akaikalia taratibu na kazi ikaanza huku kiuno chake kikiwa na kizi ya kuikatikia koki yangu.Gafla nikamziba mdomo baada ya kuanza kusikia mazungumzo mengine ya watu wanao onekana kuchoka na safari yao

    “Mimi nimesema huku sipo tunapo kwenda tumepotea jamani”

    “Hembu niacheni jamani na uzee huu mutaniua mimi”

    “Mkuu hembu jitahidi tambua tumeingia kwenye hii kesi kwa ajili ya kuyaokoa maisha yako sasa unapoleta habari za kuchoka unadhani tuta kuelewaje?”

    “Lakini si nana walipa?”

    “Hata kama”

    “Nyinyi nisindikizeni hadi mpakani mwa Tanzania na Kenya kisha niacheni nitajua wapi kwa kwenda ila na umri huu sipo tayari kabisa kuingia gerezani”

    “Sasa mkuu ilikuwaje hadi yule kijana akakuona?”

    “Yaani hata mimi sielewi ilikuwa kuwa vipi kwa maana ile hoteli sikudhani kama ipo siku nitakutana na mwanafunzi wangu”

    “Mmmm alafu yule dogo anajiamini”

    “Anajiamini kutokana wazazi wake ni wazito serikalini ila haki ya MUNGU nikija kumtia mikononi nitakumbukia enzi zangu za jeshini za kulenga shabaha na bunduki yaani nitahakikisha risasi zote zinamuishia mwilini mwake”

    “Utampataje wakati ndio tayari umekinukisha”

    “Hii dunia milima haikutani ila binadamu tutakutana tu”

    Gafla nikaiminya simu yangu mfukoni hukuzuia mlio wa maesseji unaoingia na kuwafanya watu wanao zungumza kukaa kimya huku wakionekana kustushwa

    “Hiyo simu ni ya nani?”

    “Ahaa ni simu yangu ni ujumbe kutoka Voda”

    Mwalimu mmoja alijibu na kuyafanya mapigo yangu ya moyo kutulia na Madam Rukia akawa anatetemeka kwa woga,Nikawachungulia na nikawaona waalimu watatu wa kiume akiwemo na mkuu wa shule akongeza idadi yao na kuwa wanne

    Nikaitoa simu yangu taratibu na nikaiweka sinlence na kuupunguza mwanga wake na nikaisoma meseji iliyo ingia nayo pia inatoka Voda

    “NDUGU MTEJA SAMAHANI KWA MTANDAO KUTOKUWAHEWANI KWA TAKRIBANI MASAA MATANO HII NIKUTOKANA NA SABABU ZILIZOPO NJE YA UWEZO WETU.ENDELEA KUFURAHIA VODACOM”

    Nikamaliza kuusoma ujumbe wa simu ulio ingia na gafla tukasikia hatua zikija upende wetu

    “Mkuu unakwenda wapi?”

    “Ninajisaidia haja ndogo mara moja”

    Mkuu wa shule na akasimama eneo tulilo jificha na Madam Rukia huku kila mmoja akiwa nguo zake amezivaa vizuri baada ya kuwasikia walimu hawa mambao walinitoroka mchana wakizungumza.Mkuu wa shule akaanza kukojoa huku akipiga mluzi akiisikilizia raha ya kukojoa na mkono wake mmoja ameshika bastola yake na gafla Madam Rukia akakohoa na kumfanya mkuu wa shule kugeuka na macho yake na yangu yakakutana huku akionekana kuto amini kuniona katika eneo hili

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akili yangu ilafanya kazi ya haraka ya kufikiri na wazo lililo nijia ni kumshika Madam Rukia na kumsukuma na akaangukia kwenye miguu ya mkuu wa shule na mimi nikanyanyuka kwa haraka na kuanza kutokomea porini.Milio ya bunduki nikaanza kuisikia kwa nyuma nikajua atakuwa ni mkuu wa shule pamoja na waalimu wengine ambao wanamuunga mkono mkuu wa shule.Nikafanikiwa kuwaacha kwa umbali mkubwa na kutokana na kuchoka sana ikanilazimu nipande juu ya mti ili niweze kujipunzisha kwani tofauti na hapo ninaweza kupata maumivu makali ya kifua yatokayono na jeraha la risasi nililo kuwa nimepigwa na Manka

    Nikajilaz akwenye tawi huku nikiangalia chini na kuumshuhudia mwalimu wa nizamu akipita kwa kasi akielekea nilipokuwa nikielekea.Ndani ya dakika moja wakapita waalimu wengine wawili wakiwa katika mwendo wa kukimbia.Nikaanza kusikia sauti ya Madam Rukia akilia na nikamshugudia mkuu wa shule akiwa amezishika nywele za Madam Rukia huku akimvuta kwa nguvu akimlazimisha atembee kwa haraka

    Mkuu wa shule na Madam Rukia wakasimama chini ya mti niliopo huku Madam Rukia akilalamika amechoka

    “Nitakuua tambua mimi sasa hivi sio mwalimu wako mkuu.Ohooo wewe niletee ufala”

    Mkuu wa shule alizungumza huku bastola yeke akiwa amaiweka kwenye sikio la Madam Rukia la upande wa kushoto.

    “Sema huyu fala mwenzako amekwenda wapi?”

    “Mimi sijui kwani si alikimbia mbele ya macho yetu”

    “Ahaaa hujui eheee?”

    “SIJUI MKUU WEWE UNANIONEA TUU”

    Mkuu wa shule akavuta kashati ka Madam Rukia na kakachanika na akabaki na sidiria kisha akaanza kumshika shika maziwa kinguvu kiasi kwamba Madam Rukia akaanza kufanya fujo ya kujitoa mikononi mwa mkuu wa shule

    “Nitakupasua hichi kichwa”

    “Nipasue ila sio kuniambukiza ukimwi wako”

    “Ahaaa sasa nakuambukiaza”

    Mkuu wa shule akaendelea kuzichana nguo za Madam Rukia kwa kutumia nguvu galfa nikastuka kuiona simu yangu ikienda chini huku ikitoa mwanga na inavyoonyesha inaita na sikujua ni kivipi imetoka mfukoni mwangu na kwabahati mbaya ikaanguka katikati ya Mkuu wa Shule na Madam Rukia.Mkuu wa shule akaiokota simu yangu na kuangalia juu haraka na kuniona.Madam Rukia akampiga mkuu wa shule kigoti cha sehemu za siri na kumfanya atoe ukulele huku akiiangusha simu aliyo ishika.Nikashuka kwenye mti kwa haraka na kumkuta bado mkuu wa shule amejikunja.

    Madam Rukia akaiokota simu yangu na mimi nikampiga teke mkuu wa shule lililo tua kwenye kifua chake na kumfanya angukie mgongo kabla sijamsogelea nikwaona waalimu wakirudi katika eneo alilopo mkuu wa shule.Nikamshika mkono Madam Rukia na kuanza kukimbia naye kurudi tulipo liacha gari

    “Eddy nimechoka?”

    “Jikaze bwana”

    “Niache wewe ndenda”

    “NINI?”

    “Eddy wewe nenda zako mimi niache hapa hapa nitajua cha kufanya”

    Nikawaona waalimu wakiwa na mwalimu mkuu wakishuka kwa kasi kwenye kilima wakija katika eneo tulipo

    “Eddy wewe nenda na chukua na simu yako”

    Mada Rukia alizungumza huku akiwa analia kwa uchungu,Nikaichukua simu nikamuachia mkono taratibu na kuanza kukumbia kwa kasi huku nikianza kuvuta kumbukumbu ni wapi nilipo liacha gari kwani miti mingi iliweza kunichanganya kiasi kwamba nikawa ninazunguka zunguka pasipo kujua ni wapi lilipo gari.Gafla nikasikia mlio wa bunduki na kunifanya nisimame gafla na akili yangu moja kwa moja ikamkumbuka Mada Rukia

    “Fuc*k wamemuua”

    Nilizungumza huku nikitazama sehemu ulipo tokea mlio wa bunduki,nikataka kurud ila nikasita na kujikuta nikishikwa na bumbuazi.Mwanga wa simu yangu ukanistua na kuigeuza na kukuta namba ngeni ikiingia kwenye simu yangu.Nikaipokea na kujibanza kwenye mti huku nikiwa ninahema kiasi kwamba hata mtu aliye nipigia simu atahisi kitu

    “Vipi kijana?’

    “Salama nani mwenzangu”

    “Mimi ni daktari wa hospiytali uliyo mleta binti wa kike na ukaniachia namba nikujulishe kitakacho endelea”

    “Ndiio nimekukumbuka dokta”

    “Hali ya Salome sio nzuri nainatubidi yumsafirishe tumpeleke Dar es Salaam kwa matibabu zaidi”

    “Kwani tatizo lake lilikuwa ni kubwa sana”

    “Ndio mishipa ya damu inayoingiza damu kwenye moyo wake imepasuka”

    “MUNGU WANGUUUU”

    “Na hapa inabidi sisi kama Hospitali kushuhulika katika garama zote kwa wakati huu ila wewe utakuja kuzilipa”

    “Saaaw........Haaaa!!!”

    Nikastukia gongo likipiga sehemu ya juu kwenye mti na nikageuka haraka na kumshuhudia mwalimu wa nidhamu ambaye siku zote huwa sipatani naye akija kwa kasi huku akiwa peke yake,Nikaiweka simu yangu mfukoni na kuipandisha juu kidogo suruali yangu ya jeanzi na kumsubiria kwa hamu mwalimu.Nikastukia mwalimu wa zamu akinipita kwa kasi kama hajaniona na sekunde kadhaa nikaona kundi la vijana wapatao kumi wakija kwa kasi huku wengine wakiwa na mapanga na magongo,

    Na mimi nikaungana na mwalimu wa zamu katika kukimbia katika njia anayo elekea huku vijana hao wakionyesha ni wachaga wakitufwata kwa kasi,Tukagawana njia mimi na mwalimu wa zamu kila mmoja akaenda upande anapo pajua yeye huku nyuma yangu wakiwepo vijana wawili wakinifwata mimi

    “Mungu wangu nisaidie”

    Nilijiesemea kimoyo moyo huku nikijikaza katika kukimbia kiasi kwamba niliaza kuhisi kuchoka huku kifua kikiniuma kwa mbali.Nikakaza mwendao huku nikiwatazama vijana wanao nifwata nikaona wakikata tama ya kunikimbiza na mwisho wa siku wakasimama na kuanza kutukana kilugha na wakarudi walipo tokea.Nikasimama na huku nikiinama na pumzi nikizihisi zikiniishia pamoja na koo langu kukauka mate.Mazingira ya eneo nililopo yakanipa matumaini kwani ndio sehemu ambayo tulifanyia mapenzi na Madam Rukia,Nikajikaza na kunyanyuka na kwenda lilipo gari na kukuta tairi moja ya mbele ikiwa haina upepo.Nikafungua buti la gari na nakuta batani ikinielekeza niminye nikaminya na ndani ya buti kukafunguka na kukuta tairii pamoja na vidungu viwili vya lita mbili mbili vya mafuta ya petrol na vinaonekana ni maalumu kwa gari hili kwani bado vina upya

    Nikalitoa taira na kuliweka chini huku nikiwa na mashaka na kila muda nikawa na kazi ya kuangalia pande zote za sehemu niliyopo.Simu yangu ikatoa mwanga ulionekana kwenye mwanga wa jeanzi yangu ikiashiria simu inaita nikaitoa mfukoni na kukuta ni Sheila ndio anapiga nikaipokea na kuibana sikioni kwa kutumia bega

    “Baby mbona nilikuwa ninakupigia hupokei?”

    “Baby weee acha tu hapa nilipo nipo kwenye matatizo”

    “Matatizo gani mume wangu?”

    “Wee acha tu nitakusimulia”

    “Saa zile nilitaka nikuambie kuwa utazame kuna mafuta ya emergence kwenye buti na sikujua kama ulielewa?”

    “Sikuelewa ila sasa hivi ndio ninayaona”

    “Fanya basi urudi dady”

    “Sawa”

    “I love you”

    “Love you too”

    Nikakata simu na kuirudisha simu ndani ya gari kisha nikaanza kazi ya kufungua tairi lililo na pancha na kulifunga tairi lililo jipya na ikanichukua kama dakika ishirini katika kuikamilisha kazi yangu.Nikayamimina mafuta kweye tanki la gari kisha nikaingia na kuliwasha na nikazifwata taratibu za uwashaji wa gari hili kisha nikaanza kuomdoka huku nikirudi katika barabara ya niliyo jia.Kutokana ni msituni mingi sikuweza kukimbiza gari kwani ninahofia kuchanganya njia,Gafla nikaona taa za gari zikija mbeke yangu kwa kasi huku zikiwasha king’ora nikatambua watakuwa ni gari la polisi.

    Dereva wa gari la polisi akaanza kuliendesa gari lake kwa fujo ya kutanda barabara nzima huku taa zake akiziwasha kwa mtindo wa zima washa kitu kilicho niumiza macho.Nikapungunza mwendo na kadri nilivyojaribu kuwakwepa kwa kubana upande mmoja wa barabara ila dereva wa gari ya polisi akanifwata upande niliopo

    “Huyu jamaa ni chizi nini?”

    Nilijiuliza kwa sauti ya juu huku gari langu nikilirudisha barabarani ili niweze kuona atanifanya nini.Na yeye akalirudisha barabarani gari lake huku akiziwasha taa zake kwa mtindo ulionikera huku akipunguza mwendo na gari zetu zikabaki zimetazamana huku dereva huyo akivuta akikanyaga mafuta kama wafanyavo madereva wa mashindano ya magari kabla hawajaruhusiwa kuanza kasi.Nikastuka baada ya kuwaona watu wawili wenye miili mikubwa wakiwa wamevalia makoti meusi na makofia yaliyo yaficha sura zao na kubaki macho wa kishuka kwenye gari ya polisi huku wakiwa na bubduki mikononi wakizielekezea kwangu.Nikairudisha gari nyuma kwa kasi ya ajabu na kuwafanya jamaa kuanza kunishambuli kwa risasi.

    ‘HALO BWANA EDDY GODWIN GARI YAKO IMEPATA ULINZI BINAFSI’

    Sauti ya kike ilisikika kupitia spika zilizopo kwenye gari ambalo kwangu kila kinacho fanyika ninaona ni kipya na sauti hii si ngeni kwangu

    ‘CHAGUA SILAHA’

    Kioo kidogo kilianza kunionyesha aina za bunduki zilizopo ndani ya gari kwa kigugumizi nikajikuta nikijiminyia kwenye silaha ambayo wala sikujua itajitokeza wapi,Gafla gari yangu ikasimama na haikurudi nyuma na nikaanza kusikia mtetemeko ndani ya gari na kuona vitu vyenye moto na vinavyokwenda kwa kasi kali vikitoka sehemu ya mbele ya gari na vikielekea lilipo gari la polisi na kulifanya lirushwe juu na kulipuka huku jamaa wanao nirushia risasi wakianguka chini

    “UPO SALAMA BWANA EDDY GODWIN UNAWEZA KUENDELEA NA SAFARI YAKO.ASANTE”

    Gari ikarudi katika hali yake ya kawaida na taratibu nikaanza kukanyaga mafuta na kufika katika sehemu ambayo wameangukia watu ambao sikujua lengo lao ni nini hadi wanisambule kwa risasi.Nikawachungulia kupitia kwenye kioo nikagundua wamefariki kwani miili yao ilijaa matobo mengi yaliyo tokana vichuma vya bomu zilizo toka kwenye gari huku damu nyingi zikivuja kwenye miili yao,Nikashuka huku nikitetemeka na kuanza kumfunua mmoja baada ya mwengine na kujikuta kumbukumbu zangu zikirudi hadi siku niliyo kamatwa pamoja na derava wetu na kuingizwa katika maabusu ya kituo cha polisi Lushoto na kulikuwa na majaamaa yenye misuli mikubwa na katika mazungumzo yetu walisema wao ni majambazi sugu wanashuhulika na utekaji wa magari.Sura mbili za majamaa wale ndizo zilizo lala chini,Sikutaka ushahidi nikaingia haraka ndani ya gari na kuondoka katika eneo hili.Baada ya lisaa nikawa nimefika mjini na muda ulio timu sasa ni saa kumi na nusu usiku.Nikafika hospitalini na kulisimamisha gari katika maengesho ya magari nikatoa simu yangu mfukoni na kuakuta missed call nyingi za Sheila.Nikafumba macho yangu na kusali kwa kumshukuru Mungu kunisaidia kutoka katika majanga yaliyo nikuta ila nafsi na moyo wangu vikajikuta vikiniuma kutokana na kifo cha madam Rukia

    Nikashuka ndani ya gari na kwenda moja kwa moja katika chuma alicholazwa Sheila ila sikumkuta na nikatoa simu na kumpigia akapokea nesi

    “Mgonjwa wangu yupo wapi?”

    “Tumemuhamisha chumba panda huku gorofani ukunje kushoto chumba namba 16 ndipo alipo mgonjwa wako”

    “Sawa”

    Nikafanya kama alivyonielekeza nesi na kuingia katika chumba namba 16 na kumkuta Sheila akiwa hana raha na baada ya kuniona akataka kushuka kitandani kuja kunikumbatia ila sindano ya dripu ilimzuia,Nikamfwata na kumkumbatia na sote tukajikuta tukitokwa na machozi ya furaha

    “Mume wangu pole”

    “Asante mke wangu”

    “Mimi kidogo hali yangu inaendele vizuri zile sindano walizo nichoma kidogo kidonda kimeanza kukauka kwa haraka”

    “Nijambo la kumshukuru Mungu”

    Nikaanza kumuadisia Sheila yaliyo nikuta ila sikumuadisia juu ya Madam Rukia kwani ninajua nilicho kitenda hakikustahili kwa mimi kumfanyia

    “Sasa huyo uliye mgonga anaendeleaje?”

    “Sijajua ila asubuhi itanibidi nikamfwatilie niweze kujua ni nani?”

    “Utampatia wapi?”

    “Nitauliza uliza na itanibidi niweze kuwa na pesa ya kumsaidia kama nitamuona na hapa sina hata pesa?”

    “Kwani ni kiasi gani cha pesa kitatosha?”

    “Sijajua ila niwe na pesa ya kutosha”

    “Basi nitakupa kadi ya benki ukachukue pesa ya kutosha”

    “Sawa mke wangu”

    Tukaendelea kuzungumza mazungumzo ya kawaida hadi asubuhi nichukua kadi moja ya Sheila na akaniambia namba zake za siri kisha nikaondoka.Sikutaka nitumie gari kuhofia watu wa eneo nililo gonga mtu jana kuweza kulijua.Nikatembea kwa miguu hadi benki na nikabaki ninashangaa baada ya kukuta salio la akaunti ya Sheila milioni miambili na themanini 280.00.

    “Huyu mwanamke kumbe anapesa kiasi hichi?”

    Nikachagua huduma ya kutoa pesa nikaanza kutoa kiasi kidogo dogo hadi ikatimu milioni moja na nusu.Nikaingia kwenye duka kubwa la nguo na kununua nguo nyingine mpya pamoja na viatu.Nikanunua begi la mgongoni na kuziweka nguo nilizo zivua pamoja na viatu kisha nikatoka nje na kuingia kwenye kihoteli kidogo nikaagizia chakula kifungua kinya na kuanza kuka taratibu huku kichwa changu kikisongwa na mawazo.Nikamaliza na kutoka kwenye mgahawa huo na moja kwa moja nikaeleka kwenye vituo vya kukodisha taksi nikaingia kwenye taksi moja na kumuomba dereva anifikishe kweye hosptali ya mkoa.Tukafika na nikamuomba derava taksi anisubiri

    “Lakini kaka itabidi pesa iongezeke”

    “Haina shinda”

    “Niachie japo advance ili nipate moyo wa kukusubiria”

    Nikatoa elfu ishirini na kumpa kisha nikaelekea kweye ofisi ya daktari wajana na kukuta foleni kubwa ya watu wakiwa wanasubiri kuingia ndani ya ofisi hiyo.Nikawasalimia wakaitikia baadhi huku wengine wakionekana wapo kwenye maumivu makali ya magonjwa yao

    “Samahani dada akitoka huyo mtu humo ndani unaweza ukanifanyia msaada niingie nikaonane na daktari mara moja?”

    “Mmm kaka yangu ni bora uakapanga foleni tuu kwani mimi nimekuja tangu saa kumi na mbili asubuhi na foleni ilikuwa kubwa kama nini?”

    “Dada mimi sio kama ninaumwa ila ninaingia mara moja kumuona huyo daktari tuu”

    “Nimesema panga foleni mbona wewe kaka sio muelewa”

    Watu waliopo nyuma ya dada wakaanza kulalamila wengine wakitaka niingie wengine wakikataa nisipishwe na dada huyo.

    “Jamani samaani kama nitakuwa nimewaudhi kwa ombi langu”

    “Ndio umetuudhi wewe utoke zako huko nyuma ulete kwato zako huku mbele,Unadhani na nina atakubaliana na ujinga kama huo kama vipi wewe ondoka”

    Jamaa mmoja alizungumza kwa hasira kiasi kwamba watu wa karibu yake wakaanza kumtuliza hasira.Nikamuangalia kwa macho ya hasira kisha nikapiga hatua na kuufungua mlango wa daktari na kuingia bila dokta na kuwaacha watu wakilalamika.Daktari alipo niona akastuka na akanitazama kwa mshangao

    “Mgonjwa wangu yupo wapi?”

    “Kijana huo sio utaratibu wa kazi kama uliwakuta wezako kwenye foleni inabidi ukae kwenye foleni”

    “Dokta hilo sio jibu nataka nijui mgojwa wangu yupo wapi?”

    “Nakuomba uwe mpole kijana.Mgonjwa wako yu....yuu”

    “Yuuu yuuu nini sema yupo wapi.....?”

    Kwa haraka haraka nikaanza kuhisi kuna kitu ambacho daktari ananificha kwani kwa jinsi anavyo zungumza ananipa wasiwasi

    “Yupo kwenye wodi ya wazazi”

    “Twende ukanionyeshe”

    Daktari akajishauri kisha akamuomba mgojwa wake niliye mkuta amsubiri anarudi ndani ya muda mchache.Tukatoka nje na kuwafanya wagonjwa wanao lalamika kukaa kimya huku wakitutumbulia mimacho ya mshangao.Tukaelekea kwenye moja ya wodi na kumkuta Madam Mery akiwa amelala kwenye moja ya kitanda huku pembeni yake akiwepo jamaa ambaye nilimuona kwenye picha za harusi yao kwa na moja kwa moja nikajua ndio mume wake.Madam Mery baada ya kuniona akastuka huku kwa ishara akiniomba nisisogee kwenye kitanda chake.

    “Mgojwa wako yule pale”

    Dokta aliniambia baada ya kuniona nimesimama

    “Pesa iliyo baki ni kiasi gani?”

    “Imeshalipwa na yule jamaa pale kwenye kitanda”

    “Powa nakushukuru dokta”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Na wewe pia nakushukuru”

    Dokta akaondoka na kuniacha nikiwa nimesimama huku macho yangu yakimtazama Madam Mery hadi jamaa yake anakaanza kuhisi kitu.Jamaa akapiga hatua za kunifwa na kabla hajanifikia nikageuka na kuondoka kwa hataua za haraka na kutoka katika wodi na kumfanya jamaa kuongeza mwendo na kuja kunishika bega

    “Kaka vipi?”

    Jamaa alinisalimia huku akinitazama machoni

    “Salama tuu vipi?”

    “Mbona umemtazama mke wnagu na ukaondoka baada ya mimi kukutazama?”

    “Kwani tatizo lako ni nini?”

    “Nahitaji kujua kama wewe unamjua mke wangu au humjui?”

    “Simjui”

    “Sasa kwanini umtazame?”

    “Wee jamaa vipi kumtizima mke wanko ni kosa?”

    “Ndio ni kosa sipendi mke wangu atazamwe...Na ukirudia kumtazama nitakutoa duniani”

    Jamaa alizungumza huku akilifunua koti la suti yake na kunionyesha bastola aliyo ichomeka kiunoni mwake.Sikutaka ugomvi naye nikageuka na kuanza kupiga hatua za kuondoka kabla sijafika mbali na sehemu niliyo kuwa nimesimama nikastukia nikivutwa tisheti na nikageuka na kumkuta mume wa Madam Mery akinitazama kwa hasira

    “Mimi ninakusemesha alafu wewe unaondoaka ina maana umenidharau si ndio?”

    Jamaa alizungumza kwa hasira na sauti ya juu na macho yangu nikayapeleka hadi kwenye kioo cha TV(Luninga) iliyopo eneo la mapumzikio ya wagonjwa na kuitazama taarifa ya habari inayorusha na shirika la utangazaji nchini Uingereza shirila la BBC inayozungumzia kupotea kwa ndege ya shirika la KLM iliyokuwa ikitokea nchini Tanzania na inavyosemekana ina viongozi wa juu wa serikali wa nchi ya Tanzania na moja kwa moja nikatambau mama yangu ni miongoni mwa viongozi hao na mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio

    Gafla nikastukia kibao kikali kikitua shavuni mwangu kikitokea kwa jaamaa na kunifanya niyumbe na kumgonga nesi mmoja anaye saidiana na mwenzake katika kusukukuma kitanda cha matairi na juu yake kuna mgonjwa ambaye sikuamini macho yangu kwani ni Manka ndiye aliyelazwa juu ya kitanda hicho kuku sura yake ikajaa michubuko na amewekewa kifaa maalumu cha kuhemea huku macho yake akiwa ameyafumba na hali yake inaonekana sio nzuri



    “Kaka kuwa makini?”

    Nesi alizungumza huku akijiweka vizuri na nikabaki nimeduwaa huku nikiwaangalia wanavyokisukuma kitanda wakielekea kwenye moja ya chumba ambacho kina maandishi mekundu makubwa juu ya malango ambayo yameandikwa ICU huku chini kukiwa na maandishi yaliyo andikwa CHUMBA CHA WAGONJWA MAHUTUTI.

    Jamaa akanishika tisheti na kunigeuza huku akirusha ngumi ambayo kabla haijanifikia nikaidaka na kumuangalia kwa macho ya kumshangaa na kuzifanya kumbukumba za tukio lake na langu linalo endelea katika sehemu hii kurudi

    “Oyaa brother vipi wewe?”

    “Sio vipi stozi zako nimezipata na utajuta kunijua”

    Jamaa alizungumza huku akilivua koki lake la suti kwa dhumuni la kupigana na mimi,Akiwa anakamilisha kazi yake ya kulivua koti lake la suti nikampiga ngumi ya pua na kumfanya atoa ukulele mkali huku akiwa ameinama na kuishika pua yake,Watu na waauguzi walipo kwenye eneo hili wakanza kujisogeza kwa haraka huku wengine wakiomba ugomvi usiendelee,

    “Wewe dogo lazima nikutafute tuu sehemu yoyote na nilazima nikuue”

    Jamaa alizungumza huku akishikwa na baadhi ya watu,sikutaka kumjibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuelekea kwenye chumba ambacho nilimuona Manka akiingizwa kabla sijakifikia madaktari wawili wakanizuia

    “Huwezi kuingia humu ndani?”

    “Kwa nini?”

    “Hichi ni chumba cha wagonjwa mahututi haturuhusu mtu wa aina yoyote kuingia humu hususani wewe ambaye umetuchafulia hewa ya hospitli”

    Daktari mmoja alizungumza huku akinitazama kwa macho makali kiasi kwamba nikajikuta nikibaki nimemtazama.Nikatoka nje na kuifungua simu yangu sehemu ya Internet na kuingia kwenye mtandao wa google na kuanza kuitafuta habari ambayo nimeiona kwenye Tv,Nikaingia kwenye tovuti ya BBC Swahili na taarifa ya kwanza kuikuta ni ambayo inahusiana na kupotea kwa ndege ambayo hadi wanakwenda mitamboni hawakujua ni wapi ilipo.Nikajikuta nikizidi kuchanganyikiwa na kuanza kuzungumza mwenyewe

    “Ila mama mimi nilikuwambia usiende ila wewe umejifanya mbishi unaona sasa yaliyo kukuta”

    Nilizungumza huku machozi yakinimwagika,Nikaingia kwenye taksi nilio kuja nayo na kumuomba dereva anipeleke kwenye hospitali aliyolazwa Sheila

    “Kaka mbona unalia?”

    “Ahaaa hakuna kitu kaka”

    “Hapana una ndugu aliye fariki nini hapo hospitalini?”

    “Hapana ila kuna mambo yangu binafsi tuu”

    “Sawa kaka ngoja nikuwashie redio usikilize muziki upunguze mawazo”

    Dereva wa taksi akawasha redio ya gari yake na tukaanza kusikiliza nyimbo kwenye stesheni moja ambayo sikujua ni stesheni ya wapi.Mara gafla miziki ikakatishwa na kukaja taarifa ya habari na sauti nzito ya muandishi wa habari ikaanza kusikika vizuri masikioni mwangu

    “TAARIFA KUTOKA IKULU ZINASEMA NDEGE ILIYOBEBA VIONGOZI WA NCHI YA TANZANIA YA SHIRIKA LA KLM IMEPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA NA INASADIKIKA KUWA IMETEKWA NA MARUBANI HAO AMBAO WAMEZIMA MITAMBO YA RADA INAYO ONYESHA SEHEMU AMBAZO NDEGE HIYO HUPITA.

    WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ANAWAOMBA WANANCHI WAWE WASIKIVU KWANI UMOJA WA MATAIFA WAMETUMA NDEGE ZA KIJESHI KWENDA KUIFWATILIA NDEGE HIYO”

    Nikajikuta nikijifunga mdomo huku machozi yakizidi kunimwagika na sura yangu nikaiinamisa chini na sikutaka dereva aelewe ni kitu gani kinacho endelea

    “Ahhh acha watekwe bwana kwa maana wamezidi kula pesa za serikali.Watu wanakaa na kujaziana matumbo yao na sisi wananchi wa hali ya chini tanazidi kufa kwa tabu kila siku vitu vinapanda bei”

    Maneno ya dereva Taksi yakazidi kuumiza moyo wangu huku hasira ikinipanda na kujikuta nikiyang’ata meno kwa nguvu ili kuizuia hasira yangu na mbaya zaidi katika maisha yangu mimi ni miongoni mwa watu wagonjwa wa hasira na siku zote huwa nikikasirika ninaweza kufanya maamuzi ambayo yatapelekae baadaye kujutia

    “Unajua hawa vionngozi wetu wamezidi kutunyanyasa hapa utakuta walikuwa wanakwenda kula bata na hao Marubani wamewapatia kweli kwa maana ni washenzi sana”

    Dereva alizidi kuzungumza huku akiongeza sauti ya redio ili asikilize majina ya viongozi sita waliomo ndani ya dege hiyo huku wengine wakitokea Kenya.Jina la mama yangu likwa ni lasita katika kutajwa na kumfanya dereva taksi kuanza kucheka

    “Haaa huyu mama naye yuopo.....Kweli Mungu hapendi dhambi kuna siku bwana alikuwa na dereva wake sasa kwa bahati mbaya nikamchomekea kwa mbele ile barabara ya kuingilia K.C.M.C nilikuwa namuwahisha mgonjwa hospitalini.Ahaaaa alikwenda kunilaza polisi hadi siku anaondoka Arusha ndio wakaniachia......Tena hao watekaji kama wanajua wamfanye wa kwanza kufa kwa maana yule mama roho mbaya sana”

    Maneno ya dereva yakazidi kunipandisha hasira hadi mwili mzima ukaanza kunitetemeka huku misuli ya mwili wangu ikikaza na kujikuta nikikunja ngumi na kuipiga kwenye sehemu niliyokuwa nimeinamisha kichwa na kusababisha kifuniko chake kuchangukuka

    “Aiiseee inakuwaje chalii wangu mbona unanaribia gari yangu,”

    “Funga bakuli lako”

    Nilizungumza huku meno yangu nikijitahidi kuyang’ata kwa nguvu kwani kiwango cha hasira kinazidi kuongezeka huku mapigo yangu ya moyo yakienda kwa kasi huku jasho likinimwagika

    “Haa wewe vipi umearibu gari yangu unaniambia ninyamaze....Kama umechanganywa na mambo yangu ndio unizingu mimi na utalipa tuu”

    “Funga bakuli lako nitakuua”

    “Wewe fala kweli nani umuue?”

    Dereva alizngumza huku akipunguza mwendo wa gari,Nikakishika kwichwa chake kwa nyuma na kukigongesha kwenye mskani mara tatu mfululizo na nikasababisha gari kuanza kuyumba na likatoka barabarani na tukajikuta likiingia kwenye mtaro na kulalia upande wa dereva huku kichwa changu kukichanwa na kioo kwenye sehemu ya paji la uso na damu zikaanza kunijaa usoni,Sikutaka kumuangalia dereva taksi anaendeleaje na nikaanza kujitahidi kuufungua mlango wa gari na watu wakaanza kukusanyika na kunisaidia katika kuufungua kwa kwa nje na kunitoa ndani ya gari.Kutokana na wenge nikataka kuondoka eneo la ajali ila wakanizuia huku wakinikalisha chini kiulazima

    “Jamani musimzunguke mpeni hewa ajisikie vizuri”

    Jamaa mmoja alizungumza huku akiwasogeza watu wanao nishangaa,dada mmoja akaanza kunifuta damu zilizo samba usoni kwangu na sikujisikia maumivu ya aina yoyote

    “Begi langu lipo wapi?”

    Niliwaauliza watu na mtu mmoja akaniletea begi langu na kuliweka sehemu niliyokaa,Nikawaona wakijitahidi kumtoa dereva taksi ambaye sikujua kama amekufa au laa,

    “Jamani tumuwahisheni hospitali”

    “Nipo salama”

    “Kaka umeumia damu zinakutoka bado”

    “Zitakata zenyewe”

    “Dada huyo mnamsemesha hapo akili sio zake cha msingi ngoja kuna teksi imekwenda kuchukuliwa tumpeleke hospitali”

    Simu yangu ikaanza kuita na dada aliyekuwa akinifuta damu akaanza kunisaidia kuitoa mfukoni na akanionyesha namba ambayo kwa ukungu ulio nitawala machoni mwangu sikuweza kuigundua kwa haraka

    “Ipokee”

    Dada akaipokea na kuisikilizia huku akiwa ameiweka laud speaker

    “Eddy upo wapi mume wangu mbona makelele?”

    “Samahani dada yangu”

    “Wee ni nani unaye ipokea simu ya mume wangu?”

    “Mimi ni masamaria mwema mume wako amepata ajali ya gari na hapa alipo hawezi kuzungumza vizuri”

    “Mungu wangu ni mzima?”

    Nikagundua ni sauti ya Sheila na kukumbuaka hali yeka aliyo nayo ikanibidi nimpokonye dada simu na kuiweka sikioni

    “Baby sijaumia sana?”

    “Eddy ni wewe?”

    “Ndio mke wagu sijaumia sana na usiwe na presha”

    “Baby usife....nitabaki na nini jamani mume wangu”

    Sheila alizungumza huku nikimsikia akiwa analia

    “Baby siwezi kufa nakuomba uache kulia si unajua hujapona vizuri utazifanya hizo nyuzi za kidonda kuachia”

    “Baby kama haujaumia basi waambiea wakulete huku hospili”

    “Sawa baby ila nyamaza kulia”

    Nikakata simu na kuiweka mfukoni na kunyanyuka nikisaidiwa na baadhi ya watua na tukaingia kwenye moja ya taksi na nikawaomba wanipeleke kwenye hospitali aliyo lazwa Sheila na madaktari wakanipokea na kuniingiza kwenye chumba ambacho wakananishona kwenye jerala langu la usoni na kunifunga bandeji.Nikaelekea kwenye chumba alicholazwa Sheila na kumkuta akiwa yupo na nesi wakiomba huku mikono yao wakiwa wameiweka juu ya Biblia na macho yao wakiwa wameyafumba.Nikawaacha wamalize kuomba na wakafumbua macho na kuniona nikiwa nimekaa pembeni ya kitanda alicho lala Sheila na akaonekana kunishangaa huku machozi yakimwagika

    “Eddy upo salama?”

    “Nipo nipo mke wangu sawa”

    “Pole mwanangu”

    Nesi ambaye ni miongoni mwa masister wa kanisa la katoliki wanaofanya kazi katika hospitali hii alinipa pole na nikamuitikia kwa sauti ya upole na yenye unyonge ndani yeke

    “Mwanangu hujaumia sana?”

    “Sijaumia sana ni hapa usoni ndio nimechanwa na kiio cha gari”

    “Eddy afandhali hujumia sana ila gari halina dhamani kwangu kuliko wewe”

    “Sikwenda na gari yetu nilikuwa nimepnda taksi”

    “Pole sana mwanangu.....ngoja niwaache ninakwenda kuendelea na shuhuli nyingine”

    Nesi akatoka ndani ya chumba na kutuacha tukiwa kimya,Nikamsogelea Sheila na kumfuta machozi taratibu na ukimya ukatawala ndani ya chumba

    “Eddy”

    “Naaamm”

    “Mbona unaonekana una mawazo?”

    “Ni mama?”

    “Amefanyaje?”

    “Ametekwa kwenye ndege?”

    “Weee”

    “Ndio”

    “Wewe umejuaje?”

    “Nmesikia kwenye taarifa ya habari”

    “Mmmm Eddy turudi Dar tukajue ni nini kinacho endelea”

    “Tutarudi hadi wewe upone”

    “Nmeshapona mume wangu?”

    “Haujapona vizuri mpaka madaktari wakikupa ruhusa ndio tutarudi Dar”

    Simu yangu ikaita na kukuta ni namba ngeni ndio inayopiaga tena ni namba ya mezani.Nikaitazama kwa muda kisha nikaipoke

    “Habari yako Eddy”

    Sauti nzito ya kiume ilisikika kutoka upande wa pili wa simu na kunifanya nistuke kidogo

    “Salama nani mwanzangu?”

    “Mimi ni mkuu wa upelelezi wa Taifa nimepewa jukumu la kukujuisha kitu kinachoendelea juu ya mama yako”

    “Sawa”

    “Nina taarifa ambayo sio nzur sana kwa mama,kwanza tunakuomba usiwe na wasiwasi kwa maana hali ya abiria wote waliomo kwenye ndege ya shirika la KLM tumegundua wanaendelea vizuri akiwemo mama yako na hapa tunafanaya juhudi za kuwaokoa na nitazidi kukujulisha kila kitakacho endelea”

    “Sawa nashukuru kwa taarifa yako”

    Nilizungumza kwa sauti ya unyonge na simu ikakatwa na nikairudisha mfukoni huku nikimtazama Sheila

    “Wamewapata?”

    “Bado”

    “Ohoo Mungu wangu msaidie mama yangu mkwe anusurike na matatizo hayo”

    Maneno ya Sheila yaliyojaa huzuni yakaamsha hisia zangu za kulia na kujikuta nikimkumbatia Sheila na akaanza kuniliwaza na maneno matamu

    “Ni wapi nimekosea kwenye maisha yangu Mungu wangu kwa nini kila siku ni mimi..Likiiasha hili linakuja hili kama ni vipi ni bora nife kuliko kupitia kipindi hichi kigumu kwenye maisha yangu”

    Nilizungumza huku machozi yakizidi kuni kunitiririka huku moyoni mwangu nikiwa nimekosa amanani na kukata tama ya kushi kabisa duniani

    “Eddy kwanini unazungumza hivyo.....Unataka mimi niishi peke yangu? Unadhani wewe ukifa mimi nitaishije ninaamini kwamba wewe unaijua historia ya maisha yangu.Sina baba,Mama,kaka,dada wala jamaa wa karibu.Eddy wewe ndio mwanga wangu...wewe ndio baba yangu..wewe ndio mama yangu.Ukifa wewe na mimi nilazima nife”

    Sheila akazidi kuniongeza uchumgu wa kulia kwani kusema kweli kila hatua ya maisha yangu ninayopitia kwangu inamikosi

    “Sheila hata mimi nikifa nakuomba usijiue...Mimi ni mwaname natambua wewe utapata mwanaume mwengine wa kukuoa ila usije ukafanya hivyo kwa ajili yangu”

    “Eddy hapana wewe ndio kila kitu kwangu kwa sasa..Japo tunamuda mfupi ila kwako nimepata tulizo la moyo wangu”

    Nikanyanyuka kitandani na kufungua dirisha na kuchungulia kwa chini nikiangalia watu wanao ingia na kutoka ndani ya hospitalini hii.Mawazo ya ajabu yakaanza kunitawala akilini mwangu na gafla nikamuona mama kwa chini akiwa amekaa pembeni ya jeneza huku akiwa amevalia nguo yeupe huku puani akiwa na pamba na akaanza kuniita huku akilia kwa uchungu kiasi kwamba nikaanza kuchanganyikiwa,Kwa nyuma yake akatokea mtu mwenye nyundo kubwa na kuinyanyua juu na kuanza kumshindilia nyondo za kichwani na kusababisha damu kuruka na mtu huyo akaanza kucheka huku akuninyooshea kidole.Kwa hasira nikapanda kwenye dirishana kabala sijajirusha nikastukia nikishikwa kwa nyuma na kuaza kuvuta na madaktari wawili wa kiume

    “Eddy mume wangu nini unataka kufanya....Kwa nini unataka kujiua,Eddy nakupenda tena nakupenda sana mume wangu kwa nini jamami?”

    Sheila alizungumza huku akilia kiasi kwamba akataka kushuka kitandani ila madaktari wakamzuia

    “Mama yangu amekufa”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Eddy mama hajafa”

    “Mama yangu amekua mimi nitaishi na nini.....Hadi sasa hivi simjui nani na baba yangu halisi”

    “Eddy mama hajafa nakuomba usimpe shetani mawazo kama hayo yakatawala kichwani kwako”

    “Sheila nimemuona mama pele chini yupo kwenye jenezaa na kuna mtu amempiga hadi amekufa”

    “Baby sio mama.....Dokta namuomba mumlete hapa”

    Madaktari wakanikalisha kwenye kitanda na Sheile hakujali kama anajeraha kifuni kwake,akanivuta na kunikumbatia kwa nguvu huku sote tukiendelea kulia

    “Mama amekufa”

    “Eddy acha kuzungumza hivyo nakuomba tafandali”

    “Sheila”

    “Mmmm”

    “Unanipenda?”

    “Eddy nakupenda tena sana”

    “Nakuomba nife”

    “Eddy ni nini unacho kizungumza?”

    “Sheila mama yangu ameshakufa sina dhamani tena duniani...Mama yangu ndio rafiki yangu wa karibu.....Sheila mimi sina upendo wa baba si...”

    Sheila akanivuta na kuanza kuninyonya mdomo kwa nguvu kunizuia nisiendelee kuzungumza,Madaktari wakatoka ndani ya chumba na kutuacha tukiendelea na kitendo ambacho kilianza kuusisimua mwili wangu.Sheila akauchukua mkono wangu na kuushikisha kwenye chuchu yake ya kushoto na nikaanza kuiminya taratibu ila nikajikuta nikimuachia Sheila

    “Sheila unaumwa sitaki tufanye sasa hivi”

    “Eddy....”

    “Hapana unaumwa”

    “Ok mume wangu asante kwa kunijali.....Alafu baby ukilia unakuwa kama yale makatuni ya Tom na Jerryjea yakilia”

    Nikajikuta nikitabasamu na kumfanya Sheila na yeye kutabasamu huku akiishika shika pua yangu na kuanza kuiminya minya kiasi kwamba furaja yangu ikaanza kunirejea taratibu

    “Na wewe ukilia unakuwa kama wale katuni wa powefull girl machozi yao yanaruka kama maji haswa yule Babon akilia machozi yanaruka hayo kama bomba lililo pasuka”

    “Jamani baby kwa hiyo machozi yangu yanaruka kama maji ya bomba lililo pasuka?”

    “Ndio unatisha kama nini?”

    “Hata wewe ukilia unatisha unakuwa kama yale mazombi ya wrong turn...Kuna ile sijui ni part one kuna kazombi kamoja kaliuliwa wacha baba mtu aanze kulia sasa yule ndio unafanana nye”

    Nikazidi kucheka huku na kujikuta nikisahau tukio lililo tokea katika dakika chache zilizo pita

    “Basi na wewe unakuwa kama yule kale kasichana kwenye wrong turn kalicho mfumania jamaa yake akiwachungulia jamaa wakifanya mapenzi....Uliona jinsi kalivyokuwa kanalia kwa hasira”

    “Mmmmmm haya baby wewe ndio umeshindi....Mume wangu unapenda nikuzalie mtoto wa kike au wa kiume”

    “Nataka wa kike ili mtu akija kumchumbia kitangulizi cha mahari nataka mabasi saba”

    “Hahaa mume wanagu hayo mabasi saba jamani mtu wa watu atayatolea wapi au ndio hivyo unataka ujipatie mtaji kupitia mtoto wako?”

    “Ndio na atakuwa mzuri kama wewe mama yao”

    “Mmmmm mimi nataka wachukue lipsi zako na macho yako?”

    “Sawa itakuwa ni vizuri pia.....Eddy nikuambie kitu?”

    “Niambie”

    “Mungu akipenda nahitaji unioe kwa ndoa ya kanisani”

    “Nikimaliza kusoma tuu nafunga ndoa na wewe”

    “Kwelu mume wangu?”

    “Kweli kwani nahitaji kuyaanza maisha mapema”

    “Kweli mume wagu...Alafu nilikuwa nimesahau,Vipi shuleni kwenu hali inaendeleaje?”

    “Mmmm hata mimi sijui inaendeleaje alafu sina namba ya simu ya mtu wa shule nikamuuliza”

    “Mume wangu ninahitaji usome na mimi baada ya kukuzalia tu mtoto nitarudi shule kusoma kwa maana nahitaji familia yetu iwe ya wasomi zaidi hata ukimuhimiza mtoto asome kweli awe anasoma kweli.....Sio mama unamumbia mtoto nenda shule wakati wewe mwenyewe shule hukuipenda”

    “Kweli mke wangu ila vipi umeshakula?”

    “Baby nilionja onja kwani muda ule nilipopiga simu na ikapokelewa na mwanamke ndio muda ambao nilikuwa ninakula chakula na baada ya simu ile hamu ya kula yote ikapotea”

    “Ngoja nikanunue chispi tuje tule...Tena nimekubuka nikakununulie na simu kabisa sipendi hivi unavyo azima azima simu za watu”

    “Sawa baby ila nakuomba usichelewe na kama unakwenda tumia gari usipande kwenye hizo ndubwasha zinazo endeshwa na wavuta bangi na ukapata ajali bure”

    “Sawa baby...ila kwa mbali ninaanza kuhisi kichwa kinaniuma”

    “Pole baby nenda ukanywe dawa kwanza ndio uende huko unaotaka kwenda”

    “Hapa dawa nitazipatia wapi?”

    “Mume wangu hospitali nzima ukose dawa za kunywa.....Sikia nenda kwenye ofisi iliyopo pale chini ya ngazi kuna masister utawakuta waombe na watakusaidia”

    “Sawa baby”

    Nikambusu Sheila mdomoni na kufungua mlango na kutoka na moja kwa moja nikashuka hadi kwenye chumba alicho nielekeza Sheila.Nikagonga mlango mara tatu na suti ya kike iliyopo ndani ya chumba hicho ikaniruhusu niingie.Nikafungua mlango na kuwakuta manesi watatu wakiwa wameshika mashavu yao huku wakionekana wanyongea na macho yao wameyaelekezea kwenye kioo cha Tv iliyopo ndani ya chumba hicho.Na mimi ikanibidi ninagalie wanacho kitazama na kukuta mipigo ya moyo yakiende kwa kasi baada ya kuiona ndege kubwa ikiwa imeanguka huku inawaka moto na kutoa moshi mwingi na mweusi huku kikosi cha zima moto ambacho sikujua ni cha nchi gani wakijitahidi kuzima moto kwa kutumia magari yao maalumu ya kuzimia moto huku baadhi ya miili inayoonekana kuwa imefariki ikitolewa ndani ya ndege hiyo



    “Karibu kaka yangu tukusaidie nini?”

    Nesi mmoja aliniuliza swali ila sikumjibu nikabaki nikiitazama taarifa inayorushwa kupitia kituo cha televishion ya SKY NEWS kinachopatikana nchini uingereza.Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio kana kwamba nimekimbia umbali mrefu pasipo kupumzika.Nikayasoma maandishi makubwa yaliopo ubavuni mwa ndege hiyo na kukuta yameandikwa Emirates kiasi kwamba nikajikuta nikishusha pumzi taratibu na manesi wote wakabaki wakinitazama

    “Kaka kaka”

    “Naam”

    “Mbona unashangaa?”

    “Ninatazama hiyo taarifa ya habari”

    “Inasikitisha sana kwa maana watu wote waliopo kwenye hiyo ndege wamefariki”

    “Imekuwaje hiyo ndege ikaanguka?”

    “Ilianguaka kipindi inapaa imesababishwa na hali ya hewa kutokuwa nzuri”

    “Imeangukia nchi gani?”

    “Imeangukia Tailand”

    Kidogo nafsi yangu ikapata unafuu na tabasanu likarudi usoni mwangu taratabu kwani nilidhani itakuwa ni ndege ambayo amepanda mama.Nikawaomba dawa za kutuliza maumivu ya kichwa wakanipatia pamoja na maji nikazinywa na kuwashukuru na kuondoka na kuwaacha wakiendelea na shughuli zao.Nikaenda kwenye maduka ya simu ambayo hayakuwa mbali sana na hopsitali na kununua simu kwa ajili ya Sheila na kupitia kwenye sehemu wanapouza chipisi.Nikanunua chips za kutosha na kurudi hospitali na kumkuta Sheila akizungumza na madaktari

    “Hali yako inazidi kuridhisha na baada ya siku kadhaa tunaweza kukupa ruhusa ya kutoka hospitali”

    “Kwani hamuwezi kunipata hata leo?”

    “Kwa leo ni vigumu inabidi umalizie dozi yako ya vidonge na sindano za kukausha kidonda na baada ya hapo tutakuwa huru katika kukuruhusu.”

    Tukakaa hospitalini siku mbili huku nikiendelea kumuuguza Sheila na ndani ya siku mbili sikuweza kupata taarifa yoyote kuhusiana na Mama juu ya kupatikana kwa ndege yao ambayo imetekwa na watu wasio julikana.Sheila akaruhusiwa kutoka hospitalini na akapewa vidonge ambavyo endapo atajisikia maumivu ameze.Nikapepeleka gari gereji kufanyiwa ukarabati wa vitu vidogo vidogo na kumuacha Sheila akijiandaa kwa ajili ya safari ya kurudi Dar es Salaam

    “Kaka hii gari umeinunua wapi?”

    “Kwa nini?”

    “Nina mwaka wa 21 tangu nianze kutengeneza magari ila sijawahi kuiona gari ya dizain hii kwa maana mmmm imekusanya mambo mengi”

    “Ahaaa hizi gari mbona zipo ukihitaji unazipata tuu”

    “Aise ila hii gari si chini ya milioni mia na kitu”

    “Imezidi zaidi ya hapo”

    Niliendelea kuzungumza na fundi mkuu wa gareji ambayo nimeileta gari yangu,Nikastukia nikiguswa bega kwa nyuma nikageuka na kukutana na sura ya Madam Rukia na kunifanya nistuke kiasi kwamba mapigo ya moyo yakaaza kunienda mbio

    “Mbona unastuka Eddy?”

    “Ha.....pana nimeshangaa tu kukuona hapa”

    “Wife(mke) unajuananaye huyo kijana?”

    Fundi gereji aliuliza swali na kujikuta nikizidi kupata kigugumizi chakuzumza kiasi kwamba nikaabaki nimekaa kimya

    “Ndio ni mwanafunzi wangu wa kidato cha tano,huyo ndio chanzo cha shele yetu kufungiwa”

    “Kaka sura yako inaonyesha mpole kumbe ni mkorofi kiasi hicho?”

    “Hapana mambo ya kawaida”

    Nilizungumza huku nikibabaika kwani kila nikimtazama Madam Rukia ninakumbuka tukio lililotokea porini na jinsi nilivyo fanya naye mapenzi kwenye kichaka isitoshe nikakumbuka niliusikia mlio wa bunduki na kujua ni lazima atakuwa ameuawa na mkuu wa shule

    “Ehee lete story Edy ile siku ilikuwaje?”

    Madam Rukia aliniuliza swali baada ya mume wake kuondoka na kuingia kwenye moja ya chumba na kuanza kuzungumza na wafanyakazi wake.Nikamuadisia Madam Rukia kuanzia tulipo achana hadi nikafika hopsitalini na yeye akaanza kuniadisia tangu tulipo achana

    “Mimi ile siku bwana nilikutana na vijana ambao ni wanakijiji cha karibu kwenye ule msitu wenyewe walikuwa wanakwenda kuwinda.....Sasa pale ulipo niacha mkuu wa shule na wezake si wakawa wananifwata basi wale vijana wakatanda ile sehemu tuliyopo na kuanza kuwashambulia waalimu na kuwatoa mbio za kufa mtu basi ikawa ndio pona pona yangu”

    “Mbona nilisikia mlio wa bunduki alipigwa nani?”

    “Ahh mkuu wa shule si alikuwa anajifanya kidume anapiga bastola juu hewani ili kuwatisha wale vijana......Wee alipigwa gongo moja la pua hata sijui ile bastola aliitupia wapi nilisikia akitoa ukulele wa uwii na kuanza kukimbia....sasa na ile miguu yake yenye matege ya kaekejea upande mmoja ungekuwepo ungecheka”

    “Mmmm sasa ulirudije mjini?”

    “Wale vijana wakaniazimisha simu na nikampigia my husband(mume wangu) nikamuelekeza nilipo akaja kunichukua na tukarudi mjini pamoja”

    “Ulimuambia jamaa kuhusiana na jinsi ulivyo fika porini?”

    “Ndio ila nilimuambia kuna majambazi ndio waliniteke...Ehee Madam Merry anaendelea vizuri amefanyiwa upasuaji na kizazi chake kimerekebishwa vizuri ila sasa hivi yupo powa”

    Madam Rukia alibadilisha mada baada ya mume wake kufika katika eneo tulilopo na sikuwa na haja ya kujiuliza ni kwanini amebadilisha mada nikajua moja kwa moja ahitaji mumu wake atambue kuwa mimi nilikuwa naye porini

    “Hivi wamesemaje kuhusiana na swala zima la shule kuendelea?”

    “Wamesema watatoa tangazo kwenye vyomba vya habari pele shule itakapo funguliwa ila kwa sasa wameunda tume ya madai yaliyopelekea shule kufungwa ambayo itachunguza kila kitu na wanafunzi walio kamatwa na polisi wapo wengine wanahojiwa”

    “Sasa hiyo tume watatumia muda gani kuchunguza hayo madai yato kwa maana siku zinakwenda mbele na masomo ndio hivyo yamesimama?”

    “Mimi wala sielewi ila kidato cha sita na cha nne wamesambazwa kwenye shule za jirani ili kuendelea na masomo hadi pale majengo yatakapo fanyiwa ukarabati nao ndio watarudi”

    “Ahaaa....”

    “Wewe sasa hivi unakwenda wapi Dar au kwa Marry?”

    “Huyo Merry mimi wala sihiaji kumsikia kwa maana mume wake amenizingu sana majuzi”

    “Wee amekuonea wapi?”

    “Si nilikwenda kumcheki hospitalini sasa nikawakuta wana mazungumzo yao basi mimi ikanibidi niwaache niondoke zao basi jamaa akanifwata na kuanza kunipiga vibao mbele za watu na mimi nikampiga basi mambo yakaharibika pale hospitali nikaamua kumpotezea”

    “Ndio ukaumia hivyo?”

    “Hapa nilipata ajali ya gari ndio maana nikafungwa huu mbadeji”

    “Pole mwaya ila yule mume wa Marry anajisikia sana”

    “Kwani anafanya kazi gani?”

    “Ni muwekezaji kwenye madini anasimamia kampuni ya baba yake kwenye kuchimba madini”

    “Tena nimekumbuka kuna kitu nahitaji unisaidie?”

    “Kitu gani?”

    “Si unamjua yule mdogo wa mke wa mwalimu Nyange”

    “Yupi?”

    “Tuye mrefu refu kiasi na nimweupe”

    “Ahaaa unamzungumzia Manka”

    “Ehee huyo huyo”

    “Mmmm yule mtoto wa watu anamatatizo sana kwani ni juzi juzi aliungua na maji ya moto usoni”

    “Kwa nini?”

    “Akili yake si imemruka yaani zinaingia na kutoka.Kuna kipindi akili yake inakuwa sawa na kuna kipindi akili yake inapote hii nikutokana na ajali iliyo mpata”

    Nikaanza kujisikia vibaya moyoni mwangu kwa maana Manka ni dada yangu japo nimefanya naye mapenzi pasipo kujua ila bado ni dada yangu

    “Hivi kwenye ajali ndugu zake walisalimika?”

    “Yaaa dada yake alipona na shemeji yake siku ya ajali wao walibaki Dar na kutokana na gari yao kujaa watu”

    “Mmmm.......nasikia alikuwa na ujauzito?”

    “Ulitoka chezea ajali wewe ila mbona unaniuliza maswali mengi ambayo ni vigumu kwa mtu kama wewe kutambua hayo mambo?”

    “Kawaida tuu”

    Madam Rukia akaondoka na mume wake wakaniacha nikilisimamaia gari langu lioshwe na mafundi wasaidizi wa mume wa madam Rukia.Wakamaliza kulisafisha gari langu nikawalipa pesa na kuingia kwenye ofisi waliyo ingia Madam Rukia na mumewe

    “Jamani mimi ndio ninaondoka zangu hivi”

    “Bwaba mdogo karibu sana”

    “Asante na pesa ya matengenezo nimewalipa vijana wako”

    “Hakuna shida nakukaribisha tena na tena”

    “Asante madam mimi ngoja niamshe popo”

    “Eddy unakiswahili cha kihuni kuamsha popo ndio nini?”

    “Maana yake ni kuondoka”

    “Ahaa sasa hembu nianchie namba yako ya simu endapo kutatokea lolote nitakujulisha”

    “Sawa”

    Nikamuandikia Madam Rukia namba yangu ya simu kwenye simu yake kisha na mimi nikajibipu na nikaisave namba yake nikaanachana nao na kurudi zangu hospitakini nikamkuta Sheila akimaliza kuagana na manesi wake ambao alishaanza kuwazoena kama dada zake na kuwafanya baadhi ya manesi kumwagikwa na machozi haswa nesi aliyekuwa akimuhudumia Sheila kwa karibu sana na ndio alikuwa akiitoa simu yake kwa ajili ya mawasiliano.Tukaondoka hospitalini na kurudi katika hoteli tuliyo fikizia na kuchukua mizigo yetu ambayo tulikuta imehifadhiwa kwenye sehemu malumu hii ni baada ya muda wetu wa vyumba tulivyo lipia ulikwisha.Safari ikaanza taratibu huku nikiendesha gari kwa umakini mkubwa kuepuka ajali zisizo na ulazima

    “Eddy nakupenda sana mume wangu”

    “Nakupenda pia mke wangu”

    “Yaani natamani hata tuishi pamoja kabisa”

    “Usijali mke wangu tutaishi pamoja”

    Tukaendelea na safari huku ukimya ukiwa umetawala ndani ya gari,Sheila akaweka vizuri siti yake aliyo kalia na kuanza kulala na kuniacha mimi nikiendelea kuendesha gari hadi tunafika Mombo mida ya saa tisa alasiri nikamuamsha Sheila na tukaingia kwenye hoteli ambayo ninapenda kuingia kwa kupata chakula nikiwa kwenye safari kati ya Dar na Arusha.Simu yangu ikaingia meseji na namba ngeni ambayo si yatanzania huku ujumbe wake ukiwa ni mfupi sana na kunistua kidogo

    ‘NIPIGIE’

    Nikabaki nikiwa nimeutazama kwa muda huku nikiwa na maswali kichwani ni nani aliye nitumia ujumbe wa namna hiyo.Nikaingia kwenye akaunti yangu ya simu na kununua muda wa kutosha wa maongezi kisha nikaipiga namba ya simu

    “Eddy mwangu hujambo”

    Nikaisikia sauti ya mama na nikajikuta nikisimama kwa haraka na kuelekea kwenye vyoo kuzungumza na simu ambayo kwangu ni muhimu sana

    “Sijambo mama shikamoo”

    “Marahaba mwanangu sina muda wa kupoteza ila ninakuomba uje nchini Iraq tupo kizuizini na hap.....”

    Nikasikia mama akitoa kelele za kupigwa na watu ambao wanazungumza kiarabu ambacho sikuwa ninakielewa na baada ya muda kidogo simu ikakata na kujikuta nikianza kupandwa na hasira huku jasho likinimwagika.Nikatoka na kwabahi mbaya kwenye mlango wa kuingilia chooni nikagongana na jamaa anaye onekana ni sharobaro na kuifanya simu yake ya gharama aliyokuwa anaichezea kuanguka chini na kupasuka kioo,Nikataka kuondoka jamaa akanishika mkono na kunivuta nirudi sehemu aliyo simama

    “Wewe fala umeangusha simu yangu hata kuniomba msamaha unaondoka ondoka”

    “Fala mwenyewe kwanza niachie mkono wangu kati ya simu hako kakopo kako ndio unakaita ni simu”

    “Kwa hiyo mimi unaniita fala si ndio”

    Jamaa alizungumza kwa hasira kiasi kwamba akanishika tisheti yangu kifuani na kuanza kuikinja huku akinivuta kiasi kwamba akazidi kunipandisha hasira.Nikaitoa mikono yake kwa nguvu kifuani kwangu na kumsukuma jamaa na akarudi nyuma kidogo na kuanza kunirushia ngumi ambazo zilinipata kifuani.Nikajirusha na bega langu kilampiga tumboni kwake kama wanavyofanya wacheza miyereka na nikamsukuma na sote tukajikuta tukiangukia mlango wa choo hadi ukavunjika.Nikanyanyuka haraka na kamkaba jamaa shingoni kwa muda na kuwafanya watu walio liona tukio kuja kutuamua

    “Eddy mume wangu ni nini unacho kifanya”

    Sheila alizunumza huku akinishika mkono akisaidiana na watu wanao amua ugomvi kuniondoa katika sehemu ya tukio

    “Wewe boya tuu kamlale mama yako ambaye ni Malaya”

    Jamaa alinitukana tusi lililoamsha hasira zangu upya na kujikuta nikiwazidi nguvu watu walio nishika na kwenda kumvaa jamaa na safari hii nikaanza kumshindilia ngumi za hasira kiasi kwamba jamaa akapasuka sehemu ya jicho lake na uso wake kujaa damu idadi ya watu ikazidi kuongezeka na kunitoa katika sehemu ya ugomvi na kuniingiza kwenye moja ya chumba kinachotumika kama ofisi ya eneo hili la hoteli.

    “Eddy mume wangu punguza hasira nakuomba tafadhali nipo chini ya miguu yako.Nakuomba baby”

    Sheila akazidi kuendelea katika kunituliza kiasi kwamba nikabaki nimekaa kimya huku mwili ukiwa unanitetemeka kwa hasira huku meno yangu nikiwa nimeyakaza kwa kuyang’ata kwa uchungu na hasira kwani katika maisha yangu kitu ambacho kinanichukiza ni mtu kumsema mama yangu vibaya

    “Eddy wangu nakuomba uachene na wapumbavu mume wangu wasikupotezee muda wako...Ehhee tulia mume wangu sawa”

    Sheila alizungumza huku akinikumbatia na kuanza kunifuta machozi yanayonitoka kwa hasira,wakaingia askari wawili na wakasimama mbele yetu huku wakijishauri kitu cha kuniuliza na mmoja wao nikamkumbuka haraka ni miongoni mwa askari walio nikamata siku Manka na familia yake walipo pata ajali na wakanipeleka kituo cha polisi mimi na dereva wa mama

    “Kaka zangu niwasaidie nini?”

    “Ahaa tulikuja kumchukua jamaa akatoe maelezo kituoni kwa tukio zima lililo tokea”

    “SIENDI KOKOTE NA OLE WAKE MTU ANIGUSE NINAKUFA NAYE”

    Askri wakakaa kimya huku wakinitazama na kumfanya Sheila awakonyeze kwa ishara ya kuniacha hadi hasira zipungue.Askari wakatoka na kuniacha na ndani ya lisaa hali yangu ikarudi kama awali hii ni baada ya Sheila kunibembeleza kwa kila aina ya maneno mazuri ya kuvutia.Tukatoka ndani ya chumba tulichopo huku Sheila akinipigisha stori za kunifurahisha na kunifanya nicheke,Nikakutana na askari waliokuja kunikamata wakanifwata kiustaarabu na kuniomba niongozane nao hadi kwenye kituo chao na sikufanya ubishi.Tukaingia kwenye gari letu na kuongozana nao huku na wao wakiwa kwenye gari lao na haikichukua muda tukafika kwenye kituo cha polisi

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikakutana na baadhi ya wazee wapatao wanne wakiwa mamevalia mashati ya kijani sura zao zikiwa zimejikunja baada ya sisi kuingia na pembeni yao akiwa amekaa kijana niliye pigana naye na sura yake ikiwa na maplasta huku ikiwa imevilia damu.Wakaanza kuzungumza lugha ya kipare ambacho ninakielewa viruzi kwani walianza kumuuliza kijana wao ni nani aliye mpiga na akawajana kwa kuninyooshea kidole kuwa mimi ndio nilio mpiga hadi akaumia sura nzima

    “Mimi ni diwani kwani umepiga mwanangu”

    Mzee mmoja mwenye kitambi cha wastani alizungumza kwa hasira na kabla sijamjiu Sheila akanifinya mkononi na kunifanya nimtazame bila ya kumjibu chochote kwani nilipanga kupa tusi ambalo asinge nisahamu maishani mwake

    “Mzee wangu ninakuomba umsamehe mume wangu kwani ni hasira tuu ndizo zilipelekea ugomvi kati yake na huyo mwenzake”

    “Wewe koma mwanamke Malaya mkubwa usiye na haya wewe unaweza ukamuita huyu kapupwe wako mume ehee kwanza sijazungumza na wewe”

    Mzee akazidi kuzungumza kwa hasira kiasi kwamba nikajikuta na mimi hasira zikaanza kunipanda taratibu na Sheila akanishika kifuni ili jazba ishuke na sikuelewa ni kwanini askari wamekaa kimya mzee akiwa anazungumza

    “Sawa mzee wangu ila ninakomba mumsamehe na kama kuna gharama zozote tupo tayari kuwalipa”

    “Wewe mwanamke huwezi kunilipa mimi....Uliza hapa mjini mzima wananijua mim ni nani?’

    “Mzee wangu naona ustaarabu umekushinda...Sijaja hapa kusikiliza kuwa wewe ni nani au unakazi gani.....Na nyinyi mumekuja kunichukua kule ili nije nikutane na wazee kama hawa wasio na aki.....”

    Sheila akaniziba mdomo ili nisimalizie nilichokuwa nikikizungumza kwani kingeamsha ugomvi upya

    “Mzee wangu tukauomba utusamehe kwa yaliyo jitokeza sema kama kuna kiasi chochote chapaesa ninaweza kukulipa”

    Kuepusha shari nikatoka kwenye kituo cha polisi na kuingia ndani ya gari na kumsubiria Sheila ambaye baada ya robo saa akatoka na kuingia ndani ya gari

    “Wamesemaje?”

    “Wametaka tuwalipe gharama za matibabu pamoja na gharama za vitu vilivyo haribika kwenye hoteli.Kumbe yule mzee ndio mmiliki wa hoteli na yule mwanaye alikuwa kama msimamizi pale”

    “Na wanataka kiasi gani cha pesa”

    “Milioni moja na nusu”

    “Waache upuuzi wao tuondoke watapewa na babu zao”

    “Eddy”

    “Tuondoke zetu wasilete uhuni yeye si amesema sisi hatuwezi kumlipa basi achana nao”

    “Edd achana kuwa mbishi mume wangu wameniomba nije kujadiliana na wewe ili tujue tunawalipa nini?”

    “Ahaa basi majadiliano yetu mimi na wewe ni kwamba hakuna swala la kuwalipa cha msingi tuondoke zetu kwanza ninahitaji tufike Dar leo hii kabla ya saa nne usiku na sasa hivi ni saa kumi na mbili jioni”

    “Eddy nakuomba tuwalipe mume wangu tuepushane na shari dhidi yao kwani watu wenyewe wanaonekana hivi hivi ni washirikina”

    “Funga mkanda wewe unaogopa wachawi?”

    “Ehhhee”

    “Na waturoge basi kama niwacawi kweli”

    Nikawasha gari na kuondoka eneo la kituo cha polisi nakuendela na safari huku gari nikiizidisha mwendo na kumfanya Sheila kuwa na wasiwasi na mwendo ninao tembea nao kwani ninatembea na zaidi ya spidi 220 ambacho ni kiwango cha juu na gari za kawaida za Tanzania mwisho wa spidi yake ni 180.

    “Eddy punguza mwendo basi”

    “Ninaharaka mke wangu”

    “Jamani baba angu haraka ya wapi wakati tunaekelekea nyumbani”

    “Nataka niwahi kufika ili nipange safari ninahitaji kwenda Iraq”

    “Eddy nimesikia vibaya au.....Unataka kwenda wapi?”

    “Iraq ndipo mama alipo kamatwa na hapa ninataka kwenda kutoa taarifa kwenye wizara ya mama wajue wananisaidiaje”

    “Mume wangu nitabaki na nini?”

    “Si nitarudi kwani ninakwenda kufa huko na hapa breki ya kwanza ni nyumbani kwetu”

    “Sawa mume wangu”

    Tukafanikiwa kufika Dar es Salaam saa tano na robo usiku na moja kwa moja tukafikizia nyumbani na kupiga honi na akatoka askari huku akiwa ameishika bunduki yake kwa umakini na kuniomba nishuke kwenye gari kwani ninahisi hakujua kama ni mimi

    “Eddy habari yako”

    “Salama vipi kaka”

    “Safi tuu nifungulie geti niingie”

    “Siwezi kufanya hivyo kwani bosi ameniambia nisimruhusu mtu yoyote kuingia ndani”

    “Bosi gani na wewe si unajua kuwa hapa ni kwetu sasa kwanini usiniruhusu?”

    “Baba yako ndio amesema nisiruhusu mtu yoyote kuingia ndani kwani anawageni humo ndani”

    “Amerudi lini?”

    “Anasiku nne tangu arudi hapa”

    “Na ha wageni ndio wamefungua mziki huo kwa sauti ya juu hivyo?”

    “Ndio”

    Nikashuka ndani ya gari kufungua geti dogo na kuingia ndani huku Sheila akinifwata kwanyuma kwa hatua za haraka,Nikaufungua mlango na kukuta wasichana nane wakiwa wamevalia chupi huku wawili wakiw uchi kabisa wakikatika mauono mbele ya baba ambaye anaonekana amelewa huku akipiga kelele za kufurahia

    “BABA....BABA”

    Baba akastuka na kuchukua rimoti ya redio na kuizima kisha akanyanyuka huku akiwa anayumba yumba na mkononi kwake akiwa ameshika chupa ya whyne na akaanza kupiga hatua za taratibbu kunifwata kwenye sehemu niliyo simama

    “Baba ni nini unacho kifanya ina maana wewe hujui kitu kilicho mpata mama na unakula raha na hawa machangudoa zako?”

    Nilizungumza kwa uchungu huku machozi yakianza kunilenga lenga

    “Wee koma kwanza ni nani aliye kupa ruhusa ya kuingia humu ndani kwangu?”

    “Kwahiyo kwenye nyumba hii mimi sina ruhusa ya kuingia?”

    Nikastukia kibao kikali kikitua kwenye shavu langu na kunifanya niyumbe na Sheila akanisaidia kisimama wima nisianguke chini

    “Huna mamlaka ya kuzungumza mbele yangu na kuanzia leo hii mama zako ni wale pale wanao cheza mbela yangu na mama yako kwanza hajui mapenzi kitandani.....Ni mzito hajui kukatika anakaa kama boga lililo ozeana”

    Maneno ya baba yakazidi kunipandisha hasira na mbaya zaidi wasichana alio kuwa nao wakaanza kucheka kwa dharau huku wakinizomea na kuongea maneno ya kejeli.Baba akanitazama kwa macho yaliyo jaa pombe nyingi na kumfwata Sheila na akatazama kwa muda na kumfanya Sheila kuanza kutetemeka na gafla akamshika ziwa na kunifanya nishindwe kuvumilia.Nikamsukuma baba na akanguka chini na akanipiga teka la kustukiza na lililonifanya nianguke kama mzigo kisha akasimama na kuanza kuruka ruka kama wapiganaji wa kick boxre na kunifanyia kidole chake akiniomba ninyanyuke ili tupigane

    “Eddy usifanye”

    Sheila akanishika mkono na kuninyanyua na kunivuta kwa nyuma huku akinizuia nisipigane na baba

    “Eddy twende zetu nyumbani”

    “Wewe malaya unataka kumpeleka wapi mwanangu”

    “Mimi sio mwanao na ninawapa hawa Malaya zako dakika mbili watoke humu ndani la sivyo nitawaua”

    “Ohhh Eddy hii ni nyumba yangu na kuhusu mama yako hawezi kurudi ndani ya hii nyumba tena kwani tayari AMESHAKUFA”

    Moyo ukaanza kuniuma baada ya kusikia mama kuwa amekufa,Sheila akanishika kiuno na tukafungua mlango na kutoka nje huku machozi yakinimwagika na chuki zidi ya baba ikazidi kunipanda kiasi kwamba nilatamani kurudi na kupiga naye ila Sheila akazidi kunionya nisifanye kitu cha namna hii

    “KUANZIA LEO HII MAMA ZAKO NI WALE PALE WANAO CHEZA MBELA YANGU NA MAMA YAKO KWANZA HAJUI MAPENZI KITANDANI.....NI MZITO HAJUI KUKATIKA ANAKAA KAMA BOGA LILILO OZENA”

    Maneno ya baba ya baba yakezidi kujirudia kichwani mwangu na kuzidi kunichanganya na kuanza kupanga mipango ya kumuua baba pale nitakapo pata nafasi,Sheila akaniingiza kwenya gari na akaingia upande wa dereva na tukaondoka katika eneno la nyumbani.Ndani ya dakika ishirini tukafika nyumbabi kwake na tukashuka kwenye gari akanifungulia mlango ni nakapitiliza mojakwa moja hadi ndani kwake na kujitupa kitandani na kumuacha akifunga miliango,Sikutegemea ata siku moja baba yangu atakuja kinidhalilisha mbele za watu mbaya zaidi ananizalilisha kuhusia na mama yangu kipenzi.Sheila hakunisesha chochote zaidi ya kuvua nguo zake na kupanda kitandani na kukaa pembeni na akaanza kunivua nguo moja baada ya nyingine na kubakiwa na boxr.Kutokana na hasira na kuchoka usingizi mzito ukanipitia na kulala fofo

    ***

    “Eddy baby kumepambazuka amka ukanywe chai”

    “Saa ngapi sasa hivi?”

    “Saa tatu”

    Sheila akaninyanyua kitandani na kunivalisha ndala na kuniingiza bafuni na kila kitu anachonifanyia Sheila sikuwahi kusanyiwa na mwanameke wa aina yoyote na taratibu nikajikuta upendo ukijijenga ndani ya moyo wangu na kujiapia kuto kumuacha Sheila.Nikamaliza kuoga na kwenda moja kwa moja mezani na tukaanza kunywa chai kwa pamoja huku akiendelea kunifariji

    “Sheila yale ndio maisha ambayo nilikuwa nikukuambia kuhusiana na baba yangu.....Na sijui ni kwanini anamfanyia mama vile na kitu kingine ambacho kinaniumiza roho ni jinsi baba alivyotembea na mfanyakazi wa ndani na kumpa mimba tena juu ya kitanda wanacholala na mama”

    “Mmmm pole mume wangu ila hapa ninahisi kuna kitu tu kinachoendelea kwenye hili swala zima la kutekwa kwa mama na ninavyo kumbuka baba yako alisema kuwa mama amefariki.......Ina maana anajua mama kuwa ametekwa”

    Nikakaa kimya na kunyanyuka kwenye kiti na kuingia ndani na kuvaa nguo kwa haraka na huku Sheila akinitazama

    “Baby unakwenda wapi?”

    “Nakwenda kutoa taari juu ya sehemu aliyopo mama kama jana alibvyo niambia kwenye simu”

    “Unaonaje tukaenda sisi wenyewe Iraq kwa maana hapa ninahisia mbaya kuhusiana na lilicho yokea kwa mama mkwe”

    “Ila ngoja kwanza niende nikazungumze nao”

    “Eddy nisikilize mimi ninakuomba twende pasipo kuzungumza na mtu wa aina yoyote kwa maana hili swala lina mikono ya watu wazito na si bure”

    Wazo la Sheila nikalikubali na akaanza kuvaa nguo zake na kuchakua hati zake za kusafiria na ikatulazimu kwenda nyumbani kuchukua hati yangu ya kusafiria kwa maana nisingeweza kwenda sehemu yoyote pasipo hati hiyo.Tukakodi taksi hadi nyumbani kwetu nikamuomba dereva kusimamisha gari mbali kidogo na ilipo nyumba yetu na nikashuka na kutembea hatua chache hadi nyumbani na kugonga geti na akatoka askari

    “Eddy umerudi tena mdogo wangu”

    “Huyu pimbi yupo humo ndani?”

    “Ametoka muda huu ameondoka na wale wadada wa jana usiku”

    “Powa naningia ndani dakika kadhaa tuu nitatoka”

    “Fanya fasta asije akakukuta”

    Nikaingia ndani na moja kwa moja nikaingia ndani kwa mama na kufugua kwenye droo yake aliyo tengenezwa kwa chuma na kujengewa ukutani na nikaingiza namba za siri na ikafunguka na kukuta vitu maalumu ambavyo ni vya siri sana pamoja na pesa ya kutosha,Nikachukua hati yangu ya kusafiria pamoja na pesa zote zipatazo dola za kimarekani laki moja na nusu ni sawa na milioni 24 za Kitanzania na kuziweka kwenye begi la mgongoni na kabla sijakifunga ndipo nikaona katatasi zilizo ambatanishwa kwa pamoja zipatazo tano huku zikiwa na maandishi makubwa na nikaanza kuzisoma haraka haraka na kukuta ni maelezo ya mama

    “MIMI GRACE J.MAPUNDA NINAANDIKA NIKIWA NA AKILI ZANGU TIMAMU PASIPO KUSHAURIWA NA MTU WA AINA YOYOTE.MALI ZOTE AMBAZO NINAZIMILIKI NI ZA MWANAGU EDDY GODWIN PALE ITAKAPOTOKEA NIMEFARIKI YEYE NDIO ATAKUWA MSIMAMIZI NA MMILIKI MKUU WA MALI ZOTE AMBAZO NI

    1.NYUMBA NINAYOISHI YENYE DHAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.5 ZA KITANZANIA PAMOJA NA NYUMBA ZANGU TANO ZA KIFAHARI ZINAZOPATIKANA ARUSHA ZIPO MBILI,MWANZA MOJA NA TANGA MOJA”

    2.MADUKA NANE.HOTEL MBILI ZILIZOPO AFRIKA KUSINI NA VITEGA UCHUMI VILIVYOPO UINGEREZA NA MAREKANI IKIWEMO HISA ASILIMI 35 ZILIZOPO KWENYE KAMPUNI YA UTENGENEZAJI WA MAGARI NCHINI MAREKANI”

    3.GARI 8 ZA KIFAHARI”

    Sikutaka kuzisoma aina za magari ambayo mama ameyaorodhesha kwa maana ninayafahamu yote na kuachana na mambo mengi ambayo mama ameyaandika na nikajikuta nikistushwa na maneno yaliyopo karatasi ya mwisho

    “MUME WANGU ASIHUSISHWE KWENYE CHOCHOTE KILICHO ANDIKWA KWENYE HUU WOSIA WANGU KWA MAANA HAJAHUSIKA KATIKA KUPANDA NILIVYO NAVYO NA SI BABA HALISI WA EDDY”

    Nikahisi nguvu zikiniishia na swala zima la nani ni baba yangu liakaanza kunijia kichwani na nikazitoa karatasi zote zilizopo ndani ya kisanduku maalumu cha mama na nikafungua droo zake na kutoa cheni na pete zake za dhahabu na vitu vyenye dhamani na kuviingiza ndani ya begi na kabla sijatoka ndani kwake nikakumbuka kubeba albamu yenye picha zake na zangu kisha nikaridhika nafsini mwangu na kuufungua mlango na kutoka kabla sijashuka kwenye ngazi nikasikia mlango ukifunguliwa na nikaisikia sauti ya baba ikizungumza na watu wa wili nikachangulia nikawaona watu wawili wakiwa wamevalia nguo za jeshi huku wakiwa wameshika nyundo na sururu mikononi mwao

    “Nimeshindwa kufungua kijidro kilichopo ukutani na huyu mwanamke amebadilisha namba za siri”

    “Kipo wapi mkuu tukushuhulikie?”

    “Kipo huku juu twendeni mukaking’oe”

    Nikaingi jikoni na kujibanza kwenye mlango na wakapita bila kuniona na kuingia chumbani kwa mama na nikatoka na kushuka kwenye ngazi kwa haraka na kutoka nje na kuanza kukumbia na kabla sijafika getini nikaisikia sauti ya baba

    “Wewe mpumbavu hapo getini mkamate huyo mshenzi”

    Sikusimama na askari wa getini akanipisha na sote kwa pamoja tukatoka getina na tukaingia kwenye taksi na kumuomba dereva aondoke kwa kasi.

    “Mbona hujanikamata?”

    “Siwezi kufanya hivyo kwa maana mama yako amanisaidia kwenye mengi na nikifanya hivyo nahisi hata mbinguni sinto kanyaga”

    “Nashukuru ndugu yangu”

    Nikafungua begi langu kutoa noti kumi za dola mia mia na kumpa askari wa getini akanishukuru kupita maelezo kwa muonekano wake tangu azaliwe hakuwahi kushika kiasi cha pesa nilicho mpatia kwa maana anaonekana kuzishangaa

    “Eddy kuna gari inatufwatwa kwa nyuma hembu iangalie sio ya baba yako?”

    Sheila aliniambia na kunifanya nigeuke na mapigo ya moyo yakanza kunienda mbio baada ya kuiona gari ya baba ikija kwa kasi nyuma yetu na gafla dereva akafunga breki za kistukiza hii ni baada ya basi dogo aina ya DSM kujaribu kilipita lori lenye tela refu na kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya VOXY iliyokuwa ikija kwa kasi kwenye upande na kusababisha ajali mbaya huku gari hizo zikiziba barabara nzima



    Nikafungua begi langu kwa haraka na kutoa noti mojaya dola mia na kumkabithi dereva taksi kisha sisi tukashuka ndani ya gari na kuanza kukimbia rukijichanganya na watu walio anza kukusanyika wakitoa misada kwa majeruhi wa gari mbili hizi.Mimi na Sheila tukapanda bodaboda za pikipiki pasipo baba na watu wake kutuona na kuwaomba boda boda kutupreleka kiwanja cha ndege cha mwalimu Julias Kambarage Nyerere pasipo baba na watu wake kujua ni wapi tulipo elekea.Tukaingia kwenye sehemu ya kutazama ratiba za ndege zilizopo kwa wakati huo na kukuta zimesalia dakika kuni na tano ndege ya shirika la Qatar Airways na nafasi za tiketi zilibakia tatu tu.Tukakata tikakata tiketi mbili na kuwa miongoni mwa abiria wa ndege hii itakayo ondoka ndani ya dakika kumi zijazo.Kwa haraka haraka tukapanda mstari na kuanza kukaguliwa na wakaguzi tulio wakuta kwenye uwanja wa ndege.

    “Wewe kijana kaa pembeni”

    Askari aliye valia sare zake za kazi huku mwili wake ukiwa umepanda juu na kujazia kwa misuli mizito aliniambia huku akininyooshea mkono wake na kunifanya nianze kupata wasiwasi.Sheila akaruhusiwa kuingia upande wa pili ili kujumuika na abiri wengine wanao iwahi ndege.Nikamkonyeza Sheila asiondoke na anisubiri kwani sikujua ni kitu gani kilicho mfanya askari huyo kuniambia nikae pembeni.Wakaja askari wengine wawili wakiwa na mbwa wakubwa na kusimama karibu yangu huku mbwa wao wakianza kunimusa nusa

    “Kijana tunakuomba utufwate tunamazungumzo na wewe”

    Askari aliye niambia nisimame pembeni alizungumza huku akiwa amelishika begi langu lenye pesa na vitu vyangu muhimu.Sikuwa na jinsi zaidi ya kuanza kumfwata kwa nyuma askari hadi kwenye moja ya chumba na kuingia naye na kukutana na askari wengine wawili wakiwa wamekaa kwenye moja ya meza moja kubwa na baada ya kumuonamwenzao wakampisha na kuanza kuuanali kwa macho ya dharau kuanzia chini hadi juu na kwaishara wakanionyesha sehemu ya kukaa na nikatii nikiwasubiria waniambie kitu ambacho wanataka kuniambia.Nikashangaa kumuona askar mmoja akilifungua begi langu na baada ya kuziona pesa zangu akaanza kushangilia kisha akavimwaga vitu vyote juu ya meza

    “Mbona munamwaga vitu vyangu?”

    “Tunakagua tunakuomba uwe mtulivu la sivyo hutotoka mikononi mwetu”

    Ikanibidi nikae kimya huku mara kea mara nikiitazama saa ya ukutani na kuona dakika zikikatika taratibu huku zikiwa zimebakia dakika tano tuu ili ndege ifungwe na kuaondoka.Wakaanza kuchagua kitu kimoja baada ya kingine na kuanza kuzisoma baadhi ya karatasi za mama nilizo ziweka kwenye begi na askari mmoja akaanza kuipisha kila karatasi kwa wezake na wakaanza kuisoma taratibu huku wakinitazama usoni

    “Hii si nyaraka ya serkali?”

    “Ndio inabdidi atueleze vizzuri kuwa hizi karatasi za mikataba amezito wapi”



    Askari wakaendelea kubishana wao kwa wao huku wakiendelea kuzitazama karatasia ambazo sikuzisoma na sikujua ni nyaraka gani wanazo zizungumzia.Ikanilazimu kuwaomna ili wanionyeshe karatasi hizo ila wakakataa

    “Wewe mikataba ya wizara ya Afya umeitoa wapi?”

    “Ehee....”

    “Umelisikia vizuri swali langu sina haja ya kulirudia”

    “Mikataba hiyo ni ya mama yangu ambeye ni waziri wa hiyo sector”

    “Aaaa kumbe nyinyi ndio munaowapelekea wazazi wenu mikataba ili wakasaini ili kuidhulumu serikali yetu si ndio?”

    “Sikia mkuu mimi sio kwamba nimeichukua hiyo mikataba kwa ajili a kwenda kumpa mama yangu.....Nyote ninaamini kuwa mujua ya kwamba mama yangu pamoja na viongozi wengine wamekamatwa na sijui kuwa nyinyi muna kazi gani kwa maana hamuonyeshi juhudi zozote katika kuwakomboa viongozi hao”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilizungumza kwa hasira huku nikinyanyuka kwenye kiti na kuwafanya askari kuchomoa virungu vyao na kuanza kunisambulia kwa kunipiga sehemu mbali mbali za mwili huku nikimshuhudia mmoja waoa akiingiza pesa zangu kwenye mifuko yake ya suruali na kujikuta nikikasirika na kumsukuma na kuanza kuminyana naye kuzichomoa pesa zangu mifukoni mwake na kuzidi kuwongezea wezake hasira na kuzidi kunipiga virungu na mateke yaliyo tua tumboni na kifuani na kuuufanya mwili wangu kunifanya nianze kutokwa na damu za mdomoni na puani

    Gafla mlango ukafunguliwa na akaingia Sheila akiwa ameongozana na waziri mkuu Bi.Maimuna Ramadhani na akaonekana kushanga na kuwafanya askari kuancha kitendo chao cha kunipiga.Nikabaki nikiwa nimejikunyata chini huku damu zikiwa zinaendelea kunimwagika huku mwili mzima ukiwa umetawaliwa na maumivu na uvimbe kwenye sehemu za kichwa chanu.Sheila akapiga magoti hukua akilia kwa uchungu na kutoa kitambaa chake na kuanza kunifuta damu zinazo nitoka

    “Hii ndio kazi muliyo agizwa na serikali kuwapiga watu kiasi hichi?”

    Swali la wa waziri mkuu likawafanya askari wote kukaa kimya na sikujua waziri mkuu imekuaje akaja katika chumba hichi ila uzuri ni kwamba ni rafiki wa mama na muda mwingi huwa wanashirikina sana katika maswala yao ya kina mama hususani katika uanzilishi wa mambo ya vikoba kwa wanamama wajasiriamali

    “Eddy Eddy”

    “Mmmmm”

    Mdomo wangu haukuweza kufunguka kutokana na kuvimba kwa mdomo ambao pia umejeruhiwa kwa kupiwgwa na askari hawa ambao sasa hivi wamejikausha kama wamemwagiwa maji ya baridi.

    “Kwahiyo hamuna majibu ya kutoa”

    Nikamnyooshea askari mmoja aliye chukua pesa zangu na kumf anya waziri mkuu kunimtazama huku akiwa haelewi ni nini kinachonifanya nimnyooshee mkono,Nikajitahidi kunyanyuka kwa msaada wa Sheila na akanikalisha kwenye kiti

    “Eddy mwanangu pole sana......”

    Waziri mkuu akamnong’oneza Sheila na kumfanaya Sheila kutoka ndani ya chumba na baada ya muda akarudi akiwa ameongozaa na mlizi wa waziri mkuu

    “Nipe simu”

    Mlinzi wa waziri mkuu akatoa simu na kumkabidhi waziri mkuu na akaminya batani na kuiweka simu yake sikioni

    “Habari yako kaka”

    “Sasa kuna vijana wako wamemjeruhi kijana wangu pasipo kuwa na sababu ya msingi sasa ni hivi ninakuomba uwafute kazi mara moja”

    “Asante”

    Waziri mkuu akampa mlinzi simu kisha akanisogelea na kunitazama kwa macho ya huruma

    “Mwanangu pole sana”

    “Asa...n.te”

    “Ulikuwa unakwenda wapi?”

    “Tulikuwa tunakwenda Iraq mama jana alimpigia simu Eddy na kumuomba amfwate”

    Sheila akajibu kwa niamba yangu kwani mdomo wangu ulivimba sana na kunifanya nishindwe kuzungumza vizuri na kumfanya waziri mkuu kuhamaki

    “Alisema you Iraq sehemu gani?”

    “Hakusema kwani alipokonywa simu na watu walio wateka”

    Waziri mkuu akaichukua simu yake na kupiga namba baadhi na kuisikiliazia simu yake na kukifanya chumba kizima kikiwa kimya tukimsikiliza

    “Shikamoo muheshimiwa Raisi”

    “Mimi nipo salama tu kuna taarifa hapa nimeipata kuwa viongozi wetu wapi Iraq na ndipo walipo shikiliwa mateka”

    “Ndio taarifa nimeipata kwa mtoto wa Grace na anadai jana alizungumza na mama yake”

    “Sawa mkuu nashukuru kwa ushirikiano wako”

    Waziri mkuu akakata simu na kuwatazama askari walio nipiga na kumuagiza mlinzi wake awaandike majina yao pamoja na namba zao za kwenye mashati

    “Wa..napes....a zan..gu”

    Nilizungumza kwa kujikaza japo ninapata maumivu makali ila ikanilazimu kufanya hivyo na Sheila akasima na kumsogelea askari niliye mnyooshea mkono kwa mara ya kwanza na akanza kumpapasa mifukoni na kuzitoa pesa zangu na kumfanya waziri mkuu kuzidi kupandwa na hasira na kumpiga kibao askari huyo na kumfanya azidi kutetemeka

    “Pumbavu...binti watazame na hao wengine”

    Sheila akaanza kumpitia askari mmoja baada ya mwengine na kuzitoa wallet zao na kuchomo pesa zote walizo kuwa nazo na nyengine hazikuwa za kwangu ila Sheila akazichukua.Akaingia mkuu wa usimamizi wa uwanja ambaye ni askari mkuu

    “Vijana wako hawa kuanzia sasa hivi sitaki kuwaona kazini.SAWA”

    “SAWA MKUU”

    Tukatoka kwenye chumba huku Sheila akinisaidi katika kutembea na baadhi ya watu wakaanza kutushangaa kila tunapopita.Tukaingia kwenye gari ya waziri mkuu na maja kwa moja wakanipeleka Hospitali ya Muhimbili na madaktari wakanipokea na kuanza kunifanyia huduma huku wakinichoma sindano za kupunguza maumivu.Waziri mkuu akatoa maagizo kwa madaktari nitibiwe katika uangalizi mzuri la sivyo watakiona cha moto kisha yeye akaondoka na kutuacha mimi na Sheila.

    Baada ya siku mbili nikapata uwezo wa kuzungumza vizuri kama awali japo kuna sehemu za mwili zina maumivu makali bado.

    “Sheila ile simu ilikuwaje wazari mkuu alikuja kwenye chumba tulichopo?”

    “Alikuwa kwenye dhiara pale uwanja wa ndee na ndio alikuwa anamaliza kuzunguka kwenye baadhi ya ofisi.Nikamfwata na kumuelezea na kwabati nzur nilivyomuelezea kuhusu wewe akanielewa ndio tukaja mule ndani”

    “Aaha nashukuru kwa hilo mke wangu”

    “Ila zile tiketi nimezirudisha na nimewaambia kuwa tumepata dharula ila hadi utakapo pona ndio tutakwenda Iraq”

    “Sawa ila waziri mkuu hakukupigia siku mbili hizi?”

    “Alinipigia na nilimuwambia kuwa unaendelea vizuri na yeye akaniambia zoezi la kuwatafuta viongozi linaendelea vizuri hatuna haja ya sisi kwenda kwa Iraq kwani itaongeza matatizo zaidi”

    “Sawa ila ndini ya mwili najisikia maumivu sana”

    “Sehemu gani?”

    “Hapa kwenye kifua kunaniuma sana nikihema hivi niihisi harufu ya damu”

    “Weee ngoja basi nimuite dakari”

    Sheila akasimama na kwenda kumuita daktari aliye kabidhiwa kwa kuniangalia kwa ukaribu sana.Sheila akaanza kumuelezea dakatari hali ninayojisikia na kumfa ya daktari kutoa agazo kwa wezake wanifanyie uchunguzi zaidi.Wakanipeleka kwenye chumba cha X-reys na wakaniweka kwenye mashine kubwa iliyokaa kama mfumo wa jeneza na kunipitisha kwenye mitambo yao na kutokea upande wa pili wa sehemu hiyo na wakanitoa kwenye kifaa chao na kunirudisha wodini na kumuomba Sheila kubaki na madaktari kwa mazungumzo zaidi.Baada ya muda Sheila akaingia huku akiwa na sura ya unyonge iliyo anza kunipa wasiwasi kiasi kwamba nikajikuta ninaaza kupata wasiwasi na mimi

    “Sheila wamekuambiaje?”

    Badala ya Sheila kunijibu akaanza kulia na kuzidi kunichanganya na sikujua ni nini kinacho mliza.

    “Eddy ninakupenda sana mume wangu”

    “Sawa hata kama unanipenda ila niambie kitu kinacho kuliza”

    “Eddy sitaki kukupoteza mume wangu bado hatujafikia malengo yetu”

    Sheila akazidi kunichanganya kiasi kwamba nikataka kunyanyuka ila kutokana na maumivu ya kifua changu nikajikuta nikurudisha kwichwa changu kwenye mto nilio uegemezea kichwa.

    “Eddy madaktari wanasema maisha yako yapo hatarini kupotea....siku yoyote”

    Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi kwamba nikajikuta ninazidi kuchananyikiwa huku jasho likinimwagika

    “Eddy kumbe ulisha wahi kupigwa risasi kwanini hukuniambia hadi leo madaktari wameniambia kuwa kidonda chako cha risasi hakikupona kikamilifu na jinsi askari waliyo kupiga imesababisha damu kuvilia kwenye mapafu na kuanza kujenga uzo kwenye moyo wako”

    Nikazidi kuchanganyikiwa na kujikuta nikitokwa na machozi na kumzidisha Sheila kulia kwa uchungu

    “Sheila kwahiyo mimi ndio nitakufa?”

    “No Eddy huwezi kufa mume wangu.....usizungumze hivyo kumbuka wewe ndio mwanga wangu we....”

    Kabla Sheila hajamaliza kuzungumza akaiingia daktari mkuu na akasimama kwa muda akitutizama huku akwa ameshika kikaratasi mkononi mwake

    “Binti umemuambia?”

    Sheila akaitikia kwa kutingisha kichwa akimuashiria daktari kuwa ndio amenimbia

    “Binti nilikuambi usimuambie hii itamsababishia matatizo zaodi kwani moyo wake kwa sasa unaweza kushindwa kufanya kazi yake muda woote kuanzi sana na inaweza ikampelekea kifo”

    Sikujua daktari kama akili zake zimekamilika vizuri au laa kwa maana kitu anacho kizungumza mbele yangu kikazidi kunichanganya zaidi ya alivyo niambia Sheila na isitoshe amemkataza Sheila kuniambia kiitu kama hicho na yeye ndio anakizungumza.

    “Sasa hapa kuna karatasi unatakiwa usaini ili tukamfanyie upasuaji mume wako”

    “Ngoja kwanza dokta ni nani munataka kumfanyia upasuaji?”

    “Ni wewe kwani maisha yako yapo hatarini”

    “Nyinyi si ndio wale mulio mpasua mgonjwa wa mguu kichwa na wakichwa mguu”

    “Hilo sio jukumu lako na mimi ni mgani.....Binti siani kwa ajili ya kuyaokoa maisha ya mume wako na kama upo tayari kumpoteza basi itakuwa hivyo”

    Sheila alachukua katatasi mikononi mwa daktari na akaifungua na kabla hajaandika chpchote nikamuomba nanionyeshe ili nipitie na mimi.

    “CHOCHOTE KINAWEZA KUTOKEA IKIWEMO KIFO”

    Maandishi madogo yaliyomo kwenye karatasi yakanichanganya sana na kujikuta nikimtazama Sheila ambaye amaeshika peni mkomoni kwa kusaini kwa niaba yangu.Sheila akasaini na kumkabidhi daktari karatasi yake na daktari akatoka kwenye chumba

    “Eddy nakuomba ujikaze mume wangu”

    “Kwenye kufa Sheila hakuna kujikaza hawa madaktari mimi sina imani nao kabisa”

    “Usijali kwa hilo mume wangu”

    “Kwani hiyo oparesheni ninafanyiwa lini?”

    “Leo hii mida na yamebaki masaa kama mawili”

    “Sasa imekuwaje na wewe ukasaini pasipo kuniambia kama ninafanyiwa leo kwa maana hapo kwenye hiyo karatasi kumeandikwa chochote kinaweza kutokea ikiwamo kifo sasa unaona ni haki kweli?”

    “Eddy acha kupanic”

    “Sio kupanic......Wewe kwanini usaini si uneniambia kuwa yamebaki masaa mawili nisinge kubali kufanyiwa ningesubiria hadi mama apatiakene ili hata nikifa nife vizuri”

    “Eddy usitake unilize sasa hivi mume wangu hembu tulia madaktari wanajua ni nini wanafanya”

    Baada ya masaa wawili wakaingia amadaktari wawili akiwemo yule daktari wa familia akaonekana kushangaa kuniona ndani ya chumba,Hakunisemesha akatoka ndani ya chumba na sikumfwatilia sana kwani manesi walianza kuniandaa kwa kunpeleke kwenye chumba cha upasuji huku wakinibadilisha nguo na kunivisha vazi maalumu kwa ajili ya upasuaji.Wakamaliza na kuniweka kwenye kitanda cha matairi na kuanza kukidukuma huku Sheila akiwa pembeni yangu na machozi yakaanza kumwagika tena

    Nikastukia nikamuona daktri anaye sukuma kitanda akisukumwa na kuanguka chini na macho yangu yakakutana na macho ya baba yaliyojaa hasira hadi yakawa mekundu.Akanishika kifuani na kunivuta na kunitupa chini na kuanukia mgongo na kusababisha maumivu makali kuzidi kunitawala kwenye mwili wangu hususani kifuani mwangu.Madaktari wakataka kumsogelea baba ila akachomoa bastola yeka na kuwafanya madaktari kusita.Mguu wa baba ukatua kifuani kwangu huku ukiwa umevalia buti lake la jesi kisha bastola yake akaikoki tayari kwa kunifyatulia risasi





    Nikastukia baba akitoa ukulele na kuanguka chini na kumuona Sheila akiwa ameshika kipande cha mbao kinachoonekana kimechomolewa kwenye benchi huku kikiwa kinavuja damu kwenye sehemu ambayo ilitua kichwani mwa baba.Sheila akaanza kutetemeka baada ya kumuona baba akiwa anavujwa na damu za kichwa,Madaktari wakaninyanyua na kunirudisha kwenye kitanda huku hali yangu ikizidi kuwa mbaya na mamcho yangu yakaanza kutawaliwa na ukungu na kwambali nikamuona Sheila akishikwa na askari wawili na wakaanza kumtoa enje akiwa ananililia kwa uchungu.Kitanda nilicho kilalia kikaanza kusukumwa taratibu na jinsi ninavyo isililizia hali yangu yenye maumivu makali ya mwili nikajikuta macho yangu yakitawaliwa na ukungu mwingi na sikujua ni kitu gani kinacho endelea

    ***

    Baridi kali ikaanza kunisumbua mwili wangu na kujikuta nikianza kufumbua macho yangu na kujikuta nikitazama sehemu ya juu ambayo kwa haraka haraka sikujua nipo wapi.Mwili wangu ukawa umebanwa kidogo na na kwa haraka haraka nikagundua kuwa nipo kama nilivyo zaliwa kwani kiwamgo cha baridi kilitawala mwili wangu mzima,nikajariu kujigeuza ila nikajikuta nikishindwa na nikaanza kujisukuma na kumbukumbu za akili yangu ikagundua kuwa sehemu niliyopo ni katika majokofu ya kuhifadhia miili ya watu walio fariki dunia.Nikajaribu kuita ila sikusikia msaada wa mtu wa aina yoyote wala kitu kikitembea nje ya majokofu hayo,Nikazidi kujitahidi huku miguu yangu nikiigonga gonga kwenye sehemu ya chini ya jokofo ambapo ndipo miguu yangu ilipo elekea na kujikuta sehemu niliyo ilalia ikienda mbele na kufunguka.Nikaendelea kujikaza huku nikizisidi kujitahidi kujitoa ndani ya jokofu hili na chakumshukuru Mungu nikafanikiwa kulifunua kwa uwazi mdogo ulio niruhusu kuitoa mikono yangu kwa nje na kujivuta na likafunguka na kupata uwezo wa kukaa na kitako na kuanza kushangaa

    Woga ukaanza kunitawala na baada ya kujikuta nikiwa nimeshonwa katikati ya kifua changu na kitu kingine kilichoizidi kuniogopesha ni miili mingi ya watu walio lala chini huku wakiwa wamefunikwa malailoni yanayo waonyesha vizuri huku miili yao ikiwa imeharibiwa sana huku wengine vichwa vyao vikiwa vimepasukwa na kurudishiwa rudishiwa kiasi kwamba wanatisa kwa muonekano wao.Nikashuka kwenye jokofu nililo kuwepo na taratibu nikaanza kuutafuta mlango wa kutokea katika chumba hichi na kabla sijauona nikastukia taa za chumba zikizima na giza kali likazidi kutawala

    Nikajikaza na sikutaka kuuruhusu woga kutawala katika mwili wangu kwa wakati huu,Nikapapasa papasa ukutani kwa dakika zaidi ya mbili na kufanikiwa kukuta mlango na kabla sijaufungua nikasikia watu wakizunumza kwa nje

    “Muambie huyo Mudi awashe hilo genereta la upande huu kuna maiti tunataka kuziingiza humu”

    “Kwani hao nao wametokea wapi?”

    “Kuna basi limeanguka na kuua watu ishirini”

    “Sasa huku ndani si kumejaa hadi maiti nyingine tumeziweka chini tutafuta ustaarabu wa kuwatoa kesho wakazikwe na manispaa kwa maana hata ndugu zao hawajitokezi”

    “Hawa tutawaweka hivyo hiyo bwana kwani hatuna seemu nyingine ya kwenda kuwaweka na hospitali zote za wilaya mochwari zao ni ndogo”

    Watu waliopo nje wakaendelea kujibishana nikataka kupiga kelele za kuomba msaada ila roho yangu ikasita na kujua ni lazima watu waliopo nje wataogopa na kukimbia na ningelisitisha zoezi zima la wao kuingiza maiti wanazo zizungumzia,Taa zikawaka na mlango nikausikia ukifunguliwa na baada ya dakika kakika moja mlango ukafunguliwa

    “Hembu shika huko vizuri usije ukamuachia”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gafla umeme ukakatika na kuwafanya watu walio ibeba maiti wanayo taka kuuingiza kuanza kutukana matusi mazito na kwakupitia uwazi mdogo wa mlango nikastukia kuona wakiondoka kwa hasira huku maiti wakiwa wameilaza chini na sikujua ni wapi wanapo elekea,Nikachungulia nje na kukuta kuna giza ila mwanga wa mbalamwezi uliweza kunisaidia kuona baadhi ya majengo na kungundua bado nipo sehemu ya Muhimbili.Nikaanza kuoiga hatua za haraka na kutoka ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti na nikafika kwenye jengo ambalo nikakuta kamba nyingi zikiwa zimeanikwa makoti meupe ya madaktari.Nikalishusha moja kwenye kamba na kulivaa kwa haraka kisha nikachukua suruali nyepe na kuivaa na muonekanao wangu ukawa kama wauduzi wa kiume kwenye hospitali hii.Nikaanza kutembea kuelekea getini huku miguuni nikiwa nipo peku peku na nikafanikiwa kutoka pasipo walinzi kunitilia mashaka ya aina yoyote.Nikatafuta sehemu na kukaa huku akili yanu ikianza kufikiria ni kitu gani kilicho wafanya madaktari hadi wakanipeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.Nikajikuta nimejishika tama na kugundua mashavu yangu yamejaa ndevu nyingi na kwaharaka haraka nikagundua ni kipindi kirefu nimekaa hospitali kwani ndevu zangu huchukua muda mwingi sana katika kuota na kuwa ndefu kama nilivyo zikuta sas

    Nikapata wazo la kwenda nyumbani kwa Sheila japo ni mbali sana na sehemu niliyopo nikaona sina budi kufanya hivyo.Nikapiga moyo konde na kunyanyuka sehemu niliyo kaa na kuanza kutembea japo njaa kali inanisumbua tomboni kwangu ila nikajitahidi kwenda kutembea kwa haraka ili niweze kufika,Nikatumia kama masaa mawili na kufika nyumbani kwake na kukuta ukimya mwingi ukiwa umetawala ila kitu kingine kilicho anza kunipa wasiwasi ni nyasi nyingi na ndefu zilizo oto nje ya geti lake na kwaharaka nikajua Sheila hayupo ndani ya nyumba yake kwa maana kama angekuwepo kusingekuwa na nyasi nyingi huku geti lake likiwa lemetawaliwa na vumbi jingi.Ikanibidi kuchungulia kwenye eti lake ili kujionea mwenyewe nikipingana na mawazo yagu ya kusema Sheila hayupo ndani ya nyumba yake.Giza lilitawala kwenye nyumba yake na hapakuwa na dalili yoyote ya mtu kushi na jinsi mlango tulivyo ufunga siku ya mwisho ndivyo jini ulivyo kwa sasa.Nikashusha pumzi nyingi huku nikitazama wapi nielekee na mbaya zaidi sikua na jirani yoyote wa Sheila ninaye mjua ambaye ninaweza kumuulizia habari za Sheila

    Hali ya uchunu ikaanza kunitawala na kwa mbali machozi yakaanza kunilenga lenga na kujikuta nikitamani utokee muujiza Sheila kusimama mbele yangu,Wazo la kuwa na mama likaanza kunijia ila kutokana na kuchoka nikashidwa kujua kama nitaweza kwenda nyumbani ambapo tulikuwa tunaishi ila woga ukaanza kunijia kwani kumbukumbu ya baba siku alivyokuwa akinipiga ikanijika kichwani kama mkanda wa video ila ukakata gafla baada ya kusikia mnguruo wa mbwa ukitoka nyuma yangu.Nikageuka na kukutana na mbwa wakubwa wawili wakiwa wananguruma huku wakinitazama kwa macho yao makali kiasi kwamba nikajikuta nikiaanza kutetemeka.Nikatulia kwa muda huku mwili wangu ukishindwa kukimbia kabisa kutokana na njaa kali iliyopelekea nguvu za mwili wangu kuniiishia.Nikasikia mlunzi wa mtu akiwaita mbwa walio karibu yangu na wakaelekea walipo itwa na kumuona mlinzi wa nyumba ya jirani akiwa amesimama huku mbwa wake wakiwa wamenzunguka na mkononi mwake akiwa ameshika bunduki yake aina ya gobore

    “Samahani kaka”

    Nilimuita mlinzi kwa sauti ya kukwaruza kwaruza huku nikianza kupiga hatua za taratibu za kumfwata sehemu alipo na kabla sijamfikia akaikoki bunduki yake na kunielekezea

    “Usipige atua nyingine ya kunfwata la sivyo nitakulipua”

    Nikasimama huku nikiwa ninamwangalia mlinzi na sikua na cha kufanya zaidi ya kuwa mnyonge mbele ya mlinzi huyo

    “Samahani kaka yangu kuna kitu ninaomba nikuulize”

    “Uliza fasta fasta”

    “Eti huyu dada aliyekuwa akiishi humu ndani yupo wapi?”

    “Kwani wewe ni nani yeke?”

    “Mimi nilikuwa ni mchumba wake?”

    “Unaudhibitisho gani kwamba wewe ulikuwa ni mchumba wake?”

    “Ninaweza kukutajia jina lake”

    “Anaitwa nani?”

    “Sheila”

    “Sasa wewe itakuwaje usijue habari za mchumba wako?”

    “Ni hstoria ndefu ndugu yangu”

    “Sasa kwa ufupi huyo demu yupo jela”

    “JELAA.....!!!?”

    “Unashangaa nini sasa.........? Wewe si ulitaka kujua ni wapi alipo huyo demu?”

    “Jela gani?”

    “Sijui yupo gereza gani ila ukweli ni kwamba amefungwa”

    “Amefungwa kwa kosa gani?”

    “Kaka mimi sio hakimu bwana kama unataka nenda Kisutu kaulizie watakuambia”

    Wasiwasi ukaanza kunijaa mwilini mwangu na kujikuta chozi likinitoka na sikutaka nilie mbele ya mlinzi

    “Kwani leo ni tarehe ngapi?”

    “Wewe jamaa umevurugwa na nini hata tarehe umesahau?”

    “Naoma tu nijue ndugu yangu”

    “Ni terehe 15 mwezi wa sita haya hadi mwezi niemkutajia unaweza ukachapa lapa kwani bosi wanu akitoka hapa akikuta ninazungumza na watu kibarua changu kinaweza kikaota mbawa bure”

    Nikajikuta nikizidi kufadhaika kwani nimiezi mine imepita tangu nilipo kutana na tatizo la kupigwa na walinzi wa uwanja wa ndage.Nikaondoka kinyone huku nikitazama tazama nyuma nikitamani nimueleze mlinzi njaa ninayo ihisi tumboni kwangu hata kama anaweza kunipatia chakula kidogo ila nikashindwa kwani tayari alishapandwa na hasira.Nikaendelea kutembea huku sijui ninapo elekea kwani mawazo mengi yanakizungusha kichwa changu kiasi kwamba ninajikuta nikiongea ongea mwenyewe.Nikakuta watu wapatao sita wakiwa wamelala kwenye maboksi nje ya baraza za maduka mengi na kujikuna mimi nikikaa kwenye moja ya baraza ambayo ukuta wake umechorwa picha za wasichana na kugundua ni saloon ya wanawake.Usingizi haukuweza kunijia na kila nilipo jaribu kuutafuta nikajikuta nikijipiga piga mwilini kuwaua mbu wanao ning’ata mwilini mwanu.Hadi kunaanza kupambazuka nikajikuta nikipitiwa a kausingizi kazito na kujikuta nikilala kwenye sakafu pembezoni mwa geti la salooni hii ya kike

    Nikastukia mguu ukinigonga gonga begani nikayafumbua macho yangu na kukuta mwanga wa jua ukiwa uemshatawala eneo zima,Macho yangu yakakutana na msichana mrembo akiwa amevalia suruali nyeupe iliyo mbana vizuri na kuyafanya makalio yake makubwa kuonekana vizuri huku sura yake akiwa ameipamba kwa vipodozi vinavyo onekana ni vyagharama.Mkononi mwake akawa amezishika funguo nyingi na tukabaki tumetazamana

    “Unanianaliangalia nini hembu nyanyua mindevu yako nahitaji kufnugua geti langu”

    Nikanyanyuka na kusogea na kukaa pembeni kidogo,akafungua geti lake la saloon na kuingia ndani na kuanza kupana vitu vyake.Watu wengi wanapita mbele ya macho yangu huku kila mmoja akionekana kuwa na mihangaiko yake ya kutafuta chochote kwa siku hii.Nikapiga miyayo ya uchovu na kusimama ila nikashindwa kupiga hatau yoyote kutokana na kuchoka sana,Nikakaa chini na kuanza kutafakari ni nini nifanye ili kuweza kupata hata kifungua kinywa nikachungulia ndani ya saloon na kumuona dada wa saloon akiendelea kufanya usafi.

    “Samahani dada ninaweza kukusaidia japo kufagia fangia”

    “Kwani nilikuomba unisaidie?”

    “Hapana ila nimeomba tuu kama ninaweza kukusaidia”

    “Usije ukawa kibaka ukaniibia vitu vyangU humu ndani”

    “Hapana dada mimi sio kibaka”

    “Haya njoo unipigie deki”

    Nikanyanyuka huku nikiwa na fauraha kidogo ya kuweza kupata chochote cha kula,akanipa tambara la deki pamoja na kindoo chenye maji kidogo na nikaanza kupiga deki taratibu huku nikijitahidi kusafisha kila sehemu ya salooni hiyo.Nikamaliza na kupiga deki kwenye eneo zima la Saloon

    “Tayari dada yangu”

    “Haya asante”

    “Dada yangu naomba japo kajipesa nikanunue kifungua kinywa”

    “Haaa kumbe ulikuwa unapiga deki ili nikulipe.......? Mimi nilidhani umenisaidia bure”

    “Hapana mimi ninaomba japo kidogo tu niweze kupata kifungua kinywa”

    Dada akafungua pochi yake na kutoa shilingi mia mbili na kunipa nikabaki nikiitazama kwa sekuende kadhaa pasipo kusema chochote na kwajinsi ya ugumu wa maisha ya Dar es Saalam yalivyo magumu kwa shilingi mia mbili siwezi kupata chochote nitakacho weza kula.

    “Dada yagnu huwezi kuniongeza japo mia tatu ili iwe mia tani niweze kupata chochote tuu”

    “Kaka yanu hiyo ndio hela niliyo nayo na kama unataka kifungua kinywa jana niliacha kiporo cha ubwabwa wa mchana unaweza kufungua hilo hotpot hapo juu ya meza utakiona chakula”

    Sikuwa na jinsi nikalisoelea hotpot alilo nelekeza na kulifungua na kukutana na harufu kali ya ubwabwa ulio chacha ambao umepikwa na nazi huku ukiwa na maharage yake.Nikakitaama kwa muda kisha nikaanza kukila haraka haraka na kunya dada wa Saloon akibaki akiwa ananitazama kwa macho ya mshangao.Ubwabwa ukaanza kuniongea ila nikajikuta ukiwa unaelekea ukingoni kwani niliufakamia fakamia kwa haraka,nikajilamba vidole vyangu kwa utamu nilio upata kisha nikasima na kunawa mikono yangu kwa maji niliyo pigia deki

    “Asante dada yangu”

    Dada wa Saloon akabaki akiwa amenitazama huku akikiangalia kifua changu na kugundua kuwa anatakuwa amestushwa na mstari wa oparesheni niliyo fanyiwa

    “Nakuomba utoke ndani ya Saloon yangu kabla sijakuitia polisi kwani unaonekana wewe ni jambazi”

    “Kwa nini?”

    “Usitake kujua kwa nini au unataka nikupigie kelele za mwizi?”

    Sikutaka makuu ya kubisha na dada wa Saloon nikaondoka huku nikiwa ninajisikia vibaya kwa jinsi maisha yangu yalivyo badilika.Nikaondokoka na kuelekea nyumbani kwetu huku nikijifariji liwalo na liwe.Nikiwa njiani nikajiku nikisimama na baadhi ya watu wanaosoma magazeti kwenye kibanda kidogo na gazeti moja lina pichwa kubwa ya Sheila huku pembeni yake kukiwa na kitanzi na juu yake kukiwa na maandishi makubwa yaliyo nistua na kujikuna nikianza kutetemeka yanayo someka

    “MUUAJI WA MTOTO WA WAZIRI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA KUNYONGWA HADI KUFA”



    “Haaa...!!”

    Nilishanga kwa sauti ya juu na kuwafanya watu walipo pembeni yangu kunishangaa kiasi kwamba nikajikuta nikitazamana nao huku wakinishangaa,Nikataka kuondoka ila dada muuza magazeti akaniita na kunifanya nirudi sehemu alipo

    “Kaka nahisi nimesha wahi kukuona sehemu?”

    “Labda utakuwa unanifananisha”

    “Hapana wewe ndio Eddy?”

    Moyo ukanistuka na kujikuta nikitaka kukimbia ila miguu ikaishiwa ujasiri wa kufanya hivyo na kujikuta nikianza kutetemeka.

    “Huyu si ndio jamaa aliyesemekana kuwa ameuliwa?”

    “Ndio huyu”

    Watu wakaanza kubishana mmoja baada ya mwengine huku kila mmoja akionekana kunishangaa hadi wakanizunguka

    “Jamani muacheni kaka wa watu aondoke munamshangaa hadi anajisikia vibaya”

    “Sasa si tunataka kujua ni nini kilicho mpata”

    “Jamani hembu acheni wanga mimi ndio nimemuita sasa kila mmoja akiwa anataka kujua ni nini kilicho mpata kaka wa watu ni umbea”

    Watu wakaendelea kubishana wenyewe kwa wenyewe na dada mwenye kibanda cha kuuza magazeti akanishika mkono na kunivuta pembeni na tukaingia kwenye moja ya duka lililopo pembei ya kibanda hicho na kumuomba muhisika wa duka hilo kutupa nafasi kidogo ya kuzungumza na muuza duka hakuwa na lakupinga akatupatia viti viwili na tukakaa

    “Najua utajiuliza ni kwani ni nimekutoa kule kukuleta huku ila ngoja kwani nijitambulishe....Mimi ninaitwa Judith na nimuuza maazeti pale kwenye kibanda ndio ofisini kwangu na mimi nimekuwa ni msomaji mkubwa sana wa stori ianyo endelea sasa kwa huyu dada Sheila kumuua mtoto wa waziri hadi jana alipo hukumiwa kunyongwa hadi kufa”

    “Ina maana Sheila ndio ameniua mimi?”

    “Kaka yangu mimi wala sijajua kama huyo dada ndio muhusika ila kwa msaada ngoja nimpiie mchumba wangu ambeye ndio muandishi wa habari yako aje hapa tujuae ukweli”

    Judidh akatoa simu yake na kumpigia mtu aliye dai ni mpenzi wake na baada ya muda jamaa akafika sehemu tulipo akitumia usafiri wa pipipiki aina ya boxer.Judith akampisha mpenzi wake kwenye kiti alicho kaa na yeye akasimama pembeni na jamaa akanipa mkono huku akionekana kunishangaa kwa jinsi nilivyo

    “Mimi ninaitwa John ni muandishi wa habari wa gazeti”

    “Nashukuru kukufahamu”

    Judidh wakabaki wakiwa wametazamana pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote kisha John akakohoa kidogo huku akiaachia tabasamu pana mdomoni mwake na kuanza kuzungumza

    “Kaka mimi ni miongoni mwa watu walio tokea kuguswa na tukio lako la kusemekana kuwa umekufa ila nikaamua kulifwatilia kina ubaga hadi sasa hivi ninaanza kupata picha ambayo itaweza kumsaidia mpenzi mpenzi wako katika kuachiwa huru.......Nilizungumza na Sheila akanielezea kisa kizima na alidai kuwa ameonewa kwa maana tangu siku ambayo wewe ulipelekwa katika chumba cha kufanyiwa oparsheni ndio siku ya yeye alipo kamatwa na polisi kwanza akashikiliwa kwa kosa la kutaka kumuua mkuu wa jeshi ila kutoka na ushaidi kutoka kwa manesi na madaktari ukamsaidia sana Sheila kuishinda kesi ya kumjerehi baba yako ambaye alitaka kukuua hadharani”

    “Ina maana baba yangu yupo hai?”

    “Ndio yupo hai na nimiongoni mwa watu walio nipa vitishi endapo nitaendelea kulifwatilia hili swala.......”

    “Mama yangu je yupo hai?”

    “Mama nilipata habari kuwa amelazwa nchini Afrika kusini kwani alipata ugonjwa wa mstuko wa moyo na hadi sasa hivi sijajua anaendeleaje”

    Nikashusha pumzi nyingi huku nikijaribau kusubiria ni nini kilitokea katika maisha yangu ila sikupata pichaya aina yoyote

    “Ishu ilikuwa hivi.......Alitengenezwa mtu anaye fanana na Sheila na kwakupitia picha rada zilizopo hospitali alionekana akitoka kwenye chumba ulichokuwa umelazwa huku akiwa ameshika sindano mkononi na kwamadai ya madaktari wakasema kuwa msichana huyo ndio amehusika kwa kukuchoma sindano ya sumu iliyo pelekea maisha yako kuwa mwisho”

    “Ngoja kwanza unataka kuniambia kuwa Sheila yeye hakuuhusika na chochote?”

    “Ndio Sheila hajausika na kiyu cha aina yoyote juu ya kukuchoma sindaono kwa maana kipindi tukio la wewe kuchomwa sindano linatokea Sheila alikuwa mikononi mwa polisi na hadi sasa hivi ninavyo zungumza Sheila ndio huyo siku zake zina hesabika”

    “Huyo daktari aliye dhibisha kuwa nimechomwa sindano ya sumu ni yupi huyo?”

    “Ngoja nikuonyeshe”

    John akatoa simu yake na kuwela upende wa video na nikamuona daktari wa familia akiwa anazungumza kwa masikitiko makubwa na mbele ya waandishi wa habari na kunifanya nibaki mdomo wazi

    “Sasa huyu mzee ndio mbaya wenu katika hii familia?”

    “Kwa nini?”

    “Yeye ndio chanzo kikubwa cha baba yako na mama yako katika kugombana?”

    “Wewe umejuaje?”

    “Mimi nilimuhoji siku akiwa amelewa sana kwa maana huyu mzee ni mjomba wangu na akanieleza vitu vingi sana juu ya familia yako”

    “Vitu gani?”

    “Kwanza yeye ndie aliye muambia baba yako kuwa wewe sio mtoto wake wa kumzaa na kitu kikubwa kilicho msababisha baba yako kuchukua uamuzi wa kutaka kumuua mama yako pamoja na wewe ili kuweza kuzirisi mali zote ambazo mama yako anazo”

    “Mmmm sasa mimi mbona ninafanana sana na baba yangu?”

    “Ndio kutokana baba yako ana pacha wake ambaye ni doto na yeye ndio baba yako wa damu na wao wanafanana sana kiasi kwamba ni vigumu sana kwa mtu kuweza kutambua kuwa wewe baba yako si huyo mkuu wa jeshi”

    Ni habari mpya katika maisha yangu kwani mama yangu hakuweza kuniambia siku hata moja kuwa baba yangu ni pacha wa baba yangu wa sasa ambaye amejenga chuki kubwa juu yangu na mama yangu,Nikajikuta machozi yakianza kunimwagika

    “Kaka jikaze usilie ila huo ni ukweli ambao mimi ninakuambia na huyu daktari mimi ni mtu wangu wa karibu ukiachilia kuwa ni mjomba wangu ila ni zaidi ya hapo kwani vitu vyake vingi huniambia kiasi kwamba vingine siwezi kuvizungumza hapa........Ila ninakuomba sasa hivi tukajaribu kuyaokoa maisha Sheila ambeye niliapa kumsaidi Sheila hadi mwisho wa maisha yake tana kuna hii sauti niliirekodi kipindi anazungumza kwa uchungu na mimi”

    ‘NI KWELI SIJAMUUA EDDY WANGU MIMI NINAMPENDA SANA NA YEYE NDIO MWANAUME WA NDOTO ZANGU.....MIMI NIPO RADHI KUFA KWA AJILI YA MUME WANGU EDDY NIKAONANE NAYE PEPONI KWA MUNGU.....JOHN NAKUOMBA USIJISUMBUE SANA KWA AJILI YANGU KWANI MIMI HUU NDIO MWISHO WA MAISHA YANGU”

    “HAPANA SHEILA USILIE MIMI NIPO TAYARI KUKUSAIDIA KUUVUMBUA UKWELI JUU YA HILI KWANI SIAMINI KAMA WEWE NDIO MUUAJI”

    “HAPANA JOHN WEWE NIACHE TU NIKAFUNGWE SINA JINSI YA KUFANYA NA HUU NDIO MWISHO WA MAISHA YANGU BAI JOHN”

    John akazima simu yake baada ya kuniona ninazidi kutokwa na mahozi mengi na akaniomba nikaze twende tupate msaada wa mwana sheria wa serikali.Tukasimama na John na kutoka nje ya duka huku sura yangu nikiwa nimeiinamisha chini ili watu wasiyaone machozi yangu,Tuakapanda kwenye pikipiki yake na moja kwa moja tukaelekea kwenye mahakama ya Kisutu na John akanipeleka kwenye ofisi za mwanasheria wa serikali aliye simamamia kesi ya kuhukumiwa kwa Sheila na kitendo cha kuingia kwenye ofisi yake kikamfanya mwana sheria huyu kustuka kiasi kwamba akanyanyuka na kubaki akinitazama

    “Mkuu samahani kwa kukuingilia ofisini kwako pasipo kuwa na taarifa maalumu ila kama unavyo one mbele yako nimekuja na Eddy ambaye inasadikika ni mfu”

    Mwanaheria wa serikali akabaki amesimama pasipo kujibu kitu cha aina yoyote na kubaki akibabaika pasipo kujibu kitu cha iana yoyote

    “Mkuu tunahitaji msaada wako wa hali na mali”

    “Ehhee umesema amefufuka?”

    “Hilo mimi sijui atasema mwenyewe kwamba amefufuka ila kidhibitisho ni kwamba Eddy mwenyewe huyu hapa na hajafa kama mulivyo mdhania ila ninakuomba uweze kutusaidi kuhairisha mauaji ya Sheila”

    “Dooo watakuwa wanakaribia kumua kwani zimebaki dakika 45 tu kabla hajanyongwa”

    Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi kwamba nikajikuta nikanza kuzunguka zunguka ndani ya ofisi ya mwanasheria wa serikali na kuwaacha John na mwanasheria wa serikali wakizungumza

    “Tunakuomba sana uweze kutausaidi kama tunaweza kwenda kumuona”

    “Ahaa sasa hiyo ni ngumu kwa maana amesha kabidhiwa kwa askari maalamu wana shuhulika na hilo swala kwa hiyo mimi siwezi kwenda”

    “Nipo chini ya miguu yako kiongozi ninakuomba twende au tuambie tu niwapi alipo”

    “Kwa hilo mimi siwezi kuzungumza chochote juu ya hilo”

    John akapia maoti huku sura yeke ikiwa ina mwagikwa na machozi na ila mwasheria akaanza kutingisha kichwa cheke akishiria hataki kukubaliana na kile anacho obwa na John.Kwa hasira nikapiga hatua hadi sehemu aliyo simama mwanasheria wa serikali na kumvuta tai yake na kumsogeza karibu na sura yangu iliyo jaa ndavu nyingi na nikamuangalia jocho kali kiasi kwamba akabaki akiwa ananitazama kiwoga

    “UNAKWENDA AU HUENDI?”

    “Mmmmm”

    Nikaishika shingo ya mwanasheria mkuu na kuinamisha kwenye meza yake kwa hasira na kwa haraka nikachukua peni iliyopo kwenye meza na kuishusha kwa kasi hadi kwenye shabu lake na kuanza kuigandamiza kwa kwa nguvu huku mwili mzima ukiwa unanitetemeka kwa hasira

    “Nakwenda nakwenda......”

    Mwanasheria mkuu alizungumza huku akitoa ukelele wa kulia,nikamnyanyua na kumuamrisha kutangulia mbele huku nikiwa ninamfwata nyumba huku nikiwa karibu yake sana endapo atajaribu kukimbia tu ningemfanya kitu ambacho asinge kisahau kwenye maisha yeke.Kila tulipo pita watu walinishangaa na hatua chache kabla mwanasheria wa serikali hatujafika kwenye maegecho ya magari akachomoka kwa kasi akikimbia kitendo kilichonifanya na mimi kukimbia kwa kasi zaidi yake na uzuri wenyewe yeye ni mnene na anakitambi likubwa

    Kwa nguvu zungu zote nikarusha teke lililo mpiga kwenye miguu yake kwa nyuma na kumfanya aanguke kama mzigo wa kuni na akaangukia pua kitendo kiliho shuhudiwa na watu wengi ikiwemo askari walio anza kukimbia wakija kwenye eneo tulilopo huku bunduki zao zikiwa mikononi mwao huku wakinimrisha nisifanye kitu cha iana yoyote na John akabaki akiwa haamini kitu alicho kiona

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikamnyanyua mwanasheria wa serikali na kumuamrisha kuelekea lilipo gari lake na askari walio kuwa wakinifwata wakajikuta wakisimama huku wakionekana kunishangaa.Ila mmoja wao akanifwata akiwa na bunduki yake na kumbukumbu zikanikumbusha kuwa ni askari wa getini ambaye mara ya mwisho alinisaidia katika kotoroka mikononi mwa baba

    “Eddy vipi tena?”

    “Safi”

    Nilizungumza huku nikumuongoza mwanasheria hadi kwenye gari lake nikamuomba funguo yake kilazima na akaitoa kabla sijaingia kwenye gari nikastukia nikiguswa bega na nikageuka nikakutana na sura ya askari wa getini

    “Kaka Eddy huyo mkuu ana nini?”

    “Si unamkumbuka yule binti niliye kuwa naye siku ile tulivyo kuwa tunatoroka home?”

    “Ndio si amehukumiwa kifuno cha maisha tayari?”

    “Ndio ila kwa kosa la kuonewa sasa ndio huyu fala ninamuomba anipeleke alipo anakazi ya kunizingua hapa”

    “Ahaa mimi ninapajua tunaweza kwenda pamoja”

    Tukaingia ndani ya gari na kumkabidhi askari wetu wa getini funguo ya gari na safari ikaanza.Kitu ambacho ninakishukuru kutoka kwa askari wetu wa getini ni kuwa mtu muelewa japo ni askari wa jeshi la polisi ila mama alipendekaza kuwa askari wa kuilinda nyumba yetu kutokana na upole na hekima aliyo nayo ni tofauti na maaskari wengine ambao wana dharau kiasi kwamba mtu unashindwa kuwadhamini katika maisha

    “Kaka Eddy unajua hata mimi niliamini kuwa umefariki dunia?”

    “Sijakufa ndugu yangu ila wee acha tuu”

    “Basi unajua habari za kifo chako zilinistua kiasi kwamba nikawa nipo njia panda kwa maana yule binti kwa muonekano anaonekana anakupenda kiasi kwamba hasikii la mtu juu yako sasa sikuelewa nilipo ambiwa kuwa amesababisha kifo chako”

    “Najua zote ni mbinu za mzee ila zitafikia mwisho”

    “JAMANI NINAOMBA MUNISIKILIZE”

    Mwanasheria wa serikali alizungumza na kutufanya sote tukae kimya na kumsikila kitu anacho taka kutuambia

    “Jamani ukweli ni kwamba Sheila hajanyongwa japo mahakama ilitoa hukumu ya namna hiyo”

    Sote tukajikuta tukiguna kila mmoja kwa mtindo anao ujua yeye mwenyewe kiasi kwamba tukabaki tukimsikilizia kitua atakacho kizungumza

    “Ukweli ni kwamba Mr Godwin alitokea kumpenda yule binti na akahitaji tuweze kumhukumu hivyo ila yeye amepanga safari ya kwenda naye kuishi visiwa vya Komoro na hapa ninavyo zungumza amenitumia meseji akidai yupo uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kuelekea visiwa vya Comoro”

    Nikajihisi nguvu za mwili zikiniiishia kiasi kwamba nikabaki nikiwa kimya nisijue nini cha kufanya na hasira kali dhidi ya baba yangu ikanipanda na kujikuta nikinyang’ata meno yangu kiasi kwamba sauti ya msuguano wake ikasikika kwa kila mtu.

    “Muheshimiwa amekuambia kuwa anaondoka na ndege ya saa ngapi?”

    “Ngoja niwaonyeshe meseji aliyo nitumia”

    Mwanasheria akatoa meseji aliyo tumiwa na baba na kuanza kumuonyesha John ambaye nikamshuhudia akishusha pumzi nyingi kiasi kwamba akionekana kuchoka na kile alicho kisoma na kabla hajamuonyesha askari wetu wa getini nikampokonya simu na kuisoma meseji iliyopo kwenye simu yake

    {MR KILONGO MIMI NIPO NIPO UWANJA WA NDEGE NINAELEKEA VISIWA VYA COMORO KULA RAHA NA HUYU MTOTO,JANA NIMEMUONJA NI MTAMU SANA.ILE PESA NIMEKUINGIZIA KWENYE AKAUNTI YAKO ASANTE KWA KAZI NZURI ULIYO IFANYA NA HAKIKISHA UNAMALIZIA JUHUDI ZA KUZIBINAFSISHA MALI ZA MKE WANGU NITAKUPA ROBO YA UTAJIRI WANGU}

    Nikabaki nikiwa ninatetemeka kwa hasira kiasi kwamba nikajihisi michuruziko ikinitoka puani kwangu na matone baadhi yakadondoka kwenye mapaja juu ya nguo za wauguzi nilizo zivaa na kugundua kuwa ni damu ndio zimenitoka puani na sikujua zimesababishwa na nini kwani ndio mara yangu ya kwanza kutokwa na damu za puani.John akanipa kiatambaa chake na kujifuta damu zinazo nitoka na askari akasimamisha gari pembeni ya barabara na wakaniomba nishuke nipigwe na upepo wa wa halisi kulilo IC iliyo tawala ndani ya gari

    Nikashuka na kuinama chini na damu zikanitoka kidogo na chakumshukuru Mungu zikakata japo kichwa nikaanza kukihisi kikiwa kimetaliwa na maumivu makali

    “Unajisikiaje?”

    “Kichwa kidogo kina gonga”

    “Noja tukakutafutie dawa”

    ”Hapana twendeni air port”

    “Utaweza kweli Eddy?”

    “John usijali kwa hilo nitaweza tu”

    Tukaingia ndani ya gari na safari ikaanza upya na kwawakati huu tukaelekea uwanja wa ndege na hatukuwa na uhakika sana kama tunaweza kuwaona baba na Sheila au laa.Tukafika uwanja wa ndege na sote tukashuka kwenye gari na mimi nikawa wa kwanza kuelekea sehemu ya abiria na nikajitahidi kuyapa wepesi macho yangu katika kuwatazama watu wengi waliopo kwenye eneo hili ili niweze kuwaona baba na Sheila ila juhudi zangu zikagonga mwamba kwani sikuweza kuwaona.Kwa kupitia kioo kikubwa kinacho onyesha sehemu ndege zilipo simama na kuwashuhudia baba akiwa amemshika Sheila kiuno wakimalizi ngazi ya mwisho kuingia ndani ya ndege na kunifanya niaze kumuita Sheila huku mkono wangu mmoja ukipiga kioo ila hawakuweza kunisikia na kuwafanya askari waliopo uwanja wa ndege kunishika na kunizui kitendo kilicho nifanya machozi kunimwagika kiasi kwamba nikaanza kupata maumivu ya kiua

    John na askari wa nyumbani kwetu wakanichukua na nikaishuhudia ndege waliyo panda Sheila na baba ikiacha ardhi na kupaa angani na kunifanya nishiwe nguvu na kujikuta nikianguaka chini.John na weza watu wengine wakaninyanyua na sikujua ni wapi wananipeleka na kujikuta nikiwa kwenye kitanda cha matairi na kuingizwa ndani ya gari ya wagonjwa na kupelekwa hospitali.Madaktari wakaanza kunifanyia uchunguzi na wakanichoma sindano ambayo sikujua inakazi gani mwili mwangu

    Ndani ya madaa matano madaktari wanipa ruhusa ya kutoka huku wakiwa wamenifungushia na baadhi ya vidonge vya kunywa pale nitakapo tokwa na damu kwani waliniambia chanzo cha damu kunitoka puani ni kutokana na kuwaza sana kiasi kwamba mishipa yangu inayopandisha damu kichwani husindwa kufanya kazi vizuri.Askari wetu wa getini akanipeleka nyumbani kwake ambapo anaiishi peke yake kwenye chumba kimoja alicho pangisha maeneo ya mbagala rangi tatu.Na tukafika kweye nyumba iliyo jaa wasichana wengi ambao kitendo cha sisi kupita mbela yao wakaanza kunong’onezana na kucheka kwa kicheko kikubwa

    “Eddy wazoee ndivyo walivyo hawa wanawake humu ndani?”

    Askari wetu wa gatini alizungumza na sikumjibu kitu cha aina yoyote na sote tukaingia ndani ya chumba chake alicho kihaza viti vingi vya dhamani

    “Eddy jisikie huru ndugu yangu”

    “Asante”

    “Hapa ninaishi peke yangu ila ni mara chache mke wangu anakuja kutokana yupo masomoni Arusha”

    “Ni mwanafunzi wa sekondari au chuo?”

    “Ni mwanafunzi wa sekondari yupo shule moja hivi ya bodi na miezi minne ya nyuma wamechoma shule yao ila wazazi wake wamempeleka shule ya wasichana Iringa”

    “Ahaaa anaitwa nani?”

    “Salome Alex Edward”

    Moyo ukanipasuka na kujikuta nikimtaza askari wetu wa getini kwani Salome anaye mzungumzia ni yule miongoni mwa wapenzi wangu japo mimi na yeye tumeachana kwa katika mazingira ya kutatanisha na mbaya zaidi ametembea na mkuu wa shule na ameambukizwa virusi vya ukimwi.

    “Yule dogo ninampenda sana hadi imefiki hatua mimi ninamlipia ada ya Advance”

    “Yupo kidato cha ngapi?”

    “Kidato cha tano japo sasa hivi anadani kuwa nimuache asome ndio tutaendelea na mapenzi imenilazimu nimsomeshe kwani familia yake ni duni sana”

    “Mmmm pole sana ndugu yangu”

    “Kwa nini unanipa pole”

    “Jukumu la kumsomesha mtu ni kubwa sana na ikitegema ndio hivyo wazazi wake hawajiwezi kiuchumi”

    “Ndio ndugu yangu si unajua mwanaume unatakiwa kujikaza na tumeubwa kupambana na ile pesa uliyonipatia kidogo ilinisaidia kumlipia ada na matibabu hospitalini”

    “Alikuwa anaumwa na ugonjwa gwani?”

    “Waliniambia kuwa ni mstuko wa moyo”

    “Ahaa ndugu yangu hongera sana”

    “Asante ndugu yangu”

    John akanionyesha nguo za kuvaa nikitoka kuoga kutokana ni uswahilini ikanilazimu kutoka na kindoo cha kuogea huku nikiwa nimeshika kopo lenye sabuni na John akanionyesha bomba la maji na nikakuta kuna kindoo kimekigwa ikanilazimu kusubiri kwa muda na kuna wamama wawili wapo pembeni wanapika vyakula vyao kwa ajili ya jioni wakaanza kunong’onezana taratibu

    “Eheeee OSAMA BIN LADEN ameingia mbagala jamani....mabomo yasije yakalipuka tena”

    “Shosti sema wewe Obama nikisema mimi Bush nitaambiwa ninakiherehere”

    “Mmmm na hayo mandevu sasa unaweza kusema kama kama paka aliye mwagikiwa na mchuzi wa moto”

    Moja kwa moja nikajua wananisema mimi kotokana na jinsi nilivyo na ndavu nyingi ambazo zimenifanya kuonekana na sura ya kutisha.Nikabaki nikiwa nimewatazama kwa jicho la hasira mpaka wakajistukia.Nikaona nikiendelea kusimama katika bomba watanikera zaidi na nilicho kifanya ni kuyamimina maji yaliyopo kwenye kindoo nilicho kikuta na kuyaweka kwenye ndoo yangu na kabla sijaondoka mama mmoja akasimama na kunifwata kwa haraka huku akubwatuka

    “Wee wee usijifanye muhuni rudisha hayo maji sehemu ulipo yatoa”

    “Kwani si nimekikinga kindoo chako si kitajaa?”

    “Koma mwanaume mzima ovyoo unazani pale nimekalisha makalio yangu bure...Nimekaa ili kindoo changu kijae maji”

    “Samahani kama nimeuudhi”

    Nikayamimina maji niliyo yatoa kwenye kindoo cha huyu mama ambeye sikujua ni kwanini amenichukia pasipo kuwa na sababu maalumu kwani ni siku yangu ya kwanza kufika atika nyumba hii ila wanaonekana kunichukia sana”

    Nikakikinga kindoo changu hadi kikajaa na kwenda nacho kweye bafu alilo nionyesha askari wetu ambaye hadi sasa hivi nilisahau jina lake kani nilisha zoea kumuita afande.Nikaoga na kumaliza na kurudi ndani kwangu na kumkuta askari wetu akivaa nguo nyingine za kazini

    “Unaondoka?”

    “Ndio kaka hapa nimepigiwa simu ninahitajika lindo si unajua nilitoaka pasipo kuaga inanilazimu kwenda kufidi muda niliokuwa sipo kazini”

    “Ahaa sawa ndangu yandu ila mbona hawa mama humu ndani wamekuwa watu wa maneno ya chini chini?”

    “Hao wamama huwa wanapenda kumpima mtu....hata mimi kipindi nilipokuwa ninakuja walikuwa wanavimaneno vya chini chini hadi kuna siku kuna mama nilimzaba makofi ndio wote wakaniheshimu”

    “Wana waume?”

    “Ndio wana waume zao ila waume zao nao ni wanaume suruali”

    “Wanaume suruali kivipi?”

    “Wanawategemea wake zoa wao kila ikifika asubuhi hukaa maskani hadi mida ya kula ndio utawaona wakirudi mmoja mmoja”

    “Mmmm ndio maana wake zao wanakuwa na dharau?”

    “Ndio hivyo ndugu yangu”

    “Kaka hivi unaitwa nani?”

    “Eddy ina maana siku zote hulijui jina langu?”

    “Silijui ndugu yangu?”

    “Mimi ninaitwa Afande Josephat”

    Josephat akanipa elfu kumi kwa ajili ya kununua chakula cha usiku kisha yeye akaondoka na mimi nikavaa nguo zake alizo nipa nizivaa kisha nikaenda kununua chipsi kwenye kibanda kisicho mbali na sehemu ya nyumba yuliyopo na nikarudi na kabla sijaingia mlangoni nikakutana na msichana ambaye sikuwahi kumuona akiwa anagonga mlango wa chumba cha Josephat

    “Mambo vipi kaka?”

    “Salama vipi?”

    “Safi tuu Jose nimemkuta?”

    “Hapana amekwenda kazini”

    “Hawezi kurudi leo?”

    “Sijajua”

    “AHaa mimi ni mgani wake ameniambia kuwa nije je nimsubiei huku kwake?”

    “Mmmm amekuambia saa ngapi?”

    “Ahha..si....sijana”

    Dada alizungumza huku akiwa anajing’ata ngat’ata kiasi kwamba sikuwa ninamuelewa ni kitu gani kilicho mleta na akapita dada mmoja na akaropoka neno lililo muudhi dada niliye simama naye

    “Wewe Asha ngedere usione chaka mavi yanakubana utakuja kufa nyoo mwanamke kila ukimuona mwanaume kidubwasha chako kina kuwasha”

    “Koma na wewe sura mbaya kama kwapa la bibi kizee”

    “Wee wee tena utaifananisha sura yangu na hilo sura lako kama ku** ya changudoa aliye kosa mteja”

    Maneno yao makali yakawafanya wapangaji waliomo kwenye yumba vyao kutoka wakiwa wanashangaa majaibizanio yao,Sikutaka kuwaingilia nisije na mimi nikavurugwa bure nilicho kifanya ni kuingia ndani na kufungua mlango na nikasikia masufuria yaliyo pangwa kwenye kordo yakianguaka huku watu wangine wakishangilia na nikagundua wanapimana lishe na nilicho kifanya nikufungulia redio yenye spika kubwa hadi mwisho na sikuzisikia sauti zao wakigombana

    Baada ya muda ugomvi wao ukaisha kisha na nikapunguza sauti ya redioa na kuanza kula nilicho kinunua huku nikiwa siamini kama ipo siku nitaishi maisha kama haya ninayo yaishi na mipango ya kwenda ikulu ikaanza kujipanga taratibu kichwani kwangu na lengo zima ni kwenda kujua ni jinsi gani wataweza kunisaidi juu ya kumpata mama.Kwa msongamano wa mawazo mengi nikajikuta nikipitiwa na usingizi kwenye sofa moja lililopo kwenye chumba hicho kilicho jaa vitu vingi na mbaya zaidi kina dirisha moja tuu

    Nikastushwa na mlango unao gongwa huku nikiisikia sauti ya Josephat ikiita nje ya mlango.Nikanyanyuka na kwenda kumfungulia mlango na akaingia huku akionekana kuwa na haraka sana

    “Kaka nimepata safari ya kikazi naelekeaa Kagera”

    “Kuna nini tena?”

    “Ni maswala ya kikazi tu na ninaweza kukaa hata wiki hapo nimekuja na wezangu wananisubiria hapo nje”

    “Ahaaa kwani ni saa ngapi saa hizi?”

    “Nane usiku”

    Afande Josephat alizungumza huku akidumbukiza nguo zake kwenye begi na la mgongoni kwa haraka akachukua vitu vyake muhimu kisha akatoa elfu hamsini na kunipatia kisha akaiiandika namba yeke ya simu pembeni na kuniambia endepo nitapata tatizo lolite nitafute simu kwa ajili ya kumpigi.Akatoka na mimi nikarudi kitandani na kujibwaga na kutokana na uchovu mwingi usingizi ukanipitia tena wa safari hii ulizidi usingizi wa mwazo

    Kwa mbali nikahisi mlango ukifunguliwa nikayafumbua macho yangu na kugundua mwanga wa juu ukiwa umetawala ndani ya chumba changu ikiashiria kumesha pambazuka.Nikayapeleka macho yangu mlangoni kumtazma mtu anaye usukuma sukuma mlango na akaingia kwa haraka

    “SAPRAIZZZZ BABY JOS........”

    Macho yangu yakakutana na Salome ambaye alishindwa kuimalizia sentensi yake na sote tukabaki tukitazamana kwa mshangao huku yeye akionekana kunishangaa zaidi



    Nikajinyanyua tararibu kitandani na kukaa kitako huku Salome naye akiliingiza begi lake la nguo na kuliweka pembeni na taratibu akakaa kwenye sofa lililopo ndani ya na kuanza kuminya minya vidole vyake vya mkononi huku sura yake akiwa ameilekezea chini akionekana kujawa na aibu kubwa ikanilazimu kuanza kumsalimia

    “Mambo”

    “Powa vipi?”

    “Salama za huko utokapo?”

    “Mmmm....?”

    “Za huko utokapo vipi?”

    “Nzuri tu”

    “Karibu mbona unaona aibu?”

    “Eheee walaa Jose yupo wapi?”

    “Ahh amesafiri kikazi”

    “Mungu wangu sijui itakuwaje?”

    “Iakuwaje nini?”

    “Mmmm hamna mwaya”

    Nikanyanyuka kitandani huku nikiwa ninawenge la usingizi kidogo na nikaanza kuvinyoosha viungo vyangu huku nikipiga miyayo na kama kawaida ya wanaume wengi walio kamilika kimaumbile pale wanapo amka ni lazima koki zao husimama kuashiria ni siku mpya hii na ndivyo ilivyo kwangu jambo lililo mpelekea Salome kuyagandisha macho yake kwenye koki yangu pasipo kuyapepesa hata kidogo.Nikawasha redio na kuifungulia sauti ya kawaida kisha nikarudi kukaa tena kitandani na Salome akatoa simu yake aina ya Samsung Galax na kuanza kuiminya minya kisha akaiweka sikioni

    “Jose jamani upo wapi?”

    “Sasa utarudi lini wakati mimi nipo kwako nilikuja kukufanyia supriz naona supriz yenyewe imeharibika”

    “Nimpe simu nani?”

    “Haya........Eddy ongea na Jose simu ipo hewani”

    “Mmmm vipi kaka Jose”

    “Safi.....sasa huyo bibie ndio hivyo kaja bila taarifa”

    “Ndio”

    “Basi ninakuomba ukatafute hata sehemu ya kujishikiza kwa hizi siku ambazo nitakuwa sipo na yeye aishi ndani humo hadi nitakapo rejea”

    “Ahaaa powa kaka”

    “Hakikisha unafanya hivyo bwana....Huyo ni Malkia wangu muache ajitanue ndani kwangu”

    “Sawa mzee......Chukua simu yako”

    “Eeehe baby”

    “Ahaa ataondoka eheee”

    “Haya kazi njema”

    “I love too mwaaaaa”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Salome akakata simu na kuachia tabasamu pana ila kwa upande wangu nikajikuta roho yangu ikiwa inauma kupita maelezo kwani kitendo cha kuambiwa kuondoka kikabaki kikiniumiza na sikuwa na jinsi ya kufanya.Nikanyanyuka kiustaarababu na kuzitoa ndala chini ya uvungu nilizo kwenda kuogea jana usiku na kuzivaa vizuri na kusimama kwenye kioo kikubwa na kujitazama jinsi sura yangu ilivyo jaa ndevu zisizo na mpangilio na kunifanya nionekane kama mzee wa miaka 70 na zaidi kumbe ni kijana mdogo tu wa miaka ishirini naa.

    “Nawatakia maisha mema wewe na mchumba wako”

    “Eddy unakwenda wapi?”

    “Sijajua ila ngoja niondoke”

    “Eddy...”

    “Salome wewe tayari umesha mpenda mtu mwengine kuwa na mimi hilo litakuwa ni ngumu”

    “Powa nenda”

    Salome akajibu kwa dharau na kunifanya nimtazame kwa muda huku machozi yakianza kunilenga lenga na kuyakumbuka mambo mema niliyo mfanyia Salome kuanzia siku ninampa pesa ya matumizi kipindi tupo shule na alipo poteza pasa yake hadi siku ninamkuta na mkuu wa shule wakitoka kwenye mlango wa chumba cha Hotel kisha taratibu nikashika kitasa cha mlango

    “Salome naamini unaijua afya yako ila ni bora ukamueleza ukweli Jose kuliko kumuua pasipo yeye kujua”

    “Nashukuru kwa ushauri wako ila ukweli ni kwamba sijaadhirika kama unavyo dhania”

    “Sawa kama ni hivyo”

    “Powa nenda usije ukanivunjia ndoa yangu na mume wangu mtarajiwa....Ila umeachwa nini na mpenzi wako mbona umechakaa hivyo kipindi kile nilivyokuwa nikikuomba msamaha ukawa unanidharau haya pole mwaya”

    Maneno ya Salome yakaniumiza kiasi kwamba nikajikuta nikitokwa na machozi kisha nikafungua mlango na kutoka nje na mtu wa kwanza kukutana naye ni yule mama wa jana aliye ninyang’anya maji yake na baada ya kuniona akaanza kucheka kwa kicheko cha kejeli

    “Heeeheee Osama na wewe pia unalia makubwa haya”

    Nikasimama na kumtazama kwa macho makali na akaendelea kujichekesha kitendo kilicho anza kunipandisha hasira na nikapiga hatua za haraka hadi alipo simama na sura yangu nikaisogeza karibu na sura yake huku ndevu zangu zikiwa zinamgusa kwenye mashavu yake na akakaaa kimya kiasi kwamba akaanza kutetemeka

    “NITAKUUA”

    Nilizungumza kwa hasira huku nikijitahidi kuizuia hasira yangu ambayo siku zote ni mbaya na taratibu nikageuka na kuondoka zangu.Na nikafika kwenye moja ya maskani na kuwasalimia watu wote nilio wakuta na mimi nikatafuta sehemu nikakaa huku nikiwasikiliza mabishano yao ya mpira dhidi ya timu za afrika zinavyo fanya vibaya kwenye kombe la dunia la mwaka huu na jinsi mabishano yao yanavyo endelea nikajikuta hasira yangu ikipungua

    “Alafu wewe jamaa ni mwera(polisi) nini?”

    “Kwa nini?”

    “Kwa maana umekuja hapa umesalimia na kuvamia vamia kijiwe cha watu usije ukawa unatuchunguza?”

    “Hapana jamani mimi mtu wa kawaida sana”

    “Sio kawaida usije ukasababisha pira(gari la polisi) likaja hapa ni kutunyanyua”

    Jamaa mmoja aliye jazia kifua akanisogelea huku akiwa na kipisi cha bangi mkononi huku kikiwa kinawaka kisha akavuta fumba kubwa la moshi na kuinama na kunipulizia usoni jambo lililo nikasirisha sana na kujikuta nikinyanyuka na kumtandika kichwa cha pua na akayumba nyumba na kuwafanya wezake wapatao wanne kunivamia na kuniangusha chini na kuanza kunishambulia kwa mangumi na kujikuta nikimdaka mmoja sikio lake na kumng’ata kwa nguvu zangu na kumfanya atoe ukelele mkubwa huku akisema anakufa na nikamuachia kumng’ata na akanyanyuka huku damu zikiwa zinamwagika kwenye masikio yake na gafla vumbi jingi la gari lililo funga breki za gafla likasimama na watu walio nishambulia wote wakakimbia na kuniacha nikiugulia kwa maumivu.

    Nikastukia askari wawili wakiwa wakininyanyua huku wakinipiga na virungu vya miguu na wakanisukumia kwenye gari lao walilo kuja nalo.Kwa wenge la maumivu sikujua ni wapi wananipeleka.Gari likasimama kwenye mtaa mwengine na kuwakuta askari wengine wapatao wanne wakiwa na bunduki mikononi wakiwaamrisha watu wapatao nane waliokuwa wamelala chini huku mikono yao wameiweka kichwani na wanavyo onekana ni wavuta bangi.Watu hao wakaamrishwa kuingi ndani ya gari hili la polisi na watu wengi tumezoea kuyaita ‘Defendar’ na sote tukajikuta tukiwa tumetosha na askari wote wakapanda na likaondoa kwa kasi.Ndani ya dakika kadhaa tukawa tumesimama kwenye moja ya geti ambalo kwa haraka nikafahamu kuwa ni gereza la Keko.

    Gari ya polisi ikaingia ndani na sote tukaamrishwa kushuka na kupanga mastari mmoja huku tukiwa tumechuchumamaa na tukaanza kuhesabu namba huku na mimi nikiwa namba tano kati ya watu tisa tuliopo kwenye eneo hili na tukasimama huku mikono tukiwa tumewekeana kwenye mabega na kunyoosha mstari mmoja na tukaaza kutembea huku tukiongozwa na askari wa magereza hadi kwenye chumba kimoja cha mahabusu na sote tukaingia ndani na mlango wake ukafungwa.Nikatafuta sehemu yangu na kukaa huku nikijutia kitu kilicho nifanya nikae kwenye ile maskani ni nini.

    “Hata nikiwaambia kuwa mama yangu ni waziri haina tija”

    Nilijisemea mwenyewe kimoyo moyo na sikuwa na uwezo huo kwa jinsi ninavyo wajua askari wangeniambia mambo ya dharau ambayo yangenikera zaidi na kunisababishia matatizo mengi zaidi.Hadi jioni inaingia sikujua ni kitu gani kinacho endelea juu ya chakula.Usiku mzima sikuweza kulala kutokana na baridi kali kwenye sakafu isitoshe tumbo langu tangu jana usiku halikuuingiza chakula cha aina yoyote.Mawazo ya jinsi nitampata mama yangu yakaanza kunitawala kichwani kwangu kwani kwa maelezo ya John aliniambia kuwa mama yangu yupo South Africa akiwa anaumwa na amelazwa.

    Hadi inatimu asububuhi sikuweza kupata usingizi na kengele kubwa likagongwa na milango ikafunguliwa na wezangu wakatoka kwa haraka na mimi ikanibidi nitoke kwa haraka na kuwafwata kwa nyuma na tukafika kwenye sehemu na kuwakuta wafungwa wengine walio valia sare wakinganyanyiana mabakuli yaliyo tengenezwa na alumuminiam na nimachafu ndani ya maji yaliopo kwenye karo na anayepata chombo chake anakimbilia kwenye sehemu unapotolewa uji.Nikabaki nikiwa nimesimama na kutokujua ni nini nifanye kwani nikahisi endapo nitakunywa uji wao ninaweza nikatapika kwani una harufu mbaya sana.

    Watu wakakanywa uji kisha sisi tulio tolewa kwenye chumba tukaamrishwa kurudi kwenye chumba tulicho toka.

    “Oya wewe ni mtoto wa mama nini?”

    Jamaa mmoja alizingumza na nikabaki nikiwa nimemtazama pasipo kukjibu kitu cha aina yoyote huku akininyooshea kidole

    “Oya wewe chok* si nanikuuliza wewe ni mtoto wa mama?”

    “Kwani wewe umezaliwa na mbwa?”

    “Ahaaa dharau sasa hizo”

    “Sio dharau unavyoniambia kuwa mimi ni mtoto wa mama ina maanisha wewe umazaliwa na mbwa tena mbwa koko”

    “Oya dogo inakuwaje anakuita mbwa koko alafu na wewe unakubali kirahisia rahisi”

    “Na wewe yasiyo kuhusu isiyaingilie ua na wewe unataka kuitwa mbwa koko?”

    Jamaa aliye ingilia mada akanifwatwa huku kifua chake akiwa amekitunisha na mimi nikasimama kwa haraka na akanisukuma kidogo na kurudi nyuma na kwanguvu zangu zote nikamrukia kwa kutumia bega langu na likatua kwenye tombo lake na kumsukuma hadi ukutani na kuanza kumshindilia mangumi na kuwafanya watu wengine kushangilia kwa nguvu.Jamaa naye hakuwa nyuma katika kuyajibu mashambulizi yangu na kusema ukweli ngumi zake ni nzito kiasi kwamba nikaanza kuona nyota nyota na kwa bahati mbaya akanisukuma na kichwa changu kikagonga kwenye nondo ya mlango na kujikuta nikianguka kama mzigo na kupotaza fahamu



    ***

    Nikastuka na kujikuta nipo kwenye kitanda cha hospitalini huku mkono mmoja nikiwa nimefungwa pingu na pembeni yangu amesimama askari wa magereza.Nikajishika kichwani kwangu na kukuta nikiwa nimefungwa na bandeji kubwa

    “Unajisikiaje?”

    Askari aliniuliza na kunifanya nikae kimya nikiwa nikimtazama kwa macho ya unyonge.Askari akafungua mlango na kumuita nesi kisha na yeye akarudi kukaa kwenye sehemu aliyokuwa umekaa hapo awali.Nesi akaingia huku akiwa amebeba kisinia chenye vifaa vingi na kukiweka pembani kwenye meza iliyopo karibu na kitanda nilicho lala na kuanza kunitazama kwenye jeraha lililopo kichwani kwangu

    “Amesha kula?”

    “Bado hajakula”

    “Ina bidi tuweze kumpatia chakula ili aweze kunywa dawa”

    “Hapa ni wapi kwenye kibanda ambacho ninaweza kumnunulia chakula?”

    “Ukitoka kwenye geti hapo utaweza kuona kibanda cha wauza chipsi na unaweza kumnunulia chakula”

    “Sawa”

    “Akimaliza kula ninaomba uniite”

    “Sawa”

    Nesi akatoka na kukiacha kisinia chake na askari akanyanyuka na kutoka nje na nikapata wazo la haraka nikaanza kutafuta kifaa kidogo kinachoweza kuingia kwenye shimo la funguo la pingu na kuchukua kijikifaa kidogo kilichopo kwenye sinia na sikujua kina kazi gani na kuanza kuifungua pingu niliyo fungwa kwa utulivu wa hali ya juu na chakumshukuru Mungu ikafunguka kisha nikashuka kitandani japo mwili umetawaliwa na maumivu makali ila nikajikaza na kuufwata mlango wa kutokea kwenye chumba nilichopo na kuwaona watu wakiwa wanaendelea na mishe zao.Nikatoka ila kitu kilicho nichanganya sikujua askari ni wapi alipo elekea,nikaanza kutembea kwa umakini huku nikifwata sehemu yenye mlango wa kutokea na kwabahati nikamuona kwa mbali askari wa magereza akija kwa mwendo wa haraka huku mkononi mwake akiwa ameshika kifuko cheusi.Nikajibanza kwenye ukuta na akapita pasipo kuniona na kwaharaka nikatoka huku miguuni nikiwa sina hata kitu chohote,Nikafanikiwa kuondoka eneo la hospitali na safari hii moja kwa moja nikaelekea nyumbani kwetu

    Japo kuna umbali kidogo ila nikajikaza kutembea na nikafanikiwa kifika na kukuta geti likiwa limefungwa,nikakumbuka kwenye sehemu ya nyuma ya ukuta wetu kuna matofali yaliyo pagnwa ya mtu mwenye kiwanja chake aye taka kujenga.Nikazunguka na kuyakuta matofi kama nilivyo tarajia

    “Hivi mwenye haya matofali amefariki dunia au?”

    Nilijisemea huku nikianza kuyapanga matofali karibu na ukuta wetu ambao ni mrefu kiasi kisha na kitu kingine kilicho niogopesha ni nyaya za umeme za ulinzi zilizo zungushiwa kwenye ukuta wa nyumba yetu sehemu ya juu.Ikanichukua kama dakika kumi na tano kutengeneza urefu wa ngazi za kuingilia kwenye nyumba yetu na nikafanikiwa kupanda ukutani huku kwa hahadhari kubwa nikizikwepa nyaya za umeme na nikafanikiwa kurukia kwa ndani na ukimya mwigi umetawala ndani ya nyumba,nikafika kwenye mlango wa mbele na kukuta umefungwa na kawaida mlango ukiwa umefungwa huwa funguo tunazificha kwenye vyungu vya udongo vyenye mau.Nikanza kutafuta kwenye chungu kimoja baada ya kingine wala sikuzikuta

    “Huyu shetani ameondoka na hizi funguo nini?”

    Nikaendelea kutafuta na kwabahati nzuri nikaziona zikiwa nimefichwa kwenye kindoo kidogo chenye maua ambayo mama siku zote huwa huyapenda na kwamadai yake ameyanunulia nchini Canada na aliyanunua kwa gharama kubwa kubwa sana.Nikafungua ndani na kukukuta vitu vikiwa vimeshanguliwa sana huku kukiwa na chupa nyingi za pombe zikiwa zimezagaa zagaa kwenye sakafu huku vijimito vidogo vya masofa vikiwa vimetupwa tupwa.Nikapanda ngazi hadi chumbani kwangu na kuingia bafuni na kuoga kisha nikapanda kitandani na kulala kutokana na uchovu mwingi sana.

    Nikaamka mida ya saa mbili usiku huku niikiwa nimechoka nikaelekea jikoni na sikukuta kitu chochote cha kula hata mafriji yote hayakuwa na kitu chochote,Nikakumbuka kwenye nyumba ya uwani kuna handaki ambalo mara nyingi nikiwa nipo likizo nilikuwa nikamuona mama akiingia na sikujua ni kitu gani anacho kifwata ndani ya handaki hilo.Nikaingia kwenye nyumba ya nyuma katika chumba ambacho kuna kitanda kimoja na kiti kisha nikasogeza pembeni kitanda na kulisogeza kapeti lilolopo ndani na kuukuta mlango wa chuma ambao ni mlango wa handaki.Nikaufungua na kukuta ngazi za kushuka chini ambapo kunagiza la kutisha sana ikanibidi nirudi tena juu kutafuta tochi.Nikafanikiwa kuiona tochi yenye uwezo mkubwa wa wa mwanga.Nikaingia tena ndani ya handaki huku tochi ikiwa inawaka,nikaanza kuona picha nyingi za kutisha zikiwa zimebandikwa kwenye kuta za handaki hili huku kukiwa na vitu vichache sana ikiwemo majoho matatu moja likiwa jeusi la pili likiwa na rangi nyeupe na jengine ni la rangi nyeusi.Sikujua ni ya kazi gani nikakifwata kitabu kikubwa kilicho jaa vumbi nilicho kikuta na kukifungua na kukuta maandishi ambayo sikujua ni ya lugha gani iliyo andikwa ndani yake

    Nikakiacha na kukiona kisanduku kidogo cha wastani kikiwa kimefungwa na kuwekwa kwenye kona ya handaki na nikakisogelea na kukifungua,Sikuamini macho yangu baada ya kukuta cheni na pete za dhahabu pamoja na vipande vaya madini.Na nikaanza kuchangua changua na kukuta pete moja ya madini ya Tanzanite ikiwa imetengenezwa kwa ustadi mkubwa huku kukiwa na vipande vingine vingi vya madini yenye dhamani kubwa na hata madini mengine sikuwahi kuyaona maishani mwangu.Nikakibeba kisanduku huki nikiwa nina furaa kubwa na nikaingia ndani ya chumba changu na kuvimwaga vitu vyote kitandani na furaha ikazidi kunitawala hata njaa sikuweza kuihisi tena na kujikuta nikiaanza kuimba nyimbo za aina mbali mbali huku nikicheza kiduku kisicho na mpangilio maalumu.

    Nikazikusanya na kuziweka kwenye kisanduku chake kisha nikaviweka chini ya uvungu wangu wa kitanda na kwenda sebleni na kuwasha Tv na kuangalia angalia miziki hadi usingizi ukanipitia.Cha kwanza baada ya kuamka asubuhi nikaoga na kuvaa nguo nyingine zilizo nipendeza na kuingia chumbani kwa mama na kuzikuta baadhi ya funguo za magari zinapo wekwa kwenye kabati na kuchukua moja kisha nikichukua dini moja la kuliweka mfukoni na kutoka nje na kuingia kwenye gari moja aina Verosa ambayo mama aliinunu kipindi zinatoka.Moja kwa moja nikaenda kwa sonara na kukutana na muhindi mmoja na tukakubaliana biashara na nikamuuzia kwa milioni kumi ambazo zinanitosha sana kwenye matumi ya kwenda nchini Afrika kusini kumuona mama.Nikaingia saluni moja kiume na kunyolewa vizuri kisha moja kwa moja nikaelekea benki ya backrays kwenye akaunti yangu ambayo ni siku ningi niliifilisi hadi ikabaki kilinda akaunti na kukiweka kiasi cha milioni saba na kubaki na tatu na nikaanza mipango ya kutengenezewa hati yangu mpya ya kusafiri

    Na ndini ya masaa machache nikawa nimefanikiwa kutokana na kuhonga sana pesa kwa watu wanao husika na utengenezaji wa hati za kusafiria na hadi ninafanikiwa kuipata nikajikuta nikiwa nimebakiwa na laki tano na nusu nusu na nikakata tiketi ya ndege ya shirika la South Africa Aur ways.Na nikaelekea kwenye ofisi za wizara ya afya na kukutana na mmoja wa masekretari wa mama ambaye nina fahamiana naye vizuri na akaonekena kunishangaa.

    “Eddy si nimesikia umefariki wewe?”

    “Nani amekuambia?”

    “Eddy kila mtu anajua kuwa wewe umeuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu kitendo kilicho mpa mama yako mstuko na tumemkimbiza Afrika kusini kwa matibabu zaidi”

    “Tena hilo ndilo nililokuwa nimekuja kulijua mama yangu amelazwa hospitali gani?”

    “Amelazwa hospital moja inaitwa Louis Pasteur ipo mji wa Pestoria”

    “Ahaaa asante kwa hilo”

    “Ila Eddy niambie ni kitu gani kilicho kupata hadi ukafufuka kwa maana mimi mwenye kwa macho yangu niliiona maiti yako ikiingizwa mochwari ila cha kustaajabu leo hii ninakuona hapa?”

    “Ni historia ndefu ila Mungu akibariki nikipata nafasi nitakuja kukusimulia ila nashukuru kwa masaada wako”

    “Usijali nakutakia safari njema”

    Kutokana tiketi ya ndege niliyo kata inaondoka saa Mbili usiku ikanilazimu kurudi nyumbani na kubeba nguo kadhaa na kurudi uwanja wa ndege kwa kutumia taksi ya kukodi.Nikatafuta sehemu yenye mgahawa na kujipatia chakula cha kutosha kwani kutokea asubuhi sikuweza kuingiza chochote kutokana na mizunguko ya kuandaa safari.Imebaki lisaa limoja kabla ya safari nikaendelea kusubiri kwenye sehemu za abiria.

    “Samahani kaka hii sehemu kuna mtu?”

    “Hapana unaweza kukaa”

    Dada mmoja aliye valia suruali ya kubana na kuyafanya makalio yake makuwa kujichora vizuri huku akiwa amejiremba na kuonekana mrembo zaidi alianiambia na baada ya kumjibu akakaa pembeni huku akiwa na pochi yake kubwa kiasi na kujikuta nikimtazama kwa jicho la kuiba.Nikaendelea kusoma gazeti hadi tulipo tangaziwa abiria shirila la ndege la South Afrika Air ways tujiandae kwa safari na tukapanga foleni na kuanza kuingia sehemu maalumu ya kukaguliwa kisha nikaingia kwenye ndege na kutafuta sehemu ilipo siti yangu na kukaa baada ya mida kidogo akingia dada aliye niuliza kuhusiana na sehemu ya kukaa kisha na yeye akakaa siti ya pembeni yangu na baada ya muda safari ikaanza pasipo kusemeshana kitu cha iana yoyote hadi katikati ya safari ndipo akaanza kuniongelesha

    “Samani kaka unaelekea wapi?”

    “Afrika kusini”

    “Ahaa mimi ninaitwa Emmy”

    “Mimi ni Eddy”

    “Ahaa nashukuru kukufahamu”

    “Na mimi pia”

    “Unakwenda South kufanya nini?”

    “Ninakwenda kumcheki bi mkubwa ni mgojwa”

    “Ahaa mimi kule ndio ninaishi ila mimi ni Mtanzania

    “Kwa hiyo wewe ni mwenyeji kule”

    “Ndio....mama yako amelazwa hospitali gani?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Inaitwa Louis Pasteur”

    “Ahaa ndipo ninapo fanyia kazi na nidaktari pale”

    “Kweli?”

    “Ndio ila nilikuwa nipo likizo ndio ninarudi hivi nilikuja kuwaona wazazi mara moja”

    “Eheee asante Mungu nimepata mwenyeji kwa maana hapa nilikuwa ninajiuliza ni jinsi gani ninaweza kumpata mama yangu”

    Safari ikaendelea kwa masaa kadhaa huku nikiwa nina amani moyoni mwangu kwani nimempata mwenyeji wangu.Ndege ikatua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo.Emmy akaniomba kwanza niende kwake ili kukipambazuka vizuri tuweze kwenda hospitali kwani yeye amebakisha siku tano za kurudi kazini.Tukafika nyumbani kwake kwenye gorofa refu moja ambalo alinieleza kuwa watu wangi wamepanga na yeye sehemu yake ni gorofa ya saba kutoka chini.

    “Eddy karibu ndani?”

    “Asante”

    Emmy akanikaribisha kwenye sehemu anayo ishi ambayo yenye vitu vingi vya dhamani ya hali ya juu.Taratibu Emmy akaanza kuvua nguo zake moja baada ya nyingine na kunifanya nibaki nikiwa nimemshangaa kwani sikujua ana maana gani na imekuwaje amevua nguo mbele yangu na kubakiwa na chupi wakati mimi na yeye hatuna mahusiano ya namna yoyote



    Emmy akachukua taulo na kujifunga kisha akaingia bafuni na kuniacha mimi nikiwa nimekaa kwenye sofa nikiyatadhimini mazingira ya ndani kwake.Baada ya muda kidogo Emmy akatoka bafuni

    “Umeshindwa hata kuwasha Tv?”

    “Ahaa hakuna tatizo sana”

    “Ok ngoja nivae nguo tuelekee hospitalini ukamuone mama”

    “Sawa”

    “Ila unajua wodi aliyo lazwa?”

    “Hapana siijui”

    “Ok basi tutajua huko huko”

    Emmy akaingia ndani kwake na akatoka akiwa amevalia mavazi mazuri kiasi kwamba tama za mapenzi zikaanza kunitawala na kujikuta nikimtazama Emmy kwa macho ya matamanio

    “Eddy twende zetu”

    “Mmmmm”

    “Twende zetu mbon unanishangaa?”

    “Ahaa hakuna kitu”

    Nikanyanyuka na nikatangulia kutoka nje ila kutokana na baridi kali ikanilazimu kumuomba Emmy koti na akarudi ndani na kunichukulia koti lake kubwa na sote tukaingia kwenye Lifti na kushuka chini gorofani.

    “Twnde huku kwenye maegesho ya magari”

    Tukafika sehemu yenye maegesho ya magari mengi na Emmy akafungua gari moja na kuniomba niingie.Safari ikaanza huku kila mmoja akiwa kimya ndani ya gari ila Emmy akaamua kuvunja ukimya

    “Hivi Tanzania wewe unafanya kazi?”

    “Mimi ni mwanafunzi wa A leve bado”

    “Ohh kumbe unasoma?”

    “Ndio”

    “Kombi gani?”

    “PCB”

    “Mungu wangu PCB wewe....Mbona unaonekana kama HKL?”

    “Hahaa PCB halisi...Aafu mbona ndege leo imetua kwenye uwanja wa Maputo international airport imekuwaje kutokana tumetua Mozambique?”

    “Ndege ilipata itilafu kwa watu kama sisi tunao jua ndio tumegundua hilo ila ukiwa ni mgeni huwezi kujua kama ndege imeshindwa kuendelea na safari”

    “Sasa si wangetulipa fidia kwa kwa abiria inakuwaje ndege inakuwa haina uwezo wa kumaliza msafara wake?”

    “Mimi niliamua tuondoke kutokana wewe umeseme unahitaji kumuona mama yako ila kwa walio baki wakisubiria ndege kutengenezwa watakuwa wamelipwa fidia na kama siku ukiondoka utakwenda kupanda ndege uwanja wa kimataifa wa Cape town”

    “Sawa”

    Safari ya kwenda hospitalini haikuchukua muda sana hii nikutokana na wingi wa barabara nyingi zinazo punguza msongamano wa magari.Tukafia hospitalini na moja kwa maja Emmy akaenda kwenye katabu kinacho onyesha orodha ya wagonjwa waliopo hapa hospitalini na nikamtajia jina la mama kishha akatumi kama dakika tano kulitafuta na akalipata

    “Kumbe mama yako ni waziri?”

    “Ndio”

    “Twende ukamuone”

    “Moja kwa moja tukealekea kwenye chumba alicho lazwa mama na kabla hatujaingia nikamkuta askari mmoja akiwa amesimama nje ya chumba alicho lazwa mama

    “Hamuruhusiwi kuingia humu ndani nyinyi ni kina nani na munahitaji nini?”

    “Mimi naitwa Dokta Emmy Samson na mfanyakazi wa hii hospitali”

    “Naomba kitambulisho chako”

    Emmy akatoa kitambulisho chake na kumpa askari aliye simama mlangoni na akakisoma kwa muda kisha akamrushu Emmy kuingia ndani na mimi nikataka kuingia ndani ila akanizuia kuingia

    “Na wewe ni nani?”

    “Mimi ni mtoto wa huyo mama huko ndani?”

    “Mbona hatuna maelezo ya aina yoyote kuhusiana kama mgonjwa ana mtoto?”

    “Mimi ni mwanaye unadhani nitafunga safari kutoka Tanzania hadi hapa nije kujipendekeza kwa mama yangu?”

    Nilizungumza kwa hasira kiasi kwamba watu walipo karibu na eneo la mlango wa kuingia kwenye chumba alicho lazwa wakaanza kunishangaa

    “Eddy kuwa mpole ngoja nikamuone mama”

    “Kijana ninakuoma usimame mbali na hili enoa la sivyo nitakuitia walinzi waje wakutoe”

    “Eddy tafadhali nakuomba uwe mpole nitazungumza na mama na utamuona tu”

    Nijaitahidi kutulia hasira zangu na kusimama pembeni kidogo na chumba alicho lazwa mama huku sura yangu ni kiwa nimeikunja.Emmy akaingia ndani ya chumba na baada ya muda akatoka na kumnong’oneza askari kisha kwa ishara Emmy akaniita na nikanyanyuka kwa haraka hadi sehemu waliyo simama kisha askari akaniruhusu kuingia ndani.Macho yangu yakatizamana na mama ambaye kwa muonekana hali yake sio nzuri sana japo nimemkuta amaekaa kitako kwa mwendo wa haraka nikamfwata mama na kumkumbatia huku machozi yakinimwagika

    Tukabaki tumekumbatiana na mama ndani ya dakika kadhaa kisha nikamuachia na kuiona sura yake ikiwa imelowana kwa machozi mengi,Mama akanishika mashavuni na kunibusu kwenye paji la uso huku akinichunguza sehemu mbali mbali za mwili mwangu na kunifanya nizidi kububujikwa na machozi

    “Eddy ni nini kilicho kupata mwanagu?”

    Mama aliniuliza huku akiwa anabubujikwa na machozi kiasi kwamba nikashindwa kulijibu swali lake hadi ndani ya dakika tano ndipo nikaanza kumuadisia kila kitu kilicho tokea na jinsi baba alivyo nifanyia kiasi kwamb hadi ninamalizia nikamshuhudia Emmy akiinama chini huku akitokwa na machozi.

    “Eddy mwanagu nakuomba unisamehe”

    “Nikusamehena nini mama?”

    “Eddy najua siku zote ulikuwa unahitaji kujua ukweli juu ya baba yako na mimi nikawa nimekuficha ila....”

    “Mama nimesha lijua hilo kuwa pacha wa baba ndio baba yangu”

    “Nani amekuambia hivyo?”

    “Mama dunia haina siri tena hili swala nimeambia na mtu baki kabisa tena ni muandishi wa habari”

    “Basi Eddy tuliache hilo mwanagu kwa maana unazidi kunipa uchungua katika hilo”

    Ikanibidi nibadilishe mada ya kuzungu na kuzungumza na kuanza kupiga story za kupoteza mawazo hadi mama na Emmy wakaanza kucheka ila sikumuambia mama kuhusiana na swala la shule yetu kuingia kwenye matatizo.

    “Emmy hapa ni wapi kwenye choo?”

    “Ukitoka hapo nje mkono wako wa kushoto utaona milango miwili imeandikwa toilet”

    “Ahaa powa”

    Nikatoka nje na kumkuta askari akiwa amesimama mbali kidogo na chumba akizungumza na simu akionekana akiwa na mazungumzo ya siri ikanibidi kulitega sikio langu kwa umakini kusikiliza ni kitu gani anacho kizungumza

    “Ndii si nimrefu kiasi na mwili wake umejazia kidogo?”

    “Basi amefika hapa kama lisaa lililo pita”

    “Amekuja na mwanamke fulani ambaye hapa ni ndakatari”

    “Basi panda ndege uje kwa maana inavyo onekana mipango yote itakwenda kuharibika”

    “Sawa Mr Godwin”

    Nikajikuta hata hamu ya kwenda kujisaidi haja ndogo ikakata na kabla hajaguka nikaingia ndani huku nikiwa ninawasiwasi hadi mama akanigundua kwa haraka

    “Una tatizo gani mwanangu?”

    “Mama hivi huju mlinzi mumemtoa wapi?”

    “Kwa nini?”

    “Wewe nijibu?”

    “Huyo amekwa na ubalozi wa Tanzania uliopo hapa nchini”

    “Unauhakika kweli ni mwema?”

    “Ni mwema kivipi?”

    “Au kuna siku ambayo baba alisha wahi kuja hapa”

    “Hajawahi kuja hapa na wala hatambui kama nipo hapa”

    “Sawa”

    Nikatoka nje na kumkuta mlinzi akiwa amesimama kwenye sehemu ambayo tulimkuta kwa mara ya kwanza na akaniangalia kwa jicho la kuiba na mimi moja kwa moja nikaelekea chooni na kumaliza haja yangu kisha nikarudi huku moyoni mwangu nikiwa na wasiwasi kiasi kwamba nikakosa amani kabisa ya kukaa ndani ya chumba alichopo mama na Emmy.

    “Emmy nakuomba mara moja nje?”

    “Kwema?”

    “Kwema tuu wewe ninakuomba”

    Emmy akatoka na nikamshika mkono hadi sehemu iliyo tulia ambayo si rahisi kwa askari kuniona

    “Hivi tunaweza kumuhamisha mama hospitali?”

    “Kwanini?”

    “Nijibu kama kuna uwezekano wa mama kuhamishwa hospitali ua hakuna?”

    “Uwezekano upo ila ni hatua zahadi yeye kuhamishwa kwenda hspitali nyingine ni ndefu kwa maana hapa ameletwa na serikali ya Tanzania....Ila ni kwanini unahitaji ahamishe kuna nini?”

    “Nafsi yangu imekosa amani kabisa juu ya mama kuendelea kuwa katika hospitali hii”

    “Wasi wasi wa nini wakati hapa maaskari wamejaa wengi na hakuna mtu atakaye weza kumdhuru mama na mimi leo nitakaa naye siku nzima humu ndani”

    “Emmy ninaamini hujui kwa undani hali ya familia yangu pale umesikiliza mamaneno machache wewe mwenyewe umejikuta ukitokwa na machozi sasa sihitaji uweze kulia zaidi ya pale ulivyo kuwa unalia?”

    “Kwa nini unakuwa unananificha kwa kitu ambacho wewe unakihisi?”

    “Kwa sasa huwezi kunielewa ila utanielewa”

    Nikaachana na Emmy na kwenda chumbani kwa mama na kumkuta akiwa anazungumza na madakatari wawili ambao wamejifunga vitambaa vya kijani usini vinavyo fanana na nguo zao walizo zivaa baada ya kuniona mimi wakaniomba nisubiri nje kwa muda.Kusema ukweli nafsi na moyo wangu vikajikuta vikishindwa kuchukua maamuvu ambayo madakatri wameniomba nitoke.Emmy akaingia na akaonekana kuwashangaa madaktari hawa ambao wamejifunga vitambaa jambo ambalo ni tofauti sana kwa madaktari tunao waona kwenye hii hospitali wakiwa wameziacha sura zao wazi

    “Nyinyi ni kina nani?”

    Madaktari wakatazamana kisha mmoja akajikoholesha kisha akaanza kuzungumza kwa sauti ya kujiamini

    “Sisi ni madakatari maalumu tumetumwa na serikali ya Tanzania kuja kuzileta dawa ambazo zinamsaidia muheshimiwa waziri katika kupona”

    “Ngoja mumesema kuwa mumetoka wapi?”

    “Tanzania?”

    “Dawa mumetumwa na nani?”

    “Na wizara ya afya”

    “Hivi nyinyi kama hizo dawa mungeziona zina faida sana si munge mpa mama yangu tangu siku akiwa yupo Tanzania akiwa anaumwa”

    “Hizi dawa kwa hapa hatuna tumeziacha ofisini”

    “Basi nendeni mukazilete”

    Madakatari wakaanza kubabaika kiasi kwamba sote tukabaki tukiwatazama kwa macho makili na hata walivyo toka hawakuga kiasi kwamba wasiwasi wangu ukaanza kupata jibu kwamba kuna mkono wa baba katika swala hili.

    “Mama ninahitaji tuhame hospitalini kwa maana baba anatufwatilia na nisipo angalia ninaweza kufa”

    “Kweli mwanangu?”

    “Basi ngoja nikaonane na daktari mkuu nitakuja muda sio mrefu”

    Emmy akatoka ndani ya chumba na kutucha mimi na mama huku akili yangu ikiwa na kazi ya kupanda nini cha kufanya kuweza kumtorosha mama katika hospitali hii.Baada ya nusu saa Emmy akarudi akiwa ameongozana na daktari mmoja wa kuzungu ambaye ni mtu wa makamo.

    “Mama huyu ndio mkuu wangu wa hapa kazini”

    Daktari mkuu akaanza kutupa mipango ya kufwata ili tuweze kumuhamisha mama katika hospitali hii jambo ambalo kwa mtazamo linachuku muda mrefu wa siku kama mbili kwani nilazima kibali kiweze kutoka katika serikali ya Tanzania na kipitie katika ubalozi wa Tanzania ndipo mama aweze kuhamishwa

    “Basi tutabubiria hadi kesho”

    “Mama Hadi kesho una uhakika na kitu unacho kizungumza?”

    “Eddy kila kitu kinakwenda kwa mpangilio wa kiserikali na ukisema uende wewe kama wewe itakuwa ni shida kumbuka kuwa mimi serikalini nina mamlaka na ninachukuliwa kama kiongozi kwahiyo nakuomba uwe mvumilivu mwanangu”

    “Mama..”

    “Eddy nielewe......Sawa daktari nimekuelewa nyinyi fanyeni hizo hatua na mukihitaji msaada wangu tutashirikiana”

    “Sawa”

    Emmy na daktari mkuu wakatoka nje na kutuacha mimi na mama huku nikiwa ninamipnago mingine ya kuto kumshorikisha mama.Emmy akarudi ndani na kukaa pembeni ya kitanda alicho lala mama

    “Eddy unaoenekana wewe ni mbishi sana”

    “Huyo mwanangu nimesha mzoa ila ana ugonjwa wa hasira kiasi kwamba akiwa anabishana na mtu huwa hapendi kushindwa”

    “Mama achilia na ugonjwa wa hasira ila kuna hatari ipo mbele yako sasa nyinyi endeleni kuniona kuwa mimi sifai”

    Tukaendelea kukaa hadi mida ya saa moja usiku nikamuomba Emmy kunielekeza ni wapi ninaweza kupata sehemu yenye benki ya Backryas na akanielekeza na haikuwa mbali sana na sehemu hospitali ilipo

    “Niwachukulie chakula gani?”

    “Mimi nina chakula changu maalumu huwa ninaletewa na madakatari wa hapa?”

    “Emmy?”

    “Mimi niletee keki na soda ya kopa ya koka”

    Nikatoka na kumkuta askari akiwa anatembea tembea huku na kule akionekana akisubiria kitu fulani kwa hamu

    “Hivi zamu yako wewe inabadilika saa ngapi?”

    “Nani mimi?”

    “Kwani hapa nina ongea na nani?”

    “Mimi zamu yangu inabadilika saa nne usiku”

    “Ahaa powa”

    Nikaachana na askari na kwenda sehemu aliyo nielekeza Emmy na kukuta ATM ya benki ya Backrays na kuchukua pesa kiasi zitakazo nisaidia katika matumizi madogo ya hapa Africa kusini.Nikaingia kwenye mgahawa uliopo karibu na hospitali na kuagizia chakula ambacho nitaweza kukila na nikatafuta sehemu ambayo ninaweza kuuona mlango wa kuingilia katika hospitli na kabla sija letewa chakula nikaona taksi ikiwa imesimama kisha nikamshuhudia baba akishuka ndani ya gari akiwa ameongozana na wanaume wawili na katika taksi nikamuona Sheila akiwa amekaa siti ya nyuma.Kwa haraka nikanyanyuka na kutoka nje ya mgahawa na kutokana na magari mengi ikanilazimu kuvunja seheria za barabara na kujikuta nikivuka kwa haraka barabara na kabla sijamalizia nikashtukia nikikumbwa na gari lililo nirusha na kuangukia pembeni ilipo simama taksi aliyopo Sheila



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikatulia chini kwa muda na kumuona Sheila akifungua mlango kwa haraka na kushuka ndani ya gari na akaonekana kunishangaa baada ya kunijua ni mimi,nikajaribu kujinyanyua ila nikajikuta nikishindwa kutokana na mguu wangu mmoja kutawaliwa na maumivu makali.Nikastuka baada ya kugundua mguu wangu wa kushoto umevunjika japo kichwani na mikononi nimepatwa na michubuko iliyosababishwa na kuaanguka na kuserereka kidogo kwenye barabara ya lami.Sheila akaoanekana kupigwa na bumbuazi kwani hakuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kubaki akinitazama hadi watu walipo anza kukusanyika na kuwaomba wauguzi wa hospitalini kunisaidia,

    Nikawawekwa kwenye machela na kuingizwa ndani pasipo Sheila kuzungumza kitu cha aina yoyote kwangu,Nikaingizwa kwenye moja ya chumba ambacho ni chaupasuaji na kwa haraka nikachomwa sindano za ganzi kwenye mguu wa kushoto ambao umevunjika na kawanipaka mafuta kisha wakamipitishia kifaa maakumu kinachotoa mwanga mwekundu wenye miyonzi mikali huku dakitazama picha inayopita kwenye Tv ndogo iliyopo ndani ya hiki chumba wakaona ni sehemu ya ambayo mguu umevunjika na wakaanza kazi ya kunihudumia

    Ndani ya lisaa moja wakamaliza upasuaji wao na kunifunga bandeji kubwa kisha majeraha madogo madogo wakayapaka dawa kisha wakanihamishia kwenye wodi kitu ambacho ninakiona ni chatofauti ni huku kufanyiwa upasuaji pasiopo kuchomwa sindano ya usingizi.Sikuweza kupata rafiki wa kunijulia afya yangu na kitu kinacho niumiza sana akili yangu ni jinsi hali ya mama ilivyo na kingine sikujua kama ameweza kusalimika mikononi mwa baba ambaye ndio amekuwa adui yetu namba moja kwenye familia yetu.Sikua ya kwanza ikakatika huku nikiwa sijui kitu kinacho endelea ila zaidi nikawa ninahudumiwa na kupewa chakula na wauguzi wa hospitalini.

    Wiki moja ikakatika na hali yangu ikaendelea kuwa nzuri zaidi na nikaanza kufanyishwa mazoezi ya kutembea na siku hii nikamuomba muuguzi kunipeleka kwenye sehemu kilipo chumba alichomo mama na hakusita na kwa mwendo wa taratibu tukafanikiwa kufika ila sikuweza kumpata mama na ikanibidi kumuuliza muuguzi huyu kwa lugha ya kingereza

    “Hivi huyu mama humu ndani amekwenda wapi?”

    “Mama yupi?”

    “Kuna mama waziri ambaye alilazwa humu chumbani”

    “Sijajua labda tukaulize sehemu zenye rekodi ya wagonjwa kwa maana mimi sihusiki katika kitngo hichi na kama unavyo iona hospitali yetu ilivyo kubwa siwezi kuwajua wagonjwa wote”

    “Sawa dada yangu basi nakuomba unifikishe hiyo sehemu wanayo angalizia orodha ya wagonjwa”

    Cha kumshukuru Mungu huyu nesi hana makuu zaidi ya alicho kifanya ni kunipeleka hadi sehemu wanayo angalizia idadi ya wagonjwa walipo kwenye hospitali hii na kadri tunavyo litafuta jina la mama kwenye kumputer yao hawakuliona na ikanibidi niweze kuuliza jina la daktari Emmy na jibu nililo lipata kutoka kwa mfanyakazi wa ofisi hii ya takwimu za hospitali likazidi kunichanganya

    “Hapa hospitalini kwetu hatuna jina la daktari anaye itwa Emmy na dokta anaye anziwa na herufi ya E ni mwanaume na anaitwa Emmanuel”

    “Kweli huyo daktari hayupo....Mbona ana hadi kitambulisho na kitambulisho kinacho muonyesha kuwa yeye ni daktari wa hii hospitali?”

    “Wewe ulikutana naye wapi?”

    “Tanzania na nikapanda naye ndege moja hadi hapa”

    “Mmmm hapa mulikuja lini?”

    “Kama wiki moja iliyo pita”

    “Ngoja kwanza”

    Msichana anayehusika na maswala ya takwimu akanyanyua mkonga wa simy ya mezani kisha akaminya baadhi ya namba na kuiweka simu yake sikioni

    “Kiongozi ninashida moja ninakumba unisaidie”

    “Kuna tatizo limejitokeza la hawa madaktari feki kuendelea kuivamia hospitali yetu na wanaendelea kufanya matukio ya ajabu”

    “Basi ninakuja sasa hivi”

    Akakata simu na kuniomba niogonzane naye huku nesi anaye nifanyisha mazoezi akinishikilia vizuri na tukaingia kwenye lifti na ikatupeleka hadi gorofa ya tatu na tukaingia kwenye chumba ambacho nikakuta tivi nyingi ndogo ndogo ambazo idadi yake kwa haraka haraka zinaweza kufika hamsini na kila Tv inaonnyesha sehemu yake na nikagundua zinaonyesha picha za kamera za ulinzi zilizo fungwa ndani ya hii hospitali

    “Una rekodi za wiki nzima?”

    “Ndio ninazo”

    “Ninaomba utuwekee za siku saba za nyuma”

    Jamaa anaye onekana ndio muongozaji wa kamera za humu hospitali akaigeukia Tv moja kubwa kama nchi 32 kisha akachuku CD ndogo na kuziingiza kwenye deki ndogo na tukaanza kuangalia video zilizo chukuliwa ndani ya wiki moja na nikajikuta nikinyoosha kidole changu kwenye moja sehemu hii ni baada ya kujiona nikiingia hapa hospitalini siku ya kwanza nikiwa na Emmy na kumfanya jamaa kuisimamisha sehemu hii kisha akaisogeza kwa ukubwa kiasi(ZOOM) na kuiangalia sura ya Emmy ambaye alizidi kunichanganya baada ya kumuona dada wa ofisi ya takwimu akitingisha kichwa huku akiibenua midomo yake

    “Mmmm hatuna daktari kama huyu”

    “Kaka hembu peleka mbele”

    Jamaa akairuhusi CD kutembea na kuanza kuangalia picha za mbele na kujiona nikiingia ndani ya chumba alichokuwa mama kipindi ninatoka kuzungumza na Emmy baada ya kuanza kuhisi hali ya ajabu,Video ikamuonyesha Emmy akizungumza na askari ambaye alikuwepo pale mlangoni kisha yeye akaingia ndani huku akiitazama camera ya ulinzi iliyokuwepo juu.

    “Hii ni Camera namba 38 ngoja niweke video zake kwani huu ni mkanda wa jumla”

    “Sawa fanya hivyo”

    “Na huyo askari hapo ni wa hapa?”

    “Askari huyo aliletwa na ubalozi wa Tanzania kumlinda huyo mama.....Kwani wewe huyo mama ni nani yako?”

    “Mama yangu mzazi”

    Jamaa akaito CD aliyokuwa ameiweka kwenye deki kisha akatafuta CD nyingine ndogo na kuuweka kwenye deki yake na tukaendelea kuona matukio yaliyo endelea eneo la nje ya chumba alicho lazwa mama baada ya mimi kuondoka kuelekea banki.Tukamuona askari akipewa soada ya kopo na Emmy na akaianza kuinywa baada ya Emmy kuingia ndani na baada ya muda akaonekana kama anaumwa na tumbo na akandoka katika eneo la nje ya chumba akielekea sehemu vilipo vyoo na baada ya muda kidogo mlango ukafunguliwa na kumshuhudia Emmy akiwa amevalia koti la kidaktari akikisukuma kitanda cha mama huku mama akiwa amefumba macho yake na kulala kama mtu aliye poteza fahamu

    Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio huku nikiema kwa hasira na kujikutani nikiyang’ata meno yangu kwa hasira kiasi kwamba nikatamani nipone kwa haraka ili niweze kumsaka Emmy sehemu yotote akatakayo kuwepo nchini Afrika kusini.Nikashusha pumzi huku nikiwa macho yangu yamebadilika na kuwa mekundu na kujikuta nikikitazama kioo kilichopo ndani ya chumba hichi kinacho nionyesha vizuri sura yangu na kila mtu akabaki akinitazama kwa umakini pasipo kuzungumza kitu chochote

    “Hemu rudisha hiyo CD ya kwanza”

    Jamaa akairudisha CD ya kwanza na kipelea mbele kidogo na kumuona Emmy akimuingiza mama ndani ya gari la wagonjwa huku akisaidiana na watu wawili ambao niliwaona wakishuku na baba huku nao kwa sasa wakiwa wamevalia makoti meupe wakionekana kama madaktari.

    “Kaka hembu simamasha kidogo hape na zoom kwenye kioo cha dereva wa hilo gari”

    Jamaa akafanya kama nilivyo muagiza na akaikuza picha ya dereva na kugundua ni baba japa amevalia miwani huku akiwa amebandika ndevu za bandia na kumfanya aonekane kama mtu wa makamo

    “Kwani Flora ina maana hawa jamaa sio wafanya kazi wa hii hospitali?”

    “Ndio”

    “Mbona wanavitambulisho kwa maana mimi hili tukio linatokea sikustushwa kwa maana ni jambo la kawaida kwa wagonjwa kuhamishwa hapa hospitalini kwetu”

    Nikamshuhudia Flora ambaye ndio muhusika kwenye ofisi ya takwimu akikuna kichwa pasipo kuzungumza kitu cha aian yoyote.

    “Je daktari wenu mkuu yopoje?”

    “Yupoje kivipi?”

    “Yaani muonekano wake?”

    “Ni mweusi kiasi kiasi na sasa yupo Captown kwenye kikao cha madaktari wakuu hapa nchini”

    “Mbona alikuja mzee wa kizungu huyo dada akasema ndio daktari mkuu?”

    “Mmmm atakuwa amekudanganya kwani ni wiki ya pili daktari mkuu yupo kwenye kikao cha madaktari kama nilivyo kuambia hapo awali”

    Sikuwa na lakuzungumza zaidi ya kuumiza kichwa ni jinsi gani ninaweza kumpata mama yangu na moja kwa moja nikajua ametekwa na baba na sikujua ni wapi alipo mpeleka.

    “Tutawasiliana na polisi kuweza kulifwatilia hili tukio”

    “Naombeni mufanye hivyo kwani mama yangu ndio kila kitu katika maisha yangu kwa maana nimetoka Tanzania kwa ajili yake na mwisho wa siku mambo yanakuwa kama hivi”

    “Usijali wa hilo”

    Nikakaa hospitali zaidi ya wiki nne na nikapona kabisa mguu wangu na kufunguliwa bandeji nililo fungwa.Habari za wapi alipo mama kila nilipojaribu kuwaulizia walio sema watalishuhulikia wakadai bado askari wanaendelea na uchunguzi ambao sikujua utaisha lini

    “Kaka gharama zako za hospitalini zimesha lipiwa”

    “Zimelipiwa na nani?”

    “Aliye kulipia ni yule aliye kugonga na gari na yupo nje anakusubiria?”

    Nikaanza kujiuliza ni nani huyu aliye ni gonga na kuwa na moyo wa kujitolea kiasi kwamba amenilipia gharama zote za ajali yangu wakati mimi ndio nilikuwa ninamakosa.Nikatoka nje pamoja na daktari aliye niambia habari hii ambayo kwangu ni nzuri kiasi japo bado akilini nimetawaliwa na wazo la wapi alipo mama.

    Daktari akanionyesha mzee mmoja aliye valia koti jeusi la suti na alinipa mgongo kwani anazungumza na simu,ikatulazimu kumsubiria amalize ndio daktari amjulishe uwepo wetu.Baada ya muda akakata simu na kugeuka na kujikuta nikihamaki kwa kiasi kikubwa kwani mtu aliyepo mbele yangu anafanana kabisa na baba yangu ambaye kwa sasa ni adui yangu namba moja.

    “Habari yako kijana”

    “Sh...ikamaoo”

    Nilipata kigugumizi cha gafla kiasi kwamba mzee naye akaanza kunitazama kwa umakini huku akionekana kunichunguza kuanzi kichwani hadi miguuni.Daktari akatutizama kwa muda na kuzungumza kitu kilicho tufanya sote tumtimame

    “HUYO NI MWANAO?”

    HAKUNA aliye lijibu swali la daktari zaidi ya kukaa kimya kimya na tukageukiana na kuendekea kutazama na kadri tulivyo zidi kutazamana ndivyo nilivyohisi ukweli wa maisha yangu juu ya baba yangu kwani kuanzia macho pua midomo na sura hakuna kilicho pishana na mwenzake kiasi kwamba machozi yakaanza kunilenga lenga huku moyoni mwangu nikijihisi amani na furaha iliyo kuba tofauti na ninavyo kuwa na baba yangu gaidi.

    “Jina lako ni nani kijana?”

    “Eddy”

    “Eddy nani?”

    “Godwin”

    Nikastukia mzee akinikumbatia kwa furaha huku akicheka kwa kicheko kikubwa cha furaha na akaninnyanyua juu kidogo na kuanza kunizungusha kisha akanisimamisha na kunitazama tena usoni huku machozi ya furaha yakimwagika na mimi nikajikuta nikiachia basabu pana

    “Dokta nahitaji vipimo vya DNA na huyu kijana”

    “Sawa ila inabidi na yeye aridhie”

    “Eddy upo tayari kwa hili?”

    “Ndio mzee”

    Sikuweza kumuita baba moja kwa moja japo tunafanana kwa asilimia 99(tisini na tisa) ila nikahofia endapo majibu yatakuwa siyo sijui sura yangu ningeiweka wapi.Tukaingia kwenye maabara nzuri na yakisasa kisha tukachukuliwa damu na kuombwa kusubiri nje.

    “Eddy mimi ninaitwa Godfrey nani Mtanzania japo sasa hivi nina uraia wa hapa Arfrika kusini hii ni kutokana na kuishi miaka mingi hapa Afrika kusini”

    “Ahaa sasa ni kwanini uliondoka Tanzania ilikuwaje?”

    “Ni historia ndefu sana iliyo nipata hadi kufikia hapa ni vikwazo na mambo mengi nilipitia ila ninamshukuru Mungu hadi leo hii nipo salama”

    “Ni kitu gani kilicho kupata?”

    “Ni mambo mengi sana yaliyo nipata na hapa sio wakati muafaka wa kulizungumzia hilo”

    Kabla sijamuuliza swali jengine mlango wa chumba cha maabara kikafunguliwa na akatoka daktari aliye tuchukua vipimo vya damu na kutuomba twende naye ofisini kwake ambapo akatupa mikono huku usoni mwake akiwa na furaha

    “MAJIBU NI ASILIMIA 100 DAMU ZENU ZINAFANA”

    Ikawa ni habari mpya yenye furaha maishani mwangu kwani siku zote kilio changu ni kuhusiana na baba yangu.Baba akanyanyuka kwa fauraha na kunikumbatia huku mkono wake mmoja akiupiga piga mgongoni mwangu,machozi ya furaha yakanibubujika na hata wazo la mama kichwani mwangu kwa wakati huu likafutika kidogo.Baba akatoa simu yake na kupiga namba fulani

    “Andaa tafrija kubwa na waalike watu wangu wa karibu kwani nina kitu cha kuzungumza nao”

    “Fanya hivyo na ndani ya lisaa nitakuwa hapo nyumbani”

    “Waambie ni saa mbili usiku”

    Sikujua baba anatoa maagizo kwa mtu gani kisha akatoa kitabu kidogo cha kuchukulia pesa na kuandika kiasi anacho kijua yeye kisha akampatia daktari na nikaondoka huku nikiwa nimebeba baasha yenye majibu yetu ya DNA.Tukatoka nje na kulekea eneo la maegesho ya magari na dereva aliye valia suti nyeusi akafungua mlango wa gari aina Astorn Martin na kidogo dereva akawa ananishangaa.Safari ikaanza huku kila nilipo tazamana na baba tukajikuta tukitabasamu ikiashiria ni furaha iliyotawala kati yetu

    Geti kubwa likajifungua na mbele yangu kwa mbali kidogo nikaliona jumba kubwa midhili ya ikulu na kuna eneo kubwa lenye kila aina ya kitu cha kuburudika pamoja na bustani kubwa zenye maua ya kupendeza sana

    “Karibu nyumbani mwanangu”

    Kwa wingi wa walinzi walioo kwenye eneo hili hadi nikaanza kuogopa japo ni baba yangu ila sikujiamini sana juu ya usalama wangu

    “Karibu sana nyumbani Eddy”

    “Asante baba”

    Tukashuka kwenye gari huku macho yangu yakitazama tazama pande zote za sehemu tuliyupo.Mlango wa kuingilia ndani ukafungulia na macho yangu yakakutana na seble inayoendelea kupambwa na wafanyakazi na akashuka mama mmoja wa kizungu kwenye ngazi na kuja kumkumbatia baba kisha akambusu mdomoni na mama huyo akabaki akinishangaa

    “Huyu ni nani?”

    “Mwanangu”

    Mama wa kizungu akanipa mkono kwa dharau kisha akaondoka huku akionekana kukasirika kwa uwepo wangu katika nyumba hii hadi nikajihisi vibaya

    “Eddy mwanangu karibu na jisikie upo huru na mwenye amani kwa maana hapa ni kwako”

    “Asante baba yangu”

    Niliitikia kwa sauti ya kinyonge ila moyoni mwangu nikaanza kuhisi kuna mapambano yatakayo endelea kati yangu na huyu mama wa kizungu.Tukaongozana hadi kwenye chumba kikubwa chenye mali nyingi za dhamani na baba akanikaribisha kwenye moja ya kiti kilicho tengenezwa kihalisi na yeye akakaa kwenye sehemu nyingine

    “Una hitaji kinywaji?”

    “Hapana”

    “Sawa Eddy kwanza ninakuomba unisamehe kwa kile ulicho kiona pale mlangoni”

    “Bila samahani kwani yule ni nani?”

    “Yule ni mke wangu wa ndoa ambaye nimefunga naye ndoa miaka mitano iliyo pita”

    “Aaaahaa sasa mbona ameonekana kuchukizwa baada ya kuniona?”

    “Ahaa nahisi hakutegemea kuupata ujio wako leo kwani hata mimi sikuwahi kumuambia kuwa mimi nina mtoto”

    “Sawa na yeye ume zaa naye?”

    “Hapana na sina mtoto mwengine zaidi yake japo yeye naye ana mtoto wa kike hayupo hapa yupo Johnsburg anasoma chuo”

    “Mama yako hivi hajambo?”

    “Siwezi kujiu kama hajambo au anaendeleaje kwa maana alikuwa yupo hospitalini na amatekwa?”

    “Ametekwa na nani?”

    “Ametekwa na baba?”

    “Ina maana kaka Godwin anaweza kumteka mke wake?”

    “Baba hiyo ni historia ndefu sana,na chanzo kikubwa cha mimi kuja huku ni yeye kwa maana alikuwa amelazwa kwenye ile hospitali uliyo nikuta”

    “Duu kweli malipo ni hapa hapa duniani?”

    “Kwa nini baba?”

    “MAMA YAKO NI KATILI SANA TENA ZAIDI YA SANA JAPO USONI MWEKE NI MWAMA KUPITILIZA”

    Maneno ya baba yakanicha mdomo wazi huku nikishangaa nisijue ni kwanini amesema mama yangu ni katili sana

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nikaendelea kumtazama baba kwa macho ya mshangao

    “Mama yako ni katili sana kiasi kwamba aliyaaribu maisha yangu kwa kiasi kikuwa....Kipindi ambacho wewe bado hujazaliwa tulikuwa tunapendana sana na kaka yangu na kwajinsi tulivyokuwa tunapenda tuliamini kwamba hakuna kitu amaco kitaweza kutuchonganisha...Ila ninanakumbuka kipindi baba yaka anaingia jeshini mimi nilifeli majaribio kutokana kipindi kile nilikuwa ninaumwa na ugonjwa wa miguu”

    “Basi baba yako akaja kukutana na mama yako na kutokana kipindi kile sisi tulikuwa ni fukara sana na wazazi wetu walisha fariki ikabidi kaka ambaye nilisha zoea kumuita kurwa aliniomba nihamie kwa mama yako amaye kwa kipindi kile alikuwa ni daktari ila kwao walikuwa ni matajiri sana kwahiyo swala la pesa kwake lilikuwa ni la kawaida......Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1991 ambapo mama yako alianza kujiingiza kwenye mambo ya vyama kwa maana uchaguzi ulikuwa unaelekea miaka ya mbeleni.....Mambo mengi sana akawa ananishirikisha kama mtu wake wa karibu sana kiasi kwamba ikafikia kipindi tukaanza mahusianao ya kimapenzi pasipo kurwa kujua na yeye kwa kipindi kile ilikuwa ni ngumu sana kuweza kujua ukweli kutokana alikuwa yupo kambini kwenye kambi ya jeshi Morogoro na sisi tulikuwa tunaishi Dar es Saalam”

    “Kuseme kweli mama yako alimpenda sana kurwa na mimi alinichukulia kama kituliza nafsi.....Ninazungumza ukweli ili uweze kumjua mama yako vizuri na yale yote aliyo nitendea”

    Nikabaki kimya huku nikiendelea kumsikiliza baba hata mat yenyewe mdomoni hayakuweza kupita sikujua ni kwanini

    “Basi kipindi alipo gundua amepeta mimba yako na ilipo kuwa na wiki mbili akaanza kutengeneza chuki juu yangu na kipindi kile kwa Tanzania masimu yetu yalikuwa ni yale ya mezani hazikuwepo kama hizi za siku hizi,Alipiga simu kambini na kumuomba kaka kuja nyumbani.Basi baada ya kaka kuja akaanza kuniumiza moyo kwa kufanya mambo yao hadharani huku mimi nikiwashuhudia.......Kitendo cha mama yako kutuchanganya kiliniuma sana na nikaapia ipo siku nitamwambia Kurwa kila kitu kinacho endelea ila kitu ambacho ninakijutia hadi leo ni kwajinsi nilivyo anza kumuambia mama yako kwamba nitamwambia kurwa ukweli wote wa mambo tuliyo yafanya na kipindi hicho tayari ujauzio wake ulisha anza kukua”

    “Kitu alicho anza kukifanya mama yako ni kuanza kufanya vitisho vya kutaka kuniua na akaniomba niweze kuondoka Tanzania kama maisha yangu ninayapenda.....Ila kutokana alikuwa na damu yangu tumboni nikawa ninavuta subra niweze kumuona mwanangu amabaye ni wewe....na nililikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwengine ambaye alikuwa amenihifadhi na baada ya mama yako kutambua kuwa ninamwanamke mwengine akatua matu na wakatuvamia sehemu ambayo sisi tunaishi na yule mwanamke....Wa...walimuua kwa kumuingiza chupa sehemu zake za siri na kumkata maziwa na kitendo hicho kilifanyika mbele yangu”

    Baba akatulia kimya huku machozi yakianza kububujika kiasi kwamba na mimi kwa mbali machozi yakaanza kunilenga lenga

    “Na mbaya zaidi yule mwanamke alikuwa na ujauzito wangu wa mwezi mmoja na nusu na akafariki na mwanangu tumboni na mimi wakanichoma sindano ya sumu kiasi kwamba sehemu hii yote ya chini ya mwili wangu ikawa haifanyi kazi,pamoja na kinywa changu kikawa kimepinda kwa na sikuweza kuzungumza kitu cha aina yoyote...Basi ninakumbuka kuna daktari wa kizungu alikuwa ni rafiki yangu sana aliweza kunisaidi na kwake kulikuwa ni huku Africa kusini....basi nilipo muelezea kuhusiana na yaliyo nikuta akaamu kunileta kuhu Afrika kusini ambapo nilifanyiwa upasuaji na ikawalazimu kunikata miguu yote miwili na kutokana yule mzee alikuwa na pesa sana akaamua kunichongeshea miguu ya bandia ambayo ni kama hii unayo iona”

    Baba akanifunulia suruali yake na kuiona miguu yake ya chuma ikifanana kama ya mwanariadha maarufu Afrika kusini ambaye naye ana miguu ya namna hii,machozi yakaanza kunimwagika huku yakiambatana na maumivu makali ya moyo.

    “Basi nilianza kufanya kazi kwa yule mzee na kipindi anafariki hakuwa na mtoto wala ndugu na mali zake zote aliniridhisha mimi na ndio maana unaniona nina mali nyingi kiasi hichi.....Hayo nileyo kueleza ni machache ila kuna mengi sana ambayo mama yako alinifanyia ila kutaoka upo hapa nitakuwa ninakuadisia kila muda utakavyo kuwa unakwenda”

    Baba akatoa kitambaa mfukoni mwake na kunipatia na kuanza kujifuta machozi ambayo yananimwagika na nikabaki nikiwa sina cha kuzungumza kwani sikuweza kuamini kama mama anaweza kumfanyia ukatili mtu aliye mbebea damu yake tumboni.Baba akasimam na kuisogelea meze iliyo jaa mizinga ya pombe kali kisha akachukua mzinga mmoja na akamimina kiasi cha kidogo cha pombe kwenye glasi kisha akapiga fumba moja la pombe hiyo huku akiikunja sura yake akionekana kuwa kitu anacho kinywa ni kikali sana kisha akaviweka mezani na kurudi sehemu aliyokuwa amekaa kisha akashusha pumzi nyingi

    “Eddy nilikutafuta sana mwanangu kupitia sehemu mbali mbali hususani mitandano ya kijamii ila kitu ambacho kilikuwa ni kigumu ni kuto kulifahamu jina lako.”

    Nikaanza kuyaamini maneno ya baba kuwa mama anaroho mbaya kutokana na jinsi alivyokuwa akimkataa Manka na kutaka kumsweka gerezani kwa kunipiga risasa na kitu kingine nilicho kikumbuka ni maneno ya yule dereva taksi ambaye nilipata naye ajali

    “HAAA HUYU MAMA NAYE YUOPO.....KWELI MUNGU HAPENDI DHAMBI KUNA SIKU BWANA ALIKUWA NA DEREVA WAKE SASA KWA BAHATI MBAYA NIKAMCHOMEKEA KWA MBELE ILE BARABARA YA KUINGILIA K.C.M.C NILIKUWA NAMUWAHISHA MGONJWA HOSPITALINI.AHAAAA ALIKWENDA KUNILAZA POLISI HADI SIKU ANAONDOKA ARUSHA NDIO WAKANIACHIA......TENA HAO WATEKAJI KAMA WANAJUA WAMFANYE WA KWANZA KUFA KWA MAANA YULE MAMA ROHO MBAYA SANA”

    Baba akanisogelea na kunishika bega na kuniomba ninyanyuke kisha akaniweka vizuri shati langu na kuniomba twende nje.Akaanza kunitembeza kwenye eneo la jumba lake la kifahari na kwaharaka haraka utajiri wa baba ni mara tano ya utaji alio nao mama.Ila moyoni mwangu sikuweza kuiruhusu chuki iliyopo kati ya wazazi wangu kunitawala moyoni mwangu ila chuki yangu kwa sasa ilibaki kwa baba mkubwa ambaye amemtekana mama akisaidia na Emmy mwanamke aliye jitambulisha kama daktari

    Baba akanionyesha chumba changu kikubwa ambacho nitakitumia kwa kulala na nikikubwa sana na kina vitu vingi sana vya kuvutia japo kwa mama ni tajiri ila baba amezidi kuwa na utajiri mkubwa.Muda wa usiku wageni ambao ni rafiki wa baba wakaanza kukusanyika kwa ajili ya sherehe na kabla ya sherehe kuanza nikawa nipo kwenye chumba maalumu huku nikiwa na mwana mitindo ambaye amenitengenezea suti nzuri inayo endana na mimi na kazi hii ameifanya ndani ya msaa machache jambo ambalo limenishangaza na hapa nikagundua kuwa wezetu wenye nchi zilizo piga hatua wamechangamka sana kwenye utendaji wao wa kazi

    “Unajionaje kijana?”

    Mwanmitindo aliniuliza baada yakuivaa suti aliyo nitengenezea huku nikiwa nimesimama mbele ya kioo nikiwa nimependeza kiasi kwamba hata mimi kimoyo moyo nikaanza kujisifia kabla sijasifiwa

    “Imenikaa vizuri?”

    “Hakuna sehemu ambayo inakupa shida kwenye kutembea au imekubana sehemu?”

    “Sina kila sehemu imekaa sawa”

    “Hembu tembea hadi pale mbele”

    Nikapiga hataa kama sita kisha akaniomba nigeuke na kurudi sehemu niliyo simama awali na hadi ninafika nikasikia makofi yakipigwa na nikageuka na kukutana na mama mke wa baba kwa sasa akiingia kwa mwendo wa madaha hadi sehemu niliyo simama

    “Unaonekena ni kijana mzuri..mtanashati eheee?”

    Sikumjibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kumtazama jinsi anavyo niangalia kuanzia chini hadi juu kwa macho ya dharau

    “Josh ninakuomba utoke na tunataka tuzungumze”

    Mwanamitindo akatoka na kutuacha tukiwa tumetazamana na mke wa baba na baada ya mlango kufungwa sura yake ikabadilika na ikakusanya mikunjo migi ya hasira.

    “Huwezi kuichukua nafasi ya mwangu mbele ya baba yako,sijui amekuokota amekununua,amekuiba ila nitahakikisha hapati chochote kwenye uridhi huu wa baba yako”

    Mke wa baba alizungumza huku sura yake akiwa ameikunja na meno yake akiwa ameyang’ata kwa hasira

    “Sikiliza wewe mwanamke hunijui sikujui sasa kama unaitaji kunijua utanijua kwa herufi kubwa sawa?”

    “Hahaa sina haja ya kukujua omba omba kama wewe usiye na wazazi na nikawaida yenu vijana masikini kama nyinyi hapa Afrika kusini kuwaparamia watu wenye fedha zao na kuwaona ni kama wazazi wenu sasa kama umtumwa na huyo mama yako Malaya aliye shindwa kukulea basi kamwambie nafasi imkwisha”

    Nikamtazama kwa hasira mke wa baba kiasi kwamba mwili mzima ukaanza kunitetemeka,

    “Na kingine nitahakikisha humalizi wiki utakuwa umeondoka ndani ya hii nyumba”

    “Etiii ehee....?”

    “Na hakuna cha Etii ehee mbwa wewe uliye kosa pa kula”

    Nikajikuta nikiunyanyu mkono wangu wa kulia kwa kasi ya ajabu nikaupeleka kwenye shavu la mke wa baba na kabla haumfikia mlango ukafunguliwa na nikamuona baba akiingia na nikaushusha chini kwa haraka na kumstukia mke wa baba akiangua kiliao huku akilishika shavu lake akidai nimepiga kitendo kilicho zidi kunipandisha hasira

    “Mume wangu umeamua kuniletea mwanao aje kuniadhiu mimi....Si ndio?”

    Mke wa baba alizungumza kwa sauti ya kufoka na kumuona baba akiwa amenywea na taratibu akaanza kupiga hatau za kumfwata mke wake

    “Pole mke wangu.....Eddy mwangu mona upo hivyo?”

    “Yaani mbele yangu unamuita huyo ngedere wako mwanao....?”

    “Mke wangu huyo sio ngedere ni mwangangu”

    “Wewe vipi kati ya watoto huyo unaweza kusema ni mtoto hembu muangalie anaonekana hivi hivi ni mama yake ni mbwa koko”

    Maneno machafu ya mke wa baba yakanizidi kunikasirisha hadi nikashindwa kuizuia hasira yangu na kwaharaka nikamchomoa mikononi mwa baba ambaye anaonekana kuwa anamdekeza mwanamke wake.Nikamvuta karibu ya sura yangu huku nikiwa nimelishika sehemu ya kifuani kwake kwenye gauni lake alilo livaa na nikamuona anayafumba macho yake kwa kuongopa

    “Nitakuua”

    Nilizungumza kwa hasira na kumsukumia sehemu aliyoo baba na akamdaka mke wake na wote wakajikuta wakianguka chini kisha mke wake akasimama haraka

    “Niue sasa kama unaweza”

    Nikapiga hataa za haraka hadi sehemu aliyo simama na nikamtisha kama ninampiga kofi akaikuja mikono yake akiuficha uso wake na kwakutuma mguu wangu wa kulia nikipiga teke miguu yake yote miwili na kumrusha juu kidogo kimo cha mbuzi na akaanguka chini kama mzigo na kuendelea kulia,nikapiga goti kwa haraka na kuishika shingo yake na kwa haraka na kumsogelea karibu

    “Usidhubutu siku hata moja kumuambia mama yangu ni Malaya na usinifananishe na mnyamwa wa aina yoyote na kama unataka kunifananisha nifananishe na shetani”

    “Eddy mwanangu ninakuomba utulize jazba msamehe bure tuu”

    Nikaisikia sauti ya baba ikizungumza kwa upole na unyenyekevu na nikamuachia na kusimama na kumaacha akikohoa kohoa

    “Baba kumbe haya ndio maisha unayo ishi na huyu mwanamke asiye na adamu....anakazi ya kukupelekesha kama boya.Wewe ni mwanaume unatakiwa kumtawala mwanamke na si mwanamke kukutawala wewe”

    “Mwanangu usizungumze hivyo”

    Baba alizungumza huku akiinama na kutaka kumpa mke wake mkono ili amnyanyue na kwa haraka nikaiwahi mikono yao na kuichanisha

    “Muache anyanyuke mwenyewe na tuone sasa kama atashindwa kunyanyuka”

    Nikamsogeza baba mbali na mke wake ambaye akanyanyuka taratibu huku sura yake ikiwa imejaa machozi na aibu na akawa ananitazama kwa macho wiziwizi na akaanza kupiga hatua za haraka kuelekea mlango ulipo na kabla hajaufikia nikamuita kwa sauti ya ukali na akasimama na nikamfwata hadi sehemu alipo simama

    “Kinacho kuliza ni nini?”

    “Mmmm hakuna kitu”

    “Futa machozi”

    Mke wa baba akaanza kufuta mchozi kwa kutumia gauni leke kisha akabaki akinitazama ninavyo hisi hakuamini kama mimi ninaweza kufanya nilicho mfanyia mbele ya mume wake

    “Nenda kajiandae na kwenye sherehe ninakuhitaji nikuone na nitakaa na wewe”

    “Sawa”

    Mke wa baba akatoka na kuufunga mlango kwa nguvu na kunifanya nianze kucheka na baba naye akanifwatia kwa kucheka

    “Baba hivi huyu mke wako unaishi naye vipi?”

    “Wee acha tuu mwanangu,Afadhali umekuja na wewe kwa maana huyu mwanamke ananipelekesha sana yaani hadi ikifikia kipindi nikirudi nyumbani tuu furaha yote inanipotea”

    “Sasa kwanini na wewe baba unakuwa hivyo?”

    “Yaani hata mimi mwenye sielewi ni kwa nini yaani akizungumza yeye huwa mimi sina la kubisha kwake”

    “Kwani umeomtoa wapi?”

    “Ahaa naye ana historia yeke ndefu tuu nitakusimulia siku nyingine...sasa hivi twende kwenye sherehe nahisi imesha anza na wanatusubiria sisi”

    “Sawa baba”

    Tukatoka na baba chumbani na kukuta mwana mitindo mlangoni na baada ya kuniona anakisimamisha na kuanza kuiziweka nguo zangu vizuri kisha akatoa viatu vinavyoendana na suti niliyo ivaa ambayo ni ya rangi ya bluu na nikavua viatu nilivyo vivaa na kuvaa alivyo nipa kisha tukaelekea sehemu yenye bustani iliyo pambwa vizuri na kukutana na watu wachache ila wamevali vizuri.Tukakaa sehemu ambayo tumeandaliwa na muongoza sherehe akaendelea na kazi yake,Macho yangu yakawa na kazi ya kutafuta ni wapi alipo mke wa baba na nikamuaga baba ninaelekea msalani(chooni) na akamuomba mlinzi wake mmoja kunifikisha msalani

    Nikapita kwenye moja ya kordo na kumuona mke wa baba akiwa amekumbatiana na jamaa mmoja huku wakiwa wananyonyana midomo yao,mlinzi naye akashuhudia tukio hilo na nikataka kwenda ila jamaa akanizuia na kuitoa simu yake mfukoni na kupiga picha kadhaa na tukaendelea na safari yetu huku moyoni mwangu nikizidi kupata maumivu nikijiuliza ni kwanini baba anaishi na mwanamke wa namna hii

    Nikamaliza haya zangu na tukarudi kwenye bustani na hatukuwaoa kwenye eneo walilo kuwepo,Nikamkuta mke wa bab akiwa amekaa pembeni ya baba huku akicheka akimtazama mchakeshaji anaye endelea kufanya yake.Nikajikausha huku mara kwa mara nikimtazama kwa macho makali na nikazidi kuumia pale anavyo mbusu busu baba machavuni na mdomoni akijifanya kama anampenda sana baba

    Wakati wa kutambulishwa ukawadia na baba akanitambulisha kama mimi ndio mridhi wake wa pekee kitendo kilicho mchukiza mke wake japo kila nilipo mtazama akatabasamu akiashiria kuwa anafuaha moyoni mwake.Sherehe ikaisha huku moyoni mwangu nikitamani kumuambia baba juu ya tukio alilo lifanya mkewe ila nikaona hatomfanya kitiu chochote.Nikaelekea chumbani kwangu na nikaoga na kupanda kitandani na mawazo ya wapi alipo mama yakanza kunitawala kichani kwangu

    Nikanyanyuka na kuisogelea meza iliyo na kumputer aina ya HP,nikaiwasha na kwabahati nzuri nikakuta imeunganishwa na hudumu ya internet.Nikaingia kwenye mtandao unao husiana na taarifa za serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Nikaanza kutafuta tafuta habari itakayo husiana na mama na nikakutana na habari ya iliyo andikwa kwa maandishi makubwa ikisema

    “WAZIRI WA AFYA ATOROSHWA HOSPITALINI HUKO AFRIKA KUSINI ALIPOKUWA AMELEZWA”

    Nikaanchana nayo kwani ni habari iliyo tolewa mwezi na nusu ulio pita na nikakutana na taarifa nyingine inayo husiana na mama

    {“BI GRACE INASADIKIKA AMETEKWA NA KUNDI LA KIGAIDI LA AL-SHABABI”}

    Mapigo ya moyo yakaanza kuniende mbio na nikaifungua taaribu hiyo na kuanza kuisoma huku mwili mzima ukinitetemeka hadi nijajikuta ninacho kisoma sikilewi.

    {“Mume wa Bi Magreti bwana Godwin amabeye ni mkuu wa jeshi kikosi maalumu amedai kuwa mke wake ametekwa na magaidi hao ambao wanahitaji kiasi cha dola za kimarekani milioni 50 kutoka kwenye serikali ya Tanzania ili kumuachia huru waziri huyo”}

    {”Raisi aishutumu serilakali ya Afrika kuwa hawapo makini katika swala la ulinzi viongozi wanao toka nchi mbalimbali wanao lazwa kwa ajili ya matibabu katika hospitali zao”}

    Nikajikuta nikijikuna kichwa kiasi kwamba nikahisi nywele nitazitoa kwa kuzivuta.Moyo kwa moja nilajua kuwa mama hajatekwa na kundi hilo la magaidi kama inavyo semekana na moja kwa moja atakuwa ni baba ambaye kwa sasa anajifanya kuwa watekaji ni kundi la Al-shababi.Nikaendelea kutafuta habai nyingine na kukutana na habari nyingine ikesema

    {“HIZI NDIZO PICHA ZINAZO MUONYESHA WAZIRI BI MAGRET AKIWA MIKONONI MWA MAGAIDI WALIO TOA SIKU KUMI NA TANO KWA SETIKALI YA TANZANIA”}

    Nikaanza kutazama picha moja baada ya nyengine na kumuona jinsi mama alivyo fungwa kitambaa cheusi machoni mwake huku kichwani mwake akiwa amewekewa mitutu kama sita ya bunduki aina ya SMG.Machozi yakaanza kunimwagika baada ya kuiona picha nyingine ya mama akiwa amechorwa maandishi ya kiarabu yenye rangi nyekundu kwenye kifufua chake huku mkono mmoja wa mtu ulio valia gloves nyeusi ukimshika kwenye sehemu ya chini ya kidevu chake huku akimminya mashavu yake kwa nguvu

    Nikajikuta mkono wangu ukielekea kwenye kitufe cha kuzimia computer na kurudi kitandani huku machozi yakinimwagika na hasira ikawa imenikaba kifuani mwangu hadi nikahisi kifua changu kinaweza kunipasuka.Sikupata usingizi hadi asubuhi na kitu cha kwanza nikamsubiria baba ili nimpe taaria hiyo.

    Baba akanikuta nimekaa sebleni nikiwa nimeshika tama na baada ya salamu nikamuomba nizungumze naye na akakubali na akakaa pembeni yangu na nikanza kumsimulia kuanzai A hadi Z kwa hali aliyo kuwa nayo mama

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa hapo tutafanyaje mwanangu?”

    “Una hizo milioni 50?”

    “Mmmm hicho ni kiasi kikuwa cha pesa japo ninacho ila ngoja kwanza tujua hiyo hali itakwenda vipi?”

    “Basi inanibidi nirudi Tanzania leo?”

    “Kwa leo mwangu siwezi kukuruhusu kurudi Tanzania ila ngoja nitwapa hiyo kazi wafanya kazi wangu hiyo kazi”

    “Wataiweza kweli?”

    “Ndio ila sio hawa una waona hapa kuna wengine nitawapa”

    “Lini utawapa?”

    “Leo ngoja tupate kifungua kinywa kisha tutakwenda kwa hao watu wangu na sipendi waje hapa kwani wanatafutwa sana kwa matukio wanayo yafanya inanibidi tuwafwate”

    “Sawa”

    Tukapata kifungua kinywa kisha nika tukajiandaa kwa ajili ya kwenda alipo ndiambia baba na tukatumia gari jengine ambao linaendesha na yule mlinzi wake wa jana sukiku,Ndani ya gari sote tukawa kimya huku akili yangu ikiwa inamuwazia mama yangu.Tukafika kwenye gorofa moja na baba akashuka

    “Eddy nisubirini nikaongee na kiongozi mmoja hapa wa jeshi kisha tutawafwata hao watu”

    “Sawa baba ila nina ombi”

    “Ombi gani mwanangu?”

    “Baba ninaomba pesa ya kununua simu kwa ajili ya mawasiliano”

    “Sawa”

    Baba akatoa kikadi cha banki na akaniandika namba zake za siri kwenye kikaratasi na kumuomba dereva wake anipeleke kwanye ATM za banki na kish yeye akaingia kweye ndani ya gorofa na sisi tukaondoka.

    “Kaka hivi simu za gharama huku nitazipata wapi?”

    “Maduka yapo mengi tuu utakapo hitaji wewe nitakupeleka”

    “Maduka yanatumia pesa aina ya dola au Rand”

    “Inategemea na duka lenyewe linatumia pesa ya aiana gani ila ninakushauri ukatoa dola ya marekani”

    “Sawa utanirushia zile picha za jana”

    “Sawa”

    Tukafika kwenye gorofa ambalo lina mashine za kutolea pesa(ATM) na tukashuka ndani ya gari na jamaa akabaki njea na mimi nikaingia ndani.Nikachukua kiasi cha pesa ya kunitosha hata kwa matumizi mengine kisha nikatoka nje na kumkuta jamaa akiminyana na dada aliye na nywele zilizo changuka huku dada huyo akiwa amenipa mgongo na mavazi yake yakiwa yamechafuka na kuchanika chanika sana.Mwili wake umejaa ukurutu na amepauka sana huku ukiwa umedhohofika sana japo anaonekana kuwa na nguvu nyingi na kwaharaka haraka nikatambua kuwa dada huyu ni kichaa

    “Eddy nenda kwenye gari ninakuja sasa hiv....khaaa”

    Jamaa alipiga kelele baada ya dada huyo kumng’ata kwanye mkono kisha akanigeukia na mimi na kujikuta nikibaki nikiwa nimesimama huku nikiwa nimemshangaa kichaa huyu kwani ni Sheila mpenzi wangu ambaye mara ya mwisho kumuona ni siku niliyo gongwa na gari.Nikiwa nimesimama Sheila akamuachia jamaa na kunirukia mimi na sote tukaanaguka chini huku nikijitahidi kumshika kichwa chake anacho taka kuning’ata kwa meno yake yaliyo machafu huku akidondosha udenda mwingi na akinguruma kama mbwa mkali mwenye njaa kali

    Mlinzi akamuwahi Sheila na kumnyanyua juaa na lipindi tukio linatokea askari waliweza kuliona na wakamkamata Sheila na kabla hawajaondoka naye nikawazuia

    “Jamani samahani kaka zangu ninamuhitaji huyo binti”

    “Huyu ni mwenda wazimu na ametoroka katika hospitali ya vichaa na karibia wiki sasa tunamtafuta”

    “Sawa nimewaelewa sijui tunaweza tukaongozana hadi sehemu ilipo hiyo hospitali?”

    “Kwani wewe unamfahamu huyu binti?”

    “Hapana ila ninahitaji kuweza kuyafahamu maendeleo yake”

    Askari wakanitazama kisha wakaniruhusu kama kuongozana nao,tukaingia kwenye gari letu na kuongozana na askari hadi kwenye hospitali ambayo ni yawatu walio pungukiwa na akili.Sheila akakabidhiwa kwa madaktari na polisi wakanionyesha sehemu ambayo ninaweza kupata kawimu za maendeleo ya Sheila,

    “Samahani dada yangu”

    Nilimuuliza nesi mmoja niliye mkuta kwenye dirisha la kuudumia wateka wanao hitaji huduma kwenye hospitali hii

    “Bila samahani”

    “Kuna mgonjwa ameletwa dakika tano zilizo pita na ninaomba kuweza kujua takwimu zake za nyuma”

    “Ahaaa juyo dada aliyeletwa hapa akiwa hajitambui na kadris siku zilivyo zidi kwenda alikuwa msumbufu anapiga wezake hadi kunasiku alimuua mwenzake mmoja kwa kumpiga kwa chupa kichwani”

    Nikajikuta nikiwa nimeuacha mdomo wangu wazi kwa mshangao kwa maana sikutegemea kusikia taarifa kama hiyo

    “Labda tatizo leke kubwa haswa ni nin?”

    “Mmmm kwa mimi siwezi kujibu labda ngoja nikukutanishe na daktari ambaye alikuwa akimuhudumia tangu siku ya kwanza alipo kuja”

    Akanyanyua mkonga wake wa simu na kuzungumza na mtu aliyo upande wa pili wa simu kisha akaniomba niweze kuingia ndani kwenye ofisi ambayo ipo upande wangu wa kushoto na ikanilazimu kumuacha nje dereva,Nikamkuta daktari wa kiume mwenye umri mkubwa kiasi na akaniruhusu nikae pembeni kwenye kiti

    “Nikusaidie nini kijana?”

    “Kuna mgonjwa ambaye ameletwa muda mchache ulio pita na sijui ninaweza kupata taarifa yake ya nyuma?”

    “Wagonjwa walio letwa muda mcha ulio pita ni wengi labda wewe unamzungumzia yupi kati ya hawa?”

    Daktari akawasha Tv yake kwa kutumi rimoti na nikaziona picha za Sheila akiwa ameshikwa na askari

    “Huyo picha namba tano”

    Nilimuonyesha daktari kwa kutumi kidole na akaizima Tv yake na kunigeukia huku akisaidiwa na kiti chake chenye uwezo wa kuzunguka

    “Huyo hapa sisi tunamuita Vaiper Lady”

    “Kwa nini?”

    “Kwanza nimkali na ninamfananisha na hao nyoka ambao wanasifa ya kung’ata sana,Pili hatulitambui jina lake halisi ni nani”

    “Sawa ila tatizo lake ni nini?”

    “Huyu binti amedhirika sana kiakili hii ni kutokana na mambo magumu ambayo ameweza kupitia huku nyuma.Pia ubongo wake umetingishika kiasi kwamba imemfanya akili zake kufyatuka”

    “Akili yake imetingishika?”

    “Ndio ina maana aliweza kupigwa kwa kitu kizito kichwani ambacho kiliipelekea akili yake kucheza kidogo na jambo kubwa la kumshukuru Mungu ni kwamba mishipa ya damu haikuweza kupasuka kichwani mwake”

    “Anaweza akapona?”

    “Mmmm sidhani kwa maana sisi tumejaribu kutumia ujuzi wetu mwingi ila tumeshindwa ila kitu kibaya zaidi huwa hapendi kuona jinsia ya kiume na alashawahi kufanya tukio la mauaji kwa….”

    “Hili nilisha ambiwa……Sasa dokta imi ninahitaji kukaa naye kwa ukaribu sana ili niweze kumtuliza”

    “Wewe kijana unahitaji kufa au…..kwa maana hataki kuona jinsia yoyote ya kiume”

    “Mimi nitaweza dokta na Mungu akibariki kesho nitakuja kwa kazi hiyo”

    “Mmmm kwa kweli si……”

    Nikachomo noti mbili za dola mimi kwenye mfuko wa suruali na kumuwekea daktari mezani na akanyamaza

    “Kaka utahitaji kiwango kingine zaidi ya hicho nitakupatia”

    Daktaria akanyamaza kimya na kushindwa kuzungumza kwa aibu na nikanyanyuka na kumuacha akiwa ananishangaa.Hali ya furaha ikanitoweka kabisa na hata ndani ya gari nikawa kimya huku nikimuwazia Sheila na sikusema kuwa ninamfahamu Sheila hii ni kuepuka maswali mengi yasiyo na msingi kwangu.Tukaingia kwenye moja ya duka la simu na kununua simu aina ya Blackbery.Tukarudi kwenye jengo ambalo baba aliingia na kumkuta akiwa anatusubiri

    “Mbona mumechelewa?”

    “Ahaa kuna sehemu sehemu nilipitia”

    “Hiyo simu umesha nunua?”

    “Ndio baba”

    “Sasa turudi nyumbai kwa maana lile swala nimesha likabidhi kwa wahusikana wameniahidi ndani ya siku mbili watanipa jibu”

    “Kweli baba?”

    “Ndio wewe kuwa na amani na kama utataka kuendelea kutazama tazama mji nipige simu nyumbani nije kuchukuliwa na gari nyingine?”

    “Hapana kwanza nimechoka ninahitaji kupumzika kidogo alafu ninaomba namba yako baba”

    “Sawa”

    Baba akanipatia namba yake ya simu na kutokana sikuwa na line ikamlazimu kunipa laini yake moja ya simu ambayo haitumii sana.Tukarudi nyumbai huku msongamano wa mawazo ukiwa umenitawala na moja kwa moja nikagundua baba wa zamani mzee Godwin ndio chanzo cha Sheila kuwa katika hali kama hii.Sikuweza kupata suingiza kabina na kila nilipo jaribu kuivuta amani kutawala usoni mwangu nikajikutani kishindwa kabisa na sura yangu ikawa imetawaliwa na mikunjo ya hasira.Nikiwa nemekaa kwenye moja ya masofa ya kupumzikia yaliyopo kwenye bustani yenye maua mengo mazuri na kuna kijibwawa kidogo chenye maji masafi na upepo mwingi nikamuoana mke wa baba akiwa na yule jamaa wa jana usiku wakiwa kwenye moja ya kijijumba kilicho kwa vioo na ndani yake kukiwa na maua mengi yanayo uteshwa kwa masaada wa mwanga wa jua

    Wakanza kushikana shikana na mwisho wa siku wakanza kupeana mambo ya chumbani bila kujali kama wanaweza wakaonekana na mtu.Nilicho kifanya ni kurekodi tukio zima mwanzo hadi mwisho hadi wanamaliza na jamaa akawa wa kwanza kutoka na baada ya dakika kama kumi mke wa baba naye akatoka huku akijifanya kunusa nusa kipande cha ua alicho toka nacho na kwabahati mbaya macho yetu yakakutana na akanipandisha na kunishu kiasi kwamba akaanza kunikera

    “Mama ninakuomba”

    Akatembea kwa mwendo wa madaha huku mdomo wake akiwa ameubenua kiasi kwamba nikaanza kujiuliza sijui kipigo cha jana amekisaha

    “Unasemaje?”

    “Hivi baba yangu ni nani kwako?”

    “Khaa wewe unamuona ni nani?”

    “Jibu nililo kuuliza”

    “Ni mume wangu”

    “Una uhakika na unacho kizungumza?”

    “Ndio kwa maana hata pete hii hapa ninayo”

    “Unajua siku zote kwenye maisha usipende kumfanyia mwenzako kile usicho penda kufanyiwa”

    “Una maana gani?”

    “Utaijua wewe nenda zako”

    Akaniandisha kuanzi chini hadi kitendo ambacho maishani mwangu sipendi mwanamke anifanyie akaachia msunyo mkali uliao nifanya ninyanyuke kwa haraka na kumfwata kwa hasira na akaanza kukimbia ila kutonaka na uwezo wangu wa kukimbia nikamdaka katika mlango wa kuingilia sebleni na kukutana na baba akiwa anatoka ndani

    “Huyu mwanao ni mwenda wazimu nini?’

    Sikumjibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kumfwata na nilipo sikia swala la uwenda wazimu na mimi nikajichetua sana na ili nionekane ni mwenda wazimu kweli.Tukaanza kazi ya kukimbizana huku tukimzunguka baba aliye kosa kitu cha kuzungumza,

    “Mume wangu mkamate mwanao atanijeruhi”

    Na mimi nikaanza kuuigilizia mlio wa Sheila alio kuwa akiningurumia na kumfanua baba kuhamako na kadri muda unavyo kwenda ndivyo nikazidi kujichetua kaisi kwamba baba akaagiza walinzi wake kunikamata na wakashauriana wanipeleke hospitali ya vichaa kwa ajili ya vipimo zaidia.Kwa bahati nzuri tukafika kwenye hospitali tuliyo toka masaa machache yaliyo pita na kwabahati nzuri daktari aliye pewa jukumu la kunipima na yule niliye mpa dola mia mbili na akawa ananishangaa kuniona nikiwa nimeletwa kama mgonjwa

    “Dokta wakikuuliza waambie kuwa itanibidi hapa nikae kwa wiki mbili”

    Nilimuambia daktari baada ya baba na watu wake kutoka nje ya chumba nilicho ingizwa

    “Saaa….saaa”

    “Dokta acha kupata kigugumizi wewe waambie hivyo kuwa mimi ni mgojwa na mutaniweka hapa kwa wiki mbili ili kunichunguza zaidi na kama ni pesa mimi nitakulipa ila hili ni dili kati yangu mimi na wewe”

    “Sawa nimekuelewa”

    Daktari akanipima pima kiuongo ili kupoteza muda kisha akatoka na baada ya muda baba akaingia huku akiwa na sura ya unyongee na kwambali machozi yanamlenga lenga

    “Ohhooo Eeeehee baba ukuwaa mkubwaa kamaaaaa John Cennaaaaaa hahaaa…babaaa huuuyoooo katokaaaa kaziiiniiiiiiiii ohooaaooa”

    Niliimba nyimbo za kuwehuka na kuzidi kumfanya baba aamini kuwa mimi nimepata kichaa

    “Dokta kweli mwangu atapona?”

    “Kama nilivyo kuambia hapo awali tunamuweka hapa ndani ya wiki mbili kisha tutaangalia jinsi maendeleo yake yanatavyo endelea”

    “Ahahaa doktaaa wiki mbiliiiii hahajhhhaa mimi takaaa kaaaa mwakaa mzimaaaa baaaabaaa lia liaaa kama totojingaaaaaa hahaahaa”

    Nikazidi kuzungumza huku nikirusha rusha miguu na mikono na ikawalazimu watu wa baba kunilaza kitandani na kunifunga mikono na miguu kwa kitumia mkanda maalumu uliopo juu ya hichi kitanda nilicho lalia

    “Ohoo Mungu wangu sijui ni kitu gani kimempata mwanangu?”

    “Usiwe na wasi wasi atapona tuu cha msingi ni kumuomba Mungu aweze kumjalia afya njema”

    Baba akanitazama kwa sura ya simanzi na akashindwa kuyazuia machozi yake na akaanza kulia na ikamlazimu mlizi wake mmoja kutoa kitambaa na kumkabidhi baba kisha akatoka naye nje na walinzi wake wengine wawili wakafwatia nyuma

    “Dokra wachungulie wamesha ondoka?”

    “Ngoja niangalie”

    Dokta akafungua mlango na kuchungulia kisha akaufunga na kunifwata kitandani huku akiwa anacheka

    “Ndio wamesha ondoka….hivi wewe kijana mbona msanii kiasi hichi?”

    “Ahaaa uanajua unapo amua kufanya kitu mtu inabidi uweze kufanya juu chini unakifanikisha hata kwa staily kama hii pia ni vyema si umeona sasa mpaka mzee ame….hahaaaa chipissssisisisisiiii oohoooo”

    Nilirudi katika hali yangu ya kuchanganyikiwa baada ya mlango kufungulia na wakaingia majamaa wawili wenye misuli na wamevalia makoti meupe na suruali nyeupe

    “Huyo naye dokta ana tatizo gani?”

    “Ahaa mchukueni mumpeleke kwenye chumba chake”

    Jamaa wakanifungua mikanda na kuninyanyua kwa nguvu na mmoja akanishika mkono wa kulia na mwengine mkono wa kustoto,tukatoka nje ya chumba na kuwaona baba na watu wake wakija kwenye ofisi ya daktari na ikanilazimu nianze kuchetuka kama kawaida huku nikijirusha rusha juu na kuwafanya majama hawa kutumia nguvu zaidi katika kunibana,Baba akawaomba wasimama kisha akasimama mbele yangu na kunitazama kwa muda huku akijikaza kuto kulia.Akanikumbatia na kuwaruhusu jamaa wanipekeleke wanapo nipeleka

    Nikaanza kupata woga kwa maana kila nilipo pita vichaa wakiume walianza kushangilia huku wengine wakiwa na sura za ajabu ajabu

    “Sasa dokta naye tulimuuliza anatatizo gani huyu hajatujibu sasa tutampeleka kwenye wodi gani?”

    “Kwa jinsi ninavyomuona tumuingize wodi namba nano itamfaa”

    Jamaa wakashauriana na kweli wakaniingiaza kwenye wodi yenye vitanda vingi na vingi vinawatu ambao kwa muonekano wao ni vichaa walio pitiliza na mbaya zaidi wengi wana miili mikubwa kupita maelezo kiasi kwamba kila nilipo pita walinitazama kwa macho makali.Jamaa wakanionyesha kitanda changu kisha wakatoka kwa haraka huku wakionekana kujishuku.Majamaa matatu yakasimama kwenye vitanda vyoa na kuanza kupiga hatua za kunifwata kitandani huku ikinguruma kama mimbwa inayo gombania mke mmoja,mapigo ya moyo yakazidi kunidunda huku kijsho kikinimwagika kiasi kwamba ubabe wangu wote ukaniishia

    Majaa yakanitazama kwa muda huku yakinguruma na yakaanza kunishika shika kichwa changu huku kila mmoja akitaka nimtazama yeye,Nikastukia kofi moja takatifu likitua kwenye sikio langu na kusababisha uwezo wa kuona vizuri ukakata na kuona vitu vyenye alama kama nyota nyota vikielea angani kiasi kwamba nikajikuta nikiona giza lililo endana na ukungu.Nikastukia nikiwa nimelala chini sakafuni wala sikujua nimeshuswaje kwenye kitanda.Makelele ya vichaa wengine yakazidi kunichanganya kiasi kwamba nikawa sielewi nini cha kufanya.Kipigo kutoka kwa haya majamaa ambayo yanaonekana ni mababe kwenye hii wodi kikanifanya nijikunyate huku nikilia kwa uchungu.Nikaingia chini ya uvungu wa kitanda ili kujinusuru kwani inadi ya vichaa wanao nishambulia ikaongezeka,Nikastukia nikivutwa miguu yangu na wakaanza kuniburuza huku wakishangilia kwa nguvu

    Maumivu makali yakazidi kuniumiza kiasi kwamba nikajuta kwa uamuzi nilio uchukua.Wakanigongesha gongesha kwenye kwenye vitanda kisha wakanilaza kwenye kordo iliyo tenganishwa na vitanda na wakanizunguka huku wakinitaza na vijamaa viwili vyembaba vikapanda juu ya vitanda nawezao wakaacha nafasi na sikujua wanataka kufanya nini,Nikastukia wa kwanza akijirusha na kunifanya nimkwepe na akapiga kichwa kwenye sakafu na kutulia tuli.Wa pili akafanya kama alivyo fanya mwenzake na akanitulia kwenye tumbo na kunifanya nitoe ukulele mkali wa maumivu huku kicha kizima kikiwa kimejaa manundu ya kipigo nilicho kipata

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikastukia wakianza kunikojolea huku wakicheka kwa furaha na kupeana mikono na kunifanya nizidi kulia kwa uchungu japo hasira imenipanda sikuwa na uwezo wa kufanya chochote dhidi yao.Wakatawanyika na kuondoka kila mmoja akarudi kawnye kitanda chake na wakaniacha nikiwa nimejilaza chini pamoja na kale kajamaa lalicho nirukia.Nikaanza kujivuta taratibu hadi kwenye kitanda changu huku mwili mzima ukiwa ninanuka mikojo pamoja na kuvimba juu na nikakaa na baada ya muda mlango ukafunguliwa na wakaanza kutoka mmoja baada ya mwengine.Akachugulia daktari mmoja na kutuona ndani ya chumba tumebaki wawili na baada ya muda wakaingia madaktari wanne ambao wawili wakanifwata mimi na wawili wakaenda kwa kale kalicho zimia

    “Huyu ni mgeni eheee?”

    “Naona”

    “Ahaaa wageni huwa wanapata shida sana”

    “Kweli kwa maana walivyo mfanya mmmm ni zaidi ya maumivu”

    Madtari wakaendelea kuzungumza huku wakinihudumia na kuniweka kwenye machela na kunihamisha kwenye na kuniingia kwenye chumba cha matibabu.

    Ndani ya siku nne nikawa nimepona vuzuri japo sio sana kwani kuna baadhi ya sehemu zinamaumivu kidogo.Nikarudishwa kwenye wodi ambayo nilitembezewa kichapo na nikaanza kazi yangu rasmi ya kumtafuta Sheila kwenye kila sehemu ya hospitali hii,Ndani ya siku mbili sikuweza kumuona Sheila na sikujua ni wapi alipo,Nikaanza kuzoeana na vichaa kadhaa ambao ni wanyonge kama mimi kwa maana jinsi watu wanavyo ishi kibabe kwenye hii hopitali inasababisha kuwemo na mgawanyiko wa vichaa wababe na vichaa wanyonge.Wakati wa kuoga ukawadia na kama kawaidi kila wodi ina mabafu yake ambayo muda wa kuoga unapo wadia ni wote tunatakiwa kufanya hivyo.

    Nikatafuta sehemu isiyo na mminyano na kusimama na kuwatazama jinsi vichaa wengine wanavyo minyana kwenye kuoga.Wakaoga wote kisha wakatoka na mimi nikanza kuvua nguo zangu na kabla sijamaliza kuzivua akaingia lile jijamaa ambalo lilinizaba makofi pamoja na wezake na baada ya kuniona likaanza kunguruma na kuanza kunifwata na nikajiandaa kwa chochote atakacho hitaji kukifanya kwangu mimi.Likanisimamia mbele yangu huku likinitazama kisha likanitisha kama ninataka kunipiga kofi na kujikuta nikiinama huku mikono yangu nikiwa nimeiweka kichwani kuziba uso wangu na nikastukia likaanza kucheka sana hadi likakaa chini kwa kucheka na ikanibidi na mimi kuanza kucheka

    Hata hamu ya kuoga ikaondoka na kujikuta nikivaa nguo zangu na kutoka bafuni.Kama kawaida muda wa michezo ukawadia na kila kichaa anaye penda mchezo wake anakwenda kwenye eneo lenye kiwanja cha mchezo wake.Nikaanza kuzunguka zunguka nikaangalia jinsi vichaa wanavyo fanya mambo ya ajabu kusema kweli inahitaji moyo wa uvumilivu kuishi nao kwa maana kama akili yako ni nzima basi ukishindwa kuvumilia unaweza ukawaambia madaktari kuwa umepona.Nikakuta wasichana watatu vichaa wakiwa wamekaa chini wakichora chora na katika kuwachunguza vizuri nikamuona Sheila akiwa katikati yao

    Na mimi nikajisogeza karibu yao na kukaa huku nikimtazama Sgeila jinsi anavyo chora chora cini kwa kkutumia kijiti huku akifuta futa.Wezake wakasimama na kuondoka zao na akabaki peke yake.Sheila hakuinyanyua sura yake kunitazama na akazidi kuchora chini huku akikigandamiza sana kijiti chini na akiwa anaonekana kama anahasira kali.Machozi yakaanza kumwagika kiasi kwamba akafuta alicho kichora kicha akaanza kuandika herufi moja moja kwa uchungu

    {I…….L…..O…….V…….E}

    Nikabaki nikimuangalia huku kwa mbali na mimi machozi yakinilenga lenga kwani afya yake imedhohifika sana isitoshe mwili wake umetawaliwa na makovu mengi sana ambayo yamemfanya azidi kuonekana mbaya.Akayafuta maandishi yake kisha akachora vikatuni viwili kimoja kikiwa cha kike huku kingine kikiwa cha kiume na akavipatia majina kwa herufi za mwazo ambacho kikatuni cha kike akakiandikia herufi kubwa ya ‘E’ huku cha kike akikiandikia kiherufi cha ‘S’.Hapo ndio nikashindwa kuzizuia hisia zangu na kujikuta nikimwagikwa na machozi na kumuona Sheila akiinyanyua sura yake tartibu na kuniangalia kwa muda kisha akairudisha sura yake chini na akanitazama tena kwa umakini huku akiwa kama mtu anaye jitahidi kuvuta kumbukumbu ya kitu fulani ila anashindwa kujua ni nini anacho kiwazia

    “Sheila…..Sheila?”

    Akaonekana kustustuka na akanikazima macho hadi akaanza kuniogopesha akajaribu kuzungumza ila akawa kama anashindwa.Aafuta vidoli vyake chini na kuandika maandishi yaliyo nistua zaidi

    {MIMI SIWEZI KUZUNGUMZA NIPO SAWA SAWA NA BUBU}

    Maumivu makali yakapenya kwenye moyo wangu na kujikuta sura nzima ikitawaliwa machozi.Nikachukua kijiti chake na kumuandikia chini

    {KWANINI HUWEZI KUONGEA?}

    Sheila akanitazama kwa macho ya mshangao kwa jinsi ninavyo lia kisha akaniandikia chini

    {SIWEZI TUU KWANI NILILISHWA MAKAA YA MAWE KWENYE MDOMO WANGU}

    Sheila akaufungua mdomo wake na kuutoa ulimi wake nje na nikajikuta nikitetemekwa kwa woga kwani ulimi wake una majeraha makubwa yanayo onyesha vika ni kweli alilishwa makaa ya moto.Sheila akasimama gafla na ni mimi nikasimama na akaanza kutembea na kujikuta nikizidi kuumia kwani hata shepu lake la nyuma lilidhohofika sana.Tukaongozana hadi kwenye moja ukumbi ambao kuna kiwanja cha mpira wa kikapu(basketball) na akazidi kunipeleka hadi kwenye moja ya mabafu na akanitazama na kulivua gauni lake

    Nikajikuta hata uwezo wa kuhema ukianza kuwa mdogo kutokana na mstuko nilio upata baada ya kuuna mwili wa Sheila ulivyo jaa majeraha makubwa ya kachanwa chwana na kutu chenye ncha kali.Akanigeukia mgongoni na kunionyesha kuvu kubwa la kutobolewa huku ngozi ya sehemu hiyo ikiwa imekunjamana na kujikuta nikizidi kuteswa na uchungu,Macho ya Sheila yakaanza kuvunjwa na machozi na akatazama tazama ndani ya bafu hili na sikujua anatafuta nini.Akafungua koki ya bomba la maji kisha akachovya kidole chake kimoja ndani ya maji na kuandika kwenye kiio kikubwa kilichopo ukutani

    {MIMI SIO KICHAA ILA WATU WANANIISI KUWA MIMI NI KICHAA ILA UKWELI NI KWAMBA NINAAKILI ZANGU VIZURI NA HAYA YOTE YAMETOKANA NA MAUMIVU MAKALI NILIYO PEWA NA MZEE MMOJA AMBAYE NI MKUU WA JESHI NA NIBABA WA MPENZI WANGU EDDY}

    Sheila akanigeukia na kuniuliza kwa ishara kama nimeelewa alicho kiandika na mimi nikatingisha kichwa nikimuashiria kuwa nimeelewa

    “Unanikumbuka?”

    Nilimuuliza Sheila na akabaki akinitazama kwa muda kisha akachovya kidole chake kwenye maji na kuandika kwenye kioo

    {HAPANA ILA NINAKUFANANISHA NA EDDY WANGU ILA SIO WEWE KWANI YEYE ANAAKILI ZAKE TIMAMU NA SIO CHIZI KAMA ULIVYO WEWE}

    Nikatulia kwa muda huku nikiyatafakari maneno ya Sheila aliyo toka kuniandikia muda mchache ulio pita.Nikamsogelea Sheila na kumkumbatia huku nikiwa ninamwagikwa na machozi.Mlango ukafunguliwa na wakaingia madaktari wawili wa kiume na walivyo tuona tumekumatiana wakanitoa mimi kwa nguvu na kuchomoa virungu vyao na kuanza kunipiga huku wakiniburuza na kunitoa nje

    “Sheila….nisaidie ninakufa mimi”

    Nilizungumza kwa sauti ya juu huku nikiwa ninalia kwa uchungu na kuzidi kuwaongezea hasira madaktari hawa na kuzidi kunipiga,Sheila kwa haraka akatoka huku akiwa na nguo ya ndani na akamsukuma dokta mmoja ana akajibamiza kichwa ukutani na akaanguka chini kisha akamshika kichwa cha gaktari na kunaza kukibamiza kwenye sakafu kwa nguvu hadi kipasukwa kwenye kisogo chake,Daktari aliye kuwa anaendelea kunipiga baada ya kumuona mwenzake akiwa anaaga dunia akaniacha na kwa nguvu zake zote akarusha kirungu chake na kikatua kichwani mwa Sheila na akadondoka chini na damu za puani zikaanza kumwagika



    Taratiu nikaanza kujiburuza chini hadi sehemu aliyo angukia Sheila huku machozi yakinimwagika na kujikuta nikijilaza juu yake na kumfanya daktari aliye mpiga akanza kunipiga tena kwenye mgongo akinimrisha nimuechie Sheila ili aendelea kumshuhulikia kwa kipigo.Kila nilipo jaribu kumtingisha Sheila sikuweza kuona dalili yoyote ya kuishi kwake na kujikuta nikizidi kumkumbatia kwa uchungu.Nikaanza kusikia makelele yakija kwa nyuma yangu,nikageuza shingo yangu na kuona kundi kubwa la vichaa wakija kwa kasi na kumfanya daktari anaye nipiga kutimka mbio na sikujua ni wapi anapo elekea na wote wakanipita na kuendeleka kumkimbiza dakrari aliye kuwa akinipiga

    Nikaona nikiendelea kujiliza haita saidi zaidi ya kumfanya Sheila kuzidi kuzidiwa na kipigo alicho kipata.Nikajikaza na kwabahati nzuri miguu yangu ina nguvu za kutosha nikanyanyuka na kujinyoosha japo nilijawa na maumivu makali ila sikuwa na jinsi.Nikanyanyua Sheila na kutokana na kudhohofika kwake kwa mwili haikuwa ngumu kwangu kumbeba hadi tukafika kwenye kwenye moja ya ofifisi na kuwakuta vichaa wakiwashambulia manesi waliomo ndani ya ofisi.Hali ya hospitali imechafuka kupita maelezo madaktari wanashambuliwa na vichaa ambao wamepandwa na hasira.Kwa bahati nzuri nikaona gari moja ya waogonjwa amayo imesimama nje kwenye maegesho huku dereva wake akichomolewa kwenye gari na kuanza kupewa kipigo kama ilivyo kwa wahudumu wengine wa hospitali ikiwemo walinzi

    Hapa ndipo nikagundua kuwa vichaa tunafahamiana kwa maana kwa kila nilipo pita huku nikiwa nimembeba Sheila hapakuwa na anaye nigusa tofauti na wanapo muona muudumu wa hospitali hii.Nikafanikiwa kufika kwenye gari la wagonjwa nakumuingiza ndani ya gari Sheila na kwenda upande wa dereva na kuanza kutafuta fungua na sikuweza kuiona ikanibidi nishuke na kuunza kuupapasa mwili wa dereva ulio lala pembezoni mwa gari na kwabahati nzuri nikaiona funguo kwenye mfuko wake wa suruali.Nikawasha gari na kuondoka hukiwasaidia vichaa kutoka ndani ya hospitali hii baada ya kuligonga geti lililokuwa kimefungwa.Kutokana sikuwa ni mwenyeji sikujua ni wapi nielekee ili kumuwahisha Sheila hospitali.Nikasimamisha gari pembezoni mwa arabara huku likiwa linawaka ving’ora na kuichukua simu iliyopo ndani ya hospitali na kuanza kubuni namba ya baba

    Kwa mara ya kwanza ikapokelewa na mwanamke ambaye hata lugha hatulewaa na nikajua nitakuwa nimekosea,nikajaribu kufikiria namba nyingi ambazo zinaweza kufanana na namba ya baba na pia namba niliyo ipiga ikapokelewa na kijana na akaanza kumwaga matusi alipoona sizungumzi kitu chochote baada ya kusema haloo.Nikajaribu zaidi ya mara saba nipo kumbukumbu ya namba za baba ziliponijia vizuri kichwani na nikaipiga ikaita kwa muda kisha ikapokelewa

    “Nani mwenzangu?”

    Ilikuwa ni sauti ya baba na kidogo tabasamu likanijia usoni

    “Mimi Eddy”

    “Eddy……!!”

    “Ndio ni mimi baba ninaomba msaada wako”

    Upo wapi mbona makelele ya king’ora?”

    “Nipo kwenye gari ya wagonjwa nimetoroka hospitalini ila mimi sio kichaa kama ulivyo dhania”

    “Ngoja kwanza umesema upo wapi?”

    “Mimi hapa wala sipajui ila kuna magorofa mafupi mafupi hii na kuna magari mengi yamesimama pembeni”

    “Umesema upo kwenye gari ya wagonjwa?”

    “Ndio”

    “Wewe ndio dereva ua kuna dereva?”

    “Mimi ndio dereva”

    “Sasa angalia kwenye upande wa kusoto kuna kijitivii kidogo….”

    “Ndio nimekiona”

    “Kiwashe kama hakija washwa na kwenye sehemu ya chini yake kuna batani nane umeziona”

    “Ndio”

    “Minya batani iliyo andikwa Map”

    Nikaiiminya batani ambayo baba aliniambia na ndani ya sekunde kadhaa kukatokea ramani yenye mistari mingi mingi huku kukiwa na kialama chekundu kikiwa kina waka waka

    “Inakisoma vipi hiyo ramani?”

    “Inasoema Cape Town, Western Cape City”

    “Subiri tunakuja sasa hivi”

    Nikakata simu na kuzima gari na kufungua kijidirisha kilichopo nyuma ya siti yanga na kumuona Sheila akiwa amejilaza huku akipumua kwa shida kidogo nikapata matumaini.Ndani ya nusu saa gari mbili zikasimama mbele ya gari nililipo na mtu wa kwanza kushuka ni baba na moja kwa moja akafika kwenye gani na akaonekana kunishangaa jinsi damu zinavyo nivuja.Watu wake wakanitoa ndani ya gari

    “Baba kuna mtu mwengine huku nyuma”

    “Ni nani?”

    “Rafiki yangu”

    Nikahakikisha wamemshusha Sheila na kumuingiza ndani ya gari ndio na mimi nikaingia.Ndani ya gari nikajikausha kimya hadi tukafika kwenye moja ya hospitali.Madaktari wakanichukua na kuniingiza kwenye chumba kingine na Sheila akaingizwa kwenye chumba kingine kwa ajili ya matibabu.Matibabu yangu hayakuchukua muda sana japo nimeumia ila kidogo ninaafadhali ni tofauti na Sheila.

    “Eddy ni kitu gani kilikupata?”

    “Wapi?”

    “Hadi ukawa kama umechanganyikiwa?”

    “Baba kusema ukweli sijachanganyikiwa ila kuna kitu nilikuwa ninakiitaji kukifanya ili niweze kumpata mtu ambaye anaweza kumjua mama ni wapi alipo?”

    “Una taka kuniambia kipindi chote hicho ulikuwa ukiigiza?”

    “Ndio ila lengo langu limefanikiwa?”

    “Kwanza mama anaendeleaje?”

    “Mama yako hadi sasa hivi bado hajapatikana japo wale watu ambao niliwapa hiyo kazi wanasema kazi yao inaendelea vizuri”

    “Sasa baba hivyo wanavyo sema kuwa inaendelea vizuri si uongo huo,mimi ninavyo jua kuwa kazi ikiendelea vizuri ni kwamba kuna majibu ya uhakika na wanacho kifanya…….Baba ninatambua fika kuwa wewe unamchukia sana mama kwa sababu ya aliyo kufanyia..ila kwangu mimi ni tofauti kabisa na wewe ninampenda mama yangu na yeye ndio kila kitu kwangu”

    Nilizungumza kwa sauti ya ukali kidogo iliyo jaa uchungu kiasi kwamba baba akabaki akitazama chini pasipo kunijibu

    “Baba….lengo langu kubwa ni wewe na mama mupatane,musameheane muwe kitu kimoja kumbuka kuwa mimi ndio mtoto wenu wa pekee.Mama hana mtoto mwengine…..wewe huna mtoto mwengine au unafurahia maisha ya manyanyaso na yule mwanake mwengine……baba simama kama baba uiokoe familia yako achana na nini kilitokea kati yako wewe na mama.Mimi peke yangu baba nitashindwa bado mimi ni mdogo nahitaji maelekezo kutoka kwenu kwanini baba inakuwa hivyo”

    Nilizungumza kwa uchungu huku machozi yakinimwagika baba akainyanyua sura yake na nikashuhudia kwa mbali machozi yakimlenga lenga

    “Eddy samahani mwanangu sikuweza kulifwatilia hilo swala la mama yako bado ninamchukia sana kupita kitu kingine chochote dunia…niangalie mimi leo hii nimekuwa ni kilema wa kila kitu maishani mwangu.Na kama sio pesa mimi leo hii nisinge weza kutembea…..”

    “Baba baba kumbuka mama alikubebea damu yako miezi tisa…..”

    “Alinitenga mbali na damu yangu.Alinifanya nisiione damu yangu na aliniulia damu yangu ni nini ambacho Eddy mwangu utaniambia nikakuelewa juu ya mama yako”

    “Haya kama baba au wewe unafurahia kuishi maisha ya kuonewa yule mwanamke asiye na heshima anakazi ya kutembea na waanya kazi wako….?”

    “Mama yako ndio chanzo wa hayo yote mwangu………Mimi sina nguvu za kumfurahisha mwanamke na sindano niliyo chomwa ndio imenipelekea kuwa hivi”

    Nikabaki mdomo wazi huku nikimuangalia baba kwa macho ya mshangao hulu machozi yakinitiririka.

    “Eddy anacho kifanya yule mwanamke ni haki yake…..tangu mimi nimchukue sijawahi kufanya naye chochote….Ndio maana mara ya kwanza nikakuambia kuwa mama yako ni katili sana na mimi ninajua kila kitua anacho kifanya mke wangu”

    “Oohh baba kwanini eeehee umemchukua wa nini sasa yule mwanamke?”

    Nilizungumza kwa sauti ya chini iliyo jaa unyonge wa hali ya juu

    “Eddy nilihitaji kuficha aibu yangu kama mtu mwenye pesa zake”

    Nikajukuta ninakosa la kuzungumza na kumfanya kunyanyuka kwenye kiti alicho kaa kilichopo pembezoni mwa kitanda changu cha hospitali kisha akanifwata kwenye kitanda nilicho kaa kisha na yeye akakaa

    “Eddy nakuomba unitunzie siri hii ambayo sipendi mtu yoyote aijue zaidi ya yako wewe na yule mwanamke”

    “Nitakutunzia baba yangu lakini nakuomba yule mwanamke aondoke pale nyumbani”

    “Eddy siwezi kuondoka kwa maana atanichafua sana kwani siri yangu sio hiyo niliyo kuambia”

    “Kwani kuna siri nyingine zaidi ya hiyo?”

    “Ndio”

    Ikanibidi nikae vizuri kitandani nimtazame baba huku nikiwa na hamu ya kusikiliza ni nini anaco taka kuniambia

    “Kipindi ambacho nilichomwa sindano ya sumu madaktari wakanitoa sehemu zangu za siri ili kuepuka kupatwa na ugonjwa wa kansa…..ila wakanishauri kitu ambacho sikuweza kubisha kwani ningekataa nisinge weza kuwa hai hadi leo”

    “Kitu gani hicho?”

    “Wakalinipandikiza sehemu za siri za jinsia ya kike kwahiyo nipo sawa na mwanamke……”

    Moyo wangu ukapiga PWAAaaa huku macho yangu nikihisi yakitaka kunichomoka usoni kwani katika maisha yangu sikuwahi kusikia kitu kama hichi ambacho baba yangu mzazi ndio ananiambia.Kulia ninatamani kuzungumza ninashindwa nikawa kama nimegandishwa kwenye Tv.Mapigo ya moyo yakaanza kupiga kwa nguvu kiasi kwamba moyo ukaanza kuniuma

    “Eddy…..Eddy”

    Baba aliniiita kumsikia ninamsikia ila kuitikia nikajikuta nikishindwa kwani kuna kitu kimenikaba koo kiasi kwamba hata kufumbua mdomo ni shuhuli pevu kwangu.Akaingia nesi akiwa ameshika kisahani cha bati huku kikiwa na vichupa pamoja na bomba la sindano hadi anaviweka juu ya meza ndio kidogo nikaanza kurudi kwenye hali yangu ya kawaida.Baba akanyanyuka na kutoka nje ya chumba na ni nikabaki na nesi na akaniomba nilale kifudi fudi na akanichoma sindano ya kutuliza maumivu kabla hajatoka nikamzuia

    “Ehee”

    “Kuna dada mmoja nilikuja naye anaendeleaje?”

    “Yupo vipi vipi?”

    “Amekondeana kidogo na mwili wake kidogo umejaa makwaruzo”

    “Ahaa…yule anaendelea vizuri tuu japo kidogo madaktari wanadai kuwa amepoteza kumbukumbu zake”

    “Eheee haya asante”

    Nesi akatoka na kujikuta akili yangu ikikosa hata cha kufikiria na ndani dakika kumi nzima sikuweza kuwaza kitu chochute.Nikajinyanyua kitandani na kuufungua mlango wa chumba na kuchungulia nje na sikumuona baba wala walinzi wake ambao aliwaacha nje.Nikatafuta sehemu yanye viti vya watu kupumzika nikapumzika huku mara kwa mara macho yangu yakielekea mlangoni mwa chumba changu,Nikamumba jamaa mmoja gazeti lake baadaya kuona taarifa ya michezo iliyo nivutia juu ya timu ya brazili kupigwa goli saba kwa moja na wajerumani.Kidogo akili yangu ikaanza kuchangamka kila nilipo yatazama makatuni yanayo fanana na wachezaji wa kibrazili yaliyo chorwa kwa utaalamu mkubwa ambao mtu ukiyatazama lazima ucheke

    “Ndugu mbona unacheka?”

    “Ahaa ni hawa makatuni walio chorwa humu kwenye hiili gazeti ndio wananifurahisha”

    “Ahaa”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikiwa nineandelea kusoma gazeti nikamuana jamaa aliye valia nguo za udaktari akiingia kwenye chumba changu na kwa haraka kumbukumbu ya wale watu walio mteka mama ikanijia kwani kichwa chake amanyoa upara na nimweusi sana.Akakaa ndani kwenye chumba kama dakika mbili kisha akatoka huku macho yake yakitazama huku na huku na ikanibidi kwa haraka nipandishe gazeti juu na kuiziba sura yangu.Nikajikaza nisitetemeke kwa woga ili jamaa mwenye gazeti lake asigundue kitu chochote kinacho endelea

    “Hembu ninaomba gazeti hilo”

    “Ehee”

    “Naliomba mara moja kuna namba ya simu nimeiandika kwenye moja ya kurasa hapo sasa sijajua ni kurasa ipi niliiandika”

    Jamaa akazidi kunichanganya kiasi kwamba nikajikuta nikiling’ang’ania kwama langu hadi jamaa akaanza kunishangaa.Nikachungulia na kumuona jamaa akizungumza na mmoja wa manesi nahisi anamuuliza ni wapi nilipo na kwa ishara nikagundua nesi alimjibu kuwa hajui ni wapi nilipo kwenda kisha jamaa akaondoka kidogo nikashusha pumzi na kumpa mwenyewe gazeti lake huku nikinyanyuka nikilichungulia jijamaa na nikamshuhudia akijichanganya kwenye watu wanao toka nje.Nikaanza kupiga hatua za kwenda kumtazama ni wapi alipo elekena nakumkuta akizungumza na mwanamke mmoja ambaye nikamtambua kuwa ni Emmy

    Wasiwasi ukaanza kunijaa kiasi kwamba amani ikatoweka moyoni mwangu kwani sikujua wamejuaje kuwa mimi nipo hapa kwenye hii hospitali.Wakaendelea kuzungumza kisha wakaanza kupiga hatua za haraka kurudi ndani.Nikajificha kwenye ya ukata na wakapitiliza na wote wakaingia kwenye chumba changu na baada ya muda wakatoka na kila mmoja akaenda upade wangu huku Emmy akija upande wangu na macho yake yakawa na kazi ya kuwachunguza watu waliomo kwenye sehemu za kupumzikia.Nikaanza kupanda ngazi za kwenda gorofani na kwabahati mbaya Emmy akaniona na ikanilazimu niweze kuongeza mwendo wa kupandisha ngazi na yeye akafanya hivyo hivyo.

    Nianza kukimbia kwenye kordo iliyo ndefu na yenye vyumba vingi na sehemu hii haina watu kabisa na Emmya naye akazidi kuongeza mwendo wa kukimbi na kwabahati mabaya mbele yangu ndipo mwisho mwa wa ukuta na hapakuwa na sehemu yoyote ya kukunja zaidi ya vyumba vilivyopo pembezoni.Nikashika kitasa cha chumba kimoja na kukuta kikiwa kimefungwa na ikanilazimu kukimbilia kwenye chumba cha mbeleni ambacho ni cha mwisho kwenye hii kordo na kwa bahati nzuri nikakuta kipo wazi na kitu cha kwanza kukiona ni bomba la chuma linalo tumika kuning’inizia dripu lililo anguka chini huku pembeni kukiwa na mgonjwa akiwa amemelala sakafuni huku kichwa chake kikiwa kimefunikwa na shuka.Nikaliokota bomba na kuchomo kipande kimoja na nikajianza kwenye mlango.

    Taratibu mlango ukaanza kufunguliwa huku mdomo wa bastola ukiwa umetangulia mbele.Kwa haraka nikaipiga mikono ya Emmy kwa kutumia bomba na bastola yake ikaanguka pembeni,nikarusha bomba ili limpiga usoni ila akaikwepa na sikujua amelichukuaje chukuaje mikononi mwangu na nilicho kistukia mimi ni mikono yangu ikiwa haina chochote.Ikawa ni kazi ya mimi kuanza kuyakwepa mabomba anayo nirushia japo kuna baadhi yalinipata vizuri ila nikajikaza na nikabahatika kumpiga ngumi ya pua na kumfanya ajishike pua na ikawa nafasi yangu kumshambulia kwa ngumi za fujo amabozo mara nyingi tunaziita ni ngumi za mtaani kwa maana hazina mfumo maakumu

    Emmy akashindwa kuhimili mashambulizi yangu kiasi kwamba akaanguka chini na nikaendelea kumshindilia magumi mfululizo yalio changanyikana na uchungu kwa uzalilishaji walio ufanya juu ya mama yangu

    “Yupo wapi mama yangu?”

    “Yupoo Yuupo?”

    Nikaishusha ngumi kwa kasi kabla haijafika usoni mwake akaniomba huku machozi yakimwagika na damu zikimtoka kwenye maeneo ya kwenye jicho.

    “Usinipige usinipige Eddy,Mama yako yupo hapa hapa Afrika kusini?”

    “Eneo gani?”

    “Kwenye hii hii hopitali ika kwa chini ndipo kuna handaki…”

    Nikashtukua kitu kizito kikitua kichwani kwa nyuma yangu na nikaanguka pembeni na macho yangu yakaanza kuingia ukungu na kwa mbali nikaliona jinamaa lenye upara likiwa limesika bomba nililokuwa nimelitumia kupambana na Emmy na nikashuhudia akitoa bastola yake na kuikoki na macho yangu yakafumba na sikujua ni nini kilicho endelea

    Nikaanza kusikia kwa mbali sauti ya vyuma vikigogwa kila nilipo jaribu kufumbua macho kutokana na ukungu ulio tawala kwenye macho yangu,nikatingisha kichwa ili kuyaweka macho yangu sawa ili kuweza kuona kitu kilichopo mbele yangu,Nikashuhudia watu wengi wakiwa wanaendelea na shuhili za utengenezaji wa magari yaliyo aribika.Nikasimama na kuhisi maumivu kwenye kichwa changu na nikajaribu kupiga hatua mbili mbele na nikastukia kitu kikinizuia kwenye mguu na nilipo chunguza vizuri nikagundua ni mnyororo ndio unao nizuia na umefungwa kwenye mguu wangu wa kuliaa.Hakuna aliye shuhulika na mimi na kila mmoja akawa anaendelea na shughuli yake na kila nilipo jaribu kumuongelesha aliye pita karibu yangu hakunisemesha kitu cha aina yoyote

    Nikaaendelea kulichunguza eneo hili na kugundua ni gereji kubwa kwa maana kila eneo limejaa magari yanayo tengenezwa na yaliyo na tayari kwa matumiazia.Baada ya muda watu wawili wanye vifua vikubwa wakanifwata sehemu nilopo na kunifungua myororo na tukaingia kwenye kitorori kinacho pita kwenye reli na tukaondoka na kuondoa kwenye eneo tulilopo huku tukupita kweye miaamba iliyo pasuliwa na sikujua ni wapi wanapo tupeleka na kila nilipo waomba wanieleze ni wapi tunapo elekea wakabaki wakinitazama huku kitoroli tulicho panda kikizidi kuongeza kasi.Ndani ya muda mchache tukafika sehemua ambayo nikakuta watu wengi wakiwa matumbo wazi,huku miili yao ikiwa imedhohofika kiasi kwamba wanatia huruma na wengi wao wanafanya kazi ngumu za kupasu miamba na wamechanganyikana wanaume na wanawake.Miili ya watu hawa imechanika chanika kama ilivyo kwa Sheila

    Wakanishusha kwenye kitorori na tukaanza kupandisha kwenye mawe yaliyo tengenezwa kama ngazi na kila nilipo pita watu nilio wakuta ndani ya hili pango kubwa wakawa na kazi ya kunisikitikia kiasi kwamba nikaanza kupata wasiwasi na walinzi waliomo kwenye hili pango wakawa na kazi ya kuwachapa kwa kutumia mkia wa taa kila mtu aliye jaribu kuniangalia.Tukaingia kweny moja ya kibanda kilicho jengwa na mawe na kukutana na jitu lililo jazia mwili na akawaamrisha wanikalishe kwenye kiti na kuwaomba jamaa walio nileta kunitoa nje

    “Eddy” aliniita na sikujua jina langu amelijuaje

    “Umelijuaje jina langu?”

    “Hahaaaa ni kitu rahisi sana kulijua jina lako kwa maana wewe tumekutafuta kwa muda mwingi sana hadi leo tumekupata kwangu ni furaha kubwa sana”

    “Wewe nani na unampango gani na mimi?”

    “Mpango wangu kwako ni ule”

    Jamaa akanyoosha kidole kwenye kiio na kunionyesha watu wanaoendelea na kazi ngumu ya kupasua miamba kwa kutumia yundo huku wakiwa wamejaa vumbi jingi hata sura zao zikiwa hazionekanani vizuri.

    “Kuanzia sasa wewe utakuwa ni mtumishi wa humu ndani”

    “Wewe unaumwa nini hembu nirudisheni sehemu muliyo nitoa”

    Jamaa akagonga meza yake na wakaingia majamaa nilio kuja nao kisha wakaninyanyua kinguvu na kunivua shati langu na kubakiwana suruali yangu kisha wakanitoa ndani ya ofisi huku wakiwa wemeibeba juu juu.Wakanikabidhi kwa askari mmoja ambaye anaonekana ndio mkubwa wa humu ndani na moja kwa moja askari niliyo kabidhiwa kwake akanipeleka kwenye mango jengine huku akiwa amenibebe begani,Nikakuta msari mrefu wa watu wakiwa wamepanga mstari na jamaa akaniangushia nyuma ya mtu wa mwisho kwenye mstari huu kisha akaondoka.

    Nikachungulia mbele na kuwaona watu hawa ambao kidogo wanaonekana ni wapya kama mimi.Nikaanza kuona kusikia kelele za watu waliopo mbele wakiaza kupiga kelele wakionekana kupata maumivu makali ikanibidi niweze kuchungulia mbele kuona ni kitu gani kinachoendelea,nikawaona watu wawili wakiwa wanalazimishwa kulishwa vitu vinavyofanana na makaa ya moto huku midomo yao ikiwa imeminywa na mijitu mikubwa myeusi ambayo kusema kweli yanatisha kupita maelezo.Mapigo ya moyo yakazidi kwenda mbio na kila muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi mstari ulivyo zidi kusogea mbele na kusema kweli sikuweza kuona sehemu yoyote ya kutoreka kwa maana katika kuta zote za pango kuna vibanda vya askari wakiwa na bunduki mikononi mwao na kila aliye jaribu kukimbia alizawadiwa zawadi ya risasi na huo ndio unakuwa mwisho wa masha yake.Wakasalia watu watano kutoka mimi nilipo na wengine wote walio pita wakawa tayari wamelishwa makaa ya mawe na wamepelekwa kwenye moja ya chumba ambacho sikujua ni nini kinacho endelea

    Tukabaki watu wawili kwenye mstari nakamshuhudia mtu aliyopo mbele yetu akachiruzikwa na na mikojo kiasi kwamba mwili wake mzima ukawa unatetemeka kiasi kwamba hali ya kutokwa na haja ndogo ikaamia na kwangu na bila ubishi nikashindwa kujizuia na mimi nikajikuta nikilowanisha suruali yangu.Gafla tukasikia filimbi zikipigwa kwa nguvu kutoka sehemu ambayo tuliwaacha watu wanao fanyishwa kazi,ikawalazimu mijamaa wanao walisha watu makaa ya mawe kutuacha na kukimbilia sehemu zinapotoka kelele za filimbi.Kwa haraka na nikachunguza sehemu zenye vibanda vyenye askari nikagundua wapo bize katika kwenda sehemu zinapo tokea kelele.Nikakimbia kuelekea sehemu zenye kelele na kwabahati nzuri sikuweza kukutana na askari yoyote.Nikakuta hali ya mvurugano kati ya askari na watu wanao tumikishwa humu ndani ya pango,Miili mingi ya watumwa ikawa imelala chini ikiwa inavuja damu kutokana na kupigwa risasi na askari waliopo ndani ya pango hili.

    Watumwa wengine waoga wakaanza kulala chini huku mikono yao wakiwa wameiweka kichwani,Nikashuhudia mwanamke mmoja akiwa amelazwa chini akipigwa kipigo kikali na askari walili wanao onekana kuwa na hasira kali sana.Roho ya huruma ikaniingia na kujikuta nikianza kukimbia na kuwakumba watu waliopo mbele yangu na kujikuta nikisimama gafla huku macho ni kiwa nimeyatoa kiasi kwamba hasira ikazi kunipanda hii ni baada ya kumkuta ni mama yangu ndio anaye pigwa na askari hawa wanao onekana hawana huruma kabiasa wa watumwa walipo ndani ya hili pango.



    Nikajirusha juu ya mwili wa mama yangua na kumkumbatia kitendo kilicho zidisha hasira ya askari hawa na wakaanza kunishambulia mimi kwa kunipiga,Sikaanza kusikia uzito mwengine ukija juu yangu na nikagundua kuwa watumwa wengine wamepatawa na roho ya huruma na wao mwaneamua kufanya kama nilivyo fanya mimi na kwa umoja wetu ikawalazimu askari kusitisha zoezi lao la kutupiga.Wakatuamuru tuweze kurudi kwenye kazi za kuvunja miamba,nikamnyanyua mama taratibu huku uso wake ukiwa umejawa na damu zilizo changanyikana na machozi mengi.Nikamshika mama huku akiwa hatambui ni nani aliye mshika na kabla sijamsemesha kitu cha ina yoyote askari mmoja anisukuma ili nimuechie mama kisha akamshika mama mkono na kuanza kumburuza kitendo kilicho zidi kunipandisha hasira ila kabla sijhamfwata nikastukia nikichapwa na fimbo aina ya mkia wa taa iliyo jizungusha kwenye tumbo langu na kunirudisha nyuma baada ya askari aliye nichapa kafanya hivyo bila ya huruma

    Nikamshuhudia mama akipotelea gizani kwenye pango pamoja na askari aliye mchukua na sikuwa na lakufanya zaidi ya kuendelea kupokea kichapo cha kuchapwa nikiamrishwa kwenda kufanya kazi upasuaji wa mame.Nikaokota moja ya nyundo huku nikiwa na hasira na uchungu mwingi na kuaza kuvunja mwamba amabao wenzangu wanaendelea kuuvunja.Kitu ambacho nimegundua ni kwamba watu wengi waliomo humu ndani wamelishwa makaa ya mawe moto ambaya sio rahisi kwa mtu kuweza kuzungumza chocheta zaidi ya kutoa miguno.Hali ya maisha ikazidi kuwa ngumu kwa upande wangu kadri ya siku zinavyo zidi kwenda sikuweza kumuona mama yangu japo ninaendelea kufanya juhudi ya kuchunguza ni wapi alipo mama na sikuwa ninafahamu kama yupo hai au tayari amesha fariki,mwili wangu ukazidi kudhohofika kutokana na chakula finyu tunacho pewa asubuhi na jiono,Asabuhi tunakunywa kikombe kidogo cha uji usio na kadha ya aina yoyote na usiku tunapewa viazi viwili vilivyo chemshwa na huo ndio mlo wa siku moja na mbaya zaidi chakula ni chakugombani usipo fanya hivyo unaweza kukaa siku mbili hadi tatu pasipo kula

    Watu wengi wanazidi kufa kutokana na njaa inayo andamana na kazi ngumu kwa upande wangu kifua kianza kuniuma sana ikafikia hatua nikaanza kukohoa na makohozi yangu yamechanganyikana na damu nyingi,

    “Hapana siwezi kufa humu ndani”

    Nimawazo ambayo yakawa yanajirudia rudia kichwani kwangu kadri siku zinavyo zidi kwenda,mbaya zaidi sikuweza kujua upi ni usiku na upi ni mchana hii ni kutokana na muda wote tuliopo ndani ya pango mataa makubwa yanawaka,Kila ninapo jitazama mwili wangu ninajikuta nikimwagikwa na machozi kwani mbavu zangu unaweza kuzihesabu,mikono na miguu yangu imekondeana sana.Nyele zangu zimekosa uhusiano mzuri kichwani vidonda vingi ambavyi vingine vimefikia hadi hatua ya kutoka na funza vikaendelea kunitesa mwili wangu.

    “Mungu wangu ninaomba unipe nguvu na juhudi katika hili”

    Nikaanza kufanya kazi ya kutafuta ni wapi ninaweza kupata njia ya kutokea na kwa bahati nzuri katika uvunjaji wangu wa miamba nikaona sehemu yenye ufana wenye kijisihimo kidogo,nikawatazama askari waliopo ndani humu na hakuna aliye nifwatiliza nikapiga hatua za taratibu na kuchungulia kwenye shimo na kuona mwanga kwa mbali na akili yangu ikatambua utakuwa ni mwanga wa jua.Kengele ya kwenda kupata chakula cha jioni ikagongwa na nikatupa sururu niliyo nayo chini na kuchomoja kwa kasi kuwania chakula ambacho nikikosa leo itakuwa siku yangu ya pili kukosa chakula.Japo mwili wangu umedhohofika nikajikaza katika kugombani viazi na kupata viazi vitatu,Nikakaa kwenye sehemu ambayo siku zote huwa ninapenda kukaa na kuanza kuvisakamia viazi kwa fujo

    Nikastukia nikiguswa mguu na binti mdogo na akaniwekea mkono kwa ishara ya kuniomba kiazi kimoja ambacho nimebaki nacho mkononi.Nikamtazama kwa jinsi alivyo kondeana hadi sura yake imejaa vishimo shimo vilivyo kosa nyma kwa kukondeana.Taratibu nikampa kijikiazi nilicho nacho na chote akakiweka mdomoni na kuanza kukitafuna kwa haraka na inavyo onyesha ana njaa kuliko mimi.Akanishukuru kwa kuikutanisha mikono yake kwa pamoja huku akiinama na akanyanyuka taratibu na kuondoka

    Tukuruhusiwa kwenda kulala kwenye mapango yetu ambayo milango yake ni ya chuma na katika chumba kimoja cha pango tunalala watu si chini ya thelathini na tangu niingie kwenye hili pango sikuwahi kuona hata siku moja watu wakienda kuoga kwahi maji tunayo kunywa ni machafu sana na yapo kwenye kijikisima kimoja kidogo.Harufu ya uchafu wa miili yetu siku zote inanikusesha raha ya kulala na hususani loe kidogo ninajambo la kuliwazia kichwani kwangu kutokana na ufana nilio uona ninaimani utanisaidia katika kutoroka ndani ya hili pango.

    Muda wa kuamshwa ukawadia na tukatoka ndani ya vyomba vyetu na kuelekea sehemu za utendaji wetu wa kazi na kitu cha kwanza kufika kwenye sehemu yangu nikawa na kazi ya kuvujunya ufa nilio uona,ugumu wa mwamba huu hakunifanya nife moyo zaidi ya nilicho kifanya ni kuendelea kuvunja hadi ikafikia kipindi matumaini yakaaza kuja,Filimbi ya dharura ikapangwa na tukakusanyika kwenye eneo la moja na askari wakaanza kutupanga mistari mitatu na tukasubiria nini tunacho taka kuambiwa.Nikawaona watu wanne walio valia vizuri na nikamgundua mmoja wao ambaye ni baba yangu mkubwa Mzee Godwin akiwa ameongozana na watu wengine watatu ambao sikuwajua.Mukuu wa askari wa eneo hili akawapokea kwa unyeyekevu mkubwa na kuanza kuwapitisha kwa kwenye mistari mmoja baada ya mwengine kama vile raisi anaye kagua gwaride la wanajeshi.

    Sura yangu nikaiinamisha chini ili asiweze kunijua kwa haraka na kabla ya kunifikia mimi akahamia kwenye mstari wa nyuma yetu na kuendelea kuwatazama watumwa wezangu tuliopo kwenye eneo hili,Wakamaliza kazi hii na wakapanda kwenye ofisi ya mkuu wa eneo hili huku wakizungumza na kucheka kwa furaha.Uchungu na maumivu makali yakaendelea kuutesa moyo wangu ila sikuwa jinsi,tukarudi kwenye sehemu zetu na kuendelea na kazi hata kengele ya uji ilivyo gonga sikuwa na haja ya kwenda kugombania uji.Nikaendelea kupasua mwamba huu na kugundua mawe haya nikiyagonganisha kwa pamoja yanaweza yakazalisha moto kutokana na chechezake.Nikawaona askari wanao tusimamia wakielekea walipo kwenda baba na wezake wakionekana kujawa na furaha hapa ndipo nikaamini kuwa baba mkubwa ndio mmiliki wa hili eneo.

    Kwa bahati nzuri nikaona kamba moja ambayo hutumia katika kubutia mawe makubwa,Nikaichukua na kwenda moja kwa moja kwenye mapipa yenye mafuta ya petrol ambayo yanatumika kuendeshea majenereta yanayo washa taa za humu ndani,Kwa haraka nikaichovya kamba kwenye pipa lenye mafuta na kabla sijaondoka eneo lenye mapipa nikaona kidungu kidogo cha maji ya lita moja na nusu.Nikakiokota na kuchota mafuta nusu na kurudi katika eneo lenye ufa,kwa uzuri ni kwaba sehemu yenye ufa juu yake ndipo zilipo ofisi za wakuu wa hii sehemu na haikuw ni raisi kwa wao kuniona kutokana nipo chini shana na pameingia ndani.Wezangu tayari wamesha toka kunywa uji na wanaendelea na kazi zao za upasuaji wa mawe na kelele za upasuaji wa mawe zikazidi kunipa moyo wa kwamba sio rahisi kwa maaskari kuweza kusikia kitu cha aina yoyote.Nikaiingiza kamba kwenye mdomo wa kidungu nilicho kiokota japo kamba ni nene kiasi ila nikajitahidi kuigandamiza hivyo hivyo na ikaingia kiasi kidogo.Nikakichomeka kidungu sehemu yenye ufa na kabla sija ondoka kwenye eneo hili msichana aliye niomba kiazi jana usiku akanifwata na kunigusa mkono na kwa ishara akaanza kunielekeza kitu ambacho haikuwa si raisi kwa mimi kuielewa

    Nikaivuta kamba yangu hadi sehemu yenye umbali kidogo na eneo lenye ufa na kuokota mawe mwili ya mwamba na kuanza kuyagonganisha kwa nguvu.Kila ninavyo endelea kuyagonganisha ndivyo jinsi msichana anavyo nisumbua kwa kunishika mkono na kunionyesha kwa ishara umbo la binadamu na kudai kuwa lipo kwenye sehemu ya pili ya sehemu ninayo ipasua.Japo ninamuelewa ila sikuwa na haja ya kusikiliza sana na nikazidi kujitahidi kuyagonganisha mawe yangu kwa nguvu na kasi ya kubwa hadi chche zikaanza kutoka na kwabahati nzuri cheche baadhi zikanasa kwenye kamba yenye mafuta ya petrol na kwa kasi ikaanza kuwaka huku ikielekea sehemu yenye kidungu cha maputa.Msichana anakigeuza ili nisome kitu alicho kiandika sehemu ya ukutani kwenye mwamba kwa kutimia jiwe.Nikakutana na maandishi yenye herufi kubwa na zilizo kaa bila mpangilio zinazosomeka

    {MAMA ULIYE MTETEA SIKU ZILEEEE YUPO SEHEMU YA PILI YA SEHEMU AMBAYO UNAPASUA HUO MWAMB…..}

    Kabla sijamalizia kusoma maandishi hayo nikastukia mlipuko mkubwa ulio sababisha mwamba kupasuka na kuanza kudondosha mawe makubwa ambayo yameanza kuwaangukia watumwa wezangu pamoja na kuta za ofisi zilizopo juu kuanza kumeguka taratibu na kuporomoka chini



    Mawe yakazidi kuporomoka huku vilio na kelele zikitawala kwenye pango zima,Binti niliye naye akanishika mkono na kuniomba nimfwate huku tukijaribu kuyakwepa mawe yanayo endelea kuanguaka,tukafanikiwa kufika kwenye moja ya kijiuchochoro na tukapita na kutokea kwenye moja ya kijimlango cha mbao na akaniomba nichungulie ndani kupitia nondo mbili zilizopo kwenye mlango.Nikamuona mama akiwa amelala chini huku panya na wadudu wengi wakiwa wanamtambalia,hali yake imedhoohofika sana mimi kidogo ninanafuu.Nikatafuta kipande cha jiwe kikubwa na kuanza kupiga kwenye mlango huu ambao ni wa mbao.Nikaendelea kusaidiana na binti niliye kuwa naye na tukafani kiwa kuipasua mbao moja ya mlango,kutokana na wembamba wangu nikafanikiwa kupennya ndani na kumkuta mama akikoroma sana akiwa anaelekea kwenye hatua za mwisho mwisho za maisha

    “Mama…..mama mama”

    Nimuita mama na akayafumua macho yake taratibu na kunitazama na hakuamini kama ni mimi ndio ninaye muita,akaachia tabasamu pana nikamnyanyua na kuanza kumpitisha kwenye kijiuwazi japo ni kwashida sana ila ikanilazimu kufanya hivyo.Tetemeko la ardhi likaanza kutikisika na woga ukazidi kunitawala,nikafanikikiwa kimtoa mama kwenye kijiupenyo cha mlango kisha na mimi nikaanza kupenya ila kabla sikamalizia kutoka nikajikita nikipiga kelele ya uchungu hii ni kutokana na jiwe lenye ncha kali kutua juu ya mguu wangu wa kushoto.Mama na msichana mdogo wakaanza kunivuta nje japo kwa mama kidogo hakuwa na nguvu sana.

    Nikatoka nje ya kijishimo na kuutazama vizuri mguu wangu na kuundua kuwa umetobolewa vibaya maeneo ya kigimbi na kipande kidogo cha jiwe kimekatikia ndani ya mguu.Kila nilipo jaribu kunyanyuka nikajikiya nikishinda na kukaa chini.Tetemeko kubwa la ardhi likaendelea kutetemesha kila eneo na mawe yakazidi kuanguka

    “E…ddy…mwan…gu jiiikazeee”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maneno ya mama yakanipa matumaini mapya ya kujiokoa,nikasimama wima huku meno yangu nikiwa nimeyang’ata nikisikilizi maumivu jinsi yanavyo vuta kwenye mguu wangu.Tukaanza kusikia mlio mkubwa wa maji na gafla tukastukia maji mengi yakija nyuma yetu kwa kasi kubwa na moja kwa moja nikatambua kuwa sehemu ambayo tupo kuna mwamba wa maji umepasuka.Mama akanikumbatia kwa nguvu na binti mdogo niliye kuwa naye ananing’ang’ania mkono na sote maji yakatunyanyua na tukaungana na watu wengi waliobebwa kwenye maji haya.

    Ikawa ni kazi ya kumuomba Mungu tunapo elekea tusikutane na kitu ambacho kitaweza kutudhuru.Mama wala binti mdogo hakuna aliye niachia na kila mmoja akajitahidi kwa uwezo weke kunishikilia kwa nguvu zake zote.Ikawa ni kazi yangu kujitahidi kupata muhumili wa kuendana na maji haya kwani watu wengine waliojiachia walijikuta wakikigonga vichwa kwenye mawe ambayao yanaendelea kupasuka na ikawa ni safari ya maisha yao japo miili yao iliendelea kuendelea kupelekwa na maji kama tunavyo pelekwa sisi.Maji yakazidi kutupekeka kwa kasi cha kumshukuru Mungu nikafanikiwa kushika maja ya jiwe lililo simama kama nguzo,Kila nilipo mtaza mama usoni nikajikuta nikipata moyo wa kuuendelea kumsaidia mama kwa moyo mmoja na wakaendelea kunishikilia japo ninapata maumivu kwenye viganja vyangu ambaco hadi kwa sasa vimeota sugu kutokana na upasuaji wa mawe ila nikajikaza kama mwanaume.

    “Bora nife mimi ila si mama yangu”

    Nilijisemea kimoyo moyo huku nikijitahidi kuikanza mikono yangu ili maji yasizidi kutupeleka mbele zaidi,Kwa bahati mbaya mwili wa mtu ukaja kutua kwenye jiwe nililo lishikikilia na kuvigandamiza viganja vyangu kwa nguvu hadi nikajihisi vidole vinaweza kukatika na taratibu nikajikuta nikachina na safari ya maji ikaanza kutupeleka huku tukiwa tumetanguliza miguu.Nikaanza kuona mwanga kwa mbali kidogo ambapo ndipo maji yanapo tokea.Wasiwasi mwingi ukaanza kuniingia na nikiwa katikati ya mawazo hayo nikastukia tukuchomolewa ndani ya pango na kuanza kwenda chini ambapo ndipo maji yanapo elekea.Nikagundua sehemu tunayo kwenda kuangukia ni kwenye bahari

    Sote tukaingia ndani ya bahari na kushuka chini kidogo na nikajihisi wepesi na nikaanza kuogelea kurudi juu,hadi ninatokeza kwenye usawa wa bahari nikajikuta nipo peke yangu sikumuona mama wala msichana mdogo.Baridi kali ikazidi kunitesa na mbaya zaidi sehemu kubwa ya bahari imezungukwa na milima mingi.Nikavuta pumzi nyingi ya kutosha na kurudi ndani ya maji na kuangaza kila sehemu ila sikuweza kumuona mama wala masichana mdogo.Nikarudi tena juu na kumuona msichana mdogo akinywa maji kwa mkupuo,kwa haraka nikaanza kuogelea hadi sehemu alipo na nikamuacha kudogo nguvu zimuishie ndipo nikaipitisha mikono yangu chini na kuushika mgongo wake ili aelele juu kidogo na macho yangu yakawa na kazi ya kutazama ni wapi alipo mama.Nikamuona mama akiibuka kwenye maji kwa mbali kidogo na kutokana na kuchoka sana sikuwa na hata na uwezo wa kumuita kwa sauti yajuu.Mama akaanza kupiga mbizi taratibi hadi nillipo mimi na akanisaidia kuipitisha mikono yake chini na ikakutana na mikono yangu kwa chini na tukashikana tukiwa hatujua nini cha kufanya kwa maana sehemu tuliyopo ni mbali sana kinho za bahari

    Jua likaanza kuzama taratibu huku baridi ikizidi kuongezeka na kwabahati nzuri tukaona boti ndogo inayo kwenda kwa kasi ikipita maeneo ya karibu nasi.Kwa hungu nikapiga kelele za kuomba msaada huku nikisaidiana na mama,Ikatupita na kujikuta tukinyamaza tukiiangalia jinsi inavyo tokomea kwenye maji na matumaini ya kuokolewa ikakata

    “Kama MUNGU aliye tusaidia tukatoka pangoni na kutufikisha hapa ninaimani yeye pia atatusaidia kupata msaada”

    Mama alizungumza huku akiutasama usawa wa biti ilipo elekea kisha akanigeukia na mimi huku machi yakianza kumlenga lenga.Unene wa kiasi wa mama yangu umepota wote,uzuri na taswira yake ya kuvutia imepotea na sura yake imeingia uzee wa gafla huku akiwa amekondeana sana

    “Haki ya Mungu nikirudi hai lazima nilipize kisasi kwa Mzee Godwin”

    Nilijiapiza kimoyo moyo huku nikimuangalia mama kwa huruma sana,msichana mdogo hali yake ikaanza kuwa mbaya.Mwili wake ulianza kutetemeka huku kmapovu mengi yakimwagika mdomoni

    “Mama ana nini huyu”

    “Ni kifafa hambe jikaze kidogo mikono yako mimi ninaachia”

    Nikafanya kama mama anavyo nihitaji na nikaikaza mikono yangu na mama akaitoa mikono yake na kuushika mdomo ya mtoto mdogo na kuanza kuziachanisha taya zake ili asiung’ate ulimi wake,Gafla kwa mbali sana nikaanza kuona kitu kikija kwa kasi huku kikiwa kimejitokeza upanga mmoja na kwaharaka nikatambua ni papa

    “Ma…”

    “Nini?”

    “Ona huko nyuma”

    Mama akatizama nyuma na nikastukia akiacha alichokuwa akikifanya kwa msichana na kwa haraka akaniomba niogelee na nimuache msicha.

    “Mama”

    “Fanya kama nilivyo kuambia okoa maisha yako kwanza huyo binti muache”

    Mama alizungumza huku akiendelea kupiga mbizi akielekea upande mwengine,roho ya huruma ikanijaa moyoni mwangu na ninakafikiria mambo machache aliyo nifanyia huyu binti kwani isinge kuwa ni yeye nisingeweza kumuona mama na kwa haraka nikamuweka mgongoni kisha nikaivua suruali yangu iliyo chakaa na kubakiwa kama nilivyo zaliwa na kumfunga vizuri ili asianguke na kuanza kuogelea kuelekea kwa haraka alipo mama.Japo kuna uzito ila nikaendelea kujikaza kama mwanaume.Na jinsi ninavyo ogelea mbele ndivyo jinsi papa aliyozidi kunikaribia na safari hii akajitokeza vizuri na kuhakikisha kweli ni papa samaki mwenye meno makali ya kumrarua binadamu anaye ingia kwenye kumi na nane zake ndio anaye nifwata kwa mwendo wa kasi na kujikuta nikipiga picha ya jinsi atakavyo nirarua pamoja na huyu msichana mdogo



    Gafla nikasikia milio mingi ya risasi iliyoanza kunichanganya hata mfumo wa kuogelea ukabadilika nikatamani maji ya bahari yabadilike na kuwa mchanga ili miguu yangu ipate uwezo wa kukimbia ila hikuwa hivyo zaidi ya milio kuzidi kuongezeka kwa kasi ya ajabu na kwakiweza sikujua hata ni wapi inapo tokea,Maji yakabadilika na kuanza kuwa na rangi nyekundu nikageuka nyuma na kukutana na boti iliyo wabeba watu wapatao wanne wenye bunduki na pembeni nikamuona papa aliyekuwa akinifwata akielea elea juu ya maji akiwa amekufa.Jamaa wenye boti yao wakaisogeza hadi pembeni na kunitazama kwa muda kisha wakanipa mkono na kunivuta kwa nguvu huku buinti mdogo akuwa mgongoni,wakanipa kitaulo cha kujifunga na kunza kumfwata mama ambaye tayari alisha fika mbali kutoka sehemu ambayo nilikuwepo mimi.Jamaa mmoja alizungumza na simu na sikuielewa luga yake kutokana anazungumza kikabila kisha akakata simu.Wakaisogeza boti yao hadi alipo mama na wakamvutia ndani ya maji.Nikawaona jamaa wakinong’onezana na kisha wakagongeana mikono ikatubidi mimi na mama tutazamane

    “Asanteni ka masaada wenu”

    Mama alizungumza huku akiwatazama usoni

    “Musijali kwa hilo”

    Jamaa wakaonekana kutawaliwa na furaha ambayo hadi wakati huu sikujua ni ya nini

    “Mbona munafurahi?”

    “Tunafurahi kwa maana tumesha kuwa ni matajiri”

    “Matajiri wa nini?”

    “Kuna tangazo lilikuwa linatolewa kwa mtu atakaye fanikisha kukupata wewe atapewa dola milioni mbili za kimarekani na baba yako na sasa ni mwezi wa tatu ndio sisi tumekupata”

    Nikatabasamu ila ikawa ni tofauti kwa mama ambaye nahisi kuwa anajua ni mume wake mzee Godwin

    “Eddy waambie wanipige risasi ili nife sipi tayari kurudi tena mikononi mwa baba yako”

    “Mama sio baba wa Tanzania?”

    “Unataka kusema wewe baba yako yupi huyo mwenye roho ya kibinadamu atakaye toa pesa yake ili amzawadie mtu?”

    “Mama sio baba unaye mjua wewe…tambua kuwa ukweli wote ninauju na ninamshukuru Mungu kuwa nimempata baba yangu ambaye yeye ndio damu yeke japo amepitia yaliyo mengi ila ninamshukuru Mungu yupo hai”

    Mama akabaki kimya huku macho yake yakiwa chini akimtazama mtoto tuliye mlaza chini,Tukaona boti nyingine kubwa ikija na kusimama karibu na sehemu ilipo boti hii ndogo,wakatuwekea kingazi na tukaanza kupanda na kuingia kwenye boti kubwa iliyo kuja na jamaa watatu wakingia na kumuacha mwezao mmoja kwenye boti ndogo.Ndani ya boti wakatupa makoti makubwa kwa ajili ya kuzui baridi kali iliyo kuwa ikitukung’uta.Wakampa msichana mdogo huduma ya kwanza na sisi wakatupatia vyakula na chai ya moto kutoa njaaa tumboni.Mimi wakanihudumia kwenye sehemu niliyo jeruhiwa na jiwe kisha wakanipa suruali mpaya,nikavua kitaulo nilicho pewa na kuivaa suruali hii.Boti ikazidi kusonga mbele huku moyoni mwangu nikijawa na amani tele ya kuweza kumpata mama yangu na kilicho salia ni kuwaunganisha baba mzazi na mama.

    “Samahani kaka nyinyi ni kina nani?”

    “Sisi ni wavuvi wa samaki wakubwa sasa yule papa tuliye muua tulikuwa tunamkimbiza alitusumbua sana na pale tumemuacha yule mwezetu akilinda sisi tutamrudia kumchukua na boti nyingine”

    “Sawa”

    Tukafika ufukweni na jamaa wakatupeleka kwenye moja ya Hotel isiyo mbali sana na bahari na kutuchukulia chumba,wakamchukua daktari maalumu na kuja kutuhudumia.Tukakaa hotelini kwa wiki moja tukijitahidi kuirudisha miili yetu katika afya zake za kawaida kwani kwa muonekano tulio nao ninaweza kujifananisha na misukule.Mudu wa wiki moja kukatika Afya yangu ikarejea kama awali japo sio sana ila kidogo niliweza kusimama mbele ya mtu au watu na kujiona ni mtu.Gharama zote zikalipwa na mama kutokana na kuwa na akaunti yake ya siri iliyopo huku Afrika kusini na kwakipindi chote hatukuwasiliana na mtu yoyote zaidi ya jamaa walio tuokoa ambao nao mama aliwakanya wasizungumze ummbea wa aina yoyote kwa mtu yoyote ili waweze kupata donge lao nono wanalo lisubiria kwa hamu kubwa kutoka kwa baba yangu mzazi

    Msichana mdogo alilazwa kwenye moja ya hospitali na madaktari wanaendelea na juhudi za kuweza kumtibu kama ataweza kuzungumza tena ili awe miongoni mwa mashaidi wa kumuhukumu baba Mzee Godwin katika kesi ya kuwatumikisha watu kikatili na kuwakatili katika kuzungumza nao

    “Mama unampango gani na baba?”

    ”Nitahakikisha ninamfunga hadi magereza yanabomoka”

    “Sawa mama je baba yangu mzazi naye una mpango gani naye?”

    “Mmmm sijui hata ni wapi nitaanzia kwa maana kwa niliyo mfanyia baba yako kidogo yananipa hata ugumu wa kusema ninaanzi wapi”

    “Ninafurahi kusikia hivyo mama ila kwa hilo ninaomba uniachie mimi kwa maana baba ananipenda sana”

    “Ila Eddy roho yangu imejawa na dukuduku kubwa ambalo sielewi siku ninamkamata Godwin nitamfanya kitu gani?”

    “Hilo mama wala lisikutie mawazo sana cha msingi ni kuweza kumuomba msamaha baba yangu ili kama ni maisha yaweze kuendelea kwa amani”

    “Sawa mwanangu nitafanya hivyo”

    “Je umewasiliana na serikali ya Tanzania?”

    “Mmmm siwezi kufanya hivyo kwanza kutokana huwezi jua baba yako ana mtandao mkubwa kiasi gani ila nitarudi kimya kimya”

    “Hapo umesema ila yule daktari wako ni mnoko sana na kama unaweza awe miongoni mwa watu wa kushuhulikiwa”

    “Kwa nini?”

    “Ana vitu vingi sana ambavyo wewe ukimuambia humuambia baba,kwa mfano swala la kuwa mimi sio mwanaye wewe siku ulipokuwa unamwambia pale sebleni kama sisi.Yeye kaenda kuyang’aza kwa lile jijambazi ndio maana likatumia uwezo wake wa kijeshi kufanya mambo ya ajabu kama haya”

    “Kumbee hapa ndio ninaanza kupata picha kwa maana siku ambayo waliniteka hospitali baba yako akawa analalamika kuwa nimemdhalilisha na lazima na mimi anidhalilishe”

    “Ndio hivyo mama je ile siku walikupeleka wapi?”

    “Walinipeleka sehemu moja hivi wala sikujua ni wapi ila nikaja kukutana na binti mmoja aliniambia anaitwa nani vileee…..”

    “Nani…..?”

    “Jina lake limenitoka mara moja alisema na yeye anatokea Tanzania na anakufahamua sana wewe na mumeshirikiana sana kwenye mambo mengi”

    “Sheila”

    “Eheee huyo huyo….yule binti alinisaidia sana kipindi nipo matesoni kweni baba yako alinipeleka kwenye jijumba chakavu msituni huko wakanifungia…cha kushukuru Mungu yule binti alikuwa akiniletea chakula kila siku usiku kwani wao walikuwa wakinipa vyakula vibaya?”

    “Kina nani?”

    “Si hilo jibaba lako na watu wake”

    “Ahaaa ila sio baba yangu”

    “Basi siku kama mbili zilipita sikumuona Sheila sasa sikujua ni wapi walimpeleka binti wa watu sijui walimuua au”

    “Hawakumuua….nilikutana naye hapa kipindi cha katikati akiwa amelishwa makaa ya mawe hawezi kuzungumza”

    “Weeee ndio maana baba yako akaamua kunipeleka kwenye lile jipango na kuniambia kuwa nitalisha keki za moto”

    “Ndio”

    “Basi nakumbuka kipindi ninaingizwa mule sikubahatika kulishwa hayo makaa na walinipiga na kuninyanyasa sana hadi ikafikia kipindi wakanitenga na wezanu na kunifungia kwenye kile kijichumba”

    “Unajua siku ya mwisho unapigwa mimi ndio niliye kusadia kuuziba mwili wako ili nipigwe mimi badala yako”

    Mama akabaki akiwa mdomo wazi na taratibu chozi likamtoka na akanivuta na kunikumbatia kwa uchungu na machozi yakaendelea kumtoka hadi akalowanisha bega langu alilo pitishia bega

    Niambembeleza mama hadi akanyamaza na akaniaga na kuingia chumbani kwake kulala na mimi nikabaki nikitazama Tv na nikapitiwa na usingizi kwenye sofa nililo kaa.Asubuhi kama ilivyo kawaida daktari maalumu anayetuhudumia akaja kututembelea na kutupa maelezo ya nini tuweze kufanya ili afya zetu ziweze kuhimarika.Nikwasiliana na jamaa walio tuokoa kili waje kutuchukua na watupeleke nyumbani kwa baba.Baada ya nusu saa jamaa wakawa wamefika na sisi tukawa tayari kwa safri,njia nzima ndani ya gari mama akawa amenishika mkono huku akiwa na futaha sana.Tukafika kwenye jumba la baba na nikamuona mama akitazama tazama kila sehemu

    “Mama mbona unashangaa?”

    “Hili jumba lote ni la kwake?”

    “Ndio”

    “Amejitahidi”

    Walinzi wakazungumza na dereva anaye endesha gari letu na baada ya kuniona mimi wakaturuhusu.Nikawa mtu wa kwanza kushuka na nikamuomba mama kusubiri ndani ya gari hadi nitakapo kuja kumuita wenyewe wazungu wanasema kumfanyia Suprize baba.Nikafungua mlango ndani huku nikiwa na shuuku kubwa sanaya kumuona baba,

    “Nimesema sitaki kumona huyo kinyago wako humu ndani”

    “Lazima…….”

    Nilizisikia kelele za baba na mke wake wakibishana ila sentesi ya baba haikumalizika na kwakasi kubwa nikashuhudia akinguka kutoka juu gorofani alipo sukumwa na mke wake na akatua kwenye meza ya kioo na kutulia kimya



    Nikabaki nikiwa nimesimama kama sekunde kadhaa huku macho yangu nikimtizama baba kisha ninayahamishia kwa mke wa baba ambaye hakuzungumza kitu cha aina yoyote,Akaondoka na kukimbilia ndani kwa haraka nikamsogelea baba na kumuwekea mkono kifuani na sikuyasikia mapigo yake ya moyo yakifanya kazi,Nikapiga kelele za kuomba msaada na walinzi wa baba wakaingia akiwemo mama na akaonekana kustuka baada ya kumkuta baba katika hali kama hii

    “Eddy amefanya nini?”

    Sikumjibu mama zaidi ya kunyanyuka na kuanza kupandisha ngazi za kuelekea gorofani na nikakutana uso kwa uso na mke wa baba akiwa ameshika begi la kuburuza huku mkono wake mmoja akiwa na bastola,Akiwa anababaika kuikoki bastola kwa haraka nikamrukia na kusukuma na akaanguka chini na bastola yeka ikaangulia pembeni.Nikamuwahi kumshika kifuani kwenye shati alilo livaa na nikamnyanyua hadi akasimama na nikumvuta karibu yangu na ngumi mbili za haraka zikatua usoni mwake,Akainama huku akiwa ameizima pua yake kwa mikono yake miwili na damu nyingi zikaanza kumtoka,sikuhitaji kumuonea huruma zaidi ya kuiacha mikono yangu kufanya kazi ya kuzichomoa ngumi zenye kasi kubwa na kutua katika mwili wa mke wa baba ambaye aliendelea kulia kama mtoto mdogo

    Mke wa baba akaanguka chini na kunipa fursa nzuri ya kuanza kumpiga mateke ya tumbo yaliyo mfanya ajikunje kama samaki mbichi huku damu zikiwa zinamwagika puani na mdomoni.Nikaikota bastola yake na kuikagua kwa haraka na kugundua kuwa ina risasi za kutosha na nikaielekeza kwake kwa hasira

    “Eddy......Eddy”

    Nikaisikia sauti ya mama ikiniita kwa nyuma

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Eddy mwangu ninakuomba usifanye hivyo baba yangu nakuomba tena sana mwanangu mpendwa usifanye hilo mwanangu”

    “Mama huyu mwanamke ndio chanzo cha baba kuanguka kutoka juu na kufa,na hana haki ya kuishi duniani kwahiyo niache nifanye ninacho kitaka kukifanya”

    Nilizungumza kwa sauti nzito na nne iliyo jaa uchungu na hasira na machozi yakiwa yametapakaa kwenye sura yangu kiasi kwamba hata mimi mwenyewe nikajishangaa ni wapi hii sauti imetokea

    “Eddy nakujua mwangu....nakuomba utulize hasira zako nakuomba mwanangu tafadhali”

    Mama alizungumza huku akinisogelea taratibu huku walinzi watutu wa baba wakiwa nyuma yake,Nikamtazama mke wa baba jinsi anavyo hema kwa tabu nikayakaza meno yangu kwa kuyang’ata na kwa hasira nikaipiga risasi moja chini karibu na eneo alilo lala na bastola yake nikaitupa pembeni na mama kwa haraka akanikumbatia na kuanza kunibembeleza huku akinipiga piga mgongoni

    “Shiii....nyamaza baba yangu usilie baba hajafa tumemuwahisha hospitalini”

    Milio miwili ya risasi ilinistua na nikatizama nyuma yangu na kumshuhudia mlinzi wa baba aliyekuwa na mahusiano na mke wa baba akianguka chini na damu nyingi zikiwa zimetapakaa kifuani mwake huku bastola ya yule mama ikiwa mkononi.Mlinzi aliye mfyatulia risasi mwenzake ni yule ambaye alinipeleka bank

    “Aitaka kuwaua”

    Jamaa alizungumza huku akiusogelea mwili wa mwezake na kuuchunguza kama kweli amefariki dunia,Mke wa baba akazidisha kulia baada ya kumuona mpenzi wake akiwa amelala chini.Mama akanishika mkono na kuniondoa katika eneo la tukio na kunitoa nje huku akiendelea kunituliza hasira hadi nikarudi katika hali yangu ya kawaida

    “Baba anaendeleaje?”

    “Wamemuwahisha hospitalini”

    “Nani amempeleka?”

    “Amepelekwa na wafanyakazi wake pamoja na wale vijana walio tusaidia,tuwasubiri warudi ndio tutajua ni hospitali gani ambayo wamempeleka”

    “Ahaa sawa”

    “Yule uliye kuwa unampiga ni nani?”

    “Si ni mke wa baba”

    “Ahaa na yule mwengine aliye pigwa risasi?”

    “Ni mshenzi mwenzake ambaye walikuwa wakitembea pamoja na kumzunguka baba”

    Tukiwa katika mzungumza ya kawaida tukazishuhudia gari mbili za polisi pamoja na gari moja za wagonjwa zikiingia kwenye geti kuu la jumba la baba na kusimama sehemu ya magari ya kusimama,Wakaingia ndani na baada ya muda madaktari wakatoka wakiwa na kitanda cha matairi na juu yake wakiwa wamemlaza mke wa baba na kumuingiza kwenye gari lao na wakaondoka huku wakiwa wanapiga ving’ora.Askari wawili wakatufwata sehemu tuliyo simama na mama na kutusalimia kwa utaratibu

    “Tunaimani na nyinyi ni miongoni mwa wahusika kwenye hii nyumba?”

    Askari mmoja alizungumza huku akituangalia usoni na mama akanitizama kisha akajibu

    “Ndio labda tuwasaidie nini?”

    “Kwa jina ninaitwa Afande Lawnrance ninawaomba kuwafanyia mahojiano ya nini kilicho tokea muda mfupi uliopita”

    “Mimi ninaitwa Afande Martin

    Kitu ambacho nimekigundua kuwa askari huyu anaukarimu mkubwa na nitofauti na baadhi ya askari wa Tanzania ambaye kwenye tukio kama hili atataka kukutingisha tingisha ilimradi iwe ni shida,Mama akashusha pumzi na kumtazama askari Lawnrence

    “Kilicho tokea kwa ufupini kwamba yule mama aliye wahishwa hospitalini alimsukuma baba wa huyu kijana kutoka gorofani hadi chini ninaimani mumeona meza ya kioo iliyo pasuka?”

    “Ndio nimeiona”

    “Yaa hilo ndio kubwa ambalo limetokea na mengine mukawahoji wale wafanyakazi wa humu ndani”

    “Asante mama je kijana una lolote la kuzugumza”

    Kwa haraka mama akaniminya mguu pasipo askari kuono tukio hilo

    “Hapana sina la kuzungumza”

    “Haya asanteni kwa maelezo yenu”

    Wakatupa mikono na wakaondoka na kuniacha nikiwa na wasiwasi mwingi juu ya tukio hili na sheria za hapa Afrika kusini hata kama una pesa kiasi gani ila kama umefanya kosa lazima ustakiwe

    “Mama si watanikama wakiujua ukweli?”

    “Ndio..ila cha kufanya sasa hivi nikupeleke kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo hapa na urudi Tanzania na mimi uniache nishuhulikie hili swala”

    “Mama wewe ubaki.....!?”

    “Ndio nahitaji kulishuhulikia kwanza hili swala la baba yako la sivyo wataanza usumbufu tena wa kukupeleka mahakamani na ikiwa hivyo ujue ni ishu nyingine tena ya kukuweka mmatatani”

    “Sasa mama....”

    “Hakuna cha sasa tena ngoja nizungumze na vijana wa hapa kazi hiyo ifanyike sasa hivi”

    Mama akamuita mmoja wa walinzi wa baba na kuwaomba atupeleke ulipo ubalozi wa Tanzania

    “Si unapajua?”

    “Ndio mama ila mimi sihusiki na maswala ya usafiri na funguo zote za magari zipo ndani”

    “Eddy si unajua sehemu zinapokaa funguo za magari?”

    “Ngoja nikatazame ndani kwa baba”

    Nikaingia ndani na kuwakuta askari wakipiga picha sehemu za matukio yalipo tokea,moja kwa moja nikaingia chumbani kwa baba na kuanza kufungua kabati moja baada ya jengine na sikufanikiwa kuona funguo hata moja.Nikafungua droo ya kitanda na kukuta funguo mbili za gari pamoja na saa mbili za dhahabu.Nikaziingiza mfukoni saa na kuzichukua funguo na kutoka nje,nikiwa ninashuka ngazi askari mmoja akanifwata na kunizuia

    “Angalia usikanyange hiyo kwenye hilo sehemu lililo chorwa”

    Alinielekeza nisipite kwenye sehemu ambayo wameichora kama ushaidi,Nikapita pembeni na kutoka nje na kuwakuta mama na mlinzi wakitusubiria.Tukafika sehemu yenye magari ya baba na kuitoa funguo moja na kuminya kitufe kilichopo kwenye gari kikiwa na matumizi ya kulifungua gari husila la funguo hiyo.Gari moja likatoa mlio na sote tukajua ndio gari husika la funguo hii.Nikamkabidhi mlizi funguo na sote tukaingia ndani ya gari na kuondoka.

    Tukafika kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania na mama akashuka na kuniomba nibaki ndani ya gari na baada ya muda akatoka na kuniita kwa ishara na sote tukangozana hadi ndani ambapo akaanza kunitambulisha kwa balozi wa Tanzania Afrika kusini bwana Marki Msuya na baadi ya wafanyakazi wa ofisi hii.

    “Tena mumekuja muda mzuri kwa maana leo ndio siku ya wale vijana wa Tanzania walio zamia huku na kukamata ndio wanarudishwa”

    “Wanatumia usafiri gani?”

    “Serikali ya hapa imetupa ndege tuwarudishe vijana wetu wapo kama 248 hivi”

    “Si kijana wangu anaweza kupata nafasi kwa maana mimi ninahitaji kubaki huku kuna ishu nitaishuhulikika kabla ya kurudi nchini”

    “Ndio nafasi zipo.....Za masiku dada yangu kwa maana ninayo taarifa kuwa umetekwa na Al Shabab?”

    “Ahaa tutazaungumza baadaye kaka yangu ila kikubwa kwanza tumshuhulikie huyu kijana wangu”

    Mipango ya mimi kurudi Tanzania ikaanza kushuhulikiwa na jina langu likawa ni miongoni mwa majinina ya vijana wanao rudishwa Tanzania kwa kuingia nchini Afrika kusini pasipo kuwa na kibali maalumu.Mida ya saa nane mchana tukafika uwanja wa ndege wa O.R. Tambo International uliopo Johannesburg na nikajumuishwa na baadhi ya vijana nilio wakuta katika sehemu za kusubiria ndege muda wa kuondoka huku wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.Mama akanikumbatia kwa ishara ya kuniaga

    “Ukirudi hakikisha humuambii mtu yoyote ni wapi nilipo na hakikisha kuwa unafwatilia nyendo zima za baba yako na utakuwa unawasiliana na mimi”

    “Nitawasilia vipi na wewe kwa maana sina simu?”

    Mama akamuita balozi wa Tanzania na akamuoma namba yake ya simu ambayo akaiindika kwenye kikaratasi na kunikabidhi mimi

    “Hiyo utaitumia kuwasiliana na mimi kwa maana mama atakuwa kwangu”

    “Sawa”

    Muda wa kuondoka ukawadia na tukaongozwa hadi kwenye ndege ambayo ndi maalu kwa sisi kuondoka na tukaanza kuingia kwa majina na mimi nikawa mtu wa mwisho kwenye orodha ya majina na kuingia ndani ya ndege na kukuta wezangu wote wamekaa kwenye siti zao.Nikaanza kutafuta siti niliyoa ambiwa na muhudumu nikae.Kila abiria akawa ananitazama na macho yangu yakagongana na macho ya Sheila akiwa amejifunga kitambaa kichwani na pembeni yake amekaa jamaa mwengine

    “Sheila?”

    “Bee”

    Nikampa mkono nikataka kuanzisha mazungumzo ya kujua ni nini kimempata ila muhudumu akaniomba nikakae kwenye siti yangu iliyopo nyuma kabisa kwani ndege imebakisha dakika chache kabla ya kuondoka.Nikakaa kwenye siti yangu na kujufunga mkanda na nisita ambayo pembeni hapakuwa namtu yoyote na mashine za ndege zikawashwa taratibu,Kwa kupitia kwenye kiio nikazishuhudia gari sita za polisi zikija katika eneo ilipo ndege na kuizuia isiondoke na katika kuchungulia vizuri nikamuona Askari Lawrance akizungumza na waongozaji wa ndege wa chini akiwaomba ndege isiondoke na wakihitaji kumshusha mmoja wa abairia wa ndege hii na kwa haraka nikajua ni mimi ndio wamenifwata na kuyafanya mapigo yangu ya moyo kuanza kwenda kasi na amani ikanitoweka moyoni mwangu



    Kutokana tayari injini za ndege zilishaanza kuata moto haikuwa rahisi kwa kuisimamisha ndege ambayo taratibu ilishaanza kuondoka kuzipisha ndege nyingine ambazo zinasubiri kutua na kila kitu katika uwanjwa huu wa ndege vinakwenda na muda wanao jipangia.Macho yangu yakashuhudia jinsi tunavyo ziacha gari za polisi na ndege inavyo ongeza mwenza na kuitafuta njia ya kurukia

    “Ehee mola niokoe mimi mja wako kwa maana mmmm”

    Nilijizungumza kimoyo moyo na kweli ndege ikakaanza kunyanyuka taratibua na kuiacha ardhi ya Afrika kusini hadi ndege inakaa sawa angani ndio nikapata amani na kajasho taratibu kakanishuka huku kwa mbali nikijasikilizia jinsi mapigo ya moyo yanavyo punguza kasi yake,safari ikaendelea kwa amani na kutokana na uchovu mwingi nikajikuta nikilala fofofo pasipo na kitu kilicho nistua ni kipaza sauti cha rubani akituomba tufunge mikanda yetu vizuri kwani ndege inajiandaa kutua katika uwanja wa Jomo Kenyata nchini Kenya

    “Mmmmmmm”

    Nikajikuta nikiguna kwani sijazoea kuziona ndege zinazo toka nchini Afrika kusini kutua Kenya ili kwenda Tanzania na isitoshe kwa maelezo niliyo yasikia wakizungumza mama na balozi wa Tanzania ni kwamba ndege inakwenda moja kwa moja Tanzania.Moyo wangu ukaanza kupoteza amani tena ikanilazimu kumiya muhudumu wa ndege na hakusita kunifwata sehemu nilipo na kunisikiliza haja yangu niliyo muitia

    “Sijui nimesikia vibaya au....? Ni kweli tutatu Kenya?”

    “Ndio kuna mzigo tunaishusha kwanza na pia kuna mmoja wa abiria nanhitajika kurudisha Afrika kusini kwahiyo tunaiwahi ndege ya shirika letu inayo ondoka Kenya saa sita usiku na tutamkabidhi abiria huyo kwa askari.”

    Moyo ukawa kama umelipuliwa na bomo,kuzungumza nikajikuta nikishindwa na kubaki nikimtazama muhudumu kama sanamu la kushangaza

    “Halloo mr”

    Nikastuka na kumtazama muhudumu wa ndege ambaye alikuwa akinipungia mkono mbele ya uso wangu baada ya kuniona nikiwa nimegandishwa kama sanamu

    “Umesema kuna mtu anashushwa?”

    “Ndio hiyo ni taarifa tuliyo powa tukiwa njiani”

    “Ni mwanume au mwanamke”

    “Kusema kweli hatujatajiwa ni jinsia gani?”

    “Nashukuru”

    “Na wewe pia”

    Muhudumu akaondoka na kuniacha nikitawaliwa na mawazo na laiti ingekuwa nipo kwenye gari nigeweza kuruka na kufilia mali.Kitu cha ndege ni ngumu sana kujirusha,rubani akatutangazia kuwa zimesalia dakika tano kwa ndege kutua na kila mto ahakikishe kuwa amejifunga vizuri mkanda wake hapo ndipo nikakumbuka na mimi kujifunga mkanda.Ndani ya dakika tano ambazo rubadi alisema ndivyo jinsi iliyo kuwa na ndege nikaanza kushuka chini kwa kasi na matairi yake yakaanza kukanyaga ardhi ila gafla tukasikia mlio wa ‘KWAAA’ kama kitu kilicho katika na kuifanya ndege kuegemea upande wangu niliopo na wezangu tulio kaa upande huu.Milio ya vyuma kukatika katika tukazidi kuisikia na si mimi mwenye niliye anza kupiga kelele za kumuomba Mungu ila hadi wezangu nao wakafanya hivyo huku kila mmoja akiomba kwa lugha anayo ijua yeye mwenyewe

    Ndege ikazidi kulala upande wetu na kazidi kuserereka na mbaya zaidi moto mwingi ukaanza kuwaka sehemu ya nyuma mita chache kutoka ilipo siti yangu na kunilazimu kuufungua mkanda ili kuyaokoa maisha yangu kama wanavyofanya wezangu.Nikawahi kuishika siti ya mbele yangu ili kujizuia na upepo mwingi unao nivuta nyuma kutoka katika sehemu ulipo moto ambao umepasua sehemu nzima ya nyuma.Nikajikaza kwenda mbele na watu walio shidwa kujishikilia walivutwa nyuma kwenye moto.Kelele na vilio vikazidi kutawala na kila sehemu na watu wengi wakawa wamebanwa na siti zao kiaisi kwamba baadhi yao walijigonga vibaya kwenye vyuma na vichwa vyao kupasuka vibaya na wengine kukatika viungo vya miili yao

    Ndege ikagonga sehemu na kusababisha mtikisiko mkubwa na kupinduka kichwa chini miguu juu jambo lililosababisha mikono yangu kushindwa kuhimili kuishikilia siti niliyo kuwa nimeishika na nikajikuta nikiachia na kuanza kuvutwa nyuma na upepo mkali uliochanganyika na moto ambao ni mkali sana,Gafla nikastukia nikidakwa mkono na kuangalia vizuri nikamkuta ni Sheila ambaye amenishika mkono huku na yeye akiwa amekaa kwenye siti yake na kuzuiwa na mkanda alio jifunga na huku mkono mmoja akiwa ameushika kwenye siti iliyopo pembeni.Nikamtazama kwa macho ya huzuni na kumuona akishindwa kuhimili uzito wangu kwani tegemezi lote la mwili wangu ni mkono wake na sikuwa na sehemu yingine ya kushikilia

    “Sheila niachie nife”

    “Eddy unasemaje?”

    “Niachie.”

    Nilizungumza huku nikimtazama Sheila machoni ambaye anatumia nguvu nyingi kunizuia nisichomolewe nje ya ndege na mbaya zaidi pembeni yangu hakuna kitu ambacho ninaweza kusema kuwa nitakishika ili kinizuie nisichomolewe nje kwani siti zote za nyuma zimechomoka na watu wake.Ndege ikaendelea kugonga majengo yaliyopo ya hapa uwanja wa ndege hadi ikasimama ndipo Sheila akaniachia mkono na mimi nikaanguka chini na kujigonga mkono wangu wa kushoto kwenye upande wa pili wa ndege.Sheila akaaanza kupata shida ya kujifungua mkanda wa siti yake na mbaya zaidi kwa jinsi ndege ilivyo anguka imemfanya awe kichwa chini miguu juu

    Nikaanza kusikia ving’ora vya gari za zimamoto zikija katika eneo la tukio na kuazna kuuzima moto unaoendelea kuiteketeza ndege,moshi mwingi ulio tawala ndani ya ndege ukanifanya nianza kukohoa na taratibu nikaanza kujivuta nje ya ndege huku mkono wangu ukitawaliwa na maumivu makali.Niavutwa nje na waokoaji na gafla mlipuko mkubwa wa ndege ukatokea na kuturusha mbali mimi pamoja na waokoaji na nikajzidi kuuegemea mkono wangu ambao ninahisi unamaumivu

    “No Sheila?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikajinyanyua na kuanza kutembea huku nikiyumba na kujitahidi kurudi kwenye ndege ila baadhi ya waaokoaji na askari wakanizuia,Machozi mengi yakaanza kunitawala kwani moja kwa moja ninatambua kuwa Sheila ni miongo mwa walio lipuka na ndege.Wazo la kwamba ninatafutwa na polisi na ninahitajika kurudishwa Afrika kusini kujibu mastaka yangu likanijia kichwani.Nikawatazama askari na waokoaji nikaona kila mmoja yupo na mihangaiko ya kuwaokoa majeruhi wengine na taratibu nikaanza kutembea kwa kujikaza pasipo kutazama pembeni wala nyuma zaidi ya kwenda mbele huku mkono wangu wa kushoto nikiwa nimeushikilia vizuri.Machela moja ikapitishwa kwa haraka pembeni yangu na waokoaji huku wakikimbia kwa kwasi na mtu waliye mmbeba juu ya machela nikamtambua ni Sheila japo mwili wake umeharibika sana kwa moto kitu kilicho nifanya nimtambue kwa haraka ni nguo zake alizo zivaa,wakamuingiza ndani ya gari ya wagonjwa na wakaondoka

    Nikabaki nikiwa na mshangao sikujua ni nini nifanye,Nikiwa ninaendelea kushangaa nikwaona askari wawili wakinifwata sehemu niliyo simama.Nikaanza kutembea kwa mwendo wa haraka huku nikigeuza geuza shingo yangu nyuma na kuwatazama askari na kuwoana nao wakiongeza mwendo wa kunifwata.Moto mkali ulio andamwa na upepe mkali ukaanza kushika majengo mengine ya uwanja wa ndege na kuwafanya watu waliopo kweye eneo hili kuaanza kukimbia kimbia ovyo kuyaokoa maisha yao.Nikajichomka katikati ya watu wanaokimbia kuokoa roho zao na nikafanikiwa kutoka nje ya uwanja wa ndege.Nikaendelea kukimbia hadi nikafanikiwa kutoka nje ya uwanja wa ndege na nilipo tizama nyuma yangu sikuweza kuwaona askari wakinifwata.Mauivu ya mkono yakazidi kunitawala na sikuwa na jinsi zaidi ya kujikaza kiume na kuendelea kutembea nisipo pajua na kunyoosha barabara ya lami ambayo nikatembea kwa umbali mkubwa na kukuta kibao kilicho andikwa Athi River na kutokana na uchovu mwingi nikatafuta sehemu nikajipuumzisha pembezoni mwa barabara,Nikapata sehemu nikajipumzisha hadi kulipo pambazuka mida ya saa kumi na moja alfajiri nikasimama barabarani na kuanza kusimamisha magari yanayo pita.Nikafanikiwa kuahatisha gari moja la watalii aina ya Landrover ikasimama

    “Where are you going young boy?”(Unakwenda wapi kijana?)

    “Am going Tanzania”(Ninakwenda Tanzania)

    “Are you a Tanzanian?”(Wewe ni mtanzania?)

    “Yes”(Ndio)

    Mama wa kizungu alinihoji maswali hayo kisha akazungumza na mume wake kwa lugha ya kireno,ambaye ni dereva wa gari lao na akanikubalia kupanda ndani ya gari lao na safari ikaanza.Ndani ya gari ukimya ukatawala huku nikiyasikilizia maumivu ya mkono wangu ambao unavuta kwa kiasi kikubwa na sikuhitaji waweze kujua juu ya kuvunjikwa kwangu mkono kwani wangenihoji maswali mengi yasiyo na msingi wowote kwangu

    “What’s your name?”(Jina lako ni nani?)

    “My name is Eddy”(Jina langu ni Eddy)

    “You have a good name as our soon”(Unajina zuri kama mtoto wetu wa kiume)

    “Thanks”(Asante)

    “My name is Madam Loren we are going Moshi”(Jina langu ni Madam Loren,tunakwenda Moshi)

    Sikutaka kujua wanakwenda Moshi kufanya nini kwani mkono wangu unaniuma kupita maelezo,Hadi tunafika Arusha Tanzani mida ya saa sita mchana hatukuweza kusimamishwa na askari njiani na tuliingilia kwa njia ya Monduli hadi tunafika Arusha mjini nikawaomba wanishushe na nikawashukuru kwa masaada wao kisha wakaendelea na safari yao kwani walinieleza wanaelekea Moshi.Nikaanza kupandisha barabara ya Old Moshi na moja kwa moja nikaenda nyumbani kwa Madam Mery.Nikafika nyumbani kwa madam Mery na kukuta mabadiliko kidogo kwani rangi ya ukuta na gati lake vilikuwa vimebadilishwa

    Niikaanza kugonga kwa kutumia mkono wa kulia na nikasikia sauti ya kike ikisema inakuja kufungua,Nikasimama kwa dakika kadhaa na gati likafunguliwa na akasimama msichana akiwa amemshika mtoto mdogo mkononi mwake akiwa anasura inayo endana na mimi

    “Nikusaidie nini kaka?”

    “Ehee madam Mery nimemkuta?”

    “Hayupo amekwenda kazini”

    “Wapi?”

    “Shuleni hapo juu...Karibu ndani”

    Nikatazama pande zote za nje kisha nikaingia ndani huku nikimtazama mtoto aliye bebwa na mtoto msichana ambaye ninahisi ni msichana wa kazi na kusema kweli kila kitu ambacho mimi ninacho kwenye sura yangu kipo kwa huyu mtoto mdogo.Binti akatangulia kuingia sebleni na akanikaribisha kwenye masofa mapya niliyo yakuta ndani ya sable hii kidogo nikashusha pumzi,Gafla macho yangu yakagongana na mume wa Madam Mery ambaye siku zote ni adui yangu na mara ya mwisho nakumuka nilimpiga kichwa na akanitolea bastola na jamaa sura yake ikabadilika gafla akanitazama kwa umakini kisha macho yake akayahamishia kwa mtoto aliye bebwa na mfanyakazi wake



    “Waooo ni muda sasa sijakuona naona umekuja kuchukua kiumbe chako si ndio?”

    Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio huku nikimtazama mume wa Madam Mery na kajasho kembamba kakaanza kunimwagika

    “Nipe huyo mtoto”

    Mfanyakazi wa ndani akamkabidhi mume wa madam Mery mtoto ambaye tayari nimegundua kuwa ni mwanangu.

    “Nenda ndani?”

    Mfanyakazi wa ndani akaondoka na kutuacha na mume wa Madam,Japo ninamaumivu ya mkono nikajaribu kunyanyuka ila niweze kujiokoa,mume wa madam Mery akamshika mwanangu kichwa chini miguu juu na kumfanya mtoto kuanza kulia kwa sauti

    “Kaa hapo hapo la sivyo huyu paka wako ninamwangamiza mbele ya macho yako”

    Nikamangalia jinsi mtoto wangu anavyolia na kujikuta roho ya huruma ikinitawala na nikakaa chini nikimtazama mume wa Madam Mery,Akatoa simu na kuipiga

    “Njoo nyum bani”

    Jamaa akakata simu na kurudisha mfukoni kisha akaniangalia machoni na kutabasamu.Akamshika mtoto vizuri na kuanza kumbembeleza huku akizunguka huku na huku ndani ya sable.Mlango ukafunguliwa na akaingia Madam Mery akiwaavalia vizuri na ule uzuri wake umezidi kuongezeka na baada ya kunioana akaonekana akistushwa.Akapitiliza hadi kwa mume wake na kumpiga busu la shavu kama ishara ya salamu

    “Nenda kakae kule”

    “Ehee”

    “Nenda kakae kwa mshenzi mwenzako”

    Jamaa alizungumza kwa hasira hukua akimsukuma Madam Mery kuja kukaa kwenye sofa ambalo nimekaa

    “Jamani Derick mume wangu si tulisha lizungumza na limeisha mbona unataka kuanzisha ugomvi?”

    “Nyamaza Malaya mkubwa wewe,hivi unajua uchungu nilio kuwa nao wewe,Au unadhani kukaa siku zote kulea kiumbe kisicho changu hivi unajua ni maumivu gani ambayo ninayo moyoni mwangu”

    Derick alizungumza huku machozi yakimwagika na mtoto wetu akiwa amemshika mikononi mwake.Madam Mery machozi yaakanza kuutawala uso wake

    “Derick nakuomba unisamehe kwa mara nyingine sito rudia tena kukusaloti mume wangu”

    “Ahaaa chagua mawili kati yangu au huyu panya wako?”

    Macho yakanitoka nilipomuona Derick akifanya kitendo cha mara ya kwanza cha kumshika mwanangu kichwa chini miguu juu huku akiwa amemuinua kwa mkono mmoja

    “Derick nyote ni muhimu sana kwangu ninakuomba mume wangu unisamehe nina kupenda sana mume wangu”

    “Wewe manamke ni muuaji,kumbuka mimi ndio nilikufanya kupata elimu yako hadi akawa mwalimu ukaona haitoshi ukanisaliti mara ya kwanza nikakusamehe......Baba yako alifariki mikononi mwangu tukimuwahisha nchini India kwa matibabu na zote zilikuwa gharama zangu senti tano kwenu mulikuwa hamuna nimevunja vibanda vyenu na kuwajengea nyumba nzuri ili nanyi muonekane watu kati ya watu ila bado umeona hatoshi kabla ya ndoa yetu umebeba mimba ambayo si yangu ni ya uyo paka hapo.”

    “Ni mara mia ungetembea na mtuu aliye kuzidi umri ila wewe ukachukua Serengeti Boy unadhani atakusaidia nini huyo mwehu wako”

    Derick aliendelea kuzungumza kwa hasira huku machozi yakiendelea kumwagika na mwanangu akiendelea kulia kwa maumivu anayo yapata.Madam Mery kapiga magoti na kuanza kuburuzika taratibu akimfwata mumewe sehemu aliyo simama

    “Rudi huko huko la sivyo ninamuua huyu paka wenu.”

    Madam Mery akaanza kurudi nyuma taratibu huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi.Kelele za mwanangu kulia kwa maumivu zikanifanya nishindwe kuvumilia huku hasira ikinipanda nikanyanyuka huku nikiwa nimeushika mkono nilio vunjika na kupiga hatua mbili mbela za kuikwepa miguu ya madam mery

    “Wewe rudisha miguu yako huko la sivyo ninamuachia huyu mtoto”

    Derick aliniambia akionekana kutokuwa na huruma kabisa na maumivu anayo yapata mwanangu,nikashindwa kuizuia miguu yangu na kujikuta nikizidi kupiga hatua kwa hasira kali iliyo nitawala mwili mzima.Derick akampiga mwanagu chini kwa nguvu na kumfanya mtoto wangu kunyamaza kimya na kelele kali ikatoka kwa madama Mery pamoja na mfanyakazi wa ndani ambaye alikuwa amejificha kwenye ukuta akishuhudia kila kinacho endelea.

    Sikujali kama mkono wangu mmoja umevunjika kwa hasira nikamrukia Derick ambaye akanikwepa na kunisindikiza kwa teke kali la mgongoni na kujigongwa kwenye uso kwenye ukuta na kuangukia pembeni ya miguu ya mfanyakazi wa ndani ambaya mkononi mwake ameshika kisu na kitunguu.Nikamuomba mafanyakazi wa ndani kisu kabla hajanipa Derick akauwahi mkono wa mfanyakazi wa ndani ulio shika kisu ikanilazimu na mimi kuuwahi mkono wa mfanyakazi kwa kuutumia mkono wangu mmoja usio vunjika.Derick akatuzidi nguvu na kumshika mfanyakazi wa ndani na kusukumia pembeni na kisu kikaanguka chini.Kabla Derick ajakiokota nikampiga teke na kuifanya miguu yake yote miwili kunyanyuka chini na akaangukia mgongo.

    Nikajisogeza kwa haraka na kabla sijakiokota kisu akanikanyaga vidole vya mkono wangu wa kulia nilio unyoosha kukiokota kisu.Derick akakipiga kisu mbali kido na eneo ambalo nililo angukia akanipiga teke la mbavu lilinifanya nijikunje huku nikigumia kwa maumivu makali.

    “Derick utamuua mtoto wa watu”

    Madam Mery alizungumza huku akimwagikwa na machozi na mikpono yake ikiwa imejaa damua na vitu vyeupe vyeupe na kugundua kuwa mwanangu amepasuka kichwa chake.Nikanyanyuka huku meno yangu nikiwa nimeyang’ata kwa nguvu.Nikajaribu kuuyanyua mkono wangu wa kushoto ulio vunjika na kuufanya kuuma kwa maumivu makali yaliyonifanya nitoe ukelel wa kuumia kwani kuna kitu kinanichoma kwa ndani.Derick akayashusha macho yake hadi kwenye mkono wangu kisha akayarudisha machoni mwangu na kwa haraka akanitisha kama ananipiga teke kwenye mkono na kuufanya niukinge mkono wangu kwa kugeuka na kumpa mgongo na kushtukia akininyanua miguu yangu na kuivuta na kuanguka kifudifudi huku mkono ulio vunjika nikiwa nimeulalia

    Derick akanikalia mgongoni na kuishika mikono yangu yote miwili na kuivuta kwa nyuma.Maumivu ninayo yapata sikuwahi kuyapata tangu nizaliwe.Madam Mery akauweka chini mwili wa mtoto wetu na kukimbilia sehemu tuliyupo na kumsukuma Derick na akaanguka kwa mbele yangu.Sikuwa na uwezo wa kunyanyuka kuokana na maumuzi makali na kubaki nikilia kwa uchungu.

    “Ni binadamyu gani usiye na huruma wewe,umenilia mwanangu kikatili ila bado unataka kumuu huyu kijana wa watu”

    “Niliapia ni lazima nimuue huyu kijana pamoja na wewe na leo ndio mwesho wenu”

    Derick alizungumza huku akinyanyuka kwa haraka na akamshika madam Mery nywele zake na kumbwaga chini kwa nguvu na kumfanya madam mery kutoa ukulele wa kulia kwa maumivu

    “Shemeji mikono yako nyoosha juu”

    Niliisikia sauti ya mfanya kazi kwa nyuma yangu na kunifanya nigeuke nyuma na kumkuta akiwa ameshika kisu huku mwili mzima ukimtetemeka.Derick akacheka kwa dharau na kumfwata mfanyakazi kwa kasi na kupiga kabali ya gafla na kumpokonya kisu na pasipo kuwa na huruma Derick akamchoma mfanya kazi wa ndani kisu cha tumbo na kumtupa chini.Derick akanisogelea huku kisu chake kikiwa kinavuja damu za mfanyakazi,akaniinamia na kunitazama kwa umakini huku akicheka

    “Nilikuumbia siku nikikutia mikononi mwangu nilazima nikuue”

    Maneno ya Derick hayakuhafikiana na moyo wangu kuyakubali kiharaka na kirahisi kama anavyo fikiria.Kwa haraka nikainyanyua miguu yangu kuikaba shingo ya Derick na kwa nguvu zote.Madam Mery akamuwahi kumshika Derick mkono ulio shika kisu na kumpokonya,Kila nilipo kumbuka jinsi mwangu alivyo anguka chini ndivyo jinsi nilivyozidi kumkaba Derick shingo yake ambaye akaanza kunishindilia ngumi za mbavu na akaubana mkono wangu uliovunjika na kuzidi kunifanya niachie ukele mkali

    “Madam nisaidieeeeeee”

    Madam akabaki akiwa ameshika kisu asijue nini afanye,Nikamuomba tena anisaidie ndipo akastuka kama yupo sehemu ya tukio la hatari,akatutizama tena kwa umakini na kwaharaka kisu akakishusha na kikatua kwenye bega la Derick na kumfanya aniachie na kunyanyuka kama mbogo na kumsukuma Madam Mery ambaye akaangukia mwili wa mtoto wetu na kutulia chini

    “Nitaendelea kukusaka”

    Derick alizungumza huku akiingia ndani kwa haraka na kutoka akiwa na begi la kuburuza na akanitazama kwa muda kisha akanipiga teke la kichwa na kizunguzungu kikali kikanitawala kikiambatana na giza kubwa lililo tanda kwenye macho yangu na nikatulia tuli

    ***

    Milio ya ndege pamoja na mwanga mkali vikanistua na kujikuta nipo kwenye chumba chene kitanda kimoja tuu.Pembeni ya kitanda kuna meza ndogo pamoja na kiti,Kila ninapojaribu kuitadhimini sehemu hii ninashindwa kujua ni wapi.Mbaya zaidi sehemu hii haifanani na hospitalini kwani kitanda nilicho lala kinaukubwa zaidi ya kitanda cha hospitalini.Nikajichunguza vizuri na kuukuta mkon wangu ukiwa umefungwa bandeji gumu(P.O.P.O).Nikashuka kitandani na kwenda dirishani na kufungua dirisha nikaona migomba mingi nikstukia kwa nyuma mlango ukifunguliwa na akaingia mama mmoja mtu mzima

    “Umeamka mwanangu?”

    “Shikamoo”

    “Marahaba,unajisikiaje?”

    “Vizuri tuu”

    Akanishika mkono na kuugeuza geuza kisha akanitazama usoni huku akiwa ameachia tabasamu pana

    “Mimi ninaitwa Mama Natujwa na hapa ulipo ni Moshi”

    “Nimefikaje?”

    “Umeletwa na rafiki yangu anaitwa Mery na tangu uje hapa huna hukuwahi kuyafumbua macho yako na ulikuwa ni mgonjwa mahututi sana”

    Ikanibidi kurudi kitandani na kukaa kwani niliaza kuhisi kizungu zungu,Mama Natujwa akakaa pembeni yangu huku akinishika shika kichwa changu na kunigeuza huku na huku

    “Mimi ni daktari wa mifupa ninamiliki hospitali yangu hapa Moshi,na kipindi Mery alipo kuleta nilikufanyia oparesheni hospitalini kwangu na tukakulaza kule kwa kipindi cha mwezi mzima huku tukikulisha kwa mipira maalumu.Nilipo kuleta hapa nyumbani kwangu tatizo lililo kuwa kubwa ni wewe kurudi katika hali yako ya kawaida”

    “Ni kipindi gani kimepita?”

    “Unakwenda mwezi wa tatu sasa,Japo Mery alikata tamaa ya kudaidi kuwa huto weza kurudi katika hali yako ya kawaida”

    “Na yeye sasa hivi yupo wapi?”

    “Yupo Arusha anaendelea na kazi...tena ngoja nimpigie simu nimjulishe kuwa umezinduka?”

    Nikamzia mama Natujwa kumpigia simu Madam Mery

    “Kwa nini unanizuia?”

    “Sihitaji alijue hili sawa”

    “Je akija?”

    “Nimekuambia sihitaji aweze kugundua jambo hilo”

    Akili na wazo juu ya mauaji ya mwanangu likanijia kichwani mwangu,Picha niyingine ya jinsi nilivyo teseka kwenye pango nchini Afrika kusini likanijia kichwani mwangu na sura ya baba yangu mkubwa Mzee Godwin ikanijia kichwani huku ikifwatiwa na sura ya Derick.

    “HII KAZI NITAIFANYA MIMI MWENYEWE”

    Nilizungumza kwa sauti ya chini na kumfanya mama Natujwa kuniuliza ninasemaje

    “Hapana sijazungumza kitu”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikaka nyumbani kwa mama Natujwa kwa wiki moja,Nilipo ridhika afya yangu ipo kamili nikamuomba ruhusa ya kuondoka na akanikubalia ila kwa kipindi chote sikumuomba asizungumze chochote kwa Madam Mery,Nikapanda basi hadi Dar es Salaam na sikufikizia nyumbani kwetu nikelekea nyumbani kwa Sheila na kukuta geti lake likiwa wazi na gari yake ikiwa imesimamishwa nje.Nikapata matumaini ya uwepo wake na moja kwa moja nikaufungua mlango wake na sikuamini macho yangu baada ya kumkuta akiwa ananyonyana denda na mwanaume mwengine ambaye kwa haraka nikamtambua ni Derick mume wa madam Mery



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog