Search This Blog

Tuesday, 17 May 2022

CHAGUO LA MOYO WANGU - 1

 







    IMEANDIKWA NA : MICHAEL MICHAEL



    *********************************************************************************



    Chombezo : Chaguo La Moyo Wangu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ilikua ni asubuhi siku ya jumatatu ambapo watu mbalimbali walikua wakiendelea na mihangaiko yao ya kila siku ili kujitafutia riziki katika mji mdogo wa zingawe,kijana mdogo ambae kwa makadirio alionekana kuwa na umri wa miaka 22 aliamka katika kitanda chake baada ya mwanga wa jua la asubuhi kupenya katika matundu yaliyo katika kuta za kibanda anachoishi na kufanya kuwe na mwanga kiasi katika kibanda hicho.

    Michael ndio jina la kijana huyo ambae alikua hana mbele wa nyuma katika maisha yake hasa baada ya kuwapoteza wazazi wake wote wawili katika ajali iliyotokea huko milima ya senkeke mkoani singida,aliamka kutoka katika kitanda chake na kuanza kupiga mihayo kutokana na njaa aliyo kua nayo tangu jana usiku,na hii ni kutokana na kutoingiza chochote tumboni kutokana na ugumu wa maisha aliokua nao,alijivuta taratibu na kwenda kufungua mlango wa kibanda alichokua anaishi,lakini alipofungua mlango alishtuka hasa baada ya kuona vijana wanne ambao walionekana ni polisi wakimuweka chini ya ulinzi,kabla hajaelewa kinachotokea,ghafla alishangaa anatiwa pingu mikononi mwake nakupandishwa katika defender ambapo safari ya kuelekea kituo cha polisi asicho kijua ilianza...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safari hiyo iliishia katika jumba moja kubwa na lakifahari ambapo defender hiyo ya polisi ilipofika ilipiga honi ambapo geti lilifunguliwa kisha gari hilo kukomea sehemu ambapo ilionekana kua na parking ya magari,na hii ni kutokana na kuonekana kwa magari kadhaa ya kifahari yakiwa sehemu hiyo,baada ya gari hilo kupaki,Michael aliteremshwa kutoka katika gari hilo na kuingizwa ndani ya jumba hilo kubwa na lakisasa,alifikishwa katika chumba kimoja ambapo mmoja wa wale polisi alibofya tarakimu kadhaa ambazo zilionekana mlangoni hapo kisha mlango ukafunguka,baada ya mlango huo kufunguka Michael aliingizwa ndani na kukalishwa katika moja ya viti vilivyo humo ndani.

    Michael alipata wasiwasi sana na kuuliza,nyie ni kina nani? na kwanini mmenileta huku wakati mliniambia nahitajika kituo cha polisi halafu mmenileta huku? hayo ni maswali mfululizo ambayo Michael aliwahoji wale watu ambao walionekana ni polisi kutokana na mavazi waliyovaa...

    kijana ni bora ukakaa kimya tuu tusije tukauondoa uhai waki,ni jibu ambalo alipewa kijana Michael na mmoja kati ya wale watu watatu ambao walionekana ni polisi.Baada ya majibu hayo,jamaa wale watatu walitoka nje nakuufunga mlango wa chumba kile ambacho ndimo walipo muhifadhi kijana Michael..

    Waliotoka na kuelekea upande wa kulia wa chumba kile ambapo kulikua na korido ndefu iliyowafikisha mpaka katika sebule moja pana kiasi ambayo ilikua na masofa pamoja na vitu kadhaa vya thamani ikiwa ni pamoja na TV flat screen ya nchi 32 na jokofu(fridge) kubwa kiasi iliyo sheheni kila aina ya kinywaji.Polisi wale watatu kama walivyoonekana kutokana na mavazi ya kipolisi waliyoyavaa,waliketi katika moja ya sofa lililokuwepo katika sebule ile kubwa na pana kiasi,baada ya dakika kama mbili kupita ndipo kijana mmoja kati ya wale watatu akatoa simu yake kisha kuandika tarakimu kadhaa nakuiweka simu ile sikioni ambapo baada ya sekunde kadhaa simu ile ilipokelewa upande wa pili.

    Mkuu tumeshakamilisha tayari, ni maneno aliyozungumza yule kijana na upande wa pili ukajibu,nusu saa tafadhali nitakua hapo,simu ikakatwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande wa Michael alianza kumuomba mungu amuepushe na matatizo yote ambayo alifikiri yanaweza kutokea muda wowote katika eneo hilo alilokuwepo.

    Baada ya nusu saa ilisikika honi ya gari nje ya geti ya jumba ambalo alikuwepo Michael ambapo geti lilifunguliwa na ikaingia gari moja aina ya hummer,baada ya kupaki eneo husika,alishuka mzee mmoja ambae alikua na makadirio ya miaka kama 60,mzee yule aliingia ndali ya jengo lile na kuelekea moja kwa moja ilipokua sebule ya jumba lile la kifahari ambapo ndipo walipo kua wameketi wale vijana watatu ambao walionekana ni polisi.

    Alipo fika katika sebule ile alisalimiana na wale polisi kisha kupelekwa sehemu ambapo polisi wale walimuhifadhi michael.

    Kazi nzuri,ni maneno aliyoyatamka mzee yule wa makamo akiwaambia polisi wale ambao aliwaita kwa majina ya Dan,Jackson na Mbuba kisha kuwakabidhi briefcase iliyojaa maburungutu ya dola za kimarekani.Nash

    ukuru boss" alijibu Jackson ambae ndie alionekana ni kiongozi wa wale polisi, “tutazidi kuwasiliana!" alijibu mzee yule aliyejulikana kwa jina la Samwel kisha mlango ule kufungwa..



    baada ya mlango ule kufungwa mzee samwel alitoka kisha kuelekea katika sebule ya jumba lake lile la kifahari,safari yake ilikomea katika jokofu(fridge) na kuchukua kilevi katika jokofu lile kisha akaketi katika moja ya sofa lililopo mle ndani na kuanza kunywa kilevi chake taratibu huku akitafakari mambo mbalimbali hasa kuhusu biashara zake,ila kubwa kabisa ni kuhusu biashara yake haramu ya usafirishaji wa madawa ya kulevya kwenda nje ya nchi.

    Kwa upande wa michael naye alikua mbali kimawazo hasa akitafakari juu ya mustakabali wa maisha yake na matukio mengi ambayo yamekua yakiandama maisha yake,kuna wakati aliwalaumu wazazi wake waliokufa miaka mingi iliyopita na wakamuacha katika hali ya dhiki huku maisha yake yakiwa hayana mbele wala nyuma na hii ni kutokana na wazazi wake kutomuachia msingi mzuri wa kimaisha,alishtuka ghafla kutoka katika mawazo hayo hasa baada ya kuhisi mlango wa chumba alichokuwepo ukifunguliwa,haikua tofauti sana na hisia zake kwani baada ya dakika moja mlango ule ulifunguliwa kisha mzee samweli akaingia ndani mule akiwa na bastola mkononi kisha mlango ule kufungwa,michael alianza kuingiwa na hofu hasa baada ya kuona bastola ile na kuanza kufikiria kuwa mwisho wa maisha yake umefika.Kijana naomba ukae na unisikilize kwa umakini sana,ni sauti iliyotoka katika kinywa cha mzee samweli,sawa alijibu samweli kwa sauti ya kitetemeshi kidogo na hii ni kutokana na woga aliokua nao,kilipita kimya kidogo na baada ya muda mzee samweli alianza kuzungumza,kijana kwanza nakupa pole kwa usumbufu ulioupata kutoka kwa vijana wangu niliowatuma waje kukukamata,aliongea mzee yule kisha kuweka nukta.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini mzee mimi nimefanya... kabla michael hajamalizia sentensi yake alishangaa bonge la kofi linatua katika shavu lake na kuhisi huenda meno yametoka hasa kulingana na uzito wa kofi hilo lililotoka kwa kwa mzee samweli,pumbavu kabisa wewe kijana,ndo mama yako alikufunza hivyo, kuongea wakati mimi bado sijamaliza kuongea? nakuuliza wewe mwanaharamu,ni maswali mfululizo ambayo mzee samweli alikua akimuuliza michael,nisamehe mzee wangu.. michael alitamka kwa unyonge.

    Mzee samweli aliendelea,kijana nimekuleta hapa sio kwa ubaya kama unavyofikiria,kwanza kabisa ujue ya kua wale waliokuja kukukamata sio polisi bali ni vijana wangu wa kazi,lakini kubwa hasa lililopelekea wewe kuletwa hapa ni kwamba nilikua nahitaji mtu kwaajili ya kunisaidia kazi za ndani,lakini kubwa zaidi ni kumsaidia binti yangu majukumu madogo madogo hapa nyumbani ambae alikua masomoni nje ya nchi na hivi masaa machache yajayo atakua hapa nyumbani,kwahiyo nahitaji jibu kutoka kwako,aliweka kituo mzee huyo na kumruhusu michael kuzungumza...

    Michael alitafakari maisha yake ya nyuma na kutafakari dhiki alizokua nazo..., ndio mzee nipo tayari,ni jibu alilotoa michael kumwambia mzee samweli,vizuri kijana sasa naomba twende nikakuonyeshe chumba chako kisha nikuonyeshe mazingira ya hapa na sehemu muhimu za kufanya usafi kila siku,aliongea mzee samweli kisha kumpeleka michael kwenye chumba chake ambacho atakua analala na kumuacha humo akijiandaa kisha yeye alielekea sebuleni ambapo alienda kumsubiri michael amalize kujiandaa ili akamuoneshe majukumu ambayo alitakiwa kuyafanya ndani ya jumba hilo la kifahari...



    Baada ya mzee samwel kumsubiri Michael kwa dakika kadhaa pale sebuleni,Michael alikuja na kisha walitoka na mzee yule ambae alianza kumtembeza Michael sehemu mbalimbali ambazo alitakiwa kuzifanyia usafi kilà ifikapo asubuhi.

    Baada ya kumaliza kumtembeza katika jumba lile,mzee samwel alimuacha Michael hapo nyumbani kisha yeye alielekea uwanja wa ndege(airport) kumfuata mwanae kipenzi,alifika uwanja wa ndege na kumkuta mwanae akimsubiri.

    Shikamoo baba alitamka binti yule aliyekua na figa matata la kibantu,marhaba mwanangu Judith,aliitikia mzee samwel huku akikumbatiana na mwanae huyo kipenzi.Baada ya salamu hiyo,mzee samwel alimpokea mwanae mizigo kisha kuelekea sehemu aliyopaki gari lake,alipakia mizigo yote kisha kumfungulia mwanae mlango wa gari ambapo mwanae aliingia,baada ya mwanae kuingia ndani ya gari mzee Samwel alifunga mlango kisha nae akaelekea upande wa dereva na kufungua mlango kisha akaingia ndani ya gari na kuufunga mlango huo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliwasha gari kisha kuingiza gia na kuanza kukanyaga mafuta taratibu ambapo gari lilianza kuondoka na safari ya kuelekea nyumbani ilianza.Baada ya dakika kumi walikua tayari wameshafika nyumbani ambapo Michael aliwasaidia kushusha mizigo kisha kuipeleka ndani,baada ya kuingiza mizigo yote ndani,Michael alitoka nje na kuendelea na kazi yake ya kupunguza nyasu katika bustani,kazi ambayo aliianza tangu mzee samwel alipoenda kumpokea mwanae uwanja wa ndege.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog