Search This Blog

Thursday, 19 May 2022

SHEMEJI INGIZA POLE POLE - 1

 





    IMEANDIKWA NA : HANS CHARLZ



    *********************************************************************************



    Chombezo : Shemeji Ingiza Pole Pole

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Naitwa Isabela ni mzaliwa katika wilaya ya kwimba mkoani Mwanza nilizaliwa mwaka 1987 katika hospitali ya rufahaa bugando. Katika Familia yangu tumezaliwa watoto Wa wili Mimi pamoja na kaka yangu Gabriel na pia wazazi wetu walitulea kwa misingi ya dini na pia wazazi wangu na sisi kwa ujumla tuliishi kwa kutegemea kilimo. Hatukufanikiwa kuishi na wazazi wote kwani mzazi mmoja akitanguria mbele za haki R I P (BABA) mwaka 1999 kipindi hicho sito kisahau kwani baba alitutoka kwenye mazingira ya kututatanisha siku hiyo ilikuwa jumapili asubuhi na mapema baba aliamka na kwenda

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    shambani basi Mimi pamoja na mama na kaka yangu Gabriel tulichelewa kwenda shambani kutokana na shuguri za asubuhi na tulipo maliza Kazi hizo tulielekea nasi tukaungane na baba yetu kwa siku hiyo. Tulifika shambani Mara moja hatukupoteza mda tulianza Kazi kwani tulikwisha muona baba yetu yuko ng'ambo ya pili akiendelea kulima. Masaa yalipita machache Mara gafra alipiga kelele na kunyamaza kimya wote tulishituka na hofu mwili mzima ilinitawala na ndipo tulielekea alipo baba yetu na tulipofika tulimkuta baba kalala chini na aongei tena yani alikuwa ameshatutoka. Tulikia sana kwani hatukujua nini kilimpata baba yetu na kupelekea mauti yake kwani alikuwa mtu mwenye afya nzuri siku hiyo. Basi tulifanya mipango ya mazishi ambayo haya kuchukua mda mwingi sana yalikamikika huku tukisaidiwa sana na wanakijiji na wana ndugu wachache walio fika kwenye msiba basi kila tulipo maliza mazishi kila mmoja alirudi na kuendelea na shuguri zake. Mama alikuwa mpweke sana kipindi hicho kwani ndiye aliyekuwa nguzo yetu na mboni yetu kwa kila kitu kwani ndiye aliyekuwa akitusomesha kwa bidii na kutusihi tusome tuutikomeze ujinga Mimi pamoja na kaka yangu Gabriel na alitutoka gafra sana kwani tulikuwa ndio tunaitimu masomo yetu darasa LA saba na ndicho kipindi tulikuwa tukisubili matokea ya kujiunga na sekondari. Matokeo yalikuja vizuri mimi pamoja na kaka yangu Gabriel tulichaguliwa kujiunga. Mama alipo pata taharifa ya kuwa sisi tumefanikiwa kujiunga na masomo ya sekondari mama.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alifulai sana japo kuwa alikuwa akifikilia juu ya pesa ambayo itaweza kutupeleka shule Mimi pamoja na kaka yangu Gabriel kwani msiba ulivyo tokea wana ndugu Wa upande Wa baba walitokea kututenga pindi msiba ulivyo kwisha kumalizika wana ndugu walihitaji Mali za baba japo kuwa mama alipambana sana na kuzibakisha ndio chanzo cha kutengwa nao. Mama alifikiria sana huku akikosa majibu na ndipo alipo fikiria juu ya kuuza shamba moja angarau APATE fedha chache ili hali mmoja wetu APATE kwenda shule. Mama aliuza shamba hilo na pesa ilipatikana chache ambayo isingeweza kukizi mahitaji yetu sote na ilitoshereza kwa mtu mmoja tu. Basi ilimbidi mama amlipie ndugu yangu Gabriel ada kwa kile kiasi cha fedha kilicho patikana ili tu APATE kuanza shule kwani mda ulikuwa umeshafika Wa sisi kulipoti shule ni. Kaka yangu Gabriel alianza masomo na Mimi nilibaki nyumbani tukiangaikia pesa ili nami nianze masomo japokuwa nilikuwa nimesha chelewa. Pesa yangu ya ada ilikuwa ngumu sana kupatikana kwani mama aliangaika huku na kule lakini hakufanikiwa siku hiyo mama alirudi nyumbani akiwa mnyonge sana na aliponikaribia aliniangalia kwa jicho huruma sana na kuingia ndani azikupita dakika alitoka na kigoda ndani na aliketi pembeni yangu na kuanza kulia.

    Mama "jamani Mimi na mkosi gani "

    Aliongea mama huku akinitazama nami machozi yalini lenga na kumuuliza!

    Isabela "kwanini mama wasema hivyo NINI kimekupata huko utokako mama yangu"

    Mama "mwanangu Isabela nimeangaika sana kwa ajili yako mwanangu lakini ninapo pita hata sipati majibu mazuri kwani wengine wanani tusi kisa Niko mjane na wengine wananisema vibaya wapendavyo lakini sito choka kwani haya yote ni kwa ajili yangu na familia yangu na nitapambana mpaka nahakikisha mwanangu mnasoma na hakika mtanisaidia mbele ni."

    Mama alikwisha kusema hayo huku nami machozi yalikuwa yameshafika chini kwani alicho kuwa akisema kilikuwa kinanihusu Mimi na familia yetu kwa ujumla. Zilipita siku kazaa huku Mimi nikimsaidia mama Kazi za nyumbani na kuangalia ili tupate fedha ya Mimi kuniwezesha kujiunga.



    "zilipita siku kaza huku mimi namsaidia mama Kazi za nyumbani na kuangaika huku na kule ili tupate fedha ya mimi" .

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kuendelea na masomo na pia kaka yangu Gabriel yeye alikuwa akiendelea na masomo vizuri kwani ilipatikana fedha yake iliomtoshereza yeye mwenyewe. Nakumbuka ilikuwa siku ya jumapili mida ya saa sita mchana alikuja mgeni nyumbani na alipofika hakumkuta mama kwani mama alikuwa kwenye mizunguko ya kutafuta na kuangaika kama ilivyo zoeleka kila siku. Alinikuta nami nilimkalibisha amsubilie mama na nilimsihi mgeni huyo kuwa mama ndio mida yake ya kurudi nyumbani. Mgeni alionekana kuwa mchangamfu na mwelewa sana nae alinikubalia atukuongea sana mara mama alitokea na alipomwona mgeni huyo kwa mbali nilimwona mama akilia na nikaisi kidonda kimetoneshwa na kumwangalia sana mgeni huyo kadri alivyokiwa akisogea mgeni nae alikuwa akimfata aliko nilitahamaki mda mrefu na kushangaa na kuona ni mchezo wa kuigiza. Sikuela kilicho kuwa mda huo kwani mgeni nae akiangua kilio kikali sana na yalipopita masaa kazaa wote walinyamaza na kila mmoja akimtazama mwenzake kwa jicho la huruma sana. Ndipo mama alimtambulisha mgeni kwangu.

    Mama "yolanda huyi ni mwanangu wa pili na wa kwanza yuko shule mda ukifika utamwona anaitwa Gabriel ndiyo ulie muacha akiwa mdogo sana na huyu ndiye aliyekuwa tumboni mwangu (mimba) anaitwa "Isabela"

    Yolanda "nashukuru kumfahamu kwani ni mda mrefu sana nimeondoka hapa mchini kuelekea masomoni ni mda mrefu pili pole kwa msiba uliokukuta kwa kumpoteza mpendwa wako"

    Mama "Asante sana ndugu yangu kwani mpendwa wangu kaniacha kwenye njia ambayo sijui iko wapi kwani naona giza lime tanda safarini". Mama alipokuwa akiongea maneno yale huku machozi yakimtoka nami ndipo nilipo msogelea karibu na kuanza kum'bembeleza.



    Mda ulipita na mama alisitisha kulia basi nilichukua jukumu la kuingia ndani ili niandae chakula cha pamoja kwani mama hakupenda mgeni aondoke bila hata ya kuweka kitu chochote mdomoni kwani ilikuwa Mira yetu mgeni akifika ni lazima aweke Baraka zake kwetu. Niliivisha chakula kwa mda mfupi tu kwani nilihitaji mgeni japo ale chakula nilicho kiandaa Mimi nilitaalisha meza na kutenga chakula ndipo nilipo chukua jukumu LA kuwakaribisha mama pamoja na mgeni (Yolanda).

    Wote walifika mezani na wote kwa pamoja tulianza kula chakula nilicho kuwa nimewaandalia Mama pamoja na mgeni (Yolanda) waliendelea kupiga stori na stori walizokuwa wakipiga nje na waki simuliana zote zilikuwa pindi walipopotezana kipindi cha nyuma katikati ya stori hizo mgeni (Yolanda) alimwambia mama

    Yolanda "kwanini nisimchukue binti yako nikaishi nae nyumbani kwangu kwani nilipojenga sasa Niko mwenyewe nyumba nzima na inabidi nikusaidie kwa kumsomesha Isabela mpaka atakapo fika elimu ya juu."

    Mama "Nitashukuru sana rafiki yangu kwani Mimi hapa nime fanya kila njia ya kumtafutia mwanangu Ada ya kujiunga na shule kiukweli sikufanikiwa mpaka mda huu nilikuwa nimetokea kwenye miangaiko hiyo ya kutafuta pesa ya Ada. Nitashukuru tena sana kama utachukua jukumu LA kumtunza na kumsomesha mwanangu nani sina uwezo Wa kukulipa japo mungu yupo atakulipa yote na ndiye pekee awezaye."

    Mgeni (Yolanda) usijali rafiki yangu tumetoka mbali sana kwani nilipo pata shida ulitia juhudi kunisaidia kipindi cha nyuma nami sita sita kwenye hili swala zito lililo kukumba rafiki yangu."

    Nilifurahi sana kusikia mgeni (Yolanda) akinitaka Mimi ili akani someshe kiukweli sikutaka kuonesha Furaha yangu mbele zao kwani nilitaka hata akitaka kuondoka mda huo tuongozane nae mpaka anapo ishi ili tu nami nianze masomo mapema kwani wenzangu walikuwa wame fika mbali mno. Tulimaliza kula chakula ndipo mama aliniomba nijiandae ili tu mgeni akitaka kuondoka niongozane nae basi nilifanya hivyo hivyo kama mama alivyo sema kwani nilifanya upesi na nikawa tayari kwa safari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulianza safari mnamo majira ya jioni kuelekea mjini alipokuwa akiishi Yolanda safari ilichukua masaa mengi kiasi licha ya tulifika salama kwake lakini ilikuwa usiku sana basi kila mmoja alionekana kuwa mchovu sana. Mimi nilipofika tu si kupenda kuficha ile ofu ya ugeni kwani nilimuomba Dada Yolanda anielekeze bafu lilipokuwa ili nipunguze uchovu niliokuwa nao kwa wakati ule.

    Aliniongoza mpaka bafuni na nilipo fika nilishangaa sana kuona maji yakitoka juu kumwagika kama mvua daaaaah! Nilibaki jicho kodoooo hofu na woga ulitawala pale Yolanda aliponiambia "OGA sasa uondoe uchovu nami nitaoga ukitoka wewe"

    Maneno yale yalinifanya kuzidi kuogopa na ndipo nilipo jitoa ufahamu na kufungulia bomba. Maji yali churuzika kwa staili yake huku nikiwa nayazoea taratibu sikutaka kuwa na papala nilioga na maji ambayo yalinifanya nichukue mda mrefu kwani Yale maji yalikuwa ya moto kiasi chake na nilinogewa mnoooo! Nilimaliza kuoga.

    Nilipo maliza kuoga Dada Yolanda alinipeleka kwenye chumba ambacho alikuwa kaniandalia kwaajili ya kulala na nilipo fika karibu na mlango alinikaribisha.

    Yolanda "hapa ndipo utakapo kuwa unalala sawa mdogo wangu

    Isabela " sawa Dada"

    Nikiitika kwa hofu sana kwani mahari nikipokuwa nimeandaliwa ili ni lale nilishangaa sana kuona vitu kama vile machoni mwangu.

    Usiku kwangu ulikuwa mkubwa sana kwani kitanda nilichokuwa nimelalia kilinifanya ni sahau kilicho nileta kuwa ni elimu na kuwaza mambo ya dunia.

    Nilichelewa siku hiyo kuamka kwani nikizoea sana nyumbani kuamka mapema sana lakini kwa usingizi niliopata kutoka kwenye kitanda kile ulikuwa Wa aina yake. .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimkuta Dada Yolanda kaisha amka na nilimkuta jikoni akiandaa chai nami nilifika na kumsaidia Kazi zilizo kuwepo chache na tulipo maliza sote tulipeleka vyakula mezani kwaajili ya kifungua kinywa kwa siku hiyo ya kwanza kwangu na chakula nilicho kula siku hiyo duuh! Kilikuwa kitamu sana mpishi alinikaribisha vizuri sana.

    Siku zilipita na maisha ya pale niliyazoea na kujikuta na fahamu mitaa mingi bila ya mwenyeji wangu Yolanda kwani Yolanda hakuwa mtu Wa kutoka na kutembea mitaa ya pale.

    Dada Yolanda alianza mipango ya kunitafutia shule ili nami nianze masomo haraka iwezekanavyo. Siku hazikupita nyingi Dada Yolanda alipata shule na kunisii nifanye maandalizi ya siku 2 nianze masomo. Ilifika majira ya mchana siku hiyo hiyo alionipatia shule na kuniomba nitoke nae kidogo tuka zurule. Alinipakiza kwenye gari lake na kuanza safari ambayo sikujui niendako nami sikuwa na hofu nae basi nilikuwa mtulivu mpaka alipo simamisha gari na kunambia.

    Yolanda "tumefika Mdogo wagu"

    Isabela "sawa dada"

    Sikuelewa mahali pale na kubaki nashangaa kuona vitu ambavyo sijawai kuona. Tuliingia kwenye Duka moja LA Nguo mjini (sahara) na tulivo ingia nae aliniambia chochote nikionacho na macho yakakipenda ni sisite kumwambia kwani dhumuni LA kunileta hapo dukani ni kunifanyia shopping.

    Turizunguka na nilichokuwa nikikiona nami siku sita kuchukua kama alivyokuwa kanambia nikionacho kizuri nijiudumie mwenyewe. Alinifanyia shopping moja kubwa sana kwani mtoko nilipata mingi sana huku nikikumbuka kilicho nileta ni elimu na siyo mambo mengine basi Dada Yolanda alilipia kile nilicho chukua dukani mule na kuanza safari ya kurudi nyumbani tulipofika nyumbani nilihisi kama miujiza imeniangukia Mimi na mwaka huuu nitakuwa mtu tofauti ("yote hayo nikijisemea moyoni").

    Nilianza shule huku siku ya kwanza nakumbuka nilikuwa muoga kwani uoga ulichangiwa na ugeni wangu shuleni hapo lakini kadri siku zilivyo kuwa zikisonga mbele nilizoeana na wanafunzi wenzangu na kuonekana kuwa kipenzi cha wote kwenye masomo yangu. Nilipo fika kidato cha pili nilifanya mtiani Wa kuingia kidato cha tatu.....

    .

    Nilifanya vizuri nikafanikiwa na masomo huku nikiweka juhudi ili nifike malengo niliokuwa nime yaweka. Miaka miwili ilipita nami nilihitimu masomo yangu ya sekondari na ni kipindi hicho hicho nilikuwa nayasubilia matokeo yangu ya kuingia ngazi ya juu (kidato cha sita). Matokeo haya kuwa mazuri kwangu kwani siku fanikiwa kuchaguliwa miongoni mwa walio fahuru kipindi hicho matokeo yalikuwa siyo mazuri kwa nchi nzima kwani yalionekana kuwa tofauti na ya miaka iliopita hivo idadi ya waliofeli turikuwa wengi mnoo!.

    Nilivyo yapokea matokeo hayo wala siku amini na kubaki nalia huku nikipata mvulugiko Wa akili kwani nilipoteza fahamu takiribani masaa mwili. Niliposhituka sura ya kwanza ukiona ilikuwa ya Dada Yolanda nae hakupenda kunivunja moyo na kunisihi sana

    Yolanda "usivunjike moyo mdogo wangu kwani kufeli siyo kufeli maisha"

    Maneno yale yalipenya mpaka ndani ya akili yangu na kukaa vizuri na kuelewa alicho kuwa akisema nami nilimjibu huku machozi yakini toka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Isabela "siamini Dada yangu kwani sikutegemea matokeo haya kwani nilipenda shule mno na nikipeleka matokeo haya nyumbani mama atanionaje Mimi?"

    Yolanda" Mdogo wangu narudia tena kufeli elimu siyo kufeli maisha hiyo weka kwenye akili yako sawa"

    Alikwisha kuongea hivyo Dada Yolanda alininyanyua na kunipeleka chumbani kupumzika.

    Nilitumia mda sana kusahau yalio tokea na maisha yaliendelea. Dada Yolanda alichukua jukumu LA kunitafutia hata sehemu nijiwekeshe kwa namna moja au nyingine ili hali nijipatie kipato.

    Alipata kazi lakini Kazi haikuwa Kazi ndipo nilipo amini ya kuwa na elimu usome sana na upate Kazi nzuri. Nilipata Kazi kwenye saloon ya rafiki yake (Yolanda). Kazi nilianza vizuri japo kuwa sikuwa mzoefu sana na Kazi za saloon na nilipata mafunzo huku nikiwa na uwezo Wa kufanya vitu vidogo kwenye saloon.

    Siku zilizidi kusogea mbele Kazi niliweza kufanya kama ilivyo kuwa inatakiwa mpaka boss wangu (Amina) Alipenda sana nilivyo kuwa najituma kwa bidii niliipenda Kazi hiyo kwa namna moja au nyingine kwani iliniingizia kipato kizuri kwa siku...



    Niliendelea hivo hivo huku boss wangu Amina alitokea kunipenda sana kwa Kazi niliokuwa nafanya kwenye saloon yake mpaka ilimpelekea yeye kutaka niame kwa rafiki yake Yolanda ili nikaishi nae kwake. Sikutaka iwe hivyo kwani nilitoka kijijini na mlezi aliye julikana kuwa atakaye nilea na kuishinae ni Dada Yolanda pekeake haikuwa rahisi kwa boss Amina kwa kile alicho kuwa akihitaji kutoka kwangu kwani nilimuomba niwe kama zamani na tokea kwa Dada Yolanda na kuelekea saloon.

    Nilivyoonesha kuwa sikubaliani nae boss Amina hakutaka kunielewa mpaka alikwenda kwa Dada Yolanda na kuzungumza nae mimi sikufaamu kuhusu jambo hilo. Siku moja boss Amina hakuonekana saloon siku nzima basi nami sikuwa na hofu kwani nilikuwa nimesha yazoea siku hiyo nilifanya Kazi siku nzima nikiwa mwenyewe saloon nzima ilipo fika jioni nilifunga na kuelekea nyumbani nilikuwa nimechoka sana niliwaza nikifika nyumbani tu chakwaza inabidi nioge na nipumzike ili niondoe uchovu Wa siku hiyo.

    Nilipo fika nyumbani niliingia ndani sijui hili wala lile mpaka sebureni nilishangaa sana kumkuta boss Amina nyumbani bila ya yeye kunijuza kuwa hata kuja kazini kwani Mimi niliisi ni mgonjwa. Sikutaka kuongea azalani ilinibidi niwape salaam yao nikipita pembeni yao na nilielekea chumbani kupumzika huku nikiwaacha wakipiga unazofanya

    Baada ya mda mfupi dada yolanda alikuja chumbani na kuniita na nikiitika wito japo sikujua nini kikiendelea huku nikiwaza Yale aliokuwa akiniambia boss Amina kuamia kwake. Nikifika sebureni na niliketi pembeni yao na kuwasikiliza

    Yolanda "aaahaa! Tumekuita hapa kuja jambo tunatakata turiweke sawa Mimi wewe na Amina boss wako"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilishituka sana alivyo sema maneno Yale huku nikiitika kwa sinto fahamu "sawaaaa Dada!

    Nikijua tu japo kuwa Dada Yolanda alikuwa hajui kama nami hilo swala nalijua sikutaka kuonesha kuwa nalijua lakini nilikuwa nikihisi ndilo hilo hilo.

    Yolanda"Isabela Mdogo wangu"

    Isabela "beeee! Dada yangu"

    Yolanda "rafiki yangu Amina alihitaji sana tena sana ukaishi nae kwake kwani katokea sana kuzipenda Kazi zako unazofanya



    Nilikubari japokuwa sikupenda iwe hivyo kwani nilikuwa nimemzoea sana Dada Yolanda lakini sikutaka kuwa na kipingamizi kwani walikuwa wakielewana ilinibidi niwape heshima yao na kuwakubalia yote waliokuwa wameafiki juu yangu kwani walipofikia tamati ya Mimi kwenda kwa boss Amina.

    Sikuwa na budi ilibidi nifate wasemayo niliwaaga pale walipokuwa wameketi sebureni na kwenda chumbani kwangu kujipanga na safari ya kuhamia kwa rafiki yake Yolanda (Amina). Nao niliwaacha sebureni huku nyuso zao kila mtu zikiwa na tabasamu huku tabasamu LA boss Amina lilikuwa limefika lengo lake.

    Nilifikiria sana pale nilipo kuwa nikipanga Nguo zangu kwa ajili ya kuhama nyumba hiyo ya dada Yolanda na kuamia kwa Amina yote Yale nilikuwa nikiwaza sikupata majibu sahihi na kuwaza kuona yote heri kwani nilikuja mjini kutafuta maisha na ilibidi nifanye Yale wasemayo.

    Kulikucha siku iliyo fuata nami nilijiandaa kwenda kwenye shuguri za kila siku yani saloon nilipo kuwa nikifanya Kazi huku nikiwa nimebeba Nguo zangu mbili tatu ili nikitoka jioni niunganishe kwa boss Amina.

    Nilipo fika saloon majira ya SAA 2 asubuhi nilianza na usafi

    Ndani ya saloon kama nilivyo kuwa nimezoea siku zote na nilipo maliza usafi ule nilipumzika kidogo na siku tumia dakika nyingi sana kupumzika alitokea mteja na aliomba nimuudumie nami sikuwa na budi ilibidi nichukue vifaa na kuanza kumuhudumia mteja huku tukipiga stori katikati ya stori zile alimuulizia Dada Amina.

    Mteja "mpaka mda huuu boss wako haijafika tuu!!?

    Isabela" ndio kwani aliniambia kuwa atachelewa kufika kutokana na majukumu mengine ya ki biashara.

    Mteja "biashara sana au zile zile tulizo zizoea kola siku Ku achana na saloon....?

    Isabela" sijui ila kwa upande wangu kaniambia hivyo!!!?

    Mteja "kuwa makini sana Mdogo wangu na boss wako?

    Isabela" kivipi Mbona waniweka njia panda Dada yangu nieleweshe...?

    Mteja "usiwe na shaka kawaida tu utakuja kujua badae kwanza wewe Fanya shuguri zako zilizokuleta hapa saloon"

    Alikwisha kusema hivyo mteja huyo huku Mimi nikiwa nimebaki na alama ya kuuliza(???) .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kichwani mwangu huku nikifikiria maneno aliyo kuwa kanipatia yalikuwa mazito huku yakionesha wazi kuwa wanafahamiana na kuna Dada Amina alikuwa tofauti na saloon lakini sikuweza kupata jibu kamili huku nikifikiria sana juu ya maneno yalikuwa magumu na yenye kukirisha MTU huku nikiwa na amini binadamu Wa siku hizi KWA kuchinganisha ni watu waliobobea tena alivyokuwa akionekana nje nilijua tu ni wale wale kasoro tarehee!!! Huku nikiwaza "labda kaona najituma sana na kutia juhudi kwenye kazi nilionayo hapo saloon labda hapendi na aniwekee sumu nipotoke" lakini kwangu hakuweza kama alikuwa na nia hiyo basi

    Nikimaliza kumuhudumia mteja huyo kwani haikuwa kazi kubwa sana ya kunifanya nichukue dakika nyingi kwake kwani ikikuwa ya kuziosha nywere zake na kuziwekea ndani.

    ili zionekane kwa nzuri na zenye kupendeza.

    Nilivyo maliza hivyo mteja aliniaga na kuondoka haikupita mda boss Amina aliingia akiwa kaongozana na MTU mwingine na waliingia na kuketi kwenye ofisi ya boss Amina na kuzungumza haikupida dakika nyingi Mara boss Amina KUTOKA huku sura yake ikiwa tofauti nae mgeni alie kuwa kaongozana nae ae alitoka huku nae sura ikiwa tofauti na alivyo ingia ndani.

    Mgeni huyo alikuwa jinsia ya kiume wala sikuelewa kikichokuwa kikiendelea kwani Dada Amina alikuwa akizunguka ndani ya saloon huku akijisemea na nilimwona yule mgeni nae akiwasha gari KWA speed na kuondoka eneo hilo.

    Dada Amina alikuwa kama kavurugukiwa akili kwani alionekana kuwa MTU mwenye jaziba kubwa hata nilipojaribu kumsemesha hakunijibu kitu nami nilimwacha atulie kidogo ndipo nitaongea nae gafra alinyanyuka alipokuwa kakaa kwenye kochi na kuniambia

    Amina "MTU yoyote akija kuniulizia mwambie sipo nimesafiri"

    Isabela "sawa Dada nitafanya hivyo"



    Amina "kuwa makini sana mdogo wangu kwani naisi kuvurugwa akili ngoja nikapunguze mawazo kidogo sehemu flani na hapa majukumu yote nimekuachia wewe nakuamini okeeey! na nitasafiri ndani ya siku tatu au mbili "

    isabela "sawa dada wala usijari kwa hilo kwani nitafanya yote ulionielekeza na wala usiwe na hofu nami".

    Dada amina aliondoka saloon huku nikiona mbeleni kuna kitu chaweza kutokea nami sikuwa na hofu huku nikiwa nafikiria juu ya dada amina hazijupita hata dakika kazaa na kuona gari zikipiga king'oraaa huku sikija kwa speed ya hatari. Walipofika walishuka ndani ya gari na kuja moja kwa moja mpaka saloon waliingia ndani huku wakiongozwa na yule mtu aliye kuja na dada amina mda mfupi uliopita nikishangaa sana na kuwaza nini kinataka kutokea nami sifahamu chochote. Niliogopa sana huku nikiwaza juu ya kukamatwa na wale polisi hawakuongea nami na kupitiliza moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya dada amina na kutafuta na walipo ona hakuna walichokuwa wakikitafuta wote walirudi nilipokuwa na kuanza kunioji huku mtu wa kwanza alikuwa ni mtu aliye kuwa na dada amina na kuniuliza kwa ukali huku akionesha chuki ndani yake imesambaaa "amina alikuambia anaelekea wapi mda huuuuu!"

    nilimjibu huku nikiwa na uoga mwingi sana hofu yangu kubwa ikikuwa ni kuulizwa maswali ambayo sijui hili wala lile pili kupelekwa kituoni niliogopa sanaaa

    Isabela "sijui kwani ulivyo toka wewe tu mda huo huo nae alijufata nyuma "

    Hapo hapo polisi waliposikia jibu langu walitoka mbio mbio na kupanda gari na kuondoka maeneo ya saloon.

    Nami kuona vile ilinibidi nichukue simu haraka haraka na kumpigia dada amina simu

    Simu iliita sana mpaka dakika ya mwisho dada amina alipokea simu

    Isabela "hallooooooooooooo dada "

    Amina "nambie mdogo wangu vipi kuna kitu nimesahau kukuachiaaaa "

    isabela"hapaana dada yangu kwani hivi navyoongea polisi wanakutafuta sana "

    amina"heeeeeh polisi wamekuambia wananitafutia nini mimi "

    Isabela "hawajaniambia kitu wameondoka mda huuu kama upo nyumbani kimbia dada yangu kwani wanaongozwaaa na yule mkaka uliye kuwa nae asubuhi."

    Amina"mmmmmmh sawa nimekuelewa"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alipokwisha kusema hivyo simu ilikatika gafra huku nikijuwa na mengine ya kuongea nae nilijaribu kupiga tena lakini simu haikuwa hewani tena niliingiwa na hofu huku nikitambua ya kuwa akikamatwa tu nami sitakuwa na mwelekeo wowote kweli siku hiyo sikuwa na amani sana huku mawazo mengi nikiwaza yale yaliotokea nafsi nao ikanambia nifunge saloon mapema na nielekee nyumbani ninakoishi na dada amina basi ikanibidi nifunge saloon na nielekee nyumbani. Nilipofika karibu gafra nilisimama huku nikishitushwa na wingi wa polisi wakishuka ndani ya gari na kuzunguka nyumba ya dada amina nami sikuweka woga wowote kwani nilikuwa nisha choka na naitaji nipumzike ilinibidi nisogee taratibu na nilipofika getini walinizuia kuingia ndani huku wakinioji maswali mengi huku dakika za mwisho walinikatalia kuingia ndani na kufunga mlango huku wakidai nyumba hiyo hawaruhusiwi kuingia mtu yoyote kuingia huku wakidai nyumba iko kwenye upelelezi.

    Walifunga mlango na kuniacha nalia sielewi pakuelekea kwa usiku huo nikiwaza kwenda kulala hotelini huku nikiwa sina pesa yoyote ya kunitosheleza mimi kwa usiku huo na ilinibidi nirudi tu saloon. Nilifika nakufungua mlango na kuingia ndani siku hiyo nililala saloon na kulipokucha niliamka kama kawaida na kuanza usafi lakini maji ya kusafishia alikuwa yameisha nami ilinibidi nichukue jukumu la kwenda kuchota maji mtaa wa pili. Nilitoka na ndooo ndogo na kuanza safari ya kuelekea kuchota maji nilipo pita mtaa wa kwanza nilishangazwa na kutaharuki kuona picha ya dada amina kila kona hiku ikioneshwa kuwa "WWANTED "

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nilianza kuzungusha macho yangu pande zote na kuona picha hiyo imetapakaaa kila mahari na ikanibidi niwe yuda kwa mda mfupi kwani watu waliokuwa wakinijua wengi wao walikuwa wakiniangalia mno huku suea zao zikiwa na hasira sana nikiogopa mnoo pindi walipokuwa wakinifata na kuniuliza maswali mengi juuu ya dada amina nami niliikana picha hiyo mara tatu nilirudi saloon haraka haraka nikiwa sina maji wala nini! na kubaki nikiwa na mawazo juu ya swala hilo kwani nilihisi nami wanaweza kuingizwa kwenye kesi hiyo..



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog