Search This Blog

Monday 16 May 2022

JAMANI MAMA MARO - 2

  







    Chombezo : Jamani Mama Maro

    Sehemu Ya Pili (2)



    Ocar baada ya kutoka Tanzania kuhudhuria arusi ya rafiki yake aliyekuwa anamuoa mwanamke ambaye yeye Oscar alimpenda na kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake.

    Alikuwa ni kati ya wanaume ambao wameumizwa sana duniani na mara nyingi alikuwa ni mtu wa mawazo lukuki. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pamoja na faraja na huduma zote ambazo Oscar alikuwa anapata kutoka kwa Michelle bado hakuweza kurudi kwenye hali ya kawaida na wakati huu alikuwa amekonda mno.

    Ilikuwa kila mara anaenda kwa fundi nguo kupunguza kiuno cha suruali zake. Mafundi walikuwa wanashangaa sana kwani baada ya nguo kupunguzwa ilikuwa haipiti hata wiki mbili bado nguo ile ililetwa tena kupunguzwa.

    Oscar alikuwa kwenye hali mbaya sana, alipoteza kabisa mvuto wake na kuwa mtu wa matukio ya ajabu sana, mara kaanguka mtaroni, mara kutapika baa na mengine mengi.

    Kama asingekuwa Michelle Oscar angekuwa hata kafariki dunia.

    Taarifa juu ya hali ya Oscar ziliifikia serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na kulazimu ahamishiwe Tanzania.

    Alipewa barua yake ambayo ilimtaka kufanya kazi kwenye ofisi ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.

    Pamoja na kupewa nafasi hiyo lakini bado hakuambiwa kazi yake maalumu japo alikuwa akipewa heshima na posho zote lakini alikuwa akienda tu ofisini bila kufanya kazi yeyote.

    Kitendo cha Oscar kuwa mbali na Michelle kilimfanya aharibikiwe zaidi kwani hakukuwa na mtu wa karibu wa kujitolea kwake kumsaidia.

    Ama kweli mapenzi hayana huruma, kama yangekuwa na huruma yangemuona Oscar hali aliyokuwa nayo na kumpunguzia adhabu.

    Oscar alikuwa haelewi chochote na hata wazazi na ndugu zake aliwasahau. Ilifika wakati akawa hataki kuonana na mtu yeyote.

    Alipenda kukaa mwenyewe na alikuwa akijinunulia mizinga ya pombe kali na kukaa nayo ndani huku akinywa usiku kucha.

    Alikuwa hapati usingizi bila kunywa pombe lakini baada ya siku kadhaa pombe zilidunda, alikuwa anakunywa sana lakini inafika saa kumi na mbili asubuhi bado usingizi haujampitia.

    Kimsingi Oscar aligeuka kuwa teja wa mapenzi.

    Siku moja akiwa anaenda super market kununua mizinga ya pombe alijisikia kizunguzungu kikali na kichwa kumuuma upande wa kushoto kama kidonda.

    Aliwasha AC ya gari mpaka mwisho lakini bado hakujisikia nafuu, aliamua kushuka kwenye gari akidhani kuwa upepo wan je utamsaidia. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipiga hatua kuelekea kwenye mti wenye kivuli uliokuwa nje ya ile supermarket lakini kabla ya kuufikia alijisikia miguu ikiishiwa nguvu na kulegea hivyo akadondoka chini kama amepigwa mtama.

    Ndani ya ile supermarket alikuwa amekaa dada mmoja mrembo sana ambaye alikuwa anazozana na pedezee mmoja aliyekuwa kapaki gari aina ya Hammer akitaka kupewa namba ya simu na Yule mrembo.

    “Nipe namba tuwasiliane nikupe maisha”

    “Nimeshakwambia mimi ni muke wa mtu, angalia pete yangu hii”

    “Sawa usiogope mimi najua kuishi na mke wa mtu, mume wako hatajua”

    “Sitaki nimekwambia, mume wangu ananitosha”

    “Murembo mume wako hatoshi, mimi sitakuweka uuze hapa, mimi nitakufungulia yakwako mwenyewe, utakuja tu kuchukua mahesabu jioni”

    “Kwani umeambiwa hii ni yanani, ninazo nyingi zaidi ya hii na kuja hapa naamua tu”

    Walikatishwa maongezi yao na mtu aliyeshuka kwenye gari na kutembea hatua chache na kuanguka chini.

    Walitoka wote kwa pamoja na kumuendea kisha wakamgeuza kwani aliangukia pua. Walivyomgusa alikuwa anahema lakini alikuwa hajitambui.

    Yule dada alimuomba Yule baba ambebe wampeleke hospitali lakini alimkatalia na kuwasha hammer yake na kutimua vumbi.

    Kwa roho aliyokuwa nayo Yule dada alishindwa kabisa kumuacha pale, alimuomba mlinzi wake wamnyanyue na kumuweka kwenye gari.

    Alivyowekwa kwenye gari ilibidi Yule dada ashuke na kuliendea gari la Oscar kwa lengo la kulizima na kuiweka sehemu yenye usalama.

    Aliingia kwenye gari na kuiwasha, wakati anaondoa gari alipiga jicho kwenye kwenye siti ya pembeni akaona komputa ndogo imewekwa pale.

    Aliifungua na kuperuz baadhi ya mafaili na kukutana na picha ambazo zilimfanya ashituke na kupigwa na butwaa.

    Aliendelea kupekua lakini aliyokuwa anakutana nayo yalimfanya apagawe zaidi. Aliweka gari sehem salama akashuka haraka na kwenda moja kwa moja kwenye gari ambalo alimuweka Oscar.

    Aliwasha gari na kulitoa mbio hadi hospitali, alipofika kabla ya kumshusha alimpekua akachukua simu pamoja na wallet yake.

    Wakati madaktari wanamchukua Oscar yeye aliwasha simu ili aangalie kama ataona namba apige lakini alikuta simu ina password.

    Alihamia kwenye wallet ambapo alipoifungua alitoa kadi mbalimbali ambazo nyingi zilikuwa ni vitambulisho mbalimbali.

    Aliposoma majina yaliyoko kwenye vitambulisho alijikuta akishika mdomo kwa hamaki, alirudisha akili yake kwa mtu aliyekuwa amembeba na kuitathmini sura na kugundua kuwa aliyeko pale hospitali ni Oscar aliyemjua vyema.

    Kilichomhuzunisha ni jinsi ambavyo huyu Oscar wa sasa alivyochoka na kuchakaa, alijikuta machozi yakimwagika bila kutaka.

    Alichukua kitambaa akajifuta na kuelekea kule alikopelekwa Oscar. Alikutana na madaktari ambao wanamhudumia Oscar.

    “Mgonjwa wako anaitwa nani?”

    “Vitambulisho vyake hivi hapa kuna kila kitu”

    Madaktari walimpima Oscar na kugundua kuwa alikuwa na presha ya juu sana na ndio iliyomuangusha,

    Ilibidi alazwe huku akiwa ametundikiwa dripu za dawa. Muda wote dada alikuwa akilia kila alipokuwa anamtazama Oscar.

    Baada ya masaa mawili Oscar alipata faham na kuamka. Alipotazama pembeni na kukutana na sura ya mdada alishtuka na kuzimia tena…





    Hallooo uko wapi”

    “nimetoka kidogo nimeenda kuangalia mzigo, kuna vinywaji hapo sisi hatuna na watu wanaviulizia sana”

    “uwahi kurudi basi mimi natoka naenda mkoani kikazi”

    “sawa narudi muda sio mrefu”

    …………………

    Baada ya Oscar kuamka na kuzimia tena baada ya kumuona Yule dada kiliwashtua madaktari ambao ilibidi wampe hudumaa nyingine ya haraka ambayo ilimzindua na kumfanya aamke na kukaa kabisa.

    “Rozina umefwata nini hapa”

    “unataka uniue kabisa, haijakutosha tu jinsi nilivyo saivi”

    “dokta ni nani aliyemuita huyu dada hapa,”

    “tunaomba utulie sawa? Huyu dada ndio amekuleta anasema ulianguka dukani kwake”

    “yeye amenileta kama nani”

    “wewe ulitaka ulivyoanguka akuache tu ufie hapo, naomba utusikilize kama unaugomvi wenu mtamalizana ila tuache hapa tufanye kazi yetu.”

    Wakati wote huu Rozina alikuwa anakaukia kwa machozi asijue amjibu nini Oscar. Baada ya maneno ya Dokta, Oscar alikaa kimya huku nae mchozi yakimchuruzika kama maji.

    “naomba unisikilize kwa umakini sana’

    “mimi naitwa Dokta Mgweno na ndio nimekupokea, tumekupima na kugundua kuwa una presha kali sana ambayo ilikuwa ni 190/90”

    “kwa presha hii inabidi tukulaze hapa mpaka tujiridhishe na hali yako, ninakuomba usahau yote yaliyokuudhi kwani inawezekana ndio yammesababisha hii hali”

    “kila kitu kinachotokea kwenye maisha kinapita hivyo usilipe jambo lolote lile uzito wa kuiathiri afya yako, tulia tukutibu kisha upone uende ukatatue matatizo yako ila usisahau maisha yanaendelea.”

    Rozina alimfwata Oscar pale kitandani akamkumbatia huku akilia na kumdondoshea machozi…

    “uncle Oscar, mimi nilikuchukulia kama mzazi wangu, sikujua kama unanipenda kimapenzi na ulitamani niwe mkeo”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mungu ni shahidi… hukuwahi kunitamkia jambo hilo kamwe, kama ungalifanya hivyo nisingeweza kukukataa kwani nilitamani uniambie kwa muda mrefu lakini hukuthubutu kufanya hivyo”

    “rafiki yako ameniwahi, amenioa, mimi ni mke wake kwa sasa, nimezaa nae mtoto kwa sasa amekua mkubwa”

    “sioni jinsi ya kukusaidia Oscar wangu, niambie nifanye nini ili urudi kwenye ubora wako? Jamii inakutegemea, wazazi wanakutegemea na wewe pia unajihitaji”

    “tafadhali Oscar nakusihi punguza stress niko bega na wewe kwa lolote”

    “nipe nafasi niwe nawe karibu kama awali, nakumis sana Oscar tafadhali kuwa kama ulivyokuwa bado ninakuthamini”

    Oscar alikosa nafasi ya kujibu chochote kwani Rozina alikuwa amembana kwa hoja nzito na maneno yenye kuchoma sana.

    Alikuwa akilia kwa kwikwi mpaka madaktari walipomtoa Rozina na kumsihi amuache mgonjwa apumzike kisha arejee baadae.

    Rozina alitoka pale hospitali akiwa hana raha hata kidogo, kazini kwake hakufika bali alimpigia dereva wake akalichukue gari la Oscar alipaki sehem salama kisha yeye akanyoosha moja kwa moja nyumbani.

    Alipofika kwake alimuandaa mmewe huku akijitahidi kuficha kadhia aliyo nayo moyoni, alimsindikiza mmewe mpaka airport nay eye akageuza mpaka hotelini ambapo alinunua vuakula vizuri maalum kwa ajili ya mgonjwa na moja kwa moja akaelekea hospitali.

    Alivyofika hospitali alimuulizia dokta aliyemhudumia Oscar na kuambiwa kuwa amemaliza muda wake na alishaondoka.

    Aliomba mawasiliano yake kisha wakaelekezana sehemu ya kuonana kisha Rozina akawasha gari na kumfwata.

    “karibu dada, hii ni ofisi yangu binafsi tofauti na kule nilikoajiriwa”

    “Hongera sana, pharmacy yako kubwa sana”

    “asanate sana”

    “dokta kama unavyojua Yule ni mgonjwa wangu ila sijapata kujua vizuri kuhusu tatizo lake”

    “ok, mgonjwa wako ana tatizo la presha ambayo imesababishwa na msongo wa mawazo, lakini pia tumegundua kuwa ana tatizo la vidonda vya tumbo ambavyo vinasababishwa na kutokula kwa muda mrefu pamoja na matumizi makubwa ya pombe kali”

    “ooh Oscar jamani”

    “ni nani kwako?”

    “acha tu dokta, ila huyu ndie alikuwa balozi wa Tanzania nchini Ghana ambaye amehamishiwa hapa nchini juzi kati”

    “wacha wewe, ndio Oscar Yule ninayemsikia mimi”

    “ndie huyo, sasa dokta nina ombi moja, naomba ahamie nyumbani kwake aondoke pale hospitali alafu uwe unakuja kumcheki nyumbani”

    Walikubaliana kisha Rozina akampa kiasi cha laki nne kama malipo ya awali na kuanzia muda huo dokta Mgweno akawa ni daktari wa Oscar.

    …………………………………………

    Nchini Ghana Michelle anakuwa hajielewi kwa kitendo cha Oscar kuhamishwa, alikuwa akimpenda sana Oscar na aliamini kuwa huko aliko anapata shida sana na hakuna wa kumsaidia kwa mapenzi kama ambavyo anggefanya yeye.

    Roho ilikuwa ikimuuma kwani alikuwa hajui jinsi ya kumpata kwani kwenye simu alikuwa hampati na hata alivyo mtumia email alikuwa hajibu.

    Ukweli ni kwamba Oscar hakuwa na muda huo hata kidogo.

    Michelle alipanga kutoroka ilia je Tanzania kumfwata Oscar, tatizo na kikwazo kilikuwa kimoja tu. Hakuwa na nauli wala fedha ya kumkimu kwa kumtafuta Oscar ambaye hakujua anapatikana Tanzania sehemu gani.

    Alipiga mahesabu yake akaona afanye jambo moja. Aibe!

    Aliamka asubuhi sana na kuwahi kazini kuliko siku zote, alipofika ofisini alimkuta secretary wa mhasibu akiwa anafanya usafi pale ndani.

    Alitumia ujanja mwingi sana wa kumuweka bize kwa story za kuvutia kisha akafanikiwa kuiba kitabu cha check na kutoka nacho hadi ofisini kwake.

    Alikijaza vyema na kuandika kiasi cha dola elfu tano ambazo ni sawa na milioni kumi za ki Tanzania kwama zitolewe.

    Alipofanikisha alikirudisha na kuinyofoa kopi kisha akaendelea na kazi zake.

    Kesho yake aliwahi sana benki na kuitoa ile check kwa teller wa benki. Aliichunguza ile check na kugundua kuwa haikuwa na utata wowote.

    “dada mbona leo umetumwa wewe kutoa hela na si mtu mwingine”

    “Yule mhasibu wetu amesafiri, mimi ndio nakaimu nafasi yake”

    “ni sawa dada lakini sisi hapa tunae mtia saini mmoja tu kwa ajili ya taasisi yenu hivyo hapa inakuwa ni ngumu, kwanini hamkusajili mtu mwingine mapema kabla huyo haja safari.”

    “tulidhani atawahi kurudi kwani safari yenyewe ilikuwa ya ghafla”

    “sawa naomba upumzike kidogo hapo hadi mafundi simu wamalize marekebisho tupige simu ofisini kwenu tujiridhishe’

    Michelle alishtuka lakini hakutaka kuonyesha mshtuko wake, alikubali akaenda kwenye kiti akakaa huku akitafakari cha kufanya.

    Alipata wazo moja kisha akatoka na kuchukua usafiri wa haraka hadi ofisini ambapo alielekea moja kwa moja ofisini kwa mhasibu na kumkuta sekretari akiwa anapanga mafaili.

    “Niambie shoga, bosi wako yuko wapi?”

    “Wako kwenye kikao kule ukumbini kuna wageni wamekuja kutoka UN”

    “Mwezangu naomba nitumie simu yenu nipige mara moja”

    “Fasta basi kabla hawajarudi”

    “Niangalizie basi hapo nje nisije bambwa mimi”

    “fanya haraka”

    Ile sekretari anatoka tu hazikupita hata dakika tatu simu iliita,

    “hapo ni ofisi za ubalozi?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “NDIO NI NANI MWENZANGU”

    “MIMI NI MENEJA WA GNCB, NAOMBA KUULIZA KAMA UNAITAMBUA CHEKI NAMBA 01/09988871777 INYOTAKA KUTOA DOLLER ELFU TANO”

    “NDIO NAITAMBUA, SAMAHANI SANA MTIA SAINI WETU AMESAFIRI ILA ATARUDI MDA SIO MREFU ILI TUMSAJILI NA HUYO DADA AMBAYE NI KAIMU WAKE.”

    Kwa asilimia tisini Michelle alikuwa amefanikiwa mpango wake. Alitoka haraka na kukabidhi ofisi ya watu kisha akatoka nje getini na kutokomea benki.

    Alipanda bodaboda ambayo ilimkimbiza haraka hadi benki ambapo alisshuka na kuwahi dirishani na kuonana na Yule teller.

    “dada ulienda wapi”

    “nilibanwa na tumbo la hedhi la ghafla ikabidi nikajiweke sawa kidogo”

    “oh pole shoga, ndio shida zetu hizo wanawake sisi”

    “asante usijali”

    “ingia kwa meneja”



    Ndani ya shirika la ndege la KLM alikuwa amekaa msichana mrefu maji ya kunde na mrembo sana, si mwingine bali ni Michelle akiwa anasafiri kuelekea Dar es salaam Tanzania.

    Kwakuwa kulikuwa hakuna ndege za moja kwa moja kutoka Ghana hadi Tanzania ilibidi akashuke kwanza afrika ya Kusini.

    Ndani ya masaa nane tayari alikuwa katika uwanja wa Oliver Thambo jijini Johannesbag. Alishuka kwenye ndege akaelekea hotelini ambapo alilala hadi usiku wa saa nane na dakika arobaini na tano kisha akaamka na kuelekea tena uwanjani kwani alikuwa na flight ya saa tisa na nusu.

    Alifika na kukuta ndege tayari iko uwanjani akafuata taratibu zote za ukaguzi kisha akazama ndani ya ndege.

    Safari ilianza rasmi na hatimaye saa tatu kamili asubuhi alikuwa jijini dar es salaam katika uwanja wa JKNIA akiwa anakuja kwa ajili ya kumtafuta mtu muhimu mno kwake (Oscar).

    Alipiga macho kuangaza angaza jiji la Dar es Salaam ambalo kamwe hakutarajia kama kuna siku atatua humu lakini leo imekuwa.

    Aliita tax na kumuomba dereva ampeleke kwenye hoteli nzuri yenye hadhi ya kimataifa, hakuwa na wasiwasi kwakuwa hela alikuwa nazo.

    Alitembezwa mpaka maeneo ya Mbezi Beach ambapo alipata hoteli nzuri iliyokuwa ufukweni mwa bahari na hapo akalipia wiki nzima.

    Alioga, akala akalala. Alipoamka kazi ikawa ni moja tu! Kutafuta namna ya kumpata Oscar. Kwakuwa Oscar alikuwa ni Balozi, Michelle alijua kabisa kuwa haitakuwa kazi ngumu kumpata. Alidhamiria ofisi za Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa ili kutafuta namna ya kuonana na Oscar.

    ………………………….

    “asante sana dokta kwa huduma yako”

    “usijali ni kazi yangu”

    “kwahiyo utakuja lini tena”

    “hapa ni mpaka kesho lakini kukiwa na haja mtanipigia simu tu, zingatieni sana lishe niliyowaambia na nasisitiza tena aache matumizi ya pombe kwa sasa kabisa”

    “sawa dokta nadhani mwenyewe pia anakusikia”

    Dokta aliondoka na kuwaacha Rozina na Oscar pale ndani. Baada tu ya dokta kuondoka kulibaki na kimya cha kitambo huku kila mmoja akiona anakosa la kumsemesha mwenzake.

    “Umesikia masharti aliyokupa dokta?”

    “Mimi hata nikifa, sioni faida ya kuishi”

    “Kwanini umekuwa hivi Oscar?”

    “Nimekuwa hivi kwasababu yako, hivi Rozina nimejitolea mangapi kwa ajili yako, nimekusubiri kwa mda gani na kukupa kila ulichotaka, nimekupenda kuliko kitu chochote lakini ukaamua kunilipa kwa kuolewa na rafiki yangu?”

    “Nyamaza Oscar, sitaki upandishe tena presha, simama nikupeleke chumbani ukapumzike”

    Rozina alimshikilia Oscar na kuelekea nae chumbani ambapo walipofika chumbani walipokelewa na harufu nzito ya uchafu wa chumba, harufu ya Pombe mikojo na matapishi.

    Rozina alishangaa sana kuona Oscar aliyefikia hatua ya kuwa balozi wan chi amekuwa mtu wa hovyo kiasi cha kuishi kwenye chumba kichafu namna ile.

    Hakutaka kuongea neon lolote isipokuwa alimuita mfanyakazi wa ndani na kumuomba vifaa vya usafi na kuanza kufanya usafi kwenye chumba cha Oscar, alifua akapiga deki, akatandika mashuka mapya, akapulizia marashi hatimaye chumba kikawa chumba kweli. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Oscar alipata faraja sana ila kila alipokuwa anauangalia urembo wa Rozina na jinsi alivyompenda roho ilikuwa inamuuma sana, kazi ya usafi ambayo Rozina aliifanya pale ndani ilimzidishia machungu na kutamani angekuwa yeye ndie mme wa Rozina.

    Kila rozina alipokuwa anapita na kufanya hili na lile Oscar alikuwa anamkata jicho la tama. Ukweli ni kuwa katika maisha yake yote ya kuishi Oscar, tangu amuone Rozina hakuweza kumtamani mwanamke mwingine.

    Ndani ya moyo wa Oscar ilikuwa ni kama vile mwanamke duniani ni Rozina peke yake.

    “amka hapo unywe uji”

    “sawa’’

    Oscar alikaa kitandaani na kunyweshwa uji wa lishe uliopozwa na kuwa wa vuguvugu,

    Sio kwamba alikuwa hawezi kunywa mwenyewe, la hasha! Rozina alitaka amtengeneze Oscar katika hali ya kujiona kuwa anapendwa ilia pone na kurudi kwenye maisha ya kawaida.

    Alikunywa uji ukaisha akaambiwa apumzike kitandani huku akiwekewa miziki ya kubembeleza kwenye tv iliyokuwa pale chumbani.

    Kwakuwa mume wa Rozina alikuwa amesafiri kwenda mkoani, Rozina aliamua kutumia nafasi hiyo kwa ajili ya kuwa na Oscar karibu ili apone kabisa.

    Walishinda pamoja kwa muda mrefu mpaka ikafika usiku ambapo walikula na ilipofika muda muda wa kulala Oscar aliingia chumbani kulala.

    Rozina aliamua kulala palepale ili aangalie kwa ukaribu hali ya Oscar na kuhakikisha kuwa hanywi pombe.

    Ilipofika mida ya saa nne usiku aliingia chumbani kwa Oscar na kujilaza kwenye kochi huku akijifunika la blanket.

    Baada ya muda kidogo walisikia kengele ya getini ikiita ambapo Oscar aliamka huku Rozina akimsindikiza kwa nyuma.

    Walipofika nje walikutana na mlinzi akiwa ameambatana na dada mmoja mrefu mwenye begi begani.

    Oscar alipotupa jicho usoni kwa Yule dada hakuamini macho yake….

    “haaa Michelle?”

    “haaaa Oscar”

    Walikumbatiana kwa furaha huku wakibaki wameshikana kwa muda mrefu. Rozina alikuwa akishangaa tu asijue Yule dada ni nani na ametoka wapi. Aliingia ndani huku akiwa amekasirika asijue amekasirishwa na nini.





    Rozina alikuwa kwake huku roho ikimuuma, alikuwa ana kitu kama wivu moyoni mwake. Ukweli ni kwamba alishawahi kumpenda Oscar na kutamani kuwa nae lakini Oscar hakumwambia kuhusu swala la Mapenzi.

    Kitendo cha Ansbert kutumia ujanja mwingi na mbinu lukuki kikamfanya aangukie kwake na kulimiliki penzi la Rozina.

    Sasa leo anapomuona Oscar akiwa katika mateso lakini sababu ikiwa ni yeye anajiona akiwa na deni lakini kwa upande mwingine anakuwa kama anaifurahia ile hali ya kuendelea kupendwa na Oscar.

    Wakati hili lineendelea na kuwa ameamua kumsaidia Oscar anatokea Michelle ambaye anafanya makusudi kumuumiza Rozina kwani alihisi ni demu wa Oscar.

    Furaha ya Rozina ilikuwa ni kumuona Oscar akiwa hana mwanamke mwingine, hakujua kwanini anakumbwa na hali hii lakini alitamani kumuona Oscar akiwa hana mwanamke. Ujio wa Michelle unamfanya ajisikie wivu.

    “Oscar Yule aliyeondoka ni nani?”

    “ni mke wa rafiki yangu”

    “unatembea nae?”

    “hapana”

    “sasa mke wa rafiki yako anakuhudumia kwa style hii ya kukaa nae chumbani, au mnaibiana, na mbona kama kakasirika kuniona hapa?”

    “Michelle acha tu kumuongelea huyu mwanamke, kanitesa sana”

    “pole unaweza ukanisimulia kidogo kuhusu wewe na yeye?”

    Oscar aliwaza kwa muda kisha akaona amuelezee Michelle kila kitu kilichotokea kati yake yeye na Rozina.

    ……………………..

    Ansbert alikaa nje ya mkoa kwa muda wa wiki moja kisha akarudi kwake, alishangaa kumuona mkewe hana raha kama alivyomzoea, mara kwa mara alikuwa anaonekana kuwa mkimya na mtu aliyezama kwenye dimbwi la mawazo.

    Ansbert hakutaka kumuuliza mkewe jambo hilo, aliamua kukaa kimya isipokuwa kufwatilia kwa ukaribu.

    Ansbert alikuwa anampenda sana mkewe, jambo lolote ambalo lilikuwa linaambatana na mkewe alikuwa halifumbii macho, alilichukulia siriazi.

    Tangu siku hiyo akajenga mazingira ya kumchunguza mkewe hususani simu yake, hii ni kwasababu aliona mkewe amekuwa na ukaribu na simu yake kuliko wakati mwingine hapo nyuma.

    Kwa siri Ansbert akawa anachunguza simu ya mkewe mara kwa mara wakati akitoka kazini na kabla hajaenda.

    Siku moja asubuhi wakati mkewe anaoga bafuni nayeye kuwa ametoka mazoezini aliingia chumbani akachukua simu ya mkewe.

    Aliiwasha na kuingia moja kwa moja kwenye call log na kupiga screenshot kisha akajitumia kwake, alifanya hivyo kwenye meseji, wasap na kumalizia na email.

    Alikuwa akifanya hili zoezi kwa wiki nzima mfululizo kisha siku moja ambayo ilikuwa ni jumapili aliamua kuchambua data zake kuanzia siku ya kwanza hadi ya mwisho.

    Alizichambua na kukumbana na namba mbili ambazo zilikuwa zikijirudia sana kwenye kupiga. Namba hizo zilionekana kupigwa asubuhi, mchana na jioni. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alichokifanya ni kuzifwatilia namba hizo ili kutambua ni za akina nani, akiwa ofisini alichukua simu ya mezani na kupiga namba moja wapo.

    “haloo samahani ninaongea na Mr Kayombo”(Ansbert aliamua kuzuga kwa kutumia jina jilo)

    “Kayombo gani,”

    “Kayambo Yule injinia wa majengo, mimi naitwa Lameck”

    “Hapana kaka, umekosea, mimi sio Injinia bali ni daktari”

    “daktari nani ndugu yangu”

    “mimi naitwa dokta Mgweno, nina duka kubwa la dawa hapa mjini maeneo ya Madukani”

    Dokta Mgweno alijitambulisha haraka kwani ilikuwa ni namna yake ya kujitaftia wateja ndio maana hakuona shida kujitambulisha.

    “basi asante sana, nitakuwa nimekosea namba”

    Ansbert alimalizana na namba hiyo kisha akachukua hiyo nyingine na kuipiga pia, iliita kwa muda mrefu lakini haikupokelewa ikabidi apige tena.

    Alivyopiga ile simu alipokea mwanamke ambaye alimjibu kwa kingereza lakini alimwambia tu kuwa unayempigia yuko na daktari anatibiwa amtafute baadae.

    Oscar aliachana na swala zima la kupiga simu, alichokifanya aliingia kwenye akaunti yake ya m-pesa na tigo pesa kuangalia majina ya wenye zile namba.

    Alipoyapata aliingia facebook, instagram na twitter kutafuta sura za wale watu.

    Alipoingia facebook mmoja kati ya wenye zile namba hakunfahamu kabisa lakini mwingine alionekana sio mgeni machoni mwake lakini kila alivyotafakari hakumfahamu.

    ………………

    Gari mbili zilikuwa zimeongozana kuelekea sehem ambayo gari ya nyuma ilikuwa haiijui ila ilikuwa inafwata ile ya mbele.

    Mbele kulikuwa na Rav 4 na nyuma kulikuwa na Prado, Rav 4 ilikuwa na Rozina na Prado ilikuwa na Ansbert.

    Ansbert alikuwa akimfwatilia Rozina anakoenda kwani alibaini mawasiliano na mtu aliyejiita dokta kuwa waonane ili ampeleke kwa mgonjwa wake.

    Ansbert alijiuliza sana kuwa iweje Rozina awe na mgonjwa ambaye yeye hamjui na hajawahi kuambiwa habari zake? Alipata wasiwasi sana na majibu ya wasiwasi wake ilikuwa ni kumfwata Rozina kule anakoenda.

    Akiwa kwa mbali lakni akiwa anaiona gari ya mkewe vyema aliishuhudia ikipaki kwenye hospital ambayo aliifaham siku nyingi kisha mwanaume mmoja akaingia na gari kuwashwa.

    Akili yote ya Ansbert ilimwambia kuwa Yule mwanaume anatembea na mkewe, alijikuta kichwa chake kikiwaka moto na moyo kumuuma.

    “Ina maana mke wangu ana mwanaume mwingine?”

    “ina maana nashiriki faragha ya mke wangu na mwanaume mwingine?”

    Ansbert aliumia kupita maelezo, wakati huu mikono ilikuwa inamtetemeka na mwili ulikuwa kama unaishiwa nguvu.

    Alimfikiria Rozina jinsi alivyo mzuri na mtamu, alimfikiria wanapokuwa nae kitandani…hakutaka kuamini kabisa kuwa kuna mtu mwingine anamvua nguo mkewe na kumaliza haja zake juu ya kifua cha mkewe.

    Mawazo yaliyokuwa yanapita kichwani kwake yalikuwa mengi mno, alifikiria kuanzia jinsi huyo mwanaume anavyoanza kufanya mapenzi na mkewe mpaka jinsi ambavyo wanamaliza.

    Alitathmini mpaka saizi ya uume wa mwanaume anayetembea na mkewe na kujikuta akifikiria… “hivi kama huyo mwanaume ana m..bo..o kubwa sana si mke wangu atakuwa ametanuliwa”



    Ansbert alikuwa anawaza mpaka mambo ya kijinga lakini yote ilikuwa ni wivu tu. Wakati anazinduka kwenye mawazo alishtuka akiwa halioni lile gari la mkewe.

    “shiiit…wamenipotelea wapi?”

    Ansbert alilipoteza lile gari kwasababu ya kuzama kwenye mawazo na kupoteza umakini wa alichokuwa anakifwatilia.

    Kwakuwa ilikuwa ni kwenye foleni aliamua kushuka na kukimbia kwa miguu yake kukagua magari yaliyoko kwenye foleni.

    Alipofika mbele kabisa aliliona gari la mkewe likiwa la kwanza kabisa kwenye foleni, alirudi mbio ili kuwahi kuingia kwenye gari lake lakini wakati anafika katikati tayari gari ziliruhusiwa na kuondoka kwa kasi.

    Magari yaliyokuwa nyuma ya Prado la Ansbert yalipiga honi nyingi yakitaka kupishwa lakini dereva hakuwepo, walianza kudaiveji na kulikwepa gari la Ansbert mpaka pale alipokuja mwenyewe na kulitoa mbio.

    Alilifukuzia gari la mkewe na kufanikiwa kulipata na kulifwata hadi pale lilipoingia njia za mitaani na kisha kupaki kwenye geti kubwa jeusi.

    Ansbert alizima gari na kushuka kisha akaanza kutembea taratibu mpaka kwenye duka lililopo karibu na hii nyumba ambayo ameingia Rozina na Yule mwanaume.

    Akili yote ya Ansbert ilimwambia kuwa ile ni gesti bubu ama ni nyumba ya Yule mwanaume hivyo mkewe anaenda kuliwa.

    Hakutaka kupoteza muda aliisogelea ile nyumba na kuona kengele pale getini. Aliibonyeza kama mara mbili hivi na kusikilizia lakini baada ya dakika kadhaa hakuona mtu kuja kumfungulia.

    Aliibonyeza tena kwa mara nyingine na kusikia hatua za mtu kule ndani akilisogelea geti, hapa akajiweka sawa na kuitoa bastola yake akaiweka tayari….





    “Hii ni nyumba ya mtu au ni gesti bubu?”

    “kaka hata salam hakuna unaanza na maswali?”

    “hujui unaongea na nani alafu unaleta jeuri, haya tangulia mbele na ole wako uniletee ubishi, nipeleke alipo mke wangu kaingia sasa hivi na mwanaume hapa”

    Ansbert alikuwa ameshikilia bastola akiwa kamuelekezea dada wa kazi wa Oscar akitaka apeekwe alipo mkewe.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huyu dada alikuwa akitetemeka kwa kuona bunduki huku aliyeishika akionekena hana masihara hata kidogo.

    “ongozaa, kinyago wewe”

    “kaka kwani mke wako ni yupi?”

    “nimekwambia kaingia sasa hivi hapa yuko na mwanaume, twendee unataka mpaka mke wangu ato…bwe kabisa!”

    Ansbert alikuwa na hasira sana, hakutaka kucheleweshwa, aliamini kuwa anavyoendelea kucheleweshwa ndio mke wake anavuliwa nguo na ku…..

    Wivu ulikiuwa umembana vya kutosha, alimpenda sana mkewe na kamwe hakutamani ashirikiane na mtu yeyote katika utamu wa penzi la mkewe.

    Alikuwa anapata maumivu kama kisu cha moto kinapitishwa moyoni.

    “hakyaMungu leo ntaua” alikuwa akijisemea moyoni.

    “Ingia chumba hiki wapo hapo” Ansbert alielekezwa sehemu alipokuwa Rozina na dokta, wakati huo Oscar alikuwa bafuni anaoga na Michelle akiandaliwa kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo na daktari pamoja na kuchomwa sindano.

    “haa Rozina mke wangu, umeamua kunisaliti kweli?”

    Ansbert alikuwa akitetemeka na kilio juu alipomuona Rozina amejilaza kwenye kochi huku docta Mgweno akiwa amekaa akimsubiri mgonjwa wake.

    “Mme wangu umefikaje hapa? Sikusaliti mme wangu niko hapa Oscar anaumwa”

    “mshenzi wewe huyu ndio Oscar, nakuuliza huyu ndio Oscar?”

    “wewe mshenzi kaa chini”

    “dokta Mgweno aliamrishwa”

    “lakini kaka…..”

    Paaa! Mlio wa risasi ulisikika, Dr Mgweno alikuwa amepigwa risasi iliyotua kwenye bega lake la mkono wa kushoto.

    Rozina aliachia ukelele mkubwa ambao uliwafanya akina Oscar pamoja na Michelle kukimbilia kwenye kile chumba alichokuwepo docta Mgweno pamoja na Rozina.

    Kilichowafanya waingie kwa tahadhari ni mlio wa risasi uliosikika, hivyo walihisi kuna majambazi. Kwakuwa Oscar nae alikuwa na bastola, aliichomoa akaitia risasi za kutosha kisha akaelekea kule ulikosikika mlio wa risasi.

    Alifungua mlango kwa tahadhari huku akichungulia kupitia kwenye kitundu cha funguo.

    Alishtuka sana kwani sura aliyoiona pale ndani alikuwa anaitambua, alivuta pumzi kisha kwa sauti ya chini akajikuta akiropoka “Ansbert…”

    Michelle alivyosikia vile nae kwa sauti ya taratibu akamuuliza Oscar …

    “unamfahamu?”

    “tulia kimya, huyo ndie mume wa Rozina, nadhani ameletwa hapa na wivu wake

    “sasa tufanyeje?”

    “tulia ngoja nikamfundishe adabu”

    “ahh… hapana usiende kufanya chochote, ngoja tuite polisi”

    “polisi?, acha ujinga wewe”

    Oscar alivamia mlango na kuingia moja kwa moja ndani huku akiwa kamnyooshea bastola Ansbert…

    “wewe mnafiki umeffwata nini hapa kwangu?”

    “haaa Oscar!”

    “unashangaa nini”

    “wewe ndio umemleta mke wangu hapa kwako, wewe ndie unamkuwadia mke wangu kwa huyu ku..m.. hapa”

    “braza mimi ni daktari tu, mkeo aliniita nimtibu huyu rafiki yake” dokta mgweno kwa kuogopa kufa alijikuta anaropoka pasi na kujua kuwa anamuweka mwenzie Oscar matatani.



    “Mme wangu mimi sikusaliti, nimekuja tu hapa kumsaidia huyu rafiki yako alikuwa na hali mbaya sana anaumwa”

    “nyamaza wewe”

    “hivi wewe Oscar, unajua ni jinsi gani mke anauma?”

    “hivi wewe Ansbert ndio wa kuniuliza huo usenge, unaona nilivyoharibikiwa maisha yangu kwa ajili ya unafiki wako, umemchukua Rozina wangu alafu leo unaniuliza maswali ya kinafiki hapa”

    “kwahiyo ndio unaamua ulipize ikiwa tayari imeshamuoa, kama angekupenda wewe si ungemuoa”

    Paaa…paaa!

    Milio ya risasi ilisikika na watu wawili walikuwa wako chini ukijumlisha na docta Mgweno wa tatu.

    Makelele pale ndani yalikuwa mengi sana, damu zilikuwa zinachuruzika bila kipimo, walikuwa wanakoroma ishara ya kukata roho kabisa.

    Gari ilikuwa kasi sana ikipita mitaa ya mjini kuelekea dukani kwa dokta Mgweno. Dereva alikuwa ni Michelle na ndani alikuwa amebeba watu watatu ambao wana majeraha ya risasi.

    Mmoja alikuwa akijitambua na wawili walikuwa hawajitambui kabisa. Wazo la kuelekea dukani kwa dokta Mgweno na sio hospitali ilikuwa ni kuukwepa mkono wa dola.

    Walipofika pale dukani waliingizwa kwenye chumba maalum ambacho dokta Mgweno hukitumia kwa kazi zake za siri.

    “Haloo dokta Kamuzu”

    “Ndio dokt Mgweno”

    “Samahani, njoo hapa ofisini kwangu sasa hivi”

    Ndani ya dakika kadhaa kijana aitwaye Kamuzu ambaye ni rafiki wa dokta Mgweno aliingia pale ofisini akiwa na briefcase ndogo.

    “Ebwana karibu sana, naomba unihudumie”

    “haaa umefanyaje dokta”

    “nihudumie kwanza, nitoe hiyo risasi begani”

    Haraka haraka dokta Kamuzu alichukua vifaa vyake akaweka mezani akachukua sindano ya ganzi na dawa akamchoma dokta Mgweno kisha akakaa kusubiria dakika kadhaa ili ganzi ishike.

    “kaka wewe endelea tu na kazi ya kutoa hiyo risasi wala usisubirie ganzi itanikuta njiani”

    “ila utaumia kaka”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “najua sana wewe fanya kazi yako.”

    Alichukua kisu akakata bega kisha damu nyeusi ikatoka kwa wingi, alichukua taulo akafuta vizuri. Wakati huu dokta Mgweno alikuwa akigugumia kwa maumivu.

    Aliposafisha vizuri alichukua mkasi akautumbukiza ndani kabisa ya shimo hili lililotobolewa na risasi mpaka akagusa kitu kama chuma.

    Aliingiza kichuma ambacho kilikuwa na sumaku mbele kisha akakivuta na kutoka na Risasi. Alifanya hivyo mara kadhaa ili kama kuna vipande vya chuma navyo vitoke.

    Baada ya zoezi la kutoa Risasi kukamilika alichukua dawa akapaka vizuri, akachukua nyuzi na sindano kisha akaanza kumshona dokta Mgweno.

    Kweli mganga hajigangi, Dokta Mgweno alikuwa kimya akisikilizia huduma anayopewa na dokta mwenzake.

    Baada ya zoezi hili kuisha alimfunga vizuri kisha akamchoma sindano ya kuzuia maumivu na kumuandikia vidonge vya kumeza.

    “dokta usiache kumeza dawa, usijifanye kwa kuwa wewe ni daktari ndio usimeze dawa”

    “hahahaaaa dokta nitameza bwana”

    “au unaogopa dawa niwaambie wawe wanakukaba”

    “acha utani dokta hebu twende huku”

    “wapi tena pumzika hapa”

    “we nifwate”

    Walifwatana dokta Mgweno na dokta Kamuzu wakaingia kwenye chumba kingine ambacho kilikuwa na giza totoro.

    Dokta mgweno aliwasha taa ambayo ilimulika pale ndani.

    “haa hawa ni akina nani”

    “shiii…kidole kilikuwa mdomoni kikiashiria kuwa dokta Kamuzu atulie kimya”

    “hawa jamaa wametwangana kwa wivu wa mapenzi, hapo wote ni mahututi ndio maana unaona wana dripu za damu na gluecose”

    “nani kawawekea”

    “ni hawa wauzaji wangu hapa, wamepitia kidogo maswala ya utabibu”

    “Mungu wangu, kwanini hujawapeleka hospitali kubwa”

    “kaka Mke wa mmoja wao amenisihi sana anaogopa ishu kuvuja na kuwafikia polisi”

    “hapana kaka hali yao inastahili hospitali kubwa”

    “kaka tuwanusuru kwanza, hivi unawajua kuwa hawa ni watu maarufu?”



    “ni akina nani hao”

    “huyu ni Yule aliyekuwa balozi wa Ghana, na huyu ni mkurugenzi wa habari Ikulu”

    “kwahiyo huyu ni Oscar na huyu ni Ansbert?”

    “Kabisa kaka”

    “haya wewe kapumzike”

    “kabla sijaondoka naomba nikwambie kitu kimoja, tuite madaktari wengine waje na vifaa hapa wawahudumie, pesa ya maana ipo”

    “poa usijali”

    Usiku kucha madaktari bingwa walikuwa wako bize kuwahudumia Oscar na Ansbert ambao wote walikuwa hawajitambui.

    Mpaka inafika asubuhi bado walikuwa hawajajitambua, madaktari hawa walikuwa na wasiwasi mwingi kwani endapo wale jamaa wangefariki basi ingekuwa ni kashfa kubwa na kisheria wangekuwa matatani.

    Tamaa ya hela nyingi iliwafanya wafanye kazi hii hatari ya kutibu nje ya sehemu inayotambulika na kukiuka miiko ya kidaktari.

    …………………

    Dokta mgweno alikuwa kwake akiugulia maumivu huku akihudumiwa na mdogo wake wa kike ambaye alikuwa anasoma chuo kikuu cha Dar Es Salaam.

    Akiwa ameamka tu na kuoga kisha akanywa chai alisikia mlango wa nyumba yake ukigongwa.

    Mdogo wake alipofungua mlango alimfanya Dokta Mgweno apigwe na butwaa na mapigo yake ya moyo kwenda kasi sana.

    Alimuona mwanamke mrembo akiingia kwake huku akiwa amevalia mavazi nadhifu na nywele zake ndefu zikiwa zimelala mpaka mgongoni.

    Dokta Mgweno alikuwa ametumbua macho kama mjusi aliyebanwa na tawi, mwanamke huyu alikuwa amevaa gauni fupi la pinki huku likionyesha miguu yake mirefu na minene.

    Alikuwa na umbo lililogawanyika kiasi na kubeba chura wa wastani kwa nyuma. Alikuwa mweupe na mwenye macho makubwa ya kulegea huku pua yake ndefu kiasi ikimfanya aonekane kuwa ni chotara kumbe alikuwa ni mwenye asili ya kitutsi kutoka Rwanda.

    “Ro..Ro..Rozina, karibu” dokta Mgweno iilikuwa ni kama mara yake ya kwanza kumuona Rozina. Aligundua kuwa mwanamke huyu ni mrembo kuliko wanawake wote aliowahi kuwaona.

    Hata Yule mdogo wake nae alibaki amemtolea macho Rozina utadhani sio mwanamke mwenzake.

    “Asante dokta, nimekuja kukucheki hali yako”

    Badala ya Dokta mgweno kujibu alijikuta akipata kigugumizi cha ghafla “hakyaMungu huyu mwanamke ni mzuri, wale jamaa wana haki ya kuuana”

    Tamaa ilikuwa imemkaba sana daktari wa watu kiasi kwamba alitamani kwa nguvu zote siku moja alale na Rozina.

    ````````````````````````````````````

    “Dokta naona huyu mmoja anahitaji kupelekwa nje ya nchi, kama tukiendelea kumhudumia hapa anakufa huyu”.

    “Sasa tufanyeje, tutawezaje kumsafirisha wakati jambo hili limefanywa siri”

    Wakati wanajadiliana mashine moja ilianza kupiga makelele kuashiria kuna mgonjwa mapigo yake ya moyo yamesimama…………



    “Mpigie Mgweno aje hapa”

    “Basi wewe mhudumie, mshtue mapigo yake”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Haloo dokta Mgweno njoo haraka”

    “Kuna nini kinaendelea”

    “Njoo tu huku hali sio nzuri”

    “Nakuja”

    Dokta mgweno aliacha kila kitu akaifunga safari kuelekea kwenye ofisi yake huku akiwa na Rozina kwenye gari.

    “Kwani wamekwambiaje?”

    “Wameniambia tu niende haraka”

    “Mungu wangu, isije kuwa mme wangu amefariki jamani, ntaishije mimi”

    Rozina alikuwa na wasiwasi na mme wake kwa sababau yeye ndiye alikuwa na hali ngumu kuliko wengine. Risasi aliyopigwa ilipita kwenye mapafu.

    Aliendesha gari kwa kasi kiasi kwamba hata dokta Mgweno pale ndani ya gari alikuwa anaogopa,mwendo ulikuwa mkali sana lakini hakumsemesha alivumilia tu huku akimuomba Mungu wafike salama.

    Kwajinsi ambavyo Rozina alikuwa anaendesha gari huku akiwa na mawazo mengi alijikuta akijisahau kabisa.

    Alijisahau kabisa na nguo yake ilikuwa imepanda juu na kuacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi. Dokta Mgweno alikuwa amekodoa macho pale kwenye mapaja ya Rozina huku udenda ukimtoka.

    Yalikuwa ni mapaja manene meupe yenye vinyweleo vilivyolala vizuri huku vikiwa vyeusi tiii…dokta Mgweno ndani ya moyo wake hakutaka kuamini kuwa kuna mwanamke mzuri hapa duniani zaidi ya Rozina.

    Alipiga mahesabu mengi kichwani jinsi ya kumpata Rozina lakini kila akijifikiria aliona kabisa kuwa nafasi hiyo hakuwa nayo. Rozina alikuwa mzuri sana na likuwa ana kila kitu, hakuna cha kumdanganyishia.

    “Ama kweli hata rais akimuona huyu mwanamke anaweza kuiweka nchi reheni” alijisemea dokta Mgweno.

    Wakati safari inaendele Dokta Mgweno alikuwa anatamani hata apitishe mkono kwenye lile paja aliguse, alikuwa akiunyanyua mkono ili aguse pale lakini akawa anakosa ujasiri na kuurudisha.

    Alimtazama Rozina kunzia juu mpaka chini akagundua kuwa hakuwa na kasoro kabisa. Wakati Rozina anaweka gia na kukanyaga mafuta aliyafanya mapaja yake kutikisika sambammba na moyo wa Mgweno.

    Kwa hali aliyokuwa nayo Mgweno alifikia hatua ya kupata ujasiri wa kutosha kushika mapaja ya Rozina, alikuwa jasiri kwasababu alishafikia kwenye hatua ya liwalo na liwe.

    Sehem zake za siri zilikuwa zimesimama kama Ngongoti na mapigo ya moyo yalikuwa juu kiasi kwamba akili yote ikawa haina uwezo wa kuzuia jaribu lililokuwa mbele yake.

    Taratibu aliunyanyua mkono wake huku unatetemeka akaanza kuupeleka eneo la Rozina, aliupeleka taratibu huku anasita sita, wakati wote huu Rozina ana mawazo tele kichwani wala haelewi chochote na ndio kwanza vazi lake linazidi kupanda juu kiasi kwamba hata dokta Mgweno aliamini kuwa Rozina hakuvaa taiti.

    Aliupeleka mkono ukaenda na mwisho ukaishia kwenye “hand brake” hii ni baada ya kuona macho ya Rozina yakimuangalia. Ujasiri ulikosekana! Hata hivyo alirudia tena jaribio lake ambapo mwishowe alifanikiwa kushika paja la Rozina.

    Alipoligusa tu alishtuka kama kashika kitu cha ajabu…alishtuka kwani alikutana na kitu cha tofauti sana, alibaini kuwa paja la Rozina lilikuwa laini na la moto kupita malezo. Mapigo ya moyo yalizidi kwenda mbio kupita awali.

    Wakati huu Rozina alikuwa hana habari na jambo lolote kwani akili yake yote ilimuwaza mumewe.

    Kitendo cha Rozina kukaa kimya kilimfanya Dokta Mgweno aamini kuwa Rozina anakubaliana na kinachoendelea.

    Ilibidi azidishe kabisa na sasa zoezi lake lilikuwa ni kupapasa kabisa mapaja ya Rozina na kuyaminya minya, alikuwa akikipeleka kiganja chake mbele na kukirudisha nyuma aliendelea na zoezi lake na sasa alikuwa anaelekea maeneo ya juu kabisa kwenye maungio.

    Hapa ndipo Rozina aliposhituka na kutaka kogongesha gari kwenye ukuta wa duka la Dokta Mgweno na kuhamaki “haaaa Dokta unafanya nini?”

    “Ah..ah..ah samahani nilikuwa nakupima homa”

    “Mshenzi mkubwa wewe, tangu lini homa ikapimwa kwa staili hii, mjinga kabisa nimekwambia nina homa mimi?”

    “Nisamehe basi nilizidiwa”

    “Umezidiwa na nini? Hivi una akili timamu kweli wewe?”Rozina alikuwa mkali kama Mbogo.

    “Nina wasiwasi hata wagonjwa wako unawafanyiaga michezo michafu”

    “Haaa hapo sasa umefika mbali, hivi unafikiri mimi nimewahi kupata mgonjwa mzuri kama wewe? Hivi ni nani anaweza kujizuia mbele yako na jinsi ulivyoacha mapaja yako wazi, si ulikuwa unanitega mwenyewe, ulitaka mimi nifanyeje”

    “Mse…ge wewe nikutege una nini wewe, sura yenyewe hiyo, niache kuwatega watu nikutege wewe kiatu…..achana na mimi kabisa, mimi sio Malaya, mimi ni mke wa mtu na ninajiheshimu”

    “Umefikia pabaya sasa, mimi sio Mse…ge, mimi ni profesheno kabisa, na naomba unisikilize…”

    “….tafuta ambulensi uwatoe wagonjwa wako hapa sawa?”

    Rozina aliposikia hivyo alijikuta akiwa mpole ghafla, alifikiria mambo mengi kisha akaamini kuwa kama mambo yakienda hivyo yeye ndio wa kuumia.

    Alitumia akili ya kuzaliwa kisha akamfwata dokta Mgweno na kumpigapiga begani kisha akamwambia….

    “Wapone kwanza…mambo mengine yatafwata”

    ……………………………………….

    “Dokta Mgweno mgonjwa mmoja amefariki”

    “Unasemaje? Nani kafariki”

    “Yule Ansbert”

    “Mungu wangu”

    Dokta Mgweno alijikuta akipata mshtuko mkubwa sana, aliingia mbio mbio mpaka pale alipokuwa amewalaza wagonjwa wake na kumuona Oscar akiwa ameamka na kukaa mwenyewe huku akinywa maziwa. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliangalia pembeni akakutana na mwili wa Ansbert ukiwa umepoa kuashiria hauna uhai. Alifikiria jisni ya kumwambia Rozina akashindwa kabisa aanze na neno gani. Wakati anawaza alimuona Rozina akiingia kwa kusukuma mlango huku akiwa na sura ya wasiwasi………………





    “niambie ukweli usinifiche chochote, Mume wangu anaendeleaje”

    “tafadhali sana Rozina, naomba utoke nje, tuko kwenye harakati za kumnusuru mume wako…usiponisikiliza ukatoka nje utaharibu kila kitu”

    Taratibu Rozina alitoka nje lakini alikuwa na wasiwasi sana moyoni mwake kuwa huenda kuna jambo anafichwa.

    Dokta Mgweno alichukua vifaa vyake na kuanza kuupima uhai wa madaktari wenzake. Aliamini siku zote kuwa jambo la kweli ni lile ambalo amelithibitisha mwenyewe pia.

    Alimpima kila sehemu anazojua yeye lakini majibu yalifanana sana nay ale aliyopewa na wenzake, alikata tama kabisa na woga ulimshika kisawasawa.

    Hakutaka kuamini moja kwa moja, alitafuta mashine yake ambayo inapima mapigo ya moyo ya chini kabisa na alipoipata akaiweka kifuani kwa Ansbert.

    Ajabu ni kwamba alisikia kwa mbali mapigo ya moyo wa Ansbert yakipigajapo kwa mbali sana. Hapo hapo alikimbia nje na kuwaita wenzake ambao nao waliingia haraka.

    “hajafa bado, mapigo yake ya moyo yako kwa mbali sana”

    “kweli? Nipe hicho kipimo”

    “haaa kweli hajafa japo nafasi yake ya kuishi ni finyu sana”

    “push kifuani kwa nguvu, ngoja kuna dawa nikachukue tumpige dripu”

    Kifua cha Ansbert kilikuwa kinashindiliwa kama mtu anajaza baiskeli upepo, ndani ya dakika kumi mashine ilianza kusoma zig zag kuashiria uhai umerudi.

    Kidogo sasa mmadaktari hawa walianza kuonyesha sura za tabasamu baada ya kuona wameweza kumrudisha Ansbert duniani.

    Mgweno alirudi kwa kasi na kukuta mashine ikisoma vyema, alishangilia moyoni kisha akachanganya dawa kwenye dripu na kulitundika huku likining’inia na kuingia kwenye mishipa ya Ansbert.

    ‘’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’

    Haikuwa kazi rahisi sana kwani usiku kucha madaktari hawa walikuwa bize kushughulikia afya ya Ansbert ambayo ilikuwa inaimarika kwa kiwango kikubwa.

    Wazo sasa la kumhamishia hospitali kubwa jijini dar es salaam lilikuwa limepitishwa kwakuwa walikuwa wanampeleka hospitali ambayo sio ya serikali.

    Taratibu zote zilikamilishwa na hatimaye Ansbert alikuwa katika hospitali inayomilikiwa na Wahindi ikiwa maeneo ya Msasani Dar es salaam.

    Oscar yeye alishafanikiwa kupona kabisa na kurudi nyumbani huku akianza kuimarika afya yake kutokana na kula vizuri, kupata matibabu fasaha na kuacha ulevi.

    Huduma ambazo alikuwa anapatiwa na Michelle zilimfanya ajisikie faraja sana na hatimaye ndani ya moyo wake alishatengeneza mapenzi kwa Michelle na kukubali kumsahau Rozina na kuamini kuwa hakuwa fungu lake.

    ‘’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’’

    Katika kipindi cha miezi miwili baadae tayari Ansbert alikuwa amepona na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwake na kuendelea na matibabu ya kawaida.

    Oscar nae alikuwa ameimarika kabisa kuanzia afya yake mpaka muonekano. Suruali alizozipunguza sasa zilikuwa hazimtoshi. Ilibidi afanye shopping upya huku akizunguka na kipenzi chake Michelle kwenye maduka mbalimbali ya Mwenge na Posta. Oscar alipendeza haswa, alikuwa na gari nzuri na tayari alishanunua nyumba nzuri maeneo ya OysterBay ambapo pia alikuwa na duka kubwa la nguo kariakoo ambalo alikuwa anauza Michelle.

    Maisha ya Oscar yalikuwa mazuri sana kiasi kwamba hata wasichana walianza kumtaka kwa kasi ila hilo halikuwa kwenye mawazo yake.

    Alimuheshimu Michelle na hakutaka kuharibu familia yake na mipango yake mingi ambayo walikuwa wamejiwekea kwa maisha yao.

    “baby nikwambie kitu”

    “niambie honey”

    “am pregnant”(nina Mimba)

    “what (nini?)”

    “nina mimba baba”

    “I cant believe your words”(siwezi kuamini maneno yako)

    “twende hospitali tukapime baba”

    …………………………………….

    Gari iliendeshwa kasi sana mpaka kwenye duka kubwa la dawa lililokuwa maeneo ya Posta mjini kabisa katikati ya jiji la dar es salaam.

    Baada tu ya kufika lilipaki na watu wawili waliopendeza walishuka huku wakiwa wameshikana mikono.

    “habari dada?”

    “nzuri tu karibuni sana”

    “asanteni sana, samahani tumemkuta Dk Mgweno”

    “yupo huko ofisini kwake”

    “Tunaweza kuonana nae?”

    “Ngoja nimjulishe kwanza”

    “Dokta samahani, kuna wageni wanakuhitaji”

    “Ni akina nani?”

    “Mwambie ni Oscar na mkewe”

    “Mnaambiwa muende ofisini kwake”

    “Ooh Oscar, karibu sana best”

    “Ahsante sana dokta”

    “naona uko na mama”

    “ndio kaka”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “habari shemeji”

    “Nzuri tu habari za kazi dokta?”

    “Salama karibuni sana mketi”

    Waliketi kwenye makochi yaliyokuwepo humu ofisini na kisha wakaletewa vinywaji walivyoagiza. Dokta Mgweno alimshangaa sana Oscar na mkewe jinsi walivyopendeza na kuwa na miili iliyonona. Zaidi sana alimshangaa Oscar kwani tangu waachane pale hospitali hawakuwahi kuonana tena.

    “aisee Oscar naomba unipe siri ya mafanikio yako, mbona umekuwa na afya nzuri kiasi hicho wakati wenzio bado tumebaki kuwa vimbaumbau”

    “hahahahaaaaaa acha masihara kaka”

    “kaka huwezi kuamini, endapo ukikutana na mtu aliyekuona kipindi kile asipoambiwa kuwa ni wewe hakika hawezi kukukumbuka….any way ngoja nisiongee sana kabla sijawasikiliza”

    “sawa dokta…naomba umpime mke wangu kwasababu ananidanganya kuwa ana Mimba”

    “anakudanganya? Umejuaje kwamba anakudananya?”

    “ah wewe si umpime ili ujue uongo wake”

    “Njoo mama Oscar”

    …………………………………..

    Hongera sana braza, inaonyesha kweli Mkeo ana Mimba ya Miezi miwili, nimempima na vipimo vimenionyesha hivyo…………

    Wakati Dokta Mgweno anamalizia sentensi yake aliingia Rozina bila hata kubisha hodi huku akionekana kushtuka baada ya kumuona Oscar na Michelle pamoja na kile alichokisikia.

    Oscar nae alishtuka kwani alipomuona tu Rozina moyo wake ulienda kasi sana na alijikuta akichanganywa na urembo alio nao Rozina.

    Dk Mgweno nae alikuwa na wasiwasi kwani kitendo cha Rozina kuingia Bila hodi kilikuwa na tafsiri tofauti kabisa.

    Rozina hali kadhalika alishtushwa na muonekano wa Oscar jinsi alivyopendeza na kujikuta akishindwa kufiicha hisia zake.

    Alishikwa na kigugumizi na kushiindwa cha kuongea kisha akamuangalia Michelle jicho la hasira na kugeuka kisha akafungua mlango na kuubamiza kwa hasira kisha akaondoka zake…..





    Pamoja na kukaa kwa muda mrefu wakilala na kuamka pamoja bado Oscar na Micchelle walikuwa hawajaingia kwenye mapenzi rasmi.

    Kila siku Michelle alikuwa akibuni mbinu za kuliteka penzi la Oscar lakini alikuwa anashindwa mbinu.

    Ukweli ni kwamba Michelle alikuwa mzuri hususani wa umbo kwani alikuwa na umbo la kuvutia sana.

    Rangi yake ya maji ya kunde na macho yake ya kulegea yalionesha kabisa kuwa alikuwa na asili ya afrika Magharibi.

    Kila siku Oscar alikuwa akimchunguza Michelle kwa lengo la kuubaini urembo wake ambao unaweza ukamvutia na kumfanya amsahau Rozina.

    Akili ya Oscar ilikuwa imetawaliwa sana na Rozina ndio maana kila mwanamke aliyekuwa anakutana nae alikuwa anamlinganisha na Rozina na kama angeona kuwa anazidiwa viwango na Rozina basi anampuuza.

    Hii ndio ilimfanya achelewe kupata mwanamke mbadala wa Rozina kwa muda mrefu kwani alitaka siku zote apate mwanamke anayefanana na Rozina.

    Uwepo wa Michelle pale ndani bado hakuujali sana japo alikuwa akimpenda ila hakufanikiwa kuwa na hisia za kimapenzi kwake.

    Hii ilikuwa ikimuumiza sana Michelle na mara kwa mara alipokuwa anamuona Rozina akija pale ndani kwa lengo la kumhudumia Oscar alikuwa anachukia sana, alikuwa anatamani siku moja amwambie Rozina kuwa asije na atakuwa anamhudumia mwenyewe lakini alihofia kumuudhi Oscar hivyo akaamua kujipa muda.

    Mapenzi, mahaba, unyenyekevu na upendo ndivyo vitu Michelle alikuwa anampa Oscar siku zote akiwa nae pale ndani.

    Taratibu afya ya Oscar iliimarika sana, alianza kunona na kupendeza, nguo zilianza kumbana na hatimaye hazikumtosha kabisa.

    Kazi ilikuwa kwa Rozina kumnunulia Oscar nguo nyingine. Oscar alipokuwa anajiangalia kwenye kioo mwenyewe alijikubali na kujiona kuwa amerejea vyema.

    Hali ya kutoishi kwa upweke pale nyumbani kwake aliifurahia sana na mapenzi pamoja na huduma alizokuwa anapata kutoka kwa Michelle zikamfanya ajione mwenye furaha.

    Walikuwa wanashinda pamoja, wanakula pamoja wanalala pamoja na kuamka pamoja, kwakweli Oscar alipata kampani ya nguvu.

    Pamoja na yote hayo hakuna hata siku moja ambayo Oscar aliwahi kumgusia michelle swala lolote la Mapenzi.

    Michelle alikuwa analala na Night Dress yake huku Oscar akilala na bukta na hawakuwa wanagusana kwani kitanda kilikuwa sita kwa sita.

    Usiku Michelle alikuwa anatamani kumkumbatia Oscar lakini alikuwa anasita, kila alipotaka kufanya hilo jaribio alikuwa anakwama kufanya maamuzi hali hii ilimuumiza kwa muda mpaka alipoamua kutumia mbinu mbadala.

    ……………………………………..

    “Baby nina maongezi na wewe”

    “Maongezi gani jamani, ya heri au shari”

    “Ah ni heri tu wala usiwe na wasiwasi”

    “Haya tuongee”

    “Hapana kunywa chai kwanza”

    “Mh ushanitia kihoro, si uniambie tu”

    “Kunywa chai kwanza bwana”

    “Mh sawa bwana”

    Oscar alikuwa na wasiwasi kwani alikuwa anajiuliza ni nini hasa ambacho Michellea anataka kukisema, alikuwa anakunywa chai nzito lakini ilikuwa haishuki vyema.

    Alijitahidi kunywa chai haraka ili amsikilize Michelle anataka kusema nini kwani tayari alikuwa na kihoro kikubwa. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Michelle nimeshamaliza chai njoo basi tuzungumze”

    “Mhhhhhh jamani, si uniache na mimi ninywe kwanza chai”

    “Haya niko chumbani basi”

    Oscar alielekea chumbani kisha akavua suruali na kubaki na bukta huku akiwa kifua wazi, aliwasha tv na kuweka muvi kisha akawasha na AC na kujilaza kwenye kochi akianagalia sinema hiyo.

    Wakati wote wa kuangalia sinema alikuwa anasubiri kwa hamu Michelle aje aseme hicho alichokipanga.

    Dakika zilisogea na hatimaye Michelle aliingia chumbani lakini hakukaa sana, alienda kuoga vizuri na kujipara vilivyo

    Alifungua begi lake na kutafuta kigauni kifupi cha kata mikono akakivaa kisha akapulizia marashi malaini na kujizungusha kwenye kioo kama mwanamitindo jukwaani.

    Alipohakikisha kuwa yuko vizuri alielekea kule aliko Oscar na kukaa mbele yake huku akiyaruhusu mapaja yake yawe wazi kwa kiasi kikubwa ili aweze kuziteka hiisia za Oscar.

    Ukweli ni kwamba Oscar alishtuka baada ya kumuona Michelle akiwa kwenye muonekano ule kwani alipendeza sana na alikuwa anavutia pia.

    Aliweza kuyatathmini mapaja ya Michelle na kugundua kuwa ujazo wake ulikuwa sio wa kitoto, alitathmini ranngi yay ale mapaja na kujikuta akiyamezea mate.

    Alipokuja kifuani kwa Michelle alikumbana na maziwa yaliyotuna vyema na kuzifanya chuchu zichomoze na kuonekana kwenye kigauni kile cha kuteleza.

    Siku hii ilikuwa kama vile ndio mara ya kwanza kumuona Michelle, taratibu alijikuta akisisimkwa na sehemu zake za chini zikaanza kunyanyuka kitu ambacho alikuwa hajakishuhudia muda mrefu sana kutokana na kuishi maisha ya stress.

    Alijikuta anasahau kumwambia Michelle aseme alichotaka na kujikuta akifikiria mambo yasiyoeleweka kwenye akili yake.

    Michelle aliligundua hili na alianza kujipa asilimia kubwa za ushindi kwenye akili yake, taratibu alikivuta kijistuli alichokuwa amekalia na kuzidi kumsogelea Oscar.

    “Oscar nashukuru kwamba afya yako inaimarika vya kutosha” kauli hii ilimzindua Oscar kwenye dimbwi la mawazo na kujiona kama alikuwa usingizini.

    “Mimi ndio natakiwa nikushukuru kwasababu huduma zako zimenifanya niwe hivi”

    “Tumshukuru na Mungu pia”

    “Nikweli tena nataka nianze kwenda kazini wiki ijayo”

    “sawa ni viizuri ila mimi nataka nikwambie kuwa kesho kutwa nataka kurudi nyumbani kwahiyo naomba ukanikatie tiketi”

    “unamaanisha uataka kurudi Ghana?”

    “ndio naomba unikatie tiket”

    Swala hili lilimshitua sana Oscar kwani alishamuona Rozina kama mtu wake wa karibu ambaye alishamzoea na hakutaraji ataondoka. Alikaa kimya kwa muda akitafakari kauli ya Michelle na jinsi kuondoka kwake kutakavyomuathiri.

    Alijisikia vibaya sana na hakutamani hilo litokee ila alikuwa akifikiria ni namna gani afanye ili kumfanya Rozina abadili maamuzi.

    “Kwanini unaondoka?”

    “sasa nitabaki hapa nifanye nini”

    “kwani huko unaenda kufanya nini?”

    “kwanza huko ndio kwetu na shughuli na mipango yangu iko huko”

    “sasa kwanini ulikuja huku?”

    “nilikuja kwasababu unaumwa na nilitaka kukuhudumia sasa umepona ni nafasi yangu sasa niondoke, hata hivyo nataka kuolewa”

    “u..ume..umesemaje?” Oscar aliuliza kwa kutetemeka.

    “nataka kuolewa, wazazi wangu wameniambia wamenitafutia mchumba”

    “lakini sio fair(haki) Michelle”

    “sio fair kivipi Oscar?”

    “ah sio fair tu bhana”

    “Ongea vizuri kwanini sio fair?”

    “sasa mimi unaniachaje? Ah..sio fair bhana”

    “sikuelewi Oscar, mbona unachoongea hakiniingii vizuri akilini”

    “yani mimi kila siku wa kuumizwa tu, kwani mimi nimekosea nini jamani”

    “umeumizwa na nani Oscar, isije ikawa unajiumiza mwenyewe”

    “mimi ntakufa tu, yani kila nikisema hapa nimepata bado nakimbiwa, kwanini nyinyi wanawake mko hivi lakini, mbona hamna huruma hata kidogo?”

    “kwani unataka nini Oscar? Sema unataka nini”

    “kwani hujui Michelle, kwani hujui?”

    Haraka sana akili ya Michelle ilifanya kazi kama umeme akawa ameshatambua ninini kinamsumbua Oscar, alijua tatizo la Oscar na tayari alifurahi ndani ya moyo wake kwani mtego wake ulikuwa uananasa kiulaini kabisa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “naomba unisikilize Oscar, najua umenizoea sana na mimi nimekuzoea pia ila naomba niondoke kwasababu mimi nahitaji kuolewa niwe na familia yangu hali kadhalika na wewe pia unapaswa kuwa na familia yako pia, tupeane nafasi kila mtu ajipange kwa maisha yake”

    “usifanye hivyo Michelle, usifanye hivyo wewe ndio tegemeo langu”

    “hivi unadhani Oscar ni nani atakubali kuwa mtumishi wako hapa kila siku bila sababu ya msingi, mimi nitakaa hapa mpaka lini, ili niwe mtumishi wako wa chumbani au? Tena naomba niondoke leo leo nikalale hotelini kesho nifwatilie tiketi maana naona huna mpango wa kunisaidia”

    Michelle baada ya kusema hivyo alichukua mabegi yake na kuanza kupanga nguo zake, alizunguka huku na kule akikusanya kila kilicho chake na kisha kuchukua simu akapiga nyumbani kwao Ghana.

    “nakuja kesho kutwa”

    “ndio”

    “sawa mwambieni nampenda pia na tutafunga ndoa”

    “sawa kabisa mwambieni aisijali



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog