Search This Blog

Monday, 16 May 2022

MTOTO WA BOSS WANGU - 1

 







    IMEANDIKWA NA : BIKORA SAIDY



    *********************************************************************************



    Chombezo : Mtoto Wa Boss Wangu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Kuna msemo usemao usilolijua litakusumbua sana na ukilijua utatuzi wake hauhitaji nguvu sana maana itakuwa vyepesi kulikwepa au kuendana nalo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hii lilidhihirika kwa kijana Wangesi mtoto wa mzee Kamau aliyejikuta akiangukia katika dimbwi la maisha magumu sana na hakujua kipi cha kufanya ili aweze kutatua hali yake maana mzee wake alianza kumdai hela yake baada ya kufeli kidato cha nne



    Huko nyumbani kwao kumbuka kuna watoto wengine husoma kwa shida sana na mzazi kupata ada ya kulipia inakuwa ni changamoto sana!



    Wangesi alisoma kwa shida sana alikuwa ni mtu mwenye ndoto zake za kufika mbali sana alitamani kufika chuo kikuu akiamini kuwa kufika huko ndio maisha yatakuwa yamenyooka alilia sana alipokuwa akiwaona wanavyuo wakivaa joho zao



    Huku akitamani na yeye awe miongoni mwao lakini hali ngumu ya maisha nyumbani kwao ilimfanya ashindwe kuendelea na shule hali ya kuwa alimaliza kidato cha nne hakufanikiwa kuendelea na shule baada ya kuwa na wastani mdogo wa ufaulu.



    Wangesi aliyachukia sana maisha yale magumu nyumbani kwao kitu kilichomfanya azame katika kufanya kazi kwa nguvu zote maana aliamini kuwa shule hawezi kuendelea tena kulingana na ufaulu wake kuwa mdogo sana alianza kulima bustani ya matunda pale nyumbani kwao



    Ambapo aliamini kuwa ndio mkomboz pekee wa maisha yake kwa muda ule alipenda sana kazi zake ziende mbele na sio kuwa mvivu hakika kijana wangesi alipenda sana kujishugulisha aliendelea na kazi ile kwa muda wa miaka kadhaa ubize wake ulimfanya kusahau kuwa duniani kuna jinsia ya kike



    Alishinda kwenye kazi zake na aliwaeza kuwakumbuka kuwa kuna jinsia ya kike mara alipokuwa akikutana nao alikuwa kujana mweusi kiasi na mwenye sura ya duaru alikuwa mfupi japo sio sana na mwenye umbo la miraba minne alijazia kifua chake sana



    Aisee mabinti wengi walipagawa na uchapakazi wa kijana wangesi mtoto wa mzee Kamau kila alipokuwa akipita aliacha maswali kwa watoto wa kike huku wakijiuliza kama ameoa au bado na kama hajaoa mchumba wake niyupi?



    Ni baadhi ya maswali waliyokuwa wakijiuliza pale tu alipokuwa akikatiza Wangesi



    Wengine walidiriki kusema huwenda jogoo hawiki ndio maana hapendi wanawake



    Wangesi alipopat habari hizo hakuweza kujali maneno aliweza kuendelea na kazi zake muda wote!.



    Baada ya miaka kadhaa Wangesi aliweza kutimiza kiasi cha fedha alichokuwa akikihitaji lengo lake ilikuwa kuendelea na shule baada ya kupata kiasi hicho wangesi aliweza kutafuta shule ya ufundi ambapo aliweza kwenda kusomea udereva na utengenezaji wa magari ( machenica)



    Aliweza kutafuta chuo hicho na mwisho wa siku aliweza kupata alilipia ada ya mwaka mmoja na alianza masomo yake muda huo chuoni pale kwa Mara ya kwanza alipata shida sana maana mazingira aliyaona magumu lakini baada ya siku kadhaa aliweza kupata marafiki maana yeye alikuwa mkimya sana hivyo alipendelea sana marafiki ambao sio walopokaji



    Alitulia sana mwisho wa siku akampata rafik wa kike aitwae Sarah

    Sarah alianza kujiweka kwa wangesi muda wote alijitahidi sana kuwa karibu yake hapo kusoma kwao kuliendelea kuwa katika hali nzuri ya upendo na heshima ilitawala katikati yao



    Wangesi hakupenda utani sana katika suala la kitu cha maana alipenda afanye kitu na kiende alivyopanga na sio kupindisha Sarah nae aliweza kumuelewa wangesi kipi anapenda na kipi hapekut

    Maisha yaliendekea na shule ilikaribia kufika ukingoni huku Sarah akijiuliza hivi wangesi jogoo anawika au hawiki?





    Sarah chumbani kwake aliwaza kwa muda sana akijiuliza kama Wangesi anasimamisha jogoo lake hakuweza kupata jibu la moja kwa moja maana wangesi alikuwa busy sana na maisha yake

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitu ambacho marafiki wa kiume walianza kumchukua kulingana na kutoungana nao katika suala la kufuatilia wasichana miezi ilienda na mwaka ulikaribia kuisha



    Mtihani wa mwisho ulifanyika wa kuhitimu ufundi wangesi alikuwa mtu wa pili kwa ufaulu mzuri wenzake wote waliokuwa wakimcheka waliangukia pua hawakuweza kufauli mtihani ule



    Sarah nae hakufanikiwa kujua ukweli kwa wangesi kama yuko sawa



    Baada ya mitihani kuisha wangesi alielekea nyumbani kwao huku akiwa na vyeti vizuri cheti cha udereva na utengenezaji magari alijisemea hapa malengo yangu yanaelekea kutimia sana maana njia hii nitahakikisha nafanya vitu vya maana .



    Wangesi alivyofika nyumbani akiendelea na kazi zake na alipokuwa akilima ilikuwa ni karibia na barabara sema tu ni barabara ambayo ilikuwa haina lami yaani yatope tu!



    Aliendekea kulima huku akiwa ameacha vyeti vyake vya udereva ndani japo akiwaza kuwa siku moja ataondoka kwenda mjini kutafuta kazi ya kufanya alianza kutafuta hela ya kutosha endapo akienda mjini asihangaike na maisha ya huko



    Wakati anaendelea kuandaa shamba muda huo ilikuja PRADO moja na muda huo mvua ilikuwa imenyesha dereva wa gari lile alishindwa kuendesha katika mazingira yale maana tope lilikuwa kubwa sana hivyo gari lilianza kurudi nyuma bahati nzuri gari lilisimama pembeni



    Dereva alishuka chini huku akiangalia tatizo ni lipi na alijua tatizo ni barabara maana kulikuwa na tope sana!



    Muda huo wangesi alimuangalia dereva wa Prado ile anavyohangaika na kutapatapa pale wangesi alitabasam na kujisemea sijui nikamsaidie yule lakini watu wa aina hii wanajiona sana hujihisi wanajua kila kitu



    Ngoja niache kwanza Wangesi aliendelea kumuangalia dereva yule mwisho alichukua upanga wake na kuelekea kwenye gari lile alipofika dereva hakuweza kumjari sana aliendelea kuwa busy na sim yake huku akitafuta msaada kutoka mjini



    Wangesi alimsalimia tena lakini dereva alimjibu kwa nyodo!



    Habari kaka alisalimia wangesi

    Fresh kwan vipi alijibu dereva

    Hapana kaka nimeona unahangaika hapa muda mrefu Mimi nilikuwa naanda shamba pale hivyo nimekuja kujua tatizo ni nini tusaidiane hat kwa mawazo

    Hata kama ukijua huwez kuwa na msaada wowote hapa kama nimeshindwa Mimi mtoto wa mjini utaweza wewe mtoto wa shamba we endelea kuandaa shamba

    Hapana kaka mawazo tu ni msaada tosha alisema wangesi

    Hebu toka kwanza huend wew unataka kuniibia alisema dereva



    Gafl sauti ya msichana ilitoka ndani ya gari lile ikilalamika majibu ya dereva wake alianza kumtetea Wangesi alisema ahaaaaaaaaaa kaka muache atusaidie bwana mbona hivo huyu ni mwenyeji wa sehemu hii huenda akawa anapafahamu vizuri embu mpe nafasi atusaidie!



    Dereva alisema na wew Monica endelea kukaa huko huku hayakuhusu Mimi niko na huyu jamaa



    Monica alisema kaka tunachelewa embu mruhusu atusaidia maana muda unaenda sana!



    Hapo dereva alimuita wangesi aliyekuwa ameshaanza kuzipiga hatua kadhaa kuelekea shambani kwake ailiita we jombaaaaaa brother nakuomba kidogo .



    Wangesi aligeuka na kusimama muda huo alirudi kwa ajili ya kumsikiliza dereva yule wangesi alifika na kuitika wito



    Dereva alianza kuomba radhi na kusema samahani kaka naomba utusaidie nisamehe kaka!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wangesi hakuweza kuongea kitu alijisemea ufundi wangu utakujibu pumbavu wew.



    Muda huo wangesi alifunua gari mbele ya bodi na alianza kutengengeneza na alikuta hitirafu kwenye betry ya gari kuna waya ulikatika hivyo aliunga kufunika tena derveva wa gari lile hakuwa na ujuzi wowote zaidi ya kuendesha tu!



    Wangesi alimaliza na aliingia ndani ili kuendesha gari lile duuuuu alipoingia alikutana na msichana nzuri sana kiasi kwamba alihisi mwili kusisimuka alijikaza na kuanza kulitoa gari mahali pale na kulipeleka sehemu nzuri



    Alifanikiwa kuliwasha na kulitoa sehemu ile muda huo Monica aliyekuwa amekaa nyuma alianza kuvutiwa na kazi nzuri ya kijana Wangesi baada ya Wangesi kuhakikisha kuwa gari liko sehemu salama alimgeukia Monica alitabasam na kusema mnaweza kuendelea na safari gari iko salama



    Monica alishukuru na dereva wake aliingia na kuanza kuendesha gari lile!

    Monica alianza kufikilia tabasam la kijana Wangesi



    Wangesi alizipiga hatua kuelekea shambani kwake!



    Muda huo Monica alizidi kufikilia tabasamu la Wangesi na alianza kuwaza atampata wapi ...ikiwezekana aweze kuongea nae lakini asingeweza kumpata maana alikuwa anapelekwa shule na huko atakaa muda mrefu sana !



    Huku wangesi aliendelea na kazi yake akiwaza kwenda mjini kutafuta kazi muda huo maana ufundi wake anaiamini na udereva wake pia siku hio ilipita alimaliza kazi zake na kurudi nyumbani kama kawaida yake hakuweza kumsimulia mtu yeyeto yaliyotokea shambani alibakia kuwaza tu uzuri wa Monica muda huo japo asingeweza kumpata



    Maana hakupatiwa namba wala yeye kuwapatia namba za simu ilifika muda akasema haitowezekana kuonana nae tena hivyo ngoja nifanye mambo yangu!



    Asubuhi mvua ilinyesha sana na muda huo mtaa wa pili kutoka kwa nyumbani kwa mzee Kamau kuna msiba ulitoke kuna binti aitwae Salome alibakwa na kufa hivyo watu walikusanyika kushuhudia tukio lile kitu ambacho kiliwasikitisha wengi na ndugu wa salome walitoa taarifa kwa ndugu na jamaa ambapo police walikuja kufanya uchunguzi na baadhi ya vijana walichukuliwa huku wengi walikimbia mazingira yale



    Muda huo Wangesi alikuwa hajui lolote kuwa police walikuja alishangaa tu anakamatwa muda huo wananchi wengi walisema huenda ni yeye maana hana mwanamke na hawajawahi kusikia kuwa mchumba wake ni yupi muda huo akichukuliwa na kupelekwa kituoni kwa ajiri ya kuchukuliwa maelezo alifikishwa na kuwekwa sehemu ya mahojiano aisee wangesi alipigwa pamoja na wenzake



    Kulingan na ukaidi alikuwa nao wangesi police walimuonea sana maana alipigwa huku alikuwa haongea chochote alijua kabisa kuwa sio yeye na hawafahamu waliofanya vile!



    Walisoteshwa kwa muda Kule police na waliweza kuhukumiwa miezi sita jera muda huo wangesi shuguli zake zilisimama na kama ujuavyo jela wangesi alionewa sana na wenzake kwa muda akiwaza kutoroka lakini akiwaza ataelekea wapi wakati alipelekwa kwa gari na hakuweza kuiona njia ya kupitia wangesi alikonda na mwili wake ulipungua sana



    Kwa muda huo aliamua kuvumilia tu maana miezi sita sio mingi japo ataharibikiwa na mambo mengi baada ya kuvumilia na hali iliyopo alianza kufanya kazi za jera akiwa na wenzake na hali ile ya ufungwa akaizoea na mwili wake ulianza kurudi



    Muda ulienda na miezi sita ilikatika watu wale waliachiwa huru baada ya kumaliza kifungo chao wangesi na wenzake waliachiwa baada ya kuonekana hawana kosa lolote



    Wangesi hakutaka kurudi nyumbani tena maana alipachukia tangu siku hio baada ya kupewa vitu vyake aliwatoroka wenzake na hawakujua ameelekea wapi waliamua kurudi zao nyumbani huku wakimuacha Wangesi mjini na dhamira ya Wangesi ulilikuwa ni kutafuta kazi ya kufanya yoyote atakayoona lazima angefanya tu!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuwatoroka wenzake Wangesi hakuwa na sehemu ya kuishi aliamua kujificha kichakani usiku huo na uaingizi ulimpitia alisinzia sana kichakani pale kulingana na maisha ya mbanano huko jera sehemu ya kulala ilikuwa mbaya sana hivyo sehemu ile alipaona ni pazuri mno



    Baada ya kusinzia kwa muda mrefu mvua ilianza kunyesha aliamka na kukimbia kuweza kutafuta sehemu ya kujibanza aliingia kibandani kwa mtu karibia na barabara na alifanikiwa kujikinga na mvua baada ya muda mvua ilikatika!



    Muda wa saa kumi na mbili asabuhi Wangesi alimshwa na fujo za kilio cha mama mmoja pembeni yake akilalamika gari lake kufeli alikuwa anaongea na Mme wake huku akitaka kulia maana alikuwa anawahi kikao cha serikali



    Baada ya dakika kadhaa wangesi alijivuta mpaka karibu na yule mama na mama yule alihisi Wangesi ni kibaka kutokana na uchafu wa nguo zake!



    Mama alijikaza na alianza kumsemesha we kijana unatafuta nini hapa..

    Mama nimesikia ukilalamika kufeli kwa gari lako nataka nikusaidie.

    Unisaidieeeeeeee???????........



    Baada ya kuambiwa anataka asaidiwe mama alimshangaa sana yule kijana maana haendani na majibu yake alikuwa amevaa nguo chafu sana bahati nzuri mama hakuwa na dharau alimuachia Uhuru wa kufanya anachokitaka



    Wangesi alizama chini kama kawaida yake hakujali tope la mvua na hakujali kama atachafuka sana mama alishangaa sana alijisemea hivi huyu kijana mbona anajilaza hivi anatoa msaada au anataka hela ya kula ..



    Wangesi aliendelea na kazi yake chini ya gari lile huku mama akiwa pembeni akiwa anaongea na fundi wake kuwa aje kumsaidia maana aliona kama wangesi hawezi kulitengeneza gari lake



    Baada ya nusu saa wangesi aliinuka na kumwambia mama ingia ujaribu kuwasha gari lako kwa sasa liko poa

    Mmmmmh!! Kijana unasema ukweli?

    Ndio mama yangu ingie uanze safari zako .

    Sawa kijana .



    Mama aliingia na kuliwasha gari lake likakubali baada ya kuwaka alishuka na kumpatia kiasi cha fedha lakini Wangesi alizikataa na kusema nashukuru mama yangu haina haja utanipatia siku nyingine!

    Mama alisema hapana kijana kwanza inaitwa nani .



    Mimi naitwa wangesi Kamau

    OK Mimi naitwa mama Rosi ni mhandisi wa maji hivyo chukua hii namba siku ukiwa na shida nitafute ukihitaji kazi niambie maana unauwezo mzuri wa kufanya kazi sawa kijana.



    Sawa mama nashukuru sana Mimi naishi hapa ukija utanikuta mama yangu

    Sawa wangesi haina shida

    Mama aliwasha gari na kuondoka huku wangesi alibakia akiwaza maana alikataa hela zile wakati hana ya kutumia lakini alijisemea haina shida bahati yangu ipo tu!



    Wangesi alika chini na kuwaza maisha yake yatakuaje kwa sababu mazingira aliyopo siyo mwenyeji sana hivyo alianza kuwaza sana mud huo!



    Mama Rose nae akielekea kwenye kikao cha wahandis wenzake alianza kuwaza kuwa nyumbani kwake hakuna mtu wa kubaki maan Rose na wadogo zake wanaishi shule pia kwa upande mwingine chakula huwa nasumbuka sana kupika ngoja nitamuambia baba rose nimchukue yule kijana



    Maana anaonekana anaweza kunisaidia na mambo mengine ya ufundi wakati mwingine huenda ni dereva mzuri nilivyomuona yule atakuwa anajua kuendesha gari!



    Wakati anawaza simu yake iliita kumbe alikuwa mme wake mama rose alinz kumuelezea jinsi alivyopew msaada na mtu asiyemjua baba Rose alisema itabid umfuate umlete nyumbani sawa huyo huenda akatusaidia kuweka mazingira sawa!



    Mama Rose alisema sawa lakini sijui kama nitaweza kumuona tena maana mazingira niloyomkuta nayo niya kimasikini sana sema nifundi magari alitengeneza yeye hili gari



    Haina shida mke wangu iko siku utakuja umuone OK

    Sawa Mme wangu



    Mama Rose aliendelea na safari yake maana ilikuwa mbali kidogo na kwake alifika na kuanza mkutano uliofanyika muda wa siku nne



    Huku wangesi aliamua kuifuata barabara ile alikopita mama Rose alikuwa anatafuta garage ili aweze kuomba kazi ya ufundi ili wamlipe hata chakula tu na sehemu ya kulala mwisho alifika sehemu ile lakini hakuweza kupata kazi maana walimdharau kulingana na mavazi Yake



    Machafu sana alijitahidi kujitetea lakini hakuna aliyekuwa akimwelewa CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wangesi baada ya kukosa kazi aliamua kukaa pembezoni kwa barabara huku akiendela kuwaza Mara alisikia fujo za mwizi wananchi wakimkimbiza kulingana na uoga wake na yeye aliamua kutimua mbio



    Baadhi ya wananchi wakaamini kuwa wangesi yuko na yule mwizi ndio maana amekimbia baadhi walianza kumkimbiza Wangesi na walimkamata huku walianza kumpiga na kutaka kumchom moto kijana Wangesi



    Bahati nzuri muda huo ulikiw muda wa chakula cha mchana wafanya kazi wengi walikuwa wanatoka maofisin na kuja kula na mama Rose alikuwa miongoni mwao alitoka na kuzitafuta hotels zilipo alipofika mbele kidogo aliona kundi la watu



    Alishuka na kwenda kutazama kuna nini baada ya kusogea alimuona wangesi akiomba msaada na ameshapigwa huku amewekewa taili za gari kwa ajili ya kuchomwa moto mama rose aliomba wamuache



    Baadhi ya watu walimuacha na wengine hawakutaka kumuacha lakini alitishia kuwaita police ndipo walimuachia Wangesi akiwa ameshaumia sana !

    Mama Rose hakusubilia alimkimbiza hospital kwanza ili apatiwe matibabu!



    Wangesi baada ya kukimbizwa hospital na mama Rose alipokelewa na madoctor walimuingiza moja kwa moja wodini na kuanza kutibiwa maana kilichomsaidia ni kujulikana kwa mama rose hospitalini pale hakuwa na haja ya kuomba kibali kutoka police maana Mama Rose ni mtu maarufu kidogo



    Wangesi alianza matibabu huku akiwa haelewi yuko sehemu gani alikuwa amezilai alikuja kupata fahamu baada ya masaa kumi na mbili ndipo aliposhangaa yeye kuwa pale alitaka kukimbia lakini doctor Sebastian alikuwa makini aliweza kumuzuia asiondoke



    Alimueleza tukio nzima na kumwambia kuna mama alikuleta hapa ukiwa hujielewi anaitwa mama Rose ni mhandisi wa maji hivyo mshukuru yeye kukuleta hapa



    Wangesi alishangaa sana mama Rose amemsaidiaje? Wakati alikuwa yuko kwenye kazi zake hakika mungu mkubwa wakati anajisemea hivo mama Rose aliingia akiwa ameshikilia mfuko wa rambo uliojaa matunda na nguo mpya kwa ajili ya wangesi



    Aliingia wodini na kumkuta wangesi amekaa kitandani mama Rose alimsalimia Wangesi alishangaa sana na kumuuliza uliniokoaje mama yangu?



    Mama Rose alisema ulikuwa unapigwa na baadhi ya wananchi baada ya wizi kutokea sehemu uliyokuwepo na walidhani kuwa na wew ni miongoni mwao kulingana na mavazi uliyokuwa umevaa hivyo nimekuletea mavazi mapya utavaa na ukipona tutaelekea kwangu sawa



    Wangesi alisema nashukuru sana mama yangu maana nyumbani kwetu sis masikini sana hivyo uwezo wa kulipia matibabu haupo watakuwa wanakulipa polepole



    Hapana kijana wangu hii ni fadhira tu maana ulinisaidia siku ile hukujali nguo zako ni safi au chafu ulilala juu ya matope na kulitengeneza gari langu hivyo kuanzia sasa tukitoka hapa tutaenda moja kwa .moja nyumbani kwangu utafanya shuguli zako ukiwa kwangu sawa



    Asante mama yangu nashukuru sana kuokoa uhai wangu sikujua kama ungeweza kunisaidia kama hivi asante sana baada ya muda doctor Sebastian alikuja na kusema mama mgonjwa wako yuko tayari anaelekea kupona hivyo unaweza kwenda nae haina shida mama yangu!



    Mama Rose alilipia matibabu na walianza kuondoka kuelekea nyumbani baada ya kumaliza kikao chake!!.



    Safari ilianza kutoka mjini na kuelekea nyumbani kwa mama Rose wangesi japo alikuwa anaumwa alimuomba mama Rose aendeshe gari lake mama Rose alishangaa sana na kusema wangesi unaweza kweli kuendesha gari?



    Wangesi alisema Mimi nifundi n dereva pia tena ninauwezo wa kuendesha magari mkubwa na madogo kama haya we niamini mama yangu



    Mama Rose aliguna na kusema sawa angalia usisababishe ajali

    Ahahahaha!! Wangesi alicheka na kusema mama siwez na kuanzia Leo Mimi nitajitolea kukupeleka kazini na kukurudisha nyumbani kama hutojali maana napenda sana kuendesha gari kuliko kazini nyingine yoyote



    Mmmmmh!! Nitaongea na Mme wangu akikubali utakuwa unanipeleka na kunirudisha au utakuwa unampeleka mwanangu shule na kumrudisha nitamtoa bordingi atakuwa anatokea nyumbani kuelekea shule .



    Haina shida mama kwani yuko kidato cha ngapi?.

    Rose yuko kidato cha tano nilimpeleka shule ya bweni baada ya kukosa dereva mwaminifu wa kumpeleka na kumrudisha shule hivyo kwa kuwa unaonekana ni mvulana mwaminifu na mpole nitakukabidhi uwe unampeleka shule na kumrudishaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wangesi alishukuru na kusema asante mama nadhani hatojuta kupelekwa shule na Mimi atakwambia tu

    Sawa wangesi



    Mama alifurahia kuendeshwa na wangesi maana alikuwa makini sana barabarani alianza kuwaza huyu atakuwa dereva mzuri atakuwa anampeleka mwanangu shule na baada ya hapo anakuja kunichukua na kunipeleka kazini kwangu



    Walifika nyumbani asubuhi sana na Mme wake alishangaa sana mke wake kuja na kijana pale nyumbani lakini mama Rose alisema huyu ndiye kijana niliyekwambia kuwa anajua kutengeneza magari na pia ni dereva mzuri sana!



    Ahaaaaaaaaaaaa!! Karibu kijana jisikie uko nyumbani nadhani nyumba yetu sasa itakuwa na furaha maana utakuwa na kazi ndogondogo tu za hapa nyumbani na nitakutafuta kazi za garage ili uwe hapo ukifanya kazi sawa kijana kwanza unaitwa nani?.



    Nashukuru mzee wangu naitwa Wangesi Kamau ni fundi magari na dereva pia mzuri tu naweza kuendesha magari mkubwa na madogo hivyo nitashukuru sana endapo nitapata sehemu ya kufanya kazi zangu!

    Usijali kijana wangu



    Walimaliza mazungumzo na kuelekea ndani duuuuuuuuuiii wangesi alishangaa sana nyumba ilivyokuwa na kila kitu ndani ukutani kuna flat screen kubwa na mziki mkubwa sana pembeni aisee hata maisha kama hakuna kufa vile ona nimeingia humu nikuwa na jasho cha ajabu limeisha uwiii !



    Wakati anashangaa Rose alikatiza pembeni yake akiwa anevaa skti fupi na hakuweza kumsalimia rose alimdharau maana alikuja kutembea ilikuwa siku ya weekend Rose alifungua friji na kuchukua kinywaji



    Alimpatia Wangesi soda ya coca cola wakati anakunya ilifurumia Rose alianza kumcheka na kusema kumbe wew mshamba wa soda eee!!.



    Wakati wangesi anajiandaa kumjibu mama rose alimuita Rose na kusema nashukuru nimekukuta hapa maana nilipanga nije shuleni kwenu kuja kukueleza kuwa unatkiwa kusoma ukiwa unatokea nyumbani



    Maana nimempata dereva wa kukupeleka na kukurudusha nyumbani wangesi huyu ndio Rose utakuwa unampeleka shule na kumrudisha nyumbani na wew Rose huyu anaitwa Wangesi tutaishi nae hapa ndio dereva wako!



    Rose alimuangalia wangesi na kusonya huku akiondoka chumbani kwake Mama Rose alisema Wangesi usijsikie vibaya huyu anahasira sana hivyo mzoee sawa



    Wangesi aliitikia hapo alionyeshwa sehemu ya kuoga na chumba chake cha kulala wangesi aliinuka na kwenda kuoga alipomaliza alienda kujilaza ili apumzike



    Rose nae alijiandaa kwenda shule kumchukua mzigo yake kwa ajili ya kutekeleza maamuzi ya wazazi wake kuwa atakuwa anasoma akitokea nyumbani.



    Baada ya muda wangesi alimaliza na kuanza kuwaza atafanyaje ili kuepuka dharau za Dada Rose? Kubwa nitajishusha na kazi itaenda gafla aliitwa kwenda kula alipotoka tu alishangaa sana kuona rose amevaa kanga moja tena laini sana



    Maana yeye ukubwa wake wote alikuwa hajawahi kuona maungo ya mwanamke kutoka na ubize wake muda wote walikaa na kuanza kula baada ya muda Rose aliinuka kwa ajili ya kwenda chumbani kuvaa ili aondoke shule



    Wangesi alishangaa kuona tena nyuma kwa Rosé pakitingishika huku makalio ya Rose yakipanda na kushuka yakisema Singida- Dodoma, singida - Dodoma......



    Wangesi aliangalia sana makalio ya Rose aliacha kutafuna kwanza chakula kilichokuwa mdomon mwake na kuanza kushangaa kwanza maumbile ya Rose aliyekuwa akitembea kuelekea chumbani kwake!



    Mama Rose alimuangalia Wangesi na kumwambia mwanangu kula ushibe maana umetoka hospital Leo tu na utapumzika wiki mbili na baada ya hapo utaanza kumpeleka Rose shule sawa



    Sawa mama nimekuelewa nitafanya hivyo baada ya dakika kadhaa Rose alitoka chumbani kwake huku akiwa amevalia sare za shule na aliaga akisema mama naendea vitu vyangu uongozi wa shule ukikubali nitakuja leo leo na ukikataa nitakuja kesho sawa mama

    Sawa mwanangu!



    Rose aliondoka zake huku mama aliachia tabasam baada ya kumwangalia mwanae akitembea kuelekea nje alijisemea mwanangu anamakusudi mmmmmh

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wangesi hakuongeza neno hapo aliinuka na kwenda kulala mchana huo huku aliwaza hivi nitamuweza huyu mwanafunzi kweli mbona kama ni shida tupu ila nitakuwa serious nadhani hatoniletea mchezo katika kazi yangu nitakuwa sitanii nae hata kidogo ngoja nianze kazi ataona..



    Rose aliwasili shule muda huo bahati nzuri alimkuta mkuu wa shule nyumbani kwake na kuanza kuongea nae alimuelezea shida yake na mahitaji ya wazazi wake mwalimu mkuu hakuwa mgumu alimruhusu Rose kuondoka nyumbani na kusema uwe unawahi shule maana tunakutegemea darasani uje uokoe darasa kwa matokeo mazuri sana sawa!



    Sawa mkuu nimekuelewa nitafanya hivyo Rose aliondoka pale na kwenda kuchukua vifaa vyake ikiwemo nguo na vitabu aliamua kuchukua usafiri na kuelekea nyumbani baada ya kuagana na marafiki zake ambao alikuwa anaishi nao bweni moja



    Ilikuwa jioni sana Rose aliwasili nyumbani na kumkuta mama yake akiwa jikoni aliingia moja kwa moja jikoni kwa mama yake na kusema mama nimerudi

    Waoooooo!! Mwanangu karibu



    Asante mama lakini mama nahisi huyu kaka ni mkorofi maana hacheki na hataki kuongea duuuuu..

    Mmmmmh Rose kumbuka amefika leo tu hivyo hajazoe mazingira isitoshe bado anaumwa siunaona alivyo na majeraha atazoea tu usijali sawa!.



    Sawa mama awe dereva mzuri nakuomba asije kunibwaga mtaloni siku moja ohoooooo bado najipenda mama yangu!

    Kijana namuamini anaweza sana tu mwanangu sema na wew uwe makini nae asije kukuharibia maisha yako sawa uwe unavaa vizuri huyu ni kaka yako mwanangu maana wew hauna kaka hivyo huyu atakuwa kaka yako.



    Mmmmmh!! Mama siwez kufanya ujinga huo unaoufikilia wew Mimi niko makini kinoma noma yani ahahahaha!! Kilikuwa ni kicheko cha mama na mtoto jikoni



    Baada ya muda chakula cha usiku kiliiva na kiliwekwa mezani wangesi aliitwa na mama Rose kwa ajili ya chakula wangesi aliinuka na kwenda kula kama kawaida alishangaa kumuona Rose mezani maana alijua atalala huko baada ya kumoana Wangesi alitabasam kwa mbali maana alipenda kumuona muda wote kusema ukweli wangesi alikuwa hajawahi kupenda wala kutamani mwanamke yeytote muda wote alikuwa seriouse na kazi zake huko kijijini



    Hivyo Rose alimdatisha Wangesi sana baada ya kumuona amevaa kanga muda huo alijikaza na alimsalimia lakini Rose aliitikia kama hataki vile kwa nyodo za hali ya huu kama mnavyojua watoto wa kishua yaani kwao maisha safi!



    Walikula chakula na baada ya chakula Baba Rose alisema kijana huyu ndie mwanangu anaitwa Rose Mimi na mama yako tumeamua uwe unampeleka shule na kumrudisha na sio vinginevyo huyu ni mwanangu mkubwa nampenda zaidi ya unavyofikilia usije kujichangavya na kufanya mengine yaliyoko nje ya kazi nitakutoa kichwa



    Mimi ni mtu mpole na msikivu ila huwa ni mkorofi unapoingia kwenye anga zangu na wew Rose nakuamini mwanangu kuwa makini na shule ufanye kilichokupeleka kule shule na sio kuwaza mengine nimekurudisha nyumbani ukae usome na sio uwaze disco za usiku na kuwa na marafiki wa ajabu!



    Mama rose nae alisema Wangesi onesha uaminifu wako kama ulivyofanya kulala juu ya matope ukitengeneza gari langu na endapo utakaa na sisi vizuri tutakujengea nyumba na utatafuta mke uoe ukiwa hapa sherehe utaifanyia hapa!



    Wangesi aliwashikuru na kusema neno moja tu wazazi wangu nitaifanya kazi yangu vizuri msiwe na shaka na Mimi!.



    Rose alitabasam na kusema nitasoma wazazi wangu msiwaze sana;.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee alisema Mimi natoa angalizo hivyo yasitokee mengine ikiwa shida baada ya mazunguzo waliondoka kulala Wangesi alienda kuoga akiwa amevaa bukta yake mama Rose alimuona na kujisemea ngoja nikamletee taulo huyu kijana aliingia ndani na kuchukua taulo mpya na kumkabidhi alimuelekeza jinsi ya kulitumia alisema utakuwa unajifutia maji baada ya kuoga



    Ukienda kuoga usiwe unaenda umevaa bukta unavua alafu unajifunga hii unaingia kuoga wangesi alikubali na kulipokea taulo lile alienda kulala na asubuhi ilivyofika wangesi alichukua mswaki na kujfunga taulo kama alivyoelekezwa usiku na mama Rose



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog