Search This Blog

Tuesday 17 May 2022

MZOEFU - 1

 





    IMEANDIKWA NA : ELISHA MSAFIRI



    *********************************************************************************



    Chombezo : Mzoefu

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    'Grrrrrrriii! grrrrrrriiii!' Huo ulikuwa ni mlio wa simu yangu ikitimiza wajibu wake wa kuniamsha saa kumi unusu za usiku.Kabla ya kulala ilinibidi nitegeshe vyema alarm ya simu yangu kukwepa usumbufu wa kulala kisungura,kungojea muda wa kuamka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hii ilibidi niamke mapema kabisa tofauti na siku nyingine,hii ni kutokana na umuhimu wa ratiba yavsiku hiyo.

    Haraka haraka nilijiandaa na takribani dakika zisizopungua ishirini nilikuwa tayari kwa kuianza safari yangu.

    "Mamaa....mamaa.....!?" Nilitaka kuondoka lakini ghafla nikakumbuka kuwa sikuaga,nikaelekea kwenye mlango wa chumba cha wazazi ,nikaanza kuita.

    Haraka haraka haina baraka,nilijiwazia mwenyewe hasa baada ya kukumbuka umuhimu wa baraka za wazazi hasa katika safari kama hii nnayohitaji kufika salaama.

    "Mbona umeamka usiku saana!?" Mama alilalama kwa sauti ya uchovu alipokuwa anakuja kufungua mlango.

    "Mama wee mwenyewe si unapajua Ubungo palivyo mbali!sikawii kuachwa na basi!" Nilijitetea na kueleweka.

    "Haya nenda salaama mwanangu mi hata sikutoi narudi zangu kulala" Aliongea mama huku akipiga miayo na kuniongezea kiasi kidogo cha fedha.

    "Hii utakunywa soda njiani na hii utawachukulia wadogo zako zawadi!" Aliongea huku akinipa pesa hizo kwa mafungu.

    "Ahsante mama,mbaki salaama!" Niliaga haraka haraka na kuanza kuondoka.

    "Wewe!..umekumbuka kusali!?" Mama aliniuliza huku akinifwata nyuma nilipokuwa nataka kutoka mlango wa nnje.

    "Ndiooo ndiooo niliomba!" Nilijibu haraka haraka huku nikiendeleaaa kufungua mlangoo.Lakini ukweli ni kwamba sikukumbuka kufanya hivyo lakini sikutaka kumpa nafasi hiyo mama kwani nilifahamu fika ni mtu wa sala ndefu lakini nikala kiapo cha moyoni kuwa sitaianza safari bila kusali mwenyewe.



    Hadi inatimu majira ya saa kumi na mbili kamili za alfajiri, tayari nilikuwa nimeshawasili Ubungo na tayari nilikuwa ndani ya basi la NBS.Basi mahususi kabisa kwa safari za Dar es salaam,Tabora.Kama kawaida nilikuwa kwenye seat ya dirishani.Nipo tayari kughairi safari kuliko kuikosa seat hiyo,Kwani mbali na kufika nnapokwenda huwa napenda sana kuangalia manthari ya nnje, huwa navutiwa sana kuona jinsi nchi hii ilivyobarikiwa achilia mbali miti kurudi nyuma.



    Baba na mama hawakuweza kutambua ni kwa nini haswa niliishupalia na kuibebea bango safari hiyo ya Tabora.Mji tulioishi miaka minne iliyopita kabla ya baba kuhamishiwa kikazi jijini Dar es salaam.Tangu ni hitimu kidato cha nne sikuwa ni wimbo mwingine zaidi ya 'nataka kwenda Tabora'.Ingawa Shule nilihitimu mkoani Kilimanjaro.Wazazi wangu walijua ningekuwa na hamu ya kukaa na kutulia Dar kipindi hicho cha kusubiria matokeo yangu ya Kidato cha nne lakini kinyume na matarajio yao walishangazwa sana na nia yangu ya kutaka kwenda Tabora.

    "Inamaana umewakumbuka sana ndugu zako wa Tabora kuliko sisi wazazi wako?"Ilifikia kipindi mama aliniuliza maswali ya namna hiyo lakini sikuwa na majibu ya msingi zaidi ya kuendelea kuwasisitiza kuwa nataka kwenda Tabora.

    Kama ilivyo ada mtoto haombi mkate akapewa jiwe.Wazazi wangu hawakuwa na kingine cha kunipa nifurahi kwa wakati huo zaidi ya nauli ya kwenda Tabora na ndivyo walivyofanya.

    Furaha ilioje kwangu.



    Hadi kufikia majira ya saa mbili asubuhi,basi lilikuwa limeshakolea mwendo na hadi kufikia muda huo tulikuwa tumeshapita mji wa Morogoro na dereva alinifurahisha sana kwa mwendo wake kwani ulikuwa na nia ya kutufikisha mapema.Mimi binafsi huwa sipendi sana kufika ugenini usiku!.



    Baada ya basi kwenda mwendo mrefu,earphone zilizokuwa zinapiga mziki zilikuwa zimeshayachosha masikio yangu.Muda huu nilihitaji kitu tofauti.Nikawaza kuanzisha mazungumzo na abiria mwenzangu tuliyeketi seat moja lakini roho ikasita nilipokumbuka kuwa hatukusalimiana alivyokuja.Hivi nani anatakiwa kuanza kumsalimia mwenzake,yule aliyekutwa ama yule aliyemkuta? Nilijiuliza swali hilo na jibu nililolipata kwa haraka ni yule aliyekukuta.Sasa kwanini huyu binti alipokuja hakunisalimia? Hilo ni swali lingine lililonigonga kichwa na kukosa majibu! Baada ya kufikiri hayo punde nilikumbuka kuwa mbali na mp 3 niliyobeba pia nilibeba na vitabu viwili vya hadithi.Huwa napenda sana kusoma vitabu mbali na kusikiliza mziki. Kumbu kumbu hiyo ikawa furaha katika kichwa changu na kujenga tabasam katika kinywa changu.Kitendo bila kuchelewa nikasimama na kuchomoa vitabu hivyo vilivyokuwa kwenye begi langu dogo nililolitoa kwenye carrier ya basi,Baada ya kukaa na vitabu hivyo kwenye seat yangu nikaviangalia punde kabla ya kuchagua kipi cha kuanzakusoma.kimoja kilikuwa ni Riwaya ya ORODHA YA SHETANI na kingine kilikuwa ni Tamthilia ya WAHUNI WA KITAA.vyote vimeandikwa na Mtunzi mahiri katika fani hiyo,Elisha Msafiri.Baada ya kuviangalia kwa muda nikaamua nianze na Orodha ya Shetani ambayo nilikuwa nimebakiza kurasa chache kabla ya kumaliza.

    "Excuse me!" Ilikuwa ni sauti nyororo ya yule binti kigoli niliyeketi naye seat moja na nilipogeuka kumtazama alikishika kitabu cha Wahuni wa kitaa akiwa na maana anakihitaji akione.

    "Nawewe ni mpenzi wa vitabu eeenh!?" Nilimuuliza huku nikiwa nimemuachia akivute kitabu hicho toka juu ya mapaja yangu kilipokuwa.

    "Yeah napenda sana kusoma!" Alinijibu kwa sauti tamu huku akiangalia kwa umakini picha ya juu ya kitabu hicho na huo ndio ukawa mwanzo wa mazungumzo yetu.

    Tulizungumza machache tu kuhusiana na uzoefu ws safari kisha kila mmoja akaendelea na yake.

    Nilipokuwa nikiendelea kusoma nilikumbuka mfukoni nna chew gum (big g )nzuri aina ya P.K.

    "Hey karibu P.K!" Nilimwambia abiria mwenzangu tuliyeketi naye seat moja,baada ya mimi kuchukua vipande viwili na yeye nilimpa viwili vilivyobaki.

    "Wow! I like this..thanks!!"(wow! Nazipenda hizi ..ahsante!) Alinishukuru baada ya kupokea kipaketi kidogo cha P.K nilichomkabidhi.

    "Mi nazipenda sana hizu huwezi kunikosa nazo mfukoni!"

    "I think me more (nafikiri mi zaidi)aisee hunishindi kwa hilo!' Aliongea binti huyo huku akipendelea zaidi kuziunda sentensi zake kiswanglishi (Nusu kiingereza nusu kiswahili)

    "You know what!?(Unajua nini?)" Nilimuuliza binti yule swali lililovuta umakini wake.

    "What!?"(nini!?) Naye alijibu kwa haraka kuonyesha kuwa ana hamu ya kutaka kusikia kutoka kwangu na ingawa alinikazia jicho kiasi cha mimi kuona haya sikusita kuendelea na nilichokusudia.

    "Unajua sijapenda kabisa nilivyokuita hey! Yaani sijapenda kiukweli!" Nilimpa maelezo hayo makusudi kwa nia ya kutaka kujua jina lake nami nashukuru akawa muelewa katika hilo.

    "Ooooh my God(Ooooh Mungu wangu) mi naitwa Beatrice au kifupi you can call me (Unaweza kuniita) Bite!" Aliongea binti yule kwa mtindo ule ule wa kiswanglish kitu kilichonifanya nifikiri atakuwa kasomea shule za English medium ama atakuwa mpenzi wa kuangalia Tamthilia.

    "Love bite sio!?" Nilimtania naye akaangua kicheko.

    "Acha utani bwana!"

    "Nimefurahi kukufahamu Bite!"

    "Nice to meet you too but you did'nt tel me your name(Nimefurahi pia kukutana na wewe lakini hujaniambia jina lako)"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ha ha ha! Nilijua hutaniita ndomana!" Nilicheka kicheko cha kutengeneza alafu nikamtania tena!.

    "Ooh! Come on!...you can't stop joking (Ah jamani huwezi kuacha utani?)"

    "Ok mi naitwa Tom!"

    "Thomas?" Aliniuliza akizani ndo kirefu cha jina langu.

    "Nop! Only Tom!" Nilimjibu kwa kiingereza cha mbwe mbwe kwasababu ndio lugha aliyeonekana kuipenda japo sikuongea kama mzungu lakini somo hilo shuleni sikuwahi kupata f.

    "Jina lako fupi nimelipenda!"

    "Ahsante!"



    Baada ya kuzungumza hayo nilibobea tena katika kitabu changu na nilipomaliza zile kurasa chache zilizokuwa zimesalia nilimuangalia tena Bite kwa jicho la wizi na nilipoona na yeye yupo bize katika kusoma kile nilichompa sikutaka kumsemesha neno nikaamua zangu kulala.



    "Tom...Tom......wee Tommmm!?" Nikiwa katika usingizi mzito nilihisi bega langu kutikiswa na kwa mbali nilisikia sauti ya kumtoa nyoka pangoni ikiniita.

    "Asee unalala bwana yani ningeamua kukuuza hata hizo hela ningekuwa nimeshatumia zimeisha!" Bite alinitania mara tu baada ya kufumbua macho.

    "Yaani ungejua nilikuwa naota nini hata usingeniamsha!" Nilichimba mkwara kupotezea mada ya mimi kulala fofofo maana usingizi ulinikamata kweli si mchezo.

    "Kwani umeota nini!?" Aliniuliza kwa hofu Bite kuonyesha kuwa ameogopa mkwara mbuzi niliomchimba.

    "Mwenzako nimeota shafika Tabora tena nilikua nasalimiana na mtu muhimu kweli!" Nilimwambia hivyo makusudi ili kumpima kama ana wivu na mimi na kweli alikuwa nao.

    "Ulikuwa unasalimiana na nani huyo!"Aliniuliza kwa upole na mimi nikajua tayari ameshafikiria kingine.

    "Sii mkuu wa mkoa!" Nilimtania tena naye hakujibu kitu zaidi ya kunipiga kikofi cha upole begani mwangu.

    "Kwani hapa ni wapi?"Nilimuuliza huku nikichungulia dirishani kana kwamba naweza kupajua.

    "Nimesikia wanasema ni Gairo,tushuke bwana tutachelewa!"

    "Sasa sikia mi siwezagi kula njiani, naomba ukishuka uniletee azam mango kubwa pamoja na...."Niliongea huku nikitoa pesa kwenye mfuko wa nyuma wa suruali yangu lakini kabla sijamaliza akanikata kauli.

    "Ah jamani mie mwenyewe naona uvivu ndomana nimekuamsha ili twende wote!" Alilalama Bite kwa sauti iliyobanwa na pua zake kisha akanishika mkono tushuke,nikajikuta nalegeza msimamo wangu wa kutokushuka.

    Baada ya kula na kuchimba dawa,tulirejea tena kwenye gari,Ndani ya muda mfupi mimi na Bite tulikuwa tumeshajenga na kuukuza urafiki wetu kiasi cha kumfanya abiria yeyote humo ndani ya basi kuzani kuwa safari yetu ilikuwa ni moja.lakini ukweli ukabaki mioyoni mwetu.



    Ingawa karibu kila mtaa wa Tabora nilikuwa na ndugu lakini nilichagua kufikia mtaa wa Mwinyi,Mtaa niliokuwa naishi na wazazi wangu kabla ya kuhamia Dar,Mtaa ambao ndio haswaa umeibeba stendi ya mji wa Tabora,Mtaa ambao wenyeji wa hapo wanapaita mjini lakini sikuamua kufikia mtaa huu tu kwajili ya umaarufu ama umashuhuri wake,Naam,ndani ya mtaa huo kulikuwa na kitu cha ziada nilichokifuata,Kitu kilichoutesa moyo wangu kwa muda wa miaka minne,Kitu ambacho niliamini ni sehemu ya maisha yangu,kitu ambacho sikuwa na uhakika kama ntakikuta ama la!,lakini hilo halikuwa neno kwangu cha msingi ilikuwa ni mimi kufika kwanza.



    Hadi majira ya saa kumi na mbili unusu za jioni, tayari basi lilikuwa limeshatia nanga ndani ya stendi ya Tabora.

    "Alhamdulilah tumefika salama!" Niliongea huku nikijishosha kivivu.

    "Mbona hushuki sasa!?" Bite aliniuliza huku na yeye akiwa bado amekaa.

    "Nasubiri wenye haraka zao washuke kwanza afu mimi ntashuka taraaatibu kwa raha zangu nna haraka gani bwana tumeshafika!" Nilimjibu Bite kwa maneno mengi na muda wote alikuwa akinitazama kwa jicho lenye alama ya ulizo lakini mimi sikutaka kufungulia mazungumzo yoyote kwa wakati huo.

    "Tom?" Bite aliniita baada ya kuniona nipo kimya.

    "Nambie!" Niliitika huku nikimtizama usoni.

    "Unakaa mtaa gani!"

    "Yaani mimi ndio nimeshafika tayari nakaa mtaa huu huu!" Kwa kuwa alishazoea kutaniwa alijua hata hili namtania lakini nilijaribu kumuhakikishia.

    "Ok! Can i get your number!(Naweza kupata namba yako)" Aliniuliza tena Bite lakini hapa nilitaka kumruka, nilijua nikiendeleza mawasiliano na yeye huenda urafiki wetu ungevuka mipaka jambo ambalo sikupenda litokee ndani ya mji huu.

    "Oh am sorry!(oh samahani) zijazishika kwa kichwa afu simu yangu imezima chaji!" Nilimdanganya huku nikiwa napapasa mifuko yangu kana kwamba naitafuta simu.

    "Ah jamani sasa itakuwaje?" Bite akawa mpole ghafla huku akionyesha kuamini nilichomwambia.

    "Wee ntajie tu zako mi ntazishika!" Nilimpa moyo baada ya kuona amezama kwenye dimbwi la mawazo ili kuipotezea mada hiyo lakini akaonekana kunishtukia.

    "Come on Tom! Za kwako tu hujazishika zangu ndo utaweza!" Point yake hiyo ingekuwa na mashiko iwapo kweli ya kwangu ningekuwa sijaishika lakini usilolijua ni sawa na kiza kinene laiti angejua hakuna mtu mwenye kichwa chepesi kwenye kushika namba kama mimi wala asingesema.lakini alikuwa sawa kwa asilimia mia kwani alifwata nilichomwambia.

    "Ok let me do something!"(sawa acha nifanye jambo fulani) Aliiongea kwa furaha na kufungua mkoba wake kisha akachana kikaratasi kidogo kwenye notebook yake na kuandika namba zake.

    "Make sure (fanya hima) unanitafuta Tom!" Alinisisitiza alipokuwa ananikabidhi kile kikaratasi.

    Nilimjibu asijali huku kimoyo moyo nikimsifu kwa kuweza kutembea na vitu muhimu kwenye mkoba wake,ni rahisi sana kukuta lipstick kwenye mkoba wa msichana kama yeye lakini si kalamu pia ni rahisi kukuta make up lakini si notebook alionyesha kidogo alikuwa ni mtu makini.



    "Byee Tom! Tutaonana siku ingine" Aliniaga Bite baada ya kushuka kwenye basi na kupanda gari la ndugu zake waliokuwa wamekuja kumpokea stendi hapo,nami sikuongea kitu ila kumpungia mkono tu kisha baada ya kumsindikiza kwa macho hadi kuhakikisha amezamia niliitoa simu yangu mfukoni na kuiwasha ili na mimi nimtafute mwenyeji wangu



    "Ama kweli dunia haina usawa yani wee ukiwa unalia njaa kali mwenzako anatafuta kiwanja ajenge ghorofa!" Nilijikuta najiwazia peke yangu wakati natafuta namba ya bamdogo wangu kwenye simu ili aje anichukue hapo stendi.Japo nilikuwa nimeishi mjini hapo kwa miaka chungu tele,Kitendo cha kuondoka miaka minne tu kilitosha kabisa kubadisha manthari na mfumo wa maisha katika mji wa Tabora.Kulikuwa na majengo mengi mapya pamoja na maduka makubwa yaliyonichanganya kiasi cha kupoteza kumbu kumbu kabisa.Si mashariki tu na magharibi hata kusini na kaskazini sikujua ziko upande gani..

    Si mazingira pekee yaliyokuwa yamebadilika bali hata watu wengi niliowaona walikuwa ni wageni machoni mwangu.Licha ya kutaka kufika nyumbani kwa mtindo wa kuwashangaza (kuwasuprize) nilishindwa kutokana na mabadiliko niliyokutananayo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "oh karibu mwanangu!!...umekuwa mrefuu!" Hiyo ilikuwa ni sauti ya bamdogo akinishangaa kwa muda kitambo kabla ya kunikumbatia kwa furaha.

    "Enhee! habari za Dar es salaam?"

    "Nzuri tu baba tunamshukuru Mungu!" Tulizungumza mawili matatu na bamdogo huku tukitembea kuelekea nyumbani safari ambayo ilituchukua dakika tatu kabla ya kufika.

    Tulipofika nyumbani mamdogo pia alifurahi sana kuniona na watoto wao wawili wadogo walikuwa wakinirukia rukia muda wote sijui ni kwajili ya kunipenda kaka yao,ama zawadi nilizowapa.



    Baada ya kusalimiana na familia hii ya baba mdogo nilionyeshwa chumba cha kulala kisha nikaandaliwa maji ya kuoga,na kama ingekuwa ni hiyari yangu basi ningechagua nisioge hasa kutokana na hali ya hewa ya baridi niliyoikuta mji huu tofauti kabisa na ya Dar ninapotokea ila kwa kuwa ni mgeni sikuwa na budi kuwaridhisha wenyeji wangu hata kama mimi moyoni sijaridhia.

    Ukiwa mgeni bhana huna tofauti na mtumwa, nilijiwazia nilipokuwa najifunga taulo kwenda bafuni.



    Baada ya kumaliza kuoga na kupumzika kidogo.Saa iliyo kuwepo ukutani ilitoa mlio mara tatu na nilipoitazama ilisema ni saa tatu za usiku.

    Naam ilikuwa ni muda muafaka kabisa wa mamdogo kuandaa chakula.

    Kuku ni mtamu lakini ladha yake inazidi mara dufu unapoambiwa umechinjiwa wewe.Jogoo nililochinjiwa pamoja na ubwabwa wenye kutiwa nazi vilinifanya niufurahie usiku ule.

    Japo Bamdogo na mkewe walifurahia uwepo wangu ndani ya mji wao,mimi nilifurahi mara mia zaidi hasa ukizingatia shughuli iliyonileta mjini hapo.



    * * * *



    nkooh! nkoooh! nkoooh!

    Ilikuwa ni sauti ya mlango wa chumba nilicholala ukilalamika baada ya kugongwa konzi kadhaa,,na lawama zake zikafika hadi kwenye ngoma za masikio yangu na kuniamsha katika usingizi mzito niliokuwa nimelala,nilijaribu kufumbua macho lakini nikayafumba haraka kutokana na kumulikwa na nuru ya mwangaza wa jua iliyosheheni chumbani hapo.

    "Hee! pamekucha mara hii!" nilijikuta nikishangaa mwenyewe baada ya kufumbua macho kwa mara ya pili na kuangalia saa iliyokuwepo kwenye simu yangu,saa iliyoniambia imetimu saa nne asabuhi.Siku hiyo nilikuwa nimelala sana,sijui ni kwajili ya uchovu wa safari ama utamu wa godoro la kitanda kipya nilichokilalia.



    "Tom!?...Tom?" yule aliyekuwa akigonga mlango sasa alikuwa hagongi tena ila alikuwa anaita na sauti yake niliweza kuitambua mara moja alikuwa ni bamdogo.Haraka nikanyanyuka toka kitandani na kuanza kutafuta pensi ya kuvaa kwani huwa nna utamaduni wa kulala na boxer pekee,huwa sipendi bughuza ya kubanwa banwa na nguo nikiwa usingizini.



    "Haya mi natoka!..nilikuwa nataka tu kujua kama umeamka salama!" Aliongea bamdogo baada ya kuona naitika tu bila kufungua mlango na mimi ikanibidi nikubaliane nae kwani hadi muda huo sikuwa nimeipata pensi na nisingeweza kufungua mlango hali nikiwa na boxer pekee.



    Nilisikia vishindo vya bamdogo akiondoka lakini pia nilisikia mtetemo (vibration) ya simu yangu ikiingiza jumbe fupi mfulululizo,nikaamua kuachana na kibarua changu cha kutafuta pensi na kuhamia kwenye simu.

    "Aarrrrgh!"nilighazibika mwenyewe mara baada ya kukuta ni jumbe (messages) za 'kufowadiwa' nikaitupa simu kitandani na kwenda kuendelea na shughuli yangu ya awali,sinaga muda wa kusoma jumbe za kufowadiwa kabisa.



    Baada ya kuipata pensi yangu nilitoka nnje kusafisha kinywa (kupiga mswaki)

    Nikiwa katika kusafisha kinywa mbele ya macho yangu niliiona nyumba ya kina Lisa.Nyumba iliyokuwepo baada ya kupita nyumba moja kisha kuvuka barabara ndogo.

    Nilisitisha kibarua cha kusafisha kinywa na akili yangu ikanirejesha miaka kadhaa nyuma.Kipindi hicho mimi nikiwa nasoma darasa la tano kwenye shule ya msingi Isike huku Lisa akiwa anasoma darasa la nne katika shule ya Westland zote zikiwa mkoani Tabora ila zikitofautishwa na hadhi.Isike ikiwa ni saint Kayumba na Westland ikiwa ni English Medium ni katika kipindi hicho ndipo tulipohamia kwenye nyumba yetu mtaa wa Mwinyi.Na bahati pekee kwangu katika mtaa huu ilikuwa ni kuishi karibu na nyumba ya kina Lisa na nyumba zetu zilikuwa zikitenganishwa na nyumba moja tu iliyokuwa katikati lakini ujirani wetu ukabaki pale pale.Mwanzo nilikuwa na marafiki wengi katika mtaa huu,lakini kadrii Urafiki wangu na Lisa ulivyozidi kukua na kukomaa ndivyo nilivyopoteza marafiki wengine.Wengi walikuwa wakimshutumu Lisa kuwa anadharau na anajidai labda kwa kuwa alikuwa akisoma international school.Lakini sababu hizo kwangu hazikuwa na mantiki yoyote kwani tangu nimemjua Lisa hakuwahi kunidharau wala kujidai mbele yangu.Hivyo niliona kuwa sababu zao hazina maana kitu kilichosababisha wanitenge na mimi,sijui ni kwa kuona wivu ama chuki binafsi kutokana na upendo wetu mimi na Lisa.Hayo yote mimi sikujali nilijali jambo moja tu,kuwa na lisa.



    Tabia hujenga mazoea,mimi na Lisa tulijenga tabia ya kuwa pamoja kila uchwao kiasi kwamba ilifikia mahali Lisa aliposhushwa na basi lao la shule alipitia kwetu kwanza na baada ya kuniona alienda kwao tu mara moja kwajili ya kubadilisha nguo za shule kisha akarudi tena tukacheza na kushinda pamoja hadi nuru ilipolikaribisha giza na usiku kututenganisha,tuliagana kishingo upande huku kila mmoja akitamani pawahi kukucha ili kesho tuonane tena.

    Upendo wetu ulishamiri kiasi cha kuwa gumzo mtaani.Wengi waliamini hakuna kilichobaki kati yetu ambacho hatujafanya na wengine wakatuchukulia kama watoto tu.Urafiki wangu na Lisa ulikula ukashiba hivyo kuzifanya hata familia zetu kuwa rafiki pia.Mimi nilishinda na hata kula kwa kina Lisa na wazazi wangu hawakuwa na shida halikadhalika Lisa alifanya vivyo hivyo kwetu na wazazi wake hawakuwa na tabu.Ilifikia hatua hata nikae chumbani na Lisa hakuna aliyekuwa na shaka yoyote na hata nimpakatie Lisa kwenye bembea hakuna aliyehoji.Pamoja na michezo mimi na Lisa tulikuwa tukishirikiana hadi kwenye masomo.Mimi nilimfundisha hesabu na yeye akanifundisha kuumba sentensi kwa kiingereza.Hakika mimi na Lisa tulipenda sana lakini hakuna aliyewahi kumwambia mwenzake kuwa anampenda ila nafsi na vitendo vilithibitisha hilo.Ilikuwa ni rahisi sana Lisa kununa iwapo ataniona na msichana mwingine halikadhalika na mimi sikujisikia vyema nilipoona kaambatana na mvulana mwingine.Hakuna kitu kinachofanywa na wapenzi ambacho mimi na Lisa hatukuwahi fanya na ingawa tulishafanyiana hadi massage tukiwa nusu uchi hatukuwahi kudiriki kufanya ngono.Naam,hayo ndiyo yalikuwa maisha yetu ya kila siku mimi na Lisa kabla ya siku moja mimi kupokea habari mbaya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nakumbuka vizuri ilikuwa ni siku moja jioni,nikiwa bado nasubiri matokeo yangu ya mtihani wa darasa la saba ndipo siku hiyo jioni baba aliponiita na kuniambia kuwa amepata uhamisho (transfer) ya kikazi hivyo mapema siku inayofuata tungekuwa safarini kuelekea Dar es salaam.

    Ingawa habari hiyo kwangu aliileta kwa kila namna ya bakshaksha na furaha lakini kwangu ilikuwa ni sawa na kumwagiwa spirit kwenye kidonda kibichi.nilihisi uchungu usioelezeka moyoni mwangu.

    "Wewe si ndio kila likizo unaliliaga kwenda Dar mbona uko hivyo sasa!" Baba aliniuliza baada ya kuniona nimepoa kama nimemwagiwa maji ya baridi.Hakujua akili yangu yote kwa muda huo ilikuwa kwa Lisa.Wapi ningempata kama Lisa.Msichana aliyetokea kuuteka moyo wangu.

    Ingawa nilikuwa simlaumu baba kwa kuhamishwa kwake kikazi lakini nilimlaumu kwa kuchelewa kunipa taarifa hiyo hadi dakika za majeruhi,Sijui alinichukulia mimi ni mtoto sipaswi kujua ama aliwaza nini.Nikataka kumkoromea juu ya hilo lakini isingesaidia kitu hasa ukizingatia sikio halizidi kichwa,Nilielekea chumbani kwangu muda huo huku machozi yakinilenga,sikumbuki kama kabla ya siku hiyo nilishawahi kupokea habari mbaya namna hiyo.

    Hadi muda huo nilikuwa bado na uwezo wa kwenda kwao Lisa na kumuaga.Lakini nilisita kufanya hivyo,nilivuta picha jinsi ambavyo Lisa angeipokea habari hiyo kwa masikitiko tele na huzuni kuu.Nikajikuta nakosa ujasiri wa kwenda kusimama mbele ya msichana mzuri kama Lisa kisha mdomo wangu kufunguka na kutamka maneno ambayo yangemtoa chozi,naam sikupenda kumuona Lisa akihuzunika na kulia mbele yangu.

    Nikaamua nitaondoka bila kumuaga japo nilijua kuwa angeumia sana baadae akijua lakini maumivu yake yasingekuwa makubwa kama ningeenda kumwambia mimi mwenyewe.

    Kama mimi mwenyewe mwanaume nimehuzunika na kughafilika kiasi hiki vipi kuhusu yeye mtoto wa kike?



    Yale niliyoambiwa siku iliyopita na kuyachukulia kama ndoto.Hatimaye alfajiri siku iliyofuata ile ndoto ikawa kweli.

    Mapema kabla ya mapambazuko ilikuja gari kubwa na kisha kupakia vitu kadhaa huku vingine baba akiahidi kuvinunulia huko huko Dar es salaam.Zoezi la kupaki vitu halikuchukua nusu saa kutokana na uhodari wa wapakiaji.Sisi nasi tulipanda kwenye gari ndogo kisha safari ya kuelekea jijini Dar es salaam ikaanza.

    Kwa mara ya kwanza chozi lilinidondoka kwajili ya Lisa,niliposoma kibao kilichoandikwa KWAHERI TABORA.maandishi niliyoweza kuyasoma kutokana na kibao hicho kumulikwa na taa za gari.Japo paliandikwa Kwaheri Tabora na macho yangu kusoma hivyo lakini moyo wangu ulikuwa tofauti kidogo wenyewe ulisoma kwaheri Lisa.

    Nitamuona tena lini Lisa? hilo ni swali lililouchafya ubongo wangu na kunipa maumivu ya kichwa ambapo hata hedex hazikunifaa kitu.



    Hatimaye tulifika Dar salama salimini japo maumivu bado yalisalia kumtima sikuwa na budi kuikubali hali hiyo na kuzoea maisha hayo mapya bila Lisa.



    Hata pawe na shida kubwa namna gani tumaini huwa halikosekani.Ingawa nilikuwa nimetengana na Lisa,bado nilikuwa na tumaini la kumuona tena.Je nitamuona vipi? hilo lilikuwa ni swali rahisi sana.Matokeo yangu ya Darasa la saba ndio ilikuwa muhimili wangu mkuu wa kumuona tena Lisa.

    Nilikuwa nikimuomba Mungu usiku na mchana kuchaguliwa kujiunga na shule za Sekondari zilizopo palepale Tabora.Sala ambazo niliamini Mungu amezisikia na atanijibu.

    Hadi muda huo nilikuwa nimeshaweza kuwashawishi baba na mama kuwa iwapo matokeo yangetoka basi ningerudi kusoma Tabora na wao walionekana kuniekewa hasa ukizingatia kuwa mji huo kulikuwa na ndugu zetu wengi.



    Muda ukaenda na masaa yakasogea.Hatimaye ule msemo usemao kuwa Binadamu wanapanga na Mungu anapanga ukatimia kwangu.Kwani licha ya kupanga kwangu kurudi tena Tabora kwa gea ya kusoma na kujiandaa kwa hilo.Mungu hakupanga hivyo,Alipanga nikasomee Moshi.

    Naam,matokeo niliyoyasubiri kwa ghamu na hamu yanikomboe.Yakanipiga tena teke,teke lililokuwa na maumivu makuu kuliko yale ya kwanza.Ama kweli ukitegemea kwendmbele hatua mbili na usiende basi unaweza kurudi nyuma hatua kumi.ndicho kilichonikuta na safari hii sikutaka tena kuumia moyo hivyo sikujiwekea mpango wowote ule wa kuonana na Lisa.

    Ingawa mtoto akifaulu nnje ya mkoa huwa ni sifa kubwa kwa familia yake na heshima kwake pia lakini wazazi wangu walishangaa kuniona bado sina raha.Nini kinachonisibu? jibu lilibaki moyoni mwangu.



    Hatimaye muda wa kwenda shule ulifika.Na mimi nikaelekea Mkoani kilimamjaro kwajili ya masomo yangu.Mji niliouona kama gereza huku shule nikiiona kama selo halikazalika walimu sikuwatofautisha hata kidogo na askari magereza,naam vyote hivyo niliviona katika mtazamo huo kwa kuwa vilikuwa vimenitenganisha na Lisa.Kipenzi cha moyo wangu,japo alikuwa maili nyingi na upeo wa macho yangu lakini daima aliishi moyoni mwangu.

    Miaka minne ambayo ningesoma shuleni hapo kwangu ilikuwa kama miaka minne ya kifungo changu katika jela ya mapenzi jela ya kutomuona Lisa.



    Nakumbuka siku moja katika kipindi cha likizo nilipokuwa nyumbani Dar es saalam alikuja ndugu yetu mmoja toka Tabora.Ndugu huyu ndiye aliyeamsha tena hamasa ya mimi kutaka kuweka mipango upya ya kurudi Tabora.

    Katika mazungumzo yetu mafupi niliweza kumdodosa juu ya habari za Lisa naye bila hiyana hakunificha jambo,alinieleza jinsi Lisa alivyokuwa na kunawiri mara elfu.Kichwani mwangu nilijaribu kuivuta picha lakini haikuja,naam ilitakiwa tena mimi niende kwa miguu yangu mwenyewe ili nimuone Lisa kwa jicho langu mwenyewe.



    Tangu hapo nilishi nikiisubiri kwa hamu ifike tena siku ya kurudi Tabora.



    Kama ilivyo kwa siku hazigandi ndivyo ilivyo kwa masaa yanavyosogea,Hatimaye nilimaliza kifungo changu cha miaka minne mkoani Kilimanjaro na sikutaka kubaki jijini Dar es salaam sasa nilikuwa mjini Tabora.Mji wa ahadi ya moyo wangu kuwa nitarudi tena kwajili ya Lisa,kipenzi cha moyo wangu.



    "Tom!....Tom!..wee Tom?" Sauti hiyo ya Mama mdogo ndiyo iliyonitoa katika dunia ya kumbukumbu nzito zilizopita kichwani mwangu kama movie na kuniacha nimeduwaa.

    "Namalizia mamdogo nakuja!" niliongea kwa sauti isiyosikika vizuri kutokana na uwepo wa mswaki kinywani mwangu kisha nikaongeza juhudi za mkono kumalizia kibarua hicho kilichonichukua dakika chungu mzima.



    Baada ya kumaliza kusafisha kinywa nilielekea moja kwa moja hadi chumba cha chakula (dining room).Hapa nilikuta mamdogo kaandaa chai nzuri ya maziwa pamoja na chapati za kumimina,Tukaendelea kunywa chai huku mamdogo akinipigia hadithi kadha wa kadha za mji huo tangu tulipouhama.

    Nani kaondoka!,nani kaja!,nani kaolewa!,nani kaoa!,nani kafilisika!,nani katajirika,nani mzima na nani kaukwaa!,Hadithi zote hizo za uongo na kweli mamdogo alinisimulia bila kubakiza neno.Masikini,Mamdogo pamoja na kukazana kwake kunisimulia hakuna lililokuwa likiniingia kichwani,japo nilikuwa nikimsikia akiongea,sikuwa naelewa haswa anasema nini,Akili yangu haikuwa pale,nilikuwa nikimuwaza sana Lisa na kitendo cha kuiona nyumba yao nilikuwa kama vile nimejiloga mwenyewe.

    Japo nilijitahidi kumsikiliza mamdogo kwa makini,hakuna nililokuwa nikiambulia na mara nyingi nilikuwa nikiitika itika,kumaanisha kuwa arudie alichosema hali iliyomfanya abaini kuwa hatuko pamoja.

    Kadri muda ulivyozidi kwenda kuna jambo niligundua.Niligundua mamdogo ameanza kununa,labda alihisi kuwa namdharau kwa yale anayosema.Kumbe mimi masikini ya Mungu nilijitahidi kweli kuenendananaye lakini fikra zikanizidi nguvu.

    Heri nusu shari kuliko shari kamili.Ingawa mamdogo alikuwa ameshaanza kununa,sikutaka anune kamili.Na ili asinune kabisa ilikuwa ni lazima nimuonyeshe ushirikiano wa hali ya juu kwa kile anachosimulia.

    "Enhee!..hivi mzee Shaka yupo kweli!?" Hatimaye nilimuuliza swali mamdogo ambapo nilijua majibu yake yatanifanya nimsikilize kwa makini.Mzee Shaka ndiye baba yake na Lisa.Mamdogo hakushangaa hata kidogo mimi kumuulizia mzee huyo kwani alikuwa ni moja kati ya watu maarufu mtaani hapo haswa kutokana na umashuhuri wa biashara zake.Taratibu mamdogo alianza kunipa habari (Michapo) ya mzee huyo, habari zilizoniwia tamu zaidi ya sukari niliyoweka kwenye chai ya maziwa ambayo nilikuwa nikiinywa muda huo.Na mamdogo hakuweza kujua kuwa janja yangu ilikuwa ni kuanzia kwa baba kuelekea kwa mwana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mmhh hivi na yule mtoto wake wa kike yupo kweli...anaitwa nani vilee!?" Hatimaye nilifikia nilipopataka na nikamuuliza swali hilo kiujanja nikijifanya simjui Lisa jina ili kumpoteza mamdogo maboyaa.

    "Nani Lisa!?!" Mamdogo naye alinijibu kwa namna ya kuuliza na mimi nikaitika kama vile sina uhakika.Laiti angejua jina hilo lilivyonikaa kichwani wala hata asingehangaika kunijibu.

    "Ah jamani alivyokuwa rafiki yako vilee umemsahau na jina!" Hatimaye mamdogo alinishushua bila yeye mwenyewe kujua.Ama kweli duniani hamna siri hadi mamdogo aliujua urafiki wangu na Lisa! Nilijiwazia moyoni mwangu huku nikiona haya kiasi kutokana na kushushuliwa.

    "Lisa yupo,amekuwa mzuri huyoo sema siku hizi anasomea Moshi!"

    "Arrghhh!!" Nilijikuta nimeghafilika ghafla na kushindwa kujizuia,niliitandika meza ngumi kali ali manusura nimwage chai yote.Nikamwacha mamdogo katika hali ya sintofahamu na mshangao wa hali ya juu.Na bahati nzuri meza ile ilitengenezwa kwa mbao imara ya mninga la sivyo ingevunjwa kwa konde lile.

    "Khaa vipi tena!?" Hatimaye mamdogo aliniuliza kwa kifupi huku sura yake ikionyesha kuwa ana swali refu.

    "Aaah samahani mama unajua ulivyonitajia Moshi,nimekumbuka na mimi nimesahau leaving certificate (cheti cha kuhitimu) yangu shule! Yaani hata sijui itakuwaje maana baba alinisisitiza sana nisiiache!" Nilijikuta nime jitetea kwa maneno mengi ya uongo ambayo hata sikujua nimeyatoa wapi,mamdogo akaungana na mimi katika hali ya kusikitika huku akijaribu kinishauri njia za kuweza kukipata.Masikini hakujua,usilolijua litakusumbua.Mimi kwa wakati huo nilikuwa nikimuwaza Lisa tu.Yaani nimejitahidi kung'ang'ana na kulazimisha safari hii ili nije nimuone kipenzi cha moyo wangu Lisa alafu leo hii naambiwa yupo Moshi.Mji ambao nilikuwa nikiwaza usiku na mchana nitaondoka lini ili nirudi Tabora,nije nimuone mpenzi wangu.Kumbe mji huo nilioukimbia ndio uliokuwa ukimuhifadhi mpenzi wangu.Ama kwa hakika ilikuwa ni habari mbaya kwangu sikuwa na tofauti na mtu aliyeitupa almasi na kufwata kipande cha chupa kinachong'ara juani.Na laiti kama nisingeipiga meza ile kupoza hasira yangu iliyonikaba koo ghafla huenda hasira hiyo ingeniua usiku usingizini.



    Hadi kufikia muda huo si chapati laini za kumimina tu bali hata chai niliyokuwa nakunywa haikuwezs kupita tena kooni.

    "Mamdogo asante sana kwa chai!"

    "Ah jamani malizia hiyo iliyobaki bwana!"

    "Yaani mama nimeshiba kweli ntakunywa tena badae!" Nilijaribu kumshawishi mamdogo lakini hakunielewa ikabidi niimalizie ile chai iliyobaki nikiwa nimekunja sura mithili ya mtu anayekunywa pombe kali.

    "Sasa mama mie nataka niusabahi mtaa kidogo unajua siku nyingi sana nimeondoka!" Hatimaye niliaga na kukubaliwa kutoka kwa sharti la kuwahi kurudi.

    Nilitembea kwa haraka kuelekea kwa kina Lisa.Sikujali ningemkuta nani huko lakini kitu pekee nilichojali muda huo ni kupata habari kamili za Lisa,Kwani si ndicho kilichonileta mji huo!?.

    Nilipiga hatua za haraka haraka hadi nilipofikia geti na kugonga mlango.Niliugonga mlango kama mara tatu hivi kwa mkupuo kisha nikasimama pembeni kusubiri ni nani atakayekuja kunifungulia.Ingawa nilisimama imara lakini kamoyo kalidunda dunda,Ukweni si parahisi hata kidogo haswa kama hujapata uhakika.

    Nikiwa bado nawaza hiki na kile nilisikia hatua za mtu kuja hapo getini nilipo.Nikaweka sawa kola ya shati yangu kisha nikajitazama tena muonekano wangu juu mpaka chini,naam,nilikuwa vizuri na baada ya kujirizia nilikohoa kidogo kusafisha koo langu tayari kwa mazungumzo na huyo anayekuja.



    "Habari yako!?" Baada ya mlango kufunguliwa kilitokeza kichwa cha binti mmoja ambaye hakuruhusu mlango kufunguka wote.Alinisalimia na kunitzama kwa makini binti yule ambaye kwa mtazamo wangu wa haraka nilihisi atakuwa mfanyakazi wa ndani (housegirl) ama ndugu yao kutoka kijijini.

    "Safi!...Mzee nimemkuta!?" Huwa sinaga nidhamu ya uoga mbele ya watu wenye wasiwasi kama yeye.Nilijibu salam yake kwa kujiamini ni sikutaka aniulize shida yangu moja kwa moja nikamuulizia baba mwenye nyumba kama vile nilikuwa namtafuta kwa udi na uvumba lakini rohoni mwangu nilipiga dua ya kimya kimya asiwepo.

    Mungu alikuwa upande wangu na kweli mzee huyo hakuwepo.alikuwepo tu mama na nikaomba kuonana naye,bila hiyana dada yule akanikaribisha ndani.

    "Ooooh! Tom jamani umekuja lini!?" Baada ya kuingia tu ndani mama yake Lisa alinipokea kwa furaha.Ingawa alikuwa amekaa kwa mtindo wa kulala kwenye sofa alitaka kunyanyuka ili anisalimie vizuri.Nililitambua hilo nikamuwahi na kumpa mkono.

    "Shikamoo mama!" Nilimsalimu huku nikiona haya kiasi flani kwasababu alikuwa akiniangalia saana.Moyoni mwangu nilifurahi sana mama Lisa kunipokea kwa mikono miwili kwani alikuwa ameniongezea sifa (credit) toka kwa yule binti aliyenifungulia mlango nilifahamu fika kama angeniona siku nyingine hata kama ndani pasinge kuwako na mtu basi angenifungulia kwa heshima na taadhima bila kuuliza swali hata moja.



    Baada ya kusalimiana na mama Lisa (mama mkwe) Nilikaa kitako na tukaanza kupiga hadithi (story) mbili tatu.Aliniuliza maswali mengi kuhusu Shule,wazazi na habari za Dar es salaam,maswali yake yote niliyajibu vizuri na kwa ufasaha mithili ya mnadi sera anayewania jimbo asilotaka kulikosa hata kidogo.Na mara kadhaa mama mkwe wangu huyo alikuwa akinisifia kuwa nimekua na kurefuka saana.Hata mimi nilimpa hongera zake kwa kuonekana kijana kila uchwao.Sifa zangu kede kede juu yake pamoja na mazungumzo yangu ya busara yalionyesha wazi kuwa amefurahia sana uwepo wangu chini ya dari ya nyumba yake.

    Hadi maji ya matunda (juice) niliyowekewa kwenye glasi yangu inaisha na mimi maswali yangu yote kichwani yalikuwa yameisha.Kitendo cha kukaa na mama mkwe wangu huyo nusu saa tu kilitosha kujua habari zote za Lisa,halikazalika na yeye alizijua za kwangu.Hivyo hapakuwa na la ziada zaidi ya kuaga na kuondoka,japo mama mkwe alinisihi sana kuwa niendelee kusalia kwake muda huo lakini sikulegeza msimamo wangu kabisa wa kutaka kuondoka. Ingawa nilipenda kupendwa na mama mkwe wangu huyo lakini sikutaka anizoee na kitendo cha kukaa naye muda mrefu huenda kingefanya hilo kutokea.Siku zote ni muhimu kuondoka mahali wakiwa bado wana hamu na wewe hiyo husababisha wasikukinai siku nyingine wanapokuona tena na ndivyo nilivyofanya.



    * * * *



    Usiku wa siku hiyo baada ya kupata chakula cha jioni bamdogo alisema ana mazungumzo na mimi,Sikuwaza sana juu ya anachotaka kuniambia bamdogo na mamdogo pamoja na watoto walipokwenda kulala,Ilikuwa ni wasaa wa Bamdogo na mimi kufanya mazungumzo hayo.

    "Mwanangu unajua hapo nnje tuna cafe (mgahawa) nzuri sana.Sema mama yako mdogo alipopata ujauzito tukaamua tuifunge ili awe na muda mzuri wa mapumziko pamoja na kuhudhuria kliniki inavyotakiwa kwasababu yeye ndiye aliyekuwa msimamizi mkuu.Si unajua tenashughuli zangu mimi si mtu wa kutulia sehem moja,Sasa unaonaje kama tukiufungua tena ili wewe usiwe idle (huna kazi).Uwe unausimamia? Hili ni wazo langu lakini kama haupo huru wee sema tu ila nakupa muda wa kufikiri hadi kesho alafu utaniambia!"

    Bamdogo akawa ameleta mada mpya kabisa kwangu ambayo sikuitarajia kwa muda.Huwa siwazi kitu bila kushirikisha uwepo wa Lisa maishani mwangu.Haraka haraka nikawaza na kuwazua kama ntakuwa msimamizi (Menager) katika mgahawa huo si nnaweza kukosa muda wa kuenjoy (kufurhia) na Lisa kweli atakaporudi.Lakini kama pia ntakuwa na muda alafu sina pesa (mwanaume suruali) si ntakuwa sina furaha kweli,Japo mapenzi sio pesa lakini pesa ni chachu ya mapenzi na mkono mtupu siku zote haulambwi.Nilishayajaribu mapenzi na kuliona hilo.Ingawa nilikuwa nimekuja na akiba ya pesa nilizojitahidi kuzitunza toka kipindi nipo shule,lakini niliamini pesa hizo zisingetosheleza mahitaji hasa ukizingatia zingekuwa za kutoka tu bila kuingia.

    "Hayaa mi nakwenda kulala asubuhi utaniambia umefikiria nini!" Bamdogo baada ya kuona nipo kimya muda mrefu akaamua kuniaga akalale lakini hakujua mimi sikunyamaza bure,ukiona kobe kainama jua anatunga sheria na ndivyo ilivyokuwa kwangu nilikuwa nikichanganua maisha yangu ya mapenzi na kazi na hadi muda huo nilikuwa nimeshapata jibu.



    "Baba mimi nipo tayari kuanza kazi hata usiku huu ila nilikuwa nataka kujua mambo kadhaa kuhusiana na cafe (mgahawa) hiyo!" Maneno hayo toka kwangu yalimfurahisha sana Bamdogo akafuta wazo la kwenda kulala na mazungumzo yakaanza upya.

    Nilimuhoji kuhusu mambo mengi sana ikiwamo jinsi walivyokuwa wanaendesha mgahawa huo.mapato yanavyopatikana,aina ya wafanyakazi waliokuwepo,bei za bidhaa na mengineyo mengi,maswali yote bamdogo alijibu vizuri pia mimi sikumwambia nimefikiria kufanya nini kutokana na majibu yake hata hivyo bamdogo alishangaa sana jinsi nilivyokuwa nikimuuliza maswali kama vile mjasiriamali mkongwe aliyebobea katika fani hiyo.Bamdogo alinizoea kuwa mimi ni mtu mwenye story nyingi za mizaha kila wakati hakujua kuwa kuna busara kubwa na maarifa ya hali ya juu yaliyojificha ndani yangu.

    Hadi kufikia majira ya saa sitta unusu za usiku tulikuwa tumemaliza kikao chetu. Na nilienda kulala nikiwa na deni la mchanganuo mpya wa uendeshaji wa mgahawa mimi kama menager (Msimamizi) mpya.Mchanganuo ambao nilitakiwa kuuwasilisha mapema asubuhi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Usiku wa deni haukawii kucha.Hatimaye mapambazuko yakalifukuza giza na jogoo wa jirani akawika kuthitibisha pamekucha.

    Naam,ilikuwa ni siku ambayo natakakiwa kuwasilisha mchanganuo wangu kwa bamdogo.Haikuwa kazi ngumu sana kwani mchanganuo tayari ulikuwepo kichwani na nilichofanya asubuhi hiyo ni kuuhamishia tuu kwenye karatasi ili wakati wa kuuwasilisha nisije nikasahau jambo.



    Mara baada ya bamdogo naye kuamka tulielekea mbele ya nyumba ambapo ndipo ulipo mgahawa.

    "Hongera bamdogo umejitahidi kutengeneza kitu cha kisasa kabisa!" Nilimsifia bamdogo mara tu baada ya kuingia ndani ya mgahawa huo uliokuwa una manthari ya kuvutia macho!.

    "Sema kama hizi kuta tutaziwekea picha nzuri za matunda na vyakula patavutia maradufu!" Nilianza kutoa ushauri wa hapa na pale huku bamdogo akiwa kachanua tabasam kubwa kuashiria kuwa alikuwa ananielewa sana.

    Baada ya kuuona mgahawa huo nilianza kutoa mchanganuo wangu rasmi.

    "Sasa bamdogo kwanza kabisa pindi tutakapoanza kazi tunatakiwa tuachane na ule mfumo wa kwnza wa kununua vitu reja reja sasa kama ni mchele tununue gunia zima kama ni unga tununue kwa viroba halikadhalika kwenye sukari na maharage tufanye vivyo hivyo.Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunapata faida kamili sio nusu nusu ya kugawana na watu pia kuna faida kuu tatu za kufanya hivyo Kwanza kabisa gharama itapungua kwa kuwa tutakuwa tumenunua kwa bei ya jumla.Pili hatutapoteza muda kila siku kuzunguka maduka kwajili ya kununua vitu hivyo na badala yake muda huo tutautumia vizuri katika kuongeza ufanisi wa kazi na kuboresha huduma na mwisho kabisa hatutokusumbua mara kwa mara eti vitu vimeisha!" Niliendelea kutoa mchanganuo wangu kama mjasiriamali mkongwe aliyebobea katika fani hiyo na muda wote nilimuacha bamdogo mdomo wazi kwa mshangao hakuweza kujua nimetoa wapi akili hiyo ya kibiashara wakati sijawahi kuuza hata pipi.



    "Swala lingine ni upande wa wahudumu.Jikoni mtamuweka yule yule mpishi wenu aliyekuwa akipika awali lakini kwa upande wa muhudumu hiyo kazi niachie mimi!" Hapa nilipasisitiza sana kwani tayari nilikuwa namjua mtu wa kumuweka.Yule binti niliyekutana naye jana wakati natoka kwa kina Lisa na kulalamika sana kuwa maisha yamemuwia magumu kutokana na kukosa ajira.Naam huyo alikuwa ni

    Sauda mrembo wa haja niliyesoma naye shule ya msingi na akashindwa kuendelea na masomo ya sekondari baada ya kufeli mtihani wa kidato cha pili mara mbili.Huyu alikuwa na mvuto wa kipekee na asingeshindwa kukaimu nafasi hiyo.Na kama ningefanikiwa kumuweka mrembo huyo mwenye mvuto wa kipekee basi kungekuwa na mvuto na kwa wateja pia.



    "Jambo la tatu bamdogo nataka tuongeze hadhi ya mgahawa kwa kupandisha vitu bei.Chai ya maziwa haitauzwa tena shilingi mia tatu kwa kikombe ila sasa itauzwa mia tano isipokuwa tu tutaiongezea ubora yaani haitakuwa tena nusu lita ya maziwa kwa lita mbili za maji ila sasa itakuwa nusu lita ya maziwa kwa nusu lita ya maji.Chai ya rangi haitauzwa tena shilingi mia mbili kwa kikombe ila sasa itauzwa mia tatu isipokuwa tu haitakuwa chai ya maji moto na majani ila sasa itaungwa kwa hiliki,mdalasini,tangawizi na mchai chai.chapati hazitauzwa tena shilingi mia tatu ila sasa zitauzwa mia tano isipokuwa hazitasukumwa mara moja tu na kukaangwa ila sasa zitasukumwa mara mbili kwa mafuta na kuongezewa ujazo halikadhalika inabidi tuongeze vitafunwa (bites) zingine kama vile vitumbua,bagia na sambusa pia supu nayo ni muhimu kuwepo ili wateja wasiopenda chai nao wasiondoke bila kula kwenye mgahawa wetu.

    Kwenye upande wa vyakula napo sahani ya wali haitauzwa tena shilingi elfu moja na mia tano ila sasa itauzwa elfu mbili na mia tano isipokuwa tu sasa hautakuwa wali wa mchele uliochemshwa kwenye maji ila mchele utakaangwa kabla ya kuchemshwa na utachanganywa na njegere ili kuongeza ladha.sahani ya ugali nayo haitauzwa shilingi elfu moja na mia mbili ila sasa itauzwa elfu mbili ila tu sasa haitakuwa na nyama za kuchemshwa,itakuwa ni nyama za kukaanga pia pembeni ya maharage na mchicha tutaongeza kachumbari pamoja na dagaa." Niliendelea kumtajia bamdogo bidhaa zote na jinsi ambavyo tungeziongezea thamani na kuzipandisha bei.Ingawa katika ajenda zangu zote alikubaliana na mimi kwa asilimia mia lakini kwa hili la kupandisha bei alilitilia shaka kidogo.



    "Sasa mwanangu watu wengi wa hapa ni wa bahili sasa tukipandisha bei situtapoteza wateja kweli!" Bamdogo alidhihirisha mashaka yake katika swali hilo.

    "Sasa bamdogo kwanza kabisa unatakiwa ujue kuwa watu wengi wa hapa sio wateja wetu kwasababu wanakula makwao.pili hapaa tupo stand centre ya kibiashara kwahiyo kukosa wateja ni ndoto sababu watu wanashuka na kupanda kutwa mzima na mwisho siri ya mafanikio ipo katika kujaribu.Na kwa kuwa bidhaa zitaongezwa ubora mara dufu kabla ya kupandishwa bei mi sioni kama kuna tatizo hapo hasa ukizingatia watu wa kileo wanaangalia ubora na sio bei" Baada ya majibu hayo ya kumtoa wasi wasi bamdogo na kumpa moyo hakuwa na swali la ziada hivyo tukafunga mjadala na kufungua utekelezaji.



    * * * *



    Wiki chache baada ya kuanza kazi rasmi.matunda yalianza kuonekana bamdogo alifurahi sana na kuniamini mara elfu.Faida iliyokuwa ikipatikana ilikuwa ni mara saba ya ile ya awali.



    Mtoto mnyang'anye kisu mpe panga.Bamdogo alifanikiwa kuninyang'anya kisu hicho.Alininyang'anya kisu kilichoitwa mapenzi na kunipa panga ambalo ni kazi.Kazi aliyonipa iliniweka mbali na mapenzi.Na mimi kuniweka mbali na mapenzi ni kunuweka mbali na Lisa kwani ndiye msichana pekee aliyeishi moyoni mwangu kwa kipindi chote.



    Siku moja usiku nikiwa nimepumzika kwenye kitanda changu nilimuwaza Lisa.Tangu niwe bize na kazi hata muda wa kumuwaza mpenzi wangu umekuwa adimu.mara nyingi nikipanda kitandani usingizi hunipita haraka kwajili ya uchovu wa pirika za mchana.Ni siku hii ndipo nilipojaribu kuvuta kumbu kumbu ili niikumbuke ile tarehe ambayo mama yake alinitajia kuwa angerudi.Kichwni zilikuwa zikipita tarehe za vitu tofauti tofauti.Nilikumbuka tarehe ya kulipa wafanyakazi mishahara,nikakumbuka tarehe ya kulipa kodi TRA,nikakumbuka tarehe ya kununua chakula kingine.Nikajikuta nakipiga kichwa changu ngumi ya hasira kwa kugoma kuniltea tarehe hiyo.Nikalala kwa hasira huku nikijua ya kuwa mara nyingi huwa nikimuwaza sana mtu kuna jambo linatokea.



    Siku iliyofuata kwenye majira ya saa nne za asubuhi nikiwa nimechafuka kiasi kutokana na kushusha kreti za soda zilizoshushwa na gari kwa mbali niliweza kuwaona walimbwende wawili wakija na njia niliyopo.

    Kadrii walivyozidi kusogea ndivyo nilivyozidi kuwatambua,naam huyu mmoja nilikuwa nikimfahamu vizuri alikuwa ni mteja wa kila siku wa vitafunwa katika mgahawa wetu hata jina nilishawahi kumuuliza akaniambia anaitwa Trace.Ingawa niliweza kumtambua Trace lakini hata huyu mrembo mwingine aliyeongozana naye hakuwa mgeni machoni mwangu.Nilishawahi kumuona mahali ila sikumbuki ni lini na wapi.

    Nikabaki nimeduwaa kwa muda nikijaribu kulifikiria hilo nishasahau kabisa kuwa jana nilimfikiria sana Lisa na mara nyingi nikimuwaza sana mtu huwa kuna jambo linatokea.



    Trace na yule mlimbwende waliyeongozana naye wakazidi kukaribia nilipo na hatimaye wakafika na kusimama mbele yangu.Pamoja na kusimama mbele yangu bado nilitawaliwa na butwaa lile lile,sikuwa na tofauti na mtu aliyepigwa shoti ya umeme na nilikuwa nikipambana kuzirejesha fahamu zangu zilizoenda mbali.Zinduka wee bwege huyo unayemuona ni Lisa.Nilisikia akili yangu ikininon'goneza kwa mbali ghafla nikashtuka na kusikia ubaridi mkali katika mifupa yangu viungo vikalegea na mwili ukakosa nguvu.Hali ya mahaba niuwe ikanikabili,nikapepesuka lakini sikuanguka,naam nilipata muhimili,nilimkumbatia Lisa kwa nguvu sana huku nikiwa na furaha kubwa moyoni.Mwili wangu ukasharabu joto lake,Nikapata nguvu na kuwa kiumbe mpya,Nikamuachia na kumuangalia sura yake tena,naam alikuwa ni mwenyewe haswa,nikamkumbatia kwa mara nyingine tena.Yote hayo niliyafanya kama chizi.Akili haikufanya kazi yake ila iliusikiliza moyo.Nilitamani kumwambia Lisa jambo lakini mdomo ukawa mzito,ulijaa mate nikajikuta tu nimemuuliza swali moja hadi anaondoka.Nilimuuliza umekuja lini naye akajibu jana usiku.Ingawa moyoni yalikuwepo mengi ya kusema mdomo ulinyamaza kimya kama vile ulikuwa haujui chochote.

    Lisa na Trace wslipoondoka niliwasindikiza kwa macho hadi wakazamia.Hata vitafunwa Trace alivyobeba sikujua alivinunua muda gani.



    Amaa kweli maji ukiyakamia huyanywi na siku ukitembea uchi ndiyo unakutana na mkweo.Sikuamini kama nimeshindwa kufurukuta kwa Lisa na neno lolote la kimapenzi hadi ameondoka yaani hata i miss you (nimekukumbuka) pamoja na hilo siku zote nimekuwa nikijitahidi kuwa smart (nadhifu) muda wote yaani leo nipo rough (mchafu) ndo Lisa anakuja.

    Nililalamika na moyo wangu huku nikijiangalia tena muonekano wangu usio wa kupendeza Lisa atakuwa ameuchukulia vipi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyo baada ya kuonana tu na Lisa nilikuwa nusu mzima nusu chizi.Yani nilikuwa hata sielewi elewi dunia inakwendaje.Yule Lisa niliyemjua utotoni hakuwa Lisa huyu mpya niliyemuona siku hiyo,kila kitu kwake kilikuwa kimebadilika.kile kifua chake kilichokuwa flat enzi hizo sasa kilikuwa kimepambwa kwa chuchu nzuri mbili zilizosimama vilivyo.Chuchu zilizokichoma kifua changu na kusababisha kunipoteza kabisa kwenye dunia hii ya kawaida pindi nilipomkumbatiaa.

    Hips zake nazo hazikuwa flat tena,vilichomoza vibastola vya ajabu kiasi cha kutishia amani ya vidume vilivyomtazama.Hata macho yake sasa aliweza kuyatumia vizuri.yalikuwa ya kicheza kutokana na maneno aliyoongea mdomoni.Hata zile nywele zake nilizozoea kuona akisuka mabutu au tatu kichwa,alikuwa kazichana vizuri na zilikuwa na mng'aro mweusi wa kupendeza.Ngozi yake nyeupe nayo iling'ara maradufu kuashiria kuwa sasa amejua kuoga na kutumia mafuta yanayofaa na walipokuwa wakiondoka niliweza kuona wezere lake lililotikisika kwa mfumo wa kusema bye bye.



    Sikuweza kuyaangalia mabadiliko hayo tu na kufurahi peke yake ila nilibaki na swali lililoniumiza kichwa.na swali hilo ndilo lililonifanya niione dunia imeongeza kasi ya kuzunguka.Kama Lisa ameweza kuwa na mabadiliko ya kimwili kwa kiasi kikubwa hivyo Je vipi kuhusu akili!? Je akili yake bado itakuwa kama ile ya utotoni kuwa anampenda sana Tom ama itakuwa imebadilika kulingana na muda na muonekano wake mpya.Swali hili ndilo lililonigonga sana kichwa na kuumiza akili yangu.



    Ukweli ni kwamba nilimpenda Lisa kwa dhati toka moyoni na sikutaka kumkosa hata kwa kufikiri tu.Pamoja na kujihusisha kimapenzi na wasichana wawili tofauti kipindi nikiwa shule lakini kati yao hapakuwa na hata mmoja ambaye aliufikia hata robo ya upendo wangu kwa Lisa.Mapenzi ya dhati yasikie kwa mwingine tu ila usiombe kupenda.



    Lile swala ambalo nililichukulia poa (rahisi) kwamba ntafika Tabora nitamkuta Lisa,Nampenda naye ananipenda pia afu maisha yataendelea sasa swala hilo lilianza kuingia uzito na halikuwa rahisi tena kama nilivyozani.



    Hivi itakuwaje kama nitamwambia Lisa nampenda alafu anijibu ah Tom acha bwana yale yalikuwa mambo ya utoto si ningekufa mimi kwa kushindwa kuvumilia jibu hilo.Jambo hilo sikutaka linitokee hata ndotoni hivyo nilitakiwa nitumie akili ya hali ya juu sana kumrudisha Lisa mikononi mwangu.



    Ingawa nilikuwa mtu wa story sana (porojo) mara baada ya chakula cha jioni.Lakini siku hiyo sikutaka story na mtu nilielekea chumbani mapema kukwepa kushtukiwa maana siku hiyo nilikuwa na mawazo tele na si mamdogo pekee hata bamdogo sikutaka ajue hali hiyo.



    Nilipanda kitandani na sikuwa na hata lepe la usingizi.Nilipanga na kupangua,kuwaza na kuwazua na yote hayo yalikuwa juu ya mrembo mmoja tu ,naye ni Lisa.Hivi kwanini timu hucheza match (mchezo) wa kirafiki kabla ya kucheza na timu husika na jibu nililolipata katikaswali hilo ni ili wajipime nguvu.Kwa hiyo na mimi natakiwa nijipime uwezo wangu wa kutongoza kabla sijasimama mbele ya Lisa eenh? Nilijiuliza swali hilo na nikaridhia kufanya hivyo.Ila nitamtongoza nani sasa!? Hilo lilikuwa ni swali lingine lililonigonga kichwa lakini nilitabasamu kwa furaha mara nilipokumbuka kikaratasi chenye namba za simu niliyepewa na abiria mrembo niliyeketi naye seat moja nikaamka toka kitandani haraka na kuanza kukitafuta kikaratasi cha binti yule ambacho nilikiweka kwenye mfuko wa begi.



    Mungu si Athumani! Nikakipata.Nikianza kuvipanga vya kuongea kabla ya kumpigia.Nikapanga kuifanya kazi hiyo kwa umakini na viwango ambavyo ningevitumia kwa Lisa.Huku nikiamini kwamba iwapo nitafanikiwa kukubaliwa na mrembo huyo basi hata Lisa hata kataa.Kwa hiyo nilichokuwa natafuta hapo ni Uzoefu,uzoefu ambao ningeutumia kumpata Lisa.Maswali atayonihoji Bite hata Lisa atanihoji hayo hayo kwani ulimwengu wa mapenzi si mmoja tu.Nijipa imani nilipokuwa naingiza namba za Bite kwenye simu yangu.

    Hatimaye kwa mara ya kwanza baada ya wiki kadhaa kupita nilinyanyua simu yangu kumpigia Bite,kadri simu ilivyoendelea kuita ndivyo mapigo yangu ya moyo yalivyoongeza kasi.



    Simu iliita mda mrefu kidogona hatimaye ilipokelewa.

    "Halloo" Hatimaye nikasikia sauti ya Bite iliyogubikwa na uzito wa usingizi.

    "Yes Bite manbo vipi!?"

    "Poa nani anaongea!?

    "Unaongea na Tom hapa!"

    "Wow Tom!...mambo vipi?" Baada ya kujua ni mimi alilegeza sauti kidogo na kuchangamka.

    "Poa tu ila nimekumiss sana!"

    "Aaaah jamani!...ila Tom tabia yako mbaya!...mbona hukunitafuta siku zote hizo?" Bite alitoa malalamiko yake lakini kwa sauti laini sana hali iliyonifanya nijione mkosaji.

    "Yaani ungejua yaliyonikuta ungenipa pole kwanza!"

    "Ulipatwa na nini tena?"

    "Yaani baada ya kunipa tu namba yako hata ilipopotelea sikujua,nimekuwa nikiitafuta kila siku hadi leo ndo nimeipata...yaani huwezi amini nilivyofurahi!" Nilimuhadaa Bite naye akakubali.

    "Jaamanii!...poleee enh! Sasa leo umeipata wapi!?" Hatimaye nikasikia swali nilillolitegemea lakini sikutaka kulijibu nami nikalipotezea kisiasa lakini Bite hakuweza kujua,tukaendelea na mazungumzo mengine na hatimaye nikamuingiza kwenye ile mada niliyoitaka.



    * * * *



    Siku iliyofuata asubuhi kwenye mishale ya saa tatu hivi nikiwa ndani ya mgahawa Lisa alikuja.

    Ingawa mwanzo nilikuwa na hamu sana ya kumuona lakini sasa nilikuwa namuogopa kama mtu anayenidai fedha nisizonazo.Baada ya kumuona Lisa nilishtuka sana kiasi cha hata kusahau nili chokuwa nafanya.Ama kwa hakika kama ningejua Lisa angefika mahali hapo muda huo ningeondoka na nisingemuona.



    "Karibu Lisa!..keti hapa!" Nilijitutumua kiume kumkaribisha Lisa huku nikimuwekea kiti vizuri.Ajaabu alikaa.

    "Enhee mambo vipi!?" Nilimuuliza baada ya mimi kukaa kiti kilichokuwa upande wa pili wa meza.

    "Poa tu za kuamka?" Alinijibu huku akiwa anachezea simu yake pengine kwa kuona haya kuniangalia.

    "Karibu chai sijui utakula na nini!?" Niliongea baada ya kufikiria neno lingine la kuongea na kukosa.

    "Ahsante mi nimeshakunywa nyumbani!?"

    "Sio vizuri ivyo kunywa kidogo na mimi!"

    "Hivi mtapata faida gani iwapo kila mtu akija atakula bure!" Lisa aliuliza swali lilinikera kiasi flani.

    "Aaah Lisa wewe si kila mtu maishani mwangu bali wewe ni mtu pekee sana na laiti ungelijua umuhimu wako kwangu wala usingesema hayo!" Hatimaye Lisa akanifanya nizungumze mambo ambayo sikutegemea kuyasema asubuhi hiyo.

    "Kwani nina umuhimu gani kwako!" Lisa aliniuliza swali ambalo lilinipa tumbo joto.Je nimueleze nnavyompenda!?.upande mmoja ukasema ndio na mwingine hapana nikabaki njia panda.

    "Nikikwambia kwa mdomo nahisi ntakudanganya hebu lete mkono wako usikie mwenyewe!" Niliongea huku nikiutwaa mkono wake wa kuume na kuuweka moyoni mwangu.

    "Enhee umesikia nini!?" Nilimuuliza mara baada ya kumuacha ausikie moyo kwa kitambo.

    "Nimesikia tu moyo wako ukidunda!"

    "moyo wangu si kitenesi Lisa kusema unadunda.Kuna jambo umekwambia labda hujaelewa tu!" Nilalama kwa sauti ndogo iliyotulia huku nikimuangalia Lisa kwa jicho la upole.

    "Sasa unasemaje!?" Aliniuliza kimitego nami nikaamua kuwa muwazi.

    "Nakupenda wewe tu,nakupenda wewe tu!" Nilimjibu kwa kufwata mdundo wa mapigo ya moyo.Akabaki na tabasam dogo bila kusema kitu.

    "Lisa!?" Nilimuita baada ya kuona yupo kimya tu ingawa hakuitika kwa mdomo,macho yake yaliniuliza unasemaje.

    "Nikuombe kitu?" Niliendelea baada ya macho yake kuniruhusu!

    "Yeah sema!'

    "Naomba niusikilize moyo wako!" Nilimuomba naye alifikiri kwa kitambo kabla ya kuniruhusu labda alihofia ningeshika ziwa lake hadharani.



    "Enhee umesikia unasemaje!?" Naye aliniuliza vile vile kama mimi nilivyomuuliza yeye.

    "Wako umeongea kifaransa naomba unitafsirie please (tafadhali)" Nilimjibu Lisa kisiasa naye akacheka kidogo nazani alitambua nilichotaka.nilitaka anithibitishie kwa mdomo wake mwenyewe kuwa ananipenda au la!.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Poa ntakwambia lakini sio sahivi!...ntakwambia badae!"

    "Je baadae tusipoonana!?" Nilihoji kwa huzuni huku hofu ikiwa imeshaanza kutanda moyoni mwangu,nikafikiri kuwa anaona haya kunitamkia kuwa hanipendi.

    "Naomba simu yako!?" Lisa aliniomba simu kwa namna ya kutaka kuziweka namba zake na mimi nikampitia.

    "Jina nisave (nihiifadhi) nani?.....nasave nyau sawa eenh!"

    "Aaasnh Lisa utasave vipi Nyau bhana?" Niling'aka kidogo kwa namna ya kughafilika na Nilifurahi kidogo nikaona binti mrembo kama Lisa kajishusha hadhi kiasi cha kujiita Nyau mbele yangu.Nikapata tumaini fulani.

    "Sasa kumbe nisave nani?" Lisa aliendelea kuhoji baada ya mimi kupingana vikali na jina la nyau!.



    "Save jina lolote zuri lakini lisiwe la kwako (Lisa)"

    Baada ya kusema hivyo Lisa alisave na kunirudishia simu kisha tukaagana na yeye kuondoka.

    Baadaye nilipokuja kuona jina alilolisave ndipo nilipo taharuki na kushikwa na butwaa.

    Nikajizuia mdomo kwa mkono wangu wa kushoto kuzuia kelele za furaha zisitoke na muda huo kijasho chembamba kilinitoka shauri ya mwili kuchemka kwa furaha.

    Lisa alikuwa amesave namba yake (ma luv) mpenzi wangu kwenye simu yangu.

    Furaha niliyokuwa nayo muda huo isingeweza kufikiwa hata na mtu aliyepewa dunia nzima aitawale.Ma luv!? Ingawa neno hilo lililomaanisha mpenzi halikuwa geni machoni mwangu lakini ndani ya dakika moja nilirudia kulisoma zaidi ya mara kumi.Kama muda huo angetafutwa mtu mwenye raha kuliko wote duniani basi ni mimi pekee ningepatikana.

    Inamana Lisa bado ananipenda eenh!? Niliuulizamoyo wangu kutafuta ushahidi nao ukanijibu ndio.

    Japo Lisa bado hakuwa amethibitisha kuwa ananipenda kwa mdomo wake mwenyewe lakini hakuna siku niliyomshukuru Mungu kama siku hiyo.Lisa alikuwa anamaanisha maisha kwangu hivyo kuwa naye kulimaanisha kuwa na maisha mazuri katika kipindi chote ntakachoishi kwenye hii dunia.Licha ya kumpenda kwa dhati toka uvungu wa moyo wangu Lisa alikuwa anavigezo vyote vya kuitwa msichana mrembo ambapo hata angekabiziwa taji la miss world (mrembo wa dunia) hakuna ambaye angejiuliza mara mbili kwa nini kapewa.Kwanini nisimshukuru sana Mungu kwa bahati hii ya mtende.Bahati ya kupewa kiumbe nilichotamani kuwa nacho siku zote za maisha yangu.Naam ndivyo nilivyofanya.



    'Lisa baby i really love you!..i will never hurt you...please belive me!'(Lisa mpenzi kweli nakupenda...sitakuumiza tafadhali niamini!".Ama kweli mapenzi hayafananishwi na kitu chochote kile yaani tangu nilipoingiza neno ma luv moyoni mwangu lililohifadhiwa na Lisa kwenye simu yangu hata utendaji wa ubongo wangu ulibadilika.Nilikuwa nikifikiria maneno mazuri ya kumwambia Lisa tena kwa lugha ya kiingereza.



    Siku hiyo ingawa sikuweza hata kula kwa furaha niliyokuwa nayo lakini niliweza kujizuia nisimpigie Lisa simu na ilipofika majira ya saa kumi na moja alasiri,Lisa alikuja tena mgahawani kwetu.Kitendo cha kumuona tu mapigo ya moyo yakaongeza kasi,hata moyo wangu ulitambua macho yalipomuona.Pamoja na mapigo ya moyo kwenda kasi lakini sasa nilikuwa na ujasiri.

    "Mambo vipi Lisa!?" Nilimsalimu huku nikimuangalia kwa jicho la huba.

    "Poa tu!....naingia hapo ndani kwenye maduka ya stend ila naogopa kwenda peke yangu!"

    Lisa aliongea kwa sauti ya kuvutia huku akichezea pindo la nguo yake kuashiria alikuwa akiona haya.

    "Kwani unaenda kununua nini!?"

    "Kuna kitu mama kanituma!"

    "Mmmh! Kwenda hapo stand tu ndo umependeza namna hiyo!?" Nilimpa Lisa sifa iliyoambatana na utani kidogo naye hakujibu kitu zaidi ya kucheka tu.

    "Stand ntakusindikiza ila tunaweza kuongea dakika mbili kabla hatujaenda au utamchelewesha mother (mama)!" Ingawa sikuwa nimepanga kitu chochote cha kuzungumza na Lisa lakini niliomba nafasi hiyo.

    "Tunaweza kuongea tu hata hivyo maa ( mama) akijua nilikuwa na wewe hawezi kumind (hatajali)!" Lisa aliongea kauli hiyo kirahisi bila kujua sentensi yake hiyo ilinifanya nijione shujaa zaidi ya mwanajeshi aliyeshinda vita vya Kagera.Yani mama mkwe hatojali akijua mwanae alikuwa na mimi!? nilijiuliza tena huku nikitoa viti viwili na kuvizungusha nyuma ya mgahawa sikutaka bughuza ya mtu yeyote yule nikifanya mazungumzo na mpenzi wangu.

    "Lisa unajua nataka kukueleza jinsi maisha yangu yalivyokuwa tangu nilipoondoka mji huu na kutengana na wewe!" Nilitoa muhtsari wa mada husika ambayo ningekwenda kuizungumzia na baada ya kumuona Lisa ananisikiliza kwa hamu na shauku kubwa niliianza habari yangu.

    Nilimsimulia kwa hisia na msisitizo wa hali ya juu huku nikidiriki kuongeza hata chumvi kwenye baadhi ya maelezo,hiyo yote ni katika kuziteka fikra zake na kumvutia kwangu zaidi kama ilivyo kwa muwamba ngoma huvutia kwake.Vyote nilimsimulia Lisa ila sikuthubutu hata kidogo kumwambia habari ya wale wasichana wawili niliowahi kujihusisha nao kimapenzi,Nashukuru hata yeye hakuniuliza swali hilo na hiyo ikawa pona yangu.Lisa hakuishia tu kunisikiliza na kukaa kimya bali na yeye mwisho wa mazungumzo yangu alianza kunisimulia hali ya upweke iliyomkabili baada ya mimi kuondoka.Alinisimulia kwa hisia na masikitiko makubwa na mimi nikaitumia fursa hiyo vyema kumsogelea karibu zaidi na kuanza kumpapasa mgongo wake taratibu kwa namna ya kumliwaza.Hakunizuia kufanya hivyo,Hivyo kadiri habari ilivyozidi kusimulia hali ya upweke ndivyo mkono wangu ulivyozidi kuzunguka maeneo mbalimbali ya mwili wake kumfariji.

    "Lisa you know what? (Unajua nini)" Nilimkatiza Lisa kwa swali hilo alipokuwa anaendelea kuongea.

    "What? (Nini)" Aliniuliza huku huku akinitazama kwa jicho la mahaba.

    "Sijawahi kupenda kama nilivyokupenda wewe!"

    "Sure? (Kweli?)" Aliniuliza huku akinitazama kwa jicho lile lile.

    "A hundred percent! (Asilimia mia)" Nilimjibu huku nikimaanisha nilichokisema.

    "Tom i love you than you did to me" (Tom nakupenda kuliko wewe unavyonipenda mimi)

    Lisa alitamka maneno yaliyopenya masikioni mwangu hadi kufika moyoni na kuzalisha hisia zisizoelezeka,taratibu nikashika kidevu chake na kuanza kusogeza mdomo wangu kwenye papi (lips) za midomo yake tayari kabisa kwa kupata busu la kiutu uzima.Tukiwa katika hali hiyo ya mahaba mazito huku wote tukiwa tumefumba macho kwaajili ya kitendo hicho kitakatifu ndipo tuliposhtuliwa ghafla na kukurupuka kabla hata ya kutimiza azma yetu.





    Kilichotushtua ilikuwa ni mtetemo mkali wa simu ya Lisa ambayo ilikazana kuita kwa juhudi na alipoitazama kwenye kioo alikuwa ni mama yake ndiye anayepiga.

    "Sasa ntamwambia nini!?" Lisa aliniomba ushauri na kabla sijamwambia neno lolote akawa ameipokea simu hiyo.

    "Mama nipo njiani nakuja!" Lisa aliongea haraka haraka baada ya kupokea simu hiyo kisha kabla upande wa pili hujajibu kitu akawa ameikata.

    "Sasa baby twende haraka haraka basi!" Lisa alinisisitiza mara baada ya kukata simu hiyo na kitendo cha kuitwa baby na mrembo huyo kikayeyusha donge langu lote la hasira lililokuwa limeanza kujikusanya kooni kutokana na kukosa ladha ya ulimi wa Lisa.

    Ama kweli mapenzi upofu yaani niliomba dakika mbili tu za kuongea na Mrembo wangu lakini tumekaa hadi giza limetukuta.Nilijiwazia mwenyewe nikipokuwa namsindikiza Lisa madukani.

    Kitendo cha kwenda kukaa nyuma ya mgahawa ilikuwa ni kama vile tumeingia kwenye ulimwengu wa kwetu peke yetu,kwani si kujua tu saa ngapi hata giza lilivyoingia hatukuliona.



    "Take care my love (Chukua tahadhari mpenzi wangu) kama mama atahoji kuchelewa kwako,mwambie ulienda maduka ya mbali sawa eenh!?"

    Nilimwambia Lisa tulipokuwa tunaagana baada ya kutoka kununua alichotumwa na yeye akajibu kuwa ameelewa kwa kutikisa kichwa.Nikampa busu la shavu kisha mie nikaanza safari ya kurudi nyumbani.



    Njia nzima nilikuwa nikitembea kwa madaha kwa mwendo wa kurukaruka kama mwana ndama.Nilikuwa nafikiria jinsi siku hiyo ilivyoniwia nzuri.Usiombe kupendwa na unayempenda sana, unaweza ukajifia kwa raha.



    Nilipofika mgahawani sikuwa na hamu tena ya kuendeleaa kukaa hapo.Siku hiyo niliruhusu wafanyakazi mapema nami nikaingia ndani kupumzika.



    Baada ya chakula cha jioni nikiwa chumbani kwangu kabla ya usingizi kunipitia.Nilipata wasaa wa kutafakari mawili matatu,nilifikitia nilpotoka na Lisa na maisha ya siku za usoni yatakavyokuwa.Nikabakiwa na tabasamu kubwa baada ya kuona mustakabali wa maisha yangu ya kimapenzi jinsi utakavyokuwa mzuri.Nikiwa katika hali hiyo ya tafakari,simu yangu iliita na kunigutusha katika dimbwi la mawazo na nilipoangalia kioo ni Bite ndiye aliyekuwa akipiga,Nikatahayari hasa baada ya kukumbuka kuwa nilikuwa na deni na mrembo huyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Yes Bite mambo vipi!?" Nilimsalimu mrembo huyo kwa uchangamfu mkubwa lakini sikuweza kumchangamsha.

    "Ah jamani mbona umenichunia hivyo!?" Bite badala ya kujibu salaam moja kwa moja alienda kwenye malalamiko yake.Kama ningemjibu nilikuwa bize asingefurahia jibu hilo na kama ningetoa sababu nyingine ningeonekana muongo,nikajikuta namumunya maneno na kukosa la kusema juu ya tuhuma hizo.

    "Haya bwana we endelea tu kunifanyia hivyo!"

    "Hamna sio hivyo Bite ila najua nikikwambia huwezi kunielewa !" Niliendelea kujigonga gonga mbele ya Bite huku nikikosa point za msingi za kupambana na mashtaka yake.

    "Enhee!! Jana uliniambia kuna kitu utaniambia leo

    So nimekupigia nikijue kabla sijalala!"

    Hatimaye Bite alinifikisha mahala ambapo nilikuwa sitaki kabisa kufika.Ukweli ni kwamba usiku uliopita nilitaka kumtongoza ili nipate uzoefu wa kusimama mbele ya Lisa bila kutetereka lakini kwa bahati mbaya mazingira

    Hayakuniruhusu kufanya hivyo kwa usiku wa jana hivyo nikamuacha na kiporo kuwa kuna kitu ntamwambia leo ili nipate mahali pa kuanzia lakini kwa bahati nzuri nyota ikawa imening'aria kwa siku hiyo na kumpata Lisa kirahisi tofauti kabisa na vile nilivyokuwa nikihangaika.Sikuwa na tofauti na mtu aliyebeba mapanga kwa mashoka kwenda kukata mti na matokeo yake akakuta umeangushwa na upepo.



    "Enhee!! nimekumbuka Bite nilitaka kukuomba nije kukutembelea weekend (mwisho wa wiki) hii!"

    "Kumbe hilo tu!...mi nikafikiria hata sijui unataka kuniambia nini!"

    "Ni hilo tu!"

    "Poa basi usiku mwema siku ukitaka kuja utaniambia!" Bite aliaga haraka haraka kuashiria kuwa hakutaka mazungumzo zaidi na mie,Mimi kwa upande wangu nikafurahi,kwakuwa nilikuwa nimeshampata Lisa nnayemtafuta,hakuna mwingine ambaye angeniumiza kichwa.

    Baada ya Bite kukata simu yake nilimuandikia mpenzi wangu Lisa ujumbe mfupi mzuri wa kumtakia usiku mwema huku nikimsisitiza kuwa nampenda sana naye akanijibu kwa ujumbe mzuri ulionifanya nikalala usingizi mzuri ulioambatana na ndoto za kupendeza,Tangu hapo penzi letu jipya mimi na Lisa likachipuka na kupendeza mithili ya bustani nzuri ya maua inayopata maji na mbolea yakutosha.

    Sasa Lisa alikuwa ni Tom na Tom alikuwa ni Lisa hadi siku moja jioni lilipotokea janga moja lililotishia kusambaratisha mahusiano yetu kabisa.



    * * * *



    Robby alikuwa rafiki yangu mkubwa kipindi cha utotoni,tulicheza,tuliwinda ndege na hata kuoga mtoni pamoja.Urafiki wetu ulianza kuingia mashaka pale nilipogundua kuwa Robby alikuwa akimpenda sana Lisa na mara kadhaa alishawahi kunitamkia wazi wazi kuwa ameshawahi kutembea(kushiriki ngono) na Lisa.

    Japo mimi nilipofanya uchunguzi yakinifu kwa Lisa niligundua kuwa Lisa hana na wala hakuwahi kuwa na hisia zozote za kimapenzi juu ya Robby.Kama ungemuuliza Lisa aseme jambo juu ya Robby basi angekwambia ni mtu apendaye sifa kwa kujitangazia vitu ambavyo hana wala hakuwahi kuwanavyo ama kwa lugha rahisi ni mtu muongo muongo.

    Kadiri urafiki wangu ulivyoendelea kushamiri na Lisa ndivyo urafiki wangu na Robby ulivyoendelea kuwa wa mashaka kabla ya kuisha

    Kabisa,hata kupishana bila salaam kwetu ilikuwa

    ni jambo la kawaida sana.Na hata tulipojaribu kuurudisha urafiki wetu ulikuwa ni wakinafki tu.Tulikaa pamoja kupiga soga na kucheka vicheko vya mdomoni huku kila mmoja moyoni mwake akiwa na mtazamo tofauti kabisa juu ya mwenzake naam! hayo ndiyo yalikuwa maisha yetu mimi na Robby kabla ya mimi kuondoka mji huu wa Tabora.



    Nakumbuka tangu nimerudi mjini hapa niliwahi kukutana na Robby mara moja tu na kusalimiana naye vizuri na kwa mara ya pili nilipokutana naye tena haikuwa na tena kwa amani kama mwanzo ila sasa ilikuwa ni kwa shari.



    Tangu tulipo renew(anza upya) penzi letu mimi na Lisa,kushinda pamoja kwetu ilikuwa ni jambo la kawaida sana.Yaani katika masaa kumi na mawili ya mchana tulitumia masaa matano hadi saba siku zingine kuwa pamoja.Lisa aliona raha kuwa karibu na mimi,na mie sikutaka abanduke kabisa ubavuni mwangu.Mda mwingine aliona uvivu hata kwenda kula kwao na tulikula pamoja mgahawani kama mke na mume.Hata masaa machache ambayo Lisa alikuwa mbali na mie sukuacha kumuwaza na kumpigia simu kila mara.



    Siku moja Lisa alikuja mgahawani majira ya saa tisa alasiri na kama ilivyokuwa desturi yetu nilizungusha viti nyuma na huko tulikaa hadi adhana ya saa moja jioni ilipotutenganisha.Nilimsindikiza Lisa kwao na dakika tano tu kupita tangu nilipomsindikiza mpenzi wangu nikiwa hata sijaingia ndani.

    Niliona kuna watu wanakuja nilipo,na kadri walivyozidi kusogea ndivyo taa zilizokuwa zimewashwa zilinisaidia kuwatambua watu hao.Naam! mmoja alikuwa ni Robby na aliambatana na wenzake wawili,nadhani walikuwa ni wapambe wake kwenye safari hiyo.

    Nikawa nawaangalia kwa makini huku nikiwa sina uhakika sana na ujio wao.Ingawa macho yangu ya kawaida yaliwachukulia kawaida jicho langu la tatu liliona mbali zaidi.naam! liliweza kutabiri shari juu ya watu hawa na ndivyo ilivyokuwa.



    "Tom...mbona unanichukulia dame (msichana ) wangu aisee!??" Robby alifika karibu nakuanza kutoa malalamiko yake kwa sauti iliyotetema labda kutokana na hasira za kuchukuliwa dame wake.

    "Dame!....dame gani huyo!?" Sikujibu swali lake na mimi nilimuhoji langu likiambatana na dharau kiasi na mshangao wa hali ya juu sana.Sikufikiria hata kidogo kuwa dame anayeongelewa hapo anaweza kuwa Lisa hivyo nikalisubiri jibu lake kwa hamu.



    "Si Lisa!" Robby alinijibu huku akionyesha kuwa hajiamini kwa hicho anachozungumza na majibu yake kichwani mwangu yalipiga kama radi,Kuongelea juu ya Lisa ni sawa na alikuwa ameongelea juu ya roho yangu.Nikajikuta taratibu napotea kwenye ulimwengu wa kawaida na kuzama kwenye uwanda wenye fikara nzito.mawazo kede kede yalikuwa yakikishambulia kichwa changu.Inamaana nilivyoondoka Robby alitumia muda huo vizuri kumshawishi na kumpata Lisa??,lakini kwanini Lisa amekubali kuwa mpenzi wangu hali yakuwa anajua yupo na Robby?? Hayo yalikuwa ni moja kati ya maswali sabini yaliyokigonga kichwa changu kila ilipotimu sekunde moja.



    "Si umeulizwa wewe!...jibu sasa?" Hilo lilikuwa ni

    swali la kipuuzi lililoulizwa na mmoja kati ya wapambe nuksi wawili ambao Robby aliambatana nao.Swali hilo ndilo lilinishtua toka katika dimbwi la mawazo na kunirudisha tena katika ulimwengu wa kawaida.Hasira kali ikaanza kwenda sawa na mapigo yangu ya moyo huku ikisambaa mwili mzima na kuamsha roho ya vita ambayo ilikuwa imelala kwa siku mingi.Taratibu nikaanza kukunja ngumi zangu huku kichwa kikipiga hesabu kuwa nianze na yupi ambaye ntamfanya wa mfano.Ingawa walikuwa watatu sikuhofia kati yao hata mmoja nakumbuka katika kipindi cha utoto Robby kila alipojaribu kupimana nguvu (kupigana)na mie mara zote aliangukia pua nakumbuka hata mpambe wake mmoja nishawahi kumtandika ngumi moja tu akazimia.Ingawa sasa muda ulikuwa umeshakwenda sana bado niliamini kwa asilimia mia kuwa Tom wa K.O (knock out) ni yule yule.Na ingawa nina sifa kubwa ya tabia ya upole,mtu akiingia anga zangu huwa natumia mithali moja tu.Heri lawama kuliko fedheha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikiwa katika harakati hizo za kutaka kuwafunza adabu jamaa hao nilishangaa kuona Lisa amekuja ingawa haikuwa kawaida yake kabisa kurudi akishaondoka majira ya usiku.Hali ya kukata tamaa ikaanza kunishambulia 

0 comments:

Post a Comment

Blog