Search This Blog

Tuesday, 17 May 2022

NIPE NIKUPE - 3

 







    Chombezo : Nipe Nikupe

    Sehemu Ya Tatu (3)





    “kazi ndogo kivipi si mpaka nisome sana ndio nije kuwa kama wewe,

    wakati anaongea vile kumbe shaitwani kashaingia kwenye mishipa ya damu ya yule kijana na kumwambia msikilize shekhe

    akisemacho, basi akapewa

    mashart matatu tu

    akiyafanya hayo atakuwa bonge la shekhe zaidi yake eti

    anywe pombe kisha aende kuzini baada ya hapo auwe astaghafir llwah,

    ni mazambi makubwa haya

    basi kwakuwa kijana tamaa ya kuwa kama yule kesho yake akadamkia kirabu cha pombe wengi walio muona wakastuka sana kumuona

    Othmani kunywa pombe kila mmoja akasema lake lakini ndio hivyo pombe ikamzidia akaenda chooni baada kuingia vyoo vya kiume akaingia vya kike akamkuta binti anajisaidia basi hakuremba akambaka yule binti akatoka chooni na kuwakuta kuna wateja wamekaa meza ile aliyo kaa yeye akaanzisha vurugu na kumpiga na chupa ya kichwani mmoja wao matokeo yake akauwa,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shetani akafurahi sana kwa kuweza kumteka yule mcha Mungu,

    Othman akakamatwa na kwenda kutumikia kifungo cha maisha jera cha kujifunza siku zote sheitwani anapenda kuongeza wafuasi katika kundi lake si ajabu kujigeuza baba yako mama yako au mtu yeyote yule wa karibu yako na kukupeleka mwenendo sio unampiga mkeo au kumdharau mumeo kisha mchepuko tu wa nnje basi shaitwani anaitaji mpeane taraka zinaa iongezeke tena katika karne hii wazazi

    washafanywa

    mambumbu kwa kutaja mahari nyingi kwa mabinti zao ili tu

    vijana washindwe kuowana

    matokeo yake wanabebeshana mimba,



    nikajichanganya na umati kuna mama mmoja akasema “jamani mpaka tumngojee huyo mganga saa ngapi si tumwambie hostadhi au shekhe hapa,

    “sasa huyo shekhe yuko

    wapi?"

    mimi hapa shekhe, nikajitaja mimi ndio shekhe kumbe sina lolote mzimu tu,

    “afadhali kumbe mkombozi yupo

    hapa hapa,

    ni maneno ya mzee mmoja hivi,

    bila kupoteza muda tukaongozana mpaka karibu na ile nyumba kufika tu wakaogopa kuingia



    mi nikazama na kumkuta

    Figisu akiongea na yule binti nikamwambia

    Figisu atoke nnje ila kwa ishara ya kwamba asionekane na yeyote wakati anatoka ni nikamsomea somea kwa kuzuga tu kisha nikatoka nnje na kuwaambia

    “jamani ndugu wana kijiji kwanza poreni kwa kushikwa na taharuki

    kingine binti hakufa kama mlivyo zania bali alipoteza fahamu tu

    kingine kuna mdudu anaitwa

    Nipe nikupe ndio alikuwa anamchezea

    baada kutaja jina la

    Nipe nikupe tu wana kijiji kila mmoja akaingiwa na hofu ya ajabu sana nikaendelea kusema “sasa basi kwa kuwa shekhe niko hapa naitaji kufahamu huyo

    Nipe nikupe nitampata wapi?"

    hakuna aliye weza kujibu zaidi ya kumuona mzee mmoja macho yake yakibadirika na kuwa mekundu yakiwaka moto hakuwa peke yake wapo kama sita hivi nikajuwa tu bila shaka wafuwasi wake hawa mbona patamu naanza nao kwanza hawa kisha nitamalizana nae yeye mwenyewe

    “ndugu zanguni naomba mtambuwe ya kwamba kuanzia leo shetani hana mamlaka tena katika himaya ya mwanaadamu sasa basi yeyote mwenye shida au matatizo wakati naongea gafla zikasikika kelele

    “jamani!!! motooo!!! kila mmoja akakimbilia kule kelele zilipo tokea kufika dahaa ile nyumba ninayo ishi mimi inawaka moto na juu ime izekwa nyasi basi wee nikatizama juu

    nikastuka!!!



    baada kutizama juu na kukutanisha macho yangu na kiumbe cha ajabu tena kinatisha vibaya mno nikastuka,

    maana ule moto haukuwa wa kawaida ni yeye ndio anaye utema nikacheki huku na kule na kujiuliza hivi

    Figisu yuko wapi sikuweza kumuona nika jaribu kuvuta hisia niweze kumuona

    Figisu nikaweza kusikia sauti ya kilio ikitokea kwenye ile nyumba inayo

    waka moto nikajivika kuvuli faster nikazama ndani huku wana kijiji waki jitahidi kuuzima moto kama ujuavyo vijumba vya kijijini nyingi zimejengwa kwa udongo juu zime ezekwa kwa nyasi nikajisemea nyie jisumbueni hapo hata zije faya mia moja huo moto hauto zimika baada kuingia ndani nikamkuta

    Figisu ana hangaika kutafuta sehemu ya kutokea

    kumbe huyu kiumbe aliye kuja ana uwezo mkubwa sana

    mpaka

    Figisu hakuwona mlango dahaa, basi nikazunguka kama feni yani kwa kasi ya ajabu upepo mkali ukavuma huko nnje na wingu zito kutanda vua kubwa ikaanza kushuka nikam beba

    Figisu na kutoka nae nnje nikacheki tena juu na kuona kile kiumbe kikijiandaa kusepa nikamwambia

    “Figisu baba naomba uningojee nitarudi sasa hivi,

    “mi naogopa kubaki peke yangu baba, “usiogope nitarudi sasa hivi!!!

    baada kumwambia vile nikapaa na kuanza kumfatilia kwa nyuma mwendo wake haukuwa kasi sana ila alipo gundua ya kwamba kuna kitu nyuma kinamfatilia akazidisha mbio ikawa mkimbize mkimbize tu mpaka tukajikuta tuna tokea sehemu moja hivi yenye magofu na kuwekana mtu kati

    kwa hasira alizo kuwa nazo akaunguruma khuu!!!!khaaa!!!

    nikamjibu kwa kuunguruma vile vile

    tukaanza mapambano ya kutupiana moto yani piga nikupige

    baada mtifuano ulio chukuwa dakika kama tano hivi na kujikuta tukivunja vunja magofu ya kale

    kila mmoja akabaki kuhema tu na kutoa moshi mzito puani tena mweusiii

    nikamuona akijiandaa kuja kunivamia kwa kasi nikajitegeshea kitu kinaitwa high volcano basi alipo nigusa tu akabaki kutetemeka huku akipiga kelele za maumivu chezea mimi wewe CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nikasikia sauti ya kitu kama upepo hivi ukivuma na kuja eneo lile basi nikacheki ni

    Figisu akija kwa kasi alipo fika tu akazama tumboni mwa yule kiumbe gafla akapasuka vipande vipande na kutawanyika

    Figisu akatoka huku akijipangusa nikabaki kushangaa kwa uwezo ule wa ajabu sana “duhuu Figisu umewezaje kufanya hivi?"

    akanijibu ya kwamba ni mambo madogo tu haya hatukuwa na kingine zaidi ya kuondoka eneo lile na kurudi kijijini tukakuta hali sio hali yani mambo si mambo kijiji kimechafuka nyumba zina dondoka kwa vua ile kila eneo mafuriko watu wana angaika kuamisha vitu kwenye vijumba vyao,

    Figisu akanipa ishala nifanye kuituliza vua maana haikuwa ya kawaida zaidi ya kutoka kuzimu

    nikafanya kama alivyo niambia kwa kunyoosha mkono juu vua ikasimama ikidosha manyunyu tu mwisho ikatulia kabisa nikabaki mimi na

    Figisu tukibaki kuwatizama

    tu maana dahaa

    kijiji majanga,



    tukiwa bado tunakodoa macho tusijuwe cha kufanya nikaweza kuiyona gari aina ya Jeep ikija pande zile baada kufika ikasimama akashuka baba na vijana kama wanne hivi wote wakiwa ndani ya combati za kijeshi na kuangaza angaza macho tu

    “hivi hii vua imenyesha huku tu kiwawa mbona kule kivinje na mavuji juwa linawaka kali tu?"

    ni maneno ya baba akiuliza hivyo basi kuna dada mmoja akamjibu ya kwamba

    “hata sisi wenyewe tuna shangaa hiki kijiji kimejaa mauza uza tu

    yani tunaabudu mizimu kwetu ndio kila kitu!!!

    “ilo ndio tatizo kubwa baada ya kumtegemea Mwenyezi Mungu nyie mna abudu mizimu pumbavu zenu!!!

    baada baba kusema vile wakapanda kwenye gari na kuondoka zao

    Figisu akaniambia hivi

    “baba hakika ya shetani ana nguvu sana basi siku moja katika pita pita zangu kule mjini nikatokea sehemu moja kuna kanisa kubwa

    sema ilikuwa usiku sana nikaweza kusikia mazungumzo kati ya shetani na mchungaji akipewa mashart ya kwamba afanye kila namna namna,

    mambo yao yaende sawa yule shetani akatamka



    “kwa hiyo nataka kusema kuwa, kuanzia sasa lazima tukaze nguvu zetu ili kuzidisha uasi katika hii dunia naitaji uikamilishe hii kazi haraka iwezekanavyo kusema kweli sauti yake ilikuwa ni kali sana yenye kutisha basi yule mchungaji akaitikia, sawa?”

    “Sawa,” kumbe hakuwa mmoja nikajaribu kuchungulia na kuuwona umati mkubwa tu wote wakiwa ndani ya vazi la kaniki nyeusi kichwani wamejifunga vitambaa vya rangi nyekundu huku mkuu wao akiwa amekaa madhabuni akaendelea kusema ya kwamba, “wote.

    nataka kuona dunia inachafuka.”“Sawa.”

    “nataka kuona binadamu wanaishi kwa wasiwasi, sawa?”

    “Sawa.”

    “nataka kuona watu hawafanikiwi katika maisha yao,sawa?”

    “Sawa.”

    “pia, nataka kuona binadamu wanatutegemea sisi kwa kila jambo. Ikitokea tatizo kidogo waende kwa waganga, sawa?”

    “Sawa.”

    hilo wote itabidi mlisimamie kikamilifu ili mambo yaende tunavyopanga. kwani majira yaliyotajwa yamekaribia sana.”binafsi nilijiuliza mengi sana pasipo kupata jibu ni majira gani hayo yaliyo tajwa na nikitu gani

    wanacho kikosa wanaadamu hawa mpaka wanaamua kumtumikia shetani huku wakijivika ngozi ya utumishi wa Mungu ole wao wafike kuzimu

    ndio watajuta na kutamani walau wapewe sec moja tu ya kurudi duniani na kutubu dhambi zao

    baada

    Figisu kusema vile akanyamaza, nikamuuliza hivi

    Figisu ni njia gani uliyo tumia kumpasua yule jamaa?"

    “vipi kwani unataka nikuonyeshe?"

    nikamjibu ndio,"

    basi akaenda mbaali kidogo kisha akajistua na kuja kwa speed akazama tumboni mwangu nikahisi anazichezea bandama zangu mara figo

    maumivu makali yaka nishika nikajikuta namwita “Figisu!!!figisu!!!

    toka bana!!! maumivu yakanizidia na kujikuta nikipoteza fahamu,



    nikaja kuzinduka na kujikuta nipo kitandani nikaitaji kujinyanyua lakini nikashindwa maana nilikuwa mzito sana dahaa nikajiuliza kwani nina nini mie mpaka siwezi kunyanyuka kitandani

    Figisu nae yuko wapi?"

    “naona umerudiwa na fahamu mtukutu ehee!!!

    nikamtizama aliye niambia vile ni bibi akaiwa kam beba paka mweusi akaja mpaka pale kitandani na kuniambia ya kwamba CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    muda mwingine acha michezo ya kipumbavu sasa basi umeweza kumuuwa mwanao mwenyewe,

    nikastuka na kuuliza “bibi what?

    “hakuna cha nati wala chapati ninacho taka kukwambia ni hivi

    Figisu hatunae tena duniani,

    “bibi unasema?"

    “sikia nikwambie mjukuu wangu Hafidhi wakati mnacheza pale mpaka

    Figisu kuingia mwilini kwako ni kwamba alishindwa kutoka kwa sababu seri ya mwili wako wewe ni tofauti

    na kiumbe chochote kile sasa basi hakuona njia matokeo yake akakosa pumzi na kupoteza maisha

    na mpaka mwili wake upo tumboni mwako kwahiyo unacho takiwa kufanya kwa sasa ni kummeza huyu paka aende kuutoa mwili wa marehemu sikuwa na jinsi zaidi ya kufanya hivyo huku mchozi ukinitoka baada ya mwili wa

    Figisu kutolewa dahaa akiwa kaungua vibaya sana



    Baada mwili wa marehemu

    Figisu kutolewa ndani ya mwili wangu ukiwa ume unguwa vibaya sana mpaka hautamaniki kwa mjeraha aliyo yapata

    nilikumbuka mengi sana tuliyo yapitia mimi na

    Figisu kwenye huzuni na furaha leo hii kwa sababu ya uzembe wangu tu nimemuuwa nikamuuliza bibi

    “hivi bibi huwezi kumrudisha tena

    Figisu duniani?" akanijibu ya kwamba

    “kwa hilo haito wezekana hata kidogo cha umuhimu ujiandae kwa kazi iliyo mbele yako mwanao kashafariki basi,"

    “bibi kwa nini unasema Figisu ni mwanangu?"

    “khaa! kumbe ulikuwa ufahamu ya kwamba huyu Figisu ni mwanao wa kumzaa kabisa

    basi nikwambie ile siku uliyo fanya mapenzi na wale wasichana wa kibinaadamu ndio siku uliyo wabebesha mimba bila wao kujuwa ila taarifa zikafika kuzimu ya kwamba kuna ujio mpya kutoka duniani

    siku ya siku ikafika kwa wale mabinti kujifungua kila mmoja kwa wakati wake

    akatokwa na damu ya hedhi mibonde mibonde ya damu mpaka mzazi wake akahofia kwa kuona binti yake yupo kwenye majanga ya kupoteza maisha wakati mganga hajafika sisi tukatuma kikundi chetu na kwenda kuwachukuwa watoto wale wakiwa mia mbili kamili,

    nikabaki kuduwaa tu na kujiuliza inakuwaje nipate watoto mia mbili kwa mabinti wawili

    Bibi akaendelea kusema najuwa unashangaa na kujiuliza umepataje wato mia mbili basi ni

    hivi kwa kawaida binaadamu akizaa mtoto mmoja jini au mzimu anazaa watoto mia moja na akifa mtoto mmoja wa kibinaadamu huku wanakufa watoto mia moja wa kijini habari ndio hiyo,



    “kwa hiyo bibi watoto wangu mia moja tayari washakufa au?"

    “hapana hawajafa aliye kufa ni huyu

    Figisu tu basi kingine ninacho itaji kukwambia jitahidi kupambana uitete dunia pamoja na wana damu maana shetani anaitaji kuikamilisha nuru yake kwa kuuteka ulimwengu pambana

    maana dunia kwa sasa imejaa imani za kishilikina si kwa wazee vijana wala watoto wote wanapotea

    vitu kama hivi vipo sana katika miji iliyo jazana watu

    maana

    wachawi wanaamini ya kwamba, katika sayari hii kuonekana kwa

    vitu visivyoonekana pia vilikuwa

    na siku sita mawazo yao katika uumbaji wa Mwenyezi

    Mungu, siku ya saba kwa ujinga wao wanazani heti

    akapumzika. na hiyo ndiyo sera

    ya mchawi mara tu baada ya

    kujiunga katika kazi hiyo iliyo laaniwa mpaka siku ya kufa kwake binaadamu

    wengi katika

    ulimwenguni kote.

    Kabla sijaondoka maana kuzimu wana ungojea mwili wa marehemu Figisu

    nataka kusema kuwa, kama

    kuna shughuli mbalimbali za

    binadamu zinazoonekana kwa

    macho ya kawaida duniani, pia

    kuna shughuli kama hizo hizo

    zisizoonekana kwa macho ya kibinaamu ya

    kawaida, lakini zinashirikisha

    wachawi na na mizimu mashetani yani viumbe vibaya vibaya mambo yao.

    Wachawi wana kila kitu, wana

    mikutano ya nchi, mikutano ya

    kimataifa, ya kanda ya mabara

    na pia wana mabenki,

    japokuwa kwa macho

    tunazungumzia mabenki ya

    pesa, wao wana mabenki yaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    damu, nyama yani ukipata bahati ya kuingia kwenye hizo bank zao mwili uta kusisimka kwa uwoga wa ajabu maana kunatisha

    kienyeji.dawa za kienyeji pia

    huwa wanakopeshana,

    wanalipana na wapo wasiotaka

    kulipa ambapo huchukuliwa

    adhabu mbalimbali kulingana

    na makosa. zipo nchi ambazo

    wachawi wake wanafukuzwa

    katika uanachama, zipo

    zinazoingizwa, wapo wakuu wa

    wachawi wa nchi

    wanaopinduliwa wengine hata

    kuuawa na pia kunakuwa na

    uchaguzi mkuu kila baada ya

    miaka mitano kuchagua

    viongozi wa kichawi wa nchi

    husika ambapo wapiga kura

    huandikisha majina yao na

    kuwa na vitambulisho vya

    kupigia kura.

    pia kuna wana bendera zao pia

    wachawi barani Afrika, Ulaya na

    duniani kote. Aidha, kila nchi ina

    bendera yake inayoonesha

    utambulisho wa kitaifa. mfano,

    bendera ya kichawi ya kilwa

    ni rangi nyekundu, nyeusi na

    kahawia, katikati ina picha ya

    mnyama Nipe nikupe ndio mfalme wao

    nchi ya nigeria, bendera yake ya

    kichawi ina rangi nyekundu bila

    mchanganyiko, katikati ina

    picha ya mkono mweusi

    umeshika kibuyu chenye

    shanga.

    kuna wachawi wanaofanya

    biashara za kimataifa, mfano

    kutoa dawa za kienyeji

    kilwa kupeleka dodoma kwa

    njia za kichawi na kule mchawi

    anaweza kununua ngozi za

    wanyama akaja kuuza kilwa au

    kenya au uganda kwa wachawi

    wengine ambao hawana mitaji

    mikubwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    naona muda una yoyoma nikwambie cha mwisho tu



    ni kwamba bila shaka umewaona wazazi wako wakija hapa leo na ujio wao unajuwa nini lengo lao ninacho weza kukwambia ni kwamba

    Nipe nikupe leo usiku huu ataenda kufukuwa kaburi na kuondoka na mwili wa mdogo wako sasa basi ni wakati wako wa kupambana na kwenda kulilinda lile kaburi usiku huu

    maana ule mwili ukitolewa kuna uwezekano mkubwa wa mdogo wako kurudi tena duniani fanya hivyo,"

    baada bibi kusema vile akapotea na kuniacha mimi na yule paka mweusi

    kama mkaa mimacho inang'aa hiyo nikainua mdomo na kumuuliza “sasa wewe unangojea nini hapa si usepe tu,"

    si akanijibu eti “mi siwezi kuondoka hapa nimeambiwa niwe mlinzi ndani ya nyumba hii,

    nikacheka sana ha!ha!h!h!

    yani wewe ulinde humu ndani kwanza unaitwa nani?"

    “naitwa Ningu!!!

    “oky Ningu je unaweza kunionyeshea mauwezo yako hata kidogo?"

    “ndio naweza boss!

    “haya anza kitendo bila kuchelewa akaanza kujibadirisha kila aina ya kiumbe hadi kunguni nikabaki kukodoa macho na kuogopa pale alipo jivika taswira ya

    Nipe nikupe maana nikawa narudi nyuma huku nikijiandaa kumtupia kombora nae kwa uboya wake akaanza kunitisha eti “wee kijana unaitaji kupambana nami sasa nakuonya ile nataka kunyoosha mkono tu akawa

    Figisu masikini mchozi ukanitoka huku akinipungia mkono mwisho akajirudi na kuwa paka vile vile na kuniambia boss

    Hafidhi j ikram time ishafika panda mgongoni twenzetu vitani kwanza nikasita kupanda ila nilipo kumbuka mauwezo yake ya kujibadilisha nikajikuta napanda basi

    Ningu akawa mkuubwa aina ya farasi mwenye mbawa na kupaa juu kupitia paa ya nyumba tukatoka nnje

    akasema hii leo ndio mwisho wa Nipe nikupe kaka nikaangaza angaza macho na kuweza kupaona makaburini kukiwa na viumbe vikiranda randa

    Ningu kama dragon vile akawasha moto kwa kuwatemea viumbe wale nami nikachumpa kutoka juu ya mgongo wa Ningu na kutuwa chini kitendo cha kutua tu upepo mkali ukavuma na miti kutingishika,,



    Baada kutua chini basi upepo mkali ukavuma na miti kutingishika maana nilikuwa tayali nisha badirika na kuwa kiumbe mwingine kabisa yani kama mmbwa mwitu vile viumbe tulivyo vikuta pale makaburini vikawa viki jihami kwa kujaribu kutupa makombola yao

    yakawa yakinigusa tu yana dunda na kuwarudia wao wenyewe na kujikuta waki tapatapa na kupiga mayowe ya maumivu tu

    Ningu nae hakuwa nyuma katika kutoa mashambulizi yake

    maana alikuwa hatari sana

    kwa kuvi chakaza vile viumbe nikajisemea “ehee hapa nime pata jembe,

    yapata takribani masaa mawili hivi tukiwa katika vita kali na wale viumbe wa kila aina maana akifa mmoja wana tokea wawili au wanne sasa ikawa kazi sio kuwa punguza bali kuwa ongeza tu miti inawaka moto katika uwanja wa machafuko usiku ule kumbuka ilikuwa ni vita ya mizimu tu,

    nikaja na hii na kutupa kombora sokomeza yani kama tsunami hivi

    Ningu nikamuomba asepe faster naitaji kuachia kitu basi kitendo bila kuchelewa nika liachia mtikisiko mkubwa sana ukatokea huku vile viumbe vikirushwa huku na kule

    baada dhuruba ile kutulia

    na hali kuwa shwar ndipo

    Ningu akarudi eneo lile huku aki kodoa kodoa macho tu asiamini kwa kile nilicho kitenda,

    usiku huo tukautumia kulinda kaburi tu la mdogo wangu basi

    ningu akanipa story ya kwamba

    “una juwa nini brother kuna vitu vingi sana vina shangaza katika hii dunia kwanza kabisa kuhusu hawa wachawi kwa kuwatoa ndugu zao au watoto wao kafara kila inapo hitajika yani mtu

    hasiti wala kuingiwa na hofu

    kumchinja mwanae

    aliye mmbeba tumboni miezi tisa

    akaenda reba tena akazaa kwa uchungu

    leo hii tu ana amrishwa amtoe sadaka nae ana kubali,

    nikamjibu kitu

    Ningu kwa kumwambia ya kwamba kazi ya uchawi hutakiwi kuwa na huruma kwa mtu yeyote yule awe baba mama n.k ukiitajika kuchinja mmoja wao wee chinja tu maana uki pindisha amri uta chinjwa wewe,

    Ningu akaendelea kusema “cheki hawa wanao jifanya watu wa Mungu sijui wachungaji mashekhe mapadri mahostadhi baazi yao ni washenzi wanzinzi matapeli mijizi tu ila wame jivika ngozi ya kondoo kumbe ndani ni chui,

    “unajuwa nini Ningu siku zote binaadamu ata mdanganya binaadamu mwenzie tu sio Mwenyezi mungu

    anae fahamu yaliyo jificha na kufi chikana ya dhahir na ya wazi kabisa ngojea nikwambie kitu ndugu yangu

    Ningu japo itakuwa kama faida kwa binaadamu siku zote,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ni kwamba, hakuna dawa kubwa ya kuushinda zaidi uchawi kama kuupuuza, mfano, unaumwa sana, umekwenda hospitali madaktari wamesema hawaoni tatizo, umekwenda kwa mabingwa wa kutibu hospitali kubwa, lakini tatizo halionekani, ukapelekwa kwenye maombi makanisani, msikitini lakini wapi dawa ni kupuuza tu.

    hapa nina maana gani, uchawi ukiupuuza toka akilini unakosa nguvu ya kufanya kazi na ndiyo maana wapo binadamu ambao hawana kinga yoyote lakini uchawi haufanyi kazi kwenye miili yao sasa hata kwa wale ambao watakuwa wamepanda daladala au basi la kichawi, ukihisi hivyo kutokana na jinsi nilivyoongea, unachotakiwa kufanya ni kupuuza tu, hakuna kingine.

    jamii imekuwa ikiangamia kwa uchawi kwa kukosa maarifa na ujasiri wa kuupuuza. mfano, utakuta mtu anarudi nyumbani kwake, mlangoni anakuta hirizi, moyo unamshtuka na kuanza kufikiria kifo au matatizo mengine ya mwili.

    Wapo ambao wanadiriki hata kuitunza hiziri hiyo isiguswe na mtu mpaka aende kwa mganga wa kienyeji akamuangalizie, hii

    ni hatari kubwa.

    Ukikuta hirizi mlangoni, ishike, ichome moto huku ukiwa na moyo uliojaa hasira, nawaambia hata kama iliwekwa kwa lengo la kumkomoa mtu au kumroga mtu haitafanya kazi. Kazi kubwa ya kichawi ni kuamini kwanza, baadaye damu ndiyo inapokea.

    Mfano mwingine, inatokea katika kijiji au mtaa, kuna mtoto ameaga dunia, wengine wanasema kwa uchawi, wengine amri ya Mungu, ni rahisi sana kujua. Utajuaje? Ilivyo ni kwamba, kifo cha mtu aliyeaga dunia kwa mapenzi ya Mungu msiba unatawaliwa na watu kucheka, nikiwa na maana majonzi si sana, lakini msiba wa mtu aliyeuawa kwa uchawi, watu wanalia sana, tena sana.

    Kingine ni kwamba, ukitaka kumjua mchawi mahali unapoishi au unapofanyia kazi, mara nyingi anakuwa na tabia isiyofanana na wengine. Mfano, asubuhi ukiamka, ukiwa unakwenda chooni, ukikutana na jirani yako ukamsalimia lakini akaitikia kwa sauti ya chini sana tena huku akiangalia ukutani, tambua huyo ni mchawi.

    Au, unakwenda kazini, kufika unakutana na mfanyakazi mwenzako, unamsalimia kwa kumpa mkono yeye anaitikia salamu lakini hakupi mkono tambua huyo ni mchawi. hakuna mchawi asiyekuwa na dalili kwenye jamii, sema tu macho ya watu yamefungwa kuona yaliyo sirini kutokana na wingi wa dhambi zetu sisi wanadamu.

    Mitaani tunapotembea, kuna viumbe vingi sana tunapishana navyo, vinatuona lakini sisi hatuvioni. Mbaya zaidi, viumbe hivi wakati mwingine vinaingia kulala kwenye majumba yetu baada ya kuchoka kwa shughuli zao za mchana kutwa.

    Sema usiri wake ni kwamba, baadhi ya viumbe havina ubaya na binadamu, hata vikiingia ndani kwako vinataka hifadhi ya malazi tu asubuhi zinaondoka.

    Umewahi kuwa peke yako usiku chumbani halafu ukajisikia hali ya kuogopa sana kiasi kwamba hutaki hata kulala na giza, unawasha taa mpaka kuna kucha? Basi tambua kwamba, kuna viumbe visivyoonekana vimeingia kulala chumbani kwako. Unaposhtuka na kuangalia dirishani vyenyewe vinakuona na kukucheka.

    Kifupi kila unachofanya vinaona ila havina dhamira ya kukuzuru.

    Sasa utajuaje kuwa ulilala na viumbe? Mara nyingi hivi viumbe humsababishia hali ya kwenda chooni mtu kila wakati. Unaweza kutoka chooni usiku mara nne, wakati si kawaida yako, jua ulilala na viumbe.

    Kikubwa, kama unahisi hatari hiyo, ukilala usifunge mlango, yaani ukae wazi. Viumbe hawa huwa hawana ubavu wa kuingia kwenye chumba au nyumba yenye mlango wazi.

    Umewahi kutembea usiku peke yako ukafika mahali kwa mbele kama kuna watu au mtu lakini ukifika hakuna? Jua maeneo hayo kuna viumbe visivyoonekana. Na mara nyingi ukikutana na hali hii lazima itaambatana na hisia za nywele kusisimka kichwa kizima.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    unaweza ukahisi nywele zinanyonyoka kwa jinsi zinavyosisimka, ujue ni maeneo yenye viumbe.

    Tabia ya viumbe hivi ambavyo asili yake ni kutoka Nchi ya Wachawi, ni kupenda maeneo yenye watu wengi, mfano, sokoni, stendi ya mabasi na vituo vya daladala. hakuna maeneo Dar es salaam yana viumbe wa ajabu kwa wingi kama stendi ya mabasi, pale ubungo na katikati ya mitaa ya k/koo.

    Kwa ubungo, unapoona watu wengi wakiingia na kutoka huku wamebeba mizigo, nyuma yao kuna viumbe hao, ndiyo maana huwa tunasema watu wengi, lakini ukweli ni kwamba tunawachanganya na viumbe.

    Sasa ubaya wao hawa viumbe ni pale wanapoamua wakati mwingine kujitokeza na kuwa watu wanaoweza kuonekana kwa macho.

    hapo ndipo wanapoweza kuharibu eneo. mfano, usidhani kilio cha mara kwa mara cha foleni jijini Dar es salaam ni cha kweli, foleni nyingine tunaongezewa na hawa viumbe baada ya kujigeuza na kuwa binadamu.

    wana uwezo wa kufanya magari yao, wakatoka k/koo kwenda kimara, kwenda mwenge au Kibamba na wanapokuwa pale magomeni na basi na wao wana jifanya kuwepo kwenye foleni wakati wana uwezo wa kufika wanakokwenda bila kuwepo kwenye foleni wala kuwa kwenye magari.

    tatizo ni kwamba, hata ukiliona gari la kiumbe kisichoonekana huwezi kulijua, lina namba za kawaida, kila kitu cha kawaida.

    Ila, mara zote abiria wa magari haya hawazidi watatu ikiwa na pamoja na dereva. Na mara zote ndani ya gari kunakuwa na utulivu, hakuna anayeongea wala kucheka, mwanzo wa safari yao hadi mwisho.

    hatari iliyopo ni kwa wale wafanyabiashara wanaouza maji, juisi, sabuni au bidhaa nyingine kwa wenye magari.

    na amini mpaka hapo ume nielewa Ningu, yaani ni kwamba, ukifika pale maeneo ya magomeni mapipa, si kuna foleni halafu kuna vijana wanauza vitu kwa watu waliomo ndani ya magari? basi wale vijana wako hatarini zaidi.

    kwa nini? Kwa sababu baadhi ya watu wengi sana wanao wauzia ni wale viumbe wasioonekana ambao siku hiyo wanakuwa ndani ya ma gari.

    wana tabia ya kuchukua damu ya vijana kama hao na kwenda kuichafua, baada ya muda utakuta kijana anakuwa mdhaifu, hana maendeleo, mwili unakuwa lege lege umechoka, vibaya sana yaani anakuwa binadamu ilimradi anaishi lakini kwa upande mwingine si binadamu kamili.

    Kifupi matukio yanayowakuta binadamu ni makubwa na mengi, yanatisha kama utasimuliwa kila siku.

    napenda kusema kuwa, mfano usiku. hakuna siku iendayo kwa Mwenyezi mungu bila kuwepo kwa watu waliopata matatizo usiku, hasa ya kichawi ambayo kesho yake mtu anaweza kushindwa kusimulia hadi zipite siku nyingi.

    Kinachowapata wanadamu wengi usiku, chanzo ni kutojua mwongozo wa kichawi, unaweza kugombana na mtu ukadhani ni wewe, kumbe wachawi wanasimamia kwa lengo la kuwapata mbele ya safari, tukiwa kati kati ya kupiga story

    gafla nika stuka

    baada kumuona

    Nipe nikupe akija kwa kasi ya ajabu sana katika eneo lile la makaburi

    mimi na

    Ningu tuka simama atesheni yani teyar teyar

    kwa mapambano tu

    kwa mara nyingine teeeeeeeeeena

    vita vipo mbele yetu huku Nipe nikupe ana hema

    na kufuka moshi kwa hasira

    Ningu akatoka kwa kasi kwenda kumfata

    Nipe nikupe gafla

    Ningu akapigwa na kitu kizito na kurushwa mbaali na eneo lile akatua chini na kuwa kimyaaa,



    Sasa tupo uso kwa uso kila mmoja akiwa na hasira na mwenzie na tumalize ubishi wa nani zaidi kila nikimcheki

    Ningu yupo kimyaa hata kutikisika hati kisiki, tuka peana ishara mimi na

    Nipe nikupe tuamie uwanja wa shule kama game ika chezwe kule nikachumpa kwa kupaa baada kumuona yeye anaenda huko sasa basi twende kazi tushafika

    Nipe nikupe aka fanya manjonjo yoote alipo kuja kufutuka akaja kuni vamia kwa speed ya ajabu sana nikajikuta narushwa hewani kwa pigo lile la kustukizwa

    nika jikuta nadondokea mti dahaaa nili jikita vibaya sana sehemu ya kiuno hayo maumivu yake haya elezeki kabla sijanyanyuka akaja kunizoa kwa kuni zungusha kama feni ikiwa katika speed ya %100 akanibwaga unajuwa mpaka hapo nikashindwa kujipanga katika kuzuuia mapigo yake

    si kanistukiza na hakutaka kunipa pumzi ya hata sec moja nikiwa bado nipo chini aka nipulizia moto uka nipata vizuri mwilini nikawa nagagaa pale chini kwa maumivu ya ajabu maana na ujanja wangu wote nalia kama mtoto

    nikiwa bado niko pale chini nika kumbuka kauri ya bibi akisema

    kuna njia nyingi sana za mapambano na mizimu maana hata wachawi wana pambana kwa kutumia nguvu za kichawi tena wana zidiana pia sasa basi jiandae kwa angushi pindi adui yako anapo kushambulia gafla tumia lanta nyori yani kipawa cha kuzuia angushi amka sasa upambane ukifeli hapo leo mdogo wako ndio bye bye,

    nika futuka kutoka pale chini na kuuzuia ule moto sasa kama ngwai na iwe ngwai nikaukusanya ule moto wake na kuwa kitu kama mpira hivi nikamtupia kitu kika enda kumpata moja kwa moja mdomoni “khooooo!!!yakhaaaaaa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akapiga ukelele kwa maumivu sasa ikawa piga nikupiga style zote tukatumia tukiwa tume choka hoi kama majogoo vile nikajiandaa kumpa zinga la kombora cha ajabu tena kwa macho yangu mawili nika shuhudia

    Nipe nikupe aki pasuka vipande vipande kwa kupigwa na miale ya umeme kutoka juu ndio ikawa nafuu yangu kwa kupumua maana dahaa

    shiida tupu kama kiu nilikuwa nacho kweli nusura nikate tamaa ya kupambana na kiumbe hiki cha ajabu chenye nguvu za kutisha mpaka

    akaweza kui tetemesha kilwa kiwawa nzima watu waka ishi kwa hofu

    ya kumuogopa yeye mbele yangu vika simama vitoto vilivyo toka juu na nikahisi bila shaka ndio walio mpasua

    Nipe nikupe kuwa cheki sura zao wote wapo kama Figisu, waka sema

    “baba tumekuja kuku saidia baba yetu

    na unahitajika haraka sana kuzimu kwenda kumzika ndugu yetu

    Figisu,'

    nika baki kuduwaa tu kumbe hawa wote ni wanangu mbona sura zao zime fanana hivi maana walikuwa wengi balaa,



    hatukuwa na kingine cha kufanya zaidi ya kusema R.I.P ndugu

    Nipe nikupe nikaondoka na wanangu mpaka kuzimu khaa nikastuka na kutoa macho pima baada kumuona

    Nipe nikupe akiwa kafungwa huku akipewa adhabu kule kuzimu nikaja kupokelewa kishu jaa baada kufanikisha kukamatwa kwa huyu zoba nikajiuliza kama

    Nipe nikupe kule ame kufa cha ajabu namkuta huku kuzimu akiwa mzima sasa kwa nini

    Figisu asiwe mzima huku, basi malkia akaja kuni kumbatia kumbuka ndio mke wangu mtarajiwa basi nikapelekwa mpaka ulipo lazwa mwili wa

    Figisu nikaubeba kwa kuupeleka sehemu ya maombi hata sisi mizimu tuna fanya maombi ndio maana tabia zetu kama binaadamu baada kufanya maombi kwa mda kidogo tukaenda kumzika

    Figisu huku mateso kwa nipe nikupe yakizidi

    nikaweza kumuona pia

    Ningu akiwa na furaha basi taratibu za ndio zika fanyika nikaweza kumuowa malkia kutoka kuzimu kazi iliyo baki ni kwenda kum rudisha Hafidhi mdogo tu nikatoka mimi na malkia mwenyewe kwenda kuifanya kazi hiyo



    yapata saa mbili hasubuhi tukakuta wachimbaji wa kaburi wakiifanya kazi ya kuchimba kaburi la mdogo wangu basi malkia akafanya jambo kwa kuivuta pumzi kwenye kiganja chake cha mkono kisha akapulizia kwenye kaburi kitendo kilicho wastusha wale walio utoa mwili ule ukiwa ndani ya sanda kwani ukaanza kupumua huku ukipiga makelele nitoeniii!!!

    hakuna aliye baki kila mmoja akatoka mbio nikamcheki malkia na kumwambia arudi nyumbani hii kazi nita ikamilisha mwenyewe kabla haja ondoka nika muuliza

    “hivi mke wangu mbona bibi siku muona kwenye mazishi ya

    Figisu?"

    “mme wangu bibi yeye ame pewa kazi na mkuu kwenda tanga kuwanasa wachawi maana ndio mkoa wao mkuu kule, “oky basi wee nenda wacha mi nifanye kazi haraka nije kujilia kitumbua changu halali kabisa basi malkia aka nisogerea tupeana mate huku niki zitomasa chuchu zake mbichi ohoooo,,,,ahaaaa,,,,“mume wangu usikawie basi kurudi mwenzako niko hoi taabani,'

    “usi jali mamy to nita wai kurudi tu



    basi tuka nyegeshana pale si unajuwa tena wana ndoa hata zile saba za mwanzo bado kila mmoja akiwa na mzuka na mwenzie baada my wife kuondoka nikabaki kuutizama ule mwili

    wa mdogo wangu pale chini nikajivika taswila ya kuwa bonge la shekhe na kuushika ule mwili ukiwa bado ndani ya sanda nikautoa akiwa bado uchi wa mchama huku nyama nyama za mwilini zikiwa hazipo na kubaki mifupa tu kwa kiasi kikubwa tu

    nilicho kifanya ni kumwita

    Ningu nazani wito wangu ulimfikia akaja faster na kuniambia “nisha fika boss niambie,'

    nikampa maagizo bila kuchelewa aende haraka hospital yeyote ile na akachukuwe nyama za mwili kutoka kwa maiti yeyote ile ila awe mwanaume kijana umri kama wa huyu,

    “sawa boss! hakuchelewa kufumba na kufumbua kaja na maiti kama tatu hivi za vijana nikafanya kuzivua ngozi na nyama na kumuwekea mdogo wangu,



    mwisho akawa fresh kabisa nika toka nae huku akiwa kama zezeta flani hivi au msukure kazi iliyo baki ni kukisaka kivuli chake maana kule kuzimu hakipo nikapiga mahesabu kipo wapi kumbe kipo tanga na bibi,



    nikamwambia ningu aende kukileta akasepa cha ajabu alipo ondoka tu wingu zito lika tanda halikuwa wingu la kawaida nikaitajika nirudi faster kuzimu ikabidi niende na ule mwili wa mdogo wangu baada kufika tu nikakuta vilio kila kona mizimu mingi ikiwa imekufa nikiwa katika hali ya sinto fahamu

    nikamuona malkia akija mbiio huku akilia na kusema

    “mume wangu CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nipe nikupe katoroka wakati narudi kutoka kule tulipo achana nikamkuta kaingizwa kwenye tanuri la moto

    anazidi kuteswa gafla sauti yako ika sikika uki muitaji Ningu kitendo cha

    Ningu kuja huko tu huku zahama ikaanza

    Nipe nikupe akatoka kwenye moto akiwa kashakata minyororo yote jeshi likaitaji kumkamata yakawa mapambano makali sana mwisho akakimbia humu amesababisha vifo vya ndugu jamaa na marafiki,

    baada kusema vile wife aka endelea kulia hasira zika nishika

    Ningu akaniambia “boss!

    Nipe nikupe hayupo mbali na hapa kwa sasa anakwenda jijini Dar es salaam

    nikatoka faster na kusema ndio kwaanza kazi imeanza,



    Kitendo cha kuambiwa ya kwamba Nipe nikupe hayupo mbali na hapa kibaya zaidi ana kwenda katika jiji la Dar es salaam nika chumpa haraka na kuanza kumfatilia huku nikiwa kasi vibaya mno kwa speed zote nilizo kwenda nazo sikuweza kumuona

    Nipe nikupe wala vumbi

    lake hata nilipo fika maeneo ya posta nikazunguka jiji zima hakuna kitu,

    nika geuza kurudi kuzimu kwa ajili ya msiba na kuangalia ni jinsi gani nitaweza kuikamilisha kazi hii ngumu,



    baada kuingia kuzimu nika pokelewa na my wife tena kwa bashasha tele na kuniuliza kwa shahuku kubwa “vipi mume wangu umempata au?"

    nika mjibu hapana sikuweza kumuona hata kivuli chake sijui kakimbilia wapi!!!

    “ohoo pore sana mume wangu lakini bibi ame shakuja tayar

    basi nikaenda moja kwa moja kuonana na bibi vizuri zaidi kaja na kile kimvuli basi tukafanya taratibu na mipango ya kuweza kumrudisha mdogo wangu baada kupita kama dakika kumi hivi mdogo wangu aka stuka na kuanza kujishangaa “jamani!!! nakufa mieee huku wapi nilipo jamani!!!



    nikapewa kazi ya kumtuliza asi zidi kupiga kelele pale nikaenda na kumuingia ndani ya mwili wake kupitia yeye niko hai na kupitia mimi yeye yupo hai je nini kifuatacho

    Hafidhi j ikram mdogo ana tujuza zaidi



    katikati ya usingizi mzito nilio kuwa nime lala nikaja kustuka baada kuhisi kitu kama maji maji hivi yaki nidondokea kutokea juu na kutua moja kwa moja kwenye maungo yangu

    siwezi kutambua ni usingizi gani huu wa kifo au vipi basi nikastuka na kujikuta nimeroa mwili mzima huku nikiwa katikati ya msitu mzito vua kubwa ikinyesha na radi pamoja na miale ya umeta iki mulika mulika eneo lile nikabaki kujiuliza nime fikaje fikaje eneo hilo nikajitahidi kuvuta kumbu kumbu niweze japo kukumbuka nitokako nikaja kukumbuka ya kwamba mara ya mwisho nili fanya mapenzi binti anae kwenda kwa jina la Mwajuma nilipo rudi nyumbani mama aka nichapa nikakimbilia porini “khaa! kumbe sijarudi nyumbani kwa bibi mpaka sasa, nikaji nyanyua pale chini na kuanza kurudi nyumbani kwa bibi nika shangaa pindi nilipo ona kila mtu ninaye kutana nae njiani ana nikimbia sikuweza kujuwa au kufahamu

    sababu ni nini hasa,



    nikazidi kusonga mbele na kufika nyumbani kwa bibi pale kibarazani hakukuwa na mtu hata mmoja zaidi ya kuwaona kuku tu wame jikunyata kujikinga na vua ile nikaugusa mlango ule wa bati na kugonga hodi,,,nikaweza kuzisikia hatua za mtu akija kufungua mlango kitendo cha kufungua tu na kuchomoza sura yake nnje aweze kujua anae gonga hodi ni nani gafla akapiga yowe zito “mamaweeeeee!!! akafunga mlango haraka sana, akazidi kupiga kelele tu mlango uka funguliwa tena akatoka baba pamoja na babu hata

    wao wali patwa na shock yani mstuko huku wakiwa hawaamini kwa kile wakio nacho mbele ya upeo wa macho yao nikiwa sitambui chochote nikaenda mbio kumkumbatia baba kabla sija mfikia nae akatoka mbio na kuingia ndani, nikabaki katika hali ya mshangao zaidi huku babu nae akiwa ana tetemeka sijui kwa sababu gani nikajaribu kumsogerea nae akatoka mbio na kukimbia hakujali vua wala nini maana ali timua mbio balaa sikuwa na jinsi zaidi ya kwenda kupiga magoti chini huku vua ikizidi kunipiga na kutamka maneno haya tena kwa sauti kubwa tu,



    "Sikuweza kufikilia wala kuwazia ya kwamba mnaweza kunitenga kisa tu kufanya mapenzi na Mwajuma kumbukeni mimi ni mtoto wenu bado kutenda kosa sio kosa bali kurudia kosa na mtoto akikunyea kwenye mkono huwezi kuukata mkono zaidi ya kuuwosha ewe mama ewe baba na bibi naomba mnipokee mimi mtoto wenu naomba mnisamehe sana

    mimi sio kama ukoma wa ku

    nigopa hivyo, nililia sana huku machozi yangu yaki ishia kumezwa na maji ya vua

    nikiwa bado nime piga magoti huku nimeinama nikaweza kugundua ya kwamba kuna mtu kasimama mbele yangu nikainua kichwa changu na kumtizama hakuwa mwingine ni mama huku akiwa analia basi akatanua mikono yake na kuitaji kuni kumbatia basi nika inuka na kuweza kukumbatia kwa furaha ya machozi “Hafidhi mwanangu ni wewe?"

    “ndio mimi mama yangu ile jana ilikuwa hasira tu ndio nikaamua kwenda kulala porini,

    “pore sana mwanangu nisamehe mimi, basi baba nae akaja kukumbatiana na sisi kila mmoja akilia kimpango wake

    basi nikaandaliwa chakula nikala nikaoga na kuvaa nguo mpya hostadhi akaja kuni somea duwa



    Usiku sikuweza kulala kwa amani baada kuota ndoto nikiwa kisimani nateka maji gafla akaja jamaa mmoja hivi handsome boy na kuniita “Hafidhi,

    “naam kaka niambie!!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “sikia nikwambie kitu nimekuja hapa kukwambia ya kwamba vita bado haijaisha, nikamuuliza

    “mbona sikuelewi una maanisha nini kusema hivyo?"

    “najuwa ndio huwezi kufahamu kwa sasa ila tambua ya kwamba mimi ni kaka yako, “nikastuka baada yule mtu kusema yeye ni kaka yangu,

    “wewe ni kaka yangu kivipi yani kiumri au?"

    “ndio kiumri pia kingine mimi na wewe ni damu moja,

    “hivi wee jamaa mbona una penda shobo tu sikia nikwambie mimi kwa wazazi wangu ni mtoto wa pekee sina kaka wala dada na kaka yangu ali shafariki kabra sija zaliwa,



    “sasa huyo kaka yako ndio mimi, nikatoa macho pima baada kusema vile aka badirika na kuwa kiumbe cha kutisha mwenye mapembe na minjino mirefu na kusema nimekuja kukuchukua basi akaruka kuja kunivamia nikajikuta napiga ukelele jamaniiiiieeeee!!! nakufaa,,,,

    nikastuka nipo kitandani jasho likini nivuja kwa fujo dahaa baba akaja mbio pamoja na mama kwa kihere here

    wakaniuliza

    “vipi tena baba kuna nini?"

    ni kauli ya mama akiniuliza nikashindwa kumjibu chochote zaidi ya kutikisa kichwa tu basi usiku ukapita kesho yake hasubuhi na mapema nika damka kwenda kupiga tizi uwanja wa shule hata hivyo hakuna aliye kuja kujiunga nami siku hiyo yani kila kijana akakimbia nikakosa raha mawazo yaka nisonga hata mzuka wa kupiga tizi sikuwa nao kabisa nikarudi zangu home nikiwa ndio naingia nyumbani nikaweza kusikia mazungumzo kati ya wazazi wangu wote wawili na bibi “sasa mtawezaje kuishi na mzimu?"

    “hilo lisikupe shida hata kidogo mama

    awe mzimu au zombie yule bado ni mtoto wetu tu

    hiki kijiji kina wachawi na ndio walio mchukuwa mwanetu kwa kumfanya msukure kwa bahati nzuri hakukatwa ulimi sie tukajuwa kafa na kwenda kuuzika mgomba dadeki,



    “walio fanya kitendo hiko sio wachawi wala nini hayo ni mambo ya

    Nipe nikupe tu, baada kusikia jina la

    Nipe nikupe basi mwili uka nisisimka kwa uoga maana hiki kiumbe nakikumbuka vizuri nikazidi kusikiliza hasa bibi alivyo sema



    mnajuwa yapata miaka miwili sasa tokea mwanenu Hafidhi j ikram afariki kama kumzika tushamzika na keshaoza huyu aliye kuja hapa sio yeye ni mzimu tu, kwa sauti yenye hasira na jazba baba akatamka

    “wee mama heshima ni kitu cha bure yule ni mwanangu mimi na wala sio mzimu kwanza yuko wapi?"

    mama akamjibu “ame toka kwenda mazoezini, “oky andaa mizigo turudi zetu mjini maana mama yako kashaanza kuleta mambo sio tusije kuonana wabaya bure au ndio mchawi mwenyewe nini?"

    “wee mwana koma mchawi mzazi wako aliye kuzaa sio mimi pumbavu wee!!!

    basi baba kwa hasira akamkunja bibi kwa kumkaba kiukweli hakuna aliye weza kumnasua bibi kwenye mikono ile ya kicommando nikaja haraka kufanya jambo japo sina ubavu nika shangaa namtoa mikono yake kama vile katoto kadogo

    baba akaniambie kuanzia leo tambua ya kwamba bibi yako si mtu mzuri kwako ame kuweka ndondocha takribani miaka miwili sasa shika begi turudi zetu mjini hakuna kukanyaga tena katika kijiji hiki,



    kauli ile ya baba ilikuwa so lias basi tukajiandaa haraka haraka na kuondoka kwenda stendi sikuweza kushangaa tena kwa kuona watu wakiulizana kila nilipo pita pale kijijini kutokana na kusikia yale

    mazungumzo kati ya baba na bibi kumbe mimi ni mfu niliye kwisha kufa kitambo tu,

    nilivyo fikilia ni jana tu kumbe ishapita miaka miwili sasa tokea nitokomee porini mawazo yaka nizidi nikiwa ndani ya bus mpaka usingizi ukanipitia na kujiona niko sehemu na kile

    kiumbe kinacho dai ni kaka yangu akinipa mafunzo jinsi ya kupambana na watu wabaya mwisho akaniambia kupitia mimi tunaweza kumuangamiza

    Nipe nikupe, nikaweza kuongea nae mambo mengi sana na kuniambia bila yeye mimi nisinge kuwa hai tena maana kafanya kazi nzito ya kupambana na

    Nipe nikupe mwisho akasepa na kwenda kusiko julikana ila kupitia mimi ata patikana tu,



    nikaja kustuka tushafika mbagala basi tukapanda DCM inayo kwenda mwenge kwakuwa ina pitia maeneo ya kinondoni nikaweza kushuhudia jinsi nyumba zilivyo bomoka bomoka maeneo ya jangwani mpaka mkwajuni huku mabondeni

    “baba mbona nyumba ziko hivi maeneo haya?"

    “dahaa mwanangu wee acha tu serikar hiyo!!!

    serikar ime fanyaje tena?" ndio walio bomoa hizo nyumba, “kisa nini hasa mpaka wana bomoa nyumba za wananchi?" “inavyo semekana wapo maeneo ya hatari zaidi yani kuna uwezekano mkubwa wa kusombwa na maji pindi mto utakapo furika maji yani mafuriko,

    “ahaa kumbe lakini si wame watafutia maeneo salama zaidi na kuwalipa gharama zao?"

    “kusema kweli sijajuwa bado ila nilivyo sikia kuna baazi ya wananchi walilipwa na kupewa viwanja huko mwagwe pande cha ajabu baazi yao wakauza viwanja walivyo pewa na kurudi tena maeneo yale yale waliyo ambiwa wahame, “duhuu kumbe Kuna watu hamnazo kabisa ehee!!!

    “ndio hivyo mwanangu ujinga wa watu wachache ina sababisha wengine wasilipwe kitu maana serikar ina hisi mambo ni yale yale,

    “sasa kwahiyo nyumba yetu hivi ipo?"

    mama akabaki kucheka tu na kusema “yani siamini mwanangu umekuwa na maswali kwa kuongea kama kagreta vile tokea tukiwa ndani ya daladala mpaka tunashuka maswali tu,

    “unajuwa nini mama, “eheee niambie CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “kipindi naondoka huku kila kitu kilikuwa shwali ila nimerudi mambo yapo hovyo hovyo kwahiyo lazima nimuulize baba anipe majibu,

    “haya karibu nyumbani, ni mama huku akifungua geti la nyumba yetu

    “mama hivi picha za marehemu kaka yangu unazo au?"

    “mmh Hafidhi wewe unataka picha za mtukutu za nini?"

    “nazitaka tu nimuone kaka yangu haya angalia ile kwanza ya ukutani naenda ndani kukuletea albaam yake,

    kitendo cha kuinua kichwa changu na kuitizama ile picha nikastuka maana ni yule yule pindi ninapo lala hunijia ndotoni cha ajabu sijui maruwe ruwe au vipi nikaona kwenye picha ananicheka mimi kisha akatoka na kuja kunishika nikapiga zinga la ukeleleee

    “mamaweeeeeeeee!!!



    Zile kelele zimkafanya baba na mama watoke mbio kuja sebureni na kuuliza kunani tena, nikakosa jibu zaidi ya kukodoa macho tu kama vile fundi saa aliye poteza nati basi baba akanishika na kuniambia nikae chini kwanya kisha akasema “mama Hafidhi bila shaka mtoto atakuwa katika mazingira magumu sana tu sasa cha umuhimu kesho tuki jaaliwa uzima wa hafya baada kutoka swalati ljumaa tumpeleke kwa shekhe mirongo akapate daawa nahisi matatizo yote yatakwisha haya, “sawa mume wangu mi sina neno maana hali ya mtoto ndio kama uionavyo, “baba!!! “naamu mwanangu, “hivi kumbe mimi nimekufa?" lile swali liliwastua sana na kushindwa kujibu huku midomo ikiwacheza nikauliza tena kwa ukali zaidi, “naomba mnijibu je mimi nilikufa!!!?

    “hapana mwanangu haukufa bali ulipotea tu katika mazingira ya utata, “baba niambie ukweli usi nifiche kitu chochote, “Hafidhi mwanangu ukweli gani unao utaka wewe?"

    “mama naomba uondoke hapa niache mimi na baba tu! basi mama akanitupia ile albaam na kuondoka zake chumbani tukiwa tume baki wanaume watupu baba hakuwa na budi zaidi ya kunipa full story mwanzo mwisho nikabaki kuduwaa tu mpaka baba alipo maliza ile story kifua changu kikawa kimeloa chapa kwa machozi na kuhisi presha ina panda presha inashuka nikakumbatina na baba kumbe mama nae hakwenda ndani zaidi ya kusimama mlangoni tu akaja kujiunga nasi basi nikaenda kuoga nikala na kwenda kulala usiku huo hata kaka alipo nijia sikuweza kuogopa tena nikapiga nae story za hapa na pale akanichukua hadi coco beach na kuzidi kunipa mafunzo ya kupambana na kila kiumbe binafsi alikuwa ni mkali wa mapigo ya kila aina taikondo karate king boxer shaollin n.k nilijifunza mengi usiku huo hasubuhi kulipo kucha nipo kitandani basi nina maumivu kila maeneo kutokana na tizi la jana usiku nikaenda kupiga mswaki nikanywa chai “Assalam alaykum ya ibnaiya, ikiwa na maana ewe mwanangu basi nikaitikia “waaleykum ssalam yaa Abiiii basi nikatoka zangu nnje kwenda maskani kwa washkaji kufika tu kila aliye niona akatoka nduki mpaka kufikia wengine kujikwaa na kudondoka vibaya sana nikawa nishatambua kinacho wakimbiza nini nikaenda kukaa kwenye benchi huku nikishika tamaa nikastuka baada kuguswa begani kucheki ni kaka kwanza nika tabasamu kwa kuweza kumuona live tena hasubuhi ile juwa lina waka basi akawa amekaa kwenye benchi kwa mbele yangu na kusema

    “popote ulipo nami nipo, nikatabasamu na kumuuliza “una maanisha nini kusema hivyo?"

    akajibu ya kwamba “mpaka sasa kuzimu tuna msaka

    Nipe nikupe hatujui yuko wapi ila kupitia wewe atajitokeza tu maana wewe ndio adui yake mkuu, “hivi kaka kwa nini usiende nyumbani ukajionesha kwa wazazi tukaishi pamoja? kusema kweli ile kauli ikamfanya kaka acheke sana

    “hahahaha! kipindi yeye anacheka nika shangaa washikaji wa kitaa wanarudi kuja kukaa pale maskani huku wakinipa tano mimi na kaka basi kijiwe kikanoga zaidi baada kaka kutupa story ya Chanduka,

    “yani kwa kifupi huyu Chanduka baada kutupwa kutoka ndani ya meri na kujikuta anatua ndani ya bahari tena kwenye kina kirefu balaa aka jitahidi sana kupiga mbizi asijuwe wapi ana kwenda gafla akahisi kuna kitu kina kuja kwa kasi ya kimbunga kucheki kwa mbaali si akauona upanga kumbe ni papa Chanduka akadata na kujuwa huu ndio mwisho wake wakati yule papa ana mkalibia kwa kitendo cha kustua akatokea zinga la joka na kumpiga kikumbo yule papa kisha akammeza Chanduka na kusepa nae wakati yote yana fanyika yeye alikuwa kashapoteza fahamu zamani tu akaja kustuka yupo misiwani ame zungukwa na watu wa ajabu ajabu akabebwa mpaka kijiji cha wale viumbe yani wanawake wa tupu hakuna mwanaume hata mmoja yani ajabu hii,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati kaka anaendeleza story nikamuona mama akija pale kijiweni kwa kitendo cha haraka kaka kuna kitu akakifanya nikajuwa bila shaka asiweze kuonekana na mama

    na kweli alipo fika kila mmoja aka muamkia na kuniambia “Hafidhi mwanangu baba yako ana kwita, nikanyanyuka kwenda kusikiliza wito huku nikimuacha kaka pale anaendelea kuwapa story washikaji

    basi nikamkuta baba amesha jiandaa kwa kupiga kanzu yenye kung'aa na barakashia yake kwakuwa nilikuwa tayari nishaoga nikavaa tu mavazi ya kuendea msikitini tukatoka zetu nilipo pita pale mskani jamaa yangu mmoja anae kwenda kwa jina la Yasini akaja mbio na kuniuliza “vipi ndio masjid au?

    nikamjibu ndio kama vipi twenzetu basi aka muamkia baba safari ikasonga kwenda masjid mtambani siku hiyo nilijisikia furaha sana kwa kuingia ndani ya nyumba ya ibada hasa shekhe kwenye khotuba yake alipo kuwa aki zungumzia kuhusu asiri ya majini maana ali nikuna sana embu tumsikilize shekhe alicho kisema



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog