Search This Blog

Tuesday, 17 May 2022

CHAGUO LA MOYO WANGU - 4

 







    Chombezo : Chaguo La Moyo Wangu

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee samwel alikurupuka baada ya kushtushwa na mlio wa simu yake,aliitoa na kuangalia mpigaji alikua nani lakini alijikuta akisita kupokea simu baada ya kuona mpigaji alikua ni mwanae judith,aliamua kukata shauri na kupokea simu ile,haloo baba umempeleka wapi michael wangu,judith alimuuliza baba yake kwa sauti ambayo ilionekana alikua akitaka kulia,mmh michael... michael amepata ajali ya gari alipokua akitoroka nyumbani hasa baada ya kugundua kua nilikua nimefahamu uchafu aliokufanyia,mzee samwel alimwambia binti yake kwa kirefu,baba tafadhali jaribu kuheshimu hisia zangu,kwani mimi pia nina haki ya kuchagua yupi ananifaa na yupi hanifai hivyo tafadhali kama unahitaji niendelee kuwa hai nieleze vizuri ni wapi ulipompeleka michael kwasababu najua kila kitu,aliongea judith kwa sauti isiyokua na masihara hata kidogo...

    mwanangu naomba unisamehe kwa niliyofanya,nikweli nimemteka michael na anapatiwa mateso kutokana na makosa aliyoyafany.. aliongea mzee samwel lakini kabla hajamaliza sentensi yake judith alimkatisha,hivi baba una akili timamu wewe? mpaka sasa umeua watu wangapi kutokana na biashara zako haramu,je ni nani aliyekupa adhabu kutokana na makosa yako? sasa nakwambia hivi ikifika saa tatu nataka nimuone michael hapa nyumbani lasivyo utakuta mwili wangu ukiwa hauna uhai,aliongea judith kisha kukata simu,hakika mzee samwel alichanganyikiwa,mzee samwel alimfungua michael haraka haraka kisha kumbeba na kumuingiza kwenye gari lake na safari ya kuelekea hospitali ilianza na wakati huo michael alikua kapoteza fahamu hasa kutokana na kupoteza damu nyingi,alikua akiendesha gari kwa mwendo kasi sana hali iliyopelekea avunje baadhi ya sheria za barabarani lakini yeye hakujali hilo,alimpenda sana mwanae judith na hakuta kufanya makosa kwani alijua kosa dogo laweza sababisha akampoteza mwanae,alifunga breki za gari katika moja ya hospitali iliyopo karibu kabisa na nyumbani kwake kisha alishuka na kuanza kupiga kelele za kuwaita madokta kuashiria kwamba mgonjwa aliyekua nae alihitaji kupatiwa huduma ya haraka kwani kuna uwezekano akapoteza maisha,manesi walitoka haraka huku wakiwa na machela,walimpakiza michael na kuanza kumkimbiza katika chumba cha wagonjwa mahututi,mzee samwel hakutaka kubanduka hospitalini hapo na mara kwa mara alikua akiitazama saa yake,ilipotimia saa mbili na dakika hamsini na tano simu ya mzee samwel ilianza kuita na mpigaji alikua ni judith,mzee samwel alijikuta akitokwa na jasho ingawa wakati huo kulikua na hali ya ubaridi.....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee samwel aliamua kuipokea simu ile huku jasho likimtoka, baba vipi ushajiandaa na kwaajili ya kuja kunizika? hilo ni swali alilokumbana nalo mzee samwel kutoka kwa judith, ha.. ha.. hap.. ana mwanangu,alijibu mzee samwel kwa kusitasita, sasa unasubiri nini mpaka muda huu kumleta michael,umeshaa

    ngalia saa yako zimebaki dakika ngapi mwili wangu utengane na uhai,ni maswali mfululizo ambayo judith alimuuliza baba yake,mwanangu tafadhali usifanye chochote kibaya kwani michael kwa sasa nipo nae hospitali anafanyiwa matibabu,mzee samwel alitoa maelezo kwa kirefu zaidi, niniiiiii... eti unasema michael yuko wapi?? aliuliza tena judith kwa sauti ya juu kana kwamba hakumsikia baba yake kwa mara ya kwanza, ndio hivyo mwanangu michael kwa sasa nipo nae hapa kwenye hii hospitali ambayo ipo jirani na hapa nyumbani anapatiwa matibabu kwani hali yake ni mbaya,mzee samwel alimuambia mwanae, nakuja sasa hivi, alijibu judith,na kweli baada ya dakika tano judith alikua tayari ameshawasili katika hospitali ambayo michael alikua amelazwa, alimkata jicho kali sana baba yake mpaka mzee huyo akajikuta akijistukia, michael amelazwa wodi gani,ni swali ambalo judith alimuuliza baba yake bila hata ya kutoa salamu, mwanangu hata salamu hujanipa tayari umeanza kwa maswali,aliongea mzee samwel kuonyesha kua alikua amechukizwa na tabia ile ambayo judith alimuonesha,naomba unijibu michael kalazwa chumba gani hiyo salamu nitakupa hata kesho,alijibu judith kwa sauti isiyokua na mzaha hata kidogo,lakini mwanangu jua kua mimi ni baba yako yakupasa uwe na adabu unapo ongea na mimi,mzee samwel alimuambia judith kwa sauti y ukali kidogo, unasemaje wewe ni baba au muuaji yani unakosa hata huruma unamtesa kijana wa watu mpaka kufikia hatua ya kulazwa kisa amelala na mimi,wewe sio mtu ni muuaji na inawezekana hata mama yangu wewe ndiye uliyemuua,aliongea judith kwa sauti ya juu ambayo iliambatana na kilio, mzee samwel baada ya kuona mambo yanataka kuharibika maana watu walikua washaanza kusogea eneo lile walilokuwepo aliamua kumuambia mwanae ni wapi michael alipolazwa,baad

    a ya judith kujua sehemu ambayo michael alikua amelazwa aliondoka kwa mwendo wa kasi mpaka katika chumba ambacho michael alikuwepo,lakini kabla hajaingia alizuiliwa na madaktari kwa kumuambia kuwa mgonjwa yupo kwenye hali mbaya hivyo hauhitajiki usumbufu wa aina yeyote ile katika chumba hicho,licha ya judith kuzuiliwa na madaktari alilazimisha kuingia ili akaone kipenzi cha moyo wake kipo kwenye hali gani ndipo mzee samwel alipoingilia kati na kuwaomba madaktari wamruhusu judith aingie kwenda kumuona michael,basi madaktari hawakua na jinsi zaidi ya kuingia na judith katika chumba ambacho michael alikua amelazwa,judith alijikuta akilia kwa taratibu baada ya kuona mwili wa michael kwa mbali ukiwa umezungushiwa bandeji katika sehemu ya kichwa na kifuani,alijikuta uvumilivu ukimshinda na kuanza kulia kwa nguvu huku akilitaja jina la michael na kumlaumu baba yake kwa kusababisha yote hayo,madaktari walijitahidi kumtoa nje lakini judith aligoma,alilia mpaka akapoteza fahamu,basi madaktari ilibidi wambebe haraka haraka na kumpandisha kwenye machela kisha kumuhamishia katika chumba kingine,mzee samwel baada ya kuona machela inatoka katika chumba cha michael alitimua mbio kuifuata ile machela na kuwauliza madaktari nini kimetokea maana haelewi elewi, madaktari walimueleza kwa kifupi kilicho tokea,baada ya kupata taarifa ile mzee samwel alipata mshtuko wa ghafla na taratibu nguvu zilimuishia na kujikuta akikaa chini kutokana na miguu kushindwa kustahimili uzito wa kiwiliwili chake,hakika alichanganyikiwa,alitamani arudishe masaa nyuma ile arekebishe yaliyotokea lakini hilo nalo kamwe halikuwezeana,alijua nini maana ya mshtuko,alijua madaktari wasipo fanya jitahada basi atampoteza mwanae,alilia kwa uchungu sana na kujikuta akijutia maamuzi ambayo aliyachukua,alizidi kulia kwa uchungu na kumuomba mungu apiganie maisha ya mwanae pamoja na michael waweze kupona,na aliapa endapo watapona basi kitakacho fuata ni mipango ya harusi na atamuozesha michael binti yake,hakuna kingine alichowaza zaidi ya hicho endapo michael na judith watapona,alishaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kubaliana na kila hali na alipanga endapo mwanae na michael watafunga ndoa atawakabidhi miradi yake karibu yote na yeye atabakia na miradi michache ambayo aliona itamsogeza mbele kwani aliamini kabisa kwa maovu aliyoyafanya siku zake za kuishi duniani zilikua zimekaribia na alikua akimuomba mungu amsamehe kwa makosa ambayo aliyafanya toka alipozaliwa mpaka hapo alipo,alionesha wazi kweli alikua akijutia makosa aliyoyafanya kipindi chote cha maisha yake,alikua akilia kama mtoto mdogo,ungeweza kumtazama siku hiyo hakika ungemuonea huruma.....



    Mzee samwel alikaa muda mrefu sana pale hospitali huku machozi yakimtiririka katika mashavu yake,alijutia sana maana maamuzi aliyoyachukua ambayo yamesababisha mapaka mwanae kipenzi judith kupata mshtuko,baada ya kukaa kwa muda mrefu huku akilia,ghafla aliacha kulia na kusimama kisha alitoa kitambaa katika moja ya mfuko uliyopo katika koti alilokua amevaa,alijifuta machozi na kisha kuwaza,mimi ni mwanaume yanipasa kusimama imara na kupigania uhai wa michael na mwanangu judith,kukaa kwangu hapa na kulia hakusaidii chochote japo kwa kiasi fulani kumenipunguzia maumvu ndani ya moyo wangu yanipasa kusimama kama mwanaume na kuhakikisha michael pamoja na judith wanapona mapema na haraka iwezekanavyo ili waweze kufunga ndoa yao ambapo na amini wataishi kwa furaha na amani, baada ya kuwaza hayo taratibu alinyanyuka sehemu ambayo alikua amekaa na kuelekea katika chumba cha daktari,alipofika aliamua kugonga mlango ambapo daktari alimruhusu aingia nae bila kupoteza mda aliingia,baada ya kuingia alirudishia mlango na kukarishwa na daktari aketi katika moja ya viti vilivyopo katika chumba kile na baada ya salamu daktari yule alimuomba mzee samwel aeleze shida yake ili kama kutakua na uwezekanao wa kumsaidia atamsaidia na kama hamna uwezekano basi watajua namna ya kufanya, baada ya daktari yule kumaliza alimtazama mzee kwa macho yalioshiria kua alikua anataka kujua shida yake na bila kupoteza muda mzee samwel alianza kujieleza na kujitambulisha kua yeye ni mzazi wa michael pamoja na judith na yupo hapo ili kutaka kujua wanae hao wawili wanaendeleaje,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    daktari yule alikohoa kidogo kisha kumuangalia mzee samwel kwa umakini mkubwa na baada hapo alianza kwa kumpa pole kwa matatizo yaliyomkuta kwani matatizo ni moja ya changamoto tunazokumbana nazo katika maisha ya kila siku,baada ya maelezo hayo aliweka kituo na kisha kuendelea,mzee wanao wanaendelea vizuri hasa yule mwanao wa kike ambae nafikiri atakua judith,yeye ameshapata fahamu na inawezekana wakamruhusu mda wa jioni, kwa upande wa michael nae hali ni nzuri japo sio sana na hii ni kutokana na kupoteza damu nyingi hasa kutokana na majeraha aliyokua nayo na nafikiri baada ya wiki moja hali yake itakua sawa,.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog