Search This Blog

Tuesday, 17 May 2022

CHAGUO LA MOYO WANGU - 5

 







    Chombezo : Chaguo La Moyo Wangu

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Daktari yule alimaliza maelezo yake marefu ambayo alikua akimwambia mzee samwel,sawa nimekuelewa daktari ila nilikua na omba kama kuna uwezekano niende sasa hivi nikawaone wanangu na bila kikwazo chochote daktari yule alisimama na kumwambia mzee samwel amfuate ili ampeleke wodini ambapo wanae ndipo walikua wamelazwa,mzee samwel alitoka na kuongozana na daktari yule ambapo safari yao ya kwa kwanza iligomea katika chumba ambacho ndani yake ndipo alipokua amelazwa michael,mzee samwel alimuomba daktari huyo amsubiri hapo nje kwani anamaongezi ya siri ambayo alikua akihitaji kuongea na mwanae michael,daktari yule kwakua alikua ni muelewa alimruhusu mzee samwel aingie na yeye alibakia nje akimsubiri ili waweze kwenda katika wodi ambayo alikua amelazwa judith,mzee samwel baada ya kuingia katika chumba alichokua amelazwa michael alisogea karibu kabisa na kitanda ambacho alikua amelala michael na bada ya kufika alipiga magoti na kumuomba michael amsamehe kwa yote aliyomfanyia kwani anajutia kwa kila kitu,michael alitingisha kichwa kumaanisha kua alikua amemsamehe mzee yule na hii ni kutokana na kushindwa kuongea kwani alikua amefungwa nyaya katika mdomo baada ya taya zake kulegea kutokana na kichapo alichopokea kutoka kwa mzee yule,baada ya kumaliza maongezi yake na michael mzee samwel alitoka na kumkuta daktari akiwa bado anamsubiri na baada ya hapo waliongozana mpaka katika wodi ya wanawake na kuelekea katika chumba ambacho judith alikua amelazwa,baada ya kufika mzee samwel alimuomba daktari amsubiri hapo nje kwani pia alitaka kuzungumza na mwanae huyo jambo la siri ambapo daktari yule alimkubalia ombi lake,mzee samwel alifungua mlango wa chumba alichokua amelazwa judith kisha kuurudishia kwa ndani,alisogea mpaka karibu na kitanda ambacho judith alikua amelazwa,judith alimtazama baba yake kwa macho yaliyojaa chuki,alitokea kumchukia sana baba yake,alimuona kama mnyama kwa kitendo alichomfanyia michael,mzee samwel alilitambua hilo kupitia katika mboni za mwanae,alipiga magoti chini huku machozi yakimtoka na kumuomba mwanae amsamehe kwa ote yaliyotokea kwani ni shetani alikua amemtawala,judith huruma ilimuingia na akajikuta anamsamehe baba yake,baada ya kusamehewa na mwanae mzee samwel alisimama na kumbusu mwanae katika paji la uso na baada ya hapo alimnong'oneza judith kitu katika sikio lake,whaaaat... baba unasema kweli au unanitania,ni maneno aliyoyasema judith baada ya kupokea taarifa ile kutoka kwa baba yake,ndio mwanangu ngoja tusubiri apone maana madaktari wamesema baada ya wiki moja afya yake itakua imetengemaa,ila nataka asijue tumfanyie surprise.. aliongea mzee samwel kumwambia mwanae, judith alifurahi mno,taarifa aliyopewa na baba yake kwamba michael akishapona wataenda kufunga pingu za maisha kwa kuwa mke na mume kwake lilikua jambo kubwa sana,hakuamini kama ndoto yake ya kuwa na michael inaenda kutimia siku za hivi karibuni,hakika alifurahi mpaka akajikuta machozi ya furaha yakimtoka,nashukuru sana baba na mungu akubariki kwa kila jambo,aliongea judith kumwambia baba yake,usijali mwanangu ni jukumu langu kuhakikisha unakua na furaha muda wote,alijibu mzee samwel kumwambia mwanae..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Judith aliongea mengi sana na baba yake mzee samwel, na kila sikualikua akimuomba Mungu amsaidie michael apone haraka, hatimae baada ya wiki moja kupita michael aliruhusiwa hospitali na mzee samwel pamoja na judith walifika hospitali hapo kwaajili ya kuja kumchukua na kumpeleka nyumbani, hakika ilkua furaha sana kwa bibie judith hasa baada ya kumuona michael akiwa mzima tena, waliamua kukaa siti za nyuma za gari na kumuacha mzee samwel akiliondoa gari kwa kasi eneo hilo, michael alipatwa na mshtuko baada ya kuona gari haliendi muelekeo wa nyumbani na akahisi huenda judith ameshakubaliana na baba yake waende wakamuue kabisa, michael alipigwa na butwaa hasa baada ya kuona gari likipaki katika moja ya duka kubwa la nguo, hapo waliambiwa na mzee samwel washuke, michael pamoja na judith walishuka na mzee samwel akawataka waingie ndani ya duka hilo na kuwaambia judith achague shela na michael achague suti nzuri kwaajili ya harusi yao ambayo itafanyika sikuya jumamosi ikiwa imebaki wiki moja tuu kufikia siku hiyo,michael na judith walichagua nguo hizo na baada ya mzee samwel kulipia waliingia kwenye gari na safari ya kuelekea nyumbani ilianza, njia nzima michael na judith walikua ni wenye furaha na walikua wakipigana mabusu huku wakishikana shikana, michael uzalendo ulimshinda na akataka afanye mapenzi na judith humo ndani ya gari lakini judith alimzuia na kumuambia asubiri wafike nyumbani kwani wakifanya mapenzi humo watamkosea heshima mzee samwel, mzee samwel ni kama aliligundua hilo na aliendesha gari kwa kasi na baada ya dakika kadhaa waliwasili nyumbani, baada ya kushuka ndani ya gari, judith na michael walielekea chumbani huku wakimuacha mzee samwel akifanya taratibu za mwisho kwaajili ya harusi ya binti yake,michael na judith walipofika chumbani hakuna kilichofuata zaidi ya wawili hao kufanya mapenzi na kuziridhisha nafsi zao.....

    *********************************************

    **********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikua siku ya jumapili ambapo barabara zote za mtaa zilikua zimefungwa, watu walijipanga katika barabara kubwa wakiwa wanaimba na kushangilia msafara wa gari aina ya VX 8 zipatazo kumi na mbili huku gari zingine zaidi ya thelathini zikiwa nyuma ya msafara huo, msafara huo ulikomea katika moja ya kanisa kubwa na baada ya gari hizo kupaki michael akiwa amevalia suti nyeusi iliyomkaa vyema aliteremka ndani ya gari na kufuatiwa na judith akiwa ndani ya shela jeupe ambalo lilimpendeza na kufanya aonekane kama miss world, waliongozana mpaka katika madhabahu ya kanisa hilo huku wakifuatiwa na nderemo na vifijo kutoka kwa kina mama waliohudhuria sherehe hiyo, mchungaji alifika na kuwafungisha ndoa michael pamoja na judith na wakawa mwili mmoja, baada ya harusi hiyo kuisha mzee samwel aliwakabidhi michael pamoja na judith baadhi ya miradi yake, nyumba pamoja na gari, huko maisha yaliendelea na kila siku judith huwa anamwambia mume wake michael kuwa anampenda sana na hatokuja kumsaliti ukizingatia magumu waliyoyapitia...



    MWISHO...

0 comments:

Post a Comment

Blog