Search This Blog

Monday, 16 May 2022

MTOTO WA BOSS WANGU - 5

 







    Chombezo : Mtoto Wa Boss Wangu

    Sehemu Ya Tano (5)



    Kikao cha dharura cha watu watatu kiliendelea pale nje ya hospital baba Rose, mam yake pamoja na kaka yake na Monica lengo kubwa ni kutaka kujua hatima ya mtoto wao Rose aliyeonesha msimamo imara wa kumtetea Wangesi akitaka kuishi nae Baba yake alichanganyikiwa kwa sababu alianza kufukiria gharama za shule hakutaka kukubaliana na matokeo alisistiza ahiwezekani tena kwa ukali sanaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mke wake alianz kuwa na hofu maana msimamo wa mme wake alihisi utamuondoa Rose duniani machozi yalianza kutirirka huku akimkumbatia mme wake na kusema mme wangu kumbuka yule ni damu yetu kwa nini unakubali tuipoteze nakuomba tuweze kuwaruhusu tu waishi wote huenda wakaw katika msimamo mzuri wa maisha



    Maana wanapendana sana mme wangu sipendi kumzika mwanangu nampenda sana embu usifikirie gharama za kusomesha japo na mimi inaniuma ila maisha yake kwnaza ona alikuwa na furaha baada ya kumona kijana yule nakuomba niko chini ya miguu yako mme wangu,



    Muda huo machozi yalianza kumtoka Baba Rose macho yalianza kuwa mekundu aliumia san maana hakutaka mtoto wake aolewe na masikini na kwa umri ule alisema mke wangu siwezi kumruhusu mwanangu kuolewa angalia umri wake ule ni wa shule kabisa tena yuko kidato cha sita hapana sikubaliani na wazo hilo kabisa nampenda mwanangu.



    Kaka yake na Monica alimshika mkono Baba yake na Rose na kusema Wangesi namfahamu japo sikutaka kufunguka mapema sna kuhofia usalma wangu na wa kwake na mimi niko tayari kumkabidhi nyumba ya kuanzia maisha naomba uwe na moyo wa kuachia tusitake yafike mbali maana huenda siku moja ukaanza kulilia maiti ya mwanao.



    Endapo atasikia habari hii ya yeye kukataliwa kumbuka mapenzi yana nguvu sana yatapelekea mwanao kupoteza uhai kama huna imani na wangesi nakuomba umpe shart moja endapo mke wake atajifungua asimuache tu nyumbani itabidi amrudishe shule please mzee okoa maisha ya kijana wako Rose.



    Hapo kidogo mzee aliinua shingo na kumfuata mke wake ambaye alikuwa amejikunja kama mtu anayehis baridi mzee alimsogelea mke wake na kusema mke wangu watoto hawa wamependana haina haja ya kuendelea kuumiza kichwa



    Nadhani wataishi vizuri Mungu atawasaidi na sis inatubidi tufanye kitu kuokoa maisha ya mama na mtoto nadhan tuna nyumba mbili moja wataenda kuishi huko huku wakijipanga kutengeneza mazingira yao na gari lile aina ya NOAH tuwakabidhi kwa ajili ya kuendesha maisha yao



    Hapo mke wake aliotabasam na kusema nashukuru mme wangu kwa kuweza kuingiwa na moyo wa ujasiri kiasi hicho Rose ndio furaha yangu na ndio mwanangu wa kwanza aliyesababisha mimi kuingia leba kwa mara ya kwanza



    Hivyo sikutaka nimpoteze mapema; Hapo walikumbatia wote wawili huku Kaka yake na Monica alitabasm na kusema hapo saw kwa Wangesi naamini wataishi vizuri tena watejenga maana ni mtu mwenye juhudi ya kutafuta,



    Walirudi wodini wote watatu na kuwakuta Wangesi na Rose wakiwa wanaongea huku Wangesi akiwa hana amani na maisha yake alistuka baada ya kuwaona wakirudi tena; Mama alitabasam na alienda kumkumbatia Rose na kusema nikutakie maisha mema wew na mmeo Mungu awe nanyi Rose alifurahi alimkubatia Mama yake kwa furaha na kusema asanteni Baba na Mama.



    Mzee nae alizungumza kwa huzuni kubwa san kitu ambacho kilimfanya Rose atoe machozi maana hakuwahi kuona baba yake akilia alianza kujihis mwenye hatia sana mbele ya baba yake lakini alipiga magoti na alimuoamba msamaha baba yake na mzee nae alimuinua na kusema



    Nimeshakusamehe na nyumba yangu ile mpya nimewakabidhi kwa muda mpaka pale mtakapo simama imara nadhani ina kila litu ndani nendeni mkayaanze maisha mapya na harusin yenu tutaiandaa baada ya wew kujifungua hivyo niawatakie maisha mema,



    Baba alichukua funguo za gari alimkabidhi wangesi na funguo za nyumba pia hapohapo aliondoka hakutaka kuongea tena,



    Mma naye aliondoka na kaka yake na Monica alienda kulipia matibabu yote aliwachukua na kuwapeleka kule walikoambiwa kwenda kuyaanza maisha mapya walifika na wlifungua nyumba ile ilikuwa kubwa san yenye kila kitu ndani Wangesi alifurahia san



    Lakin alianza kuwaza kujenga ya kwake endapo tu atapata hela zake na gari lao wangesi alianza kufanya biashara ya kubeba watu kuwapeleka sehemu tofautitofaut pale mjini'

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waliishi kwa furaha san kusema ukweli hakuna mapenzi mazuri endapo mmekutana wote mnapendana na kusikilizan wangesi maisha yalianza kubalida baada ya miezi kadhaa mwili wake ulianza kunawili na mke wake nae kila jioni wangesi alimtembeza sehemu mbalimbali kwa miguu akimfanyisha mazoezi maana ujauzito ulikuwa mkubwa alikuwa amekaribia kujifungua.



    Maisha mapya yalianza kati ya Wangesi na Rose huku ujauzito ulikuwa sana na muda wa kikaribia kujifungua ulikaribia hivyo Wangesi alikuwa na jukumu la kufanya mazoez ya kutembea yeye na mke wake hakika Wangesi alimpenda sana mke wake maana hakutaka kumkosea mke wake kulingana mazingira walitoka.



    Wangesi nae aliendelea kufanya kazi zake za kubeba abiria alifanya kwa upendo wote na hakutaka kuitunza vibaya gari walilepewa na baba yao aliitunza sana na watu wlimpenda sana kutoka na ukarimu wake



    Hivyo biashara yake ilikuwa rahisi sana kuifanya alifanya juhudi sana kwenye kazi zake na Rose nae hakutaka kumsumbua Mme wake kulingana na anavyompenda alitamani muda wote akae karibu na Mme wake na wangesi nae kila alipokuwa akitoka kazini alimletea zawadi hata kama ilikuwa ndogo alihakukisha anamletea mke wake hivyo upendo wao uliendelea vizuri.



    Muda ulienda Wangesi nae hakuwa anakula tu ovyo aliweka akiba kila alipokuwa anatoka kazini kibubu chake liliqnza kuwa na hela nyingi Sana baada ya kuona zimekuwa nyingi alijadili na mke wake kununua uwanja wao wa kujenga nyumba na walitafuta uwqnja na kununua mbali na pale walipokuwa wakiishi baba yake na Rose alifurahi sana alijisemea kumbe mwanangu amepata mwanaume mwenye akili sana ona Muda mchache tu wamenunua uwanja wao nimefurahi mke wangu



    Mama Rose nae alisema kweli Mme wangu huyo ni mwanaume mwenye malengo sana ananipa faraja sana baadae huenda wakawa kwenye mazingira mazuri sana maana kwa kasi hii ni nzuri..



    Rose nae alifurahia sana muda huo wakati Rose anaendelea kufurahi kununuliwa kwa uwanja alishikwa na uchungu wa kujufungua wangesi nae hakukawia almuweka Rose ambaye ndiye mke wake ndani ya gari na kumpeleka hospital alimuwahishq hospital na baada yq kufika alichukuliwa moja kwa moja hafi wodi ya kina mama .



    Wangesi alibakia nje huku akiomba Mungu amsaidie mke wake ajifungue salama baada ya nusu saa wangesi aliitwa na doctor alipewq hongera sana mke wako amejifungua salama umepata mtoto wa kiume.



    Wangesi alifurahi sana alipiga magoti alomshukuru Mungu kwanza maana safari ya maisha yake ilikuwa ya vikwazo sana hapo aliinuka simu na kumpiga baba yake na Rose na kumpa taarifa hii



    Baba Rose pamoja na mke wake walifurahia sana muda huo huo mama Rose aliingia ndan yq gari kwenda hospital kwenda kumuona Mtoto wake nq mjukuu alipitiq sokoni kwanza kununua nguo na vitu vingine vya Mtoto.



    Muda huo Wangesi alichukua jukumu la kukimbia nyumbani kwa ajili yq kutengeneza chakula kwa ajili ya mke wake alifurahia sana kupata mtoto na kuongeza familia yake.



    Baada ya masaa kadhaa Rose aliruhusiwa kurudi nyumbani yeye na mtoto wake huku mama yake Rose akiwa dereva wake hapo maisha ya familia ile yalizidi kuwa ya upendo na furaha muda wote.



    Muda ulienda huku Wangesi aliipenda familia yake mtoto wake aitwae Jackson aliendelea kukua baada ya mwaka wanfesi alojenga nyumba yake huku baba Riwr alimfunguliq garage yake huvyo Wangesi nae aliendelea kuwa na maisha mazuri muda huo Rose alirudi shule Kwa ajili ya kumalizia Elimu yake ya kidato cha sita na hatimae kuingia chuo kikuu



    Monica nae shuleni kwake alifukuzwa kwa ajili ya umalaya wake hakuweza kumaliza baada ya kugundulika ana ujauzito na ukimwi juu alioambukuzwa na mwalimu wake aitwae Nyambole

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wangesi maisha yalienda vizuri baafa ya kuwa msimamizi mzuri wa Mali zile hakika baba Rose alijidai sana kumpata Wangesi alijisemea mwenyeji Mungu nisamehe kwa kile nilichotenda juu ya kijana Wangesi ni mwanaume mwenye akili sana.



    Maisha ya Wangesi yalibadirika sana na alibadilisha familia nzima ya kwake na familia ya baba Rose wote waliishi Kwa upendo wa hali yq juu dharau zote ziliisha na heshima ilitawala.







    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog