Chombezo : Sema Jina Langu Mpenzi
Sehemu Ya Nne (4)
Wafuasi wengine waanze kumkimbiza baba yake moureen aliyekuwa kaganda baada ya kupata na kama mshangao baada ya kuona mfuasi wake wa pembeni kupigwa mshale wa kichwa na kudondoka papohapo.wengine wakamfuata na kumnyanyua robertson ambaye alikuwa bado anaguliwa maumivu ya kupigwa mshale wa mkono lakini kabla hata hawajaondoka naye mishale miwili ilitua katika miguu ya wale wafuasi wa robertson ambao walishafanikiwa kukimbia nakujikuta wakimuacha robertson ambaye baada ya kusikia wafuasi wake akilalamika akajikuta mwenyewe akikaza mwendo na kutaka kukunja lakini mshale mwingine wa bega mkampata na kumfanya atoe ukelele mwingine lakini hakuweza kusimama.niliendeleaa kushangaa huku nikiendeleaa kuwaangalia wafuasi wa robertson waliopigwa mishale miguuni ambao wote kwa pamoja wakati huo walikuwa wanaugulia kwa kutoa kelele za maumivu huku wote wawili wakiangaika kuichomoa mishale hiyo iliyopenya katika miguu ya kila mmoja huku kila mmoja akipigwa mguu wa kulia.nikiwa bado natafuta ni nani aliyekuwa akirusha mishale hiyo kwa kugeuka nyuma lakini kabla hata sijageuka upande mwingine mishale miwili tena ikapita tena juu ya kichwa changu na kuwapata wale wafuasi waliokuwa wakiugulia maumivu CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/mishale ya kichwa kila mmoja na kusababisha wote wafe hapo hapo.ghafla nikaguswa bega kwa nyuma na mkono ulionekana mgumu kutokana na kuniumiza pale aliponigusa kisha nikageuka na kumuangalia aliyenigusa ambaye macho yangu yakagonga katika jamaa aliyeonekana mzungu kabisa kwa macho huku akiwa kavaa kofia kubwa iliyofunika sura yake.nilimuangalia sana huku naye akiwa ananiangalia mimi pia mdomo wangu ulikuwa mzito sana kunyanyua mdomo kuongea na kujikuta nikiendelea kumuangalia mzungu huyo ambaye akanishika shika maeneo ya bega na kupandisha kwenye shingo yangu nakunibonyeza sehemu katika shingo ambapo baada ya kunibonyeza giza nene likatanda katika macho yangu na kuzimia hapo hapo.Nilishtuka na kujikuta nikiwa nimelala katika chumba chenye mwanga hafifu huku ni kibatali tu ndio nilikiona kikiwaka.jitahada zangu za kuamka ziligonga mwamba baada ya kujitonesha mwenyewe vidonda vyangu mgongoni na kunifanya nitoe ukelele wa nguvu na kuhema juu juu.nikamshuhudia mzungu huyu aliyekuwa mzee akija pale pale kwangu nakuniangalia kisha akachukua maji maji yaliokuwepo kwenye chupa na kuanza kunimwagia katika vidonda vyangu vilivyokuwepo nyuma ya mgongo na kunifanya nianze kuugulia tena kwa maumivu hali iliyomfanya hata yeye awe ananiangalia kwa kunikazia macho..
"Kijana unaitwa nani??"
"naitwa pa..blo"
"nyanyuka hebu jitahidi kunyanyuka"nilijikuta nikiingia msangao baada ya mzungu huyo mzee kuongea kiswahili fasaha kabisa huku nikifuata ushauri wake wakunyanyula kwa shida huku nikimuangalia mzee huyo ambaye naye alikuwa bize akaniangalia kwa ujasiri.
"Pablo mimi naitwa Gardner thomas ni mtalii ambaye nilikuja huku bagamoyo kutoka kwetu switzland sikufanikiwa kurudi baada ya ndugu zangu niliokuja nao kuuawa na sisi kuporwa dhahabu ambazo tulizinunua kwa kiasi kikubwa sana Mimi ni mzee licha sio mzee sana ni mimi ambaye niliweza kukimbia nakuanzisha maisha yangu hapa porini vp kwani wewe una tatizo gani.". nilimuangalia mzee gardner kwa muda kisha bila ya kuficha nikaanza kumueleza hali iliyonikuta mwanzo mwisho na kumshukuru kwa kuniokoa maisha yangu ambayo nilihisi yalikuwa hatarani kukatika.
"Usijali utakaa hapa mpaka utakapo pona kisha nitakusaidia kuweza kulipiza kisasi kwa wale wote waliokutendea ubaya." hakika baada ya gardner kunambia vile nilifarijika sana huku nikiendelea kummiminia shukrani za dhati kabisa mzee huyo.siku sita kudondosha chozi kila nilipokuwa namkumbuka moureen kutokana na kauli yake aliyoitoa robert kuwa moureen alishakufa niliendelea kuombeleza mwenyewe huku mzee gardner kuendeleza kunifariji kwa kunipa moyo huku akiendelea kunipa tiba mbadala ya vidonda vyangu.hakika siku zilichomoka na kufika mwezi ambapo kwa kutumia dawa za mitishamba vidonda vyangu vilipona kabisa tuliishi maisha ndani ya pori tukitegemea vyakula vya wanyama kama sungura na ndege kama njiwa waliokuwa wapo wengi katika pori hilo.hali yangu iliendelea kumridhisha gardner ambaye akaanza kunipa mazoezi yakurainisha viungo kwa lengo la kujiweka sawa kisha nakuniahidi kunifundisha kupambana na watu kwa lengo la kwenda kulipiza kisasi kwa wale wote walionikosea.roho ya chuki ikazidi kuniingia huku kila nikikumbuka yaliotokea nilijikuta nikishikwa na hasira za ajabu............
Mazoezi ya kukimbia umbali mrefu msituni na kuruka ruka baadhi ya mawe yaliowekwa na mzee gardner yalizidi kuniweka katika hali nyingine tofauti ya ukomavu wa mwili wangu kwa muda mchache nikajikuta nikiingiza vitu vingi katika mwili wangu zilivyonisaidia kuniweka sawa kupita kiasi.kuendelea vizuri kwangu vizuri katika mazoezi kulizidi kumfurahisha sana gardner ambaye alianza kidogo kidogo kunifundisha jinsi ya kukabiliana na adui.
"Kila kitu unachotaka kukifanya lazima uwe na nia nacho je mpaka sasa ushawai kupigana na mtu yoyote pablo."
"No mzee sijawai sikumbuki labda utotoni kwangu ila ukumba huu sijawai ooo nilishawai baada ya kushuhudia tukio la shangazi yangu kufa kama nilivyokuambia kwamba nilipata hasira iliyozidi kipimo na kujikuta nikiwazamia baadhi ya wafuasi wake robert na kuwauwa laki..."
"Ooo basi nikuambie kitu hebu attack me(nivamie mimi)"
"Eeeee unasema??
"Nivamie kijana anza kunishambulia kama unapigana na adui" mzee gardner aliniambia na mimi bila ya kusita nikajikuta nikimvamia mzee huyo na kuaanza kurusha ngumi nzito nzito zilizopanguliwa vikali kwa ustadi wa juu kisha mzee huyo akanipiga mtama na uliosababisha nidondoke.
"Simama attack me haraka kumbuka familia yako iliyouwawa kikatili kumbuka ulivyotaka kuuwawa kumbuka kwa ushampoteza mchumba wako uliyempenda kupitiliza." hakika maneno hayo ya mzee gardner yalinipandisha mori na kujikuta tena na simama na kuanza kumvamia lakini nilikuwa narudisha chini kwa mtama kila ninapojaribu kumvamia mzee huyo.alionekana kama mzee sana lakini alikuwa vizuri sana na kusababisha mimi kumvamia karibia mara hamsini lakini sikufanikiwa hata kumpata hata kidogo na kujikuta nikirusha ngumi kibao zilizokwepa kwa ufundi kisha nakudondosha.
"Nahisi utakuwa utumii akili unajua kupigana na mtu unatakiwa utumie akili huyu anakujaje anaendaje umenielewa"
"Yes nimekuelewa"
"Na kitu kingine angalia balance yako ya mwili kisha msome adui yako anakufuata vipi kamwe katika miongoni mwa sheria za kumpiga adui yako wewe unatakiwa umfuate sio yeye akufuate wewe hivi ushawai kuangalia ngumi alizokuwa anapiga tyson"
"ndio"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sasa ngoje niaanze kukufundisha" hakika maneno ya gardner yalinijenga sana kisaikolojia na kujikuta nikienda naye sawa sawa katika kila zoezi alilokuwa akinipa.Ndani ya siku saba tu nilijikuta nikiwa nimeivaa na kuanza kupamba naye mzee gardner ambaye alifurahishwa sana na kiwango changu cha upiganaji.hakika hali ya kutaka kulipiza kisasi ilizidi kuniingia katika kichwa changu huku maneno ya mzee gardner yalizidi kunishawishi kulipa kisasi.hakika mzee huyo hakuishia hapo pia alinifundisha jinsi ya kutumia mishale kulenga shabaha zoezi ambalo niliweza kuliweka kichwani kwa muda mfupi sana na kunifanya na mimi niweze kulenga shabaha kali.Siku moja mimi nikiwa nyumbani mzee gardner siku hiyo alienda porini zaidi sehemu aliniokoa mimi kwenda kuchukua dawa zake za mitishamba ambazo mara nyingi alikuwa anapendeleaa kuzitumia.nikiwa peke yangu mimi niliendelea kufanya mazoezi yakujiweka sawa kama nilivyozoea kisha nakuamia upande wa mishale na kuanza kulenga lenga vitu vilivyokuwepo hapo nje kama miti huku nikijitahidi kulengesha sehemu ambayo nilikuwa najisikia kulengesha.ghafla nikiwa katika zoezi hilo nikaanza kusikia majani yakianza kuchakarika huku na huko na kuashiria kuwa kuna kitu kibaya kinakuja bila ya kulaza damu nikaanza kujiandaa kwa kuweka mishale yangu sawa huku mwingine nikiuweka sawa kwenye upinde na kuvuta kabisa na kusubiri kinachotokea ili nifyatue.Macho yangu kakuta na mzee gardner aliyekuwa akikimbia kwa kasi na kunifanya mimi nizidi kuwa na hofu kubwa iliyosababisha nipigwa na butwaa la nguvu.
"Pablo kimbiaaaaaaa" maamrisho ya kukimbia hakuniingia kabisa nikajikuta miguu yangu ikifa ganzi na kujikuta nikiendeleaa kusimama pale pale na kuangalia nini kilichomfanya mzee gardner kukimbia.nikiwa katika mshangao ghafla gari kubwa likatokeza na kufungwa breki umbali kidogo na nyumba yetu pale kisha watu wapatao ishirini wenye kuvaa miwani meusi na suti nyeusi wakashuka huku wakiwa na silaha ambapo baada ya kushuka tu wakaanza kunimiminia mimi risasi ambazo zote hazikunipata kisha na mimi pia nikaanza kukimbia kwa kasi.nilianza kukimbia na kuanza kuita jina la gardner bila mafanikio huku kila nilipokuwa naangalia nyumba nilikuwa nafuatwa na watu wale ambao nilishawajua walikuwa ni wafuasi wa robertson.sikutaka kumpambana nao peke yangu kwa kuhofia kwamba wapo wengi.mbio zangu ziliishia katika kichaka chenye majani mengi ambayo yalinisaidia kujificha na kuanza kuangalia nini kinachofuata hakika nilipotezana na mzee gardner alitangulia kukimbia nikiwa katika hali ya kujificha bahati nzuri nilikuwa sijasahau upinde wangu na mshale ambayo nilianza kuiweka sawa baada ya kumuona jamaa mmoja ambaye alikuwa kashikilia risasi vizuri huku sura yake akiwa ameikunja kuasiria kwamba yupo kazini.ghafla mzee gardner akatokea pasipo julikana na kwenda kumkaba jamaa huyo ambaye baada ya kukabwa akatoa roba ya mzee huyo na kuanza kumtembezea kichapo kikali kilichoniogopesha sana na kujikuta nikishindwa hata kuingilia kutokana na nguvu nyingi alizokuwa nazo jamaa huyo.baada ya kuhakikisha kuwa kamdhibiti jamaa huyo akaokota bunduki aliyoidondosha wakati akipigana na mzee gardner kisha bila hata ya kuremba akafyatua risasi iliyompata sasa mzee gardner ya kichwa na kufa hapo hapo.hakika macho yangu yakanitoka ghafla nikajikuta nikipiga kelele na kutoka kichakani na kwenda kumvamia jamaa huyo kisha.............
Kilichonigharimu kuwa kwa wakati huo nikiwa na hasira ambazo zilizokuwa zimefika pomoni nikajikuta kwa hasira nikimvamia jamaa huyo ambaye baada ya kusikia kelele zangu huku nikiwa namfuata kwa mfumo wa kukimbia jamaa huyo akazunguka kwa kipiga msamba ambapo akanikwepa kisha mimi nikajikuta nikivamia mguu wake alioutegesha baada ya kupiga msamba na kusababisha mimi nijikwae katika mguu wake na kudondoka vibaya huku speed yangu ya kukimbia ikasababisha nirushwe vibaya baada ya kukwaa mguu huo.hali ya kubimbirika ndio ikafuata huku na kusababisha nipate maumivu makali sana ya mgongo.nikaanza kunyanyuka kwa shida sana huku nikiugulia lakini kabla hata sijanyanyuka ngumi kali sana ya uso iliyonitoa damu puani ikatua katika uso wangu na kunirudisha tena chini huku maumivu ya mgongo sasa yakaanza kuchanganyika na uso kutokana ngumi niliyopigwa ilikiwa ni kali sana tena ikazidi kuniua nguvu.hasira zote nilizotoka nazo zikaisha na kujikuta tena nimepoa.juhudi zangu tena zikagonga mwamba baada ya jamaa huyo huyo tena kunikalia kwa juu na kuanza kushambulia tena uso wangu kwa ngumi nyingi nyingi na kuzidi kunipasua uso wangu ambao nilijaribu sana kujiziba kwa mikono lakini jamaa huyo akafanikia tena kunikamata mikono yangu vizuri katika miguu yake na kunizidi nguvu kabisa iliyosababisha nishindwe kumtoa juu aliponikalia na kumpa nafasi ya kunisambulia kwa ngumi zilioambata na vichwa vikali vilivyozidi kuleta maafa katika sura yangu.baada ya kushindwa kabisa kutoa katika mwili wangu nikajifanya nimezimia baada ya ngumi zisizo na idadi kuzidi kumiminika nikajifanya nimepoteza fahamu na kusababisha jamaa huyo aache kunisambulia na kisha akanyanyuka.kupitia jicho langu moja niliangalia kidogo huku nikimzuga jamaa huyo ambaye alidhania nimezimia nikamuoana akichukua bunduki aliyoiyutumia kumuulia mzee gadner na kuanza kurekebisha vizuri kwa kuiweka risasi na kujiandaa kunielekezea mimi.ile kwangu ndio ilikuwa nafasi kubwa sana niliyoipata baada ya kumuona jamaa huyo akiwa anajiandaa kunipa risasi huku miguu yake akiwa kajichanua.kwa nguvu zote huku nikiwa nimelala nikampigapp jamaa huyo teke kali sana lililompata sehemu nyeti katika silaha yake anayoitumia katika uwanja wa mapenzi na kumfanya atoe ukelele mkali sana wa maumivu na kujikikuta akiachia bunduki yake aliyoishika na kuidondosha chini huku naye akadondoka chini huku akipiga magoti na mikono yake ikiwa imeshika sehemu ile niliyompiga.nikabimbirika kidogo kisha nikajibetua kwa ufundi na kusimama na kwa mwendo wa taratibu nikaenda kuichukua bunduki ile aliyoidondosha na kumuelezea huku nikimuangalia kwa jicho la hasira kali.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Fuck you fuck you Msenge wewe unasubiri nini niue sasa mrembo wew" yule jamaa akaanza kunishambulia kwa matusi huku akijaribu kunitemea mate mdomo wangu ulikuwa mzito sana kumjibu huku nikiwa na hamu kubwa sana ya kumjibu.kumbukumbu ya kukumbuka kuwa alikuwa hayupo peke yake ndio ilinishtua na kujikua nikimfyatulia risasi iliyompata sawa sawa katika kichwa na kufumua kabisa ubongo wake ulimwagika baada ya kumpiga risasi ile.nilimsogelea mzee gardner ambaye roho yake ilikuwa ishaacha mwili lakini kabla hata sijainama kumuangalia mzee gardner wafuasi wengine wapatao watano wakiwa wanakimbia nikawaona kabla hata wao hawajaiona bila ya kuchelewa kupitia bunduki ile niliyokuwa nayo kwa shabaha ya hali ya juu nikawafyatua wote watano waliopoteza maisha hapo hapo.sikutaka kwanza kushughulika na mzee gardner baada ya kukumbuka kuwa licha ya kuwauwa wafuasi sita nikakumbuka kuwa walikuwa wengi na nilikuwa sina budi kukabiliana nao sikutaka tena kuvaana nao kwa kutumia risasi nikachukua mshale niliokuwa nao kisha nikaanza kuwafuata kwa mwendo wa kujificha ficha.nikiwa katika mawindo nikawaona wafuasi wengine wakiwa wamekaa baada ya kuonekana kama walikuwa wamechoka.kwa hali ya kujificha nikaanza kuwalenga wote wanne ambao baada ya kufyatua mmoja wao mshale wa jicho ambao ulisababisha wengine wachanganyikiwe na kuanza kutaka kukimbia lakini sikuruhusu hata mmoja kunitoka machoni mwangu wote niliwashambulia kwa mishale niliyokuwa nayo na kuwauwa.hakika kila nilipokuwa nakutana nao niliendelea kuwauwa kwa mishale yangu na kusababisha vifo vya wafuasi wale wapatao ishirini ambao nilihisi kuwa walikuwa wametumwa na robertson.Baada ya kumaliza shughuli ya kuwauwa wale wafuasi wa robert nikaenda katika mwili wa mzee gardner ambapo kwa kutumia mawe nikaanza kumzika kwa kumfunikia na mawe hayo mzee huyo ambaye sitamsahau kamwe mpaka nakufa kutokana na kukaa naye katika muda mchache na kujua vitu vingi katika maisha yangu katika kipindi hicho kigumu nilichopitia.baada ya kumaliza kumzika nikamswalia na kumuombea kisha nikaanza kuondoka huku nikikumbuka kuwa kulikuwa na gari walilokuja nalo ambalo nilitaka kulitumia kwenda jijini dar ambapo nilikuwa na kazi moja tu ambayo ni ya kwenda kumuua robertson mugalula na baba yake moureen kwa kulipiza kisasi cha familia yangu,mzee gardner na moureen ambaye licha ya kuambiwa na robertson mugalula kuwa alishamuua lakini nilitaka kwenda kuhakikisha.nikajiandaa vizuri kwa kuchukua mshale ikifuataiwa na baadhi ya bunduki za wale wafuasi niliowauwa kwa kutumia mishale.baada ya kumaliza nikaelekea katika gari lile aina ya basi kubwa la wale wafuasi waliokuja lakini baada ya kulifikia karibu nilimuona mtu aliyekaa katika sehemu ya dereva huku akiwa amelala. nikanyata mpaka katika mlango wa dereva ambao baada ya kujaribu kuufungua nikagundua haujalokiwa nikiwa nimejiandaa kwa silaha nikaufungua mlango alikaa dereva yule na kumrusha kutoka kiti alichokaa mpaka chini ambapo kutokana alikuwa ana usingizi mzito akajikuta akishtuka sana na kubaki akitumbua macho.akiwa katika hali ya kushangaa nikamtandika na kitako cha bunduki kilichomzimisha kisha nikamfunga kamba na kumpandisha kwenye gari na mimi kukaa katika siti ya dereva na yeye kumueka katika sehemu ya pembeni ya siti ya dereva.sikutaka kumuua kwa sababu nilitaka msaada wake kwanza kabla ya kumuaa.Nikiwa katika harakati za kumsubiria ahamke ghafla dereva yule akaamka kwa muda wa kama lisaa na kuanza kutetemeka baada ya kuniangalia mimi nilikuwa uso wangu umetapaakaa damu kutokana na zile ngumi kali za yule jamaa zilizonipasua sana huku nikiwa nimeikunja kwa hasira.
"Pleaase naomba usiniuwe usiniuwe mimi sina hatia bado Familia yangu inaniitaji mimi dereva tu nionee hurumaa."
"Umetumwa na nani uwaendeshe hawa jamaa waje kuniua."
"tamaa tu ya pesa nimetumwa na muhesimiwa robertson mugalula naombaa usiniuwe iihiiiiiii iiiiiiiiiiiiiiiiii"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sitaki kusikia na kuona machozi yako kwa sababu una nipigia kelele nitakuua sasa hivi pumbavu wewe robertson yupo wapi"
"yupo kwake sasa hivi na familia yake wakijiandaaa mipango yao ya harusi"
"Harusi???? anamuoa nani??"
"sijui mourina"
"Whaaaaattttt???"
"ee...a..na..itw mouria..."
"Lini anamuoa"
"Kesho mkuu ila naomba usiniuee" hakika habari zile zilikaanza kunipa nguvu ya ajabu kidogo kidogo kutokana nikaanza kutoa hofu juu ya moureen ambaye nilidhania kua walishamuua na kisha nikamfungua jamaa huyo dereva aliyeitwa steven kisha nakuanza kumuelezea matukio yote ambapo kwa huruma akahidi kunisadia kwa wakati huo.nilimpisha katika siti ya udereva ili aendeshe yeye mwenyewe.Akili yangu ikaanza kuwaza kesho nakuanza kufikiria nitasimamishaje kesho yake harusi ya robertson na moureen ambayo amri mashauri yangu ya kichwa yakaanza kufikiria ulinzi utakuwepo katika harusi hiyo kutokana na kumjua vizuri robertmugalula.....
Safari yetu ikaanza kwa spidi kubwa kutokana na dereva huyo kuwa Makini sana na uwezo mkubwa wa kuendesha gari. kwa muda huo ilikuwa kama saa kumi na mbili jioni inaelekea saa moja usiku.wakati wote tukiwa barabarani dereva alikuwa anawaangalia angalia wenzake ambao kutokana na pesa kubwa aliyokuwa nayo Robert mugalula aliwaweka katika Barabara zote.Tukiwa tunakaribia kuvuka mataa ya mwenge ghafla gari yetu ikasimamishwa na waliotusimamisha walikuwa si wengine Bali ni majamaa wawili waliovaa suti safi kabisa nyeusi na miwani yao na muda wote walionekana wapo kikazi zaidi kutokana na kuonyesha katika sura zao.
"steven vp hali ya huko mmefanikiwa??" jamaa mmoja kati ya wale wawili akamuuliza swali dereva wakati huo mimi nilikuwa tayari nishajificha na nilikuwa nasikia yote yaliokuwa yanaongelewa.
"n...di..oo.mkuuu wameshamaliza kazi mbona"
"wapo wapi sasa mbona gari jeupe Maana boss robert Alikuwa anasubiri Majibu kutoka kwenu kupitia Alexandre ambaye mpaka sasa simu yake inaaita Bila ya kupokelewa"
"Aaaa siunajua wale wanapesa bana ndio wamebaki wanakunywa Mapombe yao huko huko Ila Na tumaini Waturudi....Mhesimiwa"
"Mmmh Alexandre Bana naye basi sawa wewe kapumzike mpaka kesho wewe si umepewa kadi ya Harusi??"
"Nimepewa Nitakuja" steven alimwambia Jamaa huyo ambaye baada ya kuambiwa hivyo akaturusu tuondoke hapo mimi ndio niliboibuka Baada ya kujificha.Safari yetu ndefu kutoka Bagamoyo porini ikagota katika Mitaa ya Magomeni katika Nyumba aliyopanga steven na kushuka Hapo Ambapo Bila ya hiyana steven akanikaribisha kwake.Licha ya kuniambia Alikuwa anafamilia nisimuue familia yenyewe sikuoni Hali iliyonifanya niwe na Machale machale naye.hakika kama inavyosema usimuamini mtu usiyemjua hali hiyo ya kutomwamini steven ilitawala katika kichwa changu na kujikuta Nikijiandaa Muda wote na kama kikinuka basi mimi nilikuwa tayari kabisa kukiendeleza.Nilijikuta nikikataa chakula alichopika na kumshangaza sana.
"ilikuwaje mpaka ukawa unafanya kazi na robertson"
"Ugumu wa Maisha kaka halafu mimi ni Dereva mwenye vyeti vizuri Mimi kwa robertson nilionganishiwa tu na Rafiki yangu mmoja hivi"
"Oooo kwa hiyo ushawai kuuua"
"Aaaaaa...hapana mimi..sio jambazi kaka mimi dereva tu nawapeleka wanafanya kazi zao kisha Tunarudi"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ni kazi gani wanazofanya Ambazo wewe unawapeleka"
"Kama kuua,Kwenda kuiba kwenye Mabenki haya katika shughuli za Madawa ya kulevya yote hayo" hakika siku hiyo tuliongeaa mengi Lakini kila nilipokuwa nakumbuka harusi kesho ya robert akimuoa moureen ndio ilinifanya niwe na shauku nilipomuumwambia steven yeye akaniambia atanisaidia na michogo yote nimuachie yeye.Kama kawaida mida ya saa nne nne usiku wote tukajikuta tukilala.Kwa mimi Nilizuga kama nimelala lakini ilikuwa ni kama kumzuga Steven ambaye kwa muda huo alishajua kuwa nilimuamini vya kutosha na kumuachia yeye kila kitu.katika mida ya saa sita sita hivi usiku ghafla steven dereva akaamka alipoamka akanisogelea mpaka nilipo mimi na kuanza kuniangalia kwa muda na kuanza kunitingisha tingisha vizuri kwa lengo la kujua je nimelala fofofo au la.mimi kama kawaida nilijilegeza kabisa na kujifanya nimelala usingizi mzito kwa lengo la kumzuga kabisa steven ambaye baada ya kugundua kuwa nimelala kabisa fofofo akanyata na kwenda kuchukua simu yake ya mkononi niliyomuana nayo ameishika mkononi kisha mdogomdogo akaanza kutoka nje kwa mwendo wa kunyata.Baada ya kutoka nje mwanaume kwa hasira nikanyanyuka na kunyata kisha nikaufungua Mlango polepole na kutoka nje.Macho yangu yalimshuhudia steven akiwa anabonyeza bonyeza simu mara aweke sikioni Mara andike andike namba alionekana kama aliyekuwa akimpigia alikuwa apatikani.bila ya kusita nikamsogelea kwa nyuma na kumshtua kwa kumgusa bega lako ambalo baada ya kugeuka tu akarusha ngumi kali iliyonipata sawa sawa kichwani na kuniyumbusha kidogo.nikiwa katika maandalizi ya kukaa sawa tena akaachia teke ambalo nilikwepa sawa sawa lakini nikalisahau na lingine lililotua kifuani na kunidondosha chini.nikajibetua na mfumo wa kuruka beki na kukaa sawa kisha nikaanza kumsogelea taratibu dereva steven ambaye kwa mara ya kwanza nilijua hajiwezi kabisa kumbe alikuwa naye ana gusa gusa mkono.nikamsogelea lakini kabla sijamfikia akabetuka mateke mawili dabo yaliotua kifuani kwangu na kuniyumbushia lakini safari hii sikudondoka kwa awali nilirudi nyuma kidogo.Kwa hasira nikamsogela tena na kumuacha steven tena akirusha makonde mawili makali yalionipata vizuri usoni na kunitoa damu ambazo niliishia kutema chini kisha nikaendelea kumsogelea tena kwa hasira nzito.kwa hali ile ya kudindisha kila anachonipiga na mimi kuzidi kumsogelea aniongezee kumlimshua sana dereva ambaye baada ya kunipiga mpaka
Akachoka.steven baada ya kuona hali imekuwa ngumu upande wake akaanza kuniomba msamaha huku akirudi kinyume nyume na hakusita kutoa machozi yaliozidi kunipandisha hasira kali na kuzidi kumfuata huku nikiwa tayari nishakunja ngumi kwa lengo la kumshambulia pale tu nitakapomfikia.safari ya steven kurudi kinyume nyume iligota katika mlango ambao licha ya kuusindika tu akaanza kuangaika nao kufungua kama vile umefungwa vile.bila ya kuchelewa nilipofikia tu Nikamtandika teke kali lilompeleka mpaka ndani na kumfanya aanze kupiga kelele za maumivu niliingia mpaka ndani kisha nikamuinua na kwenda kumbamiza katika tv yake ya flatscreen na kumpasua kichwa chake kidogo na kuanza kutokwa na damu kichwani.sikutaka tu kuishia hapo nikaendelea kumshambulia kwa ngumi kalo zisizokuwa na idadi mpaka nilipoona awezi kuinuka kisha nikamuachia akiwa anavuja damu huku akiugulia kimya kimya kwa maumivu.
"Nilisikia pale kwamba una kadi ya mualiko hiyo kadi ipo wapi??"
"A..aa...aa.......ka.d.dii...ipii"
"Usinifanye mtoto nitakuua nilisikia pale ulipokuwa unaongea na yule mwenzako"
"M...ssssijui"
"ok" Sikutaka kuendelea kumuongelesha kwa haraka nikajikokota mpaka katika mfuko wangu na kutoa upinde wangu wa mshale kisha nikachomeka mshale na kwa haraka nikaweka na kumfyatulia Mshale katika Mguu wa steven hali iliyomfanya apige ukelele wa juu kabisa ambao kabla hata hajaendelea tena nikawahi na kumziba mdomo.
"Hey hebu nambie kwa mara ya mwisho kabla sijakumaliza safari hii je kadi ya mualiko wa harusi ipo wapi.??"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"I...po..kwen...ye be.gi Pale..." kwa haraka nikanyanyuka na kwenda katika begi lake kisha nikalifungua na kuanza kupekenyua pekenyua na kisha kwa macho yangu nikaiona kadi na kuitoa.nilikaribishwa na picha ya moureen aliyokumbatiwa na robertson katika pozi nene lilinifanya nitoe msonyo wa hali ya juu.hakika kadi ile ilikuwa imepambwa pambwa vizuri nakaanza kuangalia kadi hiyo na kuanza kuisoma kwa umakini kidogo
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment