Chombezo : Sema Jina Langu Mpenzi
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nathan church posta..??" nililitaka jina hilo la kanisa lilinifanya nirudi nyuma kifikra kidogo baada ya kulikumbuka kanisa hilo ambalo nilishuhudia kwa Macho yangu jackline mpenzi wangu wa kwanza kuolewa na mtu mwingine.Hakika kufanyika harusi ile katika kanisa hilo lilinipa kamshangaao fulani ambao ulinionyesha ni kama kamchezo lakini kwa upande wa pili niliona ni njia rahisi kutokana na kulijua vizuri kanisa hilo.Nikaendelea pia kuangalia je ni mchungaji atakaye fungwa hiyo ndoa na kuona pia jina lake.sikutaka tena kuichukua kadi hiyo ya nikarudisha mule mule kwenye begi kisha nikakusanya mzigo wangu niliowekea upinde na mishale yangu.nilipomaliza nikaenda mpaka katika suruali ya steven na kuchukua wallet yake iliyojaa pesa iliyosababisha mpaka itune kisha nikachukua pesa kiasi bila hata ya kuzihesabu wakati huo steven alikua bado ananiangalia huku akiugulia maumivu ya mshale ule niliompiga ambao ulikuwa bado upo ndani ya paja.Nikamsogelea na kuuchomoa mshale huo na kuziba mdogo wake kwa nguvu ili asipige ukelele.
"Wahi hospitali kabla haujafa Maisha mema" nilimuaga kwa staili hiyo kisha nikatoka nje na kushika hatamu ya kwenda kutafuta gesti usiku huo huo ikiwa mida ya saa nane nane.Hakika Mipango yangu yote ilivurugika kutokana na kumuamini steven ilinibidi nibadilishe mipango na kuandaa mipango mingine ambayo ilinilazimu nifanye chini juu niweze kufika kanisani Asubuhi na Mapema kutokana na ndoa hiyo kufungwa saa Mbili Asubuhi.Nilifanikiwa kupata gesti ya mapema kabisa katika mitaa ya kariakoo mida ya saa tisa na kulala usingizi wa kushtuka shtuka kwa lengo ili nisichelewe.Nililala kidogo tu lakini niliposhtuka saa ukutani katika gesti hiyo ikaonyesha saa kumi na Moja asubuhi nikajivutavuta na kuamka kisha kwa haraka haraka nikatoka huku nikiwa na mzigo wa mishale yangu na upinde nilioweka katika mfuko mkubwa mfano wa gunia mweusi uliokuwa hauonyeshi kisha nikaubeba begani na kutoka katika chumba hicho nilichokuwa nishakilipia.kwa haraka ya mwendo wangu nikajikuta nikivuta pumzi ndefu Baada ya kufika mbele kabisa ya jengo la kanisa ambalo kwa muda huo kulikuwa na watu wachache ambao wengine walionekana wanatoka wengine wanaingia.Nikajisogeza taratibu na kuingia katika kanisa hilo kisha nikajichanganya na watu katika mkusanyiko mmoja ambao kulikuwa na muhubiri mmoja aliyekuwa anatoa neno la mungu ndani kabisa ukiingia getini.Nikiwa katika mkusanyiko huo wa watu ghafla Magari ghafla yakaanza kumiminika na kutoka watu wa heshima kutokana na suti zao walizokuwa wamevaa huki kila aliyekua anatoka Alikuwa ameambatana na mkewe.Maubiri yale ya kwetu yakasitishwa na muhubiri na kutuamuru tutoke nje ya kanisa ili tuendele sikusikiliza Amri hiyo kwa haraka haraka nikaanza kuelekea ndani ya kanisa huku nikipishana pishana na watu ambao walikuwa wanaamrishwa watoke.Nikafanikiwa kuingia ndani ya kanisa hilo na kukimbilia chooni ambapo wakati nikijiandaa kujificha nikashtulia na jamaa aliyekuwa amevaa miwani na suti.
"Mmmh wewe unafanya nini huku hebu toka haujui kwani nini kinataka kiendelee"
"Nimebanwa kidogo nataka niende nikajisaidie "CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nakuambia hakuna kwenda hausikii" Hakika yule jamaa alinizuia kuingia chooni huku akiwa ananilazimisha niondoke pale.nilimuangalia kwa muda na kuangalia usalama kwamba je kuna mtu anaona lakini Sikuona mtu katika maeneo yale.Nikazuga kama nataka kuondoka lakini nikazunguka teke kali lililompata barabara na kumdosha chini na kumfanya agune kwa maumivu.akiwa katika hali ya kujizoa zoa ili aamke nikamtandika ngumi kali ya shingo na kumzimisha kisha nikamchukua nakumuingiza chooni na kumficha katika chumba kilichopo ndani ya choo hicho kilichokuwa hakitumiki.nilitoka nikiwa nimevaa suti za yule jamaa huku nikishindilia na miwani meusi iliyonikaa vizuri katika macho yangu usoni nilionyesha tabasamu hafifu baada ya kuona nina Asilimia kubwa kabisa kuzuia Harusi isifungwe.Nikaendelea kuzunguka zunguka upande huo ambao mara kwa mara watu waliokuwa wamefavaa nao suti kama yangu na miwani waliokuwa wananipigia saluti kila wanapopita ikiashiria kama ishara yao pindi wakutanapo.Nikiwa nazuga zuga kama Mfuasi wa robertson nikiwa Nalinda Maeneo hayo.Mtu alivaa suti kama mimi akaja mpaka pale nilipokuwa nazunguka zunguka na kunipigia saluti kisha akanishika bega langu la kulia.
"sikia taarifa zilizotufikia punde kwamba dereva steven amekufa yule aliyekuwa akiwaendesha ma agent wengine kwenda kuwamaliza Yule pablo na mzee yule aliyemuokoa Nahisi taarifa ulishapata awali pia na wale walioendaa nao Mpaka sasa wale ishirini wamekutwa nao wamekufa.Sasa hapa pameshazurugika na tunahisi kwamba hawa Majamaa wanaweza kuvuruga harusi ambayo imebaki nusu saa tu ifungwe sasa kwani wewe daraja ngapi dah..aa kumbe c nimeona kwenye mfuko wako sasa basi Macho yako yawe makini sana kwa nguvu mmoja tuhakikishe boss wetu anafunga ndoa.." hakika wayasemayo wahenga usilo lijua ni sawasawa na usiku wa giza ndio hali iliyotokea baada ya jamaa yule kudhania kuwa mimi mfuasi mwenzake na kuniambia vitu ambavyo nilivisababisha mimi mwenyewe Huku mimi nikiwa ndio adui wao mkubwa.ilinibidi nimuitikie kwa katikisa kichwa na kumuacha jamaa huyu akiondoka huku akigeuka geuka nyuma na kuangalia mfuko wangu mkuukuu ambao ulikuwa mchafu lakini akajikuta akipotezea na kuniacha mimi palepale.hakika nilijikuta kwa muda mchache nikiingia katika dimbwi kubwa la mawazo yaliosababishwa na mauwaji niliyoyafanya kwa muda mfupi.hakika moyo wangu uliniuma sana kufanya vile lakini nilikuwa sina jinsi ya kufanya vile ilinibidi niuwe ili nimalize vizingiti vyote vilivyokuwepo.Nikiwa katika mawazo nikajikuta nikishtusha na matarumbeta flani yaliambatana na Nyimbo ya dini ambayo ulinioamasishwa nitoke pale chooni na kujiongeza mpaka katika kanisa lenyewe.Moyo wangu ukadunda ghafla mapigo ya moyo ambayo yalisababishwa baada ya kumuona moureen akiwa anatembea kuelekea kwa robertson aliyekuwa tayari ameshapanda kwenye kajukwaa cha kufungia ndoa.Hakika moureen uzuri wake ulizidi maradufu na alikuwa akitembea akisindikizwa nyuma na wapambe wake waliokuwa wamemsaidia kushikilia shela lake alilovaa lililokuwa likiburuzika.macho yangu yakaanza kuangaza na kuwaangalia miongoni mwa wafuasi ambao wote walikuwa wanamuangalia bibi harusi moureen wakati huo kama kawaida nikatoa upinde wangu na kuchukua mishale kama miwili na kuanza kuiandaa huku nikiificha kwa kuelekezea chini.Niliukabali msemo subira ya vuta kheri sikutaka nianzishe timbwili kwa muda huo nilisubiri kwanza misa kuu kabisa ya ndoa iishe ndio nianze kazi yangu iliyonipeleka pale...
Macho na masikio ya watu wote waliokuwepo ndani ya kanisa hilo yalikuwa katika mchungaji alikuwa anafungisha ndoa hiyo huku akiambatana na Moureen na robertson mugalula waliokuwepo pembezoni kabisa mwa mchungaji kasolo mimi niliyekuwa nimeshashika mishale yangu miwili katika upinde kwa lengo la kuifyatua yote muda utapofika.Misa fupi ya mchungaji ilionyesha kuwakuna kabisa wasikilizaji ambao walikuwa makini kabisa kumsikiliza.Wakati huo shingo yangu ilikuwa ikicheza pande zote za kanisa huku nikiangalia ni nani na nani aliyekuwa ananiangalia na kukuta Hata wafuasi wote wa baba moureen na robertson Mugalula walikuwa Wameshakamatwa na Misa ya Mchungaji aliyekuwa Na maneno matamu yaliomkuna kila mtu.Baada ya kumaliza misa mchungaji aliwaambia moureen na robertson waangaliane huku na wapambe wa robertson na wa moureen wakiwa wanakazi ya kuwafuta futa majasho licha ya kuwa hawakuwa na majasho yoyote.
"Haya bwana robertson Mugalula shika hii Pete ya Ndoa Nitakachokisema ndicho utakachokifatisha kisha baada ya kumaliza utauchukua mkono wa kushoto wa bibie moureen na kumvalisha pete hii ninayokupa sasa hivi ya ndoa."
"Sawa mchungaji" yale maneno ya mchungaji yalinisababisha nikae tayari kabisa huku taratibu nikiaanza kupandisha taratibu upinde wangu wa mshale uliokuwa na mishale miwili juu Baada ya kuficha chini Huku nikiwa tayari kabisa nishajiandaa.
"Mimi robert Mugalula"
"Mimi robert Mugalula"
"Nafunga ndoa Mbele ya ushahidi wa kanisa na pete hii ya ndoa kwa kumuoa bibie moureen"
"Nafunga ndoa Mbele ya ushahidi wa kanisa na pete hii ya ndoa kwa kumuoa bibie moureen"
"Na kuwa mke wangu halali kabisa na kufunga naye pingu za maisha Mpaka kifo kitakapotutenganisha"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Na kuwa mke wangu halali kabisa na kufunga naye pingu za maisha mpaka kifo kitakopotutenganisha" Baada ya robert mugalula kumaliza kuongea Akaipokea pete kutoka kwa mchungaji na kuchukua mkono wa kushoto wa moureen aliyekuwa analia wakati huo na kumnyoosha vidole ambavyo kwa mara ya kwanza alikuwa kavikunja kwa lengo la kumvalisha pete hiyo.Hapo ndio sehemu niliyekuwa naitaka mimi kuanzisha timbili.kabla hata robert mugalula ajamvalisha moureen pete ile anataka kumvalisha tu Nikafyatua mishale miwili ile haraka sana na mmoja kumpata robert mkononi iliyomfanya aidondoshe pete aliyoshika na kumuachia moureen kisha mwingine ukatua katika Paja lake la kulia hali iliyomfanya aruke kidogo na kudondoka chini huku akishikiria sehemu ile ya mguu niliyompiga huku akionekana kusahau kuugulia maumivu mengine ya mshale wa mkono uliomtoboa na kufanya mshale ubaki katika kiganja.Hali ya mshangaoo wenye kustaajabisha ndio ukachukua nafasi yake huku kelele za watu walizokuwanatoa kwa uoga huku wengine wakiwa katika harakati za kutaka kukimbia ndizo zilizoniwezesha mimi kwa kasi kufika katika jukwaa lile walilokuwepo Moureen na robertson.wakati ule moureen alibaki akishangaa tu naye pia alionyeshwa kushangazwa na tukio lile lililomfanya miguu yake ife ganzi.hata baba moureen na mama moureen nao walikuwa katika pia harakati za kutaka kukimbia.Baada ya kukanyaga katika jukwaa nikakutana na mabest man wa robertson waliokuwa wanajaribu kumpa msaada wa kwanza kwa kutaka kumchomoa mishale niliyomchoma.sikutaka kuwauliza bila ya kuchelewa nikajiachia Mateke Makali mawili yaliowapata wote wawili na kufanya kila mmoja aruke sehemu yake.nilisogea kwa haraka haraka na kukutana na mchungaji aliyekuwa ananiangalia kwa butwaa Nikamsogelea na kumtandika kichwa kikali cha kifua kilichomfanya atoe ukelele huku akimtaja yesu huku akidondoka kisha bila ya kupoteza muda nikamkunja roba Moureen na kumuekea bastola kichwani niliyoikuta katika suruali ya yule mfuasi ambaye niliyemuua chooni.Moureen hakusita kupiga kelele za kuomba msaada jambo lililozidi kufanya miongoni mwa watu wazidi kukimbia.Mapolisi wakiambatana na wafuasi wa robertson na baba moureen wakaanza kumiminika kwa wingi ndani ya kanisa hilo na kuanza kunisogelea mimi niliyekuwa nikitabasamu wakati huo huku nikizidi kuwaangalia kwa dharau.baba moureen alibaki akiwa anashangaa na kutojua cha kuwaamrisha wafuasi wake nini la kufanya kutokana na mimi kumshikiria Mrembo huyo na mkono wangu ulioshika bastola ulikuwa kichwani kwa moureen.Pembezoni mwangu kulikuwa na robertson mugalula ambaye Naye sumu ya mshale niliyompiga iliendeleaa kumtafuta na kubaki akiwa anagugumia kwa maumivu na kushindwa kabisa kutembea.
"Wote wekeni silaha zote chini la sivyo mali ya kichwa cha huyu binti nitakipasua sasa hivi Nahesabu mpaka tano moja!!!,Mbili!!!,Tatu!!!,Nneeeeee!!!!,Ta......"
"Jamaani wekeni silaha chini" Nikiwa nakaribia kumaliza hesabu niliyowaambia baba Moureen akawaamuru wafuasi wake na mapolisi waweke silaha chini ambapo bila ya shuruti wote wakaachia na kuzidondosha silaha zao chini.Ile nafasi ya mapolisi wale na wafuasi wale kuachia zile silaha ziliziniwezesha mimi kutoka na moureen pale jukwaani nakuanza kutembea naye haraka haraka nikitoka naye nje huku bado bastola yangu nikielekezea kichwani kwake.kwa bahati nzuri nikafanikiwa kutoka naye nje moureen huku nikisindikizwa na mapolisi na wafuasi wa robertson na wa baba moureen akiambatana na yeye mwenyewe baba moureen aliyekuwa pia na mkewe huku wakiendelea kunisisitiza nisimuue.safari yangu ya kumkokota moureen iligota katika gari jeusi ambalo lililokuwa kabisa la wafuasi wa robertson kisha nikalifungua haraka na kumuingiza Moureen na kisha mimi pia nikaingia na kwa bahati nzuri nikakuta funguo ya gari ikiwa kabisa imeshachomekwa mahala pake sikutaka kufanya ajizi kwa haraka nikakwinya funguo na kuliwasha gari kisha kwa speed ya ajabu nikaling'oa pale na kilichozidi kunisaidia ni uwepo wa geti kuwa wazi ndio ulioniwezesha nipite kwa haraka.wakatu huo huo nikiwa katika harakati hizo mapolisi na wale wafuasi baada ya kushuhudia nikianza kuendesha gari Wao waliishia kulishambulia lile gari kwa risasi kibao ambazo kwa uwezo lile gari lililokuwa hali ruhusu risasi yoyote kupenya.Speed yangu ya gari ilimshangaza kabisa moureen aliyekuwa ananiangalia sana huku machozi meusi yaliokuwa yamechanganyika na wanja aliopaka zilinifanya nijisikie vibaya.sikutaka kuanza naye kuongea kwanza kwa sababu nilikuwa ndani ya speed kubwa ya kuendesha gari kwa lengo la kuwachenga wafuasi wa robertson wakisaidia na nguvu tosha kabisa ya mapolisi waliokuwa nao wanakimbiza gari yangu na kilichozidi kunisaidia ni uwepo wa kutokuwa na Magari siku hiyo katika maeneo ya barabara zenye magari mengi na kutokuwa na matraffic.
"Moureeeen"
"Aa...b..eee"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa sikia Nielekeze Nyumbani kwenu haraka iwezekanavyo"
"Ni...mas..aki kata kushoto hapo ili tufike haraka" Hakika mipango yangu ilikuwa ipo kichwani kabisa na kwa kupita njia njia za shortcut zilifanikisha kabisa kupita bila ya wasi wasi.Bado moureen aliendelea kunishangaa na kuniuliza kwanini tunaelekea kwao lakini sikutaka kumjibu swali hilo kutokana na Mipango yangu ilikuwa inabadilika badilika kila wakati nipatapo wazo.katika kama majira ya saa sita hivi mchana saa iliyokuwa ndani ya gari ilitosha kabisa kunijulisha katika maswala ya wakati mkononi sikuwa na mshale wowote nilikuwa nimebaki na silaha tu huku nikiwa na moureen niliyejifanya kama nimemteka.Macho yangu yakatua katika lango kubwa la geti lililolembwa na vipande kama vya dhahabu dhahabu ambalo lilifanya geti hilo lipendeze Nikakanyaga breki baada ya Moureen kuniambia pale ndio palikuwa ni kwao kisha nikaanza kuendesha taratibu kuelekea katika geti hilo na kabla hata sijajiandaa kupiga honi lango lenye Automatic likajifungua na mimi nikaliingiza gari hilo.Ubaya wa gari hilo lilikuwa ni ni kioo cha nyuma tu ndio kulichokuwa kikionyesha lakini vilivyobaki vilikuwa ni tinted jambo lilinifanya niwe makini wakati wa kushuka kutokana na kuhisi nitapatwa na vizingiti kutokana na ulinzi niliohisi.Nikaanza kumtanguliza mouree aliyetoka kwa haraka na kisha kufuatia mimi lakini kabla hata sijajiandaa kutoka kabisa Ngumi nzito iliyonipata sawa sawa iliyonirudisha nyuma ikarushwa na kufanya niteme chembe chembe za damu hali ilinitia hasira kali iliyonifanya na mimi nitoke kwa style ya kurusha mateke yote mawili yaliompata yule aliyenipiga ngumi kifuani huku na mimi nikitoka kabisa nje ya gari hilo na kumfanya yule jamaa adondoke chini.wakati natoka nikakaribishwa vyema na walinzi kumi ambao kwa bahati nzuri kwa pale hawakuwa na silaha zaidi ya mikono yao iliyokuwa ishakunja ngumi tayari kabisa kupambana na mimi kutokana na wengine waliokuwa nyuma kuanza kunikimbilia.Hapo ndipo mafunzo yalioniingia kutoka kwa babu marehemu gardner ndio yalianza kutumika zoezi la kunifundisha kupambana na watu wengi ndio yalinipa hali ya kujiamini na kuanza kwenda nao sambamba.kazi hakuwa rahisi kwa sababu nao walikuwa na ujuzi kidogo ambao hakunitisha mimi ambaye niliendelea Kuwatandika mapigo makali yaliomnyong'onyesha kila aliyenisogelea na kufanikiwa kuwazimisha kama saba.huku watatu waliobaki niliishia kuwamiminia risasi za miguu kila mmoja na kufanya waanze kutoa makelele ya kuomba msaada.Baada ya kumaliza kupambana nao nikamshika moureen mkono moureen ambaye alizidi kunishangaa na kubaki akiniangalia tu na kutojua la kuniambia kutoka na kuwa na nguvu na kujiamini vya kutosha kuliko alivyonizoea.wote tukaingia ndani ya jumba hilo kubwa la kifahari ambalo lilikuwa na wafanyakazi wakike sita wa kazi za ndani.sikuwa na muda wa kuangalia angalia thamani ya vitu vya ndani na nilipofika katika sebure kubwa nikajibwaga katika kochi kubwa huku mbele yangu kukiwa na bonge la tv la flatscreen lilojaa katika ukuta wote pale.Moureen alikaa pembeni yangu akiniangalia na kutaka kuanza mazungumzo lakini alijikuta akishindwa kutokana na jicho kali nililokuwa namuangalia.
"Kwa hiyo ulikuwa unakubali kuolewa na Mwanaume usiyempenda???"
"Pablo nilikuwa sina jinsi ya kufanya hivyo ilinibidi nikubali tu"
"Ouk hivi unanipenda kweli??"
"Yes mpenzi nakupenda sana"
"Ni kweli unataka kuishi na Mimi tukiwa Mume na mke"
"Kwanini isiwe hivyo pablo Nahitaji iwe hivyo katika maisha yangu sitaki mwanaume mwingine zaidi yako pablo"
"Ouk Najua wewe ndio mtoto pekee katika familia yako nataka tucheze mchezo leoleo sasa hivi Naomba niletee hati za nyumba hii kadi zote za Benki na karatasi zake zote."
"mmmh sawa..basi nifuate huku" Nikajikuta nikipata kama mshtuko wa moyo kudunda baada moureen kukubali mpango wangu kwa kutumia ishara ya kidole akaniamrisha nimfuate jambo ambalo sikulemba nikajizoazoa kwenye kochi na kuanza kumfuata kwa haraka haraka huku naye nikimshawishi atembee haraka haraka ili tufanye vitu kwa ushapu.Moja kwa moja tukaingia katika chumba kikubwa kilichokuwa na choo chumba ambacho Baada ya kuingia nikajikuta nizungusha zungusha kichwa changu na kuanza kuangalia thamani ya vitu vingi vilivyokuwepo humo.Nikamuona moureen akisogea mpaka kwenye dressing table kubwa iliyokuwa ina vikoro koro vingi kama maperfume, mafuta na marosheni ya kila aina kisha nikamuona akifungua kamlango cha kabati la dressing table hiyo na kutoa funguo kisha alipomaliza.Moja kwa moja akaenda katika kabati kubwa la nguo lilokuwepo humohumo na kufungua kisha akakuta sanduku na kulifungua na kukuta kisanduku kingine kilichomfanya hata yeye ashangae kidogo kisha akanyanyuka pale na kuanza kama kufikiria kitu kama dakika moja hivi na kuniomba nimsaidie kuinua godoro la kitanda kilichokuwepo humo na mimi bila ya kusita nikaenda kunyanyua godoro hilo kwa kupapasa moureen akakuta funguo nyingine ambayo alienda kufungua kisanduku kingine kilichobaki na kukuta madocument ya makaratasi ya benki zikiambatana na Atm kama nne za bank zilizokuwa na kikaratasi cha namba za siri za bank zilizoandikwa katika moja ya karatasi kisha na hati miliki kabisa ya Nyumba hiyo.baada ya kutoa akarudishia vile vile kisha akanikabidhi vile vitu na mimi nikavipokea kisha akanisogelea karibu kabisa nakuanza kunipa mdomo wake kwa lengo la kunipa denda na mimi nikaupokea kwa ufundi wa hali ya juuCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Moureen!!,moureen,Si muda wake sasa subiria kama nitaweza kutoka salama"
"But..ba..by nimekumiss mpenzi ni kitambo sana ujue"
"No..sio muda wake" Nilimuambia moureen huku nikimtoa katika kifua changu alichokuwa ameegea baada ya denda la kama nusu dakika kisha nikamshika mkono na kutoka naye nje ambapo moja kwa moja tukarudi sebureni.Baada ya kufika sebereni Nikachukua dude la kuvutia sigara linaloitwa shisha na kukaa nalo karibu na kuanza kuwasha moto na kuanza kuvuta shisha hilo huku mikononi mwangu kukiwa na makaratasi yote.Nilimwambia moureen asogee karibu yangu kabisa kisha nikaitoa bastola yangu mfukoni na kumkombatia moureen kwa ule mkono uliokuwa na bunduki niliyomuelekezea kichwani na kumfanya moureen aanze kutetemeka kwa uoga huku akiniangalia kwa huruma
"So Pablo hivi ni kweli utaniua"
"Hapana sitakuua ila..."
"ila nini?? na mbona bado umekaa hapa hauoni kwamba ni hatari ambapo baba atakuja na watu wake na Mpango wako ni upi"
"Hey moureen hebu tulia kwanza usiwe na pupa subiri uone haka kamche........" Nikajikuta nashindwa kumalizia baada ya kusikia ving'ora vya magari ya polisi vilivyokuwa vikilia nje ya geti la jumba hilo vimilio vilivyopenya kabisa katika tundu zangu za masikio.Kwa madaha na utulivu nikatulia na kuvuta pumvi kwa nguvu na kumuweka moureen vizuri huku nikimuewekea bastola vizuri kichwani huku mkono mwingine nikishika makaratasi yale muhumi na kuishikilia shisa kwa wakati mmoja huku nikiendeleaa kuvuta.Haikupita hata dakika tano mlango wa pale sebureni ukafunguliwa kwa nguvu kwa kupigwa mateke na kuingia wafuasi wa baba moureen na wafuasi robert wakiambatana na mapolisi wasiokuwa na idadi ambao mikono yao ilikuwa imeshiba bunduki kali wakiongozana na baba moureen aliyekuwa na mkewe wakiwa wanahema juu juu
"Kabla hataujafanya chochote weka silaha chini na usimame juu huku ukimuachia binti kabla sheria haijachukua Mkondo wake" Moja kati ya polisi aliyekuwa mstari wa mbele huku akinionyeshea mimi bunduki aliongea na kunifanya mimi nitabasamu huku nikiendelea kutoa moshi mzito wa ile shisha Niliyokuwa Naivuta.
"Hahaha sheriaaa???,sheria gani unayozungumza wewe.Mpaka hapa Nilipo nipo tayari kwa lolote na kama mtanikamata sasa hivi basi kichwa cha huyu binti nitakipasua kwa bastola hii iliyokuwa na risasi nyingi tu."
"Hivi wewe Mbwa unataka nini??,Muachie Mwanangu kabla sijawaamrisha vibaraka wangu waanzishe vita."
"Hahaha baba moureen bado unaongea ukiwa ujui unachoongea" Nilimwambia baba moureen aliyekuwa amefura hasira kwa kuniangalia kwa jicho baya huku nikimuonyesha madocument yake ya Akiba zake za pesa huku nikimuonyesha na kadi zake za atm na kumuonyesha pia Hati miliki ya nyumba yake zilivyomfanya apate mshtuko mkubwa yeye na mke na kujikuta wote wakitumbua macho kwa mshangoo kutokana na kutoamini kabisa wanachokiona.
"Sasa basi kama unataka makaratasi haya yarudi mikononi mwako waambie wafuasi wako Pamoja na hao mapolisi watupishe kidogo watuachie tuyamaliza mimi na wewe sasa hivi" Nilimwambia baba moureen aliyekuwa kama kaduwaa na kufanya aanze kukuna kichwa na kutafakari kisha akaniangalia mimi ambaye kwa wakati huo Nilikuwa namtishia kuingiza makaratasi yale katika lile dude la kuvutia shisha ambalo lilikuwa linamoto mkali kidogo.
"Sasa vijana chukueni cheki hii ya millioni tano na mkagawane muondoke haraka nilimalizane naye na nyie vibaraka wangu nisubirieni Nje" Baba moureen kwa kujikaza akaandika cheki ya kuchukua hela na kumkabidhi yule polisi aliyekuwa akiwaongoza wenzake ambao baada ya kuambia hivyo hawakuwa na hiyana wote pamoja na wafuasi wale wakatoka na kuniacha Mimi nikibakia Na baba moureen,mke wake na moureen mwenyewe ambao wao wote hawakuwa na neno lolote la kuongea.Baada ya kuhakikisha kwa macho kuwa wote wametoka Nikajikokota kwa kuinuka kisha nikaanza kupiga hatua za taratibu na kumfuata baba moureen aliyekuwa naye ananiangalia na kumfuta kwangu kulionyesha kumpa wasiwasi kutokana alikuwa ananiangalia kiuoga
mkono wangu ulikuwa umeshika document za mali zake zote.
"Kumbuka kuwa kila mtenda baya lazima hulipwa na baya lake alilofanya kutoka na ubaya aliomfanyia mwenzake,mzee umeua familia yangu kwa kuwanyonga mbele yangu jambo ambalo linaniuma mpaka sasa,na ninavyokuona mzee baba yake halali kabisa moureen kifo kinakukalibia na nitakuua mimi mwenyewe ila kama unatafata ninachokitaka basi nitakuachia.Sasa basi umeona haya makaratasi yako nataka uandike Jina langu kama mrithi wa mali hizi"
"Whaaaaaaat haiweze..k....." kabla hata baba moureen hajamaliza kuongea nikamsogelea na kumtandika kofi nzito la uso na kumfanya ayumbe yumbe na kabla hata hajakaa sawa nikamtandika kichwa kizito cha kichwa na kufanya atoke nundu papo hapo na kusababisha moureen na mama yake waanze kupiga makelele ambayo niliyanyamazisha kwa kuwakanya kuwa kama watapiga kelele basi sitakuwa na huruma na Mzee huyo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sikia mzee sina muda wa kupoteza safari hii nakuua vp utaandika jina langu au hauandiki"
"fuck you niuee tu siandiki" jibu la baba moureen likanitia hasira na kujikuta nikimuweka sawa na kuvuta ngumi niliyoikunja kwa nguvu nikiwa na lengo la kumtandika katika mdomo wake.lakini nikiwa katika hali ya kupeleka ngumi ghafla kitu kama mshale ukapenya kwa haraka katika bega yangu ya kulia na kufanya nimuachia baba moureen niliyemkunja na kuanza kumuangalia aliyenipiga lakini kabla hata sijainua kichwa changu kumuangalia nani aliyenipiga nikazolewa kwa kupigwa kikumbo kikali mpaka katika kochi kisha zikafuatiwa na ngumi tano za nguvu zilizotuwa kifuani kwangu na kunifanya nitapike damu nzito na kunifanya nipate juhudi za kumsukumiza aliyekuwa ananishambulia jambo ambalo nilifanikiwa kumtoa.Macho yangu yakatua kwa robertson mugalula ambaye kwa Asubuhi yake nilikuwa nimempiga mishale miwili ambayo kwa hali niliyomuacha katika kanisa nilijua kabisa kwa namna moja ama nyingine sumu ya mshale ingekuwa ni silaha tosha ya kumfanya atungulie haraka mbele za haki.akiwa anachechemea mguu mmoja huku majasho mengi yaliokuwa yanamtiririka kwa kasi na kuzidi kulowesha shati akajikokota na kuchukua lile dude la shisha na kulinyanyua na kunielekezea mimi kwa lengo la kunitwanga nalo na kunifanya nibaki nimemtumbila macho huku Nikiwa najaribu kuinuka lakini maumivu ya mshale wa bega ulitosha kabisa kuniua nguvu na kubaki nikimuangalia tu Robertson aliyekuwa yupo tayari kabisa kunirushia dude lile.............................
Bila hata ya huruma robertson akanirushia lile dude la kuvutia shisa ambalo lilikuwa lina moto wa kutosha ambalo baada ya kunifikia nikalivuia kwa mkono lakini mikaa mikaa ya lile dude lilitosha kabisa kuniunguza na kujikuta nikipiga kelele kutokana na maumivu makali niliyoyapata kutokana na moto ule.Mikono yangu ndio ulikuwa imebabuka kwa moto ule ambapo baada ya robertson kunirushia akaanza kucheka kwa nguvu na kuanza kunitukana wakati huo mimi nikiwa bado nipo katika maumivu makali yaliofanya nidondoshe machozi.nikiwa katika hali hiyo teke lingine kali la shingo lililorushwa na robertson likatosha kabisa kuninyong'onyesha lakini Hali nyingine ya mshangao ikatokea baada ya Robertson Mugalula kuanza kugalagala na kuugulia mguu ule alionipiga teke kwa maumivu kutokana na mshale niliompiga na kujikuta akijisahau na kuutumia kunipigia jambo lililosababisha aanze kuugulia.hali mpya ya nguvu zikanipanga na kujikuta nikinyanyuka kwa nguvu na kasi ya ajabu iliyosababisha maumivu makali ya kubabuka kwa mikono yangu iliyounguzwa na dude la kuvutia shisha alilonipigia nalo robertson na kujikuta nikipaniki na kumfuata palepale robertson na kuanza kumshindilia ngumi nzito nzito zisizokuwa na idadi na kumfanya aanze kuvuja damu usoni kutokana na ukali wa ngumi zangu nilizokuwa nampiga kwa hasira iliyovuka kipimo.Nikiwa katika hali ile yakumsindilia ngumi hizo robert aliyekuwa amelala tu hana la kufanya kutokana na kumdhibiti vizuri Baba moureen akanichoma kisu cha mgongo kilichoingia kidogo na kunishtua kutokana shambulio hilo lilikuwa la haraka.Akiwa anajiandaa kunichoma tena nikafanikiwa kunyanyuka na kumbidua na kufanikiwa kumlaza chini na kuchukua kisu chake alichonichoma nacho cha mgongo na kuanza kumuelekezea yeye tena mwenyewe baba moureen aliyekuwa ametoa macho kutokana na kushangaa nilivyombidua na kubaki akihema juujuu na kubaki akiwa ananiangalia.kipindi hicho mama moureen na moureen mwenyewe walikuwa wanalia na kunisihi nisichukue maamuzi magumu ya kumuua jambo lililonifanya hasira zianze kupungua kidogo kidogo na kubaki nikiwa nimeshika kisu kwa lengo la kumchomoa
"Anayekufanyia ubaya sio lazima umlipizie naye ubaya Najua mpaka sasa ushanifanyia mabaya mengi yalioniharibia maisha yangu kisha tu kumpenda mwanao ambaye naye hakusita kunionyesha mapenzi ya kweli na kunipa nafasi katika moyo wake.Kwa nini humchagulie mtu atakayemuoa wakati anao uwezo wa kuchagua na yeye ampendaye na mtu sahihi wa kumuoa.Najua na wewe wala haujachagulia mtu wa kumuoa ilitokea wote mkajikuta tu mkipendana.Mzee mimi Nishakusamehe kwa yote uliyonitendea lakini kumbuku pesa yako haiwezi kuzuia penzi la dhati hata siku moja" kwa hasira iliyochanganyika na machozi yaliokuwa yananitiririka katika mashavu yangu nikamwambia baba moureen maneno yale nakukiachia kisu nilichokishika katika sakafu na kunyanyuka kisha nikamnyooshea mkono baba moureen nikiwa katika lengo la kumnyanyua ambapo naye bila ya kusita akanipa mkono wake akiwa tayari kabisa kunyanyuliwa na mimi.Ghafla kabla hata sijamnyanyua nikapigwa kikumbo kikali kikiambata na mtama ulionifanya nidondoke mzima mzima na nilipomuagalia ni nani aliyenipiga nilikuwa nishachelewa kutokana na robertson mugalula niliyedhania awezi tena kunyanyuka alikuwa kashanikalia juu yangu mkononi akiwa ameshika kisu nilichokidondosha chini akiwa kabisa lengo moja tu kukitumbukiza katika kifua changu.Hata nilipojaribu kutetereka mwili wangu ulisita kabisa ganzi kubwa ikaingia na kunifanya nikibaki nimefumba macho sikutaka kabisa kuona kwa macho kisu hicho kilichokuwa kinateremshwa taratibu na robertson mugalula.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwa herii malaya wa kiume wewe............Paaaaaaaaaaaaaaaaa" katika hali nisiyoielewa mlio wa risasi ukasikika kabisa katika mboni ya masikio yangu iliyonifanya nifumbue macho na kumuona robertson mugalula akiwa ameganda karibia kabisa na kifua changu huku kisu alichoshika kwa lengo la kunichoma kikiishia njiani.Macho yake aliyekuwa kayatoa huku domo akiuacha wazi kwa muda.Alama ya toba ya risasi ndio iliyojichora katika kichwa chake na damu nyingi zikianza kuvuja kwa kasi kisha akadondokea pembeni kwa kulala huku damu zikiendelea kuvuja.Nikajizoa zoa kuinua kichwa changu niangalie ni nani aliyempiga robertson risasi alikuwa si mwingine bali ni rafiki yake kipenzi ambaye alikubali kabisa kumpa binti yake baba yake moureen.hakika macho yangu yalipingana kabisa kuniwezesha kuamini kuwa alikuwa ni baba yake moureen ndiye alimpiga robertson risasi na kumuua jambl ambalo pia lilimuacha mdomo wazi mama yake moureen naye ambaye alikuwa kama kapigwa shoti ya umeme na kutotaka kuamini na kujikuta mikono yake akiweka kichwani na kusikitika.moureen akanifuata taratibu na kunikombatia pale pale nikiwa chini huku akiongea maneno ambayo sikuweza kuyakumbuka kutokana na mimi wakati huo nilianza kuona ukungu mwingi mweusi ulitanda katika mboni ya macho yangu na kuzimia na kutojua kilichoendeleaa wakati huo.
*-*-*-*-*-*-*-*-*-*-*-*-*-*
Macho yangu yalipofumbuka tena ikiashiria fahamu zangu zilikuwa zimerudi ilikuwa nipo hospitali iliyokuwa na mandhari yenye kumvutia mgonjwa nikiwa nimetundikwa dripu na kufungwa vungwa bandeji katika mikono yangu.ilichukua muda kidogo kukumbuka kilichonitokea nyuma mpaka pale mlango ulipofunguliwa na kuingia daktari wa kike aliyeambatana na moureen akiwa na baba yake na mama yake ambao kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilishuhudia wazazi wa moureen wakiwa wanatabasamu na kunikombatia pale pale kitandani nilipolazwa.
"Hakika yaliopitwa si ndwele tugange ya jayo kama ulivyoweza kuokoa maisha yangu kwa kusita kuniua na mimi nikamuaa kukusaidia kumua adui yako kwa lengo moja tu ili umuoe binti yangu ambaye kwa kukusubitishia utapopata ruhusa ya kutoka basi mtafunga pingu za maisha" maneno yale matamu ya baba moureen yalinifanya nitabasamu kwa kiasi kikubwa na kuanza kumshukuru mungu kimoyomoyo kutokana na miujiza ambayo kaionyesha haraka kuliko nilivyotarajia.
"mmh sasa itakuaje maana nimefanya vitu vingi mapolisi hawatanikamata??"
"haha pablo ni kama pesa yangu iliweza kufanya vile vya nyuma ambavyo sitaki tena kuvikumbuka ndio hiyo hiyo pesa ndio imefanikiwa kuzima kelele zote za hapa mapolisi hawa wanapenda pesa tu na wala usijali."
"Daaa hata siamini"
"Amini sasa mume wangu kila kitu kipo salama". Ukurasa mpya wa maisha yangu ukaanza hii ni baada ya kupona tu Nikafungua ndoa kubwa ya mimi na Mrembo Moureen iliyowaacha gumzo miongoni mwa watu waliobahatika kuhudhiria kutokana na pesa nyingi iliyotoka mfukoni mwa baba yake moureen ambaye akatuzawadia nyumba kubwa nzuri ya kuisha na Mama moureen kutoa zawadi ya Magari mawili ya bei mbaya.
"Muwe wangu nimepata ujauzito"Yalikuwa ni maneno ya moureen baada ya miezi sita kupita baada ya kufunga ndoa wakati huo tukiwa ndani ya jumba letu la kifahari tulilopewa zawadi.
"Wooow kweli moureeen"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Yeaah mpenzi"
"oooooooo jamani siamini ngojea nisikilize anavyoacheza cheza."
"Duu jamani pablo bado"
"Daa mke wangu siamini hebu sema jina langu mpenzi"
"jamani si pablo mume wangu" Hakika kilichoendelea ni utamu wa maisha ndio ulifuatia lakini haukuweza kunifanya nisahau yalionitokea ambayo kwa mara nyingi Nilitamani kujisahaulisha lakini haikuwezakana na haitawezekana mpaka nitakapo ingia kaburini.
.............MWISHO......
0 comments:
Post a Comment