Chombezo : Nifanye Na Mimi Kaka Dick
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Thank you so much and I am glad to hear that.” (Asante sana na pia nafurahi sana kusikia hivyo.)
“Ok.” (Sawa.)
“What story didi you like?” (Hadithi ipiumeipenda?)
“CHUMBA CHA MASAJI.)
“Ok.” (Sawa.)
“Ok.” (Sawa.)
Nilimaliza kuchat Instagram na Alice shabiki yangu kutoka Kenya msichana ambaye alionekana kuvutiwa na hadithi zangu.
Niliendelea kujizolea umaarufu kila siku, umahiri wangu katika kutunga na kuandika Hadithi za kimapenzi ulinifanya nizidi kupendwa sana huku wengi wao wakiwa ni wanawake ambao ndiyo walikuwa wakizifuatilia sana kazi zangu. Mpaka kufikia muda huo sikuwa nimefanikiwa kucheza filamu yoyote lakini nilibahatika kuandika hadithi iliyochezewa filamu na mtu maarufu ambaye pia nilikuwa nikitoka naye kimapenzi.
Lengo langu kubwa la kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Irine ilikuwa ni kuutafuta umaarufu wa kuandikwa magazetini na kweli katika hilo nilifanikiwa.
Mchezo wangu wa kuchat na watu haukuishia kwa Alice kutoka Kenya bali uliendelea mpaka baadhi wa Wazungu wakawa wananitafuta. Nilifahamu yote yale yaliletwa na umaarufu ambao nilikuwa nao hivyo kila kitu kilichokuwa kikiendelea hakikuweza kunitisha wala kunishangaza, nilitegemea kila kitu kilichokuwa kikitokea.
Waandishi wa habari nao hawakuwa mbali katika kutafuta habari, nilikuwa nikipata Interview nyingi kutoka katika vituo tofautitofauti vya habari ambavyo vilikuwa na lengo la kutaka kufahamu historia yangu ya maisha mpaka ikatokea nikawa katika mahusiano na Irine.
Kwa kweli lilipofikia suala la kuwaeleza ukweli wa mahusiano yangu niliamua kuficha, sikutaka kufanya ule ni ukweli ambao kila mtu angeweza kuufahamu. Nilipoulizwa swali hilo niliweza kukanusha na kudai kuwa zilikuwa ni skendo za magazeti ambayo yaliamua kuandika kwa lengo la kuyauza magazeti yao.
“Kama unavyojua tena ndugu mwandishi mtu ukishapata jina kidogo lazima mengi yatatokea. Ni kweli nimeona na nimesikia mengi kuhusu mimi na Irine lakini yote yatabaki kuwa ni maneno tu. Magazeti nayo yananichafua sana jina langu la Dick linaonekana kuwa kama la kihuni kitu ambacho si kweli. Hakuna kitu kingine kinachoendelea nyuma yangu na Irine zaidi ya kazi tu,” haya yalikuwa ni maneno yangu niliyopenda kuyatamka kila nilipokuwa nikiulizwa na waandishi wa habari kuhusu kuhusishwa kuwa kimapenzi na Irine.
Sikutaka kuyaweka wazi mahusiano yangu na Irine hasa katika kipindi kile ambacho Precious alikuwa amejifungua na tayari alikuwa ameshapata wasiwasi juu ya habari alizokuwa akizisikia kuhusu Irine.
Nilikuwa makini sana tena zaidi ya kuwa makini, kumbukumbu hazikunipotea, nilikuwa nikikumbuka kila kitu nilichokuwa nikikizungumza, sikutaka kung’atang’ata maneno, nilizungumza ukweli wa kile ambacho niliamini kisingeweza kuniumbua baadae.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****
Maisha yaliendelea huku nikiendelea kuuficha ukweli wa mahusiano yangu na Irine. Nilijaribu kumshirikisha juu ya kile nilichokuwa nikikifanya na kumuuliza kama nilikuwa sahihi au la. Alionekana kufurahishwa sana, hakutegemea kama ningeweza kufanya hivyo, hilo ndilo lililozidi kumfurahisha kiasi kwamba akazidi kunipenda kupita kawaida.
“Ujue mimi sikutegemea kama ungeweza kufanya hivyo,” aliniambia nilipokuwa nyumbani kwake Tegeta majira ya usiku, tulikuwa chumbani, wakati huo nilikuwa nimevaa bukta huku juu nikiwa kifua wazi na yeye alikuwa katika vazi la kanga laini aliyokuwa amejifunga mpaka kifuani ndani yake hakuwa amevalia chochote. Alikuwa amekilaza kichwa chake kwenye mapaja yangu.
“Hukutegemea nini sasa?”nilimuuliza huku nikimpapasa uso wake laini ambao haukuwa na chunusi hata moja.
“Mimi nilijua ungeitumia nafasi hiyo kutafuta kiki,” aliniambia kwa sauti nyororo iliyogubikwa na wimbi la jinamizi la mapenzi lililokuwa linataka kuniingia hasa kwa mapema kiasi kile, niliwahi kulikemea.
“Irine sipo na wewe kwa lengo la kutafuta umaarufu bali nipo na wewe kwa lengo moja tu,” nilimwambi kisha nikanyamaza, nikamtazama, alionekana kuwa na shahuku ya kutaka kufahamu lengo langu. Akanyanyua kichwa chake kutoka katika mapaja yangu kisha na yeye akanitazama, tukatazamana.
“Lengo gani?” aliniuliza hapa ni baada ya uvumilivu wa kutazamana kumshinda.
“Nataka kutengeneza maisha bora na wewe na si bora maisha,” nilimwambia.
“Maisha bora?” aliniuliza.
“Ndiyo Mpenzi, natamani vitu vingi sana nifanye na wewe na vyote haviwezi kutimia bila ya kitu kimoja.”
“Kitu gani?”
“Upendo yani mapenzi ya dhati.”
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha bila upendo hakuna maisha bora, bila upendo hakuna familia bora ambayo nitaweza kutengeneza na wewe, bila upendo siwezi kufunga pingu za maisha na wewe, bila upendo siwezi kufanya lolote na ndiyo maana nikakuambia natamani vitu vingi sana lakini ukikosekana upendo nitashindwa.”
“Mume wangu.”
“Niambie.”
“Kitu gani unatamani kutoka kwangu.”
“Natamani mengi sana lakini kikubwa natamani mtoto.”
“Hilo tu?”
“Ni miongoni kati ya ninavyotamani kutoka kwako.”
“Usijali mimi nitakuzalia tena sio mtoto ni watoto.”
“Nitafurahi sana nahisi ndoto yangu itakuwa imetimia.”
“Ndoto yako gani?”
“Kuwa na mtoto yani mrithi wa mali zangu.”
“Usijali Mpenzi nimeumbwa kwa ajili yako yote unayotaka nitakutimizia kama ni mtoto pia nitakupatia.”
“Kweli?”
“Ndiyo Hubby sioni sababu yoyote ya kukudanganya.”
“Mimi nafurahi na tena najivunia kukupata katika maisha yangu umekuwa mwanamke wa kitofauti sana kwangu.”
“Inamaana hao wengine walikuwaje?”
“Vivuruge tu yani pasua kichwa.”
“Hahaha! Lakini kwangu je?”
“Kwako Napata burudisho la moyo pumziko la ubongo.”
“Kwa maneno sikuwezi.”
“Huo ndiyo ukweli,” nilimwambia.
Kwa muda ambao tulimaliza mazungumzo, mikono yangu haikuacha kutulia sehemu moja, ilikuwa ikitalii sehemu mbalimbali za mwili wa Irine, kuna muda nilikuwa nikizichezea nywele zake mara nikashuka shingoni nikaitomasa, nikashuka kifuani na hatimaye nikaangukia mapajani mwake, nilikuwa katika weweseko la mapenzi, sikutulia sehemu moja kama mlinzi aliyekuwa malindoni, kila sehemu ya mwili wake ilikuwa imeumbwa ikaumbika haswaa!, hakukuwa na sehemu nilipopashika kwa muda ule kisha akawa amenyamaza kimya kama sanamu, alikuwa akitoa mguno kuashiria alikuwa akipata msisimko.
“Unataka nini tenaaaaaaa umeanzaaaa,” aliniambia kwa sauti iliyoanza kukosa uvumilivu.
“Baby nipe kidogo,” nilimwambia huku nikiifungua kanga yake, alikuwa ameifunga kizembe hivyo sikupata kazi sana ya kuifungua kilaini tu ilifunguka na sasa macho yangu yakawa ana kwa ana na vya siri alivyokuwa amevificha kangani.
Sikutaka kubaki kumshangaa kama bongo movie isipokuwa niliianza kazi yangu ya kucheza na bustani yake. Nilihakikisha mpaka anazidiwa vya kutosha ndipo ambapo niliweza kuingia mchezoni, sikutaka kumpa nafasi ya kuichezea mashine yangu ambayo na yenyewe ilikuwa tayari imezidiwa, nilimlaza chali kisha nikaanza kuingiza mashine taratibu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Aaaaaaiiiishhhhhh ooooooohhhh jamaniiiiii Dickkkk mbona tamu hivyooooo aaahhhhh ooooohhh,” aliniambia huku akitoa miguno mara baada ya kuingiza mashine yangu. Ilipoingia sikutaka kuipotezea muda wake ilianza kufanya kazi yake. Niliendelea kulisakata kabumbu mpaka pale wazungu weupe waliponibishia hodi, walikuwa wakitaka kutoka.
“Dick mwagia ndani tu…mwagiaaaa aaaahhhhh,” aliniambia huku akiendelea kutoa miguno ya kimahaba.
“Mmmmmhhhh ooooooooohh,” nilianza kutoa miguno wakati ambao wazungu walikuwa njiani kutoka nje.
“Mwagia babyyyyy babyyyyy babyyyyyy aaaaaahhhh oooooooh tamu baby tamuuuuu,” alizidi kutoa miguno huku akiwa amening’ang’ania, wakati huo nilikuwa tayari nimeshatoa wazungu weupe.
Tuliendelea kuucheza mchezo huo, tulipochoka tulipumzika, tulipopata nguvu mpya tuliendelea mpaka pale ilipofikia mwisho wa mchezo wetu wa utamu. Irine alinishukuru kwa kumridhisha usiku ule. Tulikwenda bafuni kuoga, tuliporudi tulijitupa kitandani kisha usingizi mzito uliweza kutupitia.
****
Niliamka katika siku ambayo naweza kusema ilikuwa ni siku mbaya sana kwangu, siku hiyo Magazeti yaliandika habari mbaya sana kuhusu mimi, sijui ni nini kilitokea au ni nani alitokea na kwenda kuzipeleka habari zile kwa waandishi wa habari ila nilijikuta tu! nikikumbana na skendo ambayo kwa upande wa pili wa shilingi ilikuwa na ukweli ndani yake na ni katika hiyo skendo iliweza kunipa funzo.
Ilikua ni siku ambayo magazeti yaliandika habari kuwa nilikuwa nikitembea na mke wa mtu ambaye nilibahatika kuzaa naye mtoto na kibaya zaidi waliandika kuwa hata nyumba ambayo nilikuwa nikiishi ni ya huyo Mwanamke ambaye alinihonga mara baada ya kufanikiwa kumpa ujauzito. Kwa kweli habari hizo ziliniweka katika mshangao wa hali ya juu, sikujua ni nani ambaye alihusika katika hilo, mtu wa kwanza ambaye nilimfikiria kwa wakati huo alikuwa ni Precious, niliamini Precious ndiye mtu pekee ambaye alikuwa akiufahamu ukweli huu tena aliniahidi kuwa itabaki kuwa siri kati yetu.
Sasa kwanini anisaliti?
Hili ndiyo lilikuwa swali kubwa ambalo nilijiuliza lakini sikuweza kupata jibu lolote. Kichwa changu kilitawaliwa na maswali lukuki.
“DICK KAZAA NA MKE WA MTU.”, “UKWELI KUHUSU DICK KUWA NA MTOTO.”
Hivi vilikuwa ni baadhi ya vichwa vya habari vya magazeti ya udaku yaliyopamba moto kwa habari hizo siku hiyo.
“Dick utaniambia nini kuhusu hili?”
“Hakuna kitu.”
“Hakuna kitu wakati huu ndiyo uchafu unaoufanya?”
“Irine mimi hata sielewi naona mapichapicha.”
“Mapichapicha wakati kila kitu kinaonekana hapa au unataka kuniambia waandishi wa habari ni waongo?”
“Irine hakuna ukweli wowote ulioandikwa hapa niuwongo mtupu.”
“Dick usinifanye mimi mtoto mdogo sawa naelewa kila kitu.”
“Irine huo ndiyo ukweli ambao naufahamu sina ukweli mwingine.”
“Dick kumbe na wewe haujatulia?”
“Mpenzi wangu kwanini hutaki kuniamini?”
“Sitaki kukuamini na sitakuamini Dick, najutia maamuzi yangu ya kuwa na wewe kumbe nyuma ya pazia una mtoto halafu umezaa na mke wa mtu?”
“Irine nielewe mpenzi hakuna chochote ninachokifahamu kwanza mimi mwenyewe nashangaa sijui ni nani amepanga kunichafua.”
“Unashangaa? Inamaana unataka kujifanya hujui kinachoendelea?”
“Sijui Irine kweli tena yani nimechanganyikiwa.”
“Umechanganyikiwa wakati hiyo ndiyo tabia yako. Hivi Dick ni kitu gani umekosa kwangu, ni nini ambacho umekikosa kwangu.”
“Hakuna kitu nilichokosa kwako.”
“Dick naomba uniache, niache Dick.”
“Irine mpenzi wangu nipe nafasi basi nijieleze.”
“Nikupe nafasi gani Dick, nimekupa moyo wangu lakini tayari umeshaumiza naomba uniache Dick.”
“Irine.”
(Alinyamaza kimya) huku machozi yakimdondoka.
“Irine mpenzi wangu.”
(Alinyamaza kimya)
“Nipe nafasi mpenzi wangu nijieleze,” nilimwambia lakini hakujibu lolote, alinyamaza kimya kana kwamba alikuwa bubu, nilijitahidi kumsemesha kadri niwezavyo lakini hakuna nilichoambulia zaidi ya machozi yake aliyokuwa akibubujikwa.
Nilikumbuka usiku wa siku hiyo tulitoka kufanya mapenzi tena hakukuwa na tofauti yoyote kati yetu lakini nilishangaa tukiamka katika asubuhi ya tofauti, asubuhi ambayo ilibadilisha kila kitu katika mapenzi yetu.
Tulikuwa katika ugomvi ambao uliletwa na skendo ambayo ilinihusu kwa asilimia kubwa wala hakukuwa na cha kuficha kwani kila kitu kiliwekwa wazi.
Nilijitahidi kudanganya kama ilivyokuwa kawaida yangu lakini uwongo wangu uligonga mwamba. Hakukuwa na uwongo niliouzungumza kisha ukaenda kumuingia Irine ambaye alionekana kuwa mwenye hasira sana hasa baada ya kugundua kuwa sikuwa muaminifu katika mapenzi, nilimdanganya vya kutosha.
Kitendo cha kugundua kuwa nilizaa na mwanamke mwingine nje tena mke wa mtu kilimuumiza sana, hakujua ni kwa jinsi gani alitakiwa kunieleza ili niyagundue mamivu aliyokuwa nayo. Kupitia machozi yake pamoja na ukimya alioamua kukaa baada ya kushindwa kuzungumza lolote, nilifahamu alikuwa katika wakati wa hasira, alibaki akinitazama muda wote.
“Nijibu basi mpenzi,”nilimwambia kisha nikamtazama, alionekana kuwa mwenye hasira sana.
“Naomba Dick uende, niache na maisha yangu,” aliniambia maneno ambayo alimaanisha.
Sikutaka kuwa king’ang’anizi sana kwa wakati ule kwani Irine alikuwa tayari ameshagundua ukweli wa kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Niliamua kuondoka nyumbani kwake kisha nikaelekea nyumbani kwangu huku kichwa changu kikiwa na maswali lukuki ambayo yaliniweka katika wakati wa mawazo.
Nilikuwa nikiwaza mambo mengi sana lakini mpaka nafanikiwa kufika nyumbani kwangu sikuwa nimeng’amua lolote lile, nilionekana kuchanganyikiwa kutokana na kile ambacho kilikuwa kimetokea. Sikujua ni nani ambaye alikuwa akinifuatilia undani wa maisha yangu.
Nilianza kupata mashaka na mtu ambaye nilikuwa nikimtilia mashaka alikuwa ni Precious, nilihisi yeye ndiye alikuwa amehusika kwa asilimia kubwa katika kuzisambaza habari zile kwa waandishi wa habari ili aweze kujitengenezea umaarufu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliamua kumpigia simu huku nikiwa mwenye hasira sana, nilitamani kumtukana lakini alipopokea ajabu nilishindwa kufanya hivyo, alikuwa akilia na yale aliyonieleza yalizidi kunichanganya kabisa akili yangu.
“Dick mume wangu, mume wangu Dick,” aliniambia mara baada ya kupokea simu, sauti yake ilinidhihirishia wazi kuwa alikuwa katika kilio kwa wakati huo, kilio chake kikazidi kunichanganya.
“Sasa unalia nini na mume wako amefanyaje?” nilimuuliza.
“Kwanini umeamua kunichafua kwenye magazeti kwanini Dick, mume wangu akijua huoni utaniletea matatizo kwenye ndoa yangu?”
“Precious mbona unanichanganya?”
“Nakuchanganya na nini Dick, umeamua kunichafua magazetini kwanini umenifanyia hivyo?”
“Inamaana unataka kuniambia wewe hauhusiki kabisa na tukio hili?”
“Tukio gani?”
“La kuwaambia waandishi wa habari kuhusu usiri wa jambo hili.”
“Simjui mwandishi hata mmoja hivi nitaanzaje kwenda kutangaza wakati najua kuwa hii ni siri tena tumepanga ibaki kuwa siri kati yetu,” aliniambia Precious maneno ambayo kiukweli yalizidi kuniweka katika wakati wa mawazo, mpaka kufikia wakati huo sikujua ni nani ambaye alihusika katika kuzitangaza habari zangu kwa waandishi wa habari. Nilikuwa katika wakati mgumu sana kwani ni muda mfupi ulikuwa umepita tangu nilipoweza kugombana na Irine kiasi kwamba akaamua kunifukuza nyumbani kwake.
Nilizidi kupagawa baada ya Precious kuniambia kuwa hakuhusika na lolote katika habari zile kwani kwa upande wake alikuwa katika mshangao na muda wote alikuwa akilia kwa kumuhofia mume wake endapo angeweza kuziona au kuzisikia habari zile.
“Kwani mume wako yuko wapi?” nilimuuliza swali ambalo sikumbuki kama niliwahi kumuuliza siku za karibuni, ni muda mrefu ulipita sikutaka kuzisikia habari za mume wake, niliamua kufanya hivyo kutokana na sababu za Precious kutopendelea kusikia habari za mume wake pindi anapokuwa na mimi.
“Yupo,” alinijibu kwa sauti iliyochanganyika na uwoga.
“Sasa unaogopa nini?” nilimuuliza.
“Dick mume wangu namjua na endapo akizisikia habari hizi sijui uso wangu nitauweka wapi?”
“Precious kila kitu nahisi imeharibika na sijui itakuwaje?”
“Dick kwani ni nani ameenda kuwaeleza waandishi wa habari?”
“Mimi sijui yani nimechanganyikiwa Precious.”
“Mungu Wangu.”
Mpaka kufikia hapo nilikuwa nimechanganyikiwa, nilihisi kuwa na nuksi katika siku hiyo, akili yangu haikuwa sawa na kila nilichokuwa nikikifikiria nilihisi kukosea hivyo vyote nilivipuuzia.
Kwa wakati ule nilipokuwa nikizungumza na Precious na kutoambulia lolote nilichoamua ni kukata simu. Sikuwa sawa hata kidogo. Nilikumbuka kulitafuta gazeti ambalo lilikuwa limeandika habari iliyonihusu na hapo niliamuakulitafuta jina la mwandishi aliyehusika kuiandika habari ile. Isack Mwakyonya ndiyo jina nililokutana nalo la mwandishi wa habari hiyo, niliamini kwa asilimia kubwa ukweli wa maswali yote yaliyokuwa yakinizonga akilini mwangu majibu yake alikuwa nayo yeye, niliamini kama yeye hakuhusika katika kudadisi ukweli ule basi alikuwepo mtu wa pembeni ambaye alihusika kuzitoa habari hizo kisha nay eye akaweza kuziandika. Niliinakili namba yake ya simu kisha sikutaka kupoteza muda niliamua kumpigia, simu yake ilionekana kuwa bize lakini sikukata tama, niliendelea kupiga kila mara mpaka pale nilipobahatika kumpata. Alipopokea niliwahi kujitambulisha kwa jina ambalo haikuwa rahisi kwa yeye kuweza kunifahamu.
“Nazungumza na nani?” aliniuliza kwa sauti iliyoonekana kuwa bize kiasi kwamba hata kitendo cha kupokea simu kilikuwa kikimkwaza.
“Naitwa Akilimali Kazipesa.”
“Akilimali?”
“Ndiyo.”
“Ok Akilimali niambie nikusaidie nini?”
“Bila shaka nazungumza na Isack mwandishi wa habari gazetini?”
“Ndiyo mimi bila shaka hujakosea vipi una dili la habari nini?”
“Ndiyo tena ni zaidi ya dili la habari.”
“Nipe sasa ndugu tupige pesa mjini hapa.”
“Ni kweli lakini kwa habari hii itabidi tuonane ili niweze kukueleza kila kitu.”
“Habari yenyewe inamuhusu Staa au?”
“Ndiyo tena staa wa bongo movie.”
“Ok niambie kwahiyo unataka tukutane wapi?”
“Labda wewe ndiyo uniambie unataka tukutane sehemu gani?”
“Nafikiri maeneo ya Beach itapendeza zaidi.”
“Beach gani?”
“Tukutane Sunrise Beach Resort.”
“Kwa leo itawezekana?”
“No, maybe we do tomorrow.” (Hapana, labda tufanye kesho.)
“Muda gani?”
“Mchana.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawa,” nilimjibu kisha na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mazungumzo yetu.
Kwa maongezi ambayo nilizungumza na Isack Mwakyonya alionekana kuwa mtu wa kupiga dili kupitia habari za mastaa, nililifahamu hilo baada ya kugundua kuwa na mimi nilikuwa ni miongoni kati ya wateja ambao walikuwa wakimpelekea habari za udaku jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote. Sikutaka kuufikiria ule umbali uliyokuwepo kati ya Mbezi Beach na Mji Mwema, Kigamboni ambapo ndipo ilipokuwa Sunrise Beach Resort bali nilichokuwa nikikifikiria kwa wakati huo ni kukutana na Isack kisha niitumie nafasi hiyo katika kumbaini mtu aliyehusika katika kunichunguza kiasi kwamba akaamua kunichafua magazetini.
****
Picha zangu pamoja na Precious ziliendelea kusambaa mitandaoni, kila mtu alikuwa na lake la kuandika kwa siku hiyo. Wapo waliyoitumia siku hiyo katika kunitukana na wengine waliitumia kama sehemu moja wapo ya kujiingizia kipato kupitia blog mbalimbali za kijamii.
Nilianza kupigiwa simu na waandishi wa habari kutoka sehemu tofautitofauti ambao walikuwa na lengo la kunifanyia interview kuhusu skendo ile iliyokuwa ikinikabili magazetini. Wote sikutaka kuzungumza nao, niliamini kwa kufanya hivyo nilikuwa naendelea kulilinda jina langu ambalo tayari lilikuwa limeanza kuchafuliwa na magazeti ya udaku.
Laiti kama ingetokea kama ungekutana na mimi kwa wakati ule kisha ukaniuliza kuhusu hadithi au kitu kinachohusu kazi yangu kwa kweli nisingeweza kukujibu jibu fasaha. Akili yangu haikuwa sawa hata kidogo, nilikuwa nikiwaza kitu kimoja tu! ambapo nikukutana na huyo Mwandishi wa habari na niweze kumfahamu huyo mhusika ambaye alikuwa ananifuatilia. Kuna muda nilianza kupata mashaka juu ya huyo mwandishi wa habari, nilihisi kuna mchezo alikuwa akiufanya dhidi yangu na kwa maana hiyo nisingeweza kuufahamu ukweli kwani nilikuwa naenda kukutana na mhusika mwenyewe. Hilo lilizidi kuniweka katika wakati wa mawazo, nikakumbuka ule mchezo mchafu ambao ulikuwa ukifanywa na waandishi wa habari wenye lengo la kukuchafua halafu baadae wanakuambia ili wasikuchafua inabidi uwalipe kiasi cha pesa ambapo wataweza kuipotezea habari.
Bado sikutaka kuamini kirahisi kuwa nilikuwa katikamhuo mchezo, kila nilichokuwa nikikiwaza nilikiona kuwa na uwongo ndani yake.
“Kama kweli nia yake ni kutafuta pesa kupitia hiyo skendo mbona sasa hajanitafuta?” nilijiuliza swali lililonifanya nipuuzie lile wazo lililokuwa limenijia. Kwa wakati mmoja nilikuwa nikiwaza mambo mengi sana, sikuacha kumuwaza Irine msichana ambaye alihusiika kwa asilimia kubwa katika kunipa umaarufu ambao kwa muda ule ulikuwa ukinitesa, maisha yangu yalibadilika na kuwa kama ya mnyama digidigi. Kuna muda nilijilazimisha tabasamu usoni mwangu, nikataka kutabasamu kinafki lakini tabasamu halikuja, sikuhitaji kutabasamu kwa wakati huo hivyo nilikuwa katika mkunjo wa sura.
Nilimpigia simu Irine, simu yake ilikuwa ikiita tu! bila kupokelewa, niliamini kuwa aliamua kufanya kusudi kunipokelea kutokana na tatizo lililokuwa limetokea. Wakati nikiendelea kumpigia Irine bila mafanikio akili yangu ikaanza kumuwaza Precious, sikujua alikuwa katika wakati wa aina gani wala sikujua kama mume wake alizipata habari hizi au la. Hilo sikutaka kujisahaulisha, habari ile ilikuwa ni habari mbaya lakini ilisambaa kila kona ya nchi na niliamini mpaka kufikia wakati ule hakukuwa na mtu ambaye alikuwa hafahamu kile kilichokuwa kikiendelea.
Kitendo cha kuendelea kumuwaza Precious ambaye alikuwa akilia na akimuhofia mume wake kilikuwa kikizidi kuniweka katika wakati wa maumivu, sikutakiwa kuwa katika hali hiyo kwa wakati huo. Niliamua kuacha kumuwaza japo ilikuwa ni ngumu kufuta kumbukumbu za mtu ambaye tayari alikuwa akilini mwako, nikajitoa ufahamu kisha nikampigia simu rafiki yangu Mick, alipopokea simu yangu sikutaka akuzungumza lolote zaidi ya kumwambia kuwa nilihitaji kuonana naye.
“Kuna nini?” aliniuliza.
“Nataka tuonane nitakwambia,” nilimwambia.
“Sasa tukutane wapi?” aliniuliza.
“Njoo hapa nyumbani kwangu mida hii kaka,” nilimwambia.
“Sawa nakuja,” alinijibu.
Baada ya kupita dakika kadhaa Mick aliweza kufika nyumbani kwangu, nilimkaribisha kwa kumpa juice hapa ni baada ya kudai kuwa alikuwa ameshiba chakula kisha sikutaka kupoteza muda nikaanza kumwambia kile nilichokuwa nimemuitia.
“Nimekuita hapa ndugu yangu nina tatizo.”
“Tatizo gani tena au kuna demu wa kishua umempata nini?”
“Acha masihara ndugu yangu ina maana unataka kuniambia hujasoma magazeti leo?”
“Hapana ujue mimi sio mpenzi sana na hayo magazeti hasa ya udaku nikisoma labda nimekosa kazi ya kufanya. Vipi kwani kuna nini?”
“Aisee ndugu yangu mambo yameharibika.”
“Mambo yameharibika! Mambo gani tena.”
“Waandishi wahabari tayari wameshaufahamu ukweli wangu.”
“Ukweli wako upi tena?”
“Wameniandika kuwa nimezaa na Precious yule mke wa mtu.”
“Duh! Sasa ni nani ambaye ameenda kuwaeleza waandishi wa habari.”
“Yani mimi mwenyewe sielewi hapa nimechanganyikiwa.”
“Na Irine naye imekuwaje?”
“Irine amekataa kabisa kunielewa baada ya kuziona habari hizi yani hapa ninavyokwambia hataki kabisa kuniona.”
“Umejaribu kuongea naye vizuri?”
“Yani nimeongea naye kila aina ya lugha lakini hataki kabisa kunisikia wala kuniona.”
“Duh! Sasa itakuwaje?”
“Sielewi Mick yani akili yangu imechoka.”
“Lakini rafiki yangu mimi nilikwambia huo mchezo wako unaoufanya kuna siku utakugharimu sasa umeona jinsi unavyotaabika wakati kazi ilikuwa ni ndogo tu!”
“Kazi gani?”
“Kazi ilikuwa ni kutulia na demu mmoja tena Evadia yote haya yasingekukuta.”
“Mick nimekuita hapa kwa ajili ya ushauri na si unikumbushie kuhusu huyo Malaya Evadia.”
“Evadia ndiyo Malaya au wewe mbona sijakuelewa hapo.”
“Mick embu tuachane na hiyo mada, tuongelee haya ambayo yanatuhusu.”
“Mimi kwa ushauri wangu hapo itabidi umtafute huyo mwandishi aliyeandika hiyo habari kisha fanya kuzungumza naye kirefu nadhani anaweza akakueleza ukweli kuhusu mtu au lengo la yeye kuiandika habari hiyo.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tayari nimeshafanya mawasiliano naye.”
“Anasemaje?”
“Bado sijazungumza naye ila tumepanga kukutana sehemu kwa ajili ya mazungumzo.”
“Una uhakika?”
“Ndiyo.”
“Mnaenda kukutana wapi?”
“Sunrise.”
“Mimi naamini endapo ukikutana na huyo mwandishi wa habari kila kitu kitaenda sawa hivyo jiamini.”
“Imani imepotea Mick yani nimekuwa mpole nauona mwisho wangu kwa kweli.”
“Nadhani katika hili kwako litakuwa ni funzo na tena utajifunza haswaa!” aliniambia Mick maneno yaliyopenya vyema na kuniingia akilini.
Nilimuamini sana Mick na kila ambacho alichokuwa akiniambia nilikishikilia kama ngao ambayo nilihakikisha inanikinga na kila baya ambalo lilikuwa linakwenda kunitokea. Maneno yake machache yaliyojawa na ukarimu yaliniongoza vyema japo kuna kipindi nilikuwa mkaidi nikaona ufahari kwa kubadilisha wanawake kama nguo lakini hakuacha kunisihi kuacha tabia niliyokuwa nayo.
Nilifanya yale kwa sababu ya umaarufu wangu, tangu nilipokuwa maarufu Facebook na Instagram kupitia Machombezo yangu na hatimaye nilikuwa maarufu katika kiwanda cha filamu na kuwa kama mwandishi bora wa filamu niliyekuwa napendwa zaidi.
****
Siku iliyofuata nilikwenda kukutana na Isack Mwakyonya mwandishi wa habari tuliyeahidiana kukutana Sunrise, nilipofika nilimtafuta na kumjulisha kuwa tayari nilikuwa nimeshafika lakini ajabu simu yangu hakuwa akipokea hata pale nilipomtumia ujumbe mfupi wa kumtaarifu kuwa nilikuwa nimeshafika hakuweza kunijibu lolote. Hilo lilizidi kunishangaza, nikaangalia vyema kama pale nilikuwa Sunrise kweli au la. Naam! Nilikuwa ndani ya Sunrise lakini mtu ambaye niliahidiana kukutana naye pale hakuweza kunipa ushirikiano wowote, sijui niseme katika lugha ipi ili muweze kunielewa vyema labda niseme alinidanganya au aliniuza kwa maana nyingine. Nilimsubiri eneo lile huku nikitegemea wenda angeweza kunijibu lakini haikuwa hivyo. Ukweli ni kwamba alinidanganya na baada ya kukaa masaa kadhaa bila mafanikio yoyote niliamua kuondoka.
Barabarani nilionekana kukasirishwa sana na tukio lile, sijui ni nini ila nilihisi kudharauliwa mno. Ni bora angenieleza ukweli kuliko kunidanganya. Hilo lilizidi kuniweka katika wakati wa mawazo na lawama nilizokuwa nikizitoa kama mwendawazimu.
Nakumbuka nilipofika kivuko cha Kigamboni Ferry, nilipokea ujumbe kutoka kwenye namba nisiyoifahamu, iliniandikia hivi,
“PRECIOUS AMEJIUA YEYE PAMOJA NA MTOTO WAKE.”
Nilipousoma ujumbe huo uliweza kunitatanisha, ghafla! mwili ukaanza kunyong’onyea nikaishiwa nguvu.
Kwa kweli nilikuwa nimeshaanza kuchanganyikiwa, akili yangu haikuwa sawa kabisa. Nilichoamua kukifanya ni kutafuta mahali ambapo niliweza kuegesha gari halafu nikautumia muda huo katika kuwaza kile nilichokuwa nimetumiwa katika ujumbe mfupi. Kuna muda nilijaribu kuyafumba macho yangu na kuhisi wenda nengeweza kuamka katika usingizi wa ndoto lakini haikuwa hivyo, nilikuwa katika maisha halisi, maisha ambayo tayari nilikuwa nimeanza kuyaona machungu.
“Amejiua?” nilijikuta nikijiuliza swali ambalo sikujua hata nilitakiwa kujijibuje, ni hapa ambapo nilihisi kuchanganyikiwa kabisa. Nikaichukua simu yangu kisha nikaifungua na kuingia katika kitabu cha kuhifadhi majina. Nilianza kupitia jina moja baada ya lingine, kwa wakati huo sikuwa najua hata nilikuwa natafuta nini. Nilikuwa nimeshapagawa ndugu msomaji. Niliwaza mambo mengi sana kila nililokuwa nikiliwaza sikulipatia ufumbuzi mwisho nilizidi kujiumiza kichwa.
Ghafla! Mick akawa ananipigia simu, haraka nikapokea kisha nikanyamaza kimya kumsikiliza kwa umakini.
“Dick ndugu yangu umeona sasa maisha yako ulivyoyaharibu, Aagghh! Ona sasa nimesikia yule mke wa mtu uliyezaa naye amejiua halafu sijui nani Precious kitu kama hicho yani Dar imechafuka kila kona ni habari kuhusu wewe,” aliniambia Mick maneno yaliyonifanya niingiwe na uwoga wa hali ya juu.
“Sasa ndugu yangu hapo tunafanyaje, eeehh! Utanisaidiaje ndugu yako niondokane na janga hili?” nilimuuliza Mick, yani hata sikuwa najua ni nini nilichokuwa nakizungumza. Akili yangu haikuwa kabisa pale.
“Yani hata sijui nitakusaidiaje,” aliniambia kisha akanyamaza kidogo halafu akaendelea kuzungumza.
“Kwani uko wapi sasa hivi?” aliniuliza.
“Nipo huku Ferry Kivukoni,” nilimjibu.
“Vipi yule mwandishi tayari umeshakutana naye na anasemaje?”aliniuliza.
“Hakuna nilichoambulia, ameniuza nimekuja mpaka huku nampigia simu ajabu hapokei wala hataki kujibu meseji zangu,” nilimwambia Mick kwa sauti ya kipole iliyoambatana na uwoga ndani yake.
“Dah! aisee pole sana ndugu yangu,” aliniambia Mick.
“Asante kwahiyo tunafanyaje?” nilimuuliza.
“Wewe si unarudi huku?”
“Ndiyo kaka.”
“Fanya tuonane ili tuzungumze kitu.”
“Mick nimekwama ndugu yangu sijui kama utaweza kunisaidia ili niweze kuondokana na fedhea hii iliyonikuta.”
“Kila kitu kitawezekana ila fanya tukutane pale Bamaga.”
“Bamaga?”
“Ndiyo.”
“Hapana Mick unajua wazi kabisa sasa hivi habari zangu zimesambaa kila kona sasa tukikutana hapo bamaga huoni itakuwa kama najiuzisha vile na waandishi wa habari wananitafuta kila kona.”
“Sasa wewe unataka tukutane wapi?”
“Mimi nafikiri tungekutana nyumbani kwangu tu.”
“Kweli basi tufanye hivyo,” aliniambia Mick.
Nilianza kuhisi Mick ndiye alikuwa mtu wa pekee ambaye angeweza kunisaidia kuondokana na janga hili ambalo lilikuwa limenipata, hofu yangu bado ilikuwa katika habari ambayo niliipata kuhusu kifo cha Precious, niliamini kwa asilimia kubwa kulikuwa kuna tukio lililokuwa linafuata baada ya hapo. Nikaanza kumfikiria mume wa Precious, sikujua kuwa alikuwa katika hali gani. Nilijaribu kuyapima yale maumivu ambayo angeweza kuyapata kipindi ambacho angeweza kusikia kuwa nilikuwa nikitembea na mke wake ambaye nilizaa naye mtoto aliyekuwa akimlea huku akiamini kuwa alikuwa ni mtoto wake wa damu, sikuacha pia kupima yale maumivu ya kufiwa na mke ambaye tena aliamua kujiua kwa kukiikimbia fedheha. Kwa kweli nilizidi kuziona siku za uhai wa maisha yangu zikupungua taratibu, nilikuwa nikikiona kifo changu mbele ya macho yangu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipofika nyumbani kwangu nilimkuta Mick akiwa tayari ameshafika, alionekana kunisubiria muda mrefu sana bila kuchoka. Niliposhuka kwenye gari mlinzi aliweza kunifuata na kuniletea habari nyingine ngeni kabisa. Aliniambia kulikuwa na watu watatu ambao walikuja kuniulizia, kati yao alikuwepo mwanamke mmoja aliyekuwa amembeba mtoto, mwanaume pamoja na mama mtu mzima.
Aliponiambia hivyo nikakumbuka kama kulikuwa na watu ambao nilipanga kukutana nao kwa siku hiyo, hakukuwa na mtu ambaye nilipanga kukutana naye, nikazidi kuchanganyikiwa aliponiambia kuwa kati ya hao watu pia alikuwepo mwanamke ambaye alikuwa amembeba mtoto. Kwa kweli nikazidi kuchanganyikiwa sana, sikujua ni nini kilichokuwa kikiendelea. Akili yangu ilikuwa imechoka, nikaamua kuingia ndani na Mick.
“ Vipi ndugu yangu,” aliniambia Mick.
“Dah! we acha ndugu yangu nahisi kufakufa,” nilimwambia Mick kisha akawa anacheka kwa sauti.
“Na utakufa kweli kwa huu mchezo unaoendelea aisee usipokuwa makini tunakwenda kukusahau,” aliniambia.
“Mchezo…Mchezo kivipi na kwanini useme nitakwenda kusahaulika?”
“Usijifanye huelewi kitu Dick, usijitioe ufahamu.”
“Sielewi kitu ndugu yangu ndiyo maana nauliza, sipo sawa kabisa.”
“Sasa ukisikia ukubwa au yale maneno sijui kuwa uyaone ndiyo haya, wanawake wanakwenda kukutoa roho.”
“Dah! yani nimekoma ndugu nimekomaa.”
“Huwezi kukoma bila funzo inabidi kwanza upate funzo halafu ndiyo ukome.”
“Unamaanisha nini unaposema hivyo.”
“Muda mfupi kabla hujaingia niikuwa nafuatilia habari katika website fulani hivi…nimekuta wameandika kuwa unahusikakwa namna moja ama nyingine na kifo cha Precious ambacho kimewaacha watanzania kinywa wazi….kila mtu haamini kwa kilichotokea, sijui hata utasema nini hapo.”
“Lakini..”
“Hakuna cha lakini hapo inabidi ukubaliane na kila kitu kilichotokea.”
“Siwezi, siwezi Mick lazima nipambane katika hili.”
“Huwezi nini sasa na utapambanaje kwa kitu ambacho ni kweli kinakuhusu….ukweli ni kwamba wewe ni Malaya na umalaya wako leo unakwenda kukugharimu maisha.”
“Mick.”
“Niambie Dick Mapenzi.”
“Mi naona kama hunishauri kitu hapo na lengo la mazungumzo haya ni unishauri nini nifanye ili niondokane na fedheha hii.”
“Cha kukushauri nini ufanye kwa kweli nitakudanganya labda nikwambie kitu kimoja.”
“Kitu gani?”
“Subiri dunia ikufunze kwanza maana umeshachelewa.”
“Mick unajua sikuelewi kabisa.”
“Huwezi kunielewa kwasababu akili yako haipo hapa..inawaza mambo mengi kwa wakati mmoja, sasa utawezaje kunielewa hapo,” aliniambia Mick.
Maneno ya Mick yalizidi kunifanya niiingiwe na hasira hasa baada ya kuwa nilikuwa nikimtazama wakati alipokuwa akizungumza, kuna muda nilitamani hasira zangu zote nizimalizie kwake kwa kumpiga lakini nilihisi kukosea kufanya hivyo. Nikabaki kuwa mpole nikiendelea kumsikiliza.
Sijui ni nini kilitokea ila nilishangaa Mick akakurupuka kutoka kwenye sofa alilokuwa amekaa na kuja upande niliyokuwepo huku akiwa ameishika simu yake, alikuwa akinionyesha mahojiano yaliyokuwa yakifanyika Live kupitia Application ya Hiza Tv, yalikuwa ni mahojiano kati ya mwanaume mmoja ambaye alikuwa akihojiwa na waandishi wa habari.
“Unamfahamu huyu mwanaume?” aliniuliza Mick.
“Hapana simfahamu,” nilimjibu.
“Aiisee wewe mwehu kweli inamaana hata kusoma huwezi,” aliniambia kisha nikayasoma yale maandishi ambayo yalikuwa yameandikwa kwa chini, yalikuwa ni maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa rangi nyeusi na yalikuwa yakisomeka,
“MUME WA MWANAMKE ALIYEJIUA KISA SKENDO CHAFU.” Maneno hayo yaliambatana na picha ya Precious.
Sikutaka kuamini kuwa Martine Deus jina ambalo liliandikwa pale ndiye alikuwa mume wa Precious. Moyo wangu ulizidi kuwa katika maumivu makali mno, kila nilipokuwa nikimuona Martine Deus nilihisi kuchanganyikiwa.
“Tunafanyaje?”nilimuuliza Mick.
“Hapa hakuna cha kufanya zaidi ya kutoroka, inabidi uende mbali sana ukajifiche maana inaonekana mpaka sasa unatafutwa,” aliniambia Mick kisha nikakubaliana na maneno yake. Niliamini kama ningeweza kuondoka na kwenda kujificha mbali nisingeweza kukamatwa.
“Sasa natakiwa kwenda wapi?”
“South Africa.”
“South Africa?”
“Ndiyo huko ndiyo kwenye usalama wako.”
“Naenda kufikia kwa nani?”
“Kuna ndugu yangu mmoja yuko huko nitafanya mazungumzo naye kwa njia ya Email halafu kila kitu kitakuwa sawa.”
“Una uhakika?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Niamini,” aliniambia Mick.
Siku iliyofuata Mick alianza kunihangaikia mipango ya kusafiri kwenda South Africa. Ilikuwa ni safari ya ghafla! na nilikuwa nikienda kwa kuzamia. Hakukuwa na njia nyingine niliyoiona kuwa na usalama kwangu zaidi ya kuondoka na kwenda huko mahali ambapo niliamini kulikuwa na usalama wa maisha yangu.
Hatimaye siku ya safari ikawadia, nikaenda Airport kwa kujifichaficha, Mick alikuwa akinisindikiza lakini kitu cha kushangaza tulipofika Airport tulikamatwa na watu waliyojitambulisha kuwa walikuwa ni polisi. Walikuwa na lengo la kunikamata na kunipeleka polisi, sikutaka kubisha wala kupingana na lolote lile kwa wakati huo, safari ya kwenda South Africa iliishia hapo na sasa nikakamatwa na wale watu waliojitambulisha kuwa walikuwa ni polisi, wakaniingiza katika gari lao kisha tukaondoka eneo lile. Mick tulimuacha Airport, sikutaka kujiuliza mara mbilimbili kwanini tulimuacha. Ajabu wale watu waliyojitambulisha kuwa ni polisi nilishangaa wakinipeleka sehemu nisiyoijua, ilikuwa ni sehemu tofauti na kituo cha polisi kama ambavyo waliniambia hapo awali. Tulitoka nje kidogo na jiji la Daresalaam, tuliingia katika moja ya pori ambalo kiukweli mpaka kufikia muda huo sikuwa najua lolote lililokuwa linakwenda kutokea.
“Shukaaaa,” aliniambia jamaa mmoja baada ya gari kusimama pembeni na pori lile.
“Kuna nini jamani?” niliwauliza.
“Wewe unajifanya kidume subiri sasa uoneshwe kuwa hapa mjini kutembea na mke wa mtu ni hatari,” alisema yule jamaa maneno ambayo yalinishtua sana, nilifahamu kuwa wale hawakuwa polisi kama walivyokuwa wamejitambulisha. Nilikuwa nimetekwa na wale watu nisiowafahamu kabisa, niliposhuka na wao wakashuka. Kuna muda nikatamani kukimbia eneo lile lakini nilishindwa. Wale watu walionekana kuwa katika miili iliyojengeka kimazoezi, walionekana kutisha mno kutazama na ni hapa ambapo niliamini ule ndiyo ulikuwa mwisho wa maisha yangu.
Baada ya dakika kadhaa mara likatokea gari aina ya Hummer, lilikuja na kupaki pembeni na pale ambapo nilikuwa nimesimama kisha akashuka mtu aliyevalia mavazi ya suti nyeusi, alionekana kuwa mtu nadhifu sana, nilipomtazama sura yake haikuwa ngeni, niliwahi kumuona sehemu. Alikuwa ni yule mume wa Precious. Alionekana kutawaliwa na hasira sana, uso wake ulihifadhi chuki, alionekana kunichukia sana aliponitazama.
“Ulidhani utanikimbia?” aliniuliza kisha akawa anajilazimisha kucheka kwa sauti kubwa sana huku akiwa ananipigia makofi ishara kama ya kunipongeza jambo fulani.
“Hongera sana Dick, hongera kwa kufanikiwa kummiliki mke wangu tena kwa kuuonyesha ukidume wako ukadiriki mpaka kuzaa naye,” aliniambia maneno ambayo yaliniumiza sana.
“Nadhani ulifikiri kwa mpango aliyokushauri rafiki yako ungeweza kuwa salama, ulipanga kuondoka sasa ona uko sasa hivi?” aliniuliza swali la kunikejeli kisha nikajaribu kuyalinganisha na maneno ya Mick. Kulikuwa na uhusiano, niliamini bila shaka Mick alikuwa ameniuza na kweli alifanikiwa katika hilo.
Yule mume wa Precious hakutaka kuwa muongeaji sana, alipanga kufanya vitendo kwa wakati ule. Kitu ambacho nakikumbuka aliniuliza swali moja tu, swali ambalo majibu yake yaliweza kunigharimu.
“Umetembea na mke wangu, amekuhonga nyumba, gari na kila kitu ulichokuwa unakihitaji. Hilo siwezi kukudai wala kuhusu nyumba na gari nimeamua vibaki kuwa kama zawadi yako lakini kwa muda huu nataka uchague kati ya vitu hivi vitatu ili uweze kuyaokoa maisha yako,” aliniambia.
“Vitu gani hivyo?” niliuliza huku nikionekana kuwa na hofu, wale watu waliyokuwa wamenikamata kwa wakati huo walikuwa wamenizunguka halafu mimi pamoja na mume wa Precious tulikuwa katikati.
“Chagua Kati ya kifo yani tukuue, tukuingilie kinyume na maumbile yako au tukuchome sindano ya kuua nguvu zako za kiume?” aliniuliza swali ambalo jibu lake lilikuwa gumu.
Kwa muda ambao nilikuwa nikifikiria tayari Martine alikuwa ameitoa bastola na kuninyooshea, alikuwa amedhamiria kuniua.
“No! No! usiniue,” nilimwambia kwa sauti ya uwoga kisha nikanyamaza kidogo kiasi cha kumeza fundo la mate halafu nikaendelea kuzungumza.
“Ni bora unichome sindano tu, ndiyo nipo tayari,” nilimwambia kisha akaonekana akiwapa ishara wale watu waliyokuwa wamenizunguka. Haikupita sekunde wakanikamata na kunichoma sindano.
Kwa kweli niliyasikia maumivu makali mno, nilijitahidi kuvumilia lakini uvumilivu ulinishinda mwisho nikapitiwa na usingizi wa nusu kifo.
****
Niliamka na kujikuta nipo hospitalini, sikujua niliwezaje kufika eneo lile. Waandishi wa habari walikuwa wamenizunguka kila kona. Nilipopata fahamu kila mmoja alitaka kuzungumza na mimi.
Nilijaribu kuzungumza nao ukweli wa kila kitu, sikutaka kuficha lolote na kitu kikubwa ambacho nilikizungumza ni tuhuma za kutembea na mke wa mtu, hilo niliweza kukiri wala sikutaka kuficha lolote.
Majibu ya daktari aliyokuja kunipa yaliweza kunipa wakati mgumu sana hasa wa kuweza kuamini. Nilikuwa nimepoteza nguvu za kiume, mishipa yangu ya sehemu za siri ilionekana kudhurika kwa kiasi kikubwa sana hasa baada ya sindano ya sumu niliyochomwa, nilikuwa hanithi kwa maana nyingine.
Dah!
Nayaandika haya huku machozi yakinilengalenga machoni. Najua sitakuwa na uwezo tena wa kupata mtoto hata yule ambaye nilibahatika kumpata kwa mke wa mtu hivi sasa ni marehemu yeye pamoja na mwanaye. Uhuni wa kuwatumia wanawake kama chombo cha starehe umeweza kuniacha na funzo kubwa sana katika maisha yangu. Naweza kusema haikupangwa mimi kuchagua kifo, au kuingiliwa kinyume na maumbile na wanaume wenzangu kwa kosa la kutembea na mke wa mtu. Ilipangwa yote haya yanifike ili siku moja niwe shahidi ambaye nitakusimulia kitu kilichowahi kunitokea katika maisha yangu kisha na wewe kijana mwenzangu mwenye tabia kama zangu uweze kujifunza.
Leo mimi nimekuwa hanithi na hakuna kitu kilichoniweka katika hali hii kama sio wanawake, wanawake wamenipa funzo kubwa sana katika maisha yangu.
Nimeamua kuandika kitabu changu kilichobeba uhalisia wa maisha yangu, nimekipa jina la NIFANYE NA MIMI KAKA DICK, naomba vijana wakisome ili wajifunze kitu kupitia mimi. Najua sina muda mrefu wa kuishi tena hapa duniani ile sumu imeweza kuniathiri kwa kiasi kikubwa sana na mpaka hivi ninavyokuandikia nimekutwa na Kansa ya ini. Najua naenda kufa lakini nakufa huku nikiacha elimu tosha kwa vijana. Naomba nisiwe mfano bora wa kuigwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
NB: Evadia aliweza kuolewa na mwanaume mwingine na baadae walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike.
Irine na yeye aliamua kurudiana na Juma Hiza na mapenzi yao yanaendelea mpaka leo.
MWISHO.
Nashukuruni sana kwa kulifuatilia Chombezo hili. Mungu awabariki.
0 comments:
Post a Comment