Search This Blog

Tuesday, 17 May 2022

MY SUZAN - 3

 







    Chombezo : My Suzan

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wakati nikiwa katika hali hiyo ya bumbuwazi nilipatwa na mshtuko baada ya kuona viumbe wale wakizidi kuongezeka kila baada ya sekunde kadhaa, ni kama vile mshtuko ule ulinigutua katika bumbuwazi lile na hapo ndipo nilipo usikia vyema ukulele wa yule dereva tax akiniita kwa nguvu kuwa nirudi kwenye gari ili tuweze kuondoka kwa eneo lile halikua salama kuendelea kubaki, ilifika muda yule dereva tax akashuka katika gari ili aje anivute tuingie kwenye gari, hapo niligeuka haraka baada ya kusikia ukulele mkubwa ambao aliutoa yule dereva tax kuonesha kwamba alikua katika hatari kubwa, na kweli nilipogeuka niliona chatu mwingine mkubwa kiasi akiwa anaanza kujiviringisha katika mwili wa dereva tax yule ambae alikua akipiga makelele ya uoga ili aweze kummeza, hapo nilitoka mbio mbio mpaka eneo alilokuwepo yule chatu ambae alikua anajiviringisha katika mwili wa dereva tax, hapo niliitoa pistol(bastola) yangu kisha nikaikoki vyema na kilichofuata nilisambaratisha kichwa cha yule chatu ambae alikua akijiandaa kummeza yule dereva tax, hapo nilimsaidia kujitoa kwa chatu yule ambae tayari alikua ameshapoteza uhai wake na kwakua yule dereva tax hakuwa sawa nimsaidia kumuingiza kwenye gari, hapo nilikaa sehemu ya usukani na kuliondoa gari kwa kasi ya ajabu kwani wale chatu wengine walikua wakija kwa kasi eneo lile ambalo tulikuwepo kwa lengo la kutudhuru, kutokana na mwendokasi ambao nilikua nikiutumia niliweza kufika mtwara mjini kwa kutumia dakika kumi tuu,spidi niliyoingia nayo katika barabara ya lami kila mtu aliyekuwepo barabarani aliweka mikono kichwani na wengi walitabiri kwamba tutapata ajali kwa mwendo ule, wengine walidhani kuwa huenda sisi ni majambazi tumetoka kupora mahali…

    Waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo basi laja, kama jinsi watu walivyotabiri kuwa tutapata ajali ndivyo ilivyokua, kipindi nakanyaga mafuta mpaka mwisho sikuweza kugundua kuwa mbele palikua na bamsi nah ii ni kutokana na kutokujua vyema barabara ile, ni kitendo cha ghafla tuu na kutahamaki tayari nikawa nimelifikia bamsi lile, nilijaribu kufunga breki za ghafla lakini breki zilifeli, hapo nikalivaa bamsi lile ambapo tax ile niliyokua naendesha wakati huo tukiwa wawili tuu kwenye tax ile, tax ile irushwa juu na baada ya kutua iliviringika mara tano mfululizo, yule dereva tax nilokuwa nipo nae nilishuhudia akikata roho wakati bado hatujatolewa katika gari ile na baada ya kushuhudia tukio la kukata roho kwa yule dereva tax sikujua tena kilichoendelea kwani nilipoteza fahamu” alizungumza Mr alex huku machozi yakimtoka, alitoa handkerchief(hengach­ifu/leso) yake katika moja ya mfuko wa koti la suti ambalo alikua amelivaa na kujifuta machozi…

    “Daaa aise pole sana baba kwa yaliyokukuta” alizungumza michael katika hali ya huzuni kubwa na kuumia moyoni

    “Nashukuru mwanangu nimeshapoa” alijibu Mr alex

    “Enhe baada ya hapo ikawaje baba” aliuliza tena michael na kufanya Mr alex kuendelea kusimulia kilichomkuta baada ya ajali ile mbaya kuwahi kutokea katika maisha yake..

    “Basi nilipokuja kupata fahamu nilijikuta nipo hospitalini ambapo nilikuja kugundua kuwa ilikua ni hospitali ya taifa ya muhimbili baada ya kuwauliza wahudumu ambao walikua wakipishana kuingia katika chumba ambacho nilikua nimelazwa, nilijaribu kuamka na hapo nilikumbana na maumivu makali sana ambayo yalinifanya nitoe ukulele hafifu na baada ya hapo nilipoteza tena fahamu, siku ambayo nilikuja kupata fahamu nilisikia mchakacho wa kama mtu akikimbia na baada ya hapo nikisikia sauti ya kike ikisema kwa nguvu..

    “Doktaa ameamkaaa”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hazikupita hata sekunde tano liliingia jopo la madaktari wapatao watano ambapo walipoingia walitabasamu baada ya kuona nimefungua macho, hapo nilitolewa mashine ya (Oxygen) oksijeni ambayo nafikiri ndiyo iliyokua ikinisaidia kupumua kipindi ambacho nilikua nimepoteza fahamu, baada ya mashine ile kutolewa ndipo nilipoanza kuangaza macho huku na huko, nilijaribu kuvuta kumbukumbu jinsi ilivyokua na hapo niljikuta machozi yakinitoka baada ya kukumbuka matukio yote niliyokutana nayo ambayo yalipelekea mimi kuwa hapo hospitali ya taifa ya muhimbili kwa kipindi hicho, niligeuka upande ule ambao ulikuwa na jopo la madaktari, niliwaangalia kwa awamu na hapo niliwauliza nipo wapi maana chumba ambacho nilikuwepo mara ya kwanza kilikua ni tofauti na chumba ambacho nilikuwepo kwa muda huo…

    “Tulia Mr alex kwanza pole kwa yaliyokukuta” alizungumza mmoja wa madaktari ambaye alionekana ndiye mkubwa wa jopo lile la madaktari waliokuwepo mule ndani, muda huo nilikuwa najiuliza maswali mengi sana kichwani, kwanza nilijiuliza wamejuaje jina langu na nipokumbuka kwamba nilikuwa na vitambulisho pamoja na vyeti vyangu basi nilijikuta mawazo hayo yakiisha na hapo ndipo nilipokumbuka kuwa kuna dokta alikua ananiondelesha, basi nilianza kumjibu yule dokta maswali ambayo alikua akiniuliza…

    “Pole sana Mr alex kwa yaliyokukuta” alizungumza daktari yule ambae alikua akizungumza kwa umakini wa hali ya juu..

    “Nashukuru sana dokta…”

    “Sawa naitwa dokta Hashim, wenzangu hapo ni dokta jack, dokta john,dokta abdul na dokta Razaq” alitambulisha dokta hashimu na baada ya hapo aliendelea..

    “Mimi nahusika na masuala ya mwili kwa ujumla lakini nimebobea katika kutibu magonjwa ya moyo, ini pamoja na figo, huyo dokta jack yeye amebobea katika maswala ya mifupa, dokta abdul yeye amebobea katika maswala ya ubongo na mshtuko na dokta razaq yeye amebobea katika maswala ya psychology(saikolojia) pamoja na maswala ya kizazi(reproductive issues as general)” dokta hashimu aliweka nukta na kumeza funda la mate kabla hajaendelea…

    “Nashukuru kwa utambulisho dokta, samahani kwa swali hili ambalo nataka kukuuliza” aliongea Mr alex

    “Bila samahani, unavyotuona hapa tupo kwaajili ya kukujibu maswali ambayo yatakuwa yanakutatiza” alijibu dokta hashim na kumtoa wasiwasi Mr alex

    “Tangu nimeletwa hapa nina mda gani?” Mr alex aliuliza

    “Ulifikishwa hapa muhimbili miezi miwili iliyopita, lakini mwezi mmoja kabla ya kuingizwa katika chumba hiki cha wagonjwa mahututi(ICU) ulipata fahamu lakini manesi ambao walikua zamu siku hiyo wanasema ulivyopata fahamu ulipiga ukulele na baada ya hapo ulipoteza tena fahamu, kesho yake ndipo tukakuleta huku katika wodi ya wagonjwa mahututi na hapo kwakuwa mapigo yako ya moyo yalikuwa chini tulijaribu kuyastua ambapo yalipanda kidogo na hapo ndipo tulipokuwekea mashine hiyo ya kupumulia ambayo tumekutolea muda sio mrefu, na ulidumu katika hali hiyo ya kupoteza fahamu huku ukiwa unapumulia mashine kwa muda usiopungua takribani wiki nne kasoro mpaka siku hii ya leo ambayo ndo umepata fahamu” dokta hashimu alimaliza maelezo yake aliyoyatoa kwa kirefu ambapo Mr alex alimuelewa vema…

    “Na vipi kuhusu gharama na huduma ambazo mlikuwa mnanipatia, ni nani ambae alikua anashughulika na hili?” Mr alex aliuliza tena kwani alizijua vyema hospitali za bongo, huwezi kutibiwa kama utakuwa huna pesa…CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usijali gharama zote nilizitoa mimi mpaka kufikia leo hii, nah ii nimeifanya kwa moyo kwani nilipatwa na huruma sana baada ya kuona mwili wako ukiwa katika hali mbaya, hapo nimuomba Mungu anisaidie niweze kupambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba unarudi katika hali yako ya kawaida, na ninamshukuru Mungu kwa kutenda muujiza mpaka wewe unapumua kwa wakati huu” alizungumza dokta hashim.



    Mr alex alipigwa na butwaa baada ya kusikia kua dokta hashimu alisimamia gharama zote za yeye kutibiwa kwani hakuamini kama katika dunia hii bado kulikua na watu wenye moyo kama dokta hashimu, hii ni kutokana na kuona jinsi dunia inavyoenda, watu hawasaidiani, watu wanachukiana, watu wanadharauliana, watu wanauana, wenye pesa wanawadharau masikini kwa kuwaona hawapaswi kuishi, sasa alishangaa kuona mtu mwenye moyo kama ule kuwepo katika kizazi hiki cha nyoka…

    “Nashukuru sana dokta Mungu akubariki na akuzidishie kipato chako kaka yangu” Mr alex alijikuta akizungumza maneno hayo huku machozi yakimtoka, hakika alijiona ni mwenye bahati sana, ingawa alikua ana fedha za kutosha kama pasinge tokea mtu ambae angejitolea kumsimamia mpaka hapo alipofikia, angeshakua marehemu kwani pesa alikuwa nazo sawa lakini nani akijua kwamba pesa za kujilipia matibabu alikuwa nazo ilihali yeye alikuwa kapoteza fahamu kwa muda wa miezi miwili?, hakika kama dokta hashimu asingejitolea kumlipia matibabu yake basi toka siku nyingi jina lake lingeshabadilika kutoka Mr alex mpaka kuitwa marehemu,angeshakua mfu na kwa kipindi hiki pengine wadudu kama funza na wengine wangekuwa washautoboa toboa na kuuharibu mwili wake vibaya kipindi ambacho angekuwa yupo kaburini, hakika alifarijika sana na kumshukuru mungu na kumuombea dokta hashimu na wenzake wote waliomsaidia waishi maisha marefu na kama wakija kupoteza maisha basi mungu azilaze roho zao mahali pema peponi, Mr alex alishindwa hata amshukuru mungu kwa kiasi gani kutokana na ukuu aliomtendea…

    “Oooh ahsante Mungu kwa kila jambo” aliongea Mr alex kukamilisha shukrani zake kwa Mungu…

    “Daa asee kweli bana hapo Mungu alikutendea muujiza” alizungumza Michael huku akishusha pumzi ndefu..

    “Ndo hivyo mwanangu Mungu alinitendea miujiza” alizungumza Mr alex kuthibisha alichokisema michael

    “Enhee baada ya hapo ikawaje?” aliuliza tena michael na baada ya swali hilo Mr alex aliendelea kusimulia yale yaliyomsibu mpaka kufika hapo alipofika…

    “Basi baada ya kumshukuru Dr hashim, ndipo alipovunja ukimwa tena kwa mara nyingine na kuniambia….

    “Aaaa samahani mr alex kuna tatizo limetokea ila kwa kua wewe ni mwanaume naamini utavumilia na kujikaza kiume” alizungumza dokta hashimu kumuambia mr alex

    “Tatizo gani tena dokta? Nimekua kilema nini sitaweza kutembea tena katika maisha yangu?” alizungumza Mr alex katika hali ya hamaniko…CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana mr alex haujawa kilema ila yakupasa usikilize kwa umakini sana kwani ukija kukiuka utakayoambiwa unaweza ukajisababishia matatizo makubwa sana katika maisha yako” alizungumza dokta hashimu katika hali ya utulivu wa hali ya juu sana

    “Jamani kiyu gani hicho tena mbona unanitisha dokta?” Mr alex aliuliza kwa hali ya uoga sana

    “Yakupasa utulie na utilize hofu yako, na yakupasa kuwa mtulivu na msikivu sana katika hili mr Alex” alizungumza dokta hashimu na baada ya hapo alimrusu dokta razaq ambae alikua amebobea katika masuala ya psychology(saikolojia) na masula ya kizazi kuzungumza juu ya jambo hilo.

    Kitendo cha dokta hashimu kumruhusu dokta razaq kuzungumza juu ya tatizo ambalo limemkuta mr alex, kengele ya hatari iligonga kichwani mwa mr alex alishaelewa maana yake nini kwa alishafahamu kuwa dokta razaq ni mtaalamu wa masuala ya saikologia pamoja na masuala ya kizazi hivyo alijua fika kama hatokua na tatizo la kisaikolojia basi atakua na tatizo la kizazi, na ingawa alijua fika kuwa lazima atakuwa na tatizo moja kati ya hilo aidha la kisaikolojia au linalohusu kizazi alijitahidi kumuomba mungu amuepushie na hayo matatizo, alikatishwa katika dimbwi la mawazo baada ya dokta razaq kuanza kuzungumza na hapo aliweka umakini na utulivu wa hali ya juu katika kumsikiliza ni kitu gani dokta razaq alikua akitaka kumuambia…

    “Mr alex kwanza pole kwa yaliyokukuta, japo kuwa ni makubwa yakupasa umshukuru mungu kwa kila jambo kwani binaadamu ndio sisi na haya matatizo tumeumbiwa pia sisi wanaadamu, hivyo katika hali yeyote ile litakapo kufika jambo aidha liwe jambo zuri au baya, lakusikitisha au lakuhuzunisha, lakufurahisha au lakuliza, yakupasa umshukuru mungu wako kwani yeye ndiye mpangaji wa kila jambo, hakuna jambo ambalo linashindikana kwake, yeye nduye mpangaji wa kila jambo linalotokea, yeye ndiye anayeamua leo litokee hili au leo lisitokee hili, hivyo yakupasa umshukuru mungu wako kwa kila jambo, pia kaa ukitambua na kujua ya kuwa kila neno limeshaandikwa kinachosubiriwa ni andiko litimie tuu, yakupasa ukubaliane na kila jambo ambalo tayari limeshatokea katika maisha yako, yakupasa usimame kiume na ukabiliane na changamoto ambazo utakumbana nazo katika maisha yako” yalikua na maneno ya faraja na kutia moyo ambayo alikuwa akizungumza mtaalam wa masuala ya saikolojia pamoja na kizazi dokta razaq…

    “Sawa dokta nimekuelewa na nashukuru kwa maneno yako kwani yamenitia moyo na faraja pia, mungu akubariki dokta” alizungumza mr alex

    “Usijali na karibu, ila pasina kupoteza muda kwani unahitajika kupumzika, nikwamba wakati ulipopata ajali kuna vipande vidogo vidogo vya kioo ambavyo vilifanikiwa kupenyezza katika suruali yako ambayo kwa kipindi ajali ilipotokea suruali hiyo ilichanika kwa kiwango kikubwa hivyo kusababisha eneo kubwa la mwili wako kubaki wazi, baada ya kufanya uchunguzi wa kina ndipo nilipogundua kuwa vipande hivyo vilifanikiwa kuingia katika ngozi ya korodani zako ukizingatia ngozi hiyo huwa ni laini sana hasa katika kipindi cha joto kali kama hichi, vichupa hivyo viliweza kuathiri kwa kiasi kikubwa vimirija ambavyo huwa vinatunza shahawa wa muda ambavyo vimirija hivyo vinajulikana kwa kitaalamu kama(seminiferous tubules), nilijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu na nilifanikiwa kuvitoa vipisi hivyo vya kioo ambavyo vilikuwa vimeathiri vimirija hivyo, licha ya kuvitoa tayari kuna madhara ambayo yalishatokea baada ya vipande hivyo kupenyeza katika ngozi ya korodani zako,pia nilijitahidi kukabiliana na madhara hayo ili yasije yakaendelea kutokea na nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia madhara hayo ambayo endapo yangetokea yangesababisha wewe kupata hali ya utasa ya kutoweza kumpa ujauzito mwanamke yeyote yule kwa kitaalam tunaita(infertility), sambamba na jitihada hizo pia ya kupasa kuacha kushiriki tendo la ndoa kwa muda wa miezi saba ili sehemu ambazo tulizifanyia matibabu katika vimirija hivyo viweze kupona kabisa, ila kama utakiuka hilo basi hautokuja kupata mtoto katika maisha yako yote, nafikiri utakuwa umenielewa vyema” dokta razaq aliweka nukta na kumeza funda la mate baada ya kutoa maelezo hayo marefu na yakueleweka pia…

    “Ndio dokta nimekuelewa” alijibu mr alex…

    Mr alex aliendelea kumsimulia michael kuwa baada ya maelezo hayo ya dokta razaq, jopo lile la madaktari lilitoka na kumuacha yeye akipumzika na hapo alitafakari mambo mengi sana ambayo yalitokea katika maisha yake, mwisho wa yote alimshukuru mungu kwa kila lililotokea katika maisha yake…

    “Pole sana baba, enhe baada ya hapo ikawaje?” alizungumza michael na kumuuliza swali jingine mr alex..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Niliweza kukaa hospitali kwa muda wa miezi sita ndipo hali yangu ilipotengemaa na hapo niliruhusiwa kuendelea na shughuli zangu, lakini kabla sijatoka hapo hospitali nilipitia ofisini kwa dokta hashimu ili kwenda kumpa shukrani pamoja na kumuaga, lakini nilipofika ofisini dokta hashimu alitaka nimsimulie maisha yangu kwa ufupi, niliweza kumsimulia na baada ya kumaliza simulizi hiyo dokta hashimu aliniambia haina haja ya kurudi nchini uingereza nibaki tuu Tanzania na nitaishi nae nyumbani kwake na pia atanisaidia kupata kazi ukizingatia vyeti vyangu vilikuwa na ufaulu wa hali ya juu, kwakua dokta hashimu alinibembeleza sana ukizingatia wema alionitendea niliamua kukubaliana nae na hapo nikaanza kuishi nyumbani kwa dokta hashimu maeneo ya kariakoo, wakati nikiwa nimemaliza wiki mbili tangu muda ambao niliambiwa na daktari nisishiriki tendo la ndoa, siku moja nilikua natembea tembea katika mitaa ya kariakoo, lakini nikiwa katika matembezi hayo nilikutana na msichana mmoja mrembo sana aliejitambulisha kwa jina la mery, ingawa ndio tulionana kwa mara ya kwanza kila mtu alivutiwa na mwenzake na kuanzia siku hiyo tukawa wapenzi, baada ya wiki mbili tangu tuanze mahusiano na mery, nakumbuka ilikua siku ya jumatano siku ambayo tulipanga na mery kukutana katika gesti moja iliyopo maeneo yale ya kariakoo ili tuweze kushiriki tendo la ndoa, siku hiyo nilimuaga dokta hashimu kuwa mida ya saa tisa nitatoka na kwenda kwa rafiki yangu na kwamba nitalala huko huko mpaka kesho yake ambapo dokta hashimu aliniruhusu bila ya kipingamizi ukizingatia tayari nilishakua mwenyeji katika maeneo hayo, basi siku hiyo mida ya saa tisa niliweza kukutana na mery katika gesti tuliyopanga kukutana na hapo tulishiriki tendo la ndoa na kutokana na papara zangu za kutokufanya tendo la ndoa muda mrefu, nilijikuta nikishiriki tendo la ndoa na mery pasipo kuvaa kinga(condom)” baada ya kufikia hapo Mr alex alidondosha machozi kuonesha kuna jambo ambalo nilibaya lilimkuta hasa baada ya kushiriki tendo la ndoa na mery pasina kutumia kinga(condom)…

    “Pole baba usilie, kwani ulipatwa na nini baada ya kufanya mapenzi na mery?” michael alimpa pole Mr alex na kumtupia swali jingine

    “Basi mwanangu baada ya kushiriki nae tendo lile asubuhi ya siku iliyofuata ambayo ilikua siku ya alhamisi niliweza kuacha na mery na kila mtu akaelekea eneo ambalo alikua akiishi, nilikaa kwa muda wa wiki mbili tu huku nikiwa nawasiliana na mery kupitia kwenye simu, kwa muda huo wa wiki mbili tangu niliposhiriki tendo la ndoa na mery nilianza kuona mabadiliko katika maumbile yangu ya kiume, kwani wakati nilikua nikienda haja ndogo nilikua napata maumivu makali sana, maumivu hayo yalizidi na ikafikia kipindi nikawa nikienda haja ndogo basi haja ndogo ilikua ikichanganyikana na damu, hali hiyo iliniogopesha na nilimueleza dokta hashimu mwanzo mpaka mwisho, dokta hashimu alinichukua na kunipeleka hospitali ambapo alinipima mwenyewe na hapo nilikutwa na gonjwa la ngono lijulikanalo kama kaswende, basi alinianzishia dozi na baada ya kumaliza dozi nilimleta na mery ambae nae alikutwa na gonjwa hilo ambalo kwake lilikuwa sugu hali iliyosababisha kizazi chake kuharibika na hapo madaktari hawakuwa na jinsi zaidi ya kumtoa mery kizazi na kuanzia hapo mery alianza kuishi maisha ya utasa, licha ya mery kuwa tasa nilimpenda sana na nilipanga siku nitakapo pata kazi basi nitamuoa na kuwa mke wangu kabisa, nilipomwambia mery kuhusu hilo alinikatalia na kuniambia nitafute mwanamke mwingine ambae angeishi na mimi na kunizalia watoto, hali hiyo ilinikosesha raha kabisa, sikuwa tayari kumpoteza mery hivyo nilipanga lazima nitafunga ndoa na mery, baada ya kumshauri mery kwa muda mrefu huku mery akionyesha kusuasua ndipo nilipoamua kwenda hospitali kupima kama naweza kumpa mwanamke ujauzito, majibu yaliyotoka yaliniacha kinywa wazi kwani niliambiwa kuwa sina uwezo wa kumpa mwanamke mjamzito na tatizo langu limetokea hasa baada ya kuugua ugonjwa wa kaswende, basi nilitoka hospitalini hapo na kuelekea moja kwa moja sehemu ambayo alikua akiishi mery, nilimuonesha mery majibu yale na mery alionesha kushtuka lakini alinifariji na kunitia moyo, hapo pia niliamua kumdokeza tena kuhusu suala la ndoa ambapo mery alikubali nimuoe kwakua wote tulikua hatuna uwezo wa kupata mtoto, baada ya mwezi mmoja dokta hashimu aliweza kunitafutia kazi katika benki hii ya CRDB ambapo nilipata na kutokana na vyeti vyangu kuwa vizuri niliweza kuajiriwa kama maneja msaidizi(assistance maneger), baada ya kupita miezi miwili tangu niajiriwe ndipo nilipofunga ndoa na mery na kuanzia siku hiyo nilihama nyumbani kwa dokta hashimu na kuhamia katika nyumba yangu ambayo nilizawadiwa na uongozi wa benki hiyo na nyumba hiyo ilikuwa maeneo ya kigamboni na hapo ndipo nilipoamishiwa katika tawi la posta na kuwa maneger kwa kuwa kutoka kigamboni mpaka posta kulikua hamna umbali na ndio mpaka leo nipo hapa nab ado naishi na mke wangu mery na tunapendana sana” Mr alex alimaliza simulizi yake ambayo alikuwa akimuhadithia michael…

    “Daaa aisee inasisimua sana baba” alizungumza michaelCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndo hivyo mwanangu” alizungumza mr alex na kumsihi michael amalizie chakula kwa muda wa chakula cha mchana ulikuwa unakaribia kuisha, hivyo wafanye haraka ili wakaendelee na kazi…

    ****** ******** *******



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog