Search This Blog

Tuesday, 17 May 2022

MY SUZAN - 2

 







    Chombezo : My Suzan

    Sehemu Ya Pili (2)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wakati mwingine uwe unalalamika lakini usivuke mipaka kiasi cha kumkufuru mungu namna hiyo, haijalishi nimangapi umeyapitia na mangapi utayapitia, kinachotakiwa ni wewe kumshukuru mungu kwa kila hatua unayopiga kwani huwezi jua mungu amekuandalia nini mpaka wewe upitie katika magumu hayo au huwezi kujua mungu amekuepusha na nini mpaka akaamua upitie hayo magumu, hivyo ni bora ukamshukuru mungu wako kwa kila hatua unayopiga katika maisha yako” michael aliunguruma kwa sauti nzito kiasi, suzan alikaa na kuyatafakari maneno hayo na kuona kwamba ni wazi atakua amemkosea bwana mungu wake, alifunga macho yake na kuanza kuomba kwa imani….

    “Baba katika jina yesu, nakuja mbele za uso wako saa na wakati kama huu, tazama baba mimi ni mkosaji mbele zako, naomba unisamehe kwa niliyoyafanya na kutenda baba, tazama baba katika neno lako umesema samehe saba mara sabini na mimi ni mkosaji nahitaji msamaha wako, nakwenda kumfunga muovu shetani akae mbali katika maisha yangu, naomba unitakase kwa jina lako, unilinde kwa damu ya yesu, uniweke mkono wako wa kuume baba yako, nikatika jina la yesu mnazareti mwana wa mungu aliye hai nikiomba na kushukuru, aaamen”

    Baada ya kumaliza maombi yale, suzan alishuka kitandani na kupiga magoti huku machozi yakimtoka..

    “Michael mpenzi wangu, najua nimekosea, halikuwa kusudio langu kumkufuru mungu, nilikua najaribu tuu kuelezea hisia zangu na kuonyesha ni mambo mangapi mimi nimepitia” alizungumza suzan huku akiwa na uchungu mkubwa na kuonyesha wazi kua alikua akijutia jambo ambalo alikua amelifanya…

    Michael alimuangalia mpenzi wake suzan kwa tuo alimuonea huruma pia, aliamka kitandani ambapo alikua amekaa na kumfuata na alipomfikia alimuamsha sehemu ambayo alikua amepiga magoti na kumuambia….

    “Usijali mpenzi wangu mimi nimeshakusamehe kwa kua wewe tayari umeshalijua kosa lako hivyo usijali, cha muhimu ni kukaa na kujadili ni kitu gani tukifanye kwani mimi siwezi kushindwa kukusaidia wewe ukizingatia mshahara ninaoupata ni mkubwa, na pia nikuombe samahani kwa kukup….”

    “Kabla michael hajamalizia kauli yake suzan alimuwahi mdomoni na kumpiga busu zito”

    “Wakati mwingine inabidi unipige ili nijue kwamba hapo nitakua nimevuka mipaka, nakupenda sana michael mpenzi wangu”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nakupenda pia suzan, nakupenda sana na sitopenda nikuone ukiwa katika hali ya huzuni mpenzi” michael alizungumza maneno hayo kwa hisia, baada ya hapo suzan alimrukia michael mdomoni na kuanza kubadilishana mate na kichofuata hapo ni kufanya tendo la ndoa..

    Baada ya kuridhishana katika tendo la ndoa walivuta shuka na kujifunika pamoja huku suzan akiwa amejilaza kifuani kwa michael…

    Ilipotimia saa kumi na moja alfajiri alarm ilimuamsha michael katika usingizi na wakati anaamka suzan nae alistuka kutoka usingizini na waliamka pamoja….

    “Vipi honey ulivyoamka?”

    “Aaa salama tuu, sijui wewe kipenzi cha moyo wangu?”

    “Mi nimeamka salama, mmmh nambie” aliongea michael huku akimtazama suzan usoni..

    “Baby mimi nataka cha asubuhi bana”

    “Cha asubuhi ndo nini sasa?” michael aliuliza utadhani hakujua suzan alikua anamaanisha nini…

    “Aaa bana mi nataka etii”

    “Unataka nini sasa jamani my suzan”

    “Nataka hiyo hapo” aliongea suzan huku akionesha kidole chake eneo ambalo ndipo lilipo tango la michael…

    “Mimi nimechoka banaa, mimi sitaki” aliongea michael huku akiwa anamuangalia suzan kwa jicho la huba

    “Nipe bana ujue utachelewa kazini” aliongea suzan huku akionyesha msisitizo katika hilo ikionesha wazi kuwa alikua akisikia hamu ya kufanya tendo hilo kwa wakati huo

    “Unajua suzan mi….” kabla michael hajamalizia kauli yake suzan alimrukia mdomoni na kilichosikika baada ya hapo ilikua ni miguno ya kimahaba kuonyesha kwamba kuna tendo la kiutu uzima ambalo lilikua likiendelea…

    Walichezeana na kuridhishana na baada ya kumaliza zoezi lile liliwachukua takribani nusu saa nzima, walitoka na kuelekea bafuni, huko waliogeshana na kucheza michezo yote ambayo wapenzi hucheza na baada ya kumaliza walifutana maji na michael alijiandaa tayari kwa kutoka kuelekea ofisini na muda huo tayari ilikua imeshatimia saa moja na dakika kumi na tano, baada ya michael kumaliza kuvaa, alijiaangalia katika kioo kikubwa kilichopo katika chumba chao, aligeuka baada ya kujiangalia na kujiona yupo sawa na hapo alikutana na tabasamu mwanana toka kwa mpenzi wake suzan…CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Baby nikwambie kitu, leo umetokelezeaa, yani natamani tutoke wote watu watuone jinsi tunavyoendana”

    “Mmmmh hujaacha tuu vituko vyako”

    “Nitaacha pindi ukiacha kutokelezea”

    “Na sijui kama mpenzi wangu suzan atakubali hilo litokee”

    “Umeonaee, sasa ndo unaondoka hivyo au?”

    “Yaa lakini nilikua nimesahau, ebu kaa leo utafakari ni kazi gani ambayo nikikuanzishia unaweza kuifanya na wakati wa jioni nikiwa narudi kutoka kazini basi unipatie jibu, nafikiri utakua umenielewa”



    “Mimi tena kwanini nisikuelewe wewe mahabuba wa moyo wangu”

    “Okay bana ngoja nikuache, baadae basi, love you”

    “Love you too, take care of yourself, mwaaaah” alizungumza suzan na kumshushia michael busu zito katika lipsi za midomo yake..

    “Okay bye”

    “Bye”

    Michael alitoka na kuingia kwenye gari lake aina ya mercedez benz na safari ya kuelekea ofisini kwake ilianza….

    Kutokana na kutokua na foleni siku hiyo michael alifika ofisini mapema na baada ya kupaki gari lake sehemu husika aliingia ofisini na kuwasabahi wafanyakazi wenzake na baada ya hapo alipitiliza moja kwa moja mpaka ofisi kwake ambapo ndipo huwa anafanyia kazi ili kuendelea na kazi mpya pamoja na zile ambazo hakuzimalizia jana, haukupita hata muda mrefu Mr Alex aliingia ofisini kwa michael….

    “Good morning dad” alisabahi michael akimaanisha “habari za asubuhi baba”

    “Goog morning, how are you?”

    “Am fine how about you and my mom?” alizungumza michael akimaanisha “nipo salama vipi kuhusu wewe na mama yangu”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Both we are fine too” alizungumza mr alex alimaanisha “yeye pamoja na mke wake wameamka salama”

    “May we have lunch together this day?” aliuliza mr alex akimaanisha kwamba “Tunaweza tukapata chakula cha mchana pamoja siku hii ya leo?”

    “Yes offcourse” alijibu michael akimaanisha “ndio bila shaka”

    “Okay see you later and have a nice work” alizungumza mr alex akimaanisha “Tutaonana baadae, na nakutakia kazi njema”

    “Okay fine” alijibu michael akimaanisha “Hakuna tatizo”

    Baada ya maongezi hayo mr alex alielekea ofisini kwake na kumuacha michael akiendelea na majukumu yake kama kawaida…

    Mida ya saa saba na nusu mr alex alikuwa na michael katika moja ya mgahawa uliopo karibu na benki hiyo ya CRDB wakipata chakula cha mchana huku wakijadili mambo mbalimbali kuhusu maisha na kazi pia…

    “Hivi baba ulianza kufanya kazi mwaka gani katika benki hii?” michael alianzisha mazungumzo hayo baada ya kimya cha muda mrefu..

    “Aaaa nakumbuka ilikuwa mwaka 2005”

    “Inamaana una miaka 11 tangu uanze kazi hapa?”

    “Ndiyo lakini sikuanzia kazi hapa”

    “Ulianzia kazi wapi na ilikuaje mpaka ukaja huku Dar es salaam”

    “Nakumbuka ilikua mwaka 1999 ambapo nilimaliza elimu yangu ya juu katika chuo cha Oxford kilichopo nchini marekani”

    “Ngoja kwanza baba kabla hujaendelea, huko oxford ulikua unasomea nini?”

    “Nilikua nasomea masomo haya haya ya uhasibu, lakini kule nilienda kuchukua phd(philosophical doctor)(degree ya tatu) ya uhasibu, kwani stashahada yangu ya kwanza(first degree) niliipata katika chuo cha cambrige ambapo pia kutokana na kufaulu vizuri masomoyangu waliamua kunidhani na nikapata stashahada yangu ya pili katika chuo hiko hiko, kutokana na kuendelea kufaulu vizuri masomo yangu nilidhaminiwa na chuo kwenda kuongeza elimu yangu na hapo niliambiwa nichague chuo ambacho nakipenda ili niende kusoma degree yangu ya tatu yani phd, hapo ndipo nilipochagua chuo cha oxford kwani ndio chuo ambacho nilikua nakitamani tangu nikiwa mdogo, nilisoma hapo na baaada ya kuhitimu masomo yangu niliweza kufaulu kwa kiwango cha juu sana ambacho hakijawahi kutokea tangu chuo kianzishwe na hapo ndipo nilipoitwa na uongozi wa chuo cha Cambridge wakinitaka niwe muhadhiri(lecturer) wa chuo hicho katika masomo hayo ya biashara” mr alex aliweka kituo na kupiga funda moja la juisi ya embe ambayo alikua akiitumia kwa muda huo..

    “Haa kumbe ulishawahi kuwa muhadhiri wa chuo kikuu cha Cambridge?” michael alimtupia kiswali cha uzushi mr alex..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndio tena nilifundisha kwa takribani miaka mine na baada ya hapo ndipo nilipoamua kuja nchini kwangu Tanzania kwaajili ya kuja kuwasalimu wazazi wangu kwani ni muda mrefu tangu niondoke na wao walikua kijijini huko Mtwara na wakati huo simu hizi zilikua bado hazijaenea” aliongea mr alex

    “Enhee ikawaje sasa baada ya kuamua kuja nchini?” aliuliza michael kwa staili ya kudadisi..

    “Ndo hivyo mwanangu, nilienda kwa mkuu wa chuo ( Chancellor ) na kumueleza jambo hilo na bila hiyana aliniruhusu na alinipa likizo ya miezi mitatu, basi nilikata tiketi ya ndege na baada ya hapo kesho yake nikapanda ndege na kuja nchini Tanzania, baada ya kufika nchini Tanzania nilienda moja kwa moja kijijini kwetu Mtwara na hapo sikuweza kuamini nilichokikuta” aliongea mr alex huku akionekana kulengwa lengwa na machozi…

    “Mbona kama unataka kulia baba kwani ulikuta nini nyumbani?” aliuliza michael huku akimuangalia mr alex kwa umakini wa hali ya juu…

    “Kutokana na kwetu kuwa kijijini tena ndani ndani kabisa, kiasi kwamba kutoka nyumbani mpaka kwa jirani unaweza kutumia dakika kumi mpaka kumi na tano, basi baada ya kufika huku nikiwa na zawadi zangu mkononi na wakati huo nilikua nimekodi tax kutoka mtwara mjini, sikuamini pale nilipowaona chatu wakubwa wawili wakiwa wanamalizia kuwameza wazazi wangu, hakika ilikua ni picha ya kutisha kweli, nilipiga ukulele wa uchungu na hasira pia, kwakua nilikua na bastola, nilishuka katika tax ile huku nikikimbia kuelekea eneo ambalo walikuwepo wale chatu ambao kwa wakati huo walikuwa hawawezi kutembea kutokana na kumeza viumbe wakubwa ambao walikua ni wazazi wangu, yule dereva tax alikua akinipigia ukulele kuwa nirudi kwani ilikua ni hatari kutokana na kua nilikua peke yangu tena nikiwa naonekana na umbo dogo kwani alihofia kwamba chatu wale wanaweza wakanidhuru, licha ya dereva tax yule kunipigia ukulele, sikuweza kusimama wala kumsikiliza, niliendelea kukimbia upande ule ambao ndipo walipokuwa chatu waliowameza wazazi wangu huku nikiwa na hasira na uchungu mkubwa, lakini kitu kingine ambacho kilinisukuma kufanya hivyo ni kwamba nilikua na matumaini kwamba nitawakuta wazazi wangu wakiwa ni wazima kutoka na kushuhudia tukio la kumezwa kwao, basi wakati nimewakaribia wale chatu ghafla mbele yangu umbali wa kama mita tatu walitokea chatu wengine pamoja na nyoka mkubwa aina ya kobra wakiwa wanaonekana kuja sehemu ambayo nilikua nimesimama kwasababu ya kupigwa na butwaa, na viumbe wale walionekana kabisa walikua wanania ya kunidhuru, yule dereva tax alinipigia makelele kuwa nirudi kwenye gari haraka lakini kutokana na kupigwa na bumbuwazi sikuweza kumsikia na wala sikujua nifanye nini kwa wakati huo…CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog