Search This Blog

Monday, 16 May 2022

HOUSEGIRL WA DADA - 5

  







    Chombezo : Housegirl Wa Dada

    Sehemu Ya Tano (5)



    Alice alizidi kunisimulia matukio mengi sana juu yake na matukio yalivyozid aliamua kutoroka kutoka kijijini kwao had DSM lakin mzee wake alizidi kumuandama maana alifanya kosa kubwa kupokea uchawi ule ndio maana alikuja kutafuta kazi ya kufanya mjini na nyumbani kwa Dada yangu ndio ilikuwa sehemu ya kwanza kufika na kufanya kazi .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimuuliza mbona sasa ulikuwa huli chakula sana hapa nyumbani



    Clifford chakula cha kawaida nilikuwa nakiona ni mzigo kwangu maana kila usiku nilikuwa napelekwa na baba yangu kula nyama mbichi na kunywa dam hivyo mim chakula nilikuwa sioni kama ni kitam kwangu!



    Duuuuuuu!! Alice na kunipeleka mimi huko majini na kunipeleka usiku ulikuwa unakusudia nini kwangu? Nilimuuliza



    Alianza kulia sana mbele yangu huku akiniomba msamaha maana haikuwa nia yake yeye kunifanyia vile ila mzee wake alizidi kumsakama ili aniuwe lakini bibi yake na yeye mwenyew walipenda nisiuawe kulingana nilikuwa sina kosa lolote kwao hivyo bibi yake alitamani nikabidhiwe mali miweze kuishi na mtoto wao!



    Sawa alice nimekuelewa na ulikuwa unawaza nini juu ya watu wa nyumba hii? Niliuliza!



    Clifford lengo langu lilikuwa ni kumpata huyu mtoto mdogo na mama yake lakin nilishindwa kwa sababu kila nilivyokuwa nikijaribu kuingia chumbani kwao kimiujiza nilikutana na moto mkali umewazunguka kitandani hivyo sikuwa na nguvu za kuwadhuru wote wawili ndio maana nilikuwa nalazimishwa nikuchukue wew badala ya kuwakosa hawa wawili!



    Kwani walikuwa na kosa lolote kwako hadi uwachukie alice? Niliuliza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hapana Clifford ila nilikuwa nalazimishwa sana na baba yangu mzazi nisamehe Clifford nilitamani sana nitoke kwenye hali hii lakini nilikuwa nashindwa napenda sana nisali kama wengne sipendi kuwa hivi jamani Alice aliongea kwa uchungu na huzuni kubwa sana kitu kilichonifanya nimuonee huruma sana .



    Lakin mwisho nilimuuliza umeuwa watu wangapi hadi sasa alice alinijibu watu kumi watoto nane na wavulana wawaili huku mmoja wa wavulana alikuwa ni mchumba wake duuuuuuu niliskitika sana



    kuanzia hapo walianza kuniogopa wanaume nilivyoona umenitongoza nilikuwa na furaha sana sikuweza kuamini kama nimekupata ndio maana Bibi alitaka kukupatia madaraka ya kuishi na mimi



    Alice alilia sana sana niliweza kumnyamanzisha Mara kadhaa huku tukiwa tumekaa sehem moja lakin alizidi kulia sana wakati naendelea kumbembeleza pale sebuleni Dada alikuja huki ameshika tiketi ya bus na kusema alice jiandae kesho na safari sikutaki hapa tena!





    Dada baada ya kumkabidh ticket ile Alice aliipokea na kuitunza lakin alianza kulia huku akimuomba msamaha Dada yangu kwa yote yaliyotokea alianza kusimuliz upya kwa dad yangu kwa nin alikuwa vile



    alielezea matatizo yote yaliyomkumba tangu utotoni hadi alipofika pale lakin dada yangu alikuwa mgumu kulewa na alisistiza Alice lazima uondoke maana umetufanyia mambo ya ajabu sikutaki tena nekuchoka mchawi wew



    Ahaaaaaaa!! Dada nilidakia na kusema mtu ameshakuelezea kwa nini alikuwa vile na amekili kosa yakupasa usamehe maana alikuwa sio yeye akikuwa anaendeshwa bila kujua



    dada mim nimepelekeshwa na Alice humu ndani hujui tu ila nilikiwa na wakati mgumu ningekuwa wa kukata tamaa ningekuwa nimeshaikimbia nyumba yako lakin baada ya kuombrwa na yeye ametoka kwenye hali yake ya kiuchawi yakubidi tu iangalia njia sahihi ya kumsaidia Alice na sio kumfukuza nakuomba sana dada yangu!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Siwez kumsamehe huyu siwezi aliongea dada yangu!

    Wakati tunazidi kubishana na mimi kumuombea msamaha Alice alikuja shemeji huku ameshikilia zawadi na alimkabishi dada yangu lakin alimuangalia Alice na kusema mbona unalia Alice kulikoni nakuomba kuwa huru sawa hapa ni nyumbani kwako na uzidishe maombi ili mungilu akusaidie sawa!



    Dada aliitikia na kusema kesho ataondok hapa simtaki tena maana na ticket nimeshamkatia ,

    Mme wake alidkia na kusema msamehe tu maana alikuwa hajui alitendalo akurudia tens ndio utamfukuza sawa mama!



    Nami nilimtetes na kusema msamehe hata kama amekosea kias gani na ameshakili kosa nikumsakehe na kuanza maombi ya kila siku!



    Alice alizid kumpigia magoti dada yangu huku machozi yakimtoka kitu ambacho kilimfanya asamehewe aliongea neno moja alisema ' Sawa dada unanifukuza kwa kukukosea nimefany mengi ya kukukera au kuwakela wote humu ndani lakin naomba ukumbuke nikienda huko nyumbani unategemea nitakuwa nani?



    Maana maisha magumu sana ya kijijini nakuomba dada yangu nitafanya kazi at a kama hunilipi tafadhali dada nisamesh



    Hapo dada yangu alisimama na kumshika mkono alice na kusema nimekusamehe naomba uendelee kuishi hapa mimi nitakufanyia kila kitu na.utakuwa unaenda kuombewa kila sik ili kuzifutilia mbali nguvu hizo nakupenda sana Alice walikumbatiana na maisha ya kaanza upya tena!





    Pale myumbana maisha yalianza kutawaliwa na furaha maana wote tulianza kuingia kusali na alice alikuwa serious na Mungu maana alikuwa anakaa anaomba mungu aisaidie familia yake iondokane na mambo ya kichawi

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/*

    na baada ya maombi ya muda mrefu sana Mama yake alipona na kurudi katika hali yake na baba yake alipata. Pigo la kupalalaizi upande mmoja na yeye hadi leo hafanyi kazi yoyote ni mtu wa kukaa nje na kulishwa chakula hana nguvu kabisa:



    Na sasa alice anamchumba wake na mwezi wa 11 tarhe nne ataolewa shuhuli nzima ya harusi yake iko chin ya familia yetu karibun sana kwa wale wa Dar-es- salaam maeneo ya uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere maeneo ya kipawa karibia na chuo cha ufundi veta ili muweze kushuhudia harusi hio na kuweza kuamini maana alice alikuwa mmoja wa familia yetu!



     MWISHO 

0 comments:

Post a Comment

Blog