Search This Blog

Tuesday 17 May 2022

MAMA ALIPOSHIKWA TAKO MBELE YANGU - 3

 







    Chombezo : Mama Aliposhikwa Tako Mbele Yangu

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Dr kelvin alimwendea Rafiki na kumpapasa huku no akijianda kuweka mdudu wake kwenye Eneo la Rafiki ambalo lilikuwa limeloa vya kutosha

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sam alikuwa amekaa Nairobi vya kutosha na hakuna kitu alikuwa na hamu nacho kama mkewe, alikuwa amemmiss sana Rafiki na alitamani hata angekuwa nao hapo hapo alipo na wakati huo huo lakini ndio hivyo tena haikuwezekana.

    Alichukua simu yake na kuanza kuperuz kwenye picha mbalimbali zilizokuwa kwenye simu yake hadi alipokutana na picha za mkewe.



    Alianza kufunua moja baada ya nyingine, alizikagua akaangalia picha za mkewe alizopiga akiwa kavaa kihasara hasara, picha alizoacha kifua wazi, picha nyingine kavaa mini skirt pekee, picha zingine kavaa chup tu….



    Aliendelea kuangalia picha hizo hadi anamaliza sehemu zake zilikuwa zimetutumuka vilivyo kwa hamu ya mke wake.

    Alikaa akawaza kisha akaamua kumpigia simu ikiwa ni kama majira ya saa kumi na moja jioni,



    Alipiga ikaita mara ya kwanza bila kupokelewa, akapiga mara ya pili na yatatu lakini haikupokelewa pia, wivu ulianza kumshika akiwaza mkewe atakuwa wapi na anafanya nini.

    Alivyokumbuka utamu wa mkewe nakuanza kuwaza kuwa huenda kuna mwanaume mwingine anaufaidi ndio alizidi kuchanganyikiwa kabisa.

    ….nakupigia simu hupokei, utanijibu unafanya nini na uko na nani maana wanawake nawajua nyie…..



    Sam alituma hiyo meseji kwa Rafiki lakini hata hivyo alikaa kama dakika mbili bila kujibiwa na hasira zikazidi kumlipuka, aliamua kuingia bafuni ili ajisaidie na wakati akiwa huko alisikia mlio wa meseji kwenye simu yake akarudi fasta akiamini ni mkewe katuma,



    Alipofungua ujumbe aligundua ni wa wasap na umetumwa na shemeji yake ‘Verity’

    Ujumbe ule ulikuwa umeambatana na picha ya mtoto wa kike huku ukiwa umeandikwa…. “mwenzangu kwa damu kali tu nakusifu”



    Sam ghafla mawazo yote juu ya mkewe yakapotea akaanza kuangalia ile picha ya mtoto wa Verity ambae kiukweli alikuwa amefanana nae sana.



    Mwenyewe alikiri bila wasiwasi kuwa hakika anafanana mno na Yule mtoto na uwezekano wa asilimia nyingi kuwa ni mwanae ni wa uhakika.

    Akiwa kwenye hali hiyo simu yake iliita……………

    ………………………

    Wakati simu ya Rafiki ikiita Dr Kelvin alikuwa anaiona vizuri tu lakini akawa anaiweka silent ili rafiki asisikie mpaka amalize adhma yake,



    Wakati huo Dr Kelvin anataka kumuingilia Rafiki ambaye hata hivyo analeta upinzani simu ya Rafiki iliita tena na hapa ndipo Rafiki alikurupuka kitandani na kuiendea simu ambayo ilimfanya mapigo ya moyo yaende mbio.



    Alikuwa ni mumewe anapiga…. Rafiki roho ilimsuta na kuhisi kama vile mumewe alikuwa anaona yote ambayo alikuwa anafanyiwa na Dr Kelvin.



    Alishindwa kupokea maana mapigo ya moyo yalikuwa juu sana na inawezekana angeulizwa kwanini yuko hivyo na akakosa cha kujibu.



    Alitulia kidogo kisha akakutana na ujumbe kutoka kwa SAM ambao ulizidi kumuweka roho juujuu na kisha akaamua ampigie Sam sasa wakati akiwa ametulia.

    “Haloo hubyy mambo?”

    “Uko wapi wewe” aliuliza Sam kwa sauti kali kweli



    “Niko nyumbani mume wangu kwanini unauliza hivyo?”

    “Nyumbani ipi?” Sam alikuwa anaendelea kuuliza maswali ya mtego kumpima mkewe.

    “Kwanini useme nyumbani ipi kwani kuna nyumbani ngapi?”

    “Nadhani unanielewa, nijibu uko nyumbani ipi?”



    Rafiki alianza kuogopa tena akahisi mumewe kuna jambo anajua ama kuna kitu kimempa wasiwasi.

    “Nyumbani kwetu mimi nawewe”

    “acha uongo mbona niko hapa na hakuna mtu ?”



    “Haaaa mume wangu kweli, umerudi lini” rafiki alianza kujichanganya

    “Nijibu uko wapi nakwambia niko hapa nyumbani na hakuna mtu”



    “Hebu subiri kidogo mume wangu”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Rafiki alikata simu na kuizima kabisa kisha haraka haraka akaanza kuvaa nguo zake huku akiwa na mawazo tele.

    Alifanya haraka haraka akaanza kuvaa nguo moja moja kisha akkachukua mkoba wake na kuanza kutoka…

    Wakati anatoka Dr Kelvin akamvuta mkono

    “We mjinga nini, unataka kuniharibia si ndio?”



    “Umesahau simu yako mrembo”

    Rafiki alikwapua simu akachukua boda boda kisha haraka sana akaenda kwake.

    Alipofika alishuka na kumlipa Bodaboda kisha akaingia ndani kwake haraka na kukukuta kama alivyokuacha.

    Ainyanyua simu yake akaiwasha na kuipiga tena..



    Alipiga zaidi ya mara nane lakini haikupokelewa, alipiga tena na tena lakini wapi, mwisho aliamua kupanda kitandani na kujilaza akitafakari mambo mengi ambayo yamepita kwa kasi ya umeme ndani ya siku hii ngumu

    Akiwa anawaza simu yake iliita tena na aliyekuwa anapiga ni mumewe…

    “Haloooo”

    “Ulikuwa wapi”

    “Kwanini mume wangu”

    “Kwanini nini, nasema ulikuwa wapi mke wangu?”

    “Nilikuwa kwa mama”

    “Nimempigia mama sasa hivi ameniambia haupo huko, hata kwa mdogo wako pia nimepiga, hata kazini pia nimepiga, ulikuwa wapi?”

    “Ahh Ahh Nili…likuwa sokoni mme wangu”

    “Sokoni eeenh? Na kwanini uliniambia uko nyumbani alafu tena ukaniambia ulienda kwamama?”

    “SAMAHANI mume wangu”

    “Kwakosa gani ”

    “Nimesema nilikuwa nyumbani wakati nilikuwa sokoni”

    “Sasa sikiliza nataka uandae majibu ya ukweli la sivyo utaniona mbaya, na nakwambia ukweli wako ndio dawa, ninajua kila kitu kinachoendelea na mawasiliano yako nayaona”



    …………………………………..

    Sam alishahisi kitu ambacho sio sawa kabisa kwa mke wake, alihisi huenda mkewe ameanza matendo mabaya.

    Aliwaza sana kiasi kwamba alijutia kuja hii kozi ikiwa ndoa yake bado changa na walikuwa katika harakati za kutafuta mtoto.



    Aliwaza huenda mkewe anachepuka ili azae mtoto kwani ni jambo ambalo lilikuwa linawasumbua wote hivyo akaona mkewe anaweza kuwa na wazo la kujaribu kwa wanaume wengine.

    Kwa mawazo haya Sam aliamua tena kumpigia mkewe simu….

    “Jiandae uje Nairobi weekend hii inayokuja”

    “Jamani mme wangu wewe si uko masomoni”

    “Ndio tutakuwa na mapumziko ya wiki moja”

    “Sawa nitumie nauli basi”

    “Chukua kwenye mshahara wangu”



    Sam alimuagiza mkewe ambaye alijiandaa na baada ya siku mbili akapanda ndege mpaka Nairobi akapokelewa na mme wake ambaye walielekea moja kwa moja hotelini.

    Huko hotelini mchakato ulioendelea ulikuwa ni mapenzi ya kukata na shoka.

    Kwakuwa walikuwa wamemisiana kwa miezi kadhaa hamu zao zilikuwa juuu sana kiasi ambacho hakuna alyetaka kusubiri.



    Walivyoingia chumbani tu, Sam alianza kusaula nguo za mkewe, alizisaula mpaka akambakisha na chupi tu kisha akaanza mambo ya Romansi, walichezeana kwa muda kisha Sam akambeba mkewe juujuu hadi akambwaga kitandani na kuanza kunyonya nyonyo za mkewe ambaye alikuwa kamlalia kwa juu



    Wakati huu alikuwa anaitoa nguo ya ndani ya mkewe taratibu mpaka ikatoka kwa kusindikizwa na miguu ya mkewe kisha ikadondoka chini.



    Sam alichukua tango lake na kulielekeza kwenye ikulu ya mkewe na kuizamisha taratibu kitendo kilichomfanya Rafiki aachie ukulele “aaaaaaasssssssh” kisha viuni vikaanza kazi ya Propela.



    Walifanya mapenzi kwa muda mrefu kisha kila mmoja akiwa ameridhika wakaenda kuoga wakamaliza kisha wakarudi kulala usingizi ambao uliwachukua kama lisaa limoja baadae wakaamka na kwenda hotelini ambapo waliagiza chakula na vinywaji wakaanza kunywa huku wanazungumza.



    “Mme wangu huku Nairobi nasikia wana hospitali nzuri kweli, unanonaje twende kwa ajili ya ile ishu?”

    “alafu kweli mke wangu…ngoja nikupeleke kesho wakakuchek”



    …………………………………

    Kesho yake Sam na Rafiki walikuwa Kenyatta Hospital kwa ajili ya kucheki tatizo la mkewe kutokushika Mimba.

    Walihudumiwa haraka sana baada ya kujitambulisha kuwa wao ni watanzania, walifanyiwa hivi kwani wakenya walitaka wageni waondoke na sifa nzuri kuhusu huduma zao ili wapate wateja wengi kutoka Tz.



    Vipimo vilionyesha kama kawaida rafiki hana tatizo lolote kiafya na afya yake ya uzazi ni poa kabisa.

    “Umekuja na Nani binti?” dokta alimuuliza Rafiki?

    “Nimekuja na mme wangu”

    “Oooh muite aje hapa ”

    “Rafiki alitoka kidogo akarudi na mme wake”

    “Karibu sana Mr. ”

    “Ahsante sana pole na kazi Dr.”

    “asante sasa tumempima mke wako anaonekana hana tatizo lolote, hivyo basi kwa taaluma yetu tunaona umuhimu mkubwa wa kukupima na wewe ili tujue tatizo ninini hasa ”

    “Sawa hakuna shida Dr, japo mimi niko vizuri tu”

    “Ni sawa kwasababu hata mwenzio yuko vizuri pia ila ni vizuri kujihakikishia ili kufikiria vyanzo vingine”



    Sam alichukuliwa vipimo ambavyo havikuchukua mda mrefu sana na walikuwa wanasubiria majibu ambayo baada ya nusu saa waliitwa kule kwa daktari kisha wakaambiwa waketi kwa ajili ya mrejesho wa Vipimo na majibu yake……………..



    Sam na Mkewe walikuwa wamekaa wanasubiri majibu ya Dr Otieno ambaye alikuwa ameshakaa tayari kwa kuwapa wateja wake mrejesho.



    Sam alikuwa hana wasiwasi hata kidogo, alijiamini kwa kiwangi kikubwa sana kuwa yuko vizuri na hakuwa na shida kwani hata hivyo tayari yeye ana mtoto mmoja ambaye aliamini yeye ndie kazaa na Verity.



    "Sasa jamani poleni kwa kusubiri"

    "Asante dokta wala usijali"

    Dr Otieno aliweka miwani yake vizuri kisha kwa jicho kama la kuchungulia hivi akawa anasoma ile karatasi ya majibu ya vipimo.



    "Kwanza nawapa pole kwa mara nyingine katika harakati za kutafuta mtoto, najua mmepitia mengi lakini ndivyo ilivyo"

    "Kimsingi tunapompima mwanamke ambaye amekuwa anatafuta mtoto bila mafanikio kwa kipindi cha kuishi na mumewe kwa zaidi ya mwaka mmoja huku wakifanya tendo kamili la ngono ni muhimu kumpima na mumewe pia kwani Mimba sio ya mwanamke pekee"



    "Tatizo lililopo kwenye jamii nyingi za Kiafrika ni kwamba kuna mfumo ambao tatizo la uzazi (infertility) linahesabika kuwa la mwanamke pekee na mara nyingi husababisha mwanamke kuhangaika kwenye matibabu bila mafanikio huku akionekana hana tatizo lolote lakini mimba bado haitungi"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliendelea kufafanua Dr Otieno kuwa kuna wakati mwanamke anapoonekana hapati mimba hufikia hatua ya kuachwa na mumewe kwa kigezo hicho na hatimaye huweza kuolewa na mwanamume mwingine na kufanikiwa kuzaa nae, hii huonyesha kuwa tatizo lilikuwa kwa mwanamume.



    Kitaalamu uwezo wa kuzaa na ama kutokuzaa uko 50/50 kwa mwanamume na mwanamke, hivyo basi wakati wa matibabu na vipimo wahusika wote wanatakiwa wapate.



    Kutokuhudhuria kliniki kwa wanaume kumewafanya waliowengi wasipate tiba ya matatizo yao na ama kuyafanya matatizo yao yakakomaa zaidi, ndio maana tunasisitiza sa a mwanamme na mwanamke wote wapimwe.



    Sasa basi kwa upande wa Rafiki tumeona hana tatizo lolote ila tu kuna dawa itabidi upate ili kuongeza uwezo wako wa kupata mimba zaidi na pia nitakuandikia vyakula ama diet muhimu kwa ajili ya afya ya uzazi.



    Kwa upande wako Sam tumegundua kuwa kuna tatizo kwenye uzalishaji wa mbegu zako...



    Sam baada ya kusikia hivi alishtuka sana kwani hakutarajia.



    Dr Otieno aliendelea....



    "Vipimo vimeonyesha kuwa uliwahi kupata majeraha kwenye mfuko wako wa kuzalishia mbegu kitendo kinachopelekea mbegu zisizalishwe zikiwa hai lakini pia mrija wa kupitishia mbegu una uvimbe unaozifanya zisipite kwa kasi inayotakiwa"



    " labda nikuulize Mr Sam, Je? Umewahi kujeruhiwa ama kupigwa kwa vitu vizito kwenye korodani ama sehemu ya chini ya Tumbo?"

    Sam kusikia vile alipeleka kumbukumbu zake haraka sana kwenye matukio ya kupigwa na akina afande miraji pamoja na Baba yake Mkwe yaani RPC.



    Hapo hapo machozi yalianza kumwagika usoni kwake kitendo kilichomfanya Rafiki aanza kupatwa na huzuni na kuamua kumkumbatia mumewe na kumfuta machozi.



    " usijali Sam, nitakuwa nawewe bega kwa bega"



    "Nyamaza Rafiki, baba yako ndie aliyataka haya"

    Rafiki kusikia vile alianza kunyong'onyea mwili na viungo.



    " kwahiyo unanihukumu mimi Sam?"



    Dr Otieno kuona vile ikabidi aingilie...



    "Mr Sam haimaanishi kwamba hutazaa, laah! Utazaa lakini inabidi upate matibabu kamili na baadae ndipo utaweza kupata watoto, ila hupaswi kuanzia sasa kufanya mazoezi magumu"



    Dr Mimi ni askari alafu niko kozi



    “ni sawa Mr Sam lakiini mimi naingea kitaalam kwamba ni vyema ukasitisha kazi ngumu ama mazoezi magumu mpaka upate tiba kwanza”

    “Kazi ngumu kama zipi doctor”

    “namaanisha kazi zisizo za kawaida kazi ambazo haziishii tu kwenye misuli”

    Kwa Sam huu ulikuwa ni mtihani mzito kwani alikuwa anakaribia kumaliza kozi yake ambayo ingeweza kumpa cheo kizuri tu.

    Mjadala kati ya Sam na Dk ulihitimishwa baada ya kupewa dawa za kutumia yeye na mkewe kisha wakarudi hotelini walipofikia.

    ………………………..

    Mawazo ya Sam sasa yalikuwa yanarudi kwenye mtoto aliyezaa na Verity. Alikuwa anajiuliza kama yeye ana tatizo iweje kule aambiwe Yule mtoto ni wake.

    Aliwaza ni kwanini iwe hivyo? Au Verity aliamua kumdanganya?

    Wakati anawaza haya yote aliamua kuchuka tena simu yake na kuanza kuangalia picha ambazo Verity alimtumia zikimuonyesha Yule mtoto.

    Aliichunguza moja baada ya nyingine huku akiikuza kuchunguza baadhi ya vitu kwenye muonekano wa Yule mtoto.

    Kilichomshangaza ni jinsi ambavyo Yule mtoto anafanana nae…

    Alifikia hatua akaanza kutokumuamini Yule daktari aliyewatibia kwa kudhani huenda amemdanganya.

    Rafiki alikuwa nyuma ya Sam anamuangalia jinsi ambavyo mumewe anaangalia picha ya mtoto wa Verity, roho Ilikuwa inamuuma sana anapoona kile Sam anafanya.

    Alitamani amshtue lakini akawa anasita, ghafla alimuona mumewe anafunga zile picha na kwenda kwenye upande wa meseji ambapo alilitafuta jina la Verity likiwa limeseviwa Shem Verrity.

    Alipolipata Rafiki alishuhudia meseji ikitumwa….

    “Nina maongezi na wewe”

    …………………….

    Verity alikuwa ameketi nyumbani kwake baada ya kutoka kazini akawa anacheza cheza na mtoto wake.

    Kitu kilikuwa kinamfanya atabasamu muda wote ni yuke mtoto wake…alikuwa akimuangalia jinsi alivyofanana na Sam anajikuta anatabasam tu,

    Alikuwa akimuona mwanae kama vile anamuona Sam, kwa jinsi anavyompenda mume wa DADA yake (Sam), ilitosha kabisa kufurahishwa na uufanano wa mwanae kwa Sam.

    “Bebiiii”

    “Ma..ma…ma…ma”

    Kitoto cha verity kilikuwa kinamfwata mama yake huku kinaita kwa kukatakata maneno huku kinamchekea mama yake

    Verity nae alikuwa amejiachia mpaka jino la mwisho wakati mtoto wake anamshangilia, sura na muonekano wa Sam vilikuwa juu ya huyu mtoto.

    “Bebiiiii…njoo bebiiiiii….waooooooooh”

    Verity alimkumbatia mwanae.

    “Bebiiii umefanana na baba yakoooooo, hadi raha”

    Wakati Verity anamwambia mtoto hivi mtoto nae akaanza kutamka….

    “Ba…ba….ba….ba….”

    Gwakisa alikuwa amefika nyumbani anamuangalia mkewe ambaye anacheza na mtoto pasi na wao kumuona.

    Alikuwa anafurahia jinsi mkewe anavyocheza na mtoto lakini ghafla alibadili mudi baada ya kusikia verity akimmwambia mtoto amefanana na Baba yake hadi raha.

    Hapa Gwakisa alikuwa anajiuliza ni baba yupi huyo anayefanana na mtoto wakati yeye hafanani nae hata kidogo.

    Ghafla meseji iliingia kwenye simu ya Verity ambaye aliichukua asome ile meseji

    “Nina maongezi nawewe”

    Verity aliisoma hii meseji kutoka kwa Sam, wakati anataka kuijibu alicheki pembeni na kukutana na sura ya Gwakisa akiwa ameegemea mlango.

    “Baba mbona mkimyakimya”

    “Kwni hapa si nyumbani kwangu”

    “Haya karibu baba”

    “TOTOOOOOOO…umemuona baba…njoo umsalimie”

    Verity alikuwa anamvutia mtoto kwa baba yake (Gwakisa)

    “Huyu mtoto nimefanana nae eenh?” gwakisa aliuliza

    “Mh hata hujafanana nae sana, labda pua tu mimi ndio nimefanana nae” verity alijibu bila kujua kuwa anategwa.

    “Si nimekusikia sasa hivi hapo unamwambia amefanana na baba yake hadi raha, alafu saivi unasema sijafanana nae ”

    “Mh umenisikia sangapi, mimi sijasema hivyo”

    Hapa Gwakisa alizidi kuchanganyikiwa?

    “Hujasema hivyo wakati nimekusikia? Verity kuna nini kinaendelea”

    “Aaaaah si ndio hiyo pua niliyokwambia umefanana nae”

    “Yani Pua ndio useme nimefanana nae hadi raha?”

    “Ndio, kwani mbona unauliza sana, una wasiwasi juu ya huyu mtoto”

    “Sina wasiwasi wala usijali”

    Tangia siku hiyo Gwakisa alikuwa amejenga picha mbaya sana kichwani mwake kuhusu Verity na Yule mtoto.

    Kuna roho la mauaji lilikuwa limeanza kuisonga akili yake na lilikuwa linamtuma kufanya kitu kibaya.

    ……………………………CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Rafiki alikuwa anawaza mengi sana kichwani mwake, kitendo kile alichokuwa anakiona kwa mme wake na mdogo wake kilikuwa kinampa wakati mgumu sana.

    “Vipi una maongezi gani na Verity?”

    “Kwani nimesema nina maongezi nae, yanini sasa?”

    “Mme wangu…nimekuja mda tu na nimekuona unavyomuangalia mtoto wa mdogo wangu kwenye picha kisha ukamtumia verity meseji kuwa una maongezi nae, sasa unakataa nini?”

    “AHHH kwahiyo unanichunguza? Unaanza kuniendesha kwasababu nimeambiwa nina matatizo si ndio?” sam alikuja juu.

    “Usijali Sam, matatizo yako yanatibika ila unatakiwa uwe na subira, siwezi kukuendesha wewe ni mume wangu”

    Ukweli ni kwamba Rafiki alikuwa amesoma saikolojia ya mume wake na kuona kuwa haiku sawa hakutaka kubishana nae na aliona njia nzuri ni kwenda nae polepole kwa kumbembeleza asijisikie vibaya.

    Alimuendea pale alipo akamkumbatia na kuanza kumsugua sugua mgongoni ambapo Sam alianza kuwa normal na hata ile tempa ikawa imeshuka.

    Rafiki alichukua simu ya Sam na kufungua picha za Yule mtoto na kuanza kumtania mme wake..

    “Mh mume wangu umefanana na huyu mtoto?”

    “Acha bhana sasa nifanane nae kwani ni ndugu yangu?”

    “Lbda wewe ni baba yake?”

    “Acha utani bhana, Verity si shemeji yangu, kwanza umeshaambiwa mimi nina matatizo”

    “Sasa kama matatizo uliyapata baada ya kutungisha mimba, kwani si ulipigwa ukiwa tayarii ushatembea na Verity?”

    Sam alipigwa na butwaa la mwaka kwani katika akili yake alikuwa hata siku moja hajawahi kudhani kuwa Rafiki anajua kuwa aliwahi kutembea na Verity. Alijua siri hii anaijua Verity na baba yake tu kumbe Rafiki alikuwa anajua kila kitu.

    “Ahhhh….AHHHH acha utani bwana”

    Sam alishikwa na kigugumizi kabisa na kushindwa kuongea jambo la maana.

    “Tuachane nayo tuongelee yetu, ila chondechonde usije ukaharibu ndoa ya mdogo wangu”

    Sam alitaka ajibu neon lakini Rafiki alimuwahi na kumnyonya mdomo na kuanza kufanya yao hadi walipochoka na kuamua kulala.

    ………………………………………….

    Asubuhi na mapema Verity alichukua simu yake na kutaka kumpigia Sam, simu iliita kisha Sam akapokea

    “Haloo”

    “Mambo vip”

    “Poa, umeniambia una mazungumzo na mimi”

    “Ndio ni kuhusu huyo mtoto”

    “Ana nini, si tulikubaliana hutamuulizia”

    “Sawa Verity, hivi nikuulize kitu kimoja”

    “Uliza… ”

    “Mbona hospitali nimembiwa sina uwezo wa kuzaa alafu nawewe unaniambia mtoto ni wangu?”

    Wakati Verity anataka ajibu alikutana na mumewe uso kwa uso akiwa anamuangalia

    “Haloo, halooo, halooooo” Sam aliendelea bila kujua kuwa mwenzake yuko kimya kwasababu kataitika.

    …………………………

    Rafiki alitoka nje baada ya kumuona mumewe anaongea na simu kwa kujiibiza, aligundua kuwa Sam alikuwa anaongea na Verity.

    Roho ilimuuma kiasi ambacho aliona anaweza asiweze kuvumilia…akiwa anawaza simu yake iliingia meseji, alipoifungua akakutana na meseji ya Dr Kelvin… “Nimekumiss mrembo”

    Rafiki alifikiria ile meseji na kujikuta akivuta kumbukumbu nyuma na kisha akaishia kushusha pumzi kwa nguvu na kufuta ile meseji.

    ………………………

    Gwakisa alikuwa anaemia mno moyoni, na Verity alionekana kabisa hajali….

    Gwakisa aliingia kwenye kabati la nguo na kufungua chemba yake akaitazama Bastola yake kisha akaiweka vizuri, pepo la kuua lilikuwa limekaribia kabisa na vitendo, hakupenda kudharaulika…………



    Maisha ndani ya Nairobi yalikuwa yakienda kwa kasi sana, Rafiki alikaa na mme wake kwa muda wa wiki moja huku Sam akijitahidi kumtembeza maeneo mazuri nay a starehe yaliyojazana kwenye jiji hili la Nairobi.

    Rafiki alikuwa na furaha na aliionyesha usoni lakini ndani ya moyo wake alikuwa na kinyongo kinamtafuna.

    Uhusiano kati ya Sam na Verity ulikuwa unamtesa sana, alijua baada ya ndoa kila kitu kitakuwa kimekaa sawa na Sam n verity watasahauliana lakini anashuhudia uhusiano ukiendelea kwa kupigiana simu na mawasiliano ya siri kuonyesha kuwa kuna jambo kati ya hawa watu wawili linaendelea.

    Sam nae alikuwa anajaribu kuwaza kwanini Verity amemkatia simu ia alipokumbuka kuwa Verity ni mke wa mtu aliamua kuacha na kusubiri endapo Verity angemtafuta mwenyewe.

    Siku ya siku ilifika Rfaiki akapakia kwenye ndege na safari ya kurudi dar es salaam ilikuwa imewadia. Kwa kuwa Dar es Salaam hadi Nairobi ilikuwa ni takribani lisaa limoja tu na dakika kadhaa haikumchukua muda mrefu sana Rafiki kufika.

    Alifika na kuunganisha kwa basi lililokuwa linaenda Mbeya siku hiyo hiyo, akiwa ndani ya basi alikuwa akiwaza mambo mengi sana lakini mengi yakiwa yanaihusu ndoa yake.

    Alikuwa anampenda sana mme wake na alitamani awe nae muda wote ili yale yanayowahusu wayajenge pamoja.

    Alitamani sana awe na mtoto, alitamani amzalie mume wake ili atimize majukumu yake ya ndoa lakini ndio hivyo tena, wakati mwingine alijikuta akimchukia mdogo wake kwa kudhani kuwa huenda anamdharau kwakuwa yeye amezaa na Sam ikiwa yeye mwenye mume ameshindwa kumzalia mume wake.

    Akiwa anawaza kumbukumbu zake zilienda mpaka kwa Dr Kelvin na kuamua kumtumia meseji kwani tangu alipotumiwa meseji na Dr huyo hakuwahi kuijibu.

    “pole na kazi Dr. nadhani uko mzima”

    Dr kelvin akiwa kazini kwake hakuamini kuona meseji kutoka kwa mwanamke ambaye toka aanze kazi ya udaktari huku akiwa na tabia ya kutembea na wagonjwa hakuwahi kukutana na mwanamke aina ya Rafiki. Alikuwa anavutiwa nae mno, alitamani sana alale nae hata mara mia moja ikiwezekana awe wake kabisa japo ni mke wa mtu tayari.

    Kitendo cha kutumiwa ile sms kilimfanya auone ushindi ukikaribia mlangoni kwake.

    Aliacha kila kitu na kuchukua simu kwa lengo la kumpigia kabisa Rafiki.

    ………………………………

    Sam alikuwa kwenye kituo cha mafunzo ya kiusalama ambapo pamoja na mambo mengine lakini alikuwa anasomea masuala ya teknolojia na upelelezi jeshini.

    Hizi ni kozi ambazo walikuwa wanasoma watu wachache ambao huwa wanalengwa kwa ajili ya vyeo vikubwa kwenye jeshi la Polisi.

    Pamoja na uzuri wa hii kozi lakini Sam alikuwa anateswa na masharti ya dokta kwamba asifanye kazi ngumu sana hadi atibiwe tatizo lake la kutokutungisha mimba(infertility).

    “Heeey…njoo hapa”

    Sam aliitwa na kamanda wa mafunzo…

    “Kwanini hujaenda mazoezini”

    “Najisikia kuumwa mkuu”

    “Pumbaaav….haya lala chini”

    Sama alibidi alale, ahakukuwa na namna ya kujibishana na mkuu wake.

    “Roll mpaka kuleeeee kwenye gereji”

    Sam ilibiidi aanze kujibiringisha hapo chini mpaka akafika kwenye gereji ya hapa chuoni na kuamriwa ageuze tena.

    Zoezi hilo lilipoisha alikuwa amechafuka kama aliyekuwa amezikwa.

    “Miguu juu kichwa chini tembea na huu ukuta uende na kurudi”

    Hili ni zoezi lingine ambalo Sam alikuwa analia nalo akiwa anazunguka kwenye ukuta kwa kutumia mikono huku miguu ikining’inia juu ya ukuta,

    Mateso aliyokuwa anayapata alijiona wazi akiwa anaharibu masharti ya daktari, hakuwa na namna ilibidi aendelee na zoezi lake.

    Alihenyeshwa kwa zaidi ya masaa mawili ndipo akaachiwa na kwenda kujumuika na wenzake.

    Siku ya kesho yake aliamua kumfwata mkuu wa mafunzo na kumueleza matatizo yake akiambatanisha na vielelezo kutoka kwa daktari wa Kenyatta Hospital.

    “Wewe Mtizedi shenzi sana…umewahi sikia askaria akililia kuzaa?” sam alikuwa anaambiwa maneno ambayo hakuyatarajia.

    “Kwa kukupa tu taarifa, hawa wote hapa wanaowafundisha hakuna aliyepata zaa mtoto, hakuna aliyeoa bibi” askari huyu alikuwa akiongea lafudhi ya Kikenya akimwambia Sam kuwa eti sio lazima Askari azae.

    “Wewe nenda fanya research yako alafu uniambie uliwahi ona komandoo wangapi wakizaa watoto?”

    Sam kwa wakati mwingine alikutana na mtihani mwingine. Nikweli kuwa mazoezi yale magumu sana waliyokuwa wanapewa ilikuwa sio rahisi kuwa na uwezo wa kupata watoto, yalikuwa yanaharibusana mfumo wa uzazi wa awe mwanamume ama hata mwanamke.

    Sam alijipa moyo kwamba whatever ili mradi tayari ana mtoto wake mmoja.

    “Nitahakikisha namchukua mwanangu kutoka kwa Verity, sitajali chochote hata kama ni DNA tutapima, siwezi kupoteza damu yangu” sam alikuwa anawaza kimya kimya.

    ………………………………………

    Verity alikuwa anashangazwa sana na mabadiliko ya mume wake Gwakisa, upendo uliongezeka mara dufu.

    Kila siku jioni ilikuwa ni lazima watoke wakatembee wale na kunywa kwa furaha

    Kila Gwakisa alipopata nafasi ya kutoka basi alikuwa anawaletea zawadi nyingi sana ikiwemo nguo na vitu vingine vingi tu vya kupendeza.

    Ofisini kwa Verity kila mtu alikuwa anamuonea wivu jinsi ambavyo alionekana kupendwa na mume wake.

    Alikuwa analetwa asubuhi na gari na jioni anafwatwa kurudishwa nyumbani na Gwakisa huyuhuyu bila kumtuma mtu.

    Siku zilisogea kidogo na siku moja ambayo haikuwa na taarifa Verity alishtuka kupewa funguo za gari.

    “Hii ni yako baby…utakuwa unaendesha mwenyewe kwenda kokote”

    Verity alibaki mdomo wazi akiitazama Harrier Mpya ikiwa imepaki ukumbini huku iking’aa kwa upya wake….

    “Waoooh baby mbona siamini, ni lakwangu kweli”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni lako mke wangu…I LOVE YOU” Gwakisa alimwambia Verity ambaye hakutaka kusubiri akamvaa mme wake na kuanza kumnyonya mdomoni.

    Gwakisa alikuwa ni mwanamume mwenye mwili mkubwa uliojengwa kwa mazoezi, aikuwa mrefu na mwenye misuli kiasi kwamba Verity alivyokumbatiwa alikuwa kajaa kwenye kifua cha Gwakisa na kupakatwa kama mtoto huku miguu yake ikipita kiunoni mwa Gwakisa wakinyonyana ndimi.

    Zoezi liliendelea pale nje na hatimaye likahamiia ndani ambapo Verity alinyonyolewa nguo zake na kuegeshwa ukutani kisha gwakisa nae akatoa suruali yake huku akiwa kambeba verity kifuani akauchomeka mhogo wake kwenye ikulu ya Verity ambae alianza kugugumia kwa utamu.

    Uimara wa Gwakisa ulimfanya afanye mapenzi na Verity huku akiwa kamshikilia juu juu mpaka wote wakamaliza mizunguko ndio wakaachiana na Verity akashushwa chini akiwa hajiwezi kwa furaha.

    Zoezi la kufundishwa kuendesha gari liliendelea kwa siku kadhaa huku likisimamiwa na Gwakisa mwenyewe ambapo sasa Verity alikuwa na uwezo wa kuendesha gari anaenda kazini na kurudi pamoja na kwenye mizunguko mingine.

    Sam Na Verity walikuwa wanawasiliana kwa siri kitendo ambacho Gwakisa alikishtukia lakini hakutaka kusema jambo alikaa kimya tu, mapenzi kwa mkewe na mtoto aliyazidisha mara dufu kiasi ambacho kilimpa nafasi Verity kuhisi anapendwa sana,

    Kutokana na mapenzi haya Verity alimsihi sana Sam kuwa wasitishe mawasiliano kwani hakutaka kumuudhi mme wake lakini Sam alikuwa mgumu kwa kuwa alikuwa anampango wa kumchukua mtoto.

    ……………………………………..

    Gwakisa alikuwa ndani ya Gari la mkewe huku akiwa na mtoto wanaenda matembezi. Walikuwa wamekaa sehemu wanapata vinywaji na marafiki zake huku mtoto wake akiwa anacheza gemu kaka kwenye kiti.

    Rafiki zake Gwakisa ambao walikuwa hawajui kuwa Yule ni mtoto wa Gwakisa walimuuliza…

    “Gwakisa huyu mtoto ni wa nani?”

    “Mtoto wangu huyu”

    “Kweli?”

    “Haaa , huamini au?”

    “acha masihara bhana”

    “Huamini nini sasa”

    “Mh mzuri kweli, atakuwa amefanana sana na mama yake maana ulivyo na sura ngumu angefanana na wewe sijui ingekuwaje”

    Hili lilikuwa ni dongo jingine kwa gwakisa kuhusu mtoto, roho ilikuwa inamuuma ila akawa anajikaza tu.

    Maisha yaliendelea huku Gwakisa akiwa karibu sana na mtoto wake kuliko hata mtu mwingine, kwa Verity ilikuwa ni furaha na alikuwa anapenda yale mapenzi ya Baba kwa mtoto japo alijua kuwa mtoto ni wa Sam.

    “Mimi kesho ntaenda dar mke wangu”

    “Kufanyaje?”

    “Nimeitwa makao makuu ya Jeshi”

    “Mhhh tutakumis”

    “Hata mimi nitawamis, hasa haka katotoooo”

    “Nenda nae”

    “Kweli kabisa”

    Kwa Gwakisa hili lilikuwa ni zaidi ya ushindi kwani mda wote alikuwa anatafuta ni namna gani anaweza kuondoka na mtoto.

    Kitendo cha mkewe kusema hivi kilimrahisishia na kuishia tu kufurahi huku akikimbia na mtoto chumbani kwenda kulala.

    ……………………………………………

    Gwakisa ndani ya gari anaelekea DAR huku pembeni amekaa mtoto wao ambae alikuwa na amani zote anapokuwa na baba yake.

    Walikuwa wanasuka kwenye milima ya Kitonga huku safari ikiwa imeiva kabisa, kila mara Gwakisa alikuwa anakitizama hiki kitoto na kutikisa kichwa chake tu.

    Walipofika dar kwenye mida ya saa mbili usiku aliwasiliana na watu wake ambao walikuja hapo hotelini na kufanya nao mazungumzo kisha wakaagana kwa ahadi ya kuonana tena kesho yake.



    “…dadiii ojoa..”

    “Nini ”

    “Ojoa”

    “Umekojoa?”

    Ni Gwakisa akiwa na mwanae chumbani akimwambia kuwa anataka kukojoa, Gwakisa aliamka akamchukua mtoto mpaka bafuni ambapo alimvua nguo na kumpa nafasi ya kukojoa.

    Walirudi mpaka chumbani kisha wakapanda kitandani kulala. Kabla hawajalala alimvalisha pampas vizuri na nguo za kulalia kisha akamfunika na kuanza kumbembeleza kwa kumpigapiga mgongoni ili alale.

    Wakiwa wanabembelezana simu iliita ambapo alipoangalia aligundua kuwa mpigaji alikuwa mkewe,

    “Vipi mpo salama”

    “Tuko salama sijui wewe”

    “Mimi niko poa, vipi huyo mtoto hakusumbui”

    “Wala hasumbui hapa ndio anataka alale”

    “mhh hajalala tu mpaka mida hii?”

    “Hajalala ongea nae umsikie”

    Yule mtoto ambae alikuwa anaitwa Princess alipewa simu ili aongee na mama yake

    “Kamoo mamiii”

    “Marhabaaa, hujambo”

    “Jambo mamiii”

    “Haya lala mtoto mzuriiii ee”

    “Haya mamiii”

    Walipomalizana Gwakisa aliendelea kumbembeleza mtoto wake ambae alikuwa amejikunyata huku akiwa kama kamkumbatia baba yake kitendo ambacho kilimfariji sana yeye Gwakisa mwenyewe.

    Alikuwa amemzoea sana huyu mtoto kiasi ambacho alikuwa anafarijika sana kuwa nae japo wakati mwingine alikuwa anaemia sana.

    Baada ya dakika chache usingizi uliwapitia wote na kuzama katika dimbi la usingizi hadi kulipokucha siku nyingine.

    ……………………………….

    Sam alikuwa akiwaza sana kila wakati akifikiria mustakabali wa maisha yake.

    Aliwaza ikiwa hatakuwa na uwezo wa kuzaa kabisa maisha yake yatakuwaje? Ina maana hataitwa Baba kamwe, ina maana atazeeka akiwa na mkewe tu?

    Lakini je mkewe atakubali kumvumilia mpaka mwisho bila kuzaa nae au ndio ataenda kwa wanaume wengine?

    Aliwaza sana hadi mwishowe akajikuta akiichukia kazi ya Uaskari.

    Lakini hata pamoja na kuichukia kazi ya uaskari hakuona kama ilikuwa ni njia sahihi ikiwa tayari yumo humo nay a kutokea tayari yameshatokea.

    Aliamini kilichobaki kwakuwa tayari ana mtoto wake anayeamini ni uzao wake ni lazima iwe iwavyo amchukue.

    Katika mambo aliyowaza na kuyapitisha kwenye kichwa chake ni kwamba ampigie Verity simu ajadilian nae kuhusu hilo swala.

    “Haloo”

    “Enhee unasemaje?”

    “Hata salamu hakuna Verity?”

    “Hivi lakini Shemeji Sam mbona hujiheshimu?”

    “Unamaanisha nini Verity”

    “Nimeshakwambia sitaki mawasiliano na wewe, mimi ni mke wa mtu na wewe ni mme wamtu tena mme wa dada yangu, hivi ukiharibu hizi ndoa unadhani utafaidika nini?”

    “Yani wewe Verity ndio wa kusema hivyo, wewe na mimi nani ambaye alimuingiza mwenzake kwenye haya mambo?”

    “Sasa nisikie Sam, elewa kwamba yaliyoppita yamepita, mimi nampenda sana mme wangu, sitaki unigombanishe nae”

    “Sawa namimi sina shida na hilo, mimi nataka tu mtoto wangu na sio kingine”

    “HAHAHAHAAAAAA Sam umelogwa sio bure, hivi hutaniwi? Nakuuliza hutaniwiii? Aliyekwambia Yule mtoto ni wako kakudanganya na kama ni mimi basi nilikutania tu, huna uwezo wa kuzaa Sam, ungekuwa nao ungeshamzalisha dada yangu”

    Sam kwa hasira aliamua kukata simu.

    Mawazo lukuki yalikiandama kichwa chake akaona kinataka kupasuka, kabla hajafanya lolote simu yake ikaingia meseji.

    “Nakwambia ukweli Sam, nilikutania tu kusema ukweli Yule mtoto sio wako, mtoto ni wa Gwakisa na nakuomba usimtaje tena mimi nilikwambia vile kwasababu nilitaka tuendeleze mapenzi yetu ila nimegundua nampenda sana mme wangu, please naomba uzae wa kwako, huyu sio wako”

    Sam alisonya kisha akaamka alipokuwa amekaa na kuanza kupiga ngumi ukutani kwa hasira, hakuamini maneno aliyoambiwa na Verity. Yalikuwa yamemuumiza kuliko kawaida kiasi kwamba alijikuta akikata tama kabisa.

    …………………………CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa ni saa mbili asubuhi ambapo tayari Gwakisa alikuwa ameamka na mtoto wake wanajiandaa kwa siku nyingine.

    Gwakisa alikuwa anampigisha Princess mswaki kisha akamuogesha kwa maji ya moto na yeye mwenyewe akajisafisha kisha hatimaye wakavaa vizuri na kuondoka pale chumbani.

    Walielekea moja kwa moja kwenye gari lao na hatimaye wakaenda mpaka Mikocheni kulipokuwa na hospitali moja ya kisasa kabisa iliyokuwa inamilikiwa na wajerumani.



    Alipofika walipokelewa vizuri kisha Gwakisa akapelekwa sehemu ambayo kulikuwa na wataalam wa Maabara kwa ajili ya vipimo vya DNA kama ambavyo alishaweka booking siku kadhaa nyuma.



    Walichukuliwa vipimo yeye pamoja na mtoto wake kisha wakaambiwa wakapumzike nyumbani hadi kesho yake aje achukue majibu.

    Hakukuwa na jingine isipokuwa Gwakisa aliamua kuzunguka mjini akitafuta nguo za mtoto wake, yeye mwenyewe na mama yake hadi ilipofika mchana ambapo walienda mpaka Mlimani City wakajipatia chakula cha mchana.

    Siku ilimalizika wakiwa wanatembea maeneo mbalimbali kisha wakarudi kwenye hoteli waliyofikia.

    Mawasiliano na mkewe (Verity ) yalikuwa kila wakati yanafanyika huku akimdanganya kuwa yuko Dar es Salaam kikazi ili hali sio kweli bali ameenda kupima DNA ya mtoto wake.

    ……………………………….

    Sam alikuwa bado na mawazo mengi sana akitafakari yote aliyoambiwa na Verity lakini kwa Upande mwingine Verity nae alikuwa amekosa amani kwa yale ambayo Sam alikuwa anayafanya, hakutegemea hata siku moja kuwa sam atakuja abadilike kiasi hicho juu ya mwanae.

    Kwasasa Verity aliiona hatari ambayo ilikuwa inamnyemelea endapo Gwakisa ataugundua mchezo unaoendelea.

    Alitamani hata kumuua Sam lakini kivipi alikuwa hajui, maisha yake mapya na mme wake aliyapenda sana na asingetaka mtu ayavuruge.

    Sam hakutaka kumuacha Verity na ushindi, alichokifanya aliamua nae amtumie sms

    ….nakwambia ukweli Verity, kama huyo ni mtoto wangu nitamchukua tu, kama sio wangu swadakta ila kama ni wangu siwezi kuruhusu damu yangu ilelewe na mwanaume mwingine Never, Jiandae kwa DNA, kwa hili hata mme wako nitamtaarifu ili ajue…..!

    Verity alipoiona hii sms alisikia kama kitu kinakata kutoka upande mmoja wa tumbo kwenda mwingine, hakuwahi kufikiria kuhusu DNA na hapa aliona mambo yakivurugika kabisa na ghafla mkono ukawa umepanda kwenye tama kuashiria kuwa mambo sio shwari.

    ………………………..

    Kulipokucha Gwakisa kama kawaida alimuandaa mtoto wake Princess pamoja nayeye mwenyewe kwa ajili ya kwenda kue hospitali kupokea majibu.

    Waliingia kwenye gari lao na safari ikaanza taratibu huku Gwakisa akiwa na mawazo lukuki, kuna wakati alijilaumu kwa uamuzi wake, alijiuliza hivi ikitokea kuwa Yule sio mtoto wake atamfanyaje?

    Je atamuacha mke wake? Je atamfukuza mtoto nyumbani ama atafanyaje?

    Kuna wakati alitamani asingeamua kupima akaishi tu akiamini ni mtoto wake kuliko atakapoujua ukweli kabisa.

    Alimuangalia Yule mtoto pale pembeni anavyojisikia furaha akimuona Baba yake anaendesha gari, alifikiria jinsi mtoto anavyompenda hadi kuwa nae siku zote bila kumkumbuka mama yake alafu leo aambiwe sio wake atafanyaje?

    Moyo ulimuuma sana lakini mwisho akaamua ni lazima amalize kazi aliyoianza.

    Safari ya Hospitali iliendelea na hapa tayari walikuwa Mwenge, waliendelea na barabara ya Ali Hassan Mwinyi mpaka walipofika eneo linaitwa Victoria kisha wakakunja kushoto hadi ndani ndani huko ilipokuwa hiyo hospitali.

    Alishuka kwenye gari akamchukua mtoto wake akamuweka begani kisha akafika mapokezi ambapo simu ilipigwa kwa wahusika.

    “Kaka naomba ukae wanasema utaitwa baada ya robo saa”

    Gwakisa alikaa kwenye kiti bila wasiwasi huku mwanae akiwa kamlalia mapajani.

    Baada ya dakika kama kumi hivi Yule dada pale mapokezi alimuita na kumwambia kuwa anahitajika kwa daktari wake.

    Gwakisa alimchukua mwanae kwa kumshika mkono wakatembea mpaka kule ilipokuwa ofisi ya daktari aliyewahudumia.

    “karibuni sana mketi”

    “Asante sana”

    “Totooo jambo”

    “Jambo”

    Sasa ndugu Gwakisa Ambikile majibu yako yako tayari na tunakuomba uingie chumba hiki hapa kuna wataalamu uonane nao kwanza kabla sijakupa majibu.





    Mawasiliano kati ya Sam na Rafiki yeliendelea vizuri tu japo hayakuwa imara kama awali, siku zote Rafiki alikuwa ndie wakkwanza kumtafuta Sam lakini moyo ule ulianza kupotea na alikuwa anamtafuta kutimiza wajibu tu.

    Mambo mengi yalikuwa yamemkatisha tama lakini kubwa likiwa kitendo cha Mme wake kuwa na mawasiliano ya karibu sana na Verity.

    Jambo jingine ni jinsi ambavyo hawapati mtoto na kugundulika tatizo lipo kwa mme wake, alikuwa tayari kumvumilia mpaka tatizo lile lipone lakini kinachomuumiza ni tabia ya Sam kutokuwa mwaminifu.

    Akiwa anawaza haya yote simu yake iliita na mpigaji alikuwa ni Dr Kelvin.

    Waliongea mengi sana ikiwa ni pamoja na hatua tatizo lao lilipofikia. Dr kelvin alikuwa anaongea kistaarabu sana na mpaka wanamaliza mazungumzo hakutamka jambo lolote la kimapenzi.

    Kitendo hiki hadi Rafiki alikishangaa kwani kwa jinsi alivyokuwa anamjua Dr Kelvin na tabia yake mbaya alijua basi siku hiyo angeombwa “naniliu”.

    “Haya dada nikutakie siku njema na Mungu awasaidie tatizo lenu liishe”

    Dr Kelvin alimalizia kwa kusema hivyo

    Kwenye akili ya Dr Kelvin alikuwa amepanga mkakati wa kumnasa Rafiki, katika mkakati wake aliamua kutokuwa na haraka, alijua kuwa kwa kufanya hivi ataonekana kuwa sio mtu mrahisi na mpenda hayo mambo hivyo anajenga kwanza kuaminika.

    Ukweli ni kwamba Rafiki alibaki kaduwaa kweli kweli kwani alitaka achokozwe kidogo ili apunguze machungu ya Sam japo swala la kusaliti kabisa ndoa yake bado lilikuwa gumu kuafikiwa kwenye moyo japo kuchokozwa kidogo alitamani ili nae ajione anadai.

    Kesho yake Rafiki akiwa kazini kwake alipokea simu nyingine ya Dr Kelvin.

    “Haloo niko hapa nje ya ofisini kwenu”

    “We mutu umekuja kufanya nini huku?”

    “Kwani ofisi zenu huwa hazihudumii binadamu au mimi sistahili huduma zenu”

    “Mh haya bhana, karibu”

    “Njoo hapa nje unisalimie”

    Rafiki aliwaza kidogo kisha akauliza “Uko na nani”

    “Niko na mke wangu njoo umsalimie mfahamiane”

    Rafiki kusikia vile alishtuka kidogo kisha akaona asipoenda ataeleweka vibaya ni bora aende tu.

    Alitoka nje na kukuta gari imepaki karibu na geti huku Dr Kelvin akiwa ametoa kichwa dirishani.

    Rafiki alisogea pale akamsalimia kwa adabu zote lakini cha ajabu hakumuona huyo mke wad r kelvin.

    “Huyo mkeo yuko wapi sasa?”

    “Nilikuwa nakutania bhana, mke wangu yuko nje ya nchi anasoma”

    “Hujatulia kabisa wewe”

    “Sio kweli… twende ukapate breakfast kidogo”

    Rafiki hakukataa kwasababu kwanza ndio ilikuwa mida ya chai hivyo alichoma ndani ya gari na kuelekea kwenye mgahawa ambapo walipata kifungua kinywa kilicholipwa na Dr Kelvin.

    Walipomaliza Dr Kelvin alimpeleka mpaka ofisini kisha yeye akarudi kwenye kazi yake.

    Siku hii tena Dr Kelvin wala hakumwambia Rafiki mambo yoyote mabaya, hadi Rafiki anafika ofisini alikuwa anawaza na kuamini kuwa huenda Dr Kelvin ameamua kubadilika.

    Usiku rafiki akiwa anajiandaa kulala alipigiwa simu na Dr Kelvin ambapo waliongea mambo mengi sana kisha Dr Kelvin akaanza uchokozi wake.

    “Hivi siku ile kule hospitali ulijisikiaje?” aliuliza Dr Kelvin

    “Nilijisikia vibaya”

    “Basi ungekubali tu tumalize ungejisikia vibaya zaidi”

    “Walaaa siwezi kukubali, yani nikubali ili nijisikie vibaya zaidi”

    Waliendelea kuchokozana na katika mambo ambayo Rafiki alikuwa hajui ni kwamba Dr Kelvin alikuwa mtaalam wa mapenzi mpaka ya mdomoni, yani mapenzi ya kuongea.

    Alimpelekesha Rafiki kwenye simu mpaka ikafika wakati akawa anamvua nguo moja moja anaweka pembeni, anamtomasa, anamchezea sehemu nyeti mpaka ikulu kisha anampanua miguu na kuingiza mashine yake.

    Anamkatikia viuno na kumbadililishia style mbali mbali hadi Rafiki anakojoa kabisa.

    Haya yote yanafanyika kupitia kwenye simu.

    Ilifika hatua Rafiki akakojoa kweli huku anamwambia Dr Kelvin kuwa anakojoa.

    Siku ile iliisha kwa Rafiki kuwa amejisikia rah asana kukatwa kiu yake.

    Ilifika hatua kwamba kila siku kabla Ya kulala Rafiki na Dr kelvin wanaongea na simu hata masaa matatu.

    Mchezo huu Sam aliushtukia kuwa kuna mtu anaongea na mkewe kila siku usiku tena kwa mda mrefu kwani kila alipokuwa anampigia simu ilikuwa inatumika.

    Baada ya hapo Rafiki anamtafuta na kuongea nae haraka haraka kisha anakata na hapo Sam akipiga tena anakuta inatumika kuonyesha kuwa alikata tu ili amalizane na Sam alafu aendelee na watu wake.

    Kitendo hiki kilimuumiza Sam lakini akaamua kukaa kimya tu.

    Pamoja na Dr Kelvin kuongea mengi na Rafiki kwenye simu lakini alipotaka kuomba mzigo atusue alikuwa ananyimwa. Rafiki hakuwa tayari kufanya mapenzi nje ya ndoa yake mubashara kabisa, roho ilikuwa inamsuta sana.

    Dr Kelvin nae aliendelea kukomaa na safari hii alikuja na gia ya kumzalisha.

    Katika mambo ambayo wanawake wanakosea ni kutoa siri za ndani kwao pindi wanapokuwa na mahusiano ya nje.

    Rafiki alishamuhadithia DR Kelvin kila kitu kuhusu mumewe, alishamwambia kuwa Sam ana mtoto na Verity na hapa Dr kelvin akaamua kupatumia kama mwanya wa kufungia goli.

    “Hivi mumeo asipopona unajua wewe utabaki mgumba”

    “Kwahiyo sasa”

    “Kwahiyo nini? Sema nikuzalishe allafu mumeo akija nampima namwambia kuwa amepona ilia one kuwa mimba ni yake”

    “Bado hujanishawishi”

    “Nisikilize vizuri, mwenzio yeye hana shida kwasababu tayari ana mtoto na nikwambie kila mtu ataona wewe ndio una tatizo kwasababu mwenzako tayari ana mtoto, ina maana huna hamu ya kunyonyesha wewe”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ninayo lakini lazima nizae na mume wangu, ikishindikana basi”

    “Nisikilize kwa makini, ninyi wanawake sio kama wanaume, wewe kadiri umri unavyoenda uwezo wako wa kuzaa unapungua, shauri yako mwenzako atapona wewe tayari umeshapitisha umri wa kuzaa ataenda kuzaa tena nje”

    Kwa mbali Rafiki alikuwa anaanza kutekwa na maongezi ya Dr Kelvin, alitaka kumwambia ameridhia ombi lake lakini anasita akabaki anakaa kimya tu.

    Dr Kelvin hili aliligundua hivyo alichomwambia ni kuwa ajiandae kesho jioni atampitia waende sehemu.

    Rafiki aliitikia kwa kusema “sawa” kumaanisha kuwa ameridhia.

    ………………………………..

    Gwakisa alikuwa kwenye chumba maalum cha ushauri nasaha.

    Katika mambo ambayo alikuwa hajui ni kwamba swala la DNA huwa unapewa kwanza ushauri nasaha kabla ya kupewa majibu kama vile umeenda kupima VVU.

    Alipewa ushauri mwingi unaohusiana na kama atagundua kuwa mtoto si wake ama akiwa wake ninini afanye ili asije akaleta madhara.

    Gwakisa aliitikia kwa kumaanisha ameelewa kisha akaruhusiwa kurudi kwa Dr sasa akapewe majibu yake.

    Moyo ulikuwa unamdunda sana mpaka akawa anajutia kwanini alikuja kufanya hiyo test.

    Alipokaa vizuri Yule Dr alichukua makaratasi yaliyokuwa pale mezani na kumkabidhi Gwakisa.

    Gwakisa haraka haraka alianza kupitisha macho akisoma kile kilichoandikwa lakini akawa haelewi vizuri maneno yale ya kitaaluma.

    “Dr nifafanulie”

    “Sawa usijali, sogea hapa karibu”

    Gwakisa alisogea na kuanza kusomewa maandishi yote na maana yake halisi.

    Gwakisa hakuamini masikio yake pale alipoambiwa kuwa vinasaba vyake na vya mtoto vilikuwa haviendani kabisa na hivyo mtoto Yule sio damu yake.

    “Nilijua tu” aliropoka Gwakisa.

    Yule Dr alibaki amemuangalia tu Gwakisa aliyekuwa kajiinamia huku machozi yanamwagika usoni, hakuamini kuwa mwanajeshi kama yeye tena Afisa wa Jeshi kuna wakati atatoa machozi yake.

    Alikuwa anaemia sana moyoni huku akimlaani mkewe kwanini amemfanyia mambo mabaya kama hayo.

    “Ndugu wala usilie, haya yaliyokukuta yanawakuta wanaume wengi sana, wengine huko majumbani wanalea watoto sio wao ila ni vile tu hawajapima, sasa wewe kwakuwa umejua tuliza moyo ujipange lisije likatokea tena”

    “Dadiii lia nini?” masikini ka Princess nako kalikuwa kanatoa machozi kalivyomuona baba yake analia, hakuelewa kilichokuwa kinaendelea kuwa kinamuhusu.

    Gwakisa alinyanyua uso akamwangalia Yule mtoto kisha akamnyakua na kutoka nae bila hata kuaga,

    Alipofika nje aliingia kwenye gari na kuelekea hotelini.

    Alichukua vitu vyake na hakutaka kulala siku hiyo akaamua kurudi mbeya.

    Alipofika Morogoro karibu na Stendi ya Msamvu alisimamishwa na baadhi ya vijana wakamwomba kuwa kuna dada anaomba ampakie kwani anaenda Mbeya ila amekosa Basi.

    Gwakisa alijifikiria ila alipomuona mdada mwenyewe alimkubalia kwani hata hivyo ndio kawaida ya hapo Morogoro na alishawahi kupakia watu mara nyingi tu huku wakichangia mafuta.

    Yule dada alipanda kwenye gari wakatambulishana vizuri kisha safari ikaanza, maongezi yalikuwa yanaendelea japo kwa kusua sua sana kwani Gwakisa alikuwa na mawazo yake hivyo Yule dada muda mwingi alikuwa anaongea na Princess wakichekeshana.

    Kuna wakati ulifika Gwakisa nae akawa anavutiwa na maongezi ya Princess na Yule Binti kiasi kwamba akawa anajisikia kucheka.

    Safari iliendelea huku Gwakisa akimchunguza huyu dada na kugundua kuwa alikuwa mrembo kwelikweli, alikuwa mrembo kuliko hata Verity, kuliko hata wanawake wengi aliowahi kukutana nao.

    Alipomuona nguo yake imepanda juu kidogo na sehemu ya Paja kuonekana kidogo ndio kabisa aliamini kuwa huyu dada hakuwa wa kawaida.

    Alikuwa mrembo kupitiliza, kwanza alikuwa kama chotara flani hivi.

    Gwakisa hakuweza kukaa kimya?



    “Dada umeniambia wewe ni mwenyeji wa Mbeya?”

    “Hapana niko kikazi tu?”

    “Okey unafanya kazi gani?”

    “Mimi ni askari polisi”

    “Ahhhh acha utani bhana, askari gani yuko hivyo”

    “Kwani nikoje? Tena mimi niko kikosi cha FFU”

    “Duh aloo siamini kabisa, anyway na mimi ni askari wa JWTZ”

    “aaaah nilijua tu, huo mwili wa kijeshi kabisa”

    “Kumbee najulisha kabisa”

    “Haswaaa”

    Maongezi yalikuwa yamenoga sasa kiasi kwamba ilibidi Gwakisa apunguze mwendo ilia pate muda wa kutosha kupiga story na huyu dada.

    Story zilinoga mpaka wanafika Mbeya saa tano usiku Gwakisa akaamua kumpeleka huyu dada mpaka kwake kisha akaondoka na mwanae kurudi nyumbani.

    Alipofika na kumwona Verity alijikuta hasira zikimuwaka ila akajitahidi kumsalimu na kumchangamkia kinafiki.

    Waliongea mawili matatu huku Verity akifurahia kuonana na mwanae kisha wakalala hadi asubuhi ambapo Gwakisa aliondoka kwenda kazini huku akiwa na mipango kibao kichwani kwake.

    Katika mipango yake aliyokuwa anapanga mmoja aliuona unafaa sana na akaamua kuutekeleza haraka sana.

    Alichukua simu yake akatafuta namba kisha akakutana na namba ya Yule dada aliyempakia jana yake na kumpigia simu.

    “Uko hpo kwako eenh, sawa nakuja dada, nakuja kukusalimu”



    Gwakisa alikuwa nyumbani kwa askari huyu wakike ambaye alimpakia kutoka Morogoro mpaka Mbeya.

    Alijuta kwanini alijipeleka kwani mambo aliyokuwa anafanyiwa hakuwahi kuyatazamia.



    Askari huyu alikuwa anamwekea mitego milioni kasoro, alikuwa amevaa kanga tu huku akijipitisha kila wakati mbele ya Gwakisa kwa madai kuwa anamwandalia chai.



    Gwakisa aliishia kukodoa macho tu, rangi ya nguo ya ndani aliyokuwa amevaa askari huyu ilikuwa inaonekana kabisa kuwa ni pinki.



    Kila alipokuwa anatembea kanga ilikuwa inafunuka na kuliacha paja wazi kiasi.



    Weupe wa huyu dada unaoambatana na uchotara wake ulimfanya avutie kuliko kawaida,

    Makalio yake makubwa kiasi yalikuwa yanamzidishia urembo mwingine.



    Kifuani alikuwa kachongoka kama kajitengeneza mwenyewe.



    Kila alichotaka kuongea Gwakisa alijikuta anakikosoa mwenyewe, mwisho aliibuka na swali lisilo maana...

    "Hivi wewe ni askari kweli"? Gwakisa aliuliza.



    Askari huyu kabla hajajibu alimkata Gwakisa jicho la mtego kisha akamfwata na kumpiga kijikofi shavuni huku akimchombeza...

    " nawewe bhana, usichoamini kipi sasa"



    "Kwa urembo huo unawezaje kuwa askari?"

    Gwakisa ilibidi afunguke...



    "Kunywa chai kwanza wewe afande"

    Gwakisa aliambiwa hayo huku ananawishwa mikono...

    Askari huyu alikuja akakaa kochi linalotazamana na Gwakisa na kuwa wote wanakunywa chai.



    Mapaja ya huyu dada yalikuwa nje kiasi kwamba mhogo wa Gwakisa ulikuwa ukiisukuma suruali yake ya Bakabaka kama inatobolewa vile...



    Gwakisa alipomaliza kunywa chai alinawishwa mikono na kuulizwa kama ameshiba akasema nimeshiba.



    "Basi ngojea nikaoge tutoke wote"

    Alisema yule askari.



    " ila mimi naelekea kazini"

    "Usijali kuna sehemu mimi nataka unipitishe fasta"



    Gwakisa hakuwa na cha kujibu kwa jinsi alivyomuona Huyu dada askari akipita mbele yake na kijitaulo kifupi mno...



    "Tunaweza kwenda sasa"

    Gwakisa alikuwa anapelekeshwa kama mtoto.

    "Ila umejua kunitesa leo" alifunguka Gwakisa...

    "Usijali twende kwanza"

    Gwakisa alijibiwa akajikuta mwili wote unasisimka, alikuwa anajiuliza ninini yule dada anamaanisha akashindwa kuelewa ila yeye akawa anasonga mbele tu.



    Aliyekuwa anatoa maelekezo ni yule Binti askari, kama vile lile gari amekodi.

    Gwakisa alikuwa anapelekwa tu hadi alipofikishwa kwenye jumba moja la kisasa likiwa limezungushiwa ukuta mrefu sana.



    "Njoo umsalimu kaka yangu"



    Gwakisa aliingizwa ndani nae akaingia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pale ndani hakukuta mtu yeyote isipokuwa kulionekana kuna watu wanakaa humo...



    Gwakisa alipelekwa mpaka chumbani ambapo kulikuwa na chumba kikubwa chenye vitu vya thamani mno.



    Katika hali isiyo ya kawaida yule dada alianza kusaula nguo zake akabaki na chupi tu.



    " Njoo umalize mateso yako"

    Gwakisa alivutwa akaanza kunyonywa midomo kitendo ambacho hakukiamini.



    Michezo ya mapenzi ilianza huku wakipelekeshana kwa Romance za kiitaliano, Gwakisa alikuwa hoi bin Taaban na nguo zake zote zilikuwa chini.



    "Hiki kifua na umbo lako ndio vimenifanya nikupe mwili wangu, mimi sio malaya" aliambiwa Gwakisa.



    Gwakisa hakuwa na uwezo wa kujibu lolote, alikamata mtarimbo wake mkubwa akawa anauchomeka kwa yule askari



    "No no no nooooo, vaa hizi, sikuamini"



    Gwakisa alipewa kondom, alizichukua na kuvaa kisha akachomeka mzigo, alipokelewa na joto si la kitoto na hapa makasia yakaanza kwa fujo.



    Walifanya ngono ile yenyewe kisha wakaoga na kutoka sebuleni.



    Katika hali ambayo ilimshangaza Gwakisa alikuta kuna wanaume zaidi ya kumi pale sebuleni wenye miili na vifua vikubwa kuliko yeye, alipigwa na butwaa lakini alikumbana na sentensi chache kutoka kwa mmoja wao aliyekuwa amevaa suti nyeupe pee....



    "Karibu Meja Gwakisa, usihofu, hapa ni Pesa na amani tu! jihesabie wewe ni mshirila kuanzia leo"

    Alipokelewa kwa makofi mengi kutoka kwa hawa wanaume wengine wakiongozwa na yule Dada askari

    ..........................

    Rafiki alikuwa kwenye tax anaenda kugegedwa na Dr Kelvin.



    Alikuwa na mawazo lukuki juu ya uamuzi wake lakini uamuzi wa kusaliti ulikuwa umezidi kwenye uzani.



    Wakati anaelekea huko alikuwa anaendelea kuchat na Dr Kelvin ambaye alikuwa anamchombeza kwa maneno lukuki ya kumhakikishia kuwa kila kitu kitakuwa shwari.



    Kwa maelekezo dereva wa tax aliyopewa na Dr Kelvin akawa amemfikisha sehemu muafaka.



    Rafiki alishuka ndani ya gari na kujiweka nguo yake sawa ili aelekee kule aliko Dr Kelvin akagegedwe.



    Alipogeuka upande mwingine ghafla alikutana na sura ya mwanamke akiwa kwenye gari anamuitaa



    Mrs Sam......

    Rafiki alishtuka na kabla hajajibu yule dada alishuka kwenye gari na kumfwata kwa bashasha huku akimkumbatia.



    "Waoooooh jamani mtusamehe toka mmefunga ndoa hatujawatembelea jamani"



    Huyu alikuwa matron aliyewasimamia kwenye ndoa yao...



    Rafiki alikuwa kwenye taharuki kubwa kiasi cha kumfanya ajichangamshe kwa lazima tu....



    " Roho mbaya hizo sasa, kwanini mmetutupa jamani"



    " mtusamehe bure kwakweli, Mr wangu alikuwa anaumwa kweli, nilikuwa nauguza nashukuru sasa kapona, Vipi Mr mzima"



    "Mzima tena yuko kozi Kenya"



    " haa hongera zake, haya twende ukapaone kwetu, kule tulihama,...au una safari muhimu"

    Rafiki alishindwa kukataa kwa kuhofia ataulizwa unakwenda wapi, alijikuta anakubali kupanda kwenye gari ya yule dada na safari ikaendelea.



    "Hivi mlishajaliwa mtoto au bado?"

    "Mh bado kwakweli, tunatafuta bado'

    " usijali mtapata tu, kikubwa ni muwe na subira huku mkivumiliana maana huenda mmoja ndio ana tatizo"

    "Sawa dada"

    "Unajua hata mimi nilikuwa na tatizo na nashukuru mme wangu alinivumilia miaka mitano ndio nikapona na sasa tuna wale watoto watatu unaowaona'



    " kweli?"

    " Ndio hivyo, kikubwa mvumiliane, msitangetange nje, Mungu atashusha baraka zake, yani msijeshawishika, tena wewe ndio uwe makini zaidi maana ukibeba mimba isiyo ya mume wako itakutesa maisha yote"



    Rafiki alishtuka akaona kama vile yule dada anamjua mawazo yake.



    Dr Kelvin alikuwa anapiga simu kila mara lakini ilikuwa inakatwa, Rafiki alikuwa keshabadilika.

    Mbele ya matron wake asingeweza kupokea simu na akili yake ilishavurugwa...

    ..............

    Sam alikuwa kwenye graduation ambayo ilikuwa inahitimisha mafunzo yao, alivishwa nishani na hatimaye akapanda cheo na kuvaa nyota.



    Kama masihara akiwa na umri mdogo tayari alikuwa ni afsa wa Polisi.



    Alikuwa sasa anajiandaa kurudi kwake kimya kimya bila kumtaarifu Mkewe.

    .........

    Watu watatu wenye gari aina ya Noah nyeusi walikuwa nyumbani kwa Gwakisa...

    Hakuna walichokuwa wanataka isipokuwa kumteka mtoto Princess....

    Geti liligongwa akatoka Verity aliyeshangaa kuwaona wale watu asijue wametokea wapi....



    Gwakisa alikuwa anasainishwa mikataba ambayo ilikuwa ni ya lazima huku kashikiwa Bunduki.

    Alipomaliza kusaini alipewa Kopi ambayo aliambiwa anatakiwa aiweke na iwe siri yake.



    Wakati wote huu wa hili zoezi pembeni alikuwepo Yule dada askari aliyetoka kungonoka nae akiwa amejaa tabasamu usoni kama vile kile kinachofanywa kwa Gwakisa kilikuwa na amani.

    Gwakisa alikuwa anajiuliza sana moyoni mwake ni kwanini amedakwa kirahisi namna hii aijue kuwa wenzake walikuwa wanamlia timing mda mrefu na walishajipanga kumuingiza kwenye ushirika wao kwa mikakati mingi sana ndipo wakaamua kumtumia binti huyu mrembo.



    Baada ya kila kitu kukamilika wale wanachama mule ndani walikuwa wanamshika Gwakisa mkono wa Pongezi kila mmoja kwa zamu hadi wa Mwisho akawa Yule aliyevalia suti nyeupe ambayo alipomaliza kumshika mkono alimkabidhi BriefCase na kumwambia aketi afungue aone kilichomo mule ndani.



    Gwakisa aliketi akaiifungua na kukutana na vitu vilivyoulipua moyo wake.

    Zilikuwepo pesa nyingi tena Dollar za Kimarekani zilizopangwa kwenye vibunda vingi, alipigwa na butwaaa hadi mikono ikawa inatetemeka.



    Zilikuwa mpya na zimejaa kabisa pale kwenye kile kijibegi, katika zile noti ya bei ndogo ilikuwa ni dollar mia moja ambayo ni sawa na laki mbili na zaidi za Tanzania

    “Hizi ni pesa za nani” aliuliza Gwakisa

    “Ni zako kwa ajili ya chai na soda” Alijibiwa Gwakisa

    “Yani mmenipa tuu”



    “Ndio hii ni ili uendane angalau na sisi kwenye ushirika wetu kwani kwetu hatutaki mtu wa kulia lia shida”

    Kwa Gwakisa huu ulikuwa ni muujiza tosha, ghafla akili yake ilianza kuwaza magari ya gharama, nyumba za kifahari na vitega uchumi mbalimbali.



    Alisita kujilaumu kuwajua hawa watu na kujikuta akiwa tayari kwa lolote.

    “Unaweza ukarudi kwako ila utaenda na huyu binti mkafanye jambo moja la muhimu sana” aliambiwa gwakisa na hapohapo wakaamka kwenye makochi.

    Safari ilianza na aliyekuwa anatoa maelekezo ni YULE dada askari.

    Walienda mpaka Kambini ambapo Gwakisa alibadili gari na kuchukua la Jeshi kisha moja kwamoja wakashika njia ya mpakani.



    Kote polisi hawakuwasimamisha kwasababu ya lile gari la Jeshi, walipofika mpakani askari baadhi waliwasimamisha lakini Gwakisa alitoa kitambulisho chake cha Jeshi huku Yule dada nae akitoa cha kwake cha uaskari Polisi FFU.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waliendelea mpaka mpakani na Kongo wakakutana na watu wengine waliowakabidhi mzigo na kurudi nao mpaka Mbeya mjini kisha wakaagana kwa lengo kila mtu aende kwake baada ya kufikisha mzigo panapotakiwa.



    ‘ngoja kidogo Gwakisa’



    Gwakisa alitulia asikilize anachoambiwa lakini cha ajabu alifwatwa mdomoni na kupewa denda ambalo liliibua tena hisia zake ambapo alianza kupitisha mikono yake kwenye maziwa ya Yule dada.



    “Subiri wewe hapa njiani ” aliambiwa Gwakisa na kutoa mikono yako,

    “Nenda kwako lakini utakachokutana nacho usishtuke, kama utakuwa na maswali utaniuliza siku tukikutana ila usishtuke kila kitu ni salama tu na hakuna kibaya”



    Gwakisa alianza kuogopa lakini akiwa anawaza Tayri Yule dada alishashuka na kutokomea zake.



    Kwa hofu Gwakisa aliendesha Gari mpaka kwake na kukuta kumefungwa na hakuna mtu.



    Alichukua simu yake ampigie mkewe lakini aligundua kuwa simu yake ilikuwa imezimwa, alijua kabisa walioizima ni wale jamaa kule alikotoka.



    Aliiwasha na kumtafuta mke wake ambapo alipokelewa na kilio kikali.

    “Nini wewe unalia nini” aliuliza Gwakisa

    “Mtoto wetu amepotea mume wangu uuuuuwiiiii, mamamamaaaaaaaaaa, mamaaaa mimi mwanangu jamaniiiiii” alikuwa analia Verity



    Hapo hapo Gwakisa aliwahi kituo cha Polisi ambapo alimkuta mke wake akiwa na wazazi wake wakiwa wanatoa maelezo pale na tayari taarifa zilishasambazwa kila sehemu kwenye vituo mbalimbali ili utafutwaji uanze wakifwatia maelezo ya wahusika anaowashuku Verity.



    Gwakisa hakuelewa afanye nini kwani akili yake ilishawawaza wale jamaa zake lakini akawa anashindwa kuelewa kuwa ni kwanini wamchukue Yule mtoto, yeye anahusiana nini….



    Akili yake ilimpa mawazo kwamba huenda wale watu ni washirikina na wanataka wakamtoe Yule mtoto kafara.

    Roho ilikuwa inamuuma sana, japo Yule mtoto sio wake lakini alikuwa hana mpango wa kumdhuru, mpango wake ulikuwa ni mwingine kabisa na sio kumdhuru.



    Roho ya kibinadamu na kiulezi ilikuwa inamuuma sana, alimfwata mke wake na kumnyanyua pale chini akasogea kando na kumwambia….



    “Usilie mke wangu, nitapambana na mtu yeyote mpaka mtoto apatikane.”



    ……………………………..



    Sam alikuwa njiani kurudi Tanzania kwa kutumia usafiri wa anga, ndani ya lisaa limoja tayari alikuwa Dar es salaam na mawazo yake yote yalikuwa kwa mwanae.

    Alipanga kuwa akifika tu ni lazima amchukue mtoto wake.



    Siku hiyo hiyo kwakuwa alishakata tiketi online aliunganisha ndege na kutua uwanja wa Songwe Mbeya kwa Ndege.

    Alipofika breki ya kwanza ilikuwa kwa Gwakisa na Verity ambapo alitaka amuone mwanae na waweke kila kitu wazi.



    Alipanga kuwa endapo wakikataa tu ataomba vipimo vya DNA vifanyike.

    Alipofika pale alishtushwa na uwepo wa gari la RPC pamoja na magari mengine yakiwemo yenye namba za Jeshi.

    Kwakuwa simu yake mda wote ilikuwa imezimwa kwa ajili ya safari za kwenye ndege akawa hakupata taarifa yeyote kuhusu kilichokuwa kinaendelea na mke wake alishampigia simu mara kibao bila kumpata.



    Alipofika pale alilakiwa na wakwe zake huku akisikia kilio cha Verity ambaye anamtaja mwanae .



    Sam alishindwa kuelewa haraka lakini picha aliyoipata ni huenda Princess amefariki. Mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda kwa kasi sana.

    “Kuna nini kwani”



    “Alimuuliza Mama yake Mkwe”

    “Mtoto wa Verity amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha”



    Sam alisogea kando akawaza, kisha akaibuka haraka mpaka kule ndani alikokuwa anafarijiwa Verity….



    “Nisikilize Vizuri Verity, ujanja wenu nimeshaujua, mimi ni askari by Profesheni, mmeamua kumficha mtoto wangu nisimchukue lakini mtamtoa tu huko aliko”



    Maneno ya Sam yalimshitua kila mtu na wala hakuwa na muda wa kubaki hapo, aliondoka mpaka kwake ambapo alikuta kuko kimya kwani Rafiki alikuwa kwenye harakati za kusaidia kumtafuta mtoto wa mdogo wake.



    ……………………………….

    Gwakisa aliwahi kule kwa wale jamaa zake na aliingia kama mbogo. Alikuwa anarusha ngumi nzito na mateke huku akihoji aliko mwanae.



    Ghafla mijitu minkubwa ilijitokeza mbele yake na kumkamata huku ikimpa kichapo kilichomkalisha chini hawezi hata kuamka.



    Ghafla mbele yake alitokeza Yule dada askari na kuuliza kwanini Yule Gwakisa yuko kwenye hali ile….



    “Kaja hapa analeta tabu anaulizia sijui mwanae sijui vitu gani tumempa adabu kidogo atulie”



    “Okeeeey, wewe bwege unapaswa kuwa na heshima hapa ni ikulu hupaswi kuleta fujo”



    Yule dada alimkamata Gwakisa kichwani huku akimuangalia usoni akiwa kapiga magoti.



    “Wakuu huyu nimempa mtego kidogo tu, mwanae ninae”



    Gwakisa kusikia vile alishtuka kisha akaambiwa “nifwate huku”



    Pamoja na Gwakisa kuambiwa nifwate na Yule dada hakuwa na uwezo huo kwani alipigwa kwenye viungo vya miguu, hivyo ilibidi apelekwe na wale mabaunsa.

    Alipofika alilazwa kitandani kisha Yule dada akaanza kumpa maneno….



    “Huwezi kulea mtoto ambae sio wako, hiyo ni fedheha kubwa wewe kijana, nimeamua kukusaidia hatua za kuchukua, Yule mtoto kwa sasa yupo sehemu salama na utamuona, ataenda kukaa mbali na atasoma huko huko wakati wewe unatafuta wako mwenyewe, tena nitakuzalia mimi…..”





    Gwakisa alijiuliza sana kwamba imekuwaje hadi Yule dada akajua kuwa Yule mtoto sio wake.



    Alitamani amuulize lakini akakwama namna ya kuuliza akabaki anajiuliza tu bila ya majibu.



    “Au unakataaa kuwa mtoto hujachakachuliwa?”



    “Kwanza yuko wapi?”



    “Utamuona muda ukifika wala usijali”



    “Nisijali vipi, hivi mnadhani familia yangu itatulia ikiwa mtoto hayupo?”



    “Itatulia tu wala usijali”



    “Hivi ninyi mnaofanya hivi mngependa ikiwa nanyie mngekuwa mnafanyiwa hivi”



    “Unadhani kuna jambo zuri lisilo na maumivu?”



    “Basi mimi siyataki haya maumivu na hilo jambo lenu zuri silitaki pia”



    Yule dada alimuangalia Gwakisa kwa dakika chache kisha akamwambia….

    “Kama wewe hulitaki tambua kuwa sisi tunakutaka kwenye mambo yetu, alafu pia kumbuka kuwa umesaini mkataba.”



    …………………………………

    Sam hasira alizokuwa nazo zilikuwa hazielezeki, alijua kuwa kuna mchezo anafanyiwa ili asimpate mwanae, alijipanga kwa mambo mengi ila la kwanza ilikuwa ni kumtafuta Gwakisa.

    Alirudi kule alikotoka kwa mara nyingine ili amtafute Gwakisa.



    Safari hii alienda kisataarabu sana ambapo aliegesha gari getini kisha akazama ndani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alimfwata kijana mmoja ambaye alimjua ni wa karibu nah ii familia, alimshika began a kumvuta kando kidogo.



    “Dogo hivi huyu baba wa hii familia yeye yuko wapi”

    “Yani huyu aliyepotelewa na mtoto?”

    “Ndio huyo huyo” sam aliitikia kwa sitaki nataka

    “alitoka hapa mda mrefu, nadhani yuko kwenye harakati zake za kumtafuta mwanae”

    Sam alijua moja kwa moja kuwa Gwakisa yuko sehemu na sehemu alipo itakuwa ni kwenye vyombo vya usalama wanazuga tu.



    Sam aliridhia kuwa kila kitu kwa siku hiyo kisimame mpaka kesho yake.

    Alienda kwake akamkuta mkewe ambaye alikuwa amenuna si kawaida.



    “Sam hivi kweli yani wewe ni mume wangu lakini unarudi safari hata kunitaarifu”



    “Please sitaki usumbufu rafiki niache nipumzike”



    “Hivi wewe mwanaume una matatizo gani lakini, najuta kuolewa nawewe”



    Ile Rafiki anamalizia herufi ya mwisho tu ….. ‘paaaaaaa,paaaaaaa,paaaaaaa’



    Yalikuwa ni makofi matatu mubashara yaliyokuwa yanatua kwenye shavu la Rafiki, kofi moja lilipotaka kumdondosha chini alizuiwa na kofi la upande mwingine, alipotaka kuanguka upande mwingine kofi la shavu jingine lilimbadilisha mwelekeo na kuangukia upande mwingine huku akiachia ukelele mmoja tu kisha akatulia kimya.



    Yalikuwa ni makofi matatu yaliyotua kwenye mashavu mawili kwa mtiririko yakamzimisha mtoto huyu wa RPC kimya kabisa pale chini.



    Sam alikuwa na hasira nyingi mno na kuanza kuropoka….



    “sitaki usengeeee, nasema usenge sitaki, baba yako alinipiga mpaka nimekuwa mgumba alafu unanipandishia sauti….kufaaaaaa”



    Sam alikuwa mbogo sana na alikuwa akiongea peke yake…..



    “Mimi nimehaso, nimehaso kupata haya maisha nimepitia mambo elfu kidogo, mimi ni mhuni tuuuuu, nitaua mtu yeyote lakini mwanangu nitamchukua tu”

    “Mwambie mdogo wako lazima mtoto wangu amtoeeeee”



    Sam aliongea bila kujibiwa na mtu kwani mkewe alikuwa pale chini hajitambui lakini wala hakujali na cha ajabu zaidi akamsindikiza na teke la mgongoni.

    Aliingia chumbani kwake akabadilisha nguo akaoga na kuvaa zingine, akiwa anataka kulala akakumbuka kuwa kule nje aliacha mtu.



    Alitoka akamkuta mkewe kalala pale pale alipomuacha na wala hatikisiki. Alimgeuza akamtikisa lakini wala hakuonyesha kujielewa kwa lolote.

    Sam wala hakujali na ndio hasira zilimzidi, alimburuza mpaka nje kwenye korido akamuacha humo kisha yeye akafunga milango na kuingia ndani kulala.



    Alipanda kitandani akawa anapanga mipango yake lakini ikawa haipangiki, aliamua kuwa kesho yake adamkie kwa Gwakisa wamalizane kuhusu mtoto.

    Alijaribu kuutafuta usingizi sasa ili apumzike. Kila alipojaribu hakuupata, usingizi ulikuwa mbali nayeye kabisa.

    Alijitahidi kutulia labda utakuja lakini masaa yalikuwa yanakatika tu bila kusikia lolote.



    Aliamka na kujimwagia maji bafuni akijua huenda usingizi utakuja lakini wapi, hakuambulia chochote,

    Alijifunika gubigubi na kulala huku kafumba macho lakini alipotaka tu kupitiwa na usingizi alijiwa na ndoto iliyomtisha ikabidi aamke kwa kukurupuka.



    Alianza kuwaza hatua moja hadi nyingine kuanzia alipokutana na mkewe akajikuta akianza kuingiwa na roho ya huruma na woga.



    Kwanza aliogopa akijua huenda ameua lakini pia alimuonea huruma mkewe kwani alijua kuwa mkewe anampenda sana.

    Taratibu alijikongoja mpaka sebuleni akakusanya funguo ili aanza kufungua milango akamuangalie mkewe kule nje alikomuacha.



    Alipotaka tu kufungua mlango roho ya ukatili ilimjia tena na kujikuta akijilaumu kwa zile huruma anazoanza kuwa nazo.

    Alirudi haraka mpaka ndani chumbani na kupanda kitandani kisha akalala zake.



    …………………………….

    Gwakisa alikuwa kawekwa mtu kati hafurukuti na kila alichokuwa anauliza alipewa majibu yasiyo na matumaini.

    Aliikumbuka mikataba aliyosaini akaona hana uwezo wa kuwakwepa hawa watu hivyo ikambidi akubaliane na kila kitu.

    “Basi nae naomba niende nyumbani”

    “Mkandeni hiyo miguu yake mumpeleke kwake asije akaachika” Yule dada askari alitoa amri.



    Wale jamaa walichukua dawa ya kupulizia ambayo humaliza maumivu na kumpulizia huku wakimpaka nyingine kwenye magoti na kwenye viungio vya mikono.



    Walimkanda na maji ya moto pia kisha wakamfunga vizuri na kumpakia kwenye gari mpaka nje kwake kisha wao wakarudi na gari nyingine waliyoambatana nayo.

    Jinsi gwakisa alivyoingia pale kwake kila mtu alishangaa, aliondoka bila taarifa na alipotafutwa hakupatikana alafu anarudi akiwa kwenye hali hii.



    Baba yake Mkwe na Mama yake Mkwe walimuweka chini na kumuuliza kilichomkuta kule alikoenda na hapohapo Gwakisa akajua jinsi ya kupata uongo.

    Aliwaeleza kuwa alipokuwa kwenye harakati za kumtafuta mtoto nae aliishia kutekwa na watu asiowajua wakampeleka sehemu yenye maficho kisha wakaanza kumtesa kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake.



    Aliwaeleza kuwa wale watu walimwambia kuwa endapo ataendelea kumfwatilia Yule mtoto basi wataua familia nzima.



    …………………………………………

    Asubuhi na mapema Sam aliamka ili aende kwa Gwakisa waongee kuhusu ishu ya mtoto, alijiandaa vizuri kisha akatoka nje lakini pale alipomuacha mkewe hakumuona na wala hakuhangaika kumtafuta.



    Aliondoka moja kwa moja kwa lengo la kumtafuta Gwakisa, kabla hajafika huko aliamua kumpigia kwanza simu.

    Waliongea vizuri lakini Gwakisa akamwambia kuwa hangeweza kutoka nyumbani kwani hali yake sio nzuri hivyo aje nyumbani.



    Sam hakusita, tena aliona ni vyema akimkuta Gwakisa akiwa na mke wake kwa pamoja…..



    Sam alienda mpaka hapo kwa shemeji yake na kuingiza gari ndani ya uzio na kupaki….



    Alikaribishwa ndani na kukaa sebuleni, baada ya muda kidogo alitokea Gwakisa akiwa anatembelea fimbo huku anachechemea, Sam alishtuka kuona vile akajua Gwakisa aanmuigizia.

    “Karibu ndugu, habari za nyumbani?”

    “Nzuri tu vipi hapa?”

    “Hapa ndio hivyo ni matatizo tu, afadhali umerudi kutoka masomoni utasaidia maana mimi nimejitahidi kwa siku moja tu nimeishia kufanywa hivi”

    “Kwani wamekufanyaje?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Ndugu yangu yani acha tu, wameniteka wakaanza kunipa kipigo si unaona nilivyovimba huku…wameniambia nikiendelea kufwatilia ishu za mtoto wangu wataniua kabisa”



    Kwakuwa Sam alikuwa hamuamini Gwakisa alienda akamuangalia akagundua kuwa ni kweli kavimba ila bado hakutaka kuamini moja kwa moja, alijua anachezewa mchezo….



    “Vipi shemeji yuko wapi?”

    “Ngoja nimuite”

    Aliitwa verity aliyekuwa huko chumbani kisha akaja pale walipokaa Sam na Mme wake, Verity alikuwa ana majonzi ila pia alikuwa hajiamini kutokana na hali halisi iliyokuwa pale….



    “Kwanza kabisa nawapa pole kwa kupotelewa na mtoto katika mazingira kama haya”

    “Asnte sana kaka roho inaniuma sana kwakweli nikimfikiria huyu mwanangu” alijibu Gwakisa.



    “Ila mimi naumia zaidi kuliko wewe maana Yule mtoto ni wa kwangu” alisema Sam kitendo kilichomshitua Gwakisa na kumkata jicho Sam.

    “Unasemaje wewe? Umeugua ukichaa sio?” Verity aling’aka kama mwendawazimu.



    “Mimi sio kichaa, na hilo unalijua Shemeji Verity, na unajua kuwa Yule mtoto ni wangu na sio wa Gwakisa, Hebu leo mwambie mme wako ukweli ajue”

    Gwakisa alimgeukia Verity na kumtazama kwa ishara kuwa anataka kusikia kutoka kwake



    Verity alisimama wima na kuanza kuapia kwa Mungu wake…..

    “Nakuapia mume wangu Gwakisa, Princess ni mwanao kabisa, usimsikilize huyu ni kichaa”

    Gwakisa hakujibu chochote bali alibaki amemtolea macho Verity asiyejua kuwa Gwakisa ana ushahidi wa DNA kuwa mtoto sio wake isipokuwa baba halizi wa mtoto ndio alikuwa hajamjua bado…..





    Gwakisa alifikiria cha kusema kutokana na uongo wa mkewe akashindwa afanye nini, akaishia kuguna tu.

    Jambo moja ambalo aliamini ni lazima alifanya ni kulinda heshima yake, ya familia yake, ya mke wake nay a ndoa yake…

    Japo alijua mkewe kakosea sana lakini mbele ya mwanaume mwenzake hakutaka aonekane dhaifu hata kidogo.

    Mr Sam nimekusikiliza vizuri sana, nimekusikia vizuri mnooo ila nimegundua kitu kimoja…alisema Gwakisa.

    “Kitu gani hicho” sam aliuliza

    Gwakisa alichomjibu sam ni kwamba … “nimegundua kuwa huna akili kabisa”

    “Unasemaje, mimi sina akili?”

    “Huna hata kidogooo”

    Sam alisimama wima akitaka ngumi zipigwe kwa kuona kuwa ametukanwa.

    “Ndugu yangu Sam acha hasira za kijinga, unataka upigane namimi wakati unajua naumwa. Subiri nikipona ndio uanzishe vita, hapa ukinipiga wala huna haja ya kujisifu kuwa umenipiga”

    Sam alikaa chini pale kwenye kochi huku Verity akimng’ang’aniza Sam aondoke pale nyumbani.

    “Shemeji Sam nakuomba uondoke nyumbani kwangu la sivyo nitakuunguza hata na maji ya moto”

    Sam aliamua kutulia kitendo kilichomp Gwakisa mwanya wa kuongea kidogo.

    “Ndugu yangu tena mme Mwenzangu Sam labda nikuambie tu kuwa ungekuwa na akili ungeweka juhudi zooote kumtafuta kwanza mtoto ndio uanze kumdai kuwa ni wako”

    “Mimi sio mjinga najua huyo mtoto mmemficha ili nisimchukue”

    Gwakisa akiwa na hasira alimkata jicho kali Sam akamwambia nivile tu anaumwa lakini angempa disipilini ya kutosha na wala asingerudia kukanyaga hapo nyumbani kwake.

    “Sam nashukuru sana kwa kunidhihirishia kuwa umekuwa ukitembea na mke wangu, ila nataka kukwambia kuwa mla vya wenzake na vyake huliwa, kampime mkeo ujauzito kwani inawezekana na mimi nimepanda mbegu zangu kwenye shamba lako”

    Gwakisa alisema maneno hayo ili amuumize Sam kwa kile alichomfanyia bila kujua kuwa maneno hayo yalikuwa kama mwiba kwenye moyo wa Sam.

    Sam alinyong’onyea akatahayari kwa yale aliyosikia, alioanisha mambo mengi mwisho akaamua kuondoka bila kuaga moja kwa moja kuelekea kwake.

    Akiwa njiani kuelekea kwake alipokea simu ambayo ilimtaka afike ofisini mara moja.

    Aligeuza gari na kuelekea ofisini ambapo alimkuta Bosi wake akiwa na RPC.

    Kitendo cha Sam kufika pale akatiwa Pingu na kuwekwa mahabusu.

    …………………………………………….

    Kwenye mida ya saa tisa usiku RAfiki alikuwa akijihisi baridi kali mnooo, pamoja na baridi lakini alikuwa anahisi maumivu hasa kwenye maeneo ya mbavu zake.

    Alijitahidi kufumbua macho yake akakutana na giza nene, taratibu alianza kukumbuka jambo moja baada ya jingine hadi alipofikia kukumbuka ugomvi wake na mmewe.

    Hapohapo machozi yakaanza kummwagika, alinyanyuka taratibu ili afungue miango huku akichechemea.

    Alipofika alianza kwa kutingisha grili lakini akakuta limefungwa kwa ndani, hakuamini kuwa mme wake ndie amekuwa katili kiasi kile.

    Alirudi tena pale chini kwa kujikongija na kuendelea kulia sana, alilia akachoka na kuona sio suluhisho alisogea mpaka nyuma ya dirisha kilipo chumba chao cha kulala na kuanza kumuita mmewe lakini alisikia tu sauti ya kukoroma kwani ndio muda huo Sam nae usingizi ulikuwa umemkolea baada ya kuutafuta kwa muda mrefu.

    Hakuamini kuwa pamoja na kumsubiria mme wake kwa muda mrefu kiasi hicho akitegemea mapenzi motomoto baada ya mume wake kumaliza mafunzo lakini kile ndicho alichokuwa anaambulia.

    Alijuta sana kung’ang’ana kuolewa na Mwanamume kama Sam, alijutia ndoa lakini hakuwa na uwezo wa kurudisha mambo nyuma.

    Alisubiria angalau kupambazuke ili aondoke pale nyumbani atafute sehemu yenye usalama…

    Kweli masaa yalisogea kwa mwendo wa kinyonga na hatimaye kukaanza kupambazuka na watu pamoja na magari vikawa vinasikikika vikipita huko nje.

    Aliamka kwa kujikongoja mpaka nje ya geti kisha akasubiria pikipiki akaisimamisha japo hakuwa na hela ila akapanda mpaka nyumbani kwa wazazi wake.

    Wa kwanza kumuona alikuwa ni mama yake ambaye alimshangaa sana binti yake kwa jinsi alivyokuwa,

    “Mwanangu umepatwa na nini”

    “Nomba kwanza umlipe huyo bodaboda alafu nitakwambia”

    Mama mtu alimshangaa binti yake anavyotembea kwa shida roho ikamuuma sana, alimwambia bodaboda amruhusu kisha akamshikilia bintiye na kumkongoja kwenda ndani kisha akamkalisha na kurudi kumlipa boda boda.

    Aliporudi kwa binti yake alimhoji akasimuliwa mkasa mzima kitendo kilichomfanya ashike mdomo kwa kuhamaki kuwa yani Sam waliyemjua ndio kawa vilee?

    Mama mtu hakuweza kuvumilia, alikimbilia chumbani kumsimulia mme wake ambaye nae alifadhaika sana kwa binti yake aliyempenda sana kufanyiwa yale.

    Muafaka uliofikiwa ni Rafiki apelekwe hospitali huku taarifa zikiwa zinnafika ofisini kwa Sam ili hatua zichukuliwe kwa kitendo alichokifanya.

    ……………………………..

    Dr Kelvin alikuwa anampigia sana Rafiki simu lakini alikua hampati, rafiki alizima simu yake na hata hivyo akawa ameiacha kule kwake wakati wa kuondoka baada ya ugomvi na mume wake.

    Alishakata tamaa lakini kwa jinsi alivyokuwa na usongo na Rafiki alisema kuwa atamtafuta kivyovyote amtie mikononi mke huyu wa mtu.

    Akiwa anaendelea na majukumu yake alipita korido ya mapokezi na kukuta mwanamke amejiinamia chini huku kashikiliwa na mama mmoja mtu mzima akashtuka kwani alimfananisha Yule binti.

    Alisimama na kuwasalimia kwa lengo la kuwatambua vizuri, roho yake ililipuka baada ya kuuona uso wa Rafiki lakini ukiwa umevimba.

    “Rafiki ni wewe? Mbona uko hivyo? Una matatizo gani?” dr Kelvin aliuliza maswali matatu kwa pamoja kabla hata la kwanza likiwa halijajibiwa.

    Haraka haraka alifwatilia kila kitu na Rafiki akaanza kuhudumiwa kwa uharaka.

    Kwakuwa yeye alikuwa daktari wa akina mama hakuweza kumhudumia Rafiki ila alihakikisha anampeleka kunakohusika na kwa madaktari anaowaamini ili ahudumiwe.

    Huduma alizokuwa anapata Rafiki hata mama yake alikuwa anashangaa, mama yake aliambiwa apumzike tu kwani kila kitu kilikuwa kinafanywa na wauguzi waliokuwa wanapokea amri kwa madokta.

    Tabia za madokta wa hii hospitali zilikuwa zinafanana sana kiasi kwamba ikiwa mmoja atawaambia wenzake kuwa huyu ni shemeji yenu muhudumieni vizuri basi atahudumiwa kwa ukaribu mno, na hiki ndicho kilichokuwa kinatokea kwa Rafiki.

    Japo Dr Kelvin hakuwaambia kabisa uhusiano wake na Rafiki kwni ni mke wa mtu ila wale madaktari wenzake walihisi tu na wakawa wanamhudumia vizuri sana.

    Rafiki alitibiwa na kupewa dawa huku akichomwa sindano za kuzuia maambukizi na maumivu pamoja na dawa za kupunguza uvimbe,

    Hakuwa mgonjwa wa kulazwa ila aliandikiwa kulazwa,

    Dr Kelvin siku hii alikuwa na furaha sana na alifanya kazi kwa amani mno huku kila mara akipita pale alipolazwa Rafiki.

    Alikuwa akimletea vitu vidogo vidogo vya kula na vizawadi mbalimbali kiasi kwamba hata Rafiki mwenyewe akawa anajisikia ahueni.

    Siku hii Dr Kelvin hakwenda kabisa kwenye hospitali nyingine ambazo annafanya kazi part time kwani alikuwa anataka akae na Rafiki zaidi pale hospitali.

    Ilipofika usiku alienda kule alikolazwa akakaa kitandani na kuanza kumhoji Rafiki kuhusu mambo gani yaliyompata.

    …………………………………..

    Gwakisa alikaa siku mbili kisha akajisikia nafuu kidogo na kuanza kwenda kazini, ishu ya mtoto Princess ilikuwa imeshikiiwa na Jeshi la Wananchi kwani mtoto aliyepotea ni wa Bosi wao.

    Lakini pia Jeshi la polisi lilikuwa limeikomalia kweli kweli kwani Yule mtoto alikuwa ni mjukuu wa RPC hivyo walihusianisha kupotea kwake na mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na visasi labda dhidi ya majeshi ya ulinzi na usalama.

    Ingekuwa watu waliomteka huyu mtoto wangekuwa ni wa kawaida tu basi angekuwa ameshapatikana lakini mpaka wakati huu kila walichokihisi na kukifwatilia waliishia kwenye hakuna.

    Pamoja na kutangaza dau nono kwa atakayesaidia kupatikana kwa mtoto, kutangaza magazetini kwenye TV na media zingine lakini bado hakuna kilichowezekana. Mtoto alikuwa hajapatikana bado.

    Verity ndani ya siku tatu za kupotelewa na mwanae alikuwa hali wala hanywi, alikonda ndani ya muda mfupi kwani stress zilimzidi.

    Ndoa yake nayo ilikuwa kwenye hali sio nzuri japo mume wake alikuwa mpole tu lakini alijua amani hakuna kutokana na kile ambacho Sam amefanya.

    Alijutia mengi sana lakini maumivu ya mtoto yakawa yamemeza maumivu mengine yote.

    Mmara kwa mara alikuwa anazimia kiasi kwamba ilibidi nyumbani kwao wamchukue tu ili wamuangalie kwa karibu.

    Ilikuwa ni pigo kwenye nyumba ya RPC kwani mambo yalikuwa yamepandana, huku verity kupotelewa na mtoto na huku Rafiki kupigwa na mumewe huku ndoa za watoto zikiwa kwenye sintofaham.

    …………………………………….

    Katika kitu kilikua kinawashtua maaskari ni kuiona gari ya Jeshi kila wakati ikipita kuelekea mpakani ikiwa iko na Gwakisa na askari mwingine wa Kike.

    Walianza kuhisi kuwa huenda kuna dili chafu linachezwa kupitia kwa magari ya Jeshi la wananchi hivyo wakaanza kuwachunguza kwa karibu.

    Wakiwa wamebeba mzigo mkubwa wa vitu haram kwenye gari yao ilisimamishwa na askari wanane wenye silaha nzito…



    Sam alikuwa mahabusu siku ya pili sasa, alikuwa akiteseka kwa makosa ya kumpiga na kumuumiza mke wake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa amefichwa kwenye kachumba kakwake peke yake tena kenye giza nene ambapo alikuwa haonani na mtu yeyote isipokuwa wakati wa chakula kidirisha kidogo kilikuwa kinafunguliwa na kisha chakula kinaingizwa bila kusemeshana na kisha dirisha linafungwa na kubaki giza hivyohivyo.

    Hizi zilikuwa ni adhabu za kipolisi ambazo walikuwa wanapeana polisi wenyewe ikiwa hakuna haja ya mambo ambayo yamekosewa kwenda mahakamani.

    Adhabu hizi zilikuwa zinaambatana na kushushwa cheo endapo anaehusika ana cheo katika jeshi la polisi.

    Kwa hasira alizokuwa nazo RPC juu ya Sam alikuwa anahakikisha ikiwezekana Sam anafukuzwa kazi kabisa.

    Kitu alichokuwa anakifanya alikuwa anaandaa mashitaka mpaka ya uongo ili mradi tu Sam afukuzwe kazi kabisa tena afungwe jela.

    Katika watoto wa RPC Rafiki alikuwa anapendwa kuliko wote, kitendo cha Sam kumuumiza kwa vipigo RPC likuwa anaona kama ameguswa kwa kitu chenye ncha kali ndani ya moyo wake.

    Hakuweza kabisa kuvumilia ile hali, alichoamua ni kitu kimoja tu ndani ya kichwa chake, Sam afukuzwe kazi na ama afungwe na jela kabisa.

    *************

    Asubuhi na mapema RPC akiwa ofisini kwake alimuita sekretari wake ambaye nae alikuwa ni askari mrembo na mtiifu.

    “Niitie PC kiwanuka”

    “Sawa afande!” aliitikia Yule sekretari na kwenda kumuita huyo PC KIWANUKA ambaye kwa cheo alikuwa ni mwanasheria wa Jeshi la POLISI kwa mkoa wa MBEYA.

    Lengo la RPC lilikuwa ni moja tu… kujua ni namna gani na ni sheria zipi ambazo zinamfukuzisha askari Polisi kazi na ikiwezekana afungwe jela kabisa.

    Alipoulizwa sawali hilo PC kiwanuka alishtuka kidogo lakini mbele ya Bosi wake alianza kuelezea kila kitu na sharia amazo zinakidhi takwa la bosi wake.

    Mwisho kabisa RPC alifunguka mbele ya PC huyu kwa kumwambia kuwa kuna mtu yuko mahabusu na anataka atengenezewe hayo makosa na yasainiwe kisha yaletwe kwake.

    PC Kiwanuka alikuwa ana wakati mgumu lakini alitanguliziwa hela na kisha kuahidiwa cheo akajikuta amekubali kufanya huo ushenzi.

    Sam alitafutiwa makosa yaliyoshiba na kisha akapelekewa RPC ambaye aliyasoma kisha akajikuta akichekelea maaana makosa yale yalikuwa yamekidhi kile alichokitaka.

    Kwa mara nyingine tena RPC kwa furaha aliyokuwa nayo aliamua kumuita tena Sekretari wake akiagiza aletewe kahawa ili wanywe na mwanasheria wake.

    Kahawa ililetwa kisha wakanywa huku wakipiga story mbalimbali, story zilipokwisha KIWANUKA alinyanyuka kwa lengo la kuondoka lakini RPC akamwambia atulie kwanza.

    “Hebu pitia kwa Muhasibu mwambie akuandikie cheki ya milioni tano kwa ajili ya likizo ya wiki mbili ukasalimie kwenu”

    “asante Afande”

    “Nawewe asante ila badae tukutane kwenye viti virefu nikupe kiasi kingine idogo kwa ajili ya kutunza hii siri iwe ya kwetu tu”

    ……………………………………….

    Japo Kiwanuka Roho ilikuwa inamsuta lakini hakujali sana kwani alikuwa amefaidika kwa kiwango flani, aliondoka huku moyoni akitabasamu na kuhuzunika kwa nyakati tofauti.

    Sam nae akiwa hajui lolote kule mahabusu kuwa anaundiwa kesi ya kufukuzwa kazi na kufungwa Jela alikuwa anajiuliza tum bona hatolewi, alianza kujutia kile alichokifanya na kujikuta akitamani maisha ya uraiani na kuwa huru.

    Katika vitu Sam alikuwa hajui ni Moyo wa RPC yaani baba yake mkwe, Mzee huyu alikuwa na roho nzuri nay a upole lakini endapo ukigusa maeneo muhimu kwake anakuwa na roho mbaya tena ya kuua kabisa na hapa alikuwa amempangia Sam mambo mabaya sana na tayari alikuwa ameyaweka kwenye utekelezaji.

    ……………………………..

    Fomu ya makosa aliyokuwa nayo RPC ili ipelekwe makao makuu kwa ajili ya mapendekezo ya hukumu ya Sam kupitishwa aligundua kuwa ilikuwa imekosa sahihi ya mkuu wa kitengo cha Nidhamu Katika Jeshi la Polisi.

    Hapa kichwa kilianza kumgonga maana Afisa wa polisi ambaye alikuwa anahusika na kitengo cha nidhamu walikuwa hawaivi na ingewezekana jambo hili likakwama kwenye mikono yake.

    Aliwaza sana lakini mwishoni akajipa moyo kuwa yeye ndie bosi na hivyo alitakalo lazima lifanyike.

    RPC hakutaka kumtuma mtu, aliondoka yeye mwenyewe mpaka kwenye ofisi ya huyu Afisa wa kitengo cha Nidhamu.

    Alipofika alipigiwa saluti kadhaa za heshima kisha akamkabidhi bahasha yenye zile fomu ambapo aliambiwa zinatakiwa zisainiwe haraka.

    Yule afisa wa polisi kitengo cha Nidhamu alifungua zile fomu na kuanza kuzisoma mpaka akamaliza akajikuta anachanganyikiwa.

    Makosa yaliyokuwa yameandikwa pale alikuwa hajawahi kuyasikia pale mkoani, moja kwa moja kwenye akili yake alijua kuwa kuna namna inahitajika kufanywa juu ya Sam.

    Katika watu waliokuwa wanamfahamu Sam toka anafika pale Mbeya na kuishi kwa RPC ni huyu afisa wa kitengo cha Nidhamu

    Alikuwa anamkumbuka toka alipokuwa golikipa na kufanikiwa kuwapa Kombe wakati alipokuwa hata hajawa askari.

    Haraka sana aliita watu wake anaowajua na kuanza kuulizia alipo Sam na kuambiwa kuwa amefungiwa mahabusu.

    Hakutaka kukaa tena alinyanyuka mpaka kwenye chumba alichokuwa amefungiwa sam kisha akaingia ndani na kuanza kuongea na Sam akimhoji mambo mbalimbali.

    Sam alifunguka ukweli wake wote kisha Yule AFISA wa Polisi akaamua kumpa ukweli wa mambo jinsi yanavyoenda.

    Sam alijikuta anamwaga chozi huku akitamani kupiga hata mayowe baada ya kuonyeshwa yale mashitaka. Hakuamini kabisa kuwa jambo alilofanya lingeweza kuwa na matokeo yale.

    “Sa.s..a.. nifa..nyeje” sam aliongea kwa kigugumizi huku akilia.

    “Nakutoa bila kumtaarifu na ukimbie haraka sana kule hospitali ukamuombe msamaha Yule binti kisha mhamishie huo msamaha kwa baba yake la sivyo unafungwa kijana”

    Walikubaliana kuwa aende usiku ili RPC asije akajua kuwa ametoka pale mahabusu.

    ……………………………………..

    Rafiki alikuwa analia machozi kila alipokuwa anamsimulia Dr kelvin kile ambacho mume wake amemfanyia.

    Dr Kelvin nae hakujali kuwa anachofanya ni kuvunja ndoa iliyofungwa kanisani bali alikuwa akimkandamiza Sam kuzidisha chuki kwa Rafiki kwani alikuwa na lake moyoni.

    “Huyo sio mume Rafiki, huyo ni Shetani”

    Rafiki alikuwa akilia tu kila alipokuwa anamsikiliza Dr Kelvin

    “Kweli Yule ni Shetani, yani mtu anadiriki kunipiga,alafu hajali mimi nimezimia, hajali nimelala wapi na wala haniulizii”

    Dr Kelvin kwa mbwembwe za uongo na kweli alimkalisha Rafiki kisha akamlaza kifuani kwake na kuanza kumbembeleza kwa kumpigapiga mgongoni.

    Rafiki alikuwa akijisikia amani sana kwa kile alichokuwa anafanyiwa na Dr kelvin kwani kwakweli hakuna kitu ambacho alikuwa anakihitaji kwa wakati huo kama faraja.

    Dr Kelvin alikuwa anamfuta Rafiki machozi kwa viganja vyake huku akiendelea kumpapasa mgongoni kwa mtindo wa kumbembeleza.

    Kwakuwa rafiki alikuwa amelazwa VIP alikuwa kwenye chumba chake peke yake bila kuchangamana na wagojwa wengine japo chumba kile kilikuwa na vioo vikubwa ambavyo endapo mtu amekaa anakuwa anaonekana kwa nje.

    Dr Kelvin kwa kuwa alikuwa amedhamiria makubwa alimwambia Rafiki alale ili apumzike na kweli Rafiki akalala.

    Alipolala tu Dr KELVIN nae akajiegesha kwa ubavu mmoja pale kitandani huku miguu yake kainingi’iniza chini.

    Aliendelea kumpapasa Rafuki mgongoni lakini safari hii akawa anahamia kwenye kiuno cha Binti huyu mrembo na kuwa kama anamtekenya kitendo kilichoamsha hisia za Rafiki.

    Dr Kelvin kwakuwa alikuwa amezoea haya mambo alikuwa anafanya kwa ustadi mkubwa mno.

    Alikuwa anampapasa Rafiki maeneo ambayo yalikuwa mabaya sana kwa hisia za mwanamke yeyote hususani ambaye hajagegedwa mda mrefu.

    Alifikia hatua sasa akawa anacheza na chuchu za rafiki ambaye sasa alikuwaa anajisikia utamu hadi maumivu ya kipigo akawa hayahisi tena.

    Dr Kevin sasa alikuwa amemgeuza rafiki kwa kuangalia juu kisha akawa ametumbukiza mkono tumboni kwa Rafiki na kuanza kupapasa maeneo ya kitovuni

    Rafiki alikuwa anajinyonga kwa hisia kali huku Dr Kelvin nae mhogo ukiwa uko wima unataka kutoboa koti lake jeupe.

    Dr Kelvin aliendelea kuushusha mkono wake kuelekea chini ya kitovu lakini rafiki akawa kama anauzuia kitendo kilichomfanya Dr aongeze manjonjo.

    Mwisho Rafiki alijikuta akiwa ameruhusu mikono ya Dr kelvin kushuka mpaka sehemu miguu inapoachania na kuingiza mkono ndani ya chupi ya Rafiki akitaka kuligusa eneo linalosababisha watu wauane bila huruma.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alilikuta likiwa na unyevu unyevu wa kutosha lakini Dr Kelvin hakuamini kuwa ule unyevu unatosha kupanda mbegu.

    Aliamua kuingiza kidole ndani taratibu hadi kikazama chote na kumfanya Rafiki agune Ashhhhhhhh haaaaaa….

    Dr kelvin alikitoa taratibu na kukihamishia eneo la juu kidogo lenye umbo la harage na kuanza kusugua kwa mpango maalum.

    Kitendo hiki kilimfanya Rafiki aanze kujinyonga na kutanua miguu yake huku akiwa anatamani kama vile avuliwe nguo.

    Dr kelvin alilielewa hili akaamua kuitoa chupi ya Rafiki na kupandisha nguo yake juu kisha mapaja mazuri meupe ya Rafiki yakawa wazi.

    Aliponyanyuka avue zake akakuta sura ya mtu ikiwa imekodoa macho kule ndani kwa hasira za kufura…………





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog