Search This Blog

Tuesday, 17 May 2022

UKINIPA SISEMI - 5

 







    Chombezo : Ukinipa Sisemi

    Sehemu Ya Tano (5)



    ,Kwa kweli yale Maneno ya Klinita yalinipa wasiwasi kidogo maana kama baba yake tayari alikuwa ameshapanga kutuua sisi ilikuwa vigumu yeye kumshawishi aweze kumsikiliza mwanae maana baba yake na Klinita kwa kweli hakuwa mtu wa mchezo mchezo. "Klinita Mpenzi wangu sitaki nikupoteze mimi kabla ya mimi kupotea. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Ninachokuomba nataka mimi kwenye hii dunia niwe wakwanza kuondoka ila isiwe wewe wakwanza. Naongea Hivi kwa sababu haya ambayo unataka kuyafanya yanaweza yakawa na Msaada mkubwa sana kwangu na yakakuletea matatizo ambayo yanaweza kughalimu maisha yako kabsa. Hivyo fanya vitu kwa akili sana na isizidi uwezo wako wa kufikili maana Ukifanya vikazidi uwezo wako wa kufikili kitakachofata ni kukupoteza wewe. Labda Klinita nikwambie kitu kimoja ambacho hukijui kutoka kwa baba yako. Baba yako hana Huruma kabsa na pindi anapoona mtoto wake anaenda tofauti na yeye anavyotaka hashindwi kumfanyia kitu kibaya. Magreth ingawa alikuwa mtoto wake wa kumzaa lakini alimbaka kisha kumuamlisha Mzee jonasi kumchoma sindano ya kumpotezea Kumbukumbu kisha kumuuza kwa mzungu ili akafanyiwe biashara ya Ukahaba na wala hakumkosea itakuwa wewe ambaye utakuwa umemkosea kabsa. So nenda fanya kile ambacho unahisi hakitakuletea matatizo kwenye maisha yako zaidi ya hapo naomba usifanye kitu kingine"Yalikuwa ni Maneno ambayo nilimwambia Klinita ili kumsisitizia maana Mtu ambaye alikuwa anaenda kumshawishi kutusamehe alikuwa siyo wa kawaida. Baada ya Kuongea yale Maneno Klinita alitoka kwenye kile chumba kwa Haraka sana. Alipoondoka Klinita kwenye kile chumba nilimwita yule mzee ili kumuulizia kama kuna Njia nyingine ambayo inaweza kututoa kwenye kile chumba. Mwanzo sikuwa nachachalika kabsa kuhusu kutoka kwenye kile chumba. Ila baada ya kusikia kama Masanja anapanga mbinu ya kutuua ndio nilianza kuchacharuka. Sikuwa naogopa kufa hata kidogo kwa Muda ule ila pia sikutaka kufa kwa Muda ule maana nilikuwa na Jukumu kubwa ambalo nilitakiwa kulifanya Dunia kabla ya kufa. Jukumu la kwanza ambalo nilitakiwa kufanya ni kulipiza kisasi cha kifo cha mama yangu na baba yangu ambaye mfanyaji mkuu alikuwa masanja. Kitendo cha Masanja kumuua mama yangu kwa kumkata shingo kisha kichwa kunitumia mimi kama zawadi ndicho ambacho kilikuwa kinanipa wazimu kila nilipokuwa nakumbuka. Bora kifo cha baba yangu nilisimuliwa tu pia unyama aliofanyiwa Magreth nao nilisimuliwa hivyo maumivu yalikuwa siyo kama yale ambayo nilikuwa nimeyapata kutokana na kifo cha mama yangu. Nilipomuuliza yule mzee kama kuna njia nyinge ya kutoka pale kwenye kile chumba kisha kuambiwa hakuna ndio nilizidi kuchoka zaidi. "Sam Najua utakuwa unawaza Kufanya mambo mengi sana kwa huyu Mwanaharamu Masanja. Ila nachokuomba Muda huu hauna uwezo kabsa wa kupambana na huyu mtu. Wakati naondoka Blazil mama yangu alinituma kuja kumwambia Magreth afanye haraka amuue Masanja kabla yeye hajafa maana alikuwa anamwamini maana alipitia mafunzo makali. Pia mama yangu aliniambia kama Magreth atafeli kumuua Masanja basi mimi nisithubutu kufanya kitu chochote maana Masanja siyo mtu wa kawaida kabsa. Sam ambacho nakuomba sasa hivi usikurupuke kufanya kitu chochote maana tutakufa kitu ambacho mimi sitaki kutokea. Mimi siyo kwamba kisasi nataka kulipiza kwa ajili ya kifo cha Magreth tu hapana. Kuna kitu kikubwa sana ambacho wewe hukijui Kwa nini Mama yangu Cutherbet alimtuma Magreth kuja kummaliza Masanja. Najua Magreth alikwambia tu kuwa Ametumwa kuja kumuua Masanja kama kulipiza kisasi chake pia Kumlipizia mama yangu kisasi kwa kuwa alidhurumiwa pesa. Mama yangu anapesa nyingi sana hivyo asingekaa kuwaza kulipiza kisasi kwa mtu hatari kama masanja et kisa tu kudhurumiwa pesa. Sasa siyo hayo tu lipo jingine kubwa ambalo ndio hata mimi lilinitoa Brazil kuacha kazi ili kuja kushuhudia kifo cha Masanja. Labda ngoja nikupe Mdokezo kidogo ili ujue ni kiasi gani tunatakiwa kubaki wazima ili kuweza kulipiza kisasi kwa Masanja. Baada ya Mama yangu kudhurumiwa pesa na Mchungaji masanja kwa kweli hasira zilimbana sana Baba yangu na kuamua kusafiri kuja hadi Tanzania kumuonya masanja alipe pesa. Kwa kuwa baba yangu alikuwa ananipenda sana na kila kitu ambacho kilikuwa kinafanyika alikuwa anataka mwanae nishuhudie aliamua kusafiri namimi pamoja na walinzi wake watatu. Alipokuja Tanzania baba yangu naye wala hakupoteza Muda siku hiyo hiyo ambaye alienda kumuonya masanja usiku huohuo aliuawa mbele yangu na alikatwa kichwa kabsa na mimi nilipewa kichwa cha baba yangu nimpelekee mama yangu kama wewe ulivyopewa kichwa cha mama yako. Sema Masanja amenisahau tu maana kipindi nimekuja nilikuwa na umri mdogo sana. Hivyo mimi ninahasira sana na huyu Mtu ndio maana nashindwa hata kuongea. Ila point tunatakiwa kumuomba Mungu tutoke wazima hapa"Aliongea Mzungu matonya kwa lugha yakiswahi kilichoenda shule utafikilia alikuwa Mbongo.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kiswahili ambacho aliongea Matonya kwa kweli kilikuwa kinaeleweka vizuri sana hali ambayo ilinifanya kunishitua kidogo. Ingawa kiswahili chake kiliambatana na Lafudhi ya Kizungu lakini alionekana ni mtu ambaye alikuwa anaongea sana kiswahili hali ambayo ilinifanya kushindwa kuvumilia na Kumuuliza hii lugha yeye ameifahamia wapi. "Sam kuna mambo mengi sana nimepitia mimi tena kwenye hii hii nchi ya Tanzania na ukitaka kuyajua hutayamaliza maana kwanza hatuna muda wa kuyakumbuka haya ila tunamuda wa kujadili ni namna gani tutatoka salama humu. Mimi kiswahili nilifahamia hapa Hapa Tanzania tena Magerezani nilifungwa. Ninaposema nataka kumuua Masanja ninahasira naye ndio maana navunja hata baadhi ya Amri za mungu kwa Mpumbavu mmoja. Baada ya Masanja kumuua baba yangu na walinzi na kuwatoa vichwa na kunipa mimi aliniambia niondoke. Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana baba yangu kweli niliamua kubeba vile vichwa ili kupanga namna ya kusafiri navyo au kwenda kuvizika mahali pazuri. Nilipotoka Pale Kwa Masanja wala haikunichukua hata Dakika kumi nilishangaa Gari ya Polisi inakuja kusimama na polisi waliniambia kuwa wanawasiwasi na mimi wamepata taarifa kwa wasamalia wema kuwa mimi nimehusika na mauaji ya watu wanne kisha vichwa vyao nimevibeba. Yale maneno ya polisi yalinishitua maana kweli nilikuwa na vile vichwa. Waliponikagua kweli walivikuta na walinipeleka Kituoni. Baada ya wiki Mbili nilihukumiwa kifungo cha maisha jela na kilishonishangaza sikupewa uhamisho wa kwenda kufungwa nyumbani kwetu na ilisemekana ni ni raia wa Tanzania hali iliyonifanya kugundua kuwa Masanja kanichezea game. Hivyo kiswahili mimi nimejifunzia jela Naomba tuishie hapa Sam sitaki uniulize tena kama nilifungwa Kifungo cha Maisha nilitokaje jela maana hiyo ni Story ndefu sana"Yalikuwa ni Majibu ambayo alinipa Matonya na sikuwa na swali tena kuhusu kiswahili amefahamia wapi. Kwa maelezo mafupi tu ambayo alinipa Matonya nikajumlisha maelezo aliyonipa Magreth na yote yalikuwa yanahusu unyama wa masanja kweli nilijiona kupambana na Masanja sitaweza na nilitamani kuacha kabsa hata kulipiza kisasi maana nilikuwa kama nakitamani kifo hivi. Wakati nikiwa natafakali maneno ambayo aliniambia Matonya mlango wa chumba ambacho tulikuwepo ulianza kugongwa. Kama kawaida maana ilibidiniende kufungua maana chumba ambacho tulikuwepo ilikuwa chumba ndani ya chumba. Yani chumba kilikuwa kikubwa sana ambacho kilikuwa hadi na watumishi lakini ndani ya kile chumba kulikuwa na chumba kingine ambacho ndio tulikuwa tunakaa kule. Nilipoenda kufungua kwa kweli Moyo wangu uliruka sana nilipoona mtu ambaye alikuwa anaingia Mle alikuwa masanja huku wakiwa na watu ambae walikuwa wamejazia sana. "Nimefikilia sana kuwafunga lakini nimeona kama nitakuwa naongeza uadui tu. Maana najua mnavisasi na mimi na mnauwezo wa kutoroka hata jela na kuja kutaka kuniua. Ingawa najua hakuna mtu ambaye ataniua mimi ila kujihami lazima. Hivyo kitu ambacho nimekiamua mimi ni kuwaua nyinyi ili mfatane na magreth. Ila wewe Sam naomba umsalimie Sana mama yako na mwambie nimemisi sana na kifo chake ambacho nilimuua kwa kumkata shingo nakiota kila siku ndotoni. Pia wewe mzungu Mjinga utamsalimia Sana Mwanangu Magreth mwambie baba yake nimemisi sana maana nakumbuka ile siku ambaye nilimtoa usichana wake alikuwa analia sana. Pia mnatakiwa muwahi huko mkaamulie maana najua kutakuwa na Ugomvi mkali kati ya Mwanangu magreth na Mzee Jonasi maana yeye ndio alimchomaga sindano ya sumu. Sasa mtatoka hapa kwenye nyumba yangu tukufu na nitawapeleke kwenye makazi yangu ambae ni bucha ya kuchinjia watu wajinga kama nyinyi"Yalikuwa ni maneno ambayo aliongea Masanja kwa mapozi ya hali juu sana.





     Yale maneno ambayo aliongea Masanja kwa kweli yalinifanya kujisikia vibaya sana na kujilaumu kwa nini tulikubali kizembe kizembe kumsindikiza Magreth kuja kumuua Masanja hatimae amefanya Makosa makubwa sana ambaye wote sasa tunaenda kufa na kumuacha adui yetu anaendelea kutamba Duniani. "Masanja kabla ya kutaka kuniua nataka nikuulize ni kweli unauwezo huo. Mimi nahisi unatuogopa sana ndio maana hata kutuua unatuzungusha sana hadi utupeleke mafichoni. Wewe kama kweli muuaji hatari kwa nini unamuogopa Mwanao. Kama kweli Gangstar hebu tuue wote hapa haina haja ya kutupeleka sehemu nyingine"Nilimwambia Masanja huku nikiwa nimemkazia Macho. Nilichokuwa nataka muda huo ni kuweza kumchelewesha kidogo masanja ili asitutoe mle huenda tukapata masaada maana Klinita alituhaidi kuwa anatusaidia. Hivyo kama tungeondolewa tu kwenye ile nyumba tutakuwa na wakati Mgumu sana maana Klinita wala asingetuona. "Wewe kijana kumbe ni Mjinga na akili zako zinafanana na baba yako vilevile. Yani leo nimesibitisha kuwa siku zote mtoto wa chura nichura tu wala hata siku moja hawezi kubadilika kuwa mtoto wa papa. Inamaana wewe mjinga unataka kuniambia kuwa mimi nashindwa kukuua hapa na naogopa sana hadi nikusafirishe kwenda mbali. Sasa ili nikuonyeshe kama Masanja anaweza kufanya kitu mahali popote bila kuwaza nakuua hapa hapa namaiti yako sitaibeba bali Masikini Police ndio watakuja kukutoa hapa"Aliongea CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Masanja kisha alisogea hatua tatu kurudi nyuma kisha alitoa Mguu wake wa kuku tayari kwa kutaka kunitoa dunia. nilipoona bastora kwa kweli sikumbuki jasho lilitoka wapi ambacho niliona uso tu umebadilika na kitu kama maji yakiwa yanatiririka. Woga ambao ulinikumba ulikuwa wa aina yake na hakuna siku ambayo niliogopa kama hiyo siku. Kifo bhana kisikie tu ila kamwe usikwepo kwenye tageti ya kifo hata siku moja. Kwa muda ule ambae Masanja alikuwa amekoki bastora yake huku akijiandaa kuifyatua nilikuwa nawaza neno tamu fupi lakuongea ambalo litamfanya masanja kurudisha Bunduki yake mfukoni lakini sikuwa naliona kabsa. "Hapana baba hurusiwi kufanya hivyo maana wewe ni mtu wa Mungu na Mungu anatukataza kufanya hivyo. Baba najua hawa wamekukosea sana na hata Magreth umemuua kwa kuwa ulikuwa unajilinda. Baba hawa naomba usiwauwe maana utapata dhambi kubwa sana. Ili hawa dunia iwahangaishe wabebeshe kesi ya kumuua Magreth na mimi nitakuwa mstari wa mbele kukusaidia kama watakataa hii offa ambayo utawapa ndio uwaue"Yalikuwa ni Maneno ya Klinita akiongea mara tu alipoingia chumba ambacho tulikuwepo. Masanja alipomuona mwanae kaingia kwenye kile chumba huku akiongea yale maneno alionekana kunyongonyea sana na kurudisha bastora yake kiunoni hali iliyonifanya masanja hataki mwanae ajue unyama ambae anafanya. "Mwanangu nimekusikia na nitafanya kile ambacho wewe unataka ila hawa watu wakikaidi tu kile ambacho nitawaambia nitawaua kabsa. Nikiwaacha bila kuwafunga hawa maisha yangu yatakuwa matatani sana maana watanisaka tena ili wanimalize sijui nani anawatuma. Lakini Mwanangu umejuaje kama mimi nipo kwenye hiki chumba na mimi mbona nilikukataza kuingia vyumba kama hivi"Aliongea Mzee Masanja. Maneno ya Mzee Masanja kwa kweli yalinifanya kupumua pumzi ndefu sana maana ilikuwa hafadhali kufungwa maana ipo siku nitatoka ila siyo kufa wakati bado sijafanya kile ambacho nilimuhaidi mama yangu wakati nazika kichwa chake pia bado nilikuwa sijafanya yale ambao aliniagiza magreth kabla ya kifo chake. "Baba naomba unisamehe kwa kuingia huku wakati ulikuwa umenizuia.ila baba nilipoona mimi unawatu wenye nguvu kama hawa wanaingia huku nilijua tu kuna kitu kibaya ambacho ulikuwa unawaza kufanya ndio maana nikaamua kuja kukukumbusha usifanye hivyo maana ni vibaya sana"Aliongea Klinita maneno ambayo yalimfanya baba yake kutikisa kichwa cha kukubaliana na yeye. "Sasa nyie wendawazimu Mungu bado alikuwa hajapanga nyinyi kufa na mnatakiwa kumshukuru sana mwanangu. Sasa ili kifo kiendelee kuwakosa mnatakiwa kukubaliana na mimi kwa hiki ambacho nitakisema. nitawatoa hapa hadi nje ambae kuna Gari lenu tayari nimeshalileta hadi hapa. Kwenye hilo gali nitafunga Bom ambalo nitakuwa nalimoti pia kwenye hilo gari kutakuwepo kichwa cha mzee Jonasi, kichwa cha mama yako maana wakati unakizika mimi nilienda kukitoa pia utakuwepo mwili wa magreth. Hivyo nyinyi mtapanda kwenye hilo Gari na kwenda mbali kidogo ambapo mimi nitaenda kusimama sehemu mbali na nyie na nitawapigia police kuwa kunawatu wanavichwa vya binadamu alafu mtakuja kukamatwa. Sasa mkipanda kwenye lile gari sitaki kuona mtu yeyote anashika hata mlango wa gari Ukigusa tu nalipua pia kwenye hii gari naweka microchip ambazo zitanifanya kusikia kile ambacho mtakuwa mnaongea na wale afande ambapo mtakamatwa mkipindisha tu sijui mnataka kutaja jina langu nawalipua pia"Aliongea Masanja.



    ************************************************************************** Kwa kweli maneno ambayo aliongea Masanja yalinishitua mbaya. Kwanza maelezo tu aliyotoa ilikuwa ya aina yake alafu bado anasema tena kuna kichwa cha Mama yangu kitakuwepo mle. Moyo wangu kwa kweli ulianza kuuma na kujikuta machozi yenyewe yananitoka. Yani Masanja pamoja na kumuua mama yangu kwa kumkata kichwa kisha akaniletea mimi kile kichwa na kukienda kukizika lakini bado alienda kukichimbua na kukiweka sehemu nyingine. Kwa kweli katika vitu ambavyo vilinitoa machozi katika maisha yangu ni ile hali. "Masanja kama kweli kichwa cha mama yangu kitakuwepo kwenye lile gari mimi kwa kweli siwezi kukusumbua tena nitaingia kwenye gari na kufanya kile ambacho wewe unakitaka. Ila wakati nafanya hili Jambo naomba unihaidi kitu kimoja kuwa mimi nikikamatwa na Police naomba kichwa cha mama yangu kikazikwe kwenye kaburi ambalo alizikwa mama yangu. Naomba sana hiki kichwa kisiendelee kukaa sehemu kama vile makumbusha ya kale. Pia Masanja naenda Jela kabsa ila jua nitarudi kumuoa Mwanao pia ningependa wakati naenda kumuoa mwanae huku wewe ukiwa unakata roho bila kupenda maana kabla ya Magreth kufa aliniambia kuwa mama yake alitaka wewe ufe huku ukiwa bado na hamu ya kuendelea kuishi duniani"Yalikuwa niCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Maneno ambayo yalikuwa yanatoka Mdomoni kwangu huku machozi yakiwa yananitoka. Kwa kwa kweli Muda ule nilikuwa na hasira ambazo zilikuwa hazipimika na hasira ambazo nilikuwa nazo ningeshikiwa Mzee Masanja na mtu kisha niambiwe nimuhukumu pale pale nilikuwa sina hukumu nyingine zaidi ya kuutafuna mwili wake kama nyama ya mbuzi iliyorostiwa. Maana kupiga ningehisi wala nisingeonea. "Hahaha Kijana naona unajidanganya sana kuna mambo nilikuwa naogopa kukwambia mwanangu alikuwa karibu. Hivyo kwa kuwa Mwanangu ameshatoka labda ngoja nikwambie ukweli. Wengi sana waliongea maneno kama yako lakini hakuna ambaye alitekeleza hata Mmoja mimi ndio Masanja ambae nafanya kila ninachotaka hapa Duniani na Hakuna ambaye ananihukumu. Labda ombi ambalo umeniomba nitetekeleza maana ukikamtwa kichwa cha mama yako kitachukuliwa na Police hivyo lazima wakakizike. Naomba kijana acha maneno yako kijinga ongoza twende kwenye Gari nisije kupasua Kichwa chako"Aliongea Masanja baada ya Mwanae kutoka Nje. Masanja aliposema tutoke nje wala hatukuwa na Ubishi. Tulitoka hadi Nje na Kukuta Gari ambayo tulikuwa tunatumia kweli ipo kwa Mzee Masanja wakati tulikuwa tumeiacha nyumba. Nilipanda mimi kwenye gari kisha Matonya nae alipanda kisha Masanja alienda kupandakwenye gari nyingine. Masanja alipopanda kwenye ile gari aliongea akiwa ndani ya gari yake na sisi kweli tulisikia alichokuwa anakiongea kupitia Micro chip ambazo alitegesha kwenye gari. Pia kwa mbele pia nilipoangalia vizuri baada ya masanja kunielekeza nilikuta kweli kuna Boom ambalo lilikuwa limetegeshwa tayari. "Naomba muwashe Gari wewe sam mwelekeze huyo Mzungu mwenzako hadi sehemu ile nilipokupigia simu wakati ulipofungua boksi ambalo lilikuwa kichwa cha mama yako kama zawadi na mimi nawafatilia kwa nyuma."Aliongea Masanja na sisi tulikuwa tunamsikiliza kwa Micro chip. Matonya aliposikia Maneno ya Masanja aliwasha gari na safari ilianza. Kutoka Nyumbani kwa masanja Safari ilianzishwa ya kwenda eneo lile ambalo nilikuwa napenda sana kukutana na Klinita maana ilikuwa nje kidogo ya Manispaa ya Tabora. Mwendo kama wa dakika kumi na tano tayari tulikuwa tumeshafika kwenye lile eneo. Masanja naye gari yake nilikuwa naiona kupitia kioo ambaye alipaki mbali. Kwenye lile eneo tulisimama kama muda wa dakika tano tu ghafla nilianza kusikia Ving'ora vya gari la polisi bila shaka walishapewa taarifa



     Kwa kweli kitendo cha kusikia gari za polisi zinakuja huku zikipiga ving'ora vya kutisha ndio hofu ya Kukamatwa ilizidi kuongezeka. "Sam inabidi tutoroke hawa Polisi wasitukamate. Hii kesi Sam tukikamatwa unafikilia kuna kupona kweli lazima tutafungwa Maisha na kushindwa kufanya kile ambacho wewe na mimi tunataka kukifanya. Sam wewe unajua unalipa visasi vya watu wengi sana hadi sasa na hakuna mtu ambaye utampa Jukumu la Kulipa kisasi kama utashindwa kutoroka. magreth kabla ya kufa alishapata watu wa kumsaidia kulipa Kisasi. Sasa sisi tukifa unafikili nani ambaye ataweza kufanya kitu kama hicho"Aliongea Matonya huku akiwa amechanganyikiwa mbaya. Hapo kweli niligundua Mzungu alikuwa amechanganyikiwa kweli maana alishasahau hata yale maneno ambayo alikuwa anaongea Masanja alikuwa anayasikia kupitia Micro chip na ilikuwa hatari sana kwa maisha yetu maana angelipua boom. "Wewe Mzungu unataka kuleta balaa gani hapo. Hivi umesahau tulivyokubaliana kuwa mnatakiwa kukamatwa na Polisi kuliko kufa. Sasa utaamua wewe ufe kwa mimi kulipua Bom pindi utakapotaka kutoroka au ukamatwe na Polisi ukafungwe Jela"Aliongea Masanja kwa Sauti ya Nyodo. Wakati Maongezi yote hayo yanendelea tayari Gari za polisi zilishakaribia sehemu ile ambayo tulikuwepo. Idadi ya Gari ambazo zilikuwa zinakuja kwa kweli zilikuwa nyingi sana huenda polisi waliposikia kama ndio wauji wa kutisha ambao waliwakata shingo mzee Jonasi na mama yangu waliogopa sana maana Hakuna vifo vya kutisha kama vile ambavyo vilikuwa vimetokea tabora. Kwanza vifo vile vilitikisa nchi nzima. "Sam tunatakiwa tusife kijinga mimi ni Mtaalamu wa Mabom sana hivyo Humu hakuna Mtu ambaye ametega bom hata kidogo. Pindi tu nilipopanda kwenye Hili Gari nilianza kuchunguza hili boom lakini nimegundua siyo boom original ambalo linaweza kulipuka. Sasa kama wewe unaamini boom mimi nakurusha ili masanja kama atalipua nife mimi ili mmoja abaki kulipiza kisasi maana hatuwezi kufa kizembe. Pia kama halitalipuka na mimi nitakamatwa na polisi wewe ndio utakuwa Msaada mkubwa wa kuhakikisha natoroka gerezani maana siyo kusema kunitoa. Nauhakika nikikamatwa mimi nitafungwa tu kifungo cha maisha"Aliongea Tena Mzungu kwa haraka sana na kipindi anamalizia kuongea maneno yake tayari alishafungua mlango kwa kasi ya ajabu alinisukuma. Kwa kuwa alinisukuma bila mimi CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/kujiandaa hakupata upinzani kutoka kwangu hivyo nilienda kuanguka nje ya gari. Nilipoanguka nje niliamka kwa kasi ya ajabu na akili zangu zilishahama kabsa maana niliamini kwa Asilimia mia lazima huo ndio utakuwa mwisho wa kumuona Mzungu tena hivyo macho yangu yalikuwa kuangalia Gari jinsi ambavyo litalipuka. Nilishajisahau kabsa kama Mzungu amenisukuma vile ili niweze kukimbia. Cha ajabu hata Mzungu aliponisukuma na kutua nje bado gari haikulipuka. Wakati nashangaa ile hali nilimuona Mzungu akichomoka na yeye kwenye gari kisha alitoka nduki bila hata kunisemesha. Nilipoona Matanya na yeye kachoma kwenye gari na kutimua mbio ndio kumbukumbu na mimi zilinijia na kukumbuka kama kuna kesi ya ajabu tunatakiwa kubebeshwa. Niligeuka kwa kasi na kuiangalia njia kisha mbio ilianza. Wakati natimua mbio nilianza kusikia milioa ya Risasi huku sauti ya kutuamrisha tusimame ikitawala. Nilipoisikia ile sauti ni kama ilinipa mzuka wa kukimbia zaidi maana sikutaka kabsa kukamatwa na Polisi. Wakati nikiwa nakimbia nilihisi kitu cha baridi kikipenya kwenye Mguu wangu hali iliyonifanya nianguke chini kama mzigo. Nilipoanguka chini kwa kasi ya ajabu nilitaka kuamka kuendelea kukimbia lakini Mguu wangu wa kushoto nilihisi hauna Nguvu. Ilibidi niangalia kuna nini kimefanya niwe vile. Nilipoangalia ndipo moyo wangu ulishituka zaidi maana nilikutana na Damu inatoka mbaya bila shaka nilikuwa nimepigwa Risasi. Pamoja na kujikuta nipo vile sikutaka kukata tamaa. Nilijitaidi nikaamka vile vile na kuanza kukimbia kwa Mguu mmoja. Ile haikuwa kukimbia tena bali ilikuwa kurukaruka. Kwa hali ile sikuweza hata kufika mbali polisi wakanikamata.



    Kwa kweli kitendo cha mimi kukamatwa na Polisi kiliniuma Sana na kuamini sasa kazi ya kulipa kisasi inazidi kuwa Ngumu. Ingawa wakati tunatoka kwa Masanja nilikubali kukamatwa na Polisi ili tusiuawe kama Masanja alivyosema ila kwa Muda ule sikupenda tukio kama lile litokee. Polisi waliponikamata kwanza nilianza kuambulia kichapo cha kuwasumbua. Yani hawakujali hata kama wamenipiga Risasi Mguuni wao waliponifikia kilifuata kipigo takatifu sana. Hawakuwa wanachagua watumie nini kunipigia walikuwa wanachanganya wengine walikuwa wanatumia lungu wengine makofi yani walikuwa wamenisakama sana. Maneno ambayo nilikuwa nasema kuwa siyo mimi niliyofanya hilo tukio huenda ndio yalizidi kuwapa hasira na kuzidi kunidunda zaidi. Maana walichokuwa wanahisi wao haiwezekani nikawa na mwili pamoja na vichwa vya watu kwenye gari alafu niseme siyo mimi nimefanya lile tukio. Wao hawakujua kama kuna mchezo ambao ulikuwa umechezwa na Mzee Masanja. Kipigo kiliendelea pale kama cha muda wa dakika tatu tayari nilikuwa nimeshatapakaa damu sasa maana damu ilikuwa inanitoka mguuni ambapo nilikuwa nimepigwa Risasi na nyingine puani na Mdomoni ambayo ilitokana na kipigo cha Makofi ambacho nilikuwa nalipata kutoka kwa wale Afande. Afande walipolizika na kichapo ambacho walikuwa wanakitoa kwangu yani wakahakikisha nimechoka ndipo walinibeba kwenda kunipakia kwenye Defenda kupelekwa hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya Matibabu kabla ya kupelekwa kituoni maana hali yangu ilizidi kuwa mbaya kutokana na damu ambazo zilikuwa zinanitoka. Wakati wakiwa wananibeba moyoni nilikuwa naomba kwa Mungu matonya awe ametoroka maana nilihisi ndio atakuwa msaada mkubwa kwangu. Kile ambacho nilikuwa nakiomba nahisi Hakikufanyikiwa maana Hazikupita hata dakika mbili tangu nipakiwe kwenye Gari matonya nae nilimuona akiletwa huku akiwa ametapakaa damu hafadhali ya mimi. "Jamani hakuna kitu kibaya ambacho tumekifanya sisi naomba tusikilizeni kwanza mtatuelewa na mtu ambaye amefanya hili tukio mumkamate"Yalikuwa ni maneno ambayo alikuwa anaongea Matonya huku damu zikiwa zinamtoka mdomoni na puani na kushuka kwenye shati lake maana hakuwa na uwezo wa kuzizuia maana tayari mikono yake alifungwa pingu. Maneno ya Matonya hakuna afande ambaye alimsikiliza zaidi ya kuongezewa vibao na kuambiwa hayo maelezo ataenda kutoa Kituoni. Baada ya Matonya kupakiwa Defender iliondoka kwa kasi kuelekea Tabora Mjini kupelekwa hospitalini. Kutoka Sehemu ambayo Tukio lilitokea hadi tabora mjini kulikuwa na umbali kidogo. Kwa Gari ilichukua kama Muda wa Dakika kumi na saba ndio tulifika. Tulipofika Tabora Mjini tulipelekwa kwanza Kituo cha polisi cha line polisi hapo Tabora mji vikatolewa vibari kisha tulipelekwa Hospitali ya kiteto kwenda kutibiwa huku tukiwa kwenye Ulinzi Mkali wa Polisi. Pale Hospitalini Matibabu yaliendelea kwangu kwa Muda kama wa wiki moja ili kuhakikisha kidonda ambacho nilipigwa Risasi mguuni kinaonyesha dalili ya kupona ndio niruhusiwe. Uzuri ile risasi kwa kweli iliweza kupiga nyama na haikuwa na nguvu sana hivyo haikuweza kudhuru mifupa. Mwenzangu siku ile ile tulipofikishwa alitibiwa na kurusiwa na alipelekwa Polisi huko sikujua alikuwa amepelekwa kituo gani cha polisi. Baada ya wiki kwisha tayari nilishapona Mguu wangu na kuweza kutembea ingawa ilikuwa kwa shida sana. Nakumbuka ilikuwa siku ya Juma Mosi nikiwa nimetulia Kitandani Hospitalini nikiwa nasubilia Hurusa kutoka kwa Dactari ili niweze kutolewa hospitalini na kupelekwa kituoa cha polisi tena. Nikiwa pale mgeni mmoja ambaye alikuwa ni Muhimu sana kwangu aliingia. Nilipomuona yule Mgeni kwa kweli nilishituka sana maana sikutaka kumuona akija pale. Huyu Mgeni hakuwa Mwingine bali ni Klinita. Klinita alipoingia na kuniona alishindwa kujizuia na kunikimbilia Kuja kunikumbatia huku machozi yakiwa yanamtoka. "Sam Najua upo kwenye wakati Mgumu sana ila vumilia utatoka tu. Huu wakati Mgumu unaopitia ni moja ya Mipango ya Mungu hivyo yeye mwenyewe ndio atakusafishia kwa kila kitu. Usiwe na wasiwasi kabsa utatoka Salama wala hautofungwa na utafanya kile ambacho dada yangu alikuagiza kabla ya kufa" aliongea Klinita kwa uchungu huku akiwa analia. "Klinita kama unanipenda naomba iwe mara yako ya mwisho kuja hapa. Namjua baba yako ni mtu ambaye hana huruma hata kidogo kama atagundua kuwa unakuja kuniona hapa anaweza kukufanyia kitu kibaya sana ambacho kitanifanya nikukose duniani. Hebu fikilia kama baba yako aliwezeka kumbaka mwanae Magreth ambaye hakumkosea kisha kumpeleka Brazil kumuuza na baadae kufanikiwa kumuua wewe unafikili anashindwa kukufanyia unyama zaidi. Nakupenda sana klinita sitaki nikukose kabsa hivyo kwa sasa kaa mbali na mimi"Nilimwambia Klinita.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******-********************************** Kwa kweli yale maneno ambayo nilimwambia Klinita ni kama yalimuongezea huzuni na kuzidi kulia zaidi. "Sam Najua kama baba yangu ni mtu mbaya sana lakini Kamwe siwezi kukaa mbali na wewe. Sam nipo tayari kupoteza maisha ila siyo kuwa mbali na wewe. Nazani unafahamu na unakumbuka vizuri kuwa niliacha kusomea Usister kwa ajili yako wewe lengo niwe karibu na wewe leo utaniambiaje nikae mbali kisa baba yangu. Kiufupi Sam labda elewa tu kamwe siwezi kukaa mbali hata siku moja kwa mtu ambaye nampenda kama wewe. Nakupenda Sam na nipo tayari kufanya kila kitu kwa ajili yako wewe hata kile ambacho kitasababisha maisha yangu kupotea nipo tayari"Aliongea Klinita huku Muda ule tayari alishafuta Machozi ambayo yalikuwa yanamtoka na kuongea kwa Usiliasi wa hali ya juu. Maneno ambayo alikuwa anaongea Klinita mimi nilibaini kuwa hatanii hata kidogo maana Klinita mimi nilikuwa namjua. "Nimekuelewa Klinita tena nimekuelewa sana. Klinita nimekwambia usinifatilie sana kwa kuwa wewe kuwa hai ndio furaha yangu hapa Duniani. Mama yangu na baba yangu wamekufa nimebakiwa na wewe tu wa kunifariji sasa na wewe ukifa utafikili nitabaki na nani. Klinita Nahitaji uwe nuru katika maisha yangu hasa kwenye mitihani migumu kama hii. Hivyo kwa sasahivi wewe ndio umetuokoa kwenye kifo cha kuchinjwa na kuja jela hivyo subilia uone hukumu yetu ndio utaanza kutoa Msaada tena"Nilimwambia Klinita. Kwa maneno yale Machache ambayo nilimwambia Klinita kidogo alinielewa. Klinita alinisogelea na kuja kunipiga busu la Mdomoni ambalo lilifanya Mwili wangu kushituka kama nimegusa waya wa Umeme. Baadae Klinita ilibidi aondoke na kuniacha pale Hopstalini nikisumbilia kutolewa. Muda wa Saa sita Machana Dactari ambaye alikuwa anahusika kunitibu mimi Aliniruhusu nakutolewa Hospitalini ili nipelekwe kituo cha Polisi. Nilipotolewa Hospitalini kwa kweli nje nilishangaa nilikutana na watu wengi sana ambae sikujua walikuja kufanya nini. "Alafu jamaa mwenyewe ukimwangalia hafananii kabsa na matendo ambayo aliyafanya. Kwa kweli nimeamini pesa ni mwanaharamu na Ndugu yake ni shetani. Angalia kijana alivyo mzuri lakini huwezi amini huyu ndio ambae alikata kichwa cha mama yake pamoja na kichwa cha mzee wa kanisa mzee Jonasi kisha kumuua Sister Magreth lengo tu kusaka utajiri"Nilisikia Moja ya Maneno ambayo kijana mmoja alikuwa anaongea na mzee Flani. Yale Maneno ya yule kijana kwa kweli yaliniumiza mbaya na kupata picha kumbe wale watu walikuwa wamekusanyika ili kuja kumuona Jambazi ambaye alichinja watu wawili na kuwatoa vichwa mmoja akiwa mama yake. Sikuwa na kitu cha kujibu kwa muda ule kwa yale maneno ambayo nilikuwa nayasikia zaidi ya kumuomba Mungu anitoe kwenye wakati mgumu kama ule. Nilipanda Gari na Safari ilianza ya kuelekea kituo cha polisi . Hapo Polisi line niliandikishwa vitu ambavyo nilikuwa navyo kisha nilipelekwa Gerezani Uyui ambako niliwekwa Rumande Kusubilia Kesi ambayo ilikuwa inatukabili. Huko Gerezani kwa kweli nilipofika hadi nilitamani kulia maana Nilimuona na Mwenzangu Mzungu hali yake ndani ya wiki kama moja na sehemu alikuwa amekonda hadi anatia huruma. "Sam hafadhali Umekuja hivyo muda wa kuondoka nahisi umewadia. Kwa kesi hii tulionao hakuna haja hata ya kuisikiliza maana lazima tufungwe. Hivyo muda tulionao ni kutoroka Gerezani kitu ambacho nahisi kitakuwa cha hatari sana kwetu lakini hakuna jinsi. Tuna siku chache sana za kupanga namna ya kutoroka Hapa Gerezani hakuna haja ya Kusubilia kesi"Aliongea Matonya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Maneno ya Matonya kusema kuwa tunatakiwa kutoroka Gerezani bila kusubilia kesi yetu kusomwa mimi nilimuunga Mkono. Nilikuwa najua jinsi Ugumu wa kesi jinsi ulivyo hivyo kufungwa ilikuwa Muhimu tu hali ambayo ingenikosesha mimi kulipa kisasi kwa Muda muafaka. Mwenyezimungu nilikuwa najua kabsa kama anapinga vikali mtu kuua ila Kwa Muda ule nilikuwa na Hamu ya kumuua Mchungaji masanja tena kifo cha kinyama sana. Kwa Jinsi ambavyo alimfanyia mama yangu kisha simulizi ambayo nilipewa na Magreth ukijumlisha na kifo cha Magreth mbele ya macho yetu nilitokea kumchukia Sana Masanja. Kwenye Lile Gereza uzuri tulikuwa tunalala chumba kimoja na Matonya. Chumba ambacho tulikuwa tunalala kilikuwa kizuri tu maana tulikuwa hatuchanganywi na Wafungwa wengine maana bado tulikuwa hatujafungwa tulikuwa Rumande kusubilia Kesi yatu. Ulinzi ambao Ulikuwa unatulinda sisi kwa kweli ulikuwa wa aina yake na kama Ungeendelea vile ilikuwa Vigumu sana kuweza kutoroka kwenye lile Gereza la Uyui. Kwa Muda ule prosses za kutoroka pale Gerezani zilikuwa zinaendelea kama kawaida maana uzuri mimi na Matonya tulikuwa tunalala chumba kimoja hivyo ilikuwa Rahisi kuweza kupangilia mambo yetu. Siku zilizidi kukatika pale Gerezani bila kupata nafasi kabsa ya kutoroka maana ulinzi ulikuwa Mkali sana. Tulikaa pale Gerezani kwa Muda wa mwezi mmoja na nusu bila Mafanikio hatimae siku ya kusikiliza kesi yetu ilifika. Hiyo Siku asubuh muda wa Saa nne ndio tulikuja kuchukuliwa. Hiyo Siku pili ndio tulipanga kutoroka hata kwa kuruka kutoka kwenye gari wakati tunapelekwa mahakamani gari ikiwa inakimbia. Ila hicho kitu tulipanga kitafanyika endapo askari ambao watakuwa wanatupeleka huko hawatakuwa wengi. Kwenye ile Defender Askali kwa kweli walikuwa wakutosha na wote walikuwa na siraha. Hata wakati tunapelekwa tulikuwa tumefungwa pingu na bado tulikalishwa chini ya Gari. Hadi pale kutoroka hiyo siku tulikuwa tumefeli. Tulifika Mahakamani muda wa saa nne asubuhi tulikuta watu wengi sana walikuwa wamerundikana lengo watuone sisi maana taarifa zilikuwa zimezagaa kuwa ni majambazi sugu. Tulipofika mahakamani tuliingizwa hadi ndani kisha bila kupoteza Muda hakimu alianza kusoma kesi zetu ambazo zote zilikuwa zinafanana. Hakimu alitusomea kesi kuwa tunahusika na Mauaji ya mama yangu pamoja na magreth na Mzee jonasi lengo kujipatia utajiri. Walikuwa na ushaidi kabsa kama walitukamata na vitu hivyo na bado vilikuwepo. Hakimu aliposema hata vitu vile bado vipo na viliwekwa kwenye Friji ili vikae kama ushaidi ndio niliumia zaidi. Kwa kweli kitendo cha kusikia hadi muda ule kichwa cha mama yangu bado kilikuwa kinazunguka kama pambo niliumia vibaya mno. Hakimu alipomaliza kusoma kesi yetu alitupa Muda wakuongea ambao ilikuwa kukubali au kupinga ile kesi. "Asante sana Hakimu Mtukufu kwa kunipa hii nafasi. Hakimu hata nikiongea neno gani nahisi itakuwa vigumu nyinyi kuweza kunielewa ambacho nawaomba hakimu pindi naondoka hapa mahakamani kichwa cha mama yangu naomba mkakizike kwenye kaburi la mama yangu ili kisiendelee kuteseka hivyo. Kwa kweli mimi ndio nilimuua mama yangu pamoja na hawa watu. Haya nayathibitisha kupitia mdomo wangu na hii sauti inatoka kwenye koo langu na siyo ndani ya moyo wangu. Nikisema kuwa mimi sijafanya hivi ni vigumu kunielewa kwanza mmenikamata na ushahidi na pili mmepandikizwa vitu na watu wenye uwezo wa juu kushinda mimi. Nakubali kuwa nilimkata mama yangu kichwa ili niwe tajiri. Nimekubali haya yote ili kichwa cha mama yangu mkakipumzishe salama kisiendelee kuteseka. Mama yangu yupo kaburini haoni, haiskii, hanusi, hapumui wala hapigi chafya kwani kitu ambacho kinamfanya kufanya hayo mambo bado mmekizuia huku duniani tafadhari pelekeni hicho kitu kwa mama yangu"Niliongea yale Maneno kwa sauti ya juu na yaukali kidogo hadi machozi yalianza kunitoka. Hakimu alipoona nimemaliza kuongea yale maneno alimkaribisha na Mzungu. "Najua kuwa Tanzania ni nchi ambayo inanuka rushwa hivyo mliponikamata nilijua kabsa lazima mtufunge. Nikiongea ukweli wa mambo naona sitamaliza siku mbili tayari nitakuwa nimekufa tena naweza kuuawa na polisi kabsa. Ila nathibitisha na Mungu ananisikia hicho kitu hatujafanya na aliyefanya hiki kitu muda utafika mtakuja kumjua tu. Mimi nipo tayari kwa Hukumu yeyote ambaye mtaitoa ila mtakapo nirudisha gerezani mpelekeeni salamu Mchungaji masanja atufanyie ibada sana tuweze kufia huku Jera tusitoke tena"Yalikuwa ni Maneno machache ambayo aliongea Matonya nakutulia kimya. Baada ya kumaliza kuongea yale Maneno hakimu alisema turudi wiki ijayo kwa ajili ya Hukumu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********************-************************************************ Baada ya kesi yetu kusomwa ikaisha pia sisi kupewa nafasi ya kujitetea tukajitetea hatimae hakimu kutoa wiki moja ndio Hukumu itapita ilibidi kurudishwa tena Rumande kusubilia Hukumu yetu. Kutoka Mahakamani hadi Gerezani Uyui defender ilitumia muda wa dakika tano tu tayari tulishafika. Tulipofika tulishushwa na kuwekwa Sello tena kama kawaida. Ile hali kwa kweli mimi ilikuwa hainipendezi kabsa maana bora tungehukumiwa tungekaa huru bila kulindwa muda wote. Tungehukumiwa ingawa ulinzi ungekuwepo lakini usingekuwa wa hatari kama muda huo. "Tunatakiwa kukaa miezi minne mbele ndio tutoroke inaonekana ulinzi kwetu Bado mkubwa sana. Ila kama tukihukumiwa Angalau ulinzi kwetu utapungua na kufanya maandalizi ya Kutoroka. Kiufupi siwezi lazima nitoroke kwenye hili gereza hata kama kutakuwa na ulinzi mkali wa aina gani. Nahitaji kulipiza kisasi cha kifo cha baba yangu ambae aliuawa bila hatia na Masanja kisha kesi nilitupiwa mimi. Kifo cha Magret pia ninajukumu la kulipiza kisasi hivyo kutoroka humu ni lazima"Aliongea Matonya. Yale Maneno ya Matonya kwa kweli yalinipa Amani sana na mimi kupata malengo ya kutoka Gerezani ingawa tulikuwa na kazi Kubwa sana. Kwa Gereza la Uyui ambalo lilikusanya wafungwa Watukutu wote wa Mkoa Wa Tabora kulikuwa na ulinzi Mkali kutoroka pale ilikuwa siyo kitu cha Mchezo mchezo. Maisha yaliendelea Pale Gerezani hatimae Wiki moja ambayo tulikuwa tunaisubilia iliisha na Kuja kuchukuliwa Tena Kupelekwa Mahakani. Hiyo Siku Mahakamani kila Mtu alikuwa anaingoja kwa Hamu kujua Stakabali ya maisha yake. Saa nne kamali tulishafikishwa Mahakani na nilipoingia Mahakani moyo wangu ulishituka sana nilipomuona Mzee Masanja pamoja na klinita walikuwepo. Uwepo wa Klinita pale haukunishitua maana nilijua anakuja kujua mumeo nahukumiwa miaka mingapi. Ila uwepo wa Masanja pale ilimaanisha Hukumu ambayo tungepewa ilikuwa kali. Baada ya kesi kukumbushiwa kidogo hatimae Hakimu alisimama ili kutoa hukumu "Kutokana na Sheria namba 103 inayohusu makosa ya Njinai kama kuua kwa kukusudia, kubaka pamoja na mashambulizi ya Ugaidi hukumu yake huwa kunyongwa au Kuhukumiwa kifungo cha maisha jela. Hivyo Basi namuhukumu Samweli Kifungo cha maisha Jela kwa kosa la kumuua mama yake na watu wengi kinyama tena kwa kukusudia ili apate mali. Pia namuhukumu Matonya kunyongwa kwa kosa linalofanana na kosa la Samweli ingawa katika kumbukumbu zetu Matonya siyo mara yake ya kwanza kukutwa na Hatia kwenye nchi yetu ya Tanzania. Kosa la Kwanza alimuua Baba yake Mzazi ambaye alikuwa rafiki yake na mchungaji wetu kipenzi Mzee Masanja. Sheria ya Kunyongwa bado haijapitishwa Hapa Tanzania kuwa Rasmi Hivyo ataendelea kutumikia kifungo Gerezani na Siku sheria itakapopitishwa na Rais Matonywa atatakiwa kunyongwa mara moja"Yalikuwa ni maneno ya Hakimu aliyaongea ambayo yalinifanya mapigo yangu ya Moyo kuanza kwenda mbio. Nilimwangalia Masanja yeye alionekana mtu mwenye furaha sana. Nilimwangalia Klinita nilimuonea Huruma maana yeye alikuwa anatokwa na machozi. Masanja yeye alikuwa anacheka kwa kuwa alishaona kazi imemalizika kamwe hata pata Usumbufu tena kutoka kwetu. Upande wa Matonya yeye alikuwa kimya ametulia wala hakuongea kitu chochote. Baada tu ya Hukumu kutolewa tulifungwa Pingu tena tukabakiwa kwenye Defender safari ya kupelekwa Magerezani Uyui kuwa wafungwa Rasmi ilianza





     Ndani ya Gari kipindi tunapelekwa Gerezani tulikuwa tumekalishwa chini huku ukimia ukiwa umetawala. Kila mmoja alikuwa kimya akifikilia kitu cha kufanya. Moyo kwa kweli ulikuwa unauma sana. Kijana ambaye nilikuwa na maono ya kuishi vizuri na bado nilikuwa na mchango mkubwa kwenye taifa nimejikuta nafungwa kifungo cha Maisha jela kisa kuwa na Uhusiano wa kimapenzi na Mtoto wa Masanja. Nilifikilia Maisha yangu nilipotoka hadi nilijikuta na Mwaga machozi maana ni mengi sana nilikuwa nimepitia na mengi sana yalinisubilia kufanya. Nilisoma Shule ya Seminary na kupoteza miaka kibao ili baadae niwe Padri ila katikakati ya Masomo yangu niliharibiwa na Magreth ambaye alikuwa anafanya kwa lengo la kulipiza kisasi. Nikaachana na Seminary ili kumfanya Magreth kutimiza kile anachotaka na Mimi nikaangukia kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Klinita lakini nako nikaambulia kifo cha Mama yangu kwa kuchinjwa vibaya kisha kichwa nikatumiwa kama zawadi. Katika vitu ambavyo viliniuma maishani kwangu na yananipa nguvu za kutaka kufanya mambo mabaya kwa Mchungaji masanja bila kujali ukatili wake ilikuwa kifo cha mama yangu pamoja na kile ambacho alimfanyia mama yake na Magreth mwajuma nyamilambo pamoja na ukoo wake kwa Ujumla. Simulizi ya maisha ya Magreth ambaye alinipa ilikuwa inatisha na inatia Huruma hivyo nilipaswa kumuonyesha Masanja kuwa kile ambacho anafanya siyo kizuri. Safari iliendelea hatimae tulifikishwa Gerezani tukaandiskishwa kisha tulipewa Mavazi tukapelekwa kwenye chumba ambacho tungekuwa tunaishi. Kiukweli chumba kilikuwa kichafu sana huku sehemu ya kulala kulikuwa na vipande CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/vya Godoro ambavyo vilikuwa na Rangi ya kama kunguni wanaishi mle. Mazingira ya kile chumba pamoja na Vigorodo ndio vilinipa mzuka wa kutoroka na nilikubali kabsa bora kitu chochote kibaya kinitokee lakini kutoroka kupo pale pale. Muda ule ule baada ya kuonyeshwa sehemu ambayo tungekuwa tunaangusha tulikuja kuchukuliwa kwa Ulinzi mkali na kupelekwa sehemu kufanya kazi. Kazi ambayo tulipelekwa kwa kweli ilikuwa na Ugumu wake maana ilikuwa kufyatua tofali za block ukifikilia na mimi nilikuwa Mlaini kwa kazi Ngumu kama zile nilikuwa sijazizoea. Hata pale Magerezani kitu kingine ambacho kilikuwa kinaniumiza tangia nikamatwe sikuwahi kumuona ndugu yangu hata Mmoja anakuja kunisalimia. Hii nilihisi baada ya kusikia kuwa mimi ndio nimemuua mama yangu ili kupata utajiri nahisi ndio walichukia. Maisha yaliendelea Gerezani hatimae tulimaliza miezi mitatu bado tulikuwa hatujatoroka kabsa maana ulizi kwetu ulikuwa siyo wa mchezo mchezo. Kila sehemu ambayo tulikuwa tunapelekwa kufanya kazi kulikuwa na ulinzi imara sana kitu ambacho kilikuwa kinatupa Ugumu wa sisi kufanya kazi. Hali ya afya zetu kwa kweli nazo zilipungua kwa kiasi kikubwa hii ilitokana na kazi ngumu ambayo tulikuwa tunafanya alafu unakula chakula hakieleweki na bado unakuwa na mawazo. Kwa maisha ambayo nilikuwa naishi kwa Muda ule Gerezani nilitamani kutoroka hivyo hivyo hata nikiwa kwenye ulinzi mkali. Nakumbuka ilikuwa siku ya Juma mosi tulichukuliwa kwenda kulima shamba la Mkuu wa Gereza kutokana na Udogo wa lile Shamba tulichukuliwa watu watatu tu ambao tulikuwa tunakaa chumba kimoja. Ilikuwa mimi Matonya pamoja na Mzee wa makamo Mzee Juma. Ingawa tulikuwa watatu lakini askari magereza ambao walikuwa wametupeleka hadi shambani na walikuwa na Jukumu la kulinda walikuwa zaidi ya wanne. Ile hali mimi nilishaizoea na nilijua lazima kuna mtu anasisitiza sisi kulindwa vile ili tusitoroke na alikuwa anajua tukitoroka maisha yake yatakuwa magumu sana. Tukiwa tunaendelea kulima matonya alinisogelea kama alikuwa anataka kuongea neno hivi. Maana mkiwa mnalima afande hawakai karibu sana na nyinyi wanakuwa mbali hata kama mtapiga stori kwa sauti ya chini hawawezi kusikia. "Sam nilikuwa kimya miezi hii kaza na ulikuwa unaniuliza lini hasa tunatoroka na sikukupa jibu maana nilikuwa kwenye uchunguzi. Naomba jiandae kesho saa mbili kamili wakati wafungwa wanaenda kanisani ndio muda wa sisi kusepa. Tulikuja Gerezani wawili lakini tutatoka watatu pamoja na Mzee juma nimeshaongea naye na atashirikiana na yeye kutoka Gerezani"Yalikuwa ni Maneno ambayo aliongea Matonya kwa Sauti ya chini ambayo yalinishitua kidogo. Swala la kutoroka Gerezani kwangu ndio nilikuwa nalisubilia kwa hamu kubwa sana. Hivyo niliposikia neno kutoroka kwanza nilifarijika maana. "Najua siku zote ulinzi huwa mkali sana ispokuwa siku ya juma pili ambao Askari wengi huwa wapo mapumziko na wengine huwa wapo kanisani. Leo Jioni kuna afande ataniletea bastora mmoja ambaye ndio itatusaidia kutoka Gerezani kirahisi maana walinzi watakuwa wachache. Najua Gerezani tutatoka lakini tutakuwa tunatafutwa Sana hivyo Tukishatoka Gerezani Sehemu ya kwenda kujificha itakuwa kwa adui yetu mzee Masanja na Mpenzi wako klinita ndio atatakiwa kufanya hivyo Ingawa hatujamuambia. Tukijificha kwa Masanja Vigumu sana Kugundulika na baada ya mambo kuwa shwali Tutatoroka tena kuelekea Brazil kwenda kujipanga ili kuja kupambana na Masanja"Aliongea Matonya.



    ********************************************************************************************* Maneno ambayo aliniambia Mzungu kuwa tunatoroka yalinifurahisha Sana na Muda Mwingi nilikuwa nasubilia Kitu Kama Hicho. Pia kituo ambacho alisema tutaenda kujificha kabla ya kuondoka hicho nacho nilikifurahia maana ningepata Muda wa kumuaga Klinita na kuondoka huku nikiwa na mpango wa Kuja kumuoa nikirudi kama Magreth alivyoniambia na kama mimi tulivyoahidiana na Klinita kipindi nimefukuzwa shule na yeye alikubali kuondoka na mimi na kuacha shule lengo nimuoe. Kitu ambacho kilinishitua na kunitia Wasiwasi ni Kwa nini Mzungu Alimshirikisha na Mzee Juma kutoroka Gerezani wakati ile ishu ilikuwa ya kwetu wawili na kitendo cha kumshirikisha mzee Kama yule mimi nilihisi kwa Upande Mwingine ishu itakuwa Ngumu sasa. "Bado sijakupata Ndugu matonya swala la kutoroka watatu ila nimekupata kuwa kesho ndio siku ya kutoroka hapa Gerezani. Kwa nini tusitoroke wawili tu unataka kumshirikisha na Mzee Juma hujui kama hii kazi itakuwa Ngumu"Nilimuuliza Matonya ili nijue zaidi. "Sam hujui mengi kuhusu huyu mzee ila jibu ni Fupi Huyu mzee kakaa sana Gerezani huku akiwa na mbinu ya kutoroka Gerezani. Njia nyingi anajua ambayo ukipita utakutana na ulinzi sawa lakini hautakuwa Mkali kama wa njia nyingine. Ila kama unataka kujua zaidi kwa nini mimi nataka na huyu Mzee tutoke naye Tukirudi Gerezani muulizie vizuriCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/"Alinijubu Matonya. Yale Majibu ya Matonya niliyaelewa na kujua kuwa Pamoja na Mzee Kuwa anajua njia ya kutokea Kwenye Hili Gereza Kiurahisi pia lazima kuna Jambo jingine ambalo lilimfanya mzee kuwa Humu na limemshawishi Matonya kutaka kutoka naye. Maana hata Gerezani matonya alikuwa anapenda Sana kuongea na yule mzee. Ambacho nilipanga nikienda Gerezani nilitaka kuongea kwa kina na yule mzee kwa nini Mzee kama yule alikuwa anataka kutoroka Gerezani wakati alitakiwa kusubilia tu kifungo chake kiishe awe huru. Maana nilishawahi kumuuliza bado miaka mingapi imebaki kuwa huru akanijibu miwili ambae ni sawa na Mwaka Mmoja tu kwani Gerezani usiku na mchana huwa zinahesabiwa siku Mbili. Niliendelea kufanya Kazi ya Kulima ambayo tulifanya Mpaka Muda wa saa tano tulirudi kwenda kunywa uji. Baada ya kunywa Uji tulirudi tena Shambani maana haikuwa mbali sana na kuendelea kulima. Wakati nikiwa nalima nilikuwa nawaza sana mambo ambayo nitayafanya kwa haraka kama nitafanyikiwa kutoroka Gerezani. Pia muda wote nilikuwa namuomba Mungu kuwa wakati tunatoroka tufanikiwe maana kuna kuwa na hali ya hatari sana. Tulilima kwenye lile shamba hadi Muda wa saa saba ndipo tuliondoka kurudi tena Gerezani. Tulipofika Gerezani tayari Muda wa kula ulishafika hivyo tulienda kuchukua chakula. Nilipochukua mimi niliongoza hadi kwa Mzee Juma ili kwenda kumuuliza kwa nini Matonya anataka tutoroke wote. Kweli kujua njia za Gerezani tu ndio sababu ya Matonya kutaka kutoroka na Mzee Juma au kuna kitu kingine kama alivyosema matonya kuwa sijui vitu vingi kuhusu mzee Juma. Mzee Juma tulikuwa tunalala chumba kimoja na yeye ndio alikuwa mwenyeji wetu lakini kamwe sikuwahi kumuuliza kitu gani kilimfanya kuja jela zaidi nilimuulizaga anakuwa huru lini na akanijibu bado miaka miwili. Nilipofika kwa Mzee Juma nilimtania kidogo kama kawaida yangu kisha nilikaa na kuanza kula. "Mzee Najua unafahamu fika kuwa kesho tunampango wa kutoroka Gerezani na nimepewa taarifa na Matonya kuwa na wewe utakuwa Moja ya watu ambae tutatoroka gerezani. Mzee mimi nakushauri kwa nini huo mpango wa kutoroka wewe uache maana bado mwaka mmoja tu uwe huru ukitoroka na Ukakamatwa hujui kama utajiongezea adhabu bure. Pia wewe saizi ni Mzee kitu gani unakikimbilia Uraiani kwenda kukifanya mzee wangu. Maana unapotoroka Gerezani huwa kuna mambo mawili kukamatwa na kunafanikiwa ingawa asilimia kubwa wanakamatwa. Na kama unavyojua mtu akikamatwa Wakati anatoroka adhabu huwa kubwa zaidi. Mimi nakushauri mzee wangu kama hakuna Sababu kubwa ya wewe kutoroka tulia malizia kifungo chako na sisi tuonyeshe Njia tu ya kutoka hapa gerezani" Nilimwambia Mzee yule. Nilipomwambia yale maneno yule mzee kwanza Mzee aliacha kula na kuniangalia kwa jicho la Huruma sana kwa muda kama wa dakika mbili bila kuangalia sehemu nyingine. Dakika mbili zilipoisha mzee aliangalia chini kisha akaniangalia tena. Aliponiangalia tena kwa kweli nilishituka nilipomuona Mzee Akiwa anatokwa na Machozi. "Sam wewe hujui vitu vingi sana kuhusu mimi. Ila mwenzako Matonya anajua ndio maana ananishirikisha na mimi nitoroke Gerezani. Labda nikwambie kitu kimoja kazi ambayo nyinyi mnaenda kuifanya ndio hiyo hiyo mimi natakiwa kuitimiza. Sam mimi nimefungwa jela kifungo cha maisha na siyo nimebakiza miaka miwili kama nilivyokwambia wewe. Toka nimefungwa ninampango wa Kutoroka Gerezani na huu ni mwaka wa ishirini nipo humu Gerezani. Nilishajaribu kutoroka lakini askari wananikata. Huyo Matonya ambae mnataka kuroka naye alishawahi kufungwa humu na tulikuwa tunaishi chumba kimoja na siku ya kutoroka tulitoroka wote yeye alifanikiwa na mimi nilikamatwa" Aliongea Mzee Juma kisha alipeleka Mkono wake hadi usoni akafuta machozi yaliyokuwa yanamlenga kisha alipeleka mkono kwenye shingo yake akafungua cheni mmoja ambaye alikuwa amevaa. Kwenye ile cheni kulikuwa kitu kama kimkebe kidogo hivi alifungua tena nikaona picha ya mtoto hivi alikuwa ameifadhi humo. "Huyu ni Mwanangu na Ameshakufaga siku nyingi na ndio ananipa Nguvu mimi za kutoroka kwenye hili Gereza. Sam kama Najua kuna Stori ulipewa na sister Magreth kuhusu Mama yake Mwajuma Nyamilambo ambaye alikuwa anasomea Usister na baadae alipata mimba ambaye alipewa na padri Masanja. Ile mimba Mwajuma Nyamilambo aliambiwa anitaje mimi ili siri ya padri isivuje mimi nifukuzwe Shule na yeye atakuja kuolewa. Sasa mimi ndio nilifukuzwa shule siku ile na licha ya kufukuzwa shule kuna vitu ambavyo vinaniogopesha hata kukwambia"Aliongea Mzee Juma na machozi yalianza kumtoka tena.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kweli kilio cha yule Mzee kilianza kunitia Wasiwasi na kuhisi huenda yaliyomkuta na yeye yalikuwa makubwa sana. Mpaka pale alipoongea tayari nilibaini kuwa alikuwa na Mtoto tayari ameshakufa ila sikujua muhusika wa yale mambo alikuwa nani. Nilichofanya kwa Muda ule ni kuongea maneno ya Busara na Mzee Juma ya Kumsihi asilie anisimulie kile ambacho kilimtokea. "Sam kuna mambo yamenitokea Makubwa sana nataka kwenda kuyafanya hata nikifa haitakuwa mbaya. Ila kabla sijafa natakiwa nishuhudie kifo cha watu wawili ndio nife. Nataka kushuhudia kifo cha Masanja na kifo cha Mzee Jonasi. Hawa watu wawili nikiona Wamekufa hata mimi nitafurahi sana. Hawa watu ndio wamenifanya mimi kuwa kwenye hili Jela Bila hatia. Yani huwezi Amini pamoja na kutendewa unyama Mkubwa bado mimi nae nililetwa Jela. Unajua Sama Mimi nilikuwa Nasoma Upadri shule Mmoja na mama yake na magreth ambaye baadae jina lake alianza kujiita Mwajuma Nyamilambo. Nikiwa nasoma Pale chuoni mimi nilikuwa tishio kwa akili mbaya na nilikuwa mpenzi wa kila mtu pale Shuleni. Kwenye Mitihani mtu ambaye alikuwa ananisumbua alikuwa Mwajuma Nyamirambo tu ambaye alikuwa mama yake na Magreth. Siku moja nikiwa nasoma Darasani nilifuatwa na Kijana Flani na kuniambia naitwa Ofisini. Nilienda Hadi Ofisini kwenda kusikiliza naitiwa nini. Kwa kweli nilipofika Ofisini na kusikiliza kile ambacho niliambiwa nilijikuta nachanganyikiwa mbaya. Maana niliambiwa mimi nimempa mimba Mwajuma Nyamilambo. Waliendelea kusema kwa kuwa walikuwa wananipenda sana pale shuleni wanataka walimalize lile jambo kisiri wakiwa na maana hawataki kuona mimi nafungwa. Walisema kuwa mimi nikubali kuwa nimempa mimba yule mwanafunzi mwenzangu alafu niondoke pale shuleni maana bila kufanya vile walikuwa wanasema nitafungwa kifungo cha maisha. Kwa kuwa Hata yule binti Ambaye ndio Mama Yake na Magreth alikuwa amesema mimi ndio nilimpa mimba tena mbele ya Padrid mazasanja na Mzee jonasi na Sister wengine mbalimbali sikuwa na jinsi niliamua kukubaliana. Ilibidi niende hadi Bwenini kwangu nikakusanya changu na Kurudi nyumbani. Ilikuwa Kazi ngumu Sana kuwaeleza wazazi wangu nakunielewa lakini nilijitaidi kuwaambia kuwa sikufanya kitu kama kile. Huko kitaani maisha yaliendelea huku na mimi nikijitaidi kupeleleza ni nani hasa ambaye alihusika na kumpa Mwajuma nyamilambo mimba pia kwa nini yule binti alinitaja mimi wakati anajua kabsa hata salamu tu kumpa ilikuwa ni shida. Nilikaa kama Muda wa miezi miwili nilisikia wazazi wa Mwajuma wameuawa kinyama sana na baadaa ya wiki mbili tena nilipata barua kutoka kwa Mwajuma Nyamilambo ambayo ilikuwa inaniomba Msamaha kwa kile ambacho alinifanyia na kuniambia kabsa kuwa aliyesababisha kunitaja mimi ni Mchungaji masanja na ndio amempa mimba Mwajuma pia ndio amehusika na kifo cha wazazi wake na Mwajuma. Ile baruakwa kweli ilinishitua sana na sikuamini kama Padri Masanja angefanya kitu kama kile. Niliposoma ile Barua kwa kweli sikuweza kuvumilia. Nilitamani kumuulizia padri Masanja nikweli amefanya kile kitu au binti yule anataka kumchafua tu. Pia nilijua kama nitamwambia vile Masanja nakumpa kile kimeo cha barua huenda angenipa nafasi hata ya kurudi shuleni. Nilichofanya nilitafuta namba Ya padri Masanja na Kumpigia tukaongea naye. Nilipoongea naye Padri Masanja aliongea Vizuri sana na kuniambia yule binti anataka kumchafua tu. Aliendelea kusema kuwa hata wao wamegundua kuwa Mimi sijahusika kumpa mimba Mwajuma hivyo watanirudisha shuleni. Ile hali ilinifanya kufurahi sana maana niliona naenda kutimiza lengo langu. Masanja aliendelea kusema kesho atakuja nyumbani kuja kuwaomba na wazazi wangu Msamaha na anataka wote wawepo. Baada ya kuelewana Masanja nilikata simu na kuwaelezea wazazi wangu mambo yote. Wazazi wangu kwa kweli walifurahishwa na ile taarifa. Kesho yake Masanja alikuja hadi nyumbani huku akiwa na watu ambae walionekana watumishi wazuri wa mungu maana wote walivaa Majoha. Walipofika walikaa na kuongea mambo mengi na wazazi wangu. Tukiwa Mwisho mwa maongezi namanisha wakiwa wanakula ndipo CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Masanja alibadilisha kibao kwa kutoa bundi yake na kuwaambia wazazi wangu wamejua siri yake wanatakiwa kufa. Kama mchezo mchezo masanja aliwauwa wazazi wangu. Alipowauwa wazazi wangu walimteka Mdogo wangu ambaye ndio huyu kwenye haka kamkebe na wewe nimekwambia mwanangu. Nilikuwa nampenda Sana Mdogo wangu ndio maana huwa nasema ni mwanangu. Walipomteka Mdogo wangu waliniambia ili wasimuue nifanye jambo moja. Jambo ambalo nitafanya ni kuwapigia simu na kuwatarifu askari kuwa nimewauwa wazazi wangu bahati mbaya nilikuwa napambana na majambazi walituvamia. Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana mdogo wangu niliamua kukubali na kupiga simu polisi nakuwaelezea sehemu ambayo nilikuwepo na tukio ambalo nilifanya. Nilipomaliza kupiga simu Masanja aliniambia wanaondoka na mdogo wangu hadi watakaposikia nimefungwa ndio watamuacha huru. Kweli Masanja aliondoka na Mdogo wangu huku wakinihaidi kama sitafungwa lazima wamuue na Mdogo wangu. Ile hali mimi ilizidi kunichanganya kwa kweli maana hakuna mtu ambaye nilikuwa nampenda kama mdogo wangu. Nilichokifanya ni kuwasubilia Polisi wanikamate na chochote ambacho wangeniuliza ningekubali kuwa mimi nimehusika ili tu nisimpoteze mdogo wangu. Kweli polisi walifika wakanikamata na waliponiuliza nilikubali kuwa mimi ndio nimewauwa wazazi wangu nikiwa kwenye pilikishani za kupambana na Majambazi. wiki mbili mbele mimi nilihukiwa kifungo cha maisha jela kitu ambacho kiliniumiza sana maana sikutegemea kama ningehukumiwa vile. Sikuwa na jinsi nilifungwa huku nikiwa nashukuru mungu mdogo wangu atakuwa Salama. Baada ya wiki moja kupita ndio sasa nilipatwa na pigo baada ya kupata taarifa kuwa mdogo wangu naye kakutwa amekufa ndani kwa kujipiga Bunduki. Ila baadae Masanja mwenyewe alikuja kuniambia kuwa na yule alikuwa anajua siri wameamua kumuua. Sasa Sam utaniambiaje Mimi niendelee kuwepo humu Gerezani. Nasema lazima nitoroke jela na nikamle nyama kabsa Masanja"Alinielezea Mzee Juma Huku Machozi yakiwa yanamtoka.



    Kwa kweli maelezo ya Mzee Juma yaliniumiza sana na kuamini kweli anahaki ya kutoroka gerezani. Stori ambayo nilipewa na Magreth kuwa mama yake alimtajaga mtu mwingine kuwa amempa mimba kumbe Muhusika alikuwa ni Mzee Juma. Pia nilishindwa kuelewa Masanja alikuwa mtu wa Namna Gani maana alionekana kachukua roho za watu wengi sana Duniani. "Hiki ndio kinanifanya nitoroke kesho Gerezani sam. Nilishawahi kutoroka na Huyu huyu Matonya lakini nikakamatwa na nilipata adhabu kali sana ila kesho tena natoroka wala siogopi kufa. Maana bora nife kuliko kuendelea kumuona adui yangu yupo. Unajua Sam baada ya Mdogo wangu kuuawa nilitokea hadi kubadilisha Jina na dini kutoka Yohana hadi nilianza kujiita Mzee Juma. "Aliongea Tena Mzee Juma. Kwa maelezo ambayo alitoa Mzee Juma sikuwa kabsa na neno la kuongezea zaidi nilimwambia ajiandae tu ili kesho tuchomoke. Siku hiyo tulijiandaa sana kwa safari na Jioni ilipofika Matonya alikutana na yule Afande kisha alipewa Bunduki ambaye ingetusaidia kutoroka Gerezani na kibegi kidogo kukabiliana na askari yeyote ambaye angeshitukia Dili. kesho yake saa mbili tayari mpango wa kutoroka Gerezan ulishakamilika na tulipanga Kutoroka asubuh kabsa Muda wa saa nne. Tulisubilia tu muda wa uji ambae ilikuwa saa nne ifike wakati wafungwa wanakunywa uji sisi tungekuwa tuna escape kutoka Gerezani. Saa nne ambayo tulikuwa tunaisubilia ilifika na wafungwa waliatoka kwenda kunywa uji. Wafungwa walipoenda kunywa Uji huku na sisi tulijipanga Safari ya kutoroka ilianza. Haikuwa kazi Rais kuweza kutoroka Gerezani ila kwa milango ambayo tulikuwa tunapitia kutokana na Ramani ambayo Mzee Juma alikuwa ameisomea kitambo tulifanikiwa kwa kiasi kikubwa. Baadhi ya milango tulikutana na mlinzi mmoja na wao tulimshambulia kwa kumzimisha kisha tunapita. Dakika kama tano hivi Tayari tulikuwa nje ya Gereza. Tulipotoka nje ya Gereza matonya alifungua Begi yake ndogo ambayo alikuwa naye tangia jana na alipewa na yule afande. Alipofungua alitoa nguo akatugawia nakubadilisha. Tulipo vua Nguo za wafungwa sasa tulionekana tupo huru kabsa. Tulitembea kwa kasi sana kutoka maeneo ya Gerezani huku tukipita sehemu ambazo hazikuwa na watu wengi. Tulipohakikisha sasa tupo mbali na Gerezani tulimtafuta mtu ambaye alitusaidia simu kisha nilimpigia Klinita maana namba yake ilikuwa kichwani. Klinita alipopokea simu nakumwambia kuwa mimi ni Sam nataka aje sehemu flani kunichukua alifurahi sana. Baada ya robo saa klinita alishafika sehemu ambayo tulikuwepo na kuja kutuchukua. Alipotuchukua nilimpa maelekezo kabsa kuwa tunatakiwa kwenda kujificha kwao muda wa siku kazaa kabla ya sisi kuondoka kuelekea Brazil kwenda kujipanga kwa ajili ya kuja kupambana na Masanja. Nilipomwambia vile Klinita wala hakubisha zaidi alifurahia. Tulienda hadi kwenye Nyumba ya adui yetu kisha tuliingia hadi ndani. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nje tulikutana na walinzi ila hakuna hata mmoja ambae alitushitukia maana ile nyumba ilikuwa ni kubwa na watu walikuwa wanaingia mara kw mara. Tulipoingia ndani Klinita alitupeleka hadi chumbani kwake ambako alikuwa analala na huko ndiko tulikuwa tunatakiwa kupumzika kwa siku kazaa kusoma upepo then tunaondoka. Tulikaa mle hadi muda wa saa saba ndio taarifa ya Wafungwa watatu kutoroka Gerezani ilitangazwa kwenye taarifa ya habari ikiambatana na picha zetu. Tena serikali ilihaidi donge Nono kwa wale ambao wangefanikisha sisi kukamatwa . "Nilijua kitu kama hiki kitatokea ndio maana niliwaambia tuje tupumzike kwanza huku. Waache wahangaike kwa siku kama kumi hivi hali ikiwa shwali sisi tutatoroka bila shida"Aliongea Matonya na sisi tulimuunga mkono. Tulikaa pale ndani chumbani kwa Magreth kama muda wa saa tano hivi tukipiga Stori na Magreth mara ghafla mlango ulianza kugongwa. Kwa haraka magreth alituingiza chooni maama chumba chake kilikuwa na Self cointener. Tulipoingia chooni magreth alienda kumfungulia yule mtu aliyekuwa anagonga mlango. "Mwanangu na wewe punguza kulala wewe muda wote wa kulala tu. Hivi umesikia taarifa kama sam na yule mzungu wametoroka Gerezani. Tena wametoroka wakiwa na mzee Flani. Sasa mwanangu tuwe makini maana hawa wataka kulipiza kisasi cha Magreth hivyo kuwa makini"Yalikuwa ni maneno ya Masanja ambaye alikuwa anaongea na mwanae magreth bila kujua wale watu waliotoroka walikuwa ndani kwake tena chumba kile kile ambacho alikuwa yupo. "Naenda kumuua sasa hivi huyu Mwanaharamu kamwe siwezi kumchelewesha. Huu ndio Muda wa kuondoka na hii Roho ya Mwanaharamu hakuna muda wa kusubilia mara kwenda Brazil. Naitaji kumuua ili hata mimi nikifa haina shida ila siwezi kuvumilia kumuacha huyu Mbwa"Yalikuwa ni Maneno ambayo aliongea Mzee Juma kwa hasira tena kwa sauti bila hata kuogopa. Wakati tukiwa tunashangaa kitu Gani kile alikuwa anakifanya mwenzetu tayari alishafungua Mlango wa choo kwa kasi na kwenda hadi chumbani. Ilibidi tu na sisi tutoke kwa haraka maana tulijua yule Mzee hawezi kupambana na Masanja. Tulipotoka Chooni tayari Mzee juma walishazoana na Masanja na wote walianguka hadi chini. Magreth muda ule naye hakujua afanye nini alikuwa anashangaa tu. Kwa kasi ya ajabu nilikimbia kwenda pale ambao walikuwa wameanguka masanja na mzee Juma ili nataka kumsadia mzee Juma nilisikia mlio wa Paa hali iliyonifanya nisite. Wakati natafakali kitu gani kimetokea masanja aliibuka kwa kasi ya ajabu kwa kumtupa mzee Juma pembeni kisha aliniweka chini ya ulinzi. "Hamuwezi kuniua kirahisi hivyo kama nyinyi mnavyohisi. Mimi kufa bado sana hivyo njia ambayo walipitia wenzenu ndio na nyinyi mnaifata. Haya Sam Msalimie Mwanangu Magreth mwambie na wewe nimekuwahi nimekuua kabla hata hujalipiza kisasi: "Aliongea Masanja lakini hata kabla hajamalizia kuongea Maneno yake nilishangaa kikombe ambacho kilikuwa na maji kikitua usoni mwake. Nilipoona kikombe cha maji kimetua usoni mwake nilimuwahi nakwenda kumzoa kisha wote tulianguka chini. Matonya naye aliwahi na kuja kumpiga teke la mkononi masanja hadi aliachia bastora yake na huo ndio ulikuwa masaada wangu. Kumbe wakati mimi natoka chooni kumsaidia mzee Juma matonya alibaki na huo ndio ukawa msaada wangu. Kwa haraka tulimshika vizuri masanja kisha tulimuagiza klinita kamba na kujakumfunga kisha tulimziba mdomo kwa kusokomeza tambala mdomoni na kwenda kumuweka bafuni. "Masanja hadi hapa ninao muda wa kukua ila siwezi kukuua kabsa kwa sasa maana hutakiwi kufa kwa hara. Nikikuua Ghafla kwa kweli sitakuwa nimekufanyia kitu kizuri nakuacha uendelee kuishi ngoja nikajifunze Ugaidi kwanza nitarudi"Aliongea Matonya kisha alifunga mlango wa chooni tukarudi hadi kwa mzee juma ambaye alikuwa amepigwa risasi na kumbeba ili kumkimbiza Hospitalini kwenda kutibiwa.



    Tulimbeba mzee juma huku damu zikiwa zinamtoka lengo ilikuwa kumpeleka hospitalini kwenda kuokoa maisha yake. Kwa Jinsi ambavyo nilikuwa nimechanganyikiwa nilishasahau kuwa tulitoroka Gerezani na tulikuwa tunatafutwa. "Klinita tukitoka hivi huku tukiwa tumembeba Mzee Juma lazima kutakuwa na Maswali Mengi kwa walinzi wenu. Pia hizi Sura walinzi wanaweza kuzishitukia. Ambacho nakuomba kawatoe Walinzi kijanja kisha sisi tuje kumpakia Mzee Juma kwenye Gari tumkimbize Hospitalini"Aliongea Matonya wazo ambalo hata mimi niliona bora zaidi. "Sawa mimi nitafanya Hivyo ila hata hivyo Hospitalini niachieni mimi nimpeleke huyu Mzee Juma maana kumbukeni nyinyi mnatafutwa. Hivyo Bora akamatwe Mzee Juma nyinyi mbaki mtajua Namna ya kuweza kukabiliana na kumsaidia kuliko wote tena kukamatwa"Aliongea Klinita Maneno ambayo yalinikumbusha Mimi kuwa tulikuwa tumetoroka Gerezani. "Hapana Klinita tukianza kukushirikisha wewe kwenye vitu kama hivi tutakuwa tunakutengenezea kifo kwa baba yako. Hata hapa unatakiwa kurudi kwa baba yako ukajifanye kama tulikuteka ili asigundue kama tunashirikiana na wewe. Ukifanya Msaada kama wewe unavyotaka na sisi tunampango wa kuondoka hapa Tanzania unafikili nani atakusadia zaidi ya baba yako kukuona Msaliti na Kukuua"Aliongea tena Matonya. Alipoongea yale maneno matonya hapakuwa naCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Mjadala tena maana lengo ilikuwa kuokoa maisha ya Mzee juma. Alichofanya klinita ni kutangulia nje kwa lengo la kwenda kuwarubuni walinzi ili tumtoe mzee Juma na kwenda kumpakia kwenye Gari kumpeleka hospitalini kwenda kumsaidia. Klinita alipotoka nje kuna kitu kilinijia kwenye fikra zangu. Niliwaza na kubaini sipaswi kumwacha masanja hivi hivi bila kumuwekea hata alama ya kumbukumbu. Kwa kupambana na mtu hatari kama Masanja ilikuwa kuhatarisha maisha yetu maana wengi walikuwa wanapambana na masanja wamekufa na wameacha kazi kwa wengine wamalizie. Hata mimi nilihisi huenda nikafa bila kufanikisha kile ambacho nilikuwa nataka. Kitu ambacho kilinijia akilini kwa muda ule ni kwenda kuondoka na kiungo kimoja cha masanja kumuonyesha kama mimi nilikuwa na hasira na yeye kuliko mtu yeyote duniani. Nilichofanya nilimwambia Matonya anisubilie kuna kitu muhimu sana nimesahau chumbani ambapo tulikuwepo. Sikutaka kabisa kumwambia kuwa naenda kuondoka na kiungo cha masanja hata kidogo. Nilipomwambia Vile matonya aliniruhusu na kuniambia nifanye haraka. Kwa kasi ya ajabu nilirudi mbio hadi chumbani kwa Klinita ambako kule ndio masanja alikuwepo. "Yani nyie wanaharamu wajinga kweli. Hivi ni kweli mmepata bahati ya kuniua mmeniacha mnajifanya wataalamu. Kumbuka wengi wamekufa kwa kujifanya wanataka kulipiza kisasi kitaalamu. Tena wewe mjinga yukwapi mama yako na baba yako. Yukwapi sister yako magretha ambaye alikuwa na hasira na mimi kuliko hata wewe. Tena mama yako nimemuua kinyama hadi sasa nimetenganisha kichwa chake na mwili wake. Sasa huko kaburni kama wanaenda mbinguni mama yako atakuwa kichekesho na kituko kikubwa kwani ataenda bila kichwa" Yalikuwa ni maneno ya Masanja ambaye alikuwa anaongea kwa kashifa sana huku akiwa anacheka. Yale Maneno ya masanja yalinipa hasira hadi machozi yalianza kunitoka. Niliona ambacho anakiongea huyu mjinga ni ukweli mtupu hatukupaswa kumsamehe kwa muda ule. Masanja hata alipoongea yale maneno mimi sikusema kitu chochote. Nilienda hadi kwenye meza na kutafuta haraka kitu sahihi cha kuondoka na kiungo cha Masanja hapo ndipo angeona kuwa nina hasira mbaya. Kwenye ile meza nilipata kiwembe na kuchukua kisha nilimsogelea Masanja. Nilipomfikia nilikata sikio lake bila huruma hali iliyomfanya masanja kulia kwa sauti ya juu. "Hasira ambazo ninazo siku ya kuja kukuua nitatoa kiungo kimoja kimoja. Leo nimeanza na hili sikio kama kumbukumbu yangu kwako. Masanja mimi ninahasira hadi nashindwa kuelezea ili kukuonyesha kama wewe hupaswi kuzikwa kaburini mwili wako unatakiwa kutafunwa kama nyama na kupitishiwa na maji kisha nikutolee mkunduni kama mavi naanza na hili sikio"Nilimwambia Masanja maneno machache kisha kiujasiri kabsa sikujua huo ujasiri nimeutoa wapi nilipeleka sikio la matonya mdomoni na kuanza kulitafuna. Kiukweli hiyo Siku hata mimi sikujua Nilikuwa nimefanya nini ila nilijua kufanya vile hasira zingepungua na ningemuonyesha Masanja kuwa hata mimi nilikuwa na hasira mbaya. Nilipopeleka sikio la masanja mdomoni nilitafuna mbele yake na Kulimeza huku machozi yakiwa yananitoka kwa hasira hali iliyomfanya masanja kubaki akiwa anashangaa. Nilipomeza ile sikio sikuongea kitu chochote nilienda bafuni nikaosha damu damu ili matonya asishituke na kutoka. Nilipotoka tulimbeba Mzee Juma na kwenda kumpakia kwenye Gari na Safari ya kuelekea hospitalini ilianza. Kutoka kwa Masanja hadi hosiptalini ya Wilaya kitete ilikuwa kuna umbali sana. Tukiwa Njiani Mzee Juma alifumbua Macho yake na kuonyesha hali iliyonifanya kufarijika kidogo na kuhisi kifo kwa mzee juma kilikuwa bado. "Sam kunipeleke mimi Hospitalini ni sawa na kunirudisha Gerezani tu kitu ambacho sipendi kitokee. Tena hamnirudishi mimi tu Gerezani bara hata nyie Mnaweza kurudishwa Gerezani. Ninachowaomba Niacheni mimi nife na nyinyi katafuteni maisha nchi nyingine hapa tanzania mtaishia jela tu. Ila kabla ya Kufa mimi nataka nione Masanja akifa kwanza tena nataka mnichomee Nyama ya Masanja nile ninywe na Maji ndio nife. Watu wengi sana walitaka kuona Masanja anakufa lakini wao ndio wanatangulizwa kwangu mimi sitaki itokee hivyo. Ndugu zangu nikifa mimi Kabla Masanja ajafa mimi nitaenda kumueleza nini mdogo wangu na wazazi wangu kule Kaburini. Tafadhalini sana Masanja siyo mtu wa kupewa Msamaha pindi unapopata nafasi ya kumuua. Ukimsamehe Masanja uje wewe utakufa na kumuacha. Tafadhalini Msinipeleke Hospitalini kamchukueni Masanja nije nilipe kisasi kisha mnichomee nyama yake nile ili nife nikiwa na amani. Masanja hata mkisema muende kisheria hamtamuweza hukumu yake ni kuliwa nyama tu. Au wewe Sam nambia unataka mimi nife bila kulipiza kisas. Hata Rafiki yenu Klinita kule mlikomuacha kama Masanja atafunguliwa kamba lazima atauawa maana ni msaliti aliwaingiza kwenye chumba chake na yeye ndio alileta kamba mkamfunga masanja"Aliongea Mzee Juma Maneno ambayo yalikuwa na ukweli mtu. Matonya naye alimuelewa mzee juma na kukubaliana na kile ambacho alikuwa anakitaka. Tulichofanya tuligeuza Gari letu kwa kasi ya ajabu na kurudi tena nyumbani kwa Masanja kwenda Kumaliza kazi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******************************************** Muda ule tulipanga kwenda kumalizana na Masanja kabisa na tulikuwa tunaomba Mungu Klinita awe bado hajamfungua baba yake. Muda ule ningekuwa na simu ningempigia klinita kumjulisha asimfungue masanja ila hatukuwa na Simu. Kusimama na kutafuta simu ndio tungejichelewesha zaidi. "Nashangaa mlikuwa mnataka kunipeleka Hospitalini kwanza mngeambiwa mtafute kibari kutoka polisi cha mimi kutibiwa sijui mgenikitoa wapi. Matonya ongeza Mwenda bhana kabla sijafa nile nyama ya masanja maana nahisi kifua changu kinawaka moto sijui nakaribiakufa"Aliongea Mzee Juma huku akiwa anatabasamu hali iliyonifanya kubaini kuwa mzee Juma alikuwa anapenda sana kumuona Masanja akifa. Matonya alicheza na usukani vilivyo hata dakika tano hazikwisha tayari tulishafika kwa Masanja Gheti lilifunguliwa na tuliingiza Gari hadi ndani. Yulipofika pale tulishuka na kumuacha mzee Juma kwenye Gari. Mlinzi mmoja ambaye alikuwepo pale alitukaribisha ndani sijui yeye alikuwa bado hajausoma mchezo. Kupitia Bastora moja ambaye Matonya alikuwa nayo ambaye alipewa kituoni alijiweka vizuri na kuanza kuusogelea mlango wa chumba cha Klinita. Tulipofika Mlangoni nilishitulia na Mlio wa Risasi kutoka kwenye kile chumba ingawa mlio haukusikika sana Kutokana na kile chumba kuwa gymsang bord. Ule mlio wa Risasi kwa kweli ulinilegeza na Muhusika pale Nilijua lazima alikuwa ni Klinita huenda alimfungua baba yake. Mlio wa Risasi ulitufanya kujiandaa vizuri na kusimama pembeni ya mlango ili akitoka tu analo. Ni kweli baada ya dakika moja tangu mlio usikike mlango wa chumba ulifunguliwa na Masanja alitoka. Alipotoka tu matonya alimuweka chini ya ulinzi. "Tumebadilisha Ratiba bana tumeona bora tuje kuchukua roho yako mapema maana tumeona utamaliza watu wengi. Pia Mzee juma anahamu na Nyama yako ale kabla ya kufa ili akawasimulie wazazi wake"Yalikuwa maneno machache sana aliyongea Matonya. Alipoongea vile matonya masanja alitaka kutoa bastora kiunoni kwa ajili ya kujitetea lakini Mzungu alikuwa mwepesi alimtwanga mtama ambao ulimpeleka hadi chini. Matonya hakutaka kufyatua risasi maana angewashitua walinzi ambao wengi wanakuwa ndani ya vyumba ya ile nyumba. Nilipoona Matonya amemuweza masanja mimi nilikimbia hadi ndani ya kile chumba kwenda kuangalia nani yule alikuwa amepigwa risasi. Nilipoingia kwenye kile chumba nilibaki nikiwa nimedua kwa kile ambacho nilikiona. Kwa kweli sikuamini macho yangu kama Masanja alikuwa amemuua Klinita. "Nenda salama mpenzi wangu Klinita hakika hatujafikia kile ambacho tulikuwa tunakipanga. Pia Asante kwa Kuhatarisha maisha yako ili kunitetea mimi nakupenda kuliko maelezo na Pumzika mahali pema na mimi nakuja"Niliongea Maneno machache sana kwa klinita na kutoka chumbani. Sikutaka kufikilia sana maana kwa jinsi ambavyo nilikuwa nampenda klinita ningeshindwa kufanya kazi. Nilipotoka chumbani nilimwambia Matonya kuwa klinita kafa. Tulimchukua Masanja huku akiwa chini ya ulinzi. Mlinzi naye ilibidi tumuweke chini ya ulinzi ili kuchelewesha taarifa kufika polisi. Tulienda tukawapakia hadi kwenye Gari na safari ya kuelekea Porini ambako tungeenda kula nyama ya Masanja ilianza. Tulikimbiza Gari kama muda wa Nusu saa tayari tulishaingia porini. Tulipolianza tu pori tulisimamisha gari tukamshusha yule Mlinzi na kumueleza kuwa masanja ndio amemuua mwanae na kumwambia kuwa atoe taarifa polisi kuwa wafungwa wale ndio wanaenda kumla nyama masanja kutokana unyama wa kuwauwa watu mbalimbali na kesi wakatupiwa wale wafungwa ambao sisi. Baada ya kumpa yale maelezo tuliendelea na safari. Tulitembea tena kama dakika tano ndani ya pori gari tulienda kusimamisha tukamshusha masanja na mzee juma na kuingia naye porini. Huko porini tulimfikisha masanja tukamfunga Kamba kisha tulikata Paja lake na kumchomea Haraka Mzee Juma ili ale kwani Hali yake ilikuwa mbaya. Tulikuwa tunapeleka vitu haraka ili kuwahi Mzee Juma aone wakati tunamuua masanja kama yeye alivyosema. Nyama ya masanja tuliichoma kisha tukakata vipande vidogo vidogo tukampa mzee juma na kuanza kula kwa shida maana hali yake ilikuwa mbaya sana. Wakati mzee Juma akiwa anakula nyama Huku Masanja alikuwa analia kwa uchungu kuomba msamaha kitu ambacho kilikuwa kinaniboa sana. Mzee juma alikula kama finyango tano ya nyama ya masanja huku akitabasamu kisha tulimpa maji akanywa. Alipokunywa maji tulimfungua masanja kamba na kumsogeza karibu na Mzee Juma kisha tulimpa mzee juma kisu ili alipe kisasi. Ingawa mzee Juma alikuwa amepigwa Risasi kwenye mbavu lakini alijikaza kwa nguvu zote huku machozi yakimtoka na kukipeleka kisu kwenye kifua cha Masanja. Alipopeleka kile kisu mzee juma alicheka sana hali ilimyomfanya hadi kuanguka chini na kutulia kimya. Nilipoenda kumgeuza nilikuta tayari kafa huku akiwa anacheka. Ile hali ilinisikitisha sana ila sikuwa na jinsi . CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Sisi kisasi kwa masanja tulikifanya haraka kwa kumuwekea miti akiwa vile vile bado anahema na kisu kikiwa kifuani na kuchoma moto. Baada ya kuchoma moto tulimuacha na mzee Juma pale huku tukiwa tumeandika ujumbe wa maelezo yote ya Unyama aliyofanya masanja hadi kufikia kumpa adhabu ile na kuondoka. Tulitembea Mguuu kwa mguu tena Hadi kwenye kijiji kimoja ambacho hata jina sikijui. Tulipofika kwenye kile kijiji tulinunua ijabu za kike na kuvaa lengo tusafiri kama wanawake hadi namanga Arusha huko tungevuka Mpaka wa Tanzania na kuingia kenya na kwenda kutafuta Usafiri wa kwenda brazil maana Tanzania tulikuwa tunatafutwa. Mungu siyo Athumani tulisafiri salama hadi sasa hivi Tupo Brazil naendelea na Maisha mazuri ninawatoto wawili na nimeoa binti wa kibrazil. Watoto wangu wote wakike wakwanza nimemuita klinita na wapili Magreth. One day nitarudi Tanzania tayari mmenisahau.



    ****************MWISHOOO******************

0 comments:

Post a Comment

Blog