IMEANDIKWA NA : MOONBOY
*********************************************************************************
Chombezo : Mwigizaji Balaya
Sehemu Ya Kwanza (1)
Sasa siku hio ilikua ni siku ya kikao cha usiku, baina ya watu wote.. Yaani familia nzima na alioitisha mkutano huo ni dada batuli kana kwamba ndio anataka kuliongelea lile swala la mimi kwenda Dar es Salaam...
Na mimi nilikuepo kwa pembeni nimewategea tu skio langu,...
"ndugu wazazi wangu wapendwa... Leo nimewaita hapa nina ombi moja kwenu japo sio la muhimu sana jwenu.... Aahhh kama mnavyojua kazi zangu mimi ni uigizaji, na katika tasnia yetu hua hatuweki mtu ilimladi mtu bali tunaangalia kipaji cha mtu ili aweze kukava ile nafasi husika, na nimeona kuna nafasi sheby anaiweza...."
Kila mmoja alianza kutoa macho huku mzee mwenyewe akiuliza, kua
"Uu..u..uu...unasemaje we mtoto"
"baba na ndugu zangu wote... Nataka niondoke na sheby, tukaishi Dar es Salaam ili akijue kipaji chake... "CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara mzee akaamka kwa hasira huku akisema,...
"wewe yobi wewe... Ishia hapo hapo na huko kuigiza kwako, inamaana Tanzania yooote hii umemuona sheby tu kua anaweza kukava huo ujinga wenu,... Sasa sikia ukitaka nikuachie laana ondoka na huyo kijana.. Pumbavu wewe... Nyiiiiaaaau we"
Afu mzee akaondoka zake kuelekea chumbani.... Mara na Asnati na akasema
"yaani dada yobi katka siku ulizo ongea pumba ni leo, yaani kama na mimi nina uwezo wa kukupa laana ningekupa wewe"
Hajakaa vizuri mara na sauna nae... Kaamka huku akisema
"hata mimi nimekuchukia ghafla tu dada angu, na ukitaka tuelewane muache sheby wetu"
Akiendelea kushangaa shangaa, mara na mama nae kaamka na kusema
"Huo upumbavu wako huo, upeleke huko huko dar kwenu, lakini sio sheby, wewe ni mtoto wangu lakini kwa swala hili nitakuchukia milele"
Mama aliondoka zake na kumfata mumewe huko chumbani kwao... Sasa tukabaki wenyewe, huku dada yobi akibubujikwa na machozi,... Alikua akijiuliza mengi sana lakini hakupata jibu..
"iv sheby, umeipa nini familia yangu... Nijibu umewapa nini hawa watu"
"mi sijui dada yobi"
"sheby, niambie ukweli, una mahusiano ya kimapenzi na familia yangu.. Hii sio bure kama sio mahusiano basi kuna kitu umewapa....... Sheby, umetembea na familia yangu... Si kweli ee??"
"sasa kama nimefanya mapenzi na familia... Kwaio una maanisha hadi baba yako si ndio eeee"
"Ehh basi nisamee mpenzi wangu, huko umefika mbali sana... Basi nisamee kwa maswali yangu... Ila hebu nishauri tufanyeje sasa, mana licha ya wao kukataa lakini sintokuacha hata mara moja"
"we yobnesh? Umesahau baba ako kasemaje"
"hata kama lakini sikuachi sheby wangu"
"kumbuka laana ni mbaya dada yobi"
"sawa nipo tayari kuipata... Lakini wacha niwe na maisha yangu yote.... Hebu nipe njia tufanyeje ili tuondoke... "
Nilipata wazo moja nikaona ngoja nimshauri kama atakubali
"ok... Nina wazo ila utakubaliana naloooo"
"nipo tayari hata kama linagharimu pesa kiasi gani"
"wala haliitaji hata senti tano"
"ok skia sasa.........
SASA TUENDELEE NA MWENDELEZO WAKE.... KWANI HUO ULIKUA NI MWISHO WA STORY ILIOPITA.. NIMEIWEKA NDEFU ILI ALIEANZA HAPO AIELEWE VYAMA....... SASA TWENDE KAZI
ENDELEA...........
nilitamani hata mimi niende dar es Salaam mana sijawahi kufika kabla... Hivyo hata wazo amblo ningelimpa lilikua zuri ila sijui kama angekubaliana nalo...
Wakati huo dada yobi alikua akilia sana kwa kuishangaa familia yake ikimkana kisa mimi tu, na kujiuliza maswali mengi ambayo hata majibu yake hana,... Ila kwa utamu wa dada yobi ilinifanya nami nikubali kwenda nae, tena nitaishi nae nyumba moja.. Yaani nitakua najisevia tu mwenyewe......
Nilipata wazo moja nikaona ngoja nimshauri kama atakubali
"ok... Nina wazo ila utakubaliana naloooo"
"nipo tayari hata kama linagharimu pesa kiasi gani"
"wala haliitaji hata senti tano"
"ok skia sasa.... Itabidi we uwaombe msamaha woote, afu uwaambia sawa umekubali kuniacha"
"What?.... Wazo gani sasa ilo"
"ndio... Na usiponifata mimi utalaanika kisa mapenzi".
"ok sawa... Sasa baada ya kuwaomba msamaha"
"ukishawaomba msamaha kula mtu akaridhika tena uwaambie kabisa nilikua nawapima tu imani... Alafu sasa wewe unaondoka zako na kuniacha mimi"
"Sitaki na sitaki"
"Ehh"
"hakuna cha Ehn sheby lazima tuondoke"
"sikiliza sasa..... Ukishaondoka, mimi huku naanza vibweka bweka vya hapa na pale ili nifukuzwe kazi afu wakinifukuza tu... Moja kwa moja breki nyumbani kwako Dar es Salaam"
"mmmhhh kwa upendo huu kuna kufukuzwa kweli? ..... Mi sijui"
"kua na imani litawezekana... We ulifikili nitapataje kakitu kaliko vimba kama hako"
"ahahahahaha.. Jinga wewe unamuambia dada ako ivo wewe"
Kiukweli dada yobi alidata na mimi yaani alikufa akafia kabisa na sijui ni kwanini... Basi tuliondoka sebuleni hapo yeye akaenda chumbani kwake na mimi nikaenda chumbani kwangu....
Kesho ndio siku dada yobi anaondoka zake kuelekea dar es Salaam, Hata mimi nilikua na shauku sana ya kwenda huko na natamani sana kwenda....
Leo ni siku nyingine tena ambayo ni Alhamisi, nililauka mapema sana na kuwapeleka akina asnati shuleni,..
"iv sheby, umedanganywa vipi na dada yobi uende dar?"
"Enhee hata mi namshangaa sana, yaani raha tunazokupa lakini bado huliziki sheby"
Walikua wakiniuliza kwa wote kua iv ni kweli naelekea huko, lakini mimi sikuwajibu kitu, nilikua bize na gari huku nikimuwaza dada yobi ambae ni dada yao na hawa akina asnati,
"we sheby si nakuuliza lakini mbona ivyo wewe"
Alikua ni Asnati ndio alioendelea kunisemesha,
"kwani nimeenda, mi nimekataa"
Niliwajibu hivyo huku nikiendelea kuendesha gari,..
Sauna aliposikia nimekataa alifurahi sana bila kujua kukataa huko ni kwasababu ya kuwaridhisha kwa siku mbili tatu hizi,..... Basi siku zilisonga na hatmae ule mwezi wangu wa kulipwa ulikaribia, na hapo ndipo nilipanza vituko ndani ya nyumba, yapata wiki moja sasa toka dada yobi aondoke,
"kijana wangu mbona siku hizi umebadirika kiasi hiki, yaani toka yobi aondoke umekua mtu wa tofauti sana, kwanini lakini kijana wangu"
Hayo yalikua ni malalamiko ya mzee huyo na yeye hataki niondoke maana kuna baadhi ya mirathi anataka kunirisisha, na hata katika moja ya mikataba yake ameisaini jina langu,..
"nipeni mshahara wangu, kila siku mi nagombana na mke wangu niache hii kazi lakini navumilia tu"
Ilikua ni mida ya usiku saa moja moja hivi, tukiwa sebuleni tukipata chakula, nilikua nimewaka mbaya yani nilikua staki utani hata kidogo,
Mara ghafla kwa bahati nzuri mke wangu kapiga simu muda huo huo, nami nikaiweka laudi spika ili na wao wasikie..
"haloo mke wangu habari yako mama"
"staki salamu yako, toka juzi unaniambia unaacha huo ujinga wako mbona mpaka leo hurudi... Mi nitaondoka naondoka"
"sikiliza basi mke wangu"
"sitaki endelea na hilo jim... "
Nilikata simu mana alikua anataka kusema endelea na hilo jimama lako, hivyo niliwahi kukata simu, mzee mwenyewe alikua kimya mama kashika shavu tu kwa mawazo mengi...
"ok, kijana naomba tuelekee nyumbani kwako ili tukaliweke sawa jambo hili, lakini sitaki uache kazi"
"mzeee suruhisho la kuokoa ndoa yangu ni kurudi kwangu tu, mana mke wangu kuna baadhi ya vitu kavigundua juu yangu hivyo hawezi kumuelewa mtu kabisa"
"nadhani mimi atanielewa hebu twende"
"mzee.... Naomba kuacha kazi"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliongea hivyo kisha nikawa naondoka kuelekea chumbani kwangu,
"mama yobi, mbona huongei upo kimya hivyo? Ataondoka huyu, utakesha kuleta vijana kila siku"
"muache aondoke tu"
Mama alikua hana mfupa wa kuongea sana kwasababu akiongea sana mzee anaweza kujua kua huenda kuna jambo lingine tofauti na kufanya kazi, na ni kweli jambo lipo na ndio lilionileta huku...
Siku kadhaa zilizopita na hatmae leo ndio siku ambayo nilikua nakabidhi ufunguo wao wa gari, ili niondoke kama nilivyokuja,
"yaani kijana wangu kweli unaondoka? Sawa sina jinsi mana siwezi kukulazimisha urithi usioutaka"
Sasa kumbe hili jambo la mzee kunirisisha mali zake mama halijui, sasa hapo ndio maskio yanamfunguka
"una maanisha nini baba yobi"
"ndio,... Mali zangu zote nilikua nampatia huyu kijana mana sina mtoto wa kiume"
"haaaaaa baba yobiiii jamani, wewe huna ndugu wewe"
"ninao"
"huna watoto wewe"
"ninao, ila ni wakike hawa wakiolewa na mali zote zimeolewa"
"haijalishi.... Kwahio kumbe kumbembeleza kote huko kumbe wataka umrisishe mali za wanangu.... Eeee baba sheby we nenda tu"
Mama sasa ndio akaamua kumalizia kunitimua kwa maneno baada ya kujua kua kumbe mumewe alikua anataka kuikosesha haki familia yake,
"sheby... Neeenda baba nimekuruhusu nenda"
Nilitika nikiwa naburuza zangu begi huku nikiwa nimelivaa lingine mgongoni, nilikua naelekea taarabu bila hata ya kuangalia nyuma, mana hata sipataki tena, Nilikua natembe huku nikiwaza nirudi kwa mke wangu au niende dar? Niliwaza lakini sikupata jibu sahihi... Sasa ile nakunja kona flani hivi, mara niliguswa bega, kugeuka kumbe alikua ni Sauna na dada yake nae ndio alikua anakuja ila alikua mbali kidogo...
"sheby, kweli unaondoka na kutuacha tukiwa wanyonge, lakini sitaki kukuficha kitu juu yangu... Umetembea na dada Asnati na mimi"
Nilimkatisha maongezi yake na kumwambia kua aongee Pointi mana nachelewa...
"sheby... Ukweli ni kwamba, nina mimba yako"
"Uuu.. Uuu.. U. ..... U.. Uuuu.... Uuuu... Una. Unasemaje Sauna"
"ndio, nina ujauzito wako"
Sasa huku nikiendelea kuumiza kichwa ili nijue ninafanyeje, mara ghafla Asnati kafika na kuanza kutapika mbele yangu namuona,..... Pale pale nae nikamuuliza shauku ya kujua ana nini, mana asije akaniambia na yeye ana mimba...
"Asnati?... Unaumwa na Maralia, Au ni Kaswende tu?... Sema basi unaumwa kaswende si ndio eee"
Nilikua natamani aseme hata kama anaumwa H.I.V kuliko aseme ana mimba,
"Bora ningeumwa hio kaswende au maralia kuliko ugonjwa nilionao"
"ugonjwa gani huo? Au ni gonorea"
"mbona unataja migonjwa yako tu siielewi,....Nina mimba yako"
"Tooobaaaa Yarabi Roho yangu mie, nitauweka wapi huu mwili"
Mwili wangu ulikosa nguvu juu ya jambo hilo ambalo akina Asnati wananiambia, Yaani nilihisi ni uongo lakini huenda ikawa kweli mana kati yao hakuna nilietumia nae kinga, hivyo niliamini moja kwa moja ni kweli kua wote walikua waja wazito, tena bora ingelikua kwa wanaume tofauti ingelikua afadhali kidogo lakini mwanaume ni mimi peke yangu ndio nimehusika na swala hili, Kiukweli nilihisi nimeishiwa damu vile lakini kwakua nilikua ni mtoto wa kiume hivyo nilijikaza haswa na kuzungumza nao,....... Tuliingia katika cafe moja hivi au restaurant kwa jina la kawaida.....
"Asnati na Sauna, please please please jamani, naombeni mnisaidie kwa hili"
Muda huo tupo ndani ya ki restaurant hio iitwayo MWANGA RESTAURANT haipo mbali sana na nyumbani,
"tukusaidi?... Tukusaidie kwa lipi?... Sisi ndio tunahitaji kauli kutoka kwako"
"Asnati na Sauna... Naombeni muzitoe hizo mimba zenu"
Wote waliangaliana na kusema kwa pamoja huku wakishangaa kwa wazo langu
"What???"
"yes, hakina jinsi... Bila hivyo mtanipoteza katika hii dunia, na kama mnahitaji iwe hivyo basi msizitoe"
"sheby, kweli mimi binafsi nakupenda sana tena sana... Na nipo tayari kwa hilo, lakini kwanini niue kiumbe cha watu lakini"
Huyo alikua ni Sauna akiyaongea hayo, Nilimuona Asnati akiwa kakunja sura sana kwa maneno ambayo ameyasema mdogo wake....
"kwaio wewe unampenda sana sheby si ndio"
Asnati alimuuliza mdogo wake tena kwa hasira mno....
"ndio kwani ulikua hujui"
"ivi sheby, uliingiwa na nini mpaka kutupanda wote... Nakuuliza ulikua na maana gani"
"Asnati aliuliza swali hilo huku akiwa kakasirika sana,...
"kwanza naombeni mnisamehe kwa hilo, ila kati yenu hakuna niliewahi kumtongoza hapa, wote mlinifata wenyewe, mimi ni mtoto wa maskini tu, nyie mlifikiri ningelitolea wapi nguvu ya kuwatongiza nyie watoto wa kitajiri... Ok tuachane na hayo, pointi ni kwamba hizo mimba tunazifanyaje"
"mschiuuuuuuuu.... Nikubebee mimba wewe ukiwa kama nani, nyooo kwanza umetuboa sana yani kutembea na sisi wote, tena nina wasiwasi hata dada yobi ushatembea nae wewe... Kwa taarifa yako sina mimba wala hatuna mimba.. Ila lazima tulifikishe kwa baba mana kama ni mimba ulimpa sauna na alishaitoa, sasa lazima tuseme"
Yani niliposkia kua hakuna mwenye mimba tena Asnati alionekana kunikataa tena kimapenzi, nilimshukuru mungu kimoyo moyo huku nikitabasam tu... Mana kumbe walikua wananizingua tu lakini hawakua na mimba wala nini... Nilichokifanya ni kushika begi langu kisha hatua zikaanza hapo hapo...
"sasa sheby, mbona unaniacha mimi"
Huyu alikua ni sauna mana Asnati keshakata mazoea na mimi tayari, mana Asnati ni mkubwa kuliko sauna, hivyo yeye ndio alianza kunikataa hiv hivi nami pia nimeshukuru sana kwa hilo, sasa sauna yeye ndio kama kapata nafasi mpyaa
"sauna? dada yako kajiondoa katika wimbi la mapenzi juu yangu,... So.. Ebu fanya kama alivyofanya dada yako"
"sitaki, tena nahisi penzi letu litakua tamu kuliko, mana hakuna mshakunaku tena"
"sauna... Soma mama soooma, mimi nipo tu wala sipungukiwi na kitu, utanikuta nikiwa dada kama zamani"
Wakati huo tukiyaongea hayo Asnati alikua kakaa mahali na sisi tulishamuacha kama hatua kadhaa hivi, kwahio tuanayo yaongea hayasikii labda aone kwa vitendo tu...
"we unambembeleza nini uyo kahaba tu hana lolote, mwanaume BALAYA mpaka inakera yani"
Mara sauna akamjibu dada yake
"Asnati naomba tueshmiane sawa, naomba uniache hata kama ni BALAYA kwani we anakuusu nini, kama umeshindwa kumpeti peti huyu, hata huyo utakaempata lazima umshindwe bibie"
"wewe sauna unasemaje wewe?"
"nimesema na mdomo na pua ikinong'ona"
"sawa utanikuta nyumbani"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asnati aliondoka kwa hasira sana huku akiongea maneno ya hasira hasira mara katukana, yani alikasirika kupita kiasi...
Sasa tukawa tumebaki mimi na sauna hapo rester,
"sheby mpenzi wangu, ebu niambie ukweli, unakwenda Dar es Salaam au upo hapa hapa tanga"
"nipo hapa hapa kwa ajili ya mke wangu mana anatamani nirudi nyumbani hivyo siwezi kwenda dar"
"heeeeee sheby kumbe una mke"
"sauna??... nina mke ndio, ila nilimuoa wakati nimentoa bikra yake, na wazazi wake walikua wanamkataa kama asipokuja na huyo mwanaume aliofanyia hivyo, ikabidi nioe tu"
"kwahio humpendi huyo mke si ndio"
"aah, aah, aahh, hakuna kitu ninachokipenda kama hicho, yaani nakuambia ukweli nampenda sana mke wangu, na sasa ana mimba yangu na karibuni atajifungua"
"mschiuuuuuuuu kwaio mi hunipendi si ndio ee? sawa"
"ah ah sikia basi sijamaliza kuongea"
"nini bwana.. Tatizo la watoto wa kiume mkipendwa mnalinga sana nyie"
"iv sauna, kama ningelikua sikupendi ningelikua nafanya nini mpaka sasa hivi hapa"
"sasa mbona unasema unampenda"
"Kiukweli ni kwamba nampenda sana mke wangu, narudia tena kua nampenda sana jasmini wangu na sintomuacha kamwe"
Niliongea maneno hayo mbele yake ili na yeye ajiondoe kama dada yake, japo ni kweli nampenda mke wangu.. Ila michepuko siachi,...
"basi wacha nami nifate ustaarabu wangu"
"sauna... Sawa kama umeamua hivyo hata mimi naona nitakua karibu zaidi na mke wangu"
"we mjinga nini... Ulifikiri nitakuacha kweli kisa ni hako kamke chako,.. Hata ungekua na wake wanne, sikuachi ng'oo"
"Basi hata mimi nakupenda na siendi popote kwa ajili yako,... Nikitoka kwa mke wangu naja kwako"
"safi sana... MmmmWwwAaaaHhh"
Alinikisi kwa furaha kisha nami nikamuuliza swali moja hivi....
"Eti sauna, ni kweli ulitoa mimba"
"yes, nilitoa mimba ile siku ulipokua haupo sjui ilienda wapi"
"lakini haikua yakwngu si ndio ee"
"kivipi... Ivi unajua sheby toka uje kuanza kazi kwetu, sijawahi kutoa penzi langu kwa mtu yeyote yule tofauti na wewe... Tena niligombana na mpenzi wangu kabla hata hujaja kwetu"
"kwahio unamaanisha kua hio mimba ilikua ni yangu"
"yes.... Tena nashukuru niliitoa mapema na yote ni kwa ajili ya kukupenda sheby"
"sasa huoni kua umemuua mtoto wangu"
"yes, na ningemuacha basi we ndo ungekufa"
"What??"
"yes"
"kwanini ningelikufa"
"we ulifikiri baba angekuacha"
"mmmhhh afu kweli"
"sheby??"
"naam"
"I love you"
"I love you too"
"sheby.. Please ukibadirisha number naomba unijulishe please"
"usijali..."
Tuliagana vizuri kisha kila mmoja akaanza hatua yake, mara ghafla sauna karudi tena huku akinikimbilia na kuniambia...
"sheby simama kwanza"
Ikanibidi nimsubiri na kumsikiliza... Daahh Kiukweli sauna alikua akinipenda si utani, huezi amini alitoa pesa nyingi sana yani hata kuziesabu nilihisi siwezi kwa maana zilikua hata kukaa mkao hazika, na alikua kaziweka katika mkoba wake, ni kama alizitoa zote...
"sheby, hii ni kama nauli ya, kama nitakua na shida na wewe utazitumia hizi pesa kuja nilipo sawa... Afu na hizi tumia katika matumizi yako ya kawaida"
"sauna.... Iv una akili timamu kweli"
"What"
"yes, nahisi hupo sawa kiakili"
"kwaio kukupa kwangu pesa mimi sina akili si ndio"
"sio kua huna akili, sasa hizi pesa zooote hizi karibia zinafika hata milioni tano sasa, za nini zote hizi wataka nini kwangu sauna, milioni mbili za usafiri pale unaponihitaji na milioni tatu sijui ni nne hizi eti za matumizi yangu... Mbona kama haingii akilini"
"kwaio hazitoshi au zimezidi"
Nilicheka huku nikitikisa kichwa
"kwahio unanicheka si ndio eee"
"hapana sauna sikucheki"
"sawa, chukua hilo begi zima kama hazikutoshi... "
"ah ah sasa unakwenda wapi, sauna.. Sauna... We sauna"
"staki, chukua na uende zako.. Mtu gani usioridhika na kidogo unachopewa"
"lakini mimi sikua na maana hio sauna... Njoo basi"
"sitaki.... Toyoo, toyo... Nipeleke apo mbele"
Alipanda toyo na kuondoka zake, huku begi alioniachia likionekana kua na pesa nyingi sana kuliko hata zile ambazo nimezishika mkononi... Nilichokifanya ni kuziweka zote katika lile begi, kisha nikaondoka nazo, lakini sauna alinielewa vibaya, mi nilikua namaanisha kwamba alikua akinipa pesa nyingi sana,... Sasa yeye akahisi labda naona ni kidogo,.... Basi nikapanda zangu tax mpaka nyumbani kwa mke wangu, nilipofika nilikimbilia chumbani kuzihesabu.. Nakwambia zile pesa zilikua nyingi mana nilitumia masaa mawili kuzihesabu na kuzihakiki... Zilikua zapata milioni 10 za Kitanzania... Nilikua nimefunga mlango kabisa kisha nikazificha zile pesa, hata hivyo nilipoingia mke wangu alikua hayupo,..
Sasa ndio karudi safari zake huko
"haya watoka wapi na tumbo lako ilo"
Nilimuuliza mke wangu...
"si kale kaschana kameenda mtoni sasa kamechelewa ndio ikabidi nikafate kumbe kulikua na foleni"
"ok poa"
"umekuja saa ngapi"
"muda si mrefu"
"mmmhhh poa, ila kazi si ndio umeacha, mana kazi yako ilivyo mmhh"
"umeanza sasa,.. Si ndio eee"
"wala tu, vp jimama lako halijambo"
"ebu nitokee mimi, jimama jimama, unalijua wewe"
"utajiju"
"afu jasu ntakuzaba mibao ujue"
"ukitaka kunipiga nipige tumboni ili umpige na mwanao huku"
"sawa, kwani si utajifungua... Nasubiria uwe tayari.. Yani ntakuzibua"
"utajiju mwenyewe"
"yani unanijibu mimi ivo jasu"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"usijibiwe kwani we nani... Kwanza unantia kichefu chefu"
"haaaaaaaaaa tena yamekua hayo"
"we wataka yapi"
"mmmhhhhh basi mwaya yaishe"
Aahhhhh mke wangu keshaanza kujibu nyodo, na yote hayo ni kwasababu ya hio mimba,
"yaani we ujifungue tu, mana ntakuua bure"
Basi baada ya siku hio kupita, nikiwa bado nimejilaza kitandani, na ni saa mbili hivi asubuhi, nikawa nawasha lisimu langu,.. Nilikutana na meseji nyingi zilizokua zikiingia, lakini zote sio kitu bali meseji moja kutoka kwa sauna, ilinishtua na kujikuta nimelegea hata kushika simu siwezi.. Mana nilipatwa na mshangao kutokana na hii meseji kutoka kwa Sauna,
Unajua ndugu msomaji unaweza ukashtuka sana kuhusiana na hili, lakini pia sio jambo la kushtusha, ila ni jambo la wasiwasi zaidi, katika upande wangu lilikua ni jambo la wasiwasi sana, mpaka najiuliza huyu mtoto wa kike anataka nini kwangu, na wasiwasi wangu ni kwamba hata hizi pesa huenda sii zake, bali katumwa na mtu, na mtu huyo huenda ni baba yake.....
Kwasababu begi lile jumla lilikua na shilingi milioni 10 na pointi, lakini asubuhi nilipoamka na kufungua simu yangu, nilikutana na ujumbe wa maandishi kutoka kwa sauna,.... Ukiniambia kua
"sasa kama hujatosheka na hizo, hebu njoo uchukue na hizi afu tuone kama bado hutotosheka"
Nilishtuka sana tena sanaaaa..... Huyu mtoto kapata wapi hizi pesa,... Hata kama ni mtoto wa kitajiri lakini imekuwa too much sana kwa hilo, jana nilichukua milioni kumi, leo ananiita eti kama sijaridhika nikutane nae pale pa jana ili aniongeze.... Ila sikua tayari kwa hilo mana nilihisi ananitega, niliipuuzi ile meseji yake kisha nikaendelea kulala, mke wangu na uja uzito wake tena wa mie nane kasoro, keshaamka na kuniandalia bonge la supu, japo hali ikibadirika hantaki tena, na ile tabia yake ya kupenda katoni ya juisi imeanza upyaa, yaani kweli kulea mimba si mchezo, Big up san mama angu kwa kumsumbua tumboni mpaka baba anunue vikatoni vya juice... Ona leo ni zamu yangu, mbona ntakoma walai vile...
Siku hio sikutoka kabisa hapo nyumbani na hata mke wangu alijua dhahiri kweli kua kazi ile nimeshaiacha japo kwa wakati huo nia yangu ni kumchombeza niende dar, na sijui kama atakubali jamani daaahh,... Sasa ilipofika mchana hivi muda wa lanchi tukiwa mezani watu watatu, mimi, mke wangu na mschana wa kazi, niliamka na kwenda kwenye friji na kutoa maji baridi katika friji hio... Mara ghafla simu yangu ikaita, na ipo pale mezani, afu kulikua na umbali kidogo ulionifanya nichelewe kuipokea na hatmae mke wangu aliipokea....
"heeeeee? Sauna?...... Hebu niipokee"
Nilipofika tu na mke wangu nae ndio kapokea sasa sikutaka kumpokonya ili asije akajua dhahiri kua ni mchepuko,.. Hivyo nilimuacha tu aongee nae,... Ila alichoongea huyo mtu sikua nikikisikia lakini pia mke wangu hakua akiongea, kana kwamba huyo anaeongea nae bado hajajua kua ni mtu mwingine aliokua akimsikiliza... Hivyo mke wangu alipo ipokea aliiweka moja kwa moja skioni pasina kusema HALLO hivyo na huyo mtu moja kwa moja akajua ni mimi na kuanza kuongea nae....
"kwani we ni nani"
Mke wangu aliuliza hivyo huku huku simu ikionekana kukatwa,
"nini sasa"
Niliongea hivyo kama swali kwa mke wangu,
"huyu mwanamke ni nani, mbona anakuita ukachukue pesa, au unamdai"
"aahhh hizo pesa sizitaki mke wangu"
"kwanini hutaki pesa, we fara nini"
"we jasu, shika adabu yako wewe, toka lini ukanitukana mimi"
"nisamee mume wangu, ni hasira tu za kukataa kwako pesa"
"aahaa kwaio wewe wataka kuniambia unataka pesa si ndio ee"
"ndio"
"ok poa, subiria hapo"
Niliingia chumbani na kuchukua kile kimkoba na kumpa yeye, haya chukua... Ila si utaweza kuishi mwenyewe"
"mmmhhh kivipi"
"huyo anaeniita ndio alionipa hizo pesa, na ananiitia zingine"
"heeeeee kwa kazi gani uliomfanyia"
Sikutaka kumuambia kwa vitendo na pia sikutaka kumgicha kitu ili ajue pesa anazokula zinatokana na kazi hio...
Nilikunja vidole viwili kisha nikaingiza dole gumba katikati... Mwenye akili atajua ina maana gani,
"mmhhh yani mume wangu na aikili zako zote unadiliki kuniambia huo ujinga?"
"je ningekudanganya, basi ujue ukweli ndio huo, ukila pesa jua kwamba ni kazi hio, sasa mimi naondoka ila sidhani kama nitarudi"
"haaaaa kwahio hutarudi kabisaaa mpaka kufa au ni kwa leo tu"
"yani kifupi ni hivi, nitakupigia simu... Chukua hii ni milioni 10, kaa nayo itakuseidia, ila nitarudi lakini sio leo"
"lini sasa"
"hata mi sijui"
"kwani umepata kazi nyingine"
"ndio, na haina siku maalum ya kurudi labda niibie tu"
"eee labda uibie, mana hilo limama limekushika haswaaa"
"mke wangu, nimepata kazi nzuri.. Hayo mambo ya jimama yanatokeaga tu bahati mbaya"
"sasa mi nasema hivi huendi mahari, na staki uende mahari popote, na ukikiuka tu nampigia mama simu"
"ebu ngoja basi nitarudi ili tuongee vizuri, ila hizo pesa zihifadhi"
Nilimuambia hivyo kisha nikaondoka zangu huku nikiwa sijiskii raha kwa kuto kukubaliana na mke wangu, mana nia yangu ni kumuomba... Mana hatua hii ndii hatu ya kusepa mazima yaani hii ni dar es Salaam moja kwa moja,...
Nilipotoka nyumbani niliingia pale restaurant ambako sauna alinambia tukutane, nilioofika hapo nilimpigia simu kwa bahati nzuri kumbe hakua mbali alitokea kwa pale nilipo tena alikua kashika bahasha flani hivi kubwa, ila sikujua humo ndani aliweka nini,
"mkoba wangu upo wapi"
"aaaahh sorry nimeusahau nyumbani"
"kesho nautaka"
"sawa"
"ok, jana najua ulikasirika sana labda nilikupa pesa kidogo, sasa chukua hizi milioni tano, kachanganye na zile milioni 10 upate hata gari ya kutembelea, mi spendi uwe unatembea kwa miguu"
"sauna mama? Ivi hizi pesa unatoaga wapi"
"heeeeee yani unashangaa mimi nimetoa wapi pesa,... Ila najua una wasiwasi ila jua kua sisi mimi na asnati kila mmoja ana akaunti ya benki, na kila mwezi wazazi wote wanatuingizia milioni moja kila mwe, yani kila mmoja anatoa milioni 2 kwa mtoto mmoja kwa mwizi... Na hii ilianza toka tulipoanza kidato cha kwanza.... Hivyo kwa mimi mpaka sasa sikosi kama milioni 180 hivi... Mana nimetumia tumia sana... Hivyo nataka nianze kukuwezesha wewe mpenzi wangu"
"mmmhhh sawa"
Huezi amini ile bahasha alinipatia mimi, aisee sauna alikua akinipenda sana, sikuamini macho yangu kwa pesa taslimu shilingi milioni tano... Dahhhh tuliongea mengi kisha tukatoka hapo na kuelekea katika gesti moja hivi... Nikampaka haki yake kisha tukaachana, ilikua imeshafika mida ya saa 11 hivi jioni, nikaona hapa nikienda kwa mke wangu ataleta zogo sana, hivyo dawa ni kuingia pale pale gesti nikalala mpaka kesho yake asubuhi, nikapanda Fast jet moja kwa moja mpaka dar,. Mana pesa ninazo so kwanini nisipande ndege, wakati huo nilishanunua kibegi flani kirasket, kisha zile pesa nikahamishia huko, ilituchukua lisaa limoja tu, hadi kufika huko,... Sasa nilipofika hapo Airport nikatoa simu na kumpigia dada yobi,
"haloo... "
"Eeee haloo sheby mambo"
"poa nambie"
"safi tu, vp umefika au bado"
"nimeshafika hapa Airport"
"ok nisubirie hapo dakika hii hii tu my baby"
"ok poa"
Sasa ile nakata tu simu mara polisi hao
"we vp apa"
"poa shkamoni"
Maskini ya mungu mimi nilikua mgeni wa jiji la dar, hivyo hata sheria za hapa Airport nilikua sizijui, mana nimepiga simu sehemu ambayo haikua ikiruhusiwa kwa jambo hilo,...
"ebu angalia hicho kibao hapo kimeandikwaje"
"SWICH OFF YOUR PHONE"
"sasa kwanini, umefanya kitu kinyume na sheria za hapa"
"nisameeni ndugu zangu nilikua sijakiona"
"utatoa maelezo vizuri kituoni"
"ah ah lakini broo"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"hakuna cha lakini, twendeeee"
"sawa"
"afu hili begi lina nini"
"aahhh huku ni karatasi zangu za kazi tu"
"pumbavu... Nyie ndo wapitisha madawa ya kulevya nyie... Hebu hilo begi, pumbavu wewe"
Wakati huo tulishaingia kwenye gari aina ya mando... Na polisi hao walikua wakali mno....
"lakini broo"
"hakuna cha lakini, lazima tukague hizo karatasi, siku hizi kuna karatasi feki zimeingia mjini... Hebu fungua zipu ya begi hilo"
Aaahhhh afu kwenye begi hilo kuna kitu kama milioni 4 na laki 7...mana nilishaanza kuzitumia, afu mapolisi na wanataka walione...
Lakini kabla sijaifungua zipu ya begi langu, kuna kitu nilikikumbuka kabla ya kupanda gari hilo, niliona kitu.....
Kuanzia hapo sikua na woga sana mana pia wapo ambao wameka kiraia lakini ni mapolisi, ila kwa hawa niliweza kuwagundua baada ya pale nilipokua napanda ile gari yao, kitu kilichonijulisha kua hii gari sio gari ya polisi bali ni gari binafsi kwani niliweza kunakili pleti namba za gari hio,.... Sasa kilichofuata hapo ni kua mkavu na kuyofungua zipu ya begi langu,
"kwanza naombeni vitambulisho vyenu"
Nilipoongea hivyo waliangaliana kisha wakacheka
"hahahahah, iv ana akili huyu mtoto, kwahio sisi tumekukamata tukiwa sio polisi si ndio"
"nipelekeni kituoni acheni kunizingua nyie, mliona wapi polisi hampeleki muarifu kituoni, ebu fungua mlango nisije kupiga kelele za wizi, si mnajua ni airport hapa ee? Nikisema weziii, mshakufa tayari "
"huyu dogo anajifanya anajua si ndio ee"
"fungua mlango bwana, mnazingua mi siwaelewi"
"uya dogo, tuachie ata ya kula ndugu yangu, apa ni Dar es Salaam, bila janja huishi"
"sasa ndio munifanyie janja mimi si ndio ee"
Nilipotoka ndani ya gari nikafungua begi kisha nikatoa noti moja ya elfu 10 kisha nikawapa,
"afu muache kuzingua nyie"
"sawaaa, si tumejua ni wa chuga boya wewe"
Mara ghafla kwa mbaali nikamuona dada yobi, au my baby, my hubby, my bae, my tost, my blue band, my andazi, kitumbua,.
Jamani Wanawake wana majina mengi khaaa, mbona sisi hatuitwi hivyo, mana mwanamke hata awe mkubwa vp utaskia.. CHEKI MTOTO YULE jimama kuubwa afu kijana mdogo anasema cheki mtoto yule,..... Mmmhhh heli yenu nyie watoto
Basi na yeye aliniona na kuanza kukimbiliana kwa furaha, mana mimi kuja hadi dar kulitokana na yeye kunikazania, mana huku dar sina mtu hata mmoja ninaemjua, hivyo bila yeye huku dar si kitu, japo ninayo pesa ya kujikimu zaidi kimaisha,...
"jamani sheby, nilijua uongo"
"kwanini nikudanganye dada angu"
"afu we, hilo jina la dada, utaniita tukiwa kazini huko lokesheni ila tukiwa wenyewe, I'm Your hubby"
"sawa nitalifanyia kazi"
Yaani kitendo cha kumuona tu dada yobi, nilihisi furaha ya ajabu, mana yapata wiki mbili sasa toka aondoke kule tanga kwao, basi tulipanda gari na kuondoka kwa kuelekea nyumbani kwake, mana sina pakufikia, ispokua kwake tu,.. Ilituchukua kitu kama nusu saa hivi hadi kufika kwake, Kiukweli watoto wa kitajiri ni wa kitajiri tu, mana huo mjengo wa batuli ulikua ni mkubwa, tena wa rosheni moja kwenda juu,
"hapa ulikua unaishi na nani"
"nipo na mfanyakazi wangu tu"
"wawili tu"
"ndio"
"mmmh mna mioyo yenu haswaa"
"ahahahahaha Ebu fanya mpango ukaonge twende shopping"
"eti eee"
Basi mtoto wa watu ndio nilikua nimeshawasili katika jiji la Dar es Salaam,
"jane, we Jennifer"
"abee dada"
Aliitwa mfanyakazi wa humo ndani, wakati huo nipo bafuni naskia tu
"ebu andaa chakula kitaam sana"
"sawa dada"
Nilipomaliza kuoga nilikua kweli sina hata nguo za kubadili, na ndivyo nilivyokuja mana kama unakumbuka nimekuja kwa kutoroka kule tanga,... Nimemtoroka mke wangu, Nimemtoroka sauna ambae ndio kanipa pesa nyingi sana kwa ajili ya kununua gari ya kutembelea, na hata hapa ndani nina kitu kama milioni 4 na nusu hivi katika begi hilo,
Sasa baada ya kumaliza kula nilitoka mpaka sebuleni ambapo niliweza kukuta chakula kizuuri sana, Daaahh ebana Dar wanakula vitu vya kituli tuli tu,... Basi tulikua watu wawili mezani mimi na yobi au batuli, dada yobi alikua akinitazama kwa macho flani hivi utafikiri ndio tumekutana leo, kumbe tulishawahi kukutana tena zaidi ya kukutana,..
Ilipofika saa 10 jioni tulitoka hapo na kuelekea mjini, wakati huo hata majina ya mtaa siyajui, mana ni mgeni haswa, kama ni majina ya mitaa ya dar hua naiskiaga tu, either katika maredio ama watu wakilizungumzia jiji hilo...
"huku ndio wapi huku"
"ahahaha, huku ni Kinondoni"
"Eeeebwana eee, toka nizaliwe sijawahi kufika huku"
"sasa leo si ndio umefika au"
Tulifija katika duka moja kubwaaa limeandikwa YOBI FASHION... Sio ROBBY FASHION.. .. Ni YOBI FASHION kana kwamba duka hilo lilikua ni lake, Basi tuliingia hapo, ila kibegi changu cha pesa nakumbuka nilikiacha kule chumbani kwangu,
"John mambo vp"
"safi boss karibu"
"asante, biashara vp inakwenda poa"
"ahahaha yaani boss apa mpaka kesho itabidi tulete mzigo"
"kweli eee"
"ndio, mana wanafanya kugombania"
"Okey, John? Huyu ni mdogo wangu wa tatu"
"ooohh nakumbuka hata juzi ulimuongelea hivi si ndio huyu"
"yeaahh"
"ok vp ndugu"
"safi tu, nambie broo"
"fresh,... Ebana unaelekea kufanana ee"
"ahhh kawaida tu broo"
"Ebana mi naitwa John, na hapa ndio ofisini kwangu"
"safi sana... Sheby,.. Wananiita sharbiny"
"poa poa mwanangu wacha tupige kazi"
"fresh mkali"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi baada ya kutambulishana na yule jamaa, dada yobi alinizungusha upande mwingine ambako kuna nguo za kiume,..
"haya mimi nipo ofisini, hivyo chagua viatu, nguo unazotaka then nitakuja kulipia sawa"
"sawa hubby"
"ahahaha"
Basi mtoto wa watu nikaanza kuchagua nguo katika duka hilo,.. Nakuambia nilichagua nguo nyingi sana mpaka boksa mikanda nguo aina zote... Bila kusahau viatu, viraba, visupreme, viulapa, va vingine vingi tu,...
Nilikuja kushangaa analipa shilingi laki sita, khaas, afu hata hashtuki..
"sheby"
"naam"
"nguo zimetosha"
"aahh tosha dada"
"ok, tuondoke, afu kuna mahali nimechelewa kweli yani"
"sorry dada kwa ku kuchelewesha"
"no sio wewe ulionichelewesha, nilikua kule ndani napiga mahesabu ya bidhaa na ndio maana nikachelewa"
Basi tulipanda gari yake kisha tukaondoka, sasa hapo ilikua ni mida ya saa 1 hivi jioni, jiji la Dar es Salaam ndio linaanza kuonesha ubora wake kwa taa zilitokua zikiwaka,... Kiukweli nilikua ni mshamba wa jiji lakini uzuri ni kwamba nilikua nipo na mwenyeji wangu, hivyo sikua na hofu zaidi mana nako kunasifika kwa utapeli, kama nilivyokoswa koswa Airport, Sasa tulifika katika saluni moja hivi.. Tena hata hio saluni ilikua ni yakwake mana iliandikwa YOBI HAIR DRESSING SALOON, Sasa ile nafika tu mlangoni niliona wanawake wengi humo ndani wanakwatuliwa tu,... Nilihisi aibu ya kuingia humo ndani hivyo ilinifanya nibaki nje,.. Ila dada yobi yeye alikua mbele hivyo hajui kama mimi nimebaki nyuma, na watu walikua wanazidi kuingia wake kwa waume, mana kama unavyojua jiji la Dar kujipara ni kwa kila mmoja mwenye mnyooko wa pesa.. Sasa nikiwa bado nipo hapo nje alitokea dada mmoja hivi mrembo sana,
"mambo kaka"
Dada huyo alinisalimia mana nilikua karibu na mlangoni, na yeye alikua akiingia humo ndani kwenda kujiweka sawa,.
"poa tu"
"mbona upo nje peke yako hata kampani huna why"
"we ulitaka niwe na nani"
"ok sorry, bye"
Sasa ile anaondoka akaupitisha mkono wake huku chini kwangu kama mtu aliekua anakagua hali ikoje huku,... Alafu muda huo huo na dada yobi ndio anatoke, na kitendo kile alifanikiwa kukiona live bila chenga, kwa yule dada kunishika sehemu za siri,
Sasa dada yobi si kaona ule mchezo, saa ngapi hajaanza kumuita yule mdada kwa hasira,
"we hamisi"
"abee dada, afu dada umesahau jina langu, mi si naitwa mwanaamisi"
"mimi sitaki kujua unaitwa nani,... Sikia nikuambie, Huyu ni mdogo wangu, nitakufanyia kitu kibaya wewe ooohoo"
"nisamehe dada yobi"
"naomba ukae mbali na mdogo wangu, inamaana hao wenzio wengine hawakutoshi... Nitakuharibia wewe, na uwaambie na wenzako, mbwa wewe"
"nisamee dada"
Mara wale wanawake waliokua wanasuka wakajaa pale na kuuliza.
"we Hamisi umefanya nini tena"
"jamani dada jeni, niliingia choo cha kiume afu mi mwenyewe mwanamke"
"umefanyaje"
"nilikua nimesimama na huyo kijana kumbe ni mdogo wake dada yobi"
"we nawe unezidi wewe, utapigwa we kila mwanaume wataka awe wako tu... Yobi dada msamehe tu huyu hajui atendalo"
"hamisi"
"abee dada yobi"
"shika adabu yako"
"sawa dada"
Sasa mi nilikua katika hali ya butwaa, mtu ni mwanamke afu anaitwa hamisi, ilibidi nimuulize dada yobi
"sasa sheby jamani mi nilipokua naingia we ulikua wapi"
"mi niliona aibu kuingia huko ndani"
"sheby mpenzi, sasa ukiona aibu we ulifikiri utaishije hapa mjini, ivi hata kuigiza utaweza kweli?"
"nitajitaidi.... Ila huyu mscha mbona mnamuita hamisi na ni demu huyu"
"nani huyu mjinga"
"si huyo hamisi"
"aahhhh we acha tu... Huyo ni mwanaume"
"What???... Mwanaume gani mzuri hivi"
"nini, mbona unashangaa au mmeshaahidiana nini"
"nani uyo, mimi waaalaa"
"heeeee hio waalaa nayo umeitoa wapi"
"kwani vp"
"usikute ushaambukizwa wewe, hahaha"
"mmnhhhhhh acha utanini dada yobi"
"utani wa nini sasa"
"ebu twende nikakujaribu, isije kua kweli"
"Eeeee hapo ndio umeongea neno sasa"
Basi tulikua tukiongea utani kupitia wale wanaume feki,.... tuliingia katika gari kisha tukaondoka kuelekea nyumbani, mvua ilitukuta njiani, tena mvua kubwa sana, lakini kwakua tulikua ndani ya gari, safari iliendelea hadi kufika nyumbani, mvua bado ilikua inanyesha.... Hapo nyumbani hapakua na mlinzi hivyo jeni ndio alikua tegenezi la kufungua mlango.. Dada yobi alipiga honi na geti likafunguliwa, tulipoingia ndani jeni nae alikua akifunga geti, tulipofika kwenye paking nilishuka na kuja kumseidia jeni kufunga makufuli ya geti, mana nahisi yalikua yakimpa tabu, jeni sii haba mtoto aliumbwa haswa, yani huezi jua kama ni house Girl,
Sasa kufika pale nikajikuta nimeshikwa na butwaa kwa kile nilichokiona, maskini jeni kumbe alikua ndani kalala hivyo sisi ndio tuliomuamsha.. Mana alikua kavaa kanga na ile ya ndani, hizo tu sasa kutokana na ile mvua mtoto wa watu kaloa chapa chapa, yaani mpaka ile ya ndani ilikua ikionekana kutokana na mgandamizo wa ile kanga kwa kuloa...
"samaani naomba nikuseidie kufunga"
Alikubali lakini hakutaka kuniacha, aliendelea kuniseidia na yeye mana kuna kufuli moja lilikua lina tabu, mvua ilikua ikiendelea kunyesha... Nilijikuta nikimshika mkono wake kwa ulaini aliokua nao jeni.... Tulimaliza kufunga kisha tukawa tunakimbilia ndani ila kabla ya kuingia ndani, tulibaki pale kibarazani kwa ajili ya kutoa nguo zetu ambazo zimeloa.. Mimi sikua na aibu japo kulikua na taa zilizozunguka jengo hilo lakini sikua na aibu yeyote ile, wakati dada yobi keshaingia ndani kitambo tu... Sasa nikiwa namalizia kuvua vest Ghafla jeni akawa ananiangaliaaaa bila kunipatia jibu,
"mbona unaniangalia sana"
"mmmhh samaani kaka"
Sasa sikua na nguo za kubadiri, mana nguo mpya bado zipo kwenye gari, hivyo niliogopa kumsumbua dada yobi ili niweze kufungua gari... Mana ufunguo anao yeye,
"jeni, vp huna hata ka suruali jamani"
"ninayo twende ukachukue"
Tulitoka hapo nje na kuingia moja kwa moja chumbani kwa jeni, akanipa suruali moja hivi ya jinsi, ila umbo lake lilikua kubwa kiasi, nilivaa pamoja na koti lake, sasa ile kugeuka tu nyuma hivi, nilimkuta jeni kaitoa ile kanga na kubaki na chupi tu, tena na yenyewe ilikua imeloa..
"nini ivo jeni jamani"
"jamani kaka nabadili nguo angalia ukoo"
Nikaona kuliko niangalie pembeni bora nitoke kabisa, hivyo nikawa nauelekea mlango ulipo, sasa ile nafungua tu nikaskia naitwa
"we mkaka"
"mmmnh jeni wasemaje"
"inamaana husikii baridi au"
"naskia"
"sasa unaenda wapi, mi pia naskia baridi"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mtoto wa kike aliongea huku akifikicha vidole vyake kana kwamba anaskia aibu flani hivi kutokana na kauli yake hio, ila mimi pia nilikua napenda iwe hivyo ila hofu ni kwa dada yobi, mana anaweza akanitafuta afu anikute nipo na house girl, sijui itakuaje, na house girl mwenyewe alikua ni kisu, sii sura wala umbo vyote mtoto wa watu alikua navyo tena macho yake yalikua makubwa ya kupendeza yani utajiskia raha sana pele anapokuangalia kwa kuibia ibia, mana yanakua meupee mpaka basi, mtoto jeni bado alikua akisubiri jibu toka kwangu, lakini mimi nilikua nikimhofia dada yobi,
"samaani, naomba tufanye siku nyingine but kwa leo haitowezekana kabisa"
Niliongea hivyo kwa maana tayari nilishajua nia yake ya kuniambia kua na yeye pia anaskia baridi, hivyo sikuona aibu ya kumjibu kwa usahihi... Na yeye pia baada ya kujua kua shotkati alioitumia nami nimeshaijui, aliendelee kuongea kua..
"mmhhh na wewe, kwani huyo si dada yako tu jamani kaka"
Jeni alikua akizidi kunishawishi kwa maneno huku akijifanya kama anataka kuivua na ile nyingine,..
"jeni, hata mimi napenda but please naomba iwe kesho"
"mmnhh sawa, ila leo ingekua vizuri kuliko kesho"
"hata mimi naliona hilo, ila naomba tuvumiliane tu"
"ok, usiku mwema kaka.... Afu sorry ivi unaitwa nani"
"naitwa sharbiny"
"ok.. Nikuambie kitu"
"niambie tu usijali"
"niote please"
"ok poa"
Sikua nataka kumjibu maneno mengi sana mana dada yobi akinikuta na huyu msichana, basi huenda akaikosa kazi yake hii, akajikuta ananilaumu tu, hivyo nilikua namjibu shotkati ili tuachane, na kweli alinielewa nami nikaondoka maeneo hayo ya chumbani kwake,... Nilikua nimeenda chumbani kwangu na kuendelea kulala, mana hata kula tulishakula kule kule mjini, kama unavyojua maisha ya mjini ukila kidogo tu umeshiba, sio lazima hadi ukombe safuria,...
Sasa usingizi ukiwa unaninyemelea taratibu, mara simu yangu iliita, nikaipokea,
"haloo dada yobi"
"we sheby uko wapi mbona sikuoni"
"mi mbona nipo chumbani kwangu huku"
"jamani, kwaio leo hulali na mimi"
"dada, yani leo nimechoka ile mbaya kwanini isiwe kesho"
Nia yangu ni aniache ili kesho nimfanyie kazi jeni mana ndio nimemuahidi,...
"jamni sheby mpenzi wangu, kwaio leo hii baridi nitashea na nani"
"ok poa nakuja basi... "
Nilikata simu kisha nikatoka zangu na kuelekea chumbani kwa dada yobi, niligonga mlango na alifungua mwenyewe,... Sasa ile kuingia tu dada kanirukia na kuangushana mpaka kitandani, dada alikua wamoto mpaka raha yani, basi kama unavyojua mapenzi mazito huanza na denda kama kawaida yangu mzee wa kuwaandaa mpaka wanapagawa, dada yobi alikua ana umbo la kipekee sana, mguu wake ulikua mguu wa bia ukipanda juu ya magoti yake huko kukaribia kufuli, mmmmhhh yaani alivimbiana utafikiri alikua ana ugonjwa wa miguu, kumbe ni umbo lake lilivyo...
Dada yobi alikua kavaa Night dress, kana kwamba haikua tabu kuisogeza, vikuku alivyovivaa miguuni vilikua vikinipa mie ashki ashki fulani hivi ya kuendelea kumtamani yobi wangu,....
Kama kawaida ya vijana hua tunapenda sana kuonja mboga, ila tunaponogewa, tunajikuta tunabwia mboga, kitendo cha mimi kubwia moja kati sehemu zake, zilimfanya dada awe mtu wa kukichangua kitanda chake pasina yeye kujua, alikua akilia vilio vizuri sana ambavyo vilinifanya niongeze huduma mara mbili zaidi, dada alifika mahari hataki tena mchezo huo uendelee... Nami nikamsikia vyema na kuacha ule uasherati wa kuonja mboga jikoni....
Ilituchukua masaa matatu hadi kumaliza kazi alioniitia chumbani kwake, zilizofuatia hapo zilikua ni shukrani za dhati kwangu kwa kazi nilioifanya... Sikuona tabu kulala huko, dada alilivuta shuka lake nami nikawa pembeni yake kama mke na mume, Kiukweli dada yobi alinipenda sana na sijui ni kwanini, na siii yeye tu bali ni familia yao yote ilinipenda mimi, nami sikua na pingamizi lolote kwao,...... Masaa yalisogea na sasa ni saa 12 asubuhi mida ambayo ninatakiwa kutoka ili yule beki 3 asinione mana akiniona atahoji sana kutokana na ishu hio, mana yeye anajua mimi dada yobi ni kitu na dada yake, kumbe walaa ni wapenzi tena wapenzi wazito haswaaa,.. Basi nilifika chumbani kwangu na kuendelea na usingizi wangu, nililala sana mpaka mida ya saa 2 hivi asubuhi nikakutana na bonge moja la SUPU yaani nyama kubwa maini ya kutosha,.. Afu kwa pembeni kulikua na ujumbe,..
"Spesho kwaajili yako baby wangu, pole kwa kazi ya jana"
Niliamka na kuingia bafuni, kisha nikatoka nikiwa uchovu umekwisha,... Niliikalia ile supu mpaka ikaisha nilipocheki kwa pembeni niliona begi la nguo kana kwamba tayari keshaniletea zile nguo ambazo zilikua katika gari, nilifungua begi na kuvaa vikali kali tupu, kisha nikampitia dada yobi anipe komenti,... Rumu ya dada yobi ipo rosheni ya juu na hata yangu ipo huku huku juu, kasoro jeni tu yeye ndio anaishi peke yake huku chini,
"heeeeeee waaoo sheby umezidi kua hensamu hubby wangu"
"aahhh unazingua sasa"
"kweli vile... Yaani nitaringa sana sijui nifanyeje"
"ufanyeje kivipi"
"ili wasikuone.... Mana nahisi sintokua peke yangu"
"mmhhhh dada yobi, acha wivu mamy mbona upo wewe tu"
"eti ee"
"yeaahhh"
"ok poa basi nataka tutoke now, kuna script wema kaniitia sasa ndio nataka nikaiangalie"
"wema??..... Wema yupi uyo"
"mmmhh inamana wema humjui wewe"
"huyu wema wa Sepetu"
"huyo huyo"
"waaooo must nikamuone mana sijawai kumuona"
"mmmhhh muongo wewe"
Basi tulikua tukiongea huku tukiongeza na utani kidogo, dada yobi alikua ana Headphone flani hibi aina ya NIA Headphone za kanye West,.... Za bei kweli kweli kama hujajipanga utaishia kuziona tu,.. Basi nilizichukua na kuzitupia skioni nikawa nakula ngoma taratibu bila wasi huku nikimsubiri laazizi wangu amalize kujikwatua huko ndani then atoke,.... Wakati huo ndio nilikua nashuka ili nikakae hapo sebuleni, nilipofika nilimkuta jeni akifuta futa fenicha za hapo sebuleni, kabla sijaongea nae mara yobi bibie huyo
"waaaaoooo kivazi kipya icho unabisha"
"yes, umeotea"
"mmmgggh mbona figa imetokea hivi"
"we... Angalia na maneno yako wewe asije akajua kua ni wapenzi"
"aahh hayupo keshaondoka zake"
Basi tulitoka na kuwasha gari, wakati huo nilikua nina hamu ya kumuona wema Sepetu mana namuonaga tu kwenye tv lakini live sijawahi kumuona,... Jeni alifungua geti kama kawaida yake, nasi tulitoka, kitu na mdogo wake lakini ndani yetu ni mapenzi yasiobebeka nikimaanisha mapenzi mazito kilo mia ina nafuu.....
"dada, kwanini usingeweka mlinzi"
"mmmhh niweke mlinzi kwa lipi, watu wenyewe ndio hao wa Dar es Salaam watanisafishia kila kitu humo ndani"
"kwaio unaogopa kusafishiwa"
"ndio"
"aahahahahahahahahahha"
"wacheka nini sasa"
"aahaha nacheka mana waogopa mwizi"
"weee huku Dar kuna wezi huku"
"mmmhhh kuliko Arusha"
"arusha ni majambazi tu, ila huku ni matapeli na wezi"
"nyoooooo, unasema arusha ni majambazi tu... Kule unaibiwa mchana kweupe peeee na huonewi haya na mtu"
"weeeeee"
"ooohooo"
Basi tulikua tukiongea huku tukitambiana kila mmoja mji wake upoje, sasa kwakua mimi ni mtoto wa arusha hivyo nilikua najua mengi sana kuliko....
Tuliingia kwenye hoteli moja hivi kalii ya hadhi ya maana..
Alipaki gari kisha tukashuka, nikiwa bado naendelea kula ngoma taratibu bila wasi, mara kweli we huyo.... Wakakumbatiana wenyewe pale kisha dada yobi akaanza kunitambulisha kwa wema Sepetu,
"wema rafiki yangu"
"sema huby wewe"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"he is my young brother"
"waaaooo Ona visura vile mnafanana"
"sheby, we sheby"
"naam Dada"
"unasalimiwa"
Dada yobi aliongea hivyo kisha wema akaanza kunisalimia
"mambo"
"poa shkamoo"
"marahaba ujambo"
"sijambo,..."
Nilimjibu huku nikiona aibu, wema alikua ni mzuri kumbe lile umbo ni lake kabisa mi nikajua ni umbo la video tu kumbe live ni yeye,
"we unasoma au umemaliza"
"nimeshamaliza mwaka jana"
"na ukafeli muone vile, utaigiza kama dada ako, mi nikajua wataka uwe fisadi"
Basi aliongea utani na kunichukulia kama mtoto vile mana hata sura yangu pamoja na umri ni haki kuonekana mtoto, ila balaaa lipo kwenye matendo yangu, nina matendo utafikiri nina miaka 25 kumbe kitoto cha miaka 22 hata ndevu tu nashangaa sina,
"mdogo wako ni hensamu"
"mmmhhhh weeemaaa"
"nini sasa"
"usikute naniii"
"mmmhhh jamani yooobi, uyo ni mtoto bwana siwezi fanya ivo"
Sikuelewa walichokua wakikiongelea, ila waliendelea na pointi iliowaleta eneo hilo,
Wema alitoa baadhi ya karatasi nyingi sana kumuonesha dada yobi, dada nae alizikagua sana karatasi zile, wakati huo ilishafika mida ya mchana sasa mana mida ilisogea, wema aliagiza nyama na vikorombwezo vingi tu, tukaanza kuvishuhulikia,... Dada alikula na kushiba kisha akaaga anaelekea toilet wakati huo mimi na dada wema tulikua tukivunja mifupa, na wema alikua anakula nyama huyo khaaa,.. Na kale kasura chake kama katoto,...
"we unatumia WhatsApp"
Wema aliniuliza baada ya dada yobi kuelekea toilet,
"ndio kwani vp dada"
"kuna kipande cha Script nataka nikutumie WhatsApp nawe ukipitie ili kuna sehemu flani uigize wewe"
"mmhhh kwanini usiichapishe tu ukanipa kwenye karatasi"
"ebu taja bwana namba yako, nikutumie we ulifikiri utamtegemea dada yako mpaka lini, kaa na mastaa kama sisi, tukutoe, afu hakikisha dada yako hajui sawa eee?....Haya Ebu taja sasa ni 07 ngapi vile???"
Nilikua nina wasiwasi wa kumuogopa dada yobi, mana dada yobi sio kua ni dada yangu, kama mnavyojua, sasa ikitokea kua namba ya wema ninayo katika simu yangu we ulifikiri itakuaje, na hataki kabisa namba yangu apewe kila mtu, nilikua nasita sita huku nikiangalia maeneo ya toilet kama dada yobi anakuja, ghafla simu yangu ikakwapuliwa na wema,
"Hebu lete, we ni mtoto wa kiume Why unaogopa ogopa? Huyo ni dada yako tu na atazidi kua dada yako mpaka kufa kwako"
Aliichukua simu yangu kisha akaandika Number zake na kujibipu, Simu yake ikaita kupitia simu yangu, Basi wema akawa amepata Number zangu,
"shika, nitakucheki badae sawa"
"unicheki ili twende wapi"
"kukucheki kwa phone kwani lazima tutoke? Au unapenda tutoke"
"staki"
"sasa je"
"heeeee mbona umejisevu mawese huku kwenye simu yangu"
Nilishangaa jina ambalo alilisevu kwenye simu yangu, yaani ile number yake alivyoisevu kwenye simu yangu, aliandika mawese
"yaah nimeandika hivyo ili dada yako atakapokuta neno mawese, asijue kama ni mimi, ila kwa wewe, jua hio mawese ni wema Sepetu (mawese)"
"lakini dada wema, mbona hii itakua shida kwa dada yobi"
"shida gani, afu umeshakua wewe, kwanza una miaka mingapi "
"22"
"aahh sasa mkubwa ivyo, au utamwambia kua nina namba yako"
"simwambii ila akijua je"
"hawezi kujua, mana hata huku kwangu nimekusevu Sebene badala ya sheby, hivyo ni ngumu kujua kwa hilo"
"mmmhhh sawa, ila hio Script utaituma lini, afu tukishaituma tufutiane namba"
Kiukweli nilikua namuuzi sana dada wema, mana nilikua sipendi number ya mwanamke yeyote yule, kwasababu dada yobi sio dada yangu, bali ni mpenzi wangu, hivyo siri ni yetu mimi na yeye....
"unajua utaniuzi sasa"
Mara dada yobi nae huyoo katokea hivyo maongezi yakawa kimya kwa muda,...
"eewhh nimechelewa ee?"
"heeee shost ulikua unaendesha nini?"
"we acha tu, yani toka nitoke tanga tumbo limekua la kunisumbua sana"
"sasa shost si unajua mambo ya tanga kwenu, vibuyu kwa wingi unalogwa mchana kweupeeee"
Huyo ni dada wema aliokua akimwogopesha batuli wangu, kua usikute kapigwa kipapai (zongo) huko tanga, lakini haikua kweli bali ni mchafuko wa tumbo tu,... Basi tulimaliza kula, kila mtu akawa bize na mambo yake, mimi nilikua nachati kama kawaida yangu, na wema na dada yobi walikua wakiendelea kupekua Script hio ambayo itakwenda kuigizwa muda sio mrefu, wiki hizi hizi za karibuni wataanza kushoot movie hio...
Nilihisi kuchoka sana hivyo nilitamani kwenda kupumzika mana tumekaa sana maeneo hayo, toka asubuhi mpaka sasa ni saa 8 sasa...
"dada"
"sheby ushaanza usumbufu eti ee?"
Dada yobi alikua akiongea kama kweli vile kumbe ni kipenzi chake
"Yobiiiii, msikilize mdogo wako jamni"
"ok wataka nini"
Sasa kabla dada yobi hakusema kitu mara dada wema akadakia
"oohhh kama ni pesa nitampatia"
"waaapi huyu wala tatizo lake sio pesa ni msumbufu tu, haya sema wataka nini?"
"mi nimechoka kukaa, nataka kwenda kupumzika"
"si umeona sasa? Mi nilisema ni msumbufu tu... Sasa wewe si unataka kuigiza wewe, je utawezaje kama unachoka mapema hivyo"
"aahhh nahisi leo sipo vizuri dada"
"mmhhh ok, chukua gari hapo uende afu mimi nitakuja na wema sawa"
"sawa"
Basi tukawa tumeelewana kiasi flani lakini hili swala la kuonekana mtoto silipendi dahhh,...
"mdogo wako mpoleee lakini dada mtu noma sana gaidi kweli kweli yani"
Huyo alikua ni wema ndio alikua akiongea na dada yobi kua mimi ni mpole lakini yobi ni gaidi...
"sio hivyo shost, yaani mi kuja nae sehemu kama hizi sipendi.....ok si unaijua njia?"
"ndio naifahamu"
Basi dada yobi alinipa ufunguo nami nikaondoka zangu, kweli nilikua nimechoka sio utani...
Basi nilishuka juu ya ghorofa hilo mana tulikua juu sana ya hoteli hio,... Sasa nilipofika nje hapo nikawasha gari kisha nikaianza safari ya kwenda nyumbani ambako ni kwa dada yobi, sasa nikiwa njiani nilipunguwa mkono na mrembo mmoja balaa, ila sikusimama kwa urembo wake bali nilisimama kwa kua alinitaka nisimame,... Nilisimama vizuri kisha nae akaja.. Toto toto kweli sio haba
"mambo"
Alinisalimia mtoto wa kike nami sikujivunga kwa hilo
"poa nambie"
"safi tu,... Aaahhh samahani kaka, nilikua naomba kalifti mpaka hapo mbele, samahani lakini kwa usumbufu"
"aahh bila samahani tunaweza kwenda usijali"
Basi mtoto wa kike kapanda kwenye gari na safari ikaendelea mbele, mtoto si kujisheua gani huko, mana hatulii katika siti, mara ajiangalie kwenye kioo,.... Kiukweli alikua ni mzuri sio umbo wala sio sura, hata moyo wangu ulipenda kua nae lakini nilikua namuogopa sana dada yobi,...
"samahani kaka, mimi naitwa asha, sjui kaka angu unaitwa nani"
"ok mi naitwa sharbiny "CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"mmmhhh kajina kako mbona kama kakihindi au Kiarabu hivi wewe ni mkabila gani"
"aahhh mambo gani tena ya kuulizana kabila tena?.... Ok mimi ni msambaa mpare"
"ehehehehehe asa msambaa mpare ndio nini"
"mmmhh kama bado hujajua tuyaache hayo"
Basi kaukimya kakawa kamepita kwa muda huku kajicho hakanyimwi haki yake pale ninapojifanya nabadirisha gia na wakati gari ni automatic gear,...
"heee kaka simu yako iko poa kama simu yangu"
Nikajiuliza uyu mtoto wa kike ana nini au ananijua nini mbona ananikagua hivi...
"wewe huezi kua na simu kama hio"
"weeee hiii si IPhone pia au"
"sawa ni IPhone but kuna utofauti wa IPhone"
"kwani hii yako ni ngapi"
"hio ni IPhone 7"
"ooohhh sorry.. Yangu ni IPhone 5"
"eeeehhh kifo na usingizi kabisaa"
Sasa cha ajabu mtoto wa kike kajibipu na simu yangu, hivyo namba yangu akawa ameshaijua na kuipata....
"aahhh we vp tena, mbona umefanya kitu ambacho sijakuagiza"
"mmmhhhh samahani, nilikua naitaka ila sikutaka kukusumbua mana una drive"
"hata kama aisha, sio busara kuchukua namba ya mtu bila ruksa, ivi kama ni mimi nimefanya hivyo, je ungejiskiaje"
"samahani, naifuta ukiona mwenyewe, mana niliona ni kijana mkarimu unaseidia watu but I'm so sorry my brother, nilikua nataka tu nichati na wewe"
"mi spendi bwana"
"sorry my brother"
Basi dada alionekana kuniganda kimtindo na hizi taarifa nilishapewa kua kuna wasichana ambao wanaangalia uwezo wa mwanaume ndio wataanza kumshobokea, ila sasa kwangu kama kakosea hivi mana mi mwenyewe naishi kwa mtu, sasa kama kaniona mi kifaru, atakutana na mbogo,... Sasa mara akatoa begi lake nilishangaa sana mwanadada huyu aliokosa aibu pamoja na haya,.. Kumbe huko alipotoka katoka kufanya shoping ya vinguo vyao hivi, lakini sikupenda ile hali ya kuvikunja kunja mbele yangu mana ni nguo za siri zinapaswa kufichwa sana, lakini yeye eti anazikunja hapa hapa nami nikiwa naona, Sikutaka kumuambia kitu mimi nilikua zangu bize na gari,
"ooohh sorry, naomba nishushe apo mbele aaagggg, nimepita sehemu niliotaka kushuka"
Mpaka hapo sikumjibu mana nilikua natamani ashuke tu mana vituko vyake vya dakika chache tu vimenishinda, Aliposhuka wala sikutaka kusubiria asante yake, niliwasha gari, mbele mbeleyao nilifika nyumbani muda huo ikiwa ni saa 10 jioni, nilikua sina hata raha mana nilikua nimechoka sana afu nikifikiria yule mtoto wa kike alivyo mzuri lakini kakosa adabu, sina hata hamu nae. Niliingia zangu bafuni na kuyaoga huku jeni akiniandalia kabaiti baiti hivi mana sikua nahisi njaa bali nilijiskia kutafuna tafuna tu, kama unavyojua kua jeni ana chembe chembe flani hivi za upendo juu yangu,.. Lakini kwa leo isingewezekana mana dada yobi angetokea muda wowote,....
Kesho yake asubuhi palipokucha mida ya saa 2 hivi niliamshwa na mlio wa simu ulionishtua sana katika usingizi wangu,..
Ilikua ni number ngeni ndio iliokua ikipiga, lakini sema nilichelewa kuipokea na hamae ika kata, ila ndani kulikua na meseji nayo iliingia muda sio mrefu kama dakika moja hivi, na alikua ni dada yobi ndio alinitumia meseji muda huuu..
"sheby mpenzi, kama umesha jiandaa twende kama ni chai tutakunywa mijini.. Mi natangulia kwenye gari sasa hivi, hivyo utanikuta ndani ya gari"
Sasa ile namaliza tu kusoma meseji ya dada batuli, mara ile Number ngeni ikapiga tena, sikutaka kuipotezea kabisa hivyo niliipokea fasta fasta... Lakini ghafla ikawa ni saiti ya kike...
"halooo"
"Eehh haloo kaka, samahani umeona nguo yangu hapo kwenye gari yako"
"nguo???.... Nguo gani we ulinipa mimi"
"jamani we mkaka we si ndio ulinipa lifti jana mida ya saa 9 hivi"
"aaaahhh ok, unasema umeacha nini"
"nguo zangu nilinunua pisi kumi naona hapa zipo tisa, so nadhani moja nitakua nimeisahau kwenye ile gari yako"
"unamaanisha zile nguo ulizokua unazikunja kunja pale ndani ya gari"
"ndiooo, please naomba tukutane unipatie"
"mungu wangu eeee... Ushanipa msala sasa"
Ikabidi nikurupuke tena nilikua na bukta lakini sikua na aibu japo hakukua na mtu wa kumuonea aibu, nilikua nazunguka nyuma ya nyumba hadi kwenye paking ya magari, na wakati huo simu bado ipo hewani,... Nilipofika kwenye gari tu ile nafungua mlango, kumbe na dada yobi nae ndio alikua anaingia kwenye gari, mana ukumbuka alinitumia meseji kua nitamkuta kwenye gari, sasa kwa bahati nzuri tukajikuta tunafungua milango wote, yaani yeye kafungua wakulia na mimi nikafungua wakushoto... Hamadi ile chupi ya yule mtoto wa kike hii hapa kwenye siti ila ilikua ngumu kuiokota mana dada yobi angejua naokota nini,... Hivyo nikawahi kuikalia ile siti, hivyo nikawa nimeikalia ile nguo...
"heeee we vp tena mbona ivo"
Dada yobi alinishangaa kwa kuniona nikiwa na bukta tu na vest,
"si umenitext meseji wewe au sio wewe"
"eehehehehe, sasa mi nilikuambia uje na bukta? Au umekuja kuni saplaizi jamani"
"ah ah wala tu"
Duuuuu,... Sasa jinsi ya kuitoa sasa sijui itakuaje,...
"sheby mpenzi, mbona umekuja na bukta huku nje"
"ulifikiri kuna tatizo mama, we twende tu"
"heeeee yani twende mjini ukiwa hivyo"
"yes, tena na mkanda nafunga kabisaaaa"
"muungu wangu eee sheby ushakua chizi tayari"
"kwa ajili yako ndio mana ni chizi"
"oooohhh najua umefata busu si kweli ee"
Nikaona yes hapo hapo kwenye kupeana makisi ndio pazuri pa kuitoa,.. Akajisogeza nami nikajisogeza ili tupeane mabusu moto moto,.. Lakini cha ajabu mikono yake akawa kanishika mikono yangu, kwaio nikajikuta nashindwa kuichukua ile nguo, mana nimeikalia,..
"mmmmwwwaaahhhhhh... Thenx kwa kis mpenzi wangu... Ila wahi basi ukaoge twende"
Nikawa sina pozi lolote tena mana nilitegemea lile busu lakini imeshindikana..
"sheby jamani tunachelewa location"
Yaani hapa kwenye hii siti, nikiamka tu, dada yobi ataiona hio nguo afu itazua msala.....
Sasa nifanyeje ili niweze kuichukua??
ENDELEA.......
Nilikua na mawazo mengi sana utafikiri kuna kitu kitakachonifanya nipoteze maisha, kumbe ni hicho kinguo tu, nikajishauri kua kwani akiona kuna nini, tunalisovu mambo yanaendelea kama kawaida, sasa mtoto wa kiume pamoja na kusema aone tu lakini akili yangu bado haipo sawa kwa hilo, mana akiiona itakua msala, tena usionyamazika...
Sasa nikapata wazo moja hivi
"unajua nini dada yobi"
"sijui"
"nataka tuliongelee hili swala la kunifanya mdogo wako mbele za watu mi spendi eti"
"mmmhh sasa sheby bae wangu, kwani mi nimependa iwe hivyo, unajua kama ungelikua kidogo tunaendana kiumri afadhali nikisema huyu ni mpenzi wangu, but watu watashangaa sana kama nitasema wewe ni mpenzi wangu... Na mimi nimekupendea vitu vyako vyaaa kuleeee ndani, lakini siujali umri wako na ndio mana nataka wajue wewe ni mdogo wangu... Please sheby wangu mimi pia sipendi niwe nakuongelesha kama mtoto mdogo sema inanibidi tu ili kulinda heshima yangu"
"ok basi kama ni hivyo upunguze ukali wa maneno jamani"
Mara ghafla jeni alikuja katika gari na kumuita dada yobi, mana mimi hatakiwi kuniongelesha isije julikana kua na yeye ana chembe chembe za Mapenzi kwangu.
"dada, chai ipo tayari mezani"
"ok nakuja,... Umeona sasa sheby, mimi nilitaka tukanywe chai mjini"
"lakini kwanini ukaharibu pesa wakati ndani ipo"
"mmmhhh haya tushuke basi"
"shuka tu mi nitaloock milango"
"iiii una visa wewe"
Hapo kidogo nikapata nafasi ya kuipata, mana ile amenyanyuka tu, nami nikaivuta ile nguo kisha nikaiingiza huku mbele kwangu, mana sikua na kitu chochote cha kuiweka, kwasababu nilikua nina bukta tu na boxer ya ndani basi na vest peke yake, hivyo kwakua sikua na mfuko hata wa bukata sina, hivyo niliichomeka huko ndani ndani kwangu... Kisha nikalock milango na kuongozana ila saa hio sasa ndio naanza kuona aibu mana kazi nishamaliza, nikakimbilia ndani kwenda kuvaa suruali, kisha nikaingia bafuni kama dakika 10 hivi nikawa nimemaliza kuoga na kwenda kutupia viwalo viwili vitatu vya hapa na pale, Nilikuja mezani ambako ndio chai ilipotengwa, nikiwa nipo sambamba na dada batuli kasoro house girl ndio hatujumuiki nae,
"unajua nini dada yobi"
"sijui"
"kumtenga mtu sio vizuri, nae ni binadamu anapaswa kula na familia yake"
"kwani tumemtenga nani"
"si jeni"
"wala hata siwezi kufanya hivyo, yeye mwenyewe ndio kajitenga labda anahisi nitamfokea na kwakua kipindi kabla ya wewe hujaja, yeye alikua akitangulia kula kabla yangu, kwasababu mimi nilikua nachelewa hasa tukiwa location sasa keshajijengea hayo mazoea ila sikumtenga na wala sijawahi kumwambia tusijumuike sote katika meza"
"oookey apo nimekuelewa"
"ila na wewe unapenda kudadisi"
"ehehehe nadadisi kile cha umuhimu tu"
Basi mimi na dada batuli tulimaliza kupiga chai pale kisha tukapumzika kiasi huku tukiwaza njia ya kupita kama hakutokua na jam...
"twende sasa mana naona usharidhika kula nyumbani"
"sawa tangulia mi ngoja nichukue simu yangu huku ndani"
Niliingia chumbani kwangu makusudi kisha nikaichukua ile nguo ya ndani ya yule mdada niliempaga lifti, nia yangu ni kuichukua ili nimpigie simu tukutane wapi nimpe chupi yake, mana ilikua ni mpyaaaaa.... Basi nikaiweka mfukoni kisha nikatoka zangu, na kumkuta dada yobi akiwa tayari keshawasha gari tayari kwa kuondoka, jeni alifika na kufungua geti, kisha nasi tukatoka...
"leo mnakutana wapi na wema"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"tunakwenda hapo Magomeni kuna kava tunaenda kuidizaidi, ambayo muvi yake tuliahaigiza hivyo tukwenda kupiga picha za kava tu"
"oookey"
Kweli nilikua nina shaauku ya kupajua hapo Magomeni mana napaskiaga tu katika maisha yangu hivyo, napatamani nikapajue haswa haswa, Tulifika eneo hilo nikiwa nina shauku ya kumpigia yule dada simu aje tukutane ili nimpe mzigo wake, na saa hio nilikua nina hasira nae yani nilikua natamani aje nimchape ata makofi, mana huezi kupewa lifti tu afu ukaanza kufanya ujinga ujinga ndani ya gari, sio sawa jamani wadada mjifunze jamani ukipewa lift ebu jaribu kua mpole na mstaarabu mana kama ni mapenzi yapo tu...
Sasa tulipokua ndio tunashuka katika gari, na wema nae ndio alikua anaingia, Sasa si unajua salamu za kimjini, dada yobi alishangaa sana wema kunichangamkia mimi badala ya yeye,
"waaooh jamani sheby na leo tena umekuja mambo dogo la mie"
"poa shkamoo"
"marahaba ujambo"
"sijambo"
Wema aliitikia salamu yangu tu kwakua dada yobi alikua karibu, ila hakuipenda ile salamu,
"shoti jamani mambo"
"poa mzima"
"mzima wa afya za toka jana"
"aahhh za jana nzuri,.... Vp nawe ndio unafika"
"yes"
"kumbe ningewahi bure tu"
"ulikua wataka kuwahi eee?"
"yes, tena nilikua nataka kuja kunywa chai huku mjini, yani kama sio sheby kunichelewesha ungenikuta hapa"
Basi tulikua rukiingia ndani ya studio hio ambako niliwakuta waigizaji wengi sana wakiume na wakike, Hata ray mzee wa maji nimkuta nae akiwa katika pilika pilika za hapa na pale, akina gabo, wolper, Irene Uwoya, na wengine wengi tu mana hio sehemu palikua ni studio ya filamu hivyo wasanii walikuepo hapo kwa ajili ya kukamilisha mipango yao, sasa kwakua watu walikua bize na baadhi ya watu ambao walitakiwa kupiga picha ya filamu hio bado hawajafika, ilitubidi tutoke eneo hilo kwanza tukatoka pembeni kidogo ambako palikua na restaurant flani hivi ghali sana, tukaingia hapo na kuagiza kibaiti baiti kila mmoja, na wakati huo yapata muda wa saa tano hivi asubuhi, kale kajua ka dar kama unakajua, kakali kiasi, basi kila mtu aliagiza kibaiti chake na kuanza kujisevia, tukiwa tunasubiria baadhi ya hao watu ili picha zipigwe zikiwa zenye uhalisia wa kitu cha ndani...
Ghafla simu yangu ikaita, si ikabidi niitoe sasa kumbe ule mfuko nilioekea ile nguo ndio niliwekea simu, kwahio vile nilivyotoa tu ile simu na ile nguo nayo ikatokeza nusu yake kutoka kwenye mfuko, Afu mtu mwenyewe aliopiga ndio huyo dada mwenye hio nguo,..
"haloo.."
"Eee sheby uko wapi tukutane"
"nipo Magomeni we upo wapi jamaa angu"
Niliita jamaa ili dada yobi asijui kama ni mwanamke ajue kua naongea na dume mwenzangu...
"heeeee nimekua jamaa tena"
"vunga chalii yangu we nambie uko wapi nije"
"ok nipo hapa kidarajani"
"oookeee apo kwenye hicho kighorofa hapo"
"yes, njoo hapa utanikuta"
"ok poa"
Sasa kumbe ile nguo ilivyotokeza nusu, alioiona ni dada wema, na nguo zao hua zinajulikana hata kwa macho.. Tena wenyewe ndio wanazijua ile mbaya, na dada wema yeye ndio alioiona ile nguo,... Sasa ile nataka niweke simu mfukoni mara meseji imeingi, hivyo nikajikuta nimeairisha kuiweka ili niisome hio meseji na hilo tukio la nguo kuonekana silijui... Nikashangaa mtu alietuma meseji... Alikua ni dada wema kama unakumbuka alijisevu Mawese..
"jamani umeniletea saplaizi thenks"
Mmmhhh sasa nikajiuliza nimemletea saplaizi ipi hio,... Sasa kwakua tulikua meza moja, nikamuangalia kwa jicho la kuiba ili dada yobi asijue kinachoendelea, sasa nilipomuangalia dada wema, akanikonyeza na kunionyeshea kwenye mfuko wa suruali yangu.. Nikaona kitu alichokua akikiseme, kumbe ni ile nguo ndio aliokua anasema nimemletea saplaizi, na wakati mwenyewe ndio kanipigia simu muda huu huu, anaitaka nguo yake,...
Mara meseji imeingia nyingine
"nipe bwana, hadi dada yako ajue"
Na muda huo alikua anausogeza mkoba wake eti niiweke katika mkoba huo... Mana ni zawadi yake nimemletea...
"jamani sheby asante kwa zawadi yako"
Alinipa asante hata kabla sijaamua kuiweka, na nikikataa atajua kua nina mademu wengine ambao nawanunulia nguo za ndani.... Sasa nifanyeje jamani... Aaahhh Aseee yule mtoto wa kike nikimpata nitamtia makofi... Yaani hizi karaha zisingekuepo kama sio yeye..
Mara meseji imeingia kwenye simu yangu
"jamani sheby, ivi ulijuaje kua napenda zawadi kama hizo?"
Meseji zote hakuna nilioijibu hata moja, mana bado najishauri nimpe au nisimpe, na nisipompa sifa mbaya ya kununulia watoto wa kike nguo za ndani itaanza kuepo, mana lazima atajua kua kuna demu nimemnunulia hio nguo, sasa nifanyeje mimi Jamani??
Na wakati dada yobi hajui hili wala lile, yaani yeye anaendelea kula vichipsi round na nyama, wakati huku mimi na dada wema tulikua tukiombana nguo ambayo haikua yakwake tena bora ata ningenunua mimi, lakini walaaa, sasa nikaona tukiendelea kubishana kuusiana na hilo, itafikia hadi dada yobi kujua kile tunchobishania, basi mtoto wa kiume bila hiana wala nini nikaingiza mkono mfukoni na kuiweka katika mkoba wake kisiri siri ili dada yobi asijue kitu, mana mkoba wenyewe upo chini ya meza, nikaiweka kisha nikausogeza kwa mguu huo mkoba ikawa tayari tumeshamaliza marumbano, lakini nilikua nawaza sasa nitampelekea nini yule mtoto wa watu, japo saizi ya nguo itaweza kumuenea wema mana yule mtoto wa kike na huyu dada wema hawajaachana sana kwa maumbo, ila dada wema ni shida kama unavyomjua mtoto ana umbo la kumbembeleza mwanaume hasa hasa wale marijali kamili wanaojua kuhendo vitu vyao...
Mara meseji kutoka kwa mawese,
"asante, natamani niijari apa apa yani"
Kabla sijamjibu mara simu yangu ikaita kucheki ilikua ni namba ya yule mtoto wa kike,
"ooii jamaa angu nakuja apo nisubiri"
"jamani, we mkaka mi spendi uniite jamaa"
"we vunga bana, kwani si kwa muda tu"
"ok, fanya chapu basi mbona kama nachoma mahindi vile"
"ok poa"
Nikakata simu kisha nikamuaga dada yobi
"dada nakuja mara moja kuna jama namcheki apo mbele"
"heeeeee ushakua mwenyeji sasa hivi"
Mara wema akadakia juu juu
"heeeee batuli usimbane mdogo wako ivo, kumbuka ni mtoto wa kiume uyo"
"ni sawa wema... Lakini mdogo wangu bado ni mdogo na sipendi aju niia nyingi za hapa dar"
"ok najua unampenda mdogo wako na hutaki aharibike, lakini sio kiivyo shost.. Huyo anaenda kwa rafiki zake, ina maana hujaskia mambo ya jamaa jamaa hapa.... Heeeeeee shost una wivu hata kwa mdogo wako"
"wema sasa hayo ni matusi shost"
"No simaanishi hivyo, but unambana sana mdogo wako"
"ok... Sawa.. Nenda"
"No usimruusu kishingo upande batuli, anaweza akapata hata ajali huko njiani... Be free na ruksa yako"
"niko sawa"
"ok... Sheby... Chukua gari yangu nenda nayo utanikuta hapa hapa"
Kama unavyoijua sauti ya Madam wema, anaongea utafikiri analia vile kumbe ndio kwanza anatoa macho kweli kweli, Basi dada wema alinipa nitoke na gari yake hivyo.. Sema tatizo la gari ya madam wema, Pletinamba yake Imeandikwa jina lake, WEMA SEPETU kiasi kwamba kila nitakapo pita nitaonekana kama madam wema... Ila sikujali nilipanda kwenye hio gari aina ya Lendi kluza V8 nyeusi, number yake ya usajiri ni jina lake la WEMA SEPETU nikaondoka na gari hio hadi kufika eneo hilo la darajani.. Niliangaza macho huku na kule na kumuona yule mdada, na hata yeye aliniona, hivyo alikuja fasta...
"heeeeee wewe, hili si gari ya wema hii"
"kwaio"
"una undugu na wema"
"wala ata"
"sasa unaendeshaje kama huna undugu nae"
"wewe umefata nini hapa"
"chupi yangu"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sasa ayo maswali ni ya nini ivo"
"ok nipe nguo yangu niondoke"
"mmmhh sorry kwa hilo"
"nini.... Wewe mkaka zile nguo mwenyewe nililetewa zawadi na mpenzi wangu"
"ok hio sio tabu... Unajua zinapouzwa"
"ndio ila ni bei gari"
"sawa sikatai... Nipeleke hapo mahari nikainunue"
"sawa, twende kariakoo"
Basi mtoto wa kiume nika start gari mpaka Kariakoo, tukafika kwenye hilo duka moja matata, hata wauzaji wenyewe walipoona gari ya wema walishtuka na kujihisi kua wema labda ndio alikua akija kununu viwalo hivyo mana hilo duka ni spesho kwa hizo nguo tu, hakuna suruali wala gauni hapo yani ni hizo tuuu....
Mimi skutaka kushuka na kwenda ndani ya duka hilo, bali huyu dada alishuka mwenyewe na na kumpatia kitu kama elfu 50 hivi ili akachukua zile kumi nyingine,... UKUMBUKE KUA NINA PESA NILIZOTOKA NAZO TANGA KAMA MILIONI 4 HIVI NA CHENCHI, HIVYO USIJE UKASEMA PESA NIMETOA WAPI... mtoto wa kike alishuka katika gari na kwenda kununua vitu vyake hivyo mimi nikiw ndani ya gari nacheki tv ya humo ndani, kiti kama dakika kumi hivi alimaliza kisha akarudi,... Nilichokifanya ni kumrudisha pale darajani nilipomkuta, nilikua nina hasira nae sana huyu dada lakini ziliisha kwakua nguo yake tayari nimeshampa mtu mwingine... Hivyo ikabidi niwe mpole zaidi,..
"angalia vizuri usije ukacha tena"
"iiiii nimechukua zote... Afu ile kwani ulimpa nani, au ulimpa wifi"
"hukuacha kitu bwana sema ni wenge lako tu"
"mmmhhh we sema ukweli umempa wifi"
"kwani vp si umeshapata ulichotaka"
"ndio"
"haya nenda sasa"
"ila samahani, nitakucheki na meseji jioni"
"sitaki"
"ati nini"
"sitaki tena futa namba yangu haraka"
Niliongea hivyo kisha nikaondoka bila hata ya kumuaga, Moja kwa moja mpaka Magomeni pale kwenye kile ki restaurant pale, niliwakuta tena walikua wengi pamoja na marafiki zao,..
"dada wema asante kwa usafiri"
"ok poa usijali"
Pale pale nikaona nikiaga hapa nitaleta songombingo, mana nilikua sijiskii vizuri kimwili, nikachepuka pale chapu bila hata ya kuaga,
"oya taxi"
"yes boss"
"Nipeleke hivi"
Basi nilikua naelekea nyumbani ambako ndio huko kwa dada yobi,
"niache hapo mbele"
Basi nilifika nyumbani nikaingia zangu ndani mpaka chumbani kwangu... Muda huo ikiwa ni saa 7 hivi mchana na jeni ndio alikua akipika chakula cha mchana, hivyo aliponiona tu mwenyewe alifurahi,.. Simu yangu sikutaka kuiacha on ikabidi niizime kabisa... Nilikimbilia kulala tu mana nilikua nimechoka na ile hali ya joto la dar ambalo sijalizoea, lilikua likinichosha sana yani... Nilitulia hapo kama lisaa hivi usingizi mzito ulishanipitia saa mingi sana... Ghafla mlango wa chumbani kwangu ukagongwa, yapata saa 8 hivyo kwa muda huo nikiwa nagongewa mlango,..
"nani"
Niliuliza kwa umakini wa hali ya juu sana ili niweze kumsikia mtu aliekua akigonga mlango huo, mana huenda akawa ni dada yobi karudi
"ni mimi jeni"
"ooohhh sukuma"
Aliingia jeni akiwa anaona ona aibu hivi
"sema"
"chakula kimeiva"
"ok poa, nakuja hapo mezani"
Jeni alitoka zake huku akinipa majaribu ya kidunia, lakini naweza kuyashinda kama nikiwa ngangari,... Niliamka taratibu na kusogea mpaka sebuleni kunako meza ya chakula, baada ya kufika nilimkuta jeni akiwa kashikilia jagi la kuninawishia mikono
"aaghh usijali nitanawa mwenyewe tu"
"wala tu usijali nimependa mwenyewe tu nikunawishe"
Basi mtoto wa watu nikajikuta namuangaliaaa kwa muda mrefu mpaka akaondoka kwa aibu ya macho yangu,.... Wakati huu najua dada yobi ananitafuta vibaya mno mana ni wakati wa kula chakula cha mchana, sema kwa huku dar watu wanakula chakula mapema sana unawakuta saa 6 watu washakula mchana mwema.... Lakini Arusha mpaka ngoma nane ndio mwisho wa kupata chakula cha mchana.. Sasa nikawa nimeshamaliza kula, ila nilihisi jeni alikua akiniangalia mana ile namaliza kula tu, akaja ili aninawishe mikono,..
"mbona ivo jeni, usijali mi nitanawa tu"
"kwani ni vibaya mimi kukunawisha mkono"
"sio mbaya"
Ghafla macho yangu yakatua katika kifua cha jeni, yaani mtoto utafikiri ndio anakua kwa jinsi alivyo, Alinishtukia kua nilikua nikimuangalia kifuani, hivyo alijifanya kuweka mtandio wake sawa huku akiangalia chini,.. Nilipomaliza kunawa, niliamka mezani ili nielekee chumbani kwangu, lakini ghafla nikashikwa mkono kisha nikaachiwa, alikua ni jeni alinishika mkono kisha akaniachia, kana kwamba kuna kitu anataka kusema ila anasita kusrma, jeni alikua ni mtoto mzuri alieumbika haswa, mtoto utafikiri kakiarabu kwa weupe wake,.. Sasa kwakua sikumuelewa ikabidi niondoke zangu na kuingia chumbani kwangu, na kuendelea kulala..... Kama dakika tano hivi mlango uligongwa kisha akaingia akiwa kashika grass ya maji ya kunywa, ikabidi niamke ili nimpokeee, mtoto wa watu alinikabidhi grass ile kwa heshma kubwa,... Lakini pia hakuondoka
"nasubiri grass niondoke nayo"
Aliongea hayo kisha akawa anaona aibu yaani yeye muda wote ni wakuangalia chini,
"asante "
Nilimpa grass ile ili aondoke nayo, lakini mwendo aliokua akiondoka nao ni mwendo wa kama hataki, kana kwamba hata hayo maji yenyewe kayaleta kimtego mtego tu, nikalitambua hilo mapema,.. Sasa jeni ile anafungua tu mlango nilimfuata pale mlangoni
"wewe kuna kitu unataka kusema ila sijui ni kwanini husemi"
"ni kweli lakini... Naogopa kusrma"
"we sema tu mi nitakuseidia, hata kama ni pesa nitakupa"
"wala staki pesa... Ivi nikuulize swali"
"uliza"
"ivi pesa na hisia unachagua nini"
"mmmhhh mbona swali gumu hilo"
"we nijibu tu hivyo hivyo hata kama ni gumu"
"mi nachagua vyote"
"nijibu kimoja jamani sheeeby"
Jeni alikua akiongea huku akifumba macho yaani kama mdoli vile,
"ok... Mi nachagua pesa, mana pesa ndo kila kitu mjini"
"mmhhhh basi mi naenda zangu kama wachagua pesa"
Jeni alisema anaondoka kama nimechagua pesa, lakini cha ajabu alilua haondoki...
"kwaio we ulitaka nichague nini labda"
"ungechagua hicho kingine"
"ok... Wacha nikichague kwa ajili yako"
"Eti eee?... Basi ngoja niipeleke hii grass kwanza"
Jeni alikimbia mbio kuipeleka grass ile, na mimi chumba changu kipo juu na yeye kashuka chini kwenda jikoni... Basi Mimi nikawa nanyoosha nyoosha kitanda huku nikiwa na shauku ya kumsubiri mana najya anachokitaka kwangu....
Mara ghafla mikono ya moto ilinipitia mbavuni kwangu,...
"mmhhh umerudi fasta fasta ee?"
Niliongea hivyo nikiwa bado nimegeukia kitandani na yeye yupo nyuma ya mgongo wangu,...
"nini"
Heeeeeee kumbe alikua sio jeni yule alionishika kiuno, aiseee kumbe ni dada yobi ndie aliokuja na kunishika kiuno, sasa pale pale nikabadiri maneno kua
"nasema leo umerudi fasta fasta kuliko hata jana"
"yes nimerudi kwa ajili yako..."
Sasa nilipotega skio vizuri niliskia sauti ya mtu anapanda ngazi kwa spidi kuja huku chumbani kwangu, kana kwamba huyo anaekuja ni jeni, na hajui kama dada yobi kaja,
"umeingiaje, mana sijaskia hata honi"
"nimeacha gari nje, nimeingia kwa geti ndogo"
Hapo sasa ndio kizaa zaa mana kama angepiga honi ni kwamba hata jeni asingekuja lakini hakupiga, hivyo jeni alivyoingia jikoni, na dada yobi nae ndio kaingia huku, hivyo hawakuonana,.... Mama yangu eee sasa itakuaje, na jeni nae ndio anakuja, mana naskia miguu ikija huku, na mbaya zaidi jeni anajua mimi na dada yobi ni ndugu, hivyo hatakiwi kujua kama ni wapenzi, lakini sii hivyo tu, pia jeni akiingia hapa dada yobi atamuuliza alikua anakuja kufanya nini chumbani kwangu... Nilikua nimeshikwa kiuno lakini nilihisi kama sijashikwa kiuno vile kwa huo mgongano ambao utatokea muda huu.... Sasa je nitamjulishaje jeni asije chumbani kwangu, mana dada yobi kaja... Na hata namba ya simu ya jeni sina.. Na ndio naskia anakaribia kufika
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikua natamani nipige kelele kua asije huku dada yobi keshafika, lakini nikiwa bado natafakari kuusiana na hilo, mara kuna wazo lilinijia baada ya kuona vumbi vumbi lililopo katika meza, hivyo lile vumbi ndilo lililonipa jibu la kujiseidia au kumzuia asije,
Sasa kwakua jeni alikua anakaribia kufika nilisogea kwenye ile meza ya kioo na kuigusa, ila haikua na vumbi jingi na hata hivyo lilikua vumbi la muda huu,..
"jeni, jeniii.."
Niliita mara mbili kwa haraka haraka, ili nijifanye hajasikia nimtokee,...
Nikapiga hatua ya kwanza na ya pili kisha tatu na nne, nimeshafika mlangoni... Nikampa ishara ya kwamba, dada yobi kaja yupo huku...... Afu apo apo nikaingizia na neno
"ebu njoo na dasta naona meza ina vumbi"
"sawa"
Alielewa kila kitu na swala zima likawa limeishia hapo,
"sheby, kwanini umenitoroka lakini"
"aahhh mi sikutaka kuaga afu ukaanza kutoa yale maneno yako utafikiri kweli ni mdogo wako, afu nikicheki pale mlikua wengi, nilihisi ungeniaibisha kwa kua hukawii kuniongelesha kama mdogo wako mbele za watu"
"mmhhh sorry kwa hilo, ila nikifanya hivyo ni kwamba naleta uhalisia wa kweli kua wewe ni mdogo wangu"
"sawa lakini ninapokuaga mi sioni sababu ya kunizuia,... Kwasababu watu watakuja jua kua unanizuia kwa maana gani"
"ookey nisamee basi mpenzi wangu,.. Ila kua unaniaga, na mbaya zaidi mpaka simu umezima"
"basi nisamee kwa hilo, but sababu ni wewe, mana ukiagwa hua huniruhusu bila maneno"
"okey basi tusameeane,.... Sasa ulikuja na gari gani"
"nilikuja na taxi tu"
"staki iwe hivyo, ngoja hii filamu tuimalizie kwanza then nitakununulia usafiri sawa"
"sawa my"
Basi dada yobi aliniahidi kuninunulia gari pale filamu yao itakapoisha, nami sikua na papara ya kulipa hilo gari mana kama ni usafiri sikosi popote, na hata hilo gari ni yeye ndio kapenda but kwa mimi sidhani kama nataka.....
Basi nilichukua simu yangu na kuiwasha mana niliizima muda mrefu kidogo toka nimtoroke dada yobi mpaka sasa ndio naiwasha,..
Ziliingia meseji nyingi sana za WhatsApp na zingine za kawaida,... Mawese katuma meseji kama mbili hivi,
"ona meseji zinavyoingia, watu wengi walikutafuta sana"
Sasa nikiwa naendelea kusoma meseji hizo, mara ghafla simu yangu ikaita, kucheki jina alikua ni mke wangu, aahhh sasa nikawa mzito kupokea lakini nikaipokea tu ili dada yobi asinishtukie kua simu hio ilikua ni ya mke wangu,
"haloo"
"jamani mume wangu inamana ulivyosema hurudi ni kweli"
"we ulifikiri nakutania eee"
"lakini kwanini unanifanyia hivyo... Na ni kwanini unapenda kazi za aina hio"
"mimi nilikuambia nimepata kazi lakini we hutaki nifanye kazi wataka tuangaliane tuuuu... Yaani wataka mi nirudi tena niwe FUNDI CHEREHANI? Haiwezekani kabisa"
"lakini mume wangu, tungaa chini tukaliongea"
"tuliongee na wakati hutaki"
Simu yangu haikua na sauti ya kumfanya dada yobi asikie, na hata hivyo nilikua nimewasha tv hapo chumbani kwangu, hivyo ni ngumu hata kwa kusikia kwa mbalimbali,
"okey ivi hizi pesa ulizoniachia ni kiasi gani"
"hizo pesa ni nyingi, zitakutunza mpaka utakapojifungua, ukisha jigungua usije ukategemea kua nitaleta pesa, hivyo zitumie kwa umakini sana... Mimi sileti pesa tena... Hizo ni shilingi milioni 10 na vichenchi, sasa chezea haribu fanya unachojua, afu saa unahitaji mahitaji ya mtoto staki simu nipo bize"
"oke, sawa mi nakubali, lakini basi uwe unakuja kutusalimia, kwani umepata wapi kazi"
"mama nipo Dar es Salaam"
"mtume roho yangu mie, mbali hivyo ibi utarudi kweli"
"unakumbuka nilishawahi kusema kua, naweza kurudi au nisirudi"
"mmmhhh lakini naomba uwe unakuja"
"sawa ila ondoa shaka mimi sifanyi kazi ya kutembea na watu tena, sasa hivi nipo ofisini kwa mtu sawa mama"
"sawa... Nakutakia kazi njema mume wangu"
"nawe pia"
Nilikata simu huku dada yobi akiwa ananiangaliaaa, kisha akanyanyuka na kusema.
"ivi sheby kumbe una mke na ana mimba"
"maskio yako mabovu ee"
"mabobu kivipi na wakati nimeskia sjui pesa itakuseidia mpaka utakapojifungua"
"ahahahahahaha ondoa shaka yobi... Huyo ni mama mdogo wangu, na akinitegemea mimi kwa kila mahitaji, mana mtu aliempa mimba kamkataa"
"ooohhhh maskini ya mungu, mpe pole"
"usijali"
Yaani napenda sana kumdanganya mwanamke mana anadanganyika vizuri mpaka raha yani,
Yule nimemdanganya kua kwa sasa sifanyi kazi ya kutembea na majimama, na ndicho kilichonileta mjini hiku... Huyu nae nimemdanganya kua huyo alikua ni mama yangu mdogo aliekua akinitegemea....
Muda wenyewe ulikua umekwenda kwani ilikua yapata mida ya saa 11 jioni, na hata dada yobi alikua anahitaji kutoka lakini aliposoma saa, aliairisha kutoka, hivyo akaenda zake chumbani kwake ili kujiweka mwili safi, wakati huo mimi nilikua zangu chumbani nikiwa naendelea kuangalia tv, Nilienda jikoni na kumkuta jeni akiendelea na kazi yake ya upishi kama mfanyakazi wa ndani, nilikwenda na kumtekenya, alipogeuka nikamrukia na denda zito, aisee jeni alikua alionekana kua na siku nyingi pasina kukutana na mwanaume mana hali hio ilijionyesha baada ya jeni kua na haraka ya kufanya kitu fulani, yaani alikua kama mtoto mwenye njaa ya kunyonya kwa muda mrefu,......Ghafla nikasikia mikanyago ya mtu inaelekea huku jikoni ambapo tupo mimi na jeni tena tulikua katika madhingira ya kimapenzi, nilipomuachia jeni alikua anahema juu juu utafikiri alikua akikimbizwa, ghafla dada yobi kaja.... Na ile hali ya kuhema juu juu mpaka macho kulegea iliendelea kwa kasi...
"mimi nitampiga huyu mfanyakazi wako ujue"
"ni nini jamani sheby,... Kakufanyaje kwani"
Nilijifanya nilikua nampiga mana alikua akihema juu juu na kutaka kuanguka kabisa, kwahio kwa hali hio ilinibidi nijifanye nilikua nataka kumpiga...
"saa ile mi namwambia aje afute ile meza, kaja kafuta kihuni huni afu kaondoka bado meza ina vumbi kiasi kile"
"jamani sheby usifanye ivyo lakini"
Basi dada yabi akawa kama anamtuliza, lakini dada yobi alikua kama anajiuliza mara mbilimbili kua, ni kipigo gani kinachomfanya mtu alegee na kurembua, lakini hakua akijipatia jibu kwa maana ni kila mtu kaumbwa kivyake, kuna mwingine akipigwa anacheka, na wakati anaumia sana tu lakini kilio chake ni kama kicheko....
Mimi niliondoka zangu na kuelekea chumbani kwangu kisha nikawa naendelea kutazama tv,...
Dada yobi aliingia chumbani kwani kwangu huku akiniuliza,
"ivi ulimpiga kipigo gani yule mtoto wa watu"
"si nilikua namkaba koromeo"
"jamani mtoto wa watu alikua kama anaanguka kifafa"
"atajua mwenyewe uko"
"naomba usifanye hivyo sawa mpenzi"
"sawa ila umkanye asinizoeee"
Hata hivyo jeni alikua ni mtamu kiasi flani yaani mtoto alikua ana kajoto kazuri sana kiasi kwamba, kajoto kake ni ka kipekee sana...
Dada yobi aliondoka zake na kwenda kuangalia tv sebuleni, mimi nikabaki zangu chumbani huku, nikiendelea kuchati.... Mara nikakumbuka kua simu yangu muda ule naiwasha nilipokea meseji nyingi sana, na hta za mawese zilikuwepo kama mbili hivi,... Nikaichukua simu yangu na kuitazama vizuri ili niweze kusoma zile sms ambazo sijazisoma kwa wakati ule, mana kama unakumbuka nilipigiwa simu na mke wangu na baada ya hapo sikizikumbuka tena,... Sasa kufungua meseji moja ya mawese iliandikwa
"we upo wapi dada yako anakutafuta ile mbaya"
Hii nadhani ni wakati ule nilipomtoroka,.. Sasa meseji yake ya pili iliingia huku upande wa WhatsApp, nikaingia WhatsApp na kuigungua ile meseji....
Mungu wangu eee, dada mawese kuna picha mbili alinitumia mpaka nikajikuta nafumba macho, na sijui ni kwanini aliamua kunitumia picha hizo,.. Huku zikiambatana na maneno yalioandikwa hivi...
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Inapendeza sana pale unapoamua kuziangalia, ila inachukiza sana kama hupendi kuziangalia, Kiukweli dada wema alikua ni beautiful woman, yaani dada wema alijaaliwa kua na umbo zuri la kiafrika, kipindi wakati namuona katika movie nilikua nadhani labda anavaa nguo nyingi ili kufanya umbo lionekane lakini leo ndio kanidhibitishia, dada wema alioneka yupo bedroom peke yake akiwa kavalia ile nguo ambayo alinilazimisha nimpe, nadhani unaijua nguo hio niliompa jana, na hata haikua yakwake sema nilihofia kusambaa kwa taarifa ya kwamba nina tabia ya kuwanunulia watoto wa kike nguo za ndani, hivyo ikabidi nimpe tu, sasa leo ndio naziona picha hizo alizonitumia muda si mrefu, tena inaoneka alikua akitoka bathroom,.. Maneno alio yaandika katika picha hio yalikua ni maneno ya pongezi juu yangu..
"sheby jamani, ulijuaje kiuno changu, au ulishawahi kuniota tuko wote"
Aliandika hivyo katika picha ya kwanza alafu picha ya pili akaaindika....
"imenipendeza sana, yaani natamani niivae kila siku ya mungu... Asante sana sheby... But i have a one question for you"
Aliandika hivyo kisha hakuendelea tena ila mimi nikamwambia....
"just ask"
Mawese kuwepo online WhatsApp ni kama kawaida yake,... Ghafla ikaonekana imeshasomwa na kuona.... Mawese is typing...
"sorry lakini, nimekutumia picha za kikubwa pole kama kuna maumivu eti ee"
"wala usijali... Na hata sijaumia"
"mmmhhh kwanini usiumie sheby? Ok tuyaache hayo, nina swali nikulize"
"ok uliza tu"
"nimeivaa mwenyewe but hakuna atakae ivua"
Swali hilo kwangu lilikua rahisi sana lakini likua gumu pia, nilishindwa kumjibu nikazima mpaka data ya simu na kupumzika kidogo,... Nilipitiwa na usingizi mzito hadi kufika mida ya saa mbili hivi usiku, tena niliamshwa kwa ajili ya chakula,.....
"sheby leo una nini mdogo wangu"
Dada yobi aliniuliza hivyo mbele ya jeni, unajua tukiwa wenyewe tunaitana wapenzi lakini tukiwa na zaidi ya mtu wa tatu, basi hapo atanifanya kama mdogo wake,
"asee dada leo nimechoka sana"
"iv sheby utaweza kuigiza kweli wewe"
"ndio sema hizi siku mbili tatu kidogo zimekua ngumu kwangu, si unajua kua dar mi mgeni"
Basi yalikua ni maongezi ya kawaida tu huku tukiendelea kula, wakati huo jeni alishaondoka zake, kama kawida yake ya kulia jikoni,
"sheby mpenzi"
"sema"
"leo vp utakuja"
"mmmhhh na kuchoka huku? Sidhani kama nitafanya vizuri"
"weeeeeee inamana umechoka sana"
"tena zaidi ya sana"
"basi tufanye kesho eti ee"
Ghafla simu yangi ikaita, kucheki alikua ni mawese, (wema) nilikua najishauri kupokea lakini nikapiga moyo konde na kuipokea simu hio
"haloo"
"eeeeh sheby jamani mbona hujibu swali langu"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment