Search This Blog

Thursday, 19 May 2022

WALI NAZI - 5

 





    Chombezo : Wali Nazi

    Sehemu Ya Tano (5)



    Kibaridi nacho kilisawili vizuri kwenye mwili wangu kupoza damu yangu iliyokuwa ikichemka kutokana na mtanange ule. Usingizi nao hata ulipotokea sikujua wapi ulinichukua na kuchukulika nikiwa hoi.

                                                      ________

    Maumivu makali niliyasikia punde nilipoifumbua macho yangu cha ajabu sikuwa na mdada yule. Nikiwa mahali kwengine kabisa mikono yangu ikiwa imefungwa, na si mikono hata nilipojaribu kunyanyuka pia nilishindwa. Nilikukuruka lakini wapi nilishindwa, maumivu yalianza kunisurubu. Akili yangu nayo ilikuwa ikiwaza lile nilijua tu vyovyote itakuwa bosi Mchungoma ndio atakuwa ndio mhusika wa kile.

    Joto nalo lilikuwa kali mno ndani ya chumba kile kunguni nao waliamua kufanya mwili wangu , kama wa kwao walinichezea vya kutosha hata nilipojaribu kukabiliana nao ilikuwa kazi bure. Taratibu nikaanza kuizoea michezo yao kukiwa kimya mahali pale.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kiukweli nilikuwa nimepatikana hata nilipojalizimisha kujipapasa uwenda nitakutana na simu. Ahh…. wapi! Ilikuwa hola tu, uchungu ulinikamata kiasi cha kwamba mdomo wangu uliishia kutetemeka vibaya mno. Mihemo nayo ilibadilika kutoka kuhema taratibu. Mapigo ya moyo yangu yalivyoanza kudunda kwa nguvu utafikiri gari iliyopotea njia dereva anangahika kuipa uhai wa kurudi barabarani.



    Giza nalo lilikuwa lilikuwa ukishindana na mwanga lakini lenyewe lilionekana kushinda lile. Nilitamani kulia napo machozi yalikuwa mbali licha ya maumivu makali niliyokuwa nikiyapata kutokana na kukosa nafasi ya mikono yangu na miguu yangu. Nikiwa ndani ya chumba kile, nilijikaza kisabuni nikisubiri hatima yangu wakati huo pombe ilikuwa ishakisaliti kichwa changu kama yule mdada alivyonisaliti.



    Nilijilaamu kwa nini nilikunywa vile pombe, na hata sura ya Jimama Sophi ilivyokuwa ikinijia niliona kama mzimu. Moyo wangu ulishaanza kujenga chuki dhidi yake niliamini kuwa yeye ndio alikuwa chanzo cha yale yote.

    Ahhhhhhhhhhh! Niligumia maumivu niliyokuwa nikiyasikia kwenye mwili wangu kabla ya kumkumbuka Maria nilijifonza mwenyewe . Nilimwona mtu mbaya sana kwa upande wangu, mwanamke ambaye huwezi kumdhania hata kidogo kama angekuwa na tabia za kiumbeya mbeya kiasi kile.



    Nilikukuruka kwa mara nyingine, kwa muda kidogo hatimaye macho yangu yalianza kupoteza taswira. Kwa mbali nilizisikia sauti za watu wakizungumza jambo. Maongezi yenyewe hayakuwa yakisikika vizuri kwenye masikio yangu. Dakika kadhaa maji yalisawili mwilini mwangu, ikifatiwa na sauti nzito alikuwa akitoa ndugu yule aliyekuwa moja kati ya ndugu wale walijazia miili yao.

    Nilitamani kupiga kelele, lakini niliona kelele ingekuwa kazi bure, ‘’nisameheni’’ zilinitoka kama njugu kwenye kinywa changu. Nikiwa na tetemeka baada ya ubaridi ya maji yale, samahani zangu hazikufua dafu mbele ya taswira za watu wale. Waliniachia vibao vikali kwenye mashavu yangu huku wakinitazama kwa nyuso za ukatili. Ghafla nilijikuta haja ndogo inatoka bila ya hata kujielewa , ilianza kuchulizika taratibu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndugu wale waliishia kucheka, na maneno yaliyokuwa yanawatoka yalijaa shari, hakukuwa na heri eneo lile. Mmoja alinisogelea pale nilipo akiwa anavuta sigara na kuja kunipumulia moshi,ulinifanya nikohoe kwa sekunde kadhaa. Mwili ulizidi kuchemka suala la kupona mbele ya watu wale hatakama ningekuwa sijafungwa mikono bado lingekuwa ngumu tu. Mwili wangu wa kawaida kushindana na mibaba iliyoonekana mipande ya watu ilikuwa nikujisabishia kifo wazi wazi.



    Walinifinya nikafinyika maumivu makali sasa yalicheza katika kila sehemu ya mwili wangu. Wakati huo sura yangu nilikuwa nimeinamisha chini . Nilisikikia makofi ya kipigwa na watu kadhaa wakija kuingia eneo lile. Suti kali kiatu cha mchongoko ilinifanya nijue ugeni ule ulikuwa wanani punde tu niliponyanyua sura yangu kutazama kile.



    Bosi mchongoma alikuwa mahali pale nilitamani niifiche sura yangu, jambo liliokuwa gumu. Ni ngewezaje? Roho yangu sasa nilishamkabidhi kibopa yule maumivu makali niliyokuwa nikiyasikia nilitamani nife tu kuliko kuendelea kuishi. Alipiga hatua mpaka nilipokuwepo alichukua mkongoja wake na kiinua shingo yangu iliyokuwa imelainika vibaya kutokana na kibano nilichokuwa nimekipokea kutoka kwa ile mipande ya baba. Sikuwa na neno la kusema mdomo wangu ulikuwa mzito huku baadhi ya sehemu za mwili wangu zikivuja damu.



    Nilishangaa akiniangalia kisha akitoa maigizo kwa moja ya wale watu kabla ajaondoka eneo lile.

    Moyo wangu ulidunda kweli, kifo nacho hakikuwa mbali eneo lile sikuwa na jinsi nilishakubali yote. Wakati huo wale watu walipiga hatua na kutoka na bosi Mchungoma. Kimya nacho kilichukua nafasi kwa muda mfupi kabla ya kufukuzwa na sauti za maumivu kutoka kwangu aaaaaaaaaaah.issssssssssshiiiiiiiii, niligulia maumivu kwa namna yake. Nikisubiri hatima yangu sikuweza hata kuisikia njaa japo sikuwa nimepata kitu tumboni tangia usiku wa kuamkia siku ile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maumivu yaliendelea kuunyasa mwili wangu, nikiwa pekee yangu mahali pale, vikunguni sumbufu waliendelea mchezo wao na safari hii hawakuona sehemu zingine bali walicheza sehemu zile zile nilizokuwa nikisikia maumivu makali.

    Haikuwa nusu saa wala lisaa niliweza kusikia mtu akijaa eneo lile , Mapigo wangu ya moyo walipiga kwa nguvu kwa muda mrefu hatimaye ya kapunguza kasi yakarudi katika hali yake ya kawaida akili yangu haikuwa ikifikiria kuwa ningeweza kutoka katika mdomo ule wa mamba. Hali ya hatari ndio ilikuwa ikicheza kwenye kichwa changu. Nikijiapiza kama nitafanikiwa kutoka pale Safari ya kurudi Tanga ndio ilikuwa inafatia. Sikuona haja ya kubaki eneo jiji la Dar, wakati tayari nishakuwa na maadui upande wangu.

    Nilikumbuka hadithi ya mjomba kuhusu tabia za vibosilie wengi wa kijua unatembea na wake zao. Hadithi ambayo mwanzoni alivyokuwa akiniadithia nilikuwa nikicheka. Nikiona kama porojo tu, lakini jinsi maumivu niliyokuwa nikiyapata nilikubaliana nae kabisa juu ya hadithi yake ile.



    Hadithi niliyokuwa nikiona imejaa vituko na mambo ya kubuni tu. Nilitamani hata kulia nikiwa pale hofu ya kurudiwa na watu wale kuja kunipa kibano ilinifanya nilie ndani kwa ndani huku machozi yakiendelea kuchulizika kwenye uso wangu utadhani mtoto. Makamasi nayo yakachukua nafasi ya kusindikiza kilio kile cha uchungu kikiwa kimejaa majuto. Kilio kilile cha kimya kimya kilinifanaya hata kupoteza nguvu usingizi nao ukanichukua

                                          *******

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niache… niache braza acha usifanye hivyo mungu apendi, aahhhh!!. achaaaaaaaaa. Niligumia wakati nikiwa nimezungukwa na na mipande wa mibaba. Wawili wakitumia nguvu kuniweka sawa, mwingine akivuta nguo yangu nilikuwa nimevaa kwenda chini. Nilikuruka lakini wapi walinizidi ubavu. Kabla ya kuanza kucheza na maeneo yangu ya nyuma, mkononi akiwa na kikopo cha mafuta ya kupaka. Aliyechukua na kuyapaka kwenye mtalimbo wake kabla ya kuja kuupaka maeneo yangu ya nyuma na kuanza kutafutia njia ya kupenya. Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah…. nooooooooooo!!.

    ______

    Nilijikuta napiga kelele nikiwa usingizini mule baada ya kufumbua macho kuangaza huku na huku. Nikijipapasa kwenye mwili wangu. Na kutazama kila pembembe mahali pale cha ajabu sikuona mtu. Ishhhhhhhhh! Kumbe nilikuwa nikiota ndoto ambayo sasa ilikuwa ikinitisha tangu hapo nilipokuwa kwenye usingizi mpaka nilivyokuwa nimeamka. Nikiomba Mungu bora waniue si kunifanyia mchezo ule. Nikimbuka jinsi mishindo niliyokuwa nikitoa nikutumia mbinu zangu za wali nazi. Leo mwanaume aje eti kucheza na sehemu zangu za nyuma aahhhh! Sikuwa tayari ilo kutokea . Ijapokuwa nishawai kusikia watu wakisema mara nyingi Dar wakikufumania anatembea na mke wa mtu hiyo ndio adhabu yao kubwa.



    Akili yangu haikutulia kabisa, baada ya muda, giza nalo lilizidi kuongezeka mahali pale hata ule mwanga nilikuwa nikiona kwa mbali sikuona tena .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafla nilizisikia hatua za watu wakija ndani mule. Safari hii hakuna aliyeniongelesha niliona tu wakinifungua miguu na mikono kabla ya kunivalisha kitambaa kwenye macho yangu. Nakuniamrisha niongoze wakiwa wamenishika mkono taratibu tuliongoza. Nilishangaa tunaingia kwenye gari, sikuweza kuisikia sauti ya wale na mimi nilikaa kimya huku nikiomba dua tu waweze kuniachia roho yangu. Mwendo wa lisaa na dakika kadhaa gari lile liponguza mwendo taratibu hatimaye lilipaki. Niliamrishwa kutoka kabla sijachiwa makofi kadhaa , na watu wale kuwasha gari na kuondoka eneo lile kwa kasi.



    Nilihisi kama naota vile, nilifikicha macho yangu hali ilikuwa vile japo macho yangu yalichelewa kufahamu eneo lile, lakini baada ya muda niliweza fahamu . Barabara ya vumbi ilisiwili miguu yangu pindi nilipokanyaga, kikiwa na vichaka kadhaa japo kulikuwa na giza. Mwanga wa mbala mwezi ulikuwa ukipiga kwenye macho yangu uliweza kuelekeza njia ile ilipokuwa ikielekea. Nilitafakari nikiwa na maumivu makali hatimye nilianza kusonga kueleka kule kichwa changu kilikuwa kinaniamua . Nilijivuta nikiwa na chechemea wakati huo nilikuwa na kikaputura tu. Nilipiga hatua kadhaa kwa muda kama wadakika kumi ndipo nilianza kusikia miungurumo ya magari.



    Nilitabasamu, tabasamu ambalo lilikuwa hafifu kiasi fulani kutokana na maumivu niliyokuwa nikiyasikia kwenye mwili wangu. Japo lilileta faraja kwa muda kidogo. Nakuleta matumaini ndani ya kichwa changu. Kabla sijaongeza hatua kuifata ile njia, kiuwoga nacho kilikuwa kimenitawala. Mwanaume nilijiongeza na kukaza nikiamini kama ningetakiwa kufa basi mapema ningekufa kule nilipokutana na watu katilii, ukatilii ambao nilizoea kuwona tu kwenye runinga, ama kusimuliwa na mjomba kama kwaida yake.



    Loo! Siku iyo nilikutana nao, na hapo haikuwa hadithi kama hadithi zingine. Hadithi zilizokuwa zikifanya nikinue hadi jino langu la mwisho pindi zipenyapo kwenye masikio yangu .

    Namna nilivyokuwa nikiongeza njia ile hatimaye kigiza kile cha usiku kilianza kuchanganyika na nuru kwenye macho yangu, ukaribishwaji wa nuru ile iliyokuwa ikitolewa na wenye haki ya kuitoa kwa wale waliokuwa wanauwezo wa kuipata hiyo.

    Nilijisogeza tena kwa umbali havikuwa vitu vingine bali zilikuwa ni taa ambazo zilikuwa zikitumia umeme. Umeme ambao ulikuwa ukimilikiwa na wale walikuwa wa kuitwa tanesco.



    Nuru ile ilizidi kuleta matumaini ndani ya kichwa changu, tofauti na mwanzoni nilivyokuwemo kwenye kimsitu kile nikiohofia uwepo wa wanyama wa kali, loo! kumbe hakikuwa kamsitu cha kutisha sana wala nini?.  Ni moja ya vijimisitu michache vilivyokuwa vimenusulika na wakata mkaa , kwenye hadhima yao ya kufanikisha kupata pesa kupitia kazi hiyo.



    Sauti za mingurumo ya magari safari hii nayo iliongezeka kwenye masikio yangu nakuleta nguvu kwenye miguu yangu, iliyokuwa imechoka hapo awali kutokana na shughuli niliyokuwa nimeipokea. Sasa ilipata nguvu na kuanza kuifakamia njia ile kuelekea kule ilipokuwa inasikikia miungurumo hiyo ya magari nikiamini, ingeweza walau kuleta tumaini la kufika nyumbani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Miguu nayo haikuchoka iliifakamia kweli ile njia hatimaye nilionana na njia kubwa, japo sikuona uwepo wa daladala wala magari madogo wakipita eneo lile , magari makubwa yaliendelea kupita kwa muda. Macho yangu yaliendelea kupambana kutafuta walau basi la abiria kutoka eneo lile ambalo niliweza kuhisi kusingekuwa mkoani Dar kabisa, maana hata zile gari ndogo zilikuwa zimesanifiwa na mistari kwenye mbavu za magari hayo,ikiwa mbele ya gari hizo yakiandikwa majina, kumlahisishia mwendeji huko aendapo. Macho yangu hayakuweza kuziona kabisa, niliendelea kusubiri japo ningeweza kuziona.



    Naam! muda ulienda, kibaridi nacho kiliendelea kupita kwenye mwili wangu , kuongeza maumivu yaliyokuwa yakipenya kwenye kila kona ya mwili wangu.

    Wakati nikiangahika, hatimaye macho yangu yaliona kigari cha abiria kwa mbali japo hiki hakikuwa kimechorwa kama zile zingine. Nilinyanyua kwapa kama polisi kusimamisha gari lile . Dah! kwapa nalo lilikuwa zito, likionesha usaliti mbele yangu. Maana kila nilivyokuwa nikinyanyua mkono ulikuwa kama hautaki huku nikiona gari lile likiwa linanikaribia.

    ________

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuhangahika sana hatimaye nilipata gari la kuniwezesha kurudi nyumbani, nikiwa nimaumivu makali. Siku zilizofata nilienda hospitali nikapatiwa matibabu, hatimaye jiji la Dar lilinishinda nikamua kurudi nyumbani Tanga kabla sijaona na wewe ndugu muandishi mkoani hapa Morogoro ambapo ndio maisha yangu yapo hapa, kwa sasa nimeoa na nina mtoto moja, na licha ya kuoa kwangu sikuwahi kumtamani tena mke wa mtu hata kama ikiwa kwa bure nimeamua kukaa mbali kabisa  na mimi kufanya shughuli zangu uzuri nina mke wangu, nimeamua kutoa mkasa wangu huu ili ndugu wasomaji waweze kujifunza na kujua athari za kutembea na wake za watu maana mimi naweza sema niliponyeka tu.  Sina mengi ya ziada ndugu nadhani tutazidi kuona na kutemebeleana.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog