Search This Blog

Thursday, 19 May 2022

UTAMU WA TUNDA - 5

 





    Chombezo : Utamu Wa Tunda

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilipishia.Mama alikwisha kuongea yale naye kumkaribisha kijana ili aingie chumbani mwa binti Happy naye aliingia na ndipo alipo mtazama Happy kijana yule moyo wake ulikwenda mbio sana….?, na kumsogelea kwa ukalibu binti Happy huku naye Happy alipomwona kijana Yule wala hakuwa na raha yoyote ile ila alitaka kumfurahisha nafsi yake tu..“mambo Happy!”“poa” aliitika kwa kinyonge binti Happy hukuakimtizama kijana yule ambaye hakuwai hata siku moja kumwona licha ya kuwa akisikia tu taharifa zake kipindi yuko masomoni naye,“naitwa Clinton”“nafurahi kukujua Clinton” alijibu huku akitizama chini binti Happy“okay sawa Happy natumaini tutajuana vizuri” Clinton aliongea huku akimwachia tabasamu kali binti Happy naye kutoka chumbani mwa Happy na kurudi tena sebureni alipokuwa kamwacha baba yake pamoja na wazazi wake Happy.Alifika sebureni na kukaa pembeni ya baba yake na kusonya naye kidogo huku akimsifia kuwa kamchagulia msichana mzuri“daaaaaah! Dady Happy kweli Happy kweli name nimeridhia kuwa naye binti huyu”“mmmmmmm! Kweli mwanangu!”“yah! Dady”Basi mama Happy pamoja na Baba Happy walikuwa wakimtizama Baba yake Clinton pamoja na mtoto wake wakiwa kwenye hali iliokuwa ikiwalidhisha kwani walipokuwa wakinong’onezana tabasamu kwa mbali kuonesha kuwa Clinton kampenda binti yao licha ya kumwona siku ya kwanza basi wazazi wake Happy walishikana mikono huku baba mtu akiwa kwenye tabasamu kali na mama naye huku akiwa hana furaha yoyote ile kwani alikuwa akijua kuwa binti yake anamimba ya kijana Hans, ndipo Baba yake Clinton alipoona mda wake wa kuwa pale umefika tamati ilimbidi ajiongeze kuagafamilia ya binti Happy ili wakajipange vizuri kuja kumchukua binti Happy ili akaishi na mwanae Clinton.“haaaaa! Mzee mwenzangu mimi mda umenitupa mkono kuna mahali nahitajika tutazidi kupanga na kufanikisha zoezi hili”“okay sawa mzee mwenzangu name sitakutupa mkono

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    tutalifanikisha”Walishikana mikono wawili hao na kuondoka kwa baba yake Clinton, Baba Happy alimtoa mzee mwenzake na aliporudindani mama Happy alikuwa akimsubilia kwahamu sana sebureni ili kufunguka kwa kile kilichokuwa kikiendelea nyumba ya pazia kwa binti yake.“mumewangu mwanao kama unavyo msikia kukubali kwa hili unalo taka kufanya kwa sasa”“mkewangu acha fikira hizo siku zote nakuambia mimi ni kichwa cha familia Happy atakubali tu?“mmmmmm!” ulisikika mguno wa mama Happy pembeni na kubaki akijisemea mwenyewe juuu ya jambo hilo..Happy alibaki chumbani akiwaza nini afanyejuuu ya kile baba yake anachotaka kumlazimisha kufanya huku moyoni mwake hakukuwa na makubaliano ya kitu hicho, aliwaza sana huku akibadilisha mapozi kitandani mwake na ndipo alipoona njia sahihi ni mama yake naye alitoka chumbani mwake na kuelekea sebureni na kumkuta mama kashika kichwa huku akiwaza sana naye taratibu alijisogeza mpaka pembezoni kidogo kwa mama yake alipokuwa kaka naye kumshika kwa nyuma, mama alishitukasana.“we Happy kulikoni”“hamna mama nimekuja tu nakuona uko na mawazo mengi”“ungejua mwanangu hapa nakufikilia wewe tu”“mama mimi tena!!!!!! nini hicho”“kuolewa mwanangu na kijana Clinton baba yako yuko na msimamo wa hali ya juu”“mama mimi kuolewa naolewa lakini siyo kwa mtu ambaye sijapanga kuolewa naye”Mama happy alishika kichwa chake aliposikia yale maneno yaliokuwa yakitoka kinywani mwa binti yake na kumfanya kuchanganyikiwaZaidi, na ndipo mama alipo nyanyuka mahali alipokuwa kaketi na kusimama.“mwanangu unasemaaaa nini au sijakueewa?”“mama mimi sitoolewa na mtu ambaye sijapanga kuolewa naye” Happy alijibu hukuakiwa na msisitizo“mwanangu kaa chini na fikiria sana kauli zako hii bahati mwanangu”“mama mapenzi si pesa……………..!!!!” Happy alimalizia kusema vile na kurudi chumbani mwake kuendelea kuuguza kidonda chake cha kufikilia ni jinsi gani wataweza kufanikisha kumwelewa kijana Hans na siyo Clinton.Mama alimwangalia mwanae Happy akiondoka huku akiwa na msimamo wake ule ule huku ukimfanya kuchanganyikiwaZaidi naye kujitupa kwenye sofa lililopo karibu na kupitiwa na usingizi uliochukua takiribani nusu saa, alishituliwa na mumeweee naye kuinuka na kukaa vizuri.“Happy yuko wapi” Baba Happy aliuliza“yuko chumbani mwake”“okay sawa ngoja nikazungumuze nae”..Baba Happy alizungumza na kuanza kuufuata mlango wa binti yake na alipofika aligonga mlango naye baba kuingia ndani.“Happy!!!!!!!!!!!!!!!!”“yes dady” aliitika binti Happy“umeona mambo yameiva mwanangu usiniaibishe kwa rafiki yangu”“Babaaaaaaaaaaaaaaa?”“nini”“nimekwisha kukueleza hali yote”“usitake kuniambia kuhusu yule kijana mimi nilimuruhusu akukate kiu yako tu na siyo vinginevyo”“ukisema hivyo baba unakosea”“nakosea nini basi sasa mimi ndio baba yako na nimeshapitisha Clinton akuoe”“Baba hunipi haki yangu kama mtoto wako” Happy alizungumza maneno yale na yalimfanya baba yake kumwacha hoi huku akifikilia ni kweli ila atafanya nini na ni rafiki yake.Happy alichomoka chumbani na kumwacha baba yake akiwa ajielewi naye kupita sebureni mkuku huku speed ile ilimchanganya sana mama yake nae mama kumwita akini Happy hakuweza kugeuka, baada yam da mfupi Mama Happy alimwonamumewe naye akitoka kwa speed na alipofika sebureni tu“mke wangu Happy kapita hapa?”“ndiyo tena kwa speed kali sana kulikoni”“mtoto kaishakuwa ana akili sasa duuuuuuh!!!!” Baba alijibu huku akimwangalia nje ya geti, naye hakuweza kumwona.Happy alitokomea mpaka kwa kijana Hans na alipofika getoni mwa kijana Hans aliwezakumkuta akiwa anataka kutoka kwenda kwenye mizunguko yake ya kila siku naye kijana Hans alipo mwona mpenzi wake Happy alisitisha kile alichokuwa akifanya nan a kuingia naye getoni.“mpenzi wangu!!!!!!” aliita binti Happy“yes baby”“vipi ujaenda tu kwenye shughuri zako”“yah ndio nilikuwa najiandaaa mpenzi”“Okay vizuri lakini mpenzi?” alisita kuongea alipokwisha kuongea kitu kile“lakini nini”“familia yangu mpenzi”“nilikuambia Happy wazazi wako hawapendikuniona sasa na ninavyo mwogopa mama yako si atanipeleka segerea mimi”“usifikilie hivyo Hans”“nakwambia lakini mimi ni kijana nakupendaHappy mno”“kweli nami pia Hans” Happy alijibu huku akitabasamu na kuzidi kuchanganyikiwahuku mawazo yake yote akiwaza ndiye mume sahihi atakaye kuja kumuoa na siyo Clinton……



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hans alimpapasa papasa maeneo flani mwa binti Happy huku akimfanya kuwa na Amani na furaha wakati akiwa naye, kweli kijana Hans alikuwa fundi wa mapenzi kwani alipoanza kuzichezea chezea nywere za binti Happy huku akiupandisha mkono wakena kuushusha mpaka kona zote za kichwa cha binti Happy, Happy alizidiwa na kujisikiaraha kichwani mwake na kumpelekea kulala usingizi kwenye mapaja ya kijana Hans, aliuchapa usingizi mapajani mwa kijana Hans na kumpelekea kijana huyo kushindwakwenda kwenye mizunguko yake aliokuwa kapangaaa kwani ilimbidi ampeti peti na kumpa masham! sham! Ambayo alijua fika hato chomoka kwenda kwa kijana yoyote bali ni yeye tu.Ugovi ulizuka mama pamoja na Baba Happyjuu ya kukimbia kwa mwanao Happy mahali pasipojilikana huku ikionekana kuwa baba ndiye msababishi…………….!“umefanya nini mume wangu?” mama Happyaliuliza huku akimsogelea mumeweeee“mama Happy mbona sijafanya chochote kile licha ya kile nilichokuambia tu juuu ya Clinton na Happy wetu” baba alijitetea kwa mama Happy“hapana mbona mtoto ka toka mbio hivyooooo?”“huwenda kile nilichokuwa namweleza ndicho kimemchafua”“tunampata wapi sasa maana hapa kaishatokomea”“natoka sasa kwenda kumtafuta”..Baba Happy alipokwisha kuongea naye alianza kupiga hatua kwuelekea nje ili achukue gari ili akamtafute binti yao, lakini wakati akizikaribia kuta za mlango alisikia sauti ya mama Happy ikimwita.“mumewanguuuuuu”“yes sweet”“ebu ludi na wazo hapa” baba Happy alirudi na kuitika wito wa mama Happy naye kumfata alipo, na kumsikiliza.“nimekuita mume wangu unaonaje tukimpata Happy tumrudishe kwa UINGEREZA aendelee na masomo yake”“mmmmmmh na Clinton je? Baba aliuliza kwa mshangao“mtoto ataki kuolewa na Clinton au ujamwelewa”“siyo kwamba hivyo mama Happy”“ilaaaaaa!!!”“ngoja kwanza nikamtafute nikirudi tutaongea vizuri mke wangu”“sawaaaaaa!” mama aliitikia bila y ahata kumwelekeza mahala atakapo mpata binti yaoBaba happy alichomoka ndani na kwenda kumtafuta Happy nae alipita kila kichochoroalichokuwa akijua kuwa Happy uwenda atakuwa maeneo yale ila wapi alibaki kuchoma mafuta yake na kumkosa mtoto mpaka jioni aliporudi nyumbani, aligonga mlango na kufunguliwa naye aliye mfungulia mlango ule alikuwa ni Happy mwenyewe, baba alishituka kuona sura ya mwanae mlangoni.“wewe ulikuwa wapi”“kwa rafiki yangu? Happy alijibu kwa madoido huku akiuiga mguuu wake chini“mbona nimezunguka kote sikukuona”“dady nilikuwa kwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    rafiki yangu”“sawaaaa”..Baba aliingia ndani na kwenda moja kwa moja mpaka chumbani mwake na ndipo alipo mwanzishia mke wake tifuuuu ambalo lilichukua mda kidogo kumalizika kwani baba Happy alionekana kutopenda kile kwa mwanane na kuamini ya kuwa mama yake ndio atakaye kuwa anahusika kwa kila alichokuwa akikifanya Happy.Zilipita wiki nne huku Harusi ya kijana Clinton pamoja na Happy ikipamba moto huku wana harusi hao hakuna hata moja aliekuwa akiwa na mazoea yam da mrefu na mwenzake licha ya kukutanisha mara kazaa huku mda mwingi kijana Clinton alikuwa akiutumia kutembea nab inti Happy huku akiwa hafahamu chochote juuu ya binti Happy, Clinton aliona siku zikizidi kuchelewa naye alimwomba binti Happy siku moja watoke huku naye Happy hakuwa na uwezo wa kukata ilibidi ampange siku ili waweze kukutana. Nao walipanga na siku ilipowadia wote wawili hao walikutana mahala faraga nje kidogo na kwao huku Happy mimba ikizidi kushika kasi licha haikuwa ikionekana sana naye alikuwa akivaa nguo zilizokuwa zikiendana na hali yake.“oooohoooooo! Happy nimefurahi kwa wito wangu kuutekeleza” aliongea Clinton huku akimtizama mtoto mzuri Happy“nami pia ahsante kwa kunireta mahara hapa”“lengo nililokuitia Happy ni kuhusu swala langu kwako natumaini kila kitu wakijua”“Clinton najua lakini?”“lakini nini Happy”“mimi siwezi Clinton kuolewa sasa”“Happy ukisema hivyo wakosea na ndoa imepangwa wiki hiii uoni utakuwa umenikosea mimi pamoja na wazazi wako kwa ujumla”“kweli Clinton” alijibu Happy huku akiunganisha na fundo la juisi ilikuwa mezani mwake“fikiria sana Happy napenda tuwe pamoja nawe kwani nimependezwa nae uwe mke wangu”Happy alishindwa kujibu naye alionekana kwa muoga kwani hakupenda kumsaliti mpenzi wake Hans, naye ilimbidi aombe kuondoka ili awai nyumbani kwani mda waliokuwa wamekutana ulikuwa umekwendamno, basi naye alichomoka na kurudi nyumbani na alipofika nyumbani alikuta watu wakiwa sebureni wakizungumza naye alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani mwake.Happy alifika chumbani na kuwaza sana huku akihesabu siku zilizokuwa zimebaki nakuona ni chache kwake kufanya uamuzi aliokuwa akiuona ni uamzi mgumu, ilimbidi apumzike kuondoa mawazo yote ya siku nzima naye kupitiwa na usingizi na aliposhituka tu kulikuwa kumekucha naye alichomoka asubuhi hiyo na kwenda kwa kijana Hans naye alikuwa kajilaza kwa shughuri ya siku iliopita ilionekana kuwa ngumu kwake naye binti Happy alipitiliza mpaka getoni mwa kijana Hans.“baby…..!” aliita binti Happy naye kijana Hans kuchungulia kwenye shuka na kumwona ni mpenzi wake“happy baby!”“mbona mpaka sasa uko kwenye shuka kurikoni”“uchovu tu Happy”Happy aliona kuwa ni vyema kupanda juu yakitanda ili amfanyie masaage kidogo ili kumuweka kuwa fiti, alianza kumminya minya kwenye mgongo wake…….!“umejuaje kama naitaji vitu kama hivyoooo!”“mmmmmh Hans bwana unanifanya sijui mtu akiwa kwenye hali kama yako huitaji nini”“sawa ndiyo najua leo baby”“hahahahhahaha sawa” alicheka na kumminya sehemu ambayo kijana Hans alipata raha huku akimwambia“hapo hapo Happy

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ”.“mmmmmmh wapi Hans?“juu kidogo ya kiuno………!” Hans alijibu hukuakivuta ule utamu uliokuwa ukipenyeza kwenye mgongo wakeHappy aliendelea kumpa kitu roho inapendaaaa mpaka hapo alipoona kijana karithika na kumwacha atulie kidogo, Hans aliona kuwa mbimba ya binti Happy ilikuwa ikizidi kushika kasi pale alipokuwa akiipapasaa na kuijulia hali.“Happy naona mimba inashika kasi vipi wazazi wako wanajua”“hakuna hata mmoja anayejua Zaidi yangu na wewe”“kwanini sasa Happy wafanya hivyo huku unaona kuna vitu vinataka kukwamisha ndoto zetu?”“no Hans mpenzi wangu wewe usijali”“mambo makubwa haya Happy”“yah! Najua”Hans alibaki akimwangalia Happy kwa kile alichokuwa akifanya kwa siri mdogo mdogo Hans alipata usingizi na kusahau kuwa alikuwa anatakiwa kwenda kwenye mizunguko huku Happy akizidi kuchezea mwili wa kijana Hans, Happy alikuwa kwenye kipindi kigumu huku akili yake ikiwaza sana siku ilikuwa umepangwa kufunga Harusi na kijana Clinton kufanya uamuzi ambao alikuwa akiujua mwenyewe kumsaliti kijana Hans au kumuumiza kijana Clinton. Naye yalipopita masaa kazaa huku akiwa getoni mwa kijana Hans huku akiona kuwa mda ukizidi kuyoyoma ilimbidi achomoke kurudi nyumbani, alimwacha kijana Hans huku akikoroma kitandani mwake naye kurudishia mlango na kuelekeanyumbani Happy alifika nyumbani na kuingia ndani lakini aliokuwa akikatiza kolido la sebureni naye alisikia sauti ya mama yake ikimwita.“Happy Happy Happy………………….!”“abe mama”“mbona siku hizi mbili tatu unatoka bila y ahata kuaga”“Hapana mama nilikuwa hapo kwa rafiki yangu tu”“rafikiiiiii?”“ndiyo mama”“sawa” naye Happy alijibu na kuelekea chumbani mwake..Baba Happy alirudi kutoka kwenye mizunguko yake naye alikuja na jipya pale alipomwita mama Happy pamoja na binti yao Happy nae kukaa nao wote ili wazungumze juuu ya kile kilichokuwa kikiendelea juu ya binti yao pamoja na kijana Clinton.“nimewaita hapa juu ya swala lla kijana Clinton nab inti yetu Happy”Baba alizungumuza maada ile Happy alishituka na kungoja kile kilchokuwa kikiendelea baba aliendelea tena kuongea, “tuko pamoja mpaka hapo”“ndiyo mume wangu” mama aliitikia huku Happy akiwa mdomo umejaa mate hawezi kutoa sauti yake,“jumamosi hii kwa mujibu wa upande wa piliHarusi itafungwa hiyo nikutokana na kijana Clinton kuwa likizo yake ya kukaa hapa bongo itakuwa inafikia tamati hivyo siku hiyo ndiyo imeteuliwa kuwa ya kuwaaga vijana wetu kwenye maisha yao mapya”“Baba Happy mbona mapema mno”“weeeeeeee? Mapema…” Baba aliuliza kwa jaziba huku akimtolea mama Happy macho makali, ukweli Baba Happy alitokea kubadilika sana sio kama kipendi cha nyuma mama Happy alikuwa akiwaza hayo.“ndio mume wangu”“basi ndiyo tumepanga kutokana na kijana wao kutaka kuondoka nab inti yetu”“sawa Happy tuko pamoja”Happy alishindwa kujibu na kunyanyuka kwenda chumbani mwake na alipofika alilia sana huku akiwaza “nini baba anafanya kwangu” ni maneno aliokuwa akiyatoa kinywani mwake huku akichuluzisha machozi yaliokuwa yakienda moja kwa mojampaka sakafuni, Baba Happy alibakia na mkewe sebureni huku akiendelea kutasiminijuu ya siku ya Harusi ya mtoto wao, ndipo Baba alipo mpa jukumu mkewe kwenda kumfanya mtoto wao ili asije kuwaaibisha siku ya Harusi kwani walimjua fika binti yao alivyokuwa kichaaa asiki wala kuelewa.Mama alikwenda moja kwa moja mpaka chumbani mwa Happy na kuanza kumtuliza“mwanangu kubali tu kuolewa na kijana Clinton hana neno mtoto wa watu”“mama we acha tu ujui ndio maana”“sawa lakini Baba yako anakutengenezeamazingira usije teseka mbeleni”“sawa mama” Happy aliitikia vile kumlizisha mama yake naye mama kutoka chumbani mwake...Zilipita siku kazaa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    huku ilikuwa imebakia siku moja kwenda kufanyika Harusi ya Clinton na Happy mtaa mzima ulijua kuwa binti Happy Harusi yake ni siku iliokuwa ikifuata, basi vijiweni usiku Hans katika pita pita yake alikutana na maada hiyo iliokuwa ikizungumziwa Harusi inayo kwenda kufanyika ni ya kimataifa kwani vijana waliokuwa wakizizungumza walikuwa wakitia na chumvi kiasi chake“heeeee mtoto mmoja hapo kati mzuri kishenzi kesho Harusi yake”“heeeeee yupi huyo mwanangu” kijana mmoja alidakia“si yule aliokuwa akiutikisa sana mtaaa wa hapo nyuma”“mmmmmmmh nani huyooo…?”“haaaaaaah kumbe yule binti Happy” aliitikiakijana wa pembeni“yah mwananngu ndio huyo huyo”Hans aliposikia vile aliendelea kusikiliza na kuwaza kwani siku mbili hizi hakuweza kuonana naye binti Happy na kuwaza kuwa binti Happy kaonesha udhaifu mkubwa, naye aliingilia kati mjadara ule kujua ni lini na wapi Harusi itafungwa.“hivi harusi ya huyo dada inafugwa wapi” aliuliza kijana Hans“kanisa la ushuwani…” alijibu kijana aliyekuwa akijua na mahari gani panapo fanyika harusi ileHans alitoka mdogo mdogo mpaka getoni mwake na kujitupa kitandani mwake na kuitafuta picha aliowai kumpatia kipindi cha nyumba binti Happy naye alianza kuitazamahuku akifikilia zile za chinichini alizokuwa akimpeleka binti Happy kwenye kilele, aliwaza sana ni wapi atapata kuponea kama sio kwa binti Happy alipitiwa na usingizi mpaka asubui.Kulikucha siku ya Jumamosi nayo familia yaBaba Happy ilianza maandalizi ya mwanao kwenda kanisani huku mda ulikuwa umepengwa kwa wawili hao kufunga ndoa ulikuwa ukishika kasi pale ilipofika saa sita mchana, kwa upande wa kijana Hans naye alichelewa sana kuamka kwani alikuwa kalewa chapaka chapa naye alipoona masaayakizidi kushika kasi alichomoka kitandani na kuanza kuzikamata njia za kwelekea kanisani………..Ilipofika wakati Clinton ndani ya suti pia Happy ndani ya shela huku wakisindikizwa na zigeregere na vifijo mpaka mazabauni mbele ya padre Clinton alimvua shela binti Happy ili wamalizie hatua ya mwisho, padre alianza kubaliki ndoa ile huku ikifata sauti za wawili hao kukubaliana kuwa mwili mmoja katika maisha yao…..“Clinton pamoja na Happy sogereaneni” ni maneno yaliokuwa yakitoka kwa padre“ndugu Clinton umekubali kumpokea binti Happy awe mke wako wa kufa na kuzikana….”“ndiyo nakubali” aliitikia kijana Clinton“nawe Happy unakubali kuwa na Clinton awe mume wako wa kufa na kuzikana”Ukimya ulitawala kwa binti Happy huku padre akingoja tamko la binti Happy naye alirudia kwa mara ya pili gafra sauti ilisikika ikitokea nyumaaaaaaa……



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Happy unanisalitiiii”ni sauti ya kijana Hans ilikuwa ikisikika huku akisogea eneo la tukio,Waumini na wote waliokuwa kwenye misa hiyo walipigwa na butwaa pale binti Happy aliposhindwa kuvumilia na kutoongea nae kutoka mbio mbele kwenye madhabau na kumfata kijana Hans, Nae alipomfikia kijana Hans aliwageukia waumini na wageni waalikwa nae bila y ahata woga alizungumza…..!“huyu ndiye nilie pendezwa naye” aliongea maneno yale machache bint Happy na kumshika mkono kijana Hans kutimuka wote kutoka ndani ya kanisaa.Wazazi wa pande zote mbili walibaki wakiwakwenye mshangaoo wa hali ya juuu huku mama Happy alikuwa akilaanai sana huku akimlalamikia mumeweee kwa kile alichokuwa akitaka kifanyike sasa kinawatia aibu…“mume wangu nilikuambia mtoto yule alivyoooo…!”“mke wangu sikujua haya yote”“sasa unaona hizi sura zetu tunazificha wapi?”“mke wangu mda huuu si wa kulalamiiana” Baba Happy aliongea maneno yale huku akiinamisha kichwa chake kwa ile aibu iliokuwa ikimsonga kichani mwake, basi naeilimbidi apite mlango wa nyuma ili kukimbia umati ule.Kijana Clinton alibaki akishangaaa huku akiwa na padre wakiwa madhabauni wawili hao walikuwa wakishangaana naye padre ndipo alipo muuliza kijana Clinton“kulikoni mke wako au mlikuja kuongopa mbele ya kanisa”“hapana padri mpaka sasa sijui kipi kinachoendelea”“ujui…?”“ndiyo sijui lolote mwenyezi mungu ananiona”Watu waliokuwa kwenye misa hiyo kila mmoja alitawanyika na kuiacha familia ya Clinton huku wakitafakali kile kilichotokea huku na kule walimtazama Baba yake Happywala hawakuweza kumwona kwani alikuwa ameshakwisha pita mlango wa nyuma na kuondoka..!“aibu hiii mke wangu tunaificha wapi” Baba Clinton alizungumza“kweli hiii aibu mno watu tumewapotezea mda wao wanatuona si sio wa maana”“mpaka rafiki yangu kakimbia” aliongea huku akishika kichwa naye kuchukua simu yake iliokuwa mfukoni na kumpigia Baba Happy, simu ilipokelewa naye hakuanza na salamu bali alimwagia madingo baba yake Happy mbele ya umati aliokuwa nao huku nao walikuwa wakimpandisha hasila naye kuikata simu huku akiendelea kulalamika kwa kile kilicho tokea, Basi nao walikuwa wamepoteza hela nyingi kwaajili ya kijana wao kuoa basi iliwabidi warudi nyumbani...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Happy pamoja na Hans walizdi kutimua mbio huku wakielekea mahara pa utulivu na walipofika mahali hapo walipumzika napo kulikiwa na upepo mzuri tena miti iliokuwa ikidondosha maua mazuri ambayo yaliwafanya kukaaa hapo mpaka makija ya jioni huku wakipiga story za kile kilichotokea kwa binti kutaka kumsaliti kijanHans .“Happy kwanini ulitaka kunisaliti” aliuliza kijana Hans“no Hans wala sikuwa na nia hiyoo”“inamaana nisinge kuja pale ndio ungekuwa mke halali wa yule kibalaka”“no Hans sijui tu lakini sikutamani iwe hivyokwani name nilipokuona tu nilijawa na nguvu za kuweza kuongea chochote”“mmmmmmh sawa”Mama Happy pamoja na mumewe walirudi nyumbani huku kila mmoja wao alipita njia yake…Walianza kuojiana kuhusu mtoto wao alipokimbilia basi kila mmoja wao hakuwezakujua mahali alipo naye mama alikuwa akijua mahali alipokuwa akiishi kijana Hans naye mama alitoka na kwenda kumtafuta binti yao lakini cha kushangaza hata alipofika hakuweza kumkuta mtu kwani getola kijana Hans lilikuwa limewekewa kufuri zito lilimwacha mama Happy kuwa kwenye mawazo kweli basi alianza kurudi nyumbani huku akiwa mnyonge lakini alipozidi kuiacha geto la kijana Hans alimwona Happy pamoja na kijana Hans wakiwa wanarudi naye aliwasubilia mpaka wafike kwani ndiyo ilikuwa njia ya kufika kwenye geto la kijana Hans.“Mamaaaaa! Unafata nini huku” Happy alimwona mama naye huku kijana Hans alitaka kukimbia naye Happy alipo mshika mkono wake huku akimzuia, mama alimsogelea mwanae Happy…….“Happy nini ulichofanya…?”“Mama toka mwanzo mimi niliwaambia kuwasijapendezwa naye”“hata kama mwanangu sio kwa kile ulichokionesha leo”“mama kila mtu huwa na haki ya msingi kuuseea moyo name ndivyo nilivyo fanya”“hata twende nyumbani”“mimi mama siendi nyumbani namuogopa Baba”“kwa kipi hasa unamuogopa baba yako”“si kwa tukio zima la leo”“mweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Ebu twende nyumbani”Mama aliongea huku akimtizama kijana Hans alivyokuwa kavaaa nae Happy pamoja na mama yake waliongozana kuelekea nyumbani, na walipofika walimkuta baba kichwa kikiwa kimejaa asila naye alipo mwona tu Happy alianza kupayuka ovyoo mpaka mtaa wa pili ulisikia kwa zile kelele zilizokuwa zikiendelea.“Happy nini umefanya………….”“Baba moyo wangu haukulizika na Clinton…..!”“ohooooo! Kumbe ndiyo kijana yule anakufundisha jinsi ya kujibu wazazi wako”Hapana Baba lakini sikuwa tayari kwa kile mlichokuwa mkifanya juu yangu name nilikuwa nikikataa lakini hamkuweza kunisikiliza kwa kile nilichokuwa naitaji Dady”Baba alichoka na kushusha pumzi huku akilegeza Tai aliokuwa kavaa huku akiona kuwa ikimbana sana, ndipo Mama Happy nae akaja juu huku akimlalamikia mme wakejuu ya kile alichokuwa akifanya juu ya mtotowao Happy na ndipo Baba alipo choka na kumwamulu binti yao Happy kumwita kijanaHans kwao ili aje kuwaona wazazi ili awe mume alali wa binti yao“Basi sawa namuitaji kijana huyo kesho sawa………”“kweli Baba…..”“ndio” Happy aliposikia vile moyo wake ulijawa na furaha kuwa Baba yake mzazi naye kalizika kuwa na Hans basi furaha zakezote alizikimbiza chumbani mwake huku akiuchezea mto huku akizidi kumkumbuka kijana Hans alivyokuwa akipeleka mashambulizi kwenye lango lake, kulikucha asubui sana Happy alichomoka nyumbani kwao na kuelekea kwa kijana Hans nae alipofika getoni mwa kijana Hans alipitiliza na kumkuta yuko na taulo lake basin aye alikaa pembeni yake huku akifurahi kupita kiasi huku akimtizama mara nyingi nyingi kijana Hans huku naye Hans alizidi kujiulizani kipi hasa juu ya binti Happy nae alifumbua kinywa chake nakuongea………….“Vipi Happy kulikoni furaha zote hizi…”“Ungekuwa moyono ungejua nini na furahia Hans.”“Mmmmmh nambiye

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    basi na mimi”Happy alizidi kutoa tabasamu lililozidi kumchanganya kijana Hans na ndipo alipo mtazama huku akishika nyuso yake na kuzungusha mikono yake huku akipa maneno mazuri…..“baby Baba kakubari na leo kaomba twende nyumbani mimi pamoja na wew”“heeeeeh kwenu Happy?“ndiyo baby” Happy aliongea huku akimsisitiza kijana Hans kuwa wazazi wake walikuwa wakimuuitaji….“naogopa mpenzi”“wanipenda kweli” ni maneno yaliokuwa yakimtoka binti Happy huku yakifatana…. Huku yakimuamasisha kijana Hans kujibu huku akijiamini….“ndiyo nakupenda tena sana Happy”“basi naomba fatana nami leo mpaka nyumbani”“okay sawa” Hans alijibu kwa kishingo upande huku akijua kuwa happy alikuwa akimtania…...Hans ilimbidi ajiandae vizuri naye Happy alikuwa na pesa kiasi alizokuwa kachomoa kwa wazazi wake basi waliingia mtaani kwenda kumtafutia kijana Hans japo nguo nzuri naye aonekane kuwa nazifu pindi atakapo kutana na wazazi wa binti Happy, walifanikiwa kupata mavazi yaliokuwa yakiendana na siku ile basi nao walirudi kwenye geto la kijana Hans na kubadilisha nguo ili waongozane na Happy mpaka kwaoili aonane na wazazi wa binti huyoooooo!. Walitoka na kuanza kupiga hatua kuelekea kwao na Happy huku kijana Hans alikuwa ajiamini kama ni kwelia au alikuwa akiota lakini binti Happy alionekana kuwa na nguvu lape alipokuwa akiongea nae huku akimfanya kuwa na ujasiri wa kuongea na wazazi wake licha yake kuwa muuoga…“karinu Hans…………………” Happy alimkaribisha kijana Hans mpaka ndani“asante japo mwenyeji hapa”“naomba nisubilie hapa dakika chache sawampenzi…”“sawa” Hans alijibu huku akiwa na huoga mwingi kwani alikuwa akimwogopa sana mama yake na HappyHappy alitoka na kwenda kuwaita wazazi wake waliokuwa chumbani, nao waliposikia kuwa kijana Hans kawasili basi walitoka chumbani na kwenda moja kwa moja

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mpakasebureni, na walipofika walimkuta kijana Hans akiwa tofauti na walivyokuwa wamezoea basi muonekano ule uliwafanya wazazi washituke na kumwona kuwa kijana mtanashati….“karibu kijana”“asante….” Aliitikia huku akitizama chuni huku akiwa hajiamini“kwanza hongera sana kijana umeonekana kuwa na ndamu nzuri iliompendeza mtoto wetu basi nasi tumelizia kuwa naye…….“asante baba” Hans alizidi kutojielewa mpaka wakati huo na ndipo alipoitwa HappyBasi walipomaliza kumkabizi kijana Hans nao walijumuika kwa pamoja kwa chakula kilichokuwa kimeandaliwa nab inti mzoefu Johari, basi Hans alianza kuzoea huku wakicheka na wazazi wa binti Happy. Katikati ya tafrija ile binti ndipo alipo zihilisha kuwa yuko na mimba ya kijana Hans wazazi wake walishanga japokuwa mama yake alikuwa akijua kila kilichokuwa kikiendelea basi nae Baba hakuwa na lolote la kufanya kwani alijuwa wazi binti yao kaishakuwa nae alipopewa taharifa ile wala hakuweza kuijia juu.Ulipita mwaka mmoja huku binti Happy pamoja na kijana Hans kupata mtoto mmojawa kiume huku wazazi wake Happy walisaidia sana huku waliwajengea nyumba nzuri na maisha ya kijana Hans yalibadilika pale baba Happy akimwajili kwenye kampuni yake na kumpa kitendo kijana Hans, naye Hans alizidi kuonesha juhudi kwenye kazi huku akimflaisha bosi wake mpaka alipo pandishwa cheo na kuwa na kitengo kikubwa….., Maisha yake yalikuwa mazuri huku akimfanya Happy ndiye jicho lake……………….. huku akilisamini mnooo……………………….



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog