Chombezo : Sema Jina Langu Mpenzi
Sehemu Ya Pili (2)
"oooooh aaaaaa"ni miguno ya maumivu niliyoyatoa baada ya kuamka na kujikuta nipo hospitali kichwa changu kilikua kimefungwa Bandeji kubwa iliyozunguka kichwa kizima nikajaribu kunyanyuka ili nikae kitako lakini nikazuiwa na nesi mmoja ambaye alionekana si muda mrefu alikuwa kashafisha kidonda changu kutokana na kuona baadhi ya bandeji iliyokuwa na damu damu na spirit katika chombo kama sinia flani hivi la plastic.kichwa changu kilikuwa kinauma sana huku kumbukumbu ya yote yaliotokea nikayakumbuka vizuri kabisa katika ubongo wangu.nilijikuta nikimuomba nesi japo niegeme mto kutokana nilikuwa nishachoka kulala ambapo bila ya kuchelewa alinisaidia bila ya hiyana kisha nikamuuliza.
"hivi dada kuna ndugu yangu yoyote amekuja??"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ndio pablo hebu pumzika kidogo"ilipita kama nusu saa nikiwa nipo katika dimbwi la mawazo nikiwaza je moureen yupo katika hali gani kwa sababu mara ya mwisho ni mimi ndiye niliyemsukumiza nakulivaa mimi gari.nikiwa katika hali hiyo ya mawazo ghafla mlango ukafungulia ndani ya wodi ya chumba hicho kisha macho yangu yakatua kwa shangazi yangu ambaye ndiye mlezi wangu kutokana na wazazi wangu kufa kitambo na yeye ndiye aliyenilea akiambatana na nurse,steve,rafiki yake moureen suzan na moureen mwenyewe.furaha yangu ilichomoza baada ya moureen kuniangalia kisha akachia tabasamu jambo lililonifanya kama najisikia afadhali vile kumbe bado.kila mtu akaanza kunipa pole kisha baada ya wao kuondoka moureen akaja mpaka kwangu kitandani akanibusu shavuni na kuniambia
"Thanks"kisha akaondoka.siku zilizidi kukatika huku hali yangu ikarudi kama kawaida na kuruhusiwa kuondoka katika hospitali hiyo lakini katika siku zote hizo nilizokaa moureen alikuja siku moja jambo ambalo mimi nilipoteza japo shangazi aliliulizia juujuu.shangazi akanichukua na kukaa kwake kama siku tatu hizi kisha akaridhika na kuniacha niendelee na chuo kama kawaida.hamu ya kwenda chuo ndio ilichukua nafasi na kujikuta Asubuhi na Mapema nishaamka na kujiandaa huku hamu kubwa ilikuwa kwenda kumuangalia moureen Msichana aliyeteka sana mtima wa moyo wangu.kama kawaida nilifika chuo na kuanza kuzungukazunguka ili kupoteza mida kutokana na kipindi changu kuchelewa kidogo kuanza.Ghafla nikiwa katika zungukazunguka yangu nikashtuka nikikumbatiwa kumbatio la Nguvu sana na nilipomuangalia anaye nikumbatia alikuwa si mwingine bali ni moureen jambo ambalo sikuliamini kabisa nikajikuta moyo ukidunda baada ya kuona madimpoz yake karibu kabisa ya macho yangu huku tabasamu zuri liliambatana na macho malegevu kama mtu aliyekula kungwi
"unajua katika maisha yangu sijawahi kufanyia kitu kama ulichonifanyia wewe Aa sina cha kukulipa ikafikia thamani ya upendo wako ulionionyesha kwa kuniokoa pablo thanks"
"aa...aaa...mmm...h usij..ali bana mbona kawaida..."
"Yani sasa wewe ndio rafiki yangu wa ukweli kuliko wote" Moureen alisema maneno yale huku akizidisha mbwembwe za kunikombatia jambo ambalo lilizidisha furaha kisha mdogomdogo tukaanza kutembea kuelekea darasani huku mkono wa moureen akiupita kiuoni kwangu nikafatia na mimi huku nikijikuta hisia zangu zikienda mbali baada ya kushika kiuoni cha moureen kilichovutia zaidi hapo ndipo mwanzo kabisa ya urafiki wangu na moureen.urafiki wetu ulizidi kukomaa jambo ambalo lilimkera steve na kuona nimempeperushia ndege wake baada ya moureen kuwa na mimi muda wote akiwepo chuo.chat za hapa na pale katika simu ndizo zilishamiri na nakumbuka siku moja nilirushia vocha ya laki mbili katika simu jambo ambalo lilikuwa geni kabisa katika Maisha yangu.siku moja jumamosi nakumbuka Moureen akiwa na gari lake akaamua kunitoa out tukaelekea katika moja katia ya beach nzuri za kuvutia katika maeneo ya kunduchi na kubadilishana Mawazo.hapo ndipo moureen alipoitaji kujua historia ya maisha yangu ambapo bila ya kuficha nilimuadithia mpaka kufa kwa wazazi wangu kwa ajali ya meri.Alinirudisha nyumbani kwa kutumia gari lake kisha Akaondoka lakini hakupita hata dakika kumi messeji ikaita katika simu yangu na kuonyesha kuwa ni moureen aliyetuma bila ya hiyana nikaifungua na kukuta
"Pablo katika maisha yangu nimeona wanaume wengi tu lakini kwako nimeona kitu ambacho nahisi nikiwa na wewe nitafarijika sana.ukiachilia mbali kuwa si desturi kwa msichana wa kiafrika kumtamikia moja kwa moja mvulana the way unavyojisikia lakini mimi sina budi kukuambia "Nakupenda pablo Nataka uwe mume wangu"............
Nikajikuta mara kumi kumi nikisoma messeji hiyo huku akili yangu ikiwa haimini kabisa juu ya suala hilo.kutongozwa na msichana huyo niliona kitu cha ajabu na bahati kubwa niliyopata nilihisi kama nimeokota dhahabu chooni.kwa furaha nikamjibu Moureen na kumwambia nimekubali na huo ndio ukawa mwanzo wa mahusiano yetu matamu baina ya mimi na moureen
*-*-*-*-*-*-*-*-*-*-*-*CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kelele za mashibiki ndio zilinipa hamasa kubwa ya kuuanza mpira huo uliokuwa chini ya mguu wangu ambao kwa hamu na hamasa ulikuwa ukisubiria filimbi ya mwamuzi ambaye bado alikuwa anarekebisharekebisha saa yake ya mkononi aliyoiamini kwa kuendesha dakika katika mtanange huo wa kutaka na shoka ambao kurudi kwangu uwanjani kuliwafanya mashabiki wa team yetu kuongezeka kwa furaha ya hali ya juu baada ya kukumbuka mchango wangu mkubwa kutokana na mechi sita za nyuma walifungwa kutokana na kutokuwepo kwangu.ilikuwa kama kawaida timu yetu ya orlando ilikuwa inamenyana na timu ya young bozy ambapo mshindi atachukua kitita cha shilingi laki moja ikiambatana na seti nzima ya jezi na mipira miwili.mwamuzi akapuliza kipyenga na kawa kawaida mimi nikauwanzisha mpira ule kwa mwenzagu ambaye pia naye akaurudisha nyuma kwa mabeki wengine.hakika kurudi kwangu kuliwazuia sana timu pinzani kushambulia kutokana na kuniogopa wakajikuta muda mwingi wakikaba sana na kusita kwenda mbele na kujikuta wakiniruhusu mimi kupiga kichwa baada ya kuunganisha safi krosi iliyopingwa na mwenzagu ambapo kichwa kile kilizaa goli ya kwanza na kutufanya tuongoze.rafu za hapa na pale hazikutuzia kuendelea kumiliki na kutokana na kupata mawenge nikafanikiwa kufunga goli la baada ya kuwapiga chenga mabeki wawili na kubaki na kipa na kufunga kirahisi.mechi iliendelea mpaka mwisho wa mchezo tukawatume wafunga tatu bila huku magoli yote nikifunga mimi na kwa shukrani nikakabidhiwa mpira.hakika tulishereherekea sana lakini kabla ya kuondoka uwanjani hapo nikaja kuitwa na mchezaji mwenzangu ambaye aliniambia kwamba naitwa nilipoangalia niliona gari aina ya Altezza mpya ambayo baada ya kuisogelea nikamuona moureen bila ya kusita nikapanda kisha tukaondoka hapo na kuwaacha miongoni mwa watu wakiwa wanasema yao.kabla hata hajanifikisha nyumbani simu yake ikaita na kuipokea na kuanza kuongea baada ya kumaliza akanambia
"baby leo nilitaka nikae na wewe siku nzima but nimepigia na mama inabidi niwai"siku sita kumzuia nikamuacha aende huku hatukachana hivi hivi tukanyonyana ndimi kama dakika 15 hivi kisha nikashuka kwenye gari yake na kuanza kwenda getoni kwangu ila kabla sijafika magari mawili meusi yakaniovertaking bila ya kujua wapi yalipotokea kisha wakashuka watu sita ambao bila ya kuuliza mmoja wao akanipiga na kitu kizito kichwani na kusababisha nizimie.....
Pwaaaaaaaaaaaaaa" sauti ya maji niliyomwagiwa usoni yalionishtusha kutoka katika usingizi mzito ulionikumba baada ya kuzimisha kwa kupigwa na kitu kizito ambacho kiukweli mpaka sasa sikuwa najua nini.nilifumbua macho na kujikuta nimekaa kwenye kiti huku mikono na miguu ikiwa imefungwa na kamba nzito zilizosababisha kutokuweza kufurukuta kabisa mdomo mwangu kulikuwa na plasta kubwa iliyokuwa imenizuia mimi kuongea jambo lilinifanya nianze kupata maumivu sana mdomo mwangu.maumivu ambayo pia hakusita kuniandama katika sehemu ya kichwa na mikono huku nikijikuta natamani niugulie kwa kutoa sauti lakini plasta niliyofungwa mdomo ndio ilinifanya niugulie tu kwa kuhema.kumbuku ya yaliotokea niliyakumbuka kwa haraka sana huku nikipata shauku kubwa kwa nini walikuwa wamenifanyia hivyo.macho yangu yalikuwa yakiangaza angaza sehemu hiyo niliyofungwa ambapo awali sikulitambua eneo hilo ambalo kwa kukisia tu niliona kama sehemu kama kiwandani hivi kutokana na ukubwa wa eneo hilo ambalo usafi wake kulitosha kabisa kusambaza hewa nzuri iliyonifanya Nijifariji sana kana kwamba nilikuwa tayari nina maumivu.Nikiwa bado naangaza angaza macho yangu katika eneo hilo ndipo nilipowaona watu kama saba hivi huku mmoja wao akionekana kama mtu mwenye pesa kutokana na suti yake kali aliyovaa viliambatana na viatu vyeusi vilivyong'aa na kofia safi uliyotulia kichwani kwake.Aliniangalia kisha akachia tabasamu pana na kuanza kunisogelea mpaka akanifikia akaniangalia kisha taratibu akaupeleka mkono wake katika mdomo wangu nakunifungua plasta iliyonifanya niugulie kutokana na maumivu makali sana.
"Kijana jisikie upo huru kwanza maana hapa upo mikono salama"
"we....we nani kwanza mnataka nini kwangu jamani mimi mnaniuonea tu jamani kwani nimefanya nini.."nilijikuta nikilalamika huku machozi yakinilenga hali ambayo ilimfanya yule jamaa acheke kisha akanisogelea kwa ukaribu na kunitandika kofi moja kali sana la uso lilisababisha nichanike shavuni kutokana na kucha ndefu mkononi mwake kisha akanishika mashauzi na kuniangalia kwa usoni na kunitemea mate jambo ambalo lilinitia hasira sana lakini kutokana na kufungwa nikaishia kudondosha chozi tu mashavuni kwanguCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"We fala mimi sijawai kupandishiwa na mbwa kama wewe na ukiendelea nitakupoteza Malaya wewe sasa unajua kosa lako???" akaniuliza swali ambalo kutokana na hasira ya kunitemea mate nikajikuta nikinyamaza huku bado hasira zangu zikizidi kupanda jambo ambalo pia lilizidi kumkasirisha yule jamaa ambapo kwa mara nyingine akanitandika kofi tena zito.
"Nakuuliza swali Mbona unibu swali langu je unalijua kosa lako??"
"Silijui Msenge wewe" nilimjibu kwa hasira na safari hii nikajikuta nikimtemea mimi mate jambo ambalo lilinigharimu akawaamrisha moja kati ya wafuasi wake mmoja aje kunipa ambao bila ya kuchelewa alikuja kwa kasi na kufyatua teke kali moja la kichwa lililopelekea mimi kudondoka chini kisha akaendelea kunikanyanga kanyanga tumboni na kichwani na mabuti yake ya kijeshi bila ya huruma na kunisabisha anitoe damu nyingi sana za kichwa na mdomo.aliendeleza kasi ya kunipiga mpaka yule jamaa alimuamuru akamzuia kisha akaja akaniinua na kunigisha magoti na kwa mara nyingine akavuta makoozi yake na kunitemea tena usoni. kisha akatoa picha yake mfukoni na kunionyesha.Macho yangu yalikuwa yanangalia kwa shida katika picha ile yalitua kwa mrembo mkali moureen ambaye alikuwepo katika picha hiyo jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine yalinisangaza
"unamjua huyu mwanamke"
"si.....m......ju..i"
"wewe ubishi wako ndio unakuponza hebu lete ile mashine ya shoti aruke ruke kidogo" hakupita hata dakika shoti ya umeme ikaletwa kisha ukachukuliwa waya miwili na kuchomekwa katika mbavu zangu kwa kutumia Aina fulani hivi ya kama vibanio na kisha yule jamaa akachukua rimoti na kukaa nayo.
"nakuuliza unamjua huyu mwanamke??"aliongea huku akinionyeshea picha ya moureen
"Nakwambia simjui msenge wewe!!"
"sawa bana"nilimsuhudia akabonyeza kitufe chekundu katika rimoti yake aliyoshika kisha nikaanza kutetemesha na shoti kali ya umeme huku nikipata maumivu makali sana.akaniacha na kuchukua na kuchukua bastola kisha akaiweka risasi na kuikoki akarekezea kichwani kwangu na kushababisha mimi nianze kutetemeka kutokana kuanzia nizaliwe sikuwahi kuonyeshewa bastola
"ni kwa mara ya mwisho na kuuliza unamjua huyu Mwanamke???"
"M..m....m...h..........."
"Paaaaaaaaaaaaaaaa".......
Namjuaaaaaa"nilijikuta nikiropoka kwa nguvu baada ya yule jamaa kupiga risasi karibia kabisa na mguu wangu risasi ambayo haikunipata lakini kutokana na mlio wake niliousikia vizuri kabisa katika masikio nikajikuta nakubali kutaja mwanamke Ambaye nilikuwa namjua lakini sikutaka kumwambia moja kwa moja
"Hahaha sasa unavyoringa ringa kunijibu nitakufumua ubongo mimi haya anaitwa nani..??"
"Moureen"
"oooh kumbe kweli unamjua je ni nani yako huyu"
"aaaa ni rafiki yangu tu"
"anhaaa kumbe rafiki yako basi subiri."nilimshuhudia akikoki tena bunduki na safari alionekana yupo serias kisha akaelekeza katika kichwa changu kwa lengo la kuniuma
"Subiriiiii sio rafiki yangu ni msichana wangu"
"Aaaa mbona unanisumbua kijana unajua nitakuuuua."
"Hamna usifanye hivyo"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa sikia nikwambie huyo moureen ni mwanamke wangu ambaye nasubiri muda tu Amalize kusoma nimuoe nishatoa kiasi kikubwa sana cha pesa kwa baba yake jambo ambalo hata yeye analijua sasa basi kuanzia sasa sitaki kukuona tena na moureen na kama ukikaidi ukawa hata unaongeaa naye mimi nakufutilia sana basi nitakuuua umenisikia Mimi ndio Robertson Mugalula Nakuambia Nitakuuuua" hakika maneno yale yaliniingia kabisa katika nafsi yangu huku majonzi na simanzi yaliukumba moyo wangu ambao tayari ulishazama katika penzi zito la msichana huyo.uoga wa kuuwawa na robertson Mugalula jamaa ambaye mwili wake ulikuwa wa mazoezi sana licha ya kuwa na sura nzuri ambayo ilidhirisha kabisa yeye ni handsome boy na sura yake ya Baby face.Machozi yalianza kunitiririka taratibu jambo ambalo lilimfanya robertson kuniangalia kwa dharau kubwa kisha akamuita kijana wake mmoja ambaye alimnong'oneza kitu kisha jamaa huyo akanisogelea nakunitandika ngumi kali sana ya kichwa iliyopelekea kiza kizito kinitokee macho mwangu na kuzimia.
"Oyaaaaaa Hebu Amka"ni sauti iliyoniamsha ikiambata na kofi zito la mgongo ambalo lilinipa maumivu kidogo.nilijikuta nipo katika gari ambalo vioo vyake vilionekana kama ni tinted ambavyo vilikuwa havionyeshi kabisa nje nilimuona jamaa aliyenipiga kofi akiwa kavaa miwani meusi na suti huku mwili wake ukiwa umejazia sana
"Tokaaa"
"eee...naa..aaam aya...aaa"nilijikuta nikijibu kwa kigugumizi kisha yule jamaa akafungua Mlango wa gari hilo kisha akanisukumiza kwa nguvu na kutoka katika gari hilo huku nikidondoka na kuumia mguu wangu wa kushoto kisha gari hilo haraka likaniacha mimi pale ambako baada ya kusimama nilipagundua mapema palikuwa ni pale pale waliponikamata jana yake ambapo palikuwa karibu kabisa na nyumbani.Nilifika nyumbani huku nikichechemea na kisha nikaingia haraka ndani kwangu bila mtu yoyote kuniona niliangalia saa iliyopo chumbani kwangu na kugundua ilikuwa kama saa kumi na mbili jioni.nilienda kuoga kisha nikajitupa kitandani na kuiwasha simu yangu iliyokuwa nimeiweka chini ya mto katika kitanda changu na kubonyeza kitufe cha kuwasha ambapo nikakuta missed call mia moja na messeji Themanini nikazifungua nakukuta nyingi zikiwa za moureen ambazo kwa utulivu nikaanza kuzisoma "vp baby mbona upoke na mbona ujaja chuo nimekumiss vp wewe"ilikuwa ni miongoni mwa messeji ambazo kabla hata sijaendelea simu tena ikaita na nilipoangalia nikaona jina la moureen mpenzi likitokea katika screen ya kioo cha simu yangu
"Haloo vp pablo jamani"
"Kesho nakuomba tuonane raha resort restaurant"
"lakin........"Nilikata simu kwa uchungu kisha nikamtumia sms saa ya mimi na yeye kuonana katika hotel hiyo ambayo mara nyingi tulipenda kwenda
*-*-*-*-*-*-*-*-*-*-*-*-*
Saa ziliyoyoma na giza likaachia mwanga uchomoze na kuashiria siku mpya inaanza.bila ya kupoteza muda mida ya saa nne nikiwa nimevaa nguo zangu zilizonipendezesha sana.Nikaiwasha simu yangu iliyokuwa nimeizima kutokana na moureen kunisumbua sana kisha Mdogo mdogo nikatoka na kuchukuwa bajaj ambayo hakuchukuwa hata dakika thelathini nilikuwa nimeshafika katika hotel hiyo raha resort ambayo baada kumlipa mwenye bajaji nikaingia na kuanza kumtafuta moureen ambaye alishanitumia messeji kwamba alishafika.Sura yangu ikagonga kwa mwanamke ambaye ilionyesha uzuni mkubwa katika sura yake huku mavazi aliyovaa yalimpendezesha sana nilienda na kumgusa bega ambapo bila ya hiyana akageuka na kunikombatia huku ajibenua na kupeleka mdomo wake katika mdomo wangu ambapo kwa uchungu na simanzi zito nikamtoa
"whats wrong(tatizo nini) mbona sikuelewi yani siku hizi mbili umetesa sana kwa sababu ya kukuwaza"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"oooh moureen nataka tuachane"
"sijakuelewa unasema???"
"na...taka tuach..anee"nilisema kwa shida baada ya kushuhudia kwa mara ya kwanza moureen akidondosha chozi na kuniangalia mimi hali ambayo ilipelekea na mimi chozi kunidondoka
"kisaaa...nini??"
"Ro..bert Mugalula Ndi..."nilijikuta nikisita huku jina hilo nililolitaja likamshtua kidogo moureen ambaye bado machozi yaliendelea kumtiririka huku akiniangalia
"Can i kiss you now(naweza kukubusu sasa)"moureen aliniuliza swali hilo katika hali ya sauti ya kudeka hali iliyosababisha nishindwe kujizuia na kumkombatia kwa nguvu moureen kisha wote tukaanza kudendeka huku kila moja kutojali watu ambao walionekana kushangazwa na tukio hilo lakini ghafla simu yangu ikaita jambo ambalo lilinishtua na kujikuta nikimtoa moureen ambaye hakuwa tayari kabisa kuniachia niliangalia kioo cha simu yangu na kuangalia namba inayonipigia na kukuta namba ngeni jambo ambalo lilinifanya nipokee simu kwa uoga
"Sali sala zako za Mwisho Bitch(malaya)"
................
Nilijikuta nikianza kutetemeka baada ya Namba hiyo kukata simu kabla hata sijaongea chochote.Macho yangu yalikuwa yamenitoka huku majasho yakianza kunitoka mwilini mwangu hali iliyosababisha Moureen aanze kunishangaa
"Whats wrong pablo??(tatizo nini)"moureen aliniuliza lakini sikumjibu nikaanza kurudi nyuma nyuma hali ambayo moureen bado alikuwa haelewi
"unaenda wapi sasa??"nilijikuta kama nimechanganyika na kuanza kukimbia na kuelekea nje jambo ambalo lilimfanya nae moureen naye kunikimbilia lakini kabla hata sijaufikia mlango wa kutokea Nje milio ya risasi ikanipitia karibu kabisa katika masikio yangu na kunikosa na kwenda kuwapata waliokuwa mbele yangu ambao papo hapo wakadondoka na kufa hapo hapo jambo ambalo lilishtua watu wote katika hotel na kusababisha watu kuanza kupiga makelele na kuanza kukimbia hovyo ndani ya hoteli bila ya kutojua risasi imetokea wapi.kukimbia hovyo hovyo kwa watu kulisaidia kwa kiasi kikubwa mimi kutoka nje lakini Nje ndipo kulikuwa Na magari mengi meusi ambayo baada ya kuyaona Nikajikuta nikirudi ndani na kupotezana kabisa na moureen aliyekuwa akinikimbilia lakini hakufanikiwa kunipa kutokana na hata yeye kuchanganyikiwa na milio ya risasi.niliingia ndani kabisa ya hoteli na kuelekea moja kwao moja katika Miongoni mwa meza kubwa na kujificha chini ya Meza hiyo.macho yangu yalishuhudia watu wote wakiambatana na Wafanyakazi wa hoteli hiyo wakikimbia na kuacha hoteli yote ikiwa tupu ni mimi tu ndio niliyebaki huku nikiwa nimejificha katika meza kubwa ambayo iliniwezesha kutoonekana na kuona yaliyokuwa yanaendelea.nikiwa katika hali ya kukodoa macho ghafla watu waliovaa suti kama kumi wakiongozana na Robertson mugalula wakiwa wameshika bunduki wakaingia katika hotel hiyo na kuanza kunitafuta kila pande na kilichozidi kuniogopesha walipoanza kuangalia pia chini ya meza zilizokuwa zimedondoka na kunipa hofu kubwa.nikiwa natetemeka huku Bado majasho yakiendelea kunitoka nikaanza kuomba dua ili Mungu aweze kufanya miujiza kutokana na hali kuwa Mbaya.kwa macho yangu niliona kiatu kikali aina ya foengo kikiwa kinakuja kabisa katika mezi niliyokuwa na kushababisha mimi nitulie na kujikunja tuli kama Nyoka na kuendelea kumuomba Mungu afanye miujiza yake.Alifika pale na kuianza kuishika meza hiyo ambayo mimi nikiwa chini ya meza hiyo akiwa na lengo la kuinyanyua.Akiwa katika harakati ya kuinyanyua ghafla king'ora cha mlio wa gari la polisi ulisikika kwa nguvu hali iliyomfanya aichie meza kisha kwa mwendo wa speed akanzaa kukimbia kwa kutoka nje akiambatana na wenzake.hapo ndipo na mimi nilipopata nafasi ya kutoka na kufanikiwa kuwachenga mapolisi ambao baada ya mimi kutoka ndipo walipoingia wakiwa wamejiandaa vya kutosha.hakika mihemo ya kunusurika ndio ilichukuwa nafasi yake katika mwili wangu huku nguo zangu nilizovaa zikiloa zote kutokana na majasho mengi yaliokuwa yakinitiririka.hakika ilikuwa ni jambo jipya kabisa katika maisha yangu kwa sababu sikuwahi kutokewa na msukosuko kama huu wakataka kabisa kuuliwa niliendelea kujilaumu sana kutokana na kukaidi onyo nililopewa lakini nguvu ya mapenzi ndio yalinifanya nishindwe kabisa kujihimili mwenyewe.hakika hata kwa muda huo kwenda nyumbani nilianza kupaogopa kwa sababu nilihisi kama watakuwa wanapajua.mawazo ya kwenda kwa shangazi yangu ndio yalichukua nafasi yake na kukata shauri ya kwenda kwa kuchukua bajaj ambayo nilitegemea kwa vyovyote itaweza kunifikisha haraka.nilienda kuchukua bajaj ambayo kwa haraka ikaanza kwenda huku nikiwa bado nawaza.nikiwa katika dibwi la mawazo ghalfa simu yangu ikaita nikajikuta nikiipokea bila hata ya kuangalia nani aliyekuwa anapiga.
"haloow baby vp upo salama??,upo wapi??" ilikuwa sauti ya moureen niliyosikia hakika nilivyochoka nilijikuta nikiikata simu hiyo kutokana na ukweli kwamba nilishajichokea na maisha lakini ile naikata tu messeji ikaingia kwa uvivu nikaiangalia na kukuta ni ile namba iliyonambia nisali sala zangu za mwisho na kunifanya moyo wangu tena uanze kudunda kwa kasi ya ajabu na kuchoka kabisa.kwa simanzi zito nikajikuta nikiifungua huku nikiwa na uoga kabisa wa kuisoma hiyo messeji iliyosomekaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"PABLO PABLO,UNAVYOFIKIRIA UNAWEZA UKANIZIDI AKILI HATA MIMI SASA BASI NATAKA UCHAGUE MOJA KUUA WEWE AU SHANGAZI YAKO NA FAMILIA WASIO NA HATIA HAHAHAHA CHAGUO NI LAKO" hakika macho yangu hayakuweza kuamini messeji ile iliyotumwa niliendelea kuisoma kwa kuirudia kama mara kumi hivi huku akili yangu haukataka kuamini kabisa kwamba mtego uliobaki nilikuwa siponi kabisa.Kwa haraka haraka nikamlipa mwenye bajaj na kushuka kutokana na kufikia karibu na maeneo ya nyumbani kwa shangazi nilitembea kwa tahadhari kwa kujifificha mpaka pembezoni kabisa karibia na nyumba ya shangazi.
"Eee Mungu wangu!!!!"nilijikuta nikilalamika baada ya macho yangu kutua kabisa katika nyumba ya shangazi huku njee magari kumi meusi yakiwa yamepaki nje ya nyumba yake.nilijikuta nikikata shauri ya kwenda lakini kabla hata sijanyanyua kwato zangu Nilimshuhudia robertson Mugalula akitoka ndani ya nyumba ya shangazi akiwa anasindikizwa na bodyguard zake wakiwa wamemkamata shangazi na mumewe aliambatana na mtoto wake wa kiume na kuingizwa ndani ya moja kati ya magari yale kumi meusi kisha nikaona vumbi tu likitumika baada ya magari hayo kuondoka kwa kasi ya ajabu............
Hakika nilijikuta nikiganda kama mtu aliyepigwa shoti kali sana mwili wangu uliokuwa umelowa jasho ndio ulizidi kumiminika majasho ambayo licha yakuwa hali ya hewa ni ya kawaida isiyoleta joto lakini mimi nililowa mwili mzima.Hali ya kukamatwa kwa shangazi yangu na familia yake ilileta gumzo mtaani hapo ambapo hakuchukua hata nusu saa Majirani walijaa na kila mtu akiwa anasema lake.Akili katika kichwa changu haikuweza kusoma chochote kila njia nilikuwa nikiifikiria ya kuweza kujikwamua katika hili nilikuwa sipati jibu.Siku sita kutoa machozi aliyokuwa yakinitiririka katika mashavu yangu huku nikiwa siamini kabisa kama Mapenzi ndio yalikuwa tatizo.Nikiwa katika dimbwi zito la mawazo simu yangu ya mkononi ikaita tena na kuingalia nakukuta Jina la moureen likitokea katika screen ya simu yangu nilijitutumua na kuiweka sikioni kwa hali ya unyonge
"Hey upo wapi moureen"
"baby ulitoka salama ba.."
"upo wapi??"
"nipo njiani naelekea home"
"basi njoo mitaa ya nyumbani mara moja sasa hivi"
"mm lakini..."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"lakini nini do you love me..njoo mara moja"
"love you baby nakuja"nilijikuta nikihema baada ya kumaliza na moureen ambaye nilimuambie aje nyumbani.Akili yangu ilishavurugika nakukubali liwalo na liwe kichwa changu kilikuwa kishapata usumbuzi wa tatizo hilo huku mawazo ya kuwapata shangazi na familia yake ndio ilichukua nafasi yake.niliamini sitaweza kumpata shangazi yangu bila moureen.Haraka haraka nikaenda duka la madawa na kununua dawa ya usingizi kisha haraka haraka nikachukua bodaboda ambayo kwa haraka ikaweza kunifikisha Mtani kwetu ambapo sikuweza kwenda katika nyumba yangu niliyopanga kutokana na kuogopa kupatikana kirahisi na robert mugalula.nikaenda dukani na kununua maji ambayo nikaweka ile dawa ya usingizi kisha nikaenda sehemu ambayo nilimwambia moureen aje hapo.Macho yangu yakatua katika gari kali jeusi la moureen ambalo mara ya kwanza nilitaka kukimbia kwa kuangalia vibaya labda linaweza likawa la kundi la akina robert lakini kutokana na kumjua vizuri niliweza kumtambua kupitia kioo cha gari yake.bila ya kuchelewa moureen akafunga breki na kufungua mlango wa gari yake na kuniruhusu mimi kupanda nikaingia na ukaribisho wa mabusu mazito na moureen ambaye aliyeonekana kuumisi sana mchezo huo ambayo kwa wakati huo sikuwa na hamu nao.mkononi mwangu nilikuwa nimeshika chupa yangu ya maji ambayo kwa taratibu nikapa maji hayo moureen
"moureen unaonekana una kiu hebu kunywa maji haya kidogo"
"jamani umejuaje nipe"sikutaka kuchelewa nikayafungua yale maji yenye dawa ya usingizi nakumpa moureen ambaye kwa taratibu akaanza kunywa pole pole na kuyanywa mpaka nusu huku akiniangilia kwa macho ya kurembua.
"hivi pablo nataka uniambie kwani kule hotelini ilikua....." kabla hata hajamalizia sentensi moureen akashika kichwa chake na kuanza kulalamika na hakuchukua hata muda usingizi mzito ukampitia.bila ya kupoteza muda nikaliwasha gari lake na kuanza kuliendesha huku mkononi nikichukua simu yangu nakuanza kutafuta namba ya robert Mugalula kisha nakuipiga ambayo kwa muda kidogo ikaita kisha ikapokelewa
"kijana pablo kumbuka una masaa ishirini na nne tu ya kuchagua kujisalimisha ili familia yako isiendelee kuteseka au unaweza ukaacha na tutakuleta maiti."
"Na mimi nakuambia hivi ugomvi ni mimi na wewe na kama utaiachia familia yangu basi na mimi nitamuua moureen ambaye nipo naye kwa mikono yangu."
"unasemaje kijana??".hakika nikakata simu kwa kujiamini na huku macho yangu nikimuangalia moureen ambaye wakati huo alikuwa yupo katika usingizi mzito kabisa.nilianza kuliendesha gari hilo kwa uangalifu na kwenda kulipaki sehemu ya kujificha huku na mimi nikilala humo humo ndani ya gari.hakika hali ya hofu ikaanza kunitanda baada ya kushika simu ya moureen na kukuta messeji nyingi za mapenzi baina yake na robert jambo ambalo liliniumiza sana moyo wangu.simu katika simu yake zilikuwa zikiingia kwa wingi na kunifanya niingiwe na hofu ikifuatiwa na simu yangu ambayo katika mida ya saa nne ikaingia messeji iliyozidi kuninyong'onyesha
"KIJANA KUMBUKA KWAMBA UTAPOINGIA KATIKA MIKONO YETU KICHWA CHAKO MALI YETU"maneno hayo yalinitia hofu huku nikibaki kujiamini tu na kuzidi kumuomba mungu aniwezeshe kuipata familia yangu.usiku mzima mimi na moureen ambaye kwa wakati huo alikuwa bado yupo katika usingizi tulila na katika mida ya saa mbili asubuhi nikaamka na kuanza kuelekea chuo kwa kutumia usafiri wa wake.lakini kabla hata sijafika moureen akashtuka na kujishangaa akachukua simu na kuangalia saa zilizoambata na missed call na messeji na kunifanya niwe na hofu baada ya kuniangalia kwa hasira.akachukua chupa ya maji aliyokunywa na kuinusa kisha kwa hasira akanipiga nayo.
"Pablo ndio umefanya nini sasa??"
"moureen sikia nikwambie...ya.."
"yani wewe wa kunifanyia mimi hivi Pablo unaninyesha dawa ya usingizi ili nilale na wewe mpaka...aaa sasa mbona umenitafutia matatizo nitaenda kusemaje nyumbani eee pablo nijibu..aaaa nakuomba shuka kwenye gari yangu."moureen alisema maneno yale kwa uchungu huku akinikunja shati langu kwa hasira kubwa kisha akafungua mlango la gari lake na kuanza kunifukuza hakika nilijaribu kumuelewesha lakini bado alikuwa mkali na hakutaka kusikiliza chochote.
"Nakuambia toka masikini wewe"maneno yale yaliotoka katika kinywa cha moureen yaliniumiza na kunifanya nitoke huku nikiwa na mawazo.lakini ile naangalia tu gari la moureen likiondoka kwa kasi ghafla macho yangu yakakutana na robert ambaye sura yake ilikuwa imekunjamana kwa hasira kali.nikiwa katika harakati za kuanza kukimbia nilisikia mlio wa pikipiki ambapo baada ya kugeuka nikaona pikipiki ikija kwa kasi karibu yangu na kufanya niikwepe lakini ile naikwepa tu nikapigwa rungu kubwa la kichwa na dereva huyo wa pikipiki na kuachia mlio mkali wa maumivu kisha mdogomdogo nikaenda chini na kiza kinne kikachukua nafasi yake katika mboni ya macho yangu.
*-*-*-*-*-*-*-*-*-*-*CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"oooh aaaaaaaaaaaaa" fahamu zilizirudi na huku maumivu ya kichwa kuchukua nafasi yake nakufanya nitoe ukelele wa miguno.macho yangu yalitua katika mataa taa yaliokuwepo ndani ya jumba hilo lililonipa shauku kubwa la kunyanyuka kwa sababu mpaka muda sikujua nipo wapi.nikiwa katika harakati za kurudisha kumbukumbu zangu zilizopotea wakati huo ghafla maji ya baridi yaliokuwa na barafu barafu yakatua kabisa katika mwili wangu na kunifanya nipige ukelele kutoka na baridi kali nililoanza kulisikia huku kumbukumbu ya yaliotokea nyuma yakija kabisa katika kumbukumbu zangu.nikanyanyuka haraka haraka lakini nikajikuta nikirudishwa chini na kamba ambayo ilioanza kufungwa na kuzunguka kiuoni changu.nikiwa katika tahamaki Macho yangu yakatua kwa robert ambaye wakati huo alikuwa amekombatia na moureen ambaye wakati huo alikuwa katika nyuso za uzuni.baba yake moureen alikuwepo naye akiambata na mama yake moureen aliyekuwa ananiangalia kwa dharau.
"Pablo kama umeshavua nguo hauna budi kuyaoga hahaha.......
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment