Chombezo : Mtoto Wa Hayati
Sehemu Ya Pili (2)
Mamkubwa jasu alinidanganya kwa njia hio lakini mimi sikua na akili mbovu
" we sheby, unazichukua hizo za nini"
Hio ilikua ni sauti ya shangazi akiwa kapunzika chumbani kwa mama,
"mamkubwa kanituma"
"kakutuma za nini"
"sijui"
"acha ushenzi we mtoto, utakufa masikini mshenzi wewe"
"sasa mi nitamjibu vp na nimeshamwambia zipo"
"aaaaaa nimepata wazo, nenda kazitoe fotokopi zote kisha umpelekee hio foto kopi sawa"
"sawa"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilizichukua hati zote na kutoka nazo nje, nilikwenda steshenari iliopo karibu yetu na kuzitoa foto kopi zote, ikiwemo na ile ya gari ndogo ambayo ipo kule uwani.... Baada ya hapo nikazipiga na laminesheni ili ajue ni orijino, maana hizi orijino zimewekewa laminesheni,..... Nilirudi mbio mbio mpaka chumbani kwa mama, ambako kwa sasa analala shangazi, japo mamkubwa pia alikutaka huko,.. Lakini nilipofika chumbani nilimkosa shangazi, sikuwaza chochote kile zaidi ya kuzichukua zile origino na kuziweka kwenye kibegi kidogo kama rasketi hivi, na kuzifungia kwenye droo, nilipokua natoka kuzipeleka zile feki kwa mamkubwa nilikutana na shangazi uso kwa uso,
"lete hizo funguo"
Shangazi aliniomba zile fungu za ile kabati ambayo kuna hati miliki katika droo moja ya chini, Basi nilimpa ufunguo ule kisha nikaelekea sebureni ambako ndipo nilipomkuta mamkubwa tena alikua kapitiwa na usingizi,
"mamkubwa jasu, mamkubwa"
"eee, ee baba umezipata"
"ndio, tena ilikua na hio ya gari"
"sasa mbona umechelewa"
"zilikua zipo ndani, kazificha mbaliiii"
"yaani sheby nakupenda mwanangu, asante sana, sasa hapa namuita fundi aje arekebishe nyumba vizuri"
"nyumba yetu itapendeza eee"
"yaani itapendeza hio, we ngoja utaiona tu"
Mamkubwa alionyesha furaha yake baada ya kuona hizo karatasi zenye umiliki wa mali zetu zote,. ..
"afu kule dukani kuna nani"
Aliuliza kuusu lile duka la nguo ambalo ni la mama angu,
"kule wapo wafanya kazi"
"aaaaaahhh na lini alienda kuchukua pesa, au hajawahi kwenda kabla hajafa"
"alienda siku ile alioumwa tu"
"ila si linatoa pesa nzuri"
"ndio, juzi wiki iliopita alienda kuchukua milioni 25"
"haaaaaaaaaaa kumbe linatoa pesa kiasi hicho, ngoja kesho niende"
Basi mamkubwa aliingia zake chumbani kuviweka vile vitu, mimi nilielekea jikoni ambako yupo dada fatu ambae ni kama dada yangu kabisa kutokana na jinsi alivyonilea, dada huyu ni mfanyakazi wa ndani, ila hatujawahi kumlipa bali tunaishi nae kama ndugu na mimi na wewe tumezoeana sana, kama kitu na dada yake kweli,
"we sheby, naona ulikua sebureni na mamkubwa"
"ndio, alinituma karatasi ya nyumba na gari"
"ati nini?...... Umempa?"
"ndio, kwani kuna nini"
Dada fatuma alinichapa kibao kwa kumuambia nimempa mamkubwa hizo karatasi zenye umiliki wa mali hizi
"sasa mbona unanipiga dadaa"
"tukidumu kwa miezi miwili humu uniue, mshenzi mkubwa wewe, yaani unakurupuka tu bila kuuliza, hebu ona sasa ulichokifanya kama ni kitu kizuri"
"lakini si mamkubwa wetu dada"
"Eti lakini si mamkubwa wetu dada, mshenzi wewe.... Sasa nakuambia hivi fanya juu chini uzipate na uzilete hapa au umpe shangazi"
Mara mamkubwa alitokea hapo jikoni huku akitabasamu kwa kumuangalia dada fatu
"wewe, umekuja kufanya kazi au umekuja kufatilia mambo yasiokuusu"
Mamkubwa aliongea hivyo huku akimsogelea dada fatu pale jikoni,
"samaan mamkubwa, nilikua namuambia tu"
"unamuambia ukiwa kama nani"
"nisamee mamkubwa"
Dada fatu ni mschana mkubwa mwenye umri wa miaka 19 hivi kasoro, ila na yeye alikua akimuogopa mamkubwa kutokana na ukali wake, maana mamkubwa kitu kidogo tu kafoka,
"nikusamee nini, kilichokuleta humu ni kazi tu, sasa mdomo mdomo ni wanini"
Nikaona ngoja niingilie kati ugomvi huo
"lakini mamkubwa"
"kelele na wewe, mshenzi wewe"
Mamkubwa alibadirika ghafla tu na sijui ni kwanini,. ....... Haikupita muda shangazi nae kaingia hapo jikoni,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"haya we jasu, cha kumtuma mtoto nyalaka za mali zake ni nini, kwani zinakuusu"
Huyo alikua ni shangazi ndio alikua akimpa vigongo vyake mamkubwa jasu
"heeeeeee wifi, hata wewe pia unaingilia jambo hili"
Walianza kutupiana maneno wao wenyewe maana kiumri nadhani wanalingana hivi, ila mamkubwa ana mwili kidogo kuliko shangazi saumu
"hizi mali zoooote hizo, ni za huyu mtoto hapa, sasa wewe kwanini utake hati miliki za nini, mbona mnakua walimbukeni hivyo"
"saumu, nadhani sasa unapokwenda ni pabaya, sasa mimi nasema hivi, ukiliona jua la kesho labda mimi sio jasu"
Mamkubwa aliondoka huku akiwa kakasirika mno, tena hakua akitaka masihara kabisa,....
"sheby mwanangu, kua makini sana na huyu mamkubwa wenu saweni fatuma"
"sawa shangazi"
Shangazi nae aliondoka zake na kuelekea chumbani kwake ambako ndipo alipokua akilala mama angu,.... Nilianza kulia pale jikoni baada ya kukumbuka amani na upendo uliokuepo humu ndani, kwa sasa ni kama hadithi katika nyumba hiii...... Dada fatuma au mfanyakazi wetu alinibembeleza au tukabembelezana maana wote ni familia moja na yeye pia....
Nilipotoka hapo jikoni niliiingia chumbani kwangu, ambako nilifungua kabati kisha nikaitoa ile pesa shilingi milioni tano ambayo ndio ilikua ya matibabu ya mama angu lakini kwa bahati mbaya hazikufanya kazi yake, na badala yake mama angu alifariki dunia, Nilikata fungu la shilingi milioni tatu kisha nikampelekea shangazi, "shangazi, kuna pesa ambazo zilikua ni za matibabu ya mama, lakini ndio kama hivyo hazikufanya kazi, kwahio bora ukae nazo wewe maana mimi sijui nitazifanyia nini"
"ivi shuleni hudaiwi ada, ili kama unadaiwa nikakulipie hata miaka miwili au mitatu kabisa"
"hapana wala sidaiwi shangazi, tena nililipiwa mpaka nimalize kidato cha nne"
"sawa, ngoja niziweke zitapata kazi tu"
"sawa wacha nikaendelee kujisomea maana kesho inabidi niende shule"
"sawa mwanangu soma sana baba sooma mno"
"sawa shangazi nimekuelewa"
Nilirudi zangu chumbani kwangu kisha nikaanza kuzihesabu zile milioni mbili ambazo nilizibakiza, Nilimuita dada fatu na kumuonyesha zile pesa,
"sheby umetoa wapi pesa zote hizi"
"si nilienda kutoa kwa ajili ya matibabu ya mama"
"maskini uuuuuuuwiiiiii sheby"
Dada fatu alianza kulia baada ya kusikia nimetaja mambo ya mama,
"sasa unalia nini tena we dada"
Nilishindwa kuvumilia nami nikaanza kulia, sasa tukawa tunalia wote, Haikupita muda mara mlango ulifunguliwa kwa nguvu kisha akaingia mamkubwa.....
"nyie mnapiga piga kelele za nini hapa,.... Haaaaaaaaaa nyie mmetoa wapi hizi pesa zote"
Nikaona ngoja nimjibu mimi kua ni zakwangu, lakini kabla sijamjibu, dada fatu aliwahi kumjibu
"ni mishahara yangu yote toka nianze kazi hapa"
"aaaHaaaaa kumbe una pesa eeeee? Haya leteni hapa zote hizo pumbavu nyie"
"lakini mamkubwa hizo pesa ni mishahara yake aliolipwa na mama kabla ya kufariki"
"we sheby, unaweza kunijibu mimi, nakuuliza unawezaje kunijibu mimi"
"siwezi mamkubwa"
"haya, nipeni haraka nisije kuvuruga nyuso zenu"
Huezi amini tulikua tunalia kwa majonzi ya kumkumbuka mama etu lakini kwa sasa nyuso zetu zilianza kutawaliwa na huzuni kubwa ya kukosa amani katika nyumba hiii
Tulimpa zile pesa zote akaondoka nazo,... Alipotoka nami nikakimbilia kusema kwa shangazi kua tumenyang'anywa pesa na mamkubwa jasu
Lakini nilupofika chumbani kwa shangazi sikumkuta,.... Sasa mbaya zaidi ile droo yenye zile hati miliki za mali zetu ipo wazi, nilitoa macho kuona ile droo ipo wazi,... Aisee nilitafuta kabati zima mpaka chini ya kitanda lakini hakuna kitu,... Sasa nilipofunua chini ya godoro niliona zile pesa zote nilizomuachia shangazi, nilishangaa kukuta pesa lakini hati miliki orijino hakuna,... Nilianza kulia tena kilio kikubwa kilisababisha dada fatu kuja chumbani hapo na kuniuliza sababu ya kulia....
"sheby, mbona umevuruga chumba afu unalia kuna nini"
"dada, ivi sisi tuna mikosi gani,"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"kwanini useme hivyo mdogo wangu"
"fatu, wewe ni mfanyakazi au housegirl wa nyumba hii, lakini toka uje hatujawahi kukulipa, kwa maana ya kuishi na wewe kama ndugu, na tuliiseidia familia yanu kwa kila kitu watakacho kwa ajili yako,... Lakini kwa sasa maisha ya nyumba hii nahisi yanatushinda, maana kila tunaemtegemea bado anakua adui kwetu.... Na mama aliwahi kuniambia nikueshim kama dada yangu na nisikufiche kwa chochote kile, na ni kweli nilikueshi na bado nakueshim dada yangu, lakini kwa hili la kushindwa kimaisha sitaki na wewe ushindwe dada angu,.... Dada fatu kama kuna uwezekano ukarudi nyumbani ili niteseke mwenyewe tu"
Niliongea hayo maneno huku machozi yakinitoka mfululizo,
"sheby, kauli kama hio, naomba uifute kinywani mwako, maana mama kabla ya kifo chake alishawahi kuniambia nisikuache hata hatua moja ya mateso kwani wewe ni mimi na mimi ni wewe japo hatukutoka kwenye tumbo moja,... Na mimi najijua kua ni mfanyakazi humu ndani kwenu, lakini mama ako kaniambia nisikuache popote pale nilipo, kwahio kuusu swala la mimi kuondoka kisa mabadiliko ya maisha hilo sahau, nipo tayari kuteseka na wewe mpaka mwisho mdogo wangu, na usinifiche kitu chochote kile kinachokusumbua...... Sheby mdogo wangu, hebu niambie umeona nini huku kwa shangazi"
"dada fatu, hati miliki orijino hakuna"
"we si ulimpa mamkubwa wako wewe"
"hapana, zile zilikua ni fotokopi"
"Aahaaaaa sasa hata shangazi sio wa kumuamini sana, hebu amka tupange vitu vizuri"
Baada ya kupanga chumba vizuri, maana nilikivuruga kwa kutafuta hatimiliki zetu, mimi nilienda kujisomea, hata zile pesa milioni tatu sikuzigusa, maana nilishamkabidhi, sasa kuzichukua sio sahihi..... Nilijisomea mpaka mida ya saa mbili usiku ambapo niliamshwa na fatuma kuja kula, na kwa kawaida tunakula meza moja wote, lakini nilishindwa kumuuliza shangazi kuusu zile hati miliki, maana nikimuuliza hapo, na mamkubwa nae atasanuka kua zile alizonazo kumbe ni photocopy, hivyo nikatulia tu,....... Tulipomaliza kula niliingia chumbani kwangu na kujiegemeza ili nivizie mamkubwa alale ili niende chumbani kwa shangazi kumuuliza kuusiana na hizo nyalaka,..... Lakini mungu sio asumani nilipitiwa na usingizi mzito mno
BAADA YA MASAA KADHAA
ikiwa ni mida ya saa nane usiku simu yangu ambayo ni simu ya mama angu ilikua ikiita,
"heeee shangazi anapiga simu usiku wote huu"
Nilikua nasita kuipokea maana ilikua ni usiku mno,.... Lakini inabidi tu niipokee maana haikua na jinsi,
"haloo shangazi shkamoo"
"nnnnnn nnj.... Njjj.... Nj.. Njo. Njooo nik. Niku.... Nikua.. Njooo"
Niliitupa simu na kukurupuka na usiku huo huo, nilitoka chumbani kwangu tena nilikua nina boxer tu, ila kwakua bado ni mdogo sikua nikiwaza chochote hata nikienda kwa shangazi.... Sasa nilipokua nakatiza kwenye kordo moja ambayo ndio njia ya kuendea chumbani kwa shangazi, nilikutana na mamkubwa kasimama katikati ya kile kikodro na palikua na giza maana taa zilizimwa, sasa alikua akinifata mimi, huku akiniuliza.....
"unaenda wapi saa hizi"
"naenda kwa shangazi mara moja"
Nilijibu kiujasiri na kutokuogopa maana najua mamkubwa atakua anatoka nje kujiseidia,
"kufanya nini"
"kanipigia simu, nije chumbani kwake"
"yaani unaenda kwa shangazi yako umevaa boxer, unataka ukafanye nini nae"
Mamkubwa aliniwazia mambo ambayo maskini mtoto wa watu hata siyajui, na wala sijayafikia.....
"hapana mamkubwa, shangazi alionekana kua na tatizo"
"yaani unataka ukalale na shangazi yako kweli, we mtoto kumbe ni mshenzi kiasi hicho, unaweza kunibaka hata mimi mshenzi wewe,.... Sasa kama kweli wewe ni kidume vuka ile korido pale uone moto"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikua naogopa sana tena ukizingatia ni usiku wa saa nane, hivyi nilikosa ujasiri wa kuisogelea hio korido aliosema nisiifikie, maana nilikua bado mdogo afu kwa malezi niliolelewa ni ngumu kubishana na mtu mzima, basi kwa unyinge wangu nilirudi nyuma taratibu huku nikiyatoa machozi ya huzuni, . Nilirudi chumbani na kujitupia kitandani huku machozi yakinivuja, yaani kila mara nilikua ni mtu wa kulia lia tu,... Haikufika muda dada fatu alikuja chumbani kwangu na kuanza kunibembeleza, mpaka nikalala na yeye pia alilala hapo hapo kitandani kwangu,
Ilipofika asubuhi mida ya saa 12 nilikurupuka na kwenda kwa shangazi, muda huo dada fatu alishaamka toka saa 11 kwa ajili ya usafi wa nyumba, mimi nilikimbilia chumbani kwa shangazi kumuona, Lakini sikuelewa kitu kwani Nilimkuta shangazi kanyooka nyoooo afu kakaza kama mti,
"shangazi, shangazi"
Nilikua nikimuita huku nikimsukuma mzima mzima, nilitoka nje na kumuita dada fatu, na yeye ndio alijua kua shangazi alishafariki dunia,
"sheby, nyamaza mdogo wangu"
"kwani shangazi kawaje, afu mbona ana baridi hivyo?"
"shangazi nae amekufaaaa"
Niliposikia hivyo ndio nikazidi kulia mtoto wa kiume, na wakati huo mamkubwa alikua hayupo na sikua najua alipoelekea... Mtoto wa kiume nililia bila mpangilio, huku dada akijitahidi kunibembeleza, basi kwakua dada alikua anajua na pia alikua ni mjasiri, alinfunika shangazi kisha tukatoka hapo chumbani, ila nilipokua natoka nikakumbuka zile pesa, ikabidi nirudi nyuma na kwenda kuziangalia, maana mara ya mwisho nilizikuta chini ya godoro, nilipofunua godoro sikuweza kuona zile pesa..... Hapo ndipo nilipojua kua lazima mamkubwa ndio kazichukua, lakizi mbaya zaidi shangazi amekufa bila kusema hizo nyalaka aliweka wapi,
Baada ya siku hio kupita tulikua tupo na maiti ndani, na ilikua bado haijaanza kuharibika maana ilikua ni jana tu, tulikua tunakula meza moja na mamkubwa ambapo sisi tulikua tukiogopa sana, sema hatuna tena mtu wa kumtegemea zaidi ya mamkubwa
"skieni nyie, kesho kuna gari itakuja itachukua maiti hio, wakamzike hukoo"
"wapi huko"
"usiniulize"
Nilikaa kimya huku nikitetemekwa na mwili, maana jambo la kumkosa shangazi kwetu ni pigo kubwa sana..... Nilipomaliza kula nilienda zangu chumbani kulala na dada pia aliingia zake chumbani kulala
Baada ya siku hio kupita na leo ni siku nyingine tena ambapo mida ya saa 3 hivi asubuhi kweli honi ya gari ilisikika nami nikaenda kufungua geti, ikaingia pikap moja ambayo ndani yake kulikua na sanda, gari iliingia na moja kwa moja waliingia ndani hao vijana na kumbeba shangazi, yaani familia yangu inazikwa kiajabu ajabu kweli, lakini binfsi sikua na lakufanya, maana nikiongea nitaonekana jeuri mbishi sina adabu, hivyo ikabidi nitulie tu, baada ya maiti kupakiwa katika gari, nami sikutaka kuliacha hilo gari, angalau nikajue tu kaburi lake lilipo, na muda huo mamkubwa alikuepo ndani yaani hata kuchungulia tu hajachungulia kua maiti imepakiwa vp, basi na wale jamaa waliniruusu nipande kwenye gari yao ili nikajue kaburi la shangazi yangu...
Walipokua wanakwenda kumzika ni maeneo tofauti na kule alipozikwa mama,
"eti kaka mnaenda kumzikia wapi"
"anaenda kuzikiwa makaburi ya njiro"
"haaaaa njiro tena"
"we dogo tulia tutakushusha sasa hivi"
"ah ah boka, muache dogo ana haki ya kuuliza maana ni ndugu yake"
Mmoja kati ya hao alikua ana huruma kiasi flani,
"skia dogo, sisi tumelipwa tumzike huyu mtu, na yule mwanamke katulipa pesa ya kuchimbia kaburi na pesa ya kumzika, hivyo, hapa hatubadiriki, we tulia ukamzike ndugu yako"
"sasa, broo mimi nina hiki kiasi kidogo hapa naombeni tukamzike makaburi ya stendi, alipozikwa mama angu"
"hahahahahahahaha uyu dogo vp uyu... Ni shing ngapi hio"
"elfu 50"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"we mwehu ongeza ela tugeuze gari"
Mtoto wa kiume nilikua nina elfu 80 tu mfukoni ambayo ilibakia bakia katika moja ya matumizi kabla sijapokonywa zile zingine, sasa nilitaka niwape elfu 50 ili nibakiwe hata na 30 lakini wapi, ikabidi niwape yote ili wasiende kumzika huko njiro
Basi watu hawa waligeuza gari yao na kurudi stendi
Tulipofika katika makaburi ya stendi, tuliingia kisha nikawapeleka mahali lipo kaburi la mama angu, nilishukuru kwakua wamenikubalia ombi langu, japo nimewapa pesa, kweli walianza kuchimba kaburi maeneo hayo kisha walipofikisha mita 5 tu wakamleta na kumlaza.... Yaani siwezi kuamini shangazi yangu anazikwa utafikiri kunazikwa mnyama, maana tulikua watu kama sita hivi... Wao wapo watano na mimi pamoja na watu wa pembeni waliokua wakiangalia maziko ya ajabu, mtu anazikwa na watu sita, tena hawa wengine hata sio wazikaji bali ni wafukiaji tu.....
Basi nilichota mchanga kidogo na kuumwagia katika kaburi kisha nikasoma dua zangu nilizokua nikijua kwa kumuombea shangazi yangu,...... Baada ya hapo niliruusu tumfukie shangazi, nilikua nalia kila ninapoona sanda ya shangazi,... Sasa hawa jamaa ndio maana nikakwambia sio wazikaji kabisa maana walimfukia fasta fasta kama wanazika mbwa vile, yaani kufikia walichukua dakika tano tu hadi kumaliza, yani hata kulitengenezea tu hawakulitengenezea kuonekana kama kaburi,
"dogo twende, au unabaki"
Nilikataa kuonfoka, hivyo waliondoka wenyewe maana walishamaliza kazi yao, sasa walipoondoka mimi nilianza kuukusanya mchanga vizuuri na kulitengenea ili hata lionekane kama kaburi, nilikaa hapo makaburi kwa muda mrefu sana huku nikilia machozi yasionikatika, familia yangu imekwisha, yaani alibakia shangazi tu peke yake, leo hii ndio huyu tunamzika, tena bora azikwe kama binadamu, lakini anazikwa kama anavyozikwa mbwa,..... Ilipofika mida ya saa nane mchana nilitoka hapo makaburi nikiwa nimechafuka vumbi la kaburi maana nilikua nikigala gala huku nikilitengenezea...... Niliondoka na kurudi nyumbani nilikutana na dada fatu ambae alikua akinifuta tu machozi,
"lakini si umejua kaburi la shangazi lilipo"
"ndio"
Dada fatu pia si mtu wa kukauka kulia maana janga langu ni lake, hivyo tulikua tukilia kila mara tunapokumbuka familia yetu,
"hebu niachieni kelele washenzi nyie"
Ilikua ni sauti ya mamkubwa ikitufokea kuacha kulia, tulinyamaza ghafla tu, maana tunavomuogopa ni balaa hilo,
"haya wewe ulienda wapi"
"nilienda kuzika"
"nilikuambia uende? Si nimeshawalipa watu wa kuzika"
"nisamee mamkubwa"
"heeeee mbona umechafuka hivi, ivi nikuulize unanunuaga sabuni wewe"
Sijakaa vizuri nikala kofi la uso Paaaaa
"mamkubwa msamee nitazifua mimi"
"kelele na wewe mambwa nyie, kazi kula tu humu ndani"
"nisamee mamkubwa"
"kwenda ndani kule"
Nilikimbilia ndani kisha nikaingia bafuni ambako nilioga vizuri na kutoka, nilibadiri nguo kisha nikachukua madaftari yangu na kuanza kusoma...
"fatumaaaaa"
"abeee mama"
Dada fatu aliitwa na mamkubwa kwa hasira hasira,
"huyo mshenzi mwenzio yupo wapi"
"ngoja nikamuite"
Dada alikuja kuniita kisha tukakimbia kama mbuzi mbele ya mamkubwa jasu...
"abee mama"
"yaani nyie geti linagongwa toka saa hio mlikua wapi"
"samaani mama hatujasikia"
"pumbavu zenu nyie mnakula tu na kujaza choo, haya wewe nenda kafungue geti na wewe nenda kapikie wageni chakula na uhakikishe kinaiva"
Aaaaaaaa sasa niliposikia wageni, nikajiuliza ni wageni gani hao tena, mbona tupo wenyewe humu ndani,... Niliona bora niende kufungua hilo geti kwanza kisha nidiskasi kuusu hao wageni wanaosadikiwa kupikiwa chakula kitamu... Sasa Nikiwa nakwenda kufungua geti mamkubwa alikua nyuma yangu akiangalia huyo ninaemfungulia hapo getini
Nikafungua geti ili aingie huyo mtu anaegonga, na mimi nilijua ni jirani yetu anakuja kuchota maji.....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sasa nilipofungua mlango, mtumeeee kuliingia timu ya watu
Alianza jamaa mmoja hivi mkubwa na alikua kabeba begi kana kwamba ndio anakuja, mara mwingine tena wakiume mdogo saizi yangu... Mara mwingine tena wa kike mdogo saizi yangu, akaingia na mwingine mwanamke mkubwa mkubwa kidogo, afu wote wamebeba mabegi...
"oya nyie ni wakina nani nyie"
Kuwauliza wale watu ni akina nani ilikua ni kosa kubwa sana kwa mamkubwa jasu
"he he he he, we mbwa, unawazuia na kuwauliza ukiwa kama nani"
"nisamee mama"
"haya mpeni hayo mabegi apeleke ndani"
"haaaaaaa"
"haaaa ya nyokwe, chukua mabegi hayo upeleke ndani, afu kama vyumba havitoshi jipange kulala chini"
Sikupigwa wala nini lakini machozi yalianza kunitoka mfululizo huku nikipewa mabegi ya watu wote nipeleke ndani, basi nilianza kuburuzana na mabegi yao tena hakuna hata alieniseidia kubeba, kwani waliambiwa waniachie niyabebe peke yangu, Sikuwa na hiana wala ubishi kwani huenda ndio malezi bora yanaompasa mtoto kupewa, niliburuza yale mabegi hadi ndani ambako nilishindwa pakuyaweka hivyo nikamuita mamkubwa ili nijue pakutapeleka
"mamkubwa nipeleke wapi haya mabegi"
"mmmhhh ngoja kwanza, hebu muite fatuma aje hapa niwatambulishe vizuri muwajue"
Nikaenda jikoni kumuita dada fatu kisha tukakaa sebureni sisi wote mpaka wale wageni, wageni walikua wapo wanne na sisi watatu jumla nyumba ina watu saba sasa,
Sheby na fatuma, hawa mnao waona mbele yenu ni watoto wangu, huyu wa kiume mkubwa anaitwa jamali na huyu wa kike mkubwa anaitwa sauda, hao ni mapacha na wana umri wa miaka 21 muwaheshimu sana... Na hawa wadogo nao ni mapacha vile vile, huyu wa kiume anaitwa juma na huyu wa kike anaitwa mwajuma, wana umri wa miaka 14 kama wewe sheby, kwahio hawa nao pia naombeni muwaheshimu, hasa wewe sheby ni mkorofi sana sasa Ole wako niwakute ni wanyonge utantambua"
Tukaitikia wote mimi na dada fatuma kua
"tunashukuru kuwafahamu mamkubwa"
"naaa sehemu za kulala, mimi nitalala na mwajuma wangu, kule master room, afu huyu juma atalala na sheby chumbani kwake, afu huyu sauda atalala na fatuma chumbani kwake, na huyu jamali atalala peke yake kwenye chumba alichokua akilala shangazi,.... Tumeelewana"
"ndio mamkubwa, tumekuelewa"
"haya anza kusambaza mabegi sehemu nilizokwambia"
Daahh nilianza kuwapelekea mabegi yao machumbani mwao...... Na maisha yakaanza kua hivyo
BAAD YA MWEZI MMOJA KUPITA
Maisha yangu yalikua yanazidi kua mabaya kila kukicha, yaani siku ikienda vizuri hua namuomba mungu siku hio isiishe maana najua kesho haitokua nzuri, lakini tumeshaambiwa siku hazigandi hivyo katika mwezi mzima nikisema siku nzuri zilikua labda ni mbili tu ila siku zote ni tabu kwangu, kwani nilikuja kua mfanyakazi wa ndani ghafla tu, chakula hatukua tukila kama mwanzo,... Nikiwa nimekaa hapo nje mida ya saa kumi waliingia wale watoto wakitoka shuleni, tena walipokelewa kwa shangwe na mama yao ambae ni mamkubwa......
Watoto hawa nao wanasoma kidato cha kwanza kana kwamba walihamishiwa huku mjini ili elimu yao iwe ya juu zaidikuliko kama wangesomea huko, Walioanzishwa shule ni juma na mwajuma ambao ni wale watoto saizi yangu, ila wale mapacha wakubwa ambao ni jamali na sauda sijui wamepelekwa wapi maana wanarudigi jioni tu na kutoka asubuhi, ila niliambiwa wamemaliza shule toka kijijini.... Ila kwa hapa mjini sikujua wanaendelea na shughuli gani, maana sikuambiwa na hata hawa sikuambiwa kua wanasomea wapi ila kuwaona tu najua wanasomea wapi na ni kidato cha ngapi,..... Masaa yalizidi kwenda na kufikia mida ya saa 11 jioni,.... Lakini nilishangazwa na siku ya leo ambayo sikumuona dada fatu kabisa maana, toka asubuhi mimi nilikua huku nje nafanya usafi wa gadeni,..... Sasa nikiwa najikongoja kuelekea ndani mara mlango uligongwa, kwa sasa mimi ndio mfungua mlango kwani hata mlinzi wetu alifukuzwaga kitambo tu,
Nilipofungua waliingia wale akina jamali na sauda, ila sauda alininyookea mimi na kuniambia
"ivi yule mpumbavu kule ndani kapona"
Nikashangaa huku nikimuuliza
"mpumbavu nani dada"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"si yule mfanyakazi mwenzio kule ndani"
nikajua, kumbe mie ndio nishakua mfanyakazi humu ndani, na huyo anaeumwa lazima atakua ni dada fatu, hivyo nilitoka mbio na kukimbilia chumbani kwao ambako ndipo alipolala dada fatu, Nilipofika kweli dada fatu alikua akiumwa vibaya mno tena hada kuamka alikua hawezi
"dada fatu nini shida tena"
"sheby mdogo wangu, naumwa mimi, na sijui nitapelekwa na nani hospitalini"
"usijali dada utapelekwa tu"
"sasa nitapelekwa na nani, na pesa atatoa nani"
"we usijali, vp umekula"
"sijala toka asubuhi"
Niliposikia hivyo nilikimbia mpaka jikoni ambako nilikuta hotpoti la wali samaki limetuna, basi sikulikawiza nikalibeba na kwenda kumpa dada fatu alipige lote
"shika kula"
"we sheby umetoa wapi chakula cha watu"
"dada fatu ni bora tufinywe tupigwe lakini tumeshiba"
"kwani we umekula"
"aaa ndio nimekula"
"sheby kama hukula mimi siwezi kula"
"nimekula dada"
Basi dada fatu alianza kukikandamiza kile chakula huku nikipiga maesabu ya dawa, yaani nilikua ni mtoto mdogo lakini nina majukumu ya kiutu uzima, nilipiga maesabu ya dawa lakini hayaji maana nilikua sina hata senti tano mfukoni, kwani pesa zote nilipokonywa na mamkubwa, sasa nilipokua hapo ndani nilisikia sauti ya sauda ikimuita mamkubwa
"mamaaa"
"nini wewe"
"njaa inauma"
"angalia jikoni hapo kuna chakula"
"haya"
Sasa dada fatu kusikia hivyo akaacha kula
"sheby rudisha chakula cha watu"
"dada fatu, we kula hii kesi we niachie mimi"
Mara tukaskia sauda anaulizia tena
"mama mbona hamna"
"jamani we mtoto huoni chakula kipo hapo jikoni"
"njoo uone mwenyewe"
"nione nini"
"au ndio hiki wanachokula wakina sheby"
"mtumeeee ati unasemaje"
Mamkubwa alikuja mbio mbio hadi chumbani hapo na kuanza kutuangalia...
"nyie mambwa nani kawatuma mchukue chakula kule jikoni"
"mamkubwa, dada fatu anaumwa"
"sasa kuumwa kwake mimi kunaniusu nini"
"tusameee mamkubwa"
Mamkubwa alipiga hatu ya kwenda kumpiga kofi dada fatu, ila nikaamka na kupigwa mimi
"paaaaaaaaaa"
"we nini na wewe"
"mamkubwa mimi ndio nilioenda kuchukua hicho chakula kule jikoni, hivyo dada hana makosa"
Yaani kabla sijamaliza, nilistukia tena bonge la kibao cha skio mpaka nikadondoka chini... Nikaanza kulia huku nikijikaza kiume,
"sauda, kwanini hukusema kama huyu mbwa anaumwa, litakuambukiza hili"
"nisamee mama kwa kutokuambia"
"usijali mwanangu..... We mbwa kuanzia leo naomba usilale na mwanangu mpaka utakapo pona"
Sasa mamkubwa aliposema vile nami nilirukia juu kwa juu na kuuliza kua
"sasa atalala wapi mamkubwa"
"we mshenzi tulia, nitakutoa na wewe nje sasa hivi, huyu akalale stoo"
"mamkubwaaaaaaaa, sio vizuri lakini"
"unasemaje wewe,? wewe hivyo vizuri unavijua,?.... .. sasa kwa taarifa yako utaungana nae, tokeni na muishi stoo kuanzia leo, na ni mwanzo na mwisho kuchukua chakula bila idhini yangu shuuwaini wakubwa nyie"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siwezi kuamini kwa maisha haya ambayo toka nizaliwe sijawahi kuyaona hata kwa jirani, mamkubwa alitoka zake huku akiwa na hasira ya mwanae kutokula, tena tulikula chakula cha watu ambacho kilirostiwa vibaya mno, Basi hatukua na budi ya kutoka nje, nyuma ya nyumba ila bado tupo ndani ya mjengo huo ila ni ndani ya fensi, lakini sio ndani ya nyumba, basi tulienda stoo kisha tukapaangalia marambili mbili, kana kwamba hatukuzoea stoo,
Na uzuri wa baba ni kwamba alijenga stoo mbili, stoo moja ilikua ni ya mkaa na stoo nyingine ilikua imewekewa zana za bustani, yaani vile vifaa vyote vya kutengenezea bustani, na ilikua ni rumu moja kubwa hivyo ikakatwa kati kwa kati na kutoa rumu mbili,
"dada, kutokana na shida tulionayo, aisee hapa panatufaa"
"yaani sheby siamini kama maisha yamebadirika kiasi hiki"
"hebu kaa hapo usije dondoka bure, ngoja mi nianze kutoa hivi vifaa humu"
Nilipopiga macho ndani ya hio stoo niliona godoro ambalo nakumbuka baba alimuambia mama kipindi hicho kua
"mama sheby, naomba sana hilo godoro usilitupe wala usilichome"
"kwanini baba sheby"
"mama sheby, inamaana hukumbuki tulipoanzia? Mimi binafsi nikiliona hilo godoro nakumbuka mbali sana, kwahio chonde chonde naomba tuliweke kama kumbu kumbu zetu za maisha ya nyuma kabla ya hapa"
"kweli hata mimi nakumbuka mbali sana nikiliona hili godoro, wacha nikaliweke stoo"
"afadhali uliweke huko"
Siwezi kuamini kua godoro hilo leo linakua kitanda chetu kikubwa tena tunachokitegemea kuliko chochote kile... Basi nilifungua mlango wa stoo vizuri kisha nikatoa vile vyuma vyuma, na kuviweka ndani ya banda la kuku, maana tulikua na kuku wengi sana lakini wamemalizwa na familia ya mamkubwa, kila siku wanakula kuku afu sisi tunapewa miguu na vichwa....
Baada ya muda mfupi stoo moja iling'aa vizuri maana nilipadeki kabisa, baada ya hapo nilitandika lile godoro na kumlaza dada fatu, Kwakua mie naruusiwa kuingia ndani hivyo nilienda kuchukua ndoo ya maji ya kunywa pamoja kikombe, kisha nikaja kuiweka pale ndani ambapo ndipo tunapopaswa kulala sisi, dada fatu alikua akiumwa vibaya mno... Kwani alikua akitapika mara kwa mara na kuendesha huku tumbo likimuuma kwa sana, hayo ni maelezo yake yeye alioniambia....
Masaa yalikatika hadi kufikia mida ya saa mbili usiku ambapo niliitwa nikachukue chakula... Nilitoka mbio kwenda ndani lakini kabla sijafika mlangoni nilikutana na mamkubwa akiwa kashika sahani mbili
"hiki ni chakwako na hiki ni cha huyo mbwa mwenzio"
"asante mamkubwa"
"kwenda ukooooo"
Niliondoka huku kidogo moyo wangu ukiwa umefarijika kiasi flani lakini nilipoangalia kile chakula vizuri, niligundua kuna ukoko na wali, yaani makoko nimpe dada fatu afu ule wali nile mimi, kwa jinsi mamkubwa alivyoniambia.. Nikiangalia yale makoko hayakua hata na mchuzi ila yalikua yana kichwa cha samaki... Alafu kwenye sahani yangu kulikua na wali uliojazwa mchuzi na kipisi cha samaki... Aiseee lile swala sikulipenda kabisa, na ndio hapo nilipojua kua mamkubwa hampendi dada fatu kabisa, yaani tena bora ya mimi kwasababu mimi ni mtoto wa mdogo wake, hivyo kidooooooogo kama nfsi inamsuta hivi na ndio maana kwenye upande wa chakula ananipa.....
"dada chakula hiki hapa"
Nilipa dada fatu kile chakula changu ambacho ni wali mzuri na wenye samaki, afu mimi ikabidi nile yale makoko ambayo ndio alipaswa ale dada fatu,
"we sheby umetoa wapi chakula cha watu"
"kanipa mamkubwa"
"na wewe unacho"
"ninacho si hiki hapa"
Sasa dada fatu yeye ni mpishi hivyo alipoona tu kile chakula alianza kulia huku akise
"sheby mdogo wangu, najua hicho chakula kilikua ni changu, naomba chakula changu"
"dada, mimi ndio nimepewa hiki nile mimi, na wewe umepewa hicho kwakua unaumwa"
"mh mh sio rahisi"
"we kama utaki basi lakini hiki chakula ni changu"
"lakini mamkubwa si anajua huli kichwa cha samaki, sasa kama ni chakula chako kwanini akuekee kichwa"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"dada, labda alijisaau tu, ila we kula tuhicho"
Dada fatu aliendelea kulia huku akinipa maji
"basi shika maji ushushie"
Nikachukua maji ile nishushie huo ukoko, maana nimeamua kuula badala ya dada
"lakini sheby we bado mdogo, na utumbo wako haukuzoea vitu vigumu"
"dada, hebu kula basi, we ulifikiri na maisha tulionayo tuanze kuchagua vitu vigumu na vilaini, kula bwana"
Basi mimi nilikua nikiula ule ukoko huku nikikabwa kabwa maana sikuzoea kweli kula ukoko hivyo nilikua nikiula na maji kwani haukua umewekwa mchuzi hata kidogo zaidi ya kichwa....
Tulikula na hatmae tulimaliza, lakini wazo la kupata dawa za dada fatu sina, maana sina wa kumuambia kuusina na hilo...
"sheby si ulale jamani"
"dada, kwani hata usingizi upo sasa"
"sasa tutafanyaje, maana ndio maisha tumeyaanza haya"
Ilibidi nijilaze tu ili nipumzishe akili, kwani nilikua ni mdogo lakini mawazo ya kikubwa tu....
Sasa nilipokua navuta shukua, maana dada alipoamka alitoka na shuka kule ndani hivyo ndio tunalitegemea kujifunika wote, Sasa nilipokua nalivuta shuka nikagundua dada fatu alikua ana nguo ya ndani tu peke yake, kiasi kwamba mimi ni mtoto wa kiume japo ni mdogo lakini kwahali hii siwezi kulala nae usiku wote, hivyo niliamka na kutoka nje...
"we sheby unaenda wapi saa hizi"
"apana ngoja kwa leo nilale huku juu ya mkaa"
"sasa ulale juu ya mkaakwa mpango upi"
"dada fatu mimi ni mtoto wa kiume, kwa hali ulionayo ni ngumu kulalala wote"
"sheby, inamaana hata mimi unaniogpa kisa naumwa, kwahio mimi nitakuambukiza ugonjwa si ndio"
"hapana dada sio hivyo"
"ni nini sasa"
"tatizo ni kwamba huna nguo"
Sasa nilipomwambia hivyo ndio akatulia na kujiangalia vizuri
"samaani mdogo wangu, kwani toka nilipolala jana usiku mpaka mchana wa leo sikuweza kuamka na kuvaa nguo, afu mbaya zaidi ni kwamba pale nilipokua natoka nilishindwa kuvaa nguo maana nilikua nalazimishwa kutoka, hivyo nisingeweza kuvaa nguo..... Ila isiwe sababu ya kutokulala hapa... Sheby, we sheby"
"naam"
"njoo ulale, mimi ni dada yako na wewe ni mdogo wangu huwezi kunifanya chochote sheby, plz naomba usilale kwenye mikaa"
"lakini dada"
"lakini nini, basi kama hutaki tujifunike shuka moja chukua hili shuka mi nitajifunika kanga, lakini usilale huko"
"hio kanga ipo wapi"
"niletee ipo pale kwenye kamba niliifua juzi"
"basi mi nitajifunika hio kanga, maana itakua na ubaridi afu wewe mwenyewe mgonjwa"
"sawa kaichukue, ila ulalie hapa hapa nikuone"
Basi mtoto wa kiume nilienda kuichukua hio kanga kisha nikauchapa usingizi muruuua kabisa,.....
Asubuhi palipokucha, niliamka na kwenda ndani kuchukua mishwaki,
"we sheby"
"naam mamkubwa"
"huyo mshenzi mwenzio hajapona tu"
"bado mamkubwa"
"sasa nani, atafanya usafi humu ndani"
"nitafanya mimi mamkubwa"
"fanya haraka pang'ae"
Baada ya hapo nilikuja stoo mahali nilipomuacha dada fatu akiwa bado kalala.
Sasa nikawa namuamsha ili nimpe mswaki wake,
"dada fatu, we dada fatu amka upige mswaki"
"we dada fatu weee"
Sasa ile kumgeuza, aligeuka mzima mzima, Nikajua atakua kapitiwa na usingizi hivyo nikawa namfunika shuka vizuri, sasa ile namgusa tumbo lake.. Aisee alikua ni wa baridi kuliko kawaida, mpaka nikashtuka kuona vile,
"we dada fatu,"
Machozi yalianza kunitoka bila ya kupigwa, ila ubaridi alionao nilikumbuka huu ubaridi kuna mtu alishawahi kua nao, nilivuta kumbu kumbu na kumkumbuka huyo mtu
*******************************************
Nilimkuta shangazi kanyooka nyoooo afu kakaza kama mti,
"shangazi, shangazi"
Nilikua nikimuita huku nikimsukuma mzima mzima, nilitoka nje na kumuita dada fatu, na yeye ndio alijua kua shangazi alishafariki dunia,
"sheby, nyamaza mdogo wangu"
"kwani shangazi kawaje, afu mbona ana baridi hivyo?"
"shangazi nae amekufaaaa"
***************************************
Nilipomaliza kukumbuka, nilishtuka na mapigo yangu ya moyo yakaenda mbio huku nikiendelea kumuita dada fatuma
"dada fatu, dada fatu, we dada fatuuuu"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijikuta nikianza kulia peke yangu nisijue cha kufanya, kwani hata nikipeleka taarifa kwa mamkubwa hatoseidia chochote kile ambacho kitaleta msaada kwetu, nilianza kulia huku nikiendelea kumuita dada fatu, maana yeye ndio tegemezi langu, Sasa nikiwa naendelea kulia maeneo hayo huku nikimuamsha dada angalau hata aamke lakini wapi,
"shebiiiiii"
"naam mamkubwa"
Mamkubwa aliniita, nilitoka mbio kwenda kumsikiliza kile anachoniitia,
"naam mamkubwa"
"huyo mbwa mwenzio hebu muite hapa"
"mamkubwa, dada fatu anaumwa"
"sasa nani atafanya usafi humu ndani, nguo zetu chafu vyombo vichafu nyumba chafu, nani atafanya hio kazi"
"nitafanya mimi mamkubwa"
"haya inamisha mgongo haraka na udeki vizuri mbwa wewe"
Basi mtoto wa kiume nilianza kudeki nyumba, maskini toka nizaliwe sikuwahi kudeki nyumba yaani nilikua napata tabu katika maisha ya hali hiii, lakini kudeki kwangu haikua tatizo, bali tatizo lilikua kwa dada fatu, nilikua namuwaza dada fatu kule stoo, nilikua nadeki mtoto wa kiume, sema kwa bahati nzuri nyumba yetu ilikua ni fulu tailizi, hivyo nilikua nafuta futa tu ili niwahi kuzimaliza kazi ambazo zilikua zikimhusu dada fatu, Sasa nilipomaliza kudeki nikatoka nje kwenda kumwaga maji, Mara nikasikia mtu anakohoa kule stoo, nilitupa kile kindoo na lile brashi kisha nikakimbilia huko, Nilimkuta dada fatu ndio anajitahidi kuamka, kumbe alikua ni mzima
"eeee mungu shukrani kwa kua ni mzima"
Dada fatu alikua akijitahidi kuamka
"dada pumzika dada unaenda wapi mama"
"sh sh she she sheby, naomba niend..... Niende nikafanye usafi"
"dada fatu, mimi nitafanya na tayari nimeshaanza"
"hapana, wacha nikakuseidie tu"
"mh mh mi nipo"
Sasa ghafla alitulia kimya, kana kwamba labda kalala nini, ila kushika mapigo ya moyo yalikua yakifanya kazi, kana kwamba ni uchovu wa homa ndio umemlegeza, na mbaya zaidi hakupata hata dawa, Sasa kutokana na kuamka kule nguo zake zilimshuka, kama unavyojua toka jana alilala na nguo ya ndani tu, Kiukweli nilijikaza kiume na kumuamsha hivyo hivyo akiwa na ile nguo moja tu, kisha nikaanza kumvalisha suruali yangu mimi, maana yeye hakua na suruali kutokana na madhingira aliyolelewa, hivyo nilijifanya sioni na kumvalisha suruali yangu, na dada fatu alilua ana mwili ila ilimuenea japo kifungo hakijafunga ila afadhali kidogo, baada ya kumvalisha suruali ile nilichukua na gauni lake na kumvalisha, kisha nikamfunga na kanga kwa juu, Muda huo dada fatu hakua akijitambua, na laiti kama ningelikua mtu mzima na mwenye akili potofu, basi nisingemuacha bure, maana dada fatu alikua ni mzuri na ana umbo zuri ambalo mwanaume yeyote rijali hawezi kupishana nae njiani akaacha kugeuka, yaani dada fatu alikua kaumbika vizuri mno.... Yaani kama ni mke kiukweli atakae muoa atafaidi uzuri na heshma yake,.... Kwa wenzetu waingereza wanaita "Wife Material" Basi nilifanikiwa kumvisha nguo vizuri sasa hapa naweza hata kukaa nae karibu, sasa wazo likanijia bora nimbebe nimpeleke hospitalini, japo sina pesa lakini huenda nikapata msaa wa watu, sasa ile ndio nataka kumbeba ghafla niliitwa na mamkubwa.....
Nilikimbia mara moja maana nikichelewa nitafinywa na kupigwa makwenzi,
"we mshenzi, vile vyombo pale unamuachia nani"
"nisamee mamkubwa"
"nenda kaoshe haraka sana, afu hii nyumba bado haijang'aa kabisa, maliza vyombo uje urudie"
Nikasukumwa na kibao na kudondoka chini, nilianza kulia kwa uchungu huku nikiwakumbuka wazazi wangu, kiukweli moyo ulikua ukiniuma, maana huku dada anaumwa huku mie kazi zinaniandama mwanzo mwisho afu huku watoto wake wameenda kazini na wengine shule, ila mie nimesimamishwa kwenda shule, na ada nililipiwa mwaka mzima na baba angu kabla hajafa,..... Basi kwakua nyumbani kwetu kulikua na mashine ya kufulia nguo, hivyo nilizichukua nguo zile na kuziweka kwenye mashine hio, kisha mie nikaendelea kuosha vyombo huku nguo zikifuliwa na mashine...... Vyombo vilikua ni vingi mno lakini niliweza kuvimaliza hivyo tu huku mchozi wa huzuni hauniishi kunitoka, maana hii ni mateso juu ya mateso, Nilipomaliza kuosha vyombo na huku nguo zilikua zinamalizia.....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"haaaaaaa we mbwa nani kakuambia ufue nguo zetu na mashine? Nakuulize we mwana haramu mkubwa wewe chokoraa wewe"
"lakini mamkubwa kazi ya hii mashine ni hio"
"kelele wewe mbwa mkubwa wewe, unanifubazia nguo zangu afu unaniambia kazi ya mashine, afu wewe dawa yako inachemka pumbavu mkubwa wewe"
"nisamee mamkubwa"
"toa nguo ukazianike, na leo hakuna kunywa chai humu ndani, na hata mchana nisione mtu anataka chakula hapa"
Nilipigwa vibao vya kutosha kisa nimefua nguo na washing machine, Basi nilivumilia tu maana nipo kwetu na hatuna nyumba nyingine zaidi ya hii, na pia hatuna pakwenda,... Nilipomaliza kuanika nguo zote nilitoroka na kutoka nje, safari yangu ililenga dukani kwetu, kule kwenye duka la nguo, maana toka mama alipofariki hakuna alieenda hata kuangalia maendeleo ya duka hilo, na nakumbuka hata mama mara ya mwisho kuchukua pesa ililua ni muda mrefu hata miezi miwili imepita toka achukue pesa kwa ajili ya kwenda kukusanya mzigo mpya, Ni yangu inayonipeleka dukani ni kwamba naenda kuchukua pesa ili nimpeleke dada fatu hospitalini maana sintokosa hata elfu 20..... Nililua nakaribia dukani hapo japo palikua ni mbali kweli maana tulikua tunakujaga na gari yetu lakini kwa leo nimekuja kwa miguu.... Nilikua nahema juu juu kwa kukimbia ili niwahi nyumbani, kwani hata kutembea tena nikawa siwezi tena, ila nilipoona jina la duka letu lipo mbele ya macho yangu ndipo nilipopata nguvu ya kuamka tena.....
MOON VISION CLOTHING SHOP
Hilo ndio jina la duka letu ambalo ni duka kubwa jijini hapa yaani hili ndio duka kubwa kuliko yote jijini hapa, hivyo ni duka lenye maingizo makubwa na watu walioajiriwa hapa walikua ni mwanamke na mwanaume na wananijua vizuri kua mie ni mtoto wa boss wao....
Nilifika mpaka barazani kwa duka hilo nikauangalia ule mlango wa kioo ambao nilikua najiona mie mwenyewe, nikaanza kushukuru mungu na kujipa moyo kua
"dada yangu fatu, natumai sasa umepona maana pesa ndio hio nakwenda kuipata"
Nilikua nikijisemea kimoyo moyo huku nikishika mlango huo wa Alminiamu ulioandikwa kwa neno la PUSH, nilisukuma mlango huo kisha nikaingi, kwanza kitu kilichonishangaza katika duka hilo nguo zilikua zimeisha kabisa, yaani zilizobakia ni chache mno na sio fasheni mpya hata kidogo yaani hakuna hata mzigo mpya,.... Ila kwakua kilichonileta sio ukaguzi wa duka, hivyo nilimuita braza mussa... Yaani mussa ni mmoja kati ya waajiriwa walioajiriwa katika duka hili
"broo mussa"
Niliita kwa kujiamini, maana wananifahamu, na muda huo nilipokua nawaida walikua ndani ndani ya nguo wakiendelea kutolea wateja nguo...
Sasa nikakaa kwenye kiti, wakati huo nguo zangu zilikua zikinuka mno....
Ghafla alikuja huyo mussa niliemuita, Aiseee sikuamini macho yangu kwa watu nilio waona, yaani mussa sio mussa wala batuli sio batuli, Sasa nikiwa naendelea kuwashangaa... Mara huyo jamaa akaniuliza
"sasa wewe umekuja kununua nguoo au umekuja kutuaribia hali ya hewa apa"
Aliongea hivyo huyo jamaa kisha na huyo mwanamke, akacheka huku wakigongesheana mikono....
"He heheeeeeeeee halooooooo, maakubwa,..... Ivi we mtoto kama kusoma hujui hata picha huioni?"
Nilijikuta naanza kutetemekwa na miguu yaani nguvu zote ziliniishia na kudondoka chini.... Lakini sura zinazouza hapa sio mussa wala batuli bali ni sura zingine na nazifahamu vyema kabisa......
Yaani mwili wangu ulilegea tepe tepe kwa kuchoka, kiasi kwamba hata kuona vizuri nilikua sioni kwani nilikua naona giza giza tu mbele yangu, yaani kuzimia sio kuzimia sasa sijui ilikua ni kitu gani, kilichonilegeza, watu wale walimuita mlinzi aliekuepo nje ya duka hilo nikabebwa juu na kwenda kutupwa pembeni sana ya duka hilo, ilikua ni sehemu iliokaribia na dampo, Nilipokuja kuzinduka nilikuta nimezingirwa na watu huku wenye huruma walikua wakinipepea kwa kanga na magazeti, Nilikua nalia tu maana sikua na muokozi yeyote juu yangu, zaidi kujijua mie mwenyewe, nilipoona mida imeenda nilikurupuka na kuwahi kurudi nyumbani huku wale watu wakijiuliza kua, labda walikua wakimseidia kichaa, maana niliamka bila hata ya kusalimia mtu wala kumshukuru mtu, na yote hio ni kuwahi nyumbani ili nisionekane kua nilitoka bila ya kuaga, maana mamkubwa hatakagi nitoke nje maana anahisi labda nitamletea watu wabaya,... Sasa nilipokua nikikimbia nilimuona mtu kama musa
"broo mussa, braza musa"
Aligeuka huku akiniangalia mieCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"broo musa umenisahau nini kaka"
"we sheby we, mbona umechafuka hivi wewe, ayaaa aisee unatoa harufu khaa, nini shida"
"we acha tu kaka angu, maisha hubadirika, huezi amini mie ni mtu wa kuishi maisha ambayo hayajulikani"
"ayaaa, mbona unalia sasa mdogo wangu, hebu kaa chini kwanza unielezee, afu mbona simu ya mama ako sasa hivi haipatikani kwanini"
Yaani aliposema hivyo ndio nikazidi kulia mana anaongea kitu ambacho hakipo katika ulimwengu huu
"sasa unalia nini sharbiny, eee, hebu nyamaza, kwani kuna nini"
"kaka musaa, mama baba walishakufa kitambo tu, tena baba ndio wa kwanza kufa ana miezi 7 sasa toka afariki dunia, na mama nae yapata miezi miwili sasa toka afariki dunia, sasa leo ukiniuliza habari zao nahisi kama unaniliza kaka angu"
"innalilah wa inalilah laajiun, mungu awalaze mahali pema peponi, kumbe umekua yatima mdogo wangu, lakini mimi nilijua tu, maana kuna mwanamke alikua anakujaga nae, mwisho wa siku nilishangaa tunafukuzwa mimi na batuli, afu akaweka watu wengine ambao hata siwajui"
"yule mama ni mamkubwa wangu, na wale alio waweka pale dukani ni watoto wake"
"khaaa sasa mamkubwa wako ndio unaishi hivi"
"kaka mussa bora hata ya hivi kaka angu, nyumbani ndio kwanzaa tunalala stoo"
"mungu wangu, kwanini afanye hivyo lakini"
"we acha tu, na yule dada wa kazi sasa hivi anaumwa taabani hoi hoi, lakini hatoi msaada wowote"
"basi usilie,.... Sasa huku umefata nini"
"nilikuja kule dukani kuchukua angalao pesa ya dawa, nikajua nitawakuta nyie, sasa nimeshangaa kuwakuta jamali na sauda"
"kwaio wale waliokuepo pale ni watoto wa mamkubwa wako kabisaaaa"
"kabisa, yaani mama angu mzazi na huyo mamkubwa ni ndugu wa baba mmoja mama mmoja yaani tena ni wale wa toka ntoke"
"aaaahhhhh kweli dunia imeharibika kwakweli, ila pole sana mdogo wangu, kwani mi mwenyewe ndio hivyo nami nimefukuzwa pale dukani, sina muelekeo wowote, na kama unavyojua bado nipo kwa wazazi wangu, kiukweli sina cha kukuseifia ila chukua hii elfu kumi kamnunulie huyo dada dawa"
"daaaahhh nashkuru sana kaka kwani umeniseidia sana yangu, mungu akubariki upate kazi nyingine kaka"
"usijali sharbiny we wahi kamnunulie dada dawa"
"asante wacha niwahi"
Mtoto wa kiume niliamka, na kukimbia mpaka duka la dawa
"shkamoo"
"maraaba ujambo"
"sijambo, baba nataka dawa"
"unaumwa nini mtoto mzuri"
"sio mimi ni za dada yangu"
"Ahaaa dada yako anaumwa nini"
"anaumwa na tumbo, afu anaharisha, afu anatapika afu anahisi baridi sana"
"oooke hio itakua ni Amueba hio"
"amueba ndio nini"
"hutojua kijana, ila ni ugonjwa unaosababishwa na mchafuko wa tumbo"
"ok, hii hela itatosha dozi yote"
"ndio, tena itabaki chenchi"
"nitadhukuru sana mzee nipatie"
Nilifurahi sana baada kujua ile pesa itatoshea dawa ambazo dada yangu angeweza kumeza na kupona kabisa... Kuanzia hapo moyo wangu ulianza kua mweupe pee, maana kilichokua kikinisumbua nimekipata, mzee yule ama dokta yule ambae ndio alikua akiuza dawa katika duka hilo la dawa, Alinipa chenchi ya shilingi elfu 4 kana kwamba dozi ile ingemtosha vizuri tu tena ni fulu dozi ambayo inemponya kwa kila namna... Mzee yule alipa dawa zile nami nikazipokea kwa heshma kubwa, huku nikitabasamu kwa furaha kubwa mno, Lakini dawa zile hazikua zimefungwa vizuri hivyo nilipozichukua niliziweka mfukoni moja kwa moja,
"we kijana lete tuzifunge kwanza"
"apana mzee vinatosha"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikataa kwakua nilikua nina haraka kiasi ambacho nilikua sihitaji kuchelewa kabisa, maana dada fatu yupo hoi hivyo nikichelewa huenda nikampoteza dada yangu mpendwa, wakati huo nilikua nikikimbia kwa nguvu zangu zote ili niziwahishe dawa hizo ili dada fatu apate kupona,... Mungu si asumani kweli nilifika nyumbani nikajiweka sawa hapo nje ya geti kisha nikafungua geti na kuingia ndani, ambapo nilikutana na mamkubwa uso kwa uso
"we mbwa unatoka wapi"
"ni.. Ni.. Ni... Nilienda... Nanii"
"na huko mfukoni umeweka nini?"
"hamna kitu"
"hebu nione"
"amna mamkubwa"
"unabishana na mimi"
Ilibidi tu niseme ukweli juu ya hilo ili asije akanielewa vibaya maana maisha yenyewe ndio haya, nilimuambia kua
"nimebeba dawa"
"hebu sasa nizione"
Nilimpa zile dawa huku nikiwa nimeshika kichwa maana mamkubwa havimbangi anaweza kuzichukua yeye....
"pesa ya kununulia hizi dawa umetoa wapi"
Aliuliza hilo swali lakini kwangu lilikosa majibu sahihi maana nisingejua jinsi ya kujitetea juu ya hilo, maana nikisema nimepewa itakua tabu, na kuniuliza kua labda nimekua omba omba,,
"niliioka juzi"
"wewe pumbavu zako unaniibia pesa huku ndani"
"apana mamkubwa mi sikuiba kitu"
Mara simu ya mamkubwa iliita, nikawa naomba mungu anipe tu zile dawa, lakini sasa simu aliokuaakiongea nayo ilionekana kumshitua sana mamkubwa, alipomaliza kuongea na ile simu, alinigeukia mie,
"we pumbavu nani kakuambia uende dukani"
"nisamee mamkubwa, nilikua nimeenda kutafuta ela ya dawa tu"
"we mshenzi wewe"
Alinifata na kunifinya masikio huku akinibukua kwa vibao vya mgongo, sikua nalia kwa maumivu ya vibao au kufinywa bali nilikua nalia kwa kuonewa pasipokua na kosa,
"sasa kwa taarifa yako hizi dawa huzipati afu heheheh hebu lete na hio pesa"
Aliiona ile elfu 4 iliorudi dukani kama chenchi,
"lakini mamk"
Nilikula kibao cha uso kisha akaichukua ile pesa, Nilijua anakwenda ndani lakini cha ajabu na cha kushangaza nilimuona mamkubwa akifunua chemba ya choo na kuzitumbukiza zile dawa zote katika shimo lile... Nilianza kuhuzunika na kulia kama kichaa nilikua nagala gala chini huku nikilia kwa sauti, kana kwamba kuna kitu cha muimu sana kwangu kimepotea,... Mara akina jamali na sauda waliingia, maana ilikua ni jioni mida ya kurudi shule.
"mama analia nini uyu mshenzi"
Alikua ni jamali ndio aliuliza swali hilo,
"mbwa sana huyu, kazi kuniibia pesa huku ndani afu anakwenda kununulia taka taka"
"afu umemuuliza kwanini alikuja kule dukani"
"mtoto mshenzi sana, nimemuuliza lakini hana la kusema pumbavu mkubwa shetani hili"
"ebu toka apa tutolee kelele sisi"
"kwanza kazi hajamaliza afu kakimbia, yaani na leo jioni hamuli"
Kiukweli tulikua tukiteseka sana na maisha haya, tena tulikua tukinyanyasika zaidi ya kunyanyasika, Basi nilinyanyuka maeneo yale na kuelekea zangu stoo ambako ndio chumba chetu kilipo.... Nilifika kisha nikakaa pembeni ya dada yangu huku nikiwa nimejikunja, kwa baridi, dada fatu alikua yupo macho kwani hata kuongea alikua hawezi kabisa,...
"yaani dada fatu, nilienda dukani kwetu, lakini huezi amini eti wanaofanya kazi humo ni hawa hawa akina jamali"
"E, e, e, e.... E,... Eti nini"
"ndio ivo, afu nikakutana na mussa nikamuelezea maisha yetu, akanipa elfu 10 nikaenda kununua dawa"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sa..... sa... Sasa... Sasa zikuapi hizo dawa"
"mamkubwa kazichukua na kuzitupia chooni"
"kwanini usi... Usi... Usiiii.. Usiziweke mfu... Mfukoni sheby"
"dada fatu, dawa niliziweka mfuko huu wa kulia..... Aaaaahh aisee afadhali kuna vidonge vimedokea huku"
Nilipokua natoa mfano hai, niliingiza mkono mfukoni nikashangaa kukuta vidonge vya dawa ambavyo vilidondokea kwenye mfuko, kana kwamba kumbe kule kukataa dawa zisifungwe vizuri ili zisidondoke ziliniseidia, kana kwamba dawa zilidondoka baadhi katika mfuko... Kiafya dawa ikipatwa na ubaridi hua haifai lakini kwa hali yetu ilivyo mbaya na ya kunyanyasika, nilimpa hivyo hivyo hata kama hazifai,....
BAADA YA MASAA MAWILI KUPITA
Dada fatu alipata nguvu kutokana na zile dawa, hivyo tulikua tukiongea maongezi ya hapa na pale kuusu maisha yetu,
"Enhee ulisema mamkubwa katumbukiza dawa chooni"
"ndio, tena kuna chenchi ilibakia nayo kaichukua"
"jamani mwanamke ana dhambi huyu"
"we acha tu, maana hata vibao nilikula, yani mpaka sasa hivi naskia maumivu tu"
"jamani, pole sheby... Ila umekula"
"nimekula wapi, toka asubuhi sijala, yaani hapa nataka nivizie hata masafria tule ukoko"
"jamani, na mimi sina hata shilingi, pesa zangu zote alishazichukua yule dada"
"we acha tu, mi mwenyewe sina hata pii"
Basi tulikua tumekaa nikiwa nakumbuka matukio ya nyuma tulipotokea, mara nikakumbuka kitu fulani kikubwa sana... Nikamuambia dada fatu
"dada fatu, unajua kua mimi fara"
"kwanini uwe fara"
"we niambie kweli we ni fara"
"sitaki, we niambie huo ufara wako upo wapi"
"yaani nashangaa tumekalia pesa eti"
"pesaaa"
"ndio"
"pesa gani"
"kadi ya benki si hii hapa"
"kwani hio akaunt, ina hela"
"ndio, tena ina mamilioni ya pesa"
"kweli we ni fara kweli, yaani tunateseka namna hii afu kumbe umekalia pesa tu"
"dada, we ulifikiri kwa maisha haya, nitatoa wapi wazo la kua nina pesa, nilisahau kabisa kabisa yani"
"hebu nenda katoe ununue dawa basi, afu uje na chakula"
"sawa, tena sio ya dawa tu, yaani tutahama kabisa"
"apana tusihame"
"kwanini dada, pesa inatosha na sisi kujenga nyumba yetu"
"sheby, tukihama tutapoteza haki yetu, hii nyumba ni yetu sio yao, kwanini tuhame"
"hebu ngoja nikanunue dawa na chakula kwanza ili tuongee vizuri, maana akaunt hii ina milioni mia 200 tasilimu, hii haiwezi kutuhamisha"
"haaaaaaaaa unasema kweli"
"ndiooo"
"hebu nenda kwanza kalete chakula, maana nina njaa"
Basi mtoto wa kiume nilifurahi juu ya hilo maana nilikumbuka akaunt ya wazazi wangu ilikua ina kiasi kikubwa sana cha pesa, Sasa nikawa natoka nje kwa furaha za hapa na pale, maana akaunt ina milioni mia mbili na ushenzi,
Sasa ile nataka tu kugungua geti mara mamkubwa kaniona
"wewe, unaenda wapi"
"nana, naulizia stili waya ya kuoshea vyombo"
"stili waya si zipo ndani we mtoto... Hebu njoo apa"
Mara yule mtoto wake nae akaja huku akiniangalia kwa umakini nikaificha ile kadi, maana nilikua nimeishika mkononi..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"afu mama, mbona kama alikua kashika kadi ya benki"
"kadi ya benki"
"ndio, na nilimuona alipokua anakuja"
Mamkubwa alizidi kukasirika na kukunja sura huku yule jamali akija...
"we hebu lete hicho ulichoshika mwanzo"
"amna ni kibati tu broo"
"heeebu tuone"
Mara mamkubwa akasema...
"mnyang'anye, mschiuuuu ana uwezo wa kuvimiliki huyo"
"hataki"
"we mbwa, nitawafukuza nyumbani kwangu mambwa nyie, hebu toa hicho ulificha upesi"
Yule jamaa kuona sitaki kukitoa, Alinikata bonge la kibao, sijakaa vizuri nikapigwa bonge la mtama nikadondoka chini na kuumia mkono, huku mbavu pia zikiniuma,
"achia fara wewe"
Siwezi kuamini yule jamaa aliweza kutoa ile kadi na akaichukua,
"ndio mama,.. ni yenyewe tena ni orijino kabisa"
"vip ina pesa"
"sijajua, maana ni mpaka twende benki"
"hebu nenda basi kaiangalie, au muulize ina shing ngapi"
Yule jamaa kabla hajaniuliza, alinizibua bonge la teke kisha akaniuliza
"we fara sema, hii Acount ina shing ngapi"
"mi sijui"
"ahaaa hutaki kusema ee"
"au kama hataki nenda kaiangalie mwenyewe"
"mama, kwenda sio tatizo"
"sasa kama sio tatizo unasubiri nini"
"paswadi, au namba za siri za hii Acount ndio muhimu kuliko chochote kile"
"paswadi? Paswadi ndio nini"
Mamkubwa yeye alikua ni mshamba ila watoto wake wanajua hilo swala maana wamemaliza kidato cha nne na inaonekana wanajua jua kidogo mambo ya mjini....
"mama, bila hizo siri namba zinazotakiwa hapa, hatuwezi kutoa wala kujua kilichopo ndani"
"namba si hizo hapo juu ya hio kadi"
"hapana mama, hii ni Acount number, ni kama namba ya kitambulisho tu, ila kuna hiozo zingine hazijaandikwa hapa"
"bwana wewe jamali unachelewa bwana we nenda utazipata huko huko"
"nitazipata kwa nani mama, na huyu huyu ndio anazijua huyu"
"nini?"
"ndio, huyu ndio anazijua peke yake, na hii kadi inaonekana wazi ina pesa maana ina jina la baba ake"
"haaaaaaaa, pumbavu sana hebu mwambie akupe hizo namba za siri"
Yaani niliona kama maisha yangu ndio yanakwenda kupotea maana hizo pesa zilizokuepo benki ni nyingi na ndio nazitegemea katika maisha yangu....
"we mbwa hebu taja hizo namba zinazotakiwa haraka, nisije kukuchapa saa hizi"
Nilipoangalia stoo kwa mbaali, nilimuona dada fatu anatikisa kichwa kuashiria nisikubali kuzitaja hizo namba za siri, Lakini walikua wananipiga ili tu nitaje lakini dada ananikazania nisiseme.... Na mimi nia yangu ni kusema kana kwamba labda mamkubwa atatupenda zaidi baada ya kuzipata hizo pesa.....
"hebu sema hizo namba... Ni ngapi ngapi?"
"Ni.... Ni... Ni... Ni... Nii
Nilikua nina uhakika wa kuitaja, maana naifahamu mno, na haiwezi kusahaulika kirahisi rahisi.... Ila jamali alikua akinilazimisha niitaje hio namba ambayo ingeweza kutoa pesa katika akaunt hio, hivyo mie ndio niliokua nikisubiriwa nitaje hizo namba za siri za hio ATM CARD ila kutokana na dada fatu jinsi anavyokataa, nikaona nami pia haina haja ya kuitaja, mana kama dada yangu alikua hataki kana kwamba haifai.....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"hebu sema hizo namba.. Ni ngapi ngapi? "
"Ni... Ni.. Ni... Ni.. Ni.. Nimeisahau kaka"
Nilitaamka hivyo huku nikilia, Lakini kilichoseidia ni kwamba mamkubwa alikua hajui kuusiana na hivi vitu hivyo akamfosi mwanae aachane na mie ili awahi benki huenda akapata ufumbuzi, hivyo jamali aliniacha kwa shinikizo la mama ake, maana mamkubwa hajui kua bila hio siri namba hawezi kutoa wala kujua pesa ilipo ndani, na akilazimisha kadi itamezwa na mashine mwisho waanze maswali mengi,..... Basi sikua na ujanja tena zaidi ya kurudi zangu stoo huku tukiwa tuna njaa kali ambayo hata sitegemei kula muda huu....
"sheby, mdogo wangu, kwanini usingeificha ile kadi"
"dada, mi naomba nikuulize, hivi ajali inazuilika"
"sawa, lakini bado una makosa sheby, hebu ona mi naumwa sina hata dawa, kula yenyewe hatujala toka asubuhi"
Dada fatu alikua akilalama sana, ila ukweli ni kwamba haikua na jinsi zaidi ya kutulia tu
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment